mem bulletin 94 (2).pdf

13
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 94 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Novemba 20 - 26, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz Soma habari Uk. 3 Wezi wa umeme kukiona Mmoja wa wachimbaji wadogo waliookolewa katika mgodi wa Nyangalata Amos Muhangwa akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga mara baada ya kuokolewa tarehe 15/11/2015. Walifukiwa baada ya kuopoa wenzao Wachimbaji waliofukiwa siku 41 waokolewa Kikosi cha vijana 25 waliofanikisha zoezi la uokoaji wachimbaji wadogo 6 waliofukiwa katika mgodi wa Nyangalata wakiwa katika picha mara baada ya kumaliza zoezi hilo kwa kuopoa mwili wa mchimbaji mmoja aliyefariki katika mgodi huo, Musa Spana.

Upload: jackson-m-audiface

Post on 11-Apr-2016

125 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

Habari za nisHati &madini

Toleo No. 94 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Novemba 20 - 26, 2015

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

Soma habari

Uk. 3Wezi wa umeme kukiona

Mmoja wa wachimbaji wadogo waliookolewa katika mgodi wa Nyangalata Amos Muhangwa akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga mara baada ya kuokolewa tarehe 15/11/2015.

Walifukiwa baada ya kuopoa wenzao

Wachimbaji waliofukiwa siku 41 waokolewa

Kikosi cha vijana 25 waliofanikisha zoezi la uokoaji wachimbaji wadogo 6 waliofukiwa katika mgodi wa Nyangalata wakiwa katika picha mara baada ya kumaliza zoezi hilo kwa kuopoa mwili wa mchimbaji mmoja aliyefariki katika mgodi huo, Musa Spana.

Page 2: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Teresia Mhagama na Asteria Muhozya

Wachimbaji wadogo wa madini Watano kati ya Sita waliokuwa wamefukiwa na

kifusi cha mchanga katika machimbo ya Nyangalata katika Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga wameokolewa wakiwa hai Novemba 15, 2015 baada ya kufukiwa chini ya ardhi kwa siku 41.

Hayo yameelezwa na Badra Masoud, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.

Badra aliwataja wachimbaji hao wadogo waliookolewa wakiwa hai kuwa ni Muhangwa Amos, Joseph Bulule, Chacha Wambura, Msajiri Gerald na Onyiwa Aindo huku aliyefariki dunia kuwa ni Musa Spana.

Alieleza kuwa wachimbaji hao walifukiwa katika mgodi huo tangu Oktoba 5 mwaka huu ambapo juhudi za kuwaokoa zilizoratibiwa na Wizara ya Nishati na Madini, Uongozi wa Wilaya ya Kahama na Umoja wa wachimbaji wadogo zilifanikiwa siku ya tarehe 15 Novemba 2015 kwa wachimbaji hao kupatikana wakiwa wamenasa zaidi ya mita 100 chini ya ardhi.

“Kutokana na hali ya wachimbaji hawa kudhoofika sana, walipelekwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama

mkoani Shinyanga kwa ajili ya matibabu,” alisema Badra.

Aliongeza kuwa wachimbaji hao walikaa chini ya ardhi kwa muda wa siku 41 huku hali zao zikiwa zimedhoofu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa hewa safi, kula mizizi ya miti, chura, mende na kunywa maji kidogo yaliyokuwa yakitiririka katika mgodi huo waliyokuwa wakikinga kwa kutumia kofia ngumu walizoingia nazo mgodini humo (helmet).

Vilevile taarifa zilizopatikana tarehe 19 Novemba 2015 kutoka kwa Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje zinaeleza kuwa mwili wa mchimbaji mdogo, Musa Kaspana uliokuwa umebaki katika mgodi huo tayari umeopolewa na taratibu za kusafirisha mwili huo kwenda nyumbani kwa marehemu wilayani Magu zinafanyika.

Aidha, Kaimu Kamishna pia amewashukuru wadau mbalimbali walioshiriki katika kufanikisha zoezi hilo la uokoaji wa wachimbaji hao hasa vijana 25 waliotoa mwili wa marehemu kwenye mgodi huo pamoja na wachimbaji watano waliokutwa wakiwa hai. Vijana hao walifanikisha zoezi hilo baada ya kufuata kwa umakini maelekezo waliyokuwa wakipewa na wataalam wa madini.

Wachimbaji hao walifukiwa baada ya kumaliza kuopoa miili ya wenzao waliokuwa wamefukiwa mgodini hapo.

Wachimbaji waliofukiwa siku 41 waokolewa

Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (kushoto) akizungumza na Onyiwa Aindo ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo waliookolewa katika mgodi wa Nyangalata Novemba15, 2015.

Msemaji wa Wizara, Badra Masoud akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.

Page 3: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

TahaririMEM

Na Badra Masoud

Five Pillars oF reForms

KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

Bodi ya uhariri

MharIrI Mkuu: Badra MasoudMsaNIfu: Lucas Gordon

WaaNdIshI: Veronica simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed saif, rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

increase eFFiciencyQUality delivery

oF Goods/service

satisFaction oF tHe client

satisFaction oF BUsiness Partners

satisFaction oF sHareHolders

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Tunawaombea afya njema wahanga wa Nyangalata

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Wezi wa umeme kukiona

Hivi karibuni kulikuwa na habari kwamba wachimbaji wadogo watano kati ya sita waliokuwa wamefukiwa kifusi katika mgodi wa dhahabu wa Nyangalata uliopo Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Wachimbaji hao watano walifukiwa tangu tarehe 5, Novemba 2015 ambapo jitihada za kuwatafuta zilifanyika lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kupatikana na kufanya uongozi wa Wilaya na Umoja wao wa wachimbaji wadogo kukata tamaa kama wachimbaji hao waliofukiwa watapatikana tena.

Lakini siku ya Jumapili tarehe 15 Novemba, 2015 baadhi ya wachimbaji wengine waliokuwa wakitafuta jenereta katika mgodi mwingine walipokuwa ndani ya mgodi wakiendelea na utafutaji wa jenereta hiyo walisikia sauti za watu wakiomba msaada.

Sauti hizo za wachimbaji waliofukiwa zikiomba msaada ziliwashtua wale wachimbaji wengine ambapo walitoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya pamoja na Wizara yenye dhamana na sekta ya Madini ndipo uokoaji ulipoanza katika mgodi mwingine.

Wachimbaji hao wadogo walifanikiwa kuokolewa wakiwa hai lakini afya zao zikiwa zimedhoofika kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba walikuwa wamepoteza kumbukumbu, hawaoni, wakiwa na vidonda mwilini na hawawezi hata kutembea kutokana na kukosa hewa safi, chakula na maji.

Hata hivyo, baada ya kuokolewa wachimbaji hao waliokaa kwa siku 41 chini ya mgodi huo wakiwa wamefukiwa walizua mshangao watu wengi waliuliza namna walivyoweza kuishi chini ya mgodi kwa siku zote 41.

Wahanga hao walieleza kwamba ni Mwenyezi Mungu ndiye aliyewajaalia kuishi kwa siku zote hizo lakini pia walikuwa wakila vyura, mende, magome ya miti huku wakikinga maji yaliyokuwa yanadondoka kwenye shimo hilo kwa kutumia kofia ngumu yaani helmet walizokuwa nazo.

Kwa hakika hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea nchini mwetu ambapo wachimbaji wadogo wamefukiwa na kukaa chini ya mgodi kwa siku 41 ambapo baadaye wakatolewa wakiwa hai kama ilivyotokea kwa wachimbaji hao wadogo wa Nyangalata.

Ni dhahiri kabisa wote tunaomuamini Mwenyezi Mungu lazima tumshukuru sana kwa wenzetu kuwa hai katika siku zote 41 wakiwa ndani ya mgodi uliotitia na kuanguka.

Vilevile tunawapa pole wachimbaji hao wadogo waliokolewa akina Muhangwa Amos, Joseph Bulule, Chacha Wambura, Msafiri Gerald na Onyiwa Aindo na tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye haraka na warejee katika afya kama ilivyokuwa huko nyuma kabla ya kufukiwa katika mgodi.

Aidha, tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mchimbaji mwingine aliyefukiwa marehemu Mussa Spana ambaye yeye alipoteza maisha akiwa na wenzake katika mgodi na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amen.

Kwa upande mwingine tunasihi na kuwakumbusha wachimbaji wadogo wote kuwa makini katika uchimbaji wao kwa kufuata taratibu za afya na usalama kazini ili kuepuka ajali kama ya wachimbaji hao kufukiwa katika migodi.

Pamoja na kuwakumbusha kuzingatia usalama kazini lakini pia Wizara yenye dhamana na sekta ya Madini nayo itaendelea kuwaelimisha juu ya uchimbaji wa kisasa na unaozingatia afya na usalama katika migodi hivyo wachimbaji wadogo watoe ushirikiano kwani hilo ni kwa faida yao.

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Kutokana na wizi wa umeme kukithiri na kuliingizia hasara Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wizara ya Nishati na Madini imeliagiza

Shirika hilo kuimarisha kikosi chake cha ukaguzi wa watumiaji wa umeme ili kubaini wateja wasio waaminifu wanaoiba umeme na kuwachukulia hatua za kisheria.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud alipofanya mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kuendeleza mafanikio na changamoto katika usimamizi wa sekta ya umeme.

Masoud alisema Wizara inatarajia kuunda kikosi maalum kitakachojumuisha wataalam kutoka katika taasisi mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo linalolikosesha mapato shirika la TANESCO.

Alisema kikosi hicho kitajumuisha wataalam kutoka TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na vyombo vya usalama na kuongeza kuwa hatua hii imekuja baada ya Wizara kubaini kuwa kuna baadhi ya watu wanaohujumu miundombinu ya TANESCO kama vile kuchoma nguzo za umeme, kuiba mafuta ya transfoma pamoja na nyaya za umeme na kuwataka kuacha kufanya hujuma hizo kwani watakaogundulika wataendelea kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akielezea zoezi hilo, Masoud alisema kuwa hivi sasa vyombo vya dola katika mkoa

wa Lindi vinaendelea kuwasaka na kuwatia nguvuni wale wote waliohusika kuchoma nguzo za umeme wa msongo mkubwa unaosafirisha umeme kutoka Mtwara kwenda Lindi katika vijiji vya Hingawali na Njonjo mkoani Lindi na kusababisha mikoa hiyo miwili kukosa umeme na kusababisha hasara kwa TANESCO.

Masoud alizitaka Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali kuzingatia matumizi bora ya umeme ili kudhibiti upotevu wa nishati ya umeme na kusisitiza kuwa utaratibu huu wa matumizi bora ya umeme hufanywa pia na nchi nyingi duniani kwa ajili ya kukabiliana na upotevu wa umeme.

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya taasisi huwa zinaacha umeme ukiendelea kupotea baada ya muda wa kazi kama vile kuacha viyoyozi, taa, kompyuta na vifaa vingine vinavyotumia umeme vikiendelea kutumia umeme hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa umeme ambao ungetumika katika maeneo mengine au kuokoa fedha ambazo hutumika kuzalisha umeme huo.

Akielezea hali ya upatikanaji wa umeme nchini Masoud alisema kuwa hali ya umeme nchini ni nzuri na hakuna mgawo wowote unaoendelea hivi sasa kwani hali ya uzalishaji ni nzuri pamoja na mabwawa ya maji ambayo hutumika kuzalisha umeme kukauka.

Alisisitiza kuwa kiasi cha umeme kinachopatikana kwa sasa ni megawati 1500 huku matumizi ikiwa ni kati ya megawati 800 na 900 kutokana na umeme huo kuzalishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na gesi asilia pamoja na mafuta mazito na dizeli.

Kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I jijini Dar es Salaam

Page 4: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Rhoda James

Serikali kupitia kampuni ya mafuta ya PUMA imeahidi kuendelea kutekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha

uchumi wa taifa na hatimaye wananchi na taifa kuweza kunufaika.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo wakati alipokutana na Uongozi wa Kampuni hiyo kwa lengo la kufahamiana na kujifunza juu ya utendaji wa kampuni ya mafuta ya PUMA kwa ujumla.

Aidha, Chambo aliasa uongozi wa kampuni hiyo kushirikiana na Serikali kwa karibu ili kuboresha utendaji wao kwa kuweka wazi changamoto zinazowakabili ili Serikali ifuatilie kwa karibu matatizo hayo na hivyo kuboresha utendaji.

“Kampuni hii ina ubia wa asilimia 50 kwa 50 na Serikali, hivyo basi utendaji wake lazima uwekwe wazi na ufatiliwe kwa karibu ili wananchi wafaidike na huduma zinazotokana na Kampuni hiyo”, alisema Chambo.

Vilevile Mhandisi Chambo ameahidi kutatua tatizo lililopo la kupoteza mafuta kwa wingi wakati wa kuyasafirisha au kuyapokea na kusema tatizo hilo linapelekea Serikali kuendelea kupoteza mapato.

Kwa upande wake Meneja Mwendeshaji kutoka kampuni ya PUMA, Lameck Hiliyai alisema, kampuni ya PUMA imekuwa ikifanya kazi kwa viwango na hadi sasa Kampuni hii ni ya kwanza Afrika katika utoaji wa huduma ya kuhifadhi mafuta ambayo imeongeza ukuaji wa biashara na uendeshaji wa jumla ndani ya masoko ya kikanda na kimataifa.”

Hiliyai aliongeza kuwa, hata hivyo kampuni hiyo imekuwa na changamoto ya kupoteza mafuta kutokana na kampuni hiyo kuagiza mafuta kwa wingi kwa sababu ya mfumo uliopo na kusema kuwa ni faraja kwao kuona kwamba jambo hilo hivi sasa linaelekea ukingoni.

Aidha, Hiliyai aliendelea kuelezea changamoto nyingine ikiwa ni pamoja na urasimu uliopo ambao unachangia pia katika kukosesha Serikali mapato.

Hiliyai alimaliza kwa kusema kuwa kampuni ya PUMA inaendelea kuwekeza katika biashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara kati yao na kampuni kubwa zikiwemo za madini, ndege, na hata biashara ya rejereja bila kusahau uhifadhi wa mafuta.

Kulia ni Naibu Katibu Mkuu kutoka wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja na viongozi waandamizi kutoka wizara ya Nishati na Madini na ujumbe kutoka PUMA wakiwa wanafuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya PUMA, Lameck Hiliyai.

PUMA kuchangia ukuaji Uchumi

Wa kwanza kushoto ni Meneja mwendeshaji kutoka kapuni ya PUMA, Lameck Hiliyai, kushoto kwake ni mameneja wenzake kutoka PUMA , Adam Elinewinga na Jonathan Mmari wakiwa wanafuatilia jambo katika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise (Kushoto). Wengine ni viongozi waandamizi kutoka wizara ya Nishati na Madini wakifuatila jambo kutoka kwa mtoa mada (hayupo pichani).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Omar Chambo akiwa katikati, na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Masanja, wengine katika picha ni viongozi waandamizi kutoka wizara ya Nishati na Madini na ujumbe kutoka Puma.

Page 5: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Serikali: Waliochoma nguzo wakamatwe Na Mohamed Saif

Serikali imelaani vikali uchomaji nguzo za umeme uliofanywa katika Vijiji vya Hingawali na Njonjo Mkoani Lindi na imesema inaendelea kuwasaka

ili kuwatia mbaroni wahusika.Wakizungumza na serikali za vijiji

hivyo kwa nyakati tofauti, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja walisema kitendo hicho ni uhujumu wa miundombinu na ni uhalifu hivyo sheria kali zitachukuliwa.

Awali, taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Hingawali, Kata ya Pangatena, Hamis Mshamu kwa viongozi hao, ilieleza kuwa katika vipindi tofauti ndani ya miezi sita, nguzo za umeme zipatazo tisa zimechomwa moto na watu wasiofahamika.

Mshamu alisema tukio hilo kwa kijiji hicho limetokea kwa nyakati tofauti ndani ya kipindi cha miezi sita huku juhudi za kuwatafuta waliofanya tukio hilo zikishindwa kuzaa matunda kwa madai kuwa hakuna aliyefahamika kuhusika na tukio hilo.

Alisema hapo awali, walihisi kitendo hicho kilitokana na kupita kwa nguzo hizo bila wao kupatiwa huduma

hiyo ya umeme lakini matukio hayo yameendelea hadi hivi sasa ambapo tayari Kijiji hicho kimepatiwa huduma hiyo.

“Tulidhani wananchi wamechoma kwa vile wanaona tu umeme umepita hapa kijijini lakini wao hawana; sasa hivi umeme tunao lakini juzi tu nguzo nyingine imechomwa,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu alisema Serikali haipo tayari kuona wananchi wakiteseka kwa kukosa huduma ya umeme kwa ajili ya watu wachache waliofanya hujuma hiyo kwa lengo wanalolijua wao.

“Hili ni janga, maana watu wengi wanahitaji huduma hii; shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinasimama kutokana na hujuma. Kule kuna huduma ya umeme nyie mmekata mfano hospitalini. Hili halikubaliki hata kidogo,” alisema.

Mhandisi Chambo alitoa wito kwa vijiji hivyo kuhakikisha vinawabaini na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya viongozi hao wa Kijiji. “Tunataka wiki hii, lazima waliofanya haya wapatikane,” alisema.

Alisema lengo la Serikali ni kuinua hali ya maisha ya mwananchi na kuondokana na umaskini na ndiyo lengo la huduma ya umeme.

Mhandisi Chambo alisema Serikali

haijaridhishwa na namna suala hilo linavyoshughulikiwa na uongozi wa kijiji hicho na hivyo kumtaka Mwenyekiti wa Kijiji cha Hingawali kuhakikisha waliofanya hujuma hiyo wanakamatwa mara moja na kupelekwa mahakamani.

Alisema pale diplomasia inaposhindwa, nguvu itatumika na viongozi wa kijiji ndiyo watakuwa wa kwanza kuchukuliwa hatua kwani

haiwezekani wakawa hawawafahamu waliofanya hujuma hiyo.

“Tunafahamiana, tunajuana nani ana tabia gani; haiwezekani matukio sita yatokee na nyie hamuelewi,” alisema Chambo.

Mhandisi Chambo alimalizia kwa kuwataka viongozi wa vijiji hivyo kuhakikisha waliofanya hujuma hiyo wanapatikana kabla wiki hii inayoishia Novemba, 21 haijamalizika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (aliyesimama) akizungumza na serikali ya kijiji cha Njonjo, mkoani Lindi. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja

Mtwara yatakiwa kuongeza kasi ukusanyaji maduhuliNa Mohamed Saif

Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini imepongezwa kwa ukusanyaji wa maduhuli na kutakiwa kuongeza juhudi kwenye ukusanyaji

wa madini ya ujenzi na viwandani.Pongezi na wito huo ulitolewa hivi

karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja walipotembelea Ofisi ya Madini mkoani Mtwara na kuzungumza na watumishi wa ofisi hiyo.

Mhandisi Chambo alisema kutokana na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia unaopelekea Mkoa wa Mtwara kukua kwa kasi huku viwanda vingi vikijengwa na ujenzi wa kawaida pia ukiongezeka maradufu hivyo kuitaka Ofisi hiyo kuzidisha juhudi za ukusanyaji wa maduhuli wa madini ya ujenzi na viwandani.

“Mnatakiwa muongeze juhudi, fanyeni kazi kwa weledi; makusanyo yenu yanapaswa kwenda sambamba na ukuaji wa mkoa huu; nina imani mtafanya vizuri zaidi ya hapa,” alisema Mhandisi Chambo.

Kwa upande wake Mhandisi Masanja aliipongeza Ofisi hiyo na kuwataka wasibweteke badala yake

wazidishe juhudi za ukusanyaji wa maduhuli.

Vilevile, aliwaagiza kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake watembelee maeneo ya migodi badala ya kusubiri taarifa.

Aidha, taarifa ya Ofisi ya Kanda hiyo iliyowasilishwa na Kaimu Kamishna

Msaidizi wa Madini, Masai Mahende ilieleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2015/16 lengo la ukusanyaji wa maduhuli lilikuwa ni shilingi bilioni 3 na kwamba hadi kufikia hivi sasa Kanda hiyo imekusanya asilimia 21.36 ya lengo hilo.

Mahende alisema Ofisi ya Mtwara

imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa maduhuli na kubainisha kwamba kwa mwaka wa fedha 2014/15 lengo la ukusanyaji lilikuwa ni milioni mia tisa na Ofisi hiyo ilifanikiwa kukusanya milioni mia tisa kumi na tano na hivyo kuvuka lengo lililokuwa limewekwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (katikati) na Naibu wake Mhandisi Paul Masanja (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ofisi ya Madini ya Mtwara. Kushoto kwa Katibu Mkuu ni Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise.

Page 6: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

TANESCO watakiwa kuboresha hudumaNa Mohamed Saif

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetakiwa kuboresha huduma zake pamoja na kuzidisha kasi ya ufuatiliaji na ukusanyaji wa

madeni.Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati

na Madini, Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja walitoa agizo hilo hivi karibuni walipofanya ziara kwenye ofisi za Shirika hilo za Mkoani Mtwara na kuzungumza na wafanyakazi.

Taarifa iliyosomwa na Meneja wa TANESCO Mtwara, Mhandisi Aziz Salum ilieleza kwamba hadi hivi sasa jumla ya deni la mkoa ni shilingi bilioni 6 huku sababu ikielezwa kuwa ni ulipaji wa kusuasua wa bili za umeme.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Mhandisi Chambo alisisitiza kuongeza bidii ya kufuatilia madeni hayo.

Mhandisi Chambo aliwaagiza watumishi hao kutoruhusu malimbikizo ya madeni. “Mteja ukimuachia atalimbikiza tu, kwahiyo msiruhusu mtu kulimbikiza madeni,” alisema.

Mbali na hilo, Mhandisi Chambo alitoa wito kwa watumishi hao kuwa wabunifu, kutumia elimu na maarifa walionayo, kuzingatia weledi na kushirikiana ili kukabiliana na changamoto zinazokabili ofisi hiyo.

Aidha, aliwaonya watumishi hao kuacha tabia ya kukata umeme bila kuwa na sababu maalumu. “Atakayebainika

amekata umeme kwa makusudi bila sababu maalumu atafukuzwa kazi na kushitakiwa; Suala la kukatika hovyo kwa umeme hatutaki kulisikia,” alisema.

Alieleza umuhimu wa utoaji wa taarifa kwa wananchi na kuongeza kwamba “ikitokea kukawa na hitilafu na kuna umuhimu wa kukata umeme basi wananchi wapewe taarifa mapema iwezekanavyo; hatuwezi kuvumilia wananchi wakilalamika wakati nyie mpo tu ofisini,” alisema.

Alisema Mtwara inatarajiwa kuwa na viwanda vingi hivyo inabidi kujipanga kwa kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika kwa sababu soko litaongezeka maradufu.

“Mtwara ni Kituo muhimu sana, tunahitaji kuwa na viwanda vingi hapa na chanzo cha nishati ni hapa; lazima muoneshe kwamba nyinyi ndiyo kituo cha nishati nchi nzima,” alisema.

Kwa upande wake Mhandisi Masanja aliwapongeza watumishi hao kwa juhudi wanazoendelea nazo za kutoa huduma ya nishati ya umeme kwa mikoa ya Mtwara na Lindi.

Hata hivyo, Mhandisi Masanja aliwaasa watumishi hao kutoa ushirikiano katika kubaini maeneo yote yanayosababisha shida kwa Shirika hilo ili utatuzi wa haraka upatikane.

Alisema ni muhimu watumishi hao wakatambua uwepo wao kwenye shirika hilo. “Mjitambue kuwa hampo TANESCO kwa bahati mbaya ila mmeonekana mnafaa; hivyo badilikeni acheni kufanya kazi kwa mazoea,” alisema.

Alisema lengo la Serikali ni kutengeneza TANESCO ya kusifiwa na siyo ya kuzomewa. “Anayeweza kubadilisha hili ni wewe; wananchi wanapaswa kupata huduma bora,” alisema.

Vilevile aliwagiza kuwa wabunifu badala ya kusubiri taarifa na maagizo kutoka Makao Makuu. “Nyie ndio mpo field tunatarajia ushauri wenu, msikae mkisubiri makao makuu ndio wawaletee wazo la kuboresha, anzeni nyinyi,”

alisema.Naye Kamishna wa Nishati,

Mhandisi Hosea Mbise aliwausia watumishi hao kutovunjika moyo kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili badala yake wafanye kazi kwa bidii na kuhudumia wateja kwa ufanisi. “Taswira ya TANESCO inafanana; boresheni huduma ili tuue taswira mbovu tuliyokuwa nayo,” alisema.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa TANESCO Ofisi ya mkoa wa Mtwara.

Serikali yaagiza ulinzi shirikishi kwenye Miradi ya KitaifaNa Mohamed Saif

Serikali imewataka wasimamizi wa mradi wa Gesi Asilia kushirikiana na vijiji vinavyozunguka na kupitiwa na mradi huo kwenye suala la

ulinzi.Wito huo umetolewa hivi karibuni

na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja walipotembelea Kituo cha Kupokea Gesi Asilia ya Mtwara na Lindi cha Somangafungu (Somangafungu Gas Receiving Station) kilichopo wilaya ya Kilwa, mkoa wa Lindi.

Mhandisi Chambo alisema suala la ulinzi linapaswa kuwa shirikishi na hivyo kuwaagiza kushirikiana na Serikali ya vijiji vilivyo karibu na vituo mbalimbali vya mradi pamoja na vijiji vinavyopitiwa na bomba kubwa la kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

Alisema kwa kushirikiana na wanakijiji suala la hujuma ya miundombinu ya mradi huo halitotokea kwani wanakijiji wanapaswa kuwa sehemu ya mradi.

Alisema mradi huo ni wa wananchi na wanapaswa kushirikishwa na aliagiza kuboreshwa kwa mpango wa uwajibikaji kwa jamii (corporate social responsibility) ili jamii inayozunguka ipate kunufaika na kuulinda mradi huo.

“Wananchi huwa wanahujumu miradi sababu ya kutoona manufaa ya miradi husika. Hili sitaki litokee hapa; hakikisheni jamii inanufaika na huduma mbalimbali zinazohitajika na jamii husika,” alisema.

Mhandisi Chambo alisisitiza umuhimu wa utoaji wa taarifa kwa wananchi. Alisema wananchi wanayo haki ya kuelewa kuhusu masuala

mbalimbali ya mradi.“Tumeshuhudia mradi unakwenda

vizuri, lakini je wananchi wanapata taarifa hizi?,” alihoji Chambo na kuwataka watumie vyombo vya habari pamoja na vitengo vya habari ili kuwaeleza wananchi kuhusu hatua mbalimbali za mradi.

Kwa upande wake Mhandisi Masanja, alisema suala la ulinzi linapaswa kupewa umuhimu wa kipekee kwani mradi huo umegharimu fedha nyingi lakini pia ni muhimu katika kukuza uchumi na kwa maendeleo ya Taifa.

Alisema mbali na kutumia

vyombo vya usalama katika ulinzi wa miundombinu ya mradi huo ni vyema pia wanakijiji wakashirikishwa katika suala zima la ulinzi.

“Wanakijiji ndio wapo huku kwenye mradi na kwenye maeneo linapopita bomba la gesi, kwahiyo ni muhimu sana nao wakawa sehemu ya mradi. Changieni kwenye huduma za kijamii; fanyeni nao vikao kuelewa nini wanahitaji,” alisema Mhandisi Masanja.

Naye Meneja wa Kampuni ya Gesi Asilia (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba alisema tayari mpango wa CSR upo na unaendelea kufanya kazi na wananchi kwa ukaribu huku lengo likiwa ni kufanya mradi huo kuwa sehemu ya jamii.

“Kwa kupitia mpango tulionao wa CSR tumeweza kusaidia jamii katika masuala mbalimbali. Tumechimba visima kwa baadhi ya vijiji, tumechangia kwenye masuala ya afya. Mpango huu ni endelevu na sio wa mara moja,” alisema.

Katika ziara hiyo, viongozi hao walikagua shughuli mbalimbali ziazoendelea kwenye kituo hicho na kupewa taarifa kuhusu malengo na changamoto za Kituo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa pili kushoto)akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua Mradi wa Gesi Asilia

Page 7: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Mohamed Saif

Wataalamu wa K i t a n z a n i a wanaofanya kazi kweye Mradi Mkubwa wa Gesi

Asilia nchini wametakiwa kuhakikisha wanajifunza kwa ukamilifu shughuli zote za mradi huo kabla ya kuondoka mkandarasi.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja walipofanya ziara kwenye mradi huo kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa mradi huo.

Mbali na hilo, wafanyakazi hao walielezwa umuhimu wa kutanguliza uzalendo katika shughuli zao ili kuleta tija.

Mhandisi Chambo aliwataka wafanyakazi hao kutobweteka na badala yake wawe makini kujifunza masuala yote yanayohusu mradi huo ili pale mkandarasi anapomaliza muda wake waweze kuendesha wao wenyewe bila kukwama.

“Itafika wakati lazima Mkandarasi ataondoka hivyo kama mtashindwa kujifunza kipindi hiki itawapa shida siku za usoni, kwahiyo hakikisheni mnajifunza kila anachokifanya,” aliagiza Mhandisi Chambo.

Kwa upande wake Mhandisi Masanja aliwataka viongozi wa mradi huo kuandaa utaratibu wa kuweka wazi kazi zinazofanywa na mkandarasi ili kila mfanyakazi aelewe nini kinafanyika bila kuwepo na kizuizi cha aina yoyote.

“Kusiwepo na kizuizi chochote cha nyinyi kuelewa shughuli zinazofanywa na Mkandarasi. Pale ambapo mnafikiri bado vijana hawajaiva vizuri hakikisheni mkandarasi anawaelekeza.

Vilevile aliwaagiza kuboresha mazingira ya kazi na pia kuandaa

utaratibu utakaovutia vijana hao wa Kitanzania kuendelea kulitumikia Taifa lao kupitia mradi huo wa Kitaifa.

“Mtazame namna ambayo itawavutia wataalamu wetu waendelee kufanya kazi bila kufikiria kuondoka; mnaweza kuwapatia mafunzo ukashangaa wanahama na hivyo kusababisha kudorora kwa baadhi ya shughuli,” alisema.

Naye Meneja wa Kampuni ya Gesi Asilia (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba alieleza utaratibu unaotumiwa na wafanyakazi hao katika kujifunza shughuli mbalimbali za mradi.

Alisema wanaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na mkandarasi kwa lengo la kuelewa shughuli zinazofanyika ikiwa ni pamoja na matengenezo na uendeshaji wa mitambo.

“Tupo nao kwa ukaribu sana;

wanatueleza nini watatufundisha na kwa muda gani. Tunawauliza maswali, tunatazama namna wanavyoendesha shughuli za hapa; hivyo nina imani muda wao wa kuondoka ukifika vijana wetu watakuwa wameiva vya kutosha kuweza kusimamia mradi huu,” alisema.

Lengo kuu la ziara hiyo ilielezwa kuwa ni kujionea shughuli zinazoendelea kwenye mradi huo mkubwa wa Kitaifa wa gesi asilia pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa mradi huo.

Maeneo ambayo yalitembelewa na viongozi hao ni pamoja na Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia ya Mtwara na Lindi cha Somangafungu (Somangafungu Gas Receiving Station) kilichopo wilayani Kilwa, mkoa wa Lindi; Visima vya Gesi Asilia vya Mnazi Bay na Msimbati; Sehemu

iliyoathiriwa na mmomonyoko wa ardhi ya Msimbati na Kituo cha Kuchakata gesi asilia cha Madimba cha mkoani Mtwara.

Wengine walioongozana na viongozi hao katika ziara hiyo ni Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise, Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Gesi Asilia, Mhandisi Norbert Kahyoza, Meneja wa Kampuni ya Gesi Asilia (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Ziara hiyo ni ya kwanza kwa viongozi hao tangu wameteuliwa ikielezwa kwamba huu ni miongoni mwa mikakati waliyojiwekea ya kutembelea na kukagua miradi iliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake na vilevile kuzungumza na wafanyakazi wa miradi hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) akimsikiliza Meneja wa Kampuni ya GASCO, Mhandisi Kapuulya Musomba (katikati). Wa Kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar

Chambo (kushoto) na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja mara baada ya kukagua Kituo cha Kuchakata Gesi asilia cha Madimba

Baadhi ya mitambo katika Kituo cha kuchakata Gesi Asilia cha Madimba.

Wataalamu wa Gesi watakiwa kujifunza kwa Mkandarasi

Page 8: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Serikali imeagiza wachimbaji madini nchini kufuata sheria Na Mohamed Saif

Wachimbaji wadogo wa madini nchini wamesisitizwa kufuata sheria; kulipa kodi, mrabaha na ada za

mwaka kwa kila leseni ili kuwa na tija kwenye shughuli zao.

Wito huo umetolewa hivi karibuni Mkoani Katavi na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Magharibi, Aloyce Tesha kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Rukwa na Katavi kwa kushirikiana na Ofisi ya Madini Mpanda.

Tesha alisema lengo la semina hiyo ni kuwakumbusha na kuwaelimisha wachimbaji wadogo wa madini umuhimu na wajibu wao wa kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa. “Kodi ambazo zipo ni kwa mujibu wa sheria na kwa ajili ya manufaa yetu na maendeleo ya nchi,” alisema Tesha.

Pamoja na manufaa mengine, Tesha alisema ulipaji wa kodi ni chanzo cha mapato ya Serikali, na hurudi kwa wananchi kwa njia ya mfumo wa huduma mbalimbali kama, huduma za barabara na hospitali.

Tesha alisisitiza juu ya wamiliki wa leseni kujua wajibu wao kwakuwa wao ndiyo pekee ambao Sheria ya Madini inawatambua na sio wale wenye maduara (mashimo) na hivyo kuwataka kuweka utaratibu mzuri wa usimamizi wa leseni zao.

Aliongeza kuwa “Pale ambapo kweli mchimbaji hajazalisha lakini Mamlaka ya Mapato inamdai kulipa kodi namna pekee ni kwa ushahidi wa taarifa zake za kila mwezi au kila robo mwaka alizowasilisha ofisi za madini vinginevyo atawajibika kisheria,” alisema.

Aidha, Kamishna Msaidizi huyo, aliwaomba TRA pia kufanya semina ya mafunzo kwa mlipa kodi kwa ajili ya Wafanyabiashara wa madini wakubwa na wadogo (Mineral Dealers na Brokers). Vilevile aliwashukuru wachimbaji wote kwa ujumla wao kuitika wito wa kuhudhuria semina hiyo na kuwataka

watangulize uzalendo.“Nawapongeza kwa kuja kupata

elimu juu ya ulipaji kodi, kwani zamani watu wakisikia kuhusu kodi hawajitokezi

na ninawaomba daima mtangulize uzalendo,” alisema Tesha.

Meneja wa TRA Mkoa wa Rukwa na Katavi, John Palingo alizungumzia

juu ya sheria mpya ya usimamizi wa kodi iliyoanza kufanya kazi Agosti 01 mwaka huu kuhusu wachimbaji kupata kibali cha ulipaji kodi (Tax Clearance) kabla ya kupewa leseni za uchimbaji (PMLs) na wakati wanapohuisha leseni zao.

Vilevile aliwahimiza kuwa na rejista kwa kutunza kumbukumbu zote za malipo wanayofanya kwa vibarua wao na malipo mengine yote; kuweka sawa hesabu zao ili pindi TRA watakapokuja kukagua hesabu zao, mchimbaji asikwazike na makadirio ya kodi yatakayofanyika.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Katavi (KATAREMA), William Mbogo, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Majengo, Mpanda mjini aliiomba Serikali kuwatofautisha wachimbaji na wafanyabiashara wengine.

Alisema kuwa uhalisia wa shughuli za uchimbaji ni kama wa kilimo kwa kuwa mchimbaji wa madini anaweza kuwekeza na kukosa na hivyo kupata hasara na vilevile changamoto za teknolojia zinazowakabili pamoja na uhaba wa mitaji ya kufanyia shughuli za uchimbaji.

Palingo aliwatoa hofu wachimbaji madini na kuwasisitiza wajisajili ili waweze kupata kibali cha ulipaji kodi yaani Tax Clearance na hatimaye kama ni fursa za mikopo kwa mabenki waweze kuzipata. Vilevile alihitimisha kwa kuwataka wachimbaji madini kote nchini kulipa kodi kila mmoja kwa kadri anavyopata mapato yake.

Mada zilizotolewa katika semina hiyo ni pamoja na elimu kwa mlipa kodi juu ya lengo la kukusanya kodi; kusimamia sheria za kodi; kudhibiti ulipwaji kodi usiostahili, na msisitizo kuwa Kodi ni tozo la lazima kutoka pato stahiki kwa raia na wasio raia.

Semina hiyo ya siku moja ilishirikisha wachimbaji wadogo ambao ni wanachama wa Chama cha Wachimbaji Wadogo Katavi (KATAREMA), Maofisa wa TRA na Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Magharibi, Mpanda.

Baadhi ya wachimbaji madini wa Mkoani Katavi wakifuatilia mafunzo kuhusu masuala ya ulipaji kodi kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Rukwa na Katavi kwa kushirikiana na Ofisi ya Madini Mpanda.

Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Magharibi, Aloyce Tesha akitoa ufafanuzi katika semina ya elimu kwa mlipa kodi kwa wachimbaji wa madini. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoani Katavi (KATAREMA), William Mbogo, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Majengo, Mpanda na kushoto kwake ni Meneja wa TRA wa Wilaya ya Mpanda, Michael Temu. Wa kwanza kulia ni Meneja wa TRA wa Mkoa wa Rukwa na Katavi, John Palingo.

Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Magharibi, Aloyce Tesha akifafanua jambo katika semina ya elimu kwa mlipa kodi kwa wachimbaji wa madini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Rukwa na Katavi kwa kushirikiana na Ofisi ya Madini Mpanda.

Mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu, George Karras akiuliza maswali kwenye semina ya elimu kwa mlipa kodi kwa wachimbaji wa madini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Rukwa na Katavi kwa kushirikiana na Ofisi ya Madini Mpanda.

Page 9: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

ZIARA YA VIONGOZI LINDI NA MTWARA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja (kushoto) wakimsikiliza Meneja wa Kampuni ya GASCO, Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) akiwaeleza kuhusu Kituo cha Kupokelea Gesi cha Somangafungu. Katikati ni Msimamizi wa Kituo hicho, Mhandisi Msafiri Peter

Baadhi ya mitambo katika Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia kutoka Songosongo na Mtwara kilichopo Somangafungu wilayani Kilwa Mkoani Lindi

Baadhi ya mitambo ya kupokelea gesi asilia iliyopo kwenye maeneo kilipo kisima cha gesi asilia cha Mnazi Bay Namba 3

Sehemu ya Mitambo ya kuchakata gesi asilia ya Madimba inavyoonekana wakati wa usiku. Kituo hicho cha Madimba kilitembelewa na viongozi hao na kujionea shughuli zinazoendelea kituoni hapo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa tano kutoka kushoto) na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja (wa tano kulia) katika picha ya pamoja na wataalamu wa Kituo cha Kuchakata Gesi mara baada ya kutembelea kisima cha gesi asilia cha Mnazi Bay namba 3 (MB 3).

Page 10: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Veronica Simba

Baadhi ya Wataalam wa Sekta ya Nishati nchini wamebainisha kuwa moja ya changamoto kuu zinazoikabili sekta

hiyo hususan usalama wa nishati ni upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uendelezaji wa miradi ya umeme.

Changamoto hiyo na nyingine kadhaa, zilibainishwa hivi karibuni katika warsha ya mashauriano kuhusu uendelezaji wa sera ya usalama wa nishati kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki iliyofanyika Novemba 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akifafanua kuhusu changamoto hiyo, mmoja wa washiriki wa warsha, Mhandisi Salum Inegeja kutoka Wizara ya Nishati na Madini alisema katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati, hususan inayohusu njia za kusafirisha umeme, kunahitajika ardhi ya kutosha ambayo hutakiwa kutengwa kwa mujibu wa sheria na hutofautiana kulingana na kiwango cha umeme unaokusudiwa kuzalishwa na mradi husika.

“Kwa mfano, mradi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 400 unahitaji ardhi yenye upana wa mita 90 kuanzia eneo mradi unapoanzia hadi pale unapoishia. Halikadhalika, mradi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 220 unahitaji kutengewa ardhi yenye upana wa mita 60, wakati mradi wa aina hiyo wenye msongo wa kilovoti 132 unahitaji ardhi yenye upana wa mita 40 na ule wa msongo wa kilovoti 33 unahitaji ardhi yenye upana wa mita 30,” alifafanua Mhandisi Inegeja.

Alisema, ni changamoto kubwa kupata maeneo kama hayo yasiyo chini ya umiliki wa watu binafsi au taasisi kama Msikiti, Kanisa, Shule na nyingine kama hizo.

Changamoto nyingine kuu iliyotajwa kuwa inaukabili usalama wa nishati nchini ni kiwango kikubwa cha mtaji unaotakiwa kwa uwekezaji katika ujenzi wa vituo vya umeme.

Akifafanua kuhusu changamoto hiyo, Mhandisi Inegeja alitoa mfano wa gharama za ujenzi wa mradi wa umeme wa Kinyerezi I wenye megawati 185 kuwa ni Dola za Marekani milioni 182, wakati mradi wa ujenzi wa megawati 200 za Kituo cha umeme wa makaa ya mawe

pamoja na ujenzi wa njia ya usafirishaji umeme wa kilovoti 220 unagharimu Dola za Marekani milioni 460.

Pia, Mhandisi Inegeja alitoa mfano wa mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi II wenye megawati 240 kuwa unagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 344, Mradi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 400 (Gridi ya Kaskazini Magharibi kutoka Mbeya hadi Nyakanazi) unaogharimu Dola za Marekani milioni 663.92, Mradi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 400 (Kaskazini Mashariki kutoka Dar es Salaam – Chalinze – Tanga – Arusha) wenye gharama ya Dola za Marekani milioni 693 na Upanuaji wa Gridi kwa ajili Mradi wa

Umeme Vijijini wenye msongo wa kilovoti 132 ambao unagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 805.25.

Aidha, changamoto nyingine zilizoainishwa ni pamoja na upungufu wa wataalam wa ndani wanaohitajika katika kuendeleza baadhi ya miradi ya umeme, umbali mrefu kutoka katika Vituo vya kuzalishia umeme mpaka kwenye Vituo vya kuhifadhia umeme, ukame wa maji unaotokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika Mabwawa ya kuzalishia umeme ambao huathiri uzalishaji wa umeme pamoja na wizi wa miundombinu ya kusafirishia na kusambazia umeme.

Awali, akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Nishati Mbadala, Mhandisi Leonard Ishengoma alisema kuwa nchi wanachama wa Afrika Mashariki, zimedhamiria kuhakikisha kunakuwa na nishati ya uhakika, ya bei nafuu na ya kutosha kwa nchi hizo ili kuchagiza maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika ukanda husika.

Aliongeza kwamba, katika kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa, ni lazima kuwepo na sera thabiti inayosimamia pamoja na mambo mengine usalama wa nishati.

Uendelezaji wa Sera ya Mfumo wa Usalama wa Nishati imekuja kufuatia maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa 10 wa Sekta ya Nishati uliofanyika jijini Arusha Septemba 11, mwaka huu.

Sera ya Mfumo wa Usalama wa Nishati inaendelezwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Kiuchumi Afrika, Ofisi ndogo ya eneo la Afrika Mashariki (UNECA) iliyopo Kigali.

Sera ya Mfumo wa Usalama wa Nishati inayopendekezwa inalenga kushughulikia changamotozinazokabili usalama wa nishati kwa nchi washirika.

Ardhi yatajwa kuwa changamoto kwa usalama wa nishati nchini

Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala, Mhandisi Leonard Ishengoma, akisoma hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya mashauriano kuhusu Uendelezaji wa Sera ya Usalama wa Nishati kwa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki iliyofanyika Novemba 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, akiwasilisha Mada kuhusu changamoto zinazokabili usalama wa nishati nchini katika warsha ya mashauriano kuhusu Uendelezaji wa Sera ya Usalama wa Nishati kwa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki iliyofanyika Novemba 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Page 11: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

11BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Zuena Msuya, Morogoro

Wataalam wa madini nchini wamepata elimu ya mazingira pamoja na mbinu mpya za ukaguzi wa migodi ya

Makaa ya Mawe ili kubaini uendeshaji wa migodi hiyo unaozingatia kanuni zote za afya, usalama na utunzaji wa mazingira.

Wataalam hao walipata mafunzo mjini Morogoro yakilenga kuwajengea uwezo wa kutathmini athari za mazingira katika migodi ya makaa ya mawe na kujifunza mbinu mpya za ukaguzi migodini.

Wakizungumza wakati wa mafunzo hayo, washiriki wa mafunzo hayo, Mhandisi Gabriel Senge kutoka Ofisi ya Madini Kanda ya Kati, Singida alisema kuwa, mafunzo kama hayo yanawasaidia kubaini na kudhibiti athari

mbalimbali zinazotokea katika sekta ndogo ya uchimbaji wa makaa ya mawe ambayo kwa sasa Tanzania inatarajia kuanza kuchimba katika maeneo mbalimbali.

“Tanzania hatuna uzoefu sana katika uchimbaji wa makaa ya mawe japo yapo kwa wingi nchini ukilinganisha na uchimbaji wa dhahabu, hivyo tunatakiwa kujifunza kila mbinu ili tutakapohitajika tuweze kufanya kazi hii kwa ufanisi na kuepusha madhara kutokea,” alisema Mhandisi Senge.

Kwa upande wake Kamishna Msadizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, Mhandisi David Mulabwa alisema wataalam wa madini na wakaguzi wa migodi wanatakiwa kwenda na wakati katika kufanya kazi hiyo na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.

Mulabwa aliongeza kuwa kwa

sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa ya tabia nchi duniani hivyo suala la mazingira linapaswa kupewa kipaumbele katika shughuli zote za uchimbaji ili kuepusha madhara zaidi kwa nchi na dunia kwa ujumla.

“Makaa ya mawe yanatakiwa kuchimbwa kwa umakini mkubwa kwani yanaathari kubwa katika mazingira yanayotuzunguka, na kwa kuwa nchi inatarajia kujikita zaidi huko kwa lengo la kuzalisha umeme ni vyema sasa kipaumbele kikatolewa katika kulinda mazingira na elimu zaidi ikatolewa hata kwa wananchi wanaozunguka maeneo husika,” alisema Mlabwa.

Katika mafunzo hayo wataalamu

walijifunza tathmini ya athari za mazingira na kijamii miradi ya makaa ya mawe kuanzia kwenye utafiti, uchimbaji na uzalishaji wa umeme.

Aidha katika mafunzo hayo wataalamu hao walijifunza tahadhari zote za kuchukua katika usimamizi wa madini ya makaa ya mawe pamoja na changamoto za usimamizi wa madini ya makaa ya mawe na fursa zinazoambatana na madini ya makaa ya mawe.

Mafunzo hayo ni ya pili kutolewa na Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya India( CES), ambapo mafunzo kama haya yalifanyika mwezi Juni mwaka huu 2015 mjini Bagamoyo ambayo pia yalilenga kuwajengea uwezo wakaguzi wa migodi wa Wizara ya Nishati na Madini.

Mafunzo hayo ya siku nne yamewashirikisha zaidi ya wataalam wa madini 70 wakiwemo Makamishna Wasaidizi kutoka sehemu mbalimbali nchini, pamoja na wadau wa mazingira kutoka Taasisi mbalimbali za Kiserikali.

Wataalam wa madini wapewa mbinu mpya ukaguzi migodi

Wataalamu wa madini wakifuatilia mada kuhusu tathmini ya athari za mazingira katika migodi ya makaa ya mawe

Mkaguzi wa migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini , Mhandisi Assa Mwakilembe akitoa mada wakati wa semina ya wataalam wa madini nchini iliyofanyika mjini Morogoro.( hawapo pichani).

Wataalam wa madini wakimsiliza mtoa mada wakati wa semina kuwajengea uwezo kuhusu tathmini ya athari za mazingira katika migodi ya makaa ya mawe iliyofanyika mkoani Morogoro.

Wataalam wa madini kutoka maeneo mbalimbali nchini katika picha ya pamoja wakati wa semina ya kuwajenga uwezo wataalam hao wa kuhusu tathmini ya athari za mazingira katika migodi ya makaa ya mawe iliyofanyika mkoani Morogoro.

Page 12: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Wataalam wa madini zingatieni elimu ya mazingiraNa Zuena Msuya, Morogoro

Wataalam wa madini nchini wametakiwa kuzingatia elimu i n a y o t o l e w a kuhusiana na

masuala ya tathmini ya athari za mazingira pamoja na kijamii katika miradi ya Makaa ya Mawe kuanzia kwenye utafiti, Uchimbaji ili kufanya uchimbaji salama na kulinda mazingira.

Wito huo umetolewa hivi karibuni mjini Morogoro na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka wakati wa ufunguzi wa semina iliyolenga kuwajengea uwezo wataalam wa madini na mazingira nchini kuhusu tathmini ya athari za mazingira katika migodi ya makaa ya mawe.

Mhandisi Mchwapaka alisema kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa muda muafaka kwa kuwa Tanzania sasa iko mbioni kuanza kuchimba makaa ya mawe ili kuzalisha umeme kama zinavyofanya nchi nyingine duniani ikiwemo India na Afrika Kusini.

“India inazaidi ya miaka mia moja inatumia makaa ya mawe kuzalisha umeme na kuendesha viwanda vyao na ni tegemeo kubwa la vyanzo vya umeme nchini humo, Tanzania tunayo makaa ya mawe ya kutosha na nivyema kujiandaa sasa kwani ndani ya miaka mitatu au mitano ijayo tutajikita zaidi huko ili kuzalisha umeme”, alisema Mhandisi Mchwapaka

Aliongeza kuwa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya India( CES), watakuwa wakitoa mafunzo kila wakati ili kutanua wigo wa elimu na kuwaandaa wataalam wake nchini ili kufanya uchimbaji salama na kulinda mazingira.

Pia alisema elimu hiyo itatolewa kwa wananchi ambao wanaishi maeneo yanayozunguka migodi ya makaa ya mawe ili kutambua namna

ya kulinda mazingira wao wenyewe ili kuepusha madhara; elimu hiyo itawasaidia wananchi hao kuwa mabalozi wazuri katika kuhifadhi mazingira.

Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya India( CES) Sujit Kumar Singh alisema

kuwa kwa sasa India inazalisha tani milioni 560 ya makaa ya mawe ambayo huzalisha umeme na pia kutumiwa viwandani ambapo nchi hiyo imejiwekea lengo la kuzalisha mabilioni ya tani za makaa ya mawe ifikapo mwaka 2020.

Singh alisema India imekuwa ikitegemea sana makaa ya mawe na pia imekuwa ikitumia muda mwingi kutoa elimu kwa wataalam wake na wananchi ili kuepusha madhara katika maeneo ya migodi na mazingira kwa jumla.

Hata hivyo Singh, aliipongeza Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwaandaa mapema wataalam wake katika kulinda mazingira na kutambua athari zinazoweza kutokea pindi Tanzania itakapojikita zaidi katika uchimbaji wa makaa ya mawe kwani yanaathari kubwa kimazingira endapo uchimbaji wake hautazingatia kanuni na taratibu bora za uchimbaji.

Hadi sasa Tanzania ina kiasi cha zaidi ya tani bilioni 1.5 ya makaa ya mawe yaliogundulika nchini huku tafiti mbalibali zikiendelea kufanyika ili kubaini kiasi kingine cha makaa ya mawe katika maeneo yalioonesha viashiria vya kuwepo madini hayo.

Baadhi ya maeneo ambayo yamebahatika kuwa na makaa ya mawe ni pamoja na Ngaka, Mchuchuma, Liganga pamoja na Kiwira, huku maeneo ya Ngaka tayari wameanza kuchimba makaa hayo wakati ambapo maeneo ya Kiwira yakiwa mbioni kuanza shughuli za uchimbaji na uzalishaji baada ya kusitishwa kufanya kazi hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

Mafunzo haya ni ya pili kutolewa na Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya India, mafunzo ya kwanza yalifanyika tarehe 1 - 4 Juni, 2015 mjini Bagamoyo ambayo yalilenga kuwajengea uwezo wakaguzi wa migodi wa wizara ya nishati na Madini. Katika mafunzo hayo wakaguzi walifundishwa mbinu mbalimbali ili kukagua migodi na kubaini uendeshaji wa migodi hiyo unazingatia kanuni zote za afya usalama na utunzaji wa mazingira.

Mafunzo hayo ya pili yalifanyika tarehe 16 - 19 Novemba 2015 yakilenga kujifunza sekta ya makaa ya mawe na changamoto zake. Katika mafunzo haya wataalamu walijifunza tathmini ya athari za mazingira na kijamii katika miradi ya mkaa wa mawe kuanzia kwenye utafiti, Uchimbaji na uzalishaji wa umeme. Aidha, katika mafunzo haya wataalamu waliohudhuria watajifunza tahadhari zote za kuchukua katika usimamizi wa madini ya makaa ya mawe. Changamoto za usimamizi wa madini ya makaa ya mawe na fursa zinazoambatana na madini ya makaa ya mawe.

Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka akizungumza jambo wakati akifungua semina ya wataalam wa madini nchini( hawapo pichani) iliyolenga kuwajengea uwezo wa kuhusu tathmini ya athari za mazingira katika migodi ya makaa ya mawe.

Mtoa mada katika semina ya wataalam madini inayofanyika mjini Morogoro, Sakti Banerjee kutoka Chuo cha Madini India.

Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ,Masinde Bwire akiuliza swali kwa wakufunzi wa semina hiyo wakati wa mafunzo hayo

Sehemu ya wataalam wa madini waliopata Semina kuwajengea uwezo wa kuhusu tathmini ya athari za mazingira katika migodi ya makaa ya mawe kutoka Chuo cha Madini nchini India yanayofanyika mjini Morogoro wakimsikiliza mtoa mada (hayupo pichani)

Page 13: MEM BULLETIN 94 (2).pdf

13BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Na Zuena Msuya Morogoro

Wataalam wa M a z i n g i r a wameishauri S e r i k a l i kuangalia upya

sheria ya Ardhi, Mazingira na Sekta ya madini hususan suala la fidia ili kuweka uwiano sawa na kuondoa migogoro ya ardhi na ulipaji wa fidia katika maeneo ya migodi.

Hayo yalibainishwa na baadhi ya Maafisa wa mazingira waandamizi akiwemo Masinde Bwire kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Pendo Kundya kutoa Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira( NEMC) wakati wa semina ya wataalam wa madini nchini iliyolenga kuwajengea uwezo wa kutathmini athari za mazingira pamoja na kijamii katika migodi ya makaa ya mawe iliyofanyika mkoani Morogoro hivi karibuni.

Maafisa hao wa mazingira walisema kwa sasa Tanzania imekuwa ikikabiliwa na migogoro ya mara kwa mara kuhusiana na fidia katika maeneo ya migodi ambayo yamekuwa yakisababishwa na kutokuwepo kwa kiwango maalumu cha fidia ambacho kinakidhi matakwa ya walengwa ukilinganisha na nchi ambazo ni wachimbaji na watumiaji wa wakubwa wa madini hasa makaa ya mawe kama India na Afrika kusini.

Afisa mwandamizi wa mazingira kutoka Ofisi ya Makam

wa Rais, Masinde Bwire alisema kanuni za kimazingira ni muhimu zikapitiwa upya ili kuweka mkazo hususan katika migodi ya makaa ya mawe ambayo baada ya miaka michache Tanzania inatarajia kujikita zaidi katika eneo hilo.

“ Ni muhimu kuwepo na mipango thabiti ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe na mipango hiyo ishirikishe wadau wa Mazingira, Ardhi na Sekta ya madini tangu katika hatua za awali na hii itasaidia kuweka wazi taratibu za fidia sambamba na sheria ya ardhi na pia kuondoa migogoro wakati wa kulipa fidia ili kupisha miradi hiyo ifanyike kwa wakati”, alisema Bwire .

Kwa upande wake Afisa Mazingira Mwandamizi Pendo Kundya kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira( NEMC) alisema kuna mapungufu katika sheria za Sekta madini, Mazingira na Ardhi nchini hivyo ni wakati muafaka wa kuwa na sheria, kulingana na aina ya madini inayochimbwa kama zinavyofanya nchi nyingine duniani.

Pia alisema kuwa, mamlaka husika zinatakiwa kutenganisha sheria za kulinda rasilimali hiyo na mazingira pamoja ardhi ili kila moja iweze kuwa na tija kwa wakati husika; pamoja na kuwa na uewelewa wa pamoja katika sekta zote zinazohusika ikiwemo ardhi, madini na mazingira.

“India ina sheria nyingi sana katika masuala ya madini, ardhi na mazingira na katika madini

ya makaa ya mawe sheria yake ni tofauti na madini mengine tofauti na ilivyo nchini kwa sasa na kuna sheria moja tu ya kusimamia masuala ya uchimbaji wa madini bila kujali aina ya madini husika kama makaa ya mawe, dhahabu, Tanzanite na mengine,” alisema Kundya.

Vilevile, alishauri kuwa suala kurekebisha sheria hizo liendane na kuongeza rasilimali watu ili kuweza kusimamia ipasavyo shughuli za utunzaji wa mazingira katika maeneo ya migodi kwa kuwa waliopo sasa hawakidhi

kiwango na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yao kama inavyopaswa na kutoa mwanya kwa wanaokiuka taratibu na sheria kuendelea kufanya hivyo.

Kuanzia mwaka 2013 Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC lilianza rasmi kazi ya ukaguzi migodini ambapo ilitoa adhabu ya kulipa fidia kuifungia baadhi ya migodi mikubwa mitatu nchini kwa kosa la kutokidhi viwango vya sheria za kutunza mazingira zinazotakiwa nchini ambapo adhabu hiyo ilitekelezwa.

Wataalam wabaini mapungufu sheria ya ardhi, mazingira, madini

Mhandisi Nchagwa Marwa kutoka Wakala wa ukaguzi wa madini Tanzania( TMAA) akitoa mada kuhusu utekelezaji wa sera ya kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu migodini wakati wa semina ya kuwajemga uwezo wataalam wa madini kuhusu tahmini ya athari za mazingira na jamii katika sehemu za migodini iliyofanyika mkoani Morogoro hivi karibuni..

Sehemu ya washiriki wa semina ya kutathmini athari za mazingira na jamii katika sehemu za migodi hususan makaa ya mawe iliyofanyika mjini morogoro hivi karibuni.

Baadhi ya wataalamu wa madini wakiwa katika makundi kujadili mada zilizokuwa zikitolewa na wakufunzi kutoka India wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wa kutathmnini athari za mazingira na jamii katika sehemu za migodini ili kuona namna ya kuzitekeleza.