national housing corporation (nhc) newsletter
Post on 06-Apr-2016
450 Views
Preview:
DESCRIPTION
TRANSCRIPT
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com1
NYUMBA NEWSLETTERJA R I DA L A S H I R I K A L A N Y U M B A L A TA I FA
JULAI - DESEMBA 2014TUNAJENGA TAIFA LETU
>> Rais Kikwete afungua nyumba za gharama nafuu
>> Waziri Mkuu Pinda apongeza mpango wa NHC
>> Waziri Tibaijuka azindua Bodi mpya ya NHC
>> NHC yaimarisha utendaji, Uendeshaji na udhibiti
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com1
NYUMBA NEWSLETTER
Jarida hili hutolewa na Shirika la
Nyumba la Taifa mara mbili kwa mwaka
Julai - Desemba 2014
ISSN NA. 0856-8510
BODI YA UHARIRI
Mwenyekiti
Nehemiah Kyando Mchechu
Mhariri Mkuu
Susan Omari
Mhariri Habari
Muungano K. Saguya
Yahya Charahani
Msanifu Kurasa
Arnold Njuki
Mchapishaji
Iprint Ltd
ANUANI
S.L.P 2977, Dar es Salaam.
Simu: +255 22 2105002,
Baruapepe: dg@nhctz.com,
Tovuti: www.nhctz.com.
WATAYARISHAJI
Limesanifiwa na Kutayarisha na:
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
Tahariri 2
Rais Kikwete afungua nyumba za gharama nafuu 3
Waziri Mkuu Pinda apongeza mpango wa NHC 4
Waziri Tibaijuka aizindua Bodi mpya ya NHC 5
Serikali yawahakikishia wawekezaji mazingira bora 7
NHC yaajiri wafanyakazi wapya 100 9
Wabunge watembelea Uturuki 10
Viongozi wa Shirika na Wizara wazuru Singapore 12
NHC yavutia wawekezaji nchini Dubai 12
Habari katika picha 17
NHC yafanikiwa katika utekelezaji mpango mkakati 17
Wastaafu utumishi NHC 20
Karibu NHC YALIYOMO
Page 3
Page 6Page 16
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com2
TUNAUNGA MKONO AGIZO LARAIS KIKWETE KWA HALMASHAURI
TAHARIRI
Katika nyakati tofauti wakati akifungua
nyumba za gharama nafuu zilizojengwa
na NHC katika Halmashauri mbalimbali
za Wilaya nchini, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Mrisho
Kikwete aliziagiza halmashauri zote nchini
kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya
kulipatia Shirika la Nyumba la Taifa na taasisi
zingine zinazojishughulisha na uendelezaji
miliki, ili kuwezesha ujenzi wa nyumba za
gharama nafuu.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo baada ya
kufungua miradi ya nyumba za gharama
nafuu zilizojengwa na NHC katika maeneo
ya Mkinga- Tanga, Mkuzo-Ruvuma na
Mnyakongo Kongwa. NHC inayo miradi
ya aina hii katika Halmashauri kadhaa
katika mikoa 19 hivi sasa. “jukumu la kila
halmashauri sasa ni kuhakikisha inatenga
ardhi ya kutosha na kulipatia shirika bila
gharama yoyote kwa ajili ya kukamilisha
azma yake hii njema ya kujenga nyumba za
gharama nafuu”.
Sisi Nyumba Newsletter, tunaunga mkono
na kupongeza kwa dhati agizo hilo la Rais
Kikwete kwani limeangalia hali halisi na
kuona umuhimu wa halmashauri kutenga
maeneo kwa ajili ya kujenga nyumba za
gharama nafuu. Kwa kufanya hivyo siyo
tu kutasaidia wananchi wengi kupata
makazi bora kwa gharama nafuu, bali
kutaboresha pia mandhari ya miji yetu na
kupunguza kasi ya makazi holela ambayo
inakuwa siku hadi siku kutokana na idadi
ya watu wanaohamia mijini kuongezeka
kwa kasi. Aidha, ni Halmashauri hizi hizi
zitakazonufaika na kupata kodi mbalimbali
kutokana na uwekezaji utakaofanywa
katika Halmashauri zao na waendelezaji
Miliki. Kadhalika, kuwepo kwa nyumba
katika Halmashauri hizo kutawawezesha
watumishi wa Halmashauri hizo kupata
nyumba na hivyo kupunguza hali ya
watumishi kukimbia baadhi ya maeneo ya
nchi kutokana na kukosa nyumba za kuishi.
Pamoja na kuunga mkono na kupongeza
uamuzi huo wa Rais, tunaamini kuwa
watendaji wa Halmashauri hizo
watatekeleza agizo hilo la Mheshimiwa
Rais kwa kuwa lina maslahi mapana
kwa watanzania na Halmashauri husika.
Utekelezaji wa agizo hilo kwa wakati
utaondoa changamoto nyingi zinazozikabili
Halmashauri zetu na kuziondolea
Halmashauri jukumu la kujenga nyumba za
watumishi wake kwa kuacha jukumu hilo
kwa NHC yenye dhamana ya kuwezesha
wananchi kupata nyumba.
Kwa kuzingatia yote hayo, tunaona uwe
ni utaratibu wa serikali za Miji na Wilaya
kuanzia sasa wa kutenga ardhi kwa ajili
ya waendelezaji wote wa miliki nchini ili
kuboresha mandhari ya miji, kuondoa
makazi holela na kupisha miradi mingine ya
maendeleo.
Tunaamini kuwa Halmashauri zitachukulia
uamuzi huu kama fursa ya kuongeza siyo tu
makazi bora kwa watu wake bali pia ajira na
ustawi wa maisha kwa wakazi wake.
Rais Dr. Jakaya Kikwete na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi wakikata utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkinga Tanga.
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com3
RAIS KIKWETE AFUNGUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU
UZINDUZI GHARAMA NAFUU
Na Mwandishi Wetu,
RAIS Jakaya Kikwete ameziagiza
Halmashauri za Miji na Wilaya nchini
kutenga maeneo kwa ajili ya kuwezesha
NHC na waendelezaji wengine wa nyumba
kujenga nyumba za gharama nafuu. Rais
Kikwete aliyasema hayo alipofungua kwa
nyakati tofauti miradi ya ujenzi ya nyumba
za gharama nafuu iliyojengwa na NHC
katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga
–Tanga, Mkuzo-Ruvuma na Mnyakongo –
Kongwa. Katika hafla hiyo, Rais alilazimika
kutoa agizo hilo baada ya kuelezwa kuwa
NHC inalazimika kulipa fidia ya ardhi jambo
linaloongeza gharama ya ujenzi wa nyumba
zinazojengwa. Hivyo, Rais aliziagiza
halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya
ardhi kwa ajili ya kulipatia Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) bila gharama yoyote ili
liweze kutekeleza mradi wake wa ujenzi wa
nyumba bora za gharama nafuu. “Nachukua
nafasi hii kuwapongeza NHC kwa kujenga
nyumba hizi za bei nafuu ambazo sisi
serikali tunazihitaji sana ili kuwawezesha
wananchi wetu kuishi kwenye makazi bora…
wito wangu kwa kila halmashauri sasa ni
kuhakikisha inatenga ardhi ya kutosha na
kulipatia shirika bila gharama yoyote kwa
ajili ya kukamilisha azma yake hii”, alisema.
Akiwa Mkuzo Songea Rais Kikwete alirejea
kauli yake aliyoitoa Kasera, Mkinga Tanga
kwamba Halmashauri zizipatie taasisi
zingine zinazojishughulisha na uendelezaji
miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF na LAPF
maeneo bila ya masharti ili ziweze kujenga
nyumba za gharama nafuu.
Akijibu maombi mbalimbali ya Shirika, Rais
alisema kuwa Serikali itafanyia kazi suala la
kupunguza kodi ya VAT katika nyumba mpya
kwa kuangalia uwezekano wa kuondolea
kodi hiyo ili kuwarahisishia wananchi
kuzinunua nyumba hizo.
Awali, akitoa taarifa ya Shirika katika mradi
wa Mnyakongo ulioko Kongwa, Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando
Mchechu alisema kuwa lengo la kubuniwa
kwa mradi wa nyumba za gharama nafuu
ni kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba
hususan za watu wa kipato cha kati na chini
linalowakabili wananchi katika maeneo
mbalimbali nchini. Alisema kuwa mradi huu
utasaidia juhudi za serikali za kuwaletea
wananchi maisha bora kwa kuwezesha
watumishi wa umma kuishi karibu na vituo
vyao vya kazi na kuwaondolea gharama za
usafiri.
“Ni ukweli ulio wazi kwamba hapa nchini
kuna mahitaji makubwa ya nyumba
yanayokadiriwa kufikia zaidi ya nyumba
milioni tatu hivi sasa na yanaongezeka kwa
idadi ya nyumba 200,000 kila mwaka wakati
uzalishaji wa nyumba ni kiasi cha asilimia 10
ya mahitaji ya mwaka mzima,” alisema
Bw. Mchechu alisema kuwa ujenzi wa
mradi huu unahitaji ardhi ya kutosha
ambapo alibainisha kuwa kwa sasa Shirika
linakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo
halmashauri nyingi kutokuwa na mpango
mahususi wa maendeleo ya ardhi na hivyo
kusababisha NHC kulazimika kununua
ardhi kwa fedha ya mikopo ya benki ili
kulipa fidia. Alisema hatua hiyo inaongeza
gharama ya nyumba hizo zinazoendelea
kujengwa katika halmashauri mbalimbali.
Alisema kuwa ujenzi wa nyumba za gharama
nafuu utaongeza ajira katika
Halmashauri.
Mradi huo wa nyumba za gharama nafuu
una nyumba zenye vyumba viwili na vyumba
vitatu na imewekewa huduma muhimu za
kijamii kama zahanati, shule ya chekechea
na maduka ya bidhaa za aina mbalimbali.
• Afurahishwanakasiyaujenziwa
nyumbahizokatikahalmashauri
• AziagizaHalmashaurikutengamaeneo
yaujenziwanyumbazagharamanafuu
• NHCkujenganyumbazagharama
nafuukatikaHalmashaurizote
Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu (kulia), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata utepe kwa uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za gharama nafuu, Mkuzo Songea Mjini
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com4
Na Mwandishi Wetu,
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mh.
Mizengo Kayanza Peter Pinda amezitaka
Halmashauri zote za Miji na Wilaya zilizoko
nchini kuhakikisha zinaunga mkono juhudi
za NHC za kuwapatia ajira vijana. Alizitaka
Halmashauri hizo kuhakikisha kuwa vikundi
vya vijana vya ujenzi wa nyumba nafuu
(building brigades) vilivyoundwa visaidiwe
kwa hali na mali kwa kuvifanya viwe sehemu
ya miradi ya kila Halmashauri.
Mh. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati
akizungumza na wakufunzi wanafunzi
kutoka VETA waliohitimu mafunzo
yaliyotolewa na Wakala wa Serikali wa
Utafiti wa Vifaa bora vya ujenzi (NHBRA) ya
namna ya kutumia mashine za kufungamana
kutengeneza matofali. Waziri Mkuu
alifunga mafunzo hayo yaliyotolewa Jijini
Dar es salaam kwa wakufunzi wataalam hao
waliotoka katika kila Mkoa wa Tanzania Bara
ambao sasa wanaendelea kutoa mafunzo
kwa vikundi vya vijana vilivyoko katika
Mikoa yao. Zaidi ya mashine 700 zimetolewa
na NHC kwa ajili ya kuwezesha makundi ya
vijana yaliyoundwa katika kila Halmashauri
nchini kujiajiri kwa kutengeneza matofali
kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama
nafuu.
Halmashauri hizo zimetakiwa kusaidia
mpango huu wenye nia njema kwa kutoa
maeneo kwa ajili ya vijana kuendeshea
shughuli za mpango huo. Maeneo hayo
yanapaswa kuwa na udongo unaofaa
kutengenezea matofali na kuwa karibu na
maeneo ya mjini ili kurahisisha masoko ya
matofali watakayotengeneza.
Waziri Mkuu alisema kuwa yeye binafsi
alimshawishi Mkurugenzi Mkuu wa NHC,
Bw. Nehemia Kyando Mchechu kuwa
katika ujenzi wa nyumba za gharama nafuu
nchini, ahakikishe kuwa anatafuta mbinu
za kutumia teknolojia rafiki wa mazingira
ili kuepuka janga la uharibifu wa mazingira
unaosababishwa na matumizi makubwa ya
kuni mbichi ili kuchoma matofali.
“Licha ya kuwa utengenezaji wa matofali
ya kuchoma unatekeleza azma ya Serikali
ya kutaka wananchi wake wawe na nyumba
bora, kwa kweli roho huwa inaniuma
hasa ukizingatia kiasi kikubwa cha miti
inayokatwa kuyachoma hayo matofali hadi
yawe imara, tena ikiwa mibichi,” alisema Mh.
Pinda.
Aliupongeza Wakala wa Serikali wa Utafiti
wa Vifaa Bora vya Ujenzi (NHBRA) kwa
kubuni mashine hizo ambazo alisema
zinauzwa kwa bei ambayo Halmashauri zote
zinaweza kuzimudu kuwanunulia vijana
wengine ili kupanua ajira.
“Mkurugenzi Mkuu ameniambia kila
mashine inauzwa shilingi 450,000/- na
inaweza kutengeneza matofali 700 kwa siku
moja, hayo matofali yanatumia mifuko saba
tu ya saruji. Hili ni jambo linalowezekana!”
alisisitiza. Hivyo, akawataka Wakurugenzi
wa Miji na Wilaya kushiriki kikamilifu katika
kuhakikisha kuwa mpango huu unakuwa
endelevu ili vijana wanufaike na mpango
huu. Alisema anataka Wakurugenzi hao
wachangamkie haraka kuzinunua hizo
mashine kwa sababu zinasaidia uhifadhi
wa mazingira, zinachochea ufanisi wa
teknolojia, zinapunguza gharama za
ujenzi na zinasaidia kutoa ajira kwa
vijana. Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwasihi
watakaoendesha miradi hiyo wasitoze bei
kubwa kwa matofali watakayotengeneza
ili wananchi wengi waweze kumudu bei na
wabadili hadhi za makazi yao. Waziri Mkuu
alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.
Mchechu aweke mpango wa kuendeleza
kampeni hiyo aliyoianzisha angalau kwa
miaka mitano mfululizo ili mpango huo
WAZIRI MKUU AUPONGEZA MPANGO WA NHC WA KUTOA AJIRA
WAZIRI MKUU PINDA
• Niwakusaidiavijanamashineza
kufyatuamatofali
• Unalengakutoaajirazipatazo7000
• Zaidiyamashine700zasambazwa
katikaHalmashauri
• AzitakaHalmashaurinchini
kusaidiampangohuo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya wataalam wa mashine za kutengeneza matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mafunzo hayo yaliyoanza Januari 6 mwaka huu, yaliendeshwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kushirikiana na Wakala wa Utafiti wa Vifaa Bora vya Ujenzi (NHBRA) iliyo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Nehemia Mchechu na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick na kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara.
Continued page 10 >>
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com5
BODI MPYA
Na Mwandishi Wetu,
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa
Anna Kajumulo Tibaijuka, ameagiza Bodi
ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) kuendelea na ujenzi wa nyumba
za gharama nafuu ili kuendeleza falsafa
iliyolianzisha Shirika hilo mwaka 1962 ya
kuboresha makazi ya watu wa kipato cha
chini na kati. “Ninachotaka kuwasisitizieni
Bodi mpya na Menejimenti ya NHC, Shirika
lisisahau lilipotoka liendelee na dhima
ya kuanzishwa kwake mwaka 1962 kwa
kuwajali pia wananchi kwa kujenga nyumba
za gharama nafuu, suala la nyumba lilikuwa
ni kampeni ya chama cha TANU,” alisema.
Agizo hilo alilitoa Waziri Anna Tibaijuka
Makao Makuu ya NHC, wakati alipokuwa
akizindua Bodi mpya ya Wakurugenzi
ya NHC yenye wajumbe saba hafla
iliyohudhuriwa pia na Watendaji wa
Shirika. Akizungumza katika hafla hiyo,
Waziri Tibaijuka aliagiza Shirika kuendelea
kutekeleza mabadiliko ya kuboresha
huduma za Shirika ili kuongeza tija
kubwa.“Nina imani kuwa mtaendelea na
utaratibu huu mzuri wa kujenga nyumba za
gharama nafuu ili kuwezesha Watanzania
wengi zaidi kunufaika na mipango yenu
mizuri mliyoianzisha,” alisema Tibaijuka.
Waziri Tibaijuka alisema kuwa pamoja na
kuwa hadi hivi sasa hakuna sera ya nyumba,
aliiagiza Bodi na Menejimenti ya NHC
kuhakikisha kuwa Shirika linajiendesha
kwa kufuata misingi ya ushindani, lakini
lisipoteze roho yake ya kujenga nyumba
za gharama nafuu na kuwe na vigezo
vitakavyowawezesha wenye sifa za kupata
nyumba za gharama nafuu wanufaike na
siyo wengine.
Waziri Tibaijuka alilipongeza Shirika la
Nyumba la Taifa na kubainisha kuwa hivi
sasa Shirika hilo limeimarika licha ya
kupitia katika changamoto nyingi sana huko
nyuma na kwamba Shirika linaongozwa
na Menejimenti yake huru, huku Serikali
kupitia Wizara yake ikifanya jukumu lake la
usimamizi.
Akizungumzia mabadiliko ya Sheria,
Waziri huyo alisema kuwa Serikali
ilijitahidi kubadilisha sheria mbalimbali
zilizokwamisha uwekezaji katika sekta ya
nyumba. Alizitaja sheria hizo zilizofanyiwa
marekebisho kuwa ni pamoja na sheria ya
ardhi namba 4 ya mwaka 1999, sheria ya
mikopo ya nyumba ya mwaka 2008 na sheria
ya hati pacha katika majengo ya ghorofa ya
mwaka 2008. Aidha, alisema kuwa mwaka
2010, Serikali iliagiza Shirika hili lifanyiwe
mabadiliko makubwa na lisukwe upya kwa
kulipatia uongozi mpya.
Aliiambia Bodi kuwa Wizara yake imekuwa
ikifanya mengi kuboresha sekta ya
nyumba ikiwemo kuboresha sera na sheria
mbalimbali kwa kuwa hatuwezi kuwa na
nyumba bora bila ya kuwa na mazingira bora
ya uwekezaji na sheria bora.
Alisema kuwa Bodi ambayo ameizindua
imelikuta Shirika na sekta ya uendelezaji
miliki vikiwa katika hali nzuri, hivyo akaiagiza
Bodi hiyo kuendeleza moto ule ule iliyokuwa
nayo Bodi iliyomaliza muda wake.
Alilitaka Shirika hilo kuweka uwiano
mzuri kati ya nyumba za kupangisha na
zile za kuuza ili kuweza kujilinda pindi
kunapotokea kuporomoka kwa soko la
nyumba. “Ninaomba kabisa Bodi yetu mpya
tuangalie “sustainability” ya tunayoyafanya,
washaurini hawa vijana wanunue nyumba
zinazowazunguka humu mijini ili kuwa na
vitega uchumi vilivyo katika mandhari nzuri,
siyo mbananishe maghorofa kama ilivyo
Kariakoo,”alisema.
Naye, Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia
Kyando Mchechu, alisema kuwa Shirika la
Nyumba la Taifa lina mali zenye thamani
isiyopungua shilingi trilion 1.5 hivyo
changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni
kuhakikisha wanatumia fursa zilizopo
kuwapatia Watanzania makazi bora.
Alisema kuwa Watanzania wana matumaini
makubwa na Shirika hilo ambalo hivi sasa
limedhamiria kufanya mabadiliko makubwa
hasa yenye lengo la kujiimarisha kibiashara
ikiwemo kujenga nyumba nyingi zaidi ili
kukuza uchumi wa Taifa na wa mtu mmoja
mmoja.
Alisema pamoja na jitihada hizo, Shirika
linakabiliwa na changamoto mbalimbali
kama kulazimika kununua ardhi kwa
gharama kubwa kwenye halmashauri za
Wilaya hapa nchini. Pia alisema kuwa Shirika
linalazimika kutengeneza miundombinu ya
umeme, maji na barabara katika maeneo
ya miradi na kuongeza gharama kubwa
jukumu ambalo alisema linapaswa kufanywa
na mamlaka zingine zinazohusika. Aliiomba
Serikali kuondoa kodi kwenye mauzo ya
nyumba mpya ambazo hazizidi shilingi
milioni 100 hatua itakayosaidia watu wengi
kuweza kununua nyumba kwa gharama
ndogo.
Wakizungumza katika hafla hiyo,
Wakurugenzi hao wa Bodi waliipongeza
Bodi iliyopita kwa kazi yao nzuri ya kuiongoza
Menejimenti ya Shirika. Walimshukuru Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Tibaijuka
kwa kuwapa jukumu zito la kulisimamia
Shirika na wakaahidi kuendeleza mambo
makubwa yaliyofanywa na Bodi iliyomaliza
muda wake.
Bodi hiyo inaundwa na Mwenyekiti
Mheshimiwa Zakhia Hamdani Meghji,
Bw. Diotrephes Mmari (aliyewahi kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi)ambaye ndiye
Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bibi
Subira Mchumo, Bw. Patrick Rutabanzibwa
(aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Bw.
Samson Kasalla (aliyekuwa Kamishna wa
Jeshi la Polisi), Bibi Irene Isaka (Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya
Jamii(SSRA), Bw. Bedason Shallanda kutoka
Benki Kuu ya Tanzania na Bw.Charles
Mafuru (Mkurugenzi wa Nyumba -Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi).
WAZIRI TIBAIJUKA AIZINDUA BODI MPYA YA NHC • AlipongezaShirikakwakazinzuri
• Alitakaliongezekasiyakujenganyumbazagharamanafuu
• Atakavigezovyakuuzanyumbahizokwawananchistahiliviwekwe
• Wenyewewamshukuru,waahidikufanyamakubwa
• SerikaliyaombwakuondoakodiyaVATkatikanyumbazagharamanafuu
BODI MPYA KATIKA PICHA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akizungumza na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) (hawapo pichani) kwenye uzinduzi rasmi wa Bodi mpya ya Shirika hilo uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote kwa hisani ya kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha NHC)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijuka akimkabidhi mkoba Mjumbe mpya wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , Diotrepes Mmari.
Wajumbe wapya wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijuka.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijuka akimkabidhi mikoba Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , Mama Zakhia Hamdani Meghji.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijukakatika picha ya pamoja na Mjumbe wa Bodi ya NHC, Irene Isaka.
Mjumbe mpya wa Bodi ya NHC, Charles Mafuru, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwaelekeza jambo watendaji wakuu wa Shirika la Nyumba (NHC) (hawapo pichani)
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com7
MAZINGIRA BORA
Na Mwandishi Wetu,
WADAU wa sekta ya uendelezaji miliki
nchini wamehakikishiwa mazingira
bora na salama kwa ajili ya uwekezaji katika
sekta hiyo inayokuwa kwa kasi nchini katika
siku za hivi karibuni.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa
Anna Tibaijuka jijini Dar es Salaam,
alipozungumza na wadau mbalimbali
waliohudhuria kwenye jukwaa la
wawekezaji wa ndani lililoandaliwa na
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo pia
lilishirikisha baadhi ya Wakuu wa Mikoa.
Profesa Tibaijuka alisema kuwa mazingira
bora ya uwekezaji katika sekta ya uendelezaji
miliki yameshawekwa na Serikali kwa
kuunda sheria rafiki za uwekezaji ambapo
ongezeko la uwekezaji wa moja kwa moja
kutoka nje ya nchi umekuwa na mageuzi
ya kiuchumi yamefanywa na yamewezesha
kuboreka kwa uchumi wa soko.
Alisema programu mbalimbali za mabadiliko
ya kisheria na kitaasisi yamefanywa na
serikali ambayo yana lengo la kuboresha
mazingira ya soko na uwekezaji binafsi
katika sekta binafsi.
Alisema pia kwamba maboresho ya
kitaasisi kwa kutoa vipaumbele kwa miradi
mbalimbali tayari yameshafanywa na
Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) na taasisi
nyingine za umma hali inayowarahisishia
wawekezaji kuamua mahali sahihi pa
kuwekeza.
“Ninachukua fursa hii kuwakaribisheni
wawekezaji ambao mmeshiriki kwenye
jukwaa hili, mchukue fursa hii kupata
taarifa muhimu mnazozihitaji na hatimaye
kuchukua fursa zilizopo tayari katika
uwekezaji kwenye miradi ya Usa River na
Safari Satellite City kule Arusha, na Salama
Creek Satellite City-Dar es Salaam,” alisema
Prof. Anna Tibaijuka.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia
Kyando Mchechu, alisema kuwa fursa
zilizopo katika sekta ya uendelezaji miliki
ni za kuvutia na hazina ushindani mkubwa
na ndiyo maana NHC imepanga kujenga
nyumba nyingi zaidi kwa ajili ya biashara na
makazi nchini kote.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,
sekta ya uendelezaji miliki imechukua
nafasi ya tano kati ya vivutio kumi vikuu vya
uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya
nchi yaani Foreign Direct Investment (FDI).
Bw. Mchechu alisema kuwa Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC), limedhamiria
kuyabadilisha maeneo ya jiji la Dar es Salaam
na mikoa mingine nchini baada ya kuzindua
ujenzi wa miji midogo inayojitegemea ndani
ya miji ya sasa. Alisema kuwa miradi hiyo
itakapokamilika itabadilisha mandhari ya
maeneo mbalimbali nchini na kuyafanya
kuwa ya kisasa.
Bw.Mchechu alisema ujenzi wa miradi
mitatu utaanza hivi karibuni ikiwemo ya
miji midogo katika majiji ya Dar es Salaam
na Arusha pamoja na kuendeleza nyumba
zilizobomolewa ili kupisha uendelezaji
mpya.
Alisema katika jiji la Dar es Salaam,
kutakuwa na mradi wa Salama Creek
ulioko Kigamboni na Up Town Kawe ulioko
ilipokuwa Tanganyika Packers ambayo
italifanya jiji hilo kubadilika na kuwa la kisasa
zaidi tofauti na linavyoonekana sasa.
Bw. Mchechu alisema katika miradi hiyo,
kutajengwa nyumba nyingi za kuishi,
biashara na sehemu za huduma muhimu
na kwamba itakapokamilika itabadili
muonekano wa maeneo hayo.
Alisema miradi mingine itakayotekelezwa ni
ya Usa River na Safari City itakayojengwa
Jijini Arusha na kwamba inalenga
kulibadilisha jiji hilo ili kuwa la kisasa.
Mkurugenzi Mkuu alisema kuwa mradi
mwingine ambao utatekelezwa katika Jiji
la Dar es Salaam, ni mradi wa ujenzi wa miji
mdogo wa Luguruni.
Mchechu alisema kuwa kila mradi
utagharimu dola za Marekani milioni mbili
(zaidi ya shilingi bilioni 3.4) na itakamilika
kati ya kipindi cha miaka 7 mpaka 12.
Alisema miradi mingine ambayo
itatekelezwa ni pamoja na Bagamoyo,
Dodoma, Mbeya, Mtwara, Lindi, Mwanza na
maeneo mengine nchini.
Mchechu alisema jukwaa hilo limetokana
na mkutano mkubwa wa wawekezaji
waliofanya hivi karibuni nchini Dubai
ambalo liliwahusisha wawekezaji wa nje
ili wawekeze katika sekta ya miliki nchini
Tanzania.
SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAZINGIRA BORA
• Niwawekezajiwandaniwasektayamiliki
• Sherianavivutiovingikatikasektahiyovyaboreshwa
• NHCyadhamiriakubadilishamandhariyamijinchini.
“Profesa Tibaijuka alisema
kuwa mazingira bora ya
uwekezaji katika sekta
ya uendelezaji miliki
yameshawekwa na Serikali
kwa kuunda sheria rafiki za
uwekezaji ambapo ongezeko
la uwekezaji wa moja kwa
moja kutoka nje ya nchi
umekuwa na mageuzi ya
kiuchumi yamefanywa na
yamewezesha kuboreka kwa
uchumi wa soko.
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com8
KAMATI POAC
• Afurahishwanakasiyaujenziwanyumbahizokatikahalmashauri
• AziagizaHalmashaurikutengamaeneoyaujenziwanyumbazagharamanafuu
• NHCkujenganyumbazagharamanafuukatikaHalmashaurizote
serikali tunazihitaji sana ili kuwawezesha
wananchi wetu kuishi kwenye makazi bora…
wito wangu kwa kila halmashauri sasa ni
kuhakikisha inatenga ardhi ya kutosha na
kulipatia shirika bila gharama yoyote kwa
ajili ya kukamilisha azma yake hii”, alisema.
Akiwa Mkuzo Songea Rais Kikwete alirejea
kauli yake aliyoitoa Kasera, Mkinga Tanga
kwamba Halmashauri zizipatie taasisi
zingine zinazojishughulisha na uendelezaji
miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF na LAPF
maeneo bila ya masharti ili ziweze kujenga
nyumba za gharama nafuu.
Akijibu maombi mbalimbali ya Shirika, Rais
alisema kuwa Serikali itafanyia kazi suala la
kupunguza kodi ya VAT katika nyumba mpya
kwa kuangalia uwezekano wa kuondolea
kodi hiyo ili kuwarahisishia wananchi
kuzinunua nyumba hizo.
Awali, akitoa taarifa ya Shirika katika mradi
wa Mnyakongo ulioko Kongwa, Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando
Mchechu alisema kuwa lengo la kubuniwa
kwa mradi wa nyumba za gharama nafuu
ni kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba
hususan za watu wa kipato cha kati na chini
linalowakabili wananchi katika maeneo
mbalimbali nchini. Alisema kuwa mradi huu
utasaidia juhudi za serikali za kuwaletea
wananchi maisha bora kwa kuwezesha
watumishi wa umma kuishi karibu na vituo
vyao vya kazi na kuwaondolea gharama za
usafiri.
“Ni ukweli ulio wazi kwamba hapa nchini
kuna mahitaji makubwa ya nyumba
yanayokadiriwa kufikia zaidi ya nyumba
milioni tatu hivi sasa na yanaongezeka kwa
idadi ya nyumba 200,000 kila mwaka wakati
uzalishaji wa nyumba ni kiasi cha asilimia 10
ya mahitaji ya mwaka mzima,” alisema
Bw. Mchechu alisema kuwa ujenzi wa
mradi huu unahitaji ardhi ya kutosha
ambapo alibainisha kuwa kwa sasa Shirika
linakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo
halmashauri nyingi kutokuwa na mpango
mahususi wa maendeleo ya ardhi na hivyo
kusababisha NHC kulazimika kununua
ardhi kwa fedha ya mikopo ya benki ili
kulipa fidia. Alisema hatua hiyo inaongeza
gharama ya nyumba hizo zinazoendelea
kujengwa katika halmashauri mbalimbali.
Alisema kuwa ujenzi wa nyumba za gharama
nafuu utaongeza ajira katika Halmashauri.
Mradi huo wa nyumba za gharama nafuu
una nyumba zenye vyumba viwili na vyumba
vitatu na imewekewa huduma muhimu za
kijamii kama zahanati, shule ya chekechea
na maduka ya bidhaa za aina mbalimbali.
RAIS KIKWETE AFUNGUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Cha Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing) Susan Omari (kushoto) akitoa maelezo na kisha kukabidhi kwa Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete mashine za kutengeneza matofali ya kufungamana ambazo zimekwishagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Tanga ili kuwawezesha kuanzisha vikundi vya ujenzi vya vijana. Kulia ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Galawa. Mashine hizo zilitolewa wakati wa Uzinduzi wa nyumba za bei nafuu Wilayani Mkinga
Na Mwandishi Wetu,
RAIS Jakaya Kikwete ameziagiza
Halmashauri za Miji na Wilaya nchini
kutenga maeneo kwa ajili ya kuwezesha
NHC na waendelezaji wengine wa nyumba
kujenga nyumba za gharama nafuu. Rais
Kikwete aliyasema hayo alipofungua kwa
nyakati tofauti miradi ya ujenzi ya nyumba
za gharama nafuu iliyojengwa na NHC
katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga
–Tanga, Mkuzo-Ruvuma na Mnyakongo –
Kongwa. Katika hafla hiyo, Rais alilazimika
kutoa agizo hilo baada ya kuelezwa kuwa
NHC inalazimika kulipa fidia ya ardhi jambo
linaloongeza gharama ya ujenzi wa nyumba
zinazojengwa. Hivyo, Rais aliziagiza
halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya
ardhi kwa ajili ya kulipatia Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) bila gharama yoyote ili
liweze kutekeleza mradi wake wa ujenzi wa
nyumba bora za gharama nafuu. “Nachukua
nafasi hii kuwapongeza NHC kwa kujenga
nyumba hizi za bei nafuu ambazo sisi
“Ni ukweli ulio wazi kwamba hapa nchini kuna mahitaji makubwa ya nyumba yanayokadiriwa kufikia zaidi ya nyumba milioni tatu hivi sasa na yanaongezeka kwa idadi ya nyumba 200,000 kila mwaka wakati uzalishaji wa nyumba ni kiasi cha asilimia 10 ya mahitaji ya mwaka mzima,”
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com9
WAAJIRIWA WAPYA
Na Mwandishi Wetu,
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC)
limeajiri wafanyakazi wapya 100 kutoka
wa kada mbalimbali ikiwa ni jitihada za
kuimarisha ikama na kuboresha huduma
zake kwa umma.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya
Uendelezaji Rasilimali watu imeeleza kuwa
wafanyakazi hao walioajiriwa kuanzia
Januari 2013 mpaka Oktoba 2014.
Wfanyakazi hao ni wa taaluma za Usimamizi
na Uendelezaji Miliki, Biashara, Utawala,
Manunuzi, Sheria na Ugavi.
Wafanyakazi hao ni pamoja na Mameneja
miradi ambao ni Bw. Etheldreder Koppa,
Bw. George Magembe, Bw. Samwel Metili,
Bw. Cliford Hungu na Bw. Subira Gudadi.
Maafisa Miliki walioajiriwa ni Mwasiti
Jimmy, Amon Mazanda, Dastani Mgouya,
Songoro Saidi, Lwitiko Ndigha, Emenick
Sanga, Victor Lawrence Sheushi, Edward
Haule, Amos Manyama, Costantine Yuda,
Keneth Ntulo, Fadhili Anyegile, Augustino
Sanga, Elizabeth Michael Maro, Wambura
Jafari Chege. Maafisa Miliki wengine
walioajiriwa ni Thomas Msambwa,
Mukakaro Mukakaro, Humphrey Tarimo,
Zenna Nyange, Goodluck Thomas,
Ramadhani Sadicki na Philip Gawa.
Katika kundi la Maafisa Manunuzi
waliajiriwa wamo Aman Sehaiya, Rukia
Kidasi, Fransisca Francis Michael, Kaiza
Straton, Paskalina Monko, Devina Msechu,
Victor Christopher, Evarista Mallya,
Castro Nzaye, Jimmy Mbogela, Anitha
Aloyce, Ritha Mokimirya na Olga William.
Wahasibu Wasaidizi walioajiriwa ni pamoja
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, James Rhombo akiwasilisha mada kwenye semina ya mafunzo kwa waajiriwa wapya inayofanyika kwa siku mbili kwenye hoteli ya JB Belmonte iliyoko Golden Jubilee Tower, Jijini Dar es Salaam.
Pichani baadhi ya Waajiriwa wapya kutoka kushoto Fatima Rajabu, wa tatu Clara Lumbanga, Felichism Mtenga na Lister Nyabilinyi wakisikiliza mada kutoka kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, James Rhombo wakati akiwasilisha mada kwenye semina ya mafunzo kwa waajiriwa wapya inayofanyika kwa siku mbili kwenye hoteli ya JB Belmonte iliyoko Golden Jubilee Tower, Jijini Dar es Salaam.
na Seleki Apolinary, Mussa Efata, Gloria
Otto Ringia, Lilian Reuben, Nimo William,
Salim Mbwana Salum, Benson Shabani,
Repson Yosia, Nancy Joseph na Baha j.
Nkhangaa.
Katika kada ya madereva wamo Nicholaus
Lyimo, George Kyamba, Raphael Maliva,
Anderson Fungo, Aquiline Mushi, Elias
Polepole, Aidin Stafford, Mohamed
Swanga na Abdulkher Abdallahtif.
Wafanyakazi wengine na vyeo vikiwa
kwenye mabano ni Grayson Godfrey
(Facility Manager), Rashid Omar
Amani (Msaidizi Masjala), Iddi Khalifa
Kitete (Msaidizi Masjala), Edna Lucas
Chogo (Afisa Utumishi Mwandamizi) na
Emmanuel Kabeya (Mwanasheria).
Wengine ni Godlove Godwin (Afisa
Utumishi), Gema Guerino Gamanywa
(Afisa Utumishi), Telesphori Focus (Injinia
wa Umeme), Nikundiwe Mmakasa
(Mkaguzi wa Ndani Mwandamizi) Bulla
Boma (Meneja Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu)
Tuntufye Mwambusi (Meneja Mauzo),
Emmanuel Kyarwenda (Mhasibu Kodi),
Sixtus Kilenga (Afisa Utawala Mwandamizi),
John Laswai (Mwanasheria Mwandamizi)
na Elias Mwashiuya (Meneja Huduma za
Sheria.
Pia wamo Clara Matern Lumbanga (Afisa
Mwandamizi Uendelezaji Biashara),
Fatima Adadi Rajabu (Afisa Mwandamizi
Uendelezaji Biashara), Salvatory Venant
Hinju (Afisa Mwandamizi Uendelezaji
Biashara), Getrude E. Mallya (Afisa
Utawala), Gloria E. Staki (Mapokezi),
John Temu(Mhasibu Msaidizi), Rose
Erasimus Uisso (Mhasibu Msaidizi),
Rose Michael Mwandemani (Mhasibu
Msaidizi), Khalid Maulid Mvungi(Mhasibu
Msaidizi), Felichism S. Mtenga(Mhasibu
Msaidizi),Hilda Anderson Temu(Mhasibu
Msaidizi), Lister Joseph Nyabinyili
(Mhasibu Msaidizi) na Mwita Bernard
Megabe(Mhasibu Msaidizi).
Wengine ni Domina Willbard Rwemanyila
(Afisa Huduma kwa wateja)Dyana Hatuey
Mwamba ((Afisa Huduma kwa wateja),
Jackline Kilawe (Afisa Mapokezi), Edwin
Martin Pesha (Dereva), Shija Samuel
Shimbi(Dereva), John Gustav Masika
(Dereva), Selemani A. Mashaka(Dereva),
Sadiki Muhamed Mneka(Dereva), Simon
Mhiliwa(Mhasibu Msaidizi) na Malima
Mukama(Mhasibu Msaidizi).
Menejimenti ya Shirika inawatakia
wafanyakazi hao wapya kazi njema yenye
kuliletea Shirika mafanikio zaidi hususan
wakati huu ambapo Shirika linatekeleza
mpango mkakati wake ambao unalenga
kujenga nyumba 15,000 katika kipindi cha
miaka mitano ijayo, idadi ambayo haijawahi
kufikiwa na Shirika tangu kuundwa kwake
Agosti 1, 1962.
• Niwakadambalimbalizautumishi
• Nimkakakatiwakuimarishaikamanaufanisi
NHC YAAJIRI WAFANYAKAZI WAPYA 100
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com10
Na Mwandishi Wetu,
JUMLA ya wafanyakazi arobaini
wamestaafu rasmi utumishi wao
kwa umma kwa mujibu wa sheria kwa
nyakati tofauti kati ya Januari hadi
Julai mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya
Uendelezaji Rasilimali watu imeeleza
kuwa wafanyakazi hao waliostaafu
katika kipindi hicho ni wa kada
mbalimbali hususan za Uendelezaji
Miliki, Utawala, Usimamizi Miliki na
Ubunifu Majengo.
Wafanyakazi hao na vyeo vyao
walivyotumikia vikiwa kwenye
mabano ni Joseph Mganga (Meneja
Uendeshaji Miliki), Verynice J. Nassary
(Accounts Technician), Simon Samo
(Mhandisi), Jumanne Mtuli (Fundi
Mchundo) Lusagana B. M. Lusagana
(Meneja wa Miradi ya Ubia), Dekusura
Kimaro (Karani wa Mahesabu) na
Telly Swebe (Msaidizi Mwandamizi
Utawala).
Wengine ni Traiphon Ndunguru
(Fundi Mwandamizi) , Khalfani Mhina
Juma (Dereva), Lazaro Lwanyakasura
(Fundi Mchundo), Omari Abbasi(Fundi
Mwandamizi), Alexander Nicolaus
(Msaidizi wa Ofisi) na Rajabu M.
Ngubureni(Dereva).
Pia katika orodha hiyo wamo Laurensia
Justinian (Msaidizi Mahesabu) ,
Goodnes Meresi (Msaidizi wa Ofisi),
Bakari Mnkande (Fundi Mchundo),
Augustino Joseph (Mlinzi), Cecilia
Sentala (Msaidizi masuala ya nyumba),
Leonard C. Maganga (Mkusanya
Madeni Mwandamizi).
Wastaafu wengine ni Bakari
Gumbo (Dereva), Michael Masudi
(Mlinzi), Monica Mlay (Mhudumu
Arusha), Modesta Gervas (Mhudumu
Kinondoni), Anastazia Togoro (Mpiga
chapa Shinyanga), Jane Nkwama
(Mpiga chapa Arusha), Simon
Shekigenda (Msaidizi masuala ya
nyumba), Loyce Petro (Mkadiriaji
Majengo Mwandamizi), Catherine
Fumbuka (Mhasibu), Said Mnongane
(Fundi Mchundo), Herman Kaseka
(Afisa Nyumba Kilimanjaro), Marcus
Mdugala, Sarah Mhanga (Mpiga chapa),
Twahir Chamulume (Afisa Masjala),
Allan Kabogo (Daktari wa Shirika),
Damian Hugho (Mhasibu), Seleman
Said (Afisa Stoo), Mathew Kabunga
(Mwanasheria), Ally Nangwanda
(Mhasibu Msaidizi), Alexander
Nicholaus (Mhudumu), Omari Abbasi
(Fundi) , Asubi Mwaigwisya (Fundi
Mchundo) na Mathias Chilemba (Fundi
Mchundo).
Wengine ni Ng’aranga Magai (Meneja
Mkoa –Kagera), Paul Mokimirya
(Meneja Mkoa –Ruvuma), Suresh
Dhrona – Meneja Ukaguzi wa Ndani,
Mariam Kambi- (Meneja Mkoa
Singida),Amina Salum(Mhudumu wa
Ofisi- Ilala) na Yassin Simtitu(Mhandisi
– Ruvuma).
Katika hatua nyingine wafanyakazi
watatu wa Shirika waliamua kuacha
kazi wenyewe kwa hiyari yao na
wengine kuachishwa kazi kwa sababu
mbalimbali .
Menejimenti ya Shirika inawatakia
wafanyakazi hao wastaafu maisha
mema na yenye mafanikio hasa
baada ya kushiriki vilivyo kuliletea
Shirika mafanikio makubwa hususan
wakati huu ambapo Shirika limekuwa
likitekeleza mpango mkakati wake
ambao unalenga kujenga nyumba
15,000, idadi ambayo haijawahi
kufikiwa na Shirika tangu kuundwa
kwake Agosti 1, 1962.
WASTAAFU
WASTAAFU UTUMISHI NHC•Niwakadambalimbalizautumishi
•WalilitumikiaShirikakwamafanikiomakubwa
uweze kuwa na matokeo chanya na maslahi
mapana kwa jamii.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw.
Nehemia Kyando Mchechu alisema kuwa
chini ya sera ya NHC ya kusaidia miradi
ya maendeleo inayofanywa na jamii (CSR),
Shirika limekuwa linachangia pia sekta
za afya na elimu na hivi sasa limelenga
vijana hasa ili kutoa ajira katika sekta ya
ujenzi. Aliwasihi Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri watoe
ushirikiano kwa Shirika ili mpango huo wa
kutoa ajira kwa vijana uweze kufanikiwa.
Aidha, alivitaka vikundi vya vijana vilivyoko
katika Halmashauri hizo kuunda SACCOS
zao ili kupanua shughuli zao za kiuchumi.
Katika mpango huo, kila Halmashauri
imepewa mashine nne, na kila mashine
inahudumiwa na vijana 10 kwa hiyo
itachangia ajira ya moja kwa moja kwa
vijana zaidi ya 7000. Pamoja na msaada
wa mashine, Shirika limetoa Shilingi laki
tano (500,000/=) kwa kila Halmashauri
kama kianzio cha vijana hao kununua
vifaa muhimu vya kuwezesha kazi ya
kufyatua matofali kuanza. Aidha, Shirika
limegharamia utoaji wa mafunzo kwa
vijana katika kila Halmashauri. Mpango huo
umeligharimu Shirika zaidi ya shilingi milioni
700 hadi kukamilika.
Akizungumza katika Mkutano wa Maafisa
Vijana kutoka Mikoa yote ya Tanzania
uliofanyika mjini Tabora Oktoba 16 mwaka
huu, Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa
Jamii, Bibi Susan Omari aliwaomba wasaidie
kufuatilia utekelezaji wa mpango huu.
Maafisa Vijana hao walilishukuru Shirika
kwa uamuzi huo wa kizalendo ambao
umesaidia sana kutoa ajira kwa vijana na
waliahidi kuunga mkono
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Ufundi wa utengenezaji Natofali kwakutumia teknolojia ya kisasa na kwa gharama nafuu wakimsikiliza Waziri Mkuu (hayupo pichana) wakati akiwahutubia kwenye hafla ya kufunga mafunzo yao na kuwakabidhi vyeti.
WAZIRI MKUU AUPONGEZA MPANGO WA NHC WA KUTOA AJIRA
<< Continued page 4
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com11
Na Mwandishi Wetu,
Hatua iliyopigwa na Serikali ya Uturuki
katika kupanga upya na kuyaendeleza
makazi yaliyokuwa na msongamano
mkubwa wa watu, imeonekana kuwaduwaza
wabunge wa Tanzania waliokuwapo kwenye
ziara ya mafunzo katika miji ya Ankara na
Istanbul iliyodhaminiwa na NHC.
Katika ziara hiyo, Wabunge hao walielezwa
kuwa Uturuki kupitia Mamlaka yake ya
Usimamizi na Maendeleo ya Nyumba,
iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu
(TOKI), iliwahamisha wakazi zaidi ya 6,500
waliokuwa wakiishi kwenye maeneo ya
ujenzi holela na sasa eneo hilo katika Mji wa
Ankara limepangwa na kuendelezwa upya
na baada ya kukamilika litakuwa na uwezo
wa kukaliwa na watu zaidi ya 18,000.
Ujumbe wa wabunge hao, wengi wakiwa
wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili
na Mazingira ulioongozwa na Mbunge
wa Kuteuliwa, Zakia Meghji (CCM) (sasa
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba
la Taifa), huku kwa upande wa Serikali
ukiongozwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Goodlucky Ole Medeye.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodlucky Ole Medeye (katikati), akiwa na wabunge wa Tanzania wakitembelea nyumba zilizojengwa na Serikali nchini Singapore na kuuzwa wananchi
ZIARA UTURUKI
Wengine katika ziara hiyo iliyoandaliwa
na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ni
wawakilishi kutoka Kamati za Bunge za
Bajeti na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa, pamoja na viongozi wakuu kutoka
Halmashauri ya Wilaya za Arusha na
Arumeru pamoja na Jiji la Arusha.
Katika ziara hiyo ya siku sita, ilibainika
kuwa tatizo linalokwaza uendelezaji wa
makazi Tanzania ni gharama kubwa za
ujenzi ambazo zinachangiwa na bei kubwa
ya ardhi, riba ya mikopo ya benki na kodi
ya ongezeko la thamani (VAT) baada ya
nyumba kujengwa.
Nchini Uturuki, TOKI hupewa ardhi na
Serikali kwa gharama ndogo na nyumba
zinazojengwa huuzwa pasipo kuongeza
faida wala kutozwa kodi kutokana na
Serikali kuwekeza fedha nyingi katika sekta
hiyo, huku wale wanaouziwa wakilipa fedha
hizo kwa miaka 20 bila kutozwa riba.
Meneja wa Tawi la Uhusiano wa Kimataifa
katika Idara ya Mipango miji ya TOKI, Sule
Karabey alisema gharama za nyumba kwa
ajili ya makazi yanayojengwa kwa ajili ya
watu wenye kipato cha kati na cha chini,
huuzwa kwa fedha ambazo ni sawa na
Shilingi 19.2 milioni za Tanzania.
Kiasi hicho ni zaidi ya mara mbili ya gharama
za nyumba za bei nafuu zinazojengwa na
NHC na kuuzwa kwa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia
Mchechu mara kadhaa amekuwa akieleza
kuwa gharama kubwa ya ardhi, kodi kwenye
vifaa vya ujenzi na kwenye mauzo ya
nyumba kuwa ni kikwazo kwa shirika hilo
kujenga nyumba za gharama nafuu.
Mchechu aliwaambia wabunge hao kuwa,
kikwazo kingine ni kutokuwapo kwa
huduma za jamii kama maji, umeme na
barabara katika maeneo ambayo shirika
lake linayaendeleza na kwamba wakati
mwingine NHC hugharamia huduma hizo
hivyo kusababisha gharama za nyumba
kuongezeka.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika
(Chadema), alisema tatizo lililopo ni
kukosekana kwa mawasiliano na uratibu
miongoni mwa taasisi za Serikali na kwamba
kama yangekuwapo hilo lisingekuwa tatizo.
WABUNGE WATEMBELEA UTURUKI
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com12
ZIARA SINGAPORE
• Watanzaniawatakiwakufuata
sheriazamipangomiji
• BodiyaNHCyatakiwakuitisha
mkutanowawadauwamipangomiji
• MipangomijiSingapore
imefanikiwakutokananaraiawake
namamlakazotekuzingatiasheria
zamipangomiji.
Na Mwandishi Wetu,
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. George
Simbachawene, amezitaka mamlaka
zinazosimamia mipango miji nchini
kuhakikisha kuwa sheria na taratibu zote za
mipango miji zinafuatwa na kusimamiwa.
Simbachawene alitoa kauli hiyo Jijini
Singapore alipokuwa akifanya majumuisho
ya ziara ya siku nne nchini humo mwezi
Julai,2014.
Akiwa ameandamana na watendaji wa NHC
na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Shirika, Naibu Waziri huyo alisema kuwa
Tanzania ina sheria na taratibu zinazoongoza
mipango miji kama ilivyo kwa Singapore,
lakini kinachokosekana nchini mwetu ni
usimamizi wa sheria na taratibu hizo.
Akasema kuwa ili kuleta mwafaka katika
usimamizi wa mipango miji nchini Tanzania,
ni vema Bodi ya NHC na Menejimenti ya
Shirika wakaangalia namna wanavyoweza
kuwakutanisha wadau wa mipango miji ili
kuona namna watakavyoweza kuibadili
VIONGOZI WA SHIRIKA NA WIZARA
WAZURU SINGAPORE
miji ya Tanzania kwa kuwa na mpango
kabambe wa kupanga miji hiyo. Mkutano
huo wa wadau utaweza kujadili changamoto
zilizopo katika usimamizi wa mipango
miji ya Tanzania na kupata ufumbuzi wa
changamoto hizo.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, katika
nchi ya Singapore miji ikishapangwa
kulingana na matumizi husika hakuna mtu
au taasisi yoyote inayoweza kubadilisha
kiholela mpango uliopitishwa tofauti na
ilivyo kwa Tanzania.
Hata hivyo, alisema changamoto kubwa
iliyopo nchini ili kuyafikia hayo ni kutokana
na kukosekana kwa uadilifu, nidhamu na utii
wa sheria zinazoongoza mipango miji.
Ujumbe wa NHC ukiangalia ramani ya Singapore inayoonyesha ujenzi wa miundombinu na makazi mbalimbali ya watu.
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com13
Ujumbe wa NHC ukisikiliza maelezo kutoka kwa watendaji wakuu wa Halmashauri ya jiji la Holland Bukit Panjang Singapore wanaotumia mfumo wa Kampuni Surbana katika kufanikisha na kudhibiti matengenezo ya nyumba.
Ujumbe wa NHC ukiwa katika picha ya pamoja (kutoka kushoto) ni Meneja Uendelezaji Biashara Willliam Genya, Meneja Biashara, Richard Ndeona, Meneja Huduma Miliki za Nyumba Grayson Godfrey, Meneja Fedha, Adolf Kasegenya, Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki, Hamad Abdallah, Jaffar Chege Wambura Ofisa Miliki Arusha, Meneja Mifumo ya Taarifa Suzanne Kyaruzi, Meneja Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu Bulla Boma na Emson Kabwogi Afisa wa Ukaguzi wa Ndani NHC. Walikuwa katika ofisi za Mamlaka ya Uendelezaji Miji nchini Singapore.
Ujumbe wa NHC ukisikiliza maelezo kutoka kwa watendaji wakuu wa Surbana ya Singapore.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
inayosimamia upangaji wa mji wa Singapore
ya Surbana, Tay Hang Hock Luois, alitaja
mambo mbalimbali yaliyosaidia upangaji wa
mji huo kuanzia ilipopata uhuru wake mwaka
1963, kuwa ni utii wa sheria za mipango miji,
usimamizi madhubuti wa serikali wa sheria
na taratibu za mipango miji.
Ziara hiyo ya mafunzo iliuwezesha ujumbe
huo wa Tanzania kutembelea Mamlaka ya
Mipango Miji ya Singapore na kampuni
inayosambaza majisafi na salama katika
mji wa Singapore ya Hyflux ambayo
imeonyesha nia ya kupunguza tatizo la maji
nchini Tanzania hasa maeneo zinakojengwa
nyumba mpya na NHC.
Ujumbe huo wa Tanzania ulipata pia fursa
ya kutembelea Makao Makuu ya Shirika
linalohusika na upangaji na uendelezaji miji
(Surbana); Mamlaka ya Uendelezaji upya
miji - Urban Redevelopment Authority
(URA); Housing & Development Board
(HDB na Mji mpya wa makazi eneo la
Punggol.
Shirika la Nyumba liliandaa ziara hiyo ya
mafunzo ili kuweza kuwapatia watendaji hao
uzoefu na kujifunza toka nchi zilizofanya
vizuri duniani katika masuala ya Upangaji
wa Miji, Viwango vya Majengo na Mikakati
ya Uendelezaji wa Miji Mipya (Satellite
Cities) kwa kushirikiana na Sekta binafsi.
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com14
• Niwasektayanyumba
• Wawekezajiwengiwaonyeshania
yakuwekezaTanzania
Na Mwandishi Wetu,
Katika jitihada kubwa zinazofanywa
na NHC katika kutengeneza fursa
nyingi kwenye sekta ya uendelezaji wa
makazi, Shirika limeweka historia kwenye
medani ya kimataifa kwa kufanikiwa kwa
mara ya kwanza kufanya kongamano la
uwekezaji nchini Dubai. Katika kongamano
hilo, Shirika lilifanikiwa kuonyesha fursa
zilizopo kwenye sekta ya ujenzi wa nyumba
nchini Tanzania, kwa makampuni makubwa
ya ujenzi yaliyopo Mashariki ya Kati na
kwingineko duniani ambayo yalihudhuria
katika kongamano hilo.
Tukio hili la kipekee na la kihistoria kwa
Tanzania lilizinduliwa na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dk. Mohamed Gharib Bilal
na lilihudhuriwa na makampuni makubwa
ya ujenzi Dubai kama Damac, Nahkeel,
Jumeirah na Emaar, ambayo yamehusika
na ujenzi wa majengo makubwa na maarufu
Dubai kama Burj Khalifa, Hoteli za Jumeira
na Dubai Mall.
Makampuni mengine yaliyohudhuria
yalitoka ukanda wa Guba kama Qatar na
Bahrain pamoja na nchi nyingine za Korea,
Sweden na Romania na yameonyesha
nia ya makampuni makubwa ya nchi hizo
kuwekeza kwenye sekta ya makazi Tanzania.
Akizungumzia kongamano hilo, Mkurugenzi
Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Kyando
Mchechu, alisema kuwa kongamano la
Wawekezaji Wa Sekta ya Makazi Tanzania ni
sehemu ya lengo kuu la NHC lenye dhamira
ya kupanua ukuaji wa sekta ya nyumba
nchini. Mchechu alisema kuwa kongamano
hilo lilikuwa ni mkakati wa kuionyesha
dunia kuwa Tanzania ni sehemu pekee yenye
mazingira mazuri ya uwekezaji na urudishaji
wa faida kwenye sekta ya makazi.
‘Tanzania inatoa fursa ya pekee linapokuja
suala la uwekezaji kwenye sekta ya makazi
barani Afrika na hii ni kutokana na uwazi
pamoja na utulivu wa kisiasa na amani
inayopatikana nchini, uchumi unaokua
pamoja na ushirikiano mkubwa unaotolewa
na serikali” ‘Tukio hili la kihistoria ni sehemu
tu ya mpango kamili wa kuifahamisha dunia
kuhusu fursa za uwekezaji kwenye sekta
ya makazi zinazopatikana nchini” alisema
Mchechu.
Mchechu anaamini kuwa huu ni muda
mwafaka kwa wawekezaji kuitazama
Tanzania na Afrika kwa ujumla. Alibainisha
kuwa hapo zamani ilikuwa ni vigumu kwa
wawekezaji kuwekeza Afrika na Tanzania,
lakini akasema kuwa kwa uchumi wa leo ni
hatari nchi kuwazia kutowekeza Tanzania.
Mchechu anasema kongamano hili
linalenga kupata wawekezaji wenye uwezo
wa kuanzia dola milioni 20 hadi dola nusu
bilioni. ‘Tunajua uwezo wa uwekezaji
unaotakiwa hauwezi kufikiwa kwa usiku
mmoja na ndio maana miradi yetu mingi ni
zaidi ya miaka 5 hadi 7, lakini tuna miradi
ambayo inaanzia dola milioni kumi hadi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai.
NHC YAVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI DUBAI
“Hatujawasahau dada na kaka zetu nyumbani Tanzania, wengi wao wana nafasi kubwa ya kuwekeza katika miradi ya uendelezaji wa sekta ya makazi nchini na tunataka kuhakikisha wanapata fursa hiyo pia”.
WAWEKEZAJI
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com15
Baadhi ya wajumbe waliofika kwenye kongamano la uwekezaji Dubai ambalo lilihudhuriwa na kampuni kubwa za ujenzi Dubai kama Damac, Nahkeel, Jumeirah na Emaar, ambazo zimehusika na ujenzi wa majengo makubwa na maarufu Dubai kama Burj Khalifa, Hoteli za Jumeira na Dubai Mall. Tukio hili la kipekee na kihistoria kwa Tanzania lilizinduliwa na Makamu wa Rais, Dk. MohammedGharib Bilal .
dola milioni mia, kwahiyo kiasi chochote
ambacho mwekezaji atakuwa nacho kati ya
kiwango hicho tuna fursa za kuwekeza naye’
anasema Mchechu.
Kati ya miradi ya NHC iliyoonyeshwa kwa
wawekezaji ni pamoja na miradi mitatu
ambayo itaendelezwa kwa kipindi cha miaka
5 hadi 10. Hii inajumuisha miradi miwili
ya kuendeleza Arusha inayoitwa Safari
City na USA River ambayo kwa pamoja
itakuwa na jumla ya nyumba 8000, pamoja
na mradi wa kuendeleza makazi Dar es
Salaam utakaofahamika kama Salama Creek
Satellite City ambao utakuwa na jumla ya
nyumba 9,500.
Miradi hii yote iko tayari kwa maana ya
ya kupata uwekezaji unaotakiwa.
Akizungumza katika kongamano hilo,
Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dk
Mohamed Gharib Bilal alielezea kuwa
serikali ya Tanzania imefanya kazi kubwa ya
kutengeneza fursa katika sekta ya makazi
ikiwemo kuzifanyia mabadiliko sheria
mbalimbali zinazohusu sekta hiyo. Sheria
hizo ni pamoja na sheria ya hati pacha, sheria
ya mikopo ya nyumba na uanzishwaji wa
kampuni ya kuwezesha mikopo ya nyumba
(TMRC) ambazo kwa hakika zimechangia
mabadiliko makubwa kwenye sekta ya
makazi.
‘Tanzania kwa sasa inashuhudia mafanikio
makubwa kwenye sekta ya makazi, huku
kukiwa kuna upungufu wa jumla ya nyumba
milioni 3.8 na upungufu huo unakua kwa
kiasi cha makazi 200,000 kwa mwaka,
ambayo kwa hakika inatoa changamoto
kubwa kwa Tanzania lakini ni fursa kubwa
kwa wawekezaji’ alisema Makamu wa Rais.
Naye, Balozi wa Tanzania kwenye nchi
za Falme za Kiarabu, Mheshimiwa Balozi
Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza
na wageni waalikwa alisisitiza namna sekta
ya makazi ilivyoimarika nchini Tanzania.
“Sekta ya makazi ndio sekta inayokua kwa
kasi zaidi nchini Tanzania na tunakaribisha
wawekezaji kutoka nchi za falme za Kiarabu”
alisema Mbarouk.
Kadhalika, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa
George B. Simbachawene, alisema kuwa
msingi mkuu wa kukua kwa sekta ya makazi
Tanzania umetokana na ushirikiano uliopo
baina ya serikali na sekta binafsi ambao
unaruhusu uwekezaji na ukuaji mzima wa
sekta.
Bw. Mchechu alisema kuwa wawekezaji
wa ndani ya Tanzania hawataachwa nyuma
na akabainisha kuwa nao watashirikishwa
katika kuekeza katika miradi ya ujenzi.
“Hatujawasahau dada na kaka zetu
nyumbani Tanzania, wengi wao wana
nafasi kubwa ya kuwekeza katika miradi ya
uendelezaji wa sekta ya makazi nchini na
tunataka kuhakikisha wanapata fursa hiyo
pia”.
Kongamano hili lilifanyika kwa ushirikiano
kati ya Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai,
Mheshimiwa Omary Mjenga pamoja na
Balozi Maalumu wa Mambo ya Kiuchumi,
Bwana Cleophas Ruhumbika, ambao
walishughulikia taratibu za kongamano
pamoja na kualika makampuni ya uwekezaji
ya Dubai.
“Tuna furaha kubwa kufanya kazi bega kwa
bega na Shirika la Nyumba la Taifa kwenye
tukio hili la kihistoria’ anasema Mjenga. ‘
Sehemu kubwa ya kazi yetu hapa Dubai
ni kuwezesha fursa kwa Tanzania ambayo
inaendana na wajibu wetu hapa. Pia tuna
furaha kubwa kuwa tukio limekuwa la
mafanikio makubwa na nina hakika kuwa
fursa zaidi za wawekezaji kuja Tanzania
zitazidi kufunguka’ anamalizia Mjenga.
NHC YAVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI DUBAIkuwa vibali vyote vya mradi vimepatikana
na kinachotakiwa ni kuwekeza tu na
kongamano hili lilikuwa muhimu kwa ajili
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com16
Baadhi ya maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) waliohudhuria mafunzo kazini kuhusiana na masuala ya kisheria ‘Dispute adjudication (Module 3)’ chini ya mkataba wa Shirikisho la Ushauri wa kitaalamu wa kihandisi (FIDIC). Mafunzo hayo yaliratibiwa na Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania (ACET).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijuka katika picha ya pamoja na Wajumbe mpya ya Bodi ya NHC na wakurugenzi wa NHC
Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa Nehemia Mchechu akiwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Norman Sigalla katika maandamano ya Jubilee ya miaka 50 ya shule ya sekondari Mbeya Day. Shirika la Nyumba la Taifa lilichangia kiasi cha shilingi milioni 20.
HABARI KATIKA PICHA
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com17
Mkurugenzi wa Fedha wa NHC Felix Maagi akikabidhi hati ya umiliki wa nyumba za makazi za Medeli, Dodoma kwa Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu wa BOT Bw Leonard Kisarika. BOT imenunua nyumba katika mradi huo kwa ajili ya wafanyakazi wake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi.Zakhia Meghji akizungumzakwa ufupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.
HABARI KATIKA PICHA
Wabunge na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwasili katika eneo la Kunduchi Range (Tanganyika Packers) kilichokabidhiwa kwa Shirika la Nyumba na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ) na baadaye kuelekea mradi wa Kawe City
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com20
Mwandishi Wetu,
Moja ya vigezo muhimu kwa taasisi yoyote
yenye nia ya kusonga mbele kwa kasi ya
kuridhisha ni kuwa na utawala bora kwa
maana ya utendaji, uendeshaji na uthibiti
wa rasilimali zake unaozingatia viwango
vya ubora wa hali ya juu katika kutekeleza
majukumu yake ya siku hadi siku.
Si ajabu ndio maana hata Shirika la ubora wa
viwango la kimataifa au the International
Standards Organisation (ISO) limeingiza
viwango vya utendaji kazi au utoaji huduma
kwa taasisi zisizo na majukumu ya moja kwa
moja ya uzalishaji kama ilivyo kwa NHC au
taasisi kama Shirika la Posta, Kampuni za
uchukuzi nk.
Ni kwa msingi huo Shirika la Nyumba la
Taifa limeweza kuanzisha utaratibu wa
kudhibiti matumizi ili yasizidi makadirio
ya bajeti. Mambo kadhaa yaliyoainishwa
katika mpango mkakati wa miaka mitano
yamepata mafanikio kadhaa na sasa Shirika
la Nyumba linaaminika sana katika utoaji wa
huduma zake.
Kadhalika, Shirika lilikuwa miongoni mwa
mashirika ya umma yaliyofuata taratibu
za manunuzi kwa kupata alama asilimia 86
kwa mwaka 2012/2013 zikilinganishwa na
asilimia 37 za mwaka 2009/2010. Vilevile,
Shirika limeanzisha mifumo ya mawasiliano
ya teknolojia ambayo imeongeza ufanisi
katika uendeshaji wa shughuli zake. Mifumo
hii ni pamoja na Mansoft, Document
Management System, Asset Management
System, Geographical Information System
na Fleet Management System.
Serazatayarishwakuongezaufanisi
Shirika limeanzisha sera mbalimbali ambazo
zinaliongoza katika utendaji wa shughuli
zake na zinalenga kuongeza ufanisi katika
utekelezaji wa majukumu yake. Baadhi ya
sera zilizoanzishwa ni pamoja na Sera ya
Mafunzo, Sera ya Fedha, Sera ya Uwekezaji,
Sera ya Ukaguzi, Sera ya Mawasiliano
ya Teknolojia, Sera ya Manunuzi, Sera ya
Usimamizi wa Nyumba, Sera ya Huduma
kwa Jamii, Sera ya Mawasiliano na vyombo
vya habari na Sera ya Afya.
Mfumowaudhibitinatahadhariyamajanganamatukiohasiwaanzishwa
Shirika liliweza kuanzisha mfumo wa
kutambua mapema tahadhari ya majanga
na matukio hasi na hivyo kuepukana na
gharama kubwa zinazotokana na majanga
hayo.
Lafanikiwakatikakutumiarasilimaliwatukikamilifu
Kuongeza ufanisi katika kutumia rasilimali
watu ni moja ya mikakati mipya ya NHC
katika kuhakikisha linatimiza majukumu
yake kwa ufanisi mkubwa na hivyo kukidhi
mahitaji ya wateja na matarajio ya serikali
juu ya huduma bora katika sekta ya nyumba
hapa nchini.
Ili kuweza kutumia vema rasilimali watu
iliyo nayo, Shirika liliboresha muundo wake
ili uendane na mpango mkakati pamoja na
majukumu yake yanayoendelea kupanuka.
Vilevile, Shirika linawapatia wafanyakazi
wa ngazi za chini mafunzo ya kuwaongezea
ujuzi na kuwapangia majukumu mengine
yenye tija kwa Shirika.
Pamoja na mafanikio haya, Shirika limeweza
kuajiri wataalamu wa fani mbalimbali kwa
ajili ya kuongeza tija katika utendaji. Ajira
hizi mpya, zimeweza kupandisha uwiano
kati ya wafanyakazi wenye taaluma na
wasiokuwa na taaluma kutoka asilimia 22
kwa 78 mnamo mwaka 2010 na kufikia
asilimia 51 kwa 49 hivi sasa. Lengo ni kuwa
na uwiano wa wafanyakazi wenye taaluma
asilimia 70 dhidi ya wale wasiokuwa na
taaluma asilimia 30 ifikapo Juni, 2015.
Mfumowaupimajiutendajikaziwaanzishwailikuongezaufanisi
Ili kuboresha utendaji wa kazi, Shirika
limeanzisha mfumo wa kupima utendaji wa
wafanyakazi wake (balance score card) na
kuwatambua wafanyakazi bora kila mwaka
kwa ajili ya kuwabakiza (retention) na
kuwandaa kuchukua nafasi za walio juu yao
(succession plan).
Mikatabambalimbaliyaboreshwakuletatija
Kuanzia mwaka 2010 Shirika liliweza
kupitia mikataba kati yake na wadau. Kati ya
mikataba 186 ya ubia iliyokuwepo, Shirika
lilifuta mikataba 59 ambayo haikuwa na
tija kwa NHC na Taifa. Vilevile, Shirika
lilirekebisha mikataba mingine 311. Shirika
linaendelea na marekebisho ya mikataba ya
upangaji kwa ajili ya kuiboresha ili ilete tija
kwa Shirika na wapangaji.
Marekebishoyasherianamba2yamwaka1990
Shirika kwa kushirikiana na Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
linaendelea na mchakato wa kurekebisha
Sheria Na. 2 ya mwaka 1990 iliyoliunda
upya.
Lengo la marekebisho haya ni kuliwezesha
kupanua wigo wa shughuli zake za
kuwa mwendelezaji mkuu; kuliwezesha
kuendesha shughuli zake katika mazingira
shindani; kuoanisha sheria ya Shirika na
sheria zingine na kuliwezesha kujitafutia
mitaji kwenye soko la fedha.
Lafanikiwakupunguzamashaurimahakamani
Tangu mwaka 2010 Shirika limeweza
kupunguza kesi zilizokuwa mahakamani kwa
zaidi ya asilimia 50. Aidha, Shirika lilishinda
kesi 185 kati ya kesi 190 ambazo ni sawa
na asilimia 97. Vilevile, Shirika limeweza
kubuni mikakati ya kuzuia kuibuka kwa kesi
mpya. Kwa sasa Shirika lina kesi 121 zilizopo
mahakamani katika masuala mbalimbali
na nyingi zina muelekeo wa kumalizika hivi
karibuni.
YAIMARISHA UTENDAJI
NHCYAFANIKIWAKATIKAUTEKELEZAJI MPANGO MKAKATI
• Yaimarishaudhibitiwarasilimalizake
• Serazakuongezaufanisizaanzishwa
• TaswirayaShirikayaboreshwakwakuwajaliwateja
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com21
KuboreshaTaswirayaShirika
Shirika limekuwa likitekeleza mkakati wa
kubadili mtazamo hasi juu ya shirika kwa
kuanzisha utaratibu wa kuuelimisha umma
kuhusu shughuli zake kupitia vipindi vya
televisini na redio vya Maisha ni Nyumba.
Pamoja na juhudi nyingine za kuboresha
utendaji wa Shirika, vipindi hivi vimesaidia
kuondoa mtazamo hasi wa jamii na wadau
wake na hivyo kupunguza malalamiko
dhidi ya Shirika. Mtazamo chanya wa
Shirika umeongezeka kutoka asilimia 40
mwaka 2010 na kufikia asilimia 76 mnamo
Desemba, 2013.
KuboreshamwonekanowaShirika(rebranding)
Shirika limekamilisha mchakato wa
kubadilisha mwonekano wake ili kupanua
fursa za biashara, kuondoa mtazamo hasi
wa wateja wake na kukuza soka la nyumba
za Shirika, ili kwenda sambamba na malengo
yake ya sasa.
Kuboreshaserayauwajibikajikwajamii
Kupitia sera yake ya huduma kwa jamii,
Shirika limedhamiria kuchangia katika
kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. Kwa
kushirikiana na Chuo Cha Mafunzo ya
Ufundi (VETA) cha Dar es Salaam; Wakala
wa Utafiti wa Vifaa bora vya Ujenzi na
Majengo (NHBRA); na Halmashauri za
Wilaya, Shirika linaendelea na mpango wa
mafunzo kwa vijana yanayoambatana na
kuwapatia vijana mashine za kutengeneza
matofali yanayofungamana (soil-cement
stabilized interlocking bricks) na mtaji.
Chini ya mpango huu, Shirika limetoa
mashine nne kwa kila Halmashauri nchini
kwa ajili ya kuwajengea vijana uwezo
wa kujiajiri wenyewe kupitia miradi ya
kutengeneza matofali. Katika utaratibu huu
zaidi ya mashine 700 zimetolewa katika
Halmashauri mbalimbali nchini na gharama
ya mradi huu inakadiriwa kufikia zaidi ya
shilingi milioni 700.
Mpango huu utakapokamilika utaweza
kuwapatia ajira ya moja kwa moja vijana
7000 kwa awamu ya kwanza. Lengo ni
kuendelea na mpango huu mpaka uweze
kufikisha ajira za vijana 200,000 kwa nchi
nzima.
TANZIA
Na Mwandishi Wetu,
MKURUGENZIMkuuwaShirikalaNyumbalaTaifa(NHC)anasikitikakutangaza
vifovyawafanyakaziwakewatano,vilivyotokeakwanyakatitofauti.
AkizungumziavifohivyoMkurugenziMkuu,Bw.NehemiahMchechualiwapapole
wafanyakazi wote kwa kuondokewa na wafanyakazi Fatuma Kibiki aliyefariki
mwishonimwamwaka jananaRashidJakulagizaaliyefariki usikuwakuamkia
AlhamisiyaJanuari10mwakahuu,nyumbanikwakeGongolamboto.
KifokinginenichamfanyakaziOmariIssaMalibichealiyekuwaderevaaliyefariki
dunia nyumbani kwake usiku wa kuamkia Februari 14, mwaka jana. Alizikwa
kwaoLindi.
MfanyakazimwinginewaNHCaliyeiagaDunianiAdamMwinyekulealiyekuwa
akifanyia kazi bohari yaMkoawaUpanga aliyefarikiMachi 17mwaka janana
kuzikwakwaoMbeya.
Mwaka huu Machi 25, Jeremiah Mchome aliyekuwa Mhasibu Idara ya Fedha
KinondonialifarikidunianamazishiyakeyakafanyikahukoSame,Kilimanjaro.
Mfanyakazimwingine LuanganoKikoti alifariki dunia asubuhi ya Jumamosi ya
Aprili5mwakahuukatikahospitaliyaTumaini,DaresSalaam.
Shirika pia lilimpoteza Batholomeo Brashi aliyekuwa AfisaNyumba Msaidizi
Mkoa wa Iringa aliyefariki mchana wa Oktoba 9 katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili na ambaye alizikwa kwaoMpanda. Mwingine ni Melesiana Casturi
aliyekuwamhudumuwaofisiBukoba aliyefariki tarehe21 Septemba, 2014na
Joseph Lyapula aliyekuwa Boharia Mkoani Mwanza ambaye alifariki tarehe 1
Novemba,2014katikaHospitaliyaMwananchiJijiniMwanza.Alizikwanyumbani
kwaoHekaManyoniSingidaNovemba4mwakahuu.
“Mungu amewapenda zaidi na imempendeza yeye kuwachukua wenzetu
kutanguliakatikasafariambayosotetutapitanakilamtukwawakatiwakeaujuao
MolaMaulana,”alisemaMchechu.
Amewashukuru wale wote ambao waliweza kwenda kutoa pole na kuwaona
ndugu na familia ya Marehemu katika kipindi kigumu cha maombolezo na
kwambauwepowaoulikuwaniuwakilishiwaShirikanaWafanyakaziwote.
Amewapapolewafanyakaziwote,marafikiwakaribuwaMarehemu,nduguna
jamaawote,MunguazilazerohozaMarehemumahalapemaPeponi.
AMINA!
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com22
Na Mwandishi Wetu,
Pato la ndani la Taifa lolote duniani
hutokana na mchango wa sekta
mbalimbali za uzalishaji na huduma. Katika
sekta hizi aghalabu sekta ya nyumba
imejitokeza kuwa na mchango mkubwa
katika kila nchi kutokana na ukweli kuwa
imejichukulia umuhimu wa pekee katika
maisha ya kila siku ya binadamu duniani
kote.
Ukweli huu upo dhahiri kwa kuwa huwezi
kukuta mji wowote mkubwa au mdogo
duniani kote usio na nyumba za makazi,
majengo ya biashara kama hoteli, kumbi za
mikutano, shule na vyuo. Majengo mengine
yanatumika kwa uzalishaji kama viwanda na
sehemu za kutolea huduma mbalimbali.
Ni ukweli usiopingika kuwa sekta ya
nyumba inayazunguka maisha ya kila siku ya
binadamu. Sekta hii kwa kiasi kikubwa ndio
inayomtambulisha binadamu na maendeleo
yake au ustaarabu wake kwani kama mji
au Jiji limepangwa vema na kujengeka
kikamilifu basi taswira inayojengwa kwa
watu wa Jiji lile na nchi lililopo huwa ni
chanya kwamba nchi hiyo imeendelea na
watu wake wana uchumi mzuri.
Hii ndio sababu iliyolifanya Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) kuandaa mpango
mkakati wa miaka mitano 2010/11-
2014/15 wa kuleta mapinduzi katika
sekta ya nyumba hapa nchini. Mkakati huo
umelenga kuhakikisha kuwa sekta hii inatoa
mchango mkubwa katika kukuza pato la
Taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Taarifa za kitaalamu juu ya mchango wa
sekta ya nyumba kwa pato na uchumi wa
Taifa hapa nchini zinaonyesha kuwa sekta
hiyo inatoa mchango wa asilimia 1.0 tu huku
sekta hiyo hiyo katika nchi zilizoendelea
huchangia kati ya asilimia 50 mpaka 70 ya
pato la Taifa kwa mwaka.
Katika kuhakikisha sekta ya nyumba
inachangia kwa kiasi kikubwa pato la
Taifa mpango mkakati wa NHC unalenga
kuhakikisha kuwa sekta hii inakuza pato na
uchumi wa Taifa hadi kufikia asilimia 11.
Kwa sasa Tanzania inakabiliwa na
changamoto ya uhaba mkubwa wa nyumba
bora ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya
nyumba 3,000,000 huku pengo hilo likikua
kwa takriban nyumba 200,000 kwa mwaka.
Upungufu wa nyumba ni mkubwa zaidi
sehemu za mijini ambako asilimia 37.5 ya
Watanzania ndiko wanakoishi. Shirika la
Nyumba la Taifa likiwa chombo cha Serikali,
linatarajiwa kukabiliana na changomoto hii.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kutokana na
kuongezeka kwa mahitaji ya nyumba nchini
na mchango wa nyumba katika kukuza
ustawi wa wananchi, Serikali ililiagiza
Shirika kujielekekeza zaidi kwenye ujenzi
wa nyumba badala ya usimamizi wa miliki
zake pekee. Kwa kupitia ujenzi wa nyumba
na hasa zile za gharama nafuu, Shirika
linatakiwa kuwawezesha wananchi kumiliki
nyumba kupitia fursa ya Sheria za Hati
Pacha na Mikopo ya Nyumba za mwaka
2008.
Ili kufanikiwa katika kukidhi matarajio
ya serikali kwa upande mmoja na yale
ya wananchi kwa upande wa pili, serikali
iliagiza NHC kutumia miliki zake kwa ajili
ya maendeleo na kuweza kujiendesha
kibiashara.
Shirika la Nyumba la Taifa limekuwa katika
safari ndefu ya kuleta mageuzi katika sekta
ya miliki nchini tangu Serikali ilipoamua
kufanya mageuzi katika utendaji kazi na
uendeshaji kazi wake. Katika safari hii,
Shirika limepewa jukumu la kutatua uhaba
wa nyumba pamoja na kukuza mchango wa
MCHANGO WA NYUMBA
NHC YADHAMIRIA KUONGEZA MCHANGO WA
NYUMBA KATIKA PATO LA TAIFA
Mchoro wa namna litakavyokuwa jengo la Eco Residence litakaloanza kujengwa katika kitalu namba 67 kwenye makutano ya mitaa ya Ngano na Wakulima, Dar es Salaam litakapokamilika litakuwa na ghorofa 16, sehemu za makazi 118 na kuwa makazi ya watu zaidi ya 840 wakati kabla lilikuwa makazi ya familia moja
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com23
1. Naanzakuwasalimu,wafanyakaziwanyumba
Nyoteninawaheshimu,awaongozemuumba,
Tuyashikeyamuhimu,ilitusijekuyumba
Shirikasasalapaahebutufungemikanda
2. Leonasemaukweli,siyokamanajigamba
Mamboyameshamiri,uwanjanitunatamba
Tuwesotestamili,mafanikiokuchimba
Shirikasasalapaa,hebutufungemikanda
3. Mikakatitulopanga,neemayajitokeza
Hakunawakutupinga,kwapamojatumeweza
Tumetengezamizinga,tuachanenakucheza
Shirikasasalapaa,hebutufungemikanda
4. TulipokuwaSingida,malengotumeyaweka
Tukamilishekwamuda,tusijetukabweteka
Kilamjumbeshuhuda,malengokukamilika
Shirikasasalapaa,hebutufungemikanda
5. Kwapamojatunaweza,kujenganyumbakwa
wingi
Tuwezekutekeleza,hiyoserayamsingi
Butitumeshalikaza,kujenganyumbakwawingi
Shirikasasalapaahebutufungemikanda
6. KwaspiditumeanzaMindu,UbungoKibada
KatavinakuleMwanza,MchikichiniSingida
Zakuuzanakutunza,hiyondiyoyetumada
Shirikasasalapaa,hebutufungemikanda
7. Natoamsisitizo,bidiiiwekazini
Iliujepatatuzo,kaskedikusaini
Ukiletamatatizoutajatozwafaini
Shirikasasalapaa,hebutufungemikanda
MALENGA WETU
8. Tulikotokazamanitulikuwanaaibu
Viongozinajiranihatawalemaswaibu
Tulisemahadharani,rushwaimetuaribu
Shirikasasalapaahebutufunge
mikanda
9. TumshukuruRabuki,Mchechu
katuletea
KajanusuruShirika,leotunaendelea
Rushwahaitasikika,mabaya
kutokomea
Shirikasasalapaahebutukazemikanda
10. Ewekipenzichawatu,juhudizo
endeleza
Angaliakilamtu,kipatochekuongezeka
Tupamojakilakitu,Jahazikuliongoza
Shirikasasalapaa,hebutufunge
mikanda
11. Viongoziwaridhika,ubingwa
tumeshapewa
Tusijetukapotoka,kwasifa
tunazopewa
Jahazilikitobokatutakujalaumiwa
Shirikasasalapaa,hebufungeni
mikanda
12. Tamatinimeshafika,kalamunaweka
chini
Niwaachewahusika,waingia
mitamboni
Manenohayakushikatukiwepovituoni
Shirikasasalapaa,hebutufungeni
mikanda
sekta hii ambayo mchango wake kwenye
pato la Taifa bado upo chini, ukilinganisha
na uwezo wa sekta nzima ya ujenzi wa
nyumba nchini.
Kutokana na umuhimu wa sekta ya
nyumba katika kuchangia maendeleo
ya jamii na ukuaji wa uchumi, Shirika
lilitayarisha mpango mkakati wa miaka
mitano ambao umekuwa dira ya kuleta
msukumo mpya wa sekta ya nyumba
nchini.
Kutokana na kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa kutekelezwa kwa mpango
mkakati wa 2010/11-2014/15 thamani
ya mali za shirika ambazo kwa asilimia
kubwa ni nyumba na majengo mbalimbali
inaonyesha kukua hadi kumiliki majengo
2,389 yenye sehemu ya nyumba 17,111
yenye thamani ya shilingi trilioni 2.911
Juhudi zilizofanywa za mabadiliko
ya sekta ya nyumba zilianza Machi
2010, ambapo Serikali iliteua uongozi
mpya wa Shirika kwa maana ya Bodi
ya Wakurugenzi na Menejimenti kwa
nia ya kuimarisha utendaji na ufanisi
wa Shirika ili liweze kuwa na mchango
mkubwa katika kutatua tatizo la uhaba
wa nyumba nchini.
Jukumu la kwanza la uongozi huu,
lilikuwa ni kutayarisha mpango mkakati
wa ambao umeainisha mwelekeo mpya
na malengo mapya ya Shirika.
Kwa kiasi kikubwa uongozi wa NHC
ulioteuliwa mwaka 2010 unahusika
na kuongezeka kwa kasi ya ujenzi wa
nyumba za Shirika ambazo ama zinauzwa
au kupangishwa. Ni uongozi huu ambao
umeleta chachu ya kuona kuwa sekta
ya nyumba kupitia NHC inachangia
kwa kiwango cha juu zaidi katika ukuaji
wa pato la ndani kwa kujiwekea lengo
la kuchangia asilimia 11 ya pato la Taifa
kwa kushirikisha wadau wa sekta hii
zikiwemo benki. Hivi sasa nyumba za
gharama nafuu zimejengwa katika mikoa
takriban 19 huku nyumba za vitega
uchumi na za makazi kwa ajili ya watu wa
kipato cha kati na juu zikiwa zimeshamiri
kujengwa na kuuzwa katika maeneo
mbalimbali nchini.
HEBU TUFUNGE MIKANDA
(Doctor)MOHAMMEDMNEKA
BOX2977,DARESSALAAM.
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com24
• Asisitizauadilifukatikautendaji
kaziilikuletatija
• Atakakasiyaujenziwanyumbaza
gharamanafuuiendelezwe
• Wafanyakaziwaazimiakuongeza
tijakatikautendaji
Na Mwandishi Wetu,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Alfayo Japan
Kidata amefungua kikao cha Baraza Kuu
la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC), akisisitiza uadilifu mkubwa
miongoni mwa wafanyakazi ili kuliwezesha
Shirika kutoa huduma za makazi zilizo bora
kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kikao hicho kilichofanyika kwenye Hoteli
ya Tanga Beach Resort, jijini Tanga, Bw.
Kidata alisema kuwa uadilifu ndiyo
utakaowawezesha wafanyakazi wa Shirika
kutenda kazi zao kwa ufanisi mkubwa.
Alisema kuwa wafanyakazi hao wakitenda
kazi zao kwa juhudi na maarifa huku
wakitambua umuhimu mkubwa wa sekta
ya nyumba waliyopewa dhamana ya
kuisimamia, kutalifanya Shirika hilo kuweza
kutekeleza malengo yake ya kuwajengea
Watanzania nyumba bora.
Alisema utendaji kazi wenye uwazi,
uadilifu na weledi wa hali ya juu ndiyo
utakaowaongezea heshima kubwa
wafanyakazi hao na kujenga taswira nzuri
ya Shirika katika jamii ya watanzania.
Akizungumzia kasi ya ujenzi wa nyumba
za gharama nafuu katika miji mbalimbali
ya Halmashauri za Miji na Wilaya nchini,
Katibu Mkuu huyo alilipongeza Shirika
kwa kurejesha utaratibu huo wa kizalendo
aliouanzisha Baba wa Taifa.
“ Nafahamu kuwa hivi sasa mmeshaifikia
mikoa 19 na mnayo matumaini makubwa
ya kufikia mikoa yote kufikia Desemba
mwaka huu. Utaratibu huu unaolenga
kuwawezesha wananchi wa kipato cha kati
na chini kumiliki nyumba, umepongezwa
sana na Serikali Kuu na viongozi mbalimbali
wakiwemo Waheshimiwa Wabunge.
Hivyo, mnayo dhima na jukumu kubwa la
kuusimamia mpango huu ili ndoto hiyo ya
kuwawezesha watu wengi kumiliki nyumba
iweze kutimizwa,”alisema.
Alisema kwa kufanya hivyo Shirika litakuwa
limeweka msingi mkubwa wa kukumbukwa
katika Taifa letu na vizazi vijavyo kama
tunavyomkumbuka Baba wa Taifa wa
kueneza ujenzi wa nyumba za gharama
nafuu katika miji mingi baada ya Uhuru wa
Taifa letu.
“ Ili kuzifanya nyumba hizo zinazojengwa
kuwa nafuu, narudia kusisitiza agizo
alilolitoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete kuwa Halmashauri za Miji
na Wilaya zilipatie Shirika la Nyumba na
waendelezaji wengine wa Miliki maeneo
ya kujenga nyumba hizo bila kuhitaji fidia
kubwa,” alisema.
Alisema pamoja na juhudi na ubunifu
mbalimbali uliofanywa na NHC uliosaidia
kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba za kada
zote, Serikali inaamini kuwa kasi ikiongezeka
zaidi katika ujenzi wa nyumba, licha ya
kuwa Shirika litakuwa limetekeleza ilani
ya uchaguzi ya chama tawala na litakuwa
limeisaidia pia Serikali katika juhudi zake za
kuondoa umaskini nchini.
Likiwasilisha maazimio ya Mkutano huo wa
Baraza Kuu, yaliyowasilishwa na Meneja
wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo,
wajumbe wa Baraza hilo wamemshukuru
Katibu Mkuu kwa kuwa mstari wa
mbele katika kufanikisha uandaaji wa
Mpango Mkakati wa Shirika wa miaka
kumi unaoanzia 2015. Aidha, Baraza
linamshukuru kwa kufanikisha upatikanaji
wa hati miliki ya eneo la Kawe, Tanganyika
Packers.
Kadhalika, Baraza hilo limeazimia kila
mkoa uhakikishe unaongeza mapato yake
ili kupata uwezo wa kujiendesha kibiashara.
Ili kufanikisha hilo, jitihada zitafanyika
kwa kila mkoa kuwezeshwa kupata walau
mradi mmoja wa jengo la biashara ambalo
litaongeza mapato ya mkoa husika.
Aidha, alisema kwa kuwa ujenzi wa
nyumba za gharama nafuu ni kioo cha
Shirika la Nyumba mbele ya Jamii, jitihada
zote zichukuliwe kuhakikisha kwamba
miradi yote inajengwa na kusimamiwa
BARAZA LA WAFANYAKAZI
KATIBU MKUU ARDHI AFUNGUA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI
Picha ya pamoja ya Wajumbe wa kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa kilichofanyika hoteli ya Tanga Beach Resort, Tanga
JULAI - DESEMBA 2014 /Nyumba Newsletterwww.nhctz.com25
MILIKI NYUMBA
kwa kuzingatia ubora, muda na gharama
iliyokusudiwa.
Baraza hilo liliazimia pia kuwa makusanyo
ya kodi ni uti wa mgongo wa uendeshaji
wa majukumu mbalimbali ya Shirika,
hivyo mikoa yote inawajibika kukusanya
mapato yote kwa wakati. Azimio jingine ni
kuhakikisha kuwa mikoa yote iwezeshwe
kufanya matengenezo yote ya lazima kwa
majengo ya Shirika ili kuboresha huduma
kwa wapangaji.
Azimio jingine la Baraza lililotolewa ni
kuongeza jitihada za kuuza na nyumba na
kukusanya mapato ya mauzo ya nyumba
hizo zifanyike siyo tu na kitengo cha mauzo
bali liwe jukumu nambari moja kwa kila
mfanyakazi na hasa katika kipindi hiki
ambapo Shirika limepanua wigo wa ujenzi
wa nyumba za makazi na biashara nchi
nzima.
Naye, Mkukurugenzi Mkuu wa NHC, Bw.
Nehemia Kyando Mchechu, alisema licha
ya Shirika kupata mafanikio kadhaa,, zipo
changamoto zinazoikabili sekta ya nyumba
ikiwemo gharama kubwa ya vifaa vya ujenzi
na upatikanaji wa mikopo ya nyumba ya
muda mrefu yenye riba nafuu.
Bw. Mchechu alisema kuwa, ikiwa Serikali
itapunguza kodi gharama ya nyumba
inaweza kupungua, jambo ambalo
linaweza kuwasaidia wananchi wa kawaida
kuzinunua.
“Tunaiomba Serikali kuangalia upya kodi
zilizoongezeka, kwa sababu zimechangia
kupanda kwa gharama za nyumba,”alisema
Mchechu.
Alisema, mkakati uliopo ni kuhakikisha
kuwa, miradi iliyoanzishwa inakwisha katika
kipindi kilichopangwa ili iweze kusaidia
wananchi.
1 Chukua fomu ya kununua Nyumba kutoka ofisi yoyote ya mkoa popote nchini au kwenye tovuti ya shirika.
2 Rudisha fomu iliyojazwa ikiwa na uthibitisho wa kulipiwa na malipo ya 10% (ikiwa na VAT) ya thamani ya Nyumba husika.
3 Maombi yako yatapitiwa kwa umakini ili kuhakikisha kunakuwa na usawa katika uchaguaji wa watu wanaostahili kulingana na Vigezo na masharti ya NHC na taratibu za Jamhuri ya Tanzania.
4 Kama umefanikiwa, utatumiwa barua za kuthibitishiwa kukubaliwa maombi yako. Barua zitatolewa kwa wote waliokidhi Vigezo vilivyowekwa.
5 Utatakiwa kulipa 90% iliyobaki kulingana na thamani ya nyumba husika
ndani ya siku 90 tangu umepewa.
6 Endapo ukishindwa kulipa ndani ya siku 90, NHC itatoa nyumba kwa Waombaji waliopo kwenye orodha ya wanao subiri.
7 Orodha ya wanaosubiri itakuwa na majina ya waombaji waliolipia malipo ya
mwanzo lakini wakakosa nafasi kwa kuwa nyumba zote zilishapata watu.
8 Kama ukishindwa kulipia kiasi kilichobakia, au ukakosa nafasi ukiwa kwenye orodha ya wanaosubiri, kiasi cha 10% kilicholipwa kinaweza kutumiwa kulipia kwenye miradi mingine ya NHC na waliopo kwenye orodha ya wanaosubiri au kurudishiwa pesa zao.
9 Mauzo ya nyumba za mradi husika yatatangazwa yamefungwa pindi Waombaji waliofanikiwa kupata nyumba wamemaliza kufanya malipo yao yote.
10 NHC itafanya utaratibu wa kutafuta hati za nyumba na kisha kuwapatia wanunuzi walioweza kulipia pesa zote taslimu au kupitia taratibu za mkopo. Miliki nyumba yako sasa. Kumiliki nyumba
Utaratibu huu unaolenga kuwawezesha wananchi wa kipato cha kati na chini kumiliki nyumba, umepongezwa sana na Serikali Kuu na viongozi mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Wabunge
HATUA RAHISI ZA KUMILIKI
NYUMBA YAKO LEO
Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014 www.nhctz.com26
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFAMAKAO MAKUU S.L.P 2977 SIMU: +255 22 2105002
NUKUSHI: +255 22 2105000 BARUA PEPE: dg@nhctz.com
TOVUTI: www.nhctz.com
1. MKOA WA UPANGA S.L.P 9634, Dar es Salaam SIMU: 022 2128314 022 2128305 / 022 2128306
2 . MKOA WA KINONDONI S.L.P 23200, Dar es Salaam SIMU: 022 2667150
3 . MKOA WA ILALA S.L.P 25110 Dar es Salaam SIMU: 022 2863126
4. MKOA WA TEMEKE S.L.P 45674 Dar es Salaam SIMU: 022 2866829 022 2863121
5. MKOA WA MWANZA /GEITA /SIMIYU S.L.P 1683, Mwanza SIMU: 028 2503047 028 2503048
6. MKOA WA MTWARA S.L.P 67, Mtwara SIMU: 023 23333
7. MKOA WA TABORA S.L.P 166, Tabora SIMU: 026 2604530 026 2604752
8. MKOA WA MBEYA/NJOMBE S.L.P 541, Mbeya SIMU: 025 2502482 025 2500699
9. MKOA WA ARUSHA S.L.P 883, Arusha SIMU: 027 2755052 027 2502995
10. MKOA WA KILIMANJARO S.L.P 1458, Moshi SIMU: 027 2755052 027 2754080
11. MKOA WA TANGA S.L.P 5041, Tanga SIMU: 027 2644479 027 2644480
12. MKOA WA MOROGORO S.L.P 892 Morogoro SIMU: 023 2603268 023 2604535
13. MKOA WA IRINGA S.L.P 206, Iringa SIMU: 026 2702603
14. MKOA WA MARA S.L.P 257 Musoma SIMU: 028 2622032
15. MKOA WA DODOMA S.L.P 391, Dodoma SIMU: 026 2323151
16. MKOA WA SHINYANGA S.L.P 478, Shinyanga SIMU: 028 2762045
17. MKOA WA KAGERA S.L.P 369, Bukoba SIMU: 028 2220035/36
18. MKOA WA SINGIDA S.L.P 254, Singida SIMU: 026 2502332
19. MKOA WA KIGOMA S.L.P 271, Kigoma SIMU: 028 2802844
20. MKOA WA LINDI S.L.P 206, Lindi SIMU: 023 2202054
21. MKOA WA RUVUMA S.L.P 65, Songea Ruvuma
22. MKOA WA KATAVI S.L. P 375 MPANDA,KATAVI.
TUNAJENGA TAIFA LETU
top related