mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/majadiliano-ya-randama.docx · web viewkupokea na kujadili...

12
KIKAO CHA MAJADILIANO KUHUSU UTEKELEZAJI WA RANDAMA YA MAKUBALIANO KATI YA OFISI YA RAIS -TAMISEMI NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUHUSU USIMAMIZI WA MISITU 1.0 UTANGULIZI OR Tamisemi kwa kushirikiana na Jumuiko la Maliasili Tanzania (Tanzania Natural Resource Forum, TNRF) kupitia kampeni ya Mama Misitu inayofadhiliwa na Serikali ya Ufini waliendesha mkutano wa majadiliano wenye lengo la kuboresha mashirikiano katika usimamizi na utawala endelevu wa Misitu pamoja na biashara ya mazao ya Misitu nchini. Mkutano huu ulifanyika tarehe 14 na 15 Disemba, 2016 Morogoro mjini. Mkutano huo ulijumuisha wataalamu wa Misitu kutoka OR- TAMISEMI, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Wawakilishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya za Nachingwea, Liwale, Lindi, Kilwa, Rufiji,Nachingwea, Liwale, Lindi, Kilwa, Rufiji, Urambo, Kaliua, Mlele, Mpanda na Sikonge pamoja na maafisa Misitu Mikoa ya Lindi, Pwani, Morogoro, Kigoma, Katavi na Tabora. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dk. Ezekiel Mwakalukwa ambaye alisisitiza uwazi kutoka kwa washiriki ili kuibua kero na changamoto zilizopo katika maeneo yao na kuja na mapendekezo ya kutatua kero hizo. 2.0 MALENGO NA MADHUMUNI Lengo kubwa la mkutano huu ilikuwa ni kuwezesha majadiliano baina ya OR-TAMISEMI na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuroresha mashirikiano katika usimamizi wa misitu nchini.

Upload: others

Post on 24-Jan-2021

8 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

KIKAO CHA MAJADILIANO KUHUSU UTEKELEZAJI WA

RANDAMA YA MAKUBALIANO KATI YA OFISI YA RAIS -TAMISEMI NA WIZARA

YA MALIASILI NA UTALII KUHUSU USIMAMIZI WA MISITU

1.0 UTANGULIZI

OR – Tamisemi kwa kushirikiana na Jumuiko la Maliasili Tanzania (Tanzania Natural Resource

Forum, TNRF) kupitia kampeni ya Mama Misitu inayofadhiliwa na Serikali ya Ufini

waliendesha mkutano wa majadiliano wenye lengo la kuboresha mashirikiano katika usimamizi

na utawala endelevu wa Misitu pamoja na biashara ya mazao ya Misitu nchini. Mkutano huu

ulifanyika tarehe 14 na 15 Disemba, 2016 Morogoro mjini.

Mkutano huo ulijumuisha wataalamu wa Misitu kutoka OR- TAMISEMI, Wakala wa Huduma

za Misitu Tanzania, Wawakilishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wakurugenzi wa

Halmashauri za Wilaya za Nachingwea, Liwale, Lindi, Kilwa, Rufiji,Nachingwea, Liwale, Lindi,

Kilwa, Rufiji, Urambo, Kaliua, Mlele, Mpanda na Sikonge pamoja na maafisa Misitu Mikoa ya

Lindi, Pwani, Morogoro, Kigoma, Katavi na Tabora.

Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dk. Ezekiel

Mwakalukwa ambaye alisisitiza uwazi kutoka kwa washiriki ili kuibua kero na changamoto

zilizopo katika maeneo yao na kuja na mapendekezo ya kutatua kero hizo.

2.0 MALENGO NA MADHUMUNI

Lengo kubwa la mkutano huu ilikuwa ni kuwezesha majadiliano baina ya OR-TAMISEMI na

Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuroresha mashirikiano katika usimamizi wa misitu nchini.

Katika kuboresha usimamizi wa rasilimali za misitu nchini, OR-Tamisemi na Wizara ya

Maliasili na Utalii wameingia makubaliano yenye lengo la kuboresha ushirikiano katika

usimamizi na utawala endelevu wa misitu pamoja na biashara ya mazao ya misitu.

Page 2: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

Malengo mahususi ya mkutano huo yalikuwa kama ifuatavyo:

Kupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya

Lindi, Pwani, Tabora na Katavi.

Kupata maelekezo ya namna ya kupata fedha za Mfuko wa Misitu (TaFF)

Kutengeneza mpango kazi kutokana na Randama ya makubaliano kati ya OR-

TAMISEMI na Wizara ya Maliasili na Utalii

Kuweka maazimio kulingana na changamoto zilizotokana na mijadala

3.0 WASHIRIKI WA MKUTANO

Washiriki wa mkutano huo walichaguliwa kutokana na maeneo ambayo Jumuiko la Maliasili na

wadau wake wanafanya kazi pamoja maeneo mengine ambayo yana rasilimali misitu kwa wingi

nchini. Pamoja na washiriki kutoka wilayani, mkutano huo uliwaleta wataalamu na wakuu ya

Idara kutoka katika ngazi za taifa ili kujenga uelewa wa pamoja.

Hivyo washirki wa warsha hiyo

walitokaOR-

TAMISEMIWawakilishi kutoka

Wizara ya Maliasili na Utalii,

Wakala wa Huduma za Misitu

Tanzania, Wakurugenzi wa

Halmashauri za Wilaya za

Nachingwea, Liwale, Lindi,

Kilwa, Rufiji, Urambo, Kaliua,

Mlele, Mpanda na Sikonge pamoja na maafisa Misitu Mikoa ya Lindi, Pwani, Morogoro, Katavi

na Tabora. Majina ya washiriki yameambatanishwa pamoja na taarifa hii.

Page 3: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

4.0 RATIBA YA MKUTANO

Siku ya Kwanza

Muda Tukio Mhusika0230-0300 asb Kujisajili Wote0300-0330 Kujitambulisha Wote0330-0400 Kufungua na malengo ya mkutano OR-TAMISEMI0400-0430 Mapumziko ya Chai Wote0430-0600 Mch Mawasilisho ya changamoto na mafanikio kutoka mikoani Afisa Maliasili Mkoa0600-0700 Majadiliano ya pamoja Mwenyekiti0700-0800 Chakula cha Mchana Wote0800-0900 Mawasilisho kutoka Mfuko wa Misitu (TaFF) KatibuTawala, TaFF0900-1000 Mapitio ya Randama ya Makubaliano OR-TAMISEMI1000-1030 Majadiliano kuhusu utekelezaji wa Randama Mwenyekiti10.30-1100 Kuahirisha kikao Mwenyekiti

Siku ya Pili

Muda Tukio Mhusika0230-0330 Mapitio ya siku ya kwanza (Tulichojifunza) Mwenyekiti0330-0400 Mawasilisho kutoka kwa Sekretarieti Sekretarieti0400-0430 Mapumziko ya Chai Wote0430-0530 Majadiliano katika vikundi Wote0530-0700 Mawasilisho na kuweka maazimio Wote0700-0800 Chakula cha Mchana Wote0800-0830 Kufunga Mwenyekiti0830-0900 Masuala ya utawala Mhasibu, TNRF

5.0 MAWASILISHO, MAJADILIANO NA MAAZIMIO

Maafisa Maliasili mikoa ya Katavi, Lindi, Tabora, Pwani na Morogoro walifanya mawasilisho

wa changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya misitu katika mikoa yao na kutoa

mapendekezo ya namna bora ya kukabiliana na changamoto hizo. Mawasilisho hayo yaliibua

mjadala miongoni mwa washiriki na hivyo kuleta uelewa wa pamoja juu ya changomoto zilizopo

na namna ya kukabiliana nazo.

Page 4: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

Majadiliano ya changamoto kwenye vikundi

Baadae, Katibu Tawala wa

Mfuko wa Misitu (TaFF)

aliwasilisha utaratibu na namna

Halmsahauri za Wilaya

zinavyoweza kupata fedha za

upandaji miti. Changamoto

mbalimbali zilitolewa na

Wakurugenzi wa Halmashauri

ikiwemo ucheleweshwaji wa

nyaraka zinazopaswa kupelekwa

TaFF kwa ajili ya fedha za

upandaji miti kwa Halmashauri. Pia vitendo vya baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za

Misitu kutoingiza malipo ya upandaji miti katika malipo yanayofanywa na wafanyabiashara na

hivyo kubinya fedha zinazopaswa kwenda kwa Mfuko wa Misitu (TaFF).

Shuhuda mbalimbali zilitolewa na washiriki kuhusu manufaa waliyopata katika mkutano huu.

Ndugu Hamisi Chande, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda alisema;

“ Kwa mara ya kwanza nimefahamu utaratibu wa kuomba fedha za upandaji miti kupitia

Mfuko wa Misitu (TaFF). Nimepakua fomu hizo katika tovuti ya TaFF na kuzituma katika

Halmashauri ninayoiongoza ili wachukue hatua...”

Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) alishauri Halmashauri za

wilaya kuhakikisha pesa kwa ajili ya upandaji miti zinalipwa na wafanyabiashara ili kuleta

uendelevu katika upandaji wa miti na biashara ya mazao ya misitu.

Randama ya makubaliano kati ya OR-Tamisemi na Wizara ya Maliasili na Utalii iliwasilishwa

na OR-Tamisemi ili kujenga uelewa wa washiriki kuhusu masuala yaliyokubaliwa. Baadhi ya

wajumbe walikuwa na hofu juu ya utekelezaji wake kwani hakukuwa na ushirikishwaji wa

kutosha. Mtoa mada aliwaweka sawa washiriki kuwa vipengele viliwekwa katika randama hiyo

Page 5: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

vinaakisi changamoto zilizopo na kama kutakuwa na utekelezaji katika ngazi zote mafanikio

yatapatikana.

Pamoja na mawasilisho na mijadala iliyofanyika, wajumbe walikubaliana kuwa changamoto

nyingi zilizojitokeza zilikuwa zinafanana kutoka mkoa mmoja na mwingine. Washiriki walitoa

mapendekezo ya namna ya kubabiliana nazo kwa ujumla wake kupitia michakato na taasisi

zilizopo kwa mujibu wa sheria.

Hapa chini ni baadhi ya changamoto zilizojitokeza kutokana na mawasilisho kutoka mikoani na

mijadala iliyofanyika kama ifuatavyo:-

1. Utekelezaji mdogo wa usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja (JFM)

2. Uwezeshaji mdogo kutoka serikali kuu ikiwemo Halmashauri za wilaya

3. Kukosekana kwa mipango ya usimamzi wa misitu

4. Changamoto ya Mkaa usio-endelevu; vibebeo na usafirishaji

5. Migogoro katika matumizi ya Ardhi; Mifugo, Kilimo na, Misitu

6. Taratibu za upatikanaji wa fedha zaupandaji miti kutoka TaFF; Halmashauri zinahitaji

elimu ya kutosha jinsi ya kupata fedha

7. Uchelewaji wa taarifa kuhusu fedha za upandaji miti kutoka TFS kwendaTaFF

8. Ushirikishwaji mdogo wa wadau katika kuendeleza sekta ya misitu

9. Kuchelewa utekelezaji wa Randama baina ya OR-TAMISEMI na Wizara ya Maliasili na

Utalii kunaongeza migogoro ya kiutendaji ikiwemo upatikanaji wa taarifa; Mashirikiano

hafifu

10. Baadhi ya makusanyo ya upandaji miti kutopelekwaTaFF

CHANGAMOTO NA MAAZIMIO

Page 6: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

Tatizo Kisababishi Maazimio Mhusika

Utekelezajimdogo wa usimamizishirikishi wa misitukwapamoja (JFM)

• Kukosekanakwamsukumo wa kufanikisha JFM kutokakwaSerikalikuu na LGAs

• Misituhusikaitambuliwe na maelekezoyatolewe

MNRT/FBD, PO-RALG

• Ufinyu wa bajeti • Kuhimarishaukusanyaji wa maduhuli na tozo ya fedhazaupandajimiti

RAS/MSM

• Serikalikuipakipaumbelesekta ya misitukatikautoaji wa miongozo ya uandaaji wa bajeti

OR-TAMISEMI, WMU, , Sekretarieti za Mikoa na MSM,

• Ushirikishwaji wa NGOs OR-TAMISEMI, WMU,

• Ushirikianohafifukati ya Watumishi wa TFS na watumishi wa MSM

• Kuharakishautekelezaji wa randama ya makubaliano

OR-TAMISEMI, WMU,, TFS

• Kuundwakwa TFS kuliathirimwendelezo wa jitihadaza JFM/CBFM zilizokuwepochini ya FBD

Ufuatiliajiufanyikekujuahatua ya JFM/CBFM iliyokuwaimefikiwa

OR-TAMISEMI, WMU,, TFS

• Elimundogokwajamiikwenyeuhifadhi wa

Mikakati ya kutoaelimuiandaliwe

MNRT/FBD, PO-RALG, TFS, MSM

Mkaa; vibebeo na usafirishaji (Kipimohalali cha gunia la

Kukosekanakwavibebeomaalumvya TFS

Kuandaavifungashiomaalumkwakilakanda

TFS, OR-TAMISEMI,WMU,

Page 7: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

mkaa)UwezeshwajimdogokutokaserikalikuuikiwemopiaMamlakazaserikalizamitaakukosekanakwamipango ya usimamzi wa misitu

• Ufinyu wa bajeti • Kutambuamisituyotehisiyokuwa na mipango ya usimamizi

TFS, MSM WMU

• Kuhimarishaukusanyaji wa maduhuli na kutengapesakwaajili ya kuandaamipango ya usimamizi

TFS, MSM, TaFF

• Serikalikuipakipaumbelesekta ya misitukatikautoaji wa miongozo ya uandaaji wa bajeti

OR-TAMISEMI, WMU,Sekretarieti za Mikoa, MSM

• Ushirikishwaji wa NGOs TFS, MSM

• Kufanyatathimini ya rasilimalimisitu

TFS, MSM

TaFF – upatikanaji wa fedhazaupandajimiti; halmashaurizinahitajielimu ya kutoshajinsi ya kupatafedha; Uchelewaji wa utoaji wa taarifazafedhazaupandajimitikutoka TFS-TaFF

• Baadhi ya halmashaurihazinauelewawakutoshakuhusuukusanyaji/upatikanaji wa 5% ya fedhazaupandajimiti. Kwa mfano . Kutoifahamuakaunti ya TFS na TaFF

• Mawasilianohafifubaina ya watendaji wa TFS na TaFF

• Kutozingatiautoajiwataarifazafedhakwawakati.

• Elimuitolewekwamamlakazaserikalizamitaa na wadauwenginekuhusuukusanyaji /upatikanaji wa 5% ya fedhazaupandajimiti.

• Kuboreshamawasiliano ya kiutendajikuhusiana na fedhazaupandajimitibaina ya watendaji wa TFS na TaFF.

• Taarifazafedhaziwasilishwekwawakati.

TFS, TaFF, Sekretarieti za Mikoa-, MSM na Mashirika yasiyo ya kiserikali

TFS na TaFF

Migogorokatikamatumizi ya

ardhi; wafugaji, wakulima na

misitu

• Kutokuwanamipango ya matumizi bora ya ardhi.

• Mipaka ya Misitunamaeneo ya Hifadhikutokuwa na

• Kuandaamipango ya matumizi bora ya ardhikwavijijivisivyokuwa na mipango

• Kuwekaalamakatikamipakakwe nyemaeneo ya

MSM, Sekretarieti za Mikoa na Wizara ya Ardhi , Nyumba na

Page 8: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

alama.• Kutofuatamipango

ya matumizi bora ya ardhi.

• Baaadhi ya uandaajiwamipango ya matumizi bora ya ardhikutoshirikishawadau.

• Baadhi ya watendaji wa vijijikutokuwawaadilifu

• Desturizawafugajikutakakuwanaidadikubwa ya mifugobilakuzingatiaubora.

Misitunamaeneoyote ya hifadhi.

• Kuhakikishamipango ya matumizi bora ya ardhiinafuatwa

• Kushirikishawadaumuhimukatikauandaajiwamipango ya matumizi bora ya ardhihasawafugaji.

• Kusimamia na kuwachukuliahatuawatendaji wa vijijiambaosiowaadilifu

• Wafugaji/ wakulimawapeweelimukuhusuufugaji bora wa kisasakwakuzingatiaubora wa mifugoyao na kilimo bora

Makazi , NGO’s

TFS, MSM,

MSM, Sekretarieti za Mikoa, Wizara ya Ardhi.

MSM, Sekretarieti za Mikoa, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi

MSM, Wizara Husika na NGO’s

Ushirikishwajimdogo wa

wadaukatikakuendelezasekta ya

misitu

• Uelewamdogo wa wadau

• 2.Kukosekana kwauratibu, uhusiano na ushirikiano wa pamojakwaWadau

Uhamasishaji wa wadaukupitiasera,sheria,kanuni, miongozonk.

Uwepomfumounaoratibumahusianokati ya Wadau

OR –TAMISEMI na Wizara ya Maliasili na Utalii(TFS na TaFF).

Kuchelewauandaaji wa mpangokazi na kusambazaRandamakatikangazizautekelezaji OR-TAMISEMI na Maliasili na Utalii

• Ukosefu wa Rasilimalifedhakwaajili ya kutoaelimujuu ya Randama.

• RasilimaliFedhaitafutwekwawakatimuafakakabla ya Randamakupitwa na wakati.

OR –TAMISEMI na Wizara ya Maliasili na Utalii(TFS na TaFF).

Mashirikianohafifubaina ya

• KilaTaasisiinaangaliamaslahiyake

• Kuhamasishaushirikianobaina ya Taasisi

OR –TAMISEMI

Page 9: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

watendaji wa Serikali .

• Kufuatasheria, kanunitaratibu na miongozo ya utendajikazi

na Wizara ya Maliasili na Utalii(TFS na TaFF).

Baadhi ya makusanyo ya upandajimitikutopelekwaTaFF

• Kutozingatiasheria na Utaratibu na Miongozo kwabaadhi ya Watendaji wa sekta ya Misitukatikaukusanyaji wa fedhazaupandajimiti

• KutoamaelekezokwaWatendaji.

OR –TAMISEMI na Wizara ya Maliasili na Utalii(TFS na TaFF).

6.0 MAJINA YA WASHIRIKI# JINA CHEO/MAHALI

ATOKAPOSIMU

1. Dr. Ezekiel Mwakalukwa Kaimu Mkurugenzi wa Misitu

0782232381

2. Dr. Tuli Msuya Katibu Tawala, TaFF 07843934143. Stanford Kway Mratibu4. Julius Kiiza OR-Tamisemi 07569186325. Nassoro Mzui Liwale DC 07846177366. Abushiri Mbwana Kilwa DC 07826812167. Eng. Sambo Mahona Rufiji DC 07677172988. Daniel Issara RS Pwani 07881253649. Zawadi Jilala RS Lindi 078860414210. Richard Unambwe Sikonge DC 076749424911. Husna Msagati TFS Hq 071547640812. Mathis Augustine RS Katavi 078688115513. Samwel Gunza DED Lindi 068606160014. Alex Kagunze DED Mlele 075902178815. Margareth Nakaunga Urambo DC 078453205916. Mabula Isambula Kaliua DC 078450492617. Nyassary Goshashy RS Tabora 076533274718. Ramadhani Rajabu OR-Tamisemi 076605503619. Hamisi Chande Mpanda DC 0787843639

Page 10: mamamisitu.commamamisitu.com/.../2016/08/Majadiliano-ya-Randama.docx · Web viewKupokea na kujadili hali halisi ya misitu na biashara ya mazao ya misitu kutoka mikoa ya Lindi, Pwani,

20. Ojuku Siminda Nachingwea DC 071407169721. Hassani Sengerere RBO 065752450122. Sophia Masuka TNRF 075440977623. Gwamaka Mwakyanjala TNRF 0767260010