mwezi wa rajab - qssea.net · mfano wa kijahiliya wa utukuzaji wa mwezi wa rajab. amesema abu rajaa...

15
MWEZI WA RAJAB BAINA YA KUFUATA NA KUZUA KIMEANDIKWA NA: ABU – ABDUL – BAARY AHMAD BIN EL – HAJJ KIMETAFSIRIWA NA: DARUL – KARAMAH.

Upload: dinhnguyet

Post on 26-Aug-2018

265 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

Page 1: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

MWEZI WA RAJAB

BAINA YA KUFUATA NA KUZUA

KIMEANDIKWA NA:

ABU – ABDUL – BAARY AHMAD BIN EL – HAJJ

KIMETAFSIRIWA NA:

DARUL – KARAMAH.

Page 2: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni bora zaidi, twalitupa ( la zamani) na kuchukua hilo jengine. Iwapo hatukupata jiwe, twakusanya mrundo wa mchanga, kisha twaleta mbuzi kumkama juu yake, kisha tukamzunguusha. Na uingiapo mwezi wa Rajab, twatoa mwito wa kung’oa vyembe (vya mikuki, wakati huo hatuachi mkuki ulio na chembe, wala na mshale) ulio na chembe, isipokuwa sisi (hung’oa vyembe vya mkuki na mshale) tukautupa – ufikapo mwezi wa Rajab.

Imepokewa na Imam Bukhary (4376).

Kwa Jina la MwenyeziMungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu. Ewe Mola Mkarimu, Saidia. Shukrani zote ni zenye kumthubutikia Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyeleta siku na miezi awezaye kuondoa miaka na zama, ajuaye khiyana ya macho na kilicho fichwa na nyoyo. Na Rehma na Amani zimfikie Mtume wake, na aliye mwaminifu wake juu ya wahyi wake, mbora wa kuamrisha, na mtukufu wa kuamrishwa. Ama baada ya hayo: kwa hakika miongoni mwa mambo mazito yenye madhara zaidi katika dini: ni kuzidi uzushi katika sampuli zake mbalimbali, na kutofautiana viwango vyake ambavyo vimechafua uzuri wa dini, na kuzima nuru yake, na kuharibu usafi wake na utohara wake. Hapo hawakurudi kujuwa watu wa kawaida: Ni yapi aliyo yapanga Mola katika sheria kwa waja wake na niyapi ambayo ni ya sunnah ya Mtume wake (Rehma na amani zimfikie) kwa wafuasi wake? Na niyapi ambayo yamekuwa ni mazoea katika desturi na yakupanga, mpaka zikawa hizo destrui na mambo yakupanga ndizo imani na ibada ambazo watu wanazifanya, kujikurubisha nazo kwa Mola muumba wa Ardhi na Mbingu. Na kwa hakika walisimama wanavyuoni watukufu na warithi wa Mitume waliotekeleza wajibu wao, wazamani na wasasa – Twamshukuru Allah – walisimama kidete kuilinda sunna na kuitetea, na kupambana na uzushi na kujitenga nao. Na miongoni mwa kazi yao hiyo ilikuwa: kutahadharisha watu kutokana na uzushi ambao watu waliuzowea katika mwezi wa Rajab,(1) na watu wakarithiana uzushi huo, zama baada ya zama, bila ya kupima wala kuhakikisha usawa wake! Ewe mtaka haki na ukweli, haya pokea huu uhakika kwa dakika chache, huenda Mwenyezi Mungu akakunufaisha nao, ukaweza kuiokoa nafsi yako, na ukajitolea. UHAKIKA WA KWANZA: Elewa ewe ndugu mpendwa kwamba, Mola (Aliyetukuka) amezitukuza na amezifanya bora: zama na sehemu ili waja wapate njia mbali mbali za kutenda wema na twaa na wazidishe amali njema kiasi wanavyoweza.

Page 3: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

Mola (Aliyetukuka) hahusishi wala hafadhiilishi wala halitilii mkazo jambo isipokuwa kwa MAANA MAALUM ambayo yanafuatana na uhusishaji na ufadhilishaji huo juu yake.(2) Je, mwezi mtukufu wa rajab una ubora zaidi kuliko miezi myengine? Amesema Al–Hafidh Bin–Hajar(MwenyeziMungu amrehemu):Haikupokewa hadithi sahihi ifaayo kuwa hoja,iliyo husisha ubora wa mwezi wa Rajab,wala kufunga mwezi huo, wala kufunga siku maalumu katika mwezi huo,wala kusimama usiku maalumu (kwa ajili ya ibada) katika mwezi huo. Na hakika amenitangulia kukata kauli kama hii ;Al – Imam Abu Ismael Al–harawiyyu Al–Haafidh(3), tumeipokea hadithi hii kwa mapokezi sahihi. Na vilevile tumeipokea kutoka kwa wengine.(4) Kisha akataja idadi ya hadithi dhaifu na (maudhui) za kuzua ambazo wanazitegemea wasioelewa wakawa wanazifanya ni hoja na dalili. Na kuwapotosha waja wa Mwenyezi Mungu. MIONGONI MWA HADITHI (MAU–DHUI) ZA KUZUA

(1)Ubora wa Rajab juu ya miezi myengine yote ni kama ubora wa Qur’aan juu ya (DHIKR) utajo mwengine wowote.

(2)Rajab ni mwezi wa Mwenyezi Mungu na shaabani ni mwezi wangu, na Ramadhan ni mwezi wa Ummah wangu.

(3)Rajab ni mwezi wa Mwenyezi Mungu wa kujipinda, Mwenye kufunga siku moja katika rajab kwa imani na kutaraji malipo, atawajibika kupata radhi za Allah aliye mkubwa.

(4)Atakaye funga siku tatu katika Rajab Mola humuandikia funga ya mwezi mzima na atakayefunga siku saba, milango saba ya moto hufungwa kwake (asiingie humo).

(5)Atakaye funga Rajab na akaswali rakaa nne kwenye mwezi huo, hatokufa mpaka aone makaazi yake katika pepo. Au aoneshwe.

(6)Hakika mwezi wa Rajab, ni mwezi mkubwa, atakayefunga siku moja kwenye mwezi huo,Mola humuandikia funga ya miaka elfu moja.

Page 4: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

MIONGONI MWA HADITHI DHAIFU

(7)Ewe Mola tubarikie katika Rajab na Shaabani na utufikishe Ramadhan.

(8)Hakika katika pepo kuna mto uitwao Rajab, maji yake ni meupe sana kuliko maziwa, na ni matamu sana kuliko asali, atakaye funga siku moja ya Rajab Mola atamnywesha kutokana na mto huo.

(9)Na hadithi: Kwamba Mtume (Rehma na amani zimfikie) hakufunga baada ya Ramadhan isipokuwa Rajab na Shaaban. Hili ni pori kubwa la Hadithi Dhaifu na (maudhui) kuzua ambazo nyingi hatukuzitaja lakini zimekusanywa na kuhesabiwa na kutahadharisha nazo wanavyuoni mabingwa, wachambuzi wenye ukweli na nasaha na itikadi iliyosalimika katika vitabu vyao vyenye manufaa ya kudumu, na utunzi wao wenye muongozo. Atakaye faida zaida basi anaweza kuvipitia vitabu na utunzi huu: kama kitabu kiitwacho: AL – MAUDHUUAAT–CHA BIN AL –JAWZY. Na kitabu: AL –MANAARUL – MUNIF CHA BIN AL – QAYYIM. Na kitabu: AL –FAWAA– ID AL –MAJ–MUU–AH CHA AL –SHAWKANY… Na kwa hizi sababu zote (zilizotajwa kwenye vitabu hivi) vyote, aliandika Mtunzi kwenye maelezo mafupi ya kitabu Kwamba: Atakayefunga mwezi huo kwa kuamini eti ni mwezi bora kuliko myezi myengine, atapata dhambi na ataaziriwa. Basi zingatia ewe ndugu, Mola akulinde na wala usifanye kibri! UHAKIKA WA PILI: Hakuna matukio yoyote yaliyotokea katika mwezi wa Rajab. Amesema mwanachuoni Bin Rajab Al – han – Baly (Radhi za MwenyeziMungu zimfikie). Hakika kumepokewa hadithi kuwa: kulikuwa na matukio makubwa katika mwezi wa Rajab, na hakuna hata hadithi moja ambayo ni sahihi katika hadithi hizo.6 MIONGONI MWA HADITHI HIZO – Kumepokewa kwamba Mtume (Rehma na amani zimfikie) alizaliwa usiku wa kwanza katika mwezi wa Rajab na kwa uhakika yeye Mtume (Rehma na aman zimfikie) alitumilizwa siku ya (27) katika mwezi huo. Na inasemakana alitumilizwa siku ya (5) katika mwezi huo. Hakuna usahihi wa habari hii. UHAKIKA WA TATU: Tukio la Israi na Miraaj ni miongoni mwa miujiza na ubora mkubwa wa Mtume wetu Muhammad (Rehma na amani zimfikie). Hakika imekuwa

Page 5: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

mashuhuri na imeenea katika miji mingi ya kiislamu na miji myengineo, kufanya hafla ya kuikumbuka safari hii ya Al – Israa na Miraaj usiku wa (27) katika Rajab.Na hakuna dalili juu ya kufanya Hafla siku hiyo! Amesema Bin Rajab Al – Han – Baly (MwenyeziMungu amrehemu); Hakika kumepokewa Hadithi kwa mapokezi ambayo sio sahihi kutoka kwa Qassim Bin Muhammad; kwamba (Al – Israa) kupelekwa Mtume (Rehma na amani zimfiki) hadi Baitul – Muqaddas ilikuwa (27) katika mwezi wa Rajab. Mapokezi haya yamepingwa na Ibrahim Al – Harby. (7) Amenukuu Al – Hafidh Bin Hajar kutoka kwa DIHYA neno lake: Baadhi ya watoaji visa wameeleza kuwa Al – Israa ilikuwa katika mwezi wa Rajab. Akasema AL – Hafidh: Huo ni urongo.(8) Na ametaja Abul- Fidai Ismail ibn Kathir katika(AL– BIDAYAH) Kwamba wako watu wanaodai kwamba Al–Israa ilikuwa usiku wa Ijumaa ya kwanza katika mwezi wa Rajab usiku huo ni usiku wa (Raghaib) mapendekezo ambayo ilizushwa swala mashuhuri. Na wala hayo yote hayana asli – wallahu aalam.(9) Na haki ambayo yakunjua na yatuliza moyo, ni muelekeo wa Sheikhul Islaam ibn Taimiyah (MwenyeziMungu amrehemu) namna alivyosema.;- Haikuja dalili maalum, juu ya mwezi huo wala siku kumi za mwezi huo wala katikati yake, bali hadithi zilizonukuliwa katika Rajab, ni zenye kukatika tena zatofautiana, hapana ambayo yafaa kutumika, wala hawakuwekewa sheria waislamu kuhusisha usiku huo ambao unatajwa kuwa ndio usiku wa Al–Israa,, kusimama (kufanya ibada) wala kufanya jambo jengine na hata pia hawakuwa maswahaba na wala wenye kuwafuata hao kwa wema, hawakuwa na kawaida ya kuhusisha usiku wa Al – israa kwa jambo lolote na wala walikuwa hawautaji usiku huo kwa ajili hii, haujulikani, ulikuwa usiku gani.10 Hivi ni kwamba lau kama kufanya hafla usiku huo ni jambo la kisheria angelibainisha Mtume (Rehma na amani zimfikie) kwa Ummah wake Ima kwa kusema au kwa kutenda. Na lau kungetokea kitu chochote kuhusiana na mwezi huo kingejulikana na kingekuwa mashuhuri. Na pia maswahaba wangetuandikia (wangetufikishia kutangulia). Maswahaba wamenukuu kutoka kwa Mtume wao (Rehma na Amani zimfikie) kila kitu kinacho hitajiwa na umma.Na wala hawakuacha kitu katika dini, bali wao ndio wa kwanza kutangulia kweny kila aina ya kheri.(14) Basi tuyafanye yale tuyawezayo kadiri ya uwezo wetu kama ambavyo waliyafanya wayawezayo kadiri ya uwezo wao, na tutwae wasia wao kwani wao ni watu ambao hapotoki atakayetwaa rai zao na kauli zao. JAMBO MUHIMU LA KUMALIZIA UHAKIKA HUU: Wamesema wanavyuoni: hata lau kumethubutu ushahidi sahihi waziwazi, isingefaa kwa yoyote, kwa sababu haikupatikana hadithi kutoka kwa Mtume (Rehma na amani zimikie) wala kutoka kwa maswahaba wake au Tabi– eena- kama ilivyo tangulia bayana yake na ufafanuzi wake – kuwa wao walitofautiana kwa usiku huo, au waliufanya mwezi wa Rajab – kwa ajili yake – unasifa,mbali na Munkar unaofanyika ndani yake.

Page 6: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

Mola ana hekima kubwa kwa kuwazahaulisha watu usiku huo.(11) Na wale waliochangia kusema kuwa ni uzushi kufanya hafla siku hii (1)Al – Imam Bin Al–Nahhaas (MwenyeziMungu amrehemu ) alokufa ( Hijria 814) alisema wazi kwamba kufanya hafla usiku wa Al–Israa ni(Bid’ah kubwa katika dini na ni uzushi uliozushwa na ndugu za mashetani(12). (2)Na ameeleza mwenye AL – MADKHAL 1/ 294 Kwamba: Miongoni mwa Bidah walizozizua katika mwezi wa Rajab usiku wa (27) ni yale yafanywayo usiku wa miraaj......... (3)Na imeswihi kutoka kwa Sheikh Muhammad Bin Ibrahim kwamba amesema: kufanya hafla kwa kuikumbuka siku ya Israa na Miraaj ni batili ni jambo la uzushi, hivyo ni kujifananisha na mayahudi na manaswara katika kuzitukuza siku ambazo hazikutukuzwa na sheria.13 Hivi ni kwamba lau kama kufanya hafla usiku huo ni jambo la kisheria angelibainisha Mtume (Rehma na amani zimfikie) kwa Ummah wake Ima kwa kusema au kwa kutenda. Na lau kungetokea kitu chochote kuhusiana na mwezi huo kingejulikana na kingekuwa mashuhuri. Na pia maswahaba wangetuandikia (wangetufikishia kutangulia). Maswahaba wamenukuu kutoka kwa Mtume wao (Rehma na Amani zimfikie) kila kitu kinacho hitajiwa na umma.Na wala hawakuacha kitu katika dini, bali wao ndio wa kwanza kutangulia kweny kila aina ya kheri.(14) Basi tuyafanye yale tuyawezayo kadiri ya uwezo wetu kama ambavyo waliyafanya wayawezayo kadiri ya uwezo wao, na tutwae wasia wao kwani wao ni watu ambao hapotoki atakayetwaa rai zao na kauli zao. JAMBO MUHIMU LA KUMALIZIA UHAKIKA HUU: Wamesema wanavyuoni: hata lau kumethubutu ushahidi sahihi waziwazi, isingefaa kwa yoyote, kwa sababu haikupatikana hadithi kutoka kwa Mtume (Rehma na amani zimikie) wala kutoka kwa maswahaba wake au Tabi– eena- kama ilivyo tangulia bayana yake na ufafanuzi wake – kuwa wao walitofautiana kwa usiku huo, au waliufanya mwezi wa Rajab – kwa ajili yake – unasifa,mbali na Munkar unaofanyika ndani yake. UHAKIKA WA NNE: Kufanya umra katika mwezi wa Rajab: Watu wengi wanaamini kwamba kufanya umra katika mwezi wa Rajab malipo yake ni makubwa na thawabu zake ni nyingi na haya pia hayana asili. Amepokea Imam Al – Bukhary na Muslim katika sahihi zao kutoka kwa Mujahid;amesema: Niliingia Msikitini mimi na Ur –wah Bin Zubeir mara tukamuona

Page 7: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

Abdullahi Bin Umar (Radhi za MwenyeziMungu zimfikie) amekaa kuelekea chumba cha Aisha, mara (Tukaona) Watu wanaswali msikitini swala ya Dhuha akasema Mujahidi tulimuuliza Bin Umar kuhusu swala yao hiyo akasema, Ni uzushu. Kisha akamuliza ni mara ngapi alifanya umra Mtume (Rehma na amani zimfikie) ? akasema Bwana Umar mara nne, Moja katika mara hizo, ni katika mwezi wa Rajab. Tukachukia kumrudishia jibu. Akasema Mujahid tulisikia mtafuno wa meno wa (15) Aisha mama wa waumini katika chumba, akasema Ur–wah ewe mama! Ewe mama wa waumini! Hela husikii ayasemayo Abu Abdirahman? Akasema Aisha: Yuasema nini? Akasema Ur-wah yuasema „ hakika Mtume wa MwenyeziMungu (Rehma na Amani zimfikie) alifanya umra mara nne, moja katika mara hizo ni katika mwezi wa Rajab. Akasema Aisha: Mola atamrehemu Abu Abdir Rahman,(16) Mtume hakufanya Umra yoyote isipokuwa yeye alimshuhudia, na hakufanya umra kamwe katika mwezi wa Rajab. Akasema: Na Bin Umar alikuwa yuasikia. Hakusema: laa wala hakusema naam, alinyamaza.(17) Amesema mwanafunzi wa Imam Nawawiy aitwaye Al – Atwaar (Mola amrehemu) aliyekufa 724 Hijriya; Na kutokana na yaliyonifikia kutoka kwa watu wa Makkah – Mola aizidishie utukufu – walikuwa na mazowea ya kufanya umra mara nyingi katika mwezi wa Rajab. Haya ni mazungumzo ambayo sijui asli yake inatoka wapi(18) Lakini lau mtu ataenda umra katika mwezi wa Rajab bila ya kuingiza itikadi ya aina ya ubora bali hakuwa na nafasi (uwezo) isipokuwa wakati huo, kwa hivyo, hapana ubaya Inshaallah. UHAKIKA WA TANO: Kuhusisha mwezi wa Rajab kwa kufunga na itikafu: Amesema Bin Rajabu katika kitabu LATWAIFUL – MAARIF(228) „ Ama kufunga, hakuna hadithi sahihi hata moja kutoka kwa Mtume (Rehma na amani zimfikie) wala kutoka kwa maswahaba wake iliyotaja ubora wa kuuhusisha mwezi wa Rajab. Amesema Sheikhul Islam ibn Taimiyah; Ama kuuhusisha mwezi wa Rajab kwa kufunga, hadithi zake zote ni dhaifu, bali ni ( Maudhui) za kuzua, wasomi hawazitegemei hata moja miongoni mwazo.Hadithi dhaifu hutumika katika mambo ya fadh-la ,yaliyomazuri, lakini hadithi zilizotaja ubora wa kufunga au kufanya umra katika mwezi wa Rajab , zote ni katika hadithi maudhui za urongo alizozuliwa Mtume (Rehma na Amani zimfikie). Lakini imeswihi (Athar) kwamba Umar Bin Al–Khatwab(Radhi za MwenyeziMungu zimfikie) alikuwa akipiga mikono ya watu ili waweke mikono yao kwenye chakula katika mwezi wa Rajab, (kuweka mikono kwenye chakula inamaanisha aliwalazimisha wale chakula chao na akisema: Musiufananishe na Ramadhani, sijui kama kuna amri (katika sheria).(19)

ATHARI NYENGINE ZIADA KUTOKA KWA WANAVYUONI WETU

WALIOTANGULIA. (1) Imepokewa kutoka kwa Khar –shata Bin Al–Hurri Amesema: Nilimuona Umar akiwapiga mikono wanaotarajia ( malipo ya funga ya mwezi

Page 8: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

mzima wa Rajab ili mikono yao ipate kula chakula) na akasema Umar: Kuleni hakika huo ni mwezi uliokuwa ukitukuzwa zama za jahiliya.(20) (2) Imepokewa kutoka kwa Bin Umar kuwa yeye alikuwa aonapo watu na vile wanavyouchukulia mwezi wa Rajab, alikuwa akichukia na akisema: : Fungeni na mule katika mwezi huo.(21) Na inaonyesha kuwa rai ya Bin Umar katika kuchukia funga ya Rajab mwezi wote, rai hii ilienea (ilieleweka) katika zama zake. Na baadhi ya watu walimuelewa vibaya, wakawa wanasema kuwa Bin Umar asema ni haramu funga hii Hakika alisema Abdullaahi aliyekuwa mtumwa wa Asmaa bint Abi – Bakar: alinituma Asmaa. Niende kwa Abdillahi Bin Umar, akasema Asmaa (maneno aliyomtuma Maula wake Abdullaahi akamwambie Abdullahi bin Umar) Imenifikia khabari kuwa wewe unaharamisha mambo matatu: (1) Bendera kwenye nguo. (2) Nguo yenye Rangi rangi inayomtoa mtu kwenye khushui (3) Na funga ya Rajab yote! Akaniambia Abdallah Bin Umar: ama haya uliyoyataja ya Rajab, waonaje kwa afungaye milele?(22) Na imeswihi (Athar) kutoka kwa Bin Abbass kwamba yeye alikuwa akikataza funga ya Rajab mwezi wote, ili usije ukafanywa eed.(23) Na ameandika Ibn Qudama katika kitabu chake: Al Mugh–ni (3/167) mapokezi ya Ahmad kutoka kwa Abu Bakrata kwamba yeye aliingia kwa watu wake na mbele yao kuna vikapu vipya na mtungi. Akasema hivi ni nini? Wakasema: Twafunga mwezi wa Rajab aksema: hivi mnaufanya mwezi wa Rajab ni Ramadhan? Vile vikapu akavipindua juu chini na ule mtungi akauvunja. Amesema Ibn Qudamah: Amesema Ahmad; Ambaye alikuwa akifunga sunnah, atafunga, kama si hivyo, asifunge mfulilizo, afunge na ale kwenye mwezi huo, na wala asiufananishe na Ramadhan kwa sababu kuutukuza mwezi wa Rajab ni miongoni mwa mambo yaliyozuliwa ambayo yafaa tuyaepuke, na kuufanya mwezi wa Rajab ni msimu kwa namna ya kuutenga peke yake kwa funga, hilo ni makuruhu kwa Imam Ahmad (MwenyeziMungu amrehemu) na wengineo.(24) Ametaja Ibn Al–Qayyim katika kitabu chake Al–Zaad kwamba yeye hakufunga miezi mitatu mfululizo – Rajab, Shaaban na Ramadhani ama wafanyavyo baadhi ya watu, wala hakufunga Rajab kabisa, wala hakuipendekeza funga yake. Ufupi wa mas-ala haya ni kwamba atakayekuwa na kawaida ya kufunga au kusimama au jenginelo katika Ibada zilizowekwa kisheria, hapana makosa kwake kufanya hivyo katika mwezi wa Rajab mtukufu hasahasa kufunga. Hakika imeswihi kutoka kwa Mtume kwamba yeye amesema: Funga katika miezi mitukufu na uwache. Akasema hivyo mara tatu. (25)

Iwapo atapenda mtu kufunga katika hali kwamba, yaaminika kuwa hataingia kwenye haramu na lisije likaenea ili isije ukafanywa faradhi au sunnah–basi hapana ubaya.(26) UHAKIKA WA SITA:Kutoa zaka katika mwezi wa Rajab.

Page 9: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

Na katika yale wanayo yafanya watu zama hizi katika kutoa zaka za mali ndani ya mwezi wa Rajab pasipo na nyakati nyenginezo, basi tendo hilo hali halina asili bali hukumu ya kisheria ni kwamba ni lazima kutolewa zaka za mali pale tu zinapopitiwa na mwaka kwa masharti yake sawasawa iwe katika mwezi wa Rajab au mwengineo(27). Na amesema mwanachuoni Ibn Rajab: „ Na wala jambo hilo halina asili yoyote katika mafundisho ya bwana Mtume (Rehma na Amani zimfikie).Na wala halikutambulikana na yoyote katika wanavyuoni waliotangulia......... na kwa hali yoyote itakavyo kuwa inalazimu kutoa zaka pindi tu itakapotimia mwaka na kufikia kiwango chake; na kila mtu ana mwaka wake unao muhusu kulingana na wakati wake wa kumiliki kiwango hicho cha zaka, na utakapo timu mwaka wake imelazimu kutoa zaka yake katika mwezi wowote na iwapo ataharakisha kuitoa zaka yake kabla ya kutimia mwaka basi itafaa kwa maoni ya wanavyuoni waliyo wengi. (28). UHAKIKA WA SABA: Kuchinja ndani ya mwezi huu wa rajab Jueni enyi wapendwa ya kwamba kuchinja wakati wowote katika mwezi huu inafaa na wala haikukatazwa kwa neno lake Mtume (Rehma na Amani zimfikie):Chinjeni kwa ajli ya Allah katika mwezi wowote na mumtendee wema Allah (29). Lakini watu wa zama za jaahiliyah walipokuwa wakichinja wanyama kwa ajili ya waungu au mashetani yao walikuwa wa kiwaita:A’tiirah au Rajabiya (yaani wanyama wanao chinjwa katika mwezi wa Rajab zama za jahiliya kwa lengo la kutaka kujikurubisha kwa Masanamu yao). Aliashiria Mtume (Rehma na Amani zimfikie) kwenye waungu hao kwa kusema: hakuna ibada ya kuchinja itwayo Far–a (30) wala Atiirah (31) katika Uislamu.(32) Na katika Hadithi nyengine ni kwamba Mtume(Rehma na amani zimfikie)alikataza far–a na Atiirah(33) na wala hakubatilisha Mtume (Rehma na amani zimfikie yeye)asili ya mambo haya,isipokuwa yeye amebatilisha sifa na namna inavyotekelezwa ibada hii.Na Far–a imeitwa hivyo kwa kuwa ni mnyama wa kwanza anayezaliwa na kuchinjwa ( kwa ajili ya masanamu), nayo Atiira imeitwa hivyo kwa kuwa ni kinachochinjwa huhusishwa tu katika mwezi wa Rajabu.(34) UHAKIKA WA NANE: Kuufanya mwezi huu kuwa ni msimu na siku kuu. Amesema Ibn Rajab: „ na kunafananishwa kuchinja katika mwezi wa Rajab: na kuufanya mwezi huu kuwa ni msimu maalum na siku kuu kama vile kula haluwa (vitu tamu tamu) na vyenginevyo; Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas (Radhi za MwenyeziMungu zimfikie) ya kwamba yeye alikuwa akichukia kuona mwezi wa Rajab ukifanywa kuwa ni sikukuu, na ukweli wa jambo hili ni kwamba sheria ya kiislamu haipasishi siku kuu yoyote kwa waislamu isipokuwa ile ambayo sheria imepasisha kuwa sikukuu, nayo ni siku ya Fitri ( siku ya kwanza ya mfungo mosi) na siku ya kuchinja ( siku ya kumi ya mfungo tatu) pamoja na siku tatu za Tashreeq baada ya siku hii ya kumi, nazo ni sikukuu za mwaka ukiongezea siku ya Ijumaa ambayo ni sikukuu ya wiki.Ama siku zinazofanywa kuwa ni siku kuu na msimu wa kusherehekea zisizokuwa hizo zilizotajwa, basi itakuwa ni uzushi usiokuwa na asili yoyote katika sheria.(35) Na amesema Ibn Taymiyah (MwenyeziMungu amrehemu); Na ama kujiekea msimu usiokuwa misimu yakisheria kama yalivyohusishwa baadhi ya masiku ya mwezi wa mfungo sita kuwa ni usiku wa kuamkia mazazi ya Mtume (Rehma na Amani zimfikie) au baadhi ya masiku ya mwezi wa Rajab, au tarehe kumi na nane ya mfungo tatu, au Ijumaa ya kwanza ya Rajab, au tarehe nane ya mfungo mosi ambayo wasiokuwa na elimu huuita

Page 10: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

siku kuu ya watu wema, lakini ukweli ni kwamba, kufanya hivyo ni katika uzushi ambao hawakuupendekeza na wala hawakufanya wanavyuoni wema waliotangulia.Allah Subhana ndiye ajuaye.(36) UHAKIKA WA TISA: Na miongoni mwa yale waliyo yazua watu katika mwezi huu na kuyaeneza pembe zote za ardhi: ni swala ya Raghaib! Na katika kufafanua uhakika wa swala hii (a) Tarehe ya kuzuka na kudhihiri kwake. Amesema Hajjiy Khalifah; Walitunga baadhi ya waongo hadithi ya uongo katika karne ya tatu kuhusu fadhla ya swala hiyo, kisha ikawa mashuhuri kwenye karne ya nne. Na miongoni mwa walioitolea dalili juu ya fadhila yake ni Abu Taalib Al Maky(37) na kufuatiwa na Al – Ghazaaly(38) kwa kutegemea hadithi (maudhui) (39) na amesema Imam Al–Turtuushy (MwenyeziMungu amrehemu): Na amenielezea Abu Muhamad Al maqdisy ya kwamba haikupatikana kamwe kwetu sisi katika nyumba takatifu ( Baitul Maqdis) swala ya Raghaaib hii inayo swaliwa katika mwezi wa Rajab na Shaabani, na ndicho kitu cha kwanza kilichozuka kwetu katika mwaka wa 448 Hijria,Ni kwamba alitujia mtu mmoja ndani ya nyumba takatifu kutoka Naabulsa kwa jina bin Abu-Hamraai msomaji mzuri wa Quran.Akasimama na kuswali ndani ya msikiti wa Al–Aqswa usiku wa kuamkia nusu ya mwezi wa Rajab haikuwahi kuzuka kwetu katika nyumba takatifu isipokuwa baada ya mwaka wa mia nne na thamanini(480 hijria)tulikuwa bado hatujaiona swala hiyo wala kuisikia kabla ya hapo.(40) (b) NAMNA YAKE: Imepokewa katika hadithi ya kuzua kutoka kwa Anas ya kwamba Mtume (Rehma na amani zimfikie)Amesema; Hakuna mtu yoyote atakayefunga siku ya al- khamis ( ya mwanzo wa mwezi wa Rajab kisha akaswali baina ya Isha na Atamah (yaani usiku wa kuamkia Ijumaa) rakaa kumi na mbili, akawa atasoma katika kila rakaa suratul Faatiah mara moja na (Innaa anzalnahu fii-lailatil qadr) mara tatu na ( Qul huwallahu ahad ) mara kumi na mbili akipambanua kati ya kila rakaa mbili kwa kuleta salamu na baada ya kumaliza swala yake akaniswalia mara sabiini na akasema katika sijda yake

( Subbuuhu Qudduss Rabbul malaa-ikatu walruuh) mara sabiini kisha akaenua kichwa chake na kusema;

Rabiqhfir warham watajaawaz amaa ta’lamu innaka antal Azizi Al A adhwam mara sabiini kisha asujudu mara ya pili na kusema vile alivyosema katika sajda ya kwanza, kisha akamuomba Allah (Aliyetukuka) haja yake, basi hapana shaka haja hiyo ( kukidhiwa) kutekelezewa. Amesema Mtume(Rehma na Amani zimfikie)

Page 11: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

Na apa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, hakuna mja yoyote wakiume wala wakike atakayeiswali swala hii isipokuwa Allah humsamehe dhambi zake zote hata kama zitakuwa nyingi mfano wa povu la bahari, na idadi ya mchanga, na uzani wa majabali na majani ya miti na watapata maombezi siku ya kiyama watu mia saba katika jamaa zake ambao wamestahiki kuingia motoni. Hii ni hadithi ya kuzua ameitaja mwanachuoni Al Shaukany kwenye (fawaidul Majmuua uk 47/48) Na ameitaja Ibnul Jauzy kwenye (kitabu chenye kukusanya hadithi za kuzua(2/124–125)kisha akasema; Hakika amezua aliye ziweka hadithi hizi kwani inahitajia kwa Mwenye kuiswali swala hii afunge,na huenda mchana kukawa na joto kali na lau atafunga na asipate kula mpaka kuswali swala ya maghribi kisha akasimama hapo hapo kuiswali swala hiyo ambayo inatasbihi hiyo ndefu na sijda ndefu basi atakuwa ameiudhi nafsi yake mno; nami ninaghera ya mwezi wa Ramadhan na swala yatarawehe, vipi imesongamanishwa swala hiyo ya Raghaib na hii na ya Tarawehe? Bali swala hii kwa wengi wasiojua ndiyo swala kubwa na tukufu, kwani huudhuriwa na hata asiye hudhuria swala za jamaa. Kwa hivyo ndio maana amesema Ibnul Qayyim katika kitabu chake (AL MANAR – AL MUNIIF) UK 96): Hadithi za swala ya Raghaaib usiku wa kuamkia ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Rajab zote ni za uongo na kuzuliwa Mtume (Rehma na Amani zimfikie) kwa hiyo usighurike – ewe mwenye akili – kwa fat-wa ya Imam Ibn Swalah aliyetoa wakati wake mwingi katika kuzikusanya dalili kwa ajili ya kuitetea( BID-A) Uzushi huu, kwani si jengine ila tu ni kuteteleka na kuteleza kwa mwanachuoni ambako hakuna budi. Amesema mwanachuoni Al – Hafidh Adhahaby katika kitabu chake ( SIYAR) 23/144) kuhusu mwanachuoni huyo Ibn Swalaah:Ana mas-ala mengine ambayo hana msingi nayo, amejitenga peke yake katika mas–ala hayo,nayo ni swala ya Raghaaib pamoja ya kuwa hadithi yake ni batili bila yashaka yoyote!“ na tangu kudhihirika kwa swala hii na wanavyuoni wema kuendelea kuwatahadharisha watu na swala hiyo kama vile Imam Annawawy Asshafiy (MwenyeziMungu amrehemu) aliyesema:Inampasa kila mtu kujikanya na swala hii,na kutahadharisha na kuwaepusha watu nayo, na kuifanya kuwa ni kitendo kibaya, na atangaze makatazo yake, kwani imeswihi kutoka kwa Mtume (Rehma na amani zimfiie) kwamba amesema;

Yeyote miongoni mwenu atakaye ona jambo ovu basi alizuie kwa mkono wake na ikiwa hatoweza, basi kwa kusema, na ikiwa hatoweza, basi kwa kuchukia..’ Na ni juu ya wanavyuoni kutahadharisha na kuipuza zaidi kuliko watu wengine, kwa sababu wao ndio wanaoigwa. Na wala asighurike mtu kwa kuwa swala hii imeenea na inaswaliwa na watu wengi wasiokuwa na elimu na mfano wao, kwani wakuigwa ni

Page 12: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

Mtume (Rehma na Amani zimfikie) na yale aliyoamrisha yafuatwe, na wala sikuiga na kufuata yale aliyoyakataza na kutahadharisha nayo.’(41) Na amesema Ibn Taymiyah (MwnyeziMungu amrehemu); Na ama swala ya Raghaib, haina asli yoyote, bali niuzushi haikupendekezwa kuswaliwa kwa jamaa wala kwa mtu pekeyake. Imethubutu katika swahihi Muslim ya kwamba Mtume (Rehma na amani zimfikie) amekataza kuhusishwa usiku wa kuamkia ijumaa kwa kusimama (kwa ajli ya Ibada) au siku ya ijumaa kwa kufunga, na amri iliyotajwa yakutekeleza swala hiyo ni uongo mtupu kwa makubaliano ya wanavyuoni, na wala hakuna yoyote katika watu wema waliotangulia na maimamu, aliyetaja amri hiyo hata chembe.’ (42) Na imeswihi kutoka kwa Al – Izz Ibn Abdi ssalam mfalme wa wanavyuoni ya kwamba amesema; Na kinachojulisha juu ya kuzuliwa kwa swala hii, ni kwamba wanavyuoni ambao wao ndio bendera za dini, na viongozi wa waislamu wakiwemo maswahaba , Tabeen, Tabiitabeen, na wengineo walioandika vitabu vinavyohusu sheria, wakiwa na pupa zaidi juu ya kuwafundisha watu FARADHI na SUNNAH lakini haikunukuliwa kutoka kwa yoyote miongoni mwao kuwa ameitaja swala hii wala hatakuandikwa kwenye kitabu chake wala kuigusia kwenye vikao vyake.(43) Na vipi mambo yatakuwa, pindi maovu na mambo ya haramu yatakapoungana na uzushi huu kama vile: ‚ kujumuika kwa wanawake na waume usiku katika hali ile inayotambulika kwenye mjumuiko wao na kuwa hapana budi kupatikana yasiyofaa na kuongezea kuwasha kandili na mengineo................ na mwenye kuhudhuria miongoni mwa wenye vyeo kwa upande wa dini hali ya kuwa yuajuwa jambo hilo ni jaraha lakujitakia mwenyewe ila pale atakapotubia, na ama iwapo atahudhuria kwa lengo la kuzuia na ikawa anauwezo wakufanya hivyo kwa kufuata sharti zake basi pongezi kwake.’(44) UHAKIKA WA KUMI: Nini hukumu ya kuswali swala hii Baada ya ufafanuzi huu na kulieka ( jambo hili) bayana katika hali ya kuwapaka mafuta viongozi na kutaka kuwaridhisha watu na ikawa ni kila mwaka Amesema Imam Abu Shaamah ( Allah ampe pumzi njema); Na maimamu wangapi wameniambia ya kwamba : haiswali swala hiyo ila tu, ya kutaka kuhifadhi nyoyo za watu kwake na kuendelea kuushikilia msikiti wake kwa kuhofia asije akaondolewa kwenye msikiti huo.!! Na kwa hali kama hii kuna kuingia kwenye swala bila ya nia sahihi na kufanya dharau kusimama mbele ya Allah (Aliyetukuka).Na lau hakungekuwa katika Bidaa hii jambo lolote lisilokuwa hili, basi lingetosha!! Na kila anayeiamini swala hii au kuiona kuwa ni nzuri, basi atakuwa ni mwenye kusababisha kutenda tendo hilo la uzushi,na atakuwa ni mwenye kuwaghuri watu kwa kile walicho kiamini haliyakuwa ni wenye kuizulia uongo sheria kwa sababu ya swala hii.Na lau wangeonyeshwa vyema na kujulishwa swala hii mwaka baada ya mwaka, wangelijitoa na kuivunjilia mbali, lakini uongozi wa mwenye kuipenda hiyo Bidaa kuihiuyisha huondoka. Na Allah ndiye mwenye kuafiki. Kwani viongozi wa watu waliopewa kitabu (AHLUL KITAB) walikuwa wanashindwa kuingia katika Uislamu

Page 13: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

kwa kuhofia kuondokewa na utawala wao. Na kwao wao ndio limeteremka neno(45)lake Allah

Basi adhabu kali itawapata wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao kisha wakasema; hiki kinatoka kwa Allah(wanasema uongo huo) ili wachukue thamani ndogo ya kilimwengu. Basi ole wao kwa yale waliyoyaandika kwa mikono yao (wa kasingizia kuwa ya Mungu) Na ole wao kwa yale wanayoyachuma.“ ( Al – Baqarah: 76) Haya ndiyo ya mwisho niliyo weza kuyakusanya, na kheri ndiyo niliyokusudia na nasaha nimezitoa. Allah atuafikie sisi pamoja na nyinyi kwa ajili ya kuinusuru sunnah na wafuasi wake, na kujiepusha na Bidaa na hatari yake. Na ewe Mola mrehemu na mbariki m’bora wa viumbe vyako Muhamad Ibn Abdillah na juu ya aali zake na maswahaba zake na kila aliyempenda.

Page 14: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

KIMEANDIKWA NA:

ABU ABDUL– BAARY AHMAD IBN EL – HAJJ Mwezi wa MwenyeziMungu Muharram mwaka 1422h

(1)Mwezi wa Rajab umepawa jina hili lo na maana (utukufu) kwa sababu waarabu walikuwa wakiutukuza katika zama za jahiliya, walikuwa hawapangi vita katika mwezi huu (2)Zaad Al Maad(1/59) Li ibn Qayeem (3)Kuniya yake ni Abu Ismail , naye ni katika kizazi cha Abu Ayyuob Al Ansari (Radhi za MwenyeziMungu zimfikie) amezaliwa mwaka 396h alikuwa ni mwenye kuinusuru sunnah,na akipiga vita Bid-ah (uzushi) alipatikana na mitihani mingi na aliudhiwa sana na alitaka kuuwawa mara nyingi Alikuwa amehifadhi hadthi elfu kumi na mbili kwa kuzitaja moja kwa moja..kama ilivyo katika siyaar liDhahabi (18/503-518) (4) Tabyeen al ajab(uk-8) (6)Latwaiful Maarif;(ukurasa wa 134) (7)Latwaiful Maarif(ukurasa wa 134) (8)Tbyeenul –ajab uk 6 Fat-hul baary 7/242-243 Al-Raheeqil-makhtoom uk 137 (9) Al-Bidayah ;(3/89) (10) Imenukuliwa kutoka kwa Ibn Qayeem katika zaad (1/58-59) (11) Atah-dhir minal Bid-a Libni Baaz(ukurasa 19) (12) Tanbih Al-Ghafilina ( ukurasa 37) (13) Fatawa wa Rasail Sheikh Muhammad ibn Ibrahim Aal Sheikh (3/103) wa Rasail Sheikh Muhammad ibn Ibrahim Aal Sheikh (3/103 (14) Al-Tah-dhiri minal Bid’a (ukurasa 8) (15)Mtafuno wa meno....(Annihaayah 3/401) (16)Bi-Aisha alimtaja Abu-Abdulrahman kwa jina hili;(Babake Abdulrahman) kwa kumtukuza, ikaonekano kama kwamba alisahau jina lake la uhakika(Al-Fat-hu;3/758) (17)Wamesema Ulamaa: Kunyamaza kwake kumejulisha kuwa alitatizika au alisahau au alikuwa na shaka, kwa ajili hii alinyamaza kumpinga Aisha kuyarudia maneno Nawawy 8/459 (18)Al-Musaajalatul-Ilmiyyah. (20)Al Irwai (957) (21)Al Irwai (958 22)Al Irwai (3/115) (23)Amepokea Abdulrazaq katika musanaf namba (7854)na akaiswahihisha sanad yake Hafidh katika Tabyinil ajab(uk 35 (24) Al-Iktidhaa(2/642) (25)Imepokewa na Ahmad na Abu Daud na Ibn Majah na wengineo (26) Al-Hawadith wal Bid’a ya Twartushi (uk 131) amekufa mwaka(520 h)na Twartushi ni mji Andalus. (27) Al-Musjalatul Ilmia(uk 55 (28) Latwaiful maari (uk-133) (29)Swahihi imetolewa Ahmad na Abu Daud na wengineo (30) Far-a; kizalia cha kwanza kilikuwa kikichinjiwa miungu yao (31) Atiira; kichinjwa kilikuwa kikichinjwa zama zajahiliyi katika mwezi wa Rajab-Fat-hul Baary(9/74) (32) Muttafaqun aleihi kutoka kwa Abu hureyra (33) Swahih ameitoa An Nasai na Ahmad na wengineo. (34)Al-Fat’hi (9/839) regelea Al Manahii (3/119) Lil hilali (35) Latwaiful Maarif (uk-127) (36) Al-Fatawa;(25/298) (37) Katika kitabu chake“ Kutul Qulub alikufa mwaka386 H (38) Ihyai Ulumu Ddin. Amekufa 505 (39) Kashfu Dhunun (1081 40) Alihawadith wal Bid’a (uk-103 (41) Imenukuliwa kutoka kwa Musajjalatul Ilmia (uk-47) (42) Al Fatawa(23/132) (43) AlMusajala tul Ilmiyah(uk-9) amekufa(MwenyeziMungu amrehemu) mwaka660) hijria (44) Kutoka katika masda hiyo hiyo

45) Al Baith alaa inkaril Bid’a wal hawadith (uk-105) amekufa 665h.

Page 15: MWEZI WA RAJAB - qssea.net · MFANO WA KIJAHILIYA WA UTUKUZAJI WA MWEZI WA RAJAB. Amesema Abu Rajaa Al – Utwaaridy: “ Tulikuwa tukiabudu mawe, tupatapo jiwe jengine ambalo ni

UZUNDUSHI: Nakuna uzushi mwengine mwingi ambao hatukuutaja kwa kuhofia kurefusha kuutaja miongini mwao ni Swala ya mama Daud Katika nusu ya mwezi wa Rajab, na uzushi wa kutoa sadaka kwa roho ya wafu, na vilevile kuhusisha kuyazuru makaburi katika mwezi wa Rajab na mengineyo ya uzushi na upotevun na yasiyokuwa hayo ambayo ni lazima mtu kuyaamini kuwa ni ufisadi na batili, nakuwatahadharish waislamu wasiojuwa kuingia kwenye kuingia kwenye hayo na Allah ndiye mwenye kuafiki