utungaji/uandishi - kiswahili 1...mwalimu nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni...
Post on 08-Nov-2020
40 Views
Preview:
TRANSCRIPT
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1
UTUNGAJI/UANDISHI Utungaji ni neno linalotokana na kitenzi “tunga”. Kitenzi hiki kwa mujibu wa
Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2004:414) linamaanisha “toa mawazo kutoka
ubongoni na kuyakusanya, kisha kuyadhihirisha kwa maandishi, kwa kusimulia,
kwa kuyaimba au kwa muziki.
Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa, utungaji ni kutoa mawazo binafsi kutoka akilini
mwa mtu kuhusiana na mambo mbalimbali katika jamii, kisha kuyaweka wazi kwa
njia ya mdomo au maandishi.Kile kilichotungwa na mtunzi kinaweza
kudhihirishwa kwa mitindo mbalimbali, kama vile riwaya, mashairi, tamthiliya,
insha na barua.
Dhima ya Utungaji
Utungaji huwezesha watu kutoa maelezo, mawazo au maoni kwa njia ya
maandishi au mazungumzo.
Utungaji huwezesha utumiaji wa lugha fasaha, sanifu na uwezo wa kujieleza
kwa njia ya maandishi au mazungumzo.
Utungaji huwezesha utumiaji wa mantiki, mpangilio mzuri wa mawazo,
mtiririko na matumizi sahihi na fasaha ya lugha na kanuni za fasihi.
Utungaji huwezesha kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu maisha yetu ya
kila siku. Kupitia njia ya utungaji, watu hupata taarifa kuhusu vitu
mbalimbali vinavyozunguka maisha yao ya kila siku.
Utungaji hutumika kuelimisha, kukosoa na hata kuonya. Maandishi au
mazungumzo (masimulizi) yanayotokana na utungaji huweza kuakisi hali
halisi ya maisha ya jamii, na hivyo ikawa ni kama kioo cha kujitazama na
kujirekebisha.
Utungaji, hususan unaotokana na kazi za fasihi hutumika kuburudisha
jamii. Hadithi na tanzu nyingine za fasihi zinazotokana na utungaji
huburudisha, huliwaza na kufurahisha jamii.
Utungaji hutumika kukuza lugha kwa njia ya mazungumzo au maandishi.
Mzungumzaji na msikilizaji hupata ufundi wa kujieleza zaidi kupitia
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 2
utungaji, hali kadhalika mwandishi na msomaji hupata ufundi wa kujieleza
zaidi kupitia njia ya utungaji.
Kanuni za Utungaji bora
Utungaji bora ni lazima uzingatie kanuni zifuatazo:
Matumizi mazuri ya nyakati: mfano, wakati uliopo, ujao na uliopita au hali
timilifu.
Matumizi mazuri ya lugha fasaha (lugha inayoeleweka).
Mpangilio mzuri wa mawazo na mantiki, yaani kutochanganya mawazo,
kutorudiarudia mawazo au kutosahau mawazo.
Matumizi bora ya vituo na alama za uandishi.
Matumizi bora ya sarufi ya lugha inayohusika.
Utungaji bora hugawanyika katika sehemu kuu zinazobainisha muundo wa
kazi yenyewe mf. Insha hugawanyika sehemu nne ambazo ni: Kichwa cha
insha, Utangulizi, Kiini na Hitimisho
Utungaji bora huwa na mifano ya kutosha.
Uandishi wa Insha
Insha ni utungo wenye sentensi nyingi zilizopangwa katika aya, zenye
kuzungumzia mada moja. Kwa mfano, insha zinaweza kuwa zinazungumzia
mada zifuatazo: Umuhimu wa Chakula Bora, Tiba Kutokana na Vyakula;
Ujamaa ni Imani au Jamii Inakwenda Kombo.
Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa Insha.
Bila kujali aina ya insha inayoandikwa, yapo mambo kadhaa ya kuzingatia
wakatiwa kuandika insha. Mambo hayo ni pamoja na:
(a) Kubaini mada ya kuandikia insha na kuielewa vyema.
(b) Kupanga mawazo katika mtiririko wenye mantiki
(c) Kutumia mtindo unaoendana na kusudi la insha. Kwa mfano, mtindo wa
masimulizi, unafaa kwa hadithi au insha zingine za kisanaa.
(d) Kutumia lugha fasaha na inayoeleweka
(e) Kufuata kanuni za uandishi. Kwa mfano, matumizi ya alama za uandishi,
aya, herufi kubwa na ndogo, n.k
(f) Kupanga insha katika muundo wake, yaani kichwa, utangulizi, kiini na
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 3
hitimisho.
Muundo Wa Insha Insha hugawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni:
Kichwa cha Insha
Kichwa cha insha huandikwa kwa herufi kubwa, katikati, juu ya
insha. Hakipaswi kuzidi maneno matano na hupigiwa mstari.
Utangulizi (Mwanzo)
Katika sehemu hii inampasa mwandishi atoe maelezo mafupi na
maana ya habari aliyopewa.
Kiini cha insha (Kati)
Inamlazimu mwandishi afafanue kwa mapana mada
anayoishughulikia huku akitoa mifano hai inayoendana na hali halisi.
Hitimisho (Mwisho)
Inampasa mwandishi kutoa mapendekezo (maoni) ya msingi au
kusisitiza kwa ufupi yale aliyoyaelezea katika habari yenyewe.
NB: Hitimisho sio ufupisho wa hoja zilizojadiliwa katika sehemu ya insha
yenyewe.
Aina za Insha Aina ya insha au jina la insha hujulikana kutokana na mawazo ya
mwandishi. Kuna aina nyingi za insha lakini tunaweza kuziweka aina hizo
katika makundi makuu mawili ya insha za hoja na insha za wasifu. Kila
kundi kati ya makundi haya mawili kuna insha za kisanaa na insha zisizo za
kisanaa.
Zingatia kielelezo kifuatacho
Insha za Kisanaa
Hoja
Insha zisizo za Kisanaa
Insha Insha za Kisanaa
Wasifu
Insha zisizo za Kisanaa
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 4
Insha za kisanaa hutumia vipengele mbalimbali vya fasihi katika kuwasilisha
ujumbe - mfano nahau, methali, ,misemo au tamathali za semi huweza
kutumika. Insha zisizo za kisanaa hazitumii lugha ya kifasihi katika
kufikisha ujumbe.
Insha za wasifu huelezea sifa (uzuri au ubaya) za kitu, hali au mtu fulani.
Insha za hoja ni insha ambazo hutetea mawazo ya aina fulani na kupinga
mengine kwa uthibitisho uliodhahiri. Mfano wa insha za wasifu ni Uzuri wa
bahari ya Hindi, Fahari ya Mlima Kilimanjaro, n.k. mfano wa insha za hoja
ni: Ukimwi ni Ugonjwa Hatari, Uhuru wa Bendera, n.k.
Mfano wa Insha ya Wasifu
Atukuzwe Nyerere wa Tanzania
Nyerere wa Tanzania, kiongozi shujaa wa dunia – amepata kutukuka pande zote za
dunia. Alizaliwa katika kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani
Mara. Alisoma elimu ya msingi katika shule ya Mwisenge – mojawapo ya shule za
zamani sana hapa nchini. Alipata elimu ya sekondari huko Tabora. Alijiunga na
Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda kabla ya kwenda huko Uingereza
kusomea shahada ya M.A.
Baada ya uhuru toka Uingereza, Mwalimu Nyerere alishughulika sana na suala la
ukombozi wa Tanganyika na Afrika kwa ujumla. Alionesha jitihada za wazi
kupambana na mabeberu wa Kiingereza hadi uhuru wa Tanganyika ukapatikana
tarehe 9/12/1961. Tanganyika ikawa ya kwanza kupata uhuru wake ukilinganisha
na nchi zote za Afrika ya Mashariki na kati – sifa kuu kwa Nyerere wa
Tanganyika.
Nyerere alishirikiana na Karume kuziunganisha nchi hizo na kuzaa Tanzania – jina
lililotumika na kuheshimiwa kote ulimwenguni. Wakati Nyerere akichanganya
udongo wa Tanganyika na Zanzibar alitamka maneno ya hekima yafuatayo:
“Tumeamua kuziunganisha nchi zetu ili kuimarisha umoja wa Afrika. Naamini
kuwa maadui wetu watachukia na kuhuzunika kwa kitendo hiki cha kishujaa
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 5
tulichokifanya, lakini daima hatutaogopa chochote. Muungano wetu utadumu
milele na milele. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika. Amina!”
Sifa ya pekee inayomtofautisha Mwalimu Nyerere unapomlinganisha na
wanafalsafa wengine duniani kama vile Karl Marx na Mao ni kwamba yeye
aliwapigania wanyonge wote kote ulimwenguni bila kujali ubaguzi wa rangi,
kabila, taifa au bara. Aliwatetea wanyonge wa Afrika. Aliwapigania wanyonge wa
Ulaya na Mashariki. Aliwapigania wanyonge wa bara la Asia. Hali kadhalika
aliwapigania na kuwatetea wanyonge wa bara la Amerika ya Kusini. Hivyo ni sifa
ya pekee inayofaa kumtofautisha na wanafalsafa wengine waliomtangulia.
Nyerere atatukuzwa daima kwa ushujaa wake. Alikuwa si kiongozi wa
kujikombakomba kwa mataifa mengine ya kibeberu. Alipotishiwa au kuwekewa
vikwazo/vitisho, alivunja mara moja uhusiano wa kidiplomasia na taifa
linalohusika. Kwa mfano mwaka 1965 alivunja uhusiano wa kidiplomasia na nchi
ya Uingereza baada ya nchi hiyo kuitangaza nchi ya Zimbabwe kama koloni lake
la kudumu la Walowezi. Kitendo hiki kilimpatia sifa na heshima kubwa hapa
Afrika na duniani kote – kwa wapenda amani.
Ingawa ni vigumu kuzitaja sifa zake mpaka mwisho, lakini sifa ya kupiga makelele
katika majukwaa ya kimataifa haitaweza kusahaulika. Hakuwa msomi mkimya
kama wasomi wa enzi hizi. Alitumia elimu yake ipasavyo kuitetea falsafa yake ya
Haki na Usawa kwa Binadamu Wote katika majukwaa ya kimataifa.
Wananchi wa Uganda daima humkumbuka na kumtukuza kwa jinsi alivyotumia
nguvu za kijeshi kuung‟oa utawala wa kidikteta wa Nduli Idd Amini Dada.
Wakikumbuka mateso waliyoyapata enzi za utawala huo, humtukuza na kumuenzi
Nyerere usiku na mchana.
Nyerere hataweza kusahaulika kwa jinsi alivyopinga kitendo cha viongozi
wachache wenye hila kuendelea kung‟ang‟ania kwenye madaraka. Alikuwa
kiongozi wa kwanza hapa Afrika na pengine duniani kote kung‟atuka kwenye kiti
cha Urais. Alifanya hivyo kwa hiyari ili kutoa nafasi kwa wananchi wengine
washike wadhifa huu nyeti hapa nchini kwetu.
Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa
letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa hekima na
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 6
busara. Kinywa chake daima kilinena maneno ya hekima na busara. Fikra zake
zitadumu milele kwenye vichwa vya wakulima, wasomi, wanafalsafa, mapadri,
masheikh, wachungaji, watawa na hata kwenye bongo za waovu wa Tanzania
daima watamkumbuka.
Kifo cha Mwalimu Nyerere kimeleta pengo kubwa kwa jamii yote ya wapenda
amani kote ulimwenguni. Ingekuwa mbegu ya mmea tungeipanda sote tuendelee
kuhekimika kutokana na hekima na busara zake.
Kifo cha Mwalimu Nyerere ni kama mwindaji asiye na silaha kwenye mwitu wenye
wanyama wakali kama fisi, simba, ngiri, tembo, nyoka, nyati, n.k. Je, mwindaji
atafanya nini?
Daima sifa na hekima za Mwalimu Nyerere zitukuzwe Tanzania, Afrika na
ulimwenguni kote.
Mfano wa insha ya hoja
Kijana wa leo nina balaa!!
Kilio, kilio, kilio kwa kijana wa leo, Afrika! Wakati vijana wengine wanapoombwa
kujiunga na jeshi ili kujenga na kulinda nchi yao, siyo kwangu. Kwangu
naburutwa msituni, kujiunga na jeshi kuendeleza vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Napigana na ndugu zangu ndani ya taifa moja ili matumbo machache yafaidi
almasi, dhahabu, mafuta na maliasili nyingine. Naingizwa katika vita isiyo na
maana yoyote kwangu.
Nikitaka kutafuta elimu, hakuna madarasa. Upepo umeezua paa la nyasi la shule
yetu! Nikibahatika kupata kaelimu kadogo; chini ya mti, nazuiwa kufikiri zaidi.
Naambiwa kuwa, Afrika hakuna kufikiri! Mtu mweusi hana fikra ila mtu mweupe
ndiye mwenye fikra. Natakiwa nifuate fikra zake!
Nikitaka ajira, naambiwa uzoefu miaka mitano au kumi na zaidi. Uzoefu nitaupata
wapi? Nikitamani kujiajiri mazingira hayaniruhusu: Umasikini, umasikini tena
umasikini umenikumbatia!
Nikijiunga na siasa, wimbo maarufu kote ulimwenguni ni demokrasia. Demokrasia
ina mizengwe, umajimbo, ukabila, udini, ubabe, rushwa, ubabaishaji, utapeli na
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 7
kushindana bila kukubali kushindwa. Siasa barani kwetu ni kiini macho na
matokeo yake ni „demoghasia‟ isababishayo vifo. Ubinafsi umejaa! Kujipitishia
marupurupu kibao! Ubaguzi! Majigambo! Dharau…..!
Nikitaka kusema, naambiwa mjinga, Nikidai haki, naambiwa madai yangu ni ya
kijinga. Nalazimishwa kuandika barua ya kuomba msamaha na kuahidi kuwa
sitadai haki tena! Nalazimishwa kuwa bubu. Kijana msomi nanyimwa uhuru wa
kutoa mawazo yangu mbele ya jumuiya yangu. Kijana msomi nafungwa mdomo.
Kijana msomi kukaa na kunyamaza kimya ni usaliti. Usaliti kwa jamii ya walipa
kodi ambao pesa zao zimenisomesha hadi kuitwa msomi. Kijana msomi, kutofikiri
ni dhambi nyekundu pyuuu!- isiyosameheka. Msomi kutofikiri ni kifo cha kifikra
kwangu mimi kijana wa Kiafrika.
Chochote ninachotaka kufanya kinanikatisha tamaa. Nikiwa „deiwaka‟ mpiga
debe, kila siku nitaamkia korokoroni! Nikitaka kujiburudisha na gongo au viroba -
ni kifo cha ajabu. Nikibugia unga – kwangu ni kifo cha mende wekundu!
Nikijiingiza kwenye ukahaba, natozwa kodi ya maendeleo! Nikitaka kuwa
“changudoa”, UKIMWI unaniwinda kama mamba awindavyo viumbe baharini!
Sasa nifanye nini? Balaa kubwa kwangu!
Nikiamua kuokoka, wokovu hauonekani. Nimebaki njia panda. Mchungaji
amekuwa mwongo, katu hasemi ukweli. Ananilaghai kuwa wokovu upo karibu
kuingia badala ya kuniambia kweli wokovu umekwishatoweka. Naambiwa kuwa
nijiwekee hazina mbinguni ambako kutu na wadudu hawataharibu mali
yangu…Huu ni utapeli.
Ingekuwa vizuri kama ningeelezwa wazi jiwekee akiba tumboni mwa sheikh au
tumboni mwa mchungaji au tumboni mwa padre! Naambiwa kuwa toeni
ulichonacho utabarikiwa badala ya kuambiwa kuwa kitayabariki matumbo ya
wachache!
Nakumbuka wakati mama yangu alipokuwa mwalimu katika shule ya msingi ya
Mabonde Kuinama, aliniambia kwamba, urithi wa utamaduni wetu ni mila na
desturi za Afrika. Lakini siku hizi sivyo. Siku hizi naambiwa kuwa urithi wa kizazi
kipya ni bia aina ya “Safari Larger”.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 8
Kijana wa sasa naangalia wizi wanaofanyiwa watu maskini lakini sisemi chochote.
Najinyamazia kimya. Wizi umo makanisani, misikitini, Ikulu, mahakamani na hata
bungeni. Lengo ni kuwanyanyasa, kuwadhulumu, kuwaonea, kuwanyonya na
kuwadhalilisha wanyonge. Hakika kunyamaza kwangu ni usaliti. Nimeitambua
nafasi yangu. Naahidi kupambana hadi kufa na kupona.
Uandishi wa barua na kadi za mialiko
Kuna aina mbalimbali za barua. Aina hizo hugawanywa katika makundi
makuu mawili ambayo ni Barua za kirafiki/kindugu na Barua rasmi.
(a) Barua za Kirafiki/Kindugu
Hizi ni barua zinazoandikwa kwenda kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa
madhumuni mbalimbali kama vile:
- Kusalimiana
- Kujulishana maisha yetu ya kila siku
- Kuomba msaada au kutoa shukrani kwa kutimiziwa maombi yetu.
- Kutoa hongera, rambirambi, pongezi, n.k.
Sehemu za Barua za Kirafiki/Kindugu
Anuani ya Mwandishi
Huandikwa kwenye pembe ya kulia ya karatasi. Anuani hii ndiyo
hutumiwa na mwandikiwa wakati wa kujibu barua aliyoipokea na pia
hutambulisha maskani ya mwandishi wa barua kwa wakati huo. Kwa
hiyo, ni wajibu wa mwandishi kuandika anuani yake vizuri. Ni lazima
iandikwe waziwazi.
Tarehe
Hii huandikwa mara baada ya anuani ya mwandishi. Huandikwa ili
kumjulisha mwandikiwa barua imeandikwa lini na kama imefika kwa
wakati au imechelewa. Zipo njia mbalimbali za kuandika tarehe, nazo ni:
- 20.9.2017
- 20/9/2017
- 20-9-2017
- 20 Septemba, 2017
- Septemba 20, 2017
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 9
Mwanzo wa barua
Barua za kirafiki/kindugu huanza kama ifuatavyo:
- Baba mpendwa,
- Mpendwa baba,
- Mwanangu mpendwa,
- Mama mpenzi, n.k.
Barua yenyewe
Hii ni sehemu muhimu sana. Sehemu hii ndiyo inayomfanya
mwandikiwa aelewe kusudi la mwandishi. Sehemu hii iandikwe vizuri ili
barua ieleweke kwa urahisi.
Mwisho wa barua
Mwisho wa barua ni sehemu inayostahili kuandikwa vizuri. Njia
zifuatazo ni baadhi ya zile zitumikazo kumalizia barua ya kindugu.
- Mwanao akupendaye.
- Wako wa moyoni.
- Rafiki yako akupendaye.
- Wako akupendaye.
- Wasalaam, baba yako, n.k.
Jina la Mwandishi
Ni vizuri kuandika jina lako mwishoni mwa barua ili yule
unayempelekea afahamu barua imetoka kwa nani.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 10
Mfano wa barua ya kirafiki
Shule ya Sekondari Mbezi Beach,
S.L.P 60213,
Dar Es Salaam.
03/07/2017.
Mpendwa,
Salaam sana. Natumai u mzima pamoja na jamaa na marafiki wa hapo
nyumbani. Nami ni mzima na ninaendelea na masomo yangu vizuri hapa
shuleni. Napenda kukujulisha kuwa maendeleo yangu kimasomo hapa
shuleni ni mazuri sana. Katika mtihani wa kumaliza mwaka wa pili
nimeshika nafasi ya pili kati ya wanafunzi 195 wa kidato cha tano.
Nimeamua kusomea mchepuo wa biashara ili hatimaye niwe mchumi wa
nchi yetu hivyo naomba tuzidi kuombeana heri.
Pamoja na mafanikio hayo yote, kuna tatizo kubwa sana ambalo linazidi
kuniandama hapa shuleni. Tatizo hili linanikosesha kabisa raha, kila
wakati huwa ninahuzunika. Tatizo hili huwa ni la umasikini. Sina hata
shilingi tano ya kununulia kipande cha muhogo. Hivyo, naomba uuze
yule jogoo mkubwa unitumie pesa haraka iwezekanavyo.
Wasalimie wote wanaonifahamu hapo kijijini. Msalimie sana shangazi
wangu Lilian Joackim.
Wako akupendaye,
Haidari Hamisi.
(b) Barua Rasmi
Kwa kawaida barua rasmi huandikwa kwa makusudi mbalimbali kama
vile, kutoa taarifa za tukio fulani, kuomba kazi, kuagiza vifaa au vitu,
kumwalika kiongozi katika shughuli maalumu, kutoa taarifa ya
kushindwa kufika mkutanoni, n.k.
Barua rasmi zipo za aina nyingi, lakini zinaweza kugawanywa katika
makundi matatu makubwa yafuatayo:
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 11
- Barua za kuomba kazi
- Barua za kutoa taarifa
- Barua za kuagiza au kupokea bidhaa/vitu.
Sehemu za barua rasmi
(i) Anuani ya mwandishi
Anuani hii huandikwa pembe ya juu kulia ili kutambulisha maskani ya
mwandishi na pia hutumiwa na mwandikiwa wakati wa kuijibu barua husika
inapobidi.
(ii) Tarehe
Huandikwa chini ya anuani ya mwandishi ili kumjulisha mwandikiwa kama
barua hiyo imefika mapema au imechelewa.
(iii) Kumbukumbu namba
Barua rasmi huwa na kumbukumbu namba. Huu ni utambulisho maalumu
wa barua husika. Kumbukumbu namba aghalabu huwa ni kifupi cha jina la
taasisi inakotoka barua hiyo, kule inakokwenda, hiyo ni barua ya ngapi na
mwaka husika. Mf: Mbss/crdb/02/17
(iv) Anuani ya mwandikiwa
Anuani hii hutanguliwa na cheo cha mwandikiwa na huwekwa upande wa
kushoto chini ya kumbukumbu namba. Nafasi ya mstari mmoja au zaidi
huweza kurukwa baina ya kumbukumbu namba na anuani ya mwandikiwa.
(v) Mwanzo wa barua
Sehemu hii huandikwa chini ya anuani ya mwandikiwa. Ni heshima kutaja
cheo cha mwandikiwa mwanzoni mwa barua ya namna hii, kwa mfano
Ndugu Katibu, Ndugu Ofisa Mifugo, n.k.
(vi) Kichwa cha barua
Kichwa cha barua hutaja kwa ufupi jambo linalohusu barua hiyo. Kichwa
cha barua huandikwa waziwazi katikati ya barua mara baada ya mwanzo wa
barua. Ni muhimu kiwe kifupi na chenye kueleweka waziwazi. Hufaa zaidi
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 12
kikiandikwa kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari. Hakipaswi kuzidi
maneno matano.
(vii) Barua yenyewe
Sehemu hii huandikwa mambo yote muhimu kuhusu barua yenyewe. Barua
yenyewe iwe fupi na yenye taarifa za lazima tu. Uanzaji wa barua yenyewe
umrejeshe msomaji kwenye mada ili kufupisha maelezo mengi kama vile
kwa kusema:
- Mada tajwa hapo juu inahusika
- Rejea barua yako ya tarehe…..yenye Kumb. Na….
- Husiana na mada tajwa hapo juu, n.k.
(viii) Mwisho wa barua
Mwisho wa barua huwa ni tamko la heshima la kumalizia barua. Mara
nyingi mwisho unaotumika katika barua rasmi ni kama vile:
- Wako mtiifu,
- Wako katika ujenzi wa taifa,
- Wako katika kazi, n.k.
(ix) Saini na jina la mwandishi
Mwisho wa barua mwandishi hupaswa kutia saini na jina lake kama
utambulisho wake juu ya kilichoandikwa. Saini hupaswa kutiwa kwa
mkono.
(x) Cheo cha mwandishi
Baada ya jina mwandishi hupaswa kuandika cheo chake. Cheo kinaweza
kuwa:
- Mwanakijiji
- Muombaji
- Mwalimu Mkuu
- Afisa Mtendaji, n.k
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 13
Aina za Barua Rasmi
1. Barua ya Kuomba Kazi
Barua ya kuomba kazi inahitaji uangalifu sana katika sehemu ya barua
yenyewe. Barua hii inatakiwa iandikwe kwa umakini na ujuzi mwingi.
Katika barua hii kuna mambo makuu manne ambayo ni: kutaja kazi
unayoomba, jinsi ulivyopata taarifa, elimu, ujuzi na uzoefu, maelezo binafsi
na wadhamini.
Mfano wa barua ya kuomba kazi:
Kijiji cha Mto wa Mbu,
S.L.P 4507,
Arusha.
04/7/2017
Meneja wa Kiwanda,
Kiwanda cha Kusindika Matunda,
S.L.P 0717,
Iringa.
Ndugu,
YAH : OMBI LA KAZI YA UKARANI
Husika na kichwa tajwa hapo juu. Ninayo heshima kuomba kazi ya ukarani katika
kiwanda chako kama ilivyotangazwa kupitia gazeti la “Sanifu” Uk. 3 la tarehe
20/6/2017.
Mimi nilisoma katika kituo cha Elimu ya Watu Wazima huko Mufindi. Baadaye
nilijiunga na masomo kwa njia ya posta na kuhitimu kwa ufaulu wa masomo ya
Kiswahili, Siasa na Kiingereza.
Nina umri wa miaka 45, nimeoa na nina watoto wanne. Mimi ni mwanakijiji wa
kijiji cha Magadini. Napendelea michezo na kazi za mikono. Ninaweza kusoma na
kuandika vizuri na ninayo hati nzuri.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 14
Mwalimu Mkuu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima cha Mufindi na msimamizi
wa masomo kwa njia ya posta anaweza kutoa taarifa zaidi juu ya uwezo wangu.
Nitashukuru sana iwapo ombi langu litafikiriwa na kupokelewa vema.
Wako mtiifu,
(Saini)
Matatizo Hayaishi
Mwombaji
Barua ya kupitia kwa:
Iwapo barua itapaswa kupitishwa na mtu zaidi ya mmoja kutokana na mamlaka za
kiutawala na utambuzi mwandishi atapaswa kuandika anuani za wale wanaopaswa
kuiona barua hiyo kwa kuanza na anuani ya yule atakayeiona mwisho.
Mfano:
Kijiji cha Mto wa Mbu,
S.L.P 4507,
Arusha.
04/7/2017
Meneja wa Kiwanda,
Kiwanda cha Kusindika Matunda,
S.L.P 0717,
Iringa.
K.K
Afisa Rasilimali Watu,
Kiwanda cha Kusindika Matunda,
S.L.P 0717
Iringa Ndugu,
YAH : OMBI LA KAZI YA UKARANI
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 15
Husika na kichwa tajwa hapo juu. Ninayo heshima kuomba kazi ya ukarani katika kiwanda
chako kama ilivyotangazwa kupitia gazeti la “Sanifu” Uk. 3 la tarehe 20/6/2017.
Mimi nilisoma katika kituo cha Elimu ya Watu Wazima huko Mufindi. Baadaye nilijiunga na
masomo kwa njia ya posta na kuhitimu kwa ufaulu wa masomo ya Kiswahili, Siasa na
Kiingereza.
Nina umri wa miaka 45, nimeoa na nina watoto wanne. Mimi ni mwanakijiji wa kijiji cha
Magadini. Napendelea michezo na kazi za mikono. Ninaweza kusoma na kuandika vizuri na
ninayo hati nzuri.
Mwalimu Mkuu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima cha Mufindi na msimamizi wa masomo
kwa njia ya posta anaweza kutoa taarifa zaidi juu ya uwezo wangu.
Nitashukuru sana iwapo ombi langu litafikiriwa na kupokelewa vema.
Wako mtiifu,
(Saini)
Matatizo Hayaishi
Mwombaji
2. Barua ya kutoa taarifa
Barua hizi huandikwa kwa lengo la kutoa taarifa juu ya jambo, tukio au mtu.
Taarifa huweza kutolewa kwenye taasisi fulani kama kituo cha polisi au ofisi
yoyote ya umma.
Mfano wa barua ya kutoa taarifa
Kijiji cha Jangwani,
S.L.P 1045,
Mto wa Mbu
10/7/2017.
Bwananyama wa Wilaya,
Wilaya ya Monduli,
S.L.P 1045,
Arusha.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 16
Ndugu,
YAH: TATIZO LA SIMBA KIJIJINI
Husika na mada tajwa hapo juu. Ninasikitika kukutaarifu kuwa, hapa kijijini kwetu
amezuka simba anayewinda watu. Ni simba jike na watoto watatu na ameonekana
mara tatu hapa kijijini.
Simba huyo huingia hapa kijijini kutoka katika msitu wa hifadhi ya taifa ambapo si
ruhusa kuweka mitego.
Nashukuru ikiwa utatushauri haraka jambo la kufanya mara upatapo barua hii.
Wako katika kazi,
(Saini)
Rogathe Kimario
Mtendaji wa Kijiji
3. Barua ya Mwaliko
Barua za aina hii huandikwa kwa viongozi mbalimbali kwa lengo la
kuwaalika katika shughuli mbalimbali kama mahafali, uzinduzi, ufunguzi,
n.k
Mfano wa barua ya mwaliko
Shule ya Sekondari Manyara,
S.L.P 46,
Arusha.
15/7/2017.
Mkuu wa Wilaya,
Wilaya ya Monduli,
S.L.P 12,
Arusha.
Ndugu,
YAH: MWALIKO WA KUKABIDHI VYETI
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 17
Husika na kichwa cha barua hapo juu. Ninakualika uwe mgeni rasmi katika
mahafali ya kidato cha sita yatakayofanyika hapa shuleni siku ya tarehe 20/7/2017
kuanzia saa saba za mchana hadi saa 12 jioni. Pia utatunuku vyeti vya kuhitimu
kwa wahitimu 600 katika sherehe hiyo.
Nitashukuru sana iwapo ombi letu litakubaliwa.
Wako katika ujenzi wa taifa,
(Saini)
Gambuzi Peter
Mkuu wa Shule
4. Barua ya kuagiza/kupokea bidhaa (Barua za kibiashara)
Barua hizi huandikwa kwa lengo la kuagiza bidhaa au kukiri kupokea bidhaa
zilizotumwa.
Mfano wa barua ya kuagiza bidhaa
Kijiji cha Mkwawa,
S.L.P 20,
Iringa.
12/7/2017
Meneja wa Kiwanda,
Kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya,
S.L.P 44,
Mbeya.
Ndugu,
YAH: AGIZO LA ZANA ZA KILIMO
Husika na kichwa cha barua hapo juu. Tunaomba ututumie zana za kilimo, kwani
tunakusudia kuanzisha mradi wa kilimo cha mahindi hapa kijijini. Zana
tunazohitaji kwa ajili ya mradi huu ni :
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 18
- Majembe – 6
- Mapanga – 10
- Mashoka – 6
- Slesha – 20
- Toroli – 2
Tunaomba utume kwa basi la Simama Trans linalofanya safari zake kila siku hapa
Iringa. Kabla ya kutuma, tuandikie kutuarifu tarehe utakayotuma. Malipo
yatalipwa kwa hundi.
Wako katika ujenzi wa taifa,
(Saini)
Nyanya Kitunguu
Mratibu wa Mradi
5. Kadi ya Mwaliko
Kadi ya mwaliko huandikwa kwenye karatasi maalumu inayoitwa kadi. Kadi
ya mwaliko huwa na mambo yafuatayo:
- Jina la mwalikaji na anuani
- Jina la mwalikwa
- Lengo la mwaliko
- Mahali pa tukio
- Muda wa kukutana
- Mawasiliano kwa ajili ya majibu
Familia ya Bw. & Bibi Majaliwa Maisha wa S.L.P 007 Dar es Salaam, wanayofuraha
kukuali/kuwaalika Bw. & Bibi./ Bw./ Bi./ Prof./ Dkt./ Mch./ Sheikh./……………. kwenye
mahafali ya kijana wao mpendwa ………….yatakayofanyika shuleni kwao siku ya tarehe
10/7/2017 na baadaye kwenye tafrija fupi nyumbani kwao kuanzia saa 8:00 mchana hadi
saa 12:00 jioni.
Kufika kwako ndiyo mafanikio ya tafrija yetu.
Majibu kwa wasiofika
SIMU: 0717104507
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 19
ZINGATIA: Kadi ya mwaliko huweza kujibiwa kwa kutumia muundo wa barua ya
kirafiki au barua rasmi.
6. Barua ya gazetini
Barua za magazetini ni zile zinazoandikwa na wasomaji wa magazeti fulani
fulani kwa mhariri. Barua hizi huwa na madhumuni anuai ambayo huwa na
nia mbalimbali kama vile:
- Kutoa pongezi
- Kufichua maovu
- Kutoa maoni na mapendekezo
- Kupinga madai ya barua ya awali iliyoandikwa gazetini humo
kuhusiana na mada fulani
- Kuunga mkono madai ya barua fulani iliyoandikwa gazetini
- Kulalamikia hali fulani, kwa mfano usalama wa nchi
- Kuwafahamisha wasomaji kuhusu jambo fulani, kwa mfano
umuhimu wa kompyuta katika shule za sekondari, n.k
Muundo wa barua ya gazetini
- Kichwa cha barua - huandikwa mwanzoni kabisa na huandikwa kwa
herufi kubwa na kupigiwa mstari au wino mzito
- Mwanzo wa barua – mf: ndugu mhariri
- Barua yenyewe – huwa na ufafanuzi wa hoja zenye ukweli na
ushahidi wa kutosha.
- Mwisho wa barua – mara nyingi mwisho wa barua za magazetini
huwa na ombi, maoni au mapendekezo.
- Jina la mwandishi na anuaini – huandikwa chini, upande wa
kushoto.
- Tarehe – huandikwa baada ya jina na anuani (japo si lazima)
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 20
Mfano wa barua ya gazetini:
Nakerwa na Uchafuzi Dar es Salaam
Mhariri,
Miongoni mwa mambo yanayonikera katika Jiji la Dar es Salaam ni uchafu
uliokithiri huku viongozi wake wakionesha kushindwa kabisa kukabiliana na hali
hiyo.
Ndugu mhariri, nimekuwa nikitembelea maeneo ya Kinondoni shamba, Kariakoo,
Tandale, Manzese, Buguruni pamoja na Vingunguti kutokana na shughuli zangu za
kutembeza bidhaa lakini maeneo haya kwa kweli yanatia mashaka.
Kumekuwepo na maji machafu yanayotiririka kutoka kwenye vyoo pamoja na
lundo la takataka barabarani. Jambo hili kwa kweli inaharibu taswira ya Jiji hili.
Kwa bahati mbaya viongozi wa mitaa pamoja na wajumbe wamekuwa
hawawajibiki katika kuhakikisha mazingira haya yanaboreshwa na kuwa masafi.
Matokeo yake kumekuwepo na ongezeko la watu wanaopata maradhi ya
kuambukiza ikiwa ni pamoja na kuumwa tumbo, ukurutu na kuenea kwa harufu
mbaya.
Nakumbusha mamlaka husika kwamba, kukosekana kwa afya njema ni miongoni
mwa sababu ya kushindwa kuzalisha na hivyo kudhoofisha uchumi wa nchi.
Viongozi wa serikali za mitaa pamoja na wasaidizi wao ambao ni wajumbe
wanapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.
Kwa kufanya hivyo wanaweza kuaminika kwa wananchi na hivyo kuheshimiwa
kama viongozi na hiyo ndiyo kazi ya uongozi inavyopaswa kuwa.
Ni wajibu si kwa viongozi serikalini pekee lakini hata kwa wananchi ili
kuhakikisha mazingira wanayoishi yanakuwa safi jambo litakalowezesha kusaidia
kuepuka maradhi na mambo mengi yanayotokana na uchafu.
Pamoja na hivyo, halmashauri zinapaswa kutunga sheria ndogo ndogo zinazolenga
kutunza usafi wa mazingira na kuzisimamia.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 21
Rashi S. Mbonde
simbonde@yahoo.com
Ilala, Dar es Salaam
(Kutoka gazeti la MAWIO, Alhamisi, Agosti 6-12, 2015 Uk.14)
7. Simu ya Maandishi
Simu za maandishi ni mojawapo ya mawasiliano ya haraka baina ya watu.
Waandikiwa hupata taarifa haraka iwezekanavyo ukilinganisha na barua za
kawaida. Taarifa ya simu ni fupi lakini huwa na ujumbe ulio wazi na
unaoeleweka. Ufupi wa simu za maandishi unatokana na gharama kubwa za
malipo kwa sababu gharama za simu hulipwa kulingana na idadi ya maneno
yanayoandikwa.
Barua za simu zipo za aina mbalimbali kama vile:
Barua za simu ya kawaida
Barua za simu ya haraka
Barua za simu ya kupeleka fedha
Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa barua za simu
(i) Anuani ya anayepelekewa taarifa
Anuani ya simu ya maandishi lazima iwe kamili na ya waziwazi ili kuiwezesha
barua hiyo kupelekwa haraka iwezekanavyo bila ya matatizo. Anuani ya mji ni
lazima iwe na jina la mtaa na kama inawezekana namba ya nyumba. Vilevile jina
la ofisi ya simu iliyo karibu na mahali simu hiyo inakopelekwa.
(ii) Taarifa au ujumbe wenyewe
Hapa ndipo penye kiini cha simu. Habari ielezwe kwa ufupi sana lakini ieleweke
vizuri. Epuka mambo yasiyo ya lazima.
(iii) Jina la mwandishi au mtuma simu
Jina la mwandishi huandikwa kwa ukamilifu wake ili kumjulisha mwandikiwa
barua imetoka kwa nani.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 22
Kumbuka: Ni muhimu kuandika maneno yote kwa herufi kubwa ili kurahisisha
usomaji. Barua ya simu hutumika hasa kwa ajili ya mambo ya haraka sana na
muhimu. Simu huandikwa kwenye karatasi maalumu. Karatasi hizo hupatikana
posta.
Hakuna barua ya simu ya aina yoyote ambayo itasafirishwa bila ya kulipiwa
gharama ya kuipeleka simu hiyo. Hivyo, barua ya simu huwa fupi ili kuepuka
gharama za utumaji.
Mfano wa simu ya maandishi
8. Uandishi wa Matangazo
Uandishi wa matangazo ni shughuli ya kampuni, serikali au mtu binafsi ya
kusambaza habari. Kampuni huweza kutangaza bidhaa zake, nafasi za kazi,
mabadiliko fulani katika kampuni au shughuli muhimu katika kampuni.
Matangazo ni habari zinazowekwa wazi kwa nia ya kupitishwa kwa hadhira
fulani. Matangazo huhusu jambo fulani kama vile mkutano, mashindano,
harambee, n.k.
Vyombo vya habari kama vile magazeti, televisheni hutumiwa. Matangazo
pia huweza kuwekwa kwenye mabango. Matangazo huweza kuwa na habari
za kutoa onyo au kufahamisha. Kwa mfano kampuni huweza kuwatangazia
wanunuzi wake kuhusu hatari ya kununua bidhaa zisizo na chapa ya
kampuni hiyo. Tahadhari, onyo, ilani na notisi ni aina za matangazo
yanayotekeleza majukumu mbalimbali.
JUMA ALI SLP 20 MAKUYUNI
FIKA HARAKA BABA MAHUTUTI
FARIDA BAKARI
Alama za uandishi hazitumiki isipokuwa kama nazo ni sehemu ya neno.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 23
Sifa za matangazo
Matangazo hudhamiriwa kuwanasa wasomaji/wasikilizaji. Kwa hiyo,
mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:
Yawe mafupi – matangazo marefu huchosha na kusahaulika haraka.
Yatumie lugha yenye mvuto na sahihi inayoeleweka.
Yabandikwe sehemu za wazi ili watu wayasome kwa urahisi
Kwa kawaida huandikwa kwa herufi kubwa au wino mzito unaoweza
kuvuta makini ya watu.
Huweza kuwa na picha ili kuongeza mvuto.
Matangazo huweza kuwa ya aina mbalimbali kulingana na majukumu yake.
Zifuatazo ni baadhi ya aina za matangazo:
Matangazo ya biashara
Matangazo ya tahadhari
Matangazo ya taarifa za habari
Shughuli za kampuni
Shughuli za serikali
Kuenea kwa magonjwa, n.k
Mfano:
KAMPUNI YA KAMBI YA UUZAJI WA MASHAMBA
MASHAMBA YANAUZWA BEI NAFUU!! SHILINGI 200,000
KWA EKARI MOJA! SEHEMU CHACHE ZIMESALIA
NAMBA YA SIMU : 0717104507
CHAKUBANGA
DHIMA YA MATANGAZO KATIKA JAMII
(a) Kutangaza bidhaa mbalimbali ili kukuza soko la bidhaa hizo.
(b) Kutangaza ni njia mojawapo ya kuwasiliana na njia hii inaashiria ustaarabu wa
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 24
kupeana taarifa mapema kabla ya tukio linalokusudiwa kutekelezwa siku za
usoni.
(c) Kuelimisha jamii, matangazo hutumika kama vitanabaishi vyenye kutoa
tahadhari, maarifa, ujuzi na stadi mbalimbali. Tumepata kusikia na kusoma
matangazo yanayohusu UKIMWI, malaria, wizi wa nyaya za simu na umeme.
Hii ni mifano ya matangazo ambayo dhima kubwa ni kuelimisha jamii juu ya
hayo yaliyotajwa.
(d) Kutangaza husaidia kuboresha shughuli za kiuchumi kama vile kufahamisha
jamii juu ya bidhaa mpya zilizotoka, huduma mbalimba zinazotolewa, mahali
wanapoweza kupata bidhaa au huduma hizo na mengineyo mengi yanayohusu
masoko na ongezeko la ziada kutokana na biashara. Kwa ujumla, lengo la
kutangaza ni, kushawishi, kuburudisha, kuonya, kutoa taarifa, kuuza bidhaa au
kutoa huduma, n.k
Mambo muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa matangazo
(a) Kichwa cha habari, kiandikwe kwa herufi kubwa
(b) Kutaja aina ya biashara (matangazo ya biashara)
(c) Kutaja aina ya bidhaa (matangazo ya biashara)
(d) Kutaja mahali inapopatikana hiyo bidhaa au huduma
(e) Kutaja njia za mawasiliano.
Uandishi wa matangazo ya biashara magazetini
Tangazo linapaswa kuwa na mambo yafuatayo:
(a) Kichwa cha tangazo ambacho huandikwa kwa herufi kubwa
(b) Kutaja aina ya biashara inayotangazwa
(c) Kutaja aina ya bidhaa unazouza na bei zake
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 25
(d) Kutaja mahali inapotolewa huduma husika
- mji
- mtaa
- kijiji
- kata, n.k
(e) Kutaja njia za mawasiliano
- kwa barua
- kwa simu
- kwa nukushi
- kwa wavuti, n.k
Mfano
9. Uandishi wa Hotuba
Hotuba ni maelezo ambayo hutolewa na mtu mbele ya watu. Hutolewa kwa
madhumuni maalumu. Kwa mfano, hotuba inaweza kutolewa kwa madhumuni
ya kuhimiza kazi, kufanya kampeni fulani au kutoa taarifa fulani kwa watu.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 26
Sifa za hotuba
Ukweli wa jambo linaloelezwa
Ufasaha wa lugha
Nidhamu ya mzungumzaji mbele ya watu
Mantiki nzuri
Sauti ya kusikika
Aina za hotuba
Mahubiri: hizi ni hotuba za mafundisho ya kidini, hutolewa kanisani,
msikitini au kwa njia ya redio na televisheni.
Hotuba za kisiasa na Kiserikali: hizi ni hotuba za matangazo ya taarifa za
kiserikali na chama, za kisiasa, kuhimiza na kualika watu kutenda jambo
fulani, n.k
Mihadhara au masomo ya darasani: hizi ni hotuba au mafundisho ya
mwalimu shuleni hasa anapofundisha kundi kubwa la wanafunzi na hasa
wanafunzi wa vyuo vikuu.
Muundo wa hotuba
Muundo wa hotuba huwa na mwanzo, utangulizi, kati na mwisho.
Mfano:
Mwanzo – Mwanzo wa hotuba huwa na salamu.
Mzungumzaji: - Vijana safiiii!
Wasikilizaji: - Safiii!
Mzungumzaji: - Elimu juuuu!
Wasikilizaji : - Juuu!
Hii ni sehemu muhimu sana kwa ajili ya kuwaandaa wasikilizaji kuwa makini ili
waweze kusikiliza yale yatakayotolewa kwenye hotuba na mzungumzaji.
Utangulizi
Huwa na utambulisho kulingana na vyeo. Mfano: “Mheshimiwa mgeni rasmi,
ndugu wananchi, mabibi na mabwana…….”
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 27
Licha ya utambulisho, utangulizi huwa na shukrani pamoja na muhtasari wa
hotuba itakayotolewa.
Kati
Baada ya utangulizi, kiini cha hotuba hufuata. Kiini ndicho hutoa ujumbe kwa
wasikilizaji na ndiyo sehemu muhimu sana katika hotuba. Sehemu hii mtoa hotuba
hueleza yale yote yaliyomsukuma kutoa hotuba hiyo.
Mwisho
Hapa huwa ni hitimisho, muhtasari wa yaliyoelezwa kwa ajili ya kusisitiza,
shukrani na maagizo.
Mfano wa hotuba
HOTUBA YA MGENI RASMI, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI
MHE. CHARLES M. KITWANGA, MB AKIFUNGUA KIKAO CHA KAZI
CHA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI UKUMBI WA
„JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE‟, DAR ES
SALAAM TAREHE 18 – 19 FEBRUARI 2016
Inspekta Jenerali wa Polisi, Ndugu Ernest Jumbe MANGU,
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdurahman KANIKI,
Makamishna wa Polisi,
Naibu Makamishna wa Polisi,
Wajumbe wa Mkutano,
Waandishi wa Habari,
Wageni waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 28
Habari za asubuhi!
Heri ya Mwaka Mpya!
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya
njema na kutuwezesha kukutana hapa leo hii. Pili, natumia fursa hii kumshukuru
Inspekta Jenerali wa Polisi ndugu Ernest Mangu kwa kunipa heshima hii ya kuwa
Mgeni Rasmi katika Kikao hiki muhimu. Kupitia hafla hii ninapata fursa ya
kuzungumza na viongozi wote waandamizi wa Jeshi la Polisi na makamanda wa
mikoa na vikosi ambao ni wasimamizi wakuu wa kazi za Polisi. Ninawapongeza
sana kwa utaratibu huu mliojiwekea wa kukutana kila mwaka kwa ajili ya kufanya
tathimini lakini pia kuweka mikakati ya namna ya kuboresha huduma zenu kwa
jamii pamoja na jinsi ya kuzidi kuboresha Jeshi la Polisi nchini.
Ndugu Wajumbe,
Ni matumaini yangu kuwa kikao hiki kitakuwa tofauti na vikao vilivyopita
kutokana na kasi kubwa ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli kwa Falsafa yake ya „HAPA KAZI TU‟. Ni lazima
mbadilishe mtazamo na kufanya kazi kwa kasi inayoendana na Serikali hii.
Fanyeni tathimini ya tulikotoka, upungufu, changamoto na fursa zilizopo ili
kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi. Ni muhimu kupanga mikakati mipya ya
kupambana na uhalifu kwa kuzingatia changamoto zilizopo na upungufu mliouona
kwa mustakabali wa amani na usalama wa taifa letu. Kukiwa na usalama, shughuli
za kiuchumi zitafanyika kikamilifu na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na
taifa kwa ujumla. Aidha, usalama wa nchi yetu utazidi kuwavutia wawekezaji
katika sekta mbalimbali nchini na kuongeza ajira nchini.
Ndugu Wajumbe,
Kwa kuangalia tu aina ya wajumbe wa kikao hiki, nimeridhika kuwa Kikao Kazi
hiki ni muhimu sana kwa kuwa nyinyi ndiyo msingi na dira ya utendaji kazi wa
Jeshi la Polisi nchini. Maamuzi yenu mtakayoyafanya kwenye kikao hiki na
mkiamua kuyatekeleza kwa dhati taifa litakuwa limepiga hatua kubwa katika
kukabiliana na wimbi la uhalifu nchini. Nimeambiwa kuwa kaulimbiu ya kikao
hiki ni „Badilika kifikra, acha kufanya kazi kwa mazoea‟. Kaulimbiu hii ni nzuri na
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 29
ya maana kama mtaamua kuitekeleza kwa vitendo. Malalamiko ya Wananchi
dhidi ya utendaji kazi wa Askari Polisi yatapungua kwa kiasi kikubwa sana.
Ndugu Wajumbe,
Kwa kuwa hiki ni kikao changu cha kwanza kukutana na viongozi wote wa Jeshi la
Polisi wa nchi nzima, nitumie fursa hii kutoa pongezi za dhati kwenu kwa kazi
kubwa na nzuri mliyoifanya katika kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu. Mlisimamia
kwa weledi wa hali ya juu sana Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
katika muda wote wa mchakato. Mlisimama imara kabla, wakati na baada ya
Uchaguzi Mkuu na kudumisha amani, utulivu, umoja na mshikamano kwa
watanzania wote. Hongereni sana kwa kazi nzuri.
Ndugu Wajumbe,
Pamoja na pongezi hizo, nafahamu kuwa zipo changamoto kadhaa za kiuhalifu
ambazo ziliripotiwa katika kipindi kilichopita. Takwimu zinaonesha kuwa kwa
kipindi cha mwaka 2015 makosa makubwa yaliyoripotiwa yalikuwa 68,814
ukilinganisha na makosa 70,153 yaliyoripotiwa mwaka 2014 ambayo ni pungufu
ya makosa 1,339 sawa na asilimia 1.9 %. Kwa upande wa makosa madogo mwaka
2015 yaliripotiwa makosa 450,389 ukilinganisha na makosa 458,422
yaliyoripotiwa mwaka 2014 ambayo ni upungufu wa makosa 8,033 sawa na
asilimia 1.8%.
Kutokanana takwimu hizo niwapongeze sana kwa kazi nzuri mliyoifanya kwa
kipindi cha mwaka jana, na niwasihi muongeze nguvu zaidi katika kupambana na
uhalifu huku tukijikita katika kuzuia zaidi kuliko kusubiri uhalifu utokee.
Aidha, nawakumbusha kuwa katika kuhakikisha kuwa hili linafanikiwa ni lazima
kujenga mahusiano mazuri na jamii kwani wao ndio hasa wahusika na waathirika
wa uhalifu na wanawafahamu wahalifu kwa kuwa ni sehemu ya jamii. Mahusiano
mazuri na jamii yatasaidia upatikanaji wa taarifa kwa wakati na hivyo kuwezesha
askari wetu kushughulikia matukio ya kihalifu kwa wakati, weledi na ufanisi.
Ndugu Wajumbe,
Naelewa changamoto zinazotokana na upungufu wa vitendea kazi, nyumba,
maslahi yasiyotosheleza kwa maafisa na askari, uhaba wa taaluma katika mafunzo
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 30
na askari kuishi nje ya kambi. Napenda kutumia fursa hii kuwahakikishia kwamba
Serikali itaongeza jitihada ya kuliwezesha Jeshi la Polisi na askari kwa vitendea
kazi vya kisasa kwa kadri uwezo wa bajeti utakavyoruhusu. Tutaendelea
kuwajengea uwezo na maarifa ya kiutendaji kwa kuwaelimisha watendaji ili
waendane na wakati wa sasa wa sayansi na teknolojia. Ni matarajio yangu kwamba
mtatumia fursa zilizopo katika kutatua matatizo yanayolikabili Jeshi letu la Polisi,
wakati jitihada kama nilivyoeleza hapo juu zinafanyiwa kazi kulingana na uwezo
wa kifedha wa serikali. Aidha, napenda kusisitiza kwamba hatuna budi kutunza
vizuri vifaa vilivyopo ili hivi vichache tulivyonavyo tuvitumie kwa muda mrefu
zaidi. Hivyo, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha matumizi bora ya magari,
nyumba, vifaa vya ofisini, matumizi ya umeme na maji katika makazi na ofisi. Ni
muhimu sana kulisimamia hili ili kuepusha gharama zisizo za lazima. Kwa hiyo
nawataka makamanda wote msimamie hili kwa dhati na kwa nguvu zenu zote.
Pia lipo suala la ajali za barabarani ambalo limekuwa likikua siku hadi siku hasa
ajali zinazohusisha pikipiki maarufu kama boda boda. Ninaunga mkono harakati
zinazofanywa na kitengo cha usalama barabarani katika kutoa elimu ya usalama
barabarani, lakini nawataka nguvu kubwa pia ielekezwe huko kama mlivyoelekeza
nguvu kubwa kukabiliana na ajali za barabara kwa mabasi na malori yaendayo
mikoani. Kwa mfano kwa Jiji la Dar es Salaam pekee, karibu kila siku kumekuwa
kukiripotiwa ajali zinazohusisha bodaboda na nyingi zinasababisha vifo au
ulemavu kwa madereva na hata abiria wao na wakati mwingine hata kwa
watumiaji wengine wa barabara. Ajali hizi zidhibitiwe.
Mbali na kuhusika katika ajali za barabarani, bodaboda pia zimekuwa zikihusika
sana katika matukio ya kihalifu hasa unyang‟anyi wa kutumia silaha. Ni rai yangu
kwenu kuwa baada ya mkutano huu mtoke na suluhisho kwa tatizo hili hasa
uhalifu wa kutumia silaha kwa kutumia pikipiki jijini Dar es salaam.
Ndugu Wajumbe,
Yapo malalamiko kadhaa juu ya baadhi ya askari na maafisa wachache
wanaotumia beji ya polisi vibaya kwa kuwabambikia kesi wananchi, kuomba na
kupokea rushwa, kuchelewa kufika eneo la tukio hata kama ni umbali mfupi tu,
kula njama na watuhumiwa na hivyo kuharibu vielelezo vya kesi, kuchelewesha
upelelezi wa kesi, kutokuwajali wateja (huduma bora kwa mteja) na mengi
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 31
mengineyo ambayo yamekuwa ni kero kubwa sana kwa jamii. Natambua kuwa
mmekuwa mkiwashughulikia askari na maofisa waliotuhumiwa kujihusisha na
tabia hizi kwa mujibu wa sheria, lakini nitoe rai kwenu viongozi kuongeza jitihada
zaidi katika kushughulikia matatizo haya kwa kuwasimamia ipasavyo askari wenu
kuanzia ngazi ya chini kabisa. Nawahakikishia kuwa Serikali haitafumbia macho
askari au Afisa yeyote atakayefanya mambo haya ya hovyo bila kujali cheo chake.
Tutachukua hatua kwa faida ya Watanzania.
Ninaimani kuwa kila kiongozi akijiepusha katika kulinda na uendekeza mambo ya
hovyo na akiwasimamia anaowaongoza ipasavyo na kuhakikisha kuwa
wanawajibika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi na za
nchi, malalamiko ya aina hiyo yatapungua sana kama si kumalizika kabisa.
Ndugu Wajumbe,
Mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu ndiyo jjukumu la msingi la Jeshi la
Polisi. Ninawataka makamanda wote wa mikoa kuweka mikakati ya kuimarisha
mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu katika himaya zenu ili kupunguza
uwezekano wa wahalifu kukimbilia maeneo mengine pindi wanapofanya uhalifu.
Aidha mafunzo kazini yaimarishwe ili kuwajengea askari uwezo wa kukabiliana
nauhalifu.
Mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni jukumu la kila mmoja wenu, tunasikia
taarifa za kukamatwa mirungi na bangi kwa wingi lakini dawa za kulevya za
viwandani hatuzikii zikikamatwa. Nawakumbusha kudhibiti mitandao ya madawa
ya kulevya ya viwandani. Tutapima ufanisi wenu kwa kuangalia uhalifu wa aina
zote hasa eneo hili la madawa ya kulevya. Ni wazi kuwa hii ni vita kubwa na
inahitaji umakini wa hali ya juu katika kukabiliana nayo kutokana na namna
biashara hii inavyoendeshwa. Ninawasihi katika mkutano huu mtoke na mkakati
wa namna ya kushughulika na wote wanaojihusisha na biashara hii haramu ili
kuikomesha kabisa.
Ndugu wajumbe,
Kwa kumalizia niseme tena kuwa ni matumaini yangu kikao hiki kitaleta tija kwa
taifa zima na maazimio mtakayotoka nayo ndiyo yatakuwa dira katika njia
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 32
mtakayopita mwaka huu katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku na
kuhakikisha kuwa amani tuliyonayo inadumishwa.
Ndugu IGP, Makamanda na Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi,
Mwisho ingawa si mwisho kwa umuhimu, natumia nafasi hii kuwapongeza
Makamishna Albert Nyamhanga, Nsato Marijani na Simon Sirro kwa
kupandishwa vyeo na kupewa nafasi za juu za kuwatumikia Watanzania mkiwa
Makamishna wa Polisi. Nafasi hizo ni mzigo mzito kwenu. Nawatakia kila la
kheri katika utumishi wetu. Nitoe tena shukrani za dhati kwa Inspekta Jenerali wa
Polisi kwa kunialika kusema nanyi na kufungua Kikao hiki muhimu.
Baada ya kusema hayo sasa ninatamka rasmi kuwa kikao kazi cha Maafisa
Waandamizi wa Makao Makuu ya Polisi na Makamanda wa polisi wa Mikoa na
Vikosi cha Mwaka 2016 kimefunguliwa rasmi.
ASANTE SANA KWA KUNISIKILIZA
(Imechotwa katika mtandao wa https://www.moha.go.tz/sw/blog/2016-02-19/hotuba-ya-mgeni-
rasmi)
10. Uandishi wa Risala
Maana ya risala Risala ni hotuba fupi inayosomwa mbele ya kiongozi kwa niaba ya kundi fulani la watu hasa hasa wanafunzi, wafanyakazi, washiriki, wanachama, mafundi n.k ili kutoa maelezo ya haja zao mbalimbali na mahitaji yao au kuonesha msimamo wa kundi hilo kwa kiongozi. Muundo wa risala
Utangulizi
Cheo cha kiongozi anayehusika Kundi linalowakilishwa
Kiini
Maelezo ya hali halisi ya maswala na msimamo wa kundi linalowakilishwa.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 33
Mapendekezso na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa.
Hitimisho Huwa na shukrani, msimamo pamoja na hitimisho.
Tanbihi: Kama vilivyosemwa awali risala ni hotuba fupi lakini inachukua mambo muhimu tu na kuyaeleza. Hivyo risala yenyewe huwa ni maelezo ya muhtasari kwa jambo linalohitaji maelezo marefu Katika hotuba. Utungaji wa risala unahitaji uangalifu sana na lugha ya heshima iliyo wazi kueleweka kwa kiongozi. Mfano wa risala:
Ndugu Mgeni rasmi, Walimu, Wanafunzi wenzetu, Wazazi, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana. Kwa niaba ya wanafunzi wa kidato cha nne, tunayo heshima na furaha kubwa , kukukaribisha ili ushiriki nasi katika siku hii muhimu na kusikia mafanikio mbalimbali kwa kipindi chote cha masomo yetu hapa shuleni. Shukrani zetu za pekee na za dhati ziende kwa uongozi mzima wa Shule na walimu wetu wote kwa jinsi walivyojitoa kwa moyo wa kutufundisha, hivyo tumefundishika vyema; kwasababu tupo tofauti sana na tulivyokuja hapa mwezi januari 2009. Ndugu mgeni rasmi, tulianza kidato cha kwanza tukiwa wanafunzi 120; wasichana 60 na wavulana 60. Mpaka leo tunapohitimu tupo wanafunzi 90; kati yao wavulana ni 43, na wasichana 47. Wengine wameshindwa kuhitimu nasi siku ya leo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ujauzito na kuhama shule. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema wa Baraka kwa ulinzi wake kwetu hadi leo hii tunahitimu kidato cha nne. Ndugu mgeni rasmi, elimu hii ya kidato cha nne imetupatia msingi mzuri wa kujiunga na Elimu ya juu, pia imetujengea uwezo mzuri wa kujitambua na kufikiri, kufanya kazi vizuri na kufanya maamuzi sahihi; pia imetuwezesha sisi wanafunzi kupata elimu ya mambo mbalimbali kupitia masomo tunayo fundishwa hapa shuleni, mfano; tumepata elimu ya uraia, historia ya mambo mbalimbali katika nchi yetu na dunia kwa ujumla, pia tumeweza kupata uelewa kuhusu afya na magonjwa, usalama katika mazingira yetu, Kilimo, Maumbile ya nchi, hali ya hewa, misitu, na viwanda. Vilevile tumeelewa umuhimu wa kusoma vitabu mbalimbali kwa lengo la kupata ujuzi wa kuinua uchumi wetu wa taifa. Ndugu mgeni rasmi, mafanikio hayo yamepatikana kwasababu ya ushirikiano mzuri kati yetu na walimu wetu. Tangu tujiunge na shule hii tukiwa kidato cha kwanza tumefanya majaribio na mitihani ya mara kwa mara jambo lililo tusaidia kuinua taaluma yetu.Tunawashukuru sana walimu wetu, tuna waahidi kufanya vizuri katika mitihani yetu ya Taifa ya kidato cha nne mwaka huu, na Mungu awabariki sana.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 34
Ndugu mgeni rasmi, tumepata changamoto mbalimbali wakati wa maisha yetu ya kielimu hapa shuleni, kama ifuatavyo; Ndugu mgeni rasmi, tuna changamoto ya upungufu wa vitabu vya kiada na ziada; hii imepelekea kushindwa kujisomea vizuri, kwani kitabu kimoja kinatumiwa na wanafunzi zaidi ya ishirini (20). Ndugu mgeni rasmi, changamoto nyingine ni upungufu wa vifaa vya maabara, hii inapelekea kuchangia kifaa kimoja, hivyo tuna tumia muda mwingi sana kujifunza na kumuelewa mwalimu. Ndugu mgeni rasmi, pia kuna changamoto ya upungufu wa walimu, hasa wa masomo ya sayansi; hii imepelekea kutomaliza ‘syllabus’ kwa wakati. Ndugu mgeni rasmi, pia kuna changamoto ya upungufu wa samani za shule, kama vile; madawati kwa ajili ya wanafunzi, viti na meza kwa ajili ya walimu; hii imepelekea baadhi ya wanafunzi wenzetu kukaa wawili kwenye dawati moja. Ndugu mgeni rasmi, maji ni changamoto hapa shuleni, kwani shule haina kisima cha maji, hii imepelekea shule kununua maji kwa gharama kubwa, ambayo hayatoshelezi mahitaji ya shule, kama vile usafi; hususani kwa upande wa vyoo, bila kuwa na maji ya kutosha tutapata magonjwa ya mlipuko, kama vile kipindupindu. Ndugu mgeni rasmi, changamoto ya vifaa vya michezo; kama unavyojua kuwa michezo ni afya, shule yetu ina upungufu mkubwa wa vifaa vya michezo kama vile; mipira ya miguu, pete na mikono, pia hatuna milingoti ya chuma kwaajili ya magoli ya viwanja vya michezo yote tunayocheza hapa shuleni. Ndugu mgeni rasmi, tunashukuru uongozi wa shule hii, walimu na wazazi ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya shule yetu; kwa upande wa masomo ya sayansi; shule imeweza kutenga chumba kimoja cha darasa kitumike kama maabara japo kuwa kuna upungufu mkubwa wa vifaa. Ndugu mgeni rasmi, tunayo matumaini kwamba maombi yetu umeyasikiliza na utayaatekeleza, maana tunajua kwamba wewe unaweza kupitia Hlimashauri unayo isimamia, asante sana. Mwisho tunaomba msamaha wa dhati toka moyoni mwetu kwa Walimu, Wanafunzi wenzetu na Wazazi pale tulipoenda kinyume na matazamio yenu, kwani watu wakiishi pamoja tofauti lazima ziwepo, tunatumaini mtapokea msamaha wetu, nasi hatuna jambo lolote baya kwenu.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 35
Ndugu mgeni rasmi, tuna kushukuru sana kwa kufika katika Mahafali yetu, kwani tunatambua kuwa unamajukumu mengi ambayo umeyaacha na kuwepo hapa kwaajili yetu.
11. Uandishi wa Mdahalo
Mdahalo ni majibizano yenye utaratibu maalumu. Ni kichocheo cha utafiti na
njia ya kuelimishana. Mdahalo hufanywa kwa mashindano, ambapo upande
mmoja hutoa hoja za kutetea jambo linalozungumziwa na upande mwingine
hutoa hoja za kupinga. Kila upande hujitahidi kutetea msimamo wake mpaka
mwisho.
Katika mdahalo, kunaweza kuwepo watu wa kati ambao hawafungamani na
upande wowote. Hawa huweza kutetea upande fulani wakati fulani na kupinga
uande huo huo wakati mwingine.
Mdahalo hugawanyika katika sehemu kuu tatu:
Utangulizi: huwa na maneno ya kuvuta makini ya wasikilizaji na ndimo
ufafanuzi wa mdahalo hutolewa kwa ufupi.
Mdahalo wenyewe: katika sehemu hii, mzungumzaji huonesha msimamo wake
kuhusu mada ya mdahalo, hutoa hoja za kutetea msimamo wake kwa kutoa hoja
zenye ushahidi na mifano.
Hitimisho: huwa na muhtasari wa mawazo makuu ya mdahalo. Mzungumzaji
huonesha msimamo wake kwa kutumia lugha ya kuvuta wasikilizaji.
Mambo ya kuzingatia katika kufanya mdahalo
Mzungumzaji anapaswa kuelewa mdahalo kabla ya kuanza kupinga au
kuetetea.
Mzungumzaji apange na kuandaa hoja zake za kutetea au kupinga
mdahalo. Hoja hizo zinaweza kuandikiwa maelezo mafupi.
Katika hoja za mzungumzaji, achague zilizo nzito zaidi na awe
mwangalifu asichague hoja zisizohusiana na mada.
Mzungumzaji asikilize kwa makini hoja za wengine na kati ya hizo
achague anazokubaliana nazo.
Hoja zote zipangwe kimantiki na ziwasilishwe kwa kuzingatia lafudhi
sahihi na uteuzi mzuri wa maneno.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 36
Mzungumzaji atumie lugha ya kimazungumzo katika uwasilishaji wake.
Kwa nini tunafanya midahalo?
Kwa kujitayarisha na kushiriki katika midahalo wanafunzi wanajifunza kutumia
taarifa kuunga mkono hoja zao. Wanajifunza namna ya kuwasilisha mawazo yao
kwa uwazi na kwa ushawishi mkubwa.
Kwa kushiriki katika midahalo, wanajifunza kuelewa mawazo ambayo ni tofauti na
yao kwa sababu, wakati wa kufanya mdahalo, wanaweza kujadiliana kwa kutoa
hoja kwa jambo ambalo hawakubaliani nalo kikamilifu, na wanapaswa kuelewa
mawazo ya wenzao wa timu ya wasiokubali hoja zao.
Matayarisho ya mdahalo
Wafanya midahalo wazuri hujitayarisha vizuri. Mdahalo unaofanywa darasani
unaweza usiwe rasmi, lakini unaweza kuwajenga wanafunzi katika hali
inayowafanya wanafunzi wafanye mdahalo rasmi katika mashindano.
Kabla ya kuandaa mdahalo, wafanya midahalo wanakusanya taarifa nyingi kwa
kadri iwezekanavyo, kutoka katika maktaba, magazetini, na kwa kujadiliana na
watu.
Wanafikiria hoja zote zinazounga mkono mada yao, na zile zinazopinga hoja yao.
Kwa maana nyingine ni kuwa, wanaelewa hoja za wapinzani wao pamoja na hoja
zao. Wanajitayarisha kwa maswali yoyote wanayoweza kuulizwa na wapinzani
wao, na changamoto zozote zinazoweza kutolewa.
Wafanya midahalo wazuri hutayarisha hoja zao katika muundo mzuri wa
ushawishi. Wanawasikiliza watu wengine wanaofanya mdahalo, ili wajifunze
ufundi na stadi za kufanya mdahalo. Wanajiunga na vyama vya kufanya midahalo,
na kufanya midahalo mara kwa mara.
Mchakato wa mdahalo
Kuna timu mbili, kila timu ina wazungumzaji wawili au watatu. Timu moja
(chanya) inaafiki hoja, na timu nyingine (hasi) inapinga hoja.
Kuna mwenyekiti, ambaye anaendesha utaratibu.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 37
Mdahalo na muda wa mdahalo huo unagawanywa sawasawa kwa timu zote mbili.
Kila mzungumzaji anatoa mdahalo kama upande wake umeandaa kuunga mkono
hoja zao. Pande zinazungumza kwa zamu, wakianza na anayependekeza hoja
(chanya, hasi, chanya, hasi). Kila mzungumzaji ana muda maalum wa kuzungumza
(k.m. dakika tatu au tano)
Baadaye mdahalo unaweza kufunguliwa kwa washiriki wengine, kwa wasemaji
kusimama na kutoa hoja zao za kuunga mkono au kupinga mada ya mdahalo. Kila
mzungumzaji kutoka upande wa wasikilizaji anapewa muda maalum wa
kuzungumza ( k.m. dakika moja au dakika tatu).
Kila timu inaweza pia kuzungumza kwa kujibu hoja za wapinzani wao, baada ya
kila timu kupewa muda kidogo wa mashauriano. Hii ina maana kuwa wana nafasi
ya kupinga hoja dhidi ya hoja zilizotolewa na wapinzani wao. Kila timu inaweza
kupewa nafasi ya kupinga hoja dhidi ya hoja zilizotolewa na wenzao mara moja au
zaidi. Nafasi ya kwanza ya kupinga hoja wanapewa wale wanaopinga mjadala na
nafasi ya mwisho inatolewa kwa wanaounga mkono mjadala.
Kanuni muhimu za mdahalo
Timu inayounga mkono mjadala haitakiwi kubadili hoja zao. Aidha, ile
inayopinga mjadala nayo pia hairuhusiwi kubadili hoja zao. Wanapaswa kupinga
kabisa mjadala licha ya maoni yao binafsi.
Ikiwa mzungumzaji anatoa tamko, wanatakiwa kutoa ushahidi au sababu za
kuunga mkono tamko hilo.
Taarifa zinazotolewa katika mdahalo lazima ziwe sahihi.
Wazungumzaji hawaruhusiwi kuleta hoja mpya wakati wa kujibu/kupinga hoja za
wenzao.
Hoja ya utaratibu na hoja ya taarifa
Yeyote anayehusika na mdahalo anaweza kuingilia kati wakati msemaji
akizungumza kwa kunyoosha mikono na kusema kuwa „anataka kutoa hoja‟. (Hii
ni „hoja ya utaratibu‟). Hii ina maana kuwa anataka kueleza kuwa moja ya kanuni
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 38
za mdahalo imevunjwa (k.m. mzungumzaji amezidisha muda wake wa maongezi,
au hana ushahidi wa kuthibitisha hoja zake).
Wana-mdahalo wanaweza pia kunyoosha mikono yao wakitaka kutoa „hoja ya
taarifa‟ (swali au taarifa za ziada wanazoweza kutoa). Msemaji anaweza kuamua
kumruhusu mshiriki kuzungumza, lakini halazimiki.
Uamuzi
Timu inayoshinda katika mdahalo inaamuliwa na jaji au majaji kwa kutegemea
ubora wa mjadala.
Aidha inaweza pia kuamuliwa kwa kupigiwa kura.
Mfano wa mdahalo
Asante Mwenyekiti,katibu,mtunza muda na washiriki wote. Nipo mbele yenu
kuunga mkono mada isemayo Pesa ni chanzo cha maovu yote kwa hoja zifuatazo.
Hoja ya kwanza,………
Hoja ya pili,………
Hoja ya tatu,………..
Hoja ya nne,………..
Hoja ya tano,……..
Kwa hoja hizo nahitimisha kwa kusema kuwa ni kweli kabisa kuwa pesa ndio
chanzo cha maovu yote kwa wanadamu.
12. Taarifa za kikao
Kumbukumbu za kikao ni muhtasari wa mambo yaliyojadiliwa na kukubaliwa
katika kikao. Ni muhimu kuandika kumbukumbu za kikao ili kusaidia na
kurahisisha utekelezaji wa mambo yaliyoamuliwa. Pia kumbukumbu za kikao
hutumika kwa ajili ya marejeleo kwa vizazi vya baadaye.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 39
Namna ya kuandika kumbukumbu za kikao
Katika kuandika kumbukumbu mwandishi hana budi kuzingatia mambo
yafuatayo:
(a) Kichwa cha kumbukumbu
Kichwa cha kumbukumbu kioneshe kuwa kikao kinahusu nini, kilifanyikia
wapi na tarehe gani.
(b) Mahudhurio
Mwandishi anapaswa kuandika orodha ya majina ya watu waliohudhuria kikao
na wasiohudhuria. Kama kikao kinahudhuriwa kwa mara ya kwanza
mahudhurio yatakuwa na majina ya waliohudhuria tu.
(c) Uteuzi wa viongozi
Iwapo kikao kinahudhuriwa kwa mara ya kwanza wajumbe hupaswa kuteua
viongozi wa kikao hicho ambao ni Mwenyekiti na Katibu kabla ya kuanza kwa
kikao. Kikao hakiwezi kuanza pasipo viongozi wa kusimamia mijadala yote
katika kikao husika.
(d) Ufunguzi wa kikao
Baada ya kuteua viongozi, Mwenyekiti aliyeteuliwa hufungua kikao rasmi na
kuanzisha mijadala ya kikao cha siku hiyo na siku zijazo hadi itakapokuwa
vinginevyo
(e) Ajenda
Hapa huandikwa ajenda zilizojadiliwa kwenye kikao. Mambo yaliyojadiliwa
katika kila ajenda yaandikwe kwa muhtasari. Kwa kila ajenda kauli ya
kukubaliwa au kukataliwa itamkwe wazi.
(f ) Mengineyo
Hapa huandikwa ajenda ambazo hujitokeza katika kikao lakini hazikupitia kwa
Mwenyekiti na zinastahili kujadiliwa kama ajenda.
(g) Yatokanayo
Hapa huandikwa mambo ambayo yamejitokeza katika kikao na hayana
uhusiano na ajenda za kikao. Kwa mfano masuala mtambuka kama mjumbe
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 40
kulipia gharama za kikao,taarifa ya dharura inayoweza kumfanya mjumbe
aondoke kabla ya kikao kuahirishwa, n.k
(h) Kuahirisha kikao
Baada ya majadiliano ya ajenda, Mwenyekiti huahirisha kikao. Mwandishi wa
kumbukumbu azingatie muda kikao kilipoahirishwa.
Baada ya kikao mwandishi apitie tena kumbukumbu hizo na aziandike vizuri na
kuzihifadhi kwa ajili ya marejeleo ya kikao kijacho. Kumbukumbu hizo zitiwe
saini na Mwenyekiti na Mwandishi (katibu) kisha wakati wa mkutano mwingine
zisambazwe na kusomwa na wajumbe wa mkutano. Baadaye zithibitishwe na
wajumbe na Mwenyekiti na atie saini ya kuthibitishwa huko.
Ufuatao ni mfano wa kumbukumbu za kikao kinachofanywa kwa mara ya
kwanza:
KUMBUKUMBU ZA KIKAO CHA KWANZA CHA WANAFUNZI WA
KIDATO CHA TANO KUHUSU MAHAFALI KILICHOFANYIKA
TAREHE 5/4/2017 KATIKA UKUMBI WA SHULE KUANZIA SAA 4:00
ASUBUHI HADI SAA 6:00 MCHANA.
(a) Mahudhurio
Waliohudhuria (orodhesha majina yao)
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Wasiohudhuria (orodhesha majina yao)
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 41
-
-
-
-
-
-
-
-
-
(b) Uteuzi wa viongozi
Kiranja wa darasa aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kikao na katibu wake ni
kiranja msaidizi. Wajumbe wote walikubaliana na uteuzi huo.
(c) Kufungua kikao
Kiranja wa darasa ambaye aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kikao hicho
alifungua kikao mnamo saa 4:00 asubuhi kwa kuwaeleza wajumbe madhumuni
ya kikao hicho.
(d) Ajenda
- Siku na mahali pa mahafali
- Mgeni rasmi
- Zawadi
- Michango ya sherehe
- Uteuzi wa kamati
Siku na mahali pa mahafali
Wajumbe walijadiliana na kukubaliana kwa pamoja kuwa mahafali yafanyike
jumamosi ya pili kabla ya kuanza kwa mitihani ya kitaifa ili kuwawezesha
waalikwa wote kuhudhuria lakini pia kutoa muda wa kutosha kwa wahitimu
kujiandaa kwa mitihani yao.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 42
Kuhusu mgeni rasmi
Wajumbe walikubaliana kuwa jukumu la kutafuta mgeni rasmi apewe mkuu wa
shule.
Kuhusu zawadi
Wajumbe walijadiliana na kukubaliana kuwa zawadi zitapangwa na kuamuliwa
na kamati itakayoundwa.
Michango ya sherehe
Kikao kiliazimia kwa pamoja kuwa ili kupata pesa za kufanikishia mahafali kila
mjumbe apewe fomu maalumu itakayoandaliwa ili kuchangisha toka kwa
ndugu, jamaa na marafiki kiasi chochote atakachoguswa mtu kuchangia.
Uteuzi wa kamati
Wanafunzi wafuatao walichaguliwa ili wafanye mipango ya kuandaa na
kusimamia sherehe ya mahafali yao. Wanafunzi hao ni;
- Mtungi
- Baraka
- Mujuni
- Byoma
- Shukuru
- Sikudhani
- Kachacha
- Stumai
- Tamasha
- Kaitaba
Wajumbe hao walikubaliana na uteuzi huo na wakaahidi kupeana majukumu.
(f) Mengineyo
Wajumbe walisisitiza kwamba kamati ifanye mipango kwa kuzingatia kwamba
muda uliobaki ni mfupi. Walipendekeza kwamba kufanyike mkutano wa
kuwapatia wajumbe taarifa kuhusu mgawanyo wa majukumu.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 43
(g) Yatokanayo
Mjumbe mmoja aliwaburudisha wajumbe kwa vinywaji na nyama choma ya
mbuzi katika kumbukumbu yake ya kuzaliwa.
(h) Kuahirisha kikao
Mwenyekiti aliahirisha kikao kwa kuwaomba wajumbe wengine wawe na
ushirikiano kwa wenzao katika kufanikisha mahafali hayo. Kikao liahirishwa
saa 6:00 mchana. Kikao kijacho kitakuwa 12/4/2017 kuanzia saa 9:00 mchana
hadi saa 12:00 jioni.
Mwenyekiti…………………….Tarehe…………………………........
Katibu………………………….Tarehe……………………………….
Ikiwa kikao kinafanyika kwa mara ya pili:
Kikao cha pili na kuendelea huwa na muundo ufuatao:
1. Kichwa cha kikao
2. Mahudhurio
3. Kusomwa na Kuthibitishwa taarifa za kikao kilichotangulia
4. Kufungua kikao
5. Ajenda
6. Mengineyo
7. Yatokanayo
8. Kuahirisha kikao
9. Majina & saini za viongozi
13. UANDISHI WA RIPOTI
Ripoti ni maelezo kuhusu mtu, kitu au jambo fulani lililotokea. Ni aina ya
kumbukumbu ambazo huandikwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Ripoti
inaweza kuwa ya uchunguzi wa utafiti kuhusu jambo fulani, inaweza kuwa ya
polisi, daktari au ya tume fulani.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 44
Namna ya kuandika ripoti
Kabla ya kuandika ripoti lazima kuwe na ushahidi unaohusu suala au jambo
linaloandikiwa ripoti hiyo. Kwa hiyo, ni lazima mtunzi afanye uchunguzi kwanza.
Pia mtunzi anapaswa kufahamu kiwango cha elimu na uwanja wa mtu
anayemwandikia ripoti hiyo. Kwa mfano kama ni polisi, daktari, mwanasheria,
mfanyabiashara n.k. Lugha atakayoitumia mwandishi au mtunzi izingatie
muktadha wa matumizi. Lugha itegemee aina ya ripoti.
Hatua za uandishi wa ripoti
(a) Kichwa cha ripoti
Mtunzi aandike kichwa cha ripoti ambacho kinaonesha; kiini cha ripoti- ripoti
inahusu nini, tarehe ya tukio au jambo linaloandikiwa ripoti na mahali palipotokea
jambo hilo.
(b) Utangulizi wa ripoti
Katika hatua hii mtunzi hueleza kwa muhtasari madhumuni ya ripoti
(c) Kiini cha ripoti
Mtunzi aeleze mambo aliyoyaona, chanzo chake na madhara au faida yake
(d) Hitimisho
Katika kuhitimisha ripoti mtunzi aoneshe msimamo na mapendekezo yake. Baada
ya hitimisho mtunzi aandike au aoneshe ripoti imeandikwa na nani, cheo chake
(nafasi yake hasa katika ripoti hiyo) na tarehe ripoti hiyo ilipoandikwa.
Ufuatao ni mfano wa ripoti ya mkutano wa wanafunzi
Ripoti ya kikao cha wanafunzi wa kidato cha tano uliofanyika katika ukumbi wa
shule mnamo tarehe 10/4/2017 kuhusu mahafali yao.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 45
Mnamo tarehe 10/4/2017 saa 4:00 asubuhi, wanafunzi wa kidato cha tano
walifanya mkutano kuhusu mahafali yao yatakayofanyika mwezi Mei mwaka huu.
Mambo yaliyojadiliwa siku hiyo ni pamoja na :
(i) Kuwakaribisha wazazi wao
(ii) Kuandaa michezo mbalimbali: mpira wa miguu, mpira wa
kikapu, ngonjera, nyimbo, igizo, mashairi na muziki.
(iii) Kuandaa zawadi kwa ajili ya walimu wao wa madarasa, wa
masomo na Mkuu wa shule.
(iv) Kutoa mchango wa kununulia zawadi hizo.
Wanafunzi walitoa mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na kumwomba kiranja
wao wa darasa awaeleze walimu kwamba siku hiyo wanafunzi wanaomba wasivae
sare za shule na pia waruhusiwe kuwakaribisha wanafunzi wa shule nyingine kwa
ajili ya kucheza nao dansi na wakati wa muziki pawekwe ulinzi mkali ili
wasiingiliwe na watu wa nje.
Mwisho wanafunzi wote walikubaliana kuchanga Tshs. 2000/= kila mmoja ili
kufanikisha shughuli hiyo.
Mkutano huo uliodumu kwa saa mbili ulifungwa saa 6:00 mchana na kiranja wa
darasa.
Imetayarishwa na. Saini………………………..
Jina………………………...
Tarehe………………... Cheo…………………….....
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 46
14. Uandishi wa Wasifu
Wasifu ni insha inayosimulia maisha ya mtu fulani tangu kuzaliwa kwake, elimu
yake, kazi, ujuzi wake n.k. Anayeandika wasifu ni tofauti na anayezungumziwa
katika wasifu huo.
Kuna aina tatu za wasifu:
Wasifu wa Kawaida
Tawasifu/Wasifu binafsi Wasifu-Kazi
Wasifu wa kawaida.
Wasifu wa kawaida ni masimulizi ya maisha ya mtu fulani yanayosimuliwa na mtu
mwengine.
Katika insha, mwanafunzi anaweza kuambiwa aandike wasifu wa mtu mashuhuri-
anayejulikana kama vile Nelson Mandela, Julius Nyerere au Mzee Jomo Kenyatta
n.k. mtu yeyote anayemjua - kama vile mzazi, rafiki, mwalimu wake n.k. au
kumhusu mtu wa kubuni - mwanafunzi anaweza kubuni mtu na asimulie maisha
yake.
Mfano wa wasifu wa kawaida
WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI RAIS
WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
1.0. MAISHA YAKE
Ndugu John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha
Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke na watoto saba. Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi
Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015.
Tangu ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Ana
mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona wananchi wanapata huduma bora za jamii
na kero zao zinaondoka.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 47
2.0. ELIMU NA MAFUNZO
Rais Dkt. Magufuli alianza elimu ya msingi katika Shule ya msingi Chato mwaka 1967 na kumaliza mwaka 1974. Mwaka 1975 alianza masomo ya sekondari katika Shule ya Seminari ya Katoke Mkoani Kagera. Mwaka 1977 alihamia shule ya sekondari ya Lake
iliyopo Mkoani Mwanza na kuhitimu kidato cha Nne mwaka 1978. Kuanzia mwaka 1979 hadi 1981 alifanya masomo ya kidato cha Tano na Sita katika shule ya Sekondari ya Mkwawa Mkoa wa Iringa.
Mwaka 1981 hadi 1982 alisoma Chuo cha Ualimu Mkwawa na kuhitimu Stashahada ya
Ualimu ya Masomo ya Kemia na Hisabati. Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 1983, Dkt. Magufuli alipata mafunzo ya kijeshi katika Jeshi la kujenga Taifa kikosi cha
Makutupora mkoa wa Dodoma. Mwezi Januari hadi Machi 1984 alihamishiwa kikosi cha mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni, Arusha. Mwezi huo wa Machi alihamia kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Mpwapwa Dodoma na kumaliza mafunzo mwezi Juni 1984.
Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusoma Shahada ya kwanza ya
Sayansi na Ualimu akijikita katika masomo ya Kemia na Hisabati. Alitunukiwa Shahada hiyo mwaka 1988. Mwaka 1991 hadi 1994 alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Kemia iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha
Salford cha Uingereza. Mwaka 2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika Fani ya Kemia na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2009.
3.0. UZOEFU WA NDANI YA SERIKALI
Baada ya kuhitimu masomo yake ya Stashahada ya Ualimu, mwaka 1982 hadi 1983 Dkt. Magufuli alikuwa Mwalimu katika shule ya Sekondari ya Sengerema iliyopo Mkoani
Mwanza akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1989 alijiunga na Chama Cha Ushirika cha Nyanza Mkoani Mwanza, ambapo alifanya kazi kama Mkemia Mkuu hadi mwaka 1995.
Mwaka 1995 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki Mkoa wa
Kagera. Baada ya Uchaguzi, Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2000. Mwaka 2000 alichaguliwa kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Jimbo la
Biharamulo Mashariki lakini mara hii akipita bila kupingwa. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa Wizara ya Ujenzi hadi mwaka 2005.
Mwaka 2005 Rais Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki, kwa mara nyingine akipita bila kupingwa. Baada ya uchaguzi,
Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2008 ambapo alihamishiwa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi hadi hadi mwaka
2010.
Mwaka 2010 Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya nne kuwa Mbunge lakini, kufuatia mgawanyo wa majimbo uliofanyika, mara hii katika Jimbo jipya la Chato. Baada ya uchaguzi, aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2010 hadi
mwaka 2015.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 48
Wakati akiwa Mbunge na Waziri, Dkt. Magufuli amefanya shughuli na kushika nyadhifa kadhaa ndani na nje ya nchi. Mwaka 2014, Dkt. Magufuli alishiriki katika Bunge Maalum la Kutunga Katiba Mpya akiwa ni Mjumbe wa Bunge hilo. Aidha, wakati akiwa Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza (Co-Chair) wa Mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Makazi (UN-Habitat).
Tarehe 25 Oktoba, 2015 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alichaguliwa kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tarehe 5 Novemba, 2015 aliapishwa kushika rasmi wadhifa huo.
4.0. UZOEFU WA UONGOZI NDANI YA CHAMA
Rais Dkt. Magufuli alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977. Amekuwa
Mwanachama mwaminifu na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama. Nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya,
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.
Sambamba na kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Dkt. Magufuli mara zote alijitoa kukitetea Chama na kuhakikisha kinapata ushindi. Alishiriki kikamilifu kuwafanyia
kampeni wagombea wa CCM katika Chaguzi Ndogo zilizofayika katika majimbo ya Busanda, Biharamulo Magharibi na Igunga na kupata ushindi. Katika Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 11 – 12 Novemba mwaka 2012, Dkt. Magufuli alikuwa miongoni mwa
Mawaziri wachache waliopata fursa ya kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya Mwaka 2010 – 2015. Alielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani, hususan katika sekta ya miundombinu.
Tarehe 11 mwezi Julai, 2015 Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ulimchagua na kumteua
Dkt. Magufuli kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliinadi vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015) na kukiwezesha Chama kupata ushindi mkubwa. Tarehe 25 Oktoba, 2015 alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Nafasi hiyo imemwezesha kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.
5.0. UFANISI KATIKA UONGOZI
Dkt. Magufuli ni kiongozi mnyenyekevu, aliye na hofu ya Mungu, mkweli, mtekelezaji wa ahadi, mwadilifu, shupavu, mahiri, mbunifu, mtafiti, mchapakazi na mtetezi wa
wanyonge. Ni kiongozi mpenda haki na mchukia dhuluma, rushwa, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote ile. Ni kiongozi mwenye msimamo na mtetezi wa yale anayoyaamini.
Katika nyadhifa zote alizopata kutumikia alifanya kazi kwa uadilifu na umahiri mkubwa. Amejidhihirisha na kujipambanua kuwa ni mfuatiliaji na msimamizi wa sheria. Akiwa
Mwalimu Sengerema Sekondari aliwezesha wanafunzi wote wa darasa lake kufaulu masomo ya Hesabu na Kemia aliyokuwa akiyafundisha. Akiwa Mkemia Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Nyanza alisimamia vyema ubora wa uzalishaji wa mafuta ya Pamba na
kuifanya Kampuni ya Nyanza kuwa mzalishaji mzuri wa mafuta ya Pamba. Akiwa Waziri
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 49
wa ujenzi anakumbukwa kwa kubuni na kusanifu miradi ya ujenzi wa barabara, kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati uliopangwa. Uwezo wake katika kubuni na kusanifu miradi ya
barabara uliigwa na nchi majirani, ikiwemo Kenya. Ameondoka Wizara ya Ujenzi akiwa amesimamia ujenzi wa zaidi ya Kilometa 17,000 za barabara za lami, madaraja makubwa zaidi ya 14 na madaraja madogo madogo zaidi ya 7,000 na vivuko. Aidha,
alisimamia vizuri taasisi mbalimbali za Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu na Wakadiriaji Majengo.
Dkt. Magufuli pia anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuweka kumbukumbu ya kazi
zake. Akiwa Wizara ya Ujenzi aliweza kutaja majina ya barabara zilizojengwa au zilizokuwa katika hatua za ujenzi, urefu wake, majina ya wakandarasi pamoja na gharama za ujenzi bila kusoma mahali popote. Wakati wa Rais Mstaafu Benjamini
William Mkapa alimwita “Askari wa Mwavuli”. Akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisimamia upimaji wa ardhi za vijiji na viwanja vya makazi, na kushughulikia migogoro mingi ya ardhi iliyowahusu wananchi wa maisha ya chini.
Wakati akiwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi alikuwa maarufu wa kutambua na kutaja idadi ya mifugo, kama vile samaki, ngómbe, mbuzi, kondoo, kuku, mbwa n.k. Kitendo cha kukamata meli ya kichina iliyokuwa ikivua samaki kwa
wizi ndani ya Bahari Kuu ya Hindi eneo la Tanzania kilidhihirisha uzalendo kwa Taifa lake. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Kikwete alimpachika jina maarufu la “Tingatinga”.
Sifa hizi nzuri ameendelea nazo hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais. Katika miezi
michache ya uongozi wake amethibitisha anatekeleza ahadi. Aliahidi kutoa elimu bila malipo na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi. Ameweza kusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma kwa kuondoa watumishi hewa na kuchukua hatua dhidi ya
watumishi wa umma wasio waaminifu, wala rushwa, wazembe na wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Ameweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Kwa hakika Dkt. Magufuli
anaakisi uongozi bora unaopaswa kuigwa na viongozi wengi Barani Afrika na Dunia.
6.0. DHIMA YA UONGOZI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO 2015 –
2020) NA MALENGO YAKE MAHSUSI
Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 inazielekeza serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa nne;- Kwanza kuondoa umaskini, Pili, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, Tatu, kuendeleza
vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, na Nne, kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya Watanzania na mali zao.
Sambamba na kutekeleza mambo hayo makubwa manne, kipindi cha Kampeni na wakati akizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20
Novemba, 2015 Rais Dkt. Magufuli alitaja malengo mahsusi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Malengo hayo ni haya yafuatayo:
Kudumisha Muungano, Amani na Umoja wa Tanzania. Serikali haitamwonea aibu mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano na kuvuruga amani na mshikamano katika nchi. Hili
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 50
alilidhihirisha vizuri wakati wa uchaguzi wa marudio huko Zanzibar, kwani Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu.
Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kulingana na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Viwanda vinalengwa ni vyenye kutumia nguvu kazi kubwa, malighafi za ndani ya nchi, kuzalisha bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Nia ni kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini;
Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi, hususan miundombinu ya usafiri na nishati;
Kuimarisha huduma za jamii, hususan elimu, Afya na Maji. Lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinapatakana sio tu kwa urahisi bali pia kwa ubora unaostahili ili kukabiliana na maadui ujinga, umaskini na maradhi;
Kusimamia uwajibikaji wa utumishi wa umma na kuondoa urasimu ndani ya Serikali. Lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa ueledi, uadilifu na kujituma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati;
Kuimarisha usimamizi wa rasilimali za nchi, ikiwemo kuhifadhi mazingira na kuzidisha vita dhidi ya ujangili. Lengo ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watu wote wa kizazi cha sasa na kijacho. Aidha, ukusanyaji wa mapato ya Serikali na udhibiti wa matumizi ya Serikali nao utaimarishwa;
Kusimamia utawala bora unaozingatia sheria na haki za binadamu. Jitihada za makusudi zitaelekezwa katika kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, dhuluma na uonevu wa aina yoyote. Aidha, maslahi ya makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo wanawake, wazee, watu wenye ulemavu na watoto yatalindwa. Kwa upande mwingine, wananchi watahimizwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi;
Kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kupambana na uhalifu, ikiwemo wizi, ujambazi, tatizo la dawa za kulevya n.k.
Kudumisha na kuendeleza ujirani mwema, mahusiano mema na Mataifa mengine duniani pamoja na Mashirika ya Kimataifa na Kikanda;
Kuendeleza na kusimamia vizuri shughuli za michezo, sanaa, burudani na utamaduni, ikiwemo kukuza lugha ya Kiswahili.
HITIMISHO
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kuwataka watanzania washiriki kufanya kazi kwa bidii na maarifa ndani ya falsafa ya HAPA KAZI TU. Dhamira hii
inakusudia kuwezesha Taifa letu kufikia Uchumi wa Kati unaoongozwa na Viwanda ili kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 51
Tawasifu/Wasifu binafsi
Katika tawasifu, mwandishi huwa anasimulia maisha yake mwenyewe. Hivyo basi,
tawasifu huandikwa na kusimuliwa katika nafsi ya kwanza.
Katika insha, mwanafunzi anaweza kuulizwa asimulie: maisha yake binafsi,
maisha yake miaka kadhaa ijayo, maisha ya mtu fulani kama yake binafsi k.m
ajifanye kuwa Rais wa Tanzania, halafu asimulie maisha yake tangu kuzaliwa hadi
alipo. k.m 'Umekuwa Rais wa nchi yako kwa muda wa miaka mitano, andika
tawasifu kuhusu maisha yako itakayowasaidia wananchi wako kukuelewa vyema zaidi maisha ya mhusika wa kubuni, kama yake binafsi
Kwa mfano, katika riwaya ya Siku Njema, mhusika Kongowea Mswahili
anaandika tawasifu akisimulia maisha yake tangu kuzaliwa, maisha ya nyumbani,
elimu yake, kazi alizozifanya, maono yake n.k.
Mfano wa wasifu binafsi
Katika maisha yangu, nimekuwa ni mtu wa kukata tama mara nyingi. Hali hiyo
inaponitokea hunifanya niwe kama moto uliomwagiwa maji. Nakumbuka siku
moja, nikiwa mjini katika hali ileile ya kukata tama, nilikutana na Chopeko. Ni
Chopeko tuliyekuwa tukimwita “njiti” shuleni kwa vile alikuwa mwembamba kama kamba. Pia, siku zote alikuwa ni mtu wa mwisho katika mitihani.
Basi nilihisi mtu ananigusa begani; kugeuka macho yangu yalipamia bonge la
mtu aliyekuwa na uso wa mviringo kama tikitimaji. Hatimaye, baada ya kitambo
alijitambulisha kuwa yeye ni Chopeko baada ya mimi kuwa wa mwisho katika mtihani wa kumkumbuka.
Chopeko alinieleza kuwa hivi sasa yeye ni mfanyabiashara anayesafiri kufuata
bidhaa China na Dubai. Tulizungumza mengi, kasha tukaagana baada ya kuwa
tumepeana namba za simu.
Kuanzia siku hiyo niliazimia moyoni mwangu kuwa kukata tama kwangu tena mwiko!
Wasifu-Kazi
Wasifu-kazi (Resume/Curriculum Vitae) ni stakabadhi inayotumiwa kuorodhesha
mambo muhimu katika maisha ya mtu kama vile elimu, kazi, ujuzi n.k
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 52
inayotumiwa sanasana katika kuomba kazi. Kinyume na wasifu na tawasifu
ambazo hutumia lugha natharia (ya masimulizi), wasifu-kazi hutumia muundo
fulani wa orodha na/au jedwali kuwasilisha mambo muhimu tu. Isitoshe, wasifu
kazi huwa mfupi - aghalabu ukurasa mmoja.
Tunapoorodhesha mambo fulani katika wasifu, tunaanza na yale ya hivi karibuni
hadi yale ya kitambo. Kwa mfano, anza na shule uliyosomea mwisho, iliyokuwa
imetangulia hiyo n.k hadi shule uliyoenda kwanza.
Muundo wa Wasifu-Kazi
Katika wasifu-kazi unahitajika kuonesha:
1. Jina lako
2. Namna ya mawasiliano (simu, anwani, barua pepe)
3. Elimu
orodhesha shule zote ulizozisomea kutoka shule uliyosomea mwisho
hadi shule ile uliyoihudhuria kwanza.
katika kila shule, onesha miaka uliyohudhuria k.m 1996-2000
onesha shahada (degrees) na diploma ulizozipata
4. Kazi
orodhesha kazi zote ulizozifanya kutoka kazi ya hivi karibuni hadi
kazi ulizozifanya mwanzoni
onesha cheo ulichokuwa nacho katika kazi hiyo na majukumu yake
onesha kampuni au mahali ulipofanya kazi hiyo
onesha miaka ambayo ulikuwa katika kazi hiyo
taja ujuzi au taaluma uliyoipata katika kazi hiyo
5. Ujuzi / Taaluma - taja ujuzi maalumu ulionao, taaluma au talanta zozote
ulizonazo.
6. Mapato/Mafanikio/Tuzo - taja mafanikio yoyote au tuzo zozote ulizozipata
katika maisha
7. Mapendeleo - Nini kinakupendeza katika maisha? unapenda kutumiaje muda
wako wa likizo usiokuwa wa kazi
8. Maono ya Kazi - una maono gani katika kufanya kazi? ungependa kufanya
nini?
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 53
Mfano wa Wasifu-Kazi
Taarifa binafsi
Majina: TAFUTA MAISHA USICHOKE
Utaifa: MTANZANIA
Mahali pa kuzaliwa: ARUSHA
Tarehe ya kuzaliwa: 26/11/2017
Jinsi: ME
Hali ya Ndoa: SIJAOA
Anwani ya Posta:
MBEZI BEACH
S.L.P 60213
DAR ES SALAAM
Simu: 0717104507
Barua pepe: mwalimwakiswahili@gmail.com
Sifa za kitaaluma
2006-2009: Shahada ya Sanaa katika Elimu. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
2004-2006: Cheti cha Elimu ya sekondari ya juu. Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
2000-2003: Cheti cha Elimu ya sekondari ya kawaida. Shule ya Sekondari
Manyara
1993-1999: Elimu ya Msingi. Shule ya Msingi Mto wa Mbu
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 54
Uzoefu na historia ya kuajiriwa
2013-2015: Mwandishi wa Habari za Mazingira, Mwananchi Communications
Ltd
Ujuzi na weledi
Katika sehemu hii onesha aina ya ujuzi na weledi uliowahi kuupata kupitia
warsha, semina na makongamano yalivyokusaidia kuongeza ujuzi mwepesi
unaoweza kukusaidia kuzalisha, kukuza, kubuni, kuanzisha, kusababisha,
kubadili, kuchangia mabadiliko na kuwezesha.
Onesha mahali, mwaka, shughuli husika na malengo yake kwa mtiririko wa
kuanzia hivi karibuni mpaka yale ya zamani.
Machapisho na utafiti
Kama kazi unayoomba inahusiana na masuala ya taaluma na elimu (mfano
ualimu, ukufunzi, utafiti, uhadhiri), onesha machapisho na tafiti ulizowahi
kuzifanya na kuziandika.
Hapa, utaonesha jina la chapisho husika, mchapishaji na mwaka lilipochapishwa.
Lengo ni kuonesha ushiriki wako katika kutafuta majibu ya changamoto
zinazoikabili jamii, ikiwa ni pamoja na kuchangia kukuza maarifa yaliyopo.
Tuzo au heshima
Mwajiri huvutiwa na mtu anayeweza kuonyesha namna jitihada zake
zilivyotambuliwa na wengine. Onesha namna bidii, na ari yako ya kazi ilivyowahi
kutambuliwa katika ajira zilizopita.
Siyo lazima iwe kazini tu, inawezekana kuwa katika masomo, lakini ziwe tofauti
na zile tuzo za kitaaluma moja kwa moja.
Maneno kama, nilishinda, nilituzwa na nilitambuliwa, kwa sababu ya shughuli,
majukumu, jitihada zilizowahi kufanywa, yanakuongezea nafasi ya kukubalika.
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 55
Orodha ya wadhamini
Taja watu wanaoaminika wanaoweza kutoa ushuhuda wa uwezo na weledi wako.
Orodhesha angalau watu watatu wenye nyadhifa zinazotambulika na
wanaokufahamu vizuri iwe kwa sababu wamekufundisha au waliwahi kufanya
kazi nawe.
Ni vizuri kuwasiliana nao kabla ya kuwataja kwa kuwa wanaweza kuulizwa pasipo
wewe kujua. Na wakati mwingine ni vyema kuwaomba wakuandikie barua ya
utambulisho ukazitumia inapolazimika.
MWISHO
top related