kiongozi cha utaratibu wa mafunzo elekezi ya awali … · salaam, tanzania, chini ya mkataba namba...

36
JUNI 2017 Chapisho hili limeandaliwa kwa ushirikiano na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) iliyopo Dar es Salaam, Tanzania, chini ya mkataba namba AID-621-C-15-00003 na USAID/Tanzania. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA KIONGOZI CHA UTARATIBU WA MAFUNZO ELEKEZI YA AWALI KWA WATUMISHI WAPYA WA SEKRETARIETI ZA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

Upload: others

Post on 27-Oct-2019

19 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

JUNI 2017Chapisho hili limeandaliwa kwa ushirikiano na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) iliyopo Dar es Salaam, Tanzania, chini ya mkataba namba AID-621-C-15-00003 na USAID/Tanzania.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

KIONGOZI CHA UTARATIBU WA MAFUNZO ELEKEZI YA AWALI KWA WATUMISHI WAPYA WA SEKRETARIETI ZA

MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

USAID/Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) una lengo la kuisaidia Serikali ya Tanzania kuimarisha utoaji wa huduma katika sekta mbalimbali, hasa katika jamii zenye uhitaji zaidi. Ikiongozwa na kampuni ya Abt Associates Inc., PS3 inatekelezwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Ben-jamin William Mkapa, Broad Branch Associates, IntraHealth International, Chuo cha Serikali za Mitaa – Hombolo (LGTI), Tanzania Mentors Associa-tion, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Urban Institute.

JUNI 2017 Mkataba Na: AID-621-C-15-00003

Nukuu Pendekezwa: Juni 2017. Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Bethesda, MD: Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Abt Associates.

KANUSHOChapisho hili limefanikishwa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID), kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3). Ofisi ya Rais - TAMISEMI ndiyo itakayowajibika na matokeo ya kazi hii. Chapisho hili si lazima liwakilishe maoni ya USAID au ya Serikali ya Marekani.

i

YALIYOMO

DIBAJI............................................................................................................................................iiiSHUKRANI.................................................................................................................................ivVIFUPISHO VYA MANENO...................................................................................................vTAFSIRI YA MANENO...........................................................................................................vIUTANGULIZI..............................................................................................................................1MADHUMUNI............................................................................................................................2MAJUKUMU YA WADAU MBALIMBALI..........................................................................31.0 Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora............42.0 Ofisi ya Rais – TAMISEMI................................................................................................43.0 Sekretarieti za Mikoa........................................................................................................44.0 Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.........................45.0 Wizara za Kisekta...............................................................................................................46.0 Tume ya Utumishi wa Umma.........................................................................................47.0 Tume ya Utumishi wa Walimu........................................................................................48.0 Taasisi za Elimu.....................................................................................................................49.0 Bodi za Kitaaluma...............................................................................................................510.0 Mamlaka za Serikali za Mitaa........................................................................................511.0 Taasisi za Fedha.................................................................................................................512.0 Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.............................................................................................513.0 Tarafa/Kata/Kijiji/Mtaa.....................................................................................................514.0 Vituo vya Kutolea Huduma...........................................................................................615.0 Wadau wa Maendeleo.....................................................................................................6HITIMISHO................................................................................................................................21Kiambatisho Na. A - ORODHA YA WAJUMBE WALIOSHIRIKI KATIKA KIKOSI KAZI..........................................................................................................22Kiambatisho Na. B - HADIDU ZA REJEA ZA TIMU YA MAPOKEZI YA WATUMISHI WAPYA KATIKA NGAZI YA SEKRETARIETI YA MKOA NA HALMASHAURI.....................................................................................................................24Kiambatisho Na. C - HADIDU ZA REJEA ZA TIMU YA MAPOKEZI YA WATUMISHI WAPYA KATIKA NGAZI YA KATA/KIJIJI/MTAA.............................25

ii

DIBAJI

Serikali kupitia Waraka wa Utumishi Na. 5 wa Mwaka 2011 ilielekeza watumishi wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza kupatiwa Mafunzo Elekezi ya Awali ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu kuajiriwa. Aidha, Taasisi katika Utumishi wa Umma zilielekezwa kuwafahamisha watumishi wapya mazingira ya Taasisi pindi wanapori-poti katika vituo vyao vya kazi na kuwapatia taarifa muhimu. Hata hivyo, utekelezaji wa Waraka huu umekuwa na changamoto ambapo watumishi wanaoajiriwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wamekuwa wakipokelewa kwa utaratibu unaotofauti-ana kutokana na kukosekana kwa kiongozi mahsusi cha Mafunzo Elekezi.Kutokana na changamoto hii, wadau mbalimbali wamejaribu kutengeneza utaratibu ambao ni mahsusi kwa baadhi ya kada na maeneo fulani. Mfano, Taasisi ya Benjamin William Mkapa katika kipindi cha mwaka 2013, iliandaa kitini kwa ajili ya kutoa Mafunzo Elekezi ya Awali na kuwapokea watumishi wa kada ya Afya katika Mam-laka za Serikali za Mitaa. Hali kadhalika, baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikiandaa utaratibu ambao sio rasmi wa kupokea watumishi wapya ka-tika Mamlaka hizo.Hali hii imesababisha watumishi wapya kutokuwa na uelewa mzuri juu ya haki, wajibu, sheria na kanuni za Utumishi wa Umma. Aidha, watumishi wengi wame-ingia kwenye Utumishi wa Umma bila kuyafahamu maadili yanayoongoza utumishi wa Umma, taaluma za kada zao na kukosa mbinu za kukabiliana na changamoto za mazingira ya kazi, hali ambayo imechangia katika kuathiri utendaji, uvutiaji na ukaaji wa watumishi wa Umma hususan katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.Kutokana na changamoto hii, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR -TAMISEMI) kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa lengo la kuboresha utoaji huduma katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, imeandaa Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya wanaoajiriwa katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kiongozi hiki kinaweka utaratibu maalum wa utoaji wa Mafunzo Elekezi ya Awali katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi wapya na hivyo kuwa na Utumishi wa Umma wenye tija na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.Ni matumaini yangu kuwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zitatekeleza maelekezo yaliyomo katika Kiongozi hiki ili kuleta mabadiliko chanya katika Utumishi wa Umma.

Eng. Mussa I. IyombeKATIBU MKUU

iii

SHUKRANI

Ofisi ya Rais-TAMISEMI inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wadau wote waliochangia na kufanikisha uandaaji wa Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya wanaoajiriwa ka-tika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Kiongozi hiki kimeandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo (US-AID) chini ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3). OR-TAMISEMI inatambua na kushukuru mchango uliotolewa na Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Ofisi za Wakuu wa Mikoa ya Katavi, Lindi na Shinyanga; Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro; Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero; Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo na; Chuo cha Utumi-shi wa Umma Tanzania kwa kuwaruhusu watumishi wao kufanya kazi hii muhimu.

Aidha, shukrani za pekee zinatolewa kwa Wajumbe walioshiriki katika Kikosi Kazi kilichoundwa na OR-TAMISEMI kama inavyonekana katika Kiambatisho A.

iv

VIFUPISHO VYA MANENO

BMF - Benjamin William Mkapa Foundation

GSO - Government Security Officer

HCMIS - Human Capital Management Information System

HR - Human Resource

LGTI - Local Government Training Institute

MSM - Mamlaka za Serikali za Mitaa

OPRAS - Open Performance Review and Appraisal System

OR-TAMISEMI - Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

OR-MUUUB - Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

PS3 - Public Sector Systems Strengthening

TPSC - Tanzania Public Service College

TSC - Teachers Service Commission

USAID - United States Agency for International Development

v

TAFSIRI YA MANENO:

Kiongozi Kitini kinachotumika kutoa maelekezo ya mafunzo elekezi ya awali ya watumishi wapya katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa

Wadau wa Maendeleo Mtu binafsi,Taasisi, Shirika, Asasi za Kiraia, Jumuiya, Washirika wa Maendeleo

Mafunzo Elekezi ya Awali Maelekezo ya masuala ya msingi katika Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na mapokezi ya Watumishi wapya katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa yanayotolewa wakati watumishi hao wanaajiriwa kwa mara ya kwanza kwa lengo la kuwasaidia kumudu majukumu yao na mazingira mapya ya kazi.

vi

UTANGULIZI

Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinaku-sudia kurahisisha utekelezaji wa Sera ya Mafunzo katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 2013 na Waraka wa Utumishi Na. 5 wa Mwaka 2011 unaohusu Mafunzo Elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya.

Mnamo mwezi Agosti 2016, OR-TAMISEMI ilifanya utafiti kuhusu utekelezaji wa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa watumishi wapya katika Mikoa mitano (5) na Mamlaka za Serikali za Mitaa kumi na tano (15).

Utafiti huo ulibaini changamoto mbalimbali katika utoaji wa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa watumishi wapya ambapo mafunzo haya hayatolewi kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa au hayatolewi kabisa.

Hali hii imesababisha watumishi wapya kutokuwa na uelewa mzuri juu ya haki na wajibu wao, hivyo kuathiri utendaji, uvutiaji na kuwabakiza watumishi wa Umma katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kutokana na matokeo ya utafiti huo, imeonekana kuna umuhimu wa kuandaa Kiongozi cha Mafunzo Elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kiongozi hiki kinatoa utaratibu na majukumu ya Taasisi za Umma, na wa-dau wengine wa maendeleo katika utekelezaji wa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa watumishi wote wapya katika Sekretarieti za Mikoa na Mam-laka za Serikali za Mitaa.

1

MADHUMUNIKiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa Watumishi wapya wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinaweka utaratibu wa utoaji wa mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya wanaoajiriwa katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Kiongozi hiki kinakusudia kutatua changamoto za utoaji wa mafunzo hayo kwa watumishi wapya ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi wa watumishi wapya na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Utekelezaji wa Kiongozi hiki, unatarajiwa kuleta manufaa yafuatayo kwa mtumishi mpya:-

n Kufahamu Dira, Dhima na Malengo ya Taasisi;

n Kufahamu haki na wajibu wake, viwango vya utekelezaji na utaratibu uliopo katika utekelezaji wake;

n Kufahamu mazingira na mbinu za kukabiliana na changamoto zilizopo;

n Kuimarisha maadili ya Utumishi wa Umma na kujenga mahusiano mazuri baina ya mtumishi mpya na watumishi wenzake pamoja na jamii; na

n Kuwasaidia watumishi wapya kubaki katika vituo vyao vya kazi na kutoa huduma bora kwa wananchi.

2

MAJUKUMU YA WADAU MBALIMBALI

Yafuatayo ni majukumu ya wadau mbalimbali katika utekelezaji wa kiongozi hiki. Majukumu pamoja na shughuli mahsusi zitakazotekelezwa zimefafanuliwa kwa kina katika jedwali la maelekezo ya utekelezaji wa mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya wanaoajiriwa katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;

1.0 OfisiyaRais–MenejimentiyaUtumishiwaUmmana Utawala BoraOfisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ina jukumu la kutoa miongozo ya utoaji wa mafunzo kwa watumishi wa umma na kupokea nakala ya taarifa za utekelezaji wa utoaji wa mafunzo elekezi ya awali.

2.0 OfisiyaRais–TAMISEMIOfisi ya Rais-TAMISEMI ina jukumu la kupokea taarifa, kuchambua na kutoa mrejesho kutoka katika Sekretarieti za Mikoa kuhusu mafunzo elekezi ya awali katika Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na kuratibu utoaji wa mafunzo ya awali kwa watumishi wapya wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

3.0 Sekretarieti za MikoaSekretarieti za Mikoa zina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo Elekezi ya Awali katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji na kutoa taarifa OR-TAMISEMI kuhusu utekelezaji wa Kiongozi hiki, pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu namna bora ya kuendesha mafunzo hayo kwa wa-tumishi wapya wa Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa husika.

3

4.0 OfisiyaRais–SekretarietiyaAjirakatikaUtumishiwa UmmaIna jukumu la kutoa taarifa kamili ya orodha ya watumishi wapya wa-naopangwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuziwezesha Mamlaka husika kujiandaa kwa ajili ya mapokezi na mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi hao.

5.0 Wizara za KisektaWizara za Kisekta zina jukumu la kuhakikisha Sera, Sheria Kanuni na Mion-gozo ya Kisekta inawafikia watumishi wa sekta husika ikiwa ni pamoja na watumishi wapya. Pale ambapo Wizara za Kisekta zinapopewa jukumu la kuwapangia vituo vya kazi watumishi wapya zihakikishe Watumishi hao wanakidhi sifa za Miundo ya Kiutumishi.

6.0 Tume ya Utumishi wa UmmaTume ya Utumishi wa Umma ina jukumu la kusimamia uzingatiwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na utoaji wa mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

7.0 Tume ya Utumishi wa WalimuKatika kutekeleza Kiongozi hiki Tume ya Utumishi wa Walimu ina jukumu la kuwasajili walimu wapya, kukamilisha taratibu za ajira za walimu wapya na kutoa mafunzo kuhusu Maadili na Miiko ya kazi ya Ualimu.

8.0 Taasisi za ElimuChuo cha Serikali za Mitaa – Hombolo na Chuo cha Uongozi wa Ma-hakama - Lushoto vina jukumu la kutoa mafunzo elekezi ya awali, kutoa ushauri kwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu namna bora ya kuendesha mafunzo pamoja na kufanya utafiti kuhusu utoaji wa mafunzo hayo kwa watumishi wapya katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

4

9.0 Bodi za KitaalumaJukumu la Bodi za Kitaaluma ni kutoa miongozo ya kitaaluma na kufanya usajili wa wataalam wa kada husika kwa mujibu wa vigezo vilivyopo.

10.0 Mamlaka za Serikali za MitaaMamlaka hizi zina jukumu la kutekeleza Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo Elekezi ya Awali katika Mamlaka zao, kufuatilia utekelezaji wake katika ngazi ya Kata, Kijiji, Mtaa na Vituo vya kutolea Huduma na kuku-sanya, kuchambua, kuwasilisha taarifa Mkoani pamoja na kuratibu ushiriki wa wadau mbalimbali katika utoaji wa mafunzo hayo.

11.0 Taasisi za FedhaTaasisi hizi zina jukumu la kutoa huduma za kibenki kwa watumishi wapya wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na huduma ny-inginezo kwa mujibu wa Sera ya Taasisi husika.

12.0 Mifuko ya Hifadhi ya JamiiJukumu la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni kutoa maelezo kwa watumishi wapya kuhusu mafao yanayotolewa na Mifuko hiyo, kufanya usajili wa wa-nachama, kutoa kadi za uanachama na kuelezea fursa mbalimbali zinazo-tolewa na Mifuko kwa wanachama na huduma nyinginezo kwa mujibu wa Sera ya Taasisi husika.

13.0 Tarafa/Kata/Kijiji/MtaaNgazi hizi za utawala zina jukumu la kuwapokea, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya katika vi-tuo vya kutolea huduma vilivyopo katika maeneo yao na pia kutoa taarifa katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

5

6

14.0 Vituo vya Kutolea HudumaVituo vya kutolea huduma vina jukumu la kufanya maandalizi ya ku-wapokea watumishi wapya (makazi, ofisi na vitendea kazi); kuwapokea na kuwatambulisha kwa watumishi na viongozi wa eneo husika; kuwapa taarifa muhimu kuhusu mazingira, fursa, maeneo ya huduma muhimu na tamaduni za jamii za mahali kilipo kituo cha kazi. Aidha, vituo vya ku-tolea huduma vina wajibu wa kuwapangia watumishi wapya majukumu /mgawanyo wa kazi; kumpangia mtumishi mpya mshauri (Mentor); ku-peleka taarifa ya kupokelewa na kupangiwa kazi mtumishi mpya kwenye Serikali ya Kijiji/Mtaa na Halmashauri na Sekretarieti za Mkoa husika.

15.0 Wadau wa MaendeleoMajukumu ya Wadau wa Maendeleo ni pamoja na kushiriki katika mapokezi ya watumishi wapya kwa kuwezesha upatikanaji wa makazi, usafiri, chakula, fedha na vitendea kazi ili kuchangia juhudi za Serikali za kuboresha utoaji huduma bora kwa wananchi.

Jedw

ali

la

maj

ukum

u na

m

aele

kezo

ya

ut

ekel

ezaj

i w

a M

afun

zo

Elek

ezi

ya

Aw

ali

kwa

Wat

umis

hi W

apya

wan

aoaj

iriw

a ka

tika

Sekr

etar

ieti

za M

ikoa

na

Mam

laka

za

Serik

ali z

a M

itaa.

NA

. N

GA

ZI

HA

TUA

SH

UGH

ULI

M

UDA

M

HUS

IKA

REJE

A

1W

IZA

RA

Ka

bla

ya

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

tum

a o

rod

ha

ya

wa

tum

ishi

wa

pya

n

a

ma

wa

silia

no

ya

o

(na

mb

a z

a s

imu

na

an

ua

ni z

a

ba

rua

pe

pe

) kw

a S

ekr

eta

riati

za

Mik

oa

n

a

Ma

mla

ka

za

Serik

ali

za M

itaa

Siku

14

kab

la

ya

kurip

oti

Ofis

i ya

R

ais-

Sekr

eta

rieti

ya

Ajir

a;

OR

-TA

MIS

EMI;

Wiz

ara

za

Se

kta

hu

sika

Ka

nu

ni

B.7

ya

K

an

un

i za

K

ud

um

u

zaU

tum

ishi

wa

U

mm

a z

a M

wa

ka 2

009

Ku

wa

julis

ha

wa

tum

ish

i wa

pya

Mik

oa

na

Ma

mla

kaza

Se

rika

li za

M

itaa

w

aliz

op

an

giw

a

na

m

ud

a w

a k

urip

oti

Ofis

i ya

Ra

is-

Sekr

eta

rieti

ya

Ajir

a;

OR

–TA

MIS

EMI;

Wiz

ara

za

Se

kta

hu

sika

Mw

on

go

zo

kuh

usu

M

asu

ala

ya

A

jira

ka

tika

U

tum

ish

i w

a

Um

ma

wa

Mw

aka

200

9

Ba

ad

a

ya

Ku

ripo

tika

tika

ki

tuo

c

ha

ka

zi

Ku

fan

ya

ufu

atil

iaji

wa

m

ap

oke

zi

ya

Wa

tum

ishi

wa

pya

ka

tika

Se

kre

tarie

ti za

M

iko

a n

a M

am

laka

za

Se

rika

li za

Mita

a

Siku

14

ba

ad

a

ya

uko

mo

w

a

mu

da

w

a

kurip

oti

Ofis

i ya

Ra

is-

Sekr

eta

rieti

ya

Ajir

a;

OR

–TA

MIS

EMI;

OR

–M

UU

UB

; W

iza

ra

ya

Sekt

a h

usik

a

Wa

raka

w

a

Utu

mish

i N

a.

5

wa

Mw

aka

201

1

Ku

fua

tilia

ute

kele

zaji

wa

m

afu

nzo

e

leke

zi

ya

aw

ali

katik

aSe

kre

tarie

ti za

M

iko

a

na

Ma

mla

ka

za

Serik

ali

za

Mita

a

Mie

zi

3b

aa

da

ya

ku

ripo

ti

OR

–TA

MIS

EMI;

OR

–M

UU

UB

; W

iza

ra

ya

Sekt

a h

usik

a

Ka

bla

ya

K

urip

oti

Ku

fua

tilia

taa

rifa

ya

oro

dh

a

yaw

atu

mish

i w

ap

ya

na

N

da

ni

ya

siku

14

Sekr

eta

rieti

ya

Mko

aSh

eria

ya

Ta

wa

la

za

Mik

oa

N

a. 1

9 ya

Mw

aka

199

7

7

8

NA

. N

GA

ZI

HATU

A

SHUG

HULI

MUD

A

MHU

SIKA

REJE

A

2M

KO

A

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

ma

an

da

lizi

ya

kuw

ap

oke

a

katik

a M

am

laka

za

Se

rika

li za

M

itaa

kab

la

ya

mu

da

w

a

kurip

oti

Wa

kati

wa

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

toa

ush

au

ri kw

a M

am

laka

za

Se

rika

li za

M

itaa

ku

hu

su

na

mn

a

bo

ra

ya

kue

nd

esh

a

ma

fun

zo

ya

aw

ali

kwa

w

atu

mish

i wa

pya

Nd

an

i ya

si

ku14

tan

gu

w

arip

oti

kazi

ni

Sekr

eta

rieti

ya

Mko

aSh

eria

ya

Ta

wa

la

za

Mik

oa

N

a. 1

9 ya

Mw

aka

199

7

Ku

fua

tilia

w

atu

mish

i w

ap

ya

wa

na

orip

oti

kwe

nye

M

am

laka

za

Se

rika

li za

Mita

a

Siku

14

ziliz

o

ain

ishw

a

kwe

nye

Ta

ng

azo

/b

aru

a

Sekr

eta

rieti

ya

Mko

a

She

ria

ya

Taw

ala

za

M

iko

a

Na

. 19

ya M

wa

ka 1

997

Ba

ad

a

ya

Ku

ripo

tika

tika

ki

tuo

c

ha

ka

zi

Ku

fua

tilia

u

teke

leza

ji w

a

ma

fun

zo e

leke

zi y

a a

wa

li kw

a

wa

tum

ishi

wa

pya

ka

tika

M

am

laka

za

Se

rika

li za

Mita

a

Mie

zi

3b

aa

da

ya

ku

ripo

ti

Sekr

eta

rieti

ya

Mko

aSh

eria

ya

Ta

wa

la

za

Mik

oa

N

a. 1

9 ya

Mw

aka

199

7

3SE

KR

ETA

RI

ETI

YA

M

KO

A/

HA

LMA

SHA

UR

•K

ua

nd

aa

Tim

u /

Afis

a w

a

ma

po

kezi

kw

a

kuzi

ng

atia

ka

da

na

ida

di

ya w

atu

mish

i wa

pya

;•

Ku

an

da

u

tara

tibu

w

a

kuw

ap

oke

a

wa

tum

ishi

wa

pya

kw

a

ajil

i ya

ku

wa

pa

m

ae

leke

zo

ya

aw

ali

ya m

sing

i

Siku

14

kab

la

ya

kurip

oti

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/Mku

rug

en

zi

wa

H

alm

ash

au

ri

-

9

NA

. N

GA

ZI H

ATU

A SH

UG

HU

LI

MU

DA

MH

USI

KA

RE

JEA

SEK

RET

AR

IET

I Y

A

MK

OA

/H

ALM

AS

HA

UR

I

Ka

bla

ya

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

fan

ya

ma

wa

silia

no

n

a

wa

tum

ishi w

ap

ya k

wa

njia

ya

sim

u,

tovu

ti a

u

Ba

rua

P

ep

e,

vyo

mb

o v

ya H

ab

ari

(ra

dio

, TV

n

a

ma

ga

zeti)

n

a

kuw

ap

a

ma

ele

kezo

ya

n

am

na

ya

ku

fika

ma

en

eo

hu

sika

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

-

Ku

an

da

a

Fom

u

za

ku

kam

ilish

a t

ara

tibu

za

a

jira

ka

tika

U

tum

ishi

wa

U

mm

a,

mfa

no

:-

Fom

u

ya

Taa

rifa

za

K

iutu

mis

hi

(PR

F)

Ku

dh

ibiti

A

jira

K

azi

ni

(EB

1)

Fo

mu

za

Uc

hu

ng

uzi

wa

A

fya

(Re

qu

est

fo

r M

ed

ica

l Exa

min

atio

n)

Fo

mu

za

Mka

tab

a w

a

Ajir

a y

a W

alim

u

Fo

mu

za

M

ifuko

ya

H

ifad

hi y

a J

am

ii

Fom

u

ya

Ah

ad

i ya

U

ad

ilifu

Fo

mu

ya

Bim

a y

a A

fya

(N

HIF

)

Fom

u

ya

Wa

zi

ya

Ma

piti

o n

a U

pim

aji

wa

U

ten

da

ji K

azi

(O

PR

AS )

. “H

isto

ry S

he

et”

Ka

tibu

Ta

wa

law

a

Mko

a

/Mku

rug

en

zi w

a

Ha

lma

sha

uri/

Ka

tibu

TSC

Ka

nu

ni

D.1

6,

D.3

6,

D.3

7,

D.4

2 n

a D

.64

ya K

an

un

i za

K

ud

um

u

za

Utu

mis

hi

wa

U

mm

a

za

Mw

aka

20

09;

She

ria

Na

.25

ya

M

wa

ka

2015

ya

Tu

me

ya

Utu

mish

i w

a

Wa

limu

; K

an

un

i za

Tu

me

ya

U

tum

ishi

wa

W

alim

u y

a M

wa

ka 2

016

10

NA

. N

GA

ZI H

ATU

A SH

UG

HU

LI

MU

DA

MH

USI

KA

RE

JEA

SEK

RET

AR

IET

I Y

A

MK

OA

/H

ALM

ASH

AU

RI

Ka

bla

ya

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

sha

jala

kw

a a

jili

ya z

oe

zi l

a

ma

po

kezi

ya

w

atu

mish

i w

ap

ya

katik

a

Ma

mla

ka

za

Serik

ali

za

Mita

a:-

(Sc

an

ne

r,K

om

pyu

ta,

ph

oto

co

py

ma

ch

ine

, Sta

tion

erie

s)

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

-

Ku

an

da

a

seh

em

u

ya

karib

u

ya

kuto

lea

H

ud

um

a

ya

Uc

hu

ng

uzi

wa

Afy

a

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

-

Ku

wa

pa

ng

ia

vitu

o

vya

ka

zi

wa

tum

ishi w

ap

yaK

atib

u

Taw

ala

w

a

Mko

a

/Mku

rug

en

zi w

a

Ha

lma

sha

uri

-

Ku

wa

taa

rifu

w

asi

ma

miz

i w

a

vitu

o k

ufa

nya

ma

an

da

lizi

ya

kuw

ap

oke

a

wa

tum

ishi

wa

liop

an

gw

a

katik

a

vitu

o

vya

o

na

ku

toa

n

aka

la

kwa

A

fisa

Ta

rafa

,Mte

nd

aji

Ka

ta,

Mta

a/

Kiji

ji

Siku

14

kab

la

ya

kurip

oti

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

-

Ku

an

da

a

uta

ratib

u

wa

ku

wa

pe

leka

w

atu

mish

i w

ap

ya k

we

nye

vitu

o v

ya k

azi

w

aliv

yop

an

giw

a

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

-

Ku

an

da

a s

tah

ili z

a w

atu

mish

i w

ap

ya (

Po

sho

za

Ku

jikim

u n

a

Na

uli)

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

Ka

nu

ni

J.2

(1)

(a),

L.

6 ya

K

an

un

i za

K

ud

um

u

zaU

tum

ishi

wa

U

mm

a

za

Mw

aka

20

09;

Wa

raka

wa

W

atu

mis

hi

wa

Se

rika

li N

a.4

w

a M

wa

ka 2

014

Ku

an

da

a

vite

nd

ea

ka

zi

n

a

Ka

tibu

Ta

wa

la

11

NA

. N

GA

ZI H

ATU

A SH

UG

HU

LI

MU

DA

MH

USI

KA

RE

JEA

SEK

RET

AR

IET

I Y

A

MK

OA

/H

ALM

AS

HA

UR

I

Ku

wa

taa

rifu

W

ad

au

w

a

ma

en

de

leo

,ta

asi

si z

a k

ibe

nki

n

a

M

ifuko

ya

H

ifad

hi

ya

Jam

ii ku

jian

da

a

kush

iriki

an

a

na

H

alm

ash

au

ri ku

fan

ikish

a

ma

fun

zo E

leke

zi y

a A

wa

li kw

a

Wa

tum

ish

i w

ap

ya

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

Mw

on

go

zo

wa

U

an

dik

ish

aji

Wa

na

ch

am

a w

a M

ifuko

ya

H

ifad

hi

ya

Jam

ii,

2013

K

ifun

gu

N

a.7

(T

he

So

cia

l Se

cu

rity

Sch

em

es

Me

mb

ers

hip

R

eg

istra

tion

G

uid

elin

es

of

2013

)K

ua

nd

aa

m

pa

ng

o

wa

m

afu

nzo

n

a

wa

we

zesh

aji

wa

taka

oto

a

ma

fun

zo

ya

aw

ali

kwa

wa

tum

ishi w

ap

ya

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

Sera

ya

Me

ne

jime

nti

na

A

jira

ka

tika

U

tum

ish

i w

a

Um

ma

, To

leo

la 2

(20

08)

Wa

kati

wa

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

wa

po

kea

n

a

kuw

aka

ribish

a

wa

tum

ishi

wa

pya

n

a

kuw

afa

nyi

a

uta

mb

ulis

ho

Siku

7K

atib

u

Taw

ala

w

a

Mko

a

/Mku

rug

en

zi w

a

Ha

lma

sha

uri

-

Ku

kag

ua

vy

eti

ha

lisi

vya

w

atu

mish

i na

ku

wa

silis

ian

a n

a

Ma

mla

ka h

usik

a k

wa

uh

aki

ki

zaid

i

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

-

12

NA

. N

GA

ZI H

ATU

A SH

UG

HU

LI

MU

DA

MH

USI

KA

RE

JEA

SEK

RET

AR

IET

I Y

A

MK

OA

/H

ALM

AS

HA

UR

I

Wa

kati

wa

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

wa

ele

keza

w

atu

mish

i ku

jaza

fo

mu

za

ku

kam

ilish

a

tara

tibu

za

a

jira

ka

tika

U

tum

ishi w

a U

mm

a, m

fan

o:-

Fo

mu

ya

Ta

arif

a

za

Kiu

tum

ishi,

Fom

u

ya

kud

hib

iti

Ajir

a

Serik

alin

i (E

B1)

Fo

mu

za

U

ch

un

gu

zi

wa

A

fya

(R

eq

ue

st

for

Me

dic

al E

xam

ina

tion

)

Fom

u z

a M

kata

ba

Fo

mu

ya

W

azi

ya

M

ap

itio

n

a

Up

ima

ji U

ten

da

ji K

azi

(O

PR

AS)

Fo

mu

za

M

ifuko

ya

H

ifad

hi y

a J

am

ii,

Fo

mu

ya

A

ha

di

ya

Ua

dilif

u

na

“H

isto

ry

She

et”

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri/K

atib

u w

a T

SC

Mw

on

go

zo w

a U

an

dik

isha

ji w

an

ac

ha

ma

wa

Mifu

ko y

a

Hifa

dh

i ya

Ja

mii,

20

13

Kifu

ng

u

Na

.7(T

he

So

cia

l Se

cu

rity

Sch

em

es

Me

mb

ers

hip

R

eg

istra

tion

G

uid

elin

es,

20

13);

W

ara

ka

wa

Mku

u w

a U

tum

ishi

wa

U

mm

a

Na

.2

wa

M

wa

ka

2015

; K

an

uni

D.1

6,

D.3

6,

D.3

7,

D.4

2 n

a

D.6

4 ya

K

an

un

i za

K

ud

um

u

za

Utu

mish

i w

a

Um

ma

za

M

wa

ka 2

009

Ku

wa

ele

keza

w

atu

mish

i m

ah

ali

pa

kufa

nya

U

ch

un

gu

zi w

a A

fya

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri/

Ka

tibu

wa

TSC

Ka

nu

ni

D.1

6 ya

K

an

un

i za

K

ud

um

u K

atik

a U

tum

ishi w

a

Um

ma

za M

wa

ka 2

009

13

NA

. N

GA

ZI H

ATU

A SH

UG

HU

LI

MU

DA

MH

USI

KA

RE

JEA

SEK

RET

AR

IET

I Y

A

MK

OA

/H

ALM

AS

HA

UR

I

Ku

fun

gu

a j

ala

da

kw

a a

jili

ya

utu

nza

ji w

a k

um

bu

kum

bu

za

w

atu

mish

i wa

pya

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri/

Ka

tibu

wa

TSC

She

ria y

a K

um

bu

kum

bu

na

N

yara

ka

za

Taifa

N

a.3

ya

M

wa

ka

2002

n

a

Mw

on

go

zo w

a U

tun

zaji

wa

K

um

bu

kum

bu

n

a

Nya

raka

za

K

iutu

mish

i w

a

Mw

aka

20

12;

Ka

nu

ni

C.1

9 ya

K

an

un

i za

K

ud

um

u

za

Utu

mish

i w

a

Um

ma

za

M

wa

ka 2

009

Wa

kati

wa

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

wa

tam

bu

lish

a

wa

tum

ishi

wa

pya

kw

en

ye I

da

ra n

a O

fisi

za M

koa

/Ha

lma

sha

uri

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

Wa

raka

w

a

Utu

mish

iN

a.5

w

a M

wa

ka 2

011,

Kip

en

ge

le

ch

a 5

(viii

)

Wa

tum

ish

i w

ap

ya

kufu

ng

ua

a

kau

nti

be

nki

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

-

Ku

ing

iza

na

ku

zitu

ma

ta

arif

a

za W

atu

mish

i kw

en

ye M

fum

o

wa

Ta

arif

a

za

Kiu

tum

ish

i n

a

Mish

ah

ara

(H

CM

IS-L

aw

son

)

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri/

OR

-MU

UU

B

HC

MIS

Use

r M

an

ua

ls

Ku

toa

m

ae

lezo

m

uh

imu

ku

hu

su:-

i)H

aki

n

a

wa

jibu

w

a

wa

tum

ishi;

ii)M

ae

lezo

ya

K

azi

ya

w

atu

mish

i (jo

b

de

scrip

tion

);iii

)K

an

un

i za

Ma

ad

ili

ya

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

She

ria

ya

Utu

mish

i w

a

Um

ma

Na

.8 y

a M

wa

ka 2

002

na

m

are

keb

isho

ya

ke;

Ka

nu

ni

na

M

ion

go

zo

ya

Utu

mish

i wa

Um

ma

; W

ara

ka

wa

Ma

en

de

leo

ya

Utu

mish

i w

a

Mw

aka

20

02

na

N

yon

ge

za

zake

; K

an

un

i za

14

NA

. N

GA

ZI H

ATU

A SH

UG

HU

LI

MU

DA

MH

USI

KA

RE

JEA

SEK

RET

AR

IET

I Y

A

MK

OA

/H

ALM

AS

HA

UR

I

Wa

kati

wa

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ute

nd

aji

katik

a

Utu

mish

i w

a U

mm

a(C

od

e o

f Et

hic

s a

nd

Co

nd

uc

t);

iv)M

aa

dili

ya

ki

taa

lum

a

(pro

fess

ion

al

co

de

o

f c

on

du

ct)

;v)

She

ria,

Ka

nu

ni

na

Ta

ratib

u

za k

azi

ka

tika

Utu

mish

i w

a

um

ma

;vi

)Mu

un

do

na

ma

juku

mu

ya

Se

rika

li;vi

i)M

ah

usi

an

o y

a

Serik

ali

Ku

u n

a S

erik

ali

za M

itaa

; vi

ii)M

uu

nd

o n

a m

aju

kum

u

ya M

am

laka

za

Se

rika

li za

M

itaa

,ix

)Mfu

mo

w

a

Up

ima

ji w

a

wa

zi

wa

U

ten

da

ji ka

zi

(OP

RA

S), n

ax)

Ma

ele

zo

kuh

usu

h

ud

um

a

za

kib

en

ki

na

M

ifuko

ya

H

ifad

hi y

a J

am

iixi

)Ma

sua

la

Mta

mb

uka

(U

KIM

WI,

Ru

shw

a,

Ma

zin

gira

& J

insi

a)

Ma

ad

ili

ya

Ute

nd

aji

(Co

de

o

f Et

hic

s a

nd

C

on

du

ct)

ka

tika

U

tum

ish

i w

a

Um

ma

; K

an

un

i za

U

tum

ishi

wa

U

mm

a

za

Mw

aka

20

03;

She

ria N

a.

25

ya

Tu

me

ya

U

tum

ishi

wa

W

alim

u

ya

M

wa

ka

2015

; K

an

un

i ya

Tu

me

ya

U

tum

ishi

wa

Wa

limu

ya

M

wa

ka

2016

; K

an

un

i za

Kise

kta

za

Ma

ad

ili

ya

Kita

alu

ma

; R

eje

a

ya

Sera

, Sh

eria

K

an

un

i n

a

Nya

raka

Mb

alim

ba

li ku

hu

su

ma

sua

la

ya

Ajir

a

katik

a

Utu

mish

i w

a U

mm

a;

Sh

eria

ya

Se

rika

li za

M

itaa

, 19

82

Sura

287

K

ifun

gu

174

& 2

88

Kifu

ng

u

54(a

);

Ka

tiba

ya

Ja

mh

uri

ya

Mu

un

ga

no

w

a

Tan

zan

ia

ya M

wa

ka 1

977;

K

ifun

gu

(E

)(17

4)

ch

a S

he

ria

ya T

aw

ala

za

Mik

oa

Na

. 19

ya

mw

aka

199

7 &

Sh

eria

ya

Se

rika

li za

M

itaa

, Su

ra

288

K

ifun

gu

54

(a;

She

ria

ya

Serik

ali

za

Mita

a

Su

ra

287

K

ifun

gu

174

& 2

88

Kifu

ng

u

54(a

; W

ara

ka w

a U

tum

ishi

wa

Um

ma

Na

.2 w

a M

wa

ka

2006

ku

hu

su

hu

du

ma

kw

a

15

NA

. N

GA

ZI

HA

TUA

SH

UG

HU

LI

M

UD

A

MH

USI

KA

REJE

A

wa

tum

ishi

wa

U

mm

a

wa

na

oish

i n

a

Viru

si

vya

U

kim

wi

na

w

en

ye

Uki

mw

i; Sh

eria

ya

K

up

am

ba

na

n

a

Ku

zuia

R

ush

wa

N

a.1

1 ya

M

wa

ka

2007

; Sh

eria

ya

U

sima

miz

i w

a

Ma

zin

gira

N

a.4

ya

Mw

aka

200

4; S

era

ya

M

ae

nd

ele

o

ya

Wa

na

wa

ke

na

Ji

nsia

ya

M

wa

ka

2000

n

a;

Ka

nu

ni

D.4

2 &

64

ya

K

an

un

i za

K

ud

um

u

za

Utu

mish

i w

a

Um

ma

za

Mw

aka

200

9K

ufa

nya

ma

lipo

ya

st

ah

ili z

a

kiu

tum

ishi

katik

a M

am

laka

za

Se

rika

li za

Mita

a

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

Ha

lma

sha

uri

Ka

nu

ni

ya 1

3 ya

Ka

nu

ni

za

Utu

mish

i w

a

Um

ma

za

m

wa

ka 2

003;

Ka

nu

ni

J.2

(1)

(a),

L.

6 ya

K

an

un

i za

K

ud

um

u

za

Utu

mish

i w

a

Um

ma

za

M

wa

ka

2009

; W

ara

ka w

a W

atu

mis

hi

wa

Se

rika

li N

a.4

w

a

Mw

aka

20

14K

uto

a

ma

ele

zo

kuh

usu

u

sim

am

izi

na

u

tun

zaji

wa

n

yara

ka n

a s

iri z

a S

erik

ali

na

ku

mfa

nyi

a

up

eku

zi

mtu

mish

i m

pya

Afis

a

Usa

lam

a

wa

Se

rika

li

(GSO

)

She

ria y

a U

sala

ma

wa

Ta

ifa

ya M

wa

ka 1

970;

Ka

nu

ni

D

31

ya K

an

un

i za

Ku

du

mu

za

U

tum

ish

i w

a

Um

ma

za

M

wa

ka 2

009

Ku

toa

b

aru

a

ya

kum

pa

ng

ia

mtu

mis

hi k

ituo

ch

a k

azi

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

-

SEK

RET

AR

IET

I Y

A

MK

OA

/H

ALM

AS

HA

UR

I

Wa

kati

wa

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

16

NA

. N

GA

ZI

HATU

A

SHUG

HULI

MUD

A

MHU

SIKA

REJE

A

SEK

RET

AR

IET

I Y

A

MK

OA

/H

ALM

AS

HA

UR

I

/Mku

rug

en

zi w

a

Ha

lma

sha

uri

Ku

wa

pe

leka

W

atu

mish

i ka

tika

vitu

o v

yao

vya

ka

ziK

atib

u

Taw

ala

w

a

Mko

a

/Mku

rug

en

zi w

a

Ha

lma

sha

uri

-

Ba

ad

a

ya

Ku

ripo

ti ka

tika

ki

tuo

c

ha

ka

zi

Ku

fua

tilia

m

ap

oke

zi

ya

wa

tum

ishi

wa

pya

kwe

nye

n

ga

zi

ya

kitu

o

ch

a

kazi

(n

yum

ba

,m

ga

wa

nyo

w

a

ma

juku

mu

,vite

nd

ea

ka

zi)

Siku

14

b

aa

da

ya

ku

pe

lekw

a

kitu

on

i

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

-

Ku

fua

tilia

Ma

lipo

ya

M

sha

ha

ra

ya

Wa

tum

ishi

wa

pya

kw

en

ye

mfu

mo

w

a

Taa

rifa

za

K

iutu

mis

hi

na

M

isha

ha

ra

Nd

an

i ya

m

we

zi 1

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

Ku

fua

tilia

n

a

kuw

aka

bid

hi

wa

tum

ishi

wa

pya

vi

tam

bu

lish

o

vya

K

azi

, B

eji,

K

ad

i za

U

an

ac

ha

ma

w

a

Mfu

ko w

a H

ifad

hi y

a ja

mii

na

B

ima

ya

Afy

a

Mie

zi 3

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

Ku

toa

ta

arif

a

kuh

usu

m

afu

nzo

kw

a

wa

tum

ishi

wa

pya

kw

a K

atib

u M

kuu

OR

-TA

MIS

EMI

kup

itia

kw

a K

atib

u

Taw

ala

wa

Mko

a

Mw

ezi

1

b

aa

da

ya

m

afu

nzo

Ka

tibu

Ta

wa

la

wa

M

koa

/M

kuru

ge

nzi

wa

H

alm

ash

au

ri

Wa

raka

w

a

Utu

mis

hi

Na

.5

wa

Mw

aka

201

1, K

ipe

ng

ele

5(

vi)

4TA

RA

FA/

KA

TAK

ab

la y

a

Ku

ripo

ti ka

tika

Ku

fan

ya

ura

tibu

w

a

ma

an

da

lizi

ya

kuw

ap

oke

a

wa

tum

ishi w

ap

ya

Siku

7

ka

bla

ya

ku

ripo

ti

Afis

a

Tara

fa/

Mte

nd

aji

wa

K

ata

She

ria N

a.

7 &

8 y

a M

wa

ka

1982

za

Serik

ali

za

Mita

a;

Wa

raka

w

a

Mu

un

do

w

a

17

NA

. N

GA

ZI

HATU

A

SHUG

HULI

MUD

A

MHU

SIKA

REJE

A

kitu

o

ch

a k

azi

Wa

ten

da

ji w

a

Ka

ta

wa

M

wa

ka 2

014

Wa

kati

wa

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

fan

ya

ura

tibu

w

a

ma

po

kezi

ya

wa

tum

ishi

wa

pya

wa

na

orip

oti

Siku

14

za

ku

ripo

tiA

fisa

Ta

rafa

/ M

ten

da

ji w

a

kata

-

Baa

da

ya

ku

ripo

ti ka

tika

ki

tuo

c

ha

ka

zi

Ku

fua

tilia

na

ku

toa

ta

arif

a y

a

ma

en

de

leo

ya

w

atu

mish

i w

ap

ya

wa

liop

an

giw

a

katik

a

ng

azi

ya

ka

ta

na

vi

tuo

vy

a

kuto

lea

h

ud

um

a

kwe

nye

ka

ta h

usik

a

Mie

zi 3

A

fisa

Ta

rafa

/ M

ten

da

ji w

a

Ka

ta

-

5KI

JIJI

/

MTA

A

Ka

bla

ya

K

urip

oti

katik

a

kitu

oc

ha

ka

zi

•K

uw

ata

arif

u

wa

na

jam

ii ku

hu

su u

jio w

a w

atu

mish

i w

ap

ya

kwa

ku

piti

a

Ha

lma

sha

uri

ya

Kiji

ji a

u

Mta

a;

•K

ua

nd

aa

K

am

ati

ya

ma

po

kezi

ya

W

atu

mish

i W

ap

ya;

•K

ua

nd

aa

o

rod

ha

ya

m

aka

zi

kwa

a

jili

ya

wa

tum

ishi

wa

pya

kw

aku

shiri

kia

na

n

a

jam

ii iliy

op

o

Siku

7M

ten

da

ji w

a

kijij

i/M

taa

-

Wa

kati

wa

Wa

tum

ishi

wa

pya

ku

karib

ishw

a

na

Si

ku 1

M

ten

da

ji w

a

Kiji

ji/M

taa

n

a

-

18

NA

. N

GA

ZI

HATU

A

SHUG

HULI

MUD

A

MHU

SIKA

REJE

A

Ku

ripo

ti ka

tika

ki

tuo

c

ha

ka

zi

kuta

mb

ulis

hw

a

kwa

w

atu

mish

i n

a

vio

ng

ozi

w

a k

isia

sa•

Ku

an

da

a

oro

dh

a

ya

furs

a

ziliz

op

o

za,

kija

mii

na

kiu

ch

um

i•

Ku

wa

ele

za

wa

tum

ishi

ha

li ya

m

azi

ng

ira

(Mila

, D

est

uri

na

ta

ratib

u)

ya

jam

ii in

ayo

mzu

ng

uka

na

ku

wa

on

esh

a m

ae

ne

o y

a

hu

du

ma

za

kija

mii

Mw

en

yeki

ti w

a

Kiji

ji/M

taa

Ba

ad

a

ya

kurip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

wa

pe

leka

w

atu

mish

i w

ap

ya k

we

nye

vitu

o v

ya k

azi

Siku

1

Mte

nd

aji

wa

K

ijiji/

Mta

a

Wa

raka

w

a

Utu

mish

i N

a.

5

wa

Mw

aka

200

8, U

safir

isha

ji w

a M

izig

o

6V

ITU

O

VY

A

KU

TOLE

A

HU

DU

MA

Ka

bla

ya

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

fan

ya

ma

an

da

lizi

ya

ma

kazi

, se

he

mu

ya

ku

po

kele

wa

n

a

kusa

ini

vita

bu

, o

fisi

na

vite

nd

ea

ka

zi

kwa

wa

tum

ishi w

ap

ya

Siku

7

ka

bla

ya

ku

ripo

ti

Msi

ma

miz

i w

a

Kitu

o

Ku

an

da

a o

rod

ha

ya

nyu

mb

a

kwa

ajil

i ya

wa

tum

ish

i wa

pya

ku

we

za

kup

ata

m

aka

zi

(nyu

mb

a

za

Serik

ali

au

za

w

atu

bin

afs

i)

Sera

ya

Ajir

a M

en

ejim

en

tin

a

Ajir

a

Ka

tika

U

tum

ishi

wa

U

mm

a

Tole

o

la

2 (2

008)

ki

pe

ng

ele

4.1

1(V

).

19

NA

. N

GA

ZI

HATU

A

SHUG

HULI

MUD

A

MHU

SIKA

REJE

A

VIT

UO

V

YA

K

UTO

LEA

H

UD

UM

A

Ku

an

da

a

ofis

i n

a

vite

nd

ea

ka

zi

kwa

a

jili

ya

wa

tum

ishi

wa

pya

Sera

ya

Ajir

a M

en

ejim

en

ti n

a

Ajir

a

Ka

tika

U

tum

ishi

wa

U

mm

a T

ole

o la

2 (

2008

)K

ua

nd

aa

m

sha

uri

(Me

nto

r)

kwa

a

jili

ya

kuw

ae

leke

za

wa

tum

ishi

wa

pya

m

azi

ng

ira

ya k

azi

-

Wa

kati

wa

K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

Ku

wa

po

kea

n

a

kuw

ata

mb

ulis

ha

w

atu

mish

i w

ap

ya

kwa

w

atu

mish

i w

en

gin

e

Siku

1

Msi

ma

miz

i w

a

Kitu

oW

ara

ka

wa

U

tum

ishi

Na

. 5

w

a M

wa

ka 2

011

Ku

wa

on

yesh

a

ofis

i ya

ku

fan

yia

ka

ziK

uw

ap

atia

wa

tum

ishi

wa

pya

m

ae

lezo

ya

ka

zi k

ulin

ga

na

na

m

iun

do

ya

o y

a u

tum

ishi.

Siku

1M

sim

am

izi

wa

K

ituo

Miu

nd

o y

a U

tum

ishi y

a k

ad

a

hu

sika

•K

uw

ae

leza

w

atu

mish

i w

ap

ya m

azi

ng

ira y

a k

azi

;•

Ku

pe

wa

m

ale

ng

o

ya

kitu

o

katik

a

uto

aji

wa

h

ud

um

a;

•K

uw

ae

leza

w

atu

mish

i w

ap

ya k

uh

usu

ta

ma

du

ni

za ja

mii

hu

sika

;•

Ku

wa

pa

tia

wa

tum

ish

i w

ap

ya v

iten

de

a k

azi

;•

Ku

toa

m

ae

lezo

ku

hu

su

Mfu

mo

wa

W

azi

up

ima

ji U

ten

da

ji ka

zi

katik

a

Utu

mish

i w

a

Um

ma

(O

PR

AS)

Siku

1

Wa

raka

w

a

Utu

mish

i N

a.

5

wa

Mw

aka

201

1

20

NA

. N

GA

ZI

HATU

A

SHUG

HULI

MUD

A

MHU

SIKA

REJE

A

VIT

UO

V

YA

K

UTO

LEA

H

UD

UM

A

Baa

da

ya K

urip

oti

katik

a

kitu

o

ch

a k

azi

•W

atu

mish

i w

ap

ya

kup

ew

a m

sha

uri

(Me

nto

r)

mw

en

ye u

zoe

fu;

•K

ufa

nya

ta

thm

ini

ya

msa

ad

a

alio

up

ata

m

tum

ishi

toka

kw

a

Msh

au

ri;•

Ku

pe

leka

rip

oti

ya

ute

kele

zaji

wa

m

afu

nzo

e

leke

zi k

atik

a S

eh

em

u z

a

kazi

ka

tika

O

fisi

ya

Mku

rug

en

zi

wa

H

alm

ash

au

ri ku

piti

a

mfu

mo

w

a

uto

aji

wa

ta

arif

a u

liop

o.

Mie

zi 6

M

sima

miz

i w

a

kitu

o

-

21

HITIMISHO

Wadau wote waliotajwa katika Kiongozi hiki ni muhimu wahakikishe wanatekeleza wajibu wao katika utekelezaji wa utoaji mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa lengo la kuwavutia watumishi kubaki katika Vituo na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, katika kuhakikisha mfumo huu unakua endelevu katika matumizi yake kila mwajiri anapaswa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kila robo mwaka Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kutumia mifumo ya utoaji wa taar-ifa iliyopo. Kiongozi hiki kinaweza kufanyiwa marekebisho kulingana na mahitaji yaliyopo.

22

Kia

mb

atis

ho

Na.

A-

OR

OD

HA

YA

WA

JUM

BE

WA

LIO

SH

IRIK

I K

AT

IKA

KIK

OS

I K

AZ

I

Na

JIN

A

CH

EO

T

AA

SIS

I

1 B

i. M

iria

m P

. Mm

baga

K

aim

u M

kuru

genz

i Ida

ra y

a Se

rika

li za

Mita

a O

R-T

AM

ISEM

I

2 B

i. B

eatr

ice

R. K

imole

ta

Mku

ruge

nzi

Msa

idiz

i Se

hem

u K

uzije

ngea

Uw

ezo

Sek

reta

riet

i

za M

iko

a

OR

-TA

MIS

EMI

3 B

w. M

rish

o S

. Mri

sho

M

kuru

genz

i Msa

idiz

i – S

ehem

u ya

Uta

wal

a O

R-T

AM

ISEM

I

4 D

kt. C

harl

es E

. Mhi

na

Mku

ruge

nzi M

said

izi-

Sehe

mu

ya U

toaj

i Hud

uma

OR

-TA

MIS

EMI

5 B

w. S

eush

i J. M

buri

M

kuru

genz

i Ida

ra y

a U

taw

ala

na R

asili

mal

iwat

u W

izar

a ya

Kili

mo

, M

i-

fugo

na

Uvu

vi

6 B

ibi R

oxa

na D

. B. K

ijazi

M

kuru

genz

i wa

Idar

a ya

Uen

dele

zaji

Ras

ilim

aliw

atu

OR

-MU

UU

B

7 B

w. C

harl

es T

. Rw

ekaz

a M

hadh

iri

TPS

C

8 D

kt. H

enry

Jona

than

M

hadh

iri

LGT

I

9 B

w. H

enry

P. K

ando

re

Mha

dhir

i LG

TI

10

Bib

i Cre

cens

ia J.

Sha

yo

Kat

ibu

Taw

ala

Msa

idiz

i-Uta

wal

a na

Ras

ilim

aliw

atu

Ofis

i ya

Mku

u w

a M

koa

- K

atav

i

11

Bw

. G

reys

on

H.

Mw

ai-

gom

be

Kat

ibu

Taw

ala

Msa

idiz

i –U

taw

ala

na R

asili

mal

iwat

u O

fisi y

a M

kuu

wa

Mko

a

Lind

i

12

Bw

. Moha

med

I. N

chir

a K

atib

u T

awal

a M

said

izi –

Uch

umi n

a U

zalis

haji

Ofis

i ya

M

kuu

wa

Mko

a- S

hiny

anga

Na

JIN

A

CH

EO

T

AA

SISI

13

Bw. E

linee

ma

W. M

taita

K

atib

u-T

SC

Hal

msh

auri

M

anis

paa

ya M

orog

oro

14

Bw. H

erm

an L

. Msu

ha

Mku

u w

a Id

ara

ya U

taw

ala

na R

asili

mal

iwat

u H

alm

asha

uri

Man

ispa

a

ya M

orog

oro

15

Bw. A

bdul

S. M

bim

bi

Mku

u w

a Id

ara

ya U

taw

ala

na R

asili

mal

iwat

u H

alm

asha

uri

ya W

ilaya

ya M

vom

ero

16

Bi. S

tella

M. P

asch

al

Afis

a Se

rika

li za

Mita

a M

kuu

OR

-TA

MIS

EMI

17

Bw. G

eoffr

ey G

. Luf

umbi

M

shau

ri w

a R

asili

mal

i wat

u BM

F

Sekr

etar

ieti

1 Bw

. Moh

amed

Gom

bati

Afis

a R

asili

mal

iwat

u O

R-T

AM

ISEM

I

2 Bw

. Ayo

ub J.

Kam

bi

Afis

a R

asili

mal

iwat

u O

R-T

AM

ISEM

I

3 Bw

. Afr

aha

N. H

assa

n A

fisa

Ras

ilim

aliw

atu

Mw

anda

miz

i O

R-T

AM

ISEM

I

4 Bi

. Rac

hel S

heiz

a M

kuru

genz

i wa

Prog

ram

u BM

F

5 Bi

. Jos

ephi

ne R

. Kim

aro

HR

Lea

d PS

3

6 Bw

. Rem

my

O. M

oshi

M

shau

ri w

a R

asili

mal

i wat

u PS

3

7 Bi

.Chr

istin

a M

alem

beka

A

fisa

Ras

ilim

aliw

atu

Mw

anda

miz

i BM

F

23

Kiambatisho Na. B - HADIDU ZA REJEA ZA TIMU YA MAPOKEZI YA WATUMISHI WAPYA KATIKA NGAZI YA SEKRETARIETI YA MKOA NA HALMASHAURI

1. Kuandaa ratiba ya mapokezi ya watumishi wapya katika Halmashauri husika;

2. Kuandaa bajeti ya kufanikisha mapokezi na Mafunzo Elekezi ya Awali kwa watumishi wapya katika Halmashauri husika;

3. Kuhamasisha wadau mbalimbali wa maendeleo katika eneo husika ikiwemo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Taasisi za Fedha kushiriki katika kufanikisha mapokezi na Mafunzo Elekezi ya Awali ya watumishi wapya;

4. Kuratibu ushiriki wa wadau mbalimbali katika kufanikisha mapokezi na Mafunzo Elekezi ya Awali ya watumishi wapya;

5. Kuandaa vitendea kazi mbalimbali vya kufanikisha mapokezi na Mafunzo Elekezi ya Awali ya watumishi wapya;

6. Kufanya mawasiliano na wasimamizi wa vituo kuhusu maandalizi ya kuwapokea watumishi watakaopangwa katika vituo husika;

7. Kuandaa wawezeshaji watakaotoa mada mbalimbali wakati wa Mafunzo Elekezi ya Awali;

8. Kuandaa taarifa ya mapokezi na Mafunzo Elekezi ya Awali ya watumishi wapya katika Sekretarieti ya Mkoa/Mamlaka za Serikali za Mitaa; na

9. Kazi nyingine kadri itakavyoonekana inafaa katika kufanikisha Mafunzo Elekezi ya Awali kwa watumishi wapya.

24

25

Kiambatisho Na. C - HADIDU ZA REJEA ZA TIMU YA MAPOKEZI YA WATUMISHI WAPYA KATIKA NGAZI YA KATA/KIJIJI/MTAA

1. Kuandaa ratiba ya mapokezi ya watumishi wapya katika Hal mashauri husika;

2. Kuhamasisha wadau mbalimbali wa maendeleo katika eneo husika ikiwemo Taasisi za Fedha, na Sekta Binafsi kushiriki katika kufanikisha mapokezi na Mafunzo Elekezi ya Awali ya watumishi wapya;

3. Kuratibu ushiriki wa wadau mbalimbali katika kufanikisha mapokezi na Mafunzo Elekezi ya Awali ya watumishi wapya;

4. Kufanya mawasiliano na wasimamizi wa vituo kuhusu maandalizi ya kuwapokea watumishi watakaopangwa katika vituo husika;

5. Kuandaa taarifa ya mapokezi kwa watumishi wapya na kui wasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri; na

6. Kazi nyingine kadri itakavyoonekana inafaa katika kufanikisha mapokezi kwa watumishi wapya.

KIONGOZI CHA UTARATIBU WA MAFUNZO ELEKEZI YA AWALI KWA WATUMISHI WAPYA WA SEKRETARIETI ZA

MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA