mem bulletin 113 edition

Upload: ahmad-issa-michuzi

Post on 07-Jul-2018

437 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    1/20

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM)

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 113 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Machi 31 - Aprili 6, 2016Bulletinews

     

    http://www.mem.go.tz

     

    Prof. Sospeter Muhongo

    98% Bomba la Mafutakupita Tanzania >>SOMA UK. 2

       M  p  a  n  g  o  w  a  u   t  e   k  e   l  e  z  a   j    i   w

      a  m  r  a   d   i   w  a   b  o  m   b  a   l  a   M  a   f  u   t  a

       U  g  a  n   d  a  -   T  a  n  z  a  n   i  a

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    2/20

    BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    2

    Teresia Mhagama naZuena Msuya

    Imeelezwa kuwa Tanzania inavigezo mbalimbali ambavyovinaifanya ijiamini kwa asilimia98 kuwa mradi wa bomba lakusafirishia mafuta kutoka

    Ziwa Albert nchini Uganda utapitiaKaskazini mwa Tanzania hadi Bandariya Tanga badala ya nchini Kenya.

    Hayo yameelezwa na Katibu Mkuuwa Wizara ya Nishati na Madini,Profesa Justin Ntalikwa wakati wa

    kikao chake na wafanyabiashara wamafuta nchini ambacho kililengakujadiliana nao kuhusu fursa zauwekezaji zitakazotokana na mradihuo endapo utapita nchini.

    Profesa Ntalikwa alivitaja vigezohivyo kuwa ni uzoefu wa Tanzaniakatika ujenzi wa mabomba yakusafirisha nishati mbalimbali ikiwemoBomba la Mafuta la kutoka Tanzaniahadi Zambia (TAZAMA), Bomba lakusafirisha gesi kutoka SongoSongohadi Dar es Salaam, Bomba lakusafirisha gesi kutoka eneo la MnaziBay hadi Mtwara, pamoja na Bombakuu la gesi kutoka mkoani Mtwara hadiDar es Salaam lenye kipenyo cha inchi36 hivyo uzoefu huo utasaidia katika

    kupunguza muda wa ujenzi wa bombala mafuta ambalo kipenyo chake niinchi 24.

    “Tumewaeleza wenzetu kuwaSerikali ya Tanzania pia ilishajengauwezo mkubwa katika masuala yakutwaa, kumiliki na kulipa madaiya wananchi wanaopisha miradi yamabomba na shughuli hizi zimekuwazikifanywa kwa wepesi na umakinimkubwa ikiwemo umakini katikakufuata kanuni na sheria za mazingira,hivyo haitatuwia ngumu katikakutekeleza mradi huu,” alisema ProfesaNtalikwa.

    Alitaja kigezo kingine kuwa niubora wa bandari ya Tanga ambayoimeonekana kuwa ni bora zaidi

    ukilinganisha na Bandari nyingineAfrika Mashariki kwa kuwa ina kingoza asili (naturally sheltered) na kinakirefu hivyo kupunguza muda nagharama za ujenzi kwa kuwa uchimbajiwa kuongeza kina hauhitajiki naitakuwa na uwezo wa kupakia mafutakatika kipindi cha mwaka mzima.

    Profesa Ntalikwa aliongeza kuwanjia ya kupitia Tanzania hadi Bandariya Tanga ni bora zaidi kwa upande waujenzi wa bomba hilo kwa kuwa haipitisehemu yenye makazi ya watu wengi,sehemu za hifadhi na haina miinukomikali hivyo kupunguza muda waujenzi na gharama za ujenzi.

    “Hivyo ndugu zangu tumewaitawafanyabiashara hawa wa mafuta

    nchini ili waweze kutumia fursambalimbali zitakazotokana na

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) akiwa na Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Profesa James Mdoe (wa tatu kulia), NaibuKatibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo (wa pili kulia),

    na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Norbert Kahyoza (wa kwanza kulia)wakiwa katika mkutano na wadau wa sekta ya mafuta hawapo pichani, mkutano ulilenga kuwaeleza fursa zauwekezaji zitakazotokana na mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda endapo litapita Tanzania.

    Uhakika wa Bomba la Mafuta

    kupita Tanzania ni asilimia 98

    Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini. Profesa Justin Ntalikwa ( katikati) akiongoza mkutano katiyake na wadau wa Sekta ya Mafuta katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es salaam,Mkutano wake na wadau hao ulilenga kueleza fursa za uwekezaji zitakazopatikana endapo ujenzi wa bombala mafuta kutoka nchini Uganda litapita Tanzania. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishatina Madini (Madini), Profesa James Mdoe, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi JulianaPallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Norbert Kahyoza na Mkurugenziwa Mkondo wa Chini kutoka TPDC, Dkt. Wellington Hudson.

    >> Inaendelea Uk. 3

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    3/20

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    mradi huo na kuzichangamkia nawao wamepokea vizuri suala hili nawameahidi kushirikiana na Serikalikatika kuhakikisha kwamba Tanzanianapata mradi huu muhimu,” alisemaProfesa Ntalikwa.

    Awali akizungumza kuhusu mradihuo, Mkurugenzi wa Mkondo wa Chinikutoka Shirika la Maendeleo ya PetroliTanzania (TPDC), Dkt. WellingtonHudson alieleza kuwa Uwekezaji mradiwa bomba hilo unakadiriwa kugharimuDola za Marekani bilioni 4 na kwambaBomba lote litakuwa na urefu wakilomita 1403 na kipenyo cha inchi 24.

    Alisema kuwa hatua zilizofikiwahadi sasa ni kuwa Serikali za Tanzaniana Uganda zilishatiliana sahihiMkataba wa Maelewano (MOU)arehe 12 Oktoba 2015 ambao kwaasa ndiyo mwongozo wa kukamilisha

    majadiliano ya mikataba mbalimbaliambayo inayohitajika kisheria.

    “Kwa sasa lengo ni kukamilishamazungumzo mapema na kusainiwakwa Mikataba husika, ili kuruhusuhughuli za upatikanaji wa mkuza

    na ujenzi kuanza maramoja. Ujenziunatarajiwa kukamilika ndani ya miakamitatu baada ya Mikataba yote muhimukusainiwa,” alisema Dkt. Wellington.

    Alitaja baadhi ya faidazitakazopatikana kutokana na mradihuo kujengwa Tanzania kuwa nikuchochea shughuli za utafutaji

    mafuta nchini hususani katika maeneoinapopita bomba la mafuta, Kuimarishamatumizi ya Bandari ya Tanga nahivyo kuongeza mapato ya Serikalikutoka katika bandari hiyo pamoja

    na kupatikana mkuza utakaowezakutumika siku za baadaye kwa shughulinyingine za maendeleo ikiwemokusafirisha gesi na mafuta katika mikoaya Kaskazini, Kanda ya Ziwa na nchi za

     jirani.Faida nyingine zitakazotokana na

    mradi huo ni Ujenzi wa barabara mpyatakriban kilometa 200 na uboreshaji wa barabara zilizopo takriban kilometa 150na madaraja katika maeneo linapopita

     bomba,

    Pia kuongezeka kwa fursa ya Shirikala Reli Tanzania kufanya biashara yakusafirisha kiwango cha mabombayanayokadiriwa kufikia 123,000 kupitiamiundombinu ya reli iliyopo, fursa zaajira kwa takribani watu 15,000 wakatiwa ujenzi na watu wapatao 1,000 wakati

    wa kuendesha mradi.Dkt. Wellington pia aliwaasaWatanzania kuchangamkia fursazitakazojitokeza endapo bomba hilolitapita nchini na kuzitaja baadhi ya

    fursa hizo kuwa ni kazi za kuunganishamabomba (welding), huduma za afya,huduma za mabenki, huduma za usafina kudhibiti taka, Kandarasi za kujengana za umeme, huduma za Bima,Huduma za mawasiliano na mtandao,kandarasi za ujenzi wa Mabarabara na

    Huduma za uuzaji mafuta.Alitaja fursa nyinginezitakazopatikana kuwa ni Karakana zaukarabati wa mashine mbali mbali namagari, Huduma za sheria, Hudumaza Mawasiliano na Kandarasi zakusambaa vifaa vya ujenzi.

    Kwa upande wake Mwenyekitiwa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt.Gideon Kaunda akiongea kwa niabaya wafanyabiasahara hao aliishuukuruSerikali kwa kuamua kuwashirikishakatika suala hilo muhimu kwa manufaaya nchi na kuahidi kushirikiana nayo ilikufikia lengo la Serikali la kuhakikisha

     bomba hilo la Mafuta linapita Tanzanialinafanikiwa.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Profesa Justin Ntalikwa ( katikati )akizungumza na waandishiwa habari wakati wa mkutano wake na wadau wa sekta ya mafuta (hawapo pichani)uliofanyika jijini Dar esSalaam. Mkutano ulilenga kuwaeleza fursa ya uwekezaji zitakazotokana na mradi wa bomba la mafuta kutokaUganda endapo litapita Tanzania.

    Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt. GideonKaunda (katikati ) akizungumza na waandishi wa habariwakati wa mkutano wa Wizara na wadau wa sektaa mafuta (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es

    alaam. Mkutano ulilenga kuwaeleza fursa ya uwekezajiitakazotokana na mradi wa bomba la mafuta kutoka

    Uganda endapo litapita Tanzania.

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MSANIFU: Lucas GordonWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson

    Mwase, Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    INCREASE EFFICIENCY 

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Bomba la Mafuta>> Inatoka Uk. 2

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    4/20

    4   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikiaNishati Dkt Juliana Pallangyo( katikati) akieleza jambo wakati wamkutano wa majumuisho wa wakandarasi wanaotekeleza miradi yausambazaji umeme vijijini inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini(REA). Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa SospeterMuhongo.

    Mkurugenzi wa Ufundi wa REA, Mhandisi Bengiel Msofe akifafanua jambo wakati wa mkutano wa majumuisho wa wakandarasiwanaotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini. Wengine ni Waziriwa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Naibu

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia NishatiDkt. Juliana Pallangyo (katikati)

    MCC kutoathiri miradi ya REANa Mwandishi wetu 

    Waziri wa Nishati naMadini, Profesa SospeterMuhongo amesemakuwa kwa Tanzania

    kutopatiwa fedha na Marekani kupitiaMfuko wa Changamoto za Milenia(MCC) ambazo ni Dola za Marekanimilioni 472 kwa ajili ya miradi ya

     barabara, maji na umeme hazitaathirimiradi ya usambazaji umeme vijijiniinayofadhiliwa na Wakala wa NishatiVijijini (REA).

    Aliyasema hayo jijini Dar essalaam wakati akifanya majumuishoya vikao vyake na wakandarasiwanaosambaza umeme vijijiniambavyo vilianza tarehe 29 Machi,2016 na kuhudhuriwa na watendajiwa Wizara, Shirika la Umeme Nchini(TANESCO) na REA.

    Profesa Muhongo alisema kuwafedha hizo zilikuwa haziendi mojakwa moja katika mfuko wa REA walaSerikali kuu kama inavyodaiwa nawatu wengi.

    “Tulikuwa tunakaa na MCC,tunasema bwana katusaidiekusambaza umeme mfano Shinyanga,kwa hiyo anachukua zile fedha zakeanaenda na wakandarasi wake mojakwa moja Shinyanga, huku miradi yaREA ikiendela kama ilivyopangwa,”alisema Profesa Muhongo.

    Alisema kuwa miradi ya MCCilikuwa ikisaidia juhudi za Serikalikatika kusambaza umeme vijijinina mijini lakini fedha hizo zilikuwahazipelekwi REA.

    Alisisitiza kuwa kabla ya MCCkuanza kutoa fedha za kuendelezamiradi ya umeme, Serikali tayariilikwishaanza kusambaza nishati hiyokwa wananchi na kwamba kuna

    wadau mbalimbali wanaochangiamiradi hiyo na hata kamawasipochangia, jukumu la Serikalila kuwasambazia wananchi wakeumeme linabaki kuwa pale pale.

    “Isichukuliwe kwamba fulaniasipochangia, basi Taifa zima miradiyake imekufa, hivyo dhana yakusema kwamba fedha hizo zilikuwazinapelekwa REA ni upotoshwaji wahali ya juu, kwamba REA itaathirikakwa kukosa hizo fedha si kweli,”alisema Profesa Muhongo.

    Akielezea utekelezaji wa miradiya REA Awamu ya Pili, Profesa

    Muhongo alisema awali jumla yashilingi bilioni 881 zilitengwa lakinizikaongezeka shilingi bilioni 60ambapo hadi kukamilika kwa Awamuhiyo ya Pili jumla ya vijiji 2500vinatarajiwa kupata umeme na watejawa awali 250, 000 kuunganishwana huduma hiyo hadi kufikia mweziJuni, mwaka huu ambao ni ukomowa utekelezaji wa awamu hiyo.

    Kuhusu tathmini ya wakandarasiwanaosambaza umeme vijijini,Profesa Muhongo alisema kuwawakandarasi wengi wametekelezamiradi hiyo kwa asilimia kati ya 75 na85, huku wengine wakivuka wastaniwa REA ambao ni asilimia 87.

    Katika hatua nyingine, Profesa

    Muhongo alitoa miezi miwili kwawakandarasi ambao hawajakamilishamiradi ya umeme kukamilishamiradi hiyo na kusisitiza miradi yotekukamilishwa mwezi Mei au Juni15, mwaka huu kabla ya kuanza kwaAwamu ya Tatu inayotarajiwa kuanzaifikapo Julai mosi mwaka huu.

    Aliongeza kuwa katika utekelezajiwa miradi ya umeme vijijini, Serikaliimebaini kuwa wapo wakandarasiwanaotumia vifaa hafifu kamatransfoma na nguzo na kusisitiza

    ukaguzi kufanyika na kampuniitakayobainika kutumia vifaa hafifuitafutwa mara moja kabla ya Awamuya Tatu.

    Ili kutekeleza miradi hiyo kwaufanisi, Profesa Muhongo aliitakaTANESCO kwa kushirikiana naWizara kuhamasisha wananchi hasawaishio vijijini kujiunga na hudumaya umeme, na TANESCO kusogezahuduma karibu na wananchiili kuepusha wananchi kusafiriumbali mrefu kufuata hudumaya kuunganishiwa umeme auchangamoto nyingine zinazotokana

    na nishati hiyo.Akizungumzia kuhusu malipo ya

    wakandarasi hao, Profesa Muhongoalisema kuwa Serikali imeendeleakulipa wakandarasi wote kwa wakatikulingana kazi zinazofanyika.

    Wakati huo huo Profesa Muhongoalisema kuwa mitambo ya kuzalishaumeme kwa kutumia gesi asiliaya Kinyerezi I kwa sasa inazalishaMegawati 150 na kuongeza kuwamalipo kwa ajili ya ujenzi wa mitamboya Kinyerezi II inayojengwa nakampuni ya Sumitomo kutoka nchiniJapan yamekamilika

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo(kushoto) akifafanua jambo wakati wa majumuisho ya mkutano waWakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijiniinayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), hawapo pichani.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madinianayeshughulikia Nishati Dkt Juliana Pallangyo

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    5/20

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Stamico yajizatiti kuuboresha mgodi wa TanzaniteNa Veronica Simba -Mirerani

    Imeelezwa kuwa, hatua ya Shirika

    la Madini la Taifa (STAMICO)kuweka wawakilishi wake katikaMgodi wa Tanzanite uliopo katika

    eneo la Mirerani Kitalu C, imeoneshamafanikio makubwa ikiwemo kupunguakwa wizi wa ndani na kuimarika kwamifumo ya uendeshaji Mgodi.

    Aidha, imeelezwa kuwa katikakipindi cha ubia wa Shirika hilo naKampuni ya Madini ya Tanzanite One(TML), Juni 2013 hadi Februari 2016,umla ya karati 30, 674, 250 za Tanzanite

    zimezalishwa na kuuzwa kwa thamaniya Dola za Marekani milioni 13.64.

    Kaimu Mkurugenzi Mkuu waSTAMICO, Zena Kongoi alisema hayoijini Arusha hivi karibuni, wakati wa

    ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge

    ya Nishati na Madini katika Migodimbalimbali inayochimba madiniya Tanzanite ukiwemo Mgodi waTanzanite One.

    Alisema kuwa Mgodi umewezakuchangia pato la Taifa kwa kurejeshamrabaha wa asilimia Tano (5.0) yamauzo ambayo ni sawa na Dola zaMarekani 481, 271.04 kwa Serikali.

    Vilevile, Kongoi alitaja mafanikiomengine yaliyopatikana katika Mgodihuo kwa mwezi Februari mwaka huukuwa ni pamoja na kulipa ushuru wahuduma wa asilimia 0.3 ya mauzo kwa

    Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,kiasi cha Dola za Marekani 32, 769.75.

    Akielezea zaidi kuhusu utaratibuwa Shirika hilo kusimamia kwa karibumaslahi yake na Serikali kwa ujumlakatika kuendesha na kusimamia mradihuo, Mkurugenzi huyo wa STAMICOalisema kuwa kulingana na maeneoya usimamizi kuwa mengi mgodini,kuanzia mwezi Machi mwaka huu,Shirika limeongeza idadi ya watumishiuangalizi na usimamizi kufikia Sita.

    “Awali, tulipeleka Maafisa watatukufanya kazi hiyo ya uangalizi nausimamizi. Sasa tumeongeza idadihiyo mara mbili ili kuleta ufanisi zaidi,”alisema Kongoi.

    Akizungumzia majukumu yaMaofisa hao, Kongoi alisema kuwakwa mujibu wa kifungu namba 12cha mkataba wa kuendeleza Mgodihuo, timu ya wataalam wenye fanimbalimbali iliundwa ikijumuishawahandisi, wajiolojia, wachenjuaji nawahasibu ambao jukumu lao kubwani kufuatilia, kusimamia na kushauri

     juu ya mwenendo wa uendeshaji washughuli za kila siku za Mgodi pamojana utekelezaji wa masuala ya mkatabawa ubia.

    STAMICO iliingia ubia na Kampuni

    ya Tanzanite One Mining Ltd (TML)mwaka 2013 kwa uwiano wa 50 kwa 50ili kumiliki leseni ya uchimbaji madini nakuendeleza Mgodi wa Tanzanite katikaeneo la Mirerani Kitalu C.

    Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ZenaKongoi (wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya Wajumbe wanawakewa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, muda mfupikabla ya kushuka chini ya ardhi kwa kutumia Kiberenge maalumu ilikujionea mahala kunakochimbwa madini ya Tanzanite.

    Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ZenaKongoi, akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Mgodi wa TanzaniteOne kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini hivikaribuni. Kamati hiyo ilifanya ziara Mgodini hapo kujionea namna

    unavyofanya kazi.

    Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, AllyKeissy, akiuliza swali wakati wa kikao cha majumuisho baada ya ziaraya kamati hiyo katika migodi mbalimbali inayochimba madini yaTanzanite Mirerani hivi karibuni.

    Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Susan

    Kiwanga, akiuliza swali wakati wa kikao cha majumuisho baada yaziara ya kamati hiyo katika Migodi mbalimbali inayochimba madini yaTanzanite Mirerani hivi karibuni.

    Baadhi ya Maasa wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa tayarikuwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati naMadini, kushuka chini ya ardhi kunakochimbwa madini ya Tanzanitewalipokuwa katika ziara kukagua Mgodi wa Tanzanite One hivi karibuni.Kutoka Kulia ni Fundi Mchundo wa Wakala wa Ukaguzi wa MadiniTanzania (TMAA) Zakaria Mtunya, Asa wa Bunge kutoka Wizarani AmonMarco, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini Elias Kayandabilana Mhandisi Nyanswi Mbona (TMAA).

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    6/20

    6   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Latifah Boma

    Waziri wa Nishati naMadini, ProfesaSospeter Muhongoamelitaka Shirikala Umeme nchini

    (Tanesco) liongeze juhudi katikakuhamasisha wananchi kuunganishwana huduma ya umeme.

    Aliyasema hayo katika mkutano baina yake na wawakilishi kutokakampuni inayosambaza umeme vijijiniya Derm Electronics na watendajikutoka Tanesco na Wakala wa NishatiVijijini (REA), uliofanyika katikati yawiki hii, jijini Dar es Salaam.

    Kampuni hiyo, inayosambazaumeme Mkoani Dodoma na Mara,ilieleza kuwa moja ya changamotokubwa inayoipata katika utekelezaji wakazi zake ni muamko mdogo kutokakwa wananchi kutaka kujiunga nahuduma ya umeme.

    Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni

    ya Derm Electronics, Ridhuani Mringoalisema kuwa suala hilo limewafanyawakumbwe na changamoto yakutimiza malengo yao ya kusambazaumeme kwa idadi iliyopangwa katikamakubaliano na Serikali.

    Alisema wameweza kuunganishiaumeme kwa wananchi takribani 2,000kati ya 11,000 waliotarajiwa mkoaniDodoma na wananchi takribani 3,000kati ya 14,000 mkoani Mara.

    Aidha, Profesa Muhongoaliipongeza kampuni hiyo kwa kufanyakazi nzuri kwani wameweza kumalizaasilimia 96 ya kazi yao, wakiwawameweza kuunganisha umemekatika vijiji 125 mkoani Dodoma na

    vijiji 161 mkoani Mara.Profesa Muhongo pia aliwaagizawatendaji kutoka Wakala wa NishatiVijijini (REA) kufanya ukaguzi, baadaya wiki moja katika maeneo ya kaziya wakandarasi hao wanaosambazaumeme vijijini ili kuhakikisha kuwakazi hizo zinafanyika kwa ufanisi.

    Na Devota Myombe

    K ampuni ya MBH PowerLtd inayosambazaumeme vijijini katikamikoa ya Morogoro,Lindi na Pwani, imepewa

    onyo na Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo baadaya kuonekana kusuasua katika kaziya usambazaji umeme vijijini katikamikoa hiyo.

    Onyo hilo alilitoa jijini Dar esSalaam katika ukumbi wa Wizara yaNishati na Madini wakati kampunihiyo ilipowasilisha ripoti ya utekelezajiwa miradi ya usambazaji umemevijijini. Kikao hicho pia kilihudhuriwa

    na watendaji kutoka Shirika la Umemenchini (TANESCO) na Wakala waNishati Vijijini (REA).

    Awali mwakilishi wa kampunihiyo, Thulasidas alieleza kuwawamechelewa kutekeleza miradi hiyokutokana na changamoto mbalimbaliikiwemo wananchi kuwazuiakusimamisha nguzo za umeme haliinayopelekea kazi yao kutomalizikakwa wakati na zoezi la ufungaji mita zaumeme kwa wateja kutofanyika kwawakati kwani wananchi huchelewakulipia huduma hiyo.

    Alieleza kuwa kwa mkoa wa Lindikampuni hiyo imeunganishia umemewateja wa njia moja ya umeme kwaasilimia 4.92 na asilimia 35.16 kwa

    wateja wa njia tatu za umeme.

    Kwa mkoa wa Morogoro alielezakuwa kampuni hiyo imeunganishiaumeme wateja wa njia moja ya umemekwa asilimia 22.76 na asilimia 14.63kwa wateja wa njia tatu za umeme.

    Vilevile kwa mkoa wa Morogoroalieleza kuwa kampuni hiyoimeunganishia umeme wateja wa njiamoja ya umeme kwa asilimia 11 naasilimia 5 kwa wateja wa njia tatu zaumeme.

    Kuhusu utatuaji wa changamotohizo Profesa Muhongo aliwaagizawatendaji wa TANESCO kufanyakazi kwa karibu na kampuni hiyoili kuweza kutatua changamoto haliitakayopelekea mradi huo ukamilishwekwa wakati kama makubalianoyanavyoelekeza ambapo ukomowa utekelezaji wa miradi yote yausambazaji umeme vijijini ni mweziJuni mwaka huu.

    “Nawapa miezi miwili tu yakukamilisha kazi hiyo iliyobakimkishindwa kufanya hivyo hatutawezakuwapa kazi ya kusambaza umemevijijini katika Awamu ya Tatu ambayoitaanza mara baada ya kukamilika kwaAwamu hii ya Pili”, alisema ProfesaMuhongo.

    Aidha, Profesa Muhongo aliutakauongozi wa kampuni hiyo kuachakubadilisha Mameneja mradi nawahandisi mara kwa mara katikamaeneo ya kazi kwani suala hilolinachelewa utekelezaji wa kazi hiyo.

    Profesa Muhongo awatakaTANESCO kuhamasishawananchi kuunganisha Umeme

    Kampuni ya MBHPower yapewa Onyo

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati)akimsikiliza mmoja ya watendaji kutoka Shirika la Umeme nchini(TANESCO) waliohudhuria mkutano kati ya Wizara na kampuni yaDerm Electronics uliofanyika katikati ya wiki hii, jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Kampuni yaMBH Power Ltd, Thulasidas (Kulia) akiwasilisha

    taarifa ya utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini katika mikoa ya Lindi,Morogoro na Pwani. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu waWakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya na wa pilikushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi kutoka REA, Mhandisi Bengiel Msofe.

    Baadhi ya wawakilishi kutoka kampuni ya Derm Electronics nawatendaji kutoka Shirika la Umeme nchini (Tanesco) na Wakala waNishati Vijijini (REA) wakifuatilia mkutano kati ya Wizara na kampuni

    ya Derm Electronics uliofanyika hivi karibuni, jijini Dar es Salaam. WaTatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dkt. Lutengano Mwakahesyana wa Pili kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi kutoka REA, Mhandisi BengielMsofe.

    Wawakilishi kutoka Kampuni yaMBH Power Ltd wakimsikiliza Waziriwa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)alipokuwa akiwahoji kuhusu mradi wa Awamu ya usambazaji umemevijijini katika mikoa ya Lindi, Morogoro na Pwani.

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    7/20

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Profesa Muhongo aiagiza TANESCO

    kukagua Vituo vya kupoozea UmemeRhoda James naZuena Msuya

    Mameneja wa Kandawa Shirika laUmeme Tanzania(TANESCO) pamojana Wakala wa

    Nishati Vijijini (REA) wameagizwakushirikiana ili kumaliza ukaguziwa vituo sita vya kupoozea umemevilivyojengwa na Kampuni ya ChinaTaikai wilayani Kigoma, Kasulu,Kibondo, Mbinga, Ngara na Tunduru.

    Agizo hilo limetolewa hivi karibunina Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo alipofanyamkutano na Kampuni hiyo ili kuelewahatua za utekelezaji wa miradiinayotekelezwa na kampuni hiyokatika Awamu ya Pili ya usambazajiumeme vijijini inayosimamiwa naWakala wa Nishati Vijijini (REA).

    “Fuatilieni miradi hii kwa karibuili kuhakikisha kila kituo kinafanyakazi kulingana na makubalianomliyowekeana na hii ni kwa ajiliya kuepusha matatizo yanayowezakujitokeza hapo baadaye endapo vituohivi vya kupoozea umeme vitaonekanakufanya kazi chini ya kiwango,”alisema Profesa Muhongo.

    Profesa Muhongo alisisitiza kuwakampuni hiyo ya China Taikai naKampuni nyingine zote zinazotekelezamiradi mbalimbali zikamilishe miradi

    hiyo kwa wakati na huku zikizingatiamaelekezo waliokubaliana na Serikali.

    “Wakandarasi wote lazimawamalize kazi zao kwa wakati na hiiitatumika kama kigezo katika kupatanafasi ya kushiriki tena kwenye miradiya usambazaji umeme vijijini yaAwamu ya Tatu,”

    Kwa upande wake Meneja waMasuala ya Biashara kutoka kampuniya Taikai, Wang Kai alisema kuwahadi sasa kampuni hiyo imekamilishakazi hiyo kwa asilimia 99 nakwamba changamoto zinazojitokezazinafanyiwa kazi na Wahandisi wa

    Kampuni husika.Kai aliongeza kuwa vituo vyote Sitavya kupoozea umeme vimekamilikana kueleza kuwa kituo cha Tunduruhakijakamilika kwa asilimia 100 nakusisitiza kuwa kazi zote zitakamilikakwa wakati ili kufanya majaribio yamitambo yote na uzinduzi rasmi.

    Vile vile aliishukuru Serikali yaTanzania kwa kuiamini Serikali yaChina katika kutekeleza miradi hiyona kuahidi kuendelea kuimarishaushirikiano uliopo kati ya nchi hizimbili.

    Waziri Muhongo amekuwana vikao na Wakandarasi wotewanaotekeleza miradi ya umemevijijini, Awamu ya Pili ili kujadili

    hatua za utekelezaji zilizofikiwakwenye miradi husika na changamotowanazokabiliana nazo wakandarasihao.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbelekatikati), Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo(kushoto kwa Waziri), viongozi waandamizi wa Wakala wa NishatiVijijni (REA), Viongozi wandamizi kutoka Shirika la Umeme nchini(TANESCO) na Ujumbe kutoka kampuni ya Taikai wakifuatilia taarifaya utekelezaji wa umeme vijijini iliyokuwa ikitolewa na kampuni hiyokatika kikao kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutanowa Wizara jijini Dar es Salaam.

    Waziri wa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo (kulia) na Ujumbekutoka kampuni ya China Taikaiwakimsikiliza mtendaji wa kampuniya hiyo (hayupo pichani) wakatiwalipokutana na Kampuni hiyo ili kujadilihatua za utekelezaji katika miradi yaumeme vijijini.

    Meneja wa masuala ya biashara kutokakampuni ya Taikai ya China, Wang Kaiakitoa taarifa ya utekelezaji wa umemevijijini kwa viongozi waandamizi waWizara ya Nishati na Madini, Shirikala Umeme nchini (Tanesco) pamoja naWakala wa Nishati Vijijini (REA).

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    8/20

    8   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Greyson Mwase,Dar es Salaam

    Naibu Katibu Mkuuwa Wizara ya

    Nishati na Madinianayeshughul ik iamasuala ya Nishati,

    Dkt. Jualiana Pallangyo amewatakawawekezaji binafsi nchini kujitokezakwa wingi na kuwekeza katikauzalishaji na uuzaji wa nishati yaumeme nchini ili iweze kuchangiakatika ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Dkt. Pallangyo alisema hayokwenye mkutano unaokutanishawakurugenzi wa mashirika yaumeme katika nchi zilizopo kusinimwa Afrika zinazoshirikiana katika

     biashara ya umeme. Nchi hizo nipamoja na Bostwana, Msumbiji,Afrika ya Kusini, Lesotho, Namibia,Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo,Swaziland, Zambia na Zimbabwe.Lengo la mkutano huo lilikuwa nikujadili changamoto zinazozikumbanchi wanachama katika uzalishaji nauuzaji wa umeme ikiwa ni pamoja nakubadilishana uzoefu.

    Aliongeza kuwa wawekezaji binafsi wanaweza kuzalisha umemekupitia vyanzo mbalimbali vya nishatiikiwa ni pamoja na maporomokomadogo ya maji, upepo, bayomasi na

     jua kutokana na uwezo wao.Akielezea fursa za uwekezaji

    nchini, Dkt. Pallangyo alisema kuwawawekezaji wanaweza kuwekezakupitia ujenzi wa miundombinu yausambazaji wa umeme, uendelezajiwa miradi ya umeme unaotokanana maporomoko madogo ya majina vyanzo vingine ikiwa ni pamojana jotoardhi, upepo na uanzishwajiwa viwanda vidogo kwa ajili yautengenezaji wa vifaa kwa ajili yaujenzi wa miundombinu ya umeme.

    Dkt. Pallangyo aliongeza kuwaushiriki wa sekta binafsi katikasekta ya umeme umeongezeka kila

    mwaka na kusisitiza kuwa serikali bado inaendelea na mikakati yakuwawezesha wawekezaji binafsikatika uzalishaji ya umeme nchini.

    Aliongeza kuwa serikali imewekamazingira mazuri ya uwekezaji nchiniikiwa ni pamoja na sera na sheriambalimbali zinazotumika kamamwongozo na kutaja kuwa ni pamojana sheria ya umeme ya mwaka 2008,sera ya nishati ya mwaka 2003 ambayoinahamasisha ushiriki wa sekta binafsikatika sekta ya umeme.

    Alitaja sheria nyingine kuwa nipamoja na ile ya Mamlaka ya Udhibitiwa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) ya mwaka 2001, sheria yaWakala wa Nishaji Vijijini (REA) yamwaka 2005.

    Akielezea mikakati ya serikalikatika upatikanaji wa nishati yauhakika, Dkt. Pallangyo alisemakuwa serikali imeweka mkakati wakuhakikisha kuwa ifikapo mwaka2025 asilimia 75 ya wananchi wotehasa waishio vijijini wanapata nishatiya umeme ambayo ni ya uhakika.

    “Tunatarajia kuzalisha hadimegawati 10,000 za umeme ambaoutachochea ukuaji wa uchumi wa nchikupitia viwanda na hivyo nchi kutokakatika kundi la nchi masikini dunianina kuwa katika kundi la nchi zenyekipato cha kati duniani,” alisisitizaDkt. Pallangyo.

    Akielezea hali ya upatikanaji waumeme nchini, Dk. Pallangyo alisemakuwa umeme unaozalishwa nimegawati 1461.69 huku mahitaji halisiyakiwa ni megawati 1026.

    Umoja wa nchi zinazoshirikianakatika sekta ya umeme kusini mwaAfrika (Southern African Power Pool;SAPP) ulianzishwa Agosti mwaka1995 katika Mkutano wa Umojawa Nchi zilizo Kusini mwa Jangwala Sahara (SADC) ambapo walisainimakubaliano kwa ajili ya kushirikianakatika uzalishaji na biashara yaumeme wa pamoja.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dkt. JulianaPallangyo (aliyekaa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya watendaji nawakurugenzi wa mashirika ya umeme katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katikabiashara ya umeme, mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

    Dkt. Pallangyo awakaribisha wawekezaji

    binafsi kwenye uzalishaji wa Umeme

    Mwenyekiti wa kamati ya nchi za kusini mwa Afrika zinazoshirikianakatika biashara ya umeme, Josh Chifamba (kulia) akimkabidhi zawadiNaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikiamasuala ya Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (kushoto) aliyekuwa mgenirasmi kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikiamasuala ya Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (kulia) na KaimuMkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)Mhandisi Decklan Mhaiki (kushoto) wakifuatilia maelezo yaliyokuwayanatolewa na mwenyekiti wa kamati ya nchi za kusini mwa Afrikazinazoshirikiana katika biashara ya umeme, Josh Chifamba (hayupopichani)

    Naibu Katibu Mkuu waWizara ya Nishati na Madinianayeshughulikia masuala yaNishati Dkt. Juliana Pallangyo(pichani) akifungua mkutanoulioshirikisha wakurugenziwa mashirika ya umemekatika nchi zilizopo kusinimwa Afrika zinazoshirikianakatika biashara ya umeme.

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    9/20

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mohamed Saif naNuru Mwasampeta

    K ampuni ya Sinotec ya nchiniChina inayosambazaumeme vijijini katikawilaya za Chunya, Mbeyavijijini, Mbozi, Nkasi

    na Sumbawanga Vijijini imetakiwakukamilisha kwa wakati miradinayotekeleza kwenye wilaya hizoambapo ukomo ni Mwezi Juni mwakahuu.

    Agizo hilo limetolewa hivi karibuniijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati

    na Madini, Profesa Sospeter Muhongoalipofanya mkutano na wawakilishi wakampuni hiyo ili kubaini utekelezaji wamiradi iliyo chini ya kampuni hiyo.

    Awali Mwakilishi wa kampuni hiyonchini, Zheng Minrong alitaja miradiambayo inatekelezwa na kampunihusika kuwa ni Chunya na MbeyaVijijini (Lot 11); Mbozi (Lot 13) naNkasi na Sumbawanga Vijijini (Lot18) ambayo yote kwa pamoja ilianzakutekelezwa rasmi mwezi Agosti, 2014.

    Akizungumzia hatua iliyofikiwa yautekelezaji wa miradi hiyo, Minrongalisema kwa lot 11 mradi umekamilikakwa asilimia 72, wakati lot 13 mradiumekamilika kwa asilimia 89 na hukulot 18 mradi umekamilika kwa asilimia75.

    Alisema utekelezaji wa miradihiyo umesuasua kutokana na sababumbalimbali ambazo ni pamojauchakavu wa miundombinu hususanya barabara hasa kipindi cha masika

    ambapo usafirishaji wa vifaa kuelekeamaeneo ya miradi (vijijini) unakuwamgumu.

    Mbali na sababu hiyo, Minrongalieleza sababu nyingine kuwa niugumu wa kupata wateja wenye

    kuhitaji kuunganishiwa umeme, kwaniwananchi wachache ndio waliojitokezakuunganishwa na huduma husika.

    “Kipindi cha masika inakuwangumu kusafirisha vifaa kuelekeakijijini kwani barabara nyingi zinakuahazipitiki; na vilevile ni wananchiwachache ambao wameonesha nia yakuunganishiwa umeme.”

    Hata hivyo Waziri Muhongohakuridhishwa na maelezo hayoyaliyotolewa na Mkandarasi kwanialisema hakuna sababu ya msingiiliyoelezwa na hivyo ni juu yaMkandarasi kuhakikisha anakamilishamiradi hiyo kwa muda uliopangwa.

    Alisema suala la kwamba watejani wachache halina ukweli kwaniamekuwa akipokea meseji nyingikatika simu yake ambapo wananchiambao wanahitaji huduma ya nishati yaumeme.

    “Kila siku ninapokesa ujumbemfupi wa simu kati ya 600 hadi 800kutoka kwa wananchi wakieleza uhitajiwao wa huduma ya umeme; kwahiyomsitueleze kwamba wananchi wamaeneo hayo hawana uhitaji,” alisemaMuhongo.

    Waziri Muhongo pia aliliagizaShirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kushirikiana na Wakalawa Nishati Vijijini (REA) katikakusimamia na kufuatilia kwa karibuutekelezaji wa miradi ya umeme vijijiniili ikamilike kwa wakati na kwa kiwangokinachotakiwa.

    SINOTEC YAAGIZWA KUKAMILISHA MIRADI YA REA KWA WAKATI

    Mwakilishi wa Kampuni ya Sinotec nchini Tanzania, Zheng Minrongakielezea hatua ya utekelezaji wa miradi iliyo chini ya kampuni hiyowakati wa kikao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa SospeterMuhongo (hayupo pichani) na watendaji mbalimbali kutoka Wizara yaNishati na Madini na Taasisi zilizo chini ya wizara.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya Sinotec nchini, Zheng Minrong(hayupo pichani) alipokuwa akielezea kuhusu miradi inayotekelezwa na

    kampuni husika. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masualaya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.

     

    Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha

     yenye aina mbalimbali za vito zikiwemo

    T anzanite , Ruby, Sapphire , Tsavorite ,

    Rhodolite , Spessartite , Tourmaline,

    Chrysoberyl na Almasi yanatarajiwa kuvutia  

    Zaidi ya kampuni 100 za wafanyabiashara na

     wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na

    nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini;

    na  zaidi ya wanunuzi 500 kutoka zaidi ya nchi 25

    ulimwenguni

     Jisajili na Ushiriki Sasa!!! 

     Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF 

    Simu: +255 784352299 or +255 767106773 

    Barua pepe: [email protected]

    :ama Ofisi za Madini za Kanda

     Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madinikwa kushirikiana na

    Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA) 

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    10/20

    10   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    GILAY SHAMIKA

    SENIOR ENGINEER & GEMOLOGISTTANZANIA MINERALS AUDIT AGENCY (TMAA)[email protected]

    What is Hessonite Gemstone?

    Hessonite orCinnamonStone, is a morecommon varietyof grossular

    with the general formula:Ca3Al2Si3O12. The namecomes from the Greek hesson,meaning inferior; an allusionto its lower hardness and lower

    density than most other garnetspecies varieties. Hessonite isa variety of grossularite garnetlike Tsavorite. It is also knownas Cinamon Stone in Asianmarket.

    It has a unique characteristiccalled ‘heat wave effect’ (lookslike undulating growth, burntarea or some call it scotch inwater effect) and roundedcrystals.

    In Tanzania Hessonite isavailable in different placesincludingMorogoro: Kilosa,Uluguru mount, Mngazivalley, kisitwiTanga: MlolaLushoto, Kilinga and Kihunza

    HandeniRuvuma: LikondeMbinga

    GeologyHessonite being a variety

    of Grossular is found in

    contact metamorphosedlimestones with its red-orange(honey color). A fairly rare asa gemstone, the Hessonite isa silicate of zirconium and iscommonly found in igneousrocks as well.

    Hessonite a grossularvariety, is a calcium-aluminumgarnet with the formula

    Ca3Al2(SiO4)3, thoughthe calcium may in part bereplaced by ferrous iron and thealuminum by ferric iron.

    Colour Ranges: Mediumto dark orange, yellow, yellow-green, brownish orange andcolorless.If pale it is calledgrossularite garnet and nothessonite.

    Varieties: Hessonite is avariety of grossularite garnetlike Tsavorite Garnet with thesame geological properties, thedifference being only colour.When the hessonite has palecolour, it is called grossularite

    garnet.

    HessoniteConfusewith:Citrine, Spessartite,Almandite, Zircon, Topaz,Orange Sapphire and FireOpal.

    Gemological properties of Hessonite

    Gemological Properties of Hessonite Unit of Measure

    Gem group Garnet

    Refractive Index (RI) SR 1.740 (can go up to 1.755)

    Specic gravity 3.61

    Hardness (Mohs Scale) 7.0

    Toughness Medium

    Stability to light Stable

    Treatment and Grading of Hessonite

    Heating:To improve color or clarity appearance.Lattice diffusion: This is a process of heating

    Hessonite to very high temperature in the presence of a coloring agent. The aim is either to increasecolour appearance, remove color or change to other colour.

    Hessonite Grading Explanation

    A Vivid Pure Orange Colour

    B Deep orange Colour

    C Deeporange colour with windowand impurities

    TraditionalGrading

    Gem quality A

    Near Gem B

    Industrial/Low quality C

    Rough Hessonite on its rockCut and Polished Hessonite

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    11/20

    11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Greyson Mwase,Dar es Salaam

    K ampuni inayojihusisha naujenzi wa miundombinukwa ajili ya kusambazaumeme vijijini katikamikoa ya Mwanza na

    Tabora ya Chico CCC kutoka nchiniChina imepewa muda wa miezi miwiliya kuhakikisha inakamilisha miradiyake ya umeme.

    Agizo hilo lilitolewa na Waziri waNishati na Madini Profesa Sospeter

    Muhongo alipokutana na kampunihiyo kwa ajili ya kupokea taarifa yautekelezaji wa miradi yake ya umemevijijini. Kampuni hiyo inatekelezamiradi ya umeme inayosimamiwa naWakala wa Nishati Vijijini (REA).

    Mara baada ya kupokea taarifa hiyona kutoridhishwa na kasi ya utekelezajiwa miradi ya kampuni hiyo, ProfesaMuhongo aliitaka kampuni hiyokuhakikisha inakamilisha miradi yakeifikapo mapema mwezi Mei mwakahuu.

    Alisisitiza kuwa wananchi wanahitajiumeme wa uhakika ambao ni nguzoya ukuaji wa uchumi wa nchi kupitiaviwanda, hivyo serikali haitamwoneahaya mwekezaji yeyote asiyetekeleza

    mradi wa umeme aliopewa kwa kasiinayoridhishwa.

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akielezeaumuhimu wa kutekeleza kwa wakati miradi ya umeme kwawakandarasi waliokutana naye jijini Dar es salaam. Profesa Muhongo

    anakutana na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijinikupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) kwa ajili ya kupokea taarifa yautekelezaji wa miradi hiyo.

    Mkurugenzi Mtendaji kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt.Lutengano Mwakahesya (kushoto) akisisitiza jambo katika kikao hicho.

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mbele)

    akiongoza kikao kilichohusisha wakandarasi wa miradi ya umeme vijijiniinayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na watendaji waWizara ya Nishati na Madini na taasisi zake.

    Kampuni ya Chico CCC yapewa miezi miwili

    kukamilisha miradi ya umeme Tabora, Mwanza

    Mwakilishi kutoka kampuni ya Chico CCC kutoka Nchini China, Jacky Gn, akitoa taarifa ya utekelezaji

    wa miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa waMwanza.

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    12/20

    12   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Latifah Boma naDevotha Myombe

    Waziri wa Nishati naMadini, ProfesaSospeter Muhongoa m e w a t a k aw a k a n d a r a s i

    wanaotekeleza miradi ya umeme vijijinikupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) awamu ya pili kufanya kazi kwakasi zaidi ili umeme uweze kuwafikiawalengwa kabla ya mwezi Juni mwakahuu.

    Akizungumza na watendaji kutokakampuni ya CCC International NigeriaLimited, inayosambaza umeme katikamkoa wa Manyara, Profesa Muhongo

    alisema kuwa hajaridhishwa na kasiya kampuni hiyo katika utekelezajiwa miradi ya umeme katika wilayaya Simanjiro ambapo hakuna watejawaliounganishiwa umeme.

    Pia, Profesa Muhongo amelitaka

    Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)kufanya kazi kwa karibu na wakandarasihao katika kutatua changamotozinazowakabili ili waweze kukamilishamiradi hiyo kwa wakati.

    Aliwataka Mameneja waTANESCO kuongeza juhudikatika kazi zao ikiwa ni pamoja namakusanyo, utatuaji wa changamotona uunganishaji wa umeme kwawateja, na kusisitiza kuwa Menejaatakayeshindwa kutekeleza majukumuyake ataondolewa katika nafasi yake.

    Awali, akielezea changamoto katikautekelezaji wa miradi ya umeme MenejaMradi kutoka CCC InternationalNigeria Limited

    Zhang Jiangaang, alieleza kuwa

    wamekuwa wakiibiwa vifaa vyao vyakazi kutokana na kuwepo kwa usalamamdogo hivyo kupelekea kutokamilishaMradi kwa wakati kutokana na hasarawanayoipata.

    Meneja mradi wa Kampuni ya CCC International Engineering Nigeria,Zhang Jiangaang (Mwenye shati jeupe) akiwasilisha ripoti ya maendeleoya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa NishatiVijijini (REA) Awamu ya Pili.

    Na Rhoda James

    Wakandarasi wakuuw a n a o s a m b a z aumeme vijijiniwametakiwa kufanyakazi hiyo kwa

    kushirikiana na wakandarasi wadogo(sub- contractors) ili kuweza kusambazaumeme kwa kasi na hivyo kuendanana muda uliopangwa na Serikali wakukamilisha miradi hiyo inayofikiaukomo mwezi Juni mwaka huu.

    Wito huo umetolewa hivi karibunina Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo wakatialipokutana na uongozi wa Kampuniya LTL project (PTV) ltd kutoka nchiniSrilanka inayosambaza umeme katikamikoa ya Shinyanga na Ruvuma kwa

    ufadhili wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA).“Inasemekana kuwa mahusiano

     baina yenu na wanaofanya kazi chiniyenu sio mazuri mmekuwa mkiwaajirimameneja wa miradi mnayoitekelezana kuwafukuza. Tatizo lililopo nikwamba mameneja hao wapyawanakuwa wanachukua muda mrefukujifunza hivyo kuwapotezea muda,”Alisema Profesa Muhongo.

    Aidha, Profesa Muhongo ameiagizakampuni hiyo kufanya kazi kwaviwango vilivyo katika makubalianona Serikali na kuhakikisha kuwamiundombinu ya kusambaza umemekutoka Songea hadi kituo cha Masistacha Tulia inakamilika ili kituo hicho

    kiweze kufanikisha azma yao yakuwasambazia umeme wananchi.Muhongo alieleza kuwa “kwa sasa

    kituo hicho cha Masista kinasambazaumeme wa kiasi cha megawati 5 lakini

    wataongeza hadi kufikia usambazajiwa megawati 7 na baadaye kufikiamegawati 10”.

    Kwa upande wake Meneja Mradiwa Kampuni ya LTL project (PVT)Ltd, Nishantha Amarasekara alielezahatua waliyofikia katika usambazaji waumeme vijijini ni nzuri kwani katikamradi wa Shinyanga vijijini tayariwameshaunganisha wateja 348 sawa naasilimia 42, Bariadi wateja 30 sawa naasilimia 5, Kahama wateja 713 sawa naasilimia 71, Kishapu wateja 306 sawa naasilimia 33, Meatu wateja 299 sawa naasilimia 57 ya wateja wote waliotakiwakuunganishwa na huduma ya umeme.

    Akielezea hatua waliyofikia katikausambazaji wa umeme mkoani

    Ruvuma Amarasekara alisema kuwahadi sasa katika wilaya za Mbinga naNyasa wameunganisha wateja 873sawa na asilimia 22, Songea wateja 703sawa na asilimia 45 na Tunduru wateja161 sawa na asilimia 7.

    Akizungumzia changamotozinazowakabili, Amarasekara alitajachangamoto hizo kuwa ni ubovu wa

     barabara inayopelekea usumbufu wakatiwa usafirishaji wa vifaa mbalimbali vyaujenzi na uchelewaji katika kupatikanavibali vya wataalam wao kufanya kazinchini.

    Pamoja na changamotozinazowakabili, Amarasekaraamemhakikishia Profesa Muhongokwamba wataimarisha mahusiano

     baina ya watendaji na wafanyakazi wakampuni hiyo na kwamba miradi yotemiwili itakamilishwa ifikapo 15 Juni,2016.

    Wakandarasi Wakuu wa Umeme Vijijiniwaaswa kushirikiana na Wakandarasi Wadogo

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele,katikati) akipitia ripoti ya kampuni ya LTL project (PVT) Ltd, ambayoiliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini katika

    mikoa ya Ruvuma na Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuuwa REA,Dkt. Lutengano Mwakahesya.Wengine ni watendaji kutokaWizara, TANESCO na REA.

    Meneja wa mradi wa kampuni ya LTL project (PVT) Ltd, NishanthaAmarasekara akitoa taarifa kwa Waziri wa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo (hayupo pichani), Viongozi waandamizi wa Wizaraya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Wakalawa Nishati Vijijini (REA) katika kikao hicho kilichofanyika hivi karibuni

     jijini Dar es Salaam.

    Profesa Muhongo aagiza miradiya umeme vijijini kukamilika

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    13/20

    13BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Veronica Simba -

    Mirerani

    K uwepo kwa mitobozanoya mara kwa mara bainaya wachimbaji wadogowenyewe kwa wenyewena kati ya Mgodi wa

    Tanzanite One na wachimbaji wadogowa Tanzanite katika vitalu B na D,kumeelezwa kuwa ni changamotoinayosababisha kukosekana kwausalama katika eneo la machimboya Tanzanite, Mirerani kutokanana kutumika kwa silaha za moto na

    mabomu ya kutengenezwa kienyeji.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya

    Nishati na Madini anayeshughulikiaMadini, Profesa James Mdoe aliyasema

    hayo hivi karibuni mkoani Arusha,wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumuya Bunge ya Nishati na Madini kukaguaMigodi mbalimbali inayochimba madinihayo eneo la Mirerani.

    Akielezea maana ya mitobozano,Profesa Mdoe alisema ni hali yawachimbaji kuvuka mipaka ya lesenizao na kuingia katika maeneo yawachimbaji wengine wakiwa chini yaardhi.

    Kutokana na tatizo hilo, ProfesaMdoe alisema kuwa Serikali, kupitiaWizara ya Nishati na Madini, hususanOfisi ya Madini Mirerani, inaendelea na

     juhudi za kuwaelimisha wachimbaji nawadau wote wa sekta ya madini katikakuhakikisha wanatekeleza majukumuyao kwa mujibu wa sheria za nchiikiwemo Sheria ya Madini ya Mwaka2010 na kanuni zake pamoja na Sheriaya Baruti ya mwaka 1963 na kanunizake za mwaka 1964.

    Akifafanua zaidi, Profesa Mdoealisema kuwa, mbali na kuwatakawachimbaji kufuata sheria, pia

    kumekuwepo na juhudi za

    kuwakutanisha wachimbaji wa KitaluC na Vitalu B na D ili kuweka namnaambavyo uchimbaji unaweza kufanyikakwa kuepuka mitobozano.

    Aidha, alieleza kuwa Wizara yaNishati na Madini imekuwa ikishirikianana Kamati za Ulinzi na Usalama zamikoa ya Arusha, Kilimanjaro naManyara katika kudhibiti utoroshaji waTanzanite.

    Alisema, wataalam wa Wizarakupitia Ofisi ya Madini Mirerani,Mamlaka ya Udhibiti wa MadiniTanzania (TMAA ) na Shirika la Madinila Taifa ( STAMICO), wameongezaudhibiti wa Tanzanite kwenye maeneoya uzalishaji chini mgodini.

    “Kazi hii inafanyika kwa kuhakikisha

    kuwa maafisa husika wanakuwepowakati wa uzalishaji ili kufahamu kiasikinachozalishwa, “ alisema ProfesaMdoe.

    Vilevile, alieleza hatua nyinginezinazochukuliwa na Serikali kutatuatatizo hilo kuwa ni pamoja na kuandaamaonesho ya vito ya kimataifa ambayohufanyika Arusha kila mwaka ambapowanunuzi wa kimataifa kutoka nchimbalimbali hukutana moja kwamoja na wauzaji wakubwa wa ndanihivyo kupunguza uwezekano wawafanyabiashara kuendelea kutoroshaTanzanite.

    Alisema kuwa, Serikali imeanzishamasoko ya ndani yatakayokuwayanafanyika Mirerani kila mwakana ina mpango wa kuanza ujenzi wasoko kubwa Mirerani ili madini yoteyatakayozalishwa yaweze kuuzwa,kukatwa na kusanifiwa Mirerani.

    Kwa upande wao, Wajumbe waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishatina Madini, waliitaka Serikali pamojana mambo mengine, kuhakikishamigogoro iliyopo katika machimbohayo ya Tanzanite Mirerani inatafutiwaufumbuzi wa haraka na wa kudumu.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (katikati)akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakisikiliza maelezo kutokakwa Meneja wa Mgodi wa Tanzanite, Emmanuel Mbise ulioko Kitalu B, Mirerani. Mgodi huo unamilikiwa naMchimbaji Mdogo, Ester Ndosi.

    Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Elias Kayandabila(aliyenyoosha mkono), akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, walipotembelea Mgodi

    wa madini ya Tanzanite wa Franone uliopo Kitalu D, Mirerani. Wakwanza Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe.

    Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (wa nne kushoto),akimwonyesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madinianayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (wa tatu kushoto), namnaKiberenge kinavyofanya kazi ya kushusha watu na vifaa chini ya ardhi

    kunakochimbwa madini ya Tanzanite, wakati wa ziara ya Kamati yaKudumu ya Bunge ya Nishati na Madini katika Mgodi wa Tanzanite Oneuliopo Mirerani, hivi karibuni.

    Profesa Mdoe aieleza Kamati ya Bungemikakati kutatua changamoto Sekta ya Madini

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    14/20

    14   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya yaArusha, Fadhili Nkurlu (aliyesimama), akizungumza na Wajumbe waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini walipoka osinikwake Machi 30 mwaka huu, kabla ya kutembelea Machimbo ya Tanzaniteyaliyopo Mirerani.

    Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya yaArusha, Fadhili Nkurlu (mwenye Suti nyeusi–mbele), akiwa katika pichaya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati naMadini, mara baada ya kufanya mazungumzo osini kwake Machi 30mwaka huu, wakiwa njiani kuelekea katika machimbo ya Tanzanite hukoMirerani.

    Mjiolojia Mkuu wa Mgodi unaochimba madini ya Tanzanite wa Franone,uliopo Kitalu D – Mirerani, Vitus Ndakize (Kulia), akitoa maelezo kwaWajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, jinsiMgodi huo unavyofanya kazi. Kamati hiyo ilitembelea Mgodi huo Machi30, mwaka huu.

    Baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakijadiliana jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati naMadini katika Machimbo ya Tanzanite, Mirerani hivi karibuni. Kutokakushoto ni Fundi Sanifu, Denis Mrengo, Asa wa Bunge Msaidizi(Madini) Andendekisye Mbije, na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Serana Mipango anayeshughulikia Tathmini na Ufuatiliaji, James Mganga.

    Asa Madini Mkazi wa Mirerani, Henry Mditi (katikati) akijadiliana jambona wadau wa madini wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaNishati na Madini katika migodi mbalimbali ya madini ya Tanzanite, eneo laMirerani hivi karibuni.

    Asa wa Bunge kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Amon Marco (Kulia),akijadiliana jambo na Maosa kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini

    Tanzania (TMAA), Zakaria Mtunya (katikati) na Mhandisi Nyansai Mbona,wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madinikatika Mgodi wa Tanzanite One, hivi karibuni

    ZIARA KAMATI YA BUNGE MIRERANI - MANYARA

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    15/20

    15BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati naMadini, wakijadiliana jambo, muda mfupi kabla ya kushuka chini ya ardhikunakochimbwa madini ya Tanzanite, katika Mgodi wa Tanzanite One,Mirerani.

    Picha No. 1- 4 ni baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaNishati na Madini wakipanda Kiberenge maalumu kushuka chini ya ardhi

    kunakochimbwa madini ya Tanzanite. Kamati hiyo ilifanya ziara kukaguaMgodi wa Tanzanite One na Migodi mingine kadhaa ya wachimbaji wadogonayochimba madini hayo hivi karibuni.

    ZIARA KAMATI YA BUNGE MIRERANI - MANYARA

    1

    2

    3

    4

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    16/20

    16   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    BRIKETI ZA MAKAA YA MAWE YA

    NGAKA-MAKAA BORA YA KUPIKIA 

     UTANGULIZI.eknolojia ya utengenezaji wa briketi za makaabora ya kupikia ni teknolojia inayopatikana katikamgodi wa Makaa ya Mawe ya Ngaka. Hii nibaada ya kufanyika kwa utafiti uliofanywa naKitengo cha ubora wa Makaa ya mawe kutokaancoal Energy Limited kwa ushirikiano naMbawala Women Organization mnamo mwaka2014.Matokeo ya teknolojia hii yanasaidia kujibutatizo sugu la ukataji miti kiholela kwa ajili yamatumizi ya nishati.eknolojia ya Makaa boraya briketi ni rahisi, na ni mbadala wa nishati yakuni na mkaa wa miti. Ni suluhisho kwa kerona uharibifu utokanao na matumizi ya kuni namkaa wa miti.Briketi za makaa ya mawe hutengenezwa kwamchanganyiko wa chenga chenga (vumbi) zamakaa ya mawe, udongo mfinyanzi, mabaki yamazao ya kilimo yaliyokauka, kwa kuchanganywana maji katika kiwango maalumu. 

    UWAKAJI Briketi za makaa bora ya Ngaka huwaka vizuri.Moto unapoanza kukolea hutoa ulimi mfupirangi ya bluu kutoka katika jiko la kawaida kama jiko la mkaa lililotengenezwa kwa kusilibwaudongo ndani yake (ambalo hutunza joto).Makaa haya yakishawaka na kukolea vizurihayatoi moshi wala kutengeneza masizi ambayohuchafua sufuria au vyungu vyako. Briketiya makaa huhifadhi moto kwa saa 3 hadi 4.Briketi za makaa bora baada ya moto kuwashwahuchukua takribani dakika 10 kukolea 

    • Teknolojia ya Makaa bora ya kupikiani teknolojia iliyobuniwa kuendana namazingira rafiki ya jiko la Kitanzania.eknolojia hii humruhusu mpishi/ mtumiajikutumia vyombo au sufuria za kawaida zaalumini.

    • Briketi za makaa bora ya Ngaka huwa namoto mkali wa kutosha ingawa makaahutumika kidogo sana ukilinganisha na

    nishati ya kuni na mkaa wa kawaida. Makaakidogo hutumika kupikia muda mrefu. Nirahisi kubana matumizi ukilinganisha namatumizi ya nishati ya kuni au mkaa wa miti.Nishati hii huokoa pesa, hulinda misitu, nahutunza mazingira yetu.

    Mradi huu wa kutengeneza briketi boraza kupikia za makaa ya mawe ya Ngakaunaendeshwa na shirika lisilo la kiserikalila Wanawake liitwalo Mbalawala WomenOrganization (MWO).Mbalawala Women Organization ni NGOiliyoundwa na serikali za vijiji vinavyozungukamgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka ambavyoni Ruanda na Ntunduwaro kwa kushirikiana na wawekezaji wa mgodi wa Ngaka –ancoal EnergyLimited.NGO hii imesajiliwa na kuanza kazimwaka 2012.MWO ni matokeo ya juhudi za ancoal EnergyLimited katika kuiwezesha jamii kiuchumi hasa wanawake wanaozunguka mgodi wa makaaya mawe Ngaka kupitia ajira katika miradimbalimbali ukiwemo mradi wa utengenezaji wabriketi za makaa ya mawe.

     WITOBriketi za makaa bora ya kupikia zinafaa kwamatumizi ya majumbani, viwandani na katikataasisi kama shule, vyuo, hospitali, magereza nk.

    o unawasisitiza wananchi majumbani kupikiabriketi za makaa ya maweo unazisihi taasisi kutunza mazingira kwa

    kutumia briketi za makaa ya mawe badala yakuni na mkaa wa miti

    o Ni wakati wa viwanda kuachana na kunina mkaa wa miti. unza mazingira kwaKUUMIA NISHAI YA BRIKEI Z AMAKAA YA MAWE-MAKAA BORA.

    o Wakala wa usambazaji na wauzaji wa jumla wanahitajika

    Faida ya kutumia briketi za makaa ya makaa yamawe• Gharama ya briketi za makaa ni nafuu

    ukilinganisha na mkaa wa miti• Moto wake hudumu muda mrefu, saa 3-4• Ni rahisi kutumia • Unahitaji briketi za makaa kidogo kupika

    vyakula vingi• Kiwango cha joto lake kimepimwa, huhitaji

    kutumia sufuria maalum.• Ukitumia briketi za makaa ya mawe utasaidia

    kupunguza ukataji miti holela, hivyo utatunzamazingira 

    OKOA PESA KWA KUTUMIA BRIKETIBORA ZA MAKAA YA NGAKA 

     Je ungependa kuwa msambazaji wa briketi zamakaa bora ? Wasiliana nasi.Mbawala Women OrgnizationS.L.P 450 Mbinga Simu: + 225- (0) 766-698662/ 754-285887/

    765-282809/0753-874835e-mail: [email protected] website:www.mwo.or.tz

    Mama akipika kwa kutumia mkaa wamawe katika sufuria ya kawaida

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    17/20

    17BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    BRIKETI ZA MAKAA YA MAWE YA

    NGAKA-MAKAA BORA YA KUPIKIA 

    1:0 UTANGULIZI

    eknolojia ya utengenezaji wa briketi za makaaafi ya kupikia ni teknolojia inayopatikana katika

    machimbo ya Makaa ya Mawe ya Ngaka, hii nibaada ya kufanyika kwa utafiti uliofanywa naKitengo cha ubora wa Makaa ya mawe kutokaancoal Energy Limited kwa ushirikiano naMbawala Women Organization mnamo mwaka2014Matokeo ya teknolojia hii yanatoa jibu lamatatizo yaliyodumu kwa muda mrefuyaliyotokana na ukataji miti kiholela kwa ajili yamatumizi ya nishati.eknolojia ya Makaa boraya briketi ni rahisi, na ni mbadala wa nishatiamani. Ni suluhisho kwa kero za kuni na mkaa

    kwa matatizo na mateso yatokanayo na nishatihizo zitumikazo kwa matumizi ya nyumbani nakatika taasisi mbalimbali.metengenezwa kwa mchanganyiko wa chengahenga ( vumbi) la makaa ya mawe , udongo

    mfinyanzi, virutubisho, mabaki ya mazao yakilimo yaliyokauka, huchanganywa na majikatika kiwango maalumu.

    2:0 HATUA/ MAELEKEZO YAKUTENGENEZA BRIKETI ZA MAKAA Ni rahisi. Unaweza kuitengeneza nishati hiinyumbani au katika taasisi yako. MbalawalaWomen Organization tunatengeneza nishati hiikwa kutumia mashine maalumu ya briketi za

    makaa. Mashine hii hutoa briketi katika maumbombalimbali ya vitofali kama vile umbo duara,umbo ovali na, umbo mraba. Maumbo hayahuruhusu mzunguko wa hewa katika briketi zamakaa ili kurahisisha uwakaji.Pia briketi za makaa ya mawe zawezakutengenezwa kwa mikono kwa kutumia kifaakilichotengenezwa maalum kwa bati gumu (handmolder)

    2:1 Mchanganyiko wa chenga laini /vumbiza makaa na masalio mengine huchanganywana huongezwa kemikali maalum kitaalamu ilikuondoa sumu hatarishi ya karboni kwa afya yabinadamu/ mtumiaji, hivyo kufanya briketi zamakaa kuwa salama kwa matumizi ya kupikia.

    2:2 MUDA WA KUKAUKA Briketi za makaa bora huchukua muda wa siku 2au 3 kukauka kulingana na hali ya hewa baada yakutengenezwa.

    2:3 KIPINDI CHA MASIKA/ MVUA Kipindi cha masika ni rahisi njia mbadala yakukausha nishati hii huweza kukaushwa katikatanuru, au kivulini baada ya kutengenezwa.

    3:0 UWAKAJI3:1 Briketi za makaa bora ya Ngaka huwakavizuri. Moto unapoanza kukolea hutoa ulimimfupi rangi ya bluu kutoka katika jiko lake lakawaida kama jiko la mkaa lililotengenezwa kwaudongo ndani yake. (Ambalo hutunza joto).Makaa haya yakishawaka na kukolea vizurihayatoi moshi wala kutengeneza masizi ambayoyatachafua sufuria au vyungu vyako. Vipandevidogo 34 vya briketi ya makaa huwa na uzito wakilo moja baada ya kukauka na huhifadhi motokwa saa 3 hadi 4.

    3:2 UWASHAJI WAKEi. Weka vijiti vidogovidogo vikavu katikatindani ya jiko lako sehemu ya kuwekea mkaa 

    ii. Washa vijiti na weka vipande 3-4 vya briketiviache viwake pamoja kwa muda

     wa dakika 8-15iii. Ongeza briketi zako na uziache zikolee moto

    kwa muda wa dakika 8-15iv. Briketi zitakuwa zimewaka na kutoa rangi

    nyekundu kuanzia chiniv. Waweza pia kuwasha kwa kutumia mkaa

    kidogo uliokwishawaka kwa kuweka chinisehemu ya kuwekea mkaa . Kisha wekabriketi za makaa juu yake.

    3:3 MOTO KUWAKA Briketi za makaa ya mawe baada ya motokuwashwa huchukua takribani dakika 8-15kuwaka au kukolea 3: 4 eknolojia ya Makaa ya mawe safi ya Ngakaya kupikia ni teknolojia iliyobuniwa kuendana namazingira rafiki ya jiko la Kitanzania. eknolojiahii humruhusu mpishi/ mtumiaji kutumiavyombo au sufuria za kawaida za alumini.3:5Briketi za makaa ya mawe ya Ngaka huwa namoto mkali wa kutosha ingawa makaa hutumikakidogo sana ukilinganisha na nishati ya kunina mkaa wa kawaida .Mkaa kidogo hutumikakupikia muda mrefu. Ni rahisi kubana matumiziukilinganisha na matumizi ya nishati ya kuniau mkaa. Nishati hii huokoa gharama, hulindamisitu, na hutunza mazingira yetu

    Majiko yakiwa yamewashwa

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    18/20

    18   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    PRESS RELEASE INVITATION FOR BIDS FORPROCUREMENT OF FURNITURE AND EQUIPMENT

    FOR MINES OFFICESBID NO. ME/008/SMMRP/G/80

    1. Te United Republic of anzania (hereinafter called “Borrower”) has received Additional Financing from the International Development Association (IDA)(hereinafter called “Credit”) towards the cost of the Sustainable Management ofMineral Resources Project (SMMRP) and intends to apply part of this Creditto cover eligible payments under Contract for Procurement of Furniture andEquipment for Mines Offices

    2. Te Ministry of Energy and Minerals (MEM) now invites sealed bids from eligibleand qualified bidders for the supply of Furniture and Equipment as shown below:-

    Te above items constitute FIVE LOS. Bidders may bid for one or all lots, eachlot shall be considered separately and bidders shall quote all items and respectivequantities. Bids not quoting the items and quantities will be considered non –responsive and rejected for evaluation.

    3. Bidding will be conducted through the National Competitive Bidding (NCB)procedures specified under the Public Procurement Act No.7 of 2011: (Procurementof Goods, Works, Non Consultant Service and Disposal of Public Assets byender) Regulations, 2013 –and are open to all eligible bidders as defined in theRegulations.

    4. Interested eligible bidders may obtain further information from the Secretary,Ministerial ender Board, Ministry of Energy and Minerals (MEM), 5 Samora Avenue, 6th floor Room No. 10 Wing B, 11474 Dar es Salaam and inspect thebidding documents during office hours from 09.00 to 15.00 hours local time,Mondays to Fridays inclusive, except public holidays.

    5. A complete set of Bidding Document in English language may be purchased byinterested eligible bidders upon submission of a written application to the Secretary,Ministerial ender Board, Ministry of Energy and Minerals (MEM) Samora Machel Avenue, 6th floor Room No. 10 Wing B, 11474 Dar es Salaam and upon paymentof a non–refundable fee of ZS 150,000/= (anzania Shillings One Hundred FiftyTousand only) or equivalent amount in any intefreely convertible currency. Temethod of payment will be by banker’s cheque, banker’s draft payable in favor of

    Permanent Secretary, Ministry of Energy and Minerals.

    6. Bids in one original plus two (2) copies, properly filled in and enclosed in plainenvelopes, addressed to the address below and to be delivered to the Secretary,Ministerial ender Board, Ministry of Energy and Minerals (MEM) at 5 SamoraMachel Avenue, 6th floor, Room 611, Wing A, 11474 Dar es Salaam at or before10.00 hours, East African time on Tursday 21st April, 2016. Bids will be publiclyopened in the presence of the bidders’ designated representatives and anyone whochoose to attend immediately after the deadline of bids submission.

    7. All bids must be accompanied by a Bid Securing Declaration in the format providedin the relevant bidding document.

    8. Late Bids, Portion of Bids, Electronic Bids, Bids not received, Bids not openedand not read out in public at the bid opening ceremony shall not be accepted forevaluation irrespective of the circumstances.

    Permanent Secretary,Ministry of Energy and Minerals,P. O. Box 2000,

    Dar Es Salaam, Tanzania Tel: 255-22-2121606/7 Fax: 255-22-2121606E-mail: [email protected]

    Te Ministry of Energy and Minerals and Representatives of the BusinessEnterprises of anzania convened a meeting on Monday, 28th March

    2016 in Dar es Salaam to discuss the critical role of anzania in thedevelopment of the Uganda-anzania Crude Oil Pipeline Project.Te Meeting was chaired by the Permanent Secretary of the Ministryof Energy and Minerals and was also attended by the two DeputyPermanent Secretaries and other Senior Officials of the Ministry of Energyand Minerals. Also in attendance, were senior Officials from anzaniaPetroleum Development Corporation (PDC) and from the anzania Port Authority.During the opening, the Chair emphasized the Government’s readinessand willingness to work hand-in -hand with the Private Sector to ensurethat all projects have the input of the Private Sector and thereby optimallybenefit the rapid development and transformation of anzania. Te Chairrequested the Private Sector to explore all possible ways in which theycan enhance their participation in the promotion and development of theCrude Oil Pipeline Project from Hoima, Uganda to anga, anzania. Te Chair invited the representative of the PDC to make a formal

    presentation on the said pipeline and the opportunities therein, afterthe presentation, the Private Sector was invited to make comments andcontributions.

     After intensive discussions, the meeting resolved the following:1. o establish a high level Coordinating Committee consisting of the

    representatives of the Government of the United Republic of anzaniaand the Private Enterprises in anzania, to promote and develop theCrude Oil Pipeline from Uganda to anga, anzania.

    2. o promote and develop a Regional Value Corridor that shall link theIndian Ocean to the Atlantic Ocean. Te Value Corridor shall emanatefrom anga, anzania, through Uganda, DRC and up to the Port ofBanana in the DRC.

    3. o develop within the Value Corridor other Anchor Projects such as:• A Hub Port at Tanga Region, Tanzania.• Cross-border Gas Pipeline.

    • Cross-border Freight and Passenger Railway.• Cross-border Fiber Optic.• Cross-border Multi-product Pipeline.

    4. o promote and develop key strategic locations along the ValueCorridor, new Corridor Anchor owns (CAs), designed as SpecialEconomic Zones. Te (CAs) shall be designed to act as:

    • Centres of Training and empowering Small and Medium Enterprises(SMEs) so as to create Social-economic mobility and transformation.

    • Attract Regional and international capital to further socio-economictransformation.

    In conclusion, the Private enterprises of anzania pledge their fullcommitment and support to ensure the success of the short - and long-terminterests relating to this Project and the Value Corridor.

    Issued by  PERMANENT SECRETARY MINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    LotNo.

    Brief Description of Goods unit Qty  

    1 Supply of various Furniture and fitt ings for Mtwara Each Various

    2 Supply of various Furniture and fittings for Morogoro Each Various

    3 Supply of various Furniture and fittings for unduru Each Various

    4 Supply of various Furniture and fittings for SMMRPDar es Salaam

    Each Various

    5 Supply of Standby Generator for Eastern Zone Dar Each Item

    MINISTRY OFFICIALS AND BUSINESS

    ENTERPRISES OF TANZANIA DISCUSS UGANDA-

    TANZANIA CRUDE OIL PIPELINE PROJECT

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    19/20

    19BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    China yaonesha nia kuwekeza kwenye Sekta ya Nishati

    Na Greyson Mwase,Dar es Salaam

    Wawekezaji kutokakatika kampunizinazojihusishana uzalishaji

    wa nishati ya umeme kutokanchini China, wameeleza niaya kuwekeza kwenye Sekta yaNishati nchini.

    Waliyasema hayo katikakikao baina yao na NaibuKatibu Mkuu wa Wizaraya Nishati na Madinianayeshughulikia masualaya Nishati Dkt. MhandisiJuliana Pallangyo pamoja nawataalam kutoka Wizara yaNishati na Madini pamojana taasisi mbalimbali kamaShirika la Umeme Nchini(TANESCO), Shirika laMadini la Taifa (STAMICO),Shirika la Maendeleo laTaifa (NDC) na Mamlakaya Udhibiti wa Huduma zaNishati na Maji (EWURA).

    Akizungumza katika kikaohicho Mwakilishi kutokaUmoja wa Wafanyabiasharawa Jamhuri ya Watu waChina nchini Tanzania LinZhiyong, alisema kuwa nia yawatendaji wa kampuni hizokuja Wizarani ni kubaini fursazilizopo katika Sekta ya Nishatinchini kabla ya kuamua kujakuwekeza rasmi.

    Aliongeza kuwa kunaUjumbe Maalum wa

    wawekezaji kutoka nchiniChina unaotarajiwa kuwasilinchini mapema wiki ijayokwa ajili ya kupata taarifambalimbali zenye kubainishafursa za uwekezaji nchiniikiwa ni pamoja na MpangoKabambe (master plan), sera,na mpango mkakati katikaSekta ya Nishati, kabla yakusaini makubaliano ya awalikwa ajili ya uzalishaji wanishati ya umeme.

    Zhiyong alisisitiza kuwawawekezaji kutoka Chinawako tayari kushirikiana nawawekezaji wa ndani ya nchikwenye uzalishaji wa nishati yaumeme ili taifa liweze kupatanishati ya uhakika kwa ukuajiwa uchumi wa nchi.

    Wakati huo huo, Naibu

    Katibu Mkuu wa Wizaraya Nishati na Madinianayeshughulikia Nishati Dkt.Mhandisi Juliana Pallangyoalishukuru ujumbe huona kueleza kuwa fursa zauwekezaji kwenye Sekta yaNishati ni nyingi na kuwatakakuchangamkia fursa hizo.

    “Wananchi wanahitajinishati ya uhakika ambayoni kichocheo cha ukuajiwa uchumi wa nchi, hivyotunawakaribisha kuwekezakatika uzalishaji wa umemekwa kuwa tuna vyanzo vingikama vile gesi, jotoardhi,makaa ya mawe, jua, upepo

    na mawimbi ya baharui,”alisisitiza Dkt. Pallangyo.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt.Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akisalimiana na mmoja wa wajumbe kutoka kampuniuzalishaji wa makaa ya mawe ya Shenhua Ningxia Group Co. Limited kutoka China.(kushoto). Katikati ni Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri yaWatu wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt.Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akielezea fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nishatinchini. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri yaWatu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong.

    Sehemu ya ujumbe kutoka nchini China ukifuatilia majadiliano mbalimbali yaliyokuwayanaendelea katika kikao baina ya Serikali ya Tanzania na ujumbe huo.

    Mchimbaji wa Makaa ya Mawe kutoka Nchini Tanzania,Sara Masasi akielezea uzoefu wa kampuni yakekatika uzalishaji wa makaa ya mawe nchini katikakikao baina yao na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini anayeshughulikia masuala ya NishatiDkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalamkutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja nataasisi mbalimbali kama Shirika la Umeme Nchini(TANESCO), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka yaUdhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

  • 8/18/2019 Mem Bulletin 113 Edition

    20/20

    20   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandaoya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

    tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.ImetolewanaKitengochaMawasilianoSerikalini

    Na Teresia Mhagama

    Imeelezwa kuwa wakandarasiwenye tuhuma za kutolipa

    mishahara wafanyakaziwao, kuomba rushwakwa wateja wanaotaka

    kuunganishiwa umeme nakutolipa fedha za watoa hudumawaliokuwa wakifanya nao kazikatika usambazaji umeme vijijiniAwamu ya Pili, hawatapewa kazihusika katika miradi ya REAAwamu ya Tatu.

    Hayo yameelezwa naWaziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo

     jijini Dar es Salaam wakatiakizungumza na kampunimbalimbali zinazotekeleza miradiya usambazaji umeme vijijiniAwamu ya Pili inayotarajiwa

    kukamilika mwezi Juni mwakahuu.“Kampuni zitakazopewa

    kipaumbele ni zile zilizofanyavizuri katika miradi ya REAAwamu ya Pili na kuonekanakuleta ushindani kwa kampuninyingine za ndani na nje ya nchikwa kufanya kazi waliyopewakwa bidii na kutokuwa na tuhumambalimbali ikiwemo rushwa,”alisema Profesa Muhongo.

    Awali Meneja Operesheni

    wa kampuni ya Engineering& Construction, Julius Katetiinayosambaza umeme vijijinimkoani Kagera katika wilaya za

    Ngara, Biharamulo, Misenyi,Karagwe, Kyerwa, Bukobavijijini na Muleba alimwelezaProfesa Muhongo kuwa kazi yausambazaji umeme katika mkoahuo imehusisha vijiji 451 nawanatarajia kuunganisha wateja30,000 kabla ya muda wa ukomouliowekwa na Serikali.

    Alisema kuwa katika wilayaza Ngara na Biharamulo jumlaya wateja 4385 wa njia moja yaumeme waliunganishwa kati yawateja 4554 na wateja 49 wa njiatatu za umeme waliunganishwaambapo jumla ya transfoma47 zilifungwa na kwamba kwawilaya za Ngara na Biharamulo

    wanatarajia kukamilisha kazihiyo ifikapo Aprili 20 mwakahuu na kuukabidhi mradi huokwa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO).

    Aidha alisema kuwa katikawilaya ya Karagwe jumla yatransfoma 82 zilifungwa na watejawa njia moja ya umeme wapatao3507 waliunganishwa kati yawateja 5480 na wateja 95 wa njiatatu ya umeme wameunganishwaambapo wanatarajia kukamilisha

    kazi mwezi Mei mwaka huu.“Mheshimiwa Waziri, kwa

    upande wa wilaya ya Kyerwatumeshafunga transfoma 63ambapo lengo la awali lilikuwani kufunga transfoma 53, na kwawilaya hii wateja 2044 wa njia mojaya umeme wameunganishiwaumeme kati ya wateja 3228 nawateja 30 wa njia tatu za umemewaliunganishwa na tunatarajiakuendelea kuunganisha watejahadi kufikia mwezi Juni mwakahuu,” alisema Kateti.

    Vilevile alisema kuwa katikawilaya ya Misenyi jumla yatransfoma 52 zimefungwa

    ambapo wateja 1345 wa njia mojawaliunganishwa kati ya wateja4308 na wateja waliounganishwakwa njia tatu za umeme ni 17huku wakitarajia kukamilishakazi mwezi Juni mwaka huu.

    Aliongeza kuwa kwa upandewa wilaya za Muleba na BukobaVijijini jumla ya transfoma 118zimefungwa ambapo wateja5649 wa njia moja ya umemewaliunganishwa na hudumahiyo kati ya wateja 12,703 hukuwateja waliounganishwa katikanjia tatu za umeme wakifikia 22na wanatarajia kukamilisha kazimwezi Mei mwaka huu.

    Kwa upande wa kampuni

    ya JV State Grid, Meneja Mradiwa kampuni hiyo Mhandisi A.Mwaipaja alisema kuwa kampunihiyo inasambaza umeme vijijinikatika wilaya za Rungwe, Kyela

    na Ileje mkoani Mbeya ambapokazi ya kusambaza umeme katikawilaya hizo imekamilika kwaasilimi 92 hadi kufikia katikatimwa mwezi Machi mwakahuu na wateja wapya 2,244wameunganishwa katika vijiji 65na kufunga transfoma 90 kati ya133 wanazopaswa kufunga.

    Aidha katika wilaya yaMbarali mkoani humo, JV Stateimeshakamilisha kazi kwa asilimia92 hadi kufikia tarehe 15 Machi,2016 ambapo wateja wapya1724 kati ya 4505 katika vijiji 27wameunganishwa na transfoma35 kati ya 56 zimefungwa.

    Alisema kuwa kampuni hiyopia inafanya kazi ya kusambazaumeme vijijini katika mkoawa Kigoma katika wilaya Sitaza Kigoma Vijijini, Buhigwe,Kasulu, Kibondo, Kakonko naUvinza ambapo kazi imekamilikakwa asilimia 93 hadi kufikiaMachi 2016 na jumla ya vijiji63 na wateja 2,647 kati ya 8773wameunganishwa na umemekatika wilaya hizo.

    Kwa upande wake NaibuKatibu Mkuu anayeshughulikiaNishati, Wizara ya Nishati naMadini, Dkt. Mhandisi JulianaPallangyo aliwataka wakandarasiwanaotekeleza miradi ya

    usambazaji umeme vijijinikujiepusha na masuala ya rushwakatika utekelezaji wa miradi hiyohasa katika zoezi la uunganishajiumeme kwa wateja.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo(katikati) akiwa katika kikao na kampuni ya Engineering &Construction inayosambaza umeme vijijini mkoani Kagerakatika wilaya za Ngara, Biharamulo, Misenyi, Karagwe, Kyerwa,Bukoba vijijini na Muleba kilichofanyika katika ukumbi waWizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wa kwanzakulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),Dkt. Lutengano Mwakahesya na anayemfuatia ni Meneja waTanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga.Wengine niwatendaji kutoka kampuni hiyo, Wizara na REA.

    Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt.Mhandisi Juliana Pallangyo (wa kwanza kushoto), Menejawa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga (wapili kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa NishatiVijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya (wa Tatu kushoto)wakiwa katika moja ya vikao vilivyojumuisha wakandarasiwanaosambaza umeme vijijini vilivyoanza tarehe 29 Machi nakumalizika tarehe 31 Machi, mwaka huu.

    Wakandarasi wasiolipa mishahara,madeni kutopewa kipaumbele REA III