misitu, utawala bora na maendeleo ya taifamuhtasari matokeo ya utafiti wa masuala ya misitu...

4
Andiko la Kisera AGOSTI 2016 Muhtasari Matokeo ya utafiti wa masuala ya misitu uliyofanyika kusini mwa Tanzania kabla ya mwaka 2006, yaani “Misitu, Utawala bora na na Maendeleo ya Taifa: Mafunzo yaliyotokana na Uvunaji Holela wa Magogo Kusini mwa Tanzania” yalichapishwa mwaka 2007 na kujulikana kama Ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007. Ripoti hii ilibaini kwamba sekta ya misitu ilikumbwa na udhibiti hafifu na usioendelevu. Baada ya kupokewa kwa ripoti hiyo ya TRAFFIC ya mwaka 2007, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya misitu ambayo pia yameleta uzoefu mpya, changamoto na mambo ya kujifunza. Baadhi ya mabadiliko haya ni pamoja na kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, kuongezeka kwa uwekezaji sekta ya misitu kama vile mashamba ya kupanda ya miti na Misitu ya jamii. Kuongezeka kwa mahitaji ya mbao kumelazimu uwepo wa juhudi zinazovuka mipaka za kukabiliana na biashara haramu ya mbao, ushiriki wa sekta binafsi na uimarishaji wa mijadala kuhusu utawala bora wa Misitu kati ya serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Vivyo hivyo tumeshuhudia misaada mbalimbali kutoka kwa washirika wa maendeleo katika utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu na uwezeshaji wa jamii kupitia Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa itokanayo na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) pamoja na umiliki wa misitu binafsi. Utangulizi Mwaka 2008, Kikundi Kazi cha Misitu Tanzania kilizindua awamu ya majaribio ya Kampeni ya Mama Misitu kama mwitikio wa ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007. Mama Misitu ni kampeni ya mawasiliano na uchechemuzi ya miaka mitano (2012-2016) yenye lengo la kuboresha utawala katika sekta ya misitu ili kunufaisha wananchi. Ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 iliorodhesha jumla ya mapendekezo 60, yaliyogawanwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mifumo ya uwajibikaji; usimamizi wa rasilimali watu; mapato ya kiuchumi au kifedha; udhibiti; na usimamizi wa misitu. Pamoja na mapendekezo hayo makini, utafiti wa ufuatiliaji kupitia Kampeni ya Mama Misitu uliongozwa na hadidu za rejea zilizotoa kipaumbele kwa masuala ambayo yalikuwa kipimo cha maendeleo ya utekelezaji wa mapendekezo. Lengo kuu la ufuatiliaji lilikuwa kupata ushahidi kwa kupitia kiwango cha utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 kuhusu biashara ya mbao na maendeleo ya taifa. Utafiti huu ulijielekeza katika masuala matano muhimu ili kubaini iwapo mafanikio yamepatikana katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyoibuliwa. Uwazi umeongezeka, hasa kwa upande wa miongozo na matangazo ya serikali. Mwaka 2007 mwongozo muhimu wa uvunaji wa msitu na biashara ya mbao ulitolewa katika lugha ya Kiswahili na kusambazwa nchini kote. Uhusiano kati ya Wakala wa Huduma za Misitu na Serikali za Mitaa siyo mzuri kwani Maafisa Misitu kadhaa kutoka Wilayani wanadai kuwa ushiriki wao katika kupanga bajeti ni wa ili mradi tu (tokenism). Uzoefu kutoka mahali pengine, ikiwa ni pamoja na Cameroon na Asia ya Mashariki, umeonyesha kuwa matumizi ya Ufuatiliaji Huru wa masuala yanayohusu misitu unaruhusu uwepo wa tathimini sahihi na zenye ufanisi. Pamoja na mwelekeo mzuri wa ukusanyaji wa mapato, bado mwelekeo huo unaonesha upungufu wa zaidi ya nusu ya kile kinachokusanywa. Hata hivyo, mbinu ya makusanyo inayotumiwa na Wakala wa Misitu, bado imejielekeza katika uwekaji wa malengo ya makisio ya chini bila kuweka makisio ya juu, na hii inaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa misitu. Rasilimali kidogo sana zimetengwa katika mpango kazi wa Wakala wa Misitu Tanzania kusaidia Usimamizi Shirikishi wa Misitu kwa Pamoja (JFM), ingawa nyenzo hii inawezesha ulinzi wa misitu ya hifadhi ya serikali kuu. Ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 ilibainisha jinsi Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayojihusisha na shughuli za uhifadhi wa mazingira yalivyokuwa nyuma katika ushiriki wa masuala ya utawala bora wa misitu. Tangu mwaka 2007, mashirika hayo yameendelea kujihusisha katika kukuza na kuboresha utawala wa misitu kwa niaba ya jamii. Ujumbe Muhimu Misitu, Utawala bora na Maendeleo ya Taifa Kutafakari tena mapendekezo ya kuboresha utawala wa misitu nchini Tanzania yaliyotolewa na shirika la TRAFFIC kwenye ripoti ya mwaka 2007

Upload: others

Post on 01-Mar-2020

12 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Misitu, Utawala bora na Maendeleo ya TaifaMuhtasari Matokeo ya utafiti wa masuala ya misitu uliyofanyika kusini mwa Tanzania kabla ya mwaka 2006, yaani “Misitu, Utawala bora na na

Andiko la Kisera

AGOSTI 2016

MuhtasariMatokeo ya utafiti wa masuala ya misitu uliyofanyika kusini mwa Tanzania kabla ya mwaka 2006, yaani “Misitu, Utawala bora na na Maendeleo ya Taifa: Mafunzo yaliyotokana na Uvunaji Holela wa Magogo Kusini mwa Tanzania” yalichapishwa mwaka 2007 na kujulikana kama Ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007. Ripoti hii ilibaini kwamba sekta ya misitu ilikumbwa na udhibiti hafifu na usioendelevu. Baada ya kupokewa kwa ripoti hiyo ya TRAFFIC ya mwaka 2007, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya misitu ambayo pia yameleta uzoefu mpya, changamoto na mambo ya kujifunza. Baadhi ya mabadiliko haya ni pamoja na kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, kuongezeka kwa uwekezaji sekta ya misitu kama vile mashamba ya kupanda ya miti na Misitu ya jamii. Kuongezeka kwa mahitaji ya mbao kumelazimu uwepo wa juhudi zinazovuka mipaka za kukabiliana na biashara haramu ya mbao, ushiriki wa sekta binafsi na uimarishaji wa mijadala kuhusu utawala bora wa Misitu kati ya serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Vivyo hivyo tumeshuhudia misaada mbalimbali kutoka kwa washirika wa maendeleo katika utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu na uwezeshaji wa jamii kupitia Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa itokanayo na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) pamoja na umiliki wa misitu binafsi.

UtanguliziMwaka 2008, Kikundi Kazi cha Misitu Tanzania kilizindua awamu ya majaribio ya Kampeni ya Mama Misitu kama mwitikio wa ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007. Mama Misitu ni kampeni ya mawasiliano na uchechemuzi ya miaka mitano (2012-2016) yenye lengo la kuboresha utawala katika sekta ya misitu ili kunufaisha wananchi. Ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 iliorodhesha jumla ya mapendekezo 60, yaliyogawanwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mifumo ya uwajibikaji; usimamizi wa rasilimali watu; mapato ya kiuchumi au kifedha; udhibiti; na usimamizi wa misitu. Pamoja na mapendekezo hayo makini, utafiti wa ufuatiliaji kupitia Kampeni ya Mama Misitu uliongozwa na hadidu za rejea zilizotoa kipaumbele kwa masuala ambayo yalikuwa kipimo cha maendeleo ya utekelezaji wa mapendekezo. Lengo kuu la ufuatiliaji lilikuwa kupata ushahidi kwa kupitia kiwango cha utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 kuhusu biashara ya mbao na maendeleo ya taifa. Utafiti huu ulijielekeza katika masuala matano muhimu ili kubaini iwapo mafanikio yamepatikana katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyoibuliwa.

� Uwazi umeongezeka, hasa kwa upande wa miongozo na matangazo ya serikali. Mwaka 2007 mwongozo muhimu wa uvunaji wa msitu na biashara ya mbao ulitolewa katika lugha ya Kiswahili na kusambazwa nchini kote.

� Uhusiano kati ya Wakala wa Huduma za Misitu na Serikali za Mitaa siyo mzuri kwani Maafisa Misitu kadhaa kutoka Wilayani wanadai kuwa ushiriki wao katika kupanga bajeti ni wa ili mradi tu (tokenism).

� Uzoefu kutoka mahali pengine, ikiwa ni pamoja na Cameroon na Asia ya Mashariki, umeonyesha kuwa matumizi ya Ufuatiliaji Huru wa masuala yanayohusu misitu unaruhusu uwepo wa tathimini sahihi na zenye ufanisi.

� Pamoja na mwelekeo mzuri wa ukusanyaji wa mapato, bado mwelekeo huo unaonesha upungufu wa zaidi ya nusu ya kile kinachokusanywa. Hata hivyo, mbinu ya makusanyo inayotumiwa na Wakala wa Misitu, bado imejielekeza katika uwekaji wa malengo ya makisio ya chini bila kuweka makisio ya juu, na hii inaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa misitu.

� Rasilimali kidogo sana zimetengwa katika mpango kazi wa Wakala wa Misitu Tanzania kusaidia Usimamizi Shirikishi wa Misitu kwa Pamoja (JFM), ingawa nyenzo hii inawezesha ulinzi wa misitu ya hifadhi ya serikali kuu.

� Ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 ilibainisha jinsi Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayojihusisha na shughuli za uhifadhi wa mazingira yalivyokuwa nyuma katika ushiriki wa masuala ya utawala bora wa misitu. Tangu mwaka 2007, mashirika hayo yameendelea kujihusisha katika kukuza na kuboresha utawala wa misitu kwa niaba ya jamii.

Ujumbe Muhimu

Misitu, Utawala bora na Maendeleo ya TaifaKutafakari tena mapendekezo ya kuboresha utawala wa misitu nchini Tanzania yaliyotolewa na shirika la TRAFFIC kwenye ripoti ya mwaka 2007

Page 2: Misitu, Utawala bora na Maendeleo ya TaifaMuhtasari Matokeo ya utafiti wa masuala ya misitu uliyofanyika kusini mwa Tanzania kabla ya mwaka 2006, yaani “Misitu, Utawala bora na na

Suala la 1: Taarifa za Wizara ya Maliasili na Utalii zina mapungufu, mashaka katika usahihi na zisizo chunguzwa kila mara na viongozi waandamizi, hali ambayo inaweza kusababisha kutokugundulika kwa vitendo mbalimbali visivyo ya kawaida.Ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 ililiweka suala la usimamizi wa taarifa na ufuatiliaji katika mazingira ya uwajibikaji na uwajibishwaji wa mamlaka zinazohusika na misitu nchini. Ripoti ilisema yafuatayo;

i. Mkazo juu ya ukukusanyaji wa takwimu muhimu za magogo na biashara ya mbao katika ngazi ya taifa, ulipungua katika kipindi cha miaka kabla ya 2006, kutokana na kuwepo kwa vipaumbele vingine ndani ya Wizara.

ii. Hakukuwa tu na mapengo katika taarifa, bali usahihi wa taarifa zenyewe ulikuwa wa kutiliwa mashaka sana, na ukiacha taarifa za mapato, uchunguzi na/au uchambuzi haukufanywa kabisa na viongozi waandamizi.

Faida ya ripoti ya TRAFFIC kwa muktadha huu ni kuwa imesababisha mamlaka za misitu Tanzania kufanya maboresho yanayostahili kupongezwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na;

� Mabadiliko muhimu zaidi kufanywa tangu mwaka 2007 ni uanzishwaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mwaka 2010.

� Utoaji taarifa umesanifiwa na unazingatia Mfumo wa serikali wa vipindi vya Muda wa Kati wa Matumizi.

� Mfumo wa utoaji taarifa umefungamanishwa na taarifa kutoka ofisi ya misitu katika halmashauri ya wilaya kwenda kwa Mameneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika ngazi ya wilaya, kabla ya kupeleka kwa Mameneja wa Kanda na hatimaye Makao Makuu ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

Pamoja na maboresho hayo bado kuna ukosefu wa uchunguzi na uchambuzi wa takwimu kuhusu ujazo na aina ya miti ya mbao zilizo katika biashara, ugumu wa kupata taarifa ya kiasi gani cha mbao zilizochangia mapato kwa ujumla na kiasi gani cha mapato kimetokana na misitu ya hifadhi ya asili, misitu katika maeneo ya wazi yanayomilikiwa na vijiji (Matajiwazi) na mashamba ya kupanda ya misitu. Cha kushangaza zaidi ni kwamba mchango wa mapato kutokana na mkaa, mbao kutoka misitu ya asili na mashamba makubwa ya miti haujulikani. Ratiba za utoaji wa taarifa hazizingatiwi ingawa taarifa zinapatikana kwenye Stakabadhi za serikali na leseni ya uvunaji zinatolewa katika ngazi ya wilaya.

Suala la 2: Kiwango cha chini cha uwazi wa taarifa na maamuzi huongeza hatari ya rushwa inayotokana na urasimu. Ripoti ya TRAFFIC iligundua kuwa katika miaka ya karibu na 2006 umma ulikuwa haujapata taarifa juu ya marufuku ya uvunaji, ingawa maamuzi ya usimamizi yaliyokuwa ya umuhimu mkubwa kwa umma yaliendelea kufanyika. Nyenzo mbalimbali za kuongeza uwazi zilipendekezwa, ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo ya biashara ya mbao kwa sekta binafsi ambayo ingewekwa hadharani; kufanya mikutano ya wadau mbalimbali; na kubandika taarifa kwenye mbao za matangazo.

Matokeo: Uwazi umeongezeka, hasa kwa upande wa miongozo na

matangazo ya serikali. Mwaka 2007 mwongozo muhimu wa uvunaji wa msitu na biashara ya mbao ulitolewa katika lugha ya Kiswahili na kusambazwa nchini kote. Miongozo hii ilitolewa kupitia vitini na vipeperushi na kusambazwa katika ofisi za misitu wilayani. Tangu kipindi hicho, matangazo ya Serikali hayajasambazwa tena kwa wingi. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umekuwa ukiwashirikisha watumishi wa Halmashauri za wilaya katika mikutano ya kupanga bajeti, hata hivyo, uhusiano kati ya Wakala wa Huduma za Misitu na Serikali za Mitaa siyo mzuri kwani Maafisa Misitu kadhaa kutoka Wilayani wanadai kuwa ushiriki wao katika kupanga bajeti ni wa ili mradi tu (tokenism). Mikutano ya kupanga bajeti imekuwa ikijadili malengo ya ukusanyaji mapato kuliko matumizi na uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu katika wilaya. Hakika mipango ya uvunaji na malengo ya kiwango cha chini cha mapato imeendelea kupangwa kwa makadirio ya macho tu badala ya kufanya uhakiki wa kina wa idadi ya miti iliyotayari kuvunwa.

Suala la 3: Ufuatiliaji wa Serikali wa shughuli za misitu wakati mwingine siyo sahihi au hufanya kwa upendeleo. Katika hali mahsusi, ufuatiliaji huru wa masuala yanayohusu misitu unatafsiriwa na Shirika la Global Witness kama “matumizi ya mtu huru kwa makubaliano na mamlaka ya serikali, kutoa tathmini ya utekelezaji wa sheria, na kutazama na kutoa mwongozo kuhusu mifumo rasmi ya utekelezaji wa sheria za misitu” inaweza kuwa chombo muhimu katika kuboresha utawala wa misitu na utekelezaji wa sheria (Global Witness, 2005). Ufuatiliaji Huru wa masuala ya misitu pia unajulikana kama Ufuatiliaji Huru wa Sheria za Misitu na Utawala na mara nyingi hutumika kama mkakati wa haraka na wa muda mfupi. Chini ya Ufuatiliaji Huru wa Sheria za Misitu na Utawala, ufuatiliaji wa kila siku wa uhalali wa shughuli zinazohusu misitu unatoa tathmini ya ufanisi zaidi katika utekelezaji, wakati huo taarifa inayotokana na ufuatiliaji pamoja na ushiriki wa wadau mbalimbali unaweza kuimarisha utekelezaji. Zaidi ya hayo, Ufuatilaji Huru wa masuala yanayohusu misitu unaweza kuboresha uwajibikaji, kwanza kwa kuimarisha taratibu zilizopo za ufuatiliaji na udhibiti wa taratibu za serikali, na pili kuhakikisha ushiriki wa mashirika ya kiraia, vyombo vya habari na sekta binafsi (TNRF, 2009).

Uzoefu kutoka mahali pengine, ikiwa ni pamoja na Cameroon na Asia ya Mashariki, umeonyesha kuwa matumizi ya Ufuatiliaji Huru wa masuala yanayohusu misitu unaruhusu uwepo wa tathimini sahihi na zenye ufanisi. Mwaka 2005, Waziri mwenye dhamana na misitu alikutana na wabia wa maendeleo ambapo Ufuatiliaji Huru wa masuala yanayohusu misitu ulipendekezwa. Tafiti za kuangalia uwezekano wa utekelezaji wa Ufuatiliaji Huru wa masuala ya misitu ulifanyika mwaka 2006 na 2008, na tafiti zote mbili zilihitimisha kuwa mazingira yanaruhusu utekelezaji wa Ufuatiliaji Huru wa masuala ya misitu nchini Tanzania. Hata hivyo Mwaka 2009, na baadae mwaka 2015, Waziri wa Maliasili na Utalii, licha ya kukiri kwamba Ufuatiliaji Huru wa masuala ya misitu unaweza kuwa na manufaa kwa Tanzania, lakini walisema kwamba wakati huu si muafaka kwa Ufuatiliaji Huru wa masuala yanayohusu misitu kuanzishwa.

Suala 4: Maendeleo duni katika kuongeza mapato kwa kutumia njia mbalimbali, na uwezo mdogo katika ngazi zote.Ripoti ya TRAFFIC iliainisha idadi ndogo ya watumishi, na wengi wakikaribia kustaafu, nafasi chache za ajira, kama sababu muhimu inayoathiri utendaji katika sekta ya misitu kwa serikali kuu na

Matokeo na mambo tuliyojifunza

Page 3: Misitu, Utawala bora na Maendeleo ya TaifaMuhtasari Matokeo ya utafiti wa masuala ya misitu uliyofanyika kusini mwa Tanzania kabla ya mwaka 2006, yaani “Misitu, Utawala bora na na

serikali za mitaa. Kwa kulinganisha na maeneo mengine ya nchi, watumishi wachache wako magharibi na kusini mwa Tanzania, na hakuna motisha wa kuvutia waajiriwa wapya hivi karibuni. Kutokana na idadi ndogo ya watumishi, maofisa wengi wa misitu walipewa kazi nyingi za kiutawala na kiufundi kwa wilaya nzima, ikiwa ni pamoja utoaji wa leseni za uvunaji, ukusanyaji wa mapato, ugongaji nyundo katika mbao, ukaguzi na kuendesha doria, na kutoa taarifa za kiutawala miongoni mwa kazi nyingine. Mbali na migongano na hatari zinazoweza kutokana na shughuli hizo nyingi na tofauti, ilikuwa, haiwezekani kabisa kufanya kazi zote kwa kiwango cha kuridhisha. Kama ilivyotarajiwa, ukusanyaji wa mapato ulipewa kipaumbele zaidi ya majukumu mengineyo (TRAFFIC, 2007).

Katika miaka michache iliyopita kumekuwapo na ongezeko la kuridhisha la ajira kwa watumishii wa misitu Kanda ya Kusini, na nchini kote. Pamoja na ongezeko la wafanyakazi, changamoto zinazoikabili Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni ukosefu wa vitendea kazi vya kutosha pamoja na magari. Ingawa kila wilaya katika ukanda wa kusini wamepokea pikipiki, magari yalionekana kuwa machakavu na ghali zaidi kuyaendesha, pia boti za doria nazo hazikuwa tena katika hali inayofaa, hivyo kuacha njia ya bahari kuwa wazi kwa wafanyabiashara ya magendo. Mapato yaliyokusanywa na Wakala wa Misitu Tanzania yameongezeka kwa ujumla kwa asilimia 40 katika kipindi cha miaka 4 iliyopita na hasa kwa asilimia 25 kutoka katika Shamba la Miti la Sao Hill katika kipindi hicho hicho. Pamoja na mwelekeo mzuri wa ukusanyaji wa mapato, bado mwelekeo huo unaonesha upungufu wa zaidi ya nusu ya kile kinachokusanywa. Hata hivyo, mbinu ya makusanyo inayotumiwa na Wakala wa Misitu, bado imejielekeza katika uwekaji wa malengo ya makisio ya chini bila kuweka makisio ya juu, na hii inaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa misitu.

Mapato yanayobaki kwa Wakala wa Misitu Tanzania baada ya makusanyo yanakwenda sambamba na kuongezeka kwa makusanyo ya mapato, hasa tangu mwaka 2011. Mwaka 2014, asilimia 65 ya mapato yaliyokusanywa yalibaki Wakala wa Misitu, na kiasi kilichobaki kilikwenda kwa Mfuko wa Taifa wa Misitu (TaFF) na Hazina. Mkakati wa sasa wa Wakala wa Misitu Tanzania ni kuwekeza katika mashamba ya kupanda miti na uwekaji wa mipaka misitu ya asili, hali ambayo imesababisha kupungua kwa mgao wa wa uwekezaji katika usimamizi wa misitu ya asili ya jamii. Wakala wa Misitu Tanzania inatambua kuwa vijiji vinazidi kuchagua Usimamizi Shirikishi wa misitu wa Jamii ili kudhibiti rasilimali za Misitu katika ardhi za vijiji, na hii imesababisha kuongezeka kwa udhibiti katika hifadhi za misitu ya serikali na mashamba makubwa ya kupandwa ya miti. Rasilimali kidogo sana zimetengwa katika mpango kazi wa Wakala wa Misitu Tanzania kusaidia Usimamizi Shirikishi wa Misitu kwa Pamoja (JFM), ingawa nyenzo hii inawezesha ulinzi wa misitu ya hifadhi ya serikali kuu. Sekta binafsi inaonekana kukatishwa tamaa. Wafanyabiashara wamekuwa na masikitiko namna ambavyo misitu ya asili inasimamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania na wanahitaji kuhakikishiwa uhakika wa malighafi, ili kuendelea kulipa mirahaba na kufanya uwekezaji katika kuongeza thamani ya mazao ya misitu.

Suala la 5: Changamoto ya kuhakikisha uoanishaji wa majukumu, vipaumbele na mahusiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na TAMISEMI umeendelea kuathiri usimamizi wa misitu.Ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 ilisema kumekuwa na uratibu hafifu wa majukumu kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na TAMISEMI na hivyo kuathiri mipango, ukusanyaji wa mapato, udhibiti na nidhamu.

Waandishi wa ripoti hiyo walipendekeza kuwapo kwa Mkataba wa Makubaliano (MoU), utakaofafanua majukumu na kusainiwa na wizara hizo husika. Pia ilipendekeza kuwa maafisa wa serikali kuu na serikali za mitaa washiriki katika utengenezaji wa mpango mikakati. Ripoti hiyo pia ilitaka uanzishwaji wa Kamati ya Taifa ya Ushauri kuhusu Misitu ambayo imetajwa katika sheria ya Misitu ya mwaka 2002 ili kuimarisha na kuratibu sekta hizo mtambuka.

Kwa sasa ipo miongozo inayoelekeza wajibu na majukumu ya maafisa misitu wa serikali za mitaa na serikali kuu. Hata hivyo, ukweli ni kwamba serikali za mitaa hazitoi msaada wa kifedha kusaidia usimamizi wa Misitu, na hivyo kuathiri ufanisi katika ufuatiliaji na udhibiti. Kwa sasa, uandikaji wa mipango mkakati ya Wakala wa Misitu Tanzania szinafanyika kwa utaratibu na kwa wakati, hata hivyo baadhi ya wadau wanadai kuwa utengenezaji wa mikakati hiyo siyo shirikishi. Mkataba wa Makubaliano ulisainiwa Mei 2016 unafafanua majukumu ya usimamizi wa misitu kati ya ngazi mbalimbali za serikali, lakini hauzungumzii namna ambavyo mapato yanaweza kugawanywa, makubaliano hayo hayajasambazwa kwa wadau na si mkataba kisheria.

Ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 ilibainisha jinsi Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayojihusisha na shughuli za uhifadhi wa mazingira yalivyokuwa nyuma katika ushiriki wa masuala ya utawala bora wa misitu. Tangu mwaka 2007, mashirika hayo yameendelea kujihusisha katika kukuza na kuboresha utawala wa misitu kwa niaba ya jamii. Kamati ya Taifa ya Ushauri kuhusu Misitu (FAC) imekuwepo lakini tangu mwaka 2012 haijafanya mikutano. Sheria ya misitu inataka Kamati hiyo itoe ripoti ya mwaka, ambayo itakuwa ya wazi kwa jamii. Hata hivyo, ripoti hiyo haijawahi kutolewa kwa jamii. Utafiti wa Mamlaka ya Mapato (TRA) ulipendekeza kwamba kikosi kazi cha pamoja cha Wakala wa Misitu na Mamlaka ya Mapato kianzishwe ili kushirikiana katika ukusanyaji wa mapato. Cha kusikitisha, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania haijakuwa na utayari wa kutoa taarifa za utambulisho wa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo ingeweza kusaidia ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa walipa kodi.

Page 4: Misitu, Utawala bora na Maendeleo ya TaifaMuhtasari Matokeo ya utafiti wa masuala ya misitu uliyofanyika kusini mwa Tanzania kabla ya mwaka 2006, yaani “Misitu, Utawala bora na na

Suala 1: Taarifa za Wakala wa Misitu Tanzania zina mapungufu, mashaka katika usahihi, zisizochunguzwa kila mara na viongozi waandamizi.

� Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania atengeneze kanzidata yake kwa ajili ya kuchambua takwimu zinazokusanywa;

� Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania afanye tathimini ya misitu kila baada ya miaka mitano kwa ajili ya misitu ya taifa, mameneja wa hifadhi za misitu nao wafanye tathmini kwa Misitu yao husika na Misitu ya wazi/jumla nayo ifanyiwe tathmini; na

� Uvunaji ufanyike tu katika maeneo ambayo mipango ya usimamizi imetengenezwa, kwa kuzingatia Mavuno Yaliyoruhusiwa kwa Mwaka.

Suala 2: Kiwango cha chini cha uwazi wa taarifa na maamuzi huongeza hatari ya rushwa inayotokana na urasimu

� Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kuhakikisha taarifa zote muhimu zinatolewa kwa uwazi na kwa wakati;

� Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kuandaa miongozo inayoainisha taarifa watakazopewa Maafisa Misitu wa Wilaya katika mikutano ya kanda ya kupanga mikakati, ikiwa ni pamoja na kanuni kwa ajili ya kukokotoa mavuno halali ya mwaka kwa kuzingatia kiwango cha chini na cha juu cha malengo ya mapato; na,

� Mavuno halali ya mwaka, mipango ya uvunaji na malengo ya ukusanyaji mapato ya kanda yetengenezwe kutokana katika tathimini ya kina ya msitu.

Suala la 3: Ufuatiliaji wa Serikali wa shughuli za misitu

� Mchakato wa Ufuatiliaji Huru wa masuala yanayohusu sheria za misitu uanzishwe nchini kwa lengo la kupata tathimini sahihi ya utekelezaji wa sheria.

Suala 4: Uwezo mdogo wa ukusanyaji wa mapato

� Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania inunue vitendea kazi na magari, ununuzi wa vifaa vya kitengo cha baharini upewe kipaumbele/umuhimu;

� Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania haupaswi kuweka malengo ya chini ya mapato bila uwepo wa malengo ya juu ya ukusanyaji;

� Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania itenge rasilimali zaidi kwa usimamizi misitu ya asili pamoja na kuongeza rasilimali zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu kwa Pamoja na,

� Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania itengeneze mwongozo wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika usimamizi wa misitu.

Suala la 5: Uoanishaji wa majukumu kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na TAMISEMI

� Wizara ya Maliasili na Utalii na TAMISEMI wautafsiri Mkataba wa Makubaliano kwa Kiswahili na kuusambaza katika wilaya zote.

� Utengenezaji wa Mipango Mkakati ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania inapasa kushirikisha jamii na asasi za kiraia

� Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Misitu ifufuliwe ili kushughulikia masuala ya dharura na kufuatiliwa kuona kamati hiyo inakutana mara kwa mara. Mihutasari ya vikao vya kamati ya ushauri pia iwekwe wazi.

© Kampeni ya Mama Misitu – 2016

Mapendekezo ya Kisera

Imefadhiliwa na:

Kampeni ya Mama Misitu, Namba 27 Mtaa wa Sangara - Mikocheni, Dar es Salaam.Tovuti: www.mamamisitu.com | Barua pepe: [email protected] | Simu: +255 758828398

Facebook: www.facebook.com/mamamisitu | Twitter: www.twitter.com/mamamisitu