msaada wa matibabu kwa wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/kansas rma user...

12
Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi MWONGOZO WA KUTUMIA Imeanza kutumika tar. 1 Machi 2018 ® Kampuni ya Unified Administrators, LLC KANSAS

Upload: phambao

Post on 29-Aug-2019

232 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi

MWONGOZO WA KUTUMIA Imeanza kutumika tar. 1 Machi 2018

®

Kampuni ya Unified Administrators, LLC

KANSAS

Page 2: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

Utangulizi

Kwa zaidi ya miaka 100 Kamati ya Marekani kwa Wakimbizi na Wahamiaji (USCRI)

imeendeleza haki na maisha ya watu ambao wamehama kwa kulazimishwa au kwa

hiari. USCRI hutoa fursa kwa wakimbizi na watu wengine ili kufikia yote wawezayo

nchini Marekani. Ustawi wa kimwili na kiakili, na vilevile upatikanaji wa huduma za

matibabu, ni muhimu kwa mafanikio katika maisha nchini Marekani. USCRI ina

mpango wa Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi (RMA) kwa wageni ambao kwa

sababu ya hali yao ya uhamiaji hawastahili katika mipango mingine ya Medicaid. RMA

inajumuisha manufaa ya matibabu, tiba ya meno na dawa sawa na Medicaid.

Mwongozi huu unakupa maelezo ya jinsi ya kupata manufaa ya mpango wa RMA.

Manufaa ya RMA yanatolewa na Watoa Bima wa Point Comfort, Inc. (PCU).

Page 3: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi

Je, ninastahili kupata Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi (RMA)? Ili kujua kama unastahili RMA unapaswa kukamilisha kutuma ombi kwa RMA. Msimamizi wa shauri katika shirika linalowapa wakimbizi makazi mapya mahali ulipo anaweza akakusaidia kutuma ombi. Kwa ujumla, ikiwa utatimiza masharti haya basi unastahili:

1. Hali yako ya uhamiaji ni mkimbizi au hali nyingine inayoruhusiwa.

2. Unakidhi mahitaji ya utambulisho wa hali ya uhamiaji.

3. Unatimiza masharti ya mapato.

4. Huna hadhi ya kujiunga na mpango wa Medicaid, Mpango wa Bima ya Watoto au bima nyingine yoyote ya umma au ya binafsi.

Je, naweza kusimamiwa kwa muda upi chini ya RMA? Manufaa yako ya RMA yanamalizika moja kwa moja miezi 8 baada ya kufika Marekani, isipokuwa kama wewe ni mkimbizi wa umri mdogo asiyeandamana na yeyote (URM). Ikiwa wewe ni URM, unaweza kupokea manufaa ya RMA mpaka utakapofika umri wa miaka 23. Zungumza na msimamizi wa shauri lako katika shirika linalowapa wakimbizi makazi mapya mahali ulipo ili akupe maelezo zaidi kuhusu hali yako.

Kumbuka kwamba ikiwa utaondoka jimbo la Kansas, manufaa yako ya RMA yanamalizika moja kwa moja. Utahitaji kuomba manufaa ya afya katika jimbi lako jipya.

3

Page 4: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

KADI YA KITAMBULISHO YA RMA

Kadi ya Kitambulisho cha RMA ni nini? Watu wote waliojiunga na mpango wa RMA hupokea kadi binafsi za kitambulisho za RMA. Unaweza ukapata kitambulisho chako kutoka kwa wakala wa kuwapa wakimbizi makazi mapya mahali ulipo. Unaweza pia kuomba Kadi yako ya Kitambulisho cha RMA kutoka kwa PCU. Piga tu simu au tuma barua pepe [email protected].

Kadi yako ya kitambulisho cha RMA ina jina lako, namba yako ya utambulisho na maelezo mengine muhimu kuhusu manufaa ya RMA. Ni muhimu kuwasilisha kadi yako ya kitambulisho cha RMA kila wakati unapotaka kupokea huduma. Ikiwa kuna zaidi ya mtu mmoja katika familia yako ambaye amejiunga na RMA, kadi tofauti ya kitambulisho itatolewa kwa kila mtu katika familia. Mtu aliyeandikwa kwenye Kadi ya kitambulisho pekee ndiye anayeweza kutumia kadi. Usiazime wala kumpa mtu mwingine yeyote kadi yako Kitambulisho.

Nitatumiaje kadi yangu ya kitambulisho cha RMA? Unapaswa kuwa na kadi yako ya kitambulisho cha RMA kwa wakati wote. Wasilisha kadi yako kwa daktari wako, hospitali, daktari wa meno au duka la dawa wakati unatafuta huduma. Watoaji huduma watatumia kadi hii ya kitambulisho ili kuthibitisha ustahili wako kupokea manufaa ya RMA na kupata

maelezo muhimu kuhusu ni nani atakayelipia huduma zilizotolewa kwako. Kukosa kuwasilisha kadi yako ya kitambulisho kwa watoa huduma husababisha ucheleweshaji wa kulipa madai na uwezekano wa kupoteza manufaa.

Nini kitatokea ikiwa nitapoteza Kadi ya Kitambulisho cha RMA? Unaweza kupata kadi nyingine ya kitambulisho kutoka PCU. Wasiliana na PCU katika [email protected]. Unaweza kutakiwa utoe maelezo ya binafsi ili PCU iweze kuthibitisha utambulisho wako kabla ya kukupa kadi nyingine ya kitambulisho.

Ikiwa kuna mabadiliko katika maelezo ya binafsi kama vile anwani yako ya nyumbani, namba ya simu au anwani ya barua pepe, hakikisha umeifahamisha PCU kupitia [email protected]. Hakikisha kwamba PCU ina anwani yako ya barua pepe unayotumia kila wakati.

4

Page 5: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

5

HUDUMA ZA AFYA

Ni watoa huduma gani ninaweza kuwatumia? Unaweza kutumia mtoa huduma yeyote ambaye anakubali malipo kulingana na viwango vya malipo vilivyoidhinishwa kwa ajili ya mpango wa RMA. Unaweza kupata orodha ya watoa huduma ambao wanakubali viwango hivi kwenye rma.pointcomfort.com, au kupiga simu kwa PCU ili upate usaidizi. Ikiwa unataka kutumia mtoa huduma ambaye hayupo kwenye orodha hii, unatakiwa kufanya haya:

1. Pata jina kamili, anwani na namba ya simu ya mtoa huduma unayotaka kutumia.

2. Wasilisha maelezo haya kwa PCU.

PCU itawasiliana na mtoa huduma na kujaribu kufikia makubaliano ya kutoa huduma kwa viwango vya malipo vilivyoidhinishwa. PCU itakujulisha matokeo ya majadiliano haya.

Kumbuka, unapaswa kwenda kwenye Chumba cha

Dharura kilicho karibu wakati wa dharura.

Ni huduma gani za afya zinatolewa? RMA inatoa huduma za afya wakati huduma hizo zinahitajika kimatibabu na chini ya viwango fulani. Baadhi ya huduma zinazotolewa ni zifuatazo:

HUDUMA ZA HOSPITALI • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na

huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au wadi

• Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika Chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu

• Utumiaji wa vyumba vya upasuaji, matibabu na kupata nafuu

• Mavazi, mishono ya jeraha na vifaa vingine vinavyotolewa mara kwa mara kwa wagonjwa waliolazwa

• Matibabu ya Chumba cha Dharura (lazima iwe dharura)

• Dawa unazoandikiwa ukiwa umelazwa

• Huduma za rediolojia, maabara, na mawimbi ya sauti

• Tiba ya kimwili, tiba ya mazoezi na tiba ya usemi wakati wa mgonjwa amelazwa

• Huduma za kitaaluma, ikiwa ni pamoja na madaktari

HUDUMA ZA KUTIBIWA NA KUONDOKA

HOSPITALINI/UPASUAJI NA KUONDOKA • Huduma za kitaaluma ikiwa ni pamoja na madaktari

• Mavazi, mishono ya jeraha na vifaa vingine vinavyotolewa mara kwa mara kwa wagonjwa wasiolazwa

KUTEMBELEA DAKTARI AU KLINIKI • Madaktari na wataalamu

• Tiba ya kimwili, tiba ya mazoezi na tiba

ya usemi

• Wataalamu walioidhinishwa wa Afya ya Tabia / Kiakili

• Huduma za rediolojia, maabara, na mawimbi ya sauti

• Huduma za Urekebishaji wa maungo

HUDUMA NYINGINE ZINAZOTOLEWA • Usafirishaji wa dharura wa ambulensi mahali ulipo

• Vifaa vya matibabu vya kudumu

• Huduma za matibabu nyumbani

• Huduma za faraja

• Matibabu/tiba ya Mionzi

• Tibakemikali

• Usafishaji wa damu

• Oksijeni na gesi nyingine na jinsi zinavyotolewa

• Unusukaputi na jinsi unatolewa

• Ukaguzi 1 wa mara kwa mara na jozi 1 ya miwani

• Huduma za masikio ikiwa ni pamoja na kupendekeza, kuweka au kubadili misaada ya kusikia

• Huduma za ukalimani hutolewa na daktari anayetoa matibabu

Page 6: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

Ni huduma gani za afya hazitolewi? • Gharama za ujauzito na watoto wachanga

• Vifaa binafsi vya kukufaa

• Ushauri kupitia simu au kushindwa kuzingatia mkutano uliowekwa rasmi

• Mabadiliko yoyote ya kimwili yanayofanywa ili kuboresha ustawi wa kisaikolojia, wa kiakili au wa kihisia

• Mipango ya mazoezi, ikiwa imependekezwa au haijapendekezwa na daktari

• Upasuaji wa kubadilisha mwonekano au wa mapambo

• Matibabu ya utasa, kukosa nguvu ya kujamiiana au matatizo yoyote ya ngono

• Huduma au vifaa ambavyo ni kwa ajili ya uchunguzi, majaribio au madhumuni ya utafiti

• Upasuaji wa macho ili kurekebisha kuona karibu, kuona mbali au dosari katika jicho

• Upimaji wa hali ya mwili, tiba ya burudani, usingizi au muziki

• Huduma au vifaa vinavyotolewa na mtu katika familia yako au mtu yeyote anayeishi na wewe

• Huduma au vifaa vinavyotolewa bila malipo

• Gharama za makao au usafiri

• Matibabu ya kukuza nywele, iwe imependekezwa au isiyopendekezwa na daktari

• Matibabu ili kuzuia kupoteza nywele

• Matibabu ya matatizo ya usingizi

• Huduma au zana zozote ambazo Si Lazima Kimatibabu

• Huduma ya zana ambazo manufaa au malipo hupatikana chini ya mkataba au sera yoyote

(Kati ya haya ambayo haitolewi haiwahusu watu walio chini ya umri wa miaka 21. Wasiliana na PCU kwa maelezo zaidi.)

6

Page 7: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

DAWA ZA KUANDIKIWA

Ninaweza kutumia duka gani la dawa? Unaweza kupata dawa unazoandikiwa na daktari kupitia mtandao wa maduka ya dawa ya MagellanRx Management. Mtandao huu unajumuisha maduka yote kuu, kama vile Walmart na CVS, na maduka mengi yaliyo karibu nawe. Ni sharti uwasilishe kitambulisho chako kwa mfamasia kila wakati unapotaka dawa uliyoandikiwa. Mfamasia atathibitisha ikiwa wanashiriki kwenye mtandao na ikiwa unastahili mpango wa dawa za kuandikiwa na daktari.

MATIBABU YA MENO

Ninaweza kuhudumiwa na daktari yupi wa meno? Unaweza kuhudumiwa na daktari yeyote wa meno aliye kwenye mtandao wa DenteMax. Unaweza kupata orodha ya watoa huduma wa DenteMax katika www.dentemax.com/findadentist, au piga simu kwa PCU ili upate usaidizi. Ni watoa huduma wa DenteMax pekee ndio wanaruhusiwa kufanya matibabu ya meno chini ya RMA. Unafaa kuwasilisha kadi yako ya kitambulisho kwa mtaalamu wa meno kila wakati unapohitaji huduma za meno.

Ni dawa zipi za kuandikiwa na daktari hazigharimiwi? • Dawa asili ikiwa dawa mbadala zinapatikana

• Dawa yoyote ya kuandikiwa ambayo ina gharama za matibabu ambazo hazijajumuishwa

• Dawa ambazo zinapatikana bila maagizo au bila pendekezo la daktari

• Unaweza kupata dawa za kuandikiwa zisizozidi dozi ya siku 30

Ni huduma gani za meno zinagharimiwa? • Matibabu ya dharura ya meno

yanayohitajika kutatua maumivu au kuzuia maambukizi

• Matibabu ya dharura ya meno kutokana na ajali

• Usafishaji na uchunguzi wa meno

Idhini ya kabla haihitajiki kwa matibabu ya dharura.

Ni huduma gani za meno hazitolewi? Huduma zilizoorodheshwa hapo juu pekee ndizo zinazotolewa.

7

Page 8: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

8

IDHINI YA KABLA

Ni huduma zipi zinahitaji kibali cha kabla? Huduma nyingi zinazotolewa zinapaswa kuwa na idhini ya kabla. Hiyo inamaanisha idhini kutoka kwa PCU inapaswa kupatikana kabla ya matibabu. Yafuatayo yanapaswa kuwa na idhini ya kabla:

• Utunzaji wa wagonjwa waliolazwa

• Upasuaji wowote

• Utunzaji katika kituo cha huduma za ziada

• Huduma za faraja

• Huduma ya matibabu ya nyumbani

• Huduma za urekebishaji wa maungo

• Tiba ya kimwili

• Tiba ya mazoezi

• Tiba ya usemi

• Upimaji wa mizio

• Vifaa vya matibabu vya kudumu

• Utunzaji wa afya ya kiakili/tabia

• Viungo bandia

• Vifaa vya viungo bandia

• Eksirei ya Kompyuta (Picha ya CAT)

• Upigaji Picha kwa Nguvu ya Sumaku (MRI)

• Kupandikiza Kiungo/Tishu ya binadamu

Ninawezaje kupata Idhini ya kabla? Mara tu unapogundua kuwa utahitaji huduma ambayo inahitaji idhini ya kabla, wewe au mtoa huduma wako mnapaswa kuwasiliana na PCU kupitia [email protected] au kwa simu. Utahitaji kutoa jina lako, namba ya kitambulisho, jina la mtoa huduma unayetaka kutumia na maelezo ya mawasiliano yake, na maelezo ya matibabu yaliyopangwa. Mara nyingi PCU inaweza kutoa idhini ya kabla ya mara moja; hata hivyo wakati mwingine idhini ya kabla inaweza kuchukua hadi saa 48 ili kukamilisha. Ndiyo maana ni muhimu kuwasiliana na PCU mara tu unapogundua kwamba unahitaji matibabu.

Idhini ya kabla haihitajiki kwa matibabu ya dharura; hata hivyo, unapaswa kuhakikisha umepata idhini haraka

iwezekanavyo.

Mara nyingi, mtoa huduma wako atatangulia kuitisha idhini ya kabla kwa ajili yako. Atahitaji maelezo yaliyomo katika kadi yako ya kitambulisho cha RMA.

Watoa huduma wanaweza kuwasilisha maombi ya idhini ya kabla kwa PCU kwenye pcf.pointcomfort.com.

Unatakiwa kuwasilisha kadi yako ya kitambulisho ch

RMA kila wakati unapotafuta huduma.

Itakuwaje nikitibiwa bila kupata idhini ya kabla? Ukitibiwa matibabu ambayo yanahitaji idhini ya kabla na ukose kupata idhini ya kabla, basi utagharimia huduma hiyo.

Page 9: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

9

KUKATA RUFAA

Itakuwaje ikiwa sitakubaliana na uamuzi kuhusu Idhini ya kabla au uamuzi wa madai? Unapaswa kuanza mara moja mchakato wa Rufaa kwa kufuata hatua hizi:

1. Piga simu au uandike kwa PCU na utoe maelezo kamili ya rufaa yako ndani ya siku 30 tangu tarehe ulipopokea taarifa kuhusu idhini ya kabla au uamuzi wa madai. Sharti ujumuishe majina na maelezo ya mawasiliano ya watoa huduma wote waliohusika katika matibabu yako.

2. Ndani ya siku 10 za kazi, PCU itakutumia jibu la kupokea rufaa na muda unaokadiriwa ili kukamilisha uchunguzi wowote unaohitajika.

3. Ndani ya siku 30, PCU itakupa jibu lililoandikwa lililo na maelezo kuhusu hali ya rufaa yako.

FARAGHA

Kila wakati unapotibiwa, daktari wako huandika kilichofanyika na kuiweka kwenye faili yako. Faili hii huwekwa faraghani. Daktari wako anaweza kuwapa watu wengine faili hiyo ikiwa utakubali.

PCU inatakiwa iweke kwa faragha taarifa zinazohusu huduma za matibabu unazopokea. PCU inaweza tu kuwapa watu wengine taarifa zako ikiwa utakubali.

Una haki ya kupata nakala za rekodi zako za matibabu kutoka kwa watoa huduma wako na kutoka kwa PCU. Unaweza ukaomba marekebisho yafanywe kwenye rekodi zako ikiwa kuna jambo lisilo sahihi. Unaweza ukatakiwa kumlipa mtoa huduma au PCU ada za kunakili rekodi unazotaka.

Page 10: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

10

Page 11: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

ANWANI ZA HUDUMA ZAKO ZA RMA

Maswali kuhusu ustahili au utoaji wa huduma:

[email protected]

1-844-210-2010

Maswali kuhusu mitandao ya mtoa huduma:

Matibabu ya kawaida na meno

[email protected]

1-844-210-2010 rrp.pointcomfort.com

Dawa za Kuandikiwa na Daktari:

[email protected]

1-800-424-0472

Idhini ya kabla:

[email protected]

1-844-210-2010 rrp.pointcomfort.com

Hali ya Madai:

[email protected]

1-844-210-2010 claims.pointcomfort.com

Kukata Rufaa:

[email protected]

1-844-210-2010

MASHIRIKA YA KUWAPA WAKIMBIZI MAKAZI MAPYA

Mashirika ya kuwapa wakimbizi makazi mapya:

Catholic Charities of Northeast Kansas

2220 Central Avenue

Kansas City, KS 66102

(913) 906-8937

International Rescue Committee – Wichita

1530 S. Oliver Street, Suite #270

Wichita, KS 67218

(316) 351-5495

Episcopal Migration Ministries 401

N. Emporia Avenue Wichita, KS

67202

(316) 977-9276

International Rescue Committee –

Garden City

1503 East Fulton Terrace

Garden City, KS 67846

(316) 805-6310

11

Page 12: Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi - rma.pointcomfort.comrma.pointcomfort.com/files/Kansas RMA User Guide Swahili.pdf · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi

®

Kampuni ya Unified Administrators, LLC