bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

32
Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu CHOO BORA NA MAZINGIRA SAFI WILAYA YA KONGWA

Upload: ana-ezazo

Post on 06-Apr-2016

483 views

Category:

Documents


17 download

DESCRIPTION

Katalogi hii ni matokeo maalum ya mradi”kufikia uboreshwaji wa usafi wa mazingira kwa wote ambao hawakuweza kufikia, kupitia utafiti na suluhisho sahihi”umefadhiriwa na “Water and Sanitation Systems for Development Cooperation Group” (GCSASD) of the Polytechnic University of Madrid from its ‘XIV Call for grants for university development cooperation actions 2013”. Lengo maalum ni,kutambua,kuchambua,kuendelea,kuhamasishwa unafuu, ubora na uimara wa suluhisho la usafi wa mazingira katika mazingira ya Wilaya ya Kongwa. Utekelezaji wa kazi umefanyika kwa ushirikiano kati ya GCSASD, ONGAWA na chou kikuu cha Ardhi. Mradi huu unatekelezwa ndani ya mpango wa mradi wa UMATA, ambao unafadhiriwa na GSF, Unalenga kuongeza uwezekano wa matumizi wa vifaa bora vya usafi wa mazingira na kubadili tabia mbaya za usafi wa mazingira kwa ukubwa wake. Umeanzishwa ili kuongeza kampeni ya taifa ya usafi wa mazingira Tanzania.

TRANSCRIPT

Page 1: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

choo bora Na maziNgira safiWILAYA YA KONGWA

Page 2: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

2

. UPM - Politechnic University of Madrid

. GCSASD - Grupo de Cooperación de Sistemas de Agua y Saneamiento para el Desarrollo ( Water and Sanitation Systems for Development Cooperation Group). Tsh - Tanzanian shillingi. ToT - ‘Trainings of Trainers’, inatumika kwa wale waliopata mafunzo hayo

vifupisho

. ft - futi

. ‘‘ - inchi

. m - mita

. m3 - mita na ujazo

. cm - sentimeta

. l - lita

. pipa- 200l

. Kg - Kilogram

. mchanganyo wa uwiano : simenti : mchanga : kokoto

. mbao ya frem - 1’’ x 8’’ x 12 ft

. wavu - 2,64 x 1,32 m

. nondo 12mm x 40 ft

. mfuko wa Simenti - 50Kg

. ndoo - 10l (ujazo halisi mpaka na kilima ni: 12.5l)

vizio na viPiMo

Kwa ukubwa wa tofali za simenti na za kuchoma vitumike kwa makisio kama ilivyooneshwa hapo juu, japokuwa vipimo vya ukubwa tofauti tofauti vinapatikana katika wilaya ya Kongwa.

Kwa urahisi wa kutumia, vipimo vilivyopo kwenye katalogi hii vimezingatiwa vile ambavyo hutumika kwenye mazingira yanayotuzunguka, japokuwa vipimo hivyo havifanani:

. ‘ndoo’ kwa ‘mchanga’ na ‘kokoto’ na kiasi kidogo cha maji ’pipa’ kwa kiasi kingi cha maji . ‘pipa’ for big amounts of water. ‘mfuko’ kwa ‘simenti. Kama kiasi ni kidogo, ‘Kilogramu’ itumike. ‘‘inchi’ (“) kwa vipimo ya matirio ndogo ndogo, mfano: unene wa mbao.. ‘feet’ (ft) kwa vipimo ya malighafi vikubwa, mfano: urefu wa mbao

. ndoo ya mchanga iliyo jaa katika usawa - 20.76 Kg

. ndoo ya mchanga iliyo jaa na kilima- 21.96 Kg

. ndoo ya kokoto iliyo jaa katika usawa - 20.50 Kg

. ndoo ya kokoto iliyo jaa na kilima - 22.40 Kg

30 cm

15 cm

10 cm45 cm

21 cm

15 cm

tofali ya simenti tofali ya udongo

Page 3: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

3

YALIYOMO

. Utangulizi

. Jinsi ya kutumia katalogi hii

. Mfumo wa Usambazaji

. Mawasiliano ya muhimu .Ngaziyamabadilikoyausafiwamazingira

> AINA ZA VYOO

. Choo cha kawaida cha shimo

. Choochashimokilichoboreshwa

. Choo cha kuvuta maji

> AINA mbAlImAbAlI ZA mAshImO, VIbANdA NA ghArAmA ZAke

. SHIMO

. BAMBA

. KIBANDA CHA CHOO . VITU VYA ZIADA

. VINAWIA MIKONO

4

5

6

7

8-9

10-15

11

12-13

14

16-29

16-19

20-23

24-27

28

29

Page 4: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

4

UTANGULIZI

Kwanini katalogi hii imeandikwa? :

Kwa ujumla, inajibu changamoto za usafi wa mazingira na afya ambazo sekta ya afya ilikuwa inakumbana nazo karne zilizo pita duniani kote na Tanzania.

Kwa mkoa wa Dodoma takwimu za mwisho zilizofanywa wakati wa kuanzishwa kwa mradi wa UMATA zinajieleza zenyewe. Katika wilaya tatu za Bahi, Chamwano,na Kongwa. Utafiti unaonyesha kwamba: . Asilimia 22 % tu ya kaya ndio wanapata huduma bora ya Usafi wa mazingira. . Asilimia 4 % ya watu wazima ndio wanaojihusisha na unawaji wa mikono.

Hali hii ina athari ya mojo kwa moja kwa afya ya jamii, kwa vile usambaaji wa ugonjwa wa kuha-risha ambao ni gonjwa la tatu kati ya magonjwa kumi yanoyosababisha vifo kwa watoto chini ya miaka mitano kwa Tanzania.

Ambapo ni kikwazo kikubwa sana kwa familia kuondokana na umasikini ambapo ina athiri ngu-vu kazi kufanya shughuli za kiuchumi na kupunguza muda wa kufanya shughuli za uzalishaji, na kuathiri afya za familia, maalumu ni kwa watoto ambao wana athiriwa na kina mama na watu wenye mahitaji maalumu na kupunguza utu miongoni mwao.

Wilaya zilizoonyeshwa hapo juu ni kati ya wilaya ishirini ambazo zina idadi kubwa za vifo vya watoto chini ya miaka mitano katika inchi yetu.

Kwa kutatua tatizo hili mipango kazi inatakiwa kufanya kazi kulingana na mahitaji kupitia ma-tangazo ya afya na usafi wa mazingira, lakini kwa kutoa motisha kwa wale wanaonyesha utayari wa kujenga na kuboresha huduma za usafi wa mazingira kwa bei nafuu na upatikanaji wa urahisi wa bidhaa na vifaa vitavoifikia jamii.

Kwenye sehemu ya pili ya katalogi tatizo limeonyeshwa kwa ukubwa na namna ya kutatua tatizo hili.

Njia hii iliyotumika ndio iliyoonekana ikitumika kongwa,maboresho na mapendekezo yalitolewa na mafundi.

Page 5: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

5

JINSI YA KUTUMIA KATALOGI HII

Katalogi hii imeandaliwa ili kuwasaidia mafundi na wafanyabiashara kama zana itakayowasaidia katika shughuli zao:

1. Tambua njia sahihi ya mfumo wa usambazaji, pamoja na wauzaji wa jumla (Mfumo wa usambazaji).

2. Anzisha mahusiano kati yenu na viongozi wa serikali za mitaa (Mawasiliano ya muhimu).

3. Elezea kwa wateja aina tofauti tofauti za vyoo na ipi ni nzuri kwa mahitaji yao:

Kama kazi ya kufanya ni ya kujenga au kuboresha choo fundi anaweza kumshauri mteja kwa kupitia na kumuonyesha aina za vyoo na ushauri uliotolewa kwa kila aina ya choo hususani kwa kila kurasa ya kila aina ya choo.

Hizi ni alama muhimu ambazo zimetumika katika katalogi hii (chini ya kila kurasa kwa kila choo):

4. Elezea wateja gharama zinatoka wapi na andaa gharama za awali kwa ajili ya wateja, wakati fundi na mteja wamekubaliana kazi ya kufanya , cha kwanza makadirio ya gharama yanaweza yakafanywa kwa kuangalia mada za aina mbalimbali na gharama zake . kwa ujenzi wa choo kipya moja kati ya vipengele vinne vifuatavyo vinaweza kuchukuliwa:

. Shimo . Bamba . Kibanda cha choo . Vinawia mikono

JUMLA KUU itatofautiana kulingana na aina iliyochaguliwa. Gharama halisi ya malighafi hazihu-sishi usafiri.

maji yanayohitajika kumwagia chooni ni kidogo

maji yanaweza kutu-mika mara nyingine kwa kumwagia chooni

salama kwa watoto

walemavu wanaweza kutumia aina yoyote ya choo kama vitajengwa na kuwekwa vizuri

maji yanyohitajika kumwagia chooni ni mengi sana

mtego maji unazuia harufu mbaya na inzi

bamba na kibanda vinaweza kutumika kwa mara nyingine

mfuniko utumike ili kuzuia harufu mbaya na inzi

bomba la kutolea hewa chafu lifungwe na wavu juu ili kuzuia inzi

choo kinata-kiwa kiwe na kinawia mikono

Page 6: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

6

Kijiji

Afisa wa kata

Kata na muuzaji wa jumla na duka la mfanyabiashara

Kijiji na duka la mfanyabiashara

MFUMO WA USAMBZAJI

Ramani hii inawaonyesha mafundi na wafanyabiashara wapi watapata malighafi kutoka kwa wauuzaji wa jumla kwa ajili ya kusambaza baadae kwa jamii. Wafanyabiashara wote ambao walisha-anza kufanya biashara katika vijiji pia wameonyeshwa kwenye Ramani hii.

ChitegoPingalame

ZoissaLeganga

Kinangali Mogeseni

MakawaNorini

MatongoroMlanje

Mkoka

Songambele B

Banyibanyi

MkutaniMsunjulile

Hogoro

Chamae

MsunjililiSejeli

Mbande

Vilundilo

Machenje

Mautya

Kongwa

Ibwaga

MsingisaLaikala

SagaraIjaka

Iduo-Kisimani

Ihanda

Suguta

ChamkoromaTubugwe

Mang’weta

Mseto

Mlali-Iyegu

Mlali-Bondeni

Ng’humbi

Pembamoto

Mmfukoilwa

Chigwingwili

Ndalibo

Ngomai

Mtanana A

Mtanana B

Manyata

NjogeHembahemba

Kiteto

Lenjulu

KibaigwaPandambili

Ndurungumi

Vihingo

Lengaji

Chiwe

Moleti

Majawanga

Ugogoni

Gairo

Page 7: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

7

MAWASILIANO YA MUHIMU

Andika kwa kalamu ya penseli namba za mawasiliano kwa watu wakupata ushauri, maelezo katika ngazi ya kata

PUGU (Pata Ujuzi Gawia Umma)

WEO (Ward Executive Officer - Afisa mtendaji wa kata)

WAFANYABIASHARA

VEO (Willage Executive Officer - Afisa mtendaji wa kijiji)

MAFUNDI

Kata Kijiji Jina Namba ya simu

Kata Kijiji Jina Namba ya simu

Kata Kijiji Jina Namba ya simu

Kata Kijiji Jina Namba ya simu

Kata Kijiji Jina Namba ya simuKONGWA MLANGA COSMAS MGASSA 0755 367167 / 0782 862 445SEJELI MBANDE BARAKA NHENJE 0757 390 388 / 0764489308KONGWA MLANGA ATHANASIO CHILONWA 0656 470 969UGOGONI CHIMOTOLO ISAACK MTAMBULO 0684 543 927 / 0758 216 326KONGWA KONGWA ABUBAKARI MJILI 0716 835 835 / 0759 812 982UGOGONI IBWAGA CLEMENT LUGWALU 0652 873 618

Kikundi kimeundwa na mafundi waliohudhuri mafunzo ya wakufunzi (ToT). Kikundi hiki ni wavumbuzi wa bidhaa na mifumo ya biashara, wanaweza wakatoa malighafi na ushauri kwa mafundi wanaohitaji kutoka kwao. Mafundi hawa wameunganishwa na Halmashauri ya wilaya.

Vifyatulio (KIBAO) vya mabamba vitakuwa vinatolewa na Afisa Mtendaji wa kata husika.

Afisa mtendaji wa kijiji atahusika na kuhakiki na kutia saini kwenye ripoti ya maendeleo ya kazi za mra-di katika kijiji chake.

Kazi yao maalum ni kutoa malighafi ambazo zinahitajika kutengenezea bidhaa za usafi wa mazingira na vifaa kwa kaya na mafundi.

Watajenga na kuboresha bidhaa za usafi wa mazingira na vifaa kwenye kaya na taasisi. Mafundi wa-naweza kuomba msaada wa kitaalam kwa mafundi kutoka kikundi cha PUGU.

Page 8: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

8

Ngazi hii ya usafi wa mazinguira imeandaliwa kulingana na hali ya wilaya ya Kongwa.

Ili kupanda ngazi hii ya mabadiliko ya tabia ya usafi wa mazingira kua-chana na tabia mbaya za uchafuzi wa mazingira, kaya zinatakiwa walau kutumia vinawia mikono, vyoo vyenye bamba linalosafishika, choo chenye paa na mlan-go.

Aina mbalimbali za teknolojia za vyoo vimeonyeshwa kuanzia choo cha kawaida hadi choo kilicho bora zaidi:

. Choo cha kawaida cha shimo: shimo la hapohapo na bamba lenye mfuniko, kibanda chenye paa na mlango.

. Choo cha shimo kilichoboreshwa na bomba la kutolea hewa chafu:

. Choo cha shimo la nje kilichoboreshwa chenye bamba lenye mfuniko, kibanda chenye paa na mlango.

. Choo chaa shimo la nje cha asili cha kumwagia maji, kibanda chenye paa na mlango.

. Choo cha kusukuma kinyesi na maji:

. Choo cha kusukuma kinyesi na maji chenye mtego maji, kiban-da chenye paa na mlango.

Mfano wa kila aina ya choo imeelezewa kwenye mada inayofuata.

usafi wa maziNgira ulioboreshwa

usAfI WA mAzINGIrAAmbAO hAujAbOreKA

Choo kilichoboreshwa kina kinawia mikono pamoja na sabuni au majivu

KUJISAIDIA SEHEMUZA WAZI

KUJISAIDIA KATIKA SHIMO LILILOTANABAISHWA

CHOO CHA SHIMO CHA KAWAIDA

CHOO CHA SHIMO KILICHO BORESHWA

CHOO CHA KUMWAGIA MAJI

. KIFUNIKO . SILABU INAYOSAFISHIKA NA MAJI

KWA NAMNA GANI CHOO KINAWEZA KUBORESHA

Page 9: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

9

usafi wa maziNgira ulioboreshwa

NGAZI YA MABADILIKO YA TABIA YA USAFI WA MAZINGIRA

Choo kilichoboreshwa kina kinawia mikono pamoja na sabuni au majivu

Choo kilichoboreshwa cha asili cha kumwagia maji

Choo kilichoboreshawa cha shimo la moja kwa moja na bamba

KUJISAIDIA SEHEMUZA WAZI

KUJISAIDIA KATIKA SHIMO LILILOTANABAISHWA

CHOO CHA SHIMO CHA KAWAIDA

CHOO CHA SHIMO KILICHO BORESHWA

CHOO CHA KUMWAGIA MAJI

. KIFUNIKO . SILABU INAYOSAFISHIKA NA MAJI

KWA NAMNA GANI CHOO KINAWEZA KUBORESHA

Page 10: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

10

Page 11: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

11

CHOO CHA SHIMO CHA KAWAIDA

Mfuniko unaozuia inzi na harufu mbaya

Choo kilichoboreshwa kina kifaa cha kunawia mikono sabuni au majivu

Bamba linalosafishika

Faida zake

. Bei nafuu

. Kina usiri

. Kinasafishika

. Kinadumu

. Bamba linaweza kutumika tena

. Ni salama kama kitatumika pamoja na vinawia mikono. Ni kizuri sehemu ambayo maji ni machache au hakuna

Hasara zake

. Kinyesi hakijatengwa vizuri chaweza kuonekana . Kitatoa harufu kama hakitatumika vizuri

Kama udongo sio imara shimo lijengewe na tofali za kuchoma, bloku, au mawe

Page 12: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

12

choo Kilichoboreshwa cha shimo la moJa Kwa moJa Na bamba

Faida zake

. Bei nafuu

. Kina usiri

. Uwezekano mdogo wa kupata magonjwa ambukizi. Uwezekano mdogo wa kutoa harufu mbaya na inzi ukilinganisha na choo cha shimo cha kawaida

Hasara zake

. Hakuna mtego maji

. Kibanda hakiwezi kutumika tena kama shimo limejaa

Bomba la kutolea hewa lililofungwa na wavu.Bomba laweza kuwa ndani au nje ya choo

Choo kilichoboreshwa kina kifaa cha kunawia mikono na sabuni au majivu

Kama udongo sio imara shimo lijengewe na tofali za kuchoma, bloku, au mawe

mtiririko wa hewa

Page 13: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

13

choo Kilichoboreshwa cha asili cha Kumwagia maJi

CHOO CHA SHIMO KILICHO BORESHWA

Choo kilichobores-hwa kina kifaa cha kunawia mikono na sabuni au ma-jivu

Kama udongo sio imara shimo lijengewe na tofali za kuchoma, bloku, au mawe. Na zaidi pia mianya ya kupitishia maji inashauriwa.

Bomba la kutolea hewa na kufungwa na wavu.

Bomba lenye mteremko mdogo kuelekea shimo

Mtiririko wa hewa

Faida zake

. Bei nafuu

. Kina usiri

. Maji yanoyohitajika kwa kumwagia chooni ni machache.

. Uwezekano mdogo wa kuambukizwa magonjwa ambukizi. Uwezekano mdogo wa kutoa harufu mbaya na inzi ukilinganisha na choo cha shimo cha kawaida

Hasara zake

. Hakuna mtego maji

Page 14: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

1414

Page 15: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

1515

CHOO CHA KUMWAGIA MAJI

Faida zake

. Kina usiri

. Kina mtego maji

. Hakuna harufu

. Kina dumu kwa muda mrefu

. Kuboresha afya

Hasara zake

. Maji yanayohitajika kumwagia chooni ni mengi (sio sahihi kwa sehemu ambapo hakuna maji). Ni hatari kwa maji ya ardhini

Choo kilichobo-reshwa kina kifaa cha kunawia mi-kono na sabuni au majivuKama udongo sio imara

shimo lijengewe na tofali za kuchoma, bloku, au mawe. Licha ya shimo la kawaida na mianya ya maji, mara nyngi tanki la kinyesi na tanki la pembeni la kinyesi hutumika

Mtego maji

Bomba lenye mteremko mdogo kuelekea shimo

Page 16: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

16

Ushauri:

. Fanya uchaguzi kulingana na aina ya udongo.

. Kama ardhi sio imara jengea shimo kwa matofali ya udongo, bloku au mawe. Tofali za kuchoma ndio yaliyochaguliwa maana gharama zake za ujenzi ndani ya shimo ni ndogo ukilinganisha na nyingine.. Kama ardhi ni imara jengea sehemu ya juu ya shimo kabla ya kuweka bamba.. Kina cha shimo sehemu ambayo chanzo cha maji kipo karibu, umbali kutoka kina cha shimo na chanzo cha maji kiwe 2 m.. Kinatakiwa kujengwa umbali wa 30 m kutoka chanzo cha maji.. Shimo la ndani lililojengewa linatakiwa kupandisha ipasavyo kuzuia mafuriko nsimu wa mvua.uelekeo wa upepo unabidi uangaliwe ili kupunguza harufu mbaya ndani ya nyumba.. Shimo linatakiwa kujengwa sehemu ambayo watu hawakai wala kupita.

Udongowakudumu:

. Ukubwa wa shimo uzingatie ukubwa wa choo, idadi ya watu watakaotumia.

Saizi inayokubalika (upana na urefu wa shimo unategemea na ukubwa wa silabu saizi ya bamba kubwa ni 1,5 x 1,5 m):

. Kina cha shimo 3 m na karibia na hapo . Unene washimo 1,5 m na karibia na hapo

. Ukubwa wa shimo unaweza kupimwa kwa kutumia fomula hii:

V= 4/3 x C x P x N

V = Ukubwa wa shimoC = Uwezo wa shimo kubeba uchafu ( 0.04 m3/mtu/mwaka kwa shimo lenye maji 0.06 m3/mtu/kwa shimo kavu)N = Mwaka lilipotengenezwa (mwaka)P = Wingi wa watu uliokadiriwa4/3 = Shimo lipakuliwe au linyonywe kabla halijajaa, liwe limebaki kwa kiwango cha ¾ kabla ya kujaa

. Kama shimo limejaa njia rahisi ni kuchimba shimo jingine na kuunganisha na shimo lililojaa au kama picha ya choo inavyoonekana

1 21

2

1 2 1. shimo la kwanza2. shimo lililoongezewa

Page 17: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

17

SHIMO

Ainambalimbalizamashimo:

Shimo la hapoha-po lisilojengewa

shimo la hapohapo lililojengewa

Shimo dogo la maji taka na shimo kubwa la maji taka

Zuri kwa choo cha shimo cha kawaida na choo cha shimo kilichoboreshwa chenye bomba la kutolea hewa

Shimo la hapohapo

Shimo la pembeni

Shimo la pembeni lisilojengewa

shimo la pembeni lililojengewa

Zuri kwa choo cha asili kilichoboreshwa cha kumwagia maji chenye bomba

Zuri kwa choo cha kumwaga maji

Shimo dogo la maji taka

Shimo kubwa la maji taka

Page 18: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

18

. mchanganyo wa uwiano shimo 1:7

. mchanganyo wa uwiano mfuniko 1:4:8

Shimolapembenilililojengewa(1x1x3 = 3 m3)

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*ShimoKuchimba 3 m3 15,000 TshTofali za kucho-ma

80 kipande 100 Tsh 8,000 Tsh

Simenti 10 Kg 330 Tsh 3,300 TshMchanga 5 ndoo 250 Tsh 1,250 TshMaji 4 ndoo 25 Tsh 100 TshGharama ya fundi kwa kujenga juu ya shimo 15,000 Tsh

Jumla 42,650 TshMfunikoSimenti 25 Kg 330 Tsh 8,250 TshMchanga 7 ndoo 250 Tsh 1,750 TshKokoto 13 ndoo 300 Tsh 3,900 TshMiti 8 kipande 500 Tsh 4,000 TshMfuko au line 2 kipande 200 Tsh 400 TshMaji 4 ndoo 25 Tsh 100 TshBomba PVC 4’’ 1.5 m 2,500 Tsh 3,750 TshGharama ya fundi kwa Mfuniko 3,000 Tsh

Jumla 25,150 TshJumla Kuu 67,800 Tsh

Shimolahapohapolisilojengewa(1x1x3 = 3 m3)

Shimolahapohapolililojengewa(1,2x1,2x3 = 4,3 m3)

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Kuchimba 3 m3 15,000 TshTofali za kucho-ma

80 kipande 100 Tsh 8,000 Tsh

Simenti 10 Kg 330 Tsh 3,300 TshMchanga 5 ndoo 250 Tsh 1,250 TshMaji 4 ndoo 25 Tsh 100 TshGharama ya fundi kwa kujengsa juu ya shimo (ya ghara-ma zakuchimba shimo zimetolewa)

15,000 Tsh

Jumla Kuu 42,650 Tsh

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Kuchimba 4,3 m3 20,000 TshTofali za kucho-ma

384 kipande 100 Tsh 38,400 Tsh

Simenti 2 mfuko 16,500 Tsh 33,000 TshMchanga 42 ndoo 250 Tsh 10,500 TshMaji 1.5 pipa 500 Tsh 750 TshGharama ya fundi kwa kujenga juu ya shimo (ya ghara-ma zakuchimba shimo zimetolewa)

25,000 Tsh

Jumla Kuu 127,650 Tsh

. mchanganyo wa uwiano: 1:7

. mchanganyo wa uwiano: 1:7

Page 19: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

19

SHIMO

*Gharama inaweza kubadilika kulingana na bei ya malighafi. Wilaya ya Kongwa 2014 Gharama halisi ya malighafi hazihusishi usafiri.

Shimolapembenilililojengewa(1,2x1,2x3 = 4,3 m3)

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*ShimoKuchimba 4,3 m3 20,000 TshTofali za kuchoma 384 kipande 100 Tsh 38,400 TshSimenti 2 mfuko 16,500 Tsh 33,000 TshMchanga 42 ndoo 250 Tsh 10,500 TshMaji 1.5 pipa 500 Tsh 750 TshGharama ya fundi kwa kujengea juu ya shimo 25,000 Tsh

Jumla 127,650 TshMfuniko wa shimo Simenti 25 Kg 330 Tsh 8,250 TshMchanga 7 ndoo 250 Tsh 1,750 TshKokoto 13 ndoo 300 Tsh 3,900 TshMiti 8 kipande 500 Tsh 4,000 TshMfuko ua nailoni 2 kipande 200 Tsh 400 TshMaji 4 ndoo 25 Tsh 100 TshBomba PVC 4’’ 1.5 m 2,500 Tsh 3,750 TshGharama ya fundi kwa mfuniko 3,000 Tsh

Jumla 25,150 TshJumla Kuu 152,800 Tsh

. mchanganyo wa uwiano shimo 1:7

. mchanganyo wa uwiano mfuniko 1:4:8

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Shimo la maji takadogo ( 1.2 x 2.4 x 2.4 = 7 m3 )Kuchimba 7 m3 60,000 TshTofali za kuchoma 600 kipande 100 Tsh 60,000 TshSimenti 8 mfuko 16,500 Tsh 132,000 TshMchanga 126 ndoo 250 Tsh 31,500 TshKokoto 30 ndoo 300 Tsh 9,000 TshMaji 5 pipe 500 Tsh 2,500 TshWavu 1 kipande 17,000 Tsh 17,000 TshNondo 12mm 1 kipande 16,000 Tsh 16,000 TshGharama ya fundi kwa Septic tanki 150,000 Tsh

Jumla 478,000 TshShimo la maji taka kubwa ( kipenyo = 2.5 m // kina = 3 m )Kuchimba 23.5 m3 80,000 TshTofali za kuchoma 600 kipande 100 tsh 60,000 TshSimenti 8 mfuko 16,500 Tsh 132,000 TshMchanga 126 ndoo 250 Tsh 31,500 TshKokote 30 ndoo 300 Tsh 3,000 TshMaji 5 ndoo 500 Tsh 2,500 TshWavu 1 kipande 17,000 Tsh 34,000 TshNondo 12mm 4 kipande 16,000 Tsh 64,000 TshBaindingi Waya 1 Kg 3,000 Tsh 3,000 TshMbao pana 1’’x8’’ 8 kipande 14,000 Tsh 112,000 TshMbao 2’’x4’’ 2 kipande 7,500 Tsh 15,000 TshSilingi bodi 1 kipande 15,000 Tsh 15,000 TshMisumari 2’’ 0.5 Kg 4,000 Tsh 2,000 TshGharama ya fundi kwa Soakaway 200,000 Tsh

Jumla 754,000 TshJumla Kuu 1,232,000 Tsh

Shimo dogo la maji taka na shimo kubwa la maji taka

. mchanganyo wa uwiano shimo 1:7

. mchanganyo wa uwiano mfuniko 1:4:8

Shimo la maji taka dogo

Shimo la maji taka kubwa

Page 20: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

20

Page 21: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

21

BAMBA

30cm

30cm

10cm

30cm

17cm

20º

Vipimo vinavyoonyeshwa pembeni ya mchoro huo, vitakusaidia kutengeneza kwa umakini makanyagio na miguu kwenye Bamba.

. Visigino vya miguu vinatakiwa vianzie kati-kati ya Tundu la bamba

. Umbali kati ya makanyagio na katikati ya tundu la choo uwe unakaribiana kwa nyuzi 20

. Ukubwa wa tundu la choo unashauriwa kuwa na urefu sentimeta 30 na upana sen-timeta 17

Bambakwakuboreshachoo:

. Bamba la sungura ndogo na mfuniko . Mbadala wa bamba la sungura ndogo na mfuniko

Bambakwaajiliyaujenziwachookipya:

. Bamba la asili la kumwagia maji . Bamba la sungura kubwa . Sinki

Ushaurikwaujenziwachoo:

. Ili kufanya maji yatiririke kuelekea kwenye shimo la choo, Bamba liwe na mbonyeo kuelekea kwenye shimo la choo (kwa asilimia 5%)

Mionekanombalimbliyamatunduyamabambayavyoo:

Page 22: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

22

Bamba la asili la kumwagia maji

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Simenti 12,5 Kg 330 Tsh 4,125 TshMchanga 6 ndoo 250 Tsh 1,500 TshTofali za kucho-ma

20 kipande 100 Tsh 2,000 Tsh

Udongo - - - -Maji 3 ndoo 25 Tsh 75 TshBomba PVC 4’’ 2 m 2,500 Tsh 5,000 TshGharama ya fundi 10,000 Tsh

Jumla Kuu 22,700 Tsh

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Simenti 4 Kg 330 Tsh 1,320 TshMchanga 1 ndoo 250 Tsh 250 TshKokoto 1 ndoo 300 Tsh 300 TshMaji 1 ndoo 25 Tsh 25 TshWavu 0.6 x 0.6 m2 5,718 Tsh 2,060 TshGharama ya fundi 1,500 Tsh

Jumla Kuu 5,455 Tsh

Bambalasungurandogonamfuniko

. Mfuniko au sungura unatakiwa kuwa imara ili kuhimili uzito wa watumiaji. Gharama za ziada za bamba ndogo. Inahitaji kifyatulio cha ghrama cha plastiki

. Mchanganyo wa uwiano 1:4:4

. Mchanganyo wa uwiano 1:7. Kusafisha kwa vitu vigumu vinaweza kuziba mfumo wa choo. Maji ya kufuria,kuogea au mengineyo yanaweza kutumika kumwagia chooni

Mbadalawabambalasungurandogonamfuniko

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Simenti 4 Kg 330 Tsh 1,320 TshMchanga 1 ndoo 250 Tsh 250 TshKokoto 1 ndoo 300 Tsh 300 TshMaji 1 ndoo 25 Tsh 25 TshWavu 0.6 x 0.6 m2 5,718 Tsh 2,060 TshGharama ya fundi 1,500 Tsh

Jumla Kuu 5,455 Tsh

. Mchanganyo wa uwiano 1:4:4. Mfuniko au bamba unatakiwa kuwa imara ili kuhimili uzito wa watumiaji. Gharama za ziada za bamba ndogo

Lid

Page 23: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

23

BAMBA

*Gharama inaweza kubadilika kulingana na bei ya malighafi. Wilaya ya Kongwa 2014 Gharama halisi ya malighafi hazihusishi usafiri.

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Sinki 1 kipande 18,000 Tsh 18,000 TshMtego maji (P-trap)

1 kipande 5,000 Tsh 5,000 Tsh

Simenti 20 Kg 330 Tsh 6,600 TshMchanga 3 ndoo 250 Tsh 750 TshMaji 1 ndoo 25 Tsh 25 TshBomba PVC 4’’ 3 m 2,500 Tsh 7,500 TshGharama ya fundi 15,000 Tsh

Jumla Kuu 52,875 Tsh

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Simenti 16 Kg 330 Tsh 5,280 TshMchanga 3 ndoo 250 Tsh 750 TshKokoto 3 ndoo 300 Tsh 900 TshMaji 4 ndoo 25 Th 100 TshWavu 1.2 x 1.2 m2 5,718 Tsh 8,240 TshGharama ya fundi 5,000 Tsh

Jumla Kuu 20,270 Tsh

Bambalasungurakubwa

. Inatakiwa kua imara zaidi iweze kumbeba mtuniaji

Sinki

. Kusafisha kwa vitu vigumu vinaweza kuziba mfumo wa choo. Maji ya kufuria,kuogea au mengineyo yanaweza kutumika kumwagia chooni

Mfuniko ya mbao

. Mchanganyo wa uwiano 1:2

. Mchanganyo wa uwiano 1:4:4

Jumla Kuu 3,000 Tsh

. Mfuniko unatakiwa kufunika shimolote bila kuacha nafasi ya kuingiza wadudu kama inzi na wengineo

Page 24: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

24

Kwa kawaida ukubwa wake: 1,5 x 1,5 x 2,2 m

Kibandakinajengwakulinganashimolilivyo:

. Kitako:Kama shimo ni la pembeni kibanda chake ninahitaji kujengewa kitako.Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Tofali za kucho-ma

80 kipande 100 Tsh 8,000Tsh

Simenti 10 Kg 330 Tsh 3,300 TshMchanga 5 ndoo 250 Tsh 1,250 TshMaji 3 ndoo 25 Tsh 75 TshGharama ya fundi 15,000 Tsh

Jumla Kuu 27,625 Tsh

Maelezo ya win-gui

Kimoja Bei* Kiasi*

Simenti 2 mfuko 16,500 Tsh 33,000 TshMchanga 42 ndoo 250 Tsh 11,500 TshMaji 1 pipa 500 Tsh 500 TshGharama ya fundi 20,000 Tsh

Jumla Kuu 65,000 Tsh

. Kupiga ripu (inside and outside):Inashauriwa kupiga lipu kwenye ukuta kwa uimara zaidi.

. Mchanganyo wa uwiano: 1:7

Kibanda:

Page 25: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

25

Kibanda

*Gharama inaweza kubadilika kulingana na bei ya malighafi. Wilaya ya Kongwa 2014 Gharama halisi ya malighafi hazihusishi usafiri.

Paa:

. Nondo zinatakiwa ziunganishwe vizuri na fundi kwenye ukuta ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na upepo na mvua kali.. Vyoo vya Tembe vijengwe vizuri ili kudhibiti mvua isipite wakati wa masika.. Paa la tembe ni zuri kwa maeneo ambayo upatikanaji wa miti ni rahisi.

KibandachachoonaBafu:

. Kila kibanda kwenye katalogi kinaweza kujengwa na bafu.

Mlango:

. Milango mingi ambayo hutumika hutengenezwa kwa bati (A) na mbao (B), mlango wa kwanza (A) unapendekezwa kwa sababu gharama zake ni ndogo (nusu) ukilinganisha na wa mbao.

Choo Choo na bafu

A B

Page 26: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

26

Kibandachamatofaliyaudongonatembe

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Matofali ya udongo

400 kipande 50 Tsh 20,000 Tsh

Udongo - - - -Maji 4 pipa 500 Tsh 2,000 TshNguzo 4 kipande 1,500 Tsh 6,000 TshMwanba 2 kipande 1,500 Tsh 3,000 TshMapao 4 kipande 300 Tsh 1,200 TshFito 100 kipande 30 Tsh 3,000 TshMlango wa bati na fremu

1 kipande 21,000 Tsh 21,000 Tsh

Bawaba 2 kipande 1,000 Tsh 2,000 TshKufuri 1 kipande 2,000 Tsh 2,000 TshGharama ya fundi 40,000 Tsh

Jumla Kuu 100,200 Tsh

Kibandachatopenatembe

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Udongo - - - -Maji 4 pipa 500 Tsh 2,000 TshNguzo 4 kipande 1,500 Tsh 6,000 TshMwanba 2 kipande 1,500 Tsh 3,000 TshMapao 4 kipande 300 Tsh 1,200 TshFito 100 kipande 30 Tsh 3,000 TshMlango wa bati na fremu

1 kipande 21,000 Tsh 21,000 Tsh

Mwamba 2 kipande 1,000 Tsh 2,000 TshKufuri 1 kipande 2,000 Tsh 2,000 TshGharama ya fundi 20,000 Tsh

Jumla Kuu 60,200 Tsh

udongomifuko au plastiki

nguzu

nyasi

fito

mapaomiamba

Tembe

Page 27: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

27

Kibanda

*Gharama inaweza kubadilika kulingana na bei ya malighafi. Wilaya ya Kongwa 2014 Gharama halisi ya malighafi hazihusishi usafiri.

KibandachamatofaliyasimentinabatiMaelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Matofali ya simenti na mchanga

110 kipande 1,000 Tsh 110,000 Tsh

Simenti 2,5 mfuko 16,500 Tsh 41,250 TshMchanga 51 ndoo 250 Tsh 12,750 TshMaji 4 pipa 500 Tsh 2,000 TshMbao 2’’x4’’ 2 kipande 7,500 Tsh 15,000 TshMlango wa bati na fremu

1 kipande 21,000 Tsh 21,000 Tsh

Bawaba 2 kipande 1,000 Tsh 2,000 TshBati 2 kipande 12,000 Tsh 24,000 TshMisumari 0.5 Kg 4,000 Tsh 2,000 TshKufuri 1 kipande 2,000 Tsh 2,000 TshGharama ya fundi 60,000 Tsh

Jumla Kuu 292,000 Tsh

Kibanda cha matofali ya udongo na batiMaelezo Ya wingi kwa kila Bei* Kiasi*Matofali ya udongo

400 kipande 50 Tsh 20,000 Tsh

Udongo - - - -Maji 4 pipa 500 Tsh 2,000 TshBati 2 kipande 12,000 Tsh 24,000 TshMisumari 0.5 Kg 4,000 Tsh 2,000 TshMbao 2”x4” 2 kipande 7,500 Tsh 15,000 TshBawaba 2 kipande 1,000 Tsh 2,000 TshMlango wa bati na fremu

1 kipande 21,000 Tsh 21,000 Tsh

Kufuri 1 kipande 2,000 Tsh 2,000 TshGharama ya fundi 50,000 Tsh

Jumla Kuu 138,000 Tsh

Kibanda na tofali za kuchoma na bati

. mchanganyo wa uwiano: 1:7

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Tofali za kucho-ma

400 kipande 100 Tsh 40,000 Tsh

Udongo - - - -Maji 4 pipa 500 Tsh 2,000 TshBati 2 kipande 12,000 Tsh 24,000 TshMisumari 0.5 Kg 4,000 Tsh 2,000 TshMbao 2’’x4’’ 2 kipande 7,500 Tsh 15,000 TshBawaba 2 kipande 1,000 Tsh 2,000 TshMlango wa bati na fremu

1 kipande 21,000 Tsh 21,000 Tsh

Kufuri 1 kipande 2,000 Tsh 2,000 TshGharama ya fundi 50,000 Tsh

Jumla Kuu 158,000 Tsh

Page 28: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

VITU VYA ZIADA

28

Vifaavyakufagilia:

Vituvyaziadakwawalemavu

. Ndoo yenye maji safi na vifaa vingine vya usafi.

. Ufagio na mti kwa ajili ya kufanyia usafi.

. Chombo cha kuwekea takataka.

. Walemavu wanaweza kutumia aina yoyote ya choo kama vitajengwa vizuri na kutunzwa vizuri.

. Stuli isIyotolewa

. Njia yenye alama ina-yoelekea chooni.

. Kamba iliyofungwa kuele-kea chooni.

. Walemavu wa macho

. Stuli inayoweza kutolewa: . Kiti cha mbao: 14,000 Tsh . Mishikio ya chuma: 5,000 Tsh

Sehemu ya kukanyaga yen-ye mikwaruzo kupunguza kuteleza

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Simenti 25 Kg 330 Tsh 8,250 TshMchanga 2 ndoo 250 Tsh 500 TshKokoto 2 ndoo 300 Tsh 600 TshWavu 1 m2 5,718 Tsh 5,718 Tsh

Jumla Kuu 15,068 Tsh

Page 29: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

29*Gharama inaweza kubadilika kulingana na bei ya malighafi. Wilaya ya Kongwa 2014 Gharama halisi ya malighafi hazihusishi usafiri.

vINAWIA MIKONO

Tip-tap

Ndoo iliyo na koki

Mtungiwaudongowenyetepu

Ili kuwa salama ni vyema kutumia choo chenye kinawia mikono

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Matawi ya miti 3 kipande 500 Tsh 1,500 TshChupa 1 kipande 1,500 Tsh 1,500 TahKamba 2 m 250 Tsh 500 Tsh

Jumla Kuu 3,500 Tsh

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Ndoo na koki 1 kipande 7,000 Tsh 7,000 TshStuli 1 kipande 3,000 Tsh 3,000 Tsh

Jumla Kuu 10,000 Tsh

Maelezo Wingi Kimoja Bei* Kiasi*Simenti 1 mfuko 16,500 Tsh 16,500 TshMchanga 2 ndoo 250 Tsh 500 TshMaji 4 ndoo 25 Tsh 100 TshKoki 1 kipande 7,500 Tsh 7,500 TshTofali za kucho-ma

20 kipande 100 Tsh 2,000 Tsh

Nondo 12 mm 0.25 m 1,340 Tsh 335 TshWAVU ya kuku 1 m 4,500 Tsh 4,500 TshGharama ya fundi 8,000 Tsh

Jumla Kuu 39,435 Tsh

Kwa kutumia koki inayoweza kufunguliwa na ku-fungwa kwa elbo maambukizo ya bakteria toka kwa mikono yenye maambukizo inazuilika.

Page 30: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

30

SHUKRANI

Mwandishi anatoa shukrani kwa watu wote waliompa msaada wakati wa kutengeneza katalogi hii:

Kwanza shukrani za pekee kwa wakazi wa vijiji vya wilaya ya kongwa kwa ukarimu wao wakati wa kutemblea maeneo yao kwa kuonesha ushirikiano wa ku-tosha. Kwa msaada wa viongozi wa serikali za kijiji kwa ushirikiano wao na moyo wa kujitoa kwa kutuunganisha na jamii.

Shukrani za dhati kwa washiriki wa UMATA, Mradi ambao umeleta muele-keo wa kazi hii, pia kwa LVIA kwa msaada wao wakati wa utafiti kwa kubadilisha-na mawazo na uzoefu wa eneo husika, lakini pia kwa shirika la Plan International Tanzania kwa muongozo, msaada na kuimarisha mahusiano miongoni mwa wadau mbalimbali. Pia tunapenda kuwashuku shirika la ‘Catholic Relief Services’(CRS) na ‘Social and Economic Development Initiative’ (SEDIT) kwa ushirikiano wao.

Wakati wa muendelezo wa ubunifu wa suluhisho la suala la usafi wa ma-zingira tulikuwa na bahati sana kufanya kazi pamoja na mafundi wa “UFUNDIKO” na wale ambao waliofundishwa na ONGAWA (Wakufunzi) ambao pia wametupatia ushauri wakati tunarudia toleo la kwanza.

Page 31: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

31

Kimetengenezwa kwa Ushirikiano na:

Kazi hii imethibitishwa chino ya Creative Commons Atribu-tion-NonCommercial 4.0 International Licence.

Grupo de Cooperación de Sistemas de Agua y Sanea-miento para el Desarrollo (GCSASD)

Escuela Técnica Superior de Ingeniería y Diseño Industrial.Universidad Politécnica de MadridC/Ronda de Valencia 3, 28012Madrid, España

Bsc.Environmental Engineering(EE)

Department of Environmental EngineeringSchool of Environmental Science and Technology(SEST)Ardhi UniversityP.O.BOX 35176 Dar Es Salaam, Tanzania

ONGAWA

Ingeniería para el desarrollo HumanoC/Vizconde de Matamala 17, 3ºplanta, 28028Madrid, España

Washiriki:

Ana Esteban Zazo - Catalogue Coordinator UPMClemence Mweche - Project managerAlfonso Zapico - Project manager technical advisorSteven Kiboko - Project officerTito Mwambala - Project officerPaul Thobias Seleman - Student from Ardhi University

Photographs:

ONGAWA and GCSASD kasoro ukurasa wa 28:

1-3. Water Aid/ Jane Wilbur4. Plan Indonesia / Agus Haru

12

43

Kisangalia ulthibitisho wa kopi hii tembelea http://creati-vecommons.org/licenses/by-nc/4.0/ or send a letter to Creative Commons, 444 Castro Street, Suite 900, Moun-tain View, California, 94041, USA

Page 32: Bidhaa za usafi wa mazingira kwa bei nafuu

Katalogi hii ni matokeo maalum ya mradi”kufikia uboreshwaji wa usafi wa mazingira kwa wote ambao hawakuweza kufikia, kupitia utafiti na suluhisho sahihi”umefadhiriwa na “Water and Sanitation Systems for Development Cooperation Group” (GCSASD) of the Polytechnic University of Madrid from its ‘XIV Call for grants for university development cooperation actions 2013”.

Lengo maalum ni,kutambua,kuchambua,kuendelea,kuhamasishwa unafuu, ubora na uimara wa suluhisho la usafi wa mazingira katika mazingira ya Wilaya ya Kongwa.

Utekelezaji wa kazi umefanyika kwa ushirikiano kati ya GCSASD, ONGAWA na chou kikuu cha Ardhi.

Mradi huu unatekelezwa ndani ya mpango wa mradi wa UMATA, ambao unafadhiriwa na GSF, Unalenga kuongeza uwezekano wa matumizi wa vifaa bora vya usafi wa mazingira na kubadili tabia mbaya za usafi wa mazingira kwa ukubwa wake. Umeanzishwa ili kuongeza kampeni ya taifa ya usafi wa mazingira Tanzania, ambapo kwa awamu ya kwanza unatekelezwa katika Wilaya tatu za mkoa wa Dodoma ambazo ni Bahi, Chamwino na Kongwa.

Kuandaliwa kwa katalogi hii ulianza mwezi wa sita hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka 2014 katika Wilaya ya Kongwa. Utafiti wa bidhaa za usafi wa mazingira na majaribio yake bado yanafanywa wakati huu ambao kitabu hiki kimetolewa.

Katalogi hii ipo kwa lugha ya kiingreza na kiswahili.

Wasomaji na watumiaji wote wanakaribishwa kutoa maoni na ushauri wao kadiri wawezavyo, ili toleo lijalo liweze kuboreshwa ku[pitiamaoni yao, kwa madhumuni hayo na habari zaidi tafadhari tuwa-siliane kupitia anuani hizo hapo chini.

Anuani ya posta: Grupo de Cooperación de Sistemas de Agua y Saneamiento para el Desarrollo Escuela Técnica Superior de Ingeniería y Diseño Industrial C/ Ronda de Valencia, 3 28012Simu no: +34 91 336 68 76 / 46Barua pepe: [email protected]: http://sistemasdeaguaysaneamientoparaeldesarrollo.wordpress.com

Imetolewa na “Wa ter and Sanitation Systems for Development Cooperation Group” (GCSASD) na ONGAWA.

ISBN 978-84-697-1719-6

Imefashiriwa na Polytechnic University of Madrid