sharh kitaabu cha tawhiyd - imaam muhammad ibn ´abdil-wahhaab

264
Kitaab-ut-Tawhiyd Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin エAbdil-Wahhaab 1 ﺷﺮﺡ ﻛﺘﺎﺏ ﺍﻟﺘﻮﺣﻴﺪSharh Kitaab-ut-Tawhiyd [Kiswahili] ﺍﻟﺸﻴﺦ ﺍﻹﻣﺎﻡ ﳏﻤﺪ ﺑﻦ ﻋﺒﺪ ﺍﻟﻮﻫﺎﺏash-Shaykh al-Imaam Muhammad bin エAbdil-Wahhaab Mfasiri: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Upload: wanachuoni

Post on 13-Apr-2015

855 views

Category:

Documents


23 download

DESCRIPTION

Sharh Kitaabu Cha Tawhiyd - Imaam Muhammad Ibn ´Abdil-Wahhaab

TRANSCRIPT

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

1

شرح كتاب التوحيدSharh

Kitaab-ut-Tawhiyd[Kiswahili]

الشيخ اإلمام حممد بن عبد الوهاب

ash-Shaykh al-Imaam Muhammadbin ´Abdil-Wahhaab

Mfasiri:Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

2

Utangulizi wa mfasiri............................................................................................................06Kauli za maimamu na wanachuoni kuhusu “Kitaab-ut-Tawhiyd”..............................08Mlango Wa 1: Kauli Yake (Ta´ala): Na Sikuumba majini na watu waisipokuwawaniabudu...........................................................................................................10Mlango Wa 2: Fadhila za Tawhiyd na madhambi yanayosamehewa kwayo..............18Mlango Wa 3: Mwenye Kuhakikisha Tawhiyd Ataingia Peponi Bila Hesabu............23Mlango Wa 4: Kuiogopa Shirki. ............................................................................ .............28Mlango Wa 5: Kulingania Katika Shahaadat An Laa ilaaha illa Allaah........................32Mlango Wa 6: Tafsiri Ya Tawhiyd Na Laa Ilaaha Illa Allaah.........................................38Mlango Wa 7: Kuvaa Cheni Na Uzi Na Mfano Wavyo Kwa Ajili Ya Kuzuia Balaa AuMadhara Ni Katika Shirki....................................................................................................44Mlango Wa 8: Yaliyokuja Katika Ruqyah Na Mahirizi..................................................48Mlango Wa 9: Mwenye Kutabaruku Kwa Mti Au Jiwe Na Mfano Wavyo.................54Mlango Wa 10: Yaliyokuja Katika Kuchinja Kwa Ajili Ya Asiyekuwa Allaah............59Mlango Wa 11: Hakuchinjwi Kwa Ajili Ya Allaah Mahali Ambapo KunachinjiwaKwa Ajili Ya Asiyekuwa Allaah. .......................................................................................63Mlango Wa 12: Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah Ni Katika Shirki...............66Mlango Wa 13: Kutafuta Kinga Kwa Asiyekuwa Allaah Ni Katika Shirki.................68Mlango Wa 14: Kutaka Msaada Kwa Asiyekuwa Allaah Au Kumuomba AsiyekuwaYeye Ni Katika Shirki........................................................................................................70Mlango Wa 15: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Je, wanawashirikisha (na Allaah) waleambao hawaumbi kitu na hali wao wameumbwa? Na wala hawawezi kuwanusuruna wala hawawezi kujinusuru nafsi zao”..........................................................................75Mlango Wa 16: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Mpaka itakapoondolewa khofu nyoyonimwao; watasema: “Amesema nini Mola wenu?” Watasema: (Amesema): “Ya haki”;Naye ni Al-’Aliyyul-Kabiyr” ..............................................................................................80Mlango Wa 17: Shafaa´ah (Uombezi)................................................................................85Mlango Wa 18: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Hakika wewe huwezi kumwongozaumpendaye; lakini Allaah Humwongoza Amtakaye, Naye A’lam (Anajua zaidi)waongokao”................................................................................................................... .........91Mlango Wa 19: Kuchupa Mipaka Kwa Watu Wema Ndio Lililopelekea KukufuruKwa Binadamu..................................................................................... .................................95Mlango Wa 20: Hukumu Ya Kuabudu Makaburi Au Kumuabudu Allaah KwenyeKaburi La Mtu Mwema. .......................................................................................... ...........101Mlango Wa 21: Yaliyokuja Ya Kuwa Kuchupa Mipaka Katika Makaburi Ya WatuWema Hupelekea Kuwa Masanamu Yanayoabudiwa Badala Ya Allaah..................106Mlango Wa 22: Himaya Ya Mustwafah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) KuihamiTawhiyd Na Kufunga Kila Njia Inayopelekea Katika Shirki......................................109

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

3

Mlango Wa 23: Yaliyokuja Ya Kwamba Baadhi Ya Watu Katika Ummah HuuWataabudu Masanamu.....................................................................................................112Mlango Wa 24: Yaliyokuja Kuhusu Uchawi. ................................................................119Mlango Wa 25: Ubainisho Wa Kitu Katika Aina Ya Uchawi......................................123Mlango Wa 26: Kuhusu Makuhani Na Mfano Wao.....................................................128Mlango Wa 27: Yaliyokuja Kuhusu An-Nushrah. .......................................................132Mlango Wa 28: Yaliyokuja Kuhusu Kuamini Mkosi...................................................136Mlango Wa 29: Yaliyokuja Kuhusu Unajimu. ..............................................................141Mlango Wa 30: Yaliyokuja Kuhusu Kuomba Kunyweshelezwa Kwa Sayari..........144Mlango Wa 31: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Na miongoni mwa watu wako wenyekuchukua asiyekuwa Allaah kuwa ni mungu mshirika (anaelingana na Allaah),wanawapenda kama mapenzi wanavyompenda Allaah”...........................................148Mlango Wa 32: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Hakika huyo ni shaytwaan anawakhofishamarafiki zake. Basi msiwakhofu, na nikhofuni Mimi mkiwa ni Waumini”..............153Mlango Wa 33: Kauli ya Allaah Ta´ala: “Na kwa Allaah Pekee tawakalini ikiwanyinyi ni Waumini” ...........................................................................................................158Mlango Wa 34: Kauli Ya Allaah Ta´ala: Je, wameaminisha na mipango ya Allaah?Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika...........161Mlango Wa 35: Kuwa Na Subira Kwa Yale Aliyoyakadiria Allaah Ni KatikaKumuamini Allaah........................................................................................................... ..164Mlango Wa 36: Yaliyokuja Kuhusu Riyaa.....................................................................167Mlango Wa 37: Ni Katika Shirki Mtu Kufanya ´Amali Kwa Kutaka Dunia.............170Mlango Wa 38: Mwenye Kuwatii Wanachuoni Na Watawala Katika KuharamishaAliyohalalisha Au Kuhalalisha Aliyoharamisha Allaah, Kawafanya Ni MiunguBadala Ya Allaah............................................................................................................ .....172Mlango Wa 39: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Je, huoni wale ambao wanadai kwambawao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako;wanataka wahukumiane kwa twaaghuwt na hali wameamrishwa wakanushe hiyo.Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali”................................................176Mlango Wa 40: Mwenye Kupinga Kitu Katika Majina Na Sifa Za Allaah................181Mlango Wa 41: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Wanazielewa neema za Allaah, kishawanazikanusha; na wengi wao ni makafiri” .................................................................185Mlango Wa 42: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Basi msimuwekee Allaah waliolingana naye(washirika) na hali ya kuwa nyinyi mnajua (kuwa Allaah Hana Anayelingananae)”....................................................................................... ...............................................188Mlango Wa 43: Yaliyokuja Kuhusu Yule Ambaye Hakuridhika Kuapa KwaAllaah....................................................................................................................................192Mlango Wa 44: Kauli “Akipenda Allaah Na Wewe” ...................................................187

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

4

Mlango Wa 45: Mwenye Kutukana Zama Kamtukana Allaah....................................198Mlango Wa 46: Kuitwa Qaadhi Wa Maqaadhi Na Mfano Wake................................201Mlango Wa 47: Kuheshimu Majina Ya Allaah Ta´ala Na Kubadili Jina Kwa Ajili YaHilo............................................................................................................................. ............204Mlango Wa 48: Mwenye Kufanyia Mzaha Kitu Kilichotajwa Ndani Yake Jina LaAllaah, Qur-aan Au Mtume.......................................................................................... .....206Mlango Wa 49: Yaliyokuja Kutokana Na Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”NaTunapomuonjesha Rahmah kutoka Kwetu baada ya dhara iliyomgusa, bila shakahusema: “Hii ni (kutokana na juhudi na elimu) yangu, na sidhani kama Saa(Qiyaamah) itasimama. Na nitakaporejeshwa kwa Mola wangu, hakika nina mazuriKwake.” Basi bila shaka Tutawabainishia wale waliokufuru yale waliyoyatenda, nabila shaka Tutawaonjesha adhabu nzito”........................................................................209Mlango Wa 50: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Lakini Anapowapa (mtoto mzima na)mwema, wanamfanyia (Allaah) washirika1 katika kile Alichowapa. Fata’aala-Allaahu (Ametukuka Allaah kwa Uluwwa) kutokana na yale yotewanayoshirikisha”......................................................................................... ......................214Mlango Wa 51: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Na Allaah Ana Asmaaul-Husnaa (MajinaMazuri kabisa), basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa (kwakuharibu utukufu, kukanusha, kugeuza maana, kushabahisha) katika MajinaYake”......................................................................................................................................217Mlango Wa 52: Hakusemwi As-Salaam (Amani) Iwe Juu Ya Allaah........................221Mlango Wa 53: Kauli “Ee Allaah! Nisamehe Ukitaka” ...............................................223Mlango Wa 54: Mtu Asiseme “Mja Wangu Au Kijakazi Wangu” .............................225Mlango Wa 55: Harudishwi Mwenye Kuomba Kwa Jina La Allaah.........................227Mlango Wa 56: Hakuombwi Kwa Uso Wa Allaah Isipokuwa Pepo.........................229Mlango Wa 57: Yaliyokuja Kuhusu “Lau...“ ................................................................230Mlango Wa 58: Makatazo Ya Kutukana Upepo...........................................................232Mlango Wa 59: Kauli Ya Allaah Ta´ala: ”Wakamdhania Allaah pasi na haki dhana yakijahili; wanasema: “Je, tuna amri yoyote sisi katika jambo hili?” Sema: “Hakikaamri yote ni ya Allaah” ................................................................................ ....................234Mlango Wa 60: Yaliyokuja Kwa Mwenye Kupinga Qadar.........................................238Mlango Wa 61: Yaliyokuja Kuhusu Watengeneza Picha.............................................242Mlango Wa 62: Yaliyokuja Kuhusu Kuapa Sana..........................................................248Mlango Wa 63: Yaliyokuja Katika Dhimma Ya Allaah Na Ya Mtume Wake (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam)...............................................................................................251

1 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa Aadam na Hawaa walimfanyia washirika katika utiifu na si katika´Ibaadah. Hii inaitwa Shirki ya utiifu ambayo ni Shirki ndogo.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

5

Mlango Wa 64: Yaliyokuja Kuhusu Kumuapia Allaah...............................................254Mlango Wa 65: Haombwi Allaah Kwa Viumbe Vyake...............................................256Mlango Wa 66: Yaliyokuja Kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) KuihamiTawhiyd Na Kuziba Njia Za Shirki.................................................................................258Mlango Wa 67: Yaliyokuja Katika Kauli Ya Allaah Ta´ala: “Na hawakumthaminiAllaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata (Mkononi Mwake)Siku ya Qiyaamah” .............................................................................................................260

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

6

Utangulizi wa mfasiri

Bismillaah. Himidi zote kamilifu zinamstahiki Allaah ( وسلمعلیھهللاصلى ) MmojaPekee Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake. Mwenye kukusudiwakwa haja zote asiyekuwa na mshirika wala mwenza katika Rubuubiyyah,Uluuhiyyah na Majina na Sifa Zake.

Nashahidilia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ilaAllaah Pekee, na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mja naMtume Wake wa Mwisho. Amma ba´ad:

Namhimidi Allaah ( وسلمعلیھهللاصلى ) kwa kuniwezesha kumaliza kazi hiiambayo ilinichukua muda na nguvu nyingi kidogo. Na hii ni Tafwiyq yaAllaah Pekee.

Lengo la kufasiri Kitaab-ut-Tawhiyd na Sharh yake, kwanza nilikuwanapenda kujinufaisha mwenyewe kielimu. Pili nilipoona umuhimu wakemkubwa, nikawa napendelea kheri hii isiishie kwangu mwenyewe, nikajiwana fikra ya kukifasiri na kukiweka katika mtandao ili wale wanaotumiaInternet wawe na usahali wa kuweza kukipata na kujinufaisha na waowaweze kuwafikishia wengine.

Makubwa na mambo muhimu niliyokutana nayo ndani ya kitabu hiki siwezikuyaeleza nikayamaliza, tutosheke na baadhi ya hizo kauli za maimamu nawanachuoni wakubwa tulizoweka hapo hichi kuhusu kitabu hiki.

Kama mtavyoona ndugu zangu katika imani, nimefasiri kitabu na Sharhufafanuzi wake. Lengo - kama nilivogusia hapo juu - ilikuwa ni kujinufaishamwenyewe, ndio nikaona nipendelee ndugu zangu kile ninachojipendeleakatika nafsi yangu. Nilipokuwa nasikiliza durusi za Sharh ya kitabu hichiiliyotolewa na Shaykh al-´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan (AllaahAmhifadhi) huku naandika Sharh kwa mukhtaswari, ndio ghafla nikawanimejiwa na fikra ya kuifanya Sharh kuwa ndefu kidogo huenda Allaah ( صلى

وسلمعلیھهللا ) Akajaalia ikaja kunufaisha Waislamu wengi. Hali ilikuwa namnahii. Kwa hiyo, mtu ataona kwa juu sikuandika jina la aliyekisherehesha kitabuna hilo ni kutokana na sababu niliyoitaja hapo juu kuwa nimefanya

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

7

mukhtaswari tu wa maneno ya Sharh. Kutokana na sababu hiyo nikaonakuwa itakuwa sio sahihi nikiandika kuwa kitabu kimeshereheshwa na ShaykhFawzaan kwa kuwa nimechukua baadhi ya sehemu tu ya maneno ya Shaykh,kutokana na ukubwa wa kazi ilivokuwa. Hata hivyo sehemu ya Sharhufafanuzi yote sikuweka maneno yangu bali ni maneno ya Shaykh tu, miminilichofanya ni kuyafupisha. Hali kadhalika, sehemu ya footnotes ambaponimeandika “Shaykh Fawzaan anasema” ni maneno ya Shaykh mwenyewe.Ama pengine pote ambapo nimeandika bila ya kuandika “Shaykh anasema”,hayo ni maneno yangu nimeweka kwa kutaka kuweka wazi zaidi nakumrahisishia ndugu msomaji. Nimefasiri milango yote ya kitabu isipokuwatu mlango wa 57 kwa kukosekana mkanda huo.

Napenda kutoa shukran zangu za dhati kwa mama Faatwimah bint Khaliyfahambaye yeye ndiye alikuwa karibu na mimi muda wote nilipokuwanakikifasiri kitabu hiki na isitoshe kunipa nguvu na subira. Kwa kweli,pengine yeye akaona ni dogo alilolifanya ila mimi naona ni kubwa na naombambele ya Allaah iwe hali kadhalika. Na namuomba Allaah Ajaalie wamamawengine wote Awafanye kama mama huyu ambaye lengo lake kubwa kwawatoto wake si jengine isipokuwa ni wawe wanachuoni waje kuihami Dini.Napenda pia kutoa shukran zangu kwa Ustadh wangu Abuu Bilaal ´Uthmaanbin Nu´umaan kwa mchango wake. Namuomba Allaah Awalipe malipomakubwa, wakiwemo wazazi wangu wawili na amlipe kila yule ambayeatakisambaza kitabu hiki na ajaalie ikawa ni sababu ya kuongoka na kuwa na´Aqiydah sahihi kuanzia familia yake nzima, mtaa wake mzima, jamii yakenzima na Ummah mzima wa Kiislamu. Na hilo kwa Allaah ni jepesi.

Tanbihi muhimu! Hichi ni kitabu cha kwanza kikubwa ambacho nafasiri. Namimi si mfaswaha hata kidogo wa lugha ya kiswahili. Hivyo kuna uwezekanomkubwa kukawa makosa mengi ya uandishi na udhaifu wa kilugha. Kwayeyote atakayeona hivyo, basi namuomba kwa ajili ya Allaah, kwa nia nzurina unyenyekevu anitanabahishe na nitakuwa mwenye kushukuru kwa hilo.

Wa Swalla Allaahu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihi wasallam.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

8

Kauli za maimamu na wanachuoni kuhusu “Kitaab-ut-Tawhiyd”

1) Kasema Shaykh Sulayman bin ´Abdillaah bin Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (d. 1233) – Allaah Amrehemu – kasema kuhusu ”Kitaab-ut-Tawhiyd” katika ”Taysiyr al-´Aziyz al-Hamiyd” (uk. 24):

”Ni kitabu cha kipekee katika maana yake, hakijatanguliwa huko kabla, nawala hakijafikiwa (na kitu kingine chochote kile) katika haki yake.”

2) Kasema Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Hassan bin Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (d. 1285) – Allaah Amrehemu - kasema:

”Kumekusanywa (ndani ya kitabu hichi) kwa mukhtaswari kheri zilizonyingi, na ndani yake kuna miongoni mwa dalili za Tawhiyd zinazoteshelezakwa yule ambaye Allaah Kamuwafikisha, na amebainisha ndani yake dalilikatika kuibainisha Shirki ambayo Haisamehi Allaah.”

3) Wanachuoni walikuwa wanausia kuhifadhi ”Kitaab-ut-Tawhiyd”.Miongoni mwao ni Shaykh ´Abdur-Rahman as-Sa´diy (d. 1376) – AllaahAmrehemu - kama ilivo katika ”Fataawaa as-Sa´diyyah (uk. 38).

4) Kasema Shaykh ´Abdullaah ad-Duwaysh (d. 1409) – Allaah Amrehemu -kasema:

”Kitaab-ut-Tawhiyd” kilichoandikwa na Imaam al-Mujaddiyd Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab. Allaah Amjaze kheri na thawabu.Kimeleta mambo mazuri katika maana yake na kuibainisha Tawhiyd, nayanayopingana nayo katika Shirki na kuikemea (hiyo Shirki).”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

9

5) Kahimiza Shaykh ´Abdul-Aziyz bin Baaz (d. 1420) – Allaah Amrehemu -juu ya kukihifadhi na kukiwekea umuhimu, pale aliposema:

”Nawausia ndugu zangu wanafunzi waitilie umuhimu Qur-aan na Sunnahkwa ukamilifu kwa vitabu vya ´Aqiydah na kuhifadhi (miongoni mwa vitabuvya Tawhiyd na ´Aqiydah) yale atayoweza mtu, kwa kuwa (vitabu hivyo)ndio msingi na khitimisho katika elimu ya Kitabu na Sunnah. Kwa mfano”Kitaab-ut-Tawhiyd” cha Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (AllaahAmrehemu).”

6) Kasema Shaykh ´Abdullaah al-Bassaam (d. 1423) – Allaah Amrehemu –Katika ”´Ulamaa Najdi” (1/149) kuhusu ”Kitaab-ut-Tawhiyd”:

”Ni katika vitabu vyenye thamani sana... ”

7) Kasema Shaykh Swaalih al-Fawzaan (Allaah Amhifadhi) katika kitabuchake ”I’aanat-ul-Mustafiyd Bisharhi Kitaab-it-Tawhyd” (1/18):

”Kitabu hichi ni katika vitabu vyenye thamani sana vilivyoandikwa katikamlango wa Tawhiyd, kwa kuwa kimejengeka juu ya Kitabu na Sunnah... ”

8) Kasema Shaykh Muqbil al-Waadi'iy (d. 1422) – Allaah Amrehemu - katikakitabu chake ”al-Muftarih fiy Ajwibah Ba´adhw As´ilah al-Musttwalah” (Uk.138):

”Na katika vitabu muhimu ambavyo asijitoshelezi navyo Muislamu (yaaniasivikose kabisa), ni kitabu ”Fath al-Majiyd Sharh ya Kitaab-ut-Tawhiyd”,”Kitab-ut-Tawhiyd” cha Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (AllaahAmrehemu).” Na kasema pia katika maregeleo yaliyotangulia (1/12):

”Ni katika vitabu vikubwa vya al-Imaam al-Mujaddiyd Shaykh Muhammadbin ´Abdil-Wahhaab.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

10

Mlango Wa 1

Kauli Yake (Ta´ala):

وندبعيإلا ل الإنسو الجن لقتا خمو

”Na Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu.” (ad-Dhaariyaat51:52)

Na Kauli Yake:

وا الطاغوتنبتاجو وا اللـهدباع ولا أنسر ةي كل أما فثنعب لقدو

“Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Mtume (awaamrishe watu wake)kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuwt (miungu yauongo).” (an-Nahl 15:32)

Na Kauli Yake:

وقضى ربك ألا تعبدوا إلا إياه وبالوالدين إحسانا يبلغن عندك الكبر أحدهما أو كلاهما فلا تقل لهما أف ولا تنهرهما وقل لهما إما ◌واخفض لهما جناح الذل من الرحمة وقل رب ارحمهما كما ربياني صغرياقولا كرميا

”Na Mola wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu (yeyote) isipokuwa YeyePekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wapoakifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, ‘Uff!(neno karaha hata kunena ‘Ah!’) Na wala usiwakemee; na waaambie manenoya heshima. Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme(kuomba): “Mola wangu! Warehemu (wazazi wangu wawili) kamawalivyonilea udogoni.” (Israa 17:23-24)

Na Kauli Yake:

واعبدوا اللـه ولا تشركوا به شيئا

“Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote.” (Nisaa 04:36)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

11

Na Kauli Yake:

كمليع كمبر مرا حل ما أتالوعقل ت ألا تشركوا به شيئا◌ ◌انسن إحيدالبالواو ولا تقتلوا أولادكم من إملاق◌ ◌ قكمزرن نحنماهإيو ◌طنا بما وهنم را ظهم شاحوا الفوبقرلا تو ولا تقتلوا النفس التي حرم اللـه إلا بالحق◌ كم تعقلونذلكم وصاكم به لعل◌

هدلغ أشبى يتح نسأح يي هيم إلا بالتتال اليوا مبقرلا تو ◌طسان بالقيزالمل وفوا الكيأوو لا نكلف نفسا إلا وسعها◌ ◌ مإذا قلتو فاعدلوا ولو كان ذا قربى وبعهد اللـه أوفوا◌ ـذا صراطي مستقيما فاتبعوهذلكم وصاكم به لعلكم تذكرون◌ أن هو ولا تتبعوا ◌

هبيلن سع بكم قفرل فتبالس ذلكم وصاكم به لعلكم تتقون◌

”Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Mola wenu kwenu.Kwamba: Msimshirikishe na chochote, na muwafanyie wema wazazi wawili,na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini. Sisi Tunakuruzukunipamoja nao. Na wala msikaribie fawaahish (machafu; zinaa, liwati n.k.) yaliyodhahiri na yaliyo siri. Na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah(kuiua) isipokuwa kwa haki. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayompate kutia akilini. Na wala msiikaribie mali ya yatima (kuila) isipokuwa kwanjia bora (ya kumtengenezea hicho chake) mpaka afikie kubalege. Na timizenikipimo na mizani kwa uadilifu. Hatukalifishi nafsi isipokuwa kwa wasaawake. Na mnaposema (katika kushuhudia) basi semeni kwa uadilifujapokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni Ahadi ya Allaah. Hivyo ndivyoAlivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kukumbuka (na kuwaidhika). “Nakwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate vijia(vinginevyo) vitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni(Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.” (al-An´aam 06:151-153)

Amesema Ibn Mas´uud:

“Mwenye kutaka kuona wasia wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) ambao Mtume kaweka muhuri wake, basi asome KauliYake (Ta´ala):

كمليع كمبر مرا حل ما أتالوعقل ت ألا تشركوا به شيئا◌

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

12

”Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Mola wenu kwenu.Kwamba: Msimshirikishe na chochote... ” hadi Kauli Yake (Ta´ala):

وهبعا فاتيمقتسي ماطرـذا ص أن هو

“Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni... ” (al-An´aam 06:151-153)

Na kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Nilikuwa nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu yapunda. Akaniuliza: “Ewe Mu´aadh! Je, unajua ni ipi haki ya Allaah juu wajana haki ya waja kwa Allaah?” Nikasema: “Allaah na Mtume Wake ndio wenyekujua.” Akasema: “Haki ya Allaah juu ya waja wamuabudu na walawasimshirikishe Yeye na chochote. Na haki ya waja kwa Allaah nikutomuadhibu yule ambaye hakumshirikisha Yeye na chochote.” Nikasema:“Ewe Mtume wa Allaah! Niwabashirie watu?” Akasema: “Usiwabashiriewakategemea hivyo.”

(Imepokelewa na al-Bukhaariy na Muslim)

Ufafanuzi:Hakika ´Aqiydah ya Tawhiyd ndio msingi wa Dini. Hayasihi matendo ya mtu wala ´Ibaadahya mja, na wala haokoki yeyote na Moto na kuingia Peponi isipokuwa akihakikisha Tawhiydna kaifanya ´Aqiydah yake kuwa sahihi. Baada ya mtu kuhakikisha Tawhiyd ndioatahitajika kuleta matendo mengine.

Na ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomtuma Mu´aad (RadhiyaAllaahu ´alayhi wa sallam) kitu cha kwanza alimwambia awalinganie ilikuwa ni Tawhiyd.Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Nimetumwa nipigane vita na watu mpaka waseme laa ilaaha illa Allaah hapana molaapasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, wakiisema imesalimika kwao damu yao namali yao... ”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

13

Hii ni dalili ya kwamba ´Aqiydah ya Tawhiyd ndio kitu cha kwanza mtu anatakiwa kukipaumuhimu kabla ya chengine chochote. Haki ndio haki ya Allaah kwa waja Wake.

Na kitabu hichi ni katika vitabu bora na muhimu sana kuhusiana na mada ya Tawhiyd, kwakuwa kimeegemea juu ya Kitabu na Sunnah. Katika kila mlango wa kitabu kaweka Aayahkatika Qur-aan, Hadiyth kutoka katika Sunnah Swahiyh, na maneno ya wanachuoniwaliobainisha maana ya Aayah na Hadiyth hizi. Kaenda kwa mtindo huu katika kila mlangomwanzo wa kitabu mpaka mwisho.

Katika kitabu hichi hakuna maneno au maoni ya fulani, hata mwandishi mwenyewehakujiwekea maneno yake mwenyewe. Isipokuwa ni Maneno ya Allaah na Maneno yaMtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanachuoni wa Ummah huu.

Kaanza kwa “Bismillaahi Rahmaani Rahiym” kwa kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) alipokuwa anaandika Risaalah zake anaanza kwa Bismillaahi Rahmaani Rahiym.Hali kadhalika alikuwa anaanza maneno yake pamoja na Maswahabah wake kwa kusemaBismillaahi Rahmaani Rahiym. Na kisichoanzwa kwa Bismillaahi Rahmaani Rahiymkinakuwa hakina baraka. Na Sulaymaan (´alayhis-Salaam) alipomwandikia malkia alianzakwa Bismillaahi Rahmaani Rahiym.

Hivyo, kuanza kwa Bismillaahi Rahmaani Rahiym katika mambo muhimu ya kheri;Khutbah, mawaidha, vitabu, barua, muhadhara n.k. ni jambo muhimu. Na ndio maanaAllaah Kaanza Nalo katika kila Suurah katika Qur-aan isipokuwa Suurat at-Tawbah. Amakatika maneno na mambo mabaya mtu asianze kwa neno hili. Na kuanzia hapa tunapatakujua, wale ambao katika vitabu vyao hawaanzi kwa Bismillaahi Rahmaani Rahiym nikwamba wamekhalifu Sunnah na wanaanza kama wanavyoanza wamagharibi.

Anaweza kuuliza mwenye kuuliza, kwa nini hakuanza kitabu chake kwa “Innal hamdahlillaah... “, jibu ni kwamba katosheleza kwa “Bismillaahi Rahmaani Rahiym”. Hakikainatosheleza katika kumsifu Allaah (Ta´ala) na inatosheleza kuanza nayo. Na mtu ikiwaataanza kwa “Bismillaahi... “ kisha akafuatisha kwa “Alhamdulillaahi Rabbil-´Alaamiyn... “inakuwa bora na kamili zaidi.

Na maana ya Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah (Ta´ala) kwa ´Ibaadah. Na kukipwekeshakitu ni kukifanya kuwa kimoja. Na Tawhiyd ni aina tatu:

1. Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah.

Kumpwekesha Allaah na kuamini kwamba Yeye Ndiye Muumba, Mwenye Kuruzuku,Mwenye Kuhuisha, Mwenye Kufisha na Mwenye Kuendesha mambo. Na Tawhiyd hii watuwote kukiwemo hata washirikina wameikubali. Na mtu hawezi kuwa Muislamu kwakukubali (kukiri) Tawhiyd hii peke yake.

2. Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

14

Kumpwekesha Allaah katika ´Ibaadah. Kusiombwe, kusiswaliwe, kusifungwe, kusihijiwe na´Ibaadah zingine zote isipokuwa iwe kwa ajili ya Allaah Pekee. Na Tawhiyd hii ndio ilikuwalengo la Mitume (´alayhimus-Salaam) kutumwa na vitabu Kuteremshwa na magomvi bainaya Mitume na washirikina. Walikubali aina ya kwanza ya Tawhiyd lakini hawakukubaliaina hii ya pili na ndio maana wakawa makafiri kwa kutokuacha ´Ibaadah ya asiyekuwaAllaah. Na hii ndio Tawhiyd ambayo wameikanusha watu wengi katika ardhi.

3. Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat.

Kumthibitishia Allaah yale Aliyojisifia Nafsi Yake, au aliyomthibitishia Mtume Wake(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Majina na Sifa Zake, bila ya kubadilisha maana,kukanusha maana, kuanisha maana na kufananisha. Kutokana na Kauli Yake (Ta´ala):

ليس كمثله شيء ◌ريصالب يعمالس وهو

“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye As-Samiy’ul-Baswiyr (Mwenye kusikiayote daima, Mwenye kuona yote daima).” (ash-Shuraa 42:11)

Na aina hii ya Tawhiyd wameithibitisha Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, na makundi menginewameikanusha kama Jahmiyyah, Mu´tazilah, Ashaa´irah na mengineyo. Wametofautiana tukatika kuikanusha. Ama Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wameithibitisha na kuiamini kamainavyostahiki.

Suurat adh-Dhaariyaat: Allaah Anasema Hakuwaumba majini na watu isipokuwa kwahekima ya kumuabudu Yeye, Aayah hii inafasiri neno Tawhiyd ya kwamba maana yake ni´Ibaadah.

Majini ni viumbe ambavyo hatuvioni lakini vipo, na yule anayepinga kuwepo kwa majinikwa vile hatuwaoni ni kafiri. Ni vitu vingi ambavyo tunaviamini lakini hatuvioni; kama vileakili, fikira, hisia na vitu vingine vingi tu ambavyo vipo lakini hatuvioni, hata hivyotunaviamini. Hivyo maana ya “waniabudu” maana yake ni wanipwekeshe. Na maana yakesio kukiri Rubuubiyyah kama wanavyosema Ahl-ul-Bid´ah.

Allaah Kaamrisha kumuabudu Yeye Pekee na kujiepusha na twaaghuut, maana ya twaaghuutni kila kinachoabudiwa badala ya Allaah; katika masanamu, makaburi na vingine vyote.Lakini anayeabudiwa na hayuko radhi kwa hilo haitwi kuwa ni twaaghuut, kama ´Iysa,Hasan na Husayn n.k. Lakini ile ´Ibaadah wanayofanya ndio inaitwa ´Ibaadah ya twaaghuut,yaani wanamuabudu Shaytwaan kwani yeye ndio kawaamrisha hilo. Baada ya kuamrishahaki ya Allaah (Ta´ala) Akaamrisha haki ya wazazi wawili, kwa kuwa hakuna mwenye hakizaidi na aliyekutendea wema baada ya Allaah isipokuwa ni wazazi wawili. Hivyo, haitoshimtu kumuabudu Allaah Pekee kisha mtu asijiepushe na twaaghuut. Ni lazima mtukujiepusha na twaaghuut.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

15

Ama maana ya neno ´Ibaadah – ni kama alivyosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, nineno lililokusanya kila Anachokipenda Allaah na Kukiridhia, katika matendo na kauli, zadhahiri na zilizojificha. Kama Swalah, Swawm, Zakaah, Hajj, kuamrisha mema na kukatazamabaya n.k. Mtu ajikurubishe kwa Allaah kwa yale Aliyoyawekea Shari´ah, ama yaleambayo hakuyawekea Shari´ah huitwa kuwa ni Bid´ah.

Katika Hadiyth ya Mu´aadh: Haki ya Allaah kwa waja Wake wamuabudu, na wala haitoshikumuabudu peke yake, bali wasimshirikishe na chochote. Kwa kuwa ´Ibaadah haiwi´Ibaadah isipokuwa mpaka iwe imesalimike na Shirki. ´Ibaadah ikichanganyika na Shirkikubwa, ´Ibaadah yote inaporomoka na kuharibika. Hali kadhalika ´Ibaadah haiwi ´Ibaadahisipokuwa mpaka iafikiane na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam). Lazima haya masharti mawili yapatikane. Na hii ndio maana ya laa ilaaha illa AllaahMuhammad Rasuulu Allaah. Na haki ya waja kwa Allaah ni kutomuadhibu yuleasiyemshirikisha Yeye na chochote. Na haki hii sio wajibu kwa Allaah, kwa kuwa Allaahhana haki yoyote iliyo ya wajibu Kwake kwa yeyote, isipokuwa hili ni kutokana na fadhilaZake (Subhaanahu wa Ta´ala). Mu´tazilah wao ndio wanaona kuwa ni haki ya wajibu kwaAllaah, ama Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanasema hapana. Watu wa Tawhiyd waliokuwana Tawhiyd pungufu, Akipenda Allaah Atawaadhibu kiasi cha madhambi yao waliyofanyana Akipenda Atawasamehe. Hata ikibidi kuingia Motoni, mwisho wao itakuwa Peponi.Allaah Atawatoa humo na kuwaingiza Peponi. Na kama alikuwa na Tawhiyd kamili,Atasalimika na kuingia humo Motoni kabisa na badala yake ataingia Peponi. Tofauti namadhehebu ya Khawaarij na Mu´tazilah, wao wanasema mtu wa Tawhiyd mwenyemadhambi makubwa chini ya Shirki atadumishwa Motoni milele. A´udhubi Allaah. AllaahAtukinge na madhehebu haya machafu na ya kipotofu.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Hekima ya kuumbwa majini na watu.

2. ‘Ibaadah maana yake ni Tawhiyd, kwani ndio mada kuu ya hoja (iliopo hapo juu) na ndiojambo walilogombana kwa ajili yake (Mitume na washirikina).

3. Yule ambaye haitekelezi, atakuwa hajamuabudu Allaah (Ta´ala). Katika hili kuna maanaya Kauli Yake (Ta´ala):

دبا أعون مابدع ملا أنتو“Na wala nyinyi si wenye kuabudu Yule Ninayemwabudu.” (al-Kaafiruun 109:03)

4. Hekima ya kutumwa Mitume (´alayhimus-Salaam)

5. Ujumbe wa Mitume wote (´alayhimus-Salaam) (wa Tawhiyd) umefikishwa kwa kilaUmmah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

16

6. Dini ya Mitume wote (´alayhimus-Salaam) ni moja.

7. Suala ambalo lina umuhimu mkubwa hapa ni kwamba kumuabudu Allaah hakufanyiki(hakusihi) bila ya kukanusha twaaghuut (miungu ya uongo). Na katika hili ndipo kunamaana ya Kauli Yake (Ta´ala):

بالطاغوت كفرن يفم

”Basi atakayemkanusha twaaghuwt (miungu ya uongo).” (al-Baqarah 02:256)

8. Neno “twaaghuut” limekusanya kwa ujumla kila kitu ambacho kinaabudiwa badala yaAllaah.

9. Salaf walichukulia kwamba Aayah tatu Muhkamaat2 katika Suurat al-An’aam ndio zenyeumuhimu mkubwa. Katika Aayah hizi ndani yake kuna mambo kumi, na jambo la kwanzani kukatazwa Shirk.

10. Aayah za Muhkamaat katika Suurat al-Israa na ndani yake kuna mambo kumi na nane.Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Kaanza kwa Kauli Yake:

ـها آخر فتقعد مذموما مخذولا لا تجعل مع اللـه إل

”Usifanye pamoja na Allaah ilaaha (mungu) mwengine, ukaja kushutumiwa na mwenyekutupiliwa mbali (Motoni).” (al-Israa 17:22)

Na Kamalizia kwa Kusema:

ـها آخر فتلقى في جهنم ملوما مدحوراولا تجعل مع الل ـه إل

”Na wala usifanye pamoja na Allaah ilaaha (mungu) mwengine ukaja kutupwa katika (Motowa) Jahannam hali ya kuwa mwenye kulaumiwa na kufukuziliwa mbali (ukawa mbali naRahma ya Allaah).” (al-Israa 17:39)

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Akatutanabahisha ukubwa wa masuala haya kwaKusema:

ةكمالح نم كبر كى إليحا أومم كذل

”Hayo ni miongoni mwa ambayo Amekuletea Wahy Mola wako (ee Muhammad صلى اهللا عليه وآله ”.katika Hikmah (khulqu, maadili na sifa njema) (وسلم (al-Israa 17:39)

11. Aayah ya Suurat an-Nisaa ambayo imeitwa: “Aayah yenye haki kumi” ambapo Allaah(Ta´ala) Kaanza kwa Kusema:

2 Zilizo wazi kabisa

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

17

واعبدوا اللـه ولا تشركوا به شيئا

“Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote.” (Nisaa 04:36)

12. Tanbihi ya wasia wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla yamauti yake.

13. Kujua haki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) juu yetu.

14. Kujua haki ya waja juu Yake (Allaah) ikiwa watatimiza haki Zake.

15. Jambo hili Maswahabah wengi walikuwa hawalijui.

16. Kuruhusu kuficha baadhi ya elimu kunapokuwa na maslahi (ya Kishari´ah).

17. Inapendekezeka kuwajulisha Waislamu khabari njema.

18. Khofu (ya watu) kutegemea tu wingi wa Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

19. Kauli ya mtu pindi anapoulizwa kitu asichokijua aseme: “Allaah na Mtume Wakewanajua zaidi”

20. Kujuzu kutoa baadhi ya elimu maalum kwa baadhi ya watu na asiitoe kwa wengine.

21. Unyenyekevu wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wa kupandamnyama pamoja na Swahabah nyuma yake.

22. Ni jambo linaruhusiwa kushirikiana kupanda mnyama (na mtu mwingine) ikiwa(mnyama) unaweza hilo.

23. Fadhila za Mu’adh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anhu)

24. Umuhimu mkubwa wa suala hili (la Tawhiyd)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

18

Mlango Wa 2

Fadhila Za Tawhiyd Na Madhambi Yanayosamehewa Kwayo

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

ـئك لهم الأمن وهم مهتدون الذين آمنوا ولم يلبسوا إميانهم بظلم أول

”Wale ambao wameamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma (yakumshirikisha Allaah). Hao ndio watakaopata amani nao ndio walioongoka."(al-An´aam 06 : 82)

Kutoka kwa ´Ubaadah bin Swaamit (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Kasema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):“Mwenye kushahidilia laa ilaaha illa Allaah wahdahu laa shariyka Lahu,3 wa annaMuhammad ´abduhu wa Rasuuluhu, hapana mola apasaye kuabudiwa kwa hakiisipokuwa Allaah, Mmoja na asiyekuwa na mshirika, na kwamba Muhammadni mja na Mtume Wake, na kwamba ´Iysa ni mja na Mtume Wake, na ni NenoLake4 Alilompelekea Maryam na roho iliyotoka Kwake,5 na [akashahidilia yakwamba] Pepo ni haki na Moto ni haki, basi Allaah Atamuingiza Peponi kwakufuatia ´amali zake [sawa bila kujali vovyote zitavyokuwa].”

(Wameipokea al-Bukhaariy na Muslim)

3 Shaykh Fawzaan anasema: ”Maana ya ”mwenye kushahidilia laa ilaaha illa Allaah, yaani 1) kuitamkakwa kujua manaa yake, 2) kuleta muqtadhwa wake na 3) kuifanyia kazi kimatendo. Lazimayapatikane masharti haya matatu.”4 Shaykh Fawzaan anasema: ”Neno hili ni lipi? Neno hili ni Kauli Yake Allaah: ”Kuwa! Na akawa”.Kwa kuwa ´Iysa (´alayhis-Salaam) Kaumbwa kwa Neno ”Kuwa na akawa.” Hii ndio maana ya ”NenoLake” ni kuwa alipatikana kwa Neno, na haina maana kuwa ´Iysa yeye ndiye neno. Kaitwa neno kwakuwa kapatikana kwa neno tofauti na watu wengine wao wanapatikana kupitia baba na mama.”5 Shaykh Fawzaan anasema: ”Roho iliyotoka Kwake”, hii haina maana kuwa ´Iysa katoka katika Dhatiya Allaah, hapana. Bali maana yake ni roho aliyopuliziwa kupitia Malaika Jibriyl (´alayhis-Salaam)akampulizia nayo Maryam (´alayhas-Salaam). Kama jinsi unavoweza kusema ”nguo hii imetoka kwaAllaah”, yaani Allaah ndiye Kaiumba nguo hii. Tazama pia Suurat al-Jaathiyah 45, Aayah ya 13ambapo Allaah Kasema: ”... kutoka Kwake”, yaani vyote vilivyomo mbinguni na ardhini vinatokakwa Allaah na Yeye Ndiye Kaviumba.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

19

´Itbaan (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kasema:

“Hakika ya Allaah Kamharamishia Moto mwenye kusema: “Laa ilaaha illaAllaah, hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah”akitafuta kwa hilo si jengine isipokuwa Uso wa Allaah.”

Abuu Sa´iyd al-Kudriy (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtumewa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Muusa (´alayhis-Salaam) alisema: “Ee Mola Wangu! Nifundishe kituambacho nitakukumbuka kwacho na kukuomba kwacho.” Akasema: “EeMuusa sema: “Laa ilaaha illa Allaah, hapana mola apasaye kuabudiwa kwa hakiisipokuwa Allaah.” Akasema: “Watu wote wanasema hili.” Akasema: “EeMuusa! Lau mbingu saba na vyote vilivyomo ndani yake na ardhi saba navyote vilivyomo ndani yake asiyekuwa Mimi vitawekwa kwenye kitangakimoja cha mzani, na “laa ilaaha illa Allaah, hapana mola apasaye kuabudiwakwa haki isipokuwa Allaah” ikawekwa kwenye kitanga kingine, basi “laailaaha illa Allaah, hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwaAllaah” ingevizidi uzito.”

(Kaipokea Ibn Hibbaan, na al-Haakim na kaisahihisha)

Na at-Tirmidhiy kapokea kutoka kwa Anas (Radhiya Allahu ´anhu) ambayeamesema, nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)akisema:

“Allaah (Ta´ala) Kasema: “Ewe binaadamu! Lau utanijia kwa madhambiyaliyojaa ardhi, kisha ukakutana na Mimi na hukunishirikisha Mimi nachochote, basi ningelikujia na msamaha unaofanana na kiasi na hivyo.”

Ufafanuzi:Mlango huu unabainisha fadhila za Tawhiyd na madhambi yanayofutwa kwa ajili yaTawhiyd. Baada ya Shaykh kubainisha uhakika wa Tawhiyd na maana sahihi ya Tawhiyd,ndio akawa ameweka mlango huu. Kabainisha kwanza maana sahihi ya Tawhiyd kisha ndio

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

20

akaweka fadhila zake hiyo Tawhiyd. Jambo hili linaonesha elimu na ufahamu aliyokuwanao Shaykh (Rahimahu Allaah).

Aayah ya Suurat al-An´aam: Aayah iliteremka kwa watu wa Ibraahiym (´alayhis-Salaam)waliokuwa wakiabudu nyota badala ya Allaah (´Azza wa Jalla). Allaah (Ta´ala) AkawaAmemtuma Mtume Wake Ibraahiym (´alayhis-Salaam) kuwalingania watu katika Tawhiydna kuwakataza Shirki. “Wale ambao wameamini”, yaani maana yake wamempwekesha. Namakusudio ya “dhulma” hapa ni Shirki. Na dhulma kama walivyosema wanachuoni ni ainatatu:

1. Dhulma kwa maana ya Shirki. Imeitwa dhulma kwa kuwa (mja) kaiweka ´Ibaadahmahali ambapo hapastahiki. Badala ya kumuabudu Allaah akenda kumuabuduasiyekuwa Allaah.

2. Mtu kufanya maasi ambayo ni chini ya Shirki. Kuiba, kunywa pombe, Zinaa namengineyo. Hii ni dhulma kwa kuwa mtu anaidhulumu nafsi yake kwakujisababishia kupata adhabu ya Allaah.

3. Mtu kumdhulumu mtu mwingine. Sawa iwe kwa kumchukulia mali yake, kumpiga,kuchukua haki yake na mengineyo.

Na aina ile ya kwanza Allaah Haisamehi kabisa. Aina ya pili, hii iko katika Matakwa yaAllaah, bi maana Allaah Akitaka Atamuadhibu mtu huyo na Akitaka Atamsamehe. Amaaina ya tatu Allaah Anaisamehe ikiwa mtu atatubia, kwa sharti ya mtu kumrudishia yuleuliyemdhulumu haki yake.

Maana ya laa ilaaha illa Allaah, ni hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwaAllaah. Ama ukisema maana yake ni “hapana mola isipokuwa Allaah”, huu ni upotofumkubwa. Lazima uongezee neno “kwa haki”. Kwa kuwa ukisema maana yake ni “hapanamola isipokuwa Allaah”, umefanya masanamu, makaburi, nyota na kila kinachoabudiwabadala ya Allaah umekifanya kuwa ni Allaah. Na maana ya “nashahidilia ya kwambaMuhammad ni mja wake... “, hapa kuna Radd kwa wale wanaochukulia sahali haki yake(´alayhis-Salaam). Ni mja wa Allaah – Radd kwa wale wanaopindukia mipaka kwake. Na niMtume wake – ni Radd kwa wale wanaokanusha Utume Wake. Hali kadhalika ´Iysa ni mjana Mtume wa Allaah (Ta´ala) ambaye kaumbwa bila ya baba. Ni mja wake – hapa kunaRadd kwa manaswara ambao wamemfanya ´Iysa ndio Allaah. Na ni Mtume wake – hii niRadd kwa mayahudi ambao wamekataa Utume wa Mtume ´Iysa (´alayhis-Salaam) nakumtuhumu mama yake (Maryam) kuwa alifanya Zinaa. Allaah Awaangamize. Na yuleanayemkanusha Mtume mmoja, basi kawakanusha wote. “Atamuingiza Peponi kwakufuatia ´amali zake”, hii ni Ahadi ya Allaah kwa watu wa Tawhiyd. Katika hili kunafadhila za Tawhiyd na kwamba Tawhiyd ndio sababu inayomfanya mtu kuingia Peponi.Nini maana ya “... kufuatia ´amali zake?” Wanachuoni wana kauli mbili kuhusu maanayake:

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

21

1. Atamuingiza Allaah Peponi hata kama atakuwa na madhambi chini ya Shirki. Hilohalitomkosesha kuingia Peponi, ima mwanzo wakati watu wataingia Peponi aumwisho wake.

2. Atamuingiza Allaah Peponi kwa kiasi cha ´amali zake. Kwa kuwa daraja za Peponiwatu wanaingia kwa kiasi cha ´amali zao. Daraja zinatofautia. Kuna ambazo ni za juuzaidi kuliko zingine.

Kwa yote haya kuna fadhila za Allaah, kuwa Allaah Atawaingiza Peponi waja wake waTawhiyd kwa kufuatia ´amali zao. Allaah Atawaingiza Peponi kwa sababu ya fadhila zao.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Wingi wa fadhila za Allaah.

2. Wingi wa thawabu za Tawhiyd kwa Allaah.

3. Pamoja na hivyo, Tawhiyd inafuta madhambi.

4. Tafsiri ya Aayah ya 82 iliyo katika Suurat al-A´naam.

5. Kuzingatia mambo matano yaliyotajwa katika Hadiyth ya ´Ubaadah (Radhiya Allaahu´anhu).

6. Ukijumuisha baina ya Hadiyth ya ´Ubaadah na ´Itbaan (Radhiya Allaahu ´anhumaa) nayaliyo baada yake, itakubainikia maana ya neno laa ilaaha illa Allaah na yatakubainikiamakosa ya waliodanganywa.

7. Tanbihi ya sharti inayopatikana katika Hadiyth ya ´Itbaan (Radhiya Allaahu ´anhu).6

8. Kuwa Mitume (´alayhimus-Salaam) walikuwa wakiitolea hoja kutanabahisha fadhila zalaa ilaaha illa Allaah.

9. Tanbihi ya uzito wake (laa ilaaha illa Allaah) kwa viumbe vyote, pamoja na kwamba wengiwanaoitamka mizani yao itakuwa khafifu.

10. Maandiko yanaonesha kuwa ardhi ni saba kama mbingu zilivo saba.

11. Ardhi saba na mbingu saba wamejaa viumbe ndani yake.

12. Uthibitisho wa Sifa za Allaah, tofauti na madai ya Ash´ariyyah.

6 Ya kwamba kutamka laa ilaaha illa Allaah haitoshi tu, bali inatakiwa mtu awe amefanya hivyo kwakutafuta Pepo Yake (Subhaanahu wa Ta´ala).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

22

13. Ukiifahamu Hadiyth ya Anas (Radhiya Allaahu ´anhu), basi utafahamu makusudio yakauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya ´Itbaan (Radhiya Allaahu´anhu):

“Hakika ya Allaah Kaharamishia Moto kwa mwenye kusema: “Laa ilaaha illa Allaah, hapanamola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah” akitafuta kwa hilo si jengineisipokuwa Uso wa Allaah.”

ya kwamba maana yake ni kuacha Shirki na hakuzingatiwi kuitamka tu kwenye ulimi.

14. Tafakari na uzingatie ´Iysa na Muhammad (´alayhimas-Swalaat was-Salaam) wotewawili ni waja wa Allaah na ni Mitume Wake.

15. Kujua kuwa ´Iysa (´alayhis-Salaam) ni Neno Lake Allaah.

16. Kujua kuwa ´Iysa (´alayhis-Salam) ni roho kutoka Kwake.

17. Kujua fadhila za kuamini Pepo na Moto.

18. Kujua maana ya kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “... kufuatia ´amali zake.”

19. Kujua kuwa mizani ina vitanga viwili.

20. Kujua maana ya kutajwa kwa “Uso” (wa Allaah).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

23

Mlango Wa 3

Mwenye Kuhakikisha Tawhiyd Ataingia Peponi Bila Hesabu

Kauli Yake Allaah (Ta´ala):

نيركشالم نم كي لمنيفا وح لـها لة قانتكان أم يماهرإن إب

”Hakika Ibraahiym alikuwa Imaam mtiifu kwa Allaah, haniyfaa (aliyejienguana dini potofu akaelemea Dini ya haki) na wala hakuwa miongoni mwawashirikina.” (an-Nahl 16:120)

Na Kasema (Ta´ala):

والذين هم بربهم لا يشركون

“Na wale ambao Mola wao, hawamshirikishi (na chochote).” (Muuminuun23:59)

Husayn bin ´Abdir-Rahmaan kasema:

“Nilikuwa kwa Sa´iyd bin Jubayr na akasema: “Ni nani kati yenu aliyeonanyota iliyorushwa jana?” Nikasema: “Mimi niliiona”, kisha nikasema kwambahaikuwa katika Swalah kwa kuwa nilidonolewa na nge.” Akasema: “Ulifanyanini?” Nikasema: “Nilitumia Ruqyah ili kujiponyesha.” Akasema: “Kipikilichokupelekea ufanye hivyo?” Nikasema: “Ni kutokana na Hadiythaliyotuelezea Sha´biy.” Nikasema: “Kawaeleza nini?” Nikasema: “Katuelezakutoka kwa Buraydah bin Huswayb ya kwamba kasema: “Hakuna Ruqyahisipokuwa kwa kupatwa na kijicho au kudonolewa.”7 Nikasema [Sa´iyd binJubayr]: “Amefanya vizuri kusitisha alichokisikia.8 Lakini katuhadithia Ibn´Abbaas, ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yakuwa kasema: “Ummah zote zilipitishwa mbele yangu, nikamuona Mtume

7 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hii haina maana kwamba Ruqyah inafanywa kwa mambo haya mawilipeke yake, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema hivi kwa kuonesha msisitizo wamambo haya mawili tu na umuhimu wake. Lakini mtu anaweza kufanya Ruqyah kwa mambomengine.”8 Yaani amefanya vizuri kuelezea kwa ujuzi kuliko angefanya hilo kwa ujinga.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

24

akiwa na kundi dogo la watu, na Mtume akiwa na mtu mmoja au wawili, naMtume akiwa hana mtu yeyote.9 Kisha nikaonyeshwa idadi kubwa ya watuniliodhania ni katika Ummah wangu, lakini nikaambiwa: “Huyo ni Muusa nawatu wake.” Kisha nikatazama nikaona kundi kubwa, ambalo nikaambiwa:“Hawa ni watu wako, miongoni mwao ni watu elfu sabiini watakaoingiaPeponi bila ya kufanyiwa hesabu wala adhabu.” Kisha Mtume (SwallaAllaahu 'alayhi wa sallam) akaondoka kwenda nyumbani kwake na nyumayake watu wakaanza kujadiliana ni nani hao watakaoweza kuwa? Baadhi yaowakasema: “Pengine ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu'alayhi wa sallam).” Na baadhi yao wengine wakasema: “Pengine ni walewaliozaliwa katika Uislamu na hawakumshirikisha Allaah kwa chochote.”Walipokuwa wakijadiliana, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)akatoka na kuja na wakamwambia (waliyokuwa wakiyajadili). Akasema: “Niwale ambao wasiojitibu kwa Ruqyah,10 wala kujichoma chuma cha moto, walahawaamini rajua nzuri na mbaya, bali wanamtegemea Mola Wao (Pekee).”‘Ukkaashah bin Mihswan (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliposikia alisimamaakasema: “Muombe Allaah Anijaalie kuwa mmoja wao.” Akasema (SwallaAllaahu 'alayhi wa sallam): “Wewe ni katika wao.” Kisha akasimama mtumwengine na akasema: “Muombe Allaah Anijaalie kuwa mmoja wao”.Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam): “Amekutangulia ´Ukkaashah.”11

9 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hii ni dalili kuonesha kuwa wingi sio hoja, kinachotazamwa nakuzingatiwa ni haki. Na wala hawazingatiwi wingi wa waliyoikhalifu hiyo haki.”10 Shaykh Fawzaan anasema: “Hawa ni wale ambao hawawaombi watu kuwasomea Ruqyah. Kwanini? Kwa kuwa kuwaomba watu wa kusomee Ruqyah kuna udhalili, na huku ni kutokana nakumtegemea kwao Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ni katika ukamilifu wa Tawhiyd.Maswahabah walikuwa namna, mtu alikuwa hata hawezi kumuomba mwenzake msaada wakupanda au kuteremka katika mpando kutokana na udhalili na upungufu wa Tawhiyd alivokuwaanaona kuwaomba watu. Ama mtu kujisomea mwenyewe Ruqyah au kusomea wengine, hilikalifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa ndio as-Sabiquun, ambao wamefanyamambo ya wajibu na mustahabah, na wameacha mambo ya haramu na ya makruhu na baadhi yamambo mubaahah (yanayoruhusiwa). Hawa ndio watu watakaoingia Pepo bila ya hesabu walaadhabu.”11 Shaykh Fawzaan anasema: “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kamwambia ´Ukkaashahkuwa yeye ni katika wao kutokana na daraja na manzilah yake aliyokuwa anaijua kwake. Na´Ukkaashah alikufa Shahidi. Ama mtu huyu wa pili kamwambia kuwa ´Ukkaashah kamtangulia kwakujua kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mtu huyu hastahiki manzilah hii. Hakumwambiahapana wewe hustahiki, kutokana na tabia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilivyokuwanzuri.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

25

Ufafanuzi:Maana ya kuhakikisha Tawhiyd ni kuitakasa na kila sampuli ya Shirki, sawa Shirki kubwana ndogo, pamoja na Bid´ah na maasi. Huku ndio kuhakikisha Tawhiyd.

Ama al-Muwahhid ni yule ambaye kasalimika na Shirki. Inaweza kuwa hakusalimika nabaadhi ya maasi, Shirki ndogo kwa kuwa pengine haijui, lakini akawa hakufikia katikadaraja ya waliyoihakikisha Tawhiyd. Muwahhiduun wako mafungu mawili:

1. Muwahhid.

Huyu ni yule aliyempwekesha Allaah (Ta´ala) na kasamilika na Shirki, lakini anaweza kuwahakusalimika na maasi na baadhi ya mambo anayoenda kinyume yaliyo chini ya Shirki(kubwa).

2. Anayeihakikisha Tawhiyd.

Hii ndio daraja ya juu kabisa.

Hadiyth ya Husayn: Hapa kuna dalili ya kwamba Salaf walikuwa hawafanyi kitu ila kwakupata dalili katika Kitabu au Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam). Kuna dalili vile vile ya kuwa dawa haijuzu isipokuwa kwa yale yaliyotolea dalilikutoka katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam). Ama kuwaendea wachawi, maddajjaal, wanga, makuhani na waongo ili kuwaombadawa, hili ni haramu, na inaweza kuwa Shirki kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu. Ikiwamtu atawachinjia badala ya Allaah, akawaomba badala ya Allaah n.k., anatoka katikaUislamu. Ni wajibu kwa Muislamu awe makini sana kwa mambo haya na wala asijitibuisipokuwa kwa kitu ambacho Allaah Kakiruhusu. Mtu kujitibu mwenyewe kwa Ruqyahwanachuoni wana kauli zifuatazo:

- Kuna ambao wanaona kuwa ni mubaahah (inaruhusiwa).

- Kuna ambao wanaona kuwa ni mustahabah (imependekezwa).

Kwa hali yoyote, sio jambo la haramu na wala halipunguzi Tawhiyd. Kwa kauli ya Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah Hakuteremsha maradhi yoyote isipokuwa Kateremsha dawa yake.”

na:

“Jitibuni enyi waja wa Allaah na wala msijitibu kwa haramu.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

26

Dawa ikiwa ni mubaahah, hakuna neno kujitibu nayo. Aina ya pili ya dawa ni dawa yamakruhu, hii ni dawa ambayo mpaka uwaombe watu. Hii ni dawa makruhu. Na kujitibu –sawa ikiwa mubaahah, mustahaabah au wajibu – hili halipunguzi kumtegemea Allaah.Maana kuna baadhi ya watu wanasema kuwa mtu akijitibu anakuwa hamtegemei Allaah.Hapana si sahihi. Kufanya sababu zinazoruhusiwa halipingani na kumtegemea Allaah.Mambo ambayo yanapingana na kumtegemea Allaah ni kufanya sababu ambazo ni zaharamu au makruhu. Katika Hadiyth hii kubwa tunapata dalili ya mambo yafuatayo:

- Kujuzu kwa Ruqyah kwa kupatwa na kijicho na kudonolewa.

- Fadhila za Muusa (´alayhis-Salaam) na watu wake.

- Hima ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) kwa elimu.

- Umakruhu wa kuwaomba watu, na kuwa kuwaomba watu kuna upungufu waTawhiyd. Ama kuacha kuwaomba kuna ukamilifu wa Tawhiyd.

- Kijicho kipo na ni haki, na kinatibiwa kwa Ruqyah.

- Ukweli wa Risaalah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam),kwani ´Ukkaashah ni kweli aliuawa Shahidi.

- Dalili kuwa atayehakikisha Tawhiyd ataingia Peponi bila ya hesabu wala adhabu.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Watu wamegawanyika daraja mbali mbali katika Tawhiyd.

2. Ni nini maana ya “kuhakikisha Tawhiyd”.

3. Allaah Kumsifu Kwake Ibraahiym (´alayhis-Salaam) kwa kutokuwa kwake miongonimwa washirikina.

4. Allaah Kuwasifu Kwake mawalii wengine kwa kusalimika kwao na Shirki.

5. Kule kuacha Ruqyah na kujichoma chuma cha moto ni katika kuhakikisha Tawhiyd.

6. Kuwa na sifa hizi ni Tawakkul kumtegemea Allaah.

7. Maarifa ya Maswahabah ya kina kujua kwao kuwa hawatofikia hilo isipokuwa mpakakwa ´amali.

8. Hili linaonesha bidii waliokuwa nayo (Maswahabah) katika kufanya kheri.

9. Fadhila za Ummah huu wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

27

10. Fadhila za watu wa Muusa (´alayhis-Salaam).

11. Ummah zote kupitishwa mbele yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

12. Kila Ummah utafufuliwa kivyake ukiwa pamoja na Mtume wake.

13. Uchache wa watu waliowaitikia Mitume (´alayhimus-Salaam).

14. Mtume ambaye hakuitikiwa na yeyote, atakuja (Siku ya Qiyaamah) akiwa peke yake.

15. Matunda ya ujuzi huu, nayo ni mtu kutokudanganyika na idadi ya wingi na kutokatatamaa na idadi ya udogo.

16. Ruhusa ya kutumia Ruqyah kwa kupatwa na kijicho na kudonolewa.

17. Elimu ya kina ya Salaf kwa Hadiyth: “Amefanya vizuri kusitisha alichokisikia.12 Lakinikadhaa na kadhaa... “, kinachopata kujulikana hapa ni kwamba Hadiyth ile ya kwanzahaipingani na ya pili.

18. Kujiepusha kwa Salaf kumsifu mtu (kwa mambo) asiyokuwa nayo.

19. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “´Ukkaashah, wewe ni katika wao... “ nialama katika alama za Utume.

20. Fadhila za ´Ukkaashah (Radhiya Allaahu ´anhu).

21. Kujuzu kutumia Ma´ariyd.13

23. Uzuri wa tabia yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

12 Yaani amefanya vizuri kuelezea kwa ujuzi kuliko angefanya hilo kwa ujinga.13 Yaani ni kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia yule mtuambaye alimuomba amuombee na yeye kwa Allaah Amjaalie katika wao. Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) akasema: “Amekutangulia ´Ukkaashah”. Ni dalili ya kujuzu kutumia Ma´ariyd,kusema maelezo ya wazi kwa njia au namna fulani, huku unamaanisha maana ya mbali au maananyingine.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

28

Mlango Wa 4

Kuiogopa Shirki

Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):

إن اللـه لا يغفر أن يشرك به ويغفر ما دون ذلك لمن يشاء

”Hakika Allaah Hasamehi kushirikishwa; lakini Anasamehe yasiyokuwa hayokwa Amtakae.” (Nisaa 04:48)

Na Kasema al-Khaliyl Ibraahiym (´alayhis-Salaam):

امنالأص دبعأن ن نيبني وبناجو

“Na Uniepushe na wanangu kuabudu masanamu.” (Ibraahiym 14:35)

Na imepokelewa Hadiyth ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kasema:

“Kikubwa ninachokikhofia kwenu ni Shirki ndogo.” Akaulizwa ni ipi?Akasema: “Ni Riyaa.”

Na Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Atakayekufa naye anamshirikisha Allaah na chochote ataingia Motoni.”

(Kaipokea al-Bukhaariy)

Muslim kapokea kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwambaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Mtu ambaye atakutana na Allaah naye hamshirikishi na chochote ataingiaPeponi, na atakayekutana Naye akiwa ni mwenye kumshirikisha na chochoteataingia Motoni.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

29

Ufafanuzi:Mlango huu unazungumzia Muislamu anapaswa kuigopa Shirki na wala asiwe ni mwenyekujiamini nafsi yake. Kwa kuwa anaweza kuteleza wakati wowote ilimradi bado yu hai,khaswa pale ambapo mtu atakuwa hajui uhakika wa Tawhiyd, yanayokwenda kinyume naTawhiyd ambayo ni Shirki, na yale waliyokuwemo watu kabla ya Uislamu. Na hapa ndiotunaona umuhimu mkubwa wa mtu kujifunza Dini yake na khaswa Tawhiyd. Na ndiomaana Shaykh kauleta mlango huu baada ya kuieleza na kuibainisha vizuri Tawhiyd, kishabaada ya hilo akaleta mlango wa fadhila za Tawhiyd hiyo na yule atakayeihakikisha, kishabaada ya yote haya ndio akaleta mlango huu kuhusu kuiogopa Shirki ambayo inakwendakinyume na Tawhiyd hiyo ambayo kaieleza huko mwanzo ili mtu aweze kujiepusha nayohiyo Shirki. Kwa kuwa mtu ikiwa haujui uhakika wa Shirki, kwanza mtu hawezi kuigopa nakwake itakuwa sahali sana kutumbukia humo wakati wowote. Lakini badala yake ikiwa mtuatasoma, akaijua vizuri Tawhiyd na Shirki, atakuwa mwenye kuifanyia kazi Tawhiyd nakuiogopa Shirki ukweli wa kuiogopa.

Aayah ya an-Nisaa: Allaah Anasema kuwa Hasamehi kushirikishwa na chochote. Hili nikuhusu yule ambaye kafa katika Shirki. Na katika Aayah nyingine Anasem:

ارالن اهأومة ونالج هليع اللـه مرح فقد باللـه ركشن يم هإن وما للظالمني من أنصار◌

”(Kwani) Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah,na makazi yake yatakuwa ni Motoni. Na madhalimu hawatopata mwenye kunusuruyeyote.” (al-Maaidah 05:72)

Mshirikina Kaharamishiwa Pepo na Atadumishwa Motoni milele. Hapa kuna khatari yaShirki. Hali ikishakuwa ni hivyo, ni wajibu kwa mtu aiogope. Binaadamu ni kiumbe dhaifu,na nyoyo za waja ziko baina ya Vidole Viwili katika Vidole vya Ar-Rahmaan, AnaziendeshaApendavyo.

Na maana ya Shirki, ni kumfanyia ´Ibaadah asiyekuwa Allaah, sawa iwe ni ´Ibaadah ya ainayoyote ile. Na maana yake si kama wanavyosema wapotofu na washirikina kwamba nikuitakidi ya kwamba kuna mwingine anayeshirikiana pamoja na Allaah katika Kuumba,Kuruzuku, Kuhuisha, Kufisha na Kuendesha mambo, yaani katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Subhaana Allaah! Hata washirikina wa mwanzo hawakuipinga aina hii yaTawhiyd. Walikuwa wakiiamini, lakini hata hivyo haikuwaingiza katika Uislamu.

Hivyo, Shirki ndio dhambi kubwa na Allaah Haisamehi Shirki na Kamuharamishia mwenyenayo Pepo. Ama madhambi mengine yote chini ya Shirki, mtu yuko chini ya Matakwa ya

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

30

Allaah. Akitaka Allaah Atamsamehe na kumuingiza Peponi bila ya kumuadhibu, na AkitakaAtamuadhibu kiasi cha madhambi yake na mwishoni Atamtoa na kumuingiza Peponi.

Aayah ya Ibraahiym: Hapa kipenzi cha Allaah, Ibraahiym (´alayhis-Salaam) anakhofiakuabudu masanamu ambaye alivunja masanamu na akawekwa katika moto kwa ajili yahayo masanamu, lakini pamoja na hivo anaikhofia nafsi yake kuabudu masanamu. Hapakuna funzo la kwamba mtu hatakiwi kuiamini nafsi yake, bila kujali elimu na uchaji Allaahkiasi gani ataofikia, asijiaminii nafsi yake kamwe. Kujiaminia ni dalili ya kiburi. AllaahAtukinge.

Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anawaambia Maswahabah wake kuwakikubwa anachokikhofia kwao ni Shirki ndogo pamoja na kuwa Maswahabah walikuwawameshakuwa na elimu ya kutosha na wameshakuwa madhubuti katika Dini. Shirki kubwamuumini anaweza kusalimika nayo, akawa hatochinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah,hatomsujudia asiyekuwa Allaah n.k., ama Shirki ndogo isiyomtoa mtu katika Uislamumuumini anaweza kutumbukia humo na ndio maana Mtume (´alayhis-Salaam) akasemaanaikhofia kwa Maswahabah wake.

Hadiyth ya Ibn Mas´uud: Hapa neno lake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) “...chochote” inajumuisha Shirki zote, sawa kubwa na ndogo. Hii ni Ahadi ya Allaah (Ta´ala)kama ambavyo Kawaahidi waja wake ikiwa hawatomshirikisha na chochote AtawaingizaPeponi. Hivyo inatakiwa kwa Muislamu aigope Shirki na ajiepushe nayo mbali sawa Shirkikubwa na ndogo. Na khaswa pale ambapo Shirki inakuwa nyingi, inatakiwa mtuatahadhari na aiogope sana.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Kuigopa Shirki.

2. Riyaa ni katika Shirki.

3. Riyaa ni katika Shirki ndogo.

4. Kutumbukia katika Riyaa ni kitu kikubwa kinachokhofiwa kwa watu wema.

5. Ukaribu wa Pepo na Moto.

6. Ujumuishaji wa ukaribu wa Pepo na Moto umetajwa katika Hadiyth moja kwa ´amalimoja inayokaribiana kisura.

7. Atakayekutana Naye hamshirikishi na chochote ataingia Peponi. Na atakayekutana Nayeanamshirikisha na chochote ataingia Motoni, hata kama itakuwa ni katika watuwanaomuabudu Allaah sana.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

31

8. Suala kubwa al-Khaliyl (Ibraahiym) akijiombea Du´aa yeye na wanawe kutumbukia katika´Ibaadah ya kuabudu masanamu.

9. Kukiri kwake (´alayhis-Salaam) hali ya wengi walivyotumbukia katika ´Ibaadah yakuabudu masanamu kwa kauli yake:

ريكث للنأض نهب إناسرالن نا م

“Mola wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza wengi sana katika watu.” (Ibraahiym14:36)

10. Tafsiri ya laa ilaaha illa Allaah kama alivyosema al-Bukhaariy katika Swahiyh yake.

11. Fadhila za mwenye kusalimika na Shirki.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

32

Mlango Wa 5

Kulingania Katika Shahaadat An Laa ilaaha illa Allaah

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

و إلى اللـهعي أدبيلس هـذ قل ه على بصرية أنا ومن اتبعني◌ ◌نيركشالمنا ما أنمو ان اللـهحبسو

”Sema: “Hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah, juu ya baswiyrah (ujuzi,umaizi) mimi na anayenifuata. Na Subhaana Allaah (Ametakasika Allaah),nami si miongoni mwa washirikina”.” (Yuusuf 10:108)

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kapokea ya kwamba Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipomtuma Mu´aadh Yemen.Akamwambia:

“Hakika wewe unawaendea watu katika Ahl-ul-Kitaab,14 basi iwe kitu chakwanza utakachowalingania kwacho “hapana mola apasaye kuabudiwa kwahaki isipokuwa Allaah.”

Na katika upokezi mwingine:

“... wampwekeshe Allaah Pekee. Ikiwa watakutii kwa hilo basi wafundishe yakwamba Allaah Kawafaradhishia juu yao Swalah tano kila mchana na usiku,ikiwa watakutii kwa hilo wafundishe ya kwamba Allaah Kafaradhisha juu yaoSwadaqah [Zakaah] itayochukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupewamafakiri wao, ikiwa watakutii kwa hilo tahadhari na kuwachukulia mali yao.Na iogope Du´aa ya mwenye kudhulumiwa, kwani hakika hakuna baina yakena baina ya Allaah kizuizi.”

(Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

14 Shaykh Fawzaan anasema: “Makusudio ya Ahl-ul-Kitaab ni mayahudi na manaswara, wameitwahivi kwa kuwa Allaah Kawatumia vitabu; Tawrat na Injiyl.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

33

Wapokezi wote wawili hawa wamepokea kutoka kwa Sahl bin Sa´d (RadhiyaAllaahu ´anhu), ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) kasema siku ya Khaybar:

“Kuna mtu nitampa bendera kesho, ni mtu anampenda Allaah na MtumeWake, na Allaah na Mtume Wake wanampenda. Allaah Atafungua mji kwamikono yake. Wakawa watu wanazungumza usiku ule: “Atampa nayo nani?”Ilipofika asubuhi, wakaamkia mapema kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) kila mmoja akitaraji atapewa nayo. Akasema: “Yuko wapi ´Aliybin Abiy Twaalib?” Akaambiwa: “Ni mgonjwa wa macho.” Akasema:“Nileteeni nae.” Akaletewa nae, Mtume akamtemea mate machoni mwake naakamuombea Du´aa, akapona papo hapo utadhani ya kwamba hakuwa naugonjwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akampa bendera nakusema:

“Nenda zako taratibu na kwa upole mpaka ufike katikati yao, kishauwalinganie katika Uislamu na uwaeleze yaliyo ya wajibu juu yao katika hakiya Allaah. Naapa kwa Allaah, lau Allaah Atamuongoza mtu mmoja kupitiakwako ni bora kwako kuliko ngamia wekundu”.”

Ufafanuzi:Mnasaba wa kuweka mlango huu ukilinganisha na yaliyo kabla yake itakudhihirikia wazikabisa sababu gani. Katika milango iliyopita mlango wa kwanza, kataja kuijua Tawhiyd,mlango wa pili kataja fadhila za Tawhiyd, mlango wa tatu kataja fadhila za mwenyekuihakikisha Tawhiyd, mlango wa nne kataja yanayoivunja Tawhiyd nayo ni Shirki; ikiwamwanafunzi kasoma kwa mazingatio makubwa milango hii tuliyoitaja na akaijua vizuri,jambo la kufuatia itakuwa kishakuwa tayari sasa kusimama bara bara kulingania kufanyaDa´wah katika Dini ya Allaah (´Azza wa Jalla). Kwa kuwa haijuzu kwa mtu atapojua kitu –khaswa katika mambo ya Tawhiyd na ´Aqiydah - akabaki nacho yeye mwenyewe, hapana.Yule atakayejua kitu ni lazima akieneze na awalinganie watu kwacho, kwani Ummah huu niUmmah wa Da´wah kama Alivyosema Allaah (Ta´ala). Leo miji mingi ya Waislamu imejaaShirki na kwa masikitiko makubwa Waislamu wameiikalia kimya. Hii ni khatari kubwaimekumba Ummah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

34

Aayah ya Suurat Yuunus: “... nalingania kwa Allaah”, Shaykh (Rahimahu Allaah) anasemakuwa kuna tanbihi ya kuwa na Ikhlaasw. Kwani kuna baadhi ya watu wanalingania kwamaslahi yao wenyewe. Mtu anapolingania kwa Allaah Anatakiwa asitafute jengine zaidiisipokuwa Uso wa Allaah. “... kwa ujuzi”, hii ni dalili si kila mtu anafaa kulingania kwaAllaah, inatakiwa mtu awe na elimu kabla ya kuanza kulingania. Baadhi ya Madu´aat(walinganiaji) wa leo hawana elimu, isipokuwa tu wana ufaswaha wa maneno lakini kuhusuelimu hawana kabisa. Wanapoulizwa masuala madogo kabisa ya kielimu hawajui. “... namisi miongoni mwa washirikina”, hapa kuna uwajibu wa anayelingania kwa Allaah ajiwekembali na washirikina. Ama wale wanaosema acheni ´Aqiydah za watu, sisi tunachotaka tu niUmoja na sote tukusanyike, sawa awe ni Suufiy, Qubuuriy,15 Jahmiy, Khaarijiy hatunanongo yoyote kwao, tunachotaka waje kushirikiana na wawe na sisi, hii sio Da´wah kwaAllaah. Manhaj ya Da´wah iko wazi na masharti yake yako wazi.

Hadiyth ya Mu´aadh kutumwa Yemen, katika Hadiyth hii kuna dalili ya kuifanyia kazikhabar al-Waahid khabari za mtu mmoja, na sio lazima (wapokezi) wawe watu wengi katikamambo ya misingi ya Dini kama wanavyosema Ahl-ul-Kalaam na Ahl-ul-Bid´ah. Wanasemamambo ya misingi ya Dini ni lazima khabari zake ziwe zimekuja kwa njia nyingi, Mtume(´alayhis-Salaam) kamtuma Mu´aadh Yemen peke yake akafunze watu Tawhiyd jamboambalo linatolea dalili kuwa Mtume (´alayhis-Salaam) alikuwa anakubali khabari za mtummoja katika mambo ya misingi ya Dini. Na hakuwa (´alayhis-Swalaat was-Salaam)akiwatuma Maswahabah wake kikundi, bali alikuwa anawatuma mmoja mmoja, kamaalivyomtuma ´Aliy pia, na Abuu ´Ubayd bin Jarraah na wengine wengi.

“... iwe kitu cha kwanza utachowalingania kwacho laa ilaaha illa Allaah”, hapa kuna dalilimlinganiaji anapaswa kuanza kuwalingania watu katika Tawhiyd na kuacha Shirki kabla yakitu kingine chochote. Kwa kuwa ´Ibaadah zingine zote hazisihi ikiwa mtu hakuihakikishaTawhiyd. Tofauti na Madu´aat wengi wa leo wameyapa umuhimu mambo mengine kabla yaTawhiyd, si hivyo tu bali Tawhiyd hawaitaji kamwe kana kwamba hata haipo. AllaahAtukinge. Kila Mtume kitu cha kwanza alichokuwa anaanza nacho ni kuwalingania watukatika Tawhiyd. Na katika upokezi mwingine “... wampwekeshhe Allaah”, Shaykh kawekaupokezi huu kwa kuwa unafasiri maana ya laa ilaaha illa Allaah. Katika Hadiyth hii (yaMu´aadh) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kataja nguzo tatu peke yake, na walahakutaja Swawm na Hajj, kwa nini? Jibu sahihi ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) kaishia katika nguzo kubwa ambazo ni za msingi, anauwiwa kwazo yuleanayeziacha. Nayo ni Shahaadah mbili, Swalah na Zakaah. Anasema Allaah (Ta´ala):

رصاحو مذوهخو موهمدتجث ويح نيركشلوا المفاقت مرالح رهالأش لخفإذا انسدصركل م موا لهداقعو موه فإن تابوا وأقاموا الصلاة وآتوا الزكاة فخلوا ◌مبيلهس

”Itapomalizika miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, nawachukueni (mateka) na wahusuruni, na wakalieni katika kila sehemu ya uvamizi. (Lakini)

15 Mwabudu kaburi

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

35

Wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi iacheni njia yao(waachieni).” (at-Tawbah 09:05)

“Wakitubu”, yaani wakishahidilia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa hakiisipokuwa Allaah. Katika Aayah hii Allaah Kataja nguzo ambazo makafiri wanatakiwakuuwiwa kwa ajili yazo, nazo ni Shahaadah mbili, Swalah na Zakaah.

Na isitoshe, hizi ni nguzo ambazo ni za dhahiri. Ama Swamw ni nguzo ambayo imejifichaiko baina ya mja na Allaah. Mtu anaweza kusema ameshinda na Swawm akajificha akalapasina watu kujua. Hata hivyo, mtu ikiwa atatamka Shahaadah mbili, akasimamisha Swalahna akatoa Zakaah, ataleta mwenyewe nguzo ya nne na ya tano. Katika Hadiyth hii kunafaida zifuatazo:

- Kutuma Madu´aat nje kwa ajili ya Da´wah.

- Fadhila za Mu´aadh.

- Kukubali khabari za mtu mmoja.

- Manhaj ya Da´wah. Mtu aanze kwa kitu muhimu zaidi cha msingi.

- Kuogopa Du´aa ya mdhulumiwa.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Kuwalingania watu katika Dini ya Allaah ni njia ya anayemfuata Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

2. Tanbihi ya kuwa na Ikhlaasw kwa kuwa watu wengi lau wanalingania katika haki basihulingania katika nafsi zao.

3. Katika kuwalingania watu, kuwa na Baswiyrah (elimu) ni jambo la faradhi.

4. Katika alama za Tawhiyd safi (nzuri) ni kule mtu kumtakasa Allaah kwa anayemtukana.

5. Katika ubaya wa Shirki ni kule kuwa kwake ni kumtukana Allaah.

6. Suala muhimu zaidi (katika mlango huu) Waislamu kujiweka mbali na washirikina iliasiwe katika wao hata kama hakufanya Shirki.

7. Kuwa Tawhiyd ndio wajibu wa kwanza.

8. Inaanzwa kwayo (Tawhiyd) kabla ya kila kitu, hata kabla ya Swalah.

9. Maana ya “wampwekeshe Allaah Pekee” ndio maana ya laa ilaaha illa Allaah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

36

10. Mtu anaweza kuwa katika Ahl-ul-Kitaab naye haijui (hiyo Shahaadah) au anaijua lakinihaifanyii kazi.

11. Tanbihi ya kufundisha hatua kwa hatua.

12. Kuanza kwa kitu ambacho ni muhimu zaidi kuliko kingine.

13. Jinsi ya kutoa Zakaah.

14. Mwanachuoni anatakiwa kujitahidi kuondosha utata kwa mwanafunzi.

15. Kujizuia na kuchukua mali ya watu.

16. Kuogopa Du´aa ya mwenye kudhulumiwa.

17. Tumeelezwa ya kwamba Du´aa ya mwenye kudhulumiwa haina kizuizi.

18. Yanayompitikia Kiongozi wa Mitume na baki ya mawalii wa Allaah katika mateso, njaana magonjwa ni katika dalili ya Tawhiyd.

19. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nitampa bendera hii... “ mapaka mwishowake, ni alama katika alama za Utume.

20. Kumtemea mate ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) machoni mwake ni alama vile vile katikaalama za Utume.

21. Fadhila za ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu).

22. Fadhila za Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) kwa kubaki kwao wanazungumzausiku ule (kuhusu ni nani atakayepewa bendera) na kujishughulisha kuhusiana na bisharaya kufunguliwa mji.

23. Kuamini Qadar, (bendera) kupatikana kwa ambaye hakuitafuta (´Aliy) na kutopewawaliokuwa wanaitaka (katika usiku ule).

24. Adabu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nenda zako taratibu na kwaupole... “

25. Kuwalingania watu katika Uislamu kabla ya vita.

26. Kujuzu kuwapiga vita na kuwaua wale waliolingania katika Uislamu kabla ya hilo lakiniwakakataa.

27. Kulingania katika Uislamu kwa hekima kutokana na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam): “Wajulishe yaliyo ya wajibu juu yao.”

28. Kutambua haki ya Allaah katika Uislamu.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

37

29. Thawabu za yule anayeongokewa na mtu mmoja.

30. Kuapa katika (kutoa) Fatwa.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

38

Mlango Wa 6

Tafsiri Ya Tawhiyd Na Laa Ilaaha Illa Allaah

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

ـئك الذين يدعون يبتغون إلى ربهم الوسيلة أيهم أقرب ويرجون رحمته ويخاف ون عذابهأول إن عذاب ربك كان محذورا◌

”Hao wanaowaomba (kama ‘Iysaa, ‘Uzayr, Malaika, Mawalii na wingineo, waowenyewe) wanatafuta kwa Mola wao Wasiylah (njia ya kujikurubisha kwaAllaah kwa kumtii); (na hata) walio karibu sana miongoni mwao (kamaMalaika wanafanya hivyo), na wanataraji Rahmah Yake, na wanakhofuAdhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola wako daima ni ya kutahadhari nayo.”(Israa 17:57)

Na Kauli Yake:

وجعلها كلمة باقية في عقبه لعلهم يرجعونإلا الذي فطرني فإنه سيهدينوإذ قال إبراهيم لأبيه وقومه إنني براء مما تعبدون

”Na (taja ee Muhammad صلى اهللا عليه وآله وسلم pale ) Ibraahiym alipomwambia babayake na watu wake: “Hakika mimi najitoa dhima (sina jukumu) na yalemnayoyaabudu. “Isipokuwa Yule Ameniumba, basi hakika Yeye Ataniongoa.Isipokuwa Yule Ameniumba, basi hakika Yeye Ataniongoa. Na akalifanya neno(la ilaaha illaa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea.” (az-Zukhruf 43:26-28)

Na Kauli Yake:

يوا إلا لرا أممو ميرم ناب سيحالمو اللـه ونن دا ماببأر مهانبهرو مهاربذوا أحخااتداحا وـه عبدوا إل ◌وإلا ه ـه لا إل سبحانه عما ◌يشركون

”Wamewafanya Ahbaar (Makuhani - wanavyuoni wa Kiyahudi) wao naRuhbaan (Wamonaki - watawa) wao kuwa ni miungu badala ya Allaah, na(wamemfanya mungu pia) Al-Masiyh mwana wa Maryam; na halihawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Ilaahan Waahidaa (Mungu MmojaPeke). Hapana ilaaha (Anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ila Yeye. Subhaanah!(Ametakasika) kutokana na yale yote wanayomshirkisha nayo.” (at-Tawbah

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

39

09:31)

Na Kauli Yake:

ب اللـهكح مهونبحا يادأند اللـه ونن دذ مختن ياس مالن نمو ◌لـها لبح دوا أشنآم ينالذو

”Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah kuwa nimungu mshirika (anaelingana na Allaah); wanawapenda kama mapenzi(yapasavyo) ya kumpenda Allaah.” (al-Baqarah 02:165)

Katika Swahiyh (Muslim) imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) ya kwamba kasema:

“Atakayesema “Laa ilaaha illa Allaah, hapana mola apasaye kuabudiwa kwahaki isipokuwa Allaah na akakufuru kwa vinavyoabudiwa badala ya Allaah,imeharamika mali na damu yake na hesabu yake iko kwa Allaah (´Azza waJalla)”.”

Ufafanuzi:Mlango huu unafasiri na kubainisha maana ya neno hili laa ilaaha illa Allaah ambalolimetajwa na kufafanuliwa na kubainishwa katika milango ya huko nyuma. Kwa kuwa yuleanayelingania katika kitu na anataka kutoka kwa watu wakifanye, ni wajibu kwakeawabainishie na awawekee wazi kabisa, na wala asitosheke na kuwaambia watu watamkelaa ilaaha illa Allaah, au kuwaambia watu waingie katika Uislamu. Isipokuwa ni wajibukwake kuwabainishia maana ya laa ilaaha illa Allaah na awabainishie maana ya Uislamu, nani wajibu vile vile awabainishie yanayouvunja Uislamu na yanayovunja laa ilaaha illa Allaahkatika aina za kuritadi na aina za Shirki mpaka Da´wah yake iwe ni yenye faida na watuwastafidi na Da´wah yake. Na wengi katika wale wanaofanya Da´wah leo, Madu´aat,hawajui maana sahihi ya laa ilaaha illa Allaah, hawajui maana hakika ya Uislamu na walahawajui yanayouvunja Uislamu na yanayovunja Shahaadah mbili, isipokuwa wanalinganiakatika kitu cha jumla. Na huenda kukawa watu wengine ambao wanafahamu hili, lakinihataki kuwabainishia watu mambo haya kwa kuwa – kwa madai yao – watakimbiza watu,na yeye lengo lake anataka kuwakusanya watu. Hili halimtomnufaisha na chochote.

Maana ya Tawhiyd ndio laa ilaaha illa Allaah, na maana ya laa ilaaha illa Allaah ndio Tawhiyd.Maana yake ni moja na ndio maana Shaykh kaweka lafdhi mbili katika mlango huu ilikuonesha maana yake ni moja.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

40

Aayah ya Suurat al-Israa: Wafasiri wote wamesema kuwa Aayah hii iliteremka kwa watuambao walikuwa wanamuabudu Masiyh, na mama yake, na ´Uzayr. Ndipo AlipobainishaAllaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ya kwamba watu hawa wanaowaabudu ni waja Wake, namafukara Kwake, na wanajikurubisha Kwangu kwa utiifu. Hivyo wao ni waja katika waja.Na mja haistahiki kufanywa kuwa muabudiwa. Wanataraji Rahmah ya Allaah, wanakhofuadhabu ya Allaah, hii ni dalili kuonesha kuwa viumbe vyote hivi ni dhalili mbele ya Allaahkwani haviwezi kujiletea manufaa na kujizuia na madhara. Vipi basi mtawaabudu badala yaAllaah? Na maana ya wasiylah hapa ni utiifu kwa Allaah, na maana yake si kamawanavyodhania Qubuuriyyuun16 ya kwamba wasiylah maana yake ni kuweka baina yakowewe na Allaah mtu ambaye atakuwa anakufikishia haja zako kwa Allaah. Maana yawasiylah katika Qur-aan na Sunnah ni utiifu na kufanya matendo mema. Hii ndio maana yawasiylah kwa washirikina tokea zamani mpaka sasa. Ndio maana wakawa wanawaabudubadala ya Allaah, wanawachinjia, wanawawekea nadhiri makaburi, wanapapasa na kutufukwenye makaburi kwa madai ya kwamba hawa maiti ni watu wema wanawafikishia hajazao kwa Allaah. Hii ndio maana ya wasiylah kwa watu hawa. Allaah Kawaradi kwa KauliYake:

اللـه ندا عناؤفعلاء شـؤ قولون هيو مهنفعلا يو مهرضا لا يم اللـه ونن دون مدبعيو

”Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao (hawawezi) kuwadhuru na wala (hawawezi)kuwanufaisha, na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah”.” (Yuunus 10:18)

لفى إن اللـهز ا إلى اللـهونقربيإلا ل مهدبعا ناء ميلأو ونهن دذوا مخات ينالذفونولتخي يهف ما هي مف مهنيب كمحي ◌كاذ وه ني مدهلا ي إن اللـهكفار ب

”Na wale waliojichukulia badala Yakeawliyaa (wasaidizi, miungu; wakisema):“Hatuwaabudu isipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu.” Hakika AllaahAtahukumu baina yao katika yale (yote) waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah Hamhidialiye muongo, kafiri.” (az-Zumar 39:03)

Kwa hivyo, Aayah hii (ya Israa) ndani yake kuna, katika maana laa ilaaha illa Allaah nikwamba asiombwe mwingine isipokuwa Allaah Pekee, na kwamba asiwekewe waasitwahwakati na kati baina Yake na waja Wake katika viumbe Vyake.

Aayah ya pili (Suurat az-Zukhruf), Ibraahiym (´alayhis-Salaam) anawatangazia kuwa yeyeanajiweka mbali na kuwakata kwa yale wanayoyaabudu, katika masanamu na nyota.“Isipokuwa Yule Ameniumba hakika Yeye Ataniongoa”, hii ndio maana ya laa ilaaha illaAllaah. Kauli yake ya kwanza “mimi najiweka mbali na kuwakata... “ hii ndio maana ya laailaaha, “... isipokuwa Yule Ameniumba”, hii ndio maana ya illa Allaah. Katika Aayah hii kunamaana ya laa ilaaha illa Allaah. Hivyo hapa kuna dalili ya kwamba maana ya Tawhiyd na

16 Umoja. Qubuuriy (mwabudu kaburi). Wingi. Qubuuriyyuun (waabudu makaburi)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

41

maana ya laa ilaaha illa Allaah ni kuacha ´Ibaadah ya masanamu na kujiweka nayo mbalikabisa na kumtakasia ´Ibaadah Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama yule anayesema laailaaha illa Allaah kisha hajiweki mbali na kukata vinavyoabudiwa badala ya Allaahhakuhakikisha maana yake. Kama wale wanaokwenda kwenye makaburi na kuyaomba nakutufu, huyu haitomfaa laa ilaaha illa Allaah hata ikiwa ataitamka mara elfu. Kwa kuwa laailaaha illa Allaah ni lazima mtu aihakikishe.

Aayah ya at-Tawbah: Hapa kuna dalili, yule anayewatii viumbe katika kuharamisha mamboambayo Kahalalisha Allaah, au kuhalalisha mambo ambayo Kaharamisha Allaah, basi mtuhuyo kawafanya ni miungu yao badala ya Allaah. Hakuna mwenye haki ya Kuhalalisha naKuharamisha isipokuwa Allaah Pekee. Hii ni katika maana ya laa ilaaha illa Allaah,kumpwekesha Allaah katika utiifu, bi maaana kuharamisha Aliyoharamisha na KuhalalishaAliyohalalisha.

Aayah ya al-Baqarah: “Miongoni mwa watu”, yaani washirikina. Wanawapenda kamamapenzi ya kumpenda Allaah, na mapenzi yanayokusudiwa hapa ni mapenzi ya ´Ibaadah.Washirikina wanayapenda masanamu yao na miungu yao mingine kama mapenzi yakumpenda Allaah. “Na wale ambao wameamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah”, wauminihawamshirikishi yeyote katika mapenzi tofauti na washirikina wanamshirikisha Allaahkatika mapenzi. Na Tawhiyd haisihi isipokuwa mpaka iwe kwa kutakasa mapenzikumtakasia Allaah (´Azza wa Jalla). Aayah hii Tukufu ni dalili ioneshayo, katika maana yaTawhiyd na maana ya laa ilaaha illa Allaah ni kumtakasia na kumpwekesha Allaah katikamapenzi, na wala asipendwe pamoja Naye mwengine yeyote na kusitangulizwe mapenzi yayeyote mbele ya mapenzi ya kumpenda Allaah (Ta´ala). Na hili ni kuhusu mapenzi ya´Ibaadah.

Hali kadhalika, Hadiyth ya mwisho inafasiri maana ya laa ilaaha illa Allaah. “Atakayesema“laa ilaaha illa Allaah, hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah naakakufuru kwa vinavyoabudiwa badala ya Allaah... ”, hii ndio maana ya laa ilaaha illa Allaah.Haitoshi kwa mtu kusema mimi namuamini Allaah peke yake na mimi ni Muislamu, kishaasijiweke mbali na kuwakufurisha wanaomuabudu badala ya Allaah, wanaoabudumasanamu, makaburi, Husayn, Hasan, ´Aliy, ´Abdul-Qaadir, Badawiy na kadhalika, huyusio Muislamu. Ni wajibu kukanusha kila kinachoabudiwa badala ya Allaah na kujiwekambali na kuwakata washirikina.

Masuala muhimu yaliyomo:Katika mlango huu kuna masuala makubwa na muhimu zaidi ni tafsiri ya Tawhiyd na tafsiriya laa ilaaha illa Allaah na imebainishwa kwa mambo ya wazi.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

42

Miongoni mwayo, ni Aayah ya Suurat Israa. Kumebainishwa ndani yake Radd kwawashirikina ambao wanawaomba watu wema, kuna ubainisho ndani yake ya kwamba hiindio Shirki kubwa.

Katika Aayah ya Suurat at-Tawbah kumebainishwa ndani yake ya kwamba Ahl-ul-Kitaabwamewafanya Ahbaar wao na Ruhbaan kuwa ni miungu yao badala ya Allaah. Nakukabainishwa pia ya kuwa hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu IlaahanWaahidaa (Mungu Mmoja Pekee). Hii ni tafsiri isiyokuwa na utata ndani yake ya kwambakuwatii wanachuoni na waja wengine wa Allaah katika mambo yasiyokuwa maasi(kunajuzu) na si kuwaomba.

Hali kadhalika, kauli ya Ibraahiym (´alayhis-Salaam) kuwaambia makafiri:

إلا الذي فطرنيإنني براء مما تعبدون

“Hakika mimi najitoa dhima (sina jukumu) na yale mnayoyaabudu. “Isipokuwa YuleAmeniumba… “(az-Zukhruf 43:26-27)

Kakata na kujiweka mbali na vinavyoabudiwa isipokuwa Mola Wake. Na Allaah(Subhanaahu) Kataja kuwa kuwakata kwake na kujiweka kwake mbali na Shirki ndio tafsiriya laa ilaaha illa Allaah. Akasema:

ـؤلاء وآباءهم حتى جاءهم الحق ووجعلها كلمة باقية في عقبه لعلهم يرجعون ه تعتل مببنيول مسر

”Na akalifanya neno (la ilaaha illaa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake ili wapatekurejea.” (az-Zukhruf 43:26-28)

Katika Aayah ya Suurat al-Baqarah ambapo Allaah Kasema kuhusiana na makafiri:

وما هم بخارجني من النار

”Na wala hawatokuwa wenye kutoka motoni.” (al-Baqarah 02:167)

Kataja ya kwamba wanawapenda washirika (miungu) wao kama mapenzi ya kumpendaAllaah. Ni dalili ioneshayo ya kuwa (washirikina) wanampenda Allaah mapenzi ya hali yajuu lakini hilo halikuwaingiza katika Uislamu. Vipi kwa yule atakayempenda mshirika(mungu) wake mapenzi ya hali ya juu kuliko anavyompenda Allaah? Na vipi kwa yuleasiyempenda mwingine zaidi isipokuwa mshirika (mungu) wake pekee na wala hampendiAllaah?

Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

43

“Atakayesema “Laa ilaaha illa Allaah, hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwaAllaah na akakufuru kwa vinavyoabudiwa badala ya Allaah, imeharamika mali na damuyake na hesabu yake iko kwa Allaah (´Azza wa Jalla).”

Hii ni katika dalili kubwa ibainishayo maana ya laa ilaaha illa Allaah. Hadiyth hii inaoneshawazi kabisa ya kwamba (Mtume) hakufanya kule kuitamka tu, bali hakufanya wala kulekuikubali na kutoomba kwake mwengine asiyekuwa Allaah Mmoja Pekee asiyekuwa namshirika mtu akahifadhiwa mali na damu yake. Mali yake na damu yake haviharamikimpaka aongezee juu ya hayo kukufuru kwa kila kinachoabudiwa badala ya Allaah. Akiwani mwenye shaka au akasimama, basi mali yake na damu yake haikuharamika. Masualahaya makubwa yameiweka wazi (laa ilaaha illa Allaah) na imekuwa ni hoja iliyokata mzozowote.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

44

Mlango Wa 7

Kuvaa Cheni Na Uzi Na Mfano Wavyo Kwa Ajili Ya Kuzuia Balaa AuMadhara Ni Katika Shirki

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

أر أو رهض فاتكاش نل هر هبض اللـه نيادإن أر اللـه ونن دون معدا تم متأيقل أفرهتمحر سكاتمم نل هه ةمحني براد قل ◌اللـه بيسح عليه يتوكل المتوكلون◌

”Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah; ikiwa AllaahAtanitakia dhara; je, wao wataweza kuondosha dhara Yake? Au AkinitakiaRahmah; je wao wataweza kuizuia Rahmah Yake?” Sema: “Hasbiya-Allaah (Ananitosheleza Allaah), Kwake watawakali wenye kutawakali.” (az-Zumar 39:38)

´Imraan bin Husayn (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mtu mkononi mwakekavaa kicheni [cha mfano wa pete] ya shaba. Akamuuliza: “Ni kitu ganihichi?”17 Akasema: “Kinanikinga na udhaifu.” Akasema: “Kiondoshe, kwanihakika hakikuzidishii isipokuwa udhaifu. Lau ungekufa nawe bado wakivaausingelifaulu kamwe.”

(Kaipokea Ahmad kwa isnadi isiokuwa na ubaya)

Na kapokea tena Hadiyth kutoka kwa ´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu´anhu) ambayo ni Marfu´18 ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) kasema:

17 Shaykh Fawzaan anasema: “Hapa kuna dalili ya mtu kuanza kuuliza kwanza atapomuona mtukavaa kicheni au kiuzi (na mfano wavyo). Ikiwa makusudio yake ni ya kujikinga na madharayasimpate au akaamini kina taathira yoyote ile basi amkataze mtu huyo. Ama ikiwa makusudio yakeni jambo mubaahah (la kuruhusu), asimkataze.”18 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hadiyth Marfu´ ni ile iliyonasabishwa kutoka kwa Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) na sio kwamba ni Mawquuf (maneno hayo yametoka) kwa Abuu Sa´iyd.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

45

“Yeyote atakayevaa hirizi [au atakayejiambatanisha na kitu], basi AllaahHatomtazamia matakwa yake kutimia kamwe.19 Na yule atakayevaa aukutundika chaza ndogo, Allaah Asimtie katika Amaanah Yake [hatopataamani na raha].”

Na katika upokezi mwingine:

“Yeyote atakayevaa hirizi ameshiriki.”20

Ibn Abiy Haatiym kapokea kutoka kwa Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Alimuona mtu ambaye mkononi mwake kulikuwa kipande cha uzi anatakaumponye na homa, akaukata ule uzi na kusoma Kauli Yake:

مشركونوما يؤمن أكثرهم باللـه إلا وهم

”Na wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanyashirki.”21 (Yuusuf 12:106)

Ufafanuzi:Baada ya Shaykh kuibainisha ni nini Tawhiyd, fadhila za Tawhiyd, yanayopingana naTawhiyd ambayo ni Shirki, sasa ndo akawa ameweka mlango huu. Kuvaa cheni au uzimwilini, kumvalisha mtoto, au kutundika kwenye mpando, au gari kwa kuitakidi yakwamba jambo hili linamkinga mtu na mabaya na kijicho cha anayehasidi, au tendo hilolinaikinga gari, mpando, nyumba, hii ni katika ada ya Kijaahiliyyah na bado mpaka sasa ipobali imeenea kwa sababu ya ujinga. Na kitendo hichi ni katika Shirki. Kwa kuwa Allaah(Jalla wa ´Alaa) Yeye Ndiye Mwenye kukinga madhara na Yeye Ndiye AmbayeAnapomtakia mja Wake kitu basi lazima kitu hicho kimpate, sawa ikiwa katika nafsi yake,

Maneno yakiwa yanatoka kwa Swahabah inakuwa ni Mawquuf. Na ikiwa ni ya Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) inakuwa ni Marfu´. Hii ndio tofauti kati ya Marfu´ na Mawquuf.”19 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hii ni Du´aa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)kumuombea kila yule ambaye atavaa hirizi ya aina yoyote ile. Na Du´aa ya Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) hairudishwi.”20 Shaykh Fawzaan anasema: ”Kuvaa hirizi ni Shirki kubwa au ndogo? Suala hili linahitajia ufafanuzi.Ikiwa mtu atavaa kwa kuamini kuwa manufaa na madhara yanatoka kwa Allaah na hirizi hii nikufanya sababu tu, itakuwa ni Shirki ndogo. Ama ikiwa anaitegemea hirizi hii, itakuwa ni Shirkikubwa.”21 Shaykh Fawzaan anasema: ”Maana ya Aayah hii ni kuwa, watu wengi hawamwamini Allaah ilakatika Rubuubiyyah, isipokuwa wao ni wenye kufanya Shirki katika Uluuhiyyah.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

46

mali yake na ahli zake. Na Anapomzuia mja Wake na kitu, basi hakuna yeyote awezaekumfanya kikampata. Ufalme uko Mikononi mwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Kwa hiyo, ni wajibu nyoyo zetu ziwe ni zenye kumtegemea Allaah (´Azza wa Jalla) nakumtakasia ´Ibaadah Allaah (´Azza wa Jalla) na wala mtu asimuogope au kuogopa chochoteau yeyote isipokuwa Allaah (´Azza wa Jalla). Yule ambaye moyo wake ataufanya ukawa niwenye kumtegemea Allaah Pekee na akampwekesha, hatofikwa na kitu isipokuwa kwaidhini ya Allaah (Ta´ala).

Aayah ya az-Zumar: Hapa anaambiwa aseme Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam). “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah”, katika masanamu, miti,mawe, makaburi, mawalii, watu wema na kila anayeabudiwa badala ya Allaah. “IkiwaAllaah Atanitakia dhara”, yaani kama maradhi, ufukara, mauti, je wao hao wanaowaabuduwataweza kuondosha dhara Yake? Hili ni swali la kukataza kitendo hicho. “... au AkinitakiaRahmah”, kama afya, utajiri au Rahmah nyenginezo, kuna yeyote katika waja wa Allaahanaweza kuzuia Rahmah Yake? Hakuna hata mmoja awezae hilo. Hivyo, hawawanaoshirikishwa pamoja na Allaah imebainika kuwa si waweza wa kitu. Vipi basimtawaogopa hao washirika wenu wasiwadhuru badala ya kumuogopa Allaah? Hapatunapata funzo kuwa mtu anatakiwa kumtegemea Allaah (´Azza wa Jalla) na kufanya nyoyokumtegemea Allaah Pekee. Na katika Hadiyth Mtume (´alayhis-Salaam) anamwambia´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Na tambua ya kwamba, lau watu wote watakusanyika kutaka kukunufaisha kwa kitu, basihawatokufaisha isipokuwa kwa kitu ambacho Kishakuandikia Allaah. Na lauwatakusanyika kutaka kukudhuru kwa kitu, basi hawatokudhuru isipokuwa kwa kituambacho Kishakuandikia Allaah.”

Mambo yote yako Mikononi mwa Allaah (´Azza wa Jalla). Hivyo Muislamu hatakiwikumuogopa yeyote zaidi ya Allaah Pekee. Unachotakiwa ni kuchukua sababu tu.

Hadiyth ya ´Imraan bin Husayn, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kamwambiamtu yule aliyekuwa amevaa kicheni kuwa hakimzidishii isipokuwa maradhi, tofauti namakusudio yake. Na hili ni jambo la wazi kwa wale ambao wanatumia vitu kama hivi,utawaona daima ni wenye khofu na woga, kila kunapotikisika kitu khofu inawaingia.Hivyo, hili haliwazidishii isipokuwa udhaifu mtupu. Lakini yule anayemtegemea Allaahhababaiki na lolote daima. Utamuona yuko imara na madhubuti daima. KishaAkamwambia: “Lau ungekufa nawe bado wakivaa usingelifaulu kamwe”, hapa kuna daliliya kuwa Shirki haisamehewi kabisa hata ikiwa ni Shirki ndogo. Mtu akifa ilihali hakutubia,lazima aadhibiwe Motoni. Hata kama hatoadhibiwa kama mtu wa Shirki kubwa, lakiniataadhibiwa kiasi cha dhambi yake kisha baadae atatolewa humo. Na hapa kuna dalili kuwaShirki ndogo ni dhambi kubwa kuliko madhambi makubwa, ni kubwa kuliko Zinaa, kuiba,kunywa pombe na kadhalika. Vipi tusemeje kuhusu Shirki kubwa? Allaah Atukinge.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

47

Kwa hivyo, ni juu ya Muislamu atahadhari na Shirki. Na ikiwa Shirki inawapitikia baadhi yawaumini,22 basi mtu asijiaminii nafsi yake kwa Shirki ndogo na akasema “mimi ni muuminina Muislamu na haiwezi kunipitikia Shirki”, hapana haya ni makosa. Anatakiwa kuigopaShirki na amuombe Allaah Amkinge na Shirki kubwa na ndogo.

“Ee Allaah najikinga kwako kukushirikisha na chochote ilihali ni mwenye kujua, naunisamehe kwa dhambi nisiyoijua.”23

Shirki si kama Waislamu wengi wanavyodhania kwamba ni kuabudu masanamu peke yake,Shirki sio kuabudu masanamu peke yake. Isipokuwa Shirki ni kila kile unachokiabudubadala ya Allaah. Sawa iwe Shirki ndogo au kubwa. Hivyo haijuzu kwa Muislamukuchukulia sahali suala la Shirki.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Uharamisho wa kuvaa cheni, uzi na mfano wavyo.

2. Lau Swahabah yule angelikufa naye bado anaivaa asingelifaulu. Kuna ushahidi wamaneno ya Maswahabah ya kwamba Shirki ndogo ni kubwa kuliko madhambi makubwa.

3. Hakupewa udhuru kwa ajili ya ujinga.

4. Kuvaa hirizi haimfai kidawa (kumponyesha) bali inamdhuru zaidi. Kwa kauli yake(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hakika hakikuzidishii isipokuwa udhaifu.”

5. Kukataza kwa ukali kwa mwenye kufanya kitendo kama hicho.

6. Ubainisho ya kwamba yule atakayejiambatanisha na kitu huwakilishwa kwacho.24

7. Ubainisho ya kwamba yeyote atakayevaa hirizi ameshiriki.

8. Kutundika (au kuvaa) kipande cha uzi ni katika Shirki.

9. Hudhayfah aliposoma Aayah, hii ni dalili ya kwamba Maswahabah walikuwa wanatoleadalili kwa Aayah za Shirki kubwa katika Shirki ndogo.25 Kama alivyosema Ibn ´Abbaas(Radhiya Allaahu ´anhumaa) vile vile kwa kusoma Aayah ya Suurat al-Baqarah. (02:165)

22 Kama huyo ambaye Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anhu) kakata uzi aliokuwa amevaa. Na kamajinsi ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu) alivoigopa Shirki ndogo akaenda kumuuliza Hudhayfah(Radhiya Allaahu ´anhu).23 Hii ndio Du´aa ya kafara ya Shirki ndogo24 Ni nini maana ya ”...huwakilishwa kwacho”? Anasema Shaykh Fawzaan: ”Hili ni jambo la wazikwa wale ambao wanatumia vitu kama hivi, utawaona daima ni wenye khofu na woga, kilakunapotikisika kitu khofu inawaingia. Hivyo, hili haliwazidishii isipokuwa udhaifu mtupu. Tofautina wale wanaomtegemea Allaah na wameziambatanisha nyoyo zao kwa Allaah.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

48

10. Kuvaa hirizi ili usipatwe na kijicho ni katika Shirki.

11. Du´aa (ya Mtume) kwa yule anayevaa hirizi Allaah Hatomtazamia matakwa yakekutimia kamwe. Na yule atakayevaa au kutundika chaza ndogo, Allaah Hatomtia katikaAmaanah Yake, bi maana hatopata amani na raha.

25 (12:106)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

49

Mlango Wa 8

Yaliyokuja Katika Ruqyah Na Mahirizi

Katika Swahiyh kutoka kwa Abuu Bashiyr al-Answaariy (Radhiya Allaahu´anhu):

“Alikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)katika baadhi ya safari zake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)akatuma ujumbe: “Pasiachwe katika shingo ya ngamia kidani cha kamba aumkufu isipokuwa kikatwe.”

Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema, nilimsikia Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakika ya ar-Ruqaah,26 at-Tamaaim na at-Tiwalah27 ni Shirki.”

(Kaipokea Ahmad na Abuu Daawuud)

´Abdullaah bin ´Ukaim kapokea Hadiyth ambayo ni Marfu´:

“Atakayevaa [au kujiambatanisha na] kitu28 huwakilishwa kwacho.”29

(Kaipokea Ahmad na at-Tirmidhiy)

at-Tamaaim ni kitu huvalishwa watoto ili kimkinge na madhara ya kupatwa nakijicho. Lakini ikiwa kilichotundikwa ni kitu kina (Aayah za) Qur-aan, baadhiya Salaf wameona kuwa hilo linaruhusu. Na baadhi yao wameona kuwahaliruhusu na kufanya hilo ni katika (mambo) yaliyokatazwa. Miongonimwao30 ni Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu).

26 Shaykh Fawzaan anasema: ”ar-Ruqaah ndio inayoitwa Ruqyah. Kumsomea mgonjwa Qur-aan aukatika Du´aa mubaahah zilizothibiti.”27 Dawa ya mapenzi28 Shaykh Fawzaan anasema: “Kitu chochote kile; hirizi, uzi, kakamba, cheni na kadhalika.”29 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hii ni adhabu ya Allaah (´Azza wa Jalla) kwa mtu huyu, na AllaahAkishamuwakilisha kwacho hakuna jengine zaidi isipokuwa kuangamia. Ama yule anayemtegemeaAllaah (´Azza wa Jalla) Peke Yake Allaah (Ta´ala) Humhifadhi. Ama yule atayejiambatanisha na kituchochote badala ya Allaah; sawa ikiwa ni hirizi, kaburi, mti, jiwe, jini n.k. basi huwakilishwa kwacho,bi maana huangamia.”30 Ambao wanaona kuwa kitendo hicho hakijuzu na ni haramu.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

50

ar-Ruqaah ndio ile iitwayo al-´Azaaim, ni kitendo cha kisomo n.k. Hayoyanaruhusiwa ambapo ndani yake kuna athari ya Shirki. Aliruhusu hiloMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa kupatwa nakijicho na kudonolewa (na mdudu mwenye sumu).

at-Tiwalah ni kitu kinachotengenezwa na wanadai kwamba humpendezea mkekwa mume wake au mume kwa mke wake.

Kapokea Ahmad kutoka kwa Ruwaifiy´ ambaye kasema, Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kanambia:

“Ewe Ruwaifiy´! Huenda uhai wako ukawa mrefu baada yangu, hivyowaeleze watu mtu ambaye anazifunga fundo ndevu zake, au akaweka kidanicha kamba ya upinde au kustanji31 kwa choo cha mnyama au mfupa, hakikaMuhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yuko mbali nae.

Kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr ambaye amesema:

“Mwenye kukata hirizi kutoka kwa mtu, atakuwa sawa kama mtu aliyeachamtumwa huru.”

Wakiy´ ndiye kaipokea, na kapokea kutoka kwa Ibraahiym32 ambaye kasema:

“Tulikuwa tukichukia hirizi za aina zote, sawa za Qur-aan na zisizokuwa zaQur-aan.”

Ufafanuzi:Yaliyokuja katika Ruqyah na mahirizi, yaani yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum) katika Hadiyth naAthaar kukataza mambo haya. Mlango huu unakamilisha mlango ulio kabla yake.

Hadiyth ya Abuu Bashiyr, kabla ya kuja Uislamu watu walikuwa wakitundika kidani chakamba juu ya ngamia wakiamini kuwa tendo hili linawakinga kupatwa ngamia na kijicho.

31 Kujisafisha baada ya kujisaidia haja32 Ibraahiym Nakh´iy

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

51

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akataka kuondosha ada hii ya Kijaahiliyyah nakuwahakikishia Tawhiyd.

“Hakika ya ar-Ruqaah, at-Tamaaim na at-Tiwalah ni Shirki”, hapa ilikuwa wakati ambapo´Abdullaah bin Mas´uud alimuona mwanamke amevaa kitu kwenye shingoni yake akawaamekikata, ndipo alipomsomea Hadiyth hii aliyosikia kwa Mtume wa Allaah (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam).

Kuvaa hirizi ya Qur-aan au Sunnah ya Mtume (´alayhis-salaam), Salaf wametofautiana.Kuna ambao wanaona kuwa tendo hilo linajuzu kwa vile ni Qur-aan na ni Maneno yaAllaah, akiwemo pia ´Abdullaah bin ´Aasw na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Nabaadhi yao hawakuruhusu hilo hata kama itakuwa ni Qur-aan, katika hao ni mpokezi waHadiyth hii ´Abdullaah bin Mas´uud na Ibraahiym Nakh´iy. Hapa Shaykh kataja tofauti yaSalaf katika hili. Na kauli iliyo sahihi ni kwamba haijuzu, kama alivosema pia hilo mwenyekitabu cha “Fath al-Majiyd” Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Hasan (Rahimahu Allaah).Kasema kauli yenye nguvu ni ya ´Abdullaah bin Mas´uud. Hilo ni kwa sababu ya mambomatatu:

- Ujumla wa makatazo. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)kakataza kiujumla kutundika hirizi yoyote ile.

- Kufunga mlango unaopelekea katika Shirki. Kwa kuwa ukifunguliwa mlango wakuruhu kuvaa hirizi ya Qur-aan, utanfunguliwa mlango wa mengine.

- Kuvaa hirizi ya Qur-aan ni kuipa mtihani Qur-aan. Kwa kuwa hirizi hiyoanavalishwa mtoto mdogo, na mtoto mdogo hasalimiki na najisi, au kuingia choonin.k. Hali kadhalika wale wajinga katika watu wakubwa, hawaizingatii Qur-aan kamainavyotakikana. Huku ni kuiweka Qur-aan katika mitihani. Na kuiweka Qur-aankwenye mitihani ni jambo la haramu. Kwa sababu hizi ndio maana wameoneleakuwa hata hirizi ya Qur-aan haijuzu kabisa.

Na wale ambao wamejuzisha kutundika hirizi ya Qur-aan wameweka sharti tatu:

- Hirizi iwe ya Qur-aan.

- Iwe imeandikwa kwa lugha ya kiarabu. Isiandikwe kwa lafdhi isiyoweza kusomwa.Iwe kwa kiarabu kwa uwazi mtu aweze kuisoma.

- Mtu aitakidi kuwa dawa inatoka kwa Allaah na si kutoka kwenye hii hirizi. Mtuaitakidi kuwa hii riziki ni sababu tu. Wale ambao wamejuzisha masharti waliyowekana haya.

Lakini – anasema Shaykh Fawzaan – kauli iliyo ya sahihi na ya nguvu ni kuwa hata hirizi yaQur-aan haijuzu.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

52

Ama Ruqyah, ikiwa ni katika Qur-aan na Du´aa ambazo ni mubaahah ni jambo linalojuzu.Imepokelewa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) karuhusu kutumiaRuqyah kwa kupatwa na kijicho na kudonolewa kama ilivyo katika Hadiyth hapo juu. Halikadhalika Jibriyl (´alayhis-Salaam) aliwahi kumsomea Ruqyah Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam). Anasema (Jalla wa ´Alaa):

ننيمؤلمة لمحرفاء وش وا هم آنالقر نزل مننو

”Na Tunateremsha katika Qur-aan ambayo ni shifaa na Rahmah kwa Waumini.” (al-Israa17:82)

قل هو للذين آمنوا هدى وشفاء

”Sema (ee Muhammad ”.Hii (Qur-aan) kwa walioamini ni uongofu na dawa“ :(صلى اهللا عليه وآله وسلم(al-Fuswswilat 41:44)

كاربم اهلنأنز ابتـذا ك هو

”Na hiki Kitabu Tumekiteremsha chenye baraka... ” (al-An´aam 06:92)

Na miongoni mwa baraka zake ni kuwa mtu unajitibu nayo. Hii ni katika baraka ya Qur-aan.Qur-aan ni dawa, kwa kuwa ni Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Hivyo hili ni jambolinalojuzu na sio Shirki, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliruhusu hilo.Unajitibu nayo kwa maradhi yote, sawa ikiwa ni maradhi ya kimwili au yakinafsi. Lakini nahili kwa sharti vile vile, mtu aitakidi kuwa Mponyaji ni Allaah na sio kisomo hicho. Ruqyahni kuchukua sababu tu, na si kwamba yenyewe ndio inaponyesha bali Mponyeshaji niAllaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Mtu anaweza kutotumia Ruqyah na akapona. Ama Ruqyahambazo ndani yake kunaingia Shirki, hii imekatazwa na haijuzu.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Tafsiri ya ar-Ruqaah na at-Tamaaim.

2. Tafsiri ya at-Tiwalah.

3. Kuwa mambo yote haya matatu ni katika Shirki bila ya kubagua.

4. Ruqyah kisomo kwa maneno ya haki, kwa kupatwa na kijicho na kudonolewa sio katikaShirki.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

53

5. Hirizi ikiwa ni ya Qur-aan, wanachuoni wametofautiana kama ni Shirki au hapana.

6. Kutundika kidani cha kamba juu ya mnyama dhidi ya kijicho ni katika Shirki.

7. Matishio makali kwa yule mwenye kujiambatanisha na kitu (sawa cha aina yoyote).

8. Fadhila za thawabu kwa yule mwenye kukata hirizi kutoka kwa mtu.

9. Maneno ya Ibraahiym Nakh´iy33 hayakwendi kinyume na yaliyotangulia katika tofauti,kwa kuwa makusudio yake (ya kuonelea hivyo) inarejea kwa Maswahabah wa ´Abdullaahbin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu).

33 “Tulikuwa tukichukia hirizi za aina zote sawa za Qur-aan na zisizokuwa za Qur-aan.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

54

Mlango Wa 9

Mwenye Kutabaruku34 Kwa Mti Au Jiwe Na Mfano Wavyo

Kauli Yake (Ta´ala):

ومناة الثالثة الأخرىأفرأيتم اللات والعزى

Je, mmeona Laata na ‘Uzzaa (masanamu miongoni mwa miungu ya makafiri)?Na Manaata (sanamu) mwengine wa tatu?” (an-Najm 53:19-20)

Abuu Waqid al-Laythiy kasema:

“Tulitoka pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)kuelekea kwenda Hunayn, na sisi ndio bado karibuni tulikuwa tumetokakatika ukafiri. Washirikina walikuwa na mkunazi35 wakikaa hapo nakutundika silaha zao juu, ambao ulikuwa ukiitwa Dhaat an-Waatw. Tukapitakwenye mti mwengine wa mkunazi, tukasema: “Ewe Mtume wa Allaah!Tujaalie36 na sisi Dhaat an-Waatw kama ule mti wa Dhaat an-Waatw?” AkasemaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Allaahu Akbar! Ndiozile zile njia. Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake,kwa hakika mmesema kama walivosema Banuu Israaiyl kumwambia Muusa:“Tufanyie mungu kama ambavyo wao wako na miungu.” Akasema: “Hakika,nyinyi ni watu wajinga.” (al-A´raaf 07:138) Hakika mtafuata njia za walewaliokuwa kabla yenu.”

(Kaipokea at-Tirmidhiy na kaisahihisha)

34 Shaykh Fawzaan anasema: ”Maana ta kutabaruku ni kutafuta baraka kutoka katika mti au jiwe.Hukumu ya anayefanya hivi kamshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla).”

35 Mti wa sidri36 Tufanyie

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

55

Ufafanuzi:Mlango huu unakamilisha milango ilio nyuma yake, kwa kuwa milango iliyo kabla yake nikuhusu kuvaa na kutundika hirizi cheni na uzi na mfano wavyo, au kutundika ar-Ruqaah namahirizi. Na katika mlango huu unazungumzia kutabaruku kwa mti au jiwe. Milango yotehii inahusiana na kumuamini asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa kitu aidhakinadhuru au kinanufaisha. Na Itikadi hii ni Shirki. Yule ambaye anaitakidi kutoka katikakitu ya kwamba kinazuia madhara au kinaleta manufaa badala ya Allaah (Ta´ala) hii niShirki. Kwa kuwa anayeweza kuleta manufaa na kuzuia madhara ni Allaah (Subhaanahu waTa´ala) Mmoja asiyekuwa na mshirika. Yeye Pekee Ndiye Muweza wa hilo.

Maana ya kutabaruku ni kutafuta baraka kutoka katika mti au jiwe. Anayefanya hivikamshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla). Kwa kuwa hakuna anayeleta baraka isipokuwa niAllaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Allaah Anaweza kujaalia baadhi ya vitu vikawa na baraka,kwa mfano maji ya Zamzam, Mitume (´alayhimus-Salaam), al-Ka´abah, vyote hivi AllaahNdiye Kavifanya kuwa na baraka. Ama vyenyewe (kwa dhati yavyo) sivyo ambavyovinaleta baraka. Hivyo baraka inatoka kwa Allaah (Ta´ala).

Aayah ya Suurat an-Najm: Allaah Anawaambia na kuwapa changamoto washirikinawanaoabudu masanamu. “Je, mmeona Laata na ‘Uzzaa (masanamu miongoni mwa miunguya makafiri)? Na Manaata (sanamu) mwengine wa tatu?”, je wamewanufaisha, jewamewazuia msipatwe na madhara, je wamewaletea kitu katika riziki? Hawawezi kujibukitu. Mlango umefunguliwa, ikiwa kuna mshirikina yoyote katika uso wa ardhi ambayeanaweza kujibu maswali haya ajitokeze, hakuna yeyote awezae kujibu kamwe.

Laat alikuwa mtu mwema mchaji Allaah katika mji wa Twaaif, alikuwa akiwalisha mahujajikwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah. Alipokufa wakawa wanafanya I´tikaaf katika kaburilake wakitabaruku kwalo, kama walivyofanya watu wa Nuuh pia. Kuchupa mipaka kwawatu wema, kutabaruku kwao na kujenga kwenye makaburi yao, hii ni Sunnah yaKijaahiliyyah tokea zama za Nuuh na bado itaendelea. Sanamu hili liliendelea kuabudiwabadala ya Allaah mpaka wakati Makkah ilipotekwa na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam). ´Uzzaa ilikuwa ni sanamu la watu wa Makkah. Ama Manaat ilikuwa nisanamu lililokuwa karibu na Madiynah. Na walikuwa wakifanya ´Umran kwenye sanamuhili wakati wa Hajj. Mtuma (´alayhis-Salaam) alipouteka mji wa Makkah akatumaMaswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wakenda kuyavunja na historia yake ikaisha. Laukama yangelikuwa ni miungu, kwa nini yashindwe kujitetea? Yako wapi ilihali yalikuwa nimasanamu makubwa kabisa? Tunachopata kujifunza katika Aayah hii ni ubatili wakutabaruku katika mti na jiwe. Yule atakayetabaruku leo katika mji au jiwe ni kama mfanowa yule ambaye alitabaruku katika Laat, ´Uzzaa na Manaat. Bali atakayepindukia mipakakatika kaburi, atakuwa ni mfano kama wa aliyepindukia mipaka katika Laat. Kwa kuwa Laatnaye alikuwa ni mtu mwema. Wale wanaoabudu makaburi leo, ni kama mfano wawalioabudu Laat.

Hadiyth ya Abuu Waqid al-Laythiy: Hapa watu hawa ndio walikuwa wameingia karibunikatika Uislamu na ndio maana walitumbukia katika hili. Na kasema hivi ili kuonesha

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

56

udhuru waliokuwa nao. Hii ni dalili ioneshayo ya kwamba ni wajibu kwa Waislamukujifunza ´Aqiydah sahihi. Ama wale wanaosema sisi ni Waislamu na tuko katika mji waKiislamu hatuhitajii kusoma Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi, huu ni upotofu. Hawa waliosemahivi siwalikuwa ni Maswahabah? Hawakutumbukia katika hili isipokuwa ilikuwa ni kwasababu ya ujinga ndio walikuwa wameingia katika Uislamu karibuni. Hii ni dalili kuwa nijuu ya Muislamu kujifunza ´Aqiydah sahihi. Na hakuna atakayesalimika na hili isipokuwayule aliyejifunza ´Aqiydah sahihi.

Maswahabah walipoona kitendo wanachofanya washirikina hawakukimbilia kukifanya, baliwalimuendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuuliza. Hapa kuna dalili yakuwa, mtu unapoona kitu katika Uislamu – hata kama kwako utakiona kuwa ni kizuri nakikakupendeza - hutakiwi kukimbilia kukifanya, bali unatakiwa kurejea katika Qur-aan naSunnah kwanza ukihakikishe. Usijifanyie kitu ni kitu tu katika mambo ya ´Ibaadah, hapana.Tunachopata kujifunza hapa ni kwamba, kutabaruku katika miti na mawe ni katika Sunnahya Kijaahiliyyah. Na atakayefanya hivyo anawafuata makafiri na ni kafiri kama wao.Hakuna tofauti kati ya yule anayeabudu kaburi na anayeabudu Laat na ´Uzzaa, au yuleanayetafuta baraka kutoka katika mti na anayetafuta baraka kutoka katika mji. Hakunatofauti kati ya watu hawa. Hivyo haijuzu kutabaruku kutoka katika mti wala jiwe na kuwani Shirki. Kwa nini? Kwa kuwa Muusa (´alayhis-Salaam) aliwaambia:

ـها قال أغير اللـه أبغيكم إل

”(Muwsaa) Akasema: “Je, nikutafutieni mungu asiyekuwa Allaah” (al-A´raaf 07:140)

Ni dalili ioneshayo ya kwamba atakayetabaruku kwa jiwe au mti kaufanya kuwa ndiomungu wake. Kutofautiana kwa matamshi, hakuathiri maana na makusudio. Kwa kuwaMaswahabah wao walimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) awafanyieDhaat an-Waatw, na Mtume (´alayhis-Salaam) akafanya kauli yao hii ni kama ile ya BanuuIsraaiyl waliyosema kwa uwazi kumuomba Muusa (´alayhis-Salaam) awafanyie mungu.Kutofautiana kwa matamshi hakubadili kitu, hata ikiwa mtaita kuwa ni kutawassul,mapenzi kwa watu wema, haki za mawalii juu yetu n.k., hii ndio Shirki. Ibra ni uhakika nahakutazamwi majina. Lau sumu utaiita kuwa ni asali itabadilika kuwa sumu? Hapana. Leowaabudu makaburi wanasema wanayoyafanya sio Shirki bali ni kuwapenda mawalii nawatu wema. A´udhubi Allaah.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat an-Najmiy. (53:20)

2. Kujua asli ya jambo ambalo (Maswahabah) walimuomba.

3. Hawakulifanya.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

57

4. Nia yao ilikuwa ni kujikurubisha kwa Allaah kwa hilo kwa kudhania kwao Atalipenda.

5. Ikiwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) hawakujua hilo, basi wasiokuwa wao niaula zaidi kutokujua.

6. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wana mema na ahadi ya msamaha usiokuwakwa wengine.

7. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwapa udhuru, bali aliwaradi kwa kauliyake: “Allaahu Akbar! Ndio zile zile njia. Kwa hakika mtafuata njia za wale waliokuwakabla yenu”, akaonesha uzito wake kwa mambo haya matatu.

8. Hili ni suala kubwa nalo ndilo linalokusudiwa, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)kawaambia kuwa ombi lao (Maswahabah) ni kama ombi la Banuu Israaiyl pindiwalipomwambia Muusa: “Tufanyie mungu.”

9. Kukanusha kitendo hichi ndio maana ya “laa ilaaha illa Allaah”, pamoja na kujificha kwakekwa watu wale.

10. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliapa juu ya Fatwa naye haapi isipokuwakunapokuwa na maslahi.

11. Shirki ni aina mbili; Shirki kubwa na Shirki ndogo. Kwa kuwa (Maswahabah)hawakuritadi kwa hili.

12. Kauli yake: “Na sisi ndio bado karibuni tulikuwa tumetoka katika ukafiri”, ndani yaketunapata kujua kuwa Maswahabah wengine walikuwa si wajinga kwa hilo.

13. Kusema Allaahu Akbar wakati wa kustaajabu. Tofauti na waonao kuwa ni Makruuh(jambo lenye kuchukiza)

14. Kuziba njia zote zinazopelekea katika Shirki.

15. Makatazo ya kujifananisha na Ahl-ul-Jaahiliyyah (makafiri).

16. Mwalimu anaweza kuwaghadhibikia (wanafunzi wake) wakati wa kuwafunza.

17. Kanuni ya kijumla ya watu imeonyeshwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)kwa kauli yake: “Ndio zile zile njia.”

18. Hii ni alama katika alama za Utume kwa kuwa imetokea kama alivyoeleza.

19. Hakika Allaah kila Anapowalaumu mayahudi na manaswara katika Qur-aan, Anatuonyasisi pia.

20. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakijua kanuni hii ya kwamba´Ibaadah imejengeka juu ya msingi wa amri ya moja kwa moja. Hivyo, kukawa kuna tanbihi

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

58

kuhusiana na maswali ya kwenye kaburi. Ama swali la: “Ni nani Mola Wako?” liko wazi.“Ni nani Mtume Wako?” inatokana na khabari zake kuhusu khabari za ghaibu. “Ni ipi Diniyako?” ni kutokana na kauli yao (Banuu Israaiyl) kumwambia Muusa: “Tufanyie mungu... ”

21. Njia za Ahl-ul-Kitaab ni zenye kulaumiwa kama njia za washirikina.

22. Mtu anayetoka katika upotofu ambao amekwishauzoea kama Imani na tabia haaminikikutokuwa ndani ya moyo wake na athari ya ada hiyo. Kwa kauli yao (Maswahabah): “Nasisi ndio bado karibuni tulikuwa tumetoka katika ukafiri.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

59

Mlango Wa 10

Yaliyokuja Katika Kuchinja Kwa Ajili Ya Asiyekuwa Allaah

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

نيالمب العر لـهي لاتممو اييحمي وكسني ولاتقل إن صله ريكلا ش ◌نيملسل الما أوأنو ترأم كبذلو

”Sema (ee Muhammad Hakika Swalaah yangu, na“ :(صلى اهللا عليه وآله وسلم Nusukiy(kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu) na uhai wangu na kufa kwangu ni kwaajili ya Allaah (Pekee) Mola wa walimwengu. Hana mshirika, na kwa hayondio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza (waliojisilimisha kwaAllaah).” (al-An´aam 06:162-163)

Na Kauli Yake:

بكرل لفصرحانو

”Basi swali kwa ajili ya Mola wako na (pia ukichinja) na chinja (kwa ajiliYake).” (at-Takaathur 108:02)

Kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) ambaye kasema:

“Kanieleza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusumambo mane: 1) Allaah Kamlaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwaAllaah,37 2) Allaah Kamlaani mwenye kuwalaani wazazi wake wawili, 3)Allaah Kamlaani mwenye kumpa himaya mzushi,38 4) Allaah Kamlaanimwenye kubadili alama ya kiwanja.”

(Kaipokea Muslim)

37 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hata ikiwa mtu atachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah kisha akasema”Bismillaah” kabla ya kuchinja, hii ni Shirki na kichinjo hichi sio halali. Maadamu kachinja kwa ajiliya majini, wachawi, ´Iysa (´alayhis-Salaam), makuhani n.k., hata akisema ”Bismillaah” haitosaidiakitu na kichinjo hichi ni haramu. Hali kadhalika sawa awe amechinja kwa ajili ya kujikurubisha aukwa ajili ya kutaka kula nyama, ilimradi kachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah nyama hii niharamu.”38 Shaykh Fawzaan anasema: ”Ni yule ambaye anastahiki kupewa hadd (adhabu) ya Kishari´ah. Kamaadhabu ya kufanya Zinaa, kuiba, kuritadi, kisasi n.k. mtu akampa himaya mtu huyu, atakuwaanastahiki laana ya Allaah. Na vile vile, inaweza kufasiriwa kuwa ni yule mwenye kuridhia Bid´ah naakainyamazia.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

60

Kutoka kwa Twaariq bin Shihaab kapokea ya kwamba Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Kuna mtu aliyeingia Motoni kwa sababu ya nzi, na kuna mtu mwenginealiingia Peponi kwa sababu ya nzi.” Wakasema: “Na ilikuweje ewe Mtume waAllaah?” Akasema: “Watu wawili waliwapitia watu waliokuwa na sanamuambalo ilikuwa haijuzu kwa mtu yeyote kulipita mpaka mtu alitoleeSwadaqah.39 Wale watu wakamwambia mmoja wao: “Litolee Swadaqah”.Akasema: “Sina chochote cha kutoa”. Wakamwambia: “Litolee ijapokuwa hatakama itakuwa ni nzi”. Hivyo akalitolea. Wakawa wamemwachia na akaingiaMotoni. Wakamwambia yule mwengine: “Litolee”. Akasema: “Siwezi kamwekutoa Swadaqah kwa ajili ya yeyote yule asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jalla)”.Hivyo wakawa wamemkata shingo yake na akaingia Peponi.”

(Kaipokea Ahmad)

Ufafanuzi:Mlango huu ni kama milango ya kabla yake, unabainisha aina ya Shirki wanayofanya baadhiya watu tokea zamani hadi sasa.

Aayah ya Suurat al-An´aam: Hapa anaamrishwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)awaambie watu. Kaanza kwa Swalah kwa kuonesha umuhimu wa ´Ibaadah ya Swalah nakwa kuwa ndio inayokuja baada tu ya Shahaadah. “Nusukiy” ni kile anachochinja mtu kwaajili ya kujikurubisha kwa Mola Wake; kama ´Aqiyqah, kuchinja katika Hajj n.k. Na kabla yakuja Uislamu washirikina walikuwa wakichinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah,wakiyachinjia masanamu, nyota n.k. Kuchinja kumeambatanishwa na Swalah hii ni dalilikuonesha kuwa kuchinja ni ´Ibaadah kubwa. Jambo ambalo limefanywa dogo leo, watuwanachinjia majini, wachawi kwa ajili ya kujitibu kama wanavyodai. Hii ni Shirki kubwainayomtoa mtu katika Uislamu. Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, ni kama kuswalikwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Hivyo, Mola wa walimwengu Ambaye ni Allaah Pekee NdiyeMwenye kustahiki kuabudiwa. Na Allaah Kataja ´Ibaadah mbili muhimu hapa; Swalah nakuchinja. Kwa kuwa Swalah ni ´Ibaadah ya kimatendo, na kuchinja ni ´Ibaadah kubwa yakimali ambayo alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akipenda kuifanya.

39 Kujikurubisha kwalo kwa kulitolea Swadaqah, kulichinjia

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

61

Aayah ya Suurat at-Takaathur: Kumefuatishwa kuchinja na Swalah kama ilivo katika Suuratal-An´aam, jambo ambalo linaonesha umuhimu wake. Allaah Alipompa Kawthar (mto),Akamuamrisha amshukuru Mola Wake kwa neema hii kubwa kwa kuswali na kuchinja kwaajili ya Mola Wake Pekee. Aayah hizi mbili ni dalili inaonesha kuwa kuchinja ni ´Ibaadah, naikishakuwa ni ´Ibaadah kumchinjia asiyekuwa Allaah ni Shirki.

Kuna aina tatu ya kuchinja:

1. Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah kwa ajili ya kutaka kujikurubisha. Nyama hiini haramu hata akiitajia “Bismillaah” kabla ya kuichinja, hii ni haramu kwa Ijmaa´ yaWaislamu. Na ni Shirki.

2. Kuchinja kwa ajili ya kutaka kula nyama na akataja jina la asiyekuwa Allaah. Hii sio´Ibaadah kwa kuwa amechinja kwa ajili ya nyama, lakini kule kutaja jina laasiyekuwa Allaah kafanya tendo la ´Ibaadah. Hii pia ni Shirki.

3. Kuchinja kwa ajili ya kuadhimisha. Kama kuwachinjia wafalme, maraisi n.k si kwalengo la nyama bali kwa lengo la kutaka kuwaadhimisha. Hii ni katika Shirki pia.Kwa kuwa hakuchinja kwa ajili ya kutaka nyama wala hakuchinja kwa ajili ya´Ibaadah, isipokuwa kachinja kwa ajili ya kumuadhimisha mtu fulani.

4. Kuchinja pindi mtu anapohamia katika nyumba mpya kwa kuogopa majini. Hii niShirki pia. Ama kuchinja kwa ajili ya mnasaba fulani, kama wageni, jamaa na ndugu,wakati wa furaha na kadhalika, hili halina ubaya. Kwa kuwa ni kuchinja kwa ajili yamnasaba fulani na matukio fulani ili kuwaalika ndugu muweze kukutana nyote nakufurahi.

Hivyo neno lake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Allaah Kamlaani mwenyekuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah”, kunaingia yote hayo ambayo tumeyataja hapo juu.

Na Hadiyth ya Twaariq bin Shihaab, yule mtu wa pili ambaye alitolea Swadaqah sanamuakaingia Motoni kwa ajili ya nzi, ni kwa sababu hakusema kitu na kuwaambia kuwa hii niShirki kama alivyofanya mwenzake. Hakuchukia tendo hili hata moyoni mwake kutokanana kauli yake aliposema: “Sina chochote cha kutoa”, maneno yake kana kwamba anasemamimi sina neno wala sioni ubaya wowote kulitolea Swadaqah kwani kashindwa hatakulikataza tendo hili na kulichukia na ndio maana akaingia Motoni. Hakuangaliwi udogowa alichokifanya bali kinachozingatiwa ni nia yake ndio ilimfanya kuingia Motoni.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Tafsiri ya Aayah:

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

62

قل إن صلاتي ونسكي

”Sema (ee Muhammad Hakika Swalaah yangu, na“ :(صلى اهللا عليه وآله وسلم Nusukiy... ” (al-An´aam06:162-163)

2. Tafsiri ya Aayah:

رحانو بكرل لفص

”Basi swali kwa ajili ya Mola wako na (pia ukichinja) na chinja (kwa ajili Yake).” (at-Takaathur 108:02)

3. Kuanza kulaaniwa mwenye kuchinjia kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.

4. Kulaaniwa kwa mwenye kuwalaani wazazi wake wawili. Kunaingia vile vile ambayeanatukana wazazi wa mtu mwingine kisha mtu huyo naye akakutukania wazazi wako.

5. Kulaaniwa kwa yule mwenye kumpa himaya mzushi, ni mtu ambaye kazusha kituambapo ni wajibu haki ya Allaah akatafuta himaya kwa mtu kutokana na hilo (asipeweadhabu anayostahiki).

6. Kulaaniwa kwa mwenye kubadili alama ya kiwanja, ni mipaka inayotofautisha baina yahaki yako ya kiwanja na haki ya jirani yako, ukaibadilisha sawa iwe kwa kuisogeza kwambele au kwa kuirudisha nyuma.

7. Tofauti kati ya kumlaani mtu binafsi na kulaani watu wa maasi kwa njia ya ujumla.

8. Kisa kikubwa cha nzi.

9. Mtu yule aliyelitolea Swadaqah sanamu aliingia Motoni kwa sababu ya ile nzi ambayohakuwa ameikusudia isipokuwa alifanya hivyo ili asalimike na shari yao.

10. Utambuzi wa kiwango cha jinsi ya kuichukia Shirki ni katika nyoyo za waumini, angaliajinsi mtu huyo alivyostahamili juu ya kuua lakini (pamoja na hivyo) hakukubaliana nao juuya maombi yao. Pamoja na kwamba hawakuwa wamemuomba jengine zaidi isipokuwakitendo cha nje.

11. Mtu yule aliyeingia Motoni alikuwa ni Muislamu kwa kuwa lau angelikuwa ni kafiri basiMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asingelisema: “Aliingia Motoni kwa sababu yanzi.”

12. Kuna ushahidi wa uthibitisho wa Hadiyth Swahiyh: “Pepo iko karibu zaidi na mmojawenu zaidi kuliko kambla za viatu vyake, na Moto ni kali kadhalika.”

13. Matendo ya kimoyo ndio makusudio yanayolengwa, hata kwa waabudu masanamu.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

63

Mlango Wa 11

Hakuchinjwi Kwa Ajili Ya Allaah Mahali Ambapo Kunachinjiwa Kwa AjiliYa Asiyekuwa Allaah

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

لا تقم فيه أبدا ى التقوى من أول يوم أحق أن تقوم فيهلمسجد أسس عل◌ فيه رجال يحبون أن يتطهروا◌ ◌ بحي اللـهوطهرينالم

”Usisimame (Msikitini) humo kamwe. Bila shaka Msikiti ulioasisiwa juu yataqwa (Masjid Qubaa) tokea siku ya kwanza unastahiki zaidi usimame humo.Humo mna watu wanaopenda kujitwaharisha (madhambi yao) Na AllaahAnapenda wanaojitwaharisha.” (at-Tawbah 09:108)

Kutoka kwa Thaabit bin adh-Dhwahhaak (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Kuna mtu aliweka nadhiri ya kuchinja mahali kunapoitwa Buwaanah,akamuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu hilo. Akasema:“Je, mahali hapo kulikuwepo sanamu lolote katika masanamu ya Ujaahiliyyah[kabla ya kuja Uislamu] likiabudiwa?” Akasema: “Hapana.” Akasema (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam): “Je, kulikuwepo sikukuu yoyote iliyofanywakatika sikukuu zao?” Akasema: “Hapana.” Akasema Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Tekeleza nadhiri yako. Kwani hakikahakuna kutekeleza nadhiri katika kumuasi Allaah, wala katika kitu ambachomwanaadamu hakimiliki.”40

(Kaipokea Abuu Daawuud, na isnadi yake iko kaatika masharti yauhakikishaji wa al-Bukhaariy na Muslim)

40 Shaykh Fawzaan anasema: ”Mfano wa nadhiri hii ni kama mtu kuweka nadhiri ya kuacha mtumwahuru nawe huna mtumwa wala humiliki mtumwa yoyote.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

64

Ufafanuzi:Mlango huu unafuatiwa na mlango wa kabla yake ambao ulizungumzia kuchinja kwa ajiliya asiyekuwa Allaah kuwa ni haramu na Shirki. Na mlango huu kuna kufunga njia kwakuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Hata kama mtu atachinja kwa ajili ya Allaah, haijuzukwake kuchinja kwa ajili ya Allaah mahali ambapo kunachinjiwa kwa ajili ya asiyekuwaAllaah. Kwa kuwa kuchinja mahali kama hapa – hata kama itakuwa kwa ajili ya Allaah – ninjia inayopelekea katika Shirki. Hali kadhalika kuchinja mahali kama hapa nikupaadhimisha na kusaidiana na washirikina. Kama jinsi alikataza Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) njia zingine zinazopelekea katika Shirki, kwa mfano kukataza kwakekuswali makaburini hata kama mwenye kuswali haswali ila ni kwa ajili ya Allaah, kuombaDu´aa makaburini n.k., haijuzu kwa kuwa sehemu kama hizi siyo za kufanyia ´Ibaadah. Halikadhalika kakata kuswali wakati wa kuchomoza jua, kwa kuwa ni njia inayopelekeakuliabudu. Kwa kuwa washirikina walikuwa wakifanya hivi. Kakataza hali kadhalikakuswali wakati wa kuzama kwa jua, kwa kuwa washirikina walikuwa wakilisujudialinapozama.

Aayah ya Suurat at-Tawbah: Sababu ya kuteremka Aayah hii ilikuwa pindi wanafikiwalipomuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aje kuswali kwenye Msikitiambao walikuwa wamejenga, Masjid ad-Dhwiraar. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)alikuwa na safari ya kwenda katika vita vya Tabuuk, akawaambia nikirejea nitakuja kuswalihumo. Aliporejea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka Tabuuk ndio AllaahAkawa Ameteremsha Aayah hii kumteremshia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam). Na makusudio yao wanafiki ilikuwa ni kuwakimbiza watu katika al-Masjid Quubana kuwafarakanisha Waislamu ambapo walikuwa wamekusanyika katika Masjid al-Quuba.Na namna hii wanakuwa wasaidizi wa Shaytwaan kila siku, kutaka kuwafarakanishaWaislamu. Hivyo, katika Aayah hii, kama jinsi Allaah (Ta´ala) Alivyomkataza Mtume Wake(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuswali kwa ajili ya Allaah mahali ambapokumetayarishwa kwa ajili ya kumuasi Allaah, basi vile vile haijuzu kuchinja kwa ajili yaAllaah mahali ambapo pametayarishwa kwa ajili ya maasi. Aayah hii iko wazi.

Hadiyth ya Thaabit bin adh-Dhwahhaak: Katika Hadiyth hii kuna dalili mahali ambapokulikuwa sanamu likiabudiwa badala ya Allaah au sikukuu za Kijaahiliyyah, haijuzukupafanyia ´Ibaadah kukiwemo kuchinja, bali inatakiwa kupakata na kupasusa. Kwa kuwahii ni njia inayopelekea katika Shirki.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Kauli Yake:

لا تقم فيه أبدا

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

65

”Usisimame (Msikitini) humo kamwe.” (at-Tawbah 09:108)

2. Maasi yanaweza kuathiri katika ardhi kama ambavyo utiifu unaweza kufanya halikadhalika.

3. Kuyarudisha masuala ya matatizo katika masuala yaliyo wazi ili utata utoweke.

4. Muftiy kuuliza maelezo itapohitajika kufanya hivyo.

5. Kutenga mahali maalum pakutekelezea nadhiri hakuna ubaya ikiwa hakuna makatazoyoyote ya kufanya hivyo.

6. Makatazo ya kutekeleza nadhiri mahali, ikiwa kulikuwepo sanamu katika masanamu yaUjaahiliyyah likiabudiwa hata kama (kitendo hicho) kiliisha kwa muda mrefu.

7. Makatazo ya kutekeleza nadhiri mahali, ikiwa kulikuwepo sikukuu katika sikukuu zao(washirikina) hata kama (kitendo hicho) kilisimamishwa kwa muda mrefu.

8. Nadhiri haijuzu kuitekeleza katika sehemu kama hizi kwa kuwa hii ni nadhiri ya maasi.

9. Tahadhari ya kujifananisha na makafiri katika sikukuu zao hata kama mtu hakukusudiahivyo.

10. Hakuna nadhiri katika kumuasi Allaah.

11. Hakuna nadhiri kwa mwanaadamu kwa asichokimiliki.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

66

Mlango Wa 12

Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah Ni Katika Shirki

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

يوفون بالنذر ويخافون يوما كان شره مستطريا

”(Ambao) Wanatimiza nadhiri (zao), na wanaiogopa siku ambayo shari yakeni yenye kuenea.” (al-Insaan 76:07)

Na Kauli Yake:

فإن اللـه يعلمهوما أنفقتم من نفقة أو نذرتم من نذر

”Na chochote mtoacho katika matumizi au mkiwekacho nadhiri katika nadhiri,basi Allaah Anakijua.” (al-Baqarah 02:270)

Katika Swahiyh (al-Bukhaariy), kapokea ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) yakwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Mwenye kuweka nadhiri ya kumtii Allaah, amtii; na mwenye kuwekanadhiri ya kumuasi Allaah, asimuasi.”

Ufafanuzi:Hii ni katika aina ya Shirki kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu. Kisha akaweka Aayahmbili kuonesha dalili ya kwamba kumuwekea nadhiri asiyekuwa Allaah ni katika Shirki.Shaykh haongei kitu pasina dalili, kila anapoongelea kitu anakitolea dalili. Ni kwa ajili yakukithiri kwa jambo hili leo, mpaka imefikia watu leo wanawawekea maiti nadhiri nakusema maiti hawa wanakubali nadhiri. Ndio maana Shaykh akapenda kuonya hili.

Nadhiri kilugha ni kuilazimisha nafsi yaki kitu fulani. Ama Kishari´ah nadhiri nikujilazimisha kunakokalifisha kwa kitu ambacho mtu atakifanya. Mwenye kuweka nadhirianailazimisha nafsi yake kwa nadhiri hii kuifanya. Au Kishari´ah mtu anaweza kusema piakuwa ni kujilazimisha kunakokalifisha kwa kufanya ´Ibaadah ambayo Allaah

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

67

Hakumlazimishia juu yake. Bali mtu ndio kajiwajibishia mwenyewe. Nadhiri imegawanyikasehemu mbili:

- Nadhiri ya utiifu.

Na hii ni ´Ibaadah kwa Allaah (´Azza wa Jalla).

- Nadhiri ya maasi.

Na hii ni kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla).

Allaah Kawasifia wale ambao wanatimiza nadhiri zao pale ambapo wanapoweka nadhiri. Nidalili kuonesha kuwa kutimiza nadhiri ni ´Ibaadah ya ujira mkubwa. Na nadhiri ya utiifuikishakuwa ni ´Ibaadah, kumfanyia mwengine badala Yake inakuwa Shirki. Kwa kuwa´Ibaadah haijuzu kumfanyia mwengine badala ya Allaah (Ta´ala) Pekee. Kama jinsi haijuzukuswali, kutoa Swadaqah, kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, basi ni hali kadhalika nanadhiri. Haijuzu kumuekea nadhiri asiyekuwa Allaah.

Katika Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) kuna dalili ya kwamba nadhiri zikoaina mbili; nadhiri ya utiifu na nadhiri ya maasi. Na hapa kuna dalili ya kwamba nadhiri ni´Ibaadah na inakuwa utiifu. Na ni jambo lenye kuchukiza kwa mtu kuanza kujiingiza katikanadhiri. Kwa nini? Kwa kuwa anakuwa ameilazimisha nafsi yake kwa kitu ambacho huendakikamkuwia kizito kwake au asiweze kabisa na Allaah Alikuwa Hakumlazimisha kwacho,bali yeye mwenyewe ndie kajilazimisha nafsi yake. Hivyo kujiingiza katika nadhiri ni jambolenye kuchukiza. Lakini ikiwa atajiingiza kwenye nadhiri ni wajibu kwake kuitimiza. Amaikiwa ni nadhiri ya maasi hatakiwi kuifanya.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Uwajibu wa kutimiza nadhiri.

2. Ikishathibiti ya kuwa kumuwekea Allaah nadhiri ni kumuabudu Allaah, kumuwekeaasiyekuwa Allaah ni Shirki.41

3. Nadhiri ya maasi haijuzu kuitimiza.

41 Shaykh anasema: ”Na nukta hii ndio ilikuwa makusudio ya Aayah na Hadiyth za mlango huu. Yakwamba nadhiri ikishakuwa ni utiifu kwa Allaah na ´Ibaadah, kumuwekea asiyekuwa Allaah niShirki. Yule anayewekea nadhiri kaburi, sanamu, fulani na fulani, huku ni kumshirikisha Allaah(Ta´ala).”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

68

Mlango Wa 13

Kutafuta Kinga Kwa Asiyekuwa Allaah Ni Katika Shirki

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وأنه كان رجال من الإنس يعوذون برجال من الجن فزادوهم رهقا

”Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa watu wanajikinga nawanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia mzigo (wa madhambina kufru).” (al-Jinn 72:06)

Kutoka kwa Khawlah bint Hakiym (Radhiya Allaahu ´anha) kasema,nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Yeyote atakayeingia kwenye nyumba na kusema42: “A´uudhuBikalimatillaah-it-Taammati min sharri maa Khalaq” (Najikinga kwa Manenoya Allaah yaliyotimia na maovu Aliyoyaumba), hakitomdhuru kitu mpakaatapoondoka mahala hapo).

(Kaipokea Muslim)

Ufafanuzi:Katika aina za Shirki ni kutafuta kinga kwa asiyekuwa Allaah. Kwa kuwa kujikinga ni´Ibaadah. Kujikinga ni kurejea na kushikamana na Allaah (Ta´ala) ili Akuhifadhi na shari yamaadui wako na yale unayochelea yasikudhuru. Hivyo kujikinga ni aina katika aina za´Ibaadah. Hali kadhalika kutafuta kinga kwa Maneno ya Allaah ni ´Ibaadah, kwa vile ni Sifakatika Sifa za Allaah (Ta´ala). Hivyo yule mwenye kuomba kinga badala ya Allaah, basikamshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla). Kama wale wenye kujikinga kwa watu sawa aliye haiau maiti, mtu kama huyu atakuwa amemshirikisha Allaah Shirki kubwa. Ama walewanaojikinga kwa makaburi, majini, Mashaytwaan, hii ni Shirki kubwa inayomtoa mtukatika Uislamu.

42 Wakati wa kuingia

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

69

Katika Aayah ya al-Jinn tunapata kujifunza ya kwamba kujikinga kwa jini au kitu kinginechochote badala ya Allaah ni Shirki.

Mtu anapoingia nyumba anatakiwa kusoma Du´aa hii iliotajwa na Mtume (´alayhis-Salaam).Ama wale wanaoingia nyumba au mahali mpya wanachinja mnyama kuwachinjia majini iliwasalimike na shari yao, kisha wanachukua damu ya mnyama huyo na kuimwagia kuta. Hiini Shirki kubwa. Hivyo inajuzu kujikinga kwa Maneno ya Allaah ambayo ni Qur-aan. Nahayakuumbwa kama wasemavyo Jahmiyyah. Kwa kuwa yangelikuwa yameumbwaingelikuwa haijuzu kujikinga nayo. Kwa kuwa kujikinga kwa kiumbe ni Shirki na walahaijuzu. Ni dalili ya kwamba Qur-aan haikuumbwa na ni katika Sifa za Allaah (Ta´ala).

Masuala muhimu yaliyomo:1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Jinn. (72:06)

2. Kutafuta kinga kwa asiyekuwa Allaah ni katika Shirki.

3. Kutumia Hadiyth hii kama dalili; kwa kuwa wanachuoni wanaitumia dalili ya kwambaManeno ya Allaah Hayakuumbwa. Wakasema ni kwa sababu kutafuta kinga kwa viumbe niShirki.43

4. Fadhila za Du´aa hii pamoja na ufupi wake.

5. Kule mtu kufikia manufaa ya kitu cha kudunia, kama kujizuia kutopatwa na madhara aukuleta manufaa sio dalili ya kwamba (ulichokifanya) sio katika Shirki.

43 Shaykh anasema: ”Hii ni katika dalili ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ya kwamba Qur-aan niManeno ya Allaah. Yameteremshwa na hayakuumbwa. Kuna Radd kwa Jahmiyyah na Mu´tazilahwanaosema kuwa Qur-aan imeumbwa.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

70

Mlango Wa 14

Kutaka Msaada Kwa Asiyekuwa Allaah Au Kumuomba Asiyekuwa Yeye NiKatika Shirki

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

كرضلا يو كنفعا لا يم اللـه ونن دم عدلا تو ◌نيمالظال نإذا م كفإن لتإلا فإن فع له فر فلا كاشبض اللـه كسسمإن يووه ◌هلفضل ادر فلا ريبخ كردإن يو ◌شن يم به يبصيهادبع ناء م ◌وهويمحالر فورالغ

“Na (nimeamrishwa pia kwamba): Wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa(ukimwabudu) na wala asiyekudhuru (usipomwabudu). Na ukifanya (hivyo),basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu. Na Allaah Akikugusishadhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye. Na (Allaah) Akikutakiakheri, basi hakuna wa kurudisha fadhila Yake, Anamsibu kwazo (fadhilaZake) Amtakaye katika waja Wake. Naye ni Al-Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wakughufiria - Mwenye kurehemu).” (Yuunus 10:106-107)

Na Kauli Yake:

وهدباعو قالرز اللـه ندوا عغتفاب

”Basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni (Yeye).” (al-Ankabuut 29:17)

Na Kauli Yake:

ع مهو ةاميم القوإلى ي له جيبتسن لا يم اللـه ونن دو معدن يمل مأض نملونوغاف همائعاء ن ددأع موا لهكان اسالن رشإذا حورينكاف همتادبوا بعكانو

”Na nani aliyepotea zaidi kuliko yule anayemwomba badala ya Allaah ambaohatowaitikia mpaka Siku ya Qiyaamah; nao hawatambui du’aa zao. Nawatakapokusanywa watu (Siku ya Qiyaamah; walioombwa) watakuwamaadui wao, na watakanusha ‘ibaadah zao.” (al-Ahqaaf 46:05-06)

Na Kauli Yake:

أمن يجيب المضطر إذا دعاه ويكشف السوء ويجعلكم خلفاء الأرض ـه مع ال◌ لـهأإل قليلا ما تذكرون◌

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

71

”(Wanaowashirikisha ni bora) Au Yule Anayemuitika mwenye dhikianapomwomba, na Akamuondoshea uovu (dhiki), na Akakufanyenimakhalifa wa ardhi? Je, yuko mungu (mwengine) pamoja na Allaah?(Hapana!) Ni machache (mno) mnayokumbuka (na mkapata kuzingatia).” (an-Naml 27:62)

at-Twabaraaniy kapokea katika isnadi yake:

“Katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kulikuwepomnafiki akiwaudhi Waislamu, baadhi yao44 wakasema: “Simamenitumuendee Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumtakamsaada kutokana na mnafiki huyu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)akasema: “Hakika, mimi siye niombwae msaada, isipokuwa msaadaanaombwa Allaah (Pekee).”

Ufafanuzi:Shirki inayokusudiwa hapa ni Shirki kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu na inaharibu´amali zote za mtu na kumweka mwenye nayo Motoni milele. Na katika aina zake ni mtukumuomba asiyekuwa Allaah; katika waliohai au ambao wameshakufa. ´Ibaadah haisihikumfanyia badala ya Allaah; sawa katika Malaika, Mitume, mawalii, watu wema, miti,mawe, makaburi na kadhalika.

Katika Suurat Yuunus Allaah Anamkataza Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kuomba mwengine badala ya Allaah. Na makatazo haya ni kwake yeyena kwa Ummah wake pia. Kisha Akamwambia ukifanya hivyo wewe utakuwa katikamadhalimu. Dhuluma imegawanyika sehemu tatu:

- Dhuluma ambayo ni kumshirikisha Allaah.

- Dhuluma ya kumdhulumu mtu mwengine.

- Dhuluma ya kuidhulumu nafsi yako kwa kufanya maasi.

Allaah Anasema katika Suurat al-Ahqaaf: “Ni nani aliyepotea zaidi...”, yaani hakuna yeyotealiyepotea zaidi isipokuwa ni mshirikina. Allaah Atukinge. Shirki ndio upotofu mkubwa. “...ambao hatawaitikia mpaka siku ya Qiyaamah” hii ni kwa sababu hawezi kuwaitikia.

44 Waislamu

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

72

وا لكمابجتا اسوا معمس لوو اءكمعوا دعمسلا ي موهعدإن ت

”Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, basi (wasingeliweza) kukujibuni.”(Faatwir 35:14)

Unamuomba mtu ambaye ni dhaifu na hana uwezo kuliko wewe. Ni maiti. Wewe nimwenye uwezo kuliko yeye. Haya ni maajabu. Lau utamuomba mpaka siku ya Qiyaamahkamwe hatokuitikia. Hivyo hakuna haja kabisa ya kumuomba kwani si muweza wa lolote.Kwa nini washindwa kumuomba Muweza Ambaye ni Allaah (´Azza wa Jalla) na badalayake unawaomba wasioweza kukusaidia kwa lolote? “na watakanusha ´Ibaadah zao”makusudio hapa ni Du´aa. “Na watakanusha ´Ibaadah zao” yaani Du´aa zao. Hii ni dalili yakwamba kumuomba (Du´aa) asiyekuwa Allaah ni ´Ibaadah, na yule mwenye kumuombamwengine badala ya Allaah kashirikisha. Hivyo ikiwa Du´aa ni ´Ibaadah, haijuzu kufanyiwamwengine asiyekuwa Allaah (Ta´ala).

Suurat an-Naml hapa Allaah Anawapa changamoto washirikina kwa kuwaambia kwa niniwakati wa shida na dhiki wanamtakasia ´Ibaadah Yeye na wakati wa raha wanamshirikisha?“Au Yule Anayemuitikia mwenye dhiki” hii ndio maana ya al-Istighaathah. Wakati wa dhikina shida walikuwa wakiyasahau masanamu yao na kumtakasia ´Ibaadah Allaah Pekee?.Masanamu yao yote yalikuwa hayawezi kuwasaidia kwa lolote wanapopatwa na shida. Kwadalili walikuwa ni wenye kumkimbilia Allaah na kumtakasia ´Ibaadah Yeye Pekee.Hawakusema kuwa ni masanamu yao, miti, mawe n.k. Du´aa ni haki ya Allaah Pekee sawawakati wa shida na wakati wa raha. Lakini tatizo watu hawa washirikina wanaoabudumakaburi, maiti, masanamu n.k. Qur-aah hawaizingatii. Wanaisoma tu kwa masauti mazurina kuihifadhi lakini hawaizingatii kabisa. Na ndio maana Allaah Kawaambia ni machachemnayoyakumbuka.

Hadiyth hii ambayo imepokelewa na at-Twabaraaniy yasemekana kuwa ni ´Abdullaah bin´Ubayd ambaye alikuwa ni kiongozi wa wanafiki. Walienda kumuomba Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) kwa kuwa walikuwa wanajua anaweza kuwasaidia kumkataza,kumuua n.k. kutokana na nafasi alionayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)alikuwa na uwezo wa kuwasaidia, lakini alikirihika na matamshi haya yakuombwa/kutakwa msaada. Hivyo alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatakakuwafunza Waislamu kutumia matamshi mazuri. Kwa kuwa ukifunguliwa mlango wakuombwa msaada viumbe kwa mambo wayawezayo, hii ni njia inayopelekea katika mamboambayo hawayawezi isipokuwa Allaah Pekee. Huku ni katika kufunga njia ambazozinapelekea katika Shirki. Hivyo kutumia lafdhi hii ya al-Istighaathah kuomba au kutakamsaada kutoka kwa mtu isitumiwe. Sawa ikiwa ni msaada mkubwa au mdogo.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

73

Masuala muhimu yaliyomo:1. Kuambatanisha Du´aa na al-Istighaathah kuomba msaada kupitia ushirikiano niuambatanisho wa jumla ya mambo kwa jambo lililo maalum.

2. Tafsiri ya Kauli Yake (Ta´ala):

كرضلا يو كنفعا لا يم اللـه ونن دم عدلا تو

“Na (nimeamrishwa pia kwamba): Wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa(ukimwabudu) na wala asiyekudhuru (usipomwabudu).” (Yuunus 10:106)

3. Kuwa hii ni Shirki kubwa.

4. Mtu aliyepotea zaidi ni yule anayemwomba asiyekuwa Allaah, basi mtu huyo kawa katikamadhalimu.

5. Tafsiri ya Aayah iliyo baada yake. (10:107)

6. Kumwomba asiyekuwa Allaah halinufaishi duniani, pamoja na kuwa ni kufuru.

7. Tafsiri ya Aayah. (29:17)

8. Riziki haitafutwi isipokuwa kutoka kwa Allaah, kama jinsi Pepo haitafutwi kutoka kwayeyote isipokuwa Kwake.

9. Tafsiri ya Aayah. (46:05)

10. Hakuna mpotevu zaidi kuliko yule anayemwomba asiyekuwa Allaah.

11. Anayeombwa hatambui Du´aa ya mwombaji.

12. Maombi hayo itakuwa ni sababu ya mwombwaji kumchukia muombaji na kumfanya niadui.

13. Maombi hayo yameitwa kuwa ni (kumfanyia) ´Ibaadah mwombwaji.

14. Mwombwaji atakanusha ´Ibaadah hiyo aliyofanyiwa.

15. Du´aa hii ndio sababu ya kuwa kwake mpotevu zaidi katika watu.

16. Tafsiri ya Aayah. (27:62)

17. Jambo la ajabu ambalo ni kukiri kwa waabudu masanamu ya kuwa hakunaanayemwitika mwenye dhiki anapomwomba isipokuwa ni Allaah. Kwa ajili hii, ndio maanawalikuwa wakimuomba wakati wa shida ilihai ni wenye kumtakasia Yeye Dini.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

74

18. Himaya ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuihami Tawhiyd na kuwa makini(kumuadhimisha) na Allaah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

75

Mlango Wa 15

Kauli Ya Allaah Ta´ala

صرا ولا أنفسهم ينصرونولا يستطيعون لهم نأيشركون ما لا يخلق شيئا وهم يخلقون

”Je, wanawashirikisha (na Allaah) wale ambao hawaumbi kitu na hali waowameumbwa? Na wala hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusurunafsi zao.” (al-A´raaf 07:191-192)

Kauli Yake:

ونهن دون معدت ينالذريوطمن قكون ملما يموا لكمابجتا اسوا معمس لوو اءكمعوا دعمسلا ي موهعدإن ت ويوم القيامة يكفرون ◌كمكربش ولا ينبئك مثل خبري◌

“Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki (hata) kijiwavu cha kokwa yatende. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, basi(wasingeliweza) kukujibuni. Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikinawenu, na wala hakuna atakayekujulisha kama Khabiyr (Mjuzi wavilivyodhahiri na vilivyofichikana).” (Faatwir 35:13-14)

Imepokewa katika Swahiyh (al-Bukhaariy) ya kwamba Anas (RadhiyaAllaahu ´anhu) kasema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipasuliwa siku ya Uhud nayakavunjwa meno yake mane. Akasema: “Vipi watafaulu watu ambaowamempasua Mtume wao?” Kukateremka:

ليس لك من الأمر شيء

”Si juu yako (ee Muhammad ”.katika amri (kuamua) lolote (صلى هللا علیھ وآلھ وسلم(al-´Imraan 03:128)

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) pia:

“Nilimsikia Mtume wa Allah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisemawakati akiinua kichwa chake kutoka katika Rukuu katika Rakaa ya mwisho ya

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

76

Swalah ya Fajr: “Ee Allaah Mlaani fulani na fulani!” baada ya yeye kusema´samiya Allaahu liman hamidah – Rabbanaa walakal hamd.45 AllaahAkateremsha:

ليس لك من الأمر شيء

”Si juu yako (ee Muhammad ”.katika amri (kuamua) lolote (صلى هللا علیھ وآلھ وسلم(al-´Imraan 03:128)

Na katika upokezi mwingine:

“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwaombea Swafwaan bin´Umayyah, Suhayl bin ´Amr na al-Haarith bin Hishaam.” Halafukukateremka:

ليس لك من الأمر شيء

”Si juu yako (ee Muhammad ”.katika amri (kuamua) lolote (صلى هللا علیھ وآلھ وسلم(al-´Imraan 03:128)

Imepokelewa pia katika Swahiyh al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa AbuuHurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) ambaye amesema:

“Alisimama Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakatialipoteremshiwa: “Na onya jamaa zako wa karibu (ee Muhammad صلى اهللا عليه وآله “(وسلم (ash-Shu´raa 26:214) na akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Enyi Quraysh - au neno lenye kufanana na hilo! Ziuzeni nafsi zenu (kwaImani na kumuabudu Allaah Pekee), sintokutoshelezeeni kwa Allaah nachochote. Ewe ´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib sintokutosheleza kwa Allaah nachochote. Ewe Swafiyyah mama mdogo wa Mtume wa Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sintokutosheleza kwa Allaah na chochote.Ewe Faatwimah bint Muhammad! Niombe chochote katika mali yanguutakacho, sintokutosheleza kwa Allaah na chochote.”

45 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa kuna dalili ya kujuzu kwa Qunuut wakati kumetokea jangakatika mji. Ama wakati usiokuwa wa janga haijuzu bila kujali wale waliojuzisha, kwa kuwahaikuthibiti kwa Mtume (´alayhis-Salaam) kukunuti daima katika Swalah ya Fajr isipokuwa wakatiwa janga peke yake. Na kuna dalili ingine ya kujuzu kumlaani mtu (kafiri) binafsi. Na kuna dalili yakujuzu kumlaani (kafiri) ndani ya Swalah.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

77

Ufafanuzi:Baada ya Shaykh kutaja dalili katika milango iliyopita aina za Shirki wanazofanya watuwengi, katika mlango huu kataja dalili za ubatili wa Shirki kwa sampuli zake zote. Kwakuwa Shirki ni uongo. Na uongo haujengeki isipokuwa juu ya uongo mwengine. AmaTawhiyd – kwa kuwa ni haki na ni kweli – imejengeka juu ya dalili na hoja. Tawhiyd ndioimejengeka juu ya dalili za Qur-aan na Sunnah.

Kila kinachoabudiwa badala ya Allaah; sawa awe ni Malaika, Mitume, watu wema, mawe,miti n.k. vyote haviwezi kuumba kitu. Hakuna awezae kuumba hata nzi tu. Na kilekisichoweza kuumba haistahiki kukiabudu. Mwenye Kuumba Ndiye Ambaye Anastahiki´Ibaadah. Katika Aayah ya al-A´raaf kataja dalili nne za ubatili wa Shirki:

- Ya kwanza ni kwa sababu hao wanaoombwa hawawezi kuumba kitu. Na yuleasiyeweza kuumba hastahiki kuabudiwa.

- Ya pili ni kwamba wameumbwa. Na kiumbe hawezi kuwa mshirika wa Allaah.- Ya tatu ni kwamba hawawezi kumnusuru yule anayewahitajia wakati wa shida.

Hivyo asiyeweza kukunusuru faida iko wapi ya kumuomba?- Ya nne ni kwamba hawawezi kujinusuru wao wenyewe.

Hii ni Aayah moja tu tunapata faida zote hizi. Lakini je, akili zao (washirikina) ziko wapi?

Na katika Aayah ya al-Faatwir Kasema hao wanaowaomba badala ya Allaah hawamilikihata kijiwavu cha kokwa ya tende. Isitoshe wanapowaomba hawasikii maombi yao. Vipiutamuomba mtu asiyekusikia? Faida iko wapi? Na lau hata wakiwasikia hawawezikuwaitikia. Na dalili ya nne siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wao na kuwafanyani maadui. Hizi ni dalili za ubatili wa Shirki. Na hakuna mshirikina hata mmoja anayewezakupinga dalili hizi na kuzikanusha. Allaah Kawapa changamoto na hoja imewasimamia.

Katika Aayah ya Suurat al-´Imraan Allaah Anamkemea Mtume Wake (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kwamba si juu yake katika amri lolote kwa Kujua Kwake (Allaah) yakwamba watu hawa watatu watakuja kusilimu baadae. Na wakasilimu kweli. Hapa kitumuhimu tunachopata kujifunza ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si juuyake kuamua lolote na wala hana haki yoyote ile katika ´Ibaadah. Ikiwa Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) hana haki yoyote katika ´Ibaadah vipi kwa asiyekuwa yeye? Nakuna dalili ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajui mambo ya Ghayb(yaliyofichikana). Ikiwa hali ni hivyo basi hastahiki kuabudiwa kabisa.

Katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) tunapata kujifunza ya kwambamtu asitegemee ukaribu au udugu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

78

utamuokoa Siku ya Qiyaamah. Hakuna kitachomuokoa mtu mbele ya Allaah zaidi ya ´amalizake mwenyewe. Vipi kwa yule mtu mwenye Qaswiydah ya Shirki ya Burdaa (inayosomwakatika Maulidi pia) – Allaah Amuangamize - ambaye anadai na kusema kuwa kwa vile nayeanaitwa Muhammad basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atamsaidia siku yaQiyaamah? Ikiwa hawezi kuwasaidia ndugu zake vipi atakusaidia wewe? Huyu ni ujingamkubwa. Allaah Atukinge.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah mbili. (07:120) na (35:13-14)

2. Kisa cha Uhud

3. Qunuut ya kiongozi wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya Swalah naMaswahabah kuitikia “Aamiyn”.

4. Ambao alikuwa anawaombea dhidi yao (Mtume) walikuwa ni makafiri.46

5. (Quraysh) walifanya mambo ambayo hawakufanya wengi katika makafiri; miongonimwayo ni kusababisha Mtume wao kupasuliwa na kutaka kumuua ingawa walikuwa nibinamu zake.

6. Allaah (Ta´ala) Akaremsha kwa hilo:

ليس لك من الأمر شيء

”Si juu yako (ee Muhammad ”.katika amri (kuamua) lolote (صلى هللا علیھ وآلھ وسلم (al-´Imraan03:128)

7. Kauli Yake (Ta´ala):

مهبذعي أو همليع وبتي أو

”(Bali ni juu ya Allaah) au Apokee tawbah yao, au Awaadhibu... ”(al-´Imraan 03:128)

8. Kujuzu kwa Qunuut wakati wa kupatwa na janga.

9. Kuwaita kwa majina yao wale aliokuwa akiwaombea dhidi yao kwa majina yao na majinaya baba zao ndani ya Swalah.

10. Kumlaani mtu binafsi katika Qunuut.

11. Kisha chake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Alipoteremshiwa:

46 Shaykh Fawzaan: ”Mtume (´alayhis-Salaam) hakuwa anajua kama watakuja kusilimu baadae.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

79

بنيالأقر كتريشع رأنذو

”Na onya jamaa zako wa karibu (ee Muhammad ”.(صلى اهللا عليه وآله وسلم (ash-Shu´raa 26:214)

12. Kuonesha uzito wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika jambo hili kwa kulekufanya jambo ambalo lilipelekea akaitwa kuwa ana wendawazimu, na hali itakuwa hivohivo lau Muislamu atafanya hivyo leo.47

13. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaambia watu wake wa karibu nandugu zake akiwemo Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anha): “Sintokutoshelezeni mbele yaAllaah kwa lolote.” Ikiwa kaweka hili wazi naye ndio kiongozi wa Mitume ya kwambahatomtosheleza mbora wa wanawake duniani, na mtu akaamini ya kwamba hasemi kitu(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa haki tupu, kisha uangalie yanayotokea katikanyoyo za watu wa leo, itakubainikia kwako suala la Tawhiyd na ugeni wa Dini.

47 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa ni wakati alipowaita ma-Quraysh na kuwanadi kwa sauti yake,wakamsifu kuwa ana wendawazimu na kusema kuwa ni mwendawazimu.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

80

Mlango Wa 16

Kauli Ya Allaah Ta´ala

كمباذا قال رقالوا م ن قلوبهمع ى إذا فزعتح ◌ققالوا الح ◌الكبري يلالع وهو

”Mpaka itakapoondolewa khofu nyoyoni mwao; watasema: “Amesema niniMola wenu?” Watasema: (Amesema): “Ya haki”; Naye ni Al-’Aliyyul-Kabiyr (Mwenye ‘uluwa Yuko juu ya vyote - Mkubwa wa dhati vitendo nasifa).” (Sabaa´ 34:23)

Katika Swahiyh (al-Bukhaariy) kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu´anhu) kapokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaaahu ´alayhi wa sallam) yakwamba kasema:

“Allaah Anapotoa amri huko juu ya mbingu Malaika hupiga mbawa zao kwakunyenyekevu amri48 Yake, kama vile sauti ya mnyororo juu ya jiwe.49

Huwapita amri hiyo hali wamezimia, mpaka inapoondolewa ile khofukwenye nyoyo zao wanasema: “Kasema nini Mola Wenu?” Wanasema:(Amesema): “Ya haki”; Naye ni Al-’Aliyyul-Kabiyr (Mwenye ‘uluwa Yuko juuya vyote - Mkubwa wa dhati vitendo na sifa).” (Sabaa´ 34:23) Husikia Nenohilo wale waibao kusikia na hawa wenye kuiba kusikia wanakuwa namna hii,hawa juu ya hawa. Alitaja sifa hii Sufyaan bin ´Uyaynah kwa kuipigia mfanokiganja chake alikigeuza na kupanua baina ya vidole vyake. Wenye kuibakusikia husikia neno ambalo huliagiza50 kwa aliye chini yake, kisha huyomwingine humuagizia aliye chini yake mpaka humfikishia kuhani au mchawi.Wakati mwingine humpata kimondo kabla ya kuifikisha, na wakati mwinginehuenda akaifikisha kabla ya kimondo hicho kumpata, huongezewa neno hilo51

uongo mia moja. Kunasemwa: “Kwani sialitwambia hivi na hivi siku kadhaana kadhaa?” Husadikishwa kwa neno hilo alilolisikia kutoka mbinguni.”

48 Kauli Yake (Ta´ala)49 Jiwe gumu sana kabisa50 Au humpasia neno hilo51 Na Shaytwaan

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

81

Kutoka kwa an-Nawwaas bin Sam´aan (Radhiya Allaahu ´anhu) ambayekasema, kasema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Anapotaka Allaah (Ta´ala) kumfunulia mtu amri, Hutamka Neno kwaWahyi. Kutokana na hili, mbingu hutikisika sana – au alisema radi kali – kwakumuogopa Allaah (´Azza wa Jalla). Wanaposikia hilo52 watu wa mbingu,hufikwa na mshtuko na humuangukia Allaah kwa kusujudu. Wa kwanza waoambaye hunyanyua kichwa chao anakuwa ni Jibriyl ambaye AllaahHumuongelesha kwa Wahyi kwa Ayatakayo, kisha Jibriyl anawapitia Malaikawengine katika mbingu mbali mbali, na katika kila tabaka Malaika humuuliza:“Kasema nini Mola Wetu, ewe Jibriyl?” Jibriyl anasema: (Amesema): “Yahaki”; Naye ni Al-’Aliyyul-Kabiyr (Mwenye ‘uluwa Yuko juu ya vyote -Mkubwa wa dhati vitendo na sifa).” (Sabaa´ 34:23) na wote husema vilealivyosema Jibriyl. Jibriyl huishia kwa Wahyi Alipomuamrisha Allaah (´Azzawa Jalla).”

Ufafanuzi:Mlango huu ni kama milango iliotangulia. Kuna dalili ya ubatili wa Shirki na Radd kwawashirikina ambao wanawaabudu Malaika, Mitume na watu wema kwa kudai ya kwambawanawaombea na kuwa wanawakurubisha kwa Allaah.

Ikiwa hali ya Malaika inakuwa namna hii (khofu mpaka wanazimia), vipi wataombwapamoja na Allaah? Na ilihali Malaika ndio viumbe wa kwanza wakubwa mbinguni naardhini.

Hadiyth hizi mbili (ya Abuu Hurayrah na an-Nawaas) zinaifasiri Aayah ilio juu. Ya kwambaMalaika wanasibiwa na khofu kubwa wanaposikia Maneno ya Allaah.

Makuhani wanawatumia Mashaytwaan katika kuiba maneno mbinguni yanayosemwa. NaAllaah – kutokana na Hekima Yake – Kafanya hivi Shaytwaan kuweza kuiba yasemwayombinguni ili kuwapa majaribio waja Wake ni kina nani watakaowaamini hawa makuhani nawachawi. Na Shaytwaan anaposikia neno moja mbinguni, basi neno hilo limoja huliongezeajuu yake uongo mia. Ukweli unakuwa asilimia moja kwa mia. Huu ni mtihani wa Allaah

52 Neno la Allaah

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

82

kwa waja wake. Hata kama katika maneno yao kutakuwa kitu katika ukweli, haitakiwikuwasadikisha kabisa. Na ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Atakayemwendea kuhani na akamsadikisha kwa aliyoyasema kakufuru yalealiyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Na katika Swahiyh Muslim kapokea:

“Atakayemwendea kuhani, hazitokubaliwa Swalah zake kwa siku arubaini.”

Hapa kuna makatazo ya kumwendea kuhani, uwajibu wa kuwakadhibisha na chanzo wapiwanachukua mambo yao. Mitume (´alayhimus-Salaam) wao wanachukua Wahyi kutokakwa Allaah kwa ukaakati wa Jibriyl. Ama makuhani wanachukua mambo na maneno yaokutoka kwa Shaytwaan. Hivyo, si Malaika wala mwingine yeyote haijuzu kumuomba.

Katika Hadiyth hizi kuna dalili ya uthibitisho wa Maneno ya Allaah (Subhaanahu waTa´ala). Anaongea na Kusema. Radd kwa Jahmiyyah, Mu´tazilah na Ashaa´irah na kilaanayekubaliana nao katika madhehebu yao. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anaongea kwaManeno ya Kusikika kwa herufu na sauti kwa namna inayolingana na Ukubwa na UtukufuWake. Yule Asiyeweza kutamka wala kuongea hawezi kuwa Ilaah (mungu). Vipi Atawezakukuamrisha kitu Naye Haongei? ”Mwenye ‘uluwa Yuko juu ya vyote” Hali kadhalika kunauthibitisho wa al-´Uluw (kuwa juu kwa Allaah). Hivyo katika mlango huu kuna ubatili waShirki na dalili ya ubatili wake.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah. (34:23)

2. Hoja zilizomo kuhusu ubatili wa Shirki, na hususan yanayohusiana na kuwategemea watuwema. Na Aayah hii ndio inayosemekana ya kwamba inakata mizizi ya mti wa Shirkimoyoni.

3. Tafsiri ya Kauli Yake:

ققالوا الح ◌الكبري يلالع وهو

(Amesema): “Ya haki”; Naye ni Al-’Aliyyul-Kabiyr (Mwenye ‘uluwa Yuko juu ya vyote -Mkubwa wa dhati vitendo na sifa).” (Sabaa´ 34:23)

4. Sababu ya (Malaika) kuuliza kwao kuhusu hilo.

5. Jibriyl anawajibu baada ya hilo kwa kusema: “Kasema kadhaa na kadhaa.”

6. Maelezo ya kwamba wa kwanza anayeinua kichwa chake ni Jibriyl.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

83

7. Ya kwamba anawajibu (Malaika) walioko mbinguni wote kwa kuwa wanamuuliza.

8. Ya kwamba huzimia wakazi wa mbinguni wote.

9. Kutetemeka kwa mbingu kutokana na Maneno ya Allaah.

10. Ya kwamba Jibriyl ndie mwenye kufikisha Wahyi kuupeleka kwa yule Amtakaye Allaah.

11. Uibaji wa usikivu wa Mashaytwaan.53

12. Sifa ya jinsi (Mashaytwaan) wanavyopandiana wao kwa wao.54

13. Kutumwa kwa kimondo.

14. Kuna wakati kimondo humpata kabla hajaufikisha (ujumbe) kwa mwengine, na wakatimwingine anawahi kuufikisha kwa mwenzake wa kibinaadamu kabla ya (kimondo)kumfikia.

15. Wakati mwingine huenda kuhani akasema kweli.55

16. Kuongezea kwake neno hilo uongo mia moja.56

17. Hausadikishwi uongo wake isipokuwa kwa neno hilo alilolisikia mbinguni.

18. Watu (wenye nyoyo chafu) kukubali uongo. Vipi watategemea neno moja nawasizingatie uongo mia?

19. Jinsi wanavyopasiana neno hilo wao kwa wao, wanalihifadhi na kulitumia kama dalili.57

20. Kuthibitisha kwa Sifa za Allaah, kinyume na Ash´ariyyah58 na al-Mu´attwilah.

21. Mtetemeko na mtikisiko huo (wa viumbe vilivyo mbinguni) ni kutokana na kumuogopaAllaah (´Azza wa Jalla).

53 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hili limetajwa katika Qur-aan: “Tazama Suurah ya as-Swaffaat 37:08.”54 Shaykh Fawzaan anasema: ”Allaah Kawapa Mashaytwaan uwezo, pindi wanapotaka kuiba kusikiayanayosemwa mbingu, basi hupandiana mpaka wanafika kwenye mbingu iliyo juu kabisa. Hawafikiihili isipokuwa kwa juhudi kubwa (ya kupandiana wao kwa wao).”55 Shaykh Fawzaan anasema: ”Huu ni mtihani na majaribio ya Allaah. Yeye asli yake ni muongo,lakini pengine akasema ukweli kwa neno alilosikia mbinguni.”56 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa kuna Radd kwa wale wanaowasadikisha makuhani. Vipiwatawasadikisha kwa neno wanaloliongezea juu yake uongo mia moja?”57 Shaykh Fawzaan: ”Hapa kuna dalili ya kuwa mtu wa batili (mtu wa Bid´ah) anaweza kutumia dalilikwa kitu katika haki ili apambie (na afikie) upotofu wake.”58 Shaykh Fawzaan: ”Ashaa´irah ni watu ambao wanajinasibisha kwa Abul-Hasan Ash´ariy(Rahimahu Allaah) ambaye alitubu na kujitoa katika madhehebu ya Mu´tazilah na Kullaabiyyah nakurejea katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah. Na kaandika kuhusu kurejea kwake katika kitabu ”al-Ibaanah” na ”Maqaalat al-Islaamiyyah”. Lakini Ashaa´irah (ambao ni wafuasi wake) hawakukubalikurejea kwake. Hivyo wanajinasibisha unasibisho wa batili naye yuko mbali kabisa nao.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

84

22. Malaika humteremkia Allaah kwa kusujudu.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

85

Mlango Wa 17

Shafaa´ah59

Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):

بهموا إلى ررشحافون أن يخي ينالذ به رأنذو ليس لهم من دونه ولي ولا شفيع لعلهم يتقون◌

”Na waonye kwayo (Qur-aan) wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywakwa Mola wao; hawana badala Yake mlinzi wala mwombezi ili wapatekumcha.” (al-An´aam 06:51)

Kauli Yake:

قل للـه الشفاعة جميعا

“Sema: (ee Muhammad Ash-shafaa’ah“ :(صلى اهللا عليه وآله وسلم (uombezi) wote ni wa

Allaah.” (az-Zumar 39:44)

Kauli Yake:

إلا بإذنه هندع فعشي ين ذا الذم

“Nani huyu ambaye anashufai (anayeombea) mbele Yake bila ya idhini Yake.”(al-Baqarah 02:255)

Kauli Yake:

ويرضىوكم من ملك في السماوات لا تغني شفاعتهم شيئا إلا من بعد أن يأذن اللـه لمن يشاء

”Na Malaika wangapi mbinguni haitowafaa kitu chochote shafaa’ah yao(uombezi) isipokuwa baada ya kuwa Allaah Ametolea idhini kwa Amtakayena kumridhia.” (an-Najm 53:26)

Kauli Yake:

59 Maombezi, uombezi, msamaha

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

86

اللـه ونن دم متمعز ينوا الذعقل اد ◌كون ملمن لا يم مهنم ا لهمو كرن شا ميهمف ما لهمض وي الأرلا فو اتاومي السف ةثقال ذرولا تنفع الشفاعة عنده إلا لمن أذن لهظهري

”Sema: “Ombeni wale mnadai (kuwa ni miungu) badala ya Allaah, hawamilikiuzito wa atomu (au sisimizi) mbinguni wala ardhini, na wala (wao) hawanahumo ushirika (Naye), na wala (Allaah) Hana msaidizi miongoni mwao. Nawala haitofaa shafaa’ah mbele Yake isipokuwa kwa yule Aliyempa idhini.”(Sabaa´ 34:22-23)

Kasema ´Abul-´Abbaas60: “Allaah Kakanusha vyote visivyokuwa Yeye, vyoteambavyo washirikina wamejiambatanisha navyo.61 Kwa kuwa Amekanushakwa yeyote badala Yake kuwa na mamlaka au ushirika wowote wa hilobadala Yake, au msaidizi wowote kwa Allaah, na hapakubaki isipokuwaShafaa´ah. Kabainisha ya kwamba haitomfaa yeyote isipokuwa kwa yuleambaye Mola Kampa idhini. Kama Alivyosema Allaah kuhusiana na Malaika:

ولا يشفعون إلا لمن ارتضى

“Na wala hawamuombei shafaa’ah (yeyote yule) isipokuwa kwa yule ambaye(Allaah) Amemridhia.” (al-Anbiyaa 21:28)

Na kwa sababu hii, Shafaa´ah ambayo washirikina wanaamini itakataliwa sikuya Qiyaamah, kama imevyokataliwa na Qur-aan na kama alivyoeleza Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakuja na kumsujudia Mola Wake na kumhimidi, hatoanza kwa Shafaa´ahkwanza. Kisha ndio Ataambiwa: “Nyanyua kichwa chako, sema nautasikizwa, omba na utapewa, na ombea Shafaa´ah na utapewa Shafaa´ah.”

Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam):

“Ni nani katika watu atakayekuwa na furaha kwa Shafaa´ah yako?” Akasema(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni yule atakayesema “Laa ilaaha illa

60 Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyad, Ahmad bin ´Abdil-Haliym bin ´Abdus-Salaam – tazama Fath-ul-Majiyd, uk. 16861 Katika miungu yao ya uongo

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

87

Allaah, hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, akiwa niwenye kutakasika moyoni mwake.”

Hivyo, Shafaa´ah hii ni ya watu wa Ikhlaasw, kwa idhini ya Allaah, nahaitokuwa kwa wale waliomshirikisha Allaah, na wala haitokuwa isipokuwakwa idhini ya Allaah.

Na uhakika wake (Shafaa´ah hiyo) ni kwamba Allaah (Subhaanahu) NdiyeMwenye kukubali kutoka kwa watu wa Ikhlaasw na at-Tawhiyd,Atawasamehe kupitia Du´aa za waombeaji wataopewa idhini ya kuombeakama kumpa ikramu (muombeaji) na kufikia al-Maqaam al-Mahmuud.

Shafaa´ah ambayo imekataliwa na Qur-aan ni ile ambayo iko na Shirki, na kwahili ndio maana Shafaa´ah imethibiti na kuthibiti kwa idhini Yake katikamaeneo kadhaa. Na hilo limebainishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) ya kwamba haitokuwa isipokuwa kwa watu wa Tawhiyd na Ikhlaasw.

Ufafanuzi:Shafaa´ah uombezi hapa ni kubainisha inayojuzu na isiyojuzu. Maana ya Shafaa´ah niukaakati62 katika kuomba kitu kutoka kwa yule anayekimiliki. Shafaa´ah, bi maana kuombakwa kupitia watu katika mambo ya kiduna – ikiwa ni jambo la kheri na lenye kheri, hakunaubaya. Kama kuomba kwa kupitia wafalme, matajiri na watu mfano wao ili awezekutatuliwa haja yake. Ama haja hii ikiwa ni ya kufikia jambo la haramu, haijuzu. Hii niShafaa´ah kwa baina ya watu. Allaah Anasema:

من يشفع شفاعة حسنة يكن له نصيب منها ومن يشفع شفاعة سيئة يكن له كفل منها◌

”Atakayeombeamaombezi mema, atapata fungu lake katika hayo. Na atakayeombeamaombezi mabaya atapata sehemu katika hayo.” (an-Nisaa 04:85)

Ama Shafaa´ah kwa Allaah (´Azza wa Jalla), hii haimiliki yeyote isipokuwa Allaah Pekee nawala haombwi isipokuwa kwa Allaah Pekee. Hakuna yeyote awezae kupitia kwa Allaah nakusema “msamehe fulani, mpe fulani” n.k. Lazima kwanza Allaah Atoe idhini ya huyomwenye kuombewa. Pili ni lazima huyo anayeombewa awe ni Muislamu. Hizi ndio shartimbili za Shafaa´ah. Allaah (Ta´ala) Anasema:

62 Wa kati na kati baina kiumbe na Mola Wake

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

88

إلا بإذنه هندع فعشي ين ذا الذم

“Nani huyu ambaye anashufai (anayeombea) mbele Yake bila ya idhini Yake.” (al-Baqarah02:255)

Kisha Anasema kuhusu makafiri:

طاعيع يفلا شيم ومح نم نيملظالا لم

”Madhalimu hawatokuwa na rafiki wa dhati, na wala mwombezi anayetiiwa.” (Ghaafir40:19)

Shaykh kuweka mlango huu kakusudia kuwaradi washirikina ambao wanamshirikishaAllaah katika ´Ibaadah, na wanapokatazwa wanasema hapana, sisi makusudio yetu siokuwaabudu. Kama Alivyosema Allaah:

اللـه ندا عناؤفعلاء شـؤ قولون هيو مهنفعلا يو مهرضا لا يم اللـه ونن دون مدبعيو قل أتنبئون اللـه بما لا يعلم في السماوات ولا في الأرض◌ ◌ هانحبسوتعالى عما يشركون

”Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao (hawawezi) kuwadhuru na wala (hawawezi)kuwanufaisha, na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” Sema: “Je,mnamjulisha Allaah kwa yale Asiyoyajua katika mbingu na ardhini? Subhaanahu wa Ta’ala!(Utakaso ni Wake Na Ametukuka kwa Uluwa) kwa yale yote wanayomshirikisha.” (Yuunus10:18)

Wanawachinjia, wanawawekea nadhiri, wanawaomba na kuwaabudu kwa madai yakwamba ni waombezi wao mbele ya Allaah. Na watu wengi leo wako katika madhehebuhaya ya washirikina. Wanaabudu makaburi na kuabudu badala ya Allaah kwa madai yakwamba wao wana madhambi mengi, hivyo ndio maana wanaomba kwa kupitia watu hawawema. Na kwamba wao hawaamini kuwa wananufaisha na kudhuru n.k. Kwa hivyo hayandio makusudio ya Shaykh kuweka mlango huu ili kuwaradi watu hawa.

Aayah ya Suurat al-An´aam: Radd kwa washirikina ya kuwa haitowafaa Shafaa´ah hiiwaliokuwa wakiitegemea. Wale waliokuwa wakiwaomba katika Malaika, Mitume, Manabii,mawalii na watu wema watawaka na kujiweka nao mbali kwa ´Ibaadah waliokuwawakiwafanyi na kudai kuwa ni Shafaa´ah.

Aayah ya Suurat az-Zumar: Allaah Anawaradi hapa wale ambao wanasema kuwa mawaliiwanaweza kuombea bila ya idhini ya Allaah.

Aayah ya Suurat al-Baqarah: Yaani hakuna yeyote awezae kuombea mwengine bila ya idhiniyake. Sawa awe Mtume, Manabii, mawalii, watu wema, Malaika n.k.

Aayah ya Suurat an-Najm: Hii ni dalili ya kwamba Shafaa´ah haiombwi kwa mwingineyeyote isipokuwa Allaah (´Azza wa Jalla) na wala haiombwi kwa viumbe.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

89

Aayah ya Suurat Sabaa´: Allaah hapa kabatilisha madai yote ya washirikina:

a) Vipi kwanza utaomba uombezi kwa watu wasioumiliki?b) Milki ni ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) Pekee na hana mshirika.c) Ikiwa sio mmiliki wala mshirikia (huyo unayemshirikisha pamoja na Allaah),

pengine akawa ni msaidizi wa Allaah. Na Allaah (Ta´ala) hana msaidizi Kajitoshelezana viumbe Vyake.

d) Ikiwa sio mmliki, mshirika wala msaidizi, pengine akaweza kuombea mbele yaAllaah. Na Allaah Haitofaa Kwake Shafaa´ah isipokuwa kwa yule aliyempa idhini.

Shafaa´ah hiii wanayoamini washirikina Allaah Kaikanusha. Ama Shafaa´ah sahihi AllaahHaikatai. Shafaa´ah ni aina mbili:

1. Shafaa´ah iliyokatazwa na ya batili. Na hii ndio wanayojiambatanisha nayowashirikina.

2. Shafaa´ah sahihi. Nayo ni ile imetimiza sharti mbili: 1) Kwanza idhini kutoka kwaAllaah. 2) Aridhie kwa yule anayeombewa. Na hii haitowafaa washirikina isipokuwaitawafaa Waislamu peke yao.

Na watu katika Shafaa´ah wamegawanyika mafungu matatu:

1. Kuna ambao wanapinga Shafaa´ah kabisa na kusema kwamba hakuna Shafaa´ah. Nawatu hawa ni Khawaarij ambao wanawakufurisha Waislamu kwa madhambimakubwa. Na kwa vile ni makafiri hivyo Shafaa´ah haitowafaa kitu.

2. Kundi lingine linathibitisha Shafaa´ah moja kwa moja bila ya masharti. Na hawa niwaabudu makaburi. Wanaiomba kupitia viumbe.

3. Ama walio kati na kati ni Ahl-ul-Haqq (Ahl-u-Sunnah). Ambao wameithibitishaShafaa´ah kwa masharti yake kama ilivyokuja katika Qur-aan na Sunnah.

Watu siku ya Qiyaamah wataposimamishwa miaka khamsini na kuwa katika hali ngumu,watawaendea Mitume kadhaa na kuwaomba wawaombee kwa Allaah (Ta´ala). Mitumewote watakataa na kuomba udhuru mpaka watapomfikia Mtume Muhammad (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam). Ataenda kwa Mola Wake na kumsujudia na kumuomba mpakaAllaah Atapompa idhini ya kuombea. Hii ndio al-Maqaam al-Mahmuud. Hatoenda tu nakuombea kwa kuwa Shafaa´ah sio milki yake yeye (´alayhis-Salaam). Hii ni dalili ya kwambahata Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hatoombea yeyote isipokuwakwa idhini ya Allaah (Ta´ala) kwanza.

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) hapa kuna Radd kwa Jahmiyyah,Khawaarij na wafuasi wao wanaopinga Shafaa´ah kwa kukufurisha watu kwa madhambimakubwa. Makusudio ya yule itakayemfaa Shafaa´ah hapa ni Muislamu.

Hivyo Shafaa´ah ni ya wale wanaompwekesha Allaah kwa idhini ya Allaah na haitokuwakwa wale wanaomshirikisha Allaah. Hizi ndio sharti mbili za Shafaa´ah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

90

Shafaa´ah iliyokataliwa ni ile yenye Shirki: Kuwaomba mawalii, watu wema, kuwatakamsaada, kuwachinjia na kuomba Du´aa kutoka kwao kwa madai ya Shafaa´ah.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayaat (zilizotajwa hapo juu).

2. Sifa ya Shafaa´ah iliyokanushwa.63

3. Sifa ya Shafaa´ah iliyothibitishwa.64

4. Kutajwa kwa Shafaa´ah kubwa, nayo ni al-Maqaam al-Mahmuud.

5. Melezo ya atavyofanya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba hamiliki Shafaa´ah,bali atasujudu (na kuomba). Atapopewa idhini ya kuombea ndo ataombea.

6. Ni nani mwenye furaha nayo (hiyo Shafaa´ah).

7. Haitokuwa kwa yule mwenye kumshirikisha Allaah (Ta´ala).

8. Ubainisho wa uhakika wake.65

63 Shaykh Fawzaan anasema: ”Nayo ni ile ambayo inaombwa kwa asiyekuwa Allaah, au bila ya idhiniya Allaah, au inaombwa kwa mshirikina au kafiri. Hizi zimekataliwa”64 Shaykh Fawzaan anasema: ”Nayo ni mfano wa ile Hadiyth iliyotajwa kwamba Mtume Atakuja nakumuomba kwanza Allaah kisha Allaah ndo Ampe idhini. Na si kurupuka tu na kwenda kwenyekaburi, au walii na mfano wao na kuwaomba Shafaa´ah. Hapana. Unatakiwa kuiomba kwa Allaah. Aukuomba kwa kusema: “Allaah naomba usininyime Shafaa´ah ya Mtume Wako na waja wako wema.”65 Shaykh Fawzaan anasema: ”Ni kama alivoibanisha Shaykh-ul-Islaam katika maneno yake yakwamba uhakika wake Allaah Atampa ikramu muombeaji baada ya idhini Yake na Amrehemumwenye kuombewa kwa Shafaa´ah hiyo.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

91

Mlango Wa 18

Kauli Ya Allaah Ta´ala

ـكن اللـه يهدي من يشاء إنك لا تهدي من أحببت ول ◌يندتهبالم لمأع وهو

”Hakika wewe huwezi kumwongoza umpendaye; lakini AllaahHumwongoza Amtakaye, Naye A’lam (Anajua zaidi) waongokao.” (al-Qaswasw 28:56)

Katika Swahiyh, kutoka kwa Ibn Musayyib ambaye kapokea kutoka kwa babayake aliyesema:

“Wakati mauti yalipomfikia Abuu Twaalib, alimjia Mtume wa Allaah (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) na alikuwepo ´Abdullaah bin Abiy ´Umayyah naAbuu Jahl (bin Hisham). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)akamwambia:

“Ewe mjomba! Sema: “Laa ilaaha illa Allaah, hapana mola apasaye kuabudiwakwa haki isipokuwa Allaah, ni neno ambalo litakuwa ni hoja kwangu kwaAllaah.” Wakamwambia: “Hivi kweli unataka kuacha dini ya ´Abdul-Muttwalib?” Akamrudilia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) naowawili wakamrudilia. Ikawa neno la mwisho alilosema, yeye yuko katika diniya ´Abdul-Muttwalib na akakataa kusema laa ilaaha illa Allaah. Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Nitakuombea msamaha midhalisijakatazwa.” Akateremsha Allaah (´Azza wa Jalla):

نيركشلموا لرفغتسوا أن ينآم ينالذبي ولنا كان لم

”Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombee maghfirah washirikina.”(at-Tawbah 09:113)

Na Allaah Akateremsha pia kuhusu Abuu Twaalib:

ـكن اللـه يهدي من يشاءإنك لا تهدي من أحببت ول

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

92

”Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah HumhidiAmtakaye.” (al-Qaswasw 28:56)

Ufafanuzi:Aayah ya Suurat al-Qaswasw: Sababu ya kuteremka Aayah hii, ilikuwa ni wakati babamdogo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Abuu Twaalib alipokuwa anatakakufa – kwa kuwa kulionekana kwake alama ya mauti - na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) alikuwa mbioni katika kutaka kumwongoza na kumwingiza katika Uislamu. Kwakuwa ni baba yake mdogo na mtu wake wa karibu. Hali kadhalika kwa kuwa alimfanyiawema kumtetea kutokana na washirikina. Alimlea baada ya babu yake ´Abdul-Muttwalibkufa, yeye (Abuu Twaalib) ndo akawa mlezi wake. Na wakati washirikina walipokuwawanamsakama (kutaka kumdhuru) alikuwa Abuu Twaalib anamhami na kumtetea. HivyoMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anataka kumlipiza wema. Akawaanamlingania, mpaka wakati wa kukata kwake roho hakukata tamaa Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) kwa kuongoka kwake. Akamjia na kumlingania katika Uislamu,atamke Shahaadah pengine akafa juu yake. Lakini hakuweza hili. Jambo hili liko Mikononimwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na Allaah (Subhaanahu) Anajua ni nani anayefaakuongozwa na ni nani asiyefaa.

Ibn Musayyib na Abuu Jahl hawa walikuwa ni washirikina, na kuhudhuria kwao ndioilikuwa sababu ya Abuu Twaalib kupotea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)alimwambia aseme laa ilaaha illa Allaah kwa kuwa mwenye kutamka neno hili kikweli kutokamoyoni mwake akaliamini na akafa juu yake anaingia Peponi kama alivyosema Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa washirikina ndio wakawa wamemwambia: “Je,unataka kuacha dini ya baba yako ´Abdul-Muttwalib.” Na ´Abdul-Muttwalib alikuwa juu yaShirki na ´Ibaadah ya masanamu. Wakamkataza kusema laa ilaaha illa Allaah kwa kuwawalijua akisema hivi atakuwa kajiweka mbali na dini ya washirikina. Lau ungelikuwa nikutamka tu ingelikuwa sahali, lakini makusudio ni maana yake. Ikawa neno lake la mwishoalilosema ni kuwa yeye yuko katika dini ya ´Abdul-Muttwalib na akawa amekufa juu yaShirki. Allaah Atukinge. Kwa sababu ya kuwepo kwa hawa watu wawili wabaya, akasikizamaneno yao na akakataa kusikiliza maneno ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam). Vinginevyo Abuu Twaalib alikuwa anajua kuwa Mtume Muhammad yuko juuya haki na Dini sahihi. Hii ni dalili ya tafsiri ya laa ilaaha illa Allaah. Hebu tazama!Washirikina walijua maana ya laa ilaaha illa Allaah, ya kwamba maana yake ni kujiwekambali na Shirki na washirikina. Mwenye kuisema kakanusha ´Ibaadah yoyote badala yaAllaah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

93

Waislamu wengi leo hawafahamu maana yake, wanadhani kuwa ni neno linalotamkwakwenye ulimi, mtu anatafuta baraka kupitia neno hilo lakini hawajui maana yake. Na ndiomaana utaona wanaabudu badala ya Allaah: maiti, wanaomba msaada makaburi, mawalii,watu wema naye anasema laa ilaaha illa Allaah. Natija ya kutofahamu maana yake. Natija yaujinga.

Hapa kuna Radd kwa wale wanaodai Abuu Twaalib alikufa juu ya Uislamu, katika Shiy´ahna wengineo. Abuu Twaalib alikufa juu ya Shirki kwa dalili ya Hadiyth hii Swahiyh naAayah hii.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakukata tamaa akasema atamuombea maadamuhajakatazwa na Allaah, kwa kuwa sio yeye mwenye maamuzi. Hivyo ndio Allaah AkawaAmeteremsha Aayah kumkataza. Uongofu uko Mikononi mwa Allaah (´Azza wa Jalla) na siMtume (´alayhis-Salaam). Uongofu unamiliki Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na huu ndiounaitwa uongofu wa Tawfiyq. Ama uongofu wa Da´wah, huu unamiliki Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) na kila yule mwenye elimu anayelingania katika Dini ya Allaah.Uongofu wa Da´wah yaani wanawaelekeza na kuwaonesha watu njia iliyonyooka.

”Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye.” Swali linakuja, je hivi kweli Mtumeanampenda Abuu Twaalib ambaye ni kafiri? Maana yake ni kwamba huwezi kumwongozayule ambaye wamtakia/wampendea uongofu wake, na maana yake si kwamba unampendailihali ni kafiri. Hii ni kauli ya kwanza katika kuifasiri Aayah hii. Na kauli ya pili inasema,kinachomaanishwa hapa ni mapenzi ya kimaumbile ya ujamaa na si mapenzi ya kidini.Kama jinsi mtu anampenda mke wake ilihali ni mkristo, myahudi, baba au watoto makafirin.k., haya ni mapenzi ya kimaumbile na ya ujamaa na hayahusiana na Dini.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya:

ـكن اللـه يهدي من يشاء إنك لا تهدي من أحببت ول

”Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye.” (al-Qaswasw 28:56)

2. Tafsiri ya Kauli Yake (Ta´ala):

وا أن ينآم ينالذبي ولنا كان لمنيركشلموا لرفغتس

”Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombee maghfirah washirikina.” (at-Tawbah09:113)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

94

3. Ni suala kubwa la tafsiri ya maana ya kauli (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): Sema: “Laailaaha illa Allaah” tofauti na wale wanaodai kuwa na elimu (ya Dini).66

4. Abuu Jahl na waliokuwa pamoja naye walijua makusudio ya Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) anapomwambia mtu: “Sema laa ilaaha illa Allaah”. Allaah Awateketezewatu ambao Abuu Jahl alijua asli ya Uislamu kuliko watu hawa.

5. Hamu na tamaa yake kubwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kutaka kusilimu kwamjomba wake.

6. Radd kwa mwenye kudai kuwa ´Abdul-Muttwalib na mababa zake walikuwa Waislamu.

7. Allaah Hakukubali msamaha wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), bali badalayake Kamkataza hilo.

8. Madhara ambayo yanaweza kupatikana kwa mtu kukaa na watu wabaya.67

9. Madhara ya kuwasifu mababu na watu wakubwa (wakiwa katika Shirki).

10. Shubuha za wabatilishaji katika hilo ni hoja za Kijaahiliyyah.

11. ´Amali huzingatiwa mwisho wake, kwa kuwa lau (Abuu Twaalib) angelitamka(Shahaadah) ingelimfaa.68

12. Uzingatio mkubwa wa shubuha hii katika nyoyo za wapotevu, kwa kuwa katika kisahawakukitolea hoja yoyote isipokuwa kwacho (kuwa hii ni dini ya ´Abdul-Muttwalib) lichaya jitihada zake kali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kumkariria (Shahaadah). Lakini kwasababu ya kiburi chao kikubwa (katika ukoo) wakakinaika na hilo.

66 Shaykh Fawzaan anasema: ”Wengi wanaoitamka leo hawajui maana yake, kwa masikitikomakubwa wakiwemo Ma´ulamaa ndani yao. Wanawaomba na kuwaabudu mawalii, watu wema,wanawachinjia, wanawaweka nadhiri na kuwaambia: “Tuombeeni kwa Allaah, tukurubisheni kwaAllaah na mfano wa hayo.” Hawakufahamu vizuri maana ya laa ilaaha illa Allaah kuwa ni kukanushana kuthibitisha. Na hii ndio natija ya ujinga.”67 Shaykh Fawzaan anasema: ”Abuu Jahl na ´Abdullaah bin Abiy ´Umayyah wao ndio walimzuiaAbuu Twaalib kuingia katika Uislamu. Ni dalili ya mtu kuwa na tahadhari kukaa na watu wabaya naMadu´aat wapotofu ili wasimuathiri mtu katika kukaa nao. Mtu badala yake awe na watu wa kheri.”68 Shaykh Fawzaan anasema: ”Abuu Twaalib aliishi maisha yake yote juu ya Shirki. Lakini lauangelisema laa ilaaha illa Allaah wakati wa kukata roho kabla ya kufa Allaah Angelimsamehe. ´Amalihuzingatiwa mwisho wake. Mtu anaweza kuwa katika kheri maisha yake yote kisha akamaliziavibaya akawa katika watu wa shari, na inaweza kuwa kinyume chake, mtu akawa katika kheri maishayake yote kisha akamalizia vizuri akawa katika watu wa kheri.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

95

Mlango Wa 19

Kuchupa Mipaka69 Kwa Watu Wema Ndio Lililopelekea Kukufuru KwaBinadamu

Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):

قإلا الح لى اللـهقولوا علا تو ينكمي دلوا فغاب لا تتل الكا أهي

“Enyi Ahlal-Kitaabi! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juuya Allaah isipokuwa (ukweli).” (an-Nisaa 04:171)

Katika Swahiyh (al-Bukhaariy), Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa)kaiwekea taaliki Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وقالوا لا تذرن آلهتكم ولا تذرن ودا ولا سواعا ولا يغوث ويعوق ونسرا

”Wakasema: “Msiwaache miungu yenu; na wala msimwache Waddaa, nawala Su’waa’a, na wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa”.” (Nuuh 71:23)

Akasema:

“Haya ni majina ya watu wema katika watu wa Nuuh. Walipokufa Shaytwaanaliwapendezea watu wake watengeneze masanamu na kuyaweka mahaliambapo walikuwa wakikaa na kuyapa majina yao.70 Wakafanya hivyo nahawakuyaabudu mpaka wakati watu hawa walipokufa na elimu ikasahaulika,hivyo wakaabudiwa.”

Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) kasema kuwa wengi katika Salafwamesema: “Walipokufa71 walishikamana na makaburi yao kishawakatengeneza masanamu yenye sura zao, kulipopita muda mrefuwakawaabudu.”

69 Ghuluu70 Hao watu wema waliokufa71 Wanachuoni na watu wema

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

96

´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Msipindukie kwangu kama walivyopindukia Manaswara kwa ´Iysa binMaryam. Hakika mimi ni mja, hivyo semeni “mja wa Allaah na MtumeWake.”

(Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

Kasema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Tahadharini na kupetuka mipaka. Hakika waliokuwa kabla yenuwaliangamia kwa ajili ya kupetuka mipaka.”

Katika (Swahiyh) Muslim, kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu)ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Wameangamia waliochupa mipaka.”72 Alisema hivyo mara tatu.”

Ufafanuzi:Pindi Shaykh katika milango iliopita alipotaja Shirki waliotumbukia humo watu wa zamanina wa sasa, sasa anataka kubainisha sababu iliyowapelekea katika hili. Kwa kuwa mtuakijua sababu ya shari atajitenga nayo na kuitahadharisha shari hiyo. Wewe utapotakakutatua tatizo, tafuta sababu yake. Na Shaykh katika vitabu vyake vyote hajisemei maoniyake mwenyewe, bali anasema kwa dalili katika Kitabu na Sunnah. Huu ndio mfumo waShaykh katika vitabu vyake; Kitabu, Sunnah na maneno ya Salaf-us-Swaalih. AllaahKawaumba waja Wake ili wamuabudu, ni kitu gani ambacho kimewatoa watu katika´Ibaadah hii na kuwaingiza katika Shirki? Sababu ni kuchupa mipaka kwa watu wema. Niwajibu mtu kuwa kati na kati katika haki ya watu wema, mtu asiwapetukie mipaka na walamtu asichuje na kupuuzia haki yao. Hii ni dhuluma. Tusichupe mipaka kama wakristowalivochupa mipaka kwa ´Iysa bin Maryam na kusema kuwa ni mtoto wa Allaah, au utatu,na wengine wakafikia na kuthubutu kusema yeye khaswa ndio Allaah. Mpaka sasawanasema hivi kuwa ´Iysa ndio Allaah. Allaah Awaangamize. Watu wa Nuuh walichupamipaka kwa watu wema mpaka wakawaabudu badala ya Allaah. Manaswara wamechupamipaka kwa Masiyh mpaka wakamuabudu badala ya Allaah. Na mayahudi wakachupamipaka wa ´Uzayr na kusema ni mwana wa Allaah. Lakini waliopindukia zaidi mipaka ni

72 Katika Dini

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

97

manaswara kwa Masiyh (´alayhis-Salaam). Allaah Kamnasibisha ´Iysa kwa mama yake kwakuwa Allaah Kamuumba pasina baba. Na Allaah ni Muweza wa kila jambo. KwaniKamuumba Aadam pasina baba wala mama.

مثل آدكم اللـه ندى عيسثل عإن م م قال له كن فيكونخلقه من تراب ث◌

”Hakika mfano wa ‘Iysaa kwa Allaah ni kama mfano wa Aadam. Amemuumba kutokana naudongo kisha Akamwambia: ‘Kun’ (Kuwa) basi akawa.” (al-´Imraan 03:59)

Hakuna Kinachomshinda. Hili ni katika miujiza.

Aayah ya Suurat an-Nisaa: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haabudiwi kwa haliyoyote. Anayeabudiwa ni Yule Aliyemtuma. Katika Aayah hii kuna onyo kwa Ahl-ul-Kitaabkuchupa mipaka kwa watu. Na wakati huo huo kuna tahadhari kwetu kufanya kamawalivofanya. Kuchupa mipaka kwa watu wema na kuwaabudu badala ya Allaah. Maana yaal-Ghuluu ni ziada.

Sababu ya watu wa Nuuh kutumbukia katika Shirki ni kuchupa mipaka kwa watu wema.Ilikuweje? Watu baada ya Aadam walikuwa katika Tawhiyd - kama alivyosema Ibn ´Abbaas(Radhiya Allaahu ´anhumaa) - juu ya Dini ya baba yao Aadam, kwa kipindi cha karne kumi.Na katika watu wa Nuuh kulikuwepo watu wema na wanachuoni waliokuwa juu yaTawhiyd na Dini. Walikuwa wakiwalingania watu na kuwafundisha elimu yenye manufaa.Allaah Akapanga wakawa wamekufa katika mwaka mmoja; Wadd, na Su’waa’a, naYaghuwth, na Ya’uwq na Nasraa. Walikuwa ni watu wema wanachuoni juu ya Dini ya babayao Aadam. Jamii waliokuwemo ilikuwa ya Kiislamu na watu walikuwa wakiwapenda kwawema wao. Walipokufa katika mwaka mmoja, watu wakahuzunika sana na wakawawanayatembelea makaburi yao sana na kukaa huko kwa muda kwa kuwapenda. Wakawawanalia na kuwatembelea ilihali nao wameshakufa. Shaytwaan akawa ametumia fursa hii.Akawajia na kuwaambia: “Msijisumbue kwenda kwenye makaburi yao mnajichokesha,badala yake tengenezeni picha (sura) zao na mzitundike katika vikao vyao walipokuwawanakaa wakati wa kufunza ili muweze kuwakumbuka na kuwaiga.” Shaytwaan akawajiakwa njia ya nasaha. Allaah Amwangamize. Wakawa wamefanya kama alivowashauri. Waowakafanya hivyo kwa lengo la ´Ibaadah na kwa ajili waweze kuwakumbuka na haikuwamalengo yao kupindukia mipaka kwao. Shaytwaan hakuwaamrisha pale pale wawaabudukwa kuwa alikuwa anajua kuwa bado ni wasomi. Aliwavuta kidogo kidogo. Wakati kizazihichi kilipoondoka na wakafa wanachuoni na kukaja watu wajinga. Akawajia Shaytwaankwa mara nyingine na kuwaambia: “Hakika baba zenu hawakutengeneza picha hiziisipokuwa ni kwa ajili ziabudiwe na walikuwa wakinywesheleza mvua kwazo.” Akawaametumia ujinga wao na kufa kwa wanachuoni. Hii ni dalili kuwepo kwa wanachuonikatika Ummah ni muhimu sana na kheri, na kukosekana wanachuoni ni maangamivu nakhatari kwa Ummah. Hali kadhalika wafuasi wa Shaytwaan katika wanaadamu hutumiafursa kama hii kunapokosekana wanachuoni. Hii ndio tafsiri ya Aayah hii Tukufu. Hii ndioilikuwa Shirki ya kwanza kujitokeza katika ardhi. Ilipojitokeza Shirki katika ardhi, ndio

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

98

Allaah Akawa Amemtuma Mtume Wake Nuuh (´alayhis-Salaam) aje kuwalingania watukatika Tawhiyd na waache ´Ibaadah badala Yake. Akawalingania miaka miatisa nakhamsini. Na hakuna waliomfuata isipokuwa watu wachache sana. Na wakanasihianakubakia katika Shirki na kutomtii mtu (Mtume) huyu.

ث ويعوق ونسراوقالوا لا تذرن آلهتكم ولا تذرن ودا ولا سواعا ولا يغو

”Wakasema: “Msiwaache miungu yenu; na wala msimwache Waddaa, na wala Su’waa’a, nawala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa.” (Nuuh 71:23)

Hii ni dalili ya kuwa mwenye kuabudu kitu badala ya Allaah Kakifanya kuwa Ilaah(mungu). Hivyo sababu ya watu wa Nuuh kutumbukia katika Shirki ilikuwa ni kuchupamipaka katika watu wema.

Na leo hali kadhalika, watu wanapindukia miaka katika kuadhimisha watu, maiti nakadhalika. Wanawajengea manyumba na Misikiti kwenye makaburi yao, wanawaabudu ,wanawachinjia, wanawawekea nadhiri. Alichofanya Shaytwaan kwa watu wa Nuuh ndiokile kile alichofanya kwa watu wapotofu wa Ummah huu; waabudu makaburi.Wakikatazwa wanasema kuwa nyinyi mnawachukia watu wema. Subhaana Allaah!Mwenye kukataza Shirki ndo anawachukia watu wema? Watu wema wenyewe wakwelikweli hawaridhii hili kabisa. Ama wale wanaowalingania watu kuwaabudu, hawa sio katikawatu wema bali hawa ni Mashaytwaan wakibinaadamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) anatakiwa kusifiwa, lakini iwe kwa mipaka na si kupindukia. Na hakuna mtualiyepindukia mpaka kufikia kumpa sifa za Rubuubiyyah kama yule mtu wa Qaswiydah yaBurdaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunga njia nyingi – ambazo zinginezilikuwa ni mubaahah – lakini zilikuwa zinapelekea katika Shirki.

Kutokana na haya tunapata mafunzo yafuatayo:

- Wajibu wa mtu kujifunza kwa wanachuoni ili asikumbwe na fitina.

- Mtu kuwa na msimamo wa kuifanyia kazi elimu yake, isiwe ni elimu pasinamatendo.

- Mtu kuwa na subira katika kushikamana na hilo (haki).

- Kufunga milango yote inayopelekea katika Shirki na khaswa picha. Picha ina shari nafitina. Na khaswa zile picha za watu wakubwa (wanachuoni, wafalme, wachajiAllaah n.k.).

- Kuwepo kwa wanachuoni katika jamii ni kheri kubwa na kufunga mlango wa watuwapotofu; katika Mashaytwaan wa kibinaadamu na wakijini.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

99

- Picha zote ni haramu; sawa za kuchora, kunakili, za camera na nyinginezo zote kwakauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Kila mtengeneza picha yuMotoni.”

Masuala muhimu yaliyomo:1. Yule atakayefahamu mlango huu na milango miwili baada yake, itambainikia kwakeugeni wa Uislamu na ataona Kudura ya Allaah na Hekima ya kuzibadili nyoyo.

2. Utambuzi wa kuwa Shirki ya kwanza iliyojitokeza katika ardhi ilikuwa ni kuhusiana nautata wa watu wema.

3. Kitu cha kwanza kubadilisha Dini ya Mitume (´alayhimus-Swalaat was-Salaam) na sababuya hilo, licha ya kutambua kuwa Allaah Ndiye Aliwatuma.

4. Utambuzi wa sababu ya kukubali Bid´ah pamoja na kuwa ni kinyume na Shari´ah namaumbile.

5. Sababu ya yote hayo ni haki kuchanganyikana na batili:

- Jambo la kwanza, kuchupa mipaka kuwapenda watu wema.

- Jambo la pili, kitendo kilichofanywa na baadhi ya wanachuoni na watu wema kwakukusudia kheri, lakini wakadhania waliokuja baada yao kuwa walikuwa wanakusudia kitukingine.

6. Tafsiri ya Aayah iliyo katika Suurat Nuuh. (71:23)

7. Umbile la kibinaadamu katika haki hupungua moyoni mwake na wakati upotofu unazidi.

8. Ndani yake kuna uthibitisho wa yaliyonukuliwa kutoka kwa Salaf ya kwamba Bid´ah nisababu inayopelekea katika kufuru na kuwa inapendwa zaidi na Iblisi kuliko maasi. Kwakuwa maasi mtu hutubia kwayo na Bid´ah hakutubiwi kwayo.

9. Shaytwaan alijua mwisho wa matokeo ya Bid´ah, hata kama nia ya mtendaji itakuwanzuri.

10. Utambuzi wa kanuni ya kijumla, nayo ni makatazo ya kuchupa mipaka na ujuzi wayanayopelekea katika hilo.

11. Madhara ya kubaki (kushikamana) katika kaburi hata ikiwa kwa ajili ya nia ya kutendamatendo mema.

12. Utambuzi wa makatazo ya masanamu na hekima ya kuyavunja.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

100

13. Ukubwa wa jambo ndani ya kisa hiki na shida ya kinavyohitajika (kama funzo) pamojana kughafilika nacho.

14. Ni jambo la ajabu sana! Cha kushangaza zaidi ni kwamba Ahl-ul-Bid´ah wanakisomakisa hichi katika vitabu vyao vya tafsiri na Hadiyth, pamoja na uelewa wao wa maana yake,na kule Allaah Kuweka kizuizi kati yao na kati ya nyoyo zao mpaka wakaamini kitendo chawatu wa Nuuh (kuwaabudu watu wema) ndio aina bora ya ´Ibaadah. Na wakawawameamini yale Aliyokataza Allaah na Mtume Wake ambayo ndio kufuru inayohalalishadamu na mali.

15. Ubainifu ya kwamba wao hawakutaka jengine zaidi isipokuwa watu wema wawaombee.

16. Kudhania kwao kuwa wanachuoni waliochorwa sura zao walikusudia kufanya hivyo.

17. Ubainisho mkubwa katika kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Msipindukiekwangu kama walivyopindukia Manaswara kwa ´Iysa bin Maryam.” Swalah na salaamzimshukie aliyefikisha ujumbe wa wazi.

18. Nasaha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwetu kwa kuangamia waliochupamipaka.

19. Ubainifu ya kwamba (masanamu ya watu wema) hayakuabudiwa mpaka iliposahaulikaelimu. Katika hili kuna ubainifu ya thamani ya kuwepo kwa elimu na madhara yakutoweka.

20. Sababu ya kutoweka kwa elimu ni kufa kwa wanachuoni.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

101

Mlango Wa 20

Hukumu Ya Kuabudu Makaburi Au Kumuabudu Allaah KwenyeKaburi La Mtu Mwema

Katika Swahiyh (al-Bukhaariy na Muslim) ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha)kapokea:

“Ummah Salamah (Radhiya Allaahu ´anha) alimtajia Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kanisa aliyoiona Habashah na ilikuwaimejaa mapicha. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hao ndio waleambao wanapofiwa na mtu mwema au mja mwema, hujenga kwenye kaburilake Msikiti na huchora ndani yake picha hiyo. Hao ndio viumbe waovukabisa kwa Allaah. Watu hawa wamekusanya baina ya fitina73 mbili; fitina yakuabudu makaburi na fitina ya masanamu.”74

Katika al-Bukhaariy na Muslim kumepokelewa ya kwamba ´Aaishah (RadhiyaAllaahu ´anha) kasema:

“Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anataka kufa,alikuwa akijifunika nguo usoni mwake, anapoona dhiki huifunua, husemanaye alikuwa katika hali hiyo: “Laana ya Allaah iwe juu ya Mayahudi naManaswara, wamefanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni Misikiti. Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitahadharisha kwa yale waliyokuwawakiyafanya, na lau sikuchelea hilo kaburi lake lingekuwa nje75, isipokuwayeye76 alikhofia lisije kufanywa kuwa Msikiti.”

Muslim kapokea kutoka kwa Jundub bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhu)ambaye kasema: “Nilimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kablaya siku tano kufa kwake naye akisema:

73 Uovu aina mbili74 Masanamu na mapicha75 Yaani ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) alimzika chumbani mwake kwa kuchelea kaburi la Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lisije kuabudiwa laiti angeliweka kwa nje kila mtu akaliona.76 ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

102

“Hakika mimi najitakasa kwa Allaah kuwa na Khaliyl kipenzi katika nyinyi.Hakika Allaah Kanifanya kuwa Khaliyl Wake kama Alivyomfanya Ibraahiym(´alayhis-Salaam) kuwa Khaliyl Wake. Na lau ningemchukua yeyote katikaUmmah wangu kuwa Khaliyl wangu, basi ningelimfanya Abu Bakr (RadhiyaAllaahu ´anhu) kuwa Khaliyl wangu.77 Tanabahini! Hakika wale waliokuwakabla yenu walikuwa wakiyafanya78 makaburi ya Mitume wao kuwa Misikiti.Tanabahini! Msiyafanye makaburi kuwa Misikiti, hakika mimi nawakatazenikwa hilo.”

Kakataza hili (Swalla Allaa Allaahu ´alayhi wa sallam) mwisho wa uhai wake.Baada ya makatazo haya,79 halafu akamlaani yule mwenye kufanya hivi, hatakama bado kutakuwa hakujajengwa Msikiti. Na hii ndio maana ya manenoyake (Radhiya Allaahu ´anha) “Alikhofia (kaburi) lake lisifanywe kuwaMsikiti.”

Hakika Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum ajmaa´iyn) hawakuwahikamwe kujenga kwenye kaburi lake Msikiti. Na kila nafasi ambapokunaswaliwa ndio kumefanywa kuwa Msikiti. Na kila nafasi ambapokunaswaliwa ndio kunaitwa Msikiti. Kama alivyosema (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam):

“Ardhi yote imefanywa kwangu kuwa ni Msikiti na ni Twahara.”

Ahmad kapokea kwa isnadi Hasan kutoka kwa Ibn Mas´uud (RadhiyaAllaahu ´anhu) kapokea Hadiyth Marfu´:

“Hakika waovu katika watu ni wale ambao Qiyaamah kitawakuta nao wakohai80 na wale wenye kujenga Misikiti kwenye makaburi.”81

(Na kaipokea Abuu Haatim katika Swahiyh yake)

77 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa kuna dalili ya fadhila za Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) nakwamba yeye ndiye anastahiki kuwa Khaliyfah baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”78 Wakiyageuza makaburi yao kuwa mahala pakuswalia79 Kuyafanya makaburi kuwa Misikiti80 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hili ni kwa sababu Allaah (´Azza wa Jalla) Atazichukua roho zawaumini na hakutobaki juu ya ardhi muumini zaidi ya watu waovu tu. Hakutobaki juu ya ardhimwenye kusema ”Allaah! Allaah! Hawa ndio watu waovu. Ama waumini Allaah Atawachukua kablaya hilo.”81 Yaani wanapafanya ni mahala pa kuswalia

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

103

Ufafanuzi:Huu ni mlango wa yule mwenye kumuabudu Allaah kwenye kaburi la mtu mwema; sawaikiwa kamuabudu Allaah kwa kuswali kwenye kaburi, Du´aa kwenye kaburi huku akidhanikuwa Du´aa inapokelewa kwenye kaburi, anatufu kwenye kaburi kwa kutaka kujikurubishakwa Allaah, akachinja kwa ajili ya Allaah kwenye kaburi, yote haya na mfano wake ni katikanjia zinazopelekea katika Shirki na wala matendo haya hayajuzu. Badala yake inatakiwakuyakataza na kuyakemea mambo haya.

Bila ya shaka watu wema wana cheo na manzilah, lakini hili halifanyi kuwapetukia mipakana kuitakidi ya kwamba wananufaisha au kudhuru badala ya Allaah (´Azza wa Jalla). Waosi jengine zaidi isipokuwa ni waja mafukara wa Allaah (Ta´ala). Lakini badala yake sisitunawapenda, tunawaiga na tunawaheshimu; lakini ´Ibaadah ni haki ya Allaah (´Azza waJalla) na hawashirikiani na Allaah katika hilo. Sababu ya kujitokeza Shirki katika ardhi nikwa sababu ya kuwapindukia mipaka watu wema, na ndio maana Shaykh akawa amewekamilango mitatu ya kufuatana kuhusiana na maudhui hii tu.

Fitina ya kuabudu makaburi ni fitina kubwa. Ummah huu umetumbukia katika yale yalealiyotahadharisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wengi katika walewanaojinasibisha na Uislamu wamepea mtihani wa kuabudu makaburi. Laa Hawla walaaQuwwata illa biLlaah. Na yule anayewakataza wanamwambia wewe unawachukia mawaliiwa Allaah na watu wema. Subhaana Allaah! Kuwapenda mawalii na watu wema nikuwaomba na kuwaabudu badala ya Allaah? Huku ndio kuwapenda? Hapana. Kuwapendani sisi kuwaiga, kuwaheshimu, kuwaombea na kuondosha maovu kwenye makaburi(wanayofanyiwa). Hii ndio haki yao juu yetu. Mambo haya yamezushwa na mapote mawiliyanayojinasibisha na Uislamu; Shiy´ah na Suufiyyah.

Hadiyh ya Ummah Salamah ambaye ni mama wa waumini mke wa Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam). Hapa tunapata mafunzo ya kwamba watu hawa wanaojenga Misikitikwenye makaburi ndio watu waovu kabisa kwa Allaah. Na watu hawa waabudu makaburileo wanadai kuwa wao ndio watu wema (mbele ya Allaah). Na Msikiti usiokuwa na kaburihauna thamani kwao. Wanaadhimisha Msikiti wenye kaburi tu; Msikiti wa Husayn, Msikitiwa Nafisah na fulani na fulani. Misikiti imejaa makaburi ilihali Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kakataza hili. Wamechukua njia ile ile ya manaswara. Ni juu ya viongozikubomoa Misikiti hii iliyo kwenye makaburi, ili ´Aqiydah ya Tawhiyd ibaki kama ilivokujakutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kujenga Msikiti kwenye makaburihata kama utakuwa hauna picha hii ni fitina, na kutundika picha ya watu wema hii pia ninyingine. Wamejumuisha baina ya fitina mbili, hii ni kauli ya Shaykh-ul-Islaam kainukuu.Picha inaitwa sanamu bila kujali ni ya ala gani. Kwa kuwa inamithili sura (umbile) ya mtu.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

104

Katika haya kuna mafunzo ya uharamu wa kujenga kwenye makaburi, uharamu wakutundika mapicha ya watu wakubwa. Kwa kuwa mambo haya mawili ni katika njiainayopekea katika Shirki. Na Shari´ah imekuja kufunga milango yote inayopelekea katikaShirki, na miongoni mwa milango hiyo ni picha na kujenga Misikiti katika makaburi.

Kwa nini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anataka kukata rohoakawaombea Allaah Awalaani mayahudi na manaswara? Ni kwa kuwa alikhofia Ummahhuu usije kufanya kaburi lake kama walivofanya mayahudi na manaswara katika makaburiya Mitume wao (´alayhimus-Salaam). Ni dalili ya kwamba kuyafanya makaburi kuwaMisikiti – yaani mahala pakufanyia ´Ibaadah – ni katika madhambi makubwa kwa kuwaMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawalaani wanaofanya hivyo. Kwa kuwa hii ninjia inayopelekea katika Shirki. Hakusema wamewaabudu Mitume wao, bali kasemawameyafanya makaburi yao kuwa Misikiti, yaani wanaomba kwenye makaburi yao,wanaswali kwenye makaburi yao n.k. Yule ambaye anaswali kwenye makaburi kalaaniwa,sawa ikiwa mtu huyo ni katika mayahudi, manaswara au Ummah huu hata kama atakuwaanaswali kwa ajili ya Allaah. Kwa kuwa hii ni njia inayopelekea katika Shirki. Aswalikwenye Misikiti na mahli pengine pasipokuwa na kaburi kwani Allaah Kaifanya ardhi yotekuwa safi (twahara) na mahapa pakuswalia. Hapaswaliwi Swalah za faradhi wala zaSunnah, na hili si wakati wake tu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hukumu hii mpakaQiyaamah bado itaendelea kuwepo kwani haikufutwa. Hapa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) kasisitiza sana kutofanya kama walivofanya mayahudi na manaswara, lakinimbali na hili hawakuacha makhurafi na waabudu makaburi kujenga Misikiti kwenyemakaburi. Alikhofia lisije kufanywa kaburi lake Msikiti ndio maana (´Aaishah) akawaamemzika kwenye chumba chake. Vipi leo kutajitokeza mwenye kusema kwamba Msikitiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) umejengwa kwenye kaburi lake? SubhaanaAllaah. Kaburi la Mtume liko nje ya Msikiti kwenye chumba chake, chumba ndio kiliingizwandani ya Msikiti wakati walipoupanua Msikiti katika zama za Waliyd bin ´Abdul-Maalikkatika uongozi wa Baniy ´Umayyah, na hapa alikosea bila ya shaka. Lakini hata hivyo, asliya Msikiti haukujengwa kwenye kaburi.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Aliyoyasema katika kutahadharisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusumwenye kujenga Msikiti ambao anaabudiwa Allaah ndani yake kwenye kaburi la mtumwema hata kama atakuwa na nia nzuri.

2. Makatazo ya masanamu (mapicha) na mfano wake na uzito wa suala hili.

3. Somo la makatazo yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika hilo. Jinsi alivyobainishahilo na kuliweka wazi suala hilo kwanza, kisha siku tano kabla ya kufa kwake akasemayakusema, kisha wakati wa kukata roho akatadharisha hilo tena.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

105

4. Msisitizo wa makatazo yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wa kutolifanya kaburilake kuwa Msikiti kabla ya kupatikana kwa kaburi lenyewe.

5. Kwamba kuyajengea makaburi ni katika njia ya mayahudi na manaswara.

6. Kuwalaani mayahudi na manaswara kwa hilo.

7. Makusudio yake ni kututahadharisha kuhusu kaburi lake.

8. Sababu ya kutowekwa hadharani kaburi lake.

9. Maana ya kuyafanya (makaburi) kuwa Misikiti.82

10. Kamlinganisha yule mwenye kuyafanya (makaburi) kuwa Msikiti na yule ambaye Saa(Qiyaamah) kitamkuta naye yuko hai. Akataja njia zinazopelekea katika Shirki kabla yakutokea pamoja na matukio yake.

11. Utanabahisho wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla ya kufa kwake kwa sikutano akipiga Radd mapote mawili ambayo ni mabaya zaidi katika Ahl-ul-Bid´ah, bali baadhiya wanachuoni wamewatoa katika mapote sabini na moja. Nayo ni Raafidhwah (Shiy´ah) naJahmiyyah. Na sababu ya Raafidhwah ndio kumejitokeza Shirki na ´Ibaadah ya kuabudumakaburi na wao ndio walikuwa wa kwanza kuyajengea Misikiti.

12. Mateso aliyoyapata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa uchungu wa kifo.

13. Allaah Kampa Ikramu ya kuwa Khaliyl.

14. Ubainisho kuwa Ukhaliyl ni daraja ya zaidi ya mapenzi.83

15. Ubainisho ya kwamba (Abu Bakr) asw-Swiddiyq ni Swahabah bora.

16. Uashirio wa Ukhalifah wake (Abu Bakr).

82 Shaykh Fawzaan anasema: ”Kufanya makaburi kuwa Misikiti sio kuyajengea peke yake, balikuswali kwenye makaburi linaingia katika hilo hata kama hayakujengewa.”83 Shaykh Fawzaan anasema: ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anawapenda Maswahabahwake, lakini hakumfanya hata mmoja kuwa Khaliyl wake. Ni dalili ioneshayo ya kwamba Ukhaliyl nidaraja ya juu zaidi ya mapenzi.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

106

Mlango Wa 21

Yaliyokuja Ya Kuwa Kuchupa Mipaka Katika Makaburi Ya Watu WemaHupelekea Kuwa Masanamu Yanayoabudiwa Badala Ya Allaah

Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) kapokea katika kitabu chake al-Muwattwa´ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Ee Allaah! Nakuomba usilifanye kaburi langu kuwa sanamu lenyekuabudiwa. Ghadhabu za Allaah huwa kali kwa watu ambao wameyafanyamakaburi ya Mitume (´alayhimus-Swalaat was-Salaam) wao kuwa Misikiti.”

Ibn Jariyr (at-Twabariy) kapokea kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Mansuur,kutoka kwa Mujaahid kasema kuhusiana na Aayah:

أفرأيتم اللات والعزى

”Je, mmeona Laata na ‘Uzzaa (masanamu miongoni mwa miungu yamakafiri)?” (an-Najm 53:19)

“Laat alikuwa akiwatumikia mahujaji kwa kuwatayarishia Sawiyq.84 Baada yakufa, watu wakaanza kufanya I´tikaaf katika kaburi lake.”

Namna hii ndivyo alivyosema Abul-Jawzaa (Rahimahu Allaah) kutoka kwaIbn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kapokea:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawalaani wanawakewanaozuru makaburi, na wanayoyafanya kuwa Misikiti na wanaoyatiliamataa.”

(Wameipokea Ahl-us-Sunan)

84 Ni unga mzuri wa shayiri au ngano iliyochanganyika pamoja na maji na samli

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

107

Ufafanuzi:Mlango huu ni kuhusu matishio yaliyokujua kuhusu wanaofanya hivi. Awthaan nikinachoabudiwa badala ya Allaah; katika kaburi, mti, jiwe, jengo na kadhalika. Ama sanamuni kinachoabudiwa badala ya Allaah kwa sura ya mtu au mnyama ndio huitwa sanamu.Kama masanamu aliyokuwa akitengeneza baba yake na Ibraahiym (´alayhis-Salaam). Hiindio tofauti kati ya al-Wathan na sanamu. Lakini kunapotajwa sanamu tu, basi huingia humoal-Wathan. Na kunapotajwa al-Wathan kunaingia humo sanamu. Ama vikitajwa vyote kwapamoja, kila kimoja kinakuwa na maana yake.

“Ee Allaah! Nakuomba usilijalie kaburi langu kuwa sanamu lenye kuabudiwa”, hapaMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamuomba Mola Wake Amkinge kaburi lakelisifanywe kama makaburi ya Mitume wengine (´alayhimus-Salaam) wa mwanzo. Mayahudina manaswara walivyopetuka mipaka katika makaburi yao. Hii ni dalili ya kwamba,kuchupa mipaka katika makaburi kunaligeuza kuwa sanamu kaburi hilo. Haya ndiomakusudio ya mlango huu. Na Allaah Akamuitikia Du´aa yake akawa amezikwa ndani yachumba cha ´Aaishah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na (Radhiya Allaahu ´anha).Kaburi lake Allaah Kalihifadhi tangu alipokufa mpaka hivi leo.

“Ghadhabu za Allaah huwa kali kwa watu ambao wameyafanya makaburi ya Mitume(´alayhimus-Swalaat was-Salaam) wao kuwa Misikiti”, hii ina maana wanaswali katikamakaburi, wanamuomba Allaah katika makaburi na kuyajengea. Na mwenye kufanya hivyoKalaaniwa na Allaah, Kaghadhibikiwa na Allaah na Kalijaalia kuwa ni sanamu lenyekuabudiwa badala ya Allaah. Hii ni dalili ya kuwa makaburi yaliyoko leo, wanayaomba,wanayawekea nadhiri, yanachinjiwa n.k. ni Awthaan. Hakuna tofauti kati yayo na Laat.

Laat alikuwa ni mtu mwema akiwatumikia mahujaji, alipokufa wakawa wanafanya I´tikaafkatika kaburi lake. Ikiwa kubaki na kushikamana na kaburi lake ni sababu ya kufanywasanamu kubwa miongoni mwa masanamu ya Ahl-ul-Jaahiliyyah. Hii ni dalili ioneshayokuwa kuchupa mipaka katika makaburi ya watu wema kunapelekea kuyageuza kuwaAwthaan yanayoabudiwa badala ya Allaah. Na haya ndio makusudio ya Aayah iliyotajwahapo juu.

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawalaani wanawake wanaozurumakaburi”, hii ni dalili ya uharamu wa wanawake kuzuru makaburi. Na haya ndiomadhehebu ya jamhuri ya wanachuoni. Hali kadhalika mwanamke hashindikizi janaza. Kwanini? Wamesema wanachuoni ni kwa sababu wanawake ni madhaifu na hawawezi kuzizuianafsi zao wanapoona maiti na khaswa za ndugu zao, watalia kwa kupiga kelele na mayowe.Isitoshe mwanamke ni ´Awrah, atapoenda makaburi na akachanganyika na wanaume hililitapelekea katika fitina. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kakatazawanawake kuzuru makaburi kwa sababu hizi mbili. Hali kadhalika kuyatilia makaburi

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

108

mataa daima, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kamlaani anayefanya hivi kwanihii ni njia inayopelekea katika Shirki. Hali kadhalika, kuyajenge kama ukuta, kuyaandikamaneno na tarehe na kadhalika, yote haya hayajuzu ni haramu kwa kuwa yanapelekeakatika Shirki.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya al-Awthaan.

2. Tafsiri ya ´Ibaadah.

3. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuomba kinga (kwa Mola Wake) isipokuwakwa mambo aliyochelea kutokea.

4. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kaambatanisha hili85 na kuyafanya makaburiya Mitume kuwa Misikiti.

5. Kutajwa kwa Ghadhabu kali ya Allaah (kwa wanaofanya mambo kama haya).

6. Suala muhimu zaidi ni maelezo ya jinsi ´Ibaadah ya Laat ilivoanza, ambalo ni sanamukubwa miongoni mwa masanamu (ya washirikina).

7. Utambuzi ya kuwa Laat ni kaburi la mtu mwema.

8. Laat ilikuwa ni jina la mtu aliye kwenye kaburi na kutajwa maana (ya sanamu hilo) kuitwahivyo.

9. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwalaani kwake wanawake wenye kuzurumakaburi.

10. Kuwalaani kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwenye kuyawekea mataa.

85 Yaani Du´aa: ”Ee Allaah! Ninamuomba usilijaalie kaburi langu kuwa sanamu lenye kuabudiwa.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

109

Mlango Wa 22

Himaya Ya Mustwafah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) KuihamiTawhiyd Na Kufunga Kila Njia Inayopelekea Katika Shirki

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

يمحر ءوفر ننيمؤكم بالمليع ريصح منتا عم هليع زيزع أنفسكم نول مسر اءكمج لقد

”Kwa yakini amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe, ni magumujuu yake (yanamhuzunisha) yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni (kwakukujalini), mwenye huruma (na mwenye mapenzi) kwa Waumini, na mwenyerahmah.” (at-Tawbah 09:128)

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema, Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiyajaalie86 manyumba yenu kuwa makaburi, na wala msifanye kaburilangu kuwa mahali pa sikukuu. Na niswalieni,87 hakika Swalah zenu hunifikiapopote mlipo.”

(Kaipokea Abuu Daawuud kwa isnadi Hasan na wapokezi wake niwaaminifu)

Na kutoka kwa ´Aliy bin Husayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Alimuona mtu akija kwenye kijitundu kilichokuwa mahali pa kaburi laMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili apate kuingia na kuomba.Akamkataza na kusema: “Hivi nikuhadithie Hadiyth niliyoisikia kutoka kwababa yangu,88 baba yangu kaisikia kutoka kwa babu yangu,89 kapokea kutokakwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema: “Msilifanyekaburi langu kuwa mahali pa sikukuu, wala manyumba yenu kuwa kamamakaburi, na niswalieni kwani Salaam zenu hunifikia popote mlipo”.”

86 Kuyafanya87 (Allaahumma swalli wa sallim ´alaa Nabiyyinaa Muhammad)88 Husayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa)89 ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

110

(Imepokelewa katika Mukhtaarah)90

Ufafanuzi:Hapa Shirki inayokusudiwa ni kubwa na ndogo. Na al-Mustwafah hapa anakusudiwa MtumeMuhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Muislamu anatakiwa kuchunga ´Aqiydahyake, na awe tahadhari isichanganyike na Shirki. Ikiwa mtu hakujifunza ´Aqiydah sahihiiliyojengeka juu ya Qur-aan na Sunnah kwa mfumo wa Salaf-us-Swaalih, mtu anawezakutumbukia katika Shirki ambayo inalinganiwa na kupambiwa na Madu´aat wapotofu.Kwani leo kuna makundi ambayo hamu yao kubwa na nguvu zao zote wanazitumia katikakutaka kuwapoteza watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kafungua njia zotezinazopelekea katika Shirki; kukataza kujenga kwenye makaburi, kuchupa mipaka kwa mtuna kwa kaburi. Kakataza hata kumuabudu Allaah kwenye makaburi, kumuomba Allaahkwa Du´aa kwenye makaburi. Hata kama muombaji anamkusudia Allaah (´Azza wa Jalla)Pekee, lakini kinachozingatiwa ni mahali. Kwa kuwa hii ni katika njia inayopelekea katikaShirki, asije kuadhimishwa mtu wa kaburi hili, wakachupa mipaka kwake, wakadhani yakwamba ananufaisha na kudhuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufungamlango wa ´Aqiydah hii ndio maana akawa amekataza. Kila kitu kinachopelekea katikaShirki, haramu na maasi, basi kitu hicho kimekatazwa. Na hili ni jambo liko wazi. KutazamaAliyoharamisha Allaah, kusikiliza Aliyoharamisha Allaah kama muziki na firimbi, ´Ibaadahkwenye makaburi - na hili ndio baya zaidi, kukaa na watu wa shari, yote haya yamekatazwa.Kutokana na sifa zilizotajwa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Aayahhapo juu, hastahiki kwa mtu kama yeye na wala hawezi kuwaacha watu katika upotofu bilaya kuwabainishia.

Hadiyth ya Abuu Hurayrah, yaani msiache kuswali ndani yake. Kwa kuwa maiti ndani yakaburi lake ndio haswali na wala hafanyi kitu chochote. Nyumba ambapo hakuswaliwindani yake si Swalah ya Sunnah wala hadhukuriwi Allaah ndani yake, nyumba hii ni kamakaburi. Vipi ikiwa nyumba itakuwa imejaa maasi, nyimbo na chaneli mbovu, vipi itakuwahali ya nyumba hii na watu wake? Hivyo ni muhimu nyumba iwe na muamsho kwakuswaliwa ndani yake na kudhukuriwa Allaah. Kutoyafanya makaburi mahali pa sikukuu,kukusanyika na kuyatembelea mara kwa mara. Kwa kuwa huku ni kuchupa mipaka na ninjia inayopelekea katika Shirki. Lakini yule aliyetoka katika safari, amtolee Salaam Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maswahibu zake na aende zake. Na wala asikariri hilikila anapoingia Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamtolea Salaam,hapana. Hili ni jambo halikufanywa na Salaf na walikuwa wakilikataza. Kwa kuwa nikuchupa mipaka na huenda likapelekea katika Shirki. Ikiwa hali ni namna hii kwa kaburi la

90 Ya Imaam al-Maqdisiy

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

111

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), vipi kwa makaburi ya wengine ambayoyamefanywa ni masanamu yakiabudiwa badala ya Allaah? Hivyo mtu anapaswa kumswaliaMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) popote alipo na si lazima aende kwenye kaburilake, kwani Swalah na Salaam yako inamfikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)popote utapomswalia. Kwa kuwa kwenda mara kwa mara kwenye kaburi ni njiainayopelekea katika al-Ghuluu na Shirki. Na hii (kumswalia) ni katika haki ya Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) juu yako.

Na Hadiyth ya pili ya ´Aliy bin Husayn Zayn-ul-´Aabidiyn ni kama ile ya kwanza ya AbuuHurayrah. Huyu ni katika maimamu wa Taabi´iyn. Alipoona mtu anaenda kwenye kaburi laMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ajili ya kumswalia tu, ndo akawaamemwambia Hadiyth hii. Hapa kuna faida ya kukataza maovu na kufikisha elimu kwayule ambaye haikumfikia, na kumsimamishia hoja mwenye kwenda kinyume. Huyu nikatika Ahl-ul-Bayt anakataza hili. Shiy´ah wako wapi na mafunzo haya ya kutokuwa naGhuluu kwa Ahl-ul-Bayt?

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya at-Tawbah. (09:128)

2. Kujitahidi kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuuweka Ummah wake kadiri naawezavyo mbali kabisa na Shirki.

3. Kutuhangaikia kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa huruma na rahmah.

4. Kukataza kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kulitembelea kaburi lake kwa njiamakhsus na maalum, pamoja na kwamba kumtemelea ni katika ´amali bora.

5. Kutukataza kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumtembelea sana.

6. Uhimizo wake juu yetu wa kuswali Naafilah (Swalah za Sunnah) nyumbani.

7. Kukubaliana kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum ajmaa´iyn) ya kwamba haijuzukuswali makaburini.

8. Kafasiri hilo, ya kwamba Swalah na Salaam ya mtu kwake inamfikia (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) hata akiwa mbali kiasi gani. Hivyo hakuna haja kwa yule mwenyekupindua maana ya umuhimu wa kutaka kuwa na ukaribu (wa kaburi lake).

9. Kuwa kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika al-Barzakh (kaburi) naSwalah na Salaam za Ummah wake anafikishiwa.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

112

Mlango Wa 23

Yaliyokuja Ya Kwamba Baadhi Ya Watu Katika Ummah Huu WataabuduMasanamu

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

ـؤلاء أهدى من الذين آمنوا سبيلاألم تر إلى الذين أوتوا نصيبا من الكتاب يؤمنون بالجبت والطاغوت ويقولون للذين ك وا هفر

”Je, huoni (huzingatii) wale ambao wamepewa sehemu ya Kitabu wanaaminimazimwi na twaaghuwt na wanasema juu ya wale ambao wamekufuru kuwa:“Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale ambao wameamini”.” (an-Nisaa 04:51)

Kauli Yake (Ta´ala):

اللـه ندة عثوبم كن ذلر مبئكم بشل أنقل ه ◌ن لعم دبعو ازيرنالخة ودرالق مهنل معجو هليع بغضو اللـه هنالطاغوت ـئك شر مكانا وأضل عن سواء السبيل◌ أول

”Sema: “Je, nikujulisheni yaliyo maovu zaidi kuliko hayo kwa malipo mbeleya Allaah?” Yule ambaye Allaah Amemlaani na Akamghadhibikia naAkawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe na wakaabudu twaaghuwt,hao wana mahali pabaya mno (Aakhirah) na wapotofu zaidi na njia iliyo sawa(duniani).” (al-Maaidah 05:60)

Kauli Yake (Ta´ala):

غلبوا على أمرهم لنتخذن عليهم مسجدا ينقال الذ

“Wakasema wale walioshinda katika shauri lao: “Bila shaka tutajenga Msikitijuu yao”.” (al-Kahf 18:21)

Kutoka kwa Abuu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwambaMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika, mtafuata njia za waliokuwa kabla yenu hatua kwa hatua, mpakawatapoingia shimo la mburukenge nanyi mtaingia.” Wakasema: “Ewe Mtume

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

113

wa Allaah! Je, wamaanisha Mayahudi na Manaswara?” Akasema: “Ni naniwengine [ikiwa si wao]?”

(Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

Muslim kapokea kutoka kwa at-Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anhu) yakwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Hakika Allaah Kanikunjulia ardhi nikaona mashariki na magharibi yake. Nahakika ufalme wa Ummah wangu91 utafikia kiasi na vile nilivyokunjuliwa nanimepewa hazina mbili; nyekundu92 na nyeupe.93 Na mimi nimemuombaMola Wangu Asiangamize Ummah wangu kwa njaa kubwa yenye kuenea, nawala Asiwatumie adui akawatawalia ardhi zao isipokuwa wa kutoka katikawao wenyewe. Mola Wangu Akanambia: “Ewe Muhammad! Mimi Ninapotoaamri hakika hairudi wala kurejeshwa. Na mimi Nimekupa wewe kwa ajili yaUmmah Wako ya kwamba sintowahilikisha kwa njaa kubwa na kwambaSintowatumia adui isipokuwa wenyewe kwa wenyewe watawalie nguvu zaowenyewe kwa wenyewe, hata kama watajikusanya watu wa pande zote zadunia wasingeliwapata, mpaka itakuwa baadhi yao wakiwaangamizawengine94 na wakidhulumiana wao kwa wao.”

al-Barqaaniy kaipokea Hadiyth hii katika Swahiyh yake na kaongezea:

“Na kubwa ninalolikhofia kwa Ummah wangu ni viongozi wapotevu. Nawatapoanza kusimamishiana panga95 hazitosimamishwa mpaka siku yaQiyaamah. Na hakitosimama Qiyaamah mpaka kikundi katika Ummahwangu kiwafuate washirikina, na mpaka kikundi katika Ummah wangukiabudu masanamu. Na hakika kutakuwa katika Ummah wangu waongothalathini, na kila mmoja wao atadai ya kwamba yeye ni Mtume, na mimindio muhuri wa Mitume na hakuna Mtume mwingine baada yangu. Na walahakitoacha kikundi katika Ummah kuwa juu ya haki wakiinusuru,

91 Yaani Dini ya Uislamu92 Anasema Shaykh Fawzaan: ”Hazina za warumi ambazo zilikuwa ni dhahabu.”93 Anasema Shaykh Fawzaan: ”Hazina za wafursi ambazo zilikuwa ni lulu na fedha.”94 Wao kwa wao95 Yaani watapoanza kuuana wao kwa wao

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

114

hatowadhuru yule mwenye kuwapinga na kuwakhalifu mpaka itapofikaamri96 ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala).”

Ufafanuzi:Yaliyokuja, yaani dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah kuonesha dalili kuwa baadhi yaUmmah huu wataabudu masanamu. Na hii ni Radd kwa wale wanaodai ya kwambaUmmah huu hauwezi kufanya Shirki. Na yanayofanywa kwenye makaburi na kwenginepohawayaiti kuwa ni Shirki, wanayaita kuwa ni kuwa ni tawassul, Shafaa´ah n.k., manenohaya ni kama yale ya washirikina wa mwanzo:

ينالذلفى وز ا إلى اللـهونقربيإلا ل مهدبعا ناء ميلأو ونهن دذوا مخات

”Na wale waliojichukulia badala Yakeawliyaa (wasaidizi, miungu; wakisema): “Hatuwaabuduisipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu.” (az-Zumar 39:03)

اللـه ندا عناؤفعلاء شـؤ قولون هيو مهنفعلا يو مهرضا لا يم اللـه ونن دون مدبعيو

”Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao (hawawezi) kuwadhuru na wala (hawawezi)kuwanufaisha, na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah”.” (Yuunus 10:18)

Wao wanaita Shirki inayofanywa na Ummah huu kuwa sio Shirki, bali wanafikia mpakakusema kuwa hii ndio Dini na kadhalika. Madu´aat wapotofu hawakati tamaa katikakuwalingania watu katika upotofu. Na hii ni katika Hekima ya Allaah. Mtu anapofanyaShriki wanasema kuwa hio sio Shirki kwa kuwa Ummah huu hauna Shirki. Na hakuna daliliyoyote ya hilo. Ama kauli yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika Shaytwaan kakata tamaa kuabudiwa katika ardhi hii” au Hadiyth mfano wa hii.

Hakuna dalili ya kuwa Ummah huu hauwezi kufanya Shirki, kuna khabari tu kuhusiana naShaytwaan ya kwamba pindi alipoona nguvu ya Uislamu na Tawhiyd alikata tamaa katikanafsi yake mwenyewe na si kwamba hakutatokea Shirki katika Ummah huu. Na si kwambani Ummah wote, isipokuwa ni baadhi ya watu, kwa kuwa Ummah wote hauwezikukusanyika juu ya upotofu.

96 Qiyaamah

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

115

al-Awthaan ni kila kinachoabudiwa badala ya Allaah, sawa kiwe na sura au kisiwe na sura.Ikiwa kina sura ya mnyama huitwa sanamu. Na ikiwa hakina sur - kama kaburi, mti, mawena kadhalika - huitwa Wathan. Hali kadhalika kuna Radd kwa wale wanaosema kuwa Shirkini kuabudu masanamu peke yake, vinginevyo haiwezi kuwa Shirki.

“al-Jibt” ni uchawi. Na “at-Twaaghuut” ni kila kinachoabudiwa badala ya Allaah. Washirikinawaliabudu badala ya Allaah, hivyo wakawa wameabudu Twaaghuut. Na Aayah hii97

imeteremka kuhusu mayahudi walipowashuhudia waabudu masanamu ya kwamba waondio waongofu kuliko Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na hiliwalilifanya kwa ajili ya hasadi na jeuri tu, pamoja na kwamba wanajua vizuri ni Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye aliye juu ya haki. Tunachojifunza katika Aayah hikwamba, ikiwa katika mayahudi kuko ambao wanaamini Jibt na Twaaghuut, basi kutakuwavile vile katika Ummah huu watakaoabudu al-Jibt na Twaaghuut. Kwa kuwa Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) katueleza kuwa kutajitokeza ambao watajifananisha namayahudi na manaswara, katika kuabudu badaba ya Allaah.

Aayah ya pili,98 Ahl-ul-Kitaab walikuwa wakiwakejeli na kuwaponda Waislamu pindiwanaposikia adhaana. Wanasema: “Hatujaona watu wenye Dini ya shari kama ya kwenu.”Pamoja na kwamba wanajua vizuri ya kuwa Dini ya haki ni hii ya Waislamu. Ndipo AllaahAkawaradi kwa Aayah hii na kubainisha aibu yao. Hivyo, shari ya watu kabisa ni mayahudina manaswara kwa kuwa wamemuasi Allaah kwa ujuzi. Wamelaaniwa,wameghadhibikiwa, wakafanywa miongoni mwao kuwa manyani na nguruwe na baya zaidiwakaabudu Twaaghuut.

Kichwa cha matwaaghuut ni 1) Shaytwaan, na 2) atakayeabudiwa naye akawa radhiya hilo, na 3) yule atakayewaita (lingania) watu kumuabudu, na 4) yule anayedaikujua elimu ya Ghayb na 5) yule mwenye kuhukumu kinyume na Shari´ah. Watuhawa watano ndio vichwa vya matwaaghuut. Kama alivyosema Ibn al-Qayyim(Rahimahu Allaah).

Na Aayah ya mwisho99 ni kuhusu watu wa Kahf100 ambao walijengewa Msikiti juu yamakaburi yao. Na hii ndio chanzo cha Misikiti kuanza kujengwa kwenye makaburi. Ikiwakatika Ummah zilizotangulia kulikuwepo ambao wanajenga Misikiti kwenye makaburi, halikadhalika kutakuwa katika Ummah huu watakaofanya hivyo. Hapa kuna Radd vile vilekwa wale wanaosema hakutotokea katika Ummah huu waabudu makaburi na kuyajengeamakaburi.

Na Hadiyth ya Abuu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anhu) ni khabari ya kiapo. “latattabi´unna... ”“lam” iliyopo ni ya kiapo na ikafuatiwa na “nun” ya msisitizo. Hadiyth hii ni dalili ya

97 (04:51)98 (05:60)99 (18:21)100 Kundi katika wao waliokuwa wema

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

116

maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba lazima kutakuwepo watukatika Ummah huu watakaojifananisha na Ahl-ul-Kitaab kabisa. Akakazia hilo kwa kusema“... mpaka watapoingia katika shimo la mburukenge nanyi mntaingia.” Na baya katikakujifananisha nao ni kuabudu badala ya Allaah. Na hili limetokea kabisa kamaalivyokhabarisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwani Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) haongei kwa matamanio yake. Na washirikina wa leo wanasema“hapana, hakuna Shirki.” Kana kwamba wanamkadhibsiha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam).

Hadiyth ya at-Thawbaan: Wakati Waislamu walitawala katika miji ya wafursi na warumiAllaah Aliwafanyia halali ngawira ya dola hizi mbili waufanye Uislamu kuwa na nguvukwazo na wazitoe katika njia ya Allaah, badala ya kuzitumia katika kufuru zikawazinatumika katika kueneza Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi wakati Waislamu walizitawala. Hiini khabari ya Ghayb aliyoeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baadaeikatokea. Miujiza, ishara na ukweli wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na hapa kunatahadhari ya Waislamu kutawanyika na kufarakana. Kwani wakiwa kitu kimoja adui (kafiri)hatoweza kupata nafasi ya kuwaingilia na kuwatawala. Na katika upokezi mwingineambapo kumekuja ya kwamba anakhofia juu yetu viongozi wapotevu huu ni msibamwengine. Na makusudio ni watawala, wanachuoni wapotevu na wanaoabudu wapotevu.Hawa watu watatu ndio hupoteza watu pindi wanapotea na kupinda. Na watu hawa watatuwakiwa sawa na kuongoka, Ummah pia huongoka na kuwa vizuri. Na nukta muhimuikusudiwayo katika Hadiyth ya mwisho, ni pale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)aliposema: “Na hakitosimama Qiyaamah mpaka kikundi katika Ummah wangu kiwafuatewashirikina, na mpaka kikundi katika Ummah wangu kiabudu masanamu”, kikundi katikaUmmah huu kitaritadi na kuwafuata washirikina. Na hii ni Radd kwa wale wanaosemakuwa Ummah huu hauna Shirki. Na yamekwishatokea haya aliyoyaeleza Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam).

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio muhuri wa Mitume. Hivyo yeyoteatakayejitokeza na kudai kuwa ni Mtume ni kafiri. Na yule ambaye atamsadikisha mtu huyunaye pia ni kafiri. Ama kuteremka kwa Masiyh ´Iysa (´alayhis-Salaam) atakuwa ni mwenyekumfuata Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), atakuwa akihukumu kwaShari´ah ya Uislamu ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Atakuwa ni katikaMujaddidiyn. Lakini mbali na yote haya, kutakuwepo kikundi (Jamaa´ah) kitachoendeleakubaki katika Dini sahihi mpaka Qiyaamah kifike.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

117

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat an-Nisaa101 (04:05)

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Maaidah (05:60)

3. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Kahf (18:21)

4. Faida ya nne – nayo ndio muhimu zaidi - maana ya kuamini al-Jibt na at-Twaaghuut. Je,maana yake ni kuamini kwa moyo; au maana yake ni kukubaliana na watu wake(washirikina) pamoja na kuchukia hilo na kuitakidi upotofu wake?102

5. Kauli yao (mayahudi) kuwa makafiri (wa ki-Quraysh) ambao kihakika wanajua kufuruyao kwamba wameongoka zaidi katika njia kuliko wale ambao wameamini.

6. Faida ya sita – na ndio makusudio katika mlango huu - watu kama hawa lazima wawepokatika Ummah huu wa Waislamu kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Abuu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anhu)103

7. Matukio ya tamko lake kwamba wengi katika Ummah huu wataabudu masanamu104

8. Maajabu makubwa ya kujitokeza ambao wanadai Utume; kama mfano wa Mukhtaar (binAbiy ´Ubayd ath-Thaqafiy) licha ya kutamka kwake Shahaadah mbili na tamko lake yakwamba na yeye ni katika Ummah huu na (kushahidilia kwake ya) kwamba MtumeMuhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wa haki, Qur-aan ni haki, pamoja nakuwa ndani yake kumeandikwa ya kuwa Mtume Muhammad ndio muhuri wa Mitume.Lakini pamoja na hili yeye - licha ya utata wake wa dhahiri – alikuwa anasadikisha yotehaya. al-Mukhtaar alijitokeza katika zama za mwisho za Maswahabah na kuna watu wengiwaliomfuata.105

9. Bishara njema ya kwamba haki haitopotea moja kwa moja - kama ilivyokuwepo mwanzo –bali kutakuwepo daima kipote.

101 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa tunapata kujifunza ya kwamba, yeyote ambaye atakubaliana namakafiri juu ya Shirki na kufuru – hata kama itakuwa kwa kutamka tu – anakuwa ni katikawanaoamini al-Jibt na Twaaghuut.”102 Shakh Fawzaan anasema: ”Bila ya shaka maana yake ndio hii. Yule mwenye kusifia dini yawashirikina hata kama itakuwa angalau kwa ulimi wake, anakuwa kaamini al-Jibt na Twaaghuwt.”103 Shaykh anasema: ”Kuna Radd kwa yule mwenye kusema ya kwamba Ummah huu hauwezi kuwana Shirki.”104 Kila kinachoabudiwa badala ya Allaah105 Anasema Shaykh: ”Huyu ndiye aliyemuua ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhu). Watuwakashangazwa sana na nguvu zake na wakamfuata watu wengi. Alikuwa akitawala Kuufa. Mpakahapo Waislamu walipokuja kumuua baadae.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

118

10. Ishaara kubwa ya kwamba wao pamoja na udogo wao, hawatowadhuru wale wenyekuwapinga wala kuwakhalifu.106

11. Itaendelea kuwa hivi mpaka Saa107 isimame.

12. Kuna miujiza Ishaara kubwa mbali mbali ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam). Miongoni mwazo:

- Allaah (Ta´ala) Kamkunjulia ardhi akaona mashariki na magharibi. Akamwambiamaana ya hilo, na imetokea kama alivyoelezea, kinyume na kaskazini na kusini.

- Kapewa hazina mbili.

- Du´aa zake mbili108 zimekubaliwa.

- Du´aa yake ya tatu haikukubaliwa.

- Watapoanza kusimamishiana panga (kuuana) hazitosimama mpaka Qiyaamah kitokee.

- Kutajitokeza kwa Mitume wa uongo wataodai Utume katika Ummah huu.

- Kutaendelea daima kuwepo kipote kilichonusuriwa.

- Na yote haya yametokea kama alivyoeleza ingawa kila mmoja wao ilikuwa haimuingiikabisa akilini.109

13. Khofu kwa Ummah wake juu ya viongozi wapotofu.

14. Onyo na tanbihi ya maana ya kuyaabudu masanamu.110

106 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hali kama inavyoshuhudiwa leo makafiri wanayofanya dhidi yaUislamu, pamoja na yote haya watu wa haki bado wataendelea kuwepo dhahiri wenye kunusuriwajuu ya haki.”107 Anasema tena: ”Wanachuoni wametofautiana juu ya neno “Saa”; je makusudio ni kuisha kwadunia au makusudio ni Saa pindi Allaah Atawapowafisha waumini wote na kusibaki juu ya ardhiisipokuwa makafiri na washirikina tu? Kauli hii ya pili ndio yenye nguvu. Na Allaah Anajua zaidi.”108 Shaykh anasema: ”Allaah Alimkubalia maombi yake mawili; Kutoungamize Ummah wake kwanjaa kubwa yenye kuenea na wala Asiwatumie adui akawatawalia ardhi zao isipokuwa wa kutokakatika wao wenyewe. Ombi la mwisho – la kutouana wao kwa wao – hakumkubalia.”109 Shaykh tena: ”Yaani kila mmoja katika Ummah huu. Ya kwamba Ummah huu dhaifu itamilikiardhi na itashinda dola kubwa, hili haliingii akilini. Lakini ni kutokana na Qadhwaa na Qadar yaAllaah (Ta´ala). Na kwamba Ummah huu uliokuwa dhaifu Allaah (Ta´ala) Aliwapa hazina mbili yadhahabu na fedha. Ni nani awezae kusadikisha hili? Lakini haya ni makadirio na mipango ya Allaah(Ta´ala). Na kujitokeza kwa waongo wataodai Utume, hakuna aliyekuwa anaamini hili kwa vile Qur-aan ilikuwa imeweka wazi ya kwamba Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiomuhuri wa Mitume. Pamoja na haya waongo walijitokeza na wakajitokeza waliowasadikisha.”110 Shaykh anasema: ”Maana yake ni kuwafuata washirikina, kuwasadikisha na kujifananisha nao. Namaana yake sio kuyasujudia na kuyaabudu peke yake.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

119

Mlango Wa 24

Yaliyokuja Kuhusu Uchawi

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

ولقد علموا لمن اشتراه ما له في الآخرة من خلاق

“Na kwa hakika walielewa111 kwamba atakayenunua (atayefanya biashara yauchawi) hatopata katika Aakhirah fungu lolote.” (al-Baqarah 02:102)

Na Kauli Yake:

الطاغوتو تون بالجبنمؤي

“Wanaamini mazimwi na twaaghuwt.” (an-Nisaa 04:51)

Kasema ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Jibt ni uchawi, na twaaghuut ni Shaytwaan.”

Na kasema Jaabir (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Twaaghuut ni makuhani walikuwa wakiteremkiwa na Shaytwaan na kilakabila lina mmoja.”

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwambaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Jiepusheni na madhambi saba yenye kuangamiza.” Wakasema: “Ewe Mtumewa Allaah! Ni yapi hayo?” Akasema: “1)Ni kumshirikisha Allaah, 2) uchawi,3) kuiua nafsi ambayo Allaah Kaiharamisha kuuliwa isipokuwa kwa haki, 4)kula Ribaa, 5) kula mali ya mayatima, 6) kukimbia siku ya vita na 7)kuwazulia uongo wa kuzini wanawake wa Kiislamu waliohifadhika.”

Kutoka kwa Jundub (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea Hadiyth Marfu´:

111 Yaani mayahudi

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

120

“Adhabu ya mchawi ni kuuawa kwa upanga.”

(Kaipokea at-Tirmidhiy na amesema Swahiyh ni kuwa ni Mawquuf)

Katika Swahiyh al-Bukhaariy, kutoka kwa Bajaalah bin ´Abadah ambayeamesema: “´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´alayhi wa sallam)kaandika: “Auawe kila mchawi mwanaume na mwanamke.” Bajaalahanaendelea kusema: “Tukaua wachawi watatu.”

Imesihi kutoka kwa Hafswah (Radhiya Allaahu ´anha) ya kwamba yeyealiamrisha auawe mtumishi wake ambaye alikuwa kamfanyia uchawi,akauawa.” Hali kadhalika kitendo hicho kimesihi kutoka kwa Jundub(Radhiya Allaahu ´anhu) pia.

Anasema Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) kuhusiana na Maswahabahwatatu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).112

Ufafanuzi:Uchawi ni katika aina ya Shirki inayopingana na Tawhiyd, ndio maana mwandishi akawaameweka mlango huu. Kwa kuwa mchawi hawezi kuufikia uchawi mpaka awatumieMashaytwaan na kunyenyekea kwao. Uchawi ulikuwepo tokea Ummah zilizotangulia.Kama Alivyosema Allaah kuhusu Fir´awn na watu wake na mayahudi. Na uchawiumegawanyika sehemu mbili:

- Uchawi wa kihakika.

Huu unaua, unamfanya mtu kuwa mgonjwa, unamtenganisha mume na mke, unaathiri akiliza mtu n.k.

- Uchawi wa udanganyifu (mazingaombwe).

Unawadhihirishia watu machoni mwao kuona kitu kinyume na uhakika wake.

Na uchawi wote huu ni shari, kufuru, kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla) na kuenezaufisadi katika ardhi.

112 Waliowaua wachawi; ´Umar, Jundub na Hafswah (Radhiya Allaahu ´anhum ajma´iyn)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

121

Allaah Alifanya Mashaytwaan wakawa wanamtumikia Nabii Sulaymaan (´alayhis-Salaam)kwa idhini yake kwa lile alipendalo. Mayahudi wakawa wamemtuhumu Nabii wa AllaahSulaymaan (´alayhis-Salaam) ya kwamba ni mchawi. Allaah Akawa Amemtakasa kwa hilokwa Kusema:

كفرة فلا تنتف نحا نمقولا إنى يتح دأح نم انملعا يمو

“Na (hao Malaika wawili) hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi nimtihani, basi usikufuru (kufanya uchawi)”.” (al-Baqarah 02:102)

Hii ni dalili ya kwamba uchawi ni kufuru.

ـكن الشياطني كفروا ول

“Lakini shayaatwiyn ndio waliokufuru.” (al-Baqarah 02:102)

Walikufuru kwa nini?

وتارمو وتارابل هن ببلكيلى الما أنزل عمو رالسح اسون النملعي ◌كفرة فلا تنتف نحا نمقولا إنى يتح دأح نم انملعا يمو

”Wanafundisha watu uchawi na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili (katika mji wa) BaabilHaaruwt na Maaruwt. Na (hao Malaika wawili) hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze:“Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru (kufanya uchawi)”.” (al-Baqarah 02:102)

Ni dalili ioneshayo ya kwamba kuufunza na kujifunza uchawi ni kufuru.

Makuhani ni wale wanaodai kujua mambo yaliyofichikana. Watu walikuwa wakiendakuhukumiwa kwao wakati wa zama za Uhaajiliyyah. Na matwaaghuut ndio makuhani.Hakujua mambo haya yaliyofichikana kwa uwezo wake, bali hujua mambo haya kwakupitia kwa Shaytwaan na kuwafunza uchawi.

نياطيل الشزنن تلى مع بئكمل أنيمهأث لى كل أفاكل عزنت

”Je, Nikujulisheni wanaowateremkia mashaytwaan? Wanateremka juu ya kila mzushimkubwa mwingi wa kutenda dhambi.” (ash-Shu´araa 26:221-122)

Wachawi wanachukua elimu kwa Mashaytwaan. Hii ni dalili ya kwamba uchawi nikumkufuru Allaah (´Azza wa Jalla) kwa kuwa ni katika matendo (mafunzo) ya Shaytwaan.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: “Jiepusheni na madhambi saba... “.Kujiepusha ni khatari sana kuliko Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaposemaacheni. Maana ya kujiepusha yaani mtu ajiweke mbali na asisogelee kabisa. Na katikamadhambi hayo saba kaanza kwa kusema Shirki.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

122

Katika Hadiyth ya Jundub, Bajaalah na Hafswah, hapa tunapata kujifunza ya kwambaadhabu ya mchawi ni kumuua. Kukithibiti ya kwamba ni mchawi kwa kukubali kwakemwenyewe, au kwa kumshuhudia, basi ni wajibu kumuua. Na wala hakuna kutubia,anauawa kwa hali yoyote ile ili kutokomeza mbali shari yake. Anauawa sawa akiwa nimchawi mwanaume au mwanamke. Hizi ni dalili zioneshazo ya kwamba adhabu ya mchawini kuuawa.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Baqarah. (02:102)

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat an-Nisaa. (04:51)

3. Tafsiri ya neno “al-Jibt”113 na “Twaaghuut” na tofauit kati ya hayo mawili.

4. Kuwa Twaaghuut inaweza kuwa katika jini na inaweza kuwa katika binaadamu.

5. Ujuzi wa madhambi saba yenye kuangamiza yaliyokatazwa vikali.

6. Ya kwamba mchawi anakufuru.

7. Ya kwamba anauawa na wala hakuna kutubia.114

8. Uchawi umepatikana kwa Waislamu katika zama za ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu),tusemeje baada yake?115

113 Shaykh Fawzaan anasema: ”al-Jibt ni uchawi; na Twaaghuut ni Shaytwaan.”114 Shaykh anasema tena: ”Ni kwa sababu hata ikiwa atadhihirisha kutubia kwa kutamka, hatubundani ya moyo wake kwa kuwa ni Zindiyq (mnafiki). Na Zindiyq hatubii hata ikiwa atadhihirishakutubia. Kwa kuwa moyo wake umeshaharibika.”115 Shaykh anasema tena: ”Ikiwa zama zake ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu) uchawi umepatikana,basi baada yake ni aula zaidi. Na leo uchawi na wachawi wamekuwa wengi katika ulimwengu waWaislamu. Bali wamekuwa mpaka na chaneli na kuwalingania watu katika uchawi huo kwa kutumiajina la Ruqyah. Hivyo ni wajibu kuwa na tahadhari na hili.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

123

Mlango Wa 25

Ubainisho Wa Kitu Katika Aina Ya Uchawi

Kasema Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah): “Katuhadithia Muhammad binJa´far, kapokea kutoka kwa ´Awf, kapokea kutoka kwa Haiyaan bin al-´Alaa,kapokea kutoka kwa Qatwaan bin Qabiyswah, kapokea kutoka kwa baba yakeambaye kasikia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)akisema:

“Hakika al-´Iyaafah, at-Twarq na at-Twiyarah ni katika al-Jibt.”

Kasema ´Awf (Radhiya Allaahu ´anhu):

“al-´Iyaafah ni kuachilia ndege.”116

“at-Twarq ni msitari unaochorwa kwenye ardhi.”

Hasan al-Baswriy kasema:

“al-Jibt ni sauti ya Shaytwaan.”

(Isnadi yake ni nzuri)

Hadiyth imepokelewa kutoka kwa Abuu Daawuud, an-Nasaa´iy na IbnHibbaan kupitia isnadi Hasan katika Swahiyh zao.

Kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kapokea ya kwambaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayejifunza sehemu ya elimu ya nyota atakuwa amejifunzasehemu katika uchawi. Wale ambao wanajifunza zaidi hujizidishia.”117

(Kaipokea Abuu Daawuud na isnadi yake ni Swahiyh)

116 Ndege inafungwa, halafu huachiliwa na kurushwa. Kisha kunatabiriwa matukio kutokana naupande ambao ndege yule ataruka117 Kujizidishia elimu ya uchawi na ndo madhambi yanavokuwa mengi

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

124

Katika an-Nasaa´iy, Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´an hu) imepokelewakwake kwamba kasema:

“Atakayefunga fundo kisha akalipulizia, basi atakuwa amefanya uchawi, namwenye kufanya uchawi atakuwa ameshiriki.”118 Na atakayevaa119

[kujiambatanisha na] kitu120 huwakilishwa kwacho.”

Kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Je, nikuambieni ni nini al-´Adwh? Ni kueneza uvumi baina ya watu.”121

(Kaipokea Muslim)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Hakika katika ufaswaha kuna uchawi.”122

Ufafanuzi:Alipobainisha katika mlango wa kwanza hukumu ya mchawi na uchawi, ndio akaonaabainishe uchawi ni nini na aina zake ni zipi ili mtu aweze kujiepusha nao. Kwa kuwaunapotahadharisha kitu ni lazima uwabainishie watu ili waweza kujiepusha nacho. Ndiomaana Shaykh kaweka mlango huu.

118 Amefanya Shirki119 Atakayekitegemea kitu badala ya Allaah120 Hirizi na mfano wake121 Kufitinisha122 Ufaswaha unaoigeuza haki kuwa batili, na batili kuifanya kuwa haki. Muhimu! Shaykh Fawzaananasema: ”Masuala haya wametofautiana wanachuoni kwao, kauli yake Mtume: ”Hakika katikaufaswaha kuna uchawi”, je Mtume kasema hivi kwa kulaumu (kukataza) kuwa na ufaswaha aukasema hivi kwa ajili ya kusifia? Kauli ya sahihi ni kwamba, ufaswaha unapotumiwa kwa kuinusuruhaki, kuibainisha na kulingania katika Dini ya Allaah, basi ni kheri na ni neema kutoka kwa Allaah.Ama ukitumiwa katika kueneza shari, kuwatenganisha Waislamu, uadui na kadhalika, basi ufaswahaunakuwa ni wenye kulaumiwa kwa sura hii. Mtume kasema: ”Hakika katika (miongoni) mwaufaswaha kuna uchawi” na wala hakusema kuwa ni ufaswaha wote. Ni dalili ya kuwa ufaswahayategemea.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

125

al-´Iyaafah: Katika Ujaahiliyyah walikuwa wakiangalia ndege kisha wanatabiri yatayotokeakatika Mustaqbal kutokana na harakati itayofanya ndege hiyo; kutakuwa kheri au shari. Hiindio at-Twiyyarah na ndio al-´Iyaafah. Nayo ni Shirki kama tulivyosema.

at-Twarq: Mpokezi wa Hadiyth ´Awf kafasiri kuwa ni kuchora kwenye ardhi. Kuna watuambao wanaitwa ar-Ramaaniyn. Huchora msitari kwenye ardhi – hususan wanawake – kishawanaeleza kuwa kutatokea kadhaa na kadhaa. Kwa kuwa wanaponyenyekea kwaMashaytwaan, wao ndio huwaambia haya. Mashaytwaan ndio huwaambia katikaMustaqbal kutajitokeza kadhaa na kadhaa. Pengine akapatia kweli na wakati mwingineakakosea. Kwa kuwa huku ni kubahatisha tu. Lakini kudai kujua mambo yaliyofichikana,huku ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jalla). Kwa kuwa hakuna ajuae Ghayb isipokuwaAllaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

al-Jibt ina maana nyingi kama tulivyosema. Kuna ambayo ni uchawi, kuna ambayo ni sautiya Shaytwaan ambayo anawaita kwayo watu katika upotofu. Na katika sauti ya Shaytwaanni nyimbo. Nyimbo ni katika sauti ya Shaytwaan.

Hadiyth ya Ibn ´Abbaas ni dalili kuonesha ya kwamba unajimu ni katika aina za uchawi.Unajimu ni kutabiri mambo kutokana na hali za nyota. Wanajimu wanatabiri mambo kwakutumia hali za nyota, kuchomoza kwake na kuzama kwake. Wanasema kutatokea kadhaana kadhaa. Hili ni kufuru na ni kudai kujua elimu ya mambo yaliyojificha. Na ni katika ainaza uchawi. Hii ni dalili ya uharamu wa elimu ya unajimu. Nyota Allaah Kaziumba kwamalengo matatu:

1. Mapambo ya mbigu

2. Kombora kwa Mashaytwaan

3. Alama kwa ajili ya uongozi wa mwenye kusafiri.

Hazitolei dalili ya kheri wala shari.

Ama kutumia nyota katika kuhesabu, Qiblah, wakati n.k. hili halina ubaya ni mubaahah.Allaah Kazijaalia ili kuzitumia kwa kujua hesabu.

ابسالحو السنني ددوا علمعتل

”Ili mjue idadi ya miaka na hesabu (nyingine).” (Yuunus 10:05)

Hili ni jambo lisilokuwa na ubaya wowote na mtu hufaidika kwalo. Ama elimu ya unajimu,ni kumkufuru Allaah na ni kudai kujua mambo yaliyojificha.

Kupulizia fundo ndio chanzo cha uchawi. Anasema Allaah (Ta´ala):

قدي العف فاثاتر النن شمو

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

126

“Na kutokana na shari ya wanaopuliza mafundoni.” (al-Falaq 113:04)

“Wanaoupulizia” ni wachawi wa kike. Huu ndio uchawi wa kihakika ambao unaathiri,unaua, unamfanya mtu kuwa mgonjwa, unatenganisha baina ya mke na mume. Hii ndioaina kubwa ya uchawi. Hii ni dalili ya kukufuru kwa mchawi na kwamba ni mshirikina.Kwa kuwa mchawi huwataka msaada Mashaytwaan ili aweze kufanikisha uchawi wake.

Muislamu anapaswa kumtegemea Allaah (Jalla wa ´Alaa) Pekee. Na wala asimtegemeeasiyekuwa Allaah katika mambo ambayo hakuna ayawezae isipokuwa Allaah. Amakuwataka msaada viumbe katika mambo ambayo wanayaweza; kujenga nyumba, kubebakitu n.k., haya ni katika mambo ya wema na kheri. Ama yule mwenye kumtaka msaadaasiyekuwa Allaah katika mambo ambayo hakuna ayawezae isipokuwa Allaah Pekee, kamakuponya wagonjwa, au kuleta riziki na kadhalika, hii ndio Shirki kubwa. Na mwenyekukitegemea kitu huwakilishwa kwacho.

Na katika aina za uchawi ni uvumi. Na uvumi ni kusambaza maneno kati ya watu kwalengo la kufitinisha. Anamwendea mtu na kumwambia fulani kakusema kadhaa na kadhaa.Kisha anamwendea mwengine na kusema fulani kakusema kadhaa na kadhaa iliawafitinishe. Kisha kunatokea ufisadi na matatizo makubwa. Na pengine kukatokea hatakuuana na kuchukiana baina ya Waislamu kwa sababu ya huyu mfitinishaji. Na kumekujakatika Hadiyth ya kwamba sababu moja wapo ya adhabu za kaburini ni uvumi. Uvumi nidhambi kubwa katika madhambi makubwa, unaleta machafuko baina ya watu, unaenezauadui na chuki. Unafanya kazi ya uchawi, kwa kuwa uchawi unatenganisha baina yawapendanao.

جهوزء ورالم نيب فرقون بها يا ممهنون ملمعتفي

“Basi wakajifunza kutoka kwa hao (Malaika) wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayobaina ya mtu na mkewe.” (al-Baqarah 02:102)

Uchawi unatenganisha baina ya wapendanao na unaeneza uadui. Hali kadhalika uchawi.Hivyo ni katika uchawi kwa sura hii. Kwa kuwa unatenganisha baina ya watu, kuenezauadui baina yao. Ni dalili ya kwamba uvumi ni aina katika aina za uchawi. Na yasemwakuwa mfitinishaji huleta machafuko katika saa moja machafuko ambayo mchawi angeliwezakuyaleta katika mwaka mmoja. Katika kufitinisha baina ya watu mfitinishaji ni khatarikuliko mchawi. Ni wajibu kwa Muislamu ajiepushe na uvumi.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. al-´Iyaafah, at-Twarq na at-Twiyarah ni katika al-Jibt.

2. Tafsiri ya al-´Iyaafah na at-Twarq.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

127

3. Kujifunza elimu ya unajimu ni aina ya Shirki.

4. Kufunga fundo na kulipulizia ni katika uchawi.123

5. Uvumi (kufitinisha) ni katika uchawi.124

6. Baadhi ya ufaswaha unaweza kuwa katika uchawi pia.

123 Shaykh Fawzaan anasema: ”Bali kufanya hivi ndio asli na chanzo cha uchawi.”124 Shaykh anasema tena: ”Ni kwa sura ya kwamba unatenganisha baina ya watu.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

128

Mlango Wa 26

Kuhusu Makuhani Na Mfano Wao

Muslim kapokea katika Swahiyh yake, kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kasema:

“Atakayemwendea mpiga ramli akamuuliza kwa kitu na akamsadikisha,hatokubaliwa Swalah zake kwa siku arubaini.”125

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea kutoka kwaMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Atakayemwendea kunahi na akamsadikisha kwa aliyoyasema, basi kakufurukwa yaliyoteremshwa kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

(Kapokea Abuu Daawuud)

Maimamu wanne na al-Haakim wamepokea Hadiyth hii126 na kusema nikuwa ni Swahiyh:

“Atakayemwendea mpiga ramli au kuhani na akamsadikisha kwaaliyoyasema, basi kakufuru kwa aliyoteremshiwa Muhammad (SwallaAllaahu ´alayhi wa salla).”

Na Abuu Ya´laa kapokea Hadiyth kama hii kutoka kwa Ibn Mas´uud(Radhhiya Allaahu ´anhu) kwa isnadi iliyo nzuri lakini Mawquuf.

Kutoka kwa ´Imraan bin Husayn (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea HadiythMarfu´ ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)kasema:

125 Tanbihi muhimu! Shaykh Fawzaan aliulizwa ”Je vipi mtu akitubia, Allaah Atakubali Swalah zakehizi au hukumu itabaki kama ilivyo? Akasema Shaykh: ”Allaah Ndiye Mwenye kujua zaidi.Tunaichukulia Hadiyth kama ilivyokuja.” (Sharh ad-Dur an-Nadhwiyd fiy Ikhlaasw Kalimaat at-Tawhiyd)126 Ya Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

129

“Si katika sisi yule afanyaye mikosi au akakubali neno la yule aliyefanyiwamikosi, au akafanya ukuhani au akafanyiwa ukuhani, au akafanya uchawi auakafanyiwa uchawi. Na atakayemwendea kuhani na akamsadikisha kwaaliyoyasema basi kakufuru kwa yale aliyoteremshiwa Muhammad (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam).”

(Kaipokea al-Bazzaar kwa isnadi nzuri)

Hadiyth hii hii imepokelewa na at-Twabaraaniy kwa isnadi Hasan kutokanana Hadiyth ya Ibn ´Abbaas bila ya neno “Na atakayemwendea... “ mpakamwisho.

Imaam al-Baghawiy kasema: “al-´Arraaf ni yule anayedai kuyajua mambo kwadalili zake za kabla ambazo anatolea dalili kwa yule mwenye kuibiwa, mahalipa kitu kilichopotelea na mfano wa hayo.”

Na imesemwa kuwa127 ni kuhani. Na kuhani ni yule ambaye anaelezeamambo yaliyofichikana128 katika mambo ya Mustaqbal. Na imesemekana yakwamba ni yule anayeelezea yaliyo ndani ya dhamira ya mtu.

Abul-´Abbaas Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) kasema: “al-´Arraaf ni jina lakuhani, mtabiri wa nyota,129 mwaguzi130 na mfano wao katika wanaoongeleakuyajua kuwa na elimu ya kuyajua mambo kwa njia mfano wa hizi.”

Kasema Ibn ´Abbaas kuhusu watu wanaoandika Abjaad na kutazama nyota:131

“Sionelei wanaofanya hivyo wana sehemu yoyote kwa Allaah.”

Ufafanuzi:Mlango huu unazungumzia hukumu katika Kitabu na Sunnah kuhusu makuhani na walewanaowaendea makuhani na watu mfano wao.

127 al-´Arraaf128 Mambo ya Ghayb129 al-Munajjim130 ar-Rammaal131 Wakiamini huleta taathira kwenye ardhi

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

130

Katika mlango huu tunapata faida zifuatazo:

- Uharamu wa yule anayefanya au kufanyiwa mikosi, kufanya au kufanyiwa ukuhani,kufanya au kufanyiwa uchawi na Mtume (´alayhis-Salaam) kujiweka mbali na watuwote hawa.

- Uharamu wa kuomba kufanyiwa mambo haya.

- Uharamu wa kuwaendea watu kama hawa na kukaa nao. Kwa kauli ya Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Na atakayemwendea kuhani na akamsadikishakwa aliyoyasema basi kakufuru kwa yale aliyoteremshiwa Muhammad (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam).”

- Kauli ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kuwa maana ya al-´Arraaf ni yule anayedaikujua elimu ya Ghayb.

- Uharamu

“Sionelei wanaofanya hivyo wana sehemu yoyote kwa Allaah”, hapa Ibn ´Abbaas (RadhiyaAllaahu ´anhumaa) kawahukumu ukafiri. Kwa kuwa yule asiyekuwa na fungu lolote kwaAllaah ina maana ni kafiri. Kwa kuwa muumini ana fungu mbele ya Allaah hata kamalitakuwa fungu (lake ni) dogo.

Abjaal ni herufu ambazo zinaitwa herufu za majini. Wanaziandika na kuzitolea dalili kwamambo yaliyofichikana. Wachawi, makuhani na mfano wao huwa wanaandika herufu kamahizi na wanakuwa mpaka na vitabu kabisa.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Kumuamini kuhani hakukusanyiki na kuiamini Qur-aan.

2. Ubainifu ya kuwa kufanya hivyo (kumwamini au kumwendea kuhani) ni kufuru.

3. Utajo wa aliyefanyiwa ukuhani.

4. Utajo wa aliyefanyiwa mikosi.

5. Utajo wa aliyefanyiwa uchawi.

6. Utajo wa aliyejifunza Abjaad.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

131

7. Tofauti kati ya kuhani na al-´Arraaf mpiga ramli.132

132 Shaykh Fawzaan anasema: “Hakuna tofauti baina ya watu wote hawa kama alivyosema Abul-´Abbaas (Rahimahu Allaah), kwa kuwa wote kazi wanayoifanya ni moja na wote wanadai kujuaelimu iliyojificha.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

132

Mlango Wa 27

Yaliyokuja Kuhusu An-Nushrah133

Kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu an-Nushrah, akasema: “Ni katika matendo ya Shaytwaan.”

(Kaipokea Ahmad na Abuu Daawuud kwa isnadi nzuri)

Imaam Abuu Daawuud kapokea ya kwamba aliulizwa Imaam Ahmad(Rahimahu Allaah) kuhusiana nalo,134 akasema:

“Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) anachukia135 yote haya.”

al-Bukhaariy kapokea kutoka kwa Qataadah (Rahimahu Allaah):

“Nilimwambia Ibn al-Muswayyib: “Mtu kafanyiwa uchawi au hawezikumwingilia mke wake, je ni halali kwake kutibiwa kwa kutumia an-Nushrah?” Ibn al-Muswayyib akasema: “Ndio, hakuna ubaya. Hakikawamechokusudia ni kusuluhisha. Yanayofaa hayakukatazwa.”136

Imepokelewa kutoka kwa Imaam al-Hasan (al-Baswriy) ya kwamba kasema:

“Haufungui uchawi isipokuwa mchawi.”

Kasema Ibn al-Qayyim (Rahimahu Allaah):

“an-Nushrah ni kuondoa uchawi kwa yule aliyefanyiwa uchawi. Na ni ainambili:

133 Shaykh Fawzaan anasema: “Maana ya an-Nushrah kilugha ni kuondosha kitu. Ama Kishari´ah nikama ni kama alivyosema Imaam Ibn al-Qayyim mwisho wa mlango huu. Na imegawanyika sehemumbili; kuna uondoshaji unaojuzu na wa haramu.”134 an-Nushrah135 Shaykh anasema tena: ”Maana ya “anachukia” yaani anaharamisha. Salaf walikuwa wakitumiakuchukia katika kuharamisha.”136 Tanbihi muhimu! Ibn al-Muswayyib hapa anakusudia an-Nushrah isiyokuwa na uchawi ndaniyake ambayo ni ile aina ya pili aliyosema Imaam Ibn-ul-Qayyim.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

133

1. Kuuondoa uchawi kwa kutumia uchawi mwingine. Na hili ndio katikamatendo ya Shaytwaan na ndio kunaingia kauli ya Hasan (al-Baswriy).Mchawi na anayefanyiwa uchawi wanajikurubisha kwa Shaytwaan kwawanayoyataka. Hivyo Shaytwaan anamuondolea taathira yulealiyefanyiwa uchawi.

2. Kuuondoa uchawi kwa Ruqyah; Aayah za Qur-aan na Du´aa, na dawazinazoruhusiwa.137 Hili linajuzu.

Ufafanuzi:Shaykh kaleta mlango huu baada ya mlango kuhusu uchawi na makuhani. Baadhi ya watuwanaweza kuteswa na uchawi, jambo hili likawafanya wahitajie dawa. Na ndio maanakaweka mlango huu katika kitabu cha Tawhiyd kwa kuwa watu wanahitajia dawa.

Maneno ya Ibn al-Qayyim, ni kwamba mchawi hawezi kukusaidia mpaka aidhaujikurubishe kwake kwa kitu cha maasi kumuasi Allaah; kama kumuabudu, kumsujudia,kumshirikisha Allaah, kumchinjia, kuwataka msaada majini. Ukimuitikia matakwa yakendio atakusudia, baada ya wewe kumkufuru Allaah. Hivyo, hii ni dalili ya wazi ya kwambahaijuzu kuwaendea wachawi kabisa.

Aina ya pili ni kuondosha uchawi kwa Ruqyah, Aayah za Qur-aan na Du´aa mubaahah, hilini jambo linalojuzu. Kama kumsomea mgonjwa al-Faatihah, Suurat al-Ikhlaasw, al-Mu´awwidhaat. Qur-aan ni dawa kama Alivyosema Allaah (Ta´ala):

وا هم آنالقر نزل مننوننيمؤلمة لمحرفاء وش

”Na Tunateremsha katika Qur-aan ambayo ni shifaa na Rahmah kwa Waumini.” (al-Israa17:82)

قل هو للذين آمنوا هدى وشفاء

”Sema (ee Muhammad Hii (Qur-aan) kwa walioamini ni“ :(صلى اهللا عليه وآله وسلم uongofu na dawa.”(al-Fuswswilat 41:44)

137 Mubaahah

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

134

Hii ni dawa ya kuondosha kufuru, al-Ilhaad na shubuha. Hali kadhalika ni dawa yamagonjwa. Lakini inahitajia ´Aqiydah na kuwa na nia nzuri. Lau mtu atakuwa na nia nzurina akamtegemea Allaah, inaponya na hufikiwa makusudio. Qur-aan ni dawa lakini sio kilaanayetumia Qur-aan hufikia natija. Anayosomewa mgonjwa kutoka katika Qur-aan ni:

- Anasomewa Aayah ya Suurat ash-Shu´araa. Kauli Yake (Ta´ala):

رب موسى وهارونقالوا آمنا برب العالمنيفألقي السحرة ساجدينفألقى موسى عصاه فإذا هي تلقف ما يأفكون

”Basi Muwsaa akatupa fimbo yake, tahamaki inameza vyote walivyovizua. Basi walewachawi wakaanguka wakisujdu (kwa Allaah). Wakasema: “Tumemwamini Mola wawalimwengu. Mola wa Muwsaa na Haaruwn”.” (ash-Shu´raa 26:45-48)

- Aayah katika Suurat Yuunus.

قال موسى ما جئتم به السحرفلما ألقوا أنتم ملقونفلما جاء السحرة قال لهم موسى ألقوا ما ◌لهطبيس إن اللـه ◌ينفسدلالممع حلصلا ي إن اللـه قحيوكره لوو هاتمبكل قالح وناللـهرمجالم

”Basi walipokuja wachawi, Muwsaa akawaambia: “Tupeni mnavyotaka kuvitupa.” Na AllaahAtathibitisha haki kwa Maneno Yake; japokuwa watakirihika wakhalifu.” (Yuunus 10:80-81)

- Aayah katika Suurat Twaaha.

إنما صنعوا كيد ساحر ولا يفلح الساحر حيث أتى◌

”Hakika walivyoviunda ni njama za mchawi, na wala mchawi hafaulu popote ajapo.”(Twaaha 20:69)

- Aayat al-Kursiyy, Suurat al-Ikhlaasw, Qul-A´udhubi Rabbil-falaqah na Qul-A´uudhubi Rabbin-Naas. Suurah hizi zinasomwa ndani ya chombo cha maji kishaanapewa mgonjwa anakunywa na maji yatayobaki atayaoga.

Aayah hizi anasomewa mgonjwa aliye na ´Aqiydah na nia nzuri. Dawa itapatikana kwaidhini ya Allaah. Hii ndio Ruqyah na Du´aa mubaahah. Ama kuuondoa uchawi kwakutumia uchawi mwingine, hichi ni kitendo kisichojuzu. Hata kama kuna baadhi yaMashaykh na wanafunzi ambao wametoa Fatwa kujuzisha hili, hii ni Fatwa isiyojuzu kabisana ni ya kimakosa. Kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“an-Nushrah ni katika matendo ya Shaytwaan.”

Hivyo kauli za wasomi hawa ambao wamejuzisha zinarudishwa kwa dalili ya maneno hayaya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

135

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Makatazo ya an-Nushrah.

2. Tofauti kati ya iliyokatazwa na iliyoruhusiwa katika kuondosha matatizo.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

136

Mlango Wa 28

Yaliyokuja Kuhusu Kuamini Mkosi138

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

ـكن أكثرهم لا يعلمون ألا إنما طائرهم عند اللـه ول

“Tanabahi! Hakika mkosi wao unatoka kwa Allaah (kwa ajili ya ubaya wao),lakini wengi wao hawajui.” (al-A´raaf 07:131)

Kauli Yake:

قالوا طائكمعكم مر أئن ذكرتم◌ بل أنتم قوم مسرفون◌

”(Mitume) Wakasema: “Mkosi wenu uko pamoja nanyi. Je, kwa vilemnakumbushwa (msimshirikishe Allaah ndio mnasema hivyo)? Bali nyinyi niwatu wapindukao mipaka.” (Yaasin 36:19)

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwambaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Hakuna al-´Adwaa139, at-Twiyarah140, Haamah141 wala Swafar.”142

138 at-Tatwayyur139 Kuamini kuambukizwa ugonjwa. Shaykh anasema: “Ni kuambukiza ugonjwa kutoka kwa mtukwenda kwa mwingine. Au kutoka mji hadi mwingine. Na makusudio si kwamba kunapingwakuambukizwa moja kwa moja, hapana. Kuambukiza kupo, kuna maradhi ya kuambukiza. Makusudioni waliokuwa wakiamini katika Ujaahiliyyah ya kwamba maradhi hujiambukiza yenyewekimaumbile. Maradhi yanaambukiza kwa idhini ya Allaah na makadirio Yake. Hivyo mtu anatakiwakumtegemea Allaah (Ta´ala) na afanye sababu za kujikinga na kujitibu.”140 Kuamini mkosi wa ndege; sauti yake, mlio wake n.k.141 Kuamini mkosi wa ndege ya usiku, yaani bundi. Shaykh anasema: “Katika Ujaahiliyyah walikuwawakisikia sauti yake wanasema hii ni dalili ya kuwa kutakufa mtu. Na mpaka sasa kwa watu wajingabado wanaamini mambo kama haya. Hii ni ndege tu na haina taathira yoyote katika maisha yamwanaadamu. Hivyo haitolei dalili ya mauti wala uhai. Mauti na uhai vipo Mikononi mwa Allaah.”142 Shaykh Fawzaan anasema: “Swafaar yasemekana kuwa ni maradhi yanayokuwa kwenye chakula.Na pia imesemekana vile vile ya kwamba ni (mkosi wa mwezi) wa Swafar (mfungo tano). Walikuwawakiamini kuwa kuna mkosi wa mwezi wa Swafar. Hawasafiri katika mwezi huo na wanaitakidikuwa una mkosi na mwezi wa Shawwaal pia. Mikosi yote hii ni katika mambo ya Shaytwaan

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

137

(Imepokelewa na al-Bukhaariy na Muslim)

Katika Swahiyh Muslim kumezidishwa:

“... na wala hakuna Naw-a´143 na Ghuul.”144

Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba amemsikia Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakuna al-´Adwaa, wala at-Twiyarah na inanipendeza al-Fa´l.” Akaulizwa:“Na ni nini al-Fa´l?” Akasema: “Ni neno zuri.”145

Kupitia kwa Abuu Daawuud kwa isnadi Swahiyh amepokea ya kwamba´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitajiwa at-Twiyarah146, kishaakasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nzuri yake ni al-Fa´l, na wala(ndege) haimrudishi Muislamu. Mmoja wenu anapoona jambolinalomchukiza, basi na aseme:

“Ee Allaah! Nakuna aletae mema isipokuwa Wewe, na hakuna aondoaemabaya isipokuwa Wewe! Na wala hakuna namna wala nguvu isipokuwaKwako.”147

Imepokelewa kutoka kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu)Hadiyth Marfu´:

yasiyokuwa na ukweli wowote. Na ikiwa kutapatikana kitu (cha ukweli) katika hayo, basi ajikingekwa Allaah.”143 Shaykh Fawzaan: “Ni kuamini mambo fulani kwa kuchomoza nyota na kuzama kwake. Yakwamba kutatokea mambo fulani, au kuwa mvua itanyesha kwa kuchomoza nyota fulani nakadhalika. Hizi ni katika itikadi za Kijaahiliyyah. Mvua iko Mikononi mwa Allaah na Anaiteremshawakati Apendapo mwenyewe.”144 Kuunda uongo na mara nyingi inakuwa pale ambapo hutishiwa mtoto kwa Shaytwaan, mzimun.k.145 Shaykh anasema tena: ”Ni kuwa na dhana nzuri na kutaraji kutokea mambo ya kheri. Hili nikinyume na kuamini mkosi.”146 Yaani mkosi147 “Allaahumma laa ya-ati bil-hasanaat illa anta, walaa yadfa´u sayyi-aat illa anta, wa laa Hawlaa walaa Quwwata illa bika.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

138

“at-Twiyarah ni Shirki, at-Twiyarah ni Shirki. Na wala hakuna yeyote katika sisiasiyehisi moyoni mwake kitu kama at-Twiyarah. Lakini Allaah Huindosha kwakumtegemea.”148

(Kaipokea Abuu Daawuud na at-Tirmidhiy na wameisahihisha)

Na sehemu ya maneno ya mwisho wameyafanya kuwa ni kauli ya IbnMas´uud.

Imaam Ahmad kapokea kutoka katika Hadiyth ya Ibn ´Amr:

“Mtu ambaye at-Twiyarah149 itamrudisha150 kutokwenda kufanya haja yake,basi ameshiriki.” Wakasema: “Ni nini kafara ya hilo?” Akasema:151 “Nikusema: “Ee Allaah! Hakuna kheri isipokuwa ni kheri Yako, na wala hakunaat-Twiyarah isipokuwa ni Yako, na wala hakuna mola apasaye kuabudiwaisipokuwa Wewe.”152

Fadhwl bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kapokea ya kwambakasema:

“Hakika at-Twiyarah ni kile kinachokufanya uweze kubeba (moyoni mwako)kitu au kukurudisha.”153

Ufafanuzi:Jambo hili la kuamini mkosi linaharibu ´Aqiydah na kumkosesha mtu kufanya alichokuwaanataka kukifanya. Na ni dalili ya kukosa kwake au udhaifu wake wa kumtegemea Allaah.Katika ´Aqiydah ya Muislamu sahihi ni amtegemee Allaah na wala asiathirike na mambo yamkosi.

هبسح وفه لى اللـهكل عوتن يمو

148 Kutawakali Kwake149 Kuamini mkosi150 Kumzuia kufanya jambo lake alilokuwa anataka kufanya151 Yaani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)152 ”Allaahumma laa khayra illa khayruka, walaa twayra illa twayruka, walaa ilaaha illa ghayruka.”153 Kutoweza kufanya kitu hicho

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

139

“Na yeyote (yule) anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza.” (at-Twalaq 65:03)

Hakitomdhuru kitu ikiwa atamtegemea Allaah kihakika.

Ndege haimrudishi Muislamu nyuma katika jambo lake. Ni dalili ya kwamba kuaminindege kunapingana na ukamilifu wa Uislamu au Imani. Na dawa ya ndege pindi mtuanapohisi kitu moyoni, ni mtu kumtegemea Allaah na kuendelea na jambo lake na walaisimzuie. Ni dalili ya kuwa yule ambaye ndege haikumrudisha na akapigana na hilokasalimika na Shirki.

Yule ambaye atarudishwa na kitu kwa ajili ya ndege, ni aina ya Shirki. Kwa kuwa kaaminimtu/kitu kingine badala ya Allaah kinadhuru. Ilihali kheri, shari, manufaa na kudhuru yotekatika Mikono ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tanbihi ya maana ya Aayah:

اللـه ندع مهرا طائمألا إن

“Tanabahi! Hakika mkosi wao unatoka kwa Allaah (kwa ajili ya ubaya wao).” (al-A´raaf07:131)

pamoja na Kauli Yake:

كمعكم مرطائ

“Mkosi wenu uko pamoja nanyi.” (Yaasin 36:19)

2. Ukanushaji wa madhara (waliokuwa wakiyaamini watu wa Ujaahiliyyah).

3. Ukanushaji wa kutokuwepo kwa at-Twiyarah.

4. Ukanushaji wa kutokuwepo kwa al-Haamah.

5. Ukanushaji wa kutokuwepo kwa Swafar.

6. Ya kwamba al-Fa´l sio katika hilo (at-Twiyarah) bali ni mustahabah.

7. Tafsiri ya al-Fa´l.

8. Kuingiwa moyoni na kitu katika hayo (at-Twiyarah) pamoja na kulichukia hakudhuru. BaliAllaah Huiondosha kwa kumtegemea.

9. Anachotakiwa kusema anayekutana na kitu (katika at-Tatwayyuur).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

140

10. Ubainifu ya kuwa at-Twiyarah ni Shirki.

11. Tafsiri ya at-Twiyarah mwenye kulaumiwa.154

154 Ni ile inayokurudisha, ama ile isiyokurudisha wala kukuzuia kwa jambo lako haikudhuru.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

141

Mlango Wa 29

Yaliyokuja Kuhusu Unajimu155

Imaam al-Bukhaariy kasema katika Swahiyh yake ya kwamba Qadaatahkasema:

“Allaah Kaumba nyota hizi kwa makusudio matatu: 1) Pambo la mbingu, 2)Kombora dhidi ya Mashaytwaan na 3) Alama kwa ajili ya uongozi wamwenye kusafiri. Yeyote atakayefasiri vinginevyo kakosea na kupoteza fungulake [Aakhirah] na kajikalifisha kwa kitu asichokuwa na ujuzi nacho.”

Na Qadaatah kachukizwa na kujifunza elimu ya al-Qamar mashukio ya mwezikama ambavyo Ibn ´Uyaynah hakuruhusu kujifunza hilo pia. Kapokea hiloHarb kutoka kwao. Na wameruhusu kujifunza elimu ya mashukio ya mweziAhmad na Ishaaq.

Kutoka kwa Abuu Muusa (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwambaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Watu sampuli tatu hawatoingia Peponi: 1) Mwenye kudumu kwa kunywapombe, 2) Mwenye kukata udugu na 3) Mwenye kusadikisha uchawi.”

(Kaipokea Ahmad na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake)

Ufafanuzi:Bi maana, yaliyokuja katika Kitabu na Sunnah kutahadharisha dhidi ya unajimu. Unajimu nikuitakidi mambo kutokana na nyota ya kwamba zinaathiri ulimwengu huu; sawa uhai,mauti, riziki, kujitokeza kwa mambo na kadhalika. Hivi ni viumbe katika viumbe vya Allaahna havina amri yoyote mbele ya Allaah. Muumini anatakiwa kumtegemea Allaah (Ta´ala)katika mambo yake yote. Allaah Kaviumba kwa malengo matatu:

155 at-Tanjiym; unajimu au elimu ya nyota.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

142

1. Pambo la mbingu.

وأنا لمسنا السماء فوجدناها ملئت حرسا شديدا وشهبا

”Na kwamba sisi (tulitafuta kuzifikia na) kuzigusa mbingu, basi tukazikuta zimejaa walinziwakali na vimondo.” (al-Jinn 72:08)

Mashaytwaan wanasema namna hii.

2. Kombora dhidi ya Mashaytwaan.

ولقد زينا السماء الدنيا بمصابيح وجعلناها رجوما للشياطني وأعتدنا لهم عذاب السعري◌

”Na kwa yakini Tumeipamba mbingu ya dunia kwa mataa, na Tukazijaalia kuwa ni kipigokwa mashaytwaan, na Tumewaandalia adhabu ya Moto uwakao kwa nguvu.” (al-Mulk67:05)

3. Alama kwa ajili ya uongozi wa mwenye kusafiri.

وهو الذي جعل لكم النجوم لتهتدوا بها في ظلمات البر والبحر

”Na Yeye Ndiye Ambaye Aliyekufanyieni nyota ili muongozwe kwazo (njia) katika viza vyabara na bahari.” (al-An´aam 06:97)

اتلامعو وبالنجم هم يهتدون◌

”Na (Ameweka) alama nyinginezo (za kutambulisha njia mchana), na kwa nyota (wakati wausiku) wanaojiongoza (watu njia).” (an-Nahl 16:16)

Hizo ndio faida za nyota. Ama kuamini ya kwamba zinadhuru na kunufaisha, yote haya niuongo mtupu. Nyota zimeumbwa kwa malengo haya matatu peke yake. Atakayeitakidivinginevyo kapoteza fungu yake – yaani Dini. Na wale wanaoabudu nyota ni watu waIbraahiym. Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alijadiliana nao mpaka akabatilisha hoja zao.

Na miongoni mwa sayari ni mwezi. Elimu ya mwezi na jua kwa kutaka kujua wakati waSwalah, mwezi, wakati wa kupanda na kadhalika, elimu hii imeruhusiwa kutokana na kauliyenye nguvu.

ابسالحو السنني ددوا علمعتل

”Ili mjue idadi ya miaka na hesabu (nyingine).” (Yuunus 10:05)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

143

Ama kuwa na itikadi kwa sayari ya kwamba kutajitokeza mambo kadhaa na kadhaa, nakwamba inaathiri ulimwengu huu na kadhalika, itikadi hii ni batili. Kwa hiyo ufafanuzi nihuu kutokana na elimu hizi mbili inayoruhusiwa na isiyoruhusiwa.

Hadiyth ya Abuu Muusa: Ima hawatongia Peponi kutokana na kufuru na Shirki yao, auhawatoingia kwa maasi yao na madhambi yao makubwa. Mara ya kwanza hatoingia ilabaada ya kuadhibiwa Motoni wataingizwa Peponi kwa kuwa sio makafiri isipokuwa wakona madhambi makubwa chini ya Shirki kubwa. Haya ni matishio makubwa. Nakinacholengwa katika Hadiyth hii ni: “Mwenye kusadikisha uchawi”, na katika uchawi niunajimu. Uchawi umewekwa katika mlango huu kwa kuwa unajimu ni aina ya uchawi, nahilo litakuja huko mbele.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Hekima ya kuumbwa kwa nyota.

2. Radd kwa mwenye kudai vinginevyo.

3. Yaliyotajwa kuhusu tofauti ya kujifunza vituo (vya mwezi, jua, nyota n.k.)

4. Tishio kwa mwenye kusadikisha kitu katika uchawi, hata kama ataamini kuwa ni batili.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

144

Mlango Wa 30

Yaliyokuja Kuhusu Kuomba Kunyweshelezwa Kwa Sayari156

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وتجعلون رزقكم أنكم تكذبون

”Na mnafanya (shukurani) za riziki yenu kuwa nyinyi mnakadhibisha.” (al-Waaqi´ah 56:82)

Abuu Maalik al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwambaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Mambo mane katika Ummah wangu ni miongoni mwa mambo yaUjaahiliyyah157 na hayatoachwa: 1) Kujifakhari kwa nasabu, 2) kutukaniananasabu, 3) kuomba kunyweshelezwa kwa nyota na 4) na maombolezo na kiliocha wanawake kwa ajili ya maiti.”

Na kasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanamke mpiga kilio ikiwa hakutubia kabla ya kufa kwake atafufuliwasiku ya Qiyaamah huku akiwa na mavazi ya lami cha kioevu na koti lenyekuwasha.”

(Kaipokea Muslim)

Kapokea Zayd bin Khaalid (Radhiya Allaahu ´anhu) akisema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituswalisha Swalahya Subh158 Hudaybiyah baada ya mvua iliyonyesha usiku. Alipomalizakuswali aliwaelekea watu na kusema: “Je, mnajua nini Kasema Mola Wenu?”

156 Nyota, mwezi, jua na kadhalika157 Shaykh Fawzaan anasema: ”Mambo ya Kijaahiliyyah ni yale yaliyokuwepo kabla ya kuja Uislamu.Na Ujaahiliyyah wote umekwisha kwa kutumwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam).”158 Fajr

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

145

Wakasema: “Mola na Mtume Wake ndio wanajua.” Akasema: “Katika asubuhihii kuna baadhi ya waja Wangu waliobakia kuwa waumini wa kweli nawengine makafiri. Ama yule aliyesema ya kwamba tumenyweshelezwa kwafadhila na Rahmah za Allaah, huyo ndiye aliyeniamini Mimi na kukanushasayari. Ama yule aliyesema ya kwamba tumenyweshelezwa kwa sababu yasayari kadhaa na kadhaa, huyo kanikufuru Mimi na kaamini sayari.”

(Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea Hadiyth kama hiyo kutoka kwa Ibn´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na ndani yake kuna: “Wakati baadhiyao waliposema: “Kumenyesha kwa sababu ya nyota kadhaa”, ndipo AllaahAlipoteremsha Aayah hii:

تنزيل من رب العالمنيفي كتاب مكنونلا يمسه إلا المطهرونإنه لقرآن كرميوإنه لقسم لو تعلمون عظيمفلا أقسم بمواقع النجومـذا الحديث أنتم مدهنون أفبهعجتونوبكذت كمأن قكملون رز

”Basi Naapa kwa maanguko ya nyota. Na hakika hicho ni kiapo kikubwa mnolau mngelielewa. Hakika hii (mnayosomewa) bila shaka ni Qur-aan Karimu.Katika Kitabu kilichohifadhiwa. (Lawhum-Mahfuudhw). Hakuna akigusayeisipokuwa waliotakaswa. Ni uteremsho kutoka kwa Mola wa walimwengu. Je,kwa hadithi hii nyinyi ni wenye kuibeza? Na mnafanya (shukurani) za rizikiyenu kuwa nyinyi mnakadhibisha.” (al-Waaqi´ah 56:75-82)

Ufafanuzi:Waarabu katika Ujaahiliyyah walikuwa wakinasibisha kunyesha kwa mvua kwa kuzama aukuchomoza kwa nyota. Hilo ilikuwa kwa sababu ya ujinga wao. Kwa kuwa mvua inanyeshakwa Amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na ndio maana nyota zinaweza kuzama aukuchomoza na mvua isinyeshe. Na mvua inaombwa kutoka kwa Allaah kama walivyokuwawakifanya Mitume; Muusa, Sulaymaan, Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam). Hivyo haijuzu kwa Muislamu kuitakidi itikadi hii baada ya Allaah Kumruzukuneema ya Uislamu.

Yule atakayeamini ya kwamba mvua inanyesha kwa sababu ya nyota, ikiwa anaitakidi yakwamba yenyewe ndio yenye kufanya mvua ikanyesha, hii ni Shirki kubwa. Ama ikiwaanaitakidi ya kwamba mwenye kufanya mvua ikanyesha ni Allaah na nyota ni sababu tu, hii

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

146

ni Shirki ndogo na kufuru ndogo. Kwa kuwa nyota sio sababu kabisa na wala hazinamafungamano yoyote na kunyweshelezwa mvua. Ndio maana Shaykh kaweka mlango huu.

Haya mambo mane ni katika mambo ya Kijaahiliyyah, na kinacholengwa hapa ni kuombakunyweshelezwa kwa nyota. Hili bado lipo kwa baadhi ya Waislamu. Ni wajibukutahadhari na hili na kuitakidi ya kwamba mvua inanyesha kwa Amri, fadhila na Ihsaanya Allaah.

Hadiyth ya Zayd bin Khaalid: Katika Ujaahiliyyah walikuwa wakiinasibisha kunyesha kwamvua kwa nyota. Huku ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jalla) na fadhila na neema Zake.Kwa kuwa mvua inatoka kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Anatakiwa kushukuriwa Allaah kwafadhila na Rahmah hii. Hii ndio Imani. Na muradi wa kufuru hapa ni kufuru ndogo yakukufuru neema. Kwa kuwa kufuru imegawanyika sehemu mbili:

1. Kufuru kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu.2. Kufuru ndogo isiyomtoa mu katika Uislamu lakini inadhoofisha Tawhiyd.

Katika Hadiyth hii kuna dalili kuinasibisha mvua kwa sababu nyingine badala ya Allaah nikumkufuru Allaah (´Azza wa Jalla). Ni wajibu kuinasibisha kwa Allaah (Subhaanahu waTa´ala). Ni kutokana na fadhila, Rahmah na neema Zake. Hapa kuna Radd kwa walewanaosema kunyesha kwa mvua ni jambo la kimaumbile na mfano wa hayo. Hili ni jambolisilojuzu. Na kama ingekuwa ni jambo la kimaumbile isingelikuwa inanyesha kwenye mjihuu na isinyeshe kwenye mji mwingine, watu wote, ardhi yote ingelikuwa inapata kwawakati mmoja, hii ni dalili ya kwamba mvua – na fadhila na neema zingine zote – zikoMikononi mwa Allaah. Hivyo Muislamu anatakiwa amtegemee Allaah (´Azza wa Jalla)Pekee na asiwe na itikadi sampuli hii kuhusiana na nyota. Hii ndio Tawhiyd na ´Aqiydahsahihi. Hivyo mtu asichukulie sahali masuala haya. Pengine mtu akasema neno alionalodogo likaharibu ´Aqiydah yake.

Aayah ya Suurat al-Waaqi´ah: Hapa kuna Radd kwa wale wanaosema kuwa Qur-aanimeumbwa. Imeteremshwa na haikuumbwa.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Waaqi´ah. (56:75-82)2. Kutajwa kwa mambo mane ambayo ni ya Kijaahiliyyah.3. Kukufuru kwa baadhi yake (mambo hayo).159

4. Katika kufuru kuna ambayo haimtoi mtu katika Uislamu.5. Kauli Yake: “Katika asubuhi hii kuna baadhi ya waja Wangu waliobakia kuwa waumini

wa kweli na wengine makafiri.” Kwa sababu ya kukanusha neema.

159 Shaykh Fawzaan: ”Huyu ndio yule aliyesema kuwa tumenyweshelezwa kwa nyota kadhaa nakadhaa.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

147

6. Uelewa wa Imani katika hali hiyo (wa kuinasibisha mvua kwa asiyekuwa Allaah).7. Uelewa wa kufuru katika hali hiyo.8. Uelewa wa kauli yake: “Imenyesha kwa sababu ya sayari kadha na kadha”160

9. Mafunzo ya mwanachuoni kwa mwanafunzi kwa njia ya kumuuliza maswali, kwa kauliyake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Je, mnajua nini kasema Mola Wenu?”161

10. Adhabu ya mwanamke mpiga kilio kwa ajili ya maiti.

160 Shaykh anasema tena: ”Mwenye kusema imenyesha kwa sababu ya sayari kadhaa na kadhaa, nimuongo. Kwa kuwa nyota hazina uhusiano wowote na kunyesha kwa mvua.”161 Shaykh anasema tena: ”Hii ni njia nzuri ya kumfunza mtu; njia ya kuuliza swali.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

148

Mlango Wa 31

Kauli Ya Allaah Ta´ala

ب اللـهكح مهونبحا يادأند اللـه ونن دذ مختن ياس مالن نمو

“Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah kuwa nimungu mshirika (anaelingana na Allaah), wanawapenda kama mapenziwanavyompenda Allaah.” (al-Baqarah 02:165)

Na Kauli Yake:

و كمتريشعو كماجوأزو كمانوإخو كماؤنأبو كماؤقل إن كان آب با أحهنوضرت ناكسما وهادن كسوشخة تارجتا ووهمفترال اقتوأمرهبأم اللـه يأتى يتوا حصبرفت هبيلي سف ادجهو هولسرو اللـه نكم مإلي

”Sema (ee Muhammad :(صلى اهللا عليه وآله وسلم “Ikiwa baba zenu, au watoto wenu, aundugu zenu, au wake (au waume) zenu, au jamaa zenu, au mali mliyoichumana biashara mnayoikhofia kuharibika kwake, na majumba mnayoridhika nayo,ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Mtume Wake na kufanya jihaad katikanjia Yake; basi ngojeeni mpaka Allaah Alete Amri Yake (ya adhabu).” (at-Tawbah 09:24)

Kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Mmoja wenu hatokuwa muumini mpaka mimi niwe kwake ni mpendwazaidi kuliko baba yake, watoto wake na watu wote.”

(Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea tena kutoka kwa Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Mambo matatu yakipatikana kwa mtu hupata ladha (utamu) wa Imani: 1)Allaah na Mtume Wake wawe ni wenye kupendwa zaidi kwake kuliko yeyoteyule, 2) ampende mtu asimpendei jengine isipokuwa iwe ni kwa ajili ya

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

149

Allaah, na 3) achukie kurudi katika ukafiri baada ya Kumuokoa Allaah nao162

kama anavyochukia kutupwa Motoni.”

Na katika upokezi mwingine:

“Hatopata mmoja wenu utamu wa Imani mpaka mpaka... “ mpaka mwishowake.

Kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kasema:

“Mwenye kupenda kwa ajili ya Allaah, na akachukia kwa ajili ya Allaah, nakufanya urafiki kwa ajili ya Allaah na kujenga163 uadui kwa ajili ya Allaah,hakika hupatikana urafiki164 wa Allaah kwa hilo. Na wala hatopata mja ladhaya Imani hata zikikithiri Swalah na Swawm165 zake mpaka iwe hivyo. Leowatu wanakuwa marafiki na kupendana kwa ajili ya mambo ya kidunia, hilohaliwazidishii wenye nalo kitu.”166

(Kaipokea Ibn Jariyr)

Kasema Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kuhusu Kauli Yake(Ta´ala):

اببالأس بهم تقطعتو

“Na yatawakatikia mafungamano yao.” (al-Baqarah 02:166)

Anasema (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Ni mapenzi.”167

162 Kumuokoa kumtoa katika ukafiri huo163 Au kuonesha164 Shaykh Fawzaan anasema: ”Yaani nusra na mpenzi ya Allaah (Ta´ala).”165 Hata awe ni mwenye kuswali na kufunga sana166 Yaani wanaofanya hivyo halitowanufaisha kitu siku ya Qiyaamah167 al-Mawaddah

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

150

Ufafanuzi:Mlango huu ni asli katika asli ya Imani na ´Aqiydah, nayo ni al-Walaa´ wal-Baraa. Mtuajenge urafiki na mawalii wa Allaah na ajiweke mbali na maadui wa Allaah. Ama yulemwenye kuwachukulia watu wote ni sawa – Muislamu na kafiri – huyu hapambanui bainaya Muislamu na kafiri. Muislamu anatakiwa awe na kikundi cha Allaah na asiwe na kikundicha Shaytwaan.

Hadiyth ya Anas: Mtu anatakiwa awapende wazazi wake, watoto wake na watu wote kwaujumla, haya ni mapenzi ya kimaumbile. Ila hatakiwi kutanguliza mapenzi haya kabla yamapenzi ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa nini? Kwakuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye ambaye kawaokoa wauminikuwatoka katika kufuru. Hivyo mapenzi nafasi ya kwanza yanatakiwa kuwa ya Allaah,Mtume wake kisha ndio wanakuja Waislamu. Na kauli yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam): “Mmoja wenu hatoamini... ” si kwamba anakuwa kafiri, bali Imani yakeinakuwa pungufu. Na sio katika mapenzi kuzusha Bid´ah katika Dini ya Allaah na kudaiwampenda Allaah na Mtume Wake, kama kuzusha Maulidi. Kwa kuwa Mtume mwenyewe(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuyafanya, Maswahabah, Makhalifah waongofu,Taabi´uun na waliokuja baada yao hawakuyafanya. Na huku – wallaahi – ndiokumbughudhi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa kuwa kumbughudhi Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kule mtu kupenda Bid´ah aliyokataza Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam).

Hadiyth nyingine ya Anas: Si kila muumini hufikia daraja ya kupata utamu (ladha) ya Imanihata kama atakuwa ni muumini mpaka awe na mambo haya matatu. Kila mmoja anadaikuwa anampenda Allaah na Mtume Wake, lakini alama na dalili iko wapi? Dalili ni paleambapo yeye atakuwa ni mwenye kufuata yale yaliyokuja kutoka kwa Allaah na kutokakwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na anajiweka mbali na yalewaliyokataza. Hii ndio dalili ya mtu kumpenda Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam). Dalili ya pili ni ampende mtu isiwe kwa jengine zaidi ya Allaah.Asimpende kwa ajili ya dunia, kwa ajili anampa mali na kadhalika, hapana. Anaweza kuwahana kitu kabisa, fakiri, masikini wewe ukampenda kwa ajili ya Allaah Pekee hata kamahakupi kitu. Dalili ya tatu mtu achukie kufuru na ukafiri kwa kuwa Allaah NayeAnavichukia. Hivyo awe na subira kwa yale yatayompata kutokana na Dini yake. Na hililinahitajia mtu ajifunze Dini yake – ni ipi kufuru na Shirki – ili mtu aweze kuvichukia. Kwakuwa huwezi kuchukia kitu usichokijua.

Hadiyth ya Ibn ´Abbaas: Ina maana mtu akapenda kwa ajili ya Allaah na si kwa ajili yadunia, na kuchukia kwa ajili ya Allaah na si kwa ajili hakupi chochote au kakuudhi,isipokuwa kwa ajili ya dunia. Ama yule mwenye kusema mimi nimeshakuwa Muislamuyatosha na si lazima kuchukia kufuru, huyu sio Muislamu. Kwa kuwa Muislamu anatakiwakuchukia kufuru na makafiri. Hali kadhalika achukie kurudi katika ukafiri, kwa ajili hiyoasiritadi kutoka katika Dini yake, hata kama ataunguzwa, atauawa n.k. asiritadi katika Dini

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

151

yake. Bali asubiri katika Dini yake kwa kuwa anaipenda Dini yake. Ama wale ambaowanapopatwa na shida na matatizo wanatoka katika Dini – kama wanafiki – huyu sioMuumini bali ni muongo. Dini sio Swalah na Swawm nyingi tu, hapana, haitoshi. Mapenzipekee yatayofaa siku ya Qiyaamah ni ya wale waliyopenda kwa ajili ya Allaah.

نيقتإلا الم ودض ععبل مهضعب ذئمولاء يالأخ

”Rafiki wapenzi Siku hiyo watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye kumuogopaAllaah.” (az-Zukhruf 43:70)

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Baqarah. (02:165)

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat at-Tawbah. (09:24)

3. Uwajibu wa kumpenda yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuliko jinsi mtuanavyojipenda mwenyewe, familia yake na mali yake.

4. Ukanushaji wa Imani haina maana mtu katoka katika Uislamu.168

5. Imani ina ladha; huenda mtu akaipata (ladha hiyo) na huenda mtu asiipati.

6. Matendo mane ya moyo ambayo hakupatikani mapenzi (nusra) ya Allaah na wala hapatimtu ladha ya Imani isipokuwa kwa matendo hayo.169

7. Ufahamu wa Swahabah (Ibn ´Abbaas) kuhusu uhakika wa sasa, ya kwamba watu wengiwakati wake wanapenda kwa ajili ya dunia.

8. Tafsiri ya:

اببالأس بهم تقطعتو

“Na yatawakatikia mafungamano yao.”170 (al-Baqarah 02:166)

9. Miongoni mwa washirikina kuko ambao wanampenda Allaah mapenzi makubwa.171

168 ”Hatoamini mmoja wenu mpaka... ” Shaykh Fawzaan anasema: ”Hadiyth hii haina maana mtuanakuwa kafiri, bali Imani yake haitokamilika. Kwa kuwa Imani imegawanyika mafungu mawili: 1)Imani kamilifu, na 2) Imani pungufu.”169 Shaykh anasema tena: ”Ni kupenda kwa ajili ya Allaah, kuchukia kwa ajili ya Allaah, kujengaurafiki kwa ajili ya Allaah na kujenga uadui kwa ajili ya Allaah. Ladha ya Imani haipatikaniisipokuwa kwa mambo haya mane”170 Shaykh Fawzaan anasema: ”Haya ni yale mapenzi ya wale watu waliopendana sio kwa ajili yaAllaah, yatageuka kuwa ni audui na kukatika.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

152

10. Tishio la adhabu kwa yule ambaye “mambo manane” anayapenda zaidi kuliko Diniyake.172

11. Yule mwenye kumfanyia Allaah mshirika na akafanya mapenzi yake (kwa mshirikahuyo) ni sawa na mapenda ampendayo Allaah, ni Shirki kubwa.

171 Shaykh Fawzaan anasema: ”Wanampenda, lakini wanampenda Yeye pamoja na wengine. Hii niShirki.”172 Shaykh Fawzaan anasema: ”Mambo haya maneno ni yale yaliyotajwa katika Suurat at-Tawbah:”Sema (ee Muhammad :(صلى اهللا عليه وآله وسلم “Ikiwa baba zenu, au watoto wenu, au ndugu zenu,au wake (au waume) zenu, au jamaa zenu, au mali mliyoichuma na biashara mnayoikhofiakuharibika kwake, na majumba mnayoridhika nayo, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaahna Mtume Wake na kufanya jihaad katika njia Yake; basi ngojeeni mpaka Allaah Alete AmriYake (ya adhabu).” (at-Tawbah 09:24). Mambo haya mtu anayapenda kimaumbile, lakinihatakiwi kutanguliza mapenzi ya mambo haya kabla ya mapenzi ya kumpenda Allaah naMtume Wake (´alayhis-Salaam).”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

153

Mlango Wa 32

Kauli Ya Allaah Ta´ala

ننيمؤم مإن كنت افونخو مافوهخفلا ت اءهيلأو وفخطان ييالش كما ذلمإن

”Hakika huyo ni shaytwaan anawakhofisha marafiki zake. Basi msiwakhofu,na nikhofuni Mimi mkiwa ni Waumini.” (al-´Imraan 03:175)

Kauli Yake:

خش إلا اللـهنما يعمر مساجد اللـه من آمن باللـه واليوم الآخر وأقام الصلاة وآتى الزكاة ولم يإ

”Hakika wanaoamirisha Masaajid ya Allaah ni (wale) wanaomwamini Allaahna Siku ya Mwisho, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah nahawamkhofu (yeyote) isipokuwa Allaah.” (at-Tawbah 09:18)

Na Kauli Yake:

لئو ذاب اللـهاس كعة الننتل فعج ي اللـهف يفإذا أوذ ا باللـهنقول آمن ياس مالن نموبكن رم رصاء نا ن جا كنإن قولنليكمعم ◌نيالمور العدي صا فبم لمبأع اللـه سليأو

”Na katika watu (wako) wasemao: “Tumemwamini Allaah;” lakiniwanapofanyiwa maudhi katika (njia ya) Allaah, hufanya mitihani (wa mateso,maudhi, vituko n.k.) ya watu kama kwamba ni adhabu ya Allaah. Nainapowajia nusura kutoka kwa Mola wako, bila shaka husema: “Hakika sisitulikuwa pamoja nanyi.” Je, kwani Allaah Hayajui yale yaliyomo katika vifuavya walimwengu?” (al-Ankabuut 29:10)

Abuu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea Hadiyth Marfu´:

“Hakika katika udhaifu wa yakini173 ni kuwaridhisha watu kwayanayomkasirikisha Allaah, na kuwasifu kutokana na riziki iliyoruzukuAllaah na kuwalaumu kwa kitu ambacho Hakuwaneemesha174 Allaah. Hakika

173 Shaykh Fawzaan anasema: “Makusudio hapa ni Imani. Watu wanatofautiana kwa Imani, kunaambao Imani zao ni zenye nguvu na wengine dhaifu.”174 Kuwapa

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

154

riziki ya Allaah hailetwi175 kwa mbio za mwenye kutafuta na walahairudishwi kwa chuki za mwenye kuchukia.”

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) kapokea ya kwamba Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Mtu mwenye kutaka176 Radhi za Allaah kwa yanayowachukiza watu, basiAllaah Humridhia na pia watu humridhia. Na mtu mwenye kutaka radhi zawatu kwa yanayomchukiza Allaah, basi Allaah Humkasirikia na watu piahumkasirikia.”

(Kaipokea Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake)

Ufafanuzi:´Ibaadah zinakuwa za kimoyo; kama kuwa na khofu, mapenzi, kutaraji n.k. Na kunakuwavile vile ´Ibaadah za kimwili; kama Swalah, Swawm, Hajj, ´Umrah n.k. Na kunakuwa´Ibaadah za kimali; kama Zakaah, Swadaqah, Ihsaan n.k. Na wakati mwingine ´Ibaadahinakuwa ya kimali na kimwili; kama Hajj na ´Umrah. Na makusudio katika mlango huu namlango kabla ya huyu – ambapo ilikuwa kuhusu mapenzi – na mlango huu kuhusu kuwana khofu na kuogopa – na inayokuja huko mbele – lazima iwe kwa muumini amuogopeAllaah, ampende, ataraji kutoka kwake n.k.

Yule atakayemuabudu Allaah bila ya kumuogopa, huyo ni Suufiy wanaosema kuwahatumuabudu Allaah kwa kuwa tunamuogopa wala kutaka Pepo Yake, isipokuwa tutunamuabudu Allaah kwa kuwa tunampenda. Huu ni upotevu mkubwa.

Na yule atakayemuabudu Allaah bila ya kumuogopa, atakuwa ni Khaarijiy. Haya ndiomadhehebu ya Khawaarij ambao wamechukua nususi za matishio tu na wakaacha zamatarajio.

Na yule ambaye atamuabudu Allaah kwa kutarajia kutoka kwake (Pepo) peke yake, huyu niMurjiy ambao wanachukua nususi za ahadi (Alizotoa Allaah) na wakaacha nususi zamatishio.

Hivyo ni lazima mtu amuabudu Allaah: kwa mapenzi, kuwa na khofu na kutaraji kutokaKwake mpaka mtu awe amemtakasia kikweli kweli ´Ibaadah Allaah.

175 Haiji, haipatikani176 Kutafuta

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

155

Aayah ya Suurat al-´Imraan: Tunachojifunza hapa ni uwajibu wa kumuogopa Allaah Pekee.Yule atakayemuogopa Allaah pamoja na mwengine yeyote, anakuwa ameshiriki. “... mkiwani waumini” hii ni dalili ya kwamba mtu hawi muumini ikiwa hamuogopi Allaah. Aayah hiiiliteremka katika vita vya Uhud pindi baadhi ya Maswahabah walipoasi amri ya Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kubaki juu ya mlima, ndio wakashambuliwa na makafiri.Hivyo haitakiwi kwa Muislamu kuwa na khofu na kupakana mafuta juu ya Dini yake kwasababu ya kuwaogopa makafiri.

Aayah ya pili ya at-Tawbah: Sababu ya kuteremka kwa Aayah hii ilikuwa ni wakatiwashirikina walikuwa wakiamirisha Masjid al-Haraam, Allaah Akawaradi na kuwaambiahii si kazi yenu bali ni ya Waislamu. Hapa kuna mafunzo ya kwamba Misikiti haiamirishimakafiri na washirikina (kwa ´Ibaadah). Kusijengwe humo kaburi, kufanywa Shirki nakuomba badala ya Allaah (´Azza wa Jalla), Taswawwuf n.k., hapana. Misikiti iwe Khaaliswkwa ajili ya kumtakasia ´Ibaadah Allaah (´Azza wa Jalla).

Aayah ya Suurat al-Ankabuut: Hapa tunapata funzo ya kwamba muumini bila kujalimaudhi kiasi gani atapata katika Dini yake, asubiri na awe na uvumilivu na wala asipakemafuta kwa kitu chochote katika Dini yake kwa ajili tu ya kutaka kuwaridhisha makafiri aumaadui wa Allaah. Ashikamane bara bara na Dini yake. Hii ni Hekima ya AllaahKuwajaribu waja Wake, mtu hawezi kusema mimi ni muumini tu ikaishia hapo. Hapana.Lazima Allaah Ampe mitihani ili aangalie je, ni muumini kweli au hapana? Adhabu iliyokoAakhirah ni kubwa kuliko mitihani ilioko hapa duniani. Kule kuwa kwake na subira hapaduniani ni bora kwake. Kwani adhabu ya Allaah ni kubwa kuliko adhabu za viumbe.Ingekuwa Allaah Hawapi mitihani waja wake, kusingelipambanuka baina ya muumini namnafiki, na baina ya mkweli na muongo. Allaah Kaweka mitihani ili apambanue baina yahuyu na huyu.

لهعجا فييعمج هكمرض فيعلى بع هضعبيث بل الخعجيالطيب و نبيث مالخ اللـه يزميلمنهي جف ـئك هم الخاسرون◌ أول

”Ili Allaah Apambanue khabiyth (waovu) na twayyib (wema), kisha Aweke waovu juu yawaovu wengine, kisha Awarundike pamoja Awatie katika (Moto wa) Jahannam. Hao ndiowaliokhasirika.” (al-Anfaal 08:37)

Mtu akipewa maudhi kwa sababu ya Dini Yake, Imani yake, Tawhiyd na ´Aqiydah yake naakawa mwenye kusubiri anakuwa ni mwenye kuokoka na adhabu za Allaah. Kwa sababumtu akiokoka (salimika) na fitina za watu duniani haokoki na adhabu za Allaah. Hapa namafunzo ya kumpwekesha Allaah kwa khofu na kumuogopa.

Hadiyth ya Abuu Sa´iyd: Hapa mtu anatakiwa aangalie na kupima kati ya mambo mawili:Mtu aridhishe watu na apate khasira za Allaah au amridhishe Allaah na apate Radhi zaAllaah? Huu ni mtihani Allaah Kawapa waja Wake. Ukiwaridhisha watu kwa mamboyanayomkasirikisha Allaah, basi utakuwa hukumuogopa Allaah na ni dalili ya udhaifu waImani. “Na kuwasifu kwa riziki ya Allaah... “, riziki ni ya Allaah kwa kuwa Yeye Ndiye Ar-

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

156

Razzaaq. Unatakiwa uinasibishe riziki hii kwa Allaah (Ta´ala) na si kwa mtu huyo ambayepengine kakupatia kitu. Yeye ni sababu tu – mkaakati. Mshukuru tu kadiri na wema wake.

“Yule asiyewashukuru watu hamshukuru Allaah.”

“Kuwalaumu kwa kitu ambacho hakuwaneemesha Allaah”, usiwalaumu watu kwakutofikia mahitajio yako, kwa kuwa Allaah ndiye Mwenye kutoa.

ما يفتح اللـه للناس من رحمة فلا ممسك لها ◌هدعن بم ل لهسرفلا م سكما يمو

”Rahmah yoyote (ile) ambayo Allaah Anayowafungulia watu, basi hakuna wa kuizuia, na(yoyote ile ambayo Allaah) Anaizuia, basi hakuna wa kuipeleka baada Yake.” (Faatwir35:02)

Watakiwa kuamini Qadhwaa na Qadar177 na kusema kuwa Allaah Hakuniandikia kitu hichi.Pengine kitu hichi kutokukupa nacho Allaah kuna maslahi kwako.

Sababu ya Hadiyth hii, ´Aaishah ambaye ni mama wa waumini (Radhiya Allaahu ´anha)ilikuwa ni pindi Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhu) alipomuandikia na kumuombanasaha ndo akawa amemuandikia Hadiyth hii kubwa. Alikuwa ni kiongozi wa Waislamuwakati huo. Ukimridhisha Allaah kwa yanayowachukiza watu, watu watakuridhia tu hatakama itakuwa ni baada ya muda, kwa kuwa nyoyo za waja ziko baina ya Vidole Viwili vyaAllaah. Na ukifanya kinyume chake, Allaah Hatokuridhia na watu vile vile hawatokuridhia.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-´Imraan. (03:175)

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat at-Tawbah. (09:18)

3. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Ankabuut. (29:10)

4. Yakini (Imani) inadhoofika na kuwa na nguvu.178

5. Alama za kudhoofika kwake (Imani). Na katika hayo ni haya mambo matatu.179

6. Kumpwekesha Allaah kwa khofu ni katika mambo ya faradhi (wajibu).

177 Yaliyopangwa na Kukadariwa na Allaah178 Shaykh Fawzaan anasema: ”Imani sio kitu kimoja kama wanavyosema Murji-ah; inazidi nakupungua kutokana na dalili nyingi. Imani za watu haziko sawa. Imani ya Abu Bakr (RadhiyaAllaahu ´anhu) si kama za watu wengine.”179 Shaykh anasema tena: ”Na dalili ya hilo (kudhoofika kwa Imani) ni pale ambapo utawaridhishawatu kwa mambo yanayomkasirikisha Allaah, utapowalaumu kwa mambo ambayo HakuwaneemshaAllaah, au ukaamini kwamba riziki inapatikana kwa mbio za mwenye kuikimbilia. Yote haya ni daliliya udhaifu wa Imani yako.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

157

7. Utajo wa Thawabu za mwenye kufanya hivo (kumuogopa na kumridhisha Allaah).

8. Utajo wa adhabu ya mwenye kuacha kufanya hivo (kumuogopa na kumridhisha Allaah).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

158

Mlango Wa 33

Kauli Ya Allaah Ta´ala

ننيمؤم مكلوا إن كنتوفت لى اللـهعو

“Na kwa Allaah Pekee tawakalini ikiwa nyinyi ni Waumini.” (al-Maaidah05:23)

Na Kauli Yake:

مهتادز هاتآي همليع تيلإذا تو مهقلوب جلتو اللـه رإذا ذك ينون الذنمؤا الممكلونإنوتي بهملى رعا وانإمي

”Hakika Waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao, zinajaa khofu(na hushtuka), na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia iymaan, na kwaMola wao wanatawakali.” (al-Anfaal 08:02)

Kauli Yake:

ننيمؤالم نم كعبن اتمو اللـه كبسح بيا النها أيي

”Ee Nabii! Hasbuka-Allaah (Anakutoshele za Allaah) na anayekufuatamiongoni wa Waumini.” (al-Anfaal 08:64)

Kauli Yake:

هبسح وفه لى اللـهكل عوتن يمو

“Na yeyote (yule) anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza.” (at-Twalaq 65:03)

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kasema:

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

159

“Hasbuna Allaahu wa ni´mal wakiyl”,180 neno hili kalisema Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alipotupwa ndani ya moto, na kalisema Muhammad (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) pindi alipoambiwa:

قد اسيلإن النكالو منعو ا اللـهنبسقالوا حا وانإمي مهادفز مهوشفاخ وا لكمعمج

”Wale ambao waliambiwa na watu: “Hakika watu wamejumuika dhidi yenu,basi waogopeni” (Haya) Yakawazidishia iymaan; na wakasema: “Hasbuna-Allaahu wa Ni’mal-Wakiyl (Allaah Anatutosheleza Naye ni Mbora wakumtegemea).” (al-´Imraan 03 : 173)

(Kaipokea al-Bukhaariy na an-Nasaa´iy)

Ufafanuzi:Kutegemea ni katika aina za ´Ibaadah ambayo haijuzu kumfanyia mtu mwingine badala yaAllaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Yule ambaye atamtegemea asiyekuwa Allaah, huyo nimshirikina kwa kuwa ni aina ya ´Ibaadah. Na kutegemea ni katika matendo ya moyo; nikama khofu, kupenda na kuogopa. Mambo ambayo hayawezi mwingine asiyekuwa Allaah,kama kuleta riziki, kukukinga na maadui, kuponya magojwa haijuzu kumtegemea mtumwingine asiyekuwa Allaah. Atakayetegemea mambo haya kutoka kwa mtu mwinginebadala ya Allaah inakuwa ni Shirki kubwa. Ama kuwategemea viumbe kwa mambowanayoyaweza huku unaamini kwamba watakukidhia unachokitaka – na sababu ya kituhicho ukaamini ni wao - hii ni Shirki ndogo. Ama kumuwakilisha kiumbe akukidhie haja,akununulie kitu, akuajiri hili halina ubaya. Lakini usiseme namtegemea fulani, baliwatakiwa kusema namuwakilisha fulani. Huku ni kuwakilisha na si kutegemea. KatikaAayah ya al-Maaidah tunapata dalili ya kuwa yule asiyemtegemea Allaah hawi muumini.

Neno hili “Hasbuna Allaahu wa ni´mal wakiyl” mtu analisema wakati wa shida, kishaAllaah Atakutosheleza kwa shida hii.

Aayah zote hizi ni dalili kuwa kumtegemea Allaah ni ´Ibaadah na haijuzu kumtegemea mtumwingine badala ya Allaah, na hili ni katika mambo ambayo hakuna ayawezae isipokuwaAllaah Pekee; kama kuponya maradhi, kuteremsha mvua, kupata riziki, kupata watoto, mtuasiwaendee mawalii, maiti na wengineo kama wafanyavyo watu leo. Hii ni Shirki kubwa.

180 Allaah (Pekee) Anatutosheleza na Yeye Ndiye Mbora wa kutegemewa

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

160

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Kutegemea ni katika mambo ya faradhi.

2. Ni katika sharti za kuwa na Imani.181

3. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Anfaal. (08:02)

4. Tafsiri ya Aayah mwisho wake. (08:64)

5. Tafsiri ya Aayah ya Suurat at-Twalaq. (65:03)

6. Umuhimu wa neno hili “Hasbuna Allaah wa ni´mal wakiyl” na kwamba ni kauliiliyosema Ibraahiym na Muhammad (´alayhimas-Salaam) katika shida.

181 Shaykh Fawzaan anasema: “Kwa kuwa Allaah Kasema: ”Na kwa Allaah Pekee tawakalini ikiwanyinyi ni Waumini.” Yule ambaye hakumtegemea Allaah sio muumini.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

161

Mlango Wa 34

Kauli Ya Allaah Ta´ala

اللـه كروا منأفأم فلا يأمن مكر اللـه إلا القوم الخاسرون◌

”Je, wameaminisha na mipango ya Allaah? Basi hawaaminishi mipango yaAllaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.” (al-A´raaf 07:99)

Na Kauli Yake:

ط مقنن يمالونوإلا الض بهر ةمحن ر

“Na nani anayekata tamaa na Rahmah ya Mola wake isipokuwa waliopotea.”(al-Hijr 15:56)

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kapokea:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusiana namadhambi makubwa182 halafu akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): 1)Kumshirikisha Allaah, 2) Kukata tamaa na Rahmah ya Allaah na 3)Kujiaminisha na vitimbi183 vya Allaah.”

Kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwambaMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Madhambi makubwa kabisa ni kumshirikisha Allaah, kujiaminisha navitimbi vya Allaah na kukata tamaa na Rahmah ya Allaah.”

(Kaipokea ´Abdur-Razzaaq)

182 al-Kabaair183 Adhabu ya Allaah (Ta´ala)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

162

Ufafanuzi:Makusudio ya mlango huu ni kubainisha khofu na kutaraji na kwamba ni aina moja katikaaina za ´Ibaadah haviachani, lazima mtu ajumuishe baina ya vyote viwili. Asiwe ni mwenyekhofu peke yake na akakata tamaa na Rahmah ya Allaah, haya ni madhehebu ya Khawaarij.Na wala asiwe ni mwenye kutaraji peke yake na akajiaminisha na adhabu na mipango yaAllaah kwake, na haya ndio madhehebu ya Murji-ah. Bali ni lazima ajumuishe baina ya yotemawili. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na ndio walivokuwawakifanya hata Mitume (´alayhimus-Salaam).

فإنهم كانوا يسارعون في الخيرات ويدعوننا رغبا ورهبا ◌نيعاشا خوا لنكانو

”Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri, na (walikuwa) wakituombakwa matumaini na khofu, na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.” (al-Anbiyaa 21:90)

وادعوه خوفا وطمعا

”Na muombeni kwa khofu na kwa kutumai.” (al-A´raaf 07:56)

Mtu lazima ajumuishe baina ya yote mawili. Amuombe Allaah kwa khofu na kutaraji, yotemawili. Asipunguze kimoja juu ya kingine.

Hadiyth ya Ibn Mas´uud: Madhambi yamegawanyika sehemu mbili; makubwa na madogo.Madhambi makubwa hayasamehewi isipokuwa kwa Tawbah, ama madogo yanasamehewakufanya matendo mbali mbali mema. Na madhambi makubwa yanatofautiana, dhambi yakwanza kubwa kabisa ni kumshirikisha Allaah. Kama jinsi mtu hakati tamaa na Rahmah yaAllaah, basi vile vile hali kadhalika mtu asijiaminishe na vitimbi na adhabu za Allaah. Mfanowa kujiaminisha na vitimbi vya Allaah ni kama mtu kufanya maasi na kusema “Allaah niMwingi wa Kusamehe” akategemea Rahmah ya Allaah peke yake huku akaendelea namaasi. Allaah ni Mwingi wa Kusamehe, ila pia vile vile ni Mkali wa Kuadhibu.

غافر الذنب وقابل التوب شديد العقاب

”Ghaafiri-dhambi (Anayeghufuru dhambi), Qaabilit-tawbi (Anayepokea tawbah), Shadiydil-‘Iqaabi (Mkali wa kuadhibu).” (Ghaafir 40:03)

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-A´raaf. (07:99)

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Hijr. (15:56)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

163

3. Matishio makali kwa yule anayejiaminisha na vitimbi ya Allaah.

4. Matishio makali kwa yule anayekata tamaa na Rahmah ya Allaah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

164

Mlango Wa 35

Kuwa Na Subira Kwa Yale Aliyoyakadiria Allaah Ni Katika KumuaminiAllaah

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

هقلب دهي ن باللـهمؤن يمو ◌يملء عيبكل ش اللـهو

”Na yeyote (yule) anayemuamini Allaah, (Allaah) Huuongoa moyo wake. NaAllaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi daima).” (at-Taghaabun 64:11)

Alqamah kasema:

“Mtu huyu184 ni yule ambaye anapofikwa na msiba anajua kuwa umetokakwa Allaah, basi huridhia na kujisalimisha Kwake.”

Katika Swahiyh Muslim, kumepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah(Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kasema:

“Mambo mawili miongoni mwa watu ni kiasi cha kufuru: 1) Kutukaniananasabu185 na 2) fujo za kumlilia maiti.”

Kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea kutoka kwaMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa amesema:

“Si katika sisi186 yule mwenye kujipiga makofi kwenye mashavu, akachananguo na akaita kwa mayowe187 ya Kijaahiliyyah.”

(Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

184 Aliyetajwa katika Aayah ya hapo juu185 Kutukana ukoo wa mwenzako186 Shaykh Fawzaan anasema: ”Kauli yake: ”Si katika sisi” huku ni kujiweka kwake mbali Mtume(´alayhis-Salaam) na yule mwenye kufanya hivyo. Na hii ni dalili ya kuonesha kuwa hii ni katikamadhambi makubwa.”187 Akapiga mayowe

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

165

Kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Allaah Akimtakia mja Wake kheri, Humharakishia adhabu duniani. NaAkimtakia mja Wake shari, Humcheleweshea adhabu ya dhambi yake mpakasiku ya Qiyaamah.”

Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ukubwa wa malipo ni pamoja na ukubwa wa mitihani.188 Hakika Allaah(Ta´ala) Anapowapenda watu Huwapa majaribio, yule mwenye kuridhia basihupara Radhi Zake, na yule mwenye kuchukia basi hupata khasira Zake.”

(Kaipokea at-Tirmidhiy na kasema ni Hasan)

Ufafanuzi:Imani ni kutamka kwa ulimi, na kuitakidi moyoni na matendo ya viungo vya mwili.Matendo ni katika Imani. Na matendo yamegawanyika sehemu mbili; matendo ya moyo namatendo ya viungo. Na subira ni katika matendo ya moyo; kama khofu, kutaraji, shauku,kutamani n.k. Muumini anatakiwa kuamini kuwa kila kitu kinatokea ni kwa Qadhwaa naQadar ya Allaah. Yule asiyeamini Qadar hamuamini Allaah (´Azza wa Jalla) kwa kuwakapinga nguzo katika nguzo za Imani sita. Yanayomfika muumini anatakiwa kuridhia,asilaumu na asubiri. Na subira imegawanyika sehemu tatu:

1. Subira juu ya amri za Allaah Alizomuamrisha kwazo Allaah. Awe ni mwenye subirana kuzitimiza kama Alivomuamrisha Allaah pamoja na shida na ugumu.

2. Subira juu ya Aliyomkataza Allaah. Awe na subira juu ya matamanio AliyomkatazaAllaah na mengine yote.

3. Subira kwa Qadar ya Allaah; kama maradhi, mauti, ufakiri na kadhalika.

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu): Hii kufuru inayokusudiwa hapa nikufuru ndogo. Kujitukuza kwa nasabu ni jambo ambalo halijuzu. Abuu Lahab ana kabilanzuri na tukufu, ni katika Baniy Haashim ilihali ni katika watu wa Motoni na haikumfaa kitu

188 Mabalaa, misiba, matatizo, majaribio

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

166

nasabu yake. Na Bilaal (Radhiya Allaahu ´anhu) mtu wa Habashah (Ethiopia) naye ni katikawatu wa Peponi, hali kadhalika Salmaan al-Faarisiy n.k. Hivyo yule ambaye anatukaniananasabu za wengine, kwanza hili ni katika matendo ya Kijaahiliyyah na isitoshe ni aina yakufuru ndogo. Na jambo la pili ni fujo za kumlilia maiti, kwa kuwa fujo ni kutoamini nakuwa na subira na Qadar ya Allaah. Pia hili ni katika aina ya kufuru.

Hadiyth ya Anas: Hapa kuna hekima kwa nini muumini anapewa mitihani na majaribio, nakwa nini kafiri anavutwa kidogo kidogo (katika adhabu). Anafanya matendo ya kufuru naShirki, lakini pamoja na haya anapewa neema mbali mbali duniani kwa kuwa AllaahAnamvuta kidogo kidogo (katika adhabu). Ama muumini anapopewa mitihani anatakiwakuwa na subira kwani ni katika maslahi yake yeye, ama kafiri kadiri na anavyopewa neemambali mbali na adhabu yake ndio huzidi. Baadhi ya wajinga leo wanasema kwa niniWaislamu ndio wenye matatizo chungu mzima leo na makafiri ndio wenye maisha mazurina neema mbali mbali naye (mtu huyu mjinga) hajui Hekima ya Allaah kwa hili.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat at-Taghaabun. (64:11)

2. Hili (kuwa na subira) ni katika kumuamini Allaah.

3. Kutukaniana nasabu za watu.

4. Matishio makali kwa yule mwenye kujipiga makofi kwenye mashavu, akachana nguo naakaita kwa mayowe ya Kijaahiliyyah.

5. Alama ya Allaah Kumtakia mja Wake kheri (kwa kumharakishia adhabu duniani).

6. Alama ya Allaah Kumtakia mja Wake shari (kwa kumcheleweshea adhabu mpaka siku yaQiyaamah).

7. Alama ya Mapenzi ya Allaah kwa mja Wake.189

8. Kuharamishwa kwa kupiga mayowe.190

9. Thawabu za kuridhia kwa balaa (mitihani).

189 Shaykh Fawzaan anasema: ”Utajuaje kama Allaah Anakupenda? Ni pale ambapo utakufika msiba.Hii ni dalili ya kwamba Allaah Anakupenda. Kwa kuwa Allaah Anawapa mitihani waleanaowapenda. Na ndio maana Mitume (´alayhimus-Salaam) ndio watu wenye mitihani mikubwamikubwa.”190 Shaykh anasema tena: ”Kama wafanyavyo Raafidhwah (Shiy´ah) siku ya ´Aashuurah. Wanajipigana kujichana chana, haya ni katika matendo ya Kijaahiliyyah.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

167

Mlango Wa 36

Yaliyokuja Kuhusu Riyaa

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

داحو ـه ـهكم إل قل إنما أنا بشر مثلكم يوحى إلي أنما إل ◌ بهر ةادببع ركشلا يا وحاللا صمل عمعفلي بهقاء رو لجرن كان يفمأحدا

”Sema (ee Muhammad Hakika mimi ni bin-Aadam kama“ :(صلى اهللا عليه وآله وسلم

nyinyi. (Isipokuwa tu mimi) Naletewa Wahy kwamba:Hakika Ilaaha wenu (Anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ni Ilaahun-Waahid (Mungu Mmoja). Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake, na atende‘amali njema na wala asimshirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.”(al-Kahf 18:110)

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea HadiythMarfu´ ya kwamba Allaah (Ta´ala) Kasema:

“Mimi ni Mwenye Kujitosheleza na Kutohitajia washirika. Atakayefanya´amali akanishirikisha na kitu kingine, ntamuacha na Shirki yake.”

(Kaipokea Muslim)

Abuu Sa´iyd (al-Khudriy) kapokea Hadiyth Marfu´ ya kwamba Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Je, nikwambieni kile ninachokukhofieni kuliko hata huyo Masiyh ad-Dajjaal?” Wakasema: “Ndio.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):“Ni Shirki iliyojificha, anasimama mtu kuswali na akaipamba Swalah yakekwa kuwa anaona watu wanamtizama.”

(Kaipokea Imaam Ahmad)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

168

Ufafanuzi:Kitu cha kwanza kikubwa Alichokataza Allaah ni Shirki, kama jinsi kitu cha kwanzaAlichoamrisha Allaah ni Tawhiyd. Na Shirki imegawanyika sehemu mbili:

1. Shirki kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu. Kama kuchinjia kwa ajili ya asiyekuwaAllaah, kuweka nadhiri kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kuomba msaada na kuombakinga badala ya Allaah n.k.

2. Shirki ndogo ambayo na yenyewe imegawanyika sehemu mbili: a) Shirki katikamatamshi: Kama kusema “Lau bila ya Allaah na wewe”, “Akipenda Allaah nawewe”, “Mimi namtegemea Allaah na wewe” n.k. b) Shirki ndogo iliyojifichamoyoni, nayo ni Riyaa. Mtu kujionesha kwa ´amali.

Na Riyaa imegawanyika sehemu mbili:

1. Riyaa ya wanafiki.

ون اء یر الى س ة قاموا ك ال وا إلى الص ا قام إذ و ھم ع اد خ ھو ھ و اللـ ون ادع یخ نافقین الم ق إن ھ إال اللـ ون كر یذ ال و الناس لیال

”Hakika wanafiki wanamhadaa Allaah. Na Yeye (Allaah) Atawaadhibu kwa hadaa zao. Nawanaposimama kuswali husimama kwa uvivu, wanajionyesha kwa watu na walahawamdhukuru Allaah isipokuwa kidogo tu.” (an-Nisaa 04:142)

Hii ni Shirki kubwa. Mwenye nayo atakuwa katika tabaka la chini kabisa Motoni.

2. Riyaa katika nia na makusudio. Hii huitwa ni Shirki ndogo yenye kujificha isiyomtoamtu katika Uislamu. Hii inaweza kumpitikia Muislamu (muumini). Ama ile yakwanza haiwezi kumpitikia Muislamu (muumini). Hii ndio Riyaa.

Aayah ya Suurat al-Kahf: Hapa Anaambiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)awaambie watu kuwa ni binaadamu kama nyinyi na sina haki yoyote ya Rubuubiyyah.Hapa kuna Radd kwa wale ambao wanachupa mipaka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) na kumpandisha cheo zaidi ya manzilah yake. Isitoshe wanasema kuwa Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kaumbwa kwa nuru, yaani wanasema yeye ni nuru nasio binaadamu. Ni kweli kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kaja kwa nuru,Wahyi na Qur-aan, ama kusema yeye ndio nuru hapana. Yeye ni binaadamu (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kama wengine. Na nukta inayolengwa katika Aayah ni: “Na walaasimshirikishe katika ´Ibaadah za Mola Wake yeyote”, hapa neno “yeyote” linajumuishakiumbe yeyote yule; sawa awe Malaika, Mitume, watu wema, mawalii na wengineo. Sawaiwe ni Shirki kubwa au ndogo, Allaah Haridhii kushirikishwa na yeyote.

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu): Hii ni Hadiyth al-Qudsiy ambayokaipokea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka kwa Mola Wake. Riyaa (naShirki ndogo) inaporomosha ´amali ambayo imechanganyika nayo na wala haiporomoshi

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

169

´amali zote, kama ifanyavo Shirki kubwa. Shirki kubwa inaporomosha ´amali zote za mtu.Hii ndio tofauti ya Shirki kubwa na ndogo.

Masiyh ad-Dajjaal ana fitina na shari kubwa kabisa, ni wachache sana watakaosalimika nae,isipokuwa wale Aliyowarehemu Allaah. Lakini mbali na fitina zake, Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) aliwakhofia Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum) juu ya Shirkindogo kuliko Masiyh ad-Dajjaal. Hakukhofia juu yao Shirki kubwa, bali alikhofia Shirkindogo. Kwa kuwa hii ni khatari sana. Ni juu ya Muislamu atahadhari na amtakasie MolaWake matendo yake na ajiepushe mbali na Shirki. Na akiingiwa na kitu katika Shirki ndogomoyoni mwake – kupenda sifa na matapo n.k. – akapambana nayo (hiyo Shirki ndogo)haitomdhuru. Ama ikiwa itaendelea ndani ya moyo wake, inaporomosha ´amali yake naanakuwa kajichosha bure bila ya faida.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Kahf. (18:110)

2. Jambo kubwa, nalo ni kurudishwa kwa ´amali njema ikiingiwa ndani yake na kitu badalaya Allaah.

3. Kutajwa sababu ya hilo, nayo ni kule Allaah Kujitosheleza kikamilifu.

4. Miongoni mwa sababu ni kuwa Yeye ni Bora kuliko washirika (anaoshirikishwa pamojaNaye).

5. Khofu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaogopea Maswahabaha zakeRiyaa.

6. Kafasiri hilo kwamba mtu anaswali kwa ajili ya Allaah lakini akaipamba Swalah yake kwakuwa anaona watu wanamtizama.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

170

Mlango Wa 37

Ni Katika Shirki Mtu Kufanya ´Amali Kwa Kutaka Dunia

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

ـئك الذين ليس لهم في الآخرة إلا من كان يريد الحياة الدنيا وزينتها نوف إليهم أعمالهم فيها وهم فيها لا يبخسون أولارالن وحبط ما صنعوا فيها وباطل ما كانوا يعملون◌

”Anayetaka maisha ya dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu ‘amalizao humo, nao hawatopunjwa humo. Hao ndio wale ambao hawatokuwa nachochote katika Aakhirah isipokuwa Moto. Na zitaharibika yale (yote)waliyoyafanya humo (duniani), na yatabatilika yale (yote) waliyokuwawakiyatenda.” (Huud 11:15-16)

Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Ameangamia mja wa Dinaar, ameangamia mja wa Dirham, ameangamia mjawa Khamiyswah,191 ameangamia mja wa Khamiylah.192 Akipewa huridhia nakama hakupewa hukasirika, kaangamia na kapotea, na mwiba ukimchomaasiweze kuutoa. Bishara nje kwa mja ambaye amechukua khatam za farasiwake kwa ajili ya kupigana Jihaad katika njia ya Allaah, huku kichwa chakena miguu yake vimejaa mavumbi. Anapowekwa kulichunga (jeshi) basihulichunga kikweli kweli kwa kuridhia, na anapowekwa nyuma kulichungaanalichunga kikweli kweli vizuri, hata akiombwa idhini asingeliidhinishwa,na akiombea, maombi yake yasingekubaliwa.”193

191 Ni aina ya nguo nzuri192 Masuti193 Kutokana na unyenyekevu wake

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

171

Ufafanuzi:Mlango huu makusudio ni Shirki ndogo.

Aayah ya Suurat Huud: “Anayetaka maisha ya dunia... ”, yaani anayetaka kwa matendoyake afanyayo maisha ya dunia na wala hataki Aakhirah. “ ... na mapambo yake”, mapamboya dunia ni mali (na watoto). Mtu huyu tutampa alichokikusudia kikamilifu, lakini Aakhirahhawatokuwa na jengine zaidi ya Moto. ´Amali zao zitakuwa si njema bali ni batili kutokanana makusudio na nia yake batili.

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu): “Mja wa Dinaar na Dirham”. Huyu nimtu ambaye hataki jengine zaidi ya Dinaar na Dirham. Kamwita kuwa ni mja wa Dinaar. Nidalili kuwa hii ni Shirki. Ni dalili ya kuwa kutaka Dinaar na Dirham kwa kufanya ´amalinjema kwa ajili ya tamaa ya dunia ni Shirki. Kwa kuwa Allaah Kamwita kuwa ni mja wake(hiyo Dinaar na Dirham). Hii ni Du´aa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)anamuombea mtu huyu aangamia kutokana na nia yake mbaya. Hii ndio alama ya mtumwenye kutaka dunia. Akipewa anaridhia, na kama hakupewa huchukia kweli kweli.

Ni kama mfano wa mtu kujifunza elimu ya Kishari´ah, muadhini, mswalishaji kwa ajili apatekazi nzuri kwa kukusudia dunia, huyu ana matishio makali kama haya. Ama elimu zakidunia haina neno kwa kuwa sio ´Ibaadah. Ama ´amali za Aakhirah haijuzu kuikusudiadunia.

Ama huyu mtu mwingine anataka Uso wa Allaah kwa kupigana Jihaad katika njia yaAllaah, na wala hataki kitu kingine zaidi ya Aakhirah. Hataki sifa wala matapo. Huu ndiomfano wa Mukhlisw mtu mwenye Ikhlaasw katika ´amali yake, na hii ndio ´amali yaIkhlaasw ya wazi kabisa.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Mtu kuitaka dunia kwa kufanya matendo ya Aakhirah.

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat Huud. (11:15-16)

3. Muislamu kuitwa mja wa Dinaar na Dirham na mja wa Khamiyswah.

4. Kufasiriwa hilo kuwa: “Akipewa huridhia na kama hakupewa hukasirika.”

5. Maana ya kauli yake: “Ta´isah wa Intakasah kapotea na kaangamia.”

6. Maana ya kauli yake: “Na mwiba ukimchoma asiweze kuutoa.”

7. Kusifiwa kwa mpigana Jihaad aliyesifiwa kwa sifa hizo (zilizotajwa katika Hadiyth).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

172

Mlango Wa 38

Mwenye Kuwatii Wanachuoni Na Watawala Katika KuharamishaAliyohalalisha Au Kuhalalisha Aliyoharamisha Allaah, Kawafanya Ni

Miungu Badala Ya Allaah

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) anasema:

“Kumekurubia kukushukieni mawe kutoka mbinguni! Nawaambieni:“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema... ” Na nyinyimnanambia: “Abu Bakr na ´Umar wamesema!?”194

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) anasema:

“Nashangazwa na watu ambao wanajua isnadi195 na usahihi wake, wanaiachana kufuata rai ya Suftaan (ath-Thawriy). Na Allaah (Ta´ala) Anasema:

يمأل ذابع مهيبصي ة أونتف مهيبصأن ت رهأم نفون عالخي ينذر الذحفلي

“Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah auikawasibu adhabu iumizayo.” (an-Nuur 24:63)

Unajua ni nini fitina? Fitina ni Shirki. Pengine ataporudisha baadhi ya manenoyake196 akaingiwa moyoni mwake na kitu kama mashaka na upotevuakaangamia.”

Kutoka kwa ´Adiy bin Haatiym (Radhiya Allaahu ´anhu) ambaye kapokea:

“Nilimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisoma Aayah hii:

اللـه ونن دا ماببأر مهانبهرو مهاربذوا أحخات

194 Hapa ilikuwa pindi Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alipowaambia kwamba Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kuwa kufanya hija ya al-Tamattu´ ndio bora, watuwakimjibu kwa kumwambia: ”Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) - kutokana naIjtihaad yao wao - wanaonelea kufanya hija ya al-Ifraad ndio bora. Ndio Ibn ´Abbaas (RadhiyaAllaahu ´anhumaa) akawa amewaambia hivyo.195 Shaykh Fawzaan anasema: ”Yaani kunakusudiwa Hadiyth Swahiyh.”196 Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

173

“Wamewafanya Ahbaar (Makuhani - wanavyuoni wa Kiyahudi) wao naRuhbaan (Wamonaki - watawa) wao kuwa ni miungu badala ya Allaah.” (at-Tawbah 09:31)

Nikamwambia:

“Sisi hatukuwa tunawaabudu.”

Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Je, hawakuwa wakiharamisha Aliyoyahalalisha Allaah nanyimkayaharamisha, na wakihalalisha Aliyoyaharamisha Allaah nanyimkayahalalisha?” Nikasema: “Ndio.”197 Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam): “Huku ndio kuwaabudu.”

(Kaipokea Ahmad na at-Tirmidhiy na kasema kuwa ni Hasan)

Ufafanuzi:Hapa tunapata funzo, kuwatii wanachuoni na watawala katika mambo ambayoyanakwenda kinyume na Shari´ah ya Allaah kuwa ni Shirki. Kwa kuwa kawashirikishapamoja na Allaah. Kwa kuwa kuhalalisha na kuharamisha ni haki ya Allaah (Subhaahahuwa Ta´ala) Pekee. Atakayemshirikisha yeyote pamoja na Allaah, kamfanya ni mshirika waAllaah. Na ndio maana washirikina waliposema kuwa maiti ni halali, Allaah (Jalla wa ´Alaa)Akasema:

ركونوشلم كمإن موهمتإن أطع

”Na mtakapowatii hakika mtakuwa washirikina.” (al-An´aam 06:121)

Mkiwatii katika mambo ambayo Kaharamisha Allaah. Na hii huitwa Shirki ya utiifu.

Ama kuwatii wanachuoni na watawala katika mambo ambayo yanaenda sambamba naShari´ah, hili ni jambo la wajibu. Anasema (Ta´ala):

نكمر مي الأمأولول وسوا الريعأطو وا اللـهيعوا أطنآم ينا الذها أيي

197 ´Adiy bin Haatiym (Radhiya Allaahu ´anhu)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

174

”Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.” (an-Nisaa 04:59)

“wenye madaraka” ni wale viongozi na wanachuoni katika Waislamu.

Watu wengi leo wanaofuata matamanio yao wanasema: “Maadamu masuala hayawanachuoni wametofautiana, sisi tunachukua kauli ya mwanachuoni ambayo ni sawakwetu hata kama kauli hii itakuwa ni ya makosa. Wanachuoni hawakulindwa na madhambi(na makosa) zaidi ya Mtume wa Allaah (´alayhis-Salaam). Yeye peke yake (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) ndio zinachukulia kauli zake kabisa, kwa kuwa haongei kwa matamanioyake, ama mwanachuoni anaweza kukosea. Hivyo inachukuliwa kauli ambayo ni ya sahihiiliyoafikiana na dalili, na tunaachana na ile ya makosa. Ama yule anayefuata matamanioyake au anachukua lile lililoendana na yeye na kuafiki matamanio yake, huyu anafuatamatamanio yake, kayafanya matamanio yake ndio mungu wake. Masuala haya ni khatarisana. Allaah Atawaambia siku ya Qiyaamah:

وقالوا ربنا إنا أطعنا سادتنا وكبراءنا فأضلونا السبيلايوم تقلب وجوههم في النار يقولون يا ليتنا أطعنا اللـه وأطعنا الرسولا

”Siku zitakapopinduliwa nyuso zao motoni, watasema: “Laiti tungelimtii Allaah, natungelimtii Mtume. Na watasema: “Mola wetu! Hakika sisi tumewatii (na kuwafuata)mabwana zetu, na wakuu wetu, basi wametupoteza njia (ya haki).” (al-Ahzaab 33:66-67)

Wao waliwatii katika kumuasi Allaah. Ndio maana wakawa pamoja nao Motoni.

ربنا آتهم ضعفين من العذاب والعنهم لعنا كبريا

“Mola wetu! Wape adhabu maradufu, na walaani laana kubwa.” (al-Ahzaab 33:68)

Je, lakini litawafaa hili? Hapana.

Haya ni masuala muhimu sana kwa kuwa yameenea sana leo. Watu wengi unawasikiawanasema: “Maadamu fulani kasema hivi, tunachukua kauli yake.” Hata huyo fulanikasema hivi, ni ipi dalili yake? Hili ndio muhimu.

Hadiyth ya Ibn ´Abbaas: Ikiwa Abu Bakr na ´Umar ambao ni watu bora katika Ummahwakikosea katika Ijtihaad haijuzu kwetu kuwatii na kuacha aliyotuamrisha Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), vipi kwa wasiokuwa wao ambao hawalingani nawao (Abu Bakr na ´Umar) sawa katika elimu na fadhila? Na kuleta madai tu ya tofauti kwakuwa mtu fulani kasema tunalolipenda.

Imaam Ahmad: Rai ya mwanachuoni akikosea, anapewa thawabu moja kwa kuwakajitahidi, lakini haijuzu kuifuata rai yake hiyo aliyokosea. Kisha Imaam Ahmad akasemakuwa fitina ni Shirki, kwa kuwa kawatii katika mambo ya Shari´ah ambayo kakosea.Sufyaan na maimamu wengine wanasema: “Msichukui maoni yetu mpaka mtapojua dalilizetu.” Fitina imegawanyika sehemu mbili:

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

175

1. Fitina ya matamanio (shahawa). Kama Zinaa, kunywa pombe na kadhalika.

2. Fitina ya shubuha. Allaah Atukinge, kwani hii ndio mbaya zaidi. Kwa kuwa hiihuwa katika mambo ya ´Aqiydah. Ama fitina ya matamanio, huwa katikamatendo, tabia n.k. Hii huwa ufasiki. Ama ya shubuha huwa katika ´Aqiydah.

Na kwa ajili hii wamesema wanachuoni:

“Yule mwenye kufuata mambo ya rukhusa hufanya Uzandiki.”

Na mambo ya ruhusa hapa makusudio ni kauli za wanachuoni zilizokhalifu dalili.

´Adiy bin Haatim: Yeye kusema kwake: “Tulikuwa hatuwaabudu” alifikirikinachomaanishwa ni kuwaswalia, kuwasujudia, kuwafanyia Rukuu, kuwachinjia n.k. Hivindivyo alivyokuwa amefahamu. Ndio Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaamemfafanulia maana ya kuwafanya Ahbaar na Ruhbaan. Dalili zote hizi zinatolea dalili yakwamba haijuzu kuchukua kauli ya mtu ambaye kali yake imekwenda kinyume na dalili.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat an-Nuur. (24:63)

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat at-Tawbah. (09:31)

3. Tanbihi ya maana ya ´Ibaadah ambayo alikuwa ameikanusha ´Adiy (Radhiya Allaahu´anhu).

4. Mfano uliotoa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa Abu Bakr na ´Umar, namfano uliotoa Imaam Ahmad kwa Sufyaan.198

5. Hali zimebadilika kwa uhakika huu, mpaka imekuwa kwa watu wengi kuwaabuduRuhbaan ni katika ´amali bora na wanaita kuwa ni Wilaayah, na kuwaabudu Ahbaar wanaitakuwa ndio elimu na Fiqh. Kisha hali zimebadilika mpaka kiasi ambacho imefikia wakawawanaabudiwa badala ya Allaah watu ambao sio hata katika watu wema199 na vile vilewakaabudiwa ambao ni katika wajinga.

198 Shaykh Fawzaan: ”Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ndio katika Maswahabahbora. Na Sufyaan ni katika wanachuoni bora. Lakini hata hivyo, yule atakayewatii katika mamboambayo yanakwenda kinyume na dalili kwa Ijtihaad yao, kawafanya ni miungu badala ya Allaah namawe kutoka mbinguni yanastahiku kumwangukia.”199 Shaykh Fawzaan anasema: ”Si kwamba wameishia kuwaabudu watu wema na mawalii peke yao,bali wamefikia hata kuwaabudu ambao ni katika mawalii wa Shaytwaan; wachawi na huku wanadaikuwa wana karama.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

176

Mlango Wa 39

Kauli Ya Allaah Ta´ala200

ون أن يريدي كلن قبا أنزل ممو كا أنزل إليوا بمنآم مهون أنمعزي ينإلى الذ رت ألم وا بهكفروا أن يرأم قدو وا إلى الطاغوتاكمحتويريد الشيطان أن يضلهم ضلالا بعيدا

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwakwako (ee Muhammad (صلى اهللا عليه وآله وسلم na yale yaliyoteremshwa kabla yako;wanataka wahukumiane kwa twaaghuwt na hali wameamrishwa wakanushehiyo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali.” (an-Nisaa 04:60)

Kauli Yake:

وإذا قيل لهم لا تفسدوا في الأرض قالوا إنما نحن مصلحون

”Na wanapoambiwa: “Msifanye uharibifu katika ardhi”. Husema: “Hakikasisi ni watengenezaji.” (al-Baqarah 02:11)

Kauli Yake:

تفسدوا في الأرض بعد إصلاحها وادعوه خوفا وطمعاولا ◌سننيحالم نم قريب اللـه تمحإن ر

”Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake; namuombeni kwa khofu na kwa kutumai. Hakika Rahmah ya Allaah iko karibuna watendao wema.” (al-A´raaf 07:56)

Kauli Yake:

أفحكم الجاهلية يبغون ومن أحسن من اللـه حكما لقوم يوقنون◌

”Je, wanataka (uwahukumu kwa) hukumu ya kijaahiliyyah? Na nani mborazaidi kuliko Allaah katika kuhukumu. (Yanafahamika haya) kwa watu wenyeyakini.” (al-Maaidah 05:50)

200 Hukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah (Ta´ala)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

177

´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtumewa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Hatoamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yawe ni yenye kufuata yaleniliyokuja nayo.”

(Kasema an-Nawawiy kwamba Hadiyth ni Swahiyh, kaipokea “Kitaab al-Hujjah” kwa isnadi Swahiyh)

Sha´biy kasema:

“Kulikuwa ugomvi baina ya watu wawili mnafiki na myahudi. Akasema yulemyahudi: “Twende kwa Muhammad atuhukumu”; kwa kuwa alijua201 kuwahachukui rushwa. Yule mnafiki akasema: “Twende kwa mayahudiwatuhukumu”; kwa kujua kwake202 kuwa wao wanachukua rushwa. Hivyowote wawili wakakubaliana kumwendea kuhani Juhaynah ili awahukumu.Ndipo kukateremka:

“Je, huoni wale ambao wanadai “ (an-Nisaa 04:60) mpaka mwisho waAayah”.”

Na yasemekana iliteremka baina ya watu wawili waliogombana. Mmoja waoakasema: “Wacha tumpelekee kesi yetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) aihukumu.” Lakini yule mwengine akasema: “Wachatumpelekee Ka´b bin al-Ashraf. Kisha wakamshtakia ´Umar (Radhiya Allaahu´anhu), mmoja wao akamueleza ´Umar kisa kilivyokuwa.203 Akamuuliza204

yule ambaye hakuridhia ipelekwe kesi kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam): “Ni hivyo (yaani ni kweli ulisema hivo)?” Akasema:“Ndio.” ´Umar akampiga kwa upanga na akamuua.”

201 Myahudi huyo kuwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hachukui rushwa202 Huyo mnafiki203 Mpaka kumfikia ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu)204 ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

178

Ufafanuzi:Ni lazima matamanio ya mtu yawe ni yenye kufuata Qur-aan na Sunnah. Mtu asiwe namatamanio ambayo yanakwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Aridhie hukumu yaAllaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ajisalimishe.

ما مجرح ي أنفسهموا فجدلا ي ثم مهنيب رجا شيمف وكمكحى يتون حنمؤلا ي بكرافلا ويملسوا تملسيو تيا قض

”Basi Naapa kwa Mola wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu (mwamuzi)katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasione katika nyoyo zao uzitokatika uliyohukumu na wajisalimishe kwa unyenyekevu.” (an-Nisaa 04:65)

Asiwe katika nafsi yake na uzito kwa hayo. Na ndio maana Akasema:

ون أن يريدي كلن قبا أنزل ممو كا أنزل إليوا بمنآم مهون أنمعزي ينإلى الذ رت ألموا إلى الطاغوتاكمحت

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (eeMuhammad وآله وسلمصلى اهللا عليه ) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; wanataka wahukumianekwa twaaghuwt.” (an-Nisaa 04:60)

Watu hawa wanadai kuwa wana Imani, na lau wangelikuwa ni wakweli katika Imani zaowangehukumiana kwa Qur-aa na Sunnah na wasingelihukumiana kwa Twaaghuut. Hii nidalili kuwa ´amali ni katika Imani. Kwa kuwa kuhukumiana ni katika Imani.

أفغير اللـه أبتغي حكما وهو الذي أنزل إليكم الكتاب مفصلا

”(Sema): “Je, nitafute hakimu asiyekuwa Allaah (atuhukumu baina yetu) Naye NdiyeAmbaye Aliyekuteremshieni Kitabu kinachofafanuliwa?” (al-An´aam 06:114)

Hili ndio lengo la kuteremshwa Kitabu. Magomvi yote na tofauti zinarudishwa katika Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Sha´biy: Hapa kuna dalili mnafiki akidhihirisha unafiki wake, anauawa. Ama maadamuhajadhihirisha unafiki wake, tunamwachia Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) alikubali hili na kukateremka Aayah kuhusu hilo. Hapa kuna dalili ya kuachakanuni na sheria zinazotunga binaadamu, hata ´Umar ambaye ni mbora katika Maswahabahhaijuzu kuhukumiwa kwake na kuacha Qur-aan na Sunnah, vipi tusemeje wengine katikamatwaaghuut? Hakuna anayefanya hivi isipokuwa mnafiki. Ama muumini wa kwelihuridhia hukumu ya Allaah.

باللـه وبالرسول وأطعنا ثم يتولى فريق منهم من بعد ذلكويقولون آمنا ◌ننيمؤبالم كـئ وإذا دعوا إلى اللـه ورسوله ليحكم بينهم إذا فريق منهم وما أولمعرضون

”Na (wanafiki) wanasema: “Tumemwamini Allaah na Mtume, na Tumetii.” Kisha hugeukakundi miongoni mwao baada ya hayo. Na (wala) hao si wenye kuamini. Na wanapoitwa

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

179

kwa Allaah na Mtume Wake ili Awahukumu baina yao, mara hapo kundi miongoni mwaowanakengeuka (kukataa).” (Nuur 24:47-48)

Haki na hukumu ikiwa kwao, wanaridhia. Ama haki na hukumu ikiwa dhidi yao,wanakasirika na wala hawaridhii. Hii ndio sifa ya wanafiki. Ama muumini anaridhiahukumu ya Allaah, sawa hukumu ikiwa yake au dhidi yake, na wala hawezi kabisa kwendakwenye makanuni na mfano wa hayo. Ni juu ya Waislamu watanabahi kwa jambo hili. Kwakuwa makafiri wanachotaka ni kuwatoa Waislamu waache kuhukumiana katika Kitabu chaAllaah na badala yake wachukue kanuni na sheria zao. Hili kamwe. Hii ndio Imani naTawhiyd. Kwa kuwa kuhukumiana kwa Shari´ah ya Allaah, hii ndio Tawhiyd. Amakuhukumiana kinyume na Shari´ah ya Allaah, hili ni katika kufuru na unafiki.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat an-Nisaa (04:60) pamoja na msisitizo wa uelewa wa maana yatwaaghuut.

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Baqarah:

وإذا قيل لهم لا تفسدوا في الأرض

”Na wanapoambiwa: “Msifanye uharibifu katika ardhi... ” 205 (al-Baqarah 02:11)

3. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-A´raaf:

بعد إصلاحها ولا تفسدوا في الأرض

”Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake... ” 206 (al-A´raaf 07:56)

4. Tafsiri ya Aayah ya al-Maaidah:

أفحكم الجاهلية يبغون

”Je, wanataka (uwahukumu kwa) hukumu ya kijaahiliyyah?” 207 (al-Maaidah 05:50)

205 Shaykh Fawzaan anasema: ”Yaani hawa ni wanafiki, wanapoambiwa msifanye uharibifu katikaardhi kwa maasi na kuhukumiana kinyume na Shari´ah ya Allaah. Wanasema: ”Sisi niwatengenezaji.” Ni dalili ya kwamba hukumu kwa Aliyoteremsha Allaah ni kutengeneza katikaardhi, na hukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah ni kueneza ufisadi katika ardhi.”206 Shaykh anasema tena: ”Allaah Kaitengeza ardhi kwa kutuma Mitume na Kuteremsha Vitabu,kuhukumu kwa Shari´ah. Watu wakihukumu kinyume na Shari´ah na badala yake wakachukuakanuni na sheria za kibinaadamu, huku ndio kueneza ufisafi katika ardhi hata kama watadai kuwahuku ni kutengenza, maendeleo, mambo ya kisasa na kadhalika.”207 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa Allaah Kaita hukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah kuwani hukumu ya kijaahiliyyah ambayo ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jalla).”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

180

5. Aliyosema Sha´biy kuhusu sababu ya kuteremka Aayah ya kwanza.

6. Tafsiri ya Imani ya kweli na ya uongo.208

7. Kisa cha ´Umar na mnafiki.

8. Imani haifikiwi kwa mtu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale aliyokujanayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

208 Shaykh anasema tena: ”Imani ya kweli ni kule kuhukumiana kwa Shari´ah ya Allaah, na Imani yauongo ni kule kuhukumiana kinyume na Shari´ah.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

181

Mlango Wa 40

Mwenye Kupinga Kitu Katika Majina Na Sifa Za Allaah

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

ـن محون بالركفري مهو ◌كلتوت هليع وإلا ه ـه وإليه متابقل هو ربي لا إل

”Nao wanamkanusha Ar-Rahmaan. Sema: “Yeye Ndiye Mola wangu;Hapana ilaaha (Anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ila Yeye. Kwake natawakalina Kwake ni marejeo yangu.” (ar-Ra´d 13:30)

Katika Swahiyh al-Bukhaariy, kasema ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Waeleze209 watu kwa wanayoyajua. Je, mnataka210 Akadhibishwe Allaah naMtume Wake?”

Kapokea ´Abdur-Razzaaq kutoka kwa Ma´mar kutoka kwa Ibn Twaawuuskutoka kwa baba yake kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Ya kwamba alimuona211 mtu kasisimuka wakati aliposikia Hadiyth kutokakwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) iliotaja Sifa za Allaah akipingahilo. Akasema:212 “Ni kitu gani kinachowatia uoga watu gawa!? Wanatiliauoga Aayah zilizo wazi na wanaegamia kwa Aayah za kushabihiyana.”213

Na pindi Quraysh walipomsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) akitaja “Ar-Rahmaan”, wakapinga hilo.214 Allaah Akawateremshia:

ي مهـنو محون بالركفر

209 Wazungumzie210 Mtaridhia, mtaona raha (na hili ni khaswa pale ambapo unaowaeleza wenyewe ni wajinga aumustawa wao kielimu ni wa chini sana wa unayowaeleza)211 Yaani yeye Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa)212 Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa)213 Aayah za Muhkam na Aayah za Mutashaabih214 Sifa hii Tukufu ya Allaah (Ta´ala)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

182

”Nao wanamkanusha Ar-Rahmaan.” (ar-Ra´d 13:30)

Ufafanuzi:Tawhiyd kama inavyojulikana imegawanyika vigawanyo vitatu:

1. Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah.

Ni kumpwekesha Allaah (´Azza wa Jalla) kwa Matendo Yake; Kuumba, Kuruzuku,Kuhuisha, Kufisha na Kuendesha ulimwengu.

2. Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.

Kumpwekesha Allaah (Subhaanahu) kwa matendo ya waja ambayo wanajikurubisha kwayoKwake kwa yale Aliyowawekea katika Shari´ah.

3. Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat.

Kumthibitishia Allaah yale Aliyojithibitishia Nafsi Yake, au akamthibitishia Mtume Wake(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Majina na Sifa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kataja kuwana Majina mengi katika Kitabu Chake. Na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayh wa sallam)kamthibitishia kuwa na Majina mengi. Na katika kila jina kunatolewa Sifa ya Allaah(Subhaanahu wa Ta´ala). Hivyo ni lazima kuthibitisha Tawhiyd kwa aina zake zote tatu.

Aina ya kwanza Tawhiyd haikupinga kiumbe yeyote isipokuwa tu mfanya kiburi na mkaidakama Fir´awn, Mu´attwilah. Na watu hawa wanakubali hili ndani ya nafsi zao isipokuwa tuwanalikanusha kwa uinje. Ama aina ya pili wamelikanusha na kulipinga viumbe wengi. Nakwa ajili hii Allaah (Ta´ala) Katuma Mitume na Kateremsha vitabu kwa ajili ya Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ili wawaamrishe viumbe kumuabudu Allaah Pekee Mmoja asiyekuwa namshirika na kumtakasia ´Ibaadah. Wawaamrishe Tawhiyd na wawakataze na Shirki.

Ama aina ya tatu wameipinga Ahl-udh-Dhwalaal; katika Jahmiyyah, Mu´tazilah,Ashaa´irah, Maaturiydiyyah na waliowafuata katika kupinga Majina na Sifa za Allaah, aukupinga Sifa za kukubali Jina, au kupinga Majina na kukubali baadhi ya Sifa kamawalivofanya Ashaa´irah. Wametofautiana kwa hili lakini kwa jumla ni kwamba wamepingahili ima baadhi ya Sifa au zote. Na watu hawa wanaopinga Majina na Sifa za Allaah, wakona watangu wao waliotangulia katika washirikina kama itavyokuja huko mbele.

Aayah ya Suurat ar-Ra´d: Hapa ilikuwa wakati wa suluhu ya Hudaybiyah, Mtumeakamuamrisha ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) aandike “Bismillaahi, Ar-Rahmaan Ar-Rahiym.” Washirikina wakasema: “Ama Ar-Rahmaan hatulijui”, andika badala yake:

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

183

“Bismika Allaahumma.” Wakapinga Jina la Ar-Rahmaan ndipo Allaah Akateremsha Aayahhii.

Hali kadhalika Makkah kabla ya Hijrah, mwanzoni mwa Utume wakati Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaswali usiku wanakuja baadhi ya makafiri nakusikiliza Swalah na Qur-aan yake, wakamsikia anasema: “Yaa Allaah! Yaa Ar-Rahmaan”.Wakasema: “Mtazame huyu! Anadai kuwa ana Mola Mmoja ilihali anaomba miungu miwili,anasema: “Allaah! Ar-Rahmaan”. Allaah Akawa Ameteremsha:

ـن محوا الرعأو اد وا اللـهعقل اد أيا ما تدعوا فله الأسماء الحسنى◌

”Sema; “Iteni (mwombeni kwa jina la) Allaah au iteni (mwombeni kwa Jina la) Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah). Vyovyote mtakavyoita (au kuomba) basi Yeye Ana Al-Asmaaul-Husnaa (Majina Mazuri).” (al-Israa 17:110)

Kwa hivyo yule mtu ambaye atajinasibisha na Uislamu akapinga Majina na Sifa za Allaah,basi huyo anajifananisha na washirikina (makafiri) ambao walipinga baadhi yake. AllaahAna Majina mengi, hakuna ayajuae yote isipokuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Sio Jina limoja,mawili mia, hapana. Ni mengi sana. Na katika kila Jina hutolewa humo Sifa inayooneshaUkamilifu Wake (Subhaanahu wa Ta´ala).

Hadiyth ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu): Hapa ilikuwa pindi kulikithiri wapiga visa nawatoa mawaidha, walikuwa wakitegemea visa na stori na hadisi ambazo haziwaingii watuakilini. Ndio kiongozi wa waumini akawa amewaambia namna hii. Na visa vinakuwa kwaKitabu na Sunnah na haviwi kwa kutunga na mambo ya kipuuzi watu wakaja kuyapinga.Hapa kuna mafunzo ya mtu kuongea na watu kwa kiwango chao kielimu.

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anumaa): Hapa ilikuwa wakati alikuwa anawahadithiawanafunzi wake kuhusiana na Majina na Sifa za Allaah. Kwa kuwa Aayah zinazozungumziaMajina na Sifa za Allaah ni Muhkam na sio Mutashaabih kama wanavyodai wapotevu.Wanaacha za Muhkam na kuchukua za Mutashaabih. Hapa kuna Radd kwa wale wanaojaaliaMajina na Sifa za Allaah ni katika Aayah za Mutashaabih ili tu kutaka kupinga maana yakehata kama watakubali lafdhi yake. Nukta muhimu hapa ni kwamba Majina na Sifa za Allaahsio katika Mutashaabih, bali ni katika Muhkam zilizo wazi.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Yeyote anayekanusha kitu katika Majina na Sifa hana Imani.215

215 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hili ni kwa sababu Allaah Kasema: ”Nao wanamkanusha Ar-Rahmaan.” (ar-Ra´d 13:30) Hii ni dalili ya kwamba kukanusha Majina na Sifa za Allaah ni katikakufuru.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

184

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat ar-Ra´d. (13:30)

3. Mtu aache kuelezea (kuhadithia) yale asiyoyafahamu msikilizaji.

4. Kutajwa sababu gani, ya kwamba hili litapelekea kukadhibishwa Allaah na Mtume Wake(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kama hakukusudia hivyo mpingaji.216

5. Onyo ya ´Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa yule mwenye kukanusha kitukatika Majina na Sifa za Allaah na kwamba ameangamia.

216 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa kuna funzo, usizungumze na ´Awwaam kamaunavyozungumza na wanachuoni, na usizungumze na wanachuoni kama unavyozungumza na´Awwaam. Kila mmoja kwa kiwango chake. Hii ndio njia sahihi.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

185

Mlango Wa 41

Kauli Ya Allaah Ta´ala

يعرفون نعمت اللـه ثم ينكرونها وأكثرهم الكافرون

”Wanazielewa neema za Allaah, kisha wanazikanusha; na wengi wao nimakafiri.” (an-Nahl 16:83)

Mujaahid anasema kuhusu maana yake:

“Ni mtu kusema: “Mali hii ni yangu. Nimeirithi kutoka kwa wazazi wangu.”

´Awn bin ´Abdillaah anasema:217

“Lau bila ya fulani nisingelikuwa hivi na hivi.”

Ibn Qutaybah anasema:

“Wanasema haya ni kutokana na baraka za maombezi ya waungu wetu.”

Baada ya Hadiyth ya Zayd bin Khaalid218 ambayo ndani yake kuna: “Katikaasubuhi hii kuna baadhi ya waja Wangu waliobakia kuwa waumini wa kwelina wengine makafiri... ” Abdul-´Abbaas (Ibn Taymiyyah) kasema:

“Na haya yamekuja sehemu nyingi katika Kitabu na Sunnah. Allaah(Subhaanahu) Anawalaumu wale ambao wanazinasibisha neema Zake kwaasiyekuwa Yeye na wanamshirikisha.”

Wamesema baadhi ya Salaf ni kwa mfano kusema:

“Upepo ulikuwa mzuri”219, “Huyu baharia alikuwa na hekima na uzoefu.” Namfano wa maneno kama hayo ambayo hupitikia kwenye ndimi za watuwengi.

217 Kuhusu maana ya Kauli ya Allaah (Ta´ala) hapo juu218 Ukurasa wa

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

186

Ufafanuzi:Suurah hii (al-An´aam) Allaah Kataja neema Zake nyingi na ndio maana ikaitwa “Suurah yaneema”. La wajibu ni mtu kunasibisha neema alizonazo kwa Allaah hili ni katika Tawhiyd.Kwa kuwa neema zote ni za Allaah. Na kunasibisha neema kwa mwingine badala Yake, hilini katika Shirki. Ndio maana Shaykh kaweka mlango huu.

Mujaahid ni katika wanafunzi wakubwa wa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).Kasema maana yake ni kusema “hii ni mali yangu”. Allaah Anapompa neema hamshukuruAllaah (´Azza wa Jalla) na badala yake anasema “hii ni mali yangu”, badala ya kusema ni yaAllaha. Kisha anainasibisha kwa baba zake na kukanusha neema ya Allaah (´Azza wa Jalla)na hili ni katika Shirki.

´Awn bin ´Abdillaah ni katika Taabi´iyn na baba yake ni Swahabah. Anasema maana yake ni“lau bila ya fulani nisingelikuwa hivi”, badala ya kumshukuru Allaah (´Azza wa Jalla). Bilaya fulani nisingelipata kazi hii, neema hii, mali hii na kadhalika. Anainasibisha neema hiyokwa kiumbe. Huku ni kumkufuru Allaah (Ta´ala).

Ibn Qutaybah: Wananasibisha neema za Allaah kwa waungu wao ambao wanawaabudubadala ya Allaah, katika maiti, makaburi, watu wema, mawalii na waungu wao wengine. Nahili pia ni katika Shirki.

Baadhi ya Salaf wamesema: “Upepo ulikuwa mzuri”, yaani hapa ni pindi wanapookoka nakuzama baharini hawanasibishi hili kwa Allaah badala yake wananasibisha hili kwa upepoambao unasukuma safina, kwa kuwa wakati huo safini ilikuwa inapelekwa na upepo. Hatasasa kuna ambao wanafanya hivi. Baada ya kuokoka na kusalimika, badala ya kumshukuruAllaah kwa kusema “Alhamdulillaah” wanasema “hii ni kwa sababu ya upepo ambaoumesukuma safina ulikuwa mzuri na wenye nguvu na mwendeshaji safina alikuwa hodarisana.” Ni kweli kwamba upepo ni sababu, lakini fadhila ni za Allaah (´Azza wa Jalla). Hukuni kukufuru neema. Hivyo ni wajibu kuinasibisha kila neema kwa Allaah (´Azza wa Jalla) nakumshukuru Allaah kwayo na wala haijuzu kuinasibisha kwa viumbe.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya uelewa wa neema na kuipinga.

219 Au maneno kama hayo; kama kusema ”Upepo umeleta kheri”, ”Upepo umesababisha hivi... ”,”Upepo umefanya hivi” na kadhalika

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

187

2. Hili hupitika katika ndimi za watu wengi (kunasibisha neeam kwa asiyekuwa Allaah).

3. Maneno haya kuitwa (na Allaah) kuwa ni kukanusha (kukufuru) neema.

4. Mambo mawili yanayokwenda kinyume kukutana moyoni.220

220 Shaykh Fawzaan anasema: ”Mambo hayo mawili ni: ”Wanazielewa neema za Allaah, kishawanazikanusha.” (16:83)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

188

Mlango Wa 42

Kauli Ya Allaah Ta´ala

فلا تجعلوا للـه أندادا وأنتم تعلمون

“Basi msimuwekee Allaah waliolingana naye (washirika) na hali ya kuwanyinyi mnajua (kuwa Allaah Hana Anayelingana nae).” (al-Baqarah 02:22)

Kasema Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kuhusu Aayah hii:

“al-Andaad (washirika) ina maana ya Shirki. Ni yenye kujificha zaidi kulikomdudu mchungu apitae juu ya jiwe jeusi katika usiku wa giza. Nako nikusema: “Kwa Jina la Allaah221 na kwa uhai wako ewe fulani.” Na kusema:“Na kwa uhai wangu.”222 Na kusema: “Lau si kijibwa hichi mwiziangelitujia.”, “Na lau si bata ya nyumbani wezi wangelitujia.”, na kauli ya mtukumwambia mwenzake: “Akipenda Allaah na wewe.”223, na kauli ya mtu:“Lau si Allaah na fulani.” Usimtaje Allaah na mwengine yeyote kwa kuwayote haya ni Shirki.”

(Kaipokea Ibn Abiy Haaatim)

´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwambaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah amekufuru au kushiriki.”

(Kaipokea at-Tirmidhiy kaisahihisha na al-Haakim kasema kuwa ni Hasan)

Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Kuapa kwa Allaah hali ya kuwa ni mwenye kudanganya, inanipendeza zaidikwangu kuliko kuapa kwa asiyekuwa Allaah hali ya kuwa ni mwenyekusema ukweli.”

221 Wallaahi222 Wahayaatiy223 Mashaa Allaah wa shi-it

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

189

Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea kutoka kwa Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) ya kuwa kasema:

“Msiseme: “Akipenda Allaah na fulani”, lakini semeni: “Akipenda Allaahkisha224 akapenda fulani.”

(Kaipokea Abuu Daawuud kwa isnadi Swahiyh)

Imekuja kutoka kwa Ibraahiym Nakhaiy ya kwamba alikuwa akichukia mtukusema:

“Najikinga kwa Allaah na kwako”, lakini inajuzu kusema: “Najikinga kwaAllaah kisha kwako.” Akasema: “Sema: “Lau si kwa ajili ya Allaah kishafulani” na wala usiseme: “Lau si kwa ajili ya Allaah na fulani.”

Ufafanuzi:Aayah ya Suurat al-Baqarah: Huu ndio wito wa kwanza katika msahafu, Mola wawalimwengu Kuwanadi watu wote na Kuwaamrisha wamuabudu kwa kuwa AllaahKawaumba ili wamuabudu. Kama Alivyosema:

وندبعيإلا ل الإنسو الجن لقتا خمو

”Na Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu.” (adh-Dhaariyaat 51: 52)

´Ibaadah ni neno lililokusanya kila Anachokipenda Allaah na Kukiridhia, katika matendo namaneno sawa yaliyo dhahiri na yaliyojificha. Ni mambo yote anayojikurubisha kiumbe kwaMola Wake au kwa viumbe wengine. Allaah Kawaumba watu kwa lengo hili. Hakuwaumbaili wamnufaishe au wamruzuku, hapana. Kawaumba ili wamuabudu na maslahi yanarudikwa kiumbe mwenyewe. Ama mwenye kumuabudu asiyekuwa Allaah, katoka katikaUislamu na kuwa mshirikina. Aayah hii imeteremka kuhusu Shirki kubwa, na Ibn ´Abbaas(Radhiya Allaahu ´anhumaa) akaitumia katika kutolea dalili Shirki ndogo, kwa kuwa Aayahhii imejumuisha Shirki kubwa na ndogo. Kuinasibisha neema ya Allaah kwa mwinginebadala Yake. Kama kusema “lau bila ya Allaah na wewe nisingelipata kitu kadhaa”, “lau bilaya Allaah na wewe nisingefikiwa na hili.” Akamfanya ni mshirika wa Allaah kwa kuletwaneema. Kwa kuwa “na” inajumuisha. Lafdhi sahihi ni kusema “lau bila ya Allaah kishawewe”, akamfanya kiumbe ni baada ya Muumba na asimfanye akawa pamoja na Allaah

224 Au halafu

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

190

katika kuleta riziki au kuzuia madhara. Ni kweli kwamba kiumbe anaweza kuwa sababu yakuzuia madhara au kuleta madhara, lakini hawi mwenye kufanya hivyo isipokuwa kwaUwezo wa Allaah (Ta´ala) Kumuweza na kumsahilishia. Hivyo inakuwa jambo hililinamrudilia Allaah (Jalla wa ´Alaa).

Hali kadhalika anapopata amani ndani ya nyumba kutokana na wezi na majambazi, asifanyehili ni kwa ajili ya mbwa au bata. Akasema “lau bila ya kijibwa hichi wezi wangelitujia”,“lau bila ya bata wazi wangelitujia”, badala yake anatakiwa kusema “lau bila ya Allaah(Subhaanahu wa Ta´ala)”. Asifanye neema yoyote chanzo ikawa ni kiumbe. Kiumbe yeye nisababu tu na mkaakati tu. Hili ni katika ukamilifu wa Tawhiyd, mtu kujiepusha na Shirkikubwa na ndogo. Shirki kubwa inamtoa mtu katika Uislamu na ndogo inaipunguzaTawhiyd. Na Shirki ndogo inaweza kuwa njia inayompelekea katika Shirki kubwa. Halikadhalika kusema “lau si Allaah na fulani”, kwa kuweka “na” ni katika shirki ya matamshi.Lau mtu ataitakidi hivi moyoni inakuwa Shirki kubwa. Kwa hivyo, lafdhi sahihi inatakiwakusema “lau bila ya Allaah”, au kusema ”lau bila ya Allaah kisha filani... ” kwa kuongezea“kisha”. Ama ukisema “na” inakuwa Shirki katika matamshi (Shirki ndogo) isipokuwa tukama mtu ataitakidi hilo moyoni ndio inakuwa Shirki kubwa.

Miongoni mwa Shirki ndogo ni kuapa kwa asiyekuwa Allaah, kwa kuwa kuapa nikumuadhimisha yule unayemuapia. Na kuadhimishwa inakuwa kwa Allaah Pekee. Hivyo,akiadhimishwa kiumbe kashrikishwa pamoja na Allaah. Haijuzu kuapa kwa asiyekuwaAllaah kwani hili ni katika aina ya Shirki ndogo. Sawa awe Mtume wala mwingine yeyote,kamwe haijuzu kuapa kwa asiyekuwa Allaah (Ta´ala). Na watu wengi leo wanaapa kwaasiyekuwa Allaah na khaswa kwa kusema “Bin-Nabiy” (naapa kwa Mtume), “Hayaatiy”(wewe ndiye maisha yangu), yote haya ni katika Shirki. Ni juu ya Muislamu ajifunzeTawhiyd, aifunze wengine na awabainishie, aijali na kuichunga ´Aqiydah yake. Huu ndiowajibu wa wanafunzi kuwafunza watu na wasiwaache katika ujinga wao na Shirki.

Kauli ya Ibn Mas´uud, kasema hivi kwa kuwa kuapa kwa asiyekuwa Allaah ni Shirki, nakuapa kwa Allaah hali ya kuwa ni mwenye kudanganya ni dhambi kubwa katika madhambimakubwa. Kwa kuwa Shirki Haisamehi Allaah. Ama dhambi kubwa Akipenda AllaahAtamsamehe mwenye nayo na Akipenda Atamuadhibu lakini hatomdumisha Motoni milele.Hii ni Fiqh ya Ibn Mas´uud. Ni juu ya Muislamu kujiepusha na matamshi sampuli yote hii.

Kwa hiyo, ni wajibu kwa Muislamu ajifunze mambo haya, aihifadhi ´Aqiydah yake. Nahaitakiwi kwa mtu kuchukulia sahali na kusema hii ni Shirki ndogo haidhuru na mfano wahayo, Shirki ndogo ni kubwa kuliko madhambi makubwa ambayo yako chini ya Shirki.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya neno al-Andaad (washirika) katika Suurat al-Baqarah. (02:22)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

191

2. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakitumia kuzifasiri Aayahzilizoteremka juu ya Shirki kubwa katika Shirki ndogo.

3. Kuapa kwa asiyekuwa ni Shirki.

4. Kuapa kwa asiyekuwa Allaah hali ya kuwa mtu ni mkweli ni jambo kubwa kuliko kuapakwa Allaah ilihali mtu anadanganya.

5. Tofauti kati ya wa (na) na thummah (kisha/halafu).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

192

Mlango Wa 43

Yaliyokuja Kuhusu Yule Ambaye Hakuridhika Kuapa Kwa Allaah

Kutoka wa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kapokea ya kwambaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Msiape kwa baba zenu. Atakayeapa kwa Allaah basi na aseme kweli. Naatakayeapiwa kwa Allaah na aridhie, na yule ambaye hakuridhia sio katikaAllaah.”225

(Kaipokea Ibn Maajah kwa isnadi Hasan)

Ufafanuzi:Kama jinsi ni wajibu kutoapa kwa mwingine zaidi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), vilevile inatakiwa kwa mwenye kuapa kukinaika na kuridhia kwa Allaah Pekee na asiwe namashaka. Na huku ni katika kumuadhimisha Allaah pia mtu akakinai kuapa kwa Allaah. Nakutokinai kuapa kwa Allaah (´Azza wa Jalal) Pekee, huku ni kutomuadhimisha Allaah(Subhaanahu wa Ta´ala).

Hadiyth ya Ibn ´Umar: Ilikuwa ni katika ada za watu wa watu wa wakati wao kuapa kwababa zao, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa amewakataza hili. Haijuzukuapa kwa asiyekuwa Allaah sawa awe ni kiumbe yeyote yule. Kataja baba kwa kuwa ndoilikuwa katika ada yao. Atakayeapa kwa Allaah basi aseme kweli, haijuzu kuapa kwa Allaahna kusema uongo. Kwa kuwa hili, kwanza kusema uongo ni haramu, na isitoshe nikutoithamini haki ya Allaah (´Azza wa Jalla). Na katika sifa ya wanafiki ni kwambawanaapa kwa kusema uongo nao wanajua. Na atakayeapiwa kwa Allaah basi aridhie, nayule asiyeridhia basi huyo Allaah Kajiweka nae mbali. Na haya ni matishio makubwayanayoonesha mtu anatakiwa aridhie anapoapiwa Allaah na uharamisho wa kutokinaika.Yule ambaye hakuridhia kuapiwa kwa Allaah na akataka aapiwe wengine badala ya Allaah,basi Allaah Kajiweka mbali na mtu huyu.

225 Allaah Anajiweka nae mbali kabisa.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

193

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Makatazo ya kuapa kwa mababa.

2. Maamrisho ya yule anayeapiwa kwa Allaah aridhie.

3. Adhabu ya yule asiyeridhia (kwa kuapiwa kwa Allaah).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

194

Mlango Wa 44

Kauli “Akipenda Allaah Na Wewe”

Kutoka kwa Qutaylah kapokea:

“Myahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema:“Hakika nyinyi mnafanya Shirki pindi mnaposema: “Akipenda Allaah naukipenda wewe”, na mnasema: “Naapa kwa al-Ka´abah.” Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) akawa amewaamrisha226 wanapotaka kuapawaseme: “Naapa kwa Mola227 wa al-Ka´abah” na waseme: “Akipenda Allaahkisha wewe.”

(Kaipokea an-Nasaa´iy na kaisahihisha)

an-Nasaa´iy kapokea pia Hadiyth kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu´anhumaa):

“Kuna mtu alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):“Akipenda Allaah na ukapenda wewe.” Akasema: “Umenifanya mimi kuwamshirika wa Allaah?” Watakiwa kusema: “Akipenda Allaah Pekee.”

Ibn Maajah kapokea kutoka kwa Twufayl ambaye ni kaka wa ´Aaishah(Radhiya Allaahu ´anha) kwa upande wa mama yake, kasema:

“Nimeona ndotoni ambapo niliwapitia kundi la Mayahudi na kuwaambia:“Nyinyi ni watu wazuri ikiwa hamtodai ya kwamba ´Uzayr228 ni mwana waAllaah.” Wakasema: “Nanyi ni watu wazuri pia ikiwa hamtosema: “AkipendaAllaah na akapenda Muhammad.” Baada ya hapo, nikawapitia kundi katikaManaswara na kuwaambia: “Nyinyi ni watu wazuri ikiwa hamtodai yakwamba al-Masiyh (´Iysa bin Maryam) ni mwana wa Allaah.” Wakasema:“Nanyi ni watu wazuri pia ikiwa hamtosema: “Akipenda Allaah na akapenda

226 Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum ajmaa´iyn)227 Muumbaji228 Shaykh Fawzaan anasema: ”´Uzayr kuna wanachuoni ambao wamesema kuwa ni katika Mitumewao, na wengine wakasema ni katika watu wema wanachuoni wao. Wakapindukia kwa ´Uzayrmpaka wakafikia kusema kuwa ni mwana wa Allaah. Katakasika Allaah na wayasemayo.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

195

Muhammad.” Kulipopambazuka, nikamweleza niliyemweleza, kishanikampitia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumueleza.Akasema: “Je, umemweleza hili yeyote?” Akasema: “Ndio.” AkamhimidiAllaah na kumshukuru229 kisha akasema “amma ba´ad, hakika Twufayl kaonandoto na kishamweleza aliyemweleza. Hakika nyinyi mlikuwa mkisemamaneno kadhaa na kadhaa ambayo yalikuwa yakinitatiza nikawa nashindwakuwakataza nayo, hivyo msiseme: “Akipenda Allaah na akapendaMuhammad”, lakini semeni: “Akipenda Allaah Pekee.”

Ufafanuzi:Hali kadhalika miongoni mwa Shirki ndogo ni Shirki katika matamshi, mtu kusema“akipenda Allaah na wewe”. Kwa kuwa “na” inajumuisha mashirikiano. Mtu akisema“akipenda Allaah na wewe” kamfanya kiumbe ni mshirika pamoja na Allaah hata kama mtuatakuwa hakukusudia hivo. Ni kweli kwamba mtu ana matakwa, lakini yasijumuishwepamoja na Matakwa ya Allaah kwa kuweka “na”, isipokuwa mtu anaweza kuweka “kisha”,kwa kuwa kisha inakuja kwa mpangilio tofauti “na” ambayo inakuja kwa mashirikiano nandio maana ikakatazwa.

Hadiyth ya Qutaybah ambaye ni Swahabah mwanamke, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) kakubali haki hata kama imetoka kwa myahudi na hakumkadhibisha. Hii ni dalili yakuwa Muislamu anatakiwa kukubali haki kutoka kwa yeyote ambaye amekuja nayo hatakama atakuwa ni adui. Ni dalili ioneshayo ya kwamba haijuzu kusema “akipenda Allaah nawewe”, kwa kusema “na”, bali inatakiwa kuweka “kisha” – kama tulivofafanua hapo juu.Hali kadhalika Ka´abah haijuzu kuiapia hata kama ni Nyumba ya Allaah (´Azza wa Jalla),kwani haijuzu kuapia kiumbe chochote kile. Haijuzu kuiadhimisha Ka´abah kamaAnavyoadhimishwa Allaah (´Azza wa Jalla) na wala haijuzu kutabaruku kwa Ka´abah. Kulekuswali kwenye Ka´abah, kutufu na mengineyo yote yanayofanywa kwenye Ka´abah siokwa ajili ya Ka´abah, bali anafanyiwa Allaah (´Azza wa Jalla).

Hadiyth ya Twufayl: Baada ya kuwaambia aibu yao, nao wakaona watafute aibu yaWaislamu, na wakawa hawakupata isipokuwa kosa hili tu dogo. Wao wanatafuta aibu zawengine hata kama itakuwa ndogo na wala hawatazami aibu yao hata kama itakuwa nikubwa ya kumnasibishia Allaah mwana. Na namna hii ndivo anavyokuwa mtu anayefuata

229 Shaykh Fawzaan anasema: “Hii ni kama ada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindialipokuwa anataka kufundisha au kutanabahisha au kuamrisha kitu, anaanza kwa kumshukuruAllaah na kumsifu.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

196

matamanio ya nafsi yake, mtu namna hii huwa hatazami aibu zake isipokuwa yeye badalayake hujishughulisha kutafuta aibu za wengine. Ni kweli kwamba Muhammad (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) na mja mwingine yeyote huwa na matakwa, lakini matakwa yaohayashirikiani na Matakwa ya Allaah, bali matakwa ya waja huja baada ya Matakwa yaAllaah kwa kuweka “kisha”. Kama Alivyosema (Jalla wa ´Alaa):

إلا أن يشاء اللـه رب العالمنيوما تشاءون

”Na hamtotaka isipokuwa Atakaye Allaah Mola wa walimwengu.” (at-Takwiyr 81:29)

Hii ndio Tawhiyd na Ikhlaasw. Neno hili ni kosa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)kakubali kutanabahishwa. Na namna hii muumini anatakiwa kukubali haki na nasaha hatakama itakuwa imetoka kwa adui. Asiwe na kiburi ya kukubali haki.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Utambuzi wa mayahudi wa Shirki ndogo.230

2. Kumfahamu mtu ikiwa yuko na hawaa (matamanio).231

3. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Je, umenifanya mimi kuwa ni mshirikawa Allaah?” Vipi kwa mwenye kusema:

“Ewe mbora wa viumbe, sina mwingine ninayeomba kinga kwake wakati wa dhiki zaidiyako.”232

4. Hili sio katika Shirki kubwa kutokana na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):“Mlikuwa mkisema maneno kadhaa na kadhaa ambayo yalikuwa yakinitatiza nikawanashindwa kuwakataza nayo”233

230 Shaykh Fawzaan anasema: ”Mayahudi ni wanachuoni kwa kuwa wamepewa Kitabu. Lakinihawakifanyii kazi na ndio maana wamelaaniwa. Allaah Atukinge. Wanajua Shirki ndogo lakinipamoja na hivyo wametumbikia katika Shirki kubwa. Allaah Atukinge”231 Shaykh anasema tena: ”Mayahudi na manaswara wameona kosa hili lidogo kwa Waislamu nawakasahau wanayoyafanya, wanayoyasema na wanayoyaitakidi katika kufuru ya wazi na Shirkikubwa. Kwa kuwa matamanio yao kuwachukia Waislamu na kuwabughudhi, haya ndio yamefanyakuona (kutafuta) kosa hili lidogo kwa Waislamu. Pamoja na hivo, hili ni kwa maslahi ya Waislamu.”232 Shaykh anasema tena: “Kukilinganishwa matamshi hayo aliyoyakemea Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) na Suufiyyah wanaopindukia mipaka kwake leo kukiwemo shairi hili la Burdaa laal-Buswiriy. Anasema: “Ikiwa hukunisaidia Aakhirah basi nimeangamia.” Yaani kamsahau Allaah(Subhaanahu wa Ta´ala) na kumuomba Mtume? Huku ndio kupindukia mipaka kabisa. Huyukapindukia mipaka zaidi kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zaidi hata yamanaswara walivyopindukia mipaka kwa ´Iysa. Tunamuomba Allaah afya.”233 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hii ni dalili kuonesha kuwa ni Shirki ndogo. Kwani lau ingekuwa niShirki kubwa, asingeliinyamazia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusita kulikataza.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

197

5. Ndoto njema (nzuri) ni aina (sehemu) ya Wahyi.

6. Ndoto nje inaweza kuwa sababu ya kuwekea baadhi ya hukumu katika Shari´ah.234

Pamoja na hivyo hakuliacha bali alilikataza na kukubali haki kutoka kwa maadui ambao ni mayahudina manaswara.”234 Shaykh anasema tena: ”Ni kama mfano wa ndoto hii (ya Twufayl). Imekuwa ni sababu kwa Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kukataza matamshi haya kwa sababu ya ndoto hii. Na ndoto hiyo– hata kama ni njema (nzuri) inapaswa kukubaliwa na Mtume kwanza, ama ambayo haikukubaliwana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haiweza kuwekea hukumu katika Shari´ah, kwa kuwaShari´ah inathibiti kwa Wahyi na wala hakuna Wahyi baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam).”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

198

Mlango Wa 45

Mwenye Kutukana Zama Kamtukana Allaah

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

رها إلا الدكنلها يما ويحنو وتما نينا الدناتيإلا ح يا هقالوا مو وما لهم بذلك من علم◌

”Na wakasema: “Haya sisi chochote isipokuwa ni maisha yetu dunia,tunakufa na tunahuika, na hakuna cha kutuangamiza isipokuwa dahari.” Nawala hawana kwayo ujuzi wowote.” (al-Jaathiyah 45:24)

Katika Swahiyh (al-Bukhaariy) kapokea Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu´anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: “AllaahKasema:

“Ananiudhi binaadamu kwa kutukana ad-Dahr235 ilihali na Mimi Ndiye Ad-Dahr. Nageuza usiku na mchana.” Na katika upokezi mwingine: “Msitukanead-Dahr kwani hakika ya Allaah Ndiye Ad-Dahr.”

Ufafanuzi:Hakika ya ´Aqiydah ya Tawhiyd inatakiwa kuyanasibisha mambo kwa Allaah (Subhaanahuwa Ta´ala), kwa kuwa Yeye Ndiye Mwendesha ulimwengu huu na Mola Wake naAliyeviumba. Hana mshirika katika hilo. Na hii ndio Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Nayo nikumpwekesha Allaah kwa Matendo Yake. Na mingoni mwa Shirki katika Rubuubiyyah, nikuyanasibisha mambo kwa zama, usiku na mchana. Zama ni kiumbe katika viumbe vyaAllaah. Hupitisha (Subhaanahu wa Ta´ala) humo Akitakacho, katika usiku na mchana. Nasio zama yenyewe inayopitisha mambo haya, isipokuwa Anayepitisha mambo humo niAllaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ndio maana ya kauli yake Shaykh. Kutukana zama nikumtukana Allaah. Kwa nini? Kwa kuwa zama imeumbwa, na yenyewe haina juu yakelolote katika maamuzi. Yule anayetukana yanayopitika humo katika mambo ambayo

235 Zama

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

199

yanamuudhi, huyu anamtukana Allaah na kumponda Mola (Subhaanahu wa Ta´ala). Nikumponda na kumtukana Mola (´Azza wa Jalla). Kwa kuwa Yeye Ndiye Mtendaji naMwendeshaji.

Aayah ya Suurat al-Jaathiyyah: Dahriyyah wamegawanyika sehemu nne:

1. Dahriyyah Malaahidah. Hawa ni wale ambao hawaamini kuwepo kwa Muumba(Subhaanahu wa Ta´ala) na wanayanasibisha mambo kwamba yanafanyika nakutendeka kimaumbile. Wanakanusha kuwepo kwa Allaah na uendeshaji Wake waulimwengu. Hawa ndio Malaahidah, katika wanafalsafa na wengine.

2. Baadhi ya washirikina wa kiarabu. Hawa ni wale wanaopinga kufufuliwa.Wanamuamini Allaah, na kuwa Yeye Ndiye Mwendeshaji, Muumba, MwenyeKuruzuku, Mwenye Kufisha na Kuhuisha. Wanamuamini, lakini wanapingakufufuliwa. Kwa kuwa wanaona kuwa maiti baada ya kufa ni jambo lisilowezekanakuweza kufufuliwa tena mara ya pili. Hawa ndio ambao Allaah Kawakusudia katikaAayah hapo juu. Wanapinga hakuna maisha mengine baada ya haya, si Pepo walaMoto.

3. Wanaomuamini Allaah na kufufuliwa, lakini ananasibisha mambo mabaya (yakuudhi) kwa zama na kuilaumu. Na hii ni aina katika Shirki. Kwa kuwa kamjaaliaAllaah mshirika katika uendeshaji. Ni aina katika Shirki.

4. Wanamuamini Allaah, kufufuliwa na anaamini mambo yako Mikononi mwa Allaah(´Azza wa Jalla), lakini anailaumu zama kwa njia ya kutukana. Huyu anamuudhiAllaah (Subhaanahu wa Ta´ala) lakini sio Shirki. Yule mwenye kutukana zamaKamtukana Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Je, katika Majina ya Allaah ni Ad-Dahr? Hapana sio katika Majina ya Allaah. Bali maanayake – ni kama ilivokuja katika Hadiyth:

“Anaitukana ad-Dahr ilihali na Mimi Ndiye Ad-Dahr. Nageuza usiku na mchana.”

Maana ya “Mimi Ndiye ad-Dahr ni kwamba Allaah Ndiye Mwendeshaji na Yeye NdiyeAnageuza usiku na mchana. Zama inaendeshwa. Hivyo inatakiwa Muislamu kuwa naadabu na achunge ulimi wake kwa maneno kama haya na wala asitukane zama kamwe.Ama Kauli ya Allaah (Ta´ala):

إنا أرسلنا عليهم رحيا صرصرا في يوم نحس مستمر

”Hakika Sisi Tumewapelekea upepo wa dhoruba wenye sauti kali katika siku ya nuksiinayoendelea.” (al-Qamar 54:19)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

200

Huku sio kutukana zama, isipokuwa ni kuisifu zama. Katika zama kunakuwa na mambomagumu na kunakuwa na mambo rahisi. Mtu atofautishe baina ya kuisifia siku nakuilaumu. Ni mambo mawili tofauti.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Makatazo ya kutukana zama.

2. Kuita kuwa kufanya hivyo ni kumuudhi Allaah.

3. Taamuli ya Kauli Yake (Ta´ala): “Kwani hakika ya Allaah Ndiye Ad-Dahr.”

4. Wakati mwingine inaweza kuwa kutukana hata kama mtu hakuitakidi hivyo moyonimwake.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

201

Mlango Wa 46

Kuitwa Qaadhi Wa Maqaadhi Na Mfano Wake

Katika Swahiyh (al-Bukhaariy na Muslim) kutoka kwa Abuu Hurayrah(Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) kuwa kasema:

“Jina linalochukizwa sana236 kwa Allaah ni mtu kujiita al-Malik al-Amlaak.237

Hakika hakuna Maalik isipokuwa Allaah.”

Sufyaan (bin ´Uyaynah) kasema: “Mfano wake ni kama mtu kujiitaShahaanshah.”238

Katika upokezi mwingine:

“Mtu atakayekasirikiwa na Allaah sana siku ya Qiyaamah na kuonekanamchafu ni yule aliyejiita kwa jina hilo.”

Na neno lake Akhnaa´ yaani aliyedharauliwa sana.

Ufafanuzi:Katika ukamilifu wa Tawhiyd ni mtu kunyenyekea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).Kwa kuwa kuwa na kiburi na kujiweka juu ni vya Allaah Pekee. Na Ufalme ni wa AllaahPekee. Na waja hawamiliki chochote isipokuwa kile Alichowamilikisha Allaah (´Azza waJalla). Ni wajibu kwa waja wajiweke chini na kunyenyekea mbele ya Allaah (´Azza wa Jalla).Allaah Akiwapa ufalme, elimu, mali na jaha wanyenyekee Kwake (´Azza wa Jalla). Kwakuwa yeye ni mja daima vovyote awavyo ni mja na dhaifu. Hii ndio sifa ya mja kwa MolaWake. Na yule mwenye kujiweka chini, Allaah Humnyanyua. Kuwa na kiburi na kujiweka

236 Jina baya zaidi237 Mfalme wa wafalme238 Shaykh Fawzaan anasema: ”Jina hili hutumiwa na watu wasiokuwa waarabu, na maana yake nimfalme wa wafalme. Kila neno lenye kuleta maana kama hii sawa kwa lugha yoyote ni lenyekulaumiwa.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

202

juu ni vya Allaah Pekee na Ufalme ni wa Allaah Pekee na hana mshirika katika hayo. Kujiitakwa jina ambalo ndani yake kuna kujiweka juu, hili ni jambo limekatazwa na kulaumiwa.Mfano wa majina hayo ni kama hili, Qadhi wa Maqadhiy, hili ni Jina la Allaah (Subhaanahuwa Ta´ala). Yeye Ndiye Huwahukumu viumbe vyote, wafalme, maqadhi n.k. Badala yakemtu anatakiwa kusema “raisi wa maqadhi”, “mrejelewa wa maqadhi”. Na mfano wa majinakama hayo ambayo yanahusiana na kazi yake lakini hayampandishi juu hivo.

Hali kadhalika haijuzu kuijiita kwa jina la mfalme wa wafalme, mtu anaweza kusema maaliktu. Na neno mfalme limekuja katika Qur-aan katika Suurat Yuusuf. Au mfalme, kiongozi namfano wa hayo. Kwa kuwa Mfalme wa wafalme ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ufalmena umiliki wa kabisa ambao hakuna juu yake kitu ni wa Allaah Peke Yake.

تاء وشن تم زعتاء وشن تمم لكالم نزعتاء وشن تم لكي المتؤت لكالم كالم ماءقل اللـهشن تل مذ ◌ريالخ كدبي ◌يرء قديلى كل شع كإن

”Sema: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, naUnamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na UnamdhalilishaUmtakaye, Kheri imo Mikononi Mwako. Hakika Wewe ni Qadiyrwa kila kitu. (Muwezadaima).” (al-´Imraan 03:26)

Na Siku ya Qiyaamah Allaah Atajiita kuwa ni Maalik (Mfalme).

موالي لكن الممل

“Ufalme ni wa nani leo?” (Ghaafir 40:16)

Hakuna mtu hata mmoja atakayejibu.

Kisha Atasema Allaah (Jalla wa ´Alaa) Akijijibu Mwenyewe:

للـه الواحد القهار

“Ni wa Allaah Pekee Al-Waahidil-Qahhaar (Mmoja Pekee - Mshindi Mwenye kudhibiti nakudhalilisha).” (Ghaafir 40:16)

Ama ufalme wa mtu ni wa mipaka, pamoja na hivyo ni wa Allaah.

تؤتي الملك من تشاء وتنزع الملك ممن تشاء وتعز من تشاء وتذل من تشاء ◌ريالخ كدبي

”Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na UnamtukuzaUmtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, Kheri imo Mikononi Mwako.” (al-´Imraan 03:26)

Ni wajibu kujiepusha na matamshi kama haya ambayo yanamfanya mtu kuwa na kiburi.Hata kama mtu mwenyewe yeye hakujiita hivyo, asiridhie yeye akaitwa hivyo bali akataze.Huku ni kunyenyekea kwa Allaah (´Azza wa Jalla).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

203

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Makatazo ya kujiita Mfalme wa wafalme.

2. Makatazo yake mfano wake (kumwita mwingine yeyote) ni kama alivyosema Sufyaan.239

3. Uelewa wa uzito (wa makatazo) yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mfano wakelicha ya kwamba mtu hakukusudia hilo moyoni mwake.

4. Uelewa ya kuwa (makatazo ya jambo hili) ni kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu).

239 Shaykh Fawzaan anasema: ”Mfano wake ni kama alivyosema Sufyaan, ni kila jina ambalo ndaniyake kuna kujiweka juu, kiburi na kujifakhari ni wajibu kuliacha.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

204

Mlango Wa 47

Kuheshimu Majina Ya Allaah Ta´ala Na Kubadili Jina Kwa Ajili Ya Hilo 240

Abuu Shurayh kapokea:

“Ya kwamba Kunyah yake ilikuwa ni Abul-Hakam. Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) akamwambia: “Allaah Ndiye Al-Hakam241 Kwakehurudishwa hukumu.” Kisha Abuu Shurayh akasema: “Hakika watu wanguwanapotofautiana kwa kitu hunijia na huwahukumu baina yao na pande zotembili huridhika.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni uzuriulioje huu. Kwani huna mtoto? Nikasema: “Shurayh, Muslim na ´Abdullaah.”Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni nani mkubwa wao?”Nikasema: “Shurayh.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Basiwewe ni Abuu Shurayh.”

(Kaipokea Abuu Daawuud na wengineo)

Ufafanuzi:Mlango huu ni ukamilisho wa mlango uliotangulia, alichozidisha tu ni kubadilisha jina(kichwa cha mlango). Abuu Shurayh mwanzoni jina lake la asli alikuwa anaitwa Abdul-Hakam, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akambadilisha kwa kumpa jina la AbuuShurayh. Kisha Abuu Shurayh akasema sababu ya kwamba sio yeye ndiye kajiita hivyo,isipokuwa ni watu ndio waliomwita hivyo. Abuu Shurayh alikuwa akiwahukumu watu kwaShari´ah, na hakuwa anatumia kanuni wala hukumu za kibinaadamu. Ama yuleanayewahukumu watu kwa kanuni za kibinaadamu au za kikabila n.k. hii ni hukumu yaTwaaghuut (Kishaytwaan). Hukumu imegawanyika sehemu tatu:

- Hukumu ya Allaah (´Azza wa Jalla). Bi maana kuhukumu kwa kutumia Shari´ah.

- Hukumu ya Twaaghuut.

240 Kwa yule ambaye yuko na jina la Allaah (Ta´ala)241 Mwenye Kuhukumu

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

205

- Hukumu ya kusuluhisha baina ya watu. Na aina hii inaingia katika aina ile yakwanza kwa kuwa Allaah Kaiamrisha na kuikubali. Na Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kaikubali katika Hadiyth hii.

Faida tunazopata katika Hadiyth hii:

- Haijuzu kuitwa kwa Majina ambayo ni hususan ni ya Allaah.

- Kusuluhisha baina ya Waislamu ni jambo linalojuzu. Isipokuwa suluhu yakuhalalisha haramu au kuharamisha halali.

- Kubadili jina ikiwa lina ukosefu wa adabu na Allaah na linashirikiana na Allaah.

- Mtu atapokataza kitu na akawa na badala atoe hiyo badala kumpa huyoaliyemkataza.

- Kujuzu kwa kutumia kunya. Kama mfano wa Abuu ´Abdullaah, Ummu ´Abdullaahn.k.

- Baba na mama hutumia kunya la yule mtoto wake ambaye ni wa kwanza. Amakutumia jina la mtoto ambaye sio wa kwanza, hili linaenda kinyume na Shari´ah.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Kuheshimu Sifa za Allaah na Majina ya Allaah hata kama mtu hakukusudia maana yake(katika kuyatumia).

2. Kubadili jina kwa ajili hiyo.

3. Kuchagua yule mtoto wa kwanza katika kutumia kunya.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

206

Mlango Wa 48

Mwenye Kufanyia Mzaha Kitu Kilichotajwa Ndani Yake Jina La Allaah,Qur-aan Au Mtume

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

بلعنو وضخا نا كنمإن قولنلي مهألتن سلئو قل أباللـه وآياته ورسوله كنتم تستهزئون◌

”Na ukiwauliza (kwanini wanaifanyai istihzai Dini) bila shaka watasema:“Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza.” Sema: Je, mlikuwa mnamfanyiaistihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?”.” (at-Tawbah 09:65)

Kutoka kwa Ibn ´Umar, Muhammad bin Ka´b, Zayd bin Aslam na Qadaatah(Radhiya Allaahu ´anhum ajmaa´iyn) wamepokea Hadiyth zinazoingiliana:

“Wakati wa vita vya Tabuk kuna mtu aliyesema: “Hatujapata kuona watukama wasomaji wetu hawa, matumbo yao yanapenda kula sana, ndimi zaozinasema uongo na ni waoga wakati wa mapambano – yaani anamkusudiaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wakewaliokuwa wakisoma. Akasema ´Awf bin Maalik: “Hakika umesema uongo,isipokuwa wewe tu ni mnafiki. Nitamwambia Mtume wa Allaah (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam).” ´Awf akaenda kwa Mtume wa Allaah (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia aliyoyasema akakuta Qur-aanimekwishamtangulia. Akaja yule mtu kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) akakuta Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndioanaanza kuondoka mahali hapo na kishampanda ngamia wake. Yule mtuakasema: “Ewe Mtume wa Allaah! Hakika sisi tulikuwa tunafanya mchezo natukipiga masoga ili kupitisha tu wakati safari.” Akasema Ibn ´Umar (RadhiyaAllaahu ´anhumaa) akasema: “Kama kwamba namtazama mtu huyoakishikilia kamba za ngamia wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) na huku mawe yakikwaruza miguu yake na huku anasema ”Hakikatulikuwa tunaporoja na tunacheza.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) anamwambia:

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

207

زئونهتست مكنت هولسرو هاتآيو أباللـهانكمإمي دعم بتكفر وا قدرذتعلا ت

”Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (at-Tawbah09:65-66) Na Mtume hakugeuka kumtazama wala kuzidisha juu ya hayo”.”

Ufafanuzi:Mwenye kufanyia mzaha kitu ambacho kimetajwa ndani yake jina la Allaah, Qur-aan auMtume amekufuru. Shaykh hakusema hili isipokuwa ni kwa sababu limetajwa katikaAayah. Huku ni kukufuru baada ya mtu kuwa Muislamu. La wajibu ni kumuabudu Allaah,kumheshimu na kumuadhimisha. Hali kadhalika Mitume (´alayhimus-Swalaat was-Salaam)na khaswa wa mwisho wao Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa kuwa waoni wafikishaji ujumbe kutoka kwa Allaah. Inatakiwa kuwaadhimisha, kuwaheshimu,kuwapenda na kuwaiga. Na ni wajibu kuiheshimu Qur-aan na vitabu vilivyoteremshwakutoka kwa Allaah (´Azza wa Jalla), kwa kuwa ni Maneno na Shari´ah ya Allaah.Kuviheshimu ni kumheshimu Allaah (Jalla wa ´Alaa). Hali kadhalika kuwaheshimuwanachuoni, kwa kuwa wanachuoni ndio warithi wa Mitume (´alayhimus-Salaam),kuheshimu ile elimu wanayofunza. Yule ambaye anafanyia istihzai mambo haya anakufuru.Allaah Atukinge. Hii ni khatari kubwa. Na ni mambo ambayo yameenea sana leo, watuwanafanya maskhara na Allaah, Mtume Wake, Qur-aan, Shari´ah na wanachuoni. Kwakuwa yote haya yanakwenda kinyume na matamanio yao. Mashaytwaan wakijini nawakibinaadamu wanapiga vita Qur-aan na Sunnah, wanachuoni na Dini yote kwa ujumla.Ni juu ya mtu kumuomba Allaah (´Azza wa Jalla) uthabiti kwa kupinda huku na upotofukama huu.

Aayah hii (ya Suurat at-Tawbah) imewateremkia watu ambao walikuwa pamoja na Mtume(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika vita vya Tabuuk wametoka kupigana Jihaadpamoja na Mtume. Waliporejea katika njia kuelekea Madiynah, wakatua kwenye nyumba.Wakakusanyika watu, kulikuwemo mtu huyu katika kikao hichi, Allaah Atukinge. Akasemamaneno haya machafu ya kashfa, wakimkusudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)na Maswahabah zake. Watu hawa waliongea maneno haya katika kikao, lakini leo kwamasikitiko makubwa maneno kama haya yanaandikwa kabisa mpaka katika kitabu nakinasomwa na kuenezwa. Jambo hili ni khatari sana. Ni wajibu kutanabahi kwa jambo hilina kulitahadharisha.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

208

Hapa aliyesema maneno ya kashfa na machafu ni mtu mmoja, lakini wamejumuishwa wotewaliokuwa wakikaa katika kikao hicho kwa kuwa hawakukataza isipokuwa kijana mmoja tu´Awf bin Maalik ndiye alikemea na kumkadhibisha ilihali wengine walikaa kimya. AllaahKawajumuisha wote waliokuwa katika kikao na kunyamazia hili. Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) hakujali kabisa udhuru wake. Hapa kuna mafunzo ya kuwakata(kuwasusa) watu sampuli hii kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).Pamoja na kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mpole, rahiym na alikuwa nimwenye tabia nzuri. Lakini pamoja na hivyo, hakumjali mtu huyu. Alimkata na kumsusa nahakumjali. Kakufuru baada ya kuamini kwake, ni dalili ya kwamba alikuwa hajakuwamnafiki wa asli mwanzo, isipokuwa kawa mnafiki sasa. Ni dalili ya kuwa muumini anawezakugeuka akawa mnafiki. Kwa kuwa wanafiki wako aina mbili:

1. Mnafiki wa asli.

2. Mnafiki ambaye ameingiwa na unafiki baadae. Alikuwa muumini kisha akafanyaunafiki (mkubwa) na kukufuru. Allaah Atukinge.

Ni dalili ya kwamba istihzai (mzaha) katika Dini haukubaliwi na wala hapewi udhurumwenye kufanya hivyo, sawa ikiwa mtu anamaanisha kweli au anafanya mzaha. Hata kamahakuwa anakusudia hivyo.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Jambo la kwanza nalo ndio jambo kubwa, yule mwenye kufanya mzaha katika mambohaya ni kafiri.

2. Hii ndio tafsiri ya Aayah (09:65) inamgusa yule mwenye kufanya hivyo yeyote awae.

3. Tofauti baina ya uvumi na baina ya nasaha kwa Allaah na kwa Mtume Wake (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam).242

4. Tofauti baina ya msamaha Anaoupenda Allaah na baina ya khasira katika kuamiliana namaadui wa Allaah.

5. Miongoni mwa nyudhuru kuna usiokubalika.243

242 Shaykh Fawzaan anasema: ”´Awf bin Maalik alienda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) kwa lengo la kutoa nasaha na haikuwa kwa lengo la kueneza uvumi na kusengenya. Ni dalilikwa yule ambaye anafanya mambo kama haya ashtakiwe kwa kiongozi wa Waislamu ili awachukuliehatua.”243 Shaykh anasema tena: ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mengi ambayo alikuwaanafanyiwa alikuwa ni mwenye kuyasamehe, lakini kunapovukwa mipaka ya Allaah alikuwaanakasirika na kulipa kisasi kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jalla) na wala hasamehi hili, kwa kuwa siokatika haki yake. Haki ya Allaah hakuna cha kuisamehe.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

209

Mlango Wa 49

Yaliyokuja Kutokana Na Kauli Ya Allaah Ta´ala

نلئولئة ومة قائاعالس ا أظنمي وـذا ل ه قولنلي هتساء مرض دعن با منة ممحر اهأذقن هندي عبي إن لإلى ر تجعن ر للحسنى ◌م مهيقنذلنلوا وما عوا بمكفر ينالذ بئننفلنيظذاب غلع ن

”Na Tunapomuonjesha Rahmah kutoka Kwetu baada ya dhara iliyomgusa,bila shaka husema: “Hii ni (kutokana na juhudi na elimu) yangu, na sidhanikama Saa (Qiyaamah) itasimama. Na nitakaporejeshwa kwa Mola wangu,hakika nina mazuri Kwake.” Basi bila shaka Tutawabainishia walewaliokufuru yale waliyoyatenda, na bila shaka Tutawaonjesha adhabu nzito.”(Fuswswilat 41:50)

Mujaahid kasema (katika kuifasiri Aayah hii):

“Hili ni kutokana na matendo yangu mimi ndiye mwenye haki nayo.”

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kasema maana yake ni:

“Anataka kutoka kwangu.”

Na Kauli Yake:

قال إنما أوتيته على علم عندي

”(Qaaruwn) Akasema: “Hakika nimepewa haya (mali) kwa sababu ya elimuyangu.” (al-Qaswasw 28:78)

Qataadah kasema (kuifasiri Aayah hii):

“Mali hii nimepewa kwa sababu ya sifa na uzoefu wangu wa kujuakuchuma.”

Na wengine244 wakasema:

244 Wanachuoni

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

210

“Ni kutokana na Elimu ya Allaah kwa sababu mimi ndiye mwenyekuistahiki.”

Na hii ndio maana ya kauli ya Mujaahid:

“Nimeipewa kwa sababu ya cheo changu.”

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba alimsikiaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Watu watatu katika Banuu Israaiyl: Mwenye ukoma, kipara na kipofu.Akataka Allaah Kuwapa mtihani. Akawatumia Malaika, akamuendea yulealiyekuwa na ukoma na kumwambia: “Kitu gani unachokipenda?” Akasema:“Napenda niwe na rangi nzuri na ngozi nzuri, na yaniondoka haya ambayowatu huniona ni mchafu kwayo.” Akasema: “Malaika yule akampapasa nauchafu wake ukawa umeondoka, akapewa rangi nzuri na ngozi nzuri.Akamuuliza: “Mali ipi unayopenda?” Akasema: “Ngamia au ng´ombe.”Akapewa ng´ombe walio na mimba ya miezi kumi. Kisha Akamwambia:245

“Allaah Akubarikie ngamia hawa.”

Akamuendea yule wa kipara na kumuuliza: “Ni kitu gani unachokipenda?”Akasema: “Kuwa na nywele nzuri na yaniondoke haya ambayo watu hunionamchafu kwayo.” Malaika akampapasa. Ukaondoka uchafu wake na akapewanywele nzuri. Akamuuliza: “Mali ipi unayopenda?” Akasema: “Ng´ombe aungamia.” Akampa ng´ombe mwenye mimba na kumwambia: “AllaahAkubarikie ngombe wako hawa.”

Akamuendea kipofu na kumuuliza: “Ni kitu gani unachokipenda?” Akasema:“Allaah Kunirudishia macho yangu niweze kuwaona watu.” AkampapasaAllaah Akawa Amemrudishia macho yake. Kisha akamuuliza: “Ni mali ipiunayopenda?” Akasema: “Kondoo.” Akapewa kondoo wenye mimba. Baadaewale wanyama wote watatu wakashika mimba na kuzaana, huyu akawa nazizi la ngamia, huyu akawa na zizi la ng´ombe na huyu zizi la kondoo.

Anasema:246

245 Huyo Malaika246 Yaani anaendelea kuelezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

211

“Halafu Malaika alimuendea yule wa ukoma katika sura na umbo lake lile lilela kwanza na kumwambia: “Mimi ni mtu masikini na sina njia nyingineyoyote katika safari yangu. Sina cha kunifikisha leo isipokuwa kwa msaadawa Allaah kisha wako. Ninakuomba kwa Jina la yule Aliyekupa rangi nzuri,ngozi nzuri na mali unipe ngamia moja atakayenifikisha katika safari yangu.”Akasema:247 “Nina haki nyingi.” Malaika akamwambia: “Kana kwamba miminakujua, kwani hukua na ukoma watu wakawa wanakuchukia kwa uchafutena fakiri kisha Allaah ndo Akakupa mali?” Akasema: “Mimi nimeirithi malihii kutoka kwa babu wa babu.” Malaika akasema: “Ikiwa umesema uongo,basi Allaah Akurudishe katika hali uliokuwa nayo mwanzo.”

Akasema:

“Malaika alimuendea yule wa kipara kwa sura yake na umbo lile lile nakumwambia kama alivyomwambia huyu wa kwanza, na akamrudisha kamaalivyomrudisha huyu.248 Akamwambia: “Ikiwa umesema uongo, basi AllaahAkurudishe katika hali uliokuwa nayo mwanzo.”

Akasema:

“Akamuendea yule kipofu kwa sura yake na uombo lile lie na kumwambia:“Mimi ni mtu masikini na sina njia nyingine yoyote katika safari yangu. Sinacha kunifikisha leo isipokuwa kwa msaada wa Allaah kisha wako.Ninakuomba kwa Jina la yule Aliyekurudishia macho yako unipe kondoomoja atakayenifikisha katika safari yangu.” Akasema: “Kwanza nilikuwakipofu Allaah Akanirudishia macho yangu, chukua unachokitaka na uombeunachokitaka. Wallaahi sintokuzuia kuchukua chochote (unachohitajia)kutoka katika mali yangu umekichukua kwa ajili ya Allaah.” Malaika yuleakamwambia: “Shika mali yako. Hakika mmepewa majaribio na AllaahKakuridhia wewe na Kawakasirikia wenzako wawili.”

(Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

247 Yule bwana wa ukoma ambaye kwa sasa ni tajiri248 Wa mwanzo wa ukoma

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

212

Ufafanuzi:Mlango huu yaani ni yaliyokuja kuifasiri Aayah hii Tukufu na zinazofanana nazo katikaAayah za Qur-aan katika kuinasibisha neema kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na wajibuwa kuishukuru. Na kuinasibisha neema kwa Allaah na kuwa mwenye kuishukuru, hili nikatika Tawhiyd. Ama kuinasibisha kwa wengine, hili ni katika Shirki na kukufuru neema.Kama mtu kuinasibisha kwake mwenyewe, kutokana na ujuzi wake n.k., au kuinasibishakwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Anasema Allaah (Ta´ala):

اللـه نفم ةمن نعا بكم ممو

”Na neema yoyote mliyo nayo, basi ni kutoka kwa Allaah.” (an-Nahl 16:53)

Neema zote, za dhahiri na zilizojificha, zinatoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Mtuanatakiwa kutumia neema hizi katika kumtii, kwa kuwa shukurani ni katika Tawhiyd na´Ibaadah. Na kukufuru neema ni katika Shirki. Na shukurani ina nguzo tatu:

1. Nguzo ya kwanza mtu kuihadithia dhahiri. Uihadithie neema ya Allaah kwa njia yakumshukuru Allaah.

2. Kuijua kwa undani moyoni, haitoshi kwa ulimi peke yake.

3. Kuitumia katika kumtii Allaah na katika ´Ibaadah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).Ukiitumia katika maasi, huku itakuwa ni kukufuru neema.

Huku ndio kushukuru neema.

Maneno ya Mujaahid, hii ni haki yangu yaani ndiye mwenye kustahiki na hili na Allaahhana lolote katika haya na maneno mfano wa haya. Huku ni kuikufuru neema. Vile vilekusema Allaah Kanipa mali hii kwa kuwa anajua kuwa mimi ndiye mwenye kuistahiki, aukusema mali hii nimeipata kutokana na ujuzi wangu, sampuli ya meneno yote haya nikufuru.

Hadiyth ya Abuu Hurayrah: Watu hawa watatu Allaah Aliwaneemesha, wawili katika waowakaikanusha neema ya Allaah na wakainasibisha mali yao kwa asiyekuwa Allaah. Amayule mtu watatu (kipofu) kaijua neema ya Allaah, akamshukuru Allaah na akaitumia malikatika kumtii Allaah, hivyo Allaah Akawa Radhi naye na Akawakasirikia wenzake wawili.Watu hawa watatu ni katika Baniy Israaiyl watu waliokuwa kabla yenu. Malaika aliwajiakwa umbile la kibinaadamu kwa kuwa watu hawawezi kumuona Malaika kwa umbile lao lakihakika Alilowaumba kwalo Allaah, hawawezi hili. Allaah Kawapa Malaika uwezo wakujigeuza umbile la kibinaadamu. Walipoulizwa kuomba wote walianza kwa kuomba afyanjema, kwa kuwa afya njema kwa binaadamu ni kitu muhimu sana. Hapa katika Hadiyth hiitunapata kujifunza ya kwamba, yule anayeishukuru neema ya Allaah, Allaah Humzidishia,Humbarikia na Humsalimishia mali. Na kinyume chake, kukufuru neema kunasababisha

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

213

kupata Khasira za Allaah. Na katika Hadiyth kuna dalili ya kuwa watu wenye kushukuru niwachache. Na kushukuru neema ni katika Tawhiyd, na kuikanusha ni katika Shirki nakufuru.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Fuswswilat. (41:50)

2. Maana ya:

ـذا لي ه قولنلي

“Hii ni (kutokana na juhudi na elimu) yangu.” (al-Fuswswilat 41:50)

3. Maana ya:

إنما أوتيته على علم عندي

“Hakika nimepewa haya (mali) kwa sababu ya elimu yangu.” (al-Qaswasw 28:78)

4. Ibra inayopatikana katika kisa hiki kikubwa.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

214

Mlango Wa 50

Kauli Ya Allaah Ta´ala

فلما آتاهما صالحا جعلا له شركاء فيما آتاهما فتعالى اللـه عما يشركون◌

”Lakini Anapowapa (mtoto mzima na) mwema, wanamfanyia (Allaah)washirika249 katika kile Alichowapa. Fata’aala-Allaahu (Ametukuka Allaah kwaUluwwa) kutokana na yale yote wanayoshirikisha.” (al-A´raaf 07:190)

Anasema Ibn Hazm (Rahimahu Allaah) ya kwamba wanachuoniwamekubaliana juu ya kuharamisha kila jina linaloabudiwa badala ya Allaah.Kama ´Abd-´Umar,250 ´Abd al-Ka´abah,251 na yanayofanana na hayo isipokuwatu ´Abdul-Muttwalib.

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kasema kuhusiana na maana yaAayah hapo juu:

“Aadam alipomuendea mkewe alishika ujauzito. Wakati huyo Iblisi akawajiana kuwaambia: “Mimi ndiye yule niliyesababisha mkatolewa Peponi. Nitiini,vinginevyo nitamfanya mtoto wenu kuwa na pembe mbili za paa na atatokatumboni mwako huku nimelipasua, ntafanya hivyo ntafanya hivyo, akawatiakhofu, mtapomzaa muiteni ´Abdul-Haarith,252 wakakataa kumtii, akatoka253

hali ya kuwa ni maiti.

Kisha akabeba ujauzito mwingine akawajia na kuwaambia kamaalivyowaambia mara ya kwanza. Wakakataa kumtii na mtoto akawa ametokahali ya kuwa ni maiti.

249 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa Aadam na Hawaa walimfanyia washirika katika utiifu na sikatika ´Ibaadah. Hii inaitwa Shirki ya utiifu ambayo ni Shirki ndogo.”250 Mja wa ´Umar251 Mja wa al-Ka´abah252 Mja wa mkulima ardhi253 Ndani ya tumbo

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

215

Kisha akabeba ujauzito mwingine na akawajia na kuwaambia kamaalivyowaambia, na hapo kishawatia mapenzi ya kumpenda mtoto na wakawawamemwita ´Abdul-Haarith. Na hio ndio maana ya Kauli Yake:

جعلا له شركاء فيما آتاهما

”Wanamfanyia (Allaah) washirika katika kile Alichowapa.” (al-A´raaf 07:190)

(Kaipokea Ibn Abiy Haatim)

Naye254 kapokea kwa isnadi Swahiyh kutoka kwa Qataadah (Radhiya Allaahu´anhu) ya kwamba kasema255:

“Shurakaaa (washirika) walimshirikisha Allaah katika utiifu256 na sio katikakumuabudu badala Yake.”

Naye257 kapokea kwa isnadi Swahiyh kutoka kwa Mujaahid (Radhiya Allaahu´anhu) kasema kuhusiana na Kauli Yake:

لئن آتيتنا صالحا

“Ukitupa (mtoto mzima na) mwema bila.” (al-A´raaf 07:189)

akasema:

“Walichelea258 mtoto asijekuwa si mtu.” Maana kama hiyo imethibiti pia kwaHasan, Sa´iyd na wasiokuwa wao.

254 Ibn Abiy Haatim255 Muhimu kujua. Hadiyth iliyotajwa hapo juu yasemekana ya kwamba ni dhaifu. al-Haafidhw IbnKathiyr na al-Imaam al-Albaaniy kaona pia kuwa ni dhaifu.Shaykh Fawzaan anasema: ”Kuna tofauti kuhusiana na Hadiyth hii, kuna ambao wanaona kuwa nidhaifu na wengine wanaona kuwa ni sahihi. Anaendelea kusema: ”Hii (Hadiyth ndio) tafsiri sahihi yaAayah aliyoichagua Ibn Jariyr na wanachuoni wengine, na inasapotiwa na Hadiyth zenye nguvu nakauli za Taabi´uun na maimamu. Hii ndio kauli yenye nguvu kuhusiana na tafsiri ya Aayah. Na kunaambao wanaona kuwa Aayah yote hii inamhusu binaadamu na sio Aadam, na hii pia ndio kauli yaIbn Kathiyr. Lakini kauli yenye nguvu ni ile ya kwanza na ndio aliyochukua mwandishi (RahimahuAllaah).”256 Kumtii Shaytwaan257 Ibn Abiy Haatim258 Adaam na Hawaa

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

216

Ufafanuzi:Huu ni mlango yaliyokuja kuifasiri Aayah hii Tukufu, ya kwamba kujiita kwa majina ya ujakwa asiyekuwa Allaah ni Shirki. Kama kuitwa ´Abdul-Husayn (mja wa Husayn), ´Abdul-Amiyr (mja wa Amiyr), ´Abdul-Fulani (mja wa fulani) katika viumbe. Hii ni Shirki, lakinihaifikii Shirki kubwa isipokuwa ni Shirki katika matamshi ikiwa mtu hakukusudia uja wauhakika. Ama mtu akikusudia uja wa uhakika inakuwa Shirki kubwa. Ama kujiita kwa jinakama hilo tu bila ya kuitakidi, hii ni Shirki ndogo. Haijuzu kujiita kwa majina ya uja kwaasiyekuwa Allaah. Na hili ni haramu na ni aina ya Shirki kwa Ijmaa´. Badala yake anatakiwamtu kujiita, ´Abdullaah, ´Abdul-Hakiym na mfano wa hayo, aufanye uja uwe kwa AllaahPekee. Na majina mazuri kabisa - kama ilivyokuja katika Hadiyth - ni ´Abdullaah na ´Abdur-Rahmaan.

Hadiyth ya Ibn ´Abbaa: Hapa tunapata dalili na mafunzo ya kwamba haijuzu kuchukuliasahali katika mambo ya ´Aqiydah hata kama itakuwa kwa matamshi tu. Haijuzu. Vipi kwawale wanaokwenda kwa wachawi, Mashaytwaan na wanawaamrisha kuchinja kwa ajili yaasiyekuuwa Allaah na kuwatia khofu ya kwamba watakufa ikiwa hawakufanya kadhaa,kwa kupenda maisha na kusamilika wanawatii wachawi na makuhani. Allaah Atukinge. Niwajibu kutahadhari na hilo.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Uharamisho wa kila jina linaloabudiwa badala ya Allaah.

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-A´raaf. (07:189)

3. Hii imeitwa kuwa ni Shirki kule kumwita (mtoto wao hivo) hata kama mtuhawakukusudia uhakika wake.

4. Allaah Kumpa mtu mtoto aliye salama ni katika neema.

5. Salaf wametofautisha baina ya Shirki katika utiifu (ndogo) na Shirki katika ´Ibaadah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

217

Mlango Wa 51

Kauli Ya Allaah Ta´ala

وللـه الأسماء الحسنى فادعوه بها ◌هائمي أسون فدلحي ينوا الذذرو

”Na Allaah Ana Asmaaul-Husnaa (Majina Mazuri kabisa), basi muombenikwayo. Na waacheni wale wanaopotoa (kwa kuharibu utukufu, kukanusha,kugeuza maana, kushabahisha) katika Majina Yake.” (al-A´raaf 07:180)

Ibn Abiy Haatim kapokea kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu´anhumaa) ya kwamba kasema:

“wanaopotoa katika Majina Yake”,259 yaani wanamshirikisha.”

Na imepokelewa kwake tena:

“Wametoa jina la al-Laat260 kutoka kwenye Al-Ilaah na al-´Uzza261 kutokakwenye Al-´Aziyz.

A´mash kasema (kuhusu maana yake):

“Wanaopotoa katika Majina ya Allaah yasiyokuwemo ndani yake.”

Ufafanuzi:Huu ni mlango umekuja kuifasiri Aayah hii Tukufu. Kakusudia Shaykh kwa mlango huutawassul inayoruhusiwa na kujuzu na tawassul iliyokatazwa. Kwa kuwa masuala hayayamewatatiza watu wengi kutokana na ujinga au matamanio. Tawassul maana yake nikujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jalla) na ni njia inayomkurubisha mtu kwa Allaah

259 Yulhiduuna fiy Asmaaihi260 Moja ya masanamu ya washirikina makubwa261 Lilikuwa ni sanamu pia la washirikina

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

218

(Subhaanahu wa Ta´ala). Njia Aliyoiwekea Allaah Shari´ah ni kujikurubisha Kwake kwakumtii na kuacha kumuasi.

يا أيها الذين آمنوا اتقوا اللـه وابتغوا إليه الوسيلة

”Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na tafuteni Kwake Al-Wasiylah (njia za 'ibaadahkumkurubia).” (al-Maaidah 05:35)

Maana yake yaani jikurubisheni Kwake kwa kumtii na kwa yanayomkurubisha mtu Kwake.Maana ya “Al-Wasiylah” ni yale yanayowakurubisha kwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala).

Kauli ya Allaah:

وللـه الأسماء الحسنى فادعوه بها

”Na Allaah Ana Asmaaul-Husnaa (Majina Mazuri kabisa), basi muombeni kwayo.” (al-A´raaf07:180)

Huu ni ubainifu kwa anayotakiwa mtu kutawassul kwayo kwa Allaah na kwa AnayoombwaAllaah kwayo, nayo ni Majina na Sifa Zake. Hivyo, mtu anatakiwa kumuomba Allaah kwaMajina na Sifa Zake. Usimuombe Allaah kwa fulani, wasiylah ukaakati wa fulani, uombeziwa fulani kama wafanyavyo washirikina ambao wanaabudu badala ya Allaah.

اللـه ندا عناؤفعلاء شـؤ قولون هيو مهنفعلا يو مهرضا لا يم اللـه ونن دون مدبعيو

”Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao (hawawezi) kuwadhuru na wala (hawawezi)kuwanufaisha, na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah”.” (Yuunus 10:18)

Na wanasema:

والذين اتخذوا من دونه أولياء ما نعبدهم إلا ليقربونا إلى اللـه زلفى

”Na wale waliojichukulia badala Yakeawliyaa (wasaidizi, miungu; wakisema): “Hatuwaabuduisipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu”.”(az-Zumar 39:03)

Huku ndio kutawassul kwao. Wanatawaasul kwa kuweka watu baina yao na Allaah. AllaahAnakurubiwa kwa yale Anayoyaridhia (Subhaanahu wa Ta´ala) – kwa utiifu, kumuabudu,Majina na Sifa Zake. Kama mfano wa kusema: “Ee Ar-Rahmaan Nirehemu”, “Ee GhaffuurNisamehe”, “Ee At-Tawwaab Nisamehe”, “Ee Ar-Razzaaq Niruzuku” n.k. Mtu atawassulkwa Majina Yake.

Vile vile inajuzu kutawassul Kwake kwa matendo mema, mtu anatawassul Kwake kwamatendo yake mema aliyoyafanya kwa kujikurubisha Kwake. Kwa mfano: “Ee Allaah

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

219

nakuomba unisamehe kwa sababu nimefanya hivi na hivi... ”. Kama wale watu wa pangoniwaliotawassul kwa Allaah kwa matendo yao mwema.

ول فاكتسا الرنعباتو لتا أنزا بمنا آمنبرينداهالش عا منب

“Mola wetu, tumeamini Uliyoyateremsha na tumemfuata Mtume, basi tuandike pamoja nawanaoshuhudia.” (al-´Imraan 03:53)

Wametawassul kwa Allaah kwa kumuamini kwao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam). Na vile vile kwa kuamini kwako Qur-aan na Sunnah.

Vile vile inajuzu kutawassul kwa Allaah kwa Du´aa ya watu wema, waliopo tena hai. Kwamfano kusema: “Ewe fulani! Niombee kwa Allaah Anisamehe, Aniruzuku, Aniponye n.k.”Ukamuomba ndugu yako akuombee.

Ama tawassul iliokatazwa ni kutawassul kwa Allaah kwa jaha ya mtu, au dhati yake. Kamakwa mfano kusema: “Ee Allaah ninakuomba kwa jaha ya Muhammad”, au kutawassul kwawema wa fulani. Wema huu ni wa kwake na wewe haukufai kitu. Kitachokufaa ni wemawako wewe mwenyewe. Tawassul kwa Allaah kwa wema wako na si kwa wema wawengine.

لتخ ة قدأم لكت ◌متبا كسلكم مو تبا كسا مله ولا تسألون عما كانوا يعملون◌

”Huo ni ummah kwa hakika umeshapita, una uliyoyachuma nanyi mna mliyoyachuma, nawala hamtoulizwa waliyokuwa wakitenda.” (al-Baqarah 02:141)

Kila mmoja ataulizwa binafsi juu ya matendo yake.

Vile vile inajuzu kutawassul kwa Majina na Sifa za Allaah. Na Majina ya Allaah yote nimazuri. Na Majina ya Allaah ni mengi hakuna anayejua idadi yake isipokuwa YeyeMwenyewe. Ama Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah Ana Majina 99, yule mwenye kuyadhibiti ataingia Peponi.”

Haina maana ni haya tu, ana Majina zaidi ya 99. Hayakuwekewe mpaka Majina haya (yaAllaah) kwa kuwa ni mengi sana. Wewe chagua Jina ambalo linaendana na haja yako. Kwasharti jina hilo ulilochagua liwe limethibiti katika Qur-aan au Sunnah za Mtume (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam). Na maana ya “mwenye kuyadhibiti”: yaani 1) kayahifadhi, 2)akajua maana yake na 3) akamuomba Allaah kwayo. Kuna ambayo katueleza na kunaambayo hakutwambia nayo. Na haijuzu kumwita Allaah kwa jina ambalo Hakujiita naloYeye Mwenyewe au Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

220

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Uthibitisho wa Majina (ya Allaah).

2. Kuwa Kwake Mazuri.262

3. Maamrisho ya kumuomba kwayo.

4. Kumuacha katika wale waliyoyapa mgongo katika wajinga na Mulhiduun.

5. Tafsiri ya kuyafanyia Ilhaad Majina ya Allaah.

6. Adhabu ya mwenye kuyafanyia Ilhaad.

262 Shaykh Fawzaan anasema: “Majina yote ya Allaah ni Mazuri. Ar-Rahmaan ni dalili ioneshayo yakwamba Allaah ni Mwingi wa Rahmah, Al-´Aziyz ni dalili ioneshayo Utukufu Wake, Al-´Aliym nidalili ioneshayo kuwa ana Elimu (Ujuzi), Al-Hakiym ni dalili ioneshayo kuwa ana Hekima. Kila Jinakatika Majina Yake kunatolewa ndani yake Sifa katika Sifa Zake (Subhaanahu wa Ta´ala).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

221

Mlango Wa 52

Hakusemwi As-Salaam (Amani) Iwe Juu Ya Allaah

Imepokelewa katika Swahiyh (al-Bukhaariy na Muslim) kutoka kwa IbnMas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba kasema:

“Tulikuwa tunapokuwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katikaSwalah tunasema: “as-Salaam ´alaa Allaahi min ´Ibaadihi amani iwe juu yaAllaah kutoka kwa waja Wake, as-Salaam ´alaa fulaan wa ´alaa fulaan amani iwejuu ya fulani na fulani.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:“Msiseme “as-Salaam ´alaa Allaah amani iwe juu ya Allaah, kwani AllaahNdiye As-Salaam Amani.”

Ufafanuzi:Haya ni makatazo. Kuna matamshi imekatazwa kuyasema kwa haki ya Allaah (Subhaanahuwa Ta´ala) kwa kuwa yanaipunguza Tawhiyd. Ndio maana Shaykh akawa amewekamlango huu. Neno “As-Salaam” lina maana mbili: Maana ya kwanza ni katika Majina yaAllaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Maana ya pili ni kwamba ni Du´aa, na Allaah HaombewiDu´aa awe na amani kwa kuwa Yeye Allaah Ndiye mwenye kutoa amani na kuzuia amanikwa waja. Hivyo Allaah Haombewi Du´aa, kwa kuwa hili linaashiria mapungufu.

Hadiyth ya Ibn Mas´uud, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakataza wasisemihivyo, na badala yake akawafunza waseme “at-Tahiyyatu liLlaahi was-Swalawaat wat-Twayyibaat... ” Namna hii ndio aliwafunza waseme katika Tashahhud. AllaahAnaadhimishwa na wala hatolewi Salaam, yaani kuombewa Du´aa (Subhaanahu wa Ta´ala).Unapomtolea mtu Salaam unakuwa umemuombea Du´aa, ikiwa umekusudia “Jina la Allaahliwe juu yako” unakuwa umemuombea Allaah Amhifadhi na Amsalimishe na madhara. Naikiwa umekusudia “amani” unakuwa umemuombea amani iwe juu yake. Na maana zotehizi mbili haistahiki kuambiwa kwa haki ya Allaah. Na Waislamu kutoleana Salaam sawaikiwa mtu unamjua au humjui ni katika haki ya Muislamu juu ya Muislamu mwingine. NaMtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema hamtoingia Peponi mpaka mpendane,na akasema kutoleana Salaam ndio jambo ambalo litawafanya Waislamu wapendane.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

222

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya As-Salaam.

2. As-Salaam ni at-Tahiyyah maamkizi.

3. As-Salaam haistahiki kulitumia kwa Allaah.

4. Sababu ya kukataza hilo ni kwa kuwa Allaah Mwenyewe Ndiye Salaam.

5. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawafunza at-Tahiyyah maamkizi yanayofaakutumiwa kwa Allaah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

223

Mlango Wa 53

Kauli “Ee Allaah! Nisamehe Ukitaka”263

Katika Swahiyh (al-Bukhaariy na Muslim) kutoka kwa Abuu Hurayrah(Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kasema:

“Asiseme mmoja wenu: “Ee Allaah! Nisamehe ukitaka. Ee Allaah! Nirehemuukitaka.” Akate azimio la maombi bila ya kuvua kitu, kwani Allaah hakunaamtenzae nguvu.”264

Imepokelewa katika Muslim:

“Na aazimie raghbah shauku yake, kwani Allaah Hakioni kikubwa kwa kileAlichokitoa.”

Ufafanuzi:Katika matamshi ambayo haifai kuyatumia kwa haki ya Allaah, ni matamshi haya. Kwakuwa kuna aina ya mapungufu kwa haki ya Allaah. Hivyo haijuzu mtu kusema: “AllaahNisamehe Ukitaka.” Kwa nini? Kwa kuwa ni moja kati ya mawili:

- Ima mwenye kusema hivi kana kwamba hahitajii msamaha wa Allaah. Yaaniutadhani anamlazimisha Allaah Amsamehe.

- Akadhani mtu ya kwamba Allaah Anachukia (Kerahika) Kumsamehe, kama walivyoviumbe.

Viumbe wao hawapenda kuombwa, na wakati mwingine ukimuomba sana anaweza hatakukasirika. Allaah Hufurahi (Subhaanahu wa Ta´ala) Anapoombwa. Kiumbe anawezakukupa lakini huku akawa ni mwenye kuchukia kwa hilo. Ama Allaah (Jalla wa ´Alaa)Anakupa na ni Mwenye Kuridhia na Anafurahi kwa waja Wake kumuomba. Na Anawapa

263 Allaahummaa ighfirliy inshi-it264 Dhidi ya Matakwa Yake

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

224

mara nyingi hata bila ya kumuomba. Na hakipungui Kwake chochote Anapokupa(Subhaanahu wa Ta´ala). Ama viumbe vinapungua kwa vile anavyovimiliki. Ndio maanalafdhi hii imekatazwa.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Makatazo ya kubagua katika kuomba Du´aa.

2. Ubainisho wa sababu ya kutofanya hivyo.

3. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aombe kwa kuazimia.

4. Muombe Allaah lolote utakalo.

5. Sababu ya jambo hili (kwa kuwa Allaah hakuna amtenzae nguvu).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

225

Mlango Wa 54

Mtu Asiseme “Mja265 Wangu Au Kijakazi Wangu”

Katika Swahiyh (Muslim) kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu´anhu) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)kasema:

“Asiseme mmoja wenu: “Mlishe Rabbaka mola wako”, “Mtawadhishe Rabbakamola wako”, bali na aseme badala yake: “as-Sayyidiy bwana wangu au Maulaaibosi wangu”, na wala asiseme mmoja wenu: “´Abdiy mja wangu wakiume au´Amatiy mja wangu wakike, na aseme badala yake: “Fataai,266 Fataatiy267 kijanachangu na Ghulaamiy mvulana wangu.”268

Ufafanuzi:Katika matamshi ambayo yanakatazwa kutokana na Shirki na lafdhi yaliyo nayo ni mtukusema “mja wangu” na “kijakazi wangu”, kwa kuwa uabudiwa ni wa Allaah (Subhaanahuwa Ta´ala). Watu wote ni waja wa Allaah, sawa wanaume na wanawake. Hivyo, haitakiwikuleta matamshi ambayo ndani yake kuna uabudiwa kwa kiumbe. Kule kutamka tu haijuzuhata kama mtu hakukusudiwa maana yake. Na mafunzo haya ni kwa ajili ya kuwawekawatu mbali kabisa na Shirki na wawe na ukamilifu wa Tawhiyd. Ikiwa matamshi kama hayatu yanakatazwa kwa ajili ya kuihami Tawhiyd, vipi kwa Shirki ya wazi katika kuomba kwaasiyekuwa Allaah, kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah? Badala ya mtu kusema “mjawangu” aseme “kijana changu”. Kijana changu maana yake ni mtumishi. Kuna matamshiyasiyokuwa ndani yake na utata.

Hali kadhalika haijuzu kumwambia mtumishi “mlishe mola wako”, “mtawadhishe molawako”- maana ya mola wako hapa yaani ni bwana wako. Kwa kuwa kunaposemwa neno

265 ´Abdiy mja wangu au mtumwa wangu266 Akiwa ni mwanaume267 Akiwa ni mwanamke268 Mvulana wangu

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

226

“Mola” ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Ndiye Mola wa walimwengu. Haya ni matamshiya Shirki katika Rubuubiyyah. Mtu anatakiwa kujiepusha na matamshi kama haya.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Makatazo ya kusema “mja wangu-wakike” au “mja wangu-wakiume”.

2. Asiseme mtu “mola wangu”, na wala asiambiwe “mlishe mola wako.”

3. Kumfunza bwana badala yake aseme “kijana changu” (badala ya kusema mja wangu).

4. Kumfunza mtumishi badala yake aseme “bwana wangu” na “bosi wangu”.

5. Hekima ya masisitizo (makatazo) haya ni kuihakikisha Tawhiyd hata katika matamshi.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

227

Mlango Wa 55

Harudishwi Mwenye Kuomba Kwa Jina La Allaah

Kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kasema, kasema Mtumewa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Anayeomba kwa Jina la Allaah mpeni, anayejikinga kwa Jina la Allaahmkingeni, anayekuiteni muitikieni, anayekufanyieni wema mlipeni wema. Naikiwa hamkupata cha kumlipa muombeeni Du´aa mpaka muone ya kuwammemlipa.”

(Kaipokea Abuu Daawuud na an-Nasaa´iy kwa isnadi Swahiyh)

Ufafanuzi:Katika ukamilifu wa Tawhiyd ni kwamba yule anayeomba kwa Jina la Allaah ajibiwe nakupewa maombi yake ilimradi maombi yake sio kitu cha haramu au kisichojuzu, ikiwaanaomba kitu ambacho kinaruhusiwa inatakiwa kujibiwa (kupewa) kumuadhimisha YuleAliyeomba kwa Jina Lake Naye ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Katika kumuadhimishaAllaah ni kumjibia yule anayeomba kwa Jina la Allaah kwa sharti mbili:

- Iwe anachokuomba ni kitu kinachojuzu.

- Uwe ni mwenye uwezo wa kumpa kitu hicho.

Na kuomba kwa Jina la Allaah maana yake ni kumuapia Allaah.

Vile vile mwenye kusema “najikinga kwa Allaah kwa shari yako, najikinga kwa Allaah kwakadha, najikinga kwa Allaah kwa madhara yako” n.k., unatakiwa kumkinga, kwani kufanyahivyo ni kumuadhimisha Allaah aliyejikinga Naye. Na hili ni katika ukamilifu wa Tawhiyd.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

228

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Kumkinga yule mwenye kujikinga kwa Jina la Allaah.

2. Kumpa mwenye kuomba kwa Jina la Allaah.

3. Kuitikia wito wake.269

4. Kulipiza wema kwa aliyekufanyia wema.

5. Ikiwa mtu hawezi kulipiza wema basi Du´aa ni fidia yake.

6. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “... mpaka muone ya kuwa mmemlipa.”

269 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hili linahitajia ufafanuzi; wito unaweza kuwa wajibu, mustahabah auharamu. Ikiwa ni sehemu ya maovu na mambo ya haramu na wala huwezi kuondosha maovu haya,itakuwa ni haramu kwako kumwitikia wito wake.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

229

Mlango Wa 56

Hakuombwi Kwa Uso Wa Allaah Isipokuwa Pepo

Kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea, kasema Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna kinachoombwa kwa Uso wa Allaah isipokuwa Pepo.”270

(Kaipokea Abuu Daawuud)

Ufafanuzi:Kuomba kwa Uso wa Allaah jambo jengine zaidi ya Pepo haijuzu hili kabisa. Hakuombwikwa Uso wa Allaah mambo ya kidunia. Hakuombwi kwa Uso wa Allaah ispokuwa Pepo auyanayomfikisha mtu Peponi. Uso wa Allaah hakuombwi kwa ajili Yake mambo ya kidunia.Sababu ya kutoomba kwa Uso wa Allaah kitu kingine zaidi ya Pepo ni kwa kuwa kunaudhalili kwa kufanya hivyo kwa Uso wa Allaah. Uso Mtukufu wa Allaah ni zaidi ya hayo.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Makatazo ya kuomba kwa Uso wa Allaah zaidi ya lengo kubwa (Pepo).

2. Uthibitisho wa Sifa ya Allaah kuwa na Uso.

270 Tanbihi muhimu! Shaykh Fawzaan aliulizwa swali lifuatalo: “Ulisema katika darsa iliopita kuwahaijuzu kuomba kwa Uso wa Allaah (mambo) ya kidunia. Vipi ikiwa nitamuomba Allaah kwa Nuruya Uso Wake jambo la kidunia na Aakhirah? Akajibu: “Ukimuomba Allaah jambo katika mambo yadunia na Aakhirah hakuna ubaya. Kilichokatazwa ni kuomba cha kidunia tu. Hilo ndo halijuzu.” (ad-Dur an-Nadhwiyd fiy Ikhlaasw Kalimaat at-Tawhiyd)

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

230

Mlango Wa 57

Yaliyokuja Kuhusu “Lau...“

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

يقولون لو كان لنا من الأمر شيء ما قتلنا هاهنا

“Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa.”(al-´Imraan 03:154)

Kauli Yake:

أطاعونا ما قتلوا وا لودقعو انهموإخقالوا ل ينالذ

“Wale ambao waliwaambia ndugu zao nao wakakaa (hawakwenda vitani):“Lau wangelitutii basi wasingeliuawa”.” (al-´Imraan 03:168)

Imepolekewa katika Swahiyh (Muslim) kutoka kwa Abuu Hurayrah (RadhiyaAllaahu ´anhu) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) kasema:

“Pupia kwa yale yanayokufaa271 na muombe Allaah Akusaidie na walausishindwi. Na utapofikwa na jambo usiseme: “Lau ningelifanya kadhaaingelikuwa kadhaa na kadhaa”, lakini badala yake sema: “Hivi ndivyoAlivyokadiria Allaah na Hufanya Atakavyo,272 kwani hakika ya “lau... ”hufungua matendo ya Shaytwaan.”

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah mbili katika Suurat al-´Imraan. (03:154) na (03:168)

271 Kwa kesho Aakhirah272 “Qaddara Allaahu wa mashaa fa´al”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

231

2. Makatazo ya wazi ya kusema: “Lau... “ unapofikwa na jambo.

3. Sababu ya hilo ni kwa kuwa hilo linafungua matendo ya Shaytwaan.

4. Muelekezo wa kusema maneno mazuri (badala ya lau).

5. Maamrisho ya kupupia kwa yanayofaa (Aakhirah) pamoja na kuomba msaada kwaAllaah.

6. Makatazo ya kufanya kinyume na hivyo (kuomba msaada kwa asiyekuwa Allaah) ambaloni udhaifu.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

232

Mlango Wa 58

Makatazo Ya Kutukana Upepo

´Ubayd bin Ka´b (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Msitukane upepo, mtapoona mnachokichukia semeni:

“Ee Allaah! Tunakuomba kheri za upepo huu, na kheri zilizomo ndani yake,na tunajikinga Kwako na shari ya upepo huu na shari ya shari uliyoamrishia.”

(Kaisahihisha at-Tirmidhiy)

Ufafanuzi:Mlango huu ni kama milango mingine iliyo kabla, ndani yake kuna makatazo yakunasibisha mambo kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa kuwa AllaahNdiye Mwenye Kuendesha ulimwengu na Yeye Ndiye Mwenye kuleta upepo. Anauleta kwakheri na kwa shari. Hivyo, upepo ni wenye kuendeshwa na haujiendeshi, kwa kuwa niupepo ni kiumbe katika viumbe vya Allaah na unaenda kwa amri ya Allaah. Ukija kwashari, hii ni katika amri ya Allaah (Ta´ala). Hivyo wewe usitukane au kuulaumu, kwa kuwahilo linamrudilia Allaah Ambaye Kauuamrisha, Kuutuma na Kuundesha. Ni wajibu kwawaja warejee kwa Allaah na Awaomba Allaah Awaepushe na shari yake na awape kheriyake. Kama jinsi upepo unaweza kuja kwa shari, vile vile unaweza kuja kwa kheri. Hili nikatika ukamilifu wa Tawhiyd, na ndio maana mwandishi akawa ameweka mlango huukatika Kitabu cha Tawhiyd. Kutukana upepo ni katika mambo yanayopunguza Tawhiyd. Nahapa ni pindi mtu anapoitakidi kuwa Allaah Ndiye Mwendeshaji lakini akawa mwenyekulaumu upepo kwa njia ya kuuchukia. Ama ikiwa anaitakidi ya kwamba upepo ndiowenye kuumba, na ndio unaendesha mambo haya, hii ni Shirki kubwa. Lakini watu wengiwako katika aina ya kwanza (ya kuutukana na kuulaumu upepo). Kwa hiyo, wajibu kwawatu kurejea kwa Allaah na wajue kuwa yale yanayowasibu ni kwa sababu ya madhambiyao na si kwa sababu ya upepo tu. Watubu kwa Allaah na wamuombe msamaha.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

233

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Makatazo ya kutukana upepo.

2. Maelekezo ya maneno yenye faida pindi mtu anapoona anachokichukia (katika upepo).

3. Upepo ni wenye kuamrishwa (kwa amri ya Allaah).

4. Unaweza kuamrishwa kwa kheri na unaweza kuamrishwa kwa shari.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

234

Mlango Wa 59

Kauli Ya Allaah Ta´ala

ةيلاهالج ق ظنالح رغي ون باللـهظني يقولون هل لنا من الأمر من شيء◌ ◌لـهل كله رقل إن الأم يخفون في أنفسهم ما لا ◌ون لكدبي ◌ء مير شالأم نا مكان لن قولون لوايناها هلنا قت قل لو كنتم في بيوتكم لبرز الذين كتب عليهم القتل إلى ◌هماجعضم ◌ي قلوبكما فم صحميلو وركمدي صا فم اللـه يلتبيلو واللـه عليم بذات الصدور◌

”Wakamdhania Allaah pasi na haki dhana ya kijahili; wanasema: “Je, tunaamri yoyote sisi katika jambo hili?” Sema: “Hakika amri yote ni ya Allaah”Wanaficha katika nafsi zao yale wasiyokubainishia. Wanasema: “Lautungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa”. Sema:“Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale ambaowameandikiwa kuuwawa kwenye mahali pa kuangukia.” Ili Allaah Ayajaribuyale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyozenu. Na Allaah ni ‘Aliym kwa yaliyomo vifuani. (Mjuzi).” (al-´Imraan 03:154)

Kauli Yake:

الظانني باللـه ظن السوء عليهم دائرة السوء◌

”Wanaomdhania Allaah dhana ovu utawafikia mgeuko uovu.” (al-Fath 48:06)

Kasema Ibn al-Qayyim (Rahimahu Allaah) kuhusu Aayah ya kwanza:

“Imefasiri dhana hii kuwa ya kwamba Yeye (Subhaanahu) HatomnusuruMtume Wake na kwamba amri yake itaangamizwa.

“Na imefasiriwa ya kwamba yaliyomsibu haikuwa kwa Qadar ya Allaah nakwa Hekima Yake.”

“Na imefasiriwa kwa kupinga Hekima na kupinga Qadar na kukanushakutimia kwa amri ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nakwamba itazidi dini zingine zote. Na hii ndio adh-Dhwan as-Saui273 waliokuwawakiidhania wanafiki na washirikina iliyotajwa katika Suurat al-Fath. Hii

273 Dhana ovu au dhana mbaya

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

235

imekuwa ni adh-Dhwan as-Saui kwa kuwa wamedhania kinyume nayanayolingana na Yeye (Subhaanahu). Bali hayalingani hata na Hekima Yakena Sifa Zake Tukufu na Ahadi Yake ya kweli. Yeyote mwenye kudhani yakwamba batili274 itaizidi haki kwa kuendelea na itasababisha haki kutoweka,au akapinga yaliyotokea ni kwa Qadhwaa na Qadar Yake, au akapinga yakuwa Qadar Yake ni kwa Hekima Yake kubwa inayostahiki kuhimidiwa nakufikiria ya kwamba hayo hutendeka kwa matakwa ya kiholela: Basi hayandio dhana ya wale waliokufuru. Basi adhabu kali itawapata walewaliokufuru ya Moto.”

Na watu wengi wanamfikiria Allaah dhana mbaya kwa yanayowasibu nakwa Anayowafanyia wengine. Na wala hakuna anayesalimika kwa hiloisipokuwa yule aliyemjua Allaah kwa Majina Yake na Sifa Zake na akajuaumuhimu wa Hekima Yake na Sifa Zake. Hebu yule mwenye akili na apokeenasaha nzuri hizi akiinasihi nafsi yake kwa hili na atubu kwa Allaah nakumuomba msamaha kwa kumdhania Mola Wake dhana mbaya. Lau kamaungeliangalia kwa karibu (watu) ungeliona wako na dhiki na kero kwa Qadarna kuilaumu, na kufikiria ilikuwa inatakikana badala yake kuwa kadhaa nakadhaa. Katika dhana hii, baadhi wana kiwango kidogo na wengine kikubwa.Ichunguze nafsi yako mwenyewe: “Je, wewe umesalimika kwa dhana kamahii? Kasema mshairi: “Ikiwa umesalimika kwayo (dhana ovu/mbaya) basi utakuwaumesalimika kwa msiba mkubwa. La sivyo mimi siwezi kukuthibitishia ya kwambautaokoka”.”

Ufafanuzi:Aayah hii iliteremka katika vita vya Uhud. Wakati Waislamu walipofikwa na majaribio namitihani, wakauawa katika wao waliouawa, wakaongea wanafiki maongezi kama haya nahii ndio ada yao mpaka Qiyaamah kisimame. Ada ya wanafiki ni kwamba wakati wa shidawanaongea yanayowasibu Waislamu, na wala hawasemi kuwa hili limetoka kwa Allaah, auhili ni kwa sababu ya madhambi yetu, na hili lina kheri kwa Waislamu, na kumjengea dhananzuri Allaah, na kwamba Allaah Ataunusuru Uislamu na Waislamu. Wanafiki wanakuwanamna hii daima. Hii ni dalili kuwa kumdhania Allaah vizuri ni katika Tawhiyd na Imani au

274 Shaytwaan, washirikina, makafiri n.k.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

236

Qadhwaa na Qadar. Na kumdhania Allaah vibaya ni kufuru na kupinga Qadhwaa na Qadar.Ndio maana mwandishi akawa ameweka mlango huu katika kitabu cha Tawhiyd.

Hali kadhalika katika suluhu ya Hudaybiyah, wakati makafiri walipowazuia Waislamukuingia Makkah, wanafiki hawakutoka pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) na kwenda Hudaybiyah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka pamojana Waislamu kwenda Hudaybiyah kwa ajili ya kufanya ´Umrah, wanafikiwakajichelewesha, kwa kuwa walidhania ya kwamba Mtume na Waislamu hawatorudia.Kisha alipokuja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakaja ilihali ni wenye kutoaudhuru kwake.

شغلتنا أموالنا وأهلونا فاستغفر لنا ◌ي قلوبهمف سا ليهم متقولون بألسنيل ظنب ي قلوبكمف كذل ينزا ودأب يهملون إلى أهنمؤالمول وسالر بنقلأن لن ي منتوظننتم ظن السوء وكنتم قوما بورا

“Yametushughulisha mali zetu na ahli zetu, basi tuombee maghfirah.” Wanasema kwandimi zao yasiyokuweko nyoyoni mwao. “Bali mlidhania kwamba Mtume na Wauminihawatorudi kwa ahli zao abadan (watauawa vitani). Na wakapambiwa hayo nyoyoni mwao,na mkadhania dhana ovu, na mkawa watu wanaoangamia.” (al-Fath 48:11-12)

Hii yote ni natija ya kumdhania vibaya Allaah (´Azza wa Jalla). Wanasema “Muhammad nawatu wake hawakwenda huko isipokuwa kujiangamiza tu na hawatorudi.” Hawakutoshekana kujibakiza kwao nyuma, bali walikuja na kudanganya.

شغلتنا أموالنا وأهلونا فاستغفر لنا ◌ي قلوبهمف سا ليهم متقولون بألسني ي قلوبكمف كذل ينزا ودأب يهملون إلى أهنمؤالمول وسالر بنقلأن لن ي منتل ظنب

“Yametushughulisha mali zetu na ahli zetu, basi tuombee maghfirah.” Wanasema kwandimi zao yasiyokuweko nyoyoni mwao. “Bali mlidhania kwamba Mtume na Wauminihawatorudi kwa ahli zao abadan (watauawa vitani). Na wakapambiwa hayo nyoyonimwao.” (al-Fath 48:11-12)

Na watu wengi wanamdhania Allaah vibaya isipokuwa watu wa Imani na wakweli waohumdhania Allaah vizuri kwa lolote linalowasibu, na wala hawakati tamaa kwa fadhila naRahmah ya Allaah. Na wakisibiwa na kitu hawalaumu Qadar, bali wanazilaumu nafsi zaona wajirejea kwa waliyoyafanya.

Kwa hiyo, ni wajibu kwa Waislamu wajirejee katika nafsi zao kutokana na yanayopitikakatika ulimwengu huu. Watubu kwa Allaah kwa kuwa na dhana ovu kwa Allaah (´Azza waJalla). Na Muislamu ajue ya kwamba hakupitiki kitu katika ulimwengu huu isipokuwa nikwa sababu ya hekima Yake Kubwa. Kwanza ajue kuwa hakupitiki kitu isipokuwa kwaQadhwaa na Qadar ya Allaah. Na wala asiseme sababu ya hili ni kwa kuwa fulanihakufanya vizuri jambo kadhaa na laiti ningefanya hivi na hivi ingekuwa hivi n.k., balibadala yake asema: “Qadar Allaahu wa mashaa fa´al”.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

237

- Jambo la kwanza watakiwa kujua kuwa hili ni kutokana na Qadhwaa na Qadar yaAllaah.

- Jambo la pili ujue kuwa hili ni kwa Hekima Kubwa ya Allaah.

- Jambo la tatu ujue kuwa hili ni kutokana na kasoro kwako au kwa wengine.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-´Imraan. (03:154)

2. Tafsiri ya Aayah ya Suurat al-Fath. (48:06)

3. Maelezo ya kuwa dhana ovu kwa Allaah ni ya aina isiyohesabika.

4. Hasilimiki kwa hilo isipokuwa yule aliyejua Majina na Sifa za Allaah.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

238

Mlango Wa 60

Yaliyokuja Kwa Mwenye Kupinga Qadar

Kasema Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Na naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Ibn ´Umar iko Mikononi Mwake, laumtu atakuwa na dhahabu mfano wa mlima wa Uhud kisha akazitoa katikanjia ya Allaah Hatomkubalia Allaah kutoka kwake mpaka aamini Qadar.”Kisha akatolea dalili kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):“Imani ni: 1) Kumuamini Allaah, 2) Malaika Wake, 3) Vitabu Vyake, 4)Mitume Wake, 5) Siku ya Mwisho na 6) kuamini Qadar; kheri na shari yake.”

(Kaipokea Muslim)

Imepokelewa kutoka kwa ´Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Alimwambia mwanawe: “Ewe mwangu! Hakika hutopata ladha ya Imanimpaka kwanza ujue kuwa yaliyokufika275 hayakuwa yakukukosa, nayaliyokukosa hayakuwa yakukufika. Nimemsikia Mtume wa Allaah (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Kitu cha kwanza Alichoumba Allaah nikalamu, Akaiambia: “Andika.” Ikasema: “Ee Mola Wangu na niandike nini?”Akasema: “Andika makadirio ya kila kitu mpaka kitaposimama Qiyaamah.”Ewe mwanangu! Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wasalla) akisema: “Yule atakayekufa akiamini kinyume na hivi, basi huyo sikatika mimi”.”

Katika upokezi wa Ahmad:

“Hakika kitu cha kwanza Alichoumba Allaah ni kalamu. Akaiambia:“Andika.” Basi ikaandika katika wakati ule yote yatayokuwepo mpaka siku yaQiyaamah.276

275 Yaliyokusibu276 Shaykh Fawzaan anasema: ”Kauli ya sahihi (yenye nguvu) kitu cha kwanza Alichoumba Allaahkatika viumbe ni ´Arshi. Kisha ndo Akaumba kalamu baada ya ´Arshi na Akaiamrisha kuandikayatayokuwepo.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

239

Katika upokezi mwingine kutoka kwa Ibn Wahb ambaye amesema yakwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Yeyote ambaye haamini Qadar; kheri na shari yake Allaah Atamchoma kwaMoto.”

Imepokelewa katika Musnad Ahmad na Sunan kutoka kwa Ibn ad-Daylamiyya kwamba kasema:

“Nilimuendea ´Ubay bin Ka´b (Radhiya Allaahu ´anhu) na kumwambia:“Katika nafsi yangu kuna kitu277 kutokana na Qadar. Tafadhali nieleze kwakitu pengine Allaah Akakiondosha moyoni mwangu.” Akasema: “Lau utatoadhahabu mfano wa sawa na mlima wa Uhud, Allaah Hatozikubali kutokakwako mpaka uamini Qadar. Na ujue ya kwamba yaliyokupata hayakuwayenye kukukosa, na yaliyokukosa hayakuwa yenye kukupata. Na lau utakufaukiwa na Imani kinyume na hii utakuwa mmoja katika watu wa Motoni.”Nikamuendea ´Abdullaah bin Mas´uud, Hudhayfah bin al-Yamaan na Zaydbin Thaabit (Radhiya Allaahu ´anhum ajmaa´iyn) na wote wamenieleza kwamfano wa hayo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)”.”

(Hadiyth ni Swahiyh kaipokea al-Haakim katika Swahiyh yake)

Ufafanuzi:Mlango huu unazungumzia matishio yaliyokuja kwa haki yao na kwamba hiyo ni kasorokatika Imani yao. Mnasaba wa kutaja mlango huu ni kuwa, yule mwenye kupinga Qadarkamshirikisha Allaah na kadai kuwa kuna anayeumba pamoja na Allaah (Subhaanahu waTa´ala) na kuendesha mambo pamoja na Allaah. Na akadai kuwa Allaah Hajui mambo nawala hakuyaandika katika Lawh al-Mahfuudh. Na hii ni Shirki katika Rubuubiyyah. Shirkikatika utiifu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na ndio maana Qadar ikaja katika Hadiythna kwamba ni nguzo ya sita katika nguzo za Imani.

Allaah Katueleza ya kwamba hakupitiki kitu katika ulimwengu huu isipokuwa AmeshakijuaAllaah, na kukiandika katika Lawh al-Mahfuudh, Akakiumba na Kutaka kiwe (Subhaanahuwa Ta´ala).

277 Mashaka, wasiwasi

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

240

ما أصاب من مصيبة في الأرض ولا في أنفسكم إلا في كتاب من قبل أن نبرأها

”Hakuna msiba wowote unaokusibuni katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umokatika Kitabu (Lawhum-Mahfuudhw) kabla Hatujauumba (huo msiba).” (al-Hadiyd 57:22)

Ni dalili ioneshayo kuwa Allaah Ndiye Kakiumba na kukifanya kuwepo. Na Imani kuaminiQadhwaa na Qadar kunajumuisha daraja nne:

1. Elimu (Ujuzi). Imani ya kuamini ya kuwa Allaah Anajua kila kitu. Anajua yaliyopo,na yatakayokuwepo, na yasiyokuwepo lau yangelikuwa namna yangevolikuwa.

2. Kuandikwa katika Lawh al-Mahfuudh. Hakuna kitu kinachopitika katika yalewanayoyachukia watu au kuyapenda ya kheri au shari isipokuwa yameshaandikwakatika Lawh al-Mahfuudh. Ambapo Allaah Kaandika ndani yake Makadirio ya vitu.

3. Utashi wa Allaah. Allaah Kayataka mambo haya (yawepo), na hakukuwi kituasichokitaka Allaah.

4. Uumbaji. Allaah Ndiye Kakiumba na Kavifanya kuwepo. Hakuna kitu katikaulimwengu huu isipokuwa Kakiumba Allaah na kukifanya kuwepo, hana mshirikakatika Kuumba Kwake na Kuendesha Kwake mambo.

Hizi ndio daraja za kuamini Qadhwaa na Qadar na zimechukuliwa kutoka katika Kitabu naSunnah. Anayepinga kitu katika daraja hizi, hawi mwenye kuamini Qadhwaa na Qadar.

Qadariyyah kundi linalopinga Qadar lilijitokeza wakati wa Maswahabah, ´Ibn ´Umar(Radhiya Allaahu ´anhumaa) alikutana nao. Walipokuja watu kumuuliza kuhusiana nakundi hili na wanavoamini kuhusiana na Qadar ndio akawa amesema maneno haya. Hii nidalili kuwa mtu haamini Imani sahihi mpaka aamini Qadhwaa na Qadar.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Ubainisho wa uwajibu wa kuamini Qadar.

2. Ubainisho wa namna gani ya kuamini Qadar.278

3. Uporomokaji (kuharibika kwa) matendo kwa yule ambaye hakuiamini (Qadar).

4. Hakuna yeyote anayepata ladha ya Imani mpaka aiamini.

5. Kutajwa kitu cha kwanza Alichoumba Allaah.

6. Kalamu iliandika makadirio yote kuanza wakati huo mpaka kitaposimama Qiyaamah.

278 Shaykh Fawzaan anasema: “Yaani maana yake ni kule kujua kuwa, yaliyokufika hayakuwayakukukosa na yaliyokukosa hayakuwa yakukufika.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

241

7. Kujiweka kwake mbali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yule asiyeiamini.

8. Ada ya Salaf kuondosha shubuha kwa kuwauliza wanachuoni.

9. Wanachuoni wamewajibu kwa yale yaondoshayo shubuha yao (kuhusu Qadar) kwakuwapa dalili ya maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

242

Mlango Wa 61

Yaliyokuja Kuhusu Watengeneza Picha

Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtume waAllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Allaah Kasema: “Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule ambaye anajaribukuumba mfano wa viumbe Vyangu? Waache waumbe chembe, au waumbenafaka, au waache waumbe nafaka ya shayiri.'"

(Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

Wamepokea pia kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) ya kwambaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu watakaokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale wanaoigauumbaji wa Allaah.”

Wamepokea pia kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) yakwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)akisema:

“Kila mwenye kutengeneza picha atakuwa Motoni. Ataijaalia kila pichaaliyoitengeneza nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake katika Moto wa Jahannam.”

Wamepokea (al-Bukhaariy na Muslim) tena kutoka kwa Ibn ´Abbaas (RadhiyaAllahu ´anhumaa) Hadiyth ya Marfu´:

“Atakayetengeneza picha duniani atakalifishwa kuitia roho na hatowezakufanya hivyo.”

Muslim kapokea kutoka kwa Abuu Hayyaaj (al-Asadiy) ya kwamba ´Aliy(Radhiya Allaahu ´anhu) alimwambia:

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

243

“Hivi nikutumie ujumbe kama vile alivyonituma Mtume wa Allaah (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam)? Nao ni kuwa usiache picha hata moja isipokuwaumeifutilia mbali wala kaburi lililoinuka isipokuwa ulisawazishe.”

Ufafanuzi:Mlango huu ni kuhusu matishio makali yaliyokuja kuhusu wetengeneza picha na makatazoya picha. Hilo, ni kwa sababu picha ni katika njia zinazopelekea katika Shirki.Ikiadhimishwa picha na kutundikwa – na khaswa picha za wakuu na watu wema –zikatundikwa, hakika ni katika njia zinazopelekea katika Shirki, kama ilivyokuwa katikawatu wa Nuuh.

Hakika mwanzo wa Shirki kabisa ilivoanza katika ardhi ni kwa sababu ya picha. Hapoilikuwa pindi walipokufa watu wema katika watu wa Nuuh ambao walikuwawameshikamana na ´Ibaadah, elimu na Da´wah katika Dini ya Allaah, watu hawawalipokufa wakawa na huzuni kubwa juu yao. Walikuwa katika mwaka mmoja. AkawajiaShaytwaan na kuwaambia: “Tengenezeni sura (picha) zao ili muweze kukumbuka hali zao,na ziweze kuwasaidia katika ´Ibaadah.” Alikuja kwa njia ya kuwapa nasaha kwa madaiyake. Hawakuwaambia: “Tengenezeni ili muwaabudu”, isipokuwa aliwaambia kwa sababuziweze kuwasaidia katika ´Ibaadah na kukumbuka hali zao pindi mtapoona picha zao kishamzitundika katika vikao vyenu. Yeye alikuwa anakusudia Mustaqbal kwa kujua kwakekuwa kizazi hichi hakiwezi kuabudu picha, ndani yake kulikuwemo wanachuoni. Lakinihuko mbele kutakuja kizazi cha wajinga, hapo ndipo akawajia Shaytwaan na kuwaambia:“Hakika mababa zenu hawakutengeneza picha haya isipokuwa ni kwa sababu ziko nabaraka, zinaathiri na kunufaisha.” Akawa amewadanganya namna hii ya kuwa picha hizizinanufaisha na kudhuru, kwa kuwa zimenasibishwa kwa ajili ya ´Ibaadah. Hivyo, wakawawameziabudu badala ya Allaah. Hapa ndio Shirki ikawa imeanza.

Allaah Akamtuma Mtume Wake Nuuh (´alayhis-Salaam) awalinganie katika kumuabuduAllaah Pekee asiyekuwa na mshirika na kuacha Shirki. Wakakataa.

كمتهن آلذرقالوا لا تو

”Wakasema: “Msiwaache miungu yenu.” (Nuuh 71:23)

Yaani msiache picha hizi.

ولا تذرن ودا ولا سواعا ولا يغوث ويعوق ونسرا

”Na wala msimwache Waddaa, na wala Su’waa’a, na wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

244

(Nuuh 71:23)

Haya ni majina ya watu wema ambao ziletengenezwa picha zao na wakaabudiwa badala yaAllaah. Na wakausiana kutoacha kuwaabudu na kumuasi Nuuh (´alayhis-Salaam).

Shirki ikawa imezuka kwa ajili ya picha na kuadhimisha picha. Kwa ajili hiyo, ndio maanamwandishi akawa ametenga mlango huu katika kitabu cha Tawhiyd. Kwa kuwa kitabu hichikinabainisha Tawhiyd na Shirki, sababu za Shirki na njia zake. Hii ndio sababu, ya kwambapicha ni katika njia za Shirki, kwa kuwa ni kuiga viumbe vya Allaah (´Azza wa Jalla). Kwakuwa mtengeneza picha anataka kupatikane sura inayofanana na sura Aliyoiumba Allaah.Anajaribu kufanya hivi. Kuna ushirikisho wa Allaah katika jambo ambalo ni maalum KwakePekee ambalo ni Kuumba. Kwa kuwa hakuna awezae kuumba isipokuwa Allaah (´Azza waJalla). Huyu mtengeneza picha anajaribu kushirikiana na Allaah katika Kuumba Kwake nakupatikane picha inayofanana na Aliyoumba Allaah. Hili ni jambo la khatari.

Na wala haijuzu kufanya picha kwa viumbe vyenye roho. Ama kufanya picha ya viumbevisivyokuwa na roho, kama miti, nyumba, gari na kadhalika hakuna ubaya. Kwa kuwahakuna kipingamizi. Makatazo ni kufanya picha ya kiumbe chenye roho katika wanaadamu,minyama na kila kiumbe chenye roho. Haya ndio yamekatazwa. Hii ndio sababu ya kutajwamlango huu katika kitabu cha Tawhiyd kwa kuwa picha ni katika njia zinazopelekea katikaShirki, kama ilivokuwa katika watu wa Nuuh.

Hadiyth “Allaah Kasema: “Ni nani dhalimu...”, yaani hakuna yeyote ambaye ni dhalimumkubwa kama mtu huyu. Kwa kuwa Shirki ndio aina kubwa ya dhuluma.

يمظع لظلم كرإن الش

”Hakika shirki ni dhulma kubwa mno!” (Luqmaan 31:13)

Na hii ni katika njia ya Shirki. Yaani mtu huyu anatengeneza picha na anataka kutoka katikapicha hiyo kufananisha na viumbe vya Allaah (´Azza wa Jalla). Picha hiyo anaifanya kuwana kiwiliwili, uso, macho, mdomo n.k. kama kilivo kiumbe cha Allaah (´Azza wa Jalla).Namna hii. Yaani anaumba sura, anataka kuumba kama kiumbe cha Allaah. Huyu ndiyedhalimu mkubwa. Mtengeneza picha ndiye dhalimu mkubwa. Allaah Atukinge. AllaahKawapa changamoto na Kuwaambia: “Waache waumbe chembe, au waumbe nafaka, auwaache waumbe nafaka ya shayiri.'" Pengine wakatengeneza picha, lakini hawawezikuipulizia roho na kuifanya ikawa kama kiumbe cha Allaah, kinatembea, kinachukua kitu,kinaongea. Hawawezi kufanya hivi. Wanachoweza ni kuigiza tu. Hawawezi hilo.

“Watu watakaokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale wanaoiga uumbaji waAllaah.” Na haya ni matishio mengine. Ya kwanza ilikuwa kwamba wao ndio madhalimuwakubwa, na haya ya pili ni kwamba ndio watu watakaokuwa na adhabu kali siku yaQiyaamah. Mtengeneza picha. Huyu ndiye atakayekuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah,

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

245

kwa kuwa kitendo chake hichi ni njia inayopelekea katika Shirki na kutaka kushirikianapamoja na Allaah katika kuumba Kwake.

“Kila mwenye kutengeneza picha atakuwa Motoni. Ataijaalie kila picha aliyoitengenezanafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam.” Haya ni matishio ya tatu kwawale wenye kutengeneza picha. Kasema kila mtengeneza picha, sawa ikiwa katengeneza(kafanya picha hiyo) kwa kunakili, au katengeneza picha kwa kuchora na mkono, au kwakifaa cha Camera. Kila mtengeneza picha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)hakubagua katika hao yeyote katika wanaotengeneza picha, sawa ikiwa katumia njia yoyoteile ya kufanya picha. Wale wanaosema kuwa picha za Digital Camera hazina ubaya,inawafedhehesha Hadiyth hii. Kwa kuwa Mtume hapa hakubagua. Kasema “kilamtengeneza picha”, kila mwenye kufanya picha bila kujali katumia njia ipi. Kapewa tishio laMoto.

“Kila mwenye kutengeneza picha atakuwa Motoni. Ataijaalia kila picha aliyoitengenezanafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam.” Hili ni tishio la nne.Ataijaalia kila picha aliyoitengeneza kuipa nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Motowa Jahannam. Ataadhibiwa kwa kila picha aliyoitengeneza. Ikiwa alitengeneza picha mia,atazijaalia nafsi elfumoja. Ikiwa alitengeneza picha milioni, atazijaalia nafsi milioni. Kwa kilapicha ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam. Allaah Atukinge. Je, hivikweli kuna matishio makali zaidi ya haya? Mtu yuko katika afya, Alhamdulillaah, asiingizenafsi yake katika yaharamu. Mtu aache mambo ya picha. Hili ni jambo la khatari sana.Kadiri ya idadi ya wingi wa picha ndio jinsi adhabu itakuwa kubwa.

“Atakayetengeneza picha duniani atakalifishwa kuitia roho na hatoweza kufanya hivyo.”Hili ni tishio la tano. Ya kwamba mpiga picha siku ya Qiyaamah ataambiwa: “Kitie rohoulichokiumba, kipulizie roho.” Na hatoweza kufanya hivi kwa kuwa roho.

ويسألونك عن الروح قل الروح من أمر ربي ◌

”Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: “Roho ni katika amri ya Mola wangu.” (al-Israa 17:85)

Hakuna yeyote awazae kupulizia picha roho, akaifanya ikatembea. Hata hivyo, ataamrishwakufanya hivyo kwa ajili ya kutaka kumuadhibu.

“Hivi nikutumie ujumbe kama vile alivyonituma Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam)? Nao ni kuwa usiache picha hata moja isipokuwa umeifutilia mbali wala kaburilililoinuka isipokuwa ulisawazishe.” Hapa kuna ubainisho wa nini kinachofanywa na picha,ya kwamba ni wajibu kuichana chana. Huku ni katika kuondosha munkari. Huu ni Mtumewa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtuma ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu),akamuamrisha na kumuusia asiache picha hata moja isipokuwa aifutilie mbali. Hapakamwambia “usiache picha hata moja” hakukubaguliwa hata moja. Hali kadhalika kaburilililoinuka, yaani kujengewa na kuadhimishwa isipokuwa aliwasawazishe, yaani aliweke

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

246

sawa na alifanye kama makaburi mengine ya Waislamu. Isingewe, isiandikwe kitu,isipambwe na kadhalika. Kwa kuwa hii ni njia inayopelekea katika Shirki. Wakati Shiy´ahwaliposhika utawala Misri na katika miji mingi ya Waislamu ndio kukazushwa kuyajengeamakaburi na likaenea hili katika miji ya Waislamu kwa sababu ya Shiy´ah al-Faatwimiyyuun, vinginevyo hili lilikuwa ni jambo lisilojulikana mwanzo wa Uislamu katikakarne bora. Na Shiy´ah bila ya shaka ni kampeni katika kampeni za mayahudi wanaotakakuuharibu Uislamu kwa madai ya kutumia jina la Uislamu, wanasema ni kuwapendaWaislamu na kuhifadhi athari zao na mfano wa madai kama hayo katika shubuha zaKishaytwaan. Na anayewakataza wanasema huyu ni Wahhaabiy, hii ndio Dini yaMuhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na sio Dini ya Wahhaabiyyah bali ni Dini yaMuhammad na yeye ndiye kaamrisha hili.

Hizi zote ni nususi kuhusu picha, na Hadiyth hizi zipo katika Swahiyh al-Bukhaariy naMuslim. Hakuna njia ya kuwekea shaka (Hadiyth hizi), ni Hadiyth maana yake iko wazikabisa. Lakini wanachuoni wa sasa wahakiki wamegabua zile picha ambazo ni za dharurah,itakuwa inaruhusiwa kwa dharurah, kama kwa mfano picha ya kitambulisho n.k. Hizi ni zadharurah kiasi cha dharurah itavyokuwa. Ama picha za kumbukumbu, kuadhimishawapigwa picha n.k., hizi hazijuzu kwa hali yoyote ile. Picha hupigwa wakati wa dharurahtu.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Matishio makali ya adhabu kwa watengeneza (wafanya) picha.

2. Utengenezaji wa picha ni kukosa kuwa na adabu na Allaah. Kama ilivyo katika KauliYake: “Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule ambaye anajaribu kuumba mfano wa viumbeVyangu?”

3. Tanbihi la Uwezo wa Allaah na kutokuwa kwao na uwezo na udhaifu wao (watengenezapicha) kwa Kauli Yake: “Waache waumbe chembe, au waumbe nafaka, au waache waumbenafaka ya shayiri.'"

4. Ubainisho kuwa (watengeneza picha) ndio watu watakaokuwa na adhabu kali (siku yaQiyaamah).279

5. Allaah Ataumba roho Kuipa kila picha na watengeneza picha wataadhibiwa kwa kilapicha waliotengeneza kwenye Moto wa Jahannam.

6. (Mtengeneza picha) atakalifishwa kuipulizia roho kila picha.

279 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hakuna watu wataokuwa na adhabu kali (siku ya Qiyaamah) kamawale wanaotengeneza picha, kwa kuwa wamewafungulia watu mlango wa Shirki.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

247

7. Maarisha ya kuichana kila picha unayoipata.280

280 Shaykh anasema tena: “Ni wajibu kuchana kila picha unayopata, zinazohifadhiwa tu ni zile pichaza dharurah.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

248

Mlango Wa 62

Yaliyokuja Kuhusu Kuapa Sana

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

كمانمفظوا أياحو

”Na hifadhini viapo vyenu (msiape kisha hamtimizi).” (al-Maaidah 05:89)

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema, nimemsikiaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Kumuapia (mnunuzi) kunaweza kumshawishi mnunuzi kununua bidhaa,lakini huondokewa na baraka ya chumo.”281

(Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

Kutoka kwa Salmaan (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume wa Allaah(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Watu aina tatu Hatowasemeza Allaah, Hatowatakasa na watakuwa naadhabu kali: 1) Mzee mziniifu, 2) Mtu fakiri mwenye kiburi na 3) Mtu ambayekamfanya Allaah Ndio bidhaa yake, hanunui isipokuwa kwa yamini yake(kaupa) na wala hauzi isipokuwa kwa yamini yake.”282

(Kaipokea at-Twabaraaniy kwa isnadi Swahiyh)

Na katika Swahiyh (Muslim) kutoka kwa ´Imraan bin Husayn (RadhiyaAllaahu ´anhu) kasema, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)kasema:

281 Shaykh Fawzaan anasema: “Hapa kuna mafunzo ya kutoapa wakati wa kuuza na kununua. Namtu awe mkweli tu bila ya kuwa na haja ya kuapa.”282 Yaani isipokuwa mpaka kwa kuapa. Shaykh Fawzaan anasema: “Mtu huyu ni yule ambayekafanya hawezi kupata chumo lake mpaka kwa kumuapia Allaah. Huu ni upungufu wa Tawhiyd.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

249

“Watu bora katika Ummah wangu ni wa karne yangu, kisha walewatakaowafuatia, kisha wale watakaowafuatia.” Anasema ´Imraan:“Sikumbuki alisema baada ya karne yangu mara mbili au mara tatu. Kishabaada yenu kutakuja watu wanashuhudilia (kutoa ushahidi) bila ya kuombwakufanya hivyo, na ni makhaini na wala hawatoaminiwa, na wanatia nadhiri nawala hawatekelezi na utawadhihirikia unene.”

(Kaipokea Muslim)

Kapokea tena283 kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) yakwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Bora ya watu ni wa karne yangu,284 kisha watakaowafuatia, kishawatakaowafuatia. Kisha watakuja watu inatangulia Shahaadah ya mmoja waoyamini yake, na yamini yake inatangulia Shahaadah yake.”

Ibaarahiym (Nakhiy) kasema:

“Pindi tulipokuwa wadogo walikuwa wakitupiga kwa kushuhudilia na kwakutoa ushahidi.”285

Ufafanuzi:Mlango huu unazungumzia matishio yaliyokuja kuhusu kuapa sana, na vile vile Hadiythzilizokuja kuifasiri Aayah hii. Kaupa ni kukihakikisha kitu kwa kumtaja Anayeadhimishwa.Na kumeshatangulia mlango huku nyuma ya kwamba kuapa kwa asiyekuwa Allaah niShirki, hakuapiwi isipokuwa kwa Jina la Allaah Pekee. Ama viumbe hawafai kuapiwa kwakuwa hawastahiki kuadhimishwa isipokuwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala). Kuapa kwaasiyekuwa Allaah ni Shirki au kufuru.

283 Muslim284 Shaykh Fawzaan anasema: ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema hapa ”watu borani Maswahabah wangu”, na Shiy´ah wanasema ”watu waovu kabisa ni Maswahabah”. TunamuombaAllaah afya.”285 Shaykh anasema tena: ”Salaf walikuwa wakiwalea watoto wao namna hii, wanapomsikia mtotokatoa ushahidi au kaapa wanampiga kwa kumtia adabu, ili asije kuzoe jambo hili na kulichukuliasahali. Hapa tunapata mafunzo ya jinsi ya kuwalea watoto, inapohitajika kumpiga unampiga. Namalezi ya kikafiri ya kimagharibi wanasema kuwa ni makosa kumpiga mtoto na wanapinga kumpigamtoto katika kumlea na kumfunza, mume kwa mke wake akichupa mipaka. Hili ni jambo limethibitikatika Shari´ah na ni malezi (ya Kiislamu).”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

250

Na mtu pindi anapoapa kwa Allaah, kiapo chake hichi anatakiwa akihifadhi naakiadhimishe. Na kutochunga kiapo ni dalili ya unafiki na ni upungufu katika Tawhiyd.Haijuzu kuapa sana, kwa kuwa yule mwenye kuapa sana hatoweza kuchunga viapo vyake.Kuapa sana ni dalili ya uongo. Mtu hatakiwi kuapa isipokuwa wakati wa haja tu, na walaasiape isipokuwa awe ni mkweli. Na ikibidi kuapa, basi ahifadhi kiapo chake. Hii ndio sifaya muumini ya kwamba anamuadhimisha Allaah (´Azza wa Jalla) na ni katika ukamilifu waTawhiyd.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Wasia wa kuhifadhi kiapo.

2. Khabari kwamba kuapa kunashawishi bidhaa kununuliwa lakini (jambo hilo) linaondoshabaraka.

3. Matishio makali kwa yule asiyeweza kuuza wala kununua isipokuwa mpaka aape.

4. Tanbihi ya kuwa kufanya dhambi kwa sababu ndogo au pasina haja, dhambi inaongezwakuwa kubwa.286

5. Kulaumiwa kwa wale wanaoshahidilia na hawakuombwa kufanya hivyo.287

6. Kusifu kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) karne tatu au nne, na akatajayatakayojitokeza baada ya hizo karne.

7. Kulaumiwa kwa wale wanaoshahidilia na hawakushahidiliwa.

8. Salaf kupiga kwao wadogo kwa kushahidilia na kumuadhimisha (Allaah).

286 Shaykh Fawzaan: ”Kijana mwenye shahawa nyingi akifanya kwa mfano Zinaa, inaitwa kuwa nidhambi bali ni katika madhambi makubwa. Lakini mzee mzinifu ambaye ni mzinifu shahawa zake nidhaifu pamoja na hili anafanya Zinaa, hii ni dalili ya kuchukulia kwake sahali Zinaa na kupendakwake Zinaa. Hivyo Zinaa ya mtu mkubwa ni mbaya (yenye madhambi mengi) kuliko Zinaa yamdogo.”287 Shaykh anasema tena: ”Yaani wanachukulia sahali kuapa-apa, ni dalili ioneshayo ya kwambajambo hili ni rahisi kwao.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

251

Mlango Wa 63

Yaliyokuja Katika Dhimma Ya Allaah Na Ya Mtume Wake (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam)

Kauli Yake (Ta´ala):

مدتاهإذا ع اللـه دهفوا بعأوو

“Na timizeni Ahadi ya Allaah mnapoahidi.” (an-Nahl 16:91)

Buraydah (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)anapotawalisha kiongozi kwa jeshi au askari basi humuusia kumcha Allaah nakuwafanyia wema wale Waislamu aliyo pamoja nao. Alikuwa akisema:“Anzeni kupigana288 kwa Jina la Allaah mpigane kwa ajili ya Dini ya Allaah,muueni kila mwenye kumkufuru289 Allaah, piganeni na wala msichukue kitukatika nyara,290 msivunje ahadi (mkataba), kutowakata vinofu vinofu miili yaambao wamekwishakufa, kutowaua watoto, ukikutana na adui wako katikawashirikina mlinganie katika mambo matatu. Ikiwa atakubali kwa lolotekatika haya matatu basi mkubalie na jizuie kumpiga vita: 1) Mlinganie katikaUislamu, akikukubalia hilo muitikie kisha mlinganie katika kuhama kutokakatika miji yao na kwenda katika miji ya Muhaajiruun na uwaambie yakwamba ikiwa watafanya hivyo basi wana haki zote kama walizonazoMuhaajiruun na watakuwa na kama yale waliyonayo Muhaajiruun, wakikataakuhama kutoka katika miji yao waambieni ya kwamba watakuwa na hadhikama ya mabedui wa Kiislamu, watapitishiwa hukumu ya Allaah (Ta´ala)kama inayowapitia waumini na wala hawatopata chochote katika nyara nangawira isipokuwa ikiwa watapigana Jihaad pamoja na Waislamu, ikiwawatakataa 2) waombeni Jizyah,291 wakikubali, wakubalieni na jizuienikupigana nao, na ikiwa watakataa muombeni Allaah msaada na 3) piganeninao. Utapowazingira watu waliomo ngomeni, wakakutaka uwajaalie dhimma

288 Na maadui wa Allaah (Ta´ala)289 Kumkanusha ambaye huyo ni kafiri290 Haijuzu kwa yeyote kuchukua kitu katika nyara kabla ya kugawa ngawira291 Jizyah ni ushuru unaochukuliwa kutoka kwa wakristo na mayahudi wanaoishi chini ya utawala waKiislamu.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

252

(ahadi) ya Allaah na dhimma ya Mtume Wake, usiwajaalie dhimma ya Allaahna dhimma ya Mtume Wake, lakini watie katika dhimma yako na dhimma yaMaswahabah wako. Kwani hakika mtapotaka kuvunja dhimma zenu nadhimma za Maswahabah wenu ni sahali kuliko kuvunja dhimma ya Allaah nadhimma ya Mtume Wake. Na utapowazingira watu waliomo ngomeni nawakakutaka uwateremshe katika hukumu ya Allaah, usiwateremshe katikahukumu ya Allaah, lakini badala yake wateremshe kwa hukumu yako, kwanihakika hujui utapatia kwao hukumu ya Allaah au hapana.”

(Kaipokea Muslim)

Ufafanuzi:Mlango huu unafuatiwa na mlango ulio kabla yake, kwa kuwa mlango ulio kabla yake nikuhusu kuchunga viapo na kutoapa sana. Na mlango huu ni kuhusu kuheshimu dhimma yaAllaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na makusudio ya “dhimma” niahadi inayokuwepo baina ya Waislamu na baina ya makafiri. Ahadi vile vile inachungwa nakuheshimiwa. Anasema (Jalla wa ´Alaa):

وأوفوا بعهد اللـه إذا عاهدتم ولا تنقضوا الأيمان بعد توكيدها

”Na timizeni Ahadi ya Allaah mnapoahidi, na wala msivunje viapo baada yakuvithibitisha.” (an-Nahl 16:91)

Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kaamrisha kutimiza ahadi.

دهفوا بالعأوو إن العهد كان مسئولا◌

”Na timizeni ahadi; hakika ahadi daima ni ya kuulizwa (Siku ya Qiyaamah).” (al-Israa 17:34)

Waislamu wanapopeana ahadi na makafiri, basi Waislamu wanatakiwa kuheshimu ahadi hiina wala wasiivunje, maadamu makafiri wameichunga na Waislamu wanapaswa kuitimizana kuiheshimu, kumuadhimisha Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala). Na yule anayevunja ahadi,huyu hamuheshimu Allaah (´Azza wa Jalla) na wala hamuadhimishi Allaah (´Azza wa Jalla).Ni mapungufu katika Tawhiyd. Na hii ndio sababu ya kuwekwa mlango huu katika kitabucha Tawhiyd.

Makafiri wanapowaomba makafiri kuwapa dhimma ya Allaah na dhimma ya Mtume Wake(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wasiwape hilo, lakini wawape dhimma yao ambayo ni yakiongozi wa Waislamu na wala wasiwape dhimma ya Allaah na ya Mtume Wake. Kwa nini?Kwa kuwa kunaweza kutokea kutotimiza ahadi. Hivyo hili lisiwe katika dhimma ya Allaahna ya Mtume Wake. Ikiwa katika dhimma ya kiongozi, hili ni sahali na afadhali ikiwa

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

253

hakutowezekana kutimiza ahadi kuliko kupewa dhimma ya Allaah na ya Mtume. Kulekiongozi kutoweza kutimiza dhimma yake, hili ni haramu, lakini ni afadhali kuliko kupewadhimma ya Allaah na ya Mtume Wake kisha ikavunjwa. Huku ni kuheshimu dhimma yaAllaah na ya Mtume Wake. Na ni katika ukamilifu wa Tawhiyd.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Tofauti kati ya dhimma ya Allaah na ya Mtume Wake na dhimma ya Waislamu.

2. Mwelekeo wa kuchagua kati ya mambo mawili lililo na madhara (khatari) kidogo.

3. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Anzeni kupigana kwa ajili ya Dini yaAllaah.”

4. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Muueni mwenye kumkufuru Allaah.”

5. . Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Muombeni msaada Allaah na piganeninao.”

6. Tofauti kati ya Hukumu ya Allaah na hukumu ya wanachuoni.

7. Swahabah anaweza kuhukumu wakati wa haja, kwa hukumu asiyojua imeafikiana nahukumu ya Allaah au hapana.

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

254

Mlango Wa 64

Yaliyokuja Kuhusu Kumuapia Allaah

Kutoka kwa Jundub bin ´Abdillaah (Rahiya Allaahu ´anhu) kasema, amesemaMtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kuna mtu alisema: “Wallaahi! Allaah Hatomsamehe fulani.” Akasema Allaah(´Azza wa Jalla): “Ni nani huyo anayeniapia ya kwamba sintomsamehefulani?” Mimi nimemsamehe292 na nimeziporomosha ´amali zako.”293

(Kaipokea Muslim)

Katika Hadiyth nyingine kutoka kwa Abuu Hurayrah (Rahiya Allaahu ´anhu)ya kwamba mtu aliyesema hivi alikuwa ni mwenye Imani mwenyekuamuabudu Allaah. Anasema Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Kaongea kwa maneno ambayo yameiharibu dunia yake na Aakhirah yake.”

Ufafanuzi:Kumuapia Allaah, ya kwamba mtu atafanya kadhaa na kadhaa, au hatofanya kadhaa nakadhaa kumegawanyika katika mafungu mawili:

1. Fungu la haramu na ambalo linaiharibu Tawhiyd.

Huku ni mtu kuapa ya kwamba Hatowasamehe waja Wake. Huku ni kuzuia fadhila zaAllaah (´Azza wa Jalla) na kutokuwa na adabu na Allaah. Na Shaykh kaweka mlango huukwa ajili ya fungu hili. Kwa kuwa aidha linapingana au kuipunguza Tawhiyd. Na katika

292 Huyo fulani293 Yaani ´amali za huyo aliyemuapia Allaah, Allaah Kaziporomosha (kuziharibu) zote kabisa. ShaykhFawzaan anasema: ”Hichi ni kisa cha watu wawili katika Baniy Israaiyl, mmoja wao alikuwa namsimamo anamwabudu Allaah, na mwingine alikuwa ni muumini lakini alikuwa na baadhi yamambo anakwenda kinyume na maasi chini ya Shirki. Huyo mtu mwema alikuwa anamkataza maasihayo, kisha anamuona mara ya pili akimkataza, alipoona haachani na madhambi hayo akapatwa nakhasira nyingi na kupindukia mipaka na kumwambia: ”Wallaahi Allaah Hatokusamehe na walaHatokuingiza Peponi.” Allaah Akawa Amemkasirikia na kusema: “Ni nani huyo anayeniapia yakwamba sintomsamehe fulani?” Allaah Anamsamehe mwenye kutubia, si hivyo tu, bali Anamsamehehata yule asiyetubia mwenye madhambi chini ya Shirki.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

255

hichi kinazungumzia mambo haya, mambo ambayo yanayoiharibu na kuiporomoshaTawhiyd na kubainisha mambo ambayo yanaipunguza, sawa katika matendo au kauli.

2. Fungu la pili ni kuapa kwa Allaah kuwa Atawafanyia kheri waja Wake,Atawanusuru waumini, Atateremsha mvua n.k.

Hili linajuzu na ni katika ukamilifu wa Tawhiyd. Kwa kuwa ni kuwa na dhana nzuri kwaAllaah (´Azza wa Jalla).

Mlango huu unakusudia aina ya kwanza ambayo inaiharibu Tawhiyd na ni kukosa kuwa naadabu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Ni juu ya Muslamu auhifadhi ulimu wake na wala asiongei isipokuwa mambo ya kheri tu,maneno mazuri na yenye faida, auhifadhi ulimi wake na usengenyaji na kueneza uvumi,auhifadhi ulimi wake kutokuwa na adabu na Allaah (´Azza wa Jalla). Mtu ahifadhi ulimikwa kuwa ni kitu cha khatari. Hapa tunapata mafunzo ya kuihifadhi Tawhiyd.

Masuala muhimu yaliyomo:1. Tahadhari ya kumuapia Allaah.

2. Moto uko karibu sana nasi kuliko kamba za viatu vyetu.294

3. Pepo ni mfano wa hivo.

4. Katika Hadiyth hii kuna ushahidi wa kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)(katika Hadiyth nyingine): “Hakika mtu atatamka neno, likawa nimemridhisha Allaah naAllaah Akamsamehe kwalo. Na likawa ni lenye kumkasirikisha Allaah na Allaah Akawa nimwenye kumkasirikia.”295

5. Wakati mwingine mtu anaweza kusamehewa kwa sababu ya jambo ambalo kwake yeyelikawa ni lenye kumchukiza zaidi.

294 Shaykh Fawzaan anasema: ”Mtu anaweza kutamka neno dogo akaingia nalo Motoni. Au akaongeaneno zuri akaingia nalo Peponi.”295 Shaykh anasema tena: “Mfano wa mtu huyu ni yule anayeongelea Majina na Sifa za Allaah,akakanusha na akabadilisha maana yake sahihi, huyu anaongea kuhusu Allaah pasina elimu naanamkosea adabu Allaah (´Azza wa Jalla).”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

256

Mlango Wa 65

Haombwi Allaah Kwa Viumbe Vyake

Imepokelewa kutoka kwa Jubayr bin Mutw´im (Radhiya Allaahu ´anhu)kasema:

“Alikuja bedui kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)na kumwambia: “Ewe Mtume wa Allaah! Watu wanaangamia, watoto wananjaa na mali zinaagamia. Muombe Mola Wako Atunyweshelezee. Hakika sisitunaomba maombezi kwa Allaah kupitia kwako na kwa maombi yako kwaAllaah.” Akasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “SubhaanaAllaah! Subhaana Allaah!” Hakuacha kusabihi mpaka likajulikana hilo katikanyuso za Maswahabah wake. Kisha akasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam): “Ole wako! Je, unamjua ni nani Allaah? Hakika Jambo la Allaah nikubwa zaidi kuliko hivyo. Hakika haombwi Allaah kwa yeyote yule katikaviumbe Vyake.”

(Kaipokea Abuu Daawuud)

Ufafanuzi:Shafaa´ah uombezi umethibiti katika Qur-aan kwa aina mbili:

1. Uombezi uliothibiti. Huu ni uombezi baada ya idhini ya Allaah kwa watu waTawhiyd.

2. Uombezi uliokanushwa. Huu ni uombezi kwa washirikina na makafiri. Uombeziwao haukubaliwi kwa Allaah (´Azza wa Jalla).

Mtu anaweza kuombea kwa Allaah kwa idhini Yake, na wala Yeye Allaah Haombwi kwakupitia viumbe Vyake, kwa kuwa huku ni kukosa kuwa na adabu kwa Allaah. Hililinapingana na kumuadhimisha au linapunguza kumuadhimisha Allaah (´Azza wa Jalla)jambo ambalo ni katika haki ya Tawhiyd. Ikiwa utamuomba Allaah kwa kupitia viumbe,utakuwa umemkosea adabu Allaah (´Azza wa Jalla) na umemuadhimisha kiumbe. Na hilihaliendani na Tawhiyd; Ukubwa na Uwezo wa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala).

Huyu bedui alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumshtakiayaliyowafika watu. Na hili ni jambo lisilokuwa na ubaya ndani yake. Kauli yake bedui:

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

257

“Tunaomba maombezi kwa Allaah kupitia kwako... “ haya ni makosa makubwa na ndiomaana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkataza. Ama kauli yake bedui: “... nakwa maombi yako kwa Allaah”, hili ni sahihi na halina makatazo. Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) anaweza kuombwa amuombe Allaah kwa Du´aa AwanyweshelezeeWaislamu. Hapa kuna dalili na tunapata mafunzo ya kumuadhimisha Allaah (´Azza waJalla) na kwamba haombwi Allaah kwa kiumbe Chake chochote. Kwa kuwa huku ni kamavile kamfanya huyo aliyeomba kupitia kwake ni mkubwa kuliko Allaah (´Azza wa Jalla).

Masuala muhimu yaliyomo:1. Kumkataza kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema: “Hakika sisi tunaombamaombezi kwa Allaah kupitia kwako.”

2. Kubadilika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na kauli hii kulikuwa waziambako kulijulikana hilo kwenye nyuso za Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhu).296

3. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumkataza kwa kauli yake: “Tunaombamaombi yako kwa Allaah.”297

4. Tanbihi ya maana ya “Subhaana Allaah”.298

5. Waislamu wamemuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) awaombee mvua.

296 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa kuna funzo kwa mwanachuoni ya kwamba ni wajibu abadilikeinapopunguzwa haki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kunapofanywa maovu. Muislamuanatakiwa abadilike na akataze jambo hili na alichukie.”297 Shaykh anasema tena: “Hii maana yake ni kuwa bedui anamuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhiwa sallam) awaombee kwa Allaah. Na hili linajuzu.”298 Ametakasika Allaah

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

258

Mlango Wa 66

Yaliyokuja Kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) KuihamiTawhiyd Na Kuziba Njia Za Shirki

Kutoka kwa ´Abdullaah bin ash-Shikhkhiyr (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Nilifuatana na ujumbe wa Banuu ´Aamir kwa Mtume wa Allaah (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) na tukasema: “Wewe ndiye Sayyidnah bwanawetu.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Bwana ni Allaah(Tabaaraka wa Ta´ala).” Tukasema: “Wewe ni mbora wetu kwa ubora na nimkubwa wetu kwa ukarimu.” Akasema: “Semeni kwa kauli yenu au kwabaadhi ya kauli yenu, na wala asikupotezeni Shaytwaan.”

(Kaipokea Abuu Daawuud kwa isnadi nzuri)

Imepokelea kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anhu): “Kuna watuwalisema: “Ewe Mtume wa Allaah, ewe mbora wetu, na mtoto wa mborawetu, na bwana wetu na mtoto wa bwana wetu.” Akasema: “Enyi watu!Semeni kwa kauli yenu na wala asikupotezeni Shaytwaan. Mimi niMuhammad, ni mja wa Allaah na Mtume Wake. Sipendi mnitukuze zaidi yacheo Alichonipandisha Allaah (´Azza wa Jalla).”

(Kaipokea an-Nasaa´iy kwa isnadi nzuri)

Ufafanuzi:Kitabu hichi alichoandika Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah)chote kinazungumzia kuihami Tawhiyd, kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake nakuziba njia zinazopelekea katika Shirki.

Hadiyth ya ´Abdullaah: Hapa ilikuwa wakati imefunguliwa Makkah, kabila la kiarabu –yaani Banuu ´Aamir – likaja kumuahidi utiifu na usikivu (bay´ah) juu ya Uislamu mwishowa uhai wake ndo wakawa wamemwambia hivi. Ni kweli ya kwamba Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni bwana, lakini alichelea uchupaji wa mipaka ambakokunaipunguza Tawhiyd ndio maana akawa amewakataza hilo. Akawaambia “Bwana niAllaah.” Bwana ni Maalik Mwendeshaji, na inamstahiki Allaah Yeye Ndiye Mfalme wawafalme, Mfalme wa waja, Mfalme wa uendeshaji. Ama kunaposemwa bwana wa Banuu

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

259

fulani, hakuna neno. Vinginevyo, kusema “bwana” namna hii tu, hili halijuzu. Mtu badalayake anaweza kusema “bwana wa Banuu fulani”, “bwana wa nchi fulani” kwa kufuatisha(neno mbele ya bwana). Mtu anaweza kusema bwana kumwambia mtu isipokuwa tu ikiwakutakhofiwa kuchupa mipaka hapo itakuwa haijuzu na ikatazwa. Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) alisema:

“Simameni mumpokee bwana wenu.”

Hii ni dalili kuwa inajuzu kumwambia mtu “bwana” isipokuwa tu ikiwa kama kutakhofiwakuchupa mipaka.

Hili ni katika kuziba njia zinazopelekea katika Shirki.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Kuwatahadharisha watu na kuchupa mipaka.

2. Anachotakiwa kusema yule anayeambiwa: “Wewe ni bwana wetu”.

3. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Asiwapotezeni Shaytwaan”, pamoja nakwamba hawakusema isipokuwa haki.

4. Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Sipendi mnitukuze zaidi ya manzilahyangu”299

299 Shaykh Fawzaan anasema: ”Manzilah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kuwa, yeyeni mja wa Allaah asiyeabudiwa, na Mtume Wake asiyekadhibishwa, bali anatiiwa na kufuatwa.Manzilah hizi mbili.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

260

Mlango Wa 67

Yaliyokuja Katika Kauli Ya Allaah Ta´ala

ةاميالق موي هتضا قبيعمج ضالأرو رهقد قح وا اللـهرا قدمو

”Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yoteAtaikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah.” (az-Zumar 39:67)

Kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Alikuja mwanachuoni mmoja katika wanachuoni wa kiyahudi kwa Mtumewa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia: “EweMuhammad! Sisi tunakuta kuwa Allaah Ataziweka mbingu saba juu yaKidole,300 ardhi za saba juu ya Kidole, miti juu ya Kidole, maji na vilivyokochini ya ardhi juu ya Kidole na baki ya viumbe juu ya Kidole. Kisha Atasema:“Mimi Ndiye Maalik.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)akatabasamu mpaka magego yake yakaonekana kwa kusadikisha maneno yahuyo myahudi. Kisha Akasoma:

ةاميالق موي هتضا قبيعمج ضالأرو رهقد قح وا اللـهرا قدمو

”Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yoteAtaikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah.” (az-Zumar 39:67)

Katika upokezi mwingine wa Muslim:

“Na milima na miti juu ya Kidole. Kisha Atavitikisa na Kusema: “Mimi NdiyeMaalik! Mimi Ndiye Allaah.”301

Katika upokezi mwingine wa al-Bukhaariy:

“Allaah Ataziweka mbingu juu ya Kidole, na maji na mimea juu ya Kidole, nabaki ya viumbe juu ya Kidole.”302

300 Cha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)301 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hapa kuna dalili ya Allaah kuwa na Mikono Miwili, Viganja Viwili,Kuliani na Kushotoni, kuwa na Vidole. Hizi ni Sifa za kidhati. Tunazithibitisha kwa Allaah (´Azza waJalla) kama zilivyokuja. Na si kama mikono yetu, vidole vyetu. Hili hatuwezi kulifikiria, hili ni batili.Na mtu huyu hakumthamini Allaah inavyostahiki kumthamini. Sifa Zake hakuna anayezijuaisipokuwa Yeye Mwenyewe.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

261

Katika Muslim, kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kapokeaHadiyth Marfu´:

“Allaah Atazikunja mbingu siku ya Qiyaamah, kisha Atazishika kwa MkonoWake wa Kulia. Kisha Atasema: “Mimi Ndiye Maalik. Wako wapi majabari,wako wapi waliokuwa wakifanya kiburi? Kisha Atazikunja ardhi saba, kishaAtazishika kwa Mkono Wake wa Kushoto na kisha Atasema: “Mimi NdiyeMaalik. Wako wapi majabari na wako wapo waliokuwa wakifanya kiburi?”

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) yakwamba amesema:

“Hazikuwa mbingu saba wala ardhi saba katika Kiganja cha Ar-Rahmaanisipokuwa ni kama chembe ya hardali katika kiganja chenu.”303

Na Ibn Jariyr kasema: “Kanieleza Yuunus, katueleza Ibn Wahb, katueleza IbnZayd, kanieleza baba yangu ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) kasema:

“Kursiyy304 ukiilinganisha na ´Arshi si kitu isipokuwa ni kama mfano wakijipete cha chuma kilichotupwa juu ya mgongo wa jangwa.”

Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Baina ya masafa yaliyoko baina ya dunia na inayofuatia ni miaka miatano, nabaina ya kila mbingu mpaka nyingine ni miaka miatano, na baina ya mbinguya saba na Kursiyy ni miaka miatano, na baina ya Kursiyy na maji ni miakamiatano, na ´Arshi iko juu ya maji na Allaah Yuko juu ya ´Arshi. Hakunakinachojifichika Kwake katika ´amali zenu.305

Kaipokea Ibn Mahdiy kutoka kwa Hammaad bin Salamah kutoka kwa´Aaswim kutoka kwa Zirriy kutoka kwa ´Abdullaah (Ibn Mas´uud). Nakapokea mfano wa hiyo al-Mas´uudiy kutoka kwa ´Aaswim kutoka kwa

302 Shaykh anasema tena: ”Tunathibitisha mapokezi haya kama yalivokuja na wala hatuyaingilii ndanina kutaka kujua namna yake. Na Allaah ni Muweza wa kila kitu.”303 Nyinyi binaadamu304 Anachowekea Miguu Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)305 Shaykh anasema tena: ”Viumbe vyote hivi katika Kiganja cha Ar-Rahmaan ni kama mfano wahardali. Hili linaonesha Ukubwa wa Allaah (Subhaanahu). Washirikina, Mu´attwilah katikaJahmiyyah, Mu´tazilah, Ashaa´irah, Maaturiydiyyah hawakuzingatia Ukubwa wa Allaah pindiwalipokanusha Majina na Sifa Zake kutokana na akili zao ambazo ni dhaifu, hawakumthamini Allaahinavyostahiki kuthaminiwa. Na hapa kuna dalili ya kuwa Allaah Yuko juu ya ´Arshi. Radd kwa walewanaosema kuwa yuko kila mahali na wanaosema kuwa hana mahali. Allaah Awaangamize. Haya nimaneno yasiyoweza kusema yeyote isipokuwa yule ambaye ni mwendawazimu sana. Wanaongea juuya haki ya Allaah pasina elimu. A´udhubi Allaah.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

262

Abuu Waa´iyl, kutoka kwa ´Abdullaah (Ibn Mas´uud). al-Haafidhw adh-Dhahabiy (Rahimahu Allaah) kasema kuhusiana na Hadiyth hapo juu yakwamba imekuja kwa njia nyingi.

Imepokelewa kutoka kwa ´Abbaas bin ´Abdul-Muttwalib (Radhiya Allaahu´anhu) kasema, kasema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hivi mnajua ni masafa mangapi baina ya mbingu na ardhi?” Tukasema:“Allaah na Mtume Wake ndio wanajua.” Akasema: “Baina yake kuna masafaya miaka miatano, na kutoka kwenye mbingu mpaka nyingine ni mwendo wamiaka miatano, na tumba ya kila mbingu ni mwendo wa miaka miatano, nabaina ya mbingu ya saba na ´Arshi kuna bahari kutoka chini yake mpaka juuyake ni kama mbingu baina ya mbingu na ardhi. Na Allaah (Ta´ala) Yuko juuya hilo.306 Hakuna kinachojificha katika ´amali za binaadamu.

(Kaipokea Abuu Daawuud na wengineo)

Ufafanuzi:Mwandishi kamalizia kitabu cha Tawhiyd kwa mlango huu mkubwa, mlango ambaounajumuisha mambo yaliyokuja katika kitabu hichi. Hilo ni kwa sababu, Allaah(Subhaanahu wa Ta´ala) Ana Ukubwa, Uwezo Mkamilifu kwa kila kitu. Ana Majina Mazuri,Ana Sifa Kamilifu. Allaah ni Mkubwa kabisa kuliko kila kitu, kama alivojisifia Nafsi Yakekwa hilo na akamsifu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule ambayeatampunguza Allaah (´Azza wa Jalla) na akamsifu kwa kitu ambacho Hakujisifu Nafsi Yakeau akamshirikisha katika ´Ibaadah Yake, basi huyo hakumthamini Allaah inavyostahikikuthaminiwa. Na yule mwenye kabadilisha maana sahihi ya Majina ya Allaah, auakayafasiri kinyume na maana yake sahihi hakumthamini inavyostahiki kuthaminiwa.Anayepinga Qadhwaa na Qadar, hakumthamini inavyostahiki kuthaminiwa. Mwenyekupinga Maneno ya Allaah (Ta´ala) na kusema Allaah Haongei na wala HakuteremshaKitabu wala Mtume, hakumthamini inavyostahiki kuthaminiwa. Na yule mwenye kupingaya kwamba Allaah Hatowafufua watu siku ya Qiyaamah na kuwalipa kwa matendo yao,hakumthamini inavyostahiki kuthaminiwa. Na yule anayedhani kuwa Allaah Kawaachawaja na kanuni na hukumu za kibinaadamu na Hakuwawekea Shari´ah watayotumia,hakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa. Kila yule anayempunguza Allaah kwanjia yoyote, hakumthamini inavyostahiki kuthaminiwa (Subhaanahu wa Ta´ala). Mlangohuu ni mlango mkubwa unaojumuisha mambo yote yaliyo ndani ya kitabu; Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah, Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat.

306 Shaykh Fawzaan anasema: “Allaah Yuko mbinguni juu ya ´Arshi na Elimu (Ujuzi) Yake iko kilamahali.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

263

Anasema Shaykh Fawzaan, wallaahi naapa ya kwamba kitabu cha Tawhiyd hichi ni kitabumuhimu, kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake. Kamalizia kwa mlango huu muhimuambao umejumuisha yote yaliyo katika kitabu. Allaah Amjaze mwandishi kheri, na Awajazevile vile Waislamu kheri. Kitabu Kashf-ush-Shubuhaat na Kitabu Cha Tawhiyd ni muhimusana Waislamu wote wavisome. Mtu aanze kusoma Kitabu cha Tawhiyd kisha ndio asomeKash-ush-Shubuhaat.

Masuala muhimu yaliyomo:

1. Tafsiri ya Kauli ya Allaah (Ta´ala):

ةاميالق موي هتضا قبيعمج ضالأرو رهقد قح وا اللـهرا قدمو

”Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata(Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah.” (az-Zumar 39:67)

2. Elimu hizi na mfano wake zimebaki kwa mayahudi ambao walikuwa katika zama zake(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hawakuzikataa na wala hawakuzibadili maana.307

3. Mwanachuoni wa kiyahudi alipomtajia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)alimsadikisha na kukateremka Qur-aan kusapoti hilo.

4. Kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutabasamu pindi mwanachuoniwa kiyahudi alipotaja elimu hii kubwa.

5. Ubainifu uliotajwa kuwa Allaah Ana Mikono miwili; mbingu katika Mkono wa Kulia, naardhi katika mwingine.

6. Mkono mwingine unajulikana kama wa Kulia.308

7. Kutajwa kwa (kuwapa changamoto) majabari na wenye kiburi (jeuri) wakati wa hilo.

8. Kauli yake: “Ni kama chembe ya hardali katika kiganja chenu.”309

9. Ukubwa wa Kursiyy kwa nisba ya mbingu.

10. Ukubwa wa ´Arshi kwa nisba ya Kursiyy.

11. ´Arshi, Kursiyy na maji vinatofautiana.310

307 Shaykh Fawzaan anasema: ”Elimu inayozungumzia Ukubwa na Uwezo wa Allaah, ya kwamba anaMikono Miwili, Viganja Viwili na mfano wazo, zipo kwa mayahudi ilimradi wawe hawajabadilikatika Tawrat. Zilibaki katika Tawrat mpaka katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam), na Allaah Akatuma maandiko yakuyasapoti katika Qur-aan (39:67).”308 Shaykh anasema tena: ”Allaah Anasifiwa ya kuwa Ana Mkono wa Kulia na Kushoto, lakini MkonoWake wa kushoto ni wa Kulia (Subhaanahu wa Ta´ala).309 Shaykh anasema tena: ”Hili ni kwa ajili ya kufananisha, inajuzu kupigia mfano ili kukurubishamaana ili mtu aweze kupata picha ya unachokizungumzia.”

Kitaab-ut-TawhiydShaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

264

12. Masafa ya kila mbingu hadi nyingine.

13. Masafa ya mbingu saba hadi Kursiyy.

14. Masafa kutoka kwenye Kursiyy hadi maji.311

15. ´Arshi iko juu ya maji.

16. Allaah Yuko juu ´Arshi.

17. Masafa yaliyopo baina ya mbingu na ardhi.

18. Kipenyo cha kila mbingu ni miaka mia na khamsini alfu.

19. Bahari iliyoko juu ya mbingu saba ni sawa na umbali wa miaka mia na khamsini alfu. NaAllaah Anajua zaidi.

Alhamdulillaahi Rabbil-´Aalamiyn. Swalah na salaam zimwendee Mtumewetu Muhammad na ahli zake na Maswahabah wake ajmaa´iyn.

310 Shaykh Fawzaan anasema: ”Hili ni kwa sababu, kuko ambao wanaifasiri Kursiyy na kusema ndio´Arshi, hili ni kosa. Ni vitu viwili tofauti.”311 Shaykh anasema tena: ”Maji yako juu ya Kursiyy na chini ya ´Arshi. Baina yake ni miakakhamsini.”