je, watoto wetu wanajifunza? - twaweza watoto wetu...je watoto wetu wanajifunza? 2 jambo muhimu...

34
Je, Watoto Wetu Wanajifunza? Kuhesabu na Kusoma kaka Afrika Mashariki Juni 2011

Upload: others

Post on 12-Jan-2020

31 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Je, Watoto Wetu Wanajifunza? Kuhesabu na Kusoma kati ka Afrika Mashariki

Juni 2011

Je, Watoto Wetu Wanajifunza? Kuhesabu na Kusoma katika Afrika Mashariki

Je Watoto Wetu Wanajifunza? ii

Uwezo East Africa (managed by Twaweza)P.O Box 19875, 00200 Nairobi, Kenya Tel: +254 20 3861372 Email: [email protected] Web: www.uwezo.net

Twaweza East Africa 127 Mafinga Rd, Off Kinondoni Rd P.O Box 38342, Dar es Salaam, Tanzania Tel: +255 22 266 4301. Fax +255 22 266 4308 Email: [email protected] Web: www.twaweza.org Email: [email protected] Web: www.uwazi.org

Uwezo ni juhudi katika Afrika Mashariki inayofanya kazi yake kupitia TEN/MET nchini Tanzania; WERK nchini Kenya na UNNGOF nchini Uganda, na hupata msaada wa kudhibiti ubora na usimamizi kutoka Twaweza/Hivos. Ripoti hii imeandaliwa na kitengo cha Uwazi kilichopo Twaweza. Waandishi wakuu ni Hans Hoogeveen na Dorica Andrew. Shukrani nyingi kwa Fenohasina Mareth kwa msaada wake katika kutayarisha seti za data na kutengeneza seti ya kwanza ya majedwali na michoro. Sara Ruto na Rakesh Rajani walitoa ushauri wa jumla na kusimamia ubora. Uhariri ulifanywa na Stephanie McDonald na Maggie Bangser.

Data zote zilizotumiwa katika ripoti hii zimetolewa na Uwezo na zinapatikana kutoka www.uwezo.net.

Picha kwenye ukurasa wa nje: Hisani ya Uwezo

Uwezo Afrika Mashariki (ikisimamiwa na Twaweza)S.L.P. 19875, 00200 Nairobi, KenyaSimu: +254 20 3861372Baruapepe: [email protected]. Tovuti: www.uwezo.net

Twaweza Afrika Mashariki127 Mtaa wa Mafinga, Kando ya barabara ya KinondoniS.L.P. 38342, Dar es Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 266 4301. Nukushi: +255 22 266 4308. Barua pepe: [email protected]. Tovuti: www.twaweza.orgBarua pepe: [email protected]. Tovuti: www.uwazi.org

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki iii

Dibaji

Kazi hii inatupatia matokeo yaliyotafitiwa vema kuhusu mafanikio ya mfumo wa elimu hususan katika kusoma na kuhesabu. Uwezo na Twaweza zimeonesha umadhubuti mkubwa na viwango vya juu vya ubora katika kukusanya, kuchambua na kufasiri takwimu za msingi katika elimu na uwezo wa jumla wa watoto katika kusoma na kuhesabu. Matokeo ya msingi yanaonesha ukubwa wa changamoto iliyo mbele yetu sote, na hasa kama ukanda wa Afrika Mashariki unahitaji kuongeza kasi ya maendeleo kuendana na ulimwengu wa sasa ambao umejengwa katika maarifa na ushindani mkali.

Katika ngazi ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), ushirikiano katika maendeleo ya rasilimali watu, sayansi na teknolojia ni moja ya mihimili muhimu katika kufikia malengo ya Jumuiya. Kifungu cha 102 cha Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kinaeleza bayana jinsi Nchi Wanachama walivyokubali kuchukua hatua madhubuti za pamoja kuendeleza ushirikiano katika elimu na mafunzo ndani ya Jumuiya. Ili kuchukua hatua hizo katika ngazi za kanda na nchi, taarifa nyingi zinahitajika ili kuandaa na kutekeleza sera na mikakati inayofaa.

Kwa hiyo, umuhimu wa taarifa zilizokusanywa katika taftishi hii kuhusiana na kusoma na kuhesabu katika nchi tatu za Afrika Mashariki utasaidia sana Nchi Wanachama katika juhudi zao za kuwa na mfumo wa elimu ulioandaliwa vema na kurandanishwa; hasa katika kurandanisha mitaala, mitihani, utoaji vyeti na uthibitishaji wa kitaaluma wa taasisi za elimu na mafunzo. Miongoni mwa vipengele muhimu katika ripoti hii ni jinsi inavyoshughulikia suala la jinsia, ukuzaji mitaala, kuhusika kwa sekta binafsi na viwango vya uhamasishaji kuelekea ngazi inayofuata. Maeneo yote haya ni muhimu kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zimejikita katika kutekeleza sera muhimu za elimu na mafunzo ya msingi, zaidi sana sera ya elimu kwa wote ambayo inahitaji taarifa za kina kuwasaidia watoa maamuzi kufanya uamuzi makini wakijua bayana nini wanachokifanya.

Ripoti hii inachambua zaidi uhusiano kati ya kipato cha kaya na vigezo vya elimu kama vile mafanikio, uwezekano wa kuacha masomo, uandikishaji kwa kutazama jinsia, umri n.k. Kwa miongo mingi tumetumia viwango vya uandikishaji watoto shuleni kama vigezo muhimu vya maendeleo ya elimu. Ripoti ya Uwezo inaonesha kwamba uandikishaji pekee hautoshi kwa sababu watoto walio shuleni bado hawawezi kusoma na kuhesabu, ambazo ni stadi za msingi katika kujifunza na kuendelea (kukua kimaarifa). Hata hivyo, matokeo ya ripoti hii yatakuwa muhimu katika mchakato unaoendelea wa kurandanisha sera za elimu na mafunzo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa mfano, baada ya kudhibitishwa na kupimwa ufaaji wake, taarifa zilizokusanywa katika taftishi zinaweza kutumiwa katika kufanya mapitio ya sheria na kufanya marekebisho yanayostahili katika ngazi ya kanda na kitaifa.

Ni matarajio yangu kwamba kazi hii inayostahili pongezi itatumiwa kwa mapana na marefu na pande zinazohusika na kwamba Uwezo na Twaweza kama taasisi zitaendelea kujibainisha kama wanaharakati muhimu katika eneo hili. Jambo hili pia linahusisha changamoto ya kuhakikisha ubora wa matokeo. Wakati kuongeza idadi ya watoto walio mashuleni ni muhimu, kipengele cha muhimu zaidi cha kupima mafanikio ni kuthibitisha kama watoto wanaokwenda shule kwa hakika wanajifunza au la. Hili ni eneo lingine ambalo linastahili kuchunguzwa na Uwezo na Twaweza. Vilevile, ni matumaini yangu kwamba utafiti kama huu utakaofuata utahusisha Nchi Wanachama tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Dkt Richard SeziberaKatibu MkuuJumuiya ya Afrika MasharikiJuni 2011

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 1

1. UtanguliziNi wachache wanaohoji umuhimu wa kujifunza, kama haki ya msingi na umuhimu wake katika kuandaa vizazi vijavyo kwa kuwajengea uwezo wa kuishi maisha yenye ustawi. Serikali za Tanzania, Uganda na Kenya zinaunga mkono mtazamo huu. Nchi zote tatu zinatekeleza sera ya Elimu ya Msingi bure kwa matarajio kwamba itawezesha watoto kupata elimu, ili walau wawe raia wenye uwezo wa kuhesabu na kusoma. Ili kufanikisha lengo hili kiasi kikubwa cha fedha kimewekezwa na kinaendelea kuwekezwa katika elimu ya msingi. Mathalan, katika mwaka 2009/10, Serikali ya Tanzania ilitenga asilimia 14 ya bajeti yake (sawa na asilimia 4 ya Pato la Taifa) kwa ajili ya elimu ya msingi pekee1. Kenya na Uganda nazo zinatumia kiasi kikubwa cha fedha, na katika muongo uliopita takwimu zinaonesha kwamba bajeti ya elimu imeongezeka kwa kiwango kikubwa katika nchi hizi.

Katika nchi hizi kufutwa kwa ada ya elimu ya msingi kulifuatiwa na ongezeko kubwa la idadi ya watoto wanaokwenda shule. Ukweli huu unaoneshwa na wiano za idadi ya uandikishaji watoto katika shule kama inavyoonekana katika Kielelezo cha 1 (uwiano wa jumla wa uandikishaji ni jumla ya idadi ya watoto wanaosoma katika shule za msingi ikilinganishwa na watoto wenye umri wa kwenda shule). Nchini Uganda, ambako elimu ya msingi bure ilianza kutolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1997, idadi ya jumla ya watoto walioandikishwa ilipanda kutoka pungufu kidogo ya asilimia 70 mwaka 1997 hadi kufikia zaidi ya asilimia 120 mwaka 2000. Nchini Tanzania, baada ya ada za shule kufutwa mwaka 2001, uandikishaji uliongezeka kutoka karibu asilimia 70 hadi karibu asilimia 110. Nchini Kenya, ongezeko halikuwa kubwa sana hasa kwa sababu tayari uandikishaji ulikuwa juu, lakini hata katika nchi hii, kuanzishwa upya kwa elimu ya msingi bure katika mwaka 2003 kulifanikisha uandikishaji kuongezeka hadi kufikia karibu asilimia 105.

Kielelezo cha 1: jumla ya uandikishaji katika shule za msingi 1990-2008 (katika %)

Chanzo cha data: Taasisi ya Takwimu ya UNESCO2

Mafanikio ya kuvutia yaliyopatikana katika uandikishaji watoto shuleni yalitoa fursa kwa jitihada kuelekezwa katika kusimamia kujifunza. Je, watoto wote hawa ambao sasa wanakwenda shule kweli wanafanikiwa kujenga uwezo wa kuhesabu na kusoma? Je, uwekezaji huu mkubwa unaofanywa na serikali hizi katika elimu ya msingi unazaa matunda yanayotarajiwa na watunga sera na wazazi?

Ili kutathmini kiwango cha uwezo wa kusoma na kuhesabu walichonacho watoto wa umri wa kwenda shule, Uwezo ilifanya tafiti katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda. Tafiti zilihusisha kuwapima maelfu ya watoto katika mazingira ya nyumbani. Majaribio yaliyotumika yalikuwa ya ngazi ya Darasa la 2 kwa Kiingereza, Kiswahili na Kuhesabu. Majaribio haya yalitayarishwa kwa kuzingatia mitaala ya kila nchi inayohusika. Ripoti hii inatumia data hizi ili kutathmini ustadi wa watoto wa umri wa kwenda shule kutokana na majaribio ya Uwezo yaliyofanywa katika nchi hizi tatu.

1 Basic Education Statistics in Tanzania 20102 http://stats.uis.unesco.org

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 2

Jambo muhimu ambalo upimaji huu umebaini ni kwamba uwezo wa watoto katika nchi hizi tatu ulikuwa katika kiwango cha chini sana. Wanafunzi wengi waliokuwa katika Darasa la 3, ambao wote walitarajiwa wangekuwa wamepata stadi za kusoma na kuhesabu za ngazi ya Darasa la 2, hawakufaulu majaribio ya Uwezo. Kwa kulinganisha nchi hizi tatu tunaona kwamba watoto nchini Kenya walifanya vizuri zaidi na wale wa Tanzania walifanya vibaya zaidi. Vilevile uchambuzi unaonesha kwamba karibu wanafunzi wote wa Darasa la 7 nchini Kenya na Uganda walionesha kuwa wanamudu stadi za ngazi ya Darasa la 2. Hali ni tofauti nchiniTanzania ambako ni kati ya asilimia 50 hadi 80 tu ya wanafunzi wa Darasa la 7 ndiyo walioweza kukamilisha vizuri majaribio ya ngazi ya Darasa la 2 ya Uwezo.

Ripoti hii inazingatia pia vipengele vingine. Inalinganisha fursa za upatikanaji wa elimu ya msingi katika nchi hizi tatu, inachambua na kulinganisha uwezo wa wanafunzi katika shule za serikali na zile za binafsi, na inazingatia tofauti za kijinsia, upatikanaji wa nyenzo shuleni na uwezo wa kiuchumi wa kaya.

Ripoti hii imepangwa kwa sehemu. Sehemu ya 2 ya ripoti inaeleza zaidi kuhusu mbinu ya utafiti iliyotumiwa na Uwezo, wakati na namna ulivyotekelezwa na kiwango ambacho majaribio yanalingana katika nchi hizi tatu. Sehemu ya 3 inazungumzia upatikanaji wa elimu ya msingi; na sehemu ya 4 inajadili matokeo ya ujifunzaji. Sehemu ya 5 inaangalia upatikanaji wa vifaa/nyenzo katika shule. Sehemu ya 6 na ile ya 7 zinajadili shule binafsi na tofauti za kijinsia. Wakati ambapo sehemu za 4 hadi 7 zinazingatia uhusiano baina ya vipengele mbalimbali (jinsia, madaraja ya utajiri wa kaya, kiwango cha ubora wa shule) na uwezo wa wanafunzi kwa upekee, sehemu ya 8 inawasilisha matokeo ya uchambuzi wa vipengele vilivyojadiliwa mapema katika ripoti kupitia matokeo ya ukokotozi wa kihesabu. Sehemu hii inawasilisha uchambuzi wa athari za vipengele mbalimbali katika ujumla wake. Hitimisho linawasilishwa katika sehemu ya 9.

2. Taftishi na majaribio ya Uwezo Uwezo ilifanya tafiti kubwa za kaya na kupima uwezo wa kusoma na kufanya hesabu kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 6-16 (5-16 nchini Tanzania) katika mazingira ya nyumbani. Tafiti za Uwezo ndizo zilizotumia sampuli kubwa sana kuliko tafiti nyingine zozote zilizowahi kufanywa katika kanda hii. Vilevile, timu za utafiti zilikusanya data kutoka katika shule moja katika kila kijiji.

Nchini Kenya, utafiti wa awali ulifanywa mwaka 2009. Taarifa za wilaya 70 kati ya 158 (zilizojumuishwa katika sensa) za Kenya zilikusanywa na jumla ya watoto 68,945 wenye umri wa miaka 6-16 kutoka kaya 40,286 walipimwa. Taarifa za shule zilikusanywa kutoka shule za msingi za serikali 2,030343Nchini Uganda, utafiti wa kwanza wa Uwezo ulifanyika mwaka 2010. Utafiti ulikusanya taarifa za wilaya 27 (kati ya wilaya 80 za Uganda wakati huo). Jumla ya vijiji 810 na kaya 16,200 zilitembelewa na watoto 34,752 wenye umri wa miaka 6-16 walipimwa.

Nchini Tanzania, utafiti ulifanyika mwaka 2010. Ulihusisha wilaya 38 kati ya 133, vjijiji 1,140 na kaya 22,800 zilitembelewa. Jumla ya watoto 42,033 wenye umri wa miaka 5-16 walipimwa.

Majaribio yaliyotumiwa naUwezo katika upimaji yalikuwa ya ngazi ya Darasa la 2 na yalizingatia mitaala ya kila nchi. Nchini Kenya na Tanzania, watoto walipimwa katika kuhesabu na kusoma Kiswahili na Kiingereza. Nchini Uganda watoto walipimwa katika kuhesabu na kusoma Kiingereza. Ngazi ya Darasa la 2 imechaguliwa kwa sababu kwa mujibu wa viwango vya kimataifa baada ya ngazi hiyo ya kujifunza mwanafunzi anatarajiwa kuwa amepata stadi za msingi katika kuhesabu na kusoma, stadi ambazo ni muhimu katika kujifunza masomo mengine yote katika miaka ya baadaye.

3 Kwa sasa kuna wilaya zaidi nchini Kenya, lakini wakati wa utafiti, wilaya 158 zilikuwa zimeorodheshwa katika gazeti la Serikali na kushirikishwa katika sensa ya watu ya mwaka 2009.

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 3

Jedwali la 1: Utafiti wa Uwezo nchini Kenya, Tanzania na Uganda—muhtasari wa taarifa muhimu

Kenya Tanzania Uganda

Tarehe ya utafiti Sept/Okt 2009 Mei 2010 Aprili 2010

Idadi ya wilaya 70 (kati ya 158) 38 (kati ya 133) 27 (kati ya 80)

Idadi ya kaya 40,386 22,800 16,200

Idadi ya watoto waliopimwa 68,945 43,033 34,752

Idadi ya shule zilizotembelewa 2,030 1,140 810

Ngazi za umri 6-16 5-16 6-16

Jaribio la kuhesabu Ndiyo Ndiyo Ndiyo

Jaribio la Kiswahili Ndiyo Ndiyo Hapana

Jaribio la Kiingereza Ndiyo Ndiyo Ndiyo

Chanzo cha data: Ripoti za kitaifa za Uwezo54

Majaribio yote yalitayarishwa kwa namna ambayo wanafunzi wangeweza kupimwa katika ngazi mbalimbali. Mathalani, jaribio la kusoma lililenga kubaini uwezo wa kusoma herufi mojamoja, kisha maneno, sentensi na/au aya, na mwisho hadithi iliyofuatiwa na maswali ya ufahamu. Vivyo hivyo, jaribio la hesabu lilianza na utambuzi wa namba, kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya. Watoto walipewa alama za ziada iwapo walifanya fumbo la hesabu lililojumuisha shughuli na/au vitendo vya nyumbani vya kila siku, fumbo hilo lilitolewa katika lugha aliyoipendelea mtoto.

Kwa kuwa majaribio yaliakisi mitaala ya kitaifa, hayakuweza kulinganishwa moja kwa moja. Badala yake, ulinganishaji alama za majaribio unaonesha iwapo watoto katika kila nchi wamepata stadi za ngazi ya Darasa la 2 za mtaala wa elimu wa taifa lao. Katika kila nchi, iwapo mfumo wa elimu ungekuwa mzuri, watoto wote (asilimia 100) walio katika Darasa la 3 wangekuwa wamepata stadi za ngazi ya Darasa la 2.

Japo haiwezi kulinganishwa sawasawa, matarajio ya ufahamu wa wanafunzi katika Darasa la 2 si tofauti sana katika nchi hizi tatu. Hali hii inaonekana katika Jedwali la 3 ambalo linawasilisha majaribio yaliyotumika katika upimaji kwenye kila nchi. Jaribio la Kiswahili lingeweza kulinganishwa katika nchi za Kenya na Tanzania, huku ikionekana kwamba maswali ya ufahamu kwa Tanzania yalikuwa magumu zaidi kuliko yale ya Kenya. Jaribio la Kiingereza lilikuwa sawa katika nchi zote tatu, japo hadithi ya Tanzania ilikuwa fupi na rahisi kuliko zile za Kenya na Uganda. Vilevile majaribio ya kuhesabu yalikuwa sawa, isipokuwa tu kwamba jaribio la Tanzania lilikuwa na maswali ya kujumlisha kwa kuhamisha, na maswali ya kutoa kwa kuhamisha ambayo hata hivyo hayakuulizwa Kenya na Uganda. Kwa upande mwingine, nchini Uganda na Kenya wanafunzi walifanya hesabu za kugawanya, maswali ambayo watoto wa Tanzania hawakuulizwa.

Inaweza kusemwa kwamba majaribio haya yalipima uwezo wa watoto katika kuhesabu na kusoma, na si kujifunza. Ili kupima kujifunza, ambacho ni kipimo cha kuonesha mabadiliko, mtafiti angepaswa kuchunguza tofauti katika viwango vya kufikiri tangu wakati wanafunzi wanapoanza shule katika nchi hizi zinazohusika. Kwa ujumla, inaelezwa kwamba katika nchi za Uganda na Kenya, Kiingereza kinazungumzwa kwa upana zaidi kuliko ilivyo nchini Tanzania. Kwa hiyo, kama ubora wa viwango vya ufundishaji vitabaki kuwa sawa katika nchi zote tatu, na jaribio kuwa na kiwango cha ugumu kilicho sawa, inatarajiwa kuwa watoto nchini Kenya na Uganda wangefanya vizuri zaidi katika jaribio la Kiingereza kuliko wale wa Tanzania. Kwa mantiki hiyo, hali kama hiyo inaweza kujitokeza kwa lugha ya Kiswahili ambayo inazungumzwa kwa upana zaidi nchini Tanzania kuliko Kenya na kwa kawaida haizungumzwi nchini Uganda. Pia, kiwango cha elimu ya wazazi kinaweza kusababisha tofauti wakati watoto wanapoingia shule.

Mathalan, kwa mujibu wa tafiti za idadi ya watu na afya (Demographic and Health Surveys), nchini Kenya asilimia 19 ya akina mama hawana elimu; takwimu kama hizo nchini Tanzania ni asilimia 33 na Uganda asilimia 23. Iwapo mazingira ya nyumbani yanaathiri uwezo wa watoto wakati wanapoanza shule, basi tofauti katika matokeo ya majaribio ya kuhesabu na kusoma hayamaanishi moja kwa moja uwepo wa tofauti katika kujifunza. Wakati huo huo uhusiano wa karibu unatarajiwa baina ya matokeo ya majaribio ya kuhesabu na kusoma na ujifunzaji katika shule.

4 Uwezo 2010, Are our children learning? Annual Learning Assessment Report. Kenya 2009; Uganda 2010; Tanzania 2010. Zote zinapatikana kutoka www.uwezo.

net

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 4

Ripoti hii, kwa kiasi kikubwa, inawasilisha takwimu za kitaifa. Hii ni kwa kuzingatia kwamba utaratibu wa kupata sampuli za wilaya ulikuwa wa kinasibu. Ndani ya wilaya, vijiji vilichaguliwa kinasibu, na pia ndani ya vijiji taratibu za kinasibu zilitumika (japo taratibu zilizotumika Tanzania ziliwaruhusu watafiti kwa kiasi fulani kufanya uchaguzi huru ambao huenda ulisababisha upendeleo). Ili kuthibitisha kiwango ambacho matokeo ya kitaifa ya Uwezo yanafanana na yale yaliyopatikana katika tafiti nyingine za kitaifa zilizohusisha kaya, Jedwali la 2 linawasilisha idadi ndogo ya sifa za kaya, zilizopatikana kutoka tafiti za Uwezo na nyinginezo. Ulinganishaji wa data za Uganda (ambao ulifuata kanuni kali za kinasibu) unaonesha kufanana kwa karibu kwa matokeo ya Uwezo na yale ya Taftishi za Kaya katika Mambo ya Binadamu (Demographic Household Survey (DHS)). Kumekuwa na tofauti ndogo katika umiliki wa redio na runinga lakini tofauti hizi huenda zinaakisi kipindi cha miaka minne kilichopita katikati ya tafiti hizi mbili. Vilevile kwa Kenya, matokeo ya Uwezo yanafanana na yale ya DHS. Kuna tofauti ndogo, kama ambavyo ingetarajiwa, pale zinapolinganishwa sampuli za tafiti mbili, hata hivyo tofauti hizo si kubwa.

Inaweza kusemwa, hata hivyo, kwamba sampuli ya Uwezo kwa upande wa Kenya inaonekana kuelemea zaidi kwa kaya masikini na zenye elimu ya chini. Nchini Tanzania kwa upande mwingine, tofauti kubwa zaidi zinaweza kuonekana. Katika nchi hii sampuli ya Uwezo inaonekana kuegemea zaidi kwenye kaya zenye elimu nzuri kidogo na zilizojaliwa kiuchumi. Tofauti katika kipengele cha akina mama wasio na elimu (asilimia 30 katika HBS; asilimia 14 katika utafiti wa Uwezo) inastusha zaidi. Pia ukweli kwamba Uwezo inaripoti asilimia 19 ya kaya zenye umeme dhidi ya asilimia 12 katika utafiti wa HBS ni tofauti kubwa.

Katika sehemu zinazofuata za ripoti hii masuala haya yanajadiliwa, lakini msomaji anatahadharishwa kwamba sampuli ya Tanzania inaweza kuwa imeegemea zaidi katika kaya zenye hali nzuri, na sampuli ya Kenya kuegemea zaidi kwenye kaya zenye hali duni.

Jedwali la 2: Mlinganisho wa matokeo ya kitaifa ya Uwezo na tafiti nyingine za kitaifa za kaya

Tanzania Kenya Uganda

Elimu ya mama

Uwezo

2010

HBS

2007

Uwezo 2009

DHS

2009

Uwezo 2010 DHS

2006

Hana elimu 14 30 24 19 Hakuna taarifa kuhusu elimu ya mama katika utafiti wa Uwezo Elimu ya msingi 1-4 8 9 53 60

Elimu ya msingi 5-7/8 66 52

Elimu ya sekondari 1-4 6 6 23 20

Zaidi ya sekondari 2 2

Mali &Umeme

Umeme 19 12 11 23 8 9

Redio 70 66 73 74 74 61

Runinga 18 8 22 28 13 6Chanzo cha data: Uwezo, DHS (Uganda naKenya) na HBS (Tanzania)65

5 www.measuredhs.com; Idara ya takwimu 2009; Utafiti wa Bajeti za Kaya 2007.

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 5

Jedw

ali l

a 3:

Sam

puli

za m

ajar

ibio

ya

Kuhe

sabu

, Kiin

gere

za n

a Ki

swah

ili y

aliy

otum

iwa

na U

wez

o3a

: Jar

ibio

la K

uhes

abu

Uta

mbu

zi w

a N

amba

1-9

Uta

mbu

zi w

a N

amba

10-9

9

Kuju

mlis

ha b

ila k

ubeb

a Ku

jum

lisha

na

kube

ba

Kuto

a bi

la k

ukop

a Ku

toa

na k

u-ko

paKu

zidi

sha

Kuga

wan

yaH

esab

u ze

nye

uhus

iano

na

utam

adun

i

TZ2

8

6

0

7

5

87

31

51

60

28

99

55

49

+23

+3

0

24

3

3

+71

+4

2

77

45

+25

+48

23

12

+68

+64

89

76

-42

-

33

66

48

- 55

- 4

33

62

-15

-25

70

97

-34

-48

12

1

5

x 4

x

4

11

9

x 5

x

24

Shili

ngi 3

00 +

Shi

lingi

200

= S

hilin

gi

KE3

6

2

7

4

5

16

34

33

78

50

99

32

6

0

+24

+1

5

24

4

3

+71

+51

46

59

-24

-

38

53

74

-41

-

21

3 x

4 =

5 x

2 =

3 x

2 =

5 ÷1

=

15 ÷

3 =

8 ÷2

=

Una

shi

lingi

80.

Uta

baki

na

shili

ngi n

gapi

ba

ada

ya k

unun

ua m

fuko

mm

oja

wa

unga

una

ouzw

a kw

a sh

iling

i 60?

UG

9

5

1

3

8

6

11

91

91

47

72

69

14

8

8

+12

+11

15

1

3

+13

+14

71

46

-60

-

14

66

8

9

- 15

-1

4

7 x

3 =

3 x

4 =

5 x

1 =

6 ÷2

=

2 ÷2

=

8 ÷2

=

Jane

ana

taka

kam

ba a

mba

yo in

auzw

a sh

iling

i 250

. Joh

n an

ampa

Jane

shi

lingi

30

0. Je

, Jan

e at

abak

i na

shili

ngi n

gapi

ba

ada

ya k

unun

ua k

amba

?

3b Ja

ribi

o la

Kiin

gere

za

Her

ufiM

anen

oSe

nten

si/A

yaH

adit

hi

TZe

n

d u

w

f

boy

tall

good

b

est

com

e

sing

This

is m

y ca

t.

That

dog

is b

ig.

I lik

e m

y sc

hool

.

My

hom

e is

sm

all.

Jum

a is

livi

ng in

a s

mal

l vill

age.

He

gets

a le

tter

onc

e a

mon

th. T

he le

tter

is fr

om h

is s

on M

usa.

Mus

a liv

es in

Dod

oma.

Jum

a ca

n-no

t rea

d th

e le

tter

s. H

e as

ks S

ara

to re

ad th

e le

tter

s fo

r hi

m.

Que

stion

s: 1

. Whe

re d

oes

Jum

a liv

e?

2. W

hat d

oes

Sara

read

?

3. W

hat i

s th

e na

me

of Ju

ma’

s so

n?

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 6

KEe

x

d

w

k

c

Room

fa

ce

tabl

e

dog

desk

pen

My

mot

her

wor

ks in

Lam

u.

Lam

u is

the

busy

tow

n.

The

peop

le th

ere

are

good

.

They

are

ver

y ki

nd.

Jum

a re

ads

to u

s a

stor

y fr

om h

is b

ook

ever

y da

y. H

e re

ads

the

stor

y al

oud

in c

lass

. We

enjo

y lis

teni

ng to

the

stor

ies.

Yes

terd

ay, h

e re

ad a

bout

the

sun

and

the

win

d. B

oth

of th

em li

ved

in th

e sa

me

sky.

The

win

d di

d no

t lik

e th

e su

n .It

wan

ted

to b

e th

e he

ad o

f th

e sk

y. O

ne d

ay, t

he w

ind

chas

ed th

e su

n aw

ay. I

t tol

d su

n to

go

to a

noth

er s

ky. T

he s

un d

id n

ot g

o. T

he n

ext m

orni

ng, t

he w

ind

ran

after

the

sun.

The

sun

fell

dow

n an

d st

arte

d cr

ying

. Tha

t is

how

it b

egan

to ra

in. W

e cl

appe

d fo

r Ju

ma.

Que

stion

s: 1

. Wha

t doe

s Ju

ma

do e

very

day

?

2. H

ow d

id ra

in b

egin

?

UG

i

o

w

y

s

h

cow

m

at

car

s

ing

bus

l

eg

This

is o

ur g

oat.

She

has

two

kids

.

She

likes

her

kid

s.

She

feed

s th

em w

ell.

Tom

is o

ur b

est f

ootb

all p

laye

r. H

e st

ays

far

away

from

sch

ool.

One

day

we

had

a bi

g m

atch

. Tom

had

not

com

e to

sch

ool t

hat d

ay.

The

teac

her

wen

t to

look

for

Tom

. The

teac

her

foun

d To

m w

eedi

ng c

assa

va. T

he te

ache

r ca

lled

Tom

from

the

gard

en. A

ll pu

pils

w

ere

happ

y w

hen

Tom

cam

e. O

ur s

choo

l won

the

mat

ch. W

e da

nced

the

who

le d

ay.

Que

stion

s: 1

. Whe

re w

as T

om?

2. W

hy w

ere

the

child

ren

danc

ing?

3c M

ajar

ibio

ya

Kisw

ahili

Sila

biM

anen

oA

yaH

adit

hi

TZfa

k

i

mw

a n

jo

le

c

hi

Chai

sh

ereh

e

vuta

m

aziw

a

mam

a

kak

a

Baba

am

ejen

ga n

yum

ba n

zuri

.

Nyu

mba

yet

u im

ezun

gukw

a na

m

iti.

Miti

huz

uia

upep

o m

kali.

Miti

hut

upati

a he

wa

safi.

Hap

o za

man

i za

kale

sam

aki w

aliis

hi n

chi k

avu.

Wal

iishi

kw

a ku

la w

adud

u ka

ma

vile

pan

zi, m

ende

na

sisi

miz

i. Si

ku m

oja

wad

udu

haw

a w

alik

aa k

ikao

na

kupa

nga

nam

na y

a ku

wao

ndoa

sam

aki.

Kika

o ch

ao w

engi

wal

icha

ngia

. Ika

fika

zam

u ya

sis

imiz

i. Si

sim

izi

alis

imam

a na

kus

ema,

“U

moj

a ni

ngu

vu n

a ut

enga

no n

i udh

aifu

”. W

ote

wal

isim

ama

na k

upig

a ke

lele

“sa

mak

i wau

awee

e”. S

amak

i w

alip

osik

ia h

ivi w

alik

imbi

a na

kuj

ifich

a m

ajin

i. H

adi h

ivi l

eo s

amak

i wan

aish

i maj

ini.

Mas

wal

i: 1.

Hap

o za

man

i sam

aki w

aliis

hi w

api?

2. Z

aman

i sam

aki w

alik

uwa

wan

akul

a w

adud

u ga

ni?

3. H

adith

i hii

inat

ufun

dish

a ni

ni?

KEbe

di

na

tu

ho

le

kiti

taa

soko

u

so

mal

i

choo

Mam

a an

apik

a uj

i.

Jum

a an

asom

a ki

tabu

.

Mar

ia a

nach

eza

mpi

ra.

Nay

e ba

ba a

nalim

a sh

amba

ni.

Jina

lang

u ni

Fat

uma

Abd

i. N

inai

shi N

akur

u na

fam

ilia

yetu

kw

enye

nyu

mba

kub

wa.

Bab

a ya

ngu

ni m

wal

imu

katik

a sh

ule

ya u

pili.

W

anaf

unzi

wan

ampe

nda

mam

a ya

ngu

kwak

uwa

ni m

wal

imu

mzu

ri. N

ao n

yany

a na

bab

u w

anai

shi k

ule

kijij

ini.

Wao

wan

a m

buzi

na

kon

doo

wen

gi. M

imi h

uwat

embe

lea

siku

za

likiz

o. N

yany

a hu

nipa

had

ithi n

zuri

za

kuch

ekes

ha. M

imi h

uche

ka h

adi m

bavu

zik

a-ni

uma.

Lik

izo

ikiis

ha, n

yany

a hu

nipa

maz

iwa

nim

lete

e m

ama

yang

u.

Mas

wal

i: 1.

Mam

a ya

Fat

uma

hufa

nya

kazi

gan

i?

2. F

atum

a hu

wat

embe

lea

Nya

nya

na B

abu

wak

ati g

ani?

(*) A

ngal

izo:

Wila

ya z

a Ke

nya

zina

rang

i ya

bulu

u, w

ilaya

za

Uga

ndan

i kija

ni, w

ilaya

za

Tanz

ania

ni n

yeku

ndu.

Chan

zo c

ha d

ata:

Rip

oti z

a ki

taifa

za

Uw

ezo

Kuhesabu na Kusoma Kati ka Afi ka Mashariki 7

3. Upati kanaji wa Elimu 3.1 Uandikishaji kati ka shule za msingi uko juu lakini si kila mahaliKielelezo cha 2 kinaonesha uandikishaji kati ka shule za msingi kulingana na umri wa watoto kati ka nchi zinazohusika.76Mihimili kati ka kilelelezo inaonesha tofauti kati ka mifumo ya elimu miongoni mwa nchi hizi. Nchini Kenya elimu ya msingi hutolewa kwa miaka nane na watoto wanatarajiwa kwenda shule tangu wakiwa na umri wa miaka 6 hadi 13. Kati ka nchi za Tanzania na Uganda, elimu ya msingi huchukua miaka saba. Nchini Uganda watoto wanaanza shule wanapokuwa na miaka 6 na kumaliza wanapokuwa na umri wa miaka 12, wakati nchini Tanzania wanaanza shule wanapokuwa na miaka 7 na kumaliza wakiwa na miaka 13. Kielelezo kinaonesha pia watoto walio nje ya viwango hivi vya umri.

Mihimili kati ka kielelezo inaonesha jinsi uandikishaji ulivyo wa chini sana nchini Tanzania. Bila kujali umri, idadi ya watoto waliojiunga na shule nchini Tanzania bado ni ndogo kuliko kati ka nchi nyingine. Vilevile kielelezo kinaonesha jinsi nchini Uganda, ikilinganishwa na Kenya, watoto wengi zaidi walivyoandikishwa kati ka shule za msingi walipokuwa na umri wa miaka sita. Nchini Kenya, kwa kiasi fulani kutokana na kuwa na mtaala wenye nyongeza ya mwaka mmoja zaidi, sehemu kubwa ya watoto wenye umri mkubwa (wale waliokuwa na miaka 14-16) walikwenda shule.

Kielelezo cha 2: Uandikishaji kati ka shule za msingi kwa umri

Chanzo cha data: Uwezo

3.2 Fursa za kujiandikisha zinabaki kuwa si sawa na hutegemea utajiri wa kaya Kielelezo cha 3 kinaonesha jinsi uandikishaji ndani ya nchi unavyotofauti ana kulingana na uwezo wa kimapato wa kaya ya mtoto. Madaraja matano ya viwango vya utajiri yaliainishwa: masikini zaidi, masikini, hali ya kati (kipimo cha kati ), tajiri na tajiri sana na kila daraja lilikuwa na kaya asilimia 20. Madaraja ya utajiri yaliundwa kwa kutumia data zilizokusanywa toka kati ka nchi husika, ikimaanisha kwamba inawezekana kaya masikini kati ka Kenya ni bora zaidi kuliko zile zilizo kati ka kiwango cha kati nchini Tanzania. Kielelezo hiki kinajikita kati ka uandikishaji wa watoto ndani ya umri rasmi wa kwenda shule kati ka kila nchi. Viwango vya uandikishaji vilikuwa vya chini sana kati ka Kenya (karibu asilimia 84) na juu sana kati ka Uganda (karibu asilimia 90). Kielelezo kinaonesha vilevile kwamba watoto kutoka kati ka kaya masikini walikuwa na uwezekano mkubwa wa kutoandikishwa shule. Tofauti hizi zimeonekana zaidi kati ka Kenya na kwa kiwango kidogo kati ka Uganda na Tanzania.

6 Kipengele hiki kinatokana na maswali kwa wazazi kuhusu uandikishaji mashuleni. Matokeo yake tunatumia maneno “uandikishwaji shuleni”, japokuwa inaweze-kana wazazi walielewa swali waliloulizwa kama swali kuhusu mahudhurio. Dhana ya uwezekano wa wazazi kuongelea mahudhurio wakati wameulizwa kuhusu uandikishaji inatokana na ukweli kwamba viwango vya uandikishwaji vilivyoonekana kutoka kwenye data za Uwezo vinakaribiana sana na viwango vya mahudhu-rio kama ilivyooneshwa na tafi ti za DHS (angalia mathalan takwimu kati ka www.measuredhs.com)

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 8

Kielelezo cha 3: Uandikishaji wa watoto walio kati ka umri wa lazima kwenda shule (*)kwa madaraja matano ya utajiri

13

katinchiniTanzania.Kielelezohikikinajikitakatikauandikishajiwawatotondaniyaumrirasmiwa

kwendashulekatikakilanchi.ViwangovyauandikishajivilikuwavyachinisanakatikaKenya(karibu

asilimia84)najuusanakatikaUganda(karibuasilimia90).Kielelezokinaoneshavilevilekwamba

watotokutokakatikakayamasikiniwalikuwanauwezekanomkubwawakutoandikishwashule.

TofautihizizimeonekanazaidikatikaKenyanakwakiwangokidogokatikaUgandanaTanzania.

Kielelezocha3:Uandikishajiwawatotowaliokatikaumriwalazimakwendashule(*)

kwa

madarajamatanoyautajiri

(*)NchiniKenyaumriwalazimakwendashulenimiaka6‐13;Tanzaniani7‐13naUgandani6‐12.

Chanzochadata:Uwezo

Namnanyingineyakuoneshataabuzawatotokutokakayamasikinisananikwakuangaliawatoto

ambaokamwehawakwendashuleyamsingi.KamainavyoonekanawazikatikaKielelezocha4,

watotokutokakayamasikinisanandiyowalioathirikazaidi.NchiniKenyaasilimia64yawatotowa

umriwamiaka5‐16ambaokamwehawakwendashulewalikuwakutokakayamasikinisanakatika

madarajayaumasikiniambaponchiniUgandaidadihiyoilikuwaasilimia45nanchiniTanzania

asilimia457.

7KwaTanzaniaumriulikuwakatiyamiaka5‐16.

7482 86 88 90

8287 86 87

9286 90 91 92 93

0102030405060708090

100

Maskinizaidi

Maskini

Kipim

ochakak

Tajiri

Tajirisana

Maskinizaidi

Maskini

Kipim

ochakak

Tajiri

Tajirisana

Maskinizaidi

Maskini

Kipim

ochakak

Tajiri

Tajirisana

Asi

lim

iay

aw

ato

tow

au

mri

wa

kw

en

da

sh

ule

wa

lio

an

dik

ish

wa

(*) Nchini Kenya umri wa lazima kwenda shule ni miaka 6-13; Tanzania ni 7-13 na Uganda ni 6-12.

Chanzo cha data: Uwezo

Namna nyingine ya kuonesha taabu za watoto kutoka kaya masikini sana ni kwa kuangalia watoto ambao kamwe hawakwenda shule ya msingi. Kama inavyoonekana wazi kati ka Kielelezo cha 4, watoto kutoka kaya masikini sana ndiyo walioathirika zaidi. Nchini Kenya asilimia 64 ya watoto wa umri wa miaka 5-16 ambao kamwe hawakwenda shule walitoka kaya masikini sana kati ka madaraja ya umasikini ambapo nchini Uganda idadi hiyo ilikuwa asilimia 45 na nchini Tanzania asilimia 4587.

Kielelezo cha 4: Asilimia ya watoto wenye umri wa miaka 5-16 ambao hawakuwahi kwenda shule ya msingi, kwa madaraja matano ya utajiri

Chanzo cha data: Uwezo

Kama ilivyo idadi ya watoto ambao hawakuandikishwa, idadi ya wale walioacha shule ilikuwa juu miongoni mwa kaya masikini zaidi, ingawa tofauti zilikuwa ndogo ikilinganishwa na ile ya wasioandikishwa. Miongoni mwa wale walioacha shule, nchini Kenya asilimia 61 walitoka kati ka kaya masikini au masikini zaidi ikilinganishwa na asilimia 50 kutoka Uganda na 41 kutoka Tanzania.

7 Kwa Tanzania umri ulikuwa kati ya miaka 5-16.

Kuhesabu na Kusoma Kati ka Afi ka Mashariki 9

Kielelezo cha 5: Watoto wa miaka 5 hadi 16 walioacha shule, kwa vipimo vya utajiri wa kaya

Chanzo cha data: Uwezo

Hiti misho: Licha ya ongezeko kubwa la uandikishaji kufuati a kuanzishwa kwa sera ya elimu ya msingi bure, data za utafi ti wa Uwezo zinaonesha kwamba uandikishaji haukuwa umejumuisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule. Kutegemeana na kiwango cha utajiri, kati ya asilimia 7 na 26 ya watoto wa umri wa kwenda shule walikuwa hawaendi shuleni . Viwango hivi vinalingana na viwango vya mahudhurio vilivyopati kana kati ka tafi ti nyingine. Tafi ti za DHS zinaonesha viwango vya mahudhurio vya asilimia 73 kwa Tanzania (2004/5), 79 kwa Kenya (2008/9), na 82 kwa Uganda (2006).

Watoto kutoka makundi ya kaya masikini na masikini zaidi walikuwa na uwezekano mdogo wa kuhudhuria wote shuleni ikilinganishwa na watoto wanaotoka kwenye kaya zenye kipato bora zaidi. Hivyo si tu kwamba mpango wa kufi kisha elimu kwa watoto wote haukufanikiwa kikamilifu, lakini pia fursa za kwenda shule hazikuwa sawa, na zilitegemea kiwango cha kipato cha kaya.

4. Ujifunzaji 4.1 Uwezo (umahiri) kati ka majaribio ya Kiingereza, Kuhesabu na Kiswahili Lengo kuu la jaribio la Uwezo lilikuwa kupima uwezo wa watoto kati ka stadi za kusoma na kuhesabu. Kwa kuwa majaribio yanaonesha ufahamu ambao wanafunzi walipaswa kuwa nao baada ya kukamilisha masomo ya ngazi ya Darasa la 2, watoto wote kati ka madarasa ya juu walipaswa kufaulu vizuri kati ka jaribio la Darasa la 2. Kama itakavyooneshwa kati ka sehemu hii, matokeo yalikuwa kinyume cha matarajio hayo. Jambo hili lilijidhihirika hata miongoni mwa watoto wa ngazi ya Darasa la 7, wengi hawakuwa na stadi za kuhesabu na kusoma za ngazi ya Darasa la 2.

Kiingereza: Kielelezo cha 6 kinawasilisha jinsi watoto walivyofanya kati ka jaribio la Kiingereza huku kikionesha tofauti baina ya madarasa tofauti . Kielelezo kinaonesha jinsi ambavyo kati ka kila nchi watoto wachache wa Darasa la 3 ndiyo waliokuwa na stadi za kiwango cha Darasa la 2 kati ka jaribio la kusoma. Nchini Kenya ni asilimia 28 tu ya watoto wa Darasa la 3 ndiyo waliokamilisha jaribio kwa mafanikio, yaani waliweza kusoma hadithi bila shida. Kati ka nchi za Uganda na Tanzania viwango vya ufaulu vilikuwa vya chini zaidi, asilimia 4 kwa asilimia 8 kwa mpangilio wa nchi hizo.Watoto kati ka madarasa ya juu walionekana kufanya vizuri kati ka majaribio ya Uwezo kama ilivyotarajiwa. Nchini Kenya asilimia 94 ya watoto wa ngazi ya Darasa la 7 walionesha kumudu stadi za Darasa la 2 kati ka kusoma kifungu cha maneno cha Kiingereza. Umahiri ulionekana kuimarika kulingana na ngazi ya darasa kati ka nchi za Uganda na Tanzania vilevile. Bila kuangalia darasa, asilimia ya watoto wa Kenya waliokuwa kati ka kiwango cha juu cha uelewa ilikuwa kubwa kuliko ile ya wenzao kati ka nchi za Uganda na Tanzania. Nchini Tanzania matokeo yanakati sha tamaa; ni asilimia 51 tu ya watoto kati ka Darasa la 7 ndiyo waliofaulu jaribio la Kiingereza lililokuwa kati ka kiwango cha Darasa la 2.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 10

Kadri muda wa kuwa shule unayoongezeka ndivyo tofauti kati ya Kenya na Uganda kati ka asilimia ya watoto ambao wamepata stadi za kiwango cha Darasa la 2 polepole inavyopungua. Wakati kati ka Darasa la 4 tofauti kati ka viwango vya ufaulu kati ya nchi hizi mbili ilikuwa ni asilimia 39, ilipofi ka Darasa la 7 tofauti ilikuwa imepungua hadi asilimia 14. Kwa Kenya na Tanzania hali hii haikujitokeza na karibu mara mbili ya watoto kati ka Kenya walifaulu jaribio la Kiingereza kati ka Darasa la 7 ikilinganishwa na ilivyokuwa kati ka Tanzania.

Kielelezo cha 6: Umahiri wa wanafunzi kati ka jaribio la Kiingereza la Uwezo,kwa darasa

Chanzo cha data: Uwezo

Kuhesabu: Matokeo kati ka jaribio la kuhesabu yalifanana na yale ya Kiingereza, watoto wa Kenya wakiwa wamefanya vizuri (japokuwa ‘vizuri’ ni kwa kiwango cha wastani tu) wakilinganishwa na watoto wa Uganda na Tanzania. Kama ilivyokuwa kati ka jaribio lililotangulia watoto wa Tanzania ndiyo waliofanya vibaya zaidi. Kama ilivyokuwa kati ka jaribio la Kiingereza, uwezo wa watoto uliimarika kulingana na wakati na walipofi ka Darasa la 7 wengi wao walikuwa wamepata stadi za msingi kati ka kuhesabu na walikuwa na stadi zilizotarajiwa kati ka ngazi ya Darasa la 2. Lakini hata kati ka Kenya, nchi yenye ufaulu wa juu, asilimia 12 ya watoto kati ka Darasa la 7 walishindwa kufanya vizuri kati ka mazoezi ya kuhesabu yaliyotarajiwa kati ka kiwango cha Darasa la 2.

Ikilinganishwa na kusoma Kiingereza, tofauti kiuwezo kati ka jaribio la kuhesabu kati ya Tanzania kwa upande mmoja na Kenya na Uganda kwa upande mwingine, ni dogo. Inawezekana, ingawa hii ni kwa kukisia, pengo kubwa kwa Kiingereza kuliko kuhesabu linaakisi kuwa watoto kati ka Kenya na Uganda wanaishi kati ka mazingira ambapo Kiingereza kinasikika na kinazungumzwa kwa upana zaidi. Matokeo yake watoto hao wananufaika zaidi kuliko watoto wa Tanzania ambao nje ya shule hawapati fursa hiyo na walimu wao wana uzoefu mdogo kati ka Kiingereza. Tofauti kati ka alama za kuhesabu inaonesha kwamba haya si maelezo pekee kuhusu udhaifu wa stadi walizo nazo watoto wa Tanzania. Kwa kuwa kiwango cha ufaulu kati ka majaribio yote mawili (Kiingereza na Kuhesabu) ni wa chini zaidi chini Tanzania, inaonekana kwamba huenda kwa kiasi kikubwa watoto wa Tanzania wanajifunza kwa kiasi kidogo wanapokuwa shuleni kuliko watoto wenzao kati ka nchi za Kenya na Uganda.

Kielelezo cha 7: Umahiri wa wanafunzi kati ka jaribio la kuhesabu la Uwezo, kwa darasa

Chanzo cha data: Uwezo

Kuhesabu na Kusoma Kati ka Afi ka Mashariki 11

Kiswahili: Hiti misho hili linaungwa mkono na matokeo yaliyoonekana kati ka jaribio la Kiswahili. Jaribio hili liliendeshwa kati ka nchi ya Kenya na Tanzania pekee (kwa sababu Kiswahili hakitumiwi kwa upana nchini Uganda). Ruwaza iliyoonekana awali ya matokeo mabaya kwa wanafunzi wa Darasa la 3 na hali ya uwezo kuimarika polepole jinsi watoto wanavyopanda kati ka madarasa ya juu ilijirudia. Watoto wa Kenya walifanya vizuri zaidi kuliko watoto wa Tanzania. Tofauti inayoonekana kati ka uwezo wa watoto kati ya Tanzania na Kenya kati ka Kiswahili ilikuwa ndogo kuliko ile iliyopo kati ka Kiingereza na kuhesabu (huenda matokeo haya yanaakisi ukweli kwamba Kiswahili kinazungumzwa kwa upana zaidi kati ka Tanzania ikilinganishwa na Kenya), lakini bado tofauti ilikuwepo. Hivyo hata kati ka jaribio ambalo watoto wa Tanzania wangepaswa kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufaulu kuliko wale wa Kenya, watoto wa Tanzania walifanya vibaya. Kielelezo cha 8 kinaonesha zaidi uwezo wa watoto kati ka Kiswahili, kwa darasa, kati ka Kenya na Tanzania.

Kielelezo cha 8: Umahiri wa wanafunzi kati ka jaribio la Kiswahili la Uwezo, kwa darasa

Chanzo cha data: Uwezo

4.2 Tofauti kati ka uwezo wa watoto ki-wilaya Licha ya tofauti kati ka uwezo wa watoto miongoni mwa nchi hizi tatu, kuna tofauti nyingine kubwa zilizokuwepo miongoni mwa wilaya ndani ya kila nchi. Jedwali la 5 linaonesha asilimia ya watoto kati ka Darasa la 3 wenye stadi za kuhesabu na kusoma za Darasa la 2. Nchini Tanzania asilimia 33 ya watoto kati ka wilaya ya Moshi Mjini, iliyofanya vizuri zaidi, walifaulu jaribio la Kiingereza lakini hakuna mtoto hata mmoja (asilimia 0) kati ka wilaya ya Liwale aliyefaulu jaribio hilo. Nchini Kenya, asilimia 66 ya watoto kati ka wilaya ya Kikuyu walifaulu jaribio la kuhesabu, lakini ni asilimia 5 tu ya watoto walifaulu kati ka wilaya ya Lagdera. Na nchini Uganda, asilimia 40 ya watoto kati ka wilaya ya Bushenyi walifaulu jaribio la kuhesabu, lakini ni asilimia 7 tu walifaulu kati ka wilaya ya Nakapiripirit. Tofauti hizo zinaweza kuonekana kati ka kila jaribio kati ka majaribio matatu, na kati ka kila nchi. Tofauti hizi zinaleta wasiwasi. Hakuna sababu kwa nini watoto wa Nakapiripirit, Lagdera au Liwale wafanye vibaya kuliko watoto wenzao wa Bushenyi, Kikuyu au Moshi Mjini. Mahali anapozaliwa mtoto na kwenda shule pasiathiri uwezekano wa yeye kupata stadi za msingi na uwezo wa kufanya vizuri kati ka kusoma na kuhesabu. Ukweli kwamba matokeo yako hivyo ni kiashiria cha kutosha kuonesha kwamba hakuna usawa kati ka mifumo ya elimu kati ka kila nchi.

Jedwali la 4 linawasilisha wilaya kumi zilizofanya vizuri na zilizofanya vibaya nchini Kenya, Uganda na Tanzania. Kati ka majaribio ya Kiingereza na Kuhesabu , wilaya zote 10 bora za mwanzo zilikuwa za Kenya. Kati ka zile za chini, kulikuwa pia na wilaya chache za Kenya lakini nyingi kati ya hizo zilikuwa za Uganda na Tanzania. Ruwaza ya jumla ilionesha kwamba wilaya kutoka Kenya zilikuwa juu kati ka chati , wilaya za Tanzania zilikuwa chini, na za Uganda zilikuwa kati kati .

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 12

Jedwali la 4: Wilaya zilizofanya vizuri sana na vibaya sana, wanafunzi wa Darasa la 3 katika majaribio ya Kiingereza na Kuhesabu

Jaribio la Kiingereza Jaribio la Kuhesabu Zilizofanya vizuri sana Zilizofanya

vibaya sana

Zilizofanya vizuri

sana

Zilizofanya vibaya sana

1 Kikuyu Adjumani Kikuyu Kasulu2 Naivasha Liwale Kaloleni Lagdera3 Pokot Kaskazini Katakwi Naivasha Bukoba Vijijini4 Taita Bundibugyo Meru Kusini Nakapiripirit5 Nandi Mashariki Shinyanga Vijijini Nandi Kaskazini Gulu 6 Imenti Kaskazini Gulu Mbeere Kotido7 Nyeri Kusini Kamuli Kibwezi Mwanga8 Ruiru Mayuge Gatanga Singida Vijijini9 Nakuru Kaskazini Yumbe Keiyo Mayuge10 Gatanga Amuru Imenti Kaskazini Shinyanga Vijijini

(*) Angalizo: Wilaya za Kenya ni buluu, wilaya za Uganda ni kijani, wilaya za Tanzania ni nyekundu.Chanzo cha data: Uwezo

Jedwali la 5 linaonesha kwamba wilaya zilizofanya vizuri katika jaribio moja, ziliweza pia kufanya vizuri katika majaribio mengine. Katika Tanzania, wilaya za Moshi Vijijini na Rombo zilikuwa miongoni mwa wilaya tatu bora katika kila jaribio katika majaribio matatu. Nchini Kenya, wilaya za Kikuyu na Naivasha ndizo zilizofanya vizuri katika kila jaribio, na kule Uganda wilaya za Wakiso na Masaka zimejitokeza. Je, wilaya hizi zinafanana kwa namna gani? Miongoni mwa wilaya zilizofanya vibaya kulikuwa na tofauti nyingi japo wilaya za Muleba na Kasulu katika Tanzania, na Lagdera na Wajir Mashariki katika Kenya zinaonekana zaidi ya mara moja katika orodha ya wilaya zinazofanya vibaya zaidi. Kwa ufupi inaonekana kwamba wilaya zinazofanya vizuri zote zinafanana, wilaya zinazofanya vibaya zinafanya vibaya kwa namna yao.

Jedwali la 5: Wilaya zilizofanya vizuri sana na vibaya sana kwa Darasa la 3, kwa wilaya na nchi Tanzania Kenya Uganda

Kiingereza Waliofanya vizuri sana

Waliofanya

vibaya sana

Waliofanya vizuri sana

Waliofanya vibaya sana

Waliofanya vizuri sana

Waliofanya vibaya sana

1 Moshi Mjini 33% Liwale 0% Kikuyu 64% Lagdera 4% Wakiso 12% Adjumani 0%2 Rombo 23% Shinyanga

Vijijini1% Naivasha 53% Trans Mara 9% Masaka 8% Katakwi 0%

3 Moshi Vijijini

23% Muleba 2% Pokot North

52% Rachuonyo 10% Nakason-gola

8% Bundibu-gyo

1%

Kuhesabu

1 Moshi Mjini 40% Kasulu 5% Kikuyu 66% Lagdera 5% Busheni 40% Nakapir-ipirit

7%

2 Rombo 39% Bukoba Vijijini 7% Kaloleni 65% Samburu North

14% Masaka 38% Gulu 7%

3 Moshi Vijijini

35% Mwanga 8% Naivasha 57% Wajir Mashariki

17% Wakiso 38% Kotido 8%

Kiswahili

1 Rombo 63% Muleba 9% Naivasha 68% Lagdera 4% Hawakufanya

2 Moshi Mjini 58% Mwanga 16% Taita 64% Wajir Mashariki

12%

3 Kisarawe 57% Kasulu 17% Kikuyu 62% Trans Mara 14%

(*) Angalizo: Wilaya za Kenya ni buluu, wilaya za Ugandani kijani, wilaya za Tanzania ni nyekunduChanzo cha data: Uwezo

4.3 Tofauti katika umahiri wa wanafunzi kwa mujibu wa utajiri wa kaya Sifa za kaya vilevile zilionesha kuathiri umahiri wa watoto katika majaribio. Kielelezo cha 9 na 10 hapa chini vinaonesha jinsi utajiri wa kaya unavyohusiana na uwezo wa wanafunzi. Watoto kutoka kaya tajiri sana walifanya vizuri zaidi katika majaribio ya Uwezo kuliko watoto kutoka kaya zenye hali ya chini. Mathalan, nchini Kenya karibu nusu (asilimia 47) ya watoto wa Darasa la 3 kutoka kaya tajiri sana walionesha kuwa na stadi za kusoma za Darasa la 2, kinyume na asilimia 19 tu ya watoto kutoka katika kaya maskini zaidi. Vivyo hivyo, asilimia 48 ya watoto kutoka kaya tajiri sana katika Kenya walifaulu jaribio la kuhesabu, kinyume na asilimia 28 tu ya watoto kutoka kaya maskini zaidi.

Kuhesabu na Kusoma Kati ka Afi ka Mashariki 13

Kielelezo cha 9: Ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la 3 kati ka jaribio la Kiingereza la Uwezo, kwa madaraja ya utajiri na nchi

Chanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha 10: Umahiri wa wanafunzi wa Darasa la 3 kati ka jaribio la kuhesabu, kwa madaraja ya utajiri na nchi

Chanzo cha data: Uwezo

Kulikuwa na uwezekano mdogo kwa watoto kutoka kaya masikini zaidi nchini Kenya kufaulu majaribio ya Kuhesabu na Kiingereza kuliko watoto kutoka kaya tajiri. Hata hivyo, uwezekano wa kufanikiwa ulikuwa bado juu kwa mtoto kutoka kaya masikini zaidi nchini humo kuliko mtoto kutoka kaya tajiri sana kati ka Uganda au Tanzania. Mathalani, asilimia 19 ya watoto kutoka kaya masikini zaidi nchini Kenya walifaulu jaribio la Kiingereza, ikilinganishwa na asilimia 16 ya watoto kutoka kaya tajiri sana za Uganda na asilimia 11 ya watoto kutoka Tanzania. Kwa jaribio la Kuhesabu, matokeo yanafanana, isipokuwa watoto wa Kenya kutoka kaya masikini zaidi walifaulu kwa kiwango kinachokaribiana na watoto wenzao kutoka kaya tajiri zaidi za Uganda na Tanzania.

Hiti misho: Matokeo ya utafi ti wa Uwezo yanaonesha kwamba stadi za kuhesabu na kusoma zilikuwa dhaifu kati ka nchi zote tatu na watoto walio wengi kati ka Darasa la 3 hawakufi kia stadi za kiwango cha Darasa la 2 kati ka kuhesabu na kusoma. Kati ya waliofanya vibaya, Kenya ilifanya vizuri zaidi kuliko Uganda na Tanzania. Tanzania inaonesha udhaifu mkubwa zaidi kati ka majaribio ya Uwezo. Tofauti kubwa kati ka umahiri wa watoto zimeonekana kati ka wilaya ndani na kati ya nchi na kwa watoto kutoka kaya zenye viwango tofauti vya kipato. Inawezakana kukawa na matumaini kutokana na tofauti za msingi kati ka ufaulu zilizojitokeza ndani ya kila nchi. Kuwepo kwa tofauti hizo kunaashiria kwamba umahiri wa watoto unaweza kuimarika kati ka mifumo ya elimu iliyopo sasa na inatoa fursa ya kutafuta sababu zilizopelekea kuwepo kwa tofauti hizi.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 14

5. Upati kanaji wa nyenzo shuleni Inawezekana tofauti zilizobainika kati ka umahiri wa watoto ki-wilaya ni kutokana na tofauti ya upati kanaji wa nyenzo shuleni au tofauti kati ka ufundishaji. Japokuwa utafi ti wa Uwezo haukujumuisha taarifa kuhusu ubora wa ufundishaji, taarifa kati ka dodoso la shule ziliruhusu kwa namna fulani kuangalia mahitaji yaliyokuwa yanapati kana kati ka shule. Kwa kila moja ya nchi hizi tatu dodoso la shule la Uwezo lilikusanya taarifa ambazo zingeweza kukokotolewa kuhusu idadi ya wanafunzi kwa mwalimu, wanafunzi kwa darasa, na wanafunzi kwa choo.

Ulinganishi kwa mujibu wa nchi unaonesha kwamba shule za Kenya zilikuwa na uwiano mdogo wa wanafunzi:mwalimu, wanafunzi:darasa, na wanafunzi wachache kwa vyoo kuliko shule za Uganda na Tanzania. Tofauti kati ya Kenya na Tanzania na Uganda ilikuwa kubwa. Mathalan, nchini Tanzania kulikuwa na wanafunzi 60 kwa mwalimu mmoja, nchini Kenya ni wanafunzi 38. Uganda kulikuwa na wanafunzi 83 kwa darasa, wakati Kenya ni 48. Kwa ujumla viashiria vya upati kanaji wa mahitaji ya elimu nchini Kenya vinakaribiana sana na viwango rasmi vinavyotakiwa kufi kiwa kuliko hali ilivyo kati ka nchi za Uganda na Tanzania.

Kielelezo cha 11: Viashiria vya upati kanaji wa mahitaji shuleni kwa Kenya, Uganda na Tanzania

Chanzo cha data: Uwezo

Ndani ya nchi hizi tofauti kubwa zilionekana. Tofauti hizi zinaweza kuonekana kati ka Jedwali la 6 linaloonesha nafasi za wilaya kulingana na upati kanaji wa mahitaji ya shule kwa kuzingati a wiano hizi tatu. Nafasi ya jumla ya wilaya ilipati kana baada ya kukokotoa nafasi ya wilaya kati ka kila kiashiria kwa viashiria vyote vitatu na kuzipa wilaya namba kulingana na nafasi iliyopata. Jumla ya namba zinazoambatana na nafasi zilizopata wilaya kwa viashiria vyote vitatu ndizo zinazotoa nafasi za jumla ambazo wilaya zilipewa kutoka wilaya ya juu kabisa hadi ya chini kabisa kati ka Jedwali la 6.

Jedwali linaonesha kwamba wastani ulitofauti ana sana: kutoka wanafunzi 25 kwa mwalimu (chini kabisa) kama iliyokuwa kati ka wilaya ya Imenti Kusini, Kenya, hadi wanafunzi 91 kwa mwalimu (juu kabisa) kati ka wilaya ya Muleba, Tanzania. Vilevile wiano za mwanafunzi: darasa zilitofauti ana kutoka wanafunzi 23 (chini kabisa pia) kati ka wilaya ya Imenti Kusini, hadi kufi kia 173 (juu kabisa) kati ka wilaya ya Buliisa, Uganda. Uwiano wa wanafunzi kwa choo pia ulitofauti ana, kutoka uwiano wa chini kabisa wa wanafunzi 14 kwa choo kati ka wilaya ya Nyeri Kusini, Kenya hadi kufi kia kiwango cha juu kabisa, kiasi cha wanafunzi 110 kwa choo kimoja kati ka wilaya ya Kamuli, Uganda. Hizi wiano ni wastani kati ka ngazi ya wilaya, ikimaanisha kuwa zinafi cha tofauti kubwa zaidi zilizopo baina ya shule. Kwa shule moja moja na madarasa, tofauti zilikuwa za juu zaidi. Mathalan, nchini Kenya data za Uwezo zinaonesha kwamba wiano za mwanafunzi:mwalimu zinaanzia 10:1, chini kabisa hadi kufi kia zaidi ya 200:1.

Jambo jingine lililoonekana ni kwamba wilaya za Kenya zilikuwa kati ka nafasi za juu, ambapo za Tanzania na Uganda, na chache za Kenya zilionekana kati ka nafasi za chini ya orodha. Kati ka upangaji wa nafasi uliofanywa na Uwezo kati ka Afrika Mashariki, wilaya za Kenya zilionekana kuwa kati ka nafasi 24 za juu. Wilaya ya kwanza isiyo ya Kenya ilikuwa ya Tanzania kati ka nafasi ya 25, ambapo wilaya ya kwanza ya Uganda ilionekana kati ka nafasi ya 44. Hakuna wilaya za Kenya zilizokuwa miongoni mwa zile zilizoshika nafasi 10 za chini.

Kuhesabu na Kusoma Kati ka Afi ka Mashariki 15

Jedwali la 6: Wilaya zilizofanya vizuri na vibaya sana kati ka kipimo kinachojumuisha uwiano wa mwanafunzi:mwalimu, mwanafunzi: darasa na mwanafunzi: choo

Nafasi Jina la wilaya Wanafunzi kwa mwalimuWanafunzi kwa darasa Wanafunzi kwa choo

Wilaya 10 za juu 1 Imenti Kusini 25 23 142 Mbeere 27 28 173 Meru Kusini 28 25 174 Imenti Kaskazini 28 29 235 Nyeri Kusini 33 28 146 Kericho 28 35 307 Nyandarua Kaskazini 35 33 178 Kikuyu 35 31 259 Tharaka 29 29 3910 Wareng 31 35 31

Wilaya 10 za chini

126 Muleba 91 83 79

127 Kamuli 66 86 110

128 Mayuge 64 99 100

129 Urambo 86 110 69

130 Amuru 70 117 76

131 Amuria 69 100 89

132 Budaka 69 101 87

133 Geita 83 108 92

134 Buliisa 67 173 112

135 Ilemela 87 140 107(*) Angalizo: wilaya za Kenya ni buluu, wilaya za Uganda ni kijani, wilaya za Tanzaniani nyekunduChanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha hali ya upati kanaji mahitaji shuleni kinaweza kuundwa kwa kutumia utarati bu uleule uliotumika kuunda kielelezo cha utajiri wa kaya98. Madaraja matano ya upati kanaji wa mahitaji, kila moja likiwa na asilimia 20 ya shule zilizotembelewa, yaliainishwa kwa kila nchi. Madaraja hayo matano hayakuweza kulinganishwa moja kwa moja miongoni mwa nchi zote tatu kwa kuwa viashiria tofauti vilitumika kuunda kielelezo cha kila nchi. Ndani ya nchi, kwa kiasi kikubwa ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la 3 kati ka majaribio ya Uwezo haukutofauti ana sana kulingana na daraja la hali ya mahitaji kati ka shule. Tofauti moja iliyojitokeza ni kwamba kati ka nchi za Kenya na Tanzania umahiri wa wanafunzi kati ka jaribio la Kiingereza ulikuwa mkubwa zaidi kwa watoto waliosoma kati ka shule iliyokuwa kati ka daraja la juu la upati kanaji wa mahitaji.

Kielelezo cha 12: Watoto wa Darasa la 3 wenye stadi za kusoma Kiingereza za Darasa la 2, kwa madaraja ya upati kanaji wa nyenzo shuleni

Chanzo cha data: Uwezo

8 Angalia, mathalani Filmer D na Pritchett LH. Esti mati ng wealth eff ect without expenditure data-or tears: an applicati on to educati onal enrollments in states of India. Demography 2001; 38:115-32.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 16

Kielelezo cha 13: Watoto wa Darasa la 3 wenye stadi za kuhesabu za Darasa la 2, kwa madaraja ya upati kanaji wa nyenzo shuleni

Chanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha 14 na kile cha 15 vinawasilisha ubora wa shule kwa kuzingati a hali ya upati kanaji nyenzo kati ka shule walizohudhuria watoto kutoka daraja la chini na la juu la utajiri. Inaonekana kwamba, kwa ujumla, watoto kutoka kaya masikini walihudhuria shule duni, ambapo watoto kutoka familia bora walihudhuria shule bora. Nchini Kenya, tofauti zilionekana zaidi na watoto asilimia 37 kutoka asilimia 20 ya kaya masikini zaidi walihudhuria shule duni zaidi, ambapo ni asilimia 9 tu kutoka kaya masikini zaidi ndiyo walihudhuria shule bora zaidi. Nchini Uganda, mgawanyo ulionekana kuwa wa usawa zaidi, wakati Tanzania ikichukua nafasi ya kati kati .

Kielelezo cha 14: Hali ya nyenzo kati ka shule walizosoma watoto kutoka kaya masikini zaidi

Chanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha 15: Hali ya nyenzo kati ka shule walizosoma watoto kutoka kaya tajiri zaidi

Kuhesabu na Kusoma Kati ka Afi ka Mashariki 17

Chanzo cha data: Uwezo

Hiti misho: Kuna tofauti kubwa kati ka hali ya upati kanaji wa mahitaji baina ya shule. Ubora wa shule ukitafsiriwa kwa kutumia seti ya viashiria sahili vya mahitaji (wanafunzi kwa mwalimu, wanafunzi kwa darasa, na wanafunzi kwa choo) ulionesha kuwepo kwa tofauti kubwa miongoni mwa nchi hizi tatu, kati ya wilaya ndani ya nchi, na kati ya shule zilizo kati ka wilaya moja. Kwa jumla shule nchini Kenya zilikuwa zina hali nzuri zaidi kuliko shule za Uganda na Tanzania; shule za Uganda ndizo zilizokuwa na hali duni zaidi.

Uhusiano kati ya hali ya upati kanaji mahitaji shuleni na umahiri wa watoto kati ka majaribio ya Uwezo ulionekana kuwa hafi fu. Hali hii inapaswa kuwatahadharisha wale wanaoamini kuwa utendaji kati ka shule utakuwa bora zaidi kwa kupunguza uwiano wa mwanafunzi:mwalimu au uwiano wa mwanafunzi:darasa. Data za Uwezo zinaashiria kuwa vipengele hivi ni muhimu ila vipengele ambavyo havikuangaliwa kati ka utafi ti vinaweza kuwa ni muhimu zaidi. Namna ya ufundishaji, uwajibikaji wa mwalimu na moti sha ni baadhi ya vipengele vingine muhimu vinavyoathiri ufaulu wa shule. Kwa bahati mbaya hakuna taarifa zilizokusanywa kuhusu vipengele hivi.

Mwisho, watoto kutoka kaya masikini walikuwa na mazingira magumu zaidi kwa maana si tu kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa wa wao kutokwenda shule au kuacha shule, wao vilevile walikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kusoma kati ka shule zilizo na hali duni ya mahitaji.

6. Shule binafsiMpaka sasa ripoti hii imejikita kati ka stadi za kuhesabu na kusoma kati ka shule za msingi za serikali. Lakini kuna idadi kubwa ya watoto wanaosoma kati ka shule binafsi kati ka nchi za Afrika Mashariki. Nchini Kenya asilimia 9 ya watoto wenye umri wa kwenda shule wanasoma kati ka shule binafsi na nchini Uganda watoto wanaofi kia asilimia 28 ya watoto wote walioandikishwa shule wanahudhuria shule binafsi. Tanzania ndiyo nchi ambayo ina watoto wachache zaidi wanaosoma kati ka shule binafsi (asilimia 2).

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 18

Kielelezo cha 16: Mgawanyo wa wanafunzi wa elimu ya msingi kati ka shule za serikali na binafsi

Chanzo cha data: Uwezo

Haishangazi, bila shaka, kwamba watoto walio wengi waliosoma kati ka shule binafsi walitoka kati ka kaya tajiri sana; wachache walitoka kati ka kaya masikini. Ruwaza hii ilijitokeza zaidi kati ka Tanzania, ambako watoto waliosoma kati ka shule binafsi kwa kawaida walitoka kati ka kaya zilizo kati ka madaraja mawili ya juu ya kipimo cha utajiri. Nchini Uganda, elimu kati ka shule za binafsi ilipati kana pia kwa watoto kutoka kaya masikini, ingawa watoto kutoka kaya tajiri bado ndiyo waliokuwa na nafasi kubwa zaidi ya kusoma kati ka shule hizo. Kenya inashika nafasi ya kati kati .

Kielelezo cha 17: Uandikishaji watoto kati ka shule za binafsi kwa mujibu wa madaraja ya utajiri

Chanzo cha data: Uwezo

Wanafunzi wanaosoma kati ka shule binafsi walifanya vizuri kati ka majaribio ya Uwezo kuliko wale wanaosoma kati ka shule za serikali. Matokeo haya yamejidhihirisha kati ka nchi zote tatu. Nchini Kenya asilimia 60 ya watoto kati ka shule binafsi Darasa la 3 walifaulu majaribio ya Kiingereza na Kuhesabu. Matokeo haya yalikuwa pungufu ya asilimia 100 yaliyoyatarajiwa lakini mazuri mara mbili zaidi ikilinganishwa na matokeo kati ka shule za serikali. Nchini Tanzania tofauti kati ka uwezo wa watoto wa Darasa la 3 kati ya shule za serikali na binafsi ilikuwa dhahiri zaidi. Wakati watoto chini ya asilimia 10 kati ka shule za serikali walifaulu jaribio la Kiingereza, karibu nusu ya wale waliokuwa kati ka shule binafsi walifaulu. Tofauti kama hiyo, japo ndogo ilionekana pia kati ka jaribio la kuhesabu. Pengine matokeo yanayostusha zaidi yalikuwa kutoka Uganda ambako shule binafsi zilifanya vizuri kuliko shule za serikali lakini ni asilimia 10 tu ya watoto kati ka Darasa la 3 wanaohudhuria shule binafsi ndio waliofaulu jaribio la Kiingereza. Hii ni licha ya kuwa lugha ya Kiingereza inatumiwa kwa kiasi kikubwa kati ka baadhi ya shule za Uganda. Matokeo haya ndiyo yaliyokuwa mabaya zaidi kati ka Afrika Mashariki. Miongoni mwa wanafunzi wanaosoma kati ka shule binafsi wanafunzi kati ka shule binafsi za Uganda pia walifanya vibaya sana kati ka jaribio la kuhesabu.

Kuhesabu na Kusoma Kati ka Afi ka Mashariki 19

Wakati watoto wanapokuwa wamefi ka Darasa la 7, tofauti kati ka ufulu haionekani kati ya wale wanaosoma kati ka shule za serikali na wanaosoma kati ka shule binafsi, isipokuwa kwa Tanzania ambako wanafunzi wa Darasa la 7 kati ka shule za serikali wameonekana kufanya vibaya zaidi kuliko wanafunzi wanaosoma kati ka shule binafsi. Wakati huohuo, nchini Uganda na Tanzania idadi kubwa ya wanafunzi kati ka shule binafsi kati ka Darasa la 7 waliendelea kushindwa kati ka majaribio ya Uwezo. Mathalan, mwanafunzi mmoja kati ya watano wa Darasa la 7 wa shule binafsi nchini Uganda walishindwa jaribio la hesabu la Uwezo. Nchini Tanzania, mwanafunzi mmoja kati ya watatu wa darasa la saba toka shule binafsi walishindwa jaribio la hesabu la Uwezo.

Kielelezo cha 18: Umahiri kati ka majaribio ya Uwezo ya Kiingereza na Hesabu kwa mujibu wa aina ya shule na darasa

Chanzo cha data: Uwezo

Hiti misho: Mahudhurio ya wanafunzi kati ka shule binafsi yametofauti ana sana kati ka nchi za Afrika Mashariki, kukiwa na mtoto mmoja kati ya watoto wanne anayesoma kati ka shule za binafsi nchini Uganda, na mtoto mmoja kati ya watoto 50 nchini Tanzania. Kama ilivyotarajiwa, ni watoto kutoka kaya tajiri sana ndiyo wanaosoma kati ka shule binafsi, ingawa nchini Uganda upati kanaji wa shule ulionesha mgawanyo wenye usawa zaidi miongoni mwa matabaka ya utajiri.

Umahiri wa wanafunzi wanaosoma kati ka shule binafsi kati ka majaribio ya Uwezo ulikuwa mzuri zaidi kuliko ya wale wanaosoma kati ka shule za serikali, lakini bado hayaridhishi. Wanafunzi wanaosoma kati ka shule binafsi kwa kiasi fulani walifanya vibaya hasa kati ka nchi za Tanzania na Uganda. Hata Kenya, ambako watoto kutoka shule zake za binafsi walifanya vizuri zaidi, mtoto mmoja kati ka watoto watatu wa Darasa la 3 alishindwa kati ka majaribio ya Uwezo ya kuhesabu na Kiingereza.

Matokeo mazuri ya shule binafsi yanatoa fursa ya kuchunguza ni nini hasa chanzo cha matokeo hayo mazuri. Je, shule za binafsi zina vitendea kazi bora kama vile vitabu, walimu wenye sifa bora kitaaluma, uwajibikaji, mishahara mizuri ya walimu, au vichocheo vingine? Wakati huo huo ni wazi kwamba shule binafsi zenyewe si ufumbuzi, kwa kuwa matokeo ya wanafunzi wao bado hayaridhishi sana.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 20

7. Usawa wa Kijinsia Sehemu hii inajadili usawa wa kijinsia kwenye shule. Kama ilivyojadiliwa kati ka Sehemu ya 3, zilionekana tofauti kati ka viwango vya uandikishaji kati ka nchi hizi tatu. Hata hivyo, kama Kielelezo cha 19 kinavyoonesha, nchi zote zimefanikiwa kukuza usawa wa kijinsia kati ka uandikishaji. Kati ka nchi za Uganda na Kenya uandikishaji ulikuwa juu kidogo kwa wanafunzi wavulana ukilinganishwa na ule wa wasichana, wakati Tanzania kiwango cha uandikishaji kilikuwa juu kidogo kwa wasichana.

Kielelezo cha 19: Uandikishaji kwa mujibu wa jinsia kwa watoto wenye umri wa kwenda shule

Chanzo cha data: Uwezo

Wakati ambapo tofauti za kijinsia kati ka uandikishaji wanafunzi zimepungua sana, majaribio ya Uwezo yameonesha kuwepo kwa tofauti kidogo kati ka viwango vya ufaulu baina ya wanafunzi wa kike na wa kiume kama inavyoonekana kati ka Jedwali la 20. Nchini Kenya, wanafunzi wa kike walifanya vibaya kidogo kati ka majaribio matatu ya Uwezo, wakati kati ka nchi za Uganda na Tanzania ushahidi ulichanganyika. Nchini Uganda, wanafunzi wa kike walifanya vizuri kidogo kati ka jaribio la Kiingereza tofauti na wavulana na vibaya kati ka jaribio la kuhesabu. Nchini Tanzania, wanafunzi wa kike pia walifanya vibaya kidogo kati ka jaribio la kuhesabu, vizuri kati ka jaribio la Kiingereza, na vizuri zaidi kati ka jaribio la Kiswahili.

Kuhesabu na Kusoma Kati ka Afi ka Mashariki 21

Kielelezo cha 20: Ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la 3 kati ka majaribio ya Uwezo, kwa mujibu wa jinsia

Chanzo cha data: Uwezo

Hiti misho: Ubaguzi wa kijinsia mara nyingi huonekana kati ka nyanja za siasa-jamii. Hali hii haikuonekana kati ka elimu ya msingi, angalau kati ka uandikishaji au umahiri wa wanafunzi kati ka stadi za msingi za kusoma na kuhesabu: wanafunzi wa kike na wa kiume walikuwa na ufaulu usiotofauti ana sana. Nchini Kenya, wanafunzi wa kike waliachwa nyuma kidogo kati ka uandikishaji na pia hawakufanya vizuri kati ka majaribio ya Uwezo ukilinganisha na wenzao wa kiume. Kwa upande wa Uganda na Tanzania matokeo yalichanganyika, na inaweza kuwa haki kuhiti misha kuwa kwa ujumla wasichana na wavulana walionesha umahiri sawa.

8. Ni vipengele vipi vinaathiri zaidi ufaulu wa watoto? Hadi hapa ripoti hii inaonesha kwamba stadi za msingi za kuhesabu na kusoma zilihusiana kwa karibu zaidi na darasa analosoma mtoto, iwapo alitoka kati ka kaya tajiri, na kama alisoma kati ka shule ya binafsi. Stadi za msingi za kuhesabu na kusoma hazina uhusiano wa karibu na upati kanaji wa nyenzo au mahitaji shuleni, na jinsia ya mtoto. Kwa kuwa wanafunzi waliosoma kati ka shule duni pia walitarajiwa kukabiliwa na changamoto nyingine kama vile kipato kidogo kati ka kaya, ni vigumu kuchanganua athari za hali ya upati kanaji wa nyenzo shuleni kwa mafanikio ya watoto. Kati ka sehemu hii tunachunguza uhusiano wa vipengele tulivyojadili kwa ujumla na umahiri wa wanafunzi shuleni. Tunaangalia pia vipengele vingine vinavyoweza kuwa na uhusiano na ufaulu wa wanafunzi kama vile kiwango cha elimu ya mama au umri wa mtoto. Kwa kufanya ukokotozi wa kimahesabu tunajaribu kukadiria athari ya vipengele hivi kila kimoja, kikiwa peke yake, bila kuwepo kwa athari ya kipengele kingine kati ka ufaulu wa mtoto.

Tunawasilisha matokeo kwa nchi moja moja kwa kuwa data za Uwezo zinaruhusu kuingiza vigezo tofauti tofauti kati ka kila nchi. Mathalan, kati ka utafi ti wa Uwezo nchini Uganda maswali kuhusu elimu ya mama hayakuulizwa, wakati yaliulizwa kati ka Tanzania na Kenya.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 22

Kati ka nchi zote tatu na kwa majaribio matatu tofauti , ruwaza ya kufanana inajitokeza. Darasa alilokuwa anasoma mwanafunzi ni kipengele kilichoonekana kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na uwezekano wa mtoto kuwa na stadi za msingi za kuhesabu na kusoma. Elimu ya mama nayo vilevile ilikuwa na athari kubwa kwa uwezekano wa mtoto kumudu stadi hizi za msingi lakini, na hii ilionekana dhahiri zaidi, hasa kwa kinamama wenye elimu ya sekondari na kuendelea. Ilipotokea kuwa mama ana elimu ya shule ya msingi au chini ya hapo, athari chanya kwenye umahiri wa mtoto kati ka kumudu stadi za msingi shuleni haikuonekana. Vipengele vya utajiri wa kaya na mtoto kusoma kati ka shule za binafsi vilikuwa na athari chanya kubwa kati ka ufaulu shuleni. Vipengele vya jinsia na upati kanaji wa nyenzo/mahitaji ya shule vilikuwa na athari kidogo sana.

Kielelezo cha 21: Athari za ziada kutokana na vipengele mbalimbali kwa umahiri wa wanafunzi kati ka jaribio la Uwezo: Kenya

Chanzo cha data: Uwezo

Kielelezo cha 22: Athari za ziada kutokana na vipengele mbalimbali kati ka uwezo wa wanafunzi kati ka jaribio la Uwezo:Tanzania

Chanzo cha data: Uwezo

Kuhesabu na Kusoma Kati ka Afi ka Mashariki 23

Figure 23: Athari za ziada kutokana na vipengele mbalimbali kwa umahiri wa wanafunzi kati ka jaribio la Uwezo: Uganda

Chanzo cha data: Uwezo

9. Hiti mishoMuhtasari wa matokeo makuu Ripoti hii imechunguza uwezo wa kuhesabu na kusoma kwa maelfu ya wanafunzi wenye umri wa kati ya miaka 6 na 16 kati ka nchi za Kenya, Tanzania na Uganda kwa kutumia majaribio ya Uwezo yaliyofanywa mwaka 2009/10. Kwa mujibu wa matokeo haya, watoto kati ka nchi zote tatu walifanya vibaya ikilinganishwa na viwango vya mitaala ya nchi zao. Wanafunzi wa shule za msingi za Kenya ndiyo walioonekana kuwa wanajifunza zaidi. Kati ka majaribio yote matatu–Kiswahili, Kiingereza na kuhesabu–wanafunzi wa Kenya walikuwa juu, wakifuati wa na wanafunzi wa Uganda. Wanafunzi wa Tanzania ndiyo waliofanya vibaya zaidi hata kati ka jaribio la Kiswahili, lugha ambayo watoto wa Tanzania wanaitumia zaidi kuliko watoto wa Kenya.

Wakati watoto wa Kenya wameonesha kuwa na stadi bora zaidi kati ka kuhesabu na kusoma, nao pia hawakufanya vizuri sana. Kati ka Darasa la 3, watoto kama wawili kati ya watatu hawakuweza kufaulu majaribio ya Uwezo ya Kiingereza, Kiswahili na kuhesabu. Matokeo haya yanati a wasiwasi, kwa kuwa matarajio yalikuwa asilimia 100 au watoto wote kati ka Darasa la 3 wangeweza kufaulu jaribio la Darasa la 2. Ni pale wanafunzi walipofi ka Darasa la 7 ndipo karibu wote walionesha kuwa wamepata stadi za msingi za kuhesabu na kusoma za Darasa la 2, japo kati ka Tanzania nusu ya wanafunzi wa Darasa la 7 bado hawakuweza kufanya jaribio la Kiingereza la Darasa la 2.

Shule nchini Kenya zilionekana kuwa na hali nzuri zaidi ya upati kanaji wa mahitaji ya shule (kwa kuangalia uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu; uwiano wa wanafunzi kwa darasa, na vilevile wa wanafunzi kwa choo) zikilinganishwa na shule kati ka nchi za Uganda na Tanzania. Hata hivyo, jambo muhimu tuliloliona, ukizingati a rasilimali nyingi zimewekezwa kati ka miaka ya karibuni ili kuongeza ubora wa miundo mbinu ya shule, ni kwamba upati kanaji wa nyenzo hizi ulikuwa na uhusiano mdogo sana na viwango vya ustadi wa watoto kati ka kusoma na kuhesabu. Wanafunzi kati ka maeneo yenye shule zenye miundombinu bora hawakufanya vizuri kuliko wale wanaosoma kati ka shule zenye miundombinu isiyotosheleza au kati ka madarasa yenye msongamano mkubwa.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 24

Kenya ilikuwa nchi pekee ambako tofauti za kiusawa zilionekana wazi zaidi. Miongoni wa kaya masikini zaidi, watoto wachache zaidi waliofikia umri wa lazima kwenda shule waliandikishwa katika shule za msingi za Kenya (asilimia 74) ikilinganishwa na Tanzania (asilimia 82) na Uganda (asilimia 86). Watoto masikini wa Kenya walikuwa na uwezekano mkubwa wa kusoma katika shule zenye hali ya chini kuliko watoto masikini katika nchi za Uganda au Tanzania. Watoto masikini Kenya walikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kutokwenda shule ya msingi na kuacha shule kuliko watoto wenzao wa Tanzania.

Licha ya hali hii, kwa upande wa matokeo ya kujifunza, watoto masikini nchini Kenya walikuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya vizuri katika majaribio ya Uwezo kuliko watoto kutoka kaya tajiri zaidi katika nchi ya Tanzania na Uganda.Nchini Kenya asilimia ya watoto kutoka kaya masikini katika Darasa la 3 waliofaulu jaribio la kuhesabu walikuwa asilimia 31, ikilinganishwa na asilimia 28 ya watoto kutoka kaya tajiri zaidi Uganda waliofaulu jaribio hili. Asilimia ya watoto wa Kenya kutoka kaya masikini zaidi waliofaulu jaribio la Kiingereza ilikuwa 19, ikilinganishwa na asilimia 16 ya watoto kutoka kaya tajiri sana katika Tanzania waliofaulu jaribio hili.

Nchini Uganda, watoto walifanya vibaya sana katika madarasa ya chini lakini walipofika katika madarasa ya juu waliimarika na kuweza kuonesha ustadi wa kumudu majaribio ya viwango vya Darasa la 2. Walipofika Darasa la 7, kiwango cha ufaulu cha watoto wa Uganda kilikuwa karibu sawa na cha watoto wa Kenya. Matokeo kwa upande wa watoto wa Tanzania yalikuwa tofauti: kiwango cha ufaulu wa watoto kilibadilika kwa kiasi kidogo sana kadri walivyoendelea kupanda madarasa. Matokeo yake ni kwamba, ni asilimia 51 tu ya watoto wa Tanzania katika Darasa la 7 walifaulu jaribio la Kiingereza la Uwezo na ni asilimia 68 tu katika Darasa la 7 walifaulu jaribio la kuhesabu la Darasa la 2.

Watoto wanaosoma katika shule za binafsi walifanya vizuri kiasi wakilinganishwa na wale wanaosoma katika shule za serikali. Utafiti unathibitisha kwamba elimu ya mama ilikuwa na athari kubwa katika uwezo wa mtoto shuleni iwapo mama alikuwa angalau na elimu ya sekondari. Tofauti za kijinsia katika uandikishaji au ufaulu shuleni hazikuwa kubwa.

Nini kifanyikeUkiangalia matokeo haya bila shaka utagundua kuna changamoto kubwa zinazokabili serikali za Afrika Mashariki, walimu na wazazi katika kuhakikisha kwamba watoto wanapata stadi za msingi za kuhesabu na kusoma. Tofauti katika ujifunzaji vilevile zinapunguza matumaini ya ushirikiano mkubwa na maendeleo kati ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki. Hali katika Tanzania ni mbaya zaidi, lakini matokeo ya Kenya na Uganda yanatoa faraja kidogo. Jitihada zaidi zinahitajika sana kushughulikia viwango vya watoto kutokwenda shule na kuacha shule. Vile vile kuna haja ya kuhakikisha kwamba watoto si tu waende shuleni lakini pia wajifunze wakiwa shuleni. Kimataifa inazidi kutambuliwa kuwa watoto wanahitaji kuwa shuleni na kujifunza pia.

Matokeo mabaya lazima huibua swali, nini kifanyike? Matokeo katika ripoti hii yanaashiria kwamba watunga sera wangefanya vizuri iwapo wangehoji ufanisi wa mbinu zilizotumika hadi kufikia sasa, badala ya kuendelea kutekeleza mbinu zile zile zilizozoeleka. Japo uwekezaji wa aina tofauti tofauti unaweza kuleta matokeo chanya, viwango vya ufanisi wa uwekezaji vinatofautina. Uwekezaji wa aina fulani unaweza kuleta mabadiliko bora na ya haraka zaidi kuliko mwingine, au kuonesha kuwa na manufaa zaidi kwa thamani ya matumizi ya fedha. Katika muktadha ambapo rasilimali hazitoshelezi, ni muhimu kupima ushahidi uliopo kwa uangalifu zaidi ili kutambua kile kinachoweza kuchangia zaidi katika kuleta mafanikio.

Matokeo ya Uwezo yanatoa uelekezi kidogo kuhusu mambo yanayoweza kufanyika ili kusukuma mbele maendeleo. Kwanza, kuwepo kwa uhusiano mdogo kati ya wiano za mwanafunzi:mwalimu na mwanafunzi:darasa na kujifunza ni taarifa muhimu, kwa kuwa inauliza swali iwapo vitendea kazi na fedha katika maeneo haya vitakuwa suluhisho katika kukabili hali ya hatari iliyopo. Huu ni wakati muafaka wa kushughulikia ubora wa ufundishaji na vichocheo na motisha kwa walimu. Licha ya yote, inawezekana kabisa kwamba sababu mojawapo ya watoto wanaokwenda shule kujifunza kidogo inatokana na motisha zisizowaridhisha walimu, mahudhurio ya walimu shuleni yakiwa hafifu pia. Kwa mfano, ushahidi kutoka Tanzania unaonesha kwamba asilimia 23 ya walimu hawahudhurii shuleni kila siku na hata wanapokuwa shuleni, walimu wanatumia karibu nusu ya muda wao nje ya madarasa. Matokeo yake watoto wanafundishwa kwa masaa mawili tu na dakika nne kwa siku, badala ya masaa matano yanayotarajiwa.109 Tafiti katika nchi za Uganda na Kenya zinabaini kuwepo kwa hali inayofanana na ya Tanzania.

9 Worldbank Service Delivery Indicators:Education and Health Care in Africa,iliyowasilishwa REPOA, Machi 4,2011

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 25

Tofauti zilizoonekana katika kiwango cha ufaulu wa wanafunzi miongoni mwa wilaya ndani ya kila nchi hizi tatu, na baina ya shule za serikali na zile za binafsi, zinaashiria kwamba baadhi ya shule ‘zimetafuta’ namna ya kupata matokeo mazuri katikati ya vikwazo vilivyopo. Tukichunguza kwa nini baadhi ya wilaya, na ndani ya wilaya baadhi ya shule zinafanya vizuri kuliko nyingine huenda tukapata dokezo kuhusu mambo ya msingi zaidi yanayotakiwa kufanywa ili kuboresha ujifunzaji.

Mbinu rahisi na isiyo na gharama kubwa ingekuwa kuanza kwa kubainisha ni shule zipi zinafanya vizuri (au vibaya) kuliko inavyotarajiwa ikilinganishwa na rasilimali zilizopo, kuzitembelea shule hizi na kubainisha mambo yale yanayoweza kueleza matokeo yao, na kutokana na ziara hizi, kuweza kujifunza yale mambo ya msingi yanayofanana.

Mbinu nyingine zinaweza kutumika. Kuna ushahidi mwingi kutoka Kenya unaotokana na tafiti za kimajaribio, unaoonesha kwamba programu zilizoongeza vitendea kazi vya shule kwa kiasi kikubwa hazikuleta matokeo yaliyotarajiwa katika ufanisi. Kwa mfano kuongeza vitabu na vifaa vya walimu kuandikia, havikusaidia kuongeza ubora wa uwezo wa wanafunzi, na kupunguza ukubwa wa darasa kwa kuongeza walimu vilevile hakukubadilisha matokeo. 1110Hatua zilizoongeza viwango vya ufaulu wa wanafunzi shuleni ni zile zilizobadili vichocheo kwa walimu kwa namna inayoridhisha. Hatua ya kuwalipa walimu kwa kuhudhuria kazini au kwa maksi za mitihani walizopata wanafunzi wao zilionesha matokeo mchanganyiko, na utaratibu wa kuwapa wazazi taarifa kuhusu hali ya shule vilevile haikuwa na manufaa. Lakini, programu zilizowezesha shule kuajiri walimu zaidi kwa mikataba ya muda mfupi na zile zilizozipa kamati za shule mamlaka juu ya walimu zilifanikiwa kuongeza viwango vya ufaulu wa wanafunzi. Kujaribu mbinu hizi mpya, kwa kutumia utaratibu wa majaribio yanayosimamiwa vizuri, kunaweza kuwa njia mojawapo ya kuhamasisha kuimarisha ujifunzaji katika shule.

Mbinu mojawapo kama hiyo, ambayo bado haijathibitishwa lakini mpango wake umeundwa kutokana na ushahidi kuhusu mbinu zinazoweza kuwa na matokeo yenye ufanisi, unaitwa malipo baada ya matokeo (Cash on Delivery)1211. Wazo kuu hapa ni kwamba badala ya kugharimia vitendea kazi, kuundwe mfumo ambao malipo yatatolewa kwa kufuata ufanisi katika viashiria vya matokeo vilivyoanishwa na kuthibitishwa, kwa mfano, dola 50 kwa kila mwanafunzi atakayemaliza Darasa la 2 akiwa amefaulu kwa asilimia 80 katika stadi za kusoma na kuhesabu. Mbinu hii awali ilibuniwa ili kuboresha ufanisi katika misaada iliyotolewa kwa serikali za kitaifa, lakini huenda mbinu hii ikawa na manufaa zaidi katika namna serikali za kitaifa zinavyounda vichocheo vyake ili kuboresha ufaulu katika ngazi za wilaya na shule.

Kuna hali ya hatari katika ujifunzaji Kenya, Tanzania na Uganda. Serikali zinajivunia mafanikio yake katika kupanua uandikishaji wa wanafunzi. Lakini vilevile sasa zisijifiche nyuma ya mafanikio haya, ila badala yake ziweke malengo yake katika kuhakikisha kwamba watoto wanapokwenda shule wanajifunza. Ushahidi kutoka mapitio mbalimbali na tafiti za kimajaribio zilizofanywa kwa umakini, pamoja na data za Uwezo zilizowasilishwa katika ripoti hii zinabaini kwa kiasi kikubwa kwamba kuwekeza katika vitendea kazi pekee hakutoshi, na kwamba fikra mpya zinahitajika kuhusu suala la vichocheo1312. Mabilioni ya shilingi na masaa yanayotumiwa katika elimu ya msingi kila mwaka na wazazi, serikali na wafadhili yatakuwa yametumika vizuri iwapo watoto watajifunza, na kupata stadi katika kusoma na kuhesabu. Huu ni wakati wa kulikabili sakata hili ipasavyo, na kufikiri kuhusu suluhisho linalofaa ambalo si tu lina lengo jema, bali linaweza pia kuleta mabadiliko chanya.

10 “Improving Education in the Developing World: What have we Learned from Randomized Evaluations?” Michael Kremer na Alaka Holla,Novemba 10,2008.

Inapatikana http://www.economics.harvard.edu/faculty/kremer/files/Annual_Review_081110%20-%20NO%20TRACK%20CHANGES.pdf.

11 Wazo hili lilibuniwa na Centre for Global Development, angalia katika http://www.cgdev.org/section/initiative/_active/codaid. For a comment on its strength and value in local application Angalia :http://blogs.cgdev.org/globaldevelopment/2011/04/guest-post-five-reason-i-am-a-fan-of-cash-on-delivery-and-five-ways-to-make-it-sharper.php12 Mathalan, angalia http://siteresources.worldbank.org/EDUCATION/Resources/278200-1298568319076/makingschoolwork.pdf na thamani ya mbinu za kitafiti angalia Banerjee, A and Duflo, E, Poor Economics:A radical rethinking of the way to fight global poverty, Public Affairs,2011, sana katika sura ya 4.

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 26

Kiambatisho cha 1: Ngazi za Wilaya Jina la wilaya Viashiria vya uwezo wa wanafunzi Viashiria vya upatikanaji nyenzo shuleni

Ufaulu Da-rasa la 3

Ufaulu Da-rasa la 3

Uandikishaji Nafasi ya ufaulu (*)

Uwiano wa wana-

funzi kwa mwalimu

Uwiano wa wanafunzi kwa darasa

Uwiano wa wanafunzi kwa choo

Nafasi ya shule (*)

Adjumani 0% 93% 89% 107 66 57 47 78

Amuria 2% 60% 93% 76 69 100 89 131

Amuru 2% 67% 89% 112 70 117 76 130

Apac 3% 80% 89% 94 69 97 65 119

Babati 3% 58% 92% 78 58 58 42 72

Budaka 3% 62% 91% 97 69 101 87 132

Bukoba Vijijini 1% 39% 82% 130 64 78 47 90

Bukoba Mjini 6% 36% 86% 117 36 73 62 71

Buliisa 2% 84% 92% 66 67 173 112 134

Bundibugyo 1% 49% 94% 98 65 83 108 124

Bungoma Kaskazini 7% 78% 91% 48 42 61 31 51

Bunyala 9% 83% 82% 79 43 68 37 55

Buret 25% 85% 81% 46 34 96 81 92

Bushenyi 4% 67% 91% 81 40 47 45 50

Busia 9% 80% 95% 21 48 88 49 88

Busia 2% 79% 87% 109 64 93 90 125

Butere 11% 77% 91% 39 40 45 37 39

Chunya 10% 55% 82% 115 56 73 50 83

Eldoret Mashariki 26% 92% 93% 4 28 34 36 11

Gatanga 38% 89% 94% 1 41 34 14 16

Geita 6% 59% 81% 120 83 108 92 133

Gucha 30% 95% 89% 8 43 57 40 54

Gulu 0% 90% 93% 73 59 78 63 100

Hamis 20% 84% 91% 17 37 39 53 45

Ibanda 3% 66% 91% 91 42 52 54 60

Igembe 11% 91% 89% 26 45 44 24 36

Ijara 19% 94% 79% 44 41 50 154 82

Ilemela 13% 68% 81% 105 87 140 107 135

Iment Kusini 38% 85% 88% 18 25 29 23 1

Imenti Kaskazini 36% 95% 89% 5 28 23 14 4

Kabale 2% 56% 94% 75 41 53 59 61

Kakamega Kati 14% 80% 88% 52 44 90 39 74

Kakamega Kaskazini 14% 79% 79% 85 35 44 45 34

Kaloleni 34% 95% 72% 31 60 59 104 109

Kamuli 0% 74% 92% 95 66 86 110 127

Karagwe 2% 24% 87% 128 65 78 53 99

Kasulu 4% 18% 79% 129 90 77 67 116

Katakwi 0% 88% 95% 64 63 89 84 121

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 27

Jina la wilaya Viashiria vya uwezo wa wanafunzi Viashiria vya upatikanaji nyenzo shuleni

Ufaulu Da-rasa la 3

Ufaulu Da-rasa la 3

Uandikishaji Nafasi ya ufaulu (*)

Uwiano wa wana-

funzi kwa mwalimu

Uwiano wa wanafunzi kwa darasa

Uwiano wa wanafunzi kwa choo

Nafasi ya shule (*)

Keiyo 24% 90% 83% 34 28 58 27 23

Kericho 18% 94% 85% 32 28 35 30 6

Kibaale 2% 82% 87% 113 65 107 70 123

Kibaha 7% 35% 90% 102 37 53 58 56

Kibwezi 21% 90% 91% 9 33 37 40 24

Kikuyu 53% 87% 94% 3 35 31 25 8

Kilifi 19% 96% 70% 42 57 59 68 91

Kilombero 2% 43% 91% 106 55 81 80 112

Kilosa 0% 36% 89% 124 53 85 68 108

Kinondoni 6% 48% 92% 77 38 83 120 98

Kisarawe 1% 46% 91% 114 45 41 29 38

Kisii Kusini 14% 84% 84% 58 39 45 42 41

Kisumu Magharibi 7% 81% 87% 72 35 38 59 46

Kitui Kaskazini 19% 95% 91% 7 49 39 36 47

Koibatek 16% 89% 86% 38 32 32 46 19

Kongwa 4% 46% 91% 100 59 91 82 120

Kotido 1% 14% 44% 134 92 92 52 115

Kuria East 10% 83% 84% 70 52 51 66 81

Kyenjojo 2% 78% 90% 93 64 78 65 107

Kyuso 10% 92% 79% 63 36 36 49 31

Lagdera 2% 69% 82% 118 64 38 65 76

Laikipia Kaskazini 34% 79% 61% 62 38 161 35 65

Lamu 18% 88% 91% 15 32 31 43 17

Lari 17% 59% 93% 22 37 33 13 13

Limuru 23% 66% 87% 50 42 41 78 68

Liwale 0% 16% 79% 135 57 61 50 79

Loitoktok 25% 82% 83% 51 50 46 34 52

Makueni 15% 87% 90% 24 33 37 39 21

Mandera Kati 12% 83% 74% 86 51 47 58 73

Manga 27% 91% 89% 11 31 35 31 12

Marakwet 17% 91% 87% 33 30 33 53 29

Masaba 21% 82% 92% 13 31 38 33 15

Masaka 7% 76% 92% 53 49 67 75 96

Maswa 4% 33% 84% 125 54 61 79 97

Mayuge 1% 61% 93% 87 64 99 100 128

Mbeere 35% 94% 92% 2 27 28 17 2

Mbeya Mjini 0% 50% 95% 99 40 46 51 53

Mbulu 13% 68% 84% 101 45 62 68 85

Meru Kusini 23% 95% 91% 6 28 25 17 3

Misungwi 4% 34% 91% 108 65 68 53 94

Je Watoto Wetu Wanajifunza? 28

Jina la wilaya Viashiria vya uwezo wa wanafunzi Viashiria vya upatikanaji nyenzo shuleni

Ufaulu Da-rasa la 3

Ufaulu Da-rasa la 3

Uandikishaji Nafasi ya ufaulu (*)

Uwiano wa wana-

funzi kwa mwalimu

Uwiano wa wanafunzi kwa darasa

Uwiano wa wanafunzi kwa choo

Nafasi ya shule (*)

Molo 14% 87% 90% 29 42 45 41 49

Morogoro Vijijini 1% 25% 80% 133 48 67 66 89

Morogoro Mjini 9% 32% 92% 82 49 72 78 101

Moshi Vijijini 16% 54% 87% 92 30 49 33 25

Moshi Mjini 27% 72% 89% 43 41 94 85 106

Moyale 12% 89% 83% 59 56 48 69 86

Mpanda 2% 40% 89% 119 44 90 68 103

Mpwapwa 7% 48% 89% 103 65 87 53 104

Mubende 2% 69% 91% 89 59 76 78 110

Mukono 2% 69% 88% 111 43 65 68 84

Muleba 1% 22% 84% 131 91 83 79 126

Musoma Mjini 13% 52% 91% 68 48 86 66 102

Mwala 14% 82% 93% 19 31 49 25 20

Mwanga 1% 17% 89% 127 45 44 28 40

Naivasha 41% 85% 86% 23 44 78 39 64

Nakapiripirit 2% 90% 65% 123 85 78 55 111

Nakasongoria 5% 78% 94% 49 42 55 55 63

Nakuru Kaskazini 31% 88% 84% 27 36 42 21 22

Nandi Kati 17% 87% 83% 54 33 63 39 44

Nandi Mashariki 32% 91% 88% 14 28 48 37 26

Nandi Kaskazini 37% 96% 85% 12 27 35 38 14

Narok Kaskazini 28% 91% 74% 40 37 52 35 35

Newala 2% 34% 91% 116 78 54 44 80

Ngara 5% 38% 83% 122 69 76 79 118

Njombe 6% 52% 87% 110 65 60 40 75

Nyandarua Kaskazini 18% 79% 89% 35 35 33 17 7

Nyeri Kusini 35% 93% 88% 10 33 28 14 5

Pokot Kaskazini 37% 83% 47% 56 43 93 64 95

Rachuonyo 9% 75% 88% 69 38 63 48 58

Rakai 3% 65% 93% 71 45 69 72 93

Rombo 20% 70% 91% 36 47 68 42 69

Ruiru 27% 80% 84% 45 45 43 29 37

Rukingiri 5% 76% 92% 60 70 80 64 113

Samburu Kati 18% 66% 65% 96 34 35 45 28

Samburu Kaskazini 8% 97% 69% 65 34 31 49 27

SamburuMashariki 5% 95% 56% 88 35 38 57 43

Shinyanga Vijijini 1% 27% 82% 132 71 76 82 122

Singida Vijijini 1% 39% 88% 126 68 66 48 87

Singida Mjini 4% 44% 84% 121 39 74 53 70

Sotik 12% 85% 91% 25 35 57 60 57

Kuhesabu na Kusoma Katika Afika Mashariki 29

Jina la wilaya Viashiria vya uwezo wa wanafunzi Viashiria vya upatikanaji nyenzo shuleni

Ufaulu Da-rasa la 3

Ufaulu Da-rasa la 3

Uandikishaji Nafasi ya ufaulu (*)

Uwiano wa wana-

funzi kwa mwalimu

Uwiano wa wanafunzi kwa darasa

Uwiano wa wanafunzi kwa choo

Nafasi ya shule (*)

Suba 24% 90% 85% 28 36 38 47 32

Sumbawanga 11% 45% 92% 67 70 101 54 117

Taita 31% 86% 89% 16 38 35 25 18

TanaRiver 17% 92% 66% 57 41 40 70 62

Tanga 6% 29% 93% 84 48 142 59 105

Taveta 23% 88% 86% 30 46 45 59 66

Tharaka 20% 76% 89% 37 29 29 39 9

Thika Magharibi 19% 77% 88% 47 32 66 38 42

Trans Mara 6% 81% 80% 104 41 83 53 77

Trans Nzoia Mashariki 16% 91% 84% 41 37 57 30 33

Urambo 4% 52% 92% 80 86 110 69 129

Wajir Mashariki 7% 92% 84% 55 48 42 63 67

Wajir Kaskazini 21% 69% 52% 83 43 34 51 48

Wakiso 8% 76% 91% 61 40 58 51 59

Wareng 20% 78% 75% 74 31 35 31 10

West Pokot 24% 98% 84% 20 33 40 43 30

Yumbe 0% 78% 92% 90 54 84 80 114Angalizo: Wilaya za Kenya ni buluu, wilaya za Uganda ni kijani, wilaya za Tanzania ni nyekundu(*) Faharasa hizi hizi mbili zimetengeneza kwa kujumlisha alama zinazoambatana na nafasi ya wilaya kwa kila kimoja ya viashiria vitatu vilivyozingatiwa, na kutengeneza faharasa nyingine inayoonesha nafasi ya jumla kuanzia ya chini kabisa hadi ya juu kabisa.

Chanzo cha data: Uwezo

Serikali za Kenya, Uganda na Tanzania zinatekeleza sera za elimu ya msingi kwa wote kuwawezesha watoto wote kwenda shule na angalau wajue kusoma, kuandika na kufanya hesabu. Katika muongo uliopita nchi hizi zimeongeza sana bajeti zao za elimu na mafanikio makubwa yameonekana katika kuandikisha wanafunzi. Lakini wakati watoto wengi sasa wanakwenda shule, je wanajifunza?

Uwezo ilifanya taftishi katika nchi hizi tatu, kwa kuwatembelea maelfu ya watoto majumbani kwao, na kuwapa majaribio ya kiwango cha darasa la pili kwa somo la Kiingereza, Kiswahili na Hisabati. Watoto wengi sana walishindwa majaribio haya. Katika nchi zote tatu watoto walipata matokeo ya chini sana ikilinganishwa na kiwango kinachotarajiwa katika mitaala ya nchi zao. Katika mazoezi yote matatu watoto wa Kenya walikua juu wakifuatiwa na Uganda.

Nini huchochea ujifunzaji? Taftishi ya Uwezo imegundua vitu vya kushangaza. Hali bora ya uchumi wa familia imeonekana kushabihiana na umahiri au werevu wa watoto katika stadi za msingi; watoto kutoka katika familia zenye hali nzuri walifanya vizuri zaidi. Jinsia ya mtoto haikuonekana kuwa na uhusiano na werevu wa mtoto. Matokeo toka shule binafsi yalileta sura mchanganyiko; zaidi ya kuongeza ufahamu wa lugha ya Kiingereza katika madarasa ya chini wanafunzi toka shule za binafsi hawakuonesha tofauti kubwa ya umahiri katika stadi za msingi. Kwa watunga sera matokeo muhimu zaidi ni kuwa uwekezaji katika miundombinu na uwiano wa mwalimu na wanafunzi si muarobaini wa kuboresha ufahamu wa wanafunzi. Watoto toka maeneo yenye shule zenye majengo bora hawakufanya vizuri kupindukia kuwazidi wale wanaosoma shule zenye miundombinu hafifu ama waliorundikana madarasani. Hivyo basi, wazazi, serikali na wahisani wanaweza tu kujiridhisha kuwa mabilioni ya shilingi wanazowekeza kila mwaka kwenye sekta ya elimu yametumika vizuri iwapo watoto wakimaliza shule wataingia kutika dunia yenye ushindani wakiwa na ufahamu wa kiwango cha juu wa kusoma, wakijua Hisabati na wakijiamini.

Uwezo East Africa (managed by Twaweza)P.O Box 19875, 00200 Nairobi, Kenya Tel: +254 20 3861372 Email: [email protected] Web: www.uwezo.net

Twaweza East Africa 127 Mafinga Rd, Off Kinondoni Rd P.O Box 38342, Dar es Salaam, Tanzania Tel: +255 22 266 4301. Fax +255 22 266 4308 Email: [email protected] Web: www.twaweza.org Email: [email protected] Web: www.uwazi.org

Uwezo Afrika Mashariki (ikisimamiwa na Twaweza)S.L.P. 19875, 00200 Nairobi, KenyaSimu: +254 20 3861372Baruapepe: [email protected]. Tovuti: www.uwezo.net

Twaweza Afrika Mashariki127 Mtaa wa Mafinga, Kando ya barabara ya KinondoniS.L.P. 38342, Dar es Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 266 4301. Nukushi: +255 22 266 4308. Barua pepe: [email protected]. Tovuti: www.twaweza.orgBarua pepe: [email protected]. Tovuti: www.uwazi.org