tume ya uchaguzi ya zanzibar
TRANSCRIPT
Page | 0
TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR
MUONGOZO WA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA KWA
UCHAGUZI MKUU, 2015
MEI, 2015
Page | 1
MUONGOZO WA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA KWA UCHAGUZI MKUU, 2015
Utangulizi
Kwa kuwa tunahitaji kuwa na amani, uhuru wa kampeni, na kuheshimu sheria ili kufanya
uchaguzi wa huru na wa haki. Sisi vyama vya siasa tumeamua kwa hiari yetu wenyewe
kutengeneza maadili haya ili yatuongoze katika shughuli zetu za uchaguzi na tuna
kubalina sisi kama wananchi wa Zanzibar tutahakikisha kuwa maadili haya yanajulikana
kwa wagombea, mawakala na wafuasi wetu, na kwamba tutahakikisha vifungu vyote
vinatakelezwa kikamilifu. Kwa hiyo, kwa hiari yetu tunatengeneza na kujipa wenyewe
maadili yafuatayo:-
Mamlaka 1. Maadili haya yanaanzishwa chini ya kifungu cha 130 cha Sheria ya
Uchaguzi Namba 11 ya 1984
Kuanza
kutumika
2. (1) Maadili haya yametayarishwa kwa pamoja kati ya Vyama vya
Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2015, Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na yataanza kutumika
baada ya uteuzi wa wagombea na kumalizika mwezi mmoja baada
ya uchaguzi.
(2) Maadili haya pia yatatumika katika Uchaguzi Mdogo pale
utakapojitokeza.
Madhumuni 3. Madhumuni ya Maadili haya ni kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa
Zanzibar wa mwaka 2015 unafanyika katika mazingira ya amani na
utulivu kwa kuzingatia uhuru na haki ya ushiriki wa makundi yote ya
kijamii yakiwemo wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, na
vigezo vya kimataifa vya uchaguzi wa kidemokrasia.
Haki na wajibu
wa Vyama vya
siasa.
4. (1) Sisi Vyama vya Siasa, tunaoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar
wa mwaka 2015, tukiwa wawakilishi wa wananchi tunaamini na
kukubali kuwa:
a. Kulinda usalama, utulivu na amani ya Zanzibar ni jukumu la msingi
la vyama na wananchi wote.
b. Vyama vitahakikisha ushiriki huru na ulinzi kwa wanawake, vijana
na watu wenye ulemavu kama wapiga kura au wagombea.
Page | 2
c. Kufuata maelekezo ya Sheria, Kanuni, Miongozo ya Tume, Maadili
na Taratibu za Uchaguzi ni muhimu katika kufanya uchaguzi ulio
huru na wa haki.
d. Vyama havitatumia makundi ya wanawake na vijana katika
kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi.
e. Kujiunga na Chama chochote cha siasa na kumchagua kiongozi
anayemtaka ni uhuru na haki ya kila mwananchi mwenyewe.
f. Kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa
Zanzibar wa mwaka 2015 kina haki ya kufanya kampeni kwa
mujibu wa sheria na taratibu zilizopo nchini.
Thamani utu
na haki za
binadamu
5. (1) Sisi Vyama vya Siasa kwa umoja wetu :
a Tunathibitisha kwa imani yetu kwamba, utu, thamani, na haki ya
maisha ya mwanadamu vinastahiki kulindwa kwa nguvu zote
kama ilivyoelezwa katika Katiba ya Zanzibar 1984, nchi na
maazimio ya kimataifa
b Tunapinga kwa nguvu zetu zote hujuma dhidi ya maisha ya
mwanadamu na mali zake kwa sababu ya itikadi yake ya kisiasa;
c Tutaheshimu haki ya kila Chama cha Siasa, wanachama na
wafuasi wake kutoa na kueleza maoni yao ya kisiasa na kutekeleza
shughuli zao na malengo ya kisiasa kwa mujibu wa Sheria; na
d Tutaheshimu utu wa mwanamke na mtu mwenye ulemavu kama
wagombea na wapiga kura katika mchakato wa uchaguzi.
Kupinga na
kujiepusha na
kauli za chuki,
fujo, vitisho na
vurugu
6. (1) Sisi Vyama vya Siasa kwa pamoja;-
a. Tunakataa na kupinga matumizi ya silaha za aina yoyote
kutumiwa na viongozi, mawakala, mwanachama na wafuasi wetu
kwa malengo ya kufanya hujuma katika harakati za kisiasa;
b. Tunakaa mbinu zozote zisizo halali kutumika na vyama katika
harakati za uchaguzi.
Page | 3
c. Tunakataa matumizi matumizi ya vikundi vya ulinzi vya vyama
kutumiwa kwa malengo ya kuchochea fujo na kuvuruga amani
wakati wa kampeni na uchaguzi
d. Tunaamini kuwa ni jukumu na wajibu wetu wa kuwa na jamii
yenye mahusiano mema, yasiyo ya vurugu, chuki na vitisho;
e. Tunakataa kauli na vitendo vyote vinavyopelekea kuibua hisia za
chuki, vitisho, fujo, udhalilishaji wa wanawake na watu wenye
ulemavu na kutofahamiana katika kutekeleza malengo ya kisiasa;
(2) Kwa muelekeo huo kufanya Uchaguzi wa kidemokrasia
ulioandaliwa katika mazingira ya uwazi na ukweli ni jambo muhimu
sana kwa ustawi wa Zanzibar.
Sheria,
Kanuni na
Taratibu
7. Sisi Vyama vya Siasa tunakubali kuwa:
a. Tutatekeleza shughuli zote za kisiasa kwa mujibu wa Sheria ya
Uchaguzi, Kanuni, Miongozo ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na
Taratibu zinazotawala mwenendo wa Uchaguzi Zanzibar.
b. Tunakemea vitendo vya rushwa na vyengine visivyo halali, pia
tunawasisitiza wafuasi wa vyetu na wananchi kuepuka kutoa
matangazo na matamshi yatakayochochea ubaguzi wa aina
yoyote ukiwemo rangi, kabila, jinsia, dini, ulemavu, na itikadi za
kisiasa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu;
c. Tunawataka wanachama na mawakala wetu kuheshimu haki za
wengine, ili kuhakikisha kuwa haki ya mtu kutoa mawazo yake
inaheshimiwa.
Kampeni za
utulivu, amani
na heshima
kwa wengine
8. Sisi vyama vya siasa, tuko tayari kusaidia kwa uwezo wetu wote
kufikia malengo ya Uchaguzi huru na haki na tunaahidi kufanya
yafuatayo;
a) Kukataza matumizi ya lugha za matusi, lugha sizizofaa,
vitisho na vitendo vya fujo vitavyopelekea kushawishi na
kuharibu mikutano au shughuli nyingine halali za Vyama vya
Siasa.
Page | 4
b) Kupinga uchapishwaji wa vijarida, vipeperushi, mabango ya
matangazo, katuni, katika mitandao ya kijamii au aina
nyingine za machapisho yatayobeba ujumbe unaochochea
na kuwashawishi watu kuvunja amani ya nchi au kudhalilisha
wagombea kutokana na jinsia zao au ulemavu;
c) Kukataza wagombea, wanachama na wafuasi wa vyama vya
siasa kufanya vitendo vya aina yoyote vitakavyoharibu
mikutano, maandamano au mikusanyiko ya chama chengine
cha siasa.
d) Kukataza na kupinga vikali vitendo vyote vitakavyopelekea
kuharibu picha za wagombea, kuchana matangazo na
machapisho mengine yanayowahusisha wagombea wa
vyama vyengine.
e) Kukataza mawakala na wafuasi wa Vyama vya siasa
kubandika picha, machapisho au matangazo ya wagombea
katika nyumba za ibada na za watu binafsi, vyombo vya
usafiri bila ya ridhaa za wamiliki.
f) Kila chama kuondosha katika maeneo ya wazi mabango,
picha za wagombea na matangazo yahusianayo na uchaguzi
ndani ya kipindi cha siku kumi nan nne baada ya
kutanganzwa kwa matokeo ya uchaguzi.
g) Kuhamasisha kampeni za amani na utulivu ambazo
zitapelekea kila chama kujiheshimu na kuheshimiwa;
Muda wa
Kampeni
9. Tunakubaliana kuwa kampeni za nje zitaanza saa mbili asubuhi na
kumalizika saa kumi na mbili jioni na vipaza Sauti vitumike kwa
muda uliolekezwa hapo juu.
Matumizi ya
magari ya
serikali na
rasilimali za
umma katika
kampeni
10. Sisi, Vyama vya Siasa tunakubaliana kutotumia:-
a. Gari za Serikali na rasilimali za umma katika kampeni.
b. Majengo, watumishi na Taasisi za umma katika shughuli za
kampeni za uchaguzi.
Page | 5
Kuheshimu
Sheria za
usalama
barabarani
11. Sisi vyama vya siasa tunakataza wanachama na wafuasi wa vyama
vyetu wanaosafiri kufuatilia mikutano ya kampeni, kujazana kupita
kiasi katika gari wakati wa kwenda na kurudi katika mikutano hiyo
na gari hizo hazitovunja Sheria za Usalama Barabarani.
Kuheshimu
mchakato wa
uchaguzi
12. (1) Sisi Vyama vya Siasa pamoja na wagombea, wanachama na
mawakala wa vyama vyetu:
a. Tutashirikiana na kuisaidia Tume ya Uchaguzi, watendaji na
maafisa wake katika kutekeleza majukumu na wajibu wao;
tutajizuia na lugha za matusi, vitisho na vitendo vinavyochochea
uvunjifu wa amani wakati wa shughuli za uchaguzi.
b. Tutahakikisha wagombea, mawakala na wanachama wetu
hawafanyi hila kwa njia yoyote ile katika zoezi la kupiga na
kuhesabu kura. Aidha tutawazuia kueneza uzushi kuhusiana na
matokeo ya uchaguzi.
c. Tutawaelekeza wagombea, mawakala na wanachama wetu
kutosababisha hasara ya aina yoyote katika maeneo ya uchaguzi
kwa kuondoa, kuharibu, kuchana machapisho na nyaraka mbali
mbali zinazotolewa na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar.
Wajibu wa
Tume
13. Katika kutekeleza majukumu yake Tume ya Uchaguzi pamoja na
watendaji wake itahakikisha inatekeleza majukumu yake kwa:-
a. Kufuata Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu zinazoongoza
mchakato wa Uchaguzi wa Zanzibar.
b. Kutopendelea chama chochote cha siasa au Mgombea.
c. Kushirikiana na wagombea wa vyama vyote katika
kuhakikisha maelekezo ya Sheria juu ya mchakato wa
uchaguzi yanafuatwa.
d. Kutoa taarifa, ufafanuzi, na maelezo juu ya jambo ililolifanya,
inalolifanya na inalotarajia kulifanya katika hatua za
uchaguzi.
Page | 6
e. Kuweka wazi milango yake kwa chama au mgombea kwa ajili
ya ufafanuzi, maelekezo, au taarifa inayohusiana na utendaji
wa Tume ya Uchaguzi.
Utoaji wa
Taarifa za
Uchaguzi
14. Tume ya uchaguzi inaahidi kutoa habari na taarifa za mwenendo wa
Uchaguzi kwa njia ya uhuru, uwazi na ukweli hatua kwa hatua hadi
kukamilika hatua zote za uchaguzi.
Wajibu wa
Serikali
15. Serikali itahakikisha kuwa:-
a. Inatoa huduma na nafasi sawa kwa vyama vyote vya siasa
bila ya upendeleo wa aina yoyote;
b. Inachukua hatua za kisheria kwa kiongozi yeyote wa Serikali
atakayebainika kuvuruga au kuhujumu shughuli au kampeni
ya chama cha siasa;
c. Kupitia vyombo vya usalama inasimamia usalama wa nchi na
kutoa ulinzi unaostahiki katika mikutano na kampeni na
mikusanyiko yote iliyo rasmi ya vyama vya siasa;
d. Majengo, watumishi na vyombo (Gari) vya Serikali havitumiwi
katika shughuli za vyama vya siasa kufanikisha kampeni za
vyama vyao;
e. Watendaji wa Serikali wanatoa ushirikiano kwa vyama vya
siasa katika kutekeleza majukumu yao hasa kampeni.
f. Watumishi wa Serikali hawatumii muda wa kazi kufanya
kampeni katika Ofisi zao.
Kuheshimu
Wagombea
wengine
16. Sisi Vyama vya Siasa tutahakikisha kuwa:-
a. Wagombea, mawakala, au wafuasi wetu hawatowi lugha ya
udhalilishaji kwa viongozi wengine wa Vyama ambao
wanagombea nafasi moja au vyenginevyo.
b. Wagombea, mawakala au wafuasi wetu hawatoi lugha za
kuwadhalilisha wagombea wengine kutokana na jinsia zao,
maumbile yao, rangi zao au sehemu wanazotoka.
Page | 7
Ushirikiano na
vyombo vya
ulinzi na
usalama
17. Sisi Vyama vya Siasa tutashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama
katika usimamizi wa sheria na kudumisha amani wakati wa kampeni,
upigaji kura na utangazaji wa matokeo.
Kukubali
matokeo ya
uchaguzi
18. Sisi Vyama vya Siasa tunaahidi kuyakubali matokeo halali
yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ambayo ndio
yenye mamlaka ya kutangaza matokeo kisheria
Ukiukwaji wa
maadili
19. Muhusika yeyote atakayekwenda kinyume na maadili haya
atakuwa ametenda kosa na atawajibika kwa adhabu zifuatazo:-
a. Onyo au Karipio
b. Kutanganzwa katika jamii
c. Kutakiwa kuomba msamaha kwa jamii
d. Kumsimamisha mgombea au chama kuendelea na kampeni kwa
kipindi kitakachoonekana kinafaa na kamati.
e. Faini kama zinavyoelekezwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.
Mamlaka ya
usimamizi wa
maadili
20. Maadili haya yatasimamiwa na Kamati ya maadili ya uchaguzi
iliyopo chini ya Tume ya uchaguzi ya Zanzibar. Kamati hii itakuwa
na mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa maadili haya katika
ngazi zote za uchaguzi wa Rais, wajumbe wa baraza la wawakilishi
na Madiwani.
Uwasilishwaji
wa malalamiko
21. Chama kitakachoona kuwa maadili haya yamekiukwa au kina
sababu za kutosha kuwa yatakiukwa, kina haki ya kuwasilisha
malalamiko kwa kamati ndani ya saa arobaini na nane
kabla/baada ya tukio la uvunjifu wa maadili kutokea.
Muda wa
kusikiliza
Malalamiko
22. (1) Kamati mara baada ya kupokea malalamiko, itazijulisha pande
zote mbili muda, siku na wakati wa kusilizwa lalamiko hilo.
(2) Kamati itasikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kutoa
Uamuzi ndani ya masaa sabini na mbili.
Rufaa 23. (a)Chama ambacho hakitaridhika na uamuzi wa kamati kina haki
ya kukata rufaa kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ndani ya siku
tatu.
(b)Tume itasikiliza rufaa iliyowasilishwa ndani ya kipindi cha siku
tatu na kutoa uamuzi.
Page | 8
(c)Kama Chama hakitaridhika na uamuzi wa Tume, kina ruhusiwa
kupeleka lalamiko lake mahakamani kama ilivyo katika sheria za
uchaguzi.
Kuridhia
utekelezaji
24. (1) Sisi Vyama vya Siasa, Tume ya Uchaguzi na Serikali
tunakubaliana kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maadili haya
kwa madhumuni ya kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
ambayo kwa kiasi kikubwa yatasaidia kuwa na uchaguzi huru na
haki.
(2) Kwa uthabiti wetu tutawaagiza wagombea, wanachama na
mawakala wetu na Wananchi kwa ujumla kutekeleza maadili haya
na tunajitolea kuchukuwa hatua za ziada kuakikisha elimu juu ya
maadili inatolewa nchi nzima na yanatekelezwa kwa vitendo.
Page | 9
TAMKO
SISI vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi na Serikali kwa hiari yetu tunatia saini na
kuridhia usimamizi na utekelezaji wa maadili haya.
NAM. JINA CHAMA WADHIFA SAINI
ACT
ADC
AFP
APPT MAENDELEO
CCM
CCK
CHADEMA
CHAUSTA
CUF
CHAUMA
DEMOKRASIA
MAKINI
DP
JAHAZI ASILIA
NCCR MAGEUZI
NLD
NRA
SAU
TADEA
TLP
UDP
UMD
UPDP
Page | 10
Kwa niaba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
Jina ……………………………………………………………..
Cheo…………………………………………………………….
Sahihi…………………………………………………………..
Tarehe……………………………..…………………………..
Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Jina ……………………………………………………………..
Cheo……………………………………………………………
Sahihi…………………………………………………………..
Tarehe……………………………..…………………………..
Page | 11
CHAMA CHA ALLIANCE
FOR CHANGES
CHAMA CHA ADC CHAMA CHA WAKULIMA
CHAMA CHA UMMA
CHAMA CHA APPT
MAENDELEO
CHAMA CHA MAPINDUZI
CHAMA CHA DEMOKRASIA
NA MAENDELEO
CHAMA CHA USTAWI
TANZANIA
CHAMA CHA WANANCHI
CHAMA CHA DEMOCRATIC
PARTY
CHAMA CHA JAHAZI
ASILIA
CHAMA CHA KIJAMII
DEMOKRASIA MAKINI
CHAMA CHA NCCR
MAGEUZI
CHAMA CHA NLD
CHAMA CHA SAUTI YA
UMMA
CHAMA CHA TADEA CHAMA CHA NRA
Page | 12
CHAMA CHA UDP
CHAMA CHA UMD
CHAMA CHA TLP
CHAMA CHA UPDP