sevia: kuona ni kuamini tupo wapi sasa?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 m2 sevia inaweza...

12
FEBRUARI 2019 #8 Nakala ya bure SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA? na Elijah Mwashayenyi Jina letu ‘SEVIA limekuwa sawa na uzalishaji wa mboga nchini Tanzania. Kwa kipindi cha miaka minne na nusu iliyopita, Timu nzima ya SEVIA imevuka mipaka kupitia mashamba darasa na mafunzo kuhusu uzalishaji bora wa mboga. Kuta wakati huu, tupo kwa mara nyingine tena kutoa muhtasari wa mafanikio yetu hadi sasa. Msingi mzuri wa elimu ya uzalishaji mboga Kituo cha SEVIA kilichopo Lambo Mferejini, wilaya ya Hai (karibu na Moshi mjini) kimekuwa kikitoa msingi mzuri wa elimu ya uzalishaji wa mboga ndani na nje ya Tanzania. Kituo kinaendelea na mashamba ya majaribio lakini ikiwa ni zaidi mashamba darasa. Kazi ya SEVIA inahusisha kilimo cha nje na nyumba kitalu. Kujenga uwezo juu ya uzalishaji wa mboga ni lengo kuu la SEVIA. Mashamba yaliyo kwenye kituo yamekuwa ni chanzo kikuu cha mafunzo ya wakufunzi (wataalamu na wakulima viongonzi). Mpaka sasa, SEVIA imetoa mafunzo kwa wataalamu na wakulima viongozi 1035. 1 Loveness Maleale amefanikiwa kwenye pilipili hoho katika msimu wa pili wa mwaka 2018 Frank Mazengo akizungumzia ukuzaji wa lettuce/saladi kupitia njia ya umwagiliaji wa matone Nukuu kutoka kwa wakulima: “Ninafundisha wakulima wengine nilichojifunza kupitia SEVIA. “Wakulima wenzangu wamefikia hatua ya kunibadilisha jina. Ni rahisi kunipata ukisema unamtafuta Abubakari MSEVIA.” Abubakari Saidi kutoka Babati

Upload: dinhhuong

Post on 13-May-2019

411 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

FEBRUARI 2019 #8

Nakala ya bure

SEVIA: KUONA NI KUAMINI

TUPO WAPI SASA? na Elijah Mwashayenyi

Jina letu ‘SEVIA limekuwa sawa na uzalishaji wa mboga nchini Tanzania. Kwa kipindi cha miaka minne na nusu iliyopita, Timu nzima ya SEVIA imevuka mipaka kupitia mashamba darasa na mafunzo kuhusu uzalishaji bora wa

mboga. Kuta wakati huu, tupo kwa mara nyingine tena kutoa muhtasari wa mafanikio yetu hadi sasa.

Msingi mzuri wa elimu ya uzalishaji mboga Kituo cha SEVIA kilichopo Lambo Mferejini, wilaya ya Hai (karibu na Moshi mjini) kimekuwa kikitoa msingi mzuri wa elimu ya uzalishaji wa mboga ndani na nje ya Tanzania. Kituo kinaendelea na mashamba ya majaribio lakini ikiwa ni zaidi mashamba darasa. Kazi ya SEVIA inahusisha kilimo cha nje na nyumba kitalu. Kujenga uwezo juu ya uzalishaji wa mboga ni lengo kuu la SEVIA. Mashamba yaliyo kwenye kituo yamekuwa ni chanzo kikuu cha mafunzo ya wakufunzi (wataalamu na wakulima viongonzi). Mpaka sasa, SEVIA imetoa mafunzo kwa wataalamu na wakulima viongozi 1035.

1

Loveness Maleale amefanikiwa kwenye

pilipili hoho katika msimu wa pili wa

mwaka 2018

Frank Mazengo akizungumzia ukuzaji wa lettuce/saladi kupitia

njia ya umwagiliaji wa matone

Nukuu kutoka kwa wakulima:

“Ninafundisha wakulima wengine nilichojifunza

kupitia SEVIA. “Wakulima wenzangu wamefikia hatua

ya kunibadilisha jina. Ni rahisi kunipata ukisema unamtafuta Abubakari

MSEVIA.”

Abubakari Saidi kutoka Babati

Page 2: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

Zaidi ya mashamba darasa 900 na Zaidi ya wakulima 39,000 kufikiwaDhima ya SEVIA, “Kuona ni kuamini” imefikiwa na SEVIA kupitia mashamba darasa pamoja na kutoa huduma za

ugani. Kwa kipindi cha miaka minne iliyopita tumeweka mashamba darasa 979 ambayo yametumika kwa lengo la kufundisha teknolojia mbalimnali na kutoa ujuzi kwa wakulima katika maeneo mbali mbali ya nchi. Wakulima 39,853 wamefikiwa katika mikoa 11 (wilaya 20).

Utambulisho wa aina bora za mazao na teknolojia/mbinu bunifu

Kupitia SEVIA, wakulima ndani ya wilaya 20 nchini Tanzania wamefahamishwa kuhusu mbegu zilizoboreshwa, ikiwa ni pamoja na mbegu chotara, na mbinu bora za uangalizi wa mazao. Dhima kuu ya ujuzi huu ni pamoja na uangalizi wa

kitalu, uangalizi wa mazao, uwekaji sahihi na salama wa mbolea , umwagiliaji kwa njia ya

matone, uzalishaji wa nyumba kitalu, udhibiti wa visumbufu zao, matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, utunzaji wa mazao baada ya mavuno na taarifa za masoko.

Taarifa kuhusu uzalishaji wa mbogaWakati tukijitahidi kuwapa taarifa wakulima kupitia maafisa ugani wetu, tumefanya hivyo pia kupitia majarida yetu ya misimu, miongozo ya mazao kwa wakulima na mafunzo kwa njia ya mtandao kwa wataalamu. Miongozo yetu 12 ya mazao (hadi sasa) imetengenezwa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha tafiti Wageningen na imehushisha aina 11 za mboga, imewasaidia sana wakulima. Kupitia chuo hicho pia tumeweza kuanzisha mafunzo kwa njia ya mtandao kwa wataalamu. Yanapatikana kupitia tovuti yetu www.sevia.biz.

Uhusiano wa masokoIngawa SEVIA hainunui au kutafuta soko kwa niaba ya wakulima, inatoa taarifa baadhi juu ya masoko na kujenga

uhusiano. SEVIA inafanya kazi kwa karibu na mashirika mengine kama Tanzania Horticulture Association ambayo husaidia wakulima kupata masoko. Mwaka 2017, SEVIA ilisaidiwa utafiti na Chuo Kikuu cha Ushirika

Moshi, ripoti juu ya tafiti hiyo ilionesha masoko mbadala kwa wakulima wa mboga nchini Tanzania.

UtafitiKazi yetu ya tafiti, iliyofanywa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Chuo Kikuu Ushirika Moshi (MOCU), Tari-Tengeru na World Vegetable Centre imetafiti aina 144 za mboga na kukamilisha miradi 75 juu ya mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi na viwango vya mbolea, uangalizi wa mazao, umwagiliaji,

kufungia mazao yanayotambaa, nafasi kati ya miche na kilimo cha nyumba kitalu. Baadhi ya muhtasari wa taarifa za utafiti zinapatikana kwenye tovuti yetu www.sevia.biz.

Kuboresha uchumi wa vijijiniSEVIA imeendelea kuhamasisha wakulima kuchukulia uzalishaji wa mboga kibiashara. Hii itachangia kukuza uchumi wa vijijini. Kwa kasi tunaanza kuona vijana wanajiingiza kwenye biashara ya kilimo. Hii ni zaidi hasa teknolojia inapohusika. Tunaamini kwamba uendelevu wa kilimo kwa ujumla hutokea endapo wanawake watahusika katika maamuzi na vijana kuhusika katika kilimo.

Athari ya kudumuSafari ya SEVIA inaendelea kikamilifu. Tunaona matokeo ya kazi yetu na tunaamini kuwa wadau wetu wanaona pia. Bado tuna

idadi kubwa ya wakulima na wataalamu wa kuwapa mafunzo. Hata hivyo, sisi bado tunaamini kwamba urithi wetu hautakuwa kwa idadi ya wadau tuliowafundisha, lakini matokeo katika maisha ya wakulima, familia zao na matokeo katika sekta ya mboga kwa ujumla nchini Tanzania .

2

Ladislaus Mkufya (kulia) akionyesha jinsi ya kufungia nyanya katika wilaya ya Babati

Wilfred Makange (kushoto) akielezea kilimo cha asili ndani ya nyumba kitalu ya Jecha Katunzi (kulia)

Afisa tafiti Latifa akiangalia chawa/

vithiripi katika jaribio la udhibiti

wa chawa/vithiripi

Nukuu kutoka kwa wakulima:

“Tangu nimepokea ushauri wa SEVIA, nina furaha kuwa mkulima tofauti na wengine. Kupitia kipato

ninachokipata kwa soko lenye changamoto lililopo Dar,

ninanunua pembejeo na kutoa kama mkopo kwa wakulima

wengine. Nalipwa kwa kugawana faida hivyo natengeneza kipato

cha ziada kupitia kilimo. Hiki kinanifanya kuwa mkulima

mwenye furaha.”

Ayubu Juma Makasi kutoka Lushoto

Page 3: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

Amesema Harald Peeters, ambaye ameishi Tanzania tangu mwaka 1991. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Rijk Zwaan Q-Sem/Afrisem alikuwa ni mmoja kati ya waanzilishi wa SEVIA.

Peeters anasema Tanzania ina fursa nzuri kwa kilimo cha mboga: “Wakulima wanaweza kuboresha maisha yao kwa njia tofauti: kwanza kwa kubadilisha kilimo cha mazoea kwenye mashamba yao. Kwa kutumia mbegu bora, teknolojia na kanuni bora za kilimo mavuno yanaongezeka. Ikiwa wakulima wana nyenzo za kuwekeza katika nyumba kitalu, mfumo wa umwagiliaji, matandazo au mifumo ya umwagiliaji kutumia nishati jua, au kuboresha kilimo cha mashamba yao, kwa kufanya hivyo watakuwa wajasiriamali wa kilimo, wanaweza kupata pesa nyingi. Kufundisha wakulima na kuwapa ujuzi ni muhimu! “

Ushawishi katika kubadili tabiaKati ya mbegu zote zinazouzwa nchini Tanzania asilimia 10 pekee ni mbegu chotara au mbegu za asili zilizoboreshwa. Kama vinara wa dunia wa uzalishashaji mbegu, Rijk Zwaan inalenga kupanua wigo wa kuuza mbegu nchini. “Kuna fursa kubwa ya soko” alisema Peeters, lakini kwa wakati huohuo elimu na mafunzo kwa wakulima vinatakiwa kuwa kipaumbele. “wakulima wakiona teknolojia mpya au mbegu bora, kwao vina maana kubwa, wanaweza kushawishika kubadili mitazamo na tabia katika kilimo. Katika eneo letu la Nanenane kanda ya ziwa tulifundisha wakulima jinsi ya kuunganisha miche ya nyanya ili kukabiliana na tatizo la mnyauko bakteria na kulikuwa na hamasa kubwa toka kwa wakulima. Mfano mwingine ni aina ya nyanya yetu Jarrah F1. Hii ina nguvu na inakinzana na nzi weupe ambayo inaweza kupandwa mwezi Januari na Februari ambacho ni kipindi cha joto kali kwa mwaka. Wakulima walioneshwa kuwa mazao bado yanaweza kufanya vizuri mbali ya

kuwa na mazingira magumu ya ukame. Kwa uangalizi mzuri na matumizi sahihi ya pembejeo, mavuno yanaweza kwenda hadi tani 80 kwa ekari moja. “Kuona ni kuamini.”

Vituo vinne vya Mashamba darasa ndani ya TanzaniaRijk Zwaan ina mtazamo wa kuvutiwa zaidi na wakulima wenye nyumba kitalu, lakini pia kampuni hufikia zaidi wakulima wenye mashamba ya nje: “Tunataka kuwatoa wakulima kwenye hatua moja kwenda hatua nyingine ya mafanikio. Tumegundua kwamba wakulima wengi huvutiwa kujua njia za udhibiti magonjwa na visumbufu mazao kibaolojia pamoja na matumizi sahihi ya mbolea. Pia wanataka kujua jinsi ya kukokotoa gharama za uzalishaji.” Hivi karibuni H.Peeters kaongezewa majukumu ya kazi: amekuwa Meneja kanda ya Afrika (Area Manager Africa Digital Strategy and Retail-Chain Development).

Moja kati ya mafanikio yake ya kwanza ni kufanya Rijk Zwaan kuunda ushirika na Shirika la Marekani la USAID. Msaada wa USAID ulitolewa kama mchango wa kufundishia vituo vinne vya mashamba darasa viliyoanzishwa ( nyumba kitalu na madarasa) ndani ya Morogoro, Mbeya, Iringa na Zanzibar. Nyumba kitalu ya tano imejengwa katika kituo cha SEVIA. Vituo Mashamba darasa hayo makuu vitakuwa na uwezo wa kufundisha wakulima 30 kwa siku, wakizunguka

kuanzia darasani, mashamba ya nje na nyumba kitalu. Peeters: “Kwa mafunzo yetu tunafanya kazi na wadau wenye uhakika. Kwa mfano ikiwa tunatoa mafunzo kuhusu mfumo wa umwagiliaji, lazima tuwe na wataalamu karibu.”

Kazi nzuri sanaPeeters anaithamini vipi SEVIA? Peeters: “SEVIA inafanya kazi nzuri, tunapenda kufanya kazi na watu wa SEVIA na tutaendelea kufanya hivi. Kutokana na msaada wa fedha kutoka serikali ya Uholanzi (ambao uliwezesha kufanikisha mradi wa SEVIA) vile vile uliwezesha Rijk Zwaan kufanikisha shughuli zake hapa Tanzania.” Peeters alikuwa na ujumbe kwa watunga sera wa Tanzania: “Idadi ya watu itaongezeka mara mbili ndani ya muda mfupi ujao na wote watahitaji chakula bora. Wakulima wana mchango mkubwa katika kuimarisha hali ya kijamii na kiuchumi. Kwa kuhamasisha ujasiliamali vijijini na kuwa na kipato cha uhakika, wenye vipato vya kati wataongezeka hali ambayo itapunguza hamasa ya kuhamia miji iliyoendelea kama Dar es Salaam.”

Jarrah F1 na Gamhar F1Peeters anajivunia kuhusu Rijk Zwaan kwa mchango wake ‘inazalisha mbegu kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa’: “Aina zote za nyanya Jarrah F1 na Gamhar F1 zimezalishwa Afrisem nchini Tanzania. Hii ina maana zinaendana na hali ya hewa, udongo na kukidhi mahitaji ya wakulima. Jarrah F1 ni kwa msimu wa mvua kidogo na hali ya joto wakati Gamhar ni kwa msimu wa mvua nyingi. Tangu kutambulishwa kwake sokoni, zimekubalika kwa kasi na tunaweza

kukidhi mahitaji ya wateja. Taarifa zimesambaa kwa njia ya kupashana habari kwa wateja wetu walioridhika nazo .”

1-

1-

BRED IN AFRICA FOR AFRICA RZ SEMI DETERMINANTE TOMATOES FOR DRY AND COLD SEASON

• Semi determinate plum tomato

• Good vigour and canopy cover

• Unicolor, firm fruit

• Elongated plum fruit shape

• Fruit weight : 80 - 100 gr

• Semi determinate plum tomato

• Short plant

• Open plant type

• Productive variety and jointless

• Early and concentrated harvest

• Elongated plum shape.

• Fruit weight : 100-120gr

GAHMAR RZ F1JARRAH RZ F1

FOR MORE INFORMATION AND ADVISE CONTACT US : Lake Zone : Stanslaus Silao +255 784 900 549Highlands Zone : Latifa Khamis +255 677 000 401Usambara Zone : Anania Josia +255 757 343 377Central Zone : Naiman Mollel +255 677 000 402Northern Zone : Abel Kuley +255 677 000 405

Follow us on Facebook and Instagram : Rijk Zwaan Tanzania

Join us on m-Farming : DIAL *149*50#

Sourthern Zone : Adam Lazaro +255 621 115 527Zanzibar Zone: Nurdin Mndoholele +255 688 191 820

Rijk Zwaan Afrisem Dolly Estate, Usa RiverPO Box 12345Arusha, TanzaniaT +255 789 765 [email protected]

3

KUSAIDIA WAKULIMA KUFIKIA HATUA YA MAFANIKIO na Anita van Stel

“ Tanzania ina siku 365 zenye masaa 13 ya mwanga. Endapo mkulima ana uhakika wa kupata maji, ana uwezo wa kulima mboga mwaka mzima. Ni kitu cha kushangaza kuona Tanzania inaagiza mboga kutoka nje.”

Page 4: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

4

Maswali yanayoulizwa na wakulima mara kwa mara wakati wa mafunzo na maonesho ya shamba darasa na Epaphras Milambwe

Wakati wa maonesho ya shamba darasa (siku ya wakulima) na mafunzo, wakulima wanauliza maswali mengi kwa Maafisa ugani wetu na wataalamu wengine wa SEVIA. Tumekusanya maswali kumi na moja yaliyoulizwa sana na wakulima na tunaamini utafaidika na majibu yake. Usisite kuuliza maswali mengine kwa SEVIA, popote na kwa wakati wowote!

M1 SEVIA inatusaidia vipi kupunguza tatizo la mnyauko bakteria kwenye mazao yetu hasa nyanya na pilipili hoho? SEVIA: Kwanza kabisa unapaswa kujua sababu zinazoweza sababisha kunyauka kwa mimea; mnyauko bakteria, mnyauko fuzari, mnyauko verticilium, minyoo fundo na kuumia kwa mizizi kunaweza sababisha mnyauko wa mimea. Hivyo unahitaji kutambua sababu ya mnyauko kabla ya kusema ni mnyauko bakteria. Fusarium na verticilium ni magonjwa ya vimelea vya fangasi kwenye udongo. Mnyauko bakteria: unasababishwa na vimelea vya bakteria kwenye udongo.

Jinsi ya kuzuia mnyauko bakteria?

1. Fuata mzunguko wa mazao kutoka familia tofauti kila msimu. Mnyauko bakteria unaweza kuwepo milele.

2. Chagua aina ya mbegu inayoweza kukinzana au kustahimili mnyauko.

3. Panda nyanya kwenye udongo usiotuamisha maji na wenye kiwango kizuri cha pH (kiwango cha tindikali na magadi katika udongo).

4. Ondoa na teketeza mimea iliyoathiriwa kila mwisho wa msimu.

5. Osha mikono yako baada ya kuhudumia mimea iliyoathiriwa na mnyauko.

Hakuna kiuatilifu kilichothibitika mpaka sasa kwa kukinga/kutibu mnyauko bakteria.

Page 5: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

5

M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei?

SEVIA: Kupanga uzalishaji ni muhimu kwa kila mkulima. Fikiria ni wapi na lini unategemea kupata bei nzuri?Weka makubaliano na mnunuzi kabla ya kuanza uzalishaji. Lenga mavuno ya nje ya msimu kama una chanzo kizuri cha maji. Kwa ujumla, bei za mboga kama nyanya, kitunguu, pilipili hoho, kabichi na tango ziko chini kuanzia mwezi Juni hadi Disemba na hupanda tena mwezi Disemba hadi Juni. SEVIA hainunui mazao ya mkulima lakini inatoa taarifa na dondoo za soko kupitia maafisa ugani katika wilaya mbalimbali, ikiwa pamoja na wingi wa bidhaa, ukahika wa bidhaa na ubora. Pia

tunashirikiana na mdau wetu TAHA ambaye kila siku hutoa taarifa kuhusu bei za mazao tofauti.Ukijisajili namba *149*59# ya TAHA utapata taarifa za masoko kila siku.

M3 Mbegu chotara ni ghali sana kwa wakulima wadogo, mnaweza kutusaidia vipi? Mbegu chotara ni bora kuliko za asili?SEVIA: Mbegu chotara ni ghali kuzalisha. Inachukua miaka 6 mpaka 8 au hadi miaka 12 ili kutoa mbegu chotara. Kutokana na utafiti rahisi uliofanywa na SEVIA ulionesha kuwa, wakulima hutumia pesa zaidi kwa vibarua, viuatilifu na mbolea ukilinganisha na mbegu. Mbegu chotara zina gharama zaidi kuliko za asili lakini zitakupa mavuno bora na mengi zikitunzwa vizuri. Sababu ni kwamba mbegu chotara zinaweza kustahimili baadhi ya wadudu na magonjwa na kwa ujumla hutoa mavuno mengi ukilinganisha na mbegu za asili. Wakulima wanaweza kulima mbegu chotara katika eneo dogo na bado wanapata matokeo mazuri.

M4 Aina fulani ya mbegu hupotea sokoni baada ya kuuzwa kwa muda mfupi? Tatizo ni nini?

SEVIA: Hii inaweza kuwa kweli. Makampuni mengine ya mbegu huamua kuondoa aina fulani ya mbegu katika soko baada ya kuwa na taarifa za kutosha kuwa mbegu hiyo haifanyi vizuri kwa wakulima na inaweza kuwasababishia hasara. Wakati mwingine huiondoa ili kuiboresha.

Page 6: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

M5 Mnatusaidia vipi kupata mtaji kwa ajili ya kilimo cha mboga?SEVIA: SEVIA ukiwa mradi, hautoi ufadhili wa kifedha kwa wakulima, wala hatutoi mikopo. Lakini kwa kutambua changamoto wanazokabiliana nazo wakulima wa mboga, SEVIA inawaunganisha wakulima kwa taasisi za fedha ambazo zinasaidia wakulima, taasisi hizo za fedha ni pamoja na NMB (mkopo) na EFTA (mkopo wa pembejeo). Kama mkulima, baada ya kuuza mazao yako unapaswa kutunza akiba kwa ajili ya msimu ujayo kwa ajili ya pembejeo na zana.

M6 Mnatusaidia vipi kuepuka pembejeo bandia katika maduka ya kilimo? Dawa, mbolea, mbegu?

SEVIA: Jukumu la SEVIA ni kufundisha wakulima, wauza maduka ya pembejeo na wataalamu wengine katika vipengele mbalimbali kuhusu uzalishaji wa mboga. Moja ya kipengele hicho ni uchaguzi wa mbegu bora. Kabla ya kulalamika kuwa mbegu ni bandia au la, mkulima unapaswa kujiuliza kama una ujuzi wa kutosha juu ya uhifadhi bora wa mbegu. Kwa hiyo, unahitaji kuelewa namna nzuri ya kuhifadhi mbegu. Matatizo mengi ya mbegu yanaweza kusababishwa na uhifadhi mbaya kwa mkulima au maduka ya kilimo. Ikiwa hakuna shida kwenye uhifadhi wa mbegu tunaweza kuhoji ubora wa mbegu kwa kampuni husika ya mbegu kwa kutumia namba za utambulisho zilizopo kwenye kibandiko cha maelezo ya mbegu.

M7 Je! Tunaweza kuchanganya viuatilifu ili kuokoa muda?

SEVIA: Jibu ni hapana. Kuchanganya viuatilifu hairuhusiwi labda kama imeshauriwa kitalaamu kuwa viuatilifu hivyo vinaweza kuchanganywa. Kuchanganya kunaweza kutengeneza sumu zaidi au kufanya viuatilifu hivyo visifanye kazi vizuri, hali ambayo itaongeza gharama zaidi kununua viuatilifu vingine. Hata hivyo, kuchanganya dawa kunaweza kusababisha madhara kwa mimea na kwako mwenyewe. Bidhaa zenye mchanganyiko wa viambato amilifu zaidi ya kimoja huchukua muda kufanyiwa tafiti na mamlaka ya kudhibiti viuatilifu kama vinashabihiana ili vipewe uhalali wa kutumika. Inakuwaje wewe ndani ya dakika moja unachanganya viuatilifu bila ya utafifiti wa kina kuhusu kushabihiana kwake?

6

Page 7: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

M8 Tunaweza kumdhibiti vipi kantangaze (tuta absoluta) kwenye nyanya?

SEVIA: Kwanza kabisa unahitaji kuelewa hatua za ukuaji za kantangaze na jinsi ya kumdhibiti kwa kila hatua. Kantangaze anapitia hatua nne za ukuaji katika maisha yake; yai, funza, pupa/buu na kipepeo (mzima).

Jambo la kwanza unapaswa kuzingatia kama mkulima ni usafi wa shamba. Hakikisha mabaki yote yaliyoathiriwa na mimea mingine inakusanywa, inazikwa au inachomwa. Pia hakikisha jirani yako anazingatia usafi wa shamba. Matunda yaliyoathiriwa yanapaswa kuzikwa pia. Katika hali

ambapo unapanga kutumia kiuatilifu, hakikisha unaelewa lengo lako ikiwa ni kudhibiti funza, mayai, pupa au kipepeo (mzima). Ikiwa utaweza kudhibiti funza/kiwavi utakuwa umeweza kuondoa tatizo kwa kiwango kikubwa. Flubendiamide, Chlorantraniliprole, Lufenuron, Deltamethrin, Lambdacyhalothrin ni bora dhidi ya kantangaze funza na kipepeo (mzima). Hata hivyo, unatakiwa ufuate ratiba ya kunyunyiza viuatilifu. Usiruhusu funza/kiwavi wakue hatua ya kipepeo. Unaweza kunyunyiza kiuatilifu kila baada ya siku 5 hadi 7.

M9 Kuna tofauti gani kati ya kuzalisha mboga kwenye nyumba kitalu na kilimo cha nje?

SEVIA: Nyumba kitalu pekee haikufanyi wewe kuwa mkulima mzuri ila mkulima mzuri kwenye kilimo cha nje ana uwezo wa kufanya vizuri kwenye nyumba kitalu. Nyumba kitalu inalinda mazao kwa kuyakinga dhidi ya wadudu na baadhi ya magonjwa. Joto la wastani na mzunguko mzuri wa hewa unaisaidia mimea kukua vizuri kwenye nyumba kitalu. Karatasi ya plastiki na wavu vimetengenzwa ili kuzuia wadudu sumbufu wa zao hivyo hupunguza unyuizaji wa mara kwa mara na hivyo

kupunguza gharama ya viuatilifu na uzalisha. Karatasi ya plastiki pia huzuia mvua ya moja kwa moja kwennye majani, hivyo kupunguza magonjwa ya ukungu. Mazingira haya tulivu ndani ya nyumba kitalu yatakuwezesha kuvuna kwa muda mrefu zaidi ukilinganisha na kilimo cha nje. Kwa kilimo cha nje hauwezi kudhibiti athari kama wadudu waharibifu na magonjwa hivyo itakupasa kuingia gharama kununua viuatilifu mara kwa mara kwa ajili ya kunyunyiza. Mazao ya kilimo cha nje hudumu kwa muda mfupi shambani na kusababisha kipato kidogo. Chagua mazao sahihi kwa ajili ya nyumba kitalu ili upate kipato kizuri, mfano nyanya, hoho na tango.

7

Page 8: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

M10 Ni sahihi kukamua mbegu kutoka kwenye zao la mbegu chotara kwa ajili ya msimu ujao?

SEVIA: HAPANA! Mbegu chotara zinapaswa kutumika kwa mzunguko mmoja tu. Endapo ukikamua na kupanda msimu mwingine, mbegu chotara hufuata tabia ya mimea mama iliyotumika kuzalisha mbegu chotara ambayo inaweza kuwa inashambuliwa kirahisi na magonjwa na kutoa mavuno kidogo. Na pia unaweza kupata matunda yenye umbo tofauti.

M11 Je, uwekaji mbolea kimiminika kupitia majani ni bora kuliko kuweka mbolea ya chenga kwenye udongo?

SEVIA: Mbolea zinazonyunyizwa kwenye majani mara nyingi hutumika kama mbolea ya ziada kwa sababu zina kiwango kidogo cha virutubisho na kwa namna yoyote ile, matumizi ya kiwango kikubwa yanaweza yasiwe na tija. Vile vile virutubisho vidogo ambavyo mara nyingi hutumika kwenye mbolea za kwenye majani huhitajika kwa kiwango kidogo sana kwenye mmea. Haina tija

sana kutumia virubisho vikubwa (N.P.K) kupitia mbolea za kunyunyiza kwenye majani. Mara zote tunashauri kuweka mbolea ya chenga au mbolea kimiminika kwenye udongo kama una nyenzo au vifaa na ujuzi juu ya matumizi ya mbolea kimiminika kwenye udongo. Uwekaji mbolea kimiminika kupitia majani unashauriwa tu kama ziada katika hali ambayo mbolea za chenga kwenye udongo ufanisi wake siyo mzuri au zinaweza kuchukua muda mrefu kuonesha matokeo.Pia inabidi uelewe kwa kina mfumo wa uchukuaji virutubisho kupitia mizizi na majani ili kuepuka kuingia gharama za uzalishaji zisizo za lazima. Tambua ni virutubisho vipi vinaweza kuchukuliwa kwa urahisi na mmea kupitia mizizi na majani .

8

Page 9: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

BADO TUPO NA TUNAENDELEA na Anita van Stel

“Mbegu moja ya Imara F1 (nyanya) inagharimu TSH 20. Mavuno ya mche mmoja ni kilo 4 hadi 5. Katika soko, mkulima anaweza kuuza kilo moja kwa TSH 1,000. Huna haja ya kupiga hesabu kujua faida, “anasema Samson Meshack, Meneja Masoko East-West Seed, kampuni yenye ushirika na SEVIA.

Tunza pesa baadayeKwa nini wakulima nchini Tanzania wanaendelea kununua mbegu za asili au kutumia mbegu zilizoandaliwa shambani na wakati mbegu chotara zina uhakika wa mavuno bora? Coen Everts, Meneja Mkuu East-West Seed nchini Tanzania, anaelewa kusita kwa wakulima: “Wakulima wanapaswa kutumia pesa kununua mbegu: hawajalizoea hili, kwa sababu mbegu asili wanazoandaa kutoka kwenye nyanya au tikiti hazina gharama yoyote. Kama wameamua kununua mbegu za asili ni rahisi kuliko chotara. Tunauza mbegu za asili kwa kiasi kikubwa, lakini tunasisitiza sana mbegu chotara. Kwa kuchagua mbegu chotara wakulima watatunza pesa baadaye. Kivipi? Kwa sababu mbegu chotara zina mavuno mengi na zina uwezo wa kukabiliana na baadhi ya magonjwa, kama aina yetu ya nyanya Kipato F1 inaweza kukabiliana na tatizo la mnyauko wa bakteria. Hivyo huwafanya wakulima kupunguza gharama ya madawa na mbolea. Watahitaji kidogo ukilinganisha na pembejeo zitazotumika kuilinda mimea iliyozalishwa kwa kutumia mbegu za asili na zilizoandaliwa shambani. Meshack anasema faida zingine za kulima mazao ya mbegu chotara: “Matunda ni mazuri, yana ukubwa unaofanana, usafirishaji wake ni rahisi na yanaweza kukaa muda mrefu bila kuharibika. Wakulima wanaona uwezo huu.”

Uendeshwaji wa East-West SeedMwaka 2017 Everts alianza kulisimamia tawi la East-West Seed nchini Tanzania. Linahusisha uzalishaji mkubwa wenye nyumba vitalu taneli 350, ambapo marigolds kwa soko la Asia inalimwa, inafungwa na kusafirishwa. Mbegu za mboga hufungwa upya kwa ajili ya usambazaji. Katika tawi hili, East-West Seed imeajiri watu 250 kutoka vijiji jirani. Kwa kitengo maalumu cha mauzo kampuni ina ofisi Moshi mjini. Everts hana historia ya kilimo, lakini kuunda mfumo mzuri wa usambazaji na kujenga mahusiano mazuri na wateja, ni malengo ambayo alikamilisha katika kazi zake za kimataifa zilizopita.

Anauhakika kuhusu uendeshwaji wa East-West Seed Tanzania: “Tupo na tunaendelea kujijenga katika hili. Tunawekeza ili kukuza biashara ya mbegu za mboga. East-West Seed inaamini kwamba katika kila kituo, Idara ya Utafiti, Maendeleo na

Uzalishaji inapaswa kuwekwa. Hivi karibuni tumeanza kushirikiana na mzalishaji mbegu na

tunatarajia kujikita katika uzalishaji wa mboga za majani, kama vile Sukumawiki, sukumawiki

jamii ya Ethiopia na mnafu.”

Pamoja na kuendelea kutoa ujuziIdadi ya watu Afrika na Tanzania inakua kwa kasi na mahitaji ya mboga yanaongezeka. Utafiti wa TAHA umeonesha kuwa soko la mbegu za mboga kwa Tanzania linakuwa kwa asilimia 8 hadi 15 kwa mwaka. Nchini Tanzania asilimia 85 ya wakulima wote (wastani wa milioni 10) ni wakulima wadogo. Everts anasema malengo ya kampuni ni kuwa wasambazaji namba moja wa mbegu nchini Tanzania, kwa kuuza mbegu chotara na kuinua kilimo cha mboga. “Wakulima wadogo ni wateja wanaoheshimiwa na East-West Seed.”

Everts anaamini maafisa ugani wa SEVIA wametoa mchango mkubwa kufanya mbegu chotara kukubalika. “Kutambulisha kwa mbegu chotara kwa wakulima kunapaswa kwenda pamoja na kutoa elimu kuhusu mbinu za kilimo. Unatakiwa kuwaambia na kuwaonesha wakulima, kitu ambacho hufanywa vizuri na SEVIA”, anasema. “Hata hivyo, ndio tumeanza. SEVIA imefikia wakulima 40,000, lakini kuna wengi zaidi wanasubiri ushauri sahihi. “

Mkombozi“Umesikia kuhusu aina yetu mpya ya tikiti”, Everts aliuliza. “Inaitwa Mkombozi F1, ambayo pia inamaanisha mwokozi”, Meshack aliongezea. “Ukubwa wa tunda unaenda mpaka kilo 15 na ladha bado ni nzuri. Ni kubwa zaidi ni zuri, wanunuzi wanatuambia. Hivi karibuni tumelitambulisha Zanzibar na linafanya vizuri .”

9

Samson Meshack na Coen Everts

Page 10: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

610

Tangu awali, SEVIA imekuwa na maono ya kupanua wigo kufikia Afrika nzima. Kutokana na shughuli za mradi nchini Tanzania, mradi wa SEVIA haukuweza kufikia nchi zingine katika kipindi cha muda mfupi (toka mwaka 2014 hadi sasa). Hata hivyo, SEVIA imeweza kuonesha uwezo wake nje ya mipaka yake kwa kushirikiana na wadau wetu. Mara baada ya kuanza shughuli za ugani katika nchi zingine, ujuzi wa SEVIA umeongezeka na kuwa wenye manufaa zaidi. Kufuatia mwaliko wa wadau (kwa gharama zao) tumekuwa na furaha zaidi kutoa ujuzi wetu. Tunajivunia kuonesha mfano mahususi (dhahiri sio yote) kwa ushirikiano wetu.

Pamoja na Chuo cha Wageningen nchini UgandaUshirikiano ulianza na Integrated Seed Services Development (ISSD) ya chuo kikuu cha Wageningen. Mwaka 2016 SEVIA ilitoa ushirikiano kwa kuweka shamba la majaribio Lira nchini Uganda ambayo ilikuwa ni hatua ya awali kujifunza kuhusu mradi mpya wa mboga. Cate Nakatugga, mratibu, na maafisa ugani walitembelea SEVIA ili kupata uzoefu. Mara baada ya mradi wa mboga ISDD nchini Uganda kuanzishwa, wadau wanaohusika walianza rasmi kuufanyia kazi. East-West Seed Knowledge Transfer (EWS KT) iliweka timu maalum. SEVIA ilitoa mafunzo kwa maafisa tisa wa kwanza wa EWS KT na ISSD. Baadaye Annet Kizza, Meneja wa EWS KT nchini Uganda na Ruth Ardzard kutoka EWS KT nchini Nigeria walifika SEVIA kwa mafunzo. Marten Hermes wa Greentech Holland, akiwakilisha Rijk Zwaan nchini Uganda na anaefanya kazi pia na ISSD, pia alitembelea SEVIA ili kubadilishana uzoefu.

Kufanya kazi na GhanaZakari Musah kutoka Tikola Ghana Limited (msambazaji wa East-West Seed), alikuja SEVIA kwa ajili ya mafunzo. Tikola Ghana limited haitoi tu mbegu bora zinazoweza kustawi Ghana kutoka East-West Seed International, lakini pia mafunzo bora jinsi ya kupata mavuno mengi. Januari 2019 SEVIA ilimpokea Helen Gyasi, mfanyakazi wa Rijk Zwaan Ghana, kwa ajili ya mafunzo.

Rijk Zwaan na wakulima kutoka Magharibi, Mashariki na Kusini mwa AfrikaSEVIA ilibadilishana ujuzi juu ya kilimo cha mboga na kundi la wakulima na wataalamu kutoka Magharibi, Mashariki na Kusini mwa Afrika waliohudhuria maonesho ya shamba darasa ya Rijk Zwaan.

Nuffic na MsumbijiSEVIA iliongea na Nuffic (Shirika la Uholanzi la kimataifa linalotoa ufadhili wa elimu) kuhusu mahitaji ya mafunzo kwa vijana nchini Tanzania. Kwa kuongezea, Nuffic iliandaa wajumbe kutoka Msumbiji (wahadhiri nane kutoka vyuo vikuu na taasisi za mafunzo ya kilimo) waliokuja SEVIA kwa mafunzo. Placido Jacinto Jofrice Da Costa, moja ya washiriki wenye elimu ya kilimo, alisema: “Shukrani kwa SEVIA kwa kutuonyesha teknolojia ambazo ni tofauti sana na za nchini Msumbiji.”

Wanafunzi mjini MoshiSEVIA imepokea wanafunzi hamsini kutoka vyuo mbalimbali vya kilimo na Chuo Kikuu Sokoine nchini Tanzania, na wawili kutoka Chuo Kikuu Wageningen (Uholanzi).

Wafanyakazi wa SEVIA nchini Uganda na NigeriaLadislaus Mkufya alipelekwa EWS KT nchini Uganda kwa muda wa miezi mitatu ili kuwasaidia maafisa ugani wa awamu ya pili. Muda wake mwingi ulitumika kuangalia shamba darasa la mafunzo ambalo lilitumika kama nyenzo ya kufundishia. “Moja kati ya changamoto ni kwamba wakulima wengi huzalisha mboga kwa kutegemea mvua. Msimu mmoja wa mvua una

mvua kidogo. Niliwashauri wenzangu wa Uganda wahamasishe kilimo cha umwagiliaji, “ aliripoti Ladilaus.

Kilomita 4000 kutoka Magharibi mwa Nigeria, Mary

Maganga na Mseti Mwita wa SEVIA walitoa mafunzo kwa wadau sita wa timu mpya ya EWS KT.

Jukwaa letu la kimataifaTunaweza kuwa hatujaanzisha vituo vingine vya mradi wa SEVIA nchi zingine za Afrika lakini tumeweza kuwafikia wakulima na wataalam nje ya mipaka yetu. Huenda ikatokea baadae, hakuna anaefahamu. Ambacho tunauhakika nacho kwa upande wetu, haijalishi matokeo ila tumeweza kuifanya SEVIA itambulike kimataifa .

Mseti (fulana ya njano) akieleza jinsi ya kuhamishia miche shambani na utunzaji wake

Ruth Ardzard na Mary Maganga wa SEVIA

walitembelea shamba darasa la familia ya Uronu kutoka

Machame

SEVIA yavuka mipaka kimataifa na Elijah Mwashayenyi

Page 11: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

“Nilikuwa natumia aina moja ya mbolea kwa hatua zote za ukuaji wa nyanya, hii ilisababisha kudondoka kwa maua, kuoza kitako cha tunda na mavuno haba. Sasa nina elimu kubwa,” alisema Paul Lyimo.

Paul Lyimo (46) kutoka Managha wilaya ya Babati anajihusisha na kilimo kama shughuli yake kuu tangu mwaka 2004. Alianza na mahindi, mbaazi na nyanya ila sasa amejikita kwenye nyanya, pilipili hoho na tango kwenye eneo hilo hilo.

Kila kitu kilibadilika baada ya kutambulishwa kwa Ladislaus Mkufya (afisa ugani wa Babati). Alichaguliwa kuhudhuria mafunzo ya wakulima katika kituo cha mafunzo SEVIA kilichopo wilaya ya Hai karibu na Moshi na alijifunza umuhimu wa mbegu zilizoboreshwa , utunzaji wa kitalu, nafasi sahihi kati ya miche, kufungia mazao yanayotambaa na uangalizi wa

mazao kwa ujumla.

Miezi miwili baada ya kurudi Babati, Paul aliweka shamba darasa la nyanya na tango. Alifurahi zaidi kujifunza kuhusu uwekaji wa mbolea kwenye nyanya. “Nilikuwa natumia aina moja ya mbolea kwenye kila hatua ya ukuzaji wa nyanya, hii ilisababisha kudondoka kwa maua, kuoza kitako cha tunda na mavuno haba. SEVIA wamenifundisha mbolea sahihi katika kila

hatua ya ukuaji na niliweza kupata mavuno bora”, alisema.

Paul ameamua kutumia mbinu za kilimo alizojifunza SEVIA. “Sasa nina furaha na kiasi cha mavuno nachozalisha kwenye mazao tofauti. Mimi na majirani zangu tumekuwa tukipata matokeo mazuri kupitia ushauri wa kilimo uliotolewa na SEVIA.”

Paul ameishauri SEVIA iendelee kufikia wakulima wengi zaidi kwani mafunzo yanayotolewa yana manufaa katika kukuza ujuzi kwa wakulima wote nchini .

11

“Nilianza biashara ya kuuza miche. Nilianza na miche 2000 na baadae nikaongeza.” Joseph Mbuji amekuwa mfanyabiashara kupitia kilimo na anafanya vizuri sana.

Joseph Mbuji (42) ni mkulima wa mboga kutoka Kerege wilayani Bagamoyo. Amejihusisha na kilimo tangu mwaka 2013, akilima kabichi, pilipili hoho, chainizi kabichi, tikiti maji, pilipili kali, bilinganya na nyanya chungu. Alipoanza kilimo, alikabiliwa na changamoto kama upatikanaji wa soko, mavuno kidogo na magonjwa kwenye mazao.

Mwaka 2016 Joseph Mbuji alikutana na Nurdin Mndoholele (afisa ugani wa zamani SEVIA Bagamoyo) ambaye alimchagua kama mkulima wa mfano anaemiliki shamba darasa la nyanya (Kipato F1) na pilipili hoho (Red Jet F1). Joseph alipewa ushauri wa masoko na Thobias Mkamate (afisa ugani wa zamani wa Moshi). Na baadae Joseph alifunga mfumo wa umwagiliaji wa matone kwa msaada wa mtaalamu wa SEVIA George Kisamo. Kupitia shamba darasa lililoandaliwa vizuri, alijifunza ufanisi wa mbegu chotara, uwekaji mzuri wa mbolea, taratibu za uangalizi wa mazao na alianza kutumia mbinu hizi.

Joseph aliamua kuuza mazao yake kwenye supermarket ambapo alipata bei nzuri. “SEVIA ilinipa angalizo ambalo

lilinifanya nibadili mfumo wangu wa kilimo moja kwa moja. Nilianza kwa kuongeza ukubwa wa shamba ili kukuza uzalishaji wangu. Ila sasa ninaamini kwamba mbinu bora za kilimo na aina nzuri ya mbegu vinanipa uzalishaji mzuri.”

Joseph alifikiria jinsi ya kujitengenezea kipato cha ziada nje ya kilimo. “nilianza biashara ya kuuza miche. Nilianza na miche 2000 ambayo ilikubalika kwa

wateja wangu. Baadae nikaongeza. Mauzo ya hii biashara yalinishangaza. Niliweza kutengeneza nyumba wavu ya kukuzia miche ili kupata miche yenye afya zaidi.”

Hadi mwaka 2018, Joseph aliweza kutengeneza nyumba wavu sita maalumu kwa kukuzia miche, duka moja la pembejeo na kuwa na sehemu ya kuuzia vinywaji. Anauza miche kwa wakulima na baadhi ya taasisi.

Joseph anaendelea na uzalishaji wa mboga na anatumia mashamba yake kufundishia wakulima wengine. Anaipongeza SEVIA kwa jitihada za kufundisha wakulima kupitia mashamba darasa na anaushauri mradi upanue wigo wake ili kufikia wakulima wengi zaidi. “Sina namna ya kuishukuru SEVIA kwa jinsi ujuzi wake ulivyonitoa kutoka hatua moja kwenda nyingine” alisema kwa furaha.

MATOKEO YA KUTUMIA MBINU ZA KILIMO

UJASIRIAMALI NJE YA KILIMO

Habari kutoka shambani na Halima Jumanne

Joseph Mbuji akiwa katika kitalu chake

Paul Lyimo na Paskalina Simon (mkewe)

Page 12: SEVIA: KUONA NI KUAMINI TUPO WAPI SASA?sevia.biz/media/com_acymailing/upload/...5 M2 SEVIA inaweza kutusaidiaje changamoto ya soko la mazao yetu? Kupanda na kushuka kwa bei? SEVIA:

12

Kona ya utafiti

Mapendekezo ya kitalu bora na nyumba kitaluMiaka michache iliyopita SEVIA imefanyia kazi mchanganyiko mbalimbali wa udongo ili kupata mbadala wa udongo wa viwandani, kama vile peat moss na cocopeat. Ikiwa udongo wa viwandani una viwango sahihi, huu ni mbadala wake unaoweza kuutengeneza nyumbani:

AJENDA FEBRUARI MACHI APRILI MEI JUNI JULAI AUGOSTI SEPTEMBA OKTOBA NOVEMBA DISEMBA

Mafunzo kwa wakulima na wataalamu

Mafunzo ya uongozi kwa wataalamu wa SEVIA

Mwanzo wa msimu mpya wa mazao

27: Maonyesho ya shamba darasa ya SEVIA

1 to 8: NANENANE

Jumla hadi sasa Jumla (malengo) kufikia 2020

Muhtasari wa maendeleo dhidi ya malengo ya mradi

0 200 400 600 800 1,000 40,000

Idadi ya vituo vyaSEVIA vilivyoanzishwa

Idadi ya vitabu vya mazaovilivyotengenezwa

Idadi ya vitabu vyaushauri vilivyotengenezwa

Idadi ya miradi ya kiteknolojiailiyofanywa na SEVIA

Idadi ya miradi nataasisi za mafunzo

Idadi ya aina ya mazaoyaliyofanyiwa jaribio

Idadi ya mbegu chotarazilizozalishwa (Afrisem)

Idadi ya wataalamuwaliofundishwa

Idadi ya shambadarasa (maeneo)

Idadi ya wakulimawaliofikiwa 30,000

39,853

1,0001,035

1,000979

3020

100144

5042

5033

3012

103

11

Wilaya 15 ndaniya Mikoa 10

SEVIA ina jumla ya wafanyakazi 45

26,743 13,110

Kwa kitalu cha trei

• Mchanganyiko wa mbolea ya asili 50%, udongo 25% na mchanga 25%

• Au ndoo 2 za mbolea ya asili kwa kila ndoo moja ya udongo na mchanga

Kutumia mifuko kwa uzalishaji wa nyumba kitalu

• Udongo 75% na pumba za mchele zilizochomwa 25%

• Au ndoo 3 za udongo kwa kila ndoo ya pumba za mchele zilizochomwa

Je, unataka kupokea nakala za bure za awali za jarida hili? Tafadhali tuma barua pepe au soma jarida katika tovuti yetu www.sevia.biz

WACHANGIAJI Michango ya jarida hili ni kutoka kwa• Halima Jumanne • Epaphras Milambwe • Elijah Mwashayenyi • Herman de Putter• John Kazuba• Anita van Stel

Anuani ya posta SEVIA, P.O. Box 7211, MoshiAnuani ya kutembeleaLambo, MferejiniTanzania+255 685 942 364www.sevia.biz

WahaririHalima JumanneElijah MwashayenyiAnita van StelUbunifuMooizo Design

• SEVIA • Wageningen University & Research

• Public Relations officer East-West Seed Tanzania

• Communications consultant

Wanafunzi wa mazoezi kwa vitendo

wakichoma pumba za mchele

Florah Yangole akimuelekeza Mary

Hassan viwango sahihi

Angalizo: Chombo kinachotumika kwa ajili ya kipimo sio muhimu. Muhimu ni kuzingatia viwango sahihi. Pia zingatia kuwa, kuuchoma udongo ni muhimu ikiwa kuna tatizo la mnyauko bakteria.

Muhtasari wa

maendeleo dhidi ya

malengo ya mradi