mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/mkulima-v1-swahili.pdf ·...

36
Mkulima ulimwengu wa JANUARI 2012 TOLEO 1 ISSN: 1821 - 8245 farmer’s world Kuimarisha usawa wa kijinsia katika kilimo MABADILIKO YAMEKUJA UKWELI KUHUSU MHOGO UZALISHAJI WA NISHATI UOTO www.ansaf.or.tz

Upload: others

Post on 05-Oct-2019

32 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

Mkulimaulimwengu wa

JANUARI 2012 TOLEO 1ISSN: 1821 - 8245farmer’s world

Kuimarisha usawa wakijinsia katika kilimo

MabadilikoyaMekuja

ukweli kuhusu Mhogo

uzalishaji wanishati uoto

www.ansaf.or.tz

Page 2: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

Tanzania ni nchi yenye fursa lukuki za uwekezaji.

Msukumo wa kisiasa wa viongozi wa juu wa Tanzania katika kuvutia wawekezaji wa ndani na nje na katika kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji binafsi ni thabiti na utaendelea kuwa hivyo.

Sekta ya kilimo ni mojawapo ya sekta ambazo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinawakaribisha wawekezaji kuwekeza. Sekta hii ndiyo inaongoza kwa kuchangia asilimia 26 ya pato la taifa. Inachangia asilimia 45 ya mapato yote yatokanayo na mauzo ya nje na huajiri takribani asilimia 80 ya nguvu kazi yote Tanzania.

Kuna kila sababu kwa TIC kuhamasisha uwekezaji katika kilimo nchini Tanzania. Tanzania ina takribani hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo lakini ni takribani hekta milioni 10.1 tu (asilimia 23) inayolimwa kwa mwaka. Ukubwa wa eneo la Tanzania unatoa fursa muhimu kama za maji, ardhi na tabia nzuri ya nchi kwa ajili ya uzalishaji wa kilimo chenye ushindani. Kwa wastani, mvua kwa mwaka ni kati ya 600mm – 1100 mm.

Pamoja na matatizo yanayoikabili sekta hii, kuna fursa kadhaa ambazo zinaweza kutumiwa katika uendelezaji wa sekta. Tanzania inazo sifa za kuwezesha uzalishaji karibu wa mazao yote yanayouzwa nje pamoja na ufugaji. Sifa hii inaweza kuboreshwa kwa matumizi ya njia bora za uzalishaji na ufanisi wa soko.

TIC yakaribisha Wawekezaji KATIKA KILIMO

Page 3: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

YaliYomo

Neno toka kwa mkurugenzi

Kutoka meza ya mhariri

Neno la mgeni: aNSaF – msingi wa Kujengea mapinduzi ya kilimo

mabadiliko yamekuja

Uzalishaji wa nishati uoto na athari yake kwa wakulima wadogo

Viinitete vyasambaa Tanzania

Ukweli kuhusu mhogo Nchini Nigeria na Tanzania

Wiki ya mhogo Tanzania

Wajibu wa mViWaTa

Uzoefu wa VECo katika kuendeleza mnyororo wa kuongezea

thamani muhogo nchini Tanzania

Kuimarisha usawa wa kijinsia katika kilimo

Kutambuliwa: Siku ya Kimataifa ya Wanawake wa vijijini

Wasifu wa miriam mkosamali

Taarifa kwa Ufupi

Samoye ibrahim

Joyce Hiza

Kupata na kutumia taarifa za masoko – Ni kitendawili kwa wakulima wadogo

Wafugaji wa kuku wa kienyeji wamewezeshwa

5678

1011121314

23252728323334

35

4

14 21

917

Page 4: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

4 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Neno toka kwa Mkurugenzi

TumejiToa kuhakikisha kuwa jarida

hili linakuwa la manufaa

kwa kuandika masuala ya

msingi.

Karibu katika toleo hili muhimu sana la Jarida la Ulimwengu wa Mkulima. Jarida hili la Ulimwengu wa Mkulima ni moja ya mikakati yetu ya kuwafikia wadau wetu wengi zaidi, hususan

wakulima wadogo wadogo. Jarida hili ni kiashiria cha mageuzi makubwa kutoka Jarida la Ukulima Endelevu lililokuwa linafadhiliwa na wabia kupitia ANSAF. ANSAF inaamini kwamba kuna maarifa mengi ambayo hayajasambazwa. Kuna fursa zisizo na kikomo za wadau kuweza kufahamishana. Wakulima wadogo wadogo wanakabiliwa na changamoto kubwa katika upataji wa taarifa sahihi. Jarida la Ulimwengu wa Mkulima linajaribu kukata hiyo kiu ya taarifa. Tumejitoa kuhakikisha kuwa Jarida hili linakuwa la manufaa kwa kuandika masuala ya msingi. Tunawakaribisha wanachama na wadau wengine kulitumia Jarida hili la Ulimwengu wa Mkulima kuwafahamisha wengine kuhusu teknolojia ambazo zimethibitishwa, fursa katika masoko, upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya kilimo na kuhusu wapi pa kupata zana za kilimo, vifaa vya kuongeza ubora wa mazao na mambo mengine mengi. Tutachapisha muhtasari wa matokeo ya tafiti, mapitio ya utekelezaji wa sera na simulizi za mafanikio. Tutatumia jukwaa hili kusambaza taarifa ambazo zitawawezesha wadau kuchukua hatua. ANSAF inalenga kutoa Jarida hili kila robo ya mwaka likiwemo chapisho la kingereza. Katika kila toleo, tumekusudia kuendelea kuchapisha masuala nyeti yanayowahusu wasomaji wetu. Utafurahia kufuatilia masuala yaliyoibuliwa katika toleo hili. Masuala yaliyomo yanagusa maeneo mengi – kuanzia mnyororo wa kuongeza thamani hadi mikakati ya masoko. Katika toleo hili, tunatoa mifano ya mafanikio katika kilimo cha baadhi ya mazao kama mhogo na mahindi kutoka Nigeria and Tanzania. Aidha tumegusia masuala ya usawa, tukilenga zaidi kwenye eneo la jinsia, kwa kuzingatia muktadha na hali ya Tanzania. Lengo ni kuwahamasisha wadau mbalimbali kuwaunga mkono wanawake – ambao ndio kundi kubwa zaidi la wazalishaji wa chakula nchini Tanzania. Tunatarajia kupokea mchango wenu wa uzoefu na taarifa mbalimbali kwa ajili ya kuzisambaza zaidi. Tunapenda kuwashukuru wabia wetu, hususan GORTA, IRISH AID na Swiss Agency for International Cooperation (SDC) kwa kutupatia msaada. Toleo hili linasambazwa bure kote nchini Tanzania. Wanachama wa ANSAF wanahamasishwa kuwasiliana na ofisi zetu kwa ajili ya kujipatia nakala za Jarida.Karibuni

Audax RukongeKatibu Mtendaji wa ANSAF

Ndugu msomaji wetu mpendwa,

Page 5: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

5UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Kuzaliwa kwa mtoto ni furaha kubwa katika familia. Familia ya ANSAF inatangaza ujio wa mtoto wake mpya, Jarida la Ulimwengu wa Mkulima.

Wazo la kuanzisha jarida hili liliibuka kama mwaka mmoja uliopita. Maandalizi ya maudhui yake yalichukua miezi miwili. Leo hii, tunasherehekea kuzaliwa kwa jarida hili ambalo limesubiriwa kwa muda mrefu kwa ajili na linaloihusu Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF). Jarida hili linalenga kuanzisha na kuongoza mijadala juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya kilimo. Ulimwengu wa Mkulima litatumika kama zana ya kuchanganyia maarifa na kama chombo cha kusambazia taarifa duniani kote. Wakati mrengo wa jarida hili utabaki kwenye sekta ya kilimo na hususan wakulima wadogo wadogo, lakini pia litaangazia sera zenye athari kwa maisha ya watu na utekelezaji wake. Litakuwa mstari wa mbele katika kutetea uboreshaji wa maisha ya wakulima wadogo wadogo na ulinzi wa mazingira nchini Tanzania. Katika toleo hili, tunajikita katika masuala yahusuyo uwezeshaji, ushirikiano, maendeleo ya mnyororo wa masoko na usawa wa kijinsia. Jarida pia linaangazia uzoefu wa makundi mbalimbali na kuchochea vipaji vilivyolala ndani ya wasomaji. Kwa kuwa toleo hili ni sawa na mtoto mchanga, tunatarajia wasomaji watatuma “kadi za pongezi kwa kuzaliwa kwake” zikiwa na ujumbe na mapendekezo juu ya namna gani tunaweza kumfanya mtoto akue. Kwa hakika, mchango kutoka kwa wasomaji – wanachama na wasio wanachama wa ANSAF itamfanya mtoto akue na awe na afya. Jarida la Ulimwengu wa Mkulima linahamasisha uchanganyaji wa mawazo mbalimbali kutoka maeneo tofauti. Mgongano wa mawazo ndio unaowezesha ubunifu kutokea. ANSAF inatarajia kwamba wasomaji wa toleo hili watakuwa mabalozi wazuri wa Ulimwengu wa Mkulima. Eneza habari kuwa mtoto amezaliwa.

Alawiya Mohamed & Mbarwa Kivuyo

Kutoka Meza ya Mhariri

bodi ya uhaRiRi

MkuRugenzi Mtendajiaudax rukonge

MhaRiRi Mkuualawiya mohammed

MhaRiRi MshauRimbarwa kivuyo

Mwandishi Mgeni Mwalikwajuma salum shamte

waChangiajiaudax rukonge

juma salum shamtealawiya mohammed

mbarwa kivuyoelias mtinda

michael farrellyisla gilmore

katrine PlesnerCleophas rwechungura

michael goldwater

usaMbazaji, Mauzo na Masokoalawiya mohammed

MChaPishaji:agricultural non state actors forum

169 regent estates.l.P 6370

dar es salaam, Tanzaniasimu: +255 22 2700327

nukushi: +255 22 2700318Barua pepe: [email protected]

Tovuti: www.ansaf.or.tz

MsaniFu na MPiga ChaPa iPrint (T) ltd

s.l.P: 10009, dar es salaamsimu: (+255 22) 286 5810

Barua pepe: [email protected]

Mkulimaulimwengu wa

JANUARI 2012 TOLEO 1

ISSN: 1821 - 8245

farmer’s world

Kuimarisha usawa wa

kijinsia katika kilimo

MabadilikoyaMekuja

ukweli kuhusu

Mhogo

uzalishaji wa

nishati uoto

www.ansaf.or.tz

Page 6: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

6 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Msingi

Hivi karibuni, sekta ya kilimo Tanzania imepitia mabadiliko makubwa kutokana na mchanganyiko wa mikakati mbalimbali ambayo imekuwa

ikiibuliwa. Mikakati hiyo imeenda sambamba na jitihada za kikanda zilizojengwa kwenye Mpango madhubuti wa uendelezaji ya sekta ya kilimo Afrika. (Comprehensive Africa Agriculture Development Program (CAADP) hata kabla ya kuja kwa kauli mbiu ya ‘Kilimo Kwanza’. Katika kutekeleza malengo ya maendeleo ya kitaifa yaliyomo katika Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA), ni muhimu kuwaweka wadau mstari wa mbele. Agriculture Non State Actors Forum (ANSAF) ni kiungo muhimu kati ya watunga sera, wafadhili, makundi mbalimbali na wakulima ambao maisha yao yanategemea sana kilimo. Jukwaa hili ndilo linasaidia kuunganisha jitihada za kimaendeleo katika ngazi za taifa, mikoa na wilaya ili kuwezesha kufikiwa kwa “Dira ya Taifa ya 2025.” ANSAF inawaleta pamoja wadau mbalimbali ambao ndio huongoza na kuhamasisha maendeleo ya kilimo nchini Tanzania. ANSAF imetengeneza jukwaa ambalo hutumika kupeana uzoefu mbalimbali kwa wadau wengi zaidi. Ongezeko la jitihada za sekta binafsi, Asazi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ndizo zinashuhudia hilo.

ANSAF ni jukwaa la majadiliano kuhusu mafanikio mbalimbali na kuhusu masuala muhimu katika maendeleo ya kilimo. Jukwaa hili linawaleta pamoja wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na kuwawezesha kupanga malengo na vipaumbele vya pamoja vyenye uwezo wa kuwa na faida kubwa kwa wakulima na mazingira yao. Kwa kutumia matukio, kumbukumbu, tafiti na tovuti, ANSAF inaweza kusambaza taarifa sio tu kwa wakulima bali pia na kwa makundi mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na umma kwa ujumla. Jarida la “Ulimwengu wa Mkulima” ni toleo linalokaribishwa sana kwa sababu linatoa fursa kwa wadau mbalimbali kubadilishana taarifa kwa njia ya makala, tafiti na uzoefu. Kwa kuwa kilimo ni sekta pana sana, kuanzia kwenye mazao hadi ufugaji, mabadiliko ya tabia nchi hadi mnyororo wa masoko, dhana kadhaa zimejadiliwa katika Jarida hili. Tunatarajia kwamba Jarida hili litalenga masuala kadhaa mahsusi na mengine ya kiujumla ambayo ni ya muhimu kwa maendeleo ya kilimo hapa nchini. Jarida linatoa taarifa ambazo ni halisi, lakini muhimu zaidi, ni rejeo lenye taarifa zote kuhusiana na maendeleo ya kilimo Tanzania.

Juma S. ShamteMakala hii imeandikwa na Mwandishi

mgeni mwalikwa kutoka Katani Ltd, Tanga

MApInduzI yA KILIMOaNSaF – msingi wa Kujengea

aNSaF inawaleta pamoja wadau mbalimbali ambao ndio huongoza na kuhamasisha maendeleo ya kilimo nchini Tanzania.

Page 7: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

7UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Mabadiliko

Regina Salaganda ni mmoja wa wanawake wengi wanaojishughulisha na kilimo cha mkonge wilayani Kishapu.

Anawalea watoto wake peke yake kwa sababu ametalikiwa. “Watoto wangu wanahitaji chakula, mavazi na mahali pa kulala, na muhimu zaidi, elimu. Huo ndio uti wao wa mgongo,” anaeleza Regina Salaganda. Wanawake katika Wilaya ya Kishapu huunda vikundi vidogo vidogo vya uzalishaji katika maeneo yao, huku wakimiliki karibu mnyororo mzima wa uzalishaji. Huunda vikundi vya watu 15. Waliunda vikundi hivyo kwa sababu maisha sio safari rahisi, hususan kwa wanawake wa vijijini nchini Tanzania. Kiwango cha ukandamizaji kiko juu japokuwa kampeni kadhaa za masuala ya jinsia zimejenga uelewa. Vikundi hutoa fursa kwa wanawake kukabiliana na ukandamizaji. Kupitia mipango ya ukopeshaji ya ndani ya jamii, wanawake wamefanikiwa kuendesha maisha yao. Wanaweka akiba na kuwakopesha wengine. Hapa ndipo wanawake wanaofanya kazi kwa bidii wanahamasishwa kuwa wajasiri na wakakamavu katika kuleta mabadiliko

maishani mwao. Salaganda alijiunga na kikundi kama sehemu ya utekelezaji wa jitihada za uwezeshaji wa wanawake. Alipewa mafunzo ya ujasiriamali, utunzaji wa kumbukumbu, ubunifu na ushonaji. Aliporudi nyumbani, Salaganda alijipanga na kuunda kikundi chake binafsi cha ushonaji. Kikundi chake hushona nguo za watoto na za wanawake. Tofauti na shughuli za ushonaji, Salaganda pia analima mkonge. “Mkonge ndio shughuli yangu kuu. Kwa kuanzia, nilipanda miche 400 ya mkonge. Najua ninahitaji miaka kama miwili ili nianze kuvuna. Baada ya hapo nitakuwa napata fedha zaidi. Kwa sasa, napata fedha kutokana na kilimo cha nyanya, vitunguu na kabichi za kichina,” alieleza Salaganda. Kwa sasa anaweza kulipa ada za watoto wake. Mabadiliko ni mchakato. Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha maisha yake mwenyewe. Lakini kwa kutumia mafunzo aliyopewa, kwa sasa anaweza kuhudumia familia yake. Kama ukimuelimisha mwanamke mmoja utakuwa umeielimisha jamii nzima.

“Hapo mwanzo sikujua ni namna gani ninaweza kuanzisha chanzo changu cha mapato, ilikuwa vigumu.”

mabadiliko HAyA HApA

Page 8: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

8 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Uzalishaji wa Nishati uoto nchini Tanzania ulianza kufuatia utafiti uliofadhiliwa na GTZ

kuhusu Nishati uoto mwaka 2005. Kwa sasa, nchi inakabiliwa na ongezeko la uhitaji na shauku ya kupata ardhi. Kuna makampuni kadhaa ya kigeni kutoka Ulaya yanayopora ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa Nishati uoto na matumizi mengine. Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) kimeainisha hekta takribani million 2.5 ambazo ‘zinafaa’ kwa miradi ya uwekezaji na hadi kufikia mwaka 2009 tayari hekta 640,000 zilikuwa zimekwishatengwa kwa ajili ya uzalishaji wa Nishati uoto. Kutokana na ruzuku kubwa zinazotolewa kwenye uzalishaji wa Nishati uoto, makampuni ya Ulaya

Nishati Uoto ni suala geni nchini Tanzania huususani itokanayo na mimea.

Uzalishaji wa Nishati uoto na athari zake kwaWAKuLIMA WAdOgO WAdOgO

yanajinyakulia ardhi katika nchi zinazoendelea kwa kasi ya kutisha kwa matarajio kuwa matumizi ya Nishati uoto yataongezeka ifikapo mwaka 2020.

Kwa ujumla, uporaji wa ardhi una athari kubwa kwa haki za ardhi za wakulima wadogo

wadogo. Ijapokuwa sheria inaagiza kufanyika kwa mashauriano na jamii zinazohusika, katika utekelezaji utaratibu huo huwa haufuatwi kama inavyotakiwa. Fidia huwa haitoshi, haijadiliwi na kukubaliwa na pande zinazohusika na wakati mwingine huwa hailipwi kwa wakati. Mipango na makubaliano ya manunuzi inakuwa na mapungufu (ufisadi, udanganyifu na taarifa potofu). Taarifa ya utafiti

nishati uoto

uzalishaji wa nishaTi uoTo

nChini Tanzania ulianza

kufuaTia uTafiTi uliofadhiliwa na gTz kuhusu

nishaTi uoTo mwaka 2005

Page 9: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

9UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

wa ActionAid Tanzania kuhusu “Athari ya Uzalishaji wa Nishati uoto katika Usalama wa Chakula Tanzania” pamoja na taarifa nyingine kuhusiana na suala hilo zinaonesha kwamba maamuzi ya wanavijiji kutoa ardhi kwa wawekezaji huwa yamejengwa kwenye taarifa potofu au matarajio yasiyo sahihi. Wakati serikali ikiendelea kuhamasisha uwekezaji kwenye Nishati uoto nchini, hakuna sera wala sheria inayosimamia na kuongoza uzalishaji huo. Uwekezaji kwenye Nishati uoto umekuwa ukilaumiwa na umma kwa kusababisha kuondolewa kwa wakulima wadogowadogo katika ardhi zao. Kwa mujibu wa taarifa ya ActionAid Tanzania, jumla ya wakulima wadogo wadogo 173 wamekwishaondolewa katika mashamba yao huko Kisarawe, Lindi na Kilwa. Wengine hawakufidiwa na wengine walipunjwa fidia yao. Kadhalika mchakato wenyewe haukuwa wazi. Wawekezaji huenda moja kwa moja kujadiliana na jamii za vijijini kuhusiana na ardhi jambo ambalo ni kinyume cha taratibu na pia halifai kwa kuzingatia uwezo wa jamii hizo kuweza kujadiliana. Ardhi inayochukuliwa na makampuni ya uwekezaji haijachoka kama inavyodaiwa na baadhi ya makampuni. Ardhi hiyo ni nzuri na inafaa kwa uzalishaji wa mazao ya chakula. Bonde la Mto Rufiji, kwa mfano, ni zuri na linafaa sana kwa uzalishaji ambapo, likitumiwa vizuri, linaweza kulisha taifa zima. Pia, ardhi inayochukuliwa kwa ajili ya uzalishaji wa Nishati uoto iko karibu na maji ambayo yangeweza kutumiwa kwa ajili ya umwagiliaji na uzalishaji wa mazao ya chakula na hivyo kuongeza uhakika wa chakula lakini cha kushangaza maji hayo hutumika kumwagilia mashamba kwa ajili ya Nishati uoto. Uwekezaji mkubwa kwa ajili ya Nishati uoto katika maeneo kama Kilwa na Kisarawe huhusisha ufyekaji wa uoto wa asili na viumbe hai wake jambo ambalo husababisha upotevu wa baioanuai, hususan miti ya miombo na misitu ya pwani. Kutokana na changamoto hii na athari yake pana kwa maisha ya wakulima wadogo wadogo na taifa kwa ujumla, ActionAid Tanzania pamoja na wadau wengine na Asasi za Kiraia wanafanya

ushawishi wa kutaka serikali itunge sera na sheria za kusimamia uwekezaji ambao hautaathiri usalama wa chakula. Mwezi Oktoba 2010 wakati wa Siku ya Chakula Duniani, ActionAid Tanzania kwa kushirikiana na Oxfam GB na HakiArdhi waliandaa mdahalo wa siku moja chini ya mada isemayo: “Zuia Uporaji wa Ardhi: Wekeza kwa Wakulima Wadogo”. Mdahalo huo uliwapa fursa washiriki zaidi ya 100 kutoka vikundi vya wakulima wadogo

wadogo, Asasi za Kiraia, vyombo vya habari na maofisa wa Serikali kujadili masuala ya haki za ardhi ikiwa ni pamoja na suala la uporaji wa ardhi na athari zake kwa wakulima wadogo wadogo. Taarifa ya ActionAid iitwayo “Uzalishaji wa Nishati uoto na Athari zake kwa Usalama wa Chakula” ilizinduliwa wakati wa mdahalo huo. Taarifa ilisisitiza haja ya serikali kushughulikia madhara ya uzalishaji wa Nishati uoto.

nishati uoto

Page 10: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

10 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Hapo mwanzo Tanzania haikuwa na viini tete, lakini sasa imefungua

milango kwa teknolojia ya vinasaba. Utafiti kuhusiana na mhogo na mahindi yaliyobadilishwa vinasaba umeshaanza. Miongozo na kanuni za usalama wa vinasaba vya uoto zimekwishapitishwa na mchakato wa kutengenezwa kwa sheria unaharakishwa ili kufungua mlango kwa majaribio na uuzaji wa mazao hayo. Wakati huo huo, Taarifa ya Dunia ya Kilimo (IAASTD) 2009, iliyotengenezwa na wanasayansi 400 na kuridhiwa na serikali 61 ikiwemo ya Tanzania inatoa wito kwa serikali na mashirika ya kimataifa kubadilisha muelekeo na kuongeza rasilimali katika kuchochea mapinduzi ya kilimo ambayo yanafaa kwa mazingira. Ujumbe mkuu wa taarifa hiyo ni kwamba kuna haja ya haraka ya kuachana na kilimo chenye uharibifu na kinachotegemea sana kemikali na kuanza kutumia njia rafiki kwa mazingira ambazo zinafaa kwa bioanuai na katika kuziendeleza jamii pia. Taarifa hiyo ilihitimisha kwamba mbinu za kilimo zinazotumia uhandisi vinasaba sio suluhisho kwa bei za vyakula zinazozidi kupanda njaa wala umaskini. Taarifa hiyo pia inamulika uwezo mdogo wa Afrika katika kufanya tathmini ya athari: “Masuala nyeti

katika utumiaji wa teknolojia ya baiotiki na hususan uhandisi vinasaba ni uchakachuaji wa mbegu zilizohifadhiwa na wakulima na tishio kwa baioanuai katika maeneo husika. Athari za kimazingira na ushahidi wa athari za kiafya Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara vinamaanisha kwamba suala la uwezo wa Afrika kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na utafiti wa teknolojia hiyo, maendeleo yake, usambazaji na utumiaji wake ni nyeti sana, inaelezea taarifa ya IAASTD. Teknolojia ya ubadilishaji vinasaba imekuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi kwa wakulima wa mashamba makubwa, hususan huko Marekani, lakini tafiti zinaonesha kuwepo kwa manufaa kidogo sana kwa wakulima wadogo wadogo. Uchunguzi umebaini pia kuwa tija ya matumizi ya teknolojia hii ni ndogo ukilinganisha na matumizi ya njia za kawaida za kilimo. Matumizi ya teknolojia hii yanahamasisha utumiaji mkubwa wa kemikali zenye sumu; ni aghali sana kwa kuwa huwa na manitaji makubwa; hupunguza baioanuai; huongeza utegemezi wa wakulima kwenye biashara ya kilimo; huweza kuwa na athari za kiafya zisizojulikana wakati huo huo matumizi haya yakielekeza rasilimali muhimu (kama watu, muda na pesa) mbali na mahitaji halisi ya wakulima wadogo wadogo.

Ubadilishaji NasabaWASAMBAA HAdI TAnzAnIA

Vinasaba

Athari za matumizi ya teknolojia ya ubadilishaji vinasaba kwa wakulima wadogo nchini India ziliibuliwa na gazeti la Uingereza la Daily Mail likieleza kuwa: “Shankara, kama ilivyo kwa mamilioni ya wakulima wengine India, alikuwa ameahidiwa kuwa atapata mavuno mengi na mapato mengi kupita alivyowahi kutarajia iwapo angehama kutoka kwenye matumizi ya mbegu za asili kwenda kwenye mbele zilizoboresha kijenetikia. Kwa kushawishiwa na ahadi hizo za utajiri mkubwa, alikopa pesa ili kununulia mbegu zilizobadilishwa vinasaba. Lakini mazao yalipokwama kuota kama alivyotarajia alibaki na mzigo mkubwa wa madeni – akiwa hana kipato. Shankara alijinyonga na kuwa mmoja wa wakulima wa Kihindi wapatao 125,000 waliojinyonga kutokana na athari za hatua ya kuitumia India kama eneo la majaribio ya matumizi ya viinitete.” Wakulima na wafanya maamuzi wa Kitanzania wanapaswa kuelewa kwa undani athari mbaya zinazoweza kutokana na matumizi ya teknolojia hii na haja ya kuhakikisha kwamba maoni ya asasi za kiraia yanazingatiwa wakati wa kutengenezwa kwa sheria ya usalama wa kibaiotiki. Ni jambo lililo bayana kwamba makampuni makubwa ya kibiashara za kilimo yanatoa mapendekezo yasiyo halisi kuhusu suluhisho la matatizo ya uhaba wa chakula na umaskini barani Afrika. Lakini ni wazi kwamba matatizo ya wakulima wa Kitanzania yana sura nyingi sana ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa ardhi, maji, mikopo na uwekezaji, teknolojia zilizojaribiwa na kuthibitishwa, zana za kilimo, mafunzo, masoko, barabara, nishati na huduma. Badala tu ya kushawishiwa kwa ahadi za mbegu za miujiza zenye teknolojia ya juu, masuala hayo hapo juu yanayowakabili wakulima ndiyo yanapaswa kuwa kiini cha jitihada na matumizi ya rasilimali.

Na: Michael Farrelly , Afisa MipangoTanzania Organic Agriculture

Movement

Page 11: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

11UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Wakati watu wengine wanachukulia muhogo kama zao la sehemu

zilizokumbwa na ukame, watu wa Nigeria muhogo kwao ni “mgodi wa dhahabu nyeupe ya Nigeria.”

UZALISHAJI WA MUHOGO 2002

ENEO Tani za Ujazo

Uzalishaji Duniani 186.5

Uzalishaji Afrika 99.1

Uzalishaji Asia 51.5

Uzalishaji Amerika Kusini 33.2

Uzalishaji Tanzania 5.1

Msaidizi Maalum wa zamani wa Rais Olusegun Obasanjo kuhusu masuala ya usalama wa chakula anasema mchanganyiko wa kiikolojia pamoja na ubora wa ardhi na tabia nchi ndizo huifanya Nigeria kuwa na uwezo zaidi wa kuzalisha mazao mengi mchanganyiko ikiwa ni pamoja na mhogo, mchele, mtama, ulezi, viazi vikuu, soya, karanga, viazi vitamu na maembe. Bi. Oluwatoyin Adetunji ambaye ndiye mshauri maalum wa sasa wa Waziri ya Kilimo Nigeria kuhusu sera alisema Jijini Dar es Salaam kuwa

Ukweli kuhusu MHOgO

ukweli

Nigeria inauchukulia mhogo kuwa ni zao muhimu la biashara na “uhakika wa chakula Afrika.” Takwimu zilizopo zinaonesha kwamba asilimia 50 ya mhogo unaozalishwa duniani kote huzalishwa katika nchi tano ambazo ni Nigeria, Thailand, Brazil, Indonesia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Nigeria huzalisha asilimia 19 ya mhogo yote inayozalishwa duniani. Matumizi ya mhogo pia ni mengi sana. Yanaanzia kwenye chakula hadi mali ghafi za viwandani. Asilimia 52 ya watu wanaoishi Nigeria wanaishi vijijini na wanategemea sana mhogo katika maisha yao. Wakati kwa Tanzania kilimo kinachangia asilimia 25 tu ya pato la taifa na huajiri takribani asilimia 80 ya nguvu kazi, sekta hiyo hiyo huko Nigeria huchangia asilimia 40 ya pato la taifa na hutoa zaidi ya asilimia 60 ya ajira. Kutokana na mchango huu wa kiuchumi na kijamii wa mhogo kwa watu wa Nigeria, Rais wa Nigeria kwa wakati huo, Obasanjo, mwaka 2002 aliitisha mkutano mkubwa wa kutengeneza mkakati ambao ungeliwezesha taifa kupata fedha za kigeni kutokana na mauzo ya nje na matumizi ya ndani ya mazao ya mhogo. Lengo kuu la jitihada hii

“matumizi ya mhogo ni mengi sana. Yanayoanzia kwenye chakula hadi kwenye mali ghafi za viwandani.”

ya Rais kuhusu Kuongeza Uzalishaji, Uboreshaji na Uuzaji nje wa Mhogo (PIC) lilikuwa “kutathimini umuhimu mpana wa mhogo kama mojawapo ya zana za kupanulia uchumi wa taifa,”alieleza Bi. Adetunji. Akiongea katika Wiki ya Mhogo Dar es Salaam, Bi. Adetunji alisema utekelezaji wa PIC katika kuongeza manufaa ya uzalishaji wa mhogo, uongezaji ubora, masoko na matumizi yake ulijengwa katika tathmini ya fursa, vikwazo, uwezo na udhaifu uliokuwepo katika sekta ya mhogo nchini Nigeria. Tathmini hiyo ilionesha kuwa uzalishaji wa mhogo ulikuwa na ushindani kibiashara kwa sababu kulikuwa na ardhi kubwa ambayo ingeweza kulimwa na kulikuwa na masoko yaliyo tayari. Baadhi ya changamoto zilizobainishwa zilikuwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya ujasiriamali, uhaba wa msaada wa kitaalam na uchache au kukosekana kwa usimamizi mzuri kwenye mnyororo wa uzalishaji na utumiaji wa zao hilo. Changamoto hizi haziikabili Nigeria tu. Nchi kama Tanzania inaweza pia kujinufaisha na faida hizi za mhogo, lakini jambo hili halijafanyika bado. Dhana inayochangia katika kukwamisha utumiaji mkubwa wa mhogo ni mtazamo kwamba zao hilo ni kwa ajili ya “maeneo yenye hali ya jangwa” na kwamba huzalishwa kama zao la ziada tu pale nafaka zinapokuwa hazikustawi. Uzoefu tunaoupata Nigeria unatuonesha kwamba utashi wa kisiasa unatakiwa sana katika jitihada yoyote ya kutumia mhogo kwa faida.

Ukweli kuhusu Muhogo Na Mbarwa Kivuyo

Page 12: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

12 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Mhogo ulikuwa hauchukuliwi kama chanzo cha mapato katika familia na kama zao

lenye mchango kwa pato la taifa. Shirika liitwalo IITA lililenga kuchochea fikra za watu na kuwaonesha kuwa mhogo ni zao lenye uwezo mkubwa kama yalivyo mazao mengine ya biashara. Wiki ya kwanza kabisa ya mhogo nchini Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam kutoka Septemba 12 hadi 16, 2011. Kutokana na mafanikio ya maadhimisho hayo, wadau wamekubaliana kwa pamoja kuyafanya maadhimisho hayo kuwa ni tukio la kila mwaka. Lengo kuu ni kujenga uelewa kuhusu faida nyingi za mhogo ambazo hazijatambuliwa na kutumiwa. Mhogo huchangia katika usalama wa chakula, hutengeneza ajira, huongeza kipato na kuboresha maisha ya wakulima wadogo wadogo vijijini. Kadhalika mhogo huokoa pesa nyingi za kigeni kwa kupunguza uagizaji wa mali ghafi za viwandani kutoka nje.

Kwa muda mrefu sana, mhogo haukuchukuliwa na Watanzania wengi kama zao muhimu ambalo linaweza kuwanufaisha watu wengi maskini.

Wiki ya muhogoTAnzAnIA

muhogo huChangia kaTika usala wa Chakula, huTengeneza ajira,

huongeza kiPaTo na kuBoresha

maisha...

uzalishaji

UZALISHAJINa: Alawiya Mohammed

 

Kauli mbiu ya Wiki ya Mhogo ya mwaka isemayo “Chakula na Kipato kwa Wote” ililenga katika kuuelimisha umma kwamba mhogo sio zao la chakula tu bali pia ni zao la biashara. Uzinduzi rasmi wa Wiki ya Mhogo ulihudhuriwa na wakulima kutoka nchi nzima, asasi za kiraia, wawakilishi wa balozi mbalimbali, sekta binafsi na idara za serikali. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Prof. Jumanne Maghembe.

Maelezo kuhusu Muhogo:1. Ni zao la pili kwa umuhimu nchini

Tanzania ambalo linachangia katika kipato na chakula kwa zaidi ya watu milioni 10. Ni zao linalobebeka kwa urahisi na lenye kutegemewa ambalo hutoa mazao mazuri hata wakati wa hali mbaya ya hewa kama ukame au kwenye ardhi isiyo na rutuba.

2. Ni chanzo cha mali ghafi yenye ubora wa hali ya juu kama unga, wanga na makopa ya mhogo ambayo hutumika katika kutengeneza vifaa vya kufungashia vyakula, madawa, utengenezaji wa vyakula na malighafi katika viwanda vya vyakula vya mifugo.

3. Kwa viwanda vya utengenezaji wa vyakula pekee, Tanzania inaweza ikaokoa takribani dolla za Kimarekani milioni 20 zinazotumika kuagiza malighafi kutoka nje iwapo itatumia mhogo unaozalishwa nchini.

4. IITA na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika wametengeneza mbegu mpya za mhogo ambazo zina uwezo wa kuvumilia magonjwa mengi na uwezo wa kuzalisha hadi tani 35 kwa hekta. Mbinu mbali mbali za kibunifu za kuongeza ubora kwenye mhogo zinaendelea kutumiwa katika maeneo mengi Tanzania.

5. Serikali ya Tanzania kwa sasa iko makini katika zao hili na mwaka 2011 ilizindua Jukwaa la Kitaifa la Uratibu wa Mhogo.

 

Page 13: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

13UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) kwa miaka

mingi umekuwa ukifanya kazi ya kuwaunganisha wakulima kote nchini. Miongoni mwa wanachama wa MVIWATA walioshiriki Wiki ya Mhogo mwaka 2011 ni kundi la Jitegemee B kutoka Mtwara, Kundi la Wambato kutoka Muheza, Kundi la Juhudi kutoka Korogwe na Kundi la Mwavuli kutoka Masasi. Makundi haya huuza bidhaa zao duniani kote kutokana na mahitaji ya walaji wanazopata sokoni au kupitia mtandao. Hutekeleza mnyororo wa thamani tangu uzalishaji, uongezaji wa thamani ya bidhaa na utumiaji. Pamoja na msaada wanaoupata kutoka sehemu mbalimbali, kuna changamoto ambazo bado zinawakabili katika kujaribu kuutumia uwezo wao kikamilifu katika mnyororo wa thamani za mazao yao. Wakati wa Kusanyiko la Wiki ya Mhogo, walibainisha kuwa baadhi ya changamoto zinazowakabili ni uchache wa mashine za kuongezea ubora, vifaa duni vya kufungashia, mvua nyingi ambazo huweza kuathiri wingi wa mazao, miundombinu mibovu ya usafirishaji na magonjwa ya mazao. Picha zinaonesha baadhi ya shughuli ambazo hufanywa na wakulima.

Na: Alawiya Mohammed

Wakulima hawawezi kufikia malengo yao kama hakuna chombo kinachowaunganisha katika kuutumia uwezo walio nao.

Nafasi ya mViWaTa katika kuendelezaMnyORORO WA THAMAnI KATIKA KILIMO

Maendeleo

 

 

 

 

kikundi cha sululu Bungu Rufiji kikundi hiki huzalisha kiasi cha kilo 800-1000 za muhogo kwa siku ambazo ni sawa na kilo 200 - 300 za unga wa muhogo kwa siku

Juma Mtete ni mkulima hodari aliyezaliwa na kukulia katika kijiji cha Bungu, mwanzoni alifanya kazi kama mwajiriwa katika kikundi cha sululu, baadae aliona umuhimu wa kuanzisha kikundi chake cha uwakala kama sehemu ya kujiongezea kipato zaidi

Page 14: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

14 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

uzoefu

Imekuwa ni tabia au utani wa muda mrefu kwa watu wa bara (nchini Tanzania) kuwachukulia

watu wa maeneo ya pwani kama watu wavivu, watu wasiotaka kufanya kazi, wanaopendelea kucheza mdundiko na bao. Baadhi ya watu huwaita mamwinyi. Msemo huu unaweza kuwa na ukweli katika baadhi ya maeneo kama ilivyo kwenye maeneo mengine ya bara pia. Baadhi ni wachapakazi na baadhi sio. Watu husema hivi kutokana na kwamba eneo hili lilikaliwa na Waarabu wakati wa ukoloni. Waarabu hawa walikuwa matajiri ambao walikuwa hawajishughulishi na shughuli nyingine ngumu zaidi ya shughuli za uwekezaji. Hali hii inaweza ikasaidia kuelezea kihistoria kwa nini watu wengi wa maeneo ya pwani hawataki kujishughulisha na shughuli ngumu

Hapa chini ni uzoefu kutoka VECo afrika mashariki ,mradi wa Tanzania uliowasilishwa katika simulizi tatu za uendelezaji wa mhogo, alizeti na kuku huko mkuranga, Chunya na Same.

Uzoefu wa VECo katika kuendeleza mnyororo waTHAMAnI KATIKA KILIMO nCHInI TAnzAnIA

SIMULIZI yA 1: NANI ALISEMA WATU WA pWANI HAWAfANyI kAZI kWA bIdII?

na badala yake wanapenda shughuli nyepesi ambazo mtu anaweza kuzifanya bila usumbufu. Wakati VECO Tanzania ilipoanza kutekeleza yake ya miaka sita wilayani Mkuranga, ni kweli kwamba mtazamo wa watu kuhusu kazi ulikuwa umejawa na uzembe. Ilikuwa ni vigumu kwa wakulima kujishughulisha na kilimo cha mhogo cha kibiashara. Walizoea kusema kilimo ni kigumu na ni shughuli isiyowezekana katika maeneo yao kwa sababu walikuwa maskini – hawana mtaji wa kuweza kuwekeza katika kilimo cha kibiashara. Hata hivyo, VECO Tanzania ilipozindua programu yake, hali ilianza kubadilika kidogo kidogo. Kwa kutumia mpango wake wa Uendelezaji wa Mnyororo wa Kilimo Endelevu (SACD), shirika hili la

Kibelgiji lenye lengo la kuboresha hali za maisha ya familia za wakulima walio katika vikundi, lilianza kwa kutengeneza jukwaa la wadau mbalimbali kwa ajili ya kujadiliana masuala anuai yahusianayo na zao la mhogo. Wadau walitathmini matokeo ya utafiti kuhusiana na mnyororo wa zao la mhogo. Fursa na vikwazo vilipimwa na wahusika muhimu katika mnyororo mzima walijadiliwa kwa madhumuni ya kutaka kutumia vizuri fursa ambazo tayari zipo katika mnyororo wa zao la mhogo. Matokeo yake ilikuwa kutengenezwa kwa mbinu mbadala za kukabiliana na changamoto zilizobainika. Mbinu zilikuwa ni pamoja na kuwapa mafunzo wakulima juu ya hatua sahihi za kilimo cha mhogo kibiashara zinazopaswa kuchukuliwa ili kuongeza uzalishaji katika kila eneo. Maudhui ya mafunzo hayo yalikuwa mengi na yaligusia maeneo anuai tangu uandaaji wa shamba, upandaji, uchaguaji wa mbegu, kulima kwa kina sana, upaliliaji na uvunaji. Kisha yalifanyika mafunzo kuhusu usindikaji wa unga wa mhogo, uandaaji wa bidhaa mbalimbali za mhogo kama vitafunwa, ujasiriamali na ziara kadhaa za mafunzo kwenda kuwaona wakulima wengine waliokwisha kufanikiwa. Watu wazima hujifunza vizuri zaidi kwa vitendo. Kujifunza kwa vitendo kuliwasaidia watu kuelewa na kufurahia kile walichokuwa wanafundishwa kwa nadharia. Vile vile miradi hii iliwahamasisha wakulima kuwekeza kwenye vifaa vya usindikaji kama sehemu ya kuwajengea uwezo. Kivutio kikubwa kwa wakulima kuwekeza kwenye mbinu bora za kilimo na vifaa vya kuongezea ubora ni ongezeko kubwa la faida inayopatikana ukilinganisha na ile wanayoipata kwa kuuza mhogo kutoka shambani.

UZOEfU kUTOkA SHIrIkA LA WAkULIMA WA kIbIASHArA kIZApALAKijiji cha Kizapala ni moja ya vijiji ambako VECO Tanzania inatekeleza programu yake ya mhogo ya miaka sita iliyo katika awamu mbili za miaka mitatu-mitatu (tangu 2008 hadi 2013). Kijiji hiki kiko katika kata ya Mkamba wilayani Mkuranga. Kuna vikundi vinne vyenye wanachama 44. Vikundi

Mjumbe wa CFFO Hadija Silonga akikusanya udongo kwa ajili ya ujenzi

Page 15: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

15UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

uzoefu

vinavyoshiriki kwenye mnyororo wa mhogo vilijiunga na kuunda shirika la kijiji liitwalo Commercial Family Farmers Organization (CFFO) mwaka 2009. Shirika hili lilianzishwa baada ya wanavikundi kubaini kuwa vikundi vyao kimoja kimoja visingeweza kukidhi mahitaji ya soko. Jukumu kubwa la CFFO ni kusimamia jitihada za pamoja kama uongezaji ubora, ukusanyaji mazao kwa wingi, utafutaji masoko na utafutaji wa fedha za mtaji. Makundi yanabaki na jukumu la kuhamasisha na kusaidia uzalishaji wa mhogo katika shamba moja moja. Vikundi husaidia kutoa mafunzo ya kilimo kwa njia ya mashamba-darasa na maeneo ya maonesho, kusambaza vifaa vya kupandia na kufuatilia maendeleo ya mashamba

ya wanachama. Ili kufikia lengo la kufanya kazi kwa pamoja, shirika la CFFO lilianza kukusanya pesa kwa ajili ya kujenga kituo cha ukusanyaji, usindikaji na uuziaji. Kila mwanachama alichangia TZS 80,000/= kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ikiwa ni pamoja na ununuaji wa eneo lenye ukubwa wa ekari mbili. Kila mwanachama alishiriki katika ujenzi wa kituo kwa kusomba mchanga, kokoto, kuchota maji, kujenga kuta na kuwasaidia mafundi wakati wa ujenzi. Mchango wa kila mwanachama (wa hali na mali) unaweza kuzidi TZS 250,000/=. Wakati wa mojawapo ya mikutano ya uhamasishaji, mmoja wa wanachama wa CFFO aliishukuru VECO kwa kuwaamsha. “Tunaenda kuwaonesha

watu kuwa sio watu wote wa pwani ni wavivu. Wakihamasishwa vizuri na kuoneshwa faida za uwekezaji, wako tayari muda wote kutoa rasilimali zao kwa ajili ya kazi husika.” Jengo lina vyumba vitano ambavyo vitatumika kwa usindikaji, ghala, chumba cha mikutano na ofisi mbili. Baada ya kuona jitihada za wanakikundi katika kujenga kituo hicho, VECO Tanzania iliamua kulisaidia shirika hilo kwa kununua mabati, saruji, madirisha na milango kwa ajili ya kumalizia ujenzi. Ili kusindika mhogo, mtu anatakiwa kuwa na mashine. Shirika la CFFO lilitafuta pesa za kununulia mashine ya kukatia mhogo yenye thamani ya TZS 950,000/= na mashine ya kusaga yenye thamani ya TZS 1,650,000/=. Katika baadhi ya maeneo ambako VECO ilikuwa ikitekeleza programu hii, baadhi ya vikundi vilitarajia VECO itawanunulia vifaa hivyo. Lakini kwa wakulima wa Kizapala, hilo ni “tatizo la utegemezi.” Katibu wa kikundi Bw. Juma Nyamgunda alisema, “baada ya kupewa mafunzo ya ujasiriamali tuligundua kuwa tunachokifanya sasa ni biashara na kama tunataka kujua iwapo tunapata faida au hasara tunahitaji kuzingatia gharama zetu pia. Hii inatusaidia kufahamu gharama halisi za kuandaa bidhaa,” aliongeza. Mweka hazina wa CFFO Bi. Fauzia Ufune lisema “tumeamua kutumia rasilimali zetu wenyewe kwa sababu tunataka kuwa na hisia za umiliki miongoni mwa wanachama.” Alisema kuwa wanachama wanapokuwa hawachangiiwanakuwa hawaichukulii biashara kama ya kwao. “Imekuwa ni tabia kwamba pale uwekezaji unapokuwa umefanyika wote kwa msaada, wanachama wa kikundi wanakuwa hawawajibishi viongozi wao kwa matumizi mabaya ya mali za kikundi.” Shirika la Kizapala CFFO sasa limeanza kuona faida za uwekezaji. Kwa sasa linatengeneza makopa ya mhogo, wanga na unga. Wanachama binafsi kwa sasa wanaweza kutengeneza pia spaghetti, keki, chapati, donati, maandazi na kisamvu. Shughuli hizi zote hufanyika katika kituo cha vikundi hivyo. Mboga za majani kutoka kwenye kikundi hiki huuzwa TZS 2,000/= kwa kilo,

Kituo kikiwa katika hatua ya ujenzi

Baadhi ya wajumbe wa bodi wakiwa mbele ya jengo la kituo cha kuzalisha na kuifadhi mazao yao

Page 16: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

16 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

na kilo moja ya unga wa mhogo huuzwa kwa TZS 800/= hadi 1,000/= kwa unga ambao haujafungashwa. Unapofungashwa kwenye vifungashio bora, unga huuzwa kwa TZS 1,000/= hadi 1,200/= kwa kilo. Kikundi huwa kina oda za bidhaa za mhogo kila wiki kutoka masoko ya Dar es Salaam, Mkuranga mjini na shule za vijiji. VECO ilisaidia utengenezaji wa vifaa vya kufungashia ambavyo baadaye vitakuwa vinanunuliwa na CFFO. Vifaa vya kufungashia vitaisaidia CFFO kuingia katika masoko mengi zaidi kama maduka makubwa ya rejareja (supermarket) katika miji mikubwa. Masimulizi ya mafanikio yao yalivutia wadau wengi zaidi katika mnyororo huo. Shirika la misaada ya kiufundi la Kibelgiji (BTC) liliamua kuchimba kisima ili kusaidia kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji kwa ajili ya shughuli za usindikaji wa mhogo. Kisima hiki kiko katika hatua zake za mwisho za utengenezaji na kitatumiwa na CFFO katika kuongeza ubora wa mhogo. Mabomba mawili mengine yatawekwa ili kutoa maji kwa ajili ya matumizi ya wanakijiji wengine. Hata hivyo, watu watakuwa wanalipia huduma hiyo ya maji na CFFO itazikusanya na kuzitumia pesa hizo kwa ajili ya ukarabati na utunzaji wa kisima hicho. Mwanachama mwingine wa CFFO Bw. Rajabu Nyamgunda alisema: “Tunajivunia kile ambacho tumekifanya kwa sababu tumeanza

kupata mapato na tuna uhakika wa chakula. Tunafahamika na watu wengi sana kwa sababu tunatembelewa na wageni kutoka ndani na nje ya nchi. Watu wengi wanataka kufanya kazi na sisi. Biashara hii imetutengenezea ajira na wakulima wengi kwa sasa wanataka kujiunga na CFFO baada ya kubaini kwamba tuko hatua nyingi sana mbele yao kimafanikio. Pamoja na mafanikio hayo, Nyamgunda anasema shirika lao linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kukaushia makopa ya mhogo. Anasema, “tunategemea sana ukaushaji kwa kutumia jua.” Mafanikio ya jamii ya Kizapala yanakanusha dhana potofu kwamba watu wa pwani ni wavivu. Mafanikio ya jitihada yoyote “yanategemea sana mbinu za uhamasishaji zinazotumiwa na wawezeshaji katika kuelewesha dhana husika na iwapo mkakati husika una manufaa halisi,” anamalizia

Nyamgunda.

SIMULIZI YA 2: MIKAKATI YA PAMOJA YA JAMII KATIKA KUIMARISHA MNYORORO WA THAMANI YA ALIZETI WILAYANI CHUNYAVECO Tanzania imekuwa ikiunga mkono na kusaidia jitihada za pamoja za kuboresha hali ya maisha ya watu maskini, hususan wakulima wadogo wadogo. Jitihada za pamoja zinawawezesha wakulima kuchanganya rasilimali pamoja, kuongeza upatikanaji na huduma za masoko, kupunguza gharama za uendeshaji katika masoko, kuongeza upatikanaji wa taarifa, kuongeza uwezo wa kujadiliana na kupata fursa mpya na kubwa zaidi za kuongeza ubora wa bidhaa na kuongeza ujuzi. Vile vile, jitihada za pamoja huwawezesha wakulima wadogo wadogo kwa kiasi kikubwa sana kuwa na sauti ya kushawishi taasisi

uzoefu

Wajumbe wa kizapala CFFO wakisaidiana na mtaalam kufunga mashine ya kusaga

Bidhaa za muhogo katika kifungashio bora

Page 17: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

17UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

zinazosimamia masoko. Jitihada za pamoja katika uzalishaji, usindikaji na/au uuzaji huwezesha wanakikundi kujikita katika stadi fulani mahsusi, kupata taarifa na maarifa na kutengeneza mikakati ya kuboresha vipato vyao, kudhibiti hatari zinazoweza kujitokeza pamoja na kupunguza gharama. VECO, ambalo ni shirika la Kibelgiji linalofanya kazi na wakulima wadogo vijijini katika Wilaya za Simanjiro, Same, Mkuranga na Chunya, lina dhima kuu ya kusaidia Wanafamilia Wakulima Waliojiunga pamoja (OFFs), wa kike na wa kiume, katika kuboresha hali za maisha yao na kuongeza vipato vyao kupitia Uendelezaji wa Mnyororo wa Kilimo Endelevu (SACD). Programu ya VECO inalenga kufikia dhima hii kwa kuwawezesha wakulima kupitia ushirikiano unaoongeza uwezo wao ili waweze kutoka katika kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kilimo cha kibiashara katika mazao husika. Huko Chunya mkoani Mbeya, programu ya VECO Tanzania inatekeleza mpango wa miaka mitano (Mei 2009 - Mei 2014) wa Usalama Endelevu wa Chakula (Sustainable Food Security Programme (SFSP) ambao unahamasisha uendelezaji wa zao la alizeti. Lengo ni kuboresha hali ya maisha katika kaya wilayani Chunya kwa kuongeza uhakika wa chakula na kipato kupitia ushiriki wa wakulima katika uzalishaji na

mnyororo mzima wa zao la alizeti. Kwa kupitia mpango wake wa SACD, VECO imekuwa ikisaidia uzalishaji na mnyororo wa zao la alizeti katika kata sita kati ya kata 23 za Wilaya ya Chunya. Baadhi ya mikakati ambayo imekuwa ikitumiwa na VECO ili kufikia malengo yake ni pamoja na kuhamasisha Wanafamilia Wakulima Waliojiunga pamoja (OFF) kuunda Mashirika ya Wakulima ya Kibiashara (Commercial Farmers Organizations (CFOs), kuimarisha mashirika haya ili yaweze kutekeleza shughuli zao kwa pamoja na kuyasaidia mashirika kwa mikopo ya zana za kilimo na vifaa vya kuongezea ubora wa mazao kama mashine za kukamua alizeti. Mashirika ya CFO yanawajibika kuhakikisha kwamba wanachama wake wanaleta rasilimali zao pamoja

ili kuwezesha upatikanaji wa mazao mengi yanayoweza kukidhi mahitaji ya soko, kuongeza ubora na kutafuta masoko kwa pamoja. Hadi sasa mashirika haya yameshaonesha umuhimu wa watu kuwa na jitihada za pamoja katika kukusanya rasilimali. Hapa chini ni simulizi ya shirika moja la CFO ambalo limeanzisha jitihada za pamoja za ujenzi wa kiwanda cha alizeti chenye sehemu za kuongezea ubora, ghala, uuziaji na ofisi. Kiwanda hiki ni mali ya CFO.

MFANO WA SHIRIKA LA MATUNDAS CFO KATIKA KUFIKIA LENGO LA KUONGEZA UBORA NA KUPATA MASOKO KWA PAMOJAMatundas ni mojawapo ya programu 19 za VECO katika vijiji vya Wilaya ya Chunya ambako OFF wamehamasishwa kuunda CFO. Mashirika ya CFO yameimarishwa kwa kujengewa uwezo katika maeneo kadhaa ya usimamizi wa mashirika, ujasiriamali na usimamizi wa biashara. Mbinu kubwa ya CFO ni jitihada za pamoja katika kupanga, kutekeleza na kufanya maamuzi katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa shirika. Jukumu kubwa la CFO katika mnyororo mzima wa alizeti ni kuleta rasilimali pamoja. CFO huandaa zana za kilimo, uzalishaji, ukusanyaji, uongezaji wa ubora, kuunganisha wazalishaji na masoko na kuwawezesha kuyafikia. Shughuli hizi zote hufanyika katika ngazi ya shirika.

uzoefu

Uchimbaji wa kisima cha maji safi

Tanki la kuhifadhia maji safi

Page 18: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

18 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Katika jitihada zao za kupata mafanikio ya kiuchumi, CFO ilibaini kuwa hawakuwa na vifaa vya kutosha kuwezesha utekelezaji wa shughuli zao zihusianazo na alizeti. Walipungukiwa vifaa vya usindikaji, vifaa vya kuhifadhia na ofisi. Hivyo CFO iliomba ardhi kutoka serikali ya kijiji kwa ajili ya kujenga jengo ambalo litatumika kuwekea mashine za usindikaji na kuhifadhia mbegu za alizeti za wanachama wakati wakisubiri bei nzuri sokoni. CFO ya Matundas kwa pamoja walijenga kiwanda kidogo cha alizeti.

WANACHAMA WA MATUNDAS CFO WALIWEZAJE KUKUSANYA RASILIMALI ZA KUJENGEA VITUO VYA UONGEZAJI WA UBORA?Shirika la Matundas CFO liliundwa rasmi mwezi Mei 2010 na makundi mawili madogo madogo ya kiuchumi. Kundi la Wanawake la Upendo lenye wanachama 30 na kikundi chenye wanachama mchanganyiko 25 (wanawake 13 na wanaume 12) kiitwacho NUKIA yaliunda CFO moja yenye wanachama 55. Mkutano wa wanachama wote wa kila mwezi hufanyika kwa ajili ya kuweka mipango ya utekelezaji na mikakati ya ukusanyaji wa rasilimali.

Matundas CFO inapata fedha zake kutoka kwenye vyanzo tofauti kama faini, uuzaji wa hisa, ada za uanachama za mwezi na za mwaka. Viwango viko kama ifuatavyo: • Ada ya Uanachama ya mwaka

TZS10,000/= • AdayaMweziTZS2,000/=• Mauzo ya hisa tatu kwa mwaka

zenye thamani ya TZS 30,000/=• NguvukazikwasikuTZS10,000/=• Wachelewaji kwenye vikao TZS

1,000/=• Utoro kwenye vikao kwa kutoa

udhuru TZS 2,000/=• Wachelewaji kwenye kazi TZS

1,000/= • UtorokwenyekaziTZS10,000/=

Vyanzo hivi vya fedha vimeridhiwa na wanachama wote na fedha zinazopatikana zimewekezwa katika ununuaji wa vifaa vya ujenzi kama matofali, mchanga, mawe na mbao ambazo hutumika katika ujenzi wa kiwanda. Kila mwanachama wa Matundas CFO hujitolea kutengeneza

matofali 250. Akinyooshea kidole lundo la matofali, Katibu wa Matundas CFO alisema, “leo tumetengeneza zaidi ya matofali 10,000 na tumeanza kuyapanga kwenye tanuru kwa ajili ya kuchomwa kama unavyoona.”

UKUSANYAJI/UTUNZAJI WA MBEGU ZA ALIZETI HUFANYIKAJE?Uhifadhi hufanyika katika ngazi ya kaya. Hata hivyo, taarifa kutoka kwa viongozi wa CFO ya kijiji cha Matundas zinasema mfumo wa sasa

uzoefu

Wajumbe wa Matundas CFFO wakikusanya matofali kwenye tanuru tayari kwa kuchomwa

Wajumbe wakihesabu na kupanga matofali kwenye tanuru

Wajumbe wa CFFO wakikusanya kuni kutoka katika msitu wa karibu tayari kwa kuchoma tanuru la matofali

Page 19: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

19UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

umekuwa ukiwashawishi wakulima kuuza alizeti zao kwa madalali ambao huwadanganya kuwaongezea faida.

MPANGO WA BAADAYE WA MATUNDAS CFFOMatundas CFFO ilipanga kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha alizeti ifikapo Oktoba 2011. VECO inachangia CFFO hiyo kwa kiwango cha asilimia 70 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa kiwanda hicho. CFFO huchangia asilimia 30 ya gharama. VECO itanunua mtambo wa kukamua alizeti na kuufunga pamoja na umaliziaji mwingine ili kukidhi viwango vya Mamlaka ya Udhibiti wa Vyakula na Dawa (TFDA).

SIMULIZI YA 3: UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KWA AJILI YA UWEZESHAJI WA KIUCHUMI NA KIJAMII KATIKA JAMII ZA VIJIJINI TANZANIA: MFANO WA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI WILAYANI SAME.

utangulizi na historiaUboreshaji na uzalishaji unaolenga mahitaji ya soko vina nafasi kubwa sana ya kuongeza kipato cha wafugaji wadogo wadogo wa kuku katika jamii za vijijini. Hili limethibitishwa na mchango wa utekelezaji wa programu ya VECO wilayani Same. Mwaka 2007 VECO Tanzania ilisaidia mipango ya miaka mitano inayolenga Usalama wa Chakula wilayani Simanjiro na Same yenye lengo la kukifanya kilimo kuwa kazi yenye tija na faida kwa jamii za vijijini. Mipango ilipitiwa upya mwaka 2008 ili iendane na mabadiliko ya mbinu za VECO zinazolenga katika kuongeza uhakika wa chakula kwa familia za wakulima. Mbinu mpya ya mnyororo

endelevu wa masoko (SACD) ilianza kutumiwa na mipango hiyo na hivyo ikabadilishwa jina na kuwa Social and Economic Empowerment Programme for Simanjiro and Same Districts (SEEP for SiSa) ikimaanisha Mipango ya Uwezeshaji wa Kiuchumi na Kijamii kwa Wilaya za Simanjiro na Same. Mbinu hii inaangalia uendelezaji wa zao kwa sura pana; wadau wote wanaohusika moja kwa moja na wale wasiohusika moja kwa moja katika shughuli zilizoko kwenye mnyororo huo ni wanufaika wa shughuli za programu. Mbinu ya awali ya Kilimo endelevu kwa ajili ya uhakika wa chakula ilibainika kuwa finyu sana. Ilikuwa inaangalia maslahi ya familia za wakulima tu na kuacha nje baadhi ya mambo mengine ya msingi bila utatuzi. Mipango ya SEEP for SiSa ilianza kutumia mbinu ya SACD mwezi Julai 2008 na kuendelea. Ili kufikia malengo yake, VECO wilayani Same ilianza kusaidia uendelezaji wa ufugaji wa kuku. Mipango hii ilisaidia makundi ya familia za wakulima wa kata ya Kihurio, Makanya, Maore na Same. Huu ulikuwa ni mpango mkakati wa miaka mitatu kwa ajili ya kusaidia Familia za Wakulima Zilizoungana (OFF) ili kuboresha maisha yao. VECO kwa kushirikiana na mdau wake Halmashauri ya Wilaya ya Same waliwezesha uunganishaji na uimarishaji wa vikundi vya wakulima jambo ambalo lilirahisisha utoaji wa huduma za ughani, mafunzo, mafunzo ya vitendo na kupunguza gharama za uendeshaji. Mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na ufugaji bora wa wanyama, hususan ufugaji na usimamiaji wa kuku, masoko, utunzaji wa kumbukumbu, stadi za usimamizi wa biashara

pamoja na uundaji na uimarishani wa vikundi. Mafunzo hayo yaliwezesha wakulima kuongeza wingi na ubora wa kuku wa kienyeji na kuufanya ufugaji huo kuwa wa kibiashara. Pia yaliboresha stadi zao za ujasiriamali na kuwajengea uwezo katika biashara ya kuku. Ujasiriamali kwa wafugaji wa kuku uligeuka kuwa ni stadi mpya na mtindo wa kimaisha kwao. Wakulima hawakupewa tu mafunzo ya ufugaji na uuzaji wa kuku bali pia walijifunza namna ya kuziendeleza biashara zao zisife. Wakulima wamekuwa wakitumia stadi na ujuzi huu kuboresha hali za maisha ya familia na jamii zao kwa ujumla na pia wanaendelea kuwekeza katika kupanua biashara zao. Ufugaji wa kuku kwa sasa ni kazi inayosukumwa na soko. Wajasiriamali wanajikita zaidi katika kukidhi mahitaji ya wateja yanayobadilika kila leo. Vifaranga wenye umri wa siku moja hadi miezi miwili wanahitajika zaidi kuliko mayai. Kutokana na uhitaji huu mkubwa wa vifaranga, wakulima wadogo wadogo kwa sasa wanawekeza zaidi kwenye utotoaji wa vifaranga, biashara ambayo ndiyo inaonekana kuwa na faida zaidi. Matokeo makuu ya muda mrefu ya kusaidia vikundi vya familia za wakulima katika kuendesha shughuli husika, zaidi tu ya manufaa ya kiuchumi, ni kwamba sehemu kubwa ya jamii inaondolewa kutoka kwenye umaskini uliokithiri. Baadhi ya shuhuda za mafanikio zinahusisha mradi wa ufugaji wa kuku ambao umebadilisha maisha ya watu. Shuhuda hizi tatu hapa chini zinaonesha mabadiliko hayo.

uzoefu

Mjumbe wa Matundas CFFO, Mr. Limber Andrea akiwa katika stoo yake ya kuhifadhia alizeti wakati akisubiri kupata bei nzuri katika soko

Page 20: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

20 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

kisa Mkasa: 1

Danstan Kihedu ni mkulima anayeishi na mkewe na watoto wao watatu katika kijiji cha Mpirani, Kata ya Maore Wilayani Same.

Amekuwa akifuga kuku kama shughuli ya kawaida anayoipendelea tu tangu mwaka 1998. Kama alivyosema: “Nilikuwa nafuga kuku ili ikitokea nahitaji mayai au nyama kwa ajili ya familia nipate. Sikuwahi kufuga zaidi ya kuku watano kwa wakati mmoja. Sikuwahi kufikiri kwamba kuku wa kienyeji wanaweza kuwa na manufaa ya kiuchumi katika maisha yangu. Ghafla, mradi wa kuku ulibadilisha maisha kabisa. Shukrani nyingi ziende kwenye mradi.” Bw. Kihedu alijiunga na kikundi cha Muungano mapema mwaka 2008. Kwa kupitia kikundi na kwa msaada wa mradi wa VECO katika kata ya Maore, alibadilisha ufugaji wake kutoka ufugaji wa kujikimu hadi ufugaji wa kibiashara. Hii ilikuwa baada ya kupewa mafunzo ya kiufundi kuhusu ufugaji wa kuku kibiashara kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Same. Anasema kuwa ufugaji wa kibiashara umepanua uelewa na ujuzi wake. Kipato cha Kihedu kiliongezeka na sasa amekuwa muelimishaji rika. Mwishowe aligeuka na kuwa msambazaji wa vifaranga katika kijiji chake na katika vijiji vingine vya jirani nje ya Kata ya Maore. Soko kuu la vifaranga wake ni Same,

Hedaru na Makanya. Anaweza akauza

vifaranga wapatao 400 kwa mkupuo mmoja. Huwapatia chanjo vifaranga wake kabla hajawauza na wateja wake wamekuwa na imani kubwa sana kwake. “Pia huwa ninawapatia ushauri juu ya namna ya kuwatunza,” aliongeza. Biashara hii imebadilisha maisha yake. Amejenga nyumba mbili na sasa anaweza kulipa ada ya watoto wake. Kihedu anasema: “Kuku ni mali.”

kisa Mkasa:2

Bw. Shogholo ni mkulima anayeishi na familia yake katika Kata ya Same Wilayani Same. Alianza kufuga kuku mwishoni mwa mwaka 2008 baada

ya kujiunga na kikundi cha Umoja. Alijiunga baada ya kuona baadhi ya wana kikundi wananufaika na mafunzo pamoja na huduma nyingine zilizokuwa zinatolewa chini ya programu ya VECO kwa vikundi. Mwanzoni hakuwa mfugaji wa kuku kwa hiyo alikuwa mgeni kabisa kwenye ufugaji. Baada ya kuhudhuria mafunzo na kufanya ziara kadhaa za kujifunza alianza kufuga kuku kama 10 hivi. Taratibu, mradi ulianza kupanuka kutokana na kuongezeka kwa vifaranga waliokuwa wanatotolewa ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa usimamizi na matunzo. Kwa sasa anamiliki kama kuku 300 kwa wakati mmoja. Anauza mayai, kuku na vifaranga. Anaweza akapata hadi kufikia TZS 350,000/= kwa mwezi kutokana na biashara hiyo. Kutokana na kipato hicho anaweza kukidhi mahitaji ya familia yake kama chakula na ada za wanafunzi. Pia amejenga nyumba kwa ajili ya familia yake. Anapanga kuipanua biashara yake kwa kuongeza aina za kuku – tangu vifaranga wa siku moja hadi kuku wakubwa wa mayai. Kati ya manufaa makubwa aliyoyapata kutokana na mradi huo ambayo hatayasahau ni mafunzo ya ufundi stadi kuhusu ufugaji wa kuku kibiashara. Anasema kutokana na mafunzo hayo na uzoefu, amepata maarifa na ujuzi ambavyo anaamini ni vya thamani zaidi kuliko pesa. Anamaliza kwa kuelezea kuwa “Ufahamu na ujuzi alioupata ndio mbegu za mafanikio ya kiuchumi na kijamii.”

uzoefu

Page 21: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

21UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

kisa Mkasa:3

Bi. Magreth S. Mashambo ni mkulima anayeishi Same na watoto wake watano,

wasichana wawili na wavulana watatu. Alianza kufuga kuku baada ya kuhamasishwa na mradi mwaka 2008. Mwanzoni, alikuwa akifuga kuku kama chanzo cha mayai na nyama kwa ajili ya familia yake. Baadaye, ufugaji huu wa kuku wa kienyeji kibiashara ndio uligeuka na kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa mama huyu mjane. “Tunaishi kwa kuitegemea hii kazi. Watoto wanapata mahitaji yao yote ya shule kutokana na kazi hii. Biashara hii imeniajiri.” Bi. Mashambo ni mmoja wa wanachama waanzilishi wa kikundi cha OFF kiitwacho Muungano. Kikundi hiki kilianzishwa mwaka 2008 kwa msaada wa Halmshauri ya Wilaya ya Same na mradi wa VECO. Kikundi kina wanachama 30, wanawake 25 na wanaume watano. Kupitia mafunzo mbalimbali ya kiufundi kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara, Bi. Mashambo aliweza kuanzisha mradi wake wa ufugaji wa kuku. Alianza na kuku wapatao 50. Mradi wa SEEP for SiSa ulimsaidia kupata mabanda mazuri ya kuku ambapo yeye alichangia matofali, maji na wafanyakazi na VECO ikachangia saruji, mabati na mbao za kujengea. Ujenzi wa banda hilo uliwezesha kupanuka kwa uzalishaji. Aliweza kuongeza wingi wa kuku wake kufikia 150 wakiwemo majogoo.

Jogoo hufugwa kwa miezi matatu hadi mine kabla ya kuuzwa kwa TZS 8,000/= kila mmoja. Anaweza kufuga hadi jogoo 15 kwa wakati mmoja. Kwa kupitia mikopo midogo midogo kutoka kwenye Benki Jamii ya Kijiji (Village Community Bank) aliweza kuiendesha biashara yake vizuri. Vile vile aliweka mtambo mdogo wa kutotolea vifaranga wenye uwezo wa kutotolesha vifaranga 50 kila mwezi. “Ninauza mayai pia. Ninaweza kupata hadi trei nne za mayai kwa mwezi. Kila trei inauzwa kwa TZS 7,500/= hivyo ninapata TZS 30,000/= kutokana na mayai, wakati vifaranga, hususan wenye siku moja wanauzwa kwa TZS 1000/= kila mmoja. Huwa ninapata kiwango cha chini cha TZS 50,000/= kwa kuuza vifaranga.” Anasema kwa wastani anaweza kupata hadi TZS 150,000/= kwa mwezi. Watoto wake wawili wako sekondari – mvulana na msichana. Mvulana yuko kidato cha tatu wakati msichana yuko kidato cha kwanza. “Biashara hii imenisaidia sana kwa kuwa mume wangu aliniacha na watoto. Watoto wananitegemea mimi kwa kila kitu.” Mume wa Bi. Mashambo alienda Morogoro kutafuta kazi mwaka 2007 na hakurudi tena. Pamoja na hali hiyo katika ndoa yake, Bi. Mashambo aliweza kuwapeleka watoto wake shule ya sekondari. Pia ameikarabati nyumba yao.

uzoefu

Page 22: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

22 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Msemo usio rasmi wa Miaka Kumi ya Kimataifa ya Wanawake (1976-1985)

ulikuwa “wanawake hufanya theluthi mbili ya kazi duniani, hupata asilimia 10 ya kipato cha dunia na humiliki asilimia moja ya nyenzo za uzalishaji.” Miaka 25 baadaye, wakati Umoja wa Afrika ukizindua Muongo wa Wanawake wa Afrika (2010- 2020), nchini Tanzania hali inaonekana kuwa imebadilika kwa kiwango kidogo sana. Mwendo kama wa masaa mawili kwa gari kusini mwa Mbeya, kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa ndipo lilipo eneo maarufu la Kyela. Kyela

Jinsia

Kisa mkasa cha jinsia na Zao la Kakao Kyela

Kuimarisha Usawa waKIJInSIA KATIKA KILIMO

 

inafahamika kwa mchele wake wenye ubora wa hali ya juu na kilimo hai cha kakao. Karibu robo tatu ya wakulima 120,000 wa Kyela huzalisha kakao, zao ambalo kwa mara ya kwanza lililetwa na Rais wa Ghana Kwame Nkrumah kama kumbukumbu ya urafiki wake na Mwalimu Julius Nyerere. Taasisi ya Kilimo-Hai Tanzania (Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM) iliombwa na mshirika wake HIVOS kuandaa kisa mkasa kuhusu athari ya utoaji hati ya ubora kwenye mahusiano ya kijinsia huko Kyela ikiwa ni sehemu ya Mpango wa Kimataifa wa Masuala ya Jinsia na

Viwango (International Gender and Global Standards Initiative). Mkakati huu unalenga kuhakikisha kwamba wanawake na wanaume wanapata mafao sawa kulingana na mchango wao katika uzalishaji, uvunaji na usindikaji wa mazao. “Wanawake hufanya kazi zaidi ya wanaume lakini hulipwa kidogo zaidi ya wanaume.” Utafiti huo ulibaini kuwa wanawake wa Kyela hufanya kazi masaa matatu zaidi ya wanaume. Pamoja na kufanya kazi shambani, pia huwa wanatakiwa kufanya usafi, kupika na kulea watoto. Kwa bahati mbaya, wanaume ndio huuza kakao na

Page 23: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

23UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Jinsia

ndio huwa na sauti ya mwisho kuhusu matumizi ya fedha zinazopatikana. Kwa bahati nzuri, kwa kuwa zao la kakao kwa njia ya kilimo hai limepata hati ya ubora, mapato ya wakulima yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka wastani wa TZS 300/= kwa kilo hadi TZS 2,800/= kwa kilo jambo ambalo limewanufaisha wanawake na wanaume kwa pamoja katika jamii nzima. Kwa sasa familia zina nyumba za matofali zilizoezekwa kwa mabati na hupata huduma nzuri za elimu na afya. Baadhi zina luninga zenye kutumia setilaiti na hutumia umeme wa jua. Mwanaume mmoja mkulima wa kakao aliiambia timu ya watafiti: “Pesa zilikuwa kidogo sana hivyo nilikuwa sioni sababu ya kumuonesha mke wangu au kumueleza namna zilivyotumika. Nilitumia kile kiasi kidogo nilichokipata kwa kunywea pombe. Lakini siku hizi huwa tunajadili na tunaamua kwa pamoja namna ya kutumia mapato yetu kama familia.” Matatizo huanza pale wanaume wanapokuwa hawawapi sehemu ya pesa wake zao au wanapokuwa hawawashirikishi katika kufanya maamuzi. Mwanamke mmoja alisema “Wanawake huvuna na kuuza kakao mbichi na ambayo haijasindikwa kwa madalali (mjemuka) ili kupata pesa za kuendeshea familia zao. Huuza kwa madalali kwa bei ya chini kwa sababu wakiuza kwa makampuni yaliyosajiliwa waume zao wanaweza kubaini.” Migogoro ya kifamilia inayotokana na mapato ya kakao huweza kuibua ugomvi wa kijinsia. Wakati mwingine mwanamke akimuuliza mumewe taarifa kuhusu mapato yaliyotokana na mauzo ya kakao huweza kutishiwa au hata kupigwa iwapo ataendelea kufuatilia. Pale wanawake wanapohusishwa sio tu katika uzalishaji bali pia katika mafunzo na katika kufanya maamuzi, ubora na kiwango cha uzalishaji huongezeka. Mchakato wa utoaji hati ya ubora umeongeza majukumu kwa kiasi fulani lakini wanawake wanasema mafao yaliyoongezeka kwa familia ni makubwa mno na yanastahili kwa jitihada za ziada wanazotakiwa kuziongeza.

WANAWAKE WANAMILIKI ARDHI NA NYUMBA CHACHE SANAUtoaji hati haujawa na athari katika usawa wa kijinsia kwenye umiliki wa ardhi. Mara chache sana wanawake

humiliki ardhi kwa sababu ardhi hurithishwa kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto wa kiume. Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa mapato, siku hizi wanawake wengi zaidi huko Kyela wanaonekana wakiendesha baiskeli na wakitumia simu za mkononi.

UTOAJI HATI UNAWEZA KUWASAIDIA WANAWAKETimu ya watafiti ilibaini kuwa aina tofauti tofauti za utoaji hati ya ubora huwa na athari tofauti kwenye mahusiano ya kijinsia. Japokuwa kulikuwa na athari kidogo sana iliyotokana na utoaji hati ya ubora kwa kilimo hai, timu hiyo ilibaini kuwepo kwa athari fulani iliyotokana na utoaji hati za “biashara ya haki.” Kama meneja mmoja wa mauzo ya kakao alivyosema: “Tunalazimishwa na viwango kufanya hivyo.” Kampuni yake inachukua hatua nyingi katika kushughulikia usawa wa kijinsia, kwa kuwaajiri wanawake wengi zaidi na kuhakikisha kuwa wanawake wakulima–-kama ilivyo kwa wanaume wakulima--wanapewa mafunzo pia. Uzoefu huo umemfundisha mambo mbalimbali, kama alivyoelezea, “Wanawake hawadhani kama wanaweza lakini ni wafanyakazi wazuri, wako makini. Waajiri wengine huweza kudhani hawawezi kutegemewa.” Ni jambo zuri kuhakikisha kuwa wanawake wanahusishwa ipasavyo. Wako makini, wanawajibika na wepesi wa kujifunza, wanawake huwa na hamasa kubwa ya kufanya

kazi kwa manufaa ya familia zao. Ukiweza kutumia hiyo hamasa utaweza kuongeza sana tija, ubora na kipato. Mkulima mmoja mwanamke alieleza kuwa “uelewa zaidi unatakiwa kujengwa miongoni mwa watu ili kutambua kwamba wanawake na wanaume wanachangia katika kuzalisha kakao na hivyo suala la nafasi sawa katika umiliki na sauti katika matumizi ya fedha zinazopatikana ni la muhimu.” Akizindua Muongo wa Wanawake wa Afrika, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mzaliwa wa Songea, Asha-Rose Migiro alisema, “Suala la kuwawezesha wanawake ni la lazima kimaadili, ni suala la haki za msingi za binadamu. Vile vile ni sera sahihi. Kuwekeza kwa wanawake na wasichana ni mojawapo ya uwekezaji mkubwa sana tunaoweza kuufanya. Ni lazima tuhakikishe kwamba wanawake wa vijijini wanaweza wakapata msaada wa kisheria, kifedha na kiteknolojia wanaouhitaji ili kuhama kutoka kwenye kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye kilimo cha kibiashara. Tukubali katika fikra zetu na katika sheria zetu kwamba wanawake ni wabia wenye haki sawa na walio sawa – kulindwa, kuheshimiwa na kusikilizwa.”

(Mpango wa Gender and Global Standards Initiative unatekelezwa na mashirika manne ya Uholanzi: Hivos, Oxfam Novib, Solidaridad na The Royal Tropical Institute.)

Page 24: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

24 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Kiwango cha watu wanaoishi maeneo ya vijijini kinafikia robo tatu ya wakazi wake

wote. Sehemu kubwa ya watu maskini huishi katika maeneo haya, mbali kabisa na miji na majiji. Wengi huendesha maisha yao kwa kulima katika mashamba madogo madogo. Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, wanawake wa vijijini barani Afrika wanafikia asilimia 33 ya nguvu kazi yote na huchangia asilimia 70 ya nguvu kazi katika kilimo. Kwa baadhi ya kazi kama shughuli za awali za uongezaji ubora kwenye vyakula, uchotaji maji na utafutaji kuni, kulima kwa jembe la mkono na upaliliaji, wanawake hufanya karibu asilimia 100 ya kazi. Hata hivyo, mara nyingi huwa wanapata sehemu ndogo sana ya mapato yatokanayo na kazi zao. Wanawake hawa wa vijijini barani Afrika sio wazalishaji tu wa chakula, bali pia ni sehemu muhimu ya jamii zao, ni mama wazazi na walezi wa familia – malezi ambayo huenda mbali zaidi na kuwagusa watu wengine katika jamii zao. Majukumu haya tofauti na mengi ya wanawake husaidia sana maisha ya mamilioni ya watu barani Afrika na nje ya hapo. Lakini wanawake hawa mara nyingi sana huishi na kuendesha maisha yao kwa kutumia vipato vidogo sana. Haya ni matokeo ya ongezeko la umaskini na mwelekeo usio sahihi wa serikali na wafadhili.

KUSHEREHEKEA SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKEShirika la Concern Worldwide Tanzania, mnamo tarehe 15 Oktoba 2011 liliadhimisha maisha ya wanawake wa vijijini Tanzania, mashujaa hawa wasiovuma wa maisha ya Tanzania. Wao ndio chanzo kikubwa cha uwepo wa shirika hilo na matarajio yake ya mustakabali wa taifa. Maadhimisho hayo yalifanyika Wilayani Kibondo. Nchini Tanzania ambapo kuna watu milioni 42, asilimia 74 (milioni 31) wanaishi maeneo ya vijijini. Wanawake ni zaidi kidogo ya nusu ya idadi hiyo, jambo ambalo linajenga sababu nzuri zaidi na ya msingi ya kuelekeza jitihada za kimaendeleo katika usawa wa kijinsia. Hili ni suala la msingi sana hususan kwa kuzingatia kuwa wanawake ndio walezi wakubwa wa watoto (chini ya

Kutambuliwa

KuwaadhimishaSIKu yA KIMATAIFA yA WAnAWAKE WA VIJIJInIZaidi ya nusu ya watu wote duniani huishi katika maeneo ya vijijini na katika nchi maskini.

Kutoka kushoto Janet Wivaha, 56; Edita Enock, 40; na Renatha Kahwili, 46

Page 25: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

25UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Kutambuliwa

miaka 18) ambao ni zaidi ya asilimia 50 (milioni 22) ya raia wote Tanzania.Wanawake wa vijijini bado wanakabiliwa na changamoto na vikwazo vingi katika kupata elimu na mafanikio kwa ujumla, katika kushiriki kwenye ufanyaji wa maamuzi yanayoathiri maisha yao, na katika kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya familia zao hapa Tanzania. Wanakabiliwa na changamoto ya kubaguliwa waziwazi na kwa siri pamoja na usumbufu mkubwa wa kupata zana za uzalishaji mali kama ardhi, mikopo, mafunzo stadi na teknolojia na kwa namna hiyo hawafurahii fursa sawa za kiuchumi. Jitihada kadhaa zinaendelea kufanyika kitaifa na kimataifa kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia pamoja na haki nyingine zinazingatiwa na kupewa kipaumbele katika mipango ya maendeleo. Mchango wa Concern Tanzania katika jitihada hizi uko katika programu kuu mbili – maendeleo ya kilimo na maji, afya na mazingira. Kipaumbele kikuu cha jitihada hizo ni kuongeza usawa wa kijinsia katika maeneo ya vijijini nchini Tanzania. Concern Tanzania ilianza kufanya kazi na wanawake huko Iringa tangu mwaka 1979 katika shughuli zao za kilimo na uzalishaji wa mapato. Renatha Kahwili kutoka kijiji cha Mangawe anaelezea hali ilikuwaje hapo mwanzo: “Hapo zamani hali ilikuwa ya kutisha kila siku. Hatukuwa na elimu, tulikuwa hatukai na watu muhimu na tulikuwa hatuwezi kuelezea fikra zetu. Tusingeweza hata kuthubutu kupiga kura kwenye uchaguzi wa kijiji, kwa sababu tu sisi ni wanawake, ebu fikiri.” Concern Tanzania iliunda makundi ya wanawake katika kijiji cha Renatha. Wanakijiji wa Renatha waliieleza kwa furaha Concern kuhusiana na faida za muda mrefu za mradi huo – jinsi mbinu bora za kilimo kama matumizi ya mbolea ya mboji, uandaaji wa ardhi na upandaji wa aina tofauti za mazao, utumiaji wa plau katika kilimo na ufugaji mdogo mdogo wa mifugo ambavyo umeongeza uzalishaji wao hata wakati wa ukame. Vile vile walieleza jinsi stadi kama za utengenezaji wa majiko sanifu, lishe bora na ushonaji ambavyo zimewasaidia kuboresha afya zao na kuwaongezea kipato. “Hatukuwahi kuwa na kikundi kama hicho hapa

kijijini. Zaidi tu ya kuongeza uzalishaji na mapato yetu, tumejifunza pia umuhimu wa kuwa na Mwenyekiti, Mweka Hazina na Katibu. Tulijifunza kuhusu uongozi, usimamizi wa fedha na uwajibikaji. Ndio maana kikundi hiki bado kinaendelea hadi leo – miongo kadhaa baadaye. Kabla ya elimu tusingeweza kuthubutu kuwa wajumbe wa baraza la kijiji; lakini kundi letu lina mafanikio na sasa hatumuogopi mtu yeyote. Tumechaguliwa kwenye baraza la kijiji kwa sababu ya kazi yetu nzuri na sasa tunao uhuru wa kuelezea fikra zetu.” Siku hizi Concern, kwa kupitia wabia wake katika maeneo husika, hufanya kazi na mamia ya maelfu ya wanawake wakulima Tanzania. Miradi ya kilimo ya shirika hili imejengwa kwenye haki mbili za binadamu – haki ya chakula na ya ardhi – na inalenga katika kuongeza sauti na ushawishi wa wakulima kupitia uhamasishaji wa kijamii na uwezeshaji. Jambo hili ni la muhimu sana kwa jamii ya kitanzania, hususan wanawake, ambao ni mara chache sana hushiriki katika ufanyaji wa maamuzi. Kupitia ushiriki wao katika mifumo ya kiutawala na uwakilishi katika ngazi za chini hadi taifa, kwa mfano katika mashirika ya wakulima au serikali za mitaa, wanawake na wakulima wadogo wadogo kwa ujumla wanaweza kudai uwekezaji zaidi katika miundombinu na huduma ambazo zinaweza kuongeza mapato yao. Kwa kujiunga katika makundi, wakulima wanaweza kupata zana nyingi zaidi wanazopungukiwa na kujenga mahusiano na taasisi nyingine na serikali ili kuwezesha matakwa yao kufanyiwa kazi. Umoja wa Ulaya huifadhili Concern Tanzania ili kuongeza uelewa wa haki kama za ardhi, urithi, ndoa, kuboresha mbinu za kilimo, kuwezesha wakulima hususan wanawake kupata hati zao za ardhi na kusaidia mifumo ya kiutawala katika ngazi ya vijiji na wilaya kusimamia maendeleo ya jamii. Huko magharibi mwa nchi, timu ya wataalam wa maji na afya ya mazingira wa Concern Tanzania, wakiwa pamoja na watafiti kutoka London School of Hygiene and Tropical Medicine na Chuo Kikuu cha Durham, Uingereza, wanatafuta suluhisho la afya duni ya mazingira na kupunguza mzigo wa kuchota maji kwa akina mama na watoto.

Suala la kuhakikisha usawa wa kijinsia – katika bodi za watumiaji wa maji, kwenye serikali na kamati za vijiji na katika makundi ya wakulima – halihitaji majadiliano. Mary Rwegasira, mshauri wa usawa wa Concern Tanzania anasema: “Kwa sababu bado kuna elimu na ujuzi kidogo sana miongoni mwa wasichana baada ya kumaliza elimu ya msingi ukilinganisha na wavulana, jambo hili huwafanya wanawake kuwa ombaomba wa mazao yao wenyewe. Huwakabidhi waume zao pesa zote walizopata kwa jitihada zao kwa kuwa huamini hawawezi kusimamia fedha na hawawezi kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na maisha yao na familia zao. “Kwa bahati mbaya, huwarithisha na mabinti zao pia imani hiyo. Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini yanaweza kusaidia kuwasilisha ujumbe kuhusu uhaba wa fursa ya elimu kwa wanawake na madhara ya baadhi ya mila na desturi. Iwapo maadhimisho haya yataandaliwa vizuri na kuwahusisha wanaume, siku hii inaweza kuwaonesha wanaume wa kila umri kwamba wanatakiwa kubadilisha namna wanavyowachukulia wanawake wanaowazunguka.” Concern Tanzania inajua kuwa inafanya kazi yake pale mwanamke anapochaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji; pale mazao yanapokuwa mazuri na ziada inatumika kulipa ada za watoto; pale wanawake wanapoongea waziwazi na kwa ujasiri katika mikutano; pale maji safi na salama yanapotiririka katika vijiji na shule za vijijini na pale wanavijiji wanapoongoza njia. Muda kadhaa utapita kabla maendeleo kamili hayajawa mikononi mwa jamii, lakini kwa kadri muda unavyoenda, jitihada na msaada kutoka serikalini na kwa wafadhili unavyozidi kuongezeka, itafikia mahali jamii za vijijini Tanzania na wanawake pia watakuwa na sauti.

Vyanzo: Africa’s Smallholder Farmers Group (ASFG) report ‘Approaches that work for viable livelihoods’ 2010; Concern Worldwide UK’s Marginal Farmers campaign 2008; UN Report: ‘Improvement of the situation of women in rural areas’, 2009.

Page 26: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

26 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

 

Jina langu ni Mariam Mkosamali. Nina umri wa miaka 48 na nina watoto watano. Mume wangu ana

wake wawili. Japokuwa mimi ndiye mke mkubwa, sipati msaada wowote kutoka kwake. Yeye anaishi na mkewe mdogo mjini, mimi na watoto wangu tunaishi kijijini na huwa hatumuoni. Maisha yangu yalikuwa magumu na nilikuwa maskini. Chakula kilikuwa shida na tulikuwa tunahangaika sana kupata milo miwili kwa siku. Kaka yangu alimchukua mtoto wangu wa kwanza kunisaidia kumlea kwa sababu sikuwa na jinsi. Ninamkumbuka sana na huwa ninamfikiria sana kila siku. Wakati huo sikuwa na ufahamu wa kutosha na sikujua namna nzuri ya kuendesha kilimo. Kilimo kilikuwa cha kawaida mara zote – mahindi na maharage, pasipo mazao ya biashara. Sikuwa na fedha za kununulia ardhi kubwa kwa hiyo mara zote nilitumia ekari yangu moja niliyokuwa nayo. Watoto wangu walikuwa wakinisaidia. Nilijua namna ya kutengeneza mikeka lakini kila mtu hapa kwetu anajua namna ya kutengeneza kwa hiyo hakukuwa na wa kumuuzia. Kwa ujumla nilikuwa sijui ni nini ninaweza kufanya ili kubadilisha hali yangu ya kimaisha. Kulikuwa na wakulima waliokuwa na ujuzi wa kutosha lakini walikuwa hawataki kutufundisha, walikuwa wanataka tu kututumia kama wafanyakazi bure, hilo tu. Nilikuwa nikivuna mazao ya chakula tu na nilikuwa ninalima mashamba ya watu wengine kwa masaa tisa hadi 10 na kulipwa TZS 1,000/=. Nilidhani Mungu ndiye anataka mimi niendelee kuwa hivi. Mwaka 2007 Concern Tanzania

“Nimetoka mbali naSITAACHA KunIA MAKuBWA zAIdI”Na Isla GilmoreConcern Tanzania

na Relief to Development Society (REDESO) walinisaidia. Nilijiunga na kuwa mwanachama wa kikundi cha shamba darasa. Watu 250 kutoka kijijini kwetu tulijitolea hivyo wakatugawanya katika makundi ya watu 25 kila moja. Kila kikundi kilikuwa na kipande kidogo cha ardhi kwa ajili ya mazoezi. Tulipewa mbegu za mahindi na maharage kwa ajili ya kujifunza mbinu mpya. Pia tulipewa mbegu za karanga ili kutufundisha uzalishaji wa mazao ya biashara. Stadi hizi zilikuwa na manufaa na zilileta mabadiliko – kama kuacha nafasi, upandaji wa kwenye mistari na upaliliaji sahihi. Nilipouza mazao yangu niliyoyapata pamoja na marafiki zangu watano, niliweka TZS 150,000/= kwenye SACCOS na tulipata TZS 300,000 , hivyo tuliongeza fedha mara mbili hapo hapo. Tulizitumia fedha hizo kununulia madebe 30 ya maharage – sawa na kilo 600. Tuliyatunza maharage hayo hadi bei za maharage sokoni zilipoongezeka ndipo tukayauza. Fedha zetu ziliongezeka mara mbili tena na tukalipa deni kwenye SACCOS pamoja na riba ya TZS 50,000/=. Tulibakiwa na TZS 250,000/= na hivyo tukazitumia kwa kilimo tena. Tulilima mchele na tulipopata fedha tuliziwekeza tena kwenye SACCOS. Tulianzisha biashara nyingine. Zamu hii ilikuwa ni kununua na kuuza mbao. Tunapata fedha na tunaendelea kufanya kazi pamoja. Hivyo REDESO na Concern walituomba tujiunge na kundi lingine la watu waliokuwa na hali ngumu kijijini ili kuwapatia ujuzi na uzoefu wetu. Kundi hili lilikuwa na

wajane, yatima, wazee, walemavu na mtu mmoja alikuwa anaishi na VVU. Halmashauri ya kijiji ilitupatia ekari 48 kwa ajili ya kilimo na tulipewa mbegu kwa ajili ya ekari 28. Ndio tumeanza kulima na tunatarajia kuvuna mhogo mwingi. Bado ninaendelea kulima na kundi la wenzangu watano. Hadi sasa nimekwisha kupata TZS 800,000/= kutokana na biashara hizo. Maisha yangu yamebadilika. Mwanzoni maisha yalikuwa ya chini sana lakini kwa sasa yamepanda hadi kufikia hali nzuri kiasi. Nilikuwa ninaishi kwenye nyumba ya tope iliyoezekwa kwa nyasi lakini sasa nina nyumba nzuri ambayo najivunia kuishi ndani yake. Imejengwa kwa matofali ya kuchoma na imeezekwa kwa mabati. Mtoto wangu wa tatu amemaliza kidato cha nne. Na sasa sote tunakula milo mitatu kwa siku. Nimetumia sehemu kubwa ya fedha zangu kwa kujengea nyumba yangu mpya, kununulia vitu vya ndani na kulipia ada za watoto wangu. Kwa kuwa sasa nimeyainua maisha yangu kufikia kwenye hii hatua mpya, natakiwa kuanza kuwaza kuhusu mustakabali wangu. Ili kufanikisha hili, nahitaji mtaji. Nitajitahidi kwa kadri niwezavyo nipate mtaji kwa ajili ya kuanzishia biashara tena na kuzipanua. Mariam alibainisha ndoto zake: Anataka kutafuta mkopo ili kuanzisha biashara nyingine na kupangilia maisha yake ya baadaye. Mwezi mmoja baada ya kufanya mahojiano haya Mariam alipata hitaji lake – kikundi chake kilipata mkopo wa zaidi ya TZS milioni moja kwa ajili ya shughuli zao.

Wasifu

FRABHO ENTERPRISES LTDPlot 311 block B kiwalani Area,

P.O.Box 22557, Dar es Salaam, Tanzania, East AfricaTle: +255 22 277 1213, Fax: +255 22 277 1212, Cell: +255 784 411 818

E-mail: [email protected]

FRABHO ENTERPRISES LTD is a privately owned small and growing agro-processingcompany that performs value addition on crops such as Maize, Rice, Soya, Finger Millet, Sorghum, Cassava, Peanuts and Cashewnut, located at Kiwalani area in Dar es Salaam. It is a sales and marketing channel for resource poor small holder farming group

The Company sources raw materials from different small holder farming groups and traders and process Maize meal, Rice, Soya powder, Soy mix - Lishe, Finger millet flour, Sorghum-Cassava flour, High Quality Cassava Flour (HQCF). We are also roasters of Peanuts and Cashewnuts, pack in internationally accepted standards and market them both locally and regionally.

CASSAVA WEALTH UNFOLDING( You name it, Cassava can do it )

Value for Nutritious food value for Money

The production, processing and marketing of cassava can provide a major source of income to cassava farming households that constitute a very big population of poor farm families in the country. For long the crop has been seen as famine reserve, in recent years however, the potential wealth creating ability that is held in cassava has begun to unfold. The recognition of various uses of cassava as industrial raw material is stimulating increased production and processing. Some Commercial application of processed cassava include Animal feed, Glucose syrups, Bakery, Paperboard / Plywood, Pharmaceutical and Cosmetic industries.

The opportunity for wider markets for Cassava value addition is currently restricted by the small scale farming and processing. If large enterprises start processing, if large enterprises start using High Quality Cassava Flour and large numbers of small holder farmers can supply this new demand, therefore a substantial number of sustainable, market led, new livelihood opportunities will be created in terms of new jobs in farms and processing and utilization industries.

FRABHO enterprises is among the value chain actors dealing with semi processed cassava ( cassava grits ) purchased from small holder farmer processors in Mtwara region and process to produce High Quality Flour for sale to various end users. The Company is working closely with Cassava Adding Value for Africa (CAVA) project, which is the initiative to support the sustainable and equitable High Quality Cassava Flour Value chain.

Distribution for our products works mainly through Supermarkets such as SHOPRITE, GAME, UCHUMI to mention few, wholesale and some retail outlets. In the future our focusis to process food products for local, regional and international markets.

High Quality Cassava Flour (HQCF)

By: JULIUS WAMBURAChief Operating Officer

Cassava processing at Naliendele in Mtwara

MARIAM MKOSAMALI

Page 27: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

FRABHO ENTERPRISES LTDPlot 311 block B kiwalani Area,

P.O.Box 22557, Dar es Salaam, Tanzania, East AfricaTle: +255 22 277 1213, Fax: +255 22 277 1212, Cell: +255 784 411 818

E-mail: [email protected]

FRABHO ENTERPRISES LTD is a privately owned small and growing agro-processingcompany that performs value addition on crops such as Maize, Rice, Soya, Finger Millet, Sorghum, Cassava, Peanuts and Cashewnut, located at Kiwalani area in Dar es Salaam. It is a sales and marketing channel for resource poor small holder farming group

The Company sources raw materials from different small holder farming groups and traders and process Maize meal, Rice, Soya powder, Soy mix - Lishe, Finger millet flour, Sorghum-Cassava flour, High Quality Cassava Flour (HQCF). We are also roasters of Peanuts and Cashewnuts, pack in internationally accepted standards and market them both locally and regionally.

CASSAVA WEALTH UNFOLDING( You name it, Cassava can do it )

Value for Nutritious food value for Money

The production, processing and marketing of cassava can provide a major source of income to cassava farming households that constitute a very big population of poor farm families in the country. For long the crop has been seen as famine reserve, in recent years however, the potential wealth creating ability that is held in cassava has begun to unfold. The recognition of various uses of cassava as industrial raw material is stimulating increased production and processing. Some Commercial application of processed cassava include Animal feed, Glucose syrups, Bakery, Paperboard / Plywood, Pharmaceutical and Cosmetic industries.

The opportunity for wider markets for Cassava value addition is currently restricted by the small scale farming and processing. If large enterprises start processing, if large enterprises start using High Quality Cassava Flour and large numbers of small holder farmers can supply this new demand, therefore a substantial number of sustainable, market led, new livelihood opportunities will be created in terms of new jobs in farms and processing and utilization industries.

FRABHO enterprises is among the value chain actors dealing with semi processed cassava ( cassava grits ) purchased from small holder farmer processors in Mtwara region and process to produce High Quality Flour for sale to various end users. The Company is working closely with Cassava Adding Value for Africa (CAVA) project, which is the initiative to support the sustainable and equitable High Quality Cassava Flour Value chain.

Distribution for our products works mainly through Supermarkets such as SHOPRITE, GAME, UCHUMI to mention few, wholesale and some retail outlets. In the future our focusis to process food products for local, regional and international markets.

High Quality Cassava Flour (HQCF)

By: JULIUS WAMBURAChief Operating Officer

Cassava processing at Naliendele in Mtwara

Page 28: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

28 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Habari kwa ufupi

Habari Kwa UFUPI

UFUPIZoezi la kutengeneza Mpango Mkakati wa ANSAF 2012-2016

ambalo liliongozwa na mtaalam kutoka nje liligawanywa katika maeneo makuu mawili. Sehemu ya kwanza

iliwahusisha watu wawili kutoka Sekretariat ya ANSAF, Audax Rukonge na Alawiya Mohammed. walihudhuria warsha ya siku tatu iliyofanyika Arusha kuanzia Septemba 21 hadi 23, 2011. Warsha hii iliangalia zaidi masuala ya ndani ya Sekretariat ya ANSAF. Pia yalifanyika mapitio ya uwezo wa wafanyakazi wa ANSAF na mifumo yake. Mchakato huo pia uliangalia uhusiano wa wanachama na wafadhili na uongozi wa ANSAF. Matokeo ya mapitio haya ndiyo yaliyozaa sehemu ya pili ya mchakato huo ambayo iliwaleta pamoja wafanyakazi katika Sekretariati ya ANSAF na wanachama wa ANSAF. Rasimu rasmi ya mwisho ya Mpango Mkakati itakuwa tayari mnamo mwishoni mwa mwaka 2011. Picha zifuatazo zinaonesha mchakato uliopitiwa kuelekea kwenye utengenezaji wa mpango mkakati wa ANSAF.

Page 29: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

29UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Habari kwa ufupi

KUJA PAMOJA KUPITIA MAZUNGUMZO YA MEZANI … Majadiliano ya mezani yaliwezesha mjadala wa kina wakati wa Jukwaa la Kujifunza na Kushirikishana la mwaka 2010. Kauli mbiu ya “Kuendeleza Mnyororo wa Kuongeza Thamani nchini Tanzania: Jinsi ya Kuamsha Masoko ya Ndani” ilionekana kuwa inawahusu sana wanachama wa ANSAF hususan kupitia kwenye mawasilisho yao yaliyohusu uzoefu wao na utafiti walioufanya katika maeneo yao ya kazi. Huu ulikuwa mwendelezo wa masuala yaliyojitokeza mwaka 2009 ambapo ilibainika kuwa uzalishaji wa wakulima wadogo hauzingatii hali ya soko. Ilibainika kuwa huduma za ughani zilizopo zilikuwa zimejengwa kwenye mtazamo kwamba “unapaswa kuzalisha kwanza kisha ndipo utafute soko.” Miongoni mwa washiriki kwenye jukwaa hilo walikuwa ni wabia wa maendeleo, maafisa wa serikali, wawakilishi wa wakulima na wawakilishi wa Asasi Zisizo za Kiserikali na sekta binafsi. Katika majadiliano ilibainika kuwa kulikuwa na mabadiliko ya kimwelekeo. Hali ilivyo sasa ni kwamba michakato ya uzalishaji inaongozwa na ubora, wingi na mahali kutokana na mahitaji ya soko. Mojawapo ya changamoto zilizobainishwa ni ukosefu wa maarifa na taarifa kuhusiana na mnyororo mzima wa thamani ya mazao na mahitaji ya soko. Ni jambo la muhimu kuhakikisha kuwa mabadiliko ya soko yanafahamika kwa haraka na yanazingatiwa mara zote. Mnyororo wa thamani unafanya kazi chini ya kanuni za soko kwa kuzingatia miundo ya kibiashara ya sekta binafsi huku ukiingiza na kuzingatia mahitaji ya wadau. Majadiliano hayo pia yaligusia masuala yanayohusiana na upunguzaji wa umaskini, uhamasishaji wa ukuaji wenye kuzingatia ulinganifu, ushiriki wa wanawake katika mnyororo mzima wa thamani pamoja na wanawake kuwa katika nafasi za uongozi na ufanyaji maamuzi kwenye ngazi ya kaya. Masuala haya yote yalikuwa ni ya muhimu kwa makundi ya wazalishaji na kwenye ngazi ya taasisi.

Page 30: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

30 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Kutambuliwa

KUJA PAMOJA KWA WADAU WA KILIMOMafunzo ya siku tano ya “Mabingwa wa Mabadiliko” yaliyofanyika Morogoro tarehe 24 hadi 28 Oktoba, 2011 yalitaka kupanuliwa kwa mkakati wa Usalama wa Chakula unaotekelezwa Afrika kwa msaada wa United States Agency for International Development (USAID). Mbali na kujenga uwezo wa viongozi wa Kiafrika, warsha hii ililenga katika kujenga uelewa wa masuala ya mradi mahsusi ya Mpango madhubuti wa uendelezaji ya sekta ya kilimo Afrika Comprehensive Africa Agriculture Development Programme (CAADP), mpango wa USAID ya “mpango wa lisha vizazi vijavyo” na hali ilivyo sasa kuhusiana na maendeleo ya TAFSIP. Mafunzo hayo pia yaliwasaidia washiriki kujifunza hatua za utengenezaji wa miradi, usimamizi, kutambua vipengele muhimu kwa wafadhili, mifumo ya utunzaji wa kumbukumbu za fedha, mbinu za ufuatiliaji na tathmini na kanuni za USAID katika usimamizi wa fedha. Washiriki pia walifundishwa misingi ya uhusiano wa kazi na ufadhili, uongozi na hatimaye namna ya kutengeneza mpango kazi. USAID inatoa mafunzo kwa mashujaa wa mabadiliko katika kuhakikisha usalama wa chakula Afrika kwenye jitihada yake ya kuwezesha CAADP na mkakati wa Feed the Future (FtF) kufikia malengo yake. CAADP ni mkakati

 

 

Wadau wa kilimo kutoka mashirika mbali mbali.

kutoka kushoto ni Yona Mbwana kutoka ADRA, Herman kutoka VECO Tanzania, Alawiya kutoka ANSAF na David kutoka Afica Lead.

Page 31: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

31UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Kutambuliwa

   

 

ulioanzishwa Afrika ili kuboresha kilimo na uhakika wa chakula. Mataifa mbalimbali ya Afrika yameridhia kuitekeleza programu hii. Kila taifa linatengeneza mpango kazi wake kwa ajilli ya kutekeleza CAADP. Tanzania ilitengeneza rasimu yake ya utekelezaji iitwayo Tanzania Agriculture and Food Security Implementation Plan (TAFSIP) iliyoratibiwa na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikishirikiana kwa karibu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Rais Obama alianzisha mpango uitwao “Feed the Future” unaolenga kushughulikia tatizo la chakula kwa kuwezesha utekelezaji wa CAADP. Shirika la USAID lina nafasi kubwa sana katika utekelezaji wa mkakati huo.

KANUNI ZA USAID KUHUSU USIMAMIZI WA FEDHAWashiriki walisaidiwa kutambua tofauti za CFR, FAR na AIDAR. Vile vile walisadiwa kuelewa kanuni zinazotumika

katika usimamizi wa baadhi ya miradi, kuelezea kanuni za msingi za gharama, kutambua viwango vya malipo ya awali vinavyokubalika na gharama zinazokubalika chini ya ufadhili wa USAID. Maelezo zaidi kuhusiana na CFR, FAR na AIDAR yanapatikana kutoka www.usaid.gov . Kuanzia Juni 2011, iliamuliwa huko Washington kwamba mashirika yanaweza kuomba ruzuku moja kwa moja kutokea huko ili USAID iweze kujikita zaidi katika mambo yanayofanyika kwenye nchi husika na sio kushughulika na mawakala wa Kimarekani. Kuna njia mbili za kuweza kusimamia ruzuku: Ya kwanza ni pale ambapo USAID inaweza kuyapa fedha mashirika ya kimaendeleo kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kimaendeleo na pili, USAID inaweza kuipa jukumu taasisi nyingine kufanya kazi ambazo na USAID inazishiriki pia. Kabla ya kuomba ufadhili kutoka USAID inashauriwa upitie nyaraka hizi kwa makini:

• Tathminiyaawalikablayakupewaruzuku• ADS303–ruzukunamakubalianoyaushirikiano• ADS302–mikataba• ADS305–Serikali–Nchimwenyeji• 22CFR226–Ruzukunamakubalianoyaushirikiano• ADS303–Ruzukuyamajukumuyasiyohamishika

Tovuti za muhimu kuzitembelea unapotafuta ruzuku kutoka USAID

www.usaid.govwww.FedBizOpps.gov – funding

www.arnet.gov/far (FAR)www.gpoaccess/cfr/index.html (CFR)

www.usaid.gov/policy/ads/300/aidar (AIDAR)www.grants.gov – funding

Wanaharakati wa kike katika sekta ya kilimo.

Wadau wakiwa kwenye mafunzo.

Page 32: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

32 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Joyce Hiza ni mkulima mkazi wa kijiji cha Rusesa, Wilaya ya Kasulu, magharibi ya Tanzania. Anakaa na wapwa zake watano ambao ni yatima. Mvua hunyesa sana huko Kasulu, kwa hiyo baada ya kujifunza mbinu na stadi

mpya za kilimo kutoka kwenye mashamba darasa yaliyoanzishwa na serikali au mashirika mengine kama Concern Tanzania, wakulima kama Joyce wanaanza taratibu kutumia ujuzi huo kwenye mashamba yao kwa ajili ya kupata mazao zaidi. Joyce anasema, “Kinachotukwamisha sisi ni upatikanaji wa zana za kilimo, hususan mbegu bora. Inatulazimu kusafiri hadi mjini Kasulu (mwendo wa masaa manne) kwa ajili ya kununua mbegu na wengi wetu hatuwezi kuzimudu.” Ili kukabiliana na tatizo hili, Joyce na wakulima wengine walianzisha kikundi cha uzalishaji mbegu huko Rusesa na kwenye vijiji vya jirani. “Tunataka kuwasaidia wakulima wenzetu na kwa jinsi hii tunaweza kujipatia pesa, hivyo ni jambo zuri kwa kila mtu,” anasema Joyce. Kundi hili lilianza uzalishaji wa mbegu za mahindi na alizeti msimu wa kilimo mwaka 2009/2010. Mbegu zao za awali zilipewa hati mwaka 2010. Mahindi yalithibitishwa kuwa yalikuwa halisi kwa kiwango 99.9% na 93% kwa kiwango cha umeaji. Alizeti ilikuwa halisi kwa kiwango cha 99.8% na 93% kwa kiwango cha umeaji. Mwaka 2010, kikundi kilizalisha mbegu za mahindi kilo 517 na kilo 399 za mbegu za alizeti. “Huwa tunalima pia kwa ajili ya chakula, na mwaka huu tuna furaha kwa sababu tuna mbegu za kutosha kwa ajili ya mashamba yetu kutokana na mavuno mazuri,” Joyce anaelezea. “Uzalishaji wa mbegu umetusaidia kupata pesa zaidi kuliko kuuza nafaka,” anaongeza Joyce. Kila mwanakikundi ana mpango wake wa namna ya kutumia faida yake. “Nitanunua vifaa vya shule kwa ajili ya wapwa zangu.” Inakadiriwa kwamba watu wapatao 2,500 watanufaika na mradi huo wa mbegu. “Tunajivunia kwamba tumeleta suluhisho la tatizo la ukosefu wa mbegu Rusesa.”

“Sina chaguo. maisha haya ndio pekee niliyo nayo,

“nInAzALISHA MBEgu KWA AJILI yA JAMII”

nI LAzIMA nIyATuMIE KIKAMILIFu”

Wasifu

Mtwara, Kusini mwa Tanzania, 2010

Somoye hajui umri wake. Anadhani alikuwa ana umri wa miaka mitano wakati

Tanzania inapata uhuru wake mwaka 1961; anaonekana bado kijana sana. Ni mlemavu, labda kutokana na pepopunda, ila hana uhakika. Alizaa watoto tisa na sita kati yao bado wako hai. Mwanzoni unaweza kudhani Somoye ana dunia nzima mikononi mwake. Ana kicheko cha kujiachia ambacho kinatufanya na sisi tucheke pamoja naye. Anatuvutia kwa uwezo mkubwa wa kuelezea mambo kwa hisia huku akiwa wazi kujibu maswali yote tunayomtupia. Hafichi kitu chochote na humwambia mtu yeyote aliye tayari kumsikiliza, huku akitabasamu. Lakini maisha ya Somoye si ya furaha na mafanikio kama anavyoonesha usoni. Anatokea kwenye eneo lenye ukame nchini Tanzania na uwezo wake wa kulima

umekuwa ukizidi kupungua siku hadi siku hivyo amebaki kuwa mtegemezi wa misaada ya chakula kutoka kwenye familia nyingine. Katika miaka ya hivi karibuni alipokea msaada fulani kutoka kwenye serikali ya kijiji na kutoka kwenye shirika moja la kijamii linalosaidiwa na Concern Tanzania. Lakini kila kitu alichopewa, mumewe alikiiba, akakiuza ili apate pesa za kununulia pombe. Mwishowe alipata ujasiri wa “kumfukuzia mbali” yule mumewe hajawahi kujutia uamuzi wake huo. “Sijui aliko na wala sitarajii kama atarudi tena. Watoto wangu wako mbali na huwa wanarudi nyumbani iwapo tu kuna kitu wanahitaji lakini sina kitu chochote cha kuwapa.” Akiwa ni mwanamke nchini Tanzania, Somoye anakabiliwa na mzigo wa kubaguliwa, huku akiwalea watoto

wake peke yake pamoja na kazi ngumu ambazo mara nyingi huwa na manufaa kidogo sana. Ulemavu wake unamuongezea mzigo mwingine mzito juu ya ile ambayo tayari anayo kama mwanamke. Hulima kwenye mashamba ya watu wengine ili alipwe japokuwa kimwili amechoka. Anasema: “Hii ndo kazi ninayoweza kuifanya vizuri zaidi” na kwamba ni lazima aendelee kuifanya. Alipoulizwa ni kwa nini anaonekana mwenye furaha kiasi hicho anasema “Sina chaguo. Maisha haya ndio maisha pekee niliyo nayo, ni lazima niyatumie kikamilifu.”

 

Joyce Hiza akiwa na mfuko wa mbegu bora za mahindi zilizozalishwa na kikundi, 2010

Page 33: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

33UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

TAP ni ushirikiano wa wadau kutoka sekta binafsi ya umma. Hushughulikia masuala yote

yanayohusu mnyororo wa kilimo kama upatikanaji wa mikopo, upatikanaji wa zana za kilimo na huduma za ughani, mfumo wa vocha na masoko. Mbinu kuu ya TAP ni kutumia miundo na mifumo ya wadau wengine iliyopo tayari. Huyaangalia masuala kwa ujumla wake na kila mdau huleta kitu fulani katika ushirikiano huo. Chini ya programu hii ambayo hutekelezwa katika wilaya 25, wakulima na wauzaji wa zana na pembejeo za kilimo huwezeshwa kuboresha uwezo wao wa kitaalam na kibiashara.

TAARIFA ZA BEI ZA MAZAOMara zote wakulima huhamasishwa kulima sana pale wanapokuwa

Kupata na Kutumia Taarifa za masoko:KITEndAWILI KWA WAKuLIMA WAdOgO

Baraza la Kilimo Tanzania (aCT) linasimamia mipango maalum iitwayo Ushirikiano Katika Kilimo Tanzania (Tanzania agricultural Partnership (TaP).

ushirikiano

wanatarajia bei nzuri za mazao yao. Lakini mara nyingi taarifa za masoko huwa hazipatikani kwa urahisi, na matokeo yake wakulima wengi huuza mazao kwa bei za kutupa. Ndio maana TAP imejikita katika kampeni ya kuwafunza wakulima namna ya kupata na kutumia taarifa za bei. Hivi karibuni mratibu wa mnyororo wa thamani ya chakula wa TAP (TAP Food Value Chain Coordinator) aliendesha semina za mafunzo katika Wilaya 13. Mafunzo hayo ambayo yalitokana zaidi na mahitaji ya waliokuwa wanafundishwa, hayakuangalia suala moja kwa upekee wake. Mafunzo hayo yaliangazia pia masuala mengine kama matumizi ya mbinu bora za kilimo. Hii ni kwa sababu pasipo kuzalisha mazao yenye ubora wa

hali ya juu jitihada za kupata masoko zitakuwa kazi bure. Katika hali ya kawaida, wakulima wa Tanzania hulima ekari kidogo sana, hupata mazao kidogo na hawajajipanga vizuri. Katika zoezi la awali, zaidi ya wakulima 2600 walipewa mafunzo katika vipindi vinne tofauti vyenye siku tatu kila kimoja katika kila wilaya miongoni mwa zile Wilaya 13. Kila kipindi kilihusisha wakulima 50. Upangaji na utekelezaji ulifanyika kwa kuwashirikisha waratibu wa Wilaya wa TAP pamoja na wadau wengine kwenye wilaya husika, hususan RUDI, Faida Mali na TRACE. Kipaumbele kiliwekwa kwenye vijiji ambako TAP ina karakana zilizokarabatiwa. Mafunzo yalikuwa shirikishi na yenye kuzingatia uhalisi na

Page 34: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

34 UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

uwezekano wa kutekelezeka kwa kadri ilivyowezekana. Matokeo chanya ya mafunzo inaweza kupimwa kwa kuangalia wingi wa washiriki waliojitokeza na jinsi walivyoonesha kuridhishwa na mafunzo. Katika baadhi ya maeneo, idadi ya washiriki ilizidi ile iliyokuwa imekadiriwa wakati wa kupanga. Mkulima mmoja kutoka Igomaa, wilaya ya Mufindi alisema: “Tunashukuru sana kualikwa kwenye mafunzo haya muhimu. Kwa kuangalia mchanganyiko wa washiriki, tunaona wazi kuwa TAP inawajali wakulima maskini na walio pembezoni. Hii ni tofauti na mafunzo mengine yaliyofanyika hapa kijijini kwetu.” Mwanamke huyo ni mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wanaoishi na virusi vya UKIMWI. Naye Bw. Zefania, mkulima kutoka kijiji cha Ngaresh- Lasheine, Wilayani Monduli alisema: “Mafunzo haya yametusaidia sana. Ardhi yetu inabadilika kutoka hali mbaya kuwa mbaya zaidi. Inazidi kuwa kavu na isiyozaa. Japokuwa tunategemea sana kilimo, hatujui namna ya kulima kwa manufaa. Mafunzo haya yanatusaidia kutafakri upya kuhusu kilimo chetu na kutumia teknolojia za gharama nafuu.” Masuala mengine yaliyogusiwa kwenye mafunzo hayo ni ujasiriamali na stadi za majadiliano. Washiriki

walifanya maigizo kuhusu majadiliano ya kuwawezesha kupata bei nzuri ya mazao yao na kutumia mizani. Walishangaa baada ya kuona ni kiasi gani cha mapato walikuwa wanakipoteza kutokana na vipimo. Mara nyingi, wanunuzi huwa na madebe tofauti–kwa ajili ya kuuzia na kununulia. Madebe ya kuuzia huwa ni madogo na ya kununulia huwa ni makubwa. Ni jambo la kawaida kuona gunia la mkulima likibeba madebe saba ya mahindi (ambayo hujulikana zaidi kama lumbesa), wakati gunia la mfanyabiashara hubeba madebe sita–ikimaanisha kwamba hupata debe moja bure kutoka kwa mkulima. Baada ya kukokotoa gharama za kilimo ikilinganishwa na mapato wanayoyapata kwa kuuza mazao yao, wakulima wengi walishtuka na kuumia sana walipobaini hasara waliyokuwa wakiipata. Mafunzo bora yaliwawezesha wakulima kubaini namna gani wanaweza kubadilisha hasara kuwa faida. Afisa Mazao wa Wilaya ya Mufindi Bi. Nyanzali alielezea: “Mafunzo yaliyofanyika mwanzoni yalilenga katika masoko tu, wakati mafunzo haya yamelenga katika mchanganyiko wa masuala mbalimbali ambayo mkulima anakabiliana nayo na namna ya kuyashughulikia kikamilifu.” Mafunzo haya yalikuwa mazuri na yenye kufaa

kwa mkulima yeyote bila kujali alikuwa na ufahamu na ujuzi kiasi gani wakati anaanza na bila kujali anatokea shirika gani au umbali kiasi gani. TAP kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wanaoshughulikia masuala ya masoko (RUDI, TRACE na Faida Mali) walifanya kazi kwa pamoja kutengeneza muongozo ambao ulitumiwa katika wilaya zote ambako Ruzuku ya Mfuko wa Chakula ya EC (ambayo TAP ilipewa na Umoja wa Ulaya) ilikuwa inatumiwa. Sambamba na mafunzo, TAP iliwapa kazi Match Makers Associates kuchambua mifumo ya zamani na ya sasa ya taarifa za masoko (Market Information Systems (MIS) nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Taarifa hiyo itakuwa inapatikana www.tap.or.tz.

“Tunashukuru sana kualikwa

kwenye mafunzo haya

muhimu

ushirikiano

Mbomole Investment wilayani Njombe ipo tayari kufanya kazi na wakulima wote waliopata mafunzo ya taarifa za masoko

Page 35: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

35UlimwengU wa mkUlima • janUari 2012

Mbinu mbalimbali hutumika katika kutengeneza uwezekano wa kuwafanya

wakazi wa vijijini waingizwe kwenye mfumo wa kawaida wa maisha. Hii huhusisha uundaji wa vikundi vidogo vidogo vya wakulima. Vikundi husaidia katika kutengeneza mitandao na kurahisisha uwezeshaji. Deogratius William wa kijiji cha Handuki wilayani Maswa ni mmoja wa wale waliopata mafunzo ya ufugaji wa kuku wa kienyeji. “Sikuwa na wazo kwamba siku moja ufugaji wa kuku wa kienyeji ungeweza kubadilisha maisha yangu. Sikuwahi kufikiri kwamba siku moja ningeufanya ufugaji wa kuku wa kienyeji kuwa ndio kazi yangu kuu,”

anaelezea William. William alihudhuria mafunzo ya mnyororo wa kuongeza thamani ambako alifundishwa namna ya kujenga banda la kuku, namna ya kutunza taarifa za kifedha na namna ya kuwachanja kuku. “Nilianza mwaka 2010 nikiwa na jogoo wawili na kuku watatu,” alielezea William ambaye kwa sasa anamiliki kuku 50. Kuku mmoja wa kienyeji huuzwa kati ya TZS 8,000/= na TZS 10,000/=. Kuna kituo ambapo wao huuzia kuku wao na mayai. Wafugaji wa kuku wa kienyeji wamewezeshwa kupitia kwenye vikundi. Madalali hawafurahii kuundwa kwa vikundi vya wakulima kwa

sababu wanakuwa hawawezi tena

kuwanyonya. Pamoja na mafanikio,

wafugaji wa kuku wa kienyeji bado

wanakabiliwa na changamoto

kadhaa. Mbali na magonjwa ya

kuku, masoko pia sio ya kutegemewa

sana. William anasema wafugaji

wenzake katika wilaya jirani ya

Kishapu wamefanikiwa kuishawishi

Halmashauri ya Wilaya kutenga siku

maalum ya soko la kuku. Anasema

kwa msaada wa wahamasishaji wa

wakulima, wafugaji wa kuku wa

kienyeji wilayani Maswa wanajaribu

kuishawishi Halmashauri ya Wilaya

kutenga siku maalum ya soko la kuku.

Kuwezesha

Wafugaji wa Kuku waKIEnyEJI WAMEWEzESHWAWatu duniani kote wanapambana ili kuutokomeza umaskini. Wanaoishi vijijini nao wanapambana ili kupata riziki kwa ajili ya familia zao.

Page 36: Mkulima - dev.ansaf.or.tzdev.ansaf.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Mkulima-V1-Swahili.pdf · Huchukua muda mpaka kuyaona matokeo. Mwanzoni, Salaganda hakuwa na uwezo hata wa kuendesha

AgRICuLTuRAL nOn STATE ACTORS FORuM, 169 Regent EstateS.L.p 6370, dar es Salaam, Tanzania

Simu: +255 22 2700327, nukushi: +255 22 2700318Barua pepe: [email protected]

Tovuti: www.ansaf.or.tz