cdf report / ripoti ya cdf

16
Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao Ripoti ya CDF

Upload: african-woman-child-feature-service

Post on 28-Mar-2016

275 views

Category:

Documents


8 download

DESCRIPTION

A Swahili report on how the Constituency Development Fund (CDF) can be used for development in Kenya Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao.

TRANSCRIPT

Page 1: CDF Report / Ripoti ya CDF

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia

CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Ripoti ya CDF

Page 2: CDF Report / Ripoti ya CDF
Page 3: CDF Report / Ripoti ya CDF

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Ripoti ya CDF

Page 4: CDF Report / Ripoti ya CDF

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

2

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

Hazina hii ya CDF ni mpango wa Serikali ya Kenya iliyotenga shilingi milioni 20 kwa kila eneo la ubunge nchini kila mwaka. Dhamira ama lengo la hazina hii ni kurahisisha miradi ya maendeleo ama ustawi katika maeneo hayo. Huidhinishwa ama kupitishwa na she-ria za Bunge kisha pesa hizo hutolewa kwa Kamati ya Kitaifa kupitia akaunti ya benki maeneo hayo.

Aina ya Miradi• Miradi yote ya maendeleo sharti iwe ni

ile ya manufaa kwa jamii nzima• Pesa hizo pia zinaweza kutumiwa kughar-

amia ama kulipia ujenzi na uwekaji vi-faa vya afisi hiyo ya miradi.(Haitapaswa

Page 5: CDF Report / Ripoti ya CDF

3

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

iwe ni afisi ya kisisasa ya Mbunge).• Mradi wa ujenzi wa afisi, kadhalika

vifaa vilivyomo humo kama viti, meza, kabati na kadhalika, vyote hivyo vitachukuliwa kama mradi wa maendeleo

• Mpango wa kutoa msaada wa kifed-ha kwa elimu, utachukuliwa kama wa kimaendeleo, lakini hautapa-ta zaidi ya asilimia 10% ya hazina ya kila mwaka kwa kila eneo la ubunge.

Miradi Inayoanzishwa na JamiiHazina hii, KAMWE sio ya kufaidi makundi ama shughuli za kisiasa wala hata za kidi-

ni, ila tu pale kama iwapo makundi hayo yanatoa huduma kama wawakilishi. Mira-di ya kufaidi watu binafsi, pia imeachwa nje ya mpango huu.

Utaratibu na Uandikishaji wa Mapendekezo ya MiradiOrodha ya mapendekezo ya miradi itakayopaswa kushughulikiwa, itapaswa itumwe kwa katibu mkuu wa bunge na Mbunge mhusika. Kuna fomu maalum itakayopaswa ijazwe kwanza. Hii ita-paswa ifanywe kabla ya mwezi wa Feb-ruari, kila mwaka, ama mwezi mwingine wowote kama anavyoweza kuamua Waziri wa Fedha.

Page 6: CDF Report / Ripoti ya CDF

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

4

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

Orodha hiyo itakuwa ni pamoja na mi-radi na gharama zao. Hayo yote, hata hivyo, yatachujwa na kamati ya Bunge na kamati ya hazina ya eneo la ubunge, ambazo baadaye zitapendekeza map-endekezo hayo yafikishwe kwa Waziri wa Fedha.

Miradi hiyo yote, zitapewa nambari ili kuhakikisha kwamba kila mradi fulani unahifadhi namba ile ile hadi shughuli zake zimekamilika.

Kutekelezwa kwa MiradiMiradi yote iliyokusudiwa itapaswa kutekelezwa na idara za serikali wilay-

ani. Iwapo mradi fulani utahusu idara mbalimbali za serikali, idara iliyota-jwa kwenye mapendekezo ya bajeti, itakuwa mstari wa mbele kwa utekele-zaji wa mradi kama huo.

Iwapo mradi utahusisha ununuzi wa vifaa, basi, vifaa hivyo vitabakia kwa utumizi mahsusi ya eneo hilo la ubunge. Kamati ndogo ya lokesheni pamoja na ingine ya ustawi zinaweza kuanzishwa kwa madhumuni ya kuchunguza jinsi kazi inavyondelea ama inavyofanya na kamati ya maendeleo katika sehemu kama hiyo.

Page 7: CDF Report / Ripoti ya CDF

5

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

Kazi zote zinazohusiana na mradi zita-paswa kufuata utaratibu ulioko wa seri-kali wa ununuzi wa vifaa. Maombi yote ya tenda yatapaswa kuwasilishwa kwan-za mbele ya kamati ya mipango wilayani ambapo wakuu wa idara ya wizara inay-ohusika katika kila wilaya watapaswa kuchunguza jinsi miradi iliyoko chini yao inayotekelezwa, kwa kuhakikisha kwamba wanahifadhi rekodi zote za ma-tumizi ya fedha kwa miradi kama hiyo.

Afisa wa maendeleo wilayani katika kila wilaya atapaswa kuweka rekodi ya risiti zote na jinsi fedha zilivyotumika kila mwezi na kwa kila mradi, kisha kuwasili-

sha akaunti yake kwa kamati ya kitaifa. Iwapo jamii itaomba, itaweza kuwateua wawakilishi wao kuangalia masilahi yao kwa mradi wowote ule unaoendelea ka-tika sehemu yao.

MashartiFedha zilizotengwa kwa minajili ya mra-di fulani hazitapaswa kamwe zipelekwe kwingineko wakati wa msimu wa fedha za serikali kwa shughuli nyinginezo ka-tika eneo la ubunge ama kwingineko. Iwapo mradi umefutiliwa mbali waka-ti wa msimu huo wa fedha za serikali, pesa hizo zitapaswa kurejeshwa kwenye hazina kuu ya serikali lakini kutakuwepo

Page 8: CDF Report / Ripoti ya CDF

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

6

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

na rekodi ya kuonyesha mahali ambako pesa hizo zilitolewa.

Gharama za kuwa na afisi maeneo ya ubunge na marupurupu mengineyo hazitapaswa ziwe zaidi ya asilimia 3% ya jumla ya fedha zinazotolewa kila mwaka, (Ksh.600,000). Asilimia 5% ama shilingi milioni moja ya jumla inayotolewa kwa kila eneo la ubunge hazitatengwa ila kubakia kama ‘hazina ya dharura’ ambapo pesa kama hizo zinaweza kutolewa iwapo kumezuka hali ya dharura inayohitaji msaada ka-tika eneo la ubunge.Mpango ambapo mtu fulani atapaswa

kuzawadiwa kifedha ama kwa njia yoy-ote ile, hautaruhusiwa. Kamati ya CDF itahakikisha kwamba mashauri ya ku-faa yanafanywa kati yake na idara za serikali zinazohusika kuhakikisha kuwa makadirio ya gharama zitakazohusi-ka ni sahihi na ya ukweli. Cheki ama hundi zote za malipo zitapaswa zifuate utaratibu uliowekwa na serikali, kabla malipo yoyote kutolewa.

Akaunti ya benki itakuwa tofauti na ile ya kawaida ya wilayani. Fedha zita-tolewa tu wakati zinapohitajika baada ya rezolusheni ya kamati ya maendeleo ya CDF, kupitishwa. Fedha zote zitaba-

Page 9: CDF Report / Ripoti ya CDF

7

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

kia kwenye akaunti ya CDF na hakuna uwekezaji mwingine wowote utaruhusi-wa kwa dhamira ya kutumiwa kwa fedha kama hizo.

Itapaswa ikumbukwe kuwa hakuna Mbunge wala Diwani yeyote atakuwa na saini yake kwenye hazina hiyo. Mtu yeyote yule ambaye atafuja fedha kama hizo atakuwa akivunja sheria ambayo adhabu yake ni kifungo cha hata kufi-kia miaka mitano gerezani ama faini Ksh 200,000 ama zote pamoja.

Wenye Kutia Saini Kwenye Cheki/HundiNi watu watatu tu ndio wanaoruhusiwa kutia saini ya malipo kwa cheki ama hundi za CDF. Kati ya hao ni mteuzi kutoka kwa kamati ya miradi wilayani na mwingine mteuzi wa CDF.

Kamati ya Maendeleo Eneo la Ubunge (CDC)

• Kamati hii itapaswa ichaguliwe na Mbunge kwa muda wa siku 30 wakati wa kufunguliwa kwa bunge jipya

• Wanachama wake hawatapaswa kuzidi idadi ya watu 15

Page 10: CDF Report / Ripoti ya CDF

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

8

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

Wanaokusudiwa Kuwemo• Mbunge – akiwa kama mwenyekiti

na mwenye mamlaka ya uteuzi • Madiwani wawili kutoka eneo

lake• Afisa Tawala (DO) mmoja wa se-

hemu hiyo• Wawakilishi wawili wa kundi la

kidini katika sehemu hiyo• Wawakilishi wawili wa kiume ka-

tika eneo hilo• Wawakilishi wawili wa kike se-

hemu hiyo• Mwakilishi mmoja wa vijana ka-

tika eneo hilo• Wateuzi wawili kutoka shirika

maarufu lisilo la kiserikali (NGO) kwenye eneo hilo.

Utendaji KaziMbunge wa kuchaguliwa atapaswa mara moja, kila mwaka kuandaa mikutano ya maendeleo sehemu za lokesheni

• Kila lokesheni itapaswa ilete orodha ya miradi yake inayopaswa kushughulikiwa haraka mbele ya kamati hii

• Kamati ya CDC itapaswa iwe iki-jadili orodha kama hiyo kuona ni mradi gani utapaswa kupewa ki-pau mbele wakati huo na ni gani utashughulikiwa baadaye kisha

Page 11: CDF Report / Ripoti ya CDF

9

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

kuwasilisha ripoti hiyo kwa bunge• Kushauriana na idara za serikali zi-

nazohusika kuhakikisha kwamba

makadirio ya fedha za mradi/mi-radi ni ya kweli

Kamati ya Miradi WilayaniWajibu:

• Kushirikisha utekelezaji wa miradi iliyonufaika na fedha za CDF na shu-ghuli nyinginezo ambazo zimepend-ekezwa na kamati ya Kitaifa.

• Kamati ya miradi wilayani, inawe-za wakati wa kutekeleza shughuli zake chini ya Kanuni hii ya bunge,

kuzuru kwa ghafla sehemu ambako miradi kama hiyo ya maendeleo in-ashughulikiwa

Wanachama• Wabunge wote wilayani aidha wa

kuchaguliwa ama kuteuliwa.• Wenyeviti/Mameya wa mabaraza

ya wilaya.• Mkuu wa wilaya (DC)• Afisa wa maendeleo wilayani (DDO)

ambaye atakuwa ndiye katibu wa kamati ya miradi wailayani

• Mwenyekiti wa kamati ya maen-deleo eneo la ubunge (CDC) am-baye atapaswa awe ni Mbunge

Page 12: CDF Report / Ripoti ya CDF

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

10

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

• Mhasibu mkuu wa wilaya. Wakuu wa idara ya serikali wanaweza pia kuhudhuria mikutano kama maafi-sa waalikwa

• Muda wa kuhudumu miongoni mwa Wabunge ama Madiwani walio-chaguliwa kwa kipindi cha miaka miwili hadi mwisho wa msimu wa bunge

• Kila Mbunge atapaswa awe akiorod-hesha orodha ya miradi atakayo-taka zishughulikiwe

• Kamati ya miradi wilayani ita-paswa kuhakikisha kwamba miradi zitakazoshughulikiwa hazifanani katika eneo moja na kwamba kila

mradi utakuwa manufaa kwa jamii nzima wilayani.

• Kupendekeza orodha ya miradi kwa katibu mkuu wa bunge kupitia kwa Mbunge kutoka kila eneo na ambaye hatapaswa kukalia map-endekezo kama hayo bila sababu

Kamati Teule ya Bunge kuhusu HazinaKamati hii ilibuniwa chini ya sheria za bunge kama kamati teule

UanachamaWanachama wake watakuwa sawa na kamati zingine teule za bunge, kwa

Page 13: CDF Report / Ripoti ya CDF

11

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

mfano, kuwepo kwa mwenyekiti na sio zaidi ya Wabunge 10 ambao si mawaziri/wasaidizi wa mawaziri. Uwakilishi wa usawa kwa vyama vya kisiasa bungeni, utapaswa kuwepo.

Utendaji Kazi• Kufikiria juu ya mapendekezo ya mi-

radi sehemu za wilayani kisha kutoa mapendekezo hayo kwa katibu mkuu wa bunge

• Kutoa mapendekezo ya majina ya watu watakaohitajika na ambao wataidhinishwa na bunge chini ya sheria za CDF

• Kuhakikisha kuwa sheria hiyo ime-

fuatwa, na kuweza pia kupendekeza kufanywa kwa mabadiliko kisha ku-wasilisha ripoti kwa bunge kila baa-da ya miezi sita

• Kuchunguza kuona kuwa maongozi yaliyowekwa ya kutekelezwa kwa mi-pango hii yameshughulikiwa haraka

Wanachama wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi ya Ustawi Maeneo ya Ubunge

• Mwenyekiti (kutoka Wizara ya Fed-ha), Katibu Mkuu Wizara ya Mipango ya Uchumi

• Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Mikoa

Page 14: CDF Report / Ripoti ya CDF

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

12

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika

maeneo yao

• Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo• Katibu Mkuu wa Bunge• Watu wanane walioteuliwa na

waziri kutoka Kenya Farmers Union na Institute of Engineers of Kenya

• Kenya National Chamber of Com-merce, Kanisa Katoliki, KNUT, Baraza la Mashirika yasiyo ya kiseri-kali (NGO), Baraza Kuu la Waislamu nchini (SUPKEM), afisa mmoja mtu-mishi wa umma kusimamia hazina (kama mteule na vile vile katibu)

• Majina na maelezo ya wanachama wa kamati ya kitaifa yataidhinish-wa na rais.

Wajibu waoKuhakikisha kwamba fedha zimetolewa kwa usawa kwa kila eneo la ubunge na kwamba kuna usimamizi boraKutayarisha ripoti na rekodi zote kutoka maeneo ya ubunge kisha kuziwasilisha kwa bunge.Katibu wa kamati hii atachunguza na kuhakikisha kwamba anasimamia vilivyo shughuli za siku hadi siku za matumizi ya fedha hizo huku akihakikisha kuwa rekodi zote za kifedha ziko sawa kabla hatimaye kuzituma kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za fedha serikalini.

Page 15: CDF Report / Ripoti ya CDF
Page 16: CDF Report / Ripoti ya CDF

Imehaririwa na kuchapishwa

na AWC Feature Service.

Imedhaminiwa na shirika la Swedish International Development

Cooperation Agency (SIDA).