bunge la tanzania majadiliano ya bunge mkutano wa...

143
3 APRILI, 2018 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kwanza – Tarehe 3 Aprili, 2018 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA D U A Naibu Spika (Mhe. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae, Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: KIAPO CHA UAMINIFU Waheshimiwa Wabunge wafuatao waliapa:- Mhe. Dkt. Godwin O. Mollel Mhe. Maulid S. A. Mtulia NAIBU SPIKA: Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: TAARIFA YA SPIKA NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nitasoma kwenu taarifa ya Mheshimiwa Spika ambayo imetolewa chini ya Kanuni ya 33 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2016.

Upload: others

Post on 27-Oct-2019

6 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Kwanza – Tarehe 3 Aprili, 2018

(Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi)

WIMBO WA TAIFA

D U A

Naibu Spika (Mhe. Tulia Ackson) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Tukae, Katibu.

NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE:

KIAPO CHA UAMINIFU

Waheshimiwa Wabunge wafuatao waliapa:-

Mhe. Dkt. Godwin O. MollelMhe. Maulid S. A. Mtulia

NAIBU SPIKA: Katibu.

NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE:

TAARIFA YA SPIKA

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nitasomakwenu taarifa ya Mheshimiwa Spika ambayo imetolewa chiniya Kanuni ya 33 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka2016.

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

2

Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano wa 10 waBunge, Bunge lilipitisha Miswada miwili ya Sheria ya Serikalikama ifuatavyo:-

Muswada wa kwanza ulikuwa ni Muswada wa Sheriaya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 5 wa mwaka 2017(The Written Laws Miscellaneous (Amendments) No. 5 Bill, 2017).Muswada wa pili ni Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhiya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa mwaka 2017 (ThePublic Service Social Security Fund, Bill, 2017).

Waheshimiwa Wabunge, kwa taarifa hii MheshimiwaSpika analiarifu Bunge hili Tukufu kwamba tayari Miswadahiyo miwili imepata kibali cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania na kuwa sheria za nchizinazoitwa:-

Kwanza, Sheria ya Marekebisho ya Sheria MbalimbaliNa. 1 ya mwaka 2018 (The Written Laws Miscellaneous(Amendments) Act No. 1, 2018).

Pili; Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishiwa Umma Na. 2 ya mwaka 2018 (The Public Service SocialSecurity Fund Act, No. 2 of 2018).

Waheshimiwa Wabunge, hiyo ndiyo taarifa yaMheshimiwa Spika. Tutaendelea, Katibu.

NDG. STEPHEN KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:-

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU:

Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

3

Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zilizo chiniyake, kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS(MUUNGANO NA MAZINGIRA):

Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chiniya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mkataba waMabadiliko ya Tabianchi (The Paris Agreement Under the UNFramework Convention on Climate Change).

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA - MAKAMUMWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA):

Maoni ya Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingirakuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chiniya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko yaTabianchi (The Paris Agreement under the UN FrameworkConvention on Climate Change).

MHE. JOYCE B. SOKOMBI (K.n.y. MHE. ALLY SALEH ALLY- MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA OFISI YAMAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA):

Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzanijuu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingirakuhusu Azimio la Bunge kuridhia Makubaliano ya Paris chiniya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko yaTabianchi (The Paris Agreement under the UN FrameworkConvention on Climate Change)

NAIBU SPIKA: Ahsante. Tunaendelea, Katibu.

NDG. STEPHEN KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE:

MASWALI NA MAJIBU

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

4

Na.1

Kasi ya kupambana na Dawa za Kulevya Nchini

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA (K.n.y) MHE. MWANTUMUDAU HAJI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inarejeshakasi ya kupambana na dawa za kulevya?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa MantumuDau haji, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeongeza kasi naharakati za kupambana na biashara haramu ya dawa zakulevya nchini baada ya Bunge lako Tukufu kutunga Sheriampya ya Kudhibiti na Kupamabana na Dawa za Kulevya Na.5 ya mwaka 2015. Sheria hii imeipa Serikali Mamlaka yakuanzisha chombo chenye nguvu cha kudhibiti nakupambana na dawa za kulevya, ambacho kiliundwa rasmimwezi Februari mwaka 2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mamlaka hiyo imepewanguvu Kisheria ya kuweza kukamata, kupekua, kuzuia malina kuchunguza mashauri yote ya dawa za kulevya namakosa mengine yanayohusiana nayo ikiwemo malizitakazothibitika kupatikana kutokana na dawa za kulevya.Hata hivyo, Serikali katika kuongeza kasi ya kupambana nadawa za kulevya, mwaka 2017 ilifanya marekebishomakubwa ya sheria hiyo na kuipa nguvu maradufu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa takribani mwakammoja sasa tangu kuundwa kwake hadi kufikia mweziFebruari mwaka 2018, Mamlaka imekwishakamata jumla yawatuhumiwa 11,071; kati ya hao, watuhumiwa 3,486 niwafanyabiashara wa dawa za kulevya na tayari

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

5

wameshafikishwa Mahakamani. Kutokana na kuongezekakwa kasi ya kupambana na dawa za kulevya imesababishakupungua kwa kiasi kikubwa cha matumizi ya madawa yakulevya nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa wito kwaWaheshimiwa Wabunge wote kushiriki kikamilifu katika juhudiza Serikali za kupambana na dawa za kulevya kwanimadhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo kwanamna moja ama nyingine yanatuathiri sote kwa njiambalimbali ikiwemo kuongeza vitendo vya uhalifu, matumiziya Serikali katika kuwahudumia waathirika pia.

NAIBU SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Asha AbdullahJuma, swali la nyongeza.

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri yaliyotolewa naMheshimiwa Anthony Mavunde, Naibu Waziri anayehusika namasuala haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni kwamba,kutokana na kwamba bado hakujawa na udhibiti wakutosha wa kuzuia madawa ya kulevya yasipenye nakutokana na tulivyomsikia Mkuu anayeshughulika na udhibitiwa madawa ya kulevya kwamba kule Zanzibar badokunatumika kama kipenyo cha kupitisha madawa haya yakulevya. Je, Serikali imejipangaje kuongeza ushirikiano naSerikali ya Mapinduzi ili kudhibiti na kuhakikisha kwamba kuleZanzibar hakuwi mlango wa kupitisha madawa haya yakulevya?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya WaziriMkuu, Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli baada yajitihada na juhudi kuwa kubwa sana Tanzania Bara, hasa kazi

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

6

kubwa sana ambayo ilifanywa na Mamlaka ambayoimewafanya wafanyabiashara wengi sana wa dawa zakulevya nchini na wengine kukimbilia Zanzibar, ni kweli sasaZanzibar imeanza kutumika kama sehemu ya uchochoro wawafanyabiashara ambao wanakimbia kutoka Tanzania Bara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi inayofanyika hivi sasani kuhakikisha kwamba tunaanza kufanya kazi kwa pamojana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kwanza kutengenezamfumo mzuri wa kusaidia katika kuhakikisha kwambatunawabaini wafanyabiashara hata hao wanaokwenda njeTanzania Bara ambao wanakwenda Zanzibar. Piavimekuwepo vikao vya mara kwa mara kati ya Mamlaka nawataalam kutoka kule Zanzibar, lengo lake kubwa nikuhakikisha kwamba tunatengeneza mfumo mzuri waudhibiti.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimwondoleehofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kazi hiyo inaendelea natayari tatizo hilo limebainika, naamini muda siyo mrefu sanamaridhiano yakikamilika basi tutafanya kazi pia kuhakikishakwamba tunazuia na upande wa Zanzibar.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Shomari, swali la nyongeza.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kuniona. Kwa kuwa, Serikali inajizatitikuzuia suala hili la madawa ya kulevya, Je, itatuhakikishiavipi kufanya kila Mkoa wa Tanzania kuwa na sober house ilikudhibiti matatizo haya?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya WaziriMkuu, Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika mikakati ambayotumejiwekea ya kupambana na kudhibiti dawa za kulevya,moja ya mkakati ni kitu ambacho kinaitwa harm reduction.Harm reduction ni kupunguza madhara kwa watumiaji wa

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

7

madawa ya kulevya hasa wale ambao wanatumia madawaya heroin ambao wanakwenda kutibiwa kwa kutumiaMethadone.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa Serikali pamoja nakuwa na mpango wa kuweka vituo vingi vya Sober houseslakini tunatumia hospitali katika Mikoa yetu kuwa namadirisha maalum kwa ajili ya kuwahudumia watu ambaowameathirika na madawa ya kulevya. Kwa hiyo, naaminihuduma itasambaa Nchi nzima na wengi watapata hudumahiyo kupitia katika hospitali za Mikoa katika maeneo husika.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu, majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU: Mheshimiwa NaibuSpika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwanzanimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibumazuri ambayo ameyatoa hivi punde.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue nafasihii kwanza niliarifu Bunge lako Tukufu kwamba Tanzaniatumepewa heshima ya kuwa ni kati ya nchi chache ndani yaBara la Afrika ambayo inafanya vizuri, kuwa na sheria nzurina inasimamia vizuri udhibiti wa dawa za kulevya katika nchiya Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hali hiyo, Umoja waMataifa umekubaliana kwamba mwaka huu wa 2018, nchizote za Bara la Afrika, Viongozi wanaosimamia Sheria zaKudhibiti Dawa za Kulevya katika nchi zao watakuwa namkutano wao mkubwa sana lakini utafanyika ndani yaTanzania ili waweze kujifunza zaidi ni kwa kiasi gani Tanzaniaimefanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikiongeza kuhusu suala hilila kutengeneza mfumo wa utengemaa kwa waathirika wadawa za kulevya, Serikali kupitia Mamlaka kazi kubwa

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

8

tuliyoifanya katika kipindi hiki kifupi ni kuandaa miongozona utaratibu wa uendeshaji wa sober houses katika nchi yetuya Tanzania; miongozo hiyo sasa ipo tayari.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Serikali kwa kuanzakujifunza model nzuri ya sober houses katika nchi yetu yaTanzania tumetengeneza tayari tumeshajenga naMheshimiwa Waziri Mkuu mwaka jana amezindua NationalRehabilitation Center katika Mji wa Dodoma na itaanzakufanya kazi baada ya muda siyo mrefu, hiyo itakuwa nimodel ya Sober houses na rehabilitation centers nyingineambazo tunazihitaji katika nchi ya Tanzania za kuwasaidiahawa waraibu wa dawa za kulevya kurudi katika hali yao.Hivyo, Serikali inafanya kazi kubwa sana katika eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Zainab Amirswali la nyongeza.

MHE. ZAINAB M. AMIR: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Tunaona jitihada kubwa zinazofanywa naSerikali katika kudhibiti suala hili la madawa ya kulevya nawakati yanapokamatwa tunaoneshwa. Je, ni kwa ninicocaine na heroin wakati zinateketezwa hatuoneshwitunaoneshwa bangi? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya WaziriMkuu, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuruMheshimiwa Mbunge kwamba amekiri amekuwa akionauteketezaji wa mashamba ya bangi ambao kwa kipindi chaJanuari, 2017 mpaka Disemba, 2017 takribani ekari 542 zabangi zimeteketezwa na hii ikiwa ni kazi nzuri ambayoimefanywa na mamlaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake alitakakujua kwa nini hatuoni uteketezwaji wa madawa mengine

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

9

aina ya cocaine na heroin. Kwa nature ya madawa yenyewenamna uteketezaji wake uko tofauti na utaratibuunaotumika ni utaratibu ambao kwanza kabisa utahakikishatunalinda afya na mazingira vilevile upo utaratibu ambaomamlaka unautumia katika uteketezaji huu ambao kwakiwango kikubwa sana haijawa rasmi kwamba inaoneshwakila wakati, lakini ni kweli kazi kubwa imefanyika katika eneohili.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka ninapozungumzahivi sasa takribani kilo 196 za heroin zimeteketezwa ikiwa nikazi nzuri ambayo inafanywa na mamlaka. Kwa hiyo, siyokwamba kazi hii haifanyiki inafanyika lakini kwa uangalizimkubwa sana, inahitaji pia kuangalia na athari za mazingira.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi naambiwa hapa ulikuwa umesimama.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jibulake sahihi na niunge mkono kwamba ni kweli madawamengine yanateketezwa kwa uangalifu sana kwa sababuhata bangi tu nilienda kuteketeza nilipotoka pale ilibidiniende kwa Daktari kuangalia kama haijaniingia na Daktarialiniambia sijavuta. (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea naOfisi ya Rais, TAMISEMI; Mheshimiwa Livingstone Joseph LusindeMbunge wa Mtera, sasa aulize swali lake.

Na. 2

Ufanisi wa TARURA

MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE aliuliza:-

Serikali iliunda chombo kinachosimamia barabara zaVijijini na Mijini kinachoitwa TARURA:-

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

10

Je, chombo hicho kitaanza lini kufanya kazi kwaufanisi mkubwa kwani barabara hizi ni mbaya sana hasawakati wa masika?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali laMheshimiwa Livingstone Joseph Lusinde, Mbunge wa Mtera,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakala wa Barabara zaVijijini na Mijini (TARURA) ilianzishwa kwa Sheria za Wakala zaSerikali, Sura 445 na kutangazwa katika Gazeti la Serikali Na.211 la tarehe 12 Mei, 2017. TARURA imeanza rasmi tarehe MosiJulai, 2017, kwa ajili ya utekelezaji wa matengenezo yabarabara zenye urefu wa kilometa 108,946.2 katika mwakawa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, TARURA imeidhinishiwashilingi bilioni 230.8 kwa ajili ya matengenezo ya barabarazenye urefu wa kilometa 34,024. Kati ya fedha hizo, shilingibilioni 98.5 zimetolewa na kutumika kujenga barabara zenyeurefu wa kilometa 4,188.31, madaraja 35, makaravatimakubwa 43 na makaravati madogo 364.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2017/2018, barabara zilizojengwa katika Jimbo la Mtera zinaurefu wa kilometa 93.3 kwa gharama ya Sh.356,737,115.80.Barabara hizo ni:-

Handali – Chanhumba – Igandu - Nghahalezi(kilometa nne); Nghahalezi – Miganda – Idifu - Iringa Mvumi -Mlowa barabarani (kilometa tano); na Nagulomwitikila - Huzi- Ilangali (kilometa 17) kwenda Nhinhi - Wiliko (kilometa 20);Mlowa barabarani - Makangw’a (kilometa 12); Manzase –Sasajila - Ilowelo (kilometa 21.3); Chipogolo - Loje - Igungili(kilometa 14). Wakandarasi wanaendelea kufanyakazi nawanatarajia kukamilisha kazi hiyo Mei, 2018.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

11

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2018/2019, TARURA imeomba kutengewa kiasi cha shilingibilioni 243.3 kwa ajili ya ujenzi wa barabara zenye urefu wakilometa 23,465.05, ukarabati wa madaraja 117, mifereji yamvua yenye urefu wa mita 67,844 na makaravati 1,881 kwanchi nzima.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Livingstone Lusinde, swalila nyongeza.

MHE. LIVINGSONE J. LUSINDE: Mheshimiwa NaibuSpika, namshukuru Naibu Waziri kwa majibu, hata hivyonapenda kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; urefu wabarabara alizotaja na milioni 350 kweli hapo kunamatengenezo ya barabara kwa kiwango cha changaraweau ni kwa kiwango cha tope?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwamvua za mwaka huu Mungu ametupa neema zimekuwanyingi na zimetusaidia sana kwa upande wa kilimo, vilevilezimeleta uharibifu mkubwa sana wa barabara na madaraja,Mheshimiwa Waziri anatuambiaje juu ya matengenezomazuri na yenye maana kwa ajili ya wananchi kuwezakupitisha mazao yao ambayo wanategemea kuyavuna iliwaweze kujiletea maendeleo?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Mheshimiwa Josephat Kandege, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, anaulizia juu ya idadi ya kilometa ambazonimezitaja na kiasi cha fedha ambacho kimetumika je,tumetengeneza kwa ubora uliotarajiwa au tumeyatengenezakwa kutumia tope.

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

12

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza hatujatumia topekwa sababu yeye mwenyewe ni shuhuda kwambatumehama kutoka katika matengenezo yaliyokuwayanafanywa na Halmashauri pale ambapo kila MheshimiwaDiwani alikuwa akiomba angalau apate hata kilometa mojaau kalivati moja katika aeneo lake, mwisho wake inakujainafikia kwamba hata ile thamani ya pesa ambayoimetumika haikuweza kuonekana na hivyo tukawa tunarudiakila mwaka katika matengenezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishieMheshimiwa Lusinde na bahati nzuri na yeye ni shuhudaamekuwa akifanya kazi nzuri ya kupita kwenye Jimbo lakehebu akalinganishe kazi ambayo imefanywa na chombo hikicha TARURA linganishe na jinsi ambavyo kazi zilikuwazinafanyika hapo awali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la piliameongelea neema ya mvua ambayo tumepata na sisi sotetukiwa ndani ya Mkoa wa Dodoma ni mashuhuda, tumepatamvua ya kutosha, mvua ni neema, lakini kila neema nayoinakuja na dhahama yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, naombanimhakikishie chini ya TARURA na ndiyo maana kuna maeneoambayo kumekuwa na mataengenezo na maombi maalumili kuhakikisha kwamba barabara hizi zinapitika vipindi vyotena kiasi cha pesa ambacho chombo hiki kimeombewakama Bunge lako Tukufu itaidhinisha chini ya usimamizimadhubuti hakika barabara zitatengenezwa kwa kiwangokizuri na kitakachoweza kupita katika vipindi vyote.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri hebu angaliahawa Wabunge wote wana maswali na TARURA.Mheshimiwa Mary Chatanda, swali la nyongeza:

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kuniona. Kwanza napongeza TARURAkwamba wameanza kazi vizuri hususani katika Mji wanguwa Korogwe, lakini napenda kujua je, Wizara ina mpango

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

13

gani sasa wa kuwawezesha hawa TARURA hususani kwenyehizi Halmashauri za Miji pamoja na kwamba wanawapafedha za kujenga barabara zile kwa kiwango chachangarawe, sasa wapewe fedha za kutengeneza ile miferejikwa kiwango cha kutumia mawe ili kusudi wasiweze kurudiamara kwa mara kutengeneza zile barabara? Wana mpangogani wa kuwatengea fedha ili Miji hii iweze kuwa na barabarazilizo imara kwa kupitia kuweka mawe misingi yao? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu mazuri yoteya msingi ya mwanzo yaliyoweza kutolewa. Naombanimpongeze mama Mary Chatanda ni miongoni mwaWabunge ambao tulipambana sana katika ujenzi wabarabara na stendi yake ya pale Korogwe Mjini.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa utengenezajikatika Halmashauri za Mji kwanza tunatumia mradi wa UGLSPambao tunagusa takribani Manispaa na Halmashauri zoteza Mji. Kwa hiyo, naomba niwahakikishie Wabunge woteambao wako katika Halmashauri za Miji na Manispaampango wetu mkakati ni kuhakikisha maeneo hayatunayabadilisha kwa ajili ya ujenzi katika maeneo haya kwatabaka la lami. Huu ndiyo mpango wa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, katika ile MijiMikuu Saba ambayo nimezungumza tutaaendelea kuboreshasuala la mifereji, suala la barabara kwa kiwango ambachotunajua kwamba barabara zetu tunataka guarantee yamiaka 20 ndiyo tuweze kuzifanyia service, ndiyo maanahatuko katika supervision ya hali ya juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, naomba nikirikwamba TARURA tuna mtandao wa barabara takribanikilometa 108,000 ambao ni matandao mkubwa sana, lakiniukiangalia kutokana na suala la kisera la mgawanyo wa

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

14

Mfuko wa Barabara ambao asilimia 30 inakuja TARURA naasilimia 70 inaenda TANROAD, eneo hili ndilo lina changamotokubwa. Baadaye tutaangalia nini cha kufanya, lengo letukubwa ni kwamba Halmashauri zote ziweze kupitika kwasababu wananchi huko ndiko uchumi unapojengeka.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutulie kidogo.Mheshimiwa Zuberi Kuchauka, swali la nyongeza.(Kicheko)

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Ninachotaka kujua TARURA ni chombo ambaco kimeundwahivi karibuni, nataka kujua TARURA sasa kwa sababubarabara wanazoshughulikia ni zile zilikuwa zinashughulikiwana Halmashauri chini ya Madiwani. Je, hiki chombo sasakinasimamiwa na mamlaka gani kwa niaba ya wananchi,kwa sababu hawaingii kwenye Baraza la Madiwani?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kwamba TARURA ni chombo ambachokimeanzishwa hivi karibuni. Kimsingi taarifa ya kazizinazofanyika taarifa yake inapelekwa kwenye chombokinaitwa DCC na katika DCC Waheshimiwa Wabunge wotewanakuwemo kwenye kile chombo, lakini pia kila Mwenyekitiwa Halmashauri husika anahudhuria kwenye hicho kikao nandiyo fursa ambayo kwa sasa hivi TARURA inatoa taarifa juuya utekelezaji wa kazi zake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hiyo haitoshi, hatakatika vipaumbele vya barabara ambazo zinaendakutengenezwa ni wajibu wa Halmashauri kwa kushirikianana Madiwani wote tunaidhinisha barabara ambazo nivipaumbele, lakini TARURA inapelekewa kulingana na bajeti

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

15

sasa wao ndio wanasema katika hizi barabara tunaendakutengeneza barabara zipi, lakini fursa kama forum yaWaheshimiwa Madiwani bado ipo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Abdallah Saidi Mtulia, swalila nyongeza. (Makofi)

MHE. ABDALLAH S. MTULIA: Mheshimiwa Naibu Spika,Alhamdulilah.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nakushukuru sana,lakini pia nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwakunijalia uzima, nina afya njema, akili timamu na utayari wahali ya juu ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kinondonina tunasema dua la mwewe halimpati kuku. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo letu laKinondoni na Manispaa ya Kinondoni kwa ujumla TARURAinafanya kazi vizuri, tunawapongeza sana. Hata hivyo,Manispaa yetu ya Kinondoni ina barabara za kiwango chalami siyo zaidi ya asilimia 10 za barabara zote katika Manispaaya Kinondoni na tumewaambiwa wananchi tunataka kuletaKinondoni mpya; je, TARURA ina mpango gani wakutuongezea barabara zetu katika kiwango cha lami iliangalau kufikia asil imia 50 kama siyo asil imia miamoja?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) - MHE. JOSEPH S. KANDEGE:Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi niungane na Wabungewenzangu kumpongeza sana Mheshimiwa ,welcome againuko katika nafasi iliyo sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika maeneo ambayochombo chetu TARURA kinafanya kazi vizuri ni pamoja naManispaa ya Kinondoni, nimepata fursa ya kwenda

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

16

kutembelea, Halmashauri zingine zinatakiwa kwenda kuigana kutazama kazi nzuri ambayo inafanywa na TARURAKinondoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala zima lakuongeza ili angalau tufike asilimia 50 ya barabara zote kuwaza lami, kati ya Miji ambayo ina fursa ya kupata maendeleokwa maana ya miundombinu ya barabara ni pamoja ni Jijiletu la Dar es Salaam. Naamini katika mpango mzima wakuboresha Jiji la Dar es Salaam na program zinazoendeleahakika, barabara za Kinondoni zitahama kutoka hiyo asilimiakufika asilimia 50 katika kipindi ambacho siyo kirefu sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Naibu Spika,nataka tu niongezee katika majibu mazuri sana yaMheshimiwa Naibu Waziri kwamba katika eneo la Kinondoniambako Mbunge aliyeapishwa leo Mheshimiwa Mtuliaanatoka ni kwamba hiyo coverage tutaifika haraka sanakwa sababu tuna combination mbili; tuna mradi wa DMDPambao Mheshimiwa Mbunge anaufahamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu una kazi kubwasana ya kuboresha miundombinu ya barabara za lami katikaJiji la Dar es Salaam na eneo la Kinondoni ni eneo mojawapo, lakini kuna upande mwingine upande wa TARURA,kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge aondoe hofu zile ahadializozisema kwa wananchi wake, naamini ikifika mwaka 2020zote zitakuwa zimetekelezwa tena kwa zaidi.

NAIBU SPIKA: Naamini huo utekelezaji wa ahadi zoteunahusu Majimbo yote. Mheshimiwa Dkt. Godwin OloyceMollel. (Makofi)

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa NaibuSpika, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza. Hata hivyo, nitumie fursa hii kuwashukuru

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

17

wananchi wa Siha kwa kuniamini tena na kuhakikisha hawawanaosema muda nawapiga kipigo ambacho hawajawahikukisikia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna barabara yetu yakutokea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwenda kwenye Kata yaBiriri kukutana na barabara inayotokea Sanya Juu kuelekeampaka KIA (Kilimanjaro International Airport), kwa mwakajana ni katika barabara mbili ambazo zilikuwa zipandishwehadhi kuingizwa TANROAD ikashindikana ikawa imepandabarabara moja ya Mwanga. Nataka kumuuliza Waziri mwakahuu basi isidunde kama zawadi ya watu wa Siha kwa uamuziwa busara walioufanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) - MHE. JOSEPH S. KANDEGE:Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpongeze nakumkaribisha sana Dkt. Mollel na kumhakikishia kwambayuko katika nafasi ambayo ni salama sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake lakupandisha hadhi barabara ambayo anaiongelea ili iwe chiniya TANROAD.

Mheshimiwa Naibu Spika, wewe ni shuhuda kwambaWaheshimiwa Wabunge wengi tulikuwa tunapendabarabara za Majimboni kwetu zipandishwe zichukuliwe naTANROADS, lakini ni kwa nini tulikuwa tunataka zichukuliwena TANROADS? Ni kutokana na namna ambavyo barabaraambazo ziko chini ya TANROADS zimekuwa zikihudumiwakwa namna nzuri. Ndiyo maana kama Bunge tukaonakwamba ni vizuri tukaanzisha chombo ambacho kitakuwakinafanya kazi madhubuti kama ambavyo zimekuwazikifanywa na TANROADS.

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

18

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie, kwakasi ambayo tumeanza nayo na jinsi ambavyo TARURAimeanza kufanya kazi, nimtoe mashaka, barabara ambayoanaisemea chini ya TARURA itakuwa na hadhi na ubora sawana barabara ambazo zinatengenezwa chini ya TANROADS.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, sasatutaendelea na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.Mheshimiwa Ritta Enespher Kabati, Mbunge wa Viti Maalum,sasa aulize swali lake.

Na. 3

Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Nduli

MHE. RITTA E. KABATI aliuliza:-

Kiwanja cha Ndege cha Nduli kipo katika mpango waSerikali wa Ujenzi wa viwanja 11:-

(a) Je, ni lini kiwanja hicho kitajengwa?

(b) Mpaka sasa hakuna kituo cha kujaza mafutakatika kiwanja hicho; je, ni utaratibu gani unaotumika ilikiwepo kituo cha mafuta katika kiwanja hicho?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS JOHN KWANDIKWA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, naomba kujibu swali laMheshimiwa Ritta Enespher Kabati, Mbunge wa Viti Maalum,lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:

(a) Kiwanja cha Ndege cha Nduli kililichopoMkoani Iringa ni miongoni mwa viwanja 11 vya ndegevilivyofanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kinauliomalizika mwezi Mei mwaka 2017. Katika mwaka wafedha wa 2017/2018, Serikali ilitenga fedha za ndani kwa ajili

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

19

ya maandalizi ya ujenzi wa kiwanja hicho ikiwa ni pamojana kutangaza zabuni.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kutokana na Benkiya Dunia kuonesha nia ya kufadhili ujenzi wa uwanja huu,Serikali ilisitisha taratibu za ndani za manunuzi ili kusubirimanunuzi kufanyika kwa kuzingatia taratibu za Benki yaDunia. Hivyo, uwanja huo utaanza kujengwa mara mojabaada ya taratibu hizo kukamilika.

(b) Kwa sasa kiwanja hiki hakina ndege zakutosha zinazoweza kuvutia uwekezaji wa kituo cha mafuta.Ni vema ieleweke wazi kwamba sera ya uwekezaji katikaviwanja vya ndege inatoa fursa ya kuuza mafuta ya ndegekwa makampuni binafsi yenye leseni ya Mamlaka ya Usafiriwa Anga TCAA.

Mheshimiwa Naibu Spika, Makampuni yenye lesenihizo na yaliyoingia mikataba ya biashara ya mafuta ya ndegena Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania TAA ni Puma,Oilcom, Total na Prime fuels. Kwa hiyo, ni utashi wamakampuni ya mafuta na nguvu ya soko inayosukumauwekezaji wa biashara ya mafuta katika viwanja vya ndege.Ni matumaini yangu kwamba kiwanja hiki kitakapokamilikakujengwa kitawavutia wawekezaji na hatimaye kumalizatatizo hili.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Ritta Kabati,swali la nyongeza.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswalimadogo ya nyongeza. Kwanza kabisa nianze kuipongezaSerikali ya Chama cha Mapinduzi kwa mapokezi makubwakabisa ya ndege ya Bombadier ambayo jana ilitua naMheshimiwa Rais akiwa anaongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili pia niipongezeSerikali kwa kuanza sasa kujenga kiwanja chetu cha Nduli

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

20

kwa sababu nina imani kabisa sasa hata utalii utafungukakatika Mkoa wetu wa Iringa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ndege yaBombadier ina uwezo wa kutua katika kiwanja chenye urefuwa kilometa 1.2 na kiwanja chetu cha Nduli kina urefu wakilometa 1.6, tatizo ni kipande tu kidogo cha mita kama 100ambacho ni kibovu sana ambacho hakiwezi ndege kubwakutua na hata zile ndege ndogo ambazo zinatua, zinatuakwa matatizo makubwa sana na mpaka sasa hivi kiwanjachetu kina abiria karibu 20,886,000. Je, Serikali sasa haioniumuhimu sasa wa kujenga hicho kipande kidogo cha mita100 ili tuweze kupata ndege kubwa na hizo ndogo zipatekutua vizuri wakati tunasubiri huo ujenzi wa kiwanja hicho,kwa ufadhili wa Benki ya Dunia? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; nimesikiatayari zoezi la uthamini wa mali limeshaanza katika kiwanjachetu cha Nduli. Hofu yangu kubwa ni kwamba zoezi hilihuwa linafanyika mapema kabisa lakini huwa linachukuamuda mrefu sana kwa wananchi kulipwa mali zao, ninamfano halisi kabisa wa kiwanja cha ndege cha Songeaambacho toka mwaka 2010 karibu miaka nane badohawajalipwa na vilevile hata barabara yetu ile ya mchepuoilichukua karibu miaka sita mpaka wananchi kuanza kulipwa.Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha kuwa wananchihawa ambao wanapisha hiki kiwanja wanalipwa mapemazaidi?

Mheshimiwa Naibu Sika, ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaNaibu Spika, kwanza napenda nizipokee pongezi nyingiambazo amezitoa kwa kupokea ndege ambayo janaMheshimiwa Rais ameipokea. (Makofi)

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

21

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze sanaMheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia uboreshaji wa kiwanjahiki, amekuwa akifuatilia na mimi binafsi nilifika kuona haliya uwanja. Suala la kwanza ambalo amelizungumzia juu yakuongeza urefu wa kiwanja. Ilikuwa imetengwa shilingi bilioni47 kwa ajili ya upanuzi wa kiwanja hiki lakini kwa bahatinzuri tumepata fedha kwa udhamini wa Benki yaDunia tutakwenda kujenga kwa thamani ya shilingi bilioni94.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii inaonesha kwambahuduma nyingi katika uwanja huu zitakuwa zimeongezeka.Hii ni pamoja na kuweka taa za kuongozea ndege, kuongezaurefu wa uwanja na sasa huu uwanja pamoja na taazitakapowekwa utakuwa na urefu wa mita 2,500 kwa maanautaweza kumudu kiwango hiki ambacho MheshimiwaMbunge anaomba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimwombeMheshimiwa Mbunge, wananchi wa Iringa na Watanzaniakwa ujumla tuvute subira, tunaenda kuboresha huu uwanjautakwenda kuwa wa kisasa pamoja na kuweka majengo,jengo la abiria pamoja na jengo la wafanyakazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni ushahidi toshakwamba sasa hivi compensation hazichelewi kulipwa. Vikoviwanja ambavyo vinaendelea kujengwa kule Shinyanga,compensation imelipwa lakini uthamini umeshakamilika,tunaendelea kuhakiki wenzetu wa Wizara ya Fedhawanahakiki umethaminishwa kama Sh.3,043,626,000 kwa ajiliya kulipa compensation. Nimwombe tu Mheshimiwa Mbungeuvute subira, uhakiki unafanyika na mara uhakiki ukikamilikafedha hizi zitalipwa kwa wananchi. Kwa hiyo, wananchiwasubiri kulipwa compensation yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Nape Moses Nnauye, swalila nyongeza.

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

22

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Pamoja na kutambua na kupongeza kazi nzuri ambayoinafanywa katika kuboresha viwanja mbalimbali vya ndegehapa nchini, naomba kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa nilizonazo nikwamba uwanja wa ndege wa Lindi umeshafanyiwaupembuzi na usanifu. Sasa, Serikali iko tayari kuanza kutengafedha za ndani badala ya kutegemea fedha za nje kwa ajiliya kuanza ukarabati wa uwanja huu wa ndege ikizingatiwauwanja ulivyokaa kimkakati, lakini historia ya uwanja huuna mahitaji ya uwanja huu kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaNaibu Spika, nimjulishe tu Mheshimiwa Mbunge kwambaavute subira wakati wa bajeti ataona kwamba tumewekafedha za kutosha kupitia mapato ya ndani. Ile asilimia yafedha ambazo tumetenga kupitia mapato ya ndani nikubwa. Kwa hiyo, ilikuwa sio vema nizungumze hapa lakinilabda kama baadaye tunaweza tukaonana nimwoneshe,lakini wakati wa bajeti tutaonesha namna ambavyo Serikaliimedhamiria kuboresha viwanja vyake kupitia mapato yandani. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maftaha, swali la nyongeza.

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Naomba kuuliza swali la nyongeza kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, uwanja wa ndege waKanda ya Kusini ni uwanja ambao upo Mtwara Mjini na uleuwanja wa Mtwara Mjini nimekuwa nazungumza sanakwenye Bunge hili kwamba ni uwanja ambao hauruhusundege kuweza kutua wakati wa usiku, miaka ya nyuma huko

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

23

taa zilikuwepo zikaondolewa. Je, mpango wa Serikali waahadi inazotoa kila mwaka wa kukarabati na kuweka taaza kuongozea ndege Mtwara Mjini kiwanja hiki cha Kandaya Kusini utaanza lini.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Maftaha kwakuendelea kufuatilia ujenzi huu wa uwanja wa ndege waMtwara. Kikubwa tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge nikwamba katika Bajeti ya fedha ya mwaka uliopita kulikuwakumetengwa fedha, pia katika mwaka huu unaokuja kwaajili ya kuongeza zile huduma ambazo zilikuwa zimepunguakatika uwanja huu tumeweka fedha za kutosha. Kwa hiyo,avute tu subira, nimefika uwanja wa ndege wa Mtwaranimeuona kwanza sasa hivi huduma zinaendelea vizuri, hilizoezi la taa litakamilika tu Mheshimiwa Mbunge asiwe nawasiwasi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Edward Franz Mwalongo,swali la nyongeza.

MHE. EDWARD F. MWALONGO: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi. Naomba niiulize Serikali,je, ni lini uwanja wa ndege wa Njombe utawekwa lami?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano. majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaNaibu Spika, uwanja wa ndege wa Njombe ni kati ya viwanja11 ambavyo viko kwenye utaratibu wa kuboreshwa.Kulikuwa kuna changamoto kidogo pale ya wale majiranikwenye uwanja Mheshimiwa Mbunge anatambua, kunawatu wameendelea kuweka majengo marefu kandokandoya uwanja huo.

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

24

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na mawazo yakuuhamisha ule uwanja ili uwe nje ya sehemu hiyo uliopo.Kwa hiyo, zoezi hilo tuliwaachia wataalam waendeleekuliangalia itakapokuwa imekamilika au itakapokuwaimeonesha tofauti basi tutaendelea na hatua ya kuujengahuu uwanja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu changamotozil izokuwepo na Mheshimiwa Mbunge tumekuwatukizungumza nae, lakini nasi tumelichukulia hatuatumewaagiza wataalam wa upande wa TAA na Mkoawaweze kukaa na kuona kama tutauhamisha huu uwanjabasi tusichelewe kuchukua hizo hatua ili tuweze kufanyaujenzi wa uwanja huu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, nashawishikakukutajia viwanja vya Wabunge waliosimama hapa kwasababu muda wetu umekwenda. Naona Mbunge wa Songeauwanja wa Songea, Mbunge wa Ileje kasimama na Singidanaona ameshasimama. Mheshimiwa Naibu Waziri naombauwatazame hawa watu ili bajeti yako itakapofika uwe namajibu ya kuwapa. Waheshimiwa Wabunge naomba tukae,muda wa swali hili umekwenda sana.

Tunaendelea na Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mheshimiwa Dkt. Steven Lemomo Kiruswa, Mbunge waLongido sasa aulize swali lake.

Mheshimiwa Kiruswa naomba utumie microphone yakiti kinachofuata kwa sababu hiyo haisikiki.

Na. 4

Mradi wa Maji kutoka Mto Simba hadi Longido

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA aliuliza:-

Upungufu wa maji safi na salama kwa matumizi yabinadamu na mifugo ni moja ya kero kubwa kwa wananchi

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

25

wa Wilaya ya Longido. Vyanzo vya maji vilivyoko ni vichachena ni vya muda (seasonal) na mahali pengine hakunakabisa:-

(a) Je, utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuletamaji ya bomba kutoka Mto Simba ulioko Siha, MkoaniKilimanjaro hadi Mji wa Longido kilometa 64 unaogharimushilingi bilioni 16 umefikia hatua gani?

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuendelezausambazaji wa maji hayo ili yawafikie wananchi wapatao23,000 waishio katika Kata Kimokouwa na Namanga piaKiserain ambazo zipo umbali wa kuanzia kilometa 15 - 25 tutoka Longido Mjini?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naUmwagiliaji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. StevenKiruswa, Mbunge wa Longido, lenye sehemu (a) na (b), kamaifuatavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatekeleza mradiwa uboreshaji wa huduma ya upatikanaji wa maji katika Mjiwa Longido. Mradi huo umegawanyika katika vipande vinne.Utekelezaji wa kipande cha kwanza unagharimu shilingi bilioni10.89. Hadi mwezi Machi 2018, utekelezaji wa kipande hichoumefikia asilimia 15. Utekelezaji wa kipande cha piliunagharimu shilingi bilioni 2.54.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi mwezi Machi 2018utekelezaji wa kipande hicho umefikia asilimia 40. Kipandecha tatu kinagharimu shilingi milioni 276.36. Hadi mwezi Machi2018 utekelezaji wa kipande hicho umefikia asilimia 90.Kipande cha nne kinahusu ulazaji wa mabomba yausambazaji maji katika Mji wa Longido kwa gharama yashilingi bilioni 2.09 ambapo utekelezaji wa kipande hichoumefikia asilimia 85.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu umesanifiwakutoa huduma kwa Kata za Longido, Engikaret na Orbomba

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

26

zenye jumla ya wakazi 16,712 kwa takwimu ya sensa ya watuwa makazi ya mwaka 2012, ambapo Kata ya Longido inawakazi 2,285; Kata ya Orbomba 7,900; na Engikaret ya wakazi6,527; na inatazamiwa idadi ya watu ikafika 26,145 kwa Katazote tatu ifikapo mwaka 2024 kwa ongezeko la asilimia 3.8kwa mwaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, Kata za Kimokouwa,Namanga na Kiserian zitaingizwa katika mpango wa awamuya pili ya uzambazaji maji baada ya mradi huu kukamilika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kiruswa, swali lanyongeza.

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana na naomba niulize maswali mawilimadogo ya nyongeza. Kabla ya yote nipende kuishukuruSerikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli kwakutupatia mradi huu mkubwa wa kutuletea maji safi nasalama kwa ajili ya binadamu na mifugo toka MlimaKilimanjaro Mto Simba.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwawananchi wa hizi Kata tatu zilizolengwa na mradi huu wanashauku kubwa ya kupata maji haya ikizingatiwa kwambaWilaya hii ni kame, Je, mradi huu unategemewa kukamilikalini?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kufahamuuhaba wa maji katika Wilaya ya Longido Mheshimiwa Waziriwa Maji na Umwagiliaji alipotembelea Longido mwaka janaaliwaahidi wananchi wa Kijiji cha Wosiwosi wanaoishipembezoni mwa Ziwa Natron lenye maji yasiyofaa kwamatumizi ya binadamu pamoja na wananchi wa Kata yaTingatinga katika Kijiji cha Tingatinga kwamba atawapatiamabwawa ya maji; je, ahadi hii ataitimiza lini?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

27

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii kumpongeza sanaMheshimiwa Mbunge kwa namna ya kipekeeanavyowatetea wananchi wake wa Longido. Kubwa tuitambulike kutokana na changamoto kubwa sana kwa Mjiule wa Longido katika suala zima la maji, Wizara yetu ikaonahaja ya kuwapatia wananchi wale maji safi na salama naya kuwatosheleza, lakini anataka kujua ni lini mradi uleunakamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi ule unakamilikamwishoni mwa mwezi Mei. Mimi kama Naibu Waziri nilipatanafasi ya kufika pale katika kuhakikisha tunausukuma mradiule ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, nilipofika katika uleutekelezaji wa mradi nimemkuta Mkandarasi amelala,nilimtikisa kwa mujibu wa mkataba ili mwisho wa sikuwananchi wake wapate maji. Nataka nimhakikishietutashirikiana ili wananchi wake waweze kupata maji safina salama kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la ahadi yaMheshimiwa Waziri ya mabwawa, nataka nimhakikishieahadi ni deni. Sisi kama Wizara ya Maji kwa kuwa MheshimiwaWaziri ameahidi tutatekeleza kwa wakati katika kuhakikishawananchi wake wanapata maji.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Stephen Ngonyani, kwasababu lazima upande wa Upinzani wapewe nafasi jamani.(Kicheko)

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Kwa niaba ya Kambi Mbadala, kwanzaniwapongeze Wizara hii ya Maji kwa kufanya kazi vizuri hasamdogo wangu kwa kubeba ndoo kichwani. Kule Mnyuzikatika Kijiji cha Lusanga kuna mradi mkubwa wa maji ambaoupembuzi yakinifu umeshafanyika na maji hayo yangewezakufika mpaka Shamba Kapori; je, mradi huu mpaka sasa hiviumefikia wapi?

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

28

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana. Hata hivyo,nimpongeze Kaka yangu Mheshimiwa Maji Marefu kwanamna anavyowapigania wananchi wake wa Jimbola Korogwe Vijijini. Nataka nimhakikishie yeye ni jembewembe!

Mheshimiwa Naibu Spika, kikubwa kama alivyokuwaamesema, upembuzi yakinifu umeshakamilika, kubwanimwombe tu Mhandisi wa Maji wa Korogwe Vijijini asilale.Ahakikishe kwamba anatangaza ile kazi ili mwisho wa sikuMkandarasi apatikane na utekelezaji wa mradi uanze maramoja na Wizara ya Maji hatutokuwa kikwazo katikakuhakikisha tunawapa fedha ili mradi ule ukamilike kwawakati. Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Martha Mlata, swali lanyongeza.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Kwanza niipongeze Serikali kwa mkakati mkubwainayoweka kuhakikisha wananchi wote kwenye vij i j iwanapata maji. Hata hivyo, tukirudi nyuma historia nikwamba Serikali ilipochimba visima iliachia Kamati za Majikuendesha visima hivyo. Je, Serikali kwa sababu imejizatitikupeleka maji kila kata na vijiji, ina mpango gani ya kuchukuawale wanafunzi wenyeji waliomaliza Kidato cha Nnewakajifunze Chuo cha Maji kwa ajili ya kuja kusimamia visimahivyo ili viweze kutumika kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni hilo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu.

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

29

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru. Pia nimshukuru sanaMheshimiwa Mbunge, mama yangu, kwa swali zuri, lakinikikubwa na sisi tumepokea ushauri. Tulivyoanzisha miradi yamaji na kuhakikisha wananchi wanapata maji, lakini lazimakuwe na usimamizi, tukaona haja ya kuwashirikisha wananchikatika kuhakikisha kwamba, kunakuwa na jumuiya zawatumiaji maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pamoja na nia njemaya kuweka jumuiya ya watumiaji maji, lakini kumekuwa nachangamoto za aina yake. Sisi kama Wizara ya Majitumekuwa na Chuo cha Maji kipo pale Ubungo; ni fursa pianiwahamasishe vijana wenzangu wapate nafasi ya kufikapale na sisi kama Wizara tutaangalia namna ya kuwezakuwasaidia katika kuhakikisha na wao wawe sehemu yakumiliki miradi ile ya maji. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Musa Ntimizi, swali lanyongeza.

MHE. MUSA R. NTIMIZI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru na nashukuru kwa majibu mazuri ya MheshimiwaNaibu Waziri, lakini shida ya ya maji Longido ni sawasawana shida ya maji iliyopo Jimbo la Igalula. Maeneo mengi yaJimbo la Igalula maji chini hayapatikani kwa urahisi, visimavingi vimechimbwa lakini havitoi maji na kusababishakupotea fedha nyingi za Serikali; lakini yako maeneo mengiambayo yanaweza yakachimbwa mabwawa na yakasaidiaupatikanaji wa maji katika Jimbo la Igalula.

Mheshimiwa Naibu Spika, utafiti umeshafanyika,upembuzi yakinifu na usanifu katika Kata ya Goweko naIgalula umeshafanyika, lakini mpaka sasa miradi hiihaijafanyika na miradi hii ilikuwa kwenye bajeti ya Serikali yamwaka 2016/2017, lakini mpaka sasa hakuna kinachofanyika.Sasa naomba kujua miradi hii ni lini itatekelezwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

30

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru. Moja tu, ukimwonamtu mzima analia ujue kuna jambo. Sasa mpaka MheshimiwaNtimizi analia maana yake Igalula kuna hali mbaya sanakatika suala zima la maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Wizara ya Maji nakwa kuwa, sisi si Wizara ya ukame, tupo tayari kushirikiananae katika kuhakikisha tunawachimbia mabwawa iliwananchi wake waweze kupata maji kwa wakati. Ahsantesana.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwatunaendelea, Mheshimiwa Lucy Fidelis Owenya Mbunge waViti Maalum, swali lake litaulizwa kwa niaba na MheshimiwaMarwa Ryoba Chacha, Mbunge wa Serengeti.

Na. 5

Mradi wa Maji wa Kata ya Old Moshi

MHE. MARWA R. CHACHA (K.n.y. MHE. LUCY F.OWENYA) aliuliza:-

Mradi wa Maji Vijijini katika Kata ya Old MoshiMagharibi katika Kijiji cha Mande haujatekelezwa kuanziamwaka 2008;

Je, ni sababu zipi zi l izosababisha mradi huokutokamilika?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaji na Umwagiliaji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa LucyFidelis Owenya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

31

Mheshimiwa Naibu Spika, katika awamu ya kwanzaya utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji(WSDP I) Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ilipanga kutekelezamiradi ya maji katika vijiji 12. Kati ya vijiji hivyo ujenzi wa miradiumekamilika katika vijiji sita vya Korini Juu, Korini Kati, KoriniKusini, Kilima Juu, Kilima Kati na Golo na utekelezaji wa miradiiliyobaki unaendelea kufanyika katika awamu ya pili yaProgramu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP II).

Mheshimiwa Naibu Spika, usanifu wa mradi wa majiwa Tela Mande ulikamilika mwaka 2013. Mkandarasialiyeteuliwa hakuweza kuanza kazi na ulichelewakutekelezwa kutokana na ufinyu wa bajeti. Halmashauri yaWilaya ya Moshi iliutangaza mradi huu katika mwaka wafedha 2017/2018 na kwa sasa mradi huo upo kwenye hatuaya tathmini (evaluation) ili kumpata mkandarasi wa ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, uUtekelezaji wa mradi huuunategemea kuanza mwezi Mei, 2018. Mradi huuutakapokamilika utahudumia wakazi 5,141 kulingana nasensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kwa Vijiji vya Telana Mande.

NAIBU SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Marwa RyobaChacha swali la nyongeza.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa NJaibu Spika,nina maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, mradi huuumechukua muda mrefu sana. Ukiangalia kwenye swali lamsingi ni tangu 2008, lakini ukija kwenye majibu anasemausanifu umekamilika tangu 2013. Pamoja na kwamba Serikaliinasema wako kwenye evaluation wananchi wa Wilaya yaMoshi na hususan wa Kata ya Tela wanataka kujua, huu mradiumetengewa shilingi ngapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; katika Wilayaya Serengeti kuna miradi ya maji kwenye Vij i j i vyaNyagasense, Rung’abure na Kibanchebanche. Mradi waNyagasense hautoi maji na walishalipa retention yote. PiaMradi wa Rung’abure hautoi maji. Mradi wa Kibanchebanche

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

32

mkandarasi ametokomea na nimemwambia MheshimiwaWaziri twende Serengeti, hatukwenda mpaka leo,wameshalipa mpaka retention lakini miradi haitoi maji. Ninini tamko la Wizara dhidi ya matatizo haya ambayoyametokea, wamelipwa fedha zote miradi haitoi maji?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, swali la nyongeza la kwanza linahitaji takwimu.Kama unazo unaweza kujibu kama huna kikanuni utampaMheshimiwa Mbunge majibu baadaye, lakini karibu kwamajibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimjibu swali kaka yanguMheshimiwa Marwa Chacha, moja alitaka kujua gharamaya mradi; gharama ya mradi itagharimu kiasi cha milioni mianane ishirini na mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili;kuna baadhi ya miradi ambayo imeshalipwa fedha za Serikalilakini haitoi maji. Nataka nimhakikishie sisi kama Wizara yaMaji na kama viongozi; maana unapokuwa Naibu Waziri, nijukumu lako kuhakikisha wananchi wanapata maji. Sisihatutamwonea haya yeyote ambaye amefanya ubadhirifuwa fedha za Serikali. Kama kweli kuna fedha ambazo kunamtu amezila, basi ajiandae kuzitapika ili wananchi wawezekupata maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Shally Raymond, swali lanyongeza.

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Naomba kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwahali ya kusuasua kwa huu mradi wa Mande, Tela kunafananakabisa na miradi mingine iliyo katika maeneo ya tambarareya Mkoa wa Kilimanjaro, ukiweko ule mradi wa Mwangampaka kule Hedaru mpaka Mombo. Ni lini sasa Serikali itatupamuda muafaka wa kukamilika kwa miradi hiyo?

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

33

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru. Tunapozungumziasuala la maji, maji hayana mbadala, si kama wali, ukikosawali eti utakula ugali. Kwa hiyo kuna haja kubwa sana yakuhakikisha wananchi wanapata maji kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa sisi kama Wizara yaMaji katika kuhakikisha wananchi wanapata maji kwawakati lazima kuwe na ufuatiliaji na usimamizi wa karibu.Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, sisi kama Wizaraya Maji tumejipanga katika kufuatilia na kusimamia miradihii kwa wakati ili wananchi waweze kupata maji kwa mudamuafaka uliopangwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mary Nagu

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipa fursa. Naomba niipongezeWizara na Serikali kwa kutengea fedha Mradi wa Endasak,Endagao na Endeshwal na Mradi wa Malama.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hivyo miradi hiimiwili imepangiwa shilingi bilioni 1.31 na bilioni 1.2 mradi wapili na naishukuru Serikali kwa kuanza kutekeleza mradi, lakiniimechukua muda mrefu sana. Naomba kujua kutoka kwaMheshimiwa Waziri, ni lini kasi itaongezeka ili miradi hii miwiliiweze kukamilika kwa sababu Wilaya ya Hanang ilivyo chiniya Rift Valley ina ukame na watu wanapata shida kubwasana ya kutafuta maji?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

34

hii lakini nimpongeze sana Mheshimiwa Mary Nagu, mamayangu kwa namna anavyowapigania wananchi wake.Kubwa ni kwamba sisi kama Wizara ya Maji jukumu letu nikuwapatia wananchi maji. Zipo changamoto ambazotumekumbana nazo, moja ni wakandarasi ambaowamekuwa wakifanya kazi kwa kusuasua.

Mheshimiwa Naibu Spika, labda nimhakikishieMheshimiwa Mbunge, sisi kama Wizara tumejipanga kwamkandarasi ambaye atatuchelewesha katika kuhakikishawananchi wanapata maji, hatuna sababu ya kujadiliananaye, tutamwondoa, tutamweka mtu ambaye atawezakufanya kazi kwa wakati ili wananchi waweze kupata majikwa muda uliopangwa. Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabungetutaendelea na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Jaffar Sanya Jussa, Mbunge wa Paje, sasa aulizeswali lake. Swali lake litaulizwa kwa niaba na MheshimiwaUssi Pondeza.

Na. 6

Hitaji la Samani na Gari kwa Vituo vya PolisiPaje na Jambiani

MHE. USSI SALUM PONDEZA (K.n.y. MHE. JAFFAR SANYAJUSSA) aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itavipatia Vituo vya Polisi vya Pajena Jambiani samani za ofisi pamoja na magari kwa ajili yapatrol?

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Jaffar Jussa, Mbunge wa Paje, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna uhaba wamagari pamoja na samani katika Vituo vya Polisi vya Paje

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

35

na Jambiani, kama ilivyo kwenye maeneo mengine hapanchini. Kwa sasa Vituo vya Polisi cha Paje na Jambianivinapata huduma za doria kutoka kwa OCD wa Makunduchi,hali inayosababisha kuwa na changamoto katika utekelezajiwa majukumu ya kiusalama.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jeshi la Polisi lipo katikamchakato wa kupokea magari mapya yaliyonunuliwa naSerikali ambayo yatagawawiwa kwa kuzingatia kiwango chauhalifu, idadi ya watu na ukubwa wa eneo katika kamandihusika. Aidha, Jeshi la Polisi litaendelea kutumia bajetiinayotengwa kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwalinakuwa na vitendea kazi vya kutosha, ikiwa ni pamoja namagari na samani katika vituo vya Polisi kote nchini.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ussi Pondeza, swali lanyongeza.

MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Vile vile nampongeza Mheshimiwa Waziri kwamajibu yake mazuri, lakini nina swali moja la nyongeza. Tatizola samani katika vituo vya Zanzibar, zaidi katika Majimbo yaChwaka, lakini yako katika Wilaya nyingi za Zanzibar yote.Jimboni kwangu kuna Kituo cha Chumbuni ambachokinahudumia wilaya mbili, Wilaya ya Magharibi na Wilaya yaMjini, lakini kituo hiki hakina samani, hakina gari, kinahudumiawatu zaidi ya 70,000 na kinavuja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeshalisemea sana sualahili na nimeshaliuliza zaidi ya mara tatu, mara nne nanikaahidiwa kitatengenezwa na huduma zitapatikana, lakinimpaka leo hali iko vile vile. Je, Mheshimiwa Wazirianatuambia nini wananchi wa Chumbuni kuhusu suala letuhili?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

36

kwa kuwa mfuatiliaji sana wa masuala ya jimbo lake namasuala yanayohusu Vituo vya Polisi vilivyoko katika Jimbolake. Amekuja Mara kadhaa akisemea jambo hilo natulishatuma wataalam wetu wafanye tathmini ili tuwezekujua namna tunavyoweza kulishughulikia. Kwa kuwatunaelekea kwenye bajeti niendelee tu kumhakikishiakwamba, punde bajeti inavyoruhusu tutaweka kipaumbelekwenye jambo hilo ambalo amekuwa akilisemea mara kwamara.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anne Kilango Malecela,swali la nyongeza.

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kupata nafasi. Kwa kuwa mwaka 2015nilipokuwa Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki nilitoaufadhili wa gari la golisi kwenye Kituo cha Kata ya Maorekwa ajili ya Jimbo la Same Mashariki; nina uhakika Serikaliinalifahamu hilo. Kwa kuwa, lile gari sasa halina matairi,linahitaji kufanyiwa maintainance kubwa. Je, Serikali mnatoaahadi gani leo hapa ili wananchi wa Same Mashariki wasikie?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mhesimiwa MbungeAnne Kilango Malecela kwa kusaidia kazi za Ofisi ya Polisikatika Jimbo la Same Mashariki kuweza kufanya kazi nawanakukumbuka sana. Nimefika mwenyewe Same nimeonawakikukumbuka.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba Serikaliinatambua jitihada alizofanya Mheshimiwa Mbunge natutaongea na Kamanda wa Polisi wa Mkoa ili tuweze kuonanamna ambavyo tunaweza tukaunga mkono jitihada hizoambazo Mheshimiwa Mbunge ulizifanya. Hata hivyoniendelee kukuomba uendelee kuwakumbuka wananchi wa

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

37

Same kwani wanakukumbuka sana ili vitu kama vile matairiwasiendelee kuvikosa, waendelee kupata kama ulivyokuwaunafanya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Masoud, swali la nyongeza.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru. Kituo cha Polisi cha Kingeja, Jimbo laMtambire ni kibovu, chakavu na kimekaliwa tangu enzi yaukoloni. Kumekuwa na ahadi ya Serikali karibu miaka 13kwamba watakijenga kituo kile, lakini dalili hazioneshikwamba kuna nia njema ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali ituambieina mkakati gani wa ziada kuhakikisha kwamba, Kituo chaPolisi cha Kingeja kinajengwa sambamba na Kituo cha Polisicha Mkoani hasa ukizingatia kuna vifaa vya Polisi ambavyotayari vimewekwa katika eneo la Wilaya ya Mkoani ambavyovinatakiwa viweze kusambazwa. Je, Kituo cha Polisi chaKingeja…

NAIBU SPIKA: Hilo ni swali la pili, Mheshimiwa Masoud.Hii ni nafasi ya swali la nyongeza.

Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba nia ya Serikali ni njema na utaona kwamba, wikimoja iliyopita Mheshimiwa Makamu wa Rais alikuwa ziaranikule pamoja na Naibu Waziri. Pia utaona kwamba,wamefanya shughuli kubwa ambayo inahusu ujenzi wa vituona kazi inaendelea. Kwa hiyo kazi ile inayoendelea itafikapia mpaka Jimboni kwako pamoja na kituo kile ulichokitajana vituo vingine ambavyo vinahitaji huduma kama hiyo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Deo Sanga, swali lanyongeza.

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

38

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kuniona. Kwa kuwa, Kituo cha PolisiMakambako ni kituo cha kiwilaya na kwa sababuMakambako ndipo katikati ya kwenda Songea, Mbeya naIringa; na kwa sababu, Waziri alituahidi kutupatia kitendeakazi cha gari. Je, ahadi yake ya kutupatia gari iko pale paleili shughuli za kipolisi pale ziweze kufanyika kwa ufanisi mzuri?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli pana uhitaji mkubwa wa gari katikaKituo cha Makambako. Niendelee kusema tu kwamba,Serikali inaendelea kuweka umuhimu mkubwa wa kukipatiagari kituo kil ichopo hapo na punde magariyatakapopatikana tutaweka kipaumbele kile kamaambavyo tuliahidi.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea,Mheshimiwa Rose Cyprian Tweve, Mbunge wa Viti Maalumsasa aulize swali lake.

Na. 7

Ongezeko la Ajali za Barabarani Nchini

MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza:-

Kumekuwa na idadi kubwa ya ajali nchinizinazosababisha vifo, majeruhi na upotevu wa mali:-

(a) Je, kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia 2016– 2018 ni ajali ngapi zimetokea na kusababisha vifo aumajeruhi?

(b) Je, ni waathirika wangapi waliomba fidia nawangapi mpaka sasa wamelipwa fidia zao kutoka kampuniza bima?

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

39

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Rose Tweve, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuliarifuBunge lako Tukufu kuwa katika kipindi cha mwaka 2016 hadi2018 Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabaranililichukua hatua za makusudi kupunguza ajali ambapompaka kufikia Disemba, 2017 limefanikiwa kupunguza ajaliza barabarani kwa asilimia 43.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2016 kulitokea jumlaya ajali 9,856 ambazo zilisababisha vifo 3,256 na majeruhi2,128. Mwaka 2017 kulitokea ajali 5,310 ambazo zilisababishavifo 2,533 na majeruhi 5,355 wakati kwa kipindi cha Januarihadi Februari, 2018 zimetokea ajali 769 ambazozimesababisha vifo 334 na majeruhi 698.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi chamwaka 2016 hadi 2018 jumla ya waathirika wa ajali 1,583walilipwa fidia yenye jumla ya thamani ya fedha za kitanzaniabilioni 7.3 kutoka kampuni mbalimbali za bima.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rose Cyprian Tweve, swalila nyongeza.

MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Mheshimiwa Waziri mimi nilikuwa veryspecific kwenye swali langu la msingi, niliuliza ni watu wangapiwaliomba fidia na wangapi wamelipwa mpaka sasa hivi.Kwa maelezo yako Mheshimiwa Waziri inaonesha jumla yavifo na majeruhi ni zaidi ya elfu 14, hiyo ni kwa mwaka 2016mpaka 2018 na ambao wamelipwa fidia mpaka sasa hivi niwatu 1,583, ni kama asilimia zaidi ya 10 kidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ikumbukwe kuwa mwaka2009 Bunge lilipitisha Sheria namba 10 ili kuwalinda waathirikawa ajali hizo. Sasa Mheshimiwa Waziri hawa wenzetu ambao

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

40

wanaoshughulikia hili suala la bima hawa wenzetu wa TIRA(Tanzania Insurance Regulatory Authority) inaonesha kabisakuna upungufu. Ambao wamekuwa beneficiary wakubwawa hii issue ya bima ni hizi kampuni ambazo yanakatishabima, lakini ajali inapotokea inaonesha kabisa Watanzaniawamekuwa ni waathirika wakubwa ambao wameachiwamzigo mkubwa. Sasa Mheshimiwa Waziri huoni ni wakatimuafaka sasa tuanzishe idara maalum ambayo itakuwainatoa elimu kwa Watanzania pale ajali inapotokea ili wajuehatua stahiki ambazo wanatakiwa kuchukua ili walipwe fidiazao?

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa RoseTweve kwa ku-take serious concern ya Watanzaniawanaopata matatizo hayo na kutokupata fidia amakuchelewa kupata fidia. Niseme tu kama Serikali tunapokeawazo lake na kwa sababu tuna wataalam wazo hilolitachambuliwa kitaalam.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe rai kwa Watanzaniakuchukua hatua haraka za kufuata taratibu zinazotakiwabadala ya utaratibu ambao maeneo mengi wamekuwawakifanya panapotokea matatizo ya aina hiyo; kuamuakuchukua sheria mikononi ama kuamua kufanya taratibu zanjia za mkato ambazo zinasababisha wao kukosa kileambacho walitakiwa wapate.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Fatma Toufiq, swali lanyongeza.

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa fursa kuweza kuuliza swali lanyongeza. Kwa kuwa hizi ajali za barabarani zinatokana nauzembe wa baadhi ya madereva na baadhi ya madereva

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

41

kutumia simu wakati wakiwa wanatumia vyombo ya moto.Je, Serikali ina mkakati gani wa kurekebisha Sheria ya UsalamaBarabarani ili kuwachukulia hatua kali zaidi hawa maderevaambao wamekuwa wakitumia simu wakati wakitumiavyombo vya moto? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwambakweli kuna kiwango kikubwa cha ajali zinatokea kutokanana uzembe. Ukiangalia hata kwenye kumbukumbu zaiditakribani ya matukio zaidi ya 1,500 yanatokana na uzembe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kile alichokisema chakurekebisha sheria na kuchukua hatua tunaendelea nautaratibu huo na tunasema tunakokwenda tutaanza hatakutumia taratibu ambazo nchi zingine wanatumia kwa ku-count down dereva ambaye anapatikana sana na makosaaweze kukosa sifa za kuendelea kumiliki leseni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunalifanyia kaziwazo lake na nimpongeze sana kwa kuguswa na jambo hilikwa sababu limekuwa likisababisha hasara sana kwa familiana kwa Taifa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Goodluck Mlinga, swali lanyongeza.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Wazirikwa kazi nzuri ambayo anaifanya. Swali langu ni hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ajali zinaendelea kutokeakwa wingi, hata hivi sasa hivi ninavyoongea ukipita barabaraya Morogoro – Dodoma kuna ajali nyingi sana, lakini trafficwamegeuka agent wa TRA kazi yao ni kusimamisha magarina kutoza faini. Sasa Mheshimiwa Waziri naomba atoe tamkokuanzia leo hii matrafiki waache kutoza faini wakazane na

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

42

kutoa elimu kwa kutoa elimu kwa watumia vyombo vyamoto na wasafiri ili wajue ni haki gani watapata pindi ajalizinapotokea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, moja, sisi kama Wizara ya Mambo ya Ndani naJeshi la Polisi, kutoza faini ama kukusanya faini si kipaumbelechetu; sisi kipaumbele chetu ni maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuwa imepitamiaka mingi sana ya kutoa elimu na tunaendelea kuonakama ambavyo Mheshimiwa Mbunge alisema uzembe badouko mwingi sana ndipo tunapokwenda kwenye hatua hiyoya kutoza faini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kama Watanzaniawatazingatia kwamba wamebeba dhamana kubwa yamaisha ya Watanzania na maisha yao wao wenyewe,wakawa waangalifu hili suala la faini litakuwa limeisha, lakinikwa kuwa tunawapenda zaidi na tunapenda zaidi maishayao ndiyo maana tunakuwa hatuna njia nyingi zaidi yakuchukua sheria kali ili kuweza kuokoa maisha yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nitoe rai kwa Jeshila Polisi kuendelea kuwa strictly, kuendelea kuwa wakalipunde watu wanapofanya mzaha na huku wakiwawamebeba abiria ili kuweza kuokoa maisha yanayopoteakutokana na ajali nyingi zinazotokea barabarani. Jambo hilininalolisemea ni kwa vyombo vya moto vyote, ukianziamagari ambayo si ya abiria pamoja na bodaboda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nalisisitiza sana hili kwasababu tumeshuhudia vifo vikiwa vimetokea na paletunapokwenda kwenye kuokoa miili tunakuta watu walikuwatayari walishaandikiwa faini ikiwa ni kwamba wameambiwa

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

43

kwamba wanakwenda mwendo kasi. Hata hivyo, pamojana faini wanaendelea na mwendo kasi ama na uzembe nabaadaye inagharimu maisha ya Watanzania.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Venance Mwamoto, swalila nyongeza.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi hii na mimi niweze kuulizaswali. Kwa kuwa kuna upungufu mkubwa wa askari katikabaadhi ya sehemu na askari wengi sana kwa maana ya trafficwako barabaran, je, Serikali sasa haioni imefikia wakati wakuweza kupata kamera au teknolojia nyingine badala yakutumia askari ambao kwa kweli utendaji wao hauna tija.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Mwamoto kwajambo hilo alilolitoa. Ni kweli kuna uhitaji mkubwa sana wakuhamia kwenye teknolojia, nchi nyingi zilizoendelea ndioutaratibu unaotumika. Sisi kama Serikali wataalamwanaendelea kufanyia kazi jambo hilo ikiwepo na kufanyaupembuzi yakinifu ili kuweza kujua mahitaji pamoja namaeneo ambayo tunaweza tukaanza nayo ili kuwezakupunguza adha inayojitokeza; kwa sababu kwanza tukukaa kwenye jua kukaa kwenye mvua pamoja na uchachewa askari inasababisha ufanisi kupungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, jambo lake hilotunalifanyia kazi na nimpongeze sana kwa kuleta hoja hiyomakini, lakini nimpe pole tu kwa yeye ni ndugu yangu kwayale yaliyotokea Jumamosi, yaliyotokea tarehe moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Suleiman Ally Yussuf,Mbunge wa Mgogoni, sasa aulize swali lake.

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

44

Na. 8

Jeshi la Polisi Kukamata Watu Pasipo Ushahidi Zanzibar

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF aliuliza:-

Kuna ushahidi wa kutosha kwamba kuna watukadhaa ambao wamekuwa wakikamatwa na Jeshi la PolisiUnguja na Pemba huku baadhi yao wakifunguliwa mashtakana wengine kuachiwa:-

(a) Je, ni kwa nini Jeshi la Polisi linashindwa kufanyakazi kwa weledi na kukamata watu pasipo ushahidi kwalengo la kukomoa tu?

(b) Ili kulisafisha Jeshi la Polisi, je, Serikali haioni hajaya kuwawajibisha watendaji ambao wenye tabia yakuwakomoa wananchi kwa kuwakamata pasipo ushahidi?

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Dkt.Suleiman Ally Yussuf, Mbunge wa Mgogoni, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Jeshi la Polisi ni chombokilichoundwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria na linatekelezamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba na Sheria na kanunina taratibu zilizopo, jukumu lake kuu likiwa ni kulinda usalamawa raia na mali zao. Jeshi la Polisi limepewa mamlaka yakisheria ya kukamata, kuhoji na kuweka watuhumiwamahabusu kwa muda ulioruhusiwa kisheria endapo itabainikakuwa kuna viashiria au taarifa ya kuhusika katika kutendakosa la jinai.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa sheria nakanuni na taratibu za utendaji zinazoongoza Jeshi la Polisilinapobainika askari amebambika kesi kwa sababu zozotezile huchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu ikiwamokufukuzwa kazi.

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

45

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Suleiman Ally Yussuf,swali la nyongeza.

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: Mheshimiwa Naibuwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuulizamaswali mawili ya nyongeza. Katika jawabu la msingi laMheshimiwa Waziri amesema Jeshi la Polisi limepewamamlaka kisheria kutuhumu, kukamata, kuhoji na kuwekawatuhumiwa mahabusu kwa muda ulioruhusiwa kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, wako watu wengi ambaowanawekwa mahabusu ya polisi kwa zaidi ya siku 15,akiwemo mwanafunzi Abdul Nondo, ambao wanawekwamahabusu ya polisi kwa zaidi ya siku 15 bila ya kupelekwamahakamani. Nataka nijue ni sheria gani ambayo inatumikaau inatumiwa na polisi kuwaweka watu mahabusu ya polisikwa muda huo mrefu bila ya kuwapeleka mahakamani?Nataka kujua sheria ni sheria gani. Swali la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, ni hatua gani ambayoMheshimiwa Waziri ataichukua iwapo tutamletea orodha yawatu ambao wamebambikiziwa kesi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kama nilivyosema jeshi la polisi linafanyakazi kwa mujibu wa sheria na katika ufanyaji kazi wake kunahatua mbalimbali za kuchukua ikiwemo kufanya upelelezi,kufanya mahojiano na baadaye mambo yote yaleyakikamilika hatua nyingine ndipo huwa zinafuatia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa jambo lausalama ni kipaumbele, usalama wa mtuhumiwa lakini nausalama wa raia wengine wanaosalia, Jeshi la Polisi hutumiawajibu wake lililopewa wa kulinda usalama wa raia kuwezakuhakikisha kwamba linatimiza majukumu yake na huku watuwakiwa salama pamoja na mali zao.

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

46

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu jambo la pili, kwakuwa ni suala la takwimu nitamwomba Mheshimiwa Mbungeniweze kuwasiliana naye kuweza kumpa masuala yale yatakwimu na yeye kama ana orodha kuweza kubadilishanaorodha hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Haji.

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Napenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri, ni mudagani kisheria jeshi la polisi linaposhindwa kupeleka ushahidiwa kesi unaopeleka mahakamani naweza kupeleka maombiya kuondoa mashitaka hayo mahakamani?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi, majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, naomba kumjibu ndugu yangu Khatib wa kutokakwetu kule kwa mama, kwamba makosa ya jinai hayanaukomo kwa hiyo, inategemea kosa analolisemea ambaloanaweza akasubiria na akaenda kuomba liondolewe ni ainagani ya makosa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana hiyo kamamakosa ni yale ambayo shitaka lake halina ukomo, basi nivyema kuacha vyombo vingine ambavyo vinatoa hukumuvikatoa hukumu ndipo yeye akatambua kwamba jambo hilolimeshafika ukomo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutamaliziana Wizara ya Kilimo, Mheshimiwa Joyce Bitta Sokombi,Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. MheshimiwaMarwa Ryoba Chacha kwa niaba yake.

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

47

Na. 9

Kuwapa Kipaumbele Wananchi WanaosambuliwaMashamba yao na Tembo

MHE. MARWA R. CHACHA (K.n.y. MHE. JOYCE B.SOKOMBI) aliuliza:-

Katika Msimu wa mwaka 2017/2018, wananchi waWilaya ya Serengeti na Bunda wanaoishi kandokando yaMbuga ya Serengeti wameathirika sana kwa mashamba yaokushambuliwa na tembo na hivyo kukumbwa na baa lanjaa:-

Je, Serikali ina mpango gani wa dharura wakuyafanya maeneo hayo kuwa kipaumbele cha kuwapamsaada wa chakula?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa JoyceSokombi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala waTaifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) mnamo mwezi Mei, 2017ilichukua hatua madhubuti ya kupeleka mahindi kiasi chatani 400 kwa Wilaya ya Serengeti na tani 253.6 kwa Wilaya yaBunda na kuyauza kwa bei nafuu kwa wananchiwalioathiriwa na ukame pamoja na uharibifu wa mazaouliosababishwa na wanyamapori.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendeleakuchukua hatua stahiki na za haraka za kukabiliana naupungufu wa chakula katika maeneo mbalimbali hapa nchiniikiwemo Wilaya ya Serengeti na Bunda. Aidha, Wizara yaKilimo itashirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuwekamkakati wa pamoja wa kudhibiti tembo wanaoharibumazao ya wakulima.

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

48

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kulijulisha Bungelako Tukufu kuwa Serikali mnamo mwezi Mei, 2018 kupitiaWizara ya Kilimo ikishirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Ofisiya Taifa ya Takwimu itafanya tathimini ya awali ya uzalishajiwa mazao ya chakula kwa mwaka 2017/2018 na upatikanajiwa chakula kwa mwaka 2018/2019 (Preliminary Food CropProduction Forecast) katika Wilaya zote nchini ikiwemoWilaya ya Serengeti na Bunda ili kujua hali ya uzalishaji naupatikanaji wa chakula nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande mwingineWilaya ya Serengeti na Bunda zimekuwa zikifanya tathminiza athari za uharibifu wa mazao unaosababishwa na tembomara unapojitokeza ili kubaini ukubwa wa tatizo na idadiya wakulima walioathirika. Taarifa za tathmini hizohuwasilishwa Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo wakulimawaliobainika kuathiriwa hulipwa kifuta jasho.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mambomengine matokeo ya tathmini hii yataainisha Wilaya zenyeviashiria vinavyopelekea uwepo wa upungufu wa chakulakutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya uharibifu wamazao unaosababishwa na wanyampori.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kufuatiliakwa karibu mwenendo wa upatikanaji wa chakula katikamaeneo yatakayobainishwa kuwa na viashiria vya upungufuwa chakula na kuchukua hatua stahiki ikiwamo ya kufanyatathmini ya kina ya chakula na lishe (Comprehensive Foodand Nutrition Security Vulnerability Assessment).

Mheshimiwa Naibu Spika, tathmini ya kina itaainishahali halisi ya upatikanaji wa chakula, idadi ya watuwalioathirika, viwango vya athari, kipindi cha athari, sababuzilizosababisha na hatua stahiki za kuchukuliwa na Serikalina wadau wengine katika kipindi cha muda mfupi, mudawa kati na muda mrefu. Lengo ni kuhakikisha uwepo wahali endelevu na ya utengemano wa hali ya usalama wachakula na lishe nchini.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

49

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Chacha, swali lanyongeza.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, baada yakupata janga la tembo kuharibu mazao ya wananchi waSerengeti na Bunda nilimwomba chakula, kwa kweli tulipatamahindi nimshukuru sana. Nina maswali mawili ya nyongezalakini kimsingi swali hili lilikuwa lijibiwe na Wizara ya Maliasilina Utalii. Sasa kwa kuwa Serikali ni moja naomba niulizemaswali yafuatayo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2016, baada yatembo kuharibu mazao sana na kupiga kelele hapa Bungeniikaonekana hatua haichukuliwi nilimwandikia Spika wa Bungebarua dhidi ya madhara na hatua ambayo wananchiwalikuwa wameamua kuichukua. Mheshimiwa Spikaakamwandikia Waziri wa Maliasili na Utalii aliyekuwepo,Mheshimiwa Maghembe ambaye tuliondoka naye kwendanaye Serengeti akaona madhara makubwa naakakabidhiwa tathmini ya uharibifu wa mazao na mauajiambayo yameyosababishwa na tembo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Marwa, hizo barua kamazilielekea kwa Spika, nyingine kwa Mheshimiwa Waziriunayesema wa Maliasili, maswali unataka kumuulizaMheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo, naomba ujikite kwenyeswali la msingi uliza maswali yako nyongeza ili na yeye awezekupata kujibu kwa kikamilifu.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,swali langu ni kwamba kumekuwepo na uharibifu mkubwawa mazao na mauaji hauwezi ukaisha mwezi mtu hajauawana tembo. Mashamba yanaharibiwa kwa kiasi kikubwa naSerikali ilishaahidi kuweka uzio au fence kuzunguka makaziya wananchi, sasa miaka mitano inaelekea kwisha hakunahatua yoyote, hakuna chochote kilichofanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshaweka mpakafedha kwenye bajeti yake kuweka game posts kwenye

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

50

maeneo ya makazi ya wananchi ili kuzuia tembo, lakinimpaka leo hakuna chochote kilichofanyika. Nini tamko laSerikali dhidi ya uharibifu unaosababishwa na tembo kwenyemazao ya chakula na mauaji ya wananchi wa Serengeti,Bunda na Tarime na maeneo mengine?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimonaomba usubiri ajibu mwenye tembo wake. MheshimiwaNaibu Waziri wa Maliasili ya Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Kwanzanaomba nichukue nafasi hii kumpongeza MheshimiwaMbunge kwa swali lake zuri ambalo ameliuliza. Ni kweli kabisakumekuwa na matatizo katika maeneo mengi na hilo eneoalilolisema ni mojawapo ya maeneo ambayo kumekuwa natatizo sana la tembo kuvamia katika mashamba ya watu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi uliopita tarehe 29na tarehe 30 tulipeleka Maafisa wetu kwenda kufanyatathmini katika yale maeneo ili kuangalia uharibifu mkubwaambao umefanyika na ili tuone ni hatua gani ziwezekuchukuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu hili suala ambaloamesema kwamba tuna mpango wa kuweka uzio, naombanimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali badoinafanya jitihada kuhakikisha kwamba tunachukua hatua zatahadhari na kuona ni nini kifanyike katika kuweza kuhakikishakwamba tunawalinda wananchi wale ambao wanazungukahifadhi zetu. Kwa hiyo, tutaendelea kulifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwaswali lake dogo la nyongeza, lakini kwa niaba pia ya

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

51

Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa pongezi alizozitoa naombanizipokee. Vile vile naomba pia niongezee katika majibumazuri ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasiliamejibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la nyongeza kwasababu linahusu wakulima, mazao na chakula naombaniseme kabisa kwamba sisi kama Wizara ya Kilimo kwa vileinahusu wakulima na mazao, basi tutashirikiana na Ofisi yaRais, TAMISEMI, vile vile na Ofisi ya Maliasili na Utalii kuhakikishakwamba tunahakikisha wakulima wetu wanapewa stahikizao zinazostahili ili tatizo hili lisiweze kujitokeza tena.Nashukuru.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Agnes Mathew Marwa,swali la nyongeza.

MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Swali langu la nyongeza lilikuwa ni hiloaliloliongelea Mheshimiwa Ryoba, labda swali (b), kutokanana hizo posho kusuasua na wananchi wanakuwa hawazipatikwa muda, ni lini sasa Serikali itakaa na wale wananchi ilikuongea nao au kuwapa uhakika wa kuwapa hizo fidia kwamuda?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri naonaMheshimiwa wa fidia amesimama, ama wewe jibu kwanzahalafu ataendelea Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nijibu swali moja dogo la nyongeza la Mheshimiwamdogo wangu Agnes Marwa na wifi yangu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza sisi Wizara ya Kilimokama nilivyosema kwenye jibu langu lile la nyongeza, nikwamba hatuwezi tukafanya Wizara ya Kilimo peke yetu sisikama Wizara ya Kilimo kwa sababu inawahusu wakulima kwasababu hii inahusisha Wizara tatu; Ofisi ya Rais, TAMISEMI,Wizara ya Maliasili na Utalii.

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

52

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo ningependakuwaasa Maafisa Kilimo wetu, Maafisa Ugani wetu kulekwenye halmashauri wajaribu ku-review zile posho naviwango vya posho ambavyo huwa wanavifanyia tathminikwa wakulima wetu kabla hawajapeleka Wizara ya Maliasilina Utalii ili wakulima hawa waweze kupata haki zao stahiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, naomba kuongezea majibu kwa yaleMheshimiwa Naibu Waziri ambayo ameyajibu vizuri sana. Basikatika hili suala ambalo nimelisema Wizara ya Maliasili naUtalii sasa hivi inafanya mapitio ya zile kanuni zetu za kifutajasho za mwaka 2011 ambazo ndizo zinaongoza namna yakutoa kifuta jasho, si fidia kama inavyosomeka, ni kifuta jashokwa wale wananchi ambao wameathirika. Kwa hiyo, baadaya hizi taratibu kukamilika basi mambo yatakuwayamekwenda vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuhusu hili suala lakekwamba ni lini watalipwa, kama nilivyosema katika jibulangu la kwanza kwamba tarehe 29 na tarehe 30 mweziuliopita maafisa wetu wameshakwenda kufanya tathmini.Baada ya tathmini hiyo kukamilika basi taratibu za kuwalipahao wote walioathirika zitafanyika mara moja.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dokta Raphael Chegeni,swali la mwisho.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Suala la tembo pamoja na uharibifu wakeni suala zito sana. Linaongelewa hapa kwa juu juu lakinimadhara yake ni makubwa sana kwa wananchi na hasawanaozunguka maeneo hayo. Je, unaposema mapitio yakanuni, ni lini sasa yatakuwa tayari? Swali hilo tu kwa sababuwananchi wana shida kubwa sana.

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

53

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, nimesema kwamba sasa hivi tuko kwenye hatuaya mwisho ya kupitia hizi kanuni upya ili angalau kuwezakuvipitia hivi viwango vyote ambavyo vimekamilika. Kwahiyo nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwambamwaka huu hautakwisha hizi kanuni zitakuwazimeshakamilika.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tumefikamwisho wa kipindi chetu cha maswali na majibu. Kablasijaleta matangazo tuliyonayo mezani leo na mimi nichukuefursa hii kuwapongeza Wabunge wapya walioapishwa leona niwatakie kila la heri katika utekelezaji wa majukumuyenu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tunao wageni waliotufikialeo na tutaanza na wageni walioko jukwaa la Spika. Tunaowageni tisa wa Mheshimiwa January Makamba ambaye niWaziri Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, hawawanaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo MhandisiJoseph Malongo. Karibuni sana. (Makofi)

Tunao pia wageni sita wa Mheshimiwa Dokta HarrisonMwakyembe ambao ni viongozi wa kundi la STARTIMES lanchini wakiongozwa na Rais wa kundi hilo Ndugu Pang XinXing. Aidha ujumbe huu umeambatana na Mkurugenzi Mkuuwa Shirika la Utangazaji – TBC Dkt. Ayoub Ryoba. Karibunisana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge STARTIMES ndiyo Kampuniiliyosaidia TBC kuanza kutangaza ama kurusha matangazoyake kidigitali kutoka kwenye analojia, tunawashukuru sanakwa kazi nzuri. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tunao pia wageni ambaowamekaa kwenye majukwaa ambayo wanakaa wageni waWaheshimiwa Wabunge.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

54

Tunao wageni 44 wa Mheshimiwa Dkt. Godwin Mollelambao ni viongozi na wanachama wa CCM na familia yakekutoka Wilayani Siha. Karibuni sana wageni wetu. Hawawameongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya SihaNdgugu Wilfred Mossi. Karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tunao pia wageni 33 waMheshimiwa Maulid Said Mtulia ambao ni viongozi nawanachama wa CCM na familia yake kutoka Jijini Dar esSalaam. Karibuni sana na hawa pia wameongozwa na NaibuMeya wa Kinondoni, Mheshimiwa Gere Mangalu Manyama.Karibuni sana (Makofi na vigelegele)

Tunao pia wageni 39 wa Mheshimiwa Anna Lupembeambao ni wana maombi kutoka Mkoa wa Dodoma; karibunisana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tangazo lingine linatokaUtawala. Waheshimiwa Wabunge mnataarifiwa kwamba leokutakuwa na kikao cha briefing saa 10 kamili Ukumbi waMsekwa; siku ya leo tarehe tatu mwezi wa Nne tutakutanaWabunge wote kwenye mkutano wetu wa briefing.

Waheshimiwa Wabunge ninalo tangazo linginelinatoka kwa Katibu Msaidizi wa Wabunge wa CCM,anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote wa CCMkuwa kutakuwa na kikao cha Wabunge wote wa Chamacha Mapinduzi hivyo Waheshimiwa Wabunge wotewanaotokana na chama hiki wanaombwa kukutana Ukumbiwa White House mara baada ya kuahirisha shughuli za Bunge.Kwa hiyo, tukiahirisha shughuli za Bunge WaheshimiwaWabunge wanaohusika waelekee White House.

Waheshimiwa Wabunge tangazo lingine linatokakwa Mheshimiwa Anna Lupembe ambaye ni Mwenyekiti waibada Chapel ya Bunge anawatangazia WaheshimiwaWabunge wote kuhudhuria ibada katika Ukumbi wa PiusMsekwa Chapel Ghorofa ya pili, leo siku ya Jumanne tarehe3 Aprili, 2018 mara baada ya kusitisha shughuli za Bunge saasaba mchana.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

55

Sasa haya matangazo mawili nadhani MheshimiwaAnna Lupembe awasiliane na Uongozi wa CCM kuonanamna gani watagawana huo muda wa hivyo vikao.

Waheshimiwa Wabunge hilo ndio lilikuwa tangazoletu la mwisho tutaendelea na ratiba yetu. Katibu.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,Mwongozo!

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Naib Spika,mwongozo wa Spika.

MWONGOZO

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sixtus Mapunda.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwa kunipa nafasi ya kuomba mwongozo. Nimesimamahapa kwa kanuni ya 68 ila kutokana na muda naombanisiisome.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulipoingia hapa asubuhiya leo shughuli yetu ilianza na Wimbo wa Taifa ambao si maramoja huwa tunaanza na tukifunga Bunge tunamaliza naWimbo wa Taifa. Hata hivyo, Wimbo wa Taifa ambao marazote tumekuwa tukiuimba ndani ya Bunge lako Tukufu sio ulewimbo ambao ulikuwa wimbo rasmi uliokubalika na BAMUTAmiaka ile ya zamani kabla ya kuwa BASATA kwa sababu unamakosa makubwa matatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, una kosa la kimelodiakwenye neno na watoto, kuna kosa la rhythm kwenye nenola kwanza la Mungu halafu kuna kosa la wording. Sasa shakayangu ni kwamba huu wimbo tunaoimba sasa ni remix sijuiumekuja katika mazingira gani. Sasa naomba mwongozowako hivi ni sawa sawa sisi kuimba wimbo ambao si rasmindani ya Bunge lako Tukufu?

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

56

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Goodluck Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kikao chako cha Bungekiwe halali inatakiwa itimie nusu ya idadi ya Wabunge waBunge lako la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwahesabu yangu ya haraka haraka nimehesabu nimekutaWabunge hawajafikia nusu ya idadi ya Bunge. Mwongozowangu ni huu; je, kikao chako hiki tuliyoyafanya haya kamahesabu yangu ni ya kweli, tuliyoyafanya haya ni halali ikiwemoviapo vya Wabunge?

Mheshimiwa Naibu Spika, pil i, ni hatua ganiitachukuliwa dhidi ya wale wabunge ambao hawapo kwawakati huu Bungeni wakati walitakiwa wawepo kwa sababuwamechaguliwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, kama kikao hiki sihalali vipi kuhusu posho tutalipwa au la?

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nimeombwamiongozo miwili. Kwanza mwongozo nimeombwa naMheshimiwa Sixtus Mapunda kuhusu Wimbo wa Taifaunaoimbwa hapa Bungeni na kama wimbo huo ni rasmi amasi rasmi japokuwa kwa maelezo yake yeye ametoa maelezokwa kirefu kuonesha namna ambavyo wimbo huu si wimboule ambao ni rasmi kama ambavyo tunaufahamu na ambaoulikuwa umeshakubaliwa na vyombo vinavyohusika.

Waheshimiwa Wabunge, ili niweze kutoa mwongozoulio kamili ni lazima nijiridhishe na haya maeneo ambayoameyataja Mheshimiwa Sixtus Mapunda kama ni kweliyamekosewa ama hayajakosewa. Wakati huo huonitakapoyasikiliza maneno hayo, yale nitakayoyakutapengine hayako sawasawa nitatoa mwongozo huo hapaBungeni maana wimbo sisi kama Bunge tunapaswa kuimba

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

57

wimbo ulio rasmi. Kwa hiyo, kama kutakuwa na makosanitatoa mwongozo hapo baadaye.

Waheshimiwa Wabunge pia nimeombwa mwongozona Mheshimiwa Goodluck Mlinga akizungumzia akidi ya kikaohiki cha Bunge, japokuwa hakutaja ni kanuni gani, yeyeamesema tu kikanuni wanatakiwa kuwa nusu, lakini kanuniinayotuongoza kwa ujumla wake kuhusu akidi ni kanuni ya77. Fasili ya kwanza ukisoma mpaka ya tano inakupamwelekeo wa namna gani utasema kwamba shughuli hii nihalali ama si halali kwa kutumia akidi.

Hata hivyo, kwa ujumla Waheshimiwa Wabungekwanza Mheshimiwa Mbunge anapaswa kusimama nakusema akidi haijatimia. Akisema akidi haijatimia miminaagiza kwamba hesabu zifanywe, Wabunge Wahesabiwe,si Mbunge anayefanya kazi ya kuhesabu Wabunge wakowangapi.

Kwa hivyo alipaswa anieleze mimi kwamba akidihaijatimia kwa ajili ya jambo lililo mbele yetu. Kwa sababuukizisoma hizi kanuni kwa ujumla wake akidi si moja kwa kilajambo linalofanyika hapa ndani. Kwa hivyo unasema nenoakidi kulingana na jambo lililo mbele yetu ili sisi tujiridhishekwamba kwenye hili jambo tunalotaka kulifanya je akidiimetimia ama haijatimia ndiyo kanuni zetu kwa ujumla.

Hata hivyo, kwenye suala la hesabu alizofanya yeyena kuonesha kwamba Wabunge hawajafikia nusu suala laakidi kuulizwa kwa yeye, kwa sababu ameulizia kwa ujumlawake suala la akidi ni wakati wa kuanza kikao. Kwa hiyoMheshimiwa Goodluck kama amezipata taarifa kutoka Ofisiya Katibu kwamba wakati tukianza asubuhi kulikuwa hakunaakidi, hiyo ndiyo taarifa ninayoweza kuisikiliza, lakini taarifaanayoitoa sasa ama mwongozo anaohitaji sasa haukokikanuni.

Kwa hivyo swali lake, kwa sababu amezungumziamambo matatu; la kwanza amesema ikiwa nusu yaWabunge hawakuwepo wakati tukianza, kwa hivyo sasa

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

58

hata yale mambo ambayo tumefanya ikiwa ni pamoja nakuapisha, kuapisha kumeapishwa kihalali kabisa.Mheshimiwa Mbunge alipaswa afuate kanuniinayozungumzia akidi wakati huo, wakati tunafanya hayomaamuzi, wakati tunafanya tukio hilo.

Pia amesema hatua gani zitachukuliwa kwaWabunge ambao hawapo. Nadhani ufafanuzi wa mambohaya tulishawahi kuutoa kwa kirefu sana huko nyuma sinasababu ya kurudia kwa sababu Wabunge wakiwa hawapohapa Bungeni kuna mambo mengi. Wengine wanawezakuwa wako kwenye Kamati, ama wana kazi maalumwaliyopewa. Sasa Mheshimiwa Mbunge hajaeleza vizuri kwasababu sisi tunapochukua taarifa za Wabunge waliohudhuriatunataka kwanza kujiridhisha kwenye hilo suala la akidi lakinipia kujua kwamba wabunge wetu wako wapi. Kwa hivyo,Wabunge kama wamepewa majukumu menginewanaweza kuwa nje ya ukumbi huu wa Bunge.

Waheshimiwa Wabunge amesema pia kuhusu je,posho italipwa? Posho inalipwa kwa Wabungewaliohudhuria na kukaa hapa kufanya kazi. Kama mtuamehudhuria akaondoka zake huyo kanuni na maamuziambayo tulishatoa huko nyuma yatafanya kazi yake. Kwahiyo, kama ameingia hapa ndani akajiandikisha nakuondoka utaratibu ni uleule kwamba hatolipwa hiyo poshoinayoulizwa na Mheshimiwa Mlinga.

Baada ya kusema hayo Waheshimiwa Wabungetutaendelea. Katibu!

NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE:

UCHAGUZI WA WENYEVITI WA BUNGE

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kwa mujibuwa kazi ama majukumu tuliyonayo leo pamoja na mambomengine tunalazimika kufanya uchaguzi wa Wenyeviti waBunge na nitatoa maelezo ya Mheshimiwa Spika kuhusuuchaguzi wa Wenyeviti wa Bunge.

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

59

Waheshimiwa Wabunge, kama inavyoonekanakwenye Order Paper, moja ya shughuli za leo ni uchaguzi waWenyeviti watatu wa Bunge kufuatia kuanza kwa kipindi chapili cha maisha ya Bunge kwani hili ni Bunge la Kumi na Moja.Kanuni ya 7(1) ya Kanuni za Bunge imeweka uwepo waWenyeviti watatu wa Bunge ambao wanapatikana kwakuchaguliwa na Wabunge.

Aidha, Kanuni ya 7(2) ikisomwa pamoja na Kanuni11(1)(a) ya Kanuni za Bunge imeweka utaratibu utakaofuatwakatika kufikia upatikanaji wa Wenyeviti wa Bunge kwambaKamati ya Uongozi itapendekeza majina ya Wabunge sitaambayo yatawasilishwa Bungeni ili kupigiwa kura kutokamiongoni mwa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamatiza Kudumu za Bunge.

Waheshimiwa Wabunge, siku ya Jumatano tarehe 28Machi, 2018 Kamati ya Uongozi ilikutana pamoja na MakamuWenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuyapatamajina sita ya kuwasilisha Bungeni ili yapigiwe kura. Hatahivyo, kwa kuzingatia utendaji kazi wa wenyeviti watatuwaliokuwepo wakati wa kipindi cha kwanza cha maisha yaBunge hili na kwa mujibu wa Kanuni ya 11(2) inayotoa fursakwa Wenyeviti wa awali kuchaguliwa tena katika kipindi chapili. Wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwa kauli moja walifikiauamuzi wa kupendekeza majina matatu badala ya sita iliyaweze kuwasil ishwa Bungeni na Bunge liombwekuyathibitisha kama yalivyokubaliwa na Kamati ya Uongozi.

Waheshimiwa Wabunge, mtakumbuka pia kuwaBunge letu lilikwishaweka utaratibu kwamba katika chaguzizinazofanyika hapa Bungeni iwapo idadi ya wagombeainalingana na nafasi zilizopo na vigezo vinavyohitajikavimetimizwa basi wagombea hao wanapita bila kupingwa.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, utaratibu kama huuulitumika kwenye uchaguzi wa Wenyeviti katika kipindi chapili cha maisha ya Bunge la Kumi mwaka 2013 ambapoKamati ya Uongozi i l ipendekeza majina matatu ya

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

60

waliokuwa Wenyeviti kuwa waendelee na nafasi hizo naBunge likaridhia. (Makofi)

Hivyo kwa kuzingatia utaratibu huo, nawasilishamajina ya Wabunge waliopendekezwa na Kamati ya Uongoziambao ni Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu, MheshimiwaAndrew John Chenge na Mheshimiwa Najma Murtaza Gigaili yathibitishwe na Bunge kwa njia ya kuhoji badala yautaratibu wa kupiga kura. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya maelezo hayosasa naomba kulihoji Bunge kuridhia Mheshimiwa MussaAzzan Zungu, Mheshimiwa Andrew John Chenge naMheshimiwa Najma Murtaza Giga wathibitishwe kuwaWenyeviti wa Bunge.

(Hoja Ilitolewa Iamuliwe)(Hoja Iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Bunge liliridhia Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu,Mheshimiwa Andrew John Chenge na Mheshimiwa Najma

Murtaza Giga kuwa Wenyeviti wa Bunge)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nichukuenafasi hii kuwatangaza Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu,Mheshimiwa Andrew John Chenge na Mheshimiwa NajmaMurtaza Giga kuwa ndiyo Wenyeviti wa Bunge kuanzia sasa.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nichukue nafasi hiikuwapongeza sana Waheshimiwa Wenyeviti wetu wa Bungekwa kupata uthibitisho huo wa Bunge na niwatakie kila kherikatika utendaji wenu wa kazi wa kumsaidia MheshimiwaSpika katika majukumu yake. Naamini mtaendelea kutoaushirikiano kama ambavyo mmekuwa mkifanya hivyo sikuzote mpaka Bunge limeonesha kuwa na imani na ninyi.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada kusema hayo,tutaendelea na ratiba iliyo mbele yetu. Katibu.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

61

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:

HOJA ZA SERIKALI

Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chiniya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko yaTabianchi (The Paris Agreement under the UN Framework

Convention on Climate Change)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nakushukuru kwa kutupatia fursa ya kuwasilisha hiliAzimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini yaMkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko yaTabianchi. Pia napenda kuishukuru Kamati ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira kwa kupitia Rasimu yaAzimio hili na kuipitisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawashukuru wadau wotewa mazingira kwa kushirikiana na Ofisi yetu katika jitihadambalimbali za kuboresha Azimio hili, lakini na ushiriki wetukwenye mkataba. Pia niwashukuru wataalam katika Ofisi yaMakamu wa Rais wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi yaMakamu wa Rais, Engineer Joseph Kizito Malongo kwa kazinzuri waliyofanya ya maandalizi ya Azimio hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijawasilisha Azimiohili, napenda niwasilishe maelezo mafupi ya awali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama unavyofahamuMkutano wa Kimataifa kuhusu Binadamu na Mazingiraulifanyika huko Stockholm, Sweden mwaka 1972. Katikamkutano huo kwa mara ya kwanza kabisa Jumuiya yaKimataifa ilikubaliana kwamba masuala ya mazingira namaendeleo yanafungamana na kwamba lazima yaendesambamba. Aidha, mwanzoni mwa miaka ya 1980wanasayansi na wafuatiliaji wa hali ya hewa duniani walianzakuona na kutoa taarifa kuhusu kuongezeka kwa joto dunianikuanzia kipindi cha mapinduzi ya viwanda.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

62

Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia angalizo hilo lakuongezeka kwa joto duniani, Shirika la Umoja wa Mataifala Mazingira Duniani (UNEP) kwa kushirikiana na Shirika la Haliya Hewa Duniani walipitisha uamuzi wa kuunda jopo lakimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Lengo la jopo hilolilikuwa ni kujadili matokeo ya uchunguzi wa kisayansi kuhususababu halisi za ongezeko la joto duniani ambalo lilonekanakubadilisha mifumo ya hali ya hewa na kusababishamabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ya kwanza ya jopohilo ilitolewa mwaka 1990 na kuwasilishwa mbele ya Mkutanowa Umoja wa Mataifa (United Nations General Assembly) nakujadiliwa. Majadiliano hayo ndio yalizaa majadiliano yakuunda Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi. Kwa hiyo,mwaka 1992 Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadilikoya Tabianchi ulipitishwa huko Rio De Janeiro, Brazil wakatiwa Mkutano huo.

Naomba nirudia hapo, tarehe 5 Mei, 1992 Mkatabawa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi ulipitishwahuko Brazil wakati wa Mkutano wa Dunia kuhusu Mazingirana Maendeleo (Earth Summit).

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania iliridhia mkatabahuo wa mwaka 1992 mwaka 1996 na Itifaki yake ya Kyotomwaka 2002. Lengo la mkataba huo ilikuwa ni kuzuiaongezeko la gesijoto na athari zitokanazo na mabadiliko yatabianchi kwenye mifumo ya ikolojia ya dunia ili kuharakishamaendeleo endelevu duniani. Mabadiliko ya tabianchi nimabadiliko katika mifumo ya hali ya hewayanayosababishwa na ongezeko la joto duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu za kuongezeka kwagesijoto ni kutokana na matumizi makubwa ya nishati chafuzikwa shughuli za maendeleo zilizofanyika katika nchizilizoendelea takribani miaka 150 iliyopita. Athari zitokanazona mabadiliko hayo ni pamoja na ukame, mafuriko, kueneakwa magonjwa ya kuambukiza, kumezwa kwa visiwavidogo kwenye bahari kutokana na kuongezeka kwa ujazo

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

63

wa maji ya bahari, kuyeyuka kwa barafu katika vilele vyamilima mirefu kama vile Mlima wa Kilimanjaro, kuharibikakwa madaraja, reli, barabara na makazi kutokana namafuriko na kuongezeka kwa vimbunga. Majanga hayahuathiri zaidi nchi maskini kama ya kwetu kutokana na uwezowake mdogo wa kuhimili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambuachangamoto ya mabadiliko ya tabianchi na umuhimu kwakila Mtanzania kuishi katika mazingira bora na salama,Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa mstari wa mbelekatika uhifadhi wa mazingira na katika nchi yetu tumetengatakribani asilimia 30 ya ardhi kwa ajili ya uhifadhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi, kuridhiamakubaliano haya kutasaidia nchi yetu kufanya mikakatiyake ya maendeleo kwa namna endelevu. Tanzaniaimekuwa ikishirikiana na nchi nyingine katika utekelezaji waMkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi tangu ulipopitishwa.Katika ushirikiano huo, Tanzania imenufaika na miradi yenyethamani ya takribani shilingi bilioni 700 ambayo imesaidiakutekelezwa kwa miradi mbalimbali katika maeneombalimbali ya nchi yetu ikiwemo Mradi wa Usambazaji MajiSimiyu, tumesomesha wanafunzi takribani 200 kuhusu masualaya mabadiliko ya tabianchi katika shahada mbalimbali namambo mengineyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, manufaa mengineyatokanayo na uanachama wa Tanzania kwenye Mkatabawa Mabadiliko ya Tabianchi ni pamoja na utekelezaji wamradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika maeneoya Pwani ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Vilevile tumeweza kufanikiwa kupata mradi wakuongeza uhimili ambao uliwezesha upatikanaji wa majikatika Wilaya za Igunga (Tabora), Nyasa (Ruvuma), Misenyi(Kagera) na Wilaya ya Kaskazini A. Pia upo mradi wa vijijivya mfano (Eco Village Project) ambao umewezeshaupatikanaji wa nishati na kuandaa mipango ya matumizi yaardhi katika maeneo ya Dodoma, Morogoro na Zanzibar.

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

64

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna mradi wakurejeleza ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wachakula katika maeneo ya nyanda kame (Reversing LandDegradation Trends in Increasing Food Security in DegradedEcosystems in Semi-arid Areas of Central Tanzania). Mradi huuunalenga kurejesha mifumo ya ikolojia ya kilimo iliyoharibikaili kuongeza uzalishaji wa chakula katika maeneo kame napwani ya nchi. Mradi huo unatekelezwa katika maeneombalimbali ya nchi yetu na utekelezaji wa mradi huu nimanufaa ya uanachama na ushiriki wa Tanzania katikamkataba huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna mradi wa kuhimilimabadiliko ya tabianchi katika maeneo ya vijiji kupitiamfumo wa ikolojia (Ecosystem-Based Adaptation for RuralResilience in Tanzania). Lengo la mradi huu ni kuziongezeajamii za vijijini uwezo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchikwa kuimarisha uhimilivu wa mifumo ya ikolojia na kupatanjia mbadala za kujenga ustawi wa jamii. Mradi huuunatekelezwa katika Halmashauri tano nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile chini ya Mkatabawa Mabadiliko ya Tabianchi, tumeanzisha Kituo cha Kitaifacha Ufuatiliaji na Upimaji wa Hewa Ukaa (National CarbonMonitoring Center) kilichopo Chuo Kikuu cha Kilimo chaSokoine. Kwa ujumla, miradi yote hii imetekelezwa katikapande zote mbili za Muungano.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na faida hizo,utekelezaji wa Mkataba huu na Itifaki yake umekubwa nachangamoto mbalimbali ikiwemo kutoshirikisha nchi zotekatika upunguzaji wa gesijoto hivyo kusababisha upunguzajiwake kuwa mdogo na kuongezeka kwa gharama zakukabiliana na majanga ya athari za mabadiliko ya tabianchihasa kwa nchi maskini kama ya kwetu. Katika kukabilianana changamoto hizo, Mkutano wa 21 wa nchi wanachamawa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Paris,Desemba, 2015 ulipitisha kwa kauli moja makubaliano yaParis. Makubaliano hayo ya Paris yana malengo makuuyafuatayo:-

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

65

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kuongezaushirikishwaji wa nchi zote duniani katika juhudi zakuhakikisha kwamba joto la dunia haliongezeki zaidi yacentigrade mbili kabla ya mwisho wa karne hii na kuhakikishakwamba ongezeko la gesijoto duniani linabaki chini yacentigrade 1.5 ikilinganishwa na kabla ya maendeleo yaviwanda. Pia kuongeza uwezo wa nchi kuhimili athari zamabadiliko ya tabianchi na kuchochea upunguzaji wagesijoto usioathiri maendeleo na uhakika wa chakula kwanchi husika. Vilevile lengo lake ni kuongeza upatikanaji wafedha na teknolojia kwa ajili ya kusaidia maendeleo himilivu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania ni miongoni mwanchi zilizoathirika kwa kiasi kikubwa na mabadiliko yatabianchi katika sekta zote. Hivyo kuridhia kwa makubalianoya Paris kutasaidia nchi yetu kuongeza uwezo wa kuhimiliathari za mabadiliko ya tabianchi, kupata teknolojia safiambazo zitasaidia katika mikakati ya Serikali ya kujengauchumi endelevu wa viwanda na wenye kustahimilimabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tutanufaika nakuongeza uzalishaji na upatikanaji wa chakula, kutunzamisitu ambayo ipo hatarini kutoweka, kuandaa nakutekeleza mikakati na mipango ambayo itasaidia kuhimiliathari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta za afya, kilimo,maji na sekta nyinginezo hasa zile zinazoathirika namabadiliko ya tabianchi. Aidha, nchi yetu itapata fedha zakutekeleza programu za miradi kupitia mifuko mbalimbalikama vile Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi na taasisi zakimataifa kama vile Umoja wa Nchi za Afrika, Caribbean naPacific (ACP).

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa makubalinoya Paris utazingatia misingi ya usawa, uwezo na historia yanchi na hali yake ya uchumi. Kwa maana hiyo, nchi yetuhaitabanwa wala kulazimishwa kupunguza uzalishaji wagesijoto duniani bali itashiriki katika juhudi hizo kwa hiyari nabila kushurutishwa, ukizingatia kwamba mchango wa nchiyetu katika kuongezeka kwa gesijoto duniani ni mdogo mno.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

66

Hata hivyo, kama Tanzania ingekuwa inabanwa kisheriakupunguza uzalishaji wa gesijoto bado ina ziada ya uwezowa kunyonya gesijoto kupitia misitu yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Tanzaniainazalisha kiasi cha tani za hewa ya carbon 0.2 pekee kwamwaka wakati ina misitu takribani hekari milioni 48 ambayoina uwezo wa kunyonya kiasi cha takribani tani tisa za hewaya carbon. Aidha, ardhi ya Tanzania ina eneo la takribaniasilimia 30 ambalo limehifadhiwa kisheria na linaendeleakunyonya gesijoto zinazozalishwa duniani bila mipaka. Hatahivyo, utekelezaji wa makubaliano ya Paris ni wa hiyari,hakuna sheria za kuzibana nchi wanachama na makubalianohaya yanairuhusu nchi kujitoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na dhanakwamba nchi yetu tukiridhia makubaliano haya basitutalazimishwa kufanya maendeleo kwa namna ambayoitapunguza kasi yetu ya maendeleo. Ukweli ni kwamba kwamujibu wa mkataba huu nchi zinapaswa kuweka mipangoyake ya upunguzaji wa mchango wake kwenye gesijotoduniani kulingana na mazingira halisi ya nchi hiyo, kwa hiyo,hakuna wasiwasi huo. Sisi tunadhani kwamba manufaamakubwa zaidi yapo kwenye mchango ambao Tanzaniaitaupata kutoka kwenye Jumuiya ya Kimataifa kwenyejitihada zake za kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi(adaptation).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nchi kuwamwanachama wa Makubaliano ya Paris, Ibara ya 20inaelekeza nchi husika kuridhia makubaliano haya kama ilivyokwenye mikataba mingine ya kimataifa. Hadi kufikia tarehe21 Aprili, 2016, ambacho ni kipindi maalum kilichowekwakwa nchi kusaini, jumla ya nchi 182 zilikuwa zimesaini ikiwemoTanzania. Aidha, kufikia tarehe 28 Machi, jumla ya nchi 175zilikuwa zimeridhia.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kufikia akidi yanchi zinazohitajika kuridhia yaani nchi 55, makubaliano yaParis yameingia katika hatua ya utekelezaji kabla ya muda

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

67

uliopangwa ambao ni mwaka 2020. Kimsingi utekelezajiwake umeanza tangu tarehe 4 Novemba, 2016. Hivyo kunaumuhimu wa nchi yetu kuridhia ili iungane na nchi nyinginekatika utekelezaji na kuendelea kunufaika na fursa zilizopo.Kwa upande wa Bara la Afrika, hadi kufikia tarehe 26 Machi,2018 nchi 45 kati ya nchi 54 za Afrika zilikuwa zimeridhia.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda sasa kupitia kwaharaka vipengele muhimu vya makubaliano haya iliWaheshimiwa Wabunge waweze kufahamu kwa kina.

Kwanza Ibara ya Pili ya makubaliano inazungumzialengo na lengo kuu kwa kweli ni kushirikisha nchi zotewanachama katika jitihada za kushughulikia mabadiliko yatabianchi hasa upunguzaji wa gesijoto duniani na kusaidianchi zinazoendelea kama Tanzania kuhimili athari zamabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo lingine ni kuongezaupatikanaji wa chakula na kuchochea maendeleo endelevu.Utekelezaji wa makubalino haya utazingatia misingi yausawa, uwezo na hali ya uchumi wa nchi husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 3 inazungumziawajibu wa nchi mbalimbali katika kutekeleza makubalianohaya. Nchi zitatakiwa kuandaa na kuwasilisha taarifa kuhusujuhudi zake za kufikia malengo ya makubaliano ya Paris kamayalivyoainishwa katika Ibara za 4, 7, 9, 10, 11 na 13. Nchizilizoendelea zitawajibika kuchangia fedha za kusaidia nchizinazoendelea katika kutekeleza programu na miradi yakuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi na miradi yaupunguzaji wa gesijoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 4 inazungumziamuda wa kufikia kiwango cha juu cha upunguzaji wagesijoto. Nchi zinatakiwa kupunguza gesijoto kwa lengo lakufikia kiwango cha juu cha upunguzaji kwa kuzingatiamisingi ya usawa na maendeleo endelevu na kuondoaumaskini. Makubaliano haya yanabainisha kuwa nchizinazoendelea zitahitaji muda mrefu zaidi kufikia kiwango

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

68

cha juu cha kupunguza gesijoto. Hatutawekewa deadlineambayo hatutaweza kuimudu ya kupunguza kiwango chagesijoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya Tano inazungumziasekta ya misitu, inasema kwamba kila nchi mwanachamainahimizwa kutunza misitu inayonyonya gesijoto. Juhudi hizizikizingatiwa zitachangia kuongezeka kwa motisha na kasiya kutunza misitu ambayo huchangia upatikanaji wa mvuana kuhifadhi vyanzo vya maji nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya Sita inazungumziaushirikiano wa hiari katika utekelezaji. Nchi zitashirikiana kwahiari katika utekelezaji wa mikakati ya kupunguza gesijotona kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuchocheamaendeleo endelevu na hifadhi ya mazingira. Mfumo wakusimamia upunguzaji wa gesijoto duniani umeanzishwa ilikutoa motisha na kuchochea ushiriki wa taasisi za umma nasekta binafsi katika jitihada hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya Saba inazungumziakuhimili mabadiliko ya tabianchi, kwamba kila nchimwanachama inawajibika kuandaa na kutekeleza mipangoya kuhimili mabadiliko ya tabianchi (National Action Plan).Kuimarisha uwezo wa kuhimili athari za mabadiliko yatabianchi kutasaidia kupunguza athari za ukame, mafurikona kudhibiti kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya Tisa inazungumziaupatikanaji wa fedha za utekelezaji. Makubaliano ya Parisyanatoa haki kwa nchi zinazoendelea ambazo nimwanachama kupata fedha za kushughulikia changamotoza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia ufadhiliwa mifuko ya mabadiliko ya tabianchi na wadau wengine.Nchi zilizoendelea zitatakiwa kutoa taarifa kila baada yamiaka miwili kuhusu kiwango cha fedha walizotoa auwanazotarajia kutoa kama msaada kwa nchi ambazo zikohatarini kuathirika na mabadiliko ya tabianchi. Kamanilivyoeleza hapo awali kwamba ushiriki wetu katikaMkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi hadi sasa umewezesha

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

69

nchi kupata msaada wa takribani shilingi bilioni 700. Tunaaminikwamba tukiridhia Makubaliano ya Paris fursa hizi zitapanukana kuongezeka zaidi na hasa mchango wa nchizinazoendelea kupitia mifuko mbalimbali ya mabadiliko haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 10 inazungumziateknolojia na imeweka mfumo wa nchi zinazoendeleakupata teknolojia za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 11 inazungumziakuhusu kujengewa uwezo. Inasema kwamba nchizinazoendelea, kama nchi yetu, zina haki ya kujengewauwezo na uelewa katika kushughulikia mabadiliko yatabianchi, hali ambayo itaongeza uelewa wa jamii kuhusuhatua za kuchukua ili kupunguza athari za mabadiliko hayakatika maeneo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 13 inazungumziauwazi katika utekelezaji. Ibara hii inazitaka nchi wanachamakuwa na mfumo wa uwazi wa kupeana taarifa kuhusuutekelezaji wa makubaliano ili kuhakikisha kwamba malengoyanafikiwa. Mfumo huu umewekwa makusudi i l ikuwezesha nchi kutambua uwezo mdogo wa nchimaskini na utatekelezwa kwa hiari bila kuingilia uhuru wanchi husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 20 inazungumzakuhusu utaratibu wa uridhiaji na inasema kwamba kila nchiitaridhia kulingana na taratibu zake kama sisi tunavyofanyahivi leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 28 inazungumziauhuru wa kujitoa na inasema kwamba nchi ina haki ya kujitoakatika makubaliano hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Tanzaniainaingia kwenye uchumi wa viwanda, Makubaliano ya Parisyatasaidia kuchochea matumizi ya gesi asilia, upatikanaji wateknolojia safi, kufunza wataalam wetu na kuendelea kuwana vyanzo vya nishati endelevu ili kukabiliana na uchafuzi

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

70

wa mazingira. Aidha, Makubaliano ya Paris yataongezaushirikiano, upatikanaji wa fedha na kuchochea biashara yahewa ukaa na upashanaji wa taarifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa nchi yetukuridhia utazingatia Katiba ya nchi yetu ambayo inalipaBunge madaraka ya kujadili na kuridhia mikataba yoteinayohusu Jamhuri yetu na ambayo kwa masharti yakeinahitaji kuridhiwa. Hati ya kuridhia itawasilishwa kwa KatibuMkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ana jukumu la kupokeana kuhifadhi hati hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo,sasa naomba niwasilishe Azimio la Bunge la Kuridhia kamaifuatavyo:-

Kwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimiongoni mwa nchi wanachama wa Mkataba waMabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 1992 na Itifaki yake yaKyoto ya mwaka 1997;

Na kwa kuwa nchi yetu iliridhia mkataba huo mwaka1996 na itifaki hiyo mwaka 2002; Na kwa kuwa lengo kuu lamkataba huu na itifaki yake ni kuzuia ongezeko la gesijotona athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi kwenyemifumo ya ikolojia ya dunia ili kuhakikisha maendeleoendelevu duniani;

Na kwa kuwa mabadiliko ya tabianchiyanasababisha athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukame,mafuriko, kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza, kumezwakwa visiwa vidogo kwenye bahari kutokana na kuongezekakwa ujazo wa maji ya bahari, kuyeyuka kwa barafu kwenyevilele vya milima mirefu kama vile Kilimanjaro na uharibifuwa miundombinu ya barabara, reli, makazi kutokana namafuriko na kuongezeka kwa vimbunga;

Na kwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimiongoni mwa nchi zinazoathirika kwa kiasi kikubwa namatokeo hasi ya mabadiliko ya tabianchi;

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

71

Na kwa kuwa tangu mkataba huu na itifaki yakeiridhiwe na nchi wanachama na kuanza kutekelezwakumejitokeza changamoto katika utekelezaji wake ikiwemonchi zilizoendelea kuogopa kupoteza nguvu za kiuchumi kwasababu ya utekelezaji wa mkataba huu utaathiri uzalishajiviwandani na kupunguza matumizi ya nishati chafu,ushindani wa kiuchumi baina ya nchi zinazoendelea na zilezenye uchumi unaokua haraka, unasababisha kuongezekakwa viwanda vinavyochafua mazingira na kutoshirikisha nchizote katika upunguzaji wa gesijoto kunasababishaupunguzaji wake kuwa mdogo na kuongezeka kwagharama za kukabiliana na majanga ya mabadiliko yatabianchi, hasa kwa nchi zinazoendelea;

Na kwa kuwa nchi yetu inatambua changamoto hizona umuhimu wa kila Mtanzania kuishi katika mazingira borana safi;

Na kwa kuwa katika Mkutano wa 21 wa NchiWanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchiuliofanyika Paris (Ufaransa), Desemba, 2015 nchi wanachamawa mkataba walipitisha Makubaliano ya Paris kwa lengo lakuboresha utekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko yaTabianchi; Na kwa kuwa Makubaliano ya Paris yanalengakuboresha utekelezaji wa mkataba ule wa mwaka 1992 kwakufanya yafuatayo:-

Kwanza kutunza misitu inayonyonya joto; kuandaana kutekeleza mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi;kuwa na mifumo ya upatikanaji wa fedha na teknolojia safikwa nchi zinazoendelea kwa ajil i ya kukabiliana nachangamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuwekautaratibu wa kuzijengea uwezo nchi zinazoendelea katikakukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi;

Na kwa kuwa makubaliano haya yalitiwa saini nanchi wanachama ikiwemo Jamhuri ya Muungano waTanzania tarehe 22 Aprili, 2016 huko New York, Marekani;

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

72

Na kwa kuwa makubaliano haya yatawezesha nchiwanachama kuchukua hatua madhubuti katika kuuboreshautekelezaji wa mkataba huu ikiwa ni pamoja na kuongezaushirikishwaji wa nchi zote duniani katika juhudi zakuhakikisha kwamba joto duniani haliongezeki zaidi yacentigrade degree mbili kabla ya mwisho wa karne hii nakuongezeka kwa uwezo wa nchi kuhimili athari za mabadilikoya tabianchi na kuchochea upunguzaji wa gesijoto usioathirimaendeleo na uhakika wa chakula kwa nchi husika,kuongezeka kwa upatikanaji wa fedha na teknolojia kwaajili ya kusaidia maendeleo himilivu;

Na kwa kuwa ni muhimu kwa nchi yetu iridhiemakubaliano haya ili kuwezesha utekelezaji wake, wenyelengo la kupambana na changamoto zilizojitokeza katikautekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi wamwaka 1992 na kuendelea kunufaika na ushirikiano wakikanda na wa kimataifa katika kukabiliana na changamotoza mabadiliko ya tabianchi;

Na kwa kuwa hatua hii itasaidia kuongeza uwezowa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kupatateknolojia safi ambazo zitasaidia katika mikakati ya Serikaliya kujenga uchumi endelevu wa viwanda na wenyekustahimili mabadiliko ya tabianchi; Na kwa kuwa nchi yetukwa kuweka saini makubaliano haya na hatimayekuyatekeleza itanufaika na mambo yafuatayo:-

Kwanza, kuwa miongoni mwa nchi zilizo mstari wambele katika kupambana na athari za mabadiliko yatabianchi ili kunusuru uchumi wa nchi yetu; kuimarika kwaushirikiano baina ya nchi yetu na jumuiya ya kimataifa katikakusimamia na kutekeleza masuala yanayohusu mabadilikoya tabianchi; kuongeza upatikanaji wa fursa zilizopo na zamiradi na teknolojia safi itakayowezesha matumizi ya gesiasilia majumbani na viwandani ili kuchochea maendeleo yaviwanda kwa kutumia nishati yenye bei nafuu na kuimarishahali ya uchumi wa nchi na kujenga uchumi endelevu waviwanda na wenye kustahimili mabadiliko ya tabianchi nakuimarisha mipango ya Taifa ya kuhimili athari ya mabadiliko

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

73

ya tabianchi ili kupunguza majanga yatokanayo na atharihizo; Na kwa kuwa utekelezaji wa makubaliano hayo ni wahiari na nchi ina uhuru wa kujitoa; Na kwa kuwa katika Kikaocha Baraza la Mawaziri cha Nne cha mwaka 2017/2018kilikubali Makubaliano ya Paris kuhusu kuboresha utekelezajiwa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi yaridhiwe na Bungela Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

Hivyo basi kwa kuzingatia manufaa yatokanayo namkataba huu na itifaki yake kwa Tanzania na pia umuhimuwa manufaa ya makubaliano hayo, Bunge hili katikaMkutano wa Kumi na Moja na kwa mujibu wa Ibara ya63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yamwaka 1977 linaazimia kuridhia Makubaliano ya Paris kuhusuKuboresha Utekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko yaTabianchi. Naomba kuwasilisha.

NAIBU SPIKA: Toa hoja Mheshimiwa JanuaryMakamba.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liridhieMakubaliano ya Paris kuhusu Kuboresha Utekelezaji waMkataba wa Makubaliano ya Tabianchi (The Paris Agreementunder the United Nations Framework Convention on ClimateChange).

MAELEZO YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS(MUUNGANO NA MAZINGIRA), MHESHIMIWA JANUARY

YUSUF MAKAMBA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI AZIMIO LABUNGE LA KURIDHIA MAKUBALIANO YA PARIS CHINI YA

MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MKATABA WAMABADILIKO YA TABIANCHI (THE PARIS AGREEMENT UNDERTHE UN FRAMEWORK CONVENTION ON CLIMATE CHANGE)

KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

Mheshimiwa Spika, Mkutano wa Kimataifa kuhusuBinadamu na Mazingira ulifanyika huko Stockholm, Swedentarehe 5-16 Juni 1972. Mkutano huo ulisisitiza kuwa

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

74

maendeleo ya kiuchumi ni lazima yaende sambamba nasuala la hifadhi ya Mazingira. Aidha, mwanzoni mwa miakaya themanini wanasayansi walianza kutoa taarifa kwambajoto la dunia lilianza kuongezeka kuanzia kipindi chamapinduzi ya viwanda. Kufuatia angalizo hilo, mwaka 1988,Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) kwakushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)walipitisha uamuzi wa kuunda Jopo la Kimataifa kuhusuMabadiliko ya Tabianchi (Intergovernmental Panel on ClimateChange – IPCC). Lengo la Jopo hilo lilikuwa kujadili matokeoya uchunguzi wa kisayansi kuhusu sababu za ongezeko lajoto duniani ambalo lilionekana kusababisha mabadiliko yatabianchi. Taarifa ya kwanza ya Jopo ilitolewa mwaka 1990na kuwasilishwa mbele ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa(UN General Assembly). Baada ya kujadili taarifa hiyo Mkutanowa Umoja wa Mataifa uliunda Kamati ya Majadiliano yaKimataifa (Intergovernmental Negotiating Committee - INC)ambayo ilianzisha majadiliano ya kuunda Mkataba waMabadiliko ya Tabianchi. Tarehe 5 Mei 1992 Mkataba waUmoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi ulipitishwahuko Rio de Janeiro, Brazil wakati wa Mkutano wa Duniakuhusu mazingira na maendeleo.

Mheshimiwa Spika, Tanzania iliridhia Mkataba waUmoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi mwaka 1996na Itifaki yake ya Kyoto mwaka 2002. Lengo la Mkataba huuni kuzuia ongezeko la gesijoto na athari zitokanazo namabadiliko ya tabianchi kwenye mifumo ya ikolojia ya duniaili kuhakikisha maendeleo endelevu duniani. Mabadiliko yatabianchi ni mabadiliko katika mifumo ya hali ya hewayanayosababishwa na ongezeko la joto la dunia. Sababuza kuongezeka kwa gesijoto ni kutokana na matumizimakubwa ya nishati chafuzi kwa shughuli za maendeleozilizofanyika katika nchi zilizoendelea kwa zaidi ya miaka 150iliyopita. Athari zitokanazo na mabadiliko hayo ni pamojana ukame, mafuriko, kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza,kumezwa kwa visiwa vidogo kwenye bahari kutokana nakuongezeka kwa ujazo wa maji ya bahari, kuyeyuka kwabarafu katika vilele vya milima mirefu kama vile MlimaKilimanjaro, uharibifu wa madaraja, reli, barabara na makazi

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

75

kutokana na mafuriko na kuongezeka kwa vimbunga.Majanga haya huathiri zaidi nchi maskini kutokana na uwezowake mdogo wa kuhimili.

Mheshimiwa Spika, Kwa kutambua changamoto yamabadiliko ya tabianchi na umuhimu wa kila mtanzaniakuishi katika mazingira bora na salama, Tanzania ni miongonimwa nchi zilizoko mstari wa mbele katika uhifadhi wamazingira na imetenga zaidi ya asilimia 30 ya ardhi kwa ajiliya uhifadhi. Hivyo, kuridhia Makubaliano haya kutasaidiautekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.Tanzania imekuwa ikishirikiana na nchi nyingine katikautekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi tanguulipopitishwa. Katika ushirikiano huo Tanzania imenufaika namiradi yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni300 ambayo imesaidia yafuatayo: - ununuzi wa vifaa vyautabiri wa hali ya hewa vyenye thamani ya zaidi ya sh. 150milioni. na vitendea kazi vya Ofisi; kujenga uwezo wawataalam ambapo watanzania zaidi ya 200 wamefadhiliwakusomea masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika ngaziya shahada ya uzamili na zaidi ya 50 shahada ya uzamifu;kuongeza ushiriki na ushawishi katika agenda na mikakatiya jumuiya ya kimataifa kuhusu suala la mabadiliko yatabianchi; Kuanzisha Kituo cha Mafunzo ya Mabadiliko yaTabianchi (Centre for Climate Change Studies) katika ChuoKikuu cha Dar es Salaam; mradi wa kusambaza maji kutokaZiwa Victoria hadi Mkoa wa Simiyu.

Mheshimiwa Spika, manufaa mengine yaliyotokanana uanachama wa Tanzania kwenye Mkataba waMabadiliko ya Tabianchi ni utekelezaji wa Mradi wa KuhimiliMabadiliko ya Tabianchi Katika Maeneo ya Pwani ya TanzaniaBara na Zanzibar ambao umejenga ukuta wa fukwe katikamaeneo ya Barabara ya Obama - Ocean Road (920m) naKigamboni (Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere– 480m); ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua ili kupunguzamafuriko maeneo ya Bungoni (475m), kata ya Buguruni (Wilayaya Ilala) na Miburani – Mtoni (550m) (Wilaya ya Temeke); Mradiwa kuongeza uhimili ambao uliwezesha upatikanaji wa majikatika Wilaya za Igunga mkoani Tabora katika Vijiji vya

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

76

Nanga, Igumbi, Majengo na Itunduru, Nyasa mkoani Ruvumakijiji cha Ng’ombo, Misenyi mkoani Kagera katika vijiji vyaByeju, Mbale, Kanyigo, Kashasha, Bukwali na Kitobo na Wilayaya Kaskazini A kijiji cha Nungwi; Mradi wa Vijiji vya Mfano(Eco-villages Project) ambao umewezesha upatikanaji wanishati na kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi katikavijiji vya Chololo - Dodoma; Luguru - Morogoro; na Zanzibar.Mradi wa kurejeleza ardhi iliyoharibika na kuongeza usalamawa chakula katika maeneo kame ya nyanda za kati(Reversing land degradation trends and increasing foodsecurity in degraded ecosystems of semi-arid areas of centralTanzania). Mradi unalenga kurejesha mifumo ya ikolojia yakilimo iliyoharibika ili kuongeza uzalishaji wa chakula katikamaeneo kame na pwani ya nchi. Mradi unatekelezwa katikaKata ya Haubi (Halmashauri ya Kondoa); Kata ya Sigili(Halmashauri ya Nzega); Kata ya Mpambala (Halmashauriya Mkalama); Kata ya Sukuma (Halmashauri ya Magu); naKata ya Micheweni na Kiuyu Maziwa Ngombe, katika wilayaya Micheweni, Kaskazini Pemba.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kuhimili Mabadiliko yaTabianchi katika maeneo ya Vijijini kupitia Mfumo Ikolojia(Ecosystem-Based Adaptation for Rural Resilience in Tanzania).Lengo la mradi ni kuziongezea jamii za vijijini uwezo wakuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha uhimilivuwa mfumo-ikolojia na kupata njia mbadala za kujengaustawi wa jamii. Mradi huu utatekelezwa katika Halmashauritano (5) ambazo ni: - Kishapu (Shinyanga), Mpwapwa(Dodoma), Mvomero (Morogoro), Simanjoro (Manyara) naKaskazini Unguja, Shehia A (Unguja).

Vilevile chini ya Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchikimeanzishwa Kituo cha Kitaifa cha Ufuatiliaji na Upimaji waHewa Ukaa (National Carbon Monitoring Centre- NCMC)kilichopo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA). Kwaujumla miradi chini ya Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchiimetekelezwa katika pande zote za Muungano.

Mheshimiwa Spika, pamoja na faida hizo, utekelezajiwa Mkataba huu na Itifaki yake umekumbwa na

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

77

changamoto kadhaa zikiwemo: kutoshirikisha nchi zotekatika upunguzaji wa gesijoto hivyo kusababisha upunguzajiwake kuwa mdogo na kuongezeka kwa gharama zakukabiliana na majanga ya athari za mabadiliko ya tabianchihasa kwa nchi maskini. Katika kukabiliana na changamotohizo, Mkutano wa 21 wa Nchi Wanachama wa Mkataba waMabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Paris, Ufaransa, Desemba,2015 ulipitisha Makubaliano ya Paris. Makubaliano ya Parisyana malengo makuu yafuatayo: - kuongeza ushirikishwajiwa nchi zote duniani katika juhudi za kuhakikisha joto laDunia haliongezeki zaidi ya 2oC kabla ya mwisho wa karnehii na kuhakikisha kuwa ongezeko ya gesijoto linabaki chiniya 1.5oC ikilinganishwa na kabla ya maendeleo ya viwanda;kuongeza uwezo wa nchi kuhimili athari za mabadiliko yatabianchi na kuchochea upunguzaji wa gesijoto usioathirimaendeleo na uhakika wa chakula kwa nchi husika;kuongeza upatikanaji wa fedha na teknolojia kwa ajili yakusaidia maendeleo himilivu.

Mheshimiwa Spika, Tanzania ni miongoni mwa nchizinazoathirika na mabadiliko ya tabianchi katika sekta zote.Hivyo, kuridhia Makubaliano ya Paris kutasaidia kuongezauwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi, kupatateknolojia safi (clean technology) ambazo zitasaidia katikamikakati ya serikali ya kujenga uchumi endelevu wa viwandana wenye kustahimili mabadiliko ya tabianchi; kuongezauzalishaji na upatikanaji wa chakula; kutunza misitu ambayoiko hatarini kutoweka; kuandaa na kutekeleza mikakati namipango ambayo itasaidia kuhimili athari za mabadiliko yatabianchi katika sekta za afya, kilimo, maji na sekta nyinginezinazoathirika na mabadiliko ya tabianchi. Aidha, Tanzaniaitapata fedha za kutekeleza programu na miradi kupitiaMifuko kama vile Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi na Taasisiza Kimataifa kama vile umoja wa nchi za African Caribbeanand Pacific (ACP).

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Makubaliano yaParis utazingatia misingi ya usawa, uwezo na historia ya nchina hali ya uchumi wake. Aidha, chini ya Makubaliano hayo,Tanzania haitabanwa au kulazimishwa kupunguza uzalishaji

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

78

wa gesijoto bali itashiriki katika juhudi hizo kwa hiari bilakushurutishwa. Hata kama Tanzania ingekuwa inabanwakisheria kupunguza uzalishaji wa gesijoto bado ina ziada yauwezo wa kunyonya gesijoto kupitia misitu yake. Kwa sasaTanzania inazalisha kiasi cha tani za hewa ya kaboni 0.2pekee kwa mwaka wakati ina misitu takribani hekari 48millioni ambayo ina uwezo wa kunyonya kiasi cha tani 9 zahewa ya kaboni. Aidha, ardhi ya Tanzania ina eneo latakriban asimilia 30 ambalo limehifadhiwa kisheria nalinaendelea kunyonya gesijoto zinazozalishwa duniani bilamipaka. Hata hivyo, utekelezaji wa Makubaliano ya Paris niwa hiari, hakuna sheria za kuzibana nchi wanachama naMakubaliano haya yanaruhusu nchi kujitoa.

Mheshimiwa Spika, Kwa nchi kuwa Mwanachamawa Makubaliano ya Paris, Ibara ya 20 inaelekeza nchi husikakuridhia Makubaliano haya kama ilivyo kwa mikatabamingine ya kimataifa. Hadi kufikia tarehe 21 Aprili, 2016(Kipindi maalum kichowekwa kwa nchi kusaini), jumla ya nchi182 zilikuwa zimesaini ikiwemo Tanzania. Aidha, kufikia tarehe28 Machi, 2018 jumla ya nchi 175 zilikuwa zimeridhia. Baadaya kufikia akidi inayohitajika (55), Makubaliano ya Parisyameingia katika hatua ya utekelezaji kabla ya mudauliopangwa ambao ni mwaka 2020. Kimsingi, utekelezajiwake umeanza tangu tarehe 4 Novemba, 2016. Hivyo, kunaumuhimu wa Tanzania kuridhia ili iungane na nchi nyinginekatika utekelezaji na kuendelea kunufaika na fursa zilizopo.Kwa upande wa Bara la Afrika, hadi kufikia tarehe 26 Machi2018, nchi 45 zilikuwa zimeridhia.

Mheshimiwa Spika, vipengele muhimu vyaMakubaliano ya Paris ni kama ifuatavyo: -

Moja, Ibara ya 2: Lengo la Makubaliano. Lengo nikushirikisha nchi zote wanachama katika juhudi zakushughulikia mabadiliko ya tabianchi hasa upunguzaji wagesijoto na kusaidia nchi zinazoendelea kuhimili athari zamabadiliko ya tabianchi, kuongeza upatikanaji wa chakulana kuchochea maendeleo endelevu. Utekelezaji utazingatiamisingi ya usawa, uwezo na hali ya uchumi wa nchi husika.

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

79

Mbili, Ibara ya 3: Wajibu wa nchi katika kutekelezaMakubaliano ya Paris. Nchi itatakiwa kuandaa nakuwasilisha taarifa kuhusu juhudi zake katika kufikia malengoya Makubaliano ya Paris kama yalivyoainishwa katika Ibaraya 4, 7, 9, 10, 11 na 13. Nchi zilizoendelea zitawajibikakuchangia fedha za kusaidia Nchi zinazoendelea kutekelezaprogramu na miradi ya kuhimili athari za mabadiliko hayana miradi ya upunguzaji gesijoto.

Tatu, Ibara ya 4: Muda wa kufikia kiwango cha juucha upunguzaji gesijoto. Nchi zinatakiwa kupunguza gesijotokwa lengo la kufikia kiwango cha juu cha upunguzaji kwakuzingatia misingi ya usawa na maendeleo endelevu nakuondoa umasikini. Makubaliano yanabainisha kuwa nchizinazoendelea zitahitaji muda mrefu zaidi kufikia kiwangocha juu cha kupunguza gesijoto.

Nne, Ibara ya 5: Sekta ya misitu. Kila nchimwanachama inahimizwa kutunza misitu inayonyonyagesijoto. Juhudi hizi zikizingatiwa zitachangia kuongezekakwa motisha na kasi ya kutunza misitu ambayo huchangiaupatikanaji wa mvua na kuhifadhi vyanzo vya maji nchini.

Tano, Ibara ya 6: Ushirikiano wa Hiari katikautekelezaji. Nchi zitashirikiana kwa hiari katika utekelezaji wamikakati ya kupunguza gesijoto na kuhimili mabadiliko yatabianchi na kuchochea maendeleo endelevu na hifadhi yamazingira. Mfumo wa kusimamia upunguzaji wa gesijotoumeanzishwa ili kutoa motisha na kuchochea ushiriki wataasisi za umma na sekta binafsi katika upunguzaji wagesijoto na kuchochea maendeleo endelevu.

Sita, Ibara ya 7: Kuhimili mabadiliko ya tabianchi.Kila nchi mwanachama inawajibika kuandaa na kutekelezamipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Kuimarishauwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchiutasaidia kupunguza athari za ukame, mafuriko, na kudhibitikuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

80

Saba, Ibara ya 9: Upatikanaji wa fedha zautekelezaji. Makubaliano ya Paris yanatoa haki kwa Nchizinazoendelea ambazo ni Mwanachama kupata fedha zakushughulikia changamoto za kukabiliana na mabadiliko yatabianchi kupitia ufadhili wa Mifuko ya Mabadiliko yaTabianchi na wadau wengine. Nchi zilizoendelea zitatakiwakutoa taarifa kila baada ya miaka miwili kuhusu kiwangocha fedha walizotoa au wanatarajia kutoa kama msaadakwa nchi ambazo ziko hatarini kuathirika na mabadiliko yatabianchi.

Nane, Ibara ya 10: Teknolojia. Ibara imeweka mfumowa Nchi Zinazoendelea kupata teknolojia za kukabiliana namabadiliko ya tabianchi.

Tisa, Ibara ya 11: Kujengewa uwezo. NchiZinazoendelea zina haki ya kujengewa uwezo na uelewakatika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi. Hali ambayoitaongeza uelewa kwa jamii kuhusu hatua za kuchukua ilikupunguza athari za mabadiliko haya katika maeneo yao.

Kumi, Ibara ya 13: Uwazi katika utekelezaji. Ibarainazitaka nchi wanachama kuwa na mfumo wa uwazi wakupeana taarifa kuhusu utekelezaji wa Makubaliano ilikuhakikisha malengo yake yanafikiwa. Mfumo huuutatambua uwezo mdogo wa nchi maskini na utatekelezwakwa hiari bila kuingilia uhuru wa nchi husika.

Kumi na Moja, Ibara ya 20: Utaratibu wa uridhiaji.Kila nchi itaridhia kulingana na utaratibu wake. Pale ambapojumuiya yoyote ambayo Tanzania ni mwanachama itaamuakujiunga na Makubaliano haya, utaratibu wa mgawanyo wamajukumu ya utekelezaji utaridhiwa baina ya Tanzania najumuiya husika.

Kumi na Mbili, Ibara ya 28: Uhuru wa kujitoa. Nchiina uhuru wa kujitoa baada ya kupita miaka mitatu ya kuwamwanachama. Aidha, Nchi ikijitoa kwenye Mkataba mama(Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi) itahesabika imejitoapia kwenye Makubaliano haya.

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

81

Mheshimiwa Spika, Kwa kuwa Tanzania inaingiakwenye uchumi wa viwanda, Makubaliano ya Parisyatasaidia kuchochea matumizi ya gesi asilia; upatikanaji wateknolojia safi; kufunza watalaam wetu, na kuendelea kuwana vyanzo vya nishati endelevu ili kukabiliana na uchafuziwa mazingira. Aidha, Makubaliano ya Paris yataongezaushirikiano, upatikanaji wa fedha, kuchochea biashara yahewa ukaa na upashanaji taarifa.

Mheshimiwa Spika, Kwa Tanzania utaratibu wakuridhia utazingatia Ibara ya 63 (3) (e) ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambayo inalipamadaraka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kujadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na ambayo kwa masharti yakeinahitaji kuridhiwa. Hati ya kuridhia itawasilishwa kwa KatibuMkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ana jukumu la kupokeana kuhifadhi Hati hizo.

Mheshimiwa Spika; baada ya maelezo haya, sasanaomba kuwasilisha Azimio la Bunge la kuridhia kamaifuatavyo: -

KWA KUWA, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimiongoni mwa Nchi Wanachama wa Mkataba waMabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 1992 na Itifaki yake yaKyoto ya mwaka 1997;

NA KWA KUWA, Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniailiridhia Mkataba mwaka 1996 na Itifaki yake mwaka 2002;

NA KWA KUWA, Lengo kuu la Mkataba huu na Itifakiyake ni kuzuia ongezeko la gesijoto, na athari zitokanazo namabadiliko ya tabianchi kwenye mifumo ya ikolojia ya Duniaili kuhakikisha maendeleo endelevu diniani;

NA KWA KUWA, mabadiliko ya tabianchiyanasababisha athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukame,mafuriko, kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza, kumezwakwa visiwa vidogo kwenye bahari kutokana na kuongezeka

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

82

ujazo wa maji ya bahari, kuyeyuka kwa barafu katika vilelevya milima mirefu kama vile Mlima Kilimanjaro na uharibifuwa miundombinu ya barabara, reli na makazi kutokana namafuriko na kuongezeka kwa vimbunga;

NA KWA KUWA, Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniani miongoni mwa Nchi zinazoathirika na matokeo hasi yamabadiliko ya tabianchi;

NA KWA KUWA, tangu Mkataba huu na Itifaki yakeuridhiwe na Nchi Wanachama kuanza kutekelezwa mwaka1996 na 2002, kumejitokeza changamoto katika utekelezajiikiwa ni pamoja na: Nchi Zilizoendelea kuogopa kupotezanguvu za kiuchumi kwa sababu utekelezaji wa Mkataba huuutaathiri uzalishaji viwandani kwa kupunguza matumizi yanishati chafu; ushindani wa kiuchumi baina ya NchiZinazoendelea na zile zenye uchumi unaokua harakaunasababisha kuongezeka kwa viwanda vinavyochafuamazingira; na kutoshirikisha nchi zote katika upunguzaji wagesijoto kunasababisha upunguzaji wake kuwa mdogo nakuongezeka kwa gharama za kukabiliana na majanga yamabadiliko ya tabianchi hasa kwa Nchi Zinazoendelea;

NA KWA KUWA, Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniainatambua changamoto hizo na umuhimu wa kila Mtanzaniakuishi katika mazingira bora na salama;

NA KWA KUWA, katika Mkutano wa 21 wa NchiWanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchiuliofanyika Paris – Ufaransa Desemba, 2015, Nchi Wanachamawa Mkataba walipitisha Makubaliano ya Paris kwa lengo lakuboresha utekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko yaTabianchi;

NA KWA KUWA, Makubaliano ya Paris yanalengakuboresha utekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko yaTabianchi wa mwaka 1992 kwa kufanya yafuatayo: - kutunzamisitu inayonyonya joto; kuandaa na kutekeleza Mipangoya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi; kuwa na mifumo ya

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

83

upatikanaji wa fedha na teknolojia safi kwa NchiZinazoendelea kwa ajili ya kukabiliana na changamoto yaTabianchi; na kuweka utaratibu wa kuzijengea uwezo Nchizinazoendelea katika kukabiliana na changamoto zamabadiliko ya Tabianchi;

NA KWA KUWA, Makubaliano haya yalitiwa saini naNchi Wanachama ikiwemo Jamhuri ya Muungano waTanzania tarehe 22 Aprili, 2016 huko New York - Marekani;

NA KWA KUWA, Makubaliano haya yatawezesha NchiWanachama kuchukua hatua madhubuti katika kuboreshautekelezaji wa Mkataba ikiwa ni pamoja na kuongezaushirikishwaji wa nchi zote duniani katika juhudi zakuhakikisha joto Dunia haliongezeki zaidi ya 20C kabla yamwisho ya karne hii, kuongeza uwezo wa nchi kuhimilimabadiliko, athari za mabadiliko ya tabianchi na kuchocheaupunguzaji wa gesijoto usioathiri maendeleo na uhakika wachakula kwa nchi husika, kuongeza upatikanaji wa fedhana teknolojia kwa ajili ya kusaidia maendeleo himilivu;

NA KWA KUWA, ni muhimu nchi yetu ir idhieMakubaliano hayo, ili kuwezesha utekelezaji wake wenyelengo la kupambana na chamgamoto zinazojitokeza katikautekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi wamwaka 1992, na kuendelea kunufaika na ushirikiano waKikanda na Kimataifa katika kukabiliana na changamotoza mabadiliko ya tabianchi;

NA KWA KUWA, hatua hii itasaidia kuongeza uwezowa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi, kupatateknolojia safi (clean technology) ambazo zitasaidia katikamikakati ya Serikali ya kujenga uchumi endelevu wa viwandana wenye kustahimili mabadiliko ya tabianchi;

NA KWA KUWA, Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwa kuweka saini Makubaliano hayo na hatimayekuyatekeleza itanufaika na mambo yafuatayo: -

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

84

a) kuwa miongoni mwa nchi zilizoko mstari wa mbelekatika kupambana na tatizo la mabadiliko ya tabianchi ilikunusuru uchumi wa nchi yetu;

b) kuimarika kwa ushirikiano baina ya Nchi yetu naJumuia ya Kimataifa katika kusimamia na kutekelezamasuala yanayohusu mabadiliko ya tabianchi;

c) kuongeza upatikanaji wa fursa zilizopo za miradina teknolojia safi itakayowezesha matumizi ya gesi asiliamajumbani na viwandani ili kuchochea maendeleo yaviwanda kwa kutumia nishati yenye bei nafuu;

d) kuimarisha hali ya uchumi wa nchi na kujengauchumi endelevu wa viwanda wenye kustahimili mabadilikoya tabianchi;

e) kuimarika kwa mipango ya Taifa ya kuhimili athariza mabadiliko ya tabianchi i l i kupunguza majangayatokanayo na athari hizo;

NA KWA KUWA, utekelezaji wa Makubaliano hayo niwa hiari na nchi ina uhuru wa kujitoa;

NA KWA KUWA, Baraza la Mawaziri katika Kikao chakeNa. 4/2017 -18 lilikubali Makubaliano ya Paris kuhusu KuboreshaUtekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchiyaridhiwe na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

HIVYO BASI, kwa kuzingatia manufaa yatokanayo naMkataba huu na Itifaki yake kwa Tanzania na pia umuhimuna manufaa ya Makubaliano hayo, Bunge hili katika Mkutanowa Kumi na Moja na kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka1977, linaazimia kuridhia Makubaliano ya Paris kuhusukuboresha utekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko yaTabianchi yaani THE PARIS AGREEMENT UNDER THE UNFRAMEWORK CONVENTION ON CLIMATE CHANGE.

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

85

Mheshimiwa Spika; naomba kuwasilisha na kutoahoja.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono.

Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea na utaratibuwetu. Sasa nimuite Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda,Biashara na Mazingira, kwa niaba yake Makamu MwenyekitiMheshimiwa Innocent Bashungwa.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA - MAKAMUMWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwaniaba ya Mwenyekiti, naomba kuwasilisha maoni ya Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingirakuhusu Makubaliano ya Paris yatokanayo na utekelezaji waMkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (The Paris Agreementunder the UN Framework Convention on Climate Change).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya53(3) na (4), ikisomwa pamoja na Nyongeza ya Nane, Kanuniya 7(1)(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari,2016, hoja ya Serikali kuhusu Azimio la Bunge KuridhiaMakubaliano ya Paris yatokanayo na utekelezaji wa Mkatabawa Mabadiliko ya Tabianchi ililetwa mbele ya Kamati yaViwanda, Biashara na Mazingira kwa ajili ya kulipitia,kulichambua na hatimaye kulishauri Bunge kuliridhia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya53(6)(b) naomba kuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumuya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Azimiola Bunge Kuridhia Makubaliano ya Paris.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jamhuri ya Muungano waTanzania ni nchi mwanachama wa Mkataba wa Paris wa

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

86

Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 1992 na Itifaki yake yaKyoto ya mwaka 1997 (Kyoto Protocol). Tanzania iliridhiamkataba huu tarehe 17 Aprili, 1996 na itifaki yake mwaka2002.

Mheshimiwa Naibu Spika, chimbuko la mkataba wamabadiliko; katika kutekeleza mkataba huu na itifaki zakekumejitokeza changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:-

(i) Baadhi ya nchi wanachama kuhofia kupotezanguvu za kiuchumi kwa sababu utekelezaji wa mkataba huuutaathiri uzalishaji viwandani kwa kupunguza matumizi yanishati chafu;

(i i) Ushindani wa kiuchumi baina ya nchizinazoendelea na zile zenye uchumi unaokua harakaunasababisha kuongezeka kwa viwanda vinavyochafuamazingira; na

(iii) Kutoshirikisha nchi zote katika upunguzaji wagesijoto na kuongezeka kwa gharama za kukabiliana namajanga ya mabadiliko ya tabianchi, hasa kwa nchizilizoendelea kukwepa gharama zinazosababishwa na athariza kuongezeka kwa gesijoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kukabiliana nachangamoto tajwa, nchi wanachama wa Mkataba waMabadiliko ya Tabianchi walipitisha Makubaliano ya Paris kwalengo la kuboresha utekelezaji wa Mkataba wa Mabadilikoya Tabianchi wa mwaka 1992. Makubaliano haya yalifikiwakatika Mkutano wa 21 uliyofanyika Paris, Ufaransa tarehe 30Novemba hadi tarehe 22 Desemba, 2015 na kutiwa saini nanchi wanachama ikiwemo Jamhuri ya Muungano waTanzania tarehe 22 Aprili, 2016 huko New York, Marekani.

Mheshimiwa Naibu Spika, dhumuni la mabadilikohaya ni kuboresha utekelezaji wa mkataba kwa kuwekawajibu wa nchi wanachama kutekeleza mabadiliko ya Pariskama ifuatavyo:-

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

87

(i) Kuongeza ushirikishwaji wa nchi zote duniani katikajuhudi za kuhakikisha joto haliongezeki zaidi ya centigradembili kabla ya mwisho wa karne hii ya 21;

(ii) Kuweka utaratibu wa kuzijengea uwezo nchizinazoendelea katika kukabiliana na changamoto zamabadiliko ya tabianchi;

(iii) Nchi kuhimizwa kutunza misitu inayonyonyagesijoto; na

(iv) Kuzuia ongezeko la gesijoto na athari zitokanazona mabadiliko ya tabianchi kwenye mifumo ya ikolojia yadunia ili kuhakikisha maendeleo endelevu duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, namna Kamatiilivyoshughulikia hoja hii; katika kushughulikia Azimio hili,Kamati ilikutana na kupata maelezo ya Serikali kuhusupendekezo la kuridhia mabadiliko ya Mkataba wa Paris waMabadiliko ya Tabianchi siku ya Jumatano, tarehe 28 Machi,2018. Kabla ya kupokea na kujadili taarifa ya Serikali kuhusuAzimio hili, Kamati ilipokea na kujadili taarifa ya uchambuziwa Azimio kutoka kwa Mshauri wa Bunge wa Mambo yaSheria. Uchambuzi huo uliisaidia Kamati kuwa katika nafasinzuri kuifanyia kazi hoja hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilijiridhisha kuwamabadiliko haya hayakinzani na Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na sheria za nchi zinazohusiana nausimamizi wa uhifadhi wa mazingira. Faida zitakazopatikanakutokana na kuridhia makubaliano hayo ni pamoja na:-

(i) Kuimarisha ushirikiano miongoni mwa nchiwanachama katika kukabiliana na athari za mabadiliko yatabianchi;

(ii) Kuongeza fursa za upatikanaji wa miradi nateknolojia za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi; na

(iii) Kuogeza mipango ya Taifa katika kukabiliana naathari za mabadiliko ya tabianchi.

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

88

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilijiridhisha kuhusumaudhui ya Makubaliano ya Paris kwa kupitia vifungu vyamkataba huo. Baadhi ya vifungu muhimu katikaMakubaliano ya Paris ni pamoja na Ibara ya Tatu ambayoinaweka wajibu wa kila nchi katika kutekeleza Makubalianoya Paris ambapo kila nchi itatakiwa kuandaa na kuwasilishataarifa kuhusu juhudi zake katika kufikia malengo yamakubaliano. Katika makubaliano haya, nchi zilizoendeleazitapaswa kuchangia fedha katika kutekeleza programu namiradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchina miradi ya upunguzaji gesijoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya Sita yaMakubaliano ya Paris inazitaka nchi wanachama kuwa naushiriki wa hiari katika utekelezaji wa mikakati ya kupunguzagesijoto na kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuchocheamaendeleo endelevu na uhifadhi wa mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya Tisa yaMakubaliano ya Paris inaelezea manufaa ya makubalianohaya kifedha. Makubaliano ya Paris yameweka utaratibu wanchi zinazoendelea ambazo ni wanachama kupata fedhaza kushughulikia changamoto za kukabiliana na mabadilikoya tabianchi kupitia ufadhili wa mifuko ya mabadiliko yatabianchi na wadau wengine. Aidha, nchi zilizoendeleazitatakiwa kutoa taarifa kila baada ya miaka miwili kuhusukiwango cha fedha walichotoa au wanachotarajia kutoakwa msaada wa nchi ambazo ziko hatarini kuathirika namabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 13 ya Makubalianoya Paris inatambua uwezo mdogo wa nchi zinazoendelea,hivyo, imeweka utaratibu wa hiari katika utekelezaji pasipokuingilia uhuru wa nchi wanachama. Faida za kuridhia Azimiohili ni nyingi kuliko gharama.

Mheshimiwa Naibu Spika, maoni na ushauri waKamati; naomba sasa kutoa maoni na mapendekezo yaKamati kama ifuatavyo:-

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

89

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa lengo laMakubaliano ya Paris ni kuzuia ongezeko la gesijoto na atharizitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi;

Kwa kuwa sisi sote ni mashuhuda wa athari zamabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali nchini,ikiwa ni pamoja na ukame, mafuriko, kuenea kwa magonjwaya kuambukiza, kumezwa kwa visiwa vidogo kwenye baharina maziwa kutokana na kuongezeka kwa ujazo wa maji,kuyeyuka kwa barafu katika kilele cha Mlima Kilimanjaro nauharibifu wa miundombinu ya barabara na makazi kutokanana mafuriko;

Na kwa kuwa Makubalino ya Paris yanalengakuandaa na kutekeleza mipango ya kuhimili mabadiliko yatabia nchi na kuweka mifumo ya upatikanaji wa fedha nateknolojia safi kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwaajili ya kukabiliana na changamoto tajwa na kuwekautaratibu wa kuzijengea uwezo nchi zinazoendelea katikakukabiliana na changamoto hizo;

Hivyo basi, Kamati inalishauri Bunge lako Tukufukuridhia Makubaliano ya Paris ili kuwezesha utekelezaji wakewenye lengo la kupambana na changamoto za mabadilikoya tabia nchi kama tulivyoainisha hapo awali.

Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho; naomba nitumienafasi hii kwa niaba ya Kamati kumshukuru sana MheshimiwaSpika na wewe Mheshimiwa Naibu Spika kwa uongozi wenumahiri. Kwa niaba ya Mwenyekiti wangu MheshimiwaSuleiman Saddiq na Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati wotetunapenda kumhakikishia Mheshimiwa Spika na weweMheshimiwa Naibu Spika kuwa tutafanya kazi kwa weledina uadilifu mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue nafasihii kuwapongeza Mheshimiwa Adrew Chenge, Mheshimiwa

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

90

Mussa Zungu na Mheshimiwa Najma Giga kwa kuchaguliwakwa mara nyingine kuendelea kuliongoza Bunge letu.Naomba pia kuwapongeza Wenyeviti na Makamu Wenyevitiwote wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kuchaguliwakwao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inapendakumshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) Mheshimiwa January Makamba,Naibu Waziri wake Mheshimiwa Kangi Lugola, MakatibuWakuu pamoja na wataalam wote wa Ofisi ya Makamu waRais kwa ushirikiano walioutoa wakati wa kujadili Azimio hili.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekeekabisa, napenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamatiya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa ushirikianowaliutoa wakati wa kupitia, kuchambua na hatimayekuwasilisha maoni kuhusu Azimio hili mbele ya Bunge lakoTukufu. Orodha yao ni kama inavyosomeka hapo chini nakwa ruhusa yako, naomba majina yao yaingie kwenyeKumbukumbu Rasmi za Bunge yaani Hansard. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee,napenda kumshukuru Katibu wa Bunge, Ndugu StephenKagaigai kwa ushirikiano ambao amekuwa akiutoa kwaKamati. Pamoja na yeye namshukuru Mkurugenzi wa Idaraya Kamati Bwana Athuman Hussein, Mkurugenzi Msaidizi,Sehemu ya Fedha na Uchumi, Bwana Michael Chikokoto,Makatibu wa Kamati Bwana Wilfred Magova na Bi. ZainabuMkamba na Msaidizi wa Kamati Bi. Pauline Mavunde kwakuratibu vyema shughuli za Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha nanaunga mkono Azimio. (Makofi)

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

91

MAONI NA USHAURI WA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARANA MAZINGIRA KUHUSU MAKUBALIANO YA PARIS KUHUSU

KUBORESHA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MABADILIKO YATABIANCHI (THE PARIS AGREEMENT UNDER THE UNFRAMEWORK CONVENTION ON CLIMATE CHANGE)

KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI___________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (3)na (4) ikisomwa pamoja na Nyongeza ya Nane Kanuni ya7(1) (b), ya Kanuni za kudumu za Bunge toleo la Januari, 2016,hoja ya Serikali kuhusu Azimio la Bunge Kuridhia Makubalianoya Paris yatokanayo na utekelezaji wa Mkataba waMabadiliko ya Tabianchi (The Paris Agreement Under the UNFramework Convention on Climate Change) ililetwa mbeleya Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa ajili yakulipitia, kulichambua na hatimaye kulishauri Bunge kuliridhia.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (6)(b), naomba kuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu yaBunge ya Viwanda Biashara na Mazingira kuhusu Azimio laBunge Kuridhia Makubaliano ya Paris.

Mheshimiwa Spika, Jamhuri ya Muungano waTanzania ni nchi Mwanachama wa Mkataba wa Paris waMabadiliko ya Tabia nchi wa mwaka 1992 na Itifaki yake yaKyoto ya mwaka 1997(Kyoto Procal). Tanzania iliridhiaMkataba huu tarehe 17 Aprili, 1996 na Itifaki yake mwaka2002.

2.0 CHIMBUKO LA MKATABA WA MABADILIKO

Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza Mkataba huuna Itifaki zake kumejiotokeza changamoto mbalimbali ikiwani pamoja na;-

i) Baadhi ya nchi wanachama kuhofia kupotezanguvu za kiuchumi kwa sababu utekelezaji wa Mkataba huu

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

92

utaathiri uzalishaji viwandani kwa kupunguza matumizi yanishati chafu;

ii) Ushindani wa kiuchumi baina ya nchizinazoendelea na zile zenye uchumi unaokua harakaunasababisha kuongezeka kwa viwanda vinavyochafuamazingira; na

iii) Kutoshirikisha nchi zote katika upunguzaji wagesijoto na kuongezeka kwa gharama za kukabiliana namajanga ya mabadiliko ya tabianchi hasa kwa nchizilizoendelea kukwepa gharama zinazosabishwa na athariza kuongezeka kwa gesijoto.

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana nachangamoto tajwa nchi wanachama wa Mkataba wamabadiliko ya tabianchi walipitisha Makubaliano ya Paris kwalengo la kuboresha utekelezaji wa Mkataba wa mabadilikoya tabianchi wa mwaka 1992. Makubaliano haya yayalifikiwa katika mkutano wa ishirini na moja (21) uliofanyikaParis-Ufaransa tarehe 30 Novemba hadi 22 Disemba, 2015 nakutiwa saini na nchi wanachama ikiwemo Jamhuri yaMuungano wa Tanzania terehe 22 Aprili, 2016 huko New York-Marekani.

Mheshimiwa Spika, dhumuni la mabadiliko haya nikuboresha utekelezaji wa Mkataba kwa kuweka wajibu kwanchi wanachama kutekeleza Makubaliano ya Paris kamaifuatavyo;-

i) Kuongeza ushirikishwaji wa nchi zote dunianikatika juhudi za kuhakikisha joto haliongezeki zaidi ya nyuzi20C kabla ya mwisho wa karne hii ya 21;

ii) Kuweka utaratibu wa kuzijengea uwezo nchizinazoendelea katika kukabiliana na changamoto zamabadiliko ya tabianchi;

iii) Nchi kuhimizwa kutunza misitu inayonyonyagesijoto; na

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

93

iv) Kuzuia ongezeko la gesijoto na atharizitokanazo na mabadiliko ya tabianchi kwenye mifumo yaIkolojia ya Dunia ili kuhakikisha maendeleo endelevu duniani.

3.0 NAMNA KAMATI ILIVYOSHUGHULIKIA HOJA HII

Mheshimiwa Spika, katika kushughulikia Azimio hili,Kamati ilikutana na kupata maelezo ya Serikali kuhusupendekezo la kuridhia Mabadiliko ya Mkataba wa Paris waMabadiliko ya Tabianchi siku ya Jumatano tarehe 28 Machi,2018. Kabla ya kupokea na kujadili Taarifa ya Serikali kuhusuAzimio hili, Kamati ilipokea na kujadili Taarifa ya Uchambuziwa Azimio kutoka kwa Mshauri wa Bunge wa Mambo yaSheria. Uchambuzi huo uliisaidia Kamati kuwa katika nafasinzuri ya kuifanyia kazi hoja hii.

Mheshimiwa Spika, Kamati i l i j i r idhisha kuwamabadiliko haya hayakinzani na Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Sheria za nchi zinazohusiana nausimamizi na uhifadhi wa mazingira.

Aidha, faida zitakazopatikana kutokana na kuridhiaMakubaliano hayo ni pamoja na:-

i) Kuimarisha ushirikiano miongoni mwa nchiwanachama katika kukabiliana na athari za mabadiliko yatabianchi.

ii) Kuongeza fursa za upatikanaji wa miradi nateknolojia za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

iii) Kuongeza mipango ya Taifa katikakukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Spika, Kamati i l i j i r idhisha kuhusumaudhui ya Makubaliano ya Paris kwa kupitia vifungu vyamkataba huo. Baadhi ya vifungu muhimu katikaMakubaliano ya Paris ni pamoja na Ibara ya 3 ambayoinaweka wajibu wa kila nchi katika kutekeleza makubalianoya Paris ambapokila nchi itatakiwa kuaandaa na kuwasilisha

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

94

taarifa kuhusu juhudi zake katika kufikia malengo yamakubaliano. Katika makubaliano haya nchi zilizoendeleazitapaswa kuchangia fedha katika kutekeleza programu namiradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchina miradi ya upunguzaji gesijoto.

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 6 ya Makubaliano yaParis inazitaka nchi wanachama kuwa na ushiriki wa hiarikatika utekelezaji wa mikakati ya kupunguza gesijoto nakuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuchochea maendeleoendelevu na uhifadhi wa mazingira.

Ibara ya 9 ya Makubaliano ya Paris inaelezea manufaaya Makubaliano haya kifedha. Makubaliano ya Parisyameweka utaratibu wa nchi zinazoendelea ambazo niwanachama kupata fedha za kushughulikia changamotoza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia ufadhiliwa mifuko ya mabadiliko ya tabianchi na wadau wengine.Aidha, nchi zilizoendelea zitatakiwa kutoa taarifa kila baadaya miaka miwili kuhusu kiwango cha fedha walichotoa auwanachotarajia kutoa kama msaada wa nchi ambazo zikohatarini kuhathirika na mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 13 ya Makubaliano yaParis inatambua uwezo mdogo wa nchi zinazoendelea hivyoimeweka utaratibu wa hiari katika utekelezaji pasipo kuingiliauhuru wa nchi wanachama. Aidha, faida za kuridhia Azimiohili ni nyingi kuliko gharama.

4.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, naomba sasa kutoa maoni namapendekezo ya Kamati kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, lengo kuu laMakubaliano ya Paris ni kuzuia ongezeko la gesijoto na atharizitokanazo na mabadiiko ya tabianchi, na

Kwa kuwa, sisi sote ni mashuhuda wa athari zamabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali nchini

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

95

ikiwa ni pamoja na ukame, mafuriko, kuenea kwa magonjwaya kuambukiza, kumezwa kwa visiwa vidogo kwenye baharina maziwa kutokana na kuongezeka kwa ujazo wa maji,kuyeyuka kwa barafu katika kilele cha Mlima Kilimanjaro nauharibufu wa miundombinu ya barabara na makazikutokana na mafuriko, na

Kwa kuwa, Makubaliano ya Paris yanalenga kuandaana kutekeleza mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchina kuweka mifumo ya upatikanaji wa fedha na teknolojiasafi kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, kwa ajili yakukabiliana na changamoto tajwa na kuweka utaratibu wakuzijengea uwezo nchi zinazoendelea katika kukabiliana nachangamoto hizo,

Hivyo basi, Kamati inalishauri Bunge lako Tukufukuridhia Makubaliano ya Paris ili kuwezesha utekelezaji wakewenye lengo la kupambana na changamoto za mabadilikoya tabianchi kama tulivyo ziainisha hapo awali.

5.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana wewena Naibu Spika kwa uongozi mahiri. Binafsi nakushukuru sanaMheshimiwa Spika kwa kuniteua kuwa Mjumbe wa Kamatiya Viwanda, Biashara na Mazingira ambapo nilichaguliwakuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo.

Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hiikuwapongeza Mhe. Andrew Chenge, Mhe. Mussa Zungu naMhe. Najma Giga kwa kuchaguliwa kwa mara nyinginekuendelea kuliongoza Bunge letu.

Mheshimiwa Spika, naomba pia kuwapongezaWenyeviti na Makamu Wenyeviti wote wa Kamati za Kudumuza Bunge kwa kuchaguliwa kwao.

Mheshimiwa Spika, Kamati inapenda kumshukuruWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano naMazingira Mhe. January Makamba (Mb), Naibu Waziri wake

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

96

Mhe. Kangi Lugola (Mb) Makatibu Wakuu, pamoja nawataalamu wote wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwaushirikiano walioutoa wakati wa kujadili Azimio hili.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa,napenda kuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa ushirikiano walioutoawakati wa kupitia, kuchambua na hatimaye kuwasilishamaoni kuhusu Azimio hili mbele ya Bunge lako tukufu. Orodhayao ni kama inavyosomeka hapa chini na kwa rukhusa yakonaomba majina yao yaingie kwenye kumbukumbu Rasmi zaBunge (Hansard).

i) Mhe. Suleiman Ahmed Sadiq, Mb........................Mwenyekitiii) Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Mb ........M/Mwenyekitiiii) Mhe. David Cecil Mwambe, Mb..............................Mjumbeiv) Mhe. Balozi Dkt. Diodorus B. Kamala, Mb...............Mjumbev) Mhe. Salim Hassan Turky, Mb......................................Mjumbevi) Mhe. Gimbi Dotto Masaba, Mb................................Mjumbevii) Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mb......................Mjumbeviii) Mhe. Lucy Thomas Mayenga, Mb..........................Mjumbeix) Mhe. Kiteto Zawadi Koshuma, Mb .......................Mjumbex) Mhe. Munde Tabwe Abdalah, Mb............................Mjumbexi) Mhe. Hawa Subira Mwaifunga, Mb..........................Mjumbexii) Mhe. Munira Mustafa Khaibu, Mb.............................Mjumbexiii) Mhe. Mussa Rashid Ntimizi, Mb................................Mjumbexiv) Mhe. Godbless Jonathan Lema, Mb.......................Mjumbexv) Mhe. Omary Ahmad Badwel, Mb............................Mjumbexvi)Mhe.Kmamis Ali Vuai, Mb.........................................Mjumbexvii) Mhe. Zainab Mdolwa Amiri, Mb..............................Mjumbexviii) Mhe. Kanal (Mst.) Masoud Ali Khamis, Mb............Mjumbexix) Mhe. Ahmed Ally Salum, Mb....................................Mjumbexx) Mhe. Josephine Johnson Genzabuke, Mb..............Mjumbexxi) Mhe. Mansoor Hirani Sharif, Mb...............................Mjumbexxii) Mhe. Sylvestry F. Koka, Mb.......................................Mjumbexxiii) Mhe. Abdulaziz Mohamed Abood, Mb................Mjumbexxiv) Mhe. Gibson Blasius Meiseyeki, Mb.......................Mjumbexxv) Mhe. Shamsia Azizi Mtamba, Mb............................Mjumbexxvi) Mhe. Ahmed Juma Ngwali, Mb.............................Mjumbe

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

97

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee napendakumshukuru Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai, kwaushirikiano ambao amekuwa akitoa kwa Kamati; pamojana yeye namshukuru Mkurugenzi wa Idara ya Kamati Bw.Athumani Hussein; Mkurugenzi msaidizi Sehemu ya Fedha naUchumi Bw. Michael Chikokoto; Makatibu wa Kamati Bw.Wilfred Magova na Bi. Zainab Mkamba na Msaidizi wa KamatiBi Paulina Mavunde kwa kuratibu vema shughuli za Kamati.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naungamkono Azimio.

Innocent Lugha Bashungwa, (Mb)MAKAMU MWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA3 Aprili, 2018

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Sasa tutamsikia Msemajiwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Ofisi ya Makamuwa Rais (Muungano na Mazingira), Mheshimiwa Ally Saleh.

MHE. ALLY SALEH ALLY - MSEMAJI MKUU WA KAMBIYA UPINZANI BUNGENI KATIKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kunipa nafasiya kutoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusuAzimio la Bunge Kuridhia Makubaliano ya Paris chini yaMkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko yaTabianchi (The Paris Agreement under the UN Framework onClimate Change.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinatambua kuwa suala la mabadiliko ya tabianchi nimtambuka kwa maana kwamba madhara yanayotokanana mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri maisha ya binadamuna viumbe wengine ikiwa ni pamoja na maliasil i namazingiara yetu kwa ujumla.

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

98

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinazo taarifa kuwa Mkataba huu wa Kimataifa ulitiwa sainiDesemba, 2015 huko Paris katika Mkutano wa Kimataifa wa21 wa mabadiliko ya tabianchi. Mpaka sasa nchi 195 zimesainimkataba huu na kati ya hizo nchi 175 zimeridhia mkatabahuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania ilisaini mkatabahuu tarehe 22 Aprili, 2016 huko New York, Marekani katikahafla iliyoandaliwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja waMataifa Bwana Ban Ki-moon na kuifanya Tanzania kuwa ninchi ya tano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuridhiamkataba huu ikiungana na Burundi, Kenya, Rwanda naUganda. Kuletwa kwa Azimio hili ni ishara kuwa tunaunganana juhudi za kimataifa katika kushughulikia changamotozinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la msingi la kuhoji sikuzote ni kwa nini Serikali inachelewa kuleta Bungeni Maazimioya Kimataifa ambayo ni muhimu kwa ajili ya maisha yetu yakila siku?

Pamoja na kuwa kwa wakati huu wa Azimio hililimekuja mapema kidogo tofauti na maazimio mengine,Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuhakikisha kuwaMaazimio ya Kimataifa kama hili linalojadiliwa leo yanaletwaBungeni mapema zaidi kwa ajili ya kuridhiwa na Bunge.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maoni kuhusu Makubalianoya Paris; Makubaliano ya Paris yamekuja baada yamalalamiko ya muda mrefu ya nchi zinazoendelea kuhusunamna zinavyoathirika na mabadiliko ya tabianchi hukuuzalishaji mkubwa wa gesijoto ukifanywa na nchizinazoendelea na ambazo uchumi na ushawishi wao wakimataifa ni mkubwa. Hata wakati wa mjadala wamakubaliano haya taarifa zinaonyesha kuwa mataifayanayoendelea hayakuwa thabiti kusimamia matakwa yaokwa sababu ya kuogopa kunyimwa misaada na nchizinazoendelea duniani.

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

99

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya Tisa ya mkatabahuu inazungumzia na inatoa masharti ya namna nchizilizoendelea zinavyogharamia masuala ya kupunguza athariya mabadiliko ya tabianchi au kuondoa kabisa athari hizo.Tatizo la Ibara hii ni kuwa inazitaja nchi zilizoendelea kwaujumla wake na hata utaratibu wa kuchangia mpaka sasahaujawekwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni maoni ya Kambi Rasmiya Upinzani kuwa Ibara ya Tisa imewekwa kama kisafishamacho tu, lakini haitoi jukumu la nchi ambazo zinatakiwakuchangia nchi zinazoendelea kukabiliana na athari hizi hukuikizingatiwa kuwa nchi hizo zinakabiliwa na changamatoza kibajeti kugharamia huduma za kawaida za nchi hizo nahivyo kuwa vigumu kwao kuwa na bajeti nyingine yamabadiliko ya tabianchi. Pamoja kuridhia Azimio hili kuhusumkataba huu, ni vyema Serikali ikasisitiza na kuendeleakufanya jitihada za kuhakikisha kuwa makubaliano katikamkataba huu yanafanyiwa marekebisho ili kutoa jukumu lakisheria kwa nchi zilizoendela kutoa fedha kwa ajili yamasuala ya mabadiliko ya tabianchi kwa nchi zinazoendeleaambazo huathiriwa zaidi pamoja na kuwa wanazalishagesijoto kidogo zaidi ikilinganishwa na nchi zilizoendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kujiandaa kukabiliana namajanga; Ibara ya 8(4) ya mkataba inaainisha maeneoushirikiano ambapo pamoja na mambo mengine inasisitizakujiandaa na majanga yanayotokana na mabadiliko yatabianchi. Taarifa zinaonyesha kuwa kwa miaka 40 nchi yetuimekuwa ikikabiliwa na ukame na mafuriko katika nyakatimbalimbali mambo ambayo yanahusishwa moja kwa mojana mabadiliko ya tabianchi. Siku za hivi karibuni Mikoa yaDar es Salaam, Tanga, Morogoro, Mwanza imeathirika sanana mabadiliko ya tabianchi jambo ambalo limesababishawananchi wengi kukosa makazi. Nyakati zote za majangaSerikali imekuwa ikionekana dhaifu kutokana na kutokuwana vifaa na nyenzo za kuzuia athari hizo pamoja nakushindwa kuwasaidia kwa wakati wahanga wa majangahayo.

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

100

Mheshimiwa Naibu Spika, katika masharti ya mkatabahuu inaonekana dhahiri kuwa hakuna jukumu la moja kwamoja la kisheria kwa nchi zilizoendelea la kuwalipa fidiawananchi wanaoathirika na majanga kama haya.Ikumbukwe kuwa majanga ya mafuriko na ukame yanaathirisekta za kilimo, mifugo pamoja na miundombinu ya umemena hivyo kwa ujumla kuathiri ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.Pamoja na kutegemea fedha kutoka nje kwa maana yamichango ya nchi zilizoendelea kukabiliana na athari zamabadiliko ya tabianchi ni vyema sisi wenyewe tukajipangazaidi kukabiliana na matokeo hasi ya mabadiliko ya tabianchiambayo yanaathiri maisha yetu ya kila siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 7(5) inawekamasharti ya ushirikishwaji wa jamii ikiwa ni pamoja na uwazina masuala ya jinsia katika kukabiliana na mabadiliko yatabianchi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitizaumuhimu wa jambo hili kufanyika wakati wa utekelezaji washeria zetu tulizojiwekea kuhusu mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, ikumbukwe kuwa jamii zetukitamaduni zimekuwa na shughuli mbalimbali kwa mudamrefu na kwa vizazi na vizazi ambazo kwa namna mojaama nyingine zimekuwa zikilinda mazingira. Mathalani hukoIringa na Njombe wananchi wamekuwa wakifanya shughulizao za kilimo kwenye maeneo maarufu kama vinyungu, lakiniSerikali imekuwa ikitumia Sheria ya Maji na Mazingirakuwaelekeza kuwa wanatakiwa kufanya hivyo kwa umbaliwa mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji. Katika Mkoawa Kilimanjaro wananchi wengi wanaishi milimani kwenyevyanzo vya maji na wamekuwa wakifanya shughuli za kilimokwa miaka mingi huku wakitunza mazingira lakini baada yautaratibu wa mita 60 Serikali inaingia kwenye mgogoro nawananchi ambao ni wadau wakubwa katika masuala yamazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkataba huu umewekautaratibu wa kushirikisha jamii na tamaaduni zao kwa ajiliya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na juhudiza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ni vyema kama

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

101

nchi tukaona namna ya kushirikisha jamii zetu na tamadunizetu kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Pamoja na kuridhia Azimio hili, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali na wadau wengine wa mabadiliko yatabianchi kusisitiza uwepo wa marekebisho au itifaki nyingineambayo itatatua changamoto za masuala ya jinsia kuhusumabadiliko ya tabianchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uwekezaji na mabadilikoya tabianchi. Kambi Rasmi ya Upinzani haipingi uwekezajiwa sekta binafsi katika sekta mbalimbali za nchi. Vilevileifahamike kuwa ni muhimu uwekezaji huo kuzingatiateknolojia ambayo ni rafiki kwa mazingira na ambayo inatoagesijoto kidogo ili kuepuka madhara yanayotokana namabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 10 ya mkatabainazungumzia na kutoa masharti kuhusu ushirikiano wakimataifa kuhusu masuala ya teknolojia rafiki kwa mazingiraambayo hutoa gesijoto kidogo. Pamoja na hekaya za Serikalikuhusu uchumi wa viwanda ambao haujafanyiwa utafiti wasoko la uzalishaji wa bidhaa hizo inaelekea Serikali inaitiliamkazo kidogo sana kwenye masuala ya mabadiliko yatabianchi. Kwa hali ilivyo hasa kwenye miji mikubwa nchiniathari za mabadiliko ya tabianchi ni ya dhahiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Mkurangawananchi wameanza kulalamika kutokana na kutanda kwawingu zito la moshi unaozalishwa na viwanda. Ni vyemaSerikali ikaona namna ya kutatua kero hiyo ambayo kwanamna moja ama nyingine inaweza kuathiri wananchi zaidihuko baadae. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata katika Wilaya ya Nzegamwekezaji wa Mgodi wa Resolute baada ya kuvuna madiniameacha mashimo bila kurejesha mazingira katika hali yakeya awali na kupelekea athari kubwa ikiwemo vifo vyawananchi. Ni vyema basi kuzingatia masuala ya mazingirakatika uwekezaji kwa ujumla na matokeo chanya yauwekezaji tunatakiwa kulinda mangira yetu kwa ajili ya vizazivijavyo. (Makofi)

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

102

Mheshimiwa Naibu Spika, mapendekezo ya jumla;kwa kuridhia mabadiliko yaliyopo katika mkataba huu,kama nchi tunalo jukumu la kuzingatia masuala yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya kwanza, upatikanajiwa fedha za kuhimili na kukabiliana na mabadiliko yatabianchi. Tunatambua kwamba katika makubaliano hayaya kimataifa nchi zilizoendelea zina jukumu la kutoa fedhakwa nchi zinazoendelea ili kuweza kukabiliana na mabadilikoya tabianchi. Tunatambua kuwa fedha hizo zimekuwahazitolewi kwa kiasi cha kuridhisha na kwa wakati kamazilivyokubaliwa na zilivyoahidiwa na nchi zilizoendelea. Hivyobasi, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuhakikishakuwa inatenga fedha kutoka vyanzo vya ndani ili kuwezakukubaliana na athahri za mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali iwekemikakati madhubuti kuweza kupata fedha moja kwa moja(direct funding) kutoka mifuko mbalimbali ya kimataifa yamabadiliko ya tabianchi ikiwemo Green Climate Fund,Adaptation Fund na Global Environment Facility. Ielewekekuwa fedha nyingi zimekuwa zikipotea kwa ajili ya kulipamashirika ya kimataifa na wataalam ili kuweza kupata fedhahizo ambapo hupunguza kiasi kinachofika nchini kwautekelezaji. Suala hili linaweza kuondolewa kwa kuboreshauwezo wa taasisi za Serikali kufikia vigezo tengwa na piakujenga utashi na ushawishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kuhakikisha kuwa fedha zinazopatikanazinaelekezwa katika miradi ya vipaumbele na yenye manufaakwa nchi na vilevile kuwepo usimamizi madhubuti namatumizi ya fedha hizo i l i kuepuka ufisadi ambaoumejitokeza katika baadhi ya miradi inayotekelezwa. KambiRasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuanzisha Mfuko Maalumkwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi ili kuweza kuboreshamatumizi bora na kuepuka ufisadi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya pili, upunguzaji wautoaji gesijoto na matumizi ya vyanzo vya nishati; Kambi

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

103

Rasmi ya Upinzani inatambua kuwa Tanzania inatoa kiasikidogo cha gesijoto (greenhouse gases) ikiwa ni chini yaasilimia moja duniani. Kutokana na shughuli za kibinadamupamoja na ongezeko la watu ambavyo vyote viwilivitaongeza matumizi ya nishati kwa kiasi kikubwa, kuna hajaya kupata uwiano mzuri wa kufikia malengo yote mawili,maendeleo ya shughuli za kiuchumi ikiwemo uwekezaji nakupunguza utoaji wa gesijoto na kuwa na maendeleoendelevu. Pia Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Serikalikuhakikisha kuwa inafanya mchanganyiko mzuri wa matumiziya vyanzo vya nishati kwa kujumuisha nishati jadidifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya tatu, kujumuishamasula ya Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi katikamipango na bajeti ya Serikali; Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kujumuisha masuala ya mkataba huopamoja na masuala ya mabadiliko ya tabianchi kiujumlakatika mipango ya bajeti. Hii itasaidia kufikia shabaha zanchi katika kutekeleza mkataba huo. Serikali kupitia Ofisi yaMakamu wa Rais na Wizara ya Fedha iweke kasma maalumya mabadiliko ya tabianchi (budget expendicture code) ilikurahisisha suala hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya nne, ushirikishwajiwa wadau; Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Serikalikuhakikisha kuwa inashirikisha kikamilifu wadau woteikiwemo vyama vya siasa, asasi za kiraia, sekta binafsi nawadau wa maendeleo na jamii kwa ujumla kamatulivyoeleza ili kuweza kutekeleza vizuri masharti yaliyopokatika mkataba huu. Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekezadhana hii kujumuisha ngazi zote kuanzia katika uchaguzi wavipaumbele, tathmini ya utekelezaji na matokeo yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho; athari zamabadiliko ya tabianchi ni dhahiri na tunahitaji kuwa namipango ya ndani kukabiliana nazo na si kusubiri michangoau fedha za nchi zi l izoendelea ambazo kuzipata nichangamoto. Kambi Rasmi ya Upinzani inaunga mkono

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

104

Azimio hili lakini inaitaka Serikali kuzingatia maoni namapendekezo yaliyotolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. (Makofi)

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANIBUNGENI KATIKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA,KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA KURIDHIA MAKUBALIANO YA

PARIS CHINI YA MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSUMABADILIKO YA TABIANCHI (THE PARIS AGREEMENT UNDERTHE UN FRAMEWORK CONVENTION ON CLIMATE CHANGE)

KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

(Imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 86(6) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016)

______________

1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hiikukushukuru kwa kunipa nafasi ya kutoa maoni ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Azimio la Bunge la KuridhiaMakubaliano ya Paris chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifakuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (The Paris Agreement underthe UN Framework on Climate Change).

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinatambua kuwa suala la mabadiliko ya tabianchi ni sualamtambuka kwa maana kwamba; madhara yanayotokanana mabadiliko ya tabianchi yanaathiri maisha ya binadamuna viumbe wengine, ikiwa ni pamoja na maliasili namazingira yetu kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inazotaarifa kuwa Mkataba huu wa kimataifa ulitiwa sainimakubaliano Desemba 2015 huko Jijini Paris-Ufaransa katikaMkutano Kimataifa wa Ishirini na Moja (21) wa Mabadiliko yaTabianchi. Mpaka sasa, nchi 195 zimesaini Mkataba huu nakati ya hizo, nchi 175 zimeridhia Mkataba huu.

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

105

Mheshimiwa Spika, Tanzania ilisaini Mkataba huutarehe 22 Aprili, 2016 huko Jijini New York-Marekani katikahafla iliyoandaliwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja waMataifa – Bw. Ban Ki Moon na kuifanya Tanzania kuwa nchiya 5 katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuridhia Mkataba huuikiungana na Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.

Mheshimiwa Spika, kuletwa kwa Azimio hili ni isharakuwa tunaungana na juhudi za kimataifa katika kushughulikiachangamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.Suala la msingi la kuhoji siku zote ni kwa nini Serikaliinachelewa kuleta Bungeni Maazimio ya Kimataifa ambayoni muhimu kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa kwa wakati huuAzimio hili limekuja mapema kidogo tofauti na maazimiomengine Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikuhakikisha kuwa maazimio ya kimataifa kama hil ilinalojadiliwa leo yanaletwa Bungeni mapema zaidi kwa ajilikuridhiwa na Bunge.

2. MAONI KUHUSU MAKUBALIANO YA PARIS2.1 Nchi Zilizoendelea na Mabadiliko ya

Tabianchi

Mheshimiwa Spika, Makubaliano ya Paris yamekujabaada ya malalamiko ya muda mrefu ya nchi zinazoendeleakuhusu namna zinavyoathirika na mabadiliko ya tabianchihuku uzalishaji mkubwa wa gesijoto ukifanywa na nchizilizoendelea na ambazo uchumi na ushawishi wao kimataifani mkubwa.

Mheshimiwa Spika, hata wakati wa mjadala wamakubaliano haya, taarifa zinaonesha kuwa Mataifayanayoendelea hayakuwa thabiti kusimamia matakwa yaokwa sababu ya kuogopa kunyimwa misaada na nchizilizoendelea duniani.

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 9 ya Mkataba huuinazungumzia na inatoa masharti ya namna nchi

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

106

zilizoendelea zikavyogharamia masuala kupunguza athari zamabadiliko ya tabianchi au kuondoa kabisa athari hizo. Tatizola ibara hii ni kuwa inazitaja nchi zilizoendelea kwa ujumlawake na hata utaratibu wa kuchangia haujawekwa.

Mheshimiwa Spika, ni maoni ya Kambi Rasmi yaUpinzani kuwa ibara ya 9 imewekwa kama kisafisha machotu lakini haitoi jukumu la nchi ambazo zinatakiwa kuchangianchi zinazoendelea kukabiliana na athari hizi huku ikizingatiwakuwa nchi hizo zinakabiliwa na changamoto za kibajetikugharamia huduma za kawaida za wananchi na hivyo kuwavigumu kuwa na bajeti nyingine ya mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuridhia Azimio kuhusuMkataba huu, ni vema Serikali ikasisitiza na kuendeleakufanya jitihada za kuhakikisha kuwa Makubaliano katikaMkataba huu yanafanyiwa marekebisho ili kutoa jukumu lakisheria kwa nchi zilizoendelea kutoa fedha kwa ajili yamasuala ya mabadiliko ya tabianchi kwa nchi zinazoendeleaambazo huathiriwa zaidi pamoja na kuwa wanazalishagesijoto kidogo ukilinganisha na nchi zilizoendelea.

2.2 Kujiandaa Kukabiliana na MajangaMheshimiwa Spika, Ibara ya 8(4) ya Mkataba

inaainisha maeneo ya ushirikiano ambapo pamoja namambo mengine inasisitiza kujiandaa na majangayanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Spika, taarifa zinaonyesha kuwa kwamiaka 40 nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na ukame na mafurikokatika nyakati mbalimbali mambo ambayo yanahusishwamoja kwa moja na mabadiliko ya tabianchi. Siku za hivikaribuni Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro naMwanza imeathirika sana na mabadiliko ya tabianchi jamboambalo limesababisha wananchi wengi kukosa makazi.

Mheshimiwa Spika, nyakati zote za majanga Serikaliimekua ikionekana dhaifu kutokana na kutokuwa na vifaana nyenzo za kuzuia athari hizo pamoja na kushindwakuwasaidia kwa wakati wahanga wa majanga hayo. Katika

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

107

masharti ya mkataba huu inaonekana dhahiri kuwa hakunajukumu la moja kwa moja la kisheria kwa nchi zilizoendeleaza kuwalipa fidia wananchi wanaoathirika na majangahaya.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kuwa majanga yamafuriko na ukame yanaathiri sekta za kilimo, mifugo pamojamiundombinu ya umeme na hivyo kwa ujumla kuathiri ukuajiwa uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kutegemea fedhakutoka nje kwa maana ya michango ya nchi zilizoendeleakukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ni vemasisi wenyewe tukajipanga zaidi kukabiliana na matokeo hasiya mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaathiri maisha yetuya kila siku.

2.3 Ushirikishwaji wa KijamiiMheshimiwa Spika, Ibara ya 7(5) inaweka masharti

ya ushirikishwaji wa jamii ikiwa ni pamoja na uwazi namasuala ya jinsia katika kukabiliana na mabadiliko yatabianchi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitizaumuhimu wa jambo hili kufanyika wakati wa utekelezaji waSheria zetu tulizojiwekea kuhusu mazingira.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kuwa jamii zetukitamaduni zimekuwa na shughuli mbalimbali kwa mudamrefu na kwa vizazi na vizazi ambazo kwa namna mojaama nyingine zimekuwa zikilinda mazingira. Mathalani hukoIringa na Njombe wananchi wamekuwa wakifanya shughulizao za kilimo kwenye maeneo maarufu kama “vinyungu”lakini Serikali imekuwa ikitumia Sheria ya Maji na ya Mazingirakuwaelekeza kuwa wanatakiwa kufanya hivyo kwa umbaliwa mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji.

Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Kilimanjarowananchi wengi wanaishi milimani kwenye vyanzo vya majina wamekua wakifanya shughuli za kilimo kwa miaka mingihuku wakitunza mazingira lakini baada ya utaratibu wa mita

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

108

60 Serikali inaingia kwenye mgogoro na wananchi ambaoni wadau wakubwa katika masuala ya mazingira.

Mheshimiwa Spika, Mkataba huu umeweka utaratibuwa kushirikisha jamii na tamaduni zao kwa ajili ya kukabilianana mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na juhudi za kukabilianana mabadiliko ya tabianchi ni vema kama nchi tukaonanamna ya kushirikisha jamii na tamaduni zetu kwa ajili yakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

2.4 Kuzingatia Masuala ya JinsiaMheshimiwa Spika, ieleweke kuwa, athari za

mabadiliko ya tabiachi zinaathiri makundi mbalimbali yakijamii katika nchi yetu. Ni wazi kuwa wanawake na watotoni kati ya makundi ambayo yanaathirika zaidi na athari zamabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Spika, Makubaliano haya hayajatoa kwaupana masuala ya jinsia hasa namna wanawakewatakavyopata fedha kwa ajili kufanya miradi ya mabadilikoya tabianchi, kuwapatia na kuwaelemisha kutumia nishatijadidifu pamoja na kuwajengea uwezo kuelewa nakukabiliana na majanga yanayotokana na mabadiliko yatabianchi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuridhia azimio hili,Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali na wadau wengine wamabadiliko ya tabia kusisitiza uwepo wa marekebisho auitifaki nyingine ambayo itatatua changamoto za masualaya jinsia kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

2.5 Uwekezaji na Mabadiliko ya TabianchiMheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haipingi

uwekezaji wa sekta binafsi katika sekta mbalimbali nchini.Lakini ni vema ikafahamika kuwa ni muhimu uwekezaji huokuzingatia teknolojia ambayo ni rafiki kwa mazingira naambayo inatoa gesijoto kidogo ili kuepuka madharayanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

109

Mheshimiwa Spika , Ibara ya 10 ya Mkatabainazungumzia na kutoa masharti kuhusu ushirikiano wakimataifa kuhusu masuala ya teknolojia rafiki kwa mazingiraambayo hutoa gesijoto kidogo. Pamoja na hekaya za Serikalikuhusu uchumi wa Viwanda ambao haujafanyiwa utafiti wasoko la uzalishaji wa bidhaa hizo inaelekea Serikali inatiliamkazo kidogo sana kwenye masuala ya mabadiliko yatabianchi. Kwa hali ilivyo, hasa kwa miji mikubwa nchini,athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri.

Mheshimiwa Spika, katika Wilaya ya Mkurangawananchi wameanza kulalamika kutokana na kutanda kwawingu zito la moshi unaozalishwa na viwanda. Ni vemaSerikali ikaona namna ya kutatua kero hiyo ambayo kwanamna moja ama nyingine inaweza kuathiri wananchi zaidihuko baadae.

Mheshimiwa Spika, hata katika Wilaya ya Nzega,mwekezaji wa Mgodi wa Resolute baada ya kuvuna madiniameacha mashimo bila kurejesha mazingira katika hali yakeya awali na kupelekea athari kubwa ikiwemo vifo vyawananchi.

Mheshimiwa Spika, ni vema kuzingatia masuala yamazingira katika uwekezaji kwa kuwa pamoja na matokeochanya ya uwekezaji tunatakiwa kulinda mazingira yetu kwaajili ya vizazi vijavyo.

2.6 MAPENDEKEZO YA JUMLAMheshimiwa Spika, Kwa kuridhia Makubaliano

yaliyopo katika Mkataba huu kama nchi tunalo jukumu lakuzingatia masuala yafuatayo:

(i) Upatikanaji wa Fedha za Uhimili na Ukabiliwa mabadiliko ya tabianchi

Mheshimiwa Spika, tunatambua kwamba; katikamakubaliano haya kimataifa, nchi zilizoendelea zina jukumula kutoa fedha kwa nchi zinazoendelea ili kuweza kukabilianana mabadiliko ya tabianchi. Tunatambua kuwa fedha hizozimekuwa hazitolewi kwa kiasi cha kuridhisha na kwa wakati

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

110

kama zil ivyokubaliwa na zil ivyoahidiwa na nchi hizozilizoendelea.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kuhakikisha kuwa inatenga fedha kutoka vyanzo vyandani ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko yatabanchi.

Mheshimiwa Spika, aidha Serikali iweke mikakatimadhubuti kuweza kupata fedha moja kwa moja (DirectFunding) kutoka mifuko mbalimbali ya kimataifa yamabadiliko ya tabianchi ikiwemo Green Climate Fund (GCF),Adaptation Fund (AF) na Global Environment Facility (GEF).

Mheshimiwa Spika, ieleweke kuwa fedha nyingizimekuwa zikipotea kwa ajili ya kulipa mashirika ya kimataifana wataalam ili kuweza kupata fedha hizo ambapohupunguza kiasi kinachofika nchini kwa utekelezaji. Suala hililinaweza kuondolewa kwa kuboresha uwezo wa taasisi zaSerikali kufikia vigezo tengwa na pia kujenga utashi waushawishi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kuhakikisha kuwa fedha zinapopatikana zinaelekezwakatika miradi ya vipaumbele na yenye manufaa kwa nchina vilevile kuwepo usimamizi madhubuti wa matumizi yafedha hizo ili kuepuka ufisadi ambao umejitokeza katikabaadhi ya miradi inayotekelezwa. Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kanzisha mfuko maalum kwa ajili yamabadiliko ya tabianchi ili fedha ili kuboresha uwazi,matumizi bora na kuepuka ufisadi.

(ii) Upunguzaji wa Utoaji wa Gesijoto na Matumiziya Vyanzo vya Nishati

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinatambua kuwa Tanzania inatoa kiasi kidogo cha gesijoto(Greenhouse Gases) ikiwa ni chini ya 1% kidunia. Kutokanana shughuli za kibinadamu pamoja na ongezeko la watuambavyo vyote viwili vitaongeza matumizi ya nishati kwakiasi kikubwa, kuna haja kupata uwiano mzuri wa kufikia

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

111

malengo yote mawili – maendeleo ya shughuli za kiuchumiikiwemo uwekezaji na kupunguza utoaji wa gesijoto (kuwana maendeleo endelevu); Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kuhakikisha kuwa inafanya mchanganyiko mzuri wamatumizi ya vyanzo vya nishati kwa kujumuisha nishatijadidifu.

(iii) Kujumuisha Masuala ya Mkataba naMabadiliko ya Tabianchi katika Mipango na Bajeti za Serikali

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kujumuisha masuala ya Mkataba huu pamoja namasuala ya mabadiliko ya tabianchi kiujumla katika mipangona bajeti. Hii itasaidia kufikia shabaha za nchi katikakutekeleza Mkataba huo. Serikali, kupitia Ofisi ya Makamuwa Rais na Wizara ya Fedha, iweke kasma maalum yamabadiliko ya tabianchi (budget/expenditure code) ilikurahisisha suala hilo.

(iv) Ushirikishwaji wa Wadau

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kuhakikisha kuwa inashirikisha kikamilifu wadau wote– ikiwemo vyama vya siasa, asasi za kiraia, sekta binafsi nawadau wa maendeleo na jamii kwa ujumla kamatulivyoeleza ili kuweza kutekeleza vizuri masharti yaliyopokatika Mkataba huu.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinapendekeza dhana hii kujumuisha ngazi zote kuanzia katikauchaguzi wa vipaumbele, namna ya utekelezaji, utekelezajina tathmini ya utekelezaji na matokeo yake.

3. HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, athari za mabadiliko ya tabianchini dhahiri na tunahitaji kuwa na mipango ya ndanikukabiliana nazo na si kusubiri michango au fedha za nchizilizoendelea ambazo kuzipata ni changamoto. Kambi Rasmiya Upinzani inaunga mkono Azimio hili lakini inaitaka Serikalikuzingatia maoni na mapendekezo yaliyotolewa.

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

112

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Kambi Rasmi yaUpinzani naomba kuwasilisha.

……………………………….Ally Saleh Ally (Mb)

MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI.KATIKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS- MUUNGANO NA

MAZINGIRA3 April, 2018

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Ally Saleh,Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katikaOfisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Waheshimiwa Wabunge, ninayo orodha hapa yawachangiaji, tutaanza na Mheshimiwa George Lubelejeatafuatiwa na Mheshimiwa Yussuf Salim, Mheshimiwa Dkt.Diodorus Kamala ajiandae.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili na mimi nichangieAzimio hili ambalo ni muhimu sana katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze MheshimiwaWaziri, niipongeze Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira kwa taarifa yao nzuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu miaka ya 1960haikuwa hivi, ilikuwa nchi nzuri sana, ilikuwa na misitumikubwa na mito ambayo inatiririsha maji mwaka mzima.Kwa sababu ya shughuli za kibinadamu watu wamefyekamiti, wamechoma moto hovyo na mifugo isiyozingatiamaeneo ya malisho sasa hivi misitu mingi sana katikamaeneo yetu imekwisha. Misitu ndiyo inayoleta mvua na haliya hewa nzuri na mito ndiyo inayoleta maji.

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

113

Maji ni uhai, maji ni maendeleo na maji ni uchumi wa nchiyetu. Lakini vyote hivi uharibifu huu wa ufyekaji, uchomajimoto hovyo ndiyo umesababisha majangwa, umesababishaukame katika nchi hii kama Kamati ilivyoelezea ukame,milipuko ya magonjwa, viwanda, kemikali hizi, maji machafuyanamwagwa hovyo, madawa, makemikali yanasababishawatu wanapata magonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, sasa hivitakataka zinachomwa hovyo hata mijini utakuta mtuanachoma takataka sasa zile takataka zinatoa moshi, ulemoshi unaharibu hali ya hewa badala ya watu kuvuta oxygenwanavuta carbonmonoxide, kwa hiyo ile ni pollution of airby combustion ambayo inaleta matatizo makubwa sanasana kwa Wananchi wetu wanapata matatizo ya magonjwaya kifua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hali ya hewainabadilika kunakuwa na joto kwa sababu ya mabadilikohayo mpaka wakati fulani unakuta hata bahari maji nayoyanaongezeka. Kwa hiyo, wito wangu kwa kumuunga mkonoMheshimiwa Waziri kwamba wananchi wazingatie kutunzamazingira, bila kutunza mazingira nchi hii ndugu zangututakwenda wapi? Maji yatakwisha na bila maji dunia hiitutaishi wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimkushukuru sanaMheshimiwa Waziri kwa kuiweka Wilaya Mpwapwa, naombanisome kidogo; “Mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchikatika maeneo ya vijijini, Mfumo wa ikolojia na lengo la mradihuu ni kuongezea vijiji uwezo wa kuhimili mabadiliko yatabianchi” na Mpwapwa imo. Mpwapwa ilikuwa na misitumikubwa sana, kulikuwa na Mto Shaban Robert wotemnaufahamu mmesoma kwenye vitabu, Shaban Robert.Ulikuwa unatiririsha maji mwaka mazima, sasa hivi uko wapi?Hakuna, umekauka kwa sababu watu wamechoma, watuwamefyeka hovyo mpaka sasa hakuna na kuna baadhi yavijiji kuna ukame umeanza, barabara zinaharibika kwasababu watu wamechoma, watu wamefyeka hovyo kwahiyo, maji yanakuja kwa kasi yanaharibu barabara.

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

114

Mheshimiwa Naibu Spika, naungana kabisa naMheshimiwa Waziri kwamba azimio hili naliomba Bunge wotetukubaliane liweze kupita bila kupingwa na naunga mkonohoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Yussuf Salimatafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Diodorus Kamala,Mheshimiwa Richard Mbogo ajiandae.

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi nichangie katika azimio hililililopo mbele yetu.

Kwanza nisikitike tu kwamba Azimio lenyewe nikubwa sana na kwa lilivyopangwa na litakavyojadiliwa sionikama tumelipa thamani hiyo au uzito huo ambao inalo. Nikitu kikubwa sana na ndiyo kinagusa maisha yetu sasakujadiliwa hapa kwa siku moja sidhani kama tunalipa uzitohuo, naomba tulipe uzito sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Azimio hili nasema linagusamaisha yetu kwa sababu gani? Wamezungumza hapa katikaparagraph ya nne kwamba kuna kupotea, sasanitazungumza hii habari ya kupotea kwa visiwa na maeneoya namna hiyo, sea erosion.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna upoteajimkubwa sana, lakini siyo kwamba vile visiwa vinaisha tu auardhi inamegwa na bahari kwa sababu ya nguvu ya maji,hatuishii hapo tu lakini kuna na viumbe vinapotea ambavyovimo katika vile visiwa au katika bahari na vikiendeleakupotea viumbe na mimea ndiyo na sisi maisha yetuyanapotea vilevile.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitatoa mifano michachetu, kuna miti ambayo inapotea kwa kasi kubwa sana,xylocarpus moluccensis na xylocarpus granatum hii nimitonga, mtonga mweusi na mtonga mwekundu inapoteasasa ikipotea hiyo ina maana kizazi chetu watakuja kuonaau watakuja kusikia ni historia.

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

115

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna heritieralittoralis (msikundasi) nayo inapotea. Kizazi chetu kinachokujahii miti hawataikuta, watakapokuja hawakuti hii miti nihisotoria itakuwa nini? Itakuwa tumewajengea faida gani?Lakini siyo hivyo tu ni mazalia ya viumbe vingine hii kamakaa, chanje kama hii miti haipo katika bahari ina maana nahivyo viumbe vingine navyo vinapotea.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika visiwa vilevilekuna ndege ambao ni endemic, ni ndege muhimu hapaduniani wanapotea vilevile. Kwa mfano white eyes (chigimanjano) sisi kule Zanzibar tunaita tayari wamepoteahawapo, sawa. Kuna ndege hawa Javaspirous tayariwanapotea hawapo na yote ni kwa sababu ya kwambamabadiliko haya ya tabianchi yanapotea. Kwahiyo kupoteana kuondoka kwa visiwa siyo kwasababu tu kwmaba tunaardhi inaondoka, lakini tunapoteza na hizo mnaita wenyewesasa bioanuai sijui na nini, vitu vyote vinapotea tutakuwahatuna na kizazi chetu kitakujakurithi nchi ambayo mimeana ndege hawapo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee mbele kuna tatizolinasema kwamba mvua hizi tunapata tunaita mabadilikoya tabianchi, lakini hatuwezi kuwa na mabadiliko yatabianchi mazuri tunayoyategemea kama sisi wenyewehatujabadilika. Mwenyezi Mungu ametuleta dunianikuitawala dunia na vilivyomo ndani yake, je, sisi wenyewetunalijua hili? Tumebadilika? Kama hatujabadilika natunachokitawala katika dunia hii kitaendelea kuharibika,hakitakuwa katika namna tunayoitaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tulikuwa tunapatamvua nne kwa mwaka, leo tunapata mvua mbili kwa taabuna zikija hizo mvua basi ni laana maana yake ni mafuriko,uharibifu. Likitoka jua ni hivyo hivyo, kwanini? kwamba sisiwenyewe hatujabadilika kwa hiyo na sisi wenyewe lazimatubadilike. Oman ilikuwa jangwa, walikuwa miaka miwilihawaoni mvua, mvua ikinyesha ni ajabu leo wanapata mvuanne, kwanini? Wao wenyewe wamebadilika. Kwa hiyo na sisilazima tubadilike na tuelewe kwamba tumeletwa

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

116

ulimwenguni kwamba tuvitawalie hivi, Je tumebadilika nafsizetu? Tunalijua hilo? Kwa hiyo na sisi wenyewe lazimatubadilike na ndiyo maana sasa mvua hizi zinaleta mafuriko,zinaleta athari kubwa, kilimo kinaharibika, matokeo yake sasani hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini siyo hapo tu waduduhawa kuna wadudu sasa hivi matunda haya yote kunavidudu dudu hivi mapapai yanaharibika, maembe, ndizi,wale wadudu weupe sijui mnawaitaje sijui sigatoka, sijuiwenyewe wataalam mnawaitaje. Wataalam wa kilimo kwamiaka nenda miaka rudi hakuna mabadiliko yoyote. Yotehaya yanasababishwa na kubadilika kwa haya mabadilikoya tabianchi ambayo tunayasababisha sisi wenyewe.

Waheshimiwa Wabunge, tunasema kwamba thelujiinayeyuka katika Mlima Kilimanjaro, wenyewe Wachaga waKilimanjaro wanaita Kibo. Sasa kwa maana ile Kibo ikipoteamaana yake na Mlima Kilimanjaro unapoteza thamani yaketutakuwa tunajivunia nini kama Watanzania? Kwa hiyo,vyote hivi ni vitu ambavyo tunatakiwa tuviangalie sana.Lakini jangwa linaongezeka kwasababu sisi wenyewe ambaotumeambiwa tuitawale dunia ndiyo wakataji wakubwa wamiti, ndiyo wachomaji mkaa, ndiyo wachomaji wa motokwenye misitu, kwa hiyo, ni sisi wenyewe na ndiyo maananikasema tunalichukulia uzito kiasi gani? Sisi kama wananchi,kama binadamu ambao tmeletwa tuvitawale hivitunalichukulia hili suala la mabadiliko ya tabianchi kwathamani kiasi gani, kwa nguvu kiasi gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni nini athari yake?Wanaoathirika sana ni wakulima na wavuvi. Tabianchiikibadilika, wakulima hawa watalima hawavuni kwa sababuhizo nilizozitaja ama kwa mafuriko ama za jua ama za waduduwaharibifu hawatavuna na matokeo yake sasa tutakuwatunawasema watalaam wa kilimo, sijui madawa, sijui hatunawatu ugani lakini ni tabianchi tu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tabia hizi zikibadilika,mazingira yakibadilika, hali ya hewa ikibadilika na maradhi

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

117

yatakuja. Zanzibar nime-check mara hii pale mwezi Januarina Februari ongezeko la wagonjwa wa pressure hospitali paleni kubwa sana, kwa sababu gani? Ya joto tu limeongezeka.Kwa hiyo, hizo ni athari za moja kwa moja tunaziona lakiniwavuvi pia samaki watakosekana, wakikosekana samakiinamaana hao nao wanaathirika. Kwa hiyo, ikifa hiiecosystem yote ina maana na kizaizi chetu kinachokujahakitaona mimea na ndege na wanyama ambaowalikuwepo wa asili hapa kwa hiyo, lazima tuwe serious nahili ili tuone kwamba kizazi chetu kinakuja kufaidika kwa kiasigani, nini tufanye?

Mheshimiwa Naibu Spika, waathirika wa masualahaya duniani asilimia 20 ni wale watu maskini kabisa na ndiyohao wanaoathirika kwa sababu wao ndiyo wanaoishi hukokwenye miti, kwenye misitu na huko vijijini kwa hiyo, hao ndiyowatakaoathirika. Sasa hili suala linalozungumzwa la globalwarming basi ionekane sasa kwamba inafanyakazi vizuri naiwafikie wale walengwa. Nitatoa mfano, kwa mfano, kunahizi kaya maskini ambazo zinasaidiwa sijui shilingi 20,000 kwamwezi hivyo inamsaidia nini mtu wa kaya maskini? Yeye nimasikini unampa shilingi 20,000 kwa mwezi inamsaidia nini?Pesa ambayo hata mtoto wangu na mtoto wakoMheshimiwa Naibu Spika haimtoshi kwa mwezi kwenda shuletu.

Sasa unamsaidia mtu wa Kaya maskini sasa nadhanihizi pesa Mheshimiwa Waziri hebu zipangiwe sasa utaratibuili kama tuna tatizo sehemu fulani twende tuka-solve hilo tatizona hizi pesa tusiwe tunazigawanya kisiasa siasa tu,kupendezeshana pendezeshana tu hali ni mbaya ni lazimatuwe commited katika kuyatafutia suluhisho masuala hayavinginevyo itakuwa tunapoteza muda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nadhani natoamfano tu hapa wa TASAF kwamba hizi shilingi 20,000 hizihazisaidii kuondoa yale matatizo na badala yake zinaletamizozo tu zaidi, mnawapa mnaowajua, mnawapa watumnachangua na nini kwa hiyo, hebu hii pesa ndogo ambayo

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

118

tutaipata katika kufanya haya basi tuipeleke katika eneoambalo lina tatizo tuondoe tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna masuala haya ya socialprotection (kinga za kijamii) je, tuna alternative gani? Maanayake tusiwe tunasema tu wkamba kuna hili, Je, alternativeyetu ni ipi? Juzi nilikuwa namuangalia Dkt. Kilahamaamepunguza yaani wamefanya utafiti, wamepata mitikutoka miaka 14 kuvuna mkaratusi sasa ni miaka naneunavuna katika ubora. Kwa hiyo, solution ziwe hizi na tuzielezesasa kwa jamii moja kwa moja kwamba solution ni hii. Kwahiyo, tufanye vitu vya namna hii na tuwatumie wasomi nawatalaam wetu katika tafiti zao tufanye katika kukabilianana hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, lazima tujitathminikama Watanzania. Kama haya tunayaona leo na haya duniainayasema leo tunachukua hatua gani? Tuna gesi lakini badoasilimia 80 ya Watanzania wanatumia mkaa na kuni kamanishati. Kwa hiyo, tuendeleze elimu na tuwasaidie, tuboreshekurahisisha matumizi ya gesi ili tupunguze sasa hizi atharizinazotkana vinginevyo itakuja kuwa kama hadithi yabiashara ya utumwa. Wazungu ndiyo walioanzisha biasharaya utumwa, wakafaidika, walipopata teknolojiawakawatupia watu wengine wao wakasema ni biasharaharamu. Kwa hiyo, na sisi tusipoliangalia hili tutakujakuishiakatika historia za namna hiyo.

Kwa hiyo, naomba katika matumizi sasa gesi tunayotuhamasishe sana ili tuepuke ukataji wa miti na utumiaji wamkaa na kuni kama nishati na badala yake tuwezekuyatunza mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipanafasi hii. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Yussuf Salim.Mheshimiwa Dkt. Diodorus Kamala, tutamalizia naMheshimiwa Richard Mbogo.

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

119

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: MheshimiwaNaibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuchangiamada hii muhimu iliyo mbele yetu. Naomba nianze kwakusema kwamba naunga mkono hoja iliyo mbele yetu nanaunga mkono hoja hii kwa kutumia hoja ndogo saba.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya kwanza kwanininaunga mkono hoja hii, naunga mkono hoja hii kwa sababuitatuwezesha Tanzania kunufaika na shilingi trilioni 195ambazo tutaweza kuzipata kwa sababu tu ya kuridhiamkataba huu. Kwa nini nasema tutanufaika na sehemu yafedha hizi? Fedha hizi trilioni 195 zimetengwa kupitiamakubaliano ya Nchi za ACP pamoja na Jumuiya ya Ulayani bilioni 70 sasa ukiziweka kwa fedha za Kitanzania zinakujakwenye trilioni 195 na fedha hizi zinaelekezwa kwa nchi 78kimsingi kwa sababu nchi wanachama wa ACP ni 79, lakiniCuba yeye ni mwanachama mtazamaji, kwa hiyo, yeyehatanufaika hata na shilingi moja.

Kwa hiyo, ukigawa fedha hizi kwa nchi zote za ACPni fedha nyingi sana na fedha hizi zinalenga kuelekezwakwenye Global Climate Change Alliance ambayo inalengakatika kutekeleza huo mkataba wa Paris. Lakini pia ni fedhaambazo zitatusaidia sana katika kupambana na mazingiraukizingatia ukweli kwamba rasil imali siku zote huwahazitoshelezi, kwa hiyo, kila fursa inayojitokeza yakukuwezesha kupata rasilimali lazima tuichangamkie kwahiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja hii kwasababu najua kwamba tutaweza kunufaika na fedha hizilakini nina uhakika kabisa kwamba Wizara imejipanga,wameanzisha mfuko wa kutafuta fedha za kupambaa namazingira na najua mipango ambayo tayari wameshaiwekaya kuhakikisha wanapata fedha na ndiyo maana nalishawishihata Bunge hili katika bajeti ijayo basi tutenge fedha zakuweka kwenye huo mfuko wa mazingira ili wawezekuandaa miradi mizuri ya kuweza kunufaika na fedha hizi nafedha nyinginezo. Kwa hiyo, hiyo ni hoja ya kwanza kwa nininaunga mkono hoja hii. (Makofi)

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

120

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hoja ya pili, ukiangaliamazungumzo yaliyokuwepo kuhusiana na masuala yamazingira nakumbuka pale Brussels tulikuwa na mazungumzoya muda mrefu kuhusu mkataba huu maana mkataba huuulizungumzwa maeneo mbalimbali duniani. UlizungumzwaNew York, ulizungumzwa Brussels, ulizungumzwa Beijing hataTanzania mlizungumza wakati huo sikuwepo nilikuwa Brusselslakini tulipokuwa Brussels tulizungumza pia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo moja kubwaambalo lilichukua muda mrefu kuzungumza na kukubalianani kukubaliana kwamba ili kupambana na mabadiliko yatabianchi, kila nchi itabidi ichangie kulingana inavyoharibumazingira lakini pia kwa kuzingatia uwezo wake wakiuchumi. Hoja hii nchi zilizoendelea hazikuitaka sana lakinikwa mara ya kwanza katika dunia hii, nchi za ACP zikaunganana nchi za Ulaya ili kuwa na msimamo wa pamoja wakwamba katika uharibifu wa mazingira basi kama weweunaharibu zaidi utatakiwa uchangie zaidi katika kupambanana tabianchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni hoja iliyotuchukua mudamrefu lakini nashukuru hatimaye hoja hiyo ilipita na ilipoendaUN mataifa yote yakakubaliana na ndio maana tunaitakifungu namba mbili katika mkataba huu kinachosemamataifa yote duniani yatawajibika kupambana na mazingirakulingana na jinsi anavyochangia, ukichangia kuchafua zaidibasi uchangie zaidi katika kupambana na hayo mazingirakwa hiyo, ndio maana nasema naunga mkono hoja hii kwasababu ni hoja muhimu inatoa fursa hata kwa mataifaambayo yanachafua zaidi yaweze kuchangia zaidi katikakupambana na mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nikwanini naunga mkono haja hii ukiangalia kifungu nambatano kinasema nchi zinazoendelea zitaendelea kusaidiwakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Sasa ukisema nchizinazoendelea na nchi nyingine zenye uchumi kama wa sisini kwamba sisi tunachangia kidogo katika kuharibu

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

121

mazingira, lakini kifungu hiki kinatuhakikishia kwambatutaendelea kusaidiwa katika kupambana na mazingira.

Lakini sababu nyingine kwa nini naunga mkono hojahii ukiangalia sehemu ya pili, kifungu cha 4(2) kinasema nchizinazoendelea ziendelee kukabiliana na hatua zakupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna mabadilikoambayo hakuna mkataba ambao utasaini tu usiokupawajibu, ni kwamba makubaliano haya tuna wajibu wakufanya ni upi. Wajibu wa kufanya ni kuendelea kuwa namikakati na kuonyesha dhamira ya kuendelea kupambanana mazingira ndiyo maana tunapopitisha tunatoa ridhaamaana yake tunakubali kama Bunge kwamba tutaendeleakusaidia Wizara yetu ya Mazingira na Masuala ya Muunganokuiwezesha kuendelea kupambana na mazingira hiyo ndiomaana yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, na ukiangalia mwenendowa bajeti Wizara imekuwa ikpatiwa kila mwaka unaonakwamba ilikuwa si fedha zinazotosheleza mahitaji yao yotebasi kwa kupitisha kifungu hiki ninakuwa nina uhakikakwamba sasa tunaenda kutenga fedha za kutosha kwaWizara ya muungano na masuala ya mazingira ili kuwezakusaidia masuala mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja iliyombele yetu kwa sababu hata mataifa makubwa kamaMarekani na Japan sitawataja baadhi ya viongozi kwasababu kidiplomasia si vizuri kumtaja mtu, wapo waliosemahawatakubaliana na masuala ya Paris Agreement, lakininaomba kulithibitishia Bunge hili kwamba mataifa yotemakubwa mnayoyajua yaliyokuwa yanaoneshahayatakubaliana na kupambana na mazingira tayariyameweka sahihi na tayari yameridhia, sasa wale waliokuwana wasiwasi waliojaribu kuonesha kwamba hawatakubali,wameshakubali sioni sababu kwa nini sisi tusiridhie kwasababu sisi ni wanuifaika wakubwa wa makubaliano hayo.(Makofi)

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

122

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuridhia maana yaketutaweza kunufaika na Global Environmental Facility,Adaptation Fund, pamoja na Green Climate Fund namengineyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la mwisho hoja ya sabakwa nini hoja iliyo mbele yetu ni muhimu tukiridhia maanayake tunaiambia dunia kwamba tutaendelea kupambanana mazingira, miradi mizuri kama ya Kihansi tutaendelea nayokuna mradi mzuri sana unaendelea kutekelezwa chini ya ofisiya Makamu wa Rais mradi kama Ruaha Mkuu, kutunza RuahaMkuu kwa sababu tunazungumzia Green Stiegler’s Gorgehuwezi ukazungumzia Stiegler’s Gorge wakati unaendeleakuharibu mazingira, lakini tunaposema tunasaini, tunaiambiadunia kwamba tutatunza hata mazingira, lakini tutaendeleakutoa elimu, tutaendelea kutunza vyanzo vya maji, paleOcean Road kuna mradi mkubwa wa kutunza mazingira nazaidi ya nchi 10 kutoka dunia nzima zinakuja pale kuangaliaTanzania tunafanyaje kutunza mazingira kwa hiyo, ni mfanowa kuigwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu hizo sabanaunga mkono hoja iliyo mbele yetu kwa asilimia mia moja.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa RichardMbogo.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa nafasi moja kwa moja niseme tu kwanzanaunga mkono hoja ya kupitisha hili azimio kwa ajili yamakubaliano ya Paris kuhusu kuboresha utekelezaji wamkataba wa mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ambaloningependa kuchangia kwanza tukubaliane na hili Azimiokwa sababu tuna faida nyingi ambazo Mheshimiwa Waziriameweza kuzieleza kama nchi ambavyo tunawezakufaidika; la kwanza ni mkakati wa kutekeleza utunzaji wamazingira, upatikanaji wa fedha, masuala ya kuweza

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

123

kupanda miti ambayo itaweza kunyonya gesijoto, lakinikikubwa ni kwamba uhai wa mwanadamu upo kwenyemazingira, duniani nchi zote tunafanya shughuli zakimaendeleo lakini tunaangalia na uhai wa kwetu sisiwanadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ongezeko la joto dunianilina athari nyingi sana kama ambavyo tumeweza kuelezwapamoja ikiwa ni uchafuzi wa mazingira, kuleta ukame,magonjwa, uharibifu wa miundombinu na mambo menginemengi sasa kwa misingi hiyo tunavyokubali azimio hili na kilanchi kuweza kutaekeleza ili Azimio katika kusimamia kutunzamazingira tutaenda kuonyesha kwamba uhai wetu sisiwanadamu utakuwa na uhakika wa kuwepo na kuishi.

Sasa kutokana na vifungu mbalimbali vyamakubaliano ambavyo vimeweza kuelezwa ningependakama nchi kwa sababu haya ni mabadiliko yamepitishwamwaka 2016 basi tuombe kwenye mabadiliko ambayoyatakayofuata mbeleni katika haya maazimio tusisitizwe sanakwenye nchi ambazo zinachangia katika uharibifu na kuletajoto duniani ziweke vipengele ambavyo vitahakikishakwamba wanatekeleza utoaji wa fedha kwa ajili ya nchizinazoendelea katika kutunza mazingira.

Mheshimiwa Naibu spika, hilo litakuwa ni jambo laumuhimu sana katika kuzibana hizi nchi na pia katikamawasilisho imeonekana kuna baadhi ya nchi ambazozinakuwa haziko tayari zikiangalia kwamba zenyewezinaathirika zaidi katika shughuli zao za kiuchumi kutokanana kubanwa kwenye shughuli zao.

Kwa hiyo, tuombe katika maazimio mbeleni hukomarekebisho ambayo yatafanyika tuone namna ya kuzibanahizi nchi na hasa hizi nchi ambazo tena zilizoendeleazinazoshindana zaidi na zinakuwa zinapinga maazimio kamahaya basi tuone namna ya kuzibana ili ziweze kutekelezakwa namna ambayo na sisi ambao ndio nchi maskinitunaoendelea na ndio ambao wengi tunaotunza mazingirana dunia angalau inakuwa ya ina uhakika kwamba

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

124

tutaendelea kuishi duniani kwa sababu ya nchi hizi ambazotunazoendelea ambazo tunatunza mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano Tanzaniaasilimia 30 ya nchi yetu iko kwenye uhifadhi kwa hiyo, tunauhakika wa kuendelea kutunza na dunia ikapata nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuangaliaupande wa kimataifa naomba nije kwa upande wa kamanchi Tanzania, tunajua tunazo sheria, tuna sera, na tunauongozi, lakini ni kwa namna gani tunasimamia hizi seraupande wa mazingira na tunasimamia sheria zetu ili ziwezekutunza mazingira tumeona changamoto sehemumbalimbali za nchi yetu kumekuwa na uharibifu mkubwasana wa mazingira na hasa kufanya kazi za maendeleokutoka kwenye kingo za mito kama sheria inavyosema mita60 na mita 500 kutoka kwenye vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Naibu spika, lakini kuna wamiliki wamabonde, tunayo TAMISEMI na tunayo Wizara husika ilausimamizi katika maeneo mbalimbali huku hafifu mnomatokeo yake shughuli za kibinadamu, za mifugo, za kulimawamekuwa wanaingia mpaka maeneo ya vyanzo vya majina kingo za mito kwa hiyo inapelekea kuharibu mazingira,na kwa misingi hiyo changamoto mojawapo ninayoiona niuwezeshaji wa Halmashauri zetu kupitia hii Wizara jinsi ganiwanazishikisha katika kusimamia na kikubwa piatunashindwa kuwatumia namna fulani sijapenda kuielewaWakuu wetu wa Wilaya ambao ni Wenyeviti wa Kamati zaUlinzi na Usalama katika Wilaya kwanza hawana OC zakutosha kuweza kuzunguka na kusimamia vizuri watendajiwalio chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niombe Serikalituangalie namna gani tunaongezea OC Wakuu wetu waWilaya waweze kusimamia Halmashauri zetu katika kulindamazingira na kijumla maana imekuwa ni changamoto nampaka maeneo mengine Wakuu wetu wa Wilaya hawanavyombo vya usafiri vya kutosha au vingine vimechakaa nahavifai katika utendaji wa kazi.

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

125

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala lakiuongozi kiujumla jinsi gani tunashirikisha kuanzia Wenyevitiwa Vijiji, Wenyeviti wa Kitongoji katika kulinda mazingira elimuje, wanayo na inatumika ipasavyo kwa hiyo tuombe tenaWizara tuone namna gani tunawashirikisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la nishati katikamatumizi ya kawaida ya nyumbani mambo ya kupikia mkaana kuni ndio vinatumika kwa asilimia 98 na je, mkakati waSerikali katika kulinda mazingira nishati mbadala kwenyematumizi ya nyumbani mkakati uko namna gani, matumiziya mkaa kwa mfano Jiji la Dar es Salaam ndio linaloongozakatika nchi hii je nishati mbadala iko vipi, tuna taasisi za Serikalisasa hivi wananchi wengi na wataalam wengiwanatengeneza biogas kwa kupitia taka na vyanzo vinginena wanatumia kwenye matumizi ya nyumbani kwa ajili yakupikia, sasa mkakati wa Wizara hii husika kupitia Ofisi yaMakamu wa Rais hili fungu linalopatikana toka kwenye nchiwahisani wanaotoa kwa ajili ya kutunza mazingira watengekwa ajili ya kuelemisha na kufundisha na watu kuwawezeshakutumia biogas kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa mfano unawezaukaanza na taasisi kama Magereza, taasisi hizi kama vyuovikuu, mashule watengeneze biogas kwa ajili ya kupikia. Hizishule za bweni maana yake wanapikia wanafunzi chakulaje, wanatumia nishati gani? Pia tukienda kwenye shughuliza kilimo kwa mfano mazao ya biashara kama tumbaku sasahivi wakulima wanakausha tumbaku, wanakata miti sawaSerikali imeleta mabanio ambayo kidogo yanatumia kuni zilendogo ndogo chache, lakini wengine hawatekelezi je tunanishati mbadala tuache kukata miti?

Kwa hiyo, niombe sana Serikali kupitia hii Wizara wajewatueleze biogas na nishati mbadala tuachane na mkaana kuni katika kupikia ambayo ndio inayokata miti sanakatika nchi yetu namna gani tunaenda kuwezesha kwakupitia haya mafungu yanayotoka kwenye nchi zilizoendeleazinazotoa kwa ajili ya kusaidia kupunguza athari za ongezekola joto humu duniani. (Makofi)

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

126

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kumalizia niombe sasakwa upande wa hizi halmashauri mlizilazimishsa kwambaSerikali ilisema kila Halmashauri ipande miti 1,500,000 nawaliweka kwenye bajeti sasa utekelezaji mpaka sasa hivi kilahalmashauri wamepanda miti mingapi hiyo utakuta ni hafifuna watu hata wakipewa ile miti, je, wanaisimamiawanahakikisha kwamba na inakua kwa hiyo, usimamizikatika upande wa mazingira tuone namna gani tunaongezajuhudi ili tuhakikishe kwamba utekelezaji wake wa hayamaagizo tunayotoa yanasimamiwa ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ni Wizara yamaliasili na utalii ina maeneo mengi yaliweza kuathirikakutokana na watu kuvamia kwa shughuli za kil imombalimbali lakini je, tunahusisha vipi kuingia ubia nahalmashauri zetu kupanda miti rafiki kama ilivyo katikamaeneo mengine kwa mfano kama mazao ya korosho ilituweze kuboresha hayo maeneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, na la mwisho ni elimutumesema kwamba tupande miti ambayo itaenda kunyonyagesi je, hii miti tunayowaambia wataalamu wetu huko nawananchi wetu tunawaelimisha kwamba miti hiimnayopanda ndio ambayo itaenda kunyonya gesi elimu hiyoinatolewa na kwa kiasi gani inatolewa na fedha za kusaidiakutoa elimu Halmashauri zetu tunazozipata.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkonohoja na nashukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ofisi yaMakamu wa Rais, Mheshimiwa Kangi Lugola kwa dakikakumi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu spika,nishukuru kwa kunipa fursa na mimi kuweza kuchangia hojahii ya Azimio letu la makubaliano ya Paris chini ya Mkatabawa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabianchi.Mheshimiwa Waziri wangu atawatambua wale wote ambao

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

127

wamechangia kwenye Azimio letu, mimi nigusie baadhi yamaeneo ambayo wachangiaji wameyasema.

Kwanza kabisa chimbuko la azimio hili ni mkutanoambao ulifanyika kule Stockholm na ulikuwa unahusubinadamu na mazingira. Kwa hiyo, utaona ni kwa kiasi ganijinsi umuhimu ulivyo kati ya binadamu na mazingira jinsiwanavyotegemeana. Sheria yetu namba 20 ya mwaka 2004ya Usimamizi wa Mazingira imesheheni mambo ambayoWatanzania wakiyafuata bila shuruti tutakwenda kutunza,kuhifadhi na kulinda mazingira ya nchi yetu na tutakuwa ninchi ya mfano katika ukanda mzima wa Afrika na dunianzima.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini nasema hivyokatika sheria yetu mazingira yametajwa kwamba ni urithikatika msingi wa ile sheria kwamba mazingira ni urithi wa kizazihiki ambacho tunaishi sasa na vizazi vinavyokuja kwa hiyo,wananchi wakielewa umuhimu huo watakuwa katika fursanzuri ya kujali katika kutunza vyanzo vya maji katika nchiyetu, watajali katika kutunza miti, watajali kila wakatikupanda na kutunza miti na hivyo urithi huu ndio hoja ambayoMheshimiwa Saleh alikuwa anazungumzia masuala ya urithi,namna ambavyo baadhi ya ndege wanatoweka, baadhiya miti inatoweka, theruji kwenye Mlima Kilimanjaroinapungua kwa hiyo tutakapokuwa katika fursa hii yakujitambua kwamba mazingira tunatakiwa uwe ni urithi kwasasa na baadaye Watanzani tutakuwa katika mazingiramazuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, amezungumzia suala lakufanyika tafiti hasa kuwatumia wataalamu tafiti hii yamimea, tafiti ya miti sheria yetu ya mazingira inaanzisha mfukowa Taifa wa dhamana ya mazingira na mojawapo yamatumizi katika mfuko ule ni katika masuala ya tafiti, ni katikamasuala pia ya kuwafadhili Watanzania waweze kusomakatika maeneo haya ya mazingira.

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

128

Mheshimiwa Naibu Spika, ni imani yetu Ofisi yaMakamu wa Rais kwamba bajeti hii inayokuja tuombeWaheshimiwa Wabunge wapitishe tuweze kuwa na fedhaza kutosha katika mfuko wa Taifa wa dhamana ya mazingiraili kupitia mfuko huo tuweze kuhakikisha kwamba tunakuwana wataalam wanaofanya hizi tafiti ikiwa ni pamoja nakuwasaidia wananchi katika kusoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, sheria yetu ya mazingirakifungu cha sita kimetoa wajibu kwa Watanzania wotekuhakikisha kwamba wanatunza na kuhifadhi mazingira, kwahiyo sio suala tu la Ofisi ya Makamu wa Rais au NEMCkwamba sisi ndio tunawajibika kuhakikisha kwambawananchi wanatunza mazingira ni wananchi wote.

Niwaombe Waheshimiwa Wabunge nyinyi ndio mkomajimboni kule ambako ndiko kuna halmashauri zetukuanzia Halmashauri za Wilaya, za Miji za Manispaa na Majijina amezungumzia Mheshimiwa Richard Mbogo masuala yauelewa kwenye Vitongoji, kwenye Vijiji Waheshimiwa ninyindio Madiwani kwenye Halmashauri zenu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninawaomba kwa kuwasheria hii kuanzia kifungu cha 36 mpaka 41 kinazungumziakuwepo kwa Kamati za Mazingira kwenye ngazi za Vitongoji,Vijiji, Mitaa, Kata mpaka Wilaya na kuwepo kwa MaafisaMazingira hakikisheni kwamba Kamati hizo zipo na zinafanyakazi pale ndipo tutakuwa katika nafasi nzuri ya kulinda nakuhifadhi mazingira kwa sababu mazingira yako kule chinikabisa kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie sualalililozungumzwa sana la hasa kuanzia Kambi ya Upinzanikwamba kuwabana zile nchi ambazo zinachafua mazingiraili waweze kuleta fedha.

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

129

Katika Azimio hili kwenye mkataba imewekwabayana kabisa namna ambavyo hizi nchi zinawajibikakusaidia fedha na tumetaja Mifuko mbalimbali na Mashirikaya Kimataifa ambako sisi hupata fedha. Tumewaoneshamiradi mbalimbali, mingine ambayo Mheshimiwa Lubelejeamesema itaenda kwenye Wilaya yake na baadhi ya Wilayaza Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni matumaini yetukwamba sisi tutakapotenga fedha za ndani na tukaendeleakupata fedha hizi kutoka kwa wafadhili, ni imani yetu kwambatutakwenda kuhifadhi na kutunza mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na wasiwasiMheshimiwa Mbogo. Anasema kweli, kwenye Ilani yetuukurasa wa 213 tumezungumzia kwamba kila Halmashaurihapa nchini lazima kila mwaka wawe na miradi ya kupandamiti isiyopungua 1,500,000 na kwamba, ni kweli hiyo miti ipo?

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie kwamba mimina Mheshimiwa Waziri tumekuwa tukizunguka nchi nzimaikiwa ni pamoja na kutumia Sikukuu za Mazingira Duniani,tumekuwa tukizunguka na kuhimiza Halmashauri wawezekupanda hiyo miti na kutuonesha kwa macho. Tunajipangakama sehemu ya mkakati wa Kitaifa ili kuanzia mwakani,kama ilivyokuwa kwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Magufuli,akiwa Waziri wa Uvuvi, alikuwa na uwezo wa kujua idadi yasamaki kwenye bahari na kwenye maziwa na mito; nasitutakuwa na sensa ya miti i l i tujue kwamba hii mititunayoambiwa kwenye taarifa mbalimbali wamepanda, je,hii kweli hii miti ipo, ili tuwe na uhakika kwamba mazoezihaya yanakwenda vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mita 60 nawamezungumzia kwenye Kambi ya Upinzani vinyungu kuleIringa na Njombe; wamezungumzia kule milimani kuleKilimanjaro. Niseme tu kwamba Mheshimiwa Waziri alishatoamwongozo kwamba Halmashauri zote nchini walete orodhaya vyanzo vyote vya maji, pamoja na milima na vilima iliwachanganue kwamba vyanzo hivyo vya maji vina

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

130

changamoto gani ili sisi Ofisi ya Makamu wa Rais tuwezekutengeneza mkakati wetu wa Kitaifa ambao unaendeleakwenye task force i l i tuweze kuwabana hao ambaowanaharibu na kuchafua vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niwahakikishieWaheshimiwa Wabunge kwamba nchi hii ambayo tumekuwatukisema Mataifa yanayochafua na kuharibu mazingira, hasakwenye hewa ya ukaa ambayo inakuja mpaka huku nakuleta athari za mabadiliko ya tabianchi kwamba tuzibanezilete fedha; sisi kwa kutumia Sheria ya Mazingira tunawabanawananchi watumie fedha katika kuhifadhi na kutunzamazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunawabana wawekezajina hasa wenye viwanda kuhakikisha kwamba katikauwekezaji wao, nao wasiangalie tu sehemu ya faida,waangalie pia kuweka mifumo rafiki ambayo itahakikishakwamba wanalinda na kuhifadhi mazingira ili siku ya sikuTanzania ya viwanda ambayo Mheshimiwa Rais ni championkuhakikisha kwamba Tanzania ya Viwanda inaendasambamba na kuzingatia sheria za kutunza na kuhifadhimazingira. Kwa hiyo, tutaendelea sisi Ofisi ya Makamu waRais kuwa wakali sana kusimamia sheria hii ili Watanzaniawote wahakikishe kwamba wanatunza na kuhifadhimazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwenye sualaaliloligusia Mheshimiwa Lubeleje. Mheshimiwa Lubelejeamegusia suala la Mpwapwa. Mheshimiwa Waziri wangualishaniagiza niende Mpwapwa ambako wananchiwanaendelea kukata miti ovyo kwenye vilima, wanaharibuvyanzo vya maji na kuchoma moto ovyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna shule moja yasekondari ambayo inasemekana kuna mwananchi mmojaalienda akakata miti ya shule ambayo wao walikuwawameipanda kwa ajili ya kuhifadhi mazingira. Kwa hiyo, nitoewito kwa nchi nzima, siyo Mpwapwa tu kwa Mheshimiwa

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

131

Lubeleje, kwamba suala la kisingizio cha kwamba tunatumiakuni, tunatumia mkaa, vijijini kule wananchi wengi hawatumiimkaa, mkaa mwingi unaenda mijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi Serikaliimeshajipanga kuhakikisha kwamba kupitia Wizara ya Nishatiwanaanza kusambaza gesi katika Mji wa Dar es Salaamambapo tunaamini sasa tunaenda kuwa na nishati mbadalakwa njia ya gesi ili tuanze kupunguza matumizi ya kuni namkaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, taasisi nyingi za Serikaliyakiwemo Magereza, Hospitali na shule, tumeshawapamwongozo na maelekezo kwamba waache sasa kutumiakuni na mkaa, waende kwenye nishati mbadala. Wazo zurialilolitoa hapa Mheshimiwa Mbogo, kuwa shuleni kwenye bio-gas, kuna baadhi ya shule ambazo tayari tumeanzakuzitembelea kwamba wana-recycle, wana bio-gas ili sasakupitia Bunge lako tutakapopata uwezeshaji wa kibajeti,tuanze kupita kwenye shule na taasisi nyingine ambazonimezitaja kama majeshi na shule ili waanze kuwa na nishatihii ya bio-gas ili tupunguze ukataji wa miti.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mtoa hoja, MheshimiwaJanuary Makamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,(Mazingira na Muungano).

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MAZINGIRA NA MUUNGANO): Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nakushukuru tena, lakini pia naishukuru Kamati kwamaoni mazuri waliyoyatoa na ushauri tutauzingatia wote. Pianapenda kumshukuru Mheshimiwa Ally Saleh Msemaji waKambi Rasmi ya Upinzani kwenye masuala ya Mazingira naMuungano. Bahati nzuri yeye ni mwanamazingira mzuri,ametoa mawazo mazuri na tutayazingatia hasa la kushirikishawadau zaidi.

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

132

Mheshimiwa Naibu Spika,ia suala la baadhi yavipengele ambavyo vimezungumzwa kwa ujumla na hakunaufafanuzi kuhusu utekelezaji wake. Nataka nimweleze tukwamba majadiliano bado yanaendelea kuhusu namna yautekelezaji wa makubaliano haya. Kwa hiyo, mambomengine aliyoyazungumza yatapatiwa majawabu naufumbuzi mara pale mazungumzo kuhusu utekelezaji wamkataba huu yatakapokwisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru MheshimiwaNaibu Waziri kujibu karibu mambo yote yaliyozungumzwa nakwa kwa ufasaha kabisa na kwa kweli zaidi ya hapanampongeza, mwanzo nilisahau kumshukuru kwa mchangowake na kazi nzuri anayoifanya katika ofisi yetu ili kusaidiana.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Mheshimiwa Lubelejeamezungumza kwa hisia sana kuhusu masuala haya nanamshukuru. Wakati mwingine utu uzima unasaidia kuoneshatofauti. Asilimia 50 ya Watanzania ni watu wa umri wa chiniya miaka 18. Asilimia 44 ya Watanzania ni watoto chini yamiaka 14. Kwa hiyo, unapokuwa na Taifa la watu wengi niwenye umri mdogo, wanakuwa hawajapata kuona nchiilikuwaje miaka iliyopita na ilivyo sasa. Kwa hiyo, wanaonahuu uharibifu uliopo na hali iliyopo sasa ndivyo nchi ilivyo,kwa hiyo, wanakosa uchungu na hamasa ya hifadhi yamazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa MzeeLubeleje, amekula chumvi nyingi na anaposema hasakwamba miaka ya 1960 nchi hii haikuwa hivi, ni kweli, anaushuhuda kwa sababu ameona ilivyokuwa huko. Kwa kwelitungependa yeye na wazee kama yeye wapate nafasi hiziza kutuelimisha sisi vijana, tuone kwamba uoto wa asili nalandscape ya nchi yetu, kwa kweli inaharibika kwa harakasana katika miongo hii kadhaa aliyoishi, ambayo vijanawengi wa sasa wataishi, hali itakuwa mbaya zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunamshukurusana kwa ushuhuda wake. Kama nilivyomwelekeza NaibuWaziri, atakwenda Jimboni kwake. Kwa kweli hali ni mbaya,

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

133

ndiyo maana tumepeleka huu mradi mmoja Jimboni kwakekwa ajili ya kusaidia watu wa Mpwapwa. Nafahamu kunahabari ya makorongo mengi yanayopitisha maji na kuharibumazingira na Naibu Waziri atakuja kuyaona.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru piaMheshimiwa Salum, amezungumza kwa hisia sana na kwakweli ametufundisha na kutueleza jinsi gani baianuaiinavyopotea. Kwenye kisiwa kama cha Zanzibar ambapoeneo ni dogo na utajiri wa Zanzibar; utajiri wa Tanzania kwakweli haupo chini ya ardhi peke yake kwa maana ya madini.Utajiri ni kwenye maarifa ya Watanzania lakini pia ni kwenyeuoto na mimea na wanyama ambavyo Mungu ametujaalia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna baadhi ya nchi hapaduniani zina aina chache sana za mimea, aina chache sanaya wanyama, ndiyo maana wanakuja huku na duniainavyoenda kuna baadhi ya nchi hata sauti ya ndege watotowanaozaliwa miaka inayokuja watakuwa hawaijui mpakawaje kwetu. Sasa na sisi tukipoteza ndege wale, ina maanavizazi vijavyo tutakuwa tunahadithiana kwamba, bwanakuna ndege fulani aliishi miaka hiyo alikuwa na rangi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, utajiri mkubwakabisa wa nchi yetu ni baianuai (bio-diversity); wingi wamimea na wanyama. Sasa huu mkataba tunaouzungumzaleo, makubaliano haya yapo chini ya makubaliano ya UNFCCUnited Nations Convention of Climate Change na siku ileyale makubaliano yalivyowekwa sahihi kule Brazil kulikuwana mkataba mwingine unaitwa Mkataba wa Uhifadhi waBaianuai (Convention on Biological Diversity) ambao sisi niwanachama wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ule mkataba unatoa fursanyingi za kuhifadhi baianuai. Pia unatoa nafasi ya nchi yetukutajirika na kunufaika na baianuai yetu tuliyonayo. Baianuaisiyo kwa maana tu ya kuja kuitazama, lakini kuitumia kwenyetiba, utafiti na kadhalika. Mnafahamu madawa yoteyanatokana na miti; na mnapoharibu miti na mimea

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

134

mnapunguza uwezo wa kujitibia siku zijazo. Kwa hiyo,uharibifu wa mazingira ndugu zangu unahusu pia hata tibayetu kwa miaka inayokuja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nashukurukwamba hilo tumelizungumza na sisi kama Serikali,tunaendelea na utekelezaji wa mikataba yote hii miwili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana MheshimiwaMbunge amezungumza kwamba tubadilike. Leotunazungumza mabadiliko ya tabianchi lakini inawezekanacha kwanza kinapaswa kuwepo ni mabadiliko ya tabiamtuili tuweze kudhibiti mabadiliko ya tabianchi. Kwa sababukama mabadiliko ya tabiamtu hayatokei, itakuwa ni vigumusana kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumezungumzwa piakuhusu kuni na mkaa na Mheshimiwa Mbogo vile vileamezungumza kuhusu kuni na mkaa. Nataka nizungumzekwamba sisi tunaangalia matumizi ya nishati hizi zatungomotaka wanaita (biomass) katika suala zima ladeforestation na landscape degradation, kwamba huu uotounaouona, ardhi, mimea; hii landscape ya nchi yetuinayopendeza, kasi yake ya kuharibika ni kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo, ufugaji, utalii maji,zote zina uhusiano na hifadhi ya mazingira. Kwa hiyo,tunapopata uharibifu wa landscape, huu uoto, hizi sektanyingine zote haziwezi kufanikiwa. Kwa hiyo, uchumi wanchi yetu na ukuaji wa uchumi na umaskini na ustawi wawatu, unafungama moja kwa moja na hifadhi ya mazingira.Huwezi kutofautisha!

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sisi tunasemahapa, tunataka kuhamasisha Wabunge wote wawewanamazingira. Kama unataka kuzungumza maji Jimbonikwako, huwezi kuyapata bila hifadhi ya vyanzo vya maji, bilahifadhi ya miti na kadhalika. Kwa hiyo, nafurahi kwambawaliochangia karibu wote wamesaidia kutoa elimu nawamesaidia kuonesha hisia katika mambo haya.

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

135

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwenye matumizi yakuni na mkaa, sisi kama Serikali tunashirikiana na tutashirikianana Wizara ya Maliasil i na Utalii kuhakikisha kwambatunatengezea mpango mkubwa wa Kitaifa wa matumizi yanishati. Tayari maelekezo yametolewa kwenye Wizara yaNishati na Madini kutunga sera mpya ya nishati yatungomotaka (biomass policy) ili tuwe na mwongozo wanamna gani tunapata nishati ya kupikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa hivi kinachotokeani kwamba miti iko vijijini lakini ukataji wake unanufaisha watuwa mijini. Watu wa mjini hawana miti, lakini watu wa vijijinikuni zile wanakata matawi tu. Ili mtu wa mjini apate mkaa, nilazima akate mti wenyewe, gogo lile. Sisi kwenye shule,Magereza na Mahospitali, hatutumii kuni za matawi tu, nilazima tukate mti wenyewe. Ukienda unakuta lundo lamagogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sisi kama Ofisi yaMakamu wa Rais tumetumia kifungu cha 13 cha Sheria yetuya Mazingira ambacho kinasema kwamba Waziri mwenyedhamana ya mazingira ana uwezo wa kuelekeza mamlakazozote za kisekta, binafsi na taasisi kufanya mambo ambayoyatahifadhi mazingira. Kwa hiyo, tumetoa maelekezo kwashule, Magereza, hospitali na tumewapa mwaka mmojakwamba waondokane na matumizi ya kuni na mkaa natumeanza hapo UDOM.

Mheshimiwa Naibu Spika, UDOM pale pana wanafunzitakriban 30,000, wanapikiwa chakula mara tatu kwa siku.Sasa hebu fikiria kulisha watu 30,000 mara tatu kwa siku,kiwango cha kuni kinachotumika ni kikubwa sana. Ukiendapale utataka kutoa machozi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, waletumewaambia ndiyo watakuwa wa kwanza na bahati nzuritumekubaliana kwamba watu wanaowapa zabuni pale,wote sasa ili upate zabuni ya kupika chakula, hauwezi kupatakama unatumia mkaa au kuni. Kwa hiyo, tutaona mabadiliko

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

136

yaliyotokea pale UDOM yatatusaidia kutoa mfano kwenyetaasisi hizi kubwa zenye watu wengi kuhusu kuondokana nahili suala.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili ni jambo nikubwa, sisi kama Serikali tunalichukulia kwa uzito wake.Matumizi ya nishati nchini yanafungamana na umaskinikwamba masikini zaidi ndio wanagharamia nishati zaidi. Piatusisahau kwamba wewe unatoka Pemba; ukitazama mkaaunaopelekwa Pemba kutoka bara, haulingani na idadi yawatu walioko Pemba.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kule kwenye hizibandari za kwetu; Mbweni, Bagamoyo utaona magunia yamkaa yanaenda Pemba. Unajua yanaenda wapi? HayaendiPemba, yakifika Pemba yanaenda shimoni, Mombasa.Yakifika Mombasa yanapakiwa vizuri yanaenda Somalia auUarabuni kuchoma kondoo vizuri. Maana wale wanatakakuchoma kondoo na mkaa mzuri; na yakienda Somaliayanasaidia ku-finance Al-shabaab.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mkaa wetutunaweza tukauona hapa ni jambo la kawaida lakini unamuunganiko na value chain kubwa sana ambapo wotekama Serikali na Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo ndiyoinahusika moja kwa moja na haya mambo, inabidi tukaetupange vizuri. Kwa sababu siyo tu kwamba mkaaunaokatwa nchini unatumika nchini, unaenda nje yaTanzania vile vile. Kwa hiyo, tunakata miti yetu sisi kwamanufaa ya watu wengine huko nje ya Tanzania. Kwa hiyoni suala la kulizungumza.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia matumizi bora ya ardhi.Moja ya changamoto kubwa inayosababisha sisi tushindwekuhimili mabadiliko ya tabianchi ni kwamba tuna kilimo hikicha kuhamahama. Mtu anavamia msitu, analima mtamamisimu miwili, ardhi ikiharibika anakata tena kipande kinginecha msitu. Kwa hiyo, baada ya miaka michache unakutamsitu wote umefyekwa. Au wale wafugaji.

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

137

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa sisi kama nchi, wajibuwetu ni kuweka taratibu za kutumia vizuri ardhi. Kielelezo nashabaha ya maendeleo ni kutumia ardhi kidogo kuvuna zaidi.Nitatoa mfano, nchi ya Uholanzi, eneo lake ni dogo kulikoMkoa wa Katavi, yaani Mkoa wa Katavi ni mkubwa kulikoUholanzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Uholanzi ni nchi ya piliduniani kwa kuuza bidhaa za kilimo pamoja na kuwa naeneo dogo. Ukiondoa Marekani, inakuja Uholanzi. Uholanziwanauza dola bilioni 90 za mazao ya kilimo kwenye eneokama la Mkoa wa Katavi. Kwa hiyo, ndiyo kielelezo chamaendeleo. Nasi tunaweza kufika huko. Wanafanya hivyobila kutumia GMO wala nini, ni kilimo tu endelevu nawanahifadhi mazingira na ni kuzuri. Kwa hiyo, naaminimaendeleo yetu yatafikiwa tutakapokuwa tumefanyamambo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbogonashukuru sana kwa mchango, nimekupata. Tutashirikianana Serikali za Mitaa na tumezungumza na wenzetu wa Wizaraya Fedha, Naibu Waziri yupo ananisikia, tumependekezakwamba kila Wizara na kila Halmashauri iwe na budget codeyaani zile…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, naomba urudi ukaekidogo.

Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa Kanuni ya28 fasili ya (2), nakusudia kuongeza nusu saa ili tuwezekumaliza shughuli tulizonazo mbele yetu. Vile vile fasili hiiinanitaka niwahoji i l i tuweze kukubaliana. Kwa hiyo,nitawahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

NAIBU SPIKA: Walioafiki wameshinda. Kwa hiyo,tunaendelea ili tuweze kumaliza shughuli zetu za leo.

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

138

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira).

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika,napenda pia kutoa pendekezo kwamba, saa yetu ile palembele itengenezwe. Kumbe inakuwa sahihi mara mbili kwasiku. Naona imesimama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nasema kwamba,kuhusu mapendekezo ya Mheshimiwa Mbogo kuhusuushirikishwaji wa Halmashauri na viongozi kwenye maeneoyetu ya vij i j i , Wilaya na Halmashauri tutayachukua,tumeyazingatia.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya mipango yetukatika Ofisi yetu ya Makamu wa Rais ni kufanya kazi kwakaribu zaidi na Serikali za Mitaa. Katibu Mkuu anayomaelekezo yetu kuandaa mikutano baina ya ofisi yetu naSerikali za Mitaa kwenye level ya Mawaziri, Makatibu Wakuu,lakini pia kujaribu kutumia fursa za vikao mbalimbali vilivyopoikiwemo vikao vya RCC ili kuweza kwenda kutoa elimukwao, lakini kuweka makubaliano ya ushirikiano ikiwemoushirikiano katika kuhakikisha kwamba Sheria ya Mazingirainazingatiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata baadhi ya masualaikiwemo ya usimamizi wa sheria, ikiwemo ya kufanya hizihabari za tathmini ya athari kwa mazingira, baadhi yamambo tunafikiria kuyakasimu kwenye Serikali za Mitaa. Kwahiyo, mpango huo upo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema awalikabla sijakaa, itapendeza kama tutakubaliana ndani yaSerikali kuwa na budget code, ili kila Halmashauri katika bajetiyake iwe na sehemu inasoma namba zile, “Hifadhi yaMazingira,” ili fedha ziweze kupangwa kwa ajili ya hawaWakuu wa Wilaya, kama ulivyosema, wapate OC yakuzunguka na kusaidia kwenye hifadhi ya mazingira.

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

139

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kupanda miti,Naibu Waziri amelizungumza kwamba tutalipa msukumompya na tutafanya sensa ya miti. Pia, niseme tu kwamba,kama tulivyozungumza kwenye Azimio kwamba paleMorogoro tumeanzisha kituo kinaitwa National CarbonMonitoring Centre ambapo kuna teknolojia ya kujua kasi yauharibifu wa mazingira maeneo ambayo miti inahitajikurejeshwa. Bahati nzuri Mheshimiwa Waziri wa Maliasilini mhusika pia kuhusu masuala ya misitu, kwahiyo, tutashirikiana naye kuhakikisha kwamba tunafanyahivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kikubwa zaidi kuhusu misitu,siyo kupanda miti mipya, ni kutokata iliyopo. Katika miti yoteiliyopo Tanzania, 95% ni ile il iyokuwepo, 5% tu ndiyoiliyopandwa. Kwa hiyo, ili ufanikiwe zaidi kwenye hili jambo,usikate miti, bali uhifadhi ile ambayo haijakatwa na hiyoitatusaidia tutakapowezesha watu kutotegemea miti zaidikatika maisha yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sanaMheshimiwa Kamala kwa hoja nzuri alizoziwasilisha za sababuya kuunga mkono. Tunakushukuru na tunakubali kwamba sisikuridhia haya makubaliano kutatusaidia kuweza kupata fursa.Zaidi tunafurahi kwamba yeye kama Mbunge, anaona hajaya Serikali kuwa na rasilimali nyingi zaidi na Bunge mna wajibupia wa kupanga fedha kwa ajili ya hifadhi ya mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa fedha kwa ajili yahifadhi ya mazingira haziko kwenye bajeti peke yake, zikonamna nyingi ikiwemo Mfuko wa Taifa wa Dhamana yaMazingira ambapo kwenye sheria ile unategemea moja yavyanzo vilivyoandikwa vya Mfuko, nacho ni subventionappropriation kutoka kwenye Bunge, ukiondoa kwenyebajeti. Kwa hiyo, Bunge lina uwezo wa kuamua lenyewekwamba licha tu ya bajeti ya Serikali kwa Ofisi ya Makamuwa Rais, pia tunaweza kabisa kupangia Mfuko wa Mazingirakiasi fulani cha fedha na Mfuko huu utakapopata fedha hizo,basi utatuwezesha kufanya kazi zetu vizuri.

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

140

Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge,kwa hiyo, nadhani nimeweza kuzungumza yoteyaliyozungumzwa, lakini niseme tu kwamba, ushauriuliotolewa tutauzingatia. Tunaomba sasa utusaidie namnaya kwenda kwamba, tunatoa hoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima na taadhima,naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, Naafiki.

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono WaheshimiwaWabunge. Sasa tutaendelea na utaratibu wetu, nitawahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini yaMkataba wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mabadiliko ya

Tabianchi (The Paris Agreement Under the UNFramework Convention on Climate Change)

lilipitishwa na Bunge)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, walioafikiwameshinda. Kwa hiyo, Bunge siku ya leo limepitisha Azimiola Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris Chini ya Mkatabawa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (TheParis Agreement Under the UN Framework Convention onClimate Change).

Kwa hiyo, nachukua fursa hii kumpongezaMheshimiwa Waziri pamoja na timu yake yote kuwezakufanyia kazi Makubaliano haya na mpaka Bunge kuwezakupitisha Azimio. Tuwatakie kila la heri katika utekelezaji wamambo ambayo ni mazuri sana mliyotueleza kuhusu Azimiohili na umuhimu wake. Nasi tunaamini kwamba Serikalimtalitendea haki ikiwa ni pamoja na kutekeleza yale yoteambayo yamewekwa kwenye Azimio hil i ambalolimepitishwa na Bunge leo.

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

141

Waheshimiwa Wabunge, kwa ajil i ya kuwekakumbukumbu sawasawa; na kwa kuwa, hili jambo huwalinajitokeza kila wakati, nalazimika kutoa maelezo kidogokuhusu namna Bunge linavyofanya kazi. Kwa sababutunaelekea kwenye Bunge la Bajeti, ili Wabunge twende wotekwa uelewa mmoja ni vizuri haya maelezo ambayo yakokwenye kanuni zetu, wote tukayaelewa.

Waheshimiwa Wabunge Kanuni ya 118 inaelezakwamba kutakuwa na Kamati za Kudumu za Bunge kamazilivyoainishwa kwenye Nyongeza ya Nane ya Kanuni hizi.Ukienda kwenye Nyongeza ya Nane inazitaja Kamati zoteza Kudumu za Bunge tulizonazo. Pia inataja majukumu ya kilaKamati na Wizara ambazo Kamati zinasimamia.

Sasa Kamati hizi zimeundwa na WaheshimiwaWabunge, ndio wanaokaa kule. Wanapokuwa wanafanyakazi, wao wana muda mrefu zaidi wa kushughulika namambo ambayo yanapelekwa kwao na Wizara husika. Kwahiyo, yanapoletwa hapa ndani ni kwamba WaheshimiwaWabunge wameshafanya kazi kwenye Kamati zao. (Makofi)

Kwa hiyo, Kamati inapoleta maoni hapa, amamapendekezo, ni kwa ajili ya kututaarifu sisi ambao siosehemu ya Kamati i le tuweze sasa kuwaelewa waowamewaelewaje hao watu wa Serikali? Kama wamekataa,watatueleza kwamba jambo hilo sisi kama Kamatitunalikataa. Ama kama wamekubali, Kamati itatueleza sisiBunge zima kama wamekubali na sababu zao. Ndiyo maanani lazima Serikali ikishasema jambo lake, Kamati inakujakusema kwa niaba ya Bunge. Hapa tunaletewa kwa ajili yakufanya maamuzi. Ndiyo kanuni zetu zinavyosema. Kazi zetukubwa zinafanyika kwenye ngazi ya Kamati. (Makofi)

Kwa hiyo, isitokee mazingira yale ambayoWaheshimiwa Wabunge tunaona kwamba, tunapokaa hapandani mambo yanayoletwa na Serikali baadaye Kamatiinaleta mapendekezo yake na baadaye Kambi Rasmi yaUpinzani inapewa fursa ya kuzungumza, ni kwa sababuwamepata muda wa kutosha wa kuyapitia mambo haya.

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

142

Ninyi ni mashahidi, pale ambapo Kamati inakuwahaijakamilisha kazi zake, maana yake ni Bunge halijakamilishakazi, kwa hiyo, Mheshimiwa Spika hapangi shughuli hiyokuingia humu ndani kama Kamati haijamaliza kazi yake. Kwahiyo, inapokuja hapa ndani, hakuna muda ambaoMheshimiwa Spika analazimika kwamba jambo hili ni lazimalifanywe kwa muda fulani ili Waheshimiwa Wabunge 393tulioko humu ndani wote tupate nafasi ya kuzungumza.

Kwa hiyo, utendaji wetu wa kazi uko kikanuni; na kwahiyo, mambo yote yanayofanywa na Kamati yanafanywakwa niaba ya Bunge na kwa hiyo, ufafanuzi wote unaotolewana Kamati hapa mbele ni kwa niaba ya Bunge. Hapa ndanini kwa ajili kufanyia maamuzi yale ambayo wenzetuwameshayajadili kwenye ngazi ya Kamati. (Makofi)

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge, ukisoma hiiNyongeza ya Nane, hasa fasili ya (7) katika hiyo nyongeza,inasema hivi; “Majukumu ya Kamati za Kudumu za Bunge zaKisekta yatakuwa yafuatayo:-

“(a) Kushughulikia bajeti ya Wizarainazozisimamia.”

Maana yake bajeti inaenda kwenye Kamati.Inapoletwa hapa, Kamati inapata nafasi ya kutueleza,wamesikia nini kule? Ndio utendaji tuliokubaliana nao. Siyokwamba inapokuja hapa Bungeni ndiyo tunaanzakushughulikia moja, kwa sababu Wizara inakuwa ilishapelekakwenye Kamati. Pia, hata kwenye hil i, kwa mfanotunalishughulikia leo, (b) inasema, “Kushughulikia Miswadaya Sheria na mikataba inayopendekezwa kuridhiwa naBunge iliyo chini ya Wizara inazozisimamia.”

Kamati yetu ya Bunge ya Viwanda, Biashara naMazingira ndiyo inayosimamia Wizara hii ya Mazingira naMuungano. Kwa hiyo, inavyoleta maoni hapa ndani nikwamba Bunge limeshafanya kazi kule kwenye ngazi yaKamati. Kwa hiyo, inatuletea hapa ili sisi tujue na tufanyemaamuzi juu ya yale ambayo Kamati inapendekeza. Yako

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1523461271-3 APRILI 2018.pdf · Azimio la Bunge la Kuridhia Makubaliano ya Paris chini

3 APRILI, 2018

143

mambo mengi, Waheshimiwa Wabunge, niwashauri tuzipitiehizi kanuni vizuri ili sisi wenyewe tuwe tunaridhika na kazitunayoifanya, lakini pia, tujue mipaka yetu na majukumu yetuyanaenda mpaka wapi?

Waheshimiwa Wabunge, pia mnaruhusiwa kikanuni,kwenda kwenye Kamati yoyote unayoona wewe inajadilijambo ambalo unataka kulifahamu zaidi ama ungependakushiriki zaidi. Hakuna kanuni inayokukataza, isipokuwahutaruhusiwa kupiga kura.

Kwa hiyo, tunapoenda kwenye bajeti za hizi Wizara,usije ukaona mtu kwamba, Wizara fulani bajeti yake hapaimepangiwa siku moja ukaona ni muda mfupi; hakuna mudamfupi kwa sababu, Kamati uliyoichagua wewe ndiyoambayo imefanya kazi hiyo.

Ninavyosema umeichagua wewe, ni kwa sababu sisiwote tumekasimu mamlaka hayo kwa Mheshimiwa Spika,aliyempangia Kamati hiyo, anajua atafanya kazi nzuri kwenyelile eneo. Kwa hiyo, tunavyoletewa hapa ndani, tukipangiwasiku moja, tukipangiwa siku mbili ni kwamba kwa tathminiimeonekana Kamati hiyo imefanya hiyo kazi na siku moja hiyoinawatosha kutueleza yale ambayo wameyapitia. (Makofi)

Kwa hiyo, kwa sababu, huwa linajitokeza tokeza,naamini kwamba hata Waheshimiwa Wabunge ambaohawako pamoja nasi hapa, watapata haya maelezo ili mtuanaposimama aendelee na mchango wake kulikokulalamikia muda maana Kamati, Wabunge wale wanakuwawamefanya kazi kama Mbunge mwingine aliye kwenyeKamati nyingine. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,naahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho, tarehe 4 Aprili,2018, saa 3.00 asubuhi.

(Saa 7.15 Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Jumatano,Tarehe 4 Aprili, 2018, Saa Tatu Asubuhi)