tathmini ya mafunzo ya sam ukerewe: kuanzia tarehe 3- 10 … · 2013-01-18 · stadi zao...
TRANSCRIPT
1
Tathmini ya Mafunzo ya SAM
Ukerewe: Kuanzia tarehe 3- 10 Septemba 2012
Weka Alama ya √ (tick) katika mabano kwa kila swali hapo chini:
Swali 1
Kwa ujumla umeyaonaje mafunzo haya? 1=Safi 2=Safi sana 3=Mbaya 4=Mbaya Sana
Jedwali 1
Evaluation Response Total response %
1- Safi 5 14 35.7%
2- Safi Sana 9 14 64.3%
3-Mbaya 14
4- Mbaya Sana 14
Matokeo: Kwa upande wa maoni juu ya mafunzo haya asilimia 64.3 % ya washiriki wamesema
mafunzo haya ni safi sana wakati 35.7% ya washiriki wote wamesema mafunzo haya ni safi.Hii
inamaanisha kwamba mafunzo haya SAM yanaumuhimu mkubwa kwa jamii hususani katika
kuwawezesha kufanya ufuatiliaji juu ya matumizi ya rasilimali za jamii katika utoaji huduma
unaolenga kustawisha jamii.
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
Mafunzo yametuongezea uelewa wa kutosha kuanza kuhoji,kufuatilia,na kuishawishi jamii iweze
kuamka
Mafunzo yamekwenda vizuri kutokana na kupangiliwa vyema na wawezeshaji wazuri
Mafunzo yanasisimua nakutupa fursa ya ufuatiliaji
Mafunzo ni mazuri sana kwani ni somo ambalo ni muhimu na tunaomba liwe endelevu
Mafunzo ni mazuri kwani yamenijengea uwezo mkubwa katika mfumo wa ufuatiliaji wa
uwajibikaji kwa jamii
o Wawezeshaji walikuwa wanafundisha vizuri na walieleweka vizuri ,mada zilikuwa nzuri
na za kuvutia ila mda wamafunzo ulikuwa mdogo sana
Mafunzo ni mazuri sana kwa sababu tumeweza kujifunza mambo ya msingi ya haki za binadamu
Mafunzo haya ni safi sana kwa sababu yanalenga upatikanaji wa haki za binadamu kwa
kuzingatia uwezo wao katika jamii husika kuanzia ngazi ya chini kabisa.
2
Maada zilizotolewa zilikuwa zinalenga uhalisia wa uwajibikaji wa shughuli za umma,
wawezeshaji walikuwa na uwezo wa kutosha katika ufundishaji hata mifano iliyotolewa ilikaribia
na mazingira halisi.
Mafunzo haya ni mazuri kwasababu yanaelekeza jamii kutambua wajibu wake na wajibu wa
wasimamizi na watoa huduma ili kufikia lengo la kupata huduma bora zinazozingatia haki za
binadamu
Ni safi sana kwa sababu nimeelewa kuwa tatizo au kitu chochote kinavyoanza lazima kuanzia
kwa jamii kwanza ndo kuenda ngazi za juu
Kwa sababu yamenijengea uwezo wa uwajibikaji jamii kwa kuangalia haki za msingi za binadamu
ili zitimizwe lazima watoa huduma wazingatie uadilifu
Mafunzo haya yamenijengea uelewa wa mfumo wa uwajibikaji katika jamii
Swali 2
Je wawezeshaji walikuwa wanaeleweka wakati wa kufundisha? 1=Ndio Kwa kiwango kikubwa 2=Ndio kwa kiwango cha kawaida 3=Ndio kwa kiwango kidogo 4=Hapana kwa kiwango kikubwa 5=Hapana kwa kiwango cha kawaida 6= Hapana kwa kiwango kidogo
Jedwali 2
Evaluation Response Total response %
1- Ndio kwa kiwango kikubwa 9 14 64.3%
2- Ndio kwa kiwango cha
kawaida
5 14 35.7%
3- Ndio kwa kiwango kidogo 14
4- Hapana kwa kiwango kikubwa 14
5- Hapana kwa kiwango cha
kawaida
14
6- Hapana kwa kiwango kidogo 14
Matokeo: Kwa upande wa uelewa kwa wawezeshaji 64.3% wamesema walikuwa na uelewa wa
kiwango kikubwa wakati 35.7% ya washiriki wamesema walikuwa na uelewa wa kiwango cha
kawaida
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
Wawezeshaji walionyesha kutoa mafunzo walikuwa na uhakika na kile wanachokifundisha
Mpangilio wa mada na uwasilishaji, ufahamu wao mkubwa.
Wamekuwa waungwana na wanafuata mda na wanajali watu
Mwezeshaji ametoa mafunzo kwa umakini mzuri na amezingatia haki za msingi za binadamu
3
Walitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha ninaelewa kinachowezeshwa i.e majadiliano na
kutumia mifano halisi
Walikuwa wanaweza kushirikisha wawezeshwaji kwa kiwango cha kutosha
Maelezo yao na ufafanuzi wao ulikuwa ni wa kina pia walitumia lugha rahisi
Kwa sababu wamefundisha na kuweza kuelewa japokuwa masomo yalikuwa mengi muda mfupi
Wadau wa mafunzo hawakuonyesha kuchoka pindi mafunzo yanatolewa
Mafunzo ni mazuri sana yalihitaji muda zaidi kwa muda huu wawezeshaji imewalazimu
kufukuzana na muda ili angalau mada zote zipitiwe hivyo wameeleweka kiasi
Mafunzo ni mazuri kwa maoni yangu mafunzo sikunyingine yaongezwe muda
Maana kila mada imefundishwa kwa vitendo na maelekezo ya kina zaidi
Kwa sababu tulienda nao sambamba bila kutuacha nyuma na walituelewesha pale ambapo
hatujui lakini kitu kingine tulibadilishana uzoefu
Swali 3
Je mifano iliyotumika ilikuwa na uhusiano na mada na ili saidia kuelewa mada? 1=Ndio kwa kiwango kikubwa 2=Ndio kwa kiwango cha kawaida 3=Ndio kwa kiwango kidogo 4=Hapana kwa kiwango kikubwa 5=Hapana kwa kiwango cha kawaida 6= Hapana kwa kiwango kidogo
Jedwali 3.
Evaluation Response Total response %
1- Ndio kwa kiwango kikubwa 11 14 78.57%
2- Ndio kwa kiwango cha
kawaida
3 14 21.43%
3- Ndio kwa kiwango kidogo 14
4- Hapana kwa kiwango kikubwa 14
5- Hapana kwa kiwango cha
kawaida
14
6- Hapana kwa kiwango kidogo 14
Matokeo: Kwa upande wa uhusiano wa mifano na mada 78.57% ya washiriki wamesema mifano
iliyotumika inauhusiano kwa kiwango kikubwa na mada zinazotolewa wakati 21.43% wamesema
inauhusiano kwa kiwango cha kawaida.
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
Mifano ilifanya darasa kuchangia kwamapana zaidi
Nimefumbuka macho hasa hatua 5 zilizo ndani ya mfumo wa uwajibikaji wa jamii
Kabisaa yaani we acha tuu
4
Iliendana na mafunzo yenyewe
Mifano yote iliendana na mada na hali halisi kwa ujumla
Kwa mfano mihimili ya dola ,serikali,bunge,mahakama,baraza la madiwani
Kwa sababu ya uelewa zaidi tumeweza kujibu maswali yaliyokuwa yakitolewa ndani ya vikundi
na mmoja mmoja
Sababu ililenga jamii kwa mifano halisia
Mifano halisi ya Halmashauri za wilaya pamoja na vyombo vya usimamizi zililenga kabisa mada
husika
Ufafanuzi ulinisaidia sana baada ya kutoa aina za mifano
Ilikuwa ya kiwango, maana ilikuwa na uhalisia wa kile kilichoongelewa
Kwa sababu mifano iliyotumika ilionyesha jinsi gani mfumo wa uwajibikaji katika jamii
unavyoweza kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa kuzingatia misingi ya kazi
Swali4
Mada zilizowasilishwa zinaeleweka kwa ufasaha? 1=Ndio kwa kiwango kikubwa 2=Ndio kwa kiwango cha kawaida 3=Ndio kwa kiwango kidogo 4=Hapana kwa kiwango kikubwa 5=Hapana kwa kiwango cha kawaida 6= Hapana kwa kiwango kidogo
Jedwali 4.
Evaluation Response Total response %
1- Ndio kwa kiwango kikubwa 6 14 42.86%
2- Ndio kwa kiwango cha
kawaida
8 14 57.14%
3- Ndio kwa kiwango kidogo 14
4- Hapana kwa kiwango kikubwa 14
5- Hapana kwa kiwango cha
kawaida
14
6- Hapana kwa kiwango kidogo 14
Matokeo: Kwa upande wa mada kueleweka kwa ufasaha 42.86% ya washiriki wamesema mada
zilieleweka kwa ufasaha kiwango kikubwa wakati 57.14% wamesema mada zilieleweka kwa kiwango
cha kawaida.
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
Mada zilieleweka kwa kiwango kikubwa kwani washiriki walitoa mifano mingi iliyo hai.
Mfumo mzima umejidhihirisha siku hadi siku
5
Zinaeleweka
Zinaeleweka ila kuna maeneo mengine yanahitaji muda zaidi kwa hali halisi ya jamii na mifumo
iliyopo
Mada ni nyingi muda ni mfupi hivyo kunakuwepo na changamoto za kuweza kuyamasta kwa
ufasaha
Kwa sababu tulikuwa na uwezo wa kujibu na kutambua yaliyokuwa yanaelezwa
Kwasababu bado elimu hii inahitajika kwa walengwa zaidi mfano wanajamii madiwani na
watendaji.
Mada za taratibu/somo la kamati ya ugavi na mkaguzi wa ndani
Mada zinaeleweka isipokuwa muda wa mafunzo uongezwe kwa sababu ni mada zinazohitaji
kuelewa kwa upana zaidi hususan miongozo ya kisheria
Ndiyo kwa pale pasipoeleweka mifano ilitolewa mpaka mtu akaelewa
Nimeweza kuelewa wajibu wa kila utawala na mipaka yake na unawajibika kwa nani ili nini
kitokee
Kwa sababu mada zote zinaonyesha umuhimu wa kuwepo kwa mfumo wa uwajibikaji katika
jamii
Swali 5
Mbinu zilizotumika kuwasilisha mada zilikuwa muafaka? 1=Ndio kwa kiwango kikubwa 2=Ndio kwa kiwango cha kawaida 3=Ndio kwa kiwango kidogo 4=Hapana kwa kiwango kikubwa 5=Hapana kwa kiwango cha kawaida 6= Hapana kwa kiwango kidogo
Jedwali 5.
Evaluation Response Total response %
1- Ndio kwa kiwango kikubwa 9 14 64.29%
2- Ndio kwa kiwango cha
kawaida
5 14 35.71%
3- Ndio kwa kiwango kidogo 14
4- Hapana kwa kiwango kikubwa 14
5- Hapana kwa kiwango cha
kawaida
14
6- Hapana kwa kiwango kidogo 14
Matokeo: Kwa upande wa mbinu muafaka zilizotumika kufundisha 64.29% ya washiriki wamesema
mbinu muafaka zilitumika kwa kiwango kikubwa wakati 35.71% wamesema zilitumika kwa kiwango
cha kawaida
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
6
Mbinu zilizotumika zilieleweka Kwa urahisi kwa washiriki.
Stadi zao wawezeshaji, nyenzo za kufaa zilizo zingatia elimu ya mtu mzima “adult learning”
Kungekuwepo na video za kutosha.
Zimeniwezesha kuelewa zaidi somo lililokuwa linafundishwa
Waliweza kushirikisha na kutoa mfano hai hivyo ilikuwa ni rahisi kueleweka
Zilikuwa zikizingatia muda
Kwa sababu tumefundishwa na kuelewa mapungufu yaliyopo hasa usimamizi wa uadilifu.
Wawezeshaji wametumia lugha rahisi katika kuelekeza na katika kufafanua pia wametumia
mifano tete iliyo katika jamii zetu na kuelekeza namna ya kutatua au kufuatilia
Kwa sababu wawezeshaji waliweza kulisoma darasa /washiriki wanavyoielewa mada
Swali 6
Mada zilizowasilishwa zinauhusiano na hali halisi ya jamii yako? 1=Ndio kwa kiwango kikubwa 2=Ndio kwa kiwango cha kawaida 3=Ndio kwa kiwango kidogo 4=Hapana kwa kiwango kikubwa 5=Hapana kwa kiwango cha kawaida 6= Hapana kwa kiwango kidogo
Jedwali 6.
Evaluation Response Total response %
1- Ndio kwa kiwango kikubwa 13 14 92.86%
2- Ndio kwa kiwango cha
kawaida
1 14 7.14%
3- Ndio kwa kiwango kidogo 14
4- Hapana kwa kiwango kikubwa 14
5- Hapana kwa kiwango cha
kawaida
14
6- Hapana kwa kiwango kidogo 14
Matokeo: Kwa upande wa uhusiano wa mada na hali halisi ya jamii 92.86% ya washiriki wamesema
zinahusiana kwa kiwango kikubwa wakati 7.14% ya washiriki wamesema zihusiana kwa kiwango cha
kawaida
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
Kuonyesha zinauhusiano washiriki walichangia wakati mwingine muda ulipungua.
Hakuna usimazi madhubuti wa mfumo wa uwajibikaji jamii iwe kijiji,kata na hata halmashauri
Saana tu.
Nilibaini kuwa hata sisi kama jamii tunapaswa kuwajibika na kukemea ubadhilifu
7
Mifumo ya utawala imesababisha uwajibikaji wa jamii kukosa nguvu hivyo yameakisi hali halisi
katika jamii zetu
Kwa mfano walipokuwa wanaulizana mafikiano kuhusu utendaji kazi wa halmashauri ni duni pia
wao walikiri kuwa bajeti imeandaliwa kwa lugha ngumu sana
Kwa sababu mambo muhimu yahusuyo jamii hayatekelezeki vizuri
Kwasababu mada zote zililenga kuitendea jamii haki ili kuweza kupata huduma bora
Kwa ujumla maada zilizotolewa zinaigusa jamii sehemu kubwa kwa upande wa viongozi
madiwani /wabunge na watendaji kwa pamoja
Kutokana na elimu hii kutokuwepo katika jamii mada hizi zimekuwa na uhusiano mkubwa mno
Usimamizi wa matumizi na rasilimali zinatumika ovyo na bila kujali kuwa mali ya wanajamii
wenyewe
Mada zilizowasilishwa kwenye jamii yangu zina uhusiano halisi .
Kwa kuzingatia mfumo wa ufuatiliaji na uwajibikaji ndo kutasababisha jamii ipate huduma iliyo
bora.
Swali 7
Wawezeshaji walikuwa na uelewa wa kile walichokuwa wanafundisha? 1=Ndio kwa kiwango kikubwa 2=Ndio kwa kiwango cha kawaida 3=Ndio kwa kiwango kidogo 4=Hapana kwa kiwango kikubwa 5=Hapana kwa kiwango cha kawaida 6= Hapana kwa kiwango kidogo
Jedwali 7.
Evaluation Response Total response %
1- Ndio kwa kiwango kikubwa 12 14 85.71%
2- Ndio kwa kiwango cha
kawaida
2 14 14.29%
3- Ndio kwa kiwango kidogo 14
4- Hapana kwa kiwango kikubwa 14
5- Hapana kwa kiwango cha
kawaida
14
6- Hapana kwa kiwango kidogo 14
Matokeo: Kwa upande wa uelewa wa wawezeshaji wa kile walichokuwa wanafundisha 85.71% ya
washiriki wamesema wanauelewa wa kiwango kikubwa wakati 14.29% wamesema wanauelewa wa
kiwango cha kawaida
8
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
Kutotafuna maneno kutoa mifano ni ushahidi tosha kuwa na uelewa wa muwezeshaji.
Hakuna maelezo, wazuri, chamsingi walijitahidi sana “UWEZO WANAO”
Wanaeleweka wamesoma na kubobea vilivyo
Walikuwa makini pia waliheshimu wazo la kila mshiriki wa mafunzo
Walitoa ufafanuzi wakina kwa kila mada pia hawakuonyesha udhaifu katika kuwezesha
Waliweza kueleza vizuri na kueleweka kwa ufasaha
Mada zao zilieleweka vizuri sana na zililenga mahitaji ya jamii pia hata sisi tumeweza kujua
tufanye nini sasa baada ya mafunzo haya
Ndiyo kwa sababu mara kwa mara walikumbushia kuzingatia 3us ufafanuzi, uthibitisho na
uhalalisho
Wawezeshaji na mada zilizotolewa zinaweza kusema haya;walimu wa vyuo vikuu, maada pia
kwaajili ya watu wa diploma nk
Walijipanga kwa pamoja kwa kufundisha bila kutetereka
Walijiamini kutoa maelekezo pale walipokumbana na maswala tete (changamoto), walikuwa
wabunifu kwa kuibua mifano yenye utata nasi kuchangia kwa umakini zaidi.
Ndiyo kwasababu kile walichokuwa wanakifundisha wanauzoefunacho
Swali 8
Mafunzo haya yamekupa uelewa na dhana ya mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji wa kijamii na jinsi unavyofanya kazi? 1=Ndio kwa kiwango kikubwa 2=Ndio kwa kiwango cha kawaida 3=Ndio kwa kiwango kidogo 4=Hapana kwa kiwango kikubwa 5=Hapana kwa kiwango cha kawaida 6= Hapana kwa kiwango kidogo
Jedwali 8.
Evaluation Response Total response %
1- Ndio kwa kiwango kikubwa 8 14 57.14%
2- Ndio kwa kiwango cha
kawaida
6 14 42.86%
3- Ndio kwa kiwango kidogo 14
4- Hapana kwa kiwango kikubwa 14
5- Hapana kwa kiwango cha
kawaida
14
6- Hapana kwa kiwango kidogo 14
9
Matokeo: Kwa upande wa uelewa wa dhana ya mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii na jinsi
unavyofanya kazi 57.14% ya washiriki wamesema wamepata uelewa kwa kiwango kikubwa wakati
42.86% ya washiriki wamesema wamepata uelewa kwa kiwango cha kawaida
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
Kwa kiasi kikubwa
Nimegundua tofauti zilizopo kati ya mafunzo haya na niliyo tangulia kuyapata.
Katika sekta yangu mafunzo haya ni muafaka.
Nimepata ufahamu ya kuwa nina haki ya kufahamu na kusimamia rasilimali zetu.
Ndio kwani nina uwezo wa kupima mfumo wa uwajibikaji katika jamii yangu
Kwa sasa ninaweza kufuatisha taarifa za halmashauri /kijiji na kata yangu
Ninaweza kutambua niwajibikeje katika jamii
Mafunzo yameniwezesha kuelewa kwamba mfumo wa uwajibikaji uliopo hauzingatii haki za
binadamu ili kuweza kupata huduma bora
Kwa ufahamu nisawa lakini mifumo ya nchi bado haijaweka wazi sana uhuru wa kila raia kupewa
taarifa nyaraka.
Nitatumia 3us
Nilivyoelewa dhana nzima kama siku zingeongezeka uelewa wangu ungekuwa kwa asilimia
nyingi zaidi,lakini nimeelewa japo si kwa asilimia zote
Kwa sababu elimu niliyopata kutoka kwa wawezeshaji wetu imenijengea uelewa wa kawaida wa
namna ya ufuatiliaji na uwajibikaji katika jamii namna ya utoaji wa huduma bora
Swali 9 Ni mada ipi au zipi zimekuwia ugumu kuelewa?
Hakuna zote nimeelewa vizuri.
Mada ya uwajibikaji jamii lakini nimeelewa.
Hakuna.
Zote zimeeleweka vyema.
Kutokana na ufafanuzi wa wawezeshaji mad azote nilizielewa
Hakuna iliyokuwa ngumu kuielewa bali kwa kuwa mada zilikuwa nyingi hivyo ni vigumu kutunza
vipengele vyote kichwani
Kuhusu mgawanyo wa rasilimali Tanzania.
Vifupisho vya maneno ndivyo vinavyonisumbua kuelewa
Swali 10 Ni mada ipi au zipi umezielewa vizuri?
Ni mfumo mzima wa uwajibikaji kwa jamii.
Karibu zote.
Mada ya uchechemuzi
10
Mada ya uchechemuzi.
Uchechemuzi na ushawishi wake
Karibu zote
Mgawanyo wa rasilimali na mpango mkakati.
Nakubaliana na kitu au kukataliwa lazima mtu ajieleze kuzingatia afafanue,udhibitisho, na
uhalalisho
Mada ya mipango na mgawanyo wa rasilimali imeeleweka vizuri sana
Swali 11
Ukiwa kama raia wa kawaida au mwanaharakati, mafunzo haya yamekusaidia nini katika maisha
yako ya kila siku?
1. Yamenifumbua macho na kunipa uwezo wa kuanza kuhoji.
2. Nimezidisha uimara wa stadi za ufuatiliaji wa mfumo wa uwajibikaji wa kijamii
“NITAFUNDISHA KWA UZURI ZAIDI”
3. Yamenisaidia kujisahihisha na kuwabaini wala nchi.
4. Nimepata mwanga kuwa mimi nina nafasi ya kutoa ushawishi na utetezi
5. Yameniwezesha kutambua mfumo mzima wa uwajibikaji wa jamii pia mfumo wa
usimamizi wa fedha/mali ya umma
6. Ninao wajibu wa kushiriki katika kuwezesha mfumo wa uwajibikaji jamii ili kuhakikisha
huduma bora zinapatikana kwa mtizamo wa haki za binadamu
7. Ndiyo kwa sababu yameniongezea uelewa mkubwa wa masuala mbalimbali ya kijamii
8. Yamenifungua akili,Ninaweza kufanya kazi kwa uwezo mkubwa kulingana na
nilichokipata
9. Yameniongezea kuweza kujua haki zabinadamu zinazokiukwa
10. Kutambua haki na wajibu wa kupewa huduma kama kiongozi wa umma /asasi mbinu za
uwajibikaji
11. Mafunzo haya yamenisaidia kwenda kufanya ushawishi na uchechemuzi katika jamii ili
kufikia malengo ya upatikanaji wa huduma bora
12. Kwanza yamenijengea maamuzi mazuri kwenye familia yangu pamoja na jamii
inayonizunguka
13. Kuwajibika kusikokoma nikutanapo na vikwazo visivyo rasmi
14. Kwanza yamenifanya nizitambue haki zangu za msingi katika maisha ya kila siku ya
binadamu
11
Swali 12
Je mafunzo haya yamekujengea uwezo wa kuhoji na kuiwajibisha serikali yako au kiongozi wako katika eneo lako kama mwanaharakati wa kawaida? 1=Ndio kwa kiwango kikubwa 2=Ndio kwa kiwango cha kawaida 3=Ndio kwa kiwango kidogo 4=Hapana kwa kiwango kikubwa 5=Hapana kwa kiwango cha kawaida 6= Hapana kwa kiwango kidogo
Jedwali 12.
Evaluation Response Total response %
1- Ndio kwa kiwango kikubwa 10 14 71.43%
2- Ndio kwa kiwango cha
kawaida
4 14 28.57%
3- Ndio kwa kiwango kidogo 14
4- Hapana kwa kiwango kikubwa 14
5- Hapana kwa kiwango cha
kawaida
14
6- Hapana kwa kiwango kidogo 14
Matokeo: kwa upande wa kujenga uwezo wa kuweza kuhoji na kuiwajibisha Serikali au kiongozi
kama mwanaharakati 71.43% ya washiriki wamesema imewajengea uwezo kwa kiwango kikubwa
wakati 28.57% imewajengea uwezo kwa kiwango cha kawaida
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
Ni kweli mafunzo haya yameniwezesha sasa kuanza kuifuatilia serikali na kuhoji.
Nimeimarika zaidi kuwajibisha au kuhoji kutaendelea kwa staili mpya.
Uwajibikaji unahusisha jamii nzima hivyo nitaihamasisha jamii kushiriki katika mfumo wa
uwajibikaji kwa hatua zote na hatimaye tunaweza kuwawajibisha watendaji wanaokwenda
kinyume.
Nimeweza kutambua namna ya kuandaa mpango mkakati na utekelezaji wake na pia sharia
mbalimbali na bajeti za halmashauri yangu, mkaguzi mkuu wa serikali anavyofanya kazi.
Kwa sababu sijapata elimu ya kujua sharia namba ngapi na vifungu vyake
Kama mwanaharakati nimeongeza ujuzi
Kwa kutumia miongozo na kanuni na taratibau nimeweza kutambua kwamba ni wajibu wangu
kufanya hivyo
Taarifa ya fedha ndani ya mwaka na mwisho wa mwaka halmashauli na kijiji change
Nimekuwa na uelewa uliokuwa umefichika kwa kutoelewa kuwa viongozi wako chini ya jamii
maana wao ndio waajiri
Kwa sababu ni moja ya majukumu yangu kama jamii
12
Swali 13
Mazingira ya kufanyia mafunzo na huduma zilizotolewa ni ya kuridhisha? 1=Ndio kwa kiwango kikubwa 2=Ndio kwa kiwango cha kawaida 3=Ndio kwa kiwango kidogo 4=Hapana kwa kiwango kikubwa 5=Hapana kwa kiwango cha kawaida 6= Hapana kwa kiwango kidogo
Jedwali 13.
Evaluation Response Total response %
1- Ndio kwa kiwango kikubwa 3 14 21.43%
2- Ndio kwa kiwango cha
kawaida
8 14 57.14%
3- Ndio kwa kiwango kidogo 3 14 21.43%
4- Hapana kwa kiwango kikubwa 14
5- Hapana kwa kiwango cha
kawaida
14
6- Hapana kwa kiwango kidogo 14
Matokeo: Kwa upande wa mazingira 21.43% ya washiriki walisema yalikuwa ni ya kuridhisha kwa
kiwango kikubwa 57.14 % ya washiriki walisema mazingira ni ya kuridhisha kwa kiwango cha
kawaida na 21.43% walisema ni yakuridhisha kwa kiwango kidogo
Hapa chini ni sababu za matokeo hayo kama yalivyoandikwa na washiriki:
Kwakiasi cha kawaida yanaridhisha
Wakati mwingine kelele zilizidi kutokana na matumizi maalum ya maeneo yanayozunguka
ukumbi
Yametuwezesha kuwepo hapa kwa mda wote wa mafunzo
Ili kuweza kupata utulivu zaidi wa kujifunza ingefaa kubadilisha mazingira tuliyozoea
Chakula chai vilikuwa vizuri sana .chumba cha mafunzo kina madirisha makubwa hivyo
viliwasumbua wawezeshaji katika projection.choo cha hapa hakifai kikarabatiwe.
Nilitakiwa kuwa nje ya familia kwa maana ya kufuata ratiba jioni baada ya darasa kubadilishana
uzoefu na washiriki wengine.
Mafunzo yapewe muda wa kutosha pia yasiwe karibu na maeneo tunayoishi ili tuweze
kuhudhuria kwa kipindi chote mafunzo bila kutokatoka
Mahali pa mafunzo ni pakuridhisha /pametulia
Nimazingira yasiyo na kelele(tulivu)na salama
Kwa sababu huduma tuliyoihitaji kupewa tumepewa bila matatizo
13
Swali 14
Je ungependa kufanya zoezi la SAM baada ya mafunzo haya katika eneo lako? 1=Ndio 2=Hapana
Jedwali 14.
Evaluation Response Total response %
1- Ndio 12 14 85.75%
2- Hapana
14
0%
Fomu 2 hazikujazwa Swali
Nini matarajio yako baada ya mafunzo haya katika eneo lako?
1. Ni kusambaza elimu hii kadri ya uwezo wangu.
2. Ni uboreshaji wa shughuli za mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji wa umma.Ukusanyaji
taarifa za uwajibikaji wa umma katika sekta ya afya
3. Kuwa na uwezo wa kuhoji na kutafuta suluhu
4. Ufuatiliaji wangu kuhusu mali/fedha za umma sasa utakuwa wa kitaalamu sana
5. Kufanya ushawishi ili kubadilisha mifumo iliyopo
6. Kufanya uchechemuzi wa kina
7. Kufuatilia huduma kwenye idara ya afya
8. Kuwajibika kwa ukamilifu, kufuatilia mambo mbalimbali ambayo yanafanyika nje ya
utaratibu
9. Ninatarajia kufanya uchechemuzi ambao utaweza kuleta mabadiliko kutokana na
mapungufu yote yaliyopo
10. Kuelimisha jamii kuanzia kwenye familia /jamii inayonizunguka hadi watumishi wenzangu
11. Kufanya ushawishi na utetezi ili kuangalia kama mfumo wa ufuatiliaji na uwajibikaji katika
jamii unatakelezwa
14
Swali 16 Nini ungependa kiboreshwe kifanyike tofauti kuboresha mafunzo haya?
1. Nikuona tunafikia mwisho wa hatua zote za mafunzo haya naomba posho iongezwe.
2. Ukumbi peke yake
3. Yawepo maigizo na nyimbo za kutosha
4. Mafunzo haya yaendane na vifungu vya sheria namba 7 1982 na marekebisho yake na
memoranda ya 1997 vitatusaidia sana wakati wa kufuatilia kazi zetu
5. Mda uongezwe ,mda wa majadiliano uwe zaidi
6. Kuongeza posho ya chakula cha usiku na nauli
7. Muda wa mafunzo uongezwe na eneo la mafunzo liboreshwe
8. Mafunzo kufanyika ndani ya wilaya, mafunzo yawe nje ya wilaya, maslahi/posho
inayotolewa kwa siku ni kiasi kidogo kutokana na hali ya maisha ya sasa.
9. Muda wa mafunzo uongezwe,viambatanisho muhimu tuvipate kulingana na mada mfano
vitabu vya sheria ya utumishi, rushwa
10. Posho ningependa iboreshwe
11. Muda mchache.mafunzo ni mazuri yahitaji muda mrefu ili mada ziende kwa ufahamu zaidi
12. Ni kuzidi kutujengea uwezo wa kuelewa zaidi katika kuzitambua haki zetu za msingi