mwenendo wa miaka 5: serikali nzima - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/cag 2011 brief +...

7
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hukagua hesabu za serikali nzima, ikiwa ni pamoja na Wizara, Idara na Wakala zipatazo 57, Sekretarieti za Tawala za Mikoa 21, na Mamlaka za Serikali za Mitaa 134. Vyombo hivi vya serikali hupewa maoni ya ukaguzi kutegemeana na uzingatiaji wao wa sheria na kanuni za fedha. Kutoka nzuri sana hadi mbaya sana, kuna hati inayoridhisha, hati inayoridhisha yenye masuala ya msisitizo, hati yenye shaka, na hati isiyoridhisha. Chati za hapa chini zinaonesha namna ambavyo serikali inasafisha usimamizi wake wa fedha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Ingawa kuna kupanda na kushuka kila mwaka kwa serikali nzima, kwa ujumla mwenendo umebaki vilevile kwa kutoboreka zaidi lakini pia kutochafuka zaidi: takribani asilimia 60 zinaridhisha, asilimia 40 zenye shaka, na kiasi kidogo haziridhishi. Hata hivyo, kitu ambacho mienendo hii haioneshi ni kwamba kuna mienendo tofauti ndani ya Wizara, Idara na Wakala na Sekretarieti za Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kama inavyoonekana, wizara na serikali za mikoa zimeboresha utendaji wao kwa kuwa na matokeo yanayoridhisha, na kupunguza matokeo yenye shaka, lakini serikali za mitaa zimekuwa na matokeo mabaya zaidi kwa kupungua kwa maoni yanayoridhisha huku maoni yasiyoridhisha yakiongezeka. Serikali Kuu Serikali Kuu Serikali za Mitaa Serikali za Mitaa Nini ambacho kingekusaidia katika maisha yako sasa? Je, ni vitabu kwa ajili ya elimu ya watoto wako? Je, ni kliniki ambayo si tu kwamba iko karibu bali pia ina dawa unazohitaji? Je, ni trekta ya kulimia mashamba yako? Si ingekuwa vema kama tungejipanga wenyewe ili kuleta mabadiliko haya mazuri? Sawa, tumefanya hivyoserikali za vijiji, wilaya, mikoa, na serikali kuu ni aina za miundo ambamo wananchi wanaweza kufanya kazi pamoja ili kuboresha maisha yetu na kupata aina ya maendeleo tunayohitaji. Mojawapo ya njia muhimu ambayo wananchi wanatumia katika miundo ya utawala ili kujiletea matokeo mazuri ni kupitia uandaaji na utekelezaji wa bajeti. Kwa kifupi, lengo la msingi la bajeti ya serikali ni kuzifanya fedha zitumike vizuri ili kutoa bidhaa na huduma bora kwa wananchi, na panakuwepo na sheria na kanuni za usimamizi wa fedha hizo ili kuyafanya haya kwa ufanisi zaidi. Hapa ndipo anapokuja Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Jukumu la msingi la CAG ni kufuatilia matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha kuwa zinatumika ipasavyo. Dhamira ya CAG ni: Kutoa huduma ya ukaguzi wa hesabu yenye tija ili kuimarisha uwajibikaji na thamani ya fedha katika kukusanya na kutumia rasilimali za umma. Kila mwaka CAG hutoa ukaguzi huu, ambapo mwaka unaokaguliwa kwa sasa ni mwaka wa fedha wa 2009/10 (Julai 2009 hadi Juni 2010), lakini hauoneshi vipindi vya muda mrefu ili kuangalia kama usimamizi wa fedha wa serikali kwa ujumla unaboreka au la. Kipeperushi hiki kinabainisha baadhi ya masuala aliyoibua kwa mwaka wa fedha wa 2009/10 pamoja na mienendo ya masuala makubwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. HakiElimu Kipeperushi 11.2K Maelezo na takwimu zote zimechukuliwa kutoka kwenye Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2006-2010, na Ripoti za Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2006-2010 zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania. Kwa maelezo zaidi angalia www.nao.go.tz. Je, ni Mwisho wa Maendeleo? Je, ni Mwisho wa Maendeleo? Miaka Mitano ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Miaka Mitano ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Inayoridhisha Yenye Shaka Isiyoridhisha 0 20 40 60 80 100 Asilimia Mamlaka za Serikali za Mitaa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa Mbaya Zaidi 0 20 40 60 80 100 Asilimia Wizara, Idara na Wakala pamoja na Sekretarieti za Tawala za Mikoa Wizara, Idara na Wakala pamoja na Sekretarieti za Tawala za Mikoa kuwa Bora Zaidi 0 20 40 60 80 100 Asilimia Wizara, Idara na Wakala, Sekretarieti za Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Mwenendo wa Miaka 5: Serikali Nzima

Upload: others

Post on 15-Sep-2019

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hukagua hesabu za serikali nzima, ikiwa ni pamoja na Wizara, Idara na Wakala zipatazo 57, Sekretarieti za Tawala za Mikoa 21, na Mamlaka za Serikali za Mitaa 134. Vyombo hivi vya serikali hupewa maoni ya ukaguzi kutegemeana na uzingatiaji wao wa sheria na kanuni za fedha. Kutoka nzuri sana hadi mbaya sana, kuna hati inayoridhisha, hati inayoridhisha yenye masuala ya msisitizo, hati yenye shaka, na hati isiyoridhisha. Chati za hapa chini zinaonesha namna ambavyo serikali inasafisha usimamizi wake wa fedha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Ingawa kuna kupanda na kushuka kila mwaka kwa serikali nzima, kwa ujumla mwenendo umebaki vilevile kwa kutoboreka zaidi lakini pia kutochafuka zaidi: takribani asilimia 60 zinaridhisha, asilimia 40 zenye shaka, na kiasi kidogo haziridhishi. Hata hivyo, kitu ambacho mienendo hii haioneshi ni kwamba kuna mienendo tofauti ndani ya Wizara, Idara na Wakala na Sekretarieti za Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kama inavyoonekana, wizara na serikali za mikoa zimeboresha utendaji wao kwa kuwa na matokeo yanayoridhisha, na kupunguza matokeo yenye shaka, lakini serikali za mitaa zimekuwa na matokeo mabaya zaidi kwa kupungua kwa maoni yanayoridhisha huku maoni yasiyoridhisha yakiongezeka.

Serikali KuuSerikali Kuu Serikali za MitaaSerikali za Mitaa

Nini ambacho kingekusaidia katika maisha yako sasa? Je, ni vitabu kwa ajili ya elimu ya watoto wako? Je, ni kliniki ambayo si tu kwamba iko karibu bali pia ina dawa unazohitaji? Je, ni trekta ya kulimia mashamba yako? Si ingekuwa vema kama tungejipanga wenyewe ili kuleta mabadiliko haya mazuri? Sawa, tumefanya hivyo—serikali za vijiji, wilaya, mikoa, na serikali kuu ni aina za miundo ambamo wananchi wanaweza kufanya kazi pamoja ili kuboresha maisha yetu na kupata aina ya maendeleo tunayohitaji.

Mojawapo ya njia muhimu ambayo wananchi wanatumia katika miundo ya utawala ili kujiletea matokeo mazuri ni kupitia uandaaji na utekelezaji wa bajeti. Kwa kifupi, lengo la msingi la bajeti ya serikali ni kuzifanya fedha zitumike vizuri ili kutoa bidhaa na huduma bora kwa wananchi, na panakuwepo na sheria na kanuni za usimamizi wa fedha hizo ili kuyafanya haya kwa ufanisi zaidi.

Hapa ndipo anapokuja Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Jukumu la msingi la CAG ni kufuatilia matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha kuwa zinatumika ipasavyo. Dhamira ya CAG ni:

Kutoa huduma ya ukaguzi wa hesabu yenye tija ili kuimarisha uwajibikaji na thamani ya fedha katika kukusanya na kutumia rasilimali za umma.

Kila mwaka CAG hutoa ukaguzi huu, ambapo mwaka unaokaguliwa kwa sasa ni mwaka wa fedha wa 2009/10 (Julai 2009 hadi Juni 2010), lakini hauoneshi vipindi vya muda mrefu ili kuangalia kama usimamizi wa fedha wa serikali kwa ujumla unaboreka au la. Kipeperushi hiki kinabainisha baadhi ya masuala aliyoibua kwa mwaka wa fedha wa 2009/10 pamoja na mienendo ya masuala makubwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

HakiElim

u

Kipeperu

shi 1

1.2K

Makusanyo ya Kodi kwa Serikali za MitaaMakusanyo ya Kodi kwa Serikali za Mitaa

Maelezo na takwimu zote zimechukuliwa kutoka kwenye Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2006-2010, na Ripoti za Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2006-2010 zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania. Kwa maelezo zaidi angalia www.nao.go.tz.

Makusanyo ya Kodi KitaifaMakusanyo ya Kodi Kitaifa

Uthibitisho wa MalipoUthibitisho wa Malipo

Je, ni Mwisho wa Maendeleo?Je, ni Mwisho wa Maendeleo?

Miaka Mitano ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za SerikaliMiaka Mitano ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

0

20

40

60

80

100

Asi

lim

ia M

DA

, RA

S n

a L

GA

Mwenendo wa Miaka 5: Serikali Nzima

Inayoridhisha Yenye Shaka Isiyoridhisha

0

20

40

60

80

100

Asi

lim

ia M

am

lak

a z

aS

eri

ka

li z

a M

ita

a

Mamlaka za Serikali za Mitaakuwa Mbaya Zaidi

0

20

40

60

80

100

Asi

lim

ia W

iza

ra, I

da

ra n

a

Wa

ka

la p

am

oja

na

Se

kre

tari

eti

za

Ta

wa

la z

a M

iko

a

Wizara, Idara na Wakala pamoja na Sekretarieti za Tawala za Mikoa

kuwa Bora Zaidi

0

20

40

60

80

100

Asi

lim

ia W

iza

ra, I

da

ra n

a

Wa

ka

la, S

ek

reta

rie

ti z

a T

aw

ala

za

M

iko

a n

a M

am

lak

a z

a S

eri

kal

i za

Mit

aa

Mwenendo wa Miaka 5: Serikali Nzima

Inayoridhisha Yenye Shaka Isiyoridhisha

Kama ilivyoelezwa, maoni ya ukaguzi hutegemea usimamizi wa fedha wa Wizara au Halmashauri husika. Hii inajumuisha vitu kama mahesabu mazuri ya matumizi. Wizara au Halmashauri haipaswi kulipa fedha ovyoovyo; kila hati ya malipo haina budi kuambatana na nyaraka husika kama vile mikataba, ankara, risiti au orodha ya malipo yaliyowekwa saini. Nyaraka hizi zinapokosekana, CAG hawezi kuthibitisha kama fedha zimetumika ipasavyo. Kuanzia mwaka 2006 mpaka 2010, Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Sekretarieti za Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeonesha mwenendo mbaya wa kushindwa kuweka

mahesabu ya matumizi yao kwa usahihi. Ingawa Wizara, Idara na Wakala za Serikali pamoja na Sekretarieti za Tawala za Mikoa zimepiga hatua kubwa katika kuthibitisha malipo kwa kupunguza kutoka shilingi bilioni 37 mwaka 2006 hadi shilingi bilioni 4 mwaka 2009, CAG anatamka kuwa taasisi hizi zina kiasi cha shilingi bilioni 362 za matumizi yenye nyaraka pungufu kwa mwaka 2010. Wakati huohuo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeendelea kushindwa kutoa uthibitisho wa malipo ikiwa ni maradufu kutoka kiasi cha shilingi bilioni 2.4 mwaka 2006 hadi shilingi bilioni 5.5 mwaka 2010.

Makusanyo ya Kodi kwa Serikali za MitaaMakusanyo ya Kodi kwa Serikali za Mitaa

Katika ngazi ya serikali za mitaa, vitabu vya kukusanyia mapato “vilivyokosekana” na “vilivyopotea” pamoja na mapato yanayoibwa yamekuwa ni masuala ya muda mrefu sana. Mwaka 2010, Halmashauri 48 zilipoteza vitabu 948 vya kukusanyia mapato. Mapato ambayo yalikusanywa mwaka 2010 kwa niaba ya Halmashauri lakini hayakuwasilishwa na mawakala wanaokusanya kodi yalifikia kiwango cha juu kabisa cha shilingi bilioni 2.8. Kuanzia mwaka 2006 mpaka 2010, mawakala wa ukusanyaji kodi wametoroka na takribani shilingi billioni 5 za walipa kodi. Kama CAG anavyobainisha,

Kuna uwezekano mkubwa wa wizi wa mapato ya Halmashauri na kupotosha makisio ya mapato ya Halmashauri.

Kama ilivyoelezwa, maoni ya ukaguzi hutegemea usimamizi wa fedha wa Wizara au Halmashauri husika. Kwa upana zaidi, hali hii inagawanywa katika maeneo mawili: mapato na matumizi. Kwa kuangalia makusanyo ya mapato kitaifa, mbali na ukusanyaji mdogo katika miaka ya hivi karibuni, Mamlaka za Mapato Tanzania (TRA) inakusanya fedha nyingi zaidi kuliko wakati wowote uliopita. Japo bado mwaka 2010 ilipoteza shilingi bilioni 681 kupitia misamaha ya kodi, kiasi hiki cha misamaha ya kodi kilikuwa ni asilimia 10 pungufu ya kile cha mwaka 2009.

-

500

1,000

1,500

2,000

2,500

3,000

0

200

400

600

800

1,000

1,200

1,400

1,600 Ma

ku

san

yo

ya

siyo

wa

silishw

a(m

am

ilion

i ya

shilin

gi)V

ita

bu

vy

a K

uk

usa

ny

iaM

ap

ato

Vin

av

yo

ko

sek

an

a

Halmashauri Kukosa Vitabuvya Risiti na Mapato

Makusanyo Yasiyowasilishwa na Mawakala

Vitabu vya Kukusanyia Mapato Vinavyokosekana

Shilingi bilioni 2.8

Makusanyo ya Kodi KitaifaMakusanyo ya Kodi Kitaifa

Uthibitisho wa MalipoUthibitisho wa Malipo

Waathirika wa Mabomu ya Mbagala...Wameumizwa Zaidi? Shilingi bilioni 8 ambazo Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam anasema ziliwalipa fidia wahanga wa mabomu Mbagala hazina nyaraka za kuthibitisha, na kumfanya CAG kukiri kuwa, “usahihi wa fidia haukuweza kuthibitishwa.”

Uchumi Ulichochewa? Julai 2009, Rais Jakaya Kikwete alitangaza shilingi trilioni 1.7 kwa ajili ya kusaidia kuokoa uchumi wa Tanzania kutoka kwenye madhara ya mtikisiko wa kifedha duniani. Sehemu ya fedha hizi ilipelekwa Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuwasaidia watu kwa kutoa fidia na mikopo. Kinyume na utaratibu, orodha ya watu waliofaidika na kiasi cha shilingi bilioni 48 ya fedha hizo haikuweza kutolewa. Hivyo CAG anahitimisha kwa kusema, “Kutokana na hilo, sikuweza kujiridhisha kwamba, kiasi kilicholipwa kingeweza kusimama kama malipo sahihi ya fedha za umma.”

Madini Mbali na uharibifu wa mazingira ambao unachafua vyanzo vya maji, kuua mifugo, na kusababisha magonjwa ya ngozi yasiyotibika, ikiwa pamoja na migogoro ya mara kwa mara kati ya wananchi na polisi, ambayo mara nyingi husababisha kuuawa kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu, migodi inayomilikiwa na wageni pia inaendelea kuchunguzwa na umma kwa ukwepaji wa kulipa kodi. Ikiwa imefikia asilimia 7 tu ya misamaha yote ya kodi, hata hivyo sekta ya madini imepata aina ya pekee ya msamaha wa kodi ambao CAG anauangalia, huku ikiwa ilipata msamaha wa kodi ya serikali kiasi cha shilingi bilioni 49 kwa mwaka 2010.

0

1

2

3

4

5

Ma

tril

ion

i ya

Sh

ilin

gi

Makusanyo na Misamaha ya Kodi TRA

Makusanyo Misamaha

Je, ni Mwisho wa Maendeleo?Je, ni Mwisho wa Maendeleo?

Miaka Mitano ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za SerikaliMiaka Mitano ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Katika miaka ya karibuni, bajeti ya serikali iliyopitishwa na Bunge katika mwanzo wa mwaka ilikuwa inaonekana kufanana kwa kiasi kidogo sana na kile ambacho serikali ilichokifanya kwa kutumia fedha ilipofika mwisho wa mwaka. Hali hii ilikuwa hivyo hususani katika matumizi ya fedha za maendeleo. Matumizi ya fedha za serikali yanaweza kugawanywa katika aina mbili: matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo. Matumizi ya kawaida ni gharama za kila siku kama vile mishahara, vifaa na ukarabati, kwa ufupi ni gharama ambazo zinahitajika kwa ajili ya kuendesha shughuli za serikali. Matumizi ya maendeleo ni fedha zinazotumika kuboresha huduma za jamii, kama vile kupata vitabu madarasani, madawa kwenye kliniki, na lami barabarani. Mapato ya serikali pia yanaweza kugawanywa katika aina hizohizo mbili. Mapato ya kawaida yanaundwa kwa kiasi kikubwa na kodi inayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambayo hatimaye huenda kugharimia matumizi ya kawaida ya serikali. Mapato ya maendeleo yanajumuisha misaada ya nje na mikopo (pamoja na mikopo ya ndani) na hutumika kugharamia matumizi ya maendeleo.

Licha ya ukusanyaji mdogo wa kodi wa TRA hivi karibuni unaoathiri mapato ya kawaida, chanzo kikubwa cha kuyumba kwa bajeti hutoka kwenye mapato ya maendeleo. Mathalani, wakati mwaka 2010 TRA haikukusanya kodi kiasi cha shilingi bilioni 391 (au asilimia 8 ya lengo lake), misaada ya nje haikutolewa kwa kiasi cha shilingi trilioni 1.5 (au asilimia 39 ya makadirio ya bajeti). CAG anasema hii inaweza kutokana na Tanzania kutotimiza masharti ya misaada, wahisani kushindwa kutoa misaada kama ilivyoahidiwa au serikali kupigia mahesabu misaada ya

nje ambayo bado haijathibitishwa katika makadirio yake. Upungufu wa mapato kwa ujumla umekuwa tatizo kubwa katika miaka ya hivi karibuni (angalia chati ya kwanza hapo chini). Mwaka 2007, mapato halisi yalikuwa asilimia 9 chini ya makadirio yaliyopitishwa, wakati mwaka 2010 yalikuwa asilimia 21 chini ya makadirio!

Upungufu huu wa kukusanya mapato ni kikwazo kwa bajeti ya serikali ya Tanzania: makato ya misaada na dosari zingine za mapato zinachangia kuongezeka kwa mwenendo wa upungufu wa fedha, fedha kidogo kunamaanisha kuwa bajeti ya serikali iliyopitishwa haitatekelezwa kama ilivyopangwa, na matumizi yatapunguzwa (angalia chati ya pili hapa chini). Kwa kuwa upungufu aghalabu hutokana na dosari za mapato ya maendeleo, na kwa kuwa matumizi ya kawaida wakati yanahalalishwa kwamba ni ya lazima (pamoja na kwamba yamejaa matumizi yasiyo ya lazima kama vile safari za nje, posho kubwa mno, na semina/warsha/mafunzo yasiyo na tija na ambayo huleta matokeo kidogo kuliko inavyotarajiwa), matumizi ya maendeleo huathirika zaidi kunapokuwa na upungufu wa mapato. Kwa mfano, katika mwaka 2008/09, fedha za maendeleo zilikatwa asilimia 34 wakati fedha za matumizi ya kawaida zilikatwa asilimia 6 tu (angalia chati ya tatu hapa chini).

Hatimaye, bajeti ya serikali inayopitishwa na Bunge ni nadra sana kufanana na kinachotokea kwa fedha halisi kwa mwaka mzima, hali inayompelekea CAG kusema,

...serikali inapaswa kupanga bajeti kulingana na inachotegemea kukipata ili kuondoa usumbufu wakati wa utekelezaji wa bajeti. Kwa upande mwingine, Viwango vya Kimataifa vya Ukaguzi (ISA) kifungu cha 20 kinataka msaada wa nje utambuliwe katika taarifa za fedha pale tu unapokuwepo ushahidi wa kutosha kuwa msaada huo utapatikana. Juhudi kubwa zinapaswa kuelekezwa katika kupunguza utegemezi wa serikali kwenye misaada ya nje.

Bajeti na Hali HalisiBajeti na Hali Halisi Matumizi ya Maendeleo kwa HalmashauriMatumizi ya Maendeleo kwa Halmashauri

Je, ni Mwisho wa Maendeleo?Je, ni Mwisho wa Maendeleo?

Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo Pamoja na kupingwa na asasi za kiraia, Bunge lilipitisha Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (CDCF) mwaka 2009 unaotoa moja kwa moja kwa Wabunge fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo katika majimbo yao. Mwisho wa mwaka wa kwanza, mfuko huo ulikuwa na shilingi bilioni 1.3 ambazo hazijatumika, sababu kubwa ikiwa ni Halmashauri kutotenganisha akaunti kama inavyotakiwa na kuchelewa kutoa fedha. Katika maeneo machache ambako fedha za mfuko huo zilitumika, Kamati za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo za majimbo za Halmashauri husika hazikutoa ripoti ya kiasi cha fedha kilichopokelewa na kutumika kwa Waziri anayehusika na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

0

2

4

6

8

10

Ma

tril

ion

i ya

Sh

ilin

gi

Bajeti na Fedha Zinazotolewa:Bado Tatizo

Bajeti ya Serikali IliyopitishwaKiasi Halisi KilichotolewaNakisi ya Fedha Halisi na Bajeti

0.0

0.5

1.0

1.5

2.0

2.5

3.0

3.5

Ma

tril

ion

i ya

Sh

ilin

gi

Upungufu wa Fedha za Maendeleo:Pengo Kubwa

Bajeti ya Maendeleo IliyopitishwaKiasi Halisi cha Fedha za Maendeleo KilichotolewaNakisi ya Fedha za Maendeleo na Bajeti

0

2

4

6

8

10

12

Ma

tril

ion

i ya

Sh

ilin

gi

Ongezeko la Upungufu wa Fedha

Makadirio ya Makusanyo (Nje na Ndani)Makusanyo HalisiNakisi ya Mapato

Mnamo mwaka 2004, Serikali Kuu ilifuta kodi kadhaa ambazo Halmashauri zilikuwa zinatoza kata na vijiji. Ili kuweza kufidia pengo la mapato ambalo lingetokea kwenye bajeti za Halmashauri, Serikali Kuu ilianza kutuma ruzuku ya fidia kwenye Halmashauri, kukiwa na sharti maalum kwamba asilimia 20 ya fedha hizi zinapaswa zitumwe moja kwa moja kwenye kata na vijiji ili kufadhili shughuli za maendeleo. Hata hivyo, Halmashauri nyingi hupenda kubaki na fedha zile bila kuzipeleka kwenye kata na vijiji. Mwaka 2009, Halmashauri 23 zilizuia zaidi ya shilingi bilioni 3 kwenda kwenye kata na vijiji. Mnamo mwaka 2010, kulikuwa na maboresho kidogo, lakini Halmashauri 22 bado zilikataa kupeleka kwenye serikali za kata na vijiji zaidi ya shilingi bilioni 1.2.

Hata pale ambapo fedha za maendeleo zikiwepo, Halmashauri hazioneshi kuweza kuzitumia. Wakati ambapo Serikali Kuu hutumia takribani kiasi chote kinachotolewa, Halmashauri zinaendelea na mtindo wa kutotumia fedha za maendeleo, mwenendo ambao unaangaliwa kwa karibu zaidi na CAG katika kipindi cha mwaka 2008 mpaka 2010. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kwa wastani Halmashauri zimeshindwa kutumia asilimia 33 (theluthi nzima) ya fedha za ruzuku za maendeleo zilizopokelewa kutoka Serikali Kuu. Mwaka 2010 Halmashauri ziliweka rekodi mpya ya kutotumia shilingi bilioni 176 ya fedha za maendeleo. Kwa ujumla, katika mwaka 2008 hadi 2010, Halmashauri zimeshindwa kutumia shilingi bilioni 364 za ruzuku za maendeleo!

Bajeti na Hali HalisiBajeti na Hali Halisi Matumizi ya Maendeleo kwa HalmashauriMatumizi ya Maendeleo kwa Halmashauri

Je, ni Mwisho wa Maendeleo?Je, ni Mwisho wa Maendeleo?

Kilimo Kwanza au Umimi Kwanza? Taarifa za kuibwa kwa vocha za zana za kilimo zimeendelea kutawala vyombo vya habari. Kwa mujibu wa CAG, mwaka 2010 vocha zenye thamani ya shilingi milioni 200 ziliibwa au “kupotezwa” na Halmashauri, wakati kiasi kingine cha shilingi milioni 163 za vocha kiliachwa bila kutumika, jumla zikiwa ni vocha 33,000 zilizoibwa, kupotea au kutotumika. Kwa ujumla, kazi za Kilimo Kwanza zenye thamani ya shilingi milioni 977 hazikutekelezwa mwaka 2010.

Mfuko wa Afya ya Jamii Kupitia tafiti mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni, CAG amegundua tabia ya Halmashauri ya kutotumia fedha za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), fedha ya kununulia madawa, vifaa vya hospitali na ukarabati. Mwaka 2009, utafiti wa majaribio katika Halmashauri tatu uligundua shilingi milioni 184 ya fedha ambazo hazikutumika, ambapo mwaka 2010, utafiti katika Halmashauri kumi ulionesha shilingi milioni 383 hazikutumika. Pale ambapo fedha zilitumika, kuna wakati z i l i e n d a k a t i k a m a l e n g o yasiyokusudiwa kama vile kulipa mishahara. Halmashauri nyingi zilizokaguliwa hazina akaunti maalum ya mfuko huo na hazitayarishi taarifa za fedha za mwaka kwa ajili ya mfuko huu.

Halmashauri Zinaumiza Vijiji na KataHalmashauri Zinaumiza Vijiji na Kata

0

100

200

300

400

500

600

Ma

bil

ion

i ya

Sh

ilin

gi

Fedha za Maendeleo Zisizotumiwa na Halmashauri

Fedha za Maendeleo ZilizotolewaFedha za Maendeleo ZilizotumikaFedha za Maendeleo Zisizotumika

Shilingi bilioni 176 hazikutumika

Shilingi bilioni 48 Fedha zilizopelekwa Benki Kuu ya Tanzania

kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi lakini hazijathibitishwa

Shilingi bilioni 10.5 Fedha ya mapato ambayo haijawasilishwa kwenye serikali za mitaa na mawakala wa

kukusanya kodi (shilingi bil. 5), fedha za vijiji zilizozuiwa na Halmashauri (shilingi bil. 4.2) na

fedha za CDCF zisizotumika (shilingi bil. 1.3)

Shilingi milioni 650 Fedha za kununulia samani wizarani na mikoani

Shilingi bilioni 108 Misamaha ya kodi katika sekta ya madini

Mishahara ya mwaka kwa takribani walimu 3,000 wa shule za msingi, au karibu nusu ya

walimu wote wa shule za msingi mkoani Kigoma

Vyoo 15,000, au choo kipya katika karibu kila shule ya msingi nchini

Mikopo ya shilingi milioni 10 kila moja kwa biashara 36 katika kila wilaya Tanzania

Vitabu vipya 9 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi nchini

Nyumba za walimu 12,000, au kutosha kujenga nyumba mpya za walimu kwa 3/4 ya shule za

msingi za Tanzania

Shilingi bilioni 374 Jumla ya fedha ambazo

hazijatumiwa na Halmashauri

Kiasi kikubwa hiki cha fedha kinamaanisha nini… ...Je, fedha hizi zingefanya nini kwa miaka mitano iliyopita?

=

=

=

=

=

=

=

Shilingi bilioni 10.6 Mishahara na mikopo ya

wafanyakazi hewa

Shilingi milioni 363 Vocha za Kilimo Kwanza zisizotumika au kuibwa

Mbolea ingetosheleza kutumika katika zaidi ya ekari 20,000. Hii ni mara 2 ya

ardhi yote ya kilimo mkoani Singida

Madawati 21,667, au ingetosha kutoa madawati mapya kwa wanafunzi wote wa darasa la I kwa mikoa ya Lindi na Mtwara

Kama ilivyoelezwa mwanzo wa kipeperushi hiki, mamlaka ya CAG ni kutoa huduma za serikali za ukaguzi. Inafanya ukaguzi huu na kutoa matokeo na mapendekezo kwenye Bunge kila mwaka, ambako ndiko mamlaka ya ukaguzi ya CAG yanakoishia. CAG anayo mamlaka ya kukagua serikali na kutoa mapendekezo; hana mamlaka ya kuyafanyia kazi mapendekezo au hata kushughulikia ubadhilifu. Japo juhudi zake zinaweza kusaidiwa na Wabunge, hususan Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC) na ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mamlaka ya Kudhibiti Manunuzi ya Umma (PPRA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kazi za CAG huishia kwenye ukaguzi tu. CAG anabainisha kwa umakini kuwa,

...wakati ambapo ofisi yangu inaripoti ukiukwaji wowote wa sheria na kanuni mbalimbali na udhaifu katika kutoa taarifa za fedha na mfumo wa udhibiti wa ndani kwenye taasisi zote za sekta ya umma..., wajibu wa mwisho wa kuhakikisha kuwa kuna mfumo madhubuti na wenye ufanisi wa udhibiti wa ndani na kufuatwa unabakia kwenye usimamizi wa Maafisa Masuuli…[na] kila Mamlaka ya Serikali ya Mtaa.

Deni la TaifaDeni la Taifa

Ili kuwezesha utekelezaji wa kazi nyingi zinazopangwa, serikali hutafuta fedha zaidi. Hufanya hivyo kwa kupata fedha ndani na nje. Kwa upande wa ndani hutumika utaratibu wa kutoza kodi na kukopa mikopo kutoka kwenye mabenki ya ndani. Fedha za nje hutolewa kama ruzuku (misaada) na kukopa kutoka kwenye mabenki ya nje na taasisi za fedha za kimataifa. Mikopo yote, iwe ya ndani au nje, haina budi kulipwa, na kwa kuwa kwa kawaida fedha za mikopo hufikia takribani asilimia 20 ya bajeti ya serikali ya Tanzania kila mwaka, hali hii huongezeka na kuwa deni kubwa mno. Kila mwaka nchi inapopitisha bajeti kubwa, inapaswa ijulikane kuwa sehemu kubwa ya fedha hizi ni mzigo wa deni ambalo utabebwa na kizazi kijacho.

Mwaka uliopita katika ukaguzi wa CAG, deni la taifa lilifikia shilingi trilioni 10.6, kiasi ambacho kinakaribia bajeti nzima ya mwaka ya serikali kwa miaka ya hivi karibuni. Sehemu kubwa ya deni hili, takribani asilimia 73, ni kutoka kwenye mikopo ya nje.

Pamoja na kwamba ukubwa wa deni la Tanzania ni suala linalotia wasiwasi, jambo linalotia hofu zaidi ni kiwango cha kasi ambacho deni la Tanzania limekuwa likikua. Kama inavyoonekana kwenye chati, Tanzania ilipunguza deni lake mwaka 2007 na kuanza kuongezeka kiasi mwaka 2008 na mwaka 2009 deni la taifa likaongezeka ghafla kwa takribani asilimia 40 kati ya mwaka 2009 na 2010! Ongezeko la deni la kiasi cha asilimia 40 ni tatizo na linamfanya CAG kusema,

Kama mwenendo huu hautasimamiwa vizuri, unaweza kuipelekea Serikali kushindwa kulipa mzigo huu wa deni. Ongezeko ni kubwa mno kiasi ambacho mrundikano wa deni unaweza kulifanya liziweze kulipika….

Deni la taifa huwa linalipwa, au hulipwa kidogo, kila mwaka, lakini mchakato huu pia huathiriwa na usimamizi mbovu wa fedha. Mwaka 2009/10, idara ya Deni la Taifa na Huduma za Ujumla ilikuwa na kiasi kinachokaribia shilingi bilioni 280 za matumizi yasiyokuwa na nyaraka sahihi. Kiasi cha shilingi trilioni 1.8 ambacho kiliripotiwa kupelekwa kwa wakopeshaji wa nje hakikuwa na uthibitisho wa risiti. Bila shaka deni la taifa halitaweza kupungua kama fedha hizi hazitawafikia wakopeshaji na kuchakachuliwa kwenda kwingineko.

Posho ya Samani za Wizara Pamoja na agizo mahsusi la 2006 kutoka Ofisi ya Rais, likielezea tabia mbaya ya kuwapa maafisa wasiostahili posho ya samani, mwaka 2010 Wizara, Idara na Wakala 10 ziliendelea kufanya hivyo kwa kugawa fedha kiasi cha shilingi milioni 650 (sawa na makochi 6,500) kwa kuwapa maafisa wasiostahili samani katika nyumba zao binafsi.

Je, Mapendekezo ya CAG Yanafuatwa?Je, Mapendekezo ya CAG Yanafuatwa?

Masuala YasiyoshughulikiwaMasuala Yasiyoshughulikiwa

0

2

4

6

8

10

12

Ma

tril

ion

i ya

Sh

ilin

gi

Wimbi la Kuongezeka kwa Deni la Taifa

Deni la shilingi trilioni 10.6

Benki za Tanzania

26%

Benki na Taasisi za Fedha za

Nje73%

Je, serikali (na wewe mlipa kodi) inadaiwa na nani?

HakiElimu inwezesha wananchi

kuleta mabadiliko katika elimu na demokrasia.

SLP 79401 ● Dar es Salaam ● Tanzania Simu (255 22) 2151852/3 ● Faksi (255 22) 2152449

[email protected] ● www.hakielimu.org

Deni la TaifaDeni la Taifa

Wakati ambapo wajibu wa kutekeleza mapendekezo ya CAG hubakia kwa Maafisa Masuuli na Mamlaka za Serikali za Mitaa, wanakosa motisha kufanya hivyo ikiwa vyombo vingine vya usimamizi havitekelezi wajibu wao. Ni dhahiri kuwa mfumo huu kwa ajili ya kuboresha usimamizi wa fedha za serikali haufanyi kazi kwa kuwa mojawapo ya mapendekezo ya awali ya CAG mwaka baada ya mwaka ni kutekeleza mapendekezo yake ya mwaka uliopita.

Kiashiria kingine cha serikali kutotekeleza mapendekezo ya CAG ni masuala yasiyoshughulikiwa. Kwa kifupi, masuala yasiyoshughulikiwa ni yale ambayo CAG alibainisha kuwa yana utata mwaka uliopita lakini yamebaki bila kufanyiwa kazi. Mwaka jana Wizara, Idara na Wakala pamoja na Sekretarieti za Tawala za Mikoa zilifanikiwa kupunguza karibu nusu ya masuala yasiyoshughulikiwa kutoka shilingi trilioni 1.1 hadi shilingi bilioni 591. Lakini Halmashauri zilifanya kinyume chake: badala ya kuyafanyia kazi mapendekezo ya CAG na kupunguza masuala yasiyoshughulikiwa, zenyewe ziliyapuuza na kuyaongeza masuala yasiyoshughulikiwa hadi kufikia zaidi ya shilingi bilioni 122.

Katika jitihada za kupunguza “ubutu” wa mapendekezo ya CAG, Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008 iliongeza kipengele cha kuzitaka Wizara, Idara na Wakala, Sekretarieti za Tawala za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa taarifa jinsi zilivyoshughulikia mapendekezo ya CAG au kuwasilisha mipango kazi ya namna wanavyopanga kuyashughulikia mapendekezo. Mwaka 2010, taasisi hizi za serikali ziliandaa ripoti kama hizi japo hazikujibu mapendekezo mengi ya CAG (na zilichelewa kwa mwezi mmoja). CAG ana makaripio yanayolingana kwa serikali kuu na za mitaa kama ifuatavyo:

Mapendekezo mengi yaliyotolewa katika Ripoti Kuu mwaka uliopita juu ya Serikali Kuu hayakujibiwa, ikiwa ni ishara ya Serikali kukosa dhamira ya kutekeleza mapendekezo hayo.… Matokeo ya kutoyafanyia kazi maangalizo na mapendekezo ya wakaguzi husababisha kujirudia kwa hitilafu zilizoainishwa na wakaguzi katika miaka ya fedha inayofuata. Hali hii pia inaonesha kukosa dhamira kwa Maafisa Masuuli na usimamizi wa vitengo husika.

··· Mapendekezo mengi yaliyotolewa katika Ripoti kwa kila Mamlaka ya Serikali ya Mtaa mwaka uliopita hayakujibiwa, ikiwa ni ishara ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kukosa dhamira ya kutekeleza mapendekezo hayo. … Mwelekeo huu au tabia hii ya kutojibu maangalizo na mapendekezo ya wakaguzi inaweza kusababisha kujirudia kwa hitilafu zilizoainishwa na wakaguzi katika miaka ya fedha inayofuata. Hali hii pia inaweza kuonesha kukosa dhamira kwa upande wa usimamizi na Halmashauri husika.

Kusafisha usimamizi wa fedha za serikali hakuwezekani kama umma hautautupia jicho. Fungua zaidi kipeperushi hiki kujua nini kinaendelea katika wilaya yako. Tembelea tovuti www.nao.go.tz kusoma ripoti kamili za CAG na kujifunza mengine zaidi kuhusu masuala katika eneo lako. Washirikishe Maafisa Watendaji wa Vijiji na dai uwajibikaji Halmashauri. Ongea na Mbunge wako na sisitiza afanye wajibu wake katika Bunge ili kuleta usimamizi thabiti katika taasisi zingine za serikali. Ni kupitia kuboresha usimamizi wa fedha za serikali tu ndipo tutakapofanikiwa kifikia maendeleo tunayohitaji kuyaona.

0

50

100

150

Ma

bil

ion

i ya

Sh

ilin

gi

Masuala YasiyoshughulikiwaMasuala Yasiyoshughulikiwa

Picha kwa hisani ya: AngloGold Ashanti, protestbarrick.net, The Citizen, Kikundi cha Facebook cha Wahanga wa Mbagala, The Guardian, jtkinyagu.blogspot.com, mjengwa.blogspot.com

Wafanyakazi Hewa Baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Tawala za Mikoa, na Wizara, Idara na Wakala zimeshindwa kurekebisha orodha ya malipo ya mishahara ili kubainisha wafanyakazi waliostaafu, waliojiuzulu, waliofukuzwa kazi au waliofariki, na zinaendelea kupata mishahara yao kutoka Hazina ya Serikali Kuu. Endapo hali hii ikitokea, zinapaswa kurejesha Hazina mishahara ambayo haijalipwa, lakini, kama anavyoonesha CAG, aghalabu huzuia fedha hizi, hata kuziondoa kwenye taarifa za fedha, na mara nyingine huendelea kuwalipa wafanyakazi hewa. Kuanzia mwaka 2006 mpaka 2010, Halmashauri zilizuia shilingi bilioni 4.7 za mishahara ambayo haijalipwa badala ya kupeleka Hazina. Pia kuanzia mwaka 2008 mpaka 2010, Halmashauri zimelipa wafanyakazi hewa shilingi bilioni 1.6 ambao ama wamestaafu, kujiuzulu, kufukuzwa kazi, au kufariki. Mwaka 2010 pekee Wizara, Idara na Wakala pamoja na Sekretarieti za Tawala za Mikoa zililipa wafanyakazi hewa shilingi bilioni 1.8.

Mapendekezo ya CAG Kupuuzwa: Masuala Yasiyoshughulikiwa Halmashauri

0 0.5 1 1.5 2 2.5

H/W MwangaH/Mji MasasiH/W Longido

H/Mji KorogweH/W Kilosa

H/W Ukerewe H/M Songea

H/W Sikonge H/W Nzega

H/W Njombe H/W Ngorongoro

H/J Mwanza H/W Liwale

H/W Kishapu H/M Ilala

H/W Igunga H/W Handeni H/M Dodoma

H/W Babati H/M Mtwara

H/M Kigoma Ujiji H/W Bahi

H/W Rorya H/W Mkinga

H/W ChatoH/W Chamwino

H/M Temeke H/W Tandahimba H/M Sumbawanga

H/W Simanjiro H/W Shinyanga H/W Ruangwa

H/W RomboH/W Pangani

H/W NamtumboH/W Mvomero

H/W MtwaraH/M Moshi H/W Moshi

H/W MorogoroH/W Mkuranga H/W Misungwi

H/J Mbeya H/W Mbarali H/W Makete

H/W Lushoto H/W Korogwe

H/W KilwaH/M Iringa H/W Iringa

H/J Dar es Salaam H/Mji BabatiH/M Arusha

H/W Nanyumbu H/W Meru

H/W TarimeH/J Tanga

H/M Singida H/W Ngara

H/M MusomaH/W Musoma H/W Monduli H/W Mbinga H/W Mbeya H/W Maswa

H/W Magu H/Mji Lindi H/W Lindi

H/M Kinondoni H/W Kilombero

H/W Kilolo H/W Kilindi

H/W Kigoma H/Mji Kibaha H/W Kibaha H/W Kasulu

H/W Kahama H/W Ileje

H/W Hanang H/W Bunda

H/W Bukombe H/M Bukoba H/W Bariadi

H/W Bagamoyo H/Mji Njombe H/Mji Mpanda H/W Urambo

H/W Ulanga H/W Tabora

H/W Sumbawanga H/W Singida

H/M Shinyanga H/W Serengeti

H/W Sengerema H/W Same

H/W Rungwe H/W Rufiji H/W Nkasi

H/W Newala H/W Nachingwea

H/W Muleba H/W Muheza

H/W Mpwapwa H/W Mpanda

H/W Meatu H/W Mbozi

H/W Masasi H/W Mafia

H/W Kwimba H/W Kongwa

H/W Kiteto H/W Kisarawe H/W Kibondo

H/W Karatu H/W Karagwe

H/W Iramba H/W Geita

H/W Chunya H/W Bukoba

H/W Tunduru H/M Tabora H/W Songea

H/W Siha H/W Mufindi

H/M Morogoro H/MH/W Missenyi

H/W Mbulu H/W Manyoni H/W Ludewa

H/W Kyela H/W Hai

H/W Biharamuro H/W Arusha H/W Kondoa

0 0.5 1 1.5 2 2.5

Hesabu Jumuifu za TaifaWizara ya Mambo ya Ndani

Idara ya UhamiajiWizara ya Maliasili na Utalii

Mahakama (Mahakama ya Rufaa)Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Wizara ya Nishati na MadiniWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

HazinaJeshi la Zima Moto na Uokoaji

Deni la Taifa na Huduma za UjumlaTACAIDS

Ofisi ya Rais – Tume ya Utumishi wa UmmaJeshi la Kujenga Taifa

Wizara ya MajiWizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Wizara ya Ardhi na MakaziWizara ya Maendeleo ya Miundombinu

Wizara ya Viwanda, Biashara na MasokoWizara ya Mambo ya Ndani – Idara ya Jeshi la Polisi

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa KimataifaWizara ya Fedha na Uchumi

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na TeknolojiaMahakama ya Ardhi

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaOfisi ya Spika

Wizara ya Kazi na UwezeshajiWizara ya Habari, Utamaduni na Michezo

Wizara ya Mambo ya Ndani – Idara ya Jeshi la MagerezaWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na WatotoWizara ya Kilimo na Chakula

Tume ya Taifa ya UchaguziOfisi ya Makamu wa Rais

Msajili wa Vyama vya SiasaOfisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI

Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa UmmaOfisi ya Rais – Tume ya Mipango

Wizara ya Sheria na Mambo ya KatibaWizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Tume ya Kurekebisha SheriaMahakama ya Kazi

Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya MaadiliTume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Mwanasheria Mkuu wa SerikaliIdara ya Mhasibu Mkuu

Ofisi ya Waziri MkuuWaziri Mkuu

Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Baraza la MawaziriMahakama ya Biashara

Tume ya Kudhibiti Madawa ya KulevyaOfisi ya Makamu Wa Rais

IkuluTume ya Sheria

0 0.5 1 1.5 2 2.5

LindiManyara

TaboraRukwa

MtwaraKagera

DodomaTanga

SingidaRuvumaMwanza

MbeyaKilimanjaro

KigomaDar es Salaam

PwaniMorogoro

IringaArusha

ShinyangaMara

Je, Wilaya Yako Safi?Je, Wilaya Yako Safi?

Tafakari.Tafakari.

Chukua Hatua.Chukua Hatua.

Malipo Yalipwa kwa Wafanyakazi Hewa H/W Kilosa ni Halmashauri ambayo ni mwajiri mkubwa wa wafanyakazi waliostaafu, kujiuzulu, kufukuzwa kazi au kufariki, huku ikilipa mishahara yenye thamani ya shilingi milioni 119 kwa wafanyakazi hewa kuanzia mwaka 2009 mpaka 2010.

Hati za Malipo Kukosekana H/W Kilosa pia ni kiongozi katika kufanya malipo bila hati za malipo, ikiwa na shilingi bilioni 1 za matumizi bila kuwepo hati za malipo kwa ajili ya ukaguzi wa mwaka 2009.

Kukosekana kwa Vitabu vya Kukusanyia Mapato Kuanzia mwaka 2006 mpaka 2010, H/W Tandahimba iliongoza kwa “kupoteza” vitabu 974 vya kukusanyia mapato.

Mapato Kukosekana H/M Kinondoni kwa mwendelezo iliongoza kwa kuwa na mawakala wanaokusanya mapato bila kuwasilisha kwenye Halmashauri, ikiwa na shilingi bilioni 1.5 za walipa kodi zikienda kwenye mifuko ya mawakala hao kuanzia mwaka 2009 mpaka 2010.

Mishahara Kutolipwa na Kutorudishwa Hazina H/W Nachingwea ni bingwa kwa kutunza mishahara ya wafanyakazi walioacha kazi ambayo ilipaswa kurudishwa Hazina Kuu ya Serikali, ikitunza kiasi cha shilingi milioni 419 cha mishahara hiyo.

Fedha Kutopelekwa kwenye Kata na Vijiji Baada ya kufutwa kwa baadhi ya vyanzo vya mapato, Halmashauri hupewa ruzuku ya fidia kutoka Serikali Kuu. Asilimia 20 ya fedha za ruzuku hiyo inapaswa kupelekwa kwenye kata na vijiji. H/W Nzega ilivunja kanuni kwa kutopeleka fedha nyingi kwa kiasi cha shilingi milioni 326 kwenye kata na vijiji vyake katika mwaka 2009.

Fedha za Jimbo Kutotumika Mwaka 2010, H/M Sumbawanga haikutumia shilingi milioni 97 za fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo. Fedha hizi zilihitajika kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mfuko wa Afya ya Jamii Kubadilishwa Katika majaribio yaliyofanywa na CAG, H/W Iringa ilichukua shilingi milioni 116 kutoka kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii kwa matumizi mengine.

Wilaya YakoWilaya Yako Taifa LakoTaifa Lako

Mkoa WakoMkoa Wako

Malipo yenye Nyaraka Pungufu Mwaka 2010, H/M Ilala iliibuka bila upinzani ilipofanya malipo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.8 bila nyaraka muhimu za kuthibitisha matumizi hayo.

Fedha Kutotumika Kuanzia mwaka 2006 mpaka 2010, H/M Ilala pia iliongoza kwa kuwa na fedha nyingi ambazo hazikutumika kufikia kiasi cha shilingi bilioni 26.2.

Masuala Yasiyoshughulikiwa Hadi mwaka 2010, H/W Kilwa imeacha masuala mengi bila kufanyiwa marekebisho yakifikia kiasi cha shilingi bilioni 9 za masuala yasiyoshughulikiwa.

Je, unataka kufahamu jinsi Halmashauri ya Wilaya yako inavyosimamia fedha za umma? Je, unataka kufahamu jinsi usimamizi wa fedha katika mkoa wako unavyolingana na mikoa jirani? Je, ungependa kufahamu Wizara zipi ni safi na zipi ni chafu?

Chati zilizopo kulia zinalinganisha matokeo ya jumla ya ripoti za Mdhbiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa miaka mitano iliyopita katika Wizara, Idara na Wakala (vyombo vya kitaifa), Sekretarieti za Tawala za Mikoa (vyombo vya mikoa), na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri za Wilaya, Majiji, Manispaa, na Miji). Upande wa kulia matokeo yamewekwa rangi kulingana na aina ya matokeo, rangi ya kijani kibichi ikiashiria matokeo mazuri sana na nyekundu inaashiria mabaya sana. Kama inavyoonekana, hakuna taasisi ambayo ilipata matokeo safi sana ya ukaguzi (kijani kibichi) na hakuna iliyopata matokeo chafu sana (nyekundu).

Matokeo yaliyowekwa rangi kwenye Halmashauri za Wilaya (H/W), Halmashauri za Majiji (H/J), Halmashauri za Manispaa (H/M), na Halmashauri za Miji (H/Mji) yanawakilishwa na ramani hapa chini ikiwa pamoja na mifano ya ukiukwaji mkubwa wa usimamizi wa fedha.

Ili kuchora chati na ramani, matokeo ya ukaguzi yaliwekwa alama kama ifuatavyo:

3 = Inayoridhisha 2 = Inayoridhisha yenye masuala ya msisitizo 1 = Yenye shaka 0 = Isiyoridhisha

Safi sana (2.6-3.0)

Safi (2.1-2.5)

Chafu sana (0.0-0.5)

Chafu (0.6-1.0)

Hairidhishi (1.1-1.5)

Inaridhisha (1.6-2.0)

Maelezo na takwimu zote zimechukuliwa kutoka kwenye Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2006-2010, na Ripoti za Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2006-2010 zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania. Kwa maelezo zaidi angalia www.nao.go.tz.

Vocha za Kilimo Kwanza “Kupotezwa” Mwaka 2010, H/W Mbozi “ilipoteza” vocha nyingi za Kilimo Kwanza zenye thamani ya shilingi milioni 130.8.