teolojia ya madaraka

67
TEOLOJIA YA MADARAKA “Mipango ya Mungu ihusuyo uhusiano wake na wanadamu kupitia historia” Kimeandikwa na Chris V. Egemeier 1011 Aldon Street,Wyoming, MI 49509, USA www.vitabuvyakikristo.com

Upload: others

Post on 23-Jan-2022

6 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: TEOLOJIA YA MADARAKA

TEOLOJIA YA MADARAKA

“Mipango ya Mungu ihusuyo uhusiano wake na wanadamu kupitia historia”

Kimeandikwa na

Chris V. Egemeier

1011 Aldon Street,Wyoming, MI 49509, USA www.vitabuvyakikristo.com

Page 2: TEOLOJIA YA MADARAKA

TEOLOJIA YA MADARAKA Copyright © 2005 GMI Tanzania Publications GMI Publications ina haki zote za tafsiri ya kitabu hiki. Hairuhusiwi kuchapa na kuuza sehemu yo yote ya kitabu hiki bila ruhusa ya GMI Publications. Vilevile hairuhusiwi kuuza nakala za kikompyuta (digital copies) bila ruhusa ya GMI Publications Mfasiri – Steven Sherman Wahariri – Mch. Fraison Ismail, Martin Haule, na Steven Sherman Kama Biblia nyingine hazijatajwa, dondoo zote za kunukuu Biblia zinatumia Swahili Union Ver-sion (SUV): Haki miliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa. GMI Publications ni idara ya Grace Ministries International; misheni ifanyayo kazi na makanisa ya Neema duniani, pamoja na Wakristo wote wanaomwamini Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao.

Page 3: TEOLOJIA YA MADARAKA

YALIYOMO MAFUNDISHO YA MADARAKA ............................................................................................................. 1

UTANGULIZI .................................................................................................................................................... 1

UMUHIMU WA KUJIFUNZA KUHUSU MADARAKA ................................................................................. 2 SOMO LA KWANZA: MUNGU ANABADILISHA MIPANGO YAKE ....................................................................... 2 SOMO LA PILI: MADARAKA YA MUNGU KWA UFUPI ...................................................................................... 2 SOMO LA TATU: MADARAKA YANAPATANA NA HISTORIA YA WATU ............................................................. 3 SOMO LA NNE: KUFAHAMU MADARAKA KUNASAIDIA WAKRISTO KUYAJIBU MASWALI YAHUSUYO BIBLIA. 4 SOMO LA TANO: MAENDELEO YA UFUNUO ............................................................................................... 6

DARAKA LA USAFI ................................................................................................................................ 8 SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA USAFI ...................................................................................... 8 SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA USAFI .................................................................................................. 9 SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA USAFI ......................................................................................... 10 SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA USAFI ............................................................................................ 10 SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA USAFI......................................................................................... 11

DARAKA LA DHAMIRI ......................................................................................................................... 14 SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA DHAMIRI ............................................................................... 14 SOMO LA PILI: WATU DARAKA LA DHAMIRI ................................................................................................. 14 SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA YA DHAMIRI ................................................................................... 15 SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA DHAMIRI ....................................................................................... 16 SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA DHAMIRI ................................................................................... 17

DARAKA LA SERIKALI .......................................................................................................................... 19 SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA SERIKALI ................................................................................ 19 SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA SERIKALI ........................................................................................... 19 SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA SERIKALI ............................................................................. 20 SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA SERIKALI ................................................................................. 20 SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA SERIKALI ............................................................................. 21

DARAKA LA AHADI ............................................................................................................................. 23 SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA AHADI ................................................................................... 23 SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA AHADI ............................................................................................... 24 SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA AHADI ........................................................................................ 25 SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA AHADI ........................................................................................... 26 SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA AHADI ....................................................................................... 27

DARAKA LA SHERIA ............................................................................................................................ 29 SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA SHERIA .................................................................................. 29 SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA SHERIA .............................................................................................. 30 SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA SHERIA ....................................................................................... 30 SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA SHERIA .................................................................................... 34 SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA SHERIA ................................................................................. 36 SOMO LA SITA: MANENO YA MWISHO KUHUSU SHERIA ........................................................................ 38

DARAKA LA NEEMA ............................................................................................................................ 39 SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA NEEMA ........................................................................... 39 SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA NEEMA ........................................................................................ 39 SOMO LA TATU: UFUNUO WA SIRI KATIKA DARAKA LA NEEMA ........................................................... 41 SOMO LA NNE: WOKOVU KATIKA DARAKA LA NEEMA .......................................................................... 42 SOMO LA TANO: MWILI WA KRISTO KATIKA DARAKA LA NEEMA ........................................................ 43 SOMO LA SITA: MAAGIZO YA DARAKA LA NEEMA .................................................................................. 44 SOMO LA SABA: MAKOSA YA DARAKA LA NEEMA .................................................................................. 47 SOMO LA NANE: HUKUMU YA DARAKA LA NEEMA ................................................................................. 48 SOMO LA TISA: MATENDO YA ROHO MTAKATIFU KATIKA DARAKA LA NEEMA ................................. 49

Page 4: TEOLOJIA YA MADARAKA

DARAKA LA DHIKI KUU ....................................................................................................................... 51 SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA DHIKI KUU ..................................................................... 51 SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA DHIKI KUU ........................................................................................ 51 SOMO LA TATU: HALI YA WATU NA MAAGIZO YA DARAKA LA DHIKI KUU .......................................... 53 SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA DHIKI KUU .............................................................................. 54 SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA DHIKI KUU ........................................................................... 55

DARAKA LA UFALME .......................................................................................................................... 57 SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA UFALME ................................................................................ 57 SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA UFALME - MAHALI NA HALI YAO ............................................. 58 SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA UFALME NA HALI YAKE .............................................................. 59 SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA UFALME ........................................................................................ 60 SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA UFALME .................................................................................... 60

MAMBO YA MWISHO ......................................................................................................................... 62 MAFUNDISHO YA MADARAKA MANENO YA KUKUMBUKA ................................................................. 63

Page 5: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 1 -

MAFUNDISHO YA MADARAKA

UTANGULIZI

Katika kulielezea kusudi la kitabu hiki tunapata maelezo mazuri kutoka kwa rafiki yangu Mchungaji Samuel R. Vinton, Jr. katika kitabu chake: ELIMU KUBWA ZA BIBLIA.

“Tangu mwanzo Mungu amekuwa na watu wake, lakini jambo kubwa linalopaswa kufahamika ni hili: Mara kwa mara Mungu alizibadilisha sheria au amri zilizokuwa zikiwaongo-za watu wake. Mungu mwenyewe katika ASILI au KAWAIDA YAKE hawezi kubadilika lakini MI-PANGO NA MASHARTI yake vinaweza kubadilika. Tangu mwanzo Mungu ni mwenye haki na anaichukia dhambi. Aliichukia dhambi wakati wa Adamu na hata leo anaichukia na kuihukumu dhambi. Hii ni ASILI ya Mungu isiyoweza kubadilika. Lakini, katika matendo yake na watu kuna mabadiliko. Hii ni tofauti kati ya ASILI ya Mungu na MPANGO wake. ASILI ya Mungu haiwezi ku-badilika lakini MASHARTI (yasiyotegemea asili yake) na MIPANGO yake vinaweza kubadilika.

Mafundisho ya Madaraka (wengine wanasema UWAKILI) yanatafuta kuzitambua tofauti za maneno na maagizo katika Biblia. Tunaamini kwamba mafundisho yote matakatifu yaliandikwa kwa faida yetu, lakini si yote yanayotulenga wala yote hayakuandikwa kwa ajili yetu. Katika Warumi 15:4 tunasoma: “Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.”

Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya wanafunzi ambao walishamaliza masomo mengine ya kibiblia. Bila shaka wanafunzi wengine watawaza kwamba masomo haya ni magumu. Lakini usichoke kujifunza mafundisho haya kwa bidii, na uendelee pole pole, ili upate faida kubwa.

Usisahau kumwomba Mungu ili akupe akili ya kuyaelewa mafundisho haya.

Page 6: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 2 -

UMUHIMU WA KUJIFUNZA KUHUSU MADARAKA

SOMO LA KWANZA: MUNGU ANABADILISHA MIPANGO YAKE

Biblia inasema kwamba Mungu hawezi kubadilika. Mungu yuko vilevile tangu mwanzo hata milele.

“Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndiyo maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.” (Mal 3:6)

“Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.” (Yk 1:17)

Lakini Mungu hubadilisha mipango yake mara kwa mara kufuatana na mapenzi yake. Tena huibadilisha nia yake kulingana na matendo ya watu wake,

“BWANA akaghairi kwa kuwa amemwumba mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.” (Mwa 6:6)

“Na BWANA akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.” (Kut 32:14)

“Ikiwa taifa lile nililolitaja litageuka, na kuacha maovu yake nitaghairi, nisitende mabaya yale niliyoazimia kuwatenda.” (Yer 18:8)

Teolojia ya Madaraka inaonesha jinsi Mungu alivyoyabadilisha masharti na mipango yake tangu siku za Adamu hadi leo.

Vipindi hivi mbalimbali vyenye mipango tofauti huitwa “Madaraka” katika Biblia. Madaraka ni vipindi maalumu ambavyo Mungu alishughulika na watu wake kwa mpango na masharti maalum. Tunaona jumla ya Madaraka manane ambayo ni: 1) Usafi, 2) Dhamiri, 3) Serikali, 4) Ahadi, 5) Sheria, 6) Neema, 7) Dhiki Kuu, 8) Ufalme. Tutajifunza kuhusu Madaraka haya moja baada ya jingine. Tutaona kwamba kila Daraka lilianza na mtu fulani na lilimalizika katika hukumu. Watu hawa waliitwa na Mungu kwa neema yake. Tutaona jinsi Mungu alivyowaita na jinsi alivyowapa maagizo. Vilevile tutaona kwamba Mungu aliionesha rehema na neema yake katika kila Daraka, ijapokuwa watu walimkosea.

Tena, tutaona kwamba ufunuo wa Mungu ulikuwa na maendeleo, yaani Mungu aliufunua mpango wake njiani. Teolojia hii inaitwa “Maendeleo ya Ufunuo.” Maendeleo ya ufunuo ni jambo lililo kubwa sana ambalo litatusaidia kuyafahamu mafundisho ya Biblia. Kuyaelewa maendeleo ya ufunuo ni hatua ya kwanza ya kuielewa maana ya Biblia. Ni kama mtoto mdogo anayeenda darasani. Ni lazima aanze katika darasa la kwanza ambalo akishindwa hataweza kusoma darasa la pili na kufaulu.

Watu wakishindwa kuitambua tofauti iliyopo kati ya Madaraka mbalimbali katika Biblia, watayachanganya mambo ya sheria na mambo ya neema, mambo ya ufalme na mambo ya Kani-sa, mambo ya imani na mambo ya sheria. Kwa mfano, Waisraeli waliagizwa na Mungu kuleta sadaka ya mnyama ili kuziondoa dhambi zao. Je, Wakristo wa leo wanapaswa kufanya hivyo? Waisraeli walikatazwa kula nyama ya nguruwe. Je, Wakristo wa leo wanakatazwa kula nyama hiyo?

Tutajifunza tofauti kati ya Madaraka mbalimbali. Tutajifunza kuhusu makusudi ya Mungu kuanzia mwanzo hadi milele na tutaona jinsi Mungu alivyoyabadilisha masharti na mipango yake mara kwa mara ili apate kutuonesha rehema na neema yake.

Ninaamini kwamba ufahamu wako utaongezeka sana juu ya Neno la Mungu. Utakuwa tayari kumjibu kila mtu anayekuuliza habari ya imani yako. Ili uweze kufanya hivyo, ni lazima ujifunze kwa bidii mafundisho haya ya Teolojia ya Madaraka.

SOMO LA PILI: MADARAKA YA MUNGU KWA UFUPI

Mungu alimwumba mwanadamu apate kuwa mfano wake. Akamwumba bila upungufu, akamwita jina lake Adamu, ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza duniani. Hapakuwepo mnyama wa-la ndege wala samaki aliye katika mfano wa Mungu, bali ni Adamu tu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu.

Page 7: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 3 -

Adamu alikuwa mtu mkamilifu kabisa. Mwili wake haukuwa na kasoro yo yote. Alikuwa na akili kupita wanyama wote. Mungu alimweka Adamu ndani ya bustani ya Edeni ili apate kuilima na kuitunza. Hicho kilikuwa ni kipindi cha Daraka la Usafi.

Mungu alimwumba mwanamke kwa kuwa Adamu hakuwa na msaidizi wa kupendana naye na wa kumzalia watoto. Alimleta mwanamke kwa Adamu, na hao wawili walikuwa mume na mke, kusudi waanzishe kizazi duniani. Lakini walimwasi Mungu, nao wakafukuzwa watoke katika bustani. Jambo hilo lilileta mwanzo wa Daraka la Dhamiri.

Mungu alimwita Nuhu kwa sababu dunia ilijaa uovu. Kusudi la Mungu lilikuwa kuwahuku-mu watu wote kwa sababu ya dhambi zao. Lakini alitaka amwokoe Nuhu na jamaa yake, kwani Nuhu alikuwa mtu wa haki. Mungu alikusudia kuanza upya kumpitia Nuhu na watoto wake. Ndiyo mwanzo wa Daraka la Serikali.

Baada ya siku za Nuhu, watu walikuwa wengi tena duniani. Walikuwa wa taifa moja na lugha moja tu. Walipatana kujenga mnara ili wapate kuitawala mbingu sawa na dunia. Lakini Mungu alifanya nini? Alizichanganya lugha zao hata wasiweze kuwasiliana tena. Basi walisam-bazwa na walianzisha mataifa mbalimbali.

Mungu alimwita Ibrahimu aiache nyumba yake na asafiri mpaka nchi ya kigeni. Mungu aliona ni vizuri aanzishe taifa jipya, taifa litakaloweza kuwa watu wake. Ibrahimu alimtii, akas-afiri hata akafika nchi ya Kanaani. Mungu alimwahidi kwamba atakuwa baba wa taifa, na mwenye kuleta baraka kwa mataifa yote. Taifa jipya liliitwa Waebrenia au Waisraeli. Huu ni mwanzo wa Daraka la Ahadi.

Miaka mia nne na zaidi baada ya Ibrahimu, Mungu alimwita Musa aliyezaliwa katika nchi ya Misri. Musa alikuwa Mwebrania. Waebrania wote walikuwa watumwa huko Misri. Mungu al-ikisikia kilio chao, akamsimamisha Musa ili aweze kuwaokoa Waisraeli kutoka katika mikono ya Farao mfalme wa Misri.

Wakati Musa na wana wa Israeli walipokuwa wamekimbia kutoka Misri, na kuivuka Bahari ya Shamu, Mungu alimwita Musa katika Mlima wa Sinai. Pale, Mungu alimpa sheria na amri ku-mi ili kuyaongoza maisha ya Waisraeli. Akamwongoza vilevile aijenge Hema, yaani Nyumba ya Mungu jangwani. Kwa namna hii Daraka la Sheria lilianza.

Sheria iliendelea kwa miaka mingi sana. Hata Bwana Yesu, Mwana wa Mungu, alizaliwa chini ya sheria kama Myahudi (ambalo ni jina lingine kwa ajili ya taifa la Waebrenia au Waisraeli linalotokana na kabila moja ndani ya taifa hilo). Lakini, wakati Wayahudi walipomkataa Kristo kuwa mfalme wao, na kumwua, Mungu alimwita Sauli wa Tarso. Sauli huyu baadaye alipewa jina Paulo, na kazi yake ilikuwa kuihubiri Habari Njema ya neema ya Mungu kwa Mataifa. Kanisa lililo Mwili wa Kristo, lilianza katika utumishi wa Paulo. Na Wayahudi (taifa la Israeli) waliwe-kwa pembeni kwa muda. Huu ni mwanzo wa Daraka la Neema.

Kufuatana na maandiko ya manabii, wakati wa Dhiki Kuu utakuja hapa duniani. Tangu za-mani watu wamemwasi Mungu; wamefanya kila namna ya uovu. Basi, siku moja mtu mwovu atasimama, ataitawala dunia kwa hila, kwani watu wote wasioamini watadanganywa. Kwa hiyo, hasira ya Mungu itaanguka juu yao, hata watateswa sana. Wakati huo utakuwa wa Daraka la Dhiki Kuu.

Kwa huruma ya Mungu, wakati wa Dhiki Kuu utakuwa mfupi tu. Kwa miaka mitatu na nusu kutakuwa mateso kiasi yatakayofuatwa na miaka mitatu na nusu ya mateso makubwa. Kisha Bwana Yesu atarudi duniani na atawakanyaga adui zake chini ya miguu yake. Naye atausimamisha ufalme wake. Hakika atayatawala mataifa yote ya dunia kwa haki katika Daraka la Ufalme.

SOMO LA TATU: MADARAKA YANAPATANA NA HISTORIA YA WATU

Wakati Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, historia ya watu ilianza. Hatuna habari ya kuwepo kwa watu kabla ya Adamu na Hawa. Ijapokuwa walimu wa sayansi wanayakana maandiko ya Biblia wakisema kwamba watu walikuwepo hapa duniani miaka mingi sana kabla ya Adamu na Hawa, ukweli ni kwamba historia inaanzia kwa Adamu na Hawa. Kusema kulikuwa watu kabla ya Adamu na Hawa ni mawazo ya watu tu, yaliyo kinyume na ushuhuda wa Neno la Mungu. Kila kabila na kila taifa hutunza kumbukumbu za historia. Makabila yote yana historia

Page 8: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 4 -

inayohusu mwanzo wa dunia na mwanzo wa watu. Tukizichunguza kumbukumbu hizi mbalim-bali tunakuta wengi wanasimulia habari zinazokubaliana na ushuhuda wa Neno la Mungu.

Adamu na Hawa waliumbwa wakamilifu kwa mfano wa Mungu. Hawakuwa wenye dhambi. Hawakuwa na uovu. Waliagizwa kutenda mema siku zote ili wapate kushirikiana na Mungu. Wakati ule unaitwa “Daraka la Usafi.” Habari inayofanana na habari hii ya Biblia imeandikwa katika historia ya mataifa mengi.

Lakini Adamu na Hawa walifanya dhambi kwa kuwa walidanganywa na nyoka yule, yaani Shetani. Kwa sababu walikula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, macho yao yalifumbuliwa, wakaanza kujua uzuri na ubaya. Hakika Daraka la Usafi liliisha, na Daraka la Dhamiri lilianza baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi. Katika Daraka la Dhamiri watu waliongozwa na dhamiri zao; sauti ndogo ile iliyo ndani ya roho zao. Katika historia na desturi za makabila mengi, kuna habari ya kuanguka kwa watu katika dhambi na kutengwa kwao na Mungu.

Adamu na Hawa walipata watoto. Watoto wengi sana walizaliwa kwao. Wengine walitenda mazuri, na wengine walitenda mabaya. Watu walipoongeza sana juu ya uso wa dunia, dhambi iliwatawala wote isipokuwa Nuhu na familia yake. Historia ya makabila mbalimbali husimulia kwamba watu walikuwa wakali sana na walipigana bila huruma. Watu walishindwa kuzifuata dhamiri zao kabisa.

Mungu alimwambia Nuhu ajenge safina kwa kuwa alikusudia kuhukumu watu wa dunia kwa gharika ya maji. Ijapokuwa watu wengi wanakana habari hii, wakisema ni hadithi tu, maandishi ya historia ya mataifa mengi yanaonesha kwamba dunia ilifunikwa na gharika kubwa sana. Baada ya gharika ile, Mungu alifungua Daraka jingine kwa kusudi lake. Aliamuru watu wa-tawaliwe na serikali ya kibinadamu. Hata leo tokeo la Daraka la Serikali linaendelea, kwani wafalme na marais wanatawala katika nchi mbalimbali.

Baada ya siku za Nuhu, watu walikuwa wengi tena duniani. Lakini walikuwa wa taifa moja na walisema kwa lugha moja. Walianza kujaa kiburi, nao walipatana kujenga mnara mrefu sana kwenda juu. Walitaka kuzitawala nyota za anga, wapate kuwa sawa na Mungu. Lakini Mungu alizichanganya lugha zao mpaka kila kabila lilianza kusema kwa lugha nyingine. Basi, walisam-baa kwa sababu hawakuweza kuwasiliana. Kila kabila lilienda kule lilikotaka. Walimu wa aki-olojia waliochimba kwenye ardhi ya nchi ya Babeli, waliona msingi wa mnara uliyojengwa za-mani, kitu cha historia kinachofanana na ushuhuda wa Biblia.

Siku moja, Mungu alimwita Ibrahimu aliyekaa mji wa Uru wa Wakaldayo. Yeye alikuwa ameshaenda na baba yake Tera na jamaa zake hadi mji wa Harani. Baada ya Tera kufa, Mungu alimwita Ibrahimu, akisema,

“Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nita-kayokuonesha.” (Mwa 12:1)

Basi Ibrahimu aliitii sauti ya Mungu, akaenda hadi nchi ya Kanaani. Pale ndipo Mungu ali-pomwahidi Ibrahimu kwamba atampa nchi ile yote, yeye na uzao wake, milele (Mwa 15:18). Historia inathibitisha kuwa taifa la Waisraeli lilianza na mtu mmoja, ndiye Ibrahimu.

Waisraeli walikuwa watumwa katika nchi ya Misri. Mungu alimwita Musa na ndugu yake Haruni washindane na Farao aliye mfalme wa Misri. Walimshinda Farao kwa nguvu ya Mungu na maajabu yake. Wakavuka bahari, wakatembea jangwani hata wakafika Mlima wa Sinai. Pale Mungu alimpa Musa amri kumi na sheria nyingine za kuwaongoza Waisraeli. Hata leo, Waya-hudi wanajaribu kuzishika sheria za Mungu na mambo yote ya dini yao. Wakristo vilevile wanayaheshimu maandiko ya Musa kama sehemu ya Neno la Mungu.

SOMO LA NNE: KUFAHAMU MADARAKA KUNASAIDIA WAKRISTO KUYAJIBU MASWALI YAHUSUYO BIBLIA.

Watu wasioiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu wanasema kuna makosa mengi katika maandiko yake. Kwa mfano, katika kitabu cha Mwanzo, Mungu anamwambia Adamu,

“Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula.” (Mwa 2:16)

Lakini katika Mwanzo 9:3 Mungu alimwambia Nuhu, “Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu.”

Page 9: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 5 -

Tena, katika kitabu cha Mambo ya Walawi, Mungu alitaja majina ya wanyama walio safi, na wanyama walio najisi. Kisha Paulo aliandika katika 1 Timotheo 4:4,

“Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani.”

Wengine wanasema Biblia inapingana yenyewe kwa yenyewe kwa kuwa inatoa maagizo yanayopingana kama hayo. Lakini tofauti katika maneno hayo inaonekana kwa sababu ya Madaraka mbalimbali. Mtu akielewa jinsi Mungu alivyoyapanga Madaraka mbalimbali katika Biblia, ataona kwamba Biblia haijipingi yenyewe.

Kwa mfano, Ibrahimu na wanaume wa nyumba yake walitahiriwa kwa agizo la Mungu. Tena, Bwana Mungu alimwambia Ibrahimu,

“Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.” (Mwa 17:14)

Lakini Paulo, aliyekuwa Myahudi mwenyewe, alisema, “Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidi neno.” (Gal

5:2)

Kuna tofauti katika maneno haya kwa sababu Ibrahimu alikaa katika Daraka la Ahadi, na Paulo alikuwa wa Daraka la Neema.

Mfano mwingine ni jinsi Mungu alivyomwambia Musa, “Kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sa-

daka ya kuteketezwa mbele za BWANA; ni sadaka ya dhambi.” (Law 4:24)

Mstari huu unaeleza jinsi watu walivyosamehewa dhambi zao katika Daraka la Sheria. Lakini katika Daraka la Neema watu wanaambiwa,

“Wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; am-baye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake...”(Rum 3:24-25)

Basi, damu ya ng’ombe ilifaa kwa kusamehe dhambi chini ya Daraka la Sheria, lakini damu ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, inafaa katika Daraka la Neema.

Sasa angalia mfano wa vyakula katika Biblia. “Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama

ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema BWANA.” (Isa 66:17)

“Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.” (Mdo 10:15)

“Kila kiumbe cha Mungu ni kizuri.” (1 Tim 4:4)

Maagizo ya Mungu hutofautiana kwa sababu kuna Madaraka mbalimbali. Kama Biblia isin-gekuwa na Madaraka mbalimbali yenye mipango tofauti ya Mungu, kutii Biblia kungeleta shida kwa kuwa watu wangeshindwa kujua wafuate agizo lipi wakati maagizo yanapingana.

Angalia mfano mwingine. Waisraeli waliagizwa kushika siku zilizo muhimu kama Pasaka, Sabato, Malimbuko, Pentekoste, Baragumu, Upatanisho, Vibanda n.k. Lakini Wakristo wanashika siku ya kwanza kama siku ya Mungu na Pasaka tu (siku ya kukumbuka ufufuo wa Kristo). Tena, Paulo anasema,

“Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.” (Rum 14:5)

Mfano mwingine ni jinsi Mungu alivyotuma watu kuhubiri Habari Njema zilizo tofauti kutegemea Daraka husika. Wakati Bwana Yesu alipotuma wanafunzi wake kuhubiri Habari Njema ya ufalme, alisema,

“Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. Bali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” (Mt 10:5-6)

Lakini mtume Paulo alitumwa kuihubiri Habari Njema ya neema kwa Mataifa. Hakika Mun-gu aliubadilisha mpango wake! Hakika kuna Madaraka mbalimbali katika Biblia. Bwana Yesu Kristo alihubiri hapa duniani katika nchi ya Israeli tu. Alisema,

“Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” (Mt 4:17)

Page 10: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 6 -

Kisha alifundisha kwa mifano mingi, akisema, “Ufalme wa mbinguni unafanana na ...” (Mt 13)

Lakini mtume Paulo hakufundisha habari za ufalme wa mbinguni, bali habari za Kanisa lili-lo Mwili wa Kristo (Efe 1:22, 23; Kol 1:18). Tofauti za jumbe hizi zitaeleweka tu ukifahamu Teo-lojia ya Madaraka.

Zamani kulikuwa utengano katikati ya Waisraeli na Mataifa. Waisraeli walikuwa watu wali-ochaguliwa na Mungu. Mataifa walikuwa nje ya neema hii. Mtu wa Mataifa hakuweza kuokolewa bila kuifuata dini ya Waisraeli, yaani kutahiriwa, kuleta sadaka, kushika Sheria ya Musa n.k. Lakini sasa, Mataifa na Wayahudi wanakuwa na umoja katika Kristo Yesu kwa njia ya imani tu. Tazama Waefeso 2:11-17. Leo ni Wakristo tu waliochaguliwa na Mungu. Utofauti wa mambo hayo unaeleweka tu ukifahamu mambo ya Teolojia ya Madaraka.

Katika Agano la Kale, Mungu aliamuru Waisraeli kuwaua adui zao bila huruma. Lakini Bwa-na Yesu alifundisha,

“Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.” (Mt 5:44)

Tena, Paulo aliandika, “Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe...” (Rum 12:20)

Hakika, katika Agano la Kale, kusudi la Mungu lilikuwa kuwashinda adui zake wote mbele ya Waisraeli, lakini katika Agano Jipya, alikusudia kuwafundisha upendo na neema.

Msomaji, unaweza kuona kwamba mashaka mengi kuhusu Biblia hutokana na tofauti kati ya Madaraka mbalimbali. Bila kuyafahamu Madaraka ya Biblia watu wanaweza kufikiri maandi-ko ya Biblia yanajipinga ndani kwa ndani. Vivyo hivyo, watu watashindwa kuyatambua ma-kusudi mbalimbali ya Mungu katika nyakati zilizo tofauti. Kumbuka tena, hali ya Mungu haiwezi kubadilika, lakini mipango na maagizo yake kwa ajili ya wanadamu inabadilika mara kwa mara.

SOMO LA TANO: MAENDELEO YA UFUNUO

Hakika Biblia ni kitabu cha Mungu mwenyewe, kwani ni Neno la Mungu. Tusingeweza kum-tambua Mungu, jinsi alivyo, wala namna ya kumtumikia, bila Maandiko Matakatifu. Biblia ni ufunuo wa Mungu.

Mungu alijionesha kwa watu hata kabla hajajifunua kwa njia ya maandiko ya Biblia. Ali-jionesha kwa sauti, kwa ndoto, maono na ishara mbalimbali. Watu walioisikia sauti yake, au walioota ndoto, waliziandika baadhi ya habari hizo walizopewa na Mungu. Waliziandika habari zile ambazo Mungu alitaka waziandike. Tuseme, Mungu alijifunua kwa watu wenye imani na kisha waliitoa habari hiyo kwa watu wengine kupitia Maandiko (yaani, Neno la Mungu).

Mungu aliifunua habari ya mpango wake kuhusu taifa la Israeli kwa Ibrahimu, aliyeishi kwa imani. Ibrahimu hakuiandika habari hiyo katika Biblia lakini tunajua alimwelezea mtoto wake Isaka, na Isaka aliwafundisha Esau na Yakobo. Habari Njema wakati ule ilikuwa ahadi za Mungu kwa taifa moja tu, yaani uzao wa Ibrahimu.

Katika siku za Musa, Mungu alirudia ahadi zake alizozitoa kwa Ibrahimu, na aliongeza ufunuo mwingine mpya. Alijionesha kuwa Mungu mtakatifu, mwenye kuchukia dhambi na kila namna ya uchafu. Akatoa Sheria ya Musa na ndani yake alianzisha sheria za sadaka, siku muhi-mu, na mambo mengi ya kidini. Alimwongoza Musa kuijenga hema jangwani ipate kuwa nyum-ba ya Mungu. Kuna tofauti kubwa sana kati ya ufunuo wa Mungu kwa Ibrahimu na ule ambao Musa aliupokea.

Siku za wafalme wa Israeli, Mungu aliwainua manabii Isaya, Yeremia, Ezekieli, Danieli na wengine. Kazi yao ilikuwa kuwaonya Waisraeli kwa sababu ya dhambi zao na kutoa habari ya mambo yatakayokuja katika wakati ujao. Katika maandiko yao, Mungu alijifunua kuwa Mungu wa hukumu na Mungu wa rehema. Hukumu kwa wote waliomwasi, na rehema kwa wote wali-otubu na kumtii.

Manabii waliongozwa na Mungu kulifunua kusudi lake la kumwinua Mkombozi kwa ajili ya Waisraeli. Mkombozi huyu aliitwa Masihi kwa kuwa ataiokoa Israeli. Vilevile waliambiwa atakuwa Mfalme atakayeketi juu ya kiti cha ufalme cha Daudi. Naye ataitawala dunia kwa fimbo ya chuma.

Page 11: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 7 -

Ufunuo mpya wa Mungu ulipatikana pia katika kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo. Kristo alikuwa,

“Mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.” (Kol 1:15)

“Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana ...” (Ebr 1:1,2)

Yesu alikuja hapa duniani kutuonesha waziwazi hali ya Mungu Baba aliye juu ya yote. Bwana Yesu alifundisha mambo mengi kuhusu ufalme wa mbinguni. Alizifunua habari

nyingi mpya ambazo hazikufunuliwa kwa manabii wa zamani. Zaidi ya mambo yote Yesu alionesha upendo wa Mungu na kusudi lake la kuwaokoa watu wenye dhambi. Isitoshe, alitoa uzima wake msalabani kwa ajili yetu. Kwa jinsi hii aliufungua wokovu kwa watu wote. Tazama Yohana 3:16 na Luka 19:10. Kisha alifufuka kutoka kwa wafu ili apate kuyashinda mauti.

Habari nyingine mpya zilimjia Mtume Paulo aliyepata ufunuo wa siri kutoka kwa Bwana Yesu mwenyewe kama alivyosema,

“Nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. 12Kwa kuwa sikuipokea kwa mwana-damu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.” (Gal 1:11,12)

“…ya kwamba kwa kufunuliwa nilijulishwa siri hiyo.” (Efe 3:3)

Siri hii ni habari iliyofichwa tangu zamani. Ni habari ambayo haikujulikana katika kipindi cha Agano la Kale wala katika kipindi cha Yesu kuwepo duniani katika vitabu vya Injili. Basi, kwa njia hii, Mungu aliongeza ufunuo wake kwa wanadamu.

Wakati mtume Yohana alipokuwa mzee sana, Mungu alimfunulia mambo yatakayokuja katika wakati ujao. Kupitia ufunuo wa Mungu, Yohana aliweza kuziandika habari za hukumu ya Bwana juu ya dunia na pia juu ya Waisraeli. Aliweza kuuonesha uovu wa Mnyama yule (Mpinga-Kristo) na Nabii wa Uongo. Tena, aliweza kuonesha jinsi watu watakavyoteswa duniani kwa sababu ya maasi yao, na jinsi Yesu atakavyokuja katika utukufu wake kuwashinda adui zake na kusimamisha ufalme wake. Hakika maandiko yake (kitabu cha Ufunuo) yalikuwa ufunuo wa mwisho na yeye alikuwa nabii wa mwisho kati ya manabii wote.

Basi kwa maneno haya, tumeona namna gani Mungu alivyoongeza ufunuo wake mara kwa mara ili kuongeza ufahamu wa watu duniani juu ya mipango yake. Ndiyo sababu inaitwa “Maendeleo ya Ufunuo.” Mungu hakutoa habari zote za mipango yake mara moja bali alizitoa njiani kila wakati wanadamu walipohitaji kuzijua. Mara nyingine ufunuo mpya uliweza kubati-lisha ufunuo mwingine wa zamani. Hivyo wanadamu walipopewa maagizo mapya ya-nayopingana na maagizo ya zamani walijua wafuate maagizo yale mapya na waachane na yale ya zamani.

Page 12: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 8 -

DARAKA LA USAFI

SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA USAFI

Wakati Mungu alipoiumba dunia na viumbe vyote vya dunia, aliona ilikuwa vema. Tuseme hapakuwepo kasoro yo yote ulimwenguni. Dhambi haikuwepo wala uovu. Vitu vyote vilikuwa vyema tu.

Wanyama wote walikaa kwa amani na wanyama wengine. Ndege wote walikuwa salama. Hata wadudu hawakumezana wala kupigana. Amani ilikuwepo mahali pote.

Wakati huu ulikuwa wa zamani kabisa. Kama Biblia inavyosema, “Hapo mwanzo ...” (Mwa 1:1)

Wakati huo ulikuwa mwanzo wa historia ya watu. Kabla ya wakati huo hapakuwepo ma-taifa, makabila, watu, wala wanyama. Katika mwanzo huo wa historia Mungu alitaka kiumbe mmoja awatawale viumbe wote duniani.

“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini.” (Mwa 1:26)

Kusudi la Mungu lilikuwa wazi. Samaki, ndege na hata wanyama hawakuweza kutawala juu ya dunia. Mwanadamu tu, aliweza kufanya kazi hii.

“Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” (Mwa 1:27)

“Mfano wa Mungu” ina maana gani? Je maana yake ni kwamba wanadamu walipewa uso na mwili kama Mungu? Je, Mungu anaonekana sawa na Mtu? Hapana. Wanadamu waliumbwa kwa mfano wa Mungu kwa kuwa waliumbwa na akili, nafsi, na utakatifu. Wanyama hawana uwezo wa kufikiri (kama vile wanadamu wanavyoweza) wala kutenda haki wala kumtafuta na kum-wabudu Mungu.

Hatujui hakika ni wakati gani mtu alipoumbwa. Wengine wanasema Mungu aliwaumba wanadamu miaka elfu nne kabla Yesu Kristo hajazaliwa. Wengine wanasema Mungu aliwaumba wanadamu miaka elfu nyingi zaidi iliyopita. Wengine wanasema kwamba wanadamu walitoka kwa mnyama kufuatana na wazo la “Mabadiliko” (evolution). Lakini Biblia inasema wazi kwam-ba Mungu alimwumba mtu moja kwa moja kuwa tofauti na wanyama. Tena uone mwanadamu siyo mnyama, bali ni nafsi iliyo hai.

“BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.” (Mwa 2:7)

Mwanamke aliumbwa namna gani? Tazama, “BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake

mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.” (Mwa 2:21-22)

Na mwanamke alikuwa safi vilevile. Mtu wa kwanza aliyeitwa Adamu alimwoa Hawa, mwanamke, nao walipata kuwa mume na

mke. Waliumbwa wakiwa watu wazima. Hawakuwa na baba wala mama. Waliumbwa kama wa-tu wazima ili wapate kuanzisha makabila yote ya kibinadamu. Watu waliozaliwa baada ya Ada-mu na Hawa waliitwa wanadamu, kwani Adamu alikuwa baba wa watu wote. Walikuwa na akili nyingi hata Adamu aliweza kupanga majina ya wanyama na ndege na samaki wa kila aina.

Adamu na Hawa walitembea bustanini wakishirikiana na Mungu. Waliweza kumpendeza Mungu, kwani hawakuwa na dhambi mioyoni mwao. Hatujui muda wala siku ngapi au miaka mingapi waliishi kabla hawajatenda dhambi. Tunapaswa kukumbuka kwamba hawakuwa na saa wala kalenda siku zile.

Page 13: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 9 -

SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA USAFI

Daraka la Usafi lilianza na watu wawili tu, yaani Adamu na Hawa. Hawakuwepo watu wen-gine duniani wakati ule. Tulishaona habari ya kuumbwa kwao. Tena, tulishaona kwamba Adamu aliumbwa kama mtu mzima. Hakuzaliwa kama mtoto; kama vile tulivyozaliwa sisi. Hapana. Bali, aliumbwa mwenye mwili wa mtu mzima na mwenye akili ya mtu mzima. Hakufundishwa cho chote na mwingine ila kwa Mungu mwenyewe tu. Na Mungu alimpa akili iliyozidi akili za wan-yama wote duniani.

Katika Mwanzo 2:7, tunaona kwamba Mungu alipuliza pumzi ya uzima ndani ya pua ya Adamu, naye alikuwa nafsi iliyo hai. Katika 1 Wakorinto 15:45 tunasoma,

“Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa kiumbe aliye hai.”

Hakika Adamu, mwenye nafsi, alikuwa tofauti na wanyama kwa kuwa Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Mke wa Adamu alikuwa sehemu ya mwili wake Adamu kwa kuwa ali-umbwa kwa mfupa uliotolewa katika mifupa ya mbavu za Adamu. Hawa aliumbwa mtu mzima vilevile. Hakuwa mtoto mdogo wala binti, lakini alikuwa mwanamke aliye na hali ya utu uzima. Tunaweza kujua hivyo kwa sababu Mungu alitaka mume na mke wanaoweza kuwa wazazi wa jamaa za watu wote duniani.

Adamu na Hawa walikaa katika bustani ya Edeni, bustani iliyoumbwa na Mungu. Edeni ilikuwa mahali pazuri sana.

“BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya. BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.” (Mwa 2:8,9)

“Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vi-chwa vinne. Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndiyo unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu; na dhahabu ya nchi ile ni njema ... jina la mto wa pili ni Gihoni ... ina la mto wa tatu ni Hide-keli ... Mto wa nne ni Frati ...” (Mwa 2:10-14)

Kumbe kulikwa maji mengi tayari ya kumwagilia udongo wa bustani ya Edeni. Lakini kuna habari gani juu ya miti na mimea iliyo nje ya bustani ya Edeni? Tunapaswa kufahamu kwamba wakati ule dunia yote ilikuwa bustani.

“Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilivyoumbwa. Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na nchi hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; maji yaka-panda katika nchi, yakatia unyevu juu ya uso wote wa ardhi.” (Mwa 2:4-6)

Hakika dunia yote ilikuwa mahali pazuri sana, ila, bustani ya Edeni ilikuwa nzuri zaidi. Tulishaona Mungu aliwaumba Adamu na Hawa kuwa mume na mke, na kama mume na

mke, akawapa agizo, “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa

angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi..” (Mwa 1:28)

Hakika, Adamu na Hawa walikuwa watu walioheshimika duniani. Walikuwa kama mfalme na malkia wenye mamlaka juu ya maeneo yote na viumbe wote duniani.

Mungu alitengeneza chakula kwa kila kitu kilicho hai. “Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mmea utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia,

na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa chakula chenu; na chakula cha kila mnya-ma wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; ma-jani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.” (Mwanzo 1:29,30)

Basi, tumejifunza kwamba Adamu na Hawa waliumbwa na Mungu wakiwa watu wazima. Walikuwa watu wazuri sana kwa kuwa waliumbwa kwa mfano wa Mungu. Waliwekwa mahali pazuri kuliko mahali po pote pengine duniani. Walipewa mamlaka juu ya samaki, juu ya ndege, na juu ya wanyama. Pia, Mungu alikuwa ameshatengeneza chakula kizuri sana kutokana na mimea na miti mbalimbali. Hakika Adamu na Hawa walibarikiwa na Mungu, nao waliona furaha sana. Walikuwa watu wasio na dhambi kabisa.

“Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.” (Mwa 2:25)

Watu walio muhimu katika Daraka la Usafi ni Adamu na Hawa tu.

Page 14: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 10 -

SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA USAFI

Katika mwanzo, duniani kulikuwa na watu wawili tu: Adamu na Hawa. Sheria haikuwepo, serikali haikuwepo, na hukumu haikuwepo kwa kuwa dhambi haikuwepo. Adamu na Hawa walikuwa huru kutenda walivyotaka. Walikuwa safi. Walimjua Mungu na wakahusiana naye.

Mungu aliwaumba Adamu na Hawa wakiwa na hiari yao wenyewe. Tuseme, waliweza kumtii Mungu au kumwasi. Waliweza kusema ndiyo au hapana. Waliweza kupendana au kua-chana. Lakini, wakati ule hawakujua uzuri wala ubaya.

Basi Mungu alikusudia kuwapima Adamu na Hawa. Alitaka kuona kama wanampenda zaidi au hapana. Akawaagiza namna hii,

“BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, ‘Matunda ya kila mti wa bustani waweza ku-la, Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matun-da ya mti huo utakufa hakika.’” (Mwa 2:16,17)

Je, agizo hili lilizidi? Yaani, lilikuwa mtego ambao Adamu na Hawa wasingeweza kukwepa? Hapana, hata kidogo. Tazama, Mungu aliwapa ruhusa kula kila mti ndani ya bustani. Wali-katazwa mti mmoja tu kati ya miti yote. Mungu alitengeneza chakula cha kila namna kiasi kwamba wasingeweza kukosa chakula. Ni mti mmoja tu, walipaswa kuuacha. Tena, tunaona agizo la Mungu lilikuwa wazi.

“Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya USILE.”

Adamu na Hawa hawakuwa na udhuru. Adamu asingeweza kumwambia Mungu, “Sielewi agizo hili.” Lilikuwa wazi kabisa. Tulishaona kwamba Adamu alikuwa na akili nyingi. Alikuwa amewapa majina wanyama, ndege na samaki wa kila aina. Kazi ile ilihitaji akili nyingi. Hivyo Adamu alikuwa na uwezo kumwelewa Mungu kuhusu agizo hilo.

Pia, kuna agizo lingine ambalo Mungu aliwapa. Mungu aliwaagiza, “Mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho

juu ya nchi.” (Mwa 1:28)

Kwa hiyo Mungu aliwaagiza Adamu na Hawa maagizo mbalimbali kama vile kuzaa na kuongezeka, kuwatawala viumbe wengine wote walio hai, na, muhimu zaidi, wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA USAFI

Tulishaona Adamu na Hawa waliumbwa wakiwa watu wazima, wenye akili nyingi, nao ha-wakuwa na dhambi. Lakini Shetani, adui wa Mungu, alimtumia nyoka ili awajaribu Adamu na Hawa kwa hila zake. Kama ilivyoandikwa,

“Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu.” (Mwa 3:1)

Nyoka huyu alipewa hila yake na Shetani. Nyoka alienda kwa mwanamke kwanza, akamwambia,

“Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?”

Hakika Shetani, aliyekuwa ndani ya nyoka, aliyajua maagizo ya Mungu. Aliijua hali ya Ada-mu na Hawa ilikuwa safi. Alijua kwamba waliumbwa kwa mfano wa Mungu. Naye alitaka ku-waharibu.

Wakati Hawa aliposikia sauti ya nyoka, hakuogopa kwani hakuitambua hila ya Shetani. Akamjibu, akisema,

“Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.” (Mwa 3:2,3)

Tazama, mwanamke alisema uongo, kwa kuwa Mungu hakusema “Usiyaguse,” lakini alisema, “Usile” tu. Hawa aliongeza maneno ya Mungu. Lakini nyoka akamwambia mwanamke,

“Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” (Mwa 3:4,5)

Hakika, maneno haya yalilionesha kusudi la Shetani. Alitaka kumhuzunisha Mungu kwa njia ya kuwaangusha Adamu na Hawa.

Page 15: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 11 -

Basi mwanamke akayatazama matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Akaona kwamba “ule mti wafaa kwa chakula.” Angalia, Hawa hakujisikia njaa, hata kidogo, maana kulikuwa chakula cha kila namna katika bustani ile. Lakini alitamani kukionja chakula kingine tu, chakula kilichokatazwa kwake. Kwa mtego wa Shetani alitamani kuyaonja matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Pia, mwanamke aliona kwamba matunda ya mti ule yalikuwa matunda ya kutamanika (Mwa. 3:6) kwa kuwa Mungu alimkataza kula matunda yale. Alikumbuka neno la Shetani kupitia nyoka,

“Siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” (Mwa 3:5)

Tamaa hii ni tamaa ya kiburi cha uzima. Tangu kipindi cha Adamu na Hawa watu wengi wamejaribu kuwa kama Mungu. Wamejazwa kiburi na majivuno. Basi, Hawa aliyasikiliza mane-no ya nyoka, akayatazama matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, akajaribiwa sana. Akawa na tamaa ya macho, na ya kiburi cha uzima, naye akashindwa kabisa.

“Basi alichuma matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.” (Mwa 3:6)

Tazama, walikuwa wameshaasi maagizo ya Mungu. Maasi yaliingia bustanini. Dhambi na kifo viliingia ulimwenguni kwa njia ya kuasi kwa Adamu na Hawa (Rum 5:12). Baada ya ku-litenda tendo hilo la kula matunda ya mti, je, walipata kuwa kama Mungu? Hapana, hata kidogo, lakini,

“Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajitambua kuwa wako uchi, wakashona majani ya mtini, na kujifanyia mavazi ya kusitiri uchi wao.” (Mwa 3:7)

Mara moja walianza kujua jema na baya, nao wakaona haya kwa sababu walikuwa uchi. Adamu na Hawa walioneana haya kwa sababu ya uchi wao, je, unafikiri waliona haya kusimama mbele ya Mungu? Tazama,

“Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.” (Mwa 3:8)

Ole kwao! Kwa sababu walisikiliza sauti ya nyoka, nao walimwasi Mungu! Bila shaka walif-ikiri kwamba Mungu alikuja kuwaua! Bali, tazama sasa upendo wa Mungu. Alijua Adamu na Ha-wa walishafanya dhambi. Alijua wamemwasi. Lakini alikuja kwao ili awatafute na alitatue tatizo lao. Ijapokuwa watu wa dunia wanaukimbia uso wa Mungu, yeye mwenyewe huwatafuta ili apate kuwaokoa. Tazama,

“BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?” (Mwa 3:9)

Hili ni swali la kwanza kutoka kwa Mungu akiwauliza watu.

SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA USAFI

Mwisho wa somo la nne tuliona wito wa Mungu, “Adamu, uko wapi?” (Mwa 3:9). Kumbuka wakati Adamu alipoisikia sauti ya Mungu, yeye na Hawa, mke wake, walikuwa wamejificha katikati ya miti ya bustani. Hakika daima dhambi inamtenga mtu na Mungu. Watu wanamkimbia Mungu kwa kuwa wanaona woga na aibu kutokana na dhambi zao. Lakini Mungu huwatafuta ili awaokoe. Ndiyo maana baadaye alimtuma Mwana wake wa pekee ili awatafute wenye dhambi na kuwaokoa.

Tazama sasa jibu la Adamu wakati aliposikia sauti ya Mungu, “Akasema, Nilisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.” (Mwa

3:10)

Lakini, kusema kweli, Adamu aliogopa kwa sababu alijua kwamba aliliasi agizo la Mungu alipolitwaa na kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Nani anaweza kumdanganya Mungu? Angalia,

“Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?” (Mwa 3:11)

Mungu ni Mungu. Anajua vitu vyote na mambo yote. Alijua wazi kwamba Adamu na Hawa walitenda dhambi, lakini alitaka kusikia jibu lao. Mungu anataka sisi tutubu dhambi zetu ili

Page 16: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 12 -

apate kutuonesha upendo wake. Adamu alitambua alikuwa ameshaanguka katika mtego wa dhambi, lakini alisema,

“Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.” (Mwa 3:12)

Tazama, alitaka kumshtaki mke wake kwa kosa lake. Lakini kosa ni la Adamu, kwa kuwa Mungu alimwagiza yeye mwenyewe asile matunda ya mti ule (Mwa 2:16,17). Mtume Paulo alisema,

“Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.” (1 Tim 2:14)

“BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.” (Mwa 3:13)

Hawa alisema kweli wakati aliposema, “Nyoka alinidanganya,” lakini alidanganywa kwa tamaa yake vilevile. Kumbuka maneno ya Yakobo,

“Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Ha-lafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.” (Yk 1:14,15)

Mungu ni mwenye haki. Anapaswa aihukumu dhambi. Basi, alimwita nyoka yule ali-yemdanganya Hawa. Akamwambia,

“Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” (Mwa 3:14,15)

Sasa, tuone hukumu ya mwanamke. Mungu alimwambia, “Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata

hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.” (Mwa 3:16)

Maana ya maneno haya siyo kwamba mke anakuwa mtumwa wa mume wake. Hapana. Lakini inasema mume atakuwa kichwa cha nyumba, kama ilivyo Kristo ni kichwa cha Kanisa. Wanaume wanapaswa kuwapenda wake zao kama Kristo alivyolipenda Kanisa. Tazama Waefe-so 5:23-25.

Halafu Mungu alimhukumu Adamu. Akamwambia, “Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema,

Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.” (Mwa 3:17-19)

Ebu tuiangalie laana juu ya udongo. Ukumbuke Mungu alisema, “Ardhi imelaaniwa kwa ajili yako ... michongoma na miiba itakuzalia; nawe utakula mboga za

kondeni.” (Mwa 3:17,18).

Tangu wakati ule mpaka sasa, laana ya Mungu imebaki juu ya udongo na viumbe vyote. Ukiliacha shamba kwa miezi kumi au zaidi, utakuta magugu na miiba imeota na kuua mboga. Hata wadudu wamekuwa maadui wa wakulima. Isitoshe wanyama wanapigana, ndege wa anga-ni wanawindana, na hata wadudu wanashambuliana. Mateso ya watu yanazidi sana. Mambo haya yote ni matokeo ya dhambi.

Tazama sasa neema ya Mungu. Adamu na Hawa walikuwa uchi. Wakaona haya. Lakini, “BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.” (Mwa 3:21)

Alipata ngozi wapi? Mungu aliwaua wanyama, na akachuna ngozi zao. Tazama maana yake. Bwana Mungu aliimwaga damu ya wanyama, akazichuna ngozi zao, akaufunika uchi wa Adamu na Hawa kwa kuwavisha ngozi. Ni kusema, damu ilizifunika dhambi zao na mavazi yaliifunika aibu yao. Hakika ni mfano wa msamaha na neema ya Mungu.

Kumbuka namna Mungu alivyolipanda shamba la Edeni. Shamba lilikuwa zuri sana, bila kitu kibaya, bila laana. Lakini sasa, dhambi imeshaingia. Uovu ulionekana bustanini. Watu wali-okuwa na hali ya usafi, wamepata hali ya dhambi. Mungu alifanya nini? Alisema,

Page 17: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 13 -

“Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; kwa hiyo BWANA Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.” (Mwa 3:22,23)

Basi Mungu akawafukuza Adamu na Hawa kama hukumu yao. Walilazimika kukaa nje ya bustani mbali na mti wa uzima. Mungu aliwaweka Makerubi kuilinda bustani ili Adamu na Hawa wasipate kurudi.

JINA LA

DARAKA MTU MKUU MWANZO

WAKE MWISHO

WAKE MAANDIKO

MUHIMU Usafi Adamu Kuumbwa kwa Adamu Kula matunda na kufukuzwa

kuktoka katika Bustani ya Edeni

Mwanzo 1 – 3

Page 18: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 14 -

DARAKA LA DHAMIRI

SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA DHAMIRI

Tangu kosa la Adamu, watu waliyajua mema na mabaya. Kutokana na hali hii walianza kuishi wakiongozwa na dhamiri zao. Dhamiri ni nini? Dhamiri ni sauti ndogo ndani ya roho ya mtu inayomwambia kama tendo fulani au wazo fulani ni jema au baya.

Tangu kosa la Adamu mpaka gharika ya maji ni wakati wa Daraka la Dhamiri. Hatujui wa-kati huu ulidumu kwa miaka mingapi, lakini hakika ulikuwa muda wa vizazi vingi.

Ni vizuri tuone habari ya vizazi vilivyokuwepo hapa duniani baada ya Adamu na Hawa kufukuzwa kutoka Edeni. Kwanza walizaa watoto wao walioitwa Kaini na Abeli (Mwa sura 4). Mara moja matokeo ya dhambi yalionekana. Kaini alimwua mdogo wake kwa sababu Abeli alikuwa mwenye haki katika imani na utiifu wake kwa Mungu. Sadaka ya Abeli ilipokelewa na Mungu lakini sadaka ya Kaini ilikataliwa kwa sababu Kaini alikuwa mwovu akitaka kumpendeza Mungu kwa matunda ya kazi yake tofauti na maagizo ya Mungu (Tazama Mwanzo 4:3-8).

Baada ya kufa kwa Abeli, Hawa alizaa mtoto mwingine. Akamwita Sethi. Baadaye alizaa wa-toto wengine wa kiume na wengine wa kike. Waliweza kupata watoto wengi kwa sababu wa-liishi miaka mingi sana.

Kitabu cha Mwanzo sura ya tano kinatoa habari ya vizazi vya Adamu. Tunapoyasoma maneno hayo, tunaona watu waliishi maisha marefu sana. Hawakuwa na magonjwa na njaa ka-ma tunavyoona leo. Zaidi hawakuwa na vita vya kuuana siku zile. Watu wote walikuwa na afya nzuri sana. Hawakukosa chakula. Pia hawakuwa na serikali ya kuwatawala.

Mtu aliyeishi miaka mingi kupita watu wengine wote aliitwa Methusela, mwana wa Heno-ko. Methusela aliishi miaka 969. Ni miaka mingi sana. Yeye alikuwa babu wa Nuhu.

Ni jambo linaloshangaza kwamba watu walikuwa na miaka mia na zaidi kabla hawajazaa mtoto wao wa kwanza. Tunaweza kusema watu wa siku zile walikuwa vijana kwa miaka mingi. Leo katika sehemu nyingi za dunia, mtu anaitwa mtu mzima anapopita miaka kumi na nane tu.

Tukihesabu miaka ya kila kizazi cha Adamu tutaona ni miaka mingi tangu kosa la Adamu hadi siku za Nuhu. Tunaweza kuhesabu vizazi kumi na viwili tangu Adamu hadi Nuhu. Ingawa kumbukumbu siyo kamili, tunaona kulikuwa yapata miaka 1650 katika wakati wa Daraka la Dhamiri.

Tazama habari ya Henoko, mwana wa Yaredi (Mwa 5:18-24), “Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.”(24)

Hakika, Henoko alikuwa mtu wa Mungu wakati ule. Aliufuata uongozi wa dhamiri yake katika kutenda mema. Lakini watu wengine walitenda mabaya. Tazama kitabu cha Yuda mstari wa 14 na 15,

“Na Henoko, mtu wa kizazi cha saba toka kwa Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana yuaja na watakatifu wake, maelfu kwa maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibu wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno yote maovu ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.”

Tunaweza kuona matendo ya watu fulani katika Daraka la Dhamiri. Kaini alijenga mji. Lameki alijitwalia wake wawili. Nuhu alichukia uovu na akapenda wema.

Tulishaona watu wa wakati ule walikuwa huru. Hawakuwa na serikali wala sheria siku zile. Walifanya kwa kadiri ya mapenzi yao. Sasa, tutaangalia habari za watu wa Daraka la Dhamiri.

SOMO LA PILI: WATU DARAKA LA DHAMIRI

Daraka la Dhamiri lilianza na Adamu na lilimalizika na Nuhu. Lakini kulikuwa watu wengi walioishi kati ya vizazi hivyo. Adamu alikuwa ameshakula matunda ya mti wa kujua mema na mabaya. Dhamiri yake ilifunguliwa. Sasa alipotenda mema, dhamiri yake ilifurahi, lakini ali-potenda mabaya, dhamiri yake ilihuzunishwa. Kama tulivyosema tayari, dhamiri ni sauti ndogo ndani ya roho ya mtu inayoweza kumwongoza atende mema au kumzuia asitende mabaya.

Page 19: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 15 -

Mtoto wa kwanza wa Adamu na Hawa alikuwa Kaini. Kaini alizaliwa na dhamiri sawa na wazazi wake. Tunafikiri wakati alipokuwa mtoto aliwatii wazazi wake. Wakati alipoweza kufan-ya kazi alilima shamba. Siku moja alikataa kutoa sadaka ya mnyama jinsi ilivyoagizwa na Mun-gu, bali alileta matunda au mazao ya shamba lake. Wakati Mungu alipoikataa sadaka yake, ali-kasirika. Kisha alimwua ndugu yake Abeli. Hakika katika tendo hilo hakuitii sauti ya dhamiri yake.

Abeli alikuwa mtoto wa pili, mdogo wa Kaini. Alikuwa mchungaji wa kondoo. Dhamiri yake ilimwongoza kutoa sadaka ya mnyama kama Mungu alivyoagiza. Basi, akamchinja kondoo, akamtoa. Mungu akapendezwa, kwani, Abeli alionesha utiifu na imani yake (tazama Waebrania 11:4). Lakini ndugu yake Kaini aliona wivu, na kwa sababu hiyo akamwua Abeli.

Tunaona namna gani dhambi ya Adamu ilivyosababisha dhambi duniani. Hata watoto wake walipewa hali ya kujua mema na mabaya. Abeli alitenda haki, lakini Kaini alikuwa mwovu. Mto-to mwingine wa Adamu na Hawa alikuwa Sethi ambaye alikuwa baba wa Henoko. Sethi alikuwa mtu mwema. Yeye na watoto wake walianza kuliitia jina la Bwana (Mwa 4:26).

Lameki alitokana na vizazi vya Kaini. Yeye alikuwa mtu wa kwanza kuoa wake wawili. Wa-kati ule wanaume wote walikuwa na mke mmoja mmoja tu. Lakini Lameki alijitwalia wake wawili. Tena, aliua mtu kwa sababu alimfanyia jeuri. Akawaambia wake zake,

“Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba, Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba.” (Mwa 4:24)

Ni vizuri tuone habari ya mtu mwingine katika Daraka la Dhamiri. Jina lake ni Henoko. “Yaredi akaishi miaka mia moja na sitini na miwili, akamzaa Henoko.” (Mwa 5:18)

“Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mun-gu. Baada ya kumzaa Methusela aliishi miaka mia tatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye aka-toweka, maana Mungu alimtwaa.” (Mwa 5:21-24. Tazama vilevile habari ya Henoko katika Yud 14,15)

Methusela alikuwa mwana wa Henoko. Aliishi duniani miaka mingi kupita watu wote wen-gine waliozaliwa na wanawake. Hatujui ni sababu gani uzima wake ulikuwa mrefu zaidi. Bila shaka ni kwa sababu alikuwa mtu wa haki. Hatujui. Alimzaa Lameki wa pili aliyekuwa baba wa Nuhu.

Lameki wa pili alikuwa mtu wa haki sawa na babu yake Henoko, lakini Maandiko Matakati-fu hayasemi kwamba alitembea pamoja na Mungu. Vilevile hayasemi alitenda mabaya. Lakini tunajua baba yake alitembea karibu na Mungu na hata mwana wake, Nuhu, alitembea karibu na Mungu, hivyo tunahisi Lameki naye alitembea karibu na Mungu. Wakati alipomzaa mtoto wake Nuhu, alisema,

“Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA.” (Mwa 5:29)

Nuhu alikuwa mtu wa namna nyingine. Watu wote wengine walianguka katika dhambi. Yeye aliishika haki. Alijaribu kumtii Mungu katika mambo yote. Aliudharau uovu na kuupenda wema. Kwa sababu hii, alipata neema machoni pa Bwana (Mwa 6:7,8). Nuhu alimzaa Shemu, Hamu na Yafethi.

“Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mun-gu.” (Mwa 6:9)

Mungu alimwambia Nuhu aijenge safina. Alimpa vipimo vyote vya safina na alimwonesha jinsi ya kuitengeneza safina. Mungu alikusudia kuileta gharika ya maji juu ya nchi awaue watu wote chini ya mbingu, hata kila kitu kilicho hai duniani kife (Mwa 6:14-17).

SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA YA DHAMIRI

Tumeona wakati wa Daraka la Dhamiri watu walianza kuwa wengi duniani. Watu waliweza kuwazaa watoto wengi, kwani, waliishi miaka mingi kabla hawajafa. Tena tuliona siku zile ha-wakuwa na sheria, kama vile Sheria ya Musa, lakini watu wote waliongozwa na dhamiri zao ili wayatende matendo mema au mabaya. Lakini pamoja na hayo Mungu alikuwa amewapa maa-gizo mengine.

Page 20: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 16 -

Kwanza, Mungu aliwaagiza wayafuate maagizo hayo na kuzitii dhamiri zao. Adamu na Ha-wa walikuwa wamekula matunda ya mti wa kujua mema na mabaya. Hapo walianza kutambua tofauti kati ya haki na dhambi. Kaini na Abeli waliyajua mambo haya vilevile. Hata watu wote waliozaliwa na Adamu na Hawa waliyajua mema na mabaya kutokana na sauti ile ndogo ya dhamiri iliyowaongoza.

Wakati Bwana Mungu alipowachinja wanyama na kuwafanyia Adamu na Hawa mavazi ya ngozi ya wanyama wale, watu walifundishwa habari ya kutoa sadaka za kuteketezwa. Maana ya sadaka hizo ilikuwa kuikiri dhambi na kuomba msamaha kutoka kwa Mungu. Kutoa sadaka hizo za kuwachinja wanyama na kumwaga damu mara kwa mara, lilikuwa agizo la Mungu kwa ajili ya kupata msahama wa dhambi (Mwa 4:3,4).

Agizo la tatu kwa watu lilikuwa kuishinda au kuiacha dhambi. Tangu anguko la Adamu, wa-tu walijaribiwa ili waitende dhambi, kwani, walizaliwa katika hali ya dhambi. Hata Daudi alisema,

“Tazama, nikazaliwa nikiwa na hatia; Mama yangu akanichukua mimba nikiwa na dhambi.” (Zab 51:5)

Na Bwana Mungu alimwambia Kaini, “Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni,

nayo inakutamani wewe, lakini yapasa uishinde.” (Mwa 4:7)

Hatuoni maagizo mengine kwa miaka mingi, mpaka siku za Nuhu. Mungu alimwambia Nu-hu,

“Jitengenezee safina ya mti wa mvinje; tengeneza vyumba ukaifunike kwa lami ndani na nje.” (Mwa 6:14)

Mwisho Mungu alimwagiza Nuhu kuhusu wanyama na ndege akisema, “Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina, ku-

wahifadhi pamoja nawe; wawe mume na mke. Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna wa-takuja kwako ili uwahifadhi. Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao.” (Mwa 6:19-21)

SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA DHAMIRI

Ijapokuwa watu walikuwa na dhamiri iliyowaongoza, mara moja walianza kuizimisha sauti yake, wakataka kutenda mabaya. Maasi yao yaliongezeka kizazi hadi kizazi. Tazama habari ya Kaini. Aliona wivu kwa sababu sadaka yake ilikataliwa na Mungu, lakini sadaka ya Abeli, ndugu yake, ilikubaliwa. Basi, siku moja Kaini aliinuka juu ya ndugu yake, akamwua, akaficha maiti yake kwenye ardhi. Lakini Mungu aliijua habari hii na alimhukumu.

Lakini siyo Kaini tu, dhambi za watu wote ziliongezeka duniani hata: “Wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo

wote waliowachagua.” (Mwa 6:2)

Walimu wengi wanasema “wana wa Mungu” katika mstari huu walikuwa malaika wabaya waliopaacha mahali pao (Yud 6 na 2 Pet 2:4) kushirikiana na wanawake wa dunia. Tena, tuna-soma,

“Wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndiyo wali-okuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.” (Mwa 6:4)

Tunaiona hila ya Shetani katika mambo haya kwa sababu alitaka kuwaharibu watu wote duniani. Watu wote walikuwa wabaya siku zile kupita kiasi. Tazama,

“BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote.” (Mwa 6:5)

Tazama jinsi watu walivyojitenga na Mungu! Kama mtume Paulo alivyosema, “Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.” (Rum

3:10,11)

Page 21: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 17 -

Tena, watu wa siku za Nuhu waliudharau ushuhuda wa Nuhu. Walimcheka. Walifikiri Nuhu alikuwa mpumbavu kwa kuijenga safina katika nchi kavu kwa kuwa siku zile haikunyesha mvua yo yote. Waliyakataa mahubiri yake ingawa Petro alisema Nuhu alikuwa “Mjumbe wa haki” (2 Pet 2:5).

SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA DHAMIRI

Tumeshaona habari ya dhambi za watu katika Daraka la Dhamiri. Wote walimwacha Mun-gu na kuyafuata matakwa yao binafsi. Dunia ilijaa uovu na ujeuri. Wana wa Mungu walijitwalia binti za wanadamu. Watoto walizaliwa katika hali ya namna tofauti.

Mungu aliyatazama matendo ya watu duniani naye alihuzunishwa kabisa. Akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mwili; basi siku zake

zitakuwa miaka mia moja na ishirini.” (Mwa 6:3)

Hakika, maasi ya watu yalizidi sana! Tena, tunaona kwamba, “BWANA akaghairi kwa kuwa amemwumba mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.” (Mwa

6:6)

Tazama huzuni ya Mungu kwa sababu ya dhambi za watu. Roho wa Mungu alikataa kushin-dana na watu tena. Dhambi za watu zilimhuzunisha Bwana Mungu. Mungu alikasirika hata alikusudia kuwahukumu watu wote duniani isipokuwa Nuhu na jamaa zake tu,

“BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewaumba.” (Mwa 6:7)

Mungu akamwambia Nuhu, “Mwisho wa kila kiumbe umefika mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia maovu, basi nita-

waangamiza pamoja na dunia.” (Mwa 6:13)

Tunaweza kusema, Mungu alichoshwa na matendo maovu ya watu, hata aliyaona maasi tu kwa watu wote duniani.

Mungu alimwambia Nuhu aijenge safina. Alimpa vipimo vyote vya kazi hii. Kisha akasema, “Tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai,

kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.” (Mwa 6:17)

Tazama, hukumu hii ni hukumu kali sana. Hakika, Mungu alikasirishwa na dhambi za watu. Ijapokuwa Mungu alitaka kuwaangamiza watu wote pamoja na wanyama na ndege wote,

alikusudia kumwokoa Nuhu na jamii yake pamoja na viumbe wengine, kama alivyosema, “Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe, na

wanao, na mkeo, na wake za wanao, pamoja nawe. Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina, kuwahifadhi pamoja nawe; wawe mume na mke. (Mwa 6:18,19)

Tazama rehema ya Mungu. Kila mara alipowahukumu watu, aliwaokoa baadhi kusudi watu wote wasiondolewa kabisa duniani.

Lakini kabla hajaileta gharika ya maji, Mungu alimwongoza Nuhu katika kuijenga safina. Pia, alimwita ili alihubiri Neno la Mungu na kuwaonya watu duniani kwa miaka mingi ili wapate nafasi ya kuzitubu dhambi zao ili wamrudie Mungu. Hivyo, wakati Nuhu alipokuwa akiijenga safina, pia alikuwa akilihubiri Neno la Mungu siku hadi siku. Ingawa watu walimcheka, Nuhu aliendelea na kazi zake. Hata mtume Petro alimwita “mhubiri wa haki.”

Siku moja Bwana akamwambia Nuhu, “Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki

mbele zangu katika kizazi hiki. Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, wa kiume na wa kike; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, wa kiume na wa kike. Tena katika ndege wa an-gani saba saba, wa kike na wa kiume; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote.” (Mwa 7:1-3)

Tazama Mwanzo 7:4. Maneno haya yanatuonesha kwamba Mungu alingoja siku saba nyingine, kisha akaileta mvua juu ya dunia kwa siku arobaini mchana na usiku, apate kukiangamiza kila kitu kilicho hai.

Page 22: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 18 -

Basi Nuhu alilitii agizo la Mungu. Aliingia kwenye safina na mke wake pamoja na wanawe na wake zao. Vilevile wanyama wote walioitwa na Mungu waliingia kwenye safina. Baada ya siku saba maji ya gharika yalikuwa juu ya nchi. Hukumu ya Mungu ilikuwa imefika duniani. Kwa siku saba maji ya chemchemi zote yalibubujika, na madirisha ya mbinguni yalifunguliwa. Mvua ilikuwa juu ya dunia siku arobaini mchana na usiku (Mwa 7:7-10).

Hakika kulikuwa maangamizi duniani kwa sababu ya mvua nyingi na chemchemi zilizobu-bujika kwa wingi. Maji yalifurika mahali pote, hata milima ilifunikwa na maji. Hapakuwepo tena nchi kavu. Watu wote walikufa. Wanyama wote walikufa. Hata ndege wa angani walikufa, kwani, hawakuweza kupata mahali pa kutua, wala kupata chakula.

Habari ya Nuhu na nyumba yake? Tazama, “Maji yakazidi, yakaifanya safina ielee, ikaelea juu ya nchi. Zab 104:26 Maji yakaongezeka zaidi

juu ya nchi; na safina ikaelea juu ya uso wa maji.” (Mwa 7:17,18)

Safina iliweza kutembea juu ya uso wa maji kama merikebu. Watu na wanyama wote wali-okuwa ndani yake walikuwa salama. Lakini,

“Wakafa watu wote waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.” (Mwa 7:21,22)

Ilivyonyesha mvua duniani kwa siku arobaini mchana na usiku, maji yakawa mengi kiasi kwamba ilichukua siku nyingi kabla hayajapungua. Neno la Mungu linasema,

“Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.” (Mwa 7:24)

Dunia ilifunikwa na maji siku mia moja na hamsini. Mungu aliwezaje kuondoa maji yote haya? Tazama,

“Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua; chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa; maji yakadumu kuondoka katika nchi; na mwisho wa siku mia moja na hamsini maji yakapunguka.” (Mwa 8:1-3)

Mwisho, safina ilifika wapi? Neno la Mungu linasema, “Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati. Maji

yakapungukapunguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.” (Mwa 8:4,5)

Baada ya siku arobaini, Nuhu alifungua dirisha la safina, ili atazame nje. Halafu akatuma kunguru kutafuta nchi kavu, lakini ndege yule alirudi kwenye safina. Kisha, akamtuma hua, lakini hua vilevile hakuona nchi kavu, akarudi kwenye safina. Baada ya siku saba nyingine, Nuhu alimtuma tena hua, naye alirudi kwenye safina lakini alikuwa na majani ya mzeituni kinywani mwake. Basi, Nuhu alisadiki kwamba maji yamepungua katika nchi. Akasubiri tena siku saba nyingine, akamtuma hua ambaye hakurudi tena kwenye safina (Mwa 8:6-12).

“Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yali-kauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka. 14Na mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa kavu.” (Mwa 8:13,14)

Tazama, tarehe za matukio haya ni wazi kabisa. Nuhu, mke wake, wanawe, pamoja na wake zao, walitoka katika safina na wakasimama juu

ya nchi kavu. Wanyama wote, ndege wote, na vitu vyote vilivyokuwa vinatambaa, vilevile vika-toka kwenye safina. Wote wakashangaa kwa sababu hawakuona hata kitu kimoja kingine kilicho hai. Waliokuwemo kwenye safina, peke yao, waliokolewa dhidi ya gharika. Tazama sasa mambo yaliyomkuta Nuhu katika Waebrania,

“Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuiokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu ma-kosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.” (Ebr 11:7)

JINA LA

DARAKA MTU MKUU MWANZO

WAKE MWISHO

WAKE MAANDIKO

MUHIMU Dhamiri Adamu Kufukuzwa kwake atoke

kwenye bustani ya Edeni Gharika ya maji Mwanzo 4 -8

Page 23: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 19 -

DARAKA LA SERIKALI

SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA SERIKALI

Tumeshaona namna Mungu alivyofunga Daraka la Dhamiri kwa hukumu ya gharika ya maji. Watu wote, wanyama wote, na ndege wote, walikufa katika maji isipokuwa Nuhu, familia yake, na viumbe waliokuwemo ndani ya safina. Baada ya gharika, nchi kavu ilionekana tena, lakini vitu vyote vilikuwa vipya.

Wakati Nuhu na nyumba yake walipotoka nje ya safina, waliona kwamba wao wenyewe tu walibaki duniani. Nuhu, mke wake, wanawe, na wake zao. Hakuwepo mtu mwingine katika dunia hata mmoja. Ni watu wanane tu waliookolewa na gharika ya maji.

Tena, tunajua mwanzo wa Daraka hilo jipya lilikuwa wakati gani kwa sababu Biblia inasema Nuhu alikuwa na miaka mia sita na moja wakati alipotoka katika safina (Mwa 8:13).

Tunafikiri wanyama wote na ndege wote walisambaa kutafuta mahali pa kukaa. Lakini Nu-hu aliwachunga wanyama saba walio safi, wa kike na wa kiume.

“Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.” (Mwa 8:20)

Mungu alipendezwa na dhabihu za Nuhu, akamwambia, “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi. Kila mnyama wa nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na

kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.” (Mwa 9:1,2)

Pia, Mungu akasema moyoni mwake, “Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa

mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.” (Mwa 8:21)

SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA SERIKALI

Hakika Nuhu mwenyewe alikuwa mtu mkuu wa Daraka la Serikali. Yeye, mke wake, wana-we watatu, na wake zao, walikuwa pekee yao juu ya uso wa dunia baada ya gharika ya maji. Majina ya wana wa Nuhu yalikuwa: Shemu, Hamu, na Yafethi. Hatujui jina la mke wa Nuhu wala majina ya wake za wana wa Nuhu (Mwa 6:9,10; 7:13).

Basi Mungu alifanya agano jipya na Nuhu na wanawe akiwaambia, “Tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu; tena na kila kiumbe

hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi. Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.” (Mwa 9:9-11)

“Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.” (Mwa 9:12-15)

Nuhu alikuwa na wana watatu tu. Hakuwa na wana wengine wala binti. Lakini wake wa Shemu, Hamu na Yafethi, waliwazalia watoto wengi. Sura ya kumi ya kitabu cha Mwanzo inaonesha vizazi vya Nuhu na jamaa zao. Lakini Nuhu mwenyewe, wakati alipokuwa na miaka mia tisa na hamsini, alikufa.

Watu walianza kuwa wengi tena duniani. Makabila yote yalitokana na familia ya Nuhu. Tuseme, watoto wa Shemu walianzisha makabila mbalimbali. Vivyo hivyo, watoto wa Hamu na wa Yafethi walianzisha makabila mengine tofauti. Watu hawa waliijenga miji yao, wakaongeza ng’ombe na mifugo yao, na wao wenyewe wakaongezeka katika nchi.

Wakati ule, watu wote walikuwa na lugha moja na usemi mmoja na wakati waliposafiri kwenda mashariki, waliikuta nchi nzuri katika sehemu za Shinari. Waliamua kukaa pale (Mwa 11:1,2). Baadaye nchi ya Shinari iliitwa nchi ya Babeli.

Page 24: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 20 -

SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA SERIKALI

Baada ya gharika ya maji, Mungu aliruhusu Nuhu na familia yake kutawala juu ya kila kitu kilicho hai duniani (Mwa 9:2). Tena, aliwaambia,

“Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapa hivi vyote.” (Mwa 9:3)

Ijapokuwa Nuhu na jamaa yake waliweza kula kila kitu kilicho hai, walikatazwa kula damu ya wanyama. Tazama, Mungu aliwaambia,

“Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.” (Mwa 9:4)

Walipaswa kumchinja mnyama kwanza ili kuimwanga damu yake kabla hawajaila nyama yake. Agizo hilo liliendelea katika Sheria ya Musa, na hata katika Agano Jipya (Matendo 15:19,20).

Kama Mungu aliweza kuiheshimu damu ya mnyama basi damu ya binadamu aliiheshimu zaidi. Tazama,

“Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.” (Mwa 9:5)

Sasa, kwa jinsi hii, Mungu alikuwa ameanzisha mpango wa watu kuishi chini ya serikali. “Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana

kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.” (Mwa 9:6)

Watu walipaswa kuwachagua waamuzi ambao watawahukumu waovu na wauaji. Hakika jambo hilo lilikuwa mwanzo wa serikali.

Tena, Mungu aliwaagiza, “Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake.” (Mwa 9:7)

Kama tulivyoona, watu walikuwa wachache tu baada ya gharika ya maji; watu wanane tu. Basi, Mungu aliwataka wawe wengi tena.

Katika agano lake na Nuhu, Mungu aliahidi kwamba hataiharibu tena dunia kwa gharika ya maji. Alisema upinde aliouweka angani utakuwa ishara ya agano hili. Hivyo, wakati watu wanapouona upinde angani, wanapaswa kulikumbuka agano la Mungu alilolifunga na Nuhu (Mwa 9:8-17).

Mungu aliwaumba watu katika mfano wake. Basi watu wanapaswa kuiheshimu miili na uhai wao. Wakati Nuhu alipomlaani Kanaani kwa kosa lake, alifanya hivi katika jina la Mungu. Na wakati alipombariki Shemu, vilevile alifanya katika jina la Mungu (Mwa 9:20-27). Mara nyingi, Mungu aliwaongoza watu wake kuwabariki au kuwalaani watu wengine kufuatana na matendo yao yakiwa mema au mabaya.

Kuna agano lingine ambalo halikuandikwa wakati wa Nuhu, lakini bado lilikuwa agizo kubwa wakati wa Nuhu. Agizo hilo lilikuwa la kumwabudu na kumtii Mungu siku zote. Mungu ni Mungu. Watu walipaswa kumwabudu. Tena, walipaswa kuyatii maagizo yake na maneno yake yote. Dhambi ya kwanza ilitendeka wakati Adamu na Hawa walipomwasi Mungu kwa kutomtii. Katika nyakati zote, mtu ye yote anayekataa kumwabudu na kumtii Mungu, ni mwenye dhambi kabisa, na hasira ya Mungu iko juu yake.

SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA SERIKALI

Ijapokuwa watu wote walio waovu walikuwa wameshahukumiwa katika gharika ya maji, wakati Mungu alipoanza tena kuijaza dunia kwa wazao wa Nuhu, hali ya dhambi iliendelea kati-ka maisha ya watu.

Tunaona habari ya dhambi za watu katika Mwanzo 9:20-23. Nuhu alikunywa mvinyo kuto-ka mizabibu yake. Hamu, baba wa Kanaani, aliingia hemani mwa baba yake akaona uchi wake, kisha aliwaambia ndugu zake wawili. Alimdharau baba yake. Lakini ndugu zake Shemu na Yafethi waliingia hemani wakamfunika baba yao na vazi bila kutazama uchi wake.

Wakati watu walipoanza tena kuwa wengi, walijazwa na kiburi na walianza kumsahau Mungu, yaani, walianza kutenda tena dhambi.

Page 25: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 21 -

Mungu aliwaagiza watu wasambae mahali pote na kuijaza dunia. Lakini watu walikataa. Wakabaki pamoja na kufanya kazi kwa pamoja. Sura ya kumi katika kitabu cha Mwanzo inatu-onesha jinsi watu walivyomwasi Mungu. Walijizalia watoto wengi lakini hawakusambaa kuijaza dunia. Nao walikuwa na lugha moja tu. Tazama maandiko ya Biblia,

“Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.” (Mwa 11:1-2)

Huko Shinari ardhi ilikuwa nzuri kwa kilimo na nyasi zilikuwa nyingi kwa mifugo. Wakati watu walipofika kwenye nchi ya Shinari, walijadiliana na mwisho waliamua kukaa pale na ku-jenga mji. Wakasema,

“Na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami bada-la ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.” (Mwa 11:3,4)

Mawazo yao yalikuwa kutoachana bali kuujenga mji ili wakae kwa pamoja. Lakini watu wale hawakuujenga tu mji, bali walianza kuujenga mnara,

“…na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina.” (Mwa 11:4)

Hapa tunaona kosa kubwa la watu katika Daraka la Serikali. Hawakuwa na mtu, hata mmo-ja, wa kuwatawala na kuwaongoza katika njia ya haki. Walitenda matendo kwa matakwa yao wenyewe. Tena, watu wale walikuwa wamemsahau Mungu. Hakuna hata neno moja katika Bib-lia linalotuonesha kwamba walitaka kumwabudu Mungu. Bali walitaka kuujenga mnara kwenda juu ili wapate kuviabudu jua, mwezi, na nyota za angani na pia wajijengee jina katika kiburi chao. Isitoshe, kusudi lingine la mawazo yao ya kuujenga mnara lilikuwa,

“Tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.” (Mwa 11:4)

Kumbuka, Mungu aliwaagiza wasambae sehemu zote duniani, lakini hawakutaka. Walitaka wakae pamoja, wapate kusaidiana na kushirikiana.

Zaidi, walijaa kiburi. Walijihesabu kuwa wazuri kuliko Mungu. Hawakuliweka tumaini lao kwa Mungu bali kwa wao wenyewe. Kwa sababu hiyo walitaka kujifanyia jina; walitaka kujiinua wao wenyewe. Walitaka kuanzisha taifa moja tu katika nchi moja na wote waongee lugha moja.

Tangu Adamu na Hawa, watu wamejaribu kuwa kama Mungu mwenyewe. Wametaka kuyatukuza majina yao kuliko jina la Mungu aliye hai.

SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA SERIKALI

Wakati watu walipoanza kuujenga mji na kuujenga mnara, Bwana Mungu alishuka ili azione kazi zao. Maneno haya yatuonesha kwamba Mungu anayajua matendo yote ya wana-damu. Hakuna tendo lo lote linaloweza kufichwa kwake. Mungu akasema,

“Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafan-ya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.” (Mwa 11:6)

Maana yake ni kwamba watu wale walianza kufikiri kwamba wao wenyewe wangeweza kufanya kila kitu kwa nguvu na kwa akili zao tu bila kuomba msaada wa Mungu. Tena, Bwana alisema,

“Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.” (Mwa 11:7)

Tazama, watu wote waliongea lugha moja tu. Hawakuwa na matatizo kwa kuwa wali-fahamiana vizuri. Lakini ghafla, kila mtu hakuweza kuyaelewa matamshi ya jirani yake. Wote walishangaa kabisa. Matokeo yake kukazaliwa lugha nyingi hadi walimu wa leo wanahesabu kwamba kuna lugha elfu saba na zaidi katika dunia hii.

“Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.” (Mwa 11:8)

Kwa hukumu ya Mungu watu hawakuwa tena watu wa taifa moja, maana hawakuweza kuelewana. Basi, ushirikiano wao ulivunjwa. Hawakuweza tena kuwa marafiki pia hawakuweza kufanya kazi kwa pamoja. Mpango wao wa ujenzi ulikoma kabisa.

Page 26: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 22 -

Hata leo, katika kila nchi watu wana lugha yao. Tena katika nchi nyingi kuna lugha nyingi zaidi ya moja. Kwa mfano katika nchi ya Kongo kila kabila lina lugha yake. Kupitia historia watu wamepigana vita, taifa kwa taifa, kwa sababu ya kutoweza kuelewana kutokana na utofauti wa lugha. Shida ya lugha imefanya hali ya kutembeleana kuwa ngumu. Ni kawaida kwa mtu kutofahamu hata neno moja la kabila lingine. Tazama tena Maandiko Matakatifu,

“Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.” (Mwa 11:9)

Hukumu hiyo ya Mungu ilileta mwisho wa Daraka la Serikali. Baada ya kuwachafulia lugha na kuwasambaza, Mungu alianzisha mpango mpya katika uhusiano wake na wanadamu kum-pitia Abramu.

JINA LA

DARAKA MTU MKUU MWANZO

WAKE MWISHO

WAKE MAANDIKO

MUHIMU Serikali Nuhu Baada ya gharika Kusambazwa kutoka mnara

wa Babeli Mwanzo 9 – 11

Page 27: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 23 -

DARAKA LA AHADI

SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA AHADI

Sasa, ni vizuri kukumbuka kwamba Daraka la Usafi lilianza na Adamu, na baada ya Adamu kutenda dhambi, Daraka la Dhamiri lilianza. Daraka hilo liliendelea mpaka siku za Nuhu, nalo lilimalizika kwa hukumu ya gharika ya maji. Ndipo Daraka la Serikali lilianzishwa na Nuhu baada ya gharika. Daraka hilo liliendelea hadi wito wa Abramu.

Tangu kuumbwa kwa Adamu mpaka wito wa Abramu kulikuwa miaka mingi sana. Bila sha-ka ilikuwa miaka elfu mbili au zaidi. Hatujui kwa uhakika kwa sababu mambo yote ya historia ya watu hayakuandikwa wakati ule, bali kuna mapengo kwenye habari iliyoandikwa. Kwa sababu hiyo, walimu wa historia wanashindwa kupatana juu ya habari za miaka ya watu hawa wa za-mani.

Baada ya makabila kusambaa, kwa sababu ya kuchafuliwa lugha kule Babeli, watu waliji-jengea miji mahali pengi. Lakini wengine walibaki katika nchi ya Babeli. Nao wakajenga miji ya Babeli, Uru na Ninawi. Siku moja, mtu fulani aliyeitwa Tera, aliitwaa jamii yake, nao wakatoka katika Uru wakiwa na mpango wa kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika kwa Harani waliamua kukaa mahali pale (Mwa 11:31).

Waliosafiri na Tera walikuwa Abramu, ndiye mwana wa Tera, na Lutu, mwana wa Harani (Harani alikuwa mwana wa Tera aliyefariki kabla ya safari hiyo). Tena, Sarai, mke wa Abramu alienda pamoja nao. Nahori, mwana mwingine wa Tera, alibaki katika mji wa Uru, hakuenda pamoja na baba yake na Abramu ndugu yake (Mwa 11:27-32).

Daraka hili linaitwa Daraka la Ahadi kwa sababu ya ahadi za Mungu kwa Abramu na wazao wake. Tazama ahadi ya kwanza,

“Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.” (Mwa 12:2-3)

Siku nyingine, Mungu alimwita Abramu, akamwambia ahadi nyingine, “BWANA akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, uka-

tazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.” (Mwa 13:14-15)

Wakati Neno la Mungu lilipokuja kwa Abramu katika ndoto Abramu alipewa ahadi ya tatu, “Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye

mrithi wangu. Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali utakayemzaa ndiye ata-kayekurithi. Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.” (Mwa 15:3-5)

Basi, Abramu akamwamini Mungu na Mungu akamhesabia Abramu kuwa mwenye haki. Ahadi ya nne ilitamkwa hivi,

“Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. Nami nitafanya agano langu nawe, nami nitakuzidishia sana. Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, Hili ndilo agano langu nawe, utakuwa baba wa Mataifa mengi, wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Abrahamu, kwani nimekuweka uwe baba wa Mataifa mengi.” (Mwa 17:1-5)

Ahadi hizo, ambazo Mungu alimpa Ibrahimu (ambalo ni jina lake jipya), aliziahidi tena kwa mtoto wake Isaka na kwa Yakobo mwana wa Isaka (Mwa 2:2,4 na 28:13-15). Tangu wakati ule, Waisraeli, katika maombi yao kwa Mungu, kawaida walitamka, “Ee Mungu, Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka, na wa Yakobo.” au, “Mungu wa baba zetu.” Waliomba hivyo kwa sababu walielewa kwamba Mungu aliuanzisha uhusiano maalum na taifa lao kuanzia na Ibrahimu. Uhusiano huo maalum uliyaanzisha mabadiliko katika mpango wa Mungu kwa ajili ya wanadamu. Tena ndiyo mwanzo wa Daraka la Ahadi ambalo ndilo jina la mpango huo mpya.

Page 28: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 24 -

SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA AHADI

Ibrahimu ni mtu mkubwa wa Daraka la Ahadi. Ibrahimu alikuwa mwana wa Tera wa mji wa Uru wa Wakaldayo. Alikuwa na ndugu wawili: Nahori na Harani. Harani alikufa, lakini Ibrahimu na Nahori walioa wake. Jina la mke wa Ibrahimu lilikuwa Sarai (ambalo Mungu alibadilisha baadaye kuwa Sara), na jina la mke wa Nahori lilikuwa Mika. Sara alikuwa tasa; hakuwa na mto-to. Ibrahimu, Sara na Lutu walienda pamoja na Tera hadi mji wa Harani, nao wote walikaa pale. Tera alifariki Harani. Kisha Mungu alimwambia Ibrahimu:

“Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nita-kayokuonesha.” (Mwa 12:1)

Hakika, kwa mtu kuiacha nchi yake, nyumba ya baba yake, na ndugu zake, ili aende mbali katika nchi ya kigeni ni jambo gumu sana. Lakini Ibrahimu alipewa ahadi na Mungu, naye alili-weka tumaini lake kwa Mungu bila wasiwasi. Mara moja alianza safari yake.

“Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Ka-naani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.” (Mwa 12:5)

Ibrahimu alionesha imani ya ajabu; alienda bila kujua lengo la safari yake. Tazama, “Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi;

akatoka asijue aendako.” (Ebr 11:8)

Basi, Ibrahimu aliweza kufika katika nchi ya Kanaani. Watu wa nchi hiyo walikuwa wageni kwake, naye alikuwa mgeni kwao. Hata lugha zao zilikuwa tofauti. Lakini Biblia inatuambia,

“Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.” (Ebr 11:9)

Ibrahimu hakukaa katika nyumba, bali katika hema, kwani nchi ilikuwa wazi. Siku nyingi zilipita, lakini Sara hakumzalia mtoto, kisha akamwambia,

“Sarai akamwambia Abramu, kwa kuwa BWANA amenifunga tumbo nisizae, sasa mwingilie mjakazi wangu, labda nitapata uzao kutoka kwake.” (Mwa 16:2)

Basi Ibrahimu akaitii sauti ya Sara, akamtwaa Hajiri, kijakazi wa mke wake, awe mke wake. Kisha, Hajiri akapata mimba, amkazaa mwana, na jina lake lilikuwa Ishmaeli. Lakini mtoto huyu hakuwa mtoto wa ahadi. Wakati ule Mungu alilibadilisha jina la Abramu kuwa Ibrahimu na jina la Sarai kuwa Sara..

“BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema. Sara akapa-ta mimba akamzalia Abrahamu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. Abrahamu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia” (Mwa 21:1-3)

“Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wa-kati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.” (Ebr 11:11)

Kwa sababu Hajiri na Ishmaeli, mwana wake, walifanya fujo hemani mwa Ibrahimu, wote wawili walifukuzwa. Lakini Ibrahimu na Sara walimlea mtoto wao Isaka wakimfundisha kumtii Mungu. Wakati Isaka alipokuwa mtu mzima, baba yake alimtuma mtumishi wake amtafutie Isa-ka mke. Alimtwaa Rebeka kutoka nyumba ya Bethueli, mwana wa Milka aliyemzaa Nahori. Isaka alimpenda Rebeka, akamtwaa kuwa mke wake. Kisha, Rebeka alimzalia Isaka mapacha. Mtoto wa kwanza aliitwa Esau na wa pili Yakobo. Katika ujana wake Esau aliuza urithi wake wa kuwa mzaliwa wa kwanza kwa mdogo wake Yakobo kwa ajili ya chakula tu, kwani, alikuwa na njaa. Tendo hilo lilikuwa kosa mbele ya Mungu.

Kwa hila ya Yakobo na Mama yake Rebeka, Yakobo alibarikiwa na baba yake Isaka badala ya Esau. Lakini jambo hilo lilikuwa kusudi la Mungu, kwani, alijua Yakobo atakuwa mtu wa haki. Katika maisha yake Yakobo alipambana na mateso mengi. Alidanganywa mara nyingi na Labani, aliona hofu kwa sababu ya Esau mkubwa wake, na alipigana na malaika. Mwisho Mungu al-imbariki na kumbadilishia jina lake kuwa Israeli. Alikuwa na wake wawili na masuria wawili. Hawa walimzalia Yakobo wana wa kiume kumi na wawili na msichana mmoja.

Mmoja wa wana wa Yakobo aliitwa Yusufu. Mara kwa mara aliota ndoto zilizoonesha kwamba baba yake na ndugu zake wote watamtumikia. Ndugu zake walimchukia, na siku moja

Page 29: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 25 -

walimkamata na kumwuza kwa Waishmaeli, nao walimpeleka katika nchi ya Misri kama mtumwa. Pale walimwuza kwa Potifa, akida wa Farao. Kisha, baada ya matukio mengi mabaya, Yusufu alipata neema machoni pa Farao, naye alimfanya kuwa mkuu katika nchi. Mungu aliifun-ga mvua katika nchi ya Kanaani, na kulikuwa njaa kali sana. Kisha, Waisraeli walienda Misri kutafuta chakula, na Yusufu, mwana wa Yakobo, alijitambulisha kwao akiwasaidia sana ndugu zake.

Baada ya kufa kwa Yakobo na watoto wake, Waisraeli waliendelea kuwa wengi katika nchi ya Misri. Walikuwa wamehamia Misri moja kwa moja kutokana na njaa ya Kanaani. Farao, ali-yeonesha huruma kwa wana wa Yakobo, alikuwa amefariki naye pia. Farao mpya aliwachukia Waisraeli akaanza kuwatesa sana. Lakini Mungu alimteua mtu mwingine aliyeitwa Musa ili awaokoe.

“Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaenda akaoa binti mmoja wa Lawi. Yule mwanamke aka-chukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu.” (Kut 2:1-2)

Mama yake Musa alimficha Musa mtoni kwenye kisafina cha nyasi. Binti wa Farao akaja, akamwona mtoto, akamtwaa, akamwita jina lake Musa, kwa sababu “Nimemtoa majini” (Kut 2:5-10 BHN).

SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA AHADI

Agizo la kwanza katika Daraka la Ahadi lilikuwa kwa Ibrahimu kwenda katika nchi ya Ka-naani. Kama tulivyoliona, Ibrahimu alizaliwa katika mji wa Uru, nchi ya Ukaldayo. Baadaye ali-hama pamoja na baba yake Tera na mke wake Sara, kwenda mji wa Harani. Lakini Mungu ha-kumwacha pale, bali alimwagiza aende Kanaani. Ibrahimu na ndugu zake walikuwa na mifugo mingi kama vile punda, ngamia, ngombe, na kondoo. Wakati walipofika katika nchi ya Kanaani, Mungu aliwaagiza kuteka nchi ile yote. Mungu akamwambia Ibrahimu,

“Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.” (Mwa 13:17)

Kwa imani, Ibrahimu alipiga hema yake Kanaani na Mungu alimbariki hadi alikuwa na wa-tumishi wengi na mifugo mingi. Wakati Mungu alipolibadilisha jina la Abramu kuwa Ibrahimu, alimwambia,

“Mungu akamwambia Abrahamu, Nawe ulishike agano langu, wewe, uzao wako na vizazi vyao. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati yangu nawe, na uzao wako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi. Katika vizazi vyako vyote, kila mtoto wa kiume miongoni mwenu atatahiriwa akiwa na umri wa siku nane, awe mtumishi aliyezaliwa katika nyumba yako au uliyemnunua kwa fedha za-ko japo hakuwa wa uzao wako.” (Mwa 17:9-12)

Agizo hilo lilikuwa kubwa sana kwani lilikuwa ishara ya agano kati ya Mungu na Ibrahimu. Hata leo tohara ni ishara kwa Wayahudi mahali pote duniani.

Kabla Isaka hajazaliwa, Ibrahimu alimwomba Mungu kumbariki Ishmaeli kama mtoto wa ahadi, lakini Mungu alikataa.

“Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.” (Mwa 17:19)

Hata hivyo Mungu alimbariki Ishmaeli kwa kuwa alikuwa mtoto wa Ibrahimu kwa Hajiri. Lakini alisema wazi kwamba Isaka atakapozaliwa atakuwa mtoto wa ahadi na wa agano.

Hajiri na Ishmaeli walimdharau mwana wa Sara naye akafadhaika rohoni mwake. Sara ali-jua kwamba Isaka alikuwa mtoto wa ahadi, lakini Hajiri alimsumbua siku hadi siku mpaka Sara akamwambia Ibrahimu,

“Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwa-nangu, Isaka.” (Mwa 21:10)

Ibrahimu hakupenda kufanya vile, kwani alimpenda Ishmaeli. Lakini Mungu akamwambia, “Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila aku-

ambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.” (Mwa 21:12)

Page 30: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 26 -

Tazama, Ibrahimu alikuwa ameshamtii Mungu akiagizwa kuteka nchi ya Kanaani, alimwa-mini Mungu na akapewa mtoto wa ahadi kulingana na ahadi ya Mungu, na alilitii agizo la Mungu kuhusu mambo ya tohara kama ishara ya agano alilokuwa nalo na Mungu. Agizo lingine la Dara-ka la Ahadi lilimjia Isaka mwana wa Ibrahimu,

“Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia. Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.” (Mwa 26:2-3)

Agizo hilo ni kubwa kuliko maagizo yote katika Daraka la Ahadi.

SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA AHADI

“Basi kulikuwa na njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa kali katika nchi.” (Mwa 12:10)

Kosa moja la Ibrahimu katika Daraka la Ahadi lilikuwa kutomtii Mungu wakati alipokimbil-ia Misri. Mungu alikuwa ameahidi kumbariki katika nchi ya Kanaani lakini wakati njaa ilipoku-wa nzito, Ibrahimu hakumwamini Mungu, alikimbilia nchi ya Misri pamoja na Sara. Huko Misri Ibrahimu aliingia katika hatari kwa sababu alipatana na mke wake waseme uongo ya kwamba Sara siyo mke wake bali ni dada yake. Lakini wakati Farao alipomtaka Sara kimapenzi, Mungu alimtesa. Kwa sababu hiyo Farao alimfukuza Ibrahimu na Sara pamoja na watumishi wao wote.

Kosa lingine lilitokea wakati Ibrahimu na Sara waliposhindwa kumwamini Mungu kuhusu jinsi watakavyopata mtoto. Ibrahimu na Sara walikuwa wazee kabisa, nao hawakuwa na watoto kwa sababu Sara alikuwa tasa. Basi, Sara alimwambia mume wake ajitwalie Hajiri, kijakazi wake, ili amzalie mwana. Ibrahimu alifanya hivyo, na Hajiri alipata mimba na alimzalia mwana aliyeitwa Ishmaeli. Kufanya hivyo kulikuwa kosa katika imani ya Ibrahimu kwa sababu Mungu alikuwa ameshamwahidi Ibrahimu kwamba Sara atamzalia mtoto.

Kosa la Yakobo lilikuwa kumdanganya ndugu yake Esau. Tazama, “Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka mbugani, naye alikuwa amechoka sana.

Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu. Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza. Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi?” (Mwa 25:29-32)

Ijapokuwa Mungu alitaka Yakobo apate haki ya mzaliwa wa kwanza, Yakobo alikosea kwa kuwa aliipata kwa njia ya hila na siyo kwa njia ya Mungu.

Ingawa Yakobo alikosea wakati alipomdanganya ndugu yake, Esau alikosea vilevile kwa sababu hakuithamini haki yake ya kuwa mzaliwa wa kwanza . Hakika aliyaweka mahitaji ya mwili wake juu kuliko mahitaji ya roho yake.

Mara ya pili Rebeka na Yakobo, mwana wake, walimdanganya Isaka aliyekuwa mzee na kipofu kabisa. Isaka alimtuma Esau, mwana wake wa kwanza, kwenda porini kuwinda wanya-ma, kwani, Isaka alipenda kula nyama ya porini. Isaka alikusudia kumbariki Esau wakati ataka-porudi na chakula cha nyama ya porini. Lakini wakati Esau alipoenda porini, tazama mama yake na Yakobo walipatana kumdanganya Isaka. Rebeka alimvalisha Yakobo ngozi ya mwana -mbuzi, kwa maana Esau alikuwa mwenye nywele nyingi. Tena, Rebeka alipika mchuzi na mkate uliofanana na chakula ambacho Isaka alimwomba Esau ampikie. Mwisho, kwa sababu ya kum-danganya Isaka ili afikiri kuwa Yakobo ni Esau, Yakobo alipewa baraka ya Esau. Wakati Esau aliporudi, tazama baba yake alikuwa ameshambariki Yakobo badala yake (Mwa 27).

Yakobo alimtumikia Labani miaka saba ili apate kumwoa Raheli, lakini Labani alimdangan-ya, akampa Lea, binti yake wa kwanza. Basi Yakobo alimtumikia kwa miaka saba tena, kisha al-ipewa Raheli kuwa mke wake. Halafu alipata masuria wawili walio vijakazi wa Lea na Raheli. Wanawake hawa walimzalia wana kumi na wawili wa kiume na msichana mmoja.

Yakobo alimpenda mtoto wake Yusufu kuliko wana wote wengine. Alimfanyia vazi la rangi mbalimbali. Lakini wana wa Yakobo walimchukia Yusufu, tena waliitafuta njia ya kumwua. Siku moja, Yakobo alimtuma Yusufu akawatafute ndugu zake. Wakati alipofika kwa ndugu zake, walimkamata na kumwuza kwa Waishmaeli waliokuwa safarini kwenda Misri. Watu hawa, wa-kati walipofika Misri, walimwuza Yusufu kama mtumwa kwa Potifa, akida wa Farao. Baada ya

Page 31: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 27 -

siku nyingi na matukio mengi, Yusufu alipata neema machoni pa Farao, naye alimfanya kuwa mkuu wa nchi.

Ijapokuwa Mungu aliwaambia wana wa Israeli wakae katika nchi ya ahadi, wakati njaa ilipokuja tena Kanaani, waliamua kwenda Misri wakatafute chakula na mwisho waliamua kukaa Misri kinyume na agizo la Mungu. Hili ni kosa kubwa kuliko makosa yote katika Daraka la Ahadi. Waliidharau ahadi ya Mungu ya kuibariki nchi ya ahadi na walishindwa kulitii agizo la Mungu la kutoshukia Misri. Tokeo la kosa hilo ni uamuzi wa Mungu kuanzisha Daraka jingine.

SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA AHADI

Tunajua Mungu anahukumu dhambi zote, moja moja njiani, na pia tunajua kuna hukumu ya mwisho juu ya watu wote wanaoukataa upendo wa Mungu, wenye kuyaasi maagizo yake.

Hukumu ndogo iliwapata Ibrahimu na Sara wakati walipoenda Misri na Ibrahimu al-imwambia Farao kwamba Sara alikuwa ndugu yake. Walifukuzwa watoke katika nchi ile.

Hukumu nyingine iliwapata wakati Ibrahimu alijitwalia Hajiri, kijakazi wa Sara, kuwa mke wake. Hajiri alimzalia mwana na tokeo lake likawa fujo tupu katika nyumba ya Ibrahimu.

Yakobo alimdanganya Esau, naye akadanganywa na Labani akivuna alichokipanda. Tena, kulikuwa vita katikati ya wazao wa Yakobo na wa Esau kutokana na jinsi Yakobo alivyomtendea Esau kwa udanganyifu.

Kulikuwa makosa mengi siku zile na hukumu mbalimbali. Lakini kosa kubwa lilikuwa wa-kati Yakobo na jamaa zake walipoiacha nchi ya Kanaani, yaani nchi ya ahadi. Mungu alikuwa amewaagiza kwa uwazi wasiiache Kanaani na wasikae Misri. Mungu alikuwa amewaambia wakibaki Kanaani atakuwa pamoja nao na atawabariki sana. Lakini katika kipindi cha njaa wa-lisafiri kutafuta chakula katika nchi ya Misri na mwishoni waliamua kuhamia Misri. Mwanzoni hali yao huko Mirsi ilikuwa nzuri wakifaidika, lakini baadaye walipata mateso kwa sababu ha-wakumsikiliza Mungu na kuziamini ahadi zake. Wakajikuta wako chini ya hukumu ya Mungu badala ya baraka zake ambazo wangezikuta kama wangebaki Kanaani.

Wakati Yusufu, mwana wa Yakobo, alipokuwa mkuu wa Misri akipendwa na Farao, wana wa Israeli waliweza kukaa nchini kwa usalama. Lakini baada ya kufa kwa Yusufu, na kwa Farao aliyempenda Yusufu, maisha ya Waisraeli yalibadilika kabisa. Mateso ya Waisraeli yalianza wa-kati mfalme mpya aliposimama kuitawala nchi ya Misri. Yeye hakuwapenda Waisraeli. Aka-waambia watu wake,

“Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. Haya! Na tuwaten-dee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.” (Kut 1:9-10)

Kwa sababu hii wakawafanya Waisraeli kuwa watumwa. Waisraeli walimjengea Farao miji na majengo mbalimbali. Tena, Wamisri waliendelea kuwatesa Waisraeli. Tazama,

“Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; wakafanya maisha yao kuwa machun-gu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.” (Kut 1:13,14)

Farao alipoona kwamba Waisraeli waliongezeka katika nchi, aliamua kuwaua watoto wao wa kiume. Aliwaambia wakunga wa Waebrania,

“Wakati mnapowazalisha wanawake wa Kiebrania na kuona kuwa ni mtoto wa kiume basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto wa kike, na aishi.” (Kut 1:16)

Halafu Farao aliwaagiza watu wake wote akisema, “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto wa kike mtamhifadhi hai.”

(Kut 1:22)

Lakini wakunga hawakumtii Farao. Mungu alisikia kilio cha wana wa Israeli, naye al-imwonya Farao, lakini Farao hakumsikiliza Mungu. Bali aliwaambia watu wake,

“Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo; na waende wakatafute majani wenyewe. Lakini hesabu ya matofali waliyokuwa wakifanya tokea hapo, wawe-keeni iyo hiyo, msiipunguze hata kidogo, kwa maana ni wavivu hao; kwa hiyo wanapiga kelele, wakisema, Tupe ruhusa twende kumtolea Mungu wetu dhabihu. Wapeni watu hao kazi nzito zaidi, waitaabikie; wala wasiangalie maneno ya uongo.” (Kut 5:7-9)

Page 32: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 28 -

JINA LA

DARAKA MTU MKUU MWANZO

WAKE MWISHO

WAKE MAANDIKO

MUHIMU Ahadi Ibrahimu Kuitwa kwake Utumwa katika nchi ya Misri Mwanzo 12 – 50

Kutoka 1 - 19

Page 33: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 29 -

DARAKA LA SHERIA

SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA SHERIA

Wakati Mungu alianzisha Daraka la Sheria, Ibrahimu, Isaka na Yakobo walikuwa wameshafariki. Waisraeli walikuwa wamekaa katika nchi ya Misri yapata vizazi vinne na walikuwa watumwa chini ya Farao mbaya. Waliteswa sana, hata walimlilia Mungu na Mungu alikisikia kilio chao, naye alimwita Musa awaokoe. Alimwambia,

“Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.” (Kut 3:10)

Wakati Musa na Haruni, ndugu yake, walipomwendea Farao, walimwomba awaruhusu wana wa Israeli waende kwao. Lakini Farao alikataa, na zaidi aliongeza mateso kwa Waisraeli. Aliwaambia wasimamizi wake waizidishe kazi ya Waisraeli iwe nzito zaidi (Kut 5:6-14).

Basi Mungu alikasirika, naye aliwatuma Musa na Haruni waende nyumbani kwa Farao ma-ra kumi wakiomba rehema ya Farao kuwaruhusu Waisraeli wahame kutoka Misri. Lakini kila mara Farao alikataa, na kila mara Mungu aliipiga nchi ya Misri na pigo mpaka mapigo yalifika kumi (Kut 7-12). Lakini Waisraeli wenyewe hawakupigwa, kwani Mungu aliwatunza. Mwisho Farao alichoka, alimwogopa Mungu, na aliwaruhusu wana wa Israeli waende kwao, yaani katika nchi waliyoahidiwa na Mungu.

“Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu elfu mia sita wanaume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto. 38Na kundi kubwa la watu waliochangamana mno wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng'ombe, wanyama wengi sana.” (Kut 12:37-38)

Waliivuka Bahari ya Shamu wakitembea juu ya nchi kavu kwa sababu Mungu aligawanya maji yake. Lakini Farao na jeshi lake waliowafuata walikufa wote baharini wakati maji yalipopa-rudia mahali pake (Kut 14-15). Na wingu la Bwana liliendelea mbele ya Waisraeli.

“Kisha wakasafiri kutoka Elimu, na mkutano wote wa wana wa Israeli wakafikia jangwa la Sini, lililoko kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri.” (Kut 16:1)

Katika safari hii, Waisraeli walisikia kiu na walilalamika ili wapate maji. Mungu alimwam-bia Musa aupige mwamba kwa fimbo yake, na tazama, maji yalitoka kwenye mwamba. Wal-inung’unika tena kwa sababu walisikia njaa. Musa na Haruni waliomba kwa Mungu, na tazama, Mungu aliwapa mana kutoka mbinguni (Kut 16:1-15). Kwa jinsi hii Mungu aliwatunza watu wake katika safari yao.

Musa aliteswa sana na manung’uniko ya wana wa Israeli. Maneno yao yalimkera kabisa. Yethro, kuhani wa Midiani, mkwe wa Musa, alikuja kumwona Musa na kusanyiko la Waisraeli. Wakati alipoona namna gani Musa alivyoketi kuyasikiliza maneno ya watu tangu asubuhi hadi usiku, alimwambia achague watu wengine, wenye akili, wenye kuyajua maagizo ya Mungu, wamsaidie katika kuwaongoza Waisraeli. Musa alipendezwa na wazo hilo, aliwachagua watu wenye akili, akawaweka wawe wakuu juu ya watu (Kut 18).

Kisha, wana wa Israeli walifika Sinai. “Mwezi wa tatu baada ya Waisraeli kutoka katika nchi ya Misri, siku iyo hiyo wakafika katika

jangwa la Sinai. 2Nao walipokuwa wameondoka Refidimu na kufika jangwa la Sinai, wakatua katika lile jangwa; Israeli wakapiga kambi huko wakiukabili mlima.” (Kut 19:1-2)

Ilikuwa safari ndefu kabisa. Walienda kwa miguu, na walikuwa na mifugo pamoja nao. Mwisho walichoka na walitaka kupumzika. Mungu alikuwa tayari kukutana na wana wa Israeli katika Mlima wa Sinai. Mlima huu uliitwa “mlima mtakatifu.” Mungu akamwambia Musa:

“BWANA akamwambia Musa, Nenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao, wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika Mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote. Nawe utawawekea mipaka watu hawa pande zote, ukisema, Ji-hadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata pambizo zake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa.” (Kut 19:10-12)

Page 34: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 30 -

“Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka.” (Kut 19:16)

Wakati ule ulikuwa miaka 430 tangu siku za Ibrahimu (Gal 3:17).

SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA SHERIA

Hakika Musa alikuwa mtu muhimu kuliko wengine katika Daraka la Sheria. Musa alizaliwa katika nchi ya Misri lakini alikuwa Mlawi kwa kuwa wazazi wake walikuwa Walawi. Lawi alikuwa mmoja wa wana kumi na wawili wa Yakobo aliyeitwa Israeli. Musa aliwekwa mkononi mwa binti wa Farao wakati alipokuwa angali mtoto mchanga.

Wakati Musa alipokuwa na miaka arobaini, alimwona Mmisri mmoja akimpiga Mwebrania. Katika hasira Musa alimpiga na akamwua Mmisri huyu. Halafu Musa alikimbilia nchi ya Midiani. Aliwachunga kondoo kwa Reueli, na alioa binti yake Sipora. Baada ya kukaa Midiani miaka arobaini Musa aliitwa na Mungu kwenda kuwaokoa wana wa Israeli huko Misri.

Musa alimtii Mungu. Yeye na Haruni walikuwa hodari na walisimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri, kwa ajili ya Waisraeli walioteswa sana chini yake. Mungu alimshinda Farao kwa mapigo kumi, mwisho Waisraeli wote walivuka Bahari ya Shamu wakirudi katika nchi yao. Musa ndiye aliyewaongoza watu wale wengi sana katika safari hiyo ya hatari. Musa aliianzisha safari hiyo wakati alipokuwa na miaka themanini, naye alikufa akiwa na miaka mia moja na ishirini. Habari ya safari yao imeandikwa katika vitabu vya Kutoka, Walawi, Hesabu, na Kum-bukumbu la Torati.

Wakati wana wa Israeli walipofika Mlima wa Sinai, Mungu alimwita Musa apande juu ya mlima ili aongee naye. Hapo, Mungu alimpa sheria na maagizo kuhusu ujenzi wa hema ya kuku-tania. Musa alikuwa mtumishi wa Mungu kabisa. Aliwafundisha watu mambo yote ya sheria za Mungu, aliwahukumu watu waliotenda dhambi, na alikuwa mwombezi wao mbele ya Mungu.

Haruni alikuwa ndugu yake Musa, naye alikuwa Mlawi. Mungu alimchagua amsaidie Musa na pia ayaongoze mambo ya Ibada. Haruni alikuwa Kuhani Mkuu wa kwanza katika Israeli na wana wake walikuwa makuhani. Mungu alilichagua kabila la Walawi kuwa watumishi katika hema takatifu na uzao wa Haruni kuwa makuhani.

Wakati Waisraeli walipowashinda maadui zao na kuimiliki nchi ya Kanaani, Mungu ali-waweka waamuzi juu yao. Kazi ya waamuzi hawa ilikuwa kuwahukumu watu na kuitawala nchi hiyo. Habari hizi zimeandikwa katika kitabu cha Waamuzi. Samweli alikuwa mwamuzi wa mwi-sho.

Katika siku za Samweli, wakati alipokuwa mzee, wana wa Israeli walikuja kwake wakiomba wapewe mfalme awatawale. Kwa uongozi wa Mungu, Samweli alimchagua Sauli kuwa mfalme wa Israeli. Daudi alitawala baada ya Sauli kama mfalme, na Sulemani akatawala baada ya Daudi. Kisha, ufalme ukagawanyika katika falme mbili. Wafalme wengi wa Israeli walikuwa watu wa-baya, lakini wengine walikuwa wazuri.

Kwa sababu ya dhambi za wafalme na makosa ya watu, Mungu aliwaita manabii. Kazi yao ilikuwa kuwakumbusha Waisraeli juu ya sheria za Mungu na kuwaonya kuhusu hukumu itaka-yowaangukia wakishindwa kuzitii sheria zake. Tena, manabii walitabiri juu ya mambo yataka-yokuja kwa wakati ujao. Hakika manabii walikuwa sauti ya Mungu wakilihubiri Neno lake.

Basi, watu wa Daraka la Sheria walikuwa: 1. Musa 2. Haruni 3. Waamuzi 4. Wafalme 5. Manabii 6. Bwana Yesu Kristo.

SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA SHERIA

Katika Daraka la Sheria maagizo na amri ni nyingi sana. Wengine wamezihesabu na wanasema ziko sheria 613 ambazo Musa alipewa kwa ajili ya Waisraeli. Daraka hili lilianzishwa wakati Musa alipopanda Mlima wa Sinai kukutana na Mungu wakati alipopokea amri kumi. Waisraeli wote walikuwa wameshasafiri kutoka nchi ya Misri hadi Mlima wa Sinai. Maandiko yanasema,

“Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu BWANA alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuri, mlima wote ukatetemeka sana.” (Kut 19:18)

Page 35: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 31 -

Watu wote waliogopa sana. Mungu alimwambia Musa mlimani, “Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.”

(Kut 20:2)

Kisha, alimpa AMRI KUMI:

(1) Usiwe na miungu mingine ila mimi;

(2) Usijifanyie sanamu ya kuchonga;

(3) Usilitaje bure jina la BWANA;

(4) Ikumbuke siku ya sabato, uitakase (Kut 20:3-11).

Amri hizi nne za kwanza zilihusu dini na ibada. Zilikataza kumtendea Mungu dhambi.

(5) Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi;

(6) Usiue;

(7) Usizini;

(8) Usiibe;

(9) Usimshuhudie jirani yako uongo;

(10) Usitamani nyumba ya jirani yako; usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako (Kut 20:12-17).

Amri hizi sita za mwisho zilikataza kuwatendea watu dhambi. Mungu aliendelea kumwagiza Musa na wana wa Israeli maagizo mengi. Maagizo yanayo-

husu watumwa yameandikwa katika Kutoka 21:1-11; yanayohusu wauaji (12-17); wenye ku-wajeruhi wenzao (18-32); kuwaharibu wanyama wa wengine (33-36); adhabu ya wezi (Kut 22:1-4); adhabu ya wenye kuharibu mali za wengine (5-31); na maagizo mbalimbali (Kut 23:1-33). Ni muhimu kuelewa kwamba maagizo haya, yaliyo katika kitabu cha Kutoka, ni msingi wa sheria ya Mungu ingawa kuna maagizo mengine mengi yanayoonekana katika vitabu vya Wala-wi na Kumbukumbu la Torati.

Pia, Mungu aliyatoa maagizo yaliyohusu vipimo vyote vya hema takatifu na vyombo vyake vyote. Alianza na hema lenyewe na mambo ya sadaka. Kisha, alimwonesha Musa namna ya kutengeneza vyombo kama sanduku la agano, kiti cha rehema, meza ya mkate wa onesho, kina-ra cha dhahabu, mapazia ya hema takatifu, madhabahu, na kiwanja cha hema (Kut 25-27). Mun-gu aliendeleza maelezo mengine kuhusu vyombo katika sura ya 30 kama vile madhabahu ya ku-chomea uvumba, sadaka ya upatanisho, birika la shaba, mafuta matakatifu ya kupakaa, na uvumba.

Lakini Mungu hakumsahau Haruni na wanawe. Aliwaweka kuwa makuhani, na Haruni mwenyewe alichaguliwa kuwa kuhani mkuu. Mungu aliwapa maagizo kuhusu utakaso wao na kuhusu huduma zao (Kut 28-29). Hakika, Haruni alikuwa mfano wa Bwana Yesu Kristo.

Musa na watu wenye uwezo walilijenga hema lile, na walivitengeneza vyombo vyake sawa-sawa na maagizo ya Mungu. Mwisho, utukufu wa Bwana ulilijaza hema lile takatifu.

“Na hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani, wana wa Israeli wakaenda mbele kati-ka safari zao zote, bali kama lile wingu halikuinuliwa, wakati ule hawakusafiri hadi siku ile lilipoinu-liwa tena. Kwa maana lile wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.” (Kut 40:36-38)

Sasa tuendelee kuzitazama sheria nyingine za Mungu zilizowekwa juu ya wana wa Israeli katika Daraka la Sheria. Katika kitabu cha Walawi, sura ya 1 hadi sura ya 7, tunayaona maagizo yanyayohusu sadaka au matoleo. Mungu alimwambia Musa,

“Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa kufugwa, katika ng'ombe, kondoo na mbuzi.” (Law 1:2)

Sheria ya kwanza ilihusu sadaka ya kuteketezwa. Wanyama waliopokelewa walikuwa ng’ombe, kondoo, mbuzi, au hua, kutegemeana na agizo la Mungu.

Sheria ya sadaka ya unga inaonekana katika Walawi sura ya pili.

Page 36: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 32 -

“Na mtu atakapomtolea BWANA matoleo ya sadaka ya unga, matoleo yake yatakuwa ya unga mwembamba; naye ataumiminia mafuta, na kutia na ubani juu yake; kisha atauleta kwa wana wa Haruni, hao makuhani; naye atatwaa konzi moja katika huo unga mwembamba, na katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha kuhani atauteketeza kuwa ndiyo ukumbusho wake juu ya madhaba-hu, ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.” (Law 2:1-2)

Tena, Bwana Mungu aliagiza wasitie chachu au asali katika sadaka ya unga, lakini alisema, “Kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi.” (Law 2:11-13)

Sura ya tatu ya Walawi inaeleza habari ya sadaka ya amani. Mungu alisema, “Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia BWANA, kwamba ni katika kundi la

kondoo; dume au jike, atamtoa huyo aliye mkamilifu.” (Law 3:6)

Kisha, alisema, “Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya

kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.” (Law 3:17)

Sura ya nne ya Walawi ina sheria zinazohusu sadaka kwa ajili ya dhambi. Mungu alimwam-bia Musa,

“BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo; Law 9:2 kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kum-songeza kwa BWANA ng'ombe dume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi” (Law 4:1-3)

Makosa madogo madogo yalihitaji matoleo ya kondoo au mbuzi dume kama sadaka kwa aji-li yake.

Kisha, Mungu alimwamuru Musa kuhusu matendo ya makuhani wakati wa kutoa sadaka. Mungu alitaka kuwafundisha makuhani kwamba matoleo yalikuwa matakatifu na ndiyo maana walikatazwa kuyapokea matoleo yasiyo makamilifu.

Pia, Mungu aliagiza sheria za chakula akitofautisha wanyama walio safi na wale walio wachafu. Alitaja majina ya wanyama safi na wale walio najisi. Alisema juu ya wanyama najisi,

“Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu” (Law 11:8)

Vilevile kulikuwa sheria zilizohusu wanawake katika kuzaa. Mungu alisema, “Nena na hao wana wa Israeli, uwaambie, Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto wa

kiume, ndipo atakuwa najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya hedhi ndivyo atakavyokuwa najisi. Siku ya nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake.” (Law 12:2-3)

Katika siku za Musa watu wengi waliteswa na ukoma na magonjwa mengine ya ngozi za miili yao. Basi, Mungu alitoa maagizo kuhusu watu hawa ili wasiambukize wengine magonjwa yao. Sheria ilisema kwamba mtu mwenye ugonjwa wa ngozi alipaswa kutengwa na watu wen-gine mpaka ngozi yake iliweza kupona.

Sheria zingine ziliwekwa juu ya mwanamume au mwanamke mwenye kutokwa na usaha au damu katika mwili wake, na pia kuhusu mambo ya ndoa. Mungu alisema,

“Ni hivi mtakavyowatenga wana wa Israeli na unajisi wao; ili wasife katika unajisi wao, hapo watakapoitia unajisi maskani yangu iliyo katikati yao.” (Law 15:31)

Tuyaangalie sasa maagizo kuhusu siku kuu zilizopangwa na Mungu kwa ajili ya Waisraeli kusherehekea. Mungu alimwambia Musa,

“Nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Sikukuu za BWANA, ambazo mtazitangaza kuwa ni makusanyiko matakatifu; hizi ni sikukuu zangu. Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato kwa BWANA katika makao yenu yote.” (Law 23:1-3)

Sikukuu ya Pasaka ilikuwa siku kubwa kuliko siku zote nyingine. Mungu alisema, “Sikukuu za BWANA ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayatangaza kwa nyakati

zake. Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni, ni Pasaka ya BWANA. Na siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa BWANA ya mkate usiotiwa chachu; mtaila mikate isiyochachwa muda wa siku saba. Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu msifanye kazi yo yote ya utumishi. Lakini mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.” (Law 23:4-8).

Page 37: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 33 -

Tazama vilevile Kutoka sura 12 ili uone mwanzo wa Pasaka. Kuhusu sikukuu ya Malimbuko Mungu alimwambia Musa,

“Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika hiyo nchi niwapayo, na kuya-vuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sa-bato kuhani atautikisa.” (Law 23:10-11)

Siku ile Waisraeli waliagizwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, pamoja na sadaka ya unga. Kwa njia hii, Waisraeli walimshukuru Mungu kwa mavuno yao.

Kwa sikukuu ya Pentekoste Bwana aliagiza, “Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mliyouleta mganda wa

sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba; hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsogezea BWANA sadaka ya unga mpya. Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA. Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza wana-kondoo saba, wasio na dosari, wa mwaka wa kwanza, na ng'ombe dume mmoja, na kondoo wawili wa kiume; watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA....” (Law 23:15-21).

Sikukuu ya Baragumu. Bwana alisema, “Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi

wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga baragumu, ni kusanyiko takatifu. Msifanye kazi yo yote ya utumishi; nanyi mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto.” (Law 23:23-25)

Sikukuu kubwa hiyo ni siku ya kwanza ya mwaka katika kalenda ya Waisraeli, na kwa sababu hiyo walipiga baragumu kwa furaha kabisa.

Kuhusu sikukuu kubwa ya Upatanisho Bwana alisema, “Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu

kwenu, nanyi mtajinyima; na mtatoa sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto. Na msifanye kazi yo yote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za BWANA, Mungu wenu.” (Law 23:26-28)

Sikukuu kubwa ya Vibanda, “Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya

vibanda muda wa siku saba kwa BWANA. Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. Mtamsogezea BWANA sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamtolea BWANA sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.” (Law 23:34-36)

Siku hizo zilikuwa siku za furaha, na watu walikaa katika vibanda au mahema ili wajik-umbushe kuhusu safari ya baba zao jangwani.

Wakati wana wa Israeli walipokaribia nchi ya Kanaani Mungu aliyatoa maagizo kuhusu nchi hiyo. Aliiweka mipaka ya nchi, alisema,

“Hii ndiyo nchi yenu kama mipaka yake ilivyo kuizunguka pande zote.” (Hes 34:12)

Tena, Mungu aliagiza miji itengwe kwa ajili ya Walawi, kwa kuwa hawakupata urithi wa nchi (Hes 35:1-8). Tena, Mungu alisema,

“Na hiyo miji itakuwa kwenu kuwa makimbilio, kumkimbia mwenye kulipiza kisasi, ili asiuawe mwenye kumwua mtu, hata atakaposimama mbele ya mkutano ahukumiwe.” (Hes 35:11)

Alisema, “Mtawapa miji mitatu ng'ambo ya pili ya Yordani, na miji mitatu mtawapa katika nchi ya Ka-

naani; miji hiyo itakuwa ni miji ya makimbilio.” (Hes 35:14)

Vitabu vya sheria ni Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati. Vitabu vinavyotoa sheria nyingi zaidi ni Kutoka na Walawi. Sheria ilitolewa tena katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati kwa sababu Waisraeli wote walikuwa wamekufa jangwani kasoro Musa, Kalebu, na Yoshua. Mungu alitaka kizazi kipya kipate kusikia maagizo ya Mungu kabla ha-wajaingia katika nchi ya Kanaani.

Page 38: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 34 -

SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA SHERIA

Ijapokuwa Mungu aliwachagua wana wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, wawe watu wake, na taifa jipya, Waisraeli walimkosea Mungu kizazi hadi kizazi. Sasa, tutayaanglia makosa yao na hukumu waliyopewa kwa sababu ya dhambi zao.

Mungu alikuwa ameshawaokoa Waisraeli kutoka nchi ya Misri na alikuwa amewatunza jangwani. Mwisho aliwaongoza hadi mpaka wa nchi ya Kanaani ambayo ilikuwa nchi ya ahadi. Walipofika huko Musa aliwatuma wapelelezi kumi na wawili katika nchi na aliwaambia,

“Musa akawatuma ili waipeleleze nchi ya Kanaani, akawaambia, pandeni sasa katika Negebu mkapande milimani, mkaitazame nchi ni ya namna gani; na watu wanaokaa ndani yake, kama ni wenye nguvu au dhaifu, kama ni wengi au wachache; na nchi wanayoikaa kama ni nzuri au mbaya na kama wanakaa katika kambi au katika ngome; nayo nchi ni ya namna gani, kama ni nchi ya utaji-ri au ya umaskini; kama ina misitu au haina. Kuweni na mioyo ujasiri, mkayalete matunda ya nchi. Basi wakati ule ulikuwa wakati wa kuiva zabibu za kwanza.” (Hes 13:17-20)

Basi, wapelelezi waliingia katika nchi ile, wakatembea huku na huku ili waone ilivyo pamo-ja na watu na miji yake. Waliporudi wapelelezi kumi walitoa ripoti mbaya wakidai Waisraeli hawataweza kuteka nchi hiyo. Lakini wawili, Kalebu na Yoshua, walisema kwa nguvu ya Mungu Waisraeli wataweza kuitawala nchi hiyo. Mwisho Waisraeli waliyasikiliza maneno ya wale kumi na walikataa kuingia na kuichukua nchi. Hivyo Mungu aliwahukumu wafe jangwani ili kizazi kingine kipewe nchi hiyo ya ahadi.

Baada ya miaka arobaini Mungu alimwamuru Yoshua na Waisraeli kuingia Kanaani tena ili wawashinde maadui, waiharibu miji yao yote, na waiteke nchi yote. Yoshua na wanajeshi wa Israeli walipiga vita kwa nguvu sana. Wakawashinda maadui wengi na waliiharibu miji mingi, lakini hawakuwashinda watu wote na kuiharibu miji yote kama Mungu alivyowaambia katika Yoshua 13:1-7. Hivyo Mungu alisema,

“Wewe umekuwa mzee na miaka yako kwendelea sana, kisha inasalia nchi nyingi sana bado kumilikiwa ... nchi zote za Wafilisti, na Wageshuri wote ...” (Yos 13:1-7)

Baada ya kufa kwa Yoshua, wana wa Israelii walianza kuifuata miungu ya mataifa haya mengine ambayo hayakuangamizwa kufuatana na agizo la Mungu. Tazama,

“Wana wa Israeli walifanya mambo maovu mbele za macho ya BWANA, na wakawatumikia Mabaali. Wakamwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, waka-fuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakaji-inamisha mbele yao; wakamkasirisha BWANA, akaghadhibika.” (Amu 2:11-12)

Mungu aliwaamuru wana wa Israeli, “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kili-

cho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao.” (Kut 20:4,5)

Lakini tangu wakati walipotoka katika nchi ya Misri, Waisraeli waliendelea kujifanyia sanamu za kuabudu. Tazama,

“Bali walijichanganya na Mataifa, Wakajifunza matendo yao. Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao. Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani. Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sana-mu za Kanaani; Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.” (Zab 106:35-38)

Hata wafalme wao walifanya kila namna ya uovu wakiwaongoza Waisraeli kumkosea Mun-gu. Vitabu vya 1 na 2 Mambo ya Nyakati vinaonesha waziwazi jinsi wafalme wengi walivyokuwa wabaya, na jinsi wachache tu walitaka kumfuata Mungu aliye hai na kulitii Neno lake. Kila mara mfalme mzuri aliwakataza watu kuabudu sanamu, kumbe, wakati alipokufa, mfalme aliyefuata aliwavuta waabudu sanamu tena!

Basi, Mungu aliwateua manabii ili wawaonye wafalme na kuwaambia habari za hasira ya Mungu na hukumu itakayokuja juu yao. Lakini wafalme wengi hawakutaka kuyasikia mahubiri yao, bali waliwadharau, na mara nyingine walitaka hata kuwaua. Kwa sababu hiyo manabii wengi walifia mikononi mwa wafalme wabaya.

Kazi ya makuhani ilikuwa kuzipokea dhabihu za watu na kuwaombea mbele ya Mungu. Waliongoza ibada zote katika hema takatifu wakiwa jangwani na katika hekalu baada ya ku-

Page 39: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 35 -

jengwa kwake. Wajibu wao ulikuwa kuongoza taifa la Israeli katika mambo ya kiroho na walipaswa kuwa watu wenye haki na wenye maisha safi mbele ya watu na mbele ya Mungu. Lakini, mara nyingi hata makuhani walikuwa watu wabaya waliomdharau Mungu na maagizo yake.

Wakati Bwana Yesu alipozaliwa, Waisraeli walikuwa wangali chini ya Sheria ya Musa, ingawa njiani walikuwa wameongeza sheria nyingine nyingi walizozitunga wenyewe. Ndiyo kusema walichanganya sheria iliyotoka kwa Mungu pamoja na maagizo ya watu (Tazama Mt 23:14). Mafarisayo na waandishi walikuwa viongozi wa Israeli lakini nchi yote ilikuwa chini ya mamlaka ya Warumi. Ingawa katika kipindi hiki Waisraeli walikuwa wamejifunza kutoiabudu miungu mingine na kuitii Sheria ya Musa kwa umakini, bado mioyo yao ilikuwa mbali na Mungu.

Mungu alimtuma Yesu ili awahubirie kama vile manabii wengine waliomtangulia walivyofanya. Lakini, sawa na manabii wale wengine, Waisraeli, na hasa viongozi wao, walim-kataa Bwana Yesu Kristo, mwana wa Mungu.

“Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake; mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, Imempasa kuuawa. Ndipo wakamtemea mate usoni, wakampiga ngumi; na wengine wakampiga ma-kofi, wakisema, Ewe Kristo, tufumbulie; ni nani aliyekupiga?” (Mt 26:65-68)

Waisraeli walimpeleka Bwana Yesu kwa Warumi ili asulubishwe. “Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya

Yesu, wapate kumwua; wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa mtawala.” (Mt 27:1-2)

Ijapokuwa Pilato hakuweza kuuona uovu wo wote ndani ya Yesu, Waisraeli walitaka Kristo afe.

“Pilato akawaambia, Basi, nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulubiwe. Akase-ma, Kwa nini? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulubiwe.” (Mt 27:22-23)

Kwa maneno hayo tunaona kwamba Waisraeli wengi walimkataa Bwana Yesu kuwa Mwana wa Mungu. Waliishika Sheria ya Musa iliyosema Mungu ni mmoja tu na hawakuelewa kwamba Mungu alikuja duniani katika Bwana Yesu (2 Kor 5:1-3). Tena, walimkataa kuwa mfalme wao kama manabii wa zamani walivyotabiri, wakisema, “Sisi hatuna mfalme ila Kaisari” (Yn 19:15). Kaisari alikuwa mfalme wa Warumi.

Baada ya kumwua Yesu, Waisraeli waliwatesa wanafunzi wa Bwana Yesu. Waliwakataza kuhubiri na kufundisha katika jina la Kristo. Tazama,

“Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. Petro na Yo-hana wakawajibu wakawaambia, Kama ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe.” (Mdo 4:18-19, Tazama vilevile 5:17-18)

Isitoshe Wayahudi walimtesa mtume Paulo kila mahali alipoenda baada ya kuokolewa kwake. Tazama,

“Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba Neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawavuruga na kuwafadhaisha makutano.” (Mdo 17:13)

Tena, katika Yerusalemu, “Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika nchi,

kwa maana haifai aishi.” (Mdo 22:22)

Dhambi za Wayahudi wakati wa Agano Jipya zinatajwa katika maneno haya, “Ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu,

wala hawapatani na watu wo wote; huku wakituzuia tusiseme na Mataifa wapate kuokolewa; ili watimize dhambi zao siku zote. Lakini hasira imewafikia hata mwisho.” (1 Thes 2:15,16)

Page 40: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 36 -

SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA SHERIA

Tangu wakati Mungu alipowatoa Waisraeli kutoka katika nchi ya Misri, walianza kumwasi na kutenda dhambi. Hata wakati walipofika nchi ya ahadi, walikataa kuingia na kuitawala nchi ile kama vile Mungu alivyowaamuru. Basi, Mungu aliwahukumu. Aliwaacha watembee jangwani kwa miaka arobaini, mpaka watu wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi wakafia jangwani, isipokuwa Musa, Kalebu na Yoshua.

Walipofika kwenye nchi ya ahadi mara ya pili Waisraeli walishindwa kuwaua maadui zao wote na kuiteka nchi yao yote kufuatana na maagizo ya Mungu. Kwa sababu hii, Mungu aliru-husu maadui zao kuwatesa mara nyingi. Mungu aliwaruhusu Waisraeli hata kuingia utumwani mara kwa mara katika mikono ya maadui zao.

Lakini tena na tena Waisraeli walimwacha Mungu wakianza kuifuata miungu ya Mataifa mengine kama vile Baali na miungu mingine. Walilidharau Neno la Mungu lililosemwa na mana-bii. Kwa sababu hiyo, Mungu aliwahukumu njiani kwa upanga, tauni, na njaa. Tazama,

“Upanga uko nje, na tauni na njaa zimo ndani...” (Eze 7:15-16)

Hata mfalme Sulemani, mwana wa mfalme Daudi, alileta sanamu na miungu mingine wakati alipooa wake wengi wa Mataifa mengine. Kwa sababu hiyo, Mungu alikasirika na kuugawa ufalme wake kuwa falme mbili, ufalme wa Israeli na ufalme wa Yuda (1 Fal 11:11).

Waisraeli waliendelea kutenda dhambi na wafalme wao waliwaongoza katika matendo hayo mabaya. Katika vitabu vya 1 na 2 Wafalme, karibu wafalme wote walikuwa watu wabaya, wenye kuiabudu miungu mingine na wenye kuwavuta Waisraeli waziabudu sanamu. Basi Mun-gu aliwatesa zaidi kwa njia ya tauni, njaa, na kupigwa na maadui zao.

Wafalme wote wa ufalme wa Israeli (ufalme wa Kaskazini) walikuwa wabaya. Hakuna hata mmoja wao aliyefuata njia ya Daudi katika kutenda vizuri na kuyatii maagizo ya Mungu. Hakuna hata mmoja! Basi Mungu aliwaweka katika mkono wa mfalme wa Uashuru,

“Ndipo mfalme wa Ashuru akakwea katikati ya nchi yote, akaenda Samaria, akauhusuru miaka mitatu. Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, aka-wahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na Mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi.” (2 Fal 17:5-6)

Ijapokuwa wafalme wengine wa Yuda (ufalme wa Kusini) walikuwa watu wazuri, wengine zaidi walikuwa wabaya, wenye kumkasirisha Mungu. Hata watu wa Yuda walianguka katika dhambi wakiabudu sanamu. Basi, Mungu aliwahukumu sawasawa na jinsi alivyowahukumu Waisraeli.

“Hata mwezi wa tano, siku ya saba ya mwezi, ndiyo mwaka wa kumi na tisa wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia Yerusalemu. Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyum-ba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto. Na jeshi lote la Wakaldayo, waliokuwa pamoja na huyo kamanda wa askari walinzi, wakazibomoa kuta za Yerusalemu pande zote. Na mabaki ya watu waliosalia katika mji, nao wale walioasi, na kumkimbilia mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu wote wengine, watu hao Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawa-chukua mateka.” (2 Fal 25:8-11)

Baada ya miaka mingi, Mungu alisikia kilio cha watu wake na aliwarudisha wale waliobaki katika nchi yao. Nao wakazijenga tena kuta za Yerusalemu, nyumba zao, na hekalu la Bwana kama ilivyoandikwa katika vitabu vya Ezra na Nehemia. Hawakuziabudu sanamu tena, lakini walitenda dhambi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuoana na watu wa Mataifa. Kwa sababu hii walikuwa chini ya miguu ya Mataifa hata wakati wa Bwana Yesu.

Mwisho Waisraeli walitenda dhambi tena ya kumkataa Yesu Kristo kuwa Masihi na Mfalme wao walipompeleka kwa Warumi ili asulubiwe. Basi Mungu aliyatumia majeshi ya Warumi ku-wasambaza na kuibomoa Yerusalemu mwaka 70 B.K., kama Yesu mwenyewe alivyotabiri (Mt 23:37-39; Lk 21:24).

Baada ya kumkataa Yesu Kristo, Wayahudi waliwatesa wanafunzi wake ambao waliendelea kumhubiri Yesu. Mwisho Mungu alimwita Paulo kuitangaza habari ya wokovu kwa Mataifa, na Wayahudi, kupitia wivu wao, walijaribu kuzizuia huduma zake na mara nyingine walitaka hata kumwua. Soma Matendo 9:22-25,

“Hata siku nyingi zilipopita, Wayahudi wakafanya shauri ili wamwue.” (Mdo 9:23)

Page 41: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 37 -

Katika mji wa Antiokia wa Pisidia, Paulo na Barnaba waliwafundisha Wayahudi kuhusu umungu wa Kristo na watu wengi wa Mataifa walimwamini Yesu. Lakini Wayahudi wengine walijazwa wivu, wakafanya fujo mjini. Basi,

“Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima Neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona ninyi wenyewe kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.” (Mdo 13:46)

Wayahudi wasioamini waliendelea kuwatesa Paulo na Barnaba (Mdo 14:1-2) na katika mji wa Listra walimpiga Paulo kwa mawe. Wakafikiri amekufa, lakini Mungu alimnusuru na kumtia nguvu kusudi apate kuendelea na kazi yake (Mdo 14:19-20).

Wayahudi waliendelea kuwafuata Paulo na Baranaba katika mji wa Korintho na kushin-dana nao kuhusu Habari Njema ya Yesu.

“Walipopingana naye na kumtukana Mungu, akakung'uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa.” (Mdo 18:6)

Maneno (na hukumu) ya mwisho ya Paulo kwa Wayahudi yanaonekana katika Matendo 28:25-28. Tazama mstari wa 28,

“Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao wa-tasikia!”

Tumeona kwamba Paulo aliwaambia Wayahudi mara tatu kwamba atawaacha na kuyageukia Mataifa ili awahubiri Habari Njema (Mdo 13:46; 18:6; 28:28). Basi, alisema maneno haya kwa mamlaka ya Mungu mwenyewe, naye alieleza kusudi la Bwana katika barua yake ya Warumi.

“Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani; bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikia ile sheria. Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo.” (Rum 9:30-32)

Paulo alitumia maneno ya nabii Isaya kuonesha ugumu wa Wayahudi walioikataa neema ya Mungu.

“Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo.” (Rum 11:8)

Katika sehemu hii tumeona jinsi Mungu alivyowahukumu Waisraeli kwa kuwaweka pem-beni katika mpango wake. Walimkataa Yesu, waliwakataa mitume, na kwa ujumla waliikataa neema ya Mungu. Badala yake walijazwa wivu wakati Habari Njema ilipohubiriwa kwa Mataifa na walijitahidi kwa uwezo wao wote kuuzuia mpango wa Mungu. Kwa sababu hizo, Mungu ali-waweka pembeni ili Habari Njema ya neema ihubiriwe kwa Mataifa. Tazama,

“Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.” (Rum 11: 25)

Tumejifunza kwamba Mungu aliwahukumu Waisraeli mara kwa mara kwa sababu ya dhambi zao. Aliwahukumu kwa upanga, tauni na njaa. Mara nyingine aliwatia mikononi mwa maadui zao katika hali ya utumwa na mwisho aliwatumia askari wa kirumi kuubomoa mji wa Yerusalemu, kuliteketeza hekalu kwa moto, na kuwasambaza Wayahudi duniani.

Daraka la Neema lilianza kwa mtume Paulo. Wakati wa Paulo, katika kitabu cha Matendo, unaitwa kipindi cha mpito au kipindi cha mabadiliko. Ni historia ya mabadiliko ikieleza kipindi cha mwisho wa Daraka la Sheria na mwanzo wa Daraka la Neema. Kwa sababu ya kosa la Waya-hudi la kumkataa Yesu Kristo kama Masihi wao, Mungu aliwahukumu akiwaweka pembeni. Ndipo akauanzisha mpango mpya wa kuwageukia Mataifa. Kosa la Waisraeli lilimsababisha Mungu kulifunga Daraka la Sheria na kulianzisha Daraka la Neema. Ingawa Daraka la Sheria lilikuwa limefungwa, Wayahudi waliendelea kuzifuata kanuni zake na kuitii Sheria ya Musa.

Page 42: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 38 -

SOMO LA SITA: MANENO YA MWISHO KUHUSU SHERIA

Sheria ilikuja kwa njia ya Musa. Kusudi moja la sheria lilikuwa kuwateua wana wa Israeli kuwa taifa jipya, wateule wa Mungu. Hakika, Mungu aliuona uchafu na uovu wa mataifa yote na alitaka taifa moja safi na takatifu kwa ajili ya utukufu wake.

Kusudi lingine la sheria lilikuwa kuionesha waziwazi haki ya Mungu na dhambi za watu. Kwa njia ya sheria, Mungu alikusudia kuwafundisha watu kuhusu utakatifu wake na jinsi anavyoichukia dhambi.

Kusudi lingine la sheria lilikuwa kuwafanya Waisraeli kuwa mashahidi wa utakatifu wa Mungu mbele ya watu walioifuata miungu mingine.

Bwana Yesu alikuja duniani ili akamilishe Sheria ya Musa akileta neema na kweli. “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu

Kristo.” (Yn 1:17)

Yesu Kristo alizaliwa chini ya Daraka la Sheria (Gal 4:4) na alikuwa Myahudi mzuri aliyeitii Sheria ya Musa katika maisha yake. Yesu hakuivunja hata sheria moja. Hata wanafunzi wote wa Kristo walikuwa Wayahudi walioishi chini ya Sheria ya Musa katika Daraka la Sheria. Nao walizishika sheria kwa kadiri ya uwezo wao.

Wakati Yesu alipokufa msalabani, Kristo alitimiza sehemu za Sheria ya Musa zilizohusu taratibu za sadaka. Kwa sababu ya sadaka yake kuu ya kufa msalabani, aliweza kuufunga uta-wala wa sheria na kuufungua utawala wa neema.

“Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani.” (Kol 2:14)

Lakini Daraka la Sheria liliendelea hata baada ya msalaba wa Yesu kwa kuwa Mungu aliku-wa bado hajamaliza kushughulika na taifa la Israeli. Daraka la Sheria lilianza mlimani Sinai, ingawa sehemu ya Sheria ya Musa ilikomea msalabani, Daraka la Sheria iliendelea baada ya msalaba katika kitabu cha Matendo mpaka wakati Mungu alipolianzisha Daraka la Neema chini ya huduma ya Paulo.

Wakristo wengine hudanganywa na mgao wa Agano la Kale na Agano Jipya. Wanafikiri Agano la Kale ni lenye Sheria ya Musa na vitabu vyote vya Agano Jipya havina sheria. Lakini Daraka la Sheria halikuwepo katika Agano la Kale kabla ya kutolewa kwa sheria katika Mlima Sinai na linaendelea wakati wa vitabu vya kwanza vya Agano Jipya. Tena Wakristo wengine wanafikiri Daraka la Sheria liliisha wakati Yesu alipokufa msalabani mwishoni mwa vitabu vinne vya Injili. Lakini Mungu aliendeleza Daraka la Sheria akiendelea kuwapa Waisraeli nafasi ya kuipokea habari njema ya ufalme. Baadaye, katika kitabu cha Matendo, wakati Mungu alipoli-anzisha Daraka la Neema kupitia mtume Paulo, ndipo Daraka la Sheria liliisha.

Baada ya Daraka la Neema kuanza Wayahudi wengi walimwamini Kristo kuwa Mwokozi wao, lakini wengi wao walitaka kuendelea kuifuata Sheria ya Musa na kuichanganya na neema. Walitaka hata Mataifa kuzifuata sehemu nyingine za sheria kama vile kutahiriwa.

JINA LA DARAKA

MTU MKUU MWANZO WAKE

MWISHO WAKE

MAANDIKO MUHIMU

Sheria Musa Mlima wa Sinai na kutole-wa kwa Sheria ya Musa

Kumkataa Kristo kama Masihi na Mwokozi

Kutoka 20 hadi mwisho wa Agano la Kale; vitabu vya injili, na Matendo 1-9

Page 43: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 39 -

DARAKA LA NEEMA SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA NEEMA

Ijapokuwa neema kubwa ilikuja msalabani kupitia Bwana Yesu Kristo, Daraka la Neema halikuanza wakati ule. Tulishaonesha kwamba Kristo alizaliwa chini ya Daraka la Sheria pamoja na Wayahudi wote wa kipindi chake. Daraka la Neema halikuanza na kifo cha Kristo msalabani, bali Mungu aliendelea na taifa la Israeli chini ya Daraka la Sheria.

Baada ya kifo cha Yesu (30 B.K.), Wayahudi waligawanyika katika makundi mawili: Wale walioyafuata mafundisho ya Kristo, na wale walioifuata dini ya Waisraeli tu. Kulikuwa ubishi kati ya makundi haya, na Wayahudi wasiomwamini Yesu waliwatesa Wayahudi waliomwamini. Kwa ujumla, Makuhani na wakuu wa Wayahudi, hawakumwamini Yesu na waliwatesa Waya-hudi waliomshuhudia Kristo kuwa Masihi na Mwokozi (Mdo 4 - 5).

Wakristo wengi wanaamini kwamba Daraka la Neema lilianza siku ya Pentekoste, kwani, siku ile watu walibatizwa katika Roho Mtakatifu. Lakini sivyo, kwa sababu siku ile ilikuwa siku-kuu ya Wayahudi na watu wote waliokuwepo siku ile walikuwa Wayahudi pamoja na Waongofu (Mdo 2:9-11). Isitoshe, kuja kwa Roho Mtakatifu kulikuwa ahadi ya Yesu kwa wanafunzi wake walio chini ya taratibu za Daraka la Sheria.

Tunapaswa kukumbuka kwamba Bwana Yesu, wakati alipokuwa hapa duniani, aliifundisha habari ya ufalme wa mbinguni. Baada ya kifo cha Yesu, na hata siku yenyewe ya Pentekoste, ma-fundisho yale yaliendelea. Tazama yale Petro aliyoyahubiri siku ya Pentekoste,

“Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.” (Mdo 2:39)

“Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani.” (Mdo 3:19-20)

Petro alitaka Wayahudi kumkubali Yesu kama Masihi wao ili arudi kuuanzisha ufalme wake. Ndiyo maana ya “nyakati za kuburudishwa.” Yaani ni nyakati za ufalme.

Hakika, Daraka la Neema lilianza wakati Mungu alipomwita Sauli wa Tarso na kumtuma kuihubiri Habari Njema ya NEEMA kwa Mataifa. (Mdo 9:15; 26:15-18). Tazama,

“Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Ma-taifa, naitukuza huduma iliyo yangu.” (Rum 11:13)

Daraka la Neema lilianza na wito wa Paulo na wakati alipopewa ufunuo mpya kuhusu Daraka la Neema na Mwili wa Kristo. Daraka hilo linaendelea hata leo na litamalizika wakati Bwana Yesu atakapokuja kulinyakua Kanisa lake lililo Mwili wake,

“Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” (1 Thes 4:16-17).

“Miaka zaidi ya 2000 imeshapita tangu Daraka la Neema lilipoanza na hatujui wakati litakapokwisha kwa sababu hakuna anayejua siku ya kurudi kwa Bwana Yesu kulinyakua Kani-sa” (S.R. Vinton, Jr., katika ELIMU KUBWA ZA BIBLIA, p. 26).

SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA NEEMA

Tunaweza kusema kwa hakika kwamba mtume Paulo ni mtu mkubwa wa Daraka la Neema. Bwana Yesu mwenyewe alionesha neema ya Mungu katika maisha yake na katika kufa kwake vilevile. Lakini ufunuo, mafundisho, na mahubiri ya Daraka la Neema, yaliwekwa na Mungu mkononi mwa Paulo.

Paulo alizaliwa akiitwa Sauli wa Tarso. Alikuwa Myahudi wa kabila la Benyamini. Alifun-dishwa katika mambo yote ya dini ya Waisraeli hata akawa Farisayo, yaani mwalimu wa torati. Tazama,

“Lakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuu-tumainia mwili, mimi zaidi. Nilitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila la Ben-

Page 44: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 40 -

yamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia.” (Flp 3:4-6)

Sauli huyu wa Tarso aliwachukia sana Wakristo, hata akakubali Stefano auawe. Aliwatesa waumini katika kanisa la Yerusalemu mpaka wengi walikimbilia nchi za Yudea na Samaria (Mdo 8:1). Hakika, alikuwa mtu mkali sana na Wakristo walimwogopa sana.

Wakati Sauli aliposikia kwamba Wakristo wengi walikuwa wanakaa katika mji wa Dameski, aliwafuata huko.

“Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, wanaume kwa wanawake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.” (Mdo 9:1,2)

Lakini katika safari yake kwenda Dameski, jambo kubwa lilitokea kwake. “Wakati alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafla nuru kutoka mbinguni ikam-

wangaza kotekote. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona wanitesa? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayemtesa. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.” (Mdo 9:3-6)

Sauli alisafiri hata kufika Dameski, lakini alikuwa kipofu kwa sababu ya nguvu ya nuru ya Bwana.

“Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.” (Mdo 9:9)

Basi, Mungu alimwita Mkristo mmoja, jina lake Anania, na alimtuma kwa Sauli kumwombea apate kuona tena (Mdo 9:10-19). Anania alikuwa na mashaka, lakini alilitii neno la Bwana.

Sauli alianza mara moja kuihubiri habari ya Bwana Yesu kwa Wayahudi na kwa Mataifa vilevile. Lakini wakati Wayahudi wa Dameski waliposikia mahubiri yake walikasirika sana hata walitaka kumwua. Lakini Paulo aliwatoroka, akaenda nchi ya Arabuni. Baada ya muda, akarudi tena Dameski.

“Kisha, baada ya miaka mitatu, nilipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano. Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana.” (Gal 1:18-19)

Baadaye Sauli, aliyepata kuitwa Paulo, alizifanya safari tatu za kuihubiri Habari Njema ya Neema ya Mungu kwa Mataifa. Barnaba na Yohana Marko walienda pamoja naye katika safari ya kwanza. Sila, Luka, Timotheo na wengine walisafiri pamoja naye katika safari ya pili na ya tatu. Katika kila safari Paulo alilihubiri Neno la Mungu waziwazi, akiyaanzisha makanisa na ku-wafundisha waumini. Njiani alilazimika kushindana na Wayahudi wasiomwamini Kristo.

Paulo alipata mateso mengi katika safari zake kama alivyoandika katika 2 Wakorintho 11:24-27,

“Kwa Wayahudi mara tano nilipata mapigo arubaini kasoro moja. Mara tatu nilipigwa kwa ba-kora; mara moja nilipigwa kwa mawe; mara tatu nilivunjikiwa jahazi; kutwa kucha nimepata kukaa kilindini; katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang'anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa Mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.”

Paulo alifungwa mara nyingi. Mara nyingine alifungwa kwa siku chache kama ilivyokuwa katika Matendo 16. Lakini mara mbili alifungwa katika mji wa Rumi kwa muda mrefu. Mara ya kwanza kwa miaka miwili, na baadaye tena alifungwa Rumi mpaka kufa kwake. Lakini hata ali-pokuwa akifungwa hakuacha kumtumikia Bwana wake na kuihubiri Habari Njema kwa wa-fungwa, kwa walinzi, na hata kwa nyumba ya Kaisari (Flp 1). Tena, Paulo aliandika barua nyingi wakati akiwa mfungwa. Aliandika barua za Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, 1 na 2 Timotheo, Tito na Filemoni akiwa mfungwa kabla hajafa.

Paulo, mtume hodari na mtumishi mwaminifu wa Bwana Yesu Kristo, alikufa kwa agizo la mfalme Nero. Lakini matunda ya kazi yake yanaendelea hata leo. Tunakuwa na maandiko yake yaliyoongozwa na Roho Mtakatifu, na maandiko haya yanatufundisha elimu za Daraka la Neema na ufunuo wa siri, na habari ya Kanisa lililo Mwili wa Kristo.

Page 45: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 41 -

SOMO LA TATU: UFUNUO WA SIRI KATIKA DARAKA LA NEEMA

Tulishaona jinsi Paulo alivyokuwa mtu mkuu wa Daraka la Neema. Sasa tunataka kuonesha namna gani alivyoipata habari yake ambayo ilikuwa siri kabla haijafunuliwa kwake. Watu wen-gine wanashindwa kuuelewa utumishi wa mtume Paulo na jinsi alivyopewa ufunuo wa siri uli-yofichwa tangu mwanzo. Watu hawa huchanganya habari za ufunuo wa Paulo wakizichanganya na habari za sheria na habari za ufalme wa mbinguni.

“Kwa maana, ndugu zangu, Injili hiyo niliyowahubiria, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.” (Gal 1:11-12)

Maneno haya yanatuonesha wazi kwamba Paulo alipata Habari Njema yake kwa ufunuo tu, hakufundishwa na watu wengine.

Tena, Paulo alionesha kuwa alikuwa wa kwanza kuupokea ufunuo huo wa siri, yaani habari za siri hii hazionekani katika Biblia kabla ya Paulo.

“Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na Injili yangu na kwa kuhubiri-wa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele.” (Rum 16:25)

Tunaweza kufahamu kwamba Daraka la Neema na ufunuo wa siri ni kitu kimoja kwa saba-bu ya maandiko haya,

“Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa; ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kwa kufunu-liwa nilijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache.” (Efe 3:1-3)

Katika sura hii, Paulo anaeleza maana ya siri hiyo, “Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. Siri hiyo

hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii nyakati hizi katika Roho; ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.” (Efe 3:4-6)

Tazama, sasa, utumishi wa Paulo kutokana na wito wake. “Injili hiyo ambayo nilifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu nili-

yopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa wa-takatifu wote, nilipewa neema hii ya kuwahubiria Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika.” (Efe 3:7-8)

Mpango wa Mungu katika Daraka la Neema unaonekana katika Waefeso 3:9-11, “Na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote

ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Efe 3:9-11)

Jambo lingine kuhusu ufunuo wa siri linaonekana katika Wakolosai. Tazama, “Siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa wa-

takatifu wake; ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.” (Kol 1:26-27)

Hakika, Daraka la Neema na Daraka la Siri ni kitu kimoja, yaani Daraka moja. Ijapokuwa Mungu alionesha neema yake mara nyingi katika Agano la Kale, Daraka (au uwakili) la Neema lilianza kuhubiriwa wakati mtume Paulo alipopata ufunuo wa siri hii kutoka kwa Bwana Yesu Kristo mwenyewe. Ni katika wakati huo Mungu alianza kulitengeneza Kanisa jipya lililokuwa Mwili wa Kristo. Tazama,

“Naye (Kristo) ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.” (Kol 1:18)

Kanisa hili la Mwili wa Kristo ni Kanisa lisiloonekana. Siyo jengo, bali ni watu wote wali-omwamini Yesu Kristo na kufanywa kuwa viungo katika Mwili wake. Yesu, asiyeonekana kwa kuwa yuko mbinguni, ndiye kichwa cha Mwili huo. Tazama,

“Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwen-zake.” (Rum 12:5)

Page 46: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 42 -

Tazama pia 1 Wakorintho 12:27.

SOMO LA NNE: WOKOVU KATIKA DARAKA LA NEEMA

Wokovu ulipatikana katika Madaraka mengine kwa imani iliyothibitishwa kwa kumtii Mungu katika matendo maalum. Lakini katika Daraka la Neema, wokovu ni kwa imani tu kwa sababu ya kifo cha Yesu msalabani. Zamani, watu walikuja kwa Mungu kwa njia ya imani ili-yooneshwa kwa matendo yaliyoagizwa na Mungu. Matendo yenyewe yalikuwa kutoa dhabihu kuonesha imani yao. Basi, kwa sababu ya imani yao na utiifu wao katika kutoa dhabihu, Mungu aliwasamehe dhambi zao akiwaokoa kwa njia ya neema yake.

Lakini wakati Kristo alipokufa, dhabihu zilikoma kwa sababu Kristo mwenyewe alikuwa dhabihu au sadaka kuu kwa ajili ya dhambi zetu zote (Ebr 9:12).

Vivyo hivyo, wakati Kristo alipokufa, maandiko ya Sheria ya Musa yaliyomshtaki mwenye dhambi yalifungwa pamoja naye juu ya msalaba.

“Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani.” (Kol 2:14)

Katika Daraka la Neema mtu hawezi kumfikia Mungu kwa matendo yake ya haki wala kwa kumtolea Mungu sadaka. Yeye anaweza kumfikia Mungu kwa njia ya kuupokea wokovu na kui-kubali kazi ya Kristo aliyoifanya msalabani. Hakika, Bwana Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kama ilivyoandikwa,

“Bali Mungu aonesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” (Rum 5:8)

Mungu alimtoa Kristo, mwana wake wa pekee, apate kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi zetu. Tendo hili ni tendo la neema kabisa, na wenye dhambi katika Daraka hili wanaweza kuokolewa bila matendo yo yote. Tazama,

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Munguwala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” (Efe 2:8-9)

Mtume Paulo alikuwa mtumishi wa Mungu aliyeuhubiri wokovu huu; wokovu kwa neema kwa njia ya imani, usio kwa matendo ya haki wala kwa njia ya sheria. Paulo alibishana na Waya-hudi mara nyingi kwa sababu wengine wao, waliomwamini Kristo, walitaka kuongeza sheria juu ya imani kwa ajili ya wokovu wa Mataifa. Wengine wao, wasioamini, walitaka watu wote waifu-ate dini ya Israeli tu. Tazama,

“Lakini tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.” (Gal 2:16)

Kuna Wakristo wa siku zile waliosema kwamba mtu anapaswa kubatizwa kwa maji ili aokoke. Lakini, kufuatana na maandiko ya mtume Paulo, sivyo. Kubatizwa kwa maji ni kazi ya mikono ya watu, na Biblia inasema,

“Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.” (Tit 3:5)

Tazama, “Kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili” ni kazi ya Roho Mtakatifu, siyo kazi ya mtu. Maji hayawezi kuondoa dhambi, wala kumbadilisha mtu kuwa mpya, hata kidogo.

Kumbuka, msomaji, njia ya wokovu katika Daraka hili la Neema ni wazi:

1. Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu; 2. Tunapaswa kuiamini habari hii bila kuwa na mashaka; 3. Wokovu ni zawadi ya Mungu kwa sababu ya neema yake; 4. Matendo yo yote hayawezi kutufaa kitu katika wokovu wetu (Matendo mema

tunayoyafanya baada ya kuokoka ni matunda ya wokovu tuliyo nayo (Efe 2:10) na uthibitisho wa kwamba imani yetu ni ya kweli);

5. Sisi hatuna mali inayofaa kulipa gharama ya wokovu wetu, kwani, Bwana Yesu mwenyewe alilipa bei yake kwa damu yake msalabani. Ndiyo sababu tunapaswa

Page 47: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 43 -

kuupokea wokovu wetu kwa imani na kumshukuru Mungu. Tazama Warumi 4:24,25; 6:23; 1 Wakorinto 15:3,4; na Waefeso 1:7; 2:13.

Kifo cha Kristo ni msingi wa wokovu wetu. Vilevile ni msingi wa upatanisho kati yetu sisi wenye dhambi na Mungu mwenye haki.

“Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho.” (2 Kor 5:18)

Tazama vilevile Wakolosai 1:21-22 na Warumi 5:10.

SOMO LA TANO: MWILI WA KRISTO KATIKA DARAKA LA NEEMA

Katika kufafanua maana ya Mwili wa Kristo ni muhimu tutofautishe kundi hilo na makundi mengine ya watu wa Mungu katika Biblia. Waisraeli walikuwa taifa lililoitwa na Mungu kuwa watu wake. Taifa hilo na Mwili wa Kristo siyo kitu kimoja, bali ni makundi mawili yaliyo tofauti. Israeli ilikuwa mkusanyiko wa watu wa taifa moja tu, wakati Mwili wa Kristo ni mchanganyiko wa mataifa mengi ukiwa ni pamoja na Waisraeli. Makundi hayo yote mawili yanaitwa “kanisa” katika biblia kwa sababu “kanisa” ni neno lenye maana ya “wale walioitwa na Mungu kuku-tanika.” Ndiyo kusema kuna makanisa zaidi ya moja yanayotajwa katika Biblia. Kwa mfano kati-ka Matendo 7:38 Waisraeli waliitwa “kanisa jangwani” na hata katika Mathayo 16:18 Yesu anaita taifa la Israeli kuwa kanisa. Waisraeli walikuwa watu walioitwa na Mungu kwa ajili ya kumwabudu Mungu kwa pamoja, na ndivyo walivyofanya hata jangwani kabla hawajafika katika nchi ya Kanaani. Lakini katika kanisa hilo la jangwani watu wa mataifa walikuwa nje na ha-wakupewa ahadi za Bwana. Lakini Kanisa lililo Mwili wa Kristo ni kwa ajili ya watu wote wanaomwamini Kristo kuwa Mwokozi wao; Mataifa pamoja na Waisraeli.

Maelezo ya mwanzo wa Kanisa lililo Mwili wa Kristo yanaonekana katika Waefeso 2:14-16, “Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; aka-

kibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuumaliza ule uadui kwa huo msalaba.”

Mtu anaingia katika Mwili huo kwa njia gani? Kwanza, anapaswa kumpokea Bwana Yesu Kristo moyoni mwake kwa imani. Na mara moja anapata kuwa kiungo cha Mwili wa Kristo kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Tazama,

“Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Waya-hudi, au kwamba tu Wagiriki; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.” (1 Kor 12:13)

Ubatizo wa Roho katika mstari huo ni ubatizo ule mmoja unaotajwa katika Waefeso 4:5. Tazama,

“Kuna mwili mmoja, na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.” (Efe 4:4-6)

Kumbuka, ubatizo wa maji ni kazi ya mikono ya mtu, lakini ubatizo wa Roho ni kazi ya Mungu Roho mwenyewe ili atuingize katika Mwili wa Kristo, Kanisa la leo.

Tulishaona kuna viungo vingi katika mwili mmoja. Miili yetu inavyo viungo vingi, na Mwili wa Kristo umekuwa na viungo vingi vilevile. Wakristo wote, wakiwa watu weusi au watu weu-pe, wakubwa au wadogo, wenye akili au wasio na akili, matajiri au masikini, wa kike au wa kiume, wa kabila lo lote lile - wote ni viungo vya Mwili wa Kristo kama wamemwamini Yesu Kristo mioyoni mwao (Gal 3:28). Tazama,

“Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Unakuwa si wa mwili kwa sababu hiyo? Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si wa mwili; je! Linakuwa si la mwili kwa sababu hiyo? Kama mwili wote ukiwa jicho, ku-ko wapi kusikia? Kama wote ni sikio kuko wapi kunusa? Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.” (1 Kor 12:14-18)

Ijapokuwa Wakristo wanagawanyika katika makundi mengi au katika madhehebu mengi, Mwili wa Kristo ni mwili mmoja tu. Kwa mfano, Mkristo anaweza kuwa mtu wa kanisa la Wa-

Page 48: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 44 -

baptisti, au kanisa la Moravian, au kanisa la Anglican, au kanisa la Biblia, au kanisa la Neema, n.k. Lakini kila moja ni kiungo cha Mwili wa Kristo, Kanisa lisiloonekana, kama kweli amemwamini Yesu Kristo pekee kwa ajili ya wokovu wake. Kuna madhehebu mengi katika nchi ya Tanzania, na wanatofautiana katika elimu zao. Lakini kila mtu aliyezaliwa upya katika Kristo Yesu ameshabatizwa katika Mwili huu mmoja kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu.

Kusudi kubwa la Mwili wa Kristo ni kumtukuza Mungu. Tazama, “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuya-

wazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika kanisa na katika Kris-to Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.” (Efe 3:20,21)

Tena, “Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu.” (Kol 3:23)

Kusudi lingine ni kuonesha upendo katikati ya viungo vyote. “Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameiti-

miza sheria.” (Rum 13:8)

Wakristo wote wakipendana, ubishi na ugomvi hauwezi kuingia kanisani. Mwenye chakula anapaswa kumsaidia yeye asiye na chakula. Mwenye mali anapaswa kusaidia maskini. Matendo haya yanaonesha upendo.

Kusudi lingine la kanisa lililo Mwili wa Kristo ni kuombeana. Wakristo wanapaswa kusaidi-ana katika maombi yao. Kwa njia hii wanapaswa kuiimarisha imani yao. Kila Mkristo anafurahi kujua kwamba Mkristo mwenzake anamkumbuka katika maombi yake. Maombi yanaitia nguvu kanisani kama umeme unavyotia nuru nyumbani.

Kusudi lingine la Mwili wa Kristo ni kuitangaza Habari Njema ya Neno la Mungu katika dunia yote. Paulo alisema,

“Na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho.” (Efe 3:9,10)

Kwa ushuhuda wa Kanisa lililo Mwili wa Kristo watu wa dunia na hata malaika wa mbingu-ni wanaweza kuijua neema na hekima za Mungu. Tena, tunapaswa kulihubiri neno la upatanisho kama wajumbe wa Kristo (2 Kor 5:20).

SOMO LA SITA: MAAGIZO YA DARAKA LA NEEMA

Sisi tunaoishi katika Daraka la Neema leo, tunaagizwa kwanza kukumbuka kwamba hatuko tena chini ya Sheria, bali tuko chini ya Neema.

“Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.” (Rum 6:14)

Tena, “Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa

bure.” (Gal 2:21)

Tunaagizwa kuifahamu tofauti kati ya sheria na neema na kusimama katika uhuru wa nee-ma.

“Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa. Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.” (Gal 3:23-26)

Biblia inasema watu wote ni wenye dhambi, nao wanapaswa kumpokea Kristo kwa imani ili wapate kuokolewa. Agizo hilo la kumwamini Yesu na kazi yake msalabani, ni agizo kuu la kipindi cha Daraka la Neema.

“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Rum 3:23)

“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake” (Yn 1:12)

Page 49: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 45 -

Watu wote wanapaswa kuja kwa Mungu kwa njia ya imani. Wanapaswa kuiamini Habari Njema.

“Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.” (Yn 3:36)

“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” (Ebr 11:6)

Ni hatari kabisa kuutafuta wokovu kwa njia ya matendo ya haki, au kupitia dini ya watu. “Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja” (Rum 3:10)

“Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu” (Tit 3:5)

Hakika, mtu hawezi kuokolewa kwa matendo ya haki. Anapaswa kuupokea wokovu kwa imani tu.

Tunakatazwa kuifuata dini nyingine wala kumtafuta mwokozi mwingine ila Bwana Yesu Kristo tu.

“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Mdo 4:12)

Tunaona Mwokozi wetu ni mmoja tu, ndiye Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. “Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja

na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu?” (2 Kor 6:15-16)

Ni hatari kuidharau damu ya Kristo kuwa kitu bure. “Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadahabu kwa

yeye” (Rum 5:9)

“Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa da-mu yake Kristo” (Efe 2:13)

“Na pasipo kumwanga damu hakuna ondoleo” (Ebr 9:22)

“Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri roho wa neema?” (Ebr 10:29)

Watu wasiikose siku ya wokovu. “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. (Kwa maana

asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.)” (2 Kor 6:1-2)

Wakristo wanaagizwa wasiwe na kiburi. Tazama, “Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali

uogope. Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.” (Rum 11:20-21)

Kumbuka tuliokolewa kwa njia ya neema na siyo kwa haki yetu wala kwa uwezo wetu. Lakini baada ya kuokolewa kuna maagizo mengi tunayopaswa kuyatii kama Wakristo walio katika Mwili wa Kristo. Hatuwezi kuyataja yote lakini tutayataja baadhi kama mifano. Ila tukumbuke kwamba kuyatii maagizo hayo hakuwezi kutuokoa bali wokovu kwa njia ya imani unatuwezesha kutii. Basi tuone baadhi ya maagizo tuliyopewa,

“Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.” (2 Tim 2:15)

Tena, “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.” (Zab 119:11)

Neno la Mungu ni upanga wa Roho mikononi mwetu. Hivyo tunapaswa kulisoma na kuli-tumia katika huduma za Mungu. Pia tunapaswa kumwomba na kumsifu Mungu.

“Ombeni bila kukoma.” (1 Thes 5:17)

“Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudu-mu katika kuwaombea watakatifu wote.” (Efe 6:18, Tazama vilevile Flp 4:6-7)

Page 50: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 46 -

Tunapaswa kukutana pamoja kanisani. “Wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi

kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.” (Ebr 10:25)

Wakristo wanakusanyika pamoja kanisani ili wamwabudu Mungu pamoja, lakini pia, Wa-kristo wanakutana kwa kusudi la kushirikiana.Tunapaswa kuyashinda majaribu kwa uwezo wa Bwana.

“Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” (1 Kor 10:13)

Tazama tena, “Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanojaribiwa.” (Ebr

2:18)

Hakika, hatuwezi kushinda majaribu yote kwa uwezo wetu, ni muhimu tuliweke tumaini letu katika Bwana wetu.

Tunapaswa kuzivaa silaha za Mungu tupate kumshinda Shetani. “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,

juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” (Efe 6:12-13)

Tunapaswa kuwavuta watu wengine wampokee Bwana Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao. “Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote.”

(2 Kor 3:2)

“Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea.” (2 Kor 4:3)

Kila Mkristo ni mfano wa neema ya Mungu. Naye anapaswa kuuonesha ushuhuda mzuri kwa mwenendo wake, na kwa usemi wake. Wao walio nje wanatutazama wapate kuona kama sisi ni watu wa Mungu kweli au ni wadanganyifu tu.

Tunapaswa kuzitoa mali zetu kwa kazi ya Mungu. “Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa

ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.” (2 Kor 9:6-7)

Tunapaswa kujitoa kwa ajili ya watumishi wa Mungu na kwa wahitaji. “Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.”

(1 Kor 9:14)

“Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waamin-io.” (Gal 6:10)

“Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwa-saidie wale walio wajane kweli kweli.” (1 Tim 5:16)

Kazi ya namna hii ni kazi njema machoni pa Bwana. Wakristo wanapaswa kuyashika mafundisho yaliyo ya kweli.

“Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu...Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.” (2 Tim 2:16, 23)

Tena, “Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio

katika Kristo Yesu. Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatfu akaaye ndani yenu.” (2 Tim 1:13-14)

Kama tulivyosema, maagizo yetu katika Daraka la Neema ni mengi kiasi hatuwezi kuyataja yote hapa. Lakini tukumbuke kwamba agizo kuu la kipindi hicho ni kumwamini Bwana Yesu Kristo na kazi aliyoifanya msalabani.

Page 51: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 47 -

SOMO LA SABA: MAKOSA YA DARAKA LA NEEMA

Kosa kuu katika Daraka la Neema ni kutomwamini Yesu Kristo kama mwokozi. Ni kosa lin-aloendana na agizo kuu la Daraka hilo la kumwamini Yesu.

Baada ya Kanisa lililo Mwili wa Kristo kuanza Paulo aliendelea kuwaendea Wayahudi ili awashawishi kwamba Yesu alikuwa mwana wa Mungu na ndiye mwokozi wao wakimwamini.

“Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima Neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzi-ma wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.” (Mdo 13:46)

Lakini Wayahudi wengi zaidi (ingawa baadhi waliamini) walikataa kuyaacha mambo ya sheria na kuishika neema. Na hata wale waliomwamini Yesu bado walisumbuliwa na wazo la kuachana na sheria moja kwa moja na kumwamini Yesu tu. Kwa mfano,

“Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka.” (Mdo 15:1)

Tena, “Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima ku-

watahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa.” (Mdo 15:5)

Na Paulo aliandika, “Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; huwataka nyinyi mtahiriwe wapate

kujivunia alama hiyo mwilini mwenu. Lakini mimi sitajivunia kamwe cho chote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; maana kwa njia ya msalaba huo ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu. Kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; cha maana ni kuwa kiumbe kipya. Wanaoufuata mwongozo huo nawatakia amani na huruma.” (Gal 6:13-16 BHN)

Kama Wayahudi wengi walikataa kuiacha sheria na kumwamini Yesu tu, vivyo hivyo Ma-taifa wengi walikataa kuziacha sanamu zao. Walitaka kuitwa Wakristo, lakini walitaka kuziab-udu sanamu vilevile. Mtume Paulo aliwasihi Wakorintho,

“Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama il-ivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze...Kwa ajili ya hayo, wapen-zi wangu ikimbieni ibada ya sanamu.” (1 Kor 10:6,7,14)

Tangu mwanzo wa Kanisa lililo Mwili wa Kristo hadi leo watu wengine wamelidharau Neno la Mungu wakiitafuta haki katika mambo ya maarifa na mawazo ya watu wenye akili. Lakini, tazama maneno ya Paulo kwao,

“Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao. Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili. Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu.” (1 Kor 3:18-21)

Watu hawa wasioamini wanamkataa Bwana Yesu kuwa Mwokozi wao kwa kuwa wanategemea hekima iliyo tofauti na ile ya Neno la Mungu. Ingawa ni wasomi, bado wanapotea kwa kutokuwa na Yesu kwa sababu wamekataa maarifa ya Injili yake.

“Wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.” (2 Tim 3:7)

Tena, “Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu

amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. Na huu ndiyo ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.” (1 Yn 5:10-11)

Hawa wanayapenda matendo na maarifa ya giza kuliko ya nuru. “Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko

nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.” (Yn 3:19)

Wanajaribu kufika mbinguni kwa matendo ya haki au kwa hekima za watu kwa kuwa wanataka kujisifu katika kujiokoa. Kwa sababu hiyo wanakataa wito wa Mungu na wokovu wake wa bure .

Page 52: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 48 -

“Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.” (1 Kor 1:27-29)

Katika kiburi chao wanajiinua wenyewe ili wawe juu kuliko Bwana Yesu. Wanajitumikia wenyewe na hawataki kuwa watumishi wa Yesu.

“Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.” (Gal 6:3)

Isitoshe wanataka kuwa walimu wanaofundisha wengine elimu inayopingana na Maandiko Matakatifu.

“Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.” (2 Kor 11:13)

“Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana ali-yewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.” (2 Pet 2:1; Tazama pia Yud 3)

Kosa kubwa kuliko makosa yote katika Daraka la Neema ni kutoiamini Habari Njema ya Yesu Kristo. Yaani, ni kosa la kukataa kuamini kwamba Kristo ni Mungu na kwamba alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Hili ni kosa kubwa kuliko makosa yote katika kipindi hiki cha Neema.

SOMO LA NANE: HUKUMU YA DARAKA LA NEEMA

Wenye dhambi wanahukumiwa mara kwa mara katika maisha yao hapa duniani. Wengine wanafariki na magonjwa na wengine wanakufa kwa kuzama baharini. Wengine wanafungwa gerezani na wengine wanachapwa. Mifano ni mingi sana ya aina za hukumu ambazo watu wanapewa aidha mikononi mwa Mungu au mikononi mwa wanadamu. Lakini hukumu ya kweli itakuja juu ya kila mtu baada ya kifo chake. Tazama,

“Kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.” (Ebr 9:27)

Tena, “Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawa-

fuata.” (1 Tim 5:24)

Katika Daraka la Neema hukumu za kutolitii agizo la kumwamini Kristo ni za aina mbili. Kwanza, wote wasioamua kumwamini Kristo wataachwa hapa duniani wakati Yesu atakapokuja kulinyakua Kanisa lake. Matokeo yake ni kwamba wataendelea kuishi duniani na watakuwepo kwenye kipindi cha Dhiki Kuu ya miaka saba. Wakishindwa kumwamini Kristo katika kipindi hicho, hukumu ya pili itakuwa baadaye wakati wa hukumu ya mwisho katika kiti cha enzi kikubwa cheupe (Ufu 20:11-15). Katika hukumu hiyo ya mwisho wote ambao hawakumwamini Kristo watatupwa kwenye ziwa la moto milele.

Watu wanaoikataa Habari Njema ya neema ya Mungu wameanguka katika mtego ya Shetani.

“Lakini ikiwa Injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, wasiione nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.” (2 Kor 4:3-4)

Wakati Bwana Yesu atakapoonekana katika mawingu kulinyakua Kanisa lake (1 Thes 4:16-17), wote ambao hawajamwamini kabla ya siku hiyo watashtukia wamo katika kipindi cha Dhiki Kuu.

“Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.” (1 Thes 5:3)

“Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtum-wa, na muungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kwenye hasi-ra ya Mwana-kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kuistahimili?” (Ufu 6:15-17)

Wote waliokufa bila kumwamini Yesu, aidha kabla hajalinyakua Kanisa lake au baadaye katika kipindi cha Dhiki Kuu, watafufuliwa siku ya mwisho kwa ajili ya hukumu ya mwisho,

Page 53: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 49 -

“Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.” (Ufu 20:15)

Hukumu hii inaitwa vilevile mauti ya pili. Pamoja na mateso ya kutupwa katika ziwa la mo-to pia watatenganishwa na Mungu milele. Tazama,

“Watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake.” (2 Thes 1:9)

Ni muhimu kila mtu ajichunguze kwa maana wako watu wengi wasiojua wanaielekea hukumu ya namna hii. Wengine wanasali kanisani, wanaomba, na wanasoma Neno la Mungu, lakini hawajawahi kumwamini Kristo. Wengine wameyakataa mambo yote ya kikristo wakiya-fuata mawazo au dini zingine. Wanafikiri Mungu atawapokea siku ya mwisho lakini kumbe wa-tatengwa naye na kuhukumiwa.

SOMO LA TISA: MATENDO YA ROHO MTAKATIFU KATIKA DARAKA LA NEEMA

Kuna machafuko mengi kuhusu kazi au huduma za Roho Mtakatifu katika Daraka la Neema. Wakristo wana mawazo mbalimbali.

Katika kitabu hiki labda tutaziangalia nusu ya kazi za Roho Mtakatifu. Kwanza, kazi moja ya Roho Mtakatifu katika kipindi hiki cha Neema ni kuwavuta watu wampokee Bwana Yesu kuwa Mwokozi wao. Katika Yohana 16:7-11, tunasoma jinsi Roho Mtakatifu ataihakikishia dunia ku-husu dhambi, haki, na hukumu wakati atakapokuja duniani. Kama Paulo alivyoandika,

“Basi, jueni kwamba mtu ye yote anayeongozwa na Roho wa Mungu hawezi kusema: “Yesu alaaniwe!” Hali kadhalika, mtu ye yote hawezi kusema: “Yesu ni Bwana,” asipoongozwa na Roho Mtakatifu.” (1 Kor 12:3 BHN)

Wakati mtu anapompokea Bwana Yesu moyoni mwake, kwa imani, Roho Mtakatifu anam-weka au kumbatiza katika Mwili wa Kristo,

“Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Waya-hudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.” (1 Kor 12:13)

Vilevile Roho Mtakatifu anampa mtu anayemwamini Yesu uzima mpya, yaani anamhuisha kuwa hai kiroho. Tazama,

“Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuin-gia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” (Yn 3:5-6)

Tena, “Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa

kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.” (Tit 3:5)

Kazi nyingine ya Roho Mtakatifu ni kukaa ndani ya waumini kwa ajili ya kuwaongoza na kuwa muhuri na arabuni (1 Kor 3:16; Efe 1:13,14).

“Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?” (1 Kor 6:19)

Pia Roho Mtakatifu anatusaidia katika maombi yetu, “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo,

lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.” (Rum 8:26-27)

Tena, Roho Mtakatifu anaushuhudia umoja wetu katika Kristo. “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata

roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa saabbu ya haki...Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu.” (Rum 8:9-10, 16)

Kazi nyingine ya Roho Mtakatifu ni kuzalisha matunda mazuri katika maisha yetu. “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,upole,

kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” (Gal 5:22-23)

Page 54: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 50 -

Pia, Roho wa Mungu anatusaidia kufahamu au kuelewa Neno la Mungu. “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya

Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali ya-nayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwana-damu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatam-bua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Mana, ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.” (1 Kor 2:10-16)

Wakristo wameokolewa milele kwa sababu wanakuwa na muhuri wa Roho Mtakatifu. “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena

mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.” (Efe 1:13-14)

“Naye ndiye aliyetutia mhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.” (2 Kor 1:22)

Maana ya maneno haya ni kusema Roho Mtakatifu ni kama chapa ya Mungu juu yetu kuo-nesha kwamba sisi Wakristo ni mali ya Mungu kwa imani katika Kristo.

Basi, kulingana na maneno hayo kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu anayekaa ndani yetu, ni muhimu tutembee katika Roho.

“Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.” (Gal 5:16)

“Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.” (Gal 5:25) JINA LA

DARAKA MTU MKUU MWANZO

WAKE MWISHO

WAKE MAANDIKO

MUHIMU Neema Paulo Kuitwa kwake Kuja kwa Kristo kunyakua

Kanisa lake Matendo 9 - 28, na zaidi barua za Paulo.

Page 55: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 51 -

DARAKA LA DHIKI KUU

SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA DHIKI KUU

Daraka la Dhiki Kuu linayo majina mbalimbali. Tazama, “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu

mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.” (Mt 24:21)

“Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.” (Yer 30:7)

“Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo us-iku.” (1 Thes 5:2)

Vilevile, tunaona “Siku ya Bwana” mara nyingi katika Agano la Kale. Maandiko yanayolihusu Daraka la Dhiki Kuu ni mengi katika Agano la Kale kama vile Yere-

mia 30, Danieli 12, na Zakaria 14. Katika Agano Jipya kuna Mathayo 24 na 25, 2 Wathesalonike 2, na kitabu cha Ufunuo. Maandiko hayo yote yanatuonesha kwamba Daraka la Dhiki Kuu ni hukumu ya Mungu juu ya dunia kwa sababu ya dhambi za watu.

Daraka hili la Dhiki Kuu litaanza baada ya Kristo kulinyakua Kanisa lake. “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya

malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” (1 Thes 4:16-17)

Kanisa lililo Mwili wa Kristo halitaingia katika Daraka hili. Kama tulivyoona, Wakristo wote walio ndani ya Kristo watanyakuliwa wakutane naye katika mawingu wakienda naye hadi mbinguni milele. Majengo ya makanisa yatabaki na kila mtu anayejiita Mkristo, au mtu wa dini, ambaye hajampokea Kristo moyoni mwake kwa imani, atabaki duniani na kuingia katika Daraka la Dhiki Kuu.

Daraka la Dhiki Kuu litakuwa fupi. Litaendelea kwa miaka saba tu. Tazama, “Naye (Mpinga-Kristo) atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa

nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.” (Dan 9:27)

Maana ya “Juma” hapa ni miaka saba, siyo siku saba. Tazama vilevile Mathayo 24:22. Kutokana na Maandiko ya Danieli 9:27, tunafahamu kwamba kutakuwa miaka mitatu na

nusu ya amani na usalama kwa Waisraeli. Kisha, kutakuwa miaka mitatu na nusu ya mateso ma-kubwa kwa sababu Mnyama yule atalivunja agano lake na Waisraeli, naye ataikomesha sadaka na toleo. Waisraeli watateswa kwa siku elfu moja mia mbili na sitini, yaani, miaka mitatu na nu-su. (Dan 12:11).

Katika nusu ya kwanza ya kipindi hicho, Mungu atawasimamisha mashahidi wawili kuli-hubiri Neno lake katika mji wa Yerusalemu.

“Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, wakiwa wamevikwa magunia.” (Ufu 11:3)

Lakini baada ya siku hizo 1260, mfalme na watu wake watawaua mashahidi hawa wawili. Nusu ya pili ya Daraka hili (yaani, miaka mitatu na nusu), itatawaliwa na Mpinga-Kristo,

yaani “Mnyama.” “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya

kazi yake miezi arobaini na miwili.” (Ufu 13:5)

SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA DHIKI KUU

Wakuu katika Daraka la Dhiki Kuu ni saba tu. Ni Mnyama, Nabii wa Uongo, Mashahidi Wawili, Waisraeli, Malaika wa Bwana (wanaoonekana mara nyingi wakifanya mapenzi ya Mun-gu), na Shetani, yaani Joka, na malaika wake.

Page 56: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 52 -

Mnyama na Nabii wa Uongo wataonekana katika mwanzo wa Daraka la Dhiki Kuu, na wa-tahukumiwa mwishoni mwa Daraka hilo. Mnyama atakuwa mkuu wa serikali. Atayadanganya mataifa yote. Tazama,

“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, alikuwa na pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya kukufuru. Na yule mnyama nili-yemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake ka-ma kinywa cha simba, lile joka likampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona mojawapo wa vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” (Ufu 13:1-3)

Tunapaswa kufahamu kwamba Mnyama huyu siyo mnyama wa porini, bali ni mtu tu mwenye roho kali kama mnyama.

Katika kitabu cha Danieli, Mnyama huyu anaitwa mfalme. Tazama, “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine

ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme wa-tatu. Naye atanena maneno kinyume chake Aliye Juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye Juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa nyakati tatu na nusu.” (Dan 7:24-25)

Tazama vilevile Danieli 11:36. Mnyama wa kwanza atakuwa mkuu wa Serikali, na vivyo hivyo, Mnyama wa pili, yaani

Nabii wa Uongo, atakuwa mkuu wa dini. “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe

mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwan-za, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.” (Ufu 13:11-12)

Jambo lingine kuhusu Mnyama wa kwanza ni kwamba aliitwa, “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule

ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu.” (2 Thes 2:3)

Tena Mnyama yule anaitwa vilevile “Mpinga-Kristo.” Tazama, “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata

sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo tunajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.” (1 Yn 2:18)

Tena, “Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja

katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.” (2 Yn 1:7)

Wote wawili, Mnyama na Nabii wa Uongo, watapata uwezo wao kutoka kwa Joka; ndiye Shetani.

“Wakalisujudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake...” (Ufu 13:4)

Kuhusu Nabii wa Uongo, “Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele

ya wanadamu.” (Ufu 13:13)

Watu wa dunia watamwabudu Mnyama yule na Joka kwa sababu watazishangaa nguvu zao. “Wakalisujudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule

mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?” (Ufu 13:4)

Nabii wa Uongo atawakataza watu kumwabudu Mungu aliye juu pamoja na kumwamini Bwana Yesu.

“Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, ili ile sanamu ya mnyama iongee, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.” (Ufu 13:14-15)

“Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa wa-tumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kulia, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu

Page 57: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 53 -

awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa awe na chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya herufi za jina lake.” (Ufu 13:16-17)

SOMO LA TATU: HALI YA WATU NA MAAGIZO YA DARAKA LA DHIKI KUU

Ninataka kuwakumbusha kwamba mambo yote ya Daraka la Dhiki Kuu ni mambo yataka-yotokea katika wakati ujao, BAADA ya mwisho wa Daraka la Neema.

Katika Daraka hili la Dhiki Kuu, watu watakuwa waovu sana, sawa na watu walioishi katika siku za Nuhu.

“Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.” (Mt 24:10-11)

Tena, “Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa

Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hadi siku ile aliyoingia Nuhu katika safina.” (Mt 24:37-38)

Wengine watazifuata dini za dunia, na watamtukana Mungu aliye hai. “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani,

wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe.” (1 Tim 4:1-2)

Mambo haya yataanza katika mwisho wa Daraka la Neema na yataendelea katika Daraka la Dhiki Kuu.

Tena, watu wataasi maagizo ya Mungu. “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao

wenyewe watajikusanyia waalimu wengi, watakaowaambia yale tu masikio yao yanataka kusikia; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” (2 Tim 4:3-4)

Wayahudi wengine watamtafuta Masihi ili awaokoe, lakini wengi watamkataa Bwana Yesu Kristo kuwa Masihi wao.

“Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa ku-umbwa.” (2 Pet 3:3-4)

Hata wakati watakapoteswa na mapigo mengi kutoka mbinguni, hawatatubu, lakini wa-taendelea katika dhambi zao.

“Wanadamu wakaunguzwa na joto kali, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.” (Ufu 16:9)

Mungu atawaagiza watu wasipokee chapa ya Mnyama na Nabii wa Uongo. “Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsuju-

du huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchang-anywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya ma-laika watakatifu, na mbele za Mwana-kondoo.” (Ufu 14:9-10)

Mungu atawaagiza wamwamini Bwana Yesu na kumwabudu Mungu mwenyewe wakisikili-za ushuhuda wa wajumbe 144,000.

“Nikasikia hesabu yao waliotiwa mhuri katika kila kabila la Waisraeli, watu elfu mia moja na arubaini na nne.” (Ufu 7:4)

“Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, akiwa na Injili ya milele, awahubirie hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye ali-yezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” (Ufu 14:6-7)

Mungu atawaagiza wayavumilie mateso yao. “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” (Uf.

14:12)

Page 58: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 54 -

Hii ni sawa na jinsi Bwana Yesu alivyosema, “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye

kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.” (Mt 10:28)

SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA DHIKI KUU

Ijapokuwa Mungu ataihukumu dunia kwa mapigo makali, watu wataendelea na dhambi zao. Watayaasi maagizo ya Mungu bila woga.

“Na wanadamu waliobakia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kutembea. Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wizi wao.” (Ufu 9:20-21)

Watu wa mataifa mbalimbali watawatesa sana Wayahudi siku zile. “Joka likamkasirikia yule mwanamke, likaenda zake lifanye vita juu ya wazawa wake wali-

obakia, wanaozishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” (Ufu 12:17)

Mwanamke huyu ni mfano wa taifa la Israeli, na wana wake ni wana wa Israeli. Watu wa dunia watalitukana jina la Mungu.

“Wanadamu wakaunguzwa na joto kali, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.” (Ufu 16:9)

Wataukataa ushuhuda wa watu 144,000 waliotumwa kwao kulihubiri Neno la Mungu. Mnyama na askari wake watawaua, lakini Mungu atawafufua.

“Na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale elfu mia moja na arubaini na nne, walionunuliwa katika nchi.” (Ufu 14:3)

Maneno haya ni picha ya mbinguni, siyo duniani. Tuseme, watu waliotajwa hapo wa-lishapelekwa mbinguni.

Kwa sababu watu wa dunia wataikataa rehema ya Mungu, watakubali kuipokea chapa ya Mnyama.

“Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa wa-tumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kulia, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa awe na chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya herufi za jina lake.” (Ufu 13:16-17)

Tuseme, watamwogopa Mnyama kuliko Mungu. Wataiabudu sanamu ya Mnyama. Nabii wa Uongo,

“Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, ili ile sanamu ya mnyama iongee, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.” (Ufu 13:14-15)

Hakika, watu wengi watauona uovu wa Mnyama na Nabii wa Uongo, nao wataitafuta njia ya wokovu. Wataanza kumwamini Bwana Yesu, Mwana-Kondoo yule aliyekufa kwa ajili ya dhambi zao. Lakini watu wengi, walio watumishi wa Mnyama na Nabii wa Uongo, watawatafuta na ku-waua.

“(Mnyama) tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda.” (Ufu 13:7)

Naye atawakata vichwa watakatifu wengi sana. Tazama Ufunuo 7:13-14, na 20:4-5. Halafu watu wengi sana watakusanyika pamoja na Mnyama na Nabii wa Uongo ili wapate

kufanya vita na Mwana-kondoo na watakatifu wake. “Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni

Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndiyo walioitwa, na wa-teule, na waaminifu.” (Ufu 17:14)

Tazama vilevile Ufunuo 19:19-21.

Page 59: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 55 -

SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA DHIKI KUU

Watu walioasi maagizo ya Mungu, waliowatesa wateule wa Mungu, waliomdharau Bwana Yesu, Mwana-Kondoo wa Mungu, watapewa mateso makubwa. Mateso haya ni hukumu ya Mun-gu; ni siku ya gadhabu yake.

Hukumu ya kwanza, ni mapigo ya mihuri saba (Ufu 6:1-17 na 8:1). Maana ya mihuri saba ni hii:

• Kuonekana kwa Mpinga Kristo; • Vita; • Njaa; • Kufa kwa robo ya watu duniani; • Kufa kwa watakatifu; • Tetemeko kubwa la nchi na shida katika anga; • Kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.

Katika hukumu ya pili tunaona mapigo saba ya baragumu (Ufu 8 - 14). Maana ya baragumu saba ni hii:

• Theluthi ya dunia itanyeshewa mvua ya mawe na moto; • Theluthi ya bahari itabadilika kuwa damu na theluthi ya samaki watakufa; • Theluthi ya mito itakuwa chungu; • Theluthi ya Jua na mwezi itafanywa kuwa giza na theluthi ya nyota zitapigwa; • Nzige wakali sana watawatesa watu wasiomwamini Mungu kwa miezi mitano; • Malaika wanne wataliongoza jeshi la wenye farasi 200,000,000 kuja kuwaua theluthi ya

watu waliobaki duniani; • Sauti kubwa kutoka mbinguni itakayoitayarisha dunia kwa ajili ya mapigo ya mabakuli

saba ya dhahabu.

Halafu, kuna mapigo ya mabakuli saba ya dhahabu (Ufu 15 na 16). Mapigo haya ni:

• Majipu mabaya juu ya watu wenye chapa ya Mnyama, na wale walioiabudu sanamu yake;

• Bahari yote itafanywa kuwa damu; • Mito yote itafanywa kuwa damu; • Jua litafanywa kuwa moto mkali sana hata kuwaumiza watu; • Giza litashuka juu ya ufalme wa Mnyama; watu watateswa kwa maumivu mengi; • Mto utakaushwa kufungua njia kwa maadui wa Mnyama kupita; • Radi, sauti za ngurumo mbinguni, tetemeko kubwa na mvua ya mawe makubwa.

Mapigo haya yote yanaitwa “SIKU YA BWANA.” “Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo

utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.” (Oba 15)

Watu wa dunia watapigwa na mapigo mengi kwa sababu waliwapiga wateule wa Bwana. Soma vilevile Sefania 1:14-18.

Wayahudi wasioamini watateswa na Mnyama aliye mtumishi wa Shetani. “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako;

na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wa-kati huo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” (Dan 12:1)

Siku za mwisho za Daraka la Dhiki Kuu, Mnyama na jeshi lake wataizunguka Yerusalemu kusudi wauharibu mji ule pamoja na Wayahudi wote. Lakini watashindwa kwa sababu Bwana Yesu pamoja na majeshi yake ya watakatifu watakuja.

“Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake.” (2 Thes 2:8)

Tazama vilevile Ufunuo 19:19-21.

Page 60: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 56 -

Mnyama na Nabii wa Uongo, wawili wale waliowatendea watu wa dunia mabaya zaidi, wa-tatupwa katika ziwa la moto ili wateswe milele na milele.

“Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao hao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wakiwa hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.” (Ufu 19:20)

Joka yule (Shetani) aliyewapa Mnyama na Nabii wa Uongo uwezo wao, atafungwa katika shimo lisilo na mwisho kwa miaka elfu (Ufu 20:1-3).

JINA LA DARAKA

MTU MKUU MWANZO WAKE

MWISHO WAKE

MAANDIKO MUHIMU

Dhiki Kuu Mpinga Kristo (Mnyama)

Baada ya Kanisa kunya-kuliwa

Kuja kwa Kristo kama Mfalme Vitabu vya Danieli na Ufunuo; Mathayo 24 na 25.

Page 61: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 57 -

DARAKA LA UFALME

SOMO LA KWANZA: WAKATI WA DARAKA LA UFALME

Daraka hili linaitwa UFALME kwa sababu Bwana Yesu atarudi duniani kuisimamisha ufal-me wake.

“Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hau-taangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.” (Dan 2:44)

Tazama vilevile Ufunuo 19:16. Ufalme wa mbinguni utaanza wakati Bwana Yesu atakaposhuka kutoka mbinguni.

“Hapo ndipo atakapotokea BWANA, naye atapigana na mataifa hayo, kama anavyopigana siku ya vita. Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao Mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.” (Zek 14:3-4)

Ufalme huu utaanza baada ya Daraka la Dhiki Kuu; yaani baada ya miaka saba ile. “Lakini mara tu, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake,

na nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.” (Mt 24:29-30)

Daraka la Ufalme litaanza baada ya hukumu ya Mnyama na Nabii wa Uongo. “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye . . . hao wawili wakatupwa

wakiwa hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.” (Ufu 19:20)

“Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake.” (2 Thes 2:8)

Daraka la ufalme litaendelea kwa muda wa miaka elfu. “Huo ndiyo ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa

kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.” (Ufu 20:6)

Daraka la Ufalme litamalizika wakati Shetani atakapofunguliwa kutoka katika shimo lisilo na mwisho.

“Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake.” (Ufu 20:7)

Daraka hili litamalizika wakati waasi wote watakapohukumiwa na kuwekwa chini ya miguu ya Bwana.

“Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke adui zake wote chini ya miguu yake.” (1 Kor 15:25)

Daraka la Ufalme litamalizika wakati Mungu atakapoviharibu vitu vyote vya zamani na kui-tengeneza dunia mpya na mbingu mpya.

“Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitate-ketea. 11Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkiingojea hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.” (2 Pet 3:10-13)

Tazama Ufunuo 21:1 vilevile. Maandiko ya Biblia yanayohusu Ufalme wa Kristo ni mengi sana. Manabii wa Agano la Kale

walitabiri maneno mengi kuhusu ufalme utakaokuja. Katika vitabu vya Injili, Bwana Yesu mwenyewe alifundisha mambo mengi kuhusu Ufalme huo. Kwa mfano, tazama Mathayo sura 13. Katika Matendo 1:6, wanafunzi wa Kristo walimwuliza,

“Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?”

Page 62: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 58 -

Katika barua zao, Paulo na mitume wengine wanazifundisha habari za ufalme wa Mungu, lakini mtume Paulo alifundisha zaidi kuhusu Kanisa, Mwili wa Kristo. Pia, sura ya 20 ya Ufunuo ni habari ya ufalme.

SOMO LA PILI: WATU WA DARAKA LA UFALME - MAHALI NA HALI YAO

Hakika, mtu mkuu wa Daraka hili ni Bwana Yesu Kristo mwenyewe. “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme

utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndiyo utakaotenda hayo.” (Isa 9:6-7)

Tazama vilevile Zaburi 2:6 na Danieli 2:44; 7:14. Kristo atatawala dunia na fimbo ya chuma.

“Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako. Uta-waponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.” (Zab 2:8-9)

Maneno haya yanatuonesha Baba Mungu akisema kwa Mwana wake, yaani Yesu. Kristo atavithibitisha haki na wema duniani.

“Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye ata-miliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.” (Yer 23:5)

“Fadhili na kweli zitakutana, Haki na amani zitakumbatiana.” (Zab 85:10)

Watakatifu watatawala pamoja na Kristo kama makuhani na maliwali. “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa mamlaka ya kutoa hukumu;

nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya Neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala kuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.” (Ufu 20:4)

Tazama vilevile Ufunuo 20:6. Wanafunzi kumi na wawili wataketi juu ya viti vya ufalme kuyahukumu makabila ya

Waisraeli. “Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu

mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.” (Mt 19:28)

Ijapokuwa watu watakaoingia katika ufalme watakuwa wenye haki, bado asili ya dhambi itabaki ndani yao. Watakuwa wana wa Adamu sawa na sisi (Lakini siyo wale waliofufuliwa kutoka wafu ili waingie katika ufalme).

Watu watazaa watoto katika ufalme, na watoto wao watakuwa na asili ya dhambi vilevile, kama Daudi alivyosema katika zaburi yake.

“Tazama, nikazaliwa nikiwa na hatia; Mama yangu akanichukua mimba nikiwa na dhambi.” (Zab 51:5)

Majaribu ya kutenda dhambi hayatakuwa na nguvu sana kama ilivyokuwa katika Madaraka mengine kwa sababu Shetani atakuwa amefungwa kwa muda ule.

“Akalishika lile joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia mhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe kwa muda mfupi.” (Ufu 20:2,3).

Hata hivyo watu watavutwa kutenda dhambi wakiongozwa na asili yao ya dhambi. Hakika, tunajua mji mkubwa wa ufalme wa Kristo utakuwa Yerusalemu. Maandiko mengi

yanasema hivyo. “Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani

kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu.” (Isa 2:3)

“Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala kati-ka Mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.” (Isa 24:23)

Page 63: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 59 -

SOMO LA TATU: MAAGIZO YA DARAKA LA UFALME NA HALI YAKE

Ufalme huu utaitawala dunia nzima. “Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.” (Zab 72:11)

Tena, “Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha

zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.” (Dan 7:14)

Waisraeli wote wataokoka. “Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA;

kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.” (Yer 31:34)

“Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; At-amtenga Yakobo na maasia yake.” (Rum 11:26)

Mateso na huzuni ya Waisraeli itaisha. “Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. 2Semeni na moyo wa

Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.” (Isa 40:1-2)

Tazama vilevile Isaya sura 60 na 61:2-3. Mataifa yote watabarikiwa kwa kupitia Waisraeli. Bwana wa majeshi anasema hivi,

“BWANA wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yuko pamoja nanyi.” (Zek 8:23)

Tazama vilevile Isaya 60:3. Uovu ndani ya serikali utaondolewa na haki itatawala.

“Maana hukumu itarejea kwa wenye haki, Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.” (Zab 94:15)

“Mbele za BWANA, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.” (Zab 96:13)

Vita na kumwaga damu kutaisha katika Daraka la ufalme. “Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu

walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” (Mik 4:3)

Watu watakuwa na afya nzuri na watakuwa na miaka mingi katika ufalme. “Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto

atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.” (Isa 65:20)

Hali ya wanyama itabadilika. “Mbwamwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi;

ndama na mwanasimba na ng'ombe wanono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. 7Ng'ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng'ombe. 8Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa kunyonya atatia mkono wake katika pango la fira.” (Isa 11:6-8)

Laana juu ya udongo na mimea itaondolewa. “Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama war-

idi. Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Leba-noni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa BWANA, ukuu wa Mungu wetu.” (Isa 35:1-2, 6)

Page 64: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 60 -

Maagizo yatakuwa machache tu. Ya kwanza, watu wataagizwa wazitii amri za Mungu na kuishi kufuatana na kanuni za ufalme wake. Ya pili, watu wote wataagizwa kwenda Yerusalemu kuabudu, kwani hekalu la Mungu litakuwa pale.

“Na huo utukufu wa BWANA ukaingia ndani ya nyumba, kwa njia ya lango lile lielekealo upande wa mashariki. 5Eze 3:12; 1 Fal 8:10 Kisha Roho ikaniinua, ikanichukua mpaka katika ua wa ndani; na tazama, utukufu wa BWANA uliijaza nyumba.” (Eze 43:4,5)

Tazama vilevile Malaki 3:18.

SOMO LA NNE: MAKOSA YA DARAKA LA UFALME

Kama Waisraeli katika jangwa siku za Musa, watu wengi wataanza kunung’unika kuhusu utawala wa haki wa Bwana Yesu, Mfalme wao. Tabia ya maasi itaonekana mioyoni mwao. Haki-ka, tabia hii itaenea mahali pote.

Kumbuka kwamba watu ambao watakuwa hai wakati wa ufalme wa Kristo utakapoanza, watakuwa na asili yao ya dhambi. Watakuwa sawa na Wakristo wa leo. Wengine watakuwa wameokolewa kwa neema ya Mungu kwa kuweka imani yao ndani ya Yesu katika Daraka la Dhiki Kuu, na wengine watazaliwa katika Daraka la Ufalme lenyewe. Kati ya hawa watakaozali-wa katika Daraka la Ufalme, wengine wataukataa utawala wa Yesu na pia watakataa kumwa-mini Yesu kama mwokozi wao. Tazama Wagalatia 5:17.

Watu wengi katika ufalme wa Kristo watakataa kwenda Yerusalemu kuabudu. Ni sawa na Waisraeli wa zamani. Waliiacha nyumba ya Mungu kule Yerusalemu na waliabudu miungu min-gine na sanamu zao katika miji mingine.

Watu watataka kuwa sawa na watu wa zamani. Watataka kila nchi iwe na mfalme au rais wake. Tazama 1 Samweli 8:4-5.

Wakati Shetani atakapofunguliwa kutoka katika shimo, watu wengi duniani watakuwa tayari kumfuata. Na wakati miaka elfu ile itakapoisha Shetani atafunguliwa atoke katika kifungo chake,

“Naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, ku-wakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.” (Ufu 20:8)

Tazama, jambo hili litafanyika katika mwisho wa miaka elfu, na watu wengi duniani wa-takuwa tayari kupiga vita dhidi ya Yesu Kristo mfalme wao.

Shetani atayakusanya majeshi yake, nao wataenda Yerusalemu kupigana vita na mfalme Yesu na watakatifu wake.

“…ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa.” (Ufu 20: 8b-9a)

Mioyo ya watu itajazwa chuki kuhusu mfalme wao. Wataliweka tumaini lao kwa Shetani. Itakuwa sawa na jinsi Waisraeli walivyomchukia Bwana Yesu zamani, wakisema,

“Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.” (Lk 19:14)

Kumbuka, Adamu na Hawa waliwekwa mahali pazuri sana katika bustani ya Edeni, lakini walifanya dhambi. Vivyo hivyo, ufalme wa Kristo utakuwa na utawala mzuri katika dunia isiyo na laana juu ya ardhi, wala mimea, wala wanyama, lakini pamoja na uzuri wote huo, watu wengi watafanya dhambi.

Watu wa kwanza watakaoingia katika ufalme watakuwa wenye haki na utakatifu lakini wa-tazaa watoto, na watoto wao watazaa watoto vilevile wenye hitaji la kuamua kumfuata Yesu au la. Watoto wale watazaliwa wakiwa na asili ya dhambi na tabia za kibinadamu.Tuseme, wataw-eza kuchagua wema au ubaya. Basi, wengi wao watayachagua matendo ya uasi.

SOMO LA TANO: HUKUMU YA DARAKA LA UFALME

Wale watakaotenda dhambi katika ufalme huo watahukumiwa , kwani, Kristo atawatawala kwa fimbo ya chuma.

“Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo.” (Ufu 2:27)

Page 65: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 61 -

Tazama vilevile Ufunuo 12:5 na 19:15. Katika mwanzo wa ufalme wake, Kristo atawahukumu watu wa Mataifa katika bonde la Ye-

hoshafati. “Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Ye-

rusalemu, nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewa-tawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.” (Yoe 3:1-2)

Wakati ule ndiyo wakati ambao Bwana Yesu atakapowatenganisha kondoo na mbuzi (Mt 25:31-46).

Watu waliokataa kwenda kuabudu Yerusalemu watahukumiwa. “Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu Wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, ma-

taifa hayo wataharibiwa kabisa.”(Isa 60:12)

“Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, BWANA wa majeshi, mvua haitanyesha kwao.” (Zek 14:17)

Hata nchi ya Misri haitaweza kuikimbia hukumu ya Bwana. Tazama, “Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, am-

bayo BWANA atawapiga mataifa, wasiokwea ili kuadhimisha sikukuu ya Vibanda. Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya mataifa yote, wasiokwea ili kuadhimisha sikukuu ya Vibanda.” (Zek 14:18-19)

Watu ndani ya ufalme wenye kuasi maagizo ya mfalme watauawa. “Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala

moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.” (Isa 66:24)

Watu wa mataifa mengine, waliodanganywa na Shetani, watahukumiwa kwa ghafula. “Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.” (Ufu 20:9b)

Shetani atahukumiwa katika hukumu ya mwisho kabisa. Kwanza, kabla ya mwanzo wa Daraka la Ufalme, Shetani atafungwa na kutupwa katika shimo lisilo na mwisho. Kisha, katika mwisho wa utawala wa Kristo wa miaka elfu, atafunguliwa kwa muda mfupi. Lakini, tazama hukumu yake,

“Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.” (Ufu 20:10)

Hukumu ya kiti cheupe. “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu

zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguli-wa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, kulingana na matendo yao.” (Ufu 20:11-12, 15)

Kumbuka, hukumu hii itafanyika BAADA ya utawala wa Kristo wa miaka elfu. Lakini itaku-wa hukumu inayowahusu watu wote kutoka Madaraka yote, waliokufa katika dhambi zao bila kuupokea wokovu wa Bwana.

JINA LA DARAKA

MTU MKUU MWANZO WAKE

MWISHO WAKE

MAANDIKO MUHIMU

Ufalme Bwana Yesu Kristo

Kurudi kwa Yesu kama Mfalme na kuwashinda maadui wake.

Baada ya miaka elfu katika vita ya mwisho ya ku-wahukumu wote

Vitabu vya Manabii katika Agano la Kale; Mathayo, Marko, Luka, Ufunuo.

Page 66: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 62 -

MAMBO YA MWISHO Tazama maandiko yanayohusu mambo yatakayokuja baada ya hukumu ya kiti kikubwa

cheupe. “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote,

na mamlaka yote, na nguvu. Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke adui zake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.” (1 Kor 15:24-26)

Hali hii mpya ni ya milele kwa ajili ya wote wale waliomwamini Mungu ili wapate kuwa na furaha ya milele mbele za Mungu. Kwa wale ambao hawakuamini, kutakuwa hukumu, mateso, na kutenganishwa na Mungu milele. Tazama maneno ya Bwana Yesu,

“Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” (Ufu 22:12)

Kutakuwa na dunia mpya na mbingu mpya. Yerusalemu mpya utashuka kutoka mbinguni. Bustani itaonekana katikati ya mji mtakatifu (Ufu sura 21 na 22).

Mwanafunzi mpendwa. Kama umejifunza maneno ya kitabu hiki kwa bidii, sasa unaweza kuzielewa tofauti za Madaraka yote na habari za mipango ya Mungu katika kila Daraka. Neema ya Mungu iwe pamoja nawe.

Page 67: TEOLOJIA YA MADARAKA

- 63 -

MAFUNDISHO YA MADARAKA MANENO YA KUKUMBUKA

JINA LA DARAKA

MTU MKUU MWANZO WAKE

MWISHO WAKE

MAANDIKO MUHIMU

Usafi Adamu Kuumbwa kwa Adamu Kula matunda na kufukuzwa kutoka katika Bustani ya Edeni

Mwanzo 1 – 3

Dhamiri Adamu Kufukuzwa kwake atoke kwenye Bustani ya Edeni

Gharika ya maji Mwanzo 4 -8

Serikali Nuhu Baada ya gharika Kusambazwa kutoka mnara wa Babeli

Mwanzo 9 – 11

Ahadi Ibrahimu Kuitwa kwake Utumwa katika nchi ya Misri Mwanzo 12 – 50 Kutoka 1 - 19

Sheria Musa Mlima wa Sinai na kutole-wa kwa Sheria ya Musa

Kumkataa Kristo kama Masihi na Mwokozi

Kutoka 20 hadi mwisho wa Agano la Kale; vitabu vya Injili, na Matendo 1-9

Neema Paulo Kuitwa kwake Kuja kwa Kristo kunyakua Kanisa lake

Matendo 9 - 28, na zaidi barua za Paulo.

Dhiki Kuu Mpinga Kristo (Mnyama)

Baada ya Kanisa kunya-kuliwa

Kuja kwa Kristo kama Mfalme Vitabu vya Danieli na Ufunuo; Mathayo 24 na 25.

Ufalme Bwana Yesu Kristo

Kurudi kwa Yesu kama Mfalme kuwashinda maadui wake.

Baada ya miaka elfu katika vita ya mwisho ya ku-wahukumu wote

Vitabu vya Manabii katika Agano la Kale; Mathayo, Marko, Luka, Ufunuo.