mukhtasari wa sera - coral reef · kenya, tanzania, madagascar, indonesia, na papua new guinea....

10
Mukhtasari wa Sera Kukuza usimamizi shirikishi wa uvuvi mdogo kaka ukanda wa tropiki

Upload: others

Post on 18-Sep-2020

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Mukhtasari wa SeraKukuza

usimamizi shirikishi wa uvuvi mdogo katika ukanda wa tropiki

Page 2: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Ujumbe wa sera

• Usimamizi shirikishi unatoa fursa kwa watumiaji rasilimali kuwa na sauti moja katika kuunda na kusimamia sheria kwenye uvuvi mdogo.

• Ikiwa hili litafanyika vizuri itasaidia kufanya uvuvi kuwa endelevu na kudumisha maisha ya jamii inayotegemea bahari.

• Usimamizi shirikishi unakuwa na mafanikio zaidi kama kutakuwepo na mambo muhimu ya kijamii na kiuchumi, itazingatiwa hali halisi ya mahali pamoja na taasisi muhimu. Masharti haya yameainishwa katika mukhtasari wa sera hii.

Imetayarishwa na Joshua Cinner and Tim McClanahan

Wachangiaji wengine ni: MA MacNeil, NAJ. Graham, TM. Daw, A Mukminin, DA Feary, AL Rabearisoa, A. Wamukota, N Jiddawi, SJ Campbell, AH Baird, FA Januchowski-Hartley, S Hamed, R Lahari, T Morove, J Kuange

Picha ya kwenye gamba: Mvuvi wa Papua New Guinea. Picha na Joshua Cinner

Page 3: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Wavuvi wa Kenya wakitumia nyavu aina ya jarife katika miamba. Picha na Joshua Cinner

Jamii inategemea Bahari Kiasi ya watu wasiopungua milioni 200 wanategemea bahari kama sehemu ya mahitaji yao ya maisha yao. Wengi katika hawa wanaishi katika nchi zinazoendelea ambako uwezo wa serikali kusimamia uvuvi vizuri umekabiliwa na changamoto za uhaba wa fedha na watendaji kazi. Hii mara nyingi huchangia kuwepo na uongozi hafifu. Matatizo haya ya uongozi huweza kusababisha uvuvi uliokithiri ambao umeonyesha kubadili mazingira ya bahari kwa hali ya juu sana na kuhatarisha maisha ya jamii wanayoitegemea.

Nini usimamizi shirikishi?Serikali nyingi na taasisi za hifadhi pamoja na taasisi za jamii zinajihusisha katika kuwapanga watumizi wa rasilimali kujihusisha na usimamizi shirikishi katika hali ya kukuza uvuvi ili itowe matokeo bora kwa ajili ya jamii na mazingira wanayotegemea. Hii hujulikana kama “usimamizi shrikishi“ . Ni njia inayowapa fursa watumiaji kushiriki katika maamuzi yakusimamia rasilimali hizi. Mfano ni kamati simamizi za fukweni ambazo zimeanzishwa kiasi ya miaka kumi iliyopita na kuruhusu watumiaji kukuza na kutilia mkazo sheria ndogo ndogo zilizokuwepo. Sheria hizi zinategemea kukuza usimamizi wa uvuvi ambao kihistoria ulikuwa haulindwi vizuri. Mpango huu unadhamira ya kufanya usimamizi ulenge jamii yenyewe kwa kuzingatia hali halisi ya mazingira yake huku ikikuza uwezo wa jamii kufuata sheria ambazo wameziweka wenyewe.

Picha ya kwenye gamba: Mvuvi wa Papua New Guinea. Picha na Joshua Cinner

Page 4: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Wakati gani usimamizi shirikishi unafanya kazi? Kupanga jukwaa la mafanikioUthibitisho ya kuwa usimamizi shirikishi unasaidia kufanya mazingira kuwa endelevu unakuwa mkubwa. Hata hivyo, kuna baadhi ya wakati imeonyesha ya kuwa hata usimamizi shirikishi umesababisha ongezeko la uvunaji wa samaki uliokithiri, kuzidisha kutokuwepo kwa uwiano katika jamii, kutokuwepo makubaliano na kusababisha matokeo yasiyopendeza ya kijamii na kiikologia. Usimamizi shirikishi uliofanikiwa una taasisi, hali ya kijamii na kiuchumi na hali halisi ya mahali na uwiano mzuri ambao unahitaji kuzingatiwa na ma meneja na watungaji sera.

Kuzipanga taasisi vizuriTaasisi ziliopo ambazo zimejipanga na kufanya kazi ni muhimu sana katika kuhakikisha kama usimamizi shirikishi unafanya kazi. Sifa maalum za taasisi zinajulikana kama “mipango maalumu” zinasaidia kukuza mashirikiano baina ya watu. Mipango hii maalumu inajulikana kama:

• Daraja za pingamizi, Adhabu zilizopangika ambazo ni adhabu ambazo huengezeka kila kosa linapozidi kwa mfano mara ya kwanza kosa likitendeka mkosa anapewa onyo, mara ya pili anatoa faini na mwisowe anafungwa jela. Hii inasaidia kutoa mafunzo na kuweka uhalali katika sheria. Serikali inatoa mchango mkubwa katika makosa makubwa kwa kuweka uhakika wa ufatiliaji na kufanya kazi karibu na jamii kuhakikisha mambo yanatekelezeka.

• Mipaka maalumu na uwanachama, ambayo inasaidia jamii kuelewa wapi na kwa nani sheria zinalenga na nani anaziunda.

• Ushiriki wa hali ya juu, ambao unafanyika kwa njia za mikutano ambayo inashajiisha jamii kushiriki katika usimamizi hasa katika kutoa maamuzi.

• Njia za kutatua matatizo ni sehemu muhimu ya kulinda rasilimali. Kuwa na mipango kabla ya matatizo kutokea inasaidia kuhakikisha utatuzi wake wa haraka, na wa halali na wa upesi upesi.

• Uongozi wa uwazi na ufuatiliaji unatoa uhakika wa watu kuwekeza katika usimamizi shirikishi.

Mvuvi Zanzibar akizungukwa na vyombo vidogo vya kuvulia. Picha na Joshua Cinner

Page 5: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Sifa za uchumi jamii za watumizi wa rasilimali Watu wanakwepa kushiriki katika usimamizi kutokana na kutokuwa na muda na rasilimali (mara nyingi yanahusishwa na umasikini) na kuto kuelewa ya kuwa shughuli za binaadamu zinaweza kusababisha athari katika makaazi ya viumbe baharini. Hata hivyo matatizo haya yanaweza kumfanya meneja kuzingatia sera. Vikwazo vikubwa ni:

• Umasikini - Inaweza kuwa shida kwa watu kujitolea hata kwa muda mfupi katika usimamizi shirikishi hasa kama inakuwa vigumu kupata kipato japo kidogo cha kujikimu kimaisha.

• Elimu ya namna gani binaadamu anaweza kuathiri maeneo ya makaazi ya viumbe vya baharini - Inaweza kuwa vigumu kwa watu kukataa kuacha kutumia rasilimali kwa sababu hawaoni uhusiano baina ya shughuli za binaadamu (kama uvuvi) na hali halisi ya rasilimali au maeneo ya makaazi ya viumbe vya baharini.

• Utegemeaji wa rasilimali za baharini - Watu wanaotegemea sana uvuvi huona shida kufanya kazi nyengine. Lakini watu ambao wanategemea sana uvuvi ni rahisi kupata nia ya kushiriki na kutatua matatizo.

• Kipato na imani - Watu wanahitaji kuaminiana wao wenyewe na viongozi wao hasa ikiwa wanataka kufanya kazi kwa pamoja katika kutatua matatizo yaliyokabili uvuvi.

Wavuvi na wanunuzi Kenya wanagawana mapato. Picha na Joshua Cinner

Page 6: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Hali halisi ya mahali Mambo yanayoweza kuwafanya watu kushiriki au kutoshiriki katika usimamizi shirikishi ni:

• Idadi ya watu - inakuwa rahisi kwa vikundi vidogo vya watu kushirikiana na kujenga uelewa ambao ni muhimu kwa kutatua matatizo.

• Masoko - Hamu ya watu kuvunja sheria za usimamizi shirikishi husababishwa na urahisi wa kufikia masoko. Usimamizi shirikishi pia unaweza kukuza masoko na kuzidisha thamani ya bidhaa. Jambo hili linaweza kuvutia watu kushiriki na kukubaliana na usimamizi shirikishi kwa vizuri.

Soko katika Maronsetra, Madagascar. Picha na Joshua Cinner

Page 7: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Uchunguzi wa hali ya kijamii pamoja na taasisi zinazoweza kuongeza kwenda kwenye mtokeo ya maisha bora, maridhiano makubwa, na uvuvi mzuri uliangalia usimamizi shirikishi 42 katika Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea.

Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi shirikishi ulio mzuri na unaokubalika. Matokeo ya uchunguzi mkubwa wa usimamizi shirikishi katika uvuvi huko Afrika na Asia na Pacific ( Boksi) unaelezea mwelekeo mzuri wa sera juu ya:

1) Kufanya usimamizi shirikishi kuweza kufanya kazi kwa ajili ya maisha ya jamii

2) Kusaidi kukuza hali ya kukubali kuridhia na

3) Kuufanya uvuvi kuwa endelevu

Ramani ya maeneo yaliyochunguzwa kutoka repoti ya Cinner, J., TR. McClanahan MA MacNeil, NAJ. Graham, TM. Daw, A Mukminin, DA Feary, AL Rabearisoa, A. Wamukota, N Jiddawi, SJ Campbell, AH Baird, FA Januchowski-Hartley, S Hamed, R Lahari, T Morove, J Kuange (2012). Usimamizi shirikishi wa matumbawe Kijamii na kiikologia. Ndani ya National Academy of Sciences (PNAS). doi/10.1073/pnas.1121215109

Mama Karanga (mvuvi mwanamke) anasubiri samaki zaidi washushwe, Kenya. Picha na Joshua Cinner

Page 8: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Kuufanya usimamizi shirikishi kufanya kazi kwa sababu ya kudumisha maisha ya watu Somo hili limegunduwa ya kuwa watumizi wa rasilimali walikuwa na mwamko mzuri wa usimamizi shirikishi. Kiasi ya 54% ya watumiaji rasilimali 960 walisema ya kuwa uzimamizi shirikishi umewasaidia katika maisha yao. Kiasi ya 9% tu wamezungumzia kama hawakufaidika na waliobaki hawakuona faida wala hasara.Usimamizi shrikishi ulioonyesha mafanikio makubwa pale palipo kuwepo na: • Mpangilio mzuri wa taasisi husika (Mpangilo mzuri wa daraja za adhabu, mipaka iliyopangika, na mashirikiano makubwa katika

utoaji maamuzi); • Jamii inaelewa namna gani binaadamu anaweza kuathiri makaazi ya viumbe hai; • Jamii wameshirikishwa katika usimamizi shirikishi kwa muda mrefu; • Na jamii waliokuwa na uwezo zaidi wa kifedha zaidi.

Jambo la mwisho lililoonekana kuhusiana na namna usimamizi shirikishi unavyowapa faida matajiri umeonyesha ya kuwa usimamizi shirikishi una uwezo wa kupunguza ubaguzi wa kijamii kwa kutoa fursa kwa jamii wananchi wanaodhibiti rasilimali

Kwa kuwapa fursa watumiaji wa rasilimlai uwezo wa kusema jinsi rasili mali zinavyotumika na kugaiwa, usimamizi shirikishi unaweza kugawa ufikaji wa maenoa ya uvuvi na matajiri wanaweza kutumia fursa za mabadiliko yamatumizi haya.

Hakuna ushahidi ya kuwa isimamizi shirikishi ni mbaya kwa maisha ya jamii masikini. Kwa hivyo meneja, watafute njia za kuwapa faida jamii masikini kwa kuwahakikishia ya kuwa usimamizi shirikishi ni haki sawa

Hii itahitaji mgao sawa wa nguvu na kwa upande mwingine kutahitajiaka njia za kupunguza umasikini kama kutoa mikopo midogo midogo , Ikiwezekana haya yatasaidia kuongeza mafanikio ya muda mrefu ya usimamizi shirikishi.

Hatua za sera zinazohitajika kuchukuliwa

kuufanya usimamizi shirikishi kuboresha

maisha ya jamii ni kuondokana

kabisa na mawazo ya kawaida ya ma meneja.

Utekelezaji bora utahitaji kuwepo na mashirikiano na wana sayansi,

wafadhili, taasisi za kifedha na asai za

kijamii.

Tarakimu ya 1. Sera muhimu ambazo meneja wanaweza kuzitunga ili kushajiisha matokeo mazuri katika usimamizi shirikishi wa uvuvi.

Page 9: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Kuweka hali ya makubaliano Kuwafanya watu kukubali kufuata mambo yaliyokatazwa kufanya wakati wa matumizi ya rasilimali ni changamoto kubwa katika usimamizi wa uvuvi na hifadhi za bahari. Kwenye maeneo ambayo kuna upungufu wa nguvu kazi inakuwa ngumu kutilia mkazo sheria kwa mfano: ufuataji wa sheria katika maeneo yaliyokubalika kwa kuvua ni mdogo.Katika maeneo ambayo vyombo vya ufatiliaji hakuna kutahitajika njia zaidi za kufuatilia na kutilia mkazo.

Ulinzi shirikishi unaweka hali nzuri kwa watu wanaokubaliana ambayo inawafanya watu kufata sheria na kupunguza ufuatiliaji. Kwa kuwekeza kwenye njia za wazi na za makusudi za usimamizi shrikishi wafadhili na meneja wanaweza kujenga uhalali, fedha za jamii, na kukubalika yote ambayo yanajenga mashirikiano.

Mipango mingi ya usimamizi shirikishi hufanya kazi maeneo ambayo udhibiti rasmi upo mdogo kwa mfano boti hii ya doria mbovu ya Papua New Guinea. Picha na Joshua Cinner

Tarakimu ya 2. Sera ambazo meneja wanaweza kuzitilia mkazoili kuleta makubaliano katika usimamizi shirikish nwa maeno ya nuvuvi.

Page 10: Mukhtasari wa Sera - Coral Reef · Kenya, Tanzania, Madagascar, Indonesia, na Papua New Guinea. Masuala muhimu bado yamebaki ya nini waundaji sera wanaweza kufanya kukuza usimamizi

Kuufanya uvuvi kuwa endelevuTukio muhimu lililojitikeza katika somo la usimamizi shirikishi ya nchi tano ni ya kuwa uvunaji wa samaki baharini unachngiwa na kuwepo kwa masoko na hatua za utegemeaji wa rasilimali za bahari ambayo inatoa fursa ya kudhibitiwa na vipengele vya sera. Kuzingatia uhusiano baina ya makaazi ya viumbe vya baharini, maisha ya watu na urahisi wa kufikia masoko ni muhimu katika kukuza usimamizi shirikishi wa uvuvi endelevu. Haya yatahusisha kupunguza umasikini kwa njia ya kuweka kazi mbadala ambazo zina tija zaidi na kuboresha utawala bora wa masoko kwa njia mbali mbali kama kuwepo na hati za uvunaji rasilimali endelevu (Angalia tarakimu ya 2).

HitimishoHakuna mfumo mmoja wa kutatua matatizo yaliyokabili uvuvi duniani lakini mipango ya usimamizi shirikishi zinojaali hali za eneo lilipo zinaweza kusuaidia kuufanya uvuvi kuwa endelevu pamoja na watu wanaotegemea rasilimali hiyo. Hata kama umasikini umekithiri na kuna utawala dhaifu nchini

Uwezekano wa usimamizi shirikishi kuwa wa mafanikio huwa mkubwa kukiwepo na taasisi, uchumi jamii na uwiano mzuri. Jamii, wafadhili na ma meneja wanaweza kuufanya usimamizi shirikishi unaopendeka kwa kutumia mkakati ya eneo iliyopo ili kutatua matatizo magumu (Tarakimu. 1, 2. 3).

Mtumbwi umejaa samaki, Indonesia. Picha na Joshua Cinner

Tarakimu ya 3. Sera muhimu ambazo meneja wanaweza kuzitumia kufanya uvuvi endelevu.

Shukurani:Mukhtasari wa sera umetokana na waraka wa Cinner, J., TR. McClanahan MA MacNeil, NAJ. Graham, TM. Daw, A Mukminin, DA Feary, AL Rabearisoa, A. Wamukota, N Jiddawi, SJ Campbell, AH Baird, FA Januchowski-Hartley, S Hamed, R Lahari, T Morove, J Kuange. 2012. Usimamizi shirikishi wa maeneo yenye matumbawe, jamii na kiikologia.

Kazi hii imefadhiliwa na Australian Research Council, Western Indian Ocean Marine Science Association’s Marine Science for Management program, National Geographic Society, Christensen Fund, and Packard Foundation Grant 2009-33893.