the upper roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60daysprayer-swahili.pdf · mshumaa mweupe wa...

72
Kwa Kongamano Kuu 2016 The Upper Room za Selected from The Upper Room Disciplines with Invited Writers

Upload: others

Post on 14-Jan-2020

39 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Kwa Kongamano Kuu 2016

The Upper Room

za

Selected from The Upper Room Discip l ines with Invited Writers

Page 2: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

SIKU 60 ZA SALA

Kwa Kongamano Kuu 2016© 2016 na Upper Room Books®. Haki zote zimehifadhiwa.

Hakuna sehemu ya kitabu hiki inaweza kutumiwa au kutolewa tena kwa njia yoyote ile bila idhini isipokuwa pale ambapo manukuu mafupi yaliyo katika makala au uhakiki muhimu. Kwa maelezo, andika: Upper Room Books, 1908 Grand Avenue, Nashville, TN 37212.

Upper Room®, Upper Room Books®, na nembo za usanifu ni alama a biashara zinazomilikiwa na The Upper Room®, Nashville, Tennessee. Haki zote zimehifadhiwa.

Tovuti ya Upper Room Books: books.upperroom.org Cover design: Kielelezo cha Left Coast Design, Portland, Oregon Cover: Usanifu wa Tammy Smith

Isipokuwa vinginevyo, manukuu ya maandiko matakatifu yanatolewa kwenye Biblia ya New Re- vised Standard Version, hakimiliki © 1989 Baraza la Kitaifa la Makanisa ya Kristo nchini Marekani. Zinatumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa.

Manukuu ya maandiko matakatifu yenye alamaap ni maneno mengine ya mwandishi.

Manukuu ya maandiko matakatifu yenye alama (GNT) yanatoka Good News Translation katika Today’s English Version—Toleo la Pili Hakimiliki © 1992 na Ameri- can Bible Society. Zinatumiwa kwa ruhusa.

Manukuu ya maandiko matakatifu yenye alama kjv yametolewa kwenye King James Version.

Manukuu ya maandiko matakatifu kutoka THE MESSAGE. Hakimiliki © na Eugene H. Peterson 1993, 1994, 1995, 1996, 2000, 2001, 2002. Imetumiwa kwa idhini ya NavPress Publishing Group.

The Upper Room inatoa idhini ya kutafsiri kijitabu katika lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya watu katika nchi nyinginezo.

Chapisho ISBN: 978-0-8358-1560-4Mobi ISBN: 978-0-8358-1558-1Epub ISBN: 978-0-8358-1559-8

Taaluma za The Upper RoomKatika kitabu hiki maarufu cha ibada, waandishi 53 kutoka asili, lugha, na tamaduni mbalimbali za Wakristo wanapima vina vya andiko takatifu. Kila wiki ina mada mpya kulingana na vifungu vya andiko takatifu vilivyoteuliwa kutoka Revised Com- mon Lectionary.

Ili kuagiza Taaluma za The Upper Room, wasiliana na huduma kwa wateja kwa nambari 1-800-972-0433

This translation is provided by GCFA (General Council on Finance and Administration)

Page 3: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

3

M HUTASARI WA MATUMIZI YA-KIKUNDI KIDOGO

Huu hapa ni mpango rahisi wa mikutano ya kikundi kulingana na kusoma ibada hizi. Mtu mmoja anaweza kuigiza kama mshirikishi au jukumu linawe-za kuzungushwa miongoni mwa wanachama wa kikundi. Unaweza kuwasha mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja.

UFUNGUZI

Mshirikishi: Tuje katika uwepo wa Mungu.Wengine: Bwana Yesu Kristo, asante kwa kuwa nasi. Tusaidie kusikia neno lako kwetu tunapozunguma pamoja.

ANDIKO

Mshirikishi anasoma andiko lililopendekezwa kwa siku hiyo. Baada ya kimya cha dakika moja au mbili, mshirikishi anauliza: Ulimsikia Mungu akisema nini katika kifungu hiki? Mwito huu unahitaji jibu gan? (Wanachama wanajibu kwa zamu ama wanavyoongozwa.)

TAFAKARI

• Ni kifungu kipi cha andiko na tafakari kilikuwa na umuhimu kwako? Kwa nini? (Wanachama wanajibu kwa zamu ama wanavyoongozwa.)

• Ni hatua zipi ulizochochewa kuchukua kwa mujibu wa tafakari? (Wana-chama wanajibu kwa zamu ama wanavyoongozwa.)

• Ni wapi ulipopata changamoto katika ufuasi wako? Ni vipi ulivyok-abiliana na changamoto? (Wanachama wanajibu kwa zamu ama wana-vyoongozwa.)

KSALI PAMOJA

Mshirikishi anasema: Kulingana na majadiliano ya leo, ni watu na hali gani unataka tuombee kwa sasa na wiki ijayo? Kisha mshirikishi au mtu mwengine wa kujitolea anaombea masuala yaliyotajwa.

KONDOKA

Mshirikishi anasema: Tuende kwa amani kumtumikia Mungu na jirani zetu katika mambo yote tunayoyafanya.

Imetolewa kwenye mwongozo wa ibada ya kila siku The Upper Room, Januari–Februari 2001. © 2000 The Upper Room. Zinatumiwa kwa ruhusa.

Page 4: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Bwana,leo nipe mbingu mpya na dunia mpya.Nipe ajabu la mtoto ambaye kwa mara ya kwanza anafumbua macho yake ulimwenguni; furaha ya mtoto anayetambuaFahari yako katika kila kitu, katika kila kiumbe anachokumbana nacho, uhalisia wa utukufu Wako.

Nipe furaha ya yule ambaye hatua zake ni mpya.Nipe furaha ya yule ambaye maisha yake ni kila siku mpya na isiyo na hatia na yenye tumaini, kila siku yenye msamaha.

—Michel Bouttier, katika Sala za Kijiji Changu

Sala za Kijiji Changu na Michel Bouttier. Imetafsiriwa na Lamar Williamson. Hakimiliki © 1994. Ime-tumiwa wa idhini ya Upper Room Books.

Page 5: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

M A U D H U IMUHTASARI WA MATUMIZI YA-KIKUNDI KIDOGO / 3

KARIBU / 7

UTANGULIZI / 8

TAFAKARI KABLA YA KONGAMANO KUU

Tangaza / 10–19

Ongoza / 20–29

Lea / 30–39

Tuma / 40–49

TAFAKARI KABLA YA KONGAMANO KUU

Kama Tulivyoenda / 50, WARNER BROWN

Nenda na Utangaze / 51, GREGORY V. PALMER

Kuenda kwa Mamlaka / 52, CHRISTIAN ALSTED

Unapoenda, Jifunze / 53, SALLY DYCK

Kuenda kwa Ujasiri / 54, SUDA DEVADHAR

Upendo na Upendo Pekee / 55, DEBORAH L. KIESEY

Unapoenda, Waite Wote / 56, CYNTHIA FIERRO HARVEY

Ili Tuwe Kitu Kimoja / 57, MARY ANN SWENSON

Uovu Unaenda Pia / 58, JAMES SWANSON SR.

Nenda kwa Kondoo Aliyepotea / 59, JOHN YAMBASU

Nani Anakwenda Wapi? / 60, ELAINE J. W. STANOVSKY

TAFAKARI BAADA YA KONGAMANO KUU / 61

KTUMIA KIDOLE UTATA KATIKA SALA / 70

Page 6: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika
Page 7: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

7

Karibu

Wpendwa kaka na dada wa familia ya Muungano wa Methodisti, Tuna-fahamu kuwa sala zetu ni muhimu, na kwa uhakika huo, ninawaalika

katika safari ya sala ya siku 60 mnapojiandaa kwa Kongamano Kuu 2016.Viongozi wa kanisa, na wengine walio na haja hivi karibuni wataku-

sanyika huko Portland kusikilizana, kutambua mapenzi ya Mungu kwa Kanisa la Muungano wa Methodisti, na kufanya maamuzi yatakayoongoza Muungano wa Wamethodisti kote ulimwenguni katika kutimiza lengo letu tulilopewa na Mungu. Wakati wewe na wao mnapopanga kufungua moyo na akili zenu kwa uongozi wa Mungu, tafakari hizi zinatoa desturi ya kijamii inayokusudiwa kulea roho wa umoja na ufuasi. Sali kwa uhakika kuwa wengine wanasali sala hiyo.

Tafakari katika kijitabu hiki zinaanza wiki baada ya Pasaka, Alhamisi, Machi 31, na kuendelea hadi Jumapili, Mei 29. Zitakuongoza kwa siku arubaini kabla ya kikao cha ufunguzi, hadi siku kumi na moja za Konga-mano Kuu, na katika siku tisa baada ya tukio kukamilika. Kila tafakari wakati wa Kongamano Kuu, Mei 10–20 (bila kujumuisha Mei 17), imean-dikwa na askofu ambaye atahubiri siku hiyo—hivyo unaweza kukumbana na maarifa kutoka kwa mtangazaji wa Neno la siku hiyo.

Wafanyakazi wa The Upper Room walitoa chapisho hili kwa mwaliko wa Kamati ya Uabudu wa Tume Kuu ya Kongamano Kuu la 2016, na sisi hapa The Upper Room tunayo fahari kuaminiwa kwa kazi hii. Ninasubiri siku zetu sitini za sala pamoja.

—SARAH WILKEMchapishaji, The Upper Room

Page 8: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

8 Siku 60 za Sala

Utangulizi

Kitabu hiki cha Sala ya Siku 60 kinatumika kama jibu la ombi muhimu lililoandikwa katika andiko takatifu, “Bwana, tufunze kusali.” Tunak-

ualika ujiunge na wajumbe, maaskofu, na viongozi wa Kongamano Kuu 2016 katika maandalizi yao ya kiroho kwa tukio, kupitia tukio, na siku za baadaye.

Kila dhehebu la ndani katika kila sehemu ya ulimwengu linaweza kuomba na, na kuombea wajumbe 864 wa Kongamano Kuu. Kwa kutumia Intaneti na maandishi yanayopakulika, kila Muungano wa Methodisti uta-soma andiko takatifu sawa, kuzingatia yaliyomo sawa, na kusali sala sawa kwa siku arubaini kabla ya Kongamano Kuu 2016 huko Portland, Oregon (Machi 31 hadi Mei 9), kila siku ya Kongamano Kuu (Mei 10 hadi 20); na siku tisa kufuatia tukio (Mei 21 hadi 29). Sote tunaweza kushiriki katika hali sawa ya andiko takatifu, neno, na Roho.

Sala ni nguzo muhimu ya maisha na kazi ya Yesu na inasalia muhimu kwetu na kwa kanisa. Sala ilichukua nafasi muhimu katika kazi ambayo Mungu alianza kupitia John na Charles Wesley Uingereza ya karne ya kumi na nane. Huko Amerika ya Kaskazini, maisha ya Philip Otterbein, Jacob Albright, na Martin Boehm yote yanatoa ushahidi wa mafunzo ya John Wesley kuwa “Mungu hafanyi chochote isipokuwa sala.” Vuguvugu la Methodisiti lilipoenea hadi Karibea (1759), Sierra Leone (1792), Australia (1815), Afrika (1816), na Amerika Kusini (miaka ya 1830), sala ilitumika kama chanzo msingi cha mwelekeo na umuhimu wa kiroho. Barani Asia (1783) na Pasifiki (1822), hadithi ni ile ile.

Tunaamini kuwa Mungu anataka kuongoza na kuboresha hatma ya Kanisa la Muungano wa Methodisti kupitia sala. Mwongozo huu wa sala

• utatumika kama mwongozo wa kila siku kwa wajumbe walioteuliwa wa Kongamano Kuu 2016.

• toa njia kwa wale waliopo kwenye Kongamano Kuu kuungana, kuzin-girwa, na kusaidiwa kwa sala.

• shirikisha kila mwanamume, mwanamke, kijana, na mtoto wa Muun-gano wa Methodisti katika sala. Kila familia, kikundi kidogo, na kanisa la ndani kote ulimwenguni linawezsa kuomba na, na kuombea Konga-mano hili Kuu.

• fungua njia mpya kwa ukuaji wa kiroho na imani katika madhehebu

Page 9: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 9

yote, kwa wanachama na marafiki wote—kuungana katika sala kama mwili wa Kristo.

• anzisha mtandao wa sala ndani ya Kanisa la Muungano wa Method-isti ambao unaweza kusaidia maandalizi ya kiroho yanayohitajika kabla ya Kongamano Kuu, kuombeana kwa imani wakati wa siku za Konga-mano, na kushiriki katika utekelezaji wa maamuzi yaliyofanywa kwe-nye Kongamano Kuu.

Ni nini kitakachotendeka tunaposali pamoja? Hakuna anayejua kwa hakika. Hata hivyo, tunaamini kuwa mapenzi ya Mungu yatakuja kupitia sala na ufahamu. Kurasa zinazofuata zinatupa fursa ya kuungana katika sala ili mapenzi ya Mungu kutimizwa kwa njia ya Mungu na kwa wakati wa Mungu.

Bwana, tufunze kusali.

—TOM ALBINMkuu wa Upper Room Chapel

—DENISE MCGUINESSMkurugeni Mtendaji, Living Tree Services, P.S.

Wenyeviti wa Timu ya Sala

Page 10: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

10 Siku 60 za Sala

Kwa hivyo, Nenda!A L H A M I S I , M A C H I 3 1 • S O M A M A T H A Y O 2 8 : 1 9 - 2 0

Endelea! Ondoka hapa!” Mhubiri mgeni alikuwa ameahidi kushiriki dua yake ya heri anayoipenda. Ni hitimisho lililoje la kushangaza la

huduma ya uabudu rasmi! Ni hitimisho lililoje la kushangaza la huduma ya uabudu rasmi! Lakini Yesu ana utaalamu wa mahitimisho yanayoshangaza, na Mathayo anaidhihirisha katika Injili yake yote kuwa kumfuata Yesu si kwa wale wanaotaka imani iliyotulia. Lazima tuwe tayari kuenda!

Leo, siku tano tu kabla ya kusherehekea muujiza wa Ufufuko, tuna-jitolea kwa kuenda na Yesu kama dhehebu. “Kwa hivyo, nenda” inasalia kuwa muhimu kwa dhamira yetu kama Kanisa la Muungano wa Method-isti, na tunayo fursa ya kujiahidi kikamilifu kwa dhamira hiyo tunapoanza safari yetu ya sala ya pamoja ya Kongamano Kuu. Je, mkutano huu utatimiza nini? Ni tofauti gani utakayoleta ulimwenguni? Ni vipi tukakavyosalia kweli kwa dhamira yetu? Huku muziki wa Pasaka ukiendelea kucheza masikioni mwangu, kwa hakika ninafahamu kuhusu nguvu isiyo kipimo, isiyofikirika ya Mungu na sala.

“Kwa hivyo, nenda” pia ni muhimu kwa imani yangu kama mfuasi wa Yesu Kristo. Mara nyingi zaidi ninajaribu kuzingatia ufuasi kama kitu kingine kwenye orodha yangu ya mambo ya kufanya. Nenda huko nje, fanya mtu mmoja au wawili kuwa wafuasi, itie alama kwenye orodha yangu, na uende kwenye jukumu linalofuata! Katika kipindi chote cha uabudu kwe-nye Kongamano Kuu, tutachunguza jinsi Injili ya Mathayo inavyotambua kipengee cha “ndani yake kwa mapambano ya muda mrefu” kwenye safari yetu na Yesu. Hatujui tutakachokumbana nacho njiani. Lakini kuna habari njema: Yesu atakuwa nasi, na kanisa letu, na ulimwengu kwa safari nzima. Tuanze!

Yesu, hatuna uhakika kule ambako safari hii itatufikisha, lakini tuko ta-yari kuenda na wewe. Amina.

—LAURA JAQUITH BARTLETT

Page 11: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 11

Mambo MsingiI J U M A A , A P R I L I 1 • S O M A Y E R E M I A 3 1 : 1 0 - 1 4

Kipindi cha uhamisho huko Babeli pia huitwa utumwa wa Babeli. Watu wa Israeli walikuwa watumwa wa himaya yenye nguvu zaidi

wakati wao. Kwao lazima hali ilionekana kukosa tumaini. Ilhali nabii Yer-emia anatangaza nguvu ya Mungu itakayokomboa Israeli hata kutoka kwa mkuu huyo mwenye nguvu: “Bwana amemwokoa Yakobo, na kumkomboa kutoka kwenye mikono yenye nguvu zaidi yake.”

Nguvu nyingi zinaweza kutufanya watumwa. Lakini hakuna aliye mkuu zaidi kuliko zamani. Dhidi ya mkuu yeyote, tunaweza kuasi. Lakini zamani tusiyoweza kubadilisha, inayofanya hisia zetu za kushindwa kuwa na nguvu zaidi. Miaka imepita, na hatuna nguvu ya kutendua tulichoki-fanya au hata kurejesha muda tuliopoteza tuliposhindwa kufanya tulich-opaswa kufanya. Tunaweza kujaribu kutendua matokeo ya kale yetu—na mara nyingi tunapaswa kufanya hivyo. Lakini kale yenyewe hatuwezi kuitendua. Ipo, kwa kudumu, na uwezo tusioweza tusioweza kukabilina nao. Licha ya jitihada zetu bora, hatuwezi kuitendua. Ni kuu zaid kuliko Wababeli walivyokuwa kwa Israeli. Kama tu Yakobo (Israeli) ilifungwa kwa “mikono iliyokuwa na nguvu zaidi yake,” hivyo ndivyo tulivyolemewa kwa uzito wa ya kale tusiyoweza kubadilisha. Lakini Mungu aliyemwo-koa Yakobo kutoka kwenye “mikono iliyokuwa na nguvu zaidi yake” pia anaweza kutuokoa kutoka kwa chochote kinachotufunga—haijalishi kina nguvu kiasi gani—hata kutoka kwenye uzito wa mambo yaliyopita.

Hiyo ndiyo maana na msamaha. Mungu hutuokoa kutoka kwenye dhambi yetu, kutoka kwenye aibu ya makosa yetu, kutoka kwenye uzito wa mambo yaliyopita. Hivyo, tunapokabiliana na kazi mpya, tunaweza kufanya hivyo kwa furaha sawa na ile iliyoonyeshwa katika maneno ya Yeremia. Yasome tena, na ufurahie naye!

Mungu, tuondolee makosa na dhambi zetu zote. Tupe furaha ya wale wa-naorejea kwako kutoka kwenye uhamisho wa dhambi na hatia. Amina.

—JUSTO L. GONZÁLEZ

Page 12: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

12 Siku 60 za Sala

Ukomavu wa KirohoJ U M A M O S I , A P R I L I 2 • S O M A W A E B R A N I A 5 : 7 - 9

Waandishi wa Injili wanatupa picha ya Yesu kwenye sala. Kutoka kwao tunajifunza kuwa alilia, akapiga kite katika roho, na kupambana na

majaribu. Mwandishi wa Waebrania anaelezea kwa ujasiri “vilio vya sauti na machozi” ambavyo wakati mwingine viliandamana na sala za Yesu na utiifu aliojifunza kupitia mateso. Picha inayojitokeza inamtambua kama ali-yejihusisha sana na maisha kwa viwango vyote na kama aliyekabiliana kwa ujasiri na wito wake.

Rejeleo la “siku za mwili wake” linasisitiza hali ya mpito na udhaifu wa maisha ya mwanadamu. Bila shaka uchungu wa Gethsemani ulikuwa katika akili ya mwandishi. Katika bustani Yesu alijitolea, kwa njia ya uwakilishi na kujitoa mhanga, dhiki ya watu wote nyakati za uhitaji mkubwa. Alik-abilina na woga wa kifo, akimwomba Mungu aondoe kikombe, lakini hatimaye akakubali mapenzi ya Mungu. Katika pambano hili hatari Yesu alijifunza utiifu kwa mapenzi ya Mungu kupitia mateso aliyostahimili.

Ukomavu au “ukamilifu” katika sifa ya mwanadamu haujatulia lakini hukua kupitia makabiliano ya hali za maisha yanayoendelea kubalika. Luka 2:52 inasema kuwa “Yesu akazidi kufanya maendeleo katika hekima na ukuzi wa kimwili” akipata kibali kwa Mungu na wanadamu. Ukumba-tiaji wa utata na majukumu ya maisha kwa moyo mmoja, pamoja na kuachia maslahi ya binafsi, kuliwezesha kuzungumza maisha yake “kufanywa kuwa ya ukamilifu.” Kuishi kila siku kwa kusikiliza sauti ya Mungu ndiyo njia ambayo tunatambua woga wetu, kusali dhiki yetu, na kukua kikamilifu kama wale walioumbwa kwa mfano wa Mungu.

Zingatia sehemu ambazo Mungu anakuita ukue kupitia utiifu.

—ELIZABETH J. CANHAM

Page 13: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 13

Kipaji cha ImaniJ U M A P I L I , A P R I L I 3 • S O M A M A T H A Y O 1 4 : 2 2 - 3 3

Katika karne ya kumi na tisa, Johann Christoph Blum- hardt alihubiri katika kanisa dogo katika kijiji cha Ujerumani. Hakukuwa na cho-

chote cha kipekee kuhusu kazi yake—hamna, yaani, hadi wanandoa katika kanisa walipomwambia kuhusu matatizo waliyokuwa nayo na binti yao. Mhubiri Blumhardt alikutana nao ili kuomba na kumtembelea binti huyo. Mhubiri Blumhardt alitambua kuwa huenda anakabiliana na pepo kama wale aliokuwa amesoma katika Agano jipya. Ingawa ufadhili wa masomo wa historia muhimu wa Ujerumani ulikuwa ukijiandaa kuelezea pepo wa mbali katika ulimwengu wa sasa, hapa katik parokia ndogo ya Ujerumani, Blumhardt alitambua nguvu ya Yesu katika upungaji pepo.

Kama ilivyo siku ya Yesu, habari njema za ukombozi kutoka kwenye nguvu za pepo zilianza kuenea haraka. Watu walikuja kuona kitu kipya kilichokuwa kikitendeka—nguvu ambayo ilikuwa imetumiwa na huduma ya Mhubiri Blumhardt. Mungu alikuwa akifanya kitu kipya, na Mhubiri Blumhardt alikuwa akitaka kukiamini. Alianza kutambua kuwa watu wengi walikuja kwa sababu zisizofaa. Alianza kuambia “wanaotafuta msi-simko” kuwa upungaji pepo haukuwa uponyaji lakini ishara ilikusudia kuwaelekeza watu kwenye ufalme wa Mungu.

Muujiza wa Yesu wa kutembea juu ya maji unafuata mara moja ule wa kulisha watu elfu tano katika Injili ya Mathayo. Yesu anafahamu kile amba-cho Mhubiri wa Blumhardt alijifunza karne kadhaa baadaye: Mara nyingi sisi huvitiwa sana na ishara za miujiza ya nguvu ya Mungu kuliko tulivyo katika vuguvugu la ufalme ambazo zinatuelekeza. Yesu anawaita wafuasi oligopistoi—“wenye imani ndogo.” Anazunguza nasi sote. Ni jambo tofauti kuona nguvu ya Mungu na kujua kuwa ni halisi: na jambo jingine tofaut kabisa kumwamini Bwana anayeomba kila kitu, hata dhoruba inapoonye-sha hasira kwako.

Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, tupe imani ya kuamini maisha yetu yote vuguvugu la ufalme wako. Amina.

—JONATHAN WILSON-HARTGROVE

Page 14: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

14 Siku 60 za Sala

Kile Ambacho Imani Pekee Inaweza KuonaJ U M A T A T U , A P R I L I 4 • S O M A Z A B U R I 1 2 1

Nililala salama kama lami nyeusi na usiku unaonata kwa utulivu, mbali na sauti za magari na umbeya wa siku—hadi niliposikia mgongo mkali

kwenye zege. John, bawabu wetu wa zamu ya usiku, alikuwa amemwua nyoka mwenye sumu ambaye alikuwa amenyinyirika karibu na mlango wa mbele wa nyumbani kwetu nchini Ghana, Afrika Magharibi. Mimi na mke wangu , Safiyah, tulihudumu huko kama wamishionari. Marafiki wali-kuwa wametumbia, “Mwajirini bawabu wa usiku ili alinde nyumba yenu ili mlale usiku.”

Waisraeli walimwamini Mungu kuwalinda, uaminifu usiopatikana kwa wafuasi wa miungu mingine. Katika aya ya 3-4 ya Zaburi 121, mtunga zaburi anatangaza kuwa Mungu wa Israeli hasinzii wala kulala. Kauli hii inalingana na jirani wa Israeli ambao kwa kawaida waliamini kuwa miungu yao “ililala” majira ya baridi kali na kuamka misimu ya ukuaji.

Wakati fulani nilizuru hekalu la dini nyingine. Lilikuwa na wawakili-shi halisi w miungu iliyoabudiwa hapo na upatu. Nilipouliza madhumuni ya upatu, kiongozi alijibu “tunagonga upatu ili kuhakikisha kuwa miungu imeamka.” Mtunga zaburi alitumia kila fursa kuthibitisha imani kwa Mungu wa Israeli. Mungu huyu aliumba mbinu na dunia. Mungu huyu halali. Mungu huyu alitupa kivuli kama hifadhi. Imani kuwa Mungu ange-wapa mahujaji kivuli ilionyesha imani yao kwa Mungu mkuu anayeweza kuwapa kivuli kujikinga jua mchana na mwezi usiku. Mtunga zaburi anaendelea kusema kuwa Mungu atatukinga dhidi ya maovu yote.

Je wewe? Ni nini unachojivunia kuhusu Mungu? Ni sifa ipi kati ya sifa za Mungu unaiiga mwenyewe na wengine katika uabudu wa ushirika? Matamko yako kumhusu Mungu hukusaidia kuona maisha kwa macho yenye imani.

Mungu, kwa kuwa husinzii wala kulala kamwe, niepushe na usiku wenye wasiwasi na asubuhi zenye woga. Amina.

—KWASI KENA

Page 15: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 15

BarabaraniJ U M A N N E , A P R I L I 5 • S O M A L U K A 2 4 : 3 3 - 3 5

Kifungu hiki kilianza kwa kutamausha na mfadhaiko wa wafuasi wa Yesu, haswa wale wawili wanaosafiri kuelekea Emau. Sasa tunasonga

kwenye uthibitisho wa ufufuko wa Yesu na kushiriki kwa habari hiyo njema na wafuasi wa Yesu Kristo.

Katika kifungu, tunaona maana ya dharura. Ingawa ilikuwa jioni, watu wawili walisafiri mwendo mrefu sana kurudi Yerusalemu kukutana na wafuasi kumi na mmoja. Kukutana kwao na Yesu aliyefufuka kulikuwa kukubwa zaidi hivi kwamba wasingesubiri hata saa moja. Kwa sababu ya furaha yao, umbali haukuwa tatizo kwao, na giza halikuwazuia. Dharura hii ya kushiriki habari njema ni msingi wa uinjilisti wetu na dhamira ya kanisa. Hakuna kinachoweza kutuzuia kushiriki hali ya ufahamu ya kuku-tana na Bwana wetu aliyefufuka.

Wawili wanapowasili, wanapata wafuasi kumi na mmoja katika eneo moja. Pia wameshuhudia Kristo aliyefufuka: “Bwana amefufuka, na amem-tokea Simoni!” Hatujui ikiwa Yesu alimtokea Simoni kabla ya watu wawili barabarani kuelekea Emau. Wakati wa kutokea si muhimu. Muhimu zaidi kwao ni uthibitisho wa ufufuko wa Yesu. Kwa kweli alikuwa ameaga dunia msalabani lakini alikuwa amefufuka kama alivyoahidi na kama maandiko matakatifu yalivyotabiri. Kushiriki hali yao ya kukutana na Kristo aliyefu-fuka barabarani wakielekea Emau unakuwa mtindo wa maisha ya kanisa, na hali ya ufahamu wakati wa kumega mkate inatoa maana zaidi ya Karamu ya Bwana katika maisha ya kanisa letu.

Mungu wa ufufuko, tupe maana ya dharura ili kushiriki hali yetu ya Kris-to anayeishi na watu wengine. Amina.

—JUNG YOUNG LEE

Page 16: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

16 Siku 60 za Sala

Tumaini la UfufukoJ U M A T A N O , A P R I L I 6 • S O M A 1 P E T E R O 3 : 1 8 - 2 2

Kifungu hiki kinatumika kama msingi wa andiko la kauli katika Imani ya Mitume inyoungumzia Yesu kati ya kifo na ufufuko: “Alishuka kuz-

imu.” Mara nyingi jibu letu kwa kipengee hiki cha kakuni ya imani ni la mfadhaiko: Hili linaweza kumaanisha nini? Wakati mwingine kipengee hiki kinaachwa nje ya kanuni ya imani. Ilhali, kama maandishi kutoka kwa Petero wa Kwanza, kinatuonyesh sifa inayoshangaza ya tumaini letu kwa kusema kuwa vikwazo vyote vya upendo wa maisha kutoka kwa Mungu vinasambaratishwa msalabani.

Kikwazo kilichosambaratishwa hapa ni kile ambacho kinatenganisha wazima na wafu, wale wanaoaga dunia bila tumaini na wale wanaoishi kwa tumaini. Kifungu kinazungumzia wale walioaga dunia katika mafu-riko ambapo Mungu alitaka kutakasa dunia kwa kutiwa najisi kwa dhu-luma na ukiukaji. Wale waliosombwa hawakuwa na tumaini la mabadiliko. Ilhali ni kwa ajili ya hawa, ambapo wote waliokuwa wameaga dunia, kwa wote walio chini ya hukumu ya haki ya Mungu, ambapo Kristo anatangaza kati ya “kifo chake katika mwili” na ufufuko wake.

Kwa sababu ya kushuka kwake katika gereza la nafsi, tunathubutu kuwa na tumaini kwa wote wnaoonekana kutenganishwa na injili kupitia kifo au hukumu. Kwa kuwa si hata wala ghadhabu ya Mungu inayoweza kuzuia tangazo la neema ya tumaini kwa wote kuteemea kifo na ufufuko wa Kristo.

Tumaini letu la ufufuko ni thabiti mno hivi kwamba hatuwezi kukata tamaa ya tumaini kwa yeyote, haijalishi umbali uliopo kati yake na Kristo; iwe ni katika maisha au kifo, Kristo amesogea karibu nao.

Mungu, asante kwa tumaini katika Kristo. Amina.

—THEODORE W. JENNINGS

Page 17: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 17

MakaoA L H A M I S I , A P R I L I 7 • S O M A W A F I L I P I 3 : 1 7 – 4 : 1

Inamaanisha nini kuzungumza kuhusu nchi yetu kuwa mbinguni?Kwa sababu ya kuteseka na kuvunjika kwa maisha “katika mwili,”

dhehebu la Unostiki liliamini kuwa maisha ya kawaida ulimwenguni kwetu ni maovu. Badala yake, wanachama wake walifikiri kuwa sisi wan-adamu tulipaswa kuwa “kiroho,” kutojali kabisa ulimwengu halisi. Wengi wa Unostiki hawa walijitambua kuwa Wakristo. Walimwamini Yesu—lakini sio mwili na damu ya Yesu. Badala yake, walifikiri kuwa Yesu ali-kuwa kama pepo aliyetumwa kutupa ujumbe wa wokovu wa yake aliyeishi nje ya uumbaji ili kutuleta karibu na ulimwengu wa kiroho.

Kanisa la zamani lilipinga sana uwili huo uliokataa uzuri wa uum-baji wa Mungu na pia uhalisia wa Kufanyika kwa Mwili. Badala yake, mababu zetu Wakristo walithibitisha kuwa Mungu hakuwahi kukusudia ulimwengu wetu kuvunjika. Katika Waroma, Paulo anasisitiza kuwa uum-baji wenyewe unagumia katika aina ya utumwa unaotokana na dhambi ya mwanadamu. Mwisho wa nyakati, tutakapopokea mili ya ufufuko wetu, anasema, ulimwengu halisi pia uterejeshwa kwenye kusudi asili na upendo wa Mungu. Dunia hii iliyorejeshwa ni makao yetu. (Tazama Waroma 8:18-25.)

Muundo ambao urejeshaji huu utachukua na wakati wake sio muhimu kwetu kujua, hata hivyo, uvumi kuuhusu unaweza kutukengeusha kuto-kan na kazi halisi ya upendo na maisha ya Wakristo. Hata hivyo, tunahitaji kukumbushwa kuhusu upendo na utunzaji wa Mungu kwa ulimwengu huu huu tunaoishi ndani.

Mungu wa viumbe vyote, tufunze jinsi ya kujua ulimwengu wako kama ulivyokusudia uwe, na utusaidie kuupenda na kuishi ndani yake kama zawadi yako. Amina.

—ROBERTA C. BONDI

Page 18: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

18 Siku 60 za Sala

Siku ya BwanaI J U M A A , A P R I L I 8 • S O M A L U K A 3 : 1 - 6

Luka anaanzisha hadithi ya Yohana Mbatizaji katika historia kwa kutusimulia aliyekuwa kiongozi wa nini wakati gani. Hii inajumuisha

himaya ya Roma, gavana wa Roma ya Judea, mtawala wa Ituraea wa Gali-laya na kaka yake aliyetawala sehemu za Siria. Inakamilika kwa mtawala anayejulikana kigodo wa Abilene, wilaya ya kaskazini magharibi ya Dam-aska, na wawili wa makuhani wakuu Yerusalemu. Kwa kusoma orodha mara ya kwanza kunaonekana kuwa utangulizi wa kuchosha wa huduma ya Yohana, iliyojaa majina yasiyojulikana ambayo ni magumu kutamka. Luka ana sababu nzuri kwa kuijumuisha, hata hivyo—ile inayoenda moja kwa moja kwenye moyo wa Injili yake.

Ikiwa tungalisambaza ramani ya ulimwengu katika siku za zamano na kuweka vibanio vyekundu katika maeneo ambayo watu wenye nguvu walitawala, tungalikuwa na turubai ambalo lingalianzia Yerusalemu hadi Roma. Ingalijumuisha Wayahudi, Washami, Wagiriki, na Waroma. Ingaliju-muisha kiongozi wa jeshi mwenye mamlaka zaidi duniani, na pia viongozi wa dini wenye mamlaka zaidi katika Uyahudi na watu wote walioishi chini ya sheria yao.

Luka anaonyesha kuwa hadithi anayokusudia kusimulia inahusu yote hapo juu. Si hadithi ya ndani kuhusu mwanakarama wa Kiyahudi aliyeanzi-sha dhehebu jipya la Uyahudi. Ni hadithi ya ulimwengu kuhusu mkwozi wa Mungu aliyekuja kuubadilisha ulimwengu. Luka ananukuu mstari wa mwisho wa unaabii wa Isya kama mada yake: “Na mili yote itona wokovu wa Mungu.”

Kabla ya kanisa kuwepo, injili ilipewa watu wote. Leo hii kanisa lipo kwa wale wasiofaa.

Ni kwa njia zipi unajaribu kummiliki Yesu? Unafikiri Yesu ni wa nani, na ni nini ambacho lazima watu wafanye ili awe wao? Jaribu kufanya ali-chokifanya Mungu: Mtoe Yesu bila malipo kwa ulimwengu mzima.

—BARBARA BROWN TAYLOR

Page 19: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 19

Jangwa Litachanua MauaJ U M A M O S I , A P R I L I 9 • S O M A I S A Y A 3 5 : 5 - 7

Wanasubiri. Watu wa “jangwa.” Wale wanaozidi maneno sahihi ya kusema. Zaidi ya uwezo wetu wa kukua kijani tena. Watu, maeneo,

na hali zinakauka. Ni rahisi yaacha kwenye jangwa. Kinaonekana kuwa kitu kisichoaibisha sana kufanya.

Haya hayasubiri “mvua ya mwaka.” Yamezoea marekebisho ya haraka ambayo yamekuja na kuenda pamoja na upepo wa wa kwanza mkali. Yana-vumilia ahadi za wale wasiofahamu jangwa. Imekuwa rahisi kutarajia kuchoma mchanga badala ya maji na kufahamu kundi la mbweha. Uvu-milivu wa machungu hauumii sana. Tumaini limekuwa hudhurungi na kukauka.

Kisha Mungu anakuja. Hakuna anachogusa Mungu kinaweza kusalia vile vile. Si kijani cha ghafla. Ni unyunyizaji wa maji wa ndani, yanayope-nya kiini cha kiumbe. Ni urejeshaji wa maji ya ardhini, sio kutiririk lakini kumiminika katika mkondo ili maisha yote yabadilishwe. Mizizi inaanza kuota hadi ndani kabisa. Uvumilivu wa machungu unageuka kuwa tumaini. Pindi tu tumaini linapoota, furaha inajitokeza.

Nyika inaanza kuwa kijani hatua kwa hatua. Vidimbwi vya maji vina-onekana ambapo mchanga ulichoma nyayo zenye uchovu. Maji yanakimbia juu ya mawe yaliyojua upepo tu. Mbweha wanatafuta majangwa mengine. Macho ya vipofu yanaona. Wengine wanaanza kuona, lakini wote wanaona. Masikio ya viziwi yanazibuliwa. Wengine wanashika maji yanayokimbia, lakini wote wanasikia. Kiangazi cha muda mrefu cha roho kinaanza kuhisi, kuwa chochote anachogusa Mungu kinabadilika.

Tumemsubiri Mungu, sio kutrajia kuonekana. Na Mungu amekuja.Mkuu wa jangwa,Mungu wa yasiyowezekana na kutotabirika, wa wakati.ninyunyizie maji,kulingana na mapenzi yako. Amina.

—RAY BUCKLEY

Page 20: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

20 Siku 60 za Sala

Utambuzi na Kuwa na ImaniJ U M A P I L I , A P R I L I 1 0 • S O M A M W A N Z O 1 2 : 1 - 9

Wakati Mungu anapomwita Abrahamu, Abrahamu anaenda. Abra-hamu hasiti. Hashangai ikiwa anfanya jambo linalofaa. Hafikirii

kuhusu gharama au hatari. Anachofanya ni kufuata amri ya Bwana bila kunung`unika wala kukataa.

Maisha tunayoishi leo yanafanya kuwa vigumu kuiga mfano wa Abra-hamu. Mahusiano ya ulimwengu wa mali yanatufunga kabisa. Kushu-ghulika na kazi, familia zetu, kisha mahitaji mengi ya maisha ya kila siku, hatuwezi kufikiria kwa urahisi kuyaacha na kuenda eneo jipya kwa sababu Bwana ametuita kuenda huko.

Majaribu yetu makubwa yanakuja kwa kutomtafuta Mungu wa kweli aliyejifanya mwili katika Yesu Kristo na ambaye mapenzi yake yasiyo na wakati na timilifu yanatufunga kila wakati. Badala yake tunamtafuta mungu mdogo, mungu ambaye hatawahi kutuomba kufanya chochote tusichotaka kufanya, kuacha chochote tusichotaka kuacha, au kuenda eneo ambalo hat-utaki kuenda.

Wakati wa kuanzisha Massachusetts Bay Colony, John Winthrop ali-waambia wanakondoo wake kuwa Mungu hajali kile unachomiliki lakini ikiwa, Mungu akibisha mlangoni petu na atuamuru tuache kile ambacho tunathamini sana kwa ajili ya Bwana, tutajibu. Tukitambua kuwa hatuwezi kuacha chochote, hutamfuati Kristo. Anaweza kuamuru tuache mali yanayo-thaminiwa au misimamo ya kisiasa inayothaminiwa au cheo kinacho-thaminiwa katika jamii yetu. Lakini kitu kimoja ambacho kila Mkristo anakifahamu kwa hakika ni kuwa hivi karibuni Bwana atabisha.

Baba wa Mbinguni, nisaidie kuacha vitu vya ulimwengu huu, kusikiliza mwito wako ili kujitoa mhanga, na kuujibu kwa furaha na bila kuuza maswali. Amina.

—STEPHEN L. CARTER

Page 21: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 21

Tumeshafika?J U M A T A T U , A P R I L I 1 1 • S O M A W A E F E S O 2 : 1 - 7

Jinsi tunavyosema katika kanisa la Baptist nilipolelewa, nilioa nili-pokuwa na miaka kumi na mmoja, miongo mitano iliyopita. Kipindi

katika Shule ya Mfunzo ya Biblia kilikuwa kikiendelea. Jengo la kanisa letu lilikuwa hifadhi kwa zaidi ya njia moja. Muundo wa motofali mengi ilikuwa si tu sehemu ya kuwafunza watoto kuhusu Yesu; madarasa ya chini yalikuwa hifadhi bora mjini. Kusonga mbele hakukuwa kugumu. Kwa mtoto mchanga, lilikuwa jambo la maana sana, jambo ambalo lingalibadil-ish maisha yangu milele. Nilienda mbele kwa mwaliko na kumwambia mhubiri uamuzi wangu.

Wokovu ni neno tunaloweza kuhusisha na ufufuo wa kiroho. Waefeso inaelezea shughuli ya Mungu ya kuokoa katika Kristo. Aya tatu za kwanza zinataja tunachookolewa kutoka kwacho: kifo kupitia dhambi, kufuata njia za ulimwengu, na kuwa watoto wa ghadhabu. Mwandishi haadhibu sana kama kutukumbusha kuhusu yaliyopita ili tuwe tayari kuthamini uju-muishwaji wetu katika hidhithi ya maisha ya Mungu ya wokovu wa sasa!

Nilipokuwa na miaka kumi na mmoja, ahadi yangu ya kubadilisha mai-sha haikuhusu kubadilisha “dhambi,” zangu za zamani lakini kuhakikisha kuwa ilizua maswali mazito kuhusu jinsi ya kuwa Mkristo. Mara nyingi nilitaka kuacha kauli hiyo ya imani, lakini ahadi niliyokuwa nimetoa imeishia kunijenga. Haijawahi kunifanya kulegea, ingawa uelewa wangu wa kile inachomaanisha umebadilika kadri ninavyokomaa.

Nimetambua utajiri wa huruma na ukarimu wa Mungu. Ninathamini kujitolea kwa Mungu kuchukua hatua kwa ajili ya manufaa na wokovu wangu. Niko “hai pamoja na Kristo.” Kwa ahadi hiyo, ninajaribu kila wakati kuwa na tumaini.

Mungu, nisikie, nipe nguvu; niruhusu nikusikie. Amina.

—BILL DOCKERY

Page 22: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

22 Siku 60 za Sala

Kuitwa katika Agano na MunguJ U M A N N E , A P R I L I 1 2 • S O M A 2 S A M U E L I 7 : 1 - 1 1 , 1 6

Hata tukiwa na madhumuni yenye nia nzuri kwa kazi ya Mungu, ni vyema kufahamu kuwa lazima mapenzi ya Mungu yatawale. Uaminifu

haumanishi tu kufanya mambo mazuri kwa ajili ya Mungu lakini kusikiliza ili kutambua kile ambacho Mungu angependa tukifanye.

Mfalme Daudi anatamani sana kumfanyia Mungu jambo kubwa. Kwa kuongozwa na hisia yake ya furaha, Daudi anatmbua kuwa yeye binafsi anaishi katika nyumba ya mwerezi. Ikiwa hili linamfurahisha, kwa hakika nyumba bora kwa ajili ya safina itamfurahisha Mungu. Hili linaleta maana, sivyo? Lakini Mungu alitamani kumjengea Daudi (au “nyumba”) ukoo wa kiroho. Kutoka kwenye urithi huu Mungu angalichagua muda na mzawa ambaye angalijenga hekalu. Muhimu zaidi, kutoka kwenye ukoo wa kiroho angetokea masiha.

Ni mara ngapi katika maisha yetu tunawaza kile kitakachomfurahisha Mungu kulingana na hali zetu za wanadamu za furaha badala ya maarifa tunayopata kutoka kwenye maisha yetu ya kiroho? Tunapata maarifa ya kiroho kupitia uwazi wa kimaksudi kwa Mungu, kupitia kusikiliza na kut-ambua uwepo wa Mungu. Maarifa ya kiroho huandamana na uwazi na tara-jio kwamba Mungu ana mapenzi na madhumuni, madhumuni tunayoweza kufahamu kupitia maisha yenye sala.

Hata hivyo, neno la Mungu linamjia Daudi kupitia nabii Nathani, na Daudi anaweza kusikia. Watu wenye imani huishi kumfurahisha Mungu kupitia kuwepo kwao na vitendo vyao, kufahamu kuwa Mungu hufurahia katika kusikiliza kwa maombi sala zetu.

Mungu, ninaomba mdundo wa kila siku ujumuishe wakati wa kuwepo nawe, kukujua vizuri zaidi, na kukupenda zaidi. Amina.

—NATHAN D. BAXTER

Page 23: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 23

Hekima, Tumaini, na Ahadi ya MunguJ U M A T A N O , A P R I L I 1 3 • S O M A Y O H A N A 1 6 : 1 2 - 1 5

Hhatupokei maneno ya Mungu kwetu kila wakati. Yesu anajua kuwa wafuasi wake wengi watakuwa “baharini” bila umakini mkubwa,

uhakika kutoka kwa Yesu kabla, kwa njia ya mwili, hajaondoka kwenye dunia hii. Kwa hivyo Yesu anawaambia, “ningali na mambo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili kwa sasa. Roho wa ukweli ata-apokuja, atawaongoza katika yote ya kweli.”

Wengi kufikia leo hii bado hawaelewi ukamilifu wa ahadi hiyo. Ulisikia lini Mkristo mcha Mungu akisema kitu kama hiki: “Ninatamani Yesu asin-galichukuliwa kutoka kwetu. Ninatamani angalikwepa kuondoka huko.” Lakini kupaa kwa Yesu hakukuwa hasra kwetu; kulikuwa faida. Bwana katika kupaa kwake alipokea nguvu mpya. Wakati fulani alikuwa akiishi mbali kidogo; lakini sasa amefufuka, anapatikana kwa watu wote duniani saa zote mchana na usiku. Katika ufufuko wake alifikika kwa njia mpya. Aliyefufuka na kupaa hajazingirwa tena na vizuizi vya wakati na nafasi vinavyotuzuia sisi.

Masuala ya kiroho kwetu hayatuchanganyi sana kama yalivyokuwa wakati wa kipindi cha siku arubaini kutoka Siku ya Pasaka hadi Siku ya Kupaa Mbinguni. Kutamani kuwa ungalirudisha nyuma saa kunanyima nguvu ya Roho Mtakatifu anayeweza kuwa nasi katika furaha yetu na huzuni zetu, nyakati za majaribu na nyakati za ushindi juu y dhambi. Hivyo, furahi na ushangilie, kwa kuwa Roho anatupa zaidi kuliko kile ambacho kupaa mbinguni kwa Bwana kungaliondoa kwetu.

Hata zaidi, Roho yupo nasi na kuwa miongoni mwetu ahadi ambazo Yesu aliahidi wakati wa huduma yake ambazo tumesahau kwa kiasi kikubwa. Kile ambacho sisi na mababu zetu katika imani tusichokumbuka, Roho hutukumbusha.

Roho Mtakatifu, njoo miongoni mwetu, tuhudumie sasa na milele. Amina.

—LAURENCE HULL STOOKEY

Page 24: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

24 Siku 60 za Sala

Kufanya Roho Mtakatifu Kuwa MwiliA L H A M I S I , A P R I L I 1 4 • S O M A L U K A 3 : 1 5 - 1 6

N suala la ukomavu mdogo wa kiroho kujua kuwa mtu si Masihi. Hakuna mtu katika kipindi chote cha mafunzo ya useminari aliwahi kunionya

dhidi ya imani ya kuwa mwokozi. Badala yake, nilihimizwa kumwiga Yesu, kuwa mtumishi wa Mungu kwa watu. Katika miongo iliyofuata ya kufanya kazi na viongozi wa dini, wengi wao wakiwa wamechoka kwa kujaribu kutimiza matarajio ya wengine na yao binafsi au kuangamizwa kwa hitaji tupu la wanaparokia wao, nimetambua kuwa imani ya kuwa mwokozi, kwa watu wengi, haiwezi kutofautishwa na ahadi kwa Kristo.

Yohana Mbatizaji alijua vyema. Ingawa alikuwa maarufu zaidi kuliko Yesu wakati wa maisha yake, Yohana hakuwahi kujaribiwa kwa tuzo maa-rufu au kwa maana yake isiyopingika ya mwito kwa kujifikiria binafsi kuwa masiha. Alikuwa na wajibu mkubwa kwa Mungu, lakini hakuwahi kupanga kutambua wajibu wake na ule wa Masiha.

Martin Buber aliwahi kusema kuwa kuna kitu kisichoweza kulingan-ishwa kati ya kujifikiria kuwa masiha na kuwa masiha. Inawezekana kuwa wengi wetu hujipata wakifanya wajibu wa masiha kwa sababu hatujafia hitaji letu ili “kuwa” mtu mwingine. Inawezekana kuwa Yesu mweneyewe alikataa wajibu wa masiha ambao vizazi vya baadaye vilimpa. Majaribu yake katika nyika yanaonekana dhahiri kuwa kukataliwa kwa matumaini ya sasa ya masiha. Badala ya kujitambua na Mungu, alihusiana na Mungu. Aliupata mwito wake na kuufuata, kile ambacho vizazi vya baadaye vilim-wita.

Tunaweza kuhusiana na nguvu kama hizo za Mungu ndani yetu ambazo Yesu alihusiana nazo? Tunaweza kuwa vyombo vya uponyaji wa Mungu bila kujitambua binafsi na Mponyaji?

Mungu, nifanye niwe mimi na kufanya kile tu ulichoniita nikifanye. Am-ina.

—WALTER WINK (1949–2012)

Page 25: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 25

Kumkaribisha MunguI J U M A A , A P R I L I 1 5 • S O M A Y A K O B O 1 : 1 7 - 2 1

Swanadamu tunapaswa kufanya kilicho chema. Haiwezekani kuzua mjadala mkubwa kwa kauli hiyo.Lakini tunapaswa kuifanya vipi? Au kwa kugonga ndipo, kwa nini ni

vigumu sana kwetu kufanya jambo jema? Kuwa wema? Tukiangalia karibu nasi, hatuhitaji kuangalia mbali kuona maisha yaliyoharibiwa, unyama, ufisadi, na uovu ni vitu vilivyo sehemu kubwa ya jamii yetu, kuanzia familia ndogo na mtaa hadi ngazi za taifa na kimataifa.

Labda tumefasiri visivyo wajibu wetu katika kazi. Yakobo anatuambia kuwa matendo yote mema yana asili yake kwa Mungu. Hata Mungu ali-pouumba ulimwengu kwa neno moja: “Mungu alisema . . . na ilikuwa,” sasa katikati yetu neno la ukweli kutoka kwa Mungu linasababisha ulimwengu ulioanguka kuwa mzuri. Ikiwa mioyo yetu ina ukarimu kwa neno hilo la kweli, basi uzuri wenyewe wa Mungu unaanza kutuumba upya.

Tunastahili kujiondoa yale yote yanayopinga neno zuri, kung`oa kwe-kwe ya hasira na utendaji dhambi kama mtunza bustani mzuri ambaye ana-tamani kutafuta nafasi ya mbegu nzuri. Mbegu nzuri ni neno la Mungu. Hatuwezi kujiundia wenyewe— tafuta nafasi na ulikaribishe. Hiyo ni kazi ya kutosha.

Tupe mioyo iliyo wazi kwako, Mungu, ili neno lako lipate makao ndani yetu. Amina.

—CATHERINE GUNSALUS GONZÁLEZ

Page 26: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

26 Siku 60 za Sala

Njoo, Roho MtakatifuJ U M A M O S I , A P R I L I 1 6 • S O M A M A T E N D O 2 : 1 4 - 2 1

Petero, ambaye alikana kumjua Yesu, alikuwa jiwe ambalo Yesu alili-jenga kanisa lake. Hapa anazungumza kwa mamlaka. Huku akiwa ame-

zungukwa na mitume wake, anaangazia suala la umati. Hakuna miongoni mwao aliyelewa. Hawajawahi kuwa timamu zaidi. Anaripoti kuwa saa tatu kamili asubuhi hiyo Roho alining`inia juu yao kwa ndimi kama za moto, akawageuza kutoka ndani, na kuwafanya wajumbe wa Aliye Juu. Sio kwa maneno yake mwenyewe lakini kwa yale ya nabii Yoeli, Petero anafafanua kilichotendeka. Tusikilize unabii huu kana kwmba ni mara ya kwanza, na kugeuza matamko yake yafae.

Tunaweza kuwa wachanga au wazee, mwanamume au mwanamke, mtumwa au huru, Wa taifa jingine au Myahudi na bado tuteuliwe na Mungu kama manabii wanaokataa kuridhishwa na hali iliyopo. Maisha kama tuy-ajuavyo hubadilika. Asili yenyewe inarekodi mwisho wa enzi na mwanzo wa enzi nyingine. Mabadiliko haya yatatusafirisha na Yesu kutoka kwe-nye uchungu katika bustani, kupitia kashfa ya msalaba, hadi utukufu wa asubuhi ya Pasaka. Damu, jasho, moto, moshi na ukungu—hizi na ishara nyinginezo za misukosuko zinaashiria mabadiliko ambayo dunia na wakazi wake wanakaribia kupitia. Kwa ujio wa Roho, wokovu wetu uko karibu.

Mitume wanapopokea mwanzo mpya kwa Roho Mtakatifu, vivyo hivyo lazima tuwe Wapentekoste, kuacha miradi yote ya wokovu wa binafsi na kumruhusu Mungu kuwa Mungu katika maisha yetu. Mkao wetu unakuwa moja ya unyenyekevu uliokithiri, tukipiga magoti mbele za Aliye Juu na kuliita jina la Mungu ndipo tunapoweza kujiondoa kwenye aina zote za kuabudu sanamu na kutoa ahadi kuu ya hisani.

Njoo, Roho Mtakatifu, tumwagie kitulizo cha wokovu. Tupake mafuta ya fu-raha ili tuwe na ujasiri wa kutangaza kuwa Yesu Kristo ni Bwana. Amina.

—SUSAN MUTO

Page 27: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 27

Kiongozi au Mtumishi?J U M A P I L I , A P R I L I 1 7 • S O M A M A R K O 1 0 : 4 2 - 4 5

Kipindi kifupi kilichopita kuhusu utatanishi unaoonekana wa “uongozi wa mtumishi.” Tumepoteza thamani ya maneno na matendo ya Yesu

yanayobainisha kwamba uongozi wa kweli unahusu kuwatumikia wen-gine, sio kuwatawala. Ilhli, kwa njia nyingi tumebadilisha mabadiliko ya Yesu kwa kukubali neno kiongozi mtumishi lakini kulirejesha tena kwa mitego ya nguvu na upendeleo. Sote tunafahamu cheo cha kuhani mkuu wa Roma, “mtumishi wa watumishi wa Mungu.” Huku tukiwatukuza makuhani wanyenyekevu kwa haki, ukweli ni kuwa cheo kina mamlaka na nguvu ambayo si tofauti sana na mamlaka ya nguvu ya kiongoi yeyote w siasa.

Waprotestanti wanaweza kujihesabia haki kwa urahisi, kwa kutambua kwa kupinga fahari, nguvu, na upendeleo vilivyopew “mtumishi wa watu-mishi wa Mungu.” Lakini hatujafanya vivyo hivyo? Tumeepuka neno “mtu-mishi wa watumishi wa Mungu,” lakini tunawapa mamlaka na heshima kubwa viongozi wasimamizi kuliko wachungaji? Katika miduara ya Muun-gano wa Methodisti, maaskofu hawatwi tena kwa jina lakini kwa cheo. Na je, hatuthamini kutumikia makanisa tajiri kuliko makasina maskini? Kwa nini wachungaji wetu wengi bora wanatumwa kwenye makanisa makubwa kama zawadi ya kufanya vyema, badala ya makanisa yetu maskini zaidi ambapo wanaweza kusaidia kanisa kukua? Ikiwa kwa kweli tulithamini uongozi wa mtumishi, je, wachungaji wasingewania vyeo vijijini au mji wa ndani au makanisa maskini ambapo uongozi ungalikuwa wa kujitoa mhanga? Katika Marko 10 Yesu anabadilisha dhahiri cheo cha kijamii cha kiongozi kutoka sehemu ya mamlaka hadi sehemu ya huduma ya kujitoa mhanga, hata hadi sehemu anayoita utumwa. Kusulubiwa kwake kulizuia mabadiliko haya mbapo Mkuu aliteseka pamoja na aliye chini zaidi kwa ajili ya kumwokoa aliye chini. Sisi ni wafuasi wa Kristo.

Ni vipi tunavyolinda dhidi ya hatari za fahari ya sehemu tunapochagua mahali tunapotaka kutumikia?

—MARJORIE HEWITT SUCHOCKI

Page 28: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

28 Siku 60 za Sala

Sehemu Mpya za UtiifuJ U M A T A T U , A P R I L I 1 8 • S O M Z A B U R I 5 1 : 6 - 1 2

Daktari bora haridhishwi kamwe kwa kuangalia tu dalili za ugonjwa. Anataka kujua ni nini kinachoendelea ndani ya mgonjwa na kugundua

kinachosababisha dalili hizi. Utabibu wa kisasa umevumbua vifaa mbalim-bali vya kuchunguza mambo yanayoendelea katika mwili wa binadamu. Hivyo, ulimwengu wa tiba hutumia uyoka (eksrei), vitambazaji vya aina tofauti, na laparaskopia kuelewa mambo yanayoendelea ndani ya mili yetu.

Mungu, kama daktari mzuri, anataka kuchunguza “ndani ya mioyo yetu.” Kifaa pekee cha Mungu ni kichocheo cha kuanzisha kujitolea kwa mwan-adamu kufungua moyo. Ndio kwa maana kitabu cha Ufunuo kinamwonye-sha Yesu akisema, “Nimesimama mlangoni, nikibisha; ukisikia sauti yangu na kuufungua mlango, nitaingia ndani yako” (3:20). Mtunga zaburi anaji-tolea kuufungua mlango. Anajua kuwa Mungu anatamani “ukweli ndani ya moyo wa kiumbe” na hivyo anamwomba Mungu amfunze hekima katika wake.

Tunapotuma ombi, “Nisafishe,” Mungu huja kutusafisha. Tunaposema tu, “Nioshe,” ndipo Mungu atakapokuja na kufanya hivyo. Tunapotamka tu, “Jenga moyo safi ndani yangu,” ndipo Mungu huja “kuweka roho mpya na sahihi” ndani yetu. Mungu anapotuita sehemu mpya za utiifu, Mungu anasubiri jibu letu, “Ndiyo, Bwana.” Uwepo wa Roho Mtakatifu kwetu unatuita daima kufuata njia ya Mungu. Tunaposema ndiyo kwa Roho, tuna-gundua kuwa furaha yetu inarejeshwa na “roho ya kupenda” inadumishwa ndani yetu.

Zaburi hii haikamiliki kwa maombi ya maisha yaliyofanywa upya pekee; inakamilika kwa kumsifu Mungu na azimio la kuimba kwa sauti ukombozi wa Mungu. Tunaposema ndiyo kwa msamaha wa Mungu, tun-aimba wokovu wa Mungu sio tu kupitia maneno bali kwa maisha yetu yote.

Jenga ndani yangu moyo safi, Mungu, na uweke roho mpya na sahihi nda-ni yangu leo. Amina.

—M. THOMAS THANGARAJ

Page 29: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 29

Yule TusiyemjuaJ U M A N N E , A P R I L I 1 9 • S O M A Z A B U R I 1 2 6 : 1 - 6

Kuishi kama Wakristo ni kuishi katika hali ya ndoto. Ndoto bora ni zile ambazo hatutaki kuziamsha.

Ndani yake tunafurahia mchezo usiotelekezwa au tunapata kila kitu kwa ghafla kikiwa na maana au kufurahia sana kukumbatiwa na mpenzi. Kisha kengele inapolia katika giza la asubuhi yenye baridi kali, siku nyingine ya majukumu inaanza kutuamuru kutimiza matakwa, kutuweka katia maja-ribu ya kufumba macho na kujaribu kurefusha ndoto, ndoto tamu.

Lakini majukumu yanatuandama, na tunaweka nyayo zetu kwenye sakafu baridi na kudetea hadi bafuni. Kwa dakika chache ndoto inasahau-lika, na uhalisia kutukumba kwa matakwa, wasiwasi, na majukumu yake.

Hata hivyo, kuishi kama Waktristo ni kuendelea kuishi ndoto bora zaidi: ndoto ya pumziko la sabato lisilokwisha, tunapoweza kuacha kazi zetu; ndoto ya maisha yanayoleta maana na pale yasipoleta maana, amani na uaminifu wa kuishi katika siri; ndoto ya maisha ya kuishi katika ukum-batiaji wa upendo daima.

“Ndoto” hii ni muhimu sana hivi kwamba lazima tujitahidi kila wiki—kwa uabudu, sala, kusoma andiko takatifu—kuikumbika. Hizo zote ndizo maana za neema: mazoezi ya kutusaidia kukumbuka kuwa “uhalisia” wa mzigo- baadhi ya majukumu si halisi kama ilivyo ndoto.

Kisha, kama mtunga zaburi, tunaweza kucheka—kiasi kwa sababu ndoto ni furaha na kiasi kwetu binafsi kwa upumbavu wetu kwa kusahau ndoto haraka. Na haswa kwa sababu tunakumbushwa tena jinsi Mungu anapotushika, kila kitu kinageuzwa juu chini na ndani nje.

Bwana, weka katika akili yangu ndoto, na uweke moyoni mwangu furaha ya kufahamu uhalisia wake. Amina.

—MARK GALLI

Page 30: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

30 Siku 60 za Sala

Mteule Wa ...J U M A T A N O , A P R I L I 2 0 • S O M A 1 P E T E R O 2 : 2 - 1 0

Katika ulimwengu unaotangaza wengi wetu “kukokuwa wema kabisa,” inaweza kumaanisha nini kuamini kuwa kwa kweli sisi ni wateule,

tunu, na wapendwa? Katika darasa la wanachama wapya tulizungumzia ubatizo: wakati huu mtakatifu ambapo tumetajwa kwa neema ya Mungu kwa nguvu kama hiyo haitatenduliwa.

Fayette alikuwepo—mwanamke anayeishi mitaani, akipambana na ugonjwa wa akili na lupasi. Alipenda sehemu kuhusu ubatizo na anga-liuliza tena na tena, “Na nikishabatizwa, mimi ... ?” Baadaye tukajifunza kujibu, “Mpendwa, mtoto tunu ya Mungu, na mrembo tazama.” “Ndiyo!” angalisema, na kisha tungalirudi kwenye majadiliano yetu.

Sikukuu ilifika. Fayette aliinana chini, akainuka akipaza sauti, na akalia, “Na sasa mimi ... ?” Na sote tukasema, “Mpendwa, mtoto tunu ya Mungu, na mrembo tazama.” “Ndiyo!” akapiga kelele huku akicheza karibu na ukumbi wa ushirika.

Miezi miwili baadaye nilipigiwa simu. Fayette alikuwa amepigwa na kubakwa na alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya kaunti. Kwa hivyo nikaenda. Niliweza kumwona kwa umbali, akitembea mbele na nyuma kwa kasi. Nilipofika mlangoni, nilisikia, “Mimi ni mpendwa . . . ” Aligeuka, akaniona, na kusema, “Mimi ni mpendwa, mtoto tunu ya Mungu, na . . . ” Kwa kujiangalia kwenye kioo— nywele zikiwa zimesimama, damu na machozi vikidondoka usoni pake, nguo ikiwa imeraruka, mchafu, na vifungo bila mpangilio, alianza tena, “Mimi ni mpendwa, mtoto tunu ya Mungu, na . . . ” Aliangalia kwenye kioo tena na kusema, “ . . . na Mungu bado ananitendea. Ukirudi kesho, nitakuwa mrembo zaidi nitakushangaza!”

Bwana, nibatize katika maji ya neema yako ili nikumbuke daima mimi ni nani na Yule ambaye mimi ni wake. Amina.

—JANET WOLF

Page 31: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 31

Zawadi za UfuasiA L H A M I S I , A P R I L I 2 1 • S O M A H O S E A 1 1 : 1 - 1 1

Kusema kuwa Mungu anaumiza, Hosea anatupa dhana ya ajabu. Mungu Asiyeshindwa huhisi machungu. Mungu Msaniii Mchoraji, Mwandi-

shi wa Ulimwengu, huhisi uchungu wa mwanadamu kukataa kuonyesha upendo, upendo unaomsaidia na kumponya mtoto. Mungu huumia, hati-maye, kwa sababu mtoto wa Mungu anaumia na kuvutia maumivi zaidi.

Mtoto huvutia maumivi kwa kufuata miungu midogo inayoshawishi lakini inayodhuru. Ulafi, kama unavyoonekana kwa maafisa wa mashirika uliosababisha kuporomoka kwa uchumi wa 2008, ni moja ya miungu hiyo. Mwingine ni haki ya upendeleo, kama inavyotazamwa katika des-turi ya sasa ya kutoa adhabu kuu kwa ubaguzi kwa wale wasiobahatika. Mtu kutokuwa tayari kusamehe hutumika kama mungu mwingine jambo linalosababisha hukumu ya Mungu. Tendo lolote la tamaa, linalotumikia miungu ambayo inawadhulumu wengine kwa kutimiza maslahi ya kibin-afsi, linafanya kuwepo kwa hitaji ya Mungu.

Hitaji gani? Tabia hizi za kuabudu miungu zinahitaji zawadi ya ghad-habu kutoka kwa Mungu. Hasira ya Mungu inatumika zaidi kuliko jibu la wivu wa mzazi aliyedharauliwa. Hasira iliyoonyeshwa wakati wa kutendea vibaya inanyanyua hadhi ya anayenyanyaswa na kutoa ilani kuwa uonevu hauwezi na hautakukubaliwa kimyakimya. Hasira ya Mungu inataka jibu la kutetea maumivu, jibu linalokomesha matendo yasiyo ya fadhili.

Mungu anatamani upendo wetu, ili turidhiane na Mungu kwa kuwa-tendea wengine vizuri kwa upendo. Hosea anatukumbusha kuwa moyo wa Mungu huvunjika tunaposhindwa kupenda n kuw Mungu atazawidi kush-indwa kwetu kwa jibu la hasira. Ni tishio. Ni ahadi! Cha kushangaza, hata licha ya ahadi ya hasira, Mungu bado anaturejesha nyumbani. Upendo wa ajabu kweli—upendo wa kushukuru lakini sio wa kufanyiwa mzaha.

Mungu wa upendo, tusaidie tupende kama unavyotaka na ulivyodhihiri-sha. Tunaomba kwa jina la Yesu. Amina.

—VANCE P. ROSS

Page 32: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

32 Siku 60 za Sala

Dhambi, Watenda dhambi, Wasio na dhambi.I J U M A A , A P R I L I 2 2 • S O M A L U K A 1 5 : 3 - 1 0

Miezi kadhaa iliyopita katika uabudu, wakati wa kujiandaa kupokea Ushirika Mtakatifu, nilifahamu kwa uchungu kuhusu dhambi ya hivi

majuzi. Sikuhisi kuwa tayari kuacha dhambi hiyo, na niliifahamu. Hivyo nilisali, “Mungu, sistahili kupokea Komunyo asubuhi hii. . . . ” Haraka kama mwanga wa ghafla nilimsikia Mungu akisema moyoni mwangu, “Oh? Na nyakati hizo nyingine zote ambazo umekuwa ukipokea?” Nilistaajabu.

Tunastahili? Kamwe. Tumekaribishwa? Daima. Hiyo ndiyo hali ya Mungu kukabiliana nsi.

Kwa maneno ya Wesleyan, tunaita neema ya utangulizi wa ukaribisho wa kuwa tayari ya Mungu. Neema hii hutubeba kwa Mungu hata kabla hatujaamua kuanza safari. Ni Mungu anayetutongoza, kutupungia, kututa-futa.

Kwa kawaida Mungu haji katika maisha yetu kama mtaalam wa ubo-moaji, kuporomosha majengo ya zamani kwa mlipuko mmoja wenye nguvu. Hilio huenda likawa rahisi—kukwepa njia moja ya maisha pamoja na mata-tizo yake na mahusiano yaliyoharibika na kuanza upya. Lakini mara nyingi, Mungu hutubadilisha jinsi ambavyo kufungua madilirsha hubadilisha hewa chafu ndani ya nyumba—kidogo kidogo kubadilisha kitu cha zamani na kitu kipya, chenye afya, kinachovutia zaidi.

Na Mungu huendelea. Kama mchungaji aliye na wanyama walio tayari na wajinga, Mungu hutufuata katika mabonde yetu, kutuokoa ili baadaye tuweze kushirikiana katika mchakato wa kuokolewa. Tunaweza kujigamba kwa ujasiri wetu kuwa bora, lakini kuna swali msingi: Nini (nani) aliyetu-fanya kutoridhika na pale tulipokuwa? Mungu, mpenzi wetu mwaminifu. Na tunapoacha njia zinazotubomoa na kuchagua kitu kinachofaa, ni nani kiongozi wetu wa kushangilia mwenye furaha zaidi? Tena, Mungu.

Mungu, kwa neema yako inayonitafuta hata wakati nisipotaka kupatika-na, ninakushukuru. Amina.

—MARY LOU REDDING

Page 33: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 33

Wakati wa UponyajiJ U M A M O S I , A P R I L I 2 3 • S O M A Z A B U R I 3 0

Kunayo kabla na baada kila mara. Mtunga zaburi anatuonyesha maisha na Mungu kati ya kabla hii na baada. Tunatoka kwenye ukataji tamaa

hadi furaha, kutoka kwenye kujihisi kuwa mpweke, kuvunjwa moyo, na kusahauliwa hadi kuhisi kuinuliwa, kusaidiwa, na mwenye afya. Lazima tuwe makini ili tusifikirie hii kabla na baada ya maisha kama iliyosa-babishwa na Mungu kucheza nasi. Wala haitasaidia nafsi zetu kuona mai-sha kama mizunguko isiyo na mwisho wa kuendelea kuzunguka nyuma na mbele kwa mkanganyiko kati ya adhimu na ubovu.

Njia zote mbili za kuona maisha zinaendelea kutujaribu. Mtunga zaburi anatuonyesha Mungu ambaye hutembea nasi kwa wakati, anayeridhika kuwa nasi katika kila wakati wa maisha. Kabla hujaamka leo hii Mungu alikuwepo nawe, akisubiri kuingia ndani yake nawe. Kabla hujakumabana na vitu vinavyoweza kukutamausha au kukuumiza au kukufanya kuvun-jika moyo, Mungu yuko tayari kukuongoza siku nzima. Hata siku hii iki-kuelekea kwenye makosa yasiyomfurahisha Mungu na kumwumiza jirani yako, Mungu hatakuwacha lakini atasubiri toba yako na kurudi kwako tena kwenye njia ya imani.

Mungu ni Mungu wa tena na tena, ambaye anatamani kutuleta kwenye baada kila wakati: baada ya kuanguka, baada ya kutamausha, baada ya kuu-miza. Hii ni njia ya Mungu, kutuondoa kutoka kwenye ishara za kifo hadi palipo uhai. Kwa hivyo, tuna unajisiri kwa kusifu kwetu na malalamiko yetu kwa Mungu, tukijua kuwa wakati wowote tunaishi na Mungu mwe-nye ubora wa kusikia. Wakati kati ya kabla na baada unaweza kuonekana kutakuwa na mwisho, lakini kutakuwepo na baada, kwa sababu Mungu ni mwaminifu.

Bwana, nikumbushe katika nyakati zangu ngumu kwamba kulikuwa na kabla na ulikuwa nami wakati huo, na kutakuwepo na baada, kwa sababu uko nami hata sasa. Amina.

—WILLIE JAMES JENNINGS

Page 34: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

34 Siku 60 za Sala

Vigezo vya AjabuJ U M A P I L I , A P R I L I 2 4 • S O M A K U T O K A 1 7 : 1 - 7

Nina iona kuwa picha ya ajabu na isiyofurahisha: watu wa Mungu wana-gombana na Bwana. Katika tamaduni za Wakristo Ninajua—huria,

mhafidhina, na wa katikati—hatubishani na Mungu. Ni heri tulalamike kuhusu wenyewe kwa wenyewe.

Katika Maandiko Matakatifu ya Waebrania, lalamiko la Mungu ni uta-maduni unaoheshimika. Ayubu anampinga Mungu. Manabii hujaribu kup-inga mpango wa Mungu wakati Mungu anapowaita kwa huduma. Katika kifungu hiki cha Kutoka, kikundi kizima kinapaza sauti yake dhidi ya usi-mamizi wa Mungu wa kukaa katika jangwa hatari.

Sisi Wakristo wa leo tunamtolea Mungu maneno makali bila kutaka au kuuliza maswali kuhusu mpangilio wa Mungu. Katika Agano la Kale, mabis-hano na Mungu yanaashiria uhusiano halisi. Hasira hutawala mawasiliano na muunganisho wa hisia. Inachukua kanuni msingi ya uhusishaji: Hakimu atasikiliza mswada wa hasira na kutoa jibu, ikiwa si marekebisho.

Nina malalamiko machache binafsi kwa kikasha barua cha Mungu. Kwa nini tunaonekana kuunganishwa kwa ukabila, uaminifu mchache badala ya upendo wa jumla? Kwa nini mgawanyo huo hatari usiofaa wa utajiri na majanga na kuteseka na bahati (na maji ) kote ulimwenguni? Sisi ni tumefunikwa na siri.

Nilisoma kifungu hiki tena. Ninashangazwa kuwa uhusiano na Muumba wa ulimwengu unawezekana kabisa. Katika tatizo la hitaji la kila siku katika jangwa linalochemka, ukweli huu ndio ambao Waisraeli wali-kumbuka hatimaye. Kukatishwa tamaa na Mungu kulitoa njia kwa hali kubwa zaidi: huruma ya Mungu. Ni kile walichojifunza na kukumbuka, ambayo ndiyo sababu tunaiheshimu hata sasa.

Mungu Mtakatifu, ninaliita jina lako kwa shukrani. Kwa imani ninakuba-li kukutegemea. Kwa tumaini ninaomba baraka yako. Amina.

—RAY WADDLE

Page 35: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 35

MakaoJ U M A T A T U , A P R I L I 2 5 • S O M A Z A B U R I 8 4 : 1 - 4

Ulaini wa unyoya, joto la titi, kugeuka mwili wa ndege mdogo. . . . Haya hufanya kazi kwenye udongo, majani, matagaa, na kifaa muafaka

ili kuboresha kiota kwa ajili ya mama kuzama ndani, kwa ajili ya mayai kutokea ndani, kwa ajili ya watoto kuingia ndani.

Wazazi wanadamu huboresha nafasi ya kuzama ndani, kuifunika kwa rangi na maumbo ya kuridhisha; kujifukia katika moyo wa jamii inayo-tazama na kulinda wanapotayarisha sehemu ya kupumzikia kwa mtoto mchanga anayetarajiwa. Vivyo hivyo, nafasi za kivuli na utunzaji zina-boreshwa kwa watu wazee mwisho wa maisha.

Katika hali nzuri, wanadamu huboresha eneo linalotahadharisha la kiota kwa ajili ya hatari na udhaifu wao. Je, hayo ndiyo makao ya ukweli kabisa? Eneo lililoboreshwa kwa ajili ya vipande vyetu visivyoweza kukinga na vinavyoweza kuvunjika? Vipande hivyo vinaposhikwa na kuheshimiwa, tunaweza kuimba kuridhika kwetu kama kumeza katika eneo lililohifad-hiwa.

Tunaanza kujifunza kutoka kwa haya jinsi ya kuhifadhi nafsi zetu katika nyumba, altare, mkono, upendo wa Mungu. Tunaanza kuleta karibu vitu vya Mungu. Tunaanza kukaa, kugeuza, kujichimbia katika uwepo na mtu wa Mungu.

Tunapoanza kukaa na kuimba, ni vipi tunavyokumbuka wasiohifad-hiwa, walio hatarini katika mwili na roho—wale wanaohitaji nyumba, jamii, mwenza, au pumziko kutoka kwenye mapambano? Ni vipi tunavyo-lima, kuunda, kugeuza makao kwa chumba kinachotoshea wote, wakiemo wale waliovunjika karibu na ardhi inayotutisha?

Wakati mwingine hii humaanisha kuzamisha mikono yetu kwenye udongo na zege la mradi wa nyumba au kuzamisha mioyo yetu katika mae-neo yenye giza la hadithi ya mtu mwingine. Labda katika kuzamisha, katika kugeuza na kukaa, hifadhi inajengwa.

Mungu mjenga makao, tufunze kukaa ndani yako kwa kuacha na kukom-bolewa kabisa. Tupe nguvu ya kurembesha nafasi kwa ulivyo kwa ajili ya watoto na uumbaji wako. Amina.

—REGINA M. LAROCHE

Page 36: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

36 Siku 60 za Sala

Dini ya Ndani na NjeJ U M A T A N O , A P R I L I 2 6 • S O M A W A E B R A N I A 1 1 : 8 - 1 6

Sehemu ya dini ya ndani ni dira yetu ya siku zijazo kwa Mungu. Imani sio tu “kusadiki kwa vitu visivyoonekana,” pia ni “kiini cha vitu vinavyotu-

mainiwa” (11:1, kjv), kwa sababu vitu vinavyotumainiwa ni vitu ambavyo bado havijaonekana. Mwandishi wa barua kwa Waebrania anaendelea kufafanua hoja hii katika sura 11 yote kwa kutoa mifano ya wale walioishi katika tumaini la vitu visivyoonekana ambavyo Mungu alikuwa ameahidi. Abrahamu na Sara wanakuja kwanza: Abrahamu alienda sehemu ambayo hajawahi kuona; Sara alipata mtoto katika umri wake wa uzeeni, tukio jingine “la kisichoonekana” kabla.

Upande mwingine, mili na akili zetu vinakabiliana na wazo hili: Sinepsi zinajijenga katika akili zetu kwa namna ambayo mienendo na njia zetu za zamani za jinsi ya kufikiria zinafahamika na kuridhisha, na tunaona kuwa vigumu kufikiria zaidi ya vitu ambavyo tumezoea kuviona. Kwa upande mwingine, wanadamu wanafurahia kuvunja fikra potofu na mapatano. Seh-emu ambayo ni jukumu la sanaa ya kuona ni kuipa changamoto njia za kawaida jinsi tunavyofikiria, kufungua miunganisho na mawazo mapya na nafasi kwetu. Sanaa ya kuona hutusaidia “kuona”—sio tu kile ambacho ni cha kufikirika lakini kile ambacho bado “hakijaonekana”.

Sehemu ya nidhamu ya kawaida ya maisha ya kiroho, basi, lazima iwe kuona mistakabali mipya ambayo Mungu anakusudia kwetu. Hatujak-wama kwenye mzunguko milele: Tayari Mungu yupo mbele na matumaini na ndoto na mawazo mapya. Changamoto ya imani ni kuturuhusu wenyewe (kila mara!) kustaajabishwa na mipango ya Mungu ya kushangaza na kui-shi kulingana na imani hiyo.

Mungu, tupe neema, tufikirie mawazo mapya, kuota ndoto mpya, kutu-maini matumaini mapya—hata kama ulivyotuwazia, kutuotea na kututu-mainia. Na utupe neema ili tuweze kuishi kwa maono yako ya kushangaza. Amina.

—TED CAMPBELL

Page 37: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 37

Pale Ambapo Roho Anafanya KaziJ U M A T A N O , A P R I L I 2 7 • S O M A Y O H A N A 7 : 3 7 - 3 9

Vakati ambao ukosefu wa maji safi unaathiri watu wengi, picha ya mito inayotiririka ni yenye nguvu na kuhuzunisha. Kiu ni moja ya ukosefu

mbaya ambao ni vigumu sana kuvumilia—aina moja mateso ya kimwili ambayo Yesu alitaja katika saa zake za mwisho msalabani. Kuleta maji kwe-nye mashamba yaliyokauka au maji safi kwa mtu anayeaga dunia kutokana na kipindupindu kunawakilisha huduma yenye nguvu sana.

Yesu anatuahidi mito ya maji ya uzima katika nchi ya jangwa ambapo wasikilizaji wake wanajua umuhimu wake.

Yesu anamaanisha athari ya Roho Mtakatifu kwenye maisha na huduma ya wale wanaoweza kumsikia—na sisi. Roho hatakata kiu chetu tu au kutupa chanzo bila kipimo kinachodumisha maisha yetu; bali Roho “anapomwagwa” kwetu, tutakuwa mifereji ya maji ya uzima kwa wengine. Roho atatupa nguvu na kutuamrisha kustahimili zawadi za Mungu. Huu ndio utakatifu wa waamini wote ambao Luther alisisitiza: Mioyo yetu bin-afsi, kwa kugeuzwa kwa tendo la Roho itakuwa kama kisima cha chem-chemi ambapo maji kutoka kwenye chanzo cha kina yanaendelea kujazwa.

Tiririka ni kitenzi ambacho unapaswa kusita wakati wa kutafakari kifungu hiki na maisha katika Roho. Kile kinachotiririka kutoka kwetu huja licha la sisi wenyewe. Tunaifungua njia, na maji yanafuata mkondo wake kupitia vilima na mabonde na maeneo yenye miamba ya maisha yetu hadi ndani ya nafasi zilizo wazi ambapo wengine wanaweza kuyafikia. Roho anayekuja kama upepo na miali na Neno pia huja kama maji ambayo yanapata mkondo wake kupitia ardhi yoyote, kudumu na kuvumilia vya kutosha ili kuondoa upinzaji wa itale na kutoboa mashimo katika ukuta wowote.

Gracious God, may your living water flow through us as we act as agents of your grace and bearers of your good gifts. Amina.

—MARILYN CHANDLER MCENTYRE

Page 38: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

38 Siku 60 za Sala

Pale Ambapo Mbinu na Dunia HukutanaA L H A M I S I , A P R I L I 2 8 • S O M A L U K A 2 : 2 2 - 4 0

Katika kitabu chake Anam Cara: Kitabu cha Hekima ya Seltiki (A Book of Celtic Wisdom), John O’Donohue anashiriki wazo la hadithi fupi aliyotumai

kuandika: dhana kwamba katika safari ya maisha yetu yote, tutakutana na mtu mwingine mmoja tu. Wazo hilo linazua maswali mazito. Ikiwa tutaku-tana na mtu mmoja tu, tutajiandaaje? Ni desturi zipi ambazo tutazifanya ili kuwa tayari kwa hali kama hiyo?

Katika somo la leo tunakutana na watu wawili ambao wameyatoa mai-sha yao kwa ajili ya maandalizi ya aina hii. Simioni na Ana wameelekeza maisha yao yote kwa kusubiri, kujitayarisha kwa ajili ya Mmoja waliyem-jua atakuja. Wakati Mariamu na Yosefu wanamleta mtoto Yesu Yerusalemu ili kumwasilisha katika Hekalu, Simioni na Ana wapo hapo: Simioni, kwa kuvutwa na Roho Mtakatifu “ambaye alitua kwake”; Ana, mbaye ameishi maisha yake mengi kwenye Hekalu—mahali patakatifu. Kwa kujifunza kwa muda mrefu kusubiri, Ana na Simioni wamejiandaa kabisa ili wanapom-wona mtoto ambaye Mariamu na Yosefu wanamleta, kila mmoja wao amt-ambue Yesu. Miaka yao ya matarajio yamefika mwisho. Kusubiri kunatoa njia ya kukaribisha kwa kuwa wanamsalimia kwa baraka na furaha.

Kristo anatuita kwa aina hii ya matarajio. Ni vipi tunavyojiandaa wenyewe ili, kama Ana na Simioni, tutamtambua Kristo anapojitokeza kwa watu wanaopita njia yetu? Ni vipi tukavyojiandaa kumkaribisha kwa njia zote atakazojitokeza?

Macho yako yafunguke ili uone uso wa Kristo; masikio yako yafunguke ili usikie sauti ya Kristo; moyo wako ufunguke ili umkaribishe Kristo; mikono yako ifunguke ili umbariki Kristo kwa kila mmoja unayekutana naye.

—JAN L. RICHARDSON

Page 39: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 39

Tembea juu ya MajiI J U M A A , A P R I L I 2 9 • S O M A M A T H A Y O 1 4 : 2 8 - 3 3

Jibu la Petero lenye msukumo lakini la ukweli kuhusu kutokea kwa Yesu katika dhoruba linafanana na yale yote tunayojua kumhusu. “Niruhusu

nitembee juu ya maji kama ulivyofanya na nije kwako” (ap). Jibu lake la mwanzo limejaa ukweli. Macho yake hayatazami chochote ila Yesu. Kisha Petero anatambua uhalisia wa hali ambayo inamzingira, na moyo wake unashikwa kwa mkono baridi wenye woga. Badala ya kumwangalia yule aliyekuja kuokoa, Petero amelemewa na wazo la kile ambacho kinweza kuwa kikimtendekea. Ujasiri na uaminifu vinatoweka huku woga na shaka vikiongezeka ndani yake. Ni mkono wa Yesu tu wenye nguvu unaomwan-doa kwenye machafuko na kifo cha maji.

Mimi na wewe tumekuwa katika ziwa hili mara nyingi. Ikiwa hatu-jawahi kuwa, lazima maisha yatatupeleka huko. Wakati mwingine ni katikati tu ya upeo katika maisha yetu ambapo tunaweza kuelewa tunzo la Mungu kwetu. Lakini nyakati hizo—kifo cha mpendwa, kuteseka kwa mtoto, maumivu ya maadili ya kushuhudia dhuluma na unyanyasaji kuto-chukuliwa hatua, ahadi zisizotimizwa—ni thabiti na halisi kabisa. Sisi, kama Petero, tunayaondoa macho yetu kwa sadaka ya Mungu ya wokovu, na tunazama kama mawe.

Mungu hataki zaidi isipokuwa kutukomboa kutoka kwenye mambo ya binafsi na kutuweka huru kutoka kwa adui walio ndani yetu. Yule aliyekuwepo wakati wa uumbaji upepo na mawimbi na anayejua woga na mashaka yetu anasalia kuwa mtawala juu ya bahari na mleta neema. Kwa hivyo tunapomruhusu Mungu aje kwetu na kujikubali kuenda alipo Mungu, upepo unatulizwa na tunamjua alivyo—Mungu pamoja nasi.

Bwana tusamehe mashaka yetu, madogo na makubwa. Wakati dhoruba zinapotisha usiku, yaweke macho yetu kwako pekee. Amina.

—IMEKAMI LIKA. SALIERS

Page 40: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

40 Siku 60 za Sala

Biashara HatariJ U M A M O S I , A P R I L I 3 0 • S O M A R U T H U 4 : 1 3 - 1 7

Mungu hufanya jambo la hatari katika hali nyingi zisizowezekana, akiweka historia yote ya mwanadamu kwa wajane wawili wasio

na nyumba—mmoja mzee na aliyepitisha umri wa watoto, na mwingine mgeni. Mungu anakuja maishani mwetu kama asiyeonekana, uwepo usi-osikika, akituita kuhatarisha yote kama Mungu anavyohatarisha yote.

Hatari ya wanawake inaleta faida; wanalinda mistakabali yao Boazi anapomchukua Ruthu kuwa mke wake. Boazi pia anachukua hatari. Anaji-unga na mwanamke ambaye tayari alikuwa ameolewa, ambaye si wa nchi yake wala kulelewa katika imani yake.

Watu katika hadithi—Naomi, Ruthu, na Boazi— wanaingia katika uhu-siano wa hatari, lakini kuzaliwa kwa mwana kunaonekana kuthibitisha hekima ya kufanya jambo lenye hatari. Kama wanawake wa kijijini wana-vyofahamu, Obedi ni ishara ya baraka ya Mungu, yule ambaye atarejesha maisha ya Naomi, kumtunza uzeeni, na kuthibitisha thamani ya mkazam-wana.

Tunafahamu kuwa mtoto huyu, aliyezaliwa kwa muungano usio na uwezekano, ni uhusiano unaoendelea wa mtoto mwingine, yule ambaye atatoka kwenye muungano usio na uwezekano kabisa wa yote, yule wa Mungu na mwanadamu. Kupitia Obedi, Mungu anajenga nyumba ya Daudi, nyumba kubwa ya kutosha kujumuisha aliyetengwa, mgeni, mtenda dhambi, mhanga, aliyevunjika moyo: “Na Salmon [alikuwa] baba wa Boazi kupitia Rahabu, na Boazi baba wa Obedi kupitia Ruthu, na Obedi baba wa Yese, na Yese baba wa Mfalme Daudi” (Mat. 1:5-6).

Ni shughuli ya hatari kuamini wokovu wa ulimwengu kwa fukara na asiyeweza kujitetea. Ni shughuli ya hatari kuacha kil kitu mikononi mwa wanawake na watoto. Lakini hilo ndilo haswa ambalo Mungu amelifanya.

Tafakari kuhusu pale ambapo Mungu anafanya jambo la hatari na maisha yako. Utajibu vipi?

—MARTHA HIGHSTREET

Page 41: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 41

Mwito, Ahadi, JibuJ U M A P I L I , M E I 1 • S O M A K U T O K A 3 : 1 6 - 1 8

Hap Kutoka inarekodi mwito na ahadi ya Mungu kwa Musa na vion-gozi wa Israeli, mwito wa kuondoka Misri na na ahadi ya kuongoza

Israeli hadi nchi bora, kwa njia ya Mungu. Mwito unatokana na upendo na huruma ya Mungu. Paji la upendo wa Mungu litatubadilisha daima, iwe ni kwa misukumo ya ndani au kwa matukio ya nje, kubadilika, kukua.

“Nimeamua kuwa nitawaleta Misri” (Gnt). Misri wakati fulani ulikuwa wokovu wa Waebrania, wakati watu wa Mungu walipoitwa Misri kuo-kolewa kutokana na njaa wakiongozwa na Yosefu. Lakini sasa, kwa sababu ya Waebrania walikua wameongezeka na kuwa tishio Misri, waliishi kwa ukandamizwaji. Ulikuwa wakati wa kuacha hali ambayo wakati fulani ili-kuwa imeyaokoa maisha yao. Kwa hivyo Mungu aliwaita kwenye maisha mapya, kwenye nchi mpya “inayotiririka maziwa na asali” (Kutoka 3:8).

Kama Israeli, kanisa na kila mmoja wetu ni sehemu mahujaji. Mungu anatuita kwenye hatua moja ya maisha; tunapokomaa hapo, Mungu ana-tuita kwenye hatua nyingine. Ili kuendelea, inatubidi tuache kile amba-cho wakati fulani kilikuwa wokovu wetu. Je, kukataa kubadilika na kukua kunaashiria kukataa mwito wa Mungu, upendo wa Mungu kwetu? Mungu anatuita mara kwa mara kwenye maisha mapya na ukombozi, ndani na nje: “Mahali palipo na Roho wa Bwana, pana uhuru” (2 Ko. 3:17).

Mungu ananiita wapi sasa? Mungu anakuita wapi? Ahadi ya maisha mapya ipo wapi? Ni mienendo ipi ya zamani, njia za zamani, mahusiano ya zamani, uraibu wa zamani unatushika mateka? Lazima tufanye nini ili kuwa huru kutokana navyo, kuenda kwenye maisha mapya?

Roho Mtakatifu, niongoze. Fungua akili yangu na uimarishe moyo wangu ili niweze kuona mahali unaponiita sasa na niwe na ujasiri wa kujibu. Amina.

—THEODORE TRACY

Page 42: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

42 Siku 60 za Sala

Uhusiano Unaofaa na MunguJ U M A T A T U , M E I 2 • S O M A Z A B U R I 1 : 1 - 4

Hatuna amani hadi tuingie katika uhusiano wa kweli na Mungu, uhu-siano wa viumbe hai na maisha ya uzima. Tusipofika mahali hapo,

huenda tukahisi tusiotulia, wasiwasi, na kutoridhika katika safari ya nafsi yetu.

Zaburi 1 inaelezea uhusiano unofaa na Muumba kama mti uliopandwa kando ya mto. Mizizi inasonga palipo maji kawaida, kwa uthabiti. Ardhi yenye rutuba na maji inazaa mimea na miti mizuri.

Tunapoyaangalia maisha yetu, wakati mwingine tunajiona katika pam-bano la juu ya kilima na kuipata hali kuwa ngumu. Tunahisi kung`olewa na hatarini. Maisha yetu hayafanywi upya lakini kunyauka. Israeli inaji-pata mahali kama hapo. Mungu amefanya agano na Israeli. Israeli inajribu kusalia katika uhusiano mtakatifu na Mungu Muumba, na manabii wake wanahimiza kutotengwa tena na Mungu. Hata ingawa Waisraeli wamepo-tea kutoka kwenye uhusiano wao wa mwanzo, wanaamini kuwa neema ya ukombozi wa Mungu itapatikana kama nguvu ya urejeshaji.

“Mwenye furaha ni mtu amabye hakutembea katika shauri la waovu, na katika njia ya watenda dhambi hakusimama, na katika kiti cha wenye dhihaka hakuketi; bali mapenzi yake ni katika sheria ya Bwana, naye hui-soma sheria yake kwa sauti ya chini mchanana usiku.” Mbarikiwa ni yule anayetafakari sheria ya Bwana na kwa uaminifu kufuata uhusianao unaofaa na Mungu. Mbarikiwa ni yule anayetamani uhusiano wa kweli na Mungu.

Kwenye safari ya maisha yetu, tunaweza, kama miti iliyopandwa kando ya vijito, kuzamisha mizizi yetu ndani ya maji ya uzima. Kisha tunaweza kuzuiwa katika Roho wa Mungu na kuzaa matunda kwa amani.

Mungu Muumba, tufanye tuwe baraka kwenye dunia hii yako na vyote vili-vyo ndani yake. Tunatamani kuzaa matunda kwa neeema na wingi wako. Amina.

—HEE-SOO JUNG

Page 43: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 43

Kutambua Mwito wa UfuasiJ U M A N N E , M E I 3 • S O M A K U T O K A 3 3 : 1 8 - 2 3

Uhusikaji unatangulia nia. Kabla ya nia ya kina na ya kweli kutolewa, lazima tufanye jambo dogo la hatari ya kujihusisha. Kusubiri hali itu-

fikie kabla hatujachukua hatua muhimu za kwanza za ufuasi kunaweza kumaanisha maisha yenye uchoshi na fursa zilizopotezwa. Mwana wa kwanza mwanzo anasema la kwa mwito wa ufuasi.

Hali haimfikii. Hana nia. Baadaye, anatubu. Labd hali bado haijamfikia, lakini anahisi anapaswa kuifanya awe anahisi kufanya hivyo au la. Anaji-husisha, na ni inajitokeza baadaye. Hisia na hali zake zinafuata kutokana na matendo yake.

John Wesley aliandika kuwa alienda “shingo upande” kwenye mkutano uliokuwa Aldersgate Street. Hakuruhusu hali na hisia zake ziamue vitendo vyake. Alifany njia yake kuwa hisia. Alijibu wakati halisi, na mihemko yake ikafuata baadaye.

Ni mara ngapi tunakimbia fursa za ufuasi kwa sababu hatuhisi kama tunaotaka kujihusisha? Ni mara ngapi tumesema shingo upande ndiyo ila tu kugundua baadaye jinsi shughuli kama hiyo ilivyokuwa muhimu kwetu?

Mungu mwenye nguvu na neema, tusaidie kukufuata kwa imani sio tu wakati hali au tukio linapotupata bali nyakati zote. Amina.

—THOMAS R. HAWKINS

Page 44: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

44 Siku 60 za Sala

Chagua Maisha Kwa Moyo WoteJ U M A T A N O , M E I 4 • S O M A M A T H A Y O 5 : 1 7 - 2 0

Kutimiza sheria na manabii ni kuchagua maisha kwa moyo mmoja; kunahusu kufanya na kufunza. Mtu yeyote ambaye amewafunza wen-

gine hutambua kuwa tunajifunza zaidi tunapofunza kitu kuliko tulivyowahi kufikiria inawezekana. Hili linaweza kuwa na ukweli kiasi gani katika kufanya na kufunza amri za wema zinazopatikana katika sheria na manabii?

Lakini Yesu anahitaji kitu kingine kwa wale ambao “wataitwa wakuu katika ufalme wa mbinguni.” Anawaelekeza wafuasi wake kwa wema unaopita ule wa waandishi na Wafarisayo. Anaturudisha nyuma ya amri za kisheria na ufasiri wazo kwa makusudio msingi ya Mungu kwa ajili ya bin-adamu. Wema ambao Kristo anautaka ni kwa msingi wa mapenzi ya Mungu yenye upendo na haki kwa wote.

Kauli hii mpya ya hali ya zamani sana inamaanisha nini kwa maisha yetu?

Inamaanisha sio haswa kufanya zaidi lakini kujihusisha zaidi na mapenzi ya Mungu.

Inamaanisha kutafakari kuhusu dhambi yako binafsi kabla ya kutoa hukumu, neno la kukwaza mwingine.

Inamaanisha kuimarisha, sio kudunisha, jamii ya watu wa Mungu.Inamaanisha kuchagua maisha kupitia mifuatano ya vifo vichache vya

ubinafsi.Wema mkubwa hautokani na kufuata jambo la kawaida bali kwa kue-

ndeleza ahadi ya uhusiano wa agano na Mungu na wanadamu kwenye safari. Ni kupitia uchungu na furaha, mizigo na baraka za amri za kumpenda Mungu na jirani.

Unanionyesha, Mungu, kinachohitajika kufuata katika njia ya Yesu. Ni-saidie kuishi njia hiyo ya upendo leo. Amina.

—BARBARA B. TROXELL

Page 45: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 45

Wajumbe wa MunguA L H A M I S I , M E I 5 • S O M A L U K A 1 : 6 7 - 7 5

Zekaria hakimii tena. Kipindi chake cha kimpya kilitoa wakti wa kui-marisha roho ambapo alifahamu shughuli ya Mungu katikati yake.

“Kwa kujazwa Roho Mtakatifu,” anazungumza kwa sauti unabii kuhusu mwana wake, Yohana. Unabii unaanza kwa kumtangaza Mungu kama chanzo ambacho kimewezesha wakati wa sasa kuwa wenye furaha na anay-elinda mustakabali wa watu kwa “maarifa ya wokovu.” Zekaria anakum-buka matendo makuu ya Mungu: Mungu aliwakomboa watu, akamleta mwokozi mkuu, akazunguma kupitia manabii watakatifu, akaokoa watu kutoka kwa adui zao na kuepuka madhara yoyote. Kukumbuka yaliyopita ni tendo la roho ambalo linapata maana ya uhusiano wa sasa na Mungu. Kukumbuka yaliyopita kunazua msingi wa tumaini la mustakabali.

Zekaria, kama mjumbe wa Mungu, msafiri wa wakati. Ili kuongoza na kuhakikishia kizazi chake, anaingia katika mambo yaliyopita kupitia kukumbuka na mustakabali kupitia maono ya unabii. Katika kusikiliza ujumbe, tunasafiri katika historia ya siri, na tunasafiri mbele kwa mustak-abali unaokusudiwa sisi. Katika mustakabali huu tunamwabudu Mungu kwa uhuru, bila vitisho na unyanyasaji—mustakabali ambao tunaweza kikamilifu kuishi “katika utakatifu na wema.” Ni vipi tunavyoweza kuji-andaa kutambua na kukumbatia mustakabali huu? Labda kutafakari kuwa-sikiliza wajumbe wa Mungu katika kikao cha binafsi cha kimya kutapanua maono yako ya kiroho na kuongoza miguu yako “katika njia ya amani.”

Mungu, unajua matamanio ya mioyo yetu ya kupitia hali ya sasa na baa-daye unayotukusudia. Tuweze kutambua ujumbe wako na kukaa katika urafiki wako. Amina.

—LUTHER E. SMITH JR.Baraza la Maaskofu linaanza kukutana leo kabla ya Kongamano Kuu

2016. Tafadhali washirikishe wanachama wa baraza katika sala ili kazi yao ifanywe vizuri na kwa upendo.

Page 46: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

46 Siku 60 za Sala

Safari ya WafuasiI J U M , M E I 6 • S O M A L U K A 1 0 : 1 - 1 1

Lazima wafuasi sabini walihofu Bila onyo, Yesu anawatuma ulimwen-guni kuanza huduma yao.Katika njia nyingine, ni kile ambacho wafuasi wametamani. Kwa

kweli baadhi yao wamekuwa wakifikiria, ninataka kuwa kama Yesu. Nina-taka kufanya mambo anayofanya. Lakini ni jambo tofauti kuwa na mawazo hayo na jingine tofauti kabisa kuyatenda. Sasa wakati wa kutenda umefika. Hawawezi tena kukaa, kutazama Yesu akifunza na kufanya kazi za nguvu. Ni wakati wao wa kuchukua hatua. Kama kwamba hilo halikutosha, Yesu anaongeza jambo: Usibebe chochote.

Tungalikuwa na wakati mgumu kufuata mwelekeo wa Yesu leo. Katika maisha yetu ya kila siku, mkazo wetu kwenye ratiba, mipango, na kumiliki mali kunaacha nafasi ndogo ya kusikia jinsi Mungu anavyotaka kututumia siku hiyo. Au kwa ziara za dhamira, tutume timu za upelelezi ili kuchun-guza dhamira na kujua mahitaji yake. Kisha tupange kwa miezi, tukiku-sanya vinavyosambazwa ambavyo vitatimiza hitaji lolote ambalo timu ya dhamira inaweza kukumbana nayo. Ikiwa muhimu kwa jitihada nyingi za dhamira, fikiria uwezekano wa kuhusisha dhamira na kufuata mweleko wa Yesu: Usibebe chochote.

Usibebe chochote. Maneno haya yanatualika wakati wa kuinamia mikono ya Yesu anayesambaza mahitaji yetu. Usibebe chochote. Hii inatukumbusha kuwa nguvu yetu haitoki kwenye mali au kupanga lakini kutoka kwenye imani na ukweli wetu kwa Mwana wa Mungu aliye na nguvu mkononi mwake.

Bwana wa upendo na nuru, tukomboe kutokana na mitego ya mali na kutegemea bidii zetu binafsi zinazotuzuia kuingia katika neema na nguvu zako nyingi. Tusaidie kukupenda na kukuamini kikamilifu na kuupenda upendo huo ulimwenguni. Amina.

—CHANEQUA WALKER-BARNES

Page 47: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 47

Mungu Anapokuja Kwetu!J U M A M O S I , M E I 7 • S O M A I S A Y A 6 : 1 - 8

Katika somo la leo tunaangazia mwito wa Mungu kwa Isaya: “Kisha nika-sikia sauti ya Bwana akisema, ‘Nitamtuma nani, na nani atakayeenda

kwa ajili yetu?’” Maneno hayaonekani kusemwa na Isaya, lakini Isaya anaweza kuyasikia. Kwa sababu kaa lenye moto limeichoma midomo yake michafu, na kuficha dhambi yake na kuondoa hatia yake, Isaya anasikia sauti ya Mungu! Hata hivyo, anajibu “Mimi hapa; Nitume mimi!” Tunaijua hadithi yote kutoka aya zinazofuata: Mungu anamwita Isaya na kumwam-uru awaambie watu wa Yuda kuhusu uharibifu unaokuja. Isaya anapaswa kusema Ujumbe ambao hawatahadhari hadi nchi iharibiwe “iwe ukiwa” (6:11).

Mungu anapokuja kwetu, Mungu hutuita kuenda ulimwenguni. Tunaogopa kaa linalochoma na kazi ngumu. Tunahisi kulemewa; tunakata tamaa. Hatuwezi kuyarekebisha maisha yetu binafsi. Ni vipi tunvyoweza kusema Mungu, “Mimi hapa; Nitume mimi”?

Tunaweza kujibu ombi la Mungu kwa kukubali kwa sababu katika utakaso wa Mungu, Mungu huondoa woga wetu, upinzani wetu, ulemavu wetu; tuna kazi pekee na magumu yake—na tuna nguvu ya Mungu kwa ajili ya kazi. Tunapomshuhudia Mungu, Mungu anatusukuma katika kazi ngumu: kuwalisha wenye njaa, kuwafariji wagonjwa, kuwatembelea wafungwa, kupinga unyanyasaji, kuhubiri neno.

“Mimi hapa; nitume mimi.” Tunastahili kuenda kwa Mungu na kupi-tia moto unaoondoa dhambi yetu ili tuweze kuisikia sauti ya Mungu na kumjibu Mungu vizuri. Mungu hutuwezesha kujibu, “Mimi hapa; nitume mimi.” Kuweza kujibu na kutenda ni zawadi kutoka kwa Mungu na huleta amani.

Mungu mkombozi, tunataka kukuona, kuisikia sauti yako. Tunatambua hitaji kubwa ulimwenguni. Kwa neema yako tutajibu, “Mimi hapa; nitume mimi.” Amina.

—N. SUE VAN SANT PALMER

Page 48: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

48 Siku 60 za Sala

Mwili wa KristoJ U M A P I L I , M E I 8 • S O M A M A T H A Y O 1 0 : 4 0 - 4 2

Wafuasi huenda na machache, hivyo hawatategemea uzuri wa wengine ili kuishi. Hawawezi kuwa machagu wa chakula au malazi; watakub-

ali chochote wanachopewa kutoka kwa yeyote atakayewapa.Hatupendi kuwategemea wangine. Haswa kwa tamaduni au familia zin-

azopenda ujitoshelezaji, kupata ukarimu kunaweza kuwa kugumu kuliko kuuonyesha. Kuwapa wale walio na kidogo kunatufanya tuhisi vizuri. Kuwa wale wenye haja, haswa tusipoweza kutoa chochote kwa malipo, huipa chongamoto mioyo yetu ya kujitegemea na yenye majivuno.

Kama Yesu anavyowaamuru wafuasi wake, anatoa ahadi ya ajabu: “Yeyote anayekukaribisha ananikribisha mimi, na yeyote anayenikaribisha mimi anamkaribisha aliyenituma.” Kana kwamba anadunisha wasiwasi wa kutegemea wengine, anaahidi kuwa watakuwa mbele ya Mungu katika Kristo kwa wale wanaowapokea.

Kwa mwaka mmoja baada ya chuo kikuu, niliishi na kufunza katika nchi nyingine. Kuanzia wakati nilipowasili, wanafunzi wangu na familia zao walinionyesha ukarimu mwingi kupita kiasi. Sikuwa na chochote cha kuwapa isipokuwa uwepo na shukrani zangu, lakini niligundua kuwa labda hilo lilitosha.

Kipindi hiki cha mwisho ni kigumu na chenye furaha. Ingawa tuna-hisi kuridhika kuonyesha ukarimu, kujitolea kwetu kupokea kwa neema ni zawadi. Kama wageni wanyenyekevu, tunaweza kuwa uwepo wa Kristo kwa wale wanaotukaribisha. Tunatoa fursa ya kuwa baraka na kubarikiwa. Jamii zetu zinapojifunza kutoa na kupokea, tunakuwa mwili wa Kristo.

Mungu wa neema, asante kwa njia ambazo umetubariki kupitia kwa wen-gine. Tunaomba kupokea kile ambacho wengine wataweza kutoa ili tuwe uwepo wa Kristo katikati yao. Amina.

—BETH LUDLUM

Page 49: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 49

Wakati wa DuaJ U M A T A T U , M E I 9 • S O M A 1 W A K O R I N T H O 1 : 3

Nikiwa mchungaji, nimehisi daima kubahatika kutoa baraka, au dua, kwa watu wa Mungu. Wakati huo ninajua ninashiriki katika ibada ya

zamani kama imani ya Kristo, maneno ambayo, kwa njia moja au nyingine, yamekuwa sehemu ya uabudu wa Wakristo tangu kuzaliwa kwa kanisa. Zamani, niliamua kushiriki bahati hiyo: Niliwahimiza waumini wa muun-gano wangu kusema dua pamoja. Huku watu wetu wakiwa wameshikana mikono, kuwasiliana kwa macho, na kusemezana maneno, wakati wa dua umekuwa wakati roho mwenye nguvu sana.

Hivi ndivyo jamii inavyopaswa kuwa. Dua inakuwa sala kwa kila mmoja wetu, wakati wa kumtakia kila mmoja zawadi yenye thamani sana ambayo maisha yanaweza kumpa—zawadi ya Mungu.

Kila mara tunahatarisha imani yetu kuwa kozi ya kujiimariha au mfumo wa imani au njia ya kuufanya ulimwengu kuwa eneo bora. Yote haya yanaweza kuwa sehemu ya imani; lakini moyoni mwake, imani ina-husu kumpokea Mungu. Yesu alikuja kutupa uhusiano na Mungu aliye hai anayekuja kwetu kama Baba/Muumba, kama Mwana/Mwokozi/Bwana, na kama Roho Mtakatifu/Mfariji. Zawadi za neema na amani ambazo Paulo anazungumzia zinatoka kwenye uhusiano huu hadi ndani ya maisha yetu, na kutufanya kuwa tofauti.

Ulimwengu una salamu zake binafsi. Watu husema, “Uwe na siku njema”—ombi la upole. Wakristo husema, “Uwe na neema na amani ya Mungu”—zawadi wa wokovu. Tunatoa zawadi hii isiyo ya kawaida na ya kifikra kwa kila mmoja wetu katika dua. Hamna anayeweza kutoa neema na amani tunayotoa ila Mungu. Hamna anayeweza kuitafakari ila Yesu. Hamna anayeweza kuidumisha ila Royo Mtakatifu.

Tumia dua ya Paulo kama zawadi yako kwa wote wale unaokutana nao leo.

—PETER J. STOREY

Page 50: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

50 Siku 60 za Sala

Kama TulivyoendaJ U M A N N E , M E I 1 0 • S O M A M A T H A Y O 2 8 : 1 6 - 2 0

Rais wa Barazaa la Maaskofu, ninawakribisha wasomaji wa Siku 60 za Sala za The Upper Room kwa ajili ya Kongamano Kuu 2016. Sala na

msaada wenu wa kiroho ni muhimu kwetu sote tuliokusanyika hapa Port-land, Oregon. Kwa pamoja tunaweza kukumbuka kile ambacho wanaume na wanawake Wakristo, vijana na wazee, kote ulimwenguni wamefanya ili kutuletea injili ya Yesu Kristo. Kwa sababu wameenda kwa utiifu wa amri ya Yesu ya nenda—kuwafanya wafuasi, kubatiza, na kuwafunza kutii kila kitu ambacho Yesu alifunza kwa maneno na vitendo, tupo hapa leo.

Kwa sababu wafuasi waaminifu wa Yesu wameenda “ulimwenguni kote,” tunakusanyika hapa kutoka ulimwenguni kote. Tunakusanyika kama jamii ya ulimwengu wa waamini kwa sababu ya uaminifu wao.

Mungu wetu ni Mungu mmishionari anayewatafuta na kuwaokoa wale waliopotea. Muungano wa Methodisti ulianza kwa dhamira ya John na Charles Wesley huko Amerika Kaskazini. Sisi ni wamishionari. Tunaenda kwa jibu la imani kwa amri ya Bwana wetu ya “nenda na uwafanye wafuasi.”

Tunalishwa kwenye meza ya Bwana wetu. Katika utamaduni wetu wa Wesley, hii ni meza iliyo wazi. Wote wanakaribishwa: vijana na wazee, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini, kutoka kwa walio duni zaidi hadi wa wakuu zaidi. Kwa Kristo sisi ni watu wamoja, mwili mmoja, kasina moja. Tunashiriki tumaini moja, imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja, dhamira moja.

Tunahusika kwa ndani zaidi katika dhamira ya Bwana wetu. Hatuwezi kuanguka na hatuwezi kuacha. Kwa nini? Kwa sababu Bwana wetu anatu-hakikishia, “Nipo nanyi daima, hadi mwisho wa nyakati.”

Bwana Yesu Kristo, tuongoze, tulishe, tutume—kwa watu wote katika seh-emu zote. Amina.

—WARNER BROWN

Page 51: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 51

Nenda na UtangaeJ U M A T A N O , M E I 1 1 • S O M A M A T H A Y O 1 1 : 2 - 6

Katika wakati wa vyombo vyetu vya habari vya kutilia chumvi mara ningi ninahisi kuwa maswali yanayoweza kuusaidia umma kush-

iriki katika mjadala wa umma na kufanya maamuzi ya busara badala yake yanakusudiwa kuaibisha au kunasa. Yesu hakupinga mbinu hii— haswa kutoka kwa viongozi wa dini ambao walitaka kwa hamu kubwa sana kum-wonyesha kama laghai.

Ilhali maswali yanaweza kuzua mawazo na dhana mpya. Uchunguzi wa kweli unaokusudia kuondoa maarifa na utta huwa jambo zuri daima. Hivyo swali katika maandiko ya leo ambalo Yohana Mbatizaji wa wafuasi alim-wuliza Yes ni lile linalomruhusu Yesu kufafanua, kupanua maarifa, na kuhi-miza imani: “Wewe ndiwe unayetarajiwa kuja, au tunapaswa kumsubiri mtu mwingine?” Yesu anajibu kwa kurejelea matendo yake kwa niaba ya vipofu, walemavu, viziwi, wenye ukoma, maskini, na na hata wafu. Jibu lake ni la huruma lakini imara. Ikiwa Yohana na wafuasi wake hawana uhakika Yesu ni nani, sasa wanajua.

Yesu, kwa kweli, ndiye yule aliyetarajiwa kuja. Lakini Yesu alikuja kwa njia na mtindo tofauti, akiwa kama mtumishi kuliko masiha, watu hawakuwa na uhakika. Yesu aliwaonyesha na anatuonyesh mtazamo wa Mungu anayefanya kazi miongoni mwa waliopotea, wa mwisho, na wadogo.

Tusithubutu kumlaumu Yohana kwa kutuma swali lake la uthibit-isho. Kumbuka, Yesu alisema haya kumhusu Yohana, “Miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake hakuna aliyejitokeza kuwa mkuu kuliko Yohana Mptizaji.” Swali halisi sasa ni hili: Ni kwa njia zipi tunautangazia ulimwengu kuwa Yesu Ndiye yule ambaye amekuja kupitia huruma yetu kwa “mdogo kati ya hawa”?

Mpendwa Yesu, wewe ndiwe njia, ukweli, na uzima. Tusaidie kukujua na kuona kitu kipya unachokifanya. Amina.

—GREGORY V. PALMER

Page 52: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

52 Siku 60 za Sala

Kuenda kwa MamlakaT H U R S D A Y , M A Y 1 2 • R E A D M A T T H E W 8 : 5 - 1 3

Ninakaa katika kiti cha daktari wa meno; yuko karibu kuanza matibabu ya shimo katika mzizi wa meno. Ninapewa nusukaputi, na daktari wa

meno anaanza.Ninafamu kuwa ni mtaalam aliyepta mafunzo anayejua jinsi ya

kutekeleza utaratibu, lakini ghafla wasiwasi unaanza. Itakuwaje endapo nusu-kaputi haitafanya kazi? Itakuwaje daktari akikasirika na kuniongeza? Ndipo nina-potambua jinsi vilivyo vigumu kuacha kudhibiti.

Ugonjwa mbaya wa mtumishi mpendwa umempeleka jemedari wa Roma eneo ambalo udhibiti unakwisha na imani kuanza. Jemedari alijua jinsi ya kutumia nguvu ya mamlaka, nguvu ya woga, nguvu ya dhuluma, na nguvu ya kifo. Ajijua majeshi yake yangeheshimu kila amri. Lakini wakati wa ugonjwa wa mtumishi wake anayeaminika, nguvu yake haina nguvu. Ndipo anapomgeukia Yesu. Jemedari anaamua kujishusha na kunyenyekea kwa mamlaka makuu, akitambua kutostahili kwake kumwomba Yesu cho-chote.

Kwa kushangaza Yesu anainyanyua imani ya unyenyekevu wa kujishu-sha wa jemedari. Na anaitaja: imani thabiti ambayo ameiona kufikia sasa.

Katika siku hizi za mwanzo za Kongamano Kuu, kifungu hiki kinatu-mika kama kikumbusho bora cha kuacha kila tamaa ya nguvu na udhibiti na badala yake kupokea aina nyingine ya mamlaka kutoka kwa Kristo kutegemea sala, unyenyekevu, na msamaha. Ikiwa tunatamani kumfuata Kristo na kutembea chini ya mamlaka yake, tuache udhibiti na kujinye-nyekeza kwake, tukiamini kuwa anajua anachokifanya.

Bwana, hatustahili wewe kuja kwetu; lakini sema neno moja kwetu na tutapona. Amina.

—CHRISTIAN ALSTED

Page 53: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 53

Unapoenda, JifunzeI J U M A A , M E I 1 3 • S O M A M A T H A Y O 9 : 9 - 1 3

Tunapoenda, tunahimizwa kujifunza njia ya Mungu ya huruma. Tuji-funze huruma vipi? Vitabu vya Daudi, katika kitabu chake Mwito wa

Sifa, kinasema kuvunjika au kuteseka ndiko kunakowafanya watu kuwa na huruma. Tunajifunza huruma kupitia hali ya kuvunjika kwetu binafsi? Au tunakuwa wahanga wenye hasira? Kujifunza huruma kunamaanisha kuwa tuondoke kwenye kuvunjika kwetu sio kama wahanga lakini kama watu wanaojali vya kutosha kujitahidi kuhakikisha kuwa wengine hawapitii hali hiyo ya kuvunjika. Mara nyingi huruma hushirikisha kipengee cha haki. Kwa nini nijali kuwa “wote” inamaanisha “wote” kanisani mwetu?

Kwa sababu ninajua maana ya kukataliwa na kanisa nilipendalo. Huku dhehebu la kanisa langu la “nyumbani” likiwa limenijenga nilivyo na imani yangu, Mungu aliponiita katika huduma yake, kanisa lilo hilo lili-ukataa mwito wangu! Sasa mimi ni mkristo wa Muungano wa Methodisti “niyezaliwa upya” kwa maana kwamba ninamtaka kila mmoja apokelewe na kanisa linalokiri neema kwa wote. Watu wengi wasio idadi hukataliwa, kuepukwa, kukanwa, na wanafanywa watuhumiwa katika makanisa na jamii zetu kwa sababu ya mbari, rangi, ulemavu, mvuto wa jinsia, tofauti za uchumi na daraja—njia zote za binadamu ambazo watu wana udhibiti kidogo au hawana udhibiti kabisa dhidi yazo. Labda umekuwa uki-pokelewa vyema, kusikilizwa, kutambuliwa, na kuhimizwa wakati wote. Ikiwa ndivyo, kujifunza huruma kunaweza kuwa kugumu.

Lakini inawezekana kuwa wewe pia umekuwa na na hali ya maisha yenye machungu ambayo yamesababisha uvunjikaji. Ni nini kilichosa-babisha uvunjikaji wako na ni vipi unavyokutia moyo kuhakikish kuwa huwatendei wengine kama wema katika siku ya Kristo walivyomtendea Mathayo?

Tusaidie kujifunza huruma, Mungu, na uruhusu mtihani wa kujifunza kwetu uwe katika njia ambazo tunaonyesha huruma kwa Mathayo wa siku yetu. Amina.

—SALLY DYCK

Page 54: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

54 Siku 60 za Sala

Kuenda kwa UjasiriJ U M A M O S I , M E I 1 4 • S O M A M A T H A Y O 2 : 1 - 1 2

Kwa imani ya taaluma yao, mamajusi kwa kujitolea wanaondoka kwe-nye starehe yao na, kwa kustaajabishwa na uangavu wa nyota mpya

wanayoona, wanaanza safari. Wanabeba zawadi bora za utamaduni wao: dhahabu, manemane, na ubani.

Kuuliza kwa mamajusi kunalazimisha Herode na washauri wake wa dini kutafuta maandiko yao binafsi.

Mamajusi wanaendelea na safari yao. Ingawa nyota inaongoza kwe-nye zizi, hawakati tamaa, kwa kuwa mtoto ni muhimu zaidi kuliko mahali. Wanainama kwa kuabudu na kusujudu na kisha, kwa kutii maelekezo ya Mungu, wanarejea nyumbani kupitia njia mpya. Safari ya mamajusi inatupa changamoto ya kuuliza maswali mengi tunapofanya maamuzi ambayo yata-athiri kanisa letu katika kipindi kijacho cha miaka minne.

Kama wajumbe tulioaminiwa kufanya kazi hii takatifu, sisi, kama mamajusi, tumejitayarisha kwa panda shuka ambazo safari yetu inaweza kuwa nazo mbele yetu?

• Tunasikiliza kwa heshima sauti za kila aina na vyeo kabla ya kufanya maamuzi?

• Tunafanya mema kama wafuasi wanaostahili na waaminifu wa Yesu Kristo ili kumtukuza Mungu Muumba wetu?

• Tunajaribu kumtafuta Mungu na kushuhudia upendo wa Kristo hata majadiliano yanapotupeleka kwenye zizi? Ni vipi tulivyo tayari kutam-bua uwepo wa Mungu katika majadiliano yetu na kujifunza kutoka kwa Mungu?

• Wakati Roho Mtakatifu anapotusukuma kwenye mweleko mpya kabisa katika majadiliano yetu, tuna ujasiri wa kutosha wa kuacha ajenda zetu na kufuata wito wa Mungu?

Mungu, huenda tukawa tayari kwa misukumo ya sauti yako ndani na ku-pitia utafutaji wetu kwa mwongozo wako. Amina.

—SUDA DEVADHAR

Page 55: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 55

Upendo na Upendo PekeeJ U M A P I L I , M E I 1 5 • S O M A W A E F E S O 4 : 2 5 – 5 : 2

Kitabu cha Waefeso ni barua ya “mduara”, kumaanisha haikuelekezwa kwenye kanisa moja maalum bali ilipitishwa kutoka usharika mmoja

hadi mwingine. Katika sura za 1–3, mwandishi anashughulika na ukweli mkuu wa imani ya Wakristo, n katika sura ya 4 mwandishi anaangazia jinsi tunavyoweza kuishi ukweli huo. Waefeso 4:25-32 (Ujumbe) unasema hivi :

• Usiseme uwongo tena.• Kuwa na ghadhabu—lakini usitumie ghadhabu yako kama njia ya

kulipiza kisasi.• Chunga unavyoongea.• Usiuvunje moyo wa Mungu.• Sameheaneni.

Kanuni hizi zina maana kwenye kiwango kimoja, lakini bado tuna-tatizika kuzifuata. Mara nyingi sana hatuwaamini wale wanaotofautiana nasi na kuamua kuamini kuwa sisi pekee tuna majibu. Tunawaogopa wale walio tofauti. Tunajijali wenyewe na tamaa zeu kwanza. Na bado, ... sikiliza:

Tazama anachokifanya Mungu, kisha ukifanye.... Mara nyingi ana-chokifanya Mungu ni kukupenda. Andamana na [Mungu] na uji-funze maisha yenye upendo. Angalia jinsi Kristo alivyotupenda. Upendo wake haukuwa wa tahadhari bali usio na mipaka. Hak-upenda ili kupata kitu kutoka kwetu bali kutupa kila kitu kili-chokuwa chake. Penda hivyo.

Mwito wetu ni wa kuishi maisha yasiyo na mipaka ya upendo unaozidi vipimo vya jamii yetu, utamaduni wetu, na ulimwengu wetu. Upendo rahisi, lakini mkubwa. Upendo usio na mipaka ambao tunajitoa sisi wenyewe kwa hiari kwa ajili ya Mungu, kwa ajili ya Kristo, na kwa ajili ya ulimwengu.

Mungu mwenye upendo, tupe mioyo ya kupenda pekee ili siku yetu inapo-kamilika na kazi yetu kwisha, ni wewe unayetukuzwa. Amina.

—DEBORAH L. KIESEY

Page 56: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

56 Siku 60 za Sala

Unapoenda, Waita WoteJ U M A T A T U , M E I 1 6 • S O M A M A T H A Y O 2 2 : 1 - 1 4

Wengi siku hizi wanashiriki wagivu kwa harusi za kifalme. Watu mamilioni walitazama wakati Binti Mfalme Diana na Mwana Mfalme

Charles walipooana. Na “watazamaji” walikutana ili kuangalia harusi ya Kate Mid- dleton na Mwana mfalme William. Ungaliamua kutojibu kwa RSVP ya kukubali kuhudhuria harusi ya kifamle?

Au hebu fikiria kutuma mialiko ila kutambua baadaye siku yenyewe ya harusi kuwa hakuna anayetaka kuhudhuria?

Hapa katika Mathayo 22 tunaye mfalme, baada ya waalikwa wote kukataa, anaamua kumwalika kila mtu aliye tayari kuhudhuria—mzuri na mbaya. Unaweza kutafakari karamu iliyojaa wanaofaa na wasiofaa? Ninaweza. Mimi na wewe tunashuhudia haya kila wakati tunapokusanyika kwenye meza ya Komunyo.

Na tuna maoni gani kuhusu yule anayekuja akiwa hajavalia inavyofaa kwenye sherehe? Unaweza kufikiria kutovalia inavyofaa kwenye harusi ya kifalme? Alikataa kuvaa joho la harusi linalotolewa na mfalme kitamaduni? Inashangaza. Au sivyo?

Ni mara ngapi tumekataa kuvaa “joho la harusi”? Unakumbuka wakati tulipofikiria tulikuwa bora zaidi yao na haikutulazimu kuvaa joho la harusi? Au wakati tulipohisi hatukustahili vya kutosha kulivaa? Ukweli ni kuwa, sote tunahitaji “joho la harusi.” Kuvaa joho la harusi kunafunika dhambi nyingi sana.

Yesu anatualika sote kwenye karamu yake—sikukuu yenye zawadi bora zaidi za neema. Sikukuu kwa wanaofaa na wasiofaa! Wazuri na wabay! Mimi na wewe! Na bora zaidi, majoho ya msamaha, upendo, na ukubalifu. Majoho ambayo yanafunika uvunjikaji wetu na kutukumbusha thamani yetu yanapatikana bila gharama yoyote kwetu sote ili tuvae.

Mwenyeji wa Neema wa yale yote yaliyo mema, tunakubali mwaliko wa karamu yako kwa neema na upendo tele. Tunasimama hapa katika majoho yetu tayari kwa sherehe! Amina.

—CYNTHIA FIERRO HARVEY

Page 57: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 57

Ili Tuwe Kitu KimojaJ U M A T A N O , M E I 1 7 • S O M A Y O H A N A 1 7 : 2 0 - 2 3

Leo, Kongamano la Muungano wa Methodisti linawakaribisha vion-gozi wa ekumeni kutoka kwenye makanisa mengine ya Wakristo kote

ulimwenguni. Askofu Ivan Abrahams, Katibu Mkuu wa Baraza la Meth-odisti Ulimwenguni (shirika la Wamethodisti 80, Mweslii, na Makanisa husika Yanayounganisha na ya Muungano yenye zaidi ya wanachama mil-ioni 80 katika nchi 133 kote ulimwenguni) atatangaza neno. Mbali na hayo, viongozi ulimwenguni kutoka kwenye ushirika mwingine wa Wakristo ikiwemo makanisa ya Eastern Ortho- dox, Baptist, Pentekoste na Kanisa Katoliki la Roma watakuwepo—wote pamoja katika uabudu na sala. Sote pamoja katika Kristo. Sote pamoja katika jibu la sala ya Yesu kwa umoja.

Umoja ni zawadi kutoka kwa Mungu. Maisha, kifo, ufufuko, na sala ya Yesu hutufanya kuwa mmoja katika Kristo. Hakuna kinachoweza kututen-ganisha kutoka kwenye upando wa Mungu ndani na kupitia Yesu Kristo. Kuna Mungu mmoja, imani moja, tumaini moja, ubatizo mmoja. Tunasadiki kwa Yesu na kuliheshimu neno lake, ambalo linatuita katika umoja. Sisi ni mwili mmoja wenye wanachama wengi—uelewa muhimu. Yesu alisema kuwa umoja wetu, ushirikiano wetu, upendo wetu wa kweli na heshima kwa kila mmoja kutawezesha ulimwengu kuamini kuwa alitumwa na Mungu.

Mwaka huu, nilipowakilisha Kanisa la Muungano wa Methodisti kwe-nye Braza la Kitaifa la Makanisa, Baraza la Makanisa Ulimwenguni, na Bunge la Dini za Ulimwengu, nilishuhudia furaha na tumaini vilivyoiinua roho yangu na kuongeza uamuzi wangu wa kuishi kwa makubaliano ya sala ya Yesu. Utajiunga nami kusali, “Ili wote wawe kitu kimoja. . . . ili ulimwengu uamini kuwa ulinituma.”

Bwana Yesu mwenye upendo, tunaweka sala yetu na yako pamoja—ili tuwe kitu kimoja—ili ulimwengu ujue kuwa Mungu alikutuma kututafuta na kutuokoa sote. Amina.

—MARY ANN SWENSON

Page 58: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

58 Siku 60 za Sala

Uovu Unaenda PiaJ U M A T A N O , M E I 1 8 • S O M A M A T H A Y O 1 2 : 4 3 - 4 5

Kupanda bustani kunahitaji mtunza bustani aandae udongo, kuondoa mimea inayoweza kuzuia ukuaji wa mmea kupandwa na kukuzwa.

Kwa ulinzi w mmea uliopo, lazima mtunza bustani alinde mara kwa mara dhidi ya kwekwe zinazoota na kutaka kuibia mimea virutubisho vinavyo-hitajika ili ikomae.

Kwekwe zinazoharibu maisha na mimea inayoimarisha maisha huota katika kikataa cha shamba lile lile ikiwa mmiliki wa bustani haitunzi kwa bidii.

Wakati wa mahojiano ya Dakika 60 na manusura wa Holocaust, Yehiel Dinur, ambaye alitoa ushahidi kwenye kesi ya 1960 ya Adolf Eich- mann, Mike Wallace alimwuliza Dinur ni kwa nini alilia kisha kuanguka sakafuni wakati wa kesi. Dinur alielezea kuwa hakutarajia hisia yake. Ingawa Eich- mann alihuisha uovu, mkabiliano huo ulimfanya Dinur kutambua kuwa dhambi na uovu ni hali ya asili ya binadamu.

“Nilihofu kujihusu,” Dinur alihitimisha. “Niiona kuwa ninweza kufanya hili . . . Mimi ni ... sawa na yeye.”

Maneno ya Dinur yaliyosemwa mika 56 iliyopita bado yanazunguka akilini leo. Ikiwa hatuwezi kuyashughulikia maisha yetu, tunaweza kuruhusu uovu kuota pale tulipokusudia utakatifu. Uovu, kama kwekwe, hutafuta sehemu ya kukaa na kustawi. Tunapoacha kuyashughulikia mai-sha yetu tunakaribishwa nyumbani kwenye maovu. Mara nyingi tunafikiri watu wengi kama Eichmann na wengine kuwa “waovu.” Hata hivyo, udhaifu wetu ni zaidi ya hatua zisizofaa bila madhara; unajenga miundo ya tabia inayoharibu. Kwekwe chache zinaweza kutawala kikataa cha shamba ambacho hakijashughulikiwa. Yesu anatuonya kuyajaza maisha yetu kwa maneno, vitendo, matukio, na watu wanaoyatakasa maisha yetu.

Bwana, nisaidie kuulinda moyo wangu kutokana na maovu machache ili uovu wowote usipate nafasi maishani mwangu. Amina.

—JAMES SWANSON SR.

Page 59: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 59

Nenda kwa Kondoo AliyepoteaA L H A M I S I , M E I 1 9 • S O M A M A T H A Y O 1 0 : 5 - 1 5

Yesu anawakataza wafuasi wake kuhubiri kwa mataifa mengine na Wasamaria na kuwaelekeza kwa Wayahudi. Kwa nini atoe agizo kama

hilo la ubaguzi wa kimbari?Kwa yeye binafsi kuwa Myahudi, huenda Yesu alitamani kwanza Waya-

hudi wapokee ujumbe wa utawala wa Mungu. Au labda Yesu anatambua kuwa nguvu na udhaifu wa timu yake ya wafuasi wachanga itazuia kuingia katika himaya hatari. Kuhubiri kwa Mataifa mengine na Wasamaria kulihi-taji sifa na ujuzi fulani ambao wafuasi hawakuwa nao kikamilifu.

Kama walimu wote wazuri, Yesu anajua kuwa huduma bora inahitaji mpango unaofaa ili iwe na athari kubwa. Kwa hivyo labda anaamua kuanza kutoka kwa wanaojulikana (Wayahudi) na baadaye kuingia katika himaya isiyojulikkana na yenye changamoto sana ya Mataifa mengine na Wasa-maria.

Na kama mtaalamu wa mkakati, Yesu najua kuwa huduma bora inam-taka aweke mbele vipaumbele vyake. Kufanya mambo makubwa kupita kiasi kunaweza kuwa hatari. Kuanza kufanya kidogo na malengo machache kunaweza kutoa suluhisho bora. Kwa hivyo anaamua kuangazia Galilaya, eneo linalojulikana vizuri.

Fahamu kuwa Yesu anachagua eneo mahususi, hivyo pia anataja malengo mahususi: Kuponya wagonjwa, kufufua wafu, kutakasa wenye ukoma, na kuondoa mapepo. Wafuasi wanapaswa kuangazia wasiojiweza na wasio na tumaini katika jamii. Katika ulimwengu wa Yesu, watu hawa wanatangulia kwenye orodha vipaumbele vya Yesu. Vipaumble vya Yesu kwa huduma havijabadilika. Wala jukumu lake kwetu. Chochote kisicho miongoni mwa hayo hakikubaliki.

Mungu wa neema, tusaidie tusiwahi kusahau kuwa tunaishi katika ulimwengu wenye machungu. Tufunze ili kuweka kipaumbele vipaumubele vyetu ili tuwafikie watu wote ambao kila siku hutafuta upendo wako. Am-ina.

—JOHN YAMBASU

Page 60: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

60 Siku 60 za Sala

Nani Ankweenda Wapi?I J U M A A , M E I 2 0 • S O M A M A T H A Y O 2 7 : 6 2 – 2 8 : 8

Unafanya nini asubuhi baada ya kusulubiwa? Ikiwa wewe ni Pilato na makuhani wakuu, unatuma majeshi kuziba kaburi kabisa! Wanapenda

Yesu afe na kuzikwa. Wanataka kukandamiza uvumi kuwa anaweza kufu-fuka kutoka kwa wafu. Wanataka kuangamiza hadithi ya tumaini ili mambo yarejee kawaida.

Siku inayofuata, Mariamu wawili wanaenda kwenye eneo lile lile kuangalia kaburi. Mathayo hatuambii wanachotafuta. Labda hawajakamili-sha kumfuata Yesu. Malaika anapoliondoa jiwe ili kutambua kaburi tupu, wanakimbia kueneza neno—hofu kubwa zaidi kwa Wafarisayo. Habari njema zaidi zisingeweza kuangamizwa tu msalabani. Yesu aliendelea kuishi kupitia maisha yaliyobadilishwa: wenye njaa walilishwa, walemavu waka-ponywa, waliopotea wakapatikana, wageni wakakaribishwa. Huwezi kuli-zuia hilo! Yesu anaishi katika jamii inayopendwa. Wafuasi wanapomfuata Yesu kupita kaburi, Yesu anaishi.

Juni iliyopita, Wakristo tisa Wafrika Wamarekani waliuawa kwa kufyat-uliwa risasi katika kitendo cha kinyama cha chuki ya kimbari. Familia za waliouawa zilifanya nini? Zilienda kutazama kaburi. Zilirejea kwenye eneo la uhalifu, kanisa. Zilimsamehe mhalifu na kumwambia aombe huruma ya Mungu, zikisema, “Itakuwa sawa.” Hivyo ndivyo wafuasi wa Yesu hufanya. Wakisimama katika kivuli cha kifo wanasimulia hadithi ya “Yesu na upendo wake.” Wanageuza chuki kuwa upendo, mauti kuwa uhai.

Popote unaposimama leo kwenye siku ya mwisho ya Kongamano Kuu, jiulize unapoelekea. Umeona nini? Utasimulia hadithi ipi? Hadithi ya mauti na laana? Au ya uzima na baraka?

Mungu, niruhusu nione maua katika jangwa na nuru katika giza ili had-ithi ninayosimulia iwe ya upendo ulio na vitu vyote. Amina.

—ELAINE J. W. STANOVSKY

Page 61: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 61

Nenda Palipo na MajerahaJ U M A M O S I , M E I 2 1 • S O M A M A T H A Y O 2 8 : 1 6 - 2 0

Sitawahi kusahau siku ambayo askofu wa kanisa aliwekea mikono yake kichwani pangu na kuniambia “chukua mamlaka ya kuhubiri Neno la

Mungu na kutoa Sakramenti Takatifu”—kunijaza ujasiri wa Roho wakati huo. Nilijihisi kujawa na unyenyekevu na wasiwasi fulani. Ninafikiri wafuasi kumi na mmoja kwenye mlima ule wa Galilaya walishuhudia mchanganyiko wa moto wa ujasiri na woga Yesu alipowapa mamlaka ya kuenda kuwafanya wafuasi wa mataifa yote.

Haikunichukua muda mrefu kujifunza kuwa mamlaka ya “nenda” hay-akuwa kwenye maneno au tendo la ishara la askofu. Mamlaka yalitokana na kuenda sehemu ambazo Yesu alienda.

Yesu alienda palipokuwa na majeraha na kutangaza uponyaji. Kama wanafunzi na wataalamu wa injili, tumepewa jukumu la kuenda kwa upendo wetu kwa wale waliosahaulika. Tumepewa jukumu la kuenda pamoja na shahidi wetu wa unabii kwa wale walio hatarini ambao injili inawaita wale haki na huruma inaonekana kuondolewa katika maisha yao.

Tumepewa jukumu la kuenda kwa huduma yetu ya kichungaji kwa wale ambao wamevunjika ambao maisha yao yameathiriwa na dhoruba na ajali za maisha au maamuzi mabaya yaliyofanywa na wengine au wenyewe. Tumepewa jukumu la kwenda kwa utangazaji wetu wenye furaha kwa wale wasio na tumaini ambao nafsi zao zimepondwa kwa kukata tamaa, shaka, mfadhaiko na kisha kuomba Roho wa Mungu kuzaliwa ndani yao.

Tunaenda, kwa hivyo, pale palipo majeraha kwa upendo wetu, sha-hidi wetu wa unabii, haduma yetu ya kichungaji na utangazaji wetu wenye furaha kwa sababu hapo ndipo Yesu alipoenda na ndipo tulipoitwa twende sasa.

Mungu mwenye neema na upendo, tusaidie kuenda wakati wote, kama Yesu alivyofanya, palipo na majeraha. Amina.

—BRUCE R.OUGH

Page 62: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

62 Siku 60 za Sala

Nifuate!J U M A P I L I , M E I 2 2 • S O M A Y O H A N A 2 1 : 1 5 - 2 3

Kushindwa, ahadi zisizotimizwa, usalati, na kukataliwa—Petero ame-fanya yote baada ya kuapa hadharani kutowahi kamwe kumkana Yesu.

Wafuasi wa Yesu humtamausha na kuacha wito wao. Wafuasi waliotoroka wamevua usiku wote na hawakuvua chochote. Magharibi yanapoingia, Yesu anawaita na kuwaambia waweke wavu upande ule mwingine wa mashua. Wanawanasa samaki zaidi kuliko kiasi ambacho mashua yanaweza kubeba. Biblia inasema kuwa hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa Yesu kutokea wafuasi wake baada ya Ufufuko. Ni muujiza wa huruma. Yesu anakuja kwao, anawaongoza, anajitambulisha kwao—kisha kunatokea maelezo ya kina ya urejesho wa Petero. Kukana mara tatu, maswali matatu, uthibiti-sha mara tatu—mchakato wa uponyaji na urejeshaji unachukua muda. Ni mchakato, wakati huo na sasa.

Sote tunahitaji ufunuo, urejesho, na mwongozo. Ilhali, ndani ya dakika chache za urejesho wa Petero na jibu lake zuri kwa amri ya Yesu, “Nifuate!” anayaondoa macho yake kwa Yesu na kuangazia tabia ya mfuasi mwingine, “Bwana, je, yeye?”

Jibu la Yesu kwa Petero “Hicho ni nini kwako?” ilinijia akilini na moyoni mwangu mwaka wa 2006 nilipouliza vitendo na tabia za wengine katika Kanisa letu la Muungano wa Methodisti. “Hicho ni nini kwako, Tom? Nifuate!” Ninaamini mwito wa Yesu kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu itakuwa sawa na Jumapili hii ya Pentekoste: “Nifuate!” Mwito wa fuata unakuja kwa kila mfuasi. Licha ya maneno na vitendo vyetu, hali yetu ya kupoteza au kupata—hakuna kilicho muhimu isipokuwa maneno haya ya Bwana Yesu Kristo, “Nifuate!”

Yesu, nisamehe dhambi zangu, na haja yangu ya kutambua vitendo vya watu wengine. Niwezeshe kuwa mfuasi mwaminifu—kuwalisha wanakon-doo wako, kuwahudumia kondoo wako, na kukufuata. Amina.

—TOM ALBIN

Page 63: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 63

Kwa hivyo, Endelea Kuenda!J U M A T A T U , M E I 2 3 • S O M A M A T H A Y O 2 8 : 1 6 - 2 0

Sa imekwisha. Mijadala, saa ndefu, kuishi kwenye chumba cha hoteli, kutamaushwa, msisimko, uabudu. Haleluya! Kongamano Kuu limekwi-

sha, na ni wakati wa kurudi kwenye maisha yetu ya kawaida. Hivi ndivyo wafuasi walivyohisi baada ya Ufufuko? Imekuwa safari ndefu, lakini ime-kwisha, hivyo sote tunaweza kurudia hali ya kawaida? Injili ya Mathayo inaakisi shaka (aya ya 17) kuwa chochote kimebadilika. Kisha Yesu ana-zunguma tena, “Nenda!”

Kwa sababu sasa ni mwanzo tu. Usafishaji, matayarisho, kuripoti, kupakua. Ndiyo, kazi hiyo itafanywa, lakini ni zaidi ya hilo. Kongamano Kuu limekwisha, na sasa ni wakati wa kuelekea ulimwenguni—kurudi kwenye jamii zetu zinazotusubiri kuona kuwa kitu kimebadilika, kwamba hali ile ile sasa ni tofauti kiasi. Tunarejea kwenye mitaa yetu iliyojaa watu wanaoumia, wenye njaa, wapweke—wanaotamani neno la tumaini, ishara ya ufufuko. Kurudi kwenye makanisa yetu ambayo yanatamani sana kusikia tena mwito wa Yesu: Mimi ni tumaini lako! Mimi ni ufufuko! Nipo hapa nawe milele, wakati wote!

Uhalisia ni kuwa tuendelee safarini Yesu Kristo. Kongamano Kuu lime-kwisha, lakini tunaendelea kufanya kazi, kutembea, kuandamana, kushere-hekea habari njema za ushindi wa Mungu juu ya mauti. Yule anayetutuma nje “kwa hivyo, nenda!” ndiye Yule anayetupa kila kitu tunachohitaji kwa dhamira hii. Yule anayetuita safarini ndiye Yule anayeenda nasi na ambaye hatawahi kutuacha. Tuendelee pamoja!

Mungu wa safari, tunashukuru kwa mwito wako na uwepo wako nasi tu-napoendelea pamoja kwenye njia ya upendo na ufuasi. Amina.

—LAURA JAQUITH BARTLETT

Page 64: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

64 Siku 60 za Sala

Komboa na UazimieJ U M A N N E , M E I 2 4 • S O M A M A T H A Y O 1 8 : 2 1 - 2 2

Katika huduma yangu kama mwanasaikolojia wa kichungaji, nimeba-hatika kualikwa katika makanisa ili kuyasaidia kuponya mgogoro

ambao umekuwepo kwa muda mrefu. Kunachotawala mengi ya mambo haya ni ukweli kuwa watu wanashikilia kikiki machungu na mifarakano ya zamani, wakiogopa kutoa hisia zao za kweli kwa wale waliowatia machungu. Badala yake, wanapaza sauti zao kupitia uvumi na kuanzisha migogoro kwa siri hadi kanisani. Mazingira salama tu yanapoptikana kwa wote kusimulia majeraha yao na kuanza kusahau machungu kutokana na ukosefu wa msamaha ndipo nguvu inapotiririka kuelekea njia ya uponyaji na utimilifu

Petero anamwuliza Yesu ni mara ngapi anapaswa kumsamehe mtu anay-emdhuru. Anatambua kuwa jibu lake la saba ni ukarimu sana na linazidi tarajio la kawaida. Yesu anamshangaza kwa kusema, “Haiwezekani, saba haitoshi! Lazima uendelee kusamehe.” Yesu pia anawaamuru kupendana.

Kwa kweli tukipendana na kujipenda, tutaacha haja yoyote ya kisasi au machungu. Tutatafuta njia ya kusuluhisha migogoro moja kwa moja na yule aliyetutia machungu badala ya kulipiza kisasi au kuharibu sifa ya mtu.

Wakati tulipokuwa pamoja kwenye Kongamano Kuu, kwa kweli migogoro ilitokea. Ni wapi unaposhikilia machungu au mafarakano? Ni wapi unapohitaji kusuluhisha suala na kaka au dada? Ni wapi, kama kanisa, tunahitaji kuponya migawanyiko ili kwa hakika tuwe mwili wa Kristo, ulioungana?

Mponyaji wa neema, tusaidie ili tusamehe kama tulivyosamehewa. Tufun-ze tuonane kupitia macho ya upendo, na utujalie ujasiri wa kusuluhisha migogoro na kuacha machungu. Amina.

—DENISE MCGUINESS

Page 65: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 65

Sala ya WauminiJ U M A T A N O , M E I 2 5 • S O M A I S A Y A 5 5 : 1 - 9

Kristo mwenye upendo unayetusubiri sote kusonga mbele, ili kubadilisha ndani, kupenda nje.Subiri sasa pamoja nami ninapotamani na kujifunza kuwa zaidi kama

wewe.Niongoze nisubiri na wale waliopotea, kusimama na wale walio wanyonge, kuwahurumia wale waliovunjika moyo. Amina.

Ombea

• wale wote wanaosubiri habari kutoka kwa waliotoroka• kwa wazazi wajawazito• kwa hekima• kwa upole kwako mwenyewe na wengine siku ya leo

—PAMELA C. HAWKINSKutoka The Awkward Season

Page 66: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

66 Siku 60 za Sala

Mchungaji Mwenye UpendoA L H A M I S I , M E I 2 6 • S O M A M A T H A Y O 1 8 : 1 0 - 1 4

Sisi Wakristo tuna tabia ya kufanya urahisi wa imani yetu kuwa yenye utata mkubwa. Tunatamani kusema kwa kina kile tunachotaka kufanya,

wakati, kwa nani, mara ngapi, na tunapoweza kuacha. Kwa Yesu, kanuni zinaonyesha tu jinsi ya kuishi imani isiyoongozwa na kanuni.

Hadithi niipendayo inahusu mwanakondoo mdogo wa kijivu. Kon-doo wengine wanamtenga kwa kuwa tofauti na, kwa kuhisi kutotakikana, anaanza kuamini kuwa hana thamani ya kutakikana. Ikiwa yeye ni mpum-bvu na asiyependeka, basi haijalishi anachokifanya. Iwe ina kwa fikra au kwa ufedhuli, hatawahi kuhitajika. Uzito huu unashuka kwake hadi siku moja anapokosa kujali tena—hivyo anaanza kutangatanga. Kadri anavyo-songa mbali zaidi, ndivyo anavyokuwa na uhakika kuwa ikiwa kondoo wale wengine watatambua, itakuwa kwa kicheko cha “ni heri hivyo.” Usiku unaingia, na giza ni totoro kuliko anavyokumbuka liliwahi kuwa. Anasikia kelele za ajabu. Anahisi baridi, njaa, na anaogopa.

Lakini wakati fulani usiku huo wenye baridi, mwanakondoo anathubutu kuamini kuwa anasikia ndani ya upepo mkali sauti anayoifahamu, sauti ya jina lake haswa. Ni mchungaji ambaye amewaacha wale tisini na tisa kwa sababu yake.

Mwanakondoo aliyepotea mwenye hofu anaogopa kuwa anakaribia kupigwa au kuwa katika hali mbaya zaidi. Lakini hakuna maneno ya hasira wala konde kutoka kwa wafanyakazi wa mchungaji. Badala yake, anamnyanyua taratibu, anamfunika kwa koti lake, na baadaye ukumba-tiaji wa muda mrefu unamweka salama kwenye mabega yake, akisema, “Nimekupeza/I’ve missed you!” Mchungaji mwenyewe anaelewa kile ina-chomaanisha kudharauliwa na kudhulumiwa. Na hivyo wanaenda nyum-bani, wakifurahia upendo na joto la kila mmoja.

Mchungaji wa wote, nishike kwa ukumbatiaji wako wenye upendo na joto hadi woga wangu upunguke. Amina.

—W. PAUL JONESKutoka Kuwa Yule Ambaye Mungu Anakutaka Uwe

Page 67: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 67

Kuchagua Uzima na MunguI J U M A A , M E I 7 • S O M A M A R K O 9 : 3 3 - 3 7

Tunamjua Marko kama mwinjilisti kwenye treni ya mizigo. Kwa kusoma tu sura yake ya kwanza bila kusita kunaweza kutuacha bila pumzi. Kabla

hatujafika hapa katika Injili, sio tu kuwa matendo mengi yameshuhudiwa bali neno limeenezwa kote mara moja. Hii si hadithi ya kukaa chini. Yesu yumo safarini—akiponya, kufunza, kupunga pepo, kulisha wenye njaa, na zaidi.

Kisha kitu kinatendeka na kuyasimamisha yote. Ni vita na Wafarisayo? Ni tatizo na Baraza la wajumbe? Ni uchovu au kukata tamaa? Ni mojawapo ya vitu hivi. Katikati ya sura ya 9, kiini cha Injii, kila kitu kinasimama kwa sababu Yesu anatambua kuwa wafuasi wake wanazunguma kuhusu ukuu wao binafsi. Yesu anakaa chini—moja ya nyakati chache katika Injili yote—na kuwafunza wafuasi wake.

Ni muhimu sana kutambua kuwa kitu kimoja ambacho kinapunguza kasi ya Injili ni ushahidi wa tamaa ya ubinafsi kwa baadhi ya wafuasi wa Yesu. Nani mkuu? Nani bora? Nani yuko juu? Nani wa pekee zaidi? Yesu alipotambua kuwa hili ndilo walilokuwa wakizungumzia, alikaa chini.

Fikiria kwa muda kuhusu kinachokufanya “ukae chini.” Ni nini kina-chokufanya uache kile unachokifanya na kumwangalia mtu yule mwingine machoni? Kwa Yesu, huenda ulikuwa wasiwasi wake ambapo moyo ule ule wa ufunzaji wake na ushahidi huenda haujaeleweka vizuri, kupuuzwa, au kusahaulika.

Yesu alikaa chini, akawaita kumi na wawili wale, na akawaambia, “Yeyote anayetaka kuwa wa kwanza lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.” Hii ni muhimu. Kwa kifupi, huu ni ufuasi.

Mungu, nipe masikio ili kusikia neno hili la Yesu. Kuanzia sasa na siku hii nzima, nipe ujasiri wa kuliishi! Amina.

—PAUL L. ESCAMILLA

Page 68: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

68 Siku 60 za Sala

Omba bila KukomaJ U M A M O S I , M E I 2 8 • S O M A 1 W A T H E S A L O N I K E 5 : 1 2 - 2 8

Cmba bila kukoma. Ni kazi ngumu. Lakini sisi hapa The Upper Room tunayatanguliza mawaidha ya Paulo katika katika yote tuyafanyao.

Kwa kujiona wenyewe kama wenyeji wa eneo ambalo ulimwengu unaku-tana ili kusali, tunawezesha wimbi la kimataifa la sala linalosafiri ulimwen-guni kila siku kama tu linavyofanya jua. Na sasa kwa kuwa siku sitini za sala kwa Kanisa la Muungano wa Methodisti na Kongamano lake Kuu 2016 linakaribia kukamilika, ni fursa yangu kubwa kukualika uendelee kusali na Wakristo kote ulimwenguni na pia utafute ukamilifu.

Nini maana ya kusali bila kukoma? Aina fulani zitakuwa tofauti kwa kila mmoja wetu kwa kuwa kila mmoja ana alama ya Mungu kwa njia ya kipekee. Lakini nia ya sala zetu inatufanya kuwa kitu kimoja. Tuna-sali ili kuunganisha mioyo na akili zetu pamoja, kujitahidi kuona kupitia kwa muda hadi milele. Tunasali ili kujiunga na mwenendo wa Mungu wa wema, haki, na amani. Tunasali ili kushiriki katika uhusiano wa ndani wa Utatu Mtakatifu, kupenda zaidi kama Mungu anavyopenda.

Kwenye The Upper Room tunaamini kuwa sala inachochea miondoko ya kila siku. Tunajitahidi sio kujiondoa ulimwenguni ili kusali bali kushona sala zetu kuwa kitambaa cha maisha yetu yanayodumu kwa muda mfupi. Tunasimama kwenye makutano ya kuwa na kufanya, kuzabuni maisha ya ndani nje na maisha ya nje ndani. Mnaporejea majumbani mwenu kote ulimwenguni, tunawaalika mjiunge nasi kila siku pale ulimwengu unapo-kutana ili kusali. Tusimulie hadithi za wale wanaofanya kazi miongoni mwenu. Pumua amani katika jamii yako ambapo pana machafuko. Wasaidie wanyonge. Sali nasi na ufahamu kuwa ulimwengu unasali pamoja nawe.

—SHAWN BAKKER

Page 69: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 69

Utambuzi katika Mwili UliovunjikaJ U M A P I L I , M E I 2 9 • S O M A L U K A 1 8 : 2 6 - 2 7

Kanisa si kamilifu. Wakati mwingine tunaomba liwe. Wakati mwingine hata tunafikiri kuwa ni kamilifu. Nyakati za Kristo akitenda kupitia

kanisa zinatufanya kushukuru kwa furaha. Nyakati nyingine kwa mac-hungu zinatukumbusha kuwa kanisa limejengwa na watu kama sisi. Sisi ni Mwili wa Kristo, kanisa. Na tunabeba kila kitu ambacho ni sisi katika kanisa. Kwa hivyo haipaswi kutushangaza kuwa mwili wa Kristo umevun-jika. Migogoro, kusimamisha ufuasi, imani dhaifu, shahidi mwoga, na ahadi inayofaa ni chipukizi ya asili ya sisi ni nani kama Wakristo binafsi.

Hata ingawa tunaweza kuliangalia kanisa katika fasiri zake mbalimbali kwa furaha wakati mwingine na fadhaa wakati mwingine, lazima tukum-buke kuwa maisha mapya yanawezekana. Mageuzi yanaweza kuanza leo. Nguvu ya ufufuko inaptikana kwetu na inaweza kuwekezwa katika kanisa sasa hivi. Kwa msaada wa Mungu tunaweza kuanzisha mabadiliko leo hii!

Huu ni u kwa sababu kinga yetu ya kwanza dhidi ya uvunjikaji imo ndani ya kila mmoja wetu. Jitihada zangu za kukomesha uvunjikaji na kuchukua hatua ya kwanza ya kubadilish na kugeuza kanisa lazima zianze na mimi. Sala yangu kwa ajili ya kanisa takatifu lililo na wema na upendo inaweza kujibiwa tu ninapoyafanya maisha yangu kwa njia ya Yesu Kristo na nguvu ya Roho Mtakatifu. Mageuzi yanaanza na mimi. Wazo bora sana la ukombozi! Nina nguvu na machaguo. Kwa msaada wa Mungu ninaweza kuyatoa maisha yangu kwa nguvu inayogeuza na kutoa uhai ya Roho Mtakatifu na wakati huo huo kuanza safari ya utimilifu na uaminifu ninao-taka kuona katika kanisa.

—RUEBEN P. JOB (1928–2015)Kutoka Mwongozo wa Utambuzi wa Roho

Page 70: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

70 Siku 60 za Sala

Kutumia Njia za Mzingo za Kidole katika SalaK W A H I V Y O N E N D A • S O M A M A T H A Y O 2 8 : 1 6 - 2 0

Njia za mzingo zimewapa Wakristo namna ya kusali kwa mili yetu na pia akili zetu na roho tangu karne ya kumi na mbili. Tunapoenda kutokana

na amri ya Yesu, tunafanya safari ya roho—kukomboa, kupokea na kurudi.

MWONDOKO WAKWANZA: KUKOMBOA (MAUNGAMO)Anza kwa kuungama, kimya au kwa sauti. Unapokamilisha, sogeza kidole cha-ko polepole mbele pamoja na njia za mzingo. Sogeza kwa kasi unayotaka hadi katikati. Yaache maneno ya maungamo yako yasalie nawe.

Tuliza akili yako unaposogeza kupitia njia za mzingo. Ni nini cha kuun-gama, kubadilishwa, kusamehewa, kukabiliwa, au kuponywa maishani mwako? Komboa hali hizi kwa Mungu unaposonga mbele.

MWONDOKO WAPILI: KUPOKEA (KUWEKA KATIKATI)Ukifika katikati, pumzisha kidole chako hapo kwa muda mfupi, kisha soma andiko takatifu la siku hiyo.

Soma kifungu polepole, kana kwamba hujawahi kusoma. Weka kwa Mungu na uwe wazi kwa kile ambacho Mungu anakuambia kupitia somo. Rejesha kidole chako katikati ya njia za mzingo na utafakari kifungu.

MWONDOKO WATATU: KURUDI (SALA YA WAUMINI)Unapojiandaa kuacha njia za mzingo, weka kidole chako kwenye uwazi ule ule katikati pale ulipoweka. Anza kusogea kidole chako nyuma njia ile ile am-bayo uliyoweka. Unaporudi kutoka kwenye wakati wako na Mungu, toa sala za waumini na baraka. Mshike kila mmoja na hali katika nuru ya Kristo, kisha endelea na safari.

UKISHAKAMILISHA Iache sala yako ya njia ya mzingo iende “kwa jina la Baba na Mwana na la Roho Mtakatifu.” Amina.

Page 71: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika

Siku 60 za Sala 71

Page 72: The Upper Roomumcprays.org/wp-content/uploads/2016/01/60DaysPrayer-Swahili.pdf · mshumaa mweupe wa Kristo ili kuashiria mwanzo wa muda wako pamoja. UFUNGUZI Mshirikishi: Tuje katika