utangulizi: mradi wa usalama wa umiliki wa ardhi kwa...

19
Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa wanawake (WOLTS) E. Daley, K. Lanz, A. Mhinda, Z. Driscoll, J. Ndakaru, J. Grabham na E. Kereri Warsha ya wadau mbalimbali juu ya Jinsia, Madini na Ufugaji Tanzania 16 Novemba 2017 Arusha Maandishi © Timu ya WOLTS. Picha zote © Timu ya WOLTS.

Upload: others

Post on 22-Jul-2020

26 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa wanawake (WOLTS)

E. Daley, K. Lanz, A. Mhinda, Z. Driscoll, J. Ndakaru, J. Grabham na E. Kereri

Warsha ya wadau mbalimbali juu ya Jinsia, Madini na Ufugaji Tanzania

16 Novemba 2017

Arusha

Maandishi©TimuyaWOLTS.Pichazote©TimuyaWOLTS.

Page 2: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 2

WOLTS ni mradi wa utafiti wa kimkakati wa muda mrefu kwa nchi mbili (Tanzania na Mongolia), mradi huu una lengo la kusaidia kuboresha usawa wa kijinsia katika usimamizi wa ardhi - na hivyo kuimarisha na kulinda haki za ardhi kwa wanawake na makundi maalumu. Utafiti huu ulianza mwezi Oktoba 2015 na sasa umekamilisha miaka miwili kama mradi wa majaribio uliopitia awamu sita tofauti katika utekelezaji. Utafiti ulikua na lengo la kuchunguza mwingiliano kati ya jinsia, ardhi, uchimbaji madini na ufugaji kupitia ziara zilizofanyika nchini Mongolia na Tanzania

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

WOLTS ni nini?

Page 3: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 3

WOLTS ina malengo makuu matatu ambayo ni: •  Kuanzisha msingi wa ushahidi juu ya vitisho vya ndani na nje kwa usalama

wa ardhi kwa wanawake, katika mtazamo mpana wa uwekezaji na kuchukuliwa kwa ardhi.

•  Kuimarisha uwezo wa jamii, AZAKI na serikali za mitaa ili kulinda haki na usalama wa haki za ardhi kwa wanawake kwa njia ambayo itachochea usawa wa kijinsia katika usimamizi wa ardhi ya jamii.

•  Kuona marekebisho mazuri katika umiliki na usalama wa ardhi kwa wanawake na makundi maalumu ndani ya jamii na nchi zinazofikiwa na mradi huu, ili kushikirikishana na kusambaza taarifa za yale tuliyojifunza kupitia mradi kwa pamoja .

Malengo ya WOLTS

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 4: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 4

Mradi unaangalia mahusiano ya jinsia, ardhi, ufugaji na uchimbaji madini jambo ambalo siyo wengi wamelifikiria na kulifahamu vizuri:

•  WOLTS inachangia kujaza pengo hili la ujuzi kwa njia ya vitendo

Uzoefu uliopatikana hadi sasa unaonesha faida za kuchukua njia ya muda mrefu ili kuboresha wajibu na usawa wa kijinsia katika usimamizi wa ardhi:

•  na kuchukua mbinu madhubuti ili mabadiliko yoyote ya muda mrefu katika kanuni za jamii husika kuhusu jinsia na ardhi, yaweze kupimwa wazi

Uwezo wa kuingiza ulinzi wa haki za ardhi kwa wanawake katika ulinzi wa ardhi ya jamii huchukua muda kujengeka:

•  kuanzisha ushirikiano na AZAKi, serikali za mitaa, makampuni ya madini na jamii kwa njia ya utafiti shirikishi wa muda mrefu na mkakati wa kushirikiana inaweza kusaidia uelewa huo kukua

Mantiki ya mradi wa WOLTS Sababu/umuhimu wa WOLTS

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 5: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 5

Mbinu ya muda mrefu katika kutafuta mabadiliko halisi katika ngazi ya jamii, kwa kuzingatia ushirikiano na mashirika ya ndani.

Mafunzo na kujenga uwezo wa kulinda na kuimarisha haki za ardhi kwa wanawake na makundi maalumu ndani ya jamii.

Mbinu thabiti ya utafiti - iliyoundwa kuimarisha uelewa wa matumizi bora ya ardhi na kuchochea mazungumzo na mijadala ndani ya jamii kuhusu mabadiliko ambayo yanaweza kuhitajika na jinsi yanavyoweza kufikiwa.

Njia shirikishi, kuanzisha na kuendeleza/kuzitumia mbinu za utafiti wa majaribio ya miaka 2 ikiwa ni pamoja na kutoa mrejesho kwa jamii kwa njia ya mikutano ili kukusanya maoni ya jamii.

Njia ya mradi wa WOLTS

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 6: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 6

Utafiti wa Mradi wa WOLTS Nchini Tanzania na Mongolia

Usawa wa kijinsia kwa kuzingatia Kanuni na sheria (wanawake kuruhusiwa kuwa na / kuomba / kujiandikisha kumiliki ardhi moja kwa moja au kwa pamoja na wanaume) Shughuli za uchimbaji (mdogo, wa kati, au mkubwa) na aina za madini mbalimbali Historia na mila za ufugaji kwa wafugaji wanaohamahama (nchi nzima ya Mongolia – na kwa Tanzania - sehemu za kaskazini na za kati)

Jamii/vijiji viwili ambavyo WOLTS imefanya utafiti kwa kila Nchi: Ø  Mongolia – Kijiji cha Bornuur na Dalanjargalan

Ø  Tanzania – Kijiji cha Mundarara na Naisinyai

Mila na imani za kidini zinazo fanana kati ya jamii hizi kwenye kila nchi na idadi kubwa ni kundi la nguvu kazi

Ila utofauti ni katika viwango na ukubwa wa miradi ya uchimbaji; na aina ya mahusiano na uchumi kwa ujumla

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 7: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 7

Historia ya Tanzania

•  Historia ya muda mrefu ya biashara katika bara la Afrika na Ghuba (Sultani wa Oman huko Zanzibar)

•  1891 – Koloni la Ujerumani (Tanganyika) •  1920 – Tanganyika chini ya mamlaka ya Uingereza baada ya vita vya kwanza vya dunia •  1923 – Sheria ya Ardhi inalenga sheria ya kawaida ya Kiingereza na umiliki wa mara mbili •  1961 – Uhuru - Nyerere akiongoza (Jamhuri mwaka 1962, Tanzania mwaka 1964) •  1963 – Utaratibu na kupitishwa kwa sheria ya Kimila (ulioandaliwa sheria ya ardhi ya kitamaduni/

kimila) •  1967 – Azimio la Arusha; kuanza kwa ujamaa •  1974 – Uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa •  1995 – Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi

1999 - Sheria ya Ardhi ya vijiji - hufafanua matumizi ardhi kwa aina tofauti za ardhi:

•  Ardhi ya jumla (mijini na uwekezaji), Ardhi ya Kijiji, Ardhi iliyohifadhiwa (kwa mfano mbuga za wanyama za kitaifa)

•  Ardhi ya Kijiji inasimamiwa na serikali za vijiji ila watu binafsi wanaweza kupata hati za kimila (CCRO) ili kurasimisha ardhi zao

Marekebisho mbalimbali yalifanyika, ikiwa ni pamoja na yale ya mwaka 2004 na 2007 iliyosisitiza Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka mipango ya matumizi bora ya ardhi ya kijiji (pamoja na kutenga maeneo, yakiwemo maeneo ya malisho)

Mchakato wa marekebisho ya Sera ya Ardhi

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 8: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 8

•  Kuweka mazingira ya kitaifa na kuchagua jamii

•  Kufanya utafiti wa awali ili ujulishe shughuli za mradi kwa baadaye na utumike kama mwongozo wa kupima matokeo ya mradi kwa baadaye

•  Kufanya utafiti shirikishi wa kuendeleza uelewa wa mipango ya umiliki wa ardhi katika jamii zilizochaguliwa na kubaini vitisho/changamoto za haki za ardhi kwa wanawake na makundi maalumu

•  Kushirikisha jamii matokeo ya utafiti ili kusaidia kuandaa zana na mchakato wa kujengea uwezo

•  Kushirikishana yale tuliyojifunza kitaifa na kimataifa

Mbinu za WOLTS

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 9: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 9

•  Uchunguzi wa kina wa historia na ukaguzi wa fasihi ili kujenga msingi katika

mchakato wa uteuzi wa jamii na uchambuzi wa baadaye wa matokeo ya kazi zinazofanyika ndani ya jamii.

•  Kuweka vigezo vya kuchagua, kutembelea jamii, na kuchagua jamii za kufanyia kazi na ambazo zilionekana kuwa wazi kwa kufanya kazi na timu ya WOLTS ili kuboresha usawa wa kijinsia katika usimamizi wao wa ardhi.

Awamu ya 1 na 2 - Kuanzishwa na uchaguzi wa Jamii

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 10: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 10 Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 11: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 11

•  Takwimu za utafiti wa awali huongeza uelewa wa idadi ya watu

waliochaguliwa, ustawi wa maisha yao, mienendo ya kijinsia na mitazamo ya usalama wa umiliki wa ardhi

•  Msingi wa utafiti katika ngazi ya jamii – hulenga katika kuarifu na kuandaa jamii juu ya ujio wa utafiti shirikishi

•  Inajikita katika uchambuzi wa kina zaidi juu ya kipindi cha utafiti na ushirikiano wa jamii

Awamu ya 3 - Utafiti wa Msingi/awali

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 12: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 12

10% ya Kaya kutaka jamii zote mbili zilihojiwa : •  Naisinyai: kaya 125; kati ya hizo, kaya 103 zilichaguliwa bila kuzingatia vigezo maalumu, na kaya

22 za ziada zinazoongozwa na wanawake •  Hivyo, jumla ya kaya 28 zinaongozwa na wanawake na kaya 97 zinaongozwa na wanaume

•  Mundarara: kaya 71; kati ya hizo, kaya 57 zilichaguliwa bila kuzingatia vigezo maalumu, na kaya 14 za ziada zinazoongozwa na wanawake

•  Hivyo, jumla ya kaya 21 zinaongozwa na wanawake na 50 zinaongozwa na wanaume Taarifa nyingi zilizowasilishwa ni zile tu zilizotokana na sampuli ya watu waliochanguliwa bila kuzingatia vigezo maalumu; na taarifa kutoka kwenye kaya za ziada zinazoongozwa na wanawake zilitumika tu kutofautisha ushiriki wa kijinsia

kwa mfano kuonyesha tofauti kati ya kaya zinazoongozwa na wanaume na kaya zinazoongozwa na wanawake pamoja na tofauti kati ya ushiriki wa wanaume na wa wanawake

Idadi ya washiriki katika utafiti wa awali

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 13: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 13

•  Ugumu wa kuwapata washiriki waliochaguliwa bila kuzingatia vigezo maalumu sababu zikiwa ni changamoto ya mawasiliano (taarifa kuchelewa), watu kuwa na majukumu mengi mbalimbali na wengine kuwa mbali, n.k.

•  Hata hivyo, dodoso ziliandaliwa vizuri ila baadhi ya maswali hayakueleweka kirahisi hivyo hupelekea wale wanaotafsiri kushindwa kufafanua vizuri na hivyo wahojiwa pia hushindwa kutoa taarifa sahihi.

•  Masuala mengine ya kiujumla ya kumbukumbu, haikua rahisi kwa wahojiwa kufahamu taarifa sahihi za wanakaya wengine.

•  Ushiriki/uwepo wa wale wasioalikwa kwenye mahojiano huenda iliathiri mahojiano.

•  Upotoshwaji taarifa/kutotoa taarifa sahihi juu ya wanajamii kujihusisha na uchimbaji wa madini (utafiti wa awali)

•  Ukukusanyaji wa taarifa kwenye jamii ulitumia siku nyingi!

Changamoto za utafiti wa awali

Introduction to WOLTS – Multi-Stakeholder Workshop on Gender, Mining and Pastoralism in Tanzania, 16 November 2017, Arusha

Page 14: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 14

•  Unachangia kuelewa aina ya mahusiano ya kijinsia na mipangilio ya ardhi, na vitisho/changamoto za haki za ardhi kwa watu tofauti katika jamii zilizochaguliwa.

•  Utafiti huu uliundwa ili kujenga hoja kutokana na utafiti wa awali na kufanya uchunguzi wa ndani zaidi.

•  Zana na mbinu mbalimbali zilitumika kuhakikisha kwamba taarifa sahihi zinapatikana – ikiwa ni pamoja na ramani ya maliasili na maeneo ya kuhamia, uchambuzi wa kazi za msimu, uchambuzi wa taasisi na wadau mbalimbali.

•  Uchaguzi wa mazoezi shirikishi, mahojiano ya makundi lengwa (FGDs) na mahojiano ya mtu mmoja mmoja yaliongozwa na utafiti na uchambuzi hadi wakti huu.

Awamu 4 – Utafiti Shirikishi

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 15: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 15

Tulitaka aina tofauti za watu kwa majadiliano na mahojiano haya, ili kuwakilisha tabia tofauti za watu katika kijiji chote •  Naisinyai: mijadala ya makundi 13 na mahojiano ya watu binafsi 12, ikihusisha jumla

ya watu zaidi ya 104

•  Mundarara: mijadala ya makundi 13 na mahojiano ya watu binafsi 12, ikihusisha zaidi ya watu 92

Idadi ya washiriki kwenye utafiti shirikishi

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 16: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 16

Utafiti shirikishi ndani ya jamii – zoezi la ramani

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 17: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 17

•  Wakati mwingine ni vigumu kuyapata makundi (FGDs) maalumu kwa ajili ya kujadiliana na pia wale wahojiwa binafsi wenye sifa zilizokusudiwa ---na sababu ni pamoja na ugumu wa mawasiliano, majukumu mengi walionayo watu na wengine kuwa mbali, n.k.

•  Usuluhishi wa makini katika mijadala ya makundi (FGDs) ulikuwa muhimu ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu aliyetawala mjadala huo kuwazidi washiriki wengine.

•  Katika baadhi ya mijadala na mahojiano viongozi au waangalizi walikuwepo kwenye mijadala na hivyo ilikuwa vigumu kuchunguza jinsi washiriki wengine walivyozingatia kile walichosema, kama je! wanaweza kuwa waaminifu kabisa bila hofu? (hasa wakati wa kuzungumza juu ya rushwa)

•  Kwa ujumla, watu walikuwa wakisema nini walidhani tunataka kusikia (siyo uhalisia wa hali ilivyo)

•  Wakati mwingine ilikuwa vigumu kama watafiti kukaa tu na kusikiliza hadithi zinazotolewa, hasa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji nk

Changamoto za utafiti shirikishi

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 18: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 18

•  Kutoa mrejesho wa utafiti kwa jamii, ni muhimu ili kusaidia kuandaa zana za

utekelezaji na kuweka utaratibu wa kuimarisha usawa wa kijinsia ikizingatia mazingira yenye changamoto juu ya usalama wa ardhi.

•  Inatambua umuhimu wa kushirikishana kwa mapana na usambazaji wa zana zilizotengenezwa na yale tuliojifunza wakati wa utekelezaji katika ngazi ya kitaifa na kimataifa

Awamu ya 5 na 6 – upimaji na usambazaji wa wa zana

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.

Page 19: Utangulizi: Mradi wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi kwa ...mokoro.co.uk/.../WOLTS...Presentation_Kiswahili.pdf · Sheria ya kuwepo kwa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ambayo iliweka

Slide 19

Asanteni

Utangulizi wa WOLTS - Mkutano wa Washirika kuhusu Jinsia, Uchimbaji wa Madini na Ufugaji Tanzania, 16 Novemba 2017, Arusha.