issn 0856 - 3861 na. 1168 jamadiul awwal 1436 machi …

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436, IJUMAA , MACHI 13-19, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu facebook: [email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST Ukweli mchungu: Kamanda Boko Haram Mkristo-Prof. Ojobi Ni Abu Tijjani a.k.a Kana’ana a.k.a Maitatsine Alipelekwa Sudani akarudi na Aya, Hadith Akakusanya silaha kupeleka vijana ‘Shamba’ As’hab Kital 700 wakauliwa kuleta Boko Haram2 Boko Haram3 imechanganya Ukristo na ubeberu NI bahati mbaya bado CCM, Chimwaga inadhani kuwa njia pekee ya kuidhibiti Zanzibar ni kupitia khofu na wasiwasi miongoni mwa raia. Ndiyo tafsiri ya kauli hizi “kwamba vifaru vya jeshi vitatumika kuilinda CCM madarakani.” Lakini hikima ya kujifunza inawataka wauangalie uhalisia. Vifaru vinaendeshwa na watu. Mizinga inafyatuliwa na watu. Na ni watu pia wanaodai mabadiliko. (Uk. 6) Mwaka wa Maamuzi: CCM imeamua kuhisabu risasi kubakia madarakani Zanzibar Masheikh wa Baraza Kuu Bakwata haya hamyasikii? (2) HIJI, UFE MUISLAMU! Mtume(saw) amesema kuwa anayekufa bila kuhiji hali ya kuwa aliwahi kupata uwezo anakufa Yahudi au Nasara, na Uislamu hautomtambua Hija ni haki ya Mola wako iliyopo juu yako. Mpe Mola wako haki yake kwanza. Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437. MUHAMED Marwa aka Maitatsine. Inahitajika ‘EWURA’ ya mambo ya Dini La sivyo Qur’an ina msemo wake, “Subirini!” Mtafatuku ndani ya Baraza Rungu la Spika Kificho lafanya kazi HALI ya sintofahamu ilitawala ndani ya Kikao cha Baraza la Wawakilishi juzi. Hata hivyo, ikiacha kilichokusudiwa ambayo ni sheria ya Na Mwandishi Wetu kura ya maoni ikiwa imeridhiwa. Ilikuwa ni katika kuwasilishwa hoja ya kuridhiwa kura ya maoni ambapo baadhi ya wajumbe walipinga wakisema kuwa haina masilahi na Zanzibar. Mvutano ulikuwa baina Spika na Mh. Jussa aliyetaka hoja hiyo isiridhiwe kwa sababu tayari Katiba ya Zanzibar imeshaitangulia Sheria hiyo na imeshaweka masharti ya kura ya maoni Zanzibar. Inaendelea Uk. 8 MHESHIMIWA Jussa (kushoto) akiwa na Bimani.

Upload: others

Post on 14-Nov-2021

5 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436, IJUMAA , MACHI 13-19, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamufacebook: [email protected]

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

Ukweli mchungu:

Kamanda Boko Haram Mkristo-Prof. OjobiNi Abu Tijjani a.k.a Kana’ana a.k.a MaitatsineAlipelekwa Sudani akarudi na Aya, HadithAkakusanya silaha kupeleka vijana ‘Shamba’As’hab Kital 700 wakauliwa kuleta Boko Haram2Boko Haram3 imechanganya Ukristo na ubeberu

NI bahati mbaya bado CCM, Chimwaga inadhani kuwa njia pekee ya kuidhibiti Zanzibar ni kupitia khofu na wasiwasi miongoni mwa raia.

Ndiyo tafsiri ya kauli hizi “kwamba vifaru vya jeshi vitatumika kuilinda CCM madarakani.”

Lakini hikima ya kujifunza inawataka wauangalie uhalisia.

Vifaru vinaendeshwa na watu. Mizinga inafyatuliwa na watu. Na ni watu pia wanaodai mabadiliko. (Uk. 6)

Mwaka wa Maamuzi:

CCM imeamua kuhisabu risasi kubakia madarakani Zanzibar

Masheikh wa Baraza KuuBakwata haya hamyasikii?

(2) HIJI, UFE MUISLAMU!Mtume(saw) amesema kuwa anayekufa bila kuhiji hali ya kuwa aliwahi kupata uwezo anakufa Yahudi au Nasara, na Uislamu hautomtambua Hija ni haki ya Mola wako iliyopo juu yako. Mpe Mola wako haki yake kwanza. Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.

MUHAMED Marwa aka Maitatsine.

Inahitajika ‘EWURA’ ya mambo ya DiniLa sivyo Qur’an ina msemo wake, “Subirini!”

Mtafatuku ndani ya BarazaRungu la Spika Kificho lafanya kazi

HALI ya sintofahamu i l i tawala ndani ya Kikao cha Baraza la Wawakilishi juzi.

Hata hivyo, ikiacha k i l i c h o k u s u d i w a ambayo ni sheria ya

Na Mwandishi Wetu kura ya maoni ikiwa imeridhiwa.

I l ikuwa ni kat ika kuwasilishwa hoja ya kur idh iwa kura ya maoni ambapo baadhi ya wajumbe walipinga wakisema kuwa haina masilahi na Zanzibar.

Mvutano ulikuwa baina Spika na Mh. Jussa aliyetaka hoja hiyo isiridhiwe kwa sababu tayari Katiba ya Zanzibar imeshaitangulia Sheria hiyo na imeshaweka masharti ya kura ya maoni Zanzibar. Inaendelea Uk. 8

MHESHIMIWA Jussa (kushoto) akiwa na Bimani.

Page 2: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

2 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri

KIASI wiki tatu zilizopita t u n a e l e z w a k u w a alisimama Khatib katika Mimbar ya Msikiti mmoja maeneo ya Mikocheni akihutubu siku ya Aljumaa na kuwaambia waumini kuwa ‘wakimchinja kafir, watumie kisu kikal i na wasimkate viungo kwani wanamtesa. Mada aliyoanza nayo ilikuwa ni haki za wanyama. Kwamba hata wale wanaoliwa ikiwa unamchinja kwa ajili ya kitoweo, basi uwe na huruma. Usimtese. Tumia kisu kikali liwe tendo la mara moja.

Hata hivyo, mtoa Khutba akahama akaunganisha a k a s e m a k u wa h a t a ukimchinja kafiri, usianze kumkata viungo.

B a a d a y a s w a l a tunaambiwa kuwa mmoja wa viongozi wa msikiti a l i s i m a m a , m p a s h a habari wetu akadhani kuwa huenda utatolewa ufafanuzi juu ya khutba ile. Hata hivyo, kiongozi huyo wa msikiti akaishia kusema kuwa khutba imeeleweka, hakuna cha kuongeza, kilichobaki ni utekelezaji.

Wa t u w a l i o n d o k a hawajui, kilichoeleweka nini na kinachotakiwa kikatekelezwe ni kipi. Kwamba je, waondoke wakachinje makafiri kwa visu vikali? Huyo kafiri ni nani? Na kwa Fat’wa gani anachinjwa.

Tu l i wa h i k u a n d i k a katika gazeti hili juu ya mawaidha yaliyokuwa yanatolewa katika baadhi ya misikiti kule Mwanza yakihimza watu kuwa na silaha bila kujali zina vibali au la. Lakini pia wakihamasishwa kufanya m a m b o a m b a y o n i kinyume na Uislamu na yanayostahiki kuitwa ni jinai kwa mujibu wa sheria.

Masheikh wa Baraza KuuBakwata haya hamyasikii?

Swali letu lilikuwa moja tu, hivi jamii haisikii na haioni haya?

Hali hiyo bado inaendelea katika baadhi ya Misikiti na kama ilivyokuwa kwa wale As’hab Kital, Yan Tatsine, utaona msururu wa vijana na pikipiki wakielekea atakako kuwa kiongozi wao. Na hivi sasa umeibuka msamiati wa k we n d a S h a m b a . Haijulikani shamba ni wapi na wanakwenda kufanya nini. Anatoweka kijana, mtaani haonekani, ukiuliza u n a a m b i wa ‘ k a e n d a shamba’.

Lakini Mwanza huko huko, ndiko ambapo baadhi ya viongozi wa makansa walisambaza propaganda kuwa kuna Waislamu waliwapelekea ujumbe wa tangazo la kifo wakiwa kanisani, ila hawakuripoti polisi. Tumeshaandika pia mara kadhaa juu ya propaganda, chuki na fitna inayopandikizwa kuwa kuna kikosi cha watu waliodhamiria kuchoma m a k a n i s a n a k u u wa Maaskofu na Mapadiri. Si tabu sana kuona nini matokeo ya propaganda na fitna hii ikisindikizwa na hutba za kuchinja makafiri.

P r o f e s a D a u d a a n a z u n g u m z i a wa t u waliojifanya kusil imu kule Nigeria, wakatoweka kitambo kidogo waliporudi wa n a o n g e a K i a r a b u , wakawa makamanda wa Jihad na kuwatangazia ukafiri na unafiki Waislamu wasio wafuata. Akapata kundi katika vijana na hata watu wazima. Hao ndio binadamu. Hata Firauni aliyejiita Mungu, alipata wafuasi pia.

Mohammed Mar’wa “Mai Tatsine”, alianza

kwa kuharamisha elimu a k i wa a m b i a wa f u a s i w a k e w a t o e w a t o t o skuli. Wasinunue redio, saa wala t e l ev i sh en i na magari kwa sababu zimetokana na elimu ya kikafiri. Ila wanunue AK-47 na kuhifadhi za kutosha majumbani mwao.

M u h i m u h a p a tusiangalie ujinga wa wafuasi wenyewe kwamba walitakiwa waone kuwa kama elimu iliyotengeneza redio ni ya kikafiri, basi hata iliyotengeneza AK-47, kanzu, kilemba na mtandao wa simu kundesha biashara ya Tigo-Pesa na kununua Luk ya umeme, au CD ya kurekodi mawaidha ya ‘Abu Ismail’, itakuwa ya kikafiri pia. Tukienda kwa mwendo wa kutizama hoja ya ujinga wa wafuasi, t u t a k w e n d a k o m b o . Wekithekija na kirundu kikubaja idhitho, wanasema Wapare, ikiwa na maana kuwa ukicheza na mjinga anakupasua jicho.

Hoja hapa tutizame mfanano wa mahubiri haya na yale ya Mohammed Marwa (Boko Haram1) na balaa aliloleta. Hadi kutulia kabisa kwamba hasikiki tena mtu wa Yan Tatsine, baada ya Musa Ali Suleiman aka Musa M a k a n i k i a l i ye k u wa kiongozi wao wa mwisho kukimbil ia Cameroon mwaka 1985, watu zaidi ya 9000 walikuwa wameuliwa, Waislamu kwa Wakristo na hata polisi na wanajeshi.

Hivi sasa wanasikika ‘As’hab Kital’ wanaibuka Songea/Lindi. Wengine wa n a t a n g a z a n a m n a n z u r i y a k u c h i n j a makafiri. Mwanza wao ‘wanakwenda shamba’. Jamii kimya!!! Masheikh kimyaa!!

Yal iyotokea ya Yan Ta t s i n e , N i g e r i a n a Mohammed Marwa mpaka kuuliwa zaidi ya watu 9000, wala tusione ni mambo ya paukwa pakawa. Yapo katika maandishi, vitabu na vyaraka mbalimbali kwa anayetaka kujua ukweli.

Sasa tunadhani kwa dalili zinazojitokeza nchini, kuna haja kwa Masheikh wetu kuitisha kama tutaita semina ya pamoja au mkutano wa Masheikh kujadili mambo haya na kutoa fat’wa na mwongozo kwa Waislamu. Jambo lisemewe katika misikiti na sehemu mbalimbali. Elimu

sahihi iwafikie Waislamu, hasa vijana mitaani, shuleni na vyuoni ambao ni rahisi kukumbwa.

K a n o w a l i m p u u z a M o h a m m e d M a r w a , kustuka ana jeshi kubwa la vijana waliojaza visu, mikuki , marungu na b u n d u k i m a j u m b a n i mwao. Kilipotumwa kikosi cha polisi kikiwa askari 150 katika magari makubwa 13 Desemba 18, 1980 kuwazuia wafuasi wa Mohammed Marwa kufanya mhadhara, kufumba na kufumbua p o l i s i w a l i j i k u t a wakizidiwa nguvu kwa kuvamiwa na wafuasi hao wapatao 3000 wakiwa na silaha za kila aina. Polisi waliosalimika kuuliwa wal ik imbia wakiacha magari yao 13 yakichomwa moto. Hadi jeshi linakuja, mamia ya Masheikh na Waislamu ambao Yan Tats ine , wal iwaita ni wanafiki na makafiri , walikuwa washauliwa. Makanisa, misikiti, shule, vyuo, vituo vya polisi na ofisi za serikali zilichomwa moto.

K u t o k a n a n a h a l i i l i v y o k u w a , j e s h i walipokuja nao wakawa wanauwa watu ovyo kutokana na mchafu koge uliokuwepo. Ikieleza hali hiyo, ripoti moja inasema:

“It was a desperate time and extremely desperate measures were taken by the Nigerian government, making some costly mistakes in the process, especially with the extrajudicial killings.”

Baadhi ya wachambuzi wa tukio hilo wanasema kuwa kilichosababisha hali kuwa mbaya zaidi ni kwa sababu vi jana wa Mohammed Marwa walifundwa kusema lolote na kuambiwa kuwa wana uwezo wa kufanya lolote (kuuwa makafiri, polisi, wa n a o p e l e k a wa t o t o shule), na wasijali chochote katika kufanya hivyo kwa sababu hiyo ndiyo Jihad ya Kitali.

S a s a k u w a wameshibishwa maneno hayo kwa muda mrefu n a k i o n g o z i w a o wanayemuitakidi kuwa ni mtakatifu na aliyesahihi kuliko Masheih wengine wa Nigeria wakitizamwa kama wanafiki au makafiri sawa na makafiri wengine, i l i wa j e n g e a mo r i wa kutokujali.

Masheikh wanatuambia

kuwa uongozi ni jambo linalosisitizwa katika dini. Kwamba hata mkiwa safarini watu watatu, basi mumchague mmoja wenu awe kiongozi. Labda tuulize, nini maana ya kuwa na kiongozi?

H i v i s a s a u t a k u t a misikiti mingi ama itakuwa chini ya Bakwata, Baraza Kuu, Ansaar Sunna na taasisi kama hizo ambazo zimesajiliwa kisheria. Nini maana ya msikiti kuwa chini ya Bakwata au Baraza Kuu kama Sheikh wa Mkoa, Wilaya au Taifa, hana habari kinazungumzwa nini katika misikiti na kama kinachozungumzwa ni sawa au si sawa. Au tuseme wana habari na hizi hotuba za Ijumaa za kuchinja makafiri na wao ndio wameziidhinisha?

K w a j i n s i m a m b o yalivyovurugika katika dunia ya leo, tunadhani k u n a h a j a k u wa n a ‘ E W U R A ’ z a m a m b o ya dini, vinginevyo kila mmoja akiwa ni Sheikh na Mufti wa kila jambo, balaa kubwa linakuja. Kama ni Sheikh wa Wilaya/Mkoa (Bakwata), au Katibu na Amir wa Baraza Kuu, awajibike na udhibiti wa mambo katika eneo lake.

Yupo bwana mmoja aliwahi kisema kwamba kwa jinsi ufisadi na mambo yalivyovurugika katika nchi hii , panahitaj ika utawala wa kijeshi kuwatia watu adabu ndio turudi katika demokrasia watu wakishanyooka. Akatoa mfano wa Rwanda kasi inayopigwa ya maendeleo japo watu wanalalamika udikiteta.

Ukiacha hoja kwamba hata utawala wa kijeshi unaweza kuwa wa kifisadi, tena ukawa mbaya zaidi, lakini suala hapa ni kuwa mambo hayawezi kauchwa yakaenda holela. Lazima kuwe na udhibiti, na ndio maana Uislamu ukahimiza kuwa na uongozi. Pakiwa na uongozi madhubuti wenye sifa za Kiongozi wa Kiislamu, hapana shaka hata wakiibuka akina Abu Marwa na upotofu wao, watagundulika mapema na kuchukuliwa hatua.

Lakini kwa kukosekana hilo, sasa watu Mwanza ‘wanakwenda shamba’, tunatizama. Qur’an ina msemo wake, “Subirini!” mpaka yawafike ya Yan Tatsine.

Inahitajika ‘EWURA’ ya mambo ya DiniLa sivyo Qur’an ina msemo wake, “Subirini!”

Page 3: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

3 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Habari

KAZI nzuri inayofanywa na Msikiti wa Mtambani, imeelezwa kuwa ndio sababu ya mafanikio ya kitaaluma katika shule ya Kiislamu ya Mivumoni.

Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Taaluma Manispaa ya Kinondoni, B w . A h m a d S a i d , a k i m w a k i l i s h i w a Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.

Afisa taaluma huyo alikuwa akiongea katika hafla ya kuwapongeza wahitimu wa kidato cha nne 2014 wa Shule hiyo ya Kiislamu Mivumoni.

A l i s e m a s h u l e y a Kiislamu ya Mivumoni n i mfano wa kuigwa kitaaluma na kwamba suala la maadili linalopewa kipaumbele shuleni hapo, ndio siri ya mafanikio.

Wakati huo huo Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), Sheikh Mussa Kundecha, amesema mafanikio hayo yasingepatikana kama kusigekuwa na mabadiliko ya uongozi ambayo hapo awali yalitafisiriwa kama uvamizi wa misikiti.

A l i y a s e m a h a y o alipokuwa akizungumza katika mahafali hayo ya kuwapongeza wahitimu wa kidato cha nne (2014) wa shule hiyo, yaliyofanyika Jumapili ya wiki iliyopita katika Hoteli ya Lamada.

“ K a z i t u n a z o f a n ya katika Misikiti kama hii (Mtambani) na tafsiri t u n a z o p e w a k a t i k a harakati zetu, kiwango bora cha matokeo kama haya ya mitihani ya Taifa ni kielelezo kizuri cha ufanisi wa kazi tunazozifanya tofauti na tunavyopakwa matope katika jamii”. Alisema Amir Kundecha.

A l i s e m a s h u l e y a Kiislamu ya Mivumoni ni mfano mzuri wa kazi za vituo vya elimu Misikitini, kinyume na tafsiri na propaganda zinazoenezwa.

S h e i k h K u n d e c h a , alisema katika miaka ya 2000s aliwahi kukamatwa na Polisi, akiwa huko alishutumiwa kuwa yeye ni kiongozi wa wateka Misikiti chini ya Masjidi Mtambani.

“Niliwaambia tatizo l i l i l o p o n i k w a m b a utaratibu wa kubadilishana uongozi katika Misikiti

Mtambani Misikiti wa harakati wa kuigwaMafanikio yake ni matokeo ya uongozi bora

Na Bakari Mwakangwale h a u j a z o e l e k a k w a Waislamu na viongozi husika, hivyo inavyotokea mabadiliko hunadiwa kundi fulani la Waislamu wa n a t e k a M i s i k i t i . ” Alisema Amir Kundecha.

Alihoji kuwa dhana hiyo hiyo ya utekaji wa Misikiti, h i v i u k i k i l i n g a n i s h a Mtambani ile kabla ya mabadiliko ya uongozi na huu wa sasa hali ikoje?,

A l i s e m a m a t u n d a yanayopatikana sasa ni j i t ihada za Waislamu kujiletea maendeleo yao kuanzia Misikitini, kwa manufaa ya Waislamu na Taifa na si dhana ya kuteka Misikiti.

Amir Kundecha alisema pamoja na kuwepo dhana ya utekaji wa Misikiti na misukosuko mbalimbali, l a k i n i l e o m a t u n d a yanaonekana Mivumoni chini ya Masjid Mtambani na imekuwa miongoni mwa shule bora nchini.

Akianisha matokeo ya kidato cha nne kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa Taifa mwaka jana, Amir Kundecha ambaye pia ni muasisi wa shule hiyo alisema, katika matokeo ya mwaka jana kidato cha nne shule hiyo ilifaulisha kwa kiwango cha daraja la kwanza (Distinction) na la daraja la pili (Merits) na kufuta dhana kwamba Msikiti huo ni wa Waislamu wenye vurugu .

Amir Kundecha alisema inawezekana baadhi ya watu na viongozi wa serikali walikuwa na tafsiri mbaya na Msikiti huo kwa wakati ule, lakini akasema hakuna ushahidi mzuri kama ule utakaotolewa na adui yako.

Akifafanua kauli yake h i y o , a l i s e m a i k i wa mwakilishi wa serikali aliyefika katika shughuli h i y o a m e k i r i k u w a Serikali inafurahishwa na kuridhishwa na kazi za kituo cha Mivumoni, hadhani kama kuna mtu ataibuka na kudai kuwa wao (Masjidi Mtambani) ni watu wa fujo.

Alisema ubora mwingine wa shule hiyo umeanishwa na Mkuu wa Shule hiyo kwamba, vijana wa shule hiyo hushiriki katika shughuli za kielimu kitaifa na kudhihirisha ni kwa namna gani walivyo bora kitaaluma na kinidhamu

pia.Alisema, huo ni mfano

mzuri wa kazi ya vituo vya elimu vilivyopo katika Misikiti yao na kwamba, lengo lao ni kuzalisha wasomi wenye nidhamu w a t a k a o w e z a k u w a waadilifu katika ngazi mbalimbali za kitaaluma.

A m i r K u n d e c h a alisema jamii imekuwa ikishuhudia katika vikao vya Bunge, ambapo kila mara Taifa hubainika kuingia mikataba mibovu na kushuhudiwa wizi wa fedha za umma unaopewa misamiati mbalimbali kama vile ‘EPA’ ‘ESCROW’ na mengineyo, na kwamba yote hayo yanafanywa na

wasomi waliokosa uadilifu.“Kuwa mtaalamu mzuri

wa hesabu kunaweza kukufanya uwe mwizi na kujua hesabu kunaweza k u k u f a n y a u k a w a mtaalamu na mvumbuzi mzuri wa mtatatizo ya wanajamii.”

“ H i l i n d i l o t a t i z o linaloikabili nchi yetu kwani Taifa, tuna ma-profesa wengi, lakini wengi wao ndio wanaoongoza katika ufisadi badala ya kuongoza katika ufanisi sambamba na uadilifu.”

Hata hivyo, aliitaka serikali kuwa makini na taarifa inazopenyezewa, kuwa kuna Waislamu

wanateka Misiki t i au wavuruga amani. Badala yake itumie busara katika kuzifanyia kazi taarifa hizo kwani kinachoitwa utekaji wa Misikiti ni mabadiliko ya uongozi kuelekea katika ufanisi, unaoendana na hali ya wakati uliopo sasa.

“ Tu l i a n z a j i t i h a d a za kuboresha Msikiti , ulipokamilika tukaanzisha jitihada za kufungua shule ya awali, kisha shule ya msingi na iliposimama sawasawa, tukaanzisha shule ya sekondari na leo matokeo na mwenendo wake ni kama inavyo j i e l e z a ” . A l i s e m a Kundecha.

Mkuu wa Shule ya Kiislamu ya Mivumoni, Dadi Abdalah Hemed (kulia) wakati akikabidhiwa Zawadi na mgeni Rasmi Sheikh Abdulqadri.

AMIR wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), Sheikh Mussa Kundecha, akiongea katika hafla ya kuwapongeza wahitimu wa kidato cha nne 2014 wa Shule hiyo ya Kiislamu Mivumoni.

Page 4: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

4 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala/Tangazo

HATIMAYE Taasisi ya kijamii ya Uingereza na Tanzania (British – Tanzania Society, U K ) w a m e f a n y a semina kubwa siku ya Jumamosi wiki iliyopita katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha London, SOAS, hapa Uingereza. Semina hiyo ambayo i m e l e t a m s i s i m k o mkubwa kwa wajumbe na watu wengine mbali mbali waliouhudhuria, imejumuisha wasemaje wakuu wanne, ambao wa l i j a d i l i m a m b o tafauti yahusianayo na katiba.

Semina hiyo ambayo mwenyekiti alikuwa Bwana Andrew Coulson, ilimwaalika msemaji F r e d r i c k L o n g i n o ambaye alizungumza kwa upana matarajio ya wananchi hasa kwa upande wa bara juu ya katiba mpya. Msemaji wa pili alikuwa Profesa Abdul Paliwala ambaye alizungumza suala la katiba kwa mtazamo wa kisheria nchini Tanzania

Y u s s u f H a m a d , mhadhiri Chuo Kikuu cha London, SOAS alizungumza kuhusu nafasi ya Zanzibar na matarajio yake katika katiba pendekezwa. Mwisho alizungumza mwanablogu maarufu a m b a y e a l i k u w a m w a n a m k e p e k e e katika mjadala huu Mwanadada, Aikande K w a y u a m b a y e alizungumza kuhusu nafasi ya wanawake k a t i k a k a t i b a inayopendekezwa.

Pamoja na kutolewa kwa ho ja nzur i na wachangiaji wawili wa mwanzo, yaani, Bwana Abdul Paliwala na Dr. Longino, mjadala ambao uliamsha maswali mengi na mbishano mkubwa ni ule uliotokana na mchango na maoni yake aliyotoa kuhusu nafasi ya Zanzibar katika Katiba pendekezwa ambapo baada ya kumal iza kuwasilisha tu, alijikuta akivurumishwa maswali kutoka kwa wachangiaji.

M m o j a k a t i y a w a c h a n g i a j i w a l i o m s a k a m a n a

Yaliyojiri katika seminar kuhusu katiba ya Tanzania (UK)

kupingana vikali na maoni yake ni mwandishi wa BBC Swahili Bibi Zuhura Younis, ambaye alianza kwa kumpongeza Bwana Hamad kwa kuweza kuwasilisha hoja za muungano na katiba kutoka Zanzibar bila kuonesha kuegemea itikadi ya chama chochote cha siasa. Mara baada ya hapo Bi Zuhura alianza kwa mjadala wenye msis imko ul iotosha kuitwa mechi!

M AT C H O F T H E DAY: Yussuf Hamad Vs Zuhura Younis

Hoja: Alichokisema H a m a d n i k u w a Z a n z i b a r k i u j u m l a ilihitaji Muungano wa mkataba. Akaongezea kwa kusema kwamba Wazanzibari walihitaji katiba ambayo itaondoa k e r o z a m u u n g a n o a m b a z o z i m e k u wa zikileta sintofahamu kwa muda wa miaka zaidi ya 40.

A k a s e m a , k u w a Wazanzibari wanahitaji m u u n g a n o w e n y e kufuata mis ingi ya usawa, sio usawa wa uwiano lakini usawa wa maridhiano ya kila maamuzi yanayofanywa katika Muungano. Alitoa mifano ya kero mbali mbali za Muungano kama vile mgao wa Zanzibar wa mapato k a t i k a m u u n g a n o , mapato, bandari, petrol na mambo mengine ambayo kwa kuongezwa k w a k e y a m e k u w a

sababu ya mgogoro kati ya washirika wa Muungano.

B w a n a H a m a d a l i h i t i m i s h a k w a kusema, Wazanzibari hawaukatai Muungano ila wanahitaji Muungano wenye misingi ya usawa na kuheshimiana. Na kwa maana hiyo katiba nzuri yenye maslahi kwa Zanzibar ni i le itakayotokana na misingi ya usawa (Fairness) baina ya washirika wa Muungano. Pia alisisitiza kuwa, ili kuondoa kero nyingi na migogoro ya kikatiba isiyokwisha, ni vyema kwa Tanzania kuzingatia katiba yenye kuzingatia matakwa ya wananchi walio wengi na sio inayosimamia misingi ya kivyama, dini wala kikabila.

Idadi ya wachangiaji kutoka Zanzibar kwa bahati mbaya ilikuwa haizidi watu wanne katika ukumbi. Kwa maana hiyo, michango mingi ilitokana na watu kutoka Tanzania bara ambao walionekana kukubaliana na mengi y a l i y o z u n g u m z w a na wasemaje wote . Pia walitoa michango endelevu sana hata kuhusu hoja za nafasi y a M u u n g a n o n a Katiba kwa upande wa Zannzibar.

Hata hivyo, Bi Zuhura Y o u n u s , a m b a y e n i m m o j a k a t i y a Wazanzibari wachache w a l i o h u d h u r i a ,

alipingana na karibu h o j a z o t e . K wa n z a alianza kwa kusema kuwa Wazanz ibar i , h a s a w a u p a n d e wa pil i , wamekuwa w a k i l a l a m i k i a m u u n g a n o k i l a siku, kama kwamba Muungano huo hauna jema lolote kwa Zanzibar.

P a m o j a n a h i l o akaongezea kuwa kero ziko lakini ni ndogo ndogo sana na akasisitiza kuwa mgao wa asilimia 4 . 5 % wa n a o p a t i wa Zanzibar ni sahihi kwa sababu Zanzibar ni nchi ndogo sana kiidadi ya watu ukilinganisha na idadi ya watu walioko bara. Kwa hiyo hakuna ha ja ya kula lamika lamika.

Bi Zuhura aliisuta kauli ya Bwana Hamad kuhusu mafuta akisema, Zanzibar hakuna mafuta kamwe na kwa maana hiyo hakuna haja ya kujenga mlima kwa kichuguu cha sisimizi kwa kitu ambacho hakipo kabisa. Akihitimisha maoni na michango yake, Bi Zuhura alidai kuwa katiba iliyopo inaifaa sana Zanzibar na inalekea kwamba malalamiko makubwa ya katiba yanatokana na kelele za wapinzani ambao ni sehemu tu ya wananchi wa Zanzibar ambao nusu ni CCM na nusu ni CUF kiujumla.

Al ipopewa nafas i y a m a j u m u i s h o n a k u f a f a n u a h o j a a l izozisema na zi le zilizochangiwa, Hamad, alianza kwa kusema

kuwa kumekuwa na d h a n a i l i y o j e n g wa k w a m a k u s u d i i l i k u w a d u n i s h a watu fulani kutoka upande fu lani kwa kuwahukumu kisiasa isivyo haki na kukana hoja zao kwa misingi hiyo. Alitoa mfano kwa kusema, katika mijadala kama hii , wasemaje wengi wanapos ik ia a n a y e z u n g u m z a n i M z a n z i b a r i a u Mpemba, basi huyo h u i t wa ‘ M p i n z a n i ’ wa muungano hata ikiwa mtu huyo hana mfungamano na chama chochote.

Alifafanua pia kwa k u s e m a k w a m b a baadhi ya wanasemina walimfahamu vibaya alipozungumza neno ‘ F a i r ’ w a k i d h a n i alimaanisha ‘equality’. Kwa ufupi alichokusudia kusema ni kuwa kuwe na msingi ya haki na usawa katika kufanya maamuzi ya mambo ya muungano. Moja kati ya mambo hayo ni kuwashirikisha wananchi wa pande zote mbili kwa msingi ya ukweli na uwazi. A l i h i t i m i s h a k w a k u s e m a k w a m b a Katiba yenye kujali na kusikiliza maoni huru ya wananchi walio wengi, ndio suluhisho moja la migogoro inayoweza kuunusuru Muungano wa Tanzania.

( M a k a l a k u t o k a Mtandao wa Kijamii, Mzalendo)

Page 5: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

5 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Habari za Kimataifa/Tangazo

MEYA wa Jiji la New York nchini Marekani , Bi l l De Blasio, ametangaza kuwa shule zote za umma katika mji huo zitakuwa zikifungwa kila mwaka wakati wa Sikukuu mbili muhimu za Kiislamu za Eidul-Fitr na Eidul-Adh’ha.

Meya De Blasio amesema uongozi wa jiji la New York limeona kuwa kuna haja ya kuweko usawa katika kutambua na kuheshimu shughuli muhimu za watu wa dini mbalimbali mjini humo na kwamba hatua hiyo inalenga kuonyesha heshima kwa Sikukuu hizo mbili za Waislamu.

New York ina wanafunzi wasiopungua milioni 1.1 katika shule za umma. Majimbo kadhaa ya Marekani yakiwemo ya Massachusetts, Michigan and New Jersey katika miaka ya hivi karibuni yameorodhesha sherehe za Eidul-Fitr na Idul-Adh’ha kwenye kalenda ya matukio kwenye shule zao.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa hatua hiyo ni aina f u l a n i ya m k a k a t i wa kuwapumbaza Waislamu wa Marekani, ambao hivi sasa wanakabiliwa na mashinikizo kutoka kwa vyombo vya usalama na vya kijasusi vya nchi hiyo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. (irib).

M A A N D A M A N O makubwa yamefanyika katika miji mbalimbali ya Marekani kupinga m a u a j i m e n g i n e yaliyofanywa na polisi dhidi ya Mmarekani mweusi katika mji wa Madison.

Polisi mzungu Matt Kenny, mwenye umri wa miaka 45 siku ya Ijumaa iliyopita alimpiga risasi n a k u m u u a k i j a n a Mmarekani mweusi, Tony Robinson, mwenye umri wa miaka 19 huku akiwa hana silaha.

Waandamanaji hao wal ida i kuwa v isa vya polisi wazungu kuwaua Wamarekani weusi nchini humo bila hatia, vimeongezeka sana na sasa wanaitaka serikali ichukue hatua kukomesha ubaguzi u n a o z i d i k u k i t a mizizi katika jeshi la polisi na taasisi nyingi za kiserikali nchini Marekani.

Mauaji ya Robinson ni muendelezo wa visa vya mauaji ya Wamarekani weusi mikononi mwa polisi weupe, ambavyo vimeongezeka sana katika miezi ya hivi karibuni.

Siku ya Jumamosi, Rais Barack Obama, alisema kuwa historia chafu ya ubaguzi wa rangi na kaumu bado inaendelea Marekani l i cha ya nchi h iyo kujipiga kifua kuwa ni taifa lenye usawa na uadilifu miongoni mwa raia wake.

Itakumbukwa kuwa mwaka jana yalitokea maandamano mfululizo katika miji mbalimbali n c h i n i M a r e k a n i kufuatia vitendo vya m a a f i s a wa P o l i s i kuua raia weusi huku vyombo vya dola na vile vya sharia vikiwaachia huru maofisa hao.

Baadhi ya matukio hayo ya mauaji ya raia weusi ni kama lile la kijana Michael Brown, aliyepigwa risasi kadhaa alipokuwa akining'inia

MZIMU WA KUUA RAIA MAREKANI

Polisi waua tena Mmarekani mweusi na kuibua maandamano kwenye gari ya polisi.

K u f u a t i a t u k i o hi lo , FBI wal isema wanachunguza endapo kuna uvunjifu wa haki

za binadamu katika tukio hilo la kuuawa kwa ki jana Michael Brown.

Haukupita muda,

k i j a n a m w i n g i n e mweusi naye alipigwa risasi na polisi na kufa katika kituo cha mafuta, ikiwa ni maili chache tu

k u t o k a e n e o

alilopigwa risasi na polisi na kufa Michael Brown huko Ferguson, Missouri, Marekani.

K i j a n a h u y o a l i t a m b u l i w a n a m a m a ya k e m z a z i kuwa anaitwa Antonio Mart in 18 , ambaye aliuawa kwenye kituo cha mafuta cha Mobil, kaskazini mwa barabara ya Hanley majira ya saa saba usiku.

Kufuatia matukio hayo, polisi walijikuta wakipambana na watu wenye hasira ambapo katika vurugu hizo watu kadhaa walitiwa nguvuni.

Uhasama baina ya maofisa wa polisi na watu weusi umeonekana kuota mizizi ambapo baadae polisi mmoja naye aliuliwa nchini humo. (VOA).

Shule za New York kufungwa Sikukuu za Eid

MAAFISA usalama wa Marekani wakitoa heshima ya mwisho kwa mwili wa askari mwenzao aliyekuawa kwa risasi na mtuasiyejulikana.

W A N A W A K E w a Kiyahudi huko Israel wamefanya maandamano wakitaka kuhitimishwa dhuluma za Wazayuni dhidi ya wanawake wenzao wa Kipalestina.

Katika maandamano hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wanawake katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan na mji wa Quds, washiriki waliutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kuheshimu haki za wanawake wa Kipalestina.

M a a n d a m a n o h a y o y a l i h u d h u r i w a n a wanachama wa Harakati ya Wanawake ya Kidemokrasia huko Israel, kwa kushirikiana na Umoja wa Kijamii wa Wanawake wa Kipalestina.

Aidha wanawake hao wal iokuwa wameweka kambi kwenye ukuta wa Qalandiya, unaotenganisha maeneo ya Wapalestina na yale ya Wazayuni wa Israel, wamesema ukuta huo unachangia kukandamizwa wanawake wa Kipalestina.

Jumia ya Wanawake W a n a h a r a k a t i w a Kidemokrasia, iliasisiwa mwaka 1948 katika maeneo ya a r d h i ya Pa l e s t i n a inayokaliwa kwa mabavu.

Wanawake Israel waandamana kupinga dhulma kwa wanawake wa PalestinaUtawala wa Kizayuni

umekuwa ukidai kuwa ukuta huo ulijengwa kwa lengo la kuweka usalama, hata hivyo viongozi wa

Palestina wanaamini kuwa ukuta huo ulijengwa kwa lengo la kupora zaidi ardhi za Wapalestina. (irib).

WAZIRI Mkuu wa Israel, Binyamin Netanyahu.

Page 6: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

6 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala

WAKATI Rais Nicolae Ceauşescu wa Romania alipokuwa anakaribia kilele cha anguko lake, alimuita waziri wake wa ulinzi, Vasile Milea, kumtaka ampe tathmini ya kweli bila kumficha chochote juu ya nguvu halisi za jeshi kuhimili u p i n z a n i a m b a o ulikuwa umeshavuka mpaka wa kudhibitika. Swali hasa alilomuuliza ni ikiwa kwa hali ilivyo, inaweza kulichukua jeshi siku ngapi za ziada kumlinda?

Lakini Milea, ambaye s i k u c h a c h e b a a d a ya mkutano huo na Ceauşescu alikutikana ofisini mwake “amejiua” kwa kuj ipiga r isasi karibu na moyo, hakuwa mkweli kwa Ceauşescu, kama ambavyo hutokea m a r a k a d h a a k wa wasaidizi wa watawala m a k a t i l i . A k a m p a takwimu za uongo juu ya nguvu, silaha na idadi ya wanajeshi anaoamini walikuwa wamebakia upande wa mtawala anayeanguka.

Ceauşescu alimteua Vi c t o r S t ă n c u l e s c u kuchukuwa nafasi ya Milea, lakini Stănculescu alikubali nafasi hiyo kwa shingo upande, na matokeo yake akafanya kila kilicho kinyume na bosi wake na hivyo akachochea anguko la Ceauşescu badala ya kumsaidia kuendelea kusalia madarakani.

K w a m f a n o , a l i w a a m u r u wa n a j e s h i k u r e j e a m a k a m b i n i b a d a l a ya k u wa s h a m b u l i a w a a n d a m a n a j i a m b a o w a l i k u w a w a k i y a s h a m b u l i a makao makuu ya Chama c h a K i m o m u n i s t i , badala yake akamshauri Ceauşescu na mkewe Elena kukimbia kwa hel ikopta na hivyo kumgeuza “kiongozi a n a y e w a k i m b i a watu wake” badala y a k u s i m a m a akawaongoza. Baadaye, mwenyewe Stănculescu alikuja kukiri kwamba wakati huo ni kama

Mtawala anayeanguka huhisabu vifaru na mizingaNa Mohammed Ghassani k w a m b a a l i k u w a

anapokea amri mbili kwa wakat i mmoja – moja kutoka kwa Ceauşescu aliyekuwa akipigania utawala wake na nyengine kutoka kwa umma uliokuwa u m e c h o k a n a n a ye . Akachagua kufuata amri ya umma.

Kuelekea uchaguzi m k u u w a 2 0 1 5 visiwani Zanzibar ni kama kwamba tayari mstari umeshachorwa n a w a t a w a l a n a wameshaamua wapi lipo chaguo lao, kwa upande mmoja, na wananchi nao wameshaamua lao, kwa upande mwengine. Mstari huo unaochorwa kati ya pande mbili zinazoongoza serikali moja ya Umoja wa Kitaifa visiwani Zanzibar una maana kubwa sana kwa mwenendo wa mambo ndani ya Tanzania nzima kwa ujumla. Chama cha Mapinduzi ( C C M ) , a m b a c h o ndicho mshirika mkuu kwenye Serikal i ya Umoja wa Kitaifa – na hivyo chenye nguvu ya kikatiba kuongoza nchi kwa sera na programu y a k e – k i m e a m u a kung’ang’ania bunduki, v i faru na mizinga . Kila siku iendayo kwa Mungu kinasema wazi k u wa k i n a t e g e m e a njia moja tu kusalia kuongoza nchi – nguvu za vyombo vya dola na mawakala wao.

K i n a s e m a h i v y o kupitia ngazi zake zote za uongozi – wa chini, kati na hata wa juu. Msikilize Asha Bakari Mtama, kwa mfano, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM ngazi ya taifa, akirejelea kauli ile ile ya kila siku kuwa serikali ya Zanzibar haitapatikana kwa kupiga kura.

“Nasema na nitarudia t e n a n a s i o g o p i kusema, serikali hii ni ya kimapinduzi sio ya mchezo. Hawawezi, hawawezi, hawawezi kutupindua.”

Anasema Asha Bakari kwenye mkutano wake wa hadhara wa mikoa

miwil i ya k is iwani Pemba mapema mwaka 2014. Kauli kama hii ameshaitoa mwahala mwingi, mukiwemo kwenye Bunge Maalum la Katiba mbele ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta.

Kauli kama hii pia hure je lewa kwenye m i k u t a n o m e n g i n e kadhaa ya CCM, hasa v i s iwani Zanzibar . M a r e h e m u S a l m i n A wa d h , a l i ye k u wa mwakilishi wa jimbo l a M a g o m e n i n a mnadhimu mkuu wa CCM, aliwahi kufika umbal i wa kusema kwamba vifaru vya jeshi vitatumika kuilinda CCM madarakani.

“Sasa wao (wapinzani) kama wana ubavu, b a s i w a c h u k u w e ( s e r i k a l i ) . L a k i n i hatutotoa (madaraka ya kuongoza serikali) kwa kura. Mutapiga kura katika chaguzi zote, na Chama cha Mapinduzi kitashinda.”

Hakuna k iongozi yeyote wa juu wa CCM, si wa Zanzibar wala wa Tanzania Bara , aliyewahi kujitokeza kuwakemea wana-CCM hawa wanaoyasema haya majukwaani, na

kwa hakika mara kadhaa huwa yanasemwa mbele yao, akiwamo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana. Hilo linasema ukweli mmoja tu – CCM kwa ujumla wake imeshaamua kuhisabu mizinga yake kujilindia madaraka yake visiwani Zanzibar.

K i n y u m e c h a k e ni pale unapofuatilia mikutano ya hadhara ya mshirika mdogo kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo, Chama cha Wananchi ( C U F ) , a m b a y o i m e j i k i t a k w e n y e kuutayarisha umma kwa kile inachokiita chama hicho “Mwaka wa Maamuzi” 2015. Humo huambiwa watu wajitokeze kwa wingi kwenye kujiandikisha kupiga kura. Kwamba wasichoke kukabiliana na vikwazo vya kupata haki yao hiyo kutoka kwa masheha, ambao s a s a c h a m a h i c h o kinasema kitawapeleka m a h a k a m a n i k w a kuwazuia Wazanzibari wenye haki kupata v i t a m b u l i s h o v y a Mzanzibari Mkaazi.

H u m o u n a s i k i a umma ukiambiwa kuwa muda wa CCM kusema h a wa t o w i s e r i k a l i

na wasi towe kwel i umepita, kwani zama za mageuzi hazizuiliki. W a n a t a y a r i s h w a kuitetea na kuilinda Zanzibar kwa kura zao na kuiamini kura kuwa ndio njia pekee ya kupata madaraka ya nchi.

Ni bahat i mbaya sana kwamba bado CCM makao makuu Chimwaga inadhani kuwa njia pekee ya kuidhibiti Zanzibar ni kupitia khofu na wasiwasi miongoni mwa raia, na kwamba hilo litakuwa na athari kwa Zanzibar pekee katika wakati ambapo upinzani dhidi ya CCM hiyo hiyo ni mkubwa zaidi pia huko Bara, huku ukisaidiwa sana na kashfa za kifisadi na ukosefu wa usalama.

L a k i n i b a h a t i mbaya zaidi ni kwa wana-CCM ndani ya Z a n z i b a r ye n ye we ambao hawajang’amua k u w a a n g u k o l a Ceauşescu wa Romania linawanyemelea na wao.

Hikima ya kujifunza inawataka wauangalie u h a l i s i a . V i f a r u vinaendeshwa na watu. Mizinga inafyatuliwa na watu. Na ni watu pia wanaodai mabadiliko.

Page 7: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

7 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala

WIMBI la hivi karibuni zaidi la kuteswa Wakristo nchi za Syria na Irak na wana siasa kali wa kundi la Islamic State (IS) umeweka jamii za asili maeneo hayo katika hatar i ya kutoweka. Watu takriban 300 wa kundi la wa-Ashuru kaskazini mashariki ya Syria walitekwa katika wiki moja iliyopita na wapiganaji wa IS. Wengi kati ya waliotekwa ni watoto, wanawake na wazee. Inahofiwa kuwa mateka hao watauawa k a m a a m b a v y o wengi wa jamii yao wameshaangamia katika mikono ya wapiganaji hao.

Makada hao wa IS pia wameanzisha kampeni ya kuteketeza kazi za kisanaa muhimu za zamani na makanisa katika maeneo ya kaskazini ya Syria n a I r a k . Wa a s h u r u , Wakaldayo na Wasiriaki, ni miongoni mwa jamii za awali kanisa za Kikristo katika Mashariki ya Kati, a m b a z o z i n a f u a t i l i a kuanzishwa kwake miaka 2000 iliyopita wakati wa Yesu. Sasa wanakimbia kwa maelfu kuponya maisha yao mbele ya hasira ya kundi la IS - mtandao wa siasa kali unaotangaza khilafa inayosimama Syria na Irak.

Itikadi kali ya Wahhabi ya IS inaona dini zote nyingine kama maadui wa Mungu, wanaotafutwa na kuuawa. Makundi tofauti ya Shia na Sunni pia yanalengwa na IS, pamoja na Wakris to . Kuainisha kuenea kwa IS na ukatili wake, kundi hilo lilitoa mkanda wa video ukionyesha kuchinjwa kwa Wakristo 21 wa dhehebu la Copt na Misri huko Libya katika mji wa Sirte mwezi uliopita. Udhalimu huo umesababisha kutafuta hifadhi nje ya nchi kwa Wakristo wa dhehebu la Misri nchini Libya. Serikali ya Marekani imetoa taarifa za kulaani vikali vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya jamii hizo za Kikristo na kundi la IS, ambalo pia linajulikana kama ISIL.

Kuongoza mapambano k u i s h i n d a I S n i mwendelezo tu wa upuuzi na majigambo ambayo Marekani ni bingwa wa kuyaonyesha. Taifa hilo ambalo linajitangaza kuwa ni la kipekee, ndiyo chanzo kikuu cha kuanzishwa kwa mtandao wa IS. Kabla

'Marekani ya Kikristo' yasimamia mwisho wa Ukristo Mashariki ya KatiNa Finian Cunningham

March 05, 2015 - 'Mtandao wa kupashana habari' - SCF

ya uvamizi wa Marekani nchini Irak mwaka 2003 hapakuwa na kitu kama makundi ya Al Qaeda katika eneo hilo la dunia. Miaka kumi baadaye, maeneo makubwa ya nchi, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa pili wa Mosul, sasa iko katika mikono ya Mujahidina hao.

Marekani na washirika wake wa Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi, Saudia na Qatar, wamekuwa mstari wa mbele kuinua makundi ya Al Qaeda katika vita ya kutumia mamluki kubadili utawala nchini Syria katika miaka minne iliyopita. Mabilioni ya fedha zinazotokana na mauzo ya mafuta zilijazwa nchini Syria kuinua itikadi ya vikundi hivyo nchini Syria, katika nyanja za elimu na jamii kwa jumla, ambako ndiko IS imeinuka na kuwa kundi lenye nguvu zaidi ya mengine yote.

Jambo hili wanakiri wa k u u h u s i k a , k wa m f a n o wa t u wa w i l i muhimu waliokiri hivyo wiki iliyopita. Kamanda wa zamani wa majeshi ya NATO na Marekani, Jenerali Wesley Clark, aliviambia vyombo vya habari nchini Marekani k u wa wa s h i r i k a wa Kiarabu wa Marekani ndiyo wanaowajibika kwa kuunda mtandao wa kigaidi wa IS.

H a l a f u L a k h d a r B r a h i m i , a l i y e k u wa mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Nchi za Kiarabu nchini Syria, akaweka kando itifaki ya kidiplomasia na kusema wazi kuwa Marekani ndiyo inahusika kwa kukua kwa IS kutokana na uvamizi wa Irak muongo mmoja uliopita. "Marekani ni ya kulaumiwa. Ilijenga mazingira yaliyowezesha ISIL kukua," al isema Brahimi katika mahojiano na gazeti la Al Hayat, moja ya magazeti makubwa ya kimataifa ya Kiarabu, lenye makao yake makuu nchini Uingereza na kuchapishwa London, Beirut, New York na Riyadh.

Kwa sababu za kimbinu za kuzuia zimwi la ki-Frankenstein au kwa ajili ya kuboresha mahusiano yake kijamii, Marekani na washirika wake wa NATO wanaweza kuwa wameanza kuidondoshea mabomu IS katika miezi ya hivi karibuni. Lakini bado hakuna uwezekano wa kukwepa uhalisi kuwa tatizo la siasa kali ya Uislamu katika Mashariki ya Kati ni matokeo ya vita ya kibeberu ya Marekani katika eneo hilo.

Wimbi la hivi karibuni la utekaji nyara na mauaji dhidi ya wa-Ashuru Wakristo inadhaniwa imechangiwa na dhana ya kulipa kisasi kwa upigaji mabomu wa Irak na Syria ukiongozwa na Marekani. Uvamiaji na ukaliaj i wa Marekani n c h i n i A f g h a n i s t a n na Irak kinyume cha sheria , upigaji mabomu nchini Pakistan, Yemen na Somalia, pamoja na kuchochea vita ya makundi ya kulipwa nchini Libya na Syria, yote yana uhusiano wa karibu na kuongezeka kwa makundi ya kigaidi ya aina ya Al Qaeda. Hivyo, inabidi iwe wazi kuwa sera ya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati ndiyo hasa chanzo cha tatizo hilo.

B a d o h a t a h i v y o R a i s B a r a c k O b a m a anaendeleza hisia ya kujidanganya kuwa yeye na washirika wake wako

katika vita dhidi ya ugaidi. Akimkaribisha mtawala wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani katika Ikulu ya Marekani wiki iliyopita, Obama alisema: "Qatar ni mshirika wa dhati katika jumuiko letu la kupunguza nguvu na baadaye kuishinda ISIL. Sote tuna dhamira ya kuhakikisha kuwa ISIL inashindwa, kuhakikisha kuwa nchini Irak kuna nafasi ya watu wote kuishi pamoja kwa amani."

Njozi tata za Obama zinasukumwa na ushiriki wa wazi wa vyombo hodhi vya habari vya nchi za Magharibi, ambavyo vinapuuzia kwa makusudi mtiririko mwendelezo wa vita ukiongozwa na Marekani kote Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kuwa ndiyo chimbuko halisi la kuenea kwa makundi ya siasa kali. Uteketezaji wa kihalifu wa Irak chini ya Rais GW

Bush na Obama - ambao uligharimu maisha ya watu zaidi ya milioni moja - kwa njia moja au nyingine kunatumbukizwa katika shimo la ki-Orwell la kupoteza kumbukumbu. La kushangaza ni kuwa Marekani inaamini kuwa i n a r u k h s a m a a l u m k u t o k a k wa M u n g u "kuongoza mataifa ya dunia." Katika mazingira rasmi inajidhania kuwa ni mtetezi na mwinuaji wa hali ya juu wa maadili ya Kikristo. Wakati Ukristo wa asili unapofutiliwa mbali kutoka ramani ya Mashariki ya Kati - ilipozaliwa dini hiyo - mwasisi halisi wa hali hiyo ni Marekani inayojiamini na kujiaminisha hivyo. (Makala hii ‘Christian US’ Overseeing End o f C h r i s t i a n i t y i n Mideast, imeandikwa na Finian Cunningham n a k u t a f s i r i wa k wa Kiswahili na Anil Kija)

WAPIGANAJI wa IS.

Page 8: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

8 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala

KUMBUKUMBU ya hivi kar ibuni ya miaka 70 ya kukombolewa kwa Auschwitz i l ikuwa ni kumbushio la uovu mkuu wa ufashis t i , ambako yaliyotendwa na wafuasi wa kundi la Nazi (Ujamaa wa kitaifa nchini Ujerumani) umebaki katika hisia za dunia. Ufashisti umetunzwa kama historia, kama mkanda unaochomoza wa magwanda meusi katika gwaride, uovu wao uliokubuhu ukiwa hauna ubishi. Hata hivyo katika jamii hizo hizo za kiliberali, ambazo watawala wake wafanya vita wanatuhimiza tusisahau kamwe, kuongezeka kwa hatari ya ufashisti wa kisasa kunakandamizwa, kwani ni ufashisti wao.

" K u a n z i s h a v i t a ya uchokozi...." walisema majaji wa jopo la Nuremberg mwaka 1946, "siyo tu ni jinai ya kimataifa, ila ndiyo jinai kuu ya kimataifa, ikitofautiana na jinai nyingine kwa hali ya kuwa inaweka ndani yake uovu wote uliolimbikizwa."

Kwanini kuzuka kwa ufashisti ni tatizo tenaNa John Pilger

Februari 27, 2015 - 'Mtandao wa kupashana

Kama wafuasi wa Nazi wa s i n g e i va m i a U l a ya , Auschwitz na mauaji ya kimbari visingetokea. Kama Marekani na washirika-teja wake wasingeanzisha vita dhidi ya Irak mwaka 2003, takriban watu milioni moja wangekuwa hai leo hii, na Dola ya Kiislamu, au ISIS, isingekuwa leo inatuweka roho juu kwa ushenz i wake. Ni uzao wa ufashisti wa kisasa, uliokuzwa na mabomu, umwagaji damu na uwongo ambao ndiyo jukwaa la kusadikika liitwalo habari.

K a m a u l i v y o k u w a ufashisti wa miaka ya 1930 na 1940. uwongo mkubwa unatolewa kwa usahihi wa mashine ya saa, hasa kutokana na uwepo wa vyombo vya habari vinavyorudiarudia kilichosemwa na uchujaji m k a l i wa h a b a r i k wa kutosema. Chukua mfano wa mkasa wa Libya.

M wa k a 2 0 1 1 , N AT O ilianzisha mirusho 9,300 ya mabomu dhidi ya Libya, ambako zaidi ya theluthi moja i l ikuwa dhidi ya makazi , asasi za kirai . Milipuko na makomhora yenye urani (inayotumika k u t e n g e n e z a m a b o m u ya atomiki) yalitumika. Miji wa Miserata na Sirte

ilisawazishwa kwa mabomu. C h a m a c h a k i m a t a i f a cha Msalaba Mwekundu kiligundua makaburi ya pamoja. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, likatoa taarifa kuwa "wengi zaidi kati ya watoto waliouawa walikuwa chini ya umri wa miaka kumi."

Kuingizwa hadharani kwa kisu cha bunduki ya askari wa 'uasi' katika mwili wa Kanali Muammar Gaddafi akiwa amekufa ulishangiliwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, kwa usemi alioutoa kwa jemadari wa Roma ya kale, Juliasi Kaisari, "tulifika, tukaona, akafa."

Kuuawa kwake, kama ilivyo kuteketezwa kwa nchi yake, kulihalalishwa na uwongo mwingine wa kawaida, kuwa alikuwa anapanga mauaji ya kutisha dhidi ya watu wake mwenyewe. "Tulijua, kama tukingoja siku moja nyingine," alisema

RAIS Hassan Rouhan wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (kushoto) akiwa na Rais Barack Obama wa Marekani.

HALI ya sintofahamu i l i tawala ndani ya Kikao cha Baraza la Wawakilishi juzi.

Hata hivyo, ikiacha k i l i c h o k u s u d i w a ambayo ni sheria ya kura ya maoni ikiwa imeridhiwa.

I l ikuwa ni kat ika kuwasilishwa hoja ya kur idhiwa kura ya maoni ambapo baadhi ya wajumbe walipinga wakisema kuwa haina masilahi na Zanzibar.

Mvutano ul ikuwa baina Spika na Mh. Jussa aliyetaka hoja hiyo isiridhiwe kwa sababu tayari Katiba ya Zanzibar imeshaitangulia Sheria hiyo na imeshaweka masharti ya kura ya maoni Zanzibar.

Jussa akitilia nguvu hoja yake akasema kuwa Baraza limeshawahi kukataa mambo ya aina hio kwa mambo yasiyo na maslahi na Zanzibar.

Amesema sheria ya kura ya maoni na sheria ya mabadiliko ya katiba ni vitu viwili tofauti.

Inahitaji kujadiliwa

Mtafatuku ndani ya BarazaRungu la Spika Kificho lafanya kazi

Na Mwandishi Wetu

na kwa Zanzibar Katiba y a k e i m e s h a w e k a masharti.

Kufikia hapo akauliza

kwa nini suali hilo linataka kulazimishwa wakati huko nyuma Baraza liliwahi kukataa

mambo ya aina hiyo.Kama mambo mengine

yaliwahi kujadiliwa na yakakataliwa na Baraza

la Wawakilishi baada ya kuonekana kuwa hayana masilahi na Zanzibar, vipi la kura ya maoni linazuiwa kujadiliwa?

I l i k u w a n i h o j a i l i y o k o s a m a j i b u kutoka kwa Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

K u k o s e k a n a k wa m a j i b u m u a f a k a , kulifanya kiti kushikilia hoja ya kuuliza kuwa jambo hilo limeungwa mkono.

Na kwa utaratibu ni Mwanasheria Mkuu kutoa hoja ya kuridhia.

Hata hivyo, ilikuwa ni ndani ya makelele n a s i n t o f a h a m u mara ikasemwa hoja imeungwa mkono.

W a k a t i k e l e l e zikiendelea, Mawaziri na Manaibu Waziri wanaotokana na CUF wa k i wa wa m e t o k a kuashiria kutounga mkono.

Kuona ha l i h iyo , Waziri wa Sheria Bwana A b u b a k a r K h a m i s B a k a r y a l i s i m a m a kuomba kutoa maelezo, hata hivyo hakupata nafasi. Naye akaamua kutoka.

Inaendelea Uk. 12

MHESHIMIWA Jussa (kushoto) akiwa na Bimani.

Page 9: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

9 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala/Tangazo

Ubungo Islamic High School imeandaa mafunzo maalum kwa wanafunzi wa Kiislamu wanaorudia Mitihani ya Kidato cha Nne 2015 ambao wanatafuta sifa ‘Credit’ za kujiunga na Kidato cha Tano, 2016.

Masomo yanayofundishwa ni: Elimu ya Dini ya Kiislamu, Arabic, Kiswahili, Kiingereza, Civics, History, Geography, Basic Mathematics, Physics, Chemistry, Biology, Commerce na Book-Keeping.

Muda wa masomo: Jumatatu – Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri.Kuanzia Machi 1, 2015 hadi Septemba 30, 2015. (Kwa muda wa miezi SABA)

Uandikishaji umeanza Fika ofisi ya Mkuu wa Shule Ubungo Islamic High School kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 8:30 mchana. Fomu zinapatikana BURE.

Kwa mawasiliano zaidi: 0687 820895, 0657 350172, 0714 888557

Wahi Mapema nafasi hii adhimu

Wabillah Tawfiiq

MKUU WA SHULE

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

Ubungo Islamic High SchoolMafunzo maalum ya wanaorudia Mitihani

ya Kidato cha Nne 2015

UVIVU na tamaa ya kupata mafanikio bila jasho, kwa kiasi kikubwa kumejenga hulka kwa watu kutaka kupata utajiri wa haraka. Tamaa hiyo ya utajiri wa haraka, imewachochea watu kutafuta njia mbadala na rahisi ikiwa ni sehemu ya jitihada za kufikia mafanikio ya mapema wanayoyataka. Wengine wamekuwa wakifanya mauaji na kunyang’anya w e n z a o m a l i z a o , wengine wametumia njia za utapeli na wapo ambao wamediriki kuua mwenye nacho na kukichukua kile alichokitaka na kukifanya chake. Hata hivyo, wengi wamekuwa wakitumia njia za kishirikina kufikia malengo yao ya kutajirika haraka au kupata vyeo au uongozi, wengine wakiwa ni matajiri lakini kwa sababu ya tamaa na kutotosheka, wanajikuta wakiingia kwenye shirki wakitaka watajirike zaidi.

Pia ipo dhana kwamba w a t u m a r a n y i n g i h u l a z i m i k a k u i n g i a katika shirki kwasababu ya matatizo ya maradhi au taabu tu za maisha na masuala ya mapenzi. Lakini jinsi hali ilivyo kwa Watanzania wengi, vibanda vya waganga wa kienyeji hushehenezwa na wasaka utaj ir i na mafanikio. Kudhihirisha kukolea ushirikina maeneo mengi hususan katika maeneo ya miji, ni vigumu kutembea mwendo mrefu bila kukutana na kibao kinamtangaza mganga wa kienyeji. Baadhi ya waganga wa kienyeji nchini wamegeuza matatizo ya Watanzania kuwa mitaji yao ya kujipatia mamilioni ya fedha kwa madai kwamba wanawapatia tiba ya matatizo yao. Lakini kwa wakati huo huo wanaokwenda huko, nao wanaamini kuwa waganga hao watawaletea m a f a n i k i o m a k u b wa kimaisha, kama kupata utajiri kwa njia ya mkato na wengine wakitumaini kuongeza utajiri walio nao.

Moja ya uthibitisho wa kwamba huduma hiyo haramu huwapatia fedha

Watanzania wanahitaji kukombolewaWaache uvivu wa kufikiri, tamaa ya mali bila jasho

Na Shaban Rajab nyingi waganga hao ni kuenea kwa mabango mengi yanayotangaza kuwepo kwa waganga hao. Katika maeneo mengi ya miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya nk. huwezi kutembea mwendo mrefu bila kukutana na kibao kinamtangaza mganga wa kienyeji kutoka ndani au nje ya nchi.

Wapo wanaojitangaza kutibu watu walio na matatizo ya nguvu za kiume, wanaotaka kupata watoto, kukoleza penzi, kuvunja penzi, utajiri wa haraka, kutibu wanafunzi wa s i o k u wa n a a k i l i darasani, kuolewa au kuoa haraka, kumvuta mpenzi aliye mbali, kunenepesha makalio na kurefusha maumbile ya sehemu za siri kwa wanaume na mengineyo. Aidha wingi wa matangazo hayo unaash i r ia p ia k u wa p o k wa wa t e j a wengi wanaofurika kwa waganga hao wakiamini kuwa watawaondolea shida zao, ziwe ni za maradhi au za kutaka mafanikio. Wanaotumia huduma hizo, huwasiliana na waganga hao kwa njia ya simu zilizoandikwa kwenye matangazo yao ya kuvutia wateja.

H a t a h i v y o , k w a kuwa Watanzania wengi wamekubwa na ugonjwa wa kutofikiri kwa kina na tamaa ya kupata mafaniko kwa haraka na wakati mwingine bila hata jasho wala gharama kubwa, basi wamegeuka kuwa wateja wakubwa wa waganga hao, ambao wengi wao ni feki na wezi wakubwa, ambao hawana uwezo wala t iba i s ipokuwa wanatumia udhaidu wa wateja wao kuj ipatia mamilioni fedha, huku wakiwaacha wakiendelea kudhurika na kupata hasara.

Mganga anakotoka i m e k u w a n d i o s i f a inayokoleza ubora wa mganga na kuwa kivutio kwa wateja. “Mganga kutoka Sumbawanga, Nigeria”, imekuwa ndio sifa kubwa inayo imani watu juu ya mganga mwenyewe. Tunaamini kabisa kuwa uvivu, ujinga na upumbavu huu wa kutaka mafanikio ya

haraka, kiasi cha kuruhusu a k i l i z a Wa t a n z a n i a kulemaa na kutekwa na imani za kishirikina ili kukabili maisha, ndio chimbuko la kuendelea kuawa na kujeruhiwa wenzetu wenye matatizo ya ulemavu wa ngozi. Wa k a t i wa t u we n ye u l e m a v u w a n g o z i (Albinism) wakiendelea kushambuliwa nchini, Mauaji dhidi yao yakizidi kuongezeka, wakiwindwa k a m a m n ya m a p o r i , kiasi imefika mahali sasa wanaogopa hata kuishi nje ya vituo vyao vya hifadhi, kuna haja ya kuwakomboa Watanzania kutoka katika fikra za kivivu na za kupupia utajiri au kupata mafanikio kwa njia za mkato.

Kwa muda sasa, watu w e n y e u l e m a v u wa ngozi nchini wamekuwa wakikabiliwa na mauaji n a v i s a v ya u t e k a j i n ya r a . Wa g a n g a wa kienyeji, wasaka utajiri na hata viongozi wa k i s i a s a w a m e k u w a wakinyooshewa vidole, kuwa wamekuwa chanzo kikuu cha kuangamizwa watu hawa. Hisia za wengi juu ya biashara hii haramu ya viungo vya

watu wenye albinism, ni kwamba wanadaiwa kutumia v iungo vya watu hao kupitia imani z a k i s h i r i k i n a , k wa imani kwamba watapata mafanikio (utajiri) kwa yale waliyoyakusudia. Wakati matukio ya ukatili dhidi ya albino yakituacha katika taharuki nchini, kuna taarifa za watetezi wa haki za binadamu kwamba hivi sasa nchi jirani nazo

zimeanza kuathirika na mauaji ya watu wenye albinism, na soko kubwa la viungo vya albino hao wanauliwa katika nchi hizo za jirani ni Tanzania.

Hatua hii inadhihirisha kwamba hivi sasa Tanzania imekuwa Hub kubwa ya biashara ya viungo vya watu wenye albinism katika ukanda huu wa

Inaendelea Uk. 19

Page 10: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

10 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala

Nigeria: Mai Tatsine, Boko Haram na CAN: Ukweli mchungu…”Marwa Maitatsine alikuwa Mkristo mpaka anakufa!!!”

H i v y o n d i v y o a n a v y o a n d i k a Oloko Adeola Afeez akimnukuu Profesa Dauda Ojobi juu ya utata wa Boko Haram.

Ki la uchao, Boko Haram imekuwa ni kitendawili tata kwa wengi lakini wakati huo huo yakifumuka mambo yanayotoa mwanga kwa wanaotaka kujua ukweli. Kama yaliyofichuliwa na Prof. Dauda Ojobi yatakuwa ni kweli, basi huenda kitendawili hiki itakuwa kimeteguka japo haitakuwa mwisho wa unaodaiwa kuwa ugaidi wa Boko Haram.

Maelezo ya Profesa Dauda Ojobi ambaye awali alikuwa kiongozi wa Kanisa kabla ya kusilimu mwaka 1966 yanatoa mwanga kuwa awali ‘Boko Haram’, ilibuniwa kama mkakati wa Kanisa kupambana n a U i s l a m u . J a p o mpango na mkakati huo bado unafanya kazi, lakini limeingia jambo lingine la ubeberu ambapo, wenye masilahi ya kibeberu kutoka nje ya Nigeria na kwa kushirikiana na baadhi ya wanasiasa na watu wa dini wa Nigeria, wanapata mradi wao. Habari yenyewe ipo hivi:

Kat ika ushuhuda w a k e ( Te s t i m o n y ) u n a o p a t i k a n a k wa maandishi na video/audio, Profesa Dauda Ojobi anasema kuwa mwaka 1954, chama cha Wakristo Kaskazini mwa Nigeria (Christian A s s o c i a t i o n i n t h e Northern Niger ia ) , kiliweka mkakati wa kupeleka vi jana wa Kikristo katika nchi za

Ukweli mchungu:Kamanda Boko Haram Mkristo-Prof. Ojobi

Ni Abu Tijjani aka Kana’ana a.k.a MaitatsineAlipelekwa Sudani akarudi na Aya, HadithAkakusanya silaha kupeleka vijana ‘Shamba’As’hab Kital 700 wakauliwa kuleta Boko Haram2Boko Haram3 imechanganya Ukristo na ubeberu

Na Omar Msangi

Kiarabu, kama watu waliosilimu wakasome Uislamu na lugha ya Kiarabu, halafu wakirudi watumike kuchafua Uislamu na kupandikiza k u t o k u e l e wa n a n a machafuko miongoni mwa Waislamu kutokana na fikra potofu watakazo zipandikiza. Prof. Ojobi anasema wakati akiwa ni mmoja wa vijana wa Kikristo waliokuwa wakisomea theolojia, anakumbuka vi jana watano waliteuliwa kwenda kusoma Sudan.

Hata hivyo anasema, katika hao vijana watano, watatu walikataa kurejea Nigeria, wakasalia Sudan wakiishi huko wakiwa

Waislamu. Aliwataja waliorejea ili kutekeleza kazi waliyoandaliwa k u i f a n ya k u wa n i Muhammad Marwa n a B i r e m a . M a r wa alipelekwa kufanya kazi Kano, wakati Birema alipelekwa Niamey, Niger.

P r o f e s s o r D a u d a Ojobi, aliwahi kuwa Katibu wa chama cha Wa k r i s t o N i g e r i a -Northern Christ ian Association of Nigeria (CAN), na Profesa wa Sheria (Law sio Shariah) katika Chuo Kikuu cha Benue (Benue State University) . Aidha, alikuwa ndiye mtu wa tatu kupata cheo cha-

Reverend Father kutoka Kaskazini mwa Nigeria baada ya Paul Gindiri na GG Ganaka. Alikuwa pia raia wa kwanza wa Nigeria kuwa mlezi mkuu wa Kanisa la Baptist katika Kaduna (Baptist Church). Katika nyadhifa za kiserikali aliwahi kuwa Kamishna wa Sheria katika Jimbo la Bauchi.

Muhammad Marwa aliporejea alianzisha kikundi chake mithili ya Boko Haram ya sasa ambacho kilikuja k u j u l i k a n a k a m a Mai Tatsine. Alianza kwa kutangaza kuwa elimu ya shule na vitu v i n a v y o t o k a n a n a

tekinolojia ya elimu hiyo ni haram kwa Muislamu. Kwa hiyo pamoja na kusoma shule kuwa ni haram, akasema pia ni haram kwa Muislamu kuwa na redio, saa ya mkononi (wristwatches), televisheni, gari, basikeli n.k.

L a k i n i w a k a t i a k i h a r a m i s h a v i t u vilivyotengenezwa na tekenolojia ya kisasa, alikuwa akihimiza watu wanunue na kuhifadhi bunduki za kutosha ndani ya nyumba zao, milipuko (mabomu), visu na mapanga.

Kwake kila asiyefuata Uislamu wa mtizamo wake ni kafiri na hivyo a l i h i m i z a wa f u a s i wake kuwaweka kundi m o j a n a m a k a f i r i tayari kwa kuwauwa wakishakuwa na silaha za kutosha. Na jina hili Mai Tatsine lilitokana na maneno yake makali akitoa katika mimbari a k i l a n i Wa i s l a m u wasiofuata ‘salafi’ yake hal ikadhal ika wale wanaofuata mambo ya katiba, mabunge na taratibu za kinchi. Kwa hiyo alitangaza kuwa Wakristo, Waislamu wasio katika yeye, watu wanaofuata katiba za nchi na elimu za shule, wote hao laana ya Mungu iwe juu yao na kwamba ni halali kuwachinjilia kwa mbali.

Laana hiyo alikuwa akiitoa kwa lugha ya Kihausa akisema:

“Allah ya tsine maka albarka!”, kwa ufupi ikiwa na maana laana ya Mungu iwe juu yenu. Mungu aondoe Baraka zake juu yenu.

“ W h o e v e r u s e s wristwatches, radios or ride bicycles, Allah ya tsine maka albarka!” Yeyote anayevaa saa, m w e n y e r e d i o a u kuendesha baiskeli , laana ya Mungu iwe juu yake.

Inaendelea Uk. 11

MUHAMMED Marwa

Page 11: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

11 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 201511 AN-NUURMakala

Inaendelea Uk. 15

Inatoka Uk. 10

Kamanda Boko Haram Mkristo-Prof. OjobiKutokana na maneno

hayo ya laana akiyakariri mara kwa mara, ndio akaitwa “Mai Tatsine”, ikiwa na “anayelani, mtoa laana (‘he who curses‘, ‘the one with curses’ or ‘the one who curses’.)

Akikusanya vijana kutoka kada za chini, wasio na ajira maalum na wachache wa elimu, aliwajaza chuki na hasira za kumchukia kila asiye kuwa katika wao na kuwajenga kuwa tayari kuuwa na kufa kwa ajili ya kumtetea kiongozi wao na ‘salafia’ yao.

Baada ya mafunzo hayo ya awali, alikuja na maelekezo mengine kwamba ardhi na mali ya kafiri, unaweza kuipora tu. Kwa hiyo, hata ukitaka kujenga nyumba hakuna kuomba kiwanja serikalini au kujali ni cha nani kama mwenye nacho sio katika kundi lao.

Hilo lilipokubalika akaja na jingine, kwamba watu wote wanaosoma H a d i t h i a u v i t a b u vingine vya dini baada ya Qur’an ni makafiri. Kitabu ni Qur’an tu.

H a k u n a K a t i b a ya n c h i wa l a H a d i t h i z a M t u m e ( s . a . w ) . Anayefuata Hadith, ni mtu wa motoni. Vijana wakaamini na wafuasi wakazidi kuongezeka.

A l i p o f i k i a h a p o , baadhi ya Masheikh wakaanza kuwaeleza watu kuwa huo sio Uislamu ni ukafiri na kwamba Mohammad Marwa sio Muislamu. Haraka haraka Marwa akenda kuhiji. Akawa sasa Alhaj Muhammad Marwa. Akazidi kupata wafuasi.

Hata hivyo, Masheikh w a l i z i d i k u w a n a w a s i w a s i k u w a Muhammad Marwa alikuwa Muislamu feki. Pamoja na wasiwasi huo, aliyekuwa Amir wa Kano, Sheikh Sanusi a k a g u n d u a k u w a Muhammad Marwa a . k . a M a i Ta t s i n e alikuwa akipokea vitu mbal imbal i kutoka Vatican. Akamtimua Kano kwenye miaka ya 1960s. Hata hivyo akarejea tena Kano mwaka 1979.

Ili kuwadhibiti wafuasi wa k e , a l i wa k a t a z a k u s w a l i m i s i k i t i

Amir wao Mohammed Marwa.

Baada ya kuhakikisha kuwa ana kundi la kutosha la wafuasi, Yan Tatsine, na lililo tayari kwa lolote, aliamuru waanze kuwashambulia Waislamu wasio katika mfumo wao, Wakristo na polisi. Hiyo ilikuwa Desemba 1980, ambapo walianza kuuwa Polisi k a b l a ya k u va m i a nyumba za Waislamu walioitakidi kuwa ni wanafiki na makafiri. Hali ilikuwa mbaya h a d i i k a b i d i j e s h i kuingilia kati ambapo m p a k a m a c h a f u k o yanakomeshwa, watu zaidi ya 5000 walikuwa wameul iwa. Akiwa amejificha mahali huku vijana wakipambana huko, Alhaj Mohammed M a r w a a l i a m u a kutoroka, baada ya kuona hali mbaya. Lakini wakati akisindikizwa na kulindwa na walinzi wake wal iosheheni s i laha, al ipatwa na risasi mguuni. Kwa kushindwa kujitokeza kwenda kutibiwa, akavuja d a m u m p a k a a k a f a . Wafuasi wake wakamzika haraka haraka kando ya njia.

Yan Tatsine hawakuishia hapo, wengi walikimbilia

B u l u m k u t t u , k a r i b u na Maidaguri ambapo Oktoba 1982 walianzisha vurugu tena, watu 3000 wakauliwa. Mauwaji kama hayo yalitokea tena Yola mwaka 1984 wakiuliwa watu 1000 huku nusu ya nyumba za wakazi 60,000 wa mji huo zikiteketezwa kwa moto.

Japo yapo maelezo mengi kuhusu Alha j M o h a m m e d M a r w a yakionyesha kuwa alikuwa Muislamu tu aliyepotoka, katika ushuhuda wake Professor Dauda Ojobi, anasema kuwa alikuwa Mkristo mpaka anakufa. “Marwa Maitatsine, was a Christian until his death.” Anasema katika ushuhuda huo.

Wakati Shehu Shagari a k i wa R a i s N i g e r i a , aliunda Tume kuchunguza kadhia ya Maitatsine. Miongoni mwa watu waliohojiwa na kutoa maelezo ni Prof. Ojobi. Inaelezwa kuwa Prof. Ojobi alitoa maelezo yake kwa Tume ya Rais ikibeba jina la “Anya Goru Panel”, na kueleza kisa cha wale vijana Wakristo watano waliopelekwa kusoma Sudan ndio akapatikana M o h a m m e d M a r w a na Marwa Maitatsine.

mingine, wasijadiliane na watu na akiwataka waishi katika vijiji vyao pekee, kama ilivyokuwa kule Madina, Kilindi. Kijiji maarufu cha watu hawa Maitatsine kule Nigeria kilikuwa Yan Awaki, Kano, wakiwa na utawala wao usiojali kama kuna serikali wala mamlaka yoyote nje ya

Page 12: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

12 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 201512 MAKALA

MWILI UNA RAHA GANI (JIBU)Kalamu nimeishika, mhariri samahani,Nikuombe kuniweka, angaa hata pembeni,Nipate kulipeleka, jibu langu Visiwani,Mwili kwa wake utashi, rahaye ni starehe !

Kongole kujusurika, kukamata dada peni,Na kisha kuliandika, swali lako swahifani,Kwangu limefahamika, dhima jibu kubaini,Mwili kwa wake utashi, rahaye ni starehe !

Pole kwa kutatizika, nalo gimba la insani,Lenye tumbi patashika, baadhi ushabaini,Naamini kwa hakika, kwa jibu utasakini,Mwili kwa wake utashi, rahaye ni starehe !

Binti Mtima pulika, kwa utuvu na makini,Jibu bayana naweka, la swalilo gazetini,Kumanya lililotaka, raha ya jasadi nini,Mwili kwa wake utashi, rahaye ni starehe !

Yapaswa kufahamika, kwako na kwa ikhiwani,Badani kusahilika, kwa yaso tija na dini, Pamwe na kuthakilika, kwa ya tija yake nduni,Mwili kwa wake utashi, rahaye ni starehe !

Mwili daima wataka, kudumu stareheni,Tangu unaporauka, liamba usingizini,Hata jioni kufika, uuyapo saririni,Mwili kwa wake utashi, rahaye ni starehe !

Starehe kwa hakika, si jambo mui jamani,Ila zenye kukiuka, maamuru ya MANANI,Ndizo hulaumika, mwili kwa kuzithamini,Mwili kwa wake utashi, rahaye ni starehe !

Mwili kustareheka, wapenda tangu zamani,Tena kwa yenye hilaka, na yenye kuufitini,Pamwe na ya kuuweka, baidi na RAHMANI,Mwili kwa wake utashi, rahaye ni starehe !

Starehe huziweka, mbele hasa za Shetani,Na kwazo huzainika, na kujihisi rahani,Mwili ndo yake hulka, chungua utabaini,Mwili kwa wake utashi, rahaye ni starehe !

Kwa jibu niloandika, kwa swalilo gazetini,Nahisi utaridhika, malenga wa Visiwani,Kaditama nimefika, kalamu naweka chini,Falau hutaridhika, niarifu gazetini.

ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

Penye dhulma, muhali amani kustakiri!)Kalamu i mkononi, ukweli kuukashifu,Japo mchungu moyoni, jarima kuukhalifu,Masheikh sikilizeni, pamwe na Maaskofu,Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani itongoeni, kwa mizani adilifu,Viongozi wambieni, ukweli pasi na hofu,Huru utakuwekeni, kwa insi na kwa RAUFU,Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani hapa nchini, imekuwa mausufu,Si Bara si Visiwani, viongozi huisifu,Kwa kauli za kinywani, vitendo iso sadifu,Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani ya mdomoni, kathiru 'ishatukifu', Twataka ya matendoni, yenye tutumbi sharafu, Ninyi hilo maizini, na wao muwaarifu, Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani itazameni, kwa uyuni yakinifu, Mashekhe jihadharini, na wa fikara upofu, Ushenga uepukeni, kuridhi 'Watakatifu', Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani ichungueni, kwa mapana na marefu, Ukweli mtabaini, wenye nayo maarufu, Muhali wao sijini, kuwekwa kwa uhalifu! Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani gani ambeni, haswa mnoisharifu? 'Wasota' wenzenu 'ndani', dhamana si yao kufu! Wangapi jiulizeni, 'lupango' Maaskofu? Amani kustakiri, penye dhulma muhali.

ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

KONGAMANO LA UWAWAMWA

Itaendelea

Kwanini kuzuka kwa ufashisti ni tatizo tenaInatoka Uk. 8

Rais Obama, "Benghazi, jiji lenye ukubwa wa Charlotte, lingeweza kugubikwa na mauaji ambayo yangetikisa eneo lote hilo na kuingiza doa katika hisia za dunia."

Ni uwongo wa wapiganaji wa Kiislamu waliokuwa karibu ya kushindwa na majeshi ya serikali ya Libya. Waliliambia shirika la habari la Reuters kuwa "kutakuwa na umwaga j i mkubwa wa damu, mauaji kama yale tuliyoona Rwanda." Ulipotangazwa Machi 14, 2001, uwongo huo ulitoa i shara ya kuanza kwa jehanamu ya NATO, ambayo Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alisema ni "msaada wa kibinadamu."

Wa k i w a w a m e p a t a mafunzo na kuwapa silaha kwa siri na vikosi maalum vya Uingereza SAS. wengi kati ya 'waasi' wangekuwa kama ISIS, ambao video yao ya hivi karibuni inaonyesha kuchinjwa kwa wafanyakazi 21 wa Kanisa la Coptic (Kanisa Katoliki la Ulaya Mashariki) waliokamatwa Sirte, mji aliokulia Muammar Gaddafi ulioharibiwa kwa ajili yao na mabomu ya NATO.

Kwa Obama, Cameron na rais wa Ufaransa Francois Hollande. jinai halisi ya Gaddafi ilikuwa ni uhuru wa uchumi wa Libya na nia yake aliyoieleza ya kuacha kuuza mafuta, nchi yake ikiwa ni mzalishaji wa kwanza Afrika, kwa kutumia fedha za Marekani, dollar. Fedha za mauzo ya mafuta zinalundikwa kwa dollar, ambao ni msingi wa nguvu za kiuchumi za Marekani. Gaddafi alikuwa na mipango ya kuweka fedha hizo kuwa msingi wa fedha ya pamoja (sarafu) ya Afrika ikiwa ina hazina ya dhahabu ya kutosha, kuunda Benki Kuu ya pamoja na kuhamasisha muungano wa kiuchumi miongoni mwa nchi maskini zenye hazina ya raslimali muhimu. Kwamba hili lingefanikiwa au la, mpango kama huo ulikuwa haukubaliki kwa Marekani wakati ikijiandaa kuiweka kati Afrika na kuzihonga serikali za Afrika kwa "ushirikiano" wa kijeshi.

Baada ya shambulio la NATO likijificha nyuma ya azimio la Baraza la Usalama (la Umoja wa Mataifa), Obama, aliandika Garikai Chengu, "alikamata dola bilioni 30 kutoka Benki Kuu ya Libya, ambazo Gaddafi alikuwa ametenga kwa ajili ya kuunda Benki Kuu ya Afrika na sarafu ya dinari ya Afrika ikiwa inakingwa na hazina ya dhahabu."

"Vi ta ya msaada wa k ib inadamu" dhidi ya Libya ilikuwa inafanana na

mfano ambao wa-liberali wa magharibi wanao moyoni, hasa katika vyombo vya habari. Mwaka 1999, Bill Cl inton na Tony Blair walipeleka majeshi ya NATO kuipiga mabomu Serbia, kwani, walidanganya, wa-Serb walikuwa wakiendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wenye asili ya Albania katika jimbo lililokuwa linataka kujitenga la Kosovo. David Scheffer, balozi wa Marekani asiye na maskani maalum anayeshughulikia 'uhalifu wa kivita,' alidai kuwa wa-Albania wanaume takriban 225,000 wenye umri kati ya miaka 14 na 59 inawezekana walikuwa wameuawa. Clinton na Blair wote walikumbushia mauaji ya kimbari ya Wayahudi (wakati wa Vita Vikuu vya Pili) na mafundisho ya jumla yanayotokana na vita hivyo. Washirika mashujaa wa nchi za Magharibi walikuwa Jeshi la Ukombozi la Kosovo (KLA) ambao vitendo vyao vya kihalifu viliwekwa pembeni. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Robin Cook, aliwaambia wamwite wakati wowote kwenye simu yake ya mkononi.

Upiga j i mabomu wa NATO ukiwa umekamilika, na miundombinu ya Serbia ikiwa imeteketea, pamoja na mashule, hospitali, makazi ya watawa na kituo cha taifa cha televisheni, vikundi vya wataalamu wa mabaki ya miili waliishukia Kosovo k u t a f u t a u s h a h i d i wa "mauaji ya kimbari." Idara ya Upelelezi Jinai ya Marekani (FBI) ilishindwa kupata hata kaburi moja la watu wengi na kurudisha wapelelezi wake. Ujumbe wa kitaalamu wa H i s p a n i a u l i f a n ya hivyo hivyo, k iongozi wake akilaani upotoshaji mkubwa wa "mifumo mahiri ya propaganda ya vita." Mwaka mmoja baadaye, jopo la Mahakama ya Kimataifa ya Yugoslavia ilitanga kuwa idadi ya waliothibitishwa kufa Kosovo ni 2,788, ikiwa ni pamoja na wapiganaji wa pande zote mbili pamoja na wa-Serb na wa-Roma (kabila la wanaohamahama, wanaochukiwa) waliouawa na KLA. Hapakuwa na mauaji ya kimbari. Tangazo hi lo l i l ikuwa uwongo. S h a m b u l i z i l a N AT O lilikuwa utapeli.

N y u m a ya u w o n g o kulikuwa na dhamira ya nguvu. Yugoslavia ilikuwa nchi huru kwa namna ya pekee, nchi yenye jamii tofauti za watu ambayo ilikuwa ni daraja kati ya nchi za Magharini na Mashariki wakati wa ushindani wa kiitikadi (vita baridi). Nyingi kati ya mifumo yake ya miundombinu na viwanda vilikuwa mali ya umma. Hii

haikuwa inakubalika kwa nchi za Jumuia ya Ulaya ambazo zilikuwa zinatanua wigo wake, hasa Ujerumani i k i w a n d i y o k w a n z a imeunganishwa, ik iwa inapigania kuunganisha maeneo ya mshariki kama soko lake kimaumbile, yaani majimbo ya Croatia na Slovenia nchini Yugoslavia. Hadi wakuu wa nchi za Ulaya wanaingia mkutano wa Maastricht mwaka 1991 kuweka mipango ya sarafu balaa ya Euro, mpango wa siri ulikuwa umeshafikiwa: Ujerumani ingeitambua Croatia. Yugoslavia ikawa imekwama.

J i j i n i Wa s h i n g t o n , Marek ani i l ihak ik i sha kuwa uchumi uliokuwa unalegalega wa Yugoslavia unakataliwa mikopo ya Benki ya Dunia. NATO, wakati huo ikiwa imechoka kutokana na kutokuwepo kwa mzozo ule wa vita baridi, ikarudishiwa pumzi kama mtekelezaji wa mpango wa kupanua himaya. Katika mkutano wa 'amani' ya Kosovo huko Rambouillet nchini Ufaransa, wa-Serb waliwekwa chini ya kibano cha kibeberu. Makubaliano ya Rambouillet yalikuwa na nyongeza ya pili ya siri, ambayo ujumbe wa Marekani uliingiza katika siku ya mwisho. Ulitaka kukaliwa kijeshi kwa eneo lote la Yugoslavia - nchi ambayo ina kumbukumbu ya kina ya ukaliaji kimabavu wa mafashisti wa Nazi (wakati wa vita kuu ya pili) na kutekelezwa kwa 'uchumi wa soko huria' na kubinafsishwa kwa amana zote za serikali. Hakuna serikali huru ingeweza kutia saini. Adhabu ilifuata haraka: mabomu ya NATO yalianguka juu ya nchi isiyo na ulinzi. Ilikuwa ni kufungua pazia ya mabalaa ya Afghanistan na Irak, Syria na Libya, na Ukraine.

Ta ng u mwak a 19 45 , zaidi ya theluthi moja ya wanachama wa Umoja wa Mataifa.nchi 69, zimepitia katika mikasa ya aina hiyo au kwa njia hiyo kikamilifu katika mikono ya ufashisti wa kisasa wa Marekani. Wamevamiwa, serikali zao kupinduliwa, harakati zao za umma kukandamizwa, chaguzi zao kuvurugwa, w a t u w a o k u p i g w a mabomu na uchumi wao kuondolewa kila kinga, jamii zao kuingizwa katika uzingirwa kivita unaoitwa 'vikwazo.' Mwanahistoria wa Uingereza Mark Curtis anakisia idadi ya waliokufa katika mamilioni. Katika k i l a mo ja ya matuk io hayo, uwongo mkubwa ulisambazwa.

Page 13: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

13 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015MAKALA

DAWA UGONJWA UNAOTIBIWA1 HAIIBA DENTAL

GUARDM a u m i v u ya meno

Maambukizi ya gram positive bakteria kwenye kinywa H a r u f u m b a y a kinywani

2 HAIIBA DENTAL GUARD COMBO

M a u m i v u ya meno

Maambukizi ya gram p o s i t i v e b a k t e r i a kwenye kinywa

H a r u f u m b a y a kinywani

Magonjwa ya fizi Kujenga upya meno yenye matundu

3 HAIIBA IG Kuongeza kinga za mwili Vidonda vya tumbo Kurekebisha athari za kisukari cha ukubwani

4 H A I I B A I G COMBO

Hupunguza mzigo wa virusi vya ukimwi mwilini

5 HAIIBA TIMAMU TEA

M a u m i v u ya viungo

Kusawazisha Cholesterol

K u h i f a d h i m n y u m b u k o wa ngozi

Kupunguza shinikizo la damu

Hupunguza madhara ya kisukari cha ukubwani

Hukinga dhidi ya uharibifu wa ini

Uchovu Kupunguza k a s i y a kuzeeka

K u i m a r i s h a siha ya ngozi

Kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (Heart Attack)

Hupunguza makali ya maradhi ya kupoteza k u m b u k u m b u (Alzheimer’s disease)

Hukinga mapafu yasipate makovu

Homa za mara kwa mara

Usagaj i wa c h a k u l a tumboni

K u i m a r i s h a siha ya macho

Huboresha siha ya mishipa ya fahamu

Huharakisha kupona majeraha

Hukinga dhidi ya ugonjwa wa ngozi k u c h u j a r a n g i (vitiligo)

M f u r o (Inflammation)

Kusafisha ini Kinga dhidi ya saratani

H u o n g e z a A l k a l i mwilini

Hupunguza makali ya ugonjwa wa baridi ya yabisi (Arthritis)

Husafisha kinywa dhidi ya bacteria wasiotumia oxygen

Kinga za mwili K u b o r e s h a m z u n g u k o wa damu

Kuharibu seli z a s a r a t a n i z i l i z o k o mwilini

Huzuia cholesterol m b a y a ( L D L ) kuingiliana na oxygen na kuleta madhara

Hupunguza kasi ya ongezeko la virusi vya ukimwi

Ni kinga dhidi ya utapiamlo

DAWA UGONJWA UNAOTIBIWA6 HAIIBA GLUCOMASTER

PROGRAMMEHutibu Kisukari cha ukubwani Kurekebisha athari za kisukari

cha ukubwani

7 HAIIBA P & B Kuziba mkojo Kibofu kilicholegea8 HAIIBA C CLEAN Malaria sugu Maambukizi ya njia ya

mkojoKuondoa bacteria wabaya tumboni Saratani mbalimbali

9 H A A I B A FA M I LY BUSINESS

Kuondoa ukhanithi Kuimarisha sana uwezo wa tendo la ndoa Maumivu ya kiuno na mgongo

10 HAIIBA CLEAN UP Kusafisha tumbo na njia ya haja kubwa

Kurekebisha mfumo wa usagaji chakula Nguvu za kiume

11 HAIIBA MLONGE PACK Kinga imara dhidi ya utapiamlo Huimarisha kinga za mwili Huondoa uchovu

HERBAL IMPACTP.O.BOX 70949, DAR ES SALAAM.

SIMU: 0754281131/0655281131MOSQUE STREET, NO.1574/144, KITUMBINI DAR ES SALAAM (MKABALA NA MSIKITI WA SUNNI

'Punguza sana matumizi ya chumvi, au ikiwezekana wacha kabisa'!

H u u n i u s h a u r i wa kawaida kabisa unaopewa na madaktari pale inapobainika kuwa shinikizo lako la damu liko juu kuliko inavyopaswa.

S h i n i k i z o l a d a m u hupimwa katika ngazi mbili. Ngazi ya kwanza ni shinikizo la juu. Hili hutokea pale misuli ya moyo inapokikaza kusukuma damu iliyosheheni oksijeni kutoka kwenye mapafu kuisambaza mwilini. Ngazi ya pili ni shinikizo la chini. Hili hutokea pale misuli ya moyo inapojiachia kuruhusu damu i re j ee kwenye mapafu ili kuachia hewa chafu kutoka katika seli za mwili - hewa ukaa - itolewe ndani ya mwili

Shinikizo la juu la kawaida la damu ni 110 - 120 mmHg; na la chini la kawaida ni chini ya 80 mmHg. mmHg ambayo kirefu chake ni 'millimeters of mercury' ndiyo kipimo kinachotumika kwa kawaida k u e l e z e a k i wa n g o c h a

Sukari ni kichocheo kikubwa zaidi cha Shinikizo la Damu (Hypertension) kuliko hata chumvishinikizo la damu.

Chumvi ina tabia ya kufyonza maji. Inapoingia m w i l i n i n a k w e n y e m z u n g u k o w a d a m u huvuta maji na kusababisha ongezeko la wingi wa maji kwenye damu. Ongezeko hili hupelekea shinikizo la damu kuongezeka. Hili huwa ni ongezeko la muda tu mpaka pale kiasi cha maji kwenye mzunguko wa damu kitakapopungua. Dawa za kifamasia za kushusha shinikizo la damu hufanya kazi kwa kuzingatia kanuni hii. Dawa hizi hulazimisha mhusika akojoe sana, kitendo ambacho hushusha kiasi cha maji kwenye mzunguko wake wa damu.

Tofauti na chumvi ambayo husababisha shinikizo la damu kuongezeka kwa muda mfupi tu, sukari hujenga mazingira ya mwili kuwa na shinikizo la damu la kudumu. U n a p o k u l a s u k a r i y a mezani (sucrose), mchakato ufuatao hutokea ndani ya mwili. Molekuli ya sucrose

huvunjwa na sukari mbili tofauti zilizomo (fructose na glucose) zinazounda molekuli hii huachiwa huru, kila moja na hamsini zake.

Wa t a f i t i w a n a s e m a kuwa Fructose (moja ya hizi sukari) huchochea seli za mwili kuchoma nishati (ATP) iliyohifadhiwa humo kwa kasi ya kutisha na matokeo yake seli husika hukumbwa na 'shock'! Shock hii hupelekea DNA katika hizi seli kusambaratika! Watafiti hawa wanaongeza kuwa DNA iliyosambaratika hujiunda katika kemikali zinazojulikana kama purines, a m b a z o n a z o h u i s h i a kujiunda kuwa tindilkali ya urea, yaani uric acid!

T i n d i k a l i y a u r e a inasababisha seli za mwili k u k u m b w a n a m f u r o endelevu, na huzuia mwili kuzalisha kemikali ya Nitric oxide inayosaidia kuta za mishipa ya damu kutanuka na kusinyaa kwa wepesi. K u s h i n d w a k u t a n u k a kwa mishipa ya damu

pale inapohitajika huzaa ongezeko la shinikizo la damu. Ulaji uliopindukia wa sukari hupelekea miili yetu kuzalisha kiasi kikubwa cha uric acid muda wote hali ambayo husababisha uharibifu wa mishipa ya damu kutokea muda wote.

Ni muhimu kujua kuwa shinikizo la damu ni ugonjwa hatari sana kwa sababu kila kiungo cha ndani cha mwili huwa kinakabiliwa na shinikizo kubwa. Viungo nyetu vinavyopitiwa na mishipa mingi ya damu, mathalani macho na figo huathirika sana. Watu wengi wamepata ulemavu wa macho kwa sababi ya kile kinachoitwa shinikizo la damu la macho. Watu wengi pia wamepoteza maisha kutokana na maradhi ya figo ambayo kimsingi chimbuko lake ni shinikizo kubwa la damu. Kama unataka kujifunza zaidi, zifuatazo ni hatua mbalimbali za tatizo la shinikizo la damu ambazo mtu anaweza akapitia.

AINA1. SHINIKIZO LA JUU

(Systolic) mm Hg

1.1. Kawaida: 110 - 120 mmHg

1.2 Kuelekea kuwa na tatizo la shinikizo la

damu (Prehypertension): 120 – 139 mmHg

1.3. Tatizo la shinikizo la damu (Hypertension)

Hatua ya 1: 140-149 mmHg1.4. Tatizo la shinikizo la

damu (Hypertension) Hatua ya 2: 160 au zaidi

mmHg1.5. Shinikizo la damu

lililopindukia mipaka (Hypertensive Crisis):

Zaidi ya 180 mmHg2. SHINIKIZO LA CHINI

(Diastolic) mmHg2.1. Kawaida: Chini ya 80

mmHg2.2 Kuelekea kuwa na

tatizo la shinikizo la damu (Prehypertension):

80 – 89 mmHg 2.3. Tatizo la shinikizo la

damu (Hypertension) Hatua ya 1: 90-99 mmHg2.4. Tatizo la shinikizo la

damu (Hypertension) Hatua ya 2: 100 au zaidi

mmHg2.5. Shinikizo la damu

lililopindukia mipaka (Hypertensive Crisis):

Zaidi ya 110 mmHg

Page 14: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

14 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala

Na Ben Rijal

M A K A L A h i i itamuangalia mweledi wa safari Ibn Battuta na mchango wake katika maendeleo ya Sayari yetu hii. Ni nani Ibn Battuta? Jina hili katika uga wa elimu ya Jiografia lilihitajika lizungumzwe kwa mapana na marefu kwa nchi za Kiafrika na hata katika ulingo wa historia Ibn Battuta a n a m c h a n g o wa k e a l i o u t o a . K i n y u m e chake jina la Ibn Battuta linaonekana haliingii katika mizani kwasababu z a w a n a l o l i k a t a a wanazijua wenyewe. Aidha kinachosikitisha n i k u wa h a t a k a t i k a nchi za Kiislamu na za

Mchango wa Waislamu Katika Maendeleo ya DuniaIbn Battuta - 2

Na Ben Rijal

Kiarabu katika mitaala yao hawamzungumzi na wale wanaomzungumza hawamzungumzi anavyo stahiki.

Ibn Battuta jina lake khasa ni Abu Abdullah Muhammad Ibn Battuta mzaliwa wa Morocco. A l i z a l i wa t a r e h e 2 4 Februari mwaka wa 703 Hijria (1304 CE) wakati wa utawala uliokuwa ukijulikana kama Marinid. Akifahamika zaidi kwa jina la Shams -ad-Din. Wazazi wake ni wa kabila la Kiberber na walikuwa na utamaduni wa kabila hilo kufanya kazi za uhakimu.

B a a d a y a k u p a t a elimu nyumbani kwao Morocco ka t ika fan i ya Sheria ya Kiislamu akaamua kuondoka na kuanza safari kiguu na njia ili kuweza kuujua ulimwengu. alianza safari zake hizo akiwa kijana mwenye umri wa miaka 21. Safari yake ya mwanzo kutoka Morocco ilikuwa kuelekea Makka na kupata fursa ya kutimiza nguzo ya Hijja. Hata hivyo safari hio ilikuwa ni refu kwani ilimchukua miezi 16 kutoka

Morocco hadi Makka. Baada ya kukamilisha Hijja akaamua kutorudi nyumbani na ilimchukua m u d a wa m i a k a 2 4 kuizunguka sehemu ya dunia mpaka kurudi kwao Morocco.

Baada ya kuondoka Makka alisafiri katika m a e n e o m b a l i m b a l i ikiwa baadhi ya nchi za Kaskazini mwa Afrika akaendelea na safari zake hadi Afrika ya Magaharibi, Kusini mwa Ulaya, Ulaya ya Mashariki kwa upande wa Magharibi, Mashariki ya Kati, sehemu za India, Kusini Mashariki ya Asia na China kwa upande wa Mashariki, safari zake hizo inaaminika kuwa hakuna kati ya watangulizi wake ambaye aliwahi kupita kote huko a l ikopi ta . Ib n Ba t t u t a a l i sa f i r i kukamilisha masafa zaidi ya maili 75,000 kumpita mvumbuzi Marco Polo. Baada ya kusafiri nchi zote hizo inaelezwa kuwa mwishoni alirudi nchini Morocco na kuyaelezea yale yote aliyoyaona na kuyashuhudia kwa Ibn Juzay.

Mvumbuzi wa nchi mbalimbali Ibn Battuta

Ibn Battuta aliweza kusafiri takribana katika nchi zote zile ambazo zikikaliwa na Waislamu kwa wingi katika wakati wake. Katika safari zake akipendelea zaidi kusafiri kwa kupitia njia za nchi kavu kuliko njia za baharini kwa kuchelea kuhujumiwa

na maharamia ambao walikuwa wakitamba katika maeneo ya baharini. Alikuwa akipendelea kujiunga na misafara ya wafanya biashara.

Alipofika katika mji wa Sfax alipiga chuo na

KUTOKANA na uchafu unaotupwa baharini kunaj i tokeza a thar i mabalimbali ambazo h u a t h i r i v i u m b e vilivyo baharini. Zaidi ya asilimia thamanini ya uchafuzi wa bahari hutokea nchi kavu, kwa mfano makaro ya taka (septic tanks), mafuta machafu katika magereji ambayo huchukuliwa na maji ya mvua na kuingia katika bahari, boti zinazomwaga mafuta kat ika matengenezo au kuvuja, mbolea za kemekali zinazotumiwa mashambani nayo mabaki yake huchanganyika na maji ya mvua na kumalizikia baharini, uchimbaji wa mafuta

Jee Bahari ni Jaa Mwaga Ukitakacho Bahari Itameza?-2

Na Ben Rijal

katika bahari humwaga uchafu wa kila aina, maji machafu ya majumbani na viwandani humwaga baharini moja kwa moja n.k..

Mbali na uchafu huo ni l iokwisha kueleza , wanadamu kwa sehemu ndogo na sehemu kubwa huamua kumwaga uchafu baharini kwa kuamini ndio jaa ambalo litabeba kila kitu pasi kuwa na uharibifu wa aina yoyote ile. Tunapojenga imani hii ya kumwaga taka baharini, ni kitu gani kinacokuja k u t o k e a ? Wa n y a m a wa baharini na samaki huathirika pakubwa na uvujaji na umwagikaji wa mafuta baharini, kwani huwazuwia kushindwa kuvuta pumzi kupitia mashavu yao. Athari hizi huja kupata vizazi vyao.

Umwagikaji wa mafuta huzuwia nuru ya jua kupenya kwenye maji na kuzuia mzunguko

wa u t e n g e n e z a j i wa chakula kwa mimea na kuchangia viumbe vya baharini kokosa mlo kwa wingi. Uchafu mwingi unaomwaga baharini huwa hauozi na kuchangia upatikanaji kwa hewa ya Oxigini kupungua na Oxigini inapopungua wanyama wa baharini kama Nyangumi, papa, k asa nao huat h i r ika p a k u b w a . U c h a f u unaotoka viwandani bila ya kusafishwa huathiri wanyama wengi wa bahari na hufa. Tunapowala na sisi huathirika kidogo kidogo.

P i c h a m b a l i m b a l i zinaonyesha kuwa taka zinazotupwa baharini kwa kiwango chochote kile hujikusanya na mwishowe kuleta athari kwa viumbe vya baharini. Ndio kusema kuwa thakikishe kuwa tusitupe taka za aina yoyote ile kwenye fukwe au moja

kwa moja baharini. Aidha, tunatakiwa tujihadhari kukinga maji ya mvua kusomba mbolea au aina yoyote i le ya uchafu kuingia baharini.

Plas t ik i tunapenda kuitupa baharini na hata boti zinazosafiri baharini huwapa abiria mifuko ya plastiki ambayo baadaye h u t u p w a b a h a r i n i . Tujiulize, nini athari ya plastiki katika bahari?

Tujitahidi kwa kutotupa uchafu baharini haya yanaweza kufanyika katika ngazi mbalimbali kuanzia Serikali, Asasi zilizokuwa sio za kiserikali, walimu wa Madrasa, Maimamu katika khutba zao za Ijumaa, kuhamisha watu kupitia vyombo vya habari kutotupa taka baharini, wakazi wanaoishi kando kando na bahari kupanga mikakati yao ya kuzuwia utupwaji wa taka baharini, kuwafunza watoto wa

skuli hatari ya kutupa taka baharini, siku ya bahari duniani kupendekezwa kuwa ni siku ya kitaifa ya usafishaji wa fukwe na kuhamasishwa watu umuhimu wa kutunza bahari.

M u h i m u t u k a w a n a m a b a l o z i w a kuizungumzia bahari na namna ya kuihifadhi, haya yatasaidia pakubwa katika kuihifadhi bahari. Mashekhe wana nafasi kubwa ya kuzungumzia ufisadi na kutumia aya na hadithi za Mtume SAW, kuziangalia aya za Quran kama hii: “Ufisadi (ikiwemo uchafuzi wa mazingira) vimekithiri nchi kavu na baharini v i k i w a n i m a t o k e o ya matendo maovu ya binadamu. Ameamuru ili waonje matunda ya yale waliyoyatenda ili wapate kujirekebisha.(Qur’an 30:41.”

Inaendelea Uk. 18

Page 15: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

15 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala

Kamanda Boko Haram Mkristo-Prof. OjobiHata hivyo, inaelezwa kuwa baada ya Shehu Shagari, kusoma taarifa hiyo alisema isitolewe h a d h a r a n i m a a n a inaweza kuzusha ghasia zaidi.

Profesa Dauda baada ya kuona kuwa aliyosema yamefunikwa, alikuwa a k i t o a m i h a d h a r a kusema yote aliyosema katika Tume ya Rais. Mpaka leo hakuwahi kutokea kiongozi wa Kikristo au wale watu waliokuwa katika Tume ya Rais Shehu Shagari, kukanusha aliyosema Prof. Dauda. Professor Dauda alisilimu mwaka 1966 baada ya kurejea kutoka Rome alikokuwa anachukua masomo ya Theolojia (Christian Theology).

Baadhi ya wadadisi, w a c h a m b u z i n a wafuatiliaji wa mambo wanasema kuwa kuibuka kwa Mohammed Yusuf, kiongozi wa kwanza wa Boko Haram namba mbili (ya kwanza ikiwa ni Yan Tatsine/“Mai Tatsine”, i m e f u a t a m k o n d o huo huo. Na ushahidi ni kuwa anayetajwa kuwa mtu wa karibu sana ambaye akimtoa Polisi kila akikamatwa alikuwa ni Jerry Gana, ambaye pamoja na kuwa mwanasiasa, lakini ana nafasi kubwa katika Kanisa. Hivi karibuni ametunukiwa nishani na kanisa kwa utumishi n a m c h a n g o wa k e madhubuti kwa kanisa.

1. B a a d a y a M o h a m m e d Y u s u f k u k a m i l i s h a k a z i aliyokuwa afanye ya kutengeneza kundi la kitisho cha ugaidi wa Boko Haram, Jerry Gana aliondoa mkono wake. Kama Jonas Savimbi, ‘Ustaz Yusuf’ akauliwa kwa kudhal i l i shwa hali ambayo ilifanywa makusudi ili kutibua hasira za wafuasi wake wajitokeze. Tunasema ilifanywa makusudi

Inatoka Uk. 11 kwa sababu Yusuf alikamatwa na katika mkanda wa video ambao unapatikana k a t i k a m t a n d a o hadi leo (Tazama: “ B o k o H a r a m " leader Mohammed Yusuf Interrogation before his execution), w a n a o n e k a n a w a n a j e s h i wamemfunga pingu w a n a m h o j i h u k u w a n a p i g a p i c h a za video. Baada ya hapo wanamuuwa na maiti yake iliyojaa majeraha makubwa na matobo mengi ya risasi ikapigwa picha ikasambazwa katika mtandao.

Kama walivyokuwa wale vijana wa “Mai Tatsine”, wafuasi wa Ustaz Yusuf walingia mitaani kufanya fujo, na hapo wakauliwa z a i d i ya 7 0 0 . N a inaelezwa kuwa baada ya hapo waliosalia walikuwa wakifuatwa majumbani kwao na kuuliwa kimya kimya. Huo ukawa mwishao w a B o k o H a r a m 2. Ikazal iwa Boko Haram3 ya Abubakar Shekau. Hii imekuwa kama mzuka ambao unakimbiwa mpaka na wanajeshi.

B o k o H a r a m 3 i n a o n e k a n a k u wa mbaya zaidi kuliko ya Yusuf hata ile ya “Mai Tatsine”, kwa sababu, wakati hizo mbili za nyuma zilitegemea k u w a t i a w a z i m u vijana wasiojitambua kupata wafuasi walio tayari kufa kwa imani potofu na ufuati wa kibubusa, Abubakar Shekau amekuwa mtu hewa. Kwa Yusuf na “Mai Tatsine”, hata kama wangekuwa na wafuasi wengi kiasi g a n i , wa s i g e we z a kushinda jeshi la nchi. Lakini kwa Shekau inaonekana ni kivuli tu cha propaganda. H a t a s i k u m o j a

hutaona askari wake wakipambana au kundi la wafuasi wake. Picha utakazoziona ni zile zile za juzi na jana akionyeshwa Shekau kuwa anatoa ujumbe fulani. Inavyoonekana Boko Haram ya sasa ina vikosi viwili. Kikosi cha propagngda ambayo ni picha ya Shekau ikidaiwa kasema hili na li le, na pili washambuliaji ambao hawajulikani. Hawa wanaweza kuwa ama ni watu kutoka nje, wanashambulia na kuondoka au watu w a n d a n i a m b a o s e r i k a l i i n a wa j u a , w a k i s h a m b u l i a wanakwenda Magharibi, serikali inatuma polisi

Mashariki kuwafuatilia. Kukamatwa mara mbili ndege ya mchungaji Ayo ikitaka kuingiza silaha, inatilia nguvu hoja kuwa Boko Haram, haitokani na Waislamu.

Boko Haram ya sasa inaonekana kutimiza malengo ya aina mbili. Moja ni lile alilosema Prof. Dauda na hili ndio wanalolipigia debe watu kama Askofu David Oyedepo na Mchungaji Ayo.

P i l i , i n a t i m i z a malengo ya mabeberu ambapo mpaka sasa Nigeria imeshindwa kunufaika na mafuta yaliyo Kaskazini mwa nchi hiyo. Mafuta hayo

hivi sasa yanachimbwa na Chad na Cameroon k u w a f a i d i s h a makampuni ya Ufaransa na mengine ya nje. Lakini pia inaelezwa kuwa baadhi ya wanasiasa wa Nigeria akiwemo Rais Jonathan, wanapepea Boko Haram ili badala ya nchi kunufaika na mafuta, wanufaike wao binafsi. (Tazama: Article accuses Cameroon of helping France (a.k.a Boko Haram) access Nigeria’s oil. “Boko Haram, Big Oil And The Chad Connection”. “ T h e J a n j a w e e d Connection: Boko Haram Unraveling” and “Boko Haram: Jonathan, Ihejirika S u p e r v i s e d F o r e i g n Invasion of Nigeria’s Oil Rich Northeast”.)

KIONGOZI wa Boko Haram 2 Mohammed Yusuf aliyekifua wazi kabla ya kuuliwa baada ya kukamatwa na jeshi.

Page 16: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

16 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala/Tangazo

Ofisi ya Munazzat Al- Daawa Al- Islamiyya (MDI) Iliyopo Mbezi Beach Tangi Bovu jijini Dar es Salaam,inapenda kuwatangazia nafasi za masomo kwa wale wote wanaotaka kujiunga na chuo kikuu cha INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA, Khartoum Sudan.

Kozi zinazotolewa ni;1. Shahada ya kwanza katika Medicine, Pharmacy, Dentist, Nursing, Laboratory Sciences, Natural Petroleum and Minerals, Engineering, Electronics & Electrical Engineering, Computer Science, Pure Science, Applied Chemistry, Microbiology, Geology and Physics

2. Shahada ya kwanza katika law & Sharia, Islamic studies, Economics, Administration, Political Science, Education Administration and technology, Curriculum & Methods of Teaching, Arts (Mass communication, Arabic Geography, History and General Psychology)

Fomu za maombi zinapatikana kwa Tsh 10,000=/tu kuanzia tarehe 21 March mpaka tarehe 4 April 2015 katika vituo : Dar ES SALAAM: katika ofisi ya Munazzamat iliopo Tangibovu-Mbezi Beach. MWANZA: Msikiti wa Rufiji uliopo Mtaa wa Rufiji na ZANZIBA : Katika ofisi ya Munazzamat ( Kituo cha kusaidia mayatima) kilichopo eneo la Mpendae kwa mchina mwisho, mkabala na skuli ya kijangwani, saa 3:00 asubui mpaka saa 7:00 mchana.Awe amemaliza kidato cha nne na sita au Thanawiya kwa kupata daraja la kwanza, la pili au la tatu. Pia mwombaji lazima alete Vyeti halisi ( Original academic certificates) Siku ya kurudisha fomu Result sleep haikubaliwi.

Kwa maelezo zaidi piga simu:-Makao Makuu, Dar es Salaam: 0786 806662 au 0652 806662 au 0715249015 Kituo cha Zanzibar simu no: 0777415835 au 0715 415835Kituo cha Mwanza simu no : 0688304852

Mr. Khamisi M. LiyenikeK.N.Y Mkurugenzi, MDI, TZ

NAFASI ZA MASOMO SUDAN 2015/2016

S H U K U R A N I z o t e anastahiki Mwenyezi M u n g u p e k e y a k e na rehema na amani zimfikie yule ambaye hapana Nabi i baada yake, Nabii Muhamad (saw), ama baada ya utangulizi huu mfupi. Kwa hakika anafahamu kwa kila mwenye akili t imamu japo kidogo kwamba, dini ya Uislamu haina uhusiano kabisa na tuhuma za ugaidi na ubabe na ugaidi sio kitu kilichotengenezwa na Uislamu, unaonekana k u w a n i j a m b o l a ulimwengu mzima ambalo halina dini wala nchi na kuna wahusika wengi wa ugaidi wanajihusika nao. Wanajihusisha na kufuata dini nyingine au hawana dini kabisa na hakuna mahusiano kati ya Uislamu na vitendo vya kigaidi ambavyo vinavyofanywa na watu wachache waliopotea.

Maana ya ugaidi: Ni uadui wa kupanga mtu mmoja au watu wengi au nchi kwa nafsi za binadamu au mali za umma au za watu kwa kuwatisha na kuwaudhi na kufanya ufisadi bila ya njia ya haki.

Hukunu ya ugaidi : Ugaidi kwa maana hii ni haramu na umekatazwa kisheria, kwani huu ni u a d u i k wa wa t u n a kueneza uharibifu duniani. Amesema Mwenyezi Mungu (basi malipo ya wale wanaopigana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kufanya aliyowakataza na kufanya uovu katika nchi, kuuawa au kusulubiwa au kukatwa mkono wa kulia kwa mguu wa kushoto na mkono wa kushoto kwa mguu wa kulia au kuhamishwa katika nchi hii, ndiyo fedheha yao katika dunia na akhera watapata adhabu kkubwa) al-Maidah 33. Na amesema tena (kwa sababu hiyo tunawaandikia wana wa Israeli ya kwamba, atakayemuua mtu bila yeye kuua mtu au bila yakufanya ufisadi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote

Ugaidi hauna dini na mwenye kumwacha mtu hai kumsaidia kuishi ni kama amewaacha watu wote na bila shaka Mitume wetu waliwafikia na hoja zilizo wazi, kisha wengi katika wao baada ya haya walikuwa waharibifu sana katika nchi) Sura al-Maidah (32).

Na amesema tena (na wala msifanye ufisadi k a t i k a a r d h i b a a d a yakutengemaa) Aaraf (56). Amesema Sheikh Kurtubi, “Amekata Mwenyez i Mungu kila uharibifu (ufisadi), iwe ni kidogo au kikubwa baada ya kutengemaa kwa kubwa au dogo, naye ataingia katika kundi la uhalifu kwa maneno yenye nguvu na sahihi. Kwa yakini Uislamu na yale yaliyomo miongoni mwa vyanzo vyake vitukufu katika kitabu na sunna na maisha ya Mtume (saw) na watu wema, dini hii ina uwezo wa kujitetea yenyewe, hata kwa uchache wa somo kwa muongozo wa kielimu maalum ulio mbali na kuusifia tu, ambao anautoa m p e k u z i k u e l e k e a k we n ye u h a k i k a wa elimu na historia, nayo ni kufahamisha kuwa ugaidi sio jambo lililotengenezwa na Uislamu na haukutoka katika tumbo la Uislamu kama wanavyoda watu wa magharibi na baadhi ya vyombo vya habari vya kimagharibi.

K w a h a k i k a wameandika baadhi ya waandishi Wakristo nchini Misri, naye ni msomi mkubwa wa kikibtwi Dk. Nabil Luka Baybani, yeye ameandika kitabu ki i twacho “Ugaidi s i mambo yaliyotengenezwa na Uislamu”. Akasema mwandishi kuwa pamoja na kwamba yeye ni Mkristo waarthuzaksi, ameusoma U i s l a m u s a n a n a akamaliza kwa uyakini na kukinai kwamba Uislamu upo mbal i kabisa na tuhuma hizi za dhulma na kwamba, Uislamu haujui ubabe na wala hauukubali, bali ni kinyume chake na anaupinga ubabe na anauzuia kwani hii ni dini ya amani na salama. Huu ni ushahidi wa mwandishi ambaye si Muislamu lakini ameupa haki Uislamu, k wa h a k i k a d i n i ya Uislamu ni dini ya amani na kujuana kati ya mataifa na si dini ya ubabe na

mieleka ya kimaendeleo, naye anakiri kwamba kila taifa duniana ni wajibu kusaidiana kutambuana na si kugongana na k u i n g i a k a t i k a v i t a ambavyo havina mshindi wala mshindwa.

M w e n y e z i M u n g u mtukufu anasema (enyi, watu sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume n a m w a n a m k e n a tukakufanyeni mataifa na makabila ili mjue kwa hakika, mbora na mwema m b e l e ya M we n ye z i Mungu ni yule mwenye kumuogopa sana, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi tena ana habari) Huturati 13.

Kwa hakika kisimamo cha Uislamu katika suala la ugaidi wa hawa jamaa wababe wa ugaidi, ambao wanauvisha nguo ya Uislamu, msimamo upo wazi kwamba Uislamu

hauna mahusiano yoyote na jamaa hawa na wala Uislamu haukubaliani na matendo yao, si kwenye Qur-ani tukufu wala kwenye hadithi sahihi wala kwenye mwenendo wa watu wema waliopita kwani dini ya Uislamu ni dini ya amani na vita imefaradhiswa katika wakati wa dharura na katika hali chache tu. Uislamu unakataza vita na wale watu wa kitabu pale wanapojisalimisha na pamoja na mushirikina ambao wanafungamana na dola ya Kiislam kwa mikataba, na Uislamu haukubali ubabe wala kuifanyia uadui roho ya binadamu na viumbe wengine.

K w a h a k i k a kuunganisha kudogo kati ya yale walioyafanya Waislamu kwa wasio W a i s l a m u k a t i k a

m i j i , a m b a y o t a ya r i waliikomboa na matendo yao mazuri kwao na k u wa f a n ya k u wa n a hiayari kwao kuingia katika Uislamu bila ya kulazimishwa na kati ya kubakia katika dini yao, na kati ya yale waliyoyafanya m a t a i f a ya R o m a n i a ya Wakristo Katol iki p a m o j a n a Wa k r i s t o wenyewe miongoni mwa mauaji na mateso na vita kubwa, hii yote ni kuufahamisha kwamba U i s l a m u h a u t a m b u i ugaidi na ubabe, kwa hakika Uislamu ni neema ametuongoa Mwenyezi Mungu kwa dini.

S h u k u r a n i z o t e anastahi l i Mwenyezi M u n g u a l - A a r a f 4 3 . Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuongoe sote kuelekea kwake ili tupate furaha ya dunia na ya akhera.Makala hii imeandaliwa n a D k . A b d a l l a h Abdulhamid Daruweshi.Mwalimu wa al-Azhari Sharif tawi la Tanzania.

Page 17: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

17 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015

Makala

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:• KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL – SAME – KILIMANJARO • NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL – MWANZA • UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L – DAR ES SALAAM

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE• P.O Box 55105,Phone: 0222450069, 0784 267762, 0755 260087 & Fax 022 2450822, Dar es Salaam website :www.ipctz.org

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO – 2015/2016Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu.Shule hizi ni za bweni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana .Zipo tahasusi za masomo (Subject Combinations) ya SAYANSI, ARTS na BIASHARA. Wanafunzi wote wanafundishwa Islamic Knowledge,Introduction to Arabic na matumizi ya compyuta pamoja na kutumia mtandao

(internet) katika kujifunza.Muombaji anatakiwa awe na sifa za kujiunga na kidato cha tano ziolizotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi amabazo ni :Ufaulu wa masomo matatu (3) kwa kiwango cha ‘Credit’(yaani A,B+,B au C0 katika mtihani wa Kidato cha Nne, ns Ufaulu usiopungua Daraja la ‘Credit’ au GPA ya 1.6 katika Mtihani wa Kidato cha Nne, na Ufaulu usiopungua Gredi D kwenye masomo yote ya tahasusi (combination).AUUfaulu wa masomo matatu (3) ya tahasusi kwa kiwango cha ‘Credit’ bila kujali daraja alilopata mtahiniwa kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne.

Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.Mwsho wa kurudisha fomu ni tarehe 15 Mei 2015.

Arusha - Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni : 0783552414/0762817640.

Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha :712 216490 - Same Juhudi Studio mkabala na Benki ya NMB Same: 0757 013344. - Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 - Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054. - Ugweno – Kifula Shopping Centre- Yusuph Shanga : 078458776.

Tanga - Twalut Islamc Centre – Mabovu Darajani : 0715 894111- Uongofu Bookshop: 0784 982525 - Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007/071569008. - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533. -Handeni –Mafiga -0782 105735/0657093983

Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685.- Ofisi ya Islamic Education Panel – Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770/0714097362.Musoma - Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623Shinyanga - Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini :0752180426 - Kahama ofisi ya AN –NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi : 0753 993930/0688794040 Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School : 0756584625/0657350172 - Ofisi ya Islamic Ed. Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin : 0655144474/0787119531 Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale : 0715704380.Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0718661992Singida - Ofisi ya Islamic Education. Panel – karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784 928039. Manyara - Ofisi ya Islamic Ed. Panel – Masjid Rahma: 0784491196Kigoma - Msikiti wa Mwandiga: 0714717727 - Kibondo – Islamic Nursery School: 0766406669. - Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802.Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.Mtwara - Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264/0683670772. - Mkuzo Islamic High School :0717 348375.Mbeya - Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini – 0785425319. - Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319. Rukwa - Sumbawanga:Jengo la Haji Said –Shule ya Msingi Kizwike 0717082 072.Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566/0787237342 Nzega -Dk Mbaga-0754 576922/0784576922.Iringa - Madrastun – Najah: 0714 522 122.Pemba -Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.Unguja - Madrasatul – Fallah: 0777125074. - PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na uwanja wa LumumbaMafia - Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu : 0773580703.

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU – WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

MKURUGENZI

WABILLAH TAWFIIQ

1

Page 18: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

18 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015

Makala

Mchango wa Waislamu Katika Maendeleo ya DuniaInatoka Uk. 14

kubakia hapo kwa muda, katika mji huo wa Sfax aliponea chupuchupu k u w e z a k u p o t e z a maisha yake pale jahazi alilosafiria kuzama na alipofanikiwa kufika nchi kavu ikawa ule msemo usemao kutoka kikangoni kuangukia motoni, alikuta mapambano yaliopamba moto vikiwa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe. Alifanikiwa kuokoka.

Baada ya kukaa Sfax kwa muda aliendelea na safari zake kuujuwa ulimwengu. Safari hii alifanikiwa kuwasili katika maeneo ya Mashariki ya Kati, akateremkia Bahari Nyekundu (Red sea) kupitia mji mtakatifu wa Makka, kisha akalivuka jangwa la Uarabuni na kuendelea na safari zake zilizomfikisha nchi za Iran na Iraq. Ulipofika mwaka wa 1330 akapita kwa mara nyengine tena katika Bahari Nyekundu hadi kufika visiwa vya Zanzibar ambapo katika maandishi yake alielezea k u w a a l i k u t a n a n a watu wa kisiwa hicho wakiwa ni Waislamu. Watu walio wakarimu na akazungumza nao kwa Kiarabu akasali nao. Aidha aliyasifu maji ya hapo kwa utamu wake. Kutoka Unguja akaelekea Kilwa nako huko hakupata tabu kuwasiliana na watu wa Kilwa, aliwasiliana nao kwa lugha ya kiarabu na al ivut iwa kukuta kuwa watu wake wana ustaarabu na wanaishi katika nyumba za mbao zilizoezekwa mapaa yake kwa makuti. Alibahatika kukutana na Mtawala wa Kilwa Sultan al-Hasan ibn Sulaiman akiwa ni katika kizazi cha Ali ibn al-Hassan Shirazi. Alivutiwa na mpango wa majenzi ya Kilwa yalivyokuwa ya kimpangilio na kuelezea kama ni mji uliokuwa na maendeleo. Aliuelezea M s i k i t i M k u u w a Kilwa, Msikiti uliokuwa mkubwa wenye kuvutia uliojengwa kwa mawe ya matumbawe.

Ulipofika mwaka wa 1332 aliendelea na safari zake kuelekea India a m b a p o i l i m c h u k u a miaka 8 kuweza kufika huko India bada ya k u t o k a m a e n e o y a Afrika ya Mashariki. I n d i a a l i p o k e l e w a

Ramani inayoonyesha njia alizopita Ibn Battuta

kwa mikono miwili na Sultan wa India, baada ya kustakimu hapo kwa muda akamua kuendelea na safari zake zilizoweza kumfikisha China, katika mwaka wa 1352 mshipa wa kurudi nyumbani ulimpiga akarudia hata katika maeneo ya Bahari Nyekundu na kuelekea Magharibi ya Afrika kat ika nchi ya Mal i nchi ambayo ina urithi mkubwa wa utamaduni wa Ki is lamu, a l ikaa katika mji wa Timbuktu akaitumia maktaba kubwa ya Timbuktu kujiongezea taaluma. Mji wa Timbuktu unaringia kazi kubwa iliofanywa na Mfalme Mansa Mussa ambaye n d i o a l i o w a p e l e k a walimu kutoka Misri kwenda kusomesha watu dini na kuandika vitabu mbalimbali. (Mansa Mussa ana makala zake 2 siku za mbele nitamuelezea).

Anapozungumzwa Ibn Battuta huzungumzwa zaidi juu ya safari zake bila ya kutajwa utaalamu wa masuala ya kidunia. Mbali ya taaluma ya Jiografia alikuwa mtaalamu wa fani ya Sayansi ya mimea (Botany). Aidha alibobea katika elimu ya Sayansi ya jamii. Tunafaidika

pakubwa na kazi za Ibn Battuta kutokana na maandishi yake mengi aliyoyaandika. Fani ya uandishi kwa wasomi wa Kiislamu imepotea. Waliopita waliandika sana na maandishi yao yalitoa mchango mkubwa katika

Maandishi ya Ibn Battuta

maendeleo ya sayari yetu hii.

Maandishi yake

Baadhi ya maandishi y a k e u n a p o y a s o m a unapata ladha namna alivyokuwa anazielezea j a m i i z a K i i s l a m u zilivyokuwa zinaishi na ustaarabu waliokuwa nao, nitadokowa mawili matatu juu ya hayo. Alipokuwa nchini Syria aliona mambo yaliomvutia kabisa . Syr ia i l io jaa

utamaduni na huruma. Syria ya leo inavurugwa na kupotezewa alama zote za athari za Kiislamu. Ibn Battuta aliandika yafuatayo:

“ U t a p o j u m l i s h a matumizi ambayo serikali kat ika nchi ya Syria yakifanyika katika karne ya 14 yalikuwa hayana kifani. Kukitengwa fungu la kuwasaidia wale wote wasiokuwa na uwezo wa kwenda Kuhiji Makka sio tu kusaidiwa kufika huko bali na matumizi yao ya kula na mambo madogo madogo, aidha wakisaidiwa wale ambao hawana pesa za mahari ya kuolea, aidha kukitengwa fedha za kuwapa familia ya bibi harusi waliokuwa wanyonge hawana vitu vya kumpa bi harusi, vi levile kukitengwa f e d h a k u w a s a i d i a wasafari walioishiwa k w a k u w a s a i d i a chakula na nguo na usafiri wakuwafikisha makwao. Kulikuwa na fungu la kuwaweka huru wafungwa na kuwasaidia maisha yao baada ya kutoka gerezani, aidha kukitengwa fungu la kuweka taa za barabarani na kuimarisha njia ya wapitao kwa miguu na

vipando.”Alipofika Iraq aliandika

haya: “Kisha tukawasili Baghdad mji mkuu wa Iraq ikiwa ni mwahali paliokua na amani, mji kati ya miji ya Kiislamu. Tulizikabili daraja mbili kama Hilla, ikiwa daraja hizo watu wanazipita usiku na mchana, kike kwa kiume. Sehemu za kukogea zil i jaa watu pomoni, sehemu hizo zilijengwa kwa kiufundi kabisa na kupakwa rangi za kupendeza na kuta zake zikiwa za mramar nyeusi. Maeneo hayo ya kukogea yalikuwa yana maji ambayo yakitokea Kufa na Basra saa zote na siku zote maji hayo yakiwa yakitiririka. Sehemu hizo za kukogea zil ikuwa zikimilikiwa na watu binafsi. Unapokwenda kukoga unapewa taula za kujifutia maji tatu, mmoja ikiwa ya kujifunga k i u n o n i u n a p o i n g i a kukoga na nyengine ya kujifutia maji na nyengine kuvaa kiunoni unapotoka kukoga.”

Vi l e v i l e a l i a n d i k a mambo aliyoyayaona katika visiwa vya Uturuki, Mongolia na visiwa vya Maldives. Aliyoyaona Uturuki na Mongoloa yalimsataajabisha kuona jamii ya watu wa hapo k u wa p a u h u r u u l i o m k u b wa wa n a wa k e . Aidha ki l ichomvutia katika kisiwa cha Maldives ni kuona wanawake vivazi vyao ni nguo za ming’aro.

Baada ya safari zake za miaka mingi kwa kipindi cha miaka 24 kuwa nje ya nyumbani mshipa wa kurudi nyumbani ulianza kumpiga na ulipofika mwaka wa 1355 aliwasili Morocco katika mji wa Tangier sehemu ambayo ndio alipofia na kuzikwa katika mwaka wa 1368 na kaburi lake limewekwa kuwa alama ya mvumbuzi huyu na wengi hulizuru kama tunavyotakiwa kuzuru waliokufa na kuomba dua.

W a t a a l a m u w a Kimagharibi hawaamini kuwa Ibn Battuta alifanya safari hizi bali wakionacho nikuwa alinukuu kazi za watu wengine. Hio yote ni kuwa kila kinachohusiana na taaluma na maendeleo ni cha Mzungu. Hutajwa mvumbuzi Vasco Dagama bila ya kudhukuriwa Tiro al iokuwa mjuzi wa kuongoza safari za baharini, Tiro alikuwa mtu mweusi.

Page 19: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

19 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015Makala

Watanzania wanahitaji kukombolewaInatoka Uk. 9Afrika Mashariki, kama si Afrika kwa ujumla. Kwa kweli inasikitisha kuona kwamba kwa nchi kama Tanzania, visa vya mauaji na ukatili vimeendelea kuwalenga watu wenye ulemavu wa ngozi.

Hivi karibuni tu, mtoto mweye umri wa miaka tisa mwenye ulemavu wa ngozi, Baraka Cosmas, anayeishi na wazazi wake kijijini Kipeta, mkoani Rukwa ameponea tundu la sindano kuuawa na watu wasiojulikana, baada ya kukatwa kiganja cha mkono nyumbani kwao. Mtoto huyo huyo ambaye ni mvulana a l ikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao. Kwa bahati, kamanda wa polisi katika mkoa w a R u k w a , J a c k o b Mwaruanda alithibisha kwamba mtoto huyo a n a p a t a m a t i b a b u hospitalini na hali yake inaendelea vizuri.

Tukio hilo ni la tatu kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja baada ya kuibuka kwa matukio mengine mawili ya watoto walemavu wa ngozi katika mikoa ya Mwanza na Geita kuuliwa. Pendo Emmanuel mkazi wa Ndami wilayani Kwimba mkoani Mwanza pamoja na Yohana Bahati, mkazi wa I le lema wilayani Chato mkoani Geita, ambao ni walemavu wa ngozi walitekwa hivi karibuni kwa nyakati tofauti. Yohana alitekwa Februari 15 mwaka 2015, ambapo aliokotwa akiwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa umekatwa mikono na miguu na kisha kufukiwa kwenye shimo. Shambulio hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino.

Wakati visa vya kuuawa kwa albino vikiripotiwa za id i kutoka nch in i Tanzania, Mtandao wa DW unaeleza katika taarifa yake kwamba vyombo vya usalama nchini Malawi, vimeeleza kuwa idadi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wanaouliwa nchini humo imepanda siku za hivi karibuni. Taarifa hiyo imebainisha kuwa hivi sasa nchini Malawi, watu wenye ulemavu wa ngozi wanaishi kwa w a s i w a s i m k u b w a , wakihofu kuuliwa na viungo vyao kutumika na watu wanaoamini kuwa watajipatia utajiri au madaraka. Kwa mujibu wa chama cha Albino nchini Malawi, mwaka h u u A l b i n o wa t a t u wameuliwa kikatili nchini humo.

"Tunawindwa kama

wanyama," amenukuliwa msemaji wa chama hicho kinachotetea haki za albino wapatao 10,000 wanaoishi Malawi akisema.

T a a r i f a k u t o k a Malawi zimeeleza kuwa m w a n a m k e m m o j a alikutwa amekufa, kichwa chake, miguu na mikono ikiwa imekatwa. Mbali na kufanya upelelezi kuhusu visa vya mauaji, polisi nchini humo inawatafuta albino wengine ambao hawajulikani walipo. Inaaminika kwamba viungo vya watu wenye u l e m a v u w a n g o z i

vinakwenda kuuzwa nchi jirani ya Tanzania. Taarifa ya DW inafafanua zaidi kwamba nchini Malawi, serikali imepiga marufuku shughuli za waganga wa kienyeji, kwani wao ndio wanasadikiwa kuwaagiza wateja wao wawaletee v i o n g o v ya a l b i n o . Wanaharakati wanasema baada ya serikal i ya Ta n z a n i a k u a n z i s h a kampeni ya kudhibiti mauaji ya albino, wahalifu sasa wamehamia Malawi. Wazazi wa watoto wenye u l e m a v u wa n a e l e z a kuogopa hata kuwaruhusu

watoto wao waende shule kwani hawajui kama watarudi salama au kama watatekwa. Ta k w i m u z i n a e l e z a kwamba tangu mwaka 2000, Albino wapatao 70 wameuliwa nchini Tanzania. Inaripotiwa kuwa jijini Dar es Salaam, viungo vya albino mmoja vinafikia bei ya hadi dola za Kimarekani 75,000 ambazo ni sawa na karibu shilingi milioni 140 za Kitanzania. Taarifa hiyo imebainisha kwamba Albino wako hatarini kwenye nch i ny ing i

za Kiafrika, zikiwemo Kenya, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Senegal. Shirika la kimataifa la "Under The Same Sun" linalotetea haki za watu hao linaripoti kuul iwa kwa a lb ino 140 katika nchi 25 za Kiafrika. Wengine 219 walikatwa viongo lakini wakaachwa hai. Madhila haya yote, yanachochewa na Imani kwamba Albino ana nguvu za miujiza. Aidha inaaminika kwamba jamii nyingine, kuzaliwa mtoto albino inaonekana kama laana ya mababu na punde tu akizaliwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi anauliwa.

K i m s i n g i h a t u k a t a i kuwepo kwa waganga wa tiba za jadi. Wapo waganga makini ambao wanafanya kazi zao kitaalam na kwa kuzingatia utu, taratibu na kanuni za kimatababu. Lakini ndani mwao wapo wezi, matapeli, wauaji na wachawi ambao kwa namna moja au nyingine, hawastahili kuachwa wakaendelea n a u h a l i f u wa o h u k u wakiharibu Watanzania akili zao na kuwageuza chumo la fedha haram kwa kuwaingiza katika shirki zinazoangamiza maisha na uhai wao. Kuwa kuwa ni utaratibu wa serikali kwa wafanyabiashara kuthibitishwa na kuwa na leseni za biashara zao na wanalipa kodi ya biashara zao, na kwa kuwa waganga wa mahospitalini nao kadhalika wanatambuliwa na serikali kwa leseni zao au ajira zao na wanalipa kodi kwa serikali, kuna haja kwa serikali kwa makusudi kabisa, kufanya ukaguzi wa kina kwa waganga wa kienyeji.

W a l e a m b a o watabainika kufanya s h u g h u l i z a o b i l a kuthibitishwa na kazi zao kutambuliwa na hata kusajiliwa kwa maana ya kupewa leseni na serikali, basi hao wapigwe marufuku kufanya kazi zao hizo.

K wa m t i n d o h u u , utasa idia kuwabaini wababishaji na washirikina ambao wanasabab isha wenzetu albino wateketee k u t o k a n a n a m a a g i z o ya hovyo na potofu kwa wananchi, ambayo msingi wake ni kuvunia hela bila kujali utu.

Lakini la msingi zaidi, Watanzania wabadilike. M a f a n i k i o ya h a k i n i matokeo ya fikra, mipango, jitihada, kujituma, dhamira ya dhati, kujiamini na kutokata tamaa. Tusitaraji kupata mafanikio ya haki kwa tamaa na haraka na kwa muda mfupi bila jasho, wala tusitaraji kufanikiwa kwa kuamini na kutegemea njia za shirki na za kudhulumu nafsi za wengine hata kuifanya Tanzania kuwa nchi ya laana.

BARAKA Cosmas, anayeishi na wazazi wake kijijini Kipeta, mkoani Rukwa ameponea tundu la sindano kuuawa na watu wasiojulikana, baada ya kukatwa kiganja cha mkono nyumbani kwao.

Page 20: ISSN 0856 - 3861 Na. 1168 JAMADIUL AWWAL 1436 MACHI …

20 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 201520 MAKALA AN-NUUR

20 JAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 13-19, 2015

Soma gazeti la AN-NUUR

KWA TSH 800/=kila Ijumaa

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

KUNDI la Waislamu w a n a n e k u t o k a V i s i w a n i Z a n z i b a r wanaotuhumiwa kwa Ugaidi, katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, wamepata Wakili kutoka Star Chambers Advocates.

Wa t u h u m i w a h a o k w a m u d a m r e f u w a l i k u w a h a w a n a Wakili, sasa watatetewa na Wakili Mohammed Tibanyendera, kutoka Star Chembers Advocates ya Jijini Dar es Salaam.

Wakili huyo katika kesi hiyo ya Suleiman O t h m a n M a u l i d n a wenzake saba, yenye namba 41 ya 2014, alianza kuonekana Jumatatu ya Machi 9, 2015, siku ambayo kesi hiyo ilitajwa kwa mara nyingine katika Mahakama ya Kisutu.

Hata hivyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliahirisha kesi hiyo mpaka Jumatatu ya Machi 23, 2015, ambapo itarudi kutajwa kwa mara nyingine tena Mahakamani hapo.

A k i o n g e a n a A n nuur, Katibu wa Kamati ya Maafa ya Shura ya M a i m a m u , U s t a d h i Ally Mbaruku, alisema kuwa siku hiyo (Machi 23,2015) Mahakamani hapo pataunguruma kesi zingine zinazowakabili Waislamu, wanaosota rumande kwa tuhuma za Ugaidi.

U s t . M b a r u k u anayefatilia kwa karibu kesi hizo za Waislamu, alizitaja kuwa ni kesi ya Ustadhi Jihadi Gaibuni, Mussa Haruna Lugeye na Mkewe.

Wengine ni Ustadhi Ally Nassoro Swala pamoja na Ustadhi Juma Zuberi.

Alisema, kesi ya Sheikh Farid na wenzake itakuwa Machi 18,205 na Machi 16, 2015, itakuwa siku ya kusikilizwa kesi ya Imamu Ally Athumani wa Tegeta, Jijini Dar es Salaam, katika Mahakama hiyo ya Kisutu.

A i d h a , K a t i b u Mbaruku, pia alizitaja kesi zingine za Waislamu

Watuhumiwa wa ugaidi wapata wakili

RIPOTI mpya iliyotolewa Jumatatu wiki hii kuhusu sekta ya wanyama pori nchini imeonesha kuwa rushwa ndio sababu kuu ya kuongezeka kwa matukio ya ujangili Tanzania.

Ripoti hiyo imetolewa baada ya utafiti uliofanywa na Mtandao wa Shirika lisilo la Kiserikali la Arusha ANGONETI, likishirikiana na KEPA, Jukwaa la Shirika lisilo la Kiserikali la Finland.

Aidha baadhi ya maofisa wa huduma za wanyama pori wamehusishwa na vitendo vya ufisadi katika ripoti hiyo.

Mmoja wa watafiti Bi. Joanita Mlay, alisema kuwa watu wengi walioulizwa wakati wa mchakato wa kufanya utafiti huo, walieleza kuwa wawindaji haramu wamekuwa wanatozwa faini ndogo na kwa upande mwingine, wanajamii wa kawaida wanaohusika na makosa madogo wakitozwa faini kubwa.

A i d h a a l i b a i n i s h a kwamba hata katika baadhi ya kes i ambazo tayar i zimeshafikishwa katika m a h a k a m a n i k u h u s u kadhia hii ya uwindajio h a r a m u n a u j a n g i l i , z i me k u wa z i k i f a n y i k a katika wakati mgumu, hasa pale mahakama inapotoa dhamana kwa watuhumiwa kwa mujibu wa sheria.

A l i s e w a t u h u m i w a wanapopata dhamana, wanapata muda wa kutosha kuingilia kesi kupitia rushwa na matokeo yake kes i hutupiliwa mbali. (DW).

Rushwa sababu kuu ya kuongezeka ujangili Tanzania

Na Bakari Mwakangwale

wanaotuhumiwa kwa ugaidi, zilizopo mikoani kuwa ni kesi ya Imamu Hamza wa Jiji Mwanza, itakayo tajwa machi 23, 2015, katika Mahakama ya Wilaya Mwanza.

A m b a p o , M j i n i Morogoro, Machi 20, 2015, Mahakama ya Mjini humo itasikiliza kesi ya

uchochezi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasis i za Ki is lamu, a m b a p o M a w a k i l i w a S h e i k h P o n d a , wataendelea na utetezi wao.

P ia a l i sema, J i j in i Arusha, Ijumaa ya Machi 13, 2015 (leo) itakuwa ni siku ya kutajwa kwa

kesi ya tuhuma za ugaidi inayowakabili Waislamu takriban 60, wakiwemo Imamu Hambari, Sheikh M u s t a p h a K i h a n g o pamoja na Sheikh Abdul-azizi Shaban.

Kesi hiyo ina zaidi ya miezi sita, upelelezi haujakamilika na Wislamu hao wapo rumande.

BAADHI ya watuhumiwa wa kesi ya ugaidi kutoka Zanzibar wakiwa mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam. (Picha kutoka Maktaba yetu)

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kushoto) akiongea na wakili wake.