mazingira ya mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu...

12
Baada ya kukaa na watalaamu, viongozi, wazee, wakinababa, wakinamama na watoto wa Kijiji cha Mweka, Wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, sasa imefika wakati wa kupeana maoni na kubadilishana mawazo juu ya uhifadhi. Katika utafiti niliuliza: Je, mazingira yanabadilikaje? Je, uchumi wa Mweka unabadilikaje? Je, kuna uwezo na utalaamu gani katiaka kuboresha mazingira na uchumi kwenye Kijiji cha Mweka? Mazingira ya Mweka 2010 1 Katika historia ya Mweka, wazee wanaelezeka kwamba kwenye kipindi cha uhuru kuanzia mwaka 1961, kaya zilikuwa chache, wazee walikuwa na faida kwenye kahawa, walikuwa na nafasi kulima na kuchungia mifugo msituni, na baada ya ujamaa, kwenye eneo la Chibo. Ukame wa njaa ilitokea kila miaka kumi. Kuanzia kipindi cha vita vya Kagera mwaka wa 1978, hali imebadilika. Bei ya kahawa ilishuka kwenye soko la dunia, sera ya uchumi na kilimo ilibadilika kuondoa ruzuku na mikopo na kupandia bei ya kilimo hasa dawa ya kahawa. Vilevile sheria ya msitu wa Kilimanjaro zilianza kuzuia matumizi ya msitu hadi yakachukuliwa na Hifadhi ya Kilimanjaro kusabibishwa na uharabifu wa msitu. Wakulima wa Mweka wakafyeka mikahawa na kuotesha mahindi kwenya shamba lao na kwa sababu mahindi hayakubali vuli, wakaangusha miti mingi. Linganisha picha iliopigwa kutoka ndege mwaka wa 1962 (ukurasa wa 2) na picha iliyopigwa kutoka kwenye satelite (WorldView) za mwaka 2008 (ukurasa wa 3). Picha hizi zinaonyesha Mabadiliko ya Mazingira:

Upload: others

Post on 13-Oct-2019

37 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

Baada ya kukaa na watalaamu, viongozi, wazee, wakinababa, wakinamama na watoto wa Kijiji cha Mweka, Wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, sasa imefika wakati wa kupeana maoni na kubadilishana mawazo juu ya uhifadhi. Katika utafiti niliuliza: Je, mazingira yanabadilikaje? Je, uchumi wa Mweka unabadilikaje? Je, kuna uwezo na utalaamu gani katiaka kuboresha mazingira na uchumi kwenye Kijiji cha Mweka?

Mazingira ya Mweka 2010

1

Katika historia ya Mweka, wazee wanaelezeka kwamba kwenye kipindi cha uhuru kuanzia mwaka 1961, kaya zilikuwa chache, wazee walikuwa na faida kwenye kahawa, walikuwa na nafasi kulima na kuchungia mifugo msituni, na baada ya ujamaa, kwenye eneo la Chibo. Ukame wa njaa ilitokea kila miaka kumi. Kuanzia kipindi cha vita vya Kagera mwaka wa 1978, hali imebadilika. Bei ya kahawa ilishuka kwenye soko la dunia, sera ya uchumi na kilimo ilibadilika kuondoa ruzuku na mikopo na kupandia bei ya kilimo hasa dawa ya kahawa. Vilevile sheria ya msitu wa Kilimanjaro zilianza kuzuia matumizi ya msitu hadi yakachukuliwa na Hifadhi ya Kilimanjaro kusabibishwa na uharabifu wa msitu. Wakulima wa Mweka wakafyeka mikahawa na kuotesha mahindi kwenya shamba lao na kwa sababu mahindi hayakubali vuli, wakaangusha miti mingi. Linganisha picha iliopigwa kutoka ndege mwaka wa 1962 (ukurasa wa 2) na picha iliyopigwa kutoka kwenye satelite (WorldView) za mwaka 2008 (ukurasa wa 3). Picha hizi zinaonyesha

Mabadiliko ya Mazingira:

Page 2: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

2

Kijiji cha Mweka 1962

Page 3: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

3

Kijiji cha Mweka 2008

Page 4: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

0

50

100

150

200

250

300

350

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12

mm

Mvu

a

Mwezi

Kibosho Mission Mvua(kujumlisha kila nusu mwezi)

Kibosho 1967-1974

Kibosho 2002-2009

0

500

1000

1500

2000

1967-1974 2002-2009

341 382

1599 1362

Kibosho Mission Mvua

Masika: Jan-July

Mvuli: Aug-Dec

4

uharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa. Wakulima asilimia kubwa wamelalimika kwamba mazao yanapungua kutokana na jua kali, kukosa mvua, na ardhi kuchoka. Kwa kweli kuanzia mwaka 1920 katika Kibosho Mission mvua zimepungua asilima 39, sawa na jumla milimeta 986. Ukilinganisha wastani wa mvua kwa kipindi cha 1967 hadi 1974 na 2002 hadi 2009, zimepungua asilimia 10, sawa na jumla milimeta 195. Upunguzo umetokea kwenye mvua wa masika na kipindi cha mwezi wa 7 hadi mwezi wa 9.

Page 5: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

Mabadiliko ya Uchumi:Kwanza watu wengi wameshakata tamaa kuotesha kahawa, lakini watu wachache sana wanaweza kuotesha ndizi, mahindi na maharage ya kutosha kwenye mashamba yao. Baada ya hapo upatikanaji wa kazi za kawaida ulikuwa mgumu zaidi kwenye ukame, bei za chakula zilipanda, gharama za shule, afya, nishati na kilimo zilipanda. Vilevile maliasili kama kuni, mbao, maji na majani ya mifugo yanakuwa shida kwa sababu ya sheria na uharabifu wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, watu walianza kulima mbali na mifereji, na maeneo ya watu kuwa madogo kutokana na uongezeko kubwa la watu. Sababu moja kubwa iliyochangia

hali ya uchumi kuzorota ni ongezeko kubwa la idadi ya watu. Ongezeko hilo lilisababisha ardhi na maliasili kugawiwa mpaka hazikutosha.

Katika ukame, watu walionunua mbegu,

kukodisha mashamba porini, au kulipa vibarua kulima walipata hasara kubwa kutokana na gharama za kulima. Vilevile bei za chakula huwa zinaongezeka na kazi za kibarua zinapungua kwa ujumla. Hasara nyingine ni kwamba watu wakipata dharura au wakiwekeza fedha kwenye kilimo katika mwaka wa ukame wanaweza kukosa fedha za kulima porini katika mwaka unaofuata. Tofouti ya mahindi, kwenye ukame watu wenye miparachichi bado wanauza matunda, watu wenye uwezo ya kumwagilia maji bado wanapata ndizi pamoja na mboga, watu wenye mihogo, majimbi, na viazi huwa wanapata mazao. Vilevile kama mtu amejitahidi kuotesha miti ya vuli na mbolea shambani na kumwagia samadi na maji, ataendelea kupata faida kidogo kutoka kahawa.

5

0

200,000

400,000

600,000

800,000

1,000,000

1,200,000

1920 1940 1960 1980 2000

Idad

i ya

Wat

u

Mwaka

Idadi ya Watu wanaoishi Kilimanjaro

Page 6: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

6

Kwanza, kuna wakulima wameshaona faida ya kuotesha miti shambani, kutunza migomba, na kuotesha kahawa upya. Ni kweli hawawezi kuvuna mahindi mengi, lakini faida ya ndizi, kahawa na viazi inazidi mavuno ya mahindi. Vilevile kilimo mseto husaidia kutunza mazao mchanganyiko tofauti ya kilimo cha shamba la mahindi kwenye jua kali, ukame, na upepo mkali. Ardhi iliyolimwa na kuoteshwa mahindi inakauka haraka na haina chochote cha kuzuia upepo. Soma kwa kulinganisha picha ya kilimo mseto

na shamba la mahindi. Kwenye upande wa kushoto miti iliooteshwa mpakani wa shamba (mstali nyekundu) inleta vuli na mbolea, inazuia upepo, na inazuia momonyoko ya ardhi kwenye bonde. Kwenye upande wa kulia, mahindi na migomba inakauka na inaharibikwa na upepo.

Kwenye upande wa uchumi, historia ya familia inaweza kusabibisha umaskini hata kama mtu ni mchapakazi na yuko makini. Kwa mfano, wazee wakikaa na wajukuu wakati wazazi wao wanafanya kazi mjini, mara nyingi wanakosa nguvu ya kulima shamba. Vilevile kama mama ni mkuu wa kaya pekee yake, ni vigumu sana kwake kupata mda ya kufanya kazi, kulima shamba mbali ya nyumbani, na kushiriki kwenye maendeleo ya vikundi na kijiji. Kama kijiji kikipata semina au miradi ya maendeleo inatakiwa mtembelee kaya za wazee na wanawake ili kuwapatia taarifa.

Uwezo Wa Kuboresha Mazingira na Uchumi:

Miti ikazungusha na ikalinda shamba Shamba lililoachwa wazi bila kupandwa miti ya jua kali na upepo

Page 7: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

7

Hizi picha zilipigwa katika maeneo sawa na ya picha ya ukurasa wa 6. Kushoto: kahawa na migomba yanaota vizuri chini ya migrevelia. Kulia: mahindi na migomba

iliyopigwa na jua kali na upepo mkali.

Pili, Watanzania wanaanza kujifunza namna ya kuboresha mazao na thamani ya kahawa, hasa kutumia mfumo wa kilimo bila ya matumizi ya sumu na pia kwa kutumia mbolea ya asili. Orera Goods Community wameshaanza kuotesha kahawa upya na kushirikiana kusafisha na kuuza kahawa kwa bei nafuu. Kwanza, jaribu kuongeza mazao kwa kuotesha kahawa upya, kuchanga, na kutengeneza mbolea mkusanyiko bora.

Wakinamama wa Orera wakisafisha kahawa Orera Central Pulping Unit

Page 8: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

8

Tatu, jifunzeni kutoka kwa watalaamu wa ufugaji namna ya kufuga mifugo mbalimbali. Watu wanapaswa kujiunga na vikundi vya mifugo kwa ajili ya kugawana gharama, kubadilishana mawazo, kupata dawa na lishe bora, kutafuta soko, na kupata mikopo ya kuanzisha miradi ya mifugo. Kuna mifugo ipo kulingana na uwezo wa kila mmoja kuanzia sungura, kuku, bata, kondoo, mbuzi wa maziwa, nguruwe na ng’ombe wa maziwa.

Nne, Tunzeni vyanzo vya maji kwa kuotesha miti na nyasi kuzuia mmomonyoko wa ardhi, kuzuia uchafu usiingie kwenye maji, na kuhakikisha chemchem hazikauki. Kwa ujumla hakikisheni kwamba kila mmoja anaweza kumwagilia maji shambani. Watu wenye mifereji iliyokatwa na maendeleo kama barabara, watu waliogawiwa maeneo mbali na mifereji, na watu wenye mifereji iliyoachwa washirikiane kufikisha maji kwao kwa utengenezaji wa mfereji au kugawana

Watu wengi wanategemea Chemchem Kichao lakini

hapajatunzwa vizuri

Page 9: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

9

zamu ya kutumia mipira na pampu za kumwagilia maji. Pia, watumiaji wa mifereji wakumbuke namna ya kutumia mabwawa ya kuhifadhi maji.

Watu wanaofuga samaki wanafaida lakini kutokana na ukame na kupungua kwa maji, watu wachache wana uwezo

wa kufuga samaki. Wenye mifereji wakisaidiana kutengeneza na kutunza mabwawa, wagawane faida ya samaki.

Tano, Otesheni miti kama akiba. Ukihitaji kulipia mtoto shule, kulipia gharama ya hospitali, au kununua

chakula kwenye mwaka wa ukame, utauza mti badala kuuza kuku na kukosa mayai au kuuza mifugo na kukosa maziwa, nyama na mbolea. Changanya miti ya mda mfupi kama kabilia pamoja na miti ya mbao mgumu na bei kubwa kama teak na mahogany. Ingawa mtu anahitaji kibali cha kuangusha mti wa mahogany, mteja wa kununua mbao ndiye anayelipa. Bei ya mahogany kwenye soko la dunia inaongezeka kwa sababu hairusiwi kuangusha mahogany ya Mmarekani Kusini tena. Mbao ya mahogany ya kutengeneza gita moja inauzwa dola 150 ya marekani, na bei ya mbao ya futi moja haishuki elfu moja maeneo ya mengi Moshi.

Mzungu akasimama kwenya bwawa wa kuhifadhi maji

Mbao ya Mahogany Gita

Page 10: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

10

Sita, msikubali kuuza mali au mazao kwa bei rahisi hapa kijijini. Fanyeni utafiti juu ya soko la mali kwa kuwasiliana na rafiki na ndugu zenu mjini Moshi, Arusha na Dar es Salaam kabla hujauza chochote. Mfanyabiashara akija kwako kununa parachichi, mbao, kahawa, au chochote inamaana anapata faida zaidi. Je, kwa nini mkiwa watu wengi mnaouza maparachichi msishirikiane kuvuna na kupeleka sokoni na kubakiza faida kwenu badala kwa mfanyabiashara kutoka nje?

Saba, Kuna mradi wa kuotesha vanila umeanzishwa katika mkoa wa Kilimanjaro kwa nguvu ya shirika la Tanzania Indigenous Poverty Eradication Initiatives (TIPEI). Duniani vanila ni asili yake ni Mexico na pia imeoteshwa Madagascar,

Uganda na Indonesia. Hapa Tanzania inaoteshwa Zanzibar, Kagera, na sasa Kilimanjaro. Vanila inaota kwa kupanda mti mwingine uitwao mchimbakaburi (Jatrofa). Hauhitaji dawa na inatakiwa kimvuli, mbolea na maji yamwagiliwe lakini yasikae. Inakomaa baada ya miaka miwili hadi mitatu halafu inaendelea kutoa mazao kwa miaka kumi na tano. Inawezekana kuvuna kilo moja kutoka kila mti na bei haijawahi kushuka chini ya dola 5 kwa kilo inaweza kuzidi dola 30 kwa kilo. Vanila ikaoteshwa Zanzibar

Page 11: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

11

Nane, Roots and Shoots duniani siyo kikundi ambacho kinaweza kutengwa. Kila mmoja anaweza kuwa mshiriki akiwa na moyo na wito kufuatana na wito wa Roots and Shoots, ilivyoanzishwa na Dr. Jane Goodall na wanafunzi wa sekondari Dar es Salaam mwaka wa 1991.

1. Kujenga heshima na huruma kwa vitu vyote vinavyoishi duniani.2. Kujenga uelewano wa watu wa kila utamaduni na dini3. Kutia moyo kwa kila mmoja kutenda kuboresha dunia kwa binadamu, wanyama na mazingira.

Ina maana kila mmoja anakaribishwa kwenye Roots and Shoots kubadilishana mawazo na kujitolea kuboresha dunia. Vivyohivyo, kikundi cha watu 12 kutoka Canada, Marekani na Tanzania kilianzisha kamati ya Kilimanjaro Task Force mwezi wa 11 mwaka wa 2010. Sisi wote ni wanafunzi na watu wazima wanaojitahidi kuendeleza kujifunza na kujitolea. Tuna lengo la kuboresha uhifadhi wa mazingira ya Mlima Kilimanjaro kwa njia ya ushirikiano na wanajamii kutengeneza miradi ya uhifadhi, elimu na maendeleo ya elimu mazingira na uchumi kwa ujumla.

Wanakamati wa Kilimanjaro Conservation Site Task Force wakaanzisha kamati

Page 12: Mazingira ya Mweka 2010 - josephholler.com fileuharabifu wa mazingira kwenye eneo la msitu Kilimanjaro, maeneo karibu na msitu, mabonde na mito, vianzo via maji, na mashamba ya kahawa

12

Shukrani:

Kitabu hiki kimewezekana kwa ushirikiano ya Chuo Cha Buffalo, New York, uongozi na wanajamii wa Kijiji cha Mweka, the Jane Goodall Institute, the Kilimanjaro Conservation Site Task Force, Orera Community Group, Tanzania Commission of Science and Technology (COSTECH), Pangani Water Board, Mweka College of African Wildlife Management, GeoEye Foundation, National Science Foundation, Mark Diamond Research Fund, na Hugh Grant Applied GIS Award. Watu waliojitolea ushauri na misaada mbalimbali ni Pius Kimario, Joseph Mallya, Abubakari Sekievu, Thadeus Mrema, Dr. Makundi, Gumbo Mhandeni, Japhet Mwanang’ombe Philip Jacob na Elana Daniels. Shukrani, Joseph Holler

Dr Jane Goodall pamoja na wanakikundi akafungua maktaba ya Roots and Shoots na akasherehekea miaka 50 ya utafiti na utunzaji wa mazingira na sokwemtu wa Gombe