nafasi ya mwanafunzi katika kuboresha elimu -...

4
HakiElimu •Mtaa wa Mathuradas Na. 739 • SLP 79401 Dar es Salaam, Tanzania • Simu: +255 22 2152449 • Barua pepe: info@hakielim u.o rg • Tovuti: www.hakielimu.org Toleo la 29, 2011 | ISSN 1821 5076 SautiElimu Na Happiess Richard, Mkuu-Rombo Kwanza natoa shukrani zangu za dhati kwa mashirika yanayotoa mchango katika uboreshaji wa elimu. Hili ni jambo la busara sana hasa kwa mashirika husika. Nikiwa miongoni mwa wanaharakati wa elimu, nimefarijika sana kupata nafasi ya kuwa mwanaharakati wa HakiElimu. Yapo mambo mengi sana yanayoikumba jamii kielimu hasa nikiangalia katika mazingira ya hapa kijijini kwetu. Kuna matatizo mengi ya kiuchumi hapa kijijini ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira na wazazi wengi kuwa chini kiuchumi. Wazazi na walezi wamekuwa wakihangaika sana katika kuendeleza watoto shuleni kwa kutumia kipato kidogo kwa ajili ya malezi na malipo ya shule. Mfano mzazi anafanya kazi ya mama lishe, hapo hapo hana ushirikiano na mwenza wake. Yaani baba ambae anatakiwa kuwa mkuu wa familia hajishughulishi na kazi; mzigo wote wa utafutaji na malezi unamuangukia mama peke yake. Maisha haya duni yamekuwa yakiwakatisha tamaa watoto kuendelea mbele kimasomo. Rushwa pia ni tatizo kubwa sana katika nchi yetu. Rushwa ni kikwazo cha maendeleo katika nchi. Shule nyingi zinakosa maendeleo kutokana na kukosa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, maabara, maktaba n.k. Mabilioni ya fedha yamepotezwa kwa njia zisizoeleweka ambazo iwapo zinge ingizwa katika akiba za shule, hata kwa kusomesha wale wasiojiweza zingesaidia kuinua elimu nchini. Jamani inauma sana hasa kwa sisi wanafunzi tunaonyanyasika kielimu. Tunasoma kwa shida, tunaishi kwa shida, hata kazi hatupati japo tuna elimu ya kutosha. Vile vile wapo wazazi ambao hawapendi watoto wao wa kike wasome. Kwa mfano mtoto anafaulu kwenda Sekondari lakini mzazi anakataa kumpeleka shule kwa vile mtoto aliyefaulu ni wa kike, mzazi anaona huyo mtoto hana faida akisomeshwa. Kitu hiki siyo kizuri kabisa. Watoto wa kike wana haki ya kusoma kama wa kiume. Ubebaji wa mimba mashuleni pia ni chanzo cha ukosefu wa elimu bora. Sheria za shule haziruhusu mwanafunzi aliyebeba mimba kuendelea na masomo. Wazazi nao wanakuwa hawana uwezo wa kumuendeleza kimaisha. Matokeo yake ni kuwa mtoto huyu anaishia kutanga na njia. Ushauri wangu ni kuwa, serikali pamoja na walimu waruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo yao hadi watakapojifungua. Vile vile, ni vizuri jamii ijue nini maana ya elimu na iwe mstari wa mbele kuwasaidia watoto kupata elimu bora. Pia serikali ijaribu kuangalia ni nini chimbuko la kukosa elimu bora na ni kitu gani kifanyike ili kuboresha elimu. ...ni vizuri jamii ijue nini maana ya elimu na iwe mstari wa mbele kuwasaidia watoto kupata elimu bora.Mambo Yanayochangia Wanafunzi Kukosa Elimu Bora Ni muhimu wazazi/walezi watenge muda kwa ajili ya kukaa na watoto na kukagua kazi zao za shule Na Tumwesige Ngeiyamu, Dar es Salaam Elimu bora ni jambo la msingi sana ili kujenga taifa lenye uwezo wa kustahimili ushindani wa kibiashara usiokuwa na mipaka. Hata hivyo, katika taifa changa kama Tanzania, kunahitajika mkakati wa kipekee wa kuboresha elimu kwa kushirikisha taasisi na mashirika yanayojihusisha na elimu, serikali, wazazi, wanafunzi na jamii kwa ujumla. Wanafunzi wana wajibu mkubwa katika kujenga maadili mema wakati wako shuleni. Maadili yawe mazuri yaliyojikita katika taratibu zinazokubalika na jamii nzima kwa faida ya taifa na vizazi vijavyo. Mwanafunzi bora mwenye maadili mema hana budi kujenga utamaduni wa kujitegemea; hasa katika masomo; hili husaidia kujenga moyo wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii. Kazi kubwa ya mwalimu ni kumwelekeza mwanafunzi kisha mwanafunzi anatakiwa kufuatilia kwa undani ili kupanua ufahamu wa jambo kwa kusoma vitabu. Hili ni jambo la msingi sana kwa sababu umejengeka utamaduni hasi miongoni mwa wanafunzi wa Tanzania, wa shule za msingi hadi vyuo vikuu, kupenda kusoma kwa ajili ya kufaulu mitihani tu, tena kwa njia rahisi maarufu vyuoni iitwayo kudesa. Wanafunzi wana wajibu wa kuwapenda, kuwaheshimu na kuwasikiliza walimu wao. Siri iliyopo katika hili ni kwamba, kumheshimu mwalimu kunamfanya ajitoe zaidi na kuonesha njia iliyo bora zaidi. Huu ndio msingi wa maadili mema kwani husaidia wanafunzi kuwa na utamaduni wa kuiheshimu jamii watakayoitumikia baada ya kuhitimu masomo. Aidha, ni muhimu kwa wanafunzi kushirikiana na jamii wanayoishi nayo ili kuyajua mahitaji na changamoto zinazoikumba jamii. Mwanafunzi anapaswa kujenga utamaduni wa ushirikiano wa karibu sana na wenzake kuanzia nyumbani, shuleni kisha kushiriki shughuli za kitaifa ili jamii ishuhudie umuhimu wa elimu anayoipata. Vilevile kujikubali na kujitambua ni jambo la msingi katika kuinua elimu nchini. Wanafunzi wengi kwa sasa wanazidiwa na ushawishi wa nguvu za utamaduni wa nchi za magharibi. Wanafunzi hawa wanatakiwa kujielewa kuwa wapo katika nchi ya ulimwengu wa tatu na ili kujikwamua hawana budi kuthamini utamaduni wa nchi yao. Ni wajibu wa mwanafunzi kuhoji na kuelewa ukweli wa nguvu za ubepari wa nchi za Magharibi kwani hata ukosefu wa maadili hutokana na ushawishi wa siasa za nchi za Magharibi. Ni ukweli usiopingika kuwa maadili ni nguzo ya utamaduni wa jamii na elimu bora ni ile inayoleta manufaa kwa jamii na si vinginevyo. Nafasi ya Mwanafunzi Katika Kuboresha Elimu Ni wajibu wa wanafunzi kuhoji na kuelewa ukweli wa nguvu za ubepari wa nchi za Magharibi kwani hata ukosefu wa maadili hutokana na ushawishi wa siasa za nchi za Magharibi

Upload: others

Post on 08-Oct-2019

81 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Nafasi ya Mwanafunzi Katika Kuboresha Elimu - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/SautiElimu 29.pdf · mwalimu kunamfanya ajitoe zaidi na kuonesha njia iliyo bora zaidi

HakiElimu •Mtaa wa Mathuradas Na. 739 • SLP 79401 Dar es Salaam, Tanzania • Simu: +255 22 2152449 • Barua pepe: [email protected] • Tovuti: www.hakielimu.org

Toleo la 29, 2011 | ISSN 1821 5076

SautiElimu

Na Happiess Richard, Mkuu-Rombo

Kwanza natoa shukrani zangu za

dhati kwa mashirika yanayotoa

mchango katika uboreshaji wa

elimu. Hili ni jambo la busara sana

hasa kwa mashirika husika. Nikiwa

miongoni mwa wanaharakati wa

elimu, nimefarijika sana kupata

nafasi ya kuwa mwanaharakati wa

HakiElimu.

Yapo mambo meng i sana

yanayoikumba jamii kielimu hasa

nikiangalia katika mazingira ya hapa

kijijini kwetu. Kuna matatizo mengi

ya kiuchumi hapa kijijini ikiwa ni

pamoja na ukosefu wa ajira na

wazazi wengi kuwa chini kiuchumi.

Wazazi na walezi wamekuwa

wak ihanga ik a s ana k a t i k a

kuendeleza watoto shuleni kwa

kutumia kipato kidogo kwa ajili ya

malezi na malipo ya shule.

Mfano mzazi anafanya kazi ya

mama lishe, hapo hapo hana

ushirikiano na mwenza wake. Yaani

baba ambae anatakiwa kuwa mkuu

wa familia hajishughulishi na kazi;

mzigo wote wa utafutaji na malezi

unamuangukia mama peke yake.

Maisha haya duni yamekuwa

yakiwakatisha tamaa watoto

kuendelea mbele kimasomo.

Rushwa pia ni tatizo kubwa sana

katika nchi yetu. Rushwa ni kikwazo

cha maendeleo katika nchi. Shule

nying i z inakosa maendeleo

kutokana na kukosa vifaa vya

kufundishia na kujifunzia, maabara,

maktaba n.k. Mabilioni ya fedha

y a m e p o t e z w a k w a n j i a

zisizoeleweka ambazo iwapo zinge

ingizwa katika akiba za shule, hata

kwa kusomesha wale wasiojiweza

zingesaidia kuinua elimu nchini.

Jamani inauma sana hasa kwa sisi

wanafunzi tunaonyanyasika kielimu.

Tunasoma kwa shida, tunaishi kwa

shida, hata kazi hatupati japo tuna

elimu ya kutosha.

Vile vile wapo wazazi ambao

hawapendi watoto wao wa kike

wasome. Kwa mfano mtoto

anafaulu kwenda Sekondari lakini

mzazi anakataa kumpeleka shule

kwa vile mtoto aliyefaulu ni wa kike,

mzazi anaona huyo mtoto hana

faida akisomeshwa. Kitu hiki siyo

kizuri kabisa. Watoto wa kike wana

haki ya kusoma kama wa kiume.

Ubebaji wa mimba mashuleni pia ni

chanzo cha ukosefu wa elimu bora.

Sheria za shule haziruhusu

mwanafunzi aliyebeba mimba

kuendelea na masomo. Wazazi nao

wanakuwa hawana uwezo wa

kumuendeleza kimaisha. Matokeo

yake ni kuwa mtoto huyu anaishia

kutanga na njia.

Ushauri wangu ni kuwa, serikali

pamoja na walimu waruhusu

wanafunzi waliopata ujauzito

kuendelea na masomo yao hadi

watakapojifungua.

Vile vile, ni vizuri jamii ijue nini

maana ya elimu na iwe mstari wa

mbele kuwasaidia watoto kupata

elimu bora. Pia serikali ijaribu

kuangalia ni nini chimbuko la

kukosa elimu bora na ni kitu gani

kifanyike ili kuboresha elimu.

“...ni vizuri jamii

ijue nini maana ya elimu na iwe mstari wa mbele kuwasaidia watoto kupata elimu

bora.”

M a m b o Y a n a y o c h a n g i a W a n a f u n z i K u k o s a E l i m u B o r a

Ni muhimu wazazi/walezi watenge muda kwa ajili ya kukaa na watoto na kukagua kazi zao za shule

Na Tumwesige Ngeiyamu, Dar es Salaam Elimu bora ni jambo la msingi sana ili kujenga taifa lenye uwezo wa kustahimili ushindani wa kibiashara usiokuwa na mipaka. Hata hivyo, katika taifa changa kama Tanzania, kunahitajika mkakati wa kipekee wa kuboresha elimu kwa kushirikisha taasisi na mashirika yanayojihusisha na elimu, serikali, wazazi, wanafunzi na jamii kwa ujumla. Wanafunzi wana wajibu mkubwa katika kujenga maadili mema wakati wako shuleni. Maadili yawe mazuri ya l i yo j i k i t a k a t i k a t a ra t ibu zinazokubalika na jamii nzima kwa faida ya taifa na vizazi vijavyo. Mwanafunzi bora mwenye maadili mema hana bud i ku jenga utamaduni wa kujitegemea; hasa katika masomo; hili husaidia kujenga moyo wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

Kazi kubwa ya mwalimu ni kumwelekeza mwanafunzi kisha mwanafunzi anatakiwa kufuatilia

kwa undani ili kupanua ufahamu wa jambo kwa kusoma vitabu. Hili ni jambo la msingi sana kwa sababu umejengeka utamaduni hasi miongoni mwa wanafunzi wa Tanzania, wa shule za msingi hadi vyuo vikuu, kupenda kusoma kwa ajili ya kufaulu mitihani tu, tena kwa njia rahisi maarufu vyuoni iitwayo kudesa. Wanafunzi wana wajibu wa kuwapenda, kuwaheshimu na kuwasikiliza walimu wao. Siri iliyopo katika hili ni kwamba, kumheshimu mwalimu kunamfanya ajitoe zaidi na kuonesha njia iliyo bora zaidi. Huu ndio msingi wa maadili mema kwani husaidia wanafunzi kuwa na utamaduni wa kuiheshimu jamii watakayoitumikia baada ya kuhitimu masomo. Aidha, ni muhimu kwa wanafunzi kushirikiana na jamii wanayoishi nayo ili kuyajua mahitaji na changamoto zinazoikumba jamii. Mwanafunzi anapaswa kujenga

utamaduni wa ushirikiano wa karibu sana na wenzake kuanzia nyumbani, shuleni kisha kushiriki shughuli za kitaifa ili jamii ishuhudie umuhimu wa elimu anayoipata. Vilevile kujikubali na kujitambua ni jambo la msingi katika kuinua elimu nchini. Wanafunzi wengi kwa sasa wanazidiwa na ushawishi wa nguvu za utamaduni wa nchi za magharibi. Wanafunzi hawa wanatakiwa kujielewa kuwa wapo katika nchi ya u l imwengu wa tatu na i l i kujikwamua hawana budi kuthamini utamaduni wa nchi yao. Ni wajibu wa mwanafunzi kuhoji na kuelewa ukweli wa nguvu za ubepari wa nchi za Magharibi kwani hata ukosefu wa maadili hutokana na ushawishi wa siasa za nchi za Magharibi. Ni ukweli usiopingika kuwa maadili ni nguzo ya utamaduni wa jamii na elimu bora ni ile inayoleta manufaa kwa jamii na si vinginevyo.

Nafasi ya Mwanafunzi Katika Kuboresha Elimu

Ni wajibu wa wanafunzi kuhoji na kuelewa ukweli wa nguvu za ubepari wa nchi za Magharibi kwani hata ukosefu wa maadili hutokana na ushawishi wa siasa za nchi za Magharibi

Page 2: Nafasi ya Mwanafunzi Katika Kuboresha Elimu - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/SautiElimu 29.pdf · mwalimu kunamfanya ajitoe zaidi na kuonesha njia iliyo bora zaidi

Na Perecy Paulo Ugula, Iringa Jamii imeingia katika zama ambazo zinaitwa utandawazi uliotokana na sera za ubepari. Uhalisia wa maisha umedorora na watu wanaanguka hata kushika mafundisho ya dini. Wengine wamegeuza miili yao kuwa biashara. Agosti 12, 2011 nilikuwa na True Vision Production ya Dar es Salaam katika shule ya sekondari ya Mtwivila, mkoani Iringa tukiandaa kipindi cha Tafakari Time, kipindi maarufu katika televisheni ya TBC1, ambapo mada iliyojadiliwa ilikuwa: “Kushuka kwa maadili miongoni mwa wanafunzi mashuleni, nini kifanyike?” Katika kipindi hiki wanafunzi, walimu, wanaharakati na wanajamii walichangia na kusema kwamba kushuka kwa maadili kunahusisha mambo mengi, ikiwa ni pamoja na mavazi – wanafunzi wa kike kuvaa sketi fupi, wa kiume kuvaa suruali za kubana au kuzishusha kupita kiuno. Suala la maadili pia huhusisha wanafunzi kutowahi shuleni au kutokuwepo darasani h ivyo kutoshiriki vipindi na masomo mbalimbali, wanafunzi kuvuta bangi, sigara na madawa mengine ya kulevya, kutukana walimu na kutopeleka taarifa za maendeleo yao ya shule nyumbani n.k. Wazazi, walimu, wanafunzi, serikali na jamii nao walitajwa kuhusika na kushuka kwa maadili miongoni mwa wanafunzi. Kwa mfano ilielezwa kwamba wazazi hawataki kufika shuleni kufuatilia maendeleo ya watoto wao na pia hawashiriki mikutano ya wazazi na uongozi wa shule. Baadhi ya walimu walituhumiwa kushiriki ngono na wanafunzi wa kike. Pia baadhi ya walimu wa kike nao wana upungufu wa maadili kwa kuwatongoza wanafunzi wa kiume. Wanafunzi walisemwa kwa kuiga tabia mbaya za nchi za magharibi kupitia vyombo vya habari kama runinga, mitandao ya ngono, magazeti ya udaku na miradi ya asasi zisizokuwa za kiserikali ambayo inahimiza mikusanyiko ya wanafunzi bila udhibiti wa mienendo yao. Washiriki wa kipindi kwa waliilaumu serikali kwa kutokuwa na sheria inayotilia mkazo maadili ya vijana na kuwa kama ipo usimamizi wake ni butu. Hakuna utaratibu wa kufuatilia wanafunzi wanatumiaje teknolojia ya mawasiliano, yaani kompyuta, simu, kamera na vifaa vingine vya elekroniki vinavyoweza kubeba picha, kutuma ujumbe n.k. Jamii ililaumiwa kutowakanya wanafunzi kufika katika klabu za pombe, kutembelea maeneo ya starehe, au kufumbia macho utoro

wa wanafunzi. Katika mjadala, ilionekana kwamba upungufu wa maadili kwa mwanafunzi unaathiri maendeleo yake kimasomo. Mwanafunzi mwenye msingi bora

wa maadili huwa na maendeleo kimasomo na anafanikiwa kuvuka ngazi moja ya elimu kwenda nyingine. Maendeleo yake huwa chanya! Mwanafunzi asiye na maadili huvutwa nyuma na matendo

yake ya kimaadili. Huonekana kero katika jamii. Husutwa. Hutajwa majina ya udhalilishaji. Hulaaniwa. Hutengwa. Je, ni haki jamii kufanya hivyo kwa mtoto huyu bila yenyewe kuchukua jukumu la malezi

kwanza? Napenda kutoa wito kwa jamii kuwa ni jukumu la msingi la jamii kushiriki katika malezi ya vijana wetu na hasa wanafunzi katika ngazi zote za

elimu. Jamii irudi katika utaratibu wa zamani wa kushiriki malezi ya watoto hata kama wao si wazazi wa kuwazaa. Jamii inaposhiriki kumlea mtoto, inamjengea uzalendo na heshima ya juu ya uwajibikaji kwa jamii husika. Inamsaidia mtoto kuwa na akili ya utulivu katika kuzingatia elimu; pia kuwa mtiifu na anayejipokea. Jamii isijitenge na kukaa mbali katika kushiriki katika malezi. Malezi haya yanaweza kufanyika kwa njia na mbinu nyingi tofauti tofauti. Jamii i k a t a e w a t o t o k u o n e k a n a barabarani wakati wa saa za shule, na wakati hakuna likizo. Jamii itoe taarifa shuleni inapoona watoto wanazunguka zunguka mitaani, au mjini bila sababu maalumu. Aidha, jamii ipige kelele kwa serikali kutunga na kusimamia sheria z i n a z o h i m i z a w a n a f u n z i kutokuwepo, kutofanya, au kuangalia sinema, mitandao, na mambo yote yanayoharakisha mmomonyoko wa maadili ikiwemo miziki, picha za ngono na mavazi yasiyofaa. Halikadhalika, ziwepo kamati ndogo ndogo zinazofuatilia maendeleo na maadili ya watoto kila mara katika ngazi ya kata na kijiji, ambako jamii husika huwafahamu hawa watoto/vijana.

Maadili ya wanafunzi na elimu bora, kwa nini jamii imekaa mbali?

Na. Benezegwa Rushita, Mtwara Suala la kushuka kwa nidhamu ni suala ambalo linakua kwa kasi nchini Tanzania. Suala hil i linachangiwa na mambo mengi sana. Hii husababisha kuanguka kwa nidhamu na kushuka kwa kiwango cha taaluma. Kushuka h u k u k w a n i d h a m u kunasababishwa n mambo yafuatayo: Kukua kwa utandawazi kwa kasi. Suala hili huleta muingiliano mkubwa wa u t a m a d u n i w a n c h i mbalimbali. Vijana wengi huwa katika kipindi cha mpito ambacho ni rahisi kwao kuiga kila wanaloliona hasa yanayotoka kwa watu wenye mwito katika jamii kama vile wasanii. K u k u a k w a mawasiliano ya s i m u . P am o j a n a umuhimu mkubwa wa m a wa s i l i a n o y a s i m u , kumekuwa na matumizi mabaya sana ya simu kwa vijana kwani

wanazitumia kwa mambo ambayo si mazuri kwa jamii. Kuongezeka kwa familia za mzazi mmoja. Kwa kiasi kikubwa hali hii husababisha kupungua au hata kukosa kabisa malezi ya kutosha

h i v y o

k u m f a n y a mtoto kuwa huru kuamua lolote liwe

zuri au baya. Walimu kukosa mafunzo ya kutosha. Hili linahusu Wizara husika moja kwa moja. Ni muhimu walimu wapewe mafunzo mara kwa mara ya saikolojia ili kupata uwezo zaidi wa kutambua mabadiliko ya tabia kwa wanafunzi na kuchukua hatua haraka kabla mtoto

hajaharibika kabisa. Mila na desturi potofu. Suala hili pia linachangia kushuka kwa nidhamu ya wanafunzi pale

inapotumika vibaya. Kwa mfano kuna mila za jando na

unyago kwa makabila mengi ya kusini ambayo pamoja na mambo mazuri mengi yanayofundishwa pia

yapo ambayo hayafai kwani yanapotosha; hususani suala la

mahusiano ya mwanaume na mwanamke.

Hivyo basi suala la kushuka kwa maadili ni suala mtambuka kwani halisababishwi na mtu wala taasisi moja bali ni suala

linalogusa jamii kwa upana wake. Hivyo kuliondoa kwake linahitaji pia ushirikiano wa jamii nzima pamoja na serikali.

“Mwanafunzi asiye na maadili huvutwa nyuma na matendo yake. Huonekana kero katika jamii. Husutwa. Hutajwa majina ya udhalilishaji. Hulaaniwa. Hutengwa. Je, ni haki jamii kufanya hivyo kwa mtoto huyu bila yenyewe kuchukua jukumu la malezi kwanza?”

Tushirikiane kukabili Kushuka Kwa Nidhamu ya Wanafunzi

Page 3: Nafasi ya Mwanafunzi Katika Kuboresha Elimu - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/SautiElimu 29.pdf · mwalimu kunamfanya ajitoe zaidi na kuonesha njia iliyo bora zaidi

Na. Juma Rchard Okumu, Mara Nidhamu ni jumla ya mambo anayofanya mtu katika mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na uvaaji wa nguo, utumiaji wa lugha, salam, utanashati pamoja na tabia. Nidhamu bora ni yale matendo yote mema/mazuri anayofanya mtu katika mazingira yake kama kuvaa vizuri, lugha nzuri, tabia njema ya kupenda kusalimia watu wakubwa au wadogo, wazazi na walimu, usafi na kutii sheria za shule. Utovu wa nidhamu ni jumla ya mambo yote mabaya anayofanya mtu katika mazingira mbalimbali kama vile lugha chafu, uvaaji mbaya wa nguo, kuiba, utumiaji wa madawa ya kulevya ikiwemo bangi na sigara; hali kadhalika kudharau wengine, kutosalimia watu na kuongea na simu darasani pamoja na kuvunja sheria za shule. Vyanzo vya utovu wa nidhamu shuleni: Malezi mabaya kwa baadhi ya wazazi au walezi: Baadhi ya wazazi hasa wenye vipato hupenda kuwaridhisha watoto wao kwa kuwapa kila kitu ambacho mtoto anahitaji; mfano simu, pesa nyingi n. k. Utandawazi: Baadhi ya watoto wetu hasa waishio mijini hupenda kuangalia picha zisizofaa katika wavuti pamoja na mabanda ya video; hii huwaharibu kisaikolojia na kimaadili. Utumiaji wa madawa ya kulevya: Baadhi ya watoto wetu hupenda kutumia madawa ya kulevya zikiwemo bangi na sigara bila ya kutambua madhara yake. Hatimaye w a t o t o h a w a h u a n z a kuchanganyikiwa akili na kuanza

kuwa na tabia mbaya ya kutukana hovyo na ugomvi pasipo sababu. Kuiga mambo ya mataifa ya magharibi: Kwa kawaida mtoto huj ifunza kutokana na vitu anavyoviona. Kwa sababu ya sayansi na teknolojia hivi sasa, mtoto hufanya mambo kwa vile ameona huko Ulaya au Marekani. Mfano wavulana kuvaa ‘kata k’ na was ichana ‘ v im in i ’ wak ida i wanakwenda na wakati. Tamaa na vishawishi: Baadhi ya watoto wetu hasa wa kike, hupenda kushindana kimavazi na kujiona huyu mrembo zaidi kupita yule. Kutamani kula vizuri chipsi na kuku na kudandia lifti ambazo matokeo y a k e n i k u p a t a m i m b a

zisizotarajiwa. Aidha, baadhi ya wato to wa k ike n i rah is i kushawishiwa na kurubuniwa na wanaume. Nini kifanyike: Vikao vya mara kwa mara vya ‘school baraza’ vitasaidia kutambua matatizo waliyonayo wanafunzi na kuwapa zawadi wanafunzi wenye nidhamu bora. Hii ingesaidia kuchochea wanafunzi wengine kuwa na nidhamu nzuri hapo shuleni. Elimu ya malezi itolewe kwa wazazi na wanafunzi juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya. Kuwe na school baraza mara kwa mara sambamba na utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wenye nidhamu bora. Kutungwe sheria ndogo ndogo

zitakazodhibiti watoto kuangalia picha za ngono kwenye wavuti na mabanda ya video. Kuacha kuiga tamaduni za nje kiholela.

Na Alfonsia Samuel Mbano, Songea Elimu ni jambo lolote analoambiwa mtu au jamii kwa lengo la kuelimishwa na kuelewa. Kuna sehemu nyingi ambazo unaweza kupata elimu kwa mfano katika jamii au shuleni. Elimu ni kitu cha muhimu sana katika maisha ya binadamu kwa sababu humtoa mtu katika hali ya ujinga na kwenda katika hali ya uerevu. Usipoweza kuwa na elimu maisha yako yataweza kuwa magumu zaidi kwa sababu hutaweza kubuni au kufikiri kitu kwa haraka zaidi. Mwanafunzi n i mtu yeyote anayepata elimu au mafunzo toka kwa mwalimu au jamii husika. Zifuatazo ni baadhi ya sifa a n a z o p a s w a k u w a n a z o mwanafunzi bora: Awe na nidhamu. Hii ni moja ya sifa muhimu anazopaswa kuwa

nazo mwanafunzi bora kwa sababu mambo ya shule na nidhamu huenda pamoja. Mwanafunzi asipokuwa na nidhamu kwa mwalimu hataweza kupendwa kamwe na pia mwalimu akifundisha darasani hataweza kuelewa vizuri kwa sababu hapendani na mwalimu wake. Awe na ushirikiano. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Mwanafunzi anapaswa kuwa na ushirikiano na wenzake au na mwalimu wake ili apate kufanikiwa zaidi katika masomo. Awe mdadisi. Katika kusoma udadisi kwa wanafunzi ni muhimu sana. Hii ni kwa sababu huwezi kukaa darasani kusubiri kila kitu atafsiri au atafute mwalimu na kisha akuletee. Kutafuta baadhi ya mambo ya kielimu na kuanza kupitiapitia vitabu mbalimbali huongeza ufaulu wa darasani.

Awe na mazoea ya kuwahi s h u l e n i . M w a n a f u n z i anapochelewa shule huweza kupata adhabu za kila aina. Mfano wa adhabu hizo ni kuchimba shimo la taka, kumwagilia maua, kupigwa viboko na kadhalika. Hivyo huweza kukosa vipindi na hivyo kutokuwa mwanafunzi bora darasani. Awe na ubunifu. Katika jambo la elimu wanafunzi wengi siyo wepesi wa kutafuta vifaa ya masomo mbalimbali. Baadhi yao hukaa na kusubiri kila kitu toka kwa mwalimu. Ni nadra mwanafunzi kufanikiwa kwa kumtegemea mwalimu kwa kila kitu. Hizo ndizo sifa za mwanafunzi bora anayejali elimu. Kwa kifupi ni nidhamu, ushirikiano, udadisi, kuwahi shule na ubunifu. Bila vitu vyote hivi mwanafunzi kuvifuata hawezi kuwa mwanafunzi.

Sifa Anazopaswa Kuwa Nazo Mwanafunzi Bora

“...Vikao vya mara

kwa mara vya ‘school baraza’ vitasaidia kutambua matatizo w a l i y o n a y o

wanafunzi... ”

Nini vyanzo vya Kuporomoka Kwa Nidhamu ya Wanafunzi?

Na Rehema Ngelekele, Mkuranga Mwanafunzi akiwa hana nidhamu shuleni basi mitaani na nyumbani ndio zaidi. Hali hii ni kweli ipo na imekuwa kero kubwa kwa walimu; inafikia mwalimu anakosa amani. Pia baadhi ya walimu kutaniana na kuwatania wanafunzi inachangia mwanafunzi kutokuwa na nidhamu. Mawasiliano duni kati ya mzazi au mlezi na walimu ili kufuatilia m wa n a f un z i h u y o s h u l en i huchangia kuporomoka kwa maadil i. Baadhi ya wazazi, wamefikia hatua ya kugombana na mwal imu wanapo wakemea wanafunzi wakati makosa ni ya wanafunzi. Wanafunzi wengi wamejiingiza katika makundi mabaya, kuvuta

bangi na dawa za kulevya. Hivyo vyote vinachangia utovu wa nidhamu. Pamoja na faida za utandawazi ikiwa ni pamoja dunia kuwa kama kijiji kumekuwa na kuiga utamaduni wa nje kama Ulaya na Marekani. Hii huchangia watoto wetu kusahau mila na desturi za nyumbani. Walimu kupuuzia vipindi darasani na kutofundisha vingine kabisa huwafanya mwanafunzi kupata muda mwingi kucheza nje ya eneo la shule na pia kutosikiliza wakubwa na walimu. Uondoaji wa adhabu ya viboko mashuleni pia umesababisha kupungua kwa nidhamu kwa sababu mwanafunzi akifanya kosa lolote anajua hataadhibiwa.

Hatuwezi Kuboresha Elimu Bila Kuboresha Nidhamu

Ni wajibu wako kama mzazi kuhafahamu mtoto wako anaenda wapi na kukaa na akina nani ili kuml inda as ipoteze maadili

Frank Tobadi mwenye umri wa miaka 16 anasoma katika shule ya sekondari Msonga kidato cha pili. Amekuwa mwanafunzi bora katika shule hiyo kwa miaka miwili mfululizo akishika namba moja . Tukiwapa watoto wetu malezi bora hakuna kisichowezekana.

Page 4: Nafasi ya Mwanafunzi Katika Kuboresha Elimu - hakielimu.orghakielimu.org/files/publications/SautiElimu 29.pdf · mwalimu kunamfanya ajitoe zaidi na kuonesha njia iliyo bora zaidi

Na. Juma Richard Okumu, Mara Ningependa kuzungumzia ujumbe wangu juu ya nidhamu ya mwanafunzi katika maisha ya b inadamu yeyo te mwenye mafanikio au mwenye heshima. Duniani kote lazima ukute heshima hiyo inatokana na nidhamu aliyokuwa nayo. Lakini sasa nchini mwetu nidhamu ya mwanafunzi imekuwa ni kitu adimu sana. Chanzo cha nidhamu kushuka kwa upande wangu ni serikali pamoja na wazazi. Kwa upande wa serikali kufuta adhabu ya viboko katika shule ni moja ya sababu ya kupungua n idhamu; Ser ika l i imempa mwanafunzi uhuru mkubwa sana kiasi kwamba mwanafunzi anaweza kufanya makosa akiamini kwamba hata akiadhibiwa basi si zaidi ya

voboko vitatu. Hii kwa namna moja au nyingine huweza kumpa mwanafunzi nafasi ya kujijengea utovu wa nidhamu. Kwa upande wa wazazi ambao ndiyo asilimia kubwa sana, wameshindwa kuyasimamia maadili ya watoto wao ipasavyo na kuamua kuziachia runinga na mitandao kazi ya kuwafunza watoto wao maadili. Miaka ya nyuma mtu yeyote alikuwa na nafasi ya kusimamia nidhamu za wanafunzi. Kwa mfano mtu alipomkuta mwanafunzi mitaani nyakati za masomo alikuwa na nafasi ya kumuadhibu kwa viboko mpaka shule ama nyumbani kwao. Lakini kwa sasa mtu akijaribu kufanya hivyo hushitakiwa ama ugomvi waweza kuzuka baina yake na mzazi wa mtoto aliyeadhibiwa.

Ningependa kutoa wito kwa wazazi na serikali kudhibiti kuporomoka kwa nidhamu ya wanafunzi.

Turejee miaka ya babu zetu na tujiulize walifanya nini kujenga nidhamu. Tusiachie runinga na mitandao zijenge nidhamu za watoto wetu.

HakiElimu ni shirika la hiari linalolenga kufikia usawa, haki na demokrasia katika elimu na jamii kwa ujumla. Tunafanya hivyo kwa kuwezesha jamii kupata habari, kuboresha shule na mfumo wa uundaji wa sera, kuchochea ubunifu wa mijadala ya umma, kufanya utafiti yakinifu, uchambuzi wa sera na utetezi na kushirikiana na wadau ili kuendeleza manufaa ya pamoja na kuzingatia haki za jamii. Je una kero, kisa au mafanikio kuhusu elimu, demokrasia na haki za binadamu katika eneo lako na ungependa maoni yako yachapishwe kwenye toleo lijalo la Jarida hili la SautiElimu? Tuandikie makala nasi tutaichapisha kwenye toleo lijalo.Tutafurahi kupata makala kutoka kwako. Tuma makala kupitia anuani ifuatayo: SautiElimu-HakiElimu S. L. P 79401 Dar es Salaam Tanzania Simu: (022) 2151852 au 3 Nukushi: (022) 2152449 Barua Pepe: [email protected] Tovuti: www.hakielimu.org Shukrani kwa wachangiaji, wapiga picha, wachoraji na kwa wote walioandaa habari zilizochapishwa katika jarida hili. Unaruhusiwa kunakili sehemu yoyote ya jarida hili kwa minajili isiyo ya kibiashara. Unachotakiwa kufanya no kunukuu chanzo cha sehemu iliyonakiliwa na kutuma nakala mbili kwa HakiElimu.

Wahariri Elizabeth Missokia Robert Mihayo Mtayarishaji Wambura Wasira

Wachangiaji Agnes Mangweha Benedicta Mrema Edwin Mashasi Honoratus Swai

Picha HakiElimu Michoro Popa Matumla Lugendo

© HakiElimu 2011

Na. William J. Kalekwa, Meatu

Salam kutoka kwa Rafiki yenu.

Nimetuma maoni kutoka kwenye

baadhi ya sehemu ya Shajara ya

Marafiki wa Elimu 2011 sehemu ya

k wa n z a , i n a y o s e m a k u wa

Tuwalinde watoto wa kike.

Napenda kusema kuwa suala la

u b a k a j i k w a w a n a f u n z i

inasababishwa na makazi ya

wanafunzi kuwa mbali na shule.

Shule hujengwa mbali na makazi ya

wananchi yaani nje ya vijiji au miji.

Wanafunzi pindi wanapoenda shule

au wanaporudi nyumbani kupata

chakula shule huwa mbali, vibaka

hupata muda wa kuwanyemelea na

kuwabaka. Si hivyo tu, wanafunzi

wengine hukubaliana na watu

wazima wafanye mapenzi kwa

lengo la kujipatia fedha, hivyo

mimba za utotoni hutokea.

Ili kuwalinda wanafunzi, shule

zijengwe karibu na makazi ya watu,

na vilevile, watoto waelimishwe juu

ya athari za mimba za utotoni.

Tuwalinde watoto wa kike

Iwapo shule imejengwa mbali na makazi ya watu, serikali ijenge mabweni ili kuwalinda watoto wa kike na hatari inayoweza kuwakumba njiani wakielekea shule

T u s i a c h e R u n i n g a I j e n g e n i d h a m u y a W a t o t o W e t u

Na Fatuma Mpanga - Pwani

Nidhamu ya mwanafunzi imeshuka kwa sababu ya kufutwa kwa adhabu ya viboko shuleni. Miaka ya nyuma mwanafunzi alikuwa na nidhamu ya hali ya juu. Mwanafunzi alikuwa anaheshimu mwalimu kama anavyowaheshimu wazee wake. Alipokemewa na mwalimu alisikiliza na kutii. M w a l i m u a l i p o m u h u k u m u mwanafunzi shuleni, mwanafunzi huyo alikiri na kukubali kosa; lakini kwa sasa hali hiyo haipo. K w a s a s a m w a n a f u n z i ak i huk um iwa na m wa l im u ataondoka na kilio hadi nyumbani na kutoa malalamiko kuwa amepigwa. Na mzazi au mlezi bila ya kuuliza ataenda mbio mpaka kwa mwalimu na kuanza kubwata,

kutoa lugha chafu na kutaka kupigana na mwalimu. Uchache wa walimu shuleni na watoto kuzurura ovyo mitaani pia

huchangia kupungua kwa nidhamu. Vile vile walimu kufanya biashara kuliko kufundisha darasani pia inachangia kushuka kwa nidhamu. Tunaomba Serikali itazame suala la elimu hasa utoro wa wanafunzi na walimu wenyewe. Ukipeleleza kwa undani utaona watoto wa Wilaya ya Mkuranga hasa hao wanaosoma sekondari huzurura ovyo mitaani, ukiwauliza wanasema hakuna walimu. Vilevile kuna suala la wanafunzi wa kike wa sekondari wanaopanga uraiani. Hawa ni wepesi kupata mimba. Pia hizi shule za sekondari za kata zimekuwa nyingi mno, naomba serikali waangalie hilo.

Bila Viboko Nidhamu ya Wanafunzi hakuna

Je, ni busara mwanafunzi wa kike kupanga chumba mtaani? Akipata mimba nani alaumiwe?

PATA MACHAPISHO MAPYA!