bunge la tanzania majadiliano ya bunge mkutano wa...

217
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA TISA Kikao cha Tano – Tarehe 13 Novemba, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Maswali Waheshimiwa, tunaanza Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Ritta Kabati. Na. 54 Kuridhia Mkataba Namba 189 wa ILO MHE. RITTA E. KABATI aliuliza:- Serikali ya Tanzania ilisaini Mkataba Namba 189 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) tangu tarehe 16 Juni, 2011 na Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete alishawahi kutamka kuwa, Tanzania haina tatizo na Mkataba huo.

Upload: others

Post on 19-Oct-2019

8 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE

___________

MKUTANO WA TISA

Kikao cha Tano – Tarehe 13 Novemba, 2017

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Tukae.

Katibu!

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Maswali Waheshimiwa, tunaanza Ofisiya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Ritta Kabati.

Na. 54

Kuridhia Mkataba Namba 189 wa ILO

MHE. RITTA E. KABATI aliuliza:-

Serikali ya Tanzania ilisaini Mkataba Namba 189 waShirika la Kazi Duniani (ILO) tangu tarehe 16 Juni, 2011 na RaisMstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete alishawahikutamka kuwa, Tanzania haina tatizo na Mkataba huo.

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

Je, kuna kikwazo gani kinachokwamisha kuridhiaMkataba huo wa ILO Namba 189 wa Kazi za Staha kwaWafanyakazi wa Majumbani wakati Baraza la Wafanyakazi(LESCO) limeshapendekeza kuridhia?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa RittaKabati, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Tanzaniakama nchi mwanachama wa Shirika la Kazi Duniani ilishirikikikamilifu katika majadiliano na upitishwaji wa Mkataba yaKimataifa wa ILO wa Wafanyakazi wa Majumbani Namba189 wa mwaka 2011 ambao unalenga kukuza kazi za stahakwa wafanyakazi wa majumbani. Aidha, hadi kufikia tarehe30/08/2017 mkataba huo umeridhiwa nan chi 24 kati ya nchiwanachama 187 ambapo nchi za Afrika zilizoridhia mkatabahuu ni tatu ambazo ni Afrika Kusini, Mauritius na Guinea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha napenda nielezeekuwa Serikali inathamini mchango wa wafanyakazi wamajumbani katika kujenga uchumi wa nchi. Hii ndio maanaBunge lako Tukufu lilitunga Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini,Namba 6 ya mwaka 2004, ambayo inazitambua haki zawafanyakazi wa majumbani kama ilivyo kwa wafanyakaziwengine. Vilevile kwa upande wa Zanzibar ipo Sheria ya Ajira,Namba 11 ya mwaka 2005.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuridhia mikatabayote ya kimataifa ikiwemo ya Shirika la Kazi Duniani siku zoteSerikali imekuwa ikizingatia maslahi mapana ya nchi na ustawiwa wananchi ikiwemo wafanyakazi kwa ujumla. EndapoSerikali itajir idhisha kuwa mazingira na ustawi wawafanyakazi kwa sheria zilizopo hakuna ustahimilivu, Serikaliitafanya maamuzi stahiki.

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hil i naombanilihakikishie Bunge lako Tukufu kuwa kwa kushirikiana nawadau wote vikiwemo vyama vya wafanyakazi na vyamavya waajiri, Serikali itaendelea kuimarisha utekelezaji wa sheriaza kazi, ili kulinda haki za wafanyakazi wa majumbani pamojana kujenga uelewa wa wadau kuhusu matakwa ya mkatabana haki za sheria za wafanyakazi hao.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kabati.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali madogomawili na nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake.

Je, Serikali inasaidiaje kufuatil ia wafanyakaziwahamiaji nchi za Uarabuni na kwingineko ambakowanateseka bila kuridhia mkataba huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwatumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu ambao wamekuwawakitafutiwa kazi kupitia hizi wakala za ajira (EmploymentAgency), lakini kumekuwa na malalamiko ya kupunjwa hakizao.

Je, Serikali inachukua hatua gani ili kulinda haki zawafanyakazi ambao wanapata ajira zao kupitia wakalahawa, pamoja na madalali ambao wamekuwawakiwatafutia wafanyakazi wa majumbani?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake lakwanza, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingiya kwamba tuendelee kuangalia mazingira bora ya namnaya ku-ratify mkataba huu hasa pale ambapo kama nchitutakuwa tumejiridhisha kwamba, mazingira ni rafiki na hivyokuusaini mkataba huo ambao utasaidia sana katika kulindahaki za wafanyakazi wa ndani, lakini vilevile ambaowanatoka nje ya nchi, kwa maana ya Watanzania.

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

Mhweshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusu Wakalawa Ajira; kama nilivyokuwa nikijibu katika maswali mengineambayo yamewahi kuulizwa katika eneo hili, ni kwambapale katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kazi, Vijana naAjira, ipo taasisi ambayo inashughulikia masuala ya ajira kwamaana ya wakala wa ajira ambaye anaitwa TaESA. Na raiyetu ilikuwa ni kwamba, wafanyakazi wote wa kitanzaniaambao wanakwenda kufanya kazi nje ya nchi ni lazimawapitie TaESA, ili tuwatambue tujue na katika nchi ambazowanakwenda. Tumefanya hivyo kwa sababu wakiendakatika njia ambazo si sahihi, sisi kama Wizara si rahisi sanakuweza kufahamu akina nani wako wapi na ndio maanatunawataka kwamba wote wapitie katika ofisi zetu na sisihuwa tunaongea na Balozi husika, ili waweze kushughulikiwamatatizo pale wanapopatwa na matatizo nje ya nchi,ikiwemo ukosefu wa mikataba na haki nyingine.

Na. 55

Serikali Kusaidia Miradi ya Ujenzi wa Vituo vya Afya

MHE. EZEKIEL M. MAIGE aliuliza:-

Wananchi wa Jimbo la Msalala kwa kusaidiana naMbunge wao wameanza ujenzi wa Vituo vya Afya Bugarama,Mega, Ngaya na Isaka na miradi hiyo ipo katika hatua nzuri.

(a) Je, Serikali imejipangaje kusaidia miradi hiyo yaujenzi wa Vituo vya Afya?

(b) Je, Serikali imejipangaje kukamilisha maboma zaidiya 28 ya zahanati kwenye vijiji mbalimbli Jimboni Msalala?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ni mara yanguya kwanza kusimama hapa kujibu maswali, naombauniruhusu nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingiwa rehema kwa kunijalia afya na nguvu kuweza kusimama

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

mbele ya Bunge lako Tukufu. Pili, naomba nimshukuruMheshimiwa Spika, Naibu Spika na Uongozi wote wa Bungekwa malezi na maelekezo ambayo nimepata, bila kusahauKamati ya Bajeti, chini ya Uenyekiti wa Mheshimiwa HawaGhasia kwa malezi na ushirikiano ambao nimekuwanikiupata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee naomba nimshukuruMheshimiwa Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani yake kwangukwa kuniteua kuhudumu katika nafasi ya Naibu Waziri, Ofisiya Rais – TAMISEMI. Uteuzi uliopokelewa kwa mikono miwilikwa wananchi wa Kalambo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumlawake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya utangulizi huo,kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naombakujibu swali la Mheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige, Mbungewa Msalala, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napendakutoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Mbunge waJimbo la Msalala kwa jitihada anazofanya katikakuwahamasisha wananchi wake kuibua na kuanzisha miradimingi ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya katikaJimbo lake la Msalala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya yaMsalala ina jumla ya vituo vya afya vitatu ambavyo niLunguya, Chela pamoja na Bugarama vilivyosajiliwa kwamujibu wa sheria. Kati ya vituo hivyo, ni vituo viwili ambavyoni Kituo cha Afya cha Lunguya na Chela ndivyo vinavyotoahuduma za upasuaji wa dharura kwa akina mamawajawazito.

Aidha, ujenzi wa vituo vingine vitatu ambavyo niIsaka, Ngaya na Mega upo kwenye hatua mbalimbali zaujenzi ambapo lengo la Serikali ni kuwa ifikapo mwaka 2020vituo hivi viwe vimekamilisha miundombinu muhimuinayohitajika kustahili kuwa vituo vya afya.

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya yaMsalala ina jumla ya maboma 31. Miongoni mwa mabomahayo, matatu ni vituo vya afya tarajiwa ambavyo ni Isaka,Mega na Ngaya. Aidha, kwa sasa Vituo vya Mega na Ngayamaboma yamepauliwa katika jengo la wagonjwa wa nje(OPD) ambapo Boma la Kituo cha Afya cha Isaka lipo kwenyehatua za lenta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2016/2017 Serikali iliweza kukamilisha ujenzi wa zahanati mpyanne kwa gharama ya kiasi cha shilingi milioni 277 na sabaambazo zote zipo katika kata ambazo zilikuwa hazinahuduma za afya kabisa. Zahanati hizo zipo katika Vijiji vyaNyaminje, Mbizi, Mwanase na Mwakata ambapo kukamilikakwake kumepunguza adha ya wananchi kutembea umbalimrefu kutafuta huduma ya afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika mpango wakitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoahuduma za dharura kwa upasuaji wa akina mama,Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imepatiwa kiasi cha shilingimilioni 400 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kujenga wodi yawanawake, nyumba ya watumishi, jiko, jengo la kuhifadhiamaiti na ukarabati wa miundombinu ya nyumba za watumishiiliyochakaa katika Kituo cha Afya cha Chela. Kituo cha Afyacha Chela tayari kina jengo la upasuaji, wodi ya wazazi,maabara, kichomea taka, shimo la kutupia kondo la nyumana mfumo wa maji safi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo katikabajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetenga kiasicha shilingi 336,742,394 za ruzuku ya maendeleo( CDG) kwaajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati katika vijiji sabavya Nyamigege, Gula, Ikinda, Kalole, Jomu, Buchambagana Ndala, kati ya hayo maboma 31.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Maige.

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini naomba kwa

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

sababu ndiyo nazungumza mara ya kwanza baada ya sakatala makinikia kuwa limepata mwelekeo, nimpongeze sanaMheshimiwa Rais kwa hatua alizochukua. Hatua ambazozimekuwa ni kilio changu na kilio cha wananchi wa Msalalakwa miaka yote toka Mgodi wa Bulyanhulu ulipokuwepopale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba niulizemaswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwa sababu,wananchi kama ambavyo Mheshimiwa Waziri amesema,wameitikia vizuri sana katika kukabiliana na tatizo la uhabawa huduma za afya katika Halmashauri na jimbo lao na kwasababu, changamoto ambayo ipo ni upatikanaji wa fedhaSerikalini na kwa bahati nzuri tayari tumeshapata uhakikakwamba, tutalipwa zaidi ya bilioni 700 kutika kwenyemakinikia.

Je, Serikali inaweza sasa ikakubaliana na ombi langukwamba ni vizuri tukapata angalao shilingi bilioni 3.4 ambazozinatakiwa kuyakamilisha maboma yote haya, ili wananchihawa wasione nguvu zao zikiharibika kwa sababu mengineyana zaidi ya miaka saba toka yalipoanzishwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa tayaritumeshaletewa shilingi milioni 400 kwa ajili ya uboreshaji waKituo cha Afya cha Chela, fedha ambazo pamoja nakwamba ni nyingi, lakini bado hazitoshi kwa sababu,malengo ni makubwa zaidi. Je, Serikali inaweza ikakubalianana ushauri wangu kwamba, kwa sababu lengo nikupelekahuduma kwa wananchi wengi zaidi na kuna maboma tayarikwenye Vituo vya Afya vya Isaka, Mega na Lunguya ambavyokama alivyoeleza Mheshimiwa Waziri kwamba viko kwenyehatua mbalimbali. Je, Waziri anaweza akatukubalia ombiletu kwamba fedha hizi tuzigawanye kwenye hivi vituo, iliangalao navyo viweze kufunguliwa halafu uboreshajiutakuwa unaendelea awamu kwa awamu kadri fedhazinavyopatikana kuliko kukaa na kituo kimoja na vinginevikaishia kwenye maboma kama ilivyo sasa?

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaMwenyekiti, juu ya ombi la uwezekano wa kutizama hii bilioni3.4 zitumike ili kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya pamojana zahanati; kimsingi hitaji ni kubwa sana, lakini si rahisi kablaya kufanya hesabu kujua katika mahitaji mengine kiasi ganikiende upande wa afya, kwani vipaumbele ni vingi. Kwahiyo, ni vizuri, ni wazo jema likachukuliwa likafikiriwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juu ya shilingi milioni 400ambazo zimepelekwa, Mheshimiwa Mbunge anaombakwamba ziruhusiwe zihame kwenda kwenye maeneomengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi i l i tuwezekukamilisha kituo cha afya kwa mujibu wa standard, lazimatuwe na uhakika chumba cha upasuaji kipo, wodi ya wazazikwa maana ya akina mama na watoto, wodi ya akina babaipo, maabara, nyumba za watumishi za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachowaomba naniziagize halmashauri zote, pale ambapo pesa zimeletwana Serikali si lazima, eti pesa hiyo iishie hapo, itumike busarakuhakikisha kwamba, kwa utaratibu wa Force Accounttunatumia pesa ili ikibaki tukiwa na serving hakuna dhambiya kuhakikisha kwamba, pesa hizo zinaweza zikahamiakwenda kumaliza matatizo mengine. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Qambaloatafuatiwa na Mheshimiwa Bonny.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Ni sera ya Serikali kuwa na hospitali katika ngaziya Wilaya ili kutoa huduma ya afya kwa wananchi wetu.Wilaya ya Karatu ina umri wa zaidi ya miaka 20 na hainaHospitali ya Wilaya. Ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili yaujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karatu? Ahsante.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaMwenyekiti, kimsingi naomba niziase Halmashauri zote, niwajibu wetu wa kuhakikisha kwanza tunaanza kwa kutengamaeneo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za afya, lakini kamahiyo haitoshi, kwa kushirikisha wananchi ni vizuri tukaanzahalafu Serikali ikaleta nguvu yake. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbatia.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana. Kata ya Marangu Magharibi yenye vijiji sabahaina zahanati hata moja na hasa vijiji vya Kiraracha naKitowo wako kwenye hali mbaya sana. Mbunge kwakushirikiana na wananchi wameweka nguvu zao wanajengazahanati kwa sasa na imefikia hatua za mwisho.

Nini commitment ya Serikali angalau milioni 20 yadharura, ili kata hii iweze kupata kituo cha afya cha kisasa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaMwenyekiti, katika fursa niliyopata ya kutembelea Mkoa waKilimanjaro nilijionea. Nilienda Moshi Vijijini nikakutana nawananchi wa Kiafeni, nikakuta kwamba hawakai wakasubiriSerikali ifanye, kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge na yeyeanakiri na wana utaratibu mzuri, wanasema siku ya utawalawanakwenda kushiriki wananchi kwa ujumla wake. Nguvuambayo inatolewa na wananchi ukishirikisha na nguvu yaSerikali nina imani hata hiyo kazi ambayo imefanywa nawananchi anaosema Mheshimiwa Mbatia, hakika kwakutumia uwezo wao wa ndani, kwa maana ya commitmentkutoka katika Halmashauri, naomba niitake Halmashauriihakikishe kwamba wanajibana il i huduma ambayoinahitajika kwa wananchi iweze kufikiwa kwa kumaliziazahanati.

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Ghasia.

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,asante na mimi napenda kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la MtwaraVijijini, Kata ya Mambo Pacha Nne na Kata ya Tangazo, Kijijicha Kilambo, wameanza mchakato wa kujenga vituo vyaafya na michango ya wananchi inaenda kwa kasi kubwa.

Je, Serikali itatusaidiaje katika kukamilisha ujenzi wavituo vya afya katika Kata ya Tangazo, Kijiji cha Kilambo naKata ya Mango, Pacha Nne?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuruMheshimiwa Mbunge kwa sababu, miongoni mwa maeneoambayo alileta kama request katika Jimbo lile la Mtwara nieneo hilo kwa sababu liko linapakana na Msumbiji.

Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba, katika vipaumbele vyetu vya sasa katika programutunayoanza nayo kabla ya mwezi wa pili, maeneo yaletumeyapa kipaumbele na tumeyaingiza katika mpango wetuwa bajeti ya muda katika hizi funds ambazo tunazipatakutoka kwa wafadhili mbalimbali. (Makofi)

Na. 56

Kuboresha Miundombinu ya Elimu – Mji wa Tarime

MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:-

Kufuatia utoaji wa elimu ya msingi bure, shule zamsingi na sekondari ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarimezimekuwa na upungufu mkubwa wa madarasa namadawati hadi kufikia walimu kulazimika kufundishia chiniya mti na wanafunzi walio madarasani wanakaa kwenye

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

sakafu kwa idadi kubwa kinyume na matakwa ya Sera yaElimu.

Je, ni nini mpango wa Serikali wa kuhakikisha shulehizo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarime zinaondokanana changamoto za miundombinu ya kufundishia na kujifunziaili kutoa elimu bora?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Esther Nicholas Matiko, Mbunge wa Tarime Mjinikama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto yamiundombinu ya elimu nchini ni matokeo ya mwitikiomkubwa wa wananchi katika utekelezaji wa Mpango waElimu Bila Malipo ambao umetoa fursa kwa watoto wotewenye umri wa kwenda shule kupata fursa hiyo. Shule 30 zamsingi katika Halmashauri ya Mji wa Tarime zinahitaji vyumbavya madarasa 625, vyumba vya madarasa vilivyopo ni 215na upungufu ni vyumba vya madarasa 410. Aidha, madawatiyanayohitajika ni 8,888; madawati yaliyopo ni 6,066 naupungufu ni madawati 2,823.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule nane za sekondarikatika Halmashauri ya Mji wa Tarime zinahitaji kuwa navyumba vya madarasa 133, madarasa yaliyopo ni 104 maupungufu ni madarasa 29. Aidha, katika shule hizo kuna ziadaya madawati 421 kutokana na mwitikio mzuri wa wananchina jitihada za Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo kupitia fedhaza kuchochea Maendeleo ya Mfuko wa Jimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2017/2018 Serikali imetenga shilingi 119,000,000.00 kwa ajili yakukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 16, matundu19 ya vyoo na kuongeza madawati 154 katika shule za msingi.Vilevile Serikali imetenga shilingi 172,500,000 kupitia ruzuku ya

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

maendeleo na mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wavyumba vya madarasa 22 na matundu ya vyoo 72.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kufuatia majibu ya Mheshimiwa Waziri, ni dhahirikabisa imeonyesha ni jinsi gani miundombinu ya kujifunziana kujifunza katika Halmashauri ya Mji wa Tarime hairidhishina inapelekea matokeo mabaya kwa ufaulu wa wanafunzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa wananchi waTarime wameitikia sana wakishirikiana na wadau mbalimbaliikiwepo mimi mwenyewe Mbunge. Tumejenga madarasamengi lakini mengi yamekaa bila kuezekwa na kwa kuwakuna Shule ya Msingi Mtulu ambayo imejengwa na wananchikwa kujitolea madarasa sita pamoja na ofisi lakini Mkurugenziwa Halmashauri ya Mji amezuia ile shule wananchiwasiendelee kujenga kwa kile anachokiita kwamba nimgogoro wa ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa sasa kupitiaWizara hii ambayo ipo chini ya Ofisi ya Rais na Rais anamamlaka ya kubadilisha matumizi ya ardhi, wawatie moyowananchi wale waliojenga yale madarasa ili sasa wawezekuamuru ile shule iendelezwe ili kupunguza adha ya upungufuwa madarasa katika Halmashauri ya Mji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pil i, katikaHalmashauri ya Mji kuna shule moja ambayo inatumiwa nashule tatu, Shule za Msingi Azimio, Mapinduzi na Sabasaba.Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI kipindi hicho akiwa NaibuWaziri alitembelea sisi kama Halmashauri ya Mji tunataka ileshule ijengwe ghorofa ili sasa walimu wasikae kwenye mtikama Ofisi, wanafunzi wasifundishiwe nje chini ya mti,wanafunzi wasirundikane 120 kwenye darasa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini sasa Serikaliisiweze kutumia ile asilimia tano ambayo walisema Wazirianaweza akapeleka kwenye matumizi mbalimbali kama

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

tulivyoona ilivyoenda Chato kwenye uwanja wa ndege. Kwanini msijenge ghorofa katika shule ile kwenye zile asilimia tanoambazo ni zaidi ya shilingi trilioni 1.7 ili sasa kupunguza adhaya ukosefu wa madarasa katika Mji wa Tarime? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaMwenyekiti, wanasema ukisikia upande mmoja, hakikaupande ambao haujasikilizwa utakuwa lazima umekosa.Itakuwa ni vizuri tukajir idhisha sababu ambazozimesababisha Mkurugenzi azuie uendelezaji wa hiyo shule ilitunapokuja kutoa taarifa iwe ni taarifa ambayo iko balanced.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishiembunge, miongoni mwa maeneo ambayo nitatembelea nipamoja na kwenda kutazama uhalisia wa hiki ambachonakisema kwa sababu lengo ni kuhakikisha kwambatunapunguza msongamano wa vijana wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwaaseWaheshimiwa Wabunge na viongozi kwa ujumla, kwambakatika Wilaya ya Tarime, vijana ambao wanamaliza kuanziadarasa la kwanza mpaka darasa la saba wapo 25,000 lakinivijana ambao wanajiandaa kuingia darasa la kwanza wapo13,000; kwa hiyo, unaweza ukaona sisi kama taifa kunamambo ambayo lazima tu-address namna ya populationgrowth inavyokwenda, tukiacha tukatizama hivi tukidhanikwamba Serikali peke yake inaweza hakika haiwezekani. Nivizuri tukashirikishana pande zote ili kutatua matatizo haya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, juu ya swali lake la pili juuya ujenzi wa ghorofa, ghorofa jambo zuri na ningependa namimi nijiridhishe halafu tuone na uwezo wetu maanaunapotengeneza chakula lazima ujue na unga upo kiasi ganikwa sisi tunaokula ugali. (Makofi)

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

Mheshimiwa Mwenyekiti, na juu ya asilimia tanonitaomba niwasiliane na Mheshimiwa Mbunge tuone hiyoasilimia tano na tutayamaliza ili tatizo hili liweze kutatuliwalakini siamini kwamba asilimia tano inajenga ghorofa.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Malecela, atafuatiwa naMheshimiwa Mollel. Mheshimiwa Waziri subiri kidogo iliuyamalize yote.

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kupata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hiikuwapongeza wananchi wa Tanzania, wanajenga sanazahanati, madarasana mifereji.

Je, Serikali haiwezi kuwa na mpango Maalumkwamba wananchi wakijenga kiasi fulani Serikali nayoinakuwa na kiasi fulani inachukua kumalizia kwa sababuwatanzania wanajenga mno? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge ni kama amerudia yaleambayo nilikuwa nawaasa Waheshimiwa Wabunge,kwamba hakika kwa kushirikishana wananchi pamoja naSerikali kwa pamoja tunafika na ndiyo maana nikatoa mfanonilivyokuwa nimeenda Moshi Vijijini, Kituo cha Afya ya Kiaseninimekuta wananchi wamejitoa na Serikali nayo ikapelekanguvu, hakika tukishirikishana tutaweza kutoka. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mollel.

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nampongzaMheshimiwa Rais kwa utaratibu wa kutoa elimu bure kwaniwanufaika wakubwa ni watoto wenye ulemavu ambao sikuza nyuma hawakuweza kupata nafasi hiyo. Hata hivyo,pamoja na jitihada hizo, changamoto ndio bado zipo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende katika suala zima lamadawati, madawati ni kweli kabisa yametolewa lakinihayakuzingatia uhitaji hasa kwa watoto wenye ulemavuambao wengine bado wanalazimika kukaa chini kutokanana hali zao haziwawezeshi kukaa katika madawati hayo.

Je, Serikali ina mpango gani ili basi kuzingatia mahitajiya watoto hao wenye ulemavu ili waweze kufurahia maishana kusoma vizuri ili waweze kutimiza ndoto za? Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaMwenyekiti, ni nia thabiti ya Serikali kuhakikisha kwambamakundi yote yanazingatiwa katika kutengenezamiundombinu, na ndiyo maana katika hizi siku za karibuninilivyopata fursa ya kutembelea Mkoa wa Arusha, nikafikaKituo cha Afya Muriet, pale unakuta miundombinu kwa ajiliya walemavu nayo imewekwa. Naomba niwatakeWakurugenzi wote wa Halmashauri, jambo lolote kuhusianana miundombinu inapotengenezwa sasa hivi lazimatuhakikishe hitaji la watu maalum.

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Na. 57

Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi(OGP)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO aliuliza:-

Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa mstari wa mbelekupambana na ufisadi kiasi cha kumwagiwa sifa duniani;na moja ya silaha kubwa dhidi ya rushwa ni uwazi.

Je, ni kwa nini Serikali ya Awamu ya Tano imeamuakujiondoa kwenye Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwaUwazi (OGP)?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ruhusa yako ninaombanijibu swali la Mheshimiwa Kabwe Ruyagwa Zitto, Mbungewa Kigoma Mjini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wa KuendeshaShughuli wa Serikali kwa Uwazi (Open GovernmentPartnership) ulitokana na wazo la Rais wa Marekani wakatihuo Mheshimiwa Barack Obama aliyekuwa na nia na lengola kuzifanya nchi mbalimbali duniani kuwa wazi katikauendeshaji wa shughuli za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango huo ulizinduliwakama Taasisi Isiyo ya Kiserikali (NGO) tarehe 20 Septemba, 2011na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijiungatarehe 21 Septemba 2011 baada ya kukidhi vigezo vyakujiunga ambavyo ni pamoja na kuzingatia misingi yautawala bora. Mpango huo ni wa hiari ambapo nchi inawezakujiunga baada ya kutimiza masharti na hata kujitoa bilakuwepo na kizuizi chochote.

Hadi sasa nchi wanachama dunia nzima ziko 70 tuna kati ya nchi hizo kumi tu ndizo zinatoka Barani Afrika.

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Serikali kushirikiutekelezaji wa mpango kwa zaidi ya miaka minne imeamuakujitoa. Tanzania si nchi pekee iliyojiunga na mpango huona kisha kujitoa, nchi nyingine kama Hungary na Urusi zilijiungana baadae kujitoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, Serikali yaTanzania tangu kupata uhuru imekuwa na mashirikiano yakikanda na kimataifa katika kutekeleza falsafa ya uwazi nauwajibikaji. Katika kutekeleza falsafa hii , Serikali imejiungana kutekeleza mipango ya kikanda na kimataifa kama vileMpango wa Nchi za Kiafrika wa Kujithamini katika Nyanjaza Utawala Bora na Mapambano Dhidi ya Rushwa (APRM),Shirikisho la Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki naShirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana Rushwa kwaNchi za Jumuiya za Madola.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali yetu imesainimikataba mbalimbali ya mapambano dhidi ya rushwa kamavile African Union Advisory Board on Anti- Corruption pamojana Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Rushwa. Nimaoni ya Serikali kuwa shughuli zinazotekelezwa kupitiavyombo hivyo zinatosha kwa nchi kuendelea kujijengeamisingi imara ya uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi,kuongeza uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kulihakikishiaBunge lako Tukufu kwamba Tanzania kujitoa katika Mpangowa Kimataifa wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi(OGP) hakuna madhara yoyote. Mipango inayotekelezwandani ya nchi kama ilivyoelekezwa hapo juu inajitoshelezakuendeleza na kuimarisha misingi ya uwazi na uwajibikajina mapambano dhidi ya rushwa.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Zitto halafuMheshimiwa Khatib.

MHE. KABWE Z.R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,mifano ambayo Serikali imeitoa ya nchi za Hungary na Russia,nchi hizi ni miongoni mwa nchi ambazo duniani

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

zinatuhumiwa kwa kuendeshwa bila misingi ya kidemokrasiana kidikteta. Ni aibu sana kwamba nchi yetu inaweza ikaiganchi ambazo tayari zinaonyesha kabisa kwamba hazifuatimisingi ya kidemokrasia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, majukwaa haya yakimataifa yanatengeneza ushawishi wa nchi kwenye mataifa.Leo hii Mwenyekiti wa OGP ni nchi ya Canada, juzi Rais ame…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zitto uliza swali.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Ndio swali langu la kwanzahilo.

MWENYEKITI: Uliza swali please.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, juziRais amesema kwamba amemwandikia barua Waziri Mkuuwa Canada kuhusiana na suala la Bombardier. Je, Serikalihaioni kwamba iwapo Tanzania ingekuwa imeendelea kuwamwananchama wa OGP na Canada ndio Mwenyekiti waOGP. Ombi hili la Rais lingeshughulikiwa kwa uzito zaidi kwasababu ya mahusiano yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Manispaa ya Kigoma Ujiji nimiongoni mwa Miji 15 duniani ambayo inashiriki katika OGPkwa uhuru kabisa na haizingatiwi kama nchi iko kwenye OGPau la. Serikali inatoa kauli gani kuhusiana na ushiriki si tu waManispaa ya Kigoma Ujiji ambayo inafaidika sana kwenyeOGP lakini pia na Miji mingine ya Tanzania ambayo inatakakuingia kwenye OGP, Serikali inatoa kauli gani kuhusu hili?(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Zitto ametoa mfano wa nchizailizojitoa kwamba zinaendeshwa kwa udikteta na nini nanini. Nataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

Tanzania ilipofanya maamuzi haya, imefanya kwa kupimavigezo kwa Tanzania ilivyoona inafaa, hatujamuiga mtu. Sisini Taifa huru, linalojitawala, linalofanya maamuzi yakeyenyewe bila kushurutishwa na Taifa lolote, liwe kubwa amadogo duniani. Kwa hiyo, kwamba nchi yetu imeiga mawazohayo si sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema kwamba Raiswetu amemwandikia Rais wa Canada na kwamba Canadani Mwenyekiti wa hili, mahusiano yetu pengine jambolingekuwa hili. Nataka nimweleze ndugu yangu Zitto Kabwe,sisi na Canada ni wanachama wa Jumuiya ya Madola, sisituna ubalozi Canada, with or without OGP yaani kuwepoama bila kuwepo OGP mawasiliano yetu na Canada haiwezikuwa tatizo. Na juzi Mheshimiwa Waziri Mkuu walikuwa kuleCanada. Kwa hiyo mambo haya ya Bombardier na OGPwala sijui yanaendaje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimefurahi kweli, swalilako la pili nimefurahi sana Ndugu Zitto Kabwe anataka kujuaSerikali inatoa kauli gani juu ya ushiriki wa Kigoma Ujiji. Andikolile la mradi ule linasema nchi ikijitoa, washirika wake wotewaliomo ndani ya ile nchi na wao uanachama wao shughulizao zinakoma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inayo taarifakwamba Manispaa ya Kigoma Uji j i mpaka sasawanawasiliana na OGP na OGP wamemuandikia Waziri waMambo ya Nje kwamba wana nia ya kuendelea kushirikianana ninyi. Sasa nataka kupitia Bunge lako Tukufu kuionyaManispaa ya Kigoma Ujiji, nchi inayozingatia utawala bora,haiwezi Serikali Kuu ifanye maamuzi Baraza la Madiwaniwakasema sisi hatuta-comply, haijatokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nionye Manispaa yaKigoma waache mara moja, watekeleze maamuzi ya Serikalina wakiendelea kufanya mawasiliano kama wanavyofanyasasa Serikali itachukua hatua kali zaidi. Na ninyi mnajua Serikalikwenye Manispaa sheria kali kuliko zote ni kuvunja Baraza laMadiwani na kuweka Tume ya Manispaa. (Makofi)

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Nawaomba huko mliko Waheshimiwa Madiwani waKigoma na ndugu yangu Zitto Kabwe, msiifikishe Serikali huko.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Khatib.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Dhana ya utawala bora ni pamoja na utoaji wahaki na kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mrefu sasa katikamagereza ya nchi zetu yamejaa mrundikano ya washtakiwaambao mashtaka yao yameshindwa kuthibitishwa ndani yamahakama na kuifanya mahakama kuchelewa kutoa haki.Hii ikiwemo ni pamoja na Masheikh wa Uamsho kutokaZanzibar ambao kwa sasa wana miaka mitano wanasotamagerezani na Serikali upande wa mashtaka wameshindwakuthibitisha makosa yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali inatoa kauli ganikuhusiana na kushindwa kutekeleza utoaji wa haki na kwawakati kwa watuhumiwa waliopo magerezani? Ahasantesana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Khatib swali hil iumelichomekea, halipo katika utaratibu wa swali la msingi.Kwa hiyo, nakuomba though unaweza ukalipeleka katikahatua zingine lakini sio katika swali hili. Wizara ya Mifugo naUvuvi, Mheshimiwa Kakoso, kwa niaba ya Mheshimiwa ZainabKatimba. (Makofi)

Na. 58

Vitendea kazi kwa Wavuvi Wadogo wa Ziwa Tanganyika

MHE. ZAINAB A. KATIMBA (K.n.y. MHE. MOSHI S.KAKOSO) aliuliza:-

Wavuvi wadogo wadogo wa Ziwa Tanganyika wanatatizo la vitendea kazi.

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

Je, ni lini Serikali itawapatia wavuvi hao vitendea kazivya kutosha?

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ruhusa yako, kwanzanaomba nichukue fursa hii kumshukuru sana MwenyeziMungu, kumshukuru Mheshimiwa Spika, wananchi wenzanguwa Mkuranga na kwa namna ya kipekee kabisa kumshukuruMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli kwa kuniamini kushika nafasihii ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukrani hizo,naomba sasa kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugona Uvuvi, nijibu swali la Mheshimiwa Moshi Kakoso, Mbungewa Mpanda Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendeleakuhamasisha wadau wa uvuvi, ikiwemo sekta binafsi na jamiiya wavuvi wenyewe kuwekeza katika matumizi ya zana boraza uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuboresha mapato yao,baadhi ya mikakati iliyotekelezwa ni kuwawezesha wavuviwadogo kuanzisha vyama vya ushirika vya msingi kupitiahalmashauri husika na pia wawekezaji wakubwa kuwekezakwenye viwanda vya kutengeneza boti na zana mbalimbaliza uvuvi hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ziwa Tanganyika,tunacho Kituo chetu cha Wakala wa Elimu na Mafunzo yaUvuvi (FETA) pale Kibirizi Kigoma, ambapo tunayo mipangokama Serikali kukiimarisha ili kiweze kuunda boti za kisasa napia kuendelea kutoa mafunzo na elimu inayohusu sekta yauvuvi kwa wanafunzi na jamii za wavuvi na wadau wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali inatekeleza Sheriaya VAT ya mwaka 2007 ambayo imetoa msamaha wa kodiya zana za uvuvi na malighafi nyingine ikiwemo injini za

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

kupachika, nyuzi za kushonea nyavu na vifungashio vyake.Vilevile katika jitihada nyingine za kuwasaidia wavuvi, Serikalihii ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,katika mwaka 2015/2016 ilitenga jumla ya fedha shilingimilioni mia nne ambapo jumla ya injini za boti 73 zilinunuliwana katika hizo boti 49 zilishachukuliwa na vikundi vya wavuvimbalimbali nchini kupitia Halmshauri zao katika mtindo waruzuku ambapo Serikali inachangia asilimia 40 na vikundi vyawavuvi vinachangia asilimia 60.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka hivi sasa tunazo botitakribani 24 ambazo zinawasubiri wavuvi mbalimbaliwaliopo nchini ikiwa ni pamoja na wavuvi walioko Mpandana Ziwa Tanganyika lote kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shime kwa WaheshimiwaWabunge, tuhamasishe vikundi hivi vya wavuvi, mashine hizobado tunazo, waweze kuja kupitia halmashauri zao kwakufuata utaratibu kuzipata na kuweza kuimarisha shughulizao za uvuvi kwa ajili ya kujipatia kipato zaidi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Katimba.

MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawiliya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali imefanya jitihadagani ili kuhakikisha kwamba wavuvi wanaweza kuzifikia nakunufaika na hizi fursa alizozizungumzia Mheshimiwa NaibuWaziri?

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali imechukua hatuagani kuhakikisha inasimamia kwa ukamilifu sekta hii ya uvuviili kuhakikisha inaepusha uvuvi haramu ambao utaletauharibifu kwa mazingira?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, swali la kwanza ni jitihada gani ambazo Serikaliimeshakufanya. Kama nilivyojibu katika swali la msingi yakwamba, la kwanza, tumeendelea kuhamasisha wavuvikujiunga katika vikundi mbalimbali ili waweze kutumia fursazinazojitokeza, kama vile fursa niliyoitaja ya ruzuku ambapokatika mwaka huu wa 2017/2018 tumeshatenga shilingimilioni 100 ili kuweza kuendelea kuwasaidia wavuvi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Sheria ile ya Fedhaya mwaka 2007 tunaendelea kuisimamia kuhakikisha yakwamba zana za uvuvi zinaendelea kupatikana kwa beinafuu. Pia tunalo dirisha katika Benki yetu ya Rasilimali ambalolinahusu wakulima, wavuvi na wafugaji ili waweze kupatamikopo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni juu ya hatuagani Serikali inachukua kukomesha uvuvi haramu ili kulindarasilimali zetu. La kwanza kabisa Serikali inaendelea kutoaelimu kwa wavuvi na jamii za wavuvi ili kulinda rasilimalizetu kwa ajili yetu na vizazi vijavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali imejishirikishakatika kufanya doria mbalimbali ambazo zimeleta matundachanya ya kuhakikisha kwamba uvuvi haramu unapigwa vitaikiwa ni pamoja na uvuvi wa matumizi ya mabomu na uvuviwa nyavu zisizoruhusiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho katika kupambanana uvuvi haramu, Serikali inakusudia kuleta maboresho yaSheria yetu ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003 ili kuipa menozaidi kuhakikisha tunaendelea kulinda rasilimali za nchi yetu.Nashukuru sana.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Kemi halafuMheshimiwa Dau.

MHE. KEMILEMBE J. LWOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali dogola nyongeza.

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na tatizo kubwasana la wavuvi, hasa wa Kanda ya Ziwa na wa Ziwa Victoriakuchomewa nyavu zao na kusababishiwa hasara kubwasana na Serikali. Ni lini sasa Serikali itatoa maamuzi yakukataza nyavu hizi kutengenezwa kwenye viwanda iliwananchi wetu wasiendelee kupata hasara ya kuchomewanyavu zao? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi tu.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli Serikali itaendelea kutoa elimu yakuhakikisha kwamba wananchi wanapata kujua nyavu ganiambazo haziruhusiwi na nyavu gani ambazo zinaruhusiwa.

Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwambakupitia sheria zetu za uvuvi tutaendelea kushirikiana nawavuvi wetu na jamii yote ya wavuvi ili kuhakikisha kwambazile nyavu zisizoruhusiwa hatutaziacha, lakini nyavuzinazoruhusiwa ambazo zipo katika vipimo vya kisheriazitaendelea kutumika. Vilevile kuwahamasisha wawekezajizaidi waweze kutengeneza nyavu zinazoruhusiwa kwa ajiliya kulinda mazingira yetu.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge,naomba utulivu ndani ya Bunge. Mheshimiwa Dau atafuatiwana Mheshimiwa Lupembe.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo ya wavuviwadogo katika Ziwa Tanganyika yanafanana sana namatatizo ya wavuvi wadogo katika Kisiwa cha Mafia. Taasisiya Hifadhi ya Bahari Mafia imekuwa ikiwanyanyasa nakuwabambikia kesi wavuvi wadogo wa Mafia nakuwanyang’anya nyavu zao. Je, Mheshimiwa Waziri utakuwatayari kufanya ziara Mafia na kutukutanisha sote ili kupataufumbuzi wa tatizo hili?

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

MWENYEKITI: Jibu lake, anataka kujua tu kama ukotayari kwenda ziara.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimhakikishie kaka yangu, MheshimiwaMbaraka Dau, Mbunge jirani wa Mafia ya kwamba nipo tayarikwenda nyumbani Mafia kwa ajili ya…

MWENYEKITI: Inatosha Mheshimiwa Waziri.Mheshimiwa Lupembe, baadaye Mheshimiwa Bilago.

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi kwa ajili ya kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Ziwa Tanganyika,Kalema, Ikola pamoja na Kapalamsenga, vijana wale wakoduni sana kwa ajili ya uvuvi wa lile Ziwa Tanganyika. Je, Waziriyuko tayari kwenda na mimi ili akaone hali halisi ya vijanawale?

MWENYEKITI: Haya Mheshimiwa Waziru, uanze nasafari ya kwenda Ziwa Tanganyika kwanza.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaAnna Lupembe kwamba niko tayari kwenda Ziwa Tanganyikakuonana na wavuvi wa ziwa hilo wakati wowote baada yakumaliza shughuli za Bunge hapa.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Bilago.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa nafasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaruhusu nyavuzisizotakiwa zinaingia nchini na Serikali hiyo hiyo inachukuakodi kwa waingizaji wa nyavu ambazo hazifai, nyavuzikishauzwa anayepata hasara ni mwananchi aliyenunuanyavu zile ambazo kumbe Serikali inafahamu hazihitajiki na

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

ilichukua kodi. Sasa kama Serikali inaweza ikazuia madawaya kulevya yasiingie nchini inashindwaje kuzuia nyavu zisizofaakwa wavuvi zisiingie nchini na hivyo kuwatia hasara baadaya kuwa wameshazinunua? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu, nyavu nyingizinaingia kwa njia ya magendo.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, kimsingi jambo hili la nyavu lina mkinzano. Ziponyavu ambazo zinaruhusiwa katika bahari lakini size hiyo hiyoya nyavu inaweza isiruhusiwe katika maziwa yetu; wapowafanyabiasara ambao wanaweza kuagiza nyavu kwa niaya kusema wanazipeleka katika bahari lakini wakishafika nakuzitoa bandarini wakazipeleka kwenye maziwapasiporuhusiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hila hii wataalam wetu nasisi kama Wizara tunaendelea kukabiliana nayo na hata sasatunazo kesi mahakamani za jambo la namna hii. Sisitunaomba uungwaji mkono wa kuhakikisha kwambamkanganyiko huu tunautatua ilimradi tuhakikishe kwambawafanyabiashara wetu, wazalishaji wetu wa nyavu, wotewanakwenda kwa matakwa ya sheria, kanuni na taratibuzetu zinazo-guide shughuli nzima hii ya uvuvi. Uvuvi ni maishayetu, lakini ni lazima tuhakikishe tunalinda mazingira kwa ajiliya vizazi vya leo na vya kesho. Nashukuru sana.

Na. 59

Hitaji la Umeme wa Uhakika – Mkoa wa Mtwara

MHE. SHAMSIA A. MTAMBA aliuliza:-

Katika Mkoa wa Mtwara kuna tatizo kubwa lakukatika kwa umeme mara kwa mara jambo ambalolinaathiri wananchi ikiwemo wafanyabiashara ambaowanategemea sana umeme na hivyo kusababisha wakatimwingine biashara hizo kuharibika na kuwasababishia hasarawananchi hao.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

Je, ni lini Serikali itawahakikishia wananchi wa Mtwarakupata umeme wa uhakika?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Nishati, napenda kujibu swali la MheshimiwaShamsia Aziz Mtamba, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Serikali nikuhakikisha kuwa wananchi katika maeneo mbalimbalinchini wanapata umeme wa uhakika ili kuboresha maishayao. Serikali kupitia TANESCO imeweka jitihada kubwakuhakikisha kuwa umeme wa kutosha katika Mikoa yaMtwara na Lindi unapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua zilizochukuliwa nipamoja na kufanya ukarabati mkubwa wa mitambo yotetisa iliyopo Mtwara yenye uwezo wa kuzalisha megawati 18.Ukarabati huu ulianza mwishoni mwa mwezo Oktoba, 2017na utakamilika mapema mwezi Desemba, 2017. Gharamaya matengenezo kwa mitambo yote ni shilingi 4,800,000,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ukarabati huo,Serikali imeagiza mitambo miwili mipya kutoka Kampuni yaCaterpillar yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya megawatinne kwa gharama ya shilingi 8,300,000,000. Ufungaji wamitambo hiyo unatarajiwa kuanza mwezi Januari, 2018 nakukamilika mwezi Aprili, 2018. Mitambo hiyo itaongeza uwezowa mashine zilizopo kufikia megawati 21.75.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TANESCOimeanza utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wamegawati 300 kwa kutumia gesi asilia Mkoani Mtwara. Kaziinayoendelea kwa sasa ni kukamilisha upembuzi yakinifukupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japani (JICA).Mradi huo unategemewa kuanza mwezi Aprili, 2018 nakukamilika mwezi Desemba, 2019. Mradi huuutakapokamilika utatoa suluhisho la kudumu la upatikanaji

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

wa umeme wa kutosha katika Mikoa ya kusini ikiwa nipamoja na Lindi na Mtwara.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Shamsia.

MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswalimawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza,pamoja na kupita bomba la gesi katika maeneo mengi yaMtwara na Lindi, bado vijiji na mitaa mingi haina mtandaowa umeme. Je, ni lini REA III itamaliza tatizo hili kwa mikoaya kusini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pil i,mkandarasi aliyepewa kusambaza mtandao wa umemeMtwara yupo slow sana. Je, Serikali inachukua uamuzi ganikwa mkandarasi huyo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupisana.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Mbunge ameuliza; ni lini REA III itamaliza tatizola kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya Mkoawa Mtwara. Nataka nimfahamishe Mheshimiwa Mbungekuwa Mkandarasi wa Mkoa wa Mtwara ni JV Radi ServiceLimited na ameshalipwa asilimia kumi na yupo MkoaniMtwara akiendelea na kazi ya upimaji wa njia ya umeme,na kwa kuwa Wizara tumetoa maelekezo kwamba vifaavyote vya mradi huu REA III vipatikane ndani ya nchi,wakandarasi wanachoendelea nacho sasa ni namna yakutafuta vifaa vyote na kuagiza ndani ya nchi, nanimhakikishie kazi hii itafanyika kwa mujibu wa ratibailiyopangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anauliziahatua gani zitachukuliwa dhidi ya mkandarasi huyu. Naombanimwambie ratiba ya REA iko awamu mbili, awamu ya

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

kwanza ni 2017 hii Julai mpaka 2019, kwa hiyo mkandarasihuyu yupo ndani ya muda. Na kwa kuwa amelipwa asilimia10 na ameanza kazi, nimthibitishie tu zoezi la upelekajiumeme katika Mtwara kwa mkandarasi huyu JV Radi Serviceitakamilika kwa wakati.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Nape, ajiandaeMheshimiwa Aisharose.

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jitihada kubwazinazofanywa na Serikali katika kutatua tatizo la umeme kwaMikoa ya Lindi na Mtwara, baada ya mateso makubwatuliyoyapata katika kipindi hiki cha miezi miwili/mitatu chakukosa umeme kwa zaidi ya siku nne. Serikaliinaambatanishaje juhudi hizo na ukarabati wa miundombinuhasa nguzo, kwenye yale maeneo ambayo nguzo zake nimbovu. Kwa hiyo, hata wakikamilisha uzalishaji badousambazaji wa umeme kwenye haya maeneo ambayo nguzozake ni mbovu bado itakwama.

Sasa Serikali imejipangaje kuambatanisha juhudi hizomnazoendelea nazo na ukarabati wa nguzo kwenye yalemaeneo ambayo nguzo zimechoka?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yakemazuri. Lakini niwape pole sana Waheshimiwa Wabunge waMikoa ya Mtwara na Lindi kwa kipindi ambacho MheshimiwaNape amezungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli zipo juhudi zamakusudi ambazo sasa tunachukua kama Serikali,tuliporekebisha umeme katika Mkoa wa Mtwara tarehe 16mwezi uliopita tuliacha feeder mbili ambazo matengenezoyake yanaendelea. Wananchi wa Mkoa wa Lindi kwa sasa

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

wanapata umeme kutoka kwenye sub station ya Maumbika.Sasa sub station ya Maumbika marekebisho ya engine yakeyanakamilika kesho. Kwa hiyo wananchi wa Mtwara, Lindina maeneo mengine yategemee kupata umeme kuanziakesho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la nguzo kamaambavyo Mheshimiwa Mbunge amezungumza, tumeagizanguzo mpya kutoka hapa nchini, tumeacha sasa kuletanguzo kutoka nje ambazo zilikuwa zinakaa kwa muda mrefumipakani. Nguzo zitakuwa mpya, kwa hiyo, niwahakikishiewananchi watapata nguzo na ukarabati utaendelea vizuri.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Aisharose,ajiandae Mheshimiwa Ngombale.

MHE. AISHAROSE N. MATTEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Tatizo lililopo Mtwarahalina tofauti na tatizo lililopo katika Jimbo la SingidaKaskazini. Vijiji vingi vya Jimbo la Singida Kaskazini ambavyovilikuwa katika Mpango wa REA II mpaka sasa havijapatiwaumeme. Vijiji hivyo ni Mrama, Madasenga, Mipilo, Meria, Mitulana Msange. Kwa kuwa sasa tunaelekea kwenye Tanzania yaViwanda; je, ni lini sasa Serikali itavipatia vijiji hivyo umemeukizugatia kwamba tupo katika Mpango wa REA III? Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa muhusika.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaMkoa wa Singida mkandarasi ambaye alipewa kazi alikuwana jukumu la kukamilisha masuala ya mikataba. Taratibu zamikataba amekamilisha juzi, siku ya Ijumaa, na hivyo ataanzakuingia site kuanzia Ijumaa wiki hii, kwa hiyo wananchi waSingida na maeneo mengine watapata mkandarasi huyo.

Lakini cha pili Singida tunawapatia mkandarasialiyeshindwa kukamilisha kazi katika REA II, Kampuni yaSPENCON iliondolewa kwa hiyo, tunawapa mkandarasi

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

mwingine. Kwa hiyo, Mkoa wa Singida utapata wakandarasiwawili pamoja na mkandarasi wa REA III.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ngombale.

MHE. VEDASTO E. NGOMBALE: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi.

Kwa kuwa chanzo cha umeme pale Somanga Fungukinashindwa kufanya kazi vizuri na kupelekea matatizomakubwa ya umeme kwa Wilaya ya Kilwa na Rufiji kwasababu ya mitambo ile kuchelewa kufanyiwa ukarabati nakwa kuwa sasa tatizo hilo linaendea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itatuunganishawatu wa Kusini na Gridi ya Taifa kwasababu sasa umemeimeshafika pale Kilwa? (Makofi).

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza naomba nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge Ngombalekwamba mitambo ya Somanga Fungu inatarajia kufanyiwaukarabati hivi karibuni na kampuni ya RENCO ya Italy. NaSerikali kupitia TANESCO wameshasaini mkataba na ukarabatihuo utakamilika Desemba, 2018 ambapo mitambo itakuwana uwezo wa kuzalisha megawati 7.5 na matumizi ya Kilwani megawati tatu. Kwa hiyo naomba nimtaharifu kwambahilo linafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ameuliza nilini…

MWENYEKITI: Mjibu swali moja tu, swali moja tu hililingine yeye kachomekea, si swali la msingi, linatoshaMheshimiwa Waziri, ahsante kwa majibu mazuri.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea, MheshimiwaGodifrey Mgimwa kwa niaba ya Mheshimiwa Malongo.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Na. 60

Tatizo la Umeme Katika Baadhi ya Vijiji - Kalenga

MHE. EDWARD F. MWALONGO (K.n.y. MHE. GODFREYW. MGIMWA) aliuliza:-

Tatizo la umeme bado ni kubwa licha ya jitihadakubwa zinazofanywa na Serikali.

Je, ni lini Serikali itatatua tatizo hili na hatimayekuvipatia umeme Vijiji vya Kipera, Lupalama, Itagutwa naLyamgungwe?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati, naomba kujibu swali Mheshimiwa Godfrey WilliamMgimwa, Mbunge wa Kalenga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala waNishati Vijijini (REA) inatarajia kuvipatia umeme Vijiji vyaKipela, Lupalama, Itagutwa, Ikongwe na Lyamgungwekatika Awamu ya Tatu ya uetekelezaji wa Mradi waKusambaza Umeme Vijijini (REA III) inayoendelea kwa sasa.Aidha, kwa Mkoa wa Iringa miradi hiyo inatekelezwa namkandarasi Kampuni ya Sengerema Engineering Group natayari yupo katika eneo (site) akifanya upimaji wa awalikwenye vijiji tajwa pamoja na vijiji vingine 145 vya Mkoa waIringa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya kupeleka umemekatika vijiji hivyo tajwa inajumuisha ujenzi wa njia za umemewa msongo wa kilovolti 33 na 11 zenye urefu wa kilometa22; msongo wa kilovolti 0.4 yenye urefu wa kilometa 18; nauwekaji wa transfoma tisa pamoja na kuwaunganishaumeme wateja 215. Gharama ya kutekeleza miradi hiyo nijumla ya shilingi bilioni 2.3.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwalongo.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

MHE. EDWARD F. MWALONGO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante, nashukuru sana kwa majibu mazuri yaSerikali. Pamoja na majibu hayo naomba niulize maswalimawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Kalenga pamojana kazi nzuri inayofanyika wakandarasi hawa wanapelekaumeme lakini hawafikishi kwenye Taasisi za umma kamazahanati shule.

Je, Serikali inatoa msisitizo gani na kuwafariji hawawanchi wa Kalenga juu ya utekelezaji wa mradi huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; katika Jimbo yaNjombe Mjijini yupo mkandarasi anayetekeleza mradi waMakambako - Songea. Mradi hule ulikuwa-designed miakamingi sana, matokeo yake ni kwamba mitaa imepanuka namaeneo yamepanuka na yule anatumia mchoro wa miakamingi iliyopita.

Je, Serikali inatusaidiaje sasa ili kusudi mradi ule waMakambako - Songea inaopisha umeme katika vijiji, umemeule uweze kufika vitongoji vyote na taasisi za umma?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,swali lake la kwanza lilijielekeza kwenye taasisi za ummaambazo hazifikiwi na Mradi wa REA unaoendelea.Ningependa kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwambakwenye Mkoa wa Iringa kuna mradi wa densificationunaotekelezwa kwa ajili ya maeneo ambayo yalirukwakwenye Awamu wa Pili. Inaangalia maeneo ya umma, taasisimbalimbali, iwe hospitali, ziwe shule za msingi na kadhalika.Kwa hiyo nimuhakikishie kwamba mradi wa densificationunafanya hiyo kazi katika Mkoa wa Iringa na mkandarasianaendela na kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, aliulizia juuya mradi wa Makambako - Songea. Naomba nimthibitishie

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Mheshimiwa Mbunge kwamba kwamba katika mradi huuwa Makambako Songea ujenzi wa laini wa msongo wa KV220 kwanza kazi inaendela vizuri lakini pia swali lake alikuwaanauliza je maeneo ambayo vijiji vinavyopitiwa na msongohuo usambazaji wa umeme ukoje. Nimthibitishe MheshimiwaMbunge kwamba kazi ya kusambaza umeme itaendelae namaeneo ambayo yataachwa REA III itaendelea kuya-coverkwasababu mpango wa Serikali ya Awamu Tano nikuhakikisha kwamba vijiji vyote vinapata umeme ifikapo2020/2021. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mwamoto,atafuatiwa na Mheshimiwa Mkundi.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mradi wa REA IIItayari umeanza na vijiji vingi vimepimwa, lakini sasa hivi kunabaadhi ya vijiji ambavyo vilisahaulika na baadaye tukaletakuomba tena viingizwe.

Sasa Serikali inatuambiaje hasa katika Wilaya ya Kilolo,je, vijiji ambavyo vilisahaulika vitaongezwa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza kama nilivyosema, mradi wa REA una awamu mbili,na lengo lake ni kuvifikia vijiji 7,823. Awamu ya kwanza vijiji3,559 na awamu ya pili vijiji 4,313. Nimthibitishie MheshimiwaMbunge kwamba vijiji vyote vitafikiwa umeme ifikapomwaka 2020/2021. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mkundi.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru, maeneo ya Kakelege na eneo la uwanja wandege Kata ya Nkilizia yapo katikati ya mji wa Nansio. Lakinimaeneo haya yamerukwa na huduma ya umeme, jambo

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

linalofanya wananchi wa maeneo haya waone kamawametengwa. na Mheshimiwa Waziri nimekuwanamuwasilishia tatizo hili mara kwa mara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu natakakujua Serikali imefikia hatua ipi kuhakikisha kwamba maeneohaya yaliyo katikati ya mji wa Nansio yote yanapata hudumaza umeme?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kama nilivyosema katika maelezo yangu ya awali Serikaliinatekeleza mradi pia wa densification ambao sasa hiviAwamu ya Kwanza na ni kwa Mikoa sita. Baada ya kukamilikakwa mikoa hiyo Serikali itaendelea pamoja na wafadhili waNorway kutekeleza awamu ya pili. Nia ya mradi huu nikusambaza umeme katika maeneo kaya, vitongoji na taasisiza umma zilizorukwa. Kwa hiyo, nimuahidi MheshimiwaMbunge kwamba Awamu ya Pili ya mradi huu itafikiwa katikamaeneo ambayo ameyataja.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Kitandula.

MHE. DUNSTAN. L. KITANDULA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Serikali ilihaidi kwamba Kata yaMwakijembe ambayo iko mpakani na Kenya vijiji vyakevilisahaulika lakini kuna umuhimu wa kiulinzi vijiji vile kupataumeme. Serikali i l ihaidi kwamba kabla mkandarasihajaondoka kufanya survey wataagizwa ili jambo hilolifanyike. Je, ni lini jambo hili litakamilika?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli kwamba kata anayoitaja Mheshimiwa Mbunge yaMwakijembe ni kata ambayo iko mpakani, laikini kamaalivyosema aliliwasilisha ombi lake hilo. Kwa kutambuaumuhimu wa maeneo ambayo yako mpakani suala lakelinashughulikiwa na mkandarasi wa Mkoa wa Tanga katika

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

maeneo ambao Wilaya ya Mkinga na Wilaya zinginezo niDelimiki Electric Company Limited yupo site anaendelea nahiyo kazi. Kwa hiyo nimtoe wasi wasi Mheshimiwa Mbunge,kwamba Serikali inashughulikia. Na kwa kuwa nia yetu nikusambaza umeme katika maeneo yetu hilo jambolitafanikiwa, ahsante.

Na. 61

Sheria ya Sekta Binafsi ya Ulinzi Nchini

MHE. ALMAS A. MAIGE aliuliza:-

Sekta binafsi ya ulinzi ilianzishwa mwaka 1980 ikiwana kampuni mbili tu na ikiwa haina miongozo yoyote.

(a) Kwa kuwa sasa sekta hii ina kampuni zaidi ya 850nchini kote, je, Serikali italeta Sheria ya Sekta Binafsi ya Ulinziili pia kuanzisha mamlaka ya sekta binafsi ya ulinzi?

(b) Je, Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) inampango gani wa kushirikiana na Chama cha Sekta Binafsiya Ulinzi ili kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI)alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi napenda kujibu swali laMheshimiwa Almas Athumani Maige, Mbunge wa TaboraKaskazini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba sekta yaulinzi binafsi imekuwa sana hapa nchini na kwamba Serikaliinatambua umuhimu wa sekta hii na ilishaanza maandaliziya kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Makampuni Binafsi yaUlinzi. Katika kufanikisha jambo hili Wizara ya Mambo yaMambo ya Ndani ya Nchi iliandaa walaka kupeleka Barazala Mawaziri kwa hatua za awali. Ili kukamilisha hatua hii

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

yanahitajika maoni ya wadau kutoka pande mbili zaMuungano. Serikali imeweka utaratibu wa kupata maonikutoka katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na marayatakapopokelewa waraka huu utawasilishwa mapemaiwezekanavyo.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Inspekta Jeneraliwa Polisi imekuwa ikishikiana na sekta binafsi ya ulinzi katikanyanja mbalimbali. Kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisina Polisi Wasaidizi Namba 322 Rejeo la mwaka 2002. Jeshi lapolisi limekuwa likitoa mafunzo kwa makampuni binafsi yaulinzi, kufanya ukaguzi kuchukua alama za vidole kwawatumishi, kutoa vitambulisho na kutoa ushauri kwamakampuni hayo ili kuboresha na kuhakikisha huduma yaulinzi inatolewa katika viwango vinavyostahili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Maige.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kuniruhusu niulize maswali mawili yanyongeza. Pamoja na majibu mazuri sana ya MheshimiwaWaziri, mimi nasikitika sana Serikali haisemi kwamba mimindiye niliyeleta Muswada Binafsi wa Sekta ya Ulinzi Binafsi(Private Security Industry Bill) wa mwaka 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa je, Serikali iko tayarikunilipia kunirudishia gharama hata nusu ya ghalamaniliyoitumia katika utafiti huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, na la pili, kwa kuwamchakato wa kuipata sheria hii ya sekta ya ulinzi binafsiunakuwa mrefu sana, je, Serikali sasa iko tayari kutunga GNambayo itatumika wakati huu wa mpito kwa sababumakampuni haya yalianzishwa bila GN wala sheria yoyote?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali lake la kwanza,

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

awali napenda kuchukua furusa hii kumshukuru sanaMheshimiwa Maige kwa mchango mkubwa sana ambaoamekuwa akiutoa katika sekta binafsi ya ulunzi na hivyokama Serikali tunathamini sana mchango wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya MheshimiwaMaige kuwasilisha muswada wake binafsi hapa Bungenimajibu ya Serikali yalikuwa kwamba Serikali itafanya kazi hiyo,kwa maana ya kuleta muswada huo ili ujadiliwe mbele yaBunge na sheria hii iweze kutungwa.

Kwa hiyo, nimuombe tu Mheshimiwa Maige kwambaile kazi kubwa aliyoifanya aichukulie kama ni sehemu yamchango wake kwa Taifa hili; na yeye kama akiwamzalendo namba moja basi aone kama ni mchango wakekatika kusaidia Serikali katika kukamilisha utungwaji wa sheriahii. Ninafahamu sana kwamba Mheshimiwa huyu nimzalendo, itakuwa ni sehemu ya mchango wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, la juu ya GN,katika majibu yangu ya msingi nimesma taratibu za utungwajiwa sheria zinaelekea kukamilika na hivyo namshauriMheshimiwa Mbunge kwa sababu tumeshapitia kote huko,hatua hii ilibaki atupe nafasi Serikali kuwasilishwa muswadahuu ili sheria hii itungwe na baadaye zitakuja hizo GN zinginekwa ajili ya ku-regulate maswala ya ulinzi katika sekta binafsi.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Ruth halafuMheshimiwa Ester Mahawe.

MHE. RUTH. H. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu Serikali ndiyemsimamizi mkubwa wa usalama wa raia na mali zao,ningepa kufahamu ni kwa jinsi gani Serikali inasimamia kwauhakika hizi sekta binafsi za ulinzi ili kuhakikisha wale wotewalioajiriwa hawana historia ya uhalifu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia taasisi zakembalimbali imekuwa ikihakikisha kwamba kuanzia katikaeneo la usajili wa makampuni haya ambayo pamoja nakwamba utaratibu wa usajili wake ni kupitia BRELA, lakinibado Jeshi la Polisi nalo lina nafasi ya kuweza kupitia nakuyatathimini maombi ambayo yanapekwa ili kujihakikishia.Kwa sababu kazi ambayo inakwenda kufanywa hapa nasekta ya ulinzi binafsi ni kazi ambayo vilevile ni ya kulisaidiaJeshi la Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kwa sababu kwamujibu wa viwango vya Umoja wa Mataifa askari mmojaanapaswa kulinda watu na 450, lakini sisi kwetu askari mmojaanalinda kuanzia watu 1,150 mpaka 1,300. Kwa hiyo, ndiyomaaan kama Serikali tunatoa kipaumbele na ndiyo maanakatika shughuli mbalimbali za sekta ya ulinzi binfsitunahakikisha kwamba tunashirikiana nao katika kutoaelimu, lakini vilevile na kuzisimamia kuona kwamba zinayanyakazi ile iliyokusudiwa ili hatimaye isije ikaleta madharamakubwa kwa sababu na yenyewe pia ni sehemu ya ulinzikatika nchi yetu.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mahawe.

MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Swali langu lilikuwa kuhusu ukosefu wa nyumba zapolisi katika Mkoa wa Manyara ikiwemo Ofisi ya RPC. Ni linisasa Serikali itaona kwamba kuna umuhimu wa Jeshi la Polisikupatiwa nyumba ili waweze kufanya kazi yao kwa ufanisi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri ni swali lingine lakinilijibu kwa sababu wewe ni mtaalum na unafanya kazi vizuri.(Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tunatambua kwambatunayo changamoto kubwa sana ya ukosefu wa nyumba za

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

askari wetu, lakini katika mipango ya Wizara tumejiwekeautaratibu kwamba pindi pale bajeti itakaporuhusututahakikisha kwamba tunaifikia Mikoa yote ili kuwaondoleaadha ya ukosefu wa nyumba watumishi wa Serikali hasa waJeshi la Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondolee hofuMheshimiwa Mbunge bajeti ikikaa vizuri basi tutafikia katikamaeneo yote katika kuondoa hadha hii.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Bhagwanji.

MHE. BHAGWANJI MAGANLAL MEISURIA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kinipa nasafi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazipongeza Serikali yaZanzibar na Serikali ya Muungano kwa sababu katika Jimbolangu wamejenga kituo cha polisi Chwaka na Jozani. Lakinimimi naomba Serikali, wameniomba nizungumze Serikali yaMuungano pamoja na Zanzibar wapatiwe gari za doria,Chwaka na Jozani.

La kwanza kwa kuboresha wananchi wangu wapatehitaji lao, lakini lingine mimi mwenyewe binafsi nimetoa garimbili hospitali za Chwaka na Kongoroni. Lakini hii gari yapolisi lazima tuhudumie tupate na mimi nimesaidia Jozanipolisi walikuwa wanahitaji computer na nimewasaidia, lakinihii gari mnipatie zote mbili. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Waziri majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Bhagwanji hakuulizaswali, ilikuwa ni ombi la gari la doria na mimi tu kwa niabaya Serikali tumepokea ombi lake na tutalifanyia kazi pindipale nafasi itakaporuhusu basi tutaona namna ya kuwezakufanya.

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Na. 62

Kodi za Zimamoto kwa Wananchi Wanaopimiwa Ardhi

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza:-

Jitihada za wananchi kukaa katika maeneoyaliyopimwa zinakabiliwa na changamoto ya malipo yashil ingi 150,000 ambayo ni kodi ya zimamoto palewanapotaka kupimiwa ardhi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kufuta kodi hiyo ilikupunguza ongezeko la makazi holela?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI)alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali laMheshimiwa Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa MpandaMjini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Zimamoto na Uokoajilinafanya ukaguzi kwa mujibu wa Sheria Namba 14 Sura Na.427 (Fire and Rescue Force Act) ya mwaka 2007 kupitaiakanuni zake za ukaguzi na vyeti ya mwaka 2008 ikisomwapamoja na ya mwaka 2014 [Fire and Rescue Force; (SafetyInspections, Certificate and Fire Levy) Regulalations] za mwaka2008 na mwaka 2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni zaUkaguzi za mwaka 2014 (Fire Levy Category No. 58) kanuniinaelekeza kutozwa tozo ya usomaji na ushauri wa michoroau ramani za majengo. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni yaMajengo ya mwaka 2005 [The Fire and Rescue Force, (FirePrecautions in Buildings) Regulations], 2015 Na. 248 Jeshi lazima moto na Ukoaji limekuwa likishiriana na Halmashauriza Miji, Manispaa na Majiji kukagua ramani za ujenzi ilikuhakikisha kuwa nyumba zinajengwa kwa kuzingatia

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

tahadhari na kinga dhidi ya moto na majanga mengine.Kupitia ushauri huu Jeshi la zimamoto na uokoaji hutoza tozoambapo kiasi cha tozo huzingatia aina ya ramaniiliyowasilishwa na kukaguliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia umuhimuwa ujenzi unaozingatia tahadhari na kinga dhidi moto,Serikali haikusudii kufuta tozo hii kwa sasa. Aidha, Serikalikupitia Jeshi la Zimamoto na uokoaji inawaasa Wananchikwa kujenga nyumba zao kwa kufuata Sheria na Kanunizinazosimamia mipango miji ili kuwa na miji salama hivyokupunguza athari zitokanazo na moto na majangambalimbali na kuwezesha utoaji wa huduma za kijamii kwaurahisi zaidi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kapufi.

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa kibali cha Halmashauri kinatozwa shilingi16,000, kiwango ambacho ni nafuu, je, zimamoto kutoza150,000 haioni kwamba kiwango hicho ni kikubwa na hivyoinapelekea wananchi wengi kujenga bila kuwa na kibali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mchanganuowa tozo kwa mjenzi wa nyumba ya kawaida anatozwa hiyohiyo shilingi 150,000 sawa na mjenzi wa ghorofa, hii imekaaje?

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Waziri majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanzaametaka kujua tozo ya shilingi 150,000 kwamba ni kubwana hivyo inawafanya wananchi washindwe kupata kibali hikina hivyo kujenga majengo holela. Tozo hizi ni kwa mujibuwa Kanuni na Sheria ambazo tumejiwekea, ukiacha ileHalmashauri ambayo ni shilingi 16,000 anayosema yeye, lakini

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

kwa mujibu wa taratibu ambazo tumejiwekea kwa maanaya Sheria yetu hasa katika Kanuni ile ya [The Fire and RescueForce, (Fire Precautions in Buildings) Regulations], 2015 Na. 248imezungumza kiwango ambacho kinapaswa kutozwaukianzia katika Majiji, Halmashauri, Wilaya lakini vile vile nakatika vijiji. Kwa hiyo kiasi kilichowekwa hapa cha shilingi150,000 ni kwa mujibu wa Sheria yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ametakakujua kuhusu utofauti wa utozwaji wa tozo hizi. Tozo hizizinatofautiana kutokana na kiwango cha ukubwa wa jengoau vile vile mita za ujazo wa jengo. Kwa hiyo, haiwezi ikawakuna mfanano kwa namna ambavyo tozo hizi zimewekwa.Kikubwa kinachoangaliwa hapa ni mita za ujazo. Kwa hiyo,mita za ujazo zinavyozidi kuwa kubwa zaidi ndiyo tozozenyewe zinazidi kuongezeka.

MWENYEKITI: Ahsante. Dkt. Kikwembe.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza swalila nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na swali laMheshimiwa Kapufi kuhusiana na hizi kodi za zimamoto,ninachojiuliza na wananchi wanachojiuliza hasa wa Jimbola Kavuu wanataka kujua, kwa nini hizi tozo zimeanzakutozwa sasa, na watu gani wameshirikishwa? Kwa sababuzinaoneka zimeibuka, hata kama zilikuwepo kwa ujibu waSheria, zimeibuka kiasi kwamba hata wale wenye guesthouses sasa hivi zimamoto wamekuwa wakiwavamia nakuwa-charge hizi kodi. Kwa hiyo, tunaomba ufafanuzi nigazeti namba ngapi zilizoruhusu hizi kodi zianze kutumika?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika majibuyangu ya msingi ya awali kabisa ni kwamba tozo hizi

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

zinatokana kwa mujibu wa Sheria na Kanuni ambazotumejiwekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwasababu MheshimiwaMbunge ameonyesha interest ya kufahamu namba ya GNambayo siponayo hapa hiyo namba nitampatia, lakini nikwamba tozo hizi zinafanyika kwa mujibu wa regulationsambayo niliisema pale awali ya The fire and rescue force fireprecaution in buildings regulations ya mwaka 2015. Hivyokinachofanyika hapa hata ilikuwa ifanyike hapo awali lakiniutekelezaji wa Sheria unaendelea kuwa ni halali kwa sababuilikuwepo Kanuni hii na sasa ndiyo utekelezaji wakeunafanyika.

Na. 63

Kuutangaza Mkoa wa Tabora Kwa Utalii

MHE. MWANNE I. MCHEMBA aliuliza:-

Mkoa wa Tabora umepata usafiri wa uhakika wandege ya ATCL na kwa kuwa Tabora ina historia mbalimbalina kumbukumbu za mambo ya kale.

Je, Serikali ipo tayari kuutangaza Mkoa wa Taborakwa utalii?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii naomba kujibu swali la Mheshimiwa MwanneIsmail Mchemba, Mbunge wa viti maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Tabora umo katikaKanda ya Kati inayounganisha Mikoa ya Dodoma, Singidana Kigoma. Ni kweli kabisa kuwa Mkoa wa Tabora kamasehemu ya Kanda ya Kati una historia mbalimbali nakumbukumbu za mambo ya kale ikiwa ni pamoja na Tembelililokaliwa na missionary Dkt. Livingstone, ambaye ni mpingabiashara ya utumwa kutoka Uingereza mwaka 1871 akiwa

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

njaini kuelekea Ujiji - Kigoma. Pia kuna kituo cha njia ya katiya biashara ya utumwa na vipusa vilivypo Ulyankulu eneo laMtemi Mirambo na Gofu lililokuwa hospitali ya kwanza yaKijerumani katika Mkoa wa Tabora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tembe la Dkt. Livinstonelimekarabatiwa na kuna Watumishi ambao wanatoamaekelezo kwa wageni wanaotembelea kituo hicho. Katikamwaka wa fedha 2013 hadi 2017 kituo kilitembelewa nawageni 1,642 na jumla ya shilingi 2,292,000 zilikusanywa kutokakwa watalii wa ndani na nje. Aidha, mipango ya usimamiziwa maeneo mengine niliyoyataja hapo juu imeandaliwa iliyaendelezwe kuwa vituo vya kumbukumbu na taarifa kwamatumizi mbalimbali yakiwemo ya utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ufanisi wa utangazaji,utalii wa Mkoa wa Tabora juhudi za utangazaji zinahusuvivutio vingine zaidi ya vivutio vya mambo ya kalevinavyopatikana katika eneo hilo. Juhudi hizo zinahusuutamaduni, wanyamapori, mazao ya nyuki na historia panaya harakati mbalimbali za kijamii za nchi yetu zilizofanyikaMkoani Tabora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumhakikishiaMheshimiwa Mbunge kuwa juhudi za kuendeleza nakuutangaza Mkoa wa Tabora kiutalii zimekuwa zikiendeleahata kabla ya kuwepo kwa usafiri wa ndege ya ATCL. Kwakuwa sasa Mkoa umepata usafiri wa uhakika wa ndege yaATCL, Serikali itaongeza juhudi za kuutangaza Mkoa waTabora nje na ndani ya nchi ili kuhakikisha wageni wengiwanatembelea Mkoa huo kwa lengo la kukuza utalii nakuongeza pato la Taifa.

MWENYEKETI: Mheshimiwa Mwanne.

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza namshukuru MheshimiwaNaibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo yamekidhi lakininaomba niongeze kama ifuatavyo:-

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Mkoa wa Taborauna historia nyingi sana ukizingatia pia na historia ya Babawa Taifa, lakini wakati anajibu majibu yake Baba wa Taifahakuwepo, hawakuongeza, kwa hiyo, niombe Wizara yautalii iongeze kuitangaza historia ya Baba wa Taifa.

Lakini lingine kuna historia ya miembe ambayo inaumri wa miaka 100 nayo ipo kwenye njia ya watumwa. Kwahiyo niombe niulize maswali mawili ya nyongeza kamaifuatavyo:-

Kwa kuwa hivi sasa njia ya utmwa inatambulika, je,Serikali iko tayari kuikarabati ile njia kutoka Tabora hadiKigoma - Ujiji ili iwarahisishie watalii kupita?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lingine, je, Serikali ikotayari kuwatuma wataalam kuhakikisha vivutio vyoteambavyo vipo katika Mkoa wa Tabora vinaorodheshwa?Ukilinganisha na mapato yaliyopatikana tangu 2013 mpaka2017 ni milioni mbili, milioni mbili kuna nini? Kwa hiyo nasemakwa uchungu kwamba bado tunahitaji utangazaji wa utaliikwa Mkoa wa Tabora ni muhimu sana naomba izingatiwe,ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi,halafu ajiandae Mheshimiwa Selasini.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, suala la kukarabati hii njia ambayo inatokaTabora hadi Kigoma hili tutalifanyia kazi, tutaangalia kadriupatikanaji wa fedha utakavyokuwepo katika bajeti zetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pil i, kuhusukuorodhesha vituo, ni kweli kabisa Tabora ina historia ndefusana ikiwa ni pamoja na hiyo aliyoisema ambapo MwalimuJulius Kambarage Nyerere aliweza kusoma katika Mkoa ulena mambo mengine mengi na mimi mwenyewe nimefikakatika yale maeneo, nimetembelea na nimeyaona. Kwa hiyoorodha tuliyonayo ni kubwa na tutaendelea kuifanyia kazi,

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

kuiuhisha ili tuweze kuongeza mapato yatokanayo na utaliikatika Mkoa huu wa Tabora.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Selasini.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu ina vivutio vingisana vya utalii ukiacha mbuga zetu na mlima na kadhalika,wazee wetu wa zamani, machifu wana vitu vyao ambavyowalikuwa wanatumia. Tuna ngoma zetu na vitu hivi vinaazakupotea. Sasa Wizara hii ya Maliasili na Utalii ina mpangogani wa kuhakikisha kwamba vivutio kama hivi, miji yetukama Mji wa Kilwa vinahifadhiwa kwa ajil i ya vizazivinavyokuja?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli nchi yetu na ina vitu vingi ambavyo nivivutio vya utalii. Ni azma ya Wizara yetu kuhakikishakwamba hivi vyote vinahifadhiwa ili viweze kutumika navizazi vijavyo viweze kuvielewa na viweze kufaidika namatunda ya hivyo vitu vyote. Kwa hiyo ni azma ya Wizarayetu, itaendelea kulishughulikia, kuvilinda na kuvihifadhi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwakasaka, halafutunaendelea.

MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa nukipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza. Kwa kuwa Mkoa wa Tabora una vivutio vingi vyautalii ukiwemo uwandaji. Ni lini Serikali itafanya uhakiki wavitalu vya uwindaji vilivypo Tabora? Kwa sababu kuna taarifakwamba vitalu vya uwaindaji vilivyopo vinasomeka nivichache kuliko uhalisia wa vitalu vilivyopo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri mahibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kabisa kuna vitalu viko vingi katika nchiyetu na kazi yetu kubwa ambayo tunaifanya sasa hivi,tunapitia upya vitalu vyote ili tuweze kuvibaini na kuona vipivinafaa na vipi havifai. Kwa hiyo badaa ya kukamilisha hilozoezi ni wazi kabisa Mheshimiwa Mbunge atafahamu ni vitaluvingapi ambavyo vinapatikana katika Mkoa wa Tabora.

Na. 64

Ulipaji wa Fidia Barabara ya Morogoro

MHE. JOHN J. MNYIKA aliuliza:-

Eneo la hifadhi ya barabara ya Morogoro katikaJimbo la Kibamba ni pana kuliko barabara kuu nyingine nchinina inaingia katika makazi ya asili ya wananchi.

(a)Je, ni lini Serikali itawalipa wananchi fidia kwa ardhiya asili ya tangu kabla ya uhuru ambao walihamia wakatiwa vijiji vya ujamaa?

(b)Je, ni l ini Serikali itawasilisha Muswada waMarekebisho ya Sheria husika ili eneo la hifadhi ya barabaraiwiane na barabara kuu nyingine nchini?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano napenda kujibu swali laMheshimiwa John John Mnyika, Mbunge wa Jimbo laKibamba, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sheria yaBarabara ya mwaka 1932 (The Highway Ordinance Cap.167)kifungu namba 52 eneo la hifadhi ya barabara ya Morogorokuanzia maili 10.02 yaani kilometa 16 kutoka Posta ya Zamani

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

mpaka maili 23.12 yaani kilometa 37 ni futi 400 ambazo nisawa na takribani mita 120 kila upande kutoka katikati yabarabara. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitiaTANROADS imeweka nguzo za kuonesha mipaka ya eneo lahifadhi ya barabara katika eneo tajwa na maeneo menginenchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya barabara yaMorogorio kati ya kilometa 16 na kilometa 37 iko ndani yaJimbo la Kibamba ambapo hifadhi ya barabara ni mita 120kila upande kutoka katikati ya barabara. Hivyo Serikalihaitalipa fidia kwa mwananchi yoyote wa Jimbo la Kibambaaliyejenga au aliyefanya maendelezo yoyote ndani ya eneola hifadhi ya barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haina mpango wakuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ili kufanyaeneo la hifadhi ya barabara Morogoro liwiane na barabarakuu nyingine nchini kwa kuwa eneo la hifadhi ya barabaraya Morogoro lililotengwa linahitajika kwa ajili ya upanuzi wabarabara ili kuwaiana na mahitaji ya sasa na ya miaka ijayo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Serikali katika majibu yake imesema kwamba upana huo wamita 120 ni kwa mujibu wa Sheria ya Barabara ya mwaka1932; sheria ambayo kwa sasa haipo, kwa sababu kwamujibu wa Sheria ya Barabara ya mwaka 2007, kifungu cha62.41 sheria hiyo ya mwaka 1932 ilifutwa. Kwa hiyo, tafsiri yakenini? Serikali ilifanya bomoa bomoa haramu, ambayo nikinyume cha sheria. Sasa kwa kuwa Rais Magufuli akiwaMwanza alitoa kauli ya kibaguzi yenye kueleza kwamba…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika uliza swali

MHE. JOHN J. MNYIKA: …nauliza swali sasa.

MWENYEKITI: Uliza swali

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

MHE. JOHN J. MNYIKA: Nauliza swali, kwa kuwa Raismagufuli alitoa kauli ya kibaguzi yenye kuonesha kwambawananchi wale wa Mwanza hawatabomolewa…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika chunga lugha zako,nakuomba uchunge lugha zako.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Swali ninalotaka kuulizaSerikali; kama Mheshimiwa Rais Magufuli si mbaguzi, Serikaliitoe kauli hapa ya kuwalipa fidia wananchi wa Jimbo laKibamba waliobomolewa kwenye barabara ya Morogoro.

MWENYEKITI: Mheshimwia Waziri majibu kwa kifupi.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Swali la pili.

MWENYEKITI: Unaanza maneno mengi mpakaunanichanganya hapa. (Kicheko)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwasababu serikali imesingizia Sheria, mimi nilichukua hatuakama Mbunge Rais alipopiga Mbezi akasema kwamba kamaWabunge wanataka upana wa barabara urekebishwewapeleke Muswada wa Sheria Bungeni nilileta muswada washeria wa marekebisho ili barabara yote iwe mita 60 lakiniSerikali ikaa njama na Katibu wa Bunge aliyekuwepo Dkt.Kashililah kuzuia muswada huu. Ni lini sasa Serikali itaachanana hizi njama na itakubaliana na kauli ya Mheshimiwa Raisna muswada utaletwa hapa Bungeni ili barabara hii iwe naupana wa mita 60 kama zile barabara nyingine nchini?(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaMwenyekiti, suala la barabara limeainishwa vizuri katika

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

sheria kuanzia sheria niliyoitaja katika jibu la msingi, sheria yamwaka 1932. Vilevile nimwambie Mheshimiwa Mbungekwamba iko pia Sheria Namba 27 ya mwaka 1959, ipo SheriaNamba 40 ya mwaka 1969, pia iko Sheria Namba 13 yamwaka 2007.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria hizi zilivyokuwazikitungwa zilikuwa zinatazama maendeleo ya barabara sikuza usoni na wala siyo siku za nyuma na ukizisoma sheria hizizilikuwa zinaainisha barabara. Kwa mfano hii sheria yamwaka 1932 ilitaja kabisa barabara kutoka Dar es Salaamkwenda mpaka Ruvu na maeneo gani yawe na ukubwagani, eneo lipi liwe na ukubwa upi kwa ajili ya kuzingatiamaendeleo na ukuaji wa shughuli za kibinadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimshauriMheshimiwa Mnyika, ziko taratibu za kuhakikisha kwambakama kuna barabara inatakiwa itajwe na kufanyiwamaboresho ziko taratibu zinaanzia katika Halmashauri naMamlaka ambazo zinasimamia barabara. Atumie fursa hiyokuwasiliana na mamlaka yake upande wa Serikali yaManispaa ya Kibamba ili kweza kuleta maombi. Na kwa hiiSheria Namba 13 inampa nafasi Mheshimiwa Waziri kupitiamaombi kutoka kwenye mamlaka zinazosimamia barabarakuona kama kuna eneo linaweza likafanyiwa jambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hakuna njamayoyote na suala la fidia itakwenda kwa mujibu wa sheria.

MWENYEKITI: Ahsante, Waziri Chief Whip,Waheshimiwa kaeni chini Chief Whip amesimama.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimpongeze kwanza MheshimiwaNaibu Waziri kwa majibu mazuri sana ambayo ameyatoahivi punde. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninayo majibumachache tu ya nyongeza. Kwa mujibu wa kanuni

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

zinazoendesha Bunge sehemu ya Nne ya kanuni zetuzinaonesha mpangilio wa shughuli katika Bunge letu. Sehemuya Tano ya kanuni zetu inaonesha mpangilio wa namnamajadiliano yatakavyofanywa ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kwa faida yaWatanzania, si kweli, si kweli, si kweli kwamba Serikali ilikulanjama na Ofisi ya Bunge ili kuzuia muswada wowote ambaouliletwa katika Bunge hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwa hiyo, ili kuweka majibuya Serikali vizuri katika swali la nyongeza la MheshimiwaMnyika tunaomba tulieleze Bunge lako Tukufu kwamba swalila nyongeza lililoulizwa na Mheshimiwa Mnyika si swali ambalolina tafsiri ya ukweli wa hali halisi iliyojitokeza katika muswadawake, na Bunge hili linaongozwa kwa kuzingatia kanuni nataratibu na sisi Serikali hatuna utaratibu wowote wa kulanjama na Bunge hili.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Ahsante, Waheshimiwa tunaendelea.Mheshimiwa Felister Bura.

Na. 65

Ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa - Mpwapwa

MHE. FELISTER A. BURA aliuliza:-

Wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015aliyekuwa mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM Mhe. Dkt.John Pombe Joseph Magufuli aliwaahidi wananchi waKongwa na Mpwapwa kujenga barabara ya Mbande –Kongwa - Mpwapwa kwa kiwango cha lami.

Je, ni lini barabara hiyo itaanza kujengwa?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) alijibu:-

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano napenda kujibu swali laMheshimiwa Felister Aloyce Bura, Mbunge wa Viti Maalumkama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Mbande –Kongwa – Mpwapwa yenye urefu wa kilometa 49.19 ilifanyiwausanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami nausanifu ulikamilika mwaka 2013. Baada ya kukamilika kwausanifu Serikali imeanza ujenzi wa barabara hii kwa kiwangocha lami kwa awamu ambapo mwezi Julai, 2017 sehemu yabarabara yenye urefu wa kilometa 11.7 kutoka Mbandekuelekea Kongwa ilianza kujengwa. Hadi mwishoni wa mweziOktoba, 2017 kiasi cha kilometa tano za sehemu ya barabaraya Mbande - Kongwa zimekamilika kujenga hadi tabaka lajuu (basic course). Mkandarasi anaendelea na kazi ya ujenzikwa kiwango cha lami.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bura.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naishukuru Serikali na kuipongeza kwa kuanza ujenzi wabarabara ya Mbande – Kongwa – Mpwapwa kwa kiwangocha lami. Naamini mwaka ujao wa fedha barabara hiiitakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali; kwa kuwa mji waDodoma na viunga vyake unakua kwa kasi sana kutokanana Serikali kuhamia Dodoma, na kwa kuwa tusingependamji wa Dodoma ukawa na msongamano kama Dar esSalaam; je, Serikali iko tayari na ina mkakati gani madhubutiwa kuhakikisha kwamba barabara za mzunguko katika mjihuu zinaanza kujengwa kupunguza Msongamano unaowezakuwepo mji utakapokua?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, ni lini Serikaliitajenga barabara nyingine baada ya barabara iliyokuwainatoka Shabiby Petrol Station na Area D kufungwa kwa ajiliya upanuzi wa uwanja wa ndege na sasa wananchi wa AreaD, Mlimwa, Majengo Mapya na maeneo mengine

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

wanazunguka mpaka Swaswa ndipo waje mjini, je, ni linibarabara hiyo itaanza kujengwa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaMwenyekiti, Serikali inatambua kwamba Dodoma ndiyomakao Makuu na mpango mzima wa kuhamia Dodomaunaendelea. Pia Serikali inatambua umuhimu wa kuboreshabarabara zake ili kuondoa usumbufu ambao unawezakujitokeza kutokana na ukuaji wa mji wa Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu MheshimiwaMbunge kwamba Serikali imeshaweka mkandarasi kwa ajiliya usanifu wa barabara za mzunguko za Dodoma ambazozitakuwa na ukubwa wa kilometa 96. Tulitenga fedha kiasicha shilingi 959,812,000 kwa ajili ya kuhakikisha kwambausanifu unakamilika; na usanifu wa barabara za Dodomautakamilika mwezi wa tano mwaka 2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie tuMheshimiwa Mbunge kwamba hatua iliyofikiwa sasa hivituko zaidi ya asilimia 25 ya zoezi la usanifu na mimi ni witowangu tu kwa maana kwamba hii kazi isimamiwe vizuri naupande wa TANROADS iliusanifu ukamilike ikiwezekanamapema kabla ya muda huu ili harakati za kutafuta fedhana kujenga barabara za mzunguko wa Dodoma ziwezekufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili,tunatambua usumbufu ambao unajitokeza na sasa hivi piatunaona kuna foleni zimeanza kuonekana. Hii barabaraanayoitaja Mheshimiwa Mbunge ambayo inaleta usumbufukwa wakazi la eneo la Area D, Mlimwa na Majengo Mapyakama Mheshimiwa Mbunge alivyosema ninatambua urefuwa kilometa kama mbili; barabara hii mawanzoni ilikuwainasimamiwa na CDA kabla haijavunjwa. Kwa hiyo, upandewa Serikali tumechukua jukumu la kuhakikisha sasa kipandehiki cha barabara kinatengenezwa haraka ili Waheshimiwa

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Wabunge wakiwa Dodoma pamoja na wananchi waDodoma kwa ujumla wasipate shida kutokana na shidaambayo imejitokeza baada ya ujenzi wa uwanja ule wandege kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo zoezi la kutafutafedha kwa ajili ya kukamilisha kipande hicho pamoja nakusimamia maeneo ambayo yametengewa fedha kwa tijatutapokuwa na balance kidogo imebakia tutaanza kupelekaeneo lile ili barabara iweze kujengwa, Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante, ameshakuelewa, MheshimiwaChikambo.

MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kwanza nianzekuwapongeza Mawaziri na Manaibu Mawaziri kwa kazi nzuriwanayoifanya, Mheshimwa Rais amewaona ninyi na sisiWabunge wenzenu tuna imani na ninyi katika kutatua keroza wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niulize swali lanyongeza. Wakati wa Kampeni za Uchaguzi Makamu waRais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliahidi ujenzi wabarabara kwa kiwango cha lami, barabara inyoanziaWilayani Namtumbo katika vij i j i vya Mtorapachani,Ligusenguse na kuelekea Mchoteka na Lasi hadi Tunduru.Naomba nijue ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara hiyo?Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri anataka kujua ni linitu.

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nisemetu kwa ufupi kabisa tunaratibu ahadi zote za MheshimiwaRais, ahadi zote za Makamu wa Rais kwa maeneo ambayoyanahusu ujenzi wa barabara. Nimuahidi tu kwamba katikakipindi cha miaka mitano hivi zoezi hili litakuwa linaendeleakukamilisha barabara zote zilizoko kwenye ahadi, ahsante.

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

Na.66

Kutumia mfumo wa kununua unit katika maji nchini

MHE. SEIF K. GULAMALI aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaamua kubadili mita zote za maji iliwananchi wanunue maji kwa mfumo wa unit wao wenyewekama ilivyo kwenye umeme?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Maji na Umwagiliaji naomba kujibu swali laMheshimiwa Seif Khamis Gulamali, Mbunge wa Manongakama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na tatizosugu la baadhi ya wateja wa Mamlaka za Maji kutolipaankara za maji na kulimbikiza madeni, Wizara yangu inafanyamajaribio ya kutumia mfumo wa malipo kabla ya hudumayaani prepaid system. Kupitia mfumo huo, mteja hufungiwakifaa maalum kinachomwezesha kulipia kwanza kiasi chamaji anachohitaji kabla ya kutumia. Hata hivyo, mfumo huouna gharama kubwa kiuwekezaji na kimatunzoikilinganishwa na mfumo unaotumika sasa. Kwa sababu hiyoya gharama Wizara imeagiza baadhi ya Mamlaka kuzifungamita hizo kwa wateja wake wenye tabia ya kulimbikizamadeni ya ankara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi mwezi Oktoba, 2017jumla ya Mamlaka za maji saba zimeanza kutumia mfumohuo kwa baadhi ya wateja wao. Mamlaka hizo ni za Miji yaMakao Makuu ya Mikoa ya Iringa, Arusha, Dodoma, Mbeya,Songea, Tanga na DAWASCO ya Jiji la Dar es Salaam. Mpakasasa mfumo umeonesha mafanikio makubwa. Hata hivyo,kutokana na ukubwa wa gharama za mfumo huo, Wizaraimeziagiza Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira zaDaraja ‘A’ zinategemea kwa gharama zote za uendeshajikuhakikisha kuwa zinatenga fedha katika bajeti zao ili

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

kuwezesha kuendelea na ufungaji wa mfumo huo kwa kadrihali ya kifedha itakavyoruhusu.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Gulamali,ajiandae Mheshimiwa Bashe atafuatiwa na MheshimiwaJacqueline.

MHE. SEIF K. GULAMALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kufahamu, je, Serikali inampango gani ya kusambaza huduma hii nchi nzima hasakatika Wilaya ya Igunga na Mkoa wa Tabora na ukifuatiliakwamba katika Wilaya ya Igunga na Mkoa wa Tabora hivikaribuni tutaweza kupata maji ya Ziwa Victoria?

Mheshimiwa, la pili, nilikuwa nataka kujua juu yaWizara hii ya Maji, inatoa tamko gani kwa baadhi yaMamlaka za Maji nchini ambazo zinatoa bili kubwa kwawatumiaji wa maji kuwabambikiza bili kubwa watumiaji wamaji kuliko matumizi halisi ya wananchi wanaotumia kwenyemaji? Nataka kujua tamko la Serikali juu ya ubambikizaji wagharama za maji, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikushukuru lakininimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa namnaanavyopigania wananchi wake. Lakini kikubwa napendakujibu maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ni kuhusu suala zimala usambazaji mkakati wetu kama Serikali. Safari ni hatuana hatua tumeshaianza ya kutekeleza mamlaka saba na kwakuwa safari moja huanzisha nyingine sisi kama Serikali kwakupata nafasi ya kuweza kutekeleza mamlaka sabatunaziagiza mamlaka zote zenye uwezo wa kujitoshelezakigharama kutenga bajeti kuhakikisha kwamba

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

wanatengeneza mifumo hii ili kuweza kuyafikia maeneo yambali katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, katikabaadhi ya mamlaka kuwabambikia wananchi ama watejagharama ambazo si halisia haipendezi, wala haifurahishi,kuona baadhi ya mamlaka zinawabambikia bei wananchi.Mimi nataka niziagize mamlaka zote nchini kwamba watoebei halisia ambazo zimeidhinishwa na EWURA. Kama kunamtu au mamlaka itakayokaidi hata kama ana mapembemarefu kiwango gani tutayakata ili kuhakikisha kwambawananchi wetu wanapata huduma bila usumbufu wowote.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Bashe, atafuatiaMheshimiwa Jacqueline, halafu Mheshimiwa Mtulia.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi. Nilitaka nimuulize MheshimiwaNaibu Waziri au niombe tamko la Serikali, kwenye bajetimwaka huu tulitaka Halmashauri zote ambazo ni class threeambazo zina madeni Serikali Kuu kupitia fundszinazokusanywa na EWURA zipelekwe Wizara ya Maji ilimadeni hayo walipwe. Leo ni wiki ya pili Halmashauri ya Mjiwa Nzega imezimiwa umeme na TANESCO kwa sababu yamadeni yaliyotokana na Serikali Kuu kutokupeleka fedha zautilities kwenye Halmashauri kwa miaka mingi.

Je Serikali iko tayari leo kuitaka TANESCO iwezekuruhusu watu wa Nzega waweze kupata maji?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Nishati.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awaliya yote nichukue nafasi hii kumshukuru sana MheshimiwaBashe. Tumetoa maelekezo na tumeshakaa na wadau wotekwamba taasisi zote muhimu za Serikali; afya, maji, usalamana maeneo mengi waje tukae tuweke utaratibu. Hatukatiumeme kama tumeshaweka utaratibu, lakini tukishawekautaratibu halafu utaratibu ukakiuka kwa kweli sisi tunakataumeme. Nichukue nafasi hii tutakaa na Mheshimiwa Bashe

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

na Waheshimiwa wengine tuone namna gani ya kulifanyajambo hili ili wananchi waendelee kupata maji.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Jacqueline,ajiandae Mheshimiwa Mtulia.

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili na miminiweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto iliyoko katikaJimbo la Manonga linafanana kabisa na changamoto iliyokokatika mkoa wangu wa Ruvuma. Katika mkoa wa Ruvumakuna changamoto ambayo itaenda sambamba na tatizola kubadili mita za maji kutokana na mfumo wa kupata majikwa maana ya mita ibadilike kuwa wananchi wapate majikwa mfumo wa unit. Sambamba na hilo, iko miradi ambayonilikuwa nikisema hapa mara nyingi katika mkoa wangu waRuvuma ambayo kimsingi inaonekana kwamba imekamilikalaikini haitoi maji, na miradi hiyo inataokana na World Bank.

Mheshimiwa Mwenyekiti, World Bank wamefanya hiyokazi na miradi inaonekana kwamba sasa tayari inatoa maji,lakini katika miradi hiyo kuna mradi wa maji wa Mkako(Mbinga), Ruhuwiko (Songea Mjini), Matemanga na Ndembo(Tunduru), Litola (Namtumbo)...

MWENYETKITI: Uliza swali Mheshimiwa Jacqueline.

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: MheshimiwaMwenyekiti, Serikali ina mpango gani ya kuhakikisha miradihii inafanyiwa marekebisho ili iweze kutoa maji na wananchiwaweze kufaidika?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri subiri kwanza.

Waheshimiwa Wabunge, kuna wageni kwenyeJukwaa la Spika ambao ni Balozi mpya wa ChinaMheshimiwa Wang Ke, amefatana na Mheshimiwa Liang Leena Yang Han Chin na Ndugu Liang Lee Mkurugenzi wa Siasa

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

na Mheshimiwa Yang Han Chin ni Katibu wa Balozi. Thankyou very much for visiting the parliament in Dodoma now Ibelieve you have an appointment with Speaker, your free togo to the Speaker now thank you very much. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri endelea.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema kwamba miradiimekamilika lakini maji haitoi kwa wananchi. Lengo la Serikalikuhakikisha kwamba wananchi wanapata maji na fedhazimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ile. Lakini chakushangaza miradi imekamilika haitoi maji. Labdanimuombe Mheshimiwa Jacqueline kwamba baada yaBunge tuongozane pamoja tukaone sababu ganizinazosababisha mradi ukamilike lakini hazitoi maji? Kamakuna mtu ambaye anasababisha au kukwamisha ili maji isitoetutalala naye mbele ili wananchi wetu waweze kupata maji.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mtulia.

MHE. MAULUD S. MTULIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii na mimi kuuliza swalila nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakubaliana kwambamaji ni uhai na kila mwananchi anahitaji maji; lakinitunakubaliana pia kwamba zamani tulikuwa na mabombayetu ya Serikali ambayo wananchi walikuwa wanapata majibure, lakini sasa hayapo.

Je, Serikali ian mpango gani kuyarejesha yalemabomba yetu ili wananchi wetu wapate maji bure kwawale ambao hawana uwezo ukizingatia kwamba kuhitajimaji hakutegemei uwezo wa fedha za mtu? Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kabisa kwamba zamani kulikuwa na

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

mabomba ambayo yalikuwa yanatoa maji bure na hivyokusaidia wale watu wasiojiweza, lakini kwa sasa mamlakazote zimepewa maelekezo na zina sheria kwamba kilamamlaka kwenye mkoa inashirikiana na uongozi wa mkoakubaini wananchi wote ambao hawana uwezo kamawazee na wagonjwa, kwa hiyo wakiorodheshwawanaendelea kupata kupata huduma ya maji bure.

Na. 67

Ujenzi wa Mahakama Chemba

MHE. JUMA S. NKAMIA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya yaChemba?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NAVIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waKatiba na Sheria napenda kujibu swali la Mheshimiwa JumaSuleimani Nkamia, Mbunge wa Chemba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Serikali ni kusogezahuduma karibu na wananchi. Juhudi kubwa zinaendeleakufanyika kuhakikisha kuwa kila Wilaya nchini inakuwa namahakama. Katika mwaka wa fedha 2018/2019 Serikaliimepanga kujenga jingo la Mahakama Wilaya ya Chemba.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nkamia.

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa majibu mazuri na ya uhakika ya MheshimiwaNaibu Waziri. Nilikuwa na swali moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya Chemba ni moja katiya Wilaya kubwa sana katika Mkoa huu wa Dodoma napengine kwa Tanzania kwa ujumla. Je, Serikali wakatiinasubiri kujenga jengo la Mahakama katika Makao Makuu

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

ya Wilaya iko tayari sasa kuimarisha mahakama za Mrijo nakwa Mtoro ili kupunguza adha inayowafanya wananchikutembea zaidi ya kilometa 170 kufuata huduma zamahakama Wilayani Kondoa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NAVIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli anachokisema Mheshimiwa Mbungekwamba Wilaya ya Chemba ni kubwa sana, na kwa sababumahakama hii ya wilaya itaanza kujengwa katika kipindi chamwaka wa fedha 2018/2019 niseme tu kwamba nimepokeaombi na mawazo ya Mheshimiwa Mbunge na sisi kama Serikalitutaona namna bora ya kuweza kuimarisha huduma katikamaeneo ya Mrijo ili wananchi wasipate shida kutembeaumbali mrefu kwa sababu alipokusema huko MheshimiwaNkamia ni mbali sana mpaka kufika katika makao makuuya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama Serikalikatika mpango wetu wa kuhakikisha kwamba tunasogezahuduma hizi kwa wananchi tutahakikisha pia tunalifanyiakazi jambo hilo la kuboresha huduma za mahakama katikamaeneo hayo ili wakati tunaendelea kujipanga katika ujenziwa Mahakama ya Wilaya wananchi waendelee kupatahuduma katika maeneo ya Mrijo na maeneo mengineyo.(Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, muda wetuwa maswali umekwisha. Sasa ni muda wa wageni.

Waheshimiwa Wabunge, wageni watatu waMheshimiwa Jumaa Aweso (Mbunge), Naibu Waziri wa Majina Umwagiliaji ambao ni ndugu zake kutoka Jimboni kwakePangani Mkoani Tanga. Karibuni. (Makofi)

Wageni walikuja kwa aji l i ya mafunzo, kunawanafunzi 36 na walimu watano kutoka shule ya msingi yaMtakatifu Felister ya Mkoani Dodoma.

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Pia kuna Wachungaji 12 ambao ni wanachama waKanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania kutoka IlazoMkoani Dodoma, karibuni Dodoma. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, Idara ya Shughuli za Bungeinawatangazia Waheshimiwa Wabunge kwamba waleambao hawajachukua Kamusi Kuu ya Kiswahili katikaMkutano wa Nane wa Bunge wafike eneo la mapokezi kwaajili ya kuchukua Kamusi hizo.

Tangazo lingine ni kuwa Mwenyekiti wa Bunge SportsClub Mheshimiwa William Ngeleja anapenda kulitaarifu Bungekwamba siku ya Jumapili tarehe 12 Novemba, 2017 baadhiya Wabunge walishiriki mbio za marathon zilizofanyikakuanzia uwanja wa Jamhuri hapa Mjini Dodoma. Mbio hizoziliratibiwa na uongozi wa Mkoa wa Dodoma, zilidhaminiwana Kampuni ya Simu ya Tigo. Mgeni Rasmi alikuwa NaibuWaziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni Mheshimiwa JulianaShonza. (Makofi)

Kwa upande wa Bunge, wanaume mshindi wakwanza alikuwa Mheshimiwa Abdallah Haji Ally, wa pilialikuwa Mheshimiwa Venance Mwamoto na wa tatu alikuwaMheshimiwa William Ngeleja. Kwa upande wa wanawakemshindi alikuwa Mheshimiwa Oliver Semuguruka. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge wengine walioshirika nakujishindia medali walikuwa ni Mheshimiwa Mussa Mbarouk,Mheshimiwa Richard Mbogo, Mheshimiwa Salum Rehani,Mheshimiwa Ali Salim Khamis na Mbunge mwenyeji na NaibuWaziri Mheshimiwa Antony Mavunde. (Makofi)

Pia Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt.Kigwangalla alitia fora kwenye mbio za kilometa 21. Aidhambio hizo zilihudhuriwa na Waziri wa Mifugo na UvuviMheshimiwa Luhaga Mpina. Uongozi wa Bunge Sports Clubunawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge walioshirikimbio hizo. (Makofi)

Katibu!

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

MHE. MWITA M. WAITARA: Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Bado kuna Miongozo?

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ipo.

MWENYEKITI: Haya, Mheshimiwa Mbatia, MheshimiwaMollel na Mheshimiwa Mbarouk. Tuanze na MheshimiwaMollel.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: MheshimiwaMwenyekiti, kwa Kanuni ya 68(7) ningependa kutoa/kuelezea/kusema alichokisema hapa Mheshimiwa Mnyikakuhusu Miswada ya Wabunge na Serikali kutoruhusu kujaBungeni au kusomwa na Wabunge husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi mwenyewe ni mfano,mwezi wa pili mwaka 2016 niliandika Muswada Binafsi waKulinda Rasilimali za Umma kwa kushirikiana na wanasheriawa humu na wa nje. Ikapokelewa na Ofisi ya Katibu waBunge, lakini ikafika kwenye stage ya mawasiliano kati yaOfisi ya Mwanasheria Mkuu na Bunge kwamba MwanasheriaMkuu sasa aweze kuuleta Bungeni ili uweze kujadiliwa nanina barua zaidi ya tatu za Katibu wa Bunge akimkumbushaMwanasheria Mkuu wa Serikali kuleta huo Muswada.Kilichotokea baadaye niliona imeletwa huku kama Muswadawa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi ninachowezakusema kwa sababu dada yangu Jenista amesisitiza zaidi yamara tatu akionesha kwamba Serikali haifanyi hivyo kusemakwamba ni kweli Serikali imekuwa ikiwafanyia Wabungehivyo na mimi niliyesimama hapa nimefanyiwa hivyo. Kwahiyo kwa manufaa yetu sisi Wabunge wote, tupinge hili jambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mwongozo wakosasa. Kwanza kwa nini Serikali inafanya hivyo? Kwa nini

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

inazuia Miswada binafsi ya Wabunge na inafikiriwa nini sasakama kweli Wabunge tuko kwa ajili ya kutunga sheria nakuisaidia Serikali na Serikali yenyewe sasa imekuwainatukatisha tamaa kukaa chini na kufikiri namna ya kuisaidiaSerikali hii. Tufanye nini? Mwongozo wako ni nini? (Makofi)

MWENYEKITI: Nafikiri Serikali ilitoa majibu sahihi naalieleza kwa upana mkubwa. Lakini labda inawezekanahukuelewa. Mheshimiwa Jenista, hebu mueleze tenaakuelewe, inawezekana alikuwa...

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, tena hapa nimeshika Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Ibara ya 97(1) na mwenye Katibaningeomba aifungue na sitaki kupoteza muda kwa sababuWabunge wote wana Katiba; na wakienda Ibara ya 97(1)utaratibu wa kutunga sheria utaratibu huo umeainishwa.Hata hivyo, Katiba hiyo hiyo ya Jamhuri ya Muungano waTanzania imelipa Bunge lako Tukufu madaraka ya kusimamiashughuli zote za Serikali ndani ya Bunge kwa kuzingatia Kanuniambazo tunazitunga sisi wenyewe Wabunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwenye wajibu wa kuletaMuswada ndani ya Bunge lako si Serikali. Serikali hainamadaraka yoyote ya kutengeneza Order Paper walautaratibu wa Shughuli za Bunge na kuzileta shughuli hizo zaBunge ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninachotakakumwambia Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wenginewote ni kwamba sisi kama Serikali Miswada tunayoileta ndaniya Bunge imepata ridhaa ya kuingia ndani ya Bunge kwamujibu wa Kanuni hizi ambazo zinaliongoza Bunge lako. Sikwamba Miswada hiyo tumeileta kwa kupata ridhaa kutokakwa mtu mwingine yeyote, hapana.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pil i ninachotakakuwaeleza Waheshimiwa Wabunge, Muswada wowotebinafsi wa Mbunge yeyote na Muswada huo na wenyewekama utakuwa umekidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibuwa Kanuni hakuna haja yoyote ile ya kusema kwamba Serikaliimeuzuia Muswada ule, Muswada huo utaingia Bungeni kwamujibu wa Kanuni zinazotuongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nitaendeleakusimama na kusema kwamba si kweli kwamba Serikali kaziyetu ni kuzuia Miswada ya Waheshimiwa Wabunge kuingiaBungeni, hapana! Utaratibu wa shughuli za Bungeunaongozwa na Kanuni na unaongozwa na Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania. Niwaombe sanaWabunge wasiendelee kuibebesha Serikali mizigo ambayohaiwahusu. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante umejibu vizuri sana.Mheshimiwa Mollel nafasi yako imepita. Mheshimiwa Molleltafadhali! Ndiyo Kanuni hizi zinavyosema, sasa kama Kanunihii inakushinda hii ya miswada kweli utaiweza? (Makofi)

Mheshimiwa Mbatia, ajiandae Mheshimiwa Mbaroukhalafu Mheshimiwa Matiko.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Naomba kutumia Kanuni ya 68(7) pamoja na ileya 64(1)(a). Kwa kuokoa muda sitazisoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kuhusu swali namba 64lililojibiwa leo hapa Bungeni na Serikali la Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, The Road Act ya mwaka 2007kile kifungu cha 62(4)(1) kinasema; The Highways Act is herebyrepealed na kwenye sheria hiyo haielezei utaratibu wa upanawa barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nil ikuwa naombamwongozo wako ili kuweka kumbukumbu za Bunge vizuri.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Serikali ilivyotumia sheria kwamba ndiyo iliyoweka upana wamita 120 na 120 si sheria imeweka hiyo huwa ni regulations.Kwa hiyo, ingependeza Serikali ijibu swali hili upya ili iletetaarifa sahihi Bungeni kwa sababu taarifa hizo hazikuwasahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na (b) ni Serikali itumiehekima tu kwa wananchi wa Kibamba. Upana wa barabarawa zaidi ya robo kilometa yaani mita 240 sio jambo la kherikwa maendeleo endelevu ya Taifa letu.

MWENYEKITI: Unayo Kanuni hapo ? Ulikuwa unaisomanafikiri.

MHE. JAMES F. MBATIA: Ninayo.

MWENYEKITI: Soma Kanuni ya 45(3).

MHE. JAMES F. MBATIA: Kanuni ya 45?

MWENYEKITI: Kanuni ya 45(3).

MHE. JAMES F. MBATIA: “Iwapo Spika ataridhika kuwaswali la msingi au nyongeza halijapata majibu ya kuridhisha,ataagiza lijibiwe kwa ufasaha zaidi katika kikao kingine chaBunge.”

MWENYEKITI: Haya, tutalipokea hilo. MheshimiwaMbarouk.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. (Makofi)

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona. Mimi nimesimama ka Kanuni ya 68(7)na Mwongozo wangu kwako ni kama ufuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati likijibiwa swalinamba 63 kwenye maswali ya nyongeza lilizungumzwa sualala utalii hapa kwa vivutio ambavyo vipo katika Mkoa wa

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Tabora. Sasa katika Jiji letu la Tanga kuna kivutio kikubwaambacho ni cha kihistoria lakini pia yawezekana ikaja ikawani urithi wa dunia kwa siku za baadae cha Amboni SulphurBath. Kwa wale wenyeji wa Tanga, Amboni Sulphur Bath kwaKiswahili tunasema Amboni Maji Moto, kwamba ni majiambayo kama mtu ana ugonjwa wa ngozi au ana matatizoya tumbo akitumia yanaweza kumsaidia. Lakini naona kamavile kimesahaulika na kwa sasa hivi kufuatia ujenzi waKiwanda kile kikubwa cha Saruji kutaka kuongeza eneoyawezekana lile eneo likatolewa kwa ajili ya ujenzi waKiwanda cha Saruji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba Mwongozowako kwa Wizara ya Maliasili na Utalii. Haioni kwamba ikohaja ya kutumia chanzo kile cha kitalii na cha kihistoriakukipeleka katika UNESCO ili ikawa ni urithi wa dunia?Ahsante.

MWENYEKITI: Waheshimiwa hiki sio kipindi chamaswali na majibu, tunafanya tu mahsusi kwa sababutunajua Wabunge mnayo kiu ya kutaka kujua what ishappening! Serikali.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, hili ni suala jipya na sisi kama Serikali tunaombalije kwa utaratibu maalum il i na sisi tuweze kuwatunalifahamu vizuri. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nimesimama kwa Kanuni ya 47(1) kuhusu jambola dharura.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Wabunge wotewatakuwa aware kwamba nchi yetu sasa hivi imekuwa nasintofahamu ya usalama wa raia. Tumeshuhudia mambomengi yakiendelea kama kuokotwa kwa maiti kwenye fukweza bahari na Ziwa Victoria. Juzi waliokotwa watu watatu

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

wanaosadikika ni wafanyabiashara wamefungwa,wametupwa kandokando ya Ziwa Victoria upande wa Mkoawa Mara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Jimbo langu laTarime tumeshuhudia kuna kijana anaitwa Leonard Marwaameuawa, kafungwa na mawe katupwa kwenye Mto Msati.Juzi tumeshuhudia kijana anaitwa Hassan hapa Merriwa;mimi nakaa Merriwa; ameuawa ametupwa kwenye bonde.Lakini hatuishii hapo, kuna watu/raia wanne juzi walitekwatarehe 7 Novemba, 2017 Dar es Salaam kwenye Pub ya Sebrin;ilienda gai aina ya Noah rangi ya silver wakajitambulishakwamba ni askari polisi wakawateka hao wananchi waTanzania, Sayuni Nsoo na wenzake. Mume wa huyu raiawakafuatilia wakaenda mpaka Mabatini na kwingineko,walivyo trace simu zao zikawa zinaishia maeneo yaMikocheni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikizingatiwa kwamba Bungehili hili…

MWENYEKITI: Uliza Mwongozo wako, usianzemaelezo…

MHE. ESTHER N. MATIKO: Najenga hoja!

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili hili lililopita baadaya tukio la Mheshimiwa Lissu tuliunda Kamati teule ambayoingetoa uwanda mpana wa kuweza kujadili Kamati ya Bungeya Ulinzi na Usalama ambayo ingetoa uwanja wa kuwezakujadili usalama wa nchi yetu. Wananchi wana hofu sasahivi hata za kufanya shughuli zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipindi kile mkasemaMwenyekiti anahitaji siku tatu, lakini mpaka sasa ripoti haijaja.Kwa hiyo naomba hili jambo liwe la dharura leo, nitoe hojatu-discuss na Waheshimiwa Wabunge waniunge kwa sababunchi imekuwa tete. Kuendelea kuokota maiti, watu kutekwa.Naomba kutoa hoja ili tuweze kujadili hili jambo. (Makofi)

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

MWENYEKITI: Ahsante, Waheshimiwa WabungeMwongozo wako Mheshimwa Matiko ulishatolewa ruling naKiti. Kwa vile umetaja mambo mengi, orodha ya watu wengi,Bunge hapa tutajadili nini bila ya kuwa na taarifa sahihi. Kamauna hoja hiyo ambayo unaiona ni ya msingi ipeleke kwenyeKamati ya Ulinzi na Usalama.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Sasa ndiyo ruling ninayoisema, sasakama huitaki hiyo ruling yangu usiulize maswali kwenye Kiti.

Katibu!

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifaunaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na

Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwaMwaka wa Fedha 2018/2019

KAMATI YA MIPANGO

(Majadiliano yanaendelea)

MWENYEKITI: Kamati ya Mipango.

Tukae!

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nichukue fursa hii kuchangia Mapendekezo ya Mpango waMaendeleo ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 katikamaeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu miradi ya ubia katiya sekta ya umma na sekta binafsi, eneo hili ni muhimu

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

ambalo Serikali ililipa umuhimu mkubwa sana. Ili Serikaliijipunguzie mzigo wa kubeba miradi mingi mikubwa ambayoyote ina dhamira ya kuliletea Taifa maendeleo, mimi sionisababu kwa nini Serikali isichukulie mradi wa Daraja laKigamboni na Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi Dar esSalaam kama kielelezo cha mfano. Tatizo lipo wapi?Inaonekana wazi kuna hofu katika eneo hili ambayo hainamsingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo mifano duniani ambakonchi nyingi zimepiga hatua kupitia utaratibu huu. NaombaSerikali iwekeze katika sekta ya barabara, hospitali, kilimo,usafiri wa anga, reli pamoja na usafiri wa maji kupitia publicprivate partnership (PPP) hii njia pekee itafanya nchi isongembele, kwani nchi yote ni kubwa na kila mkoa, wilaya najimbo ina changamoto tofauti, tusipochukua hatuaitachukua miaka kama si karne kutimiza matarajio yaWatanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sekta ya kilimo,mifugo, uvuvi, wanyamapori na misitu, hili pia ni eneoambalo Serikali anabidi kuweka msisistizo ili kufanya nchiiongeze Pato la Taifa. Yapo maeneo mengi ambayo yanafursa, kama yangetumika vema basi uchumi ungeongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo mengi ya nchi yetuhasa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanalima sana mahindi.Hivi ni lini Serikali itatoa utaratibu wa kuhakikisha kuwa eneohili linakuwa eneo maalum kwa ajili ya uzalishaji wa mazaoya mahindi ili nchi izalishe kwa ajili ya ndani, pia ili tuwezekuuza nje ya nchi? Hili linawezekana tukiweka utaratibu wakulima kwa njia ya kisasa. Wananchi wa maeneo hayakupata pembejeo za kisasa, mikopo ya riba nafuu nakupatiwa ruzuku kama nchi nyingine duniani wanavyofanya.Hii pia itafanikiwa katika sekta nyingine za mifugo, uvuvi,wanyamapori na mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu bomba la mafutakutoka Hoima (Uganda)- Chongoleani (Tanga), niipongezeSerikali kwa mradi huu mkubwa ambao utatoa fursa kubwa

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

ya kiuchumi katika nchi na hasa katika mkoa wetu wa Tangaambapo bomba la mafuta litapita katika Wilaya nyingiikiwemo Wilaya ya Kilidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona Serikaliitatengeneza barabara ya kiwango cha lami kutoka Handenihadi Singida ambapo barabara hii itapita. Jambo hili ni zurisana na niipongeze Serikali. Ni dhahiri kwa ukubwa wa mradihuu na thamani si busara eneo la bomba linapopata kuwana barabara mbovu. Niiombe Serikali itenge fedha kwamwaka wa fedha 2018/2019 ili ijenge barabara hii kamailivyokusudia. Aidha, barabara hii ni kiungo muhimu chamikoa minne ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida nazipo shughuli nyingi tu za kiuchumi kwa barabara hii. Wakatimuafaka umefika kujenga barabara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Wakala wa BarabaraVijijini (TARURA), uanzishaji wa Wakala wa Barabara ya Vijijiniutasaidia kufungua mawasiliano ya barabara za vijiji vyote;hii itasaidia sana kutimiza uchumi wa wananchi wote. Niwazi maeneo mengi ya nchi yetu hususan barabara za vijijivyote bado yana changamoto za kutopitika. Niishauri Serikaliiimarishe Wakala wa TARURA kwa kupatiwa wataalam wakutosha na iongeze ujuzi wa kutosha hasa katika barabarahizi, hii itasaidia sana kuunganisha barabara za vijiji nabarabara kuu. Aidha, wakala huyu wapatiwe vitendea kazivya kutosha vinginevyo utendaji utazorota.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. JANETH M. MASSABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba tena nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua kuwa Mbunge waBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pamoja napongezi naomba nichangie Mapendekezo ya Mpango waMaendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/2019 kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu miundombinu yabarabara, naomba niipongeze Serikali kwa hatua

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

mbalimbali za kuboresha barabara zetu hapa nchini. Hatahivyo kuna dosari kadhaa ambazo zinatakiwa kupatiwaufumbuzi wa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano barabara zaMkoa wa Dar es Salaam, barabara ya Tabata Dampokuelekea Tabata Segerea - Kinyerezi - Malamba Mawili -Msigani mpaka Mbezi, barabara hii imekuwa kero kubwana adha ya foleni hasa nyakati za kuanzia saa 12.00 asubuhimpaka saa 4; na saa 10.00 jioni hadi saa 3.00 usiku, naikizingatiwa barabara ndiyo lango la kubebea mitambomikubwa ya Mradi wa Gesi Kinyerezi. Kwa sababu hizo nanyingine tunaiomba Serikali ipanue barabara hiyo kutokanana idadi kubwa ya watu na watumiaji wengine kama mradiwa Kinyerezi (Mradi wa Gesi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Segerea Shelikuelekea Seminari hadi Majumba Sita, tumeiomba Serikaliiweke barabara hii kwenye mpango wa dharura wa mudamfupi na pia iwekwe kwenye mpango wa kujenga barabarahiyo na Daraja la Seminari ili wananchi waweze kutumiabarabara hiyo kwa manufaa. Barabara hii Mheshimiwa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John PombeMagufuli, wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mkuu 2015 akiwaVingunguti aliahidi kuwa barabara ya Segerea Shelil (OilCom)kupitia Segerea Seminari hadi Majumba Sita ijengwekwa kiwango cha lami na daraja lake. Kwa muda huuyafanyike matengenezo ya dharura hasa pale eneo la Sheli(Oil Com) ambapo njia inapitika kwa shida sana. Wakaziwa eneo hilo wamekata tamaa. Kwa kuanzia angalau kifusicha mawe ili kunyanyua barabara maana pamechimbikasana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu barabara kuu nabarbara za mitaa; barabara nyingi hazifanyiwi matengenezokwa wakati, hali hii inasababisha Serikali yetu ya CCMilaumiwe. Naomba Serikali iweke kitengo madhubutikitakachofanana na kuendana na kasi ya Mheshimiwa JohnPombe Magufuli Rais wetu ili kitengo hiki cha ukaguzi wabarabara kuu na barabara za mitaani kiweze kutambua

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

tatizo mapema kuliko tatizo litolewe na vyombo vya habari.Hali hiyo huwa inaleta fedheha kubwa, ikizingatiwa kunaviongozi na watendaji katika ngazi za kata na kadhalikawalitakiwa kujua tatizo kabla. Kitengo cha ukaguzikiongezewe vitendea kazi kama magari na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la maji Dar es Salaam.ninaipongeza Serikali kwa kuboresha upatikanaji wa majikatika Mkoa wa Dar es Salaam kwa asilimia 70; wananchiwa Dar es Salaam wamefurahi sana kwa kupata maji. Hatahivyo tunaiomba Serikali iharakishe upatikanaji wa majikatika maeneo ambayo hutegemea chanzo kingine chamaji, kwa mfano wananchi wa Kipera – Pugu, Majohe,Chanika, Msongola, Kitunda, Chamazi na maeneo yaMwinuko ambao hawapati maji ya uhakika. Tunaomba kasiiongezwe zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu elimu ya ufundi naujuzi, Serikali iangalie kwa upana zaidi kwa kuanzisha vyuovingi vya ufundi ili viweze kutengeneza rasilimali watu wenyeujuzi wa fani mbalimbali kama mafundi wa mitambo midogomidogo, mafundi wa kutengeneza vifaa vya umeme, vifaavya ujenzi; vifaa ambavyo soko lake litatokana na matumiziyetu ya kila siku sisi Watanzania. Kwa mfano kutengenezavifaa vya ngozi (viatu, mikanda, mabegi, vifaa vya umemeaina zote za majumbani, vifaa vya ujenzi pamoja na vifaa(vipuri) vya mitambo midogomidogo pamoja na ujuzi waaina nyingine ambazo zinaweza kuleta mabadilikomakubwa ya kiteknolojia na kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo hili la mafunzoya ufundi na ujuzi itasaidia kuruhusu vijana wengiwanaomaliza darasa la saba, kidato cha nne na kidato chasita, kupata mafunzo na baada ya hapo kupelekwa kwenyeviwanda husika. Serikali si vibaya ikafuata mfumo uliotumikakatika nchi ya Singapore ya kufanya mapinduzi yakuwafundisha vijana wao wengi mafunzo ya ufundi na ujuzikwa kuanzisha vyuo vingi vya ufundi na ujuzi mbalimbali nawalitilie nguvu katika masuala ya vifaa vya umeme.

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Mheshimwia Mwenyekiti, naunga mkono hojapamoja na maoni yangu, nawasilisha.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze na Mradi wa Umeme wa Makaa ya MaweMchuchuma; Serikali imekuwa na kigugumizi cha kuanzautekelezaji wa mradi wa Mchuchuma. Naomba Serikali sasaianze mara moja kutekeleza Mradi wa Mchuchuma naLiganga kwa sababu ahadi zimekuwa kwa muda mrefu lakinihakuna utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu madini na gesi,naiomba Serikali ihakikishe inakusanya mapato kwenyemadini kama kodi za wawekezaji kwani tuna migodi mingilakini hatukusanyi mapato mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kodi, vyanzo vyotevya mapato vimechukuliwa na Serikali Kuu. Halmashaurizinashindwa kujiendesha kwa sababu hazirudishwi kwenyeHalmashauri. Hii inakatisha tamaa kwani watendaji wetuwanashindwa kabisa kuendesha Halmashauri; Halmashaurizinakufa. Naiomba Serikali irudishe vyanzo hivyo vya mapatokwenye Halmashauri zetu ili utendaji wake uwe bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kilimo,asilimia kubwa ya Watanzania ni wakulima. Tunapangakwenda kwenye Tanzania ya viwanda, hatuwezi kwendakwenye Tanzania hiyo kama hatujaboresha kilimo. BadoWatanzania tunalima kwa mikono, pembejeo ni gharama,bei ya vyakula ni chini. Tunawezaje kuingia kwenye ushindaniwa masoko? Kwa vyovyote vile hakuna soko tena. Matokeoyake hatuwezi kuondoa umaskini katika nchi hii. NaiombaSerikali ione namna gani itaboresha kilimo na kuwasaidiawakulima. Naiomba Serikali ipunguze bei za pembejeo napembejeo zifike mapema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafanyabiasharawananyanyasika sana, wanabanwa kila upande,wanatozwa kodi kubwa ambayo hailingani na mitaji yao,hasa wafanyabiashara wadogo. Wafanyabiashara wengi

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

wamefunga biashara zao kwa sababu ya usumbufu mkubwawanaoupata hapa nchini. Naiomba Serikali iangalie namnaya kuwatoza kodi wafanyabiashara hawa bilakuwanyanyasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Mungu kunipa nafasi ya kuchangia hoja iliyopomezani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi wanaopatanafasi ya kujiunga na masomo ya elimu ya juuwamekumbana na changamoto ya kupata mikopo, hasawanafunzi wenye mahitaji. Ninatambua pia umuhimu wakutoa fursa zaidi kwa wanafunzi wanaochukua masomokusomea taaluma zenye upungufu, sayansi etc.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapendekeza Sera ya Elimuya Juu na Kanuni zake zipitiwe upya, kwa sababu wanafunziwanaofaulu kwa kiwango cha juu kidato cha sita ni walewaliosoma shule binafsi zenye mazingira mazuri ya kujifunzia,walimu, vitabu, maabara na kadhalika, matokeo yake, haowenye uwezo ndio wanapata mikopo wakati si wahitaji.Karo za shule walizosoma ni ghali kuliko ya vyuo vikuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, lile lengo la kutoamikopo kwa wahitaji na wanaotoka kwenye familia zenyeuchumi mdogo/duni, halikufikiwa. Kwa wakati huu, utaratibuwa kutoa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ufanyiwemapitio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: MheshimiwaMwenyekiti, ripoti ya Benki ya Dunia katika uzinduzi wa Ripotiya Kumi ya Mwenendo wa Uchumi Tanzania imeonesha wazikwamba katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2017,uchumi umeshuka kutoka 7.7% hadi 6.8% ukilinganisha nakipindi kama hicho mwaka jana (2016). Ripoti hii inanipa

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

wasiwasi juu ya jinsi mpango huu unaoandaliwautakavyotekelezwa kama mapato yetu ya ndaniyatapungua siku hadi siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bandari zetu (TPA) hasa yaDar es Salaam mizigo imepungua sana kutokana naongezeko la tozo kwa mizigo iendayo nchi za jirani pamojana mifumo mibovu ya bandari yetu. TPA imeshindwakuboresha mifumo na miundombinu yake kutokana nakwamba mapato yake yanapokusanywa na TRAyanapelekwa kwenye Consolidated Fund Account na amahayarudishwi au yanarudishwa baada ya muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziriwakati atakapojibu hoja za Waheshimiwa Wabunge aelezekama fedha/mapato ya wharfage ya TPA yanarudishwa kwawakati au Mheshimiwa Waziri anaweka time frame yamapato hayo kurudishwa TPA. Vinginevyo bila modernizationya TPA, wateja wengi watapitishia mizigo yao Durban, Beiraau Maputo na matokeo yake bandari itakufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kilimo chaumwagiliaji, napenda kuunga mkono kwamba fedhazitengwe za kutosha katika sekta ya kilimo, hasa kilimo chaumwagiliaji, kilimo cha kutegemea mvua kimeongezaumaskini kwa wakulima wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sekta za mifugo nauvuvi; nchi yetu inajivunia sana kuwa na mifugo wengi, ikiwani ya pili Barani Afrika baada ya Ethiopia. Mifugo inawezakubadilisha sana kiwango cha maisha ya wafugaji kamamkazo utawekwa katika ufugaji wa kisasa. Ufugaji una faidanyingi licha ya nyama na maziwa, ngozi yake inawezakuliingizia Taifa fedha nyingi. Serikali pia inashauriwa kudhibitikwa uingizaji wa nyavu ndogo badala ya kuzichoma na hivyokuongeza kiwango cha umaskini kwa wavuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Benki ya Wanawakena Benki ya Kilimo, benki hizi mbili zingeweza kuchocheamaendeleo ya wananchi wa kima cha chini. Bahati mbaya

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

Serikali na BOT wameshindwa kuisimamia Benki ya Wanawakena hivyo mtaji wake kushuka chini ya kiwangokinachokubalika kisheria. Serikali pia imeshindwa kutimizaahadi zake za kuiongezea Benki ya Kilimo mtaji kamailivyoahidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, out of Tshs. 800 billionambazo Serikali ilikuwa iipatie TADB, ni Tshs. 60 billion tuambazo kati ya hizo, ni Tshs. 10 billion tu za kukopesha tangumwaka 2015, mpango ulikuwa TADB ipatiwe Tshs. 10 billionkila mwaka. Hii undercapitalization ya benki hii itaifanyaisiweze kukopesha wakulima na hivyo kilimo kuzorota.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kati ya hizo Tshs.10 billion, ni Tshs. 2 billion tu ndiyo wamekopeshwa wakulima.Fedha nyingine zimekopeshwa benki nyingine. Katika kujibuhoja za Waheshimiwa Wabunge, naomba Mheshimiwa Wazirialieleze Bunge kwamba atahakikishaje TADB inaongezewamtaji wa Tshs. 10 billion kila mwaka na jinsi Mheshimiwa Wazirianavyoweza kuisimamia benki hii i l i fedha ziwafikiewakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umeme wa vijijini(REA), viwanda haviwezi kuanzishwa bila kupeleka umemekwenye vijiji. Pamoja na kuanzishwa kwa Rural Energy Fund,TANESCO wameshindwa kuwasilisha fedha, kiasi cha Tshs. 7.4billion kwa Mfuko wa REA zitokanazo na levy pamoja nafaini ya ucheleweshaji. Ni vyema Mheshimiwa Waziri wa Fedhaatueleze kwa nini TANESCO hailipi deni hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mashirika ambayo Mpangohuu katika ukurasa wa 48 unalenga kuyaimarisha nakuyatumia katika kuleta mageuzi ya viwanda nchini, ni vizuriMheshimiwa Waziri akayaangalia upya kama watumishiwaliopo wanaweza kwenda na kasi ya Sera ya Viwanda.Kwa mfano SIDO, STAMICO, CARMATEC na COSTECH wanarekodi ambazo si nzuri kiutendaji. Mheshimiwa Waziriatuhakikishie kwamba taasisi/mashirika haya yanawafanyakazi wenye ujuzi, waadilifu au uwezo wa kwendana kasi ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, SIDOwameacha kilio kikubwa sana kwa wakulima wa tangawiziWilayani Same. Tangu mwaka 2012 wametengeneza mashineza kuchakata tangawizi ambayo haijafanya kazi hadi sasa,hivyo kuwatia hasara kubwa sana wakulima. CARMATECwana maeneo mengi waliyopewa kazi ya kutengenezamitambo ya biogas na uvunaji wa maji, lakinihawakukamilisha kazi hizo pamoja na kulipwa fedha zote.COSTECH walipewa kazi ya ushauri na NIDA na kazi yaohaikutumika hata baada ya kulipwa fedha nyingi; ina maanaushauri wao haukukidhi mahitaji ya NIDA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu matumizi mabaya yafedha za umma, katika kipindi kinachoishia Juni, 2016, katiya mapendekezo 3,898 yaliyotolewa na CAG, nimapendekezo 1,449 tu (37%) yaliyotekelezwa kikamilifu. Hatazile Wizara zilizobainika kutumia fedha vibaya zilizopitishwakwenye bajeti, bado Mheshimiwa Waziri wa Fedhaameendelea kuwaongezea fedha kwenye bajeti. NimuombeMheshimiwa Waziri atoe mapendekezo jinsi atakavyowezakuweka mpango madhubuti wa kuhakikisha mapendekezoya CAG yanafanyiwa kazi kwa ukamilifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusus suala lakutozingatiwa sheria ya manunuzi na mikataba mibovu.Serikali imekuwa inapoteza fedha nyingi kutokana na Wizarana taasisi zao kutozingatia Sheria ya Manunuzi, kuingiamikataba mibovu na kushindwa kuwalipa wakandarasi kwamuda wa makubaliano. Matokeo yake Serikali inapotezafedha nyingi zikiwemo za kulipa faini. Fedha hizo zingetumikakatika kuleta maendeleo. Waziri alihakikishie Bunge jinsiWizara yake itakavyosimamia jambo hili kuzuia upotevu wafedha za umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo hapo juu, naaminiyatasaidia katika kuboresha Mpango wa Maendeleo waTaifa wa mwaka 2018/2019.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

ya kuchangia katika mpango huu wa maendeleo. Napendakumpongeza Mheshimiwa Rais wetu kwa juhudi kubwaanayochukua katika kuongoza nchi hii. Namuombea Munguampe uwezo na afya njema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kumpongezaMheshimiwa Waziri wa Wizara hii ya Fedha, Naibu Waziri nawatendaji wake wote kwa umakini wa kuandika nakuwasilisha Mpango huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia Mpangohuu napenda kusisitiza maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni kuhusu kuongezauwezo wa kupambana na umaskini kwa wananchi. Miongonimwa kundi kubwa la wananchi wa Tanzania niwafanyabiashara na wakulima. Hivyo, ni vyema Serikalikuendelea kuchukua juhudi za makusudi kuwawekeamazingira mazuri ya kufanikisha shughuli zao. Serikaliinapaswa kuwawekea utaratibu maalum wa kuwapatiamikopo yenye masharti nafuu ili waweze kufanya biasharazao kwa utulivu na kuweza kujipatia kipatokuweza kupunguza umaskini, hasa wafanyabiashara waliowadogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa sekta yauvuvi, sekta hii bado haijaonesha mafanikio katikakuwaendeleza na kuwanyanyua wavuvi wa nchi hii. Badompaka leo wavuvi wanahangaika kwa kukosa vifaa vyauvuvi vya kisasa. Hivyo, naiomba Serikali ichukue juhudi zamakusudi kuwaendeleza wavuvi kwa kuwapatia zana zakisasa. Aidha, Serikali iunde benki ya wavuvi, ili iwezekuwakopesha wavuvi kwa kuweza kumudu kununua vifaavya kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu miradi yamaendeleo, Serikali ina nia nzuri katika kupanga nakutekeleza miradi ya maendeleo, lakini miradi mingi katikanchi yetu inakosa ufanisi kwa sababu kadhaa. Moja kati yasababu hizo ni upatikanaji wa fedha kwa wakati. Hivyo,

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

naiomba Serikali kupeleka pesa kwa wakati katika taasisihusika ili kuweza kwenda na wakati wa mipango kazi yamiradi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kumpongeza Waziri wa Fedha na Mipango,Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, pamoja na timu nzima yaWizara ya Fedha na Mipango kwa kuleta mapendekezomazuri ya Mpango na pia Mwongozo wa Maandalizi yaMpango na Bajeti kwa mwaka 2018/2019. Naombanipendekeze kuwa katika kipaumbele cha viwanda vyakukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi na viwandamsukumo wa kuboresha kilimo, hasa katika suala la bei nauhakika wa masoko ya mazao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuboresha kilimotutaweza kuwa na malighafi ya kutosha kwa viwanda vyetu.Pamoja na msukumo wa kuanzisha kanda maalum zakiuchumi na kuimarisha SIDO, napendekeza katika mpangokuwepo na viwanda vidogo huko vijijini ili kuongeza thamaniya mazao, uwepo msukumo wa viwanda vya kuchakatapareto kutokana na mahitaji makubwa ya duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipaumbele chakufungamanisha uchumi na maendeleo ya watu, kipaumbelehiki ni muhimu sana hasa ukizingatia kuwa kukua kwa uchumiwetu kuendane na hali za wananchi hasa vijijini. Katikampango wa mwaka 2018/2019 napendekeza Serikali iwekekatika bajeti ya maendeleo umaliziaji wa miradi iliyokwamakwa muda mrefu. Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wananchiwamejitoa sana katika ujenzi wa zahanati na vituo vya afyana pia ujenzi wa madarasa pamoja na ujenzi wa kituo chapolisi cha wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya upatikanaji wa majihairidhishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya. Kati yamiradi tisa iliyoanzishwa mwaka 2013, ni mradi mmoja tuuliokabidhiwa wakati zaidi ya shilingi bilioni 4.2 kati ya shilingi

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

bilioni 5.5 ambayo ni 84% zimelipwa, lakini wananchihawapati maji, Serikali ihakikishe miradi hii inakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo huonapendekeza mradi wa maji wa chanzo cha Mto Kiwira kwamatumizi ya Wilaya ya Mbeya. Pia kuwepo na kuunganishaMamlaka ya Maji ya Jiji la Mbeya na Mamlaka ya Maji ya MjiMdogo wa Mbalizi. Pia kuwepo kwa bajeti ya ujenzi wamabwawa kwa wafugaji wa Kata ya Mjele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipaumbele chaujenzi wa mazingira wezeshi, napendekeza msukumo uwepowa kuboresha miundombinu ya barabara vijijini. Pamoja nauchumi mzuri wa Wilaya Mbeya, hali ya barabara nichangamoto kubwa. Napendekeza msukumo uelekezwekuboresha barabara za kuunganisha mikoa, ikiwemobarabara ya Mbalizi – Makongorosi, barabara ya Mbalizi –Shigamba, barabara ya Isyonje – Kikondo – Makete – Njombe,barabara ya Mjele – Mlima Njiwa, barabara ya Kawetere –Ikukwa, barabara ya Mbalizi – Songwe – Jojo, barabara yaIlembo – Mwala, barabara ya Ilembo Isonso na pia, by passya Mlima Nyoka (Uyole) – Songwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza reli ya TAZARAiboreshwe na iende sambamba na uboreshaji wa Bandariya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari KavuInyala, Mbeya. Pamoja na uboreshaji wa reli ya TAZARA, piaiwekwe kwenye bajeti ujenzi wa Reli ya Uyole, Mbeya kwendaMalawi, ili kukabiliana na ushindani wa biashara ya Bandariyetu ya Dar es Salaam na bandari nyingine kama Beira,Msumbiji na zile za Afrika Kusini na hata Angola.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipaumbele chakuimarisha usimamizi na utekelezaji wa Mpango, napendamsukumo uwekwe kuboresha ufuatiliaji na utoaji taarifa zautekelezaji, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mfumoutakaotoa taarifa sahihi. Taarifa nyingi za miradi zimekuwahazina uhalisia na zinapotosha, taarifa za miradi ya majikatika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya zimekuwazinapotoshwa. Naunga mkono hoja.

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

MHE. OMARI A. KIGODA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza kabisa nianze kwa kuipongeza Serikali kwa juhudizake katika kuleta maendeleo katika nchi yetu, bila yakusahau kumpa pongezi kubwa sana Rais wetu, MheshimiwaJohn P. Magufuli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mipango endelevu inahitajikwanza kabisa kutokuwa na watu wajinga, maradhi namaskini. Lazima mipango hii iendane na kuwanyanyua watuna kuwasaidia katika utendaji wao wa kulinyanyua Taifa.Serikali ihakikishe huduma ya ukusanyaji kodi kwa kutumiamashine za kielektroniki inakuwepo nchi nzima. Hii itasaidiaukusanyaji wa haraka na kutopoteza muda wa kutoa kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni lazima Serikaliihakikishe huduma za jamii kama maji, umeme na mengineyozinapatikana kwa wingi ili muda mwingi watu tuutumiekwenye kujenga nchi yetu. Maendeleo ya nchi lazima tuwena manpower ya kutosha, kwa hiyo, tukihakikisha hudumaza jamii zipo itasaidia kuwa na manpower ya kutosha kujengauchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali lazima ihakikisheinazingatia suala la afya ya kila mwananchi inakaa sawa nainatibika kwa urahisi, ili kutokuwa na Taifa la wenye maradhi;hii itadhoofisha ukuaji wa uchumi wetu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni suala laamani. Lazima nchi iwe na amani, ili kila mtu awe huru katikakutekeleza kazi zake za kulijenga Taifa. Lazima Serikali isisitizewatu kufanya kazi ili tuweze kukwamuka kutoka tulipo,twende mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, infrastructures zetu lazimatuhakikishe zinatumika na lazima tuweke mazingira mazurikwa watumiaji. Mfano, gesi lazima itumike kwenye viwandavyetu ili kuwa na uzalishaji wa kutosha. Lazima barabarazetu ziwe za kupitika muda wote, hii itasaidia kwawakulima na wafugaji hata waoa huduma kufika kwenyepoint haraka.

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la elimu ni muhimusana. Taifa la wajinga haliwezi kuwa na maendeleo aukujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na jiografia yanchi yetu kuna infrastructures ambazo ni za mkakati especiallykiuchumi, kwa mfano, barabara ya Handeni – Mziha – Dumilana nyingine nyingi. Hizi infrastructures lazima tuzitengeneze iliziweze kutumika katika mzunguko wa biashara kwenye nchiyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna Taifa lililoendeleabila kuwahusisha wafanyabiashara wakubwa, pia nakuwahusisha katika uwekezaji. Hivyo, ni lazima Serikali iwekaribu na wafanyabiashara na kusikia matatizo yao nakujadiliana ili kuweka mambo sawa.

Mhershimiwa Mwenyekiti, miaka 30 iliyopita SouthKorea tulikuwanao almost sawa, lakini kwa sasa wamepigahatua sana kimaendeleo. Walichofanya ni kuhakikishawanaweka mazingira mazuri ya uwekezaji na Serikali ilibakikuchukua kodi kutokana na uwekezaji huo, piakuhakikisha hiyo kodi inatumika ipasavyo kwenye hudumaza jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho napenda kumshauriWaziri, hii mipango tunayopanga ni mizuri tu endapoutekelezaji wake utapewa kipaumbele na msisitizo wa kilamtu katika sekta yake lazima afanye kazi. Hakuna uchumiunaopanda kwenye Taifa la wavivu, lazima msisitizo wauwajibikaji usemwe mara kwa mara.

MHE. SUZANA C. MGONOKULIMA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa kuwa Tanzania inataka iwe nchi yaviwanda, tuboreshe sekta ya kilimo kwa kuhakikisha kwambamikopo kwa wakulima inapatikana. Tukifanya hivyotutakuwa tumewawezesha wakulima kulima kilimo bora.Kilimo bora kinatokana na wakulima kuwa na mbegu borana mbolea kwa wakati.

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sera ya elimu bure,ni miaka miwili kama Taifa tumeona kuwa elimu bureinaathari kutokana na kuporomoka kwa ufaulu wawanafunzi. Katika mpango huu uliopendekezwa na Waziriwa Fedha, je,kuna mkakati wa makusudi wa kutatuamatatizo yanayoikabili sekta ya elimu? Elimu ya kutoshainatakiwa kutolewa kwa wananchi wajue kuna baadhi yashughuli za elimu kama wananchi wanapaswa kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mpango huuuliopendekezwa kwa mwaka 2018/2019, hakuna sehemuiliyoonesha ukuzaji wa viwanda katika Mkoa wa Iringaambavyo vilikuwepo katika Mkoa huo. Mkoa wa Iringa miakaya nyuma ulikuwa na viwanda vya COTEX, Cocacola, IMAC,SIDO na Tyre,viwanda hivi viliwasaidia sana wananchi waMkoa wa Iringa na maeneo mengine ndani ya nchi yetukupata ajira, lakini katika mpango uliopendekezwa sijaonasehemu yoyote inayoonesha kwa mwaka 2018/2019kuhakikisha viwanda hivyo vinaimarishwa ili kupatia ajirawananchi wa Mkoa wa Iringa na maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba suala hili lipewekipaumbele.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, tulikuwa na Malengo ya Milenia (MDGs)hatukuweza kufikia malengo, tulifanikiwa maeneo matatutu na hata hivyo UNESCO ilitupatia tuzo katika uandikishajiwa watoto, kwa hilo napongeza japo hatukuweza kuwana elimu bora kwa watoto wetu japo waliandikishwa kwawingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu kwa sasa tunaSDGs ambayo malengo yake ni mengi zaidi ya MDSs. Je,katika Mpango huu Serikali imejipangaje kuhakikisha inaingizakatika Mpango huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi yoyote makini,lazima iwe na vipaumbele vichache visivyoweza kushindwakatika utekelezaji, Tanzania kwa sasa ina vipaumbele gani?

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawezaje kuwa namaendeleo na mipango bila kilimo. Viwanda bila kilimo niuti wa mgongo ni vema tukazingatia kilimo maana viwandavinategemea malighafi za kilimo.

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, awaliya yote ninampongeza sana Mheshimiwa Waziri na NaibuWaziri wenye dhamana ya Fedha na Mipango kwa kazikubwa wanayoifanya ili kuhakikisha Ilani ya CCM 2015/2020inatekelezeka. Baada ya pongezi hizi, nina maombiyafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba uangalieuwezekano wa kuutengea na kuuwekea fedha Mfuko waTaifa wa Watu Wenye Ulemavu kama ambavyo Mfuko waVijana unatengewa. Mheshimiwa Waziri, Mfuko wa Taifa waWatu Wenye Ulemavu (WWU) ni muhimu sana ukatengewafedha, hii itasaidia sana ustawi wa WWU na hasa ikizingatiwakuwa wana mahitaji mengi ikiwemo hitaji la mitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi la pili, fedha iongezwekwenye Kasma 280400 Mafunzo kwa Watu wenye Ulemavuambapo mwaka 2017/2018 Kasma hii ilitengewa shilingi600,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti,Idara ya Watu WenyeUlemavu haina sub vote, hivyo ninaomba Mheshimiwa Waziriuliangalie hili maana mchakato ulishaanza.

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa fursa hii ya kuchangia hotuba ya Waziriwa Fedha na Mipango juu ya Mapendekezo ya Mpango waMaendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/2019 na Mwongozowa mMaandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru Mungu kwakibali chake na rehema zake kwa kutuwezesha kukutanandani ya Bunge lako tukiwa na afya na nguvu ya kufanyakazi. Ninampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uteuzi wake

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

alioufanya hivi karibuni kwenye Baraza lile la Mawaziri naniwapongeze wote walioteuliwa na kuzidi kushirikiana vizurihuku nikiwaasa kuwa Hapa ni Kazi Tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hiikumshukuru Rais Magufuli kipekee kwa kutimiza ahadi kwaJimbo langu la Ileje, yeye mwenyewe kwa kutujengeabarabara kuu ya kutoka Mpemba hadi Isongole kwakiwango cha lami. Barabara ya kilometa 51.8 ambayowananchi wa Ileje wameipigia kelele kwa miaka 42 sasa.Tunaishukuru Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kutimizaahadi zake kwa Wilaya ya Ileje. Naishukuru Serikali kwakutujengea Hospitali kubwa ya Wilaya Itumba ambayoitafanya upasuaji mkubwa. Tunaiomba Serikali itusaidiekumalizia hospitali hii ambayo imesimama kwa zaidi ya miakamiwili sasa. Hospitali hii inategemewa na itasaidia hataWilaya ya jirani za Mkoa wa Songwe na Mbeya Vijijini iliimaliziwe na itazuia wananchi wa Ileje kukimbilia nchi jiraniya Malawi kupata huduma za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaishukuru Serikali yaChama cha Mapinduzi kwa kusaidia kuweka miundimbinumizuri ya maji hasa maeneo ya Isongole, Itumba, Izuba Iluluambapo kumekuwa na ukame wakati wa kiangazi nakusababisha upungufu mkubwa wa maji wakati Mto Songweuko hapo jirani kabisa. Hii imerudisha imani ya wananchi kwaSerikali kwa kiasi kikubwa sana na kuinua ari yao.Tunahamasisha Serikali kuhamasisha mipango yote ya majikama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TRA walikuwana mpango wa kujenga kituo kidogo cha forodha kwenyempaka wa Tanzania na Malawi kwenye Mto Songwe. Eneolimeshapimwa na TRA wamejenga ofisi ndogo ya forodhalakini bado haitoshelezi. Mpaka wa Tanzania hauna ofisi yaUhamiaji, Polisi, Kilimo, Jeshi la Wananchi na Idara nyinginemuhimu za Kituo cha Forodha Mpakani. Tunaiomba Wizaraitusaidie kituo hiki kijengwe kwa kwa sababu kinapunguzamsongamano wa Tunduma, kwa njia ya Ileje inapendelewana wenye magari makubwa kwa sababu hupitia Chitipa

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

upande wa Malawi kutokea Isongole Ileje kuja Mpemba nitambarare zaidi kuliko ile ya Kasumulo Kyela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia itawezesha kudhibitimpaka huu ambao umekuwa na matukio ya wakimbizi waKisomalia na wengine kuutumia. Kwa hali hiyo huwezi juaathari gani nyingine zinaweza kutokea bila kuwa na kituocha forodha sehemu muhimu hiyo ya mpaka. Aidha, hichokituo kitasidia sana pindi mradi wa Bonde la Mto Songwekati ya Malawi na Tanzania utakapoanza. Vyote hivivitachangia kwa kiasi kikubwa kuchangamsha uchumi waIleje na Wilaya za jirani ambazo kwa muda mrefu zimedumaakwa kukosa miundombinu ya kisasa na taasisi muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kumekuwa namwelekeo Wizara ya Mambo ya Ndani wana mpango wakujenga Chuo cha Uhamiaji cha Ulende katika Wilaya ya Ilejena eneo tayari limeainishwa, hii pia ingesaidia sana kujengauwezo wa Maafisa Uhamiaji wa Tanzania lakini hata walewa nchi za SADC na hii itasaidia kuinua uchumi wa Jeshi laTanzania kwa ujumla. Hii ni miradi ya kitaifa naomba Serikaliiangalie jinsi ya kutusaidia kwa kuingiza mipango yake yakipindi hiki ili Ileje nayo ipate maendeleo ya haraka zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ileje ni kati ya Wilayainayozalisha mazao ya kilimo kwa wingi sana hususanimahindi, ulezi alizeti, mpunga, kahawa, pareto, hiliki,tangawizi, ndizi, viazi mviringo, viazi vitamu, soya,maharagwe, karanga, matunda ya aina mbalimbali pamojana mazao ya misitu ikiwa ni pamoja na mbao, nyuki nakadhalika. Zaidi ya hayo Ileje ina uwezo wa kuzalisha maziwakwa wingi, mifugo midogo midogo, viungo na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na haya yote Ilejeinakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa maghala,masoko, Maafisa Ugani na kwa kiasi kikubwa mitaji kwasababu maeneo yote ya Ileje hayajapimwa na tumehusishaupungufu wa wataalam wa kupima maeneo haya.Tunaomba Serikali iweke bajeti na nguvu ya ziada na yaupendeleo kwa maeneo ya pembezoni hasa Ileje na hasa

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

kwa sababu tumejaliwa kuwa na hali ya hewa nzuri sana,udongo mzuri, mvua nyingi na za kutosha ni rahisi kwa kilimona ufugaji huwainua na kupanua uzalishaji sana kwa mazaoyote hayo na huwaondolea wananchi kwenye umaskini naukosefu wa ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nijikite katikampango na nianze kwa kuwapongeza sana Serikali kwakuwashirikisha wadau katika mchakato mzima wakutayarisha mpango na mwongozo huu, ni jambo lakupongezwa kwa sababu limekuwa shirikishi zaidi. Lakinitunaiomba Serikali iyazingatie maoni haya na kuyazingatiakatika Mpango ili uwe na tija zaidi. Maoni mengi ya wadauyanaonesha uzoefu wao kwenye soko na utekelezaji ambaoumezidi ule ambao watumishi wa Serikali ambao wana ofisitu au ni wa wananchi wanaotumiwa na masuala mbalimbalikwa hiyo, siyo ya kupuuzwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikaliimepokea na kuorodhesha maeneo waliyopata ushaurininaomba Serikali itupatie masharti ya jinsi wanapangautekelezaji na fedha itakayotumia, maoni yote yaliyo ukurasawa tano wa Mpango huu wa 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli uchumi wetuumekua vizuri kwa muda mrefu lakini bado kwa kiasi kikubwatuna utegemezi mkubwa kwa wafadhili wa fedha za njeambazo haziji zote kwa wakati. Tupate sasa wakati wakupunguza zaidi utegemezi huu na vilevile kutumia sektabinafsi zaidi kutengeneza miradi ili kupunguza utegemezi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mfumuko wa beikuendelea kuwa mdogo tumeona kuwa umepanda kidogokutokana na bei za chakula kupanda na bei zinapanda kwasababu utaratibu wa soko la mazao nchini haujawa vizurikitu kinchosababisha wakulima kukosa mapato stahiki nawateja pia wanaathirika na kuwapa faida kubwa walanguzi.Lakini kama haitoshi zao la mahindi limekuwa yatima nchini,liliachiwa na wakulima kuhangaika wenyewe wazalishemazao mengine kama korosho, pamba na kadhalika

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

kunachangiwa kwa kupatiwa pembejeo, madawa nakadhalika.

Je, ni kwa nini Serikali inaacha mazao hayayanayolisha nchi nzima na kuwawezesha wananchikunufaika kwa biashara ya mazao yao? Serikali ije namustakabali wa kuwasaidia wakulima wa mazao ya nafakana jamii za kunde na ya mbegu za mafuta ili ziwe na tija nayachangie Pato la Taifa na kuwaodolea umaskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Deni la Taifakuonesha liko himilivu, lakini tukiendelea hivi litatupelekapabaya hususani kama hatutaongeza mauzo ya kuuzwa nje(exports) ili yabadilishe balance of trade yetu Tanzania. Nchinyingi zenye deni kubwa vilevile ni nchi za viwanda zenyeuchumi mkubwa, kwa hiyo malipo ya madeni hayo hayaathirisana uendeshwaji wa uchumi. Lakini kwa Tanzania deni lilikuasana dhidi ya ukuaji wa uchumi kwa maana Pato la Taifatutafikia hatari. Tujitahidi kuboresha na kuinua viwanda,kuanzisha viwanda vingi, huongeza masharti ya uwekezaji,kupunguza viwango vya kodi ili tupate ufanisi na mwishowa madeni yote ya ndani na ya nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonesha kuwapato la ndani halitoshi hutokana na ukusanyaji mdogo wamapato ya ndani, uzembe na hata rushwa. Vilevile sektaisiyo rasmi imesahauliwa katika suala nzima la makusanyoya kodi. Sekta hii ni kubwa na ina wajasiriamali wa ainambalimbali wadogo, wa kati na wanazalisha bidhaa nahuduma za kutosha na kulipa kodi nyingi. Serikali ina mpangowa kurasimisha shughuli hizi, hili ni jambo la msingi na kwahakika zimechelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Serikali sasa hiviiweke utaratibu mzuri na ishirikishe. Aidha, Serikali ishirikishetaasisi zake zinasimamia vizuri sekta hii na kuwapatiahuduma zao za kifedha na mafunzo ya kuwawezesha kuinuashughuli zao. Hii iendane na kuwapatia maeneo ya kufanyiashughuli zao.

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaipongeza sana Serikalikwa kuanza kutengeneza miradi ya maendeleo kwa mwaka2016/2017 pamoja na kugharamia ujenzi wa awamu yakwanza wa reli ya kati kwa standard gauge kutoka Dar esSalaam kwenda Morogoro, pamoja na miradi mingine, miradihii mikubwa itakayoleta mageuzi makubwa ya kiuchumi,Serikali ianze kutayarisha watumishi wa kuhudumia reli hiimapema kwa kuwapa mafunzo stahiki ili imalizike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ya msingiinayopanuliwa iendane na ujenzi wa madarasa ya kutosha,vyuo vya kutosha, maji na vyumba vya walimu na maabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya viwanda nimuhimu sana na tuipongeze Serikali kwa kuwezesha viwandahivi kuanza uzalishaji na kudumisha mahusiano mazuri nao.Tunaomba mvisaidie hivi viwanda kupata umeme wa gesiwa uhakika na kuhakikisha hawapati ushindani usio wa hakina bidhaa kwa mfano, mali zinazoingizwa na Good Onewa China amekuwa yeye mwenyewe akiagiza na kuuzajumla na rejareja lakini huwahujumu wateja wake hao haokwa yeye kuweka bei ndogo kwenye bidhaa zake na kufanyakushindwa kuuza. Huu ni mchezo mchafu, TFC walifuatiliehil i kwa bidhaa zote zinazoingizwa na ambazo zinasababisha bidhaa za viwanda visishindwe kuuza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaiomba Serikali itengepesa za kujenga vituo vya afya Wilayani, aidha, zahanatinyingi zilizojengwa kwa nguvu za wananchi sasa zimaliziwekwa awamu hadi na kuweka vifaa na watumishi wa kutoshazimalizike zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapongeza juhudi zakuboresha huduma ya maji nchini. Tunaishauri Serikali itoekipaumbele kwenye uvunaji maji ya mvua katika maeneoyenye tatizo la umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania badotunalalamikiwa kwa urasimu mkubwa katika kuhudumiawawekezaji na bado tunachukua muda mrefu, hutoa

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

maamuzi na tunakuwa waoga kuamua. Hii inapunguza kasiya kufanya biashara Tanzania.Jina la Tanzania sio zuri nje yanchi, mwisho Serikali inatuhumiwa kuwa haizingatiimikataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaipongeza Serikali kwakuboresha huduma za afya katika Taasisi ya Moyo ya JakayaKikwete, lakini kuna haja ya kuhalalisha kuwa hospitali zoteza Wilaya, Kata, Mitaa zinapata huduma muhimu za kutoshana vifaa na watumishi ambao wanahitajika sana kwenyemaeneo yetu nchi nzima. Pesa ya kutosha hupewa kwa ajiliya huduma za afya nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa kuhitimisha natakakuiomba Serikali itufanyie kuboresha maendeleo ya kilimocha kisasa, miundombinu ya vijiji na mitaa. Wakati huo huoSerikali itoe kipaumbele katika kupima maeneo ya vijijini ilikurasimisha ardhi na kuwawezesha wazalishaji kukopa.Kilimo hakionekani kuwa kweli ni uti wa mgongo na kiletetija kubwa kwa ajili ya viwanda, ajira na mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaiomba Serika ije Bungenina mkakati wa kuanza kutekeleza miradi ya kielelezo namaeneo yale ya SEZ na EPZ ambayo yamekaa muda mrefuilhali ni miradi muhimu kwa kuviwezesha kuanza viwandakwa uhakika zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho tunaiomba Serikaliitafakari kwa kina na kuzingatia maoni ya Wabunge kwenyeMpango wa 2018/2019.

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti,niane na sekta ya uvuvi.

Katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/2018kuhusu rasilimali za uvuvi, Serikali ilitenga shilingi bilioni 2.2,na shilingi milioni 400 tu kama fedha za ndani kwa ajili yaukarabati wa miundombinu ya uvuvi pekee. Fedha hii nindogo sana ukilinganisha na matokeo tunayoyatarajia katikasekta ya uvuvi.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli usiopingika kwambaSerikali hii ya Awamu ya Tano inataka kuwekeza kidogo hukuikitarajia matokeo makubwa sana. Sekta ya uvuvi ni sektanyeti ambayo inachangia katika uchumi wa Taifa na patola mtu mmoja mmoja katika maeneo mengi ya nchiyaliyozungukwa na maji. Jambo la kushangaza jamii zawavuvi zimekuwa ni jamii zinazoishi maisha duni sanapamoja na ugumu na changamoto nyingi wanazopitiawavuvi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa zana bora na zakisasa katika kufanya uvuvi wenye tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wavuvi wamekuwawakitozwa kodi nyingi huku miundombinu ikibaki vilevile.Wavuvi wa Tanzania hususani wa Mkoa wa Mara wamekuwawakinyanyasika kwenye kulipa tozo nyingi, hawana uhakikawa mikopo na pia usalama wa kutosha wawapo katikashughuli zao usiku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi kama Norway imekuasana kiuchumi kwa kuwekeza katika sekta ya uvuvi pekee.Leo hii katika nchi za Ulaya, Norway ni nchi inayoongoza kwakuwa na GDP kubwa ambapo sehemu kuwa ya Pato la Taifahutokana na uvuvi tofauti na hapa nchini ambapo jamii yawavuvi ndio jamii maskini wa kutupwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu usafiri wa anga,uwanja wa ndege wa Musoma, katika mpango huu wamaendeleo 2017/2018 hakuna mahali panapooneshamkakati maalum wa ukarabati wa uwanja wa ndege waMusoma. Ni dhahiri uwanja huu ni muhimu sana katika kukuzasekta ya utalii kwa Kanda ya Serengeti. Uwanja wa Ndegewa Musoma ni wa muhimu sana katika kuchochea ukuajiwa uchumi wa Kanda ya Ziwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na sababu zakiuchumi uwanja wa ndege wa Musoma ni muhimu katikahistoria ya ukombozi wa nchi yetu. Uwanja huu umebebahistoria ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius KambarageNyerere. Hivyo ni muhimu kwa wageni wanaokuja nchini

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

kutembelea makazi ya Hayati Baba wa Taifa ambayealiipigania ukombozi wa nchi hii kwa gharama kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo ni vema sasa Serikaliione umuhimu wa kuuweka uwanja huu katika vipaumbelevyake ikiwa ni pamoja na kuutengea fedha za kutosha nakukamilisha ukarabati kwa wakati kama vile ilivyofanyakwenye uwanja wa ndege wa Chato. Pamoja na hilo,uwanja huu utakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi kwanihata shughuli za uchimbaji madini zinazofanyika Mkoani Marazitaimarika zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado naamini Mkoa waMara una wasafiri au watumiaji wengi wa ndegewanaofanya biashra katika maeneo mbalimbali ya ndanina nje ya nchi ikiwemo nchi j irani ya Kenya. HivyoSerikali itueleze ni lini itakamilisha uboreshaji wa uwanja huuil i wananchi hawa waweze kunufaika. Naombakuwasilisha.

MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwenye sekta ya nishati, Mpango unaonesha mpaka mwaka2020 uzalishaji wa umeme ufikie zaidi ya Mw 5000 InstalledCapacity, kwa sasa ni Mw 1358 na mradi wa Stieglers Gorgeutazalisha Mw 2100. Je, Mw 1542 itatokana na mradi upi ilikufikia lengo la Mw 5000 mpaka ifikapo mwaka 2020?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango haujaainisha kamaitashirikisha sekta binafsi au itatumia mradi upi kufikia lengo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali katika mradiwa Stieglers Gorge itumie teknolojia ya kisasa ya electricitygeneration by recycling of water ili kuepusha kusuasua kwauzalishaji wa umeme kutokana na upungufu wa kina chamaji kwenye vyanzo vya maji. Mfano wa teknolojia iliyotumikakwenye The Grand Ethiopian Renaissance Dam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa namba 14umeonesha projection ya population growth. Tanzania katikamiaka michache ijayo itakuwa na idadi kubwa ya watu. Je,

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

tumejiandaa katika mipango yetu kuhakikisha kuwaongezeko hili la watu sio tegemezi na lisiwe mzigo waSerikali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo ndiyo uti wa mgongowa uchumi wa Mtanzania. Je, Serikali imeandaa mikakatigani ya kuimarisha mazingira ya Agro Business Tanzania? Kwamfano, kuna vyombo kama Bodi ya Nafaka na MazaoMchanganyiko ambayo ni chombo cha kusaidia wakulimawanapata soko la uhakika wa mazao yao, lakini Bodi hiihaijawezeshwa kibajeti kutimiza malengo. Mfano, mwingineni Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambayo inachangamotoya mtaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali iwekekatika mipango yake namna ya kuwezesha vyombo vilivyovya kuendeleza kilimo Tanzania. Lakini Serikali iweke mipangoya makusudi ya kuwahakikishia wakulima soko la mazao yaoili kilimo kiweze kuleta tija. Pia itoe kibali kwa Bodi ya Nafakana Mazao Mchanganyiko kupata shilingi bilioni 8.9 loankutoka NSSF na kibali cha kupata mkopo wa bilioni 6kutoka Azania Bank ili Bodi ifanye kazi zake kwa mujibu washeria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefikia wapi katikakuleta Muswada wa sheria itakayoanzisha Price StabilazationFund, mfuko utakaoweza kuwa suluhisho la kumlinda mkulimapale bei za mazao zinapoanguka, kwa mfano mbaazimwaka huu?

MHE. ZAINABU M. AMIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kumpongeza Waziri wa Fedha na MipangoMheshimiwa Philip Isdor Mpango (Mbunge) kwa kuwasilishaMapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwamwaka 2018/2019 na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpangowa Bajeti kwa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo yangu namaoni yangu katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwamwaka 2018/2019utakuwa katika sehemu tatu:-

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali iwekekipaumbele katika viwanda hususani kujenga, kufufuaviwanda vyetu mfano, katika Mkoa wa Morogoro kunaviwanda kama vile Canvas, Polyster, Ceramic, Magunia,Tannaries (Kiwanda cha Ngozi), Moro Shoe, Moproco. Vyotehivi vipo katika Manispaa ya Morogoro, viwanda hivi vinginevinafanyakazi na vingine wawekezaji hawaviendelezi. HivyoSerikali isimamie na kuwapa muda wawekezaji haokuviendeleza na wakishindwa virudishwe kwa Serikali iliwapewe wawekezaji wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda hivi vikifanyakazikama miaka ya 1980 na 1990 vitaleta ajira kwa Watanzaniapia kuongeza Pato la Taifa la Tanzania, kulipa kodi ya bidhaazinazozalishwa kutokana na ujenzi wa reli itakayojengwakutoka Dar es Salaam hadi Morogoro (treni ya mwendokasiitaongeza chachu ya ajira ya wananchi wa Dar es Salaam,Mkoa wa Pwani na Morogoro ambao watapata ajira katikaviwanda hivyo vilivyopo Mkoa wa Morogoro).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kodi, niipongezeMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kukusanya kodi kwawafanyakazi hususani katika Miji Mikuu mfano Dar es Salaam.Nashauri katika kipaumbele kimojawapo Serikali iandaeutaratibu maalum ambao utamwezesha mfanyabiasharaalipe kodi kwa wakati na afurahie kuchangia Pato la Taifana siyo Serikali iwe adui kwa mlipa kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iboreshe mazingiraya mwananchi wakati wa kuanza biashara. Kuna tatizokatika utaratibu uliopo, nashauri katika Mpango waMaendeleo 2018/2019 Serikali impe muda angalau miezimitatu (grace period) mwananchi anayeanzisha biashara nabaada ya hapo ifanye makadirio kwa malipo ya mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa mfanyabiasharaanakadiriwa malipo ya kulipa kwa mwaka kabla ya kuanzabiashara na sehemu kama vile Kariakoo makadiro nimakubwa mno ambayo si chini ya milioni mbili kwa mwaka,na hii hupelekea wafanyabiashara kushindwa kulipa kodi na

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

hatimaye kufunga biashara. Hivyo maoni yangu Serikali ipitietena utaratibu huu kupunguza makadirio ili mwananchiaweze kumudu kulipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri fainiwanazotozwa wafanyabiashara ambao wanakutwa namakosa, mfano ya kutotoa risiti za EFD ni kubwa mno shilingimilioni tatu kulinganisha na bidhaa aliyouza na hii hupelekeamwananchi kushindwa kulipa faini na hatimaye kufungabiashara zao. Pia nashauri wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama wamachinga hususani waliopokatikati ya Jiji la Dar es Salaam (Kariakoo) Serikali iwasajili iliwaweze kuwa na mchango kwa Pato la Taifa kwa kulipakodi na kwenda sambamba na kauli mbiu ya Rais wetuMheshimiwa John Pombe Magufuli ya ukiuza toa risiti naukinunua dai risiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya afya Serikaliimefanya jitihada kubwa katika kutatua matatizo mbalimbaliyakiwemo kutoa madawa, vifaa tiba, ujenzi wa zahanatina vituo vya afya. Maoni yangu Hospitali ya Taifa Muhimbilini Hospitali ya Rufaa Tanzania, wakati tunaelekea katikaMpango wa Maendeleo wa Bajeti wa mwaka 2018/2019Serikali i jenge eneo ambalo litasaidia wananchiwanaowasindikiza wagonjwa wao kutoka katika mikoambalimbali Tanzania ambao hawana ndugu au jamaa JijiniDar es Salaam, waweze kupata sehemu za kufikia baada yakumkabidhi mgojwa wodini. Maana kuna baadhi yawagonjwa wanahitaji huduma za karibu kutoka kwa nduguzao ambazo wahudumu wakati mwingine ni vigumukuzifanya. Wakati mwingine wagonjwa wanaopewa rufaakuja Muhimbili ni watoto zaidi ya miaka 5 – 15 ambaowanahitaji huduma ya karibu ya mzazi au mlezi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naunga mkonohoja ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/2019.

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,mahindi ni zao la chakula na uzalishaji wake umepanda

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

kutokana na mwamko wa wakulima kutokana na hamasakubwa iliyotolewa na Serikali. Pamoja na yote hayo ukulimawa mahindi leo hii ni kama adhabu kwani hakuna soko lamahindi, bei yake ni ya chini, gunia moja ni kati ya shilingi25,000 mpaka shilingi 30,000. Je, kwa bei hiyo mkulimaatamudu kununua pembejeo, mbolea, mbegu, dawa nagharama nyingine za kuendesha kilimo?

Mheshimimwa Mwenyekiti, mkulima ataendeshajeshughuli nyingine za maisha huku tukijua kuwa zao la mahindikwa mkulima ndiyo zao la chakula na biashara. Akiuguaanategemea auze mahindi, watoto kwenda shule auzemahindi, kujenga nyumba auze mahindi na kulipa michangoauze mahindi. Hivyo, unapofungia mahindi yasipelekwe njehuoni kuwa ni kuwatesa wakulima wakati Serikali hainunuimahindi? Hivi Serikali inataka wakulima warudi kwenye jembela mkono au kilimo kwa ajili ya familia tu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kilimo hakuna viwanda.Wafanyakazi wa viwandani wanahitaji kula, viwandavinahitaji malighafi inayotokana na kilimo. Hata bidhaaitakayozalishwa viwandani lazima soko la kwanza liwewananchi wenyewe. Je, watanunuaje bidhaa kama hawanafedha kwa sababu Serikali imewafanya wawe maskini kwakutonunua mazao yao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, itakuwa ni vizuriwananchi wote wanaolima wahamie kulima korosho?Wakulima waache kulima mzao ya chakula wote wahamiemigodini kuchimba madini? Wananchi wa Tanzaniawataweza kununua chakula nje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Kilimo akumbukemaneno yafuatayo ya Mheshimiwa Rais John PombeMagufuli, alisema:-

1. Mkulima asinyanyaswe.

2. Mkulima asipangiwe bei ya mazao yakehukumsaidia kulima.

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

3. Hata kama utanunua debe moja la mahindi kwang’ombe watatu ni sawa tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais huyuanajua shida ya wakulima cha ajabu Waziri wakeanakwenda kinyume na bosi wake. Kwa hali hiyo viongozitumuelewe Mheshimiwa Rais wetu, tusimchonganishe nawananchi (wakulima).

Mheshimiwa Mwenyekiti, zuio la kuuza nje lina tafsirikama ifuatavyo:-

(i) Unapomzuia mkulima asiuze mazao yake (mahindi)nje wakati na wewe hununui maana yake ni kumpangia beiwakati hukumsaidia kulima.

(ii) Unaposema wafanyabiashara wakanunue mahindina kupeleka mikoa isiyo na chakula, je, huyo mfanyabiasharaumempatia fedha za kwenda kununua hayo mahindi kiasikwamba uwe na uhuru wa kumpangia bei ya kwendakununua hayo mahindi? Je, hao wafanyabiasharautawatafutia soko zuri la kurudisha gharama zao ili wapatefaida?

(iii) Unaposema kuuza chakula nje kwa maana yamahindi/mchele mpaka wa-process wauze unga na mchele.Je, wakulima hao wameandaliwa kuwa na uwezo huo kwasasa?

(iv) Unaposema wakulima hao kuuza nje wa-processwauze unga/mchele, je, wakulima wetu wamefikia kiwangohicho? Je, ni kila sehemu kwa sasa kumefikiwa na umeme?

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimwambieMheshimiwa Waziri wa Kilimo ni uungwana sana ukiaminiwana Rais tenda haki kwa watu wake na ukiona ngoma ni nzitosiyo vibaya kuachia ngazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu afya, nashauri kuwena mpango wa kumalizia maboma ya majengo ya zahanati

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

na vituo vya afya ambavyo tayari wananchi wametoanguvu kujenga maboma hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango haujaoneshakununua magari ya wagonjwa kwa vituo vya afya ambavyobado. Mfano, Kituo cha Afya Milepa na Laela katika Jimbola Kwela - Sumbawanga Vijijini havina magari ya kubebeawagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umeme, Mpangoueleze juhudi za makusudi kuhakikisha kila kijiji/kitongojikinapata umeme. Mfano, Jimbo la Kwela lipo nyumahalijapata umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa barabara,naishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa Daraja la MtoMomba. Naomba baada ya daraja kukamilika ianze ujenziwa barabara ya Kasansa - Kilyamatundu - Kamsamba -Mlowo kwa kiwango cha lami.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimpongeze Waziri Mpango pamoja natimu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapozungumzia mapinduziya viwanda pia hutoacha kuzungumzia mapinduzi ya kilimo.Niishauri Serikali yangu ipeleke wataalam wa kutosha katikasekta nzima ya kilimo kama Maafisa Ugani pamoja naMaafisa Maendeleo ya Jamii washirikiane kuhakikisha kuwawanatoa elimu yenye tija kwa wakulima wetu pamoja naSerikali kupeleka pembejeo na mitaji kwa walengwa ambaoni wakulima kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yote haya ni kutakakuboresha kilimo chetu ili kuwezesha malighafi nyingi zitokekwenye kilimo ambazo zitatumika katika viwanda vyetukuliko kutegemea malighafi kutoka nje. Pia katika viwandavyetu Serikali ihakikishe inasimamia viwanda vyetu vizalishebidhaa bora zenye viwango kuhakikisha tunashindana naubora wa masoko ya ndani na nje.

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ndiyo njia kuupekee ya kiuchumi. Kwa hiyo, niishauri Serikali yangu Tukufuipeleke fedha za kutosha na kuhakikisha barabarazinaunganisha Mikoa hadi Mikoa na Wilaya hadi Wilaya.Pamoja na barabara hizi muhimu ambazo ndiyo zinazotoamalighafi kutoka vijijini, Serikali ipeleke pesa za kutosha nakuwa na usimamiaji wa karibu kwa kuhakikisha zinapatikanakwa mwaka mzima kuliko ilivyo sasa hasa barabara za Jimbola Lushoto zimeharibika sana. Kwa hiyo, niiombe Serikali katikaMpango wake huu iangalie kwa jicho la huruma barabaraza Lushoto ili wakulima wetu mazao yao yasiozee shambanikama ilivyokuwa sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila afya hakutakuwa namaendeleo katika sekta zote hapa nchini. Wananchi wengiwameitikia wito wa kujitolea kujenga zahanati pamoja navituo vya afya, lakini Serikali haipeleki mafungu kwa ajili yakumalizia majengo hayo. Niishauri Serikali yangu ipeleke pesaza kutosha il i majengo yale yaweze kukamilika naWatanzania waweze kupata afya njema na kuwezakulitumikia Taifa lao. Hii iende sambamba na kupeleka vifaavyote vya afya ili kupunguza mlundikano mkubwa katikahospitali zetu za Mikoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ndiyo kila kitu katikamaisha ya binadamu. Kwa hiyo, niiombe Serikali katikaMpango wake huu wa mwaka 2018/2019 ihakikishe inamaliziamaabara zote ambazo zimeanza kujengwa bila kumaliziwapamoja na kuongeza vyumba vya madarasa, kujenga vyoopamoja na kujenga nyumba za walimu na elimu hii iendanena kujenga vyuo vya VETA kila Wilaya. Wilaya ya Lushoto tokeamkoloni hakujawahi kujengwa Chuo cha VETA. Kwa hiyo,Mheshimiwa Dkt. Mpango katika awamu hii naomba utengepesa za kujenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Lushoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia mazingiratuwe tunahakikisha tunapanda miti nchi nzima pamoja nakusimamia sheria kikamilifu il i wananchi wetu wawewanatunza vyanzo vyetu vya maji na Serikali ihakikisheinawawezesha wananchi kwa kuwapatia miche ili wapande

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

katika mashamba yao. Kwa mfano, katika Jimbo la Lushotokuna misitu imeungua moto lakini kuna kikundi cha vijanakinaitwa Friends of Usambara mpaka sasa kina miche zaidiya milioni 10 na wao wenyewe wameamua kupanda mitikatika maeneo yote ya misitu yaliyoungua. Kwa hiyo, niishauriSerikali iweze kusaidia vikundi kama hivi ambavyo vipo hapanchini na vikundi hivi ikisimamiwa vizuri tutarudisha uoto wetuwa asili uliopotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama il ivyoanzishwaTARURA, niishauri Serikali ije na mpango wa kuanzisha piawa Wakala wa Maji Vijijini na Serikali ipeleke kwa wakatiumeme vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,utaratibu wa Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 (ThePublic Finance Act, 2001 No.4) inaitaka Serikali kuleta Bungenibajeti ya nyongeza kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwafedha za awali hazikutosha. Kwa sasa kuna baadhi ya miradiya maendeleo inatekelezwa nje ya bajeti na hatujaonaSerikali ikiomba bajeti ya nyongeza, mfano, ujenzi wamabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ujenzi wabarabara za juu Dar es Salaam, ni baadhi tu. Kitendo chaSerikali kuamua kufanya matumizi bila kupata idhini ya Bungeni uvunjaji wa Katiba na sheria na kitendo hicho kinawezakuruhusu mianya ya rushwa na ubadhirifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mikopo ya elimu yajuu, katika mwaka wa fedha 2016/2017 wanafunzi waliopatamikopo walikuwa 20,183 na wanafunzi takribani 27,053walikosa mikopo. Mheshimiwa Rais katika kampeni zamwaka 2015 alisema yeye atakuwa muarobaini wa mikopoya elimu ya juu. Utolewaji wa mikopo umekuwa na ubaguzina usumbufu mkubwa, ni vyema Serikali katika Mpangowake iweke commitment ya kuandaa mfumo bora wa utoajimikopo ili kuondokana na tatizo hili. Vilevile kumekuwa natatizo au hakuna mfumo mzuri wa urejeshaji mikopo kwanisheria iliyopo inawaumiza sana waliopo katika ajira kukatwa

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

asilimia kubwa kulingana na kipato wanachopata nakushindwa kuhimili maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haionyeshi uwezokatika kuziwezesha sekta binafsi kukua ili ziweze kuipunguziaSerikali mzigo wa walio wengi kukosa ajira. Wafanyabiasharawalio wengi wamefunga biashara zao au kupunguzawafanyakazi kutokana na kushindwa kumudu gharama zauendeshaji, kushuka kwa mapato kwa baadhi yamakampuni, mfano, viwanda vya vinywaji, makampuni yakitalii, nyumba za starehe zikiwemo baa na hoteli. Mfumohuu unaangamiza kabisa sekta binafsi. Sekta binafsi ndiyoinayochangia mapato ya Serikali kupitia kodi inayokusanywakwa bidhaa na waajiriwa. Vilevile kumekuwa na tabia yakuwatishia wafanyabiashara kufunga makampuni kiholela,hii inaongeza umaskini kwa Watanzania walio wengi. Hivyo,nashauri Mpango huu uzingatie na uweke kipaumbele katikakuwezesha sekta binafsi kufanya kazi bila bughudha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wa viwanda, kamaTanzania ya viwanda ni uhalisia na siyo ndoto basi suala hililisingekuwa ni la matamko kwani hivi karibuni Waziri waTAMISEMI amenukuliwa na vyombo vya habari akieleza kuwakila mkoa kujenga viwanda 100 ambapo hadi Desemba,2018 katika Mikoa yote Tanzania Bara inatakiwa kuwa naviwanda 2,600. Kama miaka yote iliyopita imeshindikanakufufua tu viwanda vilivyokuwepo hii leo ya mwaka mmojaitawezekana? Kwa Mkoa wangu wa Iringa tu kulikuwa naviwanda vifuatavyo:-

1. Kiwanda cha Vifaa vya Nyumbani kama masufuriakiliitwa IMAC;

2. Kiwanda cha Nyuzi na Nguo (COTEX);

3. TANCUT Almasi;

4. Kiwanda cha Magurudumu ya Magari (VACULUG);

5. Kiwanda cha Tumbaku;

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

6. Kiwanda cha Coca cola; na

7. SIDO

Mheshimiwa Mwenyekiti, vyote hivyo havipo tena.Maelekezo hayo ya viwanda 100 yanashangaza kwa sababukama mikopo kwa sekta binafsi imepungua na kama Serikalihaifanyi biashara hivyo viwanda vitajengwa na nani? Serikaliinabidi ijipambanue ili kujua mfumo upi inaufuata kama niuchumi wa kijamaa au uchumi wa kibepari au soko huria iliijikite madhubuti katika mfumo itakaoamua kuufuata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo ndicho kinachotoaajira kwa Watanzania zaidi ya asilimia 70. Katika Mpangohuu bado sekta hii inaendelea kupuuzwa na matokeo yakeni kudorora kwa uchumi na hiyo Tanzania ya viwandainaendelea kuwa ndoto. Kuna changamoto kwenye kilimokwani wakulima hawapati pembejeo kwa wakati, kilimo chaumwagiliaji hakitiliwi mkazo, Maafisa Ugani hawako wakutosha, baadhi ya mabenki kutokopesha wakulima kwamadai kwamba mikopo katika sekta ya kilimo huwa hainauhakika wa kurudi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mpango huu Serikaliinatakiwa kubuni utaratibu maalum wa kuziwezesha benkiza biashara kuweza kutoa mikopo hiyo. Wanawake na vijanawakiwezeshwa hasa katika mikopo ya kilimo na ufugajiukosefu wa ajira utapungua.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na mchango wangu kwa kuzungumza nina mawazokatika kuimarisha sekta ya sukari kutokana na potential yasoko la ndani na nje. Mfano sisi tunaagiza sukari yenyethamani dola za Kimarekani milioni 60.9 (shilingi bilioni 123za Kitanzania), majirani zetu kama Angola ambao ni memberwa SADC wanaagiza sukari kwa thamani ya dola zaKimarekani milioni 161.1, Ethiopia dola za Kimarekani milioni188, haya ni masoko wazi lakini ili tuyafaidi. Pamoja na mradiwa Mkulazi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, tufikirie kuwezeshawawekezaji wa ndani kupitia benki za TIB na ile ya kilimo TAB

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

ambayo mpaka sasa ina around shilingi bilioni 164 lakiniimekopesha shilingi bilioni 3.4.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwekeza kiwanda chakuzalisha tani 150,000 inahitaji wastani wa dola za Kimarekanimilioni 80 bila kujenga facilities nyingine. Pamoja namashamba utahitaji jumla ya dola za Kimarekani milioni 150,hapo tayari una miundombinu ya nishati na barabara. Sasakumbe tutumie mfumo wa small scale growers ambapotunakuwa na factory nyingi maeneo mbalimbali kwakushirikiana na Halmashauri na sekta binafsi. Maeneopotential ya kuzalisha sukari ni pamoja na Bagamoyo tani120,000; Mkulazi tani 200,000; Ruipa tani 60,000; Rufiji tani60,000; Kasulu tani 30,000 na Mkongo – Mara tani 30,000, jumlatani 500,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida ya kutumia small scalesugar plants ni kama ifuatavyo:-

(i) Inahitaji eneo dogo kama five acres.

(ii) Inahitaji kama shamba la miwa la ekari 3,000 ilikulisha kiwanda.

(iii) Inapunguza gharama za kusafirisha miwa kwendakiwandani mfano leo hii pale Kilombero kuna miwainasafirishwa umbali hadi wa kilometa 60 lakini ikiwa ndaniya shamba la eka 3,000 huwezi kuwa na gharama kubwa yakusafirisha.

(iv) Inachukua wastani wa miezi kumi kujengakiwanda cha small scale.

(v) Inahitaji mwaka mmoja kuwaendeleza wakulimawadogo (small scale farms).

(vi) Ina promotes ushiriki wa small holder farmers.

(vii) Ni rahisi kutoa extension service na pia mwekezajihahitaji kugombania ardhi maana yeye atasaidia small holder

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

kwa mbegu na pia huduma nyingine muhimu kuwezeshakupata miwa yenye content kubwa ya sukari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muundo huu umewasaidiasana Brazil ambao wanazalisha 20% ya sukari (tani milioni 36)na wanahodhi 40% ya soko la dunia. Hivyo, potential ipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee Benki ya Kilimo.Nimeona juzi hapa benki ikiwa imepata fedha zaidi. Hatahivyo, kuna matatizo makubwa kwenye hii benki kuanziaMtendaji Mkuu mpaka Bodi. Mfano, hivi Zanzibar State TradingCorporation (ZSTC) waliomba mkopo wa shilingi bilioni 10 iliwanunue karafuu, Bodi ikapitisha lakini kwa uzembe waMtendaji Mkuu mkopo ukacheleweshwa, msimu ukapitabaadaye ZSTC wakaukataa mkopo. Tujiulize with a capitalof over 164 billion, how come wametoa mkopo wa less thanfive billion? And this is a bank na main core/function of thebank ni kukopesha. Mliangalie hili jambo ili benki hii iwenyenzo kuelekea uchumi wa viwnada. Ahsante.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kulingana na kauli mbiu ya Serikali ya viwanda ni vyematukaboresha Benki ya Kilimo na kuifikisha mikoani ili wakulimawaweze kukopesheka ili waweze kujikomboa kimaisha nakufikia malengo ya viwanda katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusu sokola uhakika la mazao, kutokana na nchi yetu kuwa na idadikubwa ya wananchi ambao ni wakulima wamejikita kwenyekilimo cha mazao ya chakula na mazao ya biashara ambayoyamekosa soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sekta binafsi, Serikaliinapaswa kushirikisha sekta hii katika taratibu za kukuzauchumi katika nchi yetu ili waweze kuwa mfano na wenginewaweze kuwekeza katika nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sekta ya maliasili nautalii, kulingana na umuhimu wa sekta hii ya utalii ni muhimuikatazamwa kwa umakini mkubwa kwani tukiwekeza kwa

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

kufanya tafiti za kutosha tutaweza kupata fedha nyingi zakigeni kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa watalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya kilimo ipewekipaumbele katika shughuli zote za maendeleo kwakuwawezesha wakulima kwa kuwapa pembejeo, mtaji naelimu ya kuachana na kilimo cha mazoea badala yake kiwecha kisasa. Kuhusu kilimo cha umwagiliaji, Serikali ijielekezekwenye kilimo cha umwagiliaji ili kuelekea kwenye nchi yaviwanda kuepuka kilimo cha msimu ambacho hakitabirikina kinaweza kisifikie malengo ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa sekta yamadini, kulingana na umuhimu wa viwanda ni vyema Serikaliikawekeza kwenye utafiti ili wanavyuo wanapomalizamasomo yao waweze kusaidia Taifa la Tanzania kwa upandewa madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Deni la Taifa, nivyema kama Taifa tukawa na utaratibu wa kukopa mikopoambayo haiwezi kuwatesa Watanzania wote. Tutawezakuepuka kero hiyo kwa kukopa kwa wazabuni wa ndaniambayo haitakuwa na kero kubwa.

MH. MARY D. MURO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nipongeze uwasilishaji wa Kamati ya Bunge na Kambi yaUpinzani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikalikuwaangalia kwa jicho la huruma wajasiriamali wadogokama wasindikaji ambao wanakutana na pingamizi kubwana kukatishwa tamaa na Taasisi za Serikali za Udhibiti. Mfano,TFDA imekuwa chanzo cha wajasiriamali kukata tamaakwani TFDA wanatoza fedha nyingi sana kwa kila product/bidhaa inayotengenezwa. Pia suala la TFDA kutoza kwa dolaimekuwa kikwazo kikubwa na inarudisha nyuma zoezi zimala wajasiriamali kukua. TFDA inatoza dola 2.5 mpaka 500 kwabidhaa ambayo mtengenezaji anaiuza kwa shilingi zaKitanzania.

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali iangalie jinsiya kupunguza urasimu kwenye usajili wa biashara kwaniurasimu ni mkubwa unapelekea watu wengi kukata tamaakwa mfano wawekezaji toka nje wanalalamikia sana kuhusuusajili hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niishauri Serikali juu ya kodikwa wafanyabiashara wanaoanza biashara kutozwa kodikabla ya biashara kuanza. Sheria ya mlipa kodi inatozwakwa kuangalia pato la biashara na si mtaji hivyo inasababishawatu wengi kushindwa biashara kwani hawana grace periodya biashara kama wageni wanavyopewa fursa hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kuwa navipaumbele kwenye mipango yake kwani Serikali ikiwa navipaumbele vichache vinavyotekelezeka itasaidiakuwezesha nchi kuondokana na utegemezi au kuongezaPato la Taifa kuliko ilivyo sasa ambapo vipaumbele ni vingikiasi kwamba utekelezaji unashindikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali katikaMpango wake wa viwanda iimarishe kilimo ambakomalighafi zitatoka. Serikali iboreshe tafiti za kilimo na watoeelimu ya kilimo ili wananchi wajue kilimo cha kisasa chenyetija na si kilimo cha mlo tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kuangaliahili suala la masoko kwa mazao, soko la ndani na la nje.Mpaka sasa wananchi wamekata tamaa ya kilimo baadaya Serikali kushindwa kununua mazao yao pia sheria yakukataza wakulima kujitafutia masoko. Wakulima wengiwamekata mitaji baada ya kulima na kukosa masoko namazao yao kuishia kuharibika. Pembejeo nazo nitatizo, hazifiki kwa wakati hivyo kupishana na msimu wakilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niishauri Serikali kuwekaviwanda vya kuchakata bidhaa zitokanazo na mifugo ikiwani pamoja na ngozi, maziwa, nyama kwani Tanzania inamifugo mingi.

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana majadiliano na nafasi za Wabunge zimeshafungwa sasatunarudi kwenye majibu ya Serikali. Tunaanza na MheshimiwaNyongo ajiandae Mheshimiwa Nditiye, ajiandae MheshimiwaEngineer Kamwelwe.

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili na mimi kwa upande waSerikali basi tuanze kutoa maelezo kwa upande huu.

Kwanza kabisa nipende kushukuru kwambaWaheshimiwa Wabunge wengi wametoa mawazo mengitofauti katika kuchangia huu mpango wa mwaka. Mawazoni mengi na nashukuru mawazo mengi ni mazuri lakini namimi kwa kujikita kwa upande wa madini kulikuwa kunamawazo machache kwa Wabunge ambayo waliyatoa hasawalijikita katika upande huu wa madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kabla sijajibu hojahizo awali ya yote nichukue nafasi hii kumpongeza sanaMheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayoifanya. Tumeonaanafanya mambo mengi ambayo kwa kweli yalikuwahayana majibu, lakini kwa uwezo wake Mheshimiwa Rais nauzalendo wake ameonesha dhahiri kwamba ana nia thabitina ya dhati kuhakikisha kwamba analinda rasilimali ya nchiyetu, anahakikisha kwamba rasilimali ya nchi yetu inakuwana tija kwa uchumi wa nchi yetu. Kwa hilo Mheshimiwa Raistunampongeza sana kwa kazi nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nichukue fursa hiikumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuanzisha hii Wizara mpyaya Madini. Wizara hii ilikuwa imeungana na Wizara ya Nishatina Madini na ukitazama ni kwamba tunatambua kwambamadini ni sekta nyeti, ni sekta ambayo ina mchango mkubwakatika uchumi wa nchi yetu. Hivyo Mheshimiwa Rais aliniteuamimi na Mheshimiwa Angellah Kairuki tuweze kuongozaWizara hii lakini ukitazama kwa kina ni kwamba MheshimiwaRais alitaka tija katika Wizara hii ya Madini. Wizara hiiimeundwa kwa maana ya kwamba tuongeze efficiency yakusimamia rasilimali ya nchi yetu.

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua mchango wauchumi katika nchi yetu rasil imali ya madini i l ikuwainachangia kiwango kidogo sana, asilimia 3.7 lakini sasa hivikwa juhudi zake Mheshimiwa Rais ni kwamba sekta ya madiniinachangia zaidi ya asilimia 4.3 katika uchumi wa nchi yetu.Hivyo basi mimi na mwenzangu tuna kazi kubwa kwakushirikiana na wataalam wa Wizara ya Madini kuhakikishakwamba tunaongeza tija kupitia hii sekta ya madinikuhakikisha kwamba uchumi wetu unaimarika natunakwenda kuimarisha uchumi kwa maana ya kwambatunakwenda kupandisha kiwango hicho kilichopo chaasilimia 4.3 na kwenda mbele zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa na Sheria ya Madiniya mwaka 2010 na tumefanya mabadiliko yake ambayo niya mwaka 2017. Mabaadiliko haya ni makubwa lakiniyalitazama sana katika sehemu nne ambazo ni muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya kwanza ilikuwani kuua ile Tanzania Mineral Auditing Agency (TMAA) najambo la pili lilikuwa ni kuunda Tume ya Madini ambayompaka sasa kama Wizara tupo katika kufanya restructuringkwa maana ya kuitengeneza hii Tume na kuianzisha ili sasaTume hii iweze kusimamia sekta ya madini inavyostahili, kwamaana ya kutoa leseni, kusimamia ku-regulate sheria nakanuni za masuala ya madini ili kusudi madini yetu yawezekuongeza tija katika uchumi wa nchi yetu. Kwa hiyo, kwamuda mfupi ujao, nadhani hadi kufikia mwisho wa mwakahuu Tume hiyo itakuwa tayari na itakuwa imeanza kazikuhakikisha kwamba inasimamia vizuri sekta hii ya madinina tuweze kupata tija kutokana na madini ambayotunachimba nchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu nyingine ya sheriahii ilikuwa ni sehemu ya kuongeza kodi ya royalty (mrabaha),kutoka asilimia nne kwenda asilimia sita na kutoka asilimiatano kwenda asilimia sita kwenye madini ya vito na madiniya metallic. Vilevile kuongeza gharama au kuongeza kodiya clearance ambayo ni asilimia moja. Mchakato huu hatakabla ya kuanzisha Tume hiyo, umeshaanza, sasa hivi

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

wachimbaji wanalipa royalty asilimia sita. Hii ni hatua kubwa,ni hatua nzuri ambayo itatuongezea kipato katika mrabahana Serikali itaweza kuneemeka zaidi na madini haya tofautina ilivyokuwa kipindi cha mwanzo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ndiyo mambo yamwanzo, naweza kusema ni utangulizi kwa ujumla wake.Ninapenda kusema na niwaeleze Watanzania kwamba,tunakwenda kudhibiti utoroshaji wa madini kwa kuundaTume hii na marekebisho ya sheria. Tunakwenda kuhakikishakwamba, madini yetu tena hayatoroshwi, hayapiti njia zapanya, hayapiti njia zisizo sahihi, tunataka kwambawachimbaji wote wapitie utaratibu unaostahili ili wawezekulipa kodi zote kwa TRA na vilevile waweze kulipa mrabahaili Serikali iweze kupata kipato chake ambacho kinastahili.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushahidi umeoneshaMheshimiwa Rais, tarehe 20 Septemba, 2017 alipokuwaMererani, alitoa amri ya kujenga ukuta unaozuia yale maeneoyote ya machimbo ya Tanzanite. Ujenzi huo umeanza tokatarehe Sita mwezi huu na ujenzi huo unakwenda kwa kasi yahali ya juu. Jeshi letu la JKT liko site linafanya kazi yaconstruction na kwa hali iliyopo sasahivi ni kwamba, kunawanajeshi pale wa kutoka JKT zaidi ya 2,000 na wanafanyakazi hiyo na wataifanya kazi hiyo kwa mkataba unavyosema,watafanya kazi ndani ya miezi sita na fedha za ujenzi waukuta huo wamekwishapewa asilimia 80. Kwa hiyo, tunahakika kwamba ukuta ule utajengwa na tutadhibiti utoroshajiwa madini kutoka eneo la Mererani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Mheshimiwa Raisalitoa amri ya kwamba, tujenge mnada ambao utakuwa niMererani ambao mnada huu utatumika kwa watu wanaokujakununua madini ya Tanzanite katika Mnada wa Mererani.Hapa tunavyozungumza pale Mererani tumeshapata eneola EPZA ambalo shilingi bilioni 2.2 imetolewa kwa ajili ya ujenziwa haraka wa mnada ule, ukishakamilika ujenzi ule kwamuda mfupi ujao, basi mnada ule utafunguliwa, madini yaTanzanite, maonesho ya madini, wanunuzi watakuja pale

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

watanunua na watalipa mrabaha, watalipa ili tuwezekupata kipato chetu kama kinavyostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika michango mbalimbalikuhusiana na utoroshaji wa madini hata sheria inasema, sasahivi tuna wataalam wazuri, wathaminishaji wa madini yetu.Ukiangalia kwenye upande wa Almasi tuna wataalamwazuri, mfano mzuri ni juzi tu hawa Wiliamson DiamondLimited (WDL) waliweza kuzalisha Almasi. Almasi ile katikakutolewa kuisafirisha Serikali kwa juhudi zake ilikamata nakuangalia, kulinganisha uthaminishaji wa mwanzo na wa pili,tukakuta thamani ya Almasi zile ni kubwa, Serikali ikazuiauuzaji wa zile Almasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, WDL waliendelea kuzalisha.Walizalisha tena carat 39,000 na zikathaminishwa kwa kiasicha shilingi bilioni nane na wataalam wetu, lakini kupelekaAlmasi ile kwenye soko la Almasi, soko la mnada la Antwerp,kwa mara ya kwanza tumeweza kuuza Almasi yetu kwa njiaya mnada kwa dola za Marekani bilioni 10. Hii ni hatua kubwaambayo Serikali imechukua na ni ya kumpa moyoMheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya. Kwa kwelihiyo ni hatua kubwa na Mheshimiwa Mwenyekiti na wewe nishahidi unalielewa hili. Kwa kweli, utoroshaji wa Almasiulikuwa ni wa hali ya juu, lakini kwa namna tunavyokwendatunakwenda kudhibiti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa yako katika ulemzigo wa pili uliokwenda kuuzwa kwa dola milioni 10, ndaniya almasi zile ilikuwepo almasi adimu ambayo inapatikanaTanzania ambayo tunasema inaitwa pink diamond, iliuzwakwa dola milioni mbili, kipande kimoja tu chenye carat tano.Kwa hiyo, tunaweza tukaona kwamba, kumbe tulikuwa napink diamonds nyingi ambazo zinakwenda bila kuwarecorded katika zile takwimu ambazo zilikuwa zinaandikwa,kwa hiyo, hiyo ni hatua kubwa tumeweza kufikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado tunaendelea na hatuaza ku-control utoroshaji wa madini. Juzi tumekamata kilonne za dhahabu katika Bandari ya Zanzibar, tumezikamata

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

dhahabu ambazo zina thamani ya milioni 500. Tunaendeleakuimarisha ulinzi mipakani kuhakikisha kwamba utoroshajiwa dhahabu unasimamishwa, lakini wakati huo huo Serikaliina juhudi ya kuanzisha minada mitano mikubwa ambayoitakuwa inauza dhahabu. Tutauza dhahabu kwa njia ya waziili watu waje wanunue dhahabu na waweze kulipa ushuru,waweze kulipa na mrabaha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile minada yetu hiitunatakiwa tuitengenezee miundombinu mizuri kwa maanaya usalama, miundombinu ya umeme, miundombinu ya maji,miundombinu ya usafirishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mjadala uliokuwaunaendelea watu wamepiga sana kelele kuhusukutengeneza Uwanja wa Ndege Chato. Kule Chato tunahitajiusafirishaji wa madini yetu, tunahitaji kusafirisha watu,tunahitaji kusafirisha vifaa, uwanja wa ndege wa Chato nimuhimu sana kujenga pale Chato. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda pale Bulyanhuluwana uwanja wa ndege. Wale mabwana wamejengauwanja wao wa ndege wa kuweza kusafirisha bidhaa zao,Kwa nini Serikali tusiwe na uwanja wetu? Kwa nini Serikalitusiweke uwanja wa kisasa wa kuweza kusafirisha bidhaazetu za madini kupitia uwanja wa Chato? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wameongelea kuhusuumbali wa kutoka Mwanza. Kutoka Mwanza hadi Geita nikilometa 185, kutoka Geita kwenda Chato ni zaidi ya kilometa120. Kwa hiyo ni kilometa 120 na hizo 180 ni zaidi ya kilometa300 kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza, hapa katikatiusafirishaji wa dhahabu ni hatari sana kusafirisha dhahabuumbali wa zaidi ya kilometa 300.

Kwa hiyo, uwanja wa Chato ni muhimu kuuweka palena hii ni kwa manufaa ya Watanzania wote na wala sio kwamanufaa ya watu wachache kama wenzetu walivyokuwawakieleza.

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naunga mkonohoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Nditiye, ajiandaeMheshimiwa Injinia Kamwelwe.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasihii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hiikumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa jitihadazake mbalimbali za kuisogeza nchi yetu katika uchumi wakati. Nampongeza vilevile Waziri wa Fedha na Mipango,Mheshimiwa Dkt. Mpango, kwa mpango mzuri sanaaliouleta, ambao ni mpango endelevu kwa ajili ya Serikali,unaolenga Mpango wa Serikali wa miaka mitano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii vilevilekuwashukuru wachangiaji mbalimbali WaheshimiwaWabunge waliochangia Mpango huu kwa nia njema kabisa,lakini niwashukuru kipekee wale waliochangia kwenye sektaya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano.

Mheshimwa Mwenyekiti, kipekee kabisa napendaniongelee masuala makuu manne, nitaongelea masuala yareli, nitaongelea masuala ya barabara, nitaongelea masualaya bandari na mwisho nitagusia kidogo masuala ya viwanjavya ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpangomkubwa sana wa ujenzi wa reli mpya kwa kiwango chastandard gauge, kila Mbunge anajua na kila mwananchianafahamu. Serikali ya Awamu ya Tano inatarajia kujengajumla ya kilometa 4,886 ambazo kiujumla kabisa zitajumuishakanda kuu tatu, tutakuwa na Ukanda wa Kati ambaoutajumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Isaka, Mwanzaambayo ni kilometa 1,219 lakini vilevile tutakuwa na Ukanda

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

wa Kaskazini ambao tutakuwa na reli ya kutoka Tanga,itapita Arusha mpaka Musoma, hizo ni kilometa 1,233 navilevile tutakuwa na Ukanda wa Kusini ambao ni wa kilometa1,092 ambao utatoka Mtwara – Mbamba Bay na matawiyake ambayo ni ya Liganga na Mchuchuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanzia na reli ya kati,tumeshaanza ujenzi wa kiwango cha standard gauge kutokaDar es Salaam mpaka Morogoro, kilometa 300 ambazozitajumlisha njia ya reli ya kawaida pamoja na trunks zakena sliding, mkandarasi mpaka sasahivi yuko site anaendeleana kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekwishapatamkandarasi vilevile kwa ajili ya kipande cha Morogoro mpakaMakutupora kilometa 422 sasa hivi yuko kwenye mobilization,wakati wowote ule ataanza kazi, sehemu nyingine zotezinaendelea na utaratibu wa upembuzi yakinifu na taratibunyingine kwa ajili ya ujenzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya gharamaitakayotumika kwa ajili ya mradi huu wa standard gaugekwa nchi yetu itakuwa ni dola za Kimarekani bilioni 3.17.Tunategemea itakapokwisha itakuwa na uwezo wa kwendaspeed ya kilometa 160 kwa saa, vilevile itabeba tani milioni17 kwa mwaka. Hiyo ni miradi kwa upande wa reli ambayoinaendelea na tumeona jitihada za Serikali katika kuhakikishakwamba hiyo reli inajengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa bandaritulikuwa na wachangiaji kadhaa ambao walizungumziasana masuala ya bandari. Serikali imekuwa na mpango mzurisana wa kuboresha bandari yetu kwanza ya Dar es Salaamkwa geti namba moja mpaka geti namba saba, ambapomoja ya shughuli zitakazofanyika itakuwa ni kuongeza kinacha bandari kwa mita 15 deep sea, halafu kuna sehemu yameli kugeuzia na yenyewe inapanuliwa kwa kiwango kizurikabisa cha kimataifa, vilevile tunaongeza sehemu yadragging and channel.

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Bandari ya Dar esSalaam itaenda kuboreshwa kwa kipindi kifupi kinachokujakuhakikisha kwamba inaweza kuhudumia meli nyingi kwawakati mmoja kwa kiwango cha kimataifa na gharamazitakazohusika katika mradi huo ni shilingi za Kitanzania bilioni335.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuna uboreshaji waBandari ya Mtwara ambapo zimetengwa jumla ya shilingi zaKitanzania bilioni 186. Tunatengeneza gati mpya pale kwaajili ya kufungua lango la Kusini kusafirisha na kupokea mizigo.Tunajua jinsi ambavyo kuna mabadiliko makubwa sanakatika Ukanda wetu wa Kusini, kuna viwanda vinaanzishwavikubwa, tunategemea tuweze kupata mizigo ya kutoshakwa ajili ya kuhudumia bandari ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Mamlaka ya BandariTanzania inaendelea kulipa fidia kwa wananchi kwa ajili yaujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo baada ya malipokukamilika tunategemea kwamba ardhi itakayokuwaimepatikana sasa atapewa mwekezaji ambaye tunaendeleana mawasiliano naye kwa ajili ya kujenga bandari hiyoambayo itasaidia sana katika kufungua lango upande waMashariki wa nchi yetu. Ni matumaini yetu kwamba,wananchi ambao wako maeneo ya Bagamoyo ambayoyako karibu na sehemu tutakakojenga bandari watatoaushirikiano wa hali ya juu kwa Serikali kuhakikisha kwambatunapata eneo hilo kwa ajili ya kujenga bandari mpya paleBagamoyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuna suala la viwanjavya ndege. Ni kweli kwamba Serikali imenunua jumla yandege sita, tunazo Bombadier Q400 ziko tatu ambazo zinauwezo wa kubeba abiria 76 na ndege mbili tayari ziko hapanchini na moja itakuja hivi karibuni. Tunayo ndege ya Q Seriesau Q300 ambayo inabeba abiria 150 mpaka 176 na yenyeweiko kwenye hatua za mwisho kabla haijaja nchini natumekwishafanya malipo ya mwanzo kwa ajili ya kupataBoeing 787 ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria262. Ndege hizo zote ni kwa ajili ya kurahisisha huduma ya

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

usafiri kwa njia ya anga ili nchi yetu iweze kupata maendeleoyanayotarajiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Serikali imeendeleakufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya upanuzi wa viwanjambalimbali hapa nchini. Tuna viwanja 11 ambavyo tayarimatengenezo yameshaanza kwa ajili ya kuvipanua, kupanuarun ways, kuna sehemu kwa ajili ya apron, kwa ajili ya sehemuza kugeuzia ndege na ku-park, lakini vilevile tumeendeleakujenga majengo ya abiria kwa ajili ya kuhudumia abiriawanaofika kwenye viwanja hivyo husika vya ndege. Kwakutaja tu, kuna uwanja wa ndege wa Kigomatumeshatangaza tender kwa ajili ya kutafuta mkandarasi wakupanua uwanja huo, kuna uwanja wa ndege waSumbawanga tumeshatangaza tender vilevile, kuna viwanjavingine mbalimbali kama Mbeya, Tabora na uwanja wandege wa Geita. Kwa hiyo, kuna maendeleo makubwaambayo Serikali inayafanya kwa ajili ya kuhakikisha kwambaviwanja vyetu vinakuwa vya ubora wa kisasa kabisa kwaajili ya kuhudumia abiria mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaongelea kwa haraka tuupande wa barabara. Waheshimiwa Wabunge wotewanaelewa wazi kwamba kuna miradi mikubwatunaendelea nayo ya ujenzi wa barabara. Kuna barabaraya TAZARA flyovers inaendelea, mkandarasi yuko pale natunategemea muda sio mrefu barabara itakuwa iko tayarikwa ajili ya matumizi, vilevile kuna Ubungo Interchangeambayo tayari maandalizi ya ujenzi yameshaanza,mkandarasi yuko kwenye site kwa ajili ya kufanya mobilizationna shughuli mbalimbali za kuhakikisha kwamba ujenziunaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Serikali imeendeleana mpango wa kuhakikisha kwamba kila Mkoa katika nchiyetu ya Tanzania unaunganishwa kwa kiwango cha lami.Sehemu zile chache zilizobakia ambazo bado hazijapatamkandarasi tunaendelea kutangaza tenda ili mkandarasiapatikane kwa ajili ya kuweza kuunganisha Mikoa yetu kwakiwango cha lami, lakini vilevile tunaunganisha Wilaya zetu

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

ndani ya Mikoa mbalimbali kwa kiwango cha lami na hatuakadhaa mbalimbali zimeshaendelea kutekelezwa.Tunashukuru sana kwa michango ya Waheshimiwa Wabungena tunawaahidi tutaendelea kuhakikisha kwambatunayachukua mawazo yao na kuyafanyia kazi kwa kadriitakavyowezekana, ili nchi yetu iweze kuwa na mtandao wabarabara nchi nzima ambao unapitika mwaka mzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuwapongezavilevile Waheshimiwa Wabunge ambao wametuleteamichango kwa njia mbalimbali na kwa sekta yetu yauchukuzi, mawasiliano na ujenzi tunawaahidi kwamba,tutafanya nao kazi kwa karibu sana, lakini tukiwakumbushakwamba ujenzi au uinuaji wa kiwango cha barabaraunategemea kwanza vikao ndani ya Halmashauri husika,baada ya hapo inekwenda kwenye RCC, baada ya hapondiyo inakuja kwenye bajeti kuu na kutengewa pesa kwaajli ya ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumza hayonaomba kuunga mkono hoja. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaInjinia Kamwelwe na Mheshimiwa Dkt. Tizeba na MheshimiwaDkt. Kalemani.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwakunijalia afya njema na kunipa pumzi. Pili nimshukuruMheshimiwa Rais, ameniamini miezi 23 katika nafasi ya NaibuWaziri, lakini baadae ameniamini zaidi na kunikabidhi nafasiya Waziri wa Maji na Umwagiliaji. Ninamshukuru sana naahadi yangu kwake na ahadi kwa wananchi wa Tanzania nikwamba nitawatumikia kuhakikisha wanapata huduma yamaji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeze sana Waziriwa Fedha, ndugu yangu Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango,kwa kuleta mpango mzuri huu ambao hauna maneno mengi,lakini ukiuangalia unatupeleka moja kwa moja kwenye

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

uchumi wa kati ili tuhakikishe kwamba, wananchi wetuwanakuwa na maisha bora. Niwashukuru sana WaheshimiwaWabunge kwa michango yenu ndani ya Wizara ya Maji naUmwagiliaji na michango hii yote kwetu ni dira, tutaifanyiakazi, tutashirikiana na ninyi na tunaomba muendelee kutu-support ili tuweze kutekeleza majukumu yaliyo mbele yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninayo michangoya kiujumla kwenye Wizara yangu ya Maji na Umwagiliaji nanianze na tatizo ambalo tumekuwanalo nab ado tunalo sasahivi kuhusiana na utoaji wa huduma ya maji vijijini na mijini,hasa kupitia katika mamlaka. Tunazo mamlaka za aina tatu,tuna mamlaka ya daraja la tatu, mamlaka daraja la pili namamlaka daraja la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, daraja la kwanzawanajihudumia kwa asilimia 100, ikiwa ni kulipa mishahara,kununua madawa na kulipa gharama za umeme. Madarajaya pili na daraja la tatu ni kwamba madaraja haya inabidiyasaidiwe hasa katika kulipa bili za umeme. Daraja la pililinasaidiwa kwa asilimia 50, daraja la tatu linasaidiwa kwaasilimia 100.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko changamoto katikamamlaka hizi, zipo mamlaka ambazo zipo chini ya Wizaraya Maji na ambazo zipo chini ya Wizara ya Tawala za Mikoana Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tulishakaa na Serikalitukayaainisha medeni na tukakubaliana kwamba Serikali sasahivi inaendelea kutafuta fedha ili iweze kulipa madeni yoteya nyuma. Tumejipanga kuhakikisha kwamba hatuendeleikuzalisha deni jingine na ndio maana tumekuja na mfumowa mita za LUKU upande wa maji i l i tukishaiwekamwananchi unalipia ndio uweze kupata huduma ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu katika hili,Waheshimiwa Wabunge na Serikali kwa ujumla ni kwambasasa tunajadili mapendekezo ya maendeleo ya mwaka ujao

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

wa fedha pamoja na mwongozo wa bajeti, Serikalituhakikishe watu wote wanatenga bajeti kwa ajili yakuzihudumia hizi mamlaka za daraja la tatu na daraja la pilii l i mwaka ujao wa fedha tena isitokee kwamba mtuanakatiwa umeme kwa sababu hajalipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua Nzega sasa hiviwamekatiwa na maeneo mengine pia lakini kamaalivyosema Mheshimiwa Waziri wa Nishati kwamba tutakaatuhakikishe kwamba wananchi hawa wanapata hudumaya maji. Changamoto ninayoipata ni kwamba umemeukikatika, maji yakikosekana hatuangalii kwamba ni umemelinarudi kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe sanahasa Serikali tuhakikishe kila mtu kwenye Taasisi yake mwakaujao wa fedha atenge bajeti kwa ajili ya kulipia gharamahizo za umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuweza kutekeleza azmaya kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata maji safina salama, bajeti ya mwaka 2006/2007 tulianzisha programuya maendeleo ya sekta ya maji. Katika programu hiyotulipanga kutekeleza miradi 1,810, hadi sasa kupitia progamuhiyo ya awamu ya kwanza ambayo ilikamilika mwezi Junimwaka 2017, tumefanikiwa kutekeleza miradi 1,423, miradiiliyobaki ni miradi 378 lakini tunaendelea na utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo ya utekelezaji wamiradi hiyo, tumetengeneza vituo 117,000 vya kuchotea maji,kama vituo vyote vingetoa maji, sasa hivi tungekuwa naasilimia 78 ya upatikanaji wa maji safi na salama katikamaeneo ya vij i j i . Bahati mbaya sana kutokana nachangamoto mbalimbali, asilimia 35 ya hivi vituo havitoi majina matokeo yake sasa huduma ya maji inayopatikana kwasasa ni asilimia 63.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia bajeti ya mwaka huuwa fedha tulionao 2017/2018 Waheshimiwa Wabunge vilevitabu mlivyopewa kwenye bajeti za Halmashauri tumeweka

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

kifungu cha fedha kwa ajili ya Halmashauri kuhakikishakwamba wanarejesha huduma kwa kukafuta vyanzo vingine.Tumeweka incentives kwamba ukirejesha huduma ya kituokutoa maji, unapata sterling pound 50 na ukiweka kituo kipyaunapata sterling pound 1,500. Fedha mnazo zimeainishwakwenye bajeti, kwa hiyo tujitahidi kuhakikisha kwambatunarejesha hiyo huduma ambayo tumeweka vituo lakini vilevituo havitoi maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ambayoimejitokeza mpaka hivyo vituo vikakosa kutoa maji hadi sasatumebaini kuna changamoto za aina tatu. Kwanza niwananchi kushindwa kuendesha miradi hasa miradi ambayounakuta kwamba mradi umewekwa katika kijiji wakawekajenereta ambayo inatumia diesel, wananchi wanafikia mahaliwanashindwa kumudu gharama ya kununua mafuta namatokeo yake ni kwamba mradi ule upo lakini hautoimaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekutana na mradi wanamna hiyo wakati wa ziara zangu nikiwa Manispaa ya Mjiwa Singida nikakuta kuna mradi una vituo vya kuchotea majizaidi ya 19, maji yapo lakini wamesitisha huduma kwasababu mashine iliyowekwa ya kusukuma maji inatumiadiesel na hawana uwezo wa kununua hiyo diesel, sasa hivitumeelekeza kwamba miradi yote ambayo inatumia jeneretaza diesel tuhakikishe kwamba tunaweka solar na ndio maanatuna bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilishangaa Manispaa hiyobajeti ya mwaka 2016/2017 walikuwa na shilingi bilioni mbililakini hawakutumia hata senti tano na bado walishindwakununua umeme wa kutumia nguvu ya jua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine nimabadiliko ya tabianchi na sisi wananchi kulima kwenyevyanzo vya maji, matokeo yake vyanzo vimekauka na miradituliyotekeleza tukiwa tunatarajia kwamba chanzo kitakuwamahali fulani, maji hakuna na matokeo yake sasa majihayatoki katika hiyo miradi.

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ya tatu nipamoja na usanifu mbaya, tumekutana na usanifu mbaya.Wataalam wanakwenda kusanifi kipindi cha mvua, kwa hiyo,kwa vyovyote maeneo yote unakuta yana maji, baada yakiangazi lile eneo ulilobaini linakuwa halina maji. Kwa hiyo,sasa hivi tunasimamia kuhakikisha usanifu unafanyika wakatiwa kiangazi ili chanzo kikipatikana kinakuwa na uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tumeanza awamuya pili ambayo itakamilika mwaka 2020. Katika awamu hiyo,tunatarajia kutumia zaidi ya dola bilioni 3.3 na tunalengakutengeneza miradi ya maji vijijini 4,015 na hadi sasa tayaritumeshasaini miradi 150 na tunaendelea vizuri kabisa. Hii nimiradi itakayotekelezwa katika vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna miradi zaidi ya 33ambayo tunatarajia tuitekeleze miradi ambayo ni mikubwa.Miradi hii ni pamoja na mradi wa ujenzi wa bwawa laKidunda, tuna mradi wa maji wa Mtwara Mikindani, tunamradi wa usambazaji wa maji kutoka visiwa vya Kimbiji naMpera na tuna miradi ya maji 17 katika miji 17 ambayoitafadhiliwa na mkopo nafuu kutoka Serikali ya India. Fedhahii imeshapatikana, taratibu za kukamilisha kusaini financialagreement ziko mbioni na wakati wowote ikishasainiwa basitutaendelea na utekelezaji wa miradi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna mradi mkubwa wamaji utakaopeleka Wilaya zote za Simiyu, huu ni mradimkubwa utakaotumia zaidi ya dola bilioni 300 na tendertumeshatangaza tayari. Kwa hiyo, tunasimamiakuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma ya maji.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunao mradi tunaendeleana usanifu wa kutoa maji Mto Malagarasi kupeleka Taborana kama tutaufanikisha mradi huu na maji yakawa mengi,tuna malengo ya kupanua huduma hii ili iweze kusambaana mikoa mingine kama tulivyofanya maji ya kutoka ZiwaVictoria. (Makofi)

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mradi wa maji wauondoaji wa majitaka katika Mji wa Dodoma nao piatunaendelea nao kutafuta fedha. Pia tuna mradi wa majikupeleka Mji wa Kisarawe na juzi meagiza ikifika mwezi watano mkataba wake uwe umeshasainiwa ili wananchi waKisarawe waweze kupata huduma ya majisafi na salama.Pia Kisarawe sasa hivi kuna eneo ambalo viwandavinaendelea kujengwa na tayari tuna kiwanda cha cementpale kinafanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mradi wa maji kwa ajiliya Mji wa Kilolo. Tuna mradi wa maji wa HTM nao pia taratibuzinaendelea…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Tizeba, ajiandaeMheshimiwa Dkt. Kalemani.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali yayote na mimi nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwakuendelea kuniamini kusimamia sekta ya kilimo hapa nchini.Pia niwashukuru sana viongozi wetu wakuu wa Serikali,Mheshimiwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa uongoziwao wanaonipa ili kutekeleza majukumu yangu sawasawa.Pia nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuniletea Msaidizikatika shughuli Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa naaminikwamba tutafanya kazi vizuri kwa matarajio ya waliotuteuana wananchi kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana nakumpongeza Mheshimiwa Dkt. Mpango na Mheshimiwa Dkt.Kijaji kwa kuleta huu mpango ambao kwa kweli unatoa diraya namna uchumi wa pamoja unavyoweza kwenda natukafikia hilo lengo letu la kuwa na uchumi wa kati ifikapomwaka 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niombe kutumia nafasihii kuishukuru sana Kamati ya Kilimo, Mifugo, Maji na Uvuvi

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

kwa sababu wamekuwa msaada mkubwa katika kutekelezamajukumu yetu. Wametushauri na tumesikiliza ushauri wao,wametuelekeza na tumetekeleza maelekezo yao. Pianiwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote ambaowamechangia kwa namna moja au nyingine kuhusu mamboya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kamati yetu, ratibaya Bunge iliyokuwa imetolewa ilikuwa tuanze kuwasilishataarifa za Wizara tarehe 30 mwezi uliopita, lakini kwa unyetiwa jambo la mahindi, Kamati ilituita mapema zaidi tarehe25 ili tujadili suala la mahindi kwa udharura. Wapo wananchiwana mahindi, hawawezi kuyauza kwa sababu ya beikushuka na kwa hivyo wanashindwa kuingia katika cyclenyingine ya kilimo kwa sababu hawana fedha kwa ajili yapembejeo na maandalizi ya mashamba yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kutokana na mjadalakatika Kamati, ndipo Serikali tulisikia na tukachukua pia hatuaza kidharura tukaelekeza Wakala wetu wa Mazao (NFRA)waanze tena kwenda kununua katika maeneo yenyeuzalishaji mkubwa, tukajipiga piga pesa ikapatikana yakuanzia na tunaendelea ku-mobilize funds ili waendeleekununua katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hivi wapowameanza manunuzi katika Mikoa ya Njombe na Ruvumalakini pesa tena tulikuwa tunazungumza na Waziri wa Fedhanyingine imepatikana sasa wataanza pia kununua katikaMkoa wa Rukwa na baadae wataingia katika Mkoa waSongwe. Kwa hiyo, hizi ni hatua ambazo tulizichukua kwaudharura ule ili kuhakikisha kwamba angalau fedha inaanzakupatikana kwa wananchi waweze kuingia katika kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya tathminitumebaini pia kwamba mahindi yaliyopo kwa wananchi nimengi sana na watu kwenye maeneo haya wasipopata sokola uhakika wengine hiyo fedha ambayo inatolewa na Serikalikupitia Wakala wake inaweza isiwafikie kabisa. Kwa hiyo,Serikali imeamua kwamba itawaruhusu wafanyabiashara

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

waweze kupeleka mazao nje ya nchi, hasa mahindi ilikutengeneza soko na kuchangamsha bei kwawafanyabiashara na wakulima wa zao hili la mahindi hapanchini. Tunaomba tu kwamba viongozi wote tushirikianekuhakikisha kwamba taratibu za kawaida za uondoshaji wamazao nje ya nchi zinafuatwa ili kulinda mipaka yetu nakulinda usalama wa chakula hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kuwaagizaWakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kote nchini kuachamara moja tabia ya kuzuia mazao kutoka katika mikoa yaokwenda mikoa mingine au kutoka katika wilaya zao kwendawilaya zingine. Tanzania ni moja na tungependa bidhaaziweze kusafiri kutoka sehemu moja ya nchi kwenda sehemunyingine ya nchi bila vikwazo vyovyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawashukuru piaWabunge wote wanaotoka maeneo yanayolima tumbakukwa jinsi ambavyo wameshughulikia suala la ukosefu wa sokola zao hili kwa umakini na kuguswa sana. Serikali ilikwishalionahili tatizo mapema la kwamba tumbaku imezalishwa zaidiya mikataba iliyokuwepo na wanunuzi wetu wa kawaidawa hapa ndani, kwa hivyo tulianza mchakato wa kutafutawanunuzi wa hii tumbaku ya ziada walioko ndani na nje yanchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jitihada kubwa zimefanyikana mpaka hapa tunapozungumza sasa zipo kampuni zandani ya hapa ya nchi walio tayari kununua hiyo tumbaku.Zipo kampuni pia ambazo zimeonyesha mwelekeo kutokanje ya nchi ambao pia wapo tayari kununua hii tumbaku.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitumie pia nafasihii kuiagiza Bodi ya Tumbaku ifanye mazungumzo namakampuni yote yaliyo tayari kununua tumbaku hii ya ziada,ifikapo kesho mchana wawe wamekwishanipa taarifa yakampuni gani inaunua wapi kiasi gani ili hii tumbaku iliyopokwa wananchi isiendelee kuharibika kwa kutunzwa vibayahasa ukizingatia kwamba sasa hivi tupo kwenye msimu wa

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

mvua na inaweza kunyeshewa na kupoteza ubora wake.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutarajie tu kwamba zoezihili litakwenda vizuri, wanunuzi watapatikana wataichukuahii tumbaku nasi tutajipanga vizuri sasa kuhakikisha kwambatunapanua wigo wa soko hili la tumbaku kwa kuingizawanunuzi wengi zaidi wa tumbaku kuliko tulionao hivi sasa.Kwa hiyo, mazungumzo yanaendelea na nchi mbalimbaliambazo zina interest ya kununua tumbaku yetu na InshallahMungu akitujaalia tutapata wanunuzi wengi zaidi katikamsimu ujao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Bajeti ilizungumziasuala la upatikanaji wa pembejeo kwa wakati. Ni kweli hililimekuwa tatizo kwa wakulima wetu hapa nchini kwa miakamingi. Pembejeo inafika mahali na hasa pale tulipokuwa namfumo wa ruzuku, pembejeo ya ruzuku inafika kwenye eneomsimu umekwisha mbolea na mbegu ndio zinafika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, sasa hivitunafanya mpango hapa nchini kupitia wizara yetu ambapotutahakikisha kwamba mbolea inakuwepo maeneo yotewakati wote. Hili tunalifanya kupitia huu utaratibu wauagizaji wambolea kwa pamoja, mbolea itakuwainaendelea kuagizwa bila kujali msimu wa kil imo il ikuhakikisha kwamba ipo madukani muda wote namwananchi akiihitaji anakwenda ananunua anafanya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo la kuaminikwamba kilimo ama pembejeo zinahitajika wakati wa mvuapeke yake sio sahihi, kwa sababu wapo pia wananchiambao wanafanya kilimo cha umwagiliaji, kwa hiyo, waohawasubiri msimu ule mvua, wanaendelea na kilimo chaomuda wote. Kwa hiyo, sasa tumeanzisha huu utaratibuambao utakuwa unatuhakikisha kwamba madukani ikombolea na inayohimilika kwa maana ya bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la bei limekuwa nitatizo au changamoto kwa wakulima wetu kwamba wengi

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

wamekuwa hawawezi kumudu bei ya mbolea hizi. Sasatulichokifanya tumeanzisha huo utaratibu ambaounatuhakikishia kushuka kwa bei ya hizi mbolea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba tena kutumiafursa hii kuwakumbusha wadau wote wahakikishe kwambabei elekezi kwa aina mbili za mbolea tulizoanza nazo katikamfumo huu yaani mbolea ya kupandia DAP na mbolea yakukuzia Urea bei elekezi zinazingatiwa kwenye maeneo yotenchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwatahadharishewafanyabiashara ambao hawataki uaminifu, wanaoendeleakuuza bei elekezi katika maduka ya jumla ya Mikoani naWilayani kwamba jambo hilo ni kuvunja sheria, kwa sababuwao katika maduka ya jumla wanatakiwa wauze kwa beichini ya bei elekezi ili bei elekezi imfikie mwananchi kijijiniambaye ananunua mbolea na kwenda shambani. Bei elekezisiyo katika maduka ya jumla isipokuwa bei elekezi ni yawakulima anayenunua na kwenda shambani. Kwa hivyo,viongozi wote wa mikoa simamieni hili jambo, viongozi wotewa wilaya wasimamie hili jambo ili wananchi wawezekunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalolimezungumziwa na Waheshimiwa Wabunge na tumeonani vema na sisi tulitolee maoni ni kuhusu uboreshaji walililokuwa Shirika letu la Usagaji la Taifa (National MillingCorporation). Niseme tu kwamba sasa hivi iliyokuwa NMCiko chini ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na bodihii imekwishaanza kazi. Ilianzishwa mwaka 2009 lakiniutekelezaji wa majukumu yake umeanza mwaka 2013 na sasahivi wanasaga na kununua mahindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasaga mahindi katikakinu cha Iringa na katika msimu huu mwanzo walikwishanunua tani 2,300 za mahindi lakini sasa hivi wamepata pesa,mkopo kutoka Shirika letu la Hifadhi ya Taifa (NSSF) shilingibilioni 8.9 na tumewaelekeza kwamba waendelee na ununuziwa mahindi katika maeneo haya ambayo yana uzalishaji

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

mkubwa ili kuondoa hiyo stress ya bei katika soko la mahindi.Pia wanafanya jitihada za ku-possess mali zao zote ambazowamepewa kwa mujibu wa sheria ili waweze sasa kufanyabiashara kama ambavyo inatarajiwa kutoka kwa wananchina Serikali kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisigongewekengele ya pili, naomba nikome hapo. Nisisitize tu kwambani ruhusa sasa kusafirisha mahindi kwenda nje ya nchi nataratibu tu za kawaida zifuatwe, pia ifikapo kesho mchanasuala la tumbaku ya ziada liwe limekwishapata suluhu kwamaana ya kwamba mnunuzi gani ananunua kiasi gani, wapiniwe nimekwishafahamishwa ili keshokutwa kama ni ununuzikuanza uanze mara moja bila kuchelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Kalemani,ajiandae Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla, ajiandaeMheshimiwa Profesa Ndalichako na ajiandae pia MheshimiwaMpina.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lubeleje, taarifa unampanani? Haya, kwa vile najua mahindi yanamsumbua kila mtusema.

T A A R I F A

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,wakati ninachangia Hoja ya Waziri wa Fedha na Mipango,nilizungumzia sana tatizo la ukame, watu ambao wana njaana chakula kimejaa kwenye ma-godown. Sasa Waziri waKilimo hakugusia hilo ni lini wataanza kugawa chakula chamsaada? Watu wanateseka na njaa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, na ninaomba nimjibu Mzee wangu,Mheshimiwa Lubeleje, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa tulizalisha kwautoshelevu wa asilimia 123. Kama ulivyosikia katika maelezoyangu sasa hivi yapo maeneo yenye ziada nchini, kule beiziko chini, wananchi wanalalamika hawana pa kuuzamahindi kiasi kwamba tumefikia turuhusu watu kupelekamahindi nje ya nchi. Lakini yapo maeneo na kwa tathminiyetu, mikoa kama 11 itakuwa na utoshelevu wa chini yakiwango na kwa hiyo tunaendelea kuwaombawafanyabiashara nchini wachukue mahindi kule ambapoyapo ya ziada wapeleke kwenye maeneo haya ambayohayana utoshelevu wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nitumie tu tenanafasi hii labda kulisemea hili, kwamba wafanyabiasharanchini na wakala zetu za Serikali wanaonunua watachukuamahindi maeneo haya yenye ziada na kwenda kuyauzakwenye maeneo ambayo yana upungufu ikiwamo pia Jimbolake la Mpwapwa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Kalemani, atafuatiaMheshimiwa Dkt. Kigwangala halafu Profesa Ndalichako.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naminianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuniaminina kuniteua kuwa Waziri kamili wa Nishati, Wizara ambayoni mpya. Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge wote, hata mimi kuwa Waziri waNishati nadhani ni kwa sababu ya mikono ya WaheshimiwaWabunge hawa, kwa jinsi ambavyo tumeshirikiana sanaawamu iliyopita katika masuala yote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nawashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge kwa juhudi ambazo mlikuwamnatupa na ushirikiano wenu, tunaamini sasa tutashirikianazaidi katika safari inayofuata. Hongereni sana WaheshimiwaWabunge.

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza Mpangowa Maendeleo wa miaka mitano, Wizara yetu mpya yaNishati inayo vipaumbele ambavyo ni vya msingi sana katikakujenga uchumi wa viwanda. Tunatambua kama Serikalikwamba uchumi ni nishati, viwanda ni nishati na maendeleoni nishati, bila nishati hakuna maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya vipaumbeleambavyo kwa kweli vimezungumzwa vizuri sana naMheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango ambavyoninapenda kurejea kwenye michango ni pamoja na miradimikubwa ya kuzalisha umeme. Hivi sasa tuna mkakatimkubwa wa kuzalisha umeme wa kujitosheleza kujengauchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa umemetulionao unatosha kwa mazingira ya sasa, lakini hauwezikutosheleza kwa mwendo kasi wa kujenga uchumitunaokwenda nao. Kwa hiyo, juhudi kubwa tumezielekezakatika kuzalisha umeme ili sasa utumike vizuri kwenye kujengauchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mkubwa wa kuzalishaumeme tulionao kwa sasa ni Mradi wa Kinyerezi Namba Mojana Kinyerezi Namba Mbili. Mradi huu tuna matarajioutakamilika soon, mwezi Agosti, 2018 miradi miwili itakamilikana kutuingizia sasa jumla ya megawati 425. Huu ni umememkubwa, kama utaingia kwenye Gridi ya Taifa utachangiasana kwenye kujenga uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuishukuru sanaSerikali kupitia kwa Mheshimiwa Rais na Serikali yetu kwakupitisha uamuzi wa kujenga umeme wa maji kupitiaStiegler’s Gorge ya Mto Rufiji. Huu ni umeme mkubwa ambaoutatuzalishia megawati 2100. Taratibu za kuanza kuujengamrdai huu zimeshaanza, hivi sasa tumeshatangaza tenderna waombaji zaidi ya 80 wamejitokeza, kesho tunaanzakufungua sasa kuanza kufanya evaluation.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matayarisho ya ujenzi wa

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

mradi huu yatakamilika mwezi Disemba mwaka huu namwezi Januari tunaanza kuujenga. Kwa hiyo, kufikia mwaka2020 tutaingiza kwenye Gridi ya Taifa megawati nyingine 2100.Tujipongeze sana kwa mradi huu mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ulichelewa kidogokwa sababu kubwa mbili; ya kwanza, kulikuwa na masualaya mazingira, katika awamu hii sio kwamba tunapuuzamambo ya mazingira, tutaenda nayo lakini huku tukiharakishaujenzi wake. Jambo la pili, mradi huu huko nyuma uliwekwachini ya RUBADA, kazi ya RUBADA kimsingi haikuwa kuzalishaumeme, ilikuwa ni ku-reserve mambo ya mazingira na vyanzovya maji lakini baada ya Serikali kuamua kwamba mradi huuupelekwe kwenye Wizara inayoshughulika na masuala yanishati, Serikali tumeuchukua na ndiyo maana tutaharakishaujenzi wake. Kwa hiyo, niwape uhakika wananchi naWaheshimiwa Wabunge kwamba mradi huu utajengwakuanzia Januari, 2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele chetu cha pili,pamoja na mambo mengine, ni ukamilishaji wa ujenzi wabomba la mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda kuja Tanga,Tanzania. Kama mnavyokumbuka, niwapongeze sanaWaheshimiwa Wabunge, mwezi Septemba 2017 mlipitishamkataba wa nchi mbili ili uanze kutekelezwa. Tunawashukurusana kwa sababu baada ya hapo ujenzi umeshaanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu kama ambavyonimeeleza ni mradi mkubwa. Hapa nchini kwetu utahusishaMikoa minane ambapo utapita katika Mikoa ya Geita,Tabora, Shinyanga, Singida, Dodoma, Manyara na hatimayeTanga. Kama ambavyo nimekuwa nikieleza mara zote, mradihuu, nasema utakuwa na impact kubwa kwa sababuunapita katika Wilaya nyingi sana, unapita katika Wilaya 24katika Mikoa niliyoitaja, kadhalika unapita katika vijiji 134 naunapita katika vitongoji 210. Sasa unaweza ukaona manufaayake itakavyokuwa kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kokote mradi utakapopitautakuwa na fursa kubwa sana za kiuchumi kwa Watanzania

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

na wawekezaji wengine. Kwa hiyo, mradi huu ujenzi wakeunaanza pia mwezi Januari utakapokamilika ndani ya miakamitatu, fursa kubwa sana za kiuchumi zitakuwazimeongezeka katika nchi yetu. Kwa hiyo, nilitaka kutoataarifa kwamba haya ni maendeleo mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na juzi tuikuwa Uganda,tumekamilisha uwekaji wa bomba na kwa upande wetutulishakamilisha, sasa kazi inayofanyika ni kukamilishamajadiliao kati ya Serikali na wawekezaji. Hatua inayofuatani kuingia mkataba wa ubia na ujenzi kuanza mara moja;huo ulikuwa ni mradi wa pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa tatu ni Mradi waUchakataji Gesi (LMG), huu ni mradi muhimu sana kamaambavyo mnausikia. Upo uvumi kwamba inawezekanamradi huu haupo, niseme kwa niaba ya Serikali; msimamowa Serikali wa kujenga mradi huu uko palepale. Sasakinachofanyika, pamoja na mambo mengine, tumeshapataeneo, tumeshafanya tathmini ya wale watakaoathirika nakutakiwa kufidiwa, lakini kazi inayofanyika sasa ni kukamilishamajadiliano ya uwekezaji, hatua inayofuata ni kuingiamakubaliano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi nyingine iliyokamilika nikupata eneo ambalo kinu kitajengwa kwa ajili ya kuchakatahiyo gesi. Kwa hiyo, hatua zinakwenda vizuri, na keshonitakutana na wadau wote watakaojenga mradi ule kamaOil4All, Big Shell na makampuni mengine ili taratibu za kuanzakujenga zianze mara moja. Kwa hiyo, ule uvumi wa kwambamradi huu umetelekezwa, Serikali iko makini sana na mradihuu na lazima utekelezwe kwa nguvu zote. Kama Waziri waWizara hii pamoja na Naibu wangu, tutausimamia mradi huukwa makini sana mpaka utakapokamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya gesi viwandani.Kama mnavyojua imechukua muda mrefu sana, hasaviwanda vya mbolea na vingine vya mkakati kupewa gesi,ninapenda kutoa taarifa kwenye kikao chako kwamba wikimbili zilizopita tumekamilisha makubaliano kati ya Serikali

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

na Ferrostaal, sasa wako tayari kuja kuwekezawamekubaliana na bei ya Serikali. Walichoomba ni kupataunafuu wa masuala machache ya kodi. Sasa tumeshaanzakukamilisha makubaliano nao, tunachofanya ni kupitiamaombi yao ili baada ya kukamilika waanze kuwekeza. Kwahiyo, maeneo ya Kilwa Masoko kutajengwa kiwandakikubwa cha mbolea chini ya ujenzi wa Ferrostaal kuanziasasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Mtwarabado tunaendelea kuzungumza na HELM na wenyewewanaonesha nia ya kukubaliana na Serikali ili sasa naowaingie katika utaratibu wa kujenga. Kwa hiyo, viwandavya kimkakati vitaanza kujengwa sasa kwa sababutunakwenda kwa kukubaliana pamoja.

Mradi mwingine ni wa usambazaji umeme vijijini waREA. Tunaposema ujenzi wa viwanda, havijengwi mjini pekeyake. Serikali imedhamiria viwanda vianze kujengwa kuanziavijijini na hakuna njia ya kujenga viwanda vijijini kamahujawapelekea wananchi umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wetu uko palepale,kama ambavyo tumeeleza, majibu mengi yametolewa naMheshimiwa Naibu Waziri, lakini mimi nifafanue kwa urefuzaidi. Kwamba mradi huu kama ambavyo tumekuwatukisema tumeanza kuutekeleza. Na nitoe rai na tamko kwawakandarasi wote, tunataka ifikapo tarehe 20 mwezi huu,wakandarasi wote wa REA wawe wamesharipoti katikamaeneo yao na mkandarasi yeyote abaye atakuwa hajafikakwenye eneo lake na kuanza kazi ifikapo tarehe 20 mwezihuu atakumbwa na kimbunga kikali kweli kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kusemakwamba Mpango wa Maendeleo wa miaka mitanokuwapelekea umeme wananchi kwa ajili ya kujenga uchumitunakwenda nao vizuri. Vijiji vyote 7,873 vitapatiwa umemekatika awamu hii ya kwanza tunaanza na vijiji 3,359 lakinibaadaye tunamalizia na vijiji 4,320, vyote vitapelekewaumeme.

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo maeneo ya mitamboya maji ambayo tumedhamiria kuyapelekea umeme ilikurahisisha shughuli zao. Kule Karatu tayari vile visimawalivyokuwa wameomba tumewapelekea umeme natunataka kupeleka visima vya maji maeneo ya Mara na mikoamingine. Lakini maeneo yote ambayo kutakuwa na mitamboya maji niwaombe sana Waheshimiwa Wabunge mtupatieorodha ya maeneo hayo ili tuanze kuyapelekea umememapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie tu na mradi wakusambaza gesi majumbani. Huu mradi ulikuwa unafanyiwatathmini, tathmini imekamilika, hivi karibuni tutatoa tendakwa ajili ya kuanza ujenzi. Kadhalika tumezungumza nawadau mbalimbali wanaounga mkono juhudi kwa ajili yakujenga viwanda hivi. Tutaanza na Mkoa wa Dar es Salaamili kupunguza matumizi ya mkaa. Tutaanza kusambaza Dares Salaam kwa kaya 3,000 na baadaye tutahamia Mtwarana Lindi na baadaye tutakwenda katika Mikoa ya Dodoma,Morogoro, Singida na hatimaye katika mikoa yote yaTanzania Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, itoshe tu kusema naungamkono hoja, Wizara ya Nishati itapambana kwa niaba yaSerikali kuhakikisha kwamba uchumi wa viwandaunajengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Dkt. Kigwangalla naMheshimiwa Profesa Ndalichako ajiandae.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa hii na miminichangie kwenye hoja hii ya Mheshimiwa Waziri wa Fedhana Mipango, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango. Kwanza,nianze kwa kuiunga mkono hoja hii, lakini pil i kwakumpongeza yeye mwenyewe binafasi na Naibu wake kwakuleta mpango huu mzuri ambao unatoa dira ya namna

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

ambavyo Serikali itatekeleza majukumu yake kwenye mwakaunaokuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, naomba nitoeufafanuzi kwenye maeneo machache ambayo yamegusasekta ya maliasili na utalii kwa ujumla wake. Lakini kabla yakufanya hivyo, nitumie nafasi hii kuwashukuru viongozi wetuwa juu wa Serikali kwa miongozo mbalimbali na maagizoambayo wamekuwa wakitupa toka wametupa dhamanaya kusimamia sekta hii. Mimi naomba niwape uhakika tu waopamoja na wananchi wa nchi yetu kwambasintowaangusha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo nimeonalimejitokeza kwa kiasi kikubwa na ambalo ninaomba nianzekwa kulitolea ufafanuzi kabla sijafika mbali ni suala la kwambaWaziri mpya wa Maliasili na Utalii ameanza kazi kwa kufukuamakaburi. Naomba niseme tu kwamba mimi siyo mashuhurisana kwa ufukuaji wa makaburi, lakini ukiwa Waziri halafuukawekwa kwenye Wizara ambayo wiki ya kwanza tu hatakabla hujaanza kazi kila mtu anasema umekalia kuti kavu,ni lazima kabla hujaanza kufanya kazi uliyopewa uanzekwanza kwa kusafisha nyumba yako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa msingi huo, tumeanzakazi ya hygiene kwenye Wizara hii na kazi hii haitakomampaka pale ambapo mitandao yote ya watu ambao wakondani ya Wizara hii wanashiriki kwenye vitendo vya ujangili,wanashiriki kwenye hujuma na wamekuwa wakitajwatajwakwenye kashfa mbalimbali za rushwa, tutashughulika naokwanza. Tukimaliza kuing’oa hii mitandao sasa tutaanza kazikubwa na pana na ya maana zaidi kwa nchi yetu yakuendelea kuongeza idadi ya watalii, lakini pia kuongezaidadi ya vivutio, pia kuendelea na kazi ya uhifadhi warasilimali hii adimu tuliyonayo kwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutafanya hivyo kwakuwekeza kwenye kanda nyingine kama Kanda ya Kusini kwamaana ya diversification ambapo kwa sasa tutaelekezanguvu zetu huko ili kuifungua corridor ya Kusini kiutalii. Serikali

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

imepata fedha, shilingi bilioni takribani juu kidogo ya 300 kwaajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kuifungua Kanda yaKusini kiutalii na ninaomba hapa nitambue mchangomkubwa wa Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango na timu yake, kwa kazi kubwa waliyofanyaya kuandika andiko la mradi huu na hatimaye kufanikishazoezi la kupata fedha hizi zaidi ya bilioni 300 kwa ajili yakufungua corridor mpya ya Kusini kitalii na ninaona kwa kweliyuko busy kutekeleza mpango wake ule uliopita na sisitunamshukuru. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla hatujafika kuanzakutekeleza hii mipango yote mizuri, nilisema ni lazima tuanzekusafisha. Katika kusafisha naomba niseme sikusudii kufukuamakaburi ya Mawaziri wazuri waliopita hapo wakapata ajalimbalimbali za kisiasa kama akina Mheshimiwa Maige,Mheshimiwa Kagasheki na Mheshimiwa Maghembe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nianze kwakuzungumzia Waziri mmoja ambaye wenzetu hawa waUpinzani walimsema sana alipokuwa Waziri wa Maliasili naUtalii na huyu si mwingine ni Mheshimiwa Lazaro Nyalandu.Ninataka niseme tu kwamba rafiki yangu, Mheshimiwa Nassarializungumza kwa mwembewe nyingi sana hapa Bungenikwamba kama Dkt. Slaa…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, order! Hebuvumilieni.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,aende kwenye Mpango.

MWENYEKITI: Mimi ndiye niliyekalia Kiti, ninaye-control,siyo wewe. Wewe Mheshimiwa Haonga kaa kimya. Huwezikujibizana na Kiti, kama msemaji atakosea mimi ndiyenitakayemrekebisha siyo wewe. Kaa kimya, itapendezaukitulia. (Kicheko)

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Unajua ukiwa unaishi kwenye nyumbaya vioo, usianzishe vita ya mawe, kuna wengine kwa walemliokuja wapya humu Bungeni mnatakiwa mjifunzemazingira ya humu ndani, kuna watu wanaguswa na kunawatu hawaguswi. Mimi ni katika watu wasioguswa na huwasipendi mambo ya kipuuzi kabisa hata siku moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu amesema nimeanzakazi kwa kuanza kufukua makaburi sasa sitakikuwakumbusha yaliyotokea huko nyuma lakini naomba tuniwape uhakika kwamba mimi huwa sichezewi chezewi. Mtualiyesema nimeanza kazi hii kwa kufukua makaburi na miminasema leo nafukua moja na ninaanza kufukua hilo mojakwa maelezo yaliyotolewa na Wabunge hawa wa Upinzanikwenye Bunge lililopita. Walisema Mheshimiwa LazaroNyalandu kazi yake ni kustarehe kwenye mahoteli ya kitalii,kazi yake ni kutembea nchi za mbali huko Marekani wapi nawarembo, wakasema alitembea alienda Marekani na AuntyEzekiel.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakasema Ndugu LazaroNyalandu anatumia helikopta za wawaekezaji kwa shughulizake binafsi za kisiasa na Mheshimiwa Nassari alisemakwamba kama yeye kama Dkt. Slaa angeshinda Urais mwaka2015 na akampa yeye Uwaziri wa Mambo ya Ndani kwa sikumoja tu, angeanza kwa kushughulika na Mawaziri wa hovyokama Mheshimiwa Lazaro Nyalandu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo ninaeleza kwambakwa nini Mheshimiwa Nassari alikuwa sahihi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Nassari alikuwasahihi kwa sababu wakati Waziri Nyalandu akistarehe kwenyeHoteli ya Serena pale Dar es Salaam akitumia helikopta yamwekezaji wa TGTS, mezani kwake…….

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa.

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nimewaonawawili upande huu ambao mnasema nje ya utaratibu waKibunge na utaratibu wa Kibunge kama unahoja unasimamana you have to catch the Speaker’s eyes, nikikuona nikuruhusukama sikuruhusu unakaa, unapendeza kwa kukaa na kamamtu anataka kuharibu kipindi hiki cha mchana, nawaambienina mapema tuanze kuharibiana. (Makofi)

Kwa hiyo, naomba kuna sauti mbili za Wabungewanawake nimeshaziona na nimeshazi-mark, si vizurikutajana majina lakini ikibidi tutasema. Kwa hiyo, naombakama mchangiaji mnamuona mimi hapa ndio referee mimisiyo kocha. Kama mlivyotulia hivyo hivyo tulieni inapendeza.Mheshimiwa Waziri endelea.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru, nilichokuwa nataka kusema ni tukwamba wakati Mheshimiwa Nyalandu Nyalandu akivinjarikwenye Hoteli ya Serena ambapo alikuwa akifanyia kazi zakeza Waziri wa Maliasili na Utalii kwenye hoteli ile na akapewachumba akawa anaishi pale kwa muda wote ule, mezanikwake kulikuwa kuna GN yaani tamko la Serikali kuhusianana kitu kinachoitwa concession fees kwenye mahoteliambayo yako ndani ya mbuga ya Serengeti.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa MwenyekitiKuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Kuhusu Utaratibu.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,hoja iliyopo mezani kwako ni kujadili Mpango wa Maendeleouliowasilishwa na Waziri wa Fedha…

MBUNGE FULANI: Kaa wewe.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: ...na katika Bunge lako hilileo ni siku ya sita tunajadili. Kwa hiyo, tunamuomba

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

Mheshimiwa Waziri ajibu hoja zilizotolewa na Wabungezilizoelekezwa kwenye Wizara yake. Haya anayotuambia yaMheshimiwa Nassari humu ndani hatuyajui na kamaalivyosema hatujayajadili na wala hayajajadiliwa kwenyeBunge la Kumi na Moja hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ajibuhoja, tunajadili suala kubwa na suala nyeti hapa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bobali unayo Kanuni hapo?Sasa nenda kasome Kanuni ya 68(10). Mheshimiwa Waziriendelea kwenye hoja yako. (Makofi)

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Bobalimimi mzoefu humu ndani, wewe unadhani mimi najibu hoja,mimi sijibu hoja mimi nachangia, mwenye hoja yuko paleWaziri wa Fedha na Mipango. (Makofi)

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Uzoefu maana yake nini?

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Muwe mnajifunzanishasema mimi huwa sichezewi chezewi.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Wewe unamtisha nani wewebwana!

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Kwa sababu najuaKanuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendeleekuchangia, ninachokisema ni kwamba wakati MheshimiwaNyalandu akifanya yote hayo kulikuwa kuna mambomakubwa mawili ambayo napenda tu kuyatolea mfanohapa.

Moja; mezani kwake kama Waziri wa Maliasili na Utaliikulikuwa kuna concession fees ambayo il ikuwaimependekezwa na TANAPA na gazeti likatengenezwalikisubiri signature ya Waziri ili Serikali ianze ku-chargeconcession fees kwenye mahoteli ya kitalii. Hilo lingeongeza

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

mapato na kwa mwaka huo wa 2014 tungeweza kukusanyabilioni 16 lakini Waziri yule hakusaini hiyo GN mpakaanaondoka madarakani, maana yake MheshimiwaNyalandu aliikosesha Serikali mapato ya takribani bilioni 32,hilo ni moja na ni jambo ambalo watu wa mahoteliwalipinga na baada ya watu wa mahoteli kupinga, Serikaliikashitakiwa Mahakamani, Serikali ikapata ushindimahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, Waziri alikuwahana lolote lile la kuamua kwa sababu kuna amri yaMahakama kwamba Serikali iko sahihi na i-charge concessionfees, lakini Waziri yule hakusaini kwa miaka miwili mpakaanatoka madarakani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo kama hayaukiniambia nafukua makaburi mniache tu niendelee kufukualazima nifukue kwa sababu bila kuweka mambo sawa, bilakujua kwa nini Mheshimiwa Nyalandu hakusaini, bila kujuaMheshimiwa Nyalandu alikuwa anashirikiana na akina nanina je, alikuwa anashirikiana nao wapo ama wameondoka?Huwezi kufanya kazi yako vizuri. Ndiyo maana hata Mawaziriwatakaowekwa pale wataendelea kutolewa tu,wataendelea kukalia kuti kavu tu, sasa mimi siko tayari kukaliakuti kavu, hata nikikaa miezi mitatu nitakuwa nimeinyooshahii sekta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili napendakuzungumzia mahusiano ya kutatanisha aliyokuwa nayoWaziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Nyalandu na wawekezajiwa taasisi maarufu inajulikana kama Friedkin FamilyFoundation ni billionea kutoka nchi ya Marekani ambayoilikuwa ina Makampuni yanayofanya kazi mbalimbali za utaliihapa na bado yapo mpaka sasa. Moja inaitwa MwibaHoldings, nyingine inaitwa Winged to Winrose na nyingineinaitwa Tanzania Game Trackers Safaris. Kampuni zote hizi,Kampuni ya TGTS ilipewa vitalu zaidi ya vitano ambazoingepaswa kupewa kwa mujibu wa sheria maana yake nikwmba hapo kuna mazingira ya kutatanisha, kuna mambohayako sawa na bado Kampuni hii ipo na inafanya kazi

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

kwenye sekta hii, ukisema nisifufue makaburi utakuwaunanionea, ni lazima nijue kwa nini waliopewa vitalu zaidiya vitano? Kwa nini wanaendelea kuwinda?

Kampuni ya Mwiba Holdings ina tuhuma za ujangilikwamba Kampuni inawinda, inafaya kazi za utalii lakiniimekamatwa na nyara za Serikali na hizi Kampuni zotezinamilikiwa na mtu mmoja anaiywa Tom Friedkin ambayeni rafiki wa Ndugu Nyalandu na Waziri huyu kamanilivyosema huko nyuma alikuwa akifanya kampeni za Uraiskipindi kile tulijaribu na sisi kuomba ridhaa ya Chamakugombea Urais, alikuwa akifanya kampeni zake, akizungukana helkopta ambayo inamilikiwa na Kampuni ya huyu NduguTom Friedkin. Sasa katika mazingira kama hayo, Waziri waMaliasili na Utalii, GN ya kusaini kuhusu kudai concession feeiko mezani kwao hausaini na unaka kwenye hoteli...

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninaomba kumpa taarifa Mheshimiwa Waziri kwamba yotehayo kama alifanya Waziri Nyalandu miaka yote hiyo, kwamuda wote huo ilipaswa awe ameshachukuliwa hatua kwamaana ya kupelekwa mahakamani kwa muda mrefu nawasingeweza kusubiri kuona amehama chama amehamiachama kingine ndiyo wanakuja na maneno mepesi mepesi,siasa nyepesi ambazo haziwezi kujenga Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ni taarifa tukwamba yoye aliyo...

MWENYEKITI: Ahsante ameshakuelewa, MheshimiwaKigwangalla.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, zama zinabadilika na uongozi pia unabadilika.Kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii sasa hivi kuna Waziri

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

ambaye anaweza kumchukulia hatua Ndugu Nyalandu, kwahivyo kama ndiyo kilio chako Ndugu Haonga mimi nitaagizahapa TAKUKURU pamoja na Jeshi la Polisi wayasikilize hayaninayosema, wachukue Hansard, wakafanye uchunguzi iliwaweze kumchukulia hatua Ndugu Nyalandu wala hilohalisumbui. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ndiyo kiu yako nawewe kama mwananchi na kama Mbunge kwamba kwanini Nyalandu hajafika mahakamani, mahakama bado zipona jinai haiishi muda, jinai hata miaka 100 ipo tu, kwa hiyovyombo vinavyohusika vichukue hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo Ndugu Nyalandualikuwa akitumia helicopter za Kampuni za huyu Ndugu TomFriedkin kufanya kampeni zake za Urais lakini pia kufanyakampeni zake za ubunge Jimboni. Katika mazingira kamahayo, dada yangu Devotha Minja ukisema nisifukue makaburiutakuwa unanionea bure tu. Mniache nifukue hayamakaburi, tuweke sawa nchi, tumsaidie Mheshimiwa Raisndiyo kazi tuliyopewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, vitalu vyauwindaji kabla ya Ndugu Nyalandu vilikuwa vikitolewa kwamakampuni mbalimbali na muda wa kuwinda ulikuwa nikatika kipindi cha miezi mitatu tu, kati ya Julai mpaka Oktobaili kuwapa nafasi wale wanyama kupumua na pia kuzaliana,lakini...

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti,ninakushukuru kwa kunipa nafasi.

Napenda kumpa taarifa Mheshimiwa Wzirianayechangia, nafikiri anaeleza kitu kizuri sana na mimininamshauri kwa kuwa ameingia kwenye Wizara hiyo,

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

tunaomba atupe taarifa za Mheshimiwa Maige, za Mzeealiyeondolewa pia wote kwa pamoja na MheshimiwaMaghembe atupatie ili tuweze kulisaidia taifa letu kusongambele. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Hiyo ni katika taarifaambazo silazimiki kuzijibu kwa sababu haina maana yoyote.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, naendelea na mchango wangu, NduguNyalandu alivyopewa tu kiti cha Waziri wa Maliasili na Utaliialichokifanya bila huruma yoyote ile, bila uzalendo wowoteule alianzisha mchakato wa kubadilisha...

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Ndalichakoajiandae Mheshimiwa Mpina.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasihii nami nichangie hoja ambayo iko mezani kwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuanza kwakumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwakuniamini na kuniteua tena niendelee kutumikia katika sektahii ya elimu. Nimhakikishie Mheshimiwa Rais na Watanzaniakwa ujumla kwamba nitafanya kazi yangu kwa uadilifu nakamwe sitawaangusha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuanzamchango wangu kwa hoja iliyoko mbele yetu ambayo niMpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2018/2019pamoja na Mwongozo wa Bajeti kwa kuanza kusemakwamba ninaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.(Makofi)

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja hiikwa sababu imeandaliwa vizuri na imeangalia maeneoambayo ni muhimu katika kusukuma maendeleo kwa Taifaletu. Napenda kumpongeza kwa dhati Waziri wa Fedha naMipango Dkt. Philip Mpango na Naibu wake kwa kazi nzuriambayo wameifanya katika kuandaa hoja hizi pamoja nawatendaji wote katika Wizara ya Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza Mpangohuu, Wizara yangu inayo mchango muhimu kwa sababuelimu ndiyo nguzo muhimu katika kuleta maendeleo ya Taifaletu. Kama ambavyo tunafahamu, Mpango wetu wamaendeleo umejikita katika kujenga uchumi wa viwandana ili tuweze kujenga uchumi wa viwanda ni lazimakuangalia kwa umakini ujuzi wa Watanzania ambao ndiyonguzo kuu ya maendeleo katika Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu katikakuhakikisha kwamba tunaweka mchango unaotakiwa katikakukuza ujuzi nchini, tumeweza kufanya mambo mbalimbali,Waheshimiwa Wabunge wamekuwa katika michango yaowanaulizia na kuonesha wasiwasi wao kama kweli hii Serikaliimejipanga kuhakikisha kwamba kunakuwa na ujuzi wakutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niseme katikampango wetu tumeonyesha kwamba ili tuweze kwenda nakasi inayotakiwa tunatakiwa tuwe na asil imia 55 yaWatanzania wenye ujuzi wa chini, asilimia 33 ya ujuzi wa katina asilimia 12 ya ujuzi wa juu.

Kwa hiyo, Serikali inao Mpango Mkakati wa KukuzaUjuzi (National Skills Development Strategy) ambao katikakutekeleza mpango huo, Wizara yangu kwa kushirikiana naOfisi ya Waziri Mkuu kuna mpango ambao tunazo dola milioni120 ambazo ni sawa na fedha za Kitanzania bilioni 250ambazo zinalenga kukuza ujuzi

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha hizi zitawezeshakuimarisha mafunzo ya ufundi stadi kwa kuimarisha

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

miundombinu katika taasisi zetu zinazotoa mafunzo ya ufundistadi hususan VETA, Arusha Technical, Dar es Salaam Instituteof Technology pamoja na taasisi nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia huu mpango waelimu na ujuzi kwa kazi zenye tija (education and skills forproductive jobs) umejikita katika kuangalia maeneo ambayoni ya kipaumbele katika mpango wetu wa maendeleoambao ni pamoja na sekta ya kilimo, utalii, usafirishaji, ujenzi,nishati pamoja na TEHAMA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namna mojawapo yakupata fedha hizi ambazo nimezisema bilioni 250 ambazoSerikali tayari inazo kwa ajili ya kutekeleza mradi huu itakuwani pamoja na kuandika maandiko ambayo ni shindani. Kwahiyo, nitumie fursa hii kuwataka Waheshimiwa Wabungetushirikiane katika kuhakikisha kwamba fedha hizi ambazotunategemea kutangaza kwa mara ya kwanza maombi kwaajili ya kupaya ufadhili (skills development fund) mwishonimwa mwezi huu tushirikiane kuhamasisha taasisi za ufundizilizoko katika maeneo yetu kwa sababu fedha zitakuwazinatolewa katika mfumo wa ushindani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ningependakuchangia ambalo Waheshimiwa Wabungewamelizungumza katika michango yao ni suala la utoaji waelimu bure na suala la changamoto zilizopo katika utoajielimu.

Kwanza niseme kwamba suala la utaoji wa elimu burekatika Nchi hii limekua na mafanikio makubwa sana. Kilamwezi Serikali inatoa kiasi cha shilingi bilioni 20.8 kwa ajili yaelimu bure na mojawapo ya vigezo ambavyo tunawezatukavitumia kusema kwamba kumekuwa na mafanikiomakubwa, ukiangalia takwimu za wanafunzi ambaowanafanya mtihani wa kidato cha pili ambao wameanzaleo hii wameongezeka kutoka wanafunzi 435,075 mwaka2016 hadi kufukia wanafunzi 521,855 ambalo ni ongezeko lawanafunzi 87,730.

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mpango waelimu bure ulianza kutekelezwa mwaka 2016, hii ina maanakwamba, wale wazazi ambao walikuwa wanashindwakuwapeleka watoto wao sekondari kwa sababu ya ada,Serikali imefungulia na ndiyo maana leo hii tunaona hataidadi ya watahiniwa wanaofanya mtihani wa kidato chapili imeongezeka sana. Niwahakikishie Watanzania kwamba,Serikali imejipanga vizuri katika kuimarisha miundombinukatika ngazi zote za elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i kukabiliana nachangamoto za ongezeko la wanafunzi tumekwishajengamadarasa 1,409 tumeshajenga matundu ya vyoo 3,394 lakinivilevile tumeongeza mabweni kwa ajili ya kuhakikishakwamba watoto wa kike wanaotoka umbali mrefuwanaweza kusoma katika mazingira ambayo ni tulivu zaidikwa hiyo, tumejenga mabweni 261.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kutambuakwamba mazingira ni muhimu kwa wananfunzi kujifunzavizuri tunafanya ukarabati wa shule zetu kongwe na mpakasasa tumekwishaanza ukarabati katika shule 42 kati ya shulekongwe 88 katika nchi hii, niwahakikishie WaheshimiwaWabunge kwamba shule zote kongwe nchini zitafanyiwaukarabati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumeboreshamiundombinu katika vyuo vyetu vya ualimu na tunaendeleakufanya hivi. Sasa hivi ninavyozungumza Vyuo vya Ualimuvya Kitangali, Mpuguso, Ndala na Shinyanga miundiombinuyake inaimarishwa kwa kiwango kikubwa, majengo ya kisasayanajengwa, hii yote ni katika kutekeleza mpango wa Serikaliambao unalenga kufungamanisha maendeleo na rasilimaliwatu, ili kufanya hivyo lazima tuhakikishe kwamba tunayorasilimali iliyobobea katika ujuzi katika kutekeleza mpangowetu wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo Wizaraimekuwa ikifanya katika kutekeleza mpango huu nikuhakikisha kwamba tunakuwa na msingi ulio imara. Kwa

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

sababu tunafahamu kwamba nyumba bora inajengwakatika msingi ulio imara, Serikali imekuwa ikiweka kipaumbelekatika elimu ya awali kuhakikisha kwamba vijana wanapatautayari wa kuanza elimu ya msingi, tumeendelea kutekelezaProgramu ya Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabuili kuwajengea vijana wetu msingi mzuri wa kuweza kupatamaarifa wanapokuwa wanaanza darasa la kwaza, la tatuhadi la nne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kufanya hivyotumekuwa tukitoa mafunzo kwa walimu wa darasa lakwanza, la pili, walimu wa darasa la tatu na la nne pamojana walimu ambao wanafundisha wananfunzi wenye mahitajimaalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia imeendeleakuweka mazingira wezeshi kwa wanafunzi wenye mahitajimaalum ambapo tumewanunulia vifaa vya kujifunzia vyenyethamani ya shilingi bilioni 3.6 lakini pia Serikali inaendeleakuimarisha ufundishaji wa sayansi kwa sababu tukipataWanasayansi wazuri ndiyo chachu muhimu ya kuweza kupatawataalam ambao wanahitajika katika fani mbalimbalinchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeendelea piakuhakikisha kwamba tunakwenda sambamba na utoaji waelimu ya juu kwa kuimarisha miundominu katika elimu ya juu.Ninapende kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba pamoja nataarifa ya Serikali ambayo niliisoma hapa Bungeni tarehe Tisapia Bodi ya Mikopo imeendelea kutoa mikopo na wananfunzizaidi ya 1,775 wamepangiwa mikopo na hivyo kufanya sasajumla ya wananfunzi ambao wameshapangiwa mikopokufikia 31,353.

Mheshsimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii kwaWanafunzi ambao hawajapata mikopo lakini wanaonabado wana uhitaji, dirisha la kukata rufaa limefunguliwa leona litafungwa tarehe 19 Novemba, 2017. Niwaombe naniwaelekeze wanafunzi wote ambao hawajapata mikopolakini wanaona wana uhitaji mkubwa, watumie fursa hiyo

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

kukata rufaa na Serikali inaendelea kujiridhisha kama Je, kweliwanafunzi wale waliopangiwa mikopo ndiyo wale ambaowana uhitaji ukilinganisha na wale ambao hawajapata ilikuhakikisha kwamba dhamira ya Serikali kuhakikisha kwambamikopo ya elimu ya juu inatolewa kwa wanafunzi tu wenyeuhitaji kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa inazingatiwa,kwa sababu hiyo tayari nimeagiza Bodi ya Wakurugenzi yaBodi ya mikopo kupitia jina moja baada ya lingine ilikujiridhisha kwamba je, wale waliopangiwa mikopo ndiyowenye uhitaji kuliko wale ambao hawajapangiwa, lakini piakupitia majina yote ya wanafunzi ambao hawajapatamikopo ili kujiridhisha kama kweli hawana vigezo kwa mujibuwa vigezo mbavyo vimewekwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwahakikishie kamanilivyosema, wanafunzi wa elimu ya juu kwamba Serikaliinatekeleza sera ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wenyeuhitaji tu na hapo Waheshimiwa Wabunge tuelewanekwamba sera yetu ya elimu ya juu ni sera ya uchangiaji.Hatujafikia mahali ambapo Serikali inatoa mikopo kwawanafunzi wote na ndiyo maana hata Sheria ya Bodi yaMikopo imeainisha wazi kwamba mikopo itatolewa kwawanafunzi wenye uhitaji, kazi ya Wizara yangu ni kusimamiana kuhakikisha kwamba wale ambao wanapangiwamikopo ni wale tu wenye uhitaji na siyo vinginevyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kushukuru kwanafasi na kama nilivyosema tangu mwanzo wakati naanzaninaunga mkono hoja hii na ningeomba Wabunge wotetuiunge mkono kwa sababu ni Mpango ambao ni mzuri sana.Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mpina.

T A A R I F A

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana na tunashukuru kwa michango ambayoinaendelea kutolewa na Mawaziri wanafanya kazi nzuri, lakiniwakati ambapo tulipokuwa tukichangia Mpango huu waMaendeleo tulikuwa tunazungumzia issues specific kwaupande mwingine wa Jamhuri ya Muungano, lakini kadri yamichango inavyoendelea kutolewa naona hakuna aspectyoyote. Kwa mfano, eneo la utalii na vilevile eneo la elimuya juu.

Kwa hiyo, Mheshimiwa naomba kutoa hiyo taarifakwamba hata Mawaziri nao wanaowajibu wa kujibu hojazile ambazo tulikuwa tumezitoa na specific kwa ajili yaupande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, hoja hizo atakujakuzijibu Waziri mwenyewe mtoa hoja Waziri wa Fedha zote.Tunaendelea na Mheshimiwa Mpina.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi hii. Na mimininamshukuru sana Mheshimiwa Rais kunipa dhamana hii yakuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na kumuahidi kabisakwamba nitaitumikia nafasi hii na kuwahakikishia Watanzaniawenzangu kwamba nitawatumikia kupitia nafasi hii kwanguvu zangu zote na kipaji chote nilichopewa na MwenyeziMungu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni Mapendekezo yaMpango wetu wa Maendeleo. Waheshimiwa Wabunge wetuwamezungumza mambo mengi sana, lakini ninachotakakusema kwa sababu haya ni mapendekezo ya mpango, zileinputs zao walizozisema tumezichukua ili sasa tuje na Mpangowenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa hatujibu sana kihivyokwa sababu tumepewa ushauri na Waheshimiwa Wabungeili tukaandae Mpango wenyewe. Hata katika mapitio hapanimeona kwenye Wizara yangu na wamependekeza mambo

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

mengi, wamezungumzia suala la bandari ya uvuvi, meli yauvuvi, umuhimu wa kuwa na viwanda vya kuchakatasamaki, umuhimu wa kuwa na viwanda vya nyama,umuhimu wa kuwa na viwanda vya maziwa, haya yote niinputs wametupa ili tukaandae Mpango wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kabisa kwamba kwamoyo mmoja, michango yote ambayo imehusu sekta yangunimeichukua ili kwenda kutengeneza Mpango wenyeweambao ndiyo baadae muda utakapofika tutauwasilishahapa Bungeni na hapo ndipo mtakapoona kwambatumefanya kufikia wapi zi le inputs ambazo ninyimmetuwekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nakwa sababu muda unakuwa hautoshi sana nitoe ufafanuziwa baadhi ya mambo machache.

Moja, limezungumza sana suala hili la uchomaji wavifaranga vya kuku 6,400 ambavyo vilikuwa vinasafirishwakuingia nchini mwetu kutoka Kenya. Tukajaribiwa kulaumiwasana kama Wizara na kama nchi wakati mwingine kwakitendo hicho tulichokifanya. Jambo moja tu niseme, hapatuko Mawaziri pamoja na Wizara yangu tumeapishwakusimamia sheria na tunatekeleza kwa misingi ya sheriailiyowekwa katika kutekeleza majukumu yetu na kwambahatuwezi kufanya vinginevyo kwa sababu tukifanyavinginevyo Bunge hili litatuuliza kwa nini tumefanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria yetu ya Magonjwa yaWanyama Namba 17 ya mwaka 2003 inatoa utaratibu wanamna ya kuingiza kuku pamoja na mazao yake ndani yanchi. Vilevile kuna mazuio ambayo yalitolewa kulingana najambo hili. Tarehe 29 Oktoba, 2017 tulipowakamata haovifaranga, tuliwachoma moto kwa sababu kubwa kwambatulikuwa na zuio ambalo tulishaliweka toka tarehe 7 Juni,2006 kwamba kutokana na tishio la ugonjwa wa mafua yandege lililokuwepo duniani tulilazimika kuzuia uingizaji wakuku pamoja na mazao yake na tukawa tumezuia mtu yeyotekufanya hivyo.

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu ndugu aliyeingiza hawavifaranga kwanza aliingiza kinyume cha utaratibu bila kibalichochote ilikuwa ni illegal importation, pili, alitaka kuingizawale kuku wakiwa hawajakaguliwa. Kwa namna yoyote ilekuingia ndani ya nchi ambako kungesababisha kero kubwa.Kwa mfano, kuku wale wangekuwa wana ugonjwa huo wamafua ya ndege maana yake tungeua ndege wetu wotewalioko hapa nchini, vilevile mafua haya ya ndegeyanambukizwa mpaka kwa binadamu tungeweza kuuabinadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuzungumza kwaurahisi jambo la vifaranga hivi kuwateketeza ukawaunazungumza tu kiurahisi kwamba unajua, sijui mambo gani!Ni lazima tuchukue hatua hizi kali kwanza kwa yule aliyefanyahivyo kuhakikisha kwamba hakuna mtu mwingine ambaeatafanya jambo kama hilo, mtaji wake tumeuteketezamaana yake kama ana njia zingine ambazo alikuwaanatumia kuingiza vifaranga nchini hawezi kurudia tena,Watanznaia watuelewe kwamba tunasimamia maslahi yaWatanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuku wakifa, biasharaTanzania imekufa ya kuku, Watanzania watakufa kwa mafuaya ndege na kama Watanzania watakufa kwa mafua yandege kutokana na uzembe wa Wizara yangu na wale askariau watu waliokuwa wanafanya inspection kamawasingewachoma kuku siku ile, ningewafukuza kazi wotesiku hiyo. (Makofi)

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWENTEKITI: Taarifa.

T A A R I F A

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kumpa taarifa Mheshimiwa Wazirikutokana na kifungu cha 68(8), Mheshimiwa anasema

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

kwamba waliogopa kwamba wale kuku walikuwa naugonjwa wa mafua ya ndege, lakini taarifa waliyoitoa mudawote walisema kwamba hawakupima. Hii ni aibu kubwasana kwa Serikali kufanya mambo kama yale yaliyofanyikakuchoma vifaranga vya watu bila kupima. Tulifikiri hata kamani Serikali inatekeleza sheria ilipaswa pia Serikali…

MWENYEKITI: Ahsante amekusikia. Mheshimiwa Waziriendelea.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, nilisema kwamba Bunge hili ndilo ambalolinatunga sheria. Utekelezaji wa sheria hauwezi ukafanyikakama Mheshimiwa Mbunge anavyopendekeza. Sheria yaMagonjwa ya Mifugo, Magonjwa ya Wanyama Na. 17 yamwaka 2013, Kifungu cha 8(2) kinasema “ni kukamata nakuteketeza” na siyo anavyozungumza yeye. Tumekamata natunateketeza na tunapelaka salamu Afrika na dunianikwamba lazima wanapotaka kufanya hivyo waangalie sheriaza nchi yetu zinasema nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili tunafanyaoperation ya mifugo kutoka nje ya nchi. Ni takribani asilimia30 ya malisho ya nchi hii yanalishwa na mifugo ya kutokanje, napo tunalalamikiwa, tumekatana ng’ombe,tumekamata, tumetaifisha na tumepiga mnada. Napendaniwambie watu ambao wanatetea mambo haya, kunajambo moja tu wanalotaka kufanya…

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa ya mwisho hiyo.

TAARIFA

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,sisi wadau wa haki za wanyama kwa kweli tumesikitishwasana na kitendo kile. Sasa kama vifaranga wamechomwa,kwa nini…

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

MWENYEKITI: Kaa chini huna taarifa! (Kicheko)

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, tunafanya operation ya kuondoa mifugo kutokanje ya nchi ambao wameingia nchini kinyume cha sheria.Hili pia limelalamikiwa na wakati mwingine wanaolalamikani watunga sheria za nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa sheria hiyoniliyoitaja Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Namba 17 yamwaka 2013 imeonesha utaratibu wa kuingiza mifugo ndaniya nchi kutoka nchi nyingine. Ukieda kinyume na huoutaratibu umevunja sheria. Sheria hiyo pia inakataza kuingizamifugo kwa ajili ya malisho. Watanzania wetu sasa ukiruhusumifugo ile kuingia hapa nchini madhara yake ni nini? Madharayake unaweza kuleta ugonjwa wa kutoka nchi jirani kuingiahapa nchini. Kwa hiyo, tumekamata ng’ombe wale 1,325wa kutoka Kenya na sasa hivi tunashikilia ng’ombe wenginezaidi ya 10,000 kutoka Rwanda na Uganda ambaotutawapiga mnada hivi karibuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafanya hivyo kwasababu gani, moja, kuhakikisha kwamba tunalinda mifugoya Watanzania isipate magonjwa, mbili, tunalindaWatanzania wasipate magonjwa kupitia mifugo hiyo,tatu;tunalinda pia malisho ya Tanzania, Tanzania haiwezi ikawamalisho ya nchi za kutoka nje, nne, tunahakikisha kwambamigogoro ya wakulima na wafugaji inayochochewa namifugo ya kutoka nje inakwisha, tano, kuhakikisha kwambatunalinda mazingira pamoja na vyanzo vyetu vya majiambavyo vinaharibiwa na makundi makubwa haya yamifugo. (Makofi)

Kwa hiyo basi, watu wanaojaribu kuhusisha…

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa!

MWENYEKITI: Nilishasema hakuna taarifa tena kaachini.

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa hawajachoma…

MWENYEKITI: Nimesema kaa chini.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: ... mahusiano yetu naKenya pamoja na nchi zingine za jirani wanatakiwawazingatie mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna ushirika wa uhalifu.Watu wanaoingiza mifugo kutoka nje ya nchi ni wahalifukwa sababu wamevunja sheria na wale wanaozungumzahivyo ni kwa sababu Waziri wa Mifugo ametangaza. Je, niWatanzania wangapi wamekamatwa Kenya leo wakolockup, wapo wamefungwa kwa kuvunja sheria nani anajuaidadi? Nani anajua Watanzania ambao wako Uganda kwakuvunja sheria leo wako mahabusu, leo wamefungwa nanianajua kuwa Rwanda, Burundi. Hivyo hivyo, mhalifu akijahapa hawezi kutetewa kwa sababu ya ushirika, ushirika wetusiyo wa uhalifu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mashirikiano yetuyanayoendelea katika nchi za Afrika Mashariki ni mazuri mno,ecellent. Mahusiano tuliyonayo na Kenya ni mazuri mno kwasababu mashirikiano yetu ni ya kisheria, mashirikiano naUganda yapo kwa sababu ni ya kisheria. Kukamatwa kwang’ombe hawa ni wavunja sheria haiwezi kuhusishwa naushirika wetu, wanashauriwa wahusika kufuata sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri nilipotangazaoperation hii ya siku saba, Waziri wa Mambo ya Nje alichukuahatua ya kuzijulisha nchi zote kwamba wawaambie watuwao kuondosha mifugo Tanzania kulingana na sheria yao.Ng’ombe wengi waliondolewa, sasa hivi nimesema tunang’ombe 10,000 tunawashikilia ambao tutawapiga mnadahivi karibuni lakini mifugo mingi imeondolewa, wale ambaowamekaidi ukweli tutapiga mnada ng’ombe zao bilahuruma, operation inaendelea na tunaendelea kuwashauriambao hatujawakata waondoe mifugo yao kwa hiari yao.(Makofi)

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge,orodha ya majibu ya Mawaziri nane tumekamilisha, tutakuwana orodha jioni, ataanza Mheshimiwa Mwakyembe, atafuataMheshimiwa Ummy na ataendelea Mheshimiwa Mwijage.

(Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nasitishashughuli za Bunge mpaka saa 11.00 jioni.

(Saa 7.00 Mchana Bunge lilisitishwa hadi Saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alikalia Kiti

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae,Katibu.

NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI- KATIBU WA BUNGE:

HOJA ZA SERIKALI

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifaunaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na

Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikalikwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

KAMATI YA MIPANGO

(Majadiliano yanaendelea)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombatukae.

Waheshimiwa Wabunge, kama tunavyokumbukakwamba katika uchangiaji wetu wa hoja ya MheshimiwaWaziri wa Fedha na Mipango ya kujadili Mpango waMaendeleo ya Taifa, tulishamaliza upande wetu sasatunaendelea na uchangiaji bado, lakini upande wa Serikali.

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Kwa hiyo, tutakuwa na wachangiaji kadhaa halafubaada ya muda siyo mrefu tutamuita Mheshimiwa NaibuWaziri wa Fedha na Mheshimiwa Waziri wa Fedha ambaokwa pamoja watakuwa na saa moja ili kuhitimisha zoezi letu.

Waheshimiwa Wabunge, kwa jinsi hiyo nitaanza namchangiaji wa kwanza ambaye ni Mheshimiwa Dkt. HarrisonMwakyembe atafuatiwa na Mheshimiwa Ummy Mwalimu,Waziri wa Afya.

Mheshimiwa Mwakyembe tafadhali.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana nanaomba nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais kwakuendelea kuniamini kumsaidia kuongoza Wizara hii yaHabari, Utamaduni na Michezo na vilevile kwa kumteuaMbunge kijana, mchapakazi na mwanamichezo hodariMheshimiwa Juliana Daniel Shonza kunisaidia kuongoza hiiWizara.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii naninampongeza sana Waziri wa Fedha na Mipango,Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango na Naibu wakeMheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kwa kazi nzuriwanayoifanya ya weledi mkubwa na katika Wizara hii nyetikatika maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijielekeze kwenyebaadhi tu ya michango iliyogusia Wizara yangu ambayoinahitaji ufafanuzi wa kina kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na madai ya Mbungewa Mbeya Mjini, Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, kwambaMkurugenzi wa Idara ya Habari ambaye vilevile ni Msemajiwa Serikali alitumia kifungu cha 54(1) cha Sheria ya Hudumaza Vyombo vya Habari kulifungia Gazeti la Tanzania Daima,kitu ambacho anasema kwamba siyo sahihi, alichotakiwakufanya si kulifungia gazeti, lakini kuwawajibisha waandishiwaliohusika.

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

Mheshimiwa Mwenyekiti, madai haya ya MheshimiwaMbilinyi yanagusia utekelezaji mzima wa sheria hii mpya, hivyonafikiri kuna umuhimu sana wa kutoa uchambuzi wa kinakidogo kuhusu sheria hii na hapa tulipofika ili tusiendeleekuwachanganya wanaotusikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukumbushane kidogo tukuwa Sheria hii ya Huduma za Vyombo vya Habari tuliipitishawenyewe hapa Bungeni tarehe 5 Novemba, 2016 na tarehe16 Novemba, 2016 Mheshimiwa Rais akaridhia hii sheria natarehe 31 Desemba sheria hii ikaanza kutumika rasmi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kurahisisha na kuwezeshautekelezaji wa sheria hii uende vizuri zaidi ikabidi tutengenezeKanuni na kanuni zenyewe pia zikawa tayari na tarehe 3Februari, 2017 zikaanza kutumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nielezee hiliwanisikilize vizuri hata wadau katika masuala ya habari vizurikwa makini kwamba chini ya sheria hii na kanuni zake kunavyombo vikuu vinne vya kusimamia uendeshaji namaendeleo ya vyombo vya habari hapa nchini ambavyovinatakiwa viundwe. Kwanza ni Independent Media Councilof Tanzania ambalo ni Baraza Huru la Habari ambalolinaundwa na wanahabari wenyewe, lakini ni wanahabariambao ni accredited walishapata ithibati. Chombo cha pilikilichotakiwa kuundwa hapa ni Bodi ya Ithibati yenyewe(Accreditation Board). Kwa sababu tulishakubaliana kwambaUandishi wa Habari sio kitu cha kubahatisha tena ni taaluma.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama zilivyo taaluma zinginelazima kiwepo chombo kinachofuatilia training ya uandishi,weledi wao na nani atambuliwe kuwa mwandishi wa habarindiyo maana tuna chombo hicho kinaitwa chombo chaithibati (Accreditation Board). Tatu ni Kamati ya Kimahakamaya malalamiko ambayo kazi yake kubwa ni kusikilizamalalamiko ya wananchi kama kuna upotofu wa maadili,kama mtu ameonewa na hicho chombo kitakuwa namamlaka kama ya Mahakama, ndiyo maana ukiona

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

hujaridhika unakwenda Mahakama Kuu kudai kwamba hakiyako kwa kweli imefinywa, pengine hukusikilizwa vizuri amakuna uvunjifu wa hizi kanuni tunaita principles of naturaljustice. Kwa hiyo, hicho chombo ni Quasi Judicial Board, nialmost kama Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, chombo cha nne ni Mfukowa Habari ambao kazi yake kubwa ni kuandaa waandishiwa habari vizuri zaidi waweze kupata weledi katika kazi navilevile kufanya utafiti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nasema hayo yotekwamba dhamira ya sheria hii ilikuwa nzuri sana, kuwavyombo hivi vinne vikifanya kazi vizuri kwa kushirikiana, siotu vyenyewe vilevile na Serikali na kwa kuzingatia maadilina sheria za nchi, basi tasnia ya habari ingeweza kujiendeshawenyewe kwa kweli bila mtu yeyote kuvisogelea Vyombovya Habari, hilo ndilo lilikuwa lengo la sheria.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kuna swali limekuwalinaulizwa mpaka kwenye Kamati kwamba, vyombo hivyoulivyovitaja mbona havijaanza kufanya kazi mpaka leo?Ndiyo ni kwa sababu kubwa mbili, sababu kwanzatumeanzisha usajili mpya wa majarida na magazeti yote,tatizo moja ni kwamba hatujapata ushirikiano mzuri kutokakwa wadau wenyewe, tumeahirisha zaidi ya mara tatudeadline ya usajili. Mwisho tumekuja kusajili tarehe 31 Oktobaambazo ni wiki mbili tulizopita na ni robo tu ya majarida namagazeti yaliyoandikishwa. Tumefungua milango wanawezakuendelea kujiandikisha. Kwa hiyo, hatuwezi kupata idadindogo ya wadau hao tukaanzisha vyombo hivi muhimukesho utaambiwa Serikali imelazimisha hivyo vitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili tukumbuke kwambakuna uwepo wa kipindi cha mpito (transition period) katikahii sheria, yote ilitokana na hoja za Wabunge hapa. Wabungewanasema hatuwezi kuwawajibisha waandishi wa habarikwa sababu kazi ya uandishi wa habari ni kazi nzito ya kutafsirimtu amesema nini, anakaa kwenye chumba cha habari,unahitaji elimu at least basic education ambayo tukubaliane

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

hapa. Ndiyo maana wote tukasema tunaiga na nchi zinginekama Uganda ambapo lazima uwe na degree mbili,tukasema lakini hapa angalau uwe na Diploma au Shahadaya Chuo Kikuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungemkasema tuwape miaka mitano tusiwe unfair kawa hawawatu tukatoa miaka mitano, wenzetu wajipange vizuriwaingie ili waweze kuwa accredited kama waandishi wahabari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo yake ni kwambautekelezaji mzima wa uanzishwaji wa vyombo hivi vinneunachelewa mpaka pale wadau wenyewe haitokuwaSerikali, wadau wenyewe walisema pale to speed up, tukotayari hata tukaanzisha kesho Media Council na walewaandishi wenye shahada na wenye diploma wanatoshahao waliopo, tukifanya hivyo kama Serikali itakuwa namgogoro mkubwa. Kwa hiyo, tunasubiri wadau wenyewewatuambie muda umefika tuitekeleze hiyo sheria sasatuepukane na transitional period, hiyo hatuwezi kuamuakama Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana namjibuMheshimiwa Mbilinyi kwamba Mkurugenzi wa Habarihajawahi hata siku moja kulifungia gazeti lolote kwa chiniya sheria hii mpya na wala hajawahi kutumia hicho kifungucha 54. Kifungu cha 54 kinatoa ufafanuzi tu wa kosa lakuchapisha habari za uongo na kuitia jamii katika hofu.Madaraka anayoyazungumzia Mheshimiwa Mbilinyi nimadaraka ya Waziri nilitaka nilieleze hili. Pamoja na sheriahii kuunda vyombo vinne ambavyo vitaweza kabisa kuletapengine nidhamu kama kweli Watanzania tutaamuakutumia vyombo hivi kuheshimu kanuni na maadili ya nchi,kuna kitu kinaitwa residual powers of the government, hizoresidual powers hatujanyanganywa na hii sherianingeshangaa sana tungenyanywa na hii sheria. Duniani koteSerikali lazima iwe na residual powers kuhakikisha kwambainalinda haki za watu wake na pili inalinda usalama wa nchihizo lazima tuwe nazo, hata kama kuna vyombo vingine

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

vinafanya hiyo kazi. Sasa hayo madaraka yamo katika sheriampya katika kifungu cha 59 ndiyo ambayo Waziri anatumia.Ukiona trend ya gazeti toka siku ya kwanza unaionya, siku yapili unaionya, siku ya tatu unamwambia bwana eeh, unaletauchochezi mara ya sita unaonya unasema aah, pengineukapumzike miezi mitatu utafakari vizuri, ndiyo hichotunachofanya ili kulinda mstakabali wa nchi yetu hii.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo hatuyafanyi Tanzaniatu iko dunia nzima na tunafanya kwa kuzingatia matakwaya Mkataba wa Kimataifa tulioingia Watanzania InternationalCovenant on Civil Political Rights ya mwaka 1966, sisi nisignatories dunia yote ni signatories na kila nchi imechukuahayo maudhui yako kwenye Ibara ya 19 ya huu mkataba nasisi tumechukua tumeingiza kwenye Katiba yetu Ibara ya 18na Ibara ya 30 kwamba hata kama una haki, hata kamauna uhuru, uhuru huo lazima uwe na mipaka kwa ajili yamaslahi ya nchi. Mipaka lazima iwepo na hata hii sheriaimeingizwa katika kifungu cha 59 kwamba pamoja nakuwaachia mjiendeshe yanapokuja maslahi ya Taifa,inapokuja kulinda usalama wa nchi, lazima Serikali iwe nasauti hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kitukimoja Mheshimiwa Saada Mkuya naye aliongelea kuhusuujenzi wa mazingira wezeshi ya michezo kuitangaza nchikimataifa. Nampongeza sana Mheshimiwa Saada Mkuya kwakuja na hilo wazo, ni wazo zuri sana. Sasa hivi tunamaliziautengenezaji wa rasimu ya Sera ya Michezo ya Taifa mpya,imefika mbali sana, nina uhakika ndani ya miezi sita tutakuwasera mpya ya michezo hapa Tanzania. Hata kabla hiyo serahaijakamilika tumeshaanza kutekeleza, kuhakikisha kwambatunatumia michezo kuitangaza nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka huu mapematumeweza kuleta timu ambayo iko kwenye Premier Leagueya Uingereza iitwayo Everton, kuja kucheza kwenye uwanjawetu wa kisasa hapa kitendo hicho tu peke yake kimewezakuinyanyua Tanzania katika macho ya ulimwengu na ndiyomaana tukaweza kupata hata ufadhili wa kutengeneza

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

kiwanja chetu upya na nitakabidhiwa nafikiri tarehe 24 namwenzangu Naibu Waziri kikiwa na nyasi ambazo zitakaakwa zaidi ya miaka kumi bila kutusumbua tena ama kupataugojwa wa moyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo asubuhi nimeingiakutoka Arusha baada ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kuniruhusukwenda kufunga michezo ya golf. Naomba nimshukuru tenaMheshimiwa Dkt. Mpango na mwenzake Mheshimiwa Dkt.Ashatu kwa kutoa pesa kuelekeza kwenye mahitaji yabarabara, hii barabara kwenda Arusha imekamilika. Hiishortcut kwenda Arusha nimetoka Arusha saa 11 asubuhinimewahi kipindi asubuhi, hayo ndiyo maendeleoMheshimiwa Mpango hongera sana, Mheshimiwa Kijajihongera sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikwenda Arusha kufungamashindano ya golf ambayo yamevutia wacheza golf wakimataifa wa mataifa 250. Nampongeza sana mwekezaji waArusha ambaye amejenga kiwanja cha golf ni MholanziMtanzania wamejenga kiwanja cha golf cha kisasa kupitavyote katika Afrika ya Mashariki na Kati. Wamekuja wageniwengi na ndiyo maana tumekubaliana na MheshimiwaWaziri wa Utalii hapa tufanye kazi kwa karibu sana kwasababu michezo sasa hivi na utalii vinaenda pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu wote dunianimichezo ya golf inachezwa na matajiri, kwa hiyo, ukivisogezakaribu na mbuga za wanyama unapata watu wazito kweli.Nimepishana tu juzi na mcheza sinema mashughuli waMarekani Harrison Ford amekaa hapo akicheza golf wikinzima, siyo yeye tu wengi wanakuja. Ndiyo maana naombanitoe wito kwa viongozi wenzangu hasa huku kwenye Wilayakama kulikuwa na kiwanja cha golf zamani naombamsivigeuza kuwa magulio, maana kulikuwa na imanikwamba hii michezo ya golf siyo yetu, hapana!

Mheshimiwa Mwenyekiti, kijana aliyeshinda golftournament ya kimataifa ya Arusha jana ni kijana waKitanzania kwa jina la Victor Joseph na ni mwanafunzi, mtoto

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

wa kawaida tu. Unajua hawa vijana ambao hawajawahikucheza golf Mungu amewapa kipaji cha ajabu, anapiga tumara moja anaingia moja kwa moja kwenye shimo utafikiriTiger Woods! Tiger Woods wapo wengi, naomba ndugu zangututenge maeneo kwa ajili ya kujenga viwanja vya kisasavitatusaidia. Ukinipa tu eneo nitatafuta Wawekezaji kamaambavyo tumefanya upande wa Arusha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kusemanaunga mkono hoja hii kwa nguvu kweli. Ahsante sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt. HarrisonMwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa naMichezo. Nakushukuru sana kwa mchango wako.

Waheshimiwa Wabunge, mmemsikia Waziri? Chezenigolf, tatizo hapa Dodoma uwanja wa golf hamna! Tulikuwatuwe na mashindano ya Afrika Mashariki ya Mabunge yotelakini inabidi yahame kwa sababu tu Dodoma hatunauwanja wa golf. Kwa hiyo, hoja yake bado iko pale pale,golf ndiyo mchezo wa watu wa aina yenu. Ahsante sanaMheshimiwa Mwakyembe. (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, nimkaribishe MheshimiwaWaziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na WatotoMheshimiwa Ummy Mwalimu, tafadhali.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nianzekwa kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli,kwa kuniamini kusimamia sekta hii ya afya na maendeleo yajamii, nimhakikishie Mheshimiwa Rais nitashirikiana naMheshimiwa Dkt. Faustine Ndungulile, Naibu Waziri ilikuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya njema na hivyokuweza kushiriki katika kuji letea maendeleo yao namaendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sanaMheshimiwa Dkt. Mpango na Naibu Waziri kwa kazi nzuri

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

wanayofanya katika eneo hili la uchumi na fedha lakini hasakwa kuleta mapendekezo ya mpango wa maendeleo yaTaifa kwa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge kwa maoni na ushauri walioutoahasa katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya nchini,ikiwemo kujenga jamii ya Watanzania inayojali na kuheshimuhaki, ustawi na maendeleo ya wanawake, wazee na watoto.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sasa kujibu baadhiya hoja za Waheshimiwa Wabunge lakini nitajikita sana kwaDada yangu Mheshimiwa Susan Kiwanga. Niliposikilizamchango wake nikasema hivi huyu amesoma huu mpangoau amesoma hajauelewa? Kwa sababu anasema kwambamipango yetu haizingatii mahitaji halisi ya Watanzania.Unasema hivi huyu anazungumzia Watanzania gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua Mheshimiwa Dkt.Mpango ataeleza uhusiano mkubwa sana kati ya ujenzi wauchumi wa viwanda na maendeleo ya watu, ikiwemokuboresha afya, ikiwemo elimu, ikiwemo vijana na kila kitu.Lakini nataka ni-summarize kwa kitu kimoja, maendeleo yawatu, maendeleo ya jamii, msingi wake mkubwa nimaendeleo ya kiuchumi. Dkt. Mpango na timu yako songenimbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua Tanzania yaviwanda ndani ya huu mpango ni halisi. Maana nimesomahotuba yao wanasema Tanzania ya viwanda uhalisia aundoto? Ni uhalisia! Tunasonga mbele wame-panic ndiyomaana sasa wanatafuta sababu zisizo na maana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ndiyo maananasema amesoma? Ukiangalia ukurasa wa 51, MheshimiwaMpango na timu yake wanasema kufunganisha maendeleoya viwanda na maendeleo ya watu, sasa niache nimuoneshekwenye sekta ya afya, wananchi wa Mlimba wanataka nini.(Makofi)

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Mlimbahawataki bora huduma, wanataka huduma bora za afya.Mheshimiwa Mpango katika kitabu hiki anasema kwambakuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba. Huundiyo Mpango! Sasa namshangaa Mheshimiwa SusanKiwanga, kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano haijaingiamadarakani Ifakara walikuwa na fedha za dawa shilingimilioni 19 tu, mwaka jana tumewapa shilingi milioni 120 zadawa, mwaka huu tunawapa shilingi milioni 164, halafuanasema Mpango huu haujazingatia mahitaji ya wananchi.Najiuliza, Dkt. Mpango mimi naunga mkono hoja kwasababu najua hata huko Mlimba, Ifakara tutaongeza fedhazaidi ya hizi ambazo umeweka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili unajiulizaanasema siyo vipaumbele vya Watanzania. Unajiuliza,Watanzania wanataka nini? Watanzania wanataka wotetutibiwe Muhimbili siyo nje ya nchi. Mheshimiwa Dkt. Mpangoanatuonesha hapa kwamba ataboresha huduma zamatibabu ya kibingwa. Ndiyo maana nimesema nikuchanganyikiwa, wanaona tunasonga mbele. Nitoe mfano,Watanzania tutatibiwa Muhimbili, nataka kutoa mfanoHospitali ya Taifa ya Muhimbili pale ICU tumeongeza vitandavya wagonjwa mahututi kutoka 21 mwaka 2015 hadi vitanda75. Tumeongeza vyumba vya upasuaji Muhimbili kutokavyumba 13 hadi vyumba 20. Watu walikuwa wanasubirimiaka miwili kufanyiwa upasuaji. Sasa hivi watu wanasubirimiezi minne na tunategemea kushusha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upasuaji wa watoto,Muhimbili walikuwa wanafanya upasuaji wa watoto 15 kwawiki, sasa hivi wanawafanyia watoto 50 kwa wiki.Mheshimiwa Dkt. Mpango anasema haya ni mapendekezo,nataka kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa. Sasaunasema mpango huu haujazingatia mahitaji halisi yawanananchi. Unajiuliza hivi huyu kweli anazungumzaanachokijua kweli? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kutoa mfanomwingine. Watanzania wanataka nini kama nilivyosema?

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Watanzania wanataka wote wapate huduma za matibabuya kibingwa. Tumeanza, kuna wazazi wana watoto wanamatatizo ya kutosikia, Muhimbili leo wamepandikiza vifaavya kusikia cochlear implants, Mtanzania gani wa kawaidaataweza kutumia shilingi milioni 80 mpaka shilingi milioni 100kwenda China? Lakini Muhimbili watapata Watanzaniawote!

Mheshimiwa Mwenyekiti, habari njema, wasiwewanasema tu, habari njema ni kwamba kabla ya tarehe 30Desemba, tunaanza upandikizaji wa figo. Watanzaniawanataka kuona huduma za matibabu ya kibingwa wotewanapata na siyo wenye fedha, huduma hizi zitapatikananchini, Dkt. Mpango hongera sana nakuunga mkono kwampango huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nani alikuwa anafahamuupasuaji lazima watu wapelekwe India? Jakaya KikweteCardiac Institute ilikuwa inapasua mgonjwa mmoja kwa siku,leo wagonjwa watatu kwa siku. Watanzania wote wanapatahuduma hizi. Haya mambo ni kuanzia mwaka 2016 mpakaleo ndani ya miaka miwili mambo makubwa sanayamefanyika katika kuboresha sekta ya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nilikuwa nasemahivi huyu anasoma nini? Watanzania wengi wanapatamatatizo ya saratani. Zamani unaenda pale Ocean Road,wana vitanda 40 tu kwa ajili ya huduma ya saratani ya maji(chemotherapy) leo kuna vitanda 100, wagonjwa 100wanatibiwa kwa wakati mmoja. Mheshimiwa Dkt. Mpangonashukuru kwamba tunaenda kununua kifaa kinaitwa PETscan kwa ajili ya tiba ya uchunguzi na uchunguzi wamatibabu ya saratani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nashangaa hivihuyu, lakini ninamshukuru sana kaka yangu MheshimiwaBobali ametoa mchango mzuri, jamani wagonjwa wengiwa saratani wanaongezeka. Mna mpango gani wakuongeza elimu? Huu ndiyo mchango ambao ninauona unalengo la kujenga. Siyo mchango wa kusema hakuna

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

vipaumbele. Kaka yangu Bobali nakushukuru sana. Natakakukuhakikishia tutaendelea kutoa elimu juu ya wananchikujikinga na saratani na tulichokifanya sasa hivi, tumeongezapia vituo vya kuwezesha hasa wanawake kwa sababusaratani kubwa inayoongoza ni saratani ya mlango wa kizazikwa asilimia 34 na saratani ya matiti asilimia 12. Kwa hiyo,Serikali ya Awamu ya Tano imeongeza vituo vya kuwezeshawananchi kupima kutoka 343 hadi 443, haya ndiyowanayotaka Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie jambo la mwisho,anazungumzia afya ya mama na mtoto wananchi wanakufa,tunajua. Lakini hivi ukijenga tu majengo ndiyo watuwatapona? Sisi tumejikita kwenye kuboresha kwanzahuduma. Tumesema kama kweli hiki ni kituo cha afyatunakitaka kiwe kituo cha afya na ndiyo maana kupitiaAwamu ya Tano, wakati Mheshimiwa Dkt. Magufuli hajaingiamadarakani, vituo vya afya 500 vya Serikali ni 109 tuvinavyotoa huduma za uzazi za dharura ikiwemo upasuaji.Mwaka wa pili wa Magufuli tunaongeza vituo 170 naWaheshimiwa Wabunge mmepata barua. Hii ndiyo tunataka,lakini kwa nini wanawake wanakufa? Kwa sababu piawanavuja damu, wana upungufu wa damu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. Mpangoanatuambia anataka kuongeza upatikanaji wa dawa nachanjo. Sasa hivi chanjo, dawa za uzazi salama (Oxytoxin)kwa ajili ya kuzuia mwanamke kuvuja damu magnesiumsulphate kwa ajili ya kuzuia kifafa cha mimba na phehol kwaajili ya kuongeza damu zinatolewa bure! Hii ndiyo wananchiwa Mlimba wanataka. Najua Mheshimiwa Jafo ataongeleaujenzi wa zahanati na vituo vya afya, lakini sisi tumejikitahizo huduma zilizokuwepo ziwe ni huduma bora siyo borahuduma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, anasema siyo vipaumbelevya wananchi. Labda Dada yangu Mheshimiwa SusanKiwanga wewe na familia mna hela, lakini Watanzanianikikutwa HIV positive nianze dawa mara moja. TumeanzaSera ya Test and Treat. Mtanzania yeyote atakayepima na

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

kukutwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI anapata dawasiku hiyo hiyo tunamwanzishia, halafu anasema Mpango huuhaujazingatiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza la mwisho,Mheshimiwa Susan Kiwanga; TB kabla Mheshimiwa Magufulihajaingia madarakani kulikuwa na kituo kimoja tu cha kutoamatibabu ya TB sugu, Kibong’oto Hospital. Leo tuna vituo 18ikiwemo Ifakara, ikiwemo Ifakara kituo cha Kibaoni. Halafumtu anauliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa FedhaDkt. Mpango nakuunga mkono kaka yangu, Naibu Wazirina wataalam wote wa sekta ya fedha. Endeleeni, mkisikiawatu wanasema sema wame-panic kwa sababu wanajuaTanzania ya viwanda inafikiwa. Kwangu tukifikia Tanzaniaya viwanda najua maendeleo ya sekta ya afya yanafikiwana Watanzania watakuwa na afya bora na ustawi na hivyokushiriki katika kujiletea maendeleo yao na maendeleo yaTaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa UmmyMwalimu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazeena Watoto, nakushukuru sana kwa mchango wako.

Waheshimiwa Wabunge, mtakumbuka kwa siku nnena nusu sisi tulikuwa tunachambua Mpango, sasa hivitunapata ufafanuzi na mchango zaidi wa Mpango. Kwa hiyo,tutulie tupate mchango sawasawa halafu Waziri mwenyeweatahitimisha. Hawa wengine wote wanachangia mpakasasa. Mheshimiwa Waziri usisahahu alizungumza habari yasaratani zile za akina mama na nini, sasa nikawaza nikasemaasisahau pia na ile saratani ya wanaume sijui inatwa tezi ninisijui ile?

WABUNGE FULANI: Tezi dume.

MWENYEKITI: Mmh, mMaana imekaa pabaya sana ile,

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

usitusahau na sisi. Mheshimiwa Charles Mwijage, Waziri waViwanda, Biashara na Uwekezaji tafadhali. (Makofi/Kicheko)

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru wewe binafsi kwakunipatia fursa ya kuchangia Mpango wa Maendeleo waTaifa kwa mwaka 2018/2019, awali ya yote nitoe shukrani napongezi kwa Mheshimiwa Rais kumaliza miaka miwili nanimshukuru kwa kuendelea kuniamini nipige filimbi ya ujenziwa Tanzania ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Waziri waFedha na Mipango na Naibu wake kwa mpango mzuriambao ninauafiki. Kwa sababu sitaki kufanya kazi yakuwasomea watu, kila Mbunge anapaswa kusoma, nitatoaufafanuzi kidogo juu ya mambo ambayo watu wanayaelewandivyo sivyo.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kukariridhima ya mpango wa pili wa miaka mitano. Dhima yampango wa pili wa miaka mitano ni ujenzi wa uchumi waviwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleoya watu. Rafiki yangu Mheshimiwa Ummy amezungumziamaendeleo ya watu ambayo yanajikita kwenye elimu,yanajikita kwenye afya, yanajikita kwenye kipato. Sasamageuzi ya kiuchumi, huu mpango ambao nauunga mkononi sehemu ya ule mpango mrefu wa miaka mitano ambayonaiunga mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda tunavyovilenga,nimesikia hoja watu hawajajua mpaka leo viwandatunavyovijenga. Sitaki kuwasomea watu lakini kwa faida,viko viwanda vya makundi manne na vyotetumevishughulikia. Kundi la kwanza ni viwandavinavyochakata mazao au malighafi ya wananchi, katikakuhamasisha ni jukumu la viongozi wote na wananchi wote,ninapopiga filimbi nawategemea na ninyi WaheshimiwaWabunge tuendelee kuhamasisha zile malighafi tuzijengeeviwanda.

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Kundi la pili ni viwanda ambavyo vinaajiri watuwengi. Yupo Mheshimiwa Mbunge ameniambia kwa niniusilete viwanda vya teknolojia ya juu, hapana! Watanzaniawote hawawezi kuendesha mitambo ya teknolojia ya Juu,Watanzania wote hawawezi kuendesha LNG Plant, kwa hiyo,nitaendelea kutengeneza viwanda vinavyoajiri walio wengiili kusudi wale wenzangu na mimi ambao waliishia darasala saba na darasa la kumi waweze kutumika pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kundi la tatu ni viwandaambavyo malighafi zake, bidhaa zinazozalishwa zinatumikasana. Katika kundi hili tumefanya vizuri sana katika viwandaambavyo nilianzisha. Tuna uwezo uliosimikwa wa kuzalishasaruji tani milioni 10.8, tunatumia mahitaji yetu tani milioni4.87 kwa hiyo tuna uwezo wa kuzalisha kuliko ambavyotunahitaji kama nchi. Tuna mahitaji sasa ya kujenga viwandavya tani milioni 10 Sinoma Tanga lakini kuna viwanda vinakujaChalinze, Mamba na mwenzake Nyati wanaweka viwandavya tani milioni tatu pale. Kwenye hiyo industry ya bidhaazinazotumika sana tumefanya vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kundi la nne ni kutumiamalighafi ambazo tumepewa faida na Mwenyezi Mungu yakipekee ndiyo inaangukia suala la viwanda vya mboleainayotumia gesi. Niwaeleze Waheshimiwa Wabungemmelizungumza, Ferrostaal ameshapewa clear line naWizara ya Nishati kwamba atengeneze mbolea. HELM yaMtwara na ninyi njooni mjadiliane tuko tayari mzalishembolea. Tunapojenga Bagamoyo Special Economic Zoneviwanda 190 kiwanda kimojawapo kitakuwa chakutengeneza mbolea. Kwa hiyo, hivyo ndivyo viwandatunavyoshughulikia. Sasa uhamasishaji ni jukumu lako miminikiwa nimetangulia kusudi tujenge Tanzania ya viwanda.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio tuliofanikiwa,tumepata mafanikio. Fanikio moja kila Mtanzania sasaanaimba viwanda. Nchi yote watu wanaimba viwanda nanil if ikir ia wakati huo nitoe dhana ya isiyokuwa.Unapozungumza Watanzania, kwa mfano viongozi

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

tunazungumza Watanzania kuanzia ngazi ya kwanza ngaziya juu, ndiyo maana mimi kiwanda kidogo hata vyerehanivinne naendelea kusema ni viwanda vidogo. Kwa hiyo,usijitambue wewe nafasi yako kwa sababu unazo, lazimatuwalee Watanzania wadogo mpaka wale Watanzaniawakubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa faida ya yule aliyeulizaswali, viwanda vidogo sana vinaajiri mtu mmoja mpakawanne na capital yake ni shilingi milioni tano. Cherehaniindustrial kinauzwa shil ingi milioni 3.5 na kinawezakukutengeneza kipato cha kukutosha wewe na familia yako.Vipo viwanda vidogo vinaajiri watu watano mpaka 49 namtaji wake ni shilingi milioni tano mpaka shilingi milioni 200.Hivi ndiyo vile viwanda vya kuchakata nyanya, viwanda vyapilipili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna viwanda vya kativinaajiri watu 50 mpaka 99, vinaanzia shilingi milioni 200mpaka shilingi milioni 800. Kuna viwanda vikubwa milioni800 na vinaajiri watu 100 na kwenda zaidi. Hiyo ndiyo naihubirikwa Watanzania walio wengi. Nikienda kwa wale wenyenazo; kiwanda kidogo wanasema ni shilingi bilioni mbili lakinitunahimiza viwanda vidogo na ukisoma Mpango waMheshimiwa Mpango anakuambia SIDO itapewa kipaumbelecha kuongoza katika ujenzi wa viwanda, kwa sababutunatambua kwamba wananchi walio wengi watawezakupata faida kwa kushiriki katika kuchakata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaeleze WaheshimiwaWabunge katika ujenzi wa viwanda sekta inayoongoza niya uchakataji (manufacturing) wanaita mediating sector,tunataka tuwalee Watanzania watoke katika uchuuziwawekeze katika kuchakata katika kutengeneza viwanda.Pale ulipo, uangalie zile factor zinazokuwezesha uwezekwenda mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma ule mpango wa piliwa miaka mitano nafasi ya sekta binafsi ndiyo mhimili kwahiyo msitegemee Serikali ihamasishe, sekta binafsi ihamasishe,

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

ni jukumu lenu ni jukumu langu na sekta binafsi ndiyo itafanyahayo mambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala ambalokuna watu wamedokeza nawaheshimu sana rafiki zangu,nitawapiga taratibu. Watu wanasema kwamba Serikalihaina mahusiano mazuri na sekta binafsi. Hamna taarifa,Serikali inakutana na sekta binafsi na jana wanaosikiliza taarifaza kiingereza katika kipindi cha This Week In Perspectivewamesema wenyewe watu wa Tanzania Private Sectorwaliokuwa pale kwamba mahusiano ni mazuri sana mpakaMheshimiwa Rais anawaita wafanyabiashara anazungumzanao. Ila ni kwamba kuna paradigm shift, mamboyamebadilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatengeneza viwanda ilimoja; tutengeneze ajira, tunatengeneza ajira, mbili; tuzalishebidhaa zenye ubora kusudi tuweze kutosheleza mahitaji yaWatanzania na kuuza nje. Lakini tunatengeneza uchumi waviwanda na viwanda ku-broaden ile tax base. Mwisho yotehaya mawili ukiyatengeneza utakwenda vizuri. Lakini mwisholazima umuone Mzee wa mpango uweze kumpa chochote.Kilicho cha Yesu mpe Yesu na cha Kaisari mpe Kaisari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie masualamaalum. Limezungumzwa suala la Mchuchuma na Liganga.Amezungumza Mheshimiwa Mpango, Mchuchuma naLiganga naisimamia mimi na ni suala la muda. Ile sheriamliyoibadilisha Bungeni ya kuhusu rasilimali zetu tupate kiasigani inahusu Mchuchuma na Liganga. Nikishamaliza mamboyangu, mwekezaji tayari ana pesa ya fidia anaanza nakuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la EPZA watuwanasema tunatumia utaratibu ambao hautumiki dunianyingine, ndiyo! Mambo mengi tunayofanya Tanzaniahayatumiki sehemu nyingine, kama la kuwakoromea walewatu wa makinikia, Marais wachache wanawezakuwakoromea, kwa hiyo, kuna mambo ni ya kwetu kwetutu! (Kicheko/Makofi)

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachofanyika kwenyeEPZA, tumekubaliana na wawekezaji wa Bagamoyo wajewalipe fidia tutengeneze ile Bagamoyo Special EconomicZone. Bagamoyo Sepcial Economic Zone Januari inaanza nanitatengeneza viwanda 190 kwa kuanzia. Tutaharakishaviwanda hivi mwaka 2020 viwe vimeanza. Mwaka 2020 kunashughuli lazima nihakikishe kwamba viwanda vile vipo ilikusudi niweze kuonesha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee. Suala linginespecific la uhusiano kati ya sekta ya kilimo na viwanda.Waheshimiwa Wabunge, Serikali (mimi ndiyo napiga filimbi)lakini siwezi kufanya kazi bila kilimo, bila mifugo, bila TAMISEMI,bila miundombinu na miundombinu wezeshi ndiyo maananahitaji umeme, nahitaji maji, nahitaji reli, nahitaji barabara.Ukijumlisha hayo ndiyo yanaitwa uchumi wa viwanda halafumimi nakuja najenga viwanda.

Kwa hiyo, wanaosubiri milingoti ya viwanda ukionareli inajengwa, viwanda vinakuja. Ukiona mabomba ya majiviwanda vinakuja, ukiona umeme unavutwa viwandavinakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ndiyo mahusiano.Serikali ihakikishe upatikanaji wa soko la mazao. Hapa ndipokuna kazi. Nimei-position kwa maelekezo ya MheshimiwaWaziri, nai-position Wizara yangu. Wizara yangu imepewamandate mpya ya kuhakikisha tunatafuta masoko yamazao, yawe kilimo, yawe wapi ni kazi yangu mpya katikahii awamu mpya kuhakikisha ninapata soko la mazao nanitatoa mwongozo zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda vyakuchakata mazao nimelizungumzia katika zile sekta tatu,watu wanauliza mbona nyama haijazungumzwa? Katikamazao ya wananchi mifugo ni mazao ya wananchi ndiyoviwanda category number one. Viwanda vya mbolea vyaFerrostaal na HELM nimevizungumzia ni kiasi cha kusubirivinakuja.

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhamasishaji nimezungumzani jukumu la sisi wote. Viwanda vilivyokufa tunavifufua nahakuna mjadala. Atakayeshindwa ampe mwenzake natunahakikisha suala hilo tunalifikiria. Ukisoma Vision 2020inaelezea kwa nini tulishindwa lakini ukisoma Mpango wa Piliunakueleza kwa nini hatutashindwa. Import substitution comeexport promotion ni mojawapo ya hatua nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie sekta ya sukarina nizungumze kuhusu Mheshimiwa Mchengerwa. Walewawekezaji wako watatu siku zao zimehesabiwa, hatutakiwatu kuatamia maeneo ya ardhi. Tutashirikiana Wizara yaArdhi na ile ya Kilimo kuhakikisha kwamba tunazalisha sukariya kutosha. Watu wa SADC wametusaidia kupata uwezo wakuzalisha sukari bila kuingiliwa. Tanzania tuna uwezo wakuzalisha tani milioni mbili kwa mwaka kwa kutumia mabondeyetu yote yaliyopo. Mheshimiwa Rais alipokuwa Kageraametoa ultimatum kwa wenye viwanda waongeze uzalishajina hilo mimi nalisimamia. Kwa hiyo, msiwe na wasiwasitutazalisha sukari lakini uzuri wa sukari uzalishaji wa sukariunatengeneza ajira nyingi. Kwa hiyo, Kigoma kwetu kulenitapeleka viwanda viwili kusudi watu wa Kigoma badala yakwenda mbali mkate miwa kwenu na mambo yawanyokee.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utendaji wa Wizaranimeshazungumzia naipanga upya, lakini jukumu la SIDOkwenye mpango ndiyo inatangulia na niwaambie naanzana Mkoa wa Geita, Katavi, Simiyu, kote huko naweka ma-shade mpya. Kwa hiyo, nataka kuwaonesha tunatengenezashade, dada tulia na Kagera nitaweka, tunatengenezashade ambazo mtu unachakata unakwenda pale, ma-shadeninayokujanayo ni mapya, unapewa shade, unafundishwana namna ya kuchakata, ukihitimu unatoka na kitu chako.Ni miaka miwili, mwaka wa tatu mtaona wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitambue mchango waMheshimiwa Saada. Na mimi nitazungumza na counterpartwangu wa Zanzibar namna ya kuweza kuchakata ile karafuukuiongezea ubora. Napenda kutumia fursa hii kuwaambia

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

kwamba watumie wataalam wangu, SIDO tutaiongezeauwezo iweze kufanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nizungumziemchango wa Mheshimiwa Mbowe, aliyezungumza kwambahatuna sera na kwamba tutengeneze sera moja, huwezikutengeneza sera moja, sera zote zilizopo ni nzuri. Ile mnayoiitafast tracking ni kuharakisha na fast tracking strategy maanayake ni nini, ni kuondoa vikwazo. Tunayo hiyo na tunayo blueprint ambayo ukisoma Easy of Doing Business tuko poorlyranked, sasa kwa sababu tuko poorly ranked tumejitambuasisi tukatengeneza blue print, ile blue print ndiyo inakwambiakasoro yako, usichelewe kutoa kibali, nenda kalipe kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale wanaposematumepimwa vibaya hata kutolipa kodi wazungu wanatuonani kasoro. Kwa hiyo, kama mnasema Easy of Doing Businesstunarudi nyuma ni kwa sababu watu hawalipi kodi. Sasahuwezi kunihukumu Mwijage eti nimerudi nyuma kwenye Easyof Doing Business ni kwa sababu watu hawakulipa kodi. Hawawatu nitaendelea kuwabembeleza mimi kusudi walipe kodiniendelee kupata ranking nzuri. Kwa hiyo, mikakati iliyopo nimizuri ila kama mtu anataka nije nimsomeshe, nimwelekezetaratibu, mikakati ile inatosha na niwahakikishie Tanzania sasatuko kwenye viwanda, siyo kwamba tutajenga viwanda.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache,naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha,tutakwenda vizuri, Mpango uko vizuri. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa CharlesMwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.Nikupongeze sana kwa kazi kubwa mnayoifanya.

Waheshimiwa Wabunge, kwenye hil i eneonilipowasikia baadhi ya Wabunge, iko shida kidogoMheshimiwa Waziri wa Fedha kwa maoni yangu lakini,kwamba baadhi ya watu wanaangalia Industrial Policy kamani Factory Policy yaani viwanda vinachukuliwa kama ni

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

factories kitu ambacho siyo sawa. Mtu akijenga shule yamsingi ni industry, mtu akijenga ya sekondari, akijenga chuokile ni kiwanda na ukiniuliza kinazalisha nini, jibu lake liko wazikabisa. Mtu akijenga hoteli ni kiwanda, kina wafanyakazi,kinalipa kodi, ile ni service industry, it is a hotel industry. Mtuakijenga hospitali kubwa kile ni kiwanda. Kina mashine humondani za bei mbaya kuliko hicho kiwanda unachosema wewekiwanda, kiwe ni cha karanga, kiwe ni cha korosho, mashinemoja tu ni shughuli. (Makofi)

Wakati yule mzee aliyeanzisha wazo na kuendeshaApollo Hospital in India, wakati huo Serikali ya India ilikuwaimeanzisha sera kama yetu ya viwanda na Wizara ya Fedhaikawa na mfuko maalum wa viwanda. Kwa hiyo, wakapelekamaombi yao ya kujenga hospitali kwa kukopa kwenye mfukowa viwanda. Serikali ya India ikamjibu huwezi kukopa kwenyemfuko wa viwanda kwa sababu hospitali siyo kiwanda.Wakafanya juhudi kubadilisha ile sheria yao, ikakubalikwamba hata hospitali ni kiwanda. Leo hii Apollo peke yakewana chain of hospitals zaidi ya 50, dunia nzima tunaendakutibiwa huko na ni utalii mkubwa wa medical tourism nakadhalika. Kwa hiyo, hata sisi huu mtazamo wetu tuutazamekwa upana huo kuliko kuutazama kwa Kongwa kuna factorygani peke yake, tuangalie katika programu hiyo ya industry.Ahsante sana. (Makofi)

Tunaendelea na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Mheshimiwa Selemani Said Jafo.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali yayote, napenda sana kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetupanguvu na uzima kwa kuweza kuhakikisha tunachangiamchango huu. Nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kunipadhamana na kuniamini kuweza kuhudumu tena katika ofisiyake nikiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Raiskwamba sitamuangusha na nitazidi kumuomba MwenyeziMungu siku zote aweze kunipa nguvu na uzima. (Makofi)

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sana kumshukurukaka yangu Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Fedhana Mipango na dada yangu, Naibu Waziri, kwanza kwa kazikubwa wanayofanya. Leo hii tunajadili Mpango, lakini mimikatika ofisi ninayoiongoza naomba kutoa shukrani za dhatisana kwa Wizara ya Fedha kwa kazi kubwa inayofanya nanishukuru kwa sababu imeendelea kuiwezesha ofisi yangukwa kipindi chote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mjadala huu waMpango wetu, kikubwa zaidi ni kuangalia j insi ganitutamwezesha mwananchi wa kawaida kuweza kukuzauchumi wake. Mpango wetu wa Taifa unaeleza dhahiri kabisakuhusu chombo ambacho kiko katika ofisi yangu,tumekianzisha mwaka huu kiitwacho TARURA. Malengo yetuni kwamba ikifika mwaka 2020 tuwe na mabadilikomakubwa sana katika suala zima la miundombinu ambayohiyo itawawezesha wananchi kukuza uchumi wao kupitiamalighafi au mazao yanayozalishwa katika maeneo yao.Nishukuru ofisi hii kwa jinsi ilivyojipanga kwa sababu katikamwaka huu wa fedha peke yake takribani shilingi bilioni 573tutazielekeza katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa bila kuwana mipango mizuri, mambo hayo hayawezi yakafanyika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kwa kiwangokikubwa, nikijielekeza katika sekta ya elimu ambayonimesikitika sana kwa sababu nimeona baadhi ya Wabungewenzetu humu ndani wengine wakibeza jambo hili kubwasana lil i loanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tano lakuwawezesha Watanzania masikini kwa kuwa na programuya elimu ambayo inagharamiwa na Serikali, lakini wenginewalikuwa wakisema maneno ya kebehi kabisa kama hakunachochote kilichofanyika. Kwa kweli, kwa dhati kabisa nawezakusema hii si haki hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiangalia katika chain yetuhii tunavyozungumza hivi sasa, tujipime sisi tuko humu ndaniya mamlaka Mwenyezi Mungu ametupa fursa tumeingiahumu Bungeni, lakini tuwaangalie Watanzania hao wadogo-

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

wadogo ambao hali yao ni tete, ni taabani, hata ilegharama ya kulipia certificate ya form four wengine walikuwawanashindwa. Leo hii programu ya elimu bure ambayotakribani shilingi bilioni 18.77 zimekuwa zinatoka, sasa hivitakribani shilingi bilioni 23 kila mwezi zinatoka, halafu kamaMbunge anasimama humu ndani anabeza kabisa kwambahakuna lolote, nadhani tuna sababu ya kufanyiwa tathminisisi wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, angalia kazi kubwailiyofanyika. Ninyi mnafahamu kipindi kirefu tumesema shulezetu za Serikali hazifanyi vizuri, leo hii Wizara ya Fedha naWizara ya Elimu kwa ujumla wetu katika suala zima lauwekezaji mkubwa tunaofanya katika sekta ya elimu, shulekongwe takribani 89 zote tunaziboresha ziweze kutoamazingira ya ushindani. Mpaka sasa tunaenda takribani shule43 ambazo hali yake ilikuwa ni hoi bin taabani. Shule hizitunabadilisha miundombinu yake lengo kubwa iwe nimiundombinu wezeshi. Katika Mpango huu unaokujatunaangalia ni jinsi gani tunaenda kukamilisha shule hizinyingine tupate shule 89 ambazo zitakuwa na level ya kisasa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe WaheshimiwaWabunge, wakati mwingine tupate fursa tutembeleemazingira yetu kuangalia tulipoanzia na wapi tunakokwenda.Nendeni Mpwapwa, Msalato, Mzumbe kwenye hizi shuleambazo Serikali imefanya investiment kubwa ya fedha zaSerikali karibu shil ingi bil ioni moja kila shule. Miminimewaambia wazi kwamba lengo letu ni kuhakikisha elimuyetu inarudi katika mstari unaokubalika na haiwezi kurudi bilakuweka mipango na mipango yenyewe ndiyo hiiinayojadiliwa humu ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme bahati nzuriMheshimiwa Mwenyekiti wewe unafahamu shule yetu yaMpwapwa zamani ilikuwa imechoka kabisa, leo hii ukifikaMpwapwa unashangaa hii shule ya aina gani! NendaMsalato hapa watoto walikuwa wakifika shuleni wiki mojamtoto anatamani aende nyumbani. Tumeenda na Kamati

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

ya Bunge kutembelea tumekuta watoto 580 wamekataakwenda likizo wote wame-register kwamba watabaki shulenikwa sababu wanasema sasa hivi tumekaa shule kama tukokatika hoteli. Hii yote ni investiment kubwa inayofanywa naSerikali. Leo Mheshimiwa Mpango amekuja na Mpango wajinsi ya kuboresha ili suala la elimu liende mbele zaidi. Naombaniseme wazi, tuwe wazalendo katika kuangalia jinsi ganitunafanya nchi yetu iende mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimesikia na bahatinzuri dada yangu Mheshimiwa Ummy Mwalimu, alizungumzakatika suala zima la sekta ya afya, kumbukeni huko tulikotokana sasa hivi tukoje. Ukiachia bajeti ya dawa MheshimiwaUmmy amezungumza, lakini ajenda ya miundombinu, ninyiwenyewe mnafahamu huko tulikotoka leo hii kupitia fedhaza World Bank, fedha za ndani na fedha kutoka Canadatunafanya investment kubwa katika nchi hii kwa mara yakwanza haijawahi kutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni tumepatakaribu shilingi bilioni 10 fedha za ziada kutokana na mipangomizuri ya Serikali, mpaka donors countries wanaridhika nautendaji wa Serikali ya Tanzania. Hivi sasa tuna-scale up hiyoprogramu, tunaenda karibu vituo 216 kutoka 172, hii ni kazikubwa inayofanyika, lakini kazi hii maana yake ni jinsi ganiSerikali imejipanga kutekelza majukumu yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba miminimpongeze Mheshimiwa Mpango, ndugu yangu usikatetamaa. Wakati mwingine safari yoyote ukiona unapigiwakelele ujue kwamba safari hiyo inaenda vizuri, chapa kazikaka na sisi tuko nyuma yako tunaenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwaambieWatanzania, Mpango wetu katika suala zima lamiundombinu, bahati nzuri juzi-juzi tulikuwa kule MwanzaWorld Bank wanatusaidia suala zima la uboreshaji wa miji hiiTanzania. Ukienda Mbeya, Tanga, Arusha na miji yote mikuutumefanya mabadiliko makubwa, lakini Manispaa zetutunafanya uwekezaji mkubwa wa kujenga barabara za lami,

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

kuweka taa na kujenga madampo ya kisasa. Mpango huuunaokuja sasa hivi unaangalia ni jinsi gani tunaenda ku-scaleup hiyo programu yetu ili kuhakikisha Miji, Halmashauri namaeneo mbalimbali yanaimarika katika miundombinu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo yote ni kutokana nasera nzuri ya Serikali inavyofanya resource mobilization nawadau wetu wanaridhika kwamba kazi zinakwenda. Juzitukiwa Mwanza, World Bank imetoa extension ya mradi wetuwa UGLSP, badala ya kuishia mwaka 2018 sasa wame-extendmpaka 2020, hii ni faraja kubwa kwa Serikali ya Tanzania.(Makofi)

Kwa hiyo, jukumu letu kubwa ni lazima tuwewazalendo tuone tulikotoka, tulipo na tunakokwenda. Kweli,unaweza ukatoa mawazo lakini siyo kukashifu kwambahakuna jambo linalofanyika. Ingekuwa nchi nyingine kamaWabunge tungesema wapi kuna gap kidogo turekebishetwende mbele zaidi, lakini sio kukashifu kama hakunakinachopatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri nimesikiaWabunge wengine walikuwa wakibeza hata suala zima lauchumi wa viwanda. Nimshukuru sana kaka yanguMheshimiwa Mwijage amefanya kazi kubwa sana na mimi niWizara wezeshi ya kumwezesha kaka yangu MheshimiwaMwijage instrument yake ifanyike vizuri. Leo hii MheshimiwaMwijage na Rais anahangaika ili tuhakikishe tunajengaviwanda ili watoto waweze kupata ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana mimi nikiwamwenye mamlaka na Serikali za Mitaa, juzi juzi wakatitunawaapisha Wakuu wa Mikoa niliwapa target nikasemaMheshimiwa Mwijage anahangaika na viwanda, lazimakama Wakuu wa Mikoa, leo katika bajeti yetu ya mwaka wafedha 2017/2018, bajeti ya own source ni karibu shilingi bilioni61.5. A unit plants ya kiwanda cha kawaida cha kubanguakorosho, ukienda Newala, Masasi, ukienda SIDO wanakupatiakiwanda cha shilingi milioni 10. Kiwanda cha kukamua mafuta

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

ya alizeti hapa Singida, uliza zile mashine SIDO zinauzwa kiasigani, average ni kati ya shilingi milioni mbili na nusu mpakamilioni sita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, own source yangu ambayoipo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa, shilingi bilioni 61, hatakama unit plants ya kiwanda kidogo ukiweka shilingi milioni10 ni sawasawa na viwanda 6,100, ni beyond expectationya viwanda 2,600 kwa mwaka. Hivi vitu ni just calculation, isjust about numbers. Kwa hiyo, sisi kama Wabunge wetu lengoletu kubwa ni jinsi gani tuna-play ile leadership position, katikamamlaka zetu jinsi gani tutafanya sasa kuhakikisha tunawekauwekezaji mkubwa tunaboresha viwanda vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana Waziri waViwanda na Biashara, juzi wakati tunazindua operation yaviwanda 100, Naibu Waziri pale alitoa sera pana sana yaviwanda. Bahati nzuri mama mwenye Mifuko ya Uwezeshaji,dada yangu Mheshimiwa Jenista Mhagama, ana mifuko 17,tumetoa fursa jinsi gani tutafanya kama Watanzania kwaajenda ya viwanda ambayo ipo, tukiungana kwa pamojatunatoka. Tatizo kubwa kuna watu wengine hawataki hilijambo lifanikiwe kwa sababu watasema kuwa Ilani yaChama cha Mapinduzi imefanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba niwaambietunaenda kushinda ushindi mkubwa kwa mafanikiomakubwa. Kikubwa zaidi kaka yangu Mheshimiwa Mpangochukua yale maoni mazuri ya Wajumbe humu, tuyaweke vizurituone jinsi gani tutasonga mbele Mpango wetu uive vizuri.Nikuhakikishie, kwa Mpango huu na juhudi ya Serikaliinavyokwenda na naomba niwahakikishie Wizara zoteambapo Wizara yangu ndiyo inakumbatia mambo mengineyote, Wizara wezeshi, tutashirikiana kwa kadriiwezekananavyo Mpango huu na mambo mengine yaendevizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matamanio yangumakubwa wafike watu nchi jirani waje Tanzania kuja kujifunzakupitia kwetu. Kuna watu wengine wanaona kwamba eti

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

kufanya ufahari kwamba lazima uende kwenye kujifunza,hapana tufike muda Tanzania lazima tuache legacy nchi yetu.Leo hii tumepata mfano katika mradi wetu wa DARTunaoendelea Dar es Salaam tumeshinda katika majiji duniani.Mwezi wa pili tunaenda New York, Marekani kuchukua tuzomaalum ni Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoenda katika sualazima la utengenezaji wa barabara za mwendo kasi awamusita tumemaliza awamu moja lakini awamu hizo zote ndizoziko ndani ya Mpango ambao leo hii ndiyo MheshimiwaMpango anau-submit hapa. Si muda mrefu sana tunaendakuhakikisha tunatekeleza mradi wa barabara ya Kilwa -Mbagala - Gongo la Mboto. Lengo ni kulifanya Jiji letu la Dares Salaam na maeneo mengine yawe rafiki kwa ajili ya sualazima la kujenga uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii Tanzania tumepataufahari mkubwa, takribani nchi sita na wengine mpaka leowanazidi kuomba kupitia kwetu TAMISEMI waje Tanzaniakujifunza mipango mizuri ya utekelezaji wa miradi yetu. Hayayote yanataka sisi Wabunge ambao ni decision makersambao tunawawakilisha wananchi hapa tufanye maamuzimazuri, tushirikiane na Serikali, pale penye upungufutuboreshe vizuri zaidi nini tufanye ili tuifikishe nchi yetu mahalisalama ambapo Watanzania watajivunia kwambawamepata viongozi ambao wako humu na wamekujakufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya maisha yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika haya yote naombaniseme wazi kwamba tunaenda vizuri. Kikubwa zaiditutaboresha kwa michango mizuri ya WaheshimiwaWabunge ndiyo maana ya Bunge lazima Wabunge watoemaoni, maoni yale yakikusanywa tunatengeneza Mpangomzuri lakini Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nikuhakikishiekwamba Tanzania ikifika mwaka 2020 kuna watu mpakawengine wataogopa kugombea humu ndani. Wasipoogopakugombea basi lazima wata-join na watu ambao wanauhakika wa kushinda, election is not a numbers. Kama

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

tunaenda katika utaratibu huu mzuri naomba niwaambiehakuna mashaka lazima tutafika mahali muafaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya niliyoyazungumza,naomba niseme wazi kwamba kama Wabunge tuunganekwa pamoja, tujenge uzalendo wa nchi yetu, tuhakikishe jinsigani tunafanya na tuweke maslahi ya wananchi mbele.Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, ubariki Mpangohuu, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Aah, leo iko kazi hapa. Huyu niMheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoana Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Selemani Said Jafo. (Makofi)

Sasa twende kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, na mimi naomba nimshukuru sana MheshimiwaRais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuniamini mimipamoja na Naibu wangu, Mheshimiwa Antony Mavundelakini vilevile kwa kututeulia Mheshimiwa Stella Ikupa, jembela nguvu kushirikiana na sisi katika kuhakikisha kwambatunamsaidia Mheshimiwa Rais katika majukumu aliyotupatia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa dhati nimshukuru sanaMheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania. Mheshimiwa Waziri Mkuu amekuwa ni kielelezo chautendaji bora wa Serikali ya Awamu ya Tano katika kusimamiamajukumu makubwa ambayo hayataki mtu aambiwe aonekazi inayofanywa na Serikali hii. Pia namshukuru MheshimiwaWaziri Mkuu pia kwa kutulea vizuri sisi Mawaziri ambao tupokatika Ofisi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuunakutakia kila la kheri na hasa pale unaposhughulika namaswali ya Waziri Mkuu hapa Bungeni umeonyesha kabisa

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

kwamba wewe ni kiongozi wetu Mawaziri wote. Nakushukuruna nakupongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuunga mkonohoja ya Mheshimiwa Dkt. Mpango. Dkt. Mpango naombanikuthibitishie usikate tamaa. Wanaouponda Mpango wakowana ajenda binafsi. Dkt. Mpango chukua mawazo mazuriya Wabunge waliotushauri sisi kwa pamoja kama Serikali,Mawaziri wote pamoja na wewe lakini yale mawazo ambayokwa dhahiri unaona yanaponda Mpango wako kwa nia ovuachana nayo. Hasa Wabunge wa CCM wamechangiamawazo mazuri sana kwenye Mpango wa Serikali yao.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wachangiaji hapawanasema Serikali yetu inakurupuka tu, inakuja hapahaijajipanga, haifanyi utafiti na inapanga mipango tuambayo haieleweki. Naomba niwaambie hao wanaosemahivyo hawajasoma Mpango wala hawajaangalia mwongozoulioletwa pamoja Mpango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kwenye sektamoja tu ya ajira, hivi unafikiaje mahali pa kujua hitaji la ajirakatika nchi yetu ya Tanzania bila kufanya utafiti nakutengeneza mpango. Leo nitawaambia, Serikali yetuinafanya utafiti na ndio inakuja na mwongozo na inakujampango. Kwa mfano, sisi tumeshafanya utafiti wa kujuanguvu kazi iliyopo katika nchi yetu ya Tanzania ni idadi ganiya Watanzania na fedha za utafiti zimetolewa naMheshimiwa Dkt. Mpango ili awe na mpango mzuri wa ajirakatika nchi ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utafiti huotumegundua Watanzania milioni 25 ndiyo nguvu kazi ya nchiyetu ya Tanzania na tunapozungumzia viwanda hawa milioni25 ndiyo watakaokwenda kuchukua ajira kwenye viwandahivyo ambavyo vitajengwa kwenye nchi yetu ya Tanzania.Nani anasema Serikali hii inakuja na mipango bila kufanyautafiti, tunafanya utafiti. Katika hiyo milioni 25 tumegunduaasilimia 56 ni vijana. (Makofi)

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tumefanya utafitimwingine, sasa kama tunataka kushughulikia tatizo la ajira,hivi ukosefu wa ajira kwa vijana katika nchi yetu ya Tanzaniaukoje. Tumegundua kwamba ukosefu wa ajira kwa vijanakwenye nchi yetu ya Tanzania unazidi kupungua, ulikuwaasilimia 11.7 sasa hivi ni asilimia 10.3 na ni kwa sababu yamipango mizuri ya Serikali na sekta nyingi za uzalishajizinavyoongezeka na upungufu wa ajira unazidi kupungua.Hiyo ndiyo mipango inayogharamiwa na Waziri wa Fedhana Mipango katika nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumegundua sekta ya kilimondiyo inayoongeza katika kutoa ajira nyingi kwenye nchi yetuya Tanzania na tumegundua asilimia 60.7 kilimo kinaongozakatika kutoa ajira. Sasa tunapofanya hivi ndipotunapowaambia Watanzania baada ya utafiti huotumemwagiza Mheshimiwa Mwijage aanzishe viwanda lakiniviwanda vitakavyotumia malighafi ya kilimo inayolimwandani ya nchi ya Tanzania ili tutatue tatizo la ajira kwa vijanawa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesema MheshimiwaMwijage kwa kushirikiana na sekta hizo nyingine zote zaumeme, maji na kadhalika atusaidie kutengeneza sera zaviwanda unazozizungumza wewe Mheshimiwa Mwenyekitiiwe ni hospitali, gereji au kitu chochote, hivyo vyote niviwanda vinatofautiana ukubwa na mazingira. Akifanyahivyo viwanda hivi vitazalisha bidhaa ambazo ndizozinazohitajika zaidi katika soko la Watanzania hapa nchinina hivyo mwisho wa siku tutakuwa tumeweza kutatua tatizola ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa tumeshafanyanini? Ili kuhakikisha vijana wa Tanzania wanaajiriwa,tumetengeneza programu maalum ya kukuza ujuzi katikanchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitasema mafanikioyaliyopatikana, kwa kutumia Mpango huu wanaoupondawa Mheshimiwa Mpango tumefanya yafuatayo:-

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, tumetambua nakurasimisha ujuzi wa vijana wa Tanzania mpaka sasa 3,900wameshamaliza mafunzo ya ujuzi katika nchi yetu, 3,440wanaendelea na mafunzo na vijana 13,432tumeshawatambua wanasubiri tuwafundishe. Sasa nanianayesimama hapa na anasema eti huu mpango fakewakati unajibu mahitaji ya Watanzania. Hawa vijana ambaotumewapa ujuzi wengine wanatoka mpaka kwenye Majimboya wapinzani, watawashangaa Wabunge wao kamahawaungi mkono Mpango huu ambao umewapa ujuzi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunao graduates wengikatika nchi yetu ya Tanzania lakini wamekosa mafunzo yavitendo ya kukuza ujuzi wao. Tumeshatengeneza programuya internship ya kuwasaidia vijana wa Kitanzania wakapateuzoefu na inalipiwa na Serikali kwa fedha za MheshimiwaMpango Waziri wa Fedha. Vijana 2,122 wameshaomba naSerikali inawapangia utaratibu wa kwenda kwenye mafunzoya vitendo, hela yote inatolewa na Mpango na iko kwenyeMpango wetu. Nataka kuwaambia Watanzania kwambatunafanya kazi na Serikali yetu inafanya kazi sana tena kwakupitia Mpango ambao unaletwa na Mheshimiwa Mpangondani ya Bunge la Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ni machache tuningeweza kusema mengi, lakini muda tu hauniruhusu.Napenda sana nizungumze jambo lingine hapa kuhusumwenendo wa shughuli za Bunge. Wabunge hapa na hasaWabunge wa Upinzani wamelidhalilisha sana Bunge lako etiBunge hili halifanyi kazi yake sawa sawa, linaingiliwa naSerikali na halina tija yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme, Ibara ya 62na nakupongeza sana wewe, Naibu Spika na Wenyeviti wotewa Bunge, ndiyo iliyokuweka wewe na Bunge lako hili Tukufuna sio mtu. Hata hivyo, unapimaje tija ya Bunge, hupimi tijaya Bunge kwa kelele nyingi ndani ya Bunge, hupimi tija yaBunge kwa kuleta fujo na kupambana na askari ndani yaBunge, hapana. Hupimi tija ya Bunge eti kwa kufunga

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

midomo ndani ya Bunge kwa plasta na kuvaa nguo nyeusi,hapana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti,…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri nakuongezea muda,kwa hiyo, endelea vizuri, endelea Mheshimiwa Waziri. (Makofi/Kicheko)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, naomba niseme unapima tija ya Bunge kwanamna Bunge linavyoongoza shughuli za Bunge na shughulizinazojadiliwa ndani ya Bunge zina manufaa kwa kiasi ganikwa Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni nani Mbunge hapaatakayesimama ambaye hatashukuru na kupongeza kazikubwa iliyofanywa na Wabunge wa Bunge la Kumi na Moja?Niwaombe Wabunge wenzangu na hasa Wabunge waChama cha Mapinduzi, bebeni ajenda ya mafanikiomakubwa ya Bunge letu ndiyo itakayotuvusha mwaka 2020.(Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mifano, wewemwenyewe umedhihirisha kwa mifano dhahiri kabisakwamba Bunge hili limefanya kazi itakayokumbukwa na vizazivyote katika nchi ya Tanzania. Umeunda Kamati hapakwenye Bunge hilihili la Kumi na Moja ambayo imewezakuisaidia Serikali kuweka mfumo wa kupata faida ya nchikwenye madini ya vito katika nchi yetu ya Tanzania. Leo hiiMbunge anapata wapi courage na kusema Bunge hili halifai,halijawa na mvuto, halifanyi kazi zake linavyotakiwa! Mbungegani huyo? Leo nitawaeleza Watanzania. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Mwenyekiti, Bunge lako hili limeweka historia ya kutungasheria ya kuhifadhi maliasili za nchi yetu ya Tanzania, ni Bungehili la Kumi na Moja chini ya uongozi wako Mheshimiwa JobNdugai na siyo mtu mwingine yeyote. Leo hii Wabungewanapata wapi courage ya kulibeza Bunge hili badala yakujisifia na kwamba ni kazi nzuri tuliyoifanya ambayo piainaendana mipango mizuri ya Serikali yetu ya Awamu ya Tano.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili limetunga sheriaya Msaada wa Sheria kwa Watanzania watakaohitajikusaidiwa kwenye masuala ya sheria hata wanyonge kwenyemaeneo ya vijijini, ni Bunge hili la Kumi na Moja. NimesemaWaheshimiwa Wabunge wenzangu tabia ya kulibeza Bungeletu na mwenendo mzima wa Bunge siyo tabia njema.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitamalizia la mwisho kwaufupi sana, wakati tunachangia humu ndani na hasa Kiongoziwa Upinzani alipokuwa anachangia humu ndani alitakakupotosha umma na kutaka kuyajadili madaraka yaMheshimiwa Rais ya uteuzi wa viongozi eti kwamba anafanyauteuzi huo kwa upendeleo, hapana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 36(1), (2), (3) na (4)inatoa mamlaka kwa Rais kuanzisha na kufuta nafasi zamadaraka ya namna mbalimbali katika utumishi ndani yanchi yetu ya Tanzania. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, Ibara hiyo haisemi Rais atakapokuwa anafanyauteuzi eti aangalie ukanda, haisemi hivyo Ibara yetu kwenyeKatiba. Ibara hiyo haisemi Rais anavyoandaa na kufanyauteuzi aangalie makabila mbalimbali kwenye nchi yaTanzania, haisemi hivyo hiyo Ibara. Ibara hii haisemi Raisatakapokuwa anafanya uteuzi eti aangalie rangi ya

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

Mtanzania, haisemi hivyo. Unasimamaje ndani ya Bungekuhoji uteuzi wa Mheshimiwa Rais wa nafasi ambazoamepewa Kikatiba, ni upotoshaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme unaonawateule wa Mheshimiwa Rais wanafanya kazi vizuri.Ameteuliwa hapa Mheshimiwa Mwanri kutoka Siha na niMkuu wa Mkoa wa Tabora, anafanya kazi nzuri sana.Ameteuliwa Mheshimiwa Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa waManyara, anafanya kazi vizuri sana. Ameteuliwa hapa Mamayetu, Mama Anne Kilango jembe la nguvu kutoka Sameanafanya kazi nzuri sana. Nina orodha ndefu nikiisema hapani ndefu kweli, lakini uteuzi huo unafuata madaraka yakikatiba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe sanaWabunge wenzangu tusiingilie madaraka ya Rais aliyopewakwa mujibu wa katiba. Anayafanya kwa utashi wa hali yajuu na ukiangalia Ibara ya 34 inamtaka ateue watuwatakaowajibika kumsaidia kubeba dhamana kwa niabayake yeye mwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwakuniongezea muda na baada ya kusema hayo, naungamkono hoja iliyopo mbele yetu asilimia mia moja, nakushukurusana. (Makofi)

MWENYEKITI: Huyo ni Waziri wa Nchi, Ofisi yaMheshimiwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Jenista JoakimMhagama. Kwa wasiofahamu huyu naye ni Seneta pia,ameingia hapa mwaka 2000 mpaka leo miaka mingapi nahajatoka yaani mfululizo. Wengine hapa wapita njia kipindikimoja tu hamrudi hapa halafu mnazomeazomea Maseneta.Kwa hiyo, tujitahidi na sisi tukirudi mara mbili, mara tatu basisasa ndiyo tunaruhusiwa kusemasema hovyo kidogo. (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, tulipokaa siku ile yamwanzo ya kuchangia Mpango niliwatia moyo sananikawaambia Wabunge fungukeni, zungumzeni habari ya

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Mpango wa Maendeleo. Sasa watoa hoja nao wanakujahapa mbele na mimi niwaombe sasa fungukeni na ninyi zamuyenu kufunguka hapa msije mkasema ilikuwa upande mmoja,sasa nasawazisha goli. Kwa hiyo, karibu sana MheshimiwaNaibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. AshatuKijaji, nakupa nusu saa uchangie. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nianze kwa kumshukuru MwenyeziMungu aliyetuwezesha kufika siku hii ya tano ya mjadala huumuhimu sana kwa maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, napenda na miminimshukuru Mheshimiwa Rais wetu kwa kuendelea kuniaminina kuniacha katika nafasi hii ya Naibu Waziri wa Fedha naMipango ili niweze kuendelea kumsaidia Mheshimiwa Waziripamoja na yeye Mheshimiwa Rais wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia nikushukuruwewe kaka yangu Job Ndugai kwa kazi nzuri ambayounaendelea kuifanya ya kuendesha Bunge letu Tukufu. Kwakweli hongera sana kaka yangu, Mwenyezi Mungu azidikukubariki ili tuweze kuifanya kazi hii tuliyoaminiwa na Taifaletu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia niwapongezeWaheshimiwa Wabunge wa Bunge lako Tukufu kwamichango yao mizuri ambayo wametupatia sisi kama Wizaraya Fedha ili kuboresha Mapendekezo ya Mpango natunapokuja mwezi wa Machi/Aprili na Mpango kamili tuwezekuja na Mpango ambao upo imara. Ninaamini wote kwapamoja wametimiza wajibu wao Kikatiba wa nini walitakiwakufanya na niwapongeze sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Wizaratumeyachukua yote, mimi na Mheshimiwa Waziri hatuwezikujibu michango yote ya Wabunge zaidi ya 100 waliochangiakwa siku 5. Tutazungumzia machache ili tuweze kuendeleambele kwenda kuandaa Mpango wetu.

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa uniruhusunianze kuchangia hoja hii iliyowekwa Mezani na MheshimiwaWaziri wa Fedha na Mipango, kaka yangu, Mheshimiwa PhilipIsdor Mpango. Nianze kwa kukupongeza Mheshimiwa Waziriwa Fedha, kazi yako ni njema sana, kazi yako ni nzuri naimeonekana ndiyo maana Mheshimiwa Rais ameendeleakukuamini, hongera sana kaka yangu, simama hivyo hivyo.(Makofi)

Sisi watumishi tulio chini yako wewe ndani ya Wizaraya Fedha na Mipango tunajivunia kufanya kazi na wewe.Kwa wale ambao walikuwa hawajui uchumi sasawanaufahamu uchumi ndani ya Wizara ya Fedha,nikupongeze sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kwanza ambayonapenda kuitolea ufafanuzi ni hoja ambayo ilisema Serikaliione umuhimu wa kufanya malipo ya wakandarasi ambaowametekeleza miradi mbalimbali ndani ya Taifa letu. Serikaliyetu ya Awamu ya Tano inatambua sana umuhimu wa kazizinazofanywa na wakandarasi, lakini pia umuhimu wakuwalipa malipo yao kwa muda mwafaka ili wawezekuendelea kufanya kazi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa2016/2017 Serikali imeweza kufanya malipo ya shilingi bilioni3,358.89 kwa ajili ya wakandarasi, kati ya hizo, shilingi bilioni1,321.47 zililipwa kama madeni ya wakandarasi waliojengabarabara zetu. Tunalipa lakini la muhimu kama ambavyotumeendelea kusisitiza lazima uhakiki ufanywe ili tujiridhishenini tunalipa kama Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya kiasi hicho nilichotaja,shilingi bilioni 1,161.32 kililipwa kwa ajili ya Mfuko wa Reli. Kamaambavyo Serikali yetu imedhamiria kuboresha miundombinundani ya Taifa letu na tumeanza kulipa, shilingi bilioni 204.90zililipwa kwa ajili ya Mfuko wa Maji kwa wakandarasi wetuambao wamefanya kazi ndani ya Wizara ya Maji. Mwenyekitihili ulilisema na Waheshimiwa Wabunge walilisema kwa wingikwamba Mheshimiwa Waziri haangalii ni maswali yapi

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

ambayo yakiulizwa wanasimama Waheshimiwa Wabungewangapi. Sasa hili naomba kulidhihirishia Bunge lako Tukufukwamba kama Serikali tumekuwa tukilipa na shilingi bilioni204 zimelipwa kwa mwaka 2016/2017. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo pialimepigiwa kelele na kama Serikali tunaendelea kulipa nanimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Nishati, amesemavizuri na ametoa order nzuri sana na kwa mwaka 2016/2017tulilipa shilingi bilioni 537.95 kwa ajili ya Mfuko wa UmemeVijijini kuhakikisha vijiji vyetu vyote vinapatiwa umeme wakutosha. Shil ingi bil ioni 133.24 tuli l ipa wakandarasiwalioshughulika na miradi ya viwanja vya ndege. Tumesikiakelele nyingi zikipigwa kwa ajili ya shilingi bilioni 39 tu, hapana,tumelipa zaidi ya hizo kwa sababu zilikuwa ndani ya bajetiyetu ya mwaka husika. Kwa hiyo, nilidhihirishie Bunge lakoTukufu kwamba tumekuwa tukifanya malipo haya kwa ajiliya wakandarasi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika robo ya kwanza yamwaka huu wa 2018/2019 tumelipa pia shilingi bilioni 562.29kwa robo ya kwanza tu kwa wakandarasi wanaohusika namiradi mbalimbali ndani ya Serikali yetu. Kwa hiyo, natakakusema kwamba dhamira ya Serikali yetu ni njema sanakatika kuhakikisha kwamba watu wote wanaofanya kazi naSerikali yetu wanalipwa malipo yao yale wanayostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jambo hili,liliongelewa pia suala la Serikali kuchukua kodi ya majengona ni kiasi gani ambacho tumeweza kukusanya kwaMamlaka ya Mapato na hili aliliongelea vizuri sana kakayangu Mheshimiwa Lubeleje.

Napenda kusema kwamba katika ukusanyaji wa Kodiya Mapato nil iambie Bunge lako Tukufu kwambahatukunyang’anya Halmashauri zetu chanzo chake chamapato. Nasema hivyo kwa sababu moja kubwa, dhamiraya Serikali ya kuchukua chanzo hiki ilikuwa ni kuongeza ufanisiwake ili sasa tuone ni jinsi gani tutaweza kuzirejesha pesa hizikatika Halmshauri zetu. Kwa mwaka 2016/2017 kwa

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

Halmashauri 30 tu tumeweza kukusanya shilingi bilioni 34.09ukilinganisha na shilingi bilioni 28 ambazo zilikusanywa naHalmashauri husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema dhamira ilikuwa nikuongeza ufanisi na ufanisi tumeuongeza zaidi ya asilimia 20lakini ukiangalia Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianzakukusanya kodi hii mwezi Oktoba. Kwa hiyo, nilidhihirishieBunge lako Tukufu kwamba kwa mwaka huu ambaotumeanza tangu mwezi Julai, mapato yetu kutoka Kodi yaMajengo yatakuwa ni mazuri sana. Mifumo yetu imekamilika,tumeanza kufanya kazi kwa umakini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo lilikuwalinaulizwa kuhusu hili ni kwamba zimerejeshwa kiasi gani?Kama nilivyosema, dhamira kuu ilikuwa kuongeza ufanisi lakinikuhakikisha pesa hizi zinarejea kwa wananchi kwendakufanya kazi. Baada ya kuzikusanya shilingi bilioni 34.09 pesazote zilirejeshwa kulingana na bajeti za Halmashauri zetukama Sheria yetu ya Fedha tuliyopitisha ilivyotuelekeza. Kwahiyo, katika hili pia napenda kulieleza Bunge lako Tukufukwamba hayo ndiyo mambo ambayo Serikali yetu ya Awamuya Tano inayafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ambayonapenda kuitolea ufafanuzi ilikuwa ni kuhusu Serikali kutoungamkono sekta binafsi kwa kuwa Mapendekezo ya Mpangohayaongelei sekta hiyo wala kuainisha miradi ambayo Serikaliitashirikiana na sekta binafsi katika kuitekeleza. Nimshukurusana Mheshimiwa Waziri wa Viwanda amelielezea suala hililakini pia niwaombe Waheshimiwa Wabunge ni muhimuwanapokuja kuchangia wawe wamepitia Mpango kuanziapage ya kwanza mpaka ya mwisho kuliko kuja kutuhumubila kuwa na facts wakizifahamu. Hilo ni jambo la msingisana. Nilichoki-note, watu wanasoma hotuba ya MheshimiwaWaziri halafu wanakuja kuchangia Bungeni, hapana, hotubaya Mheshimiwa Waziri ni summary ya kitabu kizima chaMapendekezo ya Mpango, kwa hiyo wakipitie kwa umakini.(Makofi)

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivi?Nasema hivi kwa sababu ndani ya Mapendekezo ya Mpangowa Maendeleo wa mwaka 2018/2019 tumeainisha sektabinafsi itahusika na miradi ipi na katika awamu ipi.Tumeonesha waziwazi kabisa ukurasa wa 26 hadi 28 waMapendekezo ya Mpango, tumeonesha sekta binafsiilivyoshirikiana na Serikali kutekeleza bajeti yetu ya 2017/2018.Tukatoka hapo, ukurasa wa 58 hadi 59 tukaainisha sasa kwahaya Mapendekezo ya Mpango tunayokwenda nayo,Mpango wetu unaokuja tunataka sekta binafsi ishiriki katikamiradi ipi. Kwa hiyo, ndiyo maana nimesema wawewanapitia kitabu kile tulichokileta Bungeni kwa ajili ya kujadilihili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu kwa kutambuaumuhimu wa sekta binafsi katika kuleta maendeleo,hatukuishia tu kuainisha baadhi ya miradi lakini tumekwendambele na kuainisha na mikakati ni jinsi gani sekta binafsi naSerikali zitashirikiana ili tuweze kufanya kazi pamoja. Kwa hiyo,niombe sana hilo lifanyike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika hoja hiyoliliongelewa pia suala zima la kwa nini Serikali inawekezakwenye miradi mikubwa ya maendeleo ikatolewa mfanomradi wa reli yetu ya kati (Standard Gauge Railway),ukatolewa mfano pia mradi wa Stiegler’s Gorge kwa ajili yakuzalisha nishati ya umeme. Katika hili, naomba niseme jambomoja, ipo katika dunia nzima katika uchumi kwa nchi ambazozimeendelea na sisi tunaendelea kuendelea, miradi hii yamiundombinu huwa ina sifa zake kuu tatu au nne ambazondizo zinazotoa mwelekeo kwamba ni nani atawekeza katikamiradi ya miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe WaheshimiwaWabunge hasa waliosema katika jambo hili, waendewakasome The Economics of Infrastructure Projects ili wawezekuelewa. Katika economics of infrastructure projects,Maprofesa wabobezi wa uchumi wanasema miradi yote yamiundombinu ambayo ni ya kimkakati duniani kote huwa inahatua zake tatu. Hatua ya kwanza, huwa ni planning phase,

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

hatua ya pili huwa ni construction na hatua ya tatu huwa nioperation. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika planning phasewabobezi wa uchumi wanasema miradi hii, naomba ku-quote, sifa moja katika planning phase ni nini kilichopo.Wanasema; many strategic infrastructure projects generatecash flows after many years, and the initial phase of this projectis subject to high risks. Hii ina maana kwamba miradi yetu hiiya miundombinu ya kimkakati katika initial phase huwa inarisk kubwa sana na risks hizi hakuna kampuni yoyote ya binafsiambayo iko tayari kuchukua risk hii katika initial phase yamiradi hii. Ndicho ambacho Serikali yetu imeona nini chakufanya, lazima uoneshe nia wewe kama Serikali. Tunaihitajimiradi hii, tunahitaji Standard Gauge Railway, nani wakuwekeza kwa sifa hizi, hayupo, except the government itself.Katika hili, tumeanza vizuri na imeanza Serikali yetu at theinitial phase, the planning phase, we planned, sasa hivi tukokwenye construction phase, tunafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sifa ya pili ya miradi hii yakimkakati, hasa ya miundombinu, wachumi wabobeziwanasema; even though the direct payoffs to an owner ofan infrastructure project may cover its costs, the indirectexternalities include beneficial for the economy as a whole.Nini maana yake? Inamaanisha kwamba sawa gharamazake ni kubwa na risks zake ni kubwa lakini miradi hii yamiundombinu ina faida nje ya ile sekta husika. Sasa hivitulikuwa tukilalamika mahindi yanayozalishwa Sumbawangahayawezi kusafiri, Serikali ime-invest kwenye miundombinu yabarabara sasa mahindi yetu yanaweza kusafiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kaka yangu MheshimiwaLubeleje, amelalamika asubuhi kwamba mahindi kule kwakeMpwapwa hayapo. Kwa infrastructure zilizowekezwa naSerikali ndugu zangu wa Mpwapwa watapata mahindi kwabei nafuu. Ndiyo maana ya Serikali kuwekeza katikainfrastructure projects kubwa kama standard gauge katikainitial phase na construction phase lazima Serikali iwekemkono wake. (Makofi)

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida hizi ni kubwa kamanilivyosema. Kwa hiyo, la msingi, tunapokwenda kwenyeoperational phase ambapo sasa tayari miradi hii itaanza ku-generate revenue, cash flow inaingia, ndipo utakapoyaonamakampuni binafsi yanaingia ili sasa kuweka mabehewamazuri kwa ajili ya kusafirisha wananchi wetu na bidhaa zao.Hakuna kampuni au mfanyabiashara ambaye anakujakuwekeza akijua ataishi yeye, atakufa, ataishi mtoto wakeatakufa halafu awekeze mtaji, hilo halipo. Ni Serikali tu kwasababu ya faida pana ya mradi husika kwenye uchumi,tunataka kujenga nini, uchumi wa viwanda, bila standardgauge hatuna uchumi wa viwanda. Ndiyo maana Serikaliyetu imefanya hicho ambacho tumekifanya. NiwaombeWaheshimiwa Wabunge waendelee kutu-support ili tuwezekufanya kazi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala hilo, naunganakabisa asilimia 100 na kaka yangu, Mheshimiwa Bashe,aliposema economics is not a rocket science, we agree ahundred percent. Economics is not a rocket science buteconomics is a social science, you need to understand theagency you are dealing with, the behavioral economics,unafanya kazi na watu gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wifi yangu anasema nirudie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema naungana naMheshimiwa Bashe aliposema economics is not a rocketscience, that’s quite right lakini economics is a social science,unahitaji nini, unahitaji kuelewa the social actors you aredealing with. Unakaa chini unaendelea kusubiri Stiegler’sGorge tangu alivyouanzisha Mheshimiwa Baba wa Taifa letu,Mwalimu Nyerere mpaka leo hakuna mwekezaji aliyejitokeza.(Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nasikia kelelehuko, hebu tutulie tusikilize yaani huyu ni mwalimu waMzumbe University. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Waziri, endelea.

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii Serikali imeanzakuwekeza Stiegler’s Gorge, tutakapoanza initial phase, theconstruction phase, operational phase, tutapata wawekezajina uchumi wetu utaruka, that’s where now the rocket sciencewill come, not at the initial phase. Niwaombe sana na miminapenda kusema katika jambo hili sababu tunayo, niatunayo, dhamira tunayo na uwezo tunao wa kuwekezakatika miradi mikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema dhamira tunayo,sababu tunayo na uwezo tunao kwa sababu bado hatujafikaasilimia zaidi ya 40 ya kukopa kwa ajili ya maendeleo yaWatanzania. Tukope, tuwekeze ili Watanzania wafikiwe namaendeleo kule walipo. Kama tungekuwa tunakopa nakulipana posho tungeweza kuogopa, lakini tunakopatunawekeza kwenye standard gauge tusafirishe bidhaa zetu.Tunakopa tuwekeze kwenye Stiegler’s Gorge tuzalisheumeme wa kutosha viwanda vya shemeji yangu, MheshimiwaMwijage, vifanye kazi, hatuna sababu ya kuogopa.Mheshimiwa Waziri wa Fedha, niko na wewe nitafanya kazipamoja na wewe katika jambo hili, naamini hilo limeeleweka.(Makofi)

MBUNGE FULANI: Kabisa.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, sasa niende kwenye hoja nyingine ambayoilisemwa na Kambi Rasmi ya Upinzani, wakasema kwambaSerikali inafanya matumizi ya fedha ambazo hazikuidhinishwana Bunge kinyume na utaratibu wa Sheria ya Fedha yaMatumizi ya Umma ya 2011. Napenda kwanza kukanushahiki kilichosemwa na Watanzania wafahamu Serikali yao yaAwamu ya Tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduziiko makini katika kutekeleza sheria zake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatujafanya jambo hilo,hata siku moja. Kitu ambacho wanasahau ndugu zetu hawa

Page 197: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

na kuja kudanganya wananchi, Mheshimiwa Waziri wa Fedhakapewa mamlaka ya kufanya uhamisho kutoka kifungukimoja kwenda kwenye kifungu kingine, amepewa hiyodhamana. Mheshimiwa Silinde, sikiliza nikufundishe uchumi.(Makofi)

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha amepewa hayomamlaka, anayo mamlaka, labda kama mnataka kumpokalakini anayo hayo mamlaka. (Makofi)

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Anafanyareallocation kutoka kifungu kimoja kwenda kifungu kinginendani ya bajeti ya Serikali iliyopitishwa na Bunge lako.

MWENYEKITI: Mbona hasimami huyo anayetaka kutoataarifa basi? Mheshimiwa Naibu Waziri, hebu kidogo tumpenafasi, kuna binti mmoja wa Kisukuma hapa anataka kukupataarifa.

T A A R I F A

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Ningependa kumpataarifa mzungumzaji Mheshimiwa Naibu Waziri kwambaaliyetuambia pesa za standard gauge hatujakopa niMheshimiwa Rais mwenyewe. Kwa hiyo, siyo Upinzani ndiyotumepotosha, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania John Pombe Magufuli alihutubia akasema pesaza standard gauge hatujakopa ni pesa za ndani. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa sitaruhusu tena taarifa kwa sababutaarifa iliyotolewa yaani haieleweki kabisa. Naibu Wazirianachoeleza ni kwamba kuhamisha mafungu Mheshimiwa

Page 198: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

Waziri wa Fedha ana mamlaka hayo anasimamaMheshimiwa Mbunge anaongea mengine. MheshimiwaNaibu hebu endelea (Kicheko/Makofi)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru, naomba nim-quote kaka yanguJafo alivyosema wanaanza kupata kiwewe kwamba hawezikutukamata wapi tunakwenda. Hii speed siyo ya kawaidahakuna wa kutusogelea ndugu zangu. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee kutoadarasa, Sheria ya Bajeti kifungu cha 48 kinampa mamlakahiyo Waziri wa Fedha, kikisomwa pamoja na Kanuni zake,Kanuni ya 26(1) inamwelekeza Mheshimiwa Waziri wa Fedhanini cha kufanya. Kanuni ya 26(2) inamwelekeza awezekufanya reallocation kwa kiwango gani, ndicho ambachoamekuwa akifanya Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Serikaliyetu haijawahi kutumia fedha hizi nje ya bajeti iliyopitishwana Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hiyo inaunganishwa nanaona ndicho wanachokitafuta lakini wanashindwa kufika,kwamba Serikali sasa ilete Bungeni adjustment ya bajeti kwasababu wamesahau mamlaka haya ya Waziri. Naombaniseme jambo moja, nini maana ya bajeti ya nyongeza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhamisha kifungu hiki,kupeleka kifungu hiki siyo bajeti ya nyongeza ndugu zangu.Maana ya bajeti ya nyongeza ni kwamba Serikali ndani yamwaka husika imekusanya mapato ya ziada ambayohayakupitishwa na Bunge lako Tukufu na sasa inatakakuyafanyia matumizi. Hiyo ndiyo bajeti ya nyongeza ambayoMheshimiwa Waziri wa Fedha kama anataka kutumia hayomapato ya ziada tutalazimika kuja kwenye Bunge lako lakinikwa reallocation of funds between votes tunatakiwa tutunapokuja hapa katika mid year review tu-report ninitumefanya, wala siyo kuleta bajeti ya ziada, hatuna bajetiya ziada ndugu zangu. Tuko ndani ya bajeti iliyopitishwa naBunge, ndani ya matumizi husika, tunatumia katika miradiyetu ya kipaumbele ndani ya Serikali yetu. (Makofi)

Page 199: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri tukawa na uelewawa pamoja wa Sheria tunazopitisha sisi wenyewe halafutunaposimama tuseme kwa Watanzania nini Serikali inafanyakwa niaba yao. Hilo ni jambo la msingi sana nilitaka kuliombaBunge lako Tukufu tukubaliane na hiki ambacho kiko ndaniya Sheria iliyopitishwa na Bunge lako Tukufu na siyo kuja hapana kuwadanganya Watanzania kwamba Mheshimiwa Raisanatoa order, hawezi kutoa order bila kujua hiyo pesa ipona ilipitishwa na Bunge lako Tukufu. Hilo ni jambo la msingisana katika utekelezaji wa shughuli za Serikali yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ambayoiliongelewa kwa uchungu na kwa sauti kali ilikuwa nikwamba Mipango ya Maendeleo ya mwaka 2016/2017, 2017/2018 na 2018/2019 yote inafanana. Nianze kwa kukuombakwamba tuwe tunapitia vitabu hivi ili tuweze kujua lakinitusisahau msingi wa mipango hii mitatu na sasa tumebakishamipango mingine miwili ni Mpango wa Pili wa Maendeleowa miaka mitano. Mpango wa Pili wa Maendeleo wa MiakaMitano ndiyo unatupa sisi base ya miradi ipi itekelezwe, kwakiwango kipi na imeelekezwa kabisa. Ukichukua Mpango ulewa Miaka Mitano mimi nausoma vizuri sana na baada yakusikia hili nilienda nikarudia kusoma mara mbili, mara tatukuna nini? Nikagundua miradi mingi iliyopo kwenye Mpangowa wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano inatekelezwakwa kipindi cha kuanzia miaka mitatu mpaka mitano, ninimaana yake? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016/2017 tuliletamradi ule ukiwa katika initial phase, mwaka 2017/2018tumeleta mradi ule katika hatua zake za mwanzo zautekelezaji, mwaka 2018/2019 tunaleta sasa wapi tumefikabaada ya kufika nusu ya utekelezaji wa Mpango waMaendeleo wa miaka mitano, miradi ni ile ile. Tofauti ya miradihii inayoripotiwa ni utekelezaji wake hatua moja kwendahatua nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tukianza ku-crashmiradi ambayo ipo kwenye Mipango yetu ya Maendeleo yamwaka mmoja tunawambia nini Watanzania? Hatukuwa

Page 200: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

makini kupitisha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa MiakaMitano kwa sababu hakuna sehemu Waziri wangu wa Fedhaanaweza kwenda kuchukua mradi ambao hauko kwenyeMpango wa Pili wa Maendeleo.

Kwa hiyo, lazima tulifahamu hilo, twende tusomecontent of the document not what the Minister has presentedin the Parliament, tutapata content na tutaelewa sasa wapitupo na miaka mwili inayobaki nini tutafanya, je, tutawezakutimiza kile tulichodhamiria? Hicho ndicho kilichopo,ukisoma tu bila kubeba jicho la planning ndani ya mipangohii utagundua hatuna utofauti ndani ya mipango yetu lakiniukiweka jicho la planning (the planners) utaona nini kilichopondani ya mipango yetu na wapi tunaelekea sasa katikakuhakikisha Tanzania ya viwanda tunaifikia kabla ya mwaka2020. Dhamira yetu ni moja tu, kabla ya mwaka 2025 tunahitajikuona Watanzania wenye kipato cha kati, kabla ya mwaka2020 tunadhamiria kuona Watanzania wa Tanzania yaviwanda, hilo ndiyo jambo la msingi na ndiyo kazitunayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayaniseme jambo lingine ndogo ambalo liliongelewa katika ileile hoja ya kupotosha Watanzania na nini Serikali yetuinafanya. Ilikuwa ni hoja kwamba Serikali imeendeleakudharau mamlaka ya Bunge lako Tukufu kwa kuacha kuletasheria ya kusimamia mipango tunayopitisha ndani ya Bungelako. Naomba kusema Serikali yetu ni sikivu sana hasa Serikaliya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na MheshimiwaJohn Pombe Magufuli. Ni Serikali sikivu sana na hatuna ujanjahuo wa kulidharau Bunge lako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kusema kwamba,katika hili turejee kwenye Sheria ya Bajeti Na.11 ya mwaka2015, kwa nini ilitungwa Sheria ya Bajeti, ni kusimamiamipango na bajeti tunayopitisha humu ndani. Tunahitaji sherianyingine ipi na kufanya lipi? Pia kwa kila mwaka tunaAppropriation Act kwa ajili ya kusimamia matumizi yaMpango tunaojadili leo, sasa tunahitaji sheria nyingine kufanyanini? Hatuhitaji sheria nyingine. Tunayo Sheria ya Bajeti na

Page 201: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

tunayo Appropriation Act ya kila siku. Sheria ya Bajetiinatuwezesha kubainisha kisheria majukumu na mipaka yakiutendaji ya wahusika wakuu katika mchakato mzima wakibajeti na kimpango. Sheria ya Bajeti inaweka uwiano katiya mipango yetu, mapato yetu na matumizi yetu, tunahitajisheria nyingine ya kufanya nini? Sheria ya Bajeti pia inawezakutueleza na sisi tukatambua mzunguko wa kisheria wakibajeti nini kilichopo, tungekaa tukaisoma vizuri walatusingefika sehemu ya kuja na personal issues za kumtuhumuWaziri wa Fedha hata siku moja, turejee tu kwenye sheriatunazozipitisha sisi wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,naomba nikushukuru kwa kupata nafasi hii. Kama nilivyosemamwanzo yako mengi tutayafanyia kazi kwa umakini yote kwapamoja na tutakuja na Mpango unaoakisi mapendekezomazuri yaliyotolewa na Wabunge hasa wa Chama changu,Chama cha Mapinduzi walioongea mengi kwa ajili yakuboresha Mpango wetu. Yale machache ya upande wapili tutayachukua yale mazuri, yale mabaya naombatuyaache humu humu tunapotoka tutoke na ushirikiano wetuna udugu wetu ili tuweze kutekeleza azma ya Serikali yetu naHapa Kazi Tu itafanikiwa. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Wapo rafiki zangu upande huu walikuwawanamwangalia kma vile hawamfahamu Dkt. Ashatu Kijajikwamba alaa, kumbe ana uwezo wa kujieleza kiasi hicho.Kanikumbusha miaka ya 70 palikuwa na bendi moja sijuiilikuwa inaitwa Mangelepa, sijui bendi gani, palikuwa nawimbo unaitwa sindano ya moto, leo Mheshimiwa amekuwasindano ya moto. Ahsante sana Mheshimiwa kwapresentation hiyo, hiyo shule ambaye hakuelewa basi tenajamani, ahsante sana. Katibu. (Kicheko)

NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE:Kamati ya Mpango sasa imemaliza kazi yake.

MWENYEKITI: Bunge sasa linarejea.

(Bunge lilirudia)

Page 202: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae.

Waheshimiwa Wabunge, naomba sasa nimuite mtoahoja ambaye ni Waziri wa Fedha na Mipango, MheshimiwaDkt. Philip Mpango karibu utoe hitimisho lako, una dakika45. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika,naomba na mimi nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungukwa kuniruhusu kusimama leo tena hapa jioni kuhitimisha hojaambayo niliiwasilisha tarehe 7 Novemba, 2017 kuhusuMapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa naMwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka2018/2019.

Aidha, napenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwakowewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwakusimamia vyema mjadala wa hoja. Vilevile niwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote 124 waliochangia katikamjadala huu ambapo Wabunge 103 wamechangia kwakuzungumza ikijumuisha Mawaziri na Naibu Mawaziri ambaokwa kweli mmenipa raha, lakini pia wapoWaheshimiwa Wabunge 12 ambao wamechangia kwamaandishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyobainisha katika hojayangu kuwa lengo lilikuwa ni kuomba maoni na ushauri waWaheshimiwa Wabunge wakiwa ndiyo sauti za mawazo namatakwa ya wananchi wetu kuhusu maendeleo ya nchi yao,lakini pia mgawanyo wa rasilimali fedha ili yazingatiwe katikahatua ambayo itafuata baada ya kikao hiki cha Bungeambayo itakuwa ni kazi ya kuandaa Rasimu ya Mpango waMaendeleo wa Taifa na kiwango na ukomo wa bajeti kwamwaka ujao wa fedha ambavyo kwa mujibu wa Kanuni zaBunge hili zitawasilishwa kwa Wabunge tarehe 11 Machi, 2018na kufanyiwa uchambuzi na Kamati ya Bajeti kuwezeshaukamilishwaji wa Mpango na Bajeti ambavyo vitawasilishwawakati wa Bunge la bajeti. Kwa niaba ya Serikali nakiri kuwalengo hilo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa na narudiakusema ahsanteni sana. (Makofi)

Page 203: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

Mhesimiwa Spika, niruhusu kipekee nitambuemchango wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini yaMwenyekiti wake Mheshimiwa Hawa Ghasia, Mbunge waMtwara Vijijini. Kamati ilitupatia ushauri wa msingi ambaoniliuelezea kwa kifupi wakati natoa hoja, lakini vileviletulipokea mchango uliotolewa na Mheshimiwa David ErnestSilinde, Mbunge wa Momba kwa niaba ya Msemaji wa KambiRasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha naMipango. Aidha, nawashukuru sana Waheshimiwa Mawaziriwa Wizara mbalimbali waliotoa ufafanuzi wa baadhi ya hojazilizotolewa zinazogusa sekta zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, natoa shukrani kwa Naibu Waziriwa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji kwakunisaidia kusikiliza kwa makini maoni na ushauri waWaheshimiwa Wabunge kwa siku zote tano na kutoleaufafanuzi kwa umahiri hoja zilizotolewa hapa ndani mudamfupi uliopita. Nitumie pia fursa hii kuwashukuru kwa dhatiwatendaji wote wa Wizara ya Fedha na Mipangowakiongozwa na Katibu Mkuu, Bwana Dotto Mgosha Jameskwa kuchambua na kutafuta takwimu na taarifa ambazozilihitajika kwa ajili ya kutolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali.(Makofi)

Katika majadiliano ya hoja niliyowasilisha mbele yaBunge lako Tukufu, Serikali imepokea maoni mengi sana.Naomba nitaje baadhi tu kwa kifupi maoni ambayoyalitolewa na Wabunge wengi na hii ni kuthibitisha tukwamba Serikali inasikia. Maoni hayo ni kama ifuatavyo:-

(i) Mmetushauri kwamba tuweke msukumo pekeekwenye sekta ya kilimo. (Makofi)

(ii) Mmetushauri tujumuishe mkakati mahsusi wakumaliza kilio kikubwa cha upatikanaji wa huduma za majinchini kote. (Makofi)

(iii) Mmetuambia kwamba fursa ya uwepo warasilimali kubwa ya gesi asilia nchini ni lazima sasa itumikevizuri zaidi. (Makofi)

Page 204: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

(iv) Mmetuelekeza tutekeleze kwa dhati utaratibu waubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yaani PPP.(Makofi)

(v) Mmetuelekeza na kutushauri tuongeze kasi yakutekeleza miradi ya miundombinu ya kiuchumi na kijamiiikiwa ni pamoja na ile ya Umeme Vijijini REA III lakini piabarabara muhimu za kuchochea uchumi katika mikoambalimbali. (Makofi)

(vi) Mmetushauri tuongeze kasi ya kulipa madeniyaliyohakikiwa.

(vii) Mmetushauri tuhakikishe kuwa Deni la Taifalinaendelea kubakia kuwa himilivu na kuanza kupunguza kasiya kuongezeka kwa Deni la Taifa.

(viii) Mmetushauri tukabiliane na tatizo la ukosefu waajira nchini. (Makofi)

(ix) Mmetushauri kuwekeza na kutumia kikamilifurasilimali za bahari na maziwa (the blue economy).

(x) Mmetushauri kubainisha mkakati wa kuongezaidadi ya watalii na mchango wa sekta ya utalii katika uchumi.(Makofi)

(xi) Mmetushauri kuhusu kuimarisha uhifadhi wa ardhi,kupima na kupanga matumizi yake.

(xii) Mmetushauri kuchukua hatua za kupunguza kasiya ongezeko la idadi ya watu.

Mheshimiwa Spika, hayo ni baadhi tu, ni masualakumi na mbili muhimu ambayo tumesikia ushauri wenu lakiniyako mengi sana tutayafanyia kazi. Kwa niaba ya Serikalinaahidi kuwa wakati wa kuandaa Mpango wa Maendeleowa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019tutazingatia ipasavyo maoni na ushauri uliotolewa na Bungelako Tukufu lilipokaa kama Kamati ya Mipango. (Makofi)

Page 205: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kazi yangu, kazi yaNaibu Waziri na wataalam wetu wa Wizara kwa siku hizi tanoilikuwa ni kupokea maoni na ushauri ambao tunakwendakutafakari na kufanyia kazi, nitapenda nitoe ufafanuzi kwabaadhi tu ya hoja ambazo Waheshimiwa Wabunge mlizitoa.Kwa kweli hoja ni nyingi kama nilivyosema na kwa mudaambao nimepewa si rahisi kujibu zote na naombaniwahakikishie kwamba tutawasilisha majibu na maelezo yahoja zote kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, lakini kabla sijafanya hivyo,naomba nisisitize tena mambo matatu kwa sababuyanajirudiarudia kila mwaka, ni vizuri tukawa tunaelewanakwa faida ya Taifa letu.

Kwanza, nil ichowasil isha Bungeni i le tarehe 7Novemba, 2017 siyo Mpango ni mapendekezo ya mamboya msingi na vipaumbele vinavyotakiwa kuzingatiwa katikakuandaa Mpango wenyewe na bajeti ya Serikali kwa mwakaujao wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, Mapendekezo yaMpango na Mwongozo wa kuandaa bajeti yalipitia katikahatua zote ambazo ni kupata maoni ya wadau wa ndani nanje ya Serikali, Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, Kikao chaMakatibu Wakuu (IMTC) na kupata ridhaa ya Baraza laMawaziri kabla ya kujadiliwa na Kamati ya Bajeti na hatimayeBunge. Hivyo, mapendekezo ya Mpango siyo mpango waDkt. Mpango bali ni Mapendekezo ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini jambo la tatu, Mapendekezohaya ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mpango waMaendeleo wa miaka mitano 2016/2017 - 2020/2021 kwamwaka wa tatu. Kwa hiyo, wale wanaodai ni copy and pastekutoka Mpango wa mwaka jana ni vema wakazingatia hili.

Mheshimiwa Spika, sasa baada ya maelezo haya,naomba nijielekeze kujibu baadhi ya hoja na nitaombanianze na ile hoja ambayo naiona ni muhimu sana kwambaSerikali iache kupeleka fedha kugharamia miradi mikubwa

Page 206: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

ya kielelezo kama Standard Gauge Railway, ununuzi wandege mpya, uzalishaji wa umeme Stigler’s Gorge, miradiambayo inaweza kutekelezwa kibiashara na sekta binafsi.Ilisemwa hapa kuwa utaratibu huo unapunguza fedha kwaajili ya kugharamia huduma za msingi kwa jamii kama majina afya na utapelekea kuongezeka kwa mzigo wa Deni laTaifa.

Mheshimiwa Spika, hoja hii ni vema tukaitafakarivizuri. Serikali inathamini sana mchango wa sekta binafsi natunafahamu kuwa huko ndiko kwenye pesa na mitajimikubwa na hasa ukizingatia size ndogo ya uchumi wa Taifaletu kwa hivi sasa lakini pia mahitaji makubwa ya wananchiwetu. Hata hivyo, ni muhimu mawazo hayo yapimwekiuhalisia na bila kusahau historia na uzoefu wa nchi nyingine.Wote mtakumbuka kwa tulikuwa na RITES of India hapa, hivinaomba niulize walijenga kilomita ngapi za reli? Tumesahaukwamba treni karibu zote zil isimama, mizigo ikawainasafirishwa kwa malori mpaka Serikali ilipofanya uamuzi wakuondokana na RITES of India. Hivi sasa kweli hata tukikaahapa si nalisikia linapita hapo, hatuoni treni za abiria na mizigozinatimua vumbi. Tena nasikia zinaimba kadogosa kadogosakadogosa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri wanguameeleza vizuri wazo la kuzalisha umeme eneo la Stigler’sGorge lilikuwepo kwenye makaratasi kwa miaka mingi. Hivisekta binafsi si ilikuwepo na ilikuwa inasikia kilio chakutokuwepo kwa umeme wa uhakika na wa gharama nafuuhapa nchini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tulikuwa na Kampuni hapa ya CityWater kwenye sekta ya maji mbona kilio cha maji Dar esSalaam hakijaisha? Yaliyotokea ATCL na TTCL vivyo hivyo,mbona tunasahau haraka hivi? Hata hivyo, sasa tumefanyamabadiliko na tumeanza kufaidi huduma za Bombardier kujaDodoma, Songea, Kigoma na kwingineko. Aidha, hivi sasanasubiri gawio mwaka huu shilingi bilioni moja kutoka TTCLkwa mara ya kwanza. Najiuliza hivi umeme huuutakaozalishwa Stigler’s Gorge hautaimarisha upatikanaji wa

Page 207: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

huduma za afya, elimu na maji kwa gharama nafuu zaidi?Nawasihi ndugu zangu hebu tutafakari vizuri, tusisahauhistoria, we have the experience. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwasihi sana WaheshimiwaWabunge na Watanzania kwa ujumla kuwa ni kweli kabisasekta binafsi ndiyo injini ya uchumi lakini zipo changamotokiuhalisia. Mzee Kikwete alituambia akili za kuambiwa lazimatuchanganye na za kwetu kabla hatujafika hatua ya kuwana sekta binafsi yenye nguvu. Kweli natamani sanawawekezaji wa ndani na nje watatupunguzia huu mzigo.Waheshimiwa Wabunge nilieleza mwaka 2016/2017 kujengaStandard Gauge Railway kwa bajeti ya Serikali ni mzigomkubwa mno, lakini sekta binafsi tuliyonayo bado inahitajikulelewa ili iweze kubebea jukumu hili na sekta binafsi kutokanje hawaji wakati tunapowahitaji na hata wakija wanamasharti ambayo baadhi ni magumu kwelikweli na menginehayana maslahi kwa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, miezi michache ilyopitaMheshimiwa Waziri Mkuu aliita makampuni ili watujengeemtambo wa kuchenjua makinikia na alikuwepomfanyabiashara mmoja kutoka Dubai, kitu cha kwanzaalichoanza nacho anasema pesa ninayo lakini sharti lakwanza sovereign guarantee, aah, magumu haya jamani.

Kwa hiyo, katika mazingira haya hivi kweli tutakaamiaka na miaka indefinitely tukisubiri wawekezaji washukendiyo tuijenge upya reli ya kati ambayo ina zaidi ya miaka100. Uamuzi wa Serikali ni kwamba tuanze kujenga kwavipande yaani lots wakati tunaendelea na jitihada zakuwashawishi wawekezaji na taasisi za fedha ambazozinaweza kutukopesha kwa masharti ambayo ni ahueni,hatuja-rule out private sector, hapana, lakini hatuwezikuendelea kusubiri miaka mingine 50 ndiyo tupige hatua yakujenga reli yetu ya kati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba ninong’one na Bungelako Tukufu, Mheshimiwa Rais Magufuli aliposikia huu mjadalaalinipigia simu na aliniambia hivi, Waziri mwambie ndugu

Page 208: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

yako Mheshimiwa Nape na Mheshimiwa Bashe kuwanawataka sana hao wawekezaji kwenye ujenzi wa StandardGauge Railway, wawalete hata kesho, niko tayari kuwapareli ya Kaliua - Mpanda au Isaka - Mwanza au reli ya Mtwara- Mchuchuma - Liganga wajenge. Hayo ni maneno yaMheshimiwa Rais. Natumaini Waheshimia husika will raise upto this challenge from His Excellence the President. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikwa na hoja ya Deni la Taifalinakua kwa kasi kubwa wakati uchumi unakua kwa kasindogo na kwamba hali hii itafanya ulipaji wa Deni la Taifakuwa mgumu sana. Deni la Taifa liliongezeka kutoka dola zaMarekani milioni 22,320.76 mwaka 2016 na kufikia dola zaMarekani milioni 26,115.2 mwezi Juni, 2017 ikiwa ni sawa naongezeko la asilimia 17% na deni hilo ni sawa asilimia 31.2 yaPato la Taifa ikilinganishwa na ukomo wa uhimilivu waasilimia 56. Uhimilivu wa Deni la Taifa hupimwa kwakuzingatia uwezo wa nchi kulipa deni husika katika mudamfupi, wa kati na muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kulinganisha Deni la Tanzaniana nchi nyingine za Afrika Mashariki ni kama ifuatavyo;Uganda ni asilimia 35.4, Rwanda asilimia 36.6, Burundi asilimia43.4 na Kenya asilimia 50.4. Hali hii ya nchi za Afrika Masharikibado ni nzuri ikilinganishwa na baadhi ya nchi nyingine kamaZambia ambayo ni asilimia 57.2, United Arab Emirates asilimia60.3, Marekani asil imia 73.8, Morocco asil imia 77,Uingereza asilimia 92.2, Misri asilimia 92.6, Msumbiji asilimia100.3, Italia asilimia 132.5 na Ugiriki asilimia 181.6. Kwa takwimuhizi sisi bado tuna nafasi kubwa ya kuendelea kukopa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, tutaendelea kukopa kwasababu kuu moja tu, ni kukuza uwezo wetu wa baadaye wakumudu uendeshaji wa nchi yetu na kulinda uhuru na heshimaya nchi yetu. Napenda nisisitize hakuna dhambi ya nchikukopa ili mradi nchi husika itumie fedha hizo za mkopokukuza uwezo wa uchumi, kuzalisha na kurejesha hiyomikopo, ni lazima iwe prudential borrowing. KamaMheshimiwa Rais alivyosema alipokuwa ziarani kule Kagera

Page 209: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

kwa kweli tutaendelea kukopa mpaka kieleweke ili mradiDeni la Taifa tuhakikishe linaendelea kuwa himilivu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda nitoe angalizokuwa ukokotoaji wa uhimilivu wa Deni la Taifa japokuwa siyorocket science unahitaji utaalam. Kujua hesabu za kikwetuhaitoshi kufahamu namna ya kukokotoa deni in present valueterms maana masharti ya mikopo na muda wa kuiva wamadeni haya yanatofautiana sana. Siyo suala la kujumlishamkopo fulani in nominal terms na kuamua kuwa denihalitakuwa himilivu. Namuomba Mheshimiwa Kishoa nawengine kama wanataka lecture bure kuhusu debtsustainability analysis waje pale Hazina tuko tayarikuwafundisha bila malipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuliombwa hapa tutoe ufafanuzikwa nini takwimu za Deni la Taifa katika vitabu vya Mpangovya mwaka 2016/2017, 2017/2018 na 2018/2019zinatofautiana. Katika kitabu cha Mapendekezo ya Mpangowa Maendeleo ya Taifa 2017/2018 takwimu zinaonyeshakuwa Deni la Taifa hadi kufikia Juni, 2016 ni dola za Marekanimilioni 18,614.93 wakati katika Mwongozo wa Maandalizi waMpango na Bajeti kwa mwaka 2018/2019 takwimuzinaonyesha Deni la Taifa hadi Juni, 2016 ni dola za Marekanimilioni 22,320.76. Deni la Taifa linajumuisha deni la Serikali landani na nje pamoja na deni la nje kwa sekta binafsi. Deni laSerikali la nje linajumuisha mikopo kutoka nchi wahisani,mashirika ya fedha ya Kimataifa pamoja na mabenki yakibiashara ya kimataifa. Wakati deni la ndani la Serikalilinajumuisha dhamana za Serikali za muda mfupi na hatifungani za Serikali pamoja na madeni mengineyo.

Mheshimiwa Spika, takwimu zilizopo katika kitabu chaMapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/2018 za dola za Marekani 18,614.93 ni deni la Serikali na siyoDeni la Taifa kwa kuwa halikujumuisha deni la sekta binafsi.Aidha, mtoa hoja angepitia kifungu hicho hadi mwishoangeona Deni la Taifa hadi Juni, 2016 ni dola za Marekanimilioni 23,093.3 na kiasi hiki ni tofauti na kile kilichoripotiwakatika Mwongozo wa Maandalizi na Mpango wa Bajeti wa

Page 210: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

mwaka 2018/2019 ambapo Deni la Taifa kwa kipindi hicho nidola za Marekani 22,320.76. Tofauti hii ya dola za Marekani772 inatokana na kubadilika kwa deni la sekta binafsi nakupungua kwa deni la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kufuatiakukamilika kwa uhakiki wa madeni hayo.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja ya taarifa zabenki za biashara nchini zinaonyesha kuporomoka kwa kiasikikubwa kwa mikopo binafsi, mikopo ya biashara na mikopokwa sekta za uzalishaji. Hali ya kupungua kwa kasi ya ukuajiwa mikopo imetokea katika nchi kadhaa ikiwemo Tanzaniakwa kipindi cha takribani mwaka mmoja na nusu sasa. Katikamiezi kumi na mbili iliyoishia Septemba, 2017 wastani waongezeko la mikopo kwa sekta binafsi nchini Kenya ilikuwaasilimia 3.8, Tanzania asilimia 5.0, Uganda asilimia 5.2 naRwanda asilimia 10.3. Katika nchi zote hizi ukuaji wa mikopokatika kipindi kilichotajwa ulikuwa chini ya nusu ya ukuajikatika kipindi kama hicho kilichotangulia.

Mheshimiwa Spika, kushuka huku kuna sababumbalimbali ikiwemo kupungua kwa utashi duniani yaani kwakiingereza general decline and global demand ambakokunajidhihirisha kwa bei za bidhaa duniani kuwa chinikiujumla. Hii inaathiri mapato ya sekta binafsi yaani cash flowsna kufanya zisichikue mikopo kwa kasi ile ile.

Pili, mabenki kuongeza tahadhari katika shughuli zaokutokana na hali ya wasiwasi duniani yaani globaluncertainty. Matokeo ya kuongezeka kwa hali ya wasiwasini pamoja na benki kadhaa kupoteza mahusiano na benkiza kimataifa yaani correspondent banks katika kilekinachoitwa de-risking.

Tatu, ni kupungua kwa fedha za bajeti za Serikalikutoka nje ya nchi ambako kumepunguza ukwasi uliokuwaukisababishwa na matumizi ya fedha hizo na hivyo kuathiriutashi ndani ya nchi kiujumla yaani domestic demand. Mfano,fedha za bajeti kutoka nje zilizotumika zilipungua kutokashilingi bilioni 2,711 mwaka 2013/2014 hadi kufikia shilingi bilioni1,774 mwaka 2016/2017.

Page 211: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

Mheshimiwa Spika, Serikali imechukua hatua zakuongeza ukwasi na zinafahamika, Benki Kuu imeshusha ribayake yaani discount rate kutoka asilimia 16 Machi, 2017 hadiasilimia 9 Agosti, 2017. Pia kupunguza kiwango cha kisheriacha sehemu ya amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuuna benki za biashara (Statutory Minimum Reserve Requirement- SMRR) kutoa asilimia 10 mpaka 8 Aprili, 2017. Benki Kuu piaimeendelea kutoa mikopo ya muda mfupi kwa benki zabiashara pamoja na kununua fedha za kigeni kutoka kwenyesoko la jumla la mabenki.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hatua hizi, hali yaukwasi katika mabenki imekuwa ni ya kuridhisha kuanziakipindi cha nusu ya pili ya mwaka 2016/2017 na hii inadhihirikakatika kupungua kwa riba ya mabenki yaani interbankmarket rate kutoka wastani wa asilimia 13.49 Disemba, 2016hadi asilimia 3.72 Oktoba, 2017. Kupungua huku kwa ribakatika soko la mabenki kumedhihirika pia katika soko ladhamana za Serikali ambako wastani wa riba umeshukakutoka asilimia 15.12 - Disemba, 2016 hadi asilimia 9.45 -Oktoba, 2017. Matumaini ya Serikali ni kuwa hatimayematokeo ya hatua hizi yatajionesha katika ongezeko lamikopo kwa sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwa nini BenkiKuu imeacha kutoa takwimu za uuzaji na uingizaji wa bidhaanje (import and export data). Ripoti za uchumi za Benki Kuuza kila mwezi (Monthly Economic Reviews) za Julai, Agosti naSeptemba ni kweli hazikuonesha takwimu za biashara yabidhaa nje ya nchi (trade statistics) na sababu yake nichangamoto za data (harmonization) ambazo zilijitokezakatika kukamilisha takwimu hizo baada ya kuanzakutekelezwa mpango wa Himaya Moja ya Forodha ya AfrikaMashariki yaani EAC-Single Customs Territory. Changamotohizi zinashughulikiwa na mara zitakapokuwa zimetatuliwatakwimu hizi zitaendelea kutolewa, Serikali haina sababu yakuficha chochote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, palikuwa na hoja kwambamapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa

Page 212: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

hayakugusa Zanzibar. Niseme tu kwamba tumesikia hoja hiina tutajadiliana na wenzetu upande wa Serikali ya Mapinduziya Zanzibar namna bora ya kulishughulikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Mheshimiwa aliyetoahoja anafahamu kuwa ilivyo sasa Zanzibar ina Tume yaMipango Huru lakini pia ina Ofisi ya Takwimu ambavyo siovya Muungano. Aidha, Zanzibar ina Dira yake ya Maendeleo2020 na ina Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKUZA) naMaandalizi ya Mipango ya Maendeleo ya Zanzibarinaongozwa na nyaraka hizo na taasisi nilizozitaja, of course,pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya CCM. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtakumbuka kuwa yalikuwepomawazo katika Katiba Pendekezwa kwamba Taifa lifikiriekuwa na Tume moja tu ya Taifa ya Mipango lakini mchakatohaukufika mwisho. Aidha, kuna vikao vya pamoja vya Kiwizarana Kitaifa vinavyoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kujadilichangamoto mbalimbali za Muungano wetu zikiwemo zilezinazohusu masuala ya kodi ambazo Waheshimiwa Wabungewalizisema, biashara na kadhalika na Wizara ninayoiongozatunashiriki kikamilifu.

Mheshimiwa Spika, kikao kijacho kimepangwakufanywa tarehe 17 na 18 Novemba, 2017 Dar es Salaam nanishauri tu kwamba baadhi ya mambo na hoja ambazozilisemwa ziwasilishwe kwenye jukwaa hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu Waziri wa Fedha wa Serikaliya Muungano kwenda Zanzibar napenda sana nanimekwishakwenda mara mbili na napanga kwenda hukomara baada ya kikao hiki cha Bunge. Namuomba sanaMheshimiwa Saada aniandalie urojo tu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, aidha, tumefanya vikao nawenzetu wa Zanzibar si chini ya mara nne ndani yamiaka miwili hii ikiwa ni pamoja kikao ambacho aliongozaMheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Raiswa Zanzibar, nyumbani kwake Oysterbay mwezi uliopita.(Makofi)

Page 213: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

Mheshimiwa Spika, palikuwa na hoja muhimuambayo mimi nasema ni ya msingi sana kwamba sekta yakilimo, ufugaji na uvuvi vipewe kipaumbele katika Mpangona Bajeti kwa kuwa mchango wake ni muhimu sana katikakuwezesha harakati za kufikia uchumi wa viwanda nakupunguza umaskini. Serikali inakubaliana kabisa na hoja hiina tutaizingatia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba toka mwanzona pia katika wasilisho langu wakati natoa hoja, sekta yakilimo, ufugaji na uvuvi ni moja ya maeneo ya kipaumbelekatika kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi waviwanda. Kwa msingi huo, eneo hili litafafanuliwa katikaMpango wa mwaka ujao na litahusisha maeneo yoteambayo Waheshimiwa Wabunge waliyasisitiza ikiwemoupatikanaji wa uhakika wa chakula, malighafi za viwanda,miundombinu ya umwagiliaji, upatikanaji wa pembejeo,utafiti wa kilimo na mbegu bora na pia kuboresha hudumaza ugani, usindikaji wa mazao, miundombinu, hifadhi yamasoko pia kuboresha miundombinu ya uzalishaji wa mifugona kuongeza bidhaa za mifugo na uvuvi.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, hoja ni nyingina ningependa tungepata muda zaidi wa kuzifafanua lakinitutazifafanua kwa maandishi.

Kabla ya kuhitimisha hoja yangu, napenda kwa maranyingine tena kutoa shukrani za dhati kwa WaheshimiwaWabunge wote waliochangia hoja hii ya Mapendekezo yaMpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/2019 naMwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka2018/2019. Nasema hivi kwa dhati ya moyo wangu. Aidha,naomba sana Mbunge yeyote asisite kunikosoa katika utendajiwangu wa kazi kwa maslahi ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, narudia tena, naomba sanaMbunge yeyote asisite kunikosoa katika utendaji wangu wakazi kwa maslahi ya Taifa letu. Hata hivyo, nawasihi mnikosoeau kunipongeza kwa haki na hofu ya Mungu. Namuombasana Mungu, napata kigugumizi kusema maneno haya lakini

Page 214: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

nitasema tu. Namuomba Mungu anipe moyo wa kuyapokeayale yote yaliyonenwa juu yangu pasipo kweli, japokuwakama binadamu yalinisononesha, napenda nilihakikishieBunge hili na Watanzania kwa ujumla kwamba mwenendowa mjadala wa hoja hii umeniimarisha zaidi kuendeleakutimiza wajibu wangu kwa Taifa na naamini Munguatanisaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naendelea kumsihi Munguawabariki Waheshimiwa Wabunge wote bila kuwabaguawale walionivika joho la ujeuri yaani arrogance na uziwi. Hiiimenifanya nikumbuke kuwa watoza ushuru walichukiwahata kabla ya wakati wa Yesu na hivyo mimi nikiwamsimamizi wa watoza kodi inabidi tu niyapokee. Bahati nzurini kuwa wananchi wenu ambao fedha hizi za koditunazielekeza kwenye maendeleo yao ikiwemo kununuadawa na vifaatiba, elimu msingi bure, umeme vijijini,kuboresha huduma za maji na kadhalika wamewasikia.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema hapo awali,Serikali itazingatia maoni na ushauri wa WaheshimiwaWabunge katika kukamilisha maandalizi ya Mpango na Bajetiya Serikali kwa mwaka 2018/2019. Kuthibitisha hili, napendanirudie kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa Mpango ujaoutazingatia kwa kadri inavyowezekana ushauri uliotolewa naKamati ya Bajeti na Bunge zima likikaa kama Kamati yaMipango. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siwezi kuhitimisha hoja hii bilakumshukuru kwa dhati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wakewa karne, ni chuma kweli kweli. Rais Mstaafu wa Awamu yaNne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliposema hayo hakukoseakabisa. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kunitia moyoniendelee kutekeleza majukumu yangu ya msingi yakusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kudhibitimatumizi ya fedha za umma bila uoga kwa faida yawananchi wanyonge hata pale wachache wanaponidhihakibinafsi. (Makofi)

Page 215: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

Mheshimiwa Spika, kadhalika namshukuru sanaMheshimiwa Kassim Majaliwa, Mbunge wa Ruangwa, WaziriMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nimejifunzakatika miaka hii miwili kwamba kweli Waziri Mkuu wetu nikocha na kapteni mahiri wa utendaji Serikalini kama alivyokwenye medani za mpira wa miguu. Ahsante sanaMheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuendelea kunipa confidencekatika utumishi huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wito wangu ni kwa WaheshimiwaWabunge wote kuendelea kuunga mkono Serikali ya Awamuya Tano chini ya uongozi wa Rais wetu Mheshimiwa JohnPombe Joseph Magufuli katika dhamira yake ya kujengaTanzania mpya ambapo wananchi wote watanufaika narasilimali za Taifa ili kuwaondoa kwenye lindi la umaskini.Pamoja na mambo mengine, nawaomba WaheshimiwaWabunge, kuendelea kuwahimiza wananchi kushiriki katikashughuli za maendeleo ili kuleta mabadiliko chanya katikamaisha yao na Taifa kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, rai yangu kwa Watanzania woteni kuwa tuungane kwa pamoja na kufanya kazi kwa bidii,uaminifu na uadilifu mkubwa kwa nchi yetu. Mageuzimakubwa anayoyaongoza Rais wetu ni magumu tenamagumu sana lakini ndiyo njia sahihi kuelekea Tanzaniampya. Kwa mfano, uamuzi wa kuhakikisha fedha za Serikalizinarejeshwa Serikalini ili zitumike kuwahudumia wananchihaukupokelewa vizuri na wahusika lakini ukweli utasimama.Haiwezekani, labda wasubiri nitakapoondolewa kwenyeUwaziri huu, akaunti za Serikali, mfano fedha za polisizikaendelea kushikiliwa na kampuni binafsi inaitwa MaxMalipo kwa ambao hawaijui. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaahidi kuwa yale yote yaliyochini ya mamlaka niliyopewa nitayasimamia bila kuteterekaikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa tunapiga hatua kubwazaidi katika ukusanyaji wa kodi na mapato yote ya Serikali,kudhibiti mianya ya uvujaji wa mapato na kupanua wigo wakodi sambamba na kusimamia matumizi ya fedha za ummakama Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 inavyotuongoza.

Page 216: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaSpika, naafiki.

SPIKA: Nimewaona Waheshimiwa, ahsanteni sana.Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwakuhitimisha. (Makofi)

Ahsante sana kwa wasilisho hilo muhimu sana, najuamuda ulikuwa hautoshi, Waheshimiwa Wabungewangependa kusikia kila mmoja kile ambachokimezungumzwa lakini Mheshimiwa Waziri wa Fedhaametuahidi kuwa baadhi ya mambo haya yatakuwa katikamajibu ya kimaandishi. Nitawaomba majibu hayoyakipatikana basi tusome jamani maana nina hakika wapowanaoyaacha kwenye pigeon holes pale halafu tukirudi tenamwakani yanazungumzwa yale yale kumbe baadhi yakeyanakuwa yamejibiwa vizuri.

Kwa hatua hii niwashukuru sana, mwenyewe Waziriwa Fedha, Naibu Waziri wa Fedha na timu yako yote ambayoilikuja Dodoma, najua mmekesha. Niwashukuru WaheshimiwaMawaziri wote, Naibu Mawaziri, Waheshimiwa Wabungeambao tumechangia vizuri sana katika Mpango huu. Katikakumbukumbu zangu za hivi karibuni, Mpango huu ndiyoumechangiwa kwa hamasa ya kipekee kabisa. (Makofi)

Niwahakikishieni kazi yetu haikuwa bure. Wizaraimesikia, wataalam wa Wizara wamesikia namlichokizungumza ndiyo reflection ya Watanzaniawanachokizungumza. Kwa hiyo, wameyachukua kamawalivyotuahidi hapa, wataenda kuyazingatia na ndiyomaana kwa siku ya leo sitawahoji kuhusiana na jambo hilikwa sababu tulichokuwa tukikifanya hapa ni kujadiliMapendekezo ya Mpango, kwa hiyo, hatuwezi kuhojianakuhusu Mapendekezo. Tutakaporudi wakati ule wa bajeti,utakuja sasa ule Mpango ambao unatokana namapendekezo yetu haya na bajeti yenyewe itafuatiaimmediately baada ya pale. Ndiyo maana nikasema

Page 217: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1513920767-13 NOVEMBA 2017.pdf · kitaifa wa kuboresha vituo vya afya kwa ajili ya kutoa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

nawashukuru sana wote, Waheshimiwa Wabunge tuzidikushirikiana na mpaka sasa tunaenda vizuri. Nawapongezasana wote na kipekee nawapongeza sana Mawaziri,mmevumilia kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jamani, hata upande huutuwapigieni makofi, wamekaa siku nne hapa mnapigamadongo, Mpango bado yupo. Yapo mazingira hata waupande wa pil i unampigia makofi kwamba kwa hil iumevumilia. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Tumepiga.

SPIKA: Mmepiga. Si mnaona Mheshimiwa Waziriamepungua kilo mbili hapa. Mheshimiwa Waziri, haya yoteyalikuwa kwa nia njema na ni kwa ajili ya kujenga nchi yetu.(Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, kwa jinsi hiyo, kwa sababuya muda wetu hatuwezi kuongeza shughuli yoyote. Nisemesasa kwamba naahirisha shughuli za Bunge hadi kesho saatatu kamili asubuhi.

(Saa 1.36 Jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Jumanne,Tarehe 14 Novemba, 2017, Saa Tatu Asubuhi)