jarida la sikika namba ya usajili - 00005809 toleo 8 ... · kinafanya nini nyumbani kwa daktari?...

4
Jarida la Sikika Toleo 8: Desemba, 2012 Jarida la Sikika Toleo 8: Desemba, 2012 Namba ya Usajili - 00005809 Ndani Zi wapi fedha za ujenzi kituo cha afya Shelui?................................................... 1 Mfumo wa ajira Halmashauri wadaiwa kudhoofisha uwajibikaji ...................... 2 Kondoa wamshangaa Mwenyeki kuvunja Mkutano........................................ 3 Kiteto waibua changamoto sekta ya afya.......................................................... 4 Huduma bora za afya kwa watanzania wote Haliuzwi Utangulizi Mpendwa msomaji; karibu kwenye jarida letu la 8 ili uweze kufahamu kwa muhtasari shughuli zilizofanywa na shirika letu kaka robo ya nne ya mwaka (2012). Kaka kipindi cha Septemba hadi Desemba 2012, Sikika imekuwa ikiendesha mafunzo ya Ufualiaji wa Uwajibikaji wa Jamii (Social Accountability Monitoring -SAM) kaka wilaya 5 za Kondoa, Kiteto, Mpwapwa, Singida Vijijini na Iramba kwa lengo la kufualia uwajibikaji kaka sekta ya afya. Kwa ujumla, mafunzo hayo yalilenga kukuza uelewa wa jamii, wawakilishi wa wananchi na viongozi wa dini kupia uchambuzi wa nyaraka na baje, kufualia utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopangwa na kisha kudai uwajibikaji wa watendaji. SAM pia ilihamasisha wananchi kudai ufafanuzi, uhalali na uthibisho wa namna rasilimali za umma zilivyotumika na kuchukua hatua za kurekebisha pale ambapo rasilimali hizo hazikutumika kwa ufanisi. Zoezi hilo lilishirikisha mu za SAM kutoka kila wilaya ambapo ziliundwa na watu ka ya16-18. Timu hizo ziliwakilisha makundi yafuatayo; Wananchi, Madiwani, Asasi za kiraia, Watendaji Kata, viongozi Serikali za Mitaa, Watu wanaoishi na VVU, makundi ya watu wenye ulemavu na viongozi wa dini. Jarida hili lina mkusanyiko wa habari na matukio yaliyojiri kwenye wilaya hizo waka wa mafunzo ya SAM. Vile vile litakuhabarisha jinsi zoezi la SAM lilivyoanza kubadili mitazamo ya wananchi, madiwani na watendaji kaka maeneo yao. Unaweza pia kupata taarifa zaidi kuhusu kazi za Sikika kupia tovu yetu www.sikika.or.tz, twier-@sikika1, facebook - Sikika Tanzania na blogspot - www.sikika- tz.blogspot.com. Kwa maoni tafadhali wasiliana nasi kupia [email protected] au sms 0688-493-882.

Upload: nguyendien

Post on 24-Aug-2019

225 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Jarida la Sikika Namba ya Usajili - 00005809 Toleo 8 ... · kinafanya nini nyumbani kwa daktari? Mnapaswa kubadilika… au mnataka nirudishwe Dar es Salaam, nilipotoka?” Aliahidi

Jarida la Sikika Toleo 8: Desemba, 2012

1

Jarida la SikikaToleo 8: Desemba, 2012Namba ya Usajili - 00005809

NdaniZi wapi fedha za ujenzi kituo cha afya Shelui?................................................... 1 Mfumo wa ajira Halmashauri wadaiwa kudhoofisha uwajibikaji ...................... 2 Kondoa wamshangaa Mwenyekiti kuvunja Mkutano........................................ 3 Kiteto waibua changamoto sekta ya afya.......................................................... 4

Huduma bora za afya kwa watanzania wote

Haliuzw

i

UtanguliziMpendwa msomaji; karibu kwenye jarida letu la 8 ili uweze kufahamu kwa muhtasari shughuli zilizofanywa na shirika letu katika robo ya nne ya mwaka (2012).

Katika kipindi cha Septemba hadi Desemba 2012, Sikika imekuwa ikiendesha mafunzo ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji wa Jamii (Social Accountability Monitoring -SAM) katika wilaya 5 za Kondoa, Kiteto, Mpwapwa, Singida Vijijini na Iramba kwa lengo la kufuatilia uwajibikaji katika sekta ya afya.

Kwa ujumla, mafunzo hayo yalilenga kukuza uelewa wa jamii, wawakilishi wa wananchi na viongozi wa dini kupitia uchambuzi wa nyaraka na bajeti, kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopangwa na kisha kudai uwajibikaji wa watendaji. SAM pia ilihamasisha wananchi kudai ufafanuzi, uhalali na uthibitisho wa namna rasilimali za umma zilivyotumika na kuchukua hatua za kurekebisha pale ambapo rasilimali hizo hazikutumika kwa ufanisi.

Zoezi hilo lilishirikisha timu za SAM kutoka kila wilaya ambapo ziliundwa na watu kati ya16-18. Timu hizo ziliwakilisha makundi yafuatayo; Wananchi, Madiwani, Asasi za kiraia, Watendaji Kata, viongozi Serikali za Mitaa, Watu wanaoishi na VVU, makundi ya watu wenye ulemavu na viongozi wa dini.

Jarida hili lina mkusanyiko wa habari na matukio yaliyojiri kwenye wilaya hizo wakati wa mafunzo ya SAM. Vile vile litakuhabarisha jinsi zoezi la SAM

lilivyoanza kubadili mitazamo ya wananchi, madiwani na watendaji katika maeneo yao.

Unaweza pia kupata taarifa zaidi kuhusu kazi za Sikika kupitia tovuti yetu www.sikika.or.tz, twitter-@sikika1,

facebook - Sikika Tanzania na blogspot - www.sikika-tz.blogspot.com. Kwa maoni tafadhali wasiliana nasi kupitia [email protected] au sms 0688-493-882.

Page 2: Jarida la Sikika Namba ya Usajili - 00005809 Toleo 8 ... · kinafanya nini nyumbani kwa daktari? Mnapaswa kubadilika… au mnataka nirudishwe Dar es Salaam, nilipotoka?” Aliahidi

Jarida la Sikika Toleo 8: Desemba, 2012

2

Zi wapi fedha za ujenzi kituo cha afya Shelui?

Na Chresensia Joseph, Iramba

WAKAZI wa Shelui, wilayani Iramba wamewataka viongozi wa kata hiyo kutoa maelezo ya zilipo Tshs 2,600,000/- ambazo zilichangwa na wananchi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa awali wa kituo cha afya.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliondaliwa na timu ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji wa Jamii (SAM) wilayani humo, mmoja wa wakazi hao, Bw. Bili Kitundu, alisema “ wananchi tumechanga shilingi milioni mbili na laki sita kwa ajili ya ujenzi wa kituo lakini mpaka leo hii hamna hata jiwe la msingi wala ujenzi wowote wa kituo cha afya unaoendelea, hakuna mwananchi yeyote anayejua zilipokwenda hizo pesa na tatizo lipo katika serikali ya kijiji.’’

Akijibu hoja hiyo, Kaimu Mtendaji wa Kata ya Shelui, Bw. Ally Kiunsi alijitetea kwamba hana taarifa kuhusu fedha hizo kwani yeye anakaimu tu. Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Bw. Yahaya Nawanda aliyekuwa mwenyekiti wa mkutano huo alimtaka Mtendaji huyo kutoa maelezo na kusisitiza kwamba haijalishi kama anakaimu au la, anachotakiwa ni kufahamu kila jambo linaloendelea ofisini kwake.

Diwani wa Kata hiyo, Mh. Kinota Omari Hamisi aliingilia kati na kufafanua kwamba uongozi wa kijiji ulimpa malipo ya awali mkandarasi aliyeteuliwa lakini kwa bahati mbaya mjenzi huyo alifariki kabla hajaanza kazi. Alisema, fedha zilizosalia walinunua tangi la maji, kokoto, pamoja na vifaa vingine vya ujenzi.

Baada ya maelezo hayo, Mkuu wa Wilaya aliwataka viongozi wa kata hiyo kupeleka ofisini kwake risiti na vielelezo vyote vinavyoonesha jinsi fedha hizo za

wananchi zilivyotumika. “Pesa kama zimetumika si kuna stakabadhi? Hizo ni pesa za wananchi nataka nione stakabadhi za matumizi ya hizo fedha ofisini kwangu.’’

Katika mkutano huo, wawakilishi wawili kutoka timu ya SAM ya wilaya walisoma hoja zilizotokana na ufuatiliaji wa utendaji hususan katika sekta ya afya. Baadhi ya hoja zilizoibuliwa ni pamoja na kutokuwepo kwa vifaa tiba na madawa ya kutosha, umeme wa jua (solar power) katika baadhi ya vituo vya afya na jengo la jiko kutumika kama sehemu ya malazi ya watu wanaosindikiza wagonjwa, hivyo kusababisha chakula kupikiwa chini ya miti.

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) iliyopitiwa na timu ya SAM ilionesha kuwepo kwa vyandarua 4,811 katika stoo ya hospitali ya wilaya ambavyo vilikuwa havijasambazwa. Vilevile dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya takriban Tshs milioni 8 vilikutwa vimekwisha muda wake wa kutumika.

Akijibu hoja za timu ya SAM, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) Dk. Antony Mbulu alisema kwamba vifaa vya umeme jua vimeshanunuliwa na kinachosubiriwa ni usambazaji na fedha za kufungia vifaa hivyo. Kuhusu ujenzi wa jiko, mganga huyo alisema uko katika hatua za awali. Zaidi, Dk. Mbulu alieleza kwamba vyandarua vilivyokuwa stoo vilisambazwa kwa wananchi siku nne kabla ya mkutano huo wa hadhara kufanyika.

Akifunga mkutano huo, DC Nawanda aliipongeza timu ya SAM na kuwataka watendaji kuwajibika kwa kuzifanyia kazi changamoto zilizotolewa pamoja na kero za wananchi.

Mfumo wa ajira Halmashauri wadaiwa kudhoofisha uwajibikaji

Mwandishi wetu, Mpwapwa

MADIWANI wilayani Mpwapwa wamesema mfumo wa sasa wa ajira za utumishi wa umma unadhoofisha uwajibikaji katika ngazi za Halmashauri.

Hayo yalielezwa wakati wa mafunzo ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji wa Jamii (SAM) yaliyoendeshwa na Sikika, wilayani Mpwapwa. Lengo la mafunzo ya SAM ni kuwawezesha wananchi kudai haki ya kupata huduma za jamii kwa kufuatilia na kusimamia bajeti na rasilimali za umma katika maeneo yao na kuwawajibisha watoa huduma wasiotimiza wajibu wao.

Mkuu wa wilaya ya Iramba Mh. Yahya Nawanda akisisitiza uwajibikaji wa watendaji wa halmashauri na

madiwani kwa wananchi wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wadau yaliyofanywa na Sikika wilayani humo.

Page 3: Jarida la Sikika Namba ya Usajili - 00005809 Toleo 8 ... · kinafanya nini nyumbani kwa daktari? Mnapaswa kubadilika… au mnataka nirudishwe Dar es Salaam, nilipotoka?” Aliahidi

Jarida la Sikika Toleo 8: Desemba, 2012

3

Diwani wa Kata ya Chunyu wilayani Mpwapwa, Mh. Nehemiah Kongawadodo alisema utaratibu wa sasa ambapo ajira za ngazi ya juu zinatolewa serikali kuu unadhoofisha uwajibikaji.“ Tumepewa nguvu ya kukemea watendaji lakini mwishowe, mtendaji aliyesababisha upotevu wa mamilioni ya fedha za umma kwenye halmashauri anaishia tu kuhamishwa badala ya kuwajibishwa… tunahamishia matatizo wilaya zingine.”

Diwani Kongawadodo anashauri mfumo wa ajira ubadilike ili mamlaka ya kuajiri na kufukuza yarudi kwenye halmashauri kutoka Serikali kuu, ili mtendaji anayehujumu fedha za umma na miradi ya maendeleo achukuliwe hatua za kisheria mahala alipo.

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Christopher Kangoye, aliwataka watendaji kuwa waadilifu na kutoa taarifa sahihi za mipango ya maendeleo kwa wananchi na wawakilishi wao. “Wananchi wana haki ya kujua, kuuliza na kuelezwa kwani miradi yote inapangwa kwa manufaa yao. Kazi za huduma za jamii si duka lako (mtendaji), lazima ushirikishe jamii,” anasisitiza.

Mh.Kangoye pia alitoa mfano wa kutowajibika kwa kuelezea jinsi alivyotembelea tarafa ya Mima, wilayani hapo na kuelezwa kwamba gari la wagonjwa la tarafa hiyo limeegeshwa kwa muda mrefu kwenye ofisi za halmashauri bila kutumika. Alisema, awali wananchi wa Mima waliambiwa wajenge kituo, wakajenga. Kisha wakaomba gari la wagonjwa, “lakini halikupelekwa kwa kisingizio kwamba hakuna dereva, sasa wamesema dereva wanae pale kijijini na leseni yake wametuonesha…uwajibikaji uko wapi?”

Mfano mwingine wa kutowajibika uliotolewa na Mkuu huyo ni wa karavati jipya ambalo alilikuta barabarani likiwa tayari limeanza kupasuka hata kabla ya ujenzi kukamilika. Kangoye alisema baada ya kuchunguza aligundua limejengwa kwa nondo za milimita 6 tu. “Nilishtuka, nikasema hivi huyu mkandarasi anatutakia mema? Waliopewa kazi walichakachua na wasimamizi hawakuwajibika.” Mkuu huyo aliwataka watendaji wa Halmashari ya Mpwapwa kuruhusu watu kuhoji kwa uwazi masuala yanayogusa maendeleo yao.

Kondoa wamshangaa Mwenyekiti kuvunja Mkutano

Na Jackson Sikahanga, Kondoa

Wakazi wa Kondoa wameshangazwa na kitendo cha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Abdallah Mwenda kuahirisha mkutano ulioandaliwa ili kutoa mrejesho wa taarifa ya timu ya Ufuatilia wa Uwajibikaji wa Jamii (SAM), uliofanywa wilayani humo.

Mwenyekiti huyo alichukua uamuzi baada ya wananchi kuanza kuuliza maswali mengi na kudai ufafanuzi juu ya taarifa ya ufuatiliaji wa timu ya SAM. Kuvunjika kwa mkutano huo kulizua mvutano kati ya madiwani, wananchi na mwenyekiti huyo huku baadhi ya madiwani wakihoji uhalali wa kuahirishwa mkutano badala ya kujibu hoja zilizowasilishwa.

Akitoa sababu za kuahirisha, Mwenyekiti huyo alisema kwamba timu hiyo ya SAM haikwenda ofisini kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Peter Kinyasi ili kupata majibu na ufafanuzi kwanza, kabla ya kuwasilisha hoja hizo kwa umma. Mkurugenzi huyo naye aliungana na Mwenyekiti wake kwa kusisitiza:“ Hoja zote zilizowasilishwa majibu yake tunayo, timu ya SAM ilitakiwa inione kwanza kabla ya mkutano.”

Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa timu ya SAM, Bw. Waziri Fataki alithibitisha kwamba alikuwa miongoni

mwa watu waliokwenda ofisini kwa Mkurugenzi huyo na kuomba ufafanuzi wa hoja zilizoibuliwa. “Mkurugenzi mwenyewe ndiye alitupangia hadi wakuu wa vitengo ambao walijibu hoja kabla ya mkutano,” alisisitiza na kuongeza kwamba majibu walipata na hata picha za kuthibitisha wanazo.

Awali, timu ya SAM ilitembelea vituo vya kutolea huduma 27 wilayani Kondoa na kugundua kwamba

Page 4: Jarida la Sikika Namba ya Usajili - 00005809 Toleo 8 ... · kinafanya nini nyumbani kwa daktari? Mnapaswa kubadilika… au mnataka nirudishwe Dar es Salaam, nilipotoka?” Aliahidi

Jarida la Sikika Toleo 8: Desemba, 2012

4

Nyumba Na. 69 Ada Estate, KinondoniBarabara ya TunisiaMtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 26 663 55/57

Ujumbe mfupi: 0688493882Faksi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected]: www.sikika.or.tzBlog: www.sikika-tz.blogspot.comTwitter: @sikika1Facebook: Sikika Tanzania

Nyumba Na. 340 Mtaa wa Kilimani S.L.P 1970 Dodoma, TanzaniaSimu: 026 23 21307Faksi: 026 23 21316

baadhi ya miradi katika sekta ya afya haijakamilika, licha ya ripoti za halmashauri kuonesha kwamba fedha zote zimetumika kama ilivyopangwa na kupitishwa. Baadhi ya miradi hiyo ni ukarabati wa vizimba 2 vya kuchomea takataka uliogharimu kiasi cha Tshs. 17,637,710/- lakini vizimba hivyo havikujengwa.

Mapungufu mengine yalionekana katika matumizi ya Tshs. 11,114,325/- zilizoripotiwa kutoa mafunzo kwa Kamati za Afya kwenye zahanati na vituo ingawa kazi hiyo haikufanyika. Fedha nyingine,Tshs. 23,708,000/- zilielezwa kutumika kufanya mafunzo kuhusu haki na majukumu ya watendaji wa afya lakini mafunzo hayo hayakufanyika.

Siku kadhaa baada ya mkutano huo, Bw. Kinyasi na Mwenyekiti wake walikwenda Dodoma na kuitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha hoja zote zilizotolewa na timu ya SAM. “Tumewashangaa sana, badala ya kwenda kwenye maeneo yaliyotajwa na kuhakiki hoja hizo ili wajibu, wanatumia fedha za walipa kodi kwenda kwenye vyombo vya habari! Madiwani tunajipanga kuomba mkutano wa dharura ili kujadili hoja zote zilizowasilishwa na timu ya SAM,” alisema mmoja wa madiwani, Mh. Suleiman Gawa.

Kiteto waibua changamoto sekta ya afya

Na Eugenia Madhidha, Kiteto

TIMU ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (Social Accountability Monitoring - SAM) katika wilaya ya Kiteto, imebaini changamoto ambazo zimekuwa zikiathiri upatikanaji wa huduma za afya.

Changamoto hizo zilielezwa katika mdahalo wa wazi ulioitishwa na timu ya SAM, baada ya ziara yao iliyofanyika mwishoni mwa 2012, kwenye vituo 16 vya huduma za afya wilayani humo.

Baadhi ya changamoto zilizobainika ni pamoja na benchi la kukalia kutumika kama kitanda cha kufanyia uchunguzi (examination bed) katika kituo cha afya cha Lesoit. Wakati huo huo, timu iligundua kwamba kitanda cha kufanyia uchunguzi, kilikuwa kwenye nyumba ya mganga mkuu wa kituo hicho. Ziara hiyo pia iligundua kwamba kituo cha Irkiushi pamoja na vingine havitoi huduma muda wa kazi kutokana na upungufu wa rasilimali watu, madawa na vifaa tiba.

Hoja nyingine ilikuwa ni uhaba mkubwa wa maji wilayani Kiteto, ambapo vituo vingi vya huduma za afya vilikuwa vikiwaagiza wagonjwa kubeba maji

kutoka nyumbani kabla ya kupata tiba. Katika zahanati ya Ngabolo, kwa mfano, timu ya SAM ilishuhudia choo cha maji kikiwa kimezibwa kwa mawe na mchanga kama mbadala wa maji.

Katika kituo cha Songambele, wauguzi walieleza kwamba wakati mwingine hulazimika kutumia fedha zao binafsi ili kuwanunulia wagonjwa maji ya kumezea dawa. Kwa mujibu wa timu ya SAM, ujenzi wa vyoo vya maji ni matokeo ya mipango duni. Walihoji, kwanini wilaya iamue kujenga vyoo hivyo wakati ikijua fika maji ni tatizo sugu wilayani Kiteto?

Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Kiteto, Bi. Jane Mutagurwa akijibu hoja zilizoibuliwa na timu ya SAM, alionesha kusikitishwa na ufanisi duni katika utoaji huduma za afya.“Kitanda cha kujifungulia wazazi kinafanya nini nyumbani kwa daktari? Mnapaswa kubadilika… au mnataka nirudishwe Dar es Salaam, nilipotoka?” Aliahidi kushughulikia hoja hizo na kuongeza kwamba zitabaki kuwa historia wilayani humo.

Naye mjumbe wa SAM, Bw. Assam Konge aliwalaumu madiwani kwa kushindwa kuwajibika kwa wananchi na kuwaomba wazinduke na kutekeleza wajibu wao.“Waheshimiwa madiwani mnapaswa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa afya ya jamii inaboreshwa.” Alisema, watahakikisha changamoto zilizoibuliwa zinafikishwa kwenye kikao cha baraza la madiwani.

Zahanati nyingi zimejengwa kwa kiwango cha juu lakini vyoo vyake ni duni.