kauli ya wadau kuhusu - ansaf...

4
1 Agricultural Non State Actors Forum KAULI YA WADAU KUHUSU MAENDELEO YA SEKTA YA MIFUGO TANZANIA

Upload: others

Post on 10-Jan-2020

39 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: KAULI YA WADAU KUHUSU - ANSAF Tanzaniadev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/10/COMMUNIQUE-SWAHILI.pdf · mkakati wa uchechemuzi wa kisera unaozingatia upekee na fursa za maendeleo

1

Agricultural Non State Actors Forum

KAULI YA WADAU KUHUSU

MAENDELEO YA SEKTA YA MIFUGO

TANZANIA

Page 2: KAULI YA WADAU KUHUSU - ANSAF Tanzaniadev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/10/COMMUNIQUE-SWAHILI.pdf · mkakati wa uchechemuzi wa kisera unaozingatia upekee na fursa za maendeleo

2

KAULI YA WADAU KUHUSU MAENDELEO YA SEKTA YA MIFUGO TANZANIA

Wito wa kuchukua Hatua

Katika kauli hii, wadau waliotia saini (asasi za kiraia, wafugaji, watafiti, watu binafsi, vyama vya wakulima na

wadau wengine) wanatoa wito wa kuchukua hatua pamoja na wanabainisha mapendekezo yaliyomo katika

mkakati wa uchechemuzi wa kisera unaozingatia upekee na fursa za maendeleo zilizomo katika sekta ya

mifugo nchini Tanzania.

Muhtasari

Sekta ya mifugo ni mhimili wa ukuaji wa uchumi nchini Tanzania ambako asilimia 50 ya kaya hutegemea aina

fulani ya mifugo kama chanzo cha sehemu au kipato chao chote.1

Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo barani Afrika baada ya Ethiopia na Sudan, Wakati

bidhaa mbalimbali za mifugo—kama vile maziwa, nyama, kuku, mayai na bidhaa za Ngozi—huzalishwa

Tanzania, bado nchi hii inategemea uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ili kukidhi ongezeko la mahitaji yake.

Leo hii, sekta ya mifugo inahitaji kupewa msukumo mkubwa kuliko wakati mwingine wowote ili sekta iweze

kuwa kichocheo cha ukuaji wa maendeleo jumuishi nchini.

Sekta ya mifugo inaonekana kuchangia kufikia Dira ya Maendeleo Tanzania ya mwaka 2025. Uchambuzi

uliofanywa hivi karibuni umeonesha kuwa sekta hii huchangia kati ya asilimia 7.4 hadi asilimia 10 ya pato la

taifa2, japokuwa bajeti inayotengwa kwa ajili ya maendeleo ya sekta hii imebakia kuwa ndogo na kuendelea

kushuka hadi kufikia TZS 10.6 bilioni kwa mwaka wa fedha 2016/17. 3 Sekta ya mifugo inakua na kubadilika

kwa haraka sana wakati huo huo mahitaji ya chakula na malighafi yatokanayo na mifugo ikiongezeka mara

dufu kunakochangiwa na ongezeko la idadi ya watu wa kipato cha kati pamoja na ukuaji wa miji. Uwezo na

mchango wa sekta ya mifugo katika kufikia malengo ya maendeleo ni kiashiria cha fursa ya kipekee katika

kuleta mabadiliko makubwa.

1 Ministry of Livestock and Fisheries “Smallholder Livestock Sector: A review based on the 2012/13 National Panel Survey, February 2016: http://www.mifugouvuvi.go.tz/wp-2 Ministry of Livestock and Fisheries “The State of Livestock Development in Tanzania: Evidence from the 2012/13 National Panel Survey” presentation. May 2015 TLMI Workshop3 ANSAFs analysis of the Ministry of Agriculture Food Security and Cooperatives’ (MAFSC) budget and the 2015/16 and 2016/17 livestock development budgets

Printed by iprint Ltd

Photos used byGoogle and Shutterstock

Page 3: KAULI YA WADAU KUHUSU - ANSAF Tanzaniadev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/10/COMMUNIQUE-SWAHILI.pdf · mkakati wa uchechemuzi wa kisera unaozingatia upekee na fursa za maendeleo

i

Usuli

Uzalishaji wa mifugo nchini Tanzania, kama ulivyo uzalishaji wa mazao, hufanywa zaidi na wafugaji wadogo na

wachungi wa asili, wengi wao wakiwa wanawake, wanaokumbana na changamoto za upatikanaji wa pembejeo,

huduma za ugani na masoko. Mifugo mara nyingi hutumiwa kama dhamana miongoni mwa mamilioni ya

familia wasioweza kupata huduma rasmi za kifedha pamoja na wanawake wasiomiliki ardhi.

Kwa mara nyingi ni asilimia 20 tu ya wafugaji na wakulima wadogo nchini ndio wanaoweza kupata huduma za

ugani na wachache wanamiliki mifugo walioboreshwa na wanaozalisha kwa tija. 4 Wafugaji wengi huhangaika

na magonjwa yanayozuilika kutokana na kukosa huduma za chanjo zenye viwango ambapo asilimia 50

wanaripotiwa kutofikiwa na huduma za afya ya mifugo. 5Kwa nyongeza, kumekuwa na aina mbali mbali za

sera zinazoleta madhara katika ufanisi wa sekta binafsi kwa namna tofauti tofauti na kwa sekta ya mifugo kwa

ujumla kama vile kodi zinazohusiana na ufugaji, viwanda vidogo vidogo, nishati na miundombinu, uagizwaji

wa vifaa vya uzalishaji na vifungashio.

6Uzalishaji mdogo usio wa kawaida huenda ukaathiri mahitaji ya vyakula vitokanazo na mazao ya mifugo

pamoja na maligafi yake nchini, na ukweli ni kwamba mifugo ina mchango muhimu sana katika kipato na

maisha ya familia maskini.

Sekta ya mifugo Tanzania ina nafasi kubwa katika kukuza ukuaji wa uchumi lakini kuna haja kubwa ya serikali

kuongeza uwekezaji wake pamoja na kutengeneza mazingira wezeshi kwa wafugaji wadogo na wale wa asili

kulifikia lengo hili.

Mapendekezo

Mapendekezo yaliyopo hapa chini kwa pamoja yamefanywa na kikundi cha wadau wa mifugo ikijumuisha

Asasi za Kiraia, Wafugaji, watafiti, watu binafsi, vyama vya wakulima na wadau wengine waliohudhuria mkutano

uliowezeshwa na Jukwaa huru la Wadau wa Kilimo(ANSAF) na TrustAfrica, iliyofanyika mjini Dodoma mnamo

tarehe 21 Febuari 2017.

Mapendekezo haya hutoa mfumo wa kushirikisha wakulima wadogo na wafugaji wa asili katika sekta ya

mifugo kuinua mchango wao katika kuinua uchumi wa Tanzania.

Kuutambua kwa mapana mchango mkubwa wa mifugo kwa uchumi wa taifa na hivyo kutafsiriwa katika

ongezeko la uwekezaji wa serikali na sekta binafsi kuisaidia sekta hii. Kuwekeza kwa wazalishaji wadogo

inaweza kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta ya mifugo na kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi, uhakika wa chakula

na lishe nchini, kukidhi mahitaji ya vyakula vya asili ya mifugo yanayoongezeka na kupunguza umaskini.

Mwonekano wa kimkakati wenye kujali mchango wa sekta ya mifugo katika uchumi wa Tanzania na Jumuiya

ya Afrika Mashariki lazima uwe kivutio cha kuongezeka kwa uwekezaji wa rasilimali za serikali na za sekta

binafsi pamoja na utengenezaji wa sera na mikakati za kuwezesha kuwaunganisha wote pamoja.

Kuongeza ushiriki wa wadau wasio wa serikali katika kutambua na kuunda sera za mifugo rafiki kwa wakulima

wadogo na wafugaji wa asili chini. Inafahamika dhahiri kuwa uboreshaji wa mifugo, huduma za afya na

mikakati ya malisho pamoja na upatikanaji wa huduma za ugani na masoko husaidia kuwezesha wakulima 4 Ministry of Livestock and Fisheries “Smallholder Livestock Sector: A review based on the 2012/13 National Panel Survey, February 2016: http://www.mifugouvuvi.go.tz/wp-content/

uploads/2016/04/1_MALF_Tanzania_smallholder_livestock_sector_Report.pdf5 Ministry of Livestock and Fisheries “Smallholder Livestock Sector: A review based on the 2012/13 National Panel Survey, February 2016: http://www.mifugouvuvi.go.tz/wp-content/up-

loads/2016/04/1_MALF_Tanzania_smallholder_livestock_sector_Report.pdf6 ANSAF, “Final Budget Analysis 2015-2016

Page 4: KAULI YA WADAU KUHUSU - ANSAF Tanzaniadev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/10/COMMUNIQUE-SWAHILI.pdf · mkakati wa uchechemuzi wa kisera unaozingatia upekee na fursa za maendeleo

ii

wadogo na wafugaji wa asili kuongeza uzalishaji kukidhi ongezeko la mahitaji ya bidhaa za mifugo. 7 Vivyo

hivyo, kupunguzwa kwa gharama sizizo za lazima katika mnyororo wa thamani ina manufaa kwa wakulima

wadogo na wafugaji wa asili katika kuwasaidia kukidhi ongezeko la mahitaji kupitia uzalishaji wa ndani. Kupitia

mjadala mpana na ushirikiano kati ya asasi za kiraia, serikali, sekta binafsi na wadau wengine huwezesha zaidi

taarifa za kuimarisha uthibiti wa kimazingira kwa wakulima wadogo na wafugaji wa asili kujumuishwa katika

kukuza mnyororo wa thamani na viwanda na muunganiko imara.

Ushiriki wa Wanawake na Vijana katika Mnyroro wa thamani wa mifugoWakati wanawake ni wadau wakuu katika

uzalishaji wa maziwa na kuku8, sera za mifugo hazielezi dhahiri ni kwa jinsi gani wanawake wanawezeshwa

kushiriki kiufanisi katika sekta hii. Pia, sekta ya mifugo inatoa fursa nyingi za ajira kwa vijana wajasiriamali lakini

bado hazijatumika ipasavyo. Ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika mnyororo wa thamani wa mifugo

hautaishia kuboresha maisha yao tu, bali pia utachangia kufikia malengo ya taifa ya uhakika wa chakula na

lishe bora.

Kuhakikisha uwajibikaji wa uwekezaji wa sekta binafsi katika kutekeleza ushirikishwaji wa wafugaji wadogo na

wafugaji wa asili kuhusu fursa za maendeleo katika sekta ya mifugo. Wakati sekta binafsi inaongeza uwekezaji

katika kukuza uzalishaji wa sekta ya mifugo na uwekezaji mwingine muhimu, kuna ulazima wa kuendelea

kutetea maendeleo jumuishi katika sekta ya mifugo kama vile zile zilizo chini ya Mpango wa Kuendeleza

Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania(SAGCOT) na ule Mkakati Madhubuti wa Maendeleo ya Mifugo (TLMP).

Mipango hii lazima ilete manufaa ya pamoja kwa wakulima wadogo na kwa wafugaji pia. Uzalishaji endelevu

ulio wazi ni sehemu muhimu katika kufikia uwajibikaji wa kimaendeleo wa sekta binafsi kwa sekta ya mifugo.

Waraka huu umepitishwa na makundi pamoja na watu binafsi wanaounda mtandao wa uchechemuzi unaojali

kanuni mbali mbali za kisera ili kuleta ushirikishwaji na uwazi wa mabadiliko katika sekta ya mifugo.

7 Ministry of Livestock and Fisheries “The State of Livestock Development in Tanzania: Evidence from the 2012/13 National Panel Survey” presentation. May 2015 TLMI Workshop8 Ministry of Livestock and Fisheries “The State of Livestock Development in Tanzania: Evidence from the 2012/13 National Panel Survey” presentation. May 2015 TLMI Workshop