sautielimu 24

4
Sauti Elimu ISSN 1821 5076 Na Farida Nuhu – Jangwani Sec. Dar es Salaam Elimu ni taaluma yoyote inayotolewa na watu kwenye eneo maalumu kwa lengo la kufundisha na kuelimisha. Mwanafunzi ni mtu ambaye yupo tayari kupokea elimu kutoka kwa mjuzi wa taaluma fulani. Wanafunzi wengi wana mitazamo mbalimbali kuhusu suala zima la elimu hasa matatizo mbalimbali yanayoikumba elimu. Upungufu wa walimu ni tatizo kubwa hususani vijijini, serikali haina budi kuongeza idadi ya walimu kule vijiini ambako kuna upungufu zaidi kuliko mi- jini. Pia kuboresha makazi au mazingira ya walimu kule vijijini kutasaidia katika NXÀNLD PDOHQJR \D NXSDWD ZDVRPL ZHQ gi hapo baadaye. Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa walimu kuhusiana na uhaba wa vifaa kama vile vitabu, ramani, chaki n.k. hili pia ni tatizo kubwa linaloikumba elimu yetu hapa Tanzania, hivyo serikali haina budi kuboresha hili. Walimu wanatakiwa kuongezewa kiwan- go cha mishahara ili kuinua hali yao ya maisha; hii itawafanya wafundishe kwa moyo mmoja pamoja na kuipenda kazi yao. Mishahara mizuri pia itawapa mo- tisha wale wanaotarajia kuwa walimu hapo baadaye kusomea fani hiyo. 8VDÀUL NZD ZDOLPX QD ZDQDIXQ]L QL WD WL]R OLQDORIDQ\D ZDFKHOHZH NXÀND VKX leni hivyo kupelekea kukosa vipindi vya mwanzo hususani vya asubuhi. Walimu wanaochelewa kuingia shule asubuhi, husababisha wanafunzi kukosa vipindi vya mwanzo kila siku; hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya elimu. Lugha ambayo inatumika kufundishia elimu ya juu ni lugha ya kiingereza ambayo ni tatizo kubwa kwa wanafunzi wengi hivyo ingetakiwa tuitukuze lugha yetu ya Taifa ‘Kiswahili’ ili wanafunzi wapate kumuelewa mwalimu. Mtoto anapokuwa mdogo anatakiwa kuangaliwa kipaji chake na kukikuza na sio kupelekwa shule ili mradi tu amekwenda shule, inabidi tubadilike; mtoto asome lakini pia walimu wamsai- die kukuza kipaji chake. Hatuna budi kushirikiana katika suala zima la kuboresha elimu mashuleni. 7XNLVKLULNLDQD WXQDZH]D NXÀNLVKD HOLPX ya Tanzania sehemu inapotakiwa. Na Abubakari G. Jaidi, Jitegemee Secondary School Elimu ni taaluma ambayo inampatia mtu yeyote ufahamu wa kutambua jam- bo ambalo halikutambuliwa, na elimu hii inatolewa kupitia njia ya mawasiliano hasa kufundisha. Elimu bora ni ile ambayo mtu anapata na kufaidika nayo. Elimu bora yoyote ndio inayoleta changamoto ya maen- deleo katika jamii, humuwezesha mtu kuwajibika ipasavyo na kuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali kwa faida ya ja- mii inayomzunguka. Ili tuwe na elimu bora tunahitaji uon- gozi bora ambao unatekeleza misingi yote ya uongozi. Kama vile kupokea maoni kutoka kwa wahusika ambao ni walimu, wazazi, wanafunzi na wadau wengine wote wa elimu. Inapaswa haki itolewe katika sekta zote bila kuwepo na ubaguzi. Ikiwa uongozi utakuwa bora, elimu itakuwa bora na yenye kiwango kikubwa kwa sababu italeta changamoto kwa wote wanaohusika na masuala yote ya elimu. Mafunzo ya kutosha wanayopewa wali- mu, yanaambatana na wajibu wao katika kazi na ili wapatikane walimu wengi na wa kutosha, inabidi maslahi na mazingi- UD \DR \D NXIDQ\LD ND]L NDPD YLOH XVDÀUL nyumba bora za kuishi, yawe mazuri. Hali hizi zote zikiboreshwa, elimu bora itapatikana. Vifaa bora vya kufundishia: Hapa tu- nazungumzia maabara zote ambazo zinahusiana na masomo kama vile bai- ORMLD À]LNLD na kemia na pia vitabu vya kutosha ambavyo vitamuwezesha kila mwanafunzi kupata kitabu chake ili mwalimu aweze kufundisha kwa ufa- saha. Vile vile maktaba ni muhimu ka- tika kupata elimu bora. Sera ya lugha ya kufundishia moja ya vitu muhimu sana katika kuleta elimu bora hasa kwa Tanzania ambapo sera yetu imeegemea zaidi kwenye kubore- sha lugha za kigeni kama vile kiingereza wakati nchi yetu ina lugha ya kiswahili ambayo ni lugha ya Taifa. Kama sera yetu italenga katika lugha ya kiswahili, basi naamini elimu itakuwa bora kwa sababu wanafunzi walio wengi wana- fahamu kiswahili kuliko lugha ya kiin- gereza. Kupatikana kwa chakula kizuri kwa walimu na wanafunzi shuleni: Hii inato- kana na mazingira ya yetu hapa Tanza- nia ambapo vipato vyetu vinatofautiana sana. Wengi wetu ni maskini na wach- ache ndio wanaomudu suala la chakula kwa walimu na wanafunzi. Kama serika- li ikitoa chakula shuleni, walimu watatoa elimu kwa bidii na kwa wanafunzi utoaji chakula utaondoa ubaguzi na mahudhu- rio ya wanafunzi shuleni yatakuwa ma- zuri. Elimu ya vitendo ni njia mojawapo ya kuwasaidia wanafunzi kuelewa vizuri zaidi kwani inawapatia mifano dhahiri, hivyo kutosahau katika mitihani yao, na ni njia bora ya kupata elimu bora. Uzalendo unatokana na watu walio na dukuduku la kuleta maendeleo katika nchi yetu; tukiwa wazalendo kuanzia ngazi za chini hadi juu, elimu itakuwa bora. Mtazamo Wa Wanafunzi Kuhusu Elimu Elimu Bora inapatikana vipi? Sauti Elimu

Upload: vijanaforum

Post on 22-Mar-2016

432 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

Toleo hili ni mkusanyilo wa maoni ya wananchi wakiwemo wanafunzi kuhusu hali ya elimu nchini na ushauri wa jinsi ya kuboresha elimu nchini ili kunusuru kizazi hiki na cha baadaye.

TRANSCRIPT

Sauti ElimuISSN 1821 5076

Na Farida Nuhu – Jangwani Sec.Dar es Salaam Elimu ni taaluma yoyote inayotolewa na watu kwenye eneo maalumu kwa lengo la kufundisha na kuelimisha. Mwanafunzi ni mtu ambaye yupo tayari kupokea elimu kutoka kwa mjuzi wa taaluma fulani. Wanafunzi wengi wana mitazamo mbalimbali kuhusu suala zima la elimu hasa matatizo mbalimbali yanayoikumba elimu. Upungufu wa walimu ni tatizo kubwa hususani vijijini, serikali haina budi kuongeza idadi ya walimu kule vijiini ambako kuna upungufu zaidi kuliko mi-jini. Pia kuboresha makazi au mazingira ya walimu kule vijijini kutasaidia katika

gi hapo baadaye.

Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa walimu kuhusiana na uhaba wa vifaa kama vile vitabu, ramani, chaki n.k. hili pia ni tatizo kubwa linaloikumba elimu yetu hapa Tanzania, hivyo serikali haina budi kuboresha hili. Walimu wanatakiwa kuongezewa kiwan-go cha mishahara ili kuinua hali yao ya maisha; hii itawafanya wafundishe kwa

moyo mmoja pamoja na kuipenda kazi yao. Mishahara mizuri pia itawapa mo-tisha wale wanaotarajia kuwa walimu hapo baadaye kusomea fani hiyo.

leni hivyo kupelekea kukosa vipindi vya mwanzo hususani vya asubuhi. Walimu wanaochelewa kuingia shule asubuhi, husababisha wanafunzi kukosa vipindi vya mwanzo kila siku; hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya elimu. Lugha ambayo inatumika kufundishia elimu ya juu ni lugha ya kiingerezaambayo ni tatizo kubwa kwa wanafunzi wengi hivyo ingetakiwa tuitukuze lugha yetu ya Taifa ‘Kiswahili’ ili wanafunzi wapate kumuelewa mwalimu. Mtoto anapokuwa mdogo anatakiwa kuangaliwa kipaji chake na kukikuza na sio kupelekwa shule ili mradi tuamekwenda shule, inabidi tubadilike; mtoto asome lakini pia walimu wamsai-die kukuza kipaji chake. Hatuna budi kushirikiana katika suala zima la kuboresha elimu mashuleni.

ya Tanzania sehemu inapotakiwa.

Na Abubakari G. Jaidi, JitegemeeSecondary School Elimu ni taaluma ambayo inampatia mtu yeyote ufahamu wa kutambua jam-bo ambalo halikutambuliwa, na elimu hii inatolewa kupitia njia ya mawasiliano hasa kufundisha. Elimu bora ni ile ambayo mtu anapata na kufaidika nayo. Elimu bora yoyote ndio inayoleta changamoto ya maen-deleo katika jamii, humuwezesha mtu kuwajibika ipasavyo na kuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali kwa faida ya ja-mii inayomzunguka. Ili tuwe na elimu bora tunahitaji uon-gozi bora ambao unatekeleza misingi yote ya uongozi. Kama vile kupokea maoni kutoka kwa wahusika ambao ni walimu, wazazi, wanafunzi na wadau wengine wote wa elimu. Inapaswa haki itolewe katika sekta zote bila kuwepo na ubaguzi. Ikiwa uongozi utakuwa bora, elimu itakuwa bora na yenye kiwango kikubwa kwa sababu italeta changamoto kwa wote wanaohusika na masuala yote ya elimu. Mafunzo ya kutosha wanayopewa wali-mu, yanaambatana na wajibu wao katika kazi na ili wapatikane walimu wengi na wa kutosha, inabidi maslahi na mazingi-

nyumba bora za kuishi, yawe mazuri. Hali hizi zote zikiboreshwa, elimu bora itapatikana. Vifaa bora vya kufundishia: Hapa tu-nazungumzia maabara zote ambazo zinahusiana na masomo kama vile bai-

na kemia na pia vitabu vya kutosha ambavyo vitamuwezesha kila mwanafunzi kupata kitabu chake ili mwalimu aweze kufundisha kwa ufa-saha. Vile vile maktaba ni muhimu ka-tika kupata elimu bora.

Sera ya lugha ya kufundishia moja ya vitu muhimu sana katika kuleta elimu bora hasa kwa Tanzania ambapo sera yetu imeegemea zaidi kwenye kubore-sha lugha za kigeni kama vile kiingereza wakati nchi yetu ina lugha ya kiswahili ambayo ni lugha ya Taifa. Kama sera yetu italenga katika lugha ya kiswahili, basi naamini elimu itakuwa bora kwa sababu wanafunzi walio wengi wana-fahamu kiswahili kuliko lugha ya kiin-gereza.

Kupatikana kwa chakula kizuri kwa walimu na wanafunzi shuleni: Hii inato-kana na mazingira ya yetu hapa Tanza-nia ambapo vipato vyetu vinatofautiana sana. Wengi wetu ni maskini na wach-ache ndio wanaomudu suala la chakula kwa walimu na wanafunzi. Kama serika-li ikitoa chakula shuleni, walimu watatoa elimu kwa bidii na kwa wanafunzi utoaji chakula utaondoa ubaguzi na mahudhu-rio ya wanafunzi shuleni yatakuwa ma-zuri.

Elimu ya vitendo ni njia mojawapo ya kuwasaidia wanafunzi kuelewa vizuri zaidi kwani inawapatia mifano dhahiri, hivyo kutosahau katika mitihani yao, na ni njia bora ya kupata elimu bora.

Uzalendo unatokana na watu walio na dukuduku la kuleta maendeleo katika nchi yetu; tukiwa wazalendo kuanzia ngazi za chini hadi juu, elimu itakuwa bora.

Mtazamo Wa Wanafunzi Kuhusu Elimu

Elimu Bora inapatikana vipi?

Sauti Elimu

Na Fatuma Hamisi – Dar es Salaam

kizazi kimoja kwenda kizazi kingine. Elimu hii inaweza kuwa ya asili, inayoto-kana na jamii au ya kitaaluma inayokuwa na sekta mbalimbali kama shule, taasisi na mashirika binafsi. Elimu haitolewi kwa mawe, miti au wa-nyama, elimu hutolewa kwa binadamu ambao ni wanafunzi. Kuna changamoto ambazo wanafunzi wanakutana nazo katika kupata elimu yao, changamoto hizi hutoka kwa wazazi, walimu, jamii,

Wanafunzi wanakumbana na matatizo kutoka kwa wazazi au walezi wanaoishi nao. Wazazi/walezi wako karibu sana na mwanafunzi huyu. Iwapo kutakuwa na kutoelewana kati ya watu hawa, mwa-nafunzi anaathirika kisaikolojia. Wazazi au walezi ndio msingi wa mwanafunzi huyu; wanatakiwa wamsaidie katika elimu yake. Lakini kwa bahati mbaya unaweza ukakuta wazazi hawa ndio sa-babu ya mwanafunzi kutofaulu maso-mo yake. Wazazi wanaweza kumkatisha tamaa mwanafunzi; kwa mfano mzazi, anaweza akamwambia mtoto wake aolewe au afanye kazi ili wapate pesa badala ya kusoma. Walimu ni jamii nyingine inayomzun-guka mwanafunzi. Walimu ndio wanao-tegemewa katika kumwezesha mwa-

Changamoto wanazokumbana nazo Wanafunzi

nafunzi kimasomo na kimaisha kwa kumfundisha mbinu bora za kimaisha. Mwalimu anakuwa tatizo kwa mwana-funzi pale anapokiuka maadili yake ya kazi. Mwalimu kuwa mkali sana ina-changia mwanafunzi kushindwa hata kuelezea matatizo yake, kuomba au ku-taka msaada wowote ule. Mwalimu huyu pia anaweza kuvuruga masomo ya mwa-nafunzi wake, kwa mfano kwa kumpa mimba mwanafunzi wa kike. Mwalimu anapokuwa na msimamo wa kumsaidia mwanafunzi, taifa litaendelea. Jamii ni chachu kuu inayokubaliwa na wanafunzi, jamii inaweza kumjenga au kumharibu mwanafunzi. Jamii inaweza kumshauri mwanafunzi ni jinsi gani akabili masomo yake. Lakini jamii ya Tanzania inamdharau mwanafunzi, inamshushia hadhi na kumfanya kama binadamu au raia wa chini; mfano mmo-ja ni makondakta wa daladala, wanavyo nyanyasa na kuwadharau wanafunzi. Walezi wa jamii wanawachukulia wana-funzi kuwa ni watu wasio na heshima. Pia jamii ndiyo inayotoa mafataki wao-wasumbua wanafunzi wa kike bila kusa-hau mashuga mami. Jamii hii inaharibu malengo na dira ya wanafunzi. Serikali inasaidia kuleta ahueni kwa wa-nafunzi kupata elimu bora. Lakini seri-kali hii pia inakuwa kikwazo kwa mwa-nafunzi pale inapotokea sera ngumu kwa wanafunzi, mfano mabadiliko ya

vizuri. Lakini serikali inapochelewesha mishahara huwajengea mazingira ma-gumu walimu na wanaoathirika zaidi ni wanafunzi.

katika kufaulu kwa wanafunzi. Makundi haya yanaweza kuwa tatizo kwa mwa-nafunzi iwapo yatakuwa na vishawishi hasa katika elimu, wanafunzi wanawe-za wakawa na malengo mazuri katika masomo yao lakini kwa haraka sana

hawa kwa sababu ya msongo wa rika. Ili mwanafunzi akabili matatizo ya makun-di haya, anahitaji kuwa na msimamo thabiti katika masomo yake, aishi na wa-najamii vizuri ili wasiwe vikwazo kwake.

papo kwa papo ya mitaala, mwanafunzi anasoma mada zilizopo, baada ya miezi kadhaa anaambiwa hazipo katika mtaala mpya. Inamlazimu kutafuta tena ya-

yanaathiri wanafunzi. Serikali pia ndiyo inayotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Inakuwa kikwazo pale inapochelewesha au kuto toa mikopo hiyo na kusababisha mazin-gira magumu kwa wanafunzi.

Serikali ndiyo inayosababisha mazin-gira ya kujisomea, iwapo serikali itatoa mishahara kwa walimu kwa wakati un-aostahili, walimu watakuwa na moyo wa kufundisha hivyo wanafunzi kufaulu

Ni Muhimu Wananchi Kuzifahamu Sera

Na Mtemi Zombwe

Sera ni mwongozo rasmi unatoa mwelekeo wa utendaji kwa serikali au taasisi fulani kwa kuelekeza mfumo wa mipango na mikakati mbalimbali ili ku-

sera za serikali ndio mwongozo mkuu wa utendaji, unatoa mwelekeo wa nam-

ya malengo kusudiwa. Kimsingi mikakati, mipango, sheria na kanuni mbalimbali zinazoundwa na sekta husika zinapaswa kuitafsiri sera na siyo kupingana na sera. Maana sera ndiyo dira ya ufanikishaji mipango yote na shughuli zote za kiuchumi na kijamii. Ili sera ilete tija katika jamii ni muhimu utekelezaji wake uendane na kuishiriki-sha jamii kikamilifu. Wananchi wanapas-wa kuzifahamu sera zao zote ili wawe na fursa maalumu ya kuzitekeleza. Wa-nanchi ndio wanaoweza kuzifanya sera zilete matunda au zidorore. Kama mwa-nanchi hajui sera inasema nini kuhusu namna ya kufanikisha huduma ya jamii, yeye binafsi anakosa ujasiri wa namna ya kuitekeleza vyema sera hiyo. Kwa mfano, mkulima bora anayetu-mia juhudi na rasilimali nyingi kujiletea

maendeleo kupitia kilimo ni muhimu afahamu sera inasema nini kuhusu fursa zake, pamoja na wajibu wa serikali kwa mkulima. Na fursa na misaada toka seri-kalini. Itamsaidia kuepuka ulaghai na udanganyifu wa wachache wanaoweza kutumia umbumbumbu wake juu ya sera kudhulumu haki zake.

Kwa mfano, ni watanzania wangapi wanafahamu kuwa watoto wao walio sekondari kidato cha I-II wanastahili kufundishwa na walimu waliosomea ualimu ngazi ya shahada na sio walimu wa voda fasta? Ni watanzania wan-gapi wanafahamu kuwa wanafunzi wa sekondari kuanzia kidato cha 3 hadi 6 wanapaswa kufundishwa na walimu we-nye shahada za ualimu? Hiyo ni sera ya Elimu na mafunzo ya 1995.

Wananchi tujibidiishe kuzifahamu sera zetu ili tuweze kuzitelekeza vyema na kutathmini utendaji wa viongozi wetu kupitia sera hizo. Tusipozijua sera tutas-hindwa kutathimini kama tunakwenda mbele au la. Pia tutashindwa kufuatilia uwajibikaji wa serikali yetu kwetu. Na kibaya zaidi tunakuwa na vipimo dhaifu vya elimu yetu na maendeleo yetu kwa ujumla. Tunaweza kuleta mabadiliko kwa kufuatilia sera zetu.

Barua kwa Mhariri ...

Ndugu Mhariri, Elimu ni mchakato mzima wa kuon-doa ujinga na kuongeza ufahamu juu ya mambo mbalimbali ya kimaisha na kie-limu. Elimu inaweza kuwa inayofuata au isiyofuata mfumo maalum. Ushirikiano baina ya mzazi/mlezi ni muhimu katika kumuendeleza mwanafunzi na mfumo wa Elimu: Endapo mzazi/mlezi atashirikishwa moja kwa moja katika maendeleo ya ki-jana wake, ataweza kujua ni kwa kiwan-go gani mwanafunzi anafaulu darasani, mahudhurio ya mwanafunzi na njia sa-hihi ya kumsaidia mwanafunzi aweze kutimiza malengo yake. Ushirikiano baina ya mzazi na mwana-funzi unaweza kuinua na kuendeleza elimu ya Tanzania. Hii ni kwa kuwa mfumo wa sasa wa elimu Tanzania unahitaji jitihada binafsi za kila mzazi/mlezi katika kumuwezesha mwanan-funzi kupata elimu bora. Hii ni pamoja na kwa kumpeleka shule iliyo bora kwa mazingira ya usomaji na walimu, kum-nunulia mwanafunzi nyenzo za usomaji na vitabu vya kiada na ziada. Endapo mwanafunzi na mzazi watashirikiana na mwalimu basi elimu itabadilika. Hii ni kutokana na mzazi/mlezi, mwalimu na

vilevile na mwanafunzi kutimiza wajibu

Endapo ushirikiano ni wa dhati na wenye nia thabiti ya kukuza elimu, tunaamini uwajibikaji kwa mwanafunzi utaongeze-ka na walimu wataongeza ufanisi katika ufundishaji. Hii ni kwa sababu watapata fursa ya moja kwa moja kushirikiana na mzazi/mlezi ambaye ni mwezeshaji wa mwanafunzi kwa kila upande ikiwemo maadili, nidhamu na hata uwajibikaji wa mwanafunzi kwenye fursa mbalimbali. Changamoto zinazowakabili wazazi ni kushindwa kufuatilia maendeleo ya mto-to wake shuleni. Wazazi wengi Tanza-nia wanashindwa kufuatilia maendeleo ya watoto kwa sababu ya uelewa mdogo juu ya umuhimu wa elimu, kuwaamini kupita kiasi wanafunzi, shughuli za kiu-chumi, pamoja na ulevi na uzembe. Njia sahihi ya kuondoa dhana ya utege-mezi wa mzazi au mwalimu katika kum-jenga mwanafunzi ni ushirikiano wa moja kwa moja baina ya mwanafunzi, mzazi/mlezi na mwalimu. Kama wote watatu watawajibika kwa namna zao na fursa walizonazo basi itawasaidia kum-jenga kijana bora wa kesho na kuinua kiwango cha elimu nchini Tanzania.

Joshua Mawazo – Jitegemee Sec. Dar es Salaam

Sauti ElimuTahariri

Nguvu muhimu ya kuchochea maende-leo katika jamii yeyote ni elimu bora. Elimu ambayo itawajaza wananchi

mbinu mbalimbali za kutatua matatizo, ubunifu, ujasiri wa kuhoji, kudadisi, ku-

mpya zenye kutafsiri na kuzibadili chan-gamoto kuwa fursa. Elimu ya namna hii ndiyo inajenga da-raja la maendeleo. Maana jamii kubwa ya watu itakuwa na uwezo wa kuzali-sha na kushiriki moja kwa moja katika kujenga taifa lao. Jitihada zetu za kuji-letea maendeleo hazitaweza kufanikiwa iwapo elimu ya namna hii haipo katika jamii. Na wananchi wakiwa wamelala bila kuhoji elimu yetu ya sasa inayoten-geneza vyeti bandia na wasomi bandia hali itakuwa ngumu mno.

Wananchi kwa sasa tumeridhika na hali

na ya kuiboresha elimu yetu. Tumerid-hika na vipimo dhaifu vya nini maana ya elimu na mazao yake katika jamii. Lakini ukweli unasaliti kwa kuwa na wasomi wengi wasio na tija katika jamii. Pamoja na kuelekeza jitihada zetu kwe-nye vitendeakazi kama vile majengo, madawati, sare za shule, vitabu, chaki,

pasa vilevile kuelekeza nguvu kwenye

elimu; yaani nini mtoto anapata awapo shule. Hii ni kama vile kama vile mtoto ana maarifa gani, amefahamu nini baada ya kusoma, anaweza kufanya nini, ana-jiamini, anaweza kuthubutu, anaweza kuwasiliana vizuri, anajitambua, ni mbu-nifu, ni mvumbuzi, ana jitihada za ku-fanyakazi, ni jasiri na mwadilifu.

Hivyo, watanzania tuwe makini tutu-mie muda mwingi kukaa na watoto wetu an tuwapime ili kuhakikisha wa-napata elimu kwa kutathimini viashiria vya elimu vilivyoainishwa. Na ndipo tutabaini ukweli wenyewe na kutafuta suluhisho la kudumu.

Tunajidanganya kuahirisha jukumu hili muhimu kwa kudhani kuna mtu atakuja

sawa kutokana na kunywa nadharia mfu za elimu bandia zinazothibitishwa na vipimo bandia.

Halafu eti tunaota maendeleo ndani ya utandawazi na umoja wa Afrika mashariki. Kwa mwendo huu, siku zi-jazo hakutakuwa na watanzania ndani ya soko; bali kutakuwa na vibarua, vitoweo na manamba wa kitanzania wakiwa-hudumia wageni wenye maarifa ndani ya ardhi yetu. Ndiko tunataka kuwapele-ka watoto wetu? Hapana, wananchi tu-amke tufanye mapinduzi katika elimu.

Walimu, wazazi washirikiane kuboresha elimu

Wananchi tusiridhike na elimu isiyokuwa na tija

Elimu itumike kutatua changamoto za jamii

Ndugu Mhariri,Tanzania ya leo wanafunzi ni wengi. Ukianza shule ya msingi, sekondari na vyuo vikuu wanafunzi ni wengi mno. Lakini asilimia kubwa ya wanafunzi wa-nasomea kazi, hawasomi ili waje waeli-mishe jamii na kuinua Tanzania ili iwe nchi ya wasomi.

Hii inatokana na mwanafunzi, hata kama ni wa darasa la saba ikatokea akapata kazi, basi anaona maisha ndiyo haya na ndiyo inakuwa mwisho wa ku-

hadi vyuo vikuu huwa hawaangalii nchi yao kama watanzania bali wanachojali wao ni kupata kazi yoyote ile baada ya kumaliza masomo na si kitu kingine chochote.

Utakuta watu wamesoma hadi vyuo, wametafuta kazi kwa kipindi kirefu sana

bila mafanikio. Utakuta watu hawa wa-naishi katika jamii na wanakuwa hawana tofauti na wale ambao hawajaelimika. Kwa kuwa kutokana haitumikii jamii kwa kile alichokisoma/alichojifundisha ili kuleta mabadiliko chanya.

Mwanafunzi akisoma hadi akamaliza kila kinachotakiwa kusomwa ni lazima akafanye kazi nzuri yenye mshahara mkubwa ili aweze kujikimu kimaisha. Husahau jamii inayomzunguka kwani

ndiyo hayo.

Kama wanafunzi tungekuwa tunatakiwa kusomea kazi, basi tusingesoma maso-mo yanayohusu jamii, siasa, maisha ya binadamu ya zamani, maisha tunayoishi.

Fatuma Mohamedi Kassim

Na Brigitha Dickson – Dunda Sec.Bagamoyo

Elimu ni taaluma pekee katika jamii inayogusa nyanja zote za maisha ya bi-nadamu. Inatoa mtu kwenye ujinga na kumfanya awe muelewa. Mtazamo na maoni yangu yatakuwa katika sehemu kuu tano: Kwanza, ili elimu nchini ipande inabidi mitaala ya masomo ibadilishwe mara kwa mara ili kuendana na wakati. Kuhu-su suala la ukariri, wanafunzi wengi huwa wanasoma kwa staili ua kukariri na siyo kuelewa. Hivyo mitaala ikibadil-ishwa mara kwa mara itamjengea mwa-nafunzi uelewa. Pili, serikali iongeze alama za kufaulu kutoka 30% hadi 41% ili kuwapa wana-funzi hamasa ya kujisomea. Tatu, lazima serikali ijenge maabara na maktaba na kuweka zana zote za ufundishaji katika kila shule ili kuon-

Nini Kifanyike Kuboresha Elimu?

geza ufaulu. Vitu vyote hivi vikiwepo, wanafunzi watatumia na kuelewa zaidi masomo yao na hatimaye kufanya vizuri na kupandisha kiwango cha elimu hapa nchini kama nchi za nje. Nne kuwe na walimu wenye taaluma inayotosha ili kuweza kuwafundisha wanafunzi na wakaelewa barabara na kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho bila ya kuiba au kukariri majibu ya mitihani.

Suala la tano ni kudhibiti uvujaji wa miti-hani. Siku hizi mitihani imekuwa ikivuja kutokana na uzembe na uvivu wa wana-funzi ambao hawataki kusoma na wana-taka kupata vitu kwa ulaini. Mwisho wa siku baada ya kuiba mitihani, wanahi-timu bila ujuzi na sifa. Mfano, mwalimu amehitimu chuo lakini mitihani yote ameiba halafu anapangiwa shule tayari kuanza kazi na mwalimu huyo hana sifa, hiyo itasababisha kushuka kwa elimu nchini.

© HakiElimu 2010

Elizabeth Missokia

Robert Mihayo

Agnes Mangweha

Wambura Wasira

Lilian Omary

Edwin Mashasi

HakiElimuNathan Mpangala

Unidentifi ed Artist

Tuandikie!HakiElimu SautiElimuS. L. P 79401Dar es SalaamTanzania

Maoni yako yatasaidia kuleta changamoto, kuibua mijadala na kutetea haki za wanyonge.

Simu: (022) 2151852 au 3Faksi: (022) 2152449Barua Pepe: [email protected]: www.hakielimu.org

Na Jimmy Luhende

“Kule walikuwa wanatugawia mitihani kabla ya siku ya mtihani” Maneno haya yamesemwa na mtoto ambae alikuwa anasoma shule ya binafsi ya msingi na sasa anasoma shule nyingine ya msingi inayomilikiwa na kanisa.

Nukuu ya mtoto huyu inatukumbusha kuwa lipo tatizo katika mfumo wa elimu hapa Tanzania. Nukuu imenifanya nita-fakari juu ya mchanganyiko wa sera ya elimu kwa watoto wote, elimu ya bure katika ngazi ya msingi, ushindani wa bi-ashara na maadili ya walimu.

Inapendeza kuwa na sera ya elimu in-ayotoa muongozo wa jinsi elimu itaka-vyotolewa. Pia inapendeza kuwa katika soko huria lakini inakera kuona jinsi tu-navyoshindwa kupanga sheria za mche-zo. Unawezaje kuamini kuwa elimu ya bure itatolewa na shule za umma wakati shule binafsi zinatoza ada kisha utara-jie kuwa kiwango cha elimu kitafanana. Unawezaje kuamini kuwa shule binafsi zitacheza mchezo kwa kuzingatia sheria za mchezo bila refa mwenye kiwango na kasi? Kwa haraka haraka ni lazima mtu

kidogo.

Nimesikia kuwa, katika baadhi ya shule za msingi za watu binafsi, walimu wa-napewa maelekezo kuwa ni lazima wa-nafunzi washinde mtihani wa somo lake na kuwa wanafunzi wakifaulu anaji-

hakikishia ajira yake. Kwa mantiki hiyo mwalimu huyu atajitahidi kufundisha “twisheni” na akibanwa sana au akiwa hana kiwango cha kutosha kwa sababu nae alipita kwa ujanja ujanja na ajira anaitaka, anaweza kukiuka maadili ya kazi ya ualimu. Wamiliki wa shule hizi wanahitaji kupata faida, hata mimi ni-kiwa na shule bila shaka lengo litaku-wa kutengeneza fedha kwanza. Hawa wamiliki sio tatizo langu sana. Tatizo ni kuwa sheria za mchezo hazina refa kwani nae anataka kushinda!

Kimsingi Tanzania inaweza kubadili baadhi ya sera zake. Ni lazima viongozi wetu wafanye kazi ya kutetea watoto wa Taifa hili, siyo katika majukwaa! Ni lazi-ma waoneshe ujasiri na wawe tayari ku-fanya maamuzi magumu katika sekta ya elimu. Nina imani kuwa wakisema kuwa elimu ya msingi ni bure basi iwe ni bure hata kwa hao wenye shule binafsi za msingi. Kama hawataki waache hiyo bi-ashara na wafanye biashara katika ngazi ya sekondari! Wanaweza kuwa na shule za msingi na sekondari lakini wahakiki-she kuwa elimu ya msingi ni BURE! Tunahitaji viongozi wenye ujasiri wa kusema na kulisimamia jambo hili.

Tusikubali kuwa watumwa wa ujinga na mazoea. Ni sisi wenyewe tunaoweza ku-leta mabadiliko siyo mtu mwingine ku-toka Afrika ya Kusini au China! Kama mfumo fulani hautupeleki tunakotaka ni kwa nini tuukumbatie?

Pata machapisho mapya kutoka HakiElimu. Tuandikie!

Hakelimu na jamii kwa ujumla. Tunafanya hivyo kwa kuwezesha jamii kupata habari, kubadili shule na mfumo wa uundaji wa sera; kuchochea ubunifu wa mijadala ya

wadau ili kuendeleza manufaa ya pamoja na kuzingatia haki za jamii. Shukurani kwa wachangiaji, wapiga picha, wachoraji na kwa wote walioandaa habari zilizochapishwa katika jarida hili. Unaruhusiwa kunakili sehemu yoyote ya jarida hili kwa minajili isiyo ya kibiashara. Unachotakiwa kufanya no kunukuu chanzo cha seh-emu iliyonakiliwa na kutuma nakala mbili kwa HakiElimu.

Wanatugawia mitihani kabla ya siku za mitihani