jamhuri ya muungano wa tanzania wizara ya viwanda … · 2020. 1. 13. · jamhuri ya muungano wa...

1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI Simu: +255-22-2181344, 2180113, 2180141, 2180048, Nukushi: +255-22-2180371 Barua Pepe: [email protected] [email protected] [email protected] Tovuti: www.brela.go.tz S.L.P. 9393 DAR ES SALAAM TAARIFA KWA UMMA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUHUISHA TAARIFA ZA MAKAMPUNI NA MAJINA YA BIASHARA Dar es Salam, 31 Desemba 2019 Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inapenda kuutarifu Umma kuwa imeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya zoezi la uhuishaji wa taarifa za Makampuni na Majina ya Biashara yaliyosajili- wa nje ya mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao (Online Registration System - ORS) hadi tarehe 31 Machi 2020. BRELA inawataka wadau wote waliosajili Makampuni au Majina ya Biashara nje ya mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) kukamilisha zoezi hilo ndani ya muda ulioainishwa. Aidha ili Mwombaji aweze kukamilisha uhuishaji wa taarifa anahitaji kuwa na Namba ya utambulisho wa Taifa (NIN) kwa ajili ya kufungua akaunti kwenye mfumo wa usajili (kwa raia wa Tanzania) kwa raia wa kigeni anatakiwa kuwa na namba ya Pasi ya kusafiria (Passport No.); namba ya utambulisho wa mlipa kodi TIN) kwa kila Mkurugenzi wa Kampuni; Kupakia fomu zote zinazohitajika mathalani fomu ya taarifa kutoka kwenye mtandao (Consolidated Form); taarifa ya mwaka (Annual Returns) na taarifa za mabadiliko yaliyotokea katika kampuni ambayo hayakuwasilishwa hapo awali ; kupitia na kuhakiki- sha usahihi wa taarifa kwa mujibu wa Sheria na Taratibu. Baada ya kuhuisha taarifa, BRELA itahakiki usahihi wa taarifa husika na kutoa Ankara ya malipo kwa muombaji ambayo ataitumia kufanya malipo kwa njia ya simu ya mkononi au benki. Katika hatua nyingine BRELA inasisistiza kuwa anayefungua akaunti kwenye mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) awe ni mwenye hisa katika Kampuni au Mmiliki wa Jina la Biashara husika pia kutunza Jina la utumiaji (username) kwenye mfumo pamoja na nywila (password). Uwasilishwaji wa taarifa sahihi zinazoendana na taarifa zilizopo katika Masijala ya Usajili, kuwasilisha taarifa zilizokami- lika na inashauriwa zoezi hili kufanywa na mwombaji husika au Wakala mwenye weledi na uelewa wa Sheria na Taratibu za usajili, kuambatisha nyaraka sahihi na kuzingatia maelekezo ya marekebisho kwenye maombi yanayotumwa baada ya BRELA kufanya uhakiki wa taarifa. Imetolewa na: Robertha Makinda Afisa Habari na Mawasiliano BRELA

Upload: others

Post on 14-Feb-2021

17 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

    WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI

    Simu: +255-22-2181344, 2180113, 2180141, 2180048, Nukushi: +255-22-2180371 Barua Pepe: [email protected] [email protected] [email protected]: www.brela.go.tz

    S.L.P. 9393 DAR ES SALAAM

    TAARIFA KWA UMMAKUONGEZWA KWA MUDA WA KUHUISHA TAARIFA ZA MAKAMPUNI NA

    MAJINA YA BIASHARA

    Dar es Salam, 31 Desemba 2019Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inapenda kuutarifu Umma kuwa imeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya zoezi la uhuishaji wa taarifa za Makampuni na Majina ya Biashara yaliyosajili-wa nje ya mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao (Online Registration System - ORS) hadi tarehe 31 Machi 2020. BRELA inawataka wadau wote waliosajili Makampuni au Majina ya Biashara nje ya mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) kukamilisha zoezi hilo ndani ya muda ulioainishwa.

    Aidha ili Mwombaji aweze kukamilisha uhuishaji wa taarifa anahitaji kuwa na Namba ya utambulisho wa Taifa (NIN) kwa ajili ya kufungua akaunti kwenye mfumo wa usajili (kwa raia wa Tanzania) kwa raia wa kigeni anatakiwa kuwa na namba ya Pasi ya kusafiria (Passport No.); namba ya utambulisho wa mlipa kodi TIN) kwa kila Mkurugenzi wa Kampuni; Kupakia fomu zote zinazohitajika mathalani fomu ya taarifa kutoka kwenye mtandao (Consolidated Form); taarifa ya mwaka (Annual Returns) na taarifa za mabadiliko yaliyotokea katika kampuni ambayo hayakuwasilishwa hapo awali ; kupitia na kuhakiki-sha usahihi wa taarifa kwa mujibu wa Sheria na Taratibu. Baada ya kuhuisha taarifa, BRELA itahakiki usahihi wa taarifa husika na kutoa Ankara ya malipo kwa muombaji ambayo ataitumia kufanya malipo kwa njia ya simu ya mkononi au benki.

    Katika hatua nyingine BRELA inasisistiza kuwa anayefungua akaunti kwenye mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) awe ni mwenye hisa katika Kampuni au Mmiliki wa Jina la Biashara husika pia kutunza Jina la utumiaji (username) kwenye mfumo pamoja na nywila (password). Uwasilishwaji wa taarifa sahihi zinazoendana na taarifa zilizopo katika Masijala ya Usajili, kuwasilisha taarifa zilizokami-lika na inashauriwa zoezi hili kufanywa na mwombaji husika au Wakala mwenye weledi na uelewa wa Sheria na Taratibu za usajili, kuambatisha nyaraka sahihi na kuzingatia maelekezo ya marekebisho kwenye maombi yanayotumwa baada ya BRELA kufanya uhakiki wa taarifa.

    Imetolewa na:

    Robertha MakindaAfisa Habari na Mawasiliano BRELA