taarifa kwa umma msajili wa vyama vya siasa.rtf

Download TAARIFA KWA UMMA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.rtf

If you can't read please download the document

Upload: andrewchale

Post on 06-Dec-2015

233 views

Category:

Documents


9 download

TRANSCRIPT

TAARIFA KWA UMMA

Yah: WATANZANIA TUTAMBUE AMANI YETU NI FAHARI YETU (KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI)

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, pamoja na majukumu yake ya msingi, inayo pia jukumu la kuhakikisha ukuaji wa demokrasia unakuwepo kulingana na sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kikatiba. Ukuaji wa demokrasia hauwezi kuwepo kama wananchi ambao ndio wafuasi wa vyama vya siasa wanakuwa na uelewa mdogo juu ya ushiriki wao kwenye siasa za kistarabu na zenye staha.

Ndugu Watanzania, mbali na tahadhari zinazotolewa katika kipindi hiki cha kampeni kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu wa Amani miongoni mwa jamii yakiwemo baadhi ya makundi ya wanachama, wafuasi na mashabiki wa vyama vya siasa. Makundi hayo yanadiriki Kutoa maneno ya kejeli, matusi, kuvamia, kupigana hata kujeruhi makundi mengine ambayo siyo ya upande wao. Hali hii budi iachwe mara moja ili kuiweka nchi yetu ya Tanzania katika hali ya amani na kuiepusha nchi yetu kuingia kwenye vurugu, mfarakano na machafuko yasiyokuwa na ulazima wa kutokea. Ni vyema Watanzania tutambue kwamba utofauti wa itikadi wa vyama ndio ukomavu wa demokrasia nchini hivyo ni jambo la busara kuvumiliana na kufanya siasa za kistaarabu. Kipindi hiki ni cha mpito tu tusikiruhusu kikavuruga amani yetu kwani kuna maisha baada ya uchaguzi na mwisho wa uchaguzi huu ndio mwanzo wa chaguzi zingine kama hizi.

Kila mmoja wetu kwa nafasi yake hajachelewa kuhakikisha kuwa nchi yetu inabaki salama. Kutovumiliana kwa utofauti wetu wa itikadi za kisiasa kunaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii itakayopelekea idadi kubwa ya watanzania kupata athari ikiwemo ulemavu, vifo, ukimbizi, njaa na maradhi.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaamini kuwa, Viongozi wa kisiasa wanao ushawishi mkubwa kwa wafuasi na mashabiki wa vyama vyao. Tumieni nafasi hii kusisitiza Amani. Dhamana ya nchi hii iko mikononi mwenu, ushawishi wenu kuhusu amani katika kipindi hiki ndio utakaoliokoa taifa letu la Tanzania ama italiingiza taifa katika vurugu na mfarakano. Nawaasa na kuwataka viongozi wote wa Vyama vya Siasa kutoa kauli na maelekezo kwa wafuasi na wanachama wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu wa Amani. Tumieni vyema dhamana ya uongozi mliopewa na mwenyezi Mungu kuivusha salama Tanzania yetu.

Natoa rai kwa Waaandishi wa Habari, tumieni kalamu zenu vyema kuhubiri Amani. Epukeni kuandika habari za uchochezi bali wasaidieni Watanzania kupata taarifa sahihi zitakazowasaidia kufanya maamuzi kuchagua viongozi wao. Msikubali kalamu zenu zikawa chanzo cha mfarakano na vurugu bali ziwafanye muwe mabalozi wazuri wa amani.

Mwisho natoa wito kwa watanzania wote. Dumisheni Amani na kamwe tusijiingize kwenye siasa zinazoleta mfarakano na uvunjifu wa Amani. Kumbuka kuna maisha baada ya uchaguzi na Amani ya Nchi yetu ni fahari yetu sote.

Mungu ibariki Tanzania