web viewmwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia wilaya ya hai na kupangiwa kituo cha kazi...

14
HISTORIA YA MAISHA YANGU. Mimi ninaitwa Benedicta Baltazari Swai. Nina umri wa miaka arobaini na nne, nilizaliwa tarehe 10/10/1972 katika hospitali ya Huruma iliyoko Wilaya ya Rombo. Wazazi wangu wanaishi katika kijiji cha Shimbi Mashariki katika Kata ya Shidehere Tarafa ya mkuu. Nilipokuwa na umri wa miaka saba nilipata tatizo la kuugua macho kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Wazazi wangu waliteseka na mimi sana hawakujua kama ningepona hivyo, walinipeleka hospitali mbalimbali kwa matibabu. Madaktari waliposhindwa kunitibu wazazi wangu waliamua kunipeleka kwa waganga wa kienyeji ili kunitibu tatizo langu waliahangaika na mimi sana. Mwisho Mungu aliniponya wakamshukuru sana Mungu kwa macho yangu kupona. Mwaka 1981 nilianza elimu ya msingi katika shule ya msingi Kirokomu iliyoko Tarafa ya mkuu Rombo niliendelea na masomo vizuri. Siku moja nilipokuwa darasa la sita tulipokuwa tunacheza kwa bahati mbaya nilianguka na kuvunjika mkono wangu wa kulia nikapelekwa hosipatalini kwa matibabu. Nilipata shida sana wakati wa masomo kwa kushindwa kuandika na mkono wa kushoto. Baada ya miezi mitatu nilipona nikaendelea vizuri na masomo na kuhitimu elimu ya msingi mwaka 1988. Badaye baba alinichukula fomu yakujinga na elimu ya sekondari nikaijaza na kuchaguliwa na kuanza mafunzo hayo mwaka 1989 katika shule ya

Upload: buithuy

Post on 13-Mar-2018

346 views

Category:

Documents


13 download

TRANSCRIPT

Page 1: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

HISTORIA YA MAISHA YANGU.

Mimi ninaitwa Benedicta Baltazari Swai. Nina umri wa miaka arobaini na nne, nilizaliwa

tarehe 10/10/1972 katika hospitali ya Huruma iliyoko Wilaya ya Rombo. Wazazi wangu

wanaishi katika kijiji cha Shimbi Mashariki katika Kata ya Shidehere Tarafa ya mkuu.

Nilipokuwa na umri wa miaka saba nilipata tatizo la kuugua macho kwa muda wa mwaka

mmoja na nusu. Wazazi wangu waliteseka na mimi sana hawakujua kama ningepona hivyo,

walinipeleka hospitali mbalimbali kwa matibabu. Madaktari waliposhindwa kunitibu wazazi

wangu waliamua kunipeleka kwa waganga wa kienyeji ili kunitibu tatizo langu waliahangaika

na mimi sana. Mwisho Mungu aliniponya wakamshukuru sana Mungu kwa macho yangu

kupona.

Mwaka 1981 nilianza elimu ya msingi katika shule ya msingi Kirokomu iliyoko Tarafa ya

mkuu Rombo niliendelea na masomo vizuri. Siku moja nilipokuwa darasa la sita tulipokuwa

tunacheza kwa bahati mbaya nilianguka na kuvunjika mkono wangu wa kulia nikapelekwa

hosipatalini kwa matibabu. Nilipata shida sana wakati wa masomo kwa kushindwa kuandika na

mkono wa kushoto. Baada ya miezi mitatu nilipona nikaendelea vizuri na masomo na kuhitimu

elimu ya msingi mwaka 1988. Badaye baba alinichukula fomu yakujinga na elimu ya sekondari

nikaijaza na kuchaguliwa na kuanza mafunzo hayo mwaka 1989 katika shule ya sekondari

Ibukoni. Niliendele na masomo vizuri shule yetu ilikuwa ni ya kutwa nilitembea kilometa tano

kutoka nyumbani hadi shuleni kwa muda wa miaka miwili baadaye ilikuwa na majengo ya

kulala wanafunzi nikaamua kuhamia. Niliendele vizuri na masomo, Siku moja wanafunzi

walifanya vurugu mbaya sana wakapiga nyumba za walimu kwa mawe, asubuhi yake tuliitwa

wote tulioko mabwenini na kupewa adhabu kali sana kisha tukaambiwa tuende nyumbani

tukawaite wazazi wetu. Wazazi walipokuja walimu waliita kamati ya bodi ya shule wakakaa

kikao kwa ajili ya kuzungumza tatizo hilo hatimaye kikao kiliamua shule ibaki ya kutwa.

Niliendelea na masomo vizuri na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1992

Page 2: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

. Kwa bahati nzuri matokeo yalipotoka nilifaulu vizuri bali kutokana na shule yetu ilikuwa haija

sajiliwa siku bahatika kuendelea na masomo .

Page 3: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

Hivyo, niliamua kuendelea na shughuli zangu za nyumbani, baadaye nilisika tangazo katika

vyombo vya habari kuwa kuna nafasi ya kujiunga na kozi ya ufundi na ukarani katika chuo cha

Moshi Community Centre. Niliposikia tangazo hilo nilichukuwa fomu ya maombi na kujaza

na kuituma baadaye nilichaguliwa kujiunga na kozi hiyo kwa miaka miwili. Nilianza mwaka

1994 hadi mwaka 1995 masomo niliyojifunza ni ushonaji, biashara, Kingereza, ofisi praktisi,

uchapishaji na Kifaransa. Nilihitimu tarehe 28/11/1995

Page 4: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

.

Nilibahatika kuajiriwa katika kazi ya Ukarani na kupokea hela katika kiwanda cha mashine

yakukoboa na kusaga iliyoko mjini Moshi maeneo ya Mbuyuni Ostabey kwa tajiri yangu

aliyekua anaitwa Michael Mashele anayeishi jirani na mashine ya Mzee Gogo. Nilifanya kazi hii

kwa muda wa miaka miwili kuanzia mwaka 1996 mwezi wa kwanza hadi mwaka 1998 mwezi

wa kwanza. Siku moja tulishindwa kuelewana na tajiri yangu aliye niajiri baada ya kutembelewa

na ndugu yangu anayeitwa Marietha alikua na shida nimpeleke kwa dada yetu anayeitwa Topista

aliyeolewa Kibosho Umbwe, kwani alikua ana mazungumzo naye. Nilimuomba tajiri yangu

ruhusa ili nimpeleke Kibosho kwani alikua ni mgeni kwa mazingira ya Moshi hivyo, haikua

rahisi kwenda mwenyewe na tajiri yangu hakukubali ndipo nikaamua kuondoka bila ruhusa,

niliporudi tajiri yangu hakuniruhusu kuendelea na kazi. Nilijitahidi kumuomba msamaha

ikashindikana lakini mke wake aliniomba nikae kwake ili kufanya shughuli za nyumbani

akaniahidi kunilipa mshahara wa shilingi elfu kumi kwa muda wa miezi mitano.

Page 5: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

Mwezi wa kumi na mbili mwaka 1998 niliondoka baada ya kupata kazi kwa mama mmoja

Mzambia aitwae Mujanja, aliyeishi katika jiji la Arusha mtaa wa Kijenge eneo linaloitwa

Oloriani. Aliniahidi kunilipa mshahara wa shilingi elfu thelathini kwa mwezi mmoja. Shughuli

nilizokua ninazifanya ni kazi za ndani, na kuwalea watoto wake wawili wa kike. Mmoja jina lake

ni Twambo mwenye umri wa miaka 12 na wapili jina lake ni Nikay mwenye umri wa miaka tisa.

Watoto hawa hawakunipenda, kwani walinidharau sana, lakini mimi nilivumilia na kujitahidi

Page 6: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

kuwaonyesha upendo wa dhati kwa lengo la kumtumikia kafiri ili nipate ujira wangu. Baada ya

muda wa mwaka mmoja nilishindwa kuendelea kuvumilia ndipo nilipo amua kuacha kazi na

kurudi Moshi kwa rafiki yangu Pelagia aliyekuwa anafanya kazi kwa mama Klementine

Foundation.

Mwaka 1999 mwezi wa kwanza nilipata kazi ya Ukarani kwenye Hoteli ya Pan Afrika na

mshahara wake ulikuwa wa shilingi elfu ishirini kwa mwezi mmoja. Bali nilifanya kazi bila

kulipwa mshahara inavyostahili, na badala yake alinilipa robo au nusu ya mshahara na wakati

mwingine kutokunilipa kabisa. Nilipoendelea na kazi ndani ya miezi sita bila malipo yoyote

niliamua kuacha kazi. Niliendelea kuishi kwa rafiki yangu anayeitwa Pelagia. Siku moja nilisikia

matangazo ya mkutano wa Injili uliokua unafanyika katika Kanisa la Tanzania Assemblies of

God la Amani lililoko Soweto Moshi.

Niliamua kuhudhuria huo mkutano na mwisho nilisikiliza neno la Mungu na kuamua kuokoka

na kumpa Yesu maisha yangu, mkutano ulipoisha niliamua kubatizwa Ubatizo wa maji mengi.

Niliamua kwenda kumsalimia mke wa tajiri yangu nilikokua nafanya kazi ya Ukarani kiwanda

cha mashine ya kukoboa na kusaga. Walinipokea kwa furaha sana baada ya kuwasimulia historia

ya maisha yangu walinishawishi kurudi kazini, na niliamua kukubali na kuanza kazi mwaka

Page 7: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

2000 kwa muda wa miezi sita. Dada yangu anayeishi Kibosho anafanya biashara ya kuuza nguo

na viatu katika maduka yaliyoko jirani na Benki ya Nelson Mandela, siku moja alikuja

kumsalimia tajiri yangu na kuongea na mimi kwa kunishauri kuwa nikafanye kazi dukani kwake.

Nilikubali kuacha ile kazi ya mashine na kuanza kazi ya duka kwa muda wa miaka mitatu.

Nilisikia tangazo la nafasi za kujiunga na kozi ya mafunzo ya ualimu kwenye vyombo vya

habari mwaka 2003 mwezi wa kumi na mbili. Nilipo omba nafasi hiyo na kukubaliwa kwa kweli

nilimshukuru Mungu sana kwa kunipa nafasi hiyo. Mwaka 2004 mwezi wa kwanza ndipo

nilipoanza mafunzo ya ualimu daraja la tatu A katika Chuo Cha Ualimu kilichopo katika Mkoa

wa Kilimanjaro Moshi.

Niliendelea na masomo na kuhitimu tarehe 28 /11/2004. Baada ya hapo nilipata mchumba

anayeitwa

Page 8: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

Annizeth Gasper Minde anayeishi Uru Mawela Mtaa wa Mamba. Ilipofika tarehe 3/3/ 2005

nilipangiwa kituo cha kazi kwa mafunzo ya ualimu uwanafunzi kwa vitendo kwa muda wa

mwaka mmoja, katika Mkoa wa Singida, Shule ya Msingi Mvae iliyoko Wilaya ya Singida

Vijijini na kuanza kazi 7/3/2005. Tarehe 18/12/2005 nilifunga ndoa ya Kikristo, katika Kanisa

la TAG Amani Soweto Moshi.

Mume wangu alikuwa anafanya kazi katika kiwanda cha KIBO MATCH kilichoko Magereza

Moshi Mjini. Baada ya usumbufu wa kutolipwa mshahara kwa muda mrefu aliamua kuacha kazi

na kuhamia Singida kwa shughuli za biashara, mwaka 2006. Niliajiriwa rasmi kwa cheo cha

ualimu daraja la tatu A tarehe 9/6/ 2007. Mungu alitujalia mtoto wa kike wa kwanza anayeitwa

Dorcas,

Page 9: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

kweli tulifurahi sana kupata mtoto. Niliendelea na kazi kwa muda wa miaka minne huku

nikiendelea kuomba uhamisho wa kurudi Mkoa wa Kilimanjaro Moshi kutokana na mazingira ya

kazi kuwa magumu. Mwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na

kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko Machame Kaskazini na

kufanya kazi ndani ya mwaka mmoja. Mwaka 2009 nilipata uhamisho na kuhamia shule ya

msingi Ulali iliyoko Narumu na kufanya kazi ndani ya miaka mitatu. Tarehe 19/11/2010 Mungu

alitujalia mtoto wa pili wa kiume anayeitwa Joshua

Page 10: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

tulimshukuru Mungu sana na kuendelea na kazi. Baadaye niliomba uhamisho na kuhamia Shule

ya msingi Kimashuku na kuanza kazi tarehe 22/1/2012. Lengo la kuhamia shule hiyo ni baada

ya mume wangu kuwa Mchungaji na eneo alilokua anafanya kazi kuwa mbali na eneo

ninalofanya kazi. Niliendelea na kazi kwa amani na kuishi vizuri na familia yangu kwa muda wa

miaka minne.

Baadae nilisikia tangazo katika vyombo vya habari kutoka NACTE la kozi ya mafunzo

ya Diploma ya ualimu kwa shule za msingi. Ndipo niliamua kushauriana na mume wangu na

kumsihi aendelee kuitunza familia ili mimi nikajiendeleze.

Page 11: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

Mume wangu alipokubali nilichukua fomu ya kujiunga na Chuo cha ualimu Marangu na kuijaza

na mwisho kutuma maombi hayo kwa mtandao wa Intaneti kupitia NACTE, kwa katibu mkuu

wa Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kwa kuambatanisha vyeti ambavyo ni cheti cha

kuhitimu elimu ya sekondari na cheti cha kuhitimu mafunzo ya ualimu daraja la tatu A.

Nilijibiwa ombi langu na kuchaguliwa kujiunga na Chuo cha Ualimu Marangu tarehe 2/7/2015

na kuanza rasmi mafunzo ya Stashahada ya kawaida ya elimu ya msingi.

Page 12: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

Katika Semista ya kwanza nilisoma masomo yafuatayo, English Literature, Stadi za Kazi,

Saikolojia, Stadi za Maisha, Hesabu na Sayansi. Nilifaulu vizuri Semista ya kwanza. Tarehe

02/11/2015 niliendelea na masomo ya Semista ya Pili hadi sasa yenye masomo nane ambayo ni

Hisabati, Historia, Jiografia, Siasa, Tehama, Upimaji, Mitaala na Kiswahili. Namshukuru Mungu

kwa kunijalia afya na nguvu yakuendelea vizuri na masomo yangu, na pia kuilinda familia yangu

nakuitunza vizuri. Pamoja na changamoto nyingi ninazozipitia za kifamilia na masomo kuwa

magumu bado sikati tamaa, ninatumaini la kuwa na ushindi mkubwa wa ufaulu wa masomo

yangu na pia ushindi mkubwa katika familia yangu kwani Bwana Yesu ni muweza wa yote.

Page 13: Web viewMwaka 2008 mwezi wa kwanza nilifanikiwa kuhamia Wilaya ya Hai na kupangiwa kituo cha kazi katika shule ya Msingi Sere Ufundi iliyoko

Hivyo, ni matumaini yangu kuwa nitafaulu vizuri na kurudi katika kituo changu cha kazi

cha shule ya msingi Kimashuku. Pia ninamwomba Bwana Yesu anijalie uzima, afya njema,

nguvu, hekima, busara na akili njema. Ili niendelee kushirikiana vyema na wakufunzi wangu

vizuri katika kuhitimu elimu hii. Pia nawashukuru sana wazazi wangu walio nilea kwa malezi

mema, bila kuwasahau wakufunzi wote wa Chuo cha Ualimu Marangu, walimu wengine wote,

viongozi wa Dini, wadau na walezi mbalimbali katika kunipatia elimu mpaka nikaweza kufika

hapa nilipo. Mungu awabariki sana na kuwajalia maisha marefu na mazuri.