halmashauri ya kijiji cha kagunga · 3 hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu...
TRANSCRIPT
1
HALMASHAURI YA KIJIJI CHA
KAGUNGA
RASIMU YA MPANGO WA USIMAMIZI
SHIRIKISHI WA MSITU WA HIFADHI WA
KAMPESE - KIJIJI CHA KAGUNGA
HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA
S. L. P. 1
MPANDA
i
MAELEZO YA JUMLA YA MPANGO........................................................................................................... 1
MAELEZO.................................................................................................................................................. 2
Msitu wa Hifadhi ya Kijiji cha Kagunga .................................................................................................... 2
MATUMIZI YA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI CHA KAGUNGA .................................................................. 3
KIJIJI CHA KAGUNGA ................................................................................................................................ 4
Sehemu ya tatu: ....................................................................................................................................... 5
Madhumuni ya mpango wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Kagunga.................................................. 5
ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MABA. .................................................................................................... 7
ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MAJINDO ............................................................................................... 8
ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KATUNU ................................................................................................. 8
SEHEMU YA PILI ....................................................................................................................................... 9
MPANGO WA UTEKELEZAJI...................................................................................................................... 9
Meneja Mteule ........................................................................................................................................ 9
Uwezo na Majukumu ya Kamati ya Mazingira ......................................................................................10
Majukumu ya Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili ya Kjiji .....................................................................11
Majukumu ya Katibu wa kamati ya mazingira: ......................................................................................12
Majukumu ya Mtunza hazina: ...............................................................................................................13
Msimamizi wa Doria: .............................................................................................................................13
Majukumu ya Wahusika Wengine .........................................................................................................13
Halmashauri ya Kijiji:..............................................................................................................................13
Wanakijiji ...............................................................................................................................................14
Wataalamu wa Misitu katika ngazi mbalimbali .....................................................................................14
Viongozi wa Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, na Taifa (Mtendaji kata, Diwani, Katibu Tarafa, Mkuu wa
Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji (W), Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Waziri).............................................14
UTENDAJI KAZI WA KAMATI YA MALIASILI YA KIJIJI. .............................................................................15
MAELEZO MENGINEYO ..........................................................................................................................15
UTOAJI TAARIFA .....................................................................................................................................15
UWEKAJI WA KUMBUKUMBU ...............................................................................................................15
MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA KAMATI YA MALIASILI ..............................................................16
MATARAJIO YA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA USIMAMIZI WA MSITU.........................16
UTUNZAJI KUMBUKUMBU .....................................................................................................................17
VITABU VYA KUMBUKUMBU .................................................................................................................17
KITABU CHA MAKOSA NA FAINI ............................................................................................................17
ii
KITABU CHA STAKABADHI......................................................................................................................17
VITABU VYA VIBALI ................................................................................................................................17
KITABU CHA DORIA ................................................................................................................................18
KITABU CHA AKAUNTI ............................................................................................................................18
KITABU CHA MAPATO NA MATUMIZI....................................................................................................19
USIMAMIZI WA FEDHA ..........................................................................................................................19
WAHUSIKA WAKUU; ..............................................................................................................................19
AFISA MUWAJIBIKAJI WA MASUALA YA FEDHA ....................................................................................19
MATUMIZI YANAYOIDHINISHWA; .........................................................................................................20
Mipaka ya Msitu wa hifadhi wa kijiji cha Kagunga ................................................................................21
MAELEKEZO MAALUM ...........................................................................................................................21
ULINZI NA UKAGUZI WA ENEO LA MSITU WA KIJIJI CHA KAGUNGA .....................................................21
Sifa za Walinzi wa Msitu. .......................................................................................................................22
Wajibu, Majukumu na Mafao ya Walinzi wa Msitu wa Hifadhi ya Kijiji ................................................22
OPERESHENI ...........................................................................................................................................23
ZAWADI YA PONGEZI KWA MWANA DORIA ........................................................................................23
Kanuni za Kutumia Msitu wa Hifadhi ya kijiji .........................................................................................23
Kanuni za matumizi ya msitu: ................................................................................................................24
Matumizi ya Msitu yanayohusu Ukataji wa Miti ...................................................................................24
TARATIBU NA SHERIA NYINGINEZO .......................................................................................................24
Adhabu ...................................................................................................................................................24
MCHAKATO WA KUMSHUGHULIKIA MKOSAJI NA KOSA .......................................................................24
FAINI NA ADHABU KWA KILA KOSA .......................................................................................................25
FAINI ZA KUTOWAJIBIKA ........................................................................................................................26
KUUENDELEZA MSITU ............................................................................................................................26
UTANGULIZI: ..........................................................................................................................................27
UVUNAJI WA MITI ..................................................................................................................................27
HATUA ZA HARAKA ................................................................................................................................28
UFUATILIAJI ............................................................................................................................................28
Vigezo vya Mafanikio: ............................................................................................................................28
Wafuatiliaji .............................................................................................................................................29
Taarifa ya Ufuatiliaji Itatolewa kwa: ......................................................................................................29
Muda wa Kufanya Ufuatiliaji..................................................................................................................29
RATIBA YA UTEKELEZAJI .........................................................................................................................30
Hatua za Awali za Utekelezaji: ...............................................................................................................30
iii
Hatua Zitakazofuata ...............................................................................................................................30
MUDA WA MPANGO, MAREKEBISHO NA MAPITIO YAKE: ....................................................................30
VIAMBATA ..............................................................................................................................................32
1
MPANGO WA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI CHA
KAGUNGA
SEHEMU YA KWANZA - UTANGULIZI
MAELEZO YA JUMLA YA MPANGO Mpango huu wa usimamizi umeandaliwa na timu ya Tathimini Shirikishi ya Rasilimali
za Msitu kwa kushiriana na wataalamu wa misitu wa Halmashauri ya wilaya ya
Mpanda.
Maandalizi ya mpango huu wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Kagunga umefanyika
kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Kagunga ambao ndio wamiliki wa msitu huu.
Mpango huu umepitishwa na Halmashauri ya kijiji na Mkutano Mkuu wa kijiji cha
Kagunga na kuidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya Mpanda.
Uamuzi wa kutenga na kuuhifadhi msitu huu wa kijiji cha Kagunga kuwa msitu wa
Hifadhi wa kijiji umetokana na wanakijiji wenyewe kuona umuhimu wa uhifadhi. Pia
kuweka taratibu za kisheria ili kuwezesha kijiji kupata manufaa yatokanayo na mazao
na huduma za msitu na kuepusha vizazi vijavyo kukosa kabisa rasilimali za msitu huu.
Malengo makuu ya mpango huu wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Kagunga ni
kuhifadhi, Kuuendeleza na Kutumia kwa namna endelevu kwa manufaa ya kizazi cha
sasa na kijacho cha Tanzania na dunia kwa ujumla
2
MAELEZO Msitu wa Hifadhi ya Kijiji cha Kagunga Msitu wa Hifadhi ya kijiji cha Kagunga unamilikiwa kuhifadhiwa na Halmashauri ya
Kijiji cha Kagunga kwa niaba ya wananchi wote wa kagunga. Madhumuni ya msingi
ya kuhifadhi msitu huu ni kutunza na kuhifadhi uoto wa asili uliopo kwa wingi kwenye
msitu huu, kutoa mazao ya msitu na huduma ya/za misitu kwa kuzingatia misingi ya
matumizi endelevu na kuhifadhi bioanuai muhimu zinazopatikana ndani yake kwa
manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo vya Tanzania na ulimwengu kwa jumla.
Msitu huu wa hifadhi ya kijiji ni matokeo ya zoezi la Mpango wa Matumizi Bora ya
Ardhi ya kijiji cha Kagunga lililofanyika mwezi November mwaka 2016 na kuridhiwa na
wananchi wote wa Kagunga.
Msitu huu umeenea eneo la Milima Maba na kuanzia hadi mlima Mbamba Msitu huu
una eneo la ukubwa wa hekta 5465.
Msitu huu una uoto wa miti mchanganyiko sehemu kubwa una umri mkubwa na
sehemu nyingi vilevile ambazo zina uoto mchanga. Kwa juu msitu umefunga kwa
viwango tofauti tofauti toka sehemu moja hadi nyingine. Kuna sehemu ambazo msitu
umefunga sana kwa juu hasa kando kando ya mito na makorongo marefu, sehemu
zilizofunga wastani, na sehemu zilizo wazi hasa kutokana na uvamizi wa msitu kwa
ajili ya kilimo na zile sehemu za mabonde na mbuga ambazo ni vyanzo vya maji. Ndani
ya msitu huu kuna njia za miguu zinazounganisha kijiji cha Kagunga na baadhi ya
vitongoji vyake vya Mantena na kagunga B (kalaba). Pia kuna njia nyingi zisizo halali
za miguu ambazo hutumiwa na wavamizi wa msitu kwa ajili ya kilimo, wapasua mbao
na wategaji wa wanyamapori. Mipaka ya msitu huu imewekwa alama za kudumu za
maboya ya zege (beacons).
MSITU WA HIFADHI WA KIJIJI CHA KAGUNGA;
Msitu huu umeenea Magharibi na kaskazini mwa Kijiji cha Kagunga. Msitu huu una
ukubwa wa hekta 5465 wenye bioanuai nyingi muhimu kwa kijiji na taifa kwa ujumla.
Msitu huu umeathiriwa kwa kiasi na shughuli za kibinadamu kama vile uchungiaji wa
mifugo, uchomaji moto, uvunaji holela, Kilimo na makazi holela msituni.
3
Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na
uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje ya kijiji cha kagunga.
Moto ni tishio la msitu wote wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga. Madhara ya moto ndani
ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga ni kuwa umeathiri ustawi wa uoto wa msitu
huu. Vyanzo vya moto ndani msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga ni wawindaji wa
wanyamapori, wakulima na warinaji wa asali kwa kutumia moto.
Msitu huu pia una vivutio vingine vya utalii kama vile safu za Milima na maeneo mengi
yanayopendelewa na Sokwe kwa ajili ya malazi na chakula na maporomoko ya maji.
Mmiliki mkuu wa msitu huu ni Halmashauri ya Kijiji Cha Kagunga, kutokana na
muundo wa serikali za mitaa, itaiteua kamati ya Maliasili ya Kijiji kusimamia msitu huu
kwa niaba ya wananchi wote wa kijiji cha Kagunga kwa kuwa hii ndiyo kamati
inayohusika na usimamizi wa masuala ya mazingira ya kijiji kwa ujumla.
MATUMIZI YA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI CHA KAGUNGA Kabla ya kuanza kwa utaratibu huu wa usimamizi shirikishi hapa kijijini, msitu huu
haukuwa na utaratibu wowote wa jinsi ya kutumia au kuvuna rasilimali zake, na kila
mtu aliingia kwa wakati wake na kuvuna chochote alichohitaji kwa manufaa yake na
kutoka bila ya kuhojiwa na mtu. Hali kadhalika, ndani ya msitu huu kuna wafugaji na
wakulima ambao huchangia miti midogo kupotea kabisa kama itakavyo onyeshwa
kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu.
Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji kulingana na uwezo wa msitu hupelekea
kutoweka kwa miti muhimmu kama Mninga, Mpilipili, Mkora na Msawala katika msitu
huu. Hali kadhalika uchomaji moto unaofanywa na wafugaji ili kupata nyasi mpya na
wawindaji ili kurahisisha kazi yao ya kuwinda. Vitendo hivi huua kabisa makuzi ya
machipukizi na hivyo msitu hubaki na kizazi cha miti mikubwa tu ambayo ndiyo ilikuwa
ikivunwa.
Kwa upande wa matumizi ya rasilimali za msitu huu zipo rasilimali zipatikanazo katika
msitu huu ambazo zina manufaa kwa uchumi wa kila mwananchi na kijiji kwa ujumla,
hizi ni pamoja na; -
▪ Msitu huu ni makazi ya wanyamapori ambao ni faida kwa kijiji na taifa kwa
ujumla.
4
▪ Ipo miti yenye manufaa kiuchumi kwa wananchi mfano miti ya mbao kama
Milembela, Mitundu, Mininga, Mibanga, Mikurungu, Mpilipili, ambayo ina
umuhimu kiuchumi na kwamba itakinufaisha kijiji endapo utaratibu wa uvunaji
utasimamiwa ipasavyo na kwa uaminifu,
▪ Ndani ya msitu huu kuna makorongo ambayo ni mito ya misimu na mengine
hutiririsha maji mwaka mzima, hivyo kama yakitumiwa vizurini fursa ya utalii
asilia utakao ingizia kijiji kipato.
▪ Kuni ni moja wapo ya matumizi muhimu kiuchumi toka katika msitu huu.
▪ Aidha, watumiaji wakuu wa rasilimali za msitu huu wa kijiji cha Kagunga, ni
wanakijiji wenyewe wa Kagunga, pili ni wananchi toka vijiji jirani kama
Kasekese. Watumiaji wengine ni wale wakutoka nje ya kijiji na kata hii ya
Kasekese. Pamoja na taratibu za kulipia zatakazowekwa lakini yapo mahitaji
mengine ambayo wanakijiji wa Kagunga pekee wataruhusiwa kuingia na
kuvuna bila malipo bali kwa utaratibu maalum.
KIJIJI CHA KAGUNGA Kijiji cha Kagunga ni miongoni mwa vijiji hamsini na tano (55) vya wilaya ya Mpanda.
Kipo katika Kata ya Kasekese, Tarafa ya Mwese, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.
Vijiji vingine vilivyomo kwenye kata hii ni pamoja na Kasekese na Kaseganyama. Kijiji
hiki kilianzishwa mwaka 2014, kabla ya hapo eneo hili lilikuwa chini ya kijiji cha
Sibwesa na mwaka 2009 Sibwesa ilizaa kijiji cha Kasekese na eneo la Kagunga kuwa
miongoni mwa vitongoji vya kijiji cha Kasekese. Jina Kagunga lilitokana na mtu
aliyetoka kigoma aliyejulikana kwa jina la Mtabala. Eneo ambalo kijiji hiki kinapatika
kulikua na miti mingi sana aina ya Migunga na hapo ndipo jina Kagunga lilipotokea.
Kijiji hiki kina vitongoji vinne (4) ambavyo ni Kagunga A, Kagunga B, Mantena na
Kamkola Katika upande wa Kaskazini, kijiji kinapakana na kijiji cha Katuma, upande
wa Kusini kinapakana na kijiji cha Kasekese, upande wa Mashariki kinapakana na kijiji
cha Sibwesa, Magharibi kinapakana na kijiji cha Kaseganyama.
Kijiji hiki kina mchanganyiko wa makabila kadhaa. Makabila yanayotawala katika kijiji
hiki ni Watongwe, Wabende, Wafipa Wasukuma, na waha.
5
Shughuli za kiuchumi za wakazi wa kijiji cha Kagunga zinategemea sana kilimo na
ufugaji. Kwa upande wa kilimo wananchi wa kijiji hiki hulima sana zao la Mahindi,
Maharage Mihogo, Ufuta, Tumbaku, Mpunga, Ufuta na Mtama. Mazao haya huuzwa
hapa kijijini na na mengine kwa wingi huuzwa kwa wafanyabiashara toka Kasekese
na kwingineko.
Aidha, shughuli ya ufugaji hufanywa na kabila la wasukuma, wanyamwezi na wafipa
kwa kiasi kikubwa pia mifugo midogo midogo kama mbuzi, kondoo bata na kuku
hufugwa hapa kijijini.
Sehemu ya tatu: Madhumuni ya mpango wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Kagunga Msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga ni msitu wa kijiji unaohifadhiwa kwa lengo la
kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji pamoja na kuwezesha upatikanaji wa mazao na
huduma za msitu kwa njia endelevu. Kutokana na uharibifu wa msitu unaoendelea
kufanyika madhumuni hayo ya msingi yanaendelea kuathiriwa. Hivyo dhumuni kuu la
mpango huu ni kuimarisha ulinzi, uendelezaji na utumiaji wa eneo hilo la msitu kwa
kushirikisha wananchi ili kurejesha hali nzuri ya msitu iliyokuwepo. Hii itafanikiwa kwa
kufanya yafuatayo:
▪ Kuweka taratibu / kanuni za kutumia, kulinda, na kuendeleza msitu kwa njia
endelevu.
▪ Kuboresha ushiriki wa wadau wote katika usimamizi wa msitu.
▪ Kuongeza ushirikiano kati ya wananchi, Halmashauri ya Kijiji, Halmashauri ya
Wilaya na wakala wa huduma za misitu Tanzania.
▪ Kuwaelimisha wanakijiji wa Kagunga juu ya umuhimu wa msitu kwao, Taifa na
Ulimwengu na jukumu lao la kufuata taratibu za utunzaji na matumizi
zilizowekwa na kukubalika.
▪ Kuuweka msitu wetu katika udhibiti madhubuti unaokubalika na wanakijiji wote
ili kwamba kusiwe na uvunaji holela, uvamizi wa mifugo, na ujenzi wa makazi
holela au kupanua mashamba kuingia katika msitu huu. Kwa kufanya hivi,
tutasaidia msitu huu kuwa chini ya umiliki wa kijiji chote kwa manufaa yetu na
kwamba rasilimali zilizopo zitumike katika misingi endelevu kwa faida ya kizazi
hiki na kijacho.
Msitu huu umegawanyika katika maeneo makuu Matatu ya usimamizi (3) yaitwayo
“maeneo madogo ya usimamizi” (EDU) kama ifuatavyo; -
6
▪ ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MABA (2479 ha)
▪ ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KATUNU (1498 ha)
▪ ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MAJINDO (1408ha)
7
ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MABA. Eneo hili dogo la usimamizi (EDU) la Maba (milima ya Igombe) lina ukubwa wa hekta
2479 ambalo linaanzia kusini magharibi mwa msitu wa kijiji cha Kagunga, bonde la
mama bahati, pembezoni mwa mlima Maba Usawa wa bikoni namba VF35, VF36 na
VF37 kuelekea kaskazini mashariki mwa kitongoji cha Mantena na kuvuka barabara
ya mkoloni milima ya maraha kulekea kaskazini na kuishia kwenye bikoni namba VF49
na VF50 kwenye safu ya milima ya Mngengebe. Kwa upande wa kaskazini inapakana
na EDU ya Majindo Lengo kuu la EDU hii ni “MATUMIZI” na “UHIFADHI”. Kutokana
na hali halisi ya EDU hii na uwiano wa ukubwa wa miti, uvunaji unaweza kufanyika,
pamoja na kuipa nafasi ya ukuaji wa miti muhimu ifikie kwenye kiwango cha kuweza
kuvunwa miaka ijayo. EDU hii ina jumla ya miti 493,500 wakati jumla ya miti 784 ni
miti inayofaa kuvunwa kwa ajili ya mbao, ambayo ni sawa na miti 157 kwa mwaka.
Miti hiyo ni; -
▪ Mpilipili
▪ Mlembela
▪ Mbanga
▪ Mninga
▪ Mkurungu
Pamoja na kuruhusiwa uvunaji yapo matumizi mengine yanayoruhusiwa nayo ni kama
yafuatayo; -
• Ufugaji nyuki
• Uchimbaji wa dawa za asili (miti shamba)
• Kusenya kuni kavu (si miti mibichi)
• Ukataji wa nyasi za kuezekea nyumba
• Uvunaji wa miti ya boriti (pau), fito na nguzo
8
ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MAJINDO Linaanzia mashariki mwa kijiji cha Kagunga, mpakani mwa kijiji cha Sibwesa na
katuma kwa upande wa kaskazini kwenye milima Masoso A na Masoso B, kwenye
bikoni namba VF9, VF10 hadi VF15 na VF17, kuelekea kaskazini kuvuka mlima
kampese na barabara ya mkoloni na kuishia mpakani mwa ushoroba na milima ya
Mngengebe. Kwa upande wa mashariki linapakana na Katuma na upande wa kusini
inapakana na kijiji cha Sibwesa. Ndani ya msitu huu kuna milima na maporomoko
marefu na vyanzo vya maji. Eneo hili dogo la usimamizi la Majindo lina ukubwa wa
hekta 1408. kutokana na hali ya eneo hili lilivyo, litakua la “UHIFADHI na MATUMIZI”.
Matumizi yatakayoruhusiwa katika EDU hii ni pamoja na:
▪ Ufugaji nyuki na Urinaji wa asali
▪ Uchimbaji wa dawa za asili [miti shamba]
▪ Kusenya kuni zilizokauka.
▪ Ukataji wa nyasi za kuezekea nyumba
▪ Shughuli za Utalii.
▪ Matambiko
▪ Vyanzo vya maji
▪ Utafiti
ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KATUNU Eneo hili linaanzia njia panda ya Kansalu na barabara ya mkoloni kuvuka mlima bunga
kuzunguka maeneo ya ushoroba. Eneo hili lina ukubwa wa hekta 1498. Lengo la
kutenga eneo hili ni “UHIFADHI” wa vyanzo vya maji kwa ajili ya kulisha maji eneo la
ufugaji a mbalo linapakana nalo, Uhifadhi wa wanyamapori wanaoishi humo ndani ya
msitu.
9
SEHEMU YA PILI MPANGO WA UTEKELEZAJI Meneja Mteule Katika mpango huu wa usimamizi wa msitu wa hifadhi wa Kijiji cha Kagunga, meneja
atakuwa ni Halmashauri ya kijiji cha Kagunga. Halmashauri ya kijiji cha Kagunga
itaiteua KAMATI YA MALIASILI YA KIJIJI ili kusimamia msitu huu kwa niaba yake na
wanakijiji wote kwa ujumla. Kamati hii ni ile inayoelekezwa katika muundo wa uongozi
wa vijiji. Kamati hii itakuwa na wajumbe 14 kwa mchanganuo ufuatao;
▪ Wawakilisha toka kila kitongoji cha kijiji.
▪ Skauti wa kijiji wasiopungua wawili kama hawapo basi hata askari mgambo
wanaweza kutumika badala ya Skauti wa kijiji.
▪ Mtu / watu maarufu katika kijiji wanaoweza kuchangia katika suala zima la
uhifadhi. mfano wazee maarufu na wakongwe wa kijiji n.k.
▪ Wanawake (Theluthi moja au 30% ya wajumbe wote) maalumu kwa nafasi ya
upendeleo kwa wanawake
Kamati hii itapatikana kwa kufuata utaratibu ufuatao; -
▪ Wajumbe hawa watapendekezwa na halmashauri ya kijiji
10
▪ Baada ya majina hayo kupatikana mkutano mkuu wa Kijiji huketi na
kuyathibitisha majina ya wajumbe wa kamati hii.
▪ Kamati hii itakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu (3) baada ya hapo
uchaguzi unafanyika tena. mjumbe anaweza kuchaguliwa tena kulingana na
imani ya wananchi kwake.
▪ Mwenyekiti, katibu na mweka hazina watachaguliwa miongoni mwa wajumbe
waliochaguliwa na mkutano mkuu na kuthibitishwa na Halmashauri ya kijiji.
▪ Kamati hii itapewa nguvu ya kisheria ya kusimamia sheria ya kijiji na
itawajibika kwa Halmashauri kuu ya Kijiji.
▪ Itaandika taarifa ya utekelezaji kwa Halmashauri ya kijiji mara moja kila mwezi,
yenye nakala kwa Afisa Misitu (W).
▪ Itafanya vikao vyake mara moja kila mwezi na vya dharura pale inapobidi.
▪ Itapokea, kujadili na kufuatilia taarifa za walinzi wa msitu (Kamati ya doria) na
vikundi vingine vitakavyo undwa kuisaidia Kamati ya Mazingira katika
kutekeleza majukumu yake.
Uwezo na Majukumu ya Kamati ya Mazingira ▪ Kuhakikisha kuwa mipaka yote ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga
inaeleweka waziwazi kwa wanakijiji wote wa Kagunga.
▪ Kusimamia utekelezaji wa mipango yote inayohusu utumiaji, ulinzi na
uendelezaji wa msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga.
▪ Kutunza kumbukumbu zote zinazohusu shughuli za utumiaji, ulinzi, na
uendelezaji wa msitu wa hifadhi ya kijiji. Kumbukumbu hizo ni: -
• Mihtasari ya mikutano
• Doria
• Uhalifu na faini
• Vibali vilivyotolewa
• Mapato na matumizi ya fedha za msitu
▪ Uoteshaji na upandaji miti, pia shughuli zote za uhifadhi mazingira ndani ya
maeneo ya kijiji
▪ Kuhakikisha kuwa walinzi wa msitu (timu ya doria) wanatekeleza kazi yao
kikamilifu na kuchukua hatua zinazopasa kuondoa dosari zinazojitokeza katika
kazi ya ulinzi.
11
▪ Kufanya ukaguzi wa msitu wa hifadhi ya kijiji angalau mara mbili kwa mwezi.
▪ Kuhakikisha matumizi endelevu ya msitu yanazingatiwa kulingana na kanuni za
matumizi zilizowekwa na kukubaliwa.
▪ Kuwashughulikia wahalifu wa msitu kwa mujibu wa kanuni za adhabu
zilizowekwa na kukubalika kwa ushirikiano na Halmasahauri ya kijiji.
▪ Kwa ushirikiano na Halmashauri ya kijiji, kuwahamasisha wanakiiji kushiriki
katika suala zima la uhifadhi wa msitu na mazingira ya kijiji kwa ujumla.
▪ Kutumia na kutunza vitabu vya stakabadhi vilivyoidhinishwa na Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda.
▪ Kufungua Akaunti Benki ya Kamati ya Mazingira ya kijiji kwa ajili ya kuweka fedha
za mapato ya msitu (ushuru na faini).
▪ Kuhakikisha kuwa fedha za Akaunti ya Kamati ya Mazingira zinatumika kama
zilivyokusudiwa na kuidhinishwa na Halmashauri ya kijiji cha Kagunga.
▪ Kuweka utaratibu wa utoaji wa vibali ili kuhakikisha kuwa vibali vinavyotolewa ni
vile vilivyoko katika mamlaka ya Kamati ya Mazingira na kwamba utoaji wa vibali
unakwenda sambamba na mahitaji yaliyopo na sio vinginevyo.
Majukumu ya Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili ya Kjiji ▪ Kuhakikisha kuwa mikutano ya Kamati ya Mazingira inafanyika ipasavyo kwa
kufuata ratiba iliyopangwa. (angalau mara moja kila mwezi)
▪ Kuhakikisha kuwa Mhasibu na Katibu wa Kamati ya Mazingira wanafanya kazi
zao ipasavyo kwa kuweka kumbukumbu zote za vibali, doria, faini, idadi ya
wahalifu, fedha zilizopo, matumizi n.k.
▪ Kuhakikisha kuwa Kamati ya doria ya msitu wa hifadhi ya kijiji wanafanya kazi
yao ipasavyo na wanapewa haki zao kama zilizoainishwa kwenye Mpango huu.
▪ Atakuwa mmoja wa watia sahihi wa Akaunti ya Kamati ya Mazingira wakati wa
kutoa fedha Benki kwa matumizi yaliyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji kwa
ajili ya uendelezaji wa msitu na shughuli zingine za maendeleo kijijini.
▪ Atawajibika kuhudhuria vikao vyote vya Halmashauri kuu ya kijiji na kutoa taarifa
ya utendaji kazi wa kamati.
12
Majukumu ya Katibu wa kamati ya mazingira: ▪ Atawajibika Kuweka na kutunza kumbukumbu zifuatazo: -
• Kumbukumbu za mikutano yote (Kitabu cha kumbukumbu za mikutano)
• Doria zilizofanyika, uhalifu/uharibifu ulioonekana kwenye kitabu cha
Doria.
• Uhalifu ulioonekana, wahalifu waliohusika, faini zilizotozwa, tarehe ya
uhalifu na faini zilizolipwa kwenye kitabu cha “Uhalifu na faini”
• Vibali ilivyotolewa, kwa nani, kwa ajili gani, fedha zilizolipwa, tarehe,
namba ya risiti, n.k kwenye kitabu cha Vibali
• Fedha zilizotolewa, tarehe, kwa ajili gani, namba ya risiti kwenye kitabu
cha Risiti na fedha.
▪ Atahakikisha kuwa Akaunti ya Mazingira inafunguliwa na mara kwa mara baada
ya kupokea fedha na kuziingiza kwenye vitabu vinavyohusika zinapelekwa
Benki na Mweka Hazina.
▪ Atakuwa mmoja wa watia sahihi wa Akaunti ya Kamati ya Mazingira wakati wa
kutoa fedha Benki kwa matumizi yaliyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji kwa
ajili ya uendelezaji wa msitu na shughuli zingine za maendeleo kijijini.
▪ Atawajibika kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya Kijiji na
Halmashauri kuu ya kijiji
▪ Atawajibika kuandaa taarifa ya utendaji kazi wa kamati na maendeleo ya msitu
kila mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka na kuwasilisha katika
mkutano mkuu wa kijiji wa robo mwaka baada ya kupitiwa na Halmashauri kuu
ya kijiji.
▪ Ataidhinisha doria kufanyika kwa maandishi maalumu ambayo mwenyekiti wa
kijiji pia atapaswa kujulishwa kwa wakati utakaoonekana unafaa kulingana na
mazingira.
▪ Atapokea taarifa ya doria mara baada ya kumalizika na kukagua daftari la doria.
▪ Atatunza kumbukumbu za kesi zote za wavunaji haramu wa mazao ya msitu
wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga.
▪ Atawajibika kutunza orodha ya wavunaji wote wa rasilimali za msitu wa hifadhi
ya kijiji cha Kagunga pamoja na kiasi walichovuna na kuwasilisha kwa
DFO/DED kila mwezi.
▪ Atawajibika kusimamia mapato na matumizi kwa umakini na kutoa taarifa kwa
Halmashauri ya kijiji kila inapoonekana inafaa.
13
Majukumu ya Mtunza hazina: ▪ Atawajibika kutunza kumbukumbu zote za mapato yatokanayo na leseni za
uvunaji wa mazao ya misitu na vibali mbalimbali.
▪ Atawajibika kutunza kumbukumbu za matumizi yote ya fedha zitokanazo na
maduhuli ya mazao ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga kama
ilivyoidhinishwa na vikao husika vya kijiji cha Kagunga na siyo vinginevyo.
▪ Ataandaa taarifa ya Mapato na Matumizi ya fedha ya Kamati ya Mazingira na
kuiwasilisha kwenye vikao vya Kamati ya Mazingira.
▪ Atakuwa mmoja wa watia sahihi wa Akaunti ya Kamati ya Mazingira wakati wa
kutoa fedha Benki kwa matumizi yaliyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji kwa
ajili ya uendelezaji wa msitu na shughuli zingine za maendeleo kijijini.
Msimamizi wa Doria: ▪ Atatakiwa kusimamia doria zote na kuziongoza
▪ Atatunza daftari la kila mtu atakayekamatwa katika msitu wa kijiji akivuna
mazao ya misitu bila idhini (kibali) cha kijiji.
▪ Atawajibika kumuweka chini ya ulinzi mtu yeyote pamoja na maliasili
aliyokamatwa nayo (kama ipo) na kumkabidhisha kwa mtendaji wa Kijiji kwa
hatua zaidi za kisheria.
▪ Atawajibika kuhakikisha ulinzi wa mipaka ya msitu unadumu na kuwa imara ili
msitu usivamiwe kwa kilimo, makazi au kuchungia.
Majukumu ya Wahusika Wengine Halmashauri ya Kijiji: Itakuwa mhusika mkuu katika utekelezaji wa mpango huu kwa upande wa kijiji na
itakuwa na wajibu na majukumu yafuatayo: -
▪ Kusimamia utekelezaji wa mpango
▪ Kutunga na kusimamia Sheria ndogo
▪ Kuhakikisha kuwa Kamati ya Mazingira inafanya kazi yake ipasavyo.
▪ Kushirikiana na wataalamu wa Misitu wa ngazi zote katika kuandaa mikakati
mipya ya uhifadhi misitu na mazingira kwa jumla.
▪ Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mpango huu, kwa kuwa na
agenda ya kudumu katika vikao vyake vya kila mwezi pia kutembelea msitu wa
hifadhi angalau mara moja kila mwezi.
14
Wanakijiji Watashiriki katika shughuli za utumiaji, ulinzi na uendelezaji wa msitu wa hifadhi
kama ifuatavyo: -
▪ Kuzuia na kuzima moto katika maeneo yao ya makazi, mashamba na misitu
inayowazunguka.
▪ Kusafisha mipaka ya nje ya msitu wa hifadhi ya kijiji na kuhakikisha kuwa iko
wazi wakati wote wa mwaka.
▪ Kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
▪ Kuotesha na kupanda miti kwa lengo la kupunguza utegemezi wa misitu ya asili
kwa kila zao au huduma ya msitu.
▪ Kushiriki katika mikutano na kuchangia katika kuandaa mikakati mipya ya
kutumia, kulinda na kuendeleza msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga.
▪ Kubuni na kutekeleza shughuli mbadala za kuongeza kipato ili kupunguza
umaskini kwa kutumia rasilimali zilizo ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji, zilizo
katika maeneo ya makazi. Baadhi ya mbinu hizo ni ufugaji wa nyuki kwa njia
za kisasa, usukaji wa mikeka kwa kutumia ukindu kwa ajili ya soko, Kuzingatia
matumizi ya majiko banifu, nishati mbadala na matumizi sahihi ya mazao ya
misitu.
Wataalamu wa Misitu katika ngazi mbalimbali ▪ Kutoa msaada wa kitaalam katika kubuni mikakati mipya ya kuhifadhi msitu wa
hifadhi ya kijiji cha Kagunga
▪ Kusaidia shughuli za uoteshaji na upandaji miti.
▪ Kusimamia Sera ya Misitu na Sheria ya Misitu 14, 2002.
▪ Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mpango huu wa usimamizi.
▪ Kusaidia utekelezaji wa mpango.
Viongozi wa Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, na Taifa (Mtendaji kata, Diwani, Katibu Tarafa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji (W), Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Waziri).
▪ Kutoa msukumo katika utekelezaji wa mpango
▪ Kuhakikisha kuwa Polisi na Mahakama zinatekeleza wajibu wao ipasavyo
katika utekelezaji wa Sheria ya Misitu No. 14, 2002 na Sheria zinazosimamia
rasilimali za misitu.
▪ Kushirikiana na Idara ya Misitu na Nyuki.
▪ Kutoa msukumo katika utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za kutunza na
kulinda misitu.
15
▪ Kusaidia utatuzi wa migogoro inapotokea.
UTENDAJI KAZI WA KAMATI YA MALIASILI YA KIJIJI. ▪ Itafanya kazi zile zile zilizoainishwa katika majukumu ya kamati ya kudumu ya
maliasili ya kijiji
▪ Itakutana mara moja kila mwezi
▪ Itatunza mihutasari ya mikutano yake
▪ Mkutano utafanyika iwapo tu idadi ya wajumbe imefika nusu.
▪ Katika kila mkutano watapaswa kupokea taarifa ya doria na mwenendo wa
uvunaji wa mazao ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga kutoka kwa kiongozi
wa doria.
▪ Watatakiwa kujua idadi ya leseni zilizotolewa katika mwezi husika, kiasi cha
maliasili kilichovunwa na mapato yaliyopatikana.
▪ Watapokea na kujadili maombi ya leseni za kuvuna mbao na kuwasilisha kwa
Serikali ya Kijiji.
MAELEZO MENGINEYO UTOAJI TAARIFA
▪ Kamati ya Maliasili ya kijiji itatoa taarifa ya utekelezaji kwa Halmashauri ya kijiji
mara moja kwa mwezi yenye nakala kwa Afisa Misitu wa Wilaya Mpanda.
▪ Afisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) atatoa taarifa ya maendeleo ya shughuli za msitu
wa hifadhi ya kijiji na kwa Mkutano Mkuu mara nne (4) kwa mwaka yenye
nakala kwa Afisa Mtendaji Kata (WEO) na Afisa Misitu (W).
UWEKAJI WA KUMBUKUMBU Kumbukumbu zifuatazo zitawekwa na kuhifadhiwa na Kamati ya Mazingira ya Kijiji:
▪ Mihutasari ya vikao vya kamati
▪ Uhalifu na faini zilizotozwa
▪ Doria zilizofanyika
▪ Stakabadhi ya fedha na Hati ya malipo.
16
▪ Vibali vilivyotolewa
▪ Akaunti ya Kamati ya Mazingira
▪ Mapato na matumizi ya fedha za msitu.
MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA KAMATI YA MALIASILI Mapato ya Kamati ya Mazingira yatatokana na:
▪ Faini zitakazotozwa wahalifu wa msitu wa hifadhi ya kijiji.
▪ Malipo ya mazao na huduma ya msitu yaliyoruhusiwa kwa kulipia katika
Mpango huu.
▪ Mauzo ya mazao ya msitu yaliyokamatwa na zana zilizokamatwa katika ulinzi.
▪ Wafadhili na wasamaria wema watakaotoa fedha/ msaada kwa ajili ya
Usimamizi wa msitu wa hifadhi ya kijiji.
Mapato yatokanayo na mazao na huduma za msitu wa kijiji cha Kagunga yatakua ni
mali ya kijiji cha Kagunga kwa asilimia 100% na hayatagawanywa kati yake na
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
MATARAJIO YA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA USIMAMIZI WA MSITU Katika matembezi ya kukatiza msitu vikwazo Matatizo yafuatavyo vilibainika msituni;
▪ Moto kichaa
▪ Uvunaji haramu wa mbao
▪ Uchungiaji wa mifugo
▪ Kilimo msituni
▪ Ukataji wa miti
Mpango wa usimamizi ukitekelezwa vilivyo kwa msitu huu hifadhi wa kijiji cha Kagunga
kwa kuzingatia vikwazo vilivyobainika katika matembezi ya kukatiza msitu kama
yalivyofupishwa hapo juu yafuatayo yanatarajiwa kuonekana;
▪ Kupungua au kutoweka kabisa kwa matukio ya moto
▪ Kushughulikiwa kwa watuhumiwa wa kesi za uchomaji moto hovyo msituni kwa
utaratibu wa kukubalika/kwa kufuata taratibu za nchi.
17
UTUNZAJI KUMBUKUMBU Mpango huu wa usimamizi unaainisha bayana ni kumbukumbu zipi zitatunzwa,
zitatunzwa katika vitabu gani na vitabu hivyo vitatunzwa na nani kwa utaratibu gani.
Ufuatao ni ufafanuzi; -
VITABU VYA KUMBUKUMBU Hiki ni kitabu kitakachohusika na kutunza kumbukumbu zifuatazo,
▪ Kumbukumbu za mihutasari ya vikao vya kamati
▪ Kumbukumbu za maamuzi mbalimbali ya kamati
▪ Tukio lolote linalofanywa na kamati au watu wachache waliotumwa na kamati.
▪ Matokeo ya shughuli yoyote iliyofanywa na kamati au watu wachache
walioteuliwa na kamati
▪ Kumbukumbu za ukaguzi wowote uliofanywa na kamati au baadhi ya
wanakamati waliotumwa na kamati
KITABU CHA MAKOSA NA FAINI Kumbukumbu za makosa yoyote yaliyofanywa na mhalifu dhidi ya sheria ndogo za
Kijiji cha Kagunga ya Kuhifadhi Msitu wa Kijiji.
▪ Jina la mkosaji na kosa alilokosa, Kiasi alichotozwa, tarehe aliyotozwa na
namba ya stakabadhi aliyopewa kwa faini aliyotozwa.
▪ Ionyeshwe ni katika akaunti gani pesa hiyo imeingizwa.
▪ kama idhini ya kutumika nimetolewa na mamlaka husika, onyesha hapa
imetumika kufanyia nini?
KITABU CHA STAKABADHI Hivi ni vitabu ambavyo Mtunza hazina wa Halmashauri ya Wilaya atatoa kwa kijiji,
lakini ionyeshwe nani kapewa vitabu vingapi kuvitumia ndani ya kamati.
VITABU VYA VIBALI Kazi ya kitabu hiki ni kutunza kumbukumbu za vibali vyote vilivyoidhinishwa na kamati
ya Maliasili ya Kijiji, Kitabu hiki kionyeshe mambo yafuatayo; -
▪ Kuainisha lengo la kibali, jina la aliyepewa kibali hicho,
18
▪ kiasi cha malipo aliyolipa,
▪ Namba ya stakabadhi iliyotolewa kwa mteja
▪ tarehe ya kutolewa kibali na ya kuisha kutumika kibali hicho.
▪ Pia kitabu kionyeshe jina la mjumbe atakayekagua kibali hicho na la mjumbe
atakayesimamia matumizi ya kibali hicho.
Kimsingi, leseni na vibali vitasainiwa na katibu/ Mhasibu wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji
kugongwa muhuri wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji.
KITABU CHA DORIA Hiki ni kitabu kitakachokuwa kinatunzwa na msimamizi wa doria. kinapaswa
kuandikwa mambo yafuatayo;
▪ Tarehe ya doria,
▪ Majiina ya wanaofanya doria siku hiyo,
▪ eneo ambalo watu hao watafanya doria,
▪ ni uharibifu gani umefanyika katika eneo hilo la msitu ambalo watu hao
wamepangiwa kufanya doria.
▪ Pia katika taarifa ya hao waliopangiwa kufanya doria katika eneo husika
wakiona kitu mfano, wanyamapori. wanapaswa kutoa taarifa kwa kamati ya
maliasili ya Kijiji.
KITABU CHA AKAUNTI Baada ya muda kijiji kitakuwa na fedha nyingi kutokana na mapato ya msitu, hivyo
kutakuwa na kitabu cha benki kwa ajili ya kumbukumbu za kibenki. Katika kitabu hiki
kutakuwa na majina ya watia saini. watia saini watakuwa kama ifuatavyo;
▪ mtia saini kundi ‘A’ – toka Serikali ya Kijiji,
▪ Mtia saini kundi ‘A’ – toka Kamati ya Maliasili ya Kijiji,
▪ Mtia saini kundi ‘B’ – toka Serikali ya Kijiji
▪ Mtia saini kundi ‘B’ – toka Kamati ya Maliasili ya Kijiji.
19
Izingatiwe kuwa hakuna fedha itakayo chukuliwa benki bila ya kuwa na saini za watia
saini wawili toka makundi mawili tofauti pamoja na muhtasari wa kikao cha mkutano
mkuu wa kijiji ulioidhinisha matumizi ya fedha hizo.
KITABU CHA MAPATO NA MATUMIZI Hiki ni kitabu kitakachukuwa kinatunza kumbukumbu za fedha zote zinazoingia kutoka
katika faini na ada za vibali au leseni mbalimbali. Pia kitakuwa na kumbukumbu za
matumizi yote ya fedha zinazotumika ikionyesha saini ya aliyechukuwa na
viambatanisho vya uthibitisho kuwa malipo hayo yameidhinishwa na mamlaka husika.
Mfano wa malipo ni pamoja na zawadi ya pongezi kwa wafanya doria kwa kazi nzuri
itakayokuwa imethibitishwa na kuidhinishwa kuwa wapewe kiasi kadhaa kwa
maandishi. Hapa ni lazima mpokeaji athibitishe kuwa amepokea pesa hiyo.
USIMAMIZI WA FEDHA Katika kifungu hiki sisi wanakijiji cha Kagunga tunaainisha mfumo utakaotumika
kusimamia fedha hususani katika matumizi yake.
WAHUSIKA WAKUU; Mtu atakaye husika kushika vitabu vya risiti na kupokea fedha toka kwa mlipaji
atakuwa ni mtunza fedha. Fedha hizo zitahifadhiwa kwa muda na kisha kupelekwa
benki kwenye akaunti ambayo imefunguliwa kwaajili ya fedha zitokanazo na msitu wa
hifadhi ya kijiji cha Kagunga.
AFISA MUWAJIBIKAJI WA MASUALA YA FEDHA Afisa muwajibikaji wa fedha za Msitu wa Kijiji atakuwa AFISA MTENDAJI WA KIJIJI
kwakuwa huyu ndiye anayewajibika kwa masuala yote yahusuyo fedha hapa kijijini.
Anaweza kumhoji mtunza fedha na kukagua vitabu vya fedha wakati wowote
atakapoona inafaa. Hata hivyo mtunza hazina anapaswa kutoa taarifa ya mwenendo
wa makusanyo ya fedha kila wiki.
Hata hivyo, kwa kuzingatia misingi ya uhuru wa habari na taratibu za utawala bora
mwananchi yeyote anaweza kuomba kukagua kitabu cha makusanyo. pamoja na
taratibu hizi za pekee, Mamlaka inayowajibika ya juu kabisa katika kijiji ni Mkutano
mkuu, hivyo, taarifa ya mapato na matumizi yatasomwa kila baada ya miezi mitatu
katika mikutano mkuu wa kijiji kama ilivyo desturi ya mikutano hiyo hapa kijijini.
Kwa upande wa ukiukwaji wa taratibu au tuhuma dhidi ya mtunza hazina taratibu
zifuatazo zitatumika;
20
Endapo mtunza hazina /fedha atahisiwa kuwa katumia fedha tofauti na utaratibu au
ridhaa ya wananchi hatua zifuatazo zitumike; -
▪ Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji ataitisha kikao cha kamati yake
na kumhoji juu ya tuhuma husika
▪ Ikiwa ameshindwa kutoa maelezo ya kujitosheleza na kushindwa kuondoa
mashaka hayo, Taarifa hiyo itapelekwa kwa mwenyekiti wa kijiji ambaye
anapaswa kuitisha kikao cha Serikali ya Kijiji kumhoji juu ya tuhuma husika,
kama maelezo yake hayajajitosheleza kiasi cha kuuongezea uongozi wa
kijiji mashaka, Atapewa barua ya kujieleza ikiwa ni nafasi ya kujieleza
kufuatia tuhuma au mashaka dhidi ya matumizi mbaya ya fedha ya kijiji.
▪ Endapo maelezo yake katika barua hayataondoa utata, mwenyekiti
ataitisha Halmashauri ya kijiji iliyomchagua na kuwasilisha hoja ya
kumsimamisha kazi ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake. Hoja
ikipitishwa VEO ataandika barua ya kumsimamisha kazi hadi hapo
mahakama/baraza la kata itakapo amua kuwa ana hatia ama la,
▪ Baada ya kusimamishwa kazi VEO atamfikisha mtuhumiwa
polisi/mahakamani/baraza la kata. moja ya vyombo hivyo ndicho
kitakachotoa tamko la mwisho.
▪ Akipatikana na hatia atafukuzwa kazi hiyo na kutekeleza adhabu
zilizoamriwa, na mara moja Mwenyekiti wa kijiji kufanya taratibu za kuziba
pengo la mtunza hazina aliyepita.
MATUMIZI YANAYOIDHINISHWA; Kwanza ifahamike kuwa matumizi makuu ya fedha itokanayo na uhifadhi wa msitu
wetu yatagawanyika katika makundi makuu matatu kama ifuatavyo; -
▪ 50% itatumika katika shughuli za maendeleo ya kijiji kwaajili ya wananchi wote
▪ 25% pesa hii itatumika kwaajili ya kuboresha kamati ya maliasili ya Kijiji.
▪ 25% itatumika kwaajili ya kufanya shughuli za uhifadhi wa msitu wa kijiji cha
Kagunga kuwa endelevu kama vile:
• Ununuzi wa vitabu vya kumbukumbu kama vilivyoainishwa katika
“Kugharamia marekebisho ya mipaka".
21
• Kugharamia tathimini ya Rasilimali na kuboresha Mpango huu wa
Usimamizi
• Kugharamia uendeshaji wa kesi.
• Kutoa motisha kwa kikosi cha doria na Kamati ya Maliasili ya Kijiji katika
kutekeleza majukumu yao.
• Kununua zana za doria mfano sare, mahema, tochi, makoti ya mvua n.k.
• Kugharamia mahitaji wakati wa doria kama chakula n.k.
Mipaka ya Msitu wa hifadhi wa kijiji cha Kagunga Msitu huu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga una bikoni zinazozunguka mipaka ya nje
ya msitu huu.
MAELEKEZO MAALUM Katika maelekezo haya inasisitizwa kwamba maamuzi yote kuhusu usimamizi wa
msitu wetu turejee vipengele vilivyoelekezwa na kukubaliwa na sisi wenyewe katika
mpango huu. Hatutegemei tena wataalamu toka wilayani kuja kufanya maamuzi kwa
ajili yetu bali kuwaomba ushauri katika kupambanua mkwamo fulani ili baadaye sisi
tufanye maamuzi.
ULINZI NA UKAGUZI WA ENEO LA MSITU WA KIJIJI CHA KAGUNGA Kila mwanakijiji wa Kagunga ana jukumu la kulinda na kutunza hifadhi ya msitu wa
kijiji. Hili jukumu litafanyika kwa kutekeleza yafuatayo:
▪ Kutoa taarifa za uhalifu
▪ Kutambua na kutoa taarifa za wahalifu wa msitu wa hifadhi ya kijiji na zana za
uvunaji haramu ndani na hifadhi ya msitu wa kijiji.
▪ Kuzuia moto usitokee na kuzima unapotokea.
▪ Kushiriki katika shughuli za uoteshaji miche ya miti na upandaji wa miti katika
maeneo ya makazi na mashambani.
▪ Ni wajibu wa wakazi wote wa kijiji cha Kagunga kushirikiana katika ulinzi wa
msitu wa hifadhi ya kijiji.
▪ Doria za ukaguzi katika msitu wa hifadhi ya kijiji zitafanywa na kamati ya doria
angalau mara mbili kwa mwezi.
22
▪ Walinzi wa msitu na hifadhi watachaguliwa na Halmashauri ya kijiji na
kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji kutoka katika vitongoji vyote vya kijiji
kwa uwakilishi wa Vitongoji vya Kagunga A, Kagunga B, Mantena na Kamkola.
Sifa za Walinzi wa Msitu. Zifuatazo ni miongni mwa sifa ambazo inabidi mlinzi wa msitu sharti awe nazo:
▪ Awe na tabia na mwenendo mzuri.
▪ Wenye kujituma na mwaminifu.
▪ Mkakamavu na mwenye afya nzuri.
▪ Asiwe mlevi
▪ Awe mkazi wa kijiji cha Kagunga na raia wa Tanzania.
▪ Awe na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
▪ Ajue kusoma na kuandika.
Wajibu, Majukumu na Mafao ya Walinzi wa Msitu wa Hifadhi ya Kijiji
▪ Walinzi watachagua kiongizi wao (Kamanda) kutoka miongoni mwao ambaye
atawajibika kupanga utaratibu kwa kushirikiana na walinzi wenzake wa doria
na utoaji taarifa kwa Kamati ya Mazingira.
▪ Walinzi wa msitu hawatalipwa mishahara lakini watapata motisha kama
itakavyoamuliwa na Serikali ya kijiji. Aidha walinzi husika wanaweza kupewa
25% ya faini anayotozwa mhalifu.
▪ Walinzi wa msitu wanaweza kusamehewa kazi nyingine za maendeleo kijijini.
▪ Walinzi watakaokwenda kinyume na maadili yao ya kazi wataadhibiwa kwa
kuonywa, kutozwa faini na kufukuzwa au kushitakiwa Mahakamani kutokana
na ukubwa wa kosa lililotendeka.
▪ Walinzi watatoa taarifa yao ya doria kila wanapofanya doria kwa Kamanda wao
ambaye atapaswa kutoa taarifa kwa Kamati ya Mazingira haraka iwezekanavyo
(isizidi siku moja).
▪ Walinzi waliofanya kazi nzuri watazawadiwa kila mwisho wa mwaka na
Halmashaurii ya Kijiji. Walinzi hao watapendekezwa na Kamati ya Mazingira na
kuthibitishwa na Halmashauri ya kijiji. Zawadi/ motisha kwa walinzi waliofanya
vizuri itakuwa kama ilivyopendekezwa hapo juu.
23
OPERESHENI Yapo mazingira ya pekee ambapo kikosi pekee hakitoweza kukabiliana na uhalifu
fulani wa mpito, hivyo operesheni maalumu itaandaliwa kwa idhini ya mwenyekiti wa
kijiji kupitia kamati yake ya serikali ya kijiji kwa ushauri wa kamati kuu mbili; -
▪ Kamati ya Ulinzi ya Kijiji na
▪ Kamati ya Maliasili ya Kijiji.
N.B: Maandalizi haya lazima yawe ya siri sana.
ZAWADI YA PONGEZI KWA MWANA DORIA Kutakuwa na utaratibu wa kutoa zawadi ya pongezi au motisha kwa mwana kikosi cha
doria ambaye atafanya kazi kwa ujasiri, ushujaa na uadilifu mkubwa utakao thibitishwa
na wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu ya Kijiji na Kuungwa mkono na Mkutano
Mkuu wa Kijiji. Kiasi cha pongezi au motisha kitapangwa na Halmashauri kuu ya kijiji.
zawadi hii itatolewa hadharani na kuwekwa katika kumbukumbu za vitabu husika.
Kifungu Cha Kumi Taratibu
Kanuni za Kutumia Msitu wa Hifadhi ya kijiji ▪ Mkazi yeyote wa kijiji cha Kagunga, Afisa Misitu au mtu yeyote aliyeruhusiwa
wanaweza kuingia ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji kwa idhini ya Kamati ya
Mazingira.
▪ Afisa Misitu yeyote wa Idara ya Misitu na Nyuki wakati wowote anaweza kuingia
ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji aidha akiwa peke yake au kwa kushirikiana
na Kamati ya Mazingira ya kijiji kwa lengo la kufanya ukaguzi na kutoa ushauri
kwa Kamati ya Mazingira ambao unapaswa kupokelewa na kufanyiwa kazi kwa
lengo la kuboresha uendelezaji wa eneo hilo la msitu.
▪ Sio ruksa kwa mtu yeyote kuingia msitu wa hifadhi ya kijiji bila kibali kutoka kwa
Kamati ya Mazingira isipokuwa Walinzi wa msitu, Halmashauri ya kijiji, Kamati
ya Mazingira na Afisa Misitu wanaweza kufanya hivyo bila kibali.
▪ Wageni wote wenye vibali toka Wizarani, Wilayani au wafadhili ni sharti wapite
kijijini na kuonyesha vibali vyao kwa Kamati ya Mazingira ya kijiji kabla ya
kuanza kufanya kazi yoyote ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji.
24
Kanuni za matumizi ya msitu: Mahitaji yaliyoruhusiwa yatapaswa kupatikana kutoka maeneo ya matumizi ndani ya
msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga. Maeneo yaliyohifadhiwa hayataruhusiwa
kupata mahitaji ya mbao, miti ya nguzo/miamba ya nyumba na mengineyo
yasiyoruhusiwa.
Matumizi ya Msitu yanayohusu Ukataji wa Miti Mahitaji yote yanayohusu ukataji miti aina fulani kwa ajili ya mbao, nguzo na miamba
ya nyumba ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga yanaruhusiwa katika EDU
ya Maba kwa kibali kitakachotolewa na Kamati ya Maliasili na kuwekwa alama kwa
kutumia nyundo maalum ya Idara ya Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda. Miti
husika itavunwa kwa kiwango ambacho hakitaathiri lengo la msingi la kuhifadhi msitu
ambalo ni kuhifadhi vyanzo vya maji na upatikanaji endelevu wa rasilimali na huduma
ya msitu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
TARATIBU NA SHERIA NYINGINEZO Adhabu Uwezo wa Kamati ya Mazingira ya kijiji cha Kagunga kutoza faini umetolewa kwake
na Halmashauri ya kijiji cha Kagunga kulingana na Sheria za Serikali za Mitaa (Serikali
za Vijiji) 1982 No. 7 zilizoundwa chini ya kifungu cha 120 (i) na 167.
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya matumizi ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha
Kagunga yaliyowekwa na kukubaliwa atatozwa faini kwa mujibu wa Sheria Ndogo ya
kijiji cha Kagunga ya kulinda na kutunza msitu wa hifadhi ya kijiji.
Kifungu Cha Kumi na Moja Adhabu
MCHAKATO WA KUMSHUGHULIKIA MKOSAJI NA KOSA ▪ Hairuhusiwi kwa mwanakijiji, mwanakamati, mlinzi au kiongozi yeyote kumtoza
faini mhalifu akiwa peke yake.
▪ Mazao ya misitu yaliyovunwa kinyume cha utaratibu pamoja na zana
zilizotumika katika uhalifu huo yakikamatwa ni lazima yafikishwe kwenye ofisi
ya kijiji ambapo hatua zaidi itachuliwa na Kamati ya Mazingira ya kijiji.
▪ Iwapo itabainika kuwa mtu au watu wamekiuka taratibu za matumizi ya msitu
wa hifadhi ya kijiji, mtu huyo au watu hao watafikishwa mbele ya Kamati ya
25
Mazingira ya kijiji na suala lao litashughulikiwa kwa utaratuibu ufuatao hapa
chini:
• Mhalifu/wahalifu watafikishwa katika ofisi ya kijiji ambapo Afisa Mtendaji
wa Kijiji atamuweka/atawaweka chini ya ulinzi. Afisa Mtendaji wa Kijiji
atawaarifu viongozi wa kamati/wajumbe wa Kamati ya Mazingira
angalau wawili ili kuwatoza faini wahalifu iwapo watakiri/atakiri kosa kwa
kuweka sahihi katika daftari la “makosa na faini”
• Iwapo mhalifu/mtuhumiwa atakataa kukiri kutenda kosa kwa kukataa
kuweka sahihi katika daftari, mtu huyo atatakiwa kupelekwa
mahakamani.
• Endapo mhalifu/wahalifu watakiri kutenda kosa, faini yote lazima iwe
imelipwa katika muda wa siku tatu (3) toka siku ya kukiri kutenda kosa
hilo. Hata hivyo mhalifu atalazimika kuwekewa dhamana na mtu
anayekubalika katika kijiji cha Kagunga.
▪ Katibu atapokea malipo ya faini iliyolipwa kwa kuandika stakabadhi ambayo
atampatia mhalifu. Namba ya stakabadhi iliyotolewa itaandikwa kwenye daftari
la “Makosa na Faini” na kumkabidhi Mweka Hazina azipeleke kwenye akaunti
ya Kamati ya Mazingira ya kijiji.
▪ Iwapo mtu anayetuhumiwa kutenda kosa atakataa kukiri kosa mbele ya Kamati
ya Mazingira na mbele ya Mwenyekiti wa Kijiji au Afisa Mtendji wa Kijiji basi
itabidi vyombo hivyo vya utendaji vifikishe shauri hili mahakamani kwa uamuzi
zaidi.
▪ Iwapo mhalifu atashindwa kulipa faini katika kipindi kilichokubaliwa basi Kamati
ya Mazingira au Afisa Mtendaji wa Kijiji atafikisha suala hilo mahakamani.
FAINI NA ADHABU KWA KILA KOSA Mtu yoyote atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa lolote lililoidhinishwa katika
kifungu cha 10 cha sheria ndogo hizi ataadhibiwa kama ifuatavyo:
▪ Kosa la kuingiza na kuchunga mifugo atatozwa Tshs 5000/= kwa kila
mbwa, nguruwe, ng’ombe na Punda na Tsh 2500/= kwa mbuzi na
kondoo. Atakayeshindwa kulipa mifugo yake itaifishwe kulingana na gharama
ya faini.
26
▪ Kosa la kuingia msituni bila kibali adhabu yake itakuwa ni faini isiyopungua
Tsh 10,000/= na isiyozidi Tsh 50,000/=
▪ Kosa la Kuchoma mkaa faini shilingi Tsh 50,000/= na kutaifisha mkaa huo.
▪ Kosa la Kukata miti bila kibali adhabu itatolewa kulingana na thamani ya mti
uliokatwa na faini isiyopungua Tsh 10,000/= na isizidi Tsh 50,000/= pamoja na
kutaifisha miti hiyo.
▪ Kosa la Kufanya shughuli za kilimo faini shilingi elfu hamsini (50,000/=) kwa
hekari moja, kutaifisha mazao na kupelekwa mahakamani.
▪ Kosa la Kuchoma moto faini ya isiyopungua Tsh 20,000/= na isiyozidi Tsh
50,000/= na atashitakiwa kwa mujibu wa sheria ya kosa husika.
▪ Kosa la Kufanya shughuli nyingine yoyote isiyohusika katika msitu huo
atatozwa faini Tsh 30,000/=
FAINI ZA KUTOWAJIBIKA Iwapo mjumbe yeyote katika Halmashauri ya Kijiji, Kamati ya Mazingira au walinzi wa
msitu atakiuka taratibu za kiutendaji kuhusiana na uhifadhi wa msitu wa hifadhi ya kijiji
cha Kagunga, atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria hii na atatozwa faini
itakayojulikana kama faini ya wenye dhamana/madaraka. Faini hiyo itakuwa mara
mbili ya faini zitakazotozwa kwa watu wasiokuwa na madaraka kijijini/ zilizoainishwa
hapo juu.
• Pamoja na faini hizo, makosa ya viongozi hao lazima yajadiliwe kwenye vikao
vya juu katika kijiji na kuwachukulia hatua kali kama vile barua za onyo la
maandishi, kusimamishwa na kuwaondoa kwenye nafasi zao baada ya
kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.
• Kwa wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Afisa Mtendaji Kata ataitisha Kikao
kujadili hatima ya kiongozi aliyefanya uhalifu huo.
Kifungu Cha Kumi na Mbili Kuboresha msitu na Ukarabati wake
KUUENDELEZA MSITU Kwa bahati nzuri utengaji wa msitu ulizingatia maeneo ya kulima kuchungia mifugo,
makazi n.k. hivyo hakuna mvutano wa mgogoro wa hitaji la shughuli hizi katika eneo
la msitu huu. Shughuli kama hizi zitafanyika nje ya msitu kwa kujitosheleza. Hapa
27
Mpango huu wa Usimamizi wa Msitu unapiga marufuku kufanyika shughuli za aina hii
ndani ya msitu.
Aidha, ni marufuku mtu au kikundi cha watu kupanda mti wowote wa kigeni ndani ya
msitu huu.
Aina pekee za miti zinazoruhusiwa kuvunwa na kiasi chake zimeorodheshwa katika
majedwali yaliyoambatanishwa na mpango huu. Hairuhusiwi kutumia msumeno wa
mnyororo katika msitu huu.
Kifungu Cha Kumi na Tatu Matumizi
UTANGULIZI: Msitu huu ni msitu wa matumizi na Uhifadhi hivyo uvunaji wa miti ya mbao
unaruhusiwa kwa kiwango kilicho ainishwa katika mpango huu, uvunaji wa rasilimali
za msitu unaruhusiwa katika EDU ya MABA. Lakini jambo la kuzingatia ni kiasi, wakati
na utaratibu wa uvunaji kama ilivyo ainishwa katika mpango huu. EDU ya Uhifadhi ya
KATUNU na MAJINDO haitaruhusiwa kufanyika shughuli zozote za uvunaji kwani ni
kwa ajili ya Uhifadhi na matumizi mengine yasiyokuwa ya uvunaji wa miti na kutokana
na kuwa maeneo yanayopendelewa na wanyamapori aina ya sokwe pia makorongo
marefu, vyanzo vya maji na bioanuai mbalimbali muhimu. Hivyo basi, Mahitaji
yaliyoruhusiwa yatapaswa kupatikana kutoka maeneo ya matumizi ndani ya msitu wa
hifadhi ya kijiji cha Kagunga. Maeneo yaliyozuiliwa/hifadhiwa hayataruhusiwa kupata
mahitaji ya mbao, miti ya nguzo/miamba ya nyumba na mengineyo yasiyoruhusiwa.
UVUNAJI WA MITI Uvunaji wa miti unaoruhusiwa ni kwa miti ya aina zilizoorodheshwa katika Jedwali Na
1. EDU hii ina jumla ya miti kama inavyoonyeshwa katika Jedwali (tazama katika
viambata) ikiwa ni pamoja na matumizi mengineyo ya EDU hii.
Kiasi kamili cha miti ya kuvunwa kwa kila aina ya mti vimeonyeshwa katika jedwali
namba 5 na 7. Katika majedwali haya imeonyeshwa bayana kiasi gani cha kuvunwa
kwa kila mwaka na ni aina gani ya miti. Inapaswa kuzingatiwa bila kuongeza hata
kidogo.
28
Kifungu Cha Kumi na Nne Ratiba
HATUA ZA HARAKA ▪ KAMATI YA MALIASILI KIJIJI na Timu ya Doria zinapaswa kuchaguliwa
katika mkutano mkuu wa kijiji
▪ Kamati ya Maliasili ya Kijiji inapaswa kufanya mkutano wake wa kwanza
▪ Taratibu za ununuzi wa vitabu vya kumbukumbu zinatakiwa zifanyike ili
Kamati ikutane na Mtunza Hazina wa Wilaya. zoezi hili litakamilishwa na
Hafla au mkutano utakaohudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kwa
uzinduzi rasmi.
▪ Mwezi June 2017 ni mwezi wa kuanza kazi rasmi kwa utekelezaji wa Mpango
wa Usimamizi wa Msitu huu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga.
UFUATILIAJI Vigezo vya Mafanikio: Vifuatavyo ni Vigezo vya mafanikio vitatumika katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa
Mpango huu wa Usimamizi wa msitu wa hifadhi ya kijiji:
▪ Wanakijiji kuunga mkono juhudi za uhifadhi kwa:
• Kutoa ushirikiano kwa Kamati ya Mazingira na walinzi wa msitu na
hifadhi.
• Kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
• Kuotesha na kupanda miti katika maeneo ya kaya na mashamba.
• Kuheshimu na kutekeleza taratibu za ulinzi na utunzaji Misitu.
▪ Kupungua kwa matukio ya upasuaji mbao, moto, uwindaji wa wanyama pori,
uvamizi wa msitu kwa ajili ya kilimo na ufugaji.
▪ Kupungua na kufunga kwa njia zisizoruhusiwa msituni.
▪ Kuongezeka kwa uoto wa asili na hivyo msitu kufunga hasa katika maeneo
yaliyoharibiwa.
▪ Kurejea au kuongezeka kwa wanyama pori, ndege na viumbe vingine hai katika
msitu wa kijiji.
▪ Kuongezeka kwa kiwango cha maji kwenye mito, chemchem au kufufuka kwa
chemechem zilizokufa kutokana na uharibifu.
▪ Kuongezeka kwa makundi ya nyuki ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji.
29
▪ Mipaka ya nje ya msitu wa hifadhi kuwa wazi, safi na kuonekana bila ugumu
wowote.
Wafuatiliaji Wafuatao watahusika kufanya ufuatiliaji kwa kukusanya taarifa kuhusu vigezo vya
mafanikio:
▪ Wataalamu wa Misitu wa ngazi zote.
▪ Halmashauri ya kijiji
▪ Kamati ya Mazingira ya kijiji.
Taarifa ya Ufuatiliaji Itatolewa kwa: ▪ Afisa Misitu (W)/ Afisa Misitu (M)
▪ Mkutano Mkuu wa kijiji.
▪ Mkuu wa Wilaya/Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
▪ Halmashauri ya kijiji.
Muda wa Kufanya Ufuatiliaji Kamati ya Mazingira: Itafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mpango huu mara mbili
(2) kila mwezi na kuandaa taarifa kwa Halmashauri ya kijiji mara moja kwa mwezi
yenye nakala kwa Afisa Misitu (W).
Halmasahauri ya kijiji: Itafuatilia mpango huu mara moja (1) kila mwezi
▪ kwa kutembelea msitu wa hifadhi ya kijiji angalau mara moja kila mwezi
▪ kuwa na agenda ya kudumu katika vikao vyake
▪ Kwa kutumia taarifa ya Kamati ya Mazingira.
Wataalam wa Misitu & ngazi za Eneo, (W)/ (M):
▪ Wataalam wa ngazi ya Eneo (Kata/Tarafa) watafanya ufuatiliaji wa mpango huu
mara moja kila mwezi.
▪ Wataalam wa ngazi ya Wilaya & Mkoa watafuatilia utekelezaji wa mpango huu
mara moja kila baada ya miezi mitatu (3) yaani robo mwaka.
30
IKUMBUKWE: Taarifa ya matokeo ya ufuatailiaji itajadiliwa mara baada ya kazi ya
ufuatiliaji kukamilika.
Mpango huu unaweza kufanyiwa marekekebisho baada ya miaka mitano (5) ya
utekelezaji kwa kuzingatia taarifa za ufuatiliaji na uamuzi uliofikiwa wakati wa kujadili
taarifa hiyo.
RATIBA YA UTEKELEZAJI Hatua za Awali za Utekelezaji:
▪ Kuchagua Kamati ya Mazingira na walinzi wa msitu (Kamati ya doria) itafanyika
mara baada ya mpango wa utekelezaji kupitishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji.
▪ Kikao cha kwanza cha Kamati ya Mazingira na walinzi kitafanyika siku moja
baada ya uchaguzi wao kufanyika.
▪ Kununua vitabu vya kumbukumbu itafanyika baada ya Kamati ya Mazingira
kufanya kikao chake cha kwanza.
Hatua Zitakazofuata ▪ Kuweka mabango ya matangazo.
MUDA WA MPANGO, MAREKEBISHO NA MAPITIO YAKE: Mpango huu wa utekelezaji utatumika kwa miaka mitano (5) kuanzia mwaka 2017 –
2021. Marekebisho ya mpango yatafanyika kwa kuzingatia mahitaji yatakayojitokeza
kwa lengo la kuuboresha na Kamati ya Mazingira ya kijiji itahusika kwa ushirikiano na
Afisa Misitu (W) Mpanda.
31
32
VIAMBATA
MPANGO WA UVUNAJI KWA AINA MBALIMBALI ZA MITI KATIKA EDU ZA
MABA
JEDWALI Na 1: ORODHA YA MITI YA INAYORUHUSIWA KUVUNWA - EDU YA
MABA.
MITI MUHIMU MITI MINGINEYO MATUMIZI MENGINEYO
Mkoma Mkalya Ukataji wa milala
Mbanga Mhongolo Urinaji wa asali
Mlembela Mbombo Uvunaji wa miti ya mbao
Mninga Miyenze Kukata nyasi
Mkurungu Mitonga Kukusanya kuni
Mpilipili Msongati Ukatajiwa boriti, nguzo na fito
Mtundu Msongati Matambiko
33
JEDWALI Na. 2: MAJUMUISHO YA TAKWIMU KUTOKA KATIKA PLOTI ZA SAMPULI
Forest assessment form C Kijiji Kagunga Jina la msitu Kampese Idadi ya ploti sampuli (N) 62 Jina la EDU Maba
Eneo la EDU (ha) (A) 2479 Eneo la ploti sampuli (ha) (P) 0.04
Madaraja ya vipimo (DBH)
<4 4 - 7 8 - 14 15 - 29 30 - 49 50+
Jum
la
iliyo
piu
mw
a
(T)
Jum
la
kwen
ye E
DU
(F
)
Jum
la
iliyo
pim
wa
(T)
Jum
la
kwen
ye
ED
U (
F)
Jum
la
iliyo
pim
wa
(T
)
Jum
la
kwen
ye
ED
U (
F)
Jum
la
iliyo
pim
wa
(T
)
Jum
la
kwen
ye
ED
U (
F)
Jum
la
iliyo
pim
wa
(T)
Jum
la
kwen
ye
ED
U (
F)
Jum
la
iliyo
pim
wa
(T)
Jum
la
kwen
ye
ED
U (
F)
Miti muhimu
Mninga 0 0 0 0 1 1,000 4 3,998 0 0 2 1,999
Mkurungu 5 4,998 6 5,998 12 11,995 15 14,994 5 4,998 1 1,000
Mbanga 0 0 0 0 6 5,998 3 2,999 3 2,999 1 1,000
mpilipili 0 0 0 0 1 1,000 0 0 1 1,000 0 0
Mtundu 15 14,994 2 1,999 1 1,000 4 3,998 3 2,999 2 1,999
Msawala 1 1,000 0 0 1 1,000 0 0 0 0 0
Mkola 1 1,000 1 1,000 0 0 0 0 0 0 0 0
Mlembela 0 0 0 0 3 2,999 2 1,999 2 1,999 2 1,999
Mfulu 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0
Jumla kwenye EDU Miti muhimu 21,991 8,996 24,990 27,989 13,994 7,997
Wastani wa miti / ha 9 4 10 11 6 3
Miti mingineyo
mkoma 7 6,997 8 7,997 13 12,995 15 14,994 8 7,997 9 8,996
Msongati 0 0 1 1,000 6 5,998 4 3,998 4 3,998 0 0
Mlama 6 5,998 3 2,999 3 2,999 4 3,998 2 1,999 0 0
Mtonga 5 4,998 17 16,993 43 42,983 40 39,984 19 18,992 3 2,999
34
Mtopetope 0 1 1,000 3 2,999 4 3,998 1 1,000 1 1,000
Kibhula 4 3,998 15 14,994 19 18,992 26 25,990 2 1,999 3 2,999
Mkuni 0 2 1,999 1 1,000 4 3,998 7 6,997 13 12,995
Mketya 0 2 1,999 0 0 1 1,000 0
Miyenze 0 4 3,998 5 4,998 1 1,000 3 2,999 4 3,998
Mlunguji 0 4 3,998 3 2,999 0 2 1,999 0
Kaselenge 1 1,000 4 3,998 3 2,999 0 0 0 0 0
Mgando 1 1,000 1 1,000 2 1,999 2 1,999 0 0 2 1,999
Mbarebare 0 0 1 1,000 1 1,000 3 2,999 0 0 0 0
Mgunga 0 0 1 1,000 1 1,000 0 0 0 0 0
Mtiti 0 0 2 1,999 1 1,000 1 1,000 0 0 0 0
Mputika 0 0 1 1,000 2 1,999 0 0 1 1,000 1 1,000
Mbeko 0 0 1 1,000 2 1,999 0 0 1 1,000 0 0
Chinga 0 0 1 1,000 3 2,999 4 3,998 0 0 0 0
Mwembepori 0 0 2 1,999 0 0 0 0 0 0 0 0
Mfundambogo 0 0 0 0 2 1,999 0 0 3 2,999 0 0
Mponda 0 0 0 0 0 0 0 0 4 3,998 5 4,998
Msantu 0 0 0 0 0 0 1 1,000 0 0 1 1,000
Mgumbu 0 0 0 0 0 0 1 1,000 0 0 0 0
Kafumla 0 0 0 0 0 0 1 1,000 0 0 0 0
Nyengo 2 1,999 0 0 1 1,000 2 1,999 2 1,999 0 0
Mbuguso 0 0 0 0 1 1,000 0 0 0 0 0
Mkalya 0 0 0 0 0 0 0 0 1 1,000 0 0
Mnyoso 0 0 0 0 1 1,000 1 1,000 0 0 0 0
Mpapa 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 1 1,000
Mjuguji 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0
Msulula 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0
27,989 13,994 7,997
Jumla miningeyo 25,990 70,971 115,953 113,954 60,975 42,983
35
Wastani wa miti/ha 10 29 47 46 25 17
36
JEDWALI Na 3 FOMU ‘C’ YA TATHIMINI
Form C ya Tathmini ya msitu Kijiji Jina la Msitu Idadi ya ploti za sampuli (N)
Jina la EDU Eneo la EDU (ha) (A) Plot area (ha) (P)
Madaraja ya vipenyo
<4 4 - 7 8 - 14 15 - 29 30 – 49 50+
Ju
mla
ili
yo
pim
wa
(T
)
Ju
mla
kw
en
ye
E
DU
(F
)
Ju
mla
ili
yo
pim
wa
(T
)
Ju
mla
kw
en
ye
E
DU
(F
)
Ju
mla
ili
yo
pim
wa
(T
)
Ju
mla
kw
en
ye
E
DU
(F
)
Ju
mla
ili
yo
pim
wa
(T
)
Ju
mla
kw
en
ye
E
DU
(F
)
Ju
mla
ili
yo
pim
wa
(T
)
Ju
mla
kw
en
ye
E
DU
(F
)
Ju
mla
ili
yo
pim
wa
(T
)
Ju
mla
kw
en
ye
E
DU
(F
)
Miti muhimu
Miti Mingineyo
37
Jumla (F) = A/P * T/N : A = eneo la EDU (ha),P = ukubwa wa ploti ya sampuli (ha), T = idadi ya miti iliyopimwa (kwenye ploti zote za sampuli), N = idadi ya ploti za sampuli
JEDWALI Na 4: MIHIMILI YA MSINGI KUONYESHA WINGI WA MITI KATIKA EDU YA MABA.
38
JEDWALI Na. 5:
9
4
10
11
6
3
0
2
4
6
8
10
12
<4 4 - 7 8 - 14 15 - 29 30 - 49 50+
Idad
i ya
mit
i/h
a
DBH (cm)
Miti muhimu
39
0
2000
4000
6000
8000
10000
12000
14000
16000
<4 4-7 8-14 15-29 30-49 50+
Idad
i ya
mit
i
DBH (cm)
Mihimili ya ukubwa wa miti aina ya Mkurungu - EDU ya Maba
40
JEDWALI Na 6. UFUPISHO WA MPANGO WA UVUNAJI KATIKA EDU YA MABA KWA MWAKA 2017/2018 HADI 2021/2022
DBH Idadi katika
EDU Idadi halisi Pungufu / Ziada
Iliyopo kuvunwa (50% ya ziada)
Uvunaji 5 yrs Maoni
< 4 21,991
1,127,945
(1,105,954)
(552,977) -110595
4 -7 8,996 872608
(863,612)
(431,806) -86361
8-14 24990 391682
(366,692)
(183,346) -36669
15- 29 27989 24790
3,199
1,600 320
30- 49 13994 12395
1,599
800 160
50+ 7997 4958
3,039
1,520 304
JEDWALI Na 7: ORODHA YA MITI YA INAYORUHUSIWA KUVUNWA - EDU YA MABA
MITI MUHIMU MITI MINGINEYO MATUMIZI MENGINEYO
Msawala Mbarebare Urinaji wa asali
Kabamba Msongati Uyoga na matunda pori
Mpilipili Mvinje Uvunaji wa miti ya mbao
Mkola Mhongolo Uchimbaji wa dawa za kienyeji
Mninga Mkoma Kukata nyasi
Mkurungu Mhunsa Kukusanya kuni
Mlembela Mubha Kamba za miti
Mbombo Ukataji wa boriti, nguzo na fito
41
Maji
Matambiko