naf ya anzania anzaihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/kilimo...wilaya zote tatu za...

36
TAASISI YA UTAFITI NA UTETEZI WA HAKI ZA ARDHI (HAKIARDHI) KILIMO KWANZA NA NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIA Kitini cha kujielimisha kuhusu Kilimo Kwanza, nguzo zake, changamoto na nafasi ya wazalishaji wadogo katika utekelezaji. Na. 3-2012 Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 1 5/24/13 3:01 PM

Upload: others

Post on 12-Jan-2020

8 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

i

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

TAASISI YA UTAFITI NA UTETEZI WA HAKI ZA ARDHI(HAKIARDHI)

KILIMO KWANZA NA NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIA

Kitini cha kujielimisha kuhusu Kilimo Kwanza, nguzo zake, changamoto na nafasi ya wazalishaji wadogo katika utekelezaji.

Na. 3-2012

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 1 5/24/13 3:01 PM

Page 2: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

ii

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

ISBN NO. 978 9987 626 13 7

Waandishi

1. Richard Mbunda - Mtafiti2. Cathbert Tomitho

Wahariri

1. Yefred Myenzi2. Valentine Ngorisa

Mchapishaji: HAKIARDHI

Mchapaji: Ecoprint Ltd

© HAKIARDHI 2012

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 2 5/24/13 3:01 PM

Page 3: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

iii

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

YALIYOMO

Utangulizi .................................................................................... ivSura ya Kwanza ................................................................................ 1 TAARIFA FUPI KUHUSU HAKIARDHI .............................. 1Sura ya Pili ....................................................................................... 7 DHANA NA NGUZO ZA KILIMO KWANZA ...................... 7 Utangulizi ..................................................................................... 7 Kwanini Kilimo Kwanza? ............................................................ 8 NGUZO KUU KUMI ZA KILIMO KWANZA ...................... 11 1. Dira ya taifa ya Kilimo Kwanza ........................................... 11 2. Kugharamia Kilimo Kwanza ................................................. 11 3. Muundo mpya wa taasisi kwa ajili ya usimamizi wa Kilimo Kwanza ..................................................................... 11 4. Mabadiliko ya mfumo wa kimkakati wa Kilimo Kwanza ... 12 5. Ardhi kwa ajili ya Kilimo Kwanza ....................................... 12 6. Vivutio kwa ajili ya Kilimo Kwanza .................................... 13 7. Viwanda kwa ajili ya Kilimo Kwanza .................................. 13 8. Sayansi, teknolojia na rasilimali watu kwa ajili ya Kilimo Kwanza .................................................................................. 13 9. Miundombinu kwa ajili ya Kilimo Kwanza ......................... 13 10. Uhamasishaji wa watanzania kwa ajili ya Kilimo Kwanza ... 14Sura ya Tatu ....................................................................................... 15 KUIBULIWA NA UTEKELEZAJI WA KILIMO KWANZA ... 15 Ushiriki wa wazalishaji wadogowadogo katika kuibua Kilimo Kwanza ulikuaje? ......................................................................... 15 Utekelezaji wa Kilimo Kwanza na nafasi ya wazalishaji wadogowadogo ............................................................................ 17 Upatikanaji wa mikopo kwaajili ya Kilimo Kwanza na nafasi ya wazalishaji wadogowadogo ......................................................... 18 Uhakika na upatikanaji wa pembejeo kwaajili ya Kilimo Kwanza kwa wazalishaji wadogowadogo ................................... 20 Mabadiliko ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5, 1999 katika utekelezaji wa Kilimo Kwanza. Nini hatma ya wazalishaji wadogo wadogo? .......................................................................... 22Sura ya Nne ........................................................................................ 27 MAPENDEKEZO YA KUBORESHA KILIMO KWANZA.. 27 HITIMISHO ................................................................................ 29 Marejeo ............................................................................. 30

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 3 5/24/13 3:01 PM

Page 4: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

iv

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Utangulizi

Kitini hiki cha uelewa wa mkakati wa Kilimo Kwanza ni mfululizo wa vitini ambavyo taasisi ya Utafiti na Utetezi wa haki za ardhi imekuwa ikitoa kwa lengo la kusambaza taarifa mbalimbali kwa umma zinazotokana na tafiti juu ya masuala muhimu ya ardhi. Tangu kuibuka kwa dhana hii ya Kilimo Kwanza, kumekuwa na taarifa nyingi za kitafiti na zisizokuwa za kitafiti kuhusiana na jinsi ambavyo tamko hili la serikali lililotolewa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete linakuwa nyenzo na chachu ya maendeleo kwa wananchi wanaotumia ardhi kama nguzo muhimu ya uzalishaji mali kwa maisha yao na maendeleo ya taifa. HAKIARDHI, ilifanya utafiti kuanzia mwishoni mwa mwaka 2010 hadi mwanzoni mwa 2011 kuhusiana na nafasi ya wazalishaji wadogo wadogo katika mchakato mzima wa kuibuliwa na utekelezwaji wa Kilimo Kwanza kupitia mikakati iliyo ndani ya mpango wa maendeleo ya sekta ya kilimo. Katika utafiti wake, taasisi imebaini changamoto nyingi zinazowakabili wazalishaji wadogo hususan wakulima na wafugaji kiasi cha kuwafanya wasiwe washiriki wenye tija kwenye azma hii njema ya kitaifa. Kutokana na utafiti huu, yanajadiliwa na kupendekezwa masuala kadha wa kadha ambayo siyo tu yataboresha sekta ya kilimo na kuifanya kuwa na tija zaidi bali pia yatamsaidia mzalishaji mdogo kubadili mfumo wa uzalishaji na maisha yake kwa ujumla. Ni matumaini yetu kuwa utaendelea kufurahia kusoma mfululizo wa vitini vyetu na usisite kutupatia mrejesho wako kwa kutuandikia kwa anuani zilizo nyuma ya chapisho hili.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 4 5/24/13 3:01 PM

Page 5: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

1

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

SURA YA KWANZA

TAARIFA FUPI KUHUSU HAKIARDHI

1. Usuli HAKIARDHI ni Taasisi ya kiraia iliyoundwa mwaka 1994 na kusajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali, chini ya sheria ya Makampuni, Sura ya 212 ya Sheria za Tanzania. Taasisi ilianzishwa kwa kutambua umuhimu wa kuibua na kuendeleza mijadala juu ya umilikaji ardhi, kama mojawapo ya njia za kukuza ushiriki wa wananchi, hususan wazalishaji wadogo wadogo wa vijijini na pembezoni mwa miji, katika maamuzi yanayohusu ardhi na rasilimali nyingine muhimu zilizo katika maeneo yao.

2. DiraDira ya HAKIARDHI ni kuona kuwa raia wa Tanzania hususan wazalishaji wadogo wadogo wanakuwa na uhakika wa milki ya ardhi na rasilimali zao uliojengwa katika misingi ya usawa na haki katika kupata, kutumia, kumiliki na kudhibiti ardhi na rasilimali hizo kwa ajili ya maendeleo yao na ya taifa lao kwa ujumla.

3. Lengo kuu Lengo kuu la HAKIARDHI ni kukuza ufahamu wa jamii juu ya masuala ya ardhi, kuimarisha mifumo ya utoaji wa maamuzi juu ya ardhi na kuwezesha ushiriki wa wananchi hususan wazalishaji wadogo wadogo waishio vijijini ambao ni takriban 80% ya Watanzania wote, kwenye masuala ya ardhi ili waweze kudai, kutetea, kupata na kulinda haki zao za ardhi kwa manufaa yao.

3.1 Malengo mengine ni pamoja na:

(i) Kutoa ushauri na misaada mingine ya aina hiyo kwa wazalishaji wadogo wadogo vijijini na kwenye

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 1 5/24/13 3:01 PM

Page 6: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

2

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

maeneo ya viunga vya miji, kuhusu masuala ya kumiliki ardhi, na kutoa msaada wa kisheria katika kushughulikia baadhi ya mashauri ya ardhi kwenye vyombo vinavyohusika vya kisheria na kiutawala.

(ii) Kutoa huduma zitakazosaidia katika kutatua migogoro ya ardhi pale huduma hizo zitakapohitajika.

(iii) Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali ya ardhi, kuunda na kupendekeza mbinu bora za kutatua migogoro ya ardhi miongoni mwa wazalishaji wadogo wadogo na baina ya wanavijiji.

(iv) Kuandaa na kuendesha mafunzo ya muda mfupi kuhusu masuala ya milki na haki za ardhi Taasisi ikiombwa kufanya hivyo na makundi mbalimbali ya kijamii.

(v) Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali kama ushauri huo utahitajika na kama malengo yake yanahusiana na msimamo na mwelekeo wa Taasisi.

(vi) Kuandaa na kudhamini mikutano, semina na warsha na shughuli nyingine za namna hiyo kwa ajili ya kuendeleza malengo ya kijamii na kielimu ya Taasisi.

(vii) Kukusanya fedha za kuendesha shughuli za Taasisi bila ya kuathiri uhuru wa Taasisi wa kufanya kazi zake na bila ya kuathiri malengo yake ya kielimu na kijamii.

4. Programu za TaasisiKatika jitihada za kufanikisha kufikia malengo hayo, Taasisi huandaa programu mbalimbali na kuzitekeleza kulingana na fursa na uwezo wake wa kirasilimali. Tangu

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 2 5/24/13 3:01 PM

Page 7: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

3

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

mwaka 1994 hadi 2001, mipango ya Taasisi ilijikita katika kushawishi, kutetea na kuwezesha upatikanaji wa sera na sheria zinazozingatia matakwa na maslahi ya wazalishaji wadogo wadogo nchini. Sera ya taifa ya ardhi ya 1995 na sheria za ardhi za 1999 kwa kiasi kikubwa zilizingatia matakwa hayo japo baadhi ya masuala ya msingi yangali yakijadiliwa hasa kuhusiana na aina ya mfumo wa milki ya ardhi wenyewe. Hata hivyo, kwa takribani muongo mmoja sasa tangu mwaka 2002 Taasisi imejielekeza zaidi katika kuimarisha vyombo vya utoaji maamuzi yanayohusu haki za wananchi kama vile mabaraza ya ardhi, halmashauri za vijiji na mikutano mikuu ya vijiji pamoja na kukuza ushiriki wa wananchi katika vyombo hivyo ili haki itendeke na ipatikane. Mipango hii hutekelezwa katika vitengo vitatu ambavyo ni:

4.1 KitengochaUtafiti,MachapishonaUtunzajikumbukumbu. Kitengo hiki hufanya tafiti mbalimbali ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi na za wakati ili zitumike katika ushawishi na utetezi wa sera na sheria na pia katika kuandaa machapisho kwa ajili ya mafunzo ya ardhi vijijini na uelimishaji umma kwa ujumla. Matokeo ya tafiti huchapishwa vitabu, majarida, miongozo ya mafunzo na pia husambazwa kwa wasomaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

4.2 Kitengo cha Uhusishwaji jamii na UteteziKitengo hiki huratibu shughuli zote za mafunzo ya uwezeshaji katika ngazi za vijiji hadi taifa, mafunzo ya sheria za ardhi, mijadala ya wazi, semina za kila mwezi za masuala ya ardhi na makongamano ya kitaifa na kimataifa. Pia elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na ushiriki wa Taasisi katika shughuli za asasi nyingine huratibiwa na kitengo hiki.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 3 5/24/13 3:01 PM

Page 8: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

4

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

4.3 Kitengo cha uendeshaji wa Taasisi na usimamizi wa programu Hiki kinahusika na vitengo vidogo vitatu ambavyo ni; (i) Shughuli za uendeshaji wa kila siku wa Taasisi (uratibu na usimamizi), (ii) Utafutaji wa fedha, usimamizi wa fedha na ukaguzi wa mahesabu, (iii)Ufuatiliaji wa shughuli zote za Taasisi kulingana na miongozo na viwango vya ufanisi vilivyowekwa.

5. Mafanikio (i) Utekelezaji wa mipango hiyo, umewezesha kufikiwa kwa

watanzania takribani milioni kumi na tano na kukuza uelewa wao juu ya masuala ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini tangu Taasisi ilipoanzishwa. Maeneo hayo ni pamoja na vijiji zaidi ya 1,000 katika Wilaya ambazo Taasisi imekuwa ikitekeleza programu zake kwa nyakati tofauti tofauti kama vile Mufindi, Kilolo, Newala, Rujewa, Kilwa, Kisarawe, Rufiji, Bagamoyo, Meatu, Kahama, Korogwe, Kilindi na Mkinga. Wilaya nyingine ni Kilosa, Kilombero, Morogoro vijijini, Ngorongoro, Hanang, Karatu, Kiteto na Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala.

(ii) Taasisi imefanikiwa kuibua na kuendeleza mijadala juu ya haki za ardhi katika ngazi mbalimbali za kijamii ambayo imesaidia kuimarisha mifumo ya utoaji maamuzi, kupunguza na kuepusha migogoro ya ardhi na kuwezesha upatikanaji wa haki za ardhi na haki za binadamu katika maeneo husika.

(iii) Kadhalika, Taasisi imefanikiwa kufanya tafiti, kuandaa na kusambaza taarifa mbalimbali juu ya masuala ya ardhi (kama vile uwekezaji katika ardhi za vijiji na changamoto zake kwa jamii husika, rasilimali za baoanuai, mustakabali

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 4 5/24/13 3:01 PM

Page 9: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

5

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

wa ufugaji na wafugaji nchini), na kusambaza kwenye jamii kwa kwa njia ya vitabu, majarida, vyombo vya habari na mijadala ya wazi ya kijamii.

(iv) Taasisi imekuwa ikishiriki katika michakato mbalimbali ya uandaaji wa sera na sheria kwa lengo la kutetea matakwa na maslahi ya wanyonge katika sheria hizo hususan sheria za ardhi na marekebisho yake mbalimbali.

(v) Kujenga nguvu za pamoja na washirika wengine wenye mlengo sawa na wa Taasisi kwa azma ya kuchangia jitihada za kuleta mabadiliko makubwa zaidi katika mfumo wa milki na matumizi ya ardhi ili kulinda haki na mustakabali wa wazalishaji wadogo nchini.

6. ChangamotoMabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini yametikisa mifumo ya kitaasisi na kijamii iliyokuwa ikisimamia maslahi ya moja kwa moja ya wananchi hususan wazalishaji wadogo wadogo. Katika mfumo wa sasa wa milki na matumizi ya ardhi ambao umeigeuza ardhi kuwa bidhaa ya kushindaniwa, ni dhahiri kwamba maslahi ya wazalishaji wadogo yanapaswa kuangaliwa zaidi kwa vile nguvu yao ya kushindana katika soko ni ndogo kulinganisha na makundi mengine yenye uwezo kiuchumi, kisiasa na kijamii. HAKIARDHI na asasi za aina yake zina wajibu wa kuendelea kupigania, kulinda na kutetea maslahi hayo katika sera na sheria na mifumo ya usimamizi wa haki za ardhi katika jamii.

Uhaba wa rasilimali bado ni changamoto kubwa kwani Taasisi hushindwa kufanya kazi katika maeneo makubwa zaidi. Bila shaka, upatikanaji wa rasilimali fedha zaidi

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 5 5/24/13 3:01 PM

Page 10: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

6

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

utawezesha kuwa na rasilimali watu zaidi na vitendea kazi zaidi na hivyo kuwezesha Taasisi kuwafikia watu wengi zaidi katika ngazi ya jamii.

Migogoro ya ardhi kati ya makundi mbalimbali ya kijamii bado inaendelea na athari zake zimezidi kuwa kubwa hasa kutokana na upotevu wa mali na maisha ya wananchi wasio na hatia wakiwemo wanawake, watoto na wazee. Serikali, asasi za kiraia na washirika wengine hawana budi kuendelea kuimarisha mifumo ya kiasili na ile rasmi ya utatuzi wa migogoro ili kuepusha athari zaidi kwa wananchi.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 6 5/24/13 3:01 PM

Page 11: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

7

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

SURA YA PILI

DHANA NA NGUZO ZA KILIMO KWANZA

UtanguliziKilimo kwa wananchi wa Tanzania ndio uti wa mgongo wa uchumi wa taifa kutokana na ukweli kuwa kilimo ndio sekta inayoendesha maisha ya zaidi ya asilimia 741. Idadi kubwa ya watanzania wanaotegemea kilimo moja kwa moja wanaishi vijijini. Sekta hii pia inatoa zaidi ya asilimia 90 ya chakula chote kinachotumika hapa nchini na kutoa mchango unaokaribia asilimia 30 kwenye pato la taifa. Nchi ya Tanzania kwa vipindi tofauti toka uhuru imekuwa ikitunga sera, sheria na mikakati mbalimbali katika jitihada za kukuza na kuongeza uzalishaji kwenye sekta ya kilimo. Mapema baada ya nchi kupata uhuru, serikali iliweka nguvu kubwa katika sekta ya kilimo kutokana na kutambua kuwa ukombozi pekee wa kiuchumi na kijamii kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla ulikuwa mikononi mwa sekta ya kilimo. Hata mipango ya kitaifa ya maendeleo ilijikita katika kuhakikisha kuwa kilimo kinatoa mchango mkubwa wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, jamii na hatimaye taifa kwa ujumla. Sekta ya kilimo ilitegemewa kuwa chanzo cha ajira, fedha za kigeni, mapato kwa serikali na akiba ya chakula kwa taifa.

Mikakati hii ya serikali ilidhihirishwa na shughuli mbalimbali kama vile Azimio la Arusha mwaka 1967 ambalo liliainisha wazi kuwa Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi na sekta ya kilimo ndio mhimili katika maendeleo na ukuaji wa uchumi wa nchi ukilinganisha na sekta ya viwanda na makampuni mbalimbali katika sekta nyingine kama vile madini. Serikali ya awamu ya kwanza katika kuhakikisha kuwa kilimo kinakuwa uti wa mgongo wa taifa ilianzisha Vijiji vya Ujamaa kwa lengo la kuweka wananchi wa vijijini pamoja ili kuimarisha na kukuza kilimo chenye tija kwa kuanzisha mashamba ya pamoja. Vilevile ni wakati huu

1 Ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Binadamu 2009

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 7 5/24/13 3:01 PM

Page 12: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

8

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

ambao kulianzishwa mashamba makubwa (NAFCO na NARCO) yaliyomilikiwa na kusimamiwa na sekta za umma kwa lengo la kukuza uzalishaji wa chakula na mazao mengine kwa mahitaji ya ndani ya nchi na kuuza nje ya nchi.

Pamoja na jitihada zote hizi za serikali ya awamu ya kwanza bado sekta ya kilimo ilishindwa kukua kwa kiasi cha kuwakwamua watanzania na nchi kwa ujumla kutoka katika hali ya unyonge na masikini hasa ikizingatiwa kuwa nchi ilikuwa imetoka kujikomboa kwenye unyonyaji wa kikoloni na makupe wa msimu wa mwanzo wa uhuru ambao hatimaye walitokomezwa na Azimio la Arusha. Mathalani kutokueleweka kwa dhana ya uchumi wa Ujamaa na mchakato mzima wa Vijiji vya Ujamaa na kujitegemea kulikwamisha kwa namna fulani malengo ya kufikia uchumi wenye manufaa kwa wote. Hali hii ilipelekea kwa baadhi ya wananchi waliokuwa na uwezo wa kulima wenyewe pasipo kutaka ushirikiano na wengine kugoma kuwa sehemu ya vijiji vya ujamaa na kujitegemea. Vile vile mashamba yaliyoanzishwa na serikali kupitia NAFCO na NARCO yalishindwa kutimiza malengo yake ya kukuza sekta ya kilimo na mifugo kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukithiri kwa rushwa kwa baadhi ya watendaji wa mashirika haya na utendaji mbovu pamoja na kufungua milango ya biashara huria kwenye miaka ya katikati ya themanini. Kwa ujumla, mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi kutoka ule wa kijamaa ambao ulikuwa unaruhusu serikali kufanya na kusimamia biashara kwenda katika mfumo wa kibepari ulioiondoa serikali katika mfumo huo yalichangia kwa kiasi kikubwa kuyumba kwa sekta ya kilimo.

Kwanini Kilimo Kwanza?Utangulizi wa hapo juu unatupatia mwanga wa kutosha kuhusu azima ya Kilimo Kwanza kuwa si jitihada mpya bali ni muendelezo jitihada kama hizo ambazo serikali tangu uhuru, imekuwa ikizifanya kwa namna mbalimbali kwenye sekta hii. Kumekuwa na maelezo mengi na hata tofauti ya tafsisri kuhusu nini hasa maana ya Kilimo

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 8 5/24/13 3:01 PM

Page 13: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

9

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Kwanza huku baadhi wakiita mkakati, mpango, sera na hata mbinu na wengine wakiuelezea inavyostahili kuwa ni azima ya serikali ya kuchochea mabadiliko katika sekta ya kilimo kupitia mipango iliyopo kama vile ASDP huku mfumo wake wa utekelezaji ukijitanua kwenye sekta zote za kimaendeleo. Azima hii, inaaminika na kutafsirika zaidi kwa upande wa serikali kuwa ndiyo itakayoleta suluhu ya kudumaa kwa sekta ya kilimo na kukosekana kwa tija na hata mchango hafifu kwenye pato la taifa.

Kudumaa kwa sekta ya kilimo kunapimwa kwa kulinganishwa na sekta nyingine kama vile miundombinu, fedha na huduma kutokana na ukweli kuwa sekta hizo zinakua kwa kasi kubwa zaidi. Kilimo Kwanza inachukua nafasi ya matamko mengine mbalimbali yaliyotolewa nyakati na miaka tofauti katika sekta ya kilimo. Matamko na mikakati mingine iliyokwisha kupita ni kama vile “Siasa ni Kilimo”, “Chakula ni Uhai”, na “Kilimo cha Kufa na Kupona”. Kwa mujibu wa waasisi wa Kilimo Kwanza ambao ni Baraza la Biashara la Taifa, mkakati wa Kilimo Kwanza umejizatiti katika kukabiliana na vikwazo vyote vilivyosababisha kushindwa kwa sekta ya kilimo miaka iliyopita pamoja na jitihada zote serikali ilizozionyesha. Baraza la Biashara la Taifa linaorodhesha baadhi ya mapungufu yaliyopelekea kuanguka kwa sekta ya kilimo awamu zilizopita na jinsi ambavyo Kilimo Kwanza imeandaliwa kukabiliana nayo.

Kwanza, ni dola kusimamia na kumiliki njia zote za uchumi, kilimo ikiwa mojawapo, hali hii ilichangia kudumaa na kufa kwa sekta binafsi katika sekta ya kilimo. Mikakati na mipango ya kukuza kilimo ilibuniwa na serikali na kutekelezwa na serikali yenyewe ama moja kwa moja au kupita taasisi zake. Kwa mujibu wa baraza la biashara, Kilimo Kwanza imeanzishwa wakati ambao ni wa uchumi huria unaohamasisha sekta binafsi na watu binafsi kushiriki moja kwa moja pasipo kuingiliwa na serikali.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 9 5/24/13 3:01 PM

Page 14: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

10

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Pili, sera na mikakati ilitungwa na kuanzishwa katika mfumo wa maamuzi ya kutoka juu kwenda chini pasipo ushiriki wa wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo. Mfano Ujamaa na Kujitegemea ambao ulianzishwa na chama na kutekelezwa na serikali pasipo ushiriki wowote wa wananchi. Baraza linaona kuwa uanzishwaji wa Kilimo Kwanza ni tofauti kutokana na wadau wote muhimu kushirikishwa.

Tatu, mikakati haikuwa na muunganiko wa kisekta na kiwizara, kwani kila wizara na sekta husika ilifanya kazi yake tu. Hali hii ilisababisha sekta ya kilimo kukosa ushirikiano na sekta nyingine muhimu katika kukua. Kilimo Kwanza imeweka muunganiko baina ya sekta na wizara mbalimbali katika utekelezaji wake.

Nne, mikakati iliyopita ilitegemea zaidi bajeti ya serikali ambayo kwa kiasi kikubwa haikuwa toshelevu hali iliyosababisha wakulima kushindwa kuhimili ushindani. Suala la utegemezi katika Kilimo Kwanza halipo kutokana na kuwepo uwanja mpana wa wakulima kukopa kutoka katika taasisi za fedha pamoja na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka kwa wawekezaji wakubwa. Uchambuzi huu wa baraza la biashara unaonekana kulenga katika kuleta mapinduzi kuanzia ngazi ya fikra za watungaji wa sera, wasimamizi na watekelezaji wa azima yenyewe hasa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi. Hata hivyo, haimaanishi kwamba kila kilichoainishwa ndivyo kilivyo maana tafiti mbalimbali na hata hali halisi tu inaonyesha changamoto nyingi katika hatua za mwanzo za azma hii zinazohusiana na masuala ya ushiriki wa wananchi, uratibu wa mfumo wa utekelezaji wa Kilimo Kwanza, upatikanaji na usambazaji wa rasilimali kama fedha na pembejeo na utayari wa kijamii hasa kutokana na majeraha ya kushindwa kwa jitihada kama hizo zilizotangulia.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 10 5/24/13 3:01 PM

Page 15: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

11

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

NGUZO KUU KUMI ZA KILIMO KWANZAMisingi mikuu ya kuanzishwa na kutekelezwa kwa mkakati wa Kilimo Kwanza imeainishwa na kuchambuliwa katika nguzo hizi kumi.

1. Dira ya taifa ya Kilimo KwanzaShughuli kuu za kutekelezwa chini ya nguzo hii ni pamoja na (i) Kupitisha dira ya Kilimo Kwanza na (ii) Kilimo cha wakulima wadogo, wa kati na wakubwa kiwe cha kisasa na cha kibiashara. Hata hivyo, suala la nani hasa ndiye mkulima mdogo, wa kati au mkubwa bado haliko bayana kwani haijulikana ni vigezo gani vinavyotumika kati ya ukubwa wa eneo linalotumika au kiwango cha mapato.

2. Kugharamia Kilimo KwanzaBaadhi ya shughuli za kutekelezwa chini nguzo hii ni (i) Kuongeza Bajeti ya Serikali kwa ajili ya Kilimo Kwanza, (ii)Kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), (iii) Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kuwa na dirisha maalumu la mikopo ya kilimo itakayotolewa kwa masharti nafuu, (iv) kuanzisha mfuko maalumu wa fedha kwa ajili ya Kilimo Kwanza, (v) Kuimarisha Mfuko wa Programu ya Maendeleo ya sekta ya Kilimo (ASDP) ili uweze kutumika kutekeleza Kilimo Kwanza, (vi)Kuhamasisha sekta binafsi iongeze uwekezaji katika sekta ya Kilimo kuanzia ngazi ya chini, kati na wakubwa. (vii)Kuviwezesha vyama vya ushirika na SACCOS viweze kutafuta, kusimamia na kuelekeza mitaji kwa wanachama wao ili kuimarisha uzalishaji katika kilimo. (viii)Kuimarisha uanzishaji wa mabenki ya wananchi katika mikoa yote ya Tanzania.

3. Muundo mpya wa taasisi kwa ajili ya usimamizi wa Kilimo Kwanza

Shughuli za kutekelezwa kupitia nguzo hii katika Kilimo Kwanza ni kama vile (i)Kurekebisha muundo wa kitaasisi kwa ajili ya utekelezaji wa Kilimo Kwanza, (ii)Kuanzisha utaratibu wa kuratibu

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 11 5/24/13 3:01 PM

Page 16: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

12

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

uhusiano na wizara nyingine zinazohusiana na maswala ya kilimo, (iii)Kuanzisha utaratibu wa ubia wa sekta ya umma na ya binafsi kwa ajili ya Kilimo Kwanza, (iv)Kuimarisha vyama vya wakulima kwa ajili ya kuboresha ushirikiano na serikali katika utungaji wa sera, mikakati, utekelezaji na tathmini ya utendaji kazi wa sekta ya kilimo.

4. Mabadiliko ya mfumo wa kimkakati wa Kilimo Kwanza

Katika nguzo ya nne kuna masuala mbalimbali ya kushughulikia katika kutekeleza Kilimo Kwanza, nayo ni pamoja na (i)Kubainisha maeneo ya kipaumbele kwa ajili ya vyakula muhimu ili nchi ijitosheleze kwa chakula, (ii)Kubainisha maeneo ya kipaumbele ya uzalishaji wa mazao yanayoweza kuboresha kilimo haraka kwa kutumia gharama na utaalamu mdogo na kukidhi mahitaji ya soko la ndani/nje na kuongeza ajira, (iii)Kubainisha maeneo ya kipaumbele na uzalishaji wa mazao ya kilimo cha bustani, (iv)Kutunga sheria ya kuboresha mfumo wa kilimo cha mkataba, (v)Kuanzisha kamati ya ushauri kuhusu mabadiliko ya mfumo wa kilimo.

5. Ardhi kwa ajili ya Kilimo KwanzaNguzo ya tano ina shughuli mbalimbali kama vile (i) Kurekebisha Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya 1999, (ii)Kuharakisha mfumo wa upatikanaji ardhi, (iii)Kuharakisha utatuzi wa migogoro ya ardhi, (iv)Kuboresha muundo katika usimamizi wa ardhi, (v)Kuingiza maeneo yanayofaa kwa kilimo katika mipango ya maendeleo ya miji, (vi)Kutenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo katika kile kinachoitwa benki ya ardhi, (vii)Kutumia kwa ukamilifu ardhi ambayo hivi sasa inamilikiwa na serikali na taasisi za serikali. Nguzo hii ndiyo imeonekana kuvuta hisia za watu wengi hasa kutokana na ukweli kuwa uhakika wa milki ya ardhi vijijini unakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo kushindwa kupima ardhi ya vijiji na kuwagawia wanavijiji maeneo yao, kuingiliana mamlaka za kiusimamizi kati ya serikali kuu na serikali za mitaa na ugawaji

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 12 5/24/13 3:01 PM

Page 17: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

13

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

wa holela wa ardhi kwa wawekezaji bila kujiridhisha na mahitaji ya wenyeji kwanza. Kilimo Kwanza inatafrisiwa kuwa ni njia mojawapo ya kupora ardhi kwa wenyeji na kuwapa wakulima wa ngazi ya kati na wakubwa ambao aghalabu, si wanavijiji wenyeji.

6. Vivutio kwa ajili ya Kilimo KwanzaShughuli mbalimbali zimeainishwa katika nguzo hii zikiwemo, (i)Kuainisha vivutio vya sera ya kodi na vivutio vingine ili kuchochea maendeleo ya Kilimo Kwanza, (ii)Kubuni na kutekeleza hatua za kuimarisha ushindani wa kilimo cha Tanzania, (iii)Kuondoa vikwazo vya masoko kwa mazao ya kilimo, (iv)Utumiaji wa vipimo na viwango halali katika biashara uimarishwe, (v)Kuboresha bei za mazao.

7. Viwanda kwa ajili ya Kilimo KwanzaMambo mbalimbali yameainishwa ili kutekelezwa kwaajili ya Kilimo Kwanza kupitia nguzo hii ya saba, nayo ni (i)Viwanda kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wazalishaji wa kilimo, (ii)Nyenzo za uzalishaji wa Kilimo, (iii)Kuboresha uzalishaji wa mbegu, (iv) Kuainisha na kuimarisha uwezo unaohitajika kwa kuendeleza sekta ya mifugo, (v)Kuongeza uzalishaji wa dawa za kilimo nchini, (vi)Uzalishaji wa zana na vifaa vya kilimo.

8. Sayansi, teknolojia na rasilimali watu kwa ajili ya Kilimo Kwanza

Katika nguzo ya nane shughuli iliyotajwa katika utekelezaji wa Kilimo Kwanza, ambayo ni pamoja na (i)Kuanzisha utaratibu wa kutathmini matumizi yanayokidhi mahitaji ya kisayansi, kiteknolojia na rasilimali watu kwa ajili ya Kilimo Kwanza.

9. Miundombinu kwa ajili ya Kilimo KwanzaKwenye nguzo ya tisa kuna shughuli kama vile (i)Kubaini mahitaji ya uendelezaji miundombinu kwa ajili ya Kilimo Kwanza, (ii)Vituo vya soko kwa kila kata, (iii)Kupeleka umeme vijijini kwa ajili ya kuboresha kilimo.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 13 5/24/13 3:01 PM

Page 18: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

14

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

10. Uhamasishaji wa watanzania kwa ajili ya Kilimo Kwanza

Nguzo hii ya kumi imebeba shughuli mbalimbali katika utekelezaji wa Kilimo Kwanza kama vile (i)Kuingiza Kilimo Kwanza katika vyombo na mipango ya serikali, (ii)Kufanya kampeni ya uhamasishaji Kilimo Kwanza katika ngazi ya taifa, mkoa, Wilaya kata, na vijiji (iii) Kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika Kilimo Kwanza, (iv)Viongozi kushiriki katika kilimo, (v)Ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Kilimo Kwanza

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 14 5/24/13 3:01 PM

Page 19: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

15

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

SURA YA TATU

NAFASI YA WAZALISHAJI WADOGO KATIKA UIBUAJI NA UTEKELEZAJI WA KILIMO KWANZA

Ushiriki wa wazalishaji wadogo katika kuibua Kilimo Kwanza ulikuwaje?Kimsingi, waanzilishi wa Kilimo Kwanza ni Baraza la Biashara la Taifa kupitia mojawapo ya mikutano yake hapo mwaka 2009. Wajumbe wa Baraza hili ni takribani arobaini (40) kutoka katika sekta ya umma na binafsi na wawakilishi wengine kutoka katika sekta za kijamii na kiuchumi. Ndani yake kuna mawaziri, wafanyabiashara wakubwa kutoka katika kila nyanja ya kibiashara pamoja na wasomi wabobevu kutoka vyuo vikuu nchini. Kilimo Kwanza kwa maana hiyo ni zao la utafiti uliofanywa na makundi kazi mawili ndani ya Baraza hili ambayo ni kikundi kazi cha kilimo na kikundi kazi cha kukuza uchumi. Kwa mujibu wa Baraza, kikundi kazi cha kilimo kilienda hadi ngazi ya Wilaya kujadiliana na wadau wa sekta ya kilimo ni kwa jinsi gani kilimo cha Tanzania kinaweza kuboreshwa.

Pamoja na maelezo hayo ya Baraza kuwa uanzishwaji wa Kilimo Kwanza ulikuwa shirikishi kuanzia ngazi ya chini ni dhahiri kwamba vikosi kazi hivyo viliishia kwa watu wale wale wanaotoa maamuzi kwa niaba ya wakulima na wafugaji wa vijijini kwenye mikutano ya Wilaya na mkoa kisha taarifa zikatolewa kuwa wadau walishirikishwa. Na wala hatusikii wala kuona mahali ambapo wakulima wenyewe wadogo wakiibua hoja na mawazo yao kuhusiana na changamoto zinazowakabili na namna ambavyo wangetamani kuona zinashughulikiwa. Udhaifu huu unajitokeza wazi kwenye andiko lenyewe ambamo inaonekana wazi kabisa kukosa muunganiko wa moja kwa moja na sekta nyingine zinazoambatana na sekta ya kilimo kama vile sekta za ufugaji na uvuvi. Kukosekana kwa msisitizo wa sekta hizi katika Kilimo Kwanza kunapingana moja kwa moja na tafsiri ya kilimo ambayo ni muunganiko wa sekta na kazi mbalimbali zinazohusisha makundi tofauti tofauti yanayotumia ardhi.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 15 5/24/13 3:01 PM

Page 20: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

16

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Kukosekana kwa muunganiko na sekta hizo muhimu kunabakiza mapungufu yale yale katika azma hii ambayo waasisi wake walijigamba kuwa yatabaki kuwa historia. Kinachoonekana katika Kilimo Kwanza ni kugusia tu baadhi ya maeneo ya sekta ya ufugaji kama vile kujenga na kuimarisha maeneo ya machinjio lakini kimsingi hayo sio maeneo ya kipaumbele katika sekta ya mifugo kama vile kutenga maeneo ya kutosha kwa ajili ya ufugaji ambayo yatakuwa na huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na maji, miundombinu madhubuti na majosho na masoko yenye bei nzuri kwa mifugo vitu ambavyo vinawafanya wafugaji kuhama kila siku kuvitafuta vinakopatikana hata kama ni nje ya mipaka ya nchi.

Ushiriki wa wazalishaji wadogowadogo katika Kilimo Kwanza kuanzia kuibuliwa kwake hadi utekelezaji wake unaonekana kukosekana kabisa kinyume na maelezo ya Baraza la Biashara la Taifa. Ni ukweli ulio wazi kuwa ushirikishwaji wa wazalishaji wadogowadogo ungeanzia katika vikundi mbalimbali vinavyowawakilisha wazalishaji wadogowadogo kama vile MVIWATA, SACCOS, ushirika na vinginevyo kama hivyo lakini kwa mujibu wa vikundi hivi hakuna mawazo yoyote yaliyochukuliwa kutoka kwao wakati wao wanashughulika na wakulima wengi zaidi hadi kwenye ngazi ya msingi maeneo mbalimbali nchini. Kitendo cha hawa wadau muhimu katika sekta ya kilimo kutoshirikishwa ipasavyo kinaondoa mazingira ya wakulima wadogowadogo kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake na hatimaye kunufaika na Kilimo Kwanza kama ilivyokusudiwa.

Hali hii inaendana kabisa na matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya HAKIARDHI katika Wilaya za Kisarawe, Bagamoyo, Morogoro na Kiteto ambayo pamoja na mambo mengine, yalibainisha wazi kuwa wakulima wengi vijijini wamesikia kilimo kwanza kwenye redio, na katika mikutano ya wanasiasa au semina mbalimbali za asasi za kiraia. Swali la kujiuliza ni kuwa endapo wananchi hawa walishirki kikamilifu kutoa mawazo juu ya uanzishwaji wa

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 16 5/24/13 3:01 PM

Page 21: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

17

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

azma hii ya serikali, iweje sasa katika hatua ya utekelezaji wawe wamesahau kila walichokisema wakati wa kuibua azma hii? ieleweke kwamba, wakulima wadogo wadogo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa ardhi, kukosekana kwa miundombinu ya umwagiliaji, upatikanaji wa pembejeo za kutosha na kwa wakati, miundombinu ya masoko na usafirishaji wa mazao isiyoridhisha na isiyowezekana kutumika wakati wote wa msimu. Ndio maana maneno ya mwanakijiji mmoja wa Wilaya ya Bagamoyo wakati wa mahojiano na mtafiti wa taarifa hizi yanaonekana kuwa na mantiki kabisa. Kwake yeye, Kilimo Kwanza ni mkakati ulioibuliwa na wafanyabiashara wakubwa kwa lengo la kujiendeleza wao wenyewe kwa kuwa ndio walioshiriki asilimia zote katika kuutengeneza mkakati na wasitubebeshe mzigo wowote sisi wanavijiji tunaojitafutia riziki kwa shida.

Utekelezaji wa Kilimo Kwanza na nafasi ya wazalishaji wadogoKilimo Kwanza ilizinduliwa rasmi mwezi Agosti 2009 na kuanza kutekelezwa katika hatua mbalimbali katika sekta mbalimbali kwa jinsi mpango wake wa utekelezaji unavyojitanabaisha kuhusisha idara na sekta mbalimbali za umma na binafsi. Watekelezaji wakubwa ni Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kupitia Programu ya maendeleo ya sekta kilimo (ASDP) mpango ulioanza mwaka 2006. Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo kilichofanyika hasa ni kuyapitia malengo ya ASDP ili kuhakikisha yanarandana na Kilimo Kwanza kwa lengo la kuipa nguvu ya utekelezaji azma hii vinginevyo linabaki kuwa tamko tu lisilo na maana. Pamoja na muunganiko huu wa ASDP na Kilimo Kwanza, pia bajeti maalumu kwaajili ya Kilimo Kwanza itaingia kwa kila Wizara inayohusika na utekelezaji wa Kilimo Kwanza. Wizara nyeti zinazohusika na utekelezaji wa Kilimo Kwanza ni pamoja na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika; Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko; Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi; Wizara ya Maji na Umwagiliaji; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 17 5/24/13 3:01 PM

Page 22: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

18

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya Kilimo Kwanza na nafasi ya wazalishaji wadogoKwa mujibu wa Baraza la Kilimo la Taifa (ACT) mchakato wa kuanzishwa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania unaendelea. Uanzishwaji wa benki hii pia unazungumziwa katika nguzo ya kwanza (1) ya Kilimo Kwanza kifungu cha pili (2) inayosomeka “Kuanzisha Benki ya Maendeleo ya KilimoTanzania (TADB)”. Benki hii inatarajiwa, kama itaanzishwa, kutoa mikopo kwa wawekezaji katika sekta ya kilimo. Wakati mchakato wa kuanzishwa kwa benki hiyo maalumu ukiendelea vyanzo mbalimbali vya kupata fedha za kutekelezea Kilimo Kwanza vimeanzishwa ambavyo ni pamoja na kuhamasishwa kuanzishwa kwa benki za kijamii; SACCOS, pamoja na kuitumia Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB).

Upatikanaji wa mikopo iwawezeshe wazalishaji wadogo wadogo kununua vitendea kazi vya kujikwamua na kilimo cha mkono.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 18 5/24/13 3:01 PM

Page 23: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

19

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Kupitia TIB kuna madirisha mawili ya kuweza kupatia mikopo, dirisha la kwanza ni kwa wale wanaojihusisha na uzalishaji wa mazao na mifugo, usindikaji, na uuzaji. Wakati dirisha la pili ni kwa wote ambao mikopo yao itatolewa kwa taasisi zinazojihusisha na masuala ya fedha au kilimo kama vile benki za kijamii; SACCOS; Asasi za Kiraia; VICOBA na taasisi nyingine za kifedha mbalimbali kwa mujibu wa makubaliano. Kwa upande wa riba wale wa dirisha la kwanza watatozwa asilimia tano(5%) kwa mwaka na kwa wale wa dirisha la pili watatozwa asilimia nne(4%) lakini kwa masharti kuwa wasitoze wateja watakaokuwa wanachukua mikopo kutoka kwao zaidi ya asilimia nane(8%) kwa mwaka. Uchambuzi wa kitafiti uliofanywa na wadau mbalimbali walioshiriki katika utafiti huu unaonyesha kuwa nafasi ya mzalishaji mdogo kupata mikopo hii na kunufaika nayo bila kupata matatizo ni ndogo sana hasa kutokana na ukweli kuwa mabenki mengi ya kibiashara yanaendeshwa kwa misingi ya kibiashara ili kupata faida na kujiendesha na utoaji wa mikopo si huduma kama inavyoelezewa kwa urahisi. Aidha, ni vigumu kwa benki kuendesha kwa viwango vya chini kabisa vya riba na kujiendesha bila kutegemea pesa toka serikalini kitu ambacho kitaifanya benki hii iwe mrija mwingine wa kupeleka fedha kwa kundi dogo la wazalishaji wakubwa huku wale wa ngazi ya msingi wakikosa vigezo.

i. Kiwango cha chini kinachotolewa na TIB ni milioni hamsini (50) ambacho ni kiasi kikubwa sana kwa wazalishaji wadogowadogo ambao katika uzalishaji wao hawajawahi kuwa na mtaji mkubwa kiasi hicho hata kama watajiunda katika vikundi.

ii. Aidha, wazalishaji wadogowadogo kukopa kutoka katika taasisi nyingine za kifedha nje ya TIB na kutozwa riba ya asilimia nane (8%) badala ya asilimia tano(5%) inayotozwa na TIB bado ni mzigo mzito sana hata kama watawezeshwa kukopa kiasi kidogo au cha kati.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 19 5/24/13 3:01 PM

Page 24: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

20

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

iii. Pia, suala la kuwa na mali ya kuweka rehani ili kuweza kupata mkopo, na kimsingi mali inayohitajika kwa rehani ni ardhi yenye hatimiliki. Hii ni changamoto kubwa sana kwa wazalishaji wadogowadogo ambao ni vigumu kwao kuwa na hatimiliki katika ardhi wanazozitumia kutokana na ugumu uliopo katika kuzipata hati hizo. Na hata kwa wale wenye nazo bado kuna vikwazo kutokana na mazoea tu ya mabenki ya kibiashara kutoziamini wala kupenda kuzipokea hatimiliki za kimila kwa madai kuwa hazitoi ulinzi thabiti wa mikopo inayotolewa.

iv. Kikwazo kingine kwa wazalishaji wadogowadogo kupata mikopo ni kuendesha kilimo kinachotegemea mvua za msimu wakati huo huo benki na taasisi za kifedha zikiendeshwa kwa misingi ya kibiashara isiyojali wala kuangalia kukwama kwa msimu wa kilimo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kama vile kukosekana kwa mvua. Hali hii inasababisha wazalishaji wadogowadogo kuwa na wasiwasi wa kuingia katika mtego wa kupoteza mali zao walizoziweka rehani endapo watashindwa kurejesha mikopo kwa wakati.

Uhakika na upatikanaji wa pembejeo kwaajili ya Kilimo Kwanza kwa wazalishaji wadogoKuimarisha na kukuza kilimo kuna maana ya kukifanya cha kisasa na cha kibiashara zaidi. Ili kutimiza hayo yote, suala la uwepo wa pembejeo za kisasa kwa kilimo ni jambo la muhimu sana. Hii ni kutokana na ukweli kuwa kilimo cha Tanzania kimeshindwa kukua kutokana na wakulima walio wengi kutegemea jembe la mkono ambalo halina tija katika uzalishaji kwa maeneo mengi ya nchi. Suala la kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za kisasa limepewa uzito mkubwa katika azma ya Kilimo Kwanza. Kwa mfano, kwa mujibu wa shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa maarufu kama SUMA JKT ambalo ndilo lilishinda zabuni ya kuwa wasambazaji wakubwa wa pembejeo hizi, zana zinazotolewa msukumo ni matrekta na pawa tila. Zana hizi zimeagizwa kwa wingi na shirika hili na zimekuwa zikisambazwa sehemu mbalimbali

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 20 5/24/13 3:01 PM

Page 25: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

21

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

nchini hasa kwenye halmashauri za Wilaya. Kwa mujibu wa takwimu za shirika hili la usambazaji, hadi kufikia Oktoba 2010, takribani pembejeo za aina mbalimbali mia tatu thelathini na sita (336) kama vile trekta zenye uwezo tofauti tofauti, pawa tila za uwezo mbalimbali, mashine za kupandia, mashine za kupalilia, na mashine za kuvunia zilishaingizwa nchini kwaajili ya utekelezaji wa Kilimo Kwanza.

Hata hivyo, pamoja na SUMA JKT kuwa na pembejeo za aina hii kwa wingi na kufanya matangazo ya uhamasishaji kwa wananchi kuzinunua, bado wazalishaji wadogowadogo wamekuwa si wanufaikaji wakubwa wa zana hizi kutokana na mapungufu mengi yaliyoko katika utaratibu wa upatikanaji wake, bei kuwa kubwa pamoja na uimara wa zana zenyewe. Kwa mfano, gharama za ununuzi wa trekta wakati wa utafiti huu zilikuwa kati ya milioni 40 na 50 kutegemeana na aina ya treka na uwezo wake bei ambayo wazalishaji wa kawaida vijijini hawawezi kuzimudu. Pia gharama za vipuri na matengenezo kwa ajili ya pembejeo hizi ni kubwa na hazipatikani kwa urahisi maeneo ya vijijini jambo linalozidi kuwakatisha tamaa wazalishaji wadogowadogo na kuwafanya waamini kuwa kilimo kwanza ni kwa ajili ya wazalishaji wakubwa.

Kuna mitizamo mbalimbali kutoka kwa wadau wanaojihusisha na kilimo kuhusiana na pembejeo hizi, miongoni mwao kuna wanaopongeza upatikanaji wa pembejeo na wengine wanalalamikia uimara wa pembejeo katika maeneo yao ya kilimo wakati wengine wanalalamikia bei. Wakati wa utafiti, mmoja wa wanachama wa TUNAWEZA SACCOS ya Chalinze aliipongeza SUMA JKT kwa kuwawezesha kupata pawa tila kwa bei yenye punguzo. Wakati huo huo, wanachama wa taasisi ya Kilimo Konde wakilalamika kuwa trekta na pawa tila walizonunua zimeshindwa kuhimili ardhi ya Konde na kuwasababishia hasara kubwa katika matengenezo hata kabla ya kuzalisha chochote.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 21 5/24/13 3:01 PM

Page 26: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

22

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Kutokana na hali hii, suala la pembejeo kwa ajili ya utekelezaji wa Kilimo Kwanza linaonekana kukosa uchambuzi yakinifu kuhusiana na aina na gharama za pembejeo zinazotakiwa kwa ajili ya kilimo kulingana na mazingira na hali ya udongo wa maeneo tofauti tofauti nchini. SUMA JKT na wadau wengine wanaojihusisha na uagizaji na uuzaji wa pembejeo ni muhimu kulifikiria hili kutokana na kukwamisha maendeleo ya kilimo na kuwaingiza wazalishaji wadogowadogo katika hasara kwa kushindwa kulipa mikopo wanayochukua kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo.

Mabadiliko ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5, 1999 katika utekelezaji wa Kilimo Kwanza. Nini hatma ya wazalishaji wadogo Mojawapo ya rasilimali muhimu katika maendeleo ya sekta ya kilimo ni ardhi. Sote tunatambua kuwa bila ardhi inayofaa kwa uzalishaji, hakuna kilimo hata kama yangetolewa maazimio kutoka mbinguni. Azimio la Arusha ndilo lililotambulisha dhana

Dhana za kilimo kama tractor za mkono (Power Tiller) zinaweza tu kutumika sehemu tambarare lakini sehemu za milimani hazisaidii.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 22 5/24/13 3:01 PM

Page 27: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

23

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

ya Ujamaa na Kujitegemea mwaka 1967 ambalo liliainisha wazi kuwa msingi mmojawapo wa maendeleo ya Mtanzania ni ardhi. Ukifanya uchambuzi yakinifu utagundua kuwa, tamko hili bado ni muhimu hata leo kutokana na ukweli kuwa zaidi ya asilimia 74 ya watanzania wote wanategemea kilimo kuendesha maisha yao. Kwa maana hiyo ardhi ni msingi wa maisha yao. Ardhi hii si tu kuwa ni muhimu kwa kilimo cha mazao lakini pia kwa ufugaji, madini na miundombinu.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi, Tanzania inaelezewa kuwa na ardhi ya kutosha ambayo bado haijatumika ipasavyo. Kati ya hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo cha aina mbalimbali inaelezwa kwamba ni chini ya asilima 10 ya ardhi hiyo inatumika. Wapo wasiokubaliana na takwimu hizi lakini pia wapo wanahitaji uchambuzi zaidi wa takwimu hizi ili kubainisha ni ardhi ya aina gani, iko wapi, na inafaa kwa zao gani inayozungumzwa hapa. Mtazamo wa Mtaalamu wa masuala ya kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, Daktari Damian Gabagambi ni kuwa;

Aidha, takwimu zinaonyesha kuwa ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo inapatikana vijijini na hutambulika kama ardhi ya vijiji. Kwa mujibu wa sheria ardhi ya vijiji namba 5 ya mwaka 1999 ardhi ya vijiji inamilikiwa kimila. Kumilikiwa ardhi hii kimila kwa mujibu

Kama ilivyotolewa kwenye Gazeti la The Guardian - 26/7/2011

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 23 5/24/13 3:01 PM

Page 28: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

24

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

wa sheria inazipa mamlaka za ngazi ya kijiji (Halmashauri ya Kijiji na Mkutano Mkuu wa Kijiji) madaraka ya kuhusika katika usimamizi na taratibu nyingine zote zinazoambatana na usimamizi ikiwa ni pamoja na kugawa ardhi kwa watumiaji wa ardhi wa ndani na kutoka nje ya kijiji husika.

Hali kadhalika, ili mamlaka za vijiji ziendelee kuwa na kauli ya mwisho katika ardhi za vijiji ni lazima wagawe ardhi katika viwango na kiasi fulani tu, mfano ekari hamsini (50), na ardhi hiyo sharti imilikiwe kimila kwa kupata cheti cha hatimiliki ya kimila. Ni kutokana na uwezo huu ulioko kwenye vyombo vya vijiji katika usimamizi wa ardhi ndipo Kilimo Kwanza katika nguzo ya tano (5) kifungu cha kwanza kinasomeka “Kurekebisha Sheria yaArdhiyaVijijiNa.5ya1999ilikuwezeshaupatikanajiwaardhikwauwekezajiwaKILIMOKWANZA”. Hapa ndipo linapokuja pendekezo la marekebisho ya sheria ya ardhi ya vijiji ili kuweza kupunguza au kuondoa uwezo wa vijiji katika ardhi kwa lengo la kuruhusu wawekezaji mbalimbali kupata ardhi kwa haraka na hatimiliki zinazokubalika na kuaminika kwenye taasisi za kifedha zaidi ya hatimiliki za kimila zitakazowaruhusu kuchukua mikopo

Migogoro ya ardhi ya kama ilivyotolewa kwenye Gazeti la The Guardian - 17/8/2011

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 24 5/24/13 3:01 PM

Page 29: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

25

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

kwa ajili ya utekelezaji wa Kilimo Kwanza. Utamzuiaje mwanakijiji kuamini kuwa kilimo kwanza kimekuja kupora ardhi yake wakati msisitizo wa kurekebisha sheria unalenga kuhawilisha ardhi ya vijiji kuwa ya jumla na kuiweka katika benki ya ardhi au kuwagawia wawekezaji wakubwa kama ambavyo imekuwa ikifanyika?

Kimsingi mapendekezo ya mpango wa kufanyia marekebisho sheria ya ardhi ya vijiji ni kutengeneza njia pana zaidi ya kuelekea kuukumbatia umaskini miongoni mwa wazalishaji wadogowadogo ambao rasilimali pekee na muhimu wanayoitegemea ya ardhi itaishia kwenye umiliki wa watu wachache (wawekezaji wakubwa). Ni vema kukabiliana na ukweli kuwa, vijiji vitapoteza mamlaka juu ya ardhi zao kwa kuwa ardhi ya kijiji itabidi ibadilishwe kwenda kwenye ardhi ya jumla ili mwekezaji aweze kupata hatimiliki ya ardhi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 inayosimamia ardhi ya jumla chini ya Kamishina wa ardhi. Ili kulinda haki ya mzalishaji mdogo katika ardhi ya kijiji na hata kuongeza tija katika uzalishaji wa mali kwa kutumia rasilimali ardhi, ni vema nguzo ya tano ya kilimo kwanza ikalenga katika kufanya marekebisho yafuatayo badala ya ilivyo sasa.

[ Kwanza, kuboreshwa kwa cheti cha hatimiliki ya kimila ili kitambulike katika taasisi za kifedha kwa wazalishaji wadogowadogo kupatia mikopo. Cheti hicho kinaweza kuboreshwa kwa kukipa sifa zaidi kwa maana ya ardhi yenye cheti hicho kupimwa na kuwekewa vipimo vitakavyosaidia kutambulika ukubwa wake.

[ Pili, kuondoa ukomo wa ekari hamsini katika uidhinishaji wa ardhi inayoweza kugawiwa kwa mwanachi na serikali ya kijiji ili kutoa fursa zaidi kwa wananchi kutumia maeneo yao kujiendeleza kwa njia ya kilimo. Hii inatokana na ukweli kuwa, serikali na mikutano mikuu ya vijiji imekuwa ikitumika

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 25 5/24/13 3:01 PM

Page 30: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

26

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

kuhawilisha ardhi yao ili itumiwe na watu wengine pale waombaji wanapohitaji ardhi kubwa zaidi ya ekari hamsini huku idhini hiyo ikitolewa na mamlaka za juu kama vile halmashauri ya Wilaya, ofisi ya kamishina wa ardhi na Rais mwenyewe.

[ Tatu, utekelezaji wa Mpango wa Matumizi bora ya ardhi kwenye ardhi ya vijiji ni suala la kuzingatia sana katika utekekelezaji wa Kilimo Kwanza. Ni vyema ukawa mpango wa lazima kufanyika kabla ya ardhi ya kijiji kugawiwa kwa watuamiaji wa aina yoyote. Kutekelezwa kwa mpango huu kutaondoa matatizo yaliyopo sasa yanayotokana na viongozi wa vijiji na wanavijiji wenyewe kugawa ardhi yote ya vijiji kutokana na kutofahamu ukubwa wa ardhi iliyopo katika kijiji. Hali hii ya kutozingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi imekuwa chanzo kimojawapo cha migogoro ya ardhi baina ya makundi ya watumiaji wa ardhi.

[ Nne, ni muhimu kwa sheria kutambua kuwa walinzi wa ardhi ya vijiji ni wanavijiji wenyewe kwahiyo lazima matumizi yake yawanufaishe moja kwa moja. Maana yake ni kuwa ardhi inayotolewa kwa wawekezaji kwa ajili ya kilimo basi kodi zote na mapato mengine kwa mujibu wa sheria yaende moja kwa moja kijijini ili kuboresha maisha ya wananchi wenyewe kupitia kuimarisha miundombinu na huduma mbalimbali za jamii. Hali hii itasaidia kuondoa malalamiko na migogoro ya mara kwa mara kati ya wananchi na wawekezaji katika ardhi ya kijiji.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 26 5/24/13 3:01 PM

Page 31: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

27

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

SURA YA NNE

MAPENDEKEZO NA HITIMISHO

MapendekezoKatika kitini hiki cha kujielimisha, tumeona jinsi ambavyo kilimo kwanza siyo wazo jipya bali ni mwendelezo wa jitihada za serikali katika kuhakikisha kuwa sekta ya kilimo inaongoza harakati za taifa za kujiletea maendeleo na kuwakwamua wananchi wake kutoka katika lindi la umaskini. Tumeona pia jinsi ambavyo sekta mbalimbali zimehusishwa lakini zile sekta za msingi kama ufugaji na uvuvi zikipewa msisitizo hafifu licha ya umuhimu wake kwenye jitihda hizi mpya za kuleta mapinduzi ya kijani. Uchambuzi umeonyesha kuwa, kilimo kwanza kingekuwa na tija zaidi endapo wananchi wa ngazi ya msingi ambao hasa ndio wazalishaji wadogowadogo wangehusishwa kikamilifu katika kuibua hoja na kuainisha changamoto zinazoikabili sekta hii kutokana na uzoefu wao. Kukosekana kwa vichocheo hivyo muhimu vya maendeleo endelevu kunalifanya azimio hili lililopewa kipaumbele na uzito mkubwa katika maendeleo ya sekta ya kilimo kukosa mashiko na kulipunguzia mantiki pia. Yapo mapendekezo kadha wa kadha ambayo yamekuwa yakitolewa na ambayo yakizingatiwa yatatoa tija zaidi kwa tamko hili na mapinduzi ya kijani yaliyokusudiwa. Baadhi yake kwa ufupi sana ni kama yafuatayo;

u Kuwepo chombo cha kuunganisha wazalishaji wakubwa na wadogo ili kuwainua wazalishaji wadogo kwa mitaji, teknolojia na mbinu za uendeshaji wa kilimo chenye tija kwa kutumia nyenzo na pembejeo za kisasa kama ilivyokusudiwa. Kwa ilivyo sasa, wanufaikaji wakubwa ni wazalishaji wakubwa na hawana kiunganishi chochote na wazalishaji wadogo.

u Serikali iweke mfumo utakaowezesha wanavijiji kutumia ardhi yao kama sehemu ya mtaji na kuingia ubia au mikataba na wawekezaji wakubwa ili kuweka mazingira

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 27 5/24/13 3:01 PM

Page 32: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

28

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

ya kila kundi kufaidika na rasilimali ya ardhi badala ya kundi moja la wazalishaji wakubwa kunufaika peke yao.

u Uanzishwe utaratibu utakaowawezesha wakulima kuingia mikataba ya kuzalisha mazao na kuwauzia wakulima wakubwa kwa mfumo ambao pande zote mbili zitakuwa na fursa ya kukubaliana bei kabla ya msimu wa uzalishaji kupitia chombo kitakachokubaliwa na pande zote mbili. Utaratibu huu utaongeza uzalishaji na kulinda ardhi ya wazalishaji wadogo isiondoke kwenye milki yao na kupunguza migogoro baina ya pande zote mbili.

u Suala la pembejeo za kilimo pia ni jambo linalohitaji mtazamo mpana zaidi hasa katika upatikanaji wake kwa makundi yote na uimara wa pembejeo husika kwa kuzingatia mazingira na udongo wa sehemu mbalimbali za nchi. Suala la gharama za pembejeo kuwa juu kama vile trekta na pawa tila limezidi kulalamikiwa miongoni mwa wazalishaji wadogo wadogo.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 28 5/24/13 3:01 PM

Page 33: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

29

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

HitimishoWakati mkakati wa Kilimo Kwanza unaanzishwa mapema 2009 wananchi walio wengi hasa wazalishaji wadogo wadogo walikuwa na matumaini makubwa kuwa wamekomboka kutoka katika lindi la umaskini lililowazingira kwa miaka mingi. Matumaini na matarajio ya wazalishaji wadogo wadogo hawa yameyeyuka ghafla baada ya faida walizofikiri kuwa wangezipata mapema ili kuboresha kilimo kuwa ngumu kupatikana kama vile matrekta na pawa tila pamoja na mikopo. Kinachoonekana kwa wengi sasa ni wasiwasi mkubwa walionao katika kupoteza ardhi yao kutokana na wimbi kubwa la wawekezaji wanaoingia katika ardhi za vijiji kwa ahadi nzuri zisizotekelezeka za kuboresha maisha ya wanavijiji. Pia mapendekezo yaliyoko katika mkakati wa Kilimo Kwanza ya kubadilisha sheria ya ardhi ya vijiji yanazidi kuwasha hisia za wasiwasi miongoni mwa wazalishaji wadogo wadogo kuwa ni mwendelezo wa kupoteza ardhi yao waliyoitunza kwa muda mrefu na kuitumia katika kuendesha maisha yao kwa kuwa ardhi ndio kila kitu katika maisha kwao.

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 29 5/24/13 3:01 PM

Page 34: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

30

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Marejeo

HAKIARDHI 2011 Research report on the implications of

Kilimo Kwanza to the rights to land and

other resources of the small producers

TGNP 2010: A policy brief on Kilimo Kwanza.

URT 2008: Kilimo Kwanza. Nguzo kumi za Kilimo

Kwanza na mpango wa utekelezaji wa

Kilimo Kwanza

URT 2006: Investment opportunities in the

Agricultural sector 2006

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 30 5/24/13 3:01 PM

Page 35: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

31

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 31 5/24/13 3:01 PM

Page 36: NAF YA ANZANIA ANZAihi.kazi.pro/wordpress/wp-content/uploads/2017/08/KILIMO...Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. (ii) Taasisi imefanikiwa kuibua

32

NAFASI YA MZALISHAJI MDOGO NCHINI TANZANIAKILIMO KWANZA

Kitini cha 3, Kilimo kwanza.indd 32 5/24/13 3:01 PM