(2 wakorintho 4:4) yaliyomo na msingi wa kibiblia sehemu...

21
1 KUWAOMBEA WALIOPOTEA KWA NJIA INAYOFAA “… mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini…” (2 Wakorintho 4:4) Na Lee E. Thomas 2 Yaliyomo 1. Kufahamu Manufaa 2. Msingi wa Kibiblia 3. Sehemu za Kibinafsi 4. Matakwa Yenyewe 5. Vita vya Kiroho 6. Shuhuda za Kibinafsi 7. Kufanya Ahadi Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

Upload: dangphuc

Post on 24-Feb-2018

1.054 views

Category:

Documents


21 download

TRANSCRIPT

1

KUWAOMBEA WALIOPOTEA KWA NJIA INAYOFAA “… mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini…” (2 Wakorintho 4:4) Na Lee E. Thomas

2

Yaliyomo 1. Kufahamu Manufaa 2. Msingi wa Kibiblia 3. Sehemu za Kibinafsi 4. Matakwa Yenyewe 5. Vita vya Kiroho 6. Shuhuda za Kibinafsi 7. Kufanya Ahadi

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

3

Mlango wa 1

KUFAHAMU MANUFAA

Waliopotea hawataweza na kwa kweli hawawezi kuokolewa isipokuwa mtu awaombee. Hii ni habari ya kushtua ambayo inaonekana kuwa ya kutoaminika hadi tutazame maelezo ya Biblia ya waliopotea kuwa kama: watoto wa ibilisi (Yohana 8:44), chini ya mamlaka ya Shetani (Matendo 26:18), nyumba ya mtu mwenye nguvu (Marko 3:27), wafungwa wa vita (Isaya 14:17), na waliopofushwa kwa injili (2 Wakorintho 4:3-4).

Zote hizi ni sababu za kuogofya ambazo ni lazima tuwaombee waliopotea ikiwa watakuwa na tumaini lolote la wokovu. Lakini acha tuweke mkazo tu kwa upofu wa kiroho kwa muda mfupi. 2 Wakorintho 4:3-4 inasema, “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea, ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.” Kifungu hiki kinafundisha wazi kwamba Shetani amepofusha fikira za waliopotea hasa kuwazuia kufahamu injili.

Lewis Sperry Chafer anasema, “Kupofushwa au kufunikwa kwa fikira, ambako kumetajwa katika 2 Wakorintho 4:3-4, husababisha ukosefu wa nguvu ulioenea pote wa kutambua njia ya wokovu, na imeamrishwa juu ya mtu asiyezaliwa mara ya pili na adui mkuu wa Mungu katika juhudi zake za kuzuia lengo la Mungu katika ukombozi. Ni hali ya fikira ambayo dhidi yake mwanadamu hana nguvu” (Chafer 57).

Mhubiri mmoja mkuu wa nyakati zote alikuwa Charles H. Spurgeon. Si kila anaposhiriki ushuhuda wa kuokoka kwake: “Ninakiri kwamba nilikuwa nimefunzwa kumcha Mungu, niliwekwa katika kitanda changu kwa mikono yenye uzoevu wa kuomba, na kutulizwa hadi nikalala kwa nyimbo kumhusu Yesu. Nilikuwa nimeisikia injili siku zote. Ili hali, wakati Neno la Bwana lilinijia kwa nguvu, lilikuwa jipya ni kama nilikuwa nimeishi kati ya kabila za Afrika ya Kati na nilikuwa kamwe sijasikia habari ya msingi usafishao uliojazwa kwa damu, iliyotolewa kutoka katika mishipa ya Mwokozi.

Wakati kwa mara ya kwanza niliipokea Injili na moyo wangu ukaokolewa, nilifikiri ya kwamba kamwe kwa hakika sijaisikia hapo mbeleni. Nilianza kufikiri kwamba wahubiri ambao niliwasikiliza hawakuihubiri kwa kweli. Lakini, nikitazama nyuma, ninaelekezwa kuamini kwamba nilikuwa nimeisikia Injili ikihubiriwa kikamilifu mara mia mingi mbeleni.Hii ndiyo ilikuwa tofauti: Niliisikia wakati huo ni kama sikuisikia. Wakati niliisikia, ujumbe huenda haukuwa wazi wenyewe kuliko vile ulivyokuwa wakati uliopita, lakini nguvu za Roho Mtakatifu zilikuwa pale kufungua masikio yangu na kuongoza ujumbe moyoni mwangu.

Wakati huo nilifikiri sijasikia kamwe ukweli ukihubiriwa mbeleni. Sasa ninashawishiwa kwamba nuru iliangaza kila mara machoni mwangu, lakini nilikuwa nimepofushwa; kwa hivyo,nilifikiri nuru ilikuwa haijakuja kamwe pale. Nuru ilikuwa

4

ikiangaza muda huo wote, lakini hapakuwa na nguvu ya kuipokea. Mboni ya jicho ya moyo haikuwa nyepesi kuona miali ya Mungu.” (Spurgeon 26-28).

Ushuhuda wa Spurgeon ni mfano wenye nguvu wa jinsi injili isivyofaa kwa fikira ambayo imepofushwa. Kushiriki injili na wale ambao hawajaombewa na yeyote ni kama kumtia moyo mtu ambaye ni kipofu atazame jua lakupendeza linapotua pamoja na wewe. Ni hali ya kukata tamaa, kwa sababu ni kipofu. Hawezi kuona!

Na isipokuwa Roho Mtakatifu aondoe pepo mmbaya wa upofu na kufungua fikira na moyo kwa injili, hawezi akaokolewa kwa sababu mambo ya Mungu “kwake ni upuzi” (2 Wakorintho 2:14). Neno la Kigriki la upuzi ni “moria” ambalo limetolewa neno la kiingereza moron. Webster’s anaeleza moron kama “ Mpango wa hali ya juu wa kuasi kwa akili zaidi ya mpumbavu na mpungufu wa akili.” Kwa hivyo, mtu aliyepotea anaiona injili kama upuzi na ujinga, lakini ni “mtu mwenye nguvu” katika maisha yake ambaye anasababisha hali ya kukana kuelekea injili.

Kujaribu kushiriki injili na mtu katika hali hii (ambayo inahusisha kila mtu aliyepotea ambaye hakuna yeyote anayemwombea) huenda ikasababisha madhara zaidi kuliko wema. Jessie Penn-Lewis anasema, “Hadi tumtambue mtu mwenye nguvu ambaye `ana silaha kikamilifu’ nyuma ya wazo lote la giza, na kupofushwa kuelekea Injili, hatutafanya mengi kwa upande wa kuwaleta watu kutoka nguvu ya giza kuingia ufalme wa Mwana mpendwa wa Mungu. Na hadi tujue jinsi ya kutii maonyo ya Bwana na kwanza kumfunga mtu mwenye nguvu, jitihada tunazozifanya `kuharibu uzuri wake’ kutamkasirisha tu, na kumwezesha kuimarisha silaha zake, na kulinda jumba lake kubwa kwa amani” (Penn-Lewis 42-3).

Mara tutakapofahamu umuhimu wa kuiombea mioyo iokolewe, ni lazima tujifunze ni jinsi gani ya kuifanya. Katika Januari, 1979 toleo la Fullness Magazine, Manley Beasley aliandika toleo lenye kichwa “Kuwaombea waliopotea.” Haya ndio maneno yake ya kufungua: “ Kuwaombea waliopotea ni sehemu ambayo mengi husemwa lakini machache yanajulikana au kufahamika.” Ni kama kujaribu kufungua kasha lililofungwa bila kujua mchanganyo; haidhuru ni jinsi gani vilivyomo ni vya thamani, mwishowe tunavunjika moyo na kuacha.

Lakini mioyo ya milele ambayo Kristo alikufa kwa ajili yao ni ya thamani sana kwetu kuacha. Kwa hivyo, ni lazima tujifunze ni jinsi gani ya kuwaombea kunakofaa. Jambo la hakika ni kuwa, huenda ni maombi yako ambayo yanamweka mtu nje ya kuzimu. Charles G. Finney ambaye ni mhubiri wa ufufuo maarufu alisema, “Katika hali ya rafiki mwenye moyo mgumu, sharti ambalo anaweza kuokoka kutoka kuzimu huenda ikawa ni bidii na maombi yako ya kushurutisha ya mtu huyo.” (Finney 54).

Yesu alifanya tu kile aliona Baba akifanya (Yohana 5:19). Kadhalika, tunafaa kufanya tu kile ambacho tunamwona Bwana wetu anafanya, na anafanya nini “Maana yu hai siku zote ili awaombee” (Waebrania 7:25). Tunafanya makosa makubwa kwa kuwabandika Wakristo wengine waombezi. Hii inaelekeza kuonyesha kwamba sisi wengine tumeondolewa jukumu hilo – SI HIVYO!!! Sisi sote tunafaa kufanya kile ambacho tunaona Bwana wetu akifanya – kuwaombea wengine.

Kwa hivyo, wacha tujifunze ni jinsi gani ya kuomba kunakofaa kwa waliopotea na kujiunga na Bwana wetu kwa kufanya jambo kuu.

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

5

Mlango wa 2

MSINGI WA KIBIBLIA

Njia moja yenye nguvu ya kuomba kunakofaa kunahusisha kuweka mbele ya Mungu sababu zenye nguvu ni kwa nini ni lazima maombi yetu yajibiwe. Hata anatuamrisha kufanya hivyo katika Isaya 41:21, “ Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana, toeni hoja zenu zenye nguvu…”

Sababu zenye nguvu kwa kawaida zina msingi wa Biblia, na kuna sababu kama hizo nyingi zinazohusisha maombi ya waliopotea. Ninapenda jinsi F.J. Huegel ameieleza, “Ikiwa tutapata njia ya kushirikisha maombi yetu dhaifu ya msaada kwa malengo makubwa ya Mungu katika kuitangaza Injili na kuendeleza Ufalme wa Kristo, basi tunaanza kuomba kwa roho na bidii ya Paulo au David Brainard au George Muller au Hyde mwombaji, na ni lazima tusikike na mambo makubwa yatatendeka. (Huegel 80)

Sababu ya kwanza ya kuwaombea waliopotea ni upendo wetu kwao. Maombi yameelezwa kama “Upendo katika kupiga magoti.” Bila shaka, ulikuwa upendo wa Mungu kwa wanadamu ambao ulimleta Yesu msalabani; ulikuwa ni upendo kwa ndugu zake watano ambao ulimshurutisha yule tajiri kuzimu kuwaombea “wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso” (Luka 16:27-28); na upendo utatuongoza mahali pa maombezi.

Pacific Garden Mission ya kihistoria katika Chicago imetumika kwa nguvu kwa Mungu kuokoa mamia ya mioyo ambayo inatikisika juu ya mteremko wa kuzimu. Na si ajabu kwangu ya kwamba alama ya neon yenye urefu wa futi kumi na nane yenye maandiko “PACIFIC GARDEN MISSION” inahusisha ukumbusho MAOMBI YA MAMA YAMEKUFUATA. Ni ahera tu ambayo itafichua hesabu ya kushangaza ya mioyo ambayo imeokolewa kupitia machozi na maombi ya upendo wa mama! Hakika, upendo ni mali yetu kuu ya kuokoa mioyo.

Imani ni msingi mwingine wa Biblia wa kuwaombea waliopotea. Yesu alisema, “Yote yawezekana kwake aaminiye” (Marko 9:23). Mambo yote bila shaka yanahusisha wokovu wa mioyo. Ikiwa unaweza kumwamini Mungu kwa wokovu wa mtu fulani, utapata.

Watu wanne walimleta rafiki yao aliyepooza kwa Yesu na alipoiona imani yao, Alisema, “Mwanangu umesamehewa dhambi zako (Marko 2:5). Ingawa walimleta aponywe, alipokea pia msamaha wa dhambi zake. Hili ni onyesho la ajabu la nguvu ya imani. Hakika, imani ni sarafu ya ufalme.

Sababu yangu moja ya kupendeza ya kuwaombea waliopotea ni uwezo mkubwa ambao Biblia inawekea maombi. “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii,” kulingana na Yakobo 5:16. Hatuwezi hata kuanza kufahamu jinsi gani maombi yenye nguvu yalivyo ya kushangaza, kwa vile yanatoa mvuto wa nguvu wa aina yoyote katika ulimwengu wote.

“Maombi ni kazi ya cheo cha juu sana ambayo imewekwa kupita mawazo ya wanadamu. Kwa kuwa Mkristo anapoomba, uwezo wake wa kufaulu na nguvu yake ya kutenda mema inazidishwa mara elfu, ndio mara elfu mia moja. Huku si kuongeza

6

sifa, sababu ikiwa ni kwamba wakati mtu anaomba, Mungu anafanya kazi” (Huegel 10).

Wakati bomu ya atomic iliangushwa Japan wakati wa Vita vya 2, watu 92,000 waliuawa. Lakini wakati Assyria iliizunguka Yerusalemu ikamsababisha Mfalme Hezekia kumlilia Mungu kwa niaba ya watu wake, Alituma malaika aliyewauwa askari wa Assyria 185,000 kwa usiku mmoja. Maombi ya Hezekia yalikuwa mara mbili zaidi ya bomu ya atomic!! Ikiwa maombi yana nguvu ya kuharibu majeshi, je ni mara ngapi zaidi bila shaka ilivyo nguvu yake kuokoa mioyo!

Ikiwa hatungekuwa na msingi wa Biblia wa kuwaombea waliopotea ila tu Mungu anatutarajia tufanye hivyo, hii ingekuwa ya kutosha. Mungu “alifadhaika” wakati Hangeweza kupata mwombezi mmoja wa Israeli (Isaya 59:16). Hii inaniambia ya kwamba alikuwa anatarajia kupata baadhi. Sikiliza maelezo ya Andrew Murray kuhusu Mungu akitafuta waombezi: “Mara kwa mara alishangaa na kulalamika kwamba hapakuwa na mwombezi, hakuna yeyote wa kujisogeza ili ashike nguvu Zake. Na bado anangoja na kushangaa katika siku zetu, ya kwamba hakuna waombezi zaidi, ya kwamba watoto Wake wote hawajitolei kwa kazi hii ya cheo cha juu na takatifu, ya kwamba wengi wao wanaofanya hivyo, hawajishughulishi kwa bidii nyingi na kwa uvumilivu. Anashangaa kuwapata wahudumu wa injili yake wakilalamika kwamba majukumu yao hayawaruhusu kupata wakati wa kuwa waombezi, ambayo anahesabu kuwa kazi yao ya kwanza, yao ya juu, yao ya kufurahisha, kazi yao ya pekee ya kufaa” (Murray 114). Mungu ameweka kuwaombea wengine kuwa kazi ya kwanza kuu katika maisha yetu. Sikiliza kilio cha moyo wa Mungu, “Basi kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote…. Ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua kweli” (Timotheo 2:1-4). Neno la Kigriki la kwanza ni “proton” na linaelezwa katika kamusi ya kiingereza ya Strong’s kama kuwa ya kwanza au mbele kwa wakati, mahali, taratibu au umuhimu. Kwa kuwa Mungu anatamani watu wote waokolewe na kwa kuwa hakuna anayeweza kuokoka bila maombi, je ni ajabu kwamba maombi ni ya juu katika orodha ya mambo ambayo Mungu angependa tuyafanye? Pia kati ya vishawishi vyenye nguvu kwa sisi kuwaombea waliopotea ni mifano ya Biblia. Mfano mkubwa wa yote ni Bwana Yesu mwenyewe. Unabii katika Isaya 53 unasema ya kwamba Kristo “alifanya maombi kwa wenye dhambi.” Unabii huu ulitimia wazi wakati alipokuwa msalabani Aliomba, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawalijui watendalo” (Luka 23:34). Yesu anafaa kuwa mfano wetu usiobadilika katika kuwaombea wengine kwa sababu bado Anafanya hivyo!! Ni Mwokozi na Bwana, Mfalme wa Wafalme ambaye ameketi katika kiti cha enzi mbinguni na bado anaendelea kuwaombea wengine hata sasa. Waebrania 7:25 ni pigo katika fikira zangu, “Naye kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye, maana yu hai siku zote ili awaombee.” Mtume Paulo ni mfano mzuri wa kufuata. “Nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe” ni kukiri kwake

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

7

kwenye huruma katika Warumi 10:1. Katika Born For Battle, R. Arthur Mathews anaeleza maombi yangu kama “mwisho wa kutafuta kwa kubahatisha kwa mwanadamu kusimama kwenye pengo na kuwaombea watu ambao wanaangamizwa kwa uharibifu kupitia kwa dhambi zao wenyewe na ukaidi wa kukataa mamlaka ya Mungu katika maisha yao ya asili” (Matthews 104). Swali la pekee kwetu ni, “Tutafuata mifano yao?”

Hata ingawa kuna misingi mingine mingi ya Biblia ambayo tunaweza kutaja kwa aina hii ya maombi ya kutetea, nataka kutaja moja zaidi- Mungu ameifanya jukumu letu!! Tukiwa washiriki wa “ukuhani mtakatifu” wa Mungu (1 Petro 2:5) inatufanya sisi kuwasimamia wengine kwa sababu makuhani wanawakilisha dunia na mbinguni. Kazi yetu ya kwanza ni kusimama kati ya wanadamu na Mungu tukitetea hali yao Kwake. Hivi ndivyo alivyofanya Haruni alipochunguza na kusimama kati ya walio hai na waliokufa ili kusitisha tauni ya mauti iliyosababishwa na dhambi za Waisraeli.( Hesabu 16). Kwa vile sisi sote tuliookolewa ni makuhani, sisi sote tuna jukumu la kuwaombea waliopotea, na tusipofanya hivyo watakaa milele katika ziwa la moto. Acha maneno yenye kutia uchungu yaongee kwa mioyo yetu “Siwezi nikatia shaka – sipendi sana kusema hivi, ningependa sana nisiseme ikiwa ningeangalia moyoni mwangu au mwako. Lakini siwezi kutia shaka, ya kwamba kuna watu katika dunia ile ya chini iliyopotea ambao wako kule kwa sababu mtu alikosa kuweka maisha yake ili ajuane na Mungu, na kuomba “ (Gordon 194-95). Maombi yangu ni kuwa utaruhusu sababu hizi za nguvu za Biblia zikushauri kuwaombea waliopotea kama haujafanya hivyo mbeleni.

8

Mlango wa 3

SEHEMU ZA KIBINAFSI

Kuna sehemu au masharti mawili yanayohusishwa katika kila ombi linalojibiwa – haki na imani. Haki iliyohesabiwa ya Kristo, ambayo huja kupitia kwa damu Yake iliyomwagika, ndiyo hutupatia ujasiri wakukaribia kiti chake cha enzi cha neema. Bila shaka ni sharti kwa ombi linalofaa. Lakini haki ya kibinafsi pia ni ya maana, kwa sababu Zaburi 66:18 inasema, “Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia.” Labda Yesu aliijumlisha vizuri wakati alisema, “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa” (Yohana 15:7). Katika maneno mengine Wakristo watiifu, maombi yao hujibiwa!! Sehemu nyingine ya muhimu katika ombi lote linalojibiwa ni imani. Hii ni sheria isiyovunjika katika milki ya kiroho. Kila mara huwa “Kwa kadiri ya imani yenu mpate” (Mathayo 9:29). Kutoamini kunaendelea kuwa dhambi inayotusonga na mara kwa mara si sababu ya ombi lisilojibiwa. Kwa hivyo wakati tunapowaombea waliopotea, tunahitaji haki ( iliyohesabiwa na ya kibinafsi) na imani. Lakini kuna sehemu nyingine nane ambazo ziko hasa kwa kazi hii. Ya kwanza kwa hizi ni kuvunjika. “Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha” ni sheria ya kuvuna. Hata hivyo, tunataka mavuno bila huzuni. Leonard Ravenhill wakati mmoja alisema, “Mungu hajibu maombi mengi – yamefungwa ndani ya huruma za kibinafsi au zinalenga faida za kibinafsi. Yeye hujibu maombi ambayo yamekata tamaa” (Ravenhill 110). Na hadi tutakapokata tamaa kwa mioyo, maombi yetu kwao huenda yakabaki bila kujibiwa. Kama vile Yesu alililia Yerusalemu, hivyo ni lazima nasi tulilie wapendwa wetu waliopotea ikiwa tunataka kuwaona wakiokoka. Wakati mmoja wafanyikazi wa Jeshi la Wokovu walimwandikia mkubwa wao wakisingizia kutofaa kwao katika kuvuta mioyo na kuuliza wafanye nini. Alijibu ujumbe wa maneno mawili, “Jaribu machozi.” Machozi ni nguvu sana ya kwamba yakiunganishwa na kushiriki injili, Mungu anathibitisha mavuno sana (Zaburi 126:5-6). Sehemu nyingine ya muhimu ni uchungu. Hii inaonyesha maumivu na uchungu wa kuzaa mtoto kama vile inavyoonekana katika Isaya 66:8, “… maana Sayuni alipoona utungu, alizaa watoto wake.” Kamusi ya Strong’s inaeleza utungu “Kugaagaa katika uchungu; kulemewa kwa uchungu.” Luka 22 inaongea kuhusu Yesu akiwa katika uchungu na jasho Lake kama matone makubwa ya damu. Wengi wetu hatujafika mahali hapa katika maombi yatu, ambayo ndio sababu hatuoni matokeo ya ajabu ya kuwavuta waliopotea kwa Kristo. Yesu alieleza ujuzi wa wokovu kama “kuzaliwa tena.” Kama vile mama anavyoona uchungu anapojufungua mtoto kwa kimwili, hiyo ni kweli katika milki ya kiroho. Paulo anaongea kuhusu “uchungu katika kuzaa tena” kwa Wagalatia ambao walikuwa hawajakomaa kiroho ambao alikuwa amewavuta kwa Kristo. Lakini hata vile mwanamume hawezi kufahamu kikamilifu uzito wa uchungu ambao mke wake

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

9

anaona kwa sababu hazai, vivyo hivyo Wakristo wengi hawaelewi umuhimu wa kuwa na uchungu kwa mioyo kwa vile asili mia tisini na tano ya wanaokiri kuwa wakristo hawavuta hata moyo mmoja kwa Kristo!! Mmoja wa mashujaa wangu ni John “Praying” Hyde, mmishonari huko India ambaye aliyatoa maisha yake kwa kuombea mioyo iokolewe. Katika mwaka wa 1908 aliomba Mungu ampe moyo kila siku. Mwaka huo aliwavuta zaidi ya watu mia nne kwa Kristo. Mwaka uliofuata aliomba kwa mioyo miwili kila siku (sio tu waombe ombi, bali wabatizwe na wajitenge kwa ajili ya Kristo) na akawavuta watu zaidi ya mia nane kwa Kristo. Halafu katika mwaka wa 1910, aliombea mioyo minne kwa siku na Mungu akatimiza haja yake. Lakini katika mwaka huu huku afya yake ilipokuwa ikidhoofika, rafiki yake alimsihi aende kwa daktari. Ili tufahamu hali ya kutisha ya uchungu kwa mioyo, acha tusikie ni nini daktari anamwambia: “Moyo uko katika hali ya kuogofya. Sijakutana na hali mbaya kama hii. Umesongezwa kutoka katika nafasi yake ya asili ya upande wa kushoto hadi upande wa kulia. Kupitia shida na uchovu wa akili uko katika hali mbaya ya kwamba itahitaji miezi na miezi ya utulivu kamili ili kuurudisha tena kwa kitu chochote kama hali yake ya kawaida. Umekuwa ukijifanyia nini? Usipobadilisha maisha yako yote na uache uchovu wa akili, utalipia adhabu kubwa sana katika miezi sita” (Carre 44). Kuna bei ya kulipa ikiwa tutaungana na Bwana wetu wa thamani kwa kuwa na uchungu wa ukombozi wa mioyo kutoka katika ufalme wa giza, lakini itakuwa ni ya thamani! Kwa hivyo, wacha tujiunge na kundi hilo kuu ambalo “halikupenda maisha yao hata kufa” (Ufunuo 12:11) na ushindi utakuwa ni wetu. Kupitia mifano mingi halisi katika Biblia kuhusu hali mbaya ya waliopotea, tunaweza kuona kwa urahisi ni kwa nini bidii katika maombi inakuwa ni sehemu ya muhimu. Isaya 14:17 anaeleza waliopotea kuwa wafungwa ambao Shetani anakataa kuwafungua. Matendo 26:18 inatuambia ya kwamba wako chini ya mamlaka au amri ya Shetani. Labda maelezo ya kuogofya sana ya yote ni yale ambayo yamepeanwa na Yesu katika Marko 3:27 kama nyumba ya mtu mwenye nguvu. Hata Anatuambia kwamba “hakuna mtu” anayeweza kuwasaidia wale watu hadi mtu mwenye nguvu afungwe. Badhi ya mapepo yanayotawala yana nguvu ya kwamba maombi na kufunga yanahitajika kupata ushindi (Marko 9:29). Maombi ya bidii ni ya muhimu kwa sababu ya kutotaka kwa Shetani kuwaachilia, sio kwa sababu Mungu hataki kuwaokoa!! Shetani hata anaweza kutawala nchi nzima na tamaduni. Hii ndio sababu kila mara ni vigumu kwa Wamishonari kuwa wa kufaa kufikia makundi ya watu wengine. “Ilikuwa ni baada ya miaka saba kabla Carey alimbatiza mwokovu wake wa kwanza India; ilikuwa ni baada ya miaka saba kabla Judson hajavuta mwanafunzi wake wa kwanza huko Burmah; Morrison alifanya kazi ngumu kwa miaka saba kabla Mchina wa kwanza alikuja kwa Kristo; Moffat anatangaza kwamba alingojea miaka saba kuona wazi kwa mara ya kwanza kuenda kwa Roho Mtakatifu juu ya Wabechuana wa Africa; Henry Richards alitenda kazi kwa miaka saba Congo kabla ya kupata mwokovu wa kwanza huko Benza Mantaka” (Gordon 139-40). Njia moja ya Shetani ni kufanya hali kuonekana ngumu ili tupate kushushwa moya na kuacha kuomba. Sababu inayomfanya afanye hivi ni kwa kuwa hana kinga

10

dhidi ya maombi. Msemo wa zamani ni kweli kwamba Shetani hutetemeka akimwona mtakatifu mdhaifu akiwa kwa magoti yake. Maombi yote ni vita na, ukiomba,Shetani anashindwa hata ingawa hauoni mabadiliko yoyote katika jambo. Hata hivyo, kama tungeona ni nini kinafanyika katika milki ya kiroho wakati tunaomba, tutatiwa nguvu sana. Kumbuka vile Mungu alimfumbua macho ya mtumishi wa Elisha apate kuona farasi na magari ya moto yakiwalinda kutokana na adui (2 Wafalme 6:17)? Kwa hivyo endelea kuwaombea waliopotea kama unaona matokeo au kwa sababu maombi yako yanajibiwa!! Hali hii ya kushangaza ya aina hii ya bidii inapatikana katika maisha ya George Muller. Kwa sababu alikuwa na ufanisi sana mapema katika huduma yake ya kuona mabadiliko ya ghafula ya wengi ambao alikuwa amewaombea, alipata dhana kuwa itakuwa hivyo kila mara. Lakini sikiliza ushuhuda wake kuhusu haya, “Ikiwa nitasema kwamba katika miaka hamsini na nne na miezi tisa ambayo nimekuwa mwamini katika Bwana Yesu Kristo nimekuwa na majibu elfu thelathini ya maombi, kwa saa ile ile au siku hiyo hiyo ambayo mahitaji yamefanywa, sitaenda kidogo mbali sana… Lakini mmoja au mwingine anaweza kudhania maombi yangu yote yamejibiwa bila kusita. La, sio yote. Mara kwa mara nimengojea kwa wiki, miezi, miaka mara kwa mara miaka mingi… Katika Novemba 1844, nilianza kuombea kubadilishwa kwa watu watano. Niliomba kila siku bila kutulia, niwe mgonjwa au na afya, katika nchi au baharini na hata shinikizo la shughuli zangu ziwe namna gani. Miezi kumi na minane ikapita kabla mmoja wa wale watano aokoke. Nilimshukuru Mungu na nikaendelea kuwaombea wengine. Miaka mitano ikapita wa pili akaokoka. Nikamshukuru Mungu kwa wa pili na nikaendelea kuwaombea wale watatu. Siku baada ya siku niliendelea kuwaombea, na miaka sita ikapita kabla wa tatu aokoke.Nilimshukuru Mungu kwa hao watatu na nikaendelea kuwaombea wale wengine wawili. Hawa wawili bado hawajaokoka. Mwanamume ambaye Mungu kwa utajiri wa neema Yake amepewa makumi ya maelfu ya majibu ya maombi, kwa saa ile ile au kwa siku ile ile yalitolewa, amekuwa akiomba siku baada ya siku kwa karibu miaka thelathini na sita kwa kuokolewa kwa watu hawa wawili, hata sasa wamebakia bila ya kuokoka” (Steer 246-47). Lakini huu sio mwisho wa hadithi. Aliendelea kuomba siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka halafu akasema, “ Jambo kuu ni kutokata tamaa kamwe hadi jibu lije. Nimekuwa nikiomba kwa miaka sitini na mitatu na miezi nane kwa kuokolewa kwa mtu mmoja. Hajaokolewa bado lakini ataokoka. Itakuwaje vingine…Ninaomba.”Siku ilikuja ambayo rafiki ya Muller alimpokea Yesu. Haikuja hadi jeneza la Muller lilipoteremshwa ndani ya ardhi. Hapo, karibu na kaburi lililowazi, huyu rafiki alipeana moyo wake kwa Mungu. Maombi ya uvumilivu yalikuwa yameshinda vita vingine. Ufanisi wa Muller unaweza kufupishwa kwa maneno manne ya nguvu: “He did not quit”, “Hakuacha” (Eastman 99-100). Kwa sababu maombi ni vita, ninataka kushauri ya kuwa shambulio ni muhimu katika uombezi. Mungu ametupatia mamlaka makuu (Mathayo 16:19), na ni sharti tuyatumie, hasa katika uinjilisti duniani (Mathayo 28:18-20). Sisi ni washindi (Ufunuo 12:11) na “zaidi ya washindi” (Warumi 8:37), na Mungu anatutarajia “kumshambulia” mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake na

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

11

kumshinda ili “kuharibu vitu vyake” (Luka 11:21-22). Kama vile tumeona, Shetani hushika mioyo mateka na hataiachilia bila vita! Lakini ni lazima tutambue kila wakati kwamba “silaha za vita vyetu si za kimwili bali kuu kupitia kwa Mungu” (2 Wakorintho 10:4). Tukiwa tayari kwa vita katika mavazi ya Mungu na silaha za Mungu, tunapigana kwa kuomba (Waefeso 6:10-18). Mungu kwa nguvu ameliwezesha kanisa Lake kushambulia na kushinda “milango ya kuzimu.” bali, tunakaa kwa utulivu, tukiruhusu kuzimu “kuongeza tamaa yake, na kufunua kinywa chake bila kiasi” (Isaya 5:14). Nilichochewa na njia ya Ravenhill ya kusimulia huzuni hii – “ Kuna hali ya kusongwa ya kutokuwa na bidii katika kanisa kwa hatari ya hukumu” (Ravenhill 80). Kama vile mti mdogo wa mbao unaweza kumshika ndovu mkubwa kwa sababu amefundishwa kuamini hawezi kufunguka, vivyo hivyo kanisa la Mungu aishiye limedanganywa na Shetani kuhusu nguvu zetu kuu (Waefeso 1:17-23) na mamlaka ya kwamba hatujaribu tena. Na anaendelea kuwafunga wapendwa wetu huku tukififia katika uzembe na kutoamini. Shetani anakataa kukiri kushindwa kwake kwa mwanzo, anakataa kusalimisha mamlaka yake yoyote hadi lazima; kwa ukatili na kwa ukali ashindane kila kitendo dhidi yake, akitoa tu kile ambacho amepokonywa kwa nguvu (Newell 27). Kwa hivyo, ni wakati wetu kuwa wajeuri katika vita kwa mioyo, kwa kuwa ufalme wa mbinguni “hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka” (Mathayo 11:12). Ukija wakati wa kuwaombea wengine, kutetea kunafaa. Kuna mifano mingi ya Biblia: Ibrahimu kwa sodoma (Mwanzo 18), Musa kwa Israeli (Kutoka 32), Hezekia kwa Yuda (2 Wafalme 19) na orodha inaendelea. Kutetea kuna maana ya msingi ya kwamba unaweka mbele ya Mungu ni kwa nini ajibu maombi yako. Hata Bwana anatufundisha “tutoe hoja zetu zenye nguvu” (Isaya 41:21). A.T Pierson anasema, “tunafaa kujadiliana hoja yetu na Mungu, si kwa hakika kumsadikisha, bali kujisadikisha. Kumthibitishia kwamba, kwa neno Lake na kiapo na tabia, Amejifunga kati, tunaonyesha kwa imani yetu kwamba Ametupatia haki ya kuuliza na kudai, na ya kwamba atajibu ombi letu kwa sababu hawezi akajikana” (Pierson 150). Spurgeon alitilia maanani kwa nguvu kuhusu uwezo wa kutetea.Alisema, “Ni mazoea ya imani, akiomba , kutumia mateteo. Wasemaji tu wa maombi, ambao hawaombi kabisa, wanasahau kujadiliana na Mungu; lakini wale ambao watashinda huleta mbele sababu zao na hoja zao za nguvu na wanashauriana na Bwana… Oh, ndugu acha tujifunze kuteta mafundisho, ahadi na chochote kile ambacho kitatufaa; lakini acha kila mara tuwe na jambo la kutetea. Usihesabu umeomba isipokuwa umetetea, kwa kuwa kutetea ni mafuta halisi ya maombi” (Spurgeon 49-50). George Muller alichukua maneno matatu ya kwanza ya Zaburi 68:5, “Baba wa yatima,” na kukitumia kifungu hiki mara kwa mara kuwaombea yatima wake. Haya ni maneno yake mwenyewe: “Kwa msaada wa Mungu; hii itakuwa hoja yangu mbele Yake, kuwaheshimu yatima, katika saa ya haja. Ni Baba yao, na kwa hivyo amejiahidi, kama ilivyokuwa, kuwapa riziki; na nitamkumbusha tu juu ya mahitaji ya hawa watoto maskini ili yatolewe.” (Pierson 143).

12

Nina hakika kabisa ya kwamba kuna mistari mingi ya maandiko ambayo tunaweza kutumia kwa kutetea juu ya wokovu wa mioyo, lakini kwa sababu ya wakati na nafasi niruhusu nitaje tu chache. Tunaweza kuhoji makusudi ya Mungu kwa mwanadamu (Yeremia 1:5), (Luka19:10), (2 Petro 3:9), (Matendo 26:18) na (Waefeso 2:5-7). Tunaweza kuhoji ahadi za Mungu kuhusu wokovu (Yohana 3:16), (Yohana 1:12), (Warumi 10:13) na (Yohana 6:37). Tunaweza kuhoji uwezo wa Mungu kuokoa (Waebrania 7:25), (Warumi 1:16), (1 Wakorintho 2:4-5) na (1Petro 1:3-5). Tunaweza kuhoji cheo cha Mungu katika uhusiano Wake na mwanadamu kama Muumba, Mkombozi, Baba na Bwana. Tunaweza kuhoji sifa na nia ya Mungu kumwelekea mwanadamu kama vile upendo Wake, huruma Yake, neema Yake, upole Wake na Uvumilivu Wake. Kuhoji kwangu kunakonipendeza kunahusu matendo yake ya kale katika kuokoa wengine. Ninawi (mji wenye uovu sana ya kwamba Mungu alikuwa ameuweka kuwangamiza), mwenye pepo Mgerasi (ambaye hakuvaa nguo, alikaa makaburini, alikuwa mkali wala mtu hangeweza kumkaribia, alitupiliwa mbali na jamii, amejazwa na jeshi la mapepo, mbaya zaidi kuliko yeyote tutakayemjua), Sauli wa Tarisa (akiangamiza kwa wingi kanisa) na miji yote ya Lida na Sharoni (Matendo 9:35). Sehemu nyingine ya maana ambayo inaweza kuwa ya kutatiza sana na kufanya miaka ya kuomba kabisa kuwa haifai ni madhumuni yetu! Madhumuni yetu ya msingi katika kuwaombea waliopotea ni lazima yawe ni kwa utukufu wa Mungu (Yohana 15:8). Lakini kwa wakati mwingi madhumuni yetu yametiwa sumu na kiburi na uchoyo. Wazazi wanaweza kuwa wanaombea “kondoo zao nyeusi” kutokana na kiburi juu ya jina la familia bila hata kutambua madhumuni yao ni machafu. Nilimwombea shemeji yangu kwa miaka bila kuona matokeo yoyote. Lakini alipopimwa na kupatikana na ugonjwa wa saratani na maombi yangu yakawa ya bidii, Mungu alinifunulia ya kwamba maombi hayo yote ya bure yalikuwa yametiwa mawaa na uchoyo. Unaona, sababu ya kweli ambayo nilitaka aokolewe ilikuwa ni kwa sababu ili dada yangu awe na mume bora na mpwa wangu awe na baba aliye bora. Kwa hivyo, Mungu hangeweza kuyajibu maombi yangu kwake. Hata hivyo, wakati nia yangu ilipokuwa safi, Mungu alimwokoa!! Katika koti ya sheria wakili anayepinga anaweza “kukataa” safu ya maswali, hoja fulani au kuwekwa mbele kwa ushahidi fulani ambao anaamini uko nje ya mipaka ya uhalali. Ikiwa hakimu atakubali “kupokea” madai ambayo yanafanya njia zisizo za sheria kuwa zisilofaa na bure. Hii ni kweli katika milki ya kiroho. Tunaweza kwa ufasaha tetea hali ya mpendwa wetu aliyepotea, kwa kutumia sababu nyingi zenye nguvu za msingi wa Biblia, lakini ikiwa madhumuni yetu ni mabaya, Shetani “hukataa” na Mungu ni lazima akubaliane naye, na kufanya maombi yetu yote na hoja kuwa hazifai na bure!! Na yule tunayemwombea atakufa na kuenda kuzimu ikiwa hatutapata madhumuni yetu sawa. Jambo lingine lililokamili la uombezi ni roho ya kujitolea. Tunapata hii ikiwa imeonyeshwa wazi katika mtume Paulo, ambaye alikuwa amekusudia “kuharimishwa na kutengwa na Kristo” kwa ajili ya wokovu wa watu wake Wayahudi (Warumi 9:3); katika Musa ambaye alifunga na kuomba kwa siku zingine arobaini

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

13

mchana na usiku kwa ajili ya dhambi za watu wake (Kumbukumbu 9:18-19); katika Esta ambaye alitangaza, “Nami nikiangamia, na niangamie” (Esta 4:16). Wakati nilipokuwa nikifundisha darasa katika chuo kuhusu Uinjilisti wa Kibinafsi, nilipiga chapa kadi za orodha ya maombi na maandiko “Nitaenda kuzimu kwa ajili yake.” Wazo lilikuwa kuorodhesha majina ya watu ambao tulikuwa tumejitolea kuenda kuzimu kwa niaba yao na kuomba kwa sababu hiyo. Katika mkutano mwingine wa darasa, baada ya kugawa kadi kwa wanafunzi wangu, mmoja wao, mchungaji alisema, “Sifikirii ya kwamba ninaweza kujitolea kuenda kuzimu kwa ajili ya yeyote.” Alikuwa akiongea kwa niaba yetu. Ingawa Mungu hawezi kutukubalia sisi tuchukue nafasi ya wengine kuzimu, bila shaka itaongeza kusudi la maombi yetu kwao ikiwa tutakuwa tumejitolea sana!! Vitu vyote vikiwa sawa, umoja ni sehemu yenye nguvu sana katika kuwaombea waliopotea. Kwa kawaida huleta matokeo ya papo hapo!! Kama tu vile kioo cha kuongeza ukubwa kinaweza kuwasha moto kwa kushika mwangaza uliotawanyika wa jua na kuikusanya kwa mahali fulani, Vivyo hivyo hata Wakristo wakiomba wakiwa wameungana kwa mtu fulani kumshinda mtu mwenye nguvu na kukaza uwezo wa Mwana katika maisha yake. Hiki ndicho kilichotendeka katika kuokoka kwa mwana wa William Carey Jabez. Ilikuwa ni wakati wa mkutano wa kila mwaka wa Baptist Missionary Society uliokuwa ukiandaliwa huko London Dr. Ryland, akiwa amelemewa sana kwa ajili ya Jabez alisema: “Ndugu, acheni tutume ombi la pamoja, lililoenea, na la moyo wa bidii kwa Mungu katika heshima ya utulivu kwa ajili ya wokovu wa Jabez Carey.” Kama kwamba Roho Mtakatifu alikuwa kwa ghafula ameanguka juu ya kusanyiko, mkutano wote, wa watu wasiopungua elfu mbili, walienda katika uombezi wa utulivu. Carey alipokea barua kutoka kwa Jabez ikimwambia juu ya kuokolewa kwake, “na wakati wa mwamko ulipatikana kulingana na saa uombezi huu mkubwa” (Gordon 87-88). Jim Cymbala anaelezea jinsi aliumia sana katika maombi ya binti yake Chrissy kwa miaka miwili na nusu bila matokeo yanayoonekana. Halafu wakati wa mkutano wa maombi jumanne usiku huko Brooklyn Tabernacle, mwanamke mchanga aliona moyoni mwake ya kwamba wamwombee Chrissy. Usiku huo "kanisa lilibadilika kuwa chumba cha maumivu. Kulitokea kuugua, hali ya nia ya kukata tamaa, kama kwamba kusema, Shetani, hautatwaa msichana huyu. Toa mikono yako kwake – anarudi!” Na baada ya masaa thelathini na mawili alirudi (Cymbala 63-65)! Wakati mchungaji wa kanisa la New Hope Baptist huko Jones, Louisiana, alialika mkutano wake kuandika katika karatasi jina la mtu ambaye walitaka kuona ameokolewa na wangejitolea kumwombea mtu huyo, watu kumi na wanane waliandika “Mike Doles.” Katika wiki mbili aliokolewa. Baada ya miaka kumi na minane bila matokeo ya kumwombea mume wake aokolewe, Helen Gresham alimuuliza mchungaji wake, Mickey Hudnall amsaidie kuomba. Wawili hao wakimwombea Ricky kwa pamoja, aliokolewa kwa ajabu chini ya miezi miwili! Na utachekeshwa kwa furaha wakati wote kwa vitu vyote ambavyo Mungu alifanya katika maisha yake wakati wa muda wa miezi hiyo miwili ukisoma ushuhuda wake. Hata hivyo, hakujua ya kwamba mke wake na mchungaji wake walikuwa wakimwombea.

14

Acha tusimulie nguvu ya kutisha ya kuomba kwa kuungana kwa waliopotea ilivyo na uwezo: watu elfu mbili walimwombea Jabez Carey na akaokolewa saa ile ile, mamia kadhaa walimwombea Chrissy Cymbala na alikuwa akitubu katika masaa thelethini na mawili, kumi na wanane walimwombea Mike Doles na aliokolewa katika wiki mbili, wawili walimwombea Ricky Gresham na alibadilishwa kwa ukamilifu katika chini ya miezi miwili!! Ikiwa utampata mtu fulani akusaidie kumwombea mpendwa wako, utaona matokeo ya ajabu!! Kwa kuwa wawili wanaweza kuwafukuza elfu mbili katika milki ya kiroho (Kumbukumbu 32:30) na wawili “wakikubaliana pamoja” katika maombi siku zote watapata mahitaji yao kulingana na Bwana Mwenyewe (Mathayo 18:19). Acha nikuambie ni kwa nini kuwaombea waliopotea kwa kuungana kuna nguvu sana. Kwanza na ya mbele ni thamani ya ajabu mno ambayo Mungu huweka kwa watu Wake. Hii ni tamaa ya Bwana ambayo inaonekana katika maombi Yake kwetu (Yohana 17) ambapo mara tano anaomba ya kwamba “tuwe na umoja.” Pia jambo la kwanza katika orodha ya Mungu ambalo tunafaa kulifanya ni “tuwaombee watu wote…ili waokolewe (1 Timotheo 2:1-4). Sasa, kwa vile umoja haupatikani kabisa na waombezi ni wachache kabisa (Mungu hangeweza kumpata hata mmoja katika Israeli – Isaya 59:16), ukileta hizi mbili pamoja - umoja katika uombezi – unakuwa na kitu ambacho mara mbili hakipatikani. Na Mungu hukipata cha thamani ya kwamba Anakibariki sana kupita mawazo yetu!!! Sababu ya pili ni rahisi – kuna mtu mwenye nguvu mmoja anayeyatawala maisha ya mtu. Wakati watu kadha wanakuja dhidi ya mtu mwenye nguvu mmoja, anashindwa kwa urahisi kwa sababu “yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia” (1 Yohana 4:3-4). Na halafu “kuharibu vitu vyake” ni jambo rahisi. Wakati mwingi mtu aliyepotea atakuja kwako akitafuta msaada. Hivi ndivyo ilivyokuwa na Jimbo Barrentine. Niliahidiana na mke wake Rachele katika mwezi wa Januari kumwombea. Miezi miwili baaadaye alikuwa chini ya thibitisho la hatia ya makosa lililomponda ya kwamba alikuja ofisini mwangu akinitafuta. Lakini nilikuwa Arkansas nikifundisha masomo haya katika mkutano wa maombi, kwa hivyo alienda nyumbani kwa mchungaji mwingine katika kanisa letu kupata njia ya wokovu. Hangeweza kuningojea nirudi; alitaka kuokoka wakati huo na hapo! Sababu ya tatu ni kwamba kiburi kinavunjwa.Shetani anakaa katika kiburi kama vile Mungu hukaa katika sifa. Na hadi mtu awe mnyenyekevu wa kutosha aulize msaada wa maombi, ibilisi huwa kila mara anatawala hali. Na kando ya haya, Mungu Mwenyewe “huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu” (Yakobo 4:6). Wakati mwingi nikiwa ninajaribu kumshudia mume aliyepotea, mke huanza kuniambia kuhusu tabia zake nzuri. Kiburi chake hakiwezi kumruhusu kukubali hali mbovu ya mume wake mbele ya Mungu. Kwa sababu hiyo, sikumvuta hata mmoja wa waume hao kwa Kristo.

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

15

Mlango wa 4

MAHITAJI YENYEWE

Wengi wetu tunakumbana na ugumu katika kumwombea mtu aokolewe kwa sababu kile tunajua kufanya ni kusema “Mungu, tafadhali muokoe fulani na fulani”.Tunajiona kuwa wapumbavu kwa kuomba maneno haya tena na tena, kwa hivyo tunakufa moyo na kuacha. Hata hivyo, maombi ya aina hii yanashirikisha sehemu nne; mtu mwenyewe, anayevuta moyo, neno la Mungu, na ufufuo. Wakati tunajifunza kuombea mambo yenyewe katika sehemu, kuomba kwetu kunakuwa kwa kushindaniwa na kunakofaa. Kwa kuanza, tunamwombea mtu kwa jina lake, tukimuuliza Bwana kufanya mambo matano katika maisha yake. Kwanza kabisa, tunamuuliza Bwana kumtakasa. Hii inaweza kuonekana kuwa ajabu lakini hivi ndivyo Mungu anaanza kazi yake ya ukombozi katika maisha ya kila mtu. Yeye kila mara hutakasa au “hutenga” mtu kwa wokovu kabla hajamwokoa. Biblia inafundisha wazi ukweli huu katika 1 Petro 1:2, “kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo…” Tunaona mkazo kama huu katika 2 Wathesalonike 2:13-14, “Kwa kuwa Mungu amewachaguwa tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho na kuiamini kweli…” Ni kama kwamba Mungu huchora mviringo usioonekana ukimzunguka mtu na halafu anaanza kuleta maongozi ili aweze kusongea hapo. Ni rahisi kuona kuwa chochote kinachoingia “ndani” katika mviringo mara moja na kwa wingi humbadilisha yule ambaye yuko ndani yake. Wakati Mungu mwenyewe anaingia ndani ya mviringo huo, mambo ya ajabu yanaanza kutendeka, kama vile utakavyoona ukisoma shuhuda za kibinafsi baadaye katika kitabu hiki. Ukweli huu wa ajabu ni wa kutia moyo kwetu sisi ambao tunawaombea wengine kwa sababu tunaweza kuwa na matumaini ya kwamba Roho Mtakatifu ambaye ni Bwana wa mavuno kila mara humpata mtu huyu, mara Anapomtakasa! Mwanafunzi wa chuo, akikiri kuwa hakuna Mungu, wakati mmoja alimwandikia C.S Lewis akieleza kwamba alikuwa amekutana na wanafunzi wa Kikristo ambao walikuwa wakimshuhudia kwa nguvu kuhusu imani yao. Mambo mengine ambayo walikuwa wamesema yalikuwa yanasumbua mawazo yake; alikuwa akipitia mashindano makuu. Je, Dr. Lewis alifikiria nini? Lewis alimjibu; “Nafikiri tayari uko katika mtego wa wavu – Roho Mtakatifu anakufuata. Ninaona shaka ikiwa utamtoroka” (Dunn 118). Sasa tunamuuliza Mungu ambariki. Wakati Yesu aliwatuma wanafunzi wake katika “mavuno Yake,” Aliwapatia maagizo wazi “kwanza waseme amani iwemo nyumbani humu” (Luka 10:1-5). Kwa vile kila mara ni wema wa Mungu ambao humwongoza mtu kwa toba (Warumi 2:4), ni sharti tumsihi Mungu awabariki kwa ukarimu.

16

Lakini wakati mwingine maombi yetu ya wokovu wa wengine hayaleti matokeo ya haraka, tunaelekea kuvunjika moyo na kukosa subira, kwa siri tukitamani Mungu “awafunze somo kwa kiboko cha matatizo.”Wakati kijiji fulani cha Wasamaria walimkataa Bwana, wanafunzi Wake walimtaka Mungu awaangamize papo hapo. Aliwakemea akisema, “Hamjui ni roho ya aina gani mliyo nayo. Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa” (Luka 9:52-56). Ikiwa tutamuiga Mwokozi wetu mpendwa, ni lazima tuendelee kutamani mazuri ya Mungu kwa watu wote. Tunafaa kuuliza hasa baraka Zake nzuri sana juu ya wale ambao tunawaombea. Tatu, tunamuuliza Mungu amtie hatiani mtu huyo, kwa vile kutia hatiani ni muhimu kabisa kwa wokovu. Ni Roho Mtakatifu tu ambaye anaweza kumleta mtu chini ya hatia, kwa hivyo tutafanya vizuri tukisihi Yohana 16:8-11 katika moambi yetu. Kutia hatiani kuna maana ya kujulisha kwa hatia. Hatia au kosa la aliyepotea liko katika “kutomwamini Yesu” na hii ndio DHAMBI ambayo Roho Mtakatifu anahukumu (Yohana 16:9). Watu tayari wanajua “dhambi” zao, isipokuwa dhambi ya kutomwamini Kristo. Kwa vile hii ndiyo dhambi ya pekee ambayo inamtia hatia mtu kwenda kuzimu, Shetani anawapofusha kwa hiyo. Kwa hivyo, Roho Mtakatifu anamtia hatiani au anamjulisha aliyepotea katika sehemu hii moja tu, akiwafunulia Bwana Yesu Kristo katika utukufu Wake, ili waweze kuokolewa. Hata hivyo, ni lazima tujue kwamba kuwa hatiani kwa kawaida hakuhakikishi wokovu. Kama Paulo “akitoa hoja zake katika habari ya haki, na kuwa na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akafanya…” (Matendo 24:25). Lakini hakuna dalili ya Biblia ya kwamba aliweza kuokoka. Kinachofuata, tunamuuliza Mungu amulike mawazo yake kwa kweli. Hata baada ya mtu kuja chini ya hatia juu ya haja yake ya wokovu, mawazo yake ambayo injili imepofushwa yanaweza kubakia yamefungwa kwa mwangaza wa injili tukufu ya Kristo na atabakia katika giza la kiroho (2 Wakorintho 4:6). Mara moyo na mawazo yanapofunguliwa kwa kweli, Mungu huwatumia Wakristo kumweleza injili. Ingawa towashi mkushi alikuwa mtafutaji wa kweli, na alikuja Yerusalemu kwa makusudi ya kuabudu na hata alimiliki nakala ya Maandiko, alikiri ya kwamba hangeweza kuelewa “mtu asipomwongoza” (Matendo8:26-39). Hadithi ya kuvutia sana ni ile ya Kornelio (Matendo 10). Alikuwa mtu “aliyejitoa (mtakatifu) na yule aliyemwogopa Mungu pamoja na nyumba yake yote, ambayo ilitoa sadaka kwa watu na kumwomba Mungu siku zote”. Ala, alikuwa mzuri sana kuliko wakristo wengi tunaowajua, na hata sasa, alikuwa bado amepotea – hakuelewa njia ya wokovu. Aliamuriwa na malaika kumwita Petro ambaye “angemwambia yampasayo.” Kornelio na wale aliokuwa nao walikuwa wazi kwa injili ya kwamba mara tu ya kulisikia “neno”Roho Mtakatifu aliwashukia na wakaokolewa wakati Petro alikuwa bado anahubiri!! Muulize Mungu aifungue mawazo na mioyo ya waliopotea – Atafanya! Halafu, wanaweza kuokolewa kwa utukufu.

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

17

Sasa tuko tayari kumuuliza Bwana amwokoe. Hata hivyo, ni lazima tuwe na nia ya kumwacha Mungu kufanya chochote ili kuhimiza wokovu wake, kwa kuwa Mungu hupanga matukio katika maisha yake yanayoazimia kumleta kwa toba. Kwa kufafanua juu ya Luka 19:10, “Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea,” Chafer anasema, “ Ni lazima imaanishe zaidi ya jaribio tu la kuwapata watu ambao hawajaokolewa, kwa vile wako kila upande. Neno linadokezea matayarisho ya utakatifu wa yule ambaye hajaokolewa ambayo yatamleta katika marekebisho pamoja na hali inayofaa ya wokovu” (Chafer 3-4). Familia ya Tony Fontenot ilikuwa imeombea wokovu wake kwa miaka kadha. Maombi yao yalionekana kuwa ya bure hadi Mei 22, 1982. Katika siku hiyo ya ajali aliangusha kwa kishindo ndege yake na karibu achomeke hadi kufa .Mungu alikuwa na maelekezo ya moyo wake – yaliyobakia yalikuwa rahisi! Mara mtu anapokuwa tayari kuipokea injili, ni lazima mtu fulani ashiriki naye injili. Kwa hivyo jambo la asili ni kumwomba Bwana amtume kufanya hivyo. Kwa kweli, hivi ndivyo anatuambia tufanye, “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake” (Mathayo 9:37-38). Kwa sababu watenda kazi ni wachache, ambayo inamaanisha “ni wachache katika eneo, cheo, hesabu, muda au thamani” (Kamusi ya Strong’s), ni lazima tuombe kwa msaada wa Mungu katika sehemu hii. Kwanza tumwombe awatume watenda kazi zaidi. Neno la Kigriki “ekbalo” lina wazo la kutumia nguvu – kusukuma, kuvurumisha, kutupa. Kumbuka ugumu Mungu alikumbana nao wakumshawishi Yona kwenda Ninawi kulihubiri Neno Lake? Mungu kwa kweli “alimlazimisha” aende! Hali sawa na hiyo ilifanyika wakati kanisa lilikuwa wazi halitaki kuieneza injili kupita sehemu yake ya starehe. Mungu aliruhusu “adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria” (Matendo 8:1), Lakini, “wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno” (Matendo 8:4). Kwa vile watenda kazi sio tu wachache katika hesabu bali pia wachache katika muda na thamani, tunamuuliza Bwana awafanye tayari na tabia ya asili ambayo itawafanya wawe mashahidi wanaofaa. Hata hivyo, ni lazima tuelewe ya kwamba kufanywa tayari kote huja kupitia Roho Mtakatifu wa thamani. Samuel Chadwick anasema, “ Nguvu ya Roho haitengani kutoka kwa mtu Wake… Mungu hatoi sifa Yake. Nguvu yake haiwezi kukodishwa. Haiwezi kutolewa kutoka katika uwepo Wake… Yeye si tu mpeanaji wa nguvu, huitawala. Hakuna mwingine awezaye” (Chadwick 89). Hii ndiyo sababu Yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakae Yerusalemu hadi “wabatizwe kwa Roho Mtakatifu” (Matendo 1:4-5). Halafu akawaambia, “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu hata Yerusalemu na Yudea yote, na katika Samaria, na hata mwisho wa nchi” (Matendo 1:8). Ingawa ukamilifu wa Roho Mtakatifu ni haki yetu ya kuzaliwa (Matendo 2:38-39), kanisa kwa jumla linajua machache sana juu ya “ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio” (Waefeso 1:19). Kwa sababu hiyo, pande zote mioyo

18

inatumbukia bila kufikiri katika kuzimu kwa kuwa hatuna nguvu ya kuwazuia bila ukarimu wa Roho Mtakatifu wa Mungu. Kwa hivyo, ni lazima tumwombe Mungu awajaze wafanyi kazi wake na Roho Mtakatifu, akiwafanya tayari kwa nguvu (Uwezo na bidii), ujasiri (matendo 4:31), hekima (Mithali 11:30), juhudi (Wakolosai 4:12-13), huruma (Yuda 22-23) na busara ya mambo ya Mungu (Yeremia 33:3). Na mioyo itaokolewa!!! Baada ya kuwaombea watu waokoke na wafanyi kazi kuwashuhudia, sasa tunaombea neno la Mungu ambalo litashiriki kwao. Sababu ya hii ni mara mbili: kwanza kabisa, hakuna anayeokoka bila kulisikia neno la Mungu (Warumi 10:14) na, pili, Shetani anachukia neno la Mungu, bila kikomo na kwa ukali akilishambulia katika bidii yake ya kikatili ili kuwazuia watu wasilipokee. Kwa vile neno la Mungu ni muhimu kwa kutia hatiani (Matendo 2:37), kuweka huru (Yohana 8:32), na kuokoa waliopotea (1 Petro 1:23), Shetani kwa bidii analipinga kwa mashaka (Luka 8:11-15), kutia nguvu (2 Wakorintho 10:4-5), na kubadilisha ( 2 Wakorintho 11:3-4). Neno la Mungu kwa Shetani ni kama gesi ya Kryptonite kwa Superman – humfanya kuwa dhaifu na bila nguvu. Pia hupunguza ufalme wake kwa kuwaweka huru mateka kwa kuwa “mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Lakini sikia, sio ukweli ambao unakuweka huru, bali ni ukweli ambao UNAUJUA. Kwa hivyo, Shetani hufanya kila kitu anachoweza ili kuwazuia watu ‘kuujua’ ukweli. Katika kueleza mfano wa mpanzi kwa wanafunzi wake, Yesu alisema kwamba Shetani huja MARA na kuiba neno kabla mtu hajalielewa (Marko 4:15). Hii ndiyo maana ni lazima tuliombee neno la Mungu ambalo linashirikishwa kwa waliopotea. Katika kumwomba Mungu atumie neno Lake kuwabadilisha waliopotea, tunafanya mahitaji matano yenyewe. Kwanza, ya kwamba neno Lake “liendelee” (2 Wathesalonike 3:1). Hii inamaanisha lisizuiliwe; ya kwamba Shetani hawezi kwa njia yoyote kuzuia kuendelea kwa neno la Mungu. Anajaribu kulisimamisha kwa kila njia anayoweza kufikiria, kwa kumpinga na kumhangaisha mjumbe wa neno, , hadi kwa kupotosha neno, hadi kwa kuharibu nakala zilizochapishwa za neno, hadi kwa kuweka wasiwasi kwa neno, na kadhalika! Baadaye, tunaombea neno la Mungu litukuzwe. (2 Wathesalonike 3:1). Hii ina maana ya kuwa lithaminiwe kwa hali ya juu na kuheshimiwa miongoni mwa wale watakalolisikia. Tutakuwa na uchaji mpya wa neno lake tutakapoona ya kwamba “ameikuza ahadi yake kuliko jina lako lote” (Zaburi 138:2). Hakika, Mungu ni neno Lake katika mwili. “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu…Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu…” (Yohana 1:1,14). Pia tunaliombea neno la Mungu lienee (Matendo 12:24); kwa kuwa sheria moja ya mavuno ni: “Apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu” (2 Wakorintho 9:6). Pia tunaombea neno la Mungu lishinde au litumie nguvu (Matendo19:20). Kama vile mbegu ndogo inaweza kupasua ubamba wa saruji wakati nguvu ya uhai

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

19

ambayo iko ndani yake inaanza kutokea, ndivyo ilivyo mbegu ya neno la Mungu iliyopandwa moyoni. Ombi langu la kupendeza la neno la Mungu ni kuwa liwe la kufaa. Matendo 14:1 inasema ya kwamba “na kwa vile walivyonena, kundi kubwa la Wayahudi na Wayunani wakaamini.” Tunaweza kuomba Isaya 55:11, “Ndivyo litakalokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu, halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.” Mungu anakusudia neno Lake liwe la kufaa; muulize alifanye hivyo na utakuwa ukiomba katika mapenzi yake matakatifu na maombi yako yatajibiwa!! Acha nikukumbushe ya kwamba Yuda Iskariote aliishi katika mkutano thabiti na neno lenye uhai la Mungu na bado alikufa na kwenda kuzimu na Yesu akisema , “Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa” (Marko 14:21). Mafarisayo – watu wa dini sana katika siku zao – walivaa neno la Mungu kwenye ukanda wa mkono na wangeweza kusema sehemu kubwa ya maandiko, na bado walikuwa mbali na ufalme wa Mungu. Ni lazima tuelewe ya kwamba ni wakati tu Roho Mtakatifu anahuisha neno katika moyo wa msikiaji, ndipo mtu anaweza kuokolewa. Hii ndiyo sababu ni lazima tuliombee neno la Mungu liwe la kufaa katika maisha ya wale wanalolisikia!!! Ikiwa tunataka kuona wengi wakiokoka, basi tunahitaji kuomba kwa ufufuo. Andiko bora juu ya ufufuo linaanza hivi, “Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba…” (2 Mambo ya Nyakati 7:14). Aina ya kuomba ambako kumeashiriwa hapa ni uombezi – kuwaombea wengine. Ilikuwa tu baada ya Ayubu kuwaombea (neno sawa la Kiebrania kama hapo juu) rafiki zake Mungu akaibadilisha hali yake (Ayubu 42:10). Wakati wa ufufuo, karibu ombi lote huwa tu ni la watu wengine. Duncan Campbell anaeleza ufufuo kama “ watu waliojazwa na Mungu” Edwards 26). Wakati watu wamejazwa na Mungu, wao huwa wanajishughulisha na wengine kuliko wao wenyewe. Tamaa ya mioyo inakuwa yao!! Sikiliza Finney akieleza nguvu ya maombi wakati wa ufufuo: “Nimesema zaidi ya mara moja, ya kwamba roho ya maombi ambayo ilishinda katika ufufuo huo ilikuwa ni umbo la alama sana kwao. Ilikuwa ni kawaida kwa waokovu wachanga kutumiwa sana katika maombi; na kwa wakati mwingine, sana, ya kwamba walilazimishwa kuomba usiku wote, na hadi nguvu ya miili yao ilikuwa imechoka sana, kwa ajili ya kubadilishwa kwa mioyo iliyowazunguka. Kulikuwa na shinikizo la Roho Mtakatifu juu ya akili za Wakristo; na walionekana kuuchukua mzigo wa mioyo isiyokufa... ilikuwa ni kawaida kuwapata Wakristo, kila mara wakikutana mahali popote, badala ya kujiingiza katika mazungumzo, wanaanguka kwa magoti yao na kuomba. Sio tu ya kwamba mikutano ya maombi iliongezeka sana na kuhudhuruwa sana… bali kulikuwa na roho kuu ya maombi ya siri. Wakristo waliomba kwa wingi, wengi wao wakitumia masaa katika maombi ya faragha. Ilikuwa pia hali ya wawili, au zaidi, wangechukua ahadi: ‘Ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lolote ambalo watauliza, itafanyika kwao na Baba yangu aliye mbinguni’ na kufanya mtu fulani hoja ya maombi; na ilikuwa ajabu ni eneo gani walishinda. Majibu kwa

20

maombi yaliongezeka wazi kila upande, ya kwamba hakuna ambaye angeepuka shaka ya kwamba Mungu alikuwa kila siku na kila saa akijibu maombi” (Finney 141-42).

Maneno ya haraka ya ufufuo yanaonyesha kwamba mamia, maelfu, na hata mamilioni ya mioyo hubadilishwa kwa Kristo nyakati hizi. Jonathan Edwards hata alidhania ufufuo kuwa njia kubwa ambayo Mungu hutumia kueneza ufalme Wake (Edwards 26). Kwa hivyo, ikiwa unataka kuona mioyo ikiokolewa, ombea ufufuo!!!

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

21

Mlango wa 5

VITA VYA KIROHO

Kusudi la msingi la kuwaombea waliopotea SI kumsadikisha Mungu

awaokoe kwa kuwa “hapendi mtu yeyote apotee” (2 Petro 3:9), akiwa alimtuma Kristo afe kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote (1 Yohana 2:2). Lakini, inahusu vita vya kiroho – kuwaweka huru na mvuto wa mapepo ili waweze kuokolewa.

Uchunguzi mfupi wa maelezo ya Biblia juu ya hali yao ya kukata tamaa itatusaidia kuelewa ukweli huu hatari. Waliopotea ni wafungwa ambao Shetani anakataa kuwaachilia (Isaya 14:17), watumwa chini ya mamlaka na hukumu ya Shetani (Matendo 26:18), watoto wa Ibilisi (Yohana 8:44), wamepofushwa kwa injili (2 Wakorintho 4:3-4), “wametiwa nguvu” na Shetani (Waefeso 2:2), wadhaifu walioshikwa na Shetani (1 Yohana 5:19), na nyumba ya mtu mwenye nguvu (Marko 3:27).

Maelezo machache tu juu ya baadhi ya maandiko haya yatatupatia taswira wazi. Kwa mfano, Waefeso 2:2 inasema, “ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi.” Neno la Kigriki la kazi ni energeo – “kutia nguvu.” Hii ina maana kuwa waliopotea “wanatiwa nguvu na roho ya ibilisi. Hakuna budi, mtu aliyepotea hajui hivyo, na bila shaka hawezi kukiri ikiwa anajua. Anafikiri yuko huru (hiyo ni sehemu ya upotevu wake), lakini katika kweli njia yake ya matendo inaamuriwa na mfalme wa uwezo wa anga (Dunn 120).

Acha tuangalie katika 1 Yohana 5:19 “Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu, na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.” Hii ina maana ya kuwa dunia yote (pamoja na vyote vikaavyo humo) imelala kifudifudi kabisa chini ya mwongozo wa yule mwovu. Kamusi ya Webster inaeleza kifudifudi kuwa “kulala na uso ukielekea chini katika kutii kabisa; kutiishwa kikamilifu.” Kuhusu mstari huu, Stott anasema juu ya dunia, “Iko katika ‘yule mwovu,’ katika mikono yake na chini ya utawala wake. Tena, hukaa hapo. Haionyeshwi kama inashindana kwa juhudi kuwa huru, bali ikiwa imelala ikitulia, labda hata katika usingizi bila kufahamu, katika mikono ya Shetani. Yule mwovu hamgusi Mkristo, bali dunia kwa udhaifu iko katika mikono yake” (Stott 193).

Halafu, Marko 3:27 ni kile ninaona kuwa msatari muhimu sana katika Bibia kuhusu kuwavuta waliopotea kwa Kristo. Katika msatari huu Yesu Mwenyewe anasema, “Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu, ndipo atakapoiteka nyumba yake.” Ikiwa mstari huu unamaanisha chochote, unamaanisha ya kwamba hakuna mtu aliyepotea ataweza kuokoka kamwe isipokuwa mtu amweke huru kutoka kwa mvuto wa mapepo ambao unamtawala. Hili ni hasa jambo la kwanza ambalo ni lazima lifanywe. Na hii njia ya kuwekwa huru hutimizwa kupitia maombi!!

Ili kushinda vita juu ya mioyo, kuna mambo ya msingi ambayo tunahitaji kufanya. La kwanza ni kutumia silaha zetu ambazo Mungu ametuamrisha. Wakati

22

niliandikwa na Uncle Sam, sehemu ya mafunzo yangu ya kijeshi ilijumlisha kujifunza kuhusu silaha ambazo nilitarajiwa kutumia katika vita vya Vietnam. Nilipata kuwa na mazoea ya bunduki yangu ya aina ya M-16 ambayo ningeweza kuibomoa na kuiunganisha katika giza kwa sababu tendo hili la ajabu lilionekana kama linaloweza kuokoa maisha katika sehemu ya vita.

Mungu ametoa silaha zenye nguvu kwetu tuzitumie katika vita hivi vya kiroho. “Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome” (2 Wakorintho 10:4). Shida yetu ni kuwa hatuna mazoea na silaha zetu au hakika vita vyenyewe.

Lakini kabla nikujulishe kwa silaha zako na jinsi ya kuzitumia, acha nikukumbushe ya kwamba pigano halisi ni maombi – tunapigana kwa kuomba. Nimemsikia Ndugu Mickey Bonner akisema mara mingi ya kwamba maombi yote ni vita!! Kwa hivyo, wakati hatuombi, Shetani anashinda kwa ukosefu, lakini wakati tunaomba, anashindwa kwa sababu hana kinga kabisa kwa maombi. Je, hii inaweza kuwa sababu Mungu anatutaka “Kuomba bila kukoma” (1 Wathesalonike 5:17) na sababu mitume walijitoa “kudumu katika kuomba, na kwa kulihudumia Neno” (Matendo 6:4)?

Kama vile silaha asili za vita, kama ni bomu matangi, kitu cha kutupia mshale au mkuki, makombora, bunduki na kadhalika, zinatumiwa kwa kusudi moja – kumshinda adui – kwa hivyo silaha zote za kiroho zinatumiwa kufanya hivyo! Kwa hivyo, acha tuwe na mazoea na silaha zetu kuu na kuzitumia wakati tunaomba.

Damu ya Kristo ni silaha yetu moja yenye nguvu sana. Ufunuo 12:11 inasema, “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo…” Waebrania 2:14 inatuambia ni kwa nini kuomba damu ya Kristo katika maombi ni ya nguvu: “Ili kwa njia ya mauti amuharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, ibilisi.” Kamusi ya Strong’s inaeleza kuharibu kuwa “kugeuza kuwa bure kabisa; kufanya kuwa tupu.’

Wakati Shetani alimuua Mwana wa Mungu asiye na hatia, alijiharibu mwenyewe… sio kuangamiza, bali kuharibiwa. Madai yote halali ambayo alimiliki juu ya nchi na mtu kupitia kuanguka kwa Adamu sasa yamefutiliwa mbali; tangu msalaba hana haki kabisa juu ya yeyote au chochote. Hii inamaanisha ya kwamba nguvu zote ambazo sasa anatumia anatumia tu kwa udanganyifu na kwa ulaghai (Billheimer 31).

Tunapoomba damu ya Kristo, tunamkumbusha Shetani na mapepo yake yote ya kwamba tayari wameshindwa. Hii ni muhimu hasa katika vita kwa mioyo, kwa vile kumwagika kwa damu ya Kristo Kalvari kulilipa deni ya dhambi kwa watu wote (1 Yohana 2:2) na sasa Shetani anaiteka mioyo tu kwa makosa – kwa sababu hatujasisitiza ya kwamba awaachilie!!

Silaha nyingine yenye nguvu ni jina la Yesu! Wanafunzi wa bwana, wakirudi kutoka kazi yao ya kushuhudia, kwa furaha walisema kwa sauti, “Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako” (Luka 10:17). Na wako chini yetu pia!

Kuna sababu tatu za Biblia ni kwa nini jina la Bwana wetu Yesu ni la nguvu sana katika milki ya kiroho. Kwanza, kwa sababu Yeye ni Bwana juu ya yote kupitia uumbaji: “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi au usultani,

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

23

au enzi au mamlaka, vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake” (Wakolosai 1:16).

Na pili, ni Bwana kupitia kusulubishwa. “Ili kwa njia ya mauti amuharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti yaani ibilisi, awaweke huru wale ambao kwa hofu ya mauti walikuwa watumwa katika maisha yao yote "”(Waebrania 2:14-15).

Na tatu, ni Bwana kupitia taji: “Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake” (1 Petro 3:22).

Kwa vile tunatenda kwa kutii moja kwa moja kwa amri ya Bwana Yesu katika kuwaombea waliopotea na kutaka waachiliwe huru, pepo wanaowatawala ni lazima watii kwa sababu wako chini ya jina Lake.

Neno la Mungu ni silaha nyingine kuu ambayo tunaweza kuitumia katika maombi. Kama vile tumeona tayari, kuomba maandiko kunafaa sana. Neno la Mungu hata linaitwa “upanga wa roho” (Waefeso 6:17).

Kwa vile Shetani alivuliwa enzi na mamlaka kabisa pale Kalvari (Wakolosai 2:15) (Waebrania 2:14), yote ambayo anafanya nayo kazi ni uongo. Hata hivyo, yeye ni maarufu sana nao tukiona vile anaweza “kuudanganya ulimwengu wote”” (Ufunuo 12:9). Lakini, neno la Mungu ni “kweli” na ukweli huushinda uongo KILA WAKATI. Kwa hivyo, tukiendelea kulitumia neno la Mungu katika vita vya maombi, tutashinda kila wakati na mioyo itawekwa huru!!!

Sifa ni silaha nyingine yenye nguvu, kwa sababu tukianza kumsifu Mungu, Yeye huja katika hali (Zaburi 22:3) na ni jinsi gani ilivyo ajabu kuwa na “amri jeshi mkuu” katika sehemu ya vita!! Ushuhuda wa ajabu wa nguvu za sifa ni hadithi inayopatikana katika 2 Mambo ya Nyakati 20. Yuda ilikuwa inashambuliwa na muungano wa majeshi kutoka mataifa kadha. Hali ilikuwa ya kukata tamaa ya kwamba Mfalme Yehoshafati aliagiza Yuda yote “wafunge na kuomba.” Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda, nao wakapigwa” (mstari wa 22).

Wengi wetu hatuna wazo jinsi sifa ni ya nguvu katika vita juu ya mioyo – inaweza kuwa hatujaitumia ya kutosha kuelewa nguvu yake kuu? Sikiliza vile Francis McGaw anashiriki daraka lenye maana la kusifu katika kutafuta mioyo kwa John Hyde: “Ninakumbuka John akiniambia kuwa katika siku hizo ikiwa katika siku yoyote mioyo minne haikuletwa katika zizi, usiku kutakuwa na uzito moyoni mwake ya kwamba ilikuwa uchungu kwa kweli, na hangeweza kula au kulala. Halafu katika maombi angemuuliza Mungu amwonyeshe ni nini kilikuwa kizuizi ndani yake kwa baraka hii. Alipata sawasawa siku zote ya kwamba ilikuwa upungufu wa sifa katika maisha yake. Amri hii, ambayo imerudiwarudiwa katika Neno la Mungu mara mia – hakika yote ni muhimu! Halafu atakiri dhambi yake, na kukubali msamaha kupitia kwa Damu. Halafu atauliza kwa roho wa sifa kama karama yoyote ile ya Mungu. Kwa hivyo atabadilisha jivu yake na shada la maua la Kristo, kuomboleza kwake na mafuta ya furaha ya Kristo. Moyo wake wa uzito na vazi la Kristo la sifa (wimbo wa Mwana –kondoo – kumsifu Mungu kabla ya lile ambalo angetenda), na alipokuwa akimsifu Mungu mioyo ingemjia, na hesabu ambayo haikuwako ingetengenezwa” (Carre 39).

24

Kufunga ni silaha nyingine yenye nguvu lakini inayotumiwa kidogo katika ghala letu. Imeitwa “silaha yenye nguvu sana” ambayo iko tayari kwetu. Kauli yangu binafsi ni kwamba kufunga kunaongeza uwezo wa maombi kwa haikosi mara kumi!

Kusudi la vita vyetu ni kumshinda adui na kufunga kumebuniwa kufanya hivyo kwa kufaa. Sikiliza Isaya 58:6, “Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?” Wakati mmoja wanafunzi waliposhindwa kutoa pepo kutoka kwa kijana mdogo, Yesu aliwaambia ya kwamba, “Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote, isipokuwa kwa kuomba na kufunga” (Marko 9:29).

Silaha nyingine moja ambayo hutoa nguvu katika milki ya kiroho ni upendo. Yule anayempenda Bwana kwa uhai wake wote na anapenda mioyo iliyopotea kama vile anavyojipenda mwenyewe hawezi kuzuiliwa!! Ufunuo 12:11 inasema, “Nao wakamshinda kwa damu ya mwana –kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao, ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.”

Ukimpenda mtu fulani kwa kutosha, utafanya lolote likupasalo kuwaweka nje ya kuzimu. Kwa kweli, upendo hauwezi kushindwa. Upendo “huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote… HAUPUNGUI” (1 Wakorintho 13:7-8).

Kwa hivyo ni nini hufanyika wakati tunaomba, tukizitumia silaha ambazo Mungu ametupatia? 2 Wakorintho 10:4-5 inatuambia: “Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.”

Silaha ambazo zinatawala katika maombi zimebuniwa kuvunja ngome, kuangusha fikira, na kuteka nyara fikira. Ngome ni fikira ambazo ziko kinyume na neno na mapenzi ya Mungu. Kwa hivyo tunaweza kwa haraka kuona ya kwamba uwanja wa vita ni mawazo ya mtu, kwa sababu tunajishughulisha na nia, mawazo na fikira.

Ni maana ya kwamba tuelewe hii kwa sababu yeyote anayetawala fikira anamtawala mtu. Ikiwa Shetani anaweza kuendelea kutawala fikira ya mtu ambaye hajaokoka, anaweza kumzuia kuokoka. Njia ya peke ambayo anaweza kufanya hivi ni kumpofusha mtu kwa injili, kwa vile yeyote katika akili yake “sawa” atamchagua Yesu juu ya Shetani na mbinguni juu ya kuzimu KILA wakati! Wakati legioni la mapepo lilitolewa kwa Mgerasi, na angeweza kufikiri na kuchagua mwenyewe- hakumchagua tu Yesu bali pia alikuwa Muinjilisti wa bidii Kwake. (Marko 5:15-20).

Mwanadamu ni mjumbe aliye huru, kutumia msemo wa kale, kadiri Mungu anavyohusika; kabisa huru kikamilifu. Na ni mjumbe aliyefanywa mtumwa sana duniani, kadiri dhambi na uchoyo na chuki vinavyohusika. Kusudi la kuomba kwetu si kulazimisha au kushurutisha nia yake; kamwe si hivyo. Ni kuweka huru nia yake ambayo ina mwongozo uliopotoshwa ambayo sasa inapinda upande wake. Nikutoa vumbi machoni mwake ili kuona kwake kuwe safi. Na mara anapokuwa huru, kuweza kuona sawa, kusawazisha mambo bila chuki, mwelekeo wote uko katika hisani yake ya kutumia akili kuchagua sawa pekee… Maombi yetu ni ‘mwokoe kutoka kwa yule mwovu,’ na kwa vile Yesu ni Mshindi juu ya mtekaji, wokovu utafanyika. Bila shaka yoyote tunaweza kuhakikisha kubadilishwa kwa hawa walio juu ya mioyo yetu kwa

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

25

maombi ya aina hii. Maombi katika jina la Yesu humfukuza adui kutoka uwanja wa vita kwa nia ya mtu na humwacha huru kuchagua sawa” (Gordon 192-94).

Sasa kwa kuwa tunaelewa ya kwamba Mungu hutumia maombi yetu kuvunja ngome ya Shetani, acha tuone jinsi Shetani anatumia ngome katika maisha ya watu kuwazuia kuokoka. Ngome yenye nguvu zaidi ya yote ni KUTOAMINI. Ni ngome kubwa katika kila mtu – aliyeokoka au aliyepotea!! Katika Mkristo kumebuniwa kumzuia kwa kuamini kabisa ukweli fulani katika neno la Mungu ambao utamfanya kuwa na nguvu na wa kufaa katika ufalme wa Mungu. Lakini katika yule ambaye hajaokoka kumebuniwa kumzuia kuamini katika Yesu Kristo kama Mwokozi na Bwana.

Kwa vile kutoamini ndiyo dhambi ya pekee ambayo inamhukumu mtu kuzimu, Shetani anaidhania kuwa ya thamani nyingi, akiilinda pamoja na ngome zingine. Nia yoyote ambayo iko kinyume na mapenzi ya Mungu na neno hufanya. Wakati kiongozi mmoja tajiri alikuwa kwa Yesu akimuuliza jinsi angerithi uzima wa milele, Yesu KAMWE hakumwambia jinsi ya kuokoka. Ila, alimwambia kugawa faida ya mali yake kwa maskini. Lakini kijana huyo hakuwa anataka kufanya hivyo na akaenda jinsi alivyokuja – amepotea. Yesu alijua ya kwamba ulafi ulitawala fikira na moyo wake, ulimzuia kuokoka, na hadi huo uvunjwe, injili itakuwa haifai (Marko 10).

Ngome ya mwanamke Msamaria wa Sikari ilikuwa ni tamaa. Aliongea na Bwana kuhusu mambo ya jamii na historia, akiepuka jambo la hakika katika maisha yake. Lakini wakati Yesu alimwambia wazi ya kwamba alikuwa ameolewa mara tano na sasa alikuwa anaishi na mume – alipata maelekezo ya moyo wake. Katika hali hii ngome ilivunjwa na aliokoka kwa utukufu. (Yohana 4).

Shetani mara kwa mara hutumia uchungu kuzuia ukweli wa upendo wa Mungu na kuuzuia kupokelewa. Kwa mfano, msichana mdogo akinajisiwa sasa, miaka baadaye mtu ashiriki naye injili – haitaweza kupita uchungu katika moyo wake. Ngome hiyo ni lazima iangushwe kupitia maombi kabla hajaweza kupokea habari njema ya upendo wa Mungu. Ni vigumu kuwavuta mashoga kwa kristo – si kwa sababu Mungu hawapendi au kwa sababu injili haina nguvu ya kutosha au kwa sababu haujali ya kutosha. Lakini hii ni ngome yenye nguvu ya kwamba maombi mengi, kufunga, kusisitiza, imani na kadhalika vinahitajika kuivunja. Na kwa kawaida tunavunjwa moyo na kuacha kabla ushindi haujapatikana.

Siku moja nilipokuwa nikiombea mtu mmoja, nilimuuliza Bwana anifunulie ni kwa nini aliendelea kuikataa injili. Aliingiza neno “tawala” juu ya fikira yangu. Si kuelewa kwa hakika ilikuwa na maana gani. Lakini wakati niliendelea kumjua zaidi, nilitambua ya kwamba anatawala kila kitu katika eneo la uongozi wake na kwa ugumu. Sasa ninaelewa ni kwa nini kutawala ni ngome ambayo inamzuia kwa Kristo – ili kuokoka, mtu ni lazima ajitoe Kwake!

Ingawa kiwango cha kitabu hiki hakiruhusu uchunguzi wa ndani wa ngome, ninataka kuongea kwa ufupi kwa wale ambao huenda wanamwombea mtu mwenye mazoea makubwa ya madawa ya kulevya au pombe. Mazoea haya huficha tu jambo la kweli. Shida ya kweli kwa kawaida ni nafsi iliyoharibika ambapo heshima na mfano wa mtu mwenyewe imevunjwa kwa njia fulani – kupitia kwa kukataliwa, kudhulumiwa, au kuudhiwa kwa njia kubwa katika maisha. Mazoea yenyewe hufunika

26

tu na kuficha shida. Kwa hivyo muulize Bwana akuonyeshe asili ya shida ili upate ushindi.

Wakati Eddie Smith alihitaji kujua jinsi ya kumsaidia mshauriwa fulani, alimuuliza Bwana amuonyeshe ni nini alihitaji kujua kumhusu. Alimvuta Eddie amuulize kuhusu “mchezo wa ngoma.” Wakati alifanya hivyo, mara akaanza kulia na kuongea kwa sauti kubwa, “Ni nani alikwambia kuhusu hilo?” Halafu akasimulia hadithi yake ya kwamba akiwa na miaka kumi na mitano bila kutaka aliandamana na rafiki yake kuenda kucheza ngoma. Huko alimwona mwalimu wake wa ibada ya watoto akiyumbayumba katika hali ya ulevi. Hapo na hapo alimdharau Mungu akisema, “Ikiwa haya yote ndiyo yako katika Ukristo, wacha ukae.” Halafu akamwambia Eddie, “Tangu hapo, maisha yangu yamekuwa mabaya sana. Nimekuwa na mazoea ya pombe na madawa ya kulevya vibaya sana. Nimekuwa katika ndoa nyingi, na niko katika taabu kabisa.” Akijua asili ya shida, Eddie aliweza kuomba naye na Mungu akamweka huru (Smith 71-73).

Ninadhani kuna mamia ya ngome ambazo Shetani anatumia kulinda kutoamini, lakini ukweli wa msingi ambao ni lazima tuuelewe ni kwamba kawaida kuna ngome moja kubwa katika maisha ya kila mtu ambaye hajaokoka ambayo inamzuia kuipokea injili. Vita KAMWE havipiganwi juu ya dhambi nyingi (ingawa mtu anaweza kuwa na nyingi) bali ni juu ya moja!! Ngome hiyo peke yake ni silaha ambayo mtu mwenye nguvu anategemea, lakini wakati silaha (ngome) yake imeharibiwa, anashindwa na mtu huwa tayari kwa wokovu (Luka 11:21-22).

Sehemu nyingine ya asili katika sura ya vita vya kiroho ya kuvuta mioyo ni kutumia mamlaka yetu katika Kristo. Ametupatia mamlaka ya ajabu mno (Mathayo 16:19) lakini ni lazima tuyatumie. “Kama tu vile polisi katika barabara anaweza kuongoza mlolongo wa magari kwa sababu ya mamlaka yake, hivyo mwamini anaweza kuombea mioyo ya watu ambao wamefungwa na kupofushwa na Shetani na kuisababisa kuokolewa. Nguvu za giza hupata nguvu yao imevunjwa kupitia kwa damu ya Yesu Kristo; na tunapoyatumia mamlaka yetu ndani Yake, haiwezi kamwe kutupinga… Mungu ametuita kuwa vyombo ambavyo kuvipitia anaweza kutumia mamlaka Yake. Acha kwa imani tukubali nafasi hii na kusimama imara bila kujali ushindani. Halafu Ataweza kufanya mambo kupitia kwetu ambayo hatujayaota” (Epp 108-10).

Halali, mioyo yote ni ya Kristo kwa sababu alilipia dhambi zao Kalvari (1 Yohana 2:2). Lakini Shetani, kwa njia ya haramu na kwa nguvu, anaendelea kuwashika mateka, kwa uthabiti akikataa kuacha waende. Na ataendelea kuwashika kwa lazima katika giza la kiroho hadi tuchukue nafasi yetu sawa na kutumia haki zetu za enzi kwa kudai kuachiliwa kwao mara moja kwa msingi wa damu ya Kristo iliyomwagika na kwa mamlaka tuliowekewa kutoka Kwake.

Hakuna sababu kabisa ya hata moyo mmoja ufe na uende kuzimu kwa sababu Kristo tayari alilipa bei ya kukombolewa kwao. Na sababu ya pekee ni kwa nini yeyote ataenda kuzimu ni kuwa hatujachukua nafasi yetu ya mamlaka na kumfunga mtu mwenye nguvu, tukisisitiza kwa wokovu wao. Ibilisi hawezi kuwaachilia hadi tumfanye awaachilie.

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

27

Jenerali Jonathan Wainwright, pamoja na marafiki wengine wafungwa wa vita, alitiwa kifungoni katika Kisiwa cha Formosa. Ingawa vita vilikuwa vimekwisha na mkuu wa jeshi la Japan alijua hilo, hakuwaambia wafungwa wake au kuwaachilia. Lakini muda mfupi ndege ya kirafiki ilitua katika kisiwa na habari za ushindi. Halafu Jenerali Wainwright akamtangazia mkuu wa jeshi la Japan, “Mkuu wa jeshi langu amemshinda mkuu wa jeshi lako. Sasa ni mimi nilio na mamlaka.” Na hivi ndivyo tunafanya, kumtangazia mtu mwenye nguvu (mkuu wa ibilisi katika maisha ya mtu), “Mkuu wa jeshi langu amemshinda mkuu wa jeshi lako. Ninadai kuachiliwa mara moja kwa hawa ambao wameshikwa mateka kwa haramu.” Na tukisisitiza, kuachiliwa na kuokolewa kutafanyika!!!

Sehemu ya mwisho lakini ya muhimu kabisa katika kuombea mioyo ni kuendelea KUMPINGA ibilisi. Tunashauriwa kuvaa silaha za Mungu (Waefeso 6:10-18), ili tuweze “Kuzipinga hila za ibilisi… tuweze kushinda katika siku ya uovu.” Wakati tunakuwa na bidii kuhusu wokovu wa mioyo, Shetani anatumia hali ngumu katika maisha yetu au katika wale ambao tunawaombea kwa juhudi za kutufanya kuacha. Hii ndio sababu mume au kijana ambaye mke au mama anaombea mara kwa mara anaelekea kuwa mmbaya badala ya mzuri – Shetani anawataka waache kuomba, kwa kuwa anapoteza mikono yake kwa mioyo hiyo!!

Kwa hivyo, kumpinga ibilisi kunamaanisha ya kwamba usiache tendo la kinyume, hali, na kadhalika izuie bidii yako ya kuendelea na maombi. Wakati kitu kama jiwe la nyuzinyuzi, huzuia moto usipenye hii ina maana kuwa haigeuzwi kwa moto. Kitu ambacho ni cha kuzuia maji , kina maana ya kuwa hakigeuzwi kwa maji. Kuwa kizuizi kwa Shetani kuna maana ya kwamba, haijalishi anafanya nini, haikugeuzi, unaendelea tu kuombea wokovu wa wapendwa wako waliopotea.

Picha ya ajabu yakumpinga shetani kwa ajili ya moyo iko katika ushuhuda unaofuata uliosikika na Charles Blanchard ambaye alikuwa rais wa chuo cha Wheaton kwa miaka arobaini na mitatu. Aliuthibitisha kuwa kweli na kuuandika katika kitabu chake, Getting Things From God, kama ilivyonakiliwa hapa chini:

Rafiki, kama miaka miwili na nusu au mitatu iliyopita nilikuwa hospitalini huko Philadelphia. Nilikuwa fundi wa mitambo kwa Pennsylvania lines, na ingawa nilikuwa na mke muombaji, maisha yangu yote nilikuwa mtu mwenye dhambi. Wakati huu nilikuwa mgonjwa sana, nilikuwa nimedhoofika sana. Nilikuwa na uzito wa chini ya pauni mia moja.

Mwishowe daktari ambaye alikuwa akinihudumia alimwambia mke wangu ya kwamba niilikuwa nimekufa, lakini akasema: La hajakufa. Hawezi kuwa amekufa. Nimemwombea kwa miaka ishirini na saba na Mungu ameniahidi ya kwamba ataokoka. Unafikiri Mungu atamwacha afe sasa baada ya kuomba kwa miaka ishirini na saba na Mungu ameahidi na hajaokoka?” “Vema,” daktari akajibu, “Sijui lolote kuhusu hayo, lakini najua ya kuwa amekufa.” Na pazia ikavutwa kuzunguka kitanda, ambacho hutenganisha walio hai na waliokufa hospitalini.

Kumtosheleza mke wangu, madaktari wengine waliletwa, mmoja baada ya mwingine, hadi saba walikuwa kando ya kitanda, na kila mmoja wao alipokuja na kufanya uchunguzi alithibitisha ushuhuda wa wale wote waliomtangulia. Madakatari saba walisema nilikuwa nimekufa. Wakati ule ule, mke wangu alikuwa amepiga

28

magoti kando ya kitanda changu, akisisitiza ya kwamba nilikuwa sijakufa – ya kwamba ikiwa nilikuwa nimekufa Mungu atanirudisha, kwa vile alikuwa amemuahidi nitaokoka na nilikuwa bado sijaokoka. Lakini magoti yake yakaanza kumuuma, akiwa amepiga magoti katika sakafu ya hospitali. Akamuuliza muuguzi amletee pilo na akapiga magoti juu yake. Saa moja, masaa mawili , masaa matatu yakapita. Pazia ilikuwa bado imesimama kando ya kitanda. Nilikuwa bado nimelala pale, kama kwamba nimekufa. Masaa matano, masaa sita, masaa saba, masaa kumi na matatu yakapita, na wakati huu wote mke wangu alikuwa amepiga magoti kando ya kitanda changu, na wakati watu walimshauri vingine na kumtaka aende alisema: “Hapana, anafaa kuokoka. Mungu atamrudisha ikiwa amekufa. Hawezi kufa hadi aokoke.”

Mwisho wa masaa kumi na matatu nilifungua macho yangu, na akasema , “Ungetaka nini mpenzi wangu?” Na nikasema: “Ningetaka niende nyumbani,” na akasema: “Utaenda nyumban.” Lakini wakati alitoa shauri hilo, madaktari wakainua mikono yao kwa hofu kuu. Wakasema, “Kwa nini, Itakuwa ni kujiua.” Akasema: “Mmekuwa na zamu yenu. Mlisema amekufa tayari. Nitampeleka nyumbani.”

Sasa nina uzito wa pauni 246. Bado ninaendesha gari moshi la kasi kwa Pennsylvania Lines. Nimeenda Minneapolis kwa likizo fupi, nikiwaambia watu yale ambayo Yesu anaweza kuyafanya, na nina furaha kukwambia ni nini Yesu anaweza kufanya (Blanchard 94-95).

Kuna tu sababu mbili ni kwa nini ombi lolote la wokovu wa mioyo litabaki bila kujibiwa: kuna dhambi au kutoamini katika yule anayefanya maombi, au Shetani anazuia jibu. Kwa hivyo, ikiwa utapata maisha yako kuwa sawa (Yohana 15:7) na kuendelea kuomba, jibu litakuja, kwa kuwa Shetani hawezi kuendelea kuvumilia dhidi ya vita vya kuomba kwenye ujasiri na kwa bidii!!

Sasa katika vita, mipango lazima ifanywe. Askari hawaendi tu kila mahali wakipiga bunduki kwa chochote. Jambo hili ni sawa katika maombi ya vita vya mioyo – tunahitaji maarifa ya vita. Acha nikupatie kadha ambazo ni za kufaa kabisa.

Maarifa ya kwanza ni kwa kanisa lote kujitoa siku zote kwa maombi. Kanisa la kwanza lilifanya hivi: “Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali” (Matendo 1:14) na matokeo ya kustaajibisha – “Na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu” (Matendo 2:41) na “Lakini wengi katika hao waliolisikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano” (Matendo 4:4).

Katika mkutano mwingine wa maombi “mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajawa na Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri” (Matendo 4:31) na mavuno ya kuendelea ya mioyo mingi: “wengi wanaume na wanawake” (Matendo 5:14), “na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu” (Matendo 6:7), na “na watu wote waliokaa Lida na Sharon… wakamgeukia Bwana” (Matendo 9:35). Na kuna vifungu vingine vingi katika kitabu cha Matendo vinavyoeleza visa sawasawa na hivyo. Ikiwa kanisa la leo lingefuata mfano wa maombi wa kanisa la kwanza, lingeona aina hiyo ya matokeo ya uinjilisti.

Maarifa mengine yenye kuzaa ni kutengeneza vikundi vya maombi. Mwanzo bora katika makanisa mengi ungekuwa madarasa ya shule ya jumapili au makundi ya nyumbani kwa vile tayari wanakutana kwa msingi wa kawaida.

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

29

Wanaweza kuomba kwa uthabiti na bila kubadilika kwa orodha yao iliyounganishwa ya watu waliopotea hadi wawaone wakija kwa Kristo.

Evelyn Christenson anapendekeza kuomba kwa tatu pamoja kama kuwa njia moja ya kufaa sana, tena rahisi ya maombi ya kutangulia uinjilisti. Hii inajumlisha Wakristo watatu ambao kwa hiari yao watajiongoza kuomba kila wiki kwa mioyo tisa. Anaeleza matokeo ya kufaa kabisa ya aina hii ya kuomba katika mikutano miwili ya Billy Graham huko Uingereza: Tatu pamoja ilizaa matokeo makubwa ambayo Billy Graham alikuwa amepata hadi kwa mwaka wa 1984 katika mikutano ya Mission England ambapo Wakristo 90,000 katika England walitengeneza makundi ya watu watatu kwa kuomba kabla ya mkutano. Kila mmoja wa hao Wakristo watatu alichagua wasio Wakristo watatu, na halafu walikutana pamoja mara moja kila wiki kwa mwaka uliotangulia mkutano wa kiinjilisti na kuomba kwa majina ya hao tisa kumpokea Yesu. Januari, 1989 jarida la Decision, wakitia moyo kujiandikisha kwa watatu pamoja kwa ajili ya mkutano wa Billy Mission England II, walitoa habari ya kwamba wengi wa wale waombaji wa watatu pamoja waliona wote tisa waliokuwa wakiwaombea wakimkubali Yesu kabla Billy hajafika huko! Zaidi ya makanisa 7,000 kila moja likiwa na watatu pamoja wengi kwa ajili ya Billy’s Mission England ’89, matokeo yalikuwa ya kuvunja ulimwengu. Ni njia ya nguvu namna gani ya kupiga shetani kwa ajili ya mioyo katika taifa nzima” (Christenson 110)!

Washiriki wa maombi ni maarifa mengine yenye kuzaa katika kuombea mioyo ili iokolewe. Ni rahisi sana kuwapata wawili pamoja kuliko kundi kubwa. Timu ya mume/mke ni bora kwa sababu kawaida wako pamoja kila siku, pamoja na mizigo kwa jamaa wao, marafiki, majirani na kadhalika itakuwa sawa. Lakini kuwekwa pamoja kwa washiriki wa maombi wawili wowote kutafanya kazi. Yesu hata anathibitisha maombi yao yatajibiwa (Mathayo 18:19).

Nitaje maarifa moja ambayo hufanya kazi vizuri kwa mtu anayeomba Peke yake – orodha ya maombi!! Mimi, pamoja na maelfu wengine, tumetumia orodha ya maombi kwa miaka, kwa kuwa tumeona mioyo mingi ikija kwa Kristo kupitia njia hii. Ninakuacha na hadithi ambayo ilinibariki, nikitumahi itakuwa sawa kwa wewe.

“Miaka michache iliyopita katika Springfield, Illinois, mtu mwenye juhudi alijikusanyia kundi la kuomba na kuwafanyia shauri hili: ‘Wakati utafika nyumbani leo jioni andika majina ya watu katika Springfield ambao ungetaka waokolewe, na halafu waombee kwa majina yao, mara tatu kwa siku, ya kwamba wapate kuokolewa. Halafu fanya bidii yako bora uwezavyo kuwashawishi wamgeukie Mungu kwa wokovu.’

Palikaa katika Springfield kwa wakati huo mwanamke mgonjwa ambaye kwa mwili alikuwa mdhaifu kabisa. Alikuwa mgonjwa kitandani kwa miaka kumi na saba. Alikuwa kwa muda mrefu akiomba kwa Mungu katika njia ya kawaida kuiokoa mioyo mingi. Wakati familia yake walimwambia juu ya shauri ambalo lilifanywa kwa kundi la kuomba, alisema, ‘Hapa kuna jambo ninaweza kufanya.’ Angeutumia mkono wake wa kulia. Kulikuwa na meza ya kulinganisha kando ya kitanda chake. Aliitisha kalamu na karatasi. Akaandika majina ya watu anaowajua hamsini na saba. Aliwaombea kila mmoja kwa jina mara tatu kwa siku. Aliwaandikia barua na kuwaeleza juu ya moyo wake wa upendo kwao. Pia aliwaandikia marafiki Wakristo, ambao alijua watu hawa

30

wako na imani nao, na kuwasihi waongee na watu hawa kuhusu hali ya mioyo yao na kufanya vizuri kuwabembeleza watubu na kuamini. Alikuwa na imani isiyo na shaka katika Mungu. Katika kumtegemea kwa bidii na unyenyekevu ndivyo alivyowaombea wasiookoka. Kwa wakati kila mmoja wa wale watu hamsini na saba walikiri imani yao katika Yesu Kristo kama mwokozi wao” (McClure 124-25).

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

31

Mlango wa 6

SHUHUDA ZA KIBINAFSI

Nilifundisha masomo haya katika kanisa la kibaptisti la Crestview, Farmerville, Louisiana, Mei 2002. Mchungaji, Ndugu Wayne Whiteside, aliniandikia barua akisema, “Tumeona ngome zikiraruliwa kutoka kwa maisha ya watu… Masomo uliyoyashiriki yameanza mageuzi makuu katika maisha ya wale ambao wanaweka katika mazoezi kanuni za Mungu za kuwaombea waliopotea.” Wayne ana mzigo aliopewa na Mungu kwa ajili ya wafungwa ambao wako katika hukumu ya kifo na huchukua muda mwingi katika magereza akijaribu kuwavuta kwa Kristo. Anaendelea na hadithi yake: “Ushindi mkuu unahusu mfungwa mmoja aliyehukumiwa kifo ambaye aliuawa hivi karibuni katika gereza huko Huntsville, Texas. Alikuwa ni Muislamu aliyejitolea, mwenye maadili mema kuliko Wakristo wengi ninaowajua. Nilikuwa nikifanya kazi naye kwa karibu miaka miwili, nikishiriki naye injili na kanisa langu lilimwombea – yote yalikuwa ni bure. Angeliniandikia, akimalizia barua zake na, ‘Allah awe nawe.’ Kamwe sikukata tamaa au kuwa mdhaifu juu ya hali yoyote. Halafu, kama miezi miwili kabla ya kuuawa kwake Septemba 2002, nilitia moyo kanisa letu kuomba kwa wazi kumfunga mtu mwenye nguvu wa Dini ya uongo na kukiri damu ya Kristo juu yake. Mara moja mabadiliko yakaanza kufanyika. Akaanza kuungama ya kwamba Yesu alikuwa ni mwalimu mwema na barua zake sasa alimalizia na ‘Mungu awe na nawe.’ Alinialika niwe wakati wa kuuawa kwake. Nilisafiri hadi Huntsville kumwona mara moja ya mwisho. Jinsi moyo wangu ulifurahi wakati aliniuliza, 'Lazima nifanye nini ili nimwamini Kristo kwa wokovu?’ Saa 3.05 mchana alimuuliza Bwana Yesu amwokoe. Masaa hamsini na moja na dakika kumi na mbili baadaye alikuwa amekufa. Masaa mawili tu kabla ya kuuawa kwake alinikonyezea jicho na kusema, ‘Ninakupenda na nitakungojea mbinguni.’ Na maneno ya mwisho aliyoyaongea duniani yalikuwa haya: ‘Mungu husamehe. Yeye ni mkuu sana!’ Alikufa na mtazamo wa amani kwa uso wake ya kwamba hata mlinzi alieleza juu yake. Kila kitu tulijaribu kufanya katika bidii yetu kumvuta mfungwa huyu kwa Kristo kilikuwa ni bure kabisa hadi tulipomfunga kwa nguvu mtu mwenye nguvu wa Dini ya Uongo katika maisha yake na kumfunga kupitia kwa damu ya Kristo. Halafu tukaona kuvunjika mara moja ambako kuliendelea hadi mahali alipokuwa wazi kabisa kwa injili ya kwamba aliniuliza jinsi ya kuokoka.Yuko mbinguni leo kwa sababu tulijifunza jinsi ya kuwaombea waliopotea – hasa katika eneo la kumfunga mtu mwenye nguvu jinsi Yesu alisema katika Marko 3:27. Asante kwa kuongea ukweli wa kufanywa huru kwa kusanyiko letu. Bwana akujalie ufanisi sana katika mavuno ya siku za mwisho!” Tunapoanza kuombea wokovu wa mtu, Mungu huonekana akichora mviringo ukimzunguka mtu huyo na halafu anaingia katika mviringo huo naye. Hilo ndilo lililofanyika kwa Ricky Gresham wakati mkewe Helen na mchungaji wake Mickey Hudnall walianza kumwombea. Hapa ni upande wa Ricky wa hadithi hiyo: “Ilikuwa ni

32

wakati wa miezi ya Februari na machi ya 1990 ambapo nilitumia baadhi ya siku na usiku wa taabu wa maisha yangu. Sikuelewa kwa wakati ule, nilikuwa chini ya hatia ya Roho Mtakatifu wa Mungu. Sikujua ni nini kilichokuwa kinafanyika kwangu lakini ninajua ya kwamba kila mahali niligeuka kwa hiyo miezi miwili niliona au kusikia jambo linalohusiana na Mungu. Ilikuwa ni kama kila siku nilipoamka, Mungu alikuwako. Watu niliowajua kwa miaka walikuwa sasa wakiniambia kuhusu Bwana. Nilionekana singeweza kujificha mahali popote! Ninakumbuka siku moja kwa muda fulani rafiki yangu na mimi tulikuwa tukisafiri katika gari lake na rafiki yake akatusimamisha kando ya barabara. Mtu huyu alitembea nakuja upande wangu wa gari na akaanza kuongea. Wakati wa mazungumzo, akaanza kumwongelesha rafiki yangu kuhusu Bwana, akimtia moyo amkubali Bwana kama Mwokozi wake. Mara nyingine tena, ilinibidi kusikiliza neno lingine la Mungu. Ilionekana ya kwamba singeweza kujificha. Nilikaa hapo ndani ya gari bila kuongea neno. Kwa upande mmoja nilitaka kusikia zaidi lakini kwa upande mwingine nilitaka rafiki yangu aendelee kuendesha. Mwishowe, baada ya kile kilichoonekana kama saa moja (dakika tano), aliendesha. Siku zilipoendelea kupita, Mungu alijionyesha kila mahali, siku baada ya siku – hata kazini. Wakati huo nilikuwa nimejiajiri katika duka la mashine. Kulikuwa na mwanamume mweusi ambaye angekuja na kuongea na mimi mara kwa mara. Wakati huu nilipokuwa katika hatia, alikuja dukani. Kwa kiburi changu singeenda kumuuliza mtu niliyemjua kuhusu Bwana. Mwishowe, Nikapata uhodari wa kumuuliza kuhusu Bwana. Ingawa sikuwa tayari kwa jibu lake – Yeye alikuwa! Alisema, ‘dakika moja tu,’ na akaenda kwa gari lake akarudi na Biblia ambayo ilionekana kuwa na miaka mia moja. Akaanza kufungua kurasa za Biblia hiyo, akinisomea maandiko. Sikuelewa alichokuwa akishiriki lakini kuna jambo moja nami leo ambalo sijalisahau: “Ni lazima uzaliwe tena!” Alirudia maneno hayo tena na tena na tena – hayakuacha fikira zangu! Kwa wakati huu, kitu kilikuwa kinanivuta kwa neno la Mungu. Nilikuwa na majivuno sana kumuuliza mtu kwa Biblia, kwa hivyo niliangalia neno ‘Kristo” katika kitabu cha encyclopedia, na kulikuwa na picha ya Kristo akiwa msalabani. Kitu kiliendelea kunivuta kwa picha ile ya Bwana. Usiku baada ya usiku ningejifichaficha nikiangalia picha ile. Wiki chache zilizofuata, nilijaribu kujibadilisha. Nilikuwa nimefika mahali katika maisha yangu ambapo singeacha kulaani – kila neno lingine lilikuwa ni neno la laana. Bila tumaini nilitaka kuacha lakini ilionekana kama kwamba singeitawala – ilinitawala. Mwishowe, siku moja kazini, nilipokuwa peke yangu, nilimwongelesha Mungu, ‘Bwana, siwezi kuvumilia zaidi, nisaidie Mungu. Sielewi yote aliyonitendea Yesu kwa msalaba huo, lakini nionyeshe na nitakufuata.’ Na kutokea siku hiyo, kitu ndani yangu kilibadilika. Sikuacha tu kulaani, hata nilipoteza tamaa – ilikuwa ni kama lugha hiyo haikuwako kamwe. Nililazimishwa kumwambia mtu ni nini kilikuwa kikitendeka kwangu, kwa hivyo nikamuuliza mchungaji kama ningesema jambo kanisani. Yote nilijua kusema ni

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

33

kuwa Mungu alinileta mahali pa kumpenda Bwana Yesu na nilikuwa nimejitolea kumfuata kwa maisha yangu yaliyobakia. Kile ambacho sikujua kwa miezi hiyo miwili ni kuwa mke wangu na mchungaji wake walikuwa wamejitoa kuomba kila siku kwa ajili ya wokovu wangu – kile ambacho nilikuwa ninaona ni Mungu akijibu maombi hayo. Sasa ninajua mimi ni mavuno ya maombi uaminifu, na ikiwa umekuwa hapo unajua ninachomaanisha! Sasa mimi ni mchungaji wa kanisa, na ninazidi kuona neema ya Mungu zaidi na zaidi.” Wakati tunamwomba Mungu amwokoe mtu, ni lazima tuwe tayari Mungu Afanye lolote linalotakikana kumvuta mtu huyo Kwake. Wesley Deuwel anasema, “Majibu mengi ya maombi yanahitaji nia za watu fulani kujitoa kwa mpango wa Mungu. Mungu hawageuzigeuzi watu kama checkers kwenye ubao. Yeye hubembeleza kwa hali na shinikizo nyingi ambazo huzileta juu ya watu” (Deuwel 262). Hata hivyo, shinikizo laweza kuwa na nguvu kabisa! Hivi ndivyo hali ilikuwa kwa Tony Fontenot: “Nilizaliwa katika familia ya Kikristo yenye mashujaa wa kuomba wengi, wakijumlisha mama yangu, nyanya zangu, shangazi na wajomba. Ingawa walikuwa wakiniombea kwa miaka mingi, niliendelea kufanya mambo kwa ‘njia yangu.’ Lakini Mungu anapojaribu kujishughulisha na sisi na tunaendelea kufanya njia yetu, Anaruhusu mambo kufanyika kwetu ambayo yanaweza kuwa ya kusikitisha sana. Na ninaweza kukuthibitishia ya kwamba mioyo yetu itamsikiza!! Mungu alipata moyo wangu kumsikiza Mei 22, 1982. Nilikuwa tu nimemaliza kunyunyizia dawa katika shamba la maharagwe na nilikuwa nikienda kwa ndege wakati ndege yangu ilianguka mahali palipojitenga penye miti na ikawaka moto. Nilikuwa kwenye moto pia!! Baada ya kujifingirisha kwenye ardhi kuzima moto, nilisimama na nikaona shati langu lilikuwa limechomeka kabisa na ngozi kwenye mikono yangu ilikuwa inaning’inia chini kutoka kwa vidole vyangu, ikifanana na utando wa buibui. Pia nilikuwa kipofu kwenye jicho langu la kulia na kitu kama maji kilikuwa kinatoka kwa mwili wangu – Nilijua nilikuwa katika kifungo. Nikaanza kupiga kelele kwa msaada lakini hapakuwa na yeyote wa kusikia. Nilikimbia hadi nikawa mdhaifu sana ya kwamba singeweza kuendelea. Nililala chini ya mti na hapo nikaanza kuomba. Nilimuuliza Mungu tafadhali aache mtu anipate na asiache nife. Mara moja mambo yakaanza kufanyika; ilionekana kama mtu alikuja chini na kunichukua na nguvu ikaanza kutiririka kwa mwili wangu. Nikiwa na nguvu mpya nilianza kukimbia tena, mwishowe nikaona gari. Nililikaribia gari, nikipiga kelele za msaada. Mwanamume ambaye alikuwa akifanya kwa chombo fulani akaangalia juu, alipoona hali yangu, alinipeleka haraka hospitalini. Baadaye nilihamishwa hadi kwa John Sealy Burn Center huko Galveston, Texas, nilikaa miezi miwili iliyofuata katika chumba cha wagonjwa mahututi. Kupitia katika mateso haya ya kusikitisha, mwishowe Mungu aliupata moyo wangu. Katika Novemba, 1982, Ndugu Lee Thomas alihubiri mkutano wa ufufuo katika kanisa la kibaptisti la Indiana Village. Kwa wakati huu alishiriki injili nami na nikamwamini Kristo aniokoe. Aliniambia, ‘Tony, huku kuanguka kwa ndege huenda ikawa ni jambo kubwa ambalo limetokea katika maisha yako kwa sababu kuipitia umempata Bwana.’ Nilikubali!!”

34

Oswald Chambers anasema, “Wakati tunawaombea wengine, Roho wa Mungu anafanya kazi katika makao yasiyofahamika ya nafsi yao ambayo hatujui lolote kuyahusu, lakini baada ya kupita kwa muda maisha yanayofahamika ya yule anayeombewa yanaanza kuonyesha dalili za wasiwasi na kuhangaika… Ni aina hiyo ya uombezi ambayo inafanya uharibifu mkubwa kwa ufalme wa Shetani. Ni ndogo na dhaifu katika viwango vya kwanza, ya kwamba ikiwa akili haitaunganishwa kwa nuru ya Roho Mtakatifu, hatutaitii kamwe” (Chambers 102-03). Hivi ndivyo hali ilikuwa kwa Jacob Williams. Ingawa alikuwa hatiani kwa muda mrefu, ilikuwa tu ni wakati mzigo wa maombi ya wokovu wake uliongezeka miongoni mwa familia na rafiki zake ambapo wokovu ulikuja. Hapa ni hadithi yake: “Nilikuwa katika miaka kati ya kumi na kumi na sita wakati tulihamia katika kanisa la kibaptisti la Westwood. Halafu nilikuwa hatiani mara moja, lakini niliendelea kushindana na wazo hilo kila wakati nilipoenda kanisani. Baada ya muda wazo hilo lilipotea na sikuwa na tamaa hata ya kwenda kanisani. Mama yangu alinishinikiza kuenda kanisani kwa hivyo nilikaa mbali na nyumbani kadiri niwezavyo. Pia nilihusika na uhusiano mbaya sana na msichana na mambo yalionekana kuendelea kuwa mabaya. Kwa wakati huu, familia yangu ilianza kuwa na mzigo mzito kwa ajili yangu. Ilikuwa karibu Krismasi wakati kwa hakika walianza kuniombea kwa bidii kwa ajili ya wokovu wangu. Kwa vile nilikuwa ninakuja nyumbani kama nimechelewa ili kuepuka familia yangu, wakati mwingine baba yangu angekaa ili aweze kuniongelesha kuhusu hali yangu ya kiroho. Niliendelea kumwambia ya kwamba niliokoka nikiwa na miaka kumi na mitatu, lakini sote tulijua ya kwamba huo haukuwa ukweli. Wakati huu, nilikuwa chini ya hatia kubwa – kupokea wokovu kulikuwa mara kwa mara katika fikira zangu, lakini niliendelea kupinga. Mwishowe, Februari iliyopita, singeweza kuvumilia – nilimuuliza Bwana aniokoe. Halafu, nikatambua ya kwamba watu walikuwa wakiniombea kwa wakati huo, sio tu familia yangu bali pia watu wa kanisa. Ndugu yangu mdogo Josh, hata alikuwa na kundi la vijana waliokuwa wakiniombea. Ninafuraha sana Mungu alijibu maombi yao!!” Rachele Barrentine alikuwa katika hali ya kukata tamaa wakati aliniuliza kuombea wokovu wa Mume wake. Ulevi wake na kucheza kamari na kukaa nje masaa yote ya usiku vilimfanya ashindwe kabisa – ilionekana kuwa maombi yake yalikuwa ni bure. Hata hivyo, ibilisi anataka tuone hivi ili tuache kuomba. Lakini kazi moja ya kupendeza ya Mungu ni kuleta kuhukumika kwa kumvunja mtu mara moja wakati ambapo hakuna kabisa dalili hiyo katika hali yake ya mbeleni. Hivi ndivyo ilivyofanyika kwa Jimbo Barrentine: “Ingawa nilikua katika kanisa la kibaptisti la Westwood, kila kitu kilikuwa ni mimi mwenyewe ya kwamba Mungu hakuwa na nafasi katika maisha yangu. Shida zilionekana zikinifuata. Baada ya ndoa na kuzaliwa kwa mwana wangu, nilijikuta nimerudi kanisani, lakini nilikuwa tu ninapitia mawazo. Nilikuwa nimemezwa kabisa ya kwamba talaka haiwezi kuepukika, na baada ya kupoteza familia yangu, maisha yangu yalikuwa tu kama kuzimu hapa duniani. Nilifikiri maisha yatakuwa bora baada ya kumuoa Rachele, lakini nilikosea – hayakuwa mazuri kamwe. Na kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, aliokoka! Halafu tabia yangu mbaya ikazidi kwa sababu nilikaa nje masaa yote ya usiku nikilewa na kucheza kamari ili nisiwe katika uwepo wake ulionifanya kusikia nimeukumika.

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

35

Nilikuwa nje nikilewa na kucheza kamari usiku wote Jumanne, Machi 13, 2001. Wakati nilifika nyumbani Jumatano asubuhi hiyo, nilijua nilihitaji kumpata Mungu maishani mwangu; Singeweza kuishi hivi kamwe. Nilienda kanisani kuongea na Ndugu Lee kuhusu kuokolewa, lakini alikuwa nje ya mji. Kwa hivyo niliendesha gari hadi kwa nyumba ya mjomba wangu Bob, nikijua atanisaidia kwa kuwa alikuwa mhubiri na nilijua ya kwamba yeye na shangazi Faye walikuwa wakiniombea kwa miaka mingi. Shangazi Faye (dada ya mama yangu) hata aliniambia ikiwa ningekuwa mume wake, angekuwa ameniacha zamani. Ninafuraha Rachele hakuniacha, kwa kuwa Jumatano hiyo asubuhi kwa kweli nilimuamini Kristo aniokoe na kwa ajabu ameyabadilisha maisha yangu.” Machozi yameitwa “maombi ya kumiminika.” Labda ni maombi yenye nguvu sana kushinda yote! Nilitambua jinsi yalivyo ya nguvu wakati nilikuwa nikiongoza mazishi huko Moss Bluff, Louisiana, kwa mwanamke mpendwa ambaye nilikuwa mchungaji wake kwa miaka kadha mbeleni huko Orange, Texas. Katika mazishi haya, mwanamume mmoja alinijia, akiunyosha mkono wake kwangu nimsalimie, akisema, “Hunijui sivyo?” Nikasema, “Hapana bwana, siamini ninakujua.” Akasema, “Ninakaa Buna, Texas, na nilisoma katika gazeti ya kwamba Lee Thomas ataongoza mazishi haya. Nilikuja kuona ikiwa ni Lee Thomas niliyemkumbuka.” Alinimbia hadithi hii: “Jina langu ni James Lynch. Nililelewa katika nyumba ya Kikristo, lakini nilipokuwa ninakaa Orange, Texas, nilikuwa mlevi wa kuendelea, ilikuwa ni vigumu kukaa kazini. Siku moja nilipokuwa nimekaa sebuleni mwangu nikiumwa kutokana na kunywa sana na kuchanganyikiwa kuhusu maisha, ulibisha kwa mlango wangu. Nilikukaribisha ndani na punde ulipoingia nyumbani kwangu, niliona machozi yakianza kujaa katika macho yako. Uliniambia ya kwamba Yesu alinipenda na alitaka kuniokoa, lakini pombe ilikuwa imenishika ya kwamba nilikataa toleo la Mungu la wokovu. Ulipiga magoti kando ya kiti changu na machozi yakitiririka usoni mwako, ulinisihi kumwamini Kristo aniokoe. Baada ya kumpinga Mungu kwa miaka hiyo mitatu, nilitubu na Mungu kwa utukufu akaniokoa na akaniita kuhubiri. Nimekuwa nikilihubiri Neno Lake kwa miaka kadha sasa. Ninaamini ya kwamba ikiwa haungekuja nyumbani kwangu siku hiyo, ningekuwa nimepotea bila Mungu na tayari nimekufa katika kuzimu.” Ilichukua zaidi ya miaka sitini ya kuomba kila siku kwa Goerge Muller kumleta rafiki yake kwa Kristo. Ilichukua miaka mitatu kwa machozi kumleta James Lynch kwa Kristo. Lakini, Jabez Carey alikuja kwa Kristo, saa ile ile wakristo elfu mbili walimwombea, ikithibitisha kuwa njia inayofaa sana ya kuwaombea waliopotea ni kupitia kuungana! Huu ndiyo ulikuwa ufunguo kwa wokovu wa Mike Doles. Hapa ni hadithi yake: “Nilikua katika kanisa la kibaptisti la New Hope, lakini sikumwamini kamwe Bwana aniokoe. Kama kijana niliwatazama wenzangu shuleni wakijiunga na kanisa, lakini mimi sikujiunga. Niliwatazama ndugu na dada zangu wakijiunga na kanisa,lakini mimi sikujiunga. Niliamini katika maelezo ya maisha ya milele na nilijua ya kwamba kumwamini Kristo ilikuwa jambo sawa la kufanya, lakini sikulifanya.

36

Ingawa mama yangu aliendelea kuniombea, hakuna chochote kilitendeka hadi usiku mchungaji aliuuliza mkutano uandike kwa kipande cha karatasi jina la mtu ambaye wangejitolea kumuombea aokolewe. Baadaye aliniambia ya kwamba alikusanya vipande vya makaratasi kumi na nane na ya kwamba jina langu lilikuwa kwa kila moja. Muda mfupi baada ya kuanza kuniombea, nilianza kujiona tupu na wazi ndani na hali ilizidi hadi nikaanza kusoma Biblia na kumuuliza Bwana anionyeshe nifanye nini. Nilikuwa tayari nikienda kanisani Jumapili asubuhi na Machi 1, 1998, wiki mbili baada ya hawa watu kumi na nane walianza kuniombea, Bwana aliniambia niende mbele kanisani na kuchukua hatua ya kwanza na ya kwamba atafanya yaliyobakia. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha yangu na Bwana. Ingawa niliharibu miaka yangu ya kwanza arobaini na tisa kwa kumkataa Bwana, sasa ninajua ya kwamba wajibu wetu kama Wakristo ni kutumia mali yetu yote kusaidia kueneza neno Lake. Na hii ninakusudia kufanya kwa kila nafasi analonipatia!”

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

37

Mlango wa 7

KUFANYA AHADI Kitabu hiki hakikuandikwa ili kikae kwenye rafu popote, bali kiingie moyoni mwako na ukweli huu unaochoma wa kutisha: hali ya mtu fulani ya milele iko mikononi mwako – mtu atakufa, na kuenda kuzimu isipokuwa uombe!! Andrew Murray anajadili kuwa uombezi ni wa lazima, hata ni mwanzo mkuu katika kubadilishwa kwa mioyo: “Kuna dunia na mamilioni yake wanaoangamia, na maombi kama tumaini lake la pekee. Ni kiasi gani cha upendo na kazi ni karibu na bure, kwa sababu kuna maombezi kidogo sana…Mioyo, kila mmoja wa thamani zaidi kuliko dunia, thamani isiopungua bei iliyolipwa kwao katika damu ya Kristo, na karibu kufikiwa kwa nguvu ambayo inaweza kushindwa kwa uombezi” (Murray 112). Ombi langu ni kwamba kitabu hiki kitakuwa ni rafiki yako imara ukimeza ukweli wake,na kuwa mwombezi mkuu wa mioyo iliyopotea ambaye Mungu anataka sana na kukuhitaji uwe. Unaposoma shairi hili na Sandra Goodwin, ninatumaini moyo wako utachochewa kusema, “Ndio, Bwana , Nitachukua kazi.”

KUSAFIRI KWA MAGOTI YANGU

Usiku uliopita nilisafiri Kwa nchi ng’ambo ya bahari

Sikuenda kwa meli au ndege – Nilisafiri kwa magoti yangu

Niliwaona watu wengi huko

Katika utumwa kwa dhambi zao, Na Yesu aliniambia imenipasa kuenda,

Ya kwamba kulikuwa na mioyo ya kuvuta.

Lakini nikasema, “Yesu, siwezi kuenda Kwa nchi ng’ambo ya bahari.”

Akajibu kwa haraka, “Ndio, unaweza – Kwa kusafiri kwa magoti yako.”

Alisema, “Wewe omba, Nitakutana na hitaji.

Wewe ita, na nitasikia. Ni juu yako kuhusika

Kwa mioyo iliyopotea mbali na karibu.”

Na kwa hivyo nilifanya, nilipiga magoti katika kuomba, Nikatoa baadhi ya masaa ya utulivu,

Na mwokozi kando yangu

38

Nilisafiri kwa magoti yangu.

Nilipoendelea kuomba, niliona mioyo ikiokolewa Na watu waliopotoka wakiponywa.

Niliona nguvu ya wafanyikazi wa Mungu ikifanywa upya Wakifanya kazi shambani.

Nilisema, “Ndio, Bwana nitachukua kazi.

Moyo wako ninataka kuufurahisha. Nitatii mwito wako na kuenda upesi Kwa kusafiri kwa magoti yangu.”

(Lundstrom 207-08) Mzigo wangu niliopewa na Mungu ni kuona maelfu ya watu wa Mungu wakiongezeka kuwa mashujaa wa maombi wakiombea mioyo. Na nitabarikiwa kwa njia ya ajabu ikiwa utanijulisha ya kwamba unaniunga katika huduma hii yenye utukufu, nguvu na ya kufaa zaidi ya yote – kuwaombea waliopotea!! Pia, ikiwa kuna mtu mmoja ambaye unataka sana kuona akiokolewa, nitumie jina lake na uhusiano wake na wewe, pamoja na habari yoyote ya kufaa ambayo itanipatia ujuzi katika hali na nitakubaliana nawe katika maombi ya kubadilishwa kwake kulingana na ahadi ya Bwana katika Mathayo 18:19. Lakini, ninauliza ya kwamba ufanye hivi tu ikiwa umekata tamaa ya kutosha kuomba kulingana na kanuni ambazo nimezishiriki katika kitabu hiki. Ningekuuliza pia unifahamishe juu ya kazi ya Mungu katika hali, hasa wakati wokovu unakuja! Lee E. Thomas Barua pepe: [email protected] 2314 Foster Lane Simu: 337-433-8677 Ofisi Westlake, LA 70669 337-433-2663 Nyumbani

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

39

ORODHA YANGU YA MAOMBI

(1 Samueli 12:23) “Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi”

1. ____________________________________________________________ 2. ____________________________________________________________ 3. ____________________________________________________________ 4. ____________________________________________________________ 5. ____________________________________________________________ 6. ____________________________________________________________ 8. __________________________________________________________ 9. __________________________________________________________ 10. __________________________________________________________ 11. __________________________________________________________ 12. __________________________________________________________ 13. __________________________________________________________ 14. __________________________________________________________ 15. __________________________________________________________ 16. __________________________________________________________ 17. __________________________________________________________ 18. __________________________________________________________ 19. __________________________________________________________ 20. __________________________________________________________ 21. __________________________________________________________

40

Kazi Iliyotajwa

Billheimer, Paul E. Destined to Overcome. Minneapolis: Bethany House, 1982. Blanchard, Charles. Getting Things From God. Chicago: Moody, 1934 Caree, E.G. Praying Hyde. South Plainsfield: Bridge, n.d. Chadwick, Samuel. The Way To Pentecost. Fort Washington: CLC, 2001. Chafer, Lewis S. True Evangelism. Findley: Durham, 1919. Chambers Oswald. If Ye Ask. Alexandria: Lamplighter, n.d. Christenson, Evelyn. Battling the Prince of Darkness. Wheaton: Victor, 1990. Cymbala, Jim. Fresh Wind, Fresh Fire. Grand Rapids: Zondervan, 1997. Deuwel Wesley Mighty Prevailing Prayer. Grand Rapids: Asbury, 1990. Dunn, Ronald. Don’t Just Stand There, Pray Something. Nashville: Nelson, 1992. Eastman, Dick. No Easy Road. Grand Rapids: Baker 1971. Edwards, Brian. Revival. Durham: Evangelical 1990. Epp. Theodore H. Praying with Authority. Lincoln: Bible Broadcast, 1965. Finney, Charles G. Revivals of Religion. Old Tappan: Revell, n.d. Charles G. Finney: An Autobiography. Westwood: Revell, 1876. Gordon, A.J. The Holy Spirit In Missions. New York: Revell 1893. Gordon, S.D. Quiet Talks on Prayer. New York: Revell 1903. Huegel, F.J. Prayer’s Deeper Secrets. Grand Rapids: Zondervan, 1959. Lundstrom, Lowell. How You Can Pray with Power and Get Results. Sisseton: Lundstrom Ministries, 1981. Matthews, R. Arthur Born For Battle. Wheaton: Shaw, 1978.

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)

41

McClure, James G.K. Intercessory Prayer. Chicago: Moody, 1902. Murray, Andrew. The Ministry oa Intercession. Oldtappan: Revell, n.d. Newell, Philip. Revival on God’s Terms. Chicago: Moody, 1959. Penn-Lewis, Jessie. Prayer ana Evangelism. Dorset: Overcomer, n.d. Pierson, A.T. George muller of Bristol. Old Tappan: Revell, 1899. Ravenhill, Leonard. Revival God’s Way. Minneapolis: Bethany House, 1986. Smith, Eddie. Intercessors. Houston: SpiriTruth, 1998. Spurgeon, Charles. My Conversion. Springdale: Whitaker, 1996. Twelve Sermons on Prayer. Grand Rapids: Baker, 1990. Steer, Roger. George Muller: Delighted in God. Wheaton: Shaw, 1981.

Create PDF files without this message by purchasing novaPDF printer (http://www.novapdf.com)