sehemu ya kwanza...2 5. uhalali wa mikataba ya nyumba ya serikali iliyopo kiponda inayodaiwa kwamba...
TRANSCRIPT
1
SEHEMU YA KWANZA:
1.0 UTANGULIZI:
1.1 MUUNDO WA KAMATI:
Kamati hii Teule ya Baraza la Wawakilishi imeundwa kufuatia Mkutano wa Nne wa Baraza la
Wawakilish Zanzibar, ambao ulikuwa ni maalum kwa ajili ya Bajeti ya Wizara za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa mwaka 2011/2012, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar
liliridhia kuundwa kwa Kamati Teule ya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuchunguza mambo
mbali mbali ambayo yaliibuka kwenye majadiliano ya Bajeti.
Kufuatia maamuzi hayo ya Baraza, mnamo tarehe 09/08/2011, Mhe. Spika wa Baraza la
Wawakilishi aliteua wajumbe wa Kamati Teule kwa mujibu wa kifungu cha 117 (2) cha Kanuni
za Baraza, Toleo la 2011, kwa ajili ya kazi hiyo na hivyo basi, wajumbe hao ni hawa wafuatao:
1. Mheshimiwa Omar Ali Shehe Mwenyekiti.
2. Mheshimiwa Asha Bakari Makame Mjumbe.
3. Mheshimiwa Hamza Hassan Juma Mjumbe.
4. Mheshimiwa Hija Hassan Hija Mjumbe.
5. Mheshimiwa Mbarouk Wadi Mussa (Mtando) Mjumbe.
6. Ndg. Yahya Khamis Hamad Katibu.
7. Ndg. Othman Ali Haji Katibu1.
1.2 HADIDU REJEA:
Kufuatia kuundwa kwa Kamati hii, Mheshimiwa Spika kwa mujibu wa Kanuni ya 118(4) ya
Kanuni za Baraza la Wawakilishi Toleo la 2011, alizikabidhi Hadidu Rejea zifuatazo kwa
Kamati:
1. Uhaulishwaji wa Kiwanja cha Wizara ya Miundombinu na Mawasililiano ambacho kipo
kwenye eneo ilipokuwepo Karakana na Wizara hiyo, eneo la Mtoni, Mjini, Zanzibar.
2. Suala zima la Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kuhusu ulipaji wa fidia kwa watu ambao
mali zao zimeathirika kutokana na ujenzi wa uzio wa Uwanja wa Ndege, matatizo ya
ununuzi wa jenereta, mikataba ya ukodishwaji wa sehemu za biashara kwenye eneo la
Uwanja wa Ndege na utaratibu wa ajira na utoaji wa huduma mbali mbali kwenye
maeneo ya Uwanja wa Ndege na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwa ujumla.
3. Matatizo ya uvamizi wa fukwe na uharibifu wa mazingira kwenye hoteli inayopakana na
Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar, Maruhubi, kwenye Hoteli ya Zanzibar Ocean
View, Kilimani-Zanzibar, na Hoteli ya Misali iliyopo Wesha, Pemba.
4. Uhaulishwaji wa Kiwanja kianchopakana na Livingstone House Mbuyutaifa, Mjini,
Zanzibar.
1 Ifahamike kwamba, kwa mujibu wa fasili ya 119(6) ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi, Toleo la 2011, Makatibu
wa Kamati wameteuliwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi.
2
5. Uhalali wa Mikataba ya Nyumba ya Serikali iliyopo Kiponda inayodaiwa kwamba
alipewa mwananchi na kuiuza kwa mtu mwegine.
6. Kutafuta ukweli kuhusu matatizo yaliyotokea kwenye ujenzi wa jengo jipya la Wizara ya
Fedha, Pemba.
7. Ubadilishaji wa Matumizi ya Starehe Club na Jengo la Mambomsiige ambalo lilikuwa
linatumiwa kwa shughuli za Shirika la Meli Zanzibar, Kamisheni ya Wakfu na Mali ya
Amana, Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali, Zanzibar.
8. Ukodishwaji wa Kisiwa cha Changuu kilichopo nje kidogo Magharibi ya Mji wa
Zanzibar.
9. Usambazaji wa Majenereta yaliyoletwa Zanzibar kusaidia shughuli za Usambazaji wa
maji wakati Zanzibar ilipokosa umeme kwa miezi mitatu mwishoni mwa mwaka 2009 na
mwanzoni mwa 2011.
1.3 CHIMBUKO LA KAMATI TEULE:
Katika Baraza la Nane, Mkutano wa Nne uliokuwa maalum kwa ajili ya kujadili na kupitisha
Bajeti ya Wizara za Serikali kwa mwaka 2011/2012, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar liliridhia
kuundwa kwa Kamati Teule ya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuchunguza mambo mbali
mbali ambayo yaliibuka kwenye mjadala huo. Kuibuka kwa mambo hayo kulitokana na
upitishaji wa bajeti hizo ambapo Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliibua
hoja mbali mbali ambazo zilihitaji majibu ya kina na fasaha. Hata hivyo, kutokana na majibu
waliyojibiwa na Mawaziri ama Serikali kushindwa kutuliza kiu yao, ndio wakaamua kuunda
Kamati hii ili iyachunguze mambo hayo.
Namna mambo hayo yalivyoibuka ni suala la mazingira tofauti kwa mnasaba wa mjadala wa
bajeti ulivyokuwa unaendelea, lakini jambo la msingi ni pale Mhe. Mwenyekiti wa Kamati ya
Matumizi aliyekuwa anasimamia kikao cha kupitisha bajeti hiyo, ambaye ni Spika wa Baraza la
Wawakilishi baada ya kuibuka kwa hoja nyingi zilizohitaji kuundwa kwa Kamati Teule alifika
maamuzi yafuatayo: “Ruhusa imeshatolewa isipokuwa nataka kutoa maelezo kidogo tu, ni kweli nakumbuka hata kwenye
Wizara ya Habari kulikuwa kuna habari ya mikataba na pale tuliahidi kwamba kutakuwa na wajumbe wa
kamati wafuatilie mikataba ile. Kwa hivyo, sisi kama uongozi huku tulisita kidogo kwa sababu kuja kuunda
kamati nne au tano zote teule kidogo ni jambo ambalo itakuwa sio muafaka vyema, tunapaswa wakati huo
huo tuzingatie matumizi ya fedha. Kwa hivyo, hili jengine na lile la mwanzo tutayakusanya mambo haya ili
kamati hiyo teule sasa itakayoteuliwa iweze kupewa maeneo hayo ya kufanyia kazi2.
Mhe. Spika kwa nia hii hii alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Matumizi iliyokuwa inapitisha
Mswada wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, tarehe 21/07/2011, na
baada ya Mhe. Mbarouk Wadi Mussa (Mtando) kutoa hoja ya kuundwa kwa Kamati Teule ili
ichunguze Ukodishwaji wa Kisiwa cha Changuu, na baada ya mjadala mrefu alihitimisha kwa
maamuzi yake ya busara kwa kusema: “Mimi nafikiri mkataba ambao utakuwa unafuatiliwa ni huu ambao una hoja hapa mbele ya Baraza, kwa
hiyo mkataba huu ndio ufuatiliwe na kutolewa taarifa baadae kama vile ambavyo tulikuwa tumefikia
pahala kwamba ikionekana hauna faida basi unakwenda, baada ya kutizama masharti yote na dhima zote.
Nitakalojitahidi kulifanya ni kwamba ndani ya mkataba huu juu ya wajumbe hao nitakaowapeleka kuwe na
2 Hansard ya Baraza la Wawakilishi, tarehe 29/07/2011, uk- 46.
3
wajumbe wale ambao wana sheria ndani yake na watu wanaoelewa mambo ya mahesabu na mengineyo
kama hayo. Waheshimiwa Wajumbe nitajitahidi kamati isiwe kubwa na nitazingatia yote ambayo
Waheshimiwa Wajumbe mmeyasema3.
Maneno haya ya Mhe. Spika yalilenga katika mambo yote ambayo yalileta mjadala na azma ya
kufanyiwa kazi na Kamati, ambapo kwa busara zake aliamua kwamba Kamati hiyo iliyoamuliwa
kuundwa na Baraza la Wawakilishi iyafanyie kazi maeneo yote hayo(yaani ni hizo Hadidu Rejea
tulizozieleza hapo juu). Kwa mfano, Mhe. Hamza Hassan Juma, mbali na mambo mengine
alitaka kuundwa kwa Kamati hii ili kufuatilia suala la kiwanja kinachopakana na Living Stone
alichangia kama ifuatavyo: “Mhe. Mwenyekiti, hoja yangu inakuja nilipokuwa nikichangia nilijaribu kuzungumza mambo mengi na
kuna baadhi ya mambo nilipoona kwamba kuna baadhi ya majibu kila siku yanatolewa hayaturidhishi
nikataka Mhe. Waziri kama hajanitosheleza kwa jawabu na yeye itabidi uniruhusu ukubali kuunda Kamati
ya Baraza ili tukajiridhishe. Mhe. Mwenyekiti, kwa sababu ikiwa kila siku leo Waziri huyu anatujibu hivi
ndio pale tunapopata mashaka. Kwa hivyo, Mhe. Mwenyekiti, nilikuwa nataka ufafanuzi katika hili kama
haujanitosheleza itabidi uniruhusu twende kwenye kamati kwa mujibu wa kanuni zetu4.
Mhe. Hamza aliendelea kusema:
Mimi nilitaka ufafanuzi juu ya kiwanja cha Living Stone House na hapa ingawa samahani kidogo Mhe.
Mwanasheria Mkuu aliwahi kutoa ufafanuzi alitoa hadithi ya Abaabedi, lakini Abaabedi wa zamani na wa
leo ni tofauti………5”
Suala hili lilikubaliwa moja kwa moja kuundwa kwa Kamati Teule6. Suala kama hili aliliibua
tena Mhe. Hamza Hassan Juma kwa mnasaba wa matatizo yaliyokuwepo kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanzibar pale alipozungumzia matatizo ya Idara
ya Anga katika ubebaji wa Mizigo ambapo hapa tunamnunkuu:
“Mhe. Mwenyekiti katika michango niliomba tuunde Kamati Teule ya Baraza. Hoja nilizozungumza katika
muundo wa tume ili kuchunguza na kupata ukweli. Kama Mhe. Waziri alivyosema kutoa maoni, kushauri,
kuuliza, sio kumkomoa mtu au kumchukia mtu, lakini tunajenga Serikali yetu, tunajenga usalama na haki
za wananchi wetu.
Mhe. Mwenyekiti, nikija katika suala la Idara ya Uendeshaji na Utumishi nilizungumzia suala la
mfanyakazi wa Idara ya Anga. Katika kifungu cha 06 huku waheshimiwa walikuwa wanapiga zogo
ukakipitisha mimi sijawahi kupiga buti, kwa hiyo ndio maana nikaamue nije nikizuie kwa huku mbele,
nimetumia uzoefu.
Mhe. Mwenyekiti, pale kuna mfanyakazi ambae nilileta hoja kwamba wale waliamua kufungua kampuni za
Zanzibar Emission Porters Service yaani kampuni ya ubebaji wa mizigo. Nilisema kwamba mama Yule
alishirikiana na mumewe, mumewe alikuwa ni Afisa wa Jeshi la Usalama ambaye amestaafu ameletwa pale
Uwanja wa Ndege kwa ajili ya security. Lakini Mhe. Mwenyekiti, baada ya kupeleka yale maombi ya
wakakubaliwa wakaambiwa fanyeni hivi, tafuteni sare, tutakufanyia registration zote ninazo hapa. Mhe.
Mwenyekiti, tatizo lililojitokeza kwamba wale walikuja kupigwa pute na sitaki kusema na wakubwa,
walikuja kupigwa pute na viongozi wa Idara ya Anga. Matokeo yake Yule aliyebuni mradi akaja
akaonekana kwamba yeye atafaidika matokeo yake wakubwa wakauchukua mradi ule7.
3 Hansard ya Baraza la Wawakilishi, Tarehe 21/07/2011, Uk-74 (msisitizo ni wetu).
4 Ibid, uk-41.
5 Ibid pg. 42.
6 Angalia majibu ya Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais na majibu ya Mhe. Hamza Hassan
Juma,kupitia Hansard ya Baraza la Wawakilishi, tarehe 29/07/2011, uk- 46. 7 Hansard ya Baraza la Wawakilishi, tarehe 28/06/2011, uk-88.
4
Suala jengine kwa mfano linahusu kiwanja cha Miundombinu na Mawasiliano, ambalo lilihitaji
kutolewa ufafanuzi yakinifu na Waziri wa Wizara hii, baada ya kuhojiwa na Mhe. Mbarouk
Wadi Mussa (Mtando) na mwishowe kuamulika kwamba ipo haja ya kuchunguzwa suala hili8,
na Hadidu zote zilizobakia zilikabidhiwa kwa Kamati kama inavyothibitika katika faili la Kamati
Teule liliopo Afisi ya Baraza la Wawakilishi lenye Namba BLW/K.10/18.
1.4 UTARATIBU WA KAZI ZA KAMATI:
Kamati Teule baada ya kuundwa na kukabidhiwa Hadidu rejea, ilipangiwa kufanya kazi kwa
wiki sita katika miezi tofauti na kwa kupata ridhaa ya Spika, Wajumbe wa Kamati hii walijitolea
kufanya kazi hii kwa siku zisizopungua 10 bila ya malipo yoyote, lakini kwa kujali umuhimu wa
kazi hii walijitolea kuikamilisha. Vile vile, kwa siku kadhaa Kamati ilifanya kazi hadi saa 5 za
usiku kwa mnasaba huu huu wa kuikamilisha kazi hii, kama ilivyofanya hivi hata kwa siku za
mapumziko. Kamati pia imepata muda wa kuiandaa ripoti yake na kuipitia kwa pamoja katika
utaratibu iliyoona unafaa na matokeo yake kufanikisha kwa pamoja ripoti hii kama
inavyotakiwa chini ya kanuni ya 119(1) ya Kanuni za Baraza.
Kwa ujumla, kabla Kamati haijaanza kazi, kwa kufuata maelekezo ya kanuni ya 117(3) ya
kanuni za Baraza la Wawakilishi, ilimchagua Mhe. Omar Ali Shehe kuwa Mwenyekiti wa
Kamati na baadae mnamo tarehe 05/09/2011, ilianza kufanya kazi zake kwa muda wa wiki mbili.
Baadae Kamati ilipata maelekezo ya Mhe. Spika kuendelea na kazi zake Kisiwani Pemba kwa
muda wa wiki moja, kuanzia tarehe 31/10/2011 na hatimae ilipata kibali cha kumalizia kazi zake
kwa utaratibu huu, kwa muda wa wiki tatu kuanzia tarehe 21/11/2011 kazi zilizofanyika Unguja.
Hata hivyo, kwa kupitia utaratibu wa kujitolea baada ya kupata cha kibali cha Spika, Kamati
iliendelea na kazi hadi mwishoni mwa mwezi wa Disemba 2011. Kwa kupitia utaratibu wa
kufuatilia taarifa maalum ilizozihitaji, Kamati iliendelea kuifanya kazi hii hadi mwezi wa March
2012.
Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ilifanya mahojiano na Wizara na Taasisi mbali mbali
zilizohusika pamoja na wananchi binafsi kwa mnasaba wa hadidu husika, kwa utaratibu ambao
Kamati imejipangia, kama ilivyoruhusiwa kufanya hivi kupitia kanuni ya 118(2) ya Kanuni za
Baraza la Wawakilishi Toleo la 2011. Aidha, Kamati imefanya ziara mbali mbali kwa mujibu wa
haja ilivyojitokeza katika kufuatilia hadidu rejea iliyohusika. Aidha, kwa maana hii, Kamati
imeweza kujikusanyia taarifa zake kupitia mahojiano mbali mbali iliyoyafanya; kupitia
„Nyaraka‟ (documents) mbali mbali ilizozikusanya kupitia njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na
kupitia kwa wahusika waliohojiwa ama kwa kufanya mawasiliano rasmi ya maandishi na taasisi
mbali mbali.
8 Angalia Hansard ya Baraza la Wawakilishi ya tarehe 14/07/2011, uk 92-99.
5
SEHEMU YA PILI :
UCHANGANUZI WA HADIDU REJEA HUSIKA:
HADIDU REJEA YA KWANZA:
2.0 UHAULISHWAJI WA KIWANJA CHA WIZARAYA MIUNDOMBINU NA
MAWASILIANO AMBACHO KIPO KWENYE ENEO ILIPOKUWEPO
KARAKANA NA YA WIZARA HIYO, ENEO LA MTONI, ZANZIBAR :
2.1 Utangulizi:
Kamati ilitakiwa kuchunguza Iwapo kweli Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imefanya
Uhaulishaji wa Kiwanja chake kilichokuwepo eneo la Mtoni- Zanzibar ambacho kilimilikiwa na
Wizara hii. Katika kuchunguza huko, Kamati ilitakiwa kwanza ijiridhishe kama kweli kiwanja
hicho kimeuzwa au bado kipo mikononi mwa Wizara. Aidha, kama kimeuzwa, basi ni vyema
Kamati ikafahamu sababu zilizopelekea kuuzwa kwake, lakini pia iangalie iwapo uuzwaji huo
unakubalika na ulifuata taratibu za kisheria na iwapo katika kuuzwa kwake, maslahi ya umma
yamezingatiwa.
Katika kupata ufafanuzi yakinifu, Kamati imekutana na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano tarehe 05/09/2011, katika Afisi ya Wizara iliyopo hapo Forodhani, eneo la Ofisi za
Shirika la Meli, kwa umaarufu wake huitwa, Bohari Kuu. Siku ya Jumanne, tarehe 06/09/2011
Kamati ilimwita Kaimu Meneja wa Kampuni ya Coastal Fast Ferries C. Ltd, Ndg. Ahmed Saleh
Karama ambae ndie aliehusika na utiaji wa saini wa Mkataba wa Uuzwaji wa Kiwanja hicho
kwa upande wa mnunuzi. Aidha, kwa kuwa katika Mkataba huo, mnunuzi alithibitisha ununuzi
wake kupitia Shahidi wake Ndg. Rahma Salim Hafidh, Kamati ilimwita Shahidi huyo ambae pia
ni Katibu Muhtasi katika Kampuni hiyo, ili nae kutoa ufafanuzi mbele ya Kamati juu ya ufahamu
wake wa uuzwaji wa kiwanja husika. Vile vile, katika ufatiliaji wa Hadihu hii rejea, katika kikao
cha Kamati pamoja na Uongozi wa Wizara, ilifahamika kwamba, Ndg. Feisal Ali Sultan
alitumika kufanikisha mauziano hayo kwa upande wa Mnunuzi na hivyo, Kamati ilimwita na
kumhoji tarehe 13/09/2011 siku ambayo pia Kamati ilimwita na kumhoji Ndg. Abdalla H.
Kombo ambae pia alihusika kwa namna moja ama nyengine kwa upande wa Muuzaji.
Kamati haikuishia hapo, siku hiyo hiyo tarehe 13/09/2011, ilimwita Mmiliki wa Kampuni
iliyonunua kiwanja hicho, Ndg. Said Salum Bakhressa kutoa ufafanuzi wake iwapo anafahamu
lolote juu ya mauziano hayo, na hatimae, Kamati ilimwita Mhe. Machano Othman Said,
aliekuwa Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, ambae pia alihusika katika Mkataba
wa mauziano ya Kiwanja, kuja mbele ya Kamati na kutoa ufafanuzi wake, tarehe 05/12/201,
katika Afisi ya Baraza la Wawakilishi, Mbweni Unguja. Baada ya ufafanuzi huo, ni vyema sasa
tukapata ufafanuzi wa Hadidu hii rejea kama ifuatavyo:
2.2 Uchambuzi wa Hadidu Rejea husika :
Kwa bahati nzuri, Kamati ilipokabidhiwa Hadidu hii Rejea, imekabidhiwa na hadidu ndogo
ndogo tulizoziweka katika utaratibu wa points, zinazoiongoza Kamati kuchunguza namna ya
Kiwanja kilichokuwa kinamilikiwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ambacho kipo
6
eneo la Mtoni Zanzibar kimehaulishwa kwa kuuziwa Kampuni ya Coastal Fast Feries Ltd.
Katika kutoa taarifa ya uchunguzi wake, Kamati imeona ni vyema ikatoa ufafanuzi unaohusika
kwa utaratibu huu wa Hadidu ndogo ndogo kama ifuatavyo:
2.3 Kuchunguza sababu zilizopelekea kuhaulishwa kwa kiwanja hicho.
Kamati moja kwa moja ilihoji sababu iliyoipelekea Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
kukihalisha kiwanja ambacho kilikuwa mikononi mwao, huku lengo halisi la matumizi ya
kiwanja hicho ni kujengwa Afisi ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Katika kutoa
ufafanuzi wake, Uongozi wa Wizara ulieleza kwamba, walikihaulisha kiwanja hicho kutokana na
kukosa fedha kutoka Serikalini za kuwawezesha kujenga Ofisi yao ya kudumu huku
wakikabiliwa na hali ngumu na hatarishi ya ubovu na uchakavu wa jengo walilokuwa
wanalitumia kwa matumizi ya Afisi yao, liliopo eneo la Malindi, ambalo ni jengo linalomilikiwa
na Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana. Kwa mazingira yaliyowakabili, kwa namna yoyote
ile, walilazimika kukihaulisha kiwanja hicho cha Mtoni, ili waweze kupata fedha
zitakazowawezesha kujenga Afisi nyengine eneo la Mazizini, kwani wakati huo Wizara ilikuwa
na viwanja viwili, na vyote vinaweza kutumika kwa matumizi ya aina moja, yaani kujengwa
Afisi ya Kudumu ya Wizara hii.
Hata hivyo, kabla ya Kamati kuangalia uzito wa sababu hii, inapenda kueka bayana shaka
inayoibuka ya usahihi wa maelezo ya watendaji wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
kwa mnasaba wa majibu ama sababu zilizowahi kutolewa na Viongozi wao, yaani, Waziri na
Naibu Waziri wa Wizara hii, wakati suala hili hili lilipoanza kuulizwa katika Baraza la
Wawakilishi. Mhe. Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano alipokuwa akijibu hoja
hii mbele ya Mkutano wa Nne wa Baraza la Wawakilishi, alimjibu Mhe. Mbarouk Wadi Mussa
Mtando ambae pia ni Mjumbe wa Kamati hii na hapa tunanukuu: “Mhe. Mwenyekiti, kiwanja cha Mtoni kinachozungumzwa kilikuwa ni kiwanja cha Wizara ya
Mawasiliano na uchukuzi ambayo sasa ni Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, lakini pale kilipo
ilionekana kabisa kwamba Wizara haiwezi kujenga makao makuu yake kuna sababu za msingi, Moja ni
mbali mno sana na mjini, lakini kama hilo halitoshi pale ni karibu sana na „Depot‟ ya mafuta9”
Kwa mnasaba wa majibu ya Mhe. Waziri na yale ya Watendaji Wakuu wa Wizara, utafahamu
kwamba, kuna mpishano mkubwa wa sababu sahihi ya uhaulishwaji wa Kiwanja. Ama
utashawishika na sababu za Watendaji ama za Mhe. Waziri wa Wizara hii, na wakati huo huo
kwa namna ya kupingana huko unaweza pia ukapata shaka kama kweli Mhe. Waziri alitegemea
majibu yake binafsi wakati akijibu suala hilo ama alikusudia kulidanganya Baraza na
kuwapotosha Wajumbe wake kuhusu usahihi wa suala hili ulipohitajika, ama utajiuliza iwapo
Watendaji Wakuu wa Wizara ndio waliokusudia kuidanganya na kuipotosha Kamati Teule, pale
ilipotaka ufasaha wa suala hili. Hata hivyo, hoja ya msingi Kamati inayotaka ifahamike hapa ni
kwamba, kuna tofauti kubwa ya majibu yaliyotolewa juu ya usahihi wasuala hili, wakati wa
Kamati na wakati wa mjadala wake Barazani.
Kwa namna yoyote ile, kwa kuwa maamuzi ya Wizara ni kutokitumia kiwanja hicho kwa
madhumuzi yaliyokusudiwa awali, unaweza ukajiuliza masuala mengi zaidi, lakini moja kati ya
hayo, “Je Serikali imeshindwa kujenga Ofisi ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na
9 Hansard ya Baraza la Wawakilishi, tarehe 14 Julai 2011, uk-93 (Paragrafu ya 2 kutoka juu).
7
hatimae imeruhusu kuhaulishwa kwa kiwanja hicho?”. Katika kupata ufafanuzi wa suala hili,
Kamati inapenda kutukumbusha kwamba, katika Kikao cha Bajeti ya Serikali ya mwaka
2008/2009, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano iliomba kuidhinishiwa jumla ya Tsh.
200,000,000/- kwa ajili ya Ujenzi wa Afisi yake ya Kudumu iliyokusudiwa kujengwa katika
Kiwanja hicho cha Mtoni, kabla Kiwanja hicho hakijahaulishwa. Hata hivyo, hakuna kumbu
kumbu za kutolewa pesa yoyote kati ya hii iliyoidhinishwa na kwa mnasaba wa majibu
yaliyotolewa mbele ya Kamati, Uongozi wa Wizara ulieleza kwamba, hawakuingiziwa fedha
yoyote ya ujenzi husika. Aidha, katika Mkutano wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2010/2011,
Wizara ilidhinishiwa Tsh. 100,000,000/- kwa lengo hilo hilo na hatimae Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar iliwaingizia Tsh. 49,100,000/- kama ilivyothibitishwa mbele ya Kamati na Mhasibu
Mkuu wa Wizara Ndg. Said A. Ussi. Pamoja na kuingiziwa fedha hizo ka madhumuni ya Ujenzi
wa Afisi ya Kudumu ya Wizara, Wizara ilibadilisha matumizi ya fedha, badala ya kuanza Ujenzi
angalau kwa kiwango cha fedha ilizopewa, kwa makusudi imeamua kukarabati Majengo ya
Shirika la Meli, na sasa kuwa na Ofisi ya Mhe. Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na viongozi
wengine wa Wizara. Aidha, walifanya hivi kwa lengo la kulikipunguzia mzigo wa watumiaji
jengo lao la awali, ambalo ni mali ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, ili kuliepusha
kuanguka na kuleta maafa.
Kwa mnasaba wa maelezo ya hapo juu, ni wazi kwamba, Serikali haikushidwa kutoa fedha kwa
ajili ya ujenzi wa Afisi ya Kudumu ya Wizara. Aidha, Serikali kutotoa fedha mwaka 2008/2009,
na kutoa 49.1% ya fedha zilizoidhinishwa mwaka 2009/2010, hakuhalalishi hoja ya Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano ya kulazimika kutafuta fedha nje ya Serikali kwa lengo la ujenzi
wa Afisi yake. Ilitosha kuzitumia fedha ilizopatiwa Tsh. 49,100,000/- kwa mwaka wa 2009/2010
kwa kujenga Afisi yao kama walivyokusudia, huku wakiendelea kuomba fedha hizo katika kila
muda wa Bajeti ya Serikali ya mwaka husika ama kwa namna nyengine inayokubalika kisheria.
Vile vile, pia kuna suala jengine ni la msingi sana kupata jawabu. Yaani, kwa kuwa Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano imeamua kuzitumia Tsh. 49.100,000/- kwa matumizi ya
Ukarabati wa jengo la Shirika la Meli na Uwakala kwa kujenga Afisi ya Waziri, Naibu Waziri na
ofisi za watendaji wake wakuu, ama pia kukarabati jengo la zamani wanaloendelea kulitumia
kwa matumiz ya Ofisi, ambalo ni mali ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, wakati huo
huo fedha hizo ziliidhinishwa na Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya Ujenzi wa Afisi ya Wizara
katika kiwanja cha Wizara Mtoni, imepata wapi idhini ya matumumizi hayo?
Kabla ya kujibu uhalisia wa suala hili, kwanza ni vyema tukakumbuka kwamba, kwa mujibu wa
kifungu cha 88(d) cha Katiba ya Zanzibar, Baraza la Wawakilishi lina jukumu la kuidhinisha na
kusimamia mipango ya maendeleo ya Serikali katika njia ile ile ambayo Bajeti ya mwaka
inaidhinishwa. Ufahamu wa maelezo haya ya Katiba ni kwamba, Baraza la Wawakilishi ikiwa ni
pamoja na kupitia Kamati zake, lina wajibu wa kuisimamia Serikali iweze kutumia mipango
yake ya maendeleo kwa namna ile ile Bajeti ya mipango hiyo imeidhinishwa na Baraza. Yaani,
kwa kuwa Baraza la Wawakilishi kwa kila mwaka huidhinisha mipango ya maendeleo ya
Serikali, ni wajibu wa Serikali kuitekeleza mipango hiyo kwa mujibu wa kuidhinishwa kwake na
Baraza. Hii pia ina maana, kwa kuwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2009/2010 Baraza la
Wawakilishi liliidhinisha Tsh.100,000,000/- kwa ajili ya Ujenzi wa Afisi ya Kudumu ya Wizara
ya Miundombinu na Mawasilino, basi fedha hizo ni lazima zitumike kwa matumizi ya Ujenzi wa
Afisi ya Kudumu ya Wizara na sio vyenginevyo. Au kama Wizara ililazimika kuzitumia fedha
8
hizo kinyume na namna ilivyoidhinishwa, basi suala hili ni lazima lifuate taratibu za Sheria
zilizwekwa.
Kwa mfano, kwa mujibu wa kanuni ya 51 ya Kanuni za Fedha za mwaka 2005, Waziri
anaehusika na mambo ya Fedha, amepewa uwezo wa kuhaulisha fedha za kifungu kimoja hadi
chengine (vote and sub-vote) kwa sharti la kutozidi kiwango kilichoidhinishwa na Baraza la
Wawakilishi. Lakini ruhusa hii hutolewa kwa utaratibu wa kuwepo kwa maombi ya kufanya
uhaulishaji huo, yakionesha kiwango kinachotaka kuhaulishwa na fedha za ziada zinazotaka
kutumiwa. Aidha, maombi hayo yaoneshe sababu za msingi kuomba uhaulishaji husika huku
maombi yakipelekwa kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya
Maendeleo huku kopi yake ikipelekwa kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali na Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali. Aidha, baada ya kukubalika maombi hayo, atatoa taarifa kwa
kuisani na kumpa Afisa Mhasibu (Accountig Officer) na kopi yake ikipelekwa kwa Mhasibu
Mkuu kwa kuchukua hatua.
Tunachotaka hapa kifahamike ni kwamba, kwa kuwa Wizara imeamua kufanya mabadiliko ya
matumizi ya Tsh.49,100,000/- kinyume na ilivyoidhinishwa na Baraza la Wawakilishi, ilipaswa
ifuate taratibu za kisheria, lakini kwa bahati mbaya sana, Wizara imeshindwa kuithibishia
Kamati kufuata taratibu hizo na Kamati imejiridhisha kwamba, Wizara imejiamulia kuzitumia
fedha hizo bila ya kuheshimu malekezo ya Katiba wala Sheria.
2.4 Kuchunguza iwapo taratibu za kisheria zilifuatwa katika kukihaulisha kiwanja hicho.
Kabla ya kuangalia utaratibu uliofuatwa katika uhaulishwaji wa kiwanja, kuna haja kwanza ya
kujiridhisha iwapo „Uhaulishwaji‟ huo una maana ya kuuzwa; kukodishwa; kubadilishwa kwa
kupewa kitu chengine chenye thamani inayowiyana au kuhaulishwa kwa namna ipi? Pamoja na
uzuri wa hoja hii, Kamati haikupata ufafanuzi wa wazi kuhusu suala hili wakati ilipokutana na na
Watendaji wa Wizara. Kwa mfano, wakati akijibu suala hili, Naibu Katibu Mkuu, Ndg. Msanifu
H. Mussa aliitaka Kamati ndio itoe tafsiri sahihi ya Uhaulishwaji uliofanyika. Na kwa hivyo,
katika kikao hicho, Kamati haikupata neno la moja kwa moja la kutafsiri neno „Uhaulishwaji‟
kwa maslahi ya hoja hii. Hata hivyo, wakati Kamati ilipomwita na kukutana na Kaimu Meneja,
wa Kampuni iliyohaulishiwa Ndg. Ahmad Saleh Karama wa Kampuni ya Coastal Fast Ferries
Limited, yenye sanduku la barua 744, aliithibitisha Kamati kwamba, Kiwanja hicho kimeuzwa
kutoka Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na kuuziwa Kampuni yao ya (Coastal Fast
Feries Ltd), uthibitisho kama huu pia ulitolewa na Ndg. Said Salim Bakhressa, mmiliki wa
Kampuni hii. Na kwa mazingira halisi ya kiwanja hicho kilivyohaulishwa, ushahidi ilioupata
kutoka Wizarani pamoja na uthibitisho wa mmiliki wa Kampuni, Kamati imejirisha kwamba,
tukisema kiwanja hichi kimehaulishwa, maana yake kiwanja hichi kimeuzwa kutoka Serikalini,
chini ya Usimamizi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na kuuziwa Mtu binafsi,
ambapo kisheria na kwa maslahi ya hoja hii, Kampuni ya Coastal Fast Feries Ltd.
Kwa kuwa kiwanja hicho kimeuzwa, basi kuna haja ya kujiuliza, ni sheria gani iliyotumika
katika kuuza kiwanja hicho? Watendaji wa Wizara walipolijibu suala hili walisema Sheria
iliyotumika ni Sheria ya Umiliki wa Ardhi, Namba 12 ya mwaka 1992 (Land Tenure Act, No. 12
of 1992). Majibu haya pia yanaenda sambamba na majibu ya Naibu Waziri wa Wizara hii, Mhe.
9
Issa Ussi Gavu alipokuwa akijibu hoja hii katika Baraza la Wawakilishi10
kumjibu Mhe.
Mbarouk Wadi Mussa (Mtando) kuhusu Sheria iliyotumika kuhaulisha kiwanja hicho, alijibu ni
Sheria ya Ardhi ya mwaka 1992 ambayo inampa Mamlaka Mhe. Rais kuwa mmiliki wa ardhi
yote ya Zanzibar. Kwa majibu yake, Mhe. Naibu Waziri anakusudia kuthibitisha kwamba,
Wizara imefuata taratibu zote za kisheria katika kuuza kiwanja hicho, kwa kutumia Sheria hiyo,
Namba 12 ya mwaka 1992. Aidha, kwa upande wa Kamati, hoja hii inatiliwa mashaka. Kamati
haipingani na ukweli kwamba masuala ya ardhi yanasimamiwa na Sheria hiyo, Namba 12 ya
mwaka 19992, wala haipingani na mamlaka aliyopewa Mhe. Rais katika Sheria hiyo, isipokuwa
sheria hiyo sio pekee ya kutumiwa katika kuuzwa kwa kiwanja hiki cha Wizara ya Miundombinu
na Mawasiliano. Kiwanja hiki kilikuwa ni mali ya Wizara, na Wizara inaongozwa na Viongozi
wengi katika vyombo tofauti. Hivyo, kama kuna maamuzi ya kuuzwa kwa kiwanja
tunachokizungumzia, basi maamuzi hayo hayawezi tu kutoka bila ya utaratibu wa kisheria. Kwa
mfano kabla ya Wizara kuuza kiwanja hicho, ilipaswa ikae Bodi ya Zabuni ya Wizara
inayohusika na Manunuzi na Uuzaji wa Mali za Wizara ifanye maamuzi yanayohusika. Na kwa
hali hii, kabla ya hatua ya kukiuza kwa kutumia Sheria Namba 12 ya mwaka 1992, Wizara
ilipaswa kuitumia na kufuata taratibu za Sheria ikiwa ni pamoja na Sheria ya Manunuzi na Ugavi
wa Mali za Serikali Sheria Namba 9, 2005.
2.4.1 Utangazaji wa Zabuni na Mamlaka ya Kumtafuta Mnunuzi:
Hapa kuna suala la kujiuliza: Je, Wizara ilimpataje Mwekezaji (Kampuni ya Coastal Fast Feries
Ltd, iliyouziwa kiwanja hicho)? Je ilifuata taratibu za sheria ya Manunuzi na Uuzaji wa Mali za
Serikali (The Public Procurement Act, No. 9 of 2005)? Kabla ya kulijibu suala hili ni vyema
tukakumbuka kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria hiyo, ni wajibu wa kila Afisa
Mhasibu (kwa maana ya Wizara hii, Katibu Mkuu wa Wizara) kuhakikisha kwamba Uuzaji ama
Uhaulishwaji wa mali yoyote ya Serikali ni lazima ufanywe kwa kufuata masharti yaliyoelezwa
katika sheria hii na Kanuni zake. Aidha, kwa mnasaba wa kifungu cha 10 (1) cha Sheria hii, ni
lazima kuwepo katika kila Wizara, Idara inayojitegemea, Shirika au katika Serikali za Mitaa
Bodi ya Zabuni (Tender Board) kwa ajili ya kuuza na kununua mali za Serikali, Huduma na Kazi
za Taasisi husika.
Kwa maana hiyo, moja ya utata wa suala hili ni kutofuatwa kwa masharti ya Sheria hiyo. Kamati
imethibitishiwa kwamba, hakuna kikao chochote cha Bodi ya Zabuni ya Wizara wala Serikali
Kuu kilichokaa kufanya maamuzi ya Uuzaji wa kiwanja hicho. Kama hii haitoshi, Kamati pia
imepata uhakika kwamba, hakuna kikao chochote cha Bodi ya Zabuni kilichokaa na kuthibitisha
(Approve) utaratibu wa uliotumika kumpata Mnunuzi wa Kiwanja hiki, wakati kwa mujibu wa
kifungu cha 32(2) cha Sheria Namba 9 ya mwaka 2005, kinataka lazima Bodi ya Zabuni ya
Wizara ikae na kuthibitisha njia ya kutumika kumpata Mnunuzi wa kiwanja husika. Aidha,
Kamati imethibitishiwa kwamba, haja ya kuuzwa kiwanja hicho kwa Kampuni hiyo imetokana
na Ndg. Abdalla H. Kombo, Mfanyakazi wa Wizara ambae hivi sasa ni Mkurugenzi wa
Mipango, Sera na Utafiti Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na kwa sasa ni Kaimu Mrajis
wa Meli. Ndg. Abdalla alimtafuta mmiliki wa Kampuni iliyouziwa kiwanja hicho na kukubalina
na hatimae kamfuata Mhe. Waziri wa wakati huo, Mhe. Machano Othman Said na hatimae
maamuzi ya kuuzwa kiwanja hicho yakafanyika.
10
Ibid, uk- 94-96
10
Ndg. Rajab Y. Uweje (Mkurugenzi wa Utumishi) pamoja na majibu haya kutofautiana na
Watendaji wenzake, aliieleza Kamati kwamba, kuna kikao kilichofanyika na kufikia maamuzi ya
kukiuza kiwanja hicho. Kamati ilipotaka kupatiwa kumbu kumbu za kikao hicho ilipewa ya
tarehe 19/07/2010 yenye jina „Kikao cha Wakuu wa Vitengo, Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi, Idara ya Mipango na Sera‟ na kumbu kumbu ya yatokanayo ya kikao hicho cha tarehe
14/06/2010 (Kielelezo Na.1). Vile vile, wakati Kamati ilipomwita Ndg. Abdalla H. Kombo
aliieleza Kamati kwamba, katika kila Jumatatu Wizara ilikuwa inafanya kikao cha Wakuu wake
wa Vitengo na moja katika kikao hicho walifanya maamuzi ya kukiuza Kiwanja chao cha Mtoni.
Aidha, katika kikao hicho ndio waliamua haja ya kumtafuta Mnunuzi, ingawaje kazi ya
Kumtafuta na hatimae kumbarikia Coastal Fast Ferries iliachwa kwa Mhe. Waziri, kwa sababu
aliwaeleza kwamba kazi hiyo ya kumtafuta mnunuzi alisema aachiwe yeye.
Kabla ya kuangalia uwezo wa Kikao cha Wakuu wa Kitengo cha Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano kuamua juu ya uuzwaji wa kiwanja, ni vyema kwanza tukafahamu hicho
kilichojadiliwa kwa mnasaba wa hoja yetu. Katika kikao cha tarehe 19/07/2010, Wakuu hao wa
Vitengo walikujadiliana mambo 12, moja kati ya hayo ni kuhusu Taarifa ya ubovu wa jengo.
Kwamba, Kikao hicho kilipokea taarifa kwamba, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
imepokea barua kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mji Mkongwe kwamba jengo la
Makao Makuu la Wizara limekuwa bovu na linahatarisha usalama wa wafanyakazi waliomo.
Hivyo, Malaka iliishauri Wizara kuhama katika jengo hilo na kutafuta sehemu nyengine ili
Mamlaka iweze kuchukuwa hatua za kulihami jengo hilo. Baada ya kikao kupokea taarifa hiyo,
ilifanya maamuzi yafuatayo:
o Kuandaa dokezo/pendekezo na kulipeleka kwa Mhe. Waziri ili kutaka idhini ya
kuwapa ruhusa ya kutafuta eneo jengine la kujega Ofisi ya kudumu ya Wizara”
o Kumshauri Mhe. Waziri juu ya kutafuta Mfadhili wa kubadilishana kiwanja na
kutufanyia ujenzi angalau wa ghorofa moja katika kiwanja kipya cha Wizara
kiliopo Mazizini”.
Kwa mnasaba wa maelezo ya hapo juu, ni wazi kwamba, maamuzi ya kukiuza kiwanja na
hatimae kumpata mnunuzi (Mfadhili) wa kukinunua kwa masharti ya kuwajengea ghorofa moja
katika kiwanja chao kipya cha Mazizini yametoka katika kikao cha Wakuu wa Vitengo cha
Wizara na Kamati imejitosheleza kwamba, maamuzi haya hayakufanywa na mtu mmoja. Hata
hivyo, Kamati pia imejiridhisha kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa Wizarani na kutoka kwa
Ndg. Abdalla H. Kombo kwamba maamuzi ya kumpata Coastal Fast Ferries Co. Ltd kama
mnunuzi wa kiwanja hicho hayakuamuliwa katika kikao cha Wakuu wa Vitengo, bali
yaliamuliwa na Mhe. Waziri wa Wizara hiyo, baada ya kupelekewa maamuzi ya kikao juu ya
haja yao kumuomba awaruhusu wamtafute Mfadhili wa kujenga ghorofa moja katika kiwanja
cha Mazizini kwa matarajio (consideration) ya kumuuzia kiwanja cha Mtoni.
Tunazidi kusisitiza kwamba, kwa mujibu wa maelezo hayo ya taarifa za kikao hiki, Kikao cha
Wakuu wa Vitengo cha Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano (wakati huo ikiitwa Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi) hakikufanya maamuzi yoyote kuhusu uuzwaji wa kuwanja na badala
yake kimependekeza na kuomba ushauri kwa Mhe. Waziri. Ilipaswa Mhe. Waziri achukue
sehemu yake ya kupendekeza na kutoa ushauri na sio yeye kuamua kumtafuta Mnunuzi wa
kiwanja. Hapa inatubidi tuseme kwamba, Mawaziri wa Wizara baada ya kutekeleza majukumu
yao, ndio wamegeuka madalali. Unaweza kujiuliza masuala mengi kuhusiana na sababu
11
zilizompelekea Mhe. Waziri kuamua kumtafuta Mnunuzi wa kiwanja hiki, na zaidi bila hata ya
kuwashirikisha watendaji wake. Unaweza kusema kwamba katika hali kama hii, bila ya shaka
kuna harufu ya Rushwa, venginevyo Sheria ingelifuatwa. Jambo la kushangaza hata watendaji
wakuu wa Wizara hii hawajui ni nani khaswa aliehusika kumpata mnunuzi. Kwa Mfano, wakati
wakitoa ufafanuzi huo mbele ya Kamati, viongozi hawa walisema kwamba, Ndg. Abdalla H.
Kombo ndie aliekuwa kiungo wa Mhe. Waziri katika kumtafuta Ndg. Said Salum Bakhressa na
ndie aliupeleka Mkataba wa kuuzwa kwa kiwanja hicho kutoka Wizarani hadi kwa Kampuni ya
Mnunuzi. Hata hivyo, akitoa ufafanuzi wa suala hili, Ndg. Abdalla H. Kombo aliieleza Kamati
kwamba, yeye hakuwatafuta Kampuni ya Coastal Fast Ferries Ltd, wala hajawahi hata siku moja
kuzungumza na Kampuni hiyo kuhusu kiwanja, wala hajui chochote kilichoendelea baada ya
kumfikishia Mhe. Waziri taarifa ya kikao cha Wakuu wa Vitengo kuhusu ushauri walioutoa.
Mbali na hayo, Kamati pia ilitaka kuthibitishiwa juu utaratibu wa mawasiliano uliotumika
kupeana habari na haja ya kuuzwa kwa kiwanja hicho kutoka Wizara hadi kwa Kampuni. Hii ina
maana kwamba, kwa kuwa taratibu rasmi za Serikali inapofanya mazungumzo yoyote na mtu
ama taasisi nyengine huwa inafanya kupitia mawasiliano ya maandishi, ni wazi kuwa,
kungekuwepo na mawasiliano hayo, baina ya Wizara na Kampuni hiyo, kabla ya kuingia nae
Mkataba wa kumuuzia kiwanja. Hata hivyo, pamoja na haja hii, Kamati haikupatwa taarifa
zozote za mawasiliano haya yaliyofanyika zaidi ya kuambiwa na kujiridhisha kwamba,
mazungumzo yote baina ya Wizara na Kampuni iliyouziwa kiwanja hicho yamefanywa kwa
mdomo, hakuna barua yoyote inayoelekeza ama kushauri kuuzwa kwa kiwanja hicho kutoka
Wizarani hadi kwa Mnunuzi. Aidham wakati Kamati inafanya mahojiano na Ndg. Said Salim
Bakhressa juu ya utaratibu uliotumika mpaka yeye akakinunua kiwanja hicho aliieleza Kamati
kwamba yeye ni Mfanya biashara na anakumbuka Waziri (Mhe. Machano Othman Saidi)
alimpigia simu kwamba anahitaji kukihaulisha kiwanja. Na hivyo walipatana katika ununuzi
wake kama ilivyo katika Mkataba wa Mauziano.
2.4.2 Mkataba wa Uhaulishaji:
Bado tunaendelea kutoa ufafanuzi kuhusiana na hadidu hii ndogo inayoitaka Kamati kuchunguza
iwapo taratibu za kisheria zilifuatwa katika uhaulishwaji wa kiwanja husika. Hivyo, tufahamu
kwamba, ili taratibu za kisheria ziweze kukamilika, ni lazima kuwe na Mkataba wa mauziano
baina ya Wizara ya Miundombinu na Mwasiliano na Kampuni ya Coastal Fast Ferries Co. Ltd
unaohalalisha uuzwaji huo. Hata hivyo, kabla ya kuangalia Mkataba huo ni vyema pia
tukakumbuka kwamba, kabla ya suala hili kufikishwa mbele ya Kamati Teule, lilianza
kufanyiwa kazi na Kamati ya Kuchunguza na kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (P.A.C).
Na ili kupata ufafanuzi mzuri, Kamati ya P.A.C ilitaka kupatiwa Mkataba wa Uhaulishwaji,
lakini kwa bahati mbaya sana, haikupewa Mkataba huo kwa kuambiwa kwamba, Mkataba huo
haupo. Suala hili pia lilijadiliwa tena katika Baraza la Wawakilishi, katika Mkutano wake wa
Nne wa kupitia Bajeti ya Serikali, ambapo Mhe. Omar Ali Shehe, Mwenyekiti wa Kamati ya
P.A.C alieleza namna Kamati yao ilipoenda kufanya kazi na kupewa majibu ya kutokuwepo kwa
Mkataba11
na ndio maana Kamati hii ya P.A.C iliwataka Wizara wazuie ujenzi uliokuwa
unaendelea kiwanjani hapo (Kielelezo Na.2), lakini ilipata majibu kwamba, kiwanja hicho
kimehaulishwa na Mamlaka husika na hivyo, Wizara haina uwezo wa kuuzuia ujenzi huo
(Kielelezo Na.3). Hata hivyo, tofauti na maelezo ya awali, wakati Kamati Teule inafuatilia suala
11
Ibid, uk-98.
12
hili, kwa mshangao mkubwa iliambiwa Mkakataba huo upo na kwa ushahidi zaidi ilipatiwa
Mkataba husika ambao umefungwa tarehe 20/10/2011. Pamoja na kuwepo kwake, kuna kasoro
nyingi zilizojitokeza wakati Kamati ilipoupitia Mkataba husika. Kasoro hizo ni hizi zifuatazo:
2.4.3 Mikataba Miwili kufungwa katika suala moja.
Kwa kawaida na kwa mujibu wa sheria, Mikataba inayotambulika kisheria huwa ni mmoja
ambao ungeweza kutolewa katika kopi zaidi ya moja. Tatizo lilotokea ni Kamati kupewa
mikataba miwili tofauti. Wizarani Kamati ilipewa Mkataba usiokuwa na Nembo yoyote ya
Serikali wala Muhuri wa Wizara husika. Mkataba huu una muhuri wa Mhaulishwaji (Coastal
Fast Feries Ltd) pekee (Kielelezo Na.4) huku Uongozi wa Wizara ukisisitiza kwamba, Mkataba
huo ndio sahihi na wala hakuna Mkataba mwengine uliofungwa juu ya jambo hilo. Hata hivyo,
mambo yalikuwa tofauti na maelezo ya Wizara, wakati Kamati ilipomwita Kaimu Meneja, Ndg.
Ahmad Saleh Karama wa Kampuni hii aliwasilisha Mkataba mwengine wenye mihuri yote
miwili, Muhuri wa Wizara na Kampuni yake (Kielelezo Na.5) nae akisisitiza kwamba, Mkataba
huu aliokuja nao yeye ndio Mkataba halali na hakuna mwengine uliofungwa juu ya suala hili.
Mbali na tatizo hili, ambalo kisheria linaleta utata mkubwa, jambo jengine linaloutafautisha
Mkataba uliotolewa na Wizara na Mkataba huu uliotolewa na Kampuni ya Coastal Fast Ferried
C. Ltd ni kwamba, Mkataba wa Wizara hauna saini yoyote katika ukurasa wa kwanza, wakati
Mkataba wa Kampuni una saini zote, ya Kaimu Meneja na Waziri.
Yaani, kwa kawaida katika Mikataba, mbali na kutiwa saini sehemu ya saini husika, ambayo
mara nyingi huwa ukurasa wa mwisho wa Mkataba, pia saini hizo, yaani ya Muuzaji na Mnunuzi
hutiwa katika kila ukurasa wa Mkataba, ili kuutia nguvu zaidi kisheria. Sasa kwa bahati katika
Mkataba ambao Kamati imepewa na Wizara hauna saini hizo katika ukurasa wa kwanza, kati ya
kurasa mbili za Mkataba huo, wakati katika Mkataba uliokabidhiwa na Kampuni una saini zote
mbili, za Muuzaji na Mnunizi katika kurasa ya awali ya Mkataba huo. Hichi pia ni kigezo cha
utofauti wa Mikataba hii. Aidha, katika tofauti nyengine iliyojitokeza ni kwa upande wa
Wahusika wa Mkataba (Parties to the Contract). Kwa kawaida Mikataba huwa na Wahusika
wake, ambao kisheria huitwa „Parties to the Contract‟ ambao katika mauziano kama haya,
upande wa mwenye kuuza huitwa „Muuzaji‟ na upande wa anaenunua mara nyingi huitwa
„Mnunuzi‟. Sio lazima jina hili liitwe kwa kila upande, lakini kama ni Mkataba mmoja anaeuza
ameitwa „Muuzaji‟ basi bila ya shaka jina hili kama lilivyo litaendelea kujitokeza katika kila
Mkataba ambao utarajiwa kuwa kopi ya Mkataba wa asili. Tofauti na Mikataba hii, Katika
Mkataba ambao Kamati imepewa na Wizara, (Rejea Kielelezo Na.4), jina la Wizara, ambae ndie
Muuzaji ameitwa „MHAULISHAJI‟ wakati katika Mkataba ambao Kamati imepewa na
Kampuni iliyouziwa (Rejea Kielelezo Na.5), jina hili la Wizara limeitwa „MWENYE
KIWANJA‟. Tofauti hii iko wazi na ni uthibitisho kwamba, Mikataba hii ni miwili tofauti na sio
Mkataba mmoja.
Baada ya kufahamu kasoro hizi, Kamati iliendelea kujiuliza iwapo mapungufu haya yanatokana
na Mikataba hii ilikuwa miwili na yote imefungwa juu ya jambo moja ama kulikuwa na Mkataba
mmoja tu ambao ulitolewa kopi mbili. Aidha, mbali na Kamati kupata majibu haya tuliyokwisha
yaeleza hapo kabla, kwamba wanachokifahamu Wizara ni kuwepo kwa Mkataba mmoja tu,
ambao ndio walioukabidhi kwa Kamati, Kamati haikutosheka na majibu haya na zaidi baada ya
kupokea Mkataba wa pili kutoka kwa Kaimu Meneja wa Kampuni ya Coastal Fast Ferried Co.
Ltd. Hivyo basi, wakati akijibu suala hili Kaimu Meneja wa Kampuni hii alithibitisha kwamba
13
Mkataba huo ni mmoja uliopelekwa kwake ili yeye atie saini na aliletewa kopi mbili tofauti, na
zote alitia saini. Kwa hali hii, Kaimu Meneja alitaka kuhalalisha kwamba kuna Mkataba mmoja
tu, lakini anakumbuka aliletewa kopi mbili. Pamoja na kujieleza hivi, maelezo haya ya Kaimu
Mkurugenzi wa Kampuni hii yanagongana na Shahidi wake katika Mkataba huo Ndg. Rahma
Salim Hafidh ambae alithibitisha kutia saini Mkataba mmoja tu, nao ni wa Kampuni, hivyo saini
yake kujitokeza katika Mikataba miwili tofauti ni jambo asilolifahamu.
2.4.4 Tatizo la saini katika Mkataba:
Kasoro nyengine inayotia wasi wasi usahihi wa Mkataba huu kisheria inajionesha katika saini ya
Muuzaji na Mnunuzi wa Kiwanja hicho. Tukianza na upande wa Muuzaji, Mkataba huu umetiwa
saini na aliekuwa Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Machano Othman Said
na haukutiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Ili kupata ufasaha wa hoja hii, ni vyema
kwanza tukajikumbusha kidogo kupitia Katiba ya Zanzibar ambapo kifungu cha 50(1)
kinasomeka ifuatavyo:
“Pale Makamo wa Kwanza wa Rais na Mkamo wa Pili wa Rais au Waziri yeyote
mwengine anapokuwa na dhamana ya Wizara yeyote ya Serikali, atakuwa ndiye kiongozi
na Msimamizi Mkuu na bila ya kuathiri masharti yoyote ya usimamizi, Katibu Mkuu
ambaye afisi yake itakuwa ni ya utumishi wa Serikali atakuwa ndiye Afisa Mtendaji
Mkuu wa Wizara”
Tunachotaka kieleweke hapa ni kwamba, Katibu Mkuu wa Wizara ndie Mtendaji Mkuu wa
Wizara husika na kwa utaratibu wetu wa utendaji wa Serikali kwa msingi wa kifungu
tulichokinukuu hapo juu, Katibu Mkuu huhusika na Mikataba ya Wizara yake na sio Waziri, kwa
sababu ndie Mtendaji Mkuu wa Wizara hiyo. Aidha, kwa upande wa Wizara, Katibu Mkuu wa
Wizara ndie mwenye dhamana na msimamizi Mkuu wa Rasilimali za Wizara yake, vile vile ndie
mwenye dhamana ya mawasiliano yote yanatofanyika baina ya Wizara yake na Taasisi nyengine.
Kama ni hivyo, inafahamika kwamba, ni Katibu Mkuu wa Wizara hii alietakiwa kutia saini ya
Mkataba huu, jambo ambalo halikufanyika na badala yake, Mhe. Waziri (Machano Othman
Said) ndie aliyetia saini hiyo. Jambo hili pia linaendelea kutia mashaka ya usahihi wa Mkataba
ama Makubaliano haya.
Kwa upande wa Mnunuzi, Mkataba huu umemtambua Mkurugenzi Mtendaji, Ndg. Said Salim
Awadh (Bakhressa) ambae ndie Mmiliki wa Kampuni hiyo na ndie aliehusika na ununuzi wa
kiwanja husika. Katika Mkataba huu, ama mikataba yote miwili iliyowasilishwa kwa Kamati,
saini ya Mnunuzi ilitakiwa itiwe na Ndg. Bakhressa, lakini saini hiyo imetiwa na Kaimu Meneja
Ndg.Ahmed Saleh Karama, kitendo ambacho kwa mtazamo wa Sheria za Mikataba, ni kosa
kisheria kwa mtu yeyote kutia saini isiyokuwa yake na kitendo hichi ni sawa na udanganyifu wa
Nyaraka, aidha kinaufanya Mkataba kukosa ridhaa ya Mnunuzi na ni sawa na kusema kwamba
Mkataba huu ni batili kisheria. Ili kupata ushahidi huu, Kamati ilipomwita Kaimu Mkurugenzi
huyo, Ndg. Ahmed alikiri kwamba, ametia yeye saini hiyo, kutokana na Ndg. Bakhressa
kutokuwepo na kumwambia amalize yeye hatua za mauziano. Kauli hii pia ilithibitishwa na Ndg.
Said Salum Bakhressa ambae mbele ya Kamati amekiri kwamba saini hiyo hakutia yeye na
badala yake imetiwa na Kaimu Meneja.
14
2.4.5 Uvunjwaji wa Mkataba.
Mkataba wowote wa kisheria huwa na nguvu za kisheria baada ya kutiwa saini na pande zote
mbili ili kuonesha ridhaa ya wahusika (consent of the parties). Baada ya hatua hii, kila upande
hulazimika kutekeleza yale waliyokubaliana na hakuna hata upande mmoja wenye uwezo wa
kwenda kinyume na makubalinao hayo na ikitokezea upande mmoja umekwenda kinyume,
Mkataba huo utavunjika na upande wa pili una haki ya kudai haki zake zilizoathirika na
uvunjwaji wa Mkataba dhidi ya upande uliohusika. Kwa mnasaba huu, kuna haja ya kuangalia
masharti ya Mkataba husika na namna yalivyokiukwa. Kipengele cha 8 cha Mkataba husika
kinasomeka
“Kwamba, gharama zote za uhaulishaji zitafanywa na Mhaulishaji”.
Katika sharti hilo la Mkataba inakusudiwa kwamba, Kiwanja hicho kilichouzwa kabla ya
kuuzwa kwake kilikuwa kinatumiwa na Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara (UUB), ambayo
iko katika Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, na kulikuwa na vifaa pamoja majengo
mbali mbali madogo madogo yaliyotumiwa na Idara hii, hivyo, kabla ya kukabidhiwa kiwanja
hicho kwa Mnunuzi, kwa mujibu wa sharti la kifungu cha 8 cha Mkataba, wamekubaliana
kwamba, kiwanja hicho kikabidhiwe kikiwa katika hali ya usafi, yaani baada ya kuondoshwa
kwa vifaa hivyo huku gharama hizo zikibebwa ama kufanywa na Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano ambae ndie Mhaulishaji. Kwa hivyo, ili kuona kwamba masharti ya Mkataba huu
yameheshimiwa, ni lazima Wizara ithibitishe kwamba imetumia gharama zake kufanya usafi
uliokusudiwa na isitokezee hata kauli yoyote kutoka kwa Mnunuzi kusema kwamba ametumia
ghrama zake kufanya usafi wa kuondosha vifaa hivyo. Kwa upande wa pili, maneno „gharama
zote za uhaulishaji‟ yanaweza kufahamika kwamba yanahusiana na utayarishaji wa hati za
kisharia za kuhaulisha kiwanja (Legal Instrumensts) ikiwa ni pamoja na kuandaa, Mikataba ya
Uuzaji, Warka ama Hati ya Uuzaji na nyaraka nyenginezo. Na kwa tafsiri hii, inafahamika
kwamba, ni Wizara ya kutayarisha nyaraka zote kwa ghrama zake.
Pamoja na tafsiri zaidi ya moja ya maneno hayo, Kamati imejiridhisha kwamba kilichokusudiwa
katika kifungu hiki cha Mkataba ni gharama zinazohusiana na uondoshaji wa vifaa
vilivyokuwepo katika kiwanja kilichouzwa na imejiridhisha kutokana na maelezo yaliyotolewa
na Viongozi wa Wizara, na maelezo ya namna hii pia yamethibitishwa na Viongozi wa Kampuni
iliyonunua kiwanja hicho. Kwa hali hii ndio Kamati ikataka kupatiwa taarifa za kina vipi Wizara
imegharamia kuondoshwa kwa vifaa hivyo. Wakati Wizara inajibu hoja hii, ilieleza kwamba,
Wizara haikuhusika na gharama hizo na badala yake wao walitoa msaada wa magari kwa
Mnunuzi ambae alitumia gharama zake za mafuta kufanikisha kuondosha vifaa hivyo. Kwa
jawabu hii inafahamika kwamba, kipengele cha 8 cha Mkataba huu kimekiukwa kwani
hakingemuhusisha Mhaulishwaji katika kuingia gharama zozote zile katika hatua za kukihaulisha
kiwanja hicho. Tunapenda pia ifahamike kwamba, mara tu baada ya kiwanja hicho kuuzwa,
Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara (UUB) ilitakiwa kukikabidhi kiwanja hicho kwa Coastal
Fast Ferries tarehe 29/10/2010 (Siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010) yenye
kumbu kumbu namba MOCT/K90/C3/Vol.III/13912
(Kielelezo Na.6).
12
Kumbu kumbu hii haikuwa ikionesha vizuri kwani imeandikwa kwa mkoni na kukozeshwa kwa mchanganyiko
mkubwa, wakati barua yote imeandikwa kwa chapa ya Kompyuta.
15
Kamati ilipolihoji kiasi gani cha gharama alizopata Mhaulishwaji kuhusiana na kuhamisha vifaa
vyake katika kiwanja hicho, iliambiwa ni Tsh. 5,000,000 pamoja na kutoa magari ya kuondoshea
vifaa hivyo. Kwa upande mwengine, wakati Kamati ilipomwita Kaimu Meneja wa Coastal Fast
Ferries Ltd (Ndg. Ahmad Saleh Karama) na Mkurugenzi Mtendaji wake (Ndg. Said Salim
Awadh (Bakhressa)) wote wamekiri mbele ya Kamati kwamba walitoa Tsh. 5,000,000/-
walizompa Ndg. Feisal Ali Sultan ashrikiane na Uongozi wa UUB ili waviondoshe vifaa hivyo,
nae Ndg. Feisal Ali Sultan (Mfanya biashara alietumiwa na Bakhressa kuuchukua Mkataba
kutoka Ofisi ya Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi hadi kwa Ndg. Ahmad Karama na kupewa
fedha hizo Tsh. 5,000,000) alikiri kwamba pesa hizo alizitumia kwa kukodi magari ya watu
binafsi na kutia mafuta magari ya UUB kwa ajili ya kuviondosha vifaa hivyo.
Aidha, kipengele cha 9 cha Mkataba huo kinasomeka kama ifuatavyo:
“Kwamba Mhaulishaji atalazimika kuwasilisha michoro yote kamili kwa Mhaulishwaji kabla ya kutiwa
saini makubaliano haya”.
Sharti hili halikufuatwa na Wizara husika ambayo ndio Mhaulishaji. Wizara haikuwasilisha
michoro kamili kwa Mhaulishwaji na ndio sababu ujenzi haukuweza kutekelezwa mpaka muda
huu. Kamati ilihakikishiwa mbele ya watendaji na mbele ya Mkurugenzi Mtendaji na Kaimu
Meneja wa Coastal Fast Ferries kwamba Wizara iliwahi kuwasilisha michoro kwa Mhaulishwaji
(ambayo ni pungufu) na kuichukuwa wenyewe na sasa umeshapita mwaka, michoro iliyo kamili
kama maelekezo ya Mkataba yalivyotaka, haijawasilishwa kwa Mhaulishwaji. Kinachoshangaza
ni kwamba, (kinyume kabisa na maelekezo ya kipengele hiki cha Mkataba) Mkataba
haukupaswa kutiwa saini mpaka michoro hiyo iliyokamili iwe imeshawasilishwa, lakini Wizara
haikuheshimu maelekezo ya Mkataba na kukubali Mkataba huo kusainiwa ukiwa haujafikia
muda wake (premature contract). Hapa pia panatupa wasi wasi juu ya uharaka wa kutiwa saini
makubaliano hayo, na matokeo yake, Mhaulishwaji ameshahaulishiwa na kukabidhiwa kiwanja
hicho (Kielelezo Na.7) na ameanza kukitumia kwa ujenzi wa ukuta (fance) , baada ya kuomba
kibali cha ujenzi kwa Mamlaka husika (Kielelezo Na.8) huku Wizara ikibaki na tamaa
isiyotekelezeka kisheria. Ambapo haijui ni lini itawasilisha michoro hiyo ikiwa kamili lakini
kibaya zaidi haina uhakika wa kutekelezwa Mkataba huu wa kujengewa „groud floor‟ ya Ofisi
hiyo, wakati ni Wizara iliyokwisha kuuvunja Mkataba huo kwa maslahi ya Mhaulishwaji.
2.4.6 Utatanishi wa Utekelezekaji wa Mkataba.
Pointi nyengine ambayo ingestahiki kuangaliwa kwa umakini ni baada ya kulijibu suala hili: “Je
ni kweli Wizara itajengewa Ground floor ya ofisi yake kwa mujibu wa Mkataba huu?” kwa
mujibu wa maelezo ya Watendaji, Wizara imekubali kuuza kiwanja chake kwa Costal Fast
Ferries Ltd, kwa matarajio (consideration)ya kujengewa Ground Floor yenye thamani ya Tsh.
200,000,000. Pamoja na maelezo haya, kwanza inatupasa tuzingatie uzito na uhalisia wa maelezo
haya kwa mujibu wa Mkataba husika.
Kipengele cha 2 cha Mkataba kinasomeka “Kwamba Mhaulishwaji amekubali kujenga
Foundation Floor ya jengo la Mhaulishaji kwa gharama sawa na thamani ya kiwanja wakati wa
uhaulishwaji”. Hapa tufahamu kwamba, kuna mkanganyiko wa ujenzi unaolazimika kujengwa
na Mhaulishwaji, je ni Ground Floor ama Foundation Floor? Maneno yaliyotumika katika
Mkataba ni Foundation Floor na sio Ground Floor. Na kwa maana hii ujenzi wowote hauwezi
kusimama bila ya foundation, na hata ujenzi wa ghorofa hujengwa kwa foundation. Na hii
16
inaweza kumpa uwezo mkubwa Mhaulishwaji wa kufanya ubabaifu wakati wa kutekeleza ujenzi
huo, anaweza kujenga foundation floor kama ilivyoelezwa katika Mkataba akasema kuwa tayari
ameshatumia Tsh. 200,000,000 na Wizara ikashindwa kumdhibiti kisheria na zaidi linalosikitisha
ni maelekezo ya kipengele cha 5 cha Mkataba huu “kwamba, gharama za ujenzi zinakisiwa kuwa
Tsh. 200,000,000/- (milioni mia mbili tu)”. Haitarajiwi kabisa kwa Serikali iliyo makini na
inayoumwa na uchungu wa rasilimali zake ikakubali kuingia katika Mkataba usio na maslahi
kwake wala kwa raia wake.
2.4.7 Mamlaka ya kuhaulisha ardhi ya Serikali:
Suala jengine muhimu katika Mkataba huu ni kuangalia kwa namna gani Wizara ya Mawasiliano
na Uchukuzi imejibebesha dhamana isiyo yake ya kuhaulisha ardhi ya Serikali kwa Mtu binafsi.
Kwa mujibu wa kifungu cha 7 (a) cha Sheria ya Umilikiwa Ardhi (Land Tenure Act) Nam. 12 ya
mwaka 1992, Mamlaka ya kuhalisha Ardhi yapo kwa Waziri wa Wizara inayoshughulikia
masuala ya ardhi, kwa maana Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati. Na kwa mnasaba huu,
ndio maana hata jina la uhalishwaji kutoka Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi hadi kwa
Coastal Fast Ferries Ltd, kama ilivyofanywa katika kiwanja hicho, lilifanywa na Waziri
anaehusika na ardhi. Kama Serikali ilikuwa na haja ya kukiuza kiwanja hiki ama kuikodisha
ardhi hii, basi mamlaka hayo kisheria hayahusiani kabisa na Waziri wa Miundombinu na
Mawasiliano.
Kinyume na muongozi huo wa kisheria, jambo la kushangaza Mhe. Waziri aliehusika na Wizara
ya Mawasiliano na Uchukuzi kama alivyousaini Mkataba huu, katika kipengele cha 1 cha
Mkataba huu anajibebesha jukumu lisilo lake kisheria kwa kusema “Kwamba mwenye kiwanja
(yaani Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi)13
amekubali kuhaulisha kiwanja kilichopo Mtoni
pembezoni na Azam Marine Workshop kutoka jina la Mhaulishaji kwenda kwa jina la
Mhaulishwaji”. Hapa inaonesha wazi wazi kwamba, Wizara hii ndio mmiliki wa kiwanja hicho
na ndio iliyouza, kitendo cha kutafuta ridhaa ya Wizara ya Ardhi katika kuhaulisha jina la
mmiliki kwenda kwa Mnunuzi ni suala la utaratibu tu, lakini Mkataba na faida ya Mkataba huo
yote imeelekezwa kwa Wizara hii ya Miundombinu na Mawasiliano.
2.5 Kuchunguza iwapo Wizara iliwahi kufanya maamuzi yoyote ya kisheria kuhusu
kutofaa kwa kiwanja hicho kwa matumizi ya Ofisi ya Wizara na kuziarifu Taasisi
zinazohusika juu ya kutofaa kwake.
Suala hili linatokana na ukweli kwamba, Ardhi yote inasimamiwa na Wizara inayohusika na
ardhi, ambapo kwa sasa inaitwa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kama inavyoelezwa
na kifungu cha 3 (3) cha Sheria ya Umiliki wa Ardhi, Namba 12 ya mwaka 1992 ambacho
kinasomeka;
“kwa kuzingatia masharti ya sheria hii na maelekezo yoyote ya Rais, suala la ardhi litasimamiwa na Waziri
anaehusika na Ardhi kwa mujibu wa Sheria hii, ambae kwa niaba ya Rais anaweza kuhaulisha ardhi na
kutekeleza majukumu na uwezo wote aliopewa kwa mujibu wa sheria hii”.
Kwa mujibu wa maelekezo ya sheria hii, kwa maana nyengine, Wizara ya Ardhi ndio msimamizi
mkuu wa ardhi zote zilizo chini ya Serikali na ndio yenye mamlaka ya kuhaulisha kwa njia
yoyote ile inayoonekana inafaa kwa mujibu wa sheria. Hivyo basi tuendelee kujiuliza, Kwa
13
Msisitizo ni wetu.
17
kuwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ilihaulishiwa kiwanja hicho na Wizara ya Ardhi
kwa ajili ya ujenzi wa Afisi yake, Je baada ya kuona kiwanja hicho hakina haja ya kutumiwa
kwa matumizi ya kujenga Afisi yao ya kudumu, je ni kwa nini Wizara isikirejeshe kiwanja hicho
kwa Wizara inayohusika na Ardhi, kama vile Wizara na Taasisi nyengine zinavyofanya. Aidha,
kwa kuwa Wizara imeona hakuna haja ya kuendelea na ujenzi wa Afisi husika, Je Wizara hii
ilitoa taarifa hiyo Serikalini au kwa Wizara yenye dhamana na masuala ya Ardhi hapa Zanzibar?.
Suala hili Kamati ililihoji Wizarani ambapo hakuna jawabu ya kuridhisha iliyotolewa. Wizara
ilieleza kwamba Mhe. Waziri wa Wizara hii alimshauri Mhe. Rais juu ya nia yao kwa kupitia
barua iliyomuandikia kumuomba kutoa ruhusa ya kukihaulisha kiwanja hicho kwenda kwa
Coastal Fast Ferries Ltd, ambapo Mhe. Rais kwa kupita barua ya tarehe 11/10/2010 aliridhia
uhaulishwaji huo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mtazamo wa Kamati na kwa kuzingatia utafiti ilioufanya, Wizara
haukukirejesha kiwanja hicho Serikalini wala haijamshauri Rais kwa namna inavyohitajika, bali
ni kumuomba ruhusa ya kuhaulisha kiwanja hicho kama alivyofanya. Pamoja na mambo
mengine, Kamati inafahamu kwamba barua hiyo iliyopelekwa kwa Mhe. Rais kupitia Waziri
husika haikueleza haja ya Wizara kupata ushauri kwa Mhe. Rais wala haikuwa na nia ya
kukirejesha Serikalini kwa lengo hilo. Na hoja hii inasisitizwa kwa kuzingatia maelezo
yaliyotokana na barua ya majibu iliyotiwa saini na Katibu wa Rais, Ndg. Haroub S. Mussa
ambapo moja katika maelezo yake yanasomeka “Ninapenda kukujuilisha kwamba, ruhusa
imetolewa ya kubadilisha kiwanja kama ulivyoomba” (Kielelezo Na.9).
Jambo jengine la kutia shaka linatokana na uhalali wa kisheria wa barua ya Mhe. Rais
inayoruhusu uhaulishaji wa kiwanja hicho kutoka Wizara ya Miundombinu kwenda kwa Coastal
Fast Ferries Ltd (kama ilivyonukuliwa hapo juu), kutiwa saini na Katibu wake ambae hana
uwezo huo. Katika barua hii, Ndg. Haroub S. Mussa ametoa ruhusa ya kuhaulishwa kiwanja
hicho kama yeye binafsi bila hata ya kutia saini kwa niaba ya Mhe. Rais, aidha, maelezo yake
hayaoneshi hata sehemu moja kupewa maelekezo hayo kutoka kwa Mhe. Rais, maelezo
“Ninapenda kukujuilisha kwamba, ruhusa imetolewa ya kubadilisha kiwanja hicho kama
ulivyoomba” yalaleta shaka kwamba hakupokea maelekezo hayo kutoka kwa Mhe. Rais bali ni
yake mwenyewe. Vile vile ifahamike wazi kwamba, Katibu wa Rais sio msemaji wa Rais wala
sio mtoa maelekezo yake, jukumu hili kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar limekabidhiwa kwa
Katibu Mkuu Kiongozi ambae pia ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi kama kifungu cha 49(1)
cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinavyosema na tunaomba kukinukuu:
“Kutakuwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye atakuwa pia Katibu Mkuu Kiongozi ataeteuliwa na
Rais na ambaye ndiye atakaekuwa dhamana wa Afisi ya Baraza hilo na dhamana kwa mujibu wa
maelekezo atakayopewa na Rais, kwa kupanga shughuli za mikutano pamoja na kuweka kumbukumbu ya
mikutano hiyo, na kupeleka maamuzi yanayohusika kwa watu au vyombo vinavyohusika14
na atafanya
kazi nyengine atakazopewa na Rais mara kwa mara”.
Maelezo ya Katiba tuliyoyanukuu yanatosha kuthibitisha kwamba, Katibu wa Rais hakujua
anachokifanya wakati akiandika barua hiyo. Aidha, hata kama tutaamini kwamba ameariwa na
Rais, basi ni wazi kwamba hata huyo Rais hafahamu utaratibu wa utekelezaji wa maagizo yake,
kitu ambacho kwa upande wa mtu mwenye akili timamu, hawezi kukubaliana na usahihi wa
barua hiyo kutoka kwa Mhe. Rais. Kwa lugha nyengine, kwa mnasaba wa maelezo hayo, Katibu
14
Msisitizo ni wetu.
18
wa Rais katekeleza majukumu yasiyo yake na kwa hali hii, Kamati inaendelea kuwa na mashaka
mengi kuhusiana na ruhusa hiyo ya Mhe. Rais. Kama kweli ruhusa hiyo imetolewa na Rais, kwa
nini barua isitoke kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambae kwa mnasaba wa Katiba na Sheria zetu
ndie mwenye uwezo wa kupeleka maamuzi ya kuhaulisha kiwanja hicho kutoka kwa Mhe. Rais
kwenda kwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na sio Katibu wa Rais. Inaweza pia
kufahamika kwamba, watendaji wanaopewa dhamana ya kumsaidia Mhe. Rais, waiyatumia
vibaya dhamana zao na matokeo yake hupelekea Ikulu, kama sehemu takatifu kusemwa vibaya
na kuonekana ni sehemu ya biashara na sehemu inayonukia harufu ya rushwa.
Vile vile, katika kuendelea na mahojiano ya namna gani Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano iliziarifu taasisi zinazohusika juu ya kutofaa kwa kiwanja hicho kwa matumizi ya
Ofisi, Kamati imetaka kufahamu angalau kwa taarifa tu iwapo Wizara ilitoa taarifa hiyo
Serikalini. Katika kulijibu suala hili, Wizara ilieleza kwamba, walipeleka taarifa hiyo Serikalini
yaani Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kuomba uhaulishwaji wake lakini
wakashauriwa ni lazima wapate ridhaa ya Mhe. Raisi na hivyo, ilimuandikia Mhe. Rais, kwa
barua Nam. MWMU/MM/J/Vol.5/027 ya tarehe 5 Oktoba 2010 kumuomba ruhusa ya
kubadilisha kiwanja na ruhusa hiyo imetolewa kwa mujibu wa barua ya tarehe 11 Oktoba 2010
yenye kumbu kumbu Nam. IKL/TS/WMU-17/Vol.12/104, na tarehe hiyo hiyo (11/10/2010)
Wizara ilimuandikia barua Mhe. Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi yenye kumbu kumbu
Nam. MWMU/MM/J/Vol.5/028 kuomba kuhalisha Hati ya Umiliki ya kiwanja hicho Nam. 181
kuwa mali halali ya Coastal Fast Ferries Ltd ( Kiamabatanisho Namba 10).
Pamoja na majibu yaliyotolewa na Wizara kuhusiana na hoja hii kufika katika Wizara ya Ardhi,
Makaazi, Maji na Nishati, Kamati ilitaka ipewe ushahidi vipi Wizara hii ya Miundombinu na
Mawasiliano ilipeleka taarifa ya kutofaa kwa ujenzi wa Afisi yake ya kudumu kama matumizi ya
ardhi hiyo yalivyokusudiwa awali na baada ya Seikali kupokea taarifa hiyo, iishauri Wizara
kukiuza kiwanja hicho. Ili jibu hili liweze kuridhisha, ilitakiwa Wizara kutoa ushahidi wa taarifa
hiyo na kuithibitishia Kamati maamuzi ya Serikali juu ya ushauri iliyoutoa. Hata hivyo, pamoja
na haja hii, Wizara imeshindwa kuthibitisha zaidi ya kuonesha ushahidi wa barua walizoiandikia
Wizara ya Ardhi kutaka kubadilishwa jina la Wizara kama mmiliki wa kiwanja hicho na kuwa
jina la Kampuni iliyokinunua, barua ambayo haioneshi dhamira tunayoikusudia hapa.
2.6 Kuchunguza iwapo kuna maslahi ya umma katika uhaulishwaji wa kiwanja hicho.
Katika kipengele hiki Kamati ilikuwa na wajibu wa kuangalia kama kweli Wizara imefanya
uhaulishwaji kwa kuzingatia maslahi ya Wazanzibari ama kwa ajili ya maslahi binafsi. Pengine
inakuwa vigumu kulijibu suala hili bila ya kuzingatia suala la uhaulishwaji lilivyofanyika na
namna ya ukiukwaji wa Sheria za Manunuzi ya mali za Serikali pamoja na sheria zinazohusika
na masuala ya ardhi. Kwa maana nyengine, hakuna tatizo lolote kwa Kamati kuamini kwamba,
Wizara ama taasisi yoyote ya Serikali inapaswa kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia
maslahi ya umma, lakini kwa kuzingatia namna ya uhaulishwaji wa kiwanja hicho ulivyofanyika,
Kamati inaamini kwa kauli moja kwamba uuzaji huo umefanyika kwa utashi binafsi wa baadhi
ya viongozi na watendaji wa Wizara hii. Kamati inaamini kwamba, hakukuwa na sababu ya
kukiuza kiwanja hicho kwa mtu binafsi wakati kilikuwa kinatumiwa na Idara ya Ujenzi na
Utunzaji wa Barabara (UUB), aidha, Kamati inaishangaa Wizara kujibebesha majukumu yasiyo
yake ya kuuza mali za Serikali na zaidi baada ya kutoka agizo la kusitishwa uuzwaji wa mali za
Serikali kutoka Wizara ya Fedha kupitia barua ya tarehe 25/11/2009 yenye kumbukumbu namba
MFEA/PS/M.30/4/05/69 na katika utekelezaji wa agizo hili, Wizara ya Miundombinu na
19
Mawasiliano ilizikataza Idara zake zote zisiuze mali za Serikali mpaka hapo litakapotoka tena
agizo la Serikali kuruhusu uuzwaji wa mali zake kwa barua ya tarehe 1/12/2009 yenye
kumbukumbu namba MOCT/F.10/C.1/VOL II/79 ambapo tunaziambatanisha katika ripoti hii
kuwa (Kielelezo Na.11).
Miongoni mwa hoja za Kamati kwamba uuzwaji wa kiwanja hichi umefanywa kwa maslahi
binafsi, ni pamoja na kutofanyika kwa tathmini yoyote ya thamani ya ardhi kupitia mamlaka
husika wala kutofuatwa kwa sheria na Wizara kuingia katika mkataba wenye mapungufu mengi
kisheria ambapo bado Kamati inaamini kwamba hakuna mkataba wowote wa kisheria ulioingiwa
katika uuzwaji wa kiwanja hicho, kwani Mkataba uliokabidhiwa kwake ni Mkataba feki wenye
mapungufu mengi kisheria kama tulivyokwisha eleza awali. Aidha, Kamati inashangaa namna
aliekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Machano Othman Said, alivyoshiriki kumtafuta mnunuzi
wa kiwanja hicho na hatimae kukamilisha mwenyewe mauziano hayo huku bila ya kufahamu
majukumu yake akishiriki katika kutia saini mkataba huo, hali inayoonesha wazi kwamba
amegeuka dalali wa kuuza kiwanja hicho. Vile vile, Kamati inashangazwa na haraka ya kuuzwa
kiwanja hicho na zaidi siku 2 tu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2010, wakati
Serikali ilitoa tamko la kukataza uuzwaji wa mali yoyote ya Serikali mpaka itakapotoa taarifa,
lakini makusudio makubwa yakiwa ni kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2010.
Hivyo basi, kwa kuzingatia sababu tulizozieleza hapo juu, Kamati inaamini kwamba uuzwaji wa
kiwanja hicho umefanywa zaidi kwa maslahi binafsi na sio kuzingatia maslahi ya Umma.
2.7 Kuchunguza matumizi ya kuwepo au matumizi ya fedha zilizotolewa na mwekezaji
aliyepewa kiwanja hicho na matumizi ya Tsh. 49,100,000/- zilizotolewa na Serikali
kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi hiyo.
Itakakumbukwa kwamba, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano iliomba jumla ya Tsh.
200,000,000 kwa mwaka wa fedha 2008/2009 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi yake ya kudumu
katika eneo liliopo kiwanja hicho, Mtoni Zanzibar. Kamati ilijuilishwa kwamba, Serikali
haikutoa fedha yoyote pamoja na kuidhinishwa na Baraza la Wawakilishi kwa mwaka huo wa
fedha. Hata hivyo, Wizara iliidhinishiwa tena Tsh. 100,000,000/- kwa mwaka wa fedha
2009/2010 na kufanikiwa kupewa Tsh. 49,100,000/ - sawa na asilimia 49.1 fedha ambazo
Wizara imekiri mbele ya Kamati kwamba ilizipokea na kuzitumia. Suala la msingi la kujiuliza
kuhusu matumizi haya ni kwamba, je, Wizara ilizitumia fedha hizo kwa ujenzi wa ofisi yake
katika kiwanja ilichokiuza kinyume na sheria kwa Zanzibar Coastal Fast Ferries Ltd? Na kama
haijajenga ofisi hiyo kama madhumuni ya kutolewa kwa fedha hizo, pia tunajiuliza, je fedha hizo
zimetumika kwa matumizi yepi na kwa idhini ya chombo gani chenye mamlaka ya kisheria
kuidhinisha matumizi hayo?.
Tuanze na matumizi ya fedha hizo Tsh. 49,100,000/- kwa ujenzi wa Ofisi ya Wizara.
Inafahamika kwamba, miongoni mwa kazi za Baraza la Wawakilishi ni kuidhinisha na
kusimamia mipango ya maendeleo ya Serikali katika njia ile ile ambayo Bajeti ya mwaka
inaidhinishwa15
, ambapo kwa upande wa utekelezaji wa Bajeti hiyo iliyoidhinishwa, Serikali
inalazimika kufanya matumizi yaliyoidhinishwa kwa namna ile ile ambayo imeidhinishwa na
Baraza la Wawakilishi, na ndio maana Katiba hii hii ikampa mamlaka Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi ili kuhakikisha kwamba matumizi ya fedha za
15
Katiba ya Zanzibar, 1984 kifungu cha 88(d).
20
Serikali yanafanywa kwa kufuata idhini iliyotolewa na kuhusu matumizi hayo16
. Aidha, na
Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (P.A.C) ikapewa
majukumu mengi ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi kama fedha zilizooneshwa katika
Mkadirio na Matumizi ya Serikali na Mshirika yake zimetumika kama ilivyokubaliwa; na
Matumizi yalikuwa chini ya mamlaka iliyohusika, na Matumizi yaliyofanywa yalizingatia
thamani halisi ya fedha17
.
Kwa maana hii, Wizara ilipaswa kuzitumia fedha hizo Tsh. 49,100,000/- kwa ajili ya Ujenzi wa
Ofisi yake katika kiwanja cha Maruhubi Mtoni Zanzibar jambo ambalo halikufanyika. Kwa
kudharau maelekezo yaliyotolewa na Katiba na Sheria za fedha, Wizara imezitumia fedha hizo
kukarabati jengo kongwe la Wizara hiyo liliopo Forodhani, jengo ambalo ni mali ya Kamisheni
ya Wakfu na Mali ya Amana na tayari limeshakuwa bovu na fedha nyengine kufanya ukarabati
wa Ofisi zilizochini ya Shirika la Meli, eneo la Bohari Kuu bila ya kupata ama kuomba ruhusa
hiyo kwa mamlaka zinazohusika18
. Kamati ina mashaka na matumizi ya fedha hizi na wasi wasi
zaidi unatokana na kuuzwa kwa kiwanja kilichokusudiwa kujengwa ofisi ya Wizara kwa
kisingizio cha kutafuta mfadhili wa kujenga jengo la Afisi mpya, Mazizini.
2.8 Uuzaji wa Kiwanja na Uhusiano wake wa Agizo la Kusitisha Uuzaji wa Mali za
Serikali:
Baada ya kuangalia hadidu ndogo za rejea za Hadidu hii, ni vyema sasa tukaangalia uuzaji wa
kiwanja hicho kwa mnasaba wa Agizo la Serikali kuhusu uuzaji wa mali zake. Tuanze na
kuangalia Agizo husika lilitolewa mnamo tarehe 25/11/2009, kupitia barua namba
MFEA/PS/M.30/4/05/69 na kuandikwa (kwa maslahi ya hoja yetu) kwa Katibu Mkuu wa
iliyokuwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ambayo sasa ni Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano kutoka kwa iliyokuwa Wizara ya Fedha na Uchumi ambayo sasa ni Ofisi ya Rais,
Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo19
(Kielelezo Na.12). Katika agizo hilo Serikali
imeagiza kama tunavyonukuu hapa chini:
“Naomba kuwataarifu kuwa Serikali imesitisha uuzaji wowote wa mali zake zikiwemo, majengo,
mashamba, magari, matractor, n.k hadi hapo itakapoelekezwa vyenginevyo20
.
Kwa barua hii mnaombwa pia kuwajuulisha Wakuu wa Idara/ Taasisi zote zinazojitegemea zilizo chini ya
Wizara zenu”.
Aidha, nakla ya barua hii ikielekezwa kwa Waziri wa Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi anaeshughulikia Fedha na Uchumi; Katibu Mkuu, Baraza la Mapinduzi; Katibu wa
Rais, Ikulu na Kamishna wa Uhakiki Mali na Mitaji ya Umma wa Wizara ya Fedha na Uchumi
ambae katika barua hii akiamriwa asimamie ipasavyo zoezi hili. Katika kutekeleza agizo hili,
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi (kama ilivyokuwa) kupitia kwa Katibu Mkuu wake
ilizitaarifu taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake juu ya Agizo hili kama ilivyotakiwa kufanya
hivyo.
16
Ibd kifungu cha 112 (3)(b) 17
Kanuni ya 115(3),ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi, Toleo la 2011. Msisitizo ni wetu. 18
Ifahamike kwamba, Wizara haikuweza kutoa ushahidi wowote wa kupata ruhusa ya matumizi ya fedha hizo
kinyume na matumizi yalivyoidhinishwa na Baraza la Wawakilishi katika Kikao cha Bajeti ya mwaka 2009/2010. 19
Ifahamike kwamba, Agizo hili lilitolewa na Serikali kwa kila Afisa Mhasibu anaehusika na mali za Taasisi yake. 20
Msisitizo ni wetu.
21
Suala la msingi ni kujiuliza, Jee katika Agizo hili, tunajifunza mambo gani? Hebu na tuanze na
maneno haya “Naomba kuwataarifu kuwa Serikali imesitisha uuzaji wowote wa mali zake
zikiwemo, majengo, mashamba, n.k”. Tunafahamu kwamba, mara nyingi ingelifikiriwa kwamba,
kiwanja kilichokuwa kinamilikiwa na Wizara ya Miundombinu ni mali ya Wizara na hivyo,
maneno ya Kusitisha uuzaji wa mali zake, haingehusisha kiwanja hicho. Ukifikiria hivyo
ungekuwa na hoja kwamba, kwanza kiko chini ya Wizara, lakini kubwa zaidi, kiwanja sio mali
ya Serikali, yaani sio Fixed Asset na hivyo, agizo hili halihusiki na kiwanja hicho.
Baada ya kufikiria hivyo, hebu kidogo tujikumbushe maelekezo ya Sheria inayozungumzia Mali
za Serikali, Sheria Namba 9 ya mwaka 2005, katika kifungu cha 4 cha Sheria hiyo kinaanzisha
Ndani ya Wizara inayoshughulikia Masuala ya Fedha, Kitengo cha Ukakiki Mali na Mitaji ya
Umma ambapo kwa mujibu wa kazi ilizopewa katika kifungu cha 6 cha Sheria hiyo ni pamoja na
kusimamia na kutoa taarifa juu ya ununuzi na ugavi wa Mali za Serikali unaofanywa na Wizara,
Taasisi za Serikali zinazojitegemea na hata Serikali za Mitaa ili kuhakikisha kwamba sheria za
ununuzi na ugavi zinafuatwa ipasavyo. Hapa tunajifunza hekima ya Sheria hii ni kwamba mali
zote za Serikali pamoja na kuwa chini ya Wizara ama Taasisi za Serikali zinazojitegemea, bado
ziko chini ya Wizara inayoshughulikia masuala ya fedha na chochote kinachofanywa kuhusiana
na ununuzi wake ama uuzaji wake, basi Wizara husika kupitia kitengo chake hicho ni lazima
kiarifiwe kwa utaratibu uliokuweko kisheria.
Kwa maana hii, Kiwanja kilichokuwa kinamilikiwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
kilipaswa uuzwaji wake ujuilishwe kwa Wizara inayohusika na Mali za Serikali, kitendo
ambacho hakikufanyika na matokeo yake Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imejifanyia
tu suala hili bila ya kufuata maelekezo ya Sheria hii. Kwa upande mwengine, Wizara ya Fedha
na Uchumi ilikuwa sahihi kutoa Agizo lake na kuziamuru Wizara zote pamoja na Taasisi za
Serikali ziheshimu Agizo hilo, na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ilitakiwa isikiueze
kiwanja hicho hadi pale itakapopewa agizo jengine kama barua hii ilivyoelekeza. Ama kwa
upande wa hoja ya Kiwanja kuwa ni mali ya Serikali ama laa, Kamati pia ililihoji suala hili
katika kikao chake cha pamoja na Uongozi wa Wizara na wakajenga hoja kwamba, kiwanja
hicho hakimo katika Asset za Serikali na hivyo ndio maana hawakulazimika kuheshimu ama
kufuata Sheria inayohusiana na Mali hizo. Kwa upande wa Kamati inazidi kusisitiza kwamba,
maenelezo haya hayana msingi wowote na ni sawa na kutofahamu majukumu yao, lakini pia
katika Agizo tunalolizungumzia, maneno “……mali zake zikiwemo majengo, mashamba,
magari, matractor n.k…….” yanathibitisha wazi kwamba, kiwanja kama ilivyo mashamba ni
mali za Serikali na hivyo, nacho kingeuzwa kwa kufuata maelekezo ya kisheria na ya kiutawala.
Kitu chengine cha kujifunza katika Agizo hili ni haya maeneno “……….hadi hapo
itakapoelekezwa vyenginevyo” yanakusudia kwamba, kuanzia lilipotoka Agizo hili mpaka muda
wa kuuzwa kiwanja hicho ama hadi leo, hakuna ruhusa ya Wizara ama Taasisi yoyote ya Serikali
kuuza mali za Serikali, mpaka msimamizi wa mali hizo, yaani Wizara inayoshughulikia Fedha
itakapotoa agizo jengine la kuruhusu uuzwaji huo. Kwa lugha nyengine, iwapo Wizara imefuata
taratibu za Sheria na Maelekezo ya Serikali, ilipaswa ithibitishe mbele ya Kamati kupewa agizo
jengine na Serikali la kuuza mali zake ikiwa ni pamoj na kiwanja hicho. Katika hali ya
kusikitisha, Wizara imeshindwa angalau kuieleza Kamati kwamba imepokea agizo jengine,
kibaya zaidi imeshindwa kuthibitisha. Kamati kwa kuona ni busara zaidi kupata ufafanuzi wa
suala hili, ilipokutana na Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, katika kikao
ambacho hata Idara ya Uhakiki Mali na Mitaji ya Umma ilikuwepo, ililiuliza suala hili, kama
22
waliwahi kutoa agizo jengine la kuruhusu uuzaji wa mali za Serikali, lakini nao wakaithibitishia
Kamati kwamba, Wizara haijawahi kutoa agizo jengine la kuruhusu.
Hebu pia tujifunze hekima ya Agizo hili. Itakumbukwa kwamba, agizo hili lilitoka mwisho mwa
mwaka 2009, na mwaka 2010 Zanzibar iliingia katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi wa
Octoba. Katika kila kipindi cha uchaguzi Mkuu unapokaribia, baadhi ya Watendaji wa Serikali
ikiwa kwa mashirikiano na viongozi wao huwa na tabia ya kuuza mali za Serikali kiholela na
mara nyingi hufanywa ufisadi wa uharibifu ama upotevu wa mali hizo. Ili kuondosha tatizo hili,
ndio maana Wizara inayosimamia mali hizo ikatoa agizo la kusitisha mara moja uuzwaji wowote
wa mali za Serikali. Hata hivyo, pamoja na juhudi hiyo, kwa bahati mbaya sana, Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano imeuza bila hata ya kuheshimu hekima ya agizo. Kwa mfano,
ungeweza kufikiria nini wewe mwananchi wa Zanzibar unapoona Mnunuzi wa kiwanja hicho
anakabidhiwa kiwanja siku mbili tu kabla ya Uchaguzi Mkuu. Hebu fikira hali ya kisiasa na
kiuchumi ya nchi yako, hebu fikiria fikira za viongozi wanaoondoka madarakani baada ya
kukamilika miaka mitano ya Uchaguzi wao Majimboni ama kufikia kikomo cha Uteuzi wao wa
kuwa Viongozi, lakini zaidi fikiria akili za watendaji wengi wa Serikali wanaotegemea uteuzi wa
Rais katika muda huu, huku wakiwa hawana uhakika wa kurejea tena katika nyadhifa
walizonazo kwa kutojua Uchaguzi utaamua utawala upi na wa namna gani. Bila ya shaka
utakubaliana na Kamati kwamba, uuzwaji wa kiwanja hiki umegubikwa na mazingira mengi ya
utatanishi na zaidi ukinasibisha na agizo la Serikali la kuzuia uuzwaji wa mali zake.
2.9 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari wa
mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali juu
ya hatua za kuchukuliwa.
2.9.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Kuna ukiukwaji mkubwa wa Sheria na Taratibu za Uuzaji wa Mali za Serikali:
Kamati imejiridhisha kwamba Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano haikufuata
taratibu za uuzaji wa kiwanja ilichokuwa inakimiliki na kuamua kukiuza kwa Kampuni
binafsi bila ya kufuata taratibu za Kiutawala wala Taratibu za Kisheria, hali
inayopelekea wasi wasi mkubwa wa kuwepo kwa harufu ya ubinafsi na harufu ya
rushwa, na zaidi ukizingatia thamani ya kiwanja hicho kuwa ni sawa na Tsh.
200,000,000/- bei ambayo ni ndogo kwa mujibu wa bei ya soko na kwa kuzingatia
ukubwa wa kiwanja chenyewe na eneo kilipo.
(ii) Kuna upotoshaji mkubwa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Kamati
zake kuhusiana na taarifa wanazopatiwa na Viongozi wa Wizara na Watendaji
wao wakuu.
Kamati kwa kuzingatia majibu ya Mhe. Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano na majibu yaliyotolewa kwa Kamati katika Kikao cha
pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hii, na kwa mnasaba wa taarifa
zilizowasilishwa kwa Kamati ya P.A.C ilipokuwa inafuatilia uuzwaji wa kiwanja hiki,
23
imebaini wazi kwamba, kuna taarifa nyingi zisizo za kweli zinazotolewa kwa Wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi, bila ya watoaji wa taarifa hizo kuzingatia Haki, Fursa na
Uwezo wa Wajumbe katika kupewa taarifa sahihi na zilizo za kweli.
(iii) Kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kazi na utumiaji mbaya wa madaraka.
Kamati imegundua kwamba, Viongozi wajuu wa Wizara na watendaji wao wakuu
wanatumia vibaya madaraka yao bila ya kujali maadili ya kazi zao ama bila hata ya
kujali sheria na kanuni za utumishi wao ama wadhifa wao, hali ambayo kama
itaendelea kuachiwa, itaifikisha pabaya nchi hii inayoongozwa kwa mujibu wa Katiba
na Sheria.
(iv) Kuna utumiaji mbaya wa Madaraka ya Ofisi ya Rais:
Kamati imefahamu kwamba kuna baadhi ya mawasiliano ya Mhe. Rais hayafanywi
moja kwa moja na Mhe. Rais, badala yake hufanywa na wasaidizi wake ambao ama
kwa kutofahamu majukumu yao hubeba madaraka ya Mhe. Rais mikononi mwao ama
kwa makusudi na kwa kuamini kwamba hakuna mtu mwengine wa kuhoji, hutumia
vibaya majukumu waliyopewa.
(v) Kuna matumizi mabaya ya fedha za Serikali kinyume na taratibu zake:
Kamati imegundua kwamba, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano haikutumia
fedha iliyoidhinishwa kwa ajili ya Ujenzi wa Afisi yake ya Kudumu kwa mwaka
2009/2010 badala yake imeamua kuzitumia fedha hizo kwa ukarabati wa jengo la
Bohari Kuu na Jengo la Afisi yao ya Makao Makuu ya zamani ambalo linamilikiwa na
Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana. Kosa zaidi, ni kufanya matumizi haya bila ya
kufuata taratibu za fedha ikiwa ni pamoja na kuhaulisha kisheria na matokeo yake,
Serikali imetoa fedha iliyoidhinishwa na Baraza la Wawakilishi huku fedha hizo
zikitumika kinyume na malengo yaliyokusudiwa.
(vi) Kukiukwa kwa Ushauri na maelekezo yanayotolewa na Kamati za Baraza la
Wawakilishi kunapelekea gharama zisizo za lazima kwa Serikali.
Kamati imefahamu kwamba, Hoja hii ilianza kwanza kufuatiliwa na Kamati ya
Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (P.A.C) ya Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar ilipokuwa inafuatilia Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali ya mwaka 2008/2009, ingawaje hoja hii haijaibuka moja kwa moja
katika Ripoti hiyo, lakini kwa mamlaka iliyopewa Kamati hiyo, imeliuliza suala hili na
kupewa majibu yasiyoridhisha. Hata hivyo, Kamati ilitoa agizo la kuzuia ujenzi katika
kiwanja hicho na Wizara ikajibu kwamba wamefuata taratibu zote za kisheria katika
kuhaulisha kiwanja hicho na hivyo kwa kuwa tayari wameshakiuza, hawana mamlaka
ya kuwazuia badala yake ni Serikali Kuu yenye Mamlaka ya kuzuia ujenzi huo.
Kamati hii inaamini kwamba, laiti kama Kamati ya P.A.C ingepatiwa majibu ya
kuridhisha, kusingekuwa na haja ya kuundwa kwa Kamati Teule kufuatilia jambo hili,
na matokeo yake fedha nyingi zimetumika kuunda na kusimamia Kamati hii Teule.
24
(vii) Mawaziri kuingilia majukumu ya Makatibu Wakuu wa Wizara zao:
Kamati imegundua kwamba, baadhi ya Mawaziri wa Serikali wanatekeleza majukumu
ya Makatibu Wakuu, kitendo ambacho sio tu kutekeleza majukumu yasiyo yao ambayo
hawajatumwa kisheria, lakini pia hupelekea kuwepo kwa shaka kubwa juu ya usahihi
wa utekelezaji wa majukumu hayo.
(viii) Ukiukwaji wa Maagizo na Maelekezo ya Serikali.
Kamati imejiridhisha kwamba, Wizara na Taasisi mbali mbali hazifuati maazigo na
maelekezo yanayotolewa na Serikali katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Kamati imejifunza hili kwa mnasaba wa Agizo la kuzuia uuzwaji wa mali za Serikali
ambapo Wizara ya Miundombinu halifuata maelekezo hayo.
2.9.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi tuliouonesha kapo juu, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo
zichukuliwe:
(i) Aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi (2005-2010) na
watendaji wote waliohusika katika kuingia mikataba na Kampuni ya Coastal Fast
Ferries Ltd. wawajibishwe kwa misingi ya sheria.
(ii) Kamati inapendekeza Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano waliombe radhi Baraza la Wawakilishi kwa kutaka kulipotosha
Baraza juu ya ukweli wa uuzwaji wa Kiwanja tulichokizungumzia katika hoja hii.
Aidha Watendaji mbali mbali wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
wachukuliwe hatua kwa msingi wa sheria Namba 4 ya mwaka 2007 wachukuliwe
hatua zinazofaa kwa kosa la kuzidanganya Kamati za Baraza la Wawakilishi.
(iii) Serikali ichukue hadhari kubwa na matumizi ya jina la Mhe. Rais na Ofisi yake.
(iv) Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano achukuliwe hatua za
kinidhamu kwa kutosimamia ipasavyo mali ya Serikali iliyo chini ya Wizara yake
ambapo kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Fedha (Sheria Na. 12 ya 2005 na
Kanuni zake) yeye ndio msimamizi Mkuu.
(v) Uhaulishwaji huu sio halali kisheria na kiutawala, hivyo Kamati inapendekeza
kiwanja hicho kirejeshwe Serikalini mara moja.
25
HADIDU REJEA YA PILI:
3.0 KUHUSU SUALA ZIMA LA UWANJA WA NDEGE WA ZANZIBAR KUHUSU
ULIPAJI FIDIA KWA WATU AMBAO MALI ZAO ZIMEATHIRIKA
KUTOKANA NA UJENZI WA UZIO WA UWANJA WA NDEGE, MATATIZO
YA UNUNUZI WA JENERETA, MIKATABA YA UKODISHWAJI WA SEHEMU
ZA BIASHARA KWENYE ENEO LA UWANJA WA NDEGE NA UTARATIBU
WA AJIRA NA UTOAJI WA HUDUMA MBALI MBALI KWENYE MAENEO
YA UWANJA WA NDEGE NA WIZARA YA MIUONDO MBINU KWA
UJUMLA.
3.1 Utangulizi:
Kamati Teuele ilitakiwa kuifanyia kazi hadidu hii rejea kwa kuangalia maeneo Makuu
yafuatayo:
Kuchunguza ulipwaji wa fidia wa watu walioathirika katika kufuatia ujenzi wa uzio wa Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanzibar. Katika kuchunguza suala hili,
Msisitizo ukiwekwa kwa mwananchi anaemiliki nyumba ambae bado hajahama na matokeo
yake, ukuta huo umeshindikana kuzibwa hadi hapo Mamlaka ya Uwanja wa Ndege itakapo
mlipa fidia na kuridhika kuondoka ili ukuta huo uwezekane kuzimbwa.
Kamati pia ilitakiwa kuchunguza matatizo ya ununuzi wa jenereta liliopo katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Abeid Ama Karume, Zanzibar ambapo limenunuliwa takriban mwaka
mmoja nyuma huku likiwa bado halijafungwa na muda wa „warranty‟ kumalizika. Katika hadidu
hii ndogo, Kamati ilitakiwa ichunguze iwapo jenereta hilo limenunuliwa kwa kufuata taratibu za
kisheria lakini pia sababu zilizopelekea jenereta hilo kutofungwa tokea liwasili uwanjani hapo.
Aidha, katika Hadidu hii hii, Kamati imetakiwa ichunguze Mikataba ya Ukodishwaji wa sehemu
za biashara kwenye eneo la Uwanja wa Ndege, huku msisitizo ukiwekwa kwa Makampuni ama
taasisi zote zilinazofanya biashara mbali mbali katika eneo hilo ambazo kwa namna moja ama
nyengine zimeingia katika Mkataba wa ukodishwaji. Katika hili, Kamati ilitakiwa ichunguze
iwapo wakodishwaji hao wamekodishwa kisheria na mikataba yao bado ipo kihalali na namna ya
utekelezaji wa Mikataba husika.
Vile vile, Katika Hadidu hii kuu, Kamati imetakiwa kuchunguza utaratibu wa Ajira katika
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, msisitizo ukiwekwa kwa ajira zilizoanza mwezi wa
October 2010 hadi Septemba 2011. Katika kuifanyia kazi hadidu hii, Kamati ilitakiwa
kuchunguza iwapo yupo Mfanyakazi alieajiriwa akiwa bado yupo masomoni. Ichunguze kuwepo
kwa Mfanyakazi aliajiriwa mara mbili katika uajiri wa Serikali na kwa upande wa Pemba,
Ichunguze wafanyakazi walioajiriwa kutoka Tanzania bara kupitia Pemba na kusadikiwa
kwamba wao ni Wazanzibari.
26
Na hadidu ndogo ya mwisho katika hadidu hii kuu, Kamati ilitakiwa ichunguze utaratibu wa
utoaji wa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume wa Zanzibar
huku msisitizo ukiwekwa kwa migogoro iliyopo baina ya vikundi vinavyotoa huduma uwanjani
hapo, sababu za migogoro na hatua ya kuchukuliwa kuepusha migogoro hiyo kwa lengo la
kukuza utoaji bora wa huduma katika kiwanja hicho.
Kamati iliifanyia kazi Hadidu hii rejea ndani ya miezi minne katika vipindi tofauti kwa
kuzingatia muda uliopangwa kwa Kamati kufanya kazi pamoja na mazingira mbali mbali
yaliyojitokeza ya upatikanaji wa wahusika walioitwa na kuhojiwa na Kamati kwa mujibu wa
haja inapojitokeza. Kwa kuanzia, Kamati ilikutana na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege katika Afisi ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
Zanzibar tarehe 07/09/2011 kwa lengo la kupata ufafanuzi kuhusiana na ulipwaji wa fidia kwa
watu walioathirika na ujenzi wa uzio wa Uwanja wa Ndege pamoja na ufafanuzi wa jenereta la
uwanja huo na kuanza kupata ufafanuzi wa suala la Mikataba ya ukodishwaji wa eneo hilo.
Tarehe 08/09/2011 Kamati ilifanya ziara ya eneo la mwananchi ambae ana miliki nyumba katika
Uwanja wa Ndege, baada ya Kamati kugundua kwamba hajalipwa fidia na baadae ilifanya ziara
ya maeneo ya ukodishwaji, Uwanja wa Ndege iliyoendelea tarehe 13/09/2011. Kamati pia
ilikutana na baadhi ya wamiliki mbali mbali wa maeneo yaliyokodishwa katika Uwanja wa
Ndege huo, tarehe tofauti ikiwa ni pamoja na tarehe 15/09/2011 na tarehe 05/12/2011. Na tarehe
06/12/2011 Kamati ilikutana na Bodi ya Zabuni ya Serikali na Bodi ya Zabuni ya Ofisi ya Rais,
Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo tarehe 06/12/2011 katika Afisi ya Baraza la
Wawakilishi kwa ufafanuzi wa ununuzi wa jenereta, huku kikao cha pamoja juu ya suala
kukutana na watoaji wa huduma za ubebaji wa mizigo ya wasafiri katika Uwanja huo kilifanyika
tarehe 16/09/2011 na tarehe nyengine ni 28/12/2011.
Kuhusu suala la ajira za wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Kamati
ilianza kufuatilia tarehe 16/09/2011 na kazi hii ilifanywa kwa siku tofauti iliyochukua takriban
wiki moja kuanzia tarehe hiyo, huku Kamati ikifanya kazi mpaka saa 4 hadi saa 5 za usiku kwa
lengo la kuikamilisha kazi hii. Hata hivyo, Kamati iliendelea kufanya mahojiano na baadhi ya
wafanyakazi hadi mweziwa Decemba 2011 kutokana na wafanyakazi hao kutopatikana katika
siku zilizopangwa . Kwa upande wa ajira za Pemba, Kamati imezifanyia kazi siku 2, baina ya
tarehe 03/11/ 2011 na tarehe 04/11/2011 Kisiwani Pemba. Baada ya maelezo mafupi ni vyema
sasa tukapapata uchambuzi wa kazi za Kamati kuhusiana na hadidu hii rejea kama ifuatavyo:
3.2 KUHUSU ULIPAJI FIDIA KWA WATU AMBAO MALI ZAO ZIMEATHIRIKA
KUTOKANA NA UJENZI WA UZIO WA UWANJA WA NDEGE:
Ili kufahamu namna gani waathirika mbali mbali wamelipwa fidia na zaidi Kamati kujiridhisha
kwamba, hakuna mwananchi aliekuwa hajalipwa fidia hiyo, kama ulivyokuwa Msimamo wa
Wizara hii, Kamati imefanya uchunguzi ufuatao
3.2.1 Kuchunguza iwapo ulipwaji wa fidia ulifanyika kwa watu ambao mali zao
zimeathirika kutokana na Ujenzi wa Uzio wa Uwanja wa Ndege.
Katika kuchunguza ukweli wa wananchi wote waliokuwa na mazao pamoja na mali zao mbali
mbali wamelipwa fidia ili Mamlaka ya Uwanja wa Ndege ikaweza kujenga uzio wa uwanja huo,
27
suala la mwanzo ambalo Kamati ililihoji ni uhakika wa Mamlaka husika katika ulipaji wa fidia
hiyo, na kama kweli maelezo yaliyotolewa awali kwamba hakuna mwananchi ambae hajalipwa
fidia yana ukweli wowote. Katika hali hii, iliarifiwa kwamba malipo yote yanayohusiana na fidia
hiyo yamefanyika kwa watu wote wenye mazao na majengo mbali mbali. Hata hivyo, Kamati
imeendelea kuwa na mashaka juu ya fidia hiyo na hatimae ilipatiwa orodha ya Malipo
yaliyofanyika kwa watu wenye mali mbali mbali zilizoathirika na Ujenzi huo ikiwa ni pamoja na
fedha walizolipwa waathirika hao, (Kielelezo Na.13) kinahusika. Kwa mnasaba huu, Kamati
ilithibitishiwa jumla ya watu 169 wamelipwa fidia kwa njia kuu mbili. Njia ya kwanza ni kupitia
Account za watu hao ambapo jumla ya watu 152 wamelipwa kupitia Benki na watu 17
wamelipwa kwa kupitia mkononi (cash payment). Hata hivyo, Kamati ilihitaji kupatiwa karatasi
za malipo “Payment Voucher” ili kujiridhisha kufanyika kwa malipo hayo.
Suala la kushangaza ni kwamba, katika orodha ya malipo ya watu 17 iliyoambatanishwa na
„Payment Voucher‟ Namba 153 ya tarehe 20/4/2011 ni mwananchi mmoja tu ndie alietia sahihi
kuthibitisha kwamba amepewa fedha za malipo ya mazao yake ambae ni Ndg. Amour M/Juma
Amour alielipwa Tsh. 80,000/- na kujitambulisha kwa kadi ya Mzanzibari Mkaazi Namba.
260129871 (Kielelezo Na.14). Kwa mantiki hii, hakuna uthibitisho wowote wa wananchi 16
waliobakia kulipwa thamani ya mazao yao. Aidha, Kamati pia ina mashaka na malipo ya Tsh.
3,231,500/- zilizoombwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na
kulipwa katika Account ya Songea Sacom kupita Hati ya Malipo tunayoizungumzia hapa,
Namba 153 ya tarehe 21/4/2011, kwamba hazikutumika kwa makusudio yaliyoombwa na hivyo
Kamati ina wasi wasi kwamba fedha hizo zimepotea katika mikono ya watu wachache.
Hili halipingiki kutokana na ukweli kwamba, hakuna sahihi za kupokelewa fedha hizo Tsh.
3,151,500/- na hakuna uthibitisho wa fedha hizo kutumika kwa matumizi mengine yoyote zaidi
ya yale yalioidhinishwa. Inapotokezea fedha hizo zimeshaidhinishwa na kutolewa Serikalini
lakini hakuna uthibitisho wa kupokelewa na kutumika kwake, kuna namna nyingi ya kutafsiri.
Moja ni kama tuliyokwisha ieleza hapo juu, lakini pia kwa mujibu wa Kanuni ya 92 ya Kanuni
za Fedha za mwaka 2005, Mhasibu Mkuu wa Serikali ameshindwa kutekeleza wajibu wake wa
kusimamia fedha za Serikali kwa mujibu wa Sheria. Aidha kanuni hiyo inaelekeza kama
ifuatavyo:
“Mhasibu Mkuu wa Serikali atahakikisha kwamba, malipo yaliyoambatanishwa na
Vocha yatalipwa kwa wanaohusika ndani ya masaa 2421
”
Jambo jengine la kuthibitisha kwamba kanuni za fedha hazikufuatwa katika malipo ya vocha
hiyo ni kukosekana kwa muhuri wa kulipwa “Paid” katika Vocha hii jambo ambalo linakiuka
masharti ya Kanuni ya Fedha ya 95(1) ya Mwaka 2005. Kwa maana hii, Kamati inathibitisha
kwamba, Hakuna ukweli wowote wa kauli ya Wizara wala ya Mhe. Naibu Waziri walipokuwa
wakitoa ufafanuzi wa suala hili kwamba wananchi wote waliokuwa na mazao na mali katika
eneo la uwanja wa ndege, kwamba wamelipwa fidia.
Tunasema hivi kwa sababu, katika Baraza la Nane, Mkutano wa Nne wa Baraza la Wawakilishi,
kikao cha tarehe 28/06/2011, Mhe. Abdalla Juma Abdalla, wakati akiuliza suala la nyongeza
linalotokana na suala la Msingi lililoulizwa na Mhe. Ali Salum Haji, Mwakilishi wa Jimbo la
21
Tafsiri ni yetu.
28
kwahani, linalohusiana na Mpango wa Kukipanua Kiwanja cha Ndege cha Unguja, Mhe.
Abdalla aliuliza suala lake kama ifuatavyo: “Mhe. Spika, tulipofanya ziara ya kukagua kiwanja chetu cha ndege tulipata maelezo kwamba, ndani ya ule
uzio kuna mali ya mtu ambayo hajalipwa fidia na kwa sababu hiyo ule uzio wenyewe umewekwa mlango
wa bwana Yule kuja akitizama zile mali zake ndani ya uwanja, hii ni sababu ya kupitisha ngo‟ombe wakija
mle uwanjani. Je habari hizi ni kweli na kama kweli Wizara yake ina mpango gani wa kumlipa fidia yule
bwana na ule mlango ufungwe ili ng‟ombe wasiendelee kuingia22
”
Wakati akijibu suala hili, Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Mhe. Issa
Haji Gavu alimjibu Mhe. Abdalla kama ifuatavyo: “Mhe. Spika, si kweli kwamba kuna mtu ambae hajalipwa fidia na eneo lake limo ndani ya uwanja na hiyo
milango ambayo haijazibwa ilikuwa ni kutokana na mkataba wetu na hiyo kampuni ambayo ilikuwa
ikijenga tulikubaliana nao namna ya milango ya kuweka tukiwa hatujafikia muafaka. Mhe. Spika, baada ya
kwishakukubaliana hayo maeneo ambayo unahisi yanamilango yatawekwa milango hiyo ambayo
tumekubaliana, maeneo ambayo kuna watu ambao hatujawalipa fidia ni maeneo yaliyoko kwenye makaburi
ambapo ujenzi wa uzio bado haujafika”23
Aidha, Kamati ilipokuwa inafuatilia Payment Voucher No.60 ya tarehe 23/08/2011 imethibitisha
kwamba, jumla ya wananchi 13 wamelipwa ambapo kati ya hao, 11 wamelipwa kupitia Benki na
2 wamelipwa kupitia Cash (Kielelezo Na.15). Baada ya Kamati kufuatilia orodha ya malipo
yaliyofanywa kwa wananchi hao 2, imekuwa na wasi wasi wa usahihi wa saini za malipo ya
Ndg. Tulia Said Hadi ambae ametia sahihi zote mbili, saini ya kawaida na dole gumba la kulia
(Angalia Nyuma ya Voucher hiyo, Namba 60 ya tarehe 23/08/2011) kitu ambacho, yaani
kutia saini mbili tofauti wakati mmoja, ni adimu sana katika elimu na uzoefu wa utiaji wa saini
katika masuala ya fedha na ndio maana kihekima, kikakataliwa kwa mnasaba wa kifungu cha
94(1) cha Kanuni za Fedha za mwaka 2005. Sasa na tundeleea kuzungumzia Fidia ya Mazao na
vipando mbali mbali vya wananchi husika kama zilifuata taratibu za fedha. Hebu kwa mfano
angalia Hati za Malipo (Payment Vouchers) zote zilizowasilishwa kwa Kamati zinazohusiana na
Malipo yatokanayo na mazao (Vocha Namba 60 ya tarehe 25/08/2011 yenye thamani ya Tsh.
2,090,500/- na Vocha Namba 60 ya tarehe 23/08/2011 yenye thamani ya Tsh. 4,007,800/-
zinahusika na (Kielelezo Na.15), na voucher Namba 153 ya tarehe 20/04/2011 (Rejea Kielelezo
Na.13) ndio zilizokabidhiwa kwa Kamati kama ushahidi lakini kwa bahati „Voucher‟ zote hizi
zina mapungufu ya kisheria.
Mbali na mapungufu tuliyokwisha yaeleleza hapo juu, ukifanya rejea ya „voucher‟ hizi sehemu
ya maelezo ya kima cha fedha iliyolipwa kwa maneno; sehemu ya saini ya Ofisa Mlipaji;
Shahidi wa malipo na saini ya anaelipwa hazionekani kujazwa, yaani ama kujanzwa kwa njia ya
maelezo ama kwa kutiwa saini. Kwa mfano kifungu cha 87(1) cha Kanuni za Fedha za mwaka
2005, kinamuelekeza na kumtaka Ofisa anaetia saini katika „Voucher‟ ahakikishe kwamba kila
taarifa inapatikana na ni sahihi. Aidha, Kanuni ya 89(1) inaelekeza kwamba, saini ya Maofisa
waliomo katika Hati ya Malipo (payment voucher) na satafiketi zinazohusika, zitatiwa kwa wino
au kalamu na kupigwa muhuri. Tunachotaka kusema hapa kwamba, pamoja na makosa haya
kuonekana ni madogo, kwa mtazamo wa sheria na dhamira yake, haya sio makosa madogo.
22
Hansard ya Baraza la Wawakilishi, tarehe 28/06/2011, uk-22. 23
Ibid.
29
Kabla ya kuendelea na ufafaunuzi, ni vyema tukakumbushana kwamba, pamoja na mambo
mengine, Kamati ilitumwa kuchunguza iwapo kweli kuna mwananchi ambae anamiliki nyumba
katika eneo la Uwanja wa Ndege, ambae bado hajalipwa fidia na hivyo Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege imeshindwa kumaliza Ujenzi wa Uzio kwa sababu yake. Baada ya kukumbashana,
tunapenda kwa ufupi kufahamishana kwamba mwananchi huyo anaitwa Ndg. Ali Mwinchande
Simba. Kwa lugha nyengine, kuhusiana na fidia ya Ndg. Ali Mwinchande Simba anaemiliki
nyumba, Kamati imethibitisha kwamba hakulipwa fidia yoyote ya nyumba hiyo na hivyo,
Mamlaka haina uwezo wowote wa kisheria wa kumuondosha katika eneo hilo na wala haitakuwa
na uwezo wa kumzuia kupita katika ukuta huo na kufika katika makaazi yake. Ilipokuwa
inafuatilia suala hili, Kamati ilipewa taarifa za uwongo uliothibitishwa mbele ya kikao cha
pamoja baina yake na Katibu Mkuu, Wizara ya miundombinu na Mawasiliano akisaidiwa na
Naibu Katibu Mkuu na hata Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege walieleza kwamba,
wao tayari wameshazungumza nae na wamekubaliana kumlipa na jambo lilobakia ni muda tu wa
malipo hayo.
Bila ya shaka ungependa ufahamu kwa nini Kamati imekuja na jawabu hiyo. Ni dhahiri kupitia
uchunguzi ilioufanya katika kikao cha pamoja na na Uongozi husika lakini pia kwa Kamati
kutoridhika na maelezo ya Watendaji hao na hatimae ilipofanya ziara katika eneo husika na
kufanikiwa kukutana na Ndg. Ali Mwinchande Simba akiwa nyumbani kwake, katika eneo
tunalolizungumzia. Wakati Kamati ilipokutana na Mhusika mwenyewe, alikiri mbele ya Kamati
kwamba hakupokea fidia yoyote wala hajui kwamba ilifanyika tathmini ya kulipwa Tsh.
34,750,000/- majibu ambayo Kamati ilielezwa katika kikao cha pamoja na watendaji wakuu wa
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.
Aidha, Kamati ilipotaka kuthibitisha kwamba Ndg. Ali yuko tayari kuzipokea fedha hizo, kama
ilivyoahidiwa na Uongozi wa Mamlaka na Wizara, Ndg. Ali kwa kauli moja alisema kwamba
hayuko tayari kupokea fedha hizo ambazo yeye anaona ni kidogo sana ukilinganisha na thamani
halisi ya nyumba yake.
Aidha, kuhusu uthibitisho wa Mhusika huyu kupokea fidia ya nyumba yake, Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege imeshindwa kuthibitisha wapi Ndg. Ali Mwinchande Simba amethibitika
akipokea fedha za fidia ya nyumba hiyo. Katika Nyaraka zilizowasilishwa mbele ya Kamati
kuhusiana na hoja hii, jina la mwananchi huyu limejitokeza katika Namba 127 ya orodha ya
waliolipwa fidia ya mazao na sio nyumba (Rejea Kielelezo Na.13). Vile vile, kwa upande wa
nyumba, Ripoti ya Tathmini pekee iliyofanywa na Idara ya Ardhi na Usajili ya mwaka 2008 ndio
inaonesha kwamba Ndg. Ali Mwinchande anastahiki kupewa fidia ya nyumba, ya Tsh.
34,750,000/. Kwa lugha hii, Kamati imejiridhisha kwamba mbali na ushahidi wa mhusika
mwenyewe kuithibitishia Kamati, kukosekana kwa ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba
amepokea fedha hizo za fidia kama tulivyoeleza hapo awali, inatosha Kamati huthibitisha
kwamba hakuna malipo yaliyofanyika mbali na Viongozi wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano pamoja na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kueleza vyenginevyo.
Jambo la kusikitisha ni kwamba, kutokana na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kushindwa
kumlipa mwananchi huyu, Ujenzi wa uzio wa uwanja wa ndege umeshindwa kukamilika na
matokeo yake, wanyama mbali mbali wanaingia kupitia mlangoni hapo, yaani sehemu hiyo
ambayo bado haijajengwa uzio,na wananchi wamefanya njia, kwa ujumla hali ya Uwanja huo
kiusalama hairidhishi. Pamoja na kadhia hii, kuna mambo mengi yameibuka kutokana na
30
ufuatiliaji wa hadidu hii, ikiwa ni pamoja na Kamati kuhoji Utaratibu wa Kisheria wa Kumpata
Mjenzi wa Ukuta huo, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Ujenzi na uwezo wa Kampuni kwa
mujibu wa maelekezo ya Sheria Namba 9 ya mwaka 2005. Kamati pia ina wasi wasi wa kuwepo
kwa „Master Plan‟ ya Ujenzi kwa mnasaba wa mahojiano na Ndg. Ali Mwinchange Simba
ambae alieleza awali kwamba hapo awali ramani ya uzio huo ulikuwa nje ya Nyumba yake
lakini baadae ikawa ndani ya nyumba yake, hali ambayo imechangia kadhia hii. Ama pia kwa
mnasaba wa hali halisi ya ujenzi wa ukuta mwengine unaojengwa nje ya ukuta huu katika eneo
la Uwanja wa Ndege. Kwa ujumla masuala haya pia yanahitaji kufuatiliwa kwa kina, kwani kwa
mujibu wa muda uliopewa, Kamati haikuweza kuyafuatilia masuala yote haya na kuyatolea
ufafanuzi wake.
3.2.2 Tathmini juu ya fidia za mali mbali mbali zilizoathirika na ujenzi wa uzio
wa Uwanja wa Ndege.
Kwanza tufahamu hapa kwamba, tathmini ya mali husika ni za aina mbili kuu: mali
zisizohamishika, yaani ardhi, vibanda, msikiti, Nyumba na nyenginezo, na tathmini ya pili
inahusiana na mazao na vipando mbali mbali ambavyo kwa ukweli vinahamishika. Kamati
imehoji iwapo Mamlaka ya Uwanja wa ndege ilifanya tathmini kuhusiana na malipo iliyotoa ili
kujiridhisha juu ya wale wasioridhika kupokea fidia hizo. Ili kujibika kwa suala hili, Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano kupitia Mamlaka ya Uwanja wa Ndege ina dhima ya
kuithibitishia Kamati iwapo kulikuwa na uthibitisho iwapo wananchi hao wamelipwa kwa
kuzingatia thamani halisi ya soko wakati mali zao zilipoathirika. Ili kujibika suala hili, jambo la
kwanza la msingi ni kujiuliza, Je, Mamlaka ilifanya tathmini ya mali hizo? Kwa bahati nzuri,
Kamati imepatiwa tathmini iliyofanywa na Idara ya Ardhi na Usajili ya June, 2008 (Kielelezo
Na.16) ambapo Kamati haina pingamizi na tathmini hii. Hata hivyo, Kamati ina wasi wasi juu ya
malipo yaliyofanywa kwa wananchi hao iwapo yanawiyana na tahmini iliyofanywa na Idara ya
Ardhi na Usajili. Ili kujibu suala hili, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege iliwajibika kuithibitisha
Kamati kupitia Vocha ya Malipo au ushahidi wowote wa kupokelewa malipo hayo kwa mnasaba
wa tathmini halisi iliyofanywa na Idara ya Ardhi na Usajili. Kwa mfano, katika ukurasa wa 5 wa
Tathmini hii (Rejea Kielelezo Na.16), Idara ya Ardhi na Usajili ilifanya tathmini ya Nyumba ya
Ndg. Mohammed Laka kwa Tsh. 18,020,000/- Ndg. Juma Mussa Mohammed kwa tathmini ya
Msikiti ni Tsh.19,160,000/-. Ndg. Fatma Mohammed Salima aliemiliki Ardhi na Kibanda
alipaswa alipwe Tsh. 52,495,000/-. Ndg. Ali Mwinchande Simba anaemiliki Nyumba alipaswa
alipwe Tsh. 34,750,000/-. Ndg. Charles Madai Nchunga anaemiliki Kibanda alipaswa alipwe
Tsh. 1,160,000/-. Ndg. Iddi alipaswa alipwe Tsh. 860,000/-. Ndg. Hassan Gharib Makame
aliemiliki Mkahawa angelipwa Tsh. 26,260,000/- na wengine wengi. Ili kuthibitisha kwamba,
kweli Mamlaka ya Uwanja wa Ndege imelipa fidia za Nyumba ma Mali za wananchi hao,
walilazimika kuthibitisha kwa mapokezi yake yakiwa sawa na tathmini iliyofanywa. Kwa bahati
mbaya sana, Mamlaka imeshindwa kuithibitishia Kamati, na kwa jawabu hii, Kamati haina
uwezo wa kuthibitisha ama kukubali kwamba wananchi wote wamelipwa fidia. Labda tuchukulie
ushahidi wa Kimazingira, kwamba, kwa kuwa watu wote hawa walikwisha ondoka katika eneo
husika na Kamati haikupata malalamiko zaidi ya Ndg. Ali Mwinchande Simba, iwe ni ushahidi
wa kuiridhisha Kamati kwamba malipo yamefanyika.
Aidha, kuhusiana na tathmini ya mazao, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege iliieleza Kamati
kwamba tathmini hiyo imefanywa na Idara ya Kilimo, chini ya Wizara ya Kilimo na Maliasili.
Aidha walipotakiwa wathibishe, Mamlaka iliwasilisha barua ya tarehe 23/03/2011 yenye kumbu
31
kumbu namba AR/WMGH/K/29/VOL IV/129 iliyoandikwa na Ndg. Saleh S. Masoud, Afisa
Kilimo, Wilaya ya Magharibi, Unguja (Kielelezo Na.17). Kwa mnasaba wa hoja yao hii,
walitakiwa wathibitishe kwamba, Idara ya Kilimo ilikuja kufanya tahmnini ya mazao ya
wananchi na pia Kamati iridhishwe kwamba tathmnini hiyo imefanywa kwa mnasaba wa soko
halisi ya mazao na vipando hivyo. Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana Kamati haikuridhishwa
inasvyostahili. Kwani ilipatiwa barua inayotoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magharibi na sio
Idara ya Kilimo, hivyo, sio sahihi kwamba tathmini hiyo imefanywa na Idara ya Kilimo, bali
imefanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi Unguja.
Aidha, tofauti na ile iliyofanywa kitaalamu na Idara ya Ardhi na Usajili, tathmini hii iliyofanywa
na Halmashauri haikuonesha uchambuzi wowote wa kina kuhusiana na mazao ya wananchi 169
waliorodheshwa katika orodha ya malipo ya fidia (Reja Kielelezo Na.13) isipokuwa ni
wananchi wanne tu ndio waliohusika na tathmini hiyo huku wananchi 165 hawakuonekana
kufanyiwa tathmini. Kamati inapenda kuwafahamisha wananchi hao wanne waliofanyiwa
tathmini na Halmashauri ya Wilaya ya Maghribi ni Ndg. Khamis Pandu Mmadi, aliefanyiwa
tathmini ya kulipwa Tsh. 143,000; Ndg. Makoe Sana Makuru aliefanyiwa tathmini ya kulipwa
Tsh. 2,000,000/-; Ndg. Ramadhani Ali Juma aliefanyiwa tahmini ya kulipwa Tsh. 736,000 na
Ndg. Issa Jafari aliefanyiwa tathmini ya kulipwa Tsh. 150,000/-. Hata hivyo, ukifanya rejea ya
waliolipwa, yaani Kielelezo Na.13, uttafahamu kwamba, ni Ndg. Issa Jafari pekee jina lake pia
limejitokeza katika orodha ya wananchi 169 walioorodheshwa kupokea fedha zao wakati hao
watatu wenziwe mbali na kufanyiwa tathmini ya malipo, hakuna ushahidi wa wapi walipokelea
fedha zao.
Mbali na udhaifu huo, kwa mujibu wa tathmini hiyo iliyofanywa, alistahiki kulipwa Tsh.
150,000/- tu kutokana na kumiliki minazi miwili huku kila mnazi ukiwa na thamani ya Tsh.
75,000/-, jambo linaloshangaza ni kwamba, kwa mujibu wa orodha hiyo ya wananchi 169
waliolipwa mazao na vipando vyao, Ndg. Issa Jafari amelipwa kupitia Benki ya NBC Tsh.
262,000/-. Hii inathibitisha wazi kwamba, tathmini ya mazao haikufanyika kitaalamu kwa
kutowashirikisha wahusika wa tathmini hiyo hali iliyopelekea wananchi wengi kutolipwa kwa
mujibu wa tathmini halisi ya mazao ambayo ingestahiki walipwe. Kwa lugha nyengine, Kamati
haikuridhika na utaratibu wa tathmini uliofanywa na Afisa Kilimo, Wilaya ya Maghribi hali
iliyopelekea wananchi wengi kudhulumiwa haki zao. Aidha, kwa wananchi waliobakia, mbali na
hawa waliofanyiwa tathmini na Afisa huyu wa Kilimo, Kamati imejiridhisha kwamba,
wamelipwa kinyume na kufanyiwa tathmini.
3.2.3 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii ndogo, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
3.2.3.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Utaratibu wa Ulipaji wa Fidia kwa wananchi walioathirika na Ujenzi wa Uzio wa
Uwanja wa Ndege, haukufuata taratibu za kisheria.
32
Kamati imegundua kwamba, ulipwaji wa fidia kwa wananchi walioathirika na mali zao
za kudumu pamoja na mali zao za muda, haukulipwa kwa kufuata maelekezo ya sheria
za fedha. Hali hii inaleta wasi wasi kwamba, fedha hizo inawezekana sana
hazikutumika ipasavyo.
(ii) Hakuna tathmini ya Kitaalamu iliyofanyika kwa wananchi wenye mazao na
vipando mbali mbali na wengi wao wamelipwa bila ya kufanywa kwa tathmini
yoyote.
Kutokana na ushahidi uliowasilishwa na kwa mujibu wa uchunguzi wake, Kamati
imebaini kwamba wananchi wengi wamelipwa fedha zao kupitia Benki ama kupitia
mkononi bila ya kufanyiwa tathmini yoyote ya kitaalamu, hali ambayo imepelekea
kulipwa fedha kidogo kuliko thamani halisi ya mazao na vipando vyao. Kwa upande
wa waliomiliki mali zisizohamishika, Kamati imejiridhisha kwamba tathmini halisi ya
mali kwa mnasaba wa soko imefanyika, ingawaje kasoro iliyojitokeza ni
kutoshirikishwa ipasavyo kwa wamiliki hao wakafahamu namna gani tathmini hiyo
imefanyika.
(iii) Kamati imejiridhisha kwamba, sio wananchi wote waliolipwa fidia za mali zao
huku msisitizo ukiwekwa kwa Ndg. Ali Mwinchande Simba ambae ndie sababu
ya Kamati hii kutumwa kwenda kufanya uchunguzi.
(iv) Viongozi wa Wizara, yaani Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu
na Mawasiliano kwa kosa la kulipotosha Baraza la Wawakilishi kwa kutoa
majibu yasiyo na ukweli wowote.
Kinyume na Kanuni za Baraza zinavyoelekeza, Kamati imethibitisha kwamba, Waziri
na Naibu wake walipokuwa wanatoa ufafanuzi wa suala hili walilipotosha Baraza kwa
kutoa taarifa zisizo za kweli, hali inayoonesha ama majibu haya wanayatoa kwa
kuongozwa vibaya na watendaji wao ama kwa kutofanya utafiti binafsi wakajiridhisha
juu ya usahihi wa taarifa wanazotakiwa wazitoe katika Baraza la Wawakilishi.
(v) Kamati kupatiwa taarifa za Uongo na upotoshaji.
Wakati Kamati inafuatilia suala hili, ilipatiwa taarifa zisizo za kweli kuhusiana na fidia
hiyo, hivyo, Watendaji Wakuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano pamoja na
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege walishirikiana katika kutaka kuipotosha Kamati juu ya
uchunguzi uliotakiwa ufanywe.
3.2.3.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi wa hapo juu, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:
(i) Hatua za Kinidhamu zichukuliwe dhidi ya watendaji waliohusika na malipo ya
fedha za fidia kwa wananchi walioathirika na ujenzi wa uzio, kutokana na
watendaji hao kutofuata ipasavyo taratibu za malipo hayo kwa mujibu wa sheria
za fedha (Na. 12 ya mwaka 2005 pamoja na Kanuni zake).
(ii) Mwananchi ambae bado hajalipwa fidia, Ndg. Ali Mwinchande Simba alipwe
fidia yake kwa mnasaba wa thamani ya mali zake katika wakati tulionao na sio
33
tena wakati uliopita, kwa sababu tokea muda uliofanywa tathmini hadi leo,
maisha yameshabadilika na thamani halisi ya Nyumba imeongezeka.
(iii) Kwa kutumia Kanuni za Baraza la Wawakilishi, Kamati inapendekeza Waziri na
Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, waliomberadhi
Baraza la Wawakilishi kutoa maelekezo yasiyo ya kweli kuhusiana na ulipwaji
wa fidia kwa wananchi walioathirika na Ujenzi wa Uzio, Uwanja wa Ndege.
(iv) Hatua zinazofaa kwa mujibu wa Sheria Namba 4 ya mwaka 2007, zichukuliwe
kwa Watendaji wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Mamlaka
ya Uwanja wa Ndege waliohusika na upotoshaji wa Kamati kwa kutoa taarifa
zisizo za kweli.
3.3 KUCHUNGUZA MATATIZO YA UNUNUZI WA JENERETA:
Hadidu nyengine ndogo katika Hadidu hii rejea ni hii inayohusiana na Ununuzi wa Jenereta.
Chanzo cha tatizo hili ni kwamba, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege ama Serikali imenunua
Jenereta ambalo limeshawasili takriban mwaka huku bado halijafungwa na kuanza kazi kinyume
na dhamira ya kununuliwa kwake. Hivyo basi, Kamati imetakiwa kuchunguza juu ya utaratibu
wa kununuliwa kwake pamoja na sababu zilizopelekea kutofungwa na kuanza kazi kwa jenereta
hilo. Kwa lugha nyengine, kama inavyokumbukwa kuwa tarehe 01/09/2010 Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano imenunua Jenereta kwa ajili ya kuondosha tatizo la kukatika kwa
umeme katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar lakini takriban mwaka mzima jenereta hilo
limekaa na wala halifanyi kazi. Hapa kuna haja ya kujiuliza, je tatizo hili limesababishwa na kitu
gani? Ili kupata jawabu muwafaka, ni vyema tukajiuliza masuala yafuatayo:-
3.3.1 Je, Sheria ya Manunuzi na Ugavi wa Mali za Serikali (No. 9 ya 2005) imefuatwa
katika kupatikana kwa „supplier‟ wa Jenereta hilo?
Kwanza ifahamike wazi kwamba, kwa mujibu wa Sheria Namba 9 ya mwaka 2005,
kunakohusiana na ununuzi wa mali za Serikali, ni lazima suala hili lifuate taratibu zilizowekwa
katika sheria hiyo, ambapo hatua ya msingi ni kuangalia vipi suala hili la kununuliwa kwa
jenereta kulifuata taratibu hizo, na kwa kuanzia, tuanze na kupata taarifa zinazohusiana na Bodi
ya Zabuni ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Kamati ilitaka kuthibitishiwa kwa njia
ya kumbu kumbu za vikao vya Bodi hii kama iliwahi kukaa na kuthibitisha njia ya kupatikana
kwa „supplier‟ husika kama maelekezo haya yanavyotolewa na kifungu cha 32(2) cha Sheria
No.9 ya 2005 kinachoelekeza kwamba uchaguzi wa njia yoyote ya kununua (ama kumpata
supplier) ni lazima kwanza ithibitishwe na Bodi ya Zabuni. Yaani, Kamati ilitakiwa kwanza ihoji
kama „Supplier‟ huyu kapatikana kwa utaratibu upi, je ni kwa kutangaza Zabuni (Tender) kama
inavyoelekezwa na kifungu cha 33 hadi cha 35 cha Sheria hiyo; Je Wizara imeitisha „Quotations‟
kwa kupendekeza „Supplier‟ baada ya kunasibisha bei kwa „Suppliers‟ mbali mbali kama
ilivyoelekezwa na kifungu cha 37 ama kwa kwa uchaguzi wa moja kwa moja „Direct
Procurement‟ kama inavyoelekezwa na kifungu cha 38 cha Sheria hii.
Kwa bahati nzuri sana, jawabu ya aina ya uchaguzi wa taratibu ya kupatikana kwa „Supplier‟
huyo sio lazima liulizwe hapa, linajibika baada ya kuthibitishwa na maamuzi ya Bodi ya Zabuni
34
ya Wizara kama tulivyonukuu kifungu cha 32(2) cha Sheria hiyo, hivyo katika kuhoji huko
iliitaka Wizara itoe maelezo kwa Kamati imetumia njia ipi kumpata suuplier wa jenereta hiyo,
lakini je, njia hiyo kwanza ilipata Baraka ya Bodi ya Zabuni ya Wizara?. Kwa bahati mbaya
sana, jawabu husika haikupatikana. Mamalaka ya Uwanja wa Ndege ilijinata mbele ya Kamati
kwamba Bodi ya Zabuni na Kamati zake ikiwa ni pamoja na Kamati ya Tathmini ya Mamlaka
ndio iliyokaa na kufuata taratibu zote za manunuzi kama zilivyoelekezwa katika Sheria. Lakini
pia inaelezwa kwamba, ni Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ndio
iliyofanya kazi hiyo kwa kufuata sheria husika.
Tunakiri kwamba Kamati ilipoomba kupatiwa Kumbu kumbu za Vikao vya Bodi ya Zabuni ya
Wizara kuhusiana na ununuzi wa Jenereta, ilipatiwa kumbu kumbu moja ya tarehe 29/04/2008
(Kielelezo Na.18) iliyopitisha agenda nyingi moja kati ya hizo ni hii ya Ununuzi wa „Standby
Generetor‟ la Uwanja wa Ndege Zanzibar (Iterm No. 11.0), na kwa maslahi ya hoja hii, naomba
kuinukuu: “Baada ya Mkurugenzi kuwasilisha mada hii, Bodi ilikubaliana kuwa suala hili litaingizwa katika mwaka
wa fedha wa 2008/2009 katika utaratibu wa MDRI (Multilaterals Debt Relief Initiative)”
Kwanza maelezo ya nukuu hii hayaoneshi maamuzi ya Bodi ya kumpata „supplier‟ wa jenereta
hilo isipokuwa yanaonesha azma ya wapi fedha za ununuzi wake zingelipatikana, na ndio maada
baada ya miaka miwili, ndio azma hiyo ilipotimia ya kununuliwa genereta. Katika mazingira
haya, Kamati bado inasisitiza kwamba, haikupatiwa uthibitisho wa kukaa kwa Bodi ya Zabuni na
kufanya maamuzi ya ununuzi wa jenereta hilo. Kamati pia inapata shaka kuhusiana na ukweli wa
kununuliwa kwa jenereta hilo kwa kuzingatia sheria ya manunuzi tuliyoitaja hapo juu. Aidha,
Kamati iliposhindwa kupatiwa ushahidi wowote wa kumbu kumbu za vikao vyovyote vya bodi
ya zabuni, sio tu kunaonesha kutofuatwa kwa taratibu hizo za sheria lakini pia ni kwenda
kinyume na kifungu cha 5 cha Nyongeza ya Kwanza ya Sheria Namba 9 ya 2005 kinachoelekeza
kwamba Katibu wa Bodi ya Zabuni anatakiwa kurikodi na kuhifadhi kumbu kumbu za mkutano
wowote wa Bodi ya Zabuni katika hali nzuri na kutiwa sahihi na Mwenyekiti na Katibu wa Bodi
katika mkutano wake unaofuata. Kwa kuwa Kamati haikuwapiwa kumbu kumbu hizo, haina
uwezo wa kukubali kwamba taratibu za sheria ya manunuzi zimefuatwa ipasavyo.
Hata hivyo, Kamati imekabidhiwa ripoti ya tathmini na mapendekezo ya utoaji wa mkataba ya
February 2009 (Kielelezo Na.19), ambapo „Item No. 2.0‟ imetoa ufafanuzi wa namna
alivyopatikana „supplier‟ huyo kupitia „Restricted International Bidding‟ kwa maana kuwaalika
kwa njia ya barua „suppliers‟ kutoka nje ya Zanzibar, ambao wote wametoka Dar es Salaam. Ni
sawa na kutumia kifungu cha 36(1) cha Sheria Namba 9 ya 2005, kinachoweka masharti ya
kutumika kwake ni pale ambapo thamani au mazingira hayathibitishi ama hayaruhusu kufanyika
kwa njia ya wazi „open bidding method‟. Kwa maana hii, Kamati inahoji kwa nini suala hili
lililotumia fedha nyingi za wananchi halikutumika kwa njia ya wazi ya zabuni „open
domestic/international bidding‟ ambayo inasisitizwa zaidi kisheria na inaleta ushindani wa wazi
baina ya „suupliers‟. Ili kuondosha shaka ya suala hili, angalau Wizara ingeithibitishia Kamati
kwamba njia hiyo walioyoitumia imekubaliwa na Bodi ya Zabuni.
Tukiendelea na namna alivyopatikana „supplier Mpomabiva Investment Ltd‟, Ndg. Amour S.
Omar kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege ndie alieandika barua kwa
„supplier‟ wote watatu, ambao ni Mpomabiva Investments Ltd, Merry Water, na CAR & General
(C & G), kupita barua ya tarehe 6/6/2008 yenye kumbu kumbu namba DA/E/003/2 Vol. III
35
kuwaalika katika usambazaji „supply‟ wa genereta hilo (Angalia Appendix 1 ya Kielelezo
Na.19). Kwanza tunapenda ifahamike wazi kwamba, barua hii imeandikwa na Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, kwa sababu Ndg. Amour amesaini kwa niaba yake. Hapa
tunapaswa kujiuliza, je, maamuzi ya kuwaalika suppliers hawa yametoka katika chombo chenye
mamlaka, yaani Bodi ya Zabuni, na kama ndio Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
ni mjumbe wa Bodi hiyo na amepata maelekezo hayo kutoka katika Bodi ya Zabuni ya Wizara
ya Miundombinu na Mawasiliano au ameamua yeye mwenyewe kutoa „invitation‟ kwa
„suppliers‟ tuliowataja hapo juu.
Kwa mujibu wa Nyongeza ya Kwanza ya Sheria Namba 9 ya 2005, Bodi ya Zabuni ya Wizara
itakuwa na Mwenyekiti anaeteuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara husika; Mhasibu Mkuu wa
Wizara husika ama Taasisi inayojitegemea; Wakuu wa Idara za Wizara husika, na Afisa wa
Serikali kutoka Wizara inayohusika na Fedha ambae atateuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara
inayohusika na masuala ya fedha. Kwa maana hii, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege ni mjumbe tu wa Bodi hiyo ya Zabuni hivyo, hakuwa na mamlaka ya kusaini documents
zozote za Bodi kazi ambayo ingefanywa na ama Mwenyekiti au Katibu wa Bodi kwa ruhusa ya
Bodi husika. Sasa kama hii ndio hali, bado kuna masuala mengi ya kujiuliza juu ya kitendo cha
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kuitisha „quotations‟ kinyume na mamalaka iliyopewa kisheria.
Tunasema hivi pia kwa kuzingatia ukweli kwamba, katika mwaka 2008-2010, Idara ya Anga
haikuwa Mamlaka, kwani Sheria ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, Namba 8 imetungwa na
kuanza kutumika mwaka 2011 na hivyo, haikuwa na uwezo wa kujitegemea wala kuwa na Bodi
ya Zabuni na hata ingekuwa inayo, Kamati ilipewa taarifa kwamba Bodi ya Zabuni ya Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano ndio iliyoshughulikia suala la ununuzi wa jenereta.
Kwa kuwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
imeshindwa kutoa ushahidi wa Kumbu kumbu za vikao vya „Tender Board‟ iliyoamua kuteuliwa
kwa „Mpomabiva Investments Ltd‟ kutoa huduma ya kunua na kuleta jenereta na kwa kuwa
utaratibu wa kutoa invitation na kuwaandikia barua supplier wote hao watatu haukufuata
utaratibu wa Sheria za Manunuzi na Ugavi wa Mali za Serikali, Namba 9 ya mwaka 2005,
Kamati imejitosheleza kuamini kwamba, moja kati ya matatizo ya jenereta hilo ni kununuliwa
bila ya kufuata taratibu za Kisheria, na jambo la kusikitisha ni kwamba, hata Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege Ndg. Said Ndombugani ameithibitishia Kamati
kwamba, wao kama Mamlaka ya Uwanja wa Ndege ni lazima waivunje Sheria Namba 9 ya
mwaka 2005, katika utekelezaji wa majukumu yao. Hii inaleta picha kwamba, Taasisi nyingi za
Serikali zinapuuza kutekeleza masharti ya Sheria hii.
Kuna haja pia ya kuangalia kuhusu tathmini iliyofanywa na Wizara ya Miundombinu na
Mawalisiano mpaka Mpomabiva Investment Ltd, akabarikiwa kuleta jenereta hilo. Hapa
tujiulize, Je, kuna tathmini yoyote iliyofanywa juu ya huduma na uwezo wake? Lakini, Je,
Kamati hii ya Tathmini ipo kisheria?. Kifugu cha 4.0 (item no. 4.0) ya Ripoti ya
tathmini na mapendekezo ya utoaji wa mkataba ya February 2009 (Rejea Kielelezo Na.19),
imeonesha wajumbe wa Kamati ya Tathmini ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ambao
ni Ndg. Yisambi M. Shitindi-Mwenyekiti, Ndg. Masoud S. Abdulrahman-Katibu, Ndg. Amour
S. Omar-Mjumbe na Ndg. Khamis A. Omar-Afisa Manunuzi. Ambao kwa pamoja wameifanya
kazi ya kutathmini Kampuni zote 3 na kutoa taarifa zao zinazoonekana katika ripoti husika
kuanzia „item namba 4.0 hadi 8.0 ambapo Kamati haina pingamizi juu ya tathmini hii na
36
inapongeza kazi iliyofanywa. Hata hivyo, kwa kuwa muundo wa Kamati umeelezwa katika
kanuni ya 37 (1) ya Kanuni za Manunuzi na Ugavi wa Mali za Serikali ya mwaka 2005,
kwamba Bodi ya Zabuni itaunda Kamati ya Tathmini itakayokuwa na Katibu wa Bodi ya
Zabuni, Mjumbe mmoja kutoka katika Bodi ya Zabuni, Mfanyakazi mwenye ujuzi unaohitajika
(Technical Staff) kutoka katika Kitengo cha Manunuzi na Mwanasheria.
Sasa ni vyema tukajiuliza, je wajumbe wa Kamati ya Tathmini wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano, akina Ndg. Yisambi M. Shitindi na wenzake, wameteuliwa na nani na wana sifa
zilizoelezwa katika sheria husika? Yaani, Wizara ya Miunombinu na Mawasiliano ilitakiwa
ithibitishe kwa Kamati juu ya kumbukumbu yoyote ya Bodi ya Zabuni ya Wizara yao kukaa na
kuwachagua wajumbe hawa wa Kamati ya Tathmini. Lakini kwa bahati jambo hili
limeshindikana na ni wazi kwamba hakuna uthibitisho wa Kamati hii kuwakubali kama hawa
ndio wajumbe wa Kamati ya Tathmnini kisheria. Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 48(2) cha
Sheria Namba 9 ya mwaka 2005, wajumbe wa Kamati ya Tathmini ni lazima wapendekezwe na
Kamati ya Manunuzi (Procurement Management Unit) na kuthibitishwa na Bodi ya Zabuni.
Hivyo, mbali na kuhoji kumbu kumbu za Bodi ya Zabuni, Kamati ilitaka kupatiwa kwa kumbu
kumbu za Kamati ya Manunuzi iliyokaa na kuwapendekeza wajumbe hawa na hatimae
wakathibitishwa na Bodi ya Zabuni. Kwa bahati mbaya sana, Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano pamoja na Mamlaka ya Uwanja wa ndege wameshindwa kuthibitisha na hivyo,
unaweza hata nawe ukajiuliza, kuna sababu gani tena ya Kamati hii kuamini kwamba wajumbe
hawa wamechaguliwa kisheria ? Jawabu yake ni hiyo, kwamba wamechaguliwa kinyume na
maelekezo ya sheria.
Suala jengine la kujiuliza, je Wajumbe wa Kamati ya Tathmini wametia saini Waraka wa
Maadili (Code of Ethics) na kutangaza kwamba hawana maslahi katika upatikanaji wa supplier
husika? Chanzo cha suala hili ni kifungu cha 48(6) cha Sheria Namba 9 ya mwaka 2005
kinachosema: “Wajumbe wote wa Kamati ya Tathmini watasaini Kanuni (Waraka) za Maadili kwa mujibu wa Kanuni za
Sheria hii, kutangaza kwamba wao hawana mgongano wa maslahi katika mahitaji ya ununuzi na ugavi wa
mali za Serikali24
”
Kwa mantiki hii, ni vyema Kamati ikathibitishiwa kwamba wajumbe hawa wameibarikia
Kampuni ya Uwekezaji ya Mpomabiva kwa kuzingatia maslahi ya kisheria na uthibitisho ni
kutangaza kwao kutokuwa na maslahi yoyote na kampuni hiyo.
Katika „Attachment A: Personal Covenant‟ iliyomo kuanzia ukurasa wa 10 hadi 14 wa Kielelezo
Na.19, wajumbe wote wanne wa Kamati ya Tathmini ya Wizara ya Miundombinu wametangaza
kutokuwa na mgongano wa kimaslahi kama wanavyotakiwa kisheria. Hata hivyo, Sheria
iliyonukuliwa ni Sheria Namba 21 ya mwaka 2004, sheria hii sio ya Zanzibar bali ni ya
Tanzania bara, na hivyo, pamoja na juhudi za wajumbe hawa kutangaza kutokuwa na mgongano
wa maslahi, sheria waliyoitumia kutangaza huko haitumiki Zanzibar. Aidha, sheria ya Kinga
dhidi ya Rushwa (The Prevention of Corruption Act, 1971) ambayo imenukuliwa katika
Utangazaji huo wa Maslahi binafsi ya Wajumbe wa Kamati ya Tathmini haitumiki Zanzibar, na
kwa maana hii, hakuna ubaya wowote kisheria kusema kwamba, maelekezo ya kifungu cha
48(6) cha Sheria Namba 9. ya mwaka 2005 ya Sheria ya Zanzibar, hayakufuatwa.
24
Tafsiri ni yetu.
37
Hapa tunataka tufahamishe kitu kimoja, kwamba, asili ya fedha hizi zinatokana na Msamaha wa
Madeni (MDRI) pengine sual hili kwa kiasi linamahusiano na masuala ya Muungano, lakini
fedha hiyo ni fedha ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na inapaswa itumiwe kwa mujibu wa
Sheria za Zanzibar na sio Sheria za nchi nyengine. Aidha, wakati Wizara hii inapokea maelekezo
kutoka Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kuhusu matumizi ya fedha za
msamaha wa madeni kwa mwaka wa fedha 2008/2009, ilitakiwa kutayarisha utaratibu wa
ununuzi wa jenereta hilo kama sheria Namba 9 ya mwaka 2005 inavyoelekeza na sio kufuata
sheria nyenginezo. Lugha hii kisheria, yaani kuapa kwa kutumia sheria zisizohusika, ni sawa na
kusema kwamba hakuna kiapo kilichofanyika, hivyo, na Kamati inasimamia hili kwamba,
pamoja na juhudi zilizochukuliwa na kutangaza maslahi wakati wa uteuzi wa „Supplier‟
Mpomabiva, wajumbe wa Kamati ya Tathmini hawakuwa safi ipasavyo na inawezekana pia hata
maamuzi ya uteuezi wao kwake yakawa na kasoro kadhaa.
3.3.2 Kuchunguza Mamlaka iliyohusika katika Ununuzi wa Jenereta hilo:
Baada ya kuangalia namna ya utaratibu wa uitishaji wa zabuni hadi kupatikana kwa Kampuni ya
Uwekezaji ya Mpomabiva, Kamati imeona ni vyema kupata jawabu ya Mamlaka iliyohusika na
Ununuzi wa jenereta hiyo. Bila ya shaka suala hili jawabu yake ni Kampuni ya uwekezaji ya
Mpomabiva ndiyo iliyohusika na ununuzi hadi ufikishaji wa jenereta katika eneo la Uwanja wa
Ndege. Hata hivyo, Kamati ilipohoji Wizarani kuhusu namna ununuzi wake, iliiambiwa kwamba
masuala ya ununuzi wa jenereta hilo yamefanywa na Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango
ya Maendeleo ambao ndio walioingia Mkataba wa ununuzi wake na ndio wanaojua zaidi
masuala ya „installation‟ uwekaji wa jenereta hilo.
Kwa maana hiyo, ni vyema nasi tukafahamu historia ya ununuzi wa jenereta hilo katika
mahusiano ya Ofisi hizi mbili, yaani Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi. Tarehe 2/03/2009, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo iliwaandikia Makatibu Wakuu wa Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo na
Maliasili, Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo na Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano kuzitaka kukamilisha taratibu za kisheria juu Manuzi ya vifaa mbali mbali
wanavyohitaji na vitakavyochangia moja kwa moja katika kukuza Uchumi na Kupunguza
Umasikini kupitia fedha zinazotokana na msamaha wa madeni (Kielelezo Na.20). Ambapo
kupitia barua ya tarehe 4/03/2009, yenye kumbu kumbu namba MOCT/F.10/VOL.11/21
(Kielelezo Na.21)Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ilijiibu barua ya Ofisi ya Rais, Fedha
na Uchumi wa Maendeleo kukiri kupokea barua yao na kuambatanisha na tathmini ya ununuzi
wa vifaa mbali mbali vya idara ya Anga ikiwa ni pamoja na ununuzi wa Jenereta (hata hivyo,
Kamati imepewa barua hiyo tu bila ya kuambatanishwa na tathmini husika).
Tarehe 11/01/2010 Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ilimuandikia barua
Katibu Mkuu, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kuhusu kasoro zilizojitokeza katika
mkataba uliotayarishwa na Mkurugenzi, Idara ya Anga ili Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano iufanyie marekebisho Mkataba huo upate uwende sambamba na taratibu za
matumizi ya fedha za msamaha wa madeni (Kiamtatanisho Namba 22). Baada ya marekebisho
ya kasoro hizo, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ikaingia mkataba na
38
Kampuni ya Uwekezaji ya Mpomabiva (Kielelezo Na.23). Kwa kuzingatia maelezo hayo hapo
juu, suala la aliehusika na ununzi wa jenereta hilo bado linahitaji jawabu ya ufasaha.
Kwa kuwa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege waliieleza Kamati kwamba suala la ununuzi wa
Jenereta limefanywa na Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na Kamati
ilipoiita Bodi ya Zabuni ya ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, pamoja na
Idara ya Uhakikimali na Mitaji ya Umma, Kamishna wa Fedha za Nje Ndg. Saada M. Salum
alieleza kwamba, Ununuzi huo umefanywa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa kuwa wao
ndio waliohusika na utayarishaji wa hatua zote za kupatikana kwa „Supplier‟ husika pamoja na
mkataba wa ununuzi wa jenereta hilo. Kutokana na ukweli kwamba, kila Wizara inakwepa
jukumu la ununuzi wa jenereta, ipo haja ya kuliangalia suala hili kwa mujibu wa sheria, ili
tuweze kufahamu ni nani aliehusika na ununuzi huo.
Sheria ya Mikataba (Contract Decree) Cap 149 ya mwaka 1917, kifungu cha 2(a) kinaeleza
kwamba, “Pale ambapo mtu anaonesha utayari wake kwa mtu mwengine, wa kufanya ama
kujizuia kufanya jambo lolote, kwa lengo la kupata ridhaa ya mtu huyo kutokana na kufanya ama
kujizuia kufanya, anasemwa kwamba ametoa pendekezo25
” Aidha, “wakati ambapo mtu huyo
aliepewa pendekezo ataonesha kuliridhia pendekezo hilo, pendekezo hilo husemwa kuwa
limekubalika. Pendekezo lilokubalika linakuwa miadi26
” “kila miadi na kila mkusanyiko wa
miadi inayopelekea kuwepo kwa matarajio kwa kila mtu, huwa ni makubaliano27
” “Na
makubaliano yanayoweza kutekelezwa kisheria huitwa mkataba28
”
Hapa tunachotaka kuonesha kwamba, katika mkataba wowote, wahusika katika mkataba huo
wakikubaliana juu ya jambo lolote linaloweza kutekelezwa kisheria, huitwa „parties to the
contract‟ na kila mtu huwa na wajibu na haki katika mkataba huo kisheria. Kwa mujibu wa
Mkataba uliowasilishwa kwa Kamati (Rejea Kielelezo Na.23) Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo ndio iliyotoa pendekezo (offer) ambapo katika Mkataba huu anaitwa
Mnunuzi (Purchaser) na Kampuni ya Uwekezaji ya Mpomabiva ndio iliyokubali pendekezo hilo
(offeree), ambae katika mkataba huu huitwa (supplier). Vile vile, katika kifungu cha 5.01 cha
Mkataba huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ndie
alietia saini kwa niaba ya Wizara yake. Kwa hali hii, pamoja na sababu zilizotolewa mbele ya
Kamati, Kamati inakubaliana kisheria kwamba, Mkataba huu umefungwa na Ofisi ya Rais,
Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na kama kutatokezea matatizo yoyote ikiwa ni
pamoja na kuvunjwa kwa Mkataba huu, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege haiwezi kuhusika kwa
namna yoyote. Aidha, kwa kuwa Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo
ililazimika kuhakikisha kwamba, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano inafuata taratibu zote
za Sheria ya Manunuzi kama ilivyonukuliwa katika barua yao ya tarehe 2/3/2009 (Rejea
Kielelezo Na.20), na kwa kuwa taratibu hizo za Sheria ya Manunuzi na Ugavi wa Mali za
Serikali Namba 9 ya mwaka 2009, zimekiukwa, basi ni wazi kwamba, upotevu wowote
utakaotokezea kuhusiana na Tsh. 316,922,175/- alizopewa „supplier‟ wa jenereta hilo ni sawa na
upotevu wa fedha za Serikali na umehusika na Wizara zote mbili.
25
Tafsiri ni yetu. 26
Kifungu cha 2(b), Sheria ya Mikataba, Sura 149, ya mwaka 1917. 27
Ibid kifungu cha 2(e). 28
Ibid kifungu cha 2(h).
39
3.3.3 Kuchunguza tatizo lililopelekea Jenereta hilo kutofanya kazi kwa takriban zaidi ya
mwaka toka linunuliwe:
Kamati imeelezwa kwamba baada ya jenereta hilo kuwasili katika uwanja wa ndege halijawahi
kufungwa (installation) na hii inatokana na ukweli kwamba, gharama za ufungwaji
hazikuhusishwa katika mkataba wa ununuzi. Suala la kujiuliza, je tatizo hili halikuonekana
mapema wakati wa ufuatiliaji na uagizaji wa genereta na kama ni ndio, ni nani mwenye
kuwajibika katika suala hili? Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo iliyopelekwa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano, tarehe 16/06/2010, kumbu kumbu namba MFEA/PS/D.50/1/02/ VOL III/13
(Kiamtanisho Namba 24), amekiri kwamba Wizara yake imefanya malipo ya ununuzi wa
jenereta kwa kuzingatia „pro-forma invoice‟ ambayo haikuhusisha gharama za „installation‟.
Hivyo, Wizara yake kwa kutumia barua hii inampa tahadhari (Angalizo) Katibu Mkuu, Wizara
ya Miundombinu na Mawasiliano na kumtaka atayarishe vifaa vinavyohitajika katika ufungaji
wake, mara tu litakapofika Zanzibar na hatimae liweze kufanyiwa majaribio.
Pamoja na ushauri huu uliotolewa, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano haikuweza
kutayarisha vifaa hivyo, na matokeo yake hadi leo „installation‟ haikufanyika. Hata hivyo, siku
20 baada ya jenereta hilo kuwasili, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya
Maendeleo alimuandikia tena barua Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
yenye kumbu kumbu namba MFEA/PS/D.50/1/02 VOL III/42 (Kielelezo Na.25) kumkumbushia
kumalizika kwa muda wa dhamana (Warranty) ambao ni miezi 12 kama ilivyoelezwa katika
kifungu cha 15.2 cha Mkataba wa Ununuzi wa Jenereta, huku jenereta likiwa bado halijafungwa
na kujaribiwa. Hali hii iliifanya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kuliandikia Shirika la Umeme
barua ya tarehe 29/10/2010 yenye kumbu kumbu namba DA/E/003/2 VOL III, (Kielelezo
Na.26), kutaka ushauri na ikiwezekana kazi hiyo ingefanywa na Shirika hilo, ingawaje Shirika
halikuona busara ya kufanya kazi hii na badala yake likashauri ifanywe na Kampuni iliyolileta na
wao wasimamie na kuangalia (consultation) kwa kadiri kazi itakavyokuwa inaendelea (Kielelezo
Na.27)
Kwa maana hii, mbali na kutohusika kwa fedha za „installation‟ katika mkataba wa ununuzi,
lakini pia kukosekana kwa wataalamu wazalendo wa kufanya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na
gharama kubwa za ufungaji wake zimedhoofisha juhudi za kufungwa na kujaribiwa ama
kutumika kwa jenereta hilo. Mbali na hali hii, tatizo kubwa lililogunduliwa na Kamati kwamba,
kazi hii sasa imekuwa ni mzigo mzito kwa Wizara zote mbili na kila mmoja akimsukumia
mwenzake na kujitakasa yeye peke yake. Kwa mfano, ukiangalia barua ya Mkurugenzi, Idara ya
Anga(kama ilivyokuwa) ya tarehe 26/11/2010 yenye kumbu kumbu namba DA/SF/001/19,
aliyoiandika kwa Katibu wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,
ameilaumu Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kwamba imetayarisha
Mkataba wa ununuzi wa Jenereta bila ya kuzingatia Ufungaji na Uunganishaji (Installation and
Commissioning) na matokeo yake ni kuilazimisha Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kutafuta
Kampuni ya kufanya kazi hiyo (Kielelezo Na.28).
Kwa upande wa Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo nao wanaona suala la
„installation‟ lingestahiki kufanywa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na zaidi kwa
kuzingatia barua mbali mbali walizowahi kuwaandikia (Rejea Kielelezo Na.25) inahusiana na
suala la „installation‟ lifanywe na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Kwa mantiki hii,
40
tatizo la kutofungwa na kujaribiwa kwa jenereta hilo litaendelea kwa maana, Ofisi ya Rais,
Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo haiko tayari kutoa Tsh. 71,446,320/- zilizokisiwa
kwamba zingelitosha kwa kazi hiyo iwapo ingefanywa na Kampuni ya Uwekezaji ya
Mpomabiva, ambayo pia ndio iliyohusika na „supply‟ ya jenereta hilo. Hii ina maana, baada ya
kuona kimya kirefu, Kampuni ya Mpomabiva ilimuandikia barua Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo iliyoingia nae Mkataba wakihimiza kuitwa kuja
kufanya „installation‟ pamoja na kulipwa ailimia yao 10 (10%) kama walivyokubaliana katika
Mkataba huku wakisisitiza kwamba muda wa majaribio (Warranty period) inakaribia kumalizika
(Kielelezo Na.29)
3.3.4 Kitendo cha kutofungwa na kujaribiwa kwa jenereta hilo, kuna athari gani kwa
Serikali?
Ni vyema ikafahamika wazi kwamba, kifungu cha 15.2 cha Mkataba wa Uagizaji wa Jenereta
unaeleza wazi kwamba, muda wa „warranty‟ ni miezi 12 tokea jenereta hilo lifike uwanja wa
Ndege, kwa maana kwa kuwa limefika tarehe 01/09/2010 „warranty‟ ya miezi 12 bila ya shaka
ingemalizika 01/09/2011. Na hivyo, „supplier‟ hatokuwajibika kwa lolote iwapo jenereta hilo
litashindwa kufanya kazi na kwa hali hii, Serikali ndio itakayokuwa imekula hasara na kupoteza
zaidi ya 300,000,000/-. Aidha, lengo lililokudiwa la kuwepo kwa „stadby‟ jenereta lenye uwezo
mkubwa na uhakika wa matumizi kwa lengo la kuondosha tatizo la kuzimika kwa umeme katika
Uwanja wa Ndege halikufikiwa kutokana na ukweli kwamba, genereta hilo halifanyi kazi.
3.3.5 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii ndogo, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
3.3.5.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Uzembe wa makusudi umejitokeza katika ununuzi wa Jenereta hilo:
Kamati imegundua na kujiridhisha kwamba, kumefanyika uzembe wa makusudi na
Wizara zote mbili zimehusika katika uzembe huo, yaani Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi
na Mipango ya Maendeleo na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, na matokeo
yake zaidi ya Tsh. 300,000,000/- zinaelekea kupotea huku jenereta limenunuliwa na
kushindwa kujaribiwa kwa kipindi chote cha muda wake wa majaribio. Aidha, kitendo
cha jenereta kukaa bila ya matumizi ya muda mrefu pia ni sehemu ya uharibifu wake.
Kwa mantiki hii, Kamati inafahamu kwamba, jenereta hilo limetelekezwa.
(ii) Kukiukwa kwa taratibu za Sheria ya Manunuzi na Ugavi wa Mali za Serikali.
Kamati imejiridhisha kwamba, ununuzi wa jenereta hilo haujafuata taratibu za Sheria
Namba 9 ya mwaka 2005 inayohusiana na ununuzi wa mali za Serikali.
(iii) Utata wa ununuzi wa vifaa baina ya Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya
Maendeleo na Wizara ama Taasisi nyengine za Serikali.
41
Kamati imegundua kuwepo kwa utata mkubwa katika ununuzi wa mali za Serikali
unaofanywa kwa mashirikiano baina ya Wizara ama Taasisi za Serikali na Mnunuzi
Mkuu akawa ni Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo. Hali hii
hupelekea kutokuwepo kwa mashirikiano ya karibu na kila taasisi ikikwepa lawama
pale ununuzi huo unaposhindwa kufikia lengo.
(iv) Matumizi ya Sheria za nje katika masuala ya Ununuzi wa Mali za Serikali.
Kamati imegundua kwamba, Taasisi za Serikali zinafanya manunuzi ya mali za Serikali
kwa kutumia sheria zisizo za Zanzibar hali ambayo hupelekea utata wa kisheria.
(v) Kamati imebaini kwamba, hali inayoendelea sasa ya kutokufanya kazi kwa
standby jenereta la uhakika ambalo limenunuliwa kwa kazi hiyo katika Kiwanja
chetu cha Ndege ni hatari zaidi kwa usalama wa kiwanja chetu na Mashirika ya
Ndege za ndani na za Kimataifa. Hali hii pia haitoi picha nzuri ya haiba ya
Uwanja huo.
(vi) Matumizi mabaya ya fedha za Serikali zinazotokana na Msamaha wa Madeni.
Kamati imegundua kwamba fedha zinazotoka kupitia msamaha wa madeni huwa
zinatumika bila ya uangalifu wowote. Kitu ambacho huleta picha mbaya kwa nchi
changa kama hii kupata msahama wa madeni lakini fedha hizo zikatumika bila ya
uchungu wowote na kujali.
3.3.5.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo tuliouonesha kapo juu, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo
zichukuliwe:
(i) Hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa watendaji wote waliohusika na uzembe wa
ununuzi wa jenereta hilo, huku msisitizo ukiwekwa kwa Makatibu Wakuu wa
Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano; Mkurugenzi na Meneja wa Mamlaka ya Uwanja
wa Ndege.
(ii) Ili kuondosha matatizo kama haya, Kamati inapendekeza matumizi ya fedha kama
hizi yabakie katika Wizara moja tu ambayo ndio yenye mahitaji na inayojua
upatikanaji wake.
(iii) Kamati inapendekeza ndani ya mwezi mmoja baada tu ya kutoka ripoti hii,
Jenereta hilo lifanyiwe „installation‟ ili liweze kujuulikana uzima ama ubovu
wake, na kama litakuwa bovu, Kamati inaendelea kusisitiza kwamba hatua za
kurejeshwa kwa fedha hizo ziwe dhidi ya Makatibu Wakuu wa Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo.
42
3.4 KUCHUNGUZA MIKATABA YA UKODISHWAJI WA SEHEMU ZA
BIASHARA KWENYE ENEO LA UWANJA WA NDEGE:
Sehemu ya tatu ya Hadidu hii rejea inahusiana na ukodishwaji wa maeneo ya Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanzibar ambapo Kamati imetumwa kuangalia Mikataba
ya ukodishwaji wake. Hivyo basi, jambo la mwanzo ambalo Kamati imelihoji kuhusiana na
ukodishwaji wa sehemu za biashara katika uwanja huo kujua idadi halisi ya waliokodishwa,
ambapo Kamati ilipatiwa orodha ya wafanya biashara wote jumla ya Taasisi 40, orodha ambayo
inaonesha jina la Mkodishwaji, Madhumuni ya kukodishwa, ukubwa wa eneo alilokodishwa,
muda wa Mkataba, na fedha anazolipa kodi (Kielelezo Na.30). Hata hivyo, wakati Kamati
inatembelea maeneo hayo, imegundua kuwepo Taasisi 8 za ziada ambazo haziorodheshwa katika
orodha hiyo iliwasilishwa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na hivyo pamoja na taasisi
zilizoorodheshwa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na hizo Kamati ilizogundua zinafanya
jumla ya Taasisi 48 zilizokodishwa. Taasisi hizo 8 za ziada ni IZMIR ambae anafanya biashara
ya Dula la Dawa (Pharmacy); Zanzibar Data Com, inayofanya biashara ya huduma za „Bank‟;
Arrival Bureau De Change, anaetoa huduma ya Duka na „Internet‟; As Salaam Air, inayotoa
huduma za office; Direct Maintenance, inayotoa huduma za office; Airport Telephone Buro,
huduma ya office; Ethiopian Air Line, huduma ya Office na Fly 540.Com, huduma ya office.
Kabla ya kuchunguza taasisi moja moja, ni vyema tukafahamu baadhi ya masharti ya jumla
kuhusu mikataba ya biashara husika. Kwanza ifahamike wazi kwamba, mikataba yote
iliyokabidhiwa kwa Kamati imefungwa na Serikali kwa kuwakilishwa na iliyokuwa Idara ya
Anga. Aidha, mikataba yote hiyo imetiwa saini na Manager wa Uwanja wa Ndege Ndg. Badru
Amani Juma, kwa niaba ya Mkurugenzi (Hata hivyo, mingi kati ya Mikataba hii imetiwa saini na
Meneja huyu bila ya kutambulisha kutia kwa niaba ya Mkurugenzi, hali ambayo kisheria inatia
shaka ya uhalali wa Mikataba husika) na kushuhudiwa na Maofisa wengine mbali mbali wa
Idara, ikiwa ni pamoja na Ofisa Uendeshaji, Ofisa Biashara na Mhasibu wa Idara. Aidha, ipo
baadhi yao imesainiwa na Mkurugenzi mwenyewe pia ipo iliyosainiwa na Mhasibu wa Idara
kwa niaba yake. Suala hili linaleta utata mkubwa zaidi wa kisheria kwa sababu wakati huo Idara
ya Anga ilikuwa ni miongoni mwa Taasisi za Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ambapo suala
zima la Mikataba lilipaswa lishughulikiwe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi na sio Meneja wa Uwanja wa Ndege. Kuhusu wakati wa kisheria, mikataba mingi kati
ya iliyokabidhiwa kwa Kamati tayari imeshapitwa na wakati na hivyo, haina athari yoyote
kisheria wakati Kamati ilipewa taarifa zisizo za kweli kuhusu kufanya kazi kwa mikataba hiyo
(Rejea Kielelezo Na.30).
Kwa ujumla, mikataba hii imekusanya masharti mawili, masharti maalum (specific provisions)
na masharti ya jumla (general provisions) ambapo kisheria yote haya ni sehemu ya mkataba na
hivyo yana athari sawa katika utekelezaji na usimamizi wake. Hata hivyo, kwa mujibu wa
mikataba hii, ikitokezea masharti haya kugongana, masharti ya maalum yatakuwa na nguvu dhidi
ya masharti ya jumla. Kuhusu malipo yamegawika katika sehemu mbili, gharama za kodi (rent)
inayolipwa kupitia Dola za Kimarekani (US $) ambazo pia hulipwa kwa Cheki (Crossed
Cheques) na gharama nyengine ni za uendeshaji ikiwa ni huduma ya umeme na maji (Utility
costs) zinazolipwa kwa fedha za Kitanzania kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano au kwa kutumia regista kwa Meneja wa Uwanja wa ndege. Vile vile, Mkodishwaji
yoyote haruhusiwi kuuza, kuruhusu mtu mwengine kutumia sehemu aliyokodi wala kukodisha
43
kwa mtu mwengine bila ya kupata ridhaa ya maandishi kutoka kwa Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege.
Baada ya maelezo haya, zifuatazo ni Kampuni na Taasisi mbali mbali zilizobarikiwa sehemu ya
biashara katika maeneo ya Uwanja wa Ndege, isipokuwa ifahamike kwamba kwa mikataba
mingi iliyohusika, tumeangalia zaidi maeneo muhimu ya Mikataba hiyo, ikiwa ni pamoja na
Wahusika wa Mkataba, Muda wa Mkataba, Malipo yaliyokubaliwa katika Mkataba na kwa
baadhi ya Mikataba, tuliangalia kusainiwa kwa mikataba hiyo. Hata hivyo, kwa kuwa Mikataba
yote hii tumeifanya kuwa vielelezo kwa ukamilifu wake, Msomaji atapata fursa nzuri ya
kufahamu kwa kina masharti yaliyokubaliwa katika Mikataba hii.
3.4.1 Zanzibar Aviation Services & Travel Trade Ltd (ZAT):
Kabla ya kueleza kidogo kuhusiana na Mkataba huu, ifahamike kwamba, Kampuni hii imeingia
katika Mikataba mitatu tofauti. Mikataba miwili kati ya hiyo, tutaieleza kwa mnasaba wa orodha
iliyokabidhiwa Kamati (Rejea Kielelezo Na.30) na Mkataba mmoja tutaueleza baada ya
kumaliza kueleza Mikataba hii miwili. Hivyo basi kwa kuanzia na huu Mkataba wa awali,
Kampuni hii imeingia katika Mkataba na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa ajili ya shughuli
za Ofisi na stoo (office and store). Mkataba wa ukodishwaji wa Office na Stoo,
wameyokodishwa kwa jumla ya Square metre 193.81 kwa thamani ya USD 16,920.65 kwa
mwaka, sawa na Tsh. 27,073,040/- (Dola 1 ni sawa na Tsh.1600). ZAT wameweka ofisi 5 katika
square metre walizopewa na kwa maana hii, kila ofisi moja ina lipiwa USD 3,384.13 kwa mwaka
ambazo ni sawa na Tsh. 5,414,600/- (Kielelezo Na.31)
3.4.1.1 Baadhi ya mambo muhimu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Mkataba huu:
Pamoja na ukweli wa kuwepo mikataba hii, moja kati ya matatizo ni kukiukwa katika utekelezaji
wake. Kamati imefuatilia suala hili kwa njia ya mahojiano na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege,
kutembelea maeneo yaliyokodishwa kwa ZAT pamoja na kukutana uongozi wa ZAT ili kupata
ufafanuzi wa masuala mbali mbali. Kwa maana hiyo, Kamati imechunguza na kugundua mambo
yafuatayo:
3.4.1.2 Muda wa Mkataba:
Kwa mnasaba wa kipengele cha 2.1 cha Mkataba, uhalali wa kuwepo kwa mkataba huu ni miezi
12 tu, kuanzia tarehe 1/1/2010 hadi 31/12/2010. Kwa maana hii, kwa mwaka wa 2011/2012 ZAT
inatumia huduma ya ofisi ilizopewa bila ya Mkataba wowote. Kamati ilipolihoji suala hili mbele
ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, tarehe 07/09/2011 ilipewa taarifa zisizo za kweli kwamba
mkataba wa ZAT na Mamlaka ni kuanzia 1/1/2011 hadi 1/12/2011(Rejea Kielelezo Na.30).
Hata hivyo, Kamati ilipokutana na Uongozi wa ZAT, tarehe 07/12/2011 ulieleza kwamba
mkataba wao na Serikali (kwa maana ya Mamlaka ya Uwanja wa ndege) ni miaka 30, kuanzia
1995 hadi 2025. Pamoja na majibu haya, Kamati haikupatiwa mkataba wowote wa miaka 30
kutoka Mamlaka ya Uwanja wa Ndege ingawaje imepatiwa Mkataba huo na Uongozi wa ZAT
ambao ndio tulioukusudia tuuzungumze Namba 3. Hata hivyo, hapa tutanabahishe kwamba,
Mkataba huo wa miaka 30 hauhusiani na kodi ya Ofisi hizi ambazo ndio Mkataba wake huu
tuliyokwisha ueleza uliomaliza muda wake tarahe 31/12/2010. (Rejea Kielelezo Na.31).
44
3.4.1.3 Malipo ya Ukodishwaji:
Kwa mujibu wa kipengele cha 6.1 cha Mkataba, ZAT wanalazimika kulipa gharama za namna
mbili. Gharama za kodi ya eneo lao la biashara lenye ukubwa wa Square metre 193.81, ambazo
ni USD 16,921.65 zenye thamani ya Tsh. 27,074,640 (kwa kiwango cha Dola 1 x 1600) kwa
mwaka. Kamati ilihoji malipo hayo namna yanavyoingia Serikalini, ambapo Uongozi wa ZAT
ulithibitisha kwamba wao wanalipa kila mwaka na kupatiwa risiti. Kamati ilihouhoji Uongozi wa
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, iwapo kwa mwaka 2010 kama ZAT walilipa kodi,
ilithibitishiwa kupitia Risiti Namba 224759, na hivyo, Kamati imejiridhisha kwamba wanalipa
Kodi.
Kwa malipo wanayoyafanya, ZAT wanalipa jumla za USD 16921.65 kwa kodi ya mwaka ikiwa
USD 5,695.5 ni kodi ya ofisi na USD 11,226.15 hulipwa kwa kodi ya eneo la Stoo kwa kila
mwaka na hivyo, ZAT wanalipa USD 16921.65 kwa kodi ya Ofisi pamoja na Stoo. Kwa
mnasaba wa malipo ya ukodishwaji, Kamati imehoji kuhusu malipo ya gharama za huduma za
umeme na maji (Utility Costs) ambazo kwa mujibu wa kifungu cha 6.3 cha Mkataba, malipo ya
Tsh. 150,000/- yalipaswa yalipwe na ZAT ambayo kwa kawaida hulipwa kupitia Katibu Mkuu,
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Kamati ilipouhoji Uongozi wa ZAT kuhusu malipo ya
gharama za hizi, Uongozi wa ZAT ulisema unalipia gharama za „Utility‟ pamoja na Kodi kama
ambavyo vielelezo vyake vinavyoonekana katika (Kielelezo Na.32).
Vile vile Kamati imegundua kukiukwa kwa kifungu cha 6.4 cha Mkataba kinachoutaka Uongozi
wa ZAT kulipa kodi ya pango mwanzo wa mwaka kwa maana nyengine, kwa kuwa mkataba
wao unaanzia mwezi wa January, basi kabla ya kutumia eneo lote walilokodishwa, walipaswa
walipe kwanza (payment in advance) tofauti na uhalisia kwamba wao wanalipia mwisho wa
mwaka.
3.4.2 Zanzibar Aviation Services & Travel Trade LTD (ZAT) :
Maktaba wa pili wa ZAT ni huu unaohusiana na Karakara (Workshop) (Kielelezo Na.33),
Kampuni hii imeingia Mkataba wa eneo lenye Square metre 307.37 kwa ajili ya kazi hiyo,
kuanzia tarehe 1/1/2010 hadi 31/12/2010 kwa thamani ya USD 29,200.15 kwa mwaka. Hata
hivyo, baada ya Kamati kukabidhiwa Mkataba unaohusiana na ukodishwaji huo, kuna mambo
yafuatayo ni vyema tukayarejea kuyaeleza :
3.4.2.1 Muda wa Mkataba :
Mkataba huu tayari umeshapitwa na wakati na hauna nguvu ya utekelezaji wowote kisheria. Kwa
mujibu wa kifungu cha 2.1 cha Mkataba (Rejea Kielelezo Na.33), haki na fursa za pande zote
mbili katika mkataba huo ni kuanzia tarehe 1/1/2010 na kumaliza tarehe 31/12/2010 na kwa
maana hii, Mkataba huu hauna nguvu yoyote kisheria na ni sawa kusema kwamba, kuanzia
mwezi wa January 2011 hadi leo, ZAT wanaendelea kutumia eneo lote hilo bila ya Mkataba
wowote na ni sawa kutumia eneo hilo bila ya uhalali wowote kisheria na kwa hali hii iwapo
litatokezea tatizo lolote lililo kinyume na Mkataba wa awali, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
itakuwa katika wakati mgumu sana kuthibitisha dhima (Liability) dhidi ya ZAT.
Aidha, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege haikutoa taarifa za kweli kuhusiana na hali hii (Rejea
Kielelezo Na.30), na walichofanya ni kuidanganya Kamati kwa kuieleza na kuipa taarifa
kwamba Mkataba huu unamalizika tarehe 31/12/2011, taarifa ambayo inapingana na Mkataba
45
husika. Aidha, kwa mujibu wa kifungu tulichokitaja hapo juu cha Mkataba husika, kifungu cha
2.1, Mkataba huo umeshapitwa na wakati na hauna uhai kisheria, na kwa hali hii, unaifanya
Kamati kutokuwa na ulazima wa kuchunguza zaidi Mkataba ambao kwa sasa haupo. Kwa maana
hii, vipengele kwa mfano, kifungu cha 2.2 cha Makataba kinachoelekeza ZAT kuanza kutumia
eneo walilokodishwa si zaidi ya siku 30 baada ya Mkataba huo kutiwa saini, ama malekezo ya
namna gani ZAT itatekeleza wajibu wake juu ya mambo ya ujumla yaliyoekewa masharti katika
Mkataba huu, yote hayana ulazima wa kudajiliwa kwa kutegemea Mkataba uliopitwa na wakati
na kukosa nguvu kisheria.
3.4.2.2 Malipo yanayolipwa na ZAT kuhusiana na Mkataba huo:
Uongozi wa ZAT ulilazimika kulipa kodi ya USD 29,200.15 kwa mwaka. Na kwa bahati nzuri
wanalipa kodi na hata Kamati ilipotaka kuridhishwa kwa mwaka wa 2010, ilithibitishiwa
kwamba walikwisha lipa kwa risiti namba 343399 na 224790. Hata hivyo, Kamati ilielezwa
kwamba malipo hayo yanafanyika mwisho wa kila mwaka na kwa wakati Kamati tofauti na
maelekezo ya Mkataba yanayotaka malipo hayo yalipwe mwanzo kabla ya Mkodishwaji kutumia
eneo alilokodi (Kifungu cha 6.4 cha Mkataba) .Aidha, kuhusua malipo ya gharama za umeme na
maji, Uongozi wa ZAT unalazimika kulipa Tsh. 150,000/- kwa kila mwezi kama masharti haya
yalivyoelezwa katika kifungu cha 6.3 cha Mkataba husika, ambapo Kamati imethibitishiwa
kwamba malipo hayo yamefanyika.
3.4.3 Mkataba wa Miaka 30 wa Zanzibar Aviation Services & Travel Trade LTD (ZAT) :
Mnamo tarehe 29/12/1995, Kampuni hii imeingia Mkataba na Serikali, kwa maana iliyokuwa
Wizara ya Fedha wa kuirihusu kuendesha shuguli za kutoa huduma mbali mbali za „Handling‟ na
zinazohusiana kwa masharti ya Mkataba husika (Kielelezo Na.34). Tunapenda tuuzungumze
Mkataba huu kwa sababu kuna fikira nyingi kwamba, ZAT hawapo kwa mujibu wa Mkataba
ama kwamba kuzungumzia Mikataba yao miwili ya hapo juu ambayo ishapitwa na wakati
ikafahamika kwamba Kamati haikuwatendea haki. Ni vyema basi tukapata ufafanuzi wa
Mkataba huu kama inavyofuata :
3.4.3.1 Muda wa Mkataba :
Mkataba huu ni wa miaka 30 kama tulivyokwisha eleza hapo awali, uliofungwa tarehe
29/12/1995 na unatarajia kumalizika mwaka 2025. Kwa lugha hii, Mkataba huu bado ni hai na
una guvu zote za kisheria, tofauti na Mikataba ya awali.
3.4.3.2 Matumizi ya Sehemu iliyokodishwa :
Dhamira ya ukodishwaji imeelezwa katika kifungu cha iii, cha Mkataba kwamba ZAT
wamekodishwa kufanya biashara ya utoaji wa huduma ya „handling‟ kama ni wakala peke yake
katika utoaji wa huduma hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar ndani ya miaka 30 na
ukimaliza muda huo, anaweza kuingia tena katika mkataba kwa makubaliano na Serikali. Mbali
na utoaji wa huduma za „handling‟ ikiwa ni pamoja na ubebaji wa mizigo ya abiria baada ya
kufanyiwa uchunguzi wa kiusalama hadi kwenye ndege na kutoka kwenye ndege hadi sehemu ya
kupokelea mizigo, pia wana uwezo wa kuuza tiketi na kuwatayarishia „bill‟ ya malipo
zinazohusiana na hati mbali mbali za kusafiria ; kupata sehemu ya kuhifadhi vifaaa
vinavyotumika katika ndege, yaani store na mambo mengine yaliyotajwa katika kifungu hiki.
46
Kwa ujumla, kwa mujibu wa Mkataba huu, ZAT wamepewa madaraka makubwa ya utoaji wa
huduma mbali mbali zinazohusiana na usafiri wa abiria katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Pengine ndio maana Mamlaka ya Uwanja wa Ndege pamoja na kwamba ZAT wameingia
Mkataba wa miaka 30 na Serikali na wanalipia gharama za malipo kama ilivyotakiwa katika
Mkataba huo, nao Mamlaka pia wakaingia Mkataba huu huu (Rejea Kielelezo Na.31) wa
huduma za aina moja, kwa mfano katika kifungu cha 1.2 cha Mkataba huo kuna maneno ambayo
tunayanukuu:
"In conducting its business here under, the Lessee covenants and agrees to confine its activities to
operating GROUND HANDLING only within the purview of its contract……”
Maelezo haya kwa kiasi kikubwa yanaingiliana na maelezo ya huu Mkataba wa miaka 30 na kwa
kiasi hiki ndio maana unaweza ukafahamu kwamba, Mikataba miwili inayolingana dhamira yake
imefungwa kwa Kampuni moja. Hata hivyo, suala hili lilipoulizwa kwa Uongozi wa ZAT
walisema kwamba wametakiwa walipe na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa kila mwaka na
ndio maana ikaja haja ya kuingia tena Mkataba na Mamlaka.
3.4.3.3 Malipo ya Ukodishwaji :
Kwa mujibu wa kifungu cha vi, cha Mkataba husika, ZAT wameanza kuilipa Serikali baada ya
kumalizika miaka miwili tokea kuingia Mkataba huo, yaani kuanzia April, 1997 na kwamba
malipo hayo ni kuanzia asilimia 3 (3%) ya faida inayopatikana baada ya kutoa huduma zaote za
uendeshaji ambapo baada ya miaka mitatu ndio Serikali imeruhusiwa kuongeza kwa asilimia 5
(5%) ndani ya miaka hii 30 ya ukodishwaji, lakini malipo hayo yatalipwa baina ya April na
March (from April to March) ya kila mwaka. Tunapenda tukumbushie tu kwamba, neno „from
April to March‟ lina maana nyingi lakini zaidi, ndani ya miezi 12 malipo hayo yanaweza
kufanyika, yaani ndani ya mwezi wowote kuanzia April to March. Kwa mnasaba huu, hata kama
tutawataka ZAT walipe mwanzo wa mwaka kama tulivyowataka walipe katika Mikataba miwili
iliyotngulia, katika Mkataba huu hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu wana kinga kumbwa ya
kulipa takriban ndani ya miezi 12 ambayo ndio mwaka mzima.
3.4.3.4 Ulipaji wa Kodi unaofanywa na ZAT:
Hoja hii haimo katika Mkataba ambao tumemaliza kuuzungumzia hapo juu, lakini Kamati
imeliuliza suala hili ilipokutana na Uongozi wa Kampuni hii ili kujiridhisha katika uwezo wao
wa kuendelea kutoa huduma hizo katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar. Kamati imeliuliza suala
hili, kwa sababu kuna tetesi kwamba baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano na Mamlaka ya Uwanja wa ndege wanafikiria kwamba, ZAT hawangefaa
kuendelea na huduma hizo na badala yake itafutwe Kampuni ya Nje kufanya kazi. kwa bahati
mbaya sana Kamati haina ulazima wa kutoa maamuzi ya suala hili, lakini kwa mnasaba wa
Mkataba iliyoichunguza, imeona ni vyema pia ipate taarifa kidogo hususiana na vipi Kamapuni
hii inalipa kodi kama inavyotakiwa ama vyenginevyo.
Tunachotaka kuleleza hapa ni kwamba, Kampuni ya ZAT inalipa vizuri kodi zake kwa mfano
takriban miaka mitatu nyuma, Kampuni hii imelipa ipasavyo kama inavyoonekana katika
Kielelezo Na.35, kinachoonesha kwamba wamelipa takriban ndani ya mwaka mzima. Vile vile
katika kuthibitisha malipo yao na ufanisi katika masuala ya kodi ya Mapato, Uongozi wa ZAT
47
umeihakikishia Kamati kwamba, wamepata zawadi ya ulipaji bora wa Kodi kwa mwaka 2007,
2008 na 2011 (Kielelezo Na.36).
3.4.4 Precision Air Ltd.
Kielelezo Na.tatu katika Orodha iliyowasilishwa kwa Kamati ni huu wa Kampuni ya Precision
Air Ltd ambayo imekodi ofisi kwa ajili ya kutoa huduma za „Air line‟ yenye ukubwa wa „square
meter‟ 9.25 kwa thamani ya USD 693 sawa na Tsh 1,108,800/- kwa mwaka (kwa kiwango cha
1600 kwa Dola moja), hii ina maana, kila square meter moja wanalipa USD 75 ambayo ni sawa
na Tsh. 120,000/-. Kwa ujumla, mambo yafuatayo ni vyema tukayaangalia:
3.4.4.1 Muda wa Mkataba:
Katika orodha ya Wapangaji iliyokabidhiwa kwa Kamati kutoka katika Uongozi wa Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege, Mkataba wa Precision Air Ltd unaanzia tarehe 1/1/2011 na kumalizia tarehe
31/12/2011. Hata hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha 2.1 cha Mkataba huo, muda wa uhai wake
ni kuanzia tarehe 1/1/2010 hadi Disemba 31 ya mwaka 2010. (Kielelezo Na.37) kwa maana hii,
Mkata huu umepitwa na muda kisheria.
3.4.4.2 Malipo kuhusiana na Kodi na Matumizi ya Huduma za Umeme na Maji:
Kama tulivyokwisha eleza awali kwamba, malipo ya kodi ya ofisi iliyokodiwa na Precision Air
Co. Ltd yenye ukubwa wa Square meter 9.25 ni sawa na USD 693. 75 ambayo ni sawa na Tsh.
1,108,800/- kwa mwaka. Kamati ilihoji vipi kodi ya Mkataba huu inalipwa na kutaka
kuthibitishiwa wa mwaka wa 2010, ambapo ilithibitisha kwamba, Precision Air wamelipa fedha
hizo
Aidha, kuhusu malipo ya gharama za huduma ya maji na Umeme (Utility), Precision Air Co. Ltd
hawalipi kwa kueleza kwamba wao hawatumii huduma hizo kwa gharama za Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege bali walitumia gharama zao wenyewe kuunga maji na pia kutia TUKUZA.
Vile vile kifungu cha 6.8 cha Mkataba kinaelekeza kwamba kodi ya Mkataba huo ifanyiwe
marekebisho kila baada ya mwaka mmoja. Hata hivyo, kifungu hiki hakitekelezwi kwani
Precision Air Co. Ltd wanaendelea kulipia kiwango hicho hicho cha kodi kwa takriban miaka
zaidi ya mitano sasa. Na kwa maana hii, takriban wakodishwaji wote wanalipia kodi katika
mwisho wa mwaka ama muda wanaoutaka wao, kinyume na maelekezo ya Mikataba walioingia
na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, ambapo kifungu cha 6.4 cha takriban kila Mkataba
kinawataka walipe walipe mara tu baana ya Mkataba kutiwa saini, yaani tarehe ya awali ya
kufungwa kwa mkataba wenyewe ambapo mikataba mingi kati ya hii iliyowasilishwa kwa
Kamati inaanza mwanzo wa mwaka. Hali hii inaashiria wazi kwamba, Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege imeshidwa kuwasimamia ipasavyo wakodishwaji hao, pia imeshidwa kusimamia
maelekezo ya kifungu cha 6.7 cha Mikataba hiyo kinachoelekeza athari za kukawilisha ama
kutolipa kodi na gharama za huduma zilizoainishwa katika Mkataba.
3.4.4.3 Usahihi wa Saini ya Mkodishwaji:
Katika Mkataba huu, kwa upande wa Mkodishwaji yaani Precision Air Co. Ltd, umetiwa saini na
Ndg. Bertha M. Minja, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimaliwatu na Utawala (Head of Human
Resource and Administration) na wala haukutiwa saini na Meneja Mkuu wa Kampuni hii. Jambo
tunalotaka lifahamike wazi hapa ni kwamba, Mkataba huu umeingiwa baina ya Idara ya Serikali
48
ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwakilishwa na Idara ya Anga, kwa niaba ya Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi kama Mkodishaji na Precision Air Co. Ltd akiwa Mkodishwaji. Kwa
maana hii, Precision Air Co. Ltd ni Kampuni iliyosajiliwa Dar es Salaam ama Arusha lakini sio
Zanzibar. Hapa kuna mambo mawili yanayopaswa yazingatiwe vizuri. Suala la kwanza ni nani
katika Kampuni kama sio Meneja Mkuu wa Kampuni husika mwenye mamlaka ya Kisheria wa
kutia saini.
Kwa mtazamao wa Sheria zinazohusiana na Makampuni, Mkataba huu ulipaswa utiwe saini na
Meneja Mkuu kwani yeye ndie mwenye mamlaka ya kisheria kutia saini Mkataba huo kwa niaba
ya Kampuni yake na sio Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu na Utawala. Suala la pili la
msingi ni kuangalia utaratibu wa kusainiwa kwa Mkataba huu. Kama tulivyokwisha eleza hapo
awali kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 2.1 cha Mkataba huu, uhalali wa mkataba ulikuwa
kuanzia tarehe 1/1/2010 hadi tarehe 31/12/2010, lakini jambo la kushangaza ni kwamba mkataba
huo umetiwa saini na upande wa Mkodishaji tarehe 25/02/2010, mwezi mmoja baada ya tarehe
iliyokubaliwa kuanza kutumika kwa Mkataba, na baada ya mwezi mmoja mwengine yaani tarehe
24/03/2010 ndio umesainiwa na upande wa Mkodishwaji (Precision Air Co. Ltd) , miezi mine
baadae yaani tarehe 6/07/2010 ndio umetiwa saini na shahidi wa Mkodishwaji, Ndg. Elias
Mwashivya. Kwa maana hii, takriban zaidi ya miezi 6 Mkataba huu ulikuwa haujakamilika na
uko mikononi mwa Mkodishwaji. Na kwa hali hii pia ilijitokeza wakati wa kazi za Kamati
ambapo ilipodai kupatiwa mikataba iliyo ndani na wakati, yaani ya mwaka 2011, haikuweza
kupatiwa zaidi ya maelezo yasiyo na uthibitisho kwamba mikataba ipo ila wamepewa
wakodishwaji nao bado hawajairejesha kwa Mamalaka ya Uwanja wa Ndege, kwa hali hii ni
wazi kwamba, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege ina mikataba isiyoweza kupatikana inapohitajika
na pia huwa ni sababu kuu ya mapato ya Serikali kupotea kiholela.
3.4.5 Galaxy Security Services Co. Ltd:
Kampuni hii imekodi nyumba inayomilikiwa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege iliyopo kando
kidogo ya uwanja wa Ndege Mkongwe unaotumiwa kwa safari za viongozi. Kampuni ya Galaxy
imekodishwa nyumba hiyo kwa ajili ya shughuli za ofisi kwa lengo la kuendesha biashara ya
utoaji huduma za ulinzi kwa wateja wao mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Uwanja
wa Ndege. Ukubwa wa nyumba hiyo ni square meter 30 na wanalipia USD 1,500 kwa mwaka,
sawa na Tsh. 2,400,000/- kwa mwaka na wanalazimika kulipa Tsh. 200,000 kwa mwezi kwa ajili
ya kulipia huduma za maji na umeme (Utility). Pamoja na maelezo haya, ni vyema pia
tukajikumbusha masuala yafuatayo:
3.4.5.1 Muda wa Mkataba:
Tofauti na mikataba mingi iliyopita, Nyumba hiyo imekodishwa kwa Galaxy Secutrity Services
Ltd kuanzia tarehe 1/09/2010 na kumalizia tarehe 31/8/2011. Hata hivyo, wakati Kamati
inafuatilia Hadidu hii, Mkataba huo tayari ulikuwa umeshapitwa na wakati na hivyo, hauna
athari yoyote kisheria. (Kielelezo Na.38).
3.4.5.2 Malipo ya Kodi na Huduma :
Galaxy Security Services Co. Ltd wanalipia kila square meter moja kwa USD 50 ambapo Square
30 wanalipia kwa USD 1500 kwa mwaka, ni sawa na Tsh 2,400,000/-. Hata hivyo, Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege haikuweza kuithibitishia Kamati vipi fedha hizi zinalipwa na vipi zinaingia
katika Mfuko Mkuu wa Serikali. Aidha, kwa mujibu wa Mkataba husika, fedha za kodi
49
zilitakiwa zilipwe kupitia Anuani ya KUKIMU VIWANJA VYA NDEGE-ZANZIBAR. Vile
vile katika kifungu cha 6.8 cha Mkataba huu, Kinaelekeza kwamba Mamlaka ifanye
marekebisho ya kodi hii kila baada ya miaka mitatu, jambo ambalo halifanyiki.
Kuhusu gharama za maji na umeme, Mkataba huu umempa Mamlaka makubwa Meneja wa
Uwanja wa Ndege kuamua ni kiasi gani kilipwe na Kampuni hii, yaani hakuna kima maalum
kilichoainishwa kulipwa kwa gharama hizi isipokuwa ni Meneja mwenyewe ndie atafanya
maamuzi ya kiwango kinachohitaji kulipwa.
3.4.6 Hilmy Bureau de Change:
Kwa Mkataba huu, Hilmy Bureau de Change, wamekodishwa kuendesha biashara kwa kutoa
huduma za Kibenki kwa kukodiswa square meter 4.44 na wanalipia kwa USD 399.60 kwa kila
mwaka. Katika Mkataba huu, ni vyema tukayapitia mambo yafuatayo:
3.4.6.1 Muda wa Mkataba.
Kifungu cha 2.1 cha Mkataba kinaelekeza uhalali wa Mkataba huu ni kuanzia tarehe 1/1/2010
hadi 31/12/2010 na kwa maana hii, Hakuna Mkataba mwengine ulioingiwa baina ya Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege na Hilmy Bureau de Change. Hivyo, Kamati haiwezi kuuzingatia Mkataba
ambao umeshapitwa na muda wake (Kielelezo Na.39). Kwa masikitiko makubwa Kamati
imepotoshwa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa kuiwasilishia taarifa isiyo sahihi kwamba,
Mamlaka imeingia Mkataba na Hilmy tarehe 1/1/2011 hadi tarehe 31/12/2011 taarifa ambayo sio
sahihi kwa mujibu wa Mkataba husika (Rejea Kiambatanisho 30). Aidha, Kamati ilihoji suala
hili mara kwa mara na kusisitiza kupatiwa usahihi wake, na muda wote huo ilijibiwa kwamba
Mkataba upo, lakini haikuweza kupatiwa Mkataba ulio ndani ya wakati.
3.4.6.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kama tulivyokwisha eleza awali, kwamba kwa mujibu wa Square meter 4.44 walizokodi, Hilmy
Bureau de Change wanalipa USD 399.60, sawa na Tsh. 639,360 kwa mwaka na ni sawa na
kulipa Tsh. 53,288 kwa mwezi. Kamati ilifanya uchunguzi wake kwa mwaka wa 2010 kuona
kama kweli fedha hizo zinalipwa na kufahamu kwa kupitia Risiti Namba 224244 fedha hizo
zimelipwa. Kuhusu Malipo ya gharama za umeme na maji ni Tsh. 100,000/- na inapaswa
kulipwa kwa kila mwezi, lakini kwa bahati mbaya Kamati haikupatiwa uthibitisho wa malipo
hayo.
3.4.7 Maha Tours :
Kwa mujibu wa maelezo ya Mkataba, Maha Tours wamekodishwa square meter 22.92 kwa ajili
ya kuendesha shughuli za matengenezo ya ndege (Aircraft Maintenance) kwa thamini ya USD
1,719 kwa kila mwaka ambapo kwa kila square meter moja wanailipia USD 75 kwa mwaka.
Katika Mkataba huu, Kamati imegundua masuala yafuatayo:
3.4.7.1 Muda wa Mkataba.
Mkataba huu umefungwa tarehe 01/01/2010 na kumalizika tarehe 30/06/2011 (Kielelezo Na.40)
na kwa wakati Kamati inaifanyia kazi hoja hii, Mkataba huu tayari umeshapitwa na wakati na
hivyo, hauna athari yoyote kisheria. Aidha, orodha ya wapangaji wa Uwanja wa Ndege
iliyowasilishwa kwa Kamati inaonesha kwamba, Mkataba huu umeanzia tarehe 1/1/2011 na
50
kumalizia tarehe 31/12/2011, taarifa ambazo zinapingana na maelekezo ya kifungu cha 2.1 cha
Mkataba husika.
3.4.7.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kama ilivyo kwa Mikataba mengine, Malipo ya Mkataba huu yamegawika katika sehemu mbili
kuu; Kodi ya eneo walilokodishwa, lenye ukubwa wa square meter 22.92 ambalo linalipiwa kwa
USD 1,719 kwa mwaka sawa na Tsh. 2,750,400. Kodi ambayo imethibitishwa kulipwa ndani ya
mwaka 2010 kupitia Risiti namba 343376. Kuhusu malipo ya gharama za maji, umeme na simu,
hazijuulikani ni kiasi gani zinalipwa kwa kila mwezi. Uwezo wa kuamua kima maalum cha
kulipwa upo kwa Meneja wa Uwanja wa Ndege ambae atabadilisha gharama husika muda hadi
muda. Hata hivyo, Kamati haikupata uthibitisho wa malipo hayo.
3.4.7.3 Muda wa Kusainiwa kwa Mkataba.
Pamoja na ukweli kwamba Mkataba huu umeanza kazi tarehe 1/1/2010, saini za upande wa
Mkodishaji (Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa niaba ya Serikali) imesainiwa tarehe 5/8/2010,
takriban miezi 8 baada ya tarehe ya Mkataba kuanza kazi. Aidha, kwa upande wa Mkodishwaji
(Maha Tours) wameusaini Mkataba huo miezi 2 baadae, yaani tarehe 11/10/2010 wakati ikibakia
miezi 2 tu Mkataba huu kumaliza muda wake kisheria. Vile vile kwa upande wa Mkodishwaji,
ambae ni Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, saini yake imetiwa na Mhasibu Mkuu wa Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege, Ndg. Omar M. Khamis, badala ya kutiwa saini na Mamlaka inayohusika,
yaani Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, hali hii haikubaliki kisheria.
3.4.8 Air Tanzania Co. Ltd.
Air Tanzania wamekodi ofisi yenye ukubwa wa square meter 13.69 kwa ajili ya kuendesha
biashara ya utoaji wa huduma ya usafiri wa ndege (Air Line Operator). Katika Mkataba huu, ni
vyema tukayaangalia masuala yafuatayo:
3.4.8.1 Matumizi ya sehemu iliyokodishwa.
Mkataba unaeleza kwamba, square meter 13.69 zimekodishwa kwa Kampuni ya Air Tanzania
kwa matumizi ya ofisi ya kushughulikia usafiri wa ndege hiyo. Hata hivyo, wakati Kamati
inatembelea eneo hilo, ofisi hii ilikuwa imefungwa hali ambayo imejitokeza tokea Kampuni hii
ilipositisha huduma zake Zanzibar. Kwa hali hii, kifungu cha 2.2 cha Mkataba husika
kinachoitaka Kampuni inayokodishwa kutoa huduma ama kufanya shughuli yoyote
waliyokodishiwa, ndani ya mwezi mmoja baada ya Mkataba kutiwa saini, hakikuweza
kusimamiwa ipasavyo na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na matokeo yake Mkodishwaji kuzuia
sehemu bila ya pato lolote kuingia Serikalini. Hata hivyo, katika ufafanuzi walioutoa Mamlaka
ya Uwanja wa Ndege mbele ya Kamati waliihakikishia Kamati kwamba, sehemu hiyo sasa
wameizuia kwa kuifunga huku wakisubiri kuoikodisha kwa mtu mwengine (Kielelezo Na.41).
3.4.8.2 Muda wa Mkataba.
Pamoja na ukweli kwamba sehemu iliyokodishwa ilikuwa tayari imeshafungwa muda mrefu
kabla ya kufika kwa Kamati, Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege uliipotosha Kamati
kwa kuipa taarifa isiyo sahihi kwamba Mkataba wao na Kampuni ya Air Tanzania ulianza tarehe
1/1/2011 na kumalizika tarehe 31/12/2011 wakati ukweli wa suala hili ni kwamba, kwa mujibu
wa kifungu cha 2.1 cha Mkataba husika (Rejea Kielelezo Na.41), muda wa Mkataba huo
ulikuwa kuanzia tarehe 1/1/2010 na kumalizikia tarehe 31/12/2010. Kwa maana hii, kuanzia
51
January 2011 hadi leo, bado Mamlaka ya Uwanja wa Ndege haijaingia Mkataba mwengine na
Kampuni hii.
3.4.8.3 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kwa maelezo ya kifungu cha 6.2 cha Mkataba, Kampuni ya Air Tanzania ilipaswa ilipe USD
1,026.75 kwa mwaka sawa na Tsh. 1,642,800/-, ni sawa na kulipa Tsh. 136,900 kwa kila mwezi.
Hata hivyo, Kamati imethibitishiwa kulipwa kwa fedha za kodi ya mwaka 2010 kupitia risiti
namba 224784 huku ikielezwa kwamba, malipo hayo yameanza kulipwa baada ya malumbikizo
ya muda mrefu. Kuhusu malipo ya gharama za umeme, maji na simu, Tsh.150,000 zinapaswa
zilipwe kwa kila mwezi, ingawaje Kamati haikupata uashahidi wa namna malipo hayo
yanavyofanyika.
3.4.8.4 Kuhusu saini ya Mkataba.
Takribani hali hii imejitokeza katika mikataba yote, kwamba ndani ya miezi 6 mikataba hiyo
haijakamilika kutiwa saini na pande zote mbili za Mkataba na badala yake huwa mikononi mwa
Mkodishwaji ambapo katika Mkataba huu ulioanza tarehe 1/1/2010 na kutakiwa kwa mujibu wa
Sheria kutiwa saini katika siku hiyo hiyo, ingawaje yawezekana kutiwa saini katika mazingira
tofauti, Mkataba huu baada ya kutiwa saini tarehe 25/2/2010 kwa upande wa Mkodishaji, pia
ulisainiwa terehe 16/4/2010 na upande wa Mkodishwaji.
3.4.9 Coffee Shop.
Coffee Shop wamekodi square meter 4.4 kwa ajili ya Mkahawa ili kutoa huduma ya chakula kwa
wasafiri na watumiaji mbali mbali wa Uwanja wa Ndege. Katika kuupitia Mkataba huu, Kamati
imeona ni vyema kuyafahamu mambo yafuatayo:
3.4.9.1 Matumizi Sahihi ya Eneno lililokodishwa.
Kwa mujibu wa kifungu cha 1.1 cha Mkataba (Kielelezo Na.42), Coffee Shop wamekodishwa
square meter 4.4. kwa ajili ya matumizi ya utoaji huduma za chakula kama Mkahawa (Small
Retail Kiosk) ambapo kwa mujibu wa kifungu cha 1.2 cha Mkataba, Mkodishaji, yaani Coffee
Shop analazimika kuitumia sehemu aliyokodishwa kwa matumizi ya Mkahawa tu na sio
vyenginevyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa kwa Kamati (Rejea Kielelezo Na.30),
sehemu hiyo sasa inatumika kwa kutoa huduma ya duka la Watalii kinyume na matumizi
yaliyokusudiwa. Aidha, Kamati ilipotembelea eneo hilo, imethibitisha kwamba sasa eneo hilo
linatumika kwa kuwa ni duka la vitu vya Kitalii na sio Mkahawa.
3.4.9.2 Muda wa Mkataba.
Maelezo ya kifungu cha 2.1 cha Mkataba husika kinaeleza kwamba, kuanzia tarehe 1/1/2010
hadi tarehe 31/12/2010 ndio Mkataba huu utakuwa halali kisheria, kinyume na maelekezo ya
orodha ya Wapangaji wa Uwanja wa Ndege (Rejea Kielelezo Na.30) iliyowasilishwa kwa
Kamati inayoeleza kwamba Mkataba huo umeanza tarehe 1/1/2011 hadi tarehe 31/12/2011. Ni
sawa na kusema kwamba, Mkataba huu umeshapitwa na muda kisheria.
3.4.9.3 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kifungu cha 6.2 cha Mkataba kinaeleza kwamba, jumla ya USD 176 sawa na Tsh. 281,600
zinalipwa kwa kila mwaka mmoja kama kodi ya eneo hilo, ambapo kwa kila mwezi ni sawa na
kulipia Tsh. 23,466.66. kwa mwaka 2010, Coffee Shop wamelipa USD 176 kupitia Risiti Namba
52
224242 ambapo ni sawa na maelekezo ya kifungu cha 6.2 cha Mkataba. Hata hivyo, kwa mujibu
wa Orodha iliyowasilishwa kwa Kamati (Rejea Kielelezo Na.30) imeonesha wangestahiki
kulipa USD 1,300.
3.4.10 Palm Restaurant II & Duty Free Shop II.
Mkataba huu umefungwa na Kampuni moja kwa kuendesha shughuli mbili tofauti. Shughuli ya
kwanza ni kwa ajili ya kutoa huduma ya Duka la bidhaa mbali mbali za wasafiri na watalii
wanaotumia Uwanja wa Ndege na shughuli ya Pili ni kutoa huduma ya chakula, kama
inavyoelezwa na kifungu cha 1.2 cha Mkataba huo (Kielelezo Na.43), Jumla ya square meter 10
zimekodishwa na zinalipiwa USD 400 kwa mwaka. Katika Mkataba huu, mambo yafuatayo ni
vyema tukayaangalia:
3.4.10.1 Muda wa Mkataba:
Mkataba huu upo kisheria, tofauti na Mikataba mengine iliyotangulia, kwa kuwa umesainiwa
tarehe 1/07/2010 na unatarajiwa kumalizika tarehe 30/06/2012, kama inavyoonekana katika
kifungu cha 2.1 cha Mkataba huo.
3.4.10.2 Malipo ya Kodi na Huduma :
Kifungu cha 6.2 cha Mkataba kinaeleza kwamba, Mkodishwaji atalipa Kodi ya sehemu
anayokodishwa kwa USD 400 kwa mwaka, sawa na Tsh. 640,000, ambapo ni sawa na kulipia
kwa kila mwezi Tsh. 53,333.33. Kamati imethibitishiwa kwamba Kampuni hii inalipa kodi ,
ingawaje hulipwa kwa pamoja na Maeneo mengine kwa sababu maeneo yote haya yamekodiwa
na Jamani Investment Co. Ltd, ambayo hulipa kwa pamoja. Maeneo hayo ni hii Palm Tree
Restaurant; Duty Free Shop na Departure Kioks, ambapo kwa mwaka 2010, kodi hizo zililipwa
kupitia Risiti Namba, 343369; 224756; 224795; 224796; 224201 na 224202. Aidha, kuhusu
malipo ya gharama za maji, umeme na simu hulipwa kila mwezi kwa kima ambacho Meneja wa
Uwanja wa Ndege amekiamua kwa makubaliano na Mkodishwaji, ingawaje Kamati pia
haikupatiwa uthibitisho wa ulipwaji wa fedha hizo.
3.4.11 Exotic Tours and Safari:
Mkataba baina ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na Exotic Tours and Safari unahusu kuendesha
shughuli za kitalii (Tour Operator) kwa kukodi ofisi yenye ukubwa wa square meter 8 na
hatimae kufanya shughuli za kutoa huduma za usafiri kwa watalii na wasafiri mbali mbali
pamoja na huduma za safari za kawaida kwa wananchi. Pia Mkataba huu pamoja na mambo
mengine, unahusika na mambo yafuatayo:
3.4.11.1 Muda wa Mkataba:
Mkataba huu umeshamaliza muda wake wa kutambuliwa kisheria kwa sababu ulianza kutumika
tarehe 1/1/2010 na kumalizika tarehe 31/12/2010 (Kielelezo Na.44). Hata hivyo, kwa mujibu wa
orodha iliyokabidhiwa kwa Kamati, Mkataba huo umeanza tarehe 1/1/2011 hadi 31/12/2011
(Rejea Kielelezo Na.30).
3.4.11.2 Malipo ya Kodi na Huduma :
Exotic Tours and Safari wamekodishwa sehemu yenye ukubwa wa square meter 8 kwa USD 600
kwa mwaka, sawa na Tsh. 960,000, na ni sawa na kulipia Tsh. 80,000 kwa kila mwezi. Na kwa
mwaka 2010 Kamati imethibitisha kwamba wamelipa kodi ya eneo hilo kupitia Risiti Namba
53
446683. Na kwa upande wa gharama za huduma za umeme na maji, Kampuni hii wanalipia Tsh.
150,000 kwa kila mwezi, kwa mujibu wa kifungu cha 6.3, cha Mkataba. Hata hivyo, Kamati
haikupatiwa uthibitisho wa malipo hayo namna yanavyofanyika.
3.4.11.3 Saini ya Mkataba:
Kwa tabia ile ile ya ucheleweshwaji wa kutiwa saini mikataba hii, kama tulivyokwisha eleza
hapo awali, Mkataba huu umetiwa saini na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege tarehe 25/2/2010
lakini kwa upande wa Mkodishwaji, umesainiwa tarehe 1/1/2011 sawa na miezi 11 ukiwa hauna
saini zote mbili, ya Mkodishaji na Mkodishwaji, ambapo kisheria Mkataba wa aina hii hauna
uhalali wala nguvu ya kisheria kwa muda wote ulipokosa saini ya pande zote zinazohusika.
3.4.12 Gallery Tours & Safari:
Mkataba huu unahusika na eneo la square meter 14.58 zilizokodishwa kwa Gallery Tours &
Safari kwa ajili ya biasahra ya kutoa huduma ya safari kwa watalii na wasafiri wengine (Tours
Operator). Kupita Mkataba huu, mambo yafuatayo yamejitokeza:
3.4.12.1 Muda wa Mkataba:
Mkataba huu umeanza tarehe 1/1/2010 na kumalizika tarehe 31/12/2010 (Kielelezo Na.45). Hata
hivyo, kama ilivyokuwa kwa Mikataba mingi iliyotangulia, Kamati ilipotoshwa kwa kupewa
Orodha ya Wakodishwaji inayoonesha kwamba Mkataba huu umesainiwa kuanzia tarehe
1/1/2011 hadi tarehe 31/12/2011 (Rejea Kielelezo Na.30).
3.4.12.2 Malipo ya Kodi na Huduma:
Kifungu cha 6.2 cha Mkataba kinaelekeza kwamba, Mkodishwaji atalipa USD 1,093.50 kwa
mwaka, sawa na Tsh. 1,749,600 ambazo ni sawa 145,800 kwa kila mwezi. Malipo haya ni
kutokana na square meter 14.58 za eneo lililokodishwa ambapo kila square meter moja inalipwa
kwa USD 75, ni sawa na kulipiwa Tsh. 120,000 kwa kila mwaka. Kwa mwaka 2010, ambapo
Kamati ilitaka kuthibitishiwa kama ni mfano wa malipo yanavyofanyika, Gallery Tours & Safari
wamelipa kupitia risiti namba 224246. Aidha, Gallery Tours & Safari wanapaswa kulipa
gharama za maji na umeme Tsh.150,000 kwa kila mwezi, lakini mpaka tunaandika ripoti hii,
Kamati haikupewa uthibitisho wa malipo hayo.
3.4.13 Airport Telephone Bureau de Change :
Mkataba baina ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na Airport Telephone Bureau de Change
unahusu biashara ya huduma za kibenki kupitia kubadilisha fedha kwa thamani mbali mbali ya
fedha hizo. Mkodishwaji huyu amekodishwa eneo hilo kwa shughuli hiyo, na Kamati ilipoupitia
Mkataba wa ukodishwaji wake, imegundua mambo mengi yakiwemo yafuatayo:
3.4.13.1 Matumizi sahihi ya Eneo lililokodishwa:
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kwa Kamati kutoka kwa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
ni kwamba, eneo hilo limekodishwa kwa ajili shughuli za kibenki na Kamati kupewa orodha ya
wakodishwaji ikiwa ni pamoja na Airport Telephone Bureau de Change inaoeleza kwamba,
wamekodishwa kwa shughuli hii tu. Hata hivyo, tofauti iliyopo ni kifungu cha 1.1 na 1.2 cha
Mkataba vinavyothibitisha kwamba, Mkodishwaji amekodishwa sehemu hiyo kwa ajili ya kutoa
huduma za safari ya watalii (Tour Operator) (Kielelezo Na.46). Kwa maana hii, matumizi
54
yaliyoruhusiwa katika Mkataba wa ukodishwaji ni tofauti na matumizi halisi ambayo kwa sasa
Airport Telephone Bureau de Change wamejishughulisha nayo, na kwa mujibu wa Mkataba
walioingia na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, Mkodishwaji haruhusiwi kubadilisha matumizi
sahihi ya eneo alilokodishwa na kwa maana hii, Mkodishwaji amevunja Mkataba.
Tunachotaka kufahamisha hapa ni kwamba, hapo kabla ya Mkodishwaji huyu kuchukua nafasi
hiyo, eneo hilo lilikodishwa kwa Jambo Bureau De Change ambayo wao ndio waliokodi kwa
kufanya shughuli za Kibenki kama makusudio ya Mkataba huu. Lakini baadae Jambo
waliwakodisha hawa Airport Telephone Bureau De Change bila ya idhini ya Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege na ndio maana baada ya kukodi hawakubadilisha dhati ya shughuli
iliyokodishiwa hapo awali. Hivyo basi, pamoja na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kubadilisha
jina la Mkodishaji kuwa Airport Telephone Bureau De Change badala ya Jambo Bureau De
Change, haikuingia katika Mkataba mpya na Airport Telephone Bureau De Change na ni sawa
na kusema kwamba Mkataba huu umeandaliwa kuidanganya Kamati na sio vyenginevyo.
Tunasema hivi kwa hoja zifuatazo :
Mbali na hoja tuliyoieleza hapo juu, lakini Mkataba huu hauna saini ya Mkodishwaji yaani,
Airport Telephone Bureau De Change kama tutakavyoona katika kipengele kinachohusika na
saini ya Mkataba katika ufafanuzi wa Mkodishwahi huyu. Pili, wakati Kamati ilipokutana na
Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege ilitoa Orodha ya Wapangaji hao, huku
Mkodishwaji huyu wa zamani, Jambo Bureau De Change akiwa ni namba 20 ya orodha (Rejea
Kielelezo Na.30). Na wakati wote wa majadiliano, Mamlaka ilikuwa imeficha ukweli, haijaeleza
hali halisi, isipokuwa Kamati wakati ikifanya ziara katika eneo hilo ndio imegundua ukweli na
matokeo yake Mamlaka ikakubaliana na Kamati.
3.4.13.2 Muda wa Mkataba:
Kifungu cha 2.1 cha Mkataba kinaeleza wazi kwamba, Mkataba huu umefungwa tarehe 1/1/2010
hadi 31/12/2010. Na kwa maana hii, Mkataba huu umeshapitwa na wakati pamoja na Uongozi
wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kuficha ukweli huu na kutoa taarifa zisizo za kweli kuhusiana
na muda wa Mkataba huu, kwamba umeanza tarehe 1/1/2011 na kumalizika tarehe 31/12/2011,
jambo ambalo sio kweli.
3.4.13.3 Malipo ya Kodi na Huduma:
Kwa mujibu wa maelezo ya Mkataba, Airport Telephone Bureau de Change waliwajibika kulipa
USD 300 kwa mwaka, sawa na Tsh. 480,000/- na ni sawa na malipo ya USD 25 ambazo ni sawa
na Tsh. 40,000/- kwa mwezi. Aidha, malipo hayo yamelipwa kwa mwaka 2010, kupitia risiti
namba 224235. Kuhusu gharama za maji na umeme, Mkodishwaji alipwaswa kulipa Tsh.
150,000 kwa kila mwezi. Hata hivyo, Kamati haikupatiwa uthibitisho wa malipo ya fedha hizo.
3.4.13.4 Saini ya Wahusika wa Mkataba:
Mkataba huu pamoja na ukweli kwamba umeshapitwa na muda kisheria, pia ni batili kwa kukosa
saini ya Mkodishwaji (Rejea Kielelezo Na.46). Kwa maana hii, Mkataba huu umekosa ridhaa
(consent) ya Mkodishwaji kinyume na masharti ya Mkataba halali wa kisheria.
55
3.4.14 Zanzibar Bureau de Change:
Mkataba huu umeuruhusu Uongozi wa Zanzibar Bureau de Change kufanya biashara ya huduma
za Kibenki katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Zanzibar lenye ukubwa wa square meter 4.44
kwa mwaka wa 2010. Pamoja na mambo mengine, ni vyema tukayaangalia masuala yafuatayo:
3.4.14.1 Muda wa Mkataba:
Kipengele cha 2.1 cha Mkataba huo kinaweka wazi kwamba Mkataba huo unaanza tarehe
1/1/2010 hadi 31/12/2010. Pamoja na Kamati kupewa taarifa nyengine tofauti na ukweli halisi,
ni wazi kwamba tokea mwezi wa January 2011 hadi leo, hakuna Mkataba wowote ulioingiwa
baina ya Mamlaka na Mkodishwaji pamoja na ukweli kwamba Mkodishwaji anaendelea kutumia
eneo la Mamlaka kwa shughuli za kibiashara (Kielelezo Na.47).
3.4.14.2 Malipo ya Kodi na Gharama za Huduma:
Kwa kila mwaka, Zanzibar Bureau de Change wanalipa kodi ya USD 399.60, ambapo ni sawa na
Tsh 639,360. Malipo ya gharama za maji, umeme na simu yalipaswa yalipwe kwa kila mwezi
katika kiwango ambacho kwa mujibu wa kifungu cha 6.4 cha Mkataba ni makubaliano baina ya
ya Manager wa Uwanja wa Ndege na Uongozi wa Zanzibar Bureau de Change.
3.4.15 Departure and Arrival Bureau de Change:
Mkataba huu ulimruhusu Mkodishwaji kufanya shughuli za Kibenki kwa kutoa huduma za
kubadilisha fedha (Bureau de Change) katika eneo alilokodishwa lenye ukubwa wa square meter
12.2. Katika kuupitia Mkataba huu, ni vyema tukayaangalia mambo yafuatayo:
3.4.15.1 Muda wa Mkataba:
Mkataba huu umeanza tarehe 1/1/2010 hadi 31/12/2010 kwa maana ile ile kwamba Mkataba huu
tayari umeshapitwa na wakati na kukosa sifa ya uhai kisheria.
3.4.15.2 Malipo ya Kodi na Gharama za Huduma:
Mkodishwaji alilazimika kulipa USD 1,098 kwa mwaka, sawa na Tsh. 1,756,800. Na ni sawa na
kusema, kwa kila mwezi Mkodishwaji alitakiwa kulipa USD 91.5 ambazo ni sawa na Tsh.
146,400. Kwa upande wa malipo ya gharama za maji na umeme, Mkodishwaji alilazimika kulipa
Tsh. 100,000 kwa kila mwezi (Kielelezo Na.48).
3.4.16 People‟s Bank of Zanzibar (PBZ)
Mkataba huu unairuhusu Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kufanya biashara ya kutoa huduma
za Kibenki katika eneo lenye ukubwa wa square meter 8, eneo ambalo PBZ sio tu wanatoa
huduma ya kubadilisha pesa lakini pia wameweka Mfumo wa kisasa wa Utoaji wa fedha kwa
njia ya Electroniki (ATM). Aidha, mambo yafuatayo yamejitokeza:
3.4.16.1 Muda wa Mkataba:
Tofauti na Mikataba mingi iliyopita, PBZ wameingia Mkataba na Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege kwa muda wa miaka mine, kuanzia tarehe 25/03/2009 hadi tarehe 31/03/2012 (Kielelezo
Na.49).
3.4.16.2 Malipo ya Kodi na Gharaza za Huduma:
56
Kwa muda wote wa miaka mitatu, ambayo ndio uhai wa Mkataba uliowasilishwa kwa Kamati,
PBZ hawatakuwa na jukumu la kulipa kodi yoyote kwa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, kwa
sababu PBZ walijenga „Anti Narcotic Police Unit‟ katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Aman Karume, na kwa hali hii, ujenzi huo unachukuliwa kisheria kuwa ndio
„consideration‟ ya kuhalalisha Mkataba huo. Aidha, malipo ya kodi kwa PBZ yataanza tarehe
1/4/2012 bila ya kima cha kodi hiyo kuelezwa katika Mkataba uliowasilishwa kwa Kamati.
Kuhusu ghrama za maji na umeme, PBZ wanalazimika kulipa kwa kila mwezi Tsh. 150,000
ingawaje Kamati haikupata ushahidi wa namna malipo hayo yanavyofanyika.
3.4.17 Jamani Investment Ltd- Zanzibar.
Jumla ya square meter 543.47 zimekodishwa kwa Kampuni hii kupitia Mkataba unaowaruhusu
kufanya biashara ya kutoa huduma ya chakula kupitia Mkahawa (Restaurant) inayomilikiwa na
Mkodishwaji. Katika kuupitia Mkataba huu, mambo yafuatayo ni vyema tukayatizama kwa
pamoja:
3.4.17.1 Muda wa Mkataba:
Mkataba huu ni wa miaka 10, kuanzia tarehe 1/1/2007 hadi tarehe 31/12/2017. Mkataba huu
bado una nguvu kisheria kwa sababu bado upo hai kisheria.
3.4.17.2 Malipo ya Kodi na Gharama za Huduma:
Mbali na Mkataba huu kuwa na muda mrefu, yaani miaka 10, Mkodishwaji anawajibika kulipa
kodi ya kila mwaka USD 7,200, sawa na Tsh. 11,520,000. Aidha ni sawa kulipia Tsh. 960,000
kwa kila mwezi. Kifungu cha 6.2 na 6.4 vya Mkataba (Kielelezo Na.50) vinamtaka Mkodishwaji
atangulize kulipa USD 1,800 ambazo ni sawa na Tsh. 2,880,000. Malipo haya ya kodi analipa
kama ilivyoelezwa hapo awali kuhusiana na Kampuni hii. Kuhusu gharama za maji, umeme na
simu, Mkodishwaji analazimika kulipa katika kila mwezi kwa kiwango ambacho kitaamuliwa na
Meneja wa Uwanja wa Ndege, ambapo Kamati haikupatiwa uthibitisho wa malipo hayo.
3.4.18 Jamani Ivestment Ltd-Zanzibar.
Mbali na Mkataba tulioutaja hapo juu, Kampuni ya Jamani Investement Ltd, imekodi sehemu
nyengine ya biashara katika eneno la Uwanja wa Ndege leye ukubwa wa square meter 259.54
kwa lengo la kueka Duka Huria kuuza bidhaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na vitu vya asili.
Katika kuupitia Mkataba huu, mambo yafuatayo ni vyema tukayaangalia:
3.4.18.1 Muda wa Mkataba:
Mkataba huu ni wa miaka 10, ulioanza tarehe 1/2/2007 na kumalizikia 31/12/2017. Tofauti na
mikataba mingi iliyowasilishwa mbele ya Kamati, Mkataba huu bado haujapitwa na muda na
hivyo, uko hai kisheria (Kielelezo Na.51).
3.4.18.2 Malipo ya Kodi na Gharama za Huduma:
Suala la malipo limainishwa katika kifungu cha 6.2 cha Mkataba kinachoitaka Kampuni ya
Jmani Investment Ltd kulipa Kodi ya square meter 259.54 alizokodishwa kwa USD 6,000 kwa
mwaka, sawa na Tsh. 9,600,000, ambapo utaratibu wa kulipa ni kwa kila miezi minne (quarter)
atalipa USD 1,500 katika mwezi wa kwanza wa miezi minne hiyo, huku malipo ya miezi minne
ya kwanza ikilipwa kabla ya Mkodishwaji huyu kukabidhiwa sehemu aliyokodi. Hata hivyo,
Kulazimika kulipa ndani ya miezi minne (quarterly) ama kulipa kwa mwezi (monthly) ni
57
makubaliano baada ya kushauriana na Mkodishaji. Aidha, kuhusu gharama za maji, umeme na
simu zitalipwa kwa kiwango cha kila mwezi ambacho kitapangwa na kuamuliwa na Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege katika muda hadi muda. Hata hivyo, Kamati haikuweza
kupata ushahidi sahihi wa mlipo ya maji na umeme, ingawaje imethibitisha malipo ya kodi.
3.4.18.3 Saini ya Mkataba:
Kwa tabia ile ile ya ucheleweshwaji wa kutiwa saini mikataba hii, kama tulivyokwisha eleza
hapo awali, pamoja na Mkataba huu kuelezwa kuanza tarehe 1/2/2007 na kwa mujibu wa
masharti ya kifungu cha 2.3, Mkodishwaji kutakiwa kuanza kutoa huduma kwa madhumuni ya
kukodishwa kwake, ndani ya miezi mitatu, Mkataba huu umetiwa saini na pande zote mbili,
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na Kampuni ya Jamani Investment Ltd, tarehe 8/5/2007, yaani
miezi mitatu baada ya muda uliotakiwa kusainiwa na kuanza kazi kisheria.
3.4.19 Maha Travels and Tours :
Kampuni hii ya Maha Travels and Tour Ltd, imekodi sehemu nyengine yenye ukubwa wa square
meter 4.4 kwa ajili ya kutoa huduma za Usafiri wa Watalii (Tour Operator) kwa thamani ya USD
330 kwa mwaka, ambapo kwa kila square meter moja wanailipia USD 75. Katika uchambuzi wa
Mkataba huu, mambo yafuatayo ni vyema yakafahamika:
3.4.19.1 Muda wa Mkataba.
Mkataba huu umefungwa tarehe 01/01/2010 na kumalizika tarehe 30/06/2010 (Kielelezo Na.52)
na kwa wakati Kamati inaifanyia kazi hoja hii, Mkataba huu tayari umeshapitwa na wakati na
hivyo, hauna athari yoyote kisheria. Aidha, orodha ya wapangaji wa Uwanja wa Ndege
iliyowasilishwa kwa Kamati inaonesha kwamba, Mkataba huu umeanzia tarehe 1/1/2011 na
kumalizia tarehe 31/12/2011, taarifa ambazo zinapingana na maelekezo ya kifungu cha 2.1 cha
Mkataba husika.
3.4.19.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kama ilivyo kwa Mikataba mengine, Malipo ya Mkataba huu yamegawika katika sehemu mbili
kuu; Kodi ya eneo walilokodishwa, lenye ukubwa wa square meter 4.4 ambalo linalipiwa kwa
USD 330 kwa mwaka sawa na Tsh. 528,000, na ni sawa na kulipa kila mwezi Tsh. 44,000
ambapo kila square meter moja ni sawa na USD 75 ambapo kwa mwaka ni sawa na Tsh.
120,000/-. Kwa mwaka 2010, kodi hiyo imelipwa kama ilivyoshuhudiwa kupitia risiti namba
343357. Kuhusu malipo ya gharama za maji, umeme na simu, wanalipa Tsh. 150,000 kwa kila
mwezi na gharama za kodi tulizozitaja hapo juu, lazima zilipwe kabla ya Mkodishwaji kupewa
sehemu hiyo aliyokodi. Hata hivyo, Kamati haikupata uthibitisho wa malipo hayo.
Pia na Mkodishwaji huyu ifahamike kwamba amekodisha sehemu aliyokodi kumkodisha
Kampuni ya Direct Maintance bila ya idhini ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, kitendo
ambacho kinapingana na kifungu cha 10.5 cha Mkataba huo. Na hivyo, Kamati ilipofanya ziara
haikuikuta Kampuni hii na badala yake imeikuta Direct Maintenance.
3.4.19.3 Muda wa Kusainiwa kwa Mkataba.
Pamoja na ukweli kwamba Mkataba huu umeanza kazi tarehe 1/1/2010, saini za upande wa
Mkodishaji (Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa niaba ya Serikali) imesainiwa tarehe
25/02/2010, takriban miezi 2 baada ya tarehe ya Mkataba kuanza kazi huku upande wa
58
Mkodishwaji (Maha Travel and Tours Safari) wameusaini Mkataba huo miezi 4 baadae, yaani
tarehe 13/04/2010.
3.4.20 Zee Entertainment:
Kampuni ya Zee entertainment wameingia katika Mkataaba na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
kwa kukodi square meter 12 kwa ajili ya Mkahawa ili kutoa huduma ya chakula kwa wasafiri na
watumiaji mbali mbali wa Uwanja wa Ndege (Rental Kiosk). Katika kuupitia Mkataba huu,
Kamati imeona ni vyema kuyafahamu mambo yafuatayo:
3.4.20.1 Muda wa Mkataba.
Maelezo ya kifungu cha 2.1 cha Mkataba husika kinaeleza kwamba, kuanzia tarehe 1/1/2010
hadi tarehe 31/12/2010 (Kielelezo Na.53) ndio Mkataba huu utakuwa halali kisheria, kinyume na
maelekezo ya orodha ya Wapangaji wa Uwanja wa Ndege (Rejea Kielelezo Na.30)
iliyowasilishwa kwa Kamati inayoeleza kwamba Mkataba huo umeanza tarehe 1/1/2011 hadi
tarehe 31/12/2011. Kwa maana hii, Mkataba huu tayari umeshapitwa na wakati na hauna nguvu
ya kisheria.
3.4.20.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kifungu cha 6.2 cha Mkataba kinaeleza kwamba, jumla ya USD 480 sawa na Tsh. 768,000
zinalipwa kwa kila mwaka mmoja kama kodi ya eneo hilo, ambapo kwa kila mwezi ni sawa na
kulipia Tsh. 64,000. Kamati imethibitisha kulipwa kwa kodi hiyo kwa mwaka 2010 kupitia risiti
namba 224215. Na kuhusiana na gharama za maji na umeme, Mkodishwaji huyu analipia Tsh
100,000/ kwa kila mwezi. Hata hivyo, Kamati haikupata ushahidi wa malipo yanavyofanyika.
3.4.20.3 Muda wa Kusainiwa kwa Mkataba.
Pamoja na ukweli kwamba Mkataba huu umeanza kazi tarehe 1/1/2010, saini za pande zote mbili
zimetiwa mwezi mmoja baadae, yaani tarehe 15/02/2010 kwa upande wa Mkodishwaji na
Mkodishwaji alitia saini tarehe 22/2/2010.
3.4.21 Zanzibar Datacom.
Kampuni ya Zanzibar Datacome inajishughuliha na utoaji wa huduma za duka na kutoa huduma
za intaneti (internet services) kwa wasafiri na watumiaji mbali mbali wa Uwanja wa Ndege.na
hivyo, wamekodi square meter 34. Katika kuupitia Mkataba huu, Kamati imeona ni vyema
kuyafahamu mambo yafuatayo:
3.4.21.1 Muda wa Mkataba.
Mkataba huu ni wa miaka mitano ulioanza tarehe 1/09/2009 na kumalizika tarehe 1/09/2014. Na
kwa maana hii, Mkataba huu bado uko sahihi kisheria (Kielelezo Na.54).
3.4.21.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kifungu cha 6.2 cha Mkataba kinaeleza kwamba, jumla ya USD 1,360 sawa na Tsh. 2,176,000
zinalipwa kwa kila mwaka mmoja kama kodi ya eneo hilo, ambapo kwa kila mwezi ni sawa na
kulipia Tsh. 181,333.33. Kwa sababu Mkodishwaji ametumia gharama zake katika ujenzi wa
sehemu aliyokodishiwa, Kodi yake ilianza mwaka mmoja baadae, yaani tarehe 1/09/2010, hivyo
ni kusema kati ya miaka mitano aliyokodishwa, analipia kodi miaka mine tu. Hata hivyo, kwa
59
mwaka wa 2010, alilipa kodi hiyo kupitia risiti namba 447365. Aidha, kuhusu gharama za
Umeme, Maji na Simu, Mkodishwaji huyu analazimika kulipa Tsh. 100,000 kwa kila mwezi.
Hata hivyo, Kamati haikupata ushahidi wa malipo hayo.
3.4.22 Zanzibar and Coastal Travels Ltd.
Zanzibar and Coastal Travels Ltd imekodi eneo lenye ukubwa wa square meter 12.98 kwa ajili
ya kuendesha biashara ya utoaji wa huduma ya usafiri wa ndege (Air Line Operator). Katika
Mkataba huu, ni vyema tukayaangalia masuala yafuatayo:
3.4.22.1 Muda wa Mkataba.
Ukilinganisha na orodha ya Wapangaji iliyokabidhiwa kwa Kamati kutoka katika Uongozi wa
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, Mkataba wa Zanzibar and Coastal Travels Ltd unaanzia tarehe
1/1/2011 na kumalizia tarehe 31/12/2011. Kitu ambacho ni tofauti kwa mujibu wa kifungu cha
2.1 cha Mkataba huo, muda wa uhai wake ni kuanzia tarehe 1/1/2010 hadi Disemba 31 ya
mwaka 2010. (Kielelezo Na.55) kwa maana hii, Mkata huu umepitwa na muda kisheria.
3.4.22.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kwa maelezo ya kifungu cha 6.2 cha Mkataba huu, Kampuni ya Zanzibar and Coastal Travels
Ltd, inatakiwa kulipa jumla ya USD 973.50, sawa na Tsh. 1,557,600/-kwa mwaka. Ambazo ni
sawa na kulipa Tsh. 129,800 kwa kila mwezi. Kamati imethibitisha kwamba amelipa kodi ya
mwaka 2010 kupitia risiti namba 343364. Kuhusu malipo ya gharama za umeme, maji na simu,
Tsh.150,000 zinapaswa zilipwe kwa kila mwezi, huku malipo ya kodi yakisisitizwa kulipwa
kabla ya Mkodishwaji huyu kupewa sehemu hiyo ya biashara aliyoikodi. Hata hivyo, Kamati
haijathibitishiwa malipo hayo.
3.4.23 Zanzibar and TAN WING AVIATION (T) LTD.
Kampuni ya Zanzibar and Tan Wing Aviation (T) Ltd wameingia katika Mkataba na Mamlaka
ya Uwanja wa Ndege kwa lengo la kutoa huduma ya usafiri wa ndege (Air line Operator) kwa
wasafiri mbali mbali hapa Zanzibar na ili kuendesha biashara hiyo kwa ufanisi, wamelazimika
kukodi ofisi yenye ukubwa wa square meter 9 (Kielelezo Na.56). Katika Mkataba huu, ni vyema
tukayaangalia masuala yafuatayo:
3.4.23.1 Muda wa Mkataba.
Mkama ilivyokuwa ni desturi kwa mikataba mingi iliyopita, Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja
wa Ndege (wakati huo Idara ya Anga) uliipotosha Kamati kwa kuipa taarifa isiyo sahihi kwamba
Mkataba wao na Zanzibar and TAN WING AVIATION (T) LTD, ulianza tarehe 1/1/2011 na
kumalizika tarehe 31/12/2011 wakati ukweli wa suala hili ni kwamba, kwa mujibu wa kifungu
cha 2.1 cha Mkataba husika, muda wa Mkataba huo ulikuwa kuanzia tarehe 1/1/2010 na
kumalizikia tarehe 31/12/2010.
3.4.23.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kwa maelezo ya kifungu cha 6.2 cha Mkataba, Kampuni ya Zanzibar and TAN WING
AVIATION (T) LTD, ilipaswa ilipe USD 675 kwa mwaka sawa na Tsh. 1,080,000/-, na kwa
hesabu ya kila mwezi, wanalipa USD 56.25 ambazo ni sawa na Tsh. 90,000. Kamati
imethibitishiwa kwamba wamelipa kwa mwaka 2010 kupitia risiti namba 224226. Kuhusu
malipo ya gharama za umeme, maji na simu, Tsh.150,000 zinapaswa zilipwe kwa kila mwezi,
60
lakini Kamati haijathibitishiwa malipo hayo yalivyolipwa angalau kwa mwaka 2010, kama
ilivyofanya kwa malipo ya kodi.
Vile vile tunapenda tutanabahishe kwamba Mkodishwaji huyu amekodisha sehemu aliyokodi
kwa Kampuni ya Assalaam Air bila ya idhini ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, kitendo
ambacho kinapingana na kifungu cha 10.5 cha Mkataba huo. Na hivyo, Kamati ilipofanya ziara
haikuikuta Kampuni hii na badala yake imeikuta Assalaam Air.
3.4.23.3 Kuhusu saini ya Mkataba.
Kama ilivyo kwa mikataba mingi iliyoingiwa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na
wafanyabiashara mbali mbali, Mkataba huu nao badala ya kusainiwa katika tarehe iliyokubalika
katika Mkataba, yaani 1/1/2010 umesainiwa na Mamlaka ya Uwanja wa ndege tarehe
25/02/2010 na Mkodishwaji, yaani TAN WING AVIATION (T) LTD ameusaini tarehe
15/03/2010.
3.4.24 A & Z Company Ltd:
Idara ya Anga (kama ilivyokuwa) pia iliingia Mkataba na Kampuni ya A & Z Company Ltd kwa
ajili ya kutoa huduma za „Dry Store‟. Jumla ya square meter 30 zimekodishwa kwa Kampuni hii
katika Mkataba ambao tukayafahamu mambo yafuatayo:
3.4.24.1 Muda wa Mkataba.
Mkataba huu umefungwa tarehe 01/10/2010 na kumalizika tarehe 30/09/2011. Pamoja na ukweli
kwamba, wakati Kamati inaendelea na kazi zake katika Mamlaka ya Uwanja wa Ndege,
Mkataba huu ulikuwa tayari umebakisha siku chache tu kumalizika (Kielelezo Na.57).
3.4.24.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kwa maelezo ya kifungu cha 6.2 cha Mkataba, Kampuni ya A & Z Company Ltd ilipaswa ilipe
USD 1,500 kwa mwaka sawa na Tsh. 2,400,000/-, na kwa hesabu ya kila mwezi, wanalipa USD
125 ambazo ni sawa na Tsh. 200,000/- pamoja na ukubwa wa square meter 30 walizokodi,
ambazo kwa ufupi ni nyumba nzima. Kamati imepata ushahidi wa risiti namba 445090 ya malipo
ya kodi kwa mwaka 2010. Kuhusu malipo ya gharama za umeme, maji na simu, A & Z
Company Limited wanalipa kwa kima ambacho Meneja wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
atakiamua kutoka muda hadi muda. Hata hivyo, Kamati haikupatiwa uthibitisho wa malipo haya.
3.4.25 Aerotech- Zanzibar:
Kampuni ya Aerotech ni Kampuni inayomilikiwa na Mkurugenzi wa iliyokuwa Idara ya Anga na
sasa ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, Capt. Said Ndumbogani, aliekuwa na
Share 94% wakati Kampuni hii inaanzishwa na aliendelea kumiliki share hizo mpaka Kampuni
hiyo ilipoingia Mkataba na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa kukodi Hangaer ambalo ndio
tunalolizungumzia, huku share zilizobakia, yaani share 6% zikimikiwa na Ndg. Amina Said,
ambae ni mtoto wake. Kampuni hii imekodishwa eneo lote la Hanga (Hanger) liliopo Uwanja wa
Ndege, Mkabala na Uwanja wa Ndege wa Zamani, ambamo ndani yake pia mmeanzishwa Ofisi
na kutolewa huduma za Mtengenezo ya Ndege (aircraft maintenance). Kamati inaona ni vyema
ikaweka wazi mambo kadhaa kuhusiana na Mkataba huu pamoja na mambo mengine
yanayohusiana kama ifuatavyo:
61
3.4.25.1 Uhalali na Umiliki wa Kampuni ya Aerotech:
Kama tulivyoanza na utangulizi wetu, kwamba, Kampuni ya Aerotech ni Kampuni iliyosajiliwa
Zanzibar na kumilikiwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege alieingia katika
Mkataba wa kukodi eneo lote la Hanga wakati huo huo Mkurugenzi huyu ndie mwenye dhamana
ya kusimamia wakodishwaji wote wa eneo hilo. Kwa lugha nyengine, Mkurugenzi huyu ni
mfanya biashara katika eneo lake la kazi na ni msimamizi wa kuona vipi wafanyabiashara
wenzake wanavyotekeleza masharti ya Mikataba waliyoingia na Mmiliki wa eneo walilokodi,
ambae ni Mamlaka ya Uwanja wa Ndege. Mtu yoyote akisoma maelezo haya, anaaza kupata
shaka na kujiuliza masuala mengi kuhusiana na Kampuni husika, maswala ambayo Kamati nayo
imeona ni vyema kupata ufafanuzi wake ili ijiridhishe namna gani Mikataba ya Serikali
inayosimamiwa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na jee masharti ya Mikataba hiyo
yanatekelezwa ipasavyo kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar. Hivyo basi, katika kuhakikisha
inapata majibu mazuri ya kuondosha shaka hii, Kamati ikaanza kuulizia Uhalali wa Kampuni ya
Aerotech na Umiliki wake.
Kamati ilipohoji suala hili ilipatiwa Hati za Usajili wa Kampuni hii, ambazo ni „Memorandum of
Association‟ na „Articles of Association‟ zinazoonesha uwepo na usajili wa Kampuni, malengo
yake na mambo mengine yanayohusika (Kielelezo Na.58). Kwa kuanzia na ufafanuzi wetu,
tunataka ifahamike wazi kwamba, Kampuni hii imesajiliwa Zanzibar chini ya Sheria ya
Makampuni, Sura ya 153 ya Sheria za Zanzibar mnamo tarehe 03/01/2002 kwa jina la Aerotech-
Zanzibar Company Limited. Malengo ya kunzishwa kwake ni pamoja na kufanya biashara ya
kutoa matengenezo ya ndege (maintenance and servicing repairers), huduma za kuhifandhia zana
na mashine za ndege (stores and wharehouses of aircraft and machines) na mambo mengine
yanayohusika na ndege, kufanya biashara ya matengenezo ya ndege na mambo mengine
yanayohusika na hayo.
Kwa upande wa wamiliki ni kama tulivyowataja hapo juu, Capt. Said Ndumbugani aliemiliki
share 94% za Kampuni na mwanawe Ndg. Asha Said aliemiliki share zilizobakia, 6% za share
zote. Mnamo tarehe 6/07/2009, Kampuni hii iliongeza wamiliki wake, ambapo Capt. Said
Ndumbogani alifanya „stransfer‟ ya share zake 40 kati ya „share zake 94, kwa Ndg. Abdalla
Rashid share 14; Ndg. Malik Hanif, share 12; Ndg. Amina Said share 4 na share 10 kwa Ndg.
Abdulhalym Sururu (Kielelezo Na.59) na kwa maana hiyo, Umiliki wa Kampuni hii baada ya
kikao hicho cha kufanya „transfer‟ ya „share‟ ikawa kama ifuatavyo:
1. Capt. Said Ndumbogani 54%
2. Ndg. Abdalla Rashid 14%
3. Ndg. Malik Hanif 12%
4. Ndg. Amina Said 10% na
5. Ndg. Abdulhalym Sururu 10%.
Kwa ufupi, baada ya kupitia maelezo ya hapo juu, inafahamika bila ya shaka kwamba Kampuni
hii imesajiliwa Zanzibar na mmiliki wake Mkuu ni Capt. Said Ndumbogani ambae ni
Mkurugenzi wa iliyokuwa Idara ya Anga, na sasa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege, hata kama alibadili share baadae na kubakia na 54%
62
3.4.25.2 Mkataba wa Aerotech na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege:
Baada ya kuanzisha Kampuni yake kama tulivyokwisha eleza hapo juu, Capt. Said kwa fursa
iliyokuwepo ya ukodishwaji wa eneo la biashara katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Aman Karume alifanikiwa kukodi eneo lote la Hanger mnamo tarehe 1/07/2005 na
kuingia katika Mkataba wa ukodishwaji, Mkataba huo ndio tunaoukusudia kuuzungumzia hapa
(Kielelezo Na.60). Suala la kwanza ambalo Kamati imeanza kupata wasi wasi baada ya
kukabidhiwa Mkataba husika ni juu ya uwezekano wa Mkataba huu kusimamiwa ipasavyo,
wakati umeingiwa na Kampuni ya Mkurugenzi wa Mamlaka kitu ambacho tunaweza kusema ni
kwamba ana maslahi ya pande zote mbili. Upande wa kwanza anasimama kama Mkodishaji
yani, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na upande wa pili anasimama kama
Mkodishwaji yaani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aerotech Company Ltd. Katika
kufanikisha suala hili, Kamati ilimhoji kwa vyeo vyote viwili na kwa vikao viwili tofauti. Kikao
cha kwanza, Kamati ilimhoji Mkurugenzi huyu akiwa na watendaji wenzake wa Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege katika kikao cha pamoja na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano, na kikao cha Pili Kamati ilimuita peke yake na watendaji wake wa Kampuni
anayoiongoza. Na hivyo basi ufafanuzi wa Mkataba huu pia unahusisha ufafanuzi uliotolewa
katika vikao vyote viwili na mambo yafuatayo ni vyema yakafahamika wazi:
3.4.25.3 Sheria iliyo utambua Mkataba:
Tumeona kabla ya kuangalia Mkataba wenyewe pia tujiulize kugusia kidogo kuhusiana na
Mkataba huu tunaotaka tuuzungumzie na Sheria ya Sheria ya Mikataba na kwa kuwa
Mkodiwhwaji ni Kampuni, basi pia tuangalie Sheria hizo kwa maslahi ya kufahamu udhaifu
unaojitokeza katika Mkataba husika. Kwa kawaida, Mkataba wowote wa ukodishwaji huingiwa
na pande mbili, yaani Upande wa Mkodishaji na upande wa Mkodishwaji. Pande hizi huitwa
„parties to Contract‟ na huwa na wajibu na haki kama zilivyoainishwa katika Mkataba walioingia
baina yao na kama zilivyoainishwa katika Sheria za Mikataba na Sheria nyengine zinazohusika.
Hivyo basi katika kuingia Mkataba wowote, jambo la kwanza pande hizi mbili hujitambulisha
katika kujitambulisha huko, kila upande hutakiwa kueleza taarifa zilizo za kweli ili
kutompotosha mwenzake na kila mmoja kutakiwa awe msafi kisheria kabla ya kuingia katika
Mkataba, yaani kama Mkataba ni wa Kampuni na mtu mwengine, basi Kampuni hiyo ni lazima
kwanza iwe imesajiliwa kisheria, na isajiliwe kwa mujibu wa sheria zinazohusika. Kwa lugha
nyengine na tuseme kwamba katika Mkataba wa Ukodishwaji wa Makampuni, ni lazima
Makampuni hayo yatoe taarifa za kusajiliwa kwao na anuani zao zilizo za kweli ili kutomfanya
Mkodishaji, yaani kwa hadidu yetu ni Mamlaka ya Uwanja wa Ndege katika kupokea taarifa
zisizo za kweli na za upotoshaji.
Kwa bahati mbaya sana, Kampuni hii imekiuka taratibu hizo, imetoa taarifa zisizo za kweli
katika usajili na uwepo wake kisheria. Kamati inahusisha suala hili kwa mnasaba wa Hati za
Usajili za Kampuni hii na Mkataba iliyoingia na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege. Kama
tulivyokwisha eleza hapo awali, kwamba Kampuni hii imesajiliwa Zanzibar kwa mujibu wa
Sheria za Makampuni, Sura ya 153 ya Sheria za Zanzibar na uhalali wa kuwepo kwake na
kufanya biashara ikiwa ni pamoja na kuingia katika mikataba ya ukodishwaji, kunatokana na
kwanza kusajiliwa kisheria. Lakini ukifanya marejeo ya Mkataba iliyoingia na Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege, Kampuni hii imejitambulisha kuwa imesajiliwa kwa sheria za Tanzania Bara,
yaani imesajiliwa kwa sheria ya Makampuni ya Tanzania Bara, Sura ya 168 (Company
Ordinance, cap.168). Aidha, imejieleza kwamba namba yake ya biashara iliyosajiliwa kwayo ni
63
41/2002 wakati katika Cheti cha Usajili wake Zanzibar (Certificate of Incorporation), Kampuni
hii imesajiliwa kwa namba L.1802. Kama haya hayatoshi, Taarifa zilizotolewa katika Mkataba
huo kwamba Kampuni hii imesajiliwa Tanzania Bara tarehe 27/03/2002 ni za uwongo kwa
sababu ilisajiliwa Zanzibar tarehe 3/01/2002 (Rejea Kielelezo Na.60, ukurasa wa Kwanza).
Unaweza kujiuliza, kwa nini Kamati ipoteze muda mwingi kuzungumzia kasoro hii ambayo
ungeweza kuiona ni ndogo wala haina uzito wowote. Basi kwa hadhari hiyo ndio Kamati
inapenda ifahamike wazi kwamba, kasoro hii sio ndogo katika Mikataba kama inavyofikiriwa.
Kwa mujibu wa Sheria za Mikataba, Sura ya 149 ya Sheria ya Zanzibar, kifungu cha 10(1)
kinaeleza ifuatavyo: “Makubaliano yote yatakuwa Mikataba iwapo yamefanywa kwa ridhaa iliyo huru ya wahusika
waliokuwa na uwezo wa kuingia katika Mikataba29
, kwa matarajio yaliyo halali, na kwa jambo lililo
halali, na kwa masharti ya sheria hii, hayajaelezwa kuwa batili”
Aidha, kifungu cha 14 cha Sheria hiyo kinaweka masharti ya ridhaa iliyohuru, kwamba ni ile
iliyotolewa na pande zote mbili za Mkataba ikiwa haijaathiriwa na kutolewa kwa nguvu
(coercion), kutolewa kwa ushawishi usio sahihi (undue influence); kutolewa kwa sababu ya
udanganyifu (fraud); kutolewa kwa kujifananiza isivyo haki (misrepresentation) na kutotolewa
kimakosa (mistake).
Tunachotaka kufahamisha katika sehemu hii ni kwamba, kwa mujibu wa maelezo ya kifungu cha
14(c) cha Sheria za Mikataba, Mkodishwaji amefanya udanganyifu wa kujitambulisha, kwamba
Kampuni yake imesajiliwa chini ya Sheria za Tanzania Bara wakati katika „Memorandum na
Articles of Association‟ za Kampuni hii, zinaonesha kwamba imesajiliwa Zanzibar. Hivyo,
kujieleza kwa anuani nyengine ni kumdanganya Mkodishaji. Labda hapa tueke wazi zaidi,
kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria hii ya Zanzibar Sura ya 149, Udanganyifu
maana yake na unajumuisha moja kati ya mambo yaliyoelezwa kuanzia paragrafu ya (a) hadi ya
(e), yaliyofanywa na Mhusika katika Mkataba (party to a contract) au kwa kudanganya kwake au
kwa Wakala wake, kwa nia ya kumdanganya Mhusika mwenzake wa Mkataba au kwa kupitia
kwa Wakala wake, kumfanya Mwenzake huyo kuingia katika Mkataba, ambapo katika paragrafu
ya (b) ni kule kuficha kwa ukweli ambapo Mhusika huyu anafahamu ukweli wake au anaamini
juu ya ukweli wake, aidha pia inaendana na paragrafu ya (d) inayoonesha kitendo chochote
kinachofaa kuitwa kudanganya.
Sasa tunazidi kutilia nguvu kwamba, Mkodishaji huyu sio tu kwamba kadanganya mahali
iliposajiliwa Kampuni yake na sheria iliyotumika, lakini pia udanganyifu huo unaoneka katika
nambari ya usajili, No.41/2002 na hata tarehe ya kusajiliwa huko, 27/03/2002, taarifa
zinazopigana na zilizomo katika „Memorandum and Articles of Assiciation‟ ya Kampuni hii.
Laiti kama amekosea, ilikuwa kosa moja tu kati ya matatu haya linapaswa kutendwa, lakini kwa
kuwa yeye ametenda zaidi ya makosa matatu, hii inaonesha wazi kwamba alikuwa na nia ya
kudanganya na hivyo, ni sawa na kusema kwamba Mkodishaji ameshurutishwa kuridhia
Mkataba na Mkodishaji wala sio kwa ridhaa yake (free consent). Hivyo, Mkataba huu kisheria
hauna uzito wowote, kwani hauoneshi ridhaa ya Mkodishaji kwa kuzingatia sababu tulizozitaja.
Hata hivyo, kama hoja hii haitoshi kuonesha kwamba Mkataba huu ni batili kisheria, ni vyema
tukaendelea kuangalia na hoja nyengine zinazofuata hapa chini.
29
Msisitizo ni wetu.
64
3.4.25.4 Matumizi sahihi ya Mkataba: Kwa mujibu wa Mkataba baina ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na Kampuni ya Aerotech
Limited, Kampuni hii imekodi eneo lote la Hanger kwa ajili ya kutoa huduma za parking ya
ndege (Hanger) na hivyo basi wemeruhusiwa kulitumia eneo hilo kwa kuanzisha ofisi yao
pamoja na kuweka vifaa vya matengenezo ya ndege kwa maana pia kufanya matengenezo ya
ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume. Hapa inafahamika wazi
kwamba, kwa mujibu wa Mkataba husika, matumizi yote ya Hanger husika yalipaswa yafanywe
na Kampuni hii ya Aerotech na sio mtu ama Kampuni nyengine. Na kwa hali hii, Kamati
ilimhoji Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege iwapo eneo hilo la Hanger bado
linatumiwa na Kampuni yake. Nae alikiri mbele ya Kamati kwamba wao sasa wanaitumia ofisi
tu ya eneo walilokodi ila wamewakodisha ZAN AIR ambao ndio wanashughulikia masuala ya
Hanger. Kwa maana hii, Mkodishwaji amevunja masharti ya Mkataba yanayomtaka aitumie
sehemu aliyodi kwa malengo aliyokodishwa na sio kuwapa watu wengine ama Kampuni
nyengine kwa matumizi hayo.
3.4.25.5 Kuvunjwa kwa Masharti ya Mkataba (Kodi ndani ya Kodi):
Bado Kamati inaendelea na ufafanuzi wa namna gani Mkataba huu umevunjwa na kukiukwa
masharti yake. Kwa mujibu wa kifungu cha 6.1 cha Mkataba husika, Mkodishwaji alikatazwa
kabisa kuruhusu majukumu yake kufanywa na Kampuni ama mtu mwengine, aidha alikatazwa
kumkodisha mtu ama Kampuni nyengine bila ya ridhaa ya maandishi kutoka kwa Mkodishaji.
Hata hivyo, kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aerotech
na mamlaka aliyonayo kama Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, Ndg. Said
Ndumbogani aliamua kuikodisha sehemu hiyo aliyokodishwa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
bila ya ridhaa ya maandishi kutoka kwa Mkodishaji.
Hapa pia tunataka ifahamike wazi kwamba, Capt. Said kupita Kampuni ya Aerotech
imekodishwa eneo lote la Hanger kwa USD 200 tu kwa mwezi wakati yeye ameamua
kuwakodisha ZAN AIR kwa USD 1000 kwa mwezi. Kwa maana hii unaweza kusema kwamba,
Mkurugenzi huyu wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege anaendelea kunufaika zaidi na biashara ya
Hanger aliyoikodisha kinyume na sheria kwa ZAN AIR kuliko hata mshahara anaoupata kutoka
Serikalini. Kwa bahati nzuri sana Kamati pia ilimuuliza Mkuregenzi huyu juu ya usahihi wa
kukodisha kinyume na Mkataba kuwakodisha ZAN AIR, nae alikiri mbele ya Kamati kwamba
kweli amafanya makosa hayo. Aidha alipoulizwa kama ingetokezea kulazimika ama kuacha kazi
ama kuendelea na Aerotech, alikiri kwamba hayuko tayari kuachana na Aerotech, kwani
inamnufaisha zaidi.
Aidha, pamoja na Kampuni ya Aerotech kukodisha kinyume cha Mkataba kwa kuwakodisha
ZAN AIR, jambo baya zaidi ni kutoheshimiwa kwa sheria za Mikataba ambapo, ZAN AIR nao
wamekodisha kwa Kampuni ya Zanzibar Recreation Product (ZRP) inayojishughulisha na
mafunzo ya Urubani. Yaani katika Hanger walilokodishwa Aerotech, kwanza wamewakodisha
ZAN AIR ambao wamefungua ofisi 12 zifuatazo, ikiwa ni pamoja na hiyo waliyoikodisha kwa
ZRP:
1. Ofisi ya „Chief Inspector‟ wa ZAN AIR.
2. Ofisi ya Battery Room (Lead Acid)
65
3. Ofisi ya ZAN AIR.
4. Ofisi ya Fire Point.
5. Ofisi ya Bonded Store.
6. Store Administration Technical Records.
7. Ofisi ya Chief Engineer.
8. Ofisi ya Flights Operations, Flight Watch.
9. Ofisi ya Engineering Crew.
10. Ofisi ya Aviations and Electronical Work Shop.
11. Ofisi waliyokodishwa ZRP.
Ili kujiridhisha na usahihi wa maelezo ya hapo juu, Kamati ilimuita Mkurugenzi wa Kampuni ya
ZAN AIR, ambae aliithibitishia Kamati kwamba anaitambua Kampuni ya Aerotech na ndio
iliyowakodisha na wanalipia USD 1000 kwa kila mwezi. Kama ushahidi huu hautoshi, Kamati
imepatiwa Mkataba baina ya Kampuni ya Aerotech na Kampuni ya ZAN AIR (Kielelezo Na.61)
unaoonesha wazi ukweli wa hoja hii. Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria, Mkataba huu baina ya
Aerotech na ZAN AIR ni batili kisheria na hauna mashiko yoyote, kwa sababu Aerotech hana
uwezo wa kukodisha mtu mwengine wakati yeye ni Mkodishwaji, na amefanya hivyo bila hata
kupata ridhaa ya Mkodishaji.
Pamoja na uvunjwaji huu wa Mikataba na Sheria zinazoiongoza, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
imebaki kimya na haina hatua yoyote iliyoichukua na zaidi imethubutu hata kuipotosha Kamati
juu ya usahihi wa ukweli ulivyo. Lakini bado inabakia suala la kujiuliza kila mtu, kwamba ni
kweli inawezekana kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kujichukulia
hatua dhidi yake, wakati huo huo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni iliyohusika awali na
uvunjaji wa Makatabaa, yaani Kampuni ya Aerotech.
Pamoja na hali yote tuliyoieleza juu, kuna hekima moja ameitumia Mkurugenzi huyu, nayo ni
kujiondosha katika maslahi ya Kampuni na Mamlaka ya Uwanjwa wa Ndege katiak kofia mbili
alizozivaa wakati mmoja. Hivyo basi ili kupunguza kasoro hii, Captain Said aliieleza Kamati
kwamba, hivi sasa tayari Kampuni yao imeshamchagua Ndg. Rajab Zubeir Omar kupita barua ya
tarehe 27/12/2007 yenye kumbu kumbu namba ATCL/12/01 kuwa Mkurugenzi Mtendaji na
hivyo, tayari ameshajiondoa katika nafasi ya Ukuregenzi Mtendaji wa Kampuni tokea mwaka
2007 (Kielelezo Na.62). Hivyo, hakuna haja ya kuonesha udhaifu wake wa kuwa na maslahi ya
pande zote mbili wakati mmoja. Hata hivyo, majibu haya hayajakubaliwa na Kamati na
hayawezi kukubaliwa na mtu mwengine yeyote mwenye ufahamu angalau wa kiwango cha
kawaida.
3.4.25.6 Muda wa Mkataba: Hapa hatuendelei kuzungumzia udhaifu ama ubatili wa Mkataba kisheria, lakini tunataka tueke
wazi suala la muda uliokubalika katika Mkataba huu baina ya Aerotech na Mamlaka ya Uwanja
66
wa Ndege. Kwa mujibu wa kifungu cha 2.0 cha Mkataba, Mkataba huu ni wa miaka saba, na
umeanza tarehe 1/07/2005 na kumalizika tarehe 1/07/2005. Kwa maana hii, Mkataba huu bado
uko hai kisheria na una nguvu zote zinazohusika.
3.4.25.7 Gharama za Kodi na Huduma: Pamoja na ukubwa wa eneo walilokodi, Kampuni ya Aerotech wanalipa USD 200 kwa mwezi na
ni sawa na kulipa USD 2,400, ambazo ni sawa na Tsh. 3,840,000 kwa mwaka. Pamoja na
uchache huu wa kodi inazolipa Kampuni hii, malipo hayo hayalipwi kwa wakati muafaka.
Captain Said alikiri mbele ya Kamati kwamba Kampuni yake inadaiwa miaka mitatu bila ya
kulipa, yaani tokea mwaka 2007 hadi 2010 hawajalipa, ingawaje waliendelea kulipa kuanzia
mwaka wa 2011. Hali hii inakwenda kinyume na maelekezo ya kifungu cha 1.1 cha Mkataba,
kinachoitaka Kampuni hii ilipie kodi mwanzo wa kila mwezi, kama hapa tunavyokinukuu:
“The Lessee shall pay in advance a monthly agreed rent to the lessor inclusive of any
value added taxes”.
Tofauti na ZAN AIR waliokodi kutoka kwa Aerotech, wao wanalipa kodi kila mwezi USD 1000
(Kielelezo Na.63). Hii ina maana kwamba, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
anaemiliki Kampuni ya Aerotech, hajali wajibu wa Kampuni yake kulipa kodi Serikalini na
badala yake anajali zaidi na yuko mkakamavu kuinufaisha Kampuni yake na hayuko tayari hata
siku moja Kampuni hiyo kutolipwa kodi na ZAN AIR. Wakati Kamati ilipokutana na
Mkurugenzi wa ZAN AIR, aliithibitishia Kamati kwa maneno na ushahidi wa maandishi
kwamba wao wanalipa kodi kila mwezi kwa Kampuni ya Aerotech iliyowakodisha Hanger hiyo
(Rejea Kielelezo Na.63)
Aidha, Mkurugenzi huyu alipoulizwa ni lini Kampuni yake ililipia gharama za Maji, Umeme na
Simu (Utility) alieleza kwamba hawalipii. Maelezo haya yanapinga maelekezo ya kifungu cha
3.1 cha Mkataba ambacho kinamtaka Mkodishwaji alipe gharama za Maji, Umeme na Simu
tofauti na gharama za kodi na zinatakiwa zilipwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano.
3.4.26 ZAN AIR LTD.
Pamoja na Kampuni hii ya ZAN AIR kukodi Hanger katika Mkataba iliyoingia na Kampuni ya
Aerotech-Zanzibar, pia imeingia tena na Mkataba na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa kukodi
eneo lenye ukubwa wa square meter 17.20 kwa ajili ya kuendesha biashara ya utoaji wa huduma
ya usafiri wa ndege (Air Line Operator). Katika Mkataba huu, ni vyema tukayaangalia masuala
yafuatayo:
3.4.26.1 Muda wa Mkataba.
Tofauti na Mikataba mingi iliyopita, Mkataba huu umeanza tarehe 01/01/2011 na kumalizia
tarehe 31/12/2011. Pamoja na ukweli kwamba hivi sasa, wakati tunaandika ripoti hii tayari
umeshapitwa na wakati, lakini wakati Kamati inafanya kazi zake katika Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege mwezi wa Septemba mwaka 2011, Mkataba huu ulikuwa halali na hai kisheria (Kielelezo
Na.64).
3.4.26.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kwa maelezo ya kifungu cha 6.2 cha Mkataba, Kampuni ya ZAN AIR wanalipia USD 1,290
sawa na Tsh. 2,064,000 kwa mwaka na ni sawa na kulipa Tsh. 172,000 kwa mwezi. Kamati
67
imejiridhisha kwamba wanalipa kodi hiyo kwa kuchukua kigezo cha mwaka 2010 ambapo
walilipa kupitia risiti namba 224231. Kuhusu malipo ya gharama za umeme, maji na simu,
Tsh.150,000 zinapaswa zilipwe kwa kila mwezi, ingawaje Kamati haikupata taarifa za uhakika
wa malipo hayo.
3.4.26.3 Kuhusu saini ya Mkataba.
Kama ilivyokwisha jitokeza takribani kwa mikataba yote iliyoingiwa na Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege juu ya muda wa kusainiwa kwake, Mkataba huu nao umetiwa saini na upande wa
Mkodishaji tarehe 20/05/2011 badala ya tarehe 01/01/2011 iliyoainishwa katika Mkataba na kwa
upande wa Mkodishwaji ametia saini yake tarehe 19/08/2011, takriban miezi minane ndio
Mkataba huu unakamilika kisheria wakati imebakia miezi minne tu kumaliza muda wake.
3.4.27 Tropical Air (Z) Ltd:
Kampuni ya Tropical Air (Z) Ltd imeingia katika Mikataba miwili tofauti katika eneo la Uwanja
wa Ndege na kwa hivyo, katika ufafanuzi wetu huu tutaeleza mikataba hiyo kwa mnasaba wa
kodi husika. Kwanza wamekodi square meter 10.44 kwa ajili ya kuendesha biashara ya utoaji wa
huduma ya usafiri wa ndege (Air Line Operator). Katika Mkataba huu, ni vyema tukayaangalia
masuala yafuatayo:
3.4.27.1 Muda wa Mkataba.
Kifungu cha 2.1 cha Mkataba huu, Mkataba huu umeanza tarehe 01/01/2010 na kumaliza muda
wake tarehe 31/12/2010 na kwa lugha nyengine, Mkataba huu umeshamaliza muda wake wa
kutambuliwa kisheria na hauna athari yoyote kisheria (Kielelezo Na.65). Hata hivyo, Kamati
ilipewa taarifa zisizo za kweli kwa mujibu wa orodha iliyokabidhiwa kwa Kamati, inayoonesha
kwamba Mkataba huo umeanza tarehe 1/1/2011 hadi 31/12/2011 (Rejea Kielelezo Na.30). Na
hata Kamati ilipowahoji Viongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, walisisitiza ukweli wa
maelezo ya orodha kinyume na maelezo ya Mkataba husika, na kwa kuwa Kamati ilitaka
kupatiwa Mkataba uliohai kisheria baada ya Mkataba huu kufahamu mbele ya kikao husika
kwamba tayari umeshapitwa na muda wake, Uongozi wa Mamkala ya Uwanja wa Ndege
umeshindwa kuuwasilisha.
3.4.27.2 Malipo ya Kodi na Huduma.
Kwa maelezo ya kifungu cha 6.2 cha Mkataba, Kampuni ya Tropical Air wanalipia USD 783
sawa na Tsh. 1,252,800 kwa mwaka na ni sawa na kulipa Tsh. 104,400 kwa mwezi. Kamati
imethibitishiwa kulipa kodi hiyo kwa mwaka 2010 kupitia risiti namba 224234. Kuhusu malipo
ya gharama za umeme, maji na simu, Tsh.150,000 zinapaswa zilipwe kwa kila mwezi, ingawa
Kamati haikupatiwa uthibitisho wa malipo haya.
3.4.27.3 Kuhusu saini ya Mkataba.
Kama ilivyokwisha jitokeza takribani kwa mikataba yote iliyoingiwa na Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege juu ya muda wa kusainiwa kwake, Mkataba huu nao umetiwa saini na upande wa
Mkodishaji tarehe 25/02/2010 badala ya tarehe 01/01/2010 iliyoainishwa katika Mkataba na kwa
upande wa Mkodishwaji ametia saini yake tarehe 16/03/2010, takriban miezi minane ndio
Mkataba huu unakamilika kisheria wakati imebakia miezi minne tu kumaliza muda wake.
68
3.4.28 Tropical Air (Z) Ltd:
Mkataba wa pili uliopaswa kuingiwa baina ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na Tropical Air
(Z) Ltd, ni wa ukodishaji wa Banda/Karakana la kutengenezea Ndege (Aircraft Hanger). Kabla
ya kufafanua dhana ya Mkataba husika, ni vyema ikafahamika kwamba, wakati Orodha ya
Wakodishwaji ikiwasilishwa kwa Kamati, katika kikao cha pamoja baina ya Kamati na Uongozi
wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege kilichofanyika tarehe 07/09/2011, kuanzia saa 3:00 asubuhi, Kamati ilianza kupata
maelezo yanayohusu kodi ya Tropical Air (Z) Ltd kupitia orodha hiyo ya Wakodishwaji
iliyowasilishwa kwa Kamati (Rejea Kielelezo Na.30), Mkodishwaji wa 38 katika Orodha hiyo,
ni Tropical Air, ambapo katika orodha hii hakukuwa na maelezo ya ukubwa wa eneo alilokodi,
muda wa Mkataba wake wala gharama za kodi anazolipa kwa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege,
yaani hazijaweza kuwasilishwa kwa Kamati kupitia kwenye orodha hiyo, kwa maana,
ukilinganisha na Wakodishwaji wengine, Kampuni ya Tropical Air haijuulikani imekodi ukubwa
gani wa eneo, wala Mkataba wao haujuulikani wala gharama za kukodishwa kwao, hii kwa lugha
nyengine ni kwamba, katika Kikao hicho, Mamlaka imeshidwa kuwasilisha taarifa hizo na pia
imeshindwa kuwasilisha Mkataba wa kukodisha Banda/Karakana hiyo ya Ndege (Aircraft
Hanger) walioingia na Kampuni ya Tropical Air (Z) Ltd.
Kitu cha kwanza ilichofanya Kamati ni kutembelea maeneo yote ya ukodishwaji kwa mnasaba
wa orodha iliyowasilishwa, na Kamati ilipofika katika eneo la Hanger hiyo, ilishangazwa sana
kwa Mkodishwaji huyu kujenga Ofisi 17 katika eneo hilo na eneo lililobakia akifanya shughuli
ya Hanger husika, yaani akilaza ndege na kuzifanyia matengenezo. Aidha, Kati ya ofisi hizo 17
zilifanywa (partition), Tropical Air walianzaisha Chuo cha Marubani (Flying School) na
wanaeleza kwamba kimeanza kwa muda mrefu sasa na wamefanikiwa kutoa Marubani wengi wa
ZAN AIR, TROPICAL na marubani kadhaa wazalendo na wakigeni. Aidha, Tropical Air
wameajiri wafanyakazi wengi katika Ofisi hizo, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wawili wa
Kigeni wanaofanya kazi kutoka Zimbabwe na Philipine. Kwa namna yoyote, Kamati iliona ipo
haja ya kukutana na Mmiliki wa Kampuni hii, Capt. Omar Haji Nura, Mkurugenzi wa Tropical
Air, ambapo Kamati ilifanya mahojiano nae kuhusiana na Ukodishwaji wa Hanger hiyo tarehe
15/09/2011 na Kamati ilitaka kujua kwa taratibu zipi alifanikiwa kuikodi Hanger hiyo, na hivyo,
Kamati inaona ni vyema tukafahamu, taratibu hizo vipi zilifuatwa kama ifuatavyo:
3.4.28.1 Hatua za Ujenzi wa Hanger kama zilivyochukuliwa na Capt. Omar Haji Nura:
Capt. Omar Haji Nura, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tropical Air (Z) Ltd, alikuwa na azma ya
kujenga Hanger hiyo tokea mwaka ya 2002, na hatua ya mwanzo aliyoichukua ni kuomba ruhusa
ya ujenzi wa Hanger kwa iliyokuwa Idara ya Anga, ambapo kwa mujibu wa taarifa zilizofika
kwa Kamati, mazungumzo baina ya Capt. Omar na Mkurugenzi wa Idara ya Anga yalianza
mwaka 2002, ambapo katika barua ya tarehe 8/11/2002, Ndg. M.M. Hanif, aliyekuwa
Mkurugenzi Idara ya Anga alimjibu kwa barua Mkurugenzi wa „Tropical Air‟ yenye kumbu
kumbu namba DA/FE/004/6 kwamba Idaya ya Anga ilikubali maombi yake aliyoyawasilisha
kabla, yanayohusu ujenzi wa Banda la Kutengeneza Ndege (Aircraft Hanger) kwa mnasaba wa
ramani aliyoiambatanisha na maombi hayo, kwa sharti la kufika Idarani siku ya Jumanne tarehe
12/11/2002 saa 4:00 asubuhi ili wazungumze jinsi gani hali ya ujenzi huo itakavyokamilishwa
(Kielelezo Na.66).
69
Mnamo tarehe 25/11/2002, Idara ya Anga, chini ya aliekuwa Mkurugenzi wake, Ndg. M.M.
Hanif, ilimuandikia tena barua Mkurugenzi wa Tropical Air, ikiendelea kusisitiza kwamba,
imemruhusu Mkurugenzi huo wa Tropical Air kuanza Ujenzi wa Banda la Kutengenezea Ndege
(Kielelezo Na.67). Na kwa kuzingatia barua ya tarehe 28/11/2002 yenye kumbu kumbu namba
DA/PEN/005/5, Idara ya Anga bado iliendelea na kuukubali ujenzi huo kwa masharti kwamba
Capt. Omar afanye malipo ya fidia kwa wakulima mbali mbali waliokuwa na mazao yao katika
eneo alilolikusudia kujenga Banda hilo la Hanger, kwa thamani ya Tsh. 159,575/- (Kielelezo
Na.68). Kwa kuzingatia masharti yaliyotolewa na haja ya kujenga Banda hilo, Capt. Omar
alikabidhi fedha hizo za fidia mara mbili zaidi ya fidia iliyopendekezwa na Idara ya Anga, kwa
kukabidhi Tsh. 319,150/- kupitia barua ya tarehe 02/12/2002 kwa Idara ya Anga ili zitumiwe
kuwalipa wananchi wenye vipando vyao mbali mbali (Kielelezo Na.69).
Mbali na fidia hizo zilizoelezwa hapo juu, Kampuni ya Tropical Air iliingia Mkataba na Idara ya
Anga ya kuwalipa fidia wananchi mbali mbali wenye vipando vyenye thamani ya Tsh.
2,531,250/- , Mkataba ambao pia ulielezea utaratibu utakaotumika wa kuwalipa fidia wananchi
hao. Aidha, Mkataba ulifafanua namna ya kurejeshwa kwa fedha zilizotumika kulipia fidia kwa
utaratibu wa kutolipa kodi kwa thamani ya fidia waliyoitoa na kuwalipa wananchi. Hii ina
maana, kwa kuwa Kampuni ya Tropical Air ilitumia fedha zake kulipa fidia mbili kwa wananchi,
yaani zile Tsh. 319,150 walizolipa fidia awamu ya kwanza, na Tsh. 2,531,250 waliyolipia fidia
kwa awamu ya pili, ni sawa na Tsh. 2,850,400/-, ambazo nanma ya kulipwa kwake ni
kusamehewa kodi ya miaka mitatu (kwa kodi ya Tsh. 896941.65 kwa mwaka) baada ya
kukamilisha ujenzi wa Banda hilo na kuanza kazi iliyokusudiwa katika Ardhi ambayo
iligharamiwa kwanza kwa ulipwaji wa fidia. (Kielelezo Na.70).
Hatua nyengine aliyochukuwa Capt. Omar Haji Nura, Mkurugenzi wa Tropical Air (Z) Ltd ni
kuingia Mkataba wa Ukodishwaji wa Ardhi hiyo aliyoitumia kujenga Hanger. Mkataba ambao
umeingiwa na Kampuni ya Tropical Air (Z) Ltd na iliyokuwa Idara ya Anga, tarehe 1/1/2005. Ili
tuweze kufahamu angalau kwa uchache kilichomo katika Mkataba huo, ni vyema sasa
tukauangalia Mkataba huo katika maeneo yake ya msingi.
3.4.28.2 Mkataba wa Ukodihaji Ardhi (Land Lease) Baina ya Idara ya Anga na
Kampuni ya Tropical Air (Z) Ltd: Mkataba huu ni wa miaka 16, kuanzia tarehe 1/1/2005 hadi tarehe 31/12/2021 (Kielelezo Na.71),
ambapo Kampuni ya Tropical Air, wanalipia kwa mwaka Tsh. 303,750/- sawa na Tsh. 25,312.5
kwa mwezi. Kwa lugha hii, Kampuni hii inalipia gharama za aina mbili, malipo ya kodi ya
Hanger, ambayo wamekodishwa baada ya kutumia gharama zao za ujenzi wa hanger hiyo na
gharama za fidia kwa wananchi waliokuwa na vipando vyao, kodi ambayo wangelipaswa kuilipa
baada ya miaka mitatu ya ujenzi kukamilika. Na malipo ya pili ni kodi ya ardhi (land lease)
wanayolipia Tsh. 303,750/- kwa kila mwaka, isipokuwa ifahamike wazi kwamba, kodi zote hizi
zinalipwa kwa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, wakati huo ikijuulikana, Idara ya Anga.
Jambo jengine la msingi kufahamika katika Mkataba huu wa Kodi ya Ardhi ni kwamba, kwa
mujibu wa kifungu cha 4(i) cha Mkataba huo, kodi hiyo ilitakiwa ifanyiwe mapitio na
mabadiliko kabla ya miaka mitatu tokea kuanza kwa kodi, lakini kiwango kitakacholipwa baada
ya mapitio ama mabadiliko ya kodi hiyo, ni makubaliano baina ya Mkodishaji na Mkodishwaji,
na ikishindikana kukubaliana, basi watafute Wasuluhishi wawili, ambapo kila Msuluhishi mmoja
atachaguliwa na kila upande.
70
3.4.28.3 Mamlaka ya kukodisha Ardhi ya Serikali (Lease of Public Land) kisheria:
Tunapenda kidogo tuuchambue Mkataba huo kwa mnasaba wa sheria. Katika Mkataba
uliowasilishwa kwa Kamati, maelezo ya awali ya Mkataba huu ambayo ni muhimu na
yanamtambulisha Mkodishaji yanasomeka kama ifuatavyo:
“This lease is made the FIRST JANUARY Two Thousand and five BETWEEN THE Department of
Aviation on behalf of the Ministry of Communications and Transport of P.O.BOX 266 Zanzibar
(Hereinafter referred to as lessor) on the part and Tropical Air (z) Ltd of P.O.Box 3188 Zanzibar
(Hereinafter referred to as the Company) on the other part”
Tunachotaka kifahamike katika maelezo hayo ya Mkataba ni kwamba, Mkodishaji wa Ardhi
iliyotumiwa na Kampuni ya Tropical Air kwa ajili ya Karakana ya Matengenezo ya Ndege
(Aircraft Hanger) ni Idara ya Anga (ambayo sasa ni Mamlka ya Uwanja wa Ndege) na katika
Mkataba huu, Idara hii inaiwakilisha Serikali, na katika sehemu ya kutia saini Mkataba huu, kwa
niaba ya Idara ya Anga, amesaini Mkurugenzi wa Idara hiyo. Hii ina maana Mkodishaji wa
Ardhi hii, ni Idara ya Anga.
Kwa bahati nzuri sana suala la Ardhi linasimamiwa na Sheria za Ardhi, na Sheria maarufu ni
Sheria ya Umiliki wa Ardhi, Namba 12 ya mwaka 1992. Kifungu cha 46 cha Sheria hii, kama
kilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 11 ya 2010, kifungu hicho cha 46(1) sasa
kinasomeka kama ifuatavyo:
“The Minister may lease any Public land to any person, Zanzibari or non-Zanzibari,
provided that the Minister shall not lease a public land which comprises a right of
occupancy without the consent of the holder of such right of occupancy”
Kwamba mwenye mamlaka kisheria ya kukodisha ardhi ya Serikali, ni Waziri anaeshughulikia
masuala ya Ardhi, kama alivyotafsiriwa katika kifungu cha 2 cha Sheria hiyo kwamba, „Waziri‟
Maana yake ni Waziri anaeshughulikia masuala ya Ardhi. Labda tunaweza kushughulishwa
kidogo na suala la fidia ambalo Mkurugenzi wa Tropical Air (Z) ltd amewalipa wananchi,
tukafahamu kwamba kitendo hiki kinaifanya ardhi hii isiitwe ardhi ya Serikali. Ni vyema sasa
tuondoshe ufahamu huo kwa kukafanya marejeo ya kifungu cha 3 cha Sheria hiyo, Namba 12 ya
mwaka 1992, ambayo inaeleza kwamba ardhi yote ikiwa inatumiwa na watu ama isitumiwe ni
mali ya Serikali. Na kauli hii inaweza kuepushwa kuathiri haki miliki iliyosajiliwa kisheria
ambayo inamfanya mtu aliyenayo kumiliki ardhi, lakini kwa maslahi ya kifungu hiki, haizuii
Serikali kuitumia inapotaka isipokuwa tu imewekewa utaratibu katika Sheria hii.
Jambo la msingi hapa ifahamike kwamba, ardhi hiyo ni mali ya Serikali, kitendo cha kuwalipa
fidia wananchi waliokuwa na vipando vyao, kulikofanywa na Tropical Air ni sawa na kufanywa
na Idara ya Anga, ukizingatia kwamba wamekodishwa Banda la Hanger kwa kufidia gharama
zao walizozitumia katika kulipa fidia hiyo na ndo mana kwa kipindi cha miaka mitatu,
hawakulipa kodi. Na kwa hali hii, pia ulipwaji huo wa fidia hauhalalishi kwamba ardhi hiyo ni
mali ya mtu binafsi bali ni ya Serikali. Kwa maana hii, Mamlaka ya Ukodishaji Ardhi ni ya
Serikali, inayosimamiwa na Wizara inayoshughulikia masuala ya Ardhi, na wala sion na Wizara
ya Mawasiliano na Uchukuzi wala Idara ya Anga. Hivyo basi, maamuzi ya Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi kuingia katika Mkataba wa kukodisha ardhi hiyo yamefanywa
kinyume na Sheria, kwa sababu yamekengeuka kifungu cha 46 cha Sheria Namba 12 ya mwaka
1992, Sheria ambayo hata baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 2010, imeendelea kutoa
71
malmaka ya ukodishwaji wa ardhi ya Serikali kwa Waziri anaehusika na masuala ya Ardhi kama
hapa tunavyonikuu:
“The Minister may lease any public land which does not comprise a right of occupancy to
any person, Zanzibari or non Zanzibari”.
3.4.29 BP TANZANIA LTD:
Kamapuni ya BP TANZANIA LTD imeingia Mikataba ya aina mbili. Mkataba wa kwanza
unahusiana na Ukodishwaji wa ardhi (land lease) iliyoingia na Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi (ambayo sasa ni Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano) na Mkataba wa pili ni wa
kutoa huduma ya bishara ya mafuta inayoifanya katika eneo la Uwanja wa Ndege, ambapo
wameingia na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege (wakati huo ikiwa Idara ya Anga) (Kielelezo
Na.72).
3.4.29.1 Mkataba wa Kukodi Ardhi (Land Lease):
Kama tulivyosema hapo awali, kwamba Kampuni ya BP TANZANIA LTD, imeingia Mkataba
wa kukodi ardhi kwa miaka 33, kuanzia tarehe 21/09/1993 hadi mwaka 2026. Mkataba huu
umeingiwa baina ya Wizara ya Mawasiliano na Ujenzi na Kampuni hii, ambapo katika paragrafu
ya kwanza ya Mkataba huo inasomeka kama ifuatavyo:
“The Concessionaire (BP TANZANIA LTD)30
has a Land Sub- Lease Agreement for a period of 33 years
from 21st September 1993 with the Ministry of Communications and Trasport upon land aviation fuel depot
and buildings have been construed for the purpose of supplying aviation fuel to operators in Zanzibar”
Aidha, jambo jengine la msingi kufahamika kwa mujibu wa maelezo hayo, ni kwamba, Ardhi
hiyo imekodishwa kwa Kampuni hii, kwa ajili ya kujenga kituo cha Mafuta (fuel depot) na
majengo mengine yatakayotumika katika utoaji wa huduma hiyo.
Aidha, ni vyema pia ikafahamika kwamba, Kamati haikupatiwa Mkataba wa Kukodishwa ardhi
hiyo, ingawaje ilipofanya ziara ya eneo husika na kukutana na Mhusika, Kamati iliomba
kupatiwa „Documents‟ zote zilizohusika na ukodishwaji wake, ikiwa ni pamoja na Mkataba huu,
na Kamati pia iliomba kupatiwa Mkataba huo katika kikao cha pamoja na Mamlaka ya Uwanja
wa Ndege na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Hata hivyo, Kamati
imepatiwa Mkataba huu wa Kutoa Huduma ya Mafuta (Rejea Kielelezo Na.72), ambapo katika
maelezo hayo tuliyoanukuu hapo juu, Kamati inajiridhisha kwamba maelezo kwamba BP
wamekodi ardhi ni sahihi kwa mnasaba wa Mkataba huu na kwa mujibu wa mazungumzo baina
ya Kamati na wahusika.
Jambo kubwa ambalo Kamati inaendelea kulisisitiza kwa mujibu wa maelezo ya hapo juu ni
kwamba, kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi, kifungu cha 46 cha Sheria Namba 12 ya mwaka 1992,
Mamlaka ya kukodisha ardhi ya Serikali, kama ilivyo kwa ardhi hii tunayoizungumzia, ni ya
Waziri anaeshughulikia masuala ya ardhi na wala sio Waziri ama Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi. Aidha, kwa mnasaba wa maelezo ya hapo juu, maneno “The
Concessionaire has a Land Sub-Lease Agreement….” Yanaleta tafsiri nyingi, moja kati ya hizo
ni kwamba ardhi hiyo iliyokodishwa, imekodishwa kwa mara ya pili (sub-lease), yaani kuna
wakodishwaji wawili katika ardhi moja. Kwa tafsiri hii, ama Wizara ya Mawasiliano na
30
Msisitizo ni wetu.
72
Uchukuzi imekodi ardhi hiyo nayo ilaamua kuikodisha kwa Kampuni ya AIR BP ama maelezo
haya yameingia kimakosa ikikusudiwa kwamba ni „Lease‟ ya moja kwa moja kutoka Wizara hii.
Kwa hali inayosomeka katika kifungu hicho cha Mkataba inaonesha wazi kwamba inayopingana
na maelekezo ya kifungu cha 47(3) cha Sheria Namba 12 ya mwaka 1992 kabla hakijafanyiwa
marekebisho na Sheria Namba 11 ya 2010, ambapo ilikataza ardhi inayokodishwa kukodishwa
kwa mara nyengine (sub-lease). Hii ina maana, marekebisho ya kifungu hiki yanayoruhusu sasa
Ardhi ya Serikali iliyokodishwa na kuendelezwa kuweza kukodishwa tena (sub-lease) yamekuja
mwaka 2010, wakati Mkataba huu unafungwa (1993) ilikuwa ni kosa kisheria, na kwa kuwa
Sheria hii bado haijafutwa, na matendo yaliyotendwa kabla ya marekebisho hayo ya 2010
yanauhalali kisheria, ni wazi kwamba kwa tafsiri hii, kosa limetendeka.
3.4.29.2 Mkataba Unaohusu Utoaji wa Huduma ya Mafuta wanayoifanya katika eneo
la Uwanja wa Ndege:
Mkataba wa pili tunaouzungumzia sasa ni huu wa Utoaji wa Huduma ya Mafuta ulioingiwa
baina ya Idara ya Anga na Kampuni ya AIR BP. Mkataba huu ni wa kila mwaka, unaohusiana na
huduma ya mafuta inayofanywa na Kampuni ya BP TANZANIA LIMITED, na umeingiwa
baina ya Kampuni hii na Idara ya Anga (ambayo sasa ni Mamlaka ya Uwanja wa Ndege).
Mkataba huu ni wa miaka miwili, kuanzia tarehe 1/1/2010 hadi tarehe 31/12/2012. Na kwa hali
hii, Mkataba huu bado uko hai na una nguvu zote kisheria. (Rejea Kielelezo Na.72).
Malipo yanayohusiana na Mkataba huu yanalipwa kwa kila mwaka kwa Tsh. 200 kwa kila Lita
ya mafuta wanayoiuza katika Jet A-1 na „Avgas Fuel‟ katika Uwanja wa Ndege huo, ambapo
kwa mujibu wa kifungu cha 3.1 cha Mkataba husika, malipo hayo yanalipwa katika kipindi cha
mwisho wa mwaka baada ya mapato yote yanayotokana na kazi hiyo kufahamika. Kamati
imehitaji kujiridhisha juu ya malipo hayo kwa kutaka kupatiwa ushahidi wa mwaka 2010,
ambapo iliweza kuthibitishiwa kwa njia ya risiti namba 445064.
Aidha, kuhusiana na gharama za maji, umeme na simu, Kampuni hii wanalazimika kulipa katika
muda ambao haukuelezwa katika Mkataba huu, isipokuwa kima cha kulipa kitaamuliwa na
Meneja wa Uwanja wa Ndege, muda hadi muda. Ingawaje Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
haikuithibitishia Kamati namna malipo haya yanavyofanyika, kama ilivyothibitisha kwa malipo
ya kodi.
3.4.30 E A MEDIA:
Kampuni ya E A MEDIA inajishughulisha na biashara za aina mbili katika eneo la Uwanja wa
Ndege na hali hii imeifanya kuingia katika Mikataba miwili tofauti yenye masharti
yanayotafautiana pia. Mkataba wa kwanza unahusu Matangazo ya biashara yaliyopo katika eneo
lote la Uwanja wa Ndege na Mkataba wa Pili unahusiana na utoaji wa huduma ya maegesho ya
magari (Parking). Katika utaratibu wetu huu, tutaieleza Mikataba hiyo tofauti katika maeneo
yake ya msingi ili iweze kufahamika kwa urahisi.
3.4.30.1 Mkataba wa Matangazo ya Biashara:
Mkataba huu umesainiwa tarehe 17/10/2008 baina ya Kampuni ya E A Media limited
ikiwakilishwa na Ndg. Branko Gnjatic na Ndg. Adrew Johnstone na Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Zanzibar (Zanzibar Internationaal Airport) ukiwakilishwa na Mkurugenzi wa
Uwanja wa Ndege, Ndg. Malik Mohammed Hanif na Maneja wa Uwanja wa Ndege-Ndg. Badru
Amani Juma (Kielelezo Na.73). Unaweza ukashtuka kidogo unapoambiwa kwamba Mkataba
73
huu umeingiwa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar (Zanzibar International
Airport), na suala lako la kwanza utataka kujua, je ni kweli Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Zanzibar unaweza kuingia Mkataba wa kisheria na Kampuni hiyo? Na labda ungejiuliza, je
Uwanja wa Ndege wa Zanzibar ni chombo gani na kina mamlaka gani ya kuingia katika
Mkataba wa kisheria, lakini je kimeanzishwa lini na kinafanya kazi gani?
Suala hili katika Sheria za Mkataba ni muhimu sana, kwa sababu aliepewa uwezo wa kuingia
Katika Mikataba ni mtu mwenye uwezo wa kuingia katika Mkataba (competent to contract) ama
Mamlaka (chombo cha kisheria) iliyoanzishwa kisheria (Legal person). Ukifanya rejea ya
Mikataba yote tuliyoizungumzia awali, imeingiwa na Serikali ikiwakilishwa na Idara ya Anga,
kwa maana nyengine imeingiwa na Wizara ya Mawasilaino na Uchukuzi ikiwakilishwa na Idara
ya Anga. Tunapenda kukumbushia kwamba, kama tulivyoeleza hapo awali, kwamba moja kati
ya udhaifu wa Mikataba hii ni kuingiwa na Idara ya Anga ambayo ilikuwa chini ya Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi, tena kibaya zaidi imesainiwa na Meneja wa Uwanja huo. Jambo
lililopaswa kufanywa kisheria, ni kusainiwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi. Pamoja na hali hii, Mkataba huu umezidi kukiuka taratibu hizo, kwamba umeingiwa
na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, chombo ambacho hakipo wala hakifahamiki
kisheria. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ni jina lililotumika kuitwa uwanja huo kabla ya jina
lake la sasa „Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume‟.
Tatizo hili ni wazi limesababishwa na Mkataba huu kuandaliwa na Kampuni ya E A Media
Limited, ikijiweka katika nafasi ya Ukodishaji. Mkataba huu wa pegi moja, ni tofauti hata
kimuundo na Mikataba yote iliyotangulia (ingawaje hoja hii sio ya msingi kisheria) katika hali ya
kawaida inatoa picha kwamba, umeangalia zaidi maslahi ya Kampuni ya E A Media Limited na
badala yake, Idara ya Anga ikiburuzwa kukubaliana na masharti ya Kampuni. Kama hili
halingekubalika na akili za kawaida, basi ni vyema tukazidi kuupitia Mkataba huu katika maeneo
yake ya msingi.
3.4.30.2 Matumizi ya sehemu iliyokodishwa:
Mkataba huu umeingiwa kwa matarajio ya kisheria (consideration) ya Kampuni hiyo kujenga
kenopi ya muda (temporary canopy) kwa kutumia gharama zao katika eneo la uwanja wa ndege
na baada yake wataruhusiwa kuweka matangazo ya biashara katika kenopi hiyo na kujenga
bango la kuwekea matangazo ( billboard) juu ya kenopi hiyo yenye mita 3 kwa urefu na mita 60
kwa upana. Gharama za ujenzi wa kenopi na milihimili yake ya kushikia ni Tsh. 265,986.000/
ambazo zote kwa pamoja zimegharamiwa na Kampuni ya E A Media Limited, Kampuni ya
mwanzo yenye kuendesha biashara ya matangazo ya namna hiyo yenye ofisi ya kudumu
Zanzibar. Baada ya kukamilika kwa Mkataba huo na kuanza ujenzi, kwa ufupi, mwezi wa July
2009, ndio ujenzi wa kenopi ulipokamilika.
3.4.30.3 Masharti ya Mkataba:
Katika Mkataba huo, masharti manne makuu yameainishwa na kwa kuwa Mkataba huu
unatofautiana na Mikataba iliyopita, katika Muundo na Maudhui yake, ni vyema masharti hayo
tukayaeleza yote kama ifuatavyo:
o Kwamba, Kampuni ya E A Media Limited watakamilisha ujenzi wa kenopi
tuliyoitaja hapo juu katika kiwango kinachokubalika kimataifa ili kikidhi mahitaji
74
ya abiria wanaowasili na kuondoka katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa
Zanzibar.
o Kwamba, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (Kama tulivyosema hapo juu,
ikikusudiwa Idara ya Anga) utatoa sehemu ya kutosha isiyo na vikwazo ya
kujengwa kwa kenopi hiyo ili Kampuni hiyo iweze kukamilisha na kuiimarisha
kenopi hiyo.
o Kwamba, Idara ya Anga (kama ilivyokusudiwa) itatoa kodi ya miaka 5 kwa
Kampuni hiyo na kuwa na uhuru wa kuiongeza miaka 5 ya ziada, huku
ikisamehewa kodi ya mwaka mmoja tokea siku ambayo ujenzi huo utakamilika.
(Hapa imekusudiwa kwamba, baada ya miaka 5 ya awali, Kenopi hiyo itakuwa
miliki ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege).
o Kwamba, wakati wa kukodishwa kwake, Kampuni ya E A Media Limited
itakuwa huru kukataa kuruhusu upya (renewal) tangazo lolote la biashara31
.
3.4.30.4 Mapato ya Mkataba:
Kampuni ya E A Media Limited itakuwa na haki ya kukusanya mapato yatokanayo na
matangazo yote yatakayowekwa kwenye kenopi na kwenye bango la kuwekea matangazo
„billboard‟liliopo nje ya Uwanja wa Ndege, ambapo kwa matangazo yote hayo, Idara ya Anga
(kama ilivyokusudiwa) itakuwa na haki ya kupokea USD 1,000 kwa kila mwezi. Ufafanuzi wa
maelezo haya ni kwamba, kwa matangazo yote yatakayotangazwa katika Kenopi na „billboard‟
husika ambazo zimejengwa na Kampuni hii, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege haitapokea fedha
yoyote isipokuwa USD 1000 kwa mwezi. Kwa lugha nyengine, kwa mujibu wa ufafanuzi
uliotolewa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege pamoja na Meneja wa Kampuni hii alipokutana na
Kamati, Mkataba wao kuhusiana na matangazo ni wa namna mbili. Namna ya kwanza, baada ya
mwaka mmoja wa kusamehewa kulipa kodi kutokana na kujenga kenopi hiyo kwa gharama zao,
Kampuni ya E A Media Limited italipa USD 1000 kwa kila mwezi bila ya kujali kwamba
Kampuni hiyo itapata mapato ama kukosa kutokana na matangazo yaliyopo ama
yatakayokuwepo kwenye kenopi hiyo. Kwa mfano, katika eneo la ndani ya „canopy‟ kuna
mabango ya Kampuni ya simu ya Zanteli 13, yenye ukubwa wa square meter 46.8 (urefu na
upana) na kila bango moja lina thamani ya Tsh. 150,000/- kwa mwezi, ni sawa na kusema
kwamba, Kampuni hii itapokea Tsh. 7,020,000 kwa mwezi na pia katika Kenopi hiyo hiyo
(sehemu ya nje na chini ya Kenopi, sehemu ya „Booking‟ kuna mabango 8 ya urefu square meter
5.37 urefu na upana 1.22, yenye matangazo nje na ndani, ni sawa na kuwa na square meter 104.8
na kwa thamani ya Tsh. 150,000 kwa mwezi ni sawa na Tsh. 15,720,000/- . Hivyo basi, kati ya
Tsh. 22,740,000/ zinazopatikana kwa Kampuni hii, ni Tsh. 1,500,000/- ama Tsh. 1,600,000/-
ndio malipo halali kwa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, mbali na bango kubwa la juu
linalotangaza jina la Uwanja na matangazo mengine yaliyowekwa kwenye paa la canop hiyo na
bila ya kujumuisha na Bango kubwa la nje ya Uwanja (Angalia Kielelezo Na.74 kwa ufafanuzi
zaidi).
Aina ya pili ya matangazo ni yale yote yaliyopo kwenye uwanja wa Ndege, kwamba Mamlaka
ya Uwanja wa ndege imewateua Kampuni ya E A Media Limited kuwa wakala wao, yaani
Kampuni hii itakusanya mapato yatokanayo na matangazo hayo na kwa kila tangazo inapata Tsh.
50,000/- kama ni malipo yao baada ya kukusanya malipo wanakata fedha zao na bakaa la
tangazo husika wanaliwasilisha Mamlaka ya Uwanja wa Ndege. Kwa Mfano, kwa tangazo lenye
31
Tafsiri na msisitizo ni wetu.
75
thamani ya Tsh. 150,000/-, E.A. Media wana Tsh. 50,000/- na Mamlaka inaingiza Tsh. 100,000/-
(Rejea Kielelezo Na.74 na 75). Ili kupata ufafanuzi Mzuri zaidi wa suala hili, ni vyema
tukaangalia juhudi za Kampuni ya E A Media Limited ya kutafuta biashara ya matangazo ya
biashara katika eneno hilo la Uwanja wa Ndege.
3.4.30.5 Uwakala wa kukusanya Mapato yatokanayo na Matangazo ya Biashara katika
eneo la Uwanja wa Ndege:
Kama tulivyokwisha eleza awali, kwamba mbali na Kampuni hii kuingia katika Mkataba wa
kujenga kenopi ya Uwanja wa Ndege, Mahusiano mengine baina ya Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege na Kampuni ya E A Media Limited ni kuwafanya wakala wao wa kukusanya mapato ya
kila tangazo la biashara liliopo uwanjani hapo na hatimae sehemu ya mapato hayo inaingia
katika Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na sehemu ya pili yakaingia katika Kampuni hiyo. Ili
kufahamu vizuri utaratibu huu, ni vyema tupate ufafanuzi wa hatua zilizochukuliwa na Kampuni
hadi wakaweza kufanya biashara hiyo:
3.4.30.6 Hatua zilizochukuliwa na Kampuni baada ya kukamilika kwa kenopi ya Uwanja
wa Ndege:
Tokea July, 2009, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kenopi, Kampuni ya E A Media imefanya
juhudi kubwa za kujitafutia soko kwa makampuni mbali mbali ili waje watangaze katika sehemu
ya kenopi hiyo, kama Mkataba wao na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege unavyohusika. Kwa
kuzingatia kwamba, E A Media ni Kampuni pekee Tanzania inayojishughulisha na masuala ya
matangazo na yenye Makao Makuu ya kudumu hapa Zanzibar, hali hii iliwawezesha kuendelea
kujitangaza huku wakipata msaada kutoka Mamlaka ya Uwanja wa Ndege pale wanapouhitaji.
Juhudi zao kubwa zilikuwa ni kuhakikisha kwamba wanaimarisha na kuongeza matangazo
katika Uwanja huo kufuatia kutoa huduma hiyo kwa ufanisi kwa makampuni yanayotaka
kutangaza biashara zao katika Uwanja huo.
Mnamo mwezi wa August 2010, waliingia Mkataba na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa kuwa
Wakala wao kwa kukusanya mapato yanayotokana na matangazo ya biashara yaliyopo katika
eneo la Uwanja wa Ndege. Kamati ilielezwa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwamba
walifikia maamuzi hayo kutokana na Kampuni hii kuwa fanisi katika biashara hiyo, na wakati
huo huo, wao kama Mamlaka walikuwa wanapata tabu ya kukusanya mapato hayo kutokana na
wateja wao wengi walikuwa hawalipi na hivyo walikuwa wanakosa mapato yanayohitajika. Hata
hivyo, miongoni mwa changamoto zilizowakabili Kampuni hii baada ya kuingia Mkataba huo
wa Uwakala ni namna ya kuyadhibiti Makampuni ambayo hayalipii gharama za matangazo
wakati wameshapatiwa huduma, lakini kama Kampuni inayotaka kuendelea kibiashara,
inalazimika kuwa na mahusinao nao mazuri kama wateja wao. Baada ya makubaliano hayo,
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, iliwatangazia wateja wote kuhusiana na kubadilika kwa
usimamizi wa suala hili na kuwataka waanze upya taratibu za maombi ya kuweka matangazo
hayo kwa Kampuni ya E A Media badala ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege.
3.4.30.7 Uhalisia wa Mapato ya Matangazo ya Biashara katika Uwanja wa Ndege.
Pamoja na Kamati kupata ufafanuzi wa suala hili kama tulivyokwisha eleza hapo juu, imeona
kuna haja kubwa ya kufahamu juu ya mapato halisi yanayolipwa na kuingia Serikalini kutokana
na Mkataba huu. Na hivyo basi, kama ilivyofanya kuwatambua wakodishwaji wote wa maeneo
76
ya Biashara katika Uwanja wa Ndege huo, pia ilitaka kuhakikishiwa kuna mabango mangapi
ambayo yapo na yanalipiwa kiasi ambacho Mamlaka ya Uwanja wa Ndege inaamini yapo chini
yake. Kamati ilipouhoji Uongozi wa Mamlaka la Uwanja wa Ndege kuhusiana na Mapango ya
biashara yanayolipiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, ulitoa idadi ya Makampuni 12 tu
kwamba ndio yanayolipa na ndio yaliyokubaliwa kueka mabango ya matangazo Uwanjani hapo,
huku Makampuni hayo kwa ujumla wake yakimiliki takriban Mabango 17. Aidha, katika orodha
hiyo, sehemu ya mwisho kuna Makampuni 7 yameweka mabango lakini hayalipi kodi zao, n
hivyo kufanya idadi ya mabango 24 (Kielelezo Na.75).
Jawabu hii pia imeifanya Kamati kuwa na wasi wasi wa ukweli wake. Kama vile ilivyotaka
kupotoshwa juu ya idadi ya Wafanya biashara waliokodishwa maeneo Uwanja wa Ndege, ndio
pia hapa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa mara nyengine tena imetaka kuipotosha Kamati.
Baada ya Kamati kufanya ziara ya kuhesabu mabango yote ya Uwanja wa Ndege, imegundua
mabango hayo yanafika 49 ukiacha mbali mabango ya Canop na lile la Bango kubwa pale nje,
kama tulivyoeleza awali na ukiacha mbali tangazo la City Clock ambao wanamakubaliano ya
kutolipa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege (Rejea Kielelezo Na.74).
Tunachotaka tufahamishe hapa ni kwamba, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege inakusanya tu
malipo ya mabango 17 ya Makampuni 12 waliyoyawasilisha kwa Kamati, na hii taarifa mpya ya
mabango yaliyogundulika na Kamati wao hawana habari nayo, na hivyo Kamati ilipowataka
wathibitishe malipo ya mabango hayo, walitoa orodha hiyo ya mabango 17. Hapa panafahamika
kwamba, fedha zote zinazopatikana katika mabango yote ambayo Kamati imeyagundua
inawezekana sana zinaishia mikononi mwa watendaji wachache. Lakini pia tunataka tuthibitishe
kwamba, wakati Kamati ilipoamua kujiridhisha ulipaji wa kodi za wakodishwaji wa maeneo ya
biashara kwa mwaka 2010, kwa upande wa Kampuni ya E.A. Media ililetewa risiti za
uthibitisho wa malipo wanayolipa kwa matangazo ya Canopy tu, yaani USD 1000 kwa kila
mwezi, kwa risiti namba 343400; 224773na 224791, malipo ambayo ni sawa na USD 2400,
tofauti kabisa na makubaliano ya Mkataba husika kwamba Kampuni ilipe USD 1000 kwa kila
mwezi.
Tatizo jengine ndio hili kwamba mapato ya matangazo mengine mbali na yale ya Canop
yanayopatikana kutoka kwa Kampuni hii kama Wakala wa Mamlaka, yameshidwa kuthibitishwa
kutokana na Mamlaka hii ya Uwanja wa Ndege kutowasilisha ushahidi wowote wa malipo hayo.
Na kwa hali hii, Kamati imejiridhisha kwamba, kuna uwezekano mkubwa wa fedha hizo kuishia
mikononi mwa watendaji wachache wa Mamlaka huku wakishindwa pia kumsimamia
Mwekezaji huyu, E.A Media kulipa USD 1000 kwa kila mwezi kama Mkataba wa Canopy
uliyoelekeza lakini pia kumsimamia ili wahakikishe kwamba, analipia fedha halisi iliyokubaliwa
na kazi ya Uwakala wa Mabango ya Biashara anayoifanya.
3.4.31 Mkataba wa Sehemu ya Kuegesha Magari (Parking):
Kama tulivyokwisha eleza awali, kwamba E A Medlia Ltd, imeingia mikataba miwili na Idara ya
Anga, na Mkataba wa pili kati ya hiyo ni huu unaohusu Maegesho ya Magari (Parking)
(Kielelezo Na.76). Wazo la kuanzisha „parking‟ lilianza mwezi wa August, kufuatia kwa
Kampuni hii kufanya mawasiliano na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kuhusiana na nmna
gani wangeweza kuandaa „parking‟ hiyo kupita ramani na taarifa mbali mbali walizoziwasilisha
Wizarani. Na mnamo tarehe 1/05/2010 walipokea barua kutoka Wizarani inayoeleza kwamba
wameruhusiwa na wangeliweza kuanzisha na kutoa huduma mpya za „parking‟.
77
Pamoja na ruhusa hiyo kutolewa, Kampuni hii ilipata changamoto kadhaa kuhusiana na Mradi
wao huo, ikiwa ni pamoja na wapi wangeliweka maegesho hayo (parking). Baada ya
kukubaliana ni wapi „parking‟ hiyo iwepo, walifanya maendeleo hadhaa ikiwa ni pamoja na
kuweka sakafu ya zege eneo hilo, kutia „fance‟ ya waya (yenye urefu takriban wa mita 500 kwa
urefu) na kuanzisha (kujenga) ofisi ya mpokeaji fedha na ofisi za utawala(parking cashier and
administration office) sehemu ya kutokea na ofisi ndogo sehemu ya kuingilia. Aidha, Kampuni
iliomba kuuingiwa umeme kutoka Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO), vyote hivi
wamevifanya kwa gharama zao.
3.4.31.1 Muda wa Mkataba:
Mkataba huu ni wa miaka mitano, kuanzia muda ambao ujenzi wa „parking‟ hiyo utakuwa
umeshakamilika (ifahamike wazi kwamba, Mkataba huu umesainiwa tarehe 10/08/2010),
ambapo baada ya kukamilika miaka 5 ya kwanza, pande zote mbili zitakuwa na haki ya
kukubaliana tena juu ya kuendelea kwa Mkataba husika, kwa sharti kwamba, iwapo Mkataba
huo utaendelea kwa miaka 5 ya awamu ya pili, yaani baada ya kukamilika miaka 10, Kampuni
itakuwa tayari kuhamishia umiliki wa „parking‟ hiyo kuwa milki halali ya Idara ya Anga (hivi
sasa ni Mamlaka ya Uwanja wa Ndege), bila ya kufidiwa gharama zozote ilizozitumia katika
uandaaji wake.
3.4.31.2 Malipo ya Kodi na Huduma:
Kwa kila mwisho wa mwezi, Kampuni ya E A Media inatakiwa ilipe Tsh. 1,200,000/- ambapo
iwapo haitalipwa kwa wakati, Kampuni italazimika kulipa riba kwa kiwango chochote ambacho
hakijalipwa kwa mnasaba wa kiwango kilichowekwa na Benki yoyote ya biashara, tokea siku ile
ambayo haikulipwa mpaka siku ile itakayolipwa. Kodi hiyo (ambayo ni mnasaba wa gharama za
ujenzi wa „parking‟ alizokula Kampuni) itafanyiwa marekebisho kila mwaka.
Tunachotaka hapa kifahamike ni kwamba, pamoja na Mkataba huo kuwa tayari umeshasainiwa,
lakini utekelezaji wake bado haujaanza kwa sababu huduma hiyo ya maegesho bado haijaanza
kutolewa kwa malipo. Bila ya shaka malipo yangeweza kuthibitishwa iwapo huduma imeanza
kutolewa.
3.4.32 MAENEO YALIYOKODISHWA BILA YA KUWEPO MIKATABA:
Baaada ya kuangalia uchambuzi wa Mikataba iliwayowasilishwa kwa Kamati, ni vyema
tukakumbuka kwamba, katika orodha ya Wakodishwaji wa maeneo hayo iliyowasilishwa kwa
Kamati, jumla ya Makampuni ama Taasisi 48 zimekodishwa, hivyo pamoja na Mikataba mengi
kati ya hiyo kupitwa na wakati na mingi zaidi kufungwa kinyume na utaratibu wa kisheria ama
kutosimamiwa ipasavyo, Kamati imebaini Makampuni ama Taasisi zifuatazo zinafanya biashra
katika Uwanja wa Ndege huo bila ya kuwa na Mkataba. Aidha, imebaini Makampuni ama
Taasisi ambazo hata kodi hazilipi. Tuanze na Makampuni/Taasisi ambayo hayana Mkataba.
3.4.32.1 INDIGO.
Kwa mujibu wa taarifa zilizomo kwenye Orodha ya Wakodishwaji (Rejea Kielelezo Na.30),
Kampuni hii imekodishwa eneo la Ofisi lenye ukubwa wa mita za mraba 6.24 na maelezo yao
kwamba Mkataba wao umeanzia tarehe 1/1/2011 hadi 31/12/2011 na wangestahiki kulipa USD
468 kwa mwaka. Kwa Bahati mbaya, baada ya Uchunguzi wa Kamati imegundulika kwamba,
78
Kampuni hii inaendelea na kumiliki eneo la biashara lakini hana Mkataba wa Ukodishwaji.
Aidha, Kamati imepewa uthbitisho wa malipo ya kodi kwa mwaka 2010 kupitia risiti namba
343390, lakini inabainika kwamba, sasa eneo hilo limekodishwa kwa HOT POINT, katika
utartibu ule ule wa Mamlaka kutokuwa na habari wala kutoa ruhusa ya ukodishwaji huo.
3.4.32.2 ZAN TOURS
Kamati imepatiwa taarifa za ZAN TOURS kukodishwa eneo la ukubwa wa mraba 8.4 kuanzia
tarehe 1/1/2011 hadi 31/12/2011 kwa thamani ya USD 870 kwa mwaka. Pamoja na maelezo
haya, Kamati haikupatiwa Mkataba wa Ukodishwaji wa Kampuni hii na hivyo imejiridhisha
kwamba, hakuna Mkataba wa Mkodishwaji huyu. Aidha, kuhusu malipo ya kodi kwa mwaka
2010, Kamati imethibitishiwa kwamba ZAN TOURS wamelipa kupitia risiti namba 343359.
3.4.32.3 OMAN AIR.
Kamati imepewa taarifa kupitia Orodha husika kwamba, Kampuni ya Oman Air wamekodi
ukubwa wa eneo la mita za mraba 27.52 kuanzia tarehe 16/05/2011 hadi 15/04/2012 kwa kulipia
USD 24,000 kwa mwaka. Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
imeshindwa kutoa Mkataba wake na pia kuithibitishia Kamati kodi inayolipwa na Kampuni hiyo,
kwa lugha nyengine ni kusema kwamba, mbali na kwamba Kampuni hii haina Mkataba, lakini
hata kodi hailipi.
3.4.32.4 SWAHILI BUREAU DE CHANGE.
Taarifa zilizowasilishwa kwa Kamati zinaonesha kwamba, Kampuni hii imekodi eneo lenye
ukubwa wa mraba 4.44 kuanzia tarehe 1/1/2011 hadi 31/12/2011 kwa USD 399 kwa mwaka.
Hata hivyo, Kamati haikuthibitishiwa Mkataba baina ya Kampuni hii na Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege. Aidha, kuhusu malipo ya kodi kwa mwaka 2010, Kampuni hii imelipakupitia risiti
namba 224245.
3.4.32.5 PALM TREE KIOSK.
Katika orodha ya 31, jina la Palm Tree Kiosk linajitokeza (Rejea Kielelezo Na.30) huku
ikiaminika kukodishwa eneo la ukubwa wa mita za mraba 7.5, lakini haijuulikani wamekodi
kwa muda gani wala fedha wanazolipia kodi hiyo. Kamati haikupatiwa Mkataba wa Ukodishwaji
huu na pia haikupatiwa uthibitisho wa malipo ya kodi angalau kwa mwaka 2010. Hivyo, Kamati
imejiridhisha kwamba, Palm Tree Kiosk wamekodi bila ya Mkataba na wanafanya biashara bila
ya kulipa kodi ya pango.
3.4.32.6 KEMMON COMMUNICATIONS LTD.
Kampuni hii nayo imekodi Ofisi yenye ukubwa wa mraba 9.5 lakini haijuulikani muda wa
kukodi wala fedha za kodi wanazopaswa walipie. Kwa kuwa Kamati haikupatiwa uthbitisho wa
Mkataba husika, imejiridhisha kwamba, Kemmon hawana Mkataba wa eneo la biashara hiyo.
aidha, Kamati imejiridhisha kwamba Kampuni hii hailipi kodi, kwa kutothibitishwa ulipaji wake
angalau kwa mwaka 2010.
3.4.32.7 ZANZIBAR AIR LINE NA ETHIOPIAN AIR LINE.
Kwa mujibu wa orodha iliyowasilishwa kwa Kamati imebainika kwamba Kampuni hii imekodi
Ofisi yenye ukubwa wa mraba 7.5 bila ya kujuulikana muda wa Mkataba huo wala idadi ya
fedha za kodi wanazopaswa walipie. Wakati Kamati inatembelea eneo hilo, tayari
79
limeshakodishwa kwa Kampuni ya Ethiopian Air Line kinyume na ruhusa ya Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege. Hivyo basi, Kamati imeshidwa kupatiwa Mikataba yote miwili, bainia ya
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na Zanzibar Air Line wala wa Ethiopian Air line. Vile vile,
Kamati imejiridhisha kwamba Kampuni zote hizi mbli hazilipi kodi, kwa kutothibitishwa ulipaji
wao angalau kwa mwaka 2010.
3.4.32.8 MAHA TRAVELS (CONDOR OFFICE).
Usishangae kuona kuna Kampuni mbili katika jengo moja, kwani ufasaha wake ni kwamba,
wakati Kamati ilipokutana na Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege ilipewa taarifa
kwamba Kampuni ya Maha Travels imekodi eneo lenye ukubwa wa mraba 9.5 lakini
haijuulikani wamekodi kwa muda gani wala fedha wanazolipia kodi hiyo. Hata hivyo, wakati
Kamati ilipofanya ziara iligundua kwamba eneo hilo linatumika na Kampuni ya Condor kwa
kuweka Ofisi yao. Pamoja na hali hii, Kamati haikupatiwa Mkataba wa Ukodishwaji baina ya
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na Kampuni yoyote kati ya hizi mbili. Na kwa upande wa kodi,
Kamati haikupatiwa uthibitisho wa malipo ya kodi hiyo kwa Kampuni zote mbili.
3.4.32.9 ZENITH AVIATION.
Kampuni hii imekodi Ofisi yenye ukubwa wa mraba 7.8. hata hivyo, hakuna taarifa za muda wa
kodi hiyo wala bei ya kodi husika. Kamati pia haikupatiwa Mkataba wa kuthibitisha uwepo wao
kisheria ingawaje wakati ilipofanya ziara imethibitisha eneo hilo kutumiwa kibiashara. Aidha,
Kamati haikupatiwa uthibitisho wa ulipaji wa kodi wa Kampuni hii.
3.4.32.10 NOURTH COAST TRAVEL SERVICES NA 540.COM
Kampuni hii nayo imekodishwa ofisi yenye ukubwa wa mita za mraba 9.5, ingawaje hakuna
taarifa zinazoonesha muda wa kodi yao wala gharama za malipo wanayopaswa kulipa. Mkataba
wa ukodishwaji wa Kampuni hii imeshindwa kuthibitika na kuifanya Kamati ijiridhishe kusema
kwamba Mkataba huo haupo. Aidha, mbali na kutokuwepo kwa Mkataba, Kampuni hii ya
Nourth Coast imewakodisha sehemu hiyo Kampuni nyengine ya 450.COM bila ya ridhaa ya
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, kitendo kinachokwenda kinyume kabisa na taratibu zilizopo.
Hata hivyo, Kamati haikupewa taarifa hizi mpaka pale ilipofanya ziara na kushuhudia hayo,
huku hata Mkataba wa 450.COM ukishindikana kuwasilishwa kwa Kamati. Mbali na hayo,
lakini pia Kampuni zote hizi hazilipi kodi.
Kuna jambo moja ni vyema tukaligusia, kwamba Mnano tarehe 18/04/2009 aliekuwa Kaimu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ambae sasa ni Katibu Mkuu, Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano, Ndg. Vuai I. Lila alimuandikia barua Mkurugenzi wa Idara ya
Anga yenye kumbu kumbu namba MOCT/M.185/C.13/VOL.4/200 (Kielelezo Na.77)
kumuagiza kwamba Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kufuatia mazungumzo ya pamoja na
Mhe. Waziri, yeye Kaimu Katibu na Mkurugenzi wa Idara ya Anga, imeamua Kampuni hii
540.com Kujenga Afisi yao hapo Uwanja wa Ndege huku ikisisitizwa agizo hilo litekelezwe
mara moja na Idara ya Anga wakilazimika kuandaa Mkataba utakaongoza shughuli hizo. Kwa
hiyo, hata Kamati ilipofika Afisi hiyo ya Mamlaka, ilipewa barua hii kama uthbitisho wa kuwepo
kwao kisheria. Hata hivyo, Kamati haiwezi kuichukua barua hiyo kuwa ni Mkataba wa kisheria
na zaidi hata barua yenyewe iliagiza kupatikana kwa Mkataba husika.
80
3.4.32.11 FBME BANK LTD.
Kampuni hii imekodishwa eneo la kutoa Huduma za Kibenki kupitia elekroniki (ATM) yenye
ukubwa 4.6 mita za mraba, lakini hakuna muda wa kodi hiyo ulioainishwa wala kiwango cha
kodi. Kamati haikupatiwa Mkataba husika mpaka muda wa kuandika ripoti hii. Aidha, Kamati
imejiridhisha kwamba, Mkodishwaji huyu halipi kodi kwani hakuna uthibitisho wa malipo hayo.
Kama tulivyoeleza kwa Kampuni ya 540.com, kwamba Kampuni hii ya FBME imeandika barua
yake ya tarehe 1/06/2009 yenye kumbu kumbu namba HO/bd/nd/005/22 kwa Mkurugenzi wa
Idara ya Anga kumuomba awaruhusu kuanzisha ama kukodishwa eneo la huduma hiyo. Kwa
mujibu wa barua ya tarehe 12/08/2009 yenye kumbu kumbu namba DA/M/ZIA/OP/002/17/73
Idara ya Anga iliwajibu kwa kuwaruhusu FBME Bank Ltd kwa masharti yaliyoelezwa katika
barua hiyo (Kielelezo Na.78). Kwa barua hii, ndio uthibitisho walioutoa kuonesha wao Mamlaka
ya Uwanja wa Ndege wamejiridhisha kwamba FBME Bank Ltd wapo kisheria.
3.4.32.12 IZMIR (PHARMACY)
Suala hili linahusiana na Duka la dawa (Pharmacy) lililojengwa pembeni mwa ukuta wa Uwanja
wa Ndege na kuwahi kuleta malalamiko mengi ya wananchi ikiwa ni pamoja na kupitia kwa
Wawakilishi wao. Kwa bahati hapa tumeiita IZMIR (PHARMACY), kwa sababu Kamati
haikupata taarifa zake kutoka kwa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, yaani haimo katika orodha ya
wakodishwaji iliyowasilishwa kwa Kamati lakini Kamati baada ya kufanya ziara ndio
imethibitisha kuwepo kwao na duka hili la dawa linaitwa IZMIR PHARMACY. Hatujui ni
ukubwa gani wa eneo mita za mraba walizopewa lakini pia Kamati haikupata uthibitisho wa
maombi yao ya kuomba kukodishwa sehemu hiyo wala Mkataba wa kuthibitisha kuwepo kwao.
Vile vile, Kamati haikupata uthibitisho wa kulipa kodi wa „Pharmacy‟ hii.
3.4.32.13 ARRIVAL BUREAU DE CHANGE.
Kampuni ya Arrival Bureau de Change imekodishwa eneo la biashara bila ya kuainishwa katika
orodha ya Wakodishwaji iliyowasilishwa kwa Kamati, isipokuwa ifahamike kwamba, Uongozi
wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege uliieleza Kamati kwamba, Mkataba wa Kampuni hii ni
mmoja na ule wa Departure and Arrival Bureau De Change (tulioufanya Kielelezo Na.48). Hata
hivyo, wakati Kamati inafanya ziara katika maeneo husika, ilifika katika sehemu hiyo na kuona
sehemu nyengine mbali na hii Departure and Arrival Bureau de Change, ambayo inaitwa Arrival
Bureau de Change na hatimae kumuuliza mhusika aliekuwepo katika Bureau de Change hiyo na
kuthibitisha kwamba, hizi ni taasisi mbili tofauti. Kwa mazingira hayo basi, ndio Kamati ikaja na
uamuzi ambao pia iliutangaza na kukubaliana na Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
katika kikao kilichofanyika baada ya ukaguzi huo. Kwa maana hii, bado kuna haja ya kupatiwa
Mkataba baina ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na Kampuni ya Arrival Bureau de Change,
aidha, Kamati pia haikuthibitishiwa kuhusu malipo ya kodi wanayolipa Kampuni hii.
3.4.32.14 AS SALAAM AIR.
Kampuni hii tuliizungumzia pale tulipokuwa tunafafanua Mkataba wa TAN WING (T) LTD,
kwamba sehemu hiyo baada ya kukodishwa, wao TAN WING wamekodisha kwa Kampuni ya
Assalaam Air bila ya idhini ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege. Hivyo, baada ya Kamati
kuthibitisha kwamba sehemu hiyo imekodishwa kinyume na taratibu, bado ikasimamia haja ya
kupatiwa Mkataba wa kukodishwa kwake hii Kampuni ya AS SALAAM AIR. Hata hivyo,
Mkataba huo umeshindikana na wala hakukua na ushahidi wa Kampuni hii kulipa kodi.
81
3.4.33 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii ndogo, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
3.4.33.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Mikataba takriban yote ya Ukodishwaji wa maeneo ya Uwanja wa Ndege tayari
imeshapitwa na wakati na kukosa sifa za msingi kisheria.
Kamati imegundua kwamba, asilimia kubwa ya Mikataba iliyokabidhiwa kwake tayari
ilikuwa imeshapitwa na wakati na ina kasoro nyingi za kisheria.
(ii) Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege umeshindwa kuisimamia Mikataba
kwa maslahi ya nchi.
Kamati imegundua kwamba, Mikataba hii inavunjwa kiholela bila ya kuwa na
usimamizi madhubuti wa Idara ya Anga, ambayo leo inaitwa Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege, hali ambayo inapelekea kuikosesha Serikali mapato huku kutosimamiwa kwa
mikataba hii kunatokana na uzembe na kutowajibika kwa Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege katika majukumu yao ya kazi.
(iii) Kamati imedanganywa sana na kutaka kupotoshwa juu ya ukweli halisi wa
Ukodishaji wa maeneo ya Uwanja wa Ndege.
Kamati haikupatiwa taarifa za kweli wakati inafuatilia orodha kamili ya wakodishwaji
na wafanya biashara wote wa eneo husika la Uwanja wa Ndege na wakati huo huo
kutopewa taarifa za kweli kuhusiana na masharti ya Mikataba husika.
(iv) Kuna uvujaji Mkubwa wa Mapato ya Serikali yanayotokana na Ukodishwaji wa
maeneo hayo ya Uwanja wa Ndege.
Kamati imegundua kwamba, kodi za maeneo yaliyokodishwa hazilipwi kwa wakati na
pia hazilipwi kabisa na baadhi ya Taasisi zilizokodi na kufanya biashara khususan zile
ambazo Kamati haikupatiwa Mikataba yake, kwamba Mapato yanayolipwa
hayakuweza kuthibitishwa, hali inayoifanya Kamati kuamini kwamba mapato hayo
yanavuja. Aidha, uvujaji huu pia unahusiana na Matangazo ya Biashara yaliyopo katika
Uwanja huo wa Ndege, Zanzibar.
(v) Kuna Taasisi nyingi zinaendesha biashara bila ya kuwa na Mikataba.
Kamati imegundua kwamba, Taasisi nyingi zinafanya biashara bila ya kuwa na
Mikataba, huku kukiwa na mtindo unaonekana wa kawaida kwa wanaokodishwa nao
kukodisha maeneo hayo kwa wafanya biashara wengine bila ya idhini ya Uongozi wa
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, na ni sawa na kusema kwamba, Taasisi hizi zinafanya
biashara ya kukodisha maeneo ya biashara ambayo wao wenyewe wamekodishwa na
82
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kinyume na Matakwa ya sheria za Mikataba na
masharti ya Mikataba husika.
(vi) Viongozi Wakuu wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, wakati huo Idara ya Anga
wamehusika sana katika udhaifu Mkubwa wa Mikataba hii.
Kamati imegundua kwamba, Mikataba mingi ipo kirafiki zaidi kuliko kisheria kwa
maana, miongoni mwa kasoro hizo ni kwamba, muda mwingi Mikataba hii imo
mikononi mwa wakodishwaji kwa lengo la kutafutwa saini zao, jambo ambalo liko
kinyume na masharti ya Mikataba husika. Aidha udhaifu huu unatokana na Viongozi
Wakuu wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, wakiweka mbele maslahi yao binafsi zaidi
kuliko maslahi ya Taifa.
(vii) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege anahusika na biashara
wakati huo huo yeye anawajibika kuwasimamia Wafanyabiashara wenzake
watekeleze masharti ya Mikataba, kitu ambacho hakiwezekani.
Kamati imegundua kwamba, Capt. Said Ndombugani ambae ni Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege amekodi eneo la Biashara na amekiuka masharti ya
Mkataba kwa maslahi binafsi huku akiamini hakuna mtu wa kumchukulia hatua.
Ukifanya rejea ya suala hili na kukodishwa Hanger kwa USD 200 tu kwa mwezi wakati
yeye ameamua kuwakodisha ZAN AIR kwa USD 100 kwa mwezi, ni wazi kwamba
anafaidika kwa USD 800 ambazo ni kipato kizuri kwa Kampuni yake.
3.4.33.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi tulioufanya, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:
(i) Kwa kuwa sasa Idara ya Anga ni Mamlaka Kamili ya Uwanja wa Ndege, Kamati
inapendekeza Mikataba yote inayohusiana na Ukodishwaji wa biashara mbali
mbali katika eneo la Uwanja wa Ndege ipitiwe upya ili iendane na mabadiliko ya
biashara na msisitizo ukiwekwa katika gharama za kodi husika
(ii) Kamati inapendekeza hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe kwa Watendaji
Wakuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege waliohusika na upotoshaji wa Kamati kwa kutoa taarifa zisizo
za kweli.
(iii) Fedha na malipo yote ambayo hayajalipwa na Taasisi/Makampuni
zilizokodishwa, ni Lazima zilipwe kabla Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
haijaingia tena Mkataba na Taasisi ama Kampuni hizo za biashara katika Uwanja
wa Ndege wa Zanzibar.
(iv) Watendaji wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege,wanaohusika na usimamizi wa
ukodishwaji wa maeneo ya uwanja wa Ndege (msisitizo ukiwekwa kwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwanja wa Capt. Said Ndombugani) wachukuliwe
hatua za kinidhamu kwa kushindwa kuwajibika kuisimamia Mikataba hiyo huku
baadhi yao wakigeuka ni wafanya biashara katika eneo la kazi na matokeo yake
kupoteza mapato ya Serikali.
83
3.5 KUCHUNGUZA UTARATIBU WA AJIRA KWENYE WIZARA YA
MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO (UPANDE WA UNGUJA).
Kuhusu utaratibu wa ajira, Kamati imefuatilia Hadidu hii Rejea kwa upande wa Unguja katika
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Katika kikao cha kwanza katika kulizungumzia suala
hili, Kamati iliziita pamoja Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Ofisi ya Rais,
Utumishi wa Umma na Utawala Bora inayohusika na uajiri wa wafanyakazi wa Serikali. Katika
Hadidu hii, Kamati ilichunguza juu utaratibu wa ajira katika Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano kuanzia October 2010 hadi September 2011, takriban mwaka mmoja. Ili kupata
ufafanuzi yakinifu wa suala hili, Kamati iliomba kupatiwa idadi ya wafanyakazi wote
walioajiriwa katika muda huu, ambapo hapo kabla ilipatiwa wafanyakazi 24 tu ikiambiwa
kwamba ndio walioajiriwa kwa kipindi hicho.
Aidha, ifahamike wazi kwamba, kabla ya kupitishwa Sheria No. 2 ya mwaka 2011, kwa mujibu
wa kifungu cha 9 cha Kanuni za Utumishi Serikalini za mwaka 1997, Mamlaka ya kuajiri na
Kuachisha kazi katika Utumishi wa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar pamoja na vyombo vyake
vyote (isipokuwa kwa Taasisi zinazojitegemea) yalikuwepo katika Idara ya Utumishi na Tume
ya Utumishi ya Serkali. Hivyo basi katika taratibu za uajiri huo, Idara ya Utumishi Serikalini
ilikuwa inayakusanya maombi yote ya kujaza nafasi zilizowazi na kuzipeleka kwenye Tume ya
Utumishi Serikalini, kwa ngazi zilizohusika kwa ajili ya uteuzi wa mwisho wa kujaza nafasi
hizo. Kwa maana hii, utaratibu wa ajira Serikalini kwa ngazi zote za Wataalamu na wasiokuwa
wataalamu ilikuwa ni pamoja na kutolewa kibali katika Idara ya Utumishi Serikalini, na kwa
mnasaba wa Hadidu yetu hii, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ilipeleka ombi la kujaza
nafasi tupu za Wizara kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora
kupitia barua ya tarehe 21/3/2011 yenye kumbu kumbu namba MOIC/K.90/C.1/VOL. 11,
ikiomba kupatiwa jumla ya wafanyakazi 264 kwa upande wa Unguja na Pemba, kwa maana
Unguja ni nafasi 136 na Pemba ni nafasi 128.
Katika hali ya kutoa ufafanuzi mzuri zaidi, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwa
upande wa Idara ya Uendeshaji Utumishi, Unguja iliomba nafasi 10 kama zifuatazo:
i. Afisa Uhusiano nafasi 1 akitakiwa awe na elimu ya shahada ya kwanza ya
Uhusiano wa Kimataifa/Uhusiano wa Umma au Advance Diploma katika fani
hiyo au sifa zinazolingana na hizo.
ii. Mkuu wa Maktaba Nafasi 1 akitakiwa awe na elimu ya „Advance‟ Diploma katika
fani ya Record Mnagement.
iii. Karani Maktaba nafasi 1 aliwa na elimu ya Diploma au „Certificate‟ katika fani ya
„Record Management‟.
iv. Dereva Nafasi 1 akitakiwa awe na elimu ya Kidato cha nne na cheti cha Udereva.
v. Msajili wa Mali za Wizara nafasi 1 akiwa na elimu ya „Advance‟ Diploma ya
„Procurement and Supply Management‟.
vi. Katibu Muhtasi nafasi 2 wakiwa na elimu ya Kidato cha Nne na elimu ya Cheti
cha „Secretary‟.
vii. Walinzi nafasi 3 wakiwa na elimu ya Kidato cha Nne na wawe wamepata
mafunzo ya Uaskari.
84
Kwa upande wa Mamlaka ya Usafiri Baharini, Unguja, Wizara iliomba kuajiriwa kwa nafasi nne
zifuatazo:
i. Msaidizi mkaguzi meli nafasi 2 wakiwa na elimu ya Shahada ya Kwanza ya
Marine Engineering au „Advance Diploma‟ katika fani hiyo.
ii. Mshika Fedha nafasi 1 akiwa na shahada ya kwanza au „Advance Diploma‟ ya
Uhasibu.
iii. Karani Mapato nafasi 1 akiwa na elimu ya Diploma katika fani ya Uhasibu.
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Unguja iliombewa nafasi 13 zifuatazo:
i. Fundi Umeme nafasi 3 wakiwa na Elimu ya Diploma ya FTC katika fani ya
Umeme.
ii. Wahudumu Bustani/ Usafi nafasi 3 wakiwa na elimu ya Kidato cha Nne na cheti
cha „House Keeping‟.
iii. Meneja Ufundi wa Uwanja wa Ndege nafasi 1 akiwa na shahada ya pili au ya
kwanza au Diploma katika fani ya Umeme.
iv. Wahudumu wa Uwanja wa Ndege nafasi 4 wawe wamemaliza Kidato cha nne.
v. Walinzi usalama nafasi 2 wawe wamemaliza Kidato cha sita au zaidi.
Kwa upande wa Idara ya Usafiri na Leseni Unguja iliombewa nafasi 9 zifuatazo :
i. Walinzi nafasi 3 wakiwa na elimu ya Kidato cha Nne au mafunzo ya Uaskari.
ii. Mafundi Magari nafasi 4 wakiwa na elimu ya Cheti cha FTC katika fani ya
„Mechanics‟.
iii. Fundi Umeme nafasi 1 akiwa na cheti cha FTC katika fani ya Umeme.
iv. Fundi Mitambo nafasi 1 akiwa na elimu ya Diploma ya „Automobile
Engineering‟.
Na kwa upande wa Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara Unguja iliombewa nafasi 100 za
Vibarua Stadi Ujenzi/Utunzaji wakitakiwa wawe na elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea
ambao wangelisambazwa Mkoa wa Kaskazini Unguja, nafasi 30; Mkoa wa Mjini Magharibi
nafasi 30; Mkoa wa Kusini Unguja nafasi 30, nafasi 10 zilizobakia zilikusudiwa ziwe kwa
Wapimaji nafasi 3, nafasi 1 kwa kila Fundi Magari, Mhandisi Mitambo na Dereva Zana Nzito na
walinzi nafasi 4. (Kielelezo Na.79)
Miezi miwili baadae, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora alitoa
majibu ya maombi ya ajira kutoka Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kupitia barua ya
tarehe 12/5/2011 yenye kumbu kumbu namba OR/UUU/K90/VOL. XXVII/43 ikiarifu kutolewa
ruhusa ya kuajiri wafanyakazi ama vijana 33 (Kielelezo Na.80). Ili kupata ufafanuzi wa wazi,
Kamati ilimuita na kumhoji mfanyakazi mmoja mmoja na kugundua mambo mengi ya ujumla
kuhusiana na hadidu hii ambayo tutayaeleza baada ya uchanganuzi wa kila mfanyakazi kama
inavyofuata hapa chini. Kwa kuanzia, ni vyema tuanze na wafanyakazi 7 walioruhusiwa
kuajiriwa katika Idara ya Mipango na Sera (Rejea Kielelezo Na.80):
3.5.1 NDG. FATIMA HUSSEIN MASOUD:
Ndg. Fatima Hussein Masoud ameajiriwa tarehe 1/6/2011 kufanya kazi katika Maktaba ya
Wizara ya Mundombinu na Mawasiliano kama Mkuu wa Maktaba hiyo. Ndg. Fatima amemaliza
Kidato cha Nne (Form IV), Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni mwaka 2005. Kamati
haikuwa na shaka na sifa za elimu na usahihi wa vyeti alivyoviwasilisha mbele ya Kamati baada
85
ya kutakiwa kufanya hivyo, isipokuwa, tatizo kubwa linaloonekana na Kamati kuhusiana na
mfanyakazi huyu ni kwamba, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora haikuzingatia
sifa za elimu zilizohitajika kwa kila aina ya mfanyakazi na kazi alizopangiwa. Aidha, kwa
mnasaba wa sifa zilizopendekezwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Mkuu wa
Maktaba alitakiwa awe na elimu ya „Advance Diploma au mwenye Diploma katika fani ya
„Record Management‟ (Rejea Kielelezo Na.79) na sio sifa alizonazo Mfanyakakazi huyu. Ndg.
Fatima Hussein Masoud amemaliza Kidato cha Nne katika masomo ya kawaida wala hana elimu
ya „Advance Diploma‟wala „Diploma katika fani ya Utunzaji Kumbu kumbu (Record
Management). Kwa hivyo, Mfanyakazi Kamati imeridhika kwamba, mfanyakazi huyu hakua na
sifa za kuajiriwa katika nafasi aliyopangiwa.
3.5.2 NDG. AISHA MSANIF HAJI:
Miongoni mwa wafanyakazi walioisumbua Kamati kwa kutakiwa wafike mbele ya Kamati kwa
muda mrefu bila ya kufika kwa wakati ni pamoja na Ndg. Aisha Msanif Haji. Kikao cha kwanza
cha Kamati juu ya suala hili kwa upande wa Unguja kilifanyika tarehe 21/11/2011 ambapo Ndg.
Aisha hakuweza kudhuria. Tarehe 23/11/2011 Kamati pia iliendelea na ufatiliaji wa Hadidu hii
Rejea Wizarani, ambapo Ndg. Aisha pia hakuwepo na Kamati kuelezwa kwamba, Ndg. Aisha
kapewa Likizo la Dharura kumpeleka Shangazi yake kwenye matibabu, Moshi (Kielelezo
Na.81).
Aidha, katika kikao cha tarehe 28/11/2011 Ndg. Aisha Msanif Haji aliweza kufika mbele ya
Kikao cha Kamati huku likizo yake ikibaki siku 2 tu kumalizika na alipoulizwa juu ya sababu
zilizompelekea kushindwa kuhudhuria mbele ya Kamati kwa wakati aliieleza kwamba aliomba
likizo hiyo ya dharura na kumpeleka Shangazi yake matibabuni Moshi. Hata hivyo, alipotakiwa
atoe ushahidi wowote wa tiketi za boti kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam na kurudi hadi
Zanzibar angalau na tiketi za basi kutoka Ubungo, Dar es Salaam hadi Moshi na kurudi,
alishidwa kufanya hivyo, alipotakiwa angalau atoe cheti cha hospitali aliyompeleka shangazi
yake Moshi, pia alishindwa kufanya hivyo. Kamati haikuridhishwa na majibu haya yaliyokosa
ushahidi kwani kwa wakati wote huo, Kamati ilikuwa na taarifa kwamba hakuwa Moshi. Na
wakati Kamati inajiandaa kukamilisha ripoti yake, imepata taarifa kwamba Mfanyakazi huyu
tayari amesharuhusiwa kwenda masomoni nje ya Nchi. Hii ina maana kwamba, wakati huo
alipokuwa hayupo na kutoa ushahidi wa uwongo alikuwa anafuatilia Viza na taratibu nyengine
za usafiri na baada ya kukamilika ndio amekwenda masomoni. Vile vile Kamati inakumbushia
kwamba, mfanyakazi huyu yupo katika kipindi cha Majaribio na hivyo hakuwa na haki ya
kwenda masomoni, lakini bila ya shaka uhusiano wa Naibu Katibu Mkuu, ambae ni baba wa
Mfanyakazi huyu kumesaidia sana kujenga mafanikio ya mwanawe bila ya kujali sheria za kazi.
Vile vile, katika kikao cha kumhoji mfanyakazi huyu, Kamati ilimhoji juu ya usahihi wa saini
iliyotiwa katika barua yake ya maombi ya likizo, ambapo kwa utafiti wa Kamati barua hiyo
haikuwa na sahihi yake (Rejea Kimabanisho Namba 81). Kwa upande wake alijibu kwamba
ana saini tatu na zote anazitumia wakati mmoja, jawabu ambayo inazidi kuipa mashaka Kamati
juu ya usahihi wa sababu za kutohudhuria mbele ya Kamati kwa wakati. Mbali na hayo, Kamati
pia haikuridhishwa na tabia za dharau alizozionesha mbele ya Kamati ambapo Kamati
iliwashauri watendaji wakuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kuwafundisha adabu
na heshima watendaji wake na zaidi wanapoitwa mbele ya Kamati.
86
Kwa upande wa Ndg. Aisha Msanif Haji ameajiriwa tarehe 1/6/2011 katika Idara ya Usafiri na
Leseni kama Afisa Usafiri. Kwa bahati mbaya sana, katika nafasi 9 zilizoombwa na Wizara ya
Miundobminu na Mawasiliano kwenda kwa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
hakukuwa na nafasi ya Afisa Usafiri na kwa maana hii, Kamati inapata ufahamu kwamba, Ofisi
ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeruhusu kuajiriwa Afisa Usafiri ambapo nafasi
hii haikuombwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, na kwa maana hii, Kamati pia
haikuweza kulinganisha baina ya sifa ambazo zingelihitajika kwa nafasi hii na uwezo wa kielimu
alionao Ndg. Aisha. Hata hivyo, Kamati inapenda ieleweke kwamba, pamoja na maombi ya kazi
yanayoombwa na wafanyakazi wenyewe kufika Idara ya Utumishi Serikalini, kwa mujibu wa
kifungu cha 9(b) cha Kanuni za Utumishi Serikalini, Idara hii ilitakiwa ikusanye maombi ya
kujaza nafasi zilizowazi kutoka katika Taasisi husika ya Serikali na sio kuzingatia maombi ya
mfanyakazi mwenyewe. Na kwa maana hii, Kamati inapata shaka kwa nafasi hii kama
ililazimika kujazwa, yaani kama kulikuwa na haja kutoka Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano ya kuajiri mtu wa aina hii kwa wakati huo. Katika kulitafakari hili, pia tuzingatie
kwamba, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora ililetewa maombi 136 kwa upande
wa Unguja na wao kwa sababu za ukosefu wa fedha ama uwezo wa Serikali, iliajiri vijana 34 tu,
sasa hapa mtu yoyote atajiuliza juu ya sababu za msingi za kuacha kujaza nafasi tupu
zilizoombwa na matokeo yake kujaza nafasi iliyokuwa haijaombwa.
Jee, hii haitoshi kusema kwamba, Serikali haina Mipango bora ya Rasilimali watu (Human
Resource Planning) au ni kutumia vibaya nguvu kazi (Human Resource) tuliyonayo. Au ile
dhana kwamba Idara ya Utumishi haina vipaumbele bora (priority) katika utekelezaji wa
majukumu yake? Pamoja na majibu yoyoyote yatakayowezekana, hali hii haileti picha nzuri
kwani inaweza kutia shaka kwamba kuna upendeleo na Ubinafsi wa ajira za Serikali.
Tukiendelea na Mfanyakazi huyu, Kamati ilipohoji elimu yake, imeridhika na usahihi wa „Result
Slip‟ ya Kidato cha Sita aliyoiwasilisha mbele ya Kamati. Hata hivyo, Kamati inahoji kwa nini
asiajiriwe mtu mwengine mwenye Cheti cha Kumalizia masomo ya Kidato cha Sita „Original
Certificate‟ badala yake aajiriwe yeye mwenye „Result Slip‟ (Kielelezo Na.82) ambayo kwa
kawaida haitumiki kuthibitishia elimu ya mwanafunzi yoyote Tanzania badala yake, Cheti cha
Kumalizia masomo ndio kinachotumika. Ukiangalia kwa udhati wa hoja hizi na uhalisia, unakuta
ni wazi kwamba, takriban Mfanyakazi huyu ameajiriwa kwa ubinafsi zaidi, wakati kuna
wananchi wengi wenye Degree na elimu kubwa zaidi washapeleka maombi yao muda mrefu
lakini bado hawajaajiriwa.
3.5.3 NDG. TUMU GHARIB MOH‟D:
Ndg. Tumu Gharib Mohd ameajiriwa tarehe 1/6/2011 baada ya kupeleka maombi yake ya kazi
Idara ya Utumishi Serikalini ambapo Idara hii, chini ya Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na
Utawala Bora iliruhusu aajiriwe kama Karani Maktaba. Hata hivyo, Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano bila ya taarifa yoyote kwa Idara ya Utumishi wala kumuandikia barua yoyote wala
kufuata utaratibu wowote wa kisheria ikaamua kumuajiri Karani Masjala ya Siri. Kwa mnasaba
wa sifa za Karani Maktaba zilizowasilishwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasilisno,
alitakiwa awe na elimu ya Diploma ama cheti katika fani ya „Record Management‟. Kwa bahati
mbaya sana, Ndg. Tum Gharib Moh‟d amemaliza Kidato cha Sita na pia alisomea Ualimu katika
Chuo cha Kiislamu mwaka 2009 (Kielelezo Na.83).
87
Kamati haikuwa na pingamizi na elimu ya Mfanyakazi huyu wala usahihi wa vyeti vyake
alivyoviwasilisha mbele ya kamati, jambo inalohoji ni kwa nini mfanyakazi huyu akaajiriwa
kufanya kazi ya masjala ya Siri ukizingatia nafasi hii haikuombwa na kwa mnasaba huu, Wizara
ya Miundombinu na Mawasiliano haikuwa na upungufu katika nafasi hiyo na imejibebesha
madaraka isiyo yake ya uajiri, kitendo ambacho kinapingana na maelekezo ya Kanuni ya 9 ya
Utumishi Serikalini. Aidha, ilihitaji nafasi 1 ya Karani Maktaba ambapo Ndg. Tumu Gharib
Moh‟d alikwisha ajiriwa kufanya kazi hiyo. Bila ya shaka bado ni kusisitiza kwamba, kwa
utendaji wa namna hii, inaleta shaka kwamba Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala
Bora haina mipango mizuri ya rasilimali watu na pia hali hii inaweza kuleta mashaka kwamba,
Watendaji Wakuu wa Wizara za Serikali, wanatumia hoja na taratibu za namna hii kuwatafutia
kazi ndugu zao.
3.5.4 NDG. ASHA SAID MOH‟D:
Mfanyakazi huyu amemaliza masomo yake mwaka 2000, Kidato cha Nne Skuli ya Sekondari
Mwanakwerekwe „A‟ na baadae kajiendeleza na masomo ya Ukarani, mwaka mmoja (Secretary)
Chuo cha Utawala wa Umma cha Zanzibar (The Institute of Public Administration of Zanzibar),
kuanzia mwezi July 2008 hadi June 2009. Aidha, Mfanyakazi huyu ameajiriwa katika fani
aliyoisomea ya Katibu Muhtasi. Hali hii imeifurahisha sana Kamati na kuzipongeza Wizara zote
mbili kwa kumuajiri mtu kwa mujibu wa fani aliyoisomea.
3.5.5 NDG. MCHANGA IBRAHIM ABDALLA:
Mfanyakazi huyu ameajiriwa tarehe 01/06/2011 ambapo kwa mujibu wa ruhusa kutoka Ofisi ya
Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Rejea Kielelezo Na.80) alitakiwa aajiriwe kama
Karani Kalamazoo kwa mshahara wa Tsh. 105,564/- katika ngazi ya ZOS-2, lakini kwa maamuzi
ya Wizara ya Miundobminu na Mawasiliano aliajiriwa Katibu Muhtasi. Aidha, Kamati
haikupatiwa sifa zozote zilizohitajika kwa mfanyakazi wa cheo cha Karani Kalamazoo, nafasi
ambayo haikuombwa kutoka Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwenda kwa Idara ya
Utumishi Serikalini. Kwa upande wa Katibu Muhtasi, alitakiwa awe na elimu ya Kidato cha Nne
na cheti cha Secretari, ambapo Ndg. Mchanga amemaliza Kidato cha Nne katika Skuli ya
Sekondari ya Zanzibar Commercial, mwaka 2005 lakini hajasomea mafunzo ya Usekretari.
Aidha, Ndg. Mchanga hakuweza kuithibitishia Kamati kama amepata mafunzo ya Kompyuta, na
kwa maaana hii, Kamati haikuwa na uhakika kuhusu uwezo wa mfanyakazi huyu kutumia
Kompyuta na kuweza kutekeleza majukumu ya Usekretari.
3.5.6 FAT-HIYA MOH‟D ALI:
Kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine, Ndg. Fat-hiya Moh‟d Ali ameajiriwa tarehe 01/06/2011
kama Karani Kalamazoo, nafasi ambayo pia ilitolewa kibali na Idara ya Utumishi Serikalini.
Ndg. Fat-hiya amemaliza Kidato cha Nne na kupata „D‟ moja ambapo ni sawa na kusema
kwamba Mfanyakazi huyu amekosa cheti cha Kidato cha Nne ambacho huwa hakitolewi kwa
mwanafunzi aliemaliza mtihani na kupata matokeo ya „D‟ moja tu ya masomo yake. Na ndio
maana kwa ushahidi wa kukosa cheti hicho, hata maombi yake ya kazi aliyoyapeleka Idara ya
Utumishi Serikalini kwa ajili ya kuajiriwa, aliambatanisha na „Leaving Certificate‟ ya mwaka
2004 (Kielelezo Na.84) aliyoipata Skuli ya Sekondari, Lumumba (Lumumba Centre) kama
„Private Candidate‟. Hata hivyo, baadae alijiendeleza kielimu kwa kusomea Uhasibu (Business
Account) Stage I na Stage II (Kielelezo Na.85), kwa maana hii, Ndg. Fat-hiya ameajiriwa akiwa
88
hana sifa ya kuhitimu Kidato cha Nne ila ameajiriwa kwa kuzingatiwa vyeti vyake vya „Business
Accounts.‟
Kwa kuzingatia hali hii, Kamati pia ilitaka kujiridhisha kuhusu usahihi wa chei chake cha
kuzaliwa chenye kuonesha kwamba amezaliwa tarehe 12/06/1984. Hata hivyo, katika maombi
aliyoyapeleka Idara ya Utumishi Serikalini, kopi ya cheti chake ameibadilisha ili isomeke
kazaliwa mwaka 1985, aidha miongoni mwa sababu zilizompeleka afanye udanganyifu huu, ni
kwamba alitaka kulinganisha na mwaka uliopo katika Kadi yake ya Kitambulisho cha
Mzanzibari yenye namba 300122475 kinachoonesha amezaliwa tarehe 12/06/1985 (Kielelezo
Na.86). Tafsiri iliyoipata Kamati kuhusiana na kitendo hiki ni kwamba, Ndg. Fat-hiya amefoji
cheti cha kuzaliwa na kupunguza mwaka mmoja kinyume na mwaka sahihi aliozaliwa, jambo
ambalo kiutumishi ni kosa lisilovumilika kama linavyoelezwa katika kanuni ya 132 na 134 ya
kanuni za Utumishi Serikalini na pia litamnyima haki yake ya kustaafu kwa mwaka mmoja
baada ya ule ambao angestahiki kustaafu kisheria. Hivyo uajiri wa Mfanyakazi huyu umetokana
zaidi na udanganyifu na ni wazi kwamba hakuwa na sifa za kuajiriwa katika nafasi hiyo.
3.5.7 NDG. HANIFA SALEH MOH‟D
Miongoni mwa vipengele muhimu vya Hadidu hii, ni pamoja na Kuchunguza madai ya
Mfanyakazi alieajiriwa na Taasisi mbili tofauti zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa
maana hiyo, kwa mujibu wa uchunguzi wa Kamati kama unavyofafanuliwa katika maelelezo ya
Mfanyakazi huyu, ni kuathibitisha kwamba Ndg. Hanifa Saleh Moh‟d ameajiriwa katika taasisi
hizo, yaani Shirika la Bandari pamoja na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Ili kupata
ufafanuzi yakinifu, suala la kwanza ni kujiuliza iwapo ni kweli Ndg. Hanifa Saleh Moh‟d ni
mfanyakazi wa Shirika la Bandari.
Katika kikao cha tarehe 23/11/2011, Kamati ilimuita aliekuwa Mkurugenzi wa Shirika la
Bandari, Ndg. Mustafa A. Jumbe pamoja na watendaji wake kuhusiana na madai haya, ambapo
amethibitisha kwamba Ndg. Hanifa ni Mfanyakazi wake na wanamlipa Mshahara wa Tsh.
192,480/- na hivi sasa yuko masomoni akisomeshwa na Shirika la Bandari. Aidha, Shirika la
Bandari lilipofanya juhudi za kupandisha daraja kwa wafanyakazi wake kutoka ajira ya kutwa
kwenda ajira ya muda, mfanyakazi wa pili kati ya 26, alikuwa Ndg. Hanifa Saleh Moh‟d
(Kielelezo Na.87) kwa maana hii, Kamati imeridhika na hoja iliyotolewa na Mkurugenzi wa
Shirika la Bandari kwamba Ndg Hanifa ni Mfanyakazi wa Shirika la Bandari.
Suala la pili ambalo ni muhimu ni kujiridhisha iwapo Ndg. Hanifa kwa ridhaa yake alipeleka
maombi Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwa lengo la kuajiriwa wakati huo huo
akiendelea kutumikia Shirika la Bandari. Kwa mujibu wa majibu aliyoyaeleza Ndg. Hanifa Saleh
Moh‟d alipoitwa na kuhojiwa na Kamati alikiri kwamba kwa ridhaa yake alipeleka maombi
Idara ya Utumishi Serikalini kwa lengo la kuajiriwa na kwa mkono wake bila ya kulazimishwa
na mtu yoyote alijaza fomu za Mkataba wa ajira na hati za Upimaji wa Daktrai (Kielelezo
Na.88). Vile vile suala hili lilipoulizwa kwa uongozi wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano nao pia walikiri kwamba Ndg. Hanifa aliomba kazi Wizarani hapo kwa ridhaa yake
huku akijua kwamba ni mfanyakazi wa Shirika la Bandari, sambamba na suala hili
lilipoelekezwa kwa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora hakukuwa na majibu
tofauti.
89
Suala jengine ambalo mtu wa kawaida (reasonable person) anajiuliza, je kulikuwa na mshaharaa
wake wowote uliowahi kufikishwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na nini khatma ya
Mshahara huo? Kamati ilitaka uthibitisho wa mshahara wowote kuwahi kutolewa kwa
mfanyakazi huyu, ambapo Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora
aliithibitishia Kamati kwamba, Serikali ilikwisha lipa mishahara ya miezi minne kuanzia June
hadi September 2011 yenye thamani ya Tsh. 400,972/- iliyowahi kulipwa kutoka katika Mfuko
wa Hazina na kukabidhiwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano (Kielelezo Na.89). Suala
hili pia lilithibitishwa na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwa kuwasilisha
voucher ya malipo ya wafanyakazi wake ikiwa ni pamoja na mfanyakazi huyu (Kielelezo
Na.90). Aidha, pamoja na mshahara huo kufika Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,
haukuwahi kupokelewa hata mwezi mmoja na Ndg. Hanifa na matokeo yake ulikuwa chini ya
mikono ya Mshika Fedha wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ambae kwa muda wote
wa Kamati hakuwepo na Kamati ilipata tabu kuthibitishiwa iwapo fedha hizo ziko mikononi
mwake au zipo sehemu nyengine.
Hata hivyo, hatimae ikaelezwa kwamba fedha hizo ziko mikononi mwa Mshika Fedha huyo,
ambae ndio hati za malipo pamoja na fedha hizo amezifungia ofisini na ufunguo ameuchukua
yeye wakati huo yuko likizo, Dar es Salaam akiuguliwa na mwanawe. Hata hivyo, Kamati
inaamini kwamba, kama si ujio wa Kamati hii, fedha hizo zingelimazika mikononi mwa
watendaji wa fedha wa Wizara ya Mundombinu na Mawasiliano, huku fedha za wananchi
zikiendelea kuliwa na wachache katika kivuli cha wafanyakazi hewa, aidha,kwa hali hii
inaonesha wazi kwamba, ndani ya Serikali tatizo la wafanyakazi hewa linaendelea. Hata hivyo,
Kamati iliwashauri watendaji hao kuzirejesha fedha hizo Hazina na wao mnamo tarehe
24/11/2011 walitekeleza ushauri huu wa Kamati (Kielelezo Na.91) ambapo wakati huu
tunawasilisha ripoti yetu, tayari mshahara huo wa Ndg. Hanifa Saleh Moh‟d umesharejeshwa
Serikalini. Pamoja na juhudi hizo, Kamati imejiridhisha juu ya hoja hii, kwamba Ndg. Hanifa
ameajiriwa mara mbili na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na Shirika la Bandari na
Uongozi wa Wizara zote mbili, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na Idara ya Utumishi,
chini ya Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora zinahusika na zinapaswa
kuwajibika kwa kosa hili.
Pamoja na hali hiyo, ni vyema tueleze kwamba, Mfanyakazi huyu ameisumbua Kamati kwa
kuitwa na kushidwa kuhudhuria kwa wakati, hivyo ndani ya siku 3 Kamati ilidhamiria kukutana
nae lakini kwa mafanikio ya kukutana nae yalipatikana baada ya Kamati kumuagiza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano huku ikitaka kutumia nguvu za kisheria ili
afike mbele ya Kamati kama alivyoitwa.
3.5.8 NDG. NADYA RASHID KHALFAN
Ndg. Nadya Rashid Khalfan ameajiriwa kuwa Mhudumu V.I.P tarehe 1/6/2011. Kwa upande wa
Uguja hakukuwa na nafasi tupu ya Mhudumu V.I.P iliyoombwa Idara ya Utumishi Serikalini.
Hata hivyo, kulikuwa na nafasi 3 zilizoombwa kwa Wahudumu Bustani/ Usafi kwa Uwanja wa
Ndege, ambapo kwa mujibu wa majibu yaliyotolewa na Wizara, walieleza kwamba Wahudumu
hao walioombwa Idara ya Utumishi ni pamoja na Wahudumu V.I.P. Unguja. Hoja hii
haikubaliwi na Kamati kwa sababu mbili zifuatazo : Moja, sifa za Wahudumu Usafi/ Bustani
pamoja na dhati ya kazi zao hazihusiani na majukumu ya Wahudumu V.I.P ; na hoja nyengine ni
kwamba, sifa za nafasi 4 zilizohitajika kwa Wahudumu wa Uwanja zililazimisha wawe wanaume
90
na kwa kuwa Ndg. Nadya Rashid Khalfan ni mwanamke, bila ya shaka hahusiki na sifa hizi.
Aidha, Kamati inashawishika kulinganisha sifa za Mhudumu V.I.P zilizohitajika Pemba ambapo
nafasi 4 ziliombwa kwa ajili ya Mhudumu V.I.P. (Rejea Kielelezo Na.79 kuhusu Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege Pemba).
Kwa mnasaba huu, Mhudumu wa V.I.P alitakiwa awe na elimu ya Kidato cha Nne na cheti cha
„House Keeping‟ wakati Ndg. Nadya Rashid Khalfan amemaliza masomo ya Kidato cha Pili.
Kwa maana hii, hakua na sifa ya kuajiriwa na kufanya kazi kama Mhudumu wa V.I.P.
3.5.9 NDG. JABU HAJI JUMA:
Ndg. Jabu Haji Juma ameajiriwa kuwa Mhudumu Bustani kama ruhusa ya uajiri wake
ilivyoelekeza kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hata hivyo, kwa
maoni ya Kamati Ndg. Jabu hakuwa na sifa za kuajiriwa nafasi hii kwa sababu yeye amemaliza
Kidato cha Pili, Skuli ya Sekondari ya Mwanakwerekwe „A‟ (Kielelezo Na.92). Aidha, kwa
upande wa sifa zilizohitajika kwa nafasi hii, Mhudumu Bustani/ Usafi alitakiwa awe na elimu ya
Kidato cha Nne na cheti cha „House Keeping‟.
Aidha, wakati Kamati inamhoji Ndg. Jabu kuhusu vipi aliambatanisha maombi yake na cheti cha
kumalizia masomo, alieleza kwamba hapo mwanzo maombi yake hakuyaambatanisha na cheti
ila baadae aliandikiwa barua ya mkono kutoka Idara ya Utumishi Serikalini kumtaka akipeleke
cheti hicho. Suala hili lilipoelekezwa kwa watendaji wakuu wa Idara hii, walikana kufanya hivyo
na kusisitiza kwamba, jambo hilo haliwezekani kufanywa na Idara yao. Kwa mnasaba wa hali
hii, Kamati inapenda kuweka wazi kwa mujibu wa hali hii kwamba, huu ni mfano mmoja tu wa
ushahidi wa uwongo ulivyotolewa na wafanyakazi hawa pamoja na Wizara hizi mbili
zinazohusika na ajira. Na kwa hali hii pia Kamati imejenga hofu kubwa juu ya wimbi la vyeti
vya udanganyifu zaidi kwa Kidato cha Pili, ambavyo kupatikana kwake kuna utata na ni rahisi
kwa wafanyakazi hawa kutoa fedha kwa walimu wakuu wa Skuli husika na kwa viwango vya
pasi vinavyoainishwa katika vyeti hivi bila ya shaka vingi ni vya kubuni tu bila ya kujali uhalali
wa pasi za wanafunzi husika.
3.5.10 NDG. SHADYA MMANGA BAI
Ndg. Shadya Mmanga Bai ameajiriwa kufanya kazi ya Mhudumu Bustani, tarehe 1/6/2011
ambapo kwa mujibu alivyoeleza mbele ya Kamati kwamba baada ya kupeleka maombi yake ya
kazi, alikuwa anafuatiliwa na mama yake, Mwasiti Zam anaefanya kazi Shirika la Utangazaji la
Zanzibar (ZBC). Ndg. Shadya amemaliza masomo ya Kidato cha Nne, Skuli ya Sekondari
Jang‟ombe mwaka 2008 na mwaka 2009 alifanya mtihani wa kurejea masomo hayo katika Skuli
ya Sekondari ya Haile Sellassie. Hata hivyo, kwa kuzingatia sifa zilizohitajika, Ndg. Shadya
hakusomea mafunzo ya „House Keeping‟ ambayo ni sifa ya pili muhimu katika utekelezaji wa
majukumu ya nafasi hii.
3.5.11 NDG. KOMBO WADI MAKAME
Ndg. Kombo Wadi Makame ameajiriwa kufanya kazi ya Mhudumu Mfyekaji, Mamlaka ya
uwanja wa Ndege ambapo kwa mujibu wa sifa zilizohitajika alitakiwa awe na elimu ya Kidato
cha Nne na cheti cha „House Keeping‟ wakati elimu aliyokuwa nayo Ndg. Kombo ni Kidato cha
Nne huku hakuwa na cheti cha „House Keeping‟. Hata hivyo kinyume na ruhusa ya uajiri kutoka
Idara ya Utumishi Serikalini, Ndg. Kombo Wadi Makame ameajiriwa na Wizara ya
91
Miundombinu na Mawasiliano kama Mlinzi Usalama bila ya kujali sifa zinazohitajika kwa nafasi
hii, kwamba mtu anatakiwa awe na elimu ya Kidato cha sita au zaidi. Kwa hivyo, mfanyakazi
huyu hana sifa za kufanya kazi katika nafasi aliyoajiriwa kwayo.
3.5.12 NDG. MIRAJI MABROUK IBRAHIM: Mfanyakazi huyu aliruhusiwa aajiriwe katika Idara ya Anga kama Mhudumu Mfyekaji kwa
mshahara wa Tsh. 100,000/- katika ngazi ya ZOS-1. Nafasi hii ya Mhudumu Mfyekaji (kama
ilivyo), haikuombwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na badala yake wameombwa
Wahudumu Uwanja wa Ndege na Wahudumu Bustani/ Usafi. Mfanyakazi huyu alipoulizwa lini
ameandika barua yake ya maombi, alisema ni tarehe 18/11/2010 wakati imepokelewa tarehe
12/11/2010, kitu ambacho ni muhali kuwezekana. Mfanyakazi huyu ameajiriwa katika nafasi
hiyo iliyoruhusiwa na Mamlaka ya Utumishi wa Serikali.
3.5.13 NDG. HAIDAR ABUU MUSSA:
Kibali cha kuajiriwa Mfanyakazi huyu kilitaka aajiriwe kama Fundi Maabara, katika Idara ya
Anga kwa mshahara wa Tsh. 116,006/, ngazi ya ZSS-1. Kwa bahati alipoitwa mbele ya Kamati,
alikiri kwamba ameajiriwa katika nafasi hiyo hiyo ya Fundi Maabara.
3.5.14 NDG. ALI IDARUSI SULEIMAN:
Kibali kilichotoka Idara ya Utumishi, kiliruhusu Ndg. Ali Idarusi Suleiman aajiriwe katika Idara
ya Anga akiwa ni Fundi Maabara kwa mshahara wa Tsh. 139,171 katika ngazi ya ZTS-1. Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana kwa Kamati kutoka kwa mfanyakazi huyu alipoitwa na
kuhojiwa alisema kwamba ameajiriwa Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara (UUB) (na sio
Idara ya Anga kama Fundi Maabara). Kuhusu maombi yake, alieleza kwamba aliomba mwezi
wa Septemba na pamoja na kuajiriwa UUB, sasa anafanya kazi kama Afisa Upimaji wa Ardhi
(Surveyer). Mfanyakazi huyu amesomea ualimu lakini anakiri kwamba ameajiriwa Baabara,
nafasi ambayo haikuombwa wakati Idara hii inapelekea maombi ya kujaza nafasi tupu, wakati
huo huo kwa namna yoyote ile, Fundi Maabara angekuwa na elimu ya Ufundi, lakini mfanyakazi
huyu amesomea ualimu. Bila ya shaka hakuwa na sifa za kuajiriwa katika nafasi hiyo.
3.5.15 NDG. AHMADA RAJAB MWINYI:
Kamati ilipatiwa taarifa mbili tofauti kuhusiana na Ndg. Ahmand Rajab Mwinyi. Kauli ya
kwanza iliyoelezwa na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwamba
Mfanyakazi huyu, pamoja na Ndg. Maulid Mmanga Issa na Ameir Ali Ameir hawakuajiriwa
tena na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano baada ya ruhusa yao ya kuajiriwa ilipotoka
Idara ya Utumishi. Na kauli ya pili ni kwamba Ndg. Ahmada Rajab Mwinyi ameajiriwa katika
nafasi ya Mlinzi Usalama, lakini kwa muda mrefu sasa ameondoka kazini kwenda masomoni
bila ya kupata ruhusa ya mwajiri wake na mshahara wake anaendelea kupokelea Bank. Kamati
imefahamishwa kwamba, Ndg. Ahmada aliomba ruhusa ya kwenda masomoni akiwa yumo
katika kipindi cha Majaribio ya Kazi (probation) lakini akaelezwa kwamba hawezi kwenda
masomoni kwa kuwa yumo katika kipindi cha majaribio na kutakiwa kama anataka kusoma kwa
namna yoyote hiyo, basi asome fani inayolingana na kazi yake pamoja na kuchukua likizo bila
ya malipo.
Ndg. Ahmada hakusikiliza muongozo huo na aliamua kwenda masomoni bila hata ya kuijuilisha
Wizara. Kwa upande wa Kamati imeona kitendo cha Mfanyakazi huyu ni kutoroka kazini na
92
kwa kuwa yumo katika majaribio, ifahamike wazi kwamba, kama inavyoelezwa katika Kanuni
ya 20 ya Kanuni za Utumishi Serikalini, mfanyakazi huyu amefeli ama hakufaulu majaribio na
hivyo hana haki ya kuthibitishwa kazini na kwa hatua ya awali, Kamati imeitaka Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano iuzuie mshahara wake na hatua za kutothibitishwa kazini zifuate.
Hata hivyo, ukifanya mnasaba wa Ndg. Aisha Msanif Haji, Mtoto wa Naibu Mkuu wa Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano aliruhusiwa kwenda masomoni bila ya masharti, na kesi ya
Mfanyakazi huyu, Ndg. Ahmada Rajab Mwinyi utakuta zinawinaya, tatizo la Ndg. Rajab
kaekewa masharti ya usomaji wake.
3.5.16 NDG. ASHURA IDDI ALI:
Mfanyakazi huyu amemaliza masomo yake ya Kidato cha Nne mwaka 2001, Skuli ya Secondari
ya Vikokotoni na tarehe 1/6/2011 aliajiriwa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kufanya kazi ya
Mlinzi Usalama huku akitakiwa awe amemaliza Kidato cha Sita au zaidi, wakati yeye amemaliza
Kidato cha Nne. Kwa maana hii, Ndg. Ashura Iddi Ali hakuwa na sifa ya kuajiriwa Mlinzi
Usalama kwani elimu yake ni ndogo kuliko ile iliyopendekezwa. Aidha, Ndg. Ashura
alipoulizwa vipi anatekeleza majukumu yake, aliieleza Kamati kwamba amepatiwa mafunzo ya
muda mfupi ya kulekeza namna ya kutekeleza majuku yake. Ifahamike kwamba, Kamati haina
tatizo na vyeti vyake ama elimu aliyonayo ya Kidato cha Nne, lakini inashanagaa kwa nini
asiajiriwe mtu mwenye sifa zinazohitajika wakati watu waliomaliza Kidato cha Sita au zaidi na
wenye uwezo wa kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi wapo wengi, huku ikizingatiwa
kwamba kulikuwa nab ado yapo maombi mengi ya ajira katika Idara hii ya Utumishi.
3.5.17 NDG. ASHA KOMBO MAALIM:
Ndg. Aisha Kombo Maalim amemaliza masomo ya Diploma ya Ualimu, Chuo Kikuu cha Taifa
Zanzibar (SUZA) mwaka 2010. Tatizo lake ni kwamba barua yake ya maombi aliiandika tarehe
16/11/2010, wakati tarehe ya uajiri wake ni 1/6/2010 (Kielelezo Na.93), yaani haiwezekani iwe
amepeleka maombi tarehe 16 wakati uajiri ulikuwa wiki mbili nyuma, yaani tarehe 1/6/2010. Hii
ina maana kwamba, Mfanyakazi huyu ameajiriwa bila ya kupeka maombi Idara ya Utumishi au
barua hiyo imeandikwa baada ya kupata tarifa kwamba Kamati inalifuatilia suala hili.
Mfanyakazi huyu ameajiriwa Mlinzi Usalama, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa mshahara wa
Tsh. 139,171/- kwa ngazi ya ZTS-1. Kamati haikuwa na pingamizi ya usahihi wa vyeti vyeka na
uwezo wake wa kielimu, lakini haiwezi kuvumilia udanganyifu wa maombi ya kazi na hii
inaenda sambamba na tafsiri kwamba, kuna watu wengi wamepeleka maombi yao muda mrefu
bila ya kuajiriwa, na badala yake wanaajiriwa watu ambao hata maombi yao ya kazi hayajapitia
Idara ya Utumishi Serikalini.
3.5.18 NDG. BUHETI JUMA SULEIMAN:
Mfanyakazi huyu amemaliza Kidato cha Nne nchini Uganda mwaka 2005 na kujiendeleza katika
mafunzo ya Ndege na Usafiri katika ngaz ya Diploma mwaka 2009 (Air Line and Travel
Studies) nchini Uengereza katika chuo cha „Greenwich School of Management London‟. Aidha,
mfanyakazi huyu amewasilisha mbele ya Kamati, vyeti mbali mbali vya masomo yanayohusiana
na uhudumu wa Ndege. Ndg. Buheti Juma Suleiman ameajiriwa kama Mlinzi Usalama katika
ngazi ya mshahara ZTS-1, Tsh. 139,171/- . Kamati haikuwa na pingamizi juu ya usahihi wa vyeti
na sifa za mfanyakazi huyu wala haikuwa na shaka juu uwezo wa kufanya kazi katika nafasi
aliyoajiriwa.
93
3.5.19 NDG. ALI RAMADHAN OMAR:
Ndg. Ali Ramadhan Omar alistahiki kuajiriwa kama Fundi Umeme, Mamlaka ya Uwanja wa
Ndege ambapo sifa za nafasi hii ni kuwa na elimu ya Diploma au Mafunzo ya FTC katika fani ya
Umeme (Rejea Kielelezo Na.79). Hata hivyo, kwa mujibu wa Ardhi Hali za kuingizwa kazini
(Kiambanisho Namba 94), Ndg. Ali Ramadhan Omar ameajiriwa kama Fundi Magari bdala ya
Fundi Umeme huku maamuzi haya yakifanywa bila ya kutolewa taarifa yyoyote kwa Idara ya
Utumishi Serikalini. Mfanyakazi huyu pamoja na kuajiriwa nafasi hiyo amemaliza elimu ya
Msingi (Primacy School) na ana cheti cha ufundi, Grade Three. Kwa maana hii Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano imejibebesha mamlaka ya uajiri kinyume na taratibu za Uajiri
kama ilivyoelekezwa na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Utumishi Serikalini, huku ikifahamu kwamba
mfanyakazi huyu hana sifa za kuajiriwa.
3.5.20 NDG. BUSRA ALI OTHMAN:
Ndg. Busra Ali Othman ameajiriwa katika Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kama Mlinzi ambapo
kwa mujibu wa sifa zilizohitajika, alitakiwa awe na elimu ya Kidato cha Nne na awe amepata
mafunzo ya Uaskari. Hata hivyo, kwa upande wa Ndg. Busra, amemaliza masomo ya Kidato cha
Tatu katika Skuli ya Sekondari ya Mkanyageni mwaka 1985. Miongoni mwa mambo
yaliyofahamika kwa mfanyakazi huyu ni pamoja na cheti chake cha kuzaliwa kimepatikana
tarehe 23/6/2011 (Kielelezo Na.95) wakati yeye ameajiriwa tarehe 1/6/2011, kwa maana hii,
pamoja na usahihi wa cheti hiki, Kamati inaamini kwamba, Ndg. Busra ameomba kazi akiwa
hajaambatanisha cheti hicho wakati katika maombi yake yanayoonesha ameomba kazi hiyo
tarehe 27/3/2008 na hivyo amekiwasilisha cheti hicho baada ya kuajiriwa. Hii pia inaonesha
kwamba baadhi ya taarifa za wafanyakazi walioajiriwa na Wizara hii, zilipatikana ama
zimetafutwa baada ya suala hili kujadiliwa katika Baraza la Wawakilishi, aidha tarifa nyengine
zilitengenezwa wakati Kamati ilipokuwa inafuatilia hadidu hii rejea huku Kamati ikizidi kupata
wasi wasi kwamba Wizara hii ina taarifa nyingi za udanganyifu wa wafanyakazi wake.
3.5.21 NDG. TWAHIR KASSIM SIMAI:
Ameajiriwa katika Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kama Afisa Mlinzi Usalama, ambae alitakiwa
awe na elimu ya Kidato cha Sita au zaidi. Kwa upande wa Ndg. Twahir Kassim Simai
amemaliza Kidato cha Sita mwaka 2009 katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba Kamati
haikuwa na pingamizi na Mfanyakazi huyo.
3.5.22 NDG. KHADIJA SULTAN NASSOR:
Taarifa zilizowasilishwa mbele ya Kamati na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano, kwamba Ndg. Khadija Sultan Nassor hapo kabla aliajiriwa kama Mhudumu
Mfyekaji ambae angestahiki awe amemaliza Kidato cha Nne na Cheti cha „House Keeping‟.
Hata hivyo, Ndg. Khadija amemaliza masomo ya Kidato cha Nne, Skuli ya Sekondari Mombasa
Central, mwaka 2007 na kujiendeleza mafunzo ya Kompyuta katika Chuo cha Karume Institute
of Science and Technology mwaka 2010/2011 (Kielelezo Na.96).
Mbali na hayo, Kamati imehakikishiwa kwamba Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano ilifanya mabadiliko kwa kufuta neno „Mfyekaji‟ na kuweka neno „V.I.P‟ (Kielelezo
Na.97). Ikumbukwe kwamba, nafasi hii ya Mhudumu V.I.P haikuombwa hapo awali. Kwa
maana hiyo, hata sifa za Mhudumu V.I.P hazikuorodheshwa kwatika taarifa zilizokabidhiwa kwa
Kamati. Kamati ilipohoji sababu za kubadilishwa kwake, Uongozi wa Wizara ya Miundombinu
94
na Mawasiliano ulieleza imefanya hivyo kwa kumheshimu Mdhamini wake, yaani Mhe. Hamad
Msoud Hamad (Rejea Kielelezo Na.97 AHADI–KIAPO) ambae ndie Waziri wa Wizara ya
Miundombinu na Mawasilino ndio iliyoufanya Uongozi wa Wizara hii kumbadilisha nafasi ya
kazi mfanyakazi huyu kutoka Mhudumu Mfyekaji hadi Mhudumu V.I.P.
Kamati haikuridhishwa n kitendo cha Mhe. Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mwasiliano
kumdhamini mfanyakazi wake, jambo ambalo linaleta ushawishi na upendeleo „bias‟ na matokeo
yake huathiri Kanuni za haki „principles of natural justice‟. Aidha, Kamati ilimhoji mfanyakazi
huyu juu ya uhusiano wake na Mhe. Hamad Masoud Hamad ambae alijibu hana uhusiano
wowote zaidi ya mwakilishi wake katika jimbo la Ole, maelezo ambayo yanapingana na ukweli
uliomo katika dodoso la Watumishi wa Serikali, ambapo ndg. Khadija Sultan Nassor katika
kujaza watu wa kupewa taarifa wakati wa dharura, katika watu wake wa karibu aliowajaza, mtu
wa kwanza amemwandika Mhe. Hamad Masoud Hamad ambae ni babu yake (Rejea Kielelezo
Na.97).
3.5.23 SALUM KHAMIS ABEID:
Ndg. Salum Khamis Abeid ameajiriwa kufanya kazi ya Mhudumu Mfyekaji ambapo nafasi hii
haikuwa wazi katika orodha ya nafasi zilizohitajika. Katika nafasi zilizohitajika na Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege, nafasi za wahudumu ziko namna mbili: Wahudumu wa Bustani/Usafi nafasi
3 ambao sifa zao wawe na elimu ya Kidato cha Nne na cheti cha „House Keeping‟ na wahudumu
wa pili ni Wahudumu Uwanja, nafasi 4 ambae wawe wanaume na wawe na elimu ya Kidato cha
Nne. Kwa maana hii, hakukuwa na nafasi ya Mhudumu Mfyekaji iliyoombwa na Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege na Wizara ya Miundombinu kwa ujumla. Kwa upande wa Ndg. Salum,
amemaliza Kidato cha Nne Skuli ya Sekondari ya Hurumzi na hakujiendeleza kimasomo baada
ya hapo. Hivyo, basi, kwa maana ya Mhudumu yoyote awaye, mfanyakazi huyu kuna sifa
hajazitimiza na hali hii pia imejitokeza takriban kwa wafanyakazi wote waliohusika na zoezi hili.
Aidha, jambo jengine linalohusika ni tarehe ya uajiri wa mfanyakazi huyu kwamba ameajiriwa
tarehe 1/6/2011 na barua yake ya maombi ameiandika tarehe 20/2/2011 lakini mawasiliano ya
ndani ya Idara ya Utumishi yanaonesha kwamba hatua za kuajiriwa na kukamilika kwake
zimechukuliwa tarehe 23/10/2011 (Kielelezo Na.98) kwa maana hii, Kamati imefahamau
kwamba ameajiriwa kabla ya kupeleka maombi yake ya kazi au barua hiyo imeandikwa baada ya
suala hili kujadiliwa Barazani na hatimae kufanyiwa kazi na Kamati.
3.5.24 NDG. MOH‟D BAKARI JUMA:
Ameajiriwa kufanya kazi ya Ufundi Umeme katika Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara
(UUB) ambapo kati ya nafasi 100 zilizoombwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
kwenda Idara ya Utumishi Serikalini, nafasi ya Fundi Umeme haikuombwa. Hata hivyo, Idara ya
Utumishi Serikalini ilitoa kibali cha Mfanyakazi huyu kuajiriwa kama Fundi Umeme, ambapo
nafasi hii iliombwa kwa ajili ya Idara ya Usafiri na Leseni huku ikipendekezwa kwamba mtu
atakaeajiriwa katika nafasi hii awe na cheti cha FTC katika fani ya umeme. Kwa upande wa Ndg.
Moh‟d Bakari Juma alieleza Kamati kwamba ameajiriwa akiwa na elimu ya Kidato cha Nne
aliyoipata katika Skuli ya Sekondari ya Nyuki, lakini wakuwahi kupata mafunzo yoyote kutoka
FTC katika fani hiyo ya umeme na wala hakuweza kuithibitishia Kamati hicho cheti cha Kidato
cha Nne alichosema amekipata katika Skuli ya Sekondari ya Nyuki. Hii ina maana kwamba,
Mfanyakazi huyu ameajiriwa katika nafasi ambayo hana sifa zilizohitajika.
95
3.5.25 NDG. MOH‟D OMAR MMANGA:
Kibali cha kuajiriwa mfanyakazi huyu kilielekeza aajiriwe kama Fundi Mitambo kwa mshahara
wa Tsh. 111, 643/- katika ngazi ya ZOS-3, katika Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara
(UUB). Kwa mujibu wa sifa zilizopendekezwa na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, ili
mfanyakazi aajiriwe kama fundi Mitambo ni lazima awe amemaliza Kidato cha Nne na
kuendelea. Hata hivyo, Mfanyakazi huyu alipoitwa na kuhojiwa mbele ya Kamati alikiri
kwamba amemaliza Kidato cha Pili (Form II) wakati huo huo anakiri kwamba ameajiriwa kama
Form IV. Ni wazi kwamba nafasi hii pia ingelihitaji mtu asomee ufundi wa Mitambo husika.
Kamati inaamini mfanyakazi huyu hakuwa na sifa za kuajiriwa katika nafasi hiyo.
3.5.26 NDG. AMEIR ALI AMEIR:
Idara ya Utumishi Serikalini ilitoa kibali cha kuajiriwa kwa Ndg. Ameir Ali Ameir kama Fundi
Mitambo, Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara kwa mshahara wa Tsh. 111,643 katika ngazi
ya ZOS-3. Hata hivyo, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano iliieleza Kamati kwamba
mfanyakazi huyu hakuajiriwa kwa sababu hakufuatilia tena maombi yake na hivyo inawezekana
ameakhirisha. Pamoja na maelezo hayo, kuna masuala mengi yanayoulizwa na Kamati
kuhusiana na hali hii, ikiwa ni pamoja na mshahara wake, kwa kuwa alikuwa tayari
ameshaajiriwa, je ulipokelewa na nani? Kuhusu jawabu ya suala hili, Kamati haikupata maelezo
yoyote zaidi ya kuelezwa kwamba mshahara wake umezuiliwa na haukupokelewa, bila ya
kupatiwa uthibitisho wowote wa namna Wizara hii ya Miundombinu na Mawasiliano ilivyofanya
mawasiliano na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Ofisi ya Rais, Fedha,
Uchumi na Mipango ya Maendeleo kuhusu mshahara na nafasi tupu ya mfanyakazi huyu.
Jambo la kushangaza ni kwamba, Kamati imepata ushahidi wa kutosha kwamba Ofisi ya Rais,
Utumishi wa Umma na Utawala Bora haina taarifa ya khatma ya mfanyakazi huyu na ndio
maana katika barua yake ya tarehe 31/05/2011 yenye kumbu kumbu namba
OR/UUU/K90/1/VOL.XXIX/71 (Kielelezo Na.99), ilifuta ruhusa ya uajiri wa Ndg. Moh‟d Ali
Mussa na Ndg. Maulid Mmanga Issa walioruhusiwa kuajiriwa kama Fundi Umeme na kuruhusu
kuajiriwa kwa Ndg. Saleh Said Saleh na Ndg. Ali Makungu Soud, lakini haikufuta ruhusa ya
mfanyakazi huyu wakati Kamati imejuilishwa kwamba hakuajiriwa. Na kwa hali hii, tafsiri moja
muhimu inayopatikana ni kwamba, wafanyakazi wa aina hii wapo wengi Serikalini.
3.5.27 NDG. ASMA AMEIR ALI:
Mfanyakazi huyu ameajiriwa kama Mpimaji. Aidha, miongoni mwa nafasi 3 zilizopendekezwa
kwa Wapimaji Idara ya UUB-Unguja, hakuna sifa zao zilizoainishwa, ila kwa upande wa UUB-
Pemba Mpimaji alitakiwa awe na elimu ya FTC-Civil. Ndg. Asma Ameir Ali amemaliza
masomo ya Kidato cha Sita na kupatiwa mafunzo madogo madogo ya kumjengea uwezo na
uzoefu wa kazi yake.
3.5.28 NDG. ALI JUMA ISSA:
Ndg. Ali Juma Issa ameajiriwa Mpimaji katika Idara ya UUB, tarehe 1/6/2011. Katika nafasi
zilizoombewa kwa Idara hii, mfanyakazi mmoja kati ya hao ni huyu Ndg. Ali Juma Issa, nafasi
iliyohitaji mfanyakazi wake awe na elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea. Mfanyakazi huyu
ameajiriwa kwa mujibu wa kibali kilichotoka Idara ya Utumishi, iliyo chini ya Ofisi ya Rais,
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa mshahara wa 116,006/- katika ngazi ya ZSS-1.
96
3.5.29 NDG. OTHMAN ALI OTHMAN:
Mfanyakazi huyu ameajiriwa Fundi Magari, Idara ya Usafiri na Leseni. Pamoja na sifa zote
zilizohitajika, Ndg. Othman Ali Othman ameghushi kopi ya cheti cha kuzaliwa
alichokiambatanisha na maombi yake ya kazi kwa kufuta mwaka 1983 ambao ndio aliozaliwa na
badala yake kuweka mwaka 1980 (Kielelezo Na.100) katika sehemu zote mbili zilizoainisha
mwaka huo; sehemu ya tarehe na pahala pa kuzaliwa na sehemu ya tarehe ya usajili na saini ya
Afisa Msajili wa vyeti.
Suala ambalo Kamati imejiuliza, je Wizara zote mbili zilizohusika na uajiri wake, Ofisi ya Rais,
Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,
hawakugundua udhaifu wa cheti hiki ambacho kwa kila mtu anaeona anajua kama kimeghushiwa
au kwa makusudi imeridhia udanganyifu huo, ambao pia umeoneka kwa wafanyakazi wengine
walioajiriwa. Bila ya shaka kwa upande wa Kamati imejiridhisha kwamba, Maofisa Utumishi,
Mkatibu Wakuu wa Wizara hizi pamoja na watendaji wengine kwa namna moja ama nyengine
wanahusika na suala hili. Hali hii inapelekea Serikali kuwa na wafanyakazi wasio na sifa na
matokeo mabovu ya utendaji.
3.5.30 NDG. AMERI KIROBO YUSSUF:
Kibali cha kuajiriwa Mfanyakazi huyu kimeelekeza kwamba aajiriwe kama Mlinzi katika Idara
ya Usafiri na Leseni kwa mshahara wa ngazi ya 100,000/- ZOS-1. Katika mapendekezo ya
kuajiriwa kwa nafasi hii, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano walitaka mfanyakazi huyu
awe amemaliza Kidato cha Nne na amepata mafunzo ya Uaskari. Katika maelezo yake,
Mfanyakazi huyu amesema amemaliza Skuli ya Kidongo Chekundu na hakueleza kupata
mafunzo ya Uaskari. Hivyo ni wazi kwamba, sifa zilizohitajika hazikuweza kutimizwa na
Mfanyakazi huyu.
3.5.31 NDG. MWALIM MUHSIN ALI:
Kibali cha kuajiriwa mfanyakazi huyu kilichotoka Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala
Bora kiliagiza mfanyakazi huyu aajiriwe katika nafasi ya Fundi Umeme, Idara ya Leseni. Kwa
mujibu wa maombi ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Fundi Umeme alitakiwa awe
na cheti cha FTC katika fani ya Umeme. Kwa bahati, mfanyakazi huyu amemaliza Kidato cha
Nne na alisema amemaliza pia masomo ya Umeme VETA. Kwa mnasaba huu, Kamati haina
pingamizi na mfanyakazi huyu.
3.5.32 NDG. KHAMIS OMAR SHEMEY:
Mfanyakazi huyu ni Mhandisi wa Ujenzi (Civil Engineering) aliyehamishiwa kutoka Wizara ya
Afya na kuwa mfanyakazi wa kudumu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Sababu ya
uhamisho huo, Wizara iliieleza Kamati kwamba, Wahandisi wana tabu kuwapata kutokana na
dhati ya kazi zao ni adimu n mara nyingi hulipwa mishahara mikubwa katika Taasisi Binafsi.
Kwa hekma hii, Kamati meelezwa kwamba, Wizara imefanikiwa kumpata Ndg. Khamis Omar
Shemey kutoka Wizara ya Afya ambako elimu yake hakuwa akiitumia ipasavyo. Kwa kuwa
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano inahushughulika zaidi na masuala ya uhandisi wa bara
bara. Aidha, kwa kutumia barua ya tarehe 20/7/2011 yenye kumbu kumbu namba
MOIC/U/40/1/VOL XVIII/, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano iliomba ruhusa ya
97
uhamisho wa mfanyakazi huyu pamoja na Ndg. Ali Said Ali Mwajiriwa wa Wizara ya Maji,
Ujenzi, Nishati na Ardhi wakielezea haja ya kuwatumia wafanyakazi hawa (Kielelezo Na.101).
Aidha, kwa kutumia barua ya tarehe 19/09/2011, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala
Bora ilimuandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Afya ikimtaka afanye Uhamisho wa
wafanyakazi wote hawa wawili (Kwa upande wa Ndg. Ali Said Ali, Mwajiriwa wa Wizara ya
Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, barua ilipaswa iandikwe kwa Katibu Mkuu wa Wizara hii na sio
Wizara ya Afya) (Kielelezo Na.102). Kamati haikuwa na pingamizi na Mfanyakazi huyu, Ndg.
Khamis Omar Shemey ambae alifika mbele ya Kamati na kuhojiwa. Hata hivyo, Kamati
haikupata maelezo ya Ndg. Ali Saidi Ali kwa sababu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
haikutoa ufafanuzi wowote unomhusu zaidi ya huo unaopatikana katika barua hizo.
2.4.33 RUHUSA YA WAFANYAKAZI KUAJIRIWA MARA MBILI:
Idara ya Utumishi Serikalini imetoa ruhusa mbili tofauti kufanywa kazi na mfanyakazi mmoja.
Hali hii imehusisha wafanyakazi wawili Ndg. Saleh Said Saleh na Ndg.Ali Makungu Soud
ambao wameajiriwa katika kazi mbili tofauti katika Wizara moja. Ushahidi huu unaonekana
katika Barua ya awali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala
Bora ya tarehe 12/5/2011 yenye kumbu kumbu namba OR/UUU/K90/VOLXXVIII/43 (Rejea
Kielelezo Na.80) katika ruhusa ya kuajiriwa wafanyakazi wa Idara ya Anga, sasa inafahamika
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, orodha No.5 ya wafanyakazi hao ni Ndg. Saleh Said Saleh
ambae ameruhusiwa kuajiriwa kama Mhudumu Mfyekaji kwa mshahara wa Tsh. 1000,000/-
katika ngazi ya ZOS-1. Pia ruhusa hii inamhusisha Ndg. Ali Makungu Soud, anaeonekana katika
barua hiyo hiyo, Iterm No. 11 ambae nae pia ameajiriwa kama Mhudumu Mfyekaji kwa
mshahara wa Tsh. 105,564/ katika ngazi ya ZOS-2.
Aidha, katika barua ya Wizara hii hii, ya tarehe 31/05/2011 yenye kumbu kumbu namba
OR/UUU/K90/VOLXXVIII/71, inayoendeleza ruhusa ya kujaza nafasi tupu za Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano (Rejea Kielelezo Na.99), imeruhusu tena wafanyakazi hawa
(wote wawili) kuajiriwa kama Fundi Umeme kwa mshahara wa Tsh. 105,564/- katika ngazi ya
ZOS-2. Kwa maana hii, ama Wizara hii inayohusika na utumishi wa Serikali haiweki kumbu
kumbu za kutosha ama ni moja kati ya Wizara inayochangia sana kuwepo kwa wafanyakazi
hewa wanaoingizwa kinyemela na hatimae kuiingiza Serikali katika upotevu mkubwa wa fedha
na kuongeza kasi ya Umasikini kwa wananchi wa Zanzibar.
3.5.34 ORODHA YA WAFANYAKAZI 18 WALIOBAINIKA NA KAMATI:
Baada ya kupitia wafanyakazi 33 wa awali, Kamati ilihoji kama wapo wafanyakazi wengine
waloajiriwa katika kipindi cha October 2010 hadi Septemba 2011 na kujibiwa kwa msisitizo
kwamba hakuna wafanyakazi mwengine wowote baada ya hao 33 wa awali, alieajiriwa katika
kipindi hicho. Hata hivyo, Kamati ilipata taarifa nje ya Wizara hizi kwamba wapo wafanyakazi
18 wengine waliajiriwa katika kujaza nafasi tupu zilizoombwa awali. Na baada ya suala hili
kufahamika wazi, ndipo Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ikakiri kwamba kweli wapo
waajriwa hao 18 walioajiriwa katika nafasi tupu za awali. Baadae ndio Kamati kwa utaratibu
unaofuata ilifanya mahojiano na wafanyakazi hawa kama inavyofuata hapa chini(isipokuwa pia
ifahamike kwamba, kati ya hao wafanyakazi 3 hawakuweza kupatikana). Bila ya shaka huu ni
udanganyifu wa wazi unaofanywa na watendaji kuidanganya Kamati, lakini pia ni kuficha
ukweli ambao Kamati imetumwa kuufichua.
98
3.5.34.1 NDG. SALMA MOHD ALI:
Ndg. Salma Moh‟d Ali amemaliza Kidato cha Nne, Skuli ya Sekondari ya Lumumba na
kuajiriwa Karani Maktaba. Kwa bahati sifa za Karani Maktaba zinaeleza kwamba Mfanyakazi
awe na Diploma au „Certificate‟ katika fani ya „Record Management‟. Hivyo basi, mbali na Ndg.
Salma Moh‟d Ali kumaliza masomo yake katika Kidato cha Nne, bado haikutosha kumfanya
awe na sifa za kuajiriwa kuwa Karani Maktaba, kwani ili aajiriwe katika nafasi hiyo, alitakiwa
awe na ama Diploma au Cheti cha „Record Management‟.
3.5.34.2 NDG. KHADIJA MOH‟D ALI:
Ameajiriwa kama Mhudumu Uwanja wa Ndege Zanzibar, nafasi ambayo Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano ilipoainisha sifa za wafanyakazi wanaowataka na hatimae
kuomba kibali cha uajiri wao Idara ya Utumishi Serikalini, ilipendekeza kwamba Mhudumu wa
Uwanja awe mwanamme na amemaliza elimu ya Kidato cha Nne. Aidha, wakati Kamati inapitia
vyeti vya mfanyakazi huyu, iligundua kuwa cheti chake cha Kidato cha Nne ni cha kufoji (cha
udanganyifu), kwani moja ya masomo yanayooneshwa katika „LeavingCertificate‟ ni tofauti na
masomo ya kopi ya cheti cha Kidato cha Nne alichokiwasilisha mbele ya Kamati. Aidha, Ndg.
Khadija hana cheti cha asili (original Certificate) ya cheti cha Kidato cha Nne na yeye
mwenyewe alikiri mbele ya Kamati kwamba cheti chake ni cha udanganyifu.
3.5.34.3 NDG. FARIDA ABDUL RAHMAN ABUBAKAR:
Ndg. Farida Abdul-Rahman Abubakar ameajiriwa kama Mhudumu wa Uwanja. Wakati kamati
inapitia barua na kumbu kumbu zake, imebaini kwamba saini aliyotia katika barua yake ya
maombi ya kazi inatofautiana na iliyotiwa kwenye kumbu kumbu zake binafsi ikiwa ni pamoja
na barua ya likizo aliyoomba tarehe 15/11/2011, Kumbu kumbu ya Ahadi-Kiapo ya tarehe
8/6/2011 na hata Ardhi hali ya kuingia kazini (Kielelezo Na.103). Ndg. Farida alipoulizwa suala
la utofauti wa saini katika kumbu kumbu zake, alikiri kwamba barua yake ya likizo lililoombwa
tarehe 15/11/2011 ameandikiwa, hakuandika yeye wala hakutia saini yeye. Pamoja na ufafanuzi
huo, Ndg. Farida hakuwa muwazi katika majibu yake na kuifanya Kamati ipate tabu katika
kutafuta ukweli wa jambo hili. Kwa mfano alipooulizwa kuhusu Hati ya Kiapo-Ahadi ya tarehe
8/6/2011 ni nani aliyemjazia, alijibu kwamba amejaza mwenyewe na saini zote mbili katia yeye.
Utatanishi huu unaenda sambamba na maandishi ya hati za barua hizo zinavyotofautiana sana na
hati za mkono za barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa tarehe 10/11/2004. (Rejea
Kiambanisho Namba 103), tofauti ambayo pia inapatikana katika hati zilizojazwa katika fomu
ya Ardhi Hali na Fomu za Upimaji wa Daktari. Kwa maana hii, Kamati inafahamu kwamba
mfanyakazi huyu sio tu kwamba amefoji saini katika kumbu kumbu zake mbali mbali, lakini pia
kuna uwezekano mkubwa fomu hizo na saini zilizomo zimejazwa na mtu mwengine asiyekuwa
yeye. Kitendo hiki kinapingana na maelekezo ya Kanuni ya 13(b) ya Kanuni za Utumishi
Serikalini inayoelekeza kwamba mtu anaetaka kuajiriwa anawajibika kujaza (kwa maana yeye
mwenyewe) fomu ya Ardhihali ya Kuingia Kazini. Aidha, kitendo hiki cha kujazwa na mtu
mwengine asiyekuwa yeye kimezidi kutoa fursa ya kujazwa taarifa zisizo na ukweli katika
kumbu kumbu hizo. Kwa mfano ukifanya marejeo ya Fomu ya Ardhihali ya Kuingia Kazini,
aliemjazia Ndg. Farida tarehe ya kuzaliwa kwake, ameacha kuujaza mwezi aliozaliwa Ndg.
Farida, wakati huo huo amemjazia amezaliwa mwaka 1986, wakati kwa mujibu wa Cheti chake
cha kuzaliwa, Ndg. Farida amezaliwa mwaka 1985 (Rejea Kielelezo Na.103).
99
Kwa maoni ya Kamati, udhaifu kama huu usiposhuhgulikiwa utaendelea kuleta mashaka
makubwa kuhusu usahihi wa taarifa za mfanyakazi huyu na kibaya zaidi kuleta utata wa umri
wake wa kustaafu na kupata haki zinazotokana na kustaafu kwake.
Mbali na mashaka hayo, Kamati pia imetia mashaka juu ya usahihi wa cheti chake cha kumalizia
masomo ya Kidato cha Nne kwamba ni cha udanganyifu, na kwa kuzingatia uchunguzi wa
Kamati wa cheti hicho cha asili (original), imegundua kwamba maandishi ya mwaka wa cheti
hicho hayajakoza tofauti kabisa na maandishi mengine katika cheti hicho hicho. Vile vile,
Kamati ilitaka kuangalia uwezo wa kusoma na kuandika wa Ndg. Farida, ambapo ilimtaka
asome maandishi ya lugha ya Kiswahili yaliyoandikwa katika karatasi na kumpa karatasi tupu ili
aandike maneno hayo. Kwa bahati mbaya sana, Ndg. Farida alishidwa kufanya hivyo, jambo
ambalo linaleta tafsiri nyingi, ama hajui kabisa kusoma na kuandika ama kwa khofu ameshindwa
kufanya yote aliyoagizwa. Hata hivyo, kwa ujula Kamati haikuridhika na sifa za Mfanyakazi
huyu na inaamini kwamba Wizara zote mbili zimehusika na hali hii, kwa maana Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
3.5.34.4 NDG. ASHA KHAMIS HEMED:
Mfanyakazi huyu ameajiriwa kama Mhudumu na amemaliza masomo yake katika Kidato cha
Pili, Skuli ya Sekondari ya Kidongo Chekundu, mwaka 2005. Mbali na sifa nyengine, elimu ya
msingi iliyohitajika kwa mfanyakazi huyu ni kuwa na elimu ya Kidato cha Nne, wakati Ndg.
Asha Khamis Hemed amemaliza Kidato cha Pili. Aidha, Kamati ilipomhoji vipi amekipata cheti
chake cha Kidato cha Pili, alieleza wazi kwamba alikipata Skulini hapo kupitia Mwalimu Mkuu
kwa kutoa Tsh. 5000. Vile vile Kamati ilikikagua cheti chake cha kuzaliwa na kugundua kuwa
mwaka aliozaliwa (1988) unatofautiana na ule uliojazwa katika kitambulisho chake cha
Mzanzibari yaani katika kitambulisho hiki amejaza amezaliwa mwaka 1987 (Kielelezo Na.104).
Kuhusu miaka yake, katika barua yake ya maombi ya kazi ya tarehe 15/6/2007, Ndg. Asha
alisema yeye ni kijana mwenye umri wa miaka 23 wakati amezaliwa mwaka 1988, kwa maana
hii ameficha ukweli kwa kuzingatia mwaka aliozaliwa, mwaka 2007 aliofanya maombi hayo,
alikuwa na miaka 19 na sio miaka 23 kama alivyosema (Kielelezo Na.105).
3.5.34.5 NDG. RASHID JUMA RASHID:
Ndg. Rashid Juma Rashid ameajiriwa Mlinzi Usalama ambae kwa mujibu wa sifa
zilizopendekezwa, alitakiwa awe amemaliza Kidato cha Sita au zaidi, ambapo kwa mujibu wa
mfanyakazi huyu, amemaliza Kidato cha Nne. Mfanyakazi huyu kama wafanyakazi wengine
waliofika mbele ya Kamati alitakiwa ahudhurie na vyeti vyake vya asili (original), lakini kwa
bahati mbaya aliieleza Kamati kwamba amesahau. Pamoja na yote hayo, Mfanyakazi huyu kwa
elimu aliyonayo na elimu inayotakiwa, ni wazi kwamba hakuwa na sifa za kuajiriwa kwake.
3.5.34.6 NDG. MAULID AMEIR VUAI:
Ameajiriwa Karani Masjala na amejieleza kwamba amemaliza Kidato cha Nne katika Skuli ya
Sekondari ya Mwanakwerekwe, mwaka 2003. Hata hivyo, Kamati ilipokikagua cheti hicho
imekigundua kuwa ni cha udanganyifu kwani taarifa zake zimejazwa kwa „typing‟ zikiwa ni
tofauti na vyeti vyengine. Aidha, orodha ya masomo iliyomo katika cheti hicho haikufuata
mtiririko ulio sawa, tofauti kabisa na vyeti vya kawaida (Kiambataisho Namba 106) na kwa
100
hali hii, Kamati imejiridhisha kwamba taarifa za elimu ya mfanyakazi huyu, Ndg. Maulid Ameir
Vuai ni za udanganyifu.
Kwa upande wa „Leaving Certificate‟ aliyoiambatanisha na maombi yake ya kazi, Ndg. Maulid
ameeleza kwamba amesoma somo la „Chemistry‟ lakini hakusoma somo la „Physics‟ ambayo ni
masomo ya Sayansi kwa mwanafunzi wa Kidato cha Tatu na Nne. Aidha, ameeleza amesoma
somo la Kiarabu lakini hakueleza kusoma somo la „History‟ ingawaje katika Cheti chake cha
Kidato cha Nne ameeleza kusoma somo hilo. Hii haikuwa wazi na inapingana na utaratibu wa
mwanafunzi kusoma sayansi ama art. Kwa lugha nyengine, Kamati imezidi kuingiwa na wasi
wasi na kwa uchunguzi huu imejiridhisha kwamba, vyeti vyote viwili, cha Leaving na cheti cha
Kidato cha Nne cha Mfanyakazi huyu ni vya udanganyifu (Rejea Kielelezo Na.106).
3.5.34.7 NDG. RASHID BADRU SULEIMAN:
Ameajiriwa Afisa Viwango, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege. Ndg. Rashid amemaliza masomo
yake Kidato cha Sita, Skuli ya Sekondari ya Bembella na baadae alijiendeleza kimasomo ya
Elimu Muendelezo, „Pre-University, Chuo Kikuu cha Zanzibar (Institute of Continuing
Education at Zanzibar University) mwaka 2009. Kamati haikuwa na pingamizi na elimu ya
Mfanyakazi huyu wala haikutia shaka dhidi ya usahihi wa vyeti vyake. Hata hivyo, tatizo
lililojitokeza kwa mfanyakazi huyu ni kitendo chake cha kuomba kazi akiwa bado yumo
masomoni huku akidanganya kwamba tayari ameshamaliza masomo yake ya Utawala wa
Uongozi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar. Kwa maana nyengine, Ndg. Rashid ameomba kazi
tarehe 29/09/2008 na kueleza kwenye barua yake kwamba ameshamaliza masomo ya Utawala
wa Uongozi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar wakati ukweli ni kwamba, masomo hayo
yameanza mwezi wa October 2008 na kumalizia mwezi wa July 2009 (Kielelezo Na.107). Hii
inaleta maana kwamba, Mfanyakazi huyu ameomba kazi bado akiwa mwanafunzi na
ukinasibisha na hali halisi ya kuwepo kwa wahitimu wengi wanaosubiri ajira na maombi yao ya
kazi yamefika Idarani muda mrefu, utaamini kwamba uajiri wa Mfanyakazi huyu ni wa
kimahusiano ya kirafiki ama kikazi na watendaji wanaohusika na ajira.
3.5.34.8 NDG. SHARIFA ABDULRAHMAN SEIF:
Kibali cha kumuajiri Ndg. Sharifa kilielekeza kuajiriwa kama Mhudumu Bustani, lakini Wizara
ya Miundombinu na Mawasiliano ikaamua kumuajiri Mhudumu V.I.P. Ndg. Sharifa amemaliza
masomo yake Kidato cha Nne ila alifeli na hakupata cheti hicho, na kwa maana hii, kwa kuwa
Mhudumu V.I.P alitakiwa awe amemaliza Kidato cha Nne na awe na Cheti cha „House
Keeping‟, Mfanyakazi huyu hakuwa na cheti cha Kidato cha Nne cha kuthibitisha usahihi wa
elimu yake bali alikuwa na „Leaving Certificate‟ ya kumalizia masomo Skuli ya Sekondari ya
Kiembe Samaki iliyotolewa tarehe 7/06/2011 wakati Ndg. Sharifa ameajiriwa tarehe 1/06/2011.
Kwa hali hii, Kamati imejiridhisha kwamba kuajiriwa kwake ni kuaminiwa tu kwamba
amemaliza Kidato cha Nne huku uthibitisho wa kumaliza kwake ukitegemea Leaving Certificate
ambayo pia ameiwasilisha wiki moja baada ya kuajiriwa kwake (Kielelezo Na.108). Aidha,
taarifa za Mfanyakazi huyu kujieleza kwenye barua yake ya maombi kwamba anaambatanisha
maombi yake na vivuli vya vyeti hazina ukweli kwani barua yake ya maombi ni ya tarehe
1/11/2009 wakati cheti chenyewe cha Leaving alichokiambatanisha amekipokea tarehe
07/06/2011, takriban miaka 2 baada ya kuandika barua ya maombi ya kazi. (Rejea Kielelezo
Na.108). Kamati bado inaendelea kuhoji utaratibu wa kuajiriwa kwa mfanyakazi huyu kwa
101
kutegemea „Leaving Certificate‟ wakati wako wananchi wengi tu wenye vyeti halisi na
wameomba kwa muda mrefu bila ya mafanikio.
3.5.34.9 NDG. SALUM JAFFAR JUMANNE :
Ndg. Salum ameajiriwa kama Tarishi. Ndg. Salum amekiri mbele ya Kamati kwamba amekimbia
Skuli wala hajafika Kidato cha Pili, ingawaje katika barua yake ya maombi ya kazi ameandika
amemaliza masomo, Kidato cha Pili (Form II). Kwa maana hii, Ndg. Salum Jaffar Jumanne
alikiri mbele ya Kamati kwamba amefanya udanganyifu. Mbali na hayo, Kamati imegundua
kuwa nafasi hii ya Tarishi haikuombwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kama nafasi
tupu na ndio maana pia haikupata ushahidi wowote wa sifa zilizohitajika kwa mfanyakazi wa
nafasi hii. Kwa lugha nyengine hakukuwa na haja ya uajiri wa nafasi hii.
3.5.34.10 NDG. JABU HASSAN JABU:
Ameajiriwa kufanya kazi ya Udereva. Ndg. Jabu Hassan Jabu alikiri mbele ya Kamati kwamba
yeye amekimbia Skuli ila amesomea udereva na ndio maana ameajiriwa katika nafasi hii. Hata
hivyo, kwa mujibu wa sifa zilizohitajika na Wizara hii, nafasi ya Udereva ilipaswa ijazwe na mtu
mwenye elimu ya Kidato cha Nne na Cheti cha Udereva.
3.5.34.11 NDG. KHAMIS RAMADHAN SALUM:
Mfanyakazi huyu ameajiriwa katika nafasi ya Udereva. Aidha, kama tulivyokwisha eleza hapo
awali, nafasi hii ilitakiwa ijazwe na mtu aliyemaliza Kidato cha Nne na amesomea na kupata
Cheti cha Udereva. Kwa upande wa Ndg. Khamis Ramadhan Salum amekimbia skuli kabla
hajafika hata Kidato cha Pili na kwa maana hii, hana elimu ya Kidato cha Nne iliyohitajika. Hata
hivyo, ameajiriwa kwa kigezo cha cheti cha Udereva tu.
3.5.34.12 NDG. SHEHA KISAKA SHEHA:
Ndg. Sheha Kisaka Sheha ameajiriwa kama Karani Masjala. Elimu aliyokuwa nayo ni Kidato
cha Nne aliyohitimu Skuli ya Sekondari ya Haile Selassie. Kamati haikuwa na pingamizi na
mfanyakazi huyu. Hata hivyo, kwa kukosekana sifa zilizohitajika kwa ajili ya nafasi hii, Kamati
haikuweza kulinganisha na uwezo wa Ndg. Sheha katika nafasi hiyo. Yaaani, nafasi hii
haikuhitajika pale Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ilipoomba kibali cha uajiri, lakini
kwa sababu wanazozijua Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ndio wameamua
kumuajiri katika nafasi hiyo.
3.5.34.13 NDG. SEIF ABDALLA ALI :
Ndg. Seif Abdalla Ali amemaliza Kidato cha Nne Skuli ya Sekondari ya SOS Herman Gmeiner
mwaka 2004. Kamati haikuwa na shaka na vyeti vya masomo vya mfanyakazi huyu. Hata hivyo,
jambo la kufahamika ni kwamba, kibali kilichotolewa na Idara ya utumishi Serikalini ni kwamba
aajiriwe kuwa Mlinzi Usalama lakini Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imemuajiri
kufanya kazi ya Mhudumu V.I.P.
3.5.34.14 NDG. BILESHI KHEIR KHAMIS :
Mfanyakazi huyu ameajiriwa kufanya kazi ya Mhudumu Mamlaka ya Usafiri Baharini.
Amemaliza Kidato cha Nne Skuli ya Sekondari ya Bububu mwaka 2007. Ndg. Bileshi Kheir
Khamis aliandika barua ya kuomba kazi kwa Mkurugenzi Idara ya Utumishi Serikalini tarehe
13/06/2009 lakini mpaka Kamati inakagua barua hiyo hata haikuwa na hata muhuri wa
102
kupokelewa Idarani hapo wala Muhuri mwengine wowote wa kuthibitisha kwamba barua hiyo
kweli ilipokelewa na kufanyiwa kazi (Kielelezo Na.109). Hali hii inaipa mashaka Kamati
kwamba barua hiyo kweli iliandikwa katika kipindi cha mwaka huo huku tukizingatia kwamba,
wakati wote Kamati inazipitia barua za maombi za wafanyakazi hawa 18, ilijaa shaka kwamba
barua hizo hazikuandikwa katika muda husika na hakuna muhuri uiliyotiwa kwa baadhi ya barua
kuonesha zimepokelewa na Idara ya Utumishi Serikalini. Aidha, saini ya barua yake ya kazi
inatofautiana na saini za mfanyakazi huyu katika kumbu kumbu zake nyengine.
3.5.34.15 NDG. HASSAN KUNDI JUMA :
Ameajiriwa kufanya kazi ya Tarishi. Ndg. Hassan ameieleza Kamati kwamba amemaliza Kidato
cha Pili, Skuli ya Sekondari ya Kwamtipura na cheti chake alikipata baada ya kutoa Tsh. 500/-.
Hata hivyo, kutokana na sifa za Tarishi kutowasilishwa katika hati za maombi na kibali cha
mfanyakazi huyu, kwa kuwa nafasi hii haikuombwa ni wazi pia kwamba hakukuwa na haja ya
kuajiriwa mfanyakazi huyu katika nafasi hii na zaidi kwa mnasaba wa elimu yake, ukizingatia
ukweli kwamba kazi hii ingeweza pia kufanywa na wananchi waliomaliza Kidato cha Nne.
3.5.35 MFANYAKAZI ALIEAJIRIWA AKIWA BADO NI MWANAFUNZI WA CHUO
KIKUU (NDG. MWANAKOMBO VUAI IDDI LILA)
Miongoni mwa hoja za msingi katika hadidu hii rejea ni pamoja na wasi wasi wa mfanyakazi wa
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kuajiriwa akiwa bado ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu
huku akipokea mshahara wa Mtaalamu, yaani mtu aliyemaliza masomo ya Chuo kikuu. Katika
hofu hii, Kamati ilitakiwa kufuatilia na kuchunguza iwapo madai haya yana ukweli ama hayana
usahihi wowote. Kwa hali hii, pamoja na wafanyakazi waliotajwa hapo juu, Kamati pia ilimwita
Ndg. Mwanakombo Vuai Iddi Lila baada ya kufahamu kwamba ndie Mfanyakazi anaehusika na
hoja hii na hivyo ufafanuzi wake ni kama ufuatao:
Kibali cha kuajiriwa Ndg. Mwanakombo kilitoka kisheria chini ya Idara ya Utumishi Serikalini
kupitia barua ya tarehe 3/09/2007 yenye kumbu kumbu namba UTU/AR/M.10/1/VOL.XVII/87
inayoruhusu kuajiriwa mfanyakazi huyu na wenzake watano katika Idara ya Marajis wa Meli
(Shirika la Meli) kama Afisa Tawala kwa mshahara wa Tsh. 154,395 ngazi ya ZPS-1 (Kielelezo
Na.110). Kufuatia ruhusa hiyo, mnamo tarehe 1/11/2007, Ndg. Mwanakombo aliajiriwa rasmi
katika nafasi hiyo hiyo iliyoruhusiwa na Idara ya Utumishi Serikalini na kujaza Fomu ya
Ardhihali pamoja na Fomu ya Daktari (Kielelezo Na.111), lakini hapa tunapenda ifahamike
kwamba elimu ya juu ya mfanyakazi huyu aliyoajiriwa kwayo kutoka masomoni ni Diploma ya
Ualimu aliyohitimu Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), na kwa hivyo katika maombi
yake ya kazi pia aliambatanisha vyeti vyake vya kumalizia masomo (Kielelezo Na.112).
Akiwa bado yumo katika kipindi cha majaribio (probation) Ndg. Mwanakombo aliomba ruhusa
ya kwenda masomoni mnamo tarehe 4/7/2008 na siku mbili baadae aliruhusiwa kupitia barua ya
tarehe 4/7/2008 yenye kumbu kumbu namba CAA/CCA/MW (Kielelezo Na.113). Tunaposema
„yuko katika kipindi cha majaribio‟ tukumbuke tu kwamba Mfanyakazi huyu wakati bado
hajathibitishwa kazini aliruhusiwa kwenda masomoni, kitendo ambacho ni kinyume na taratibu
za Utumishi. Hebu na tujikumbushe kifungu cha 18 cha Kanuni za Utumishi Serikalini (kama
zilivyokuwa zinatumika), Mfanyakazi huyu alilazimika kutumikia majaribio hayo kwa mwaka
mmoja na ndipo baadae taratibu za kuthbitishwa na kupewa haki nyengine zingelifuata.
Usishangae kukiukwa kwa masharti haya ya sheria na taratibu za kazi, kuna uhusiano wa karibu
103
na wa kiudugu baina ya Mfanyakazi huyu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano, ambapo kwa namna moja ama nyengine hawezi kunyimwa nafasi ya amsomo
ingawaje bado yumo katika kipindi cha majaribio.
Basi tukiendelea na ufafanuzi wa mfanyakazi huyu, wakati akiwa Chuo Kikuu cha Zanzibar
(Zanzibar University) Ndg. Mwanakombo alisoma Shahada ya Kwanza ya Uongozi wa Umma
(Public Administration) na kwa maelezo yake alimaliza tarehe 17, August 2011 (Kielelezo
Na.114). Jambo linaloshangaza ni ukweli kwamba, Shahada ya Kwanza ya Uongozi wa Umma
aliyokwenda kusomea ni ya miaka mitatu yenye Mihula sita (Six Semesters), lakini Cheti chake
cha muda cha kumalizia masomo hayo (Transcript) alichokiwasilisha mbele ya Kamati
kinaonesha amemaliza Mihula Mitano tu (Five Semesters) na kimetolewa tarehe 17/08/2011
wakati yeye mwenyewe aliripoti kazi tarehe 22/08/2011.
Pamoja na maelezo hayo, tutakumbuka kwamba moja kati ya mambo yaliyotakiwa yachunguzwe
na Kamati hii kuhusiana na hadidu hii ndogo ya rejea, ni kuhusu Mfanyakazi alieajiriwa akiwa
masomoni, ambapo kwa utafiti wa Kamati ilikuwa shaka hiyo ilihusishwa kwa Mfanyakazi
huyu. Tunapenda tuthibitishe kutokana na maelezo haya kwamba, si kweli kwamba mfanyakazi
huyu ameajiriwa akiwa masomoni, lakini kutokana na uchunguzi wa Kamati imejiridhisha
kwamba, wakati alipoajiriwa alikuwa anapokea Mshahara wa Mfanyakazi alierudi masomoni
katika ngazi ya Degree ya wakati huo. Kwa lugha hii, Kamati inathibitisha kwamba, Mfanyakazi
huyu alikuwa analipwa mshahara usiomstahikia.
Kamati baada ya mashaka haya ilitaka ipatiwe uthibitisho kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusiana na kadhia hii, ambae alithibitisha
kwamba, mfanyakazi huyu hapo alipoajiriwa alikuwa anapokea mshahara wa Mtaalamu, yaani
Tsh. 154,395 (Rejea Kiambatanisho 110), mshahara ambao ni mkubwa wa Mtaalamu mwenye
elimu zaidi ya Diploma. Aidha, kwa sababu ya kupita mgongo wa Baba yake, ambae ndio Katibu
Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, jambo hili pamoja na kinyume na taratibu
na utawala, na ni wizi wa fedha za umma, limewezekana kirahisi kabisa.
3.5.36 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii ndogo, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
3.5.36.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Kiuhalisia Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ndio iliyohusika na uajiri wa
wafanyakazi wake kuliko Mamlaka husika, Idara ya Utumishi Serikalini kutokana
na wafanyakazi hao kuajiriwa katika nafasi zilizokuwa hazijaelekezwa na
Mamlaka husika na hivyo, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano bila ya
utaratibu wowote kwa kuona wao tu inafaa, wameamua kuondosha (kutomuajiri
mfanyakazi) katika nafasi zilizoelekezwa na kujaza nafasi walizotaka wao, bila
hata ya kuangalia sifa na uwezo wa wafanyakazi hawa.
104
(ii) Idara ya Utumishi Serikalini kwa kushirikiana na Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano imewaajiri wafanyakazi wengi wasio kuwa na sifa na wengi wao
wameambatanisha katika maombi yao taarifa zisizo za kweli na za udanganyifu.
(iii) Kuna wafanyakazi wameajiriwa mara mbili katika Taasisi moja, yaani Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano huku Wizara zinazohusika zimekaa kimya bila ya
kutoa taarifa husika Serikalini.
(iv) Kitengo cha G.S.O hakikushirikishwa katika kutoa taarifa za wafanyakazi hawa,
kitendo ambacho kimezidi kupelekea udanganyifu mkubwa wa taarfa sahihi za
wafanyakazi hawa.
(v) Hakukuwa na ushahidi wowote wa kufanyiwa usaili wafanyakazi hawa kabla
hawajaajiriwa ili kuthibitisha uwezo wao, Kamati imegundua kwamba wengi wao
wameajiriwa kwa kuzingatia uenyeji.
(vi) Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
pamoja na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamehusika na
Upendeleo wa wazi wa watoto na jamaa zao katika utaratibu wa ajira na zaidi
katika utekelezaji wa majukumu ya wafanyakazi hao.
(vii) Kwa kupitia mfano huu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Kamati
imegundua kuwepo kwa matatizo makubwa ya ajira katika Utumishi wa Serikali
yaliyochangiwa sana na Idara ya Utumishi Serikalini.
(viii) Tatizo la Wafanyakazi hewa litaendelea kuisakama Serikali na ni wazi kwamba
limeshindwa kudhibitiwa.
(ix) Uajiri huu wa wafanyakazi hawa umefanywa kinyume na utaratibu kwa mujibu
wa sheria za Utumishi.
(x) Kamati ilipata taarifa kwamba Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano baada ya
kazi za Kamati, imewasumbua watendaji wake, ambao ama walitoa mashirikiano
mema kwa Kamati au wamegundulika na kasoro mbali mbali za uajiri wao,
vitendo vyote vikifanywa kabla hata ya ripoti hii kuwasilishwa Barazani.
(xi) Imethibitika kwamba, kuna mfanyakazi analipwa mshahara wa ngazi ya
Mtaalamu (msomi wa Degree) wakati bado hajafikia elimu hiyo.
3.5.36.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:
105
(i) Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara zote mbili (Wizara ya Miundombinu
na Mawasiliano na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
waliohusika na kadhia hii wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
(ii) Fedha zote alizolipwa Ndg. Mwanakombo Vuai Iddi katika ngazi ya Utaalamu
ambao hakuufikia, zirejeshwe Serikalini kwa utaratibu wa kukatwa mshahara
wake. Na hatua hizi zitumike kwa wafanyakazi wote walioajiriwa mara mbili,
ingawaje kwa wafanyakazi hawa, fedha hizo zirudishwe kupitia mishahara ya
Watendaji Wakuu wa Wizara hizi mbili zilizohusika (Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora).
(iii) Uajiri wa wafanyakazi wote ambao Kamati imegundua kwamba hawana sifa za
kuajiriwa, ufanyike upya kwa kufuata muongozo wa Sheria zilizopo sasa.
3.5.36 UTARATIBU WA AJIRA KWENYE WIZARA YA MIUNDOMBINU NA
MAWASILIANO (UPANDE WA PEMBA).
3.5.37.1 Utangulizi:
Kama ilivyotakiwa kuchunguza upande wa Unguja, vile vile Kamati ilitakiwa kuchuguza
utaratibu mzima wa ajira kisiwani Pemba, ambapo pamoja na mambo mengine, ilitakiwa
kuchunguza iwapo ni kweli kuna waajiriwa katika Wizara hii wanaotoka Tanga waliotoa taarifa
za udanganyifu kwamba wao ni Wazanzibari na hatimae wameajiriwa kama wazanzibari.
Ilitakiwa pia ichunguze sababu za uajiri wa vijana hao na iwapo Idara ya Utumishi Serikalini na
Kitengo cha Usalama (GSO) walihusika na uajiri huo. Aidha, katika kupata usahihi wa shutma
hizo, Kamati ililazimika kuchunguza wafanyakazi walioajiriwa kuanzia mwezi wa Ocotber 2010
hadi Septemba 2011 na katika uchunguzi wake ilibaini mambo mbali mbali ambayo tutayaona
baadae.
Katika kufanikisha kazi zake, Kamati ilikutana na Katibu Mkuu, Afisa Mdhamini na
wafanyakazi wengine wanaohusika wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano-Pemba, ili
kupata maelezo juu wa uajiri wa wafanyakazi kutoka Tanzania Bara kupitia Pemba. Kamati
ilifanya kazi hiyo siku ya tarehe 03/11/ 2011. Ili kuweza kupata ufafanuzi huo ni vyema kwanza
tukafahamu asili ya maombi ya kuajiriwa wafanyakazi hao:
3.5.37.2 UCHANGANUZI HUSIKA :
Kwanza ni busara ikafahamika kwamba, utaratibu wa ajira ulioutumika kuomba kujaza nafasi
tupu za Wizara, ulianzia Makao Makuu ya Wizara hii Unguja, kwa maana hii, kama
ulivyokwisha eleza hapo awali, kwamba, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano mnamo
tarehe 21/03/2011 ilipeleka maombi ya kujaza nafasi tupu, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais,
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, maombi ambayo yalikuwa na nafasi 136 Unguja na
upande wa Pemba ni nafasi 128. Na hivyo, basi sifa za waajiriwa hao zilipendekezwa katika
barua hiyo ya tarehe 21/03/2011 (Rejea Kielelezo Na.79) kama tulivyoeleza kwa upande wa
Unguja.
106
Unaweza ukajiuliza, jee, vipi maombi ya Wizara upande wa Pemba yakafanywe na Makao
Makuu, vipi upande wa Pemba ulishirikishwa ? na Jee, chanzo cha mahitaji ya wafanyakazi hao
kinatoka Unguja ama Pemba ? Kamati pia ililihoji suala hili, na katika kikao hicho Afisa
Utumishi wa Wizara hii Pemba, aliieleza Kamati kwamba, ni wao waliomuandikia Katibu Mkuu
wa Wizara hii haja ya kutaka kuajiriwa nafasi hizo kwa Upande wa Pemba ili kujaza mapengo ya
wafanyakazi waliostaafu, na kwa hali hii, chanzo cha mahitaji ya wafanyakazi hao kinatoka
Pemba na ni wazi kwamba, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba, ilishirikishwa
ipasavyo katika uajiri wa nafasi hizo. Kamati hapa haikulazimika kupata uhakika kwamba wazo
la kuajiri lilitoka Pemba ama Unguja, cha msingi ni kujiridhisha kwamba, kwa ukamilifu, Wizara
ya Miundombinu na Mawasiliano kwa upande wa Pemba, ilishirikishwa ipasavyo katika ajira
hizi na hivyo wanawajibika moja kwa moja kutoa ufafanuzi kwa Kamati, lakini pia kuhusika
katika hadidu hii rejea.
Hivyo basi, kwa upande wa Pemba, kati ya hizo nafasi 128 zilizoombwa, Idara ya Uendeshaji na
Utumishi iliombewa nafasi 1 ya Afisa Mafunzo akitakiwa awe na shahada ya kwanza au
Advance Diploma ya Utawala wa Umma au Diploma ya Ualimu. Wakati Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege, Pemba iliombewa nafasi 12 zifuatazo:
i. Dereva Trekta nafasi 1 akitakiwa awe na Cheti cha udereva wa Trekta.
ii. Karani Takwimu nafasi 1, mwenye elimu ya Kidato cha Sita.
iii. Karani Mapato nafasi 1, mwenye elimu ya Cheti cha Uhasibu.
iv. Waegesha Ndege nafasi 1, akiwa na elimu ya Kidato cha Sita.
v. Wahudumu V.I.P nafasi 4 wakiwa na elimu ya Kidato cha Nne na Cheti cha
„House Keeping‟.
vi. Walinzi Usalama nafasi 4 wakiwa na elimu ya Kidato cha Sita.
Nayo Idara ya Utunzaji Barabara, Pemba iliombewa Idadi ya Vibarua Stadi Ujenzi/ Utunzaji
nafasi 100 ambao wangelisambazwa katika Mkoa wa Kaskazini Pemba 40, na 40 wengine
wangelisambazwa katika Mkoa wa Kusini Pemba wakati Dereva Zana Nzito wakiwa na Cheti
cha Udereva waliombewa nafasi 2, nafasi 4 za watu wenye elimu ya Cheti cha „Human Resource
Management‟ zilizoombwa kwa Karani Utumishi, Mhandisi Mitambo nafasi 2 wakiwa na elimu
ya FTC-Mechanics, Wapimaji nafasi 6 wakiwa na elimu ya FTC- Civil na Fundi Magari wakiwa
na elimu ya FTC-Mechanics nafasi 6. Huku Idara ya Usafiri na Leseni Pemba iliombewa nafasi
15, nafasi 5 za Afisa Usafiri wakiwa na elimu Cheti cha Udereva na nafasi 10 za Fundi Mitambo
wenye cheti cha FTC katika fani ya Mechanics.
Mnamo tarehe 10/05/2011, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora
alimjuilisha Afisa Mdhamini, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano-Pemba, kwamba Ofisi
yake imepokea barua ya kutaka kujazwa nafasi 128 Pemba, lakini kwa uwezo alio nao, alitoa
ruhusa ya kujazwa nafasi 37, Nafasi moja ya Dereva na 36 Mafundi Stadi huku akimuomba
kushirikiana na Afisa Mdhamini- Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili
kuzijaza nafasi hizo (Kielelezo Na.115). Hivyo basi, tarehe 26/05/2011, Afisa Mdhamini wa
Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora aliijibu barua ya maombi yaliyotajwa hapo
juu, kwa barua yenye kumbu kumbu namba WN/UUU/P/U.125/3VOL.1/18 (Kielelezo Na.116),
aliyoipeleka kwa Afisa Mdhamini, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Pemba.
107
Hata hivyo, kimsingi ruhusa za barua hizi mbili zinatofautia sana katika ruhusa ya ajira husika.
Ile iliyotoka kwa Katibu Mkuu, ya tarehe 10/05/2011 iliruhusu kuajiriwa Dereva 1 tu na nafasi
zilizobakia 36 ni kwa ajili ya Vibarua Stadi, wakati hii barua iliyotoka kwa Afisa Mdhamini wa
Wizara hii hii, ya Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Pemba) kwenda kwa
Afisa Mdhamini, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano iliruhusu, wafanyakazi 2 kuajiriwa
katika Idara ya Mawasiliano ; Wafanyakazi 4 katika Idara ya Anga ; Dereva Nafasi 2 (badala ya
1) ; Idara ya UUB nafasi 2 ; Mechanic Engineers nafasi 2 ; Veta nafasi 3 ; Idara ya Utumishi na
Uendeshaji nafasi 1 ; Trafic Officer katika Idara ya Usafiri na Leseni nafasi 4 ; Fundi Rangi
nafasi 1 ;Makarani nafasi 6 ; Idara ya Usafiri Baharini nafasi 4.
Tukiendelea na utaratibu huu wa ajira ulivyofanyika, baada ya Afisa Mdhamini wa Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano kupokea barua hizo za kumruhusu kuajiri, siku moja baadae,
yaani tarehe 27/05/2011, alipeleka barua kwa Mkuu wa Usalama wa Taifa- Pemba, kuomba
ushauri wa vijana 26 kati ya vijana 37 walioruhusiwa kuajiriwa na Ofisi ya Rais, Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, ikieleza nia yake ya kuajiri vijana hao kupitia Budget ya mwaka
2011/2012 (Kielelezo Na.117), hapa inaonesha wazi kwamba, Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano-Pemba, ilipeleka wafanyakazi hao kufanyiwa „Security Vetting‟ GSO,Pemba
(Rejea Kielelezo Na.117). Kamati pia imepatiwa barua ya tarehe 02/11/2011, yenye kumbu
kumbu namba KASP/ZBO:5/7/VOL. V/513a inayotoa ufafanuzi wa upekuzi wa vijana 11
waliobakia kati ya wote wanaokusudiwa kuajiriwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,
Pemba, huku ikifanya rejea ya barua ya Wizara ya tarehe 29/05/2011 yenye kumbu kumbu
namba WMMP/C.2/vol.VI/64a (Kielelezo Namba 118). Kama ilivyofanya upande wa Unguja,
Kamati ilimwita mfanyakazi mmoja baada ya mmoja na kufanya nao mahojiano ambapo taarifa
zao ni kama hizi zifuatazo:
3.5.37.3 NDG. AHMED BAKARI SAID:
Kibali kilichotoka Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilielekeza kwamba,
mfanyakazi huyu ameajiriwa katika Idara ya Mawasiliano, Pemba, akiwa na elimu ya Diploma
na Mshahara wake ni ngazi ya ZTS.1, wa Tsh. 139,171/-, ingawaje Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano haikuomba mfanyakazi wa kitengo hiki. Aidha, Kamati ilipatiwa orodha ya
maombi yote ya ajira kwa mwaka husika, ambapo katika maombi ya Ndg. Ahmed Bakari Saidi,
amemaliza masomo yake ya Diploma katika Chuo cha New Horrizon mwaka 2010. Jina la
Mfanyakazi huyu pia lilithibitishwa katika majina 11 ya wafanyakazi yaliyopelekwa Kitengo cha
Usalama wa Taifa, Pemba.
Aidha, wakati alipotakiwa athibitishe vyeti vyake vya kumalizia masomo, Ndg. Ahmed
aliwasilisha vyeti 2 vinavyotofautiana katika mwaka wa kulipiwa kwake. Kwanza ifahamike
kwamba vyeti hivyo vilikuwa ni „leaving Certificates‟ ambapo kwa mujibu wa maelezo ya hapo
awali inaonesha kwamba amemaliza masomo yake mwaka 2010, wakati vyeti hivyo vya leaving,
kimoja kinaonesha amekilipia na kukipata tarehe 14/2/1994, wakati cheti chengine kinaonesha
amemaliza na kukilipia cheti hicho cha „leaving‟ tarehe 5/2/1999. Hivyo, ni wazi kwamba kuna
mazingira ya udanganyifu wa taarifa za mfanyakazi huyu na kwa namna yoyote Kamati
haijiridhishi kufaa kwake kuajiriwa katika nafasi hiyo.
108
3.5.37.4 NDG. SULEIMAN OMAR ALI:
Mfanyakazi huyu aliruhusiwa kuajiriwa katika Idara ya Mawasiliano huku akimaliza Kidato cha
Nne Skuli ya Shamiani, na mshahara wake ukiwa katika ngazi ya ZOS.2 Tsh. 105,564/. Hata
hivyo, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, haikuomba nafasi ya mfanyakazi katika Idara
ya Mawasiliano. Taarifa za Mfanyakazi huyu pia zimeripotiwa na GSO kwamba baada ya
kumaliza masomo amejiunga na shughuli za Ujenzi wa Taifa mwaka 2009.
3.5.37.5 NDG. MAULID DAUD HAJI:
Mfanyakazi huyu ameajiriwa Idara ya Anga akiwa amemaliza Kidato cha Nne, Skuli ya
Sekondari ya Shamiyani mwaka 1999, na ameajiriwa kwa mshahara wa Tsh. 105,564/- ngazi ya
ZOS2. Taarifa za kiusalama za mfanyakazi huyu zimethibitishwa na GSO kwamba ni mtu
mwenye kufaa kuajiriwa, katika orodha ya wafanyakazi 16 waliowasilishwa kwao.
3.5.37.6 NDG. SHADIYA JUMA ALI:
Ndg. Shadya ameajiriwa Idara ya Anga akiwa amemaliza elimu ya Kidato cha Nne, Skuli ya
Sekondari ya Shamiani mwaka 2010 na ameajiriwa akipokea mshahara wa Tsh. 105,564/- katika
ngazi ya ZOS2. Taarifa za kiusalama kutoka GSO zimethibitisha kwamba, mfanyakaz huyu hana
tatizo la kiusalama. Aidha, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano katika nafasi tupu
walizoombwa kujazwa, hakuna maombi waliyoyafanya kwa Idara ya Anga. Na kwa lugha hii,
ina maana, hakukuwa na haja ya kuajiriwa wafanyakazi katika Idara ya Anga, Pemba.
3.5.37.7 NDG. SAUMU OMAR MASOUD:
Ndg. Saumu amemaliza elimu ya Kidato cha Nne, skuli ya Sekondari ya Wawi, mwaka 2000, na
kufanikiwa kuajiriwa ldara ya Anga, Pemba kwa mshahara wa Tsh. 105,564/-. Taarifa za
Mfanyakazi huyu pia zilithibitishwa na Kitengo cha Usalama (G.S.O) kwamba hana tatizo lolote
la kiusalama, Ndg. Saumu amepeleka maombi ya ajira na yumo katika orodha ya waliopeleka
maombi wakiwa wamemaliza Kidato cha Nne, orodha ambayo pia ilikabidhiwa kwa Kamati.
Tatizo ni lile lile, kwamba Idara ya Anga hawakuomba nafasi hizo.
3.5.37.8 NDG. NEEMA ABDALLA RASHID:
Ndg. Neema aliruhusiwa kuajriwa katika idara ya Anga baada ya kumaliza masomo yake ya
Kidato cha Nne. Ndg. Neema amefanyiwa Uchunguzi wa Kiusalama katika orodha ya
wafanyakazi 26 iliyowasilishwa Kitengo cha Usalama wa Taifa, na kupendekezwa kwamba
anafaa kuajiriwa kwa sababu hakuwa na tatizo la kiusalama. Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa
za Kitengo hicho cha Usalama, Ndg. Neema alimaliza elimu ya Stashahada ya Ualimu katika
Chuo cha Kiislamu kilichopo Micheweni mwaka 2011, na sio kamaliza Kidato cha Nne kama
ilivyoarifiwa na Idara ya Utumishi. Aidha, kwa mujibu wa taarifa za Kitengo hicho cha Usalama,
mfanyakazi huyu pia alimaliza masomo yake ya kidato cha Sita katika chuo hicho hicho cha
Kiislamu cha Micheweni, mwaka 2009. Na ifahamike pia kwamba, aliomba kazi kwa kiwango
cha Kidato cha Sita.
3.5.37.9 TABIA ISSA MSELLEM:
Mfanyakazi huyu ameajiriwa kama Afisa Usalama ambae amemaliza masomo yake katika Skuli
ya Sekondari ya Haile Sellassie mwaka 2005. Katika Nafasi 12 zilizoombewa kwa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege, nafasi 4 ziliombwa kwa walinzi Usalama, ambapo Kamati imejiridhisha
kwamba, Ndg. Tabia ameajiriwa katika nafasi hizo. Kama hali ndio hii, sifa walizopendekeza
109
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa nafasi hizi, upande wa Unguja na Pemba ni kuwa na elimu
ya Kidato cha Sita, wakati mfanyakazi huyu amemaliza Kidato cha Nne. Vile vile ikumbukwe
kwamba, nafasi hizi zilihitajika 4, lakini Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora
wakaajiri wafanyakazi 6 ikiwa ni pamoja na Ndg. Tabia. Kwa mujibu wa sifa yake ya elimu, ni
wazi kwamba, mfanyakazi huyu hakuwa na sifa za kuajiriwa katika nafasi hiyo.
3.5.37.10 NDG. ALI SULEIMAN JUMA:
Mfanyakazi huyu ameajiriwa Kama Mlinzi (Afisa) Usalama, nafasi ambayo iliombwa kwa ajili
ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, Pemba, kwa mtu aliemaliza Kidato cha Sita. Aidha, Ndg. Ali
amemaliza Kidato cha Nne, Chuo cha Ufundi, Kengeja, na pia amepata mafunzo ya Kompyuta.
Ni sawa na kusema kwamba, Mfanyakazi huyu hajatimiza kigezo cha msingi cha elimu ili
kuajiriwa kama ilivyotakiwa.
3.5.37.11 ZULFA MMAKA OMAR:
Nae pia ameajiriwa kama Mlinzi (Afisa) Usalama, nafasi ambayo iliombwa kwa ajili ya
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, Pemba, kwa mtu aliemaliza Kidato cha Sita wakati Ndg. Zulfa
amemaliza Kidato cha Nne, mwaka 2006 katika Skuli ya Shamiani. Tukikumbushia sifa
zilizopendekezwa kwa Afisa (Mlinzi) Usalama kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Unguja na
Pemba, alitakiwa awe amemaliza Kidato cha Sita, na kwa kuwa Ndg. Zulfa amemaliza Kidato
cha Nne, ni wazi kwamba hana sifa ya msingi ya kuajiriwa.
3.5.37.12 JUMA ABDALLA RASHID:
Katika nafasi 6 zilizoruhusiwa kuajiriwa, ingawaje ni nafasi 4 tu zilihitajika, Ndg. Juma nae ni
miongoni mwa wafanyakazi hao. Akiajiriwa kama Mlinzi (Afisa) Usalama, Mamlaka ya Uwanja
wa Ndege Pemba kwa elimu yake ya Kidato cha Nne aliyoihitimu Skuli ya Sekondari ya Furaha,
na kwa hali ile ile ya sifa ya elimu ya msingi iliyohitajika kwamba awe amemaliza Kidato cha
Sita, Ndg. Juma hakuwa na sifa za msingi za kuajiriwa nafasi hii.
3.5.37.13 TIME KHAMIS BAKARI:
Mfanyakazi huyu ameajiriwa Mlinzi (Afisa) Usalama katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege,
Pemba katika kiwango cha elimu yake ya Kidato cha Sita na kwa mujibu wa elimu iliyohitajika,
Ndg. Time anastahiki kuajiriwa katika nafasi hiyo.
3.5.37.14 SAUMU KHAMIS MASOUD:
Nae pia ameajiriwa kama Mlinzi (Afisa) Usalama katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege,
Pemba katika kiwango cha elimu yake ya Kidato cha Nne aliyoipata katika Skuli ya Sekondari
ya Shamiani. Ingawaje kama tulivyofanya rejea hapo awali, kwamba sifa zilizohitajika kwa
nafasi hii, alitakiwa aajiriwe mtu mwenye elimu ya kuanzia Kidato cha Sita, na kwa hoja hii,
Ndg. Saumu hakuwa na sifa za kuajiriwa nafasi hiyo.
3.5.37.15 NDG. KHAMIS MGAU KOMBO:
Kwa mujibu wa maelezo ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, mfanyakazi huyu
amemaliza elimu ya Kidato cha Nne na ameajiriwa katika nafasi ya Udereva, wakati nafasi hii,
pamoja na mtu kumaliza Kidato cha Nne, alitakiwa pia awe na cheti cha Udereva, wakati Ndg.
Khamis hakuwa na cheti hicho. Aidha, Kamati ina wasi wasi na usahihi wa cheti chake cha
Kidato cha Nne kwamba ni cha kufoji kwa mazingira kwamba, amesema amekipata Skuli ya
110
Benbella, wakati ameshindwa kuthibitisha kusoma Skuli hiyo, na hata alipotakiwa kutaja
angalau walimu watatu wa skuli hiyo alishindwa kufanya hivyo. Kama hii haitoshi, taarifa
zinazofahamika kwa mfanyakazi huyu, hakuwahi kusoma Skuli hiyo.
Jambo jengine linaloleta mashaka katika uajiri wake, ni namna ya haraka ya kuajiriwa.
Mfanyakazi huyu amepeleka maombi yake, tarehe 19/05/2011 na uajiri wake ulianza tarehe
1/06/2011, yaani ndani ya siku 11 tu Mfanyakazi huyu ameajiriwa. Unaweza kupata jawabu
jepesi mno kuhusu uwezekano wa suala hili. Ndg. Khamis Mgau Kombo, kabla ya kuajiriwa
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, alikuwa ni dereva wa Mhe. Hamad Masoud Hamad,
Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Hali hii inakuwezesha kukubaliana na
Kamati kwamba, Mfanyakazi huyu hakuajiriwa kwa sifa zake, kwa sababu hakua nazo. Suala
hili hata yeye mwenyewe alisema kwamba, aliombewa na Mhe. Waziri wa Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano.
3.5.37.16 NDG. SAID NASSOR BAKAR:
Ameajiriwa katika Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara, Pemba (UUB) akiwa amemaliza elimu
ya Ufundi, Chuo cha Ufundi, Sayansi na Teknolojia (Chuo cha Karume) na kupata cheti cha
FTC. Ameajiriwa katika nafasi ambayo inaenda sambamba na sifa zilizohitajika. Na hata Kamati
imepongeza kwa uajiri wa mfanyakazi huyu.
3.5.37.17 NDG. AMOUR ABDULLA KHAMIS:
Nae ameajiriwa Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara (UUB) akiwa amemaliza Cheti na
analipwa Mshahara wa Tsh. 111,643/- katika ngazi ya ZOS3. Hata hivyo, kwa mujibu wa sifa
zilizohitajika kwa mtu kuajiriwa katika nafasi yoyote ile kati ya hizi zilizoombwa ni na UUB, ni
kwa Vibarua Stadi wameshurutishwa wawe na elimu kuanzia Kidato cha Nne, wakati
mfanyakazi huyu amemaliza Kidato cha Pili. Ni wazi kwamba hakuwa na sifa za kuajiriwa
katika nafasi hiyo.
3.5.37.18 NDG. SALMA NASSOR TALIB:
Ameajiriwa katika Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara (UUB) akiwa amemaliza Skuli ya
Karume na kufanikiwa kupata cheti cha FTC, na hivyo ameajiriwa kwa mujibu wa elimu
iliyohitajika. Hata hivyo, wakati akihojiwa na Kamati alikiri kwamba amemaliza Skuli ya
Skondari ya Kengeja na baadae akajiendeleza na masomo katika Chuo cha Ufundi, Karume
lakini aliithibitishia Kamati kwamba, hakufanikiwa kupata cheti kwa sababu aliakhirisha
masomo hayo. Ni wazi kwa hivyo kwamba, mfanyakazi huyu ameajiriwa bila ya sifa ya msingi
iliyoelezwa katika taarifa zake za awali.
3.5.37.19 NDG. SALEH ALI SALIM:
Nae ameajiriwa katika Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara (UUB) akiwa amemaliza Kidato
cha Sita na kujiendeleza katika chuo cha Ufundi cha VETA, Dar es Salaam. Kamati haina
pingamizi na mfanyakazi huyu kwa kujiridhisha kwamba ameajiriwa kwa mujibu wa sifa zake.
111
3.5.37.20 NDG. ASHA KHAMIS MOH‟D:
Ndg. Asha ameajiriwa akiwa na elimu ya Kidato cha Nne aliyoipata Chuo cha Ufundi, Kengeja
na kujiendeleza katika masomo ya Kompyuta, aidha, taarifa hizi pia zimeelezwa na Ofisi ya
Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Pamoja na maelezo hayo, Mfanyakazi huyu
alipoitwa mbele ya Kamati, alishindwa kuthibitisha cheti chake cha kumalizia masomo, na hivyo
haikuthibitika ukweli wa sifa hii ya elimu ya Kidato cha Nne.
3.5.37.21 SALIM SAID MAKAME:
Ndg. Salim Said amemaliza cheti na ameajiriwa katika nafasi ya elimu iliyohitaji angalau Kidato
cha Nne. Taarifa za mfanyakazi huyu zimeelezwa kwamba amemaliza VETA. Hata hivyo,
wakati Kamati inafanya mahojiano nae, ilithibitika kwamba amemaliza Kidato cha Pili, na hata
hicho cheti cha VETA ameshindwa kukithibitisha mbele ya Kamati. Kwa sifa hizo alizozieleza,
ni wazi kwamba Mfanykazi huyu hakuwa na sifa za kuajiriwa katika nafasi hiyo.
3.5.37.22 NDG.MBAROUK OMAR MOHD:
Ameajiriwa Mhudumu Mfyekaji, Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kwa maelezo kwamba amepata
mafunzo ya VETA. Katika nafasi hii ya Uhudumu (Uwanja wa Ndege )Ufyekaji, angalau elimu
ya Kidato cha Nne ilipendekezwa iwe ni kigezo cha kuajiriwa mfanyakazi. Hata hivyo,
Mfanyakazi huyu amemaliza Kidato cha Pili. Aidha, wakati akiajiriwa, alipangiwa kulipwa
Mshahara wa Tsh. 116,006/- ngazi ya ZSS.1, mshahara ambao ungelistahiki kulipwa kwa
mfanyakazi mwenye elimu isiyopungua Kidato cha Sita. Hata hivyo, baada ya kufahamika
kasoro hii, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, iliamua kuurekebisha na kuwa
Tsh. 111,643/- ngazi ya ZOS.3. Pamoja na hali yote hii, Mfanyakazi huyu ana sifa zisizokidhi
haja ya kuajiriwa katika nafasi aliyoajiriwa.
3.5.37.23 NDG. MAISARA OTHMAN ZAIDI.
Ndg. Maisara ameajiriwa kama Dereva na amemaliza masomo yake Kidato cha Nne aliyohitimu
Skuli ya Sekondari ya Shamiani mwaka 2004. Hakuna taarifa za kusomea Udereva kwa
kusisitiza kwamba sifa za kuajiriwa Dereva ni kusomea, na hivyo ni wazi kwamba, hakutimiza
sifa zote zilizohitajika wakati akiajiriwa.
3.5.37.24 FATMA RIYAM RASHID:
Ameajiriwa katika Idara ya Utumishi na Uendeshaji, Idara ambayo iliombewa nafasi moja ya
Afisa Mafunzo mwenye elimu ya Shahada ya Kwanza au „Advance Diploma‟ ya Utawala wa
Umma au Diploma ya Ualimu. Kwa bahati mbaya sana, Ndg. Fatma amemaliza Kidato cha Nne,
Skuli ya Sekondari ya Shamiani mwaka 1999. Hivyo ni kusema kwamba hajatimiza vigezo vya
kuajiriwa katika nafasi hiyo.
112
3.5.37.25 NDG. SAID MOH‟D FADHIL:
Ameajiriwa katika Idara ya Usafiri na Leseni (Traffic Officer), huku katika mahitaji ya Wizara,
mfanyakazi huyu alitakiwa awe na cheti cha Udereva. Kwa bahati, Ndg. Said amemaliza
masomo yake ya Kidato cha Nne, na Kamati haikupata taarifa zake za kusomea Udereva kama
ilivyohitajika. Kwa hali hii, Mfanyakazi huyu hakutimiza vigezo vyote vilivyohitajika wakati
akiajiriwa.
3.5.37.26 NDG. SHARIF ALI OTHMAN:
Nae pia ameajiriwa katika Idara ya Usafiri na Leseni (Traffic Officer) ambapo kwa mahitaji ya
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ilipokuwa inapeleka maombi ya Uajiri, ni kupata mtu
pamoja na sifa nyengine, awe na cheti cha Udereva. Kwa bahati, Ndg. Sharif amemaliza Kidato
cha Tatu na hajawahi kusomea Udereva. Kamati ilipopitia cheti cha mfanyakazi huyu, imetia
mashaka juu ya usahihi wake kwa kuzingatia kwamba jina lake katika cheti hicho limeandikwa
kwa Type, tofauti na maandiko mengine.
Kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya Rais, utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndg. Sharif
amemaliza Kidato cha Nne, tofauti na taarifa za Kiusalama za GSO kwamba amemaliza Kidato
cha Tatu. Kamati imeshawishika kwamba cheti chake cha Kidato cha Nne ni cha Udanganyifu.
Aidha, alipoulizwa juu ya barua yake ya maombi ya kazi kama aliandika yeye mwenyewe, alikiri
kaandika yeye, lakini kwa ukweli maandishi haya yanatofautiana sana na muandiko wake katika
taarifa zake nyengine. Pamoja na yote, Ndg. Sharif ni ndugu wa mama mmoja na Mhe. Waziri
wa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Mhe. Zainab Omar
Mohammed. Ni kusema tu kwa mujibu wa uchunguzi wa Kamati, mfanyakazi huyu hakuwa na
sifa za kuajiriwa.
3.5.37.27 NDG. FAIZA MOH‟D IDDI:
Ndg. Faiza ameajiriwa katika Idara ya Usafiri na Leseni (Traffic Officer) na elimu yake ni ya
Kidato cha Nne, Skuli ya Ngwachani mwaka 2010, lakini hakufanikiwa kupata Cheti. Kwa lugha
hii, hangeweza kuajiriwa kwa utambulisho wa cheti cha Kidato cha Nne, ambacho Ndg. Faiza
hajakipata. Aidha, Idara ya Usafiri na Leseni Pemba, ilihitaji nafasi 2 kuu ambazo ni nafasi 5 za
Afisa Usafiri akitakiwa wawe wamesomea Udereva na kupata cheti na nafasi 10 zilizobakia ni
Fundi Mitambo wakiwa wamepata Cheti cha F.T.C katika fani ya Mechanics. Kwa bahati
mbaya, Ndg. Faiza hakuwa na sifa zozote zilizohitajika na ni sawa na kusema kwamba
ameajiriwa bila ya kuwa na sifa zinazohitajika.
3.5.37.28 NDG. MOH‟D ALI NASSOR:
Ameajiriwa Idara ya Usafiri na Leseni baada ya kumaliza masomo ya Kidato cha Sita, Skuli ya
Sekondari ya Shamiani mwaka 2009. Hata hivyo, kwa mujibu wa sifa zilizohitajika katika Idara
113
ya Usafiri na Leseni, Pemba, ukiacha Dereva, basi ni Fundi Mitambo mwenye Cheti cha F.T.C
fani ya Mechanics, wakati Mfanyakazi huyu hakusomea fani hizo.
3.5.37.29 NDG. MUSSA RAMADHAN MOH‟D:
Amemaliza Kidato cha Pili (Form.II), kwa mujibu wa Taarifa za Ofisi ya Rais, Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, wakati taarifa za Kiusalama za G.S.O, Mfanyakazi huyu alijiendeleza
kimasomo na kumalizia Kidato cha Nne. Kwa bahati Idara hii haikuombewa kujaza nafasi ya
Fundi Rangi nafasi ambayo haikuombewa kwa Taasisi yoyote iliyo chini ya Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano, Unguja na Pemba, na Kamati haiamini uwepo wa haja ya
kuajiriwa Fundi Rangi.
Aidha, wakati anahojiwa na Kamati alieleza kwamba amezaliwa tarehe 8/5/1985 wakati cheti
chake cha Utambulisho wa Mzanzibari kinaonesha amezaliwa mwaka 1986. Kuhusu barua yake
ya maombi, alikiri mbele ya Kamati kwamba ameandikiwa ingawaje saini ya barua hiyo ametia
mwenyewe.
3.5.37.30 NDG. KULTHUM ABASS HAJI:
Ameajiriwa Karani akiwa amemaliza Kidato cha Nne. Nafasi 2 tu ziliombwa kujazwa kwa
Karani, nao ni Karani Takwimu nafasi 1 akitakiwa awe na elimu ya Kidato cha Sita na nafasi ya
2 ni Karani Mapato mwenye cheti cha Uhasibu, wote walitakiwa kuajiriwa Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege, Pemba. Aidha, kwa upande wa Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara, Karani
Utumishi waliomhitaji alitakiwa awe na Cheti cha „Human Resource‟.Kwa namna yoyote ile,
Ndg. Kulthum pamoja na kwamba hajaainishwa ni Karani wa aina gani, kwa mujibu wa mahitaji
ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, hakukamilisha sifa za msingi za kuajiriwa kwake.
3.5.37.31 NDG. MUSSA AMOUR MUSSA:
Ameajiriwa Karani huku akimaliza elimu ya Kidato cha Nne. Hata hivyo, kama tulivyokwisha
sema awali, kwamba sifa za Karani yoyote awae katika nafasi zilizoombwa, ama alitakiwa awe
na Kidato cha Sita ama Karani Mapato mwenye cheti cha Uhasibu ama kwa upande wa UUB,
alitakiwa amesomea na kupata cheti cha „Human Resorce‟. Na kwa kuwa Ndg. Mussa
amemaliza Kidato cha Nne tu, hakuwahi kuwa na sifa za kuajiriwa katika nafasi hii.
3.5.37.32 NDG. MOH‟D SULEIMAN AMOUR:
Nae Ndg. Moh‟d Suleiman Amour ameajiriwa Karani huku akiwa amemaliza Kidato cha Nne,
Skuli ya Sekondari ya Ng‟ambwa mwaka 2009. Hata hivyo, kama tulivyokwisha eleza awali
kwamba, kumaliza Kidato cha Nne tu bila ya kupata elimu zilizopendekezwa katika maombi ya
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, na kwa kuzingatia maombi ya wenye elimu kubwa
zaidi yake wapo wengi tu, kama tukirejea maombi hayo, ni wazi kwamba, Ndg. Moh‟d hakuwa
na sifa za kuajiriwa nafasi ya Ukarani, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Pemba.
114
3.5.37.33 NDG. ASHA KOMBO ALI:
Ameajiriwa kama Karani kwa kuzingatiwa elimu yake ya Kidato cha Nne mwaka 2009 wakati
huo huo sifa za Karani zilizohitajika, hazikuishia katika kiwango hicho cha elimu ya mfanyakazi
huyu, kama tulivyokwishaeleza awali, na hivyo, Mfanyakazi huyu hakuwa na sifa za kutosheleza
kuajiriwa katika nafasi hiyo na zaidi kwa kuzingatia kulikuwa na takriban maombi 37 ya
wananchi waliomaliza Diploma, „Advance Deploma‟ na Degree na maombi ya Kidato cha 6
yalikuwa 108 (Kielelezo Na.119).
3.5.37.34 NDG. FADHILA ALI MACHANO:
Nae ni miongoni mwa wafanyakazi 6 walioajiriwa Makarani huku ikizingatiwa elimu yake ya
Kidato cha Nne. Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za Kiusalama za GSO, Mfanyakazi huyu
amemaliza Kidato cha Tatu (Form III) Skuli ya Sekondari ya Shamiani mwaka 2003. Wasi wasi
zaidi unajitokeza, wakati Kamati inakipitia kopi ya cheti chake cha Kidato cha Nne
alichokiwasilisha, ilikitia wasi wasi kwamba kimeghushiwa kutokana na muandiko wa jina lake
ukiwa tofauti na maandiko mengine katika cheti hicho hicho.
Ili kujiridhisha zaidi, Kamati ilimwita tena siku ya pili yake na kumtaka aje na cheti chake cha
asili (Original Certificate), ambapo alishindwa kufika nacho kwa kusema kwamba cheti hicho
hakipo Pemba, kipo Unguja. Kamati haiwezi kuthibitisha usahihi wa cheti hicho, na kwa
kuzingatia sifa zilizohitajika kwa nafasi ya Karani, Mfanyakazi huyu hakuwa na sifa za kutosha
za uajiri wake.
3.5.37.35 MOH‟D ALI MOH‟D:
Nae ni mfanyakazi wa 6 kuajiriwa Karani akiwa na kiwango kidogo kabisa cha elimu kuliko
wenzake. Ndg. Moh‟d Ali Moh‟d amemaliza Kidato cha Pili (Form II), (huku kukiwa na
wananchi zaidi ya 1000 waliomaliza Kidato cha Nne (Kielelezo Na.120)) Skuli ya Sekondari ya
Wawi na hakuna taarifa za kujiendeleza zaidi. Wakati Kamati inamhoji Mfanyakazi huyu kuhusu
muda aliokwenda kichukua cheti hicho, alieleza kwamba alikichukua mwaka 2010, wakati
katika cheti hicho inaonesha kwamba kimetolewa tarehe 04/04/2011.
Aidha, alieleza kwamba aliomba kazi baada ya kukichukua cheti chake, yaani kwa mnasaba wa
maneno yake ya awali, alikichukua cheti mwaka 2010 na kuomba mwaka huo, wakati usahihi wa
maombi yake yamepokelewa mwezi wa March, 2011. Aidha, wakati Afisa Mdhamini akitoa
ufafanuzi wa Muajiriwa huyu, alisema kwamba, baada ya kumuona hawezi kutekeleza
majukumu yake ya kazi aliyoajiriwa kwayo, wao kama Wizara wameamua kumpeleka kwenye
kukata majani, anakusudia kusema kwamba, pamoja na kutoomba nafasi ya Mhudumu Mfyekaji
(Uwanja) katika Taasisi zote za Wizara hii upande wa Pemba, nafasi hii ilipoombewa Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Unguja, alitakiwa mwanamme mwenye elimu ya Kidato cha Nne, sifa
ambazo Ndg. Moh‟d Ali Moh‟d hana. Pamoja na maelezo yote hayo, Kamati imejiridhisha
kwamba, Mfanyakazi huyu hakuwa na sifa za uajiri wake.
115
3.5.37.36 NDG. JUMA HAMAD AHMED:
Ndg. Juma ameajiriwa katika Idara ya Usafiri Baharini, Idara ambayo haikuwa na upungufu wa
kujaza nafasi yoyote na ndio maana haikupeleka maombi yake, Ofisi ya Rais, Utumishi wa
Umma na Utawala Bora. Kwa upande wa elimu, Mfanyakazi huyu amemaliza Kidato cha Nne na
mshahara wake alioajiriwa ni Tsh. 105,564/- katika ngazi ya ZOS.2.
3.5.37.37 JUMA MUSSA MSAFIRI:
Mfanyakazi huyu ni wa pili kati ya wanne walioajiriwa katika Idara ya Usafiri Baharini,
ingawaje nafasi hii haikuhitajika kujazwa kwa sababu maombi yake hayakuwasilishwa Ofisi ya
Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa upande wa Pemba. Ndg. Juma amemaliza elimu
ya kidato cha Nne, Skuli ya Sekondari ya Shamiani. Kwa mamlaka waliyoyatumia wao, Wizara
ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba, imeamua kumuajiri kama Mhudumu V.I.P. Nafasi
ambayo ilitakiwa iajiriwe kwa mtu aliemaliza Kidato cha Nne na kusomea na hatimae kupata
cheti cha House Keeping, cheti hiki Ndg. Juma hana kwa sababu hajasomea fani hii.
3.5.37.38 NDG. MOH‟D HUSSEIN MARZOUK:
Ameajiriwa kufanya kazi Idara ya Usafiri Baharini huku ikizingatiwa elimu yake ya Kidato cha
Nne. Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za Kiusalama za GSO, mfanyakazi huyu amemaliza
mtihani tu wa Kidato cha Nne bila ya kufaulu na kupata Cheti.
3.5.37.39 NDG. KHAMIS BAKAR SALIM:
Nae ni mfanyakazi wa Nne kuajiriwa katika Idara ya Usafiri Baharini huku akiwa amemaliza
Kidato cha Nne, Skuli ya Sekondari ya Shamiani. Wakati anahojiwa na Kamati, alieleza
amezaliwa tarehe 12/03/1986 wakati usahihi wa tarehe hiyo ni 10/07/1986, alipohojiwa kuhusu
Cheti chake cha kumalizia masomo skulini hapo, yaani „Leaving Certificate‟ amesema hana na
alipotakiwa azitambue pasi zake, kwa masikitiko makubwa alisema hazikumbuki.
3.5.37.40 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii ndogo, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
3.5.37.40.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake
wa Hadidu hii Rejea:
(i) Kama ilivyofanyika Unguja, ni wazi pia kwa upande wa Pemba, Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano imehusika zaidi na uajiri wa wafanyakazi wake kuliko
Mamlaka husika, yaani Idara ya Utumishi Serikalini.
116
Hii inatokana na ruhusa za awali za wafanyakazi hao kutoka Idara ya Utumishi
zimebadilishwa na Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano bila ya taratibu za
Uhamisho wala taratibu nyengine za ajira zinazohusika. Hili limefanywa bila ya
ruhusa wala taarifa kwa Mamlaka husika.
(ii) Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano imewaajiri wafanyakazi wengi wasio kuwa na sifa na
wengi wao wameambatanisha katika maombi yao taarifa zisizo za kweli na za
udanganyifu.
(iii)Wafanyakazi wote 37 wamepeleka maombi yao ya kazi, baina ya mwezi wa March,
April na May 2011 na kuajiriwa mwezi wa June, kuna maombi mengi ambayo
yalishaombwa na wananchi wengi wenye sifa zaidi ama sawa na hawa walioajiriwa
ambao walioomba zaidi ya miaka miwili nyuma, bila ya kuzingaitiwa maombi yao.
(iv) Wafanyakazi wengi walioajiriwa ni watoto wa wakubwa ama jamaa zao wa karibu.
Hata Afisa Mdhamini aliieleza Kamati kwamba, aliombwa na aliekuwa Mhe. Ashura
Abeid Faraji na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, kuwasaidia watoto ama jamaa
zao. Aidha, wafanyakazi wengi waliobakia ni watoto na jamaa wa wafanyakazi wa
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, hali ambayo imepelekea wepesi wa
kuajiriwa kwao huku wananchi wengi wasio na wakubwa wala wazee wenye kazi
Wizarani hapo wakiendelea kusota bila ya kuajiriwa kwa muda mrefu sasa.
(v) Kamati inapongeza hatua za Wizara kuwapeleka waajiriwa hao Kitengo cha G.S.O ili
kufanyiwa uchunguzi, kitu ambacho hata Makao Makuu wameshindwa kukitekeleza.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa walizozitoa kwa wafanyakazi hao, Kamati
imegundua vigezo vya kisiasa vimetumika kushawishi ajira za wafanyakazi hao.
(vi) Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
wamehusika na Upendeleo wa wazi wa watoto na jamaa zao katika utaratibu wa ajira
na zaidi katika utekelezaji wa majukumu ya wafanyakazi hao.
3.5.40.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi hu, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:
(i) Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara zote mbili (Wizara ya Miundombinu
na Mawasiliano na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
waliohusika na kadhia hii wawajibishwe kisheria.
(ii) Uajiri wa wafanyakazi wote ambao Kamati imeona hawana sifa za kuajiriwa,
ufanyike upya kwa kufuata muongozo wa Sheria zilizopo sasa.
117
3.6 UTARATIBU WA UTOAJI WA HUDUMA MBALI MBALI KWENYE MAENEO
YA UWANJA WA NDEGE:
Sehemu ya mwisho ya Hadidu hii ndogo inahusiana na huduma muhimu za ubebaji wa mizigo
ya abiria mbali mbali wanaotaka kusafiri na wanaowasili Zanzibar, zinazopatikana na kutolewa
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanzibar. Katika kufuatilia
hoja hii, Kamati kwa mashirikiano yaliyotolewa na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege imekutana na
Vikundi vitatu vya wananchi vyenye sura mbali mbali na kuhojiana nao kwa siku mbili tofauti
na hatimae kufahamu kasoro na matatizo mbali mbali na athari zake kwa wananchi wanaotumia
uwanja huo.
Katika kuchunguza utaratibu unaotumika kutolewa huduma hizo za ubebaji wa mizigo ya abiria
kutoka katika vipando vyao hadi sehemu husika ya uchunguzi wa mizigo hiyo (Luggage
Security) na kutoka sehemu ya kutoka nje baada ya safari hadi kwenye vipando mbali mbali vya
abiria, Kamati ilivihoji vikundi hivyo vitatu ambavyo ni Ushirika wa Zanzibar Aviation Porters
(ZAP); Ndg. Khamis Mussa Juma aliyekuwa na dhamira ya kuanzisha Kampuni ya Ubebaji
Mizigo na Kampuni ya Zanzibar Porters & Aviation Services Ltd ambayo hivi sasa ndio
inayotoa huduma hizo na kufahamu mambo mbali mbali ambayo kwa namna moja ama nyengine
ni muhimu kuelezwa kwatika ripoti hii ili tuweze kufahamu kwa kina matatizo mbali mbali
yanayojitokeza kutokana na utaratibu uliopo sasa na hatimae Kamati iishauri Serikali njia bora
ya kutumika ili huduma hizi ziweze kutolewa kwa ufanisi mkubwa. Kwa hatua hii, mambo
yafuatayo ni vyema tukayatizama kwa pamoja:
3.6.1 Historia ya Utoaji wa Huduma ya Ubebaji mizigo ya Abiria wa Uwanja
wa Ndege:
kwa ujumla Kamati inakubali kwamba, historia ya utolewaji wa huduma ya ubebaji mizigo ya
abiria ni ya muda mrefu sana, lakini kwa mnasaba wa hoja hii, Historia tunayoikusudia imeanza
mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo Kamati imepokea ufafanuzi wa kina kutoka kwa
wahusika watatu tuliowaeleza hapo juu ambapo ni vyema tukapata ufafanuzi wa kila mmoja:
3.6.2 Historia Fupi ya Ushirika wa Zanzibar Aviation Porters (ZAPS):
Unapozungumzia historia ya uanzishwaji wa uliokuwa Ushirika wa Zanzibar Aviation Porters ni
lazima utamzungumzia Mzee Jaffar Moh‟d Juma ambae ndio muasisi wa Ushirika huo. Ndg.
Jaffar ameieleza Kamati kwamba kwa mwaka wa 1988 hadi 1998 alikuwa mfanyakazi wa
Uwanja wa Ndege wa Zanzibar na ilipofika karibu na kustaafu na hatimae muda wa kustaafu
ulipomfikia, aliamua kumfuata Mhe. Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Aman Abeid Aman
Karume kumueleza shida yake na haja yake ya kuanzisha umoja wa wastaafu wa uwanja wa
Ndege kutoa huduma za ubebaji mizigo ya abiria ili kuweza kujituma na kuitumikia nchi yao
wakati wameshastaafu majukumu ya kujenga nchi yao kama wafanyakazi wa Serikali. Mhe. Rais
Mstaafu kwa busara zake akamfahamisha kwamba ni vyema waanzishe Ushirika wao na pia
wawatumie vijana wao kuendesha shughuli hizo. Aidha, Mzee Jaffar alisisitiza kwamba,
mazungumzo yake na Mhe. Rais Mstaafu, yalianza tokewa akiwa Waziri wa Wizara ya
118
Mawasiliano na Uchukuzi na hivyo alipokuwa Rais ilikuwa ni hatua nzuri zaidi ya kumuwezesha
kupata msaada huo.
Mnamo tarehe 4/06/2003, Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi alimuandikia barua
Mkurugenzi wa Idara ya Anga yenye kumbu kumbu Namba WMU/1.1 Vol.V/137 (Kielelezo
Na.121) kumtaka awaruhusu Mzee Jaffar na wastafu wenzake ikiwa ni pamoja na Ndg. Khamis
MMadi, Ndg. Daudi Mwinyishehe, Ndg. Saburi Suleiman, Ndg. Haji Mikidadi na Ndg. Khamis
Waziri kufanya kazi hizo ya kubeba mizigo ya wasafiri huku ikishurutisha wawe wanafanyiwa
„Police Check‟, wavae sare zilizoandikwa „PORTER‟, wapatiwe vitambulisho na wasikiuke
taratibu na heshma za kiwanja cha Ndege cha Zanzibar. Baada ya kuendelea na kazi takriban
kwa miaka mitatu, Mzee Jaffar na Wenzake walifanikiwa kukisajili kikundi chao na kuwa
Ushirika uliosajiliwa kisheria mnamo tarehe 21/04/2006 (Kielelezo Na.122).
Suala hili pia limeenda sambamba na juhudi zao za kutafuta elimu ya uhifadhi wa fedha zao na
hatimae kufungua Akaunti ya Ushirika katika Benki ya Watu wa Zanzibar-PBZ (Kielelezo
Namba 123). Ushirika huo uliweza kuwa na vijana mbali mbali waliopata ajira na kujiendeleza
kimaisha ambapo kwa namna moja ama nyengine umewasaidiwa vijana wengi kuepuka kukaa
mitaani na kuzurura. Ili kuweka utaratibu mzuri wa kutekeleza wajibu na haki za kila mjumbe,
Ushirika ulijiwekea Kanuni Ndogo za muongozo kwa kila mjumbe (Kielelezo Na.124). Hata
hivyo, ulipofika mwaka 2008, kulianzishwa Kampuni Mpya iliyowanyima wao fursa na kazi
zao na hatiimae kuibuka migogoro mbali mbali ambapo hata Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano ikaingilia kati, lakini bado matatizo ya migogoro hiyo inaendelea hadi leo.
3.6.3 Historia Fupi ya Ndg. Khamis Mussa Juma aliyekuwa na dhamira ya kuanzisha
Kampuni ya Ubebaji Mizigo:
Katika hali isiyotarajiwa wakati Kamati inafanya uchambuzi wa hoja hii katika kikao cha pamoja
na wahusika hawa, Ndg. Khamis Mussa Juma, Mfanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano nae akaeleza kwamba ni yeye aliyekuwa muanzilishi wa awali wa wazo la
kuanzisha Kampuni ya Ubebaji wa Mizigo ya Abiria na kwa muda mrefu amefuatilia suala hilo
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege na kutumia gharama nyingi ili suala hilo lifanikiwe lakini hakuna
mafanikio yoyote na hatimae amenyang‟anywa na Ushirika huo pamoja na kuondoshwa kabisa
katika juhudi za dhamira yake, baada ya kuanzishwa na hatimae huduma hizi zikakabidhiwa kwa
Kampuni ya Zanzibar Porters & Aviation Services Ltd. Ufafanuzi wa Ndg. Khamis ni kama
ufuatao:
Kwamba, Ndg. Khamis Mussa Juma alifikiria kuanzisha Kikundi cha Uchukuzi wa Mizigo
(Porters) chenye jina la Zanzibar Aviation Porters (ZAP) na akaamua kufanya hivyo kupitia
barua yake ya tarehe 11/09/2001 aliyomuandikia Mkurugenzi, Idara ya Anga- Zanzibar kwa
dhamira ya kuwasaidia vijana ambao hawana ajira rasmi na halali katika eneo la Uwanja wa
Ndege kwa njia ya kuwaajiri, pamoja na kuwasaidia abiria wanaosafiri kupitia Uwanja huo na
huku barua hiyo akiinakili kwa Waziri, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi na Wizara ya
Vijana, Ajira na Maendeleo, Zanzibar. Barua ambayo iliandikwa tena na mwanawe wa kumzaa,
Ndg. Omar Khamis Mussa, tarehe 11/12/2001 huku akiinukuu kwa Makatibu Wakuu wa Wizara
hizo (Kielelezo Na.125).
119
Mnamo tarehe 16/01/2002 Ndg. Omar Khamis Mussa, Mtoto wa Ndg. Khamis Mussa Juma
alimuandikia barua Mkurugenzi wa Idara ya Anga, Zanzibar kumkabidhi Muundo, Kazi na
tathmini ya mapato na malipo ya mishahara ya Kikundi iwapo kitakubaliwa kutoa huduma ya
ubebaji wa mizigo kama alivyoomba tarehe 11/12/2001 (Kielelezo Na.126). Tarehe 14/02/2002
walisajili Jina la Biashara la Kikundi chao (Registration of Business Name) liitwalo „Zanzibar
Aviation Porter‟ na kumkumbusha Mkurugenzi, Idara ya Anga kupitia barua ya tarehe
19/02/2002 kwamba wameshasajili jila hilo na kuruhusiwa kisheria kufanya biashara huku
wakisisitiza kuruhusiwa kuanza kazi tarehe 01/03/2002 (Kielelezo Na.127). Na katika
matayarisho yao ya awali waliomba tena kwa Mkurugenzi wa Idara ya Anga kuwakodisha Ofisi
katika maeneo ya Uwanja wa Ndege kupitia barua yao ya tarehe 4/3/2002 (Kielelezo Na.128).
Baada ya kutojibiwa kwa maombi yao muda mrefu, huku tayari wameshatumia fedha kadhaa
wakiamini watapewa wao kazi hiyo ya kutoa huduma ya ubebaji wa mizigo na matokeo yake
wakaona vijana wengine ndio wanaofanya kazi hiyo, chini ya Ushirika wa „Zanzibar Aviation
Porter‟, ndipo wakamuandikia barua Meneja wa Uwanja wa Ndege Zanzibar, tarehe 10/3/2002
kumtaka awakataze vijana ama Ushirika huo kufanya kazi ambayo wao kwa muda mrefu
walikwishaiomba na wana matumaini ya kupewa, huku wakitoa tahadhari huenda kutokatazwa
kwa vijana hao, kukapelekea matatizo na ugomvi mkubwa katika Uwanja huo (Kielelezo
Na.129).
Ndg. Omar Khamis Mussa alimuandikia barua kali Mkurugenzi wa Idara ya Anga, mnamo
tarehe 04/06/2002 akimlaumu pamoja na Idara yake kumchelewesha pamoja na kumkatisha
tamaa katika kumpa kibali cha kumruhusu na baba yake kuanzisha mradi wa Ubebaji wa Mizigo,
huku tayari wameshakula hasara za matayarisho (Kielelezo Na.130).
Kufuatia barua hii, Mkurugenzi wa Idara ya Anga alimjibu kupitia barua ya tarehe 25/07/2002
akimtaka Ndg. Omar awe na subira huku Idara inaendelea kulishughulikia suala lake na ilipofika
tarehe 20/08/2003 baada ya Ndg. Omar kuendelea kulalamika kwa muda mrefu, Mkurugenzi wa
Idara ya Anga ndipo alipomwita Ndg. Omar akimtaka afike Idarani kuonana nae (Kielelezo
Na.131). Hata hivyo, hakuna mafanikio yoyote yaliyopatikana pamoja na juhudi za Ndg. Omar
na Baba yake na hatimae Ndg. Omar akaamua kumuandikia barua Katibu mkuu, Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi tarehe 20/11/2002 na tarehe 04/08/2003, kuendelea kutaka kupatiwa
kibali husika huku akimtaka asaidie katika ngazi ya Wizara, lakini bado hakupata ufumbuzi zaidi
ya kuahidiwa kila siku (Kielelezo Na.132).
Baada ya juhudi zake kugonga ukuta katika ngazi ya watendaji wa Wizara na kwa kuzingatia
hasara ya Tsh. 1,700,000/- aliyokuwa ameshaipata kwa wakati huo (2001-2003), Ndg. Omar
Khamis aliamua kwa makusudi kumuandikia barua Mhe. Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na
Uchukuzi, tarehe 11/09/2003 akimuomba amsaidie kupatiwa ufumbuzi wa suala hili na wakati
huo huo akilalamika kukiukwa kwa makubaliano baina yao, kwamba Wizara tayari ilikwisha
amua kumruhusu kuendesha biashara ya kutoa huduma za ubebaji wa mizigo lakini kukatokea
amri nyengine iliyowateua watu maalum ambao wengine wamo katika orodha yake ya kuwaajiri,
kufanya kazi hiyo (Kielelezo Na.133).
3.6.4 Historia Fupi ya Kampuni ya Zanzibar Aviation Porter Services Company Ltd
(ZAPS):
120
Baada ya muda mrefu wa kufanya kazi ya utoaji wa huduma ya kubeba mizigo chini ya Ushirika
wa Mzee Jaffar Moh‟d Juma na Wenzake (Zanzibar Porters Aviation), mnamo mwaka 2008,
ikatokezea Kampuni iitwayo Zanzibar Aviation Porter Services Company Ltd (ZAPS) na
kuhodhi biashara hiyo iliyojikita katika utoaji wa huduma ya Kubeba Mizigo na hatimae
migogoro ikaendelea kuongezeka. Katika Kikao cha pamoja baina ya Kamati na vikundi hivyo,
Uongozi wa Kampuni hiyo uliieleza Kamati kwamba ilipofika mwaka 2008, Uongozi wa Idara
ya Anga iliwataka watoa huduma zao kwa kubadilika kutoka katika Ushirika hadi kwenda
kwenye Kampuni ili huduma zao ziwe fanisi zaidi na pia kwa dhamira ya kuondosha tatizo la
watoaji huduma wasio fahamika (Wasio rasmi). Na kwa mnasaba wa hali hii, Mzee Jaffar Moh‟d
Juma na Wenzake wakawafuata Ndg. Hassan Gharib Makame kwa lengo la kuwasaidia mawazo
na hatimae wafanikishe kuanzisha Kampuni inayohitajika. Ndg. Hassan pamoja na Mzee Jaffar
na Wenzake walikwenda kuonana na Meneja wa Uwanja wa Ndege ili kueleza namna
waliyokubaliana ya kuanzisha Kampuni, ambapo baada ya kuulizwa na kujiridhisha,Meneja
hakuwa na pingamizi.
Hatua iliyofuata ikawa ni sharti la uanzishwaji wa Kampuni husika kuwa na „Share Holders‟
jambo ambalo liliwashinda Mzee Jaffar na Wenzake kwa umasikini wao na hatimae Ndg. Hassan
Gharib alitafuta wenzake, Ndg. Salum Suleiman Lofy na Ndg. Mohammed Ambar Hanif
kuanzisha Kampuni hiyo kama „Share Holders‟ huku Mzee. Jaffar na Wenzake hawakuwa na
nafasi yoyote ya Uongozi wala undeshaji wa Kampuni hiyo zaidi ya kupata fursa ya kuajiriwa
kama wafanyakazi wa Kampuni. Katika uchambuzi wa suala hili, ni vyema tukafuata historia
fupi ya Kampuni hiyo na nafasi yake katika utoaji wa Huduma za Uwanja wa Ndege:
Baada ya wazo la kuanzishwa kwa Kampuni kukubalika na waanzilishi wake kupatikana,
Kampuni hiyo iliaandaa taratibu za usajili kwa kuwasilisha „Memorandum of Association‟ na
„Articles of Association‟ kwa Msajili wa Makampuni Zanzibar kama inavyoelekezwa katika
Sheria ya Makampuni, Sura ya 153 ya Sheria za Zanzibar (Kielelezo Na.134). Aidha, kifungu
cha 3.2 cha „Memorandum of Association‟ ya Kampuni, kinaeleza kwamba moja kati ya
malengo ya kuanzishwa kwake ni kufanya biashara ya utoaji wa huduma ya Ubebaji wa Mizigo
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume wa Zanzibar, ikiwa ni pamoja
na kuajiri na kuwasimamia wafanyakazi wa shughuli hizo. Kampuni hiyo inamilikiwa na Share
Holders wafuatao:
2 Ndg. Hassan Gharib Makame, mwenye Hisa 70%
3 Ndg. Salum Suleiman Lofy, mwenye Hisa 20%
4 Ndg. Mohammed Ambar Hanif, mwenye Hisa 10%.
Tarehe 11/01/2008, Kampuni hiyo ilipata usajili wa kuanzishwa kwake na usajili wa ulipaji kodi
(Kielelezo Na.135). Baada ya hatua hizi kukamilika, Kampuni hii ikaanza utaratibu wa kuajiri
wachukuaji wa mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na vijana wale wale waliokuwa katika Ushirika wa
Mzee Jaffar, (Zanzibar Aviation Porters) pamoja na Mzee Jaffar Mwenyewe na utaratibu wa
kuwaajiri ilikuwa ni kuomba nafasi za kazi hizo (Kielelezo Na.136) na hatimae Kampuni
ikayajibu maombi hayo kwa barua (Kielelezo Na.137) na kuandaa mikataba ya ajira za
wafanyakazi hao (Kielelezo Na.138). Aidha, Kampuni pia ilianza kuwalipa wafanyakazi hao
mshahara wa Tsh. 60,000/- (ikiwa ni apamoja na posho la usafiri na Nyumba )kwa kila
mfanyakazi wake (Kielelezo Na.139).
121
3.6.5 NAMNA YA MGOGORO ULIVYOIBUKA:
Baada ya kuanzishwa kwa Kampuni ya Zanzibar Aviation Porter Services Company Ltd (ZAPS)
na kuajiri vijana wakiwemo wale waliokuwa wana Ushirika wa Zanzibar Aviation Porter, baadhi
ya vijana hao hawakuridhika kuajiriwa na kupata Tsh.60,000/ kwa mwezi ukizingatia walikuwa
wanapata zaidi ya hizo katika wakati ambao wamejiajiri katika Ushirika huo. Aidha, Kampuni
iliwasimamia kama wafanyakazi wao kwa kuwawekea Masharti ya kazi wakati vijana hao
walikuwa huru wakijisimamia wenyewe katika Kanuni zao za Ushirika. Kwa kuwa Kampuni
imeanzishwa zaidi kibiashara na kuona vipi wangepata faida, iliamua kuwa na idadi maalum ya
wafanyakazi na hivyo, kuna vijana wengi waliokuwa hawakuajiriwa (Kielelezo Na.140) na
matokeo yake wakawa ni chachu ya kutoridhika na ujio wa Kampuni hii. Aidha, kwa mnasaba
wa nidhamu na Kanuni za Kazi, Kampuni mara kadhaa haikuwa ikifuata vyema taratibu za kazi
na matokeo yake ikawa ikawabana zaidi wafanyakazi wake, huku wengi wao wakishindwa
kuridhika na hali hii. Katika hili, Kampuni ilitoa onyo kwa wafanyakazi kadhaa (Kielelezo
Na.141) na likizo bila ya malipo kwa wakati ambapo wafanyakazi wamekuwa wengi ama
kuwasimamisha kazi moja kwa moja (Kielelezo Na.142). Pia inafahamika wazi kwamba,
kitendo cha Kampuni kumilikiwa na kusimamiwa na watu wasiokuwa waanzilishi wa Ushirika
huo kimewafanya wazee hao waastaafu, akina Mzee Jafar na Wenzake kuona wamesalitiwa na
kutokuwa na njia nyengine isipokuwa kulazimika kuajiriwa katika Kampuni hiyo huku
wakiendeleza vugu vugu la kuipiga vita ama kujieweka kando na kuwa adui wa wazi dhidi ya
Kampuni.
Kwa upande wa Ndg. Omar Khamis Mussa pamoja na baba yake Khamis Mussa Juma
hawakuridhishwa na kitendo cha kutopewa kibali cha kuanzisha Kampuni waliyoikusudia na
ukizingatia tayari walikwisha tumia fedha nyingi huku wakipewa matumaini na Uongozi wa
iliyokuwa Idara ya Anga lakini mwisho wake hawakufanikiwa. Kwa hali hii, hawakuwa na
ridhaa ya Kuanzishwa kwa Kampuni mpya na wala Ushirika na wanaamini kwamba Uongozi wa
Idara ya Anga ulifanya upendeleo wa makusudi wa kutoa kibali kwa Ushirika na hatimae
Kampuni ya ZAPS. Kutokana na hali hii, kwa muda mrefu sasa Huduma za Ubebaji Misigo
katika Uwanja wa Ndege zimekumbwa na migogoro isiyokwisha na matokeo yake hutokea
vurugu na fitna za kila namna, jambo ambalo mara kadhaa kuleta aibu kwa Taifa kwa maana
kwamba baadhi ya siku fujo hizo hutokea hadharani. Jambo la kushangaza, ilifika wakati
huduma hizo zilitolewa na vikundi viwili tofauti vyenye ugomvi baina yao, yaani baina ya
waliojiona wana Ushirika wa ZAP na Kampuni ya ZAPS. Hali hii ilizidisha machafuko na
uhasama kiasi ya kuzidi kudhorotesha huduma za ubebaji wa mizigo Uwanjani hapo.
3.6.6 NAMNA WIZARA YA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO ILIVYOSHIRIKI
KATIKA UTATUZI WA MGOGORO HUO:
Baada ya mgogoro huu kuwa mkubwa na athari zake kuonekana wazi wazi, ndio ilipofika tarehe
04/08/2008, aliekuwa Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi aliitisha Mkutano wa
pamoja na Kikundi cha Ushirika wa Zanzibar Aviation Porters (Mzee Jaffar na Wenzake);
Uongozi wa Kampuni ya Aviation Porters & Services Limited na Uongozi wa Idara ya Anga,
kujadiliana na kutafuta suluhu ya mgogoro huo na hatimae tarehe 05/08/2008, Katibu Mkuu wa
Wizara hii, aliwaandikia barua Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirika wa Zanzibar Aviation
Porters and Mkurugenzi wa Kampuni ya Zanzibar Aviation Porters & Services Ltd kuwaelezea
122
maamuzi ya kikao hicho kilichoitishwa na Waziri ambapo kiliamua mambo yafuatayo (Kielelezo
Na.143):
Kwamba, Wastaafu sita wa Idara ya Anga Zanzibar wakiwemo Ndg.
Jaffar Moh‟d Juma; Ndg. Rajab Kheir; Ndg. Moh‟d Hussein; Ndg.
Khamis Mmadi; Ndg. Rajabu Mwinyijuma Chum na Ndg. Saburi Suleima
Haji, wameruhusiwa kuendelea kufanya kazi ya uchukuzi wa mizigo kama
walivyoruhusiwa hapo mwanzo, ruhusa ambayo imetolewa kwa wastaafu
hao kufanya kazi wenyewe tu sio vyenginevyo. Aidha, kati ya wastaafu
hao sita, wanaohisi uwezo wao wa kufanya kazi ni mdogo na watapenda
kupatiwa posho ya uzeeni na Kampuni ya ZAPS au kuajiriwa basi
wafanye hivyo.
Kwamba, Kampuni iliyopewa ruhusa ya kufanya kazi ya kubeba mizigo ni
Kampuni ya ZAPS pekee (Si Kampuni nyengine yoyote wala Mtu binafsi
ama Ushirika) na kutakiwa wakae pamoja na wanaushirika wa ZAP
SACCOS ili wanaushirika hao wapewe nafasi ya kujiunga tena katika
Kampuni ya ZAPS kwa mujibu wa taratibu za Kampuni na pia wapewe
nafasi ya kununua Hisa za Kampuni kwa wale wanaotaka kufanya hivyo.
Kamati kwa upende wake imepongeza juhudi hii ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi
kujaribu kutafuta suluhisho la Mgogoro huu na zaidi juu ya busara za Wizara hii katika
kuelekeza njia za kutumiwa na vikundi hivi vinavyozozana. Hata hivyo, pamoja na juhudi hizo,
mgogoro huu haukupata suluhu na hadi leo pamoja na shughuli za Ubebaji mizigo zinafanywa na
Kampuni ya ZAPS, bado migogoro isiyokwisha inaendelea kuisakama huduma hii, huku Kamati
ikifahamu kwamba, kwa kiasi kikubwa Idara ya Anga ilishiriki katika uwepo wake.
3.6.7 MCHANGO WA KAMATI TEULE KATIKA KUUTATUA MGOGORO HUU:
Baada ya kupitia kwa makini maelezo ya hapo juu na kwa mnasaba wa kazi iliyopewa Kamati
Teule ambayo ni kuchunguza utaratibu wa utoaji wa Huduma katika Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Aman Abeid Karume Zanzibar, utafahamu kwa uwazi kwamba, huduma za
ubebaji wa mizigo inayoongozana na wasafiri hutolewa kupita Kampuni moja iitwayo Zanzibar
Aviation Porter & Services Company Limited (ZAPS) ambapo huduma zao zinakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na migogoro isiyokwisha na wana Ushirika wa ZAP na hili
kupelekea zile taratibu nyengine zilizowekwa na Uongozi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege
kukiukwa na kwa ujumla huduma hizi huwa ni duni na ziko katika hali isiyoridhisha.
Ili kurudisha huduma nzuri na fanisi, Kamati baada ya kuchambua kwa kina inaamini jambo la
kwanza muhimu ni kuondoka kwa migogoro hiyo vyenginevyo ni kutafutwa kwa Kampuni
nyengine ya kizalendo ambayo haitahusisha Viongozi wa Kampuni ya ZAPS wala Ushirika wa
ZAP waliopo sasa itakayopewa kazi kama Wakala wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kufanya
kazi hiyo. Hata hivyo, kabla ya kufika hatua ya mwisho,Kamati kwa busara zake imewashauri
viongozi wote wa aina tatu, Uongozi wa Ushirika wa ZAP; Mzee Khamis Mussa Juma na
Uongozi wake pamoja na Uongozi wa Kampuni ya ZAPS wakae pamoja na kujadiliana na
123
hatimae wao wenyewe wakubaliane utaratibu watakaoutumia kutoa huduma hizo na bila ya ya
kuwepo mgogoro wowote.
3.6.8 HATUA ZILIZOCHUKULIWA KWA LENGO LA KUBORESHA HUDUMA
HIZO:
Mnamo tarehe 09/01/2012 Kamati Teule ilipokea taarifa kutoka kwa Zanzibar Porters &
Aviation Services ambayo inathibitisha kwamba kwa pamoja, Viongozi wa Kampuni ya ZAPS,
Viongozi wa Ushirika wa ZAP na Ndg. Khamis Mussa Juma na Mwakilishi wake walikaa na
kuzungumzia namna ya vikundi vyote kwa Ushirika wa ZAP na kikundi cha Ndg. Khamis
Mussa Juma kupewa nafasi ya kununua hisa ili kujiunga ndani ya Kampuni ya ZAPS na hatimae
Wana Ushirika wa ZAP walikubali kujiunga tena katika Kampuni ya ZAPS na kufanya kazi kwa
awamu tofauti. (Kielelezo Na.144).
Hata hivyo, kwa upande wa Wanaushirika wa ZAP hawajakubali ajenda ya kununua hisa wala
kujiunga na katika Kampuni, ingawaje Ndg. Khamis Mussa Juma amekubali kununua hisa ya
5% na hivyo, Kampuni ya ZAPS imo katika utaratibu wa kubadilisha Memorandum yao na
kuviarifu vyombo husika vya Serikali ili aweze kuwa Mjumbe wan ne katika watu wenye hisa
katika Kampuni hiyo.
3.6.9 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii ndogo, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
3.6.9.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Mamlaka ya Uwanja wa Ndege (Wakati huo Idara ya Anga) kwa kiasi kikubwa
imehusika katika mgogoro ambao wao wenyewe wameshindwa kuutatua.
(ii) Chanzo cha mgogoro huo kinahusiana zaidi kimaslahi kwamba kila kikundi
pamoja na Ndg Khamis Mussa Juma kinataka kufanya kazi hizo za ubebaji wa
mizigo peke yao bila ya kuwashirikisha wengine.
(iii) Uanzishaji wa Kampuni ya ZAPS bila ya kuwashirikisha viongozi waandamizi
Kikundi cha Ushirika wa ZAP wala kumshirikisha Ndg. Khamis Mussa Juma,
kumechangia zaidi katika migogoro isiyokwisha.
3.6.9.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo tulionesha kapo juu, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo
zichukuliwe:
(i) Pamoja na Viongozi waandamizi wa Ushirika wa ZAP na Ndg. Khamis Mussa
Juma kushindwa kununua hisa katika Kampuni hiyo kutokana na Umaskini wao
124
(Ingawaje Ndg. Khamis amenunua kwa 5%), Serikali kupitia Mamlaka
zinazohusika ziwasaidie kununua share hizo kwa asilimia 50 (50%).
(ii) Mamlaka ya Uwanja wa Ndege isijiingize katika Mgogoro huu na badala yake
iwe muangalizi (observer) au msimamizi wa majukumu ya Kampuni hii.
HADIDU REJEA YA TATU:
4.1. MATATIZO YA UVAMIZI WA FUKWE NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA
KWENYE HOTELI INAYOPAKANA NA CHUO CHA MAENDELEO YA
UTALII MARUHUBI ZANZIBAR, KWENYE HOTELI YA ZANZIBAR OCEAN
VIEW KILIMANI ZANZIBAR NA HOTELI YA MISALI ILIYOPO WESHA
PEMBA:
4.1.1 Utangulizi:
Katika kufuatilia Hadidu hii rejea, Kamati ilitakiwa kuchunguza ukweli kuhusiana na kuwepo
kwa uvamizi wa ardhi katika maeneo ya ufukwe huku ikielekezwa kuangalia namna gani ujenzi
wa Hoteli ya Maruhubi Beach Villa iliyopo Maruhubi; Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliyopo
Kilimani pamoja na Hoteli ya Misali Sunset Beach iliyopo Wesha Pemba, umehusika na uvamizi
huo na pia umeathiri Mazingira.
Kamati imelifutilia suala hili kwa muda tofauti, ikianzia na Pemba ambapo ilifanya kazi kwa
siku mbili kama tutakavyoeleza katika utangulizi wa uchambuzi wa hadidu hii, Pemba. Kwa
upande wa Unguja, Kamati ilifanya kikao cha pamoja baina ya Watendaji wote wa Taasisi
zinazohusika na Miradi hii tarehe 22/11/2011 katika Afisi za Wizara ya Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo, na tarehe 23/11/2011 Kamati ilikutana tena katika kikao cha pamoja baina ya
watendaji hawa na Mmiliki wa Hoteli ya Maruhubi Beach Villa katika eneo la hoteli husika. Na
siku hiyo hiyo kwa utaratibu kama huo, Kamati ilikutana na mmiliki wa Hoteli ya Zanzibar
Ocean View iliyopo Kilimani sehemu iliyopo hoteli hiyo. Katika kutoa ufafanuzi wa suala hili,
Kamati inaona ni vyema tukafuata utaratibu ufuatao:
4.1.2 UJENZI WA HOTELI YA MARUHUBI BEACH VILLA-UNGUJA.
Kwa kuwa hoja hii inahusiana na ujenzi wa hoteli iliyopo Maruhubi, suala la kwanza ambalo
Kamati imeona ni vyema likatambulika ni hili linalohusiana na umiliki halali wa eneo husika.
Wakati Kamati inaulizia suala hili, kuna ufafanuzi mpana ulitolewa katika vikao vyote husika na
kuifanya Kamati kulieleza kama ifuatavyo:
4.1.3 Uhalali wa Umiliki wa eneo lililojengwa Hoteli ya Maruhubi Beach Villas:
Suala la kwanza ambalo ni muhimu ni kufahamu je, Mmiliki wa Hoteli hii Ndg. Khalifa Salum
Suleiman ameipata vipi ardhi aliyoitumia kujenga Hoteli hiyo iliopo katika eneo la fukwe na
mkabala na Chuo cha Maendeleo ya Utalii. Je, anaimiliki au amekodishwa na Serikali kama
wawekezaji wengi wazalendo na wageni wanaomiliki Hoteli kwa lengo la kufanya biashara ya
huduma kwa watalii mbali mbali wanaofika nchini. Kwa upande wa ardhi hii, kama ilivyo asili
ya ardhi yoyote nchini kuwa ni milki ya Serikali chini ya Rais wa Zanzibar na mamlaka ya
125
usimamizi wake yakiachwa kwa Waziri anaehusika na masuala ya ardhi, ruhusa ya matumizi ya
Ardhi ilibarikiwa kwa Ndg. Ussi Yahya Haji kufuatia kukubaliwa ombi lake lenye namba 366/94
na hivyo kupewa Haki ya Utumiaji wa Ardhi hiyo tarehe 19/10/1994. Kama ilivyo kwa yoyote
anaeruhusiwa kutumia ardhi kisheria, Ndg. Ussi Yahya Haji aliiomba kuitumia ardhi hiyo kwa
lengo la kujenga Kituo cha kuuza vitu vya asili na utamaduni na tiba (Art Gallery) na alipewa
kisheria na Mamlaka inayohusika na ardhi kwa mujibu wa masharti yafuatayo :
1. Kwamba, aitumie kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Sanaa, Mkahawa na
Afisi (Art Gallery).
2. Kwamba, Ardhi hiyo ianze kutumiwa kwa makusudio yaliyoombewa ndani ya
miaka miwili baada ya kutolewa kwa ruhusa hiyo, yaani baada ya tarehe
19/10/1994.
3. Kwamba, Ramani ya jengo analokusudia kujenga lazima iwasilishwe kwenye
Idara ya Upimaji na Mchoraji husika kwa lengo la kuzingatia Mpango Miji.
4. Kwamba, matumizi ya ardhi hiyo lazima yazingatie sheria, kanuni za ujenzi
na za Mipango Miji na Vijiji na Sheria yoyote nyengine inayohusika na
utumiaji wa ardhi iliyoidhinishwa kisheria.
5. Kwamba, Ndg. Ussi analazimika kuiangalia vizuri ardhi aliyopewa katika
muda wote unaohusika na ahakikishe kwamba majengo yawe katika hali
inayoridhisha.
6. Kwamba, kabla ya ujenzi wowote ni lazima kwanza apate idhini ya
Halmashauri na Idara ya Majenzi.
7. Kwamba, ahakikishe anahifadhi mawe ya mipaka yaliyowekwa wakati wa
upimaji na kuyarejesha iwapo yatang‟olewa kwa kuripoti katika Idara ya
Upimaji na kugharamia kazi ya kuyarejesha mawe hayo.
8. Haruhusiwi kuigawa au kuiuza haki ya matumizi ya ardhi hiyo aliyopewa.
9. Atahitajika kulipia gharama zote za upimaji, utengenezaji wa ramani na
utengenezaji wa barua ya Haki ya Utumiaji wa ardhi na malipo mengine
yanayotakiwa na Serikali kwa muda wowote wa kuimiliki haki hiyo.
10. Kwamba haki hiyo ya matumizi ya ardhi inaweza kubatilishwa iwapo
haikutumika kwa mujibu wa masharti yaliyoelezwa hapo juu na iwapo
haijatumiwa kwa muda unaozidi miaka miwili tokea tarehe 19/10/1994 au
kwa mujibu wa sheria yoyote itakayobatilisha umilikaji kwa manufaa ya
Taifa. (Kielelezo Na.145).
Kwa maana hii, hakuna shaka yoyote kwamba suala la umiliki wa ardhi hiyo liko Serikalini,
lakini haki ya matumizi halali kwa masharti yaliyotolewa iko kwa Ndg. Ussi Yahya Haji. Kwa
lugha nyengine, Ndg. Khalifa Salum Suleiman sio mmiliki wa ardhi hiyo wala hakuwahi kupewa
haki ya matumizi. Kwa hali hii, suala jengine la msingi ni kujiuliza, Je. Ndg. Khalifa aliipataje
ardhi hiyo na je upataji wake unakubalika kisheria?
Kwa kawaida, pamoja na ukweli kwamba ardhi yote ni mali ya Serikali, Sheria hiyo hiyo
(Namba 12 ya mwaka 1992), pia imetoa ruhusa ya ardhi kumilikiwa na mtu mwengine kupitia
kuuziwa na mmiliki halali anaemiliki ardhi iliyosajiliwa kama utaratibu huu ulivyopata baraka ya
kifungu cha 7 (d) cha Sheria hii. Kwa maana hii, ingekuwa vyema iwapo baada ya Ardhi hii
kukabidhiwa Ndg. Ussi Yahya Haji, yeye ndipo aamue kuiuza kwa Ndg Khalifa Salum kwa
masharti ya Sheria husika. Hata hivyo, kufanya hivi pia ingelikuwa kukengeuka masharti ya
126
kutolewa ardhi hiyo yaliyoelezwa katika kifungu cha 8 cha masharti ya kukabidhiwa kwa Ndg.
Ussi Yahya Haji, na kwa vyovyote vile hata kama angeliamua kuiuza, basi Sheria husika
tuliyoitaja hapo juu isingebariki uuzwaji huo kwa misingi ya masharti yaliyokataza kuuzwa ama
kuigawa kwa ardhi hii kutoka mikonoi mwa Ndg. Ussi. Kwa lugha hii, Ndg. Khalifa hakuwa na
uhalali wa kumilikishwa ardhi hii na Ndg. Ussi kwa njia yoyote ile.
Hata hivyo, Kamati kwa busara zake ilimhoji Ndg. Khalifa namna alivyoipata ardhi hii ambapo
nae alijibu kwamba ameuziwa na Ndg. Ussi Yahya Haji. Kamati ilipotaka kupatiwa ushahidi wa
mauzo hayo, kwa bahati mbaya sana Ndg. Khalifa alithibitisha kwamba waliuziana kienyeji na
hata alipopewa muda wa kuwasilisha angalau maandiko yoyote ya kuthibitisha maelezo yake,
alishindwa kufanya hivyo. Na kwa maana hii, Kamati haiwezi kuthibitisha uhalali wa kuuzwa
kwa eneo hilo na hata kama ingeliuzwa, basi kwa mujibu wa masharti ya Hati ya Utumiaji wa
Ardhi aliyokabidhiwa Ndg. Ussi Yahya, kipengele cha sharti namba 8, uuzwaji huo ungelikiuka
masharti ya hati hiyo na hivyo, ingelikuwa kugengeuka kifungu cha 8 (2)(c) cha Sheria hiyo
Namba 12 ya mwaka 1992, kifungu ambacho kinabatilisha uuzaji wa namna hiyo ambayo Ndg.
Khalifa anadai ameuziwa na Ndg. Ussi Yahya Haji.
4.1.4 Je, kuna Tathmini yoyote ya Athari ya Kimazingira iliofanywa juu ya Mradi wa
Kuanzisha Maruhubi Beach Villa?
Suala jengine ambalo Kamati imelihoji ni kufanyika kwa Tathmini ya Kimazingira katika Ujenzi
wa Hoteli ya Kitalii ya Maruhubi Beach Villa inayomilikiwa na Ndg. Khalifa Salum Suleiman
ambae kwa namna moja ama nyengine alibadilisha matumizi ya asili ya matumizi ya Ardhi
aliyopewa Ndg. Ussi Yahya Haji kwa ajili ya matumizi ya „Art Galary” na hatimae yeye
mwenyewe akaamua kuitumia kwa kuanzisha Mradi wa Hoteli ya Kitalii aliyoiita „ Maruhubi
Beach Villa‟. Suala hili ni la msingi sana kutokana na kushurutishwa na Sheria Namba 2 ya
mwaka 1996, ambapo kifungu cha 38(1) kinasomeka ifuatavyo: “Hakuna mtu atakaeruhusiwa kufanya shughuli yoyote ambayo huenda ikawa na athari muhimu kwa
mazingira bila ya kwanza kupata kibali cha tathmini ya athari za kimazingira kinachotolewa kwa mujibu
wa sheria hii.
Kwa mnasaba wa maelezo ya kifungu hiki, suala la kwanza ambalo mtu yoyote anajiuliza, Je,
Ndg. Khalifa Salum Suleiman amefuata taratibu za kisheria za kupata kibali cha Tathmini ya
Athari za Kimazingira kitakachomruhusu kuendelea kupata ruhusa ya ujenzi wa Mradi wake na
je, amefuata muongozo wa kisheria katika kupata kibali hicho?
Kamati ilihitaji kupata ufafanuzi wa namna gani Bw. Khalifa aliomba kibali cha tathmini ya
kimazingira kutoka katika Mamlaka husika ambayo ni Idara ya Mazingira. Katika kutoa
ufafanuzi wa suala hili, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais,Ndg. Omar D.
Shajak aliithibitishia Kamati kwamba mnamo mwaka 2004, Idara ya Mazingira ilipokea barua
kutoka Kamisheni ya Utalii yenye kumbu kumbu namba K/UT/10/156 ya tarehe 13/07/2008
iliyoandikwa na Ndg. Issa Mlingoti kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii,
inayotaka kupata ushauri wa Kimazingira ili wao, Kamisheni ya Utalii waweze kutoa kibali cha
Biashara ya Utalii kwa Ndg. Khalifa (Kielelezo Na.146). Hii ina maana, Ndg. Khalifa Salum
Suleiman hakuomba ama hakupeleka maombi Idara ya Mazingira ili kufanyiwa Tathmini ya
127
Kimazingira na badala yake aliloona yeye la wajibu kufanywa ni kuomba Leseni ya Biashara ya
Utalii kwa Kamisheni ya Utalii. Walichofanya Kamisheni ya Utalii, kuomba maoni ya Idara ya
Mazingira juu ya Mradi husika ni sahihi kwani kifungu cha 38(2) cha Sheria Namba 2 ya mwaka
1996 kinaelekeza hivyo, kama tunavyonukuu:
“Hakuna taasisi yoyote inayohusika na kutoa leseni, ruhusa, kibali, au aina nyengine ya ruhusa kwa ajili ya
shughuli yoyote ambayo huenda ikawa na athari muhimu kwa mazingira isipokuwa (ruhusa hiyo itolewe)
baada ya kufanywa tathmini ya athari za kimazingira kwa ajili ya kufanywa shughuli hiyo.
Aidha, kwa upande wa Ndg. Khalifa, amekwenda kinyume na muongozo wa kifungu cha 39 cha
Sheria hii, kinachomtaka kuwasilisha ripoti ya tathmini ya kimazingira kwa Idara ya Mazingira
inayotoa ufafanuzi wa masuala yaliyoelezwa katika kifungu kidogo cha (1) paragrafu ya (a) hadi
(h). Pamoja na Ndg. Khalifa kushindwa kupeleka maombi ya Tathmini ya Mazingira moja kwa
moja kwa Idara husika, kwa kuwa Kamisheni ya Utalii ilipeleka maombi ya kupatiwa maoni ya
Mradi juu ya athari zake za Kimazingira kwa Idara ya Mazingira, ni vyema sasa tuangalie kwa
namna gani Ruhusa ama Kibali cha Mazingira kimepatikana kwa Ndg. Khalifa.
Hatua ya kwanza, baada ya Idara ya Mazingira kuombwa ushauri na Kamisheni ya Utalii juu ya
Mradi huo na athari zake za Kimazingira, na baada ya kutembelea katika eneo husika la Mradi,
ilijiridhisha kwamba Mradi huo una athari kubwa za Kimazingiria na hatua iliyofuata ni
kumuandikia barua Ndg. Khalifa Salum Suleiman na kumueleza kwamba Mradi wake utakuwa
na athari za kimazingira na hivyo alitakiwa aandae Ripoti ya Mazingira na kumpa muongozo wa
Ripoti hiyo na kumtaka aiwasilishe Idarani haraka iwezekanavyo(Kielelezo Na.147).
Baada ya kupokea taarifa hiyo kutoka Idara ya Mazingira, Ndg. Khalifa Salum Suleiman
aliwasilisha Idarani Tathmini yakinifu ya Mradi (Preject Write Up) (Kielelezo Na.148), ambamo
pia hakuonesha namna yoyote ya usimamizi wa mazingira (Rejea Kielelezo Na.148). Hata
hivyo, baada ya Idara ya Mazingira kutoa tena muongozo wa namna gani Mwekezaji huyo
anachotakiwa afanye, ndipo mnamo tarehe 27/08/2004, Idara ya Mazingira ilimtaka Ndg.
Khalifa kuitisha kikao cha Kupitia Ripoti hiyo na hatimae kuweza kutoa Kibali cha Mazingira
kama inavyoelezwa na kifungu cha 47 cha Sheria Namba 2 ya mwaka 1996 (Kielelezo Na.149).
Hatua iliyofuata, baada ya kikao husika, Idara ya Mazingira ilitoa kibali cha Tathmini ya Athari
za Kimazingira (Kielelezo Na.149) na hivyo, ni sawa na kusema kwamba, Ndg. Khalifa Salum
Suleiman alipata kibali cha Idara ya Mazingira kinachomruhusu kuendelea na Ujenzi wa Mradi
wake wa Hoteli ya Kitalii wa Maruhubi Beach Villa mnamo tarehe 22/10/2004, kibali ambacho
kimejumuisha masharti mbali mbali yanayomtaka kuyafuata katika kuendelea na Mradi wake.
4.1.5 Nini kilifuata kuhusiana na Uharibifu wa Mazingira baada ya Kibali hicho cha
mwaka 2004 kutolewa katika Mradi wa Maruhubi Beach Villa?
Baada ya miaka 6 kupita, na baada ya mafanikio makubwa aliyoyapata katika biashara yake kwa
kipindi chote hicho cha miaka 6, mnamo mwaka 2010, Ndg.Khalifa Salum Suleiman, mmiliki
wa Hoteli ya Maruhubi Beach Villa, aliamua kuongeza eneo la Hoteli yake kwa kufukia eneo la
128
Kaskazini mwa Hoteli hiyo (land reclamation), karibu na kingo za mto unaopita jirani na hoteli
hiyo. Wakati akitoa maelezo ya ufukiaji huu, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais, ambae kwa sasa anashughulikia masuala ya mazingira aliithibitishia Kamati kwamba
Mwekezaji huyu, Ndg. Khalifa alifukia eneo hilo la Bahari bila hata ya kuijuilisha Mamlaka
husika, yaani Idara ya Mazingira na hivyo, Idara ya Mazingira katika ziara iliyoifanya katika
eneo hilo iligundua ufukiwaji huo na hatimae ilimuandikia barua ya kusimamisha kufanya hivyo
(stop order) iliyotolewa kwa mujibu wa kifungu cha 23 (1) cha Sheria Namba 2 ya mwaka 1992
kupitia barua ya tarehe 27/04/2010 yenye kumbu kumbu namba IM/29/2/8 VOL.XII/57
(Kielelezo Na.150) kumtaka Mwekezaji huyu, Ndg. Khalifa Salum Suleiman kusimamisha zoezi
lake la kufukia eneo hilo la bahari mpaka atakapopata maelekezo mengine kutoka Idara ya
Mazingira.
Siku ya Ijumaa ya tarehe 18/03/2011, Idara ya Mazingira kwa mashirikiano na Idara Mipango
Miji na Vijiji na Idara ya Upimaji, Idara ambazo ziko chini ya Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji
na Nishati walifanya ziara nyengine katika eneo la Hoteli hiyo na kushuhudia uharibifu mkubwa
wa mazingira unaoendelea kutokana na ufukiwaji wa bahari na mnamo tarehe 21/03/2011,
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ndg. Sheha M. Juma alimuandikia barua nyengine Mmiliki
wa Maruhubi Beach Villa, Ndg. Khalifa Salum Suleiman kumfahamisha kwamba kitendo
anachoendelea nacho cha kufukia eneo la bahari kina athari kubwa kwa mazingira na
kinakwenda kinyume na Sheria za Mazingira, Sheria za Ardhi na Sheria za Mamlaka ya
Baharini ya Sheria za Zanzibar (Kielelezo Na.151). Pamoja na maelekezo haya, Ndg. Khalifa
hakusimamisha zoezi lake la kufukia bahari na aliendelea nalo bila ya kupata kibali cha Idara ya
Mazingira, huku Mamlaka zinazohusika, ikiwa ni pamoja na Idara ya Mazingira zikimtazama
bila ya kumchukulia hatua yoyote ya Kisheria.
Maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais hayakumalizia hapo, aliieleza
Kamati kwamba, mnamo February 2011, Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi
inayoshughulikia Ofisi zaViongozi wa Kitaifa, ilifanya ziara ya kutembelea maeneo ya
kimazingira yakijumuisha maeneo ya mchanga na kifusi pamoja na kutembelea Idara ya
Mazingira na wakati wa majumuisho ya Kamati, Kamati ilieleza masikitiko yake kutokana na
kadhia ya ufukiaji wa bahari unaofanywa kwenye Hoteli ya Maruhubi Beach Villa na kutoa
Muongozo wa kufanyika kwa Ukaguzi wa Kimazingira (Environmental Audit) kwenye Hoteli
hiyo. Pamoja na maelekezo hayo, Mwekezaji wa Mradi husika, Ndg. Khalifa Salum Suleiman
aliendelea na ufukiaji wa bahari hiyo bila ya kujali uwezo wa kisheria wa Mamlaka zinazohusika
wala kujali athari zitakazopatikana kwa wananchi na nchi yetu kwa ujumla na ndipo Idara ya
Mazingira ilipotoa agizo la kumzuia kwa barua tuliyoitaja hapo juu (Rejea Kielelezo Na.151).
Baada ya hatua ya kupuuza agizo la kusitisha ufukiaji wa eneo hilo la bahari takriban mwaka
mmoja, mnamo mwezi wa May, 2011 ndio mmiliki wa Hoteli hiyo, Ndg. Khalifa Salum
Suleiman alifika Idara ya Mazingira na kuomba kupewa utaratibu wa kufanya ukaguzi wa
kimazingira (Environmental Audit) na Idara ikatoa muongozo husika na Katibu Mkuu, Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais aliihakikishia Kamati kwamba, hivi sasa Wizara yake kupitia Idara
129
ya Mazingira imeshakamilisha ukaguzi wa awali (scoping exercise) na kuandaa hadidu rejea za
kufanya ukaguzi wa kimazingira ambazo zilitegemewa kuwasilishwa karibuni kwa Ndg. Khalifa
Salum Suleiman ili ajaze na hatimae kuitisha Kamati husika ili apatiwe kibali cha kuendelea
kufukia eneo hilo la bahari kwa namna kibali hicho kitakavyotolewa.
4.1.6 Kwa nini Ndg. Khalifa Salum Suleiman hakufuata amri ya kuzuia ufukiaji wa
bahari wakati alipoagizwa kufanya hivyo:
Kifungu cha 100 cha Sheria Namba 2 ya mwaka 1996 kinaeleza adhabu ya mtu asietii amri ya
zuio lililotolewa na Idara ya Mazingira chini ya kifungu cha 23(1) cha Sheria hiyo kama
kinavyosomeka hapa chini:
“Mtu yoyote anaeshindwa kutii amri ya zuio iliyotolewa chini ya kifungu cha 23 atakuwa ametenda kosa
na akipatikana na hatia atawajibika kulipa faini kama ilivyoelezwa katika Jadueli ya 4 ya sheria hii au
atawajibika kutumikia kifungo kisichopungua miezi sita au adhabu zote mbili”.
Tukumbuke tu kwamba, Ndg. Khalifa Salum Suleiman hakuwahi kuomba kibali cha mazingira
moja kwa moja Idara ya Mazingira mpaka pale Kamisheni ya Utalii iliopowasiliana na Idara ya
Mazingira kwa ajili ya ushauri wa Mradi wa Ndg. Khalifa yenyewe ilipomtaka afanye hivyo,
aidha katika mwaka 2010 aliamua kufukia bahari bila ya kupata kibali chochote cha Mazingira
huku akijua wajibu wake, na hata baada ya kupokea Agizo la kusitisha ufukiaji huo kutoka Idara
ya Mazingira alidharau na aliendelea na ufukiaji wake kwa muda wa mwaka mzima ndipo
alipoona ipo haja ya kuheshimu Mamlaka husika. Katika hali hii, kila mtu atajiuliza, Je, Ndg.
Khalifa Salum Suleiman ana nguvu gani inayompa kiburi kikubwa dhidi ya Serikali. Suala hili
pia aliulizwa mbele ya Kamati, ingawaje hakuwa muwazi kulijibu suala hili, lakini alipoulizwa
juu ya mahusiano yake na Serikali, ndipo ilipofahamika wazi kwamba, kwa hali hii, Ndg.
Khalifa alifanya kiburi hicho huku akiamini kwamba hakuna Mamlaka yoyote Zanzibar yenye
uwezo wa kumchukulia hatua. Kwa hivyo, ni vyema tukafahamu uhusiano wake na Serikali.
4.1.7 Uhusiano wa Ndg. Khalifa Salum Suleiman na Serikali:
Mnamo tarehe 19/01/2010 Ndg. Khalifa Salum Suleiman alinunua shamba katika eneo la
Shakani Buyu kutoka kwa Ndg. Abdalla Ahmed Abdalla kwa thamani ya Tsh. 10,000,000
shamba ambalo lilimilikiwa na Muuzaji pamoja na Ndg. Yanu Ahmed Abdullah ambao wote
kwa pamoja walilinunua kutoka Wakfu na Mali ya Amana tarehe 12/08/1989 kwa thamani ya
Tsh.20,000/-. (Kielelezo Na.152). Kufuatia umiliki wa shamba hilo, Ndg. Khalifa alifanikiwa
kuwa na sehemu kubwa na kuweza kufanya biashara ya usambazaji wa kifusi kinachochimbwa
kutoka katika shamba lake la Shakani na miongoni mwa wateja wake wakubwa ni Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano.
Mnamo tarehe 1/03/2011, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano iliingia Mkataba na Ndg.
Khalifa Salum Suleiman wa kusambaziwa kifusi (sub-base Materials) kwa ajili ya ujenzi wa
Barabara ya Amani-Mtoni (Kielelezo Na.153). Mkataba huu wa miezi minne ulimzidishia
130
umaarufu Ndg. Khalifa na uwezo mkubwa kutokana na malipo aliyopata kwa kazi hiyo, kiasi ya
kujiamini kuwa ni sehemu muhimu kwa Serikali (Kielelezo Na.154). Aidha, Katika mahojiano
na Kamati, Ndg. Khalifa alieleza kwamba mbali na kuuzia kifusi Serikali kupitia Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano, pia alitoa msaada mwingi kwa Idara ya Ujenzi wa Barabara
(UUB) na alieleza wazi kwamba „anawapa bure vifaa vyake watu wa UUB wanapokwama‟.
Yaani anaisadia Idara ya UUB kwa kutoa vifaa vya uchimbuaji wa Kifusi na vifaa vya
kutengenezea bara bara, msaada ambao pia unajumuisha kuwauzia kifusi kwa ajili ya utekelezaji
wa majukumu mbali mbali ya Idara. Aidha, aliieleza wazi Kamati kwamba msaada huo wa kutoa
kifusi bure, huwa pia anautoa kwa viongozi mbali mbali wa nchi hii ikiwa ni pamoja na
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Mbali na hayo, Ndg. Khalifa pia analipia gharama za kibali
cha uchukuaji wa mawe na kifusi kutoka katika Shamba lake hilo la Maungani ambalo
limetumika kwa kiasi kikubwa katika kutoa mahitaji ya ufukiaji wa bahari hiyo (Kielelezo
Na.155).
4.1.8 Namna ya Ufukiaji wa Bahari ulivyofanyika na Mchango wa Serikali katika
kufanikisha hali hii:
Ndg. Khalifa aliieleza Kamati kwamba zoezi lake la kufukia bahari bila ya kufuata utaratibu wa
kisheria wala kuwasiliana na Mamlaka yoyote husika ikiwa ni pamoja na Idara ya Mazingira,
Wizara ya Ardhi na Mamlaka nyengine husika, lilianza hatua kwa hatua , kuanzia mwaka 2004
na kumalizikia hatua aliyofikia sasa mwaka 2010/2011. Alieeleza Kamati pia kwamba, tokea
mwaka 2004 alipoanza ufukiaji huo, hakuna Taasisi yoyote ya Serikali iliyolalamika ama
kumzuia kuendelea na ufukiaji huo mpaka ilipofikia mwaka 2010, akiwa katika hatua za mwisho
ndio Idara ya Mazingira ilitoa agizo la kumzuia asiendelee.
Alipoulizwa ni „materials‟ gani ametumia katika kufukia ardhi hiyo, aliieleza Kamati kwamba
amefukia kwa kutumia kifusi chake alichokichimba katika Shamba lake la Shakani Buyu na
sehemu kubwa alitumia mapande ya zege aliyoyapata baada ya kuvunjwa kwa Bandari ya
Zamani ambayo yalikwenda kutupwa maeneo ya Buyu. Alipoulizwa kama alipata kibali ama
ruhusa ya Serikali ama Shirika la Bandar kuhusiana na mapande hayo ya zege ya Bandari,
alisema kwamba hayakuwa yakihitajika na ndio maana yalikwenda kutupwa huku yeye kwa
kuona yanamfaa katika ufukiaji wa bahari, katika hoteli yake ya Maruhubi Beach Villa, ndio
aliyaokota na kuyatumia.
Kuhusiana na kupata msaada wa Serikali katika ufukiaji huo, Ndg. Khalifa alisema kwamba
hakupata msaada wowote kutoka Serikalini, akikusudia kueleza kwamba vifaa vyote alivyotumia
katika ufukuaji na uchukuliaji wa kifusi ni mali zake mwenyewe. Hata hivyo, baada ya kuelezwa
kwamba Kamati ina ushahidi wa gari za UUB zilizoshiriki katika uchukuaji wa kifusi na
kufikisha katika eneo la tukio, alikiri kwamba Madereva watatu wa Idara ya Ujenzi wa Barabara
(UUB) walitumika kupeleka dongo ambalo kuwa halihitajiki baada ya Idara ya UUB kukarabati
Babaraba na kulitoa dongo hilo, ndio waliompelekea gari hizo kwa kuwagaia pesa kidogo.
131
Ili kujiridhisha katika hili, Kamati ilifanya ukaguzi wa kuwatambua Madereva hao katika Idara
ya UUB, na kufanikiwa kukutana na Madereva wawili kati ya watatu waliohitajika na wote
walikiri kupeleka Udongo Mchafu katika eneo lililofukiwa, kwa kutumia magari ya Serikali,
SMZ 6716 na SMZ 6713 aina ya IVECO, huku wakigaiwa pesa kidogo na Ndg. Khalifa Salum
Suleiman. Kamati pia ilitaka kujua iwapo Uongozi wa Idara hii unafahamu ama kuwaagiza
Madereva wake kupeleka kifusi ama Udongo huo Mchafu kwa Ndg. Khalifa, ambapo Ndg.
Hafidh Madawa Kinoo, Msimamizi wa Bara bara alikana kuhusika kuwatuma madereva hao
kupeleka kifusi lakini anakumbuka kupelekwa kwa udongo mchafu kwa Ndg. Khalifa, na
aliwaamrisha madereva hao kufanya hivyo, baada ya yeye kupokea amri hiyo kutoka kwa Mkuu
wa Mradi wa Ujenzi wa bara bara ya Amani-Mtoni, Engineer Mbarouk.
4.1.9 Nafasi ya Kamisheni ya Utalii katika utoaji wa kibali cha Biashara ya Utalii kwa
Mradi wa Maruhubi Beach Villa:
Kwa mujibu wa kifungu cha 4(h) cha Sheria Namba 6 ya mwaka 2009, Kamisheni ya Utalii ya
Zanzibar ina jukumu la kusajili, kutoa leseni, kutoa muongozo na kusimamia Biashara ya Utalii.
Kwa mnasaba wa kifungu hiki, mtu yoyote anaetaka kuendesha biashara ya Utalii Zanzibar, ni
lazima kwanza asajiliwe na apate kibali cha biashara hiyo kinachotolewa na Kamisheni ya Utalii,
na hivyo, kwa namna moja ama nyengine, Ndg. Khalifa Salum Suleiman, kwa kuwa amekusudia
kuanzisha biashara ya Utalii katika hoteli yake ya Maruhubi Beach Villa, ni lazima nae asajiliwe
na kupata kibali kutoka kwa Kamisheni ya Utalii. Maelezo yanayonasibiana na haya pia
yalielezwa katika Sheria ya Utalii Namba 9 ya mwaka 1996 iliyofutwa kwa Sheria Namba 6 ya
mwaka 2009. Katika Sheria hii ya mwaka 1996, kifungu cha 5(c) kimeipa Kamisheni ya Utalii
kazi ya kutoa Leseni za Biashara ya Utalii, ambapo kwa mnasaba huu, Ndg. Khalifa alipaswa
akate leseni hiyo katika Kamisheni ya Utalii na sio vyenginenvyo.
Hivyo basi, Kamati nayo katika kikao cha pamoja baina ya Kamisheni ya Utalii na Taasisi
nyengine zinazohusika, ilihitaji kufahamu kwa namna gani Kamisheni ya Utalii ilihusika katika
utekelezaji wa jukumu lake la utoaji wa Leseni ya Utalii kwa Ndg. Khalifa. Katika kufafanua
hoja ya wapi Ndg. Khalifa alipata Leseni ya kuendesha biashara ya Utalii iliyoulizwa na Kamati,
Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii, Ndg. Ali Khalil Mirza aliieleza Kamati kwamba
Kamisheni ya Utalii ilipokea maombi ya Ndg. Khalifa tokea mwaka 2004 wakati huu, bado
hajafanya ufukiaji wa bahari. Baada ya kupokelewa kwa maombi hayo, Kamisheni ya Utalii
iliyapeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkurugenzi wa Idara ya Ardhi na Usajili
na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kwa ajili ya kupata ushauri na maoni kutoka katika taasisi
hizo juu ya kufaa kwa Mwekezaji huyu kupewa Leseni ya biashara ya Utalii (Rejea Kielelezo
Na.146 Kuhusu Barua yenye kumbu kumbu namba K/UT/10/156). Na baada ya kupokea
maoni hayo kutoka kwa Idara ya Mazingira, Kamisheni haikutoa Leseni kwa Ndg. Khalifa kwa
sababu alikuwa bado hajatimiza masharti ya Kufanya Tathmini ya Athari za Kimazingira na
hivyo, alimuandikia barua Ndg. Khalifa kumpa taarifa kwamba anatakiwa afike Idara ya
Mazingira kwa ajili ya kupata ushauri wa namna ya kutayarisha udhibiti wa Mazingira
(Kielelezo Na.156).
132
Kamisheni ya Utalii ilitoa Leseni kwa Ndg. Khalifa mnamo mwaka 2005 wakati huu, tayari Ndg.
Khalifa alikwisha timiza masharti ya Athari za Kimazingira na tayari alikwishapewa Kibali na
Idara ya Mazingira (Kielelezo Na.157). Aidha, Leseni hiyo hiyo ndio iliyokuwa ikitumika kwa
miaka yote bila hata ya kuwa „renewed‟ kinyume na kifungu cha 16(2)(b) cha Sheria Namba 6
ya mwaka 2009. Kwa maana nyengine, mbali na kuharibu mazingira na kufanya maamuzi yake
kinyume na Sheria na bila ya kujali uwezo wa Serikali, Ndg. Khalifa aliendesha biashara ya
Hoteli ya Utalii kwa Kukata leseni moja tu, bila ya kuifanya iende na wakati (renew) kwa kipindi
cha Miaka mitano, huku Serikali, pamoja na hasara nyenginezo, pia inakosa mapato ya leseni
husika. Hii inaleta maana kwamba, Mwekezaji huyu hakati leseni kwa kila mwaka kama
anavyotakiwa kufanya hivyo. Mbali na hayo, ni vyema pia tukaangalia sababu zilizoipelekea
Kamisheni ya Utalii kukubali kutoa tena kibali kwa Mwekezaji huyu (kumfanyia renew ya
leseni) mwaka 2011, (Kielelezo Na.158) wakati inafahamu kwamba tayari alikwishapewa barua
ya Zuio la kuhatarisha Uharibifu wa Mazingira kutoka Idara ya Mazingira mnamo tarehe
12/04/2010.
Ili kupata uchambuzi yakinifu wa suala hili, ni vyema tuanze kwa kuangalia ulazima wa kukata
Leseni ya Utalii kwa kila Mwekezaji hapa Zanzibar. Kwa mujibu wa kifungu cha 15(1) cha
Sheria ya Utalii, Namba 6 ya mwaka 2009, Ndg. Khalifa kama alivyo mtu mwengine yoyote
Zanzibar, anakatazwa kufanya biashara ya kuendesha Hoteli ya Utalii ya Maruhubi Beach Villa,
bila ya kukata Leseni inayotolewa na Kamisheni ya Utalii, na kwa hali hii, analazimika kukata
leseni hiyo ama kuifanya iende na wakati (renew) kila mwaka. Hivyo, kitendo cha kukata Leseni
ni wajibu wake kisheria. Hata hivyo, suala letu hapa, ni kwa nini Mamlaka iliyopewa dhamana
ya Leseni, yaani Kamisheni ya Utalii ikatoa leseni hiyo ya mwaka 2011, wakati inafahamu
kwamba leseni hiyo inatakiwa itolewe kwa misingi ya Sheria za Nchi.
Sharti moja miongoni mwa masharti ya msingi yaliyoelezwa katika kifungu cha 15(3) cha Sheria
Namba 9 ya mwaka 2009 kinaishurutisha Kamisheni ya Utalii kutoa leseni kwa Mwekezaji
ambae atakaekuwa analipa kodi ipasavyo kwa Mamlaka zinazohusika na Kodi na hili lifanyike
kwa ushahidi wa malipo hayo. Katika hili, Kamati inapata mashaka na Mwekezaji huyu, kwa
sababu ilipotaka kuthibitishiwa kwamba analipa kodi, hakuna uthibitisho ambao Ndg. Khalifa
aliweza kuwasilisha kwa Kamati wala Kamisheni ya Utalii haikuweza kuthibitisha suala hili, hali
ambayo inafahamika kwa Kamati kwamba, Mwekezaji huyu halipi Kodi ipasavyo.
Sharti jengine ambalo Kamisheni inalazimika kulizingatia kabla ya kutoa leseni ni melekezo ya
kifungu cha 38(2) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu, Namba 2
ya mwaka 1996 kama tunavyonukuu:
“Hakuna taasisi yoyote inayohusika na kutoa leseni, ruhusa, kibali, au aina nyengine ya ruhusa kwa ajili ya
shughuli yoyote ambayo huenda ikawa na athari muhimu kwa mazingira isipokuwa (ruhusa hiyo itolewe)
baada ya kufanywa tathmini ya athari za kimazingira kwa ajili ya kufanywa shughuli hiyo.
Kwa lugha hii, Kamisheni ilikuwa inafahamu kwamba mwekezaji huyu amekiuka masharti ya
Utunzaji wa Mazingira na tayari Mamlaka husika ilikwisha toa zuio dhidi yake,lakini kwa
133
kutoheshimu Sheria, au kwa sababu ambazo Kamisheni inazifahamu, ndio maana wakaamua
kutoa Leseni kwa Mwekezaji ambae kisheria, hangepaswa kupewa leseni hiyo.
4.1.10 Nafasi ya Idara ya Ardhi katika Suala hili.
Kwa kuwa suala la Mradi wa Ujenzi wa Hoteli za Kitalii pia linahusiana na ardhi, kwa namna
moja ama nyengine, Kamati ililazimika kukutana na watendaji wa Idara ya Ardhi katika vikao
vitatu tofauti wakati Kamati inaifanyia kazi hadidu hii rejea. Suala kubwa ambalo Kamati ilitaka
kufahamu, ni kwa namna gani Idara ya Ardhi ilishiriki katika kukemea ama kuruhusu uharibifu
wa Mazingira uliofanywa na Mwekezaji, Ndg. Khalifa Salum Suleiman kwa kufukia sehemu ya
ardhi bila ya kibali. Kwa upande wa Idara ya Ardhi, Mkurugenzi wa Idara hiyo akitoa ufafanuzi
mbele ya Kamati akithibitisha kwamba Idara yao haimtambui mmiliki wa eneo hilo zaidi ya
Ndg. Ussi Yahya Haji aliepewa ardhi hiyo kwa matumizi ya „Art Galary‟ (kama tulivyokwisha
eleza hapo kabla). Walipoulizwa ni kwa sababu gani hawakuchukua hatua dhidi ya Mwekezaji
huyo aliefukia bahari bila hata ya taarifa yoyote wala muongozo wowote kutoka Idara yao,
alieleza kwamba wao Idara ya Ardhi hawalazimiki kisheria kufanya ukaguzi wa maendeleo ya
matumizi ya ardhi katika seckta ya Utalii mpaka pale wanapopata malalamiko kutoka kwa
wananchi. Na kwa maana hii, kwa kuwa hakukuwa na malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi,
Idara ya Ardhi pia haikuwa na kauli yoyote ya kusema dhidi ya uvamizi huo.
Idara ya Ardhi iliisaidia sana Kamati kuitambua mipaka ya asili ya ardhi hiyo na sehemu ya
bahari iliyofukiwa, ambapo kati ya alama (beacons) za kiwanja cha asili zilizokuwepo kabla ya
ujenzi huo wa hoteli ya Kitalii, ni alama moja pekee Nambari 103 imeweza kutambuliwa huku
alama mbili zilizobakia zimefukiwa na ujenzi na alama zilizobakia ndio zimefukiwa na hazipo
kabisa kutokana na ufukiaji wa bahari hiyo. Hata hivyo, Kamati iliiagiza Idara ya Ardhi
kutayarisha ramani ya kuonesha vipi ardhi hiyo ilivyokuwa kabla ya ufukiwaji na eneo hilo la
bahari, eneo gani limeongezeka kutokana na ufukiwaji huo, na ujenzi upi umejengwa katika eneo
lililofukiwa, lakini taarifa hiyo haikuweza kupatikana katika siku za kazi za Kamati. Aidha, kwa
kuwa taarifa hiyo ni ya kitaalamu na ingeweza kufanywa na wataalamu pekee kutoka Idara ya
Ardhi, Kamati ilitoa muda wa kutosha kwa Idara kutayarisha na hatimae kuikabidhi kwa Kamati,
ili itusaidie katika ripoti yetu hii, lakini kwa masikitiko makubwa mpaka tunaandika ripoti hii,
Kamati haijapokea taarifa hiyo. Kwa lugha nyengine, Kamati haikupata mashirikiano ya dhati
katika upatikanaji wa taarifa hiyo.
4.2 UJENZI WA HOTELI YA ZANZIBAR OCEAN VIEW KILIMANI.
Katika kupata ufafanuzi wa suala husika, jambo la kwanza ambalo limeonekana ni busara
kufahamika ni hili linalohusiana na ardhi iliyotumika kujenga Hoteli ya Zanzibar Ocean View-
Kilimani. Suala hili ni la msingi sana kwani kwa kadiri tutakavyolifafanua, ndio hoja zilizobakia,
za uvamizi wa ardhi katika fukwe hiyo pamoja na wajibu wa kuyatunza mazingira,
134
zitakapofahamika kwa uwazi zaidi. Kwa namna hii, ni vyema kwanza tukafahamu historia ya
umiliki wa ardhi husika.
4.2.1 Umiliki wa Ardhi iliyojengewa Hoteli ya Zanzibar Ocean View:
Kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa kwa Kamati, Mmiliki wa Hoteli hiyo Ndg. Aman
Ibrahim Makungu, alieleza kwamba hapo awali alinunua nyumba ambayo ilikuwa bado
haijamaliza kujengwa (gofu) yenye namba 13 iliyokuwepo eneo hilo (Kilimani) kutoka kwa
muuzaji Dr. Asya Ali Khamis, Msimamizi wa Kisheria (Administrix) wa Marehemu Abdul-
Wahid Masoud Borafia, aliefariki katika Hospitali ya Mhimbili ya Dar es Salaam ambae ndie
mmiliki wa nyumba inayohusika, kufuatia kesi Namba 75 ya mwaka 1974 na wasia alioutoa,
mnamo mwaka huo wa 2007, ndipo uuzaji huo ulipokamilika (Kielelezo Na.159).
4.2.2 Suala la Uvamizi wa Ardhi uliofanywa kutokana na Ujenzi wa Hoteli:
Kwa mnasaba wa maelezo ya hapo juu inaonesha wazi kwamba, Ndg. Aman Ibrahim Makungu
ni mmiliki halali wa Nyumba namba 13 na ukubwa wa eneo lililoizunguuka lenye mita za mraba
(square meter) 2227.25, na Kamati imejiridhisha juu ya uhalali huo, suala ambalo linatoa
ufafanuzi wa kazi ya Kamati ya kuangalia vipi uvamizi wa ardhi umetokea ama haukutokea.
Kwa maana nyengine, kwa mujibu wa ufafanuzi wa umiliki wa ardhi inayohusika na ujenzi wa
hoteli hii, tunaweza kuigawa ardhi husika katika maeneo mawili makuu.
Aina ya kwanza ni hiyo tuliyokwishaieleza hapo kabla, kwamba Mmiliki wa Hoteli hiyo, Ndg.
Aman Ibrahim Makungu alinunua jengo (Nyumba ama Boma) Namba 13 ya ukubwa wa mita za
mraba (square meter) 2227.25, ardhi ambayo hata Kamati haikuwa na pingamizi nayo.
Isipokuwa ieleweke kwamba, eneo lote lililojengwa hoteli hiyo ni kubwa zaidi ya mara tatu na
eneo tulilolieleza awali, sasa kama hali ndio hii, je, eneo lililobakia ambalo pia linahusika na
ujenzi wa daraja hadi ng‟ambo ya pili kulikojengwa Nyumba kadhaa za kitalii (Bungalows)
pamoja na kumbi za mikutano, je zimejengwa kwa kupata kibali kutoka Mamlaka husika na je
ardhi iliyotumika katika ujenzi huo inamilikiwa na nani na je inamilikiwa kisheria? Hili basi
ndilo eneo la pili tunalolizungumzia.
Eneo hili hili ndilo lenye mikahawa miwili maarufu (Restaurants) ambayoyote imejengwa
kwenye fukwe na karibu sana takriban mita 10 tu kutoka katika bahari, je ruhusa ya ujenzi wake
imetoka wapi? Kujibika kwa masuala haya, kutasaidia sana kupata ufafanuzi wa namna gani
uvamizi katika fukwe umetokea ama haukutokea wakati wa ujenzi wa hoteli hii.
Hivyo basi, tuanze na hili linalohusu umiliki wa eneo la ziada ya eneo la Nyumba Namba 13
ambalo kwa ufupi, ndilo lililohusika na ujenzi wa hoteli hiyo. Kamati ilianza kupata maelezo ya
eneo hilo kutoka kwa Mamlaka husika, lakini ni vyema pia kueleza kweli kwamba, ushahidi wa
umiliki wake umeweza kutolewa na Ndg. Amani Ibrahim Makungu, kwamba ameipata Ardhi
hiyo kutoka Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi kupitia njia ya „grant‟ iliyofanywa kwa
135
mamlaka ya Waziri wa Wizara hiyo chini ya kifungu cha 7 na 8 cha sheria namba 12 ya mwaka
1992. (Kielelezo Na.160)
Ardhi hiyo yenye ukubwa wa mita za mraba 4499.90, inayotambuliwa kama kiwanja namba 13,
yenye namba L.O No. Z-53/S.191/2007/13 ilitolewa tarehe 27/11/2007, kupitia Shahada ya Haki
ya Matumizi ya Ardhi (Certificate of a Right of Occupancy), ambapo Kamati pia haikuwa na
pingamizi juu ya umiliki huu. Hata hivyo, ilihoji kuhusu ruhusa ya ujenzi wa majengo mbali
mbali yaliyomo kwenye ardhi hiyo, ikiwa ni pamoja na nyumba za wageni (Bungalows), kumbi
za mikutano na majengo mengine iwapo kama mmiliki wake alipata ruhusa ya ujenzi kutoka
Mamlaka zinazohusika, nae kwa uwazi akaeleza kwamba hakukata kibali chochote katika ujenzi
wake, na hii ina maana hata ujenzi wa mikahawa hiyo iliyojengwa kando ya bahari, hakupata
kibali popote.
Kwa ufupi, Kamati imejiridhisha kwamba, Ndg. Aman Ibrahim Makungu ni mmiliki halali wa
ardhi hiyo, isipokuwa haikuridhika na namna ya ujenzi wa majengo yote ya hoteli hiyo
kujengwa bila ya kibali ama ruhusa ya ujenzi kutoka Mamlaka husika. Vile vile kwa kuwa
maelekezo ya ujenzi katika eneo la fukwe ni kuwacha angalau mita 30, wakati Mmiliki huyu,
Mikahawa yake ameijenga karibu sana na bahari, ni wazi kwamba amefanya uvamizi wa eneo la
fukwe, na hapa ndipo Kamati inaposimamia hoja yake kwamba, uvamizi wa eneo la fukwe kwa
hoteli hii umefanyika kwa hatua hiyo.
Suala jengine la msingi lililotumwa kwa Kamati, ni kuangalia athari kubwa za kimazingira kama
zimehifadhiwa katika ujenzi huo. Na ili tupate ufafanuzi yakinifu, ni vyema kwanza tukaangalia
maelezo yafuatayo:
4.2.3 Uanzishaji wa Mradi na Athari zake za Kimazingira: Kabla ya kuanza kuangalia, namna gani Mamlaka husika, zilihusika katika kufanya tathmini na
hatimae kutoa kibali cha mazingira, suala hili lilipata jawabu yake bila ya usumbufu wowote,
pale mmiliki wa Hoteli hiyo alipoulizwa suala hili na kujibu kwa mkato kwamba, yeye amekiuka
taratibu za kimazingira, yaani, kunako suala la ardhi, alieleza kwamba ni yake na wala hajafanya
uvamizi, lakini anakiri kwamba suala la mazingira hakupata kibali wala kufuata taratibu zozote
za Kimazingira alipoanzisha mradi wake. Hata hivyo, Kamati inaona ni busara kuendelea
kuangalia namna gani maelezo ya Idara ya Mazingira yanawiyana na maelezo ya mkato ya
mmiliki wa hoteli hiyo.
Katika kikao cha pamoja baina ya Kamati na Watendaji wakuu wa Ofisi ya Rais, Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais, pamoja na watendaji wengine, ilielezwa na Katibu Mkuu, Dr.
Omar D. Shajak, kwamba wao kama Idara ya Mazingira walipokea taarifa ya barua kutoka
Kamisheni ya Utalii tarehe 25/07/2008 yenye kumbu kumbu namba K/UT/2008/11/79/2
inayohusiana na ombi la kuanzisha Mradi wa “Zanzibar Ocean View Resort”, ambayo
imeambatanishwa na taarifa ya mradi wa kina (project write up) iliyokuwa inakusudia kuomba
leseni ya kundesha ama kuruhusiwa kuendesha biashara ya Utalii katika Hoteli hiyo (Kielelezo
Na.161).
Tunapenda tukumbushe kwamba, kama tumepitia vizuri maelezo ya namna hii katika Hoteli ya
Maruhubi Beach Villa ya Ndg. Khalifa Salum Suleiman, ni wazi kwamba, Wawekezaji hawa
136
wazalendo huwa hawapeleki maombi yao moja kwa moja Idara ya Mazingira kama
wanavyotakiwa kufanya, na badala yake wao kwa kutoona thamani ya Mazingira, huomba kibali
cha Utalii katika Kamisheni ya Utalii, ambapo Kamisheni hii ndio hupeleka maombi hayo Idara
ya Mazingira na taasisi nyengine zinazohusika, kwa ajili ya kuomba ushauri wa Mradi uliofika
kwao.
Kwa maana nyengine, kama sio Kamisheni ya Utalii kupeleka taarifa hizo Idara ya Mazingira,
Idara hii isingekuwa na habari yoyote ya miradi ya aina hii. Lakini pia tukumbuke kwamba,
kama tulivyokwisha eleza awali, kwamba, Kamisheni ya Utalii kutoa taarifa hizo kwa Idara ya
Mazingira ni kutekeleza wajibu wao kisheria kwa sababu Sheria ya Kusimamia Mazingira kwa
Maendeleo Endelevu ya Zanzibar, Namba 2 ya mwaka 1996, imewakataza kutoa kibali chochote
kwa mtu ama Taasisi yoyote bila ya Taasisi ama Mtu huyo kuwa na kibali cha Tathmini ya
Mazingira (EIA Certificate), maelezo ambayo yametolewa na kifungu cha 38(2) cha Sheria hiyo.
Na tunaendelea kukumbusha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha Sheria hiyo, Ndg.
Aman Ibrahim Makungu alitakiwa aombe kibali cha Mazingira Idara ya Mazingira,
akiambatanisha Ufafanuzi yakinifu wa Mradi wake (Project Write up) iliyojitosheleza kitaarifa
kama zinavyohitajika kuanzia kifungu cha 39(1)(a)-(h), jambo ambalo hakulifanya. Aidha, kwa
kusisitiza, Mmiliki huyu alitakiwa afanye hivyo, kabla ya ujenzi wake na sio baada ya
kukamilika kwa ujenzi wa hoteli na ndio kuomba kama alivyofanya kwa Kamisheni ya Utalii.
Tukiendelea na maelezo ya Dr. Shajak, kwamba, baada ya Idara yake kupokea barua kutoka
Kamisheni ya Utalii kuhusiana na ujenzi wa mradi wa hoteli hii, siku nne tu baadae, yaani tarehe
29/07/2008, Idara ya Mazingira ilifanya ukaguzi wa kawaida wa eneo hilo na kubaini ukiukwaji
wa taratibu za kimazingira kwa Mradi huu wa “Zanzibar Ocean View” na kujiridhisha kwamba
Ujenzi wa Mradi huu umefanywa bila ya kibali cha Mazingira.
Kufuatia hali hii, Idara ya Mazingira ilitekeleza vyema jukumu lake kwa kumuandikia barua
Ndg. Amani Ibrahim Makungu ya kusimamisha ujenzi wa Mradi huo hadi hapo utakapofanyiwa
„Ukaguzi wa Kimazingira‟ ya tarehe 29/07/2008, yenye kumbu kumbu namba IM/29/2/8
VOL.X. Barua hiyo iliyoeleza wazi kwa Anuani (Heading) inayosomeka “UKIUKWAJI WA
TARATIBU ZA KIMAZINGIRA KWA MRADI WA “ZANZIBAR OCEAN VIEW”. Barua
hiyo ilifanya rejea ya kifungu cha 38(1) cha Sheria Namba 2 ya mwaka 1996, na kusisitiza
kwamba, Mradi huo ulipaswa kufanyiwa Tathmini ya Kimazingira na kupewa Cheti cha
Mazingira kabla ya kuanza hatua yoyote ya ujenzi. (Kielelezo Na.162).
Ifahamike tena kwamba, Idara ya Mazingira ilipotoa agizo hilo la kuzuia ujenzi huo hadi hapo
tathmini ya mazingira inapofanywa, ni mamlaka yao kisheria. Kwa mujibu wa kifungu cha 23(1)
cha Sheria hii, Namba 2 ya mwaka 1996, Idara ya Mazingira kupitia kwa Mkurugenzi wake,
ilitakiwa kutoa taarifa ya haraka kwa Mmiliki wa Hoteli hiyo, tena yenye kueleza uvunjwaji wa
sheria na taratibu za Mazingira, jambo ambalo Idara imelifanya na hata Kamati imelipongeza
sana.
137
Kwa ufupi tulichotaka hapa kifahamike ni kwamba, Mradi huu wa Ujenzi wa Hoteli ya
„Zanzibar Ocean View‟ ulipaswa kwanza kufanywa tathmini ya kimazingira kabla ya ujenzi
wake, jambo ambalo halikufanyika, na Kamati imejiridhisha kupitia Mmiliki mwenyewe, Ndg.
Aman Ibrahim Makungu wakati akihojiwa na Kamati na hata kupitia Idara inayohusika na
usimamizi wa mazingira, na kwa namna yoyote ile, ushahidi unajionesha wazi kwamba Mmiliki
huyu hakufuata taratibu za Mazingira kabla ya Ujenzi, na hivyo, ni kusema kwamba, alipaswa
baada ya kupewa „Stop Order‟ achukuliwe hatua za kisheria kama ilivyoelezwa na kifungu cha
23(4) cha Sheria hii.
4.2.4 Hatua zilizochukuliwa baada ya uvunjwaji wa taratibu za Kimazingira: Baada ya kujiridhisha kwamba, ujenzi huu umekiuka taratibu za kimazingira, ni vyema sasa
tuendelee kujiuliza, Je nini kilifuata baada ya Mmiliki huyo kutoheshimu taratibu za nchi
zinazomuongoza na kumtaka aheshimu taratibu za utunzaji wa Mazingira katika ujenzi wa Hoteli
yake kwa kuthamini maendeleo endelevu ya watu wa nchi hii.
Ukifanya marejeo ya paragrafu ya mwisho ya kielelezo Namba 162, utakutana na maeneno
yafuatayo: “Idara ya Mazingira inakutaka ufike kwa ajili ya kupewa muongozo wa kufanya “Environmental Audit”
sambamba na kusimamisha ujenzi huo. Kinyume na hivyo, Idara ya Mazingira italazimika kuchukua
taratibu zinazofaa za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwasilisha shauri hilo katika vyombo vya kisheria”
Maelezo haya yanaweza kutafsiriwa kwa mantiki mbili tofauti; kwanza ni Kwamba Idara ya
Mazingira imetekeleza vyema wajibu wake wa kutoa zuio la ujenzi wa Mradi wa Hoteli
uliokiuka taratibu za kimazingira, na iwapo agizo hilo halitafuatwa, basi watachukua hatua za
kisheri ambazo zimeelezwa na sheria hiyo hiyo waliyoitumia kutoa agizo hilo. Na kwa maana
hii, tutaona kweli Idara imetekeleza wajibu wake na ilikuwa na udhati wa kuyalinda mazingira.
Ama mtazamo wa pili, inaweza kutafsiriwa kwamba, Idara hii haikutekeleza wajibu wake,
badala ya kumchukulia hatua mmiliki huyu kwa kosa la kujenga bila ya kibali cha mazingira,
badala yake inaendelea kumbembeleza na kutaka kuhalalisha alichokifanya, wakati tayari
ameshavunja sheria. Na kwa maana hii, kwa kuwa kosa lilifanyika awali, hakuna haja ya
kulihalalisha baadae!
Basi, sisi na tuanze kuangalia hoja ama tafsiri zote mbili: Tukianzia na ya kwanza huku
tukifahamu kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 23(1) cha Sheria ya Kusimamia Mazingira
kwa Maendeleleo Endelevu ya mwaka 1996, ilitakiwa kutoa Taarifa (Notice) kwa Ndg. Aman
Ibrahim Makungu, mmiliki wa Hoteli hiyo kumtaka azuie Ujenzi wake, kwani unaathari kubwa
za kimazingira na miongoni mwa miradi ambayo lazima ifanyiwe Tathmini ya Mazingira kabla
ya Kujengwa ama kuendelezwa kwake. Na kwa kuwa Idara imetekeleza wajibu huu, ndio maana
tunakubaliana kwamba, wametekeleza wajibu wao.
Aidha, kwa upande wa tafrsiri ya pili, hata Kamati inakubaliana kwamba, Idara ya Mazingira
imejiingiza katika kazi isiyo yake, ya kumtaka Ndg. Makungu kufika ofisini na kumpa
muongozo wa kufanya Tathmini ya Kimazingira, wakati uwezo huo hawajapewa na sheria hiyo.
Kwa mfano, kifungu cha 23(3) cha Sheria hii, kinaeleza wazi kwamba, iwapo Agizo hilo
138
halitatiiwa, Idara ya Mazingira, kupitia Mkurugenzi inaweza, bila ya kutoa taarifa nyengine
(notice) kuchukua hatua zinazofaa kupunguza madhara ya kimazingira yaliyosababishwa na
ujenzi huo na Idara hii, kwa kuwa itakuwa imetumia gharama zake katika kuchukua hatua za
kupungua athari hizo za Kimazingira, kupitia Mkurugenzi wake, itakuwa na haki ya kuchukua
hatua za kujirejeshea gharama zake kama zilivyoelezwa katika kifungu cha 101 cha Sheria hii,
ambacho kinakusudia, pamoja na mambo mengine kwa mmiliki wa Mradi huu, kulipa gharama
zote zilizochukuliwa na Idara ya Mazingira katika uchukuaji wa hatua za kupunguza madhara ya
kimazingira yaliyojitokeza, na hatua nyengine yoyote ambayo Mahakama ingeliamuru
kuchukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 101.
Aidha, kifungu cha 38(1) cha Sheria hii kinaeleza wazi kwamba,
“Mtu yoyote haruhusiwi kufanya shughuli yoyote ambayo huenda ikawa na athari kubwa za kimazingira
bila ya kupewa kibali cha Tathmini ya Kimazingira kinachotolewa kwa mujibu wa Sheria hii”.
Tunachosisitiza hapa kifahamike ni kwamba, Ndg. Amani Ibrahim Makungu, kwa mujibu wa
maelekezo ya kifungu cha Sheria cha hapo juu, alitakiwa kwanza kabla ya kujenga chochote
kupata idhini ama kibali cha mazingira, na kwa kuwa Idara ya Mazingira imekiri na kumpa
taarifa kwamba, Mradi huu ni miongoni mwa shughuli ambazo haziwezi kufanywa bila ya kibali
hicho, hakuwa na sababu nyengine yoyote ya kukiuka sheria hii. Aidha, kwa mujibu wa kifungu
cha 38(3) cha Sheria hii, Iwapo mtu yoyote aliekwenda kinyume na kifungu hiki (Kujenga bila
ya kupata kibali cha Mazingira)32
atakuwa ametenda kosa chini ya kifungu cha 95 cha Sheria hii,
na kifungu cha 95 kinaelekeza kwamba mtu huyo atashtakiwa na akipatikana na hatia
atalazimika kulipa faini kama ilivyoelezwa na Nyongeza ya Nne ya Sheria hiyo au ataadhibiwa
kwa kufungwa miezi isiyopungua sita au adhabu zote mbili, faini na kifungo.
Kwa lugha hii, Idara ya Mazingira ilijiridhisha kwamba, Ndg. Aman Ibrahim Makungu, mmiliki
na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Zanzibar Ocean View Resort Limited, iliyohusika na Ujenzi
wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliyopo Kilimani, amekiuka sheria na wanafahamu hatua za
mtu anaekiuka sheria kwa mujibu wa sheria hiyo ni kumchukulia hatua za kisheria na sio
kumbembeleza kukata kibali.
Tunapenda tena kufahamisha, kwamba, kifungu hicho cha sheria hii tunayoizungumzia, Sheria
Namba 2 ya mwaka 1996, kifungu cha 38(1) kimemtaka mtu huyo (ambapo katika hoja yetu ni
Ndg. Aman) kufanya tathmini ya mazingira ya mradi wake kabla ya kuanza hatua yoyote ya
ujenzi. Kwa kuwa Ndg. Aman hakufanya tathmini hiyo kabla ya ujenzi, kufanya tathmini hiyo
baada ya ujenzi hakungeweza kutumia muongozo wa kifungu hiki cha 38(1) ambacho hata Idara
ya Mazingira wamekitumia walipomuandikia barua ya kumzuia ujenzi na kumtaka afike ofisini
kwa ajili ya kupata muongozo wa kufanya tathmini hiyo ya mazingira.
32
Msisitizo ni wetu.
139
Kwa lugha hii, mtu yoyote mwenye akili timamu (reasonable person) anafahamu kwamba, Idara
ya Mazingira ilitaka kuhalalisha jambo ambalo kisheria tayari limeshakiukwa na kuwa batili.
Unaweza pia kujiuliza suala kama ambalo hata Kamati imeliuliza wakati wa mahojiano na
Watendaji wa Wizara hii inayohusika na Idara ya Mazingira, kwamba huu utaratibu wa Mmiliki
wa Mradi anaetakiwa afanye tathmini ya mazingira kuitisha kikao na kuwalipa wajumbe wa
Mkutano huo, pamoja na kuelezwa katika kifungu cha 42 cha Sheria hii, na kwa kuzingatia
kwamba wanatakiwa wawe wataalamu wenye sifa zilizokubaliwa na kuwekwa na Idara ya
Mazingira kama kifungu cha 43 kinavyoeleza, hautoi mwanya wa kugawana maposho na
kumfanya mmiliki huyo, ambae mara nyingi ni mwekezaji kuweza kufanyiwa kazi yake kwa
wepesi kutokana na namna gani atawawezesha wajumbe wa Kikao hicho.
Bila ya shaka, miongoni mwa jawabu zake ni pamoja na ukweli kwamba, kwa kuzingatia
ukiukwaji wa sheria za mazingira uliofanyika na bado Idara ya Mazingira inapatana kufanywa
kwa Tathmini ya Mazingira wakati sheria imeshavunjwa, na kwa kuwa Mwekezaji huyu ni
mwenye uwezo wa kuitisha Mkutano ambao pamoja na majukumu yake kisheria ungeliweza
kuwasaidia wajumbe wake kupata angalau posho la siku moja, basi ni khofu kwamba Idara ya
Mazingira imefanya hivyo kwa mantiki hiyo.
Hata hivyo, kwa kuwa katika hoja hii ndogo tulikuwa tunaangalia hatua zilizochukuliwa baada
ya ukiukwaji wa mazingira, Kamati imejitosheleza kwamba, hakukuwa na hatua yoyote ya
kisheria iliyochukuliwa dhidi ya Mjenzi wa Hoteli hiyo, isipokuwa ingeliwezekana kupewa
kibali cha mazingira baada ya kutakiwa kufika Idara ya Mazingira na kupewa muongozo wa
tathmini ya Mazingira, ingawaje Kamati haikupatiwa kibali chochote cha Mazingira
kilichotolewa kwa Ndg. Amani Ibrahim Makungu kinachomruhusu kuendelea na Mradi wake, na
kwa kuwa Kamati haikupatiwa taarifa yoyote ya kimaandishi juu ya kibali hicho, imejiridhisha
kwamba, Ndg. Aman Ibrahim Makungu hakupata kibali chochote cha Mazingira.
4.2.5 Nafasi ya Kamisheni ya Utalii katika kuuendeleza Mradi huu:
Katika hoja hii, Kamati haikusudii kusema kwamba, Kamisheni ya Utalii ni mmiliki ama ina hisa
katika Kampuni hii, isipokuwa ni kuangalia vipi Kamisheni hii, pamoja na majukumu mengine,
inayotakiwa kutoa kibali cha kuruhusu biashara na shughuli nyengine za kitalii, imetoa kibali
hicho ama haijatoa katika Mradi wa Zanzibar Ocean View. Katika kulijibu suala hili,
itakumbukwa kwamba, Sheria inayoanzisha Kamisheni ya Utalii, Namba 6 ya mwaka 2009,
imeipa majukumu mengi Kamisheni hii, ikiwa ni pamoja na kutoa leseni, kutoa muongozo na
kusimamia Biashara ya Utalii Zanzibar.
Na kwa hali hii, Ndg. Aman Ibrahim Makungu alitaka kuendesha biashara ya Utalii katika Hoteli
yake ya Zanzibar Ocean View, na hivyo ni wazi kwamba, alilazimika kwanza asajiliwe na apate
kibali cha biashara hiyo kinachotolewa na Kamisheni ya Utalii. Pengine ingelisemwa kwamba,
wakati wa kuanzishwa Mradi huu, Sheria hiyo Namba 6 ya mwaka 2009 ilikuwa bado
140
haijatungwa, lakini ikumbukwe kwamba, kabla ya sheria hii, kulikuwa na Sheria ya Kukuza
Utalii, Namba 9 ya mwaka 1996, ambayo pia ilimtaka Ndg. Aman kukata kibali cha utalii.
Sasa kwa hali hii na tuendelee kulijibu hili suala, je alikata kibali cha Utalii? Kamati ilipomhoji
Ndg. Aman, alieleza kwamba ni kweli alikata kibali ama leseni ya Utalii, na suala hili
halikupingwa mbele ya Watendaji Wakuu wa Kamisheni ya Utalii, waliohudhuria katika kikao
hicho. Kama hii haitoshi, Kamati pia imepatiwa barua ya tarehe 25/09/2009 yenye kumbu
kumbu namba K/UT/2008/11/79/18 inayotoka kwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii,
kwenda kwa Meneja Mkuu wa „Zanzibar Ocean View Resort‟ ikiruhusiwa Kampuni hii
kuanzisha Hoteli hiyo, kwa masharti yaliyoorodheshwa katika barua hiyo (Kielelezo Namba
163). Kwa ufupi, pamoja na ukweli kwamba barua hii tunaweza kueleza mengi yanayohusiana
na utata kama ni ombi la leseni ama kuanzishwa kwa mradi na mambo mengine, Kamati
imejiridhisha kwamba imekusudiwa kujibu ruhusa ya ombi la leseni, iliyoombwa na Kampuni ya
Zanzibar Ocean View Resort ya tarehe 23/06/2008 (Kielelezo Na.164).
Tunapenda kukumbusha tena kwamba, kwa mujibu wa Sheria Namba 2 ya mwaka 1996, kifungu
cha 38(2) kinaeleza kwamba “Hakuna Taasisi yoyote iliyopewa mamlaka ya kutoa leseni,
ikaruhusu, kutoa kibali au aina yoyote ya kibali kwa shughuli yoyote ambayo huenda ikawa na
athari za kimazingira, isipokuwa baada ya kuhakikisha kwamba kibali cha Tathmini ya Athari za
Kimazingira kiwe kimeshatolewa kwa shughuli hiyo” tunakumbushia maelezo haya kwa
mnasaba wa kilichofanywa na Kamisheni ya Utalii, kwamba imetoa kibali ama leseni ya utalii
bila ya kuwa na kibali kutoka Idara ya Mazingira kinachothibitisha kwamba Muwekezaji huyu
amepewa kibali cha Tathmini ya Kimazingira.
Inawezekana sana ukaamini kwamba, Kamisheni imetenda hilo kwa kupatiwa kibali cha
Mazingira kutoka kwa Mmiliki wa Mradi huu, ingawaje ufahamu pia kwamba, wakati wa kazi za
Kamati, pamoja na watendaji hawa wa Kamisheni kuhudhuria wameshindwa kuthibitisha
uhahali wao wa kutoa kibali hicho, na zaidi baada ya yeye mwenyewe Ndg. Aman kusema
kwamba hakukata kibali chochote cha Mazingira. Ama Idara ya Mazingira kuthibitisha kwamba,
Muekezaji huyu hakukata kibali cha mazingira kutoka Idarani kwao.
Kwa vyovyote vile, tulichotaka kifahamike hapa ni kwamba, Kamisheni ya Utalii imetoa kibali
cha biashara ya Utalii, mwaka 2009, bila ya taratibu zozote za kisheria. Aidha, ndani ya mwaka
huo huo wa 2009, Sheria ya Kukuza Utalii, Namba 9 ya mwaka 1996 ilifutwa na kutungwa
Sheria mpya ya Utalii, Namba 6 ya mwaka 2009, ambapo chini ya kifungu cha 15(2) na 17
vinazungumzia kufanya upya leseni hiyo (renew), kwamba inakusudiwa kwa kila mwaka, ni
lazima Mwekezaji yoyote aliyekata leseni awali, aifanyie mapitio mapya (renewal) ili iendane na
matakwa ya Sheria, pia kuiingiza mapato kwa Serikali. Pamoja na haja hii, Mwekezaji huyu,
Ndg. Aman Ibrahim Makungu hakukata „renewal‟ ya Leseni yake aliyoikata tokea 2009, yaani
Kamati haikupatiwa ushahidi mwengine wa kuonesha namna gani alifanya „renewal‟ ya leseni
yake na wala haikuipatia Kamati leseni husika zaidi ya barua tuliyokwishaieleza hapo awali. Ila
141
pia ifahamike kwamba, Kamati ilisisitiza kupatiwa taarifa zote (Documents) zinazohusika na
Mradi huu, ikiwa ni pamoja na leseni na mapitio yake ya kila mwaka (renewal).
Jambo hili pia bila ya shaka linafahamika na Kamisheni ya Utalii, Uongozi wa Kamisheni hii
ulikuwepo wakati wa vikao vyote vilivyofanywa na Kamati katika kufuatilia hoja hii, na hakuna
uthibitisho walioutoa wao wakati walipotakiwa kufanya hivyo. Hivyo, kwa mazingira yote haya,
Kamati inajiridhisha kwamba, Mwekezaji huyu hakuwa akipata leseni ya Utalii kama
inavyoelekezwa na Sheria.
4.2.6 Ujenzi wa Mikahawa miwili ya Hoteli hiyo na Athari zake Kimazingira:
Kama tulivyokwisha eleza awali, kwamba masuala mawili ya msingi iliyotumwa Kamati
kuyaangalia ni uvamizi wa fukwe na uharibifu wa mazingira. Na tulipokuwa tunatoa ufafanuzi
wa uvamizi wa fukwe, pamoja na Ndg. Aman Ibrahim Makungu kueleza kwamba ardhi hiyo
aliyoitumia kujengea Mradi wake wa Hoteli ni mali yake, kwa kununua na sehemu iliyobaki
kupewa na Serikali, bado Kamati inasimamia hoja yake kwamba, amefanya uvamizi wa fukwe
iliyotumika kujenga sehemu ya Hoteli zake, na msisitizo ukiwekwa katika Ujenzi wa Mikahawa
yake miwili (Two Restauarants). Pengine ni busara sana tukathibitisha maelezo haya kwa
mnasaba wa Mamlaka Dhamana ya Mazingira kuhusiana na ujenzi wa Mikahawa hii.
Miaka miwili baada ya kujengwa kwa Hoteli hiyo, yaani mnamo tarehe 15/09/2010, Idara ya
Mazingira ilifanya tena ukaguzi wake na kugundua kwamba Ndg. Aman anaendelea na ujenzi
wa Mikahawa yake hiyo ndani ya mita 30 za bahari suala ambalo linakwenda kinyume na
muongozo wa sheria na kwa kupitia barua ya tarehe 16/09/2010, yenye kumbu kumbu namba
IM/29/2/8 VOL.XIII, Idara hii ya Mazingira ilimpa Zuio la Ujenzi (Stop Order) (Kielelezo
Na.165), kwa kutumia Sheria Namba 2 ya mwaka 1996.
Kwa dharau aliyoionesha na kujiamini kwake, Ndg. Aman Ibrahim Makungu aliendelea na
ujenzi na kuanza kutoa huduma katika mkahawa huo kama alivyokusudia. Na wiki moja baadae,
Idara ya Mazingira ilitoa tena agizo la kuvunja Mkahawa alioujenge ndani ya fukwe, ya tarehe
27/09/2010 yenye kumbu kumbu namba IM/29/2/8 VOL.XIII (Kielelezo Na.166) ikimtaka Ndg.
Aman arejee barua ya Idara ya Mazingira iliyompa agizo la kuzuia ujenzi huo. Vile vile katika
agizo hili la kuvunjwa kwa Mkahawa huo, Idara ililitoa ndani ya siku 3 kumtaka Ndg. Aman awe
ameshakamilisha kuvunja Mkahawa huo, na akishidwa kutekeleza amri hiyo, Idara itachukua
hatua za kunusuru uharibifu wa mazingira uliofanywa ikiwa ni pamoja na kuvunja Mkahawa
huo.
Pamoja na ufafanuzi wao fasaha, Mmiliki huyu wa Hoteli hakuvunja Mkahawa wake, ambao
bado upo mpaka leo na unatoa huduma kama kawaida, na Idara ya Mazingira haikuweza
kumchukulia hatua za kisheria, si kuvunja wala hatua yoyote ya kunusuru uharibifu wa
mazingira, pamoja na nguvu hizo kupewa kisheria. Takriban miezi 9 baadae, katika wakati
ambao sasa Idara hii ya Mazingira imekuwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais,
mnamo tarehe 30/06/2011, ilimuandikia tena Meneja Mkuu wa „Zanzibar Ocean View Hotel‟
142
barua yenye kumbu kumbu namba IM/29/2/8 Vol. XV/10 (Kiamtanisho Namba 167),
ikimweleza kwamba kitendo chake cha kujenga Mkahawa wake huo ni uvamizi ulio batili na ni
sawa na ufukiaji wa fukwe kinyume na sheria. Barua hii nayo iliendelea kusisitiza kwamba,
kitendo alichokifanya mmilki huyu wa hoteli, cha kujenga Mkahawa ndani ya fukwe,
hakivumiliki na kumtaka abomoe, ila kwa kuwa hakutekeleza agizo hilo, wao wako tayari
kumchukulia hatua za kisheria.
Pamoja na juhudi za barua hii, hakuna utekelezaji wowote wa hatua za kisheria zilizochukuliwa
dhidi ya Mmiliki wa Hoteli hiyo, hali ambayo kwa namna moja ama nyengine inaleta tafsiri
nyingi, ikiwa ni pamoja na Idara hii kumuogopa Mmiliki huyu, na labda kwa sababu ya mwega
alioegemea kwa vigogo mbali mbali wa Serikali. Hali ambayo Hata Kamati imehitaji kupata
uhakika wake na katika ripoti hii, tunaeleza kwa ufasaha juu ya sababu za kuidharau Idara ya
Serikali.
4.3 UJENZI WA HOTELI YA MISALI SUNSET BEACH, ILIYOPO WESHA
PEMBA
Sehemu ya tatu ni hii inayohusu Ujenzi wa Hoteli ya Misali Sunset Beach iliyopo Wesha,
Pemba. Katika kufuatilia Hadidu hii rejea, Kamati ilikutana na Makatibu Wakuu wa Wizara ya
Habari, Utamadunu, Utalii na Michezo; Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati; Ofisi ya
Makamo wa Kwanza wa Rais; na Mkurugenzi Mtendaji – Mamlaka ya Vitega Uchumi,
Zanzibar. Pia kukutana na Mwekezaji (Mmiliki ) wa Hoteli ya Pemba Misali Sunset Beach;
kukutana na baadhi ya wakaazi wa eneo la Hoteli ambao ambao kwa namna moja au nyengine
wanaathirika na Ujenzi wa Hoteli hii; na kutembelea eneo la Hoteli na kuona athari za
kimazingira zinazolalamikiwa. Kamati ilifanya shughuli hizi siku za tarehe 31/10/2011 na tarehe
01/11/2011.
Katika kufuatilia hadidu hii ndogo, ni vyema tukapata ufafanuzi ufuatao:
4.3.1 Taarifa ya Idara ya Mazingira Juu ya Mradi wa Hoteli ya Pemba Misali Sunset
Beach
Baada ya kukutana na Viongozi husika, Kamati ilihitaji kupatia taarifa ya uharibifu wa mazingira
uliochangiwa na ujenzi wa hoteli hii, suala ambalo lilikuwa fanisi kujibiwa na Idara ya
Mazingira kwa sababu wao ndio wanaohusika. Kwa mnasaba huu, baada ya Mwenyekiti wa
Kamati kuelezea azma ya Kamati juu ya kikao hicho, alitoa nafasi kwa Ndg. Omar D.Shajak,
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na msimamizi wa Idara ya Mazingira, ili
atoe taarifa mbele ya Kamati kuhusiana na Mradi huo, nae alieleza kwamba Mradi wa Pemba
Misali Sunset Beach Hotel ambao upo katika Shehia ya Wesha, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa
wa Kusini, Pemba, unatoa huduma ya kulala wageni pamoja na huduma za uzamiaji (Scuba
Diving). Kwa ajili ya utoaji wa huduma hizo, Mradi unamiliki nyumba za wageni na boti ya fiber
iendayo kwa kasi inayotumika kupeleka wageni maeneo ya kuzamia.
143
Taarifa hiyo ya mazingira imeonyesha kuwa mnamo mwaka 2010 Idara ya Mazingira ilipokea
barua kutoka ZIPA yenye kumbu kumbu ZIPA/TH/2010/M.10/2 ya tarehe 19/01/2010 ambayo
ilitumika kuwasilisha uchambuzi yakinifu (feasibility study) ya Mradi wa “MISALI DIVERS
CO. LTD” kwa maoni na ushauri wa Idara ya Mazingira. Barua hiyo ilitumwa pia kwa taasisi
nyengine husika. Tathmini ya Idara ya Mazingira ilionyesha kuwa Mradi huo unahitaji
kufanyiwa Tathmini ya Athari ya Mazingira (Environmental Impact Assessment – EIA), pamoja
na kupata maoni ya Idara ya Uvuvi na Mazao ya Baharini. Maoni hayo ya Idara ya Mazingira
yalipelekwa ZIPA kwa barua namba IM/29/2/8 VOL. XI/123 ya tarehe 26/01/2010 (Kielelezo
Namba 168) Baada ya hapo, Idara ya Mazingira haikupata taarifa nyengine yoyote.
Mnamo mwezi wa Mei 2011, Idara ya Mazingira ilifanya ukaguzi kwenye eneo hilo na
kugundua kuwa Muwekezaji wa Mradi huo alikuwa ameshaanza kujenga majengo ya hoteli
katika eneo hilo. Kutokana na hali hiyo, mnamo tarehe 28/05/2010, Idara ya Mazingira ilitoa
amri ya kusimamisha ujenzi huo kwa barua rasmi yenye namba IM/29/2/8/ VOL. XII/
iliyotumwa kwa “Managing Director, Pemba Misali Divers Company Ltd, Wesha, Pemba”.
Barua hiyo pia ilimtaka mwekezaji kufata taratibu ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini za athari
za mazingira. Amri ambayo haikutekelezwa (Kielelezo Na.169).
Imeelezwa pia kuwa hakuna hatua nyengine yoyote ambayo Idara ya Mazingira ilichukua dhidi
ya mwekezaji huyu kwa sababu, ingawa Sheria ya Mazingira imeweka baadhi ya makosa na
adhabu zake kwenye Jadueli namba VI (Schedule VI), katika adhabu zilizoonyehwa kwenye
Jadueli hiyo hamna adhabu kwa kosa la kutotii amri ya Mkurungezi wa Mazingira iliyotolewa
chini ya Sheria ya Mazingira ya 1996. Hii limeonekana ni tatizo kubwa katika juhudi za Idara ya
mazingira ya kusimamia utekelezaji wa amri zake. Kwa sasa utatuzi wa tatizo hili utategemea
uamuzi wa Mheshimiwa Waziri husika wa kutunga kanuni ili kuokoa pengo liliopo. Maamrisho
ya kanuni yanayohitajika, ni kufanya kuwa ni kosa ndani ya kanuni kwa yeyote ambae atavunja
amri halali ya Mkurugenzi wa Mazingira chini ya sheria hii. Pia adhabu haikuainishwa kwa ajili
ya mkosaji wa kosa hilo.
Wakati taarifa ya Idara ya Mazingiza juu ya mambo haya inawasilishwa mbele ya Kamati Teule
ya Baraza, ilielezwa kuwa, pamoja na juhudi zote hizi za Idara ya Mazingira, hakuna tathmini ya
mazingira wala mpango wa kukabiliana na umwagikaji wa mafuta ambao mwekezaji amefanya
kwa ajili ya Hoteli hiyo ambayo tayari sasa inatoa huduma. Aidha, kwa maelezo yaliyotolewa na
Idara ya Mazingira kwa Kamati Teule, taarifa juu ya mambo hayo ilipaswa kuwasilishwa kwa
Idara yenyewe na kujadiliwa na wadau mbali mbali kabla Muwekezaji kukubaliwa na baadae
kutolewa cheti cha Kimazingira.
Kamati Teule ilijulishwa pia, miongoni mwa juhudi nyengine ambazo Idara ya Mazingira iliwahi
kuchukua kuhusiana na Mradi wa Hoteli ya Misali ni kufanya ukaguzi wa kawaida wa Mazingira
kwenye Hoteli hiyo. Kufuatia ukaguzi uliofanywa kwenye Hoteli hiyo na kugundua kuwa
Mmiliki wa Hoteli hiyo amepuuza miongozo yote ya kimazingiza aliyopewa na Idara ya
144
Mazingira, Idara ya Mazingira ilitoa „Stop Order‟ ili kuzuia ujenzi wowote uliokuwa unafanywa
kwenye eneo hilo (Kielelezo Na.170).
Amri hiyo ya kuzuia ujenzi ilimtaka pia Mmiliki wa Hoteli hii kuchukua hatua maalum ya
kuifanyia ardhi hiyo tahmini ya athari ya mazingira na kufuata taratibu zote zilizoelekezwa
kwenye Sheria ya Mazingira ya 1996 (ikiwa ni pamoja na kufanya „environmental assesment‟)
kabla ya ujenzi huo kuanza kushughulikiwa rasmi. Hata hivyo, hatua na amri zote hizo
zilizotolewa na Idara ya Mazingira zilipuuzwa. Mmiliki wa Hoteli hiyo akaendelea na ujenzi
kama vile hakuna chochote kilichotokea mpaka kufikia ujenzi wa nyumba kadhaa za Hoteli hiyo
kukamilika na Hoteli kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa.
Kuna haja ya kujiuliza, kwa nini amri hii halali iliyotolewa na Mamlaka halali kisheria ipuuzwe
na badala yake, Mwekezaji kuwa na jeuri ya kutotii Mamlaka husika. katika kupata jawabu ya
suala hili, Kamati ilijulishwa kuwa moja ya mambo yaliyosababisha amri hiyo ya Idara ya
Mazingira kupuuzwa ni kutokuwepo na maamrisho ya kisheria yanayoweka hatua ya
kuchukuliwa mtu anaekiuka amri ya Idara ya Mazingira. Ingawa kwenye Sheria ya Mazingira
(Nam.2 ya 1996) yapo makosa pamoja na adhabu zake yaliyoainishwa kwenye Jadueli Nam.4,
lakini mwa makosa hayo hakuna kosa la kukataa kutii amri halali inayotolewa na Idara ya
Mazingira kwa mujibu wa sheria hiyo.
Lakini pia tukumbuke kuwa, hapo kabla ya ujenzi wa hoteli hiyo, sehemu husika ilikuwa na miti
kadhaa ikiwa ni pamoja na Mikoko na miti mengine. Katika hali kama hii, kuna haja ya kupata
ufafanuzi angalau mdogo wa namna gani Idara ya Kilimo kama imewahi angalau kufanya
tathmini ya athari zinazopatikana juu ya miti hiyo iliyokatwa kupisha ujenzi wa hoteli husika.
Akijibu hoja za Kamati, Mkurugenzi wa Mazingira alieleza kuwa hana hakika kuwa Idara ya
kilimo iliwahi kufanya tathmini ya athari zilizopatikana juu ya miti na miradi mengine ya
wananchi iliyoathirika kutokana na ujenzi wa hoteli hiyo. Hata hivyo alieleza kuwa tathmini hiyo
ilipaswa ifanywe kabla ya kuanza kuimarishwa kwa mradi huo.
Baada ya kushindwa kusimamia Sheria zinazowaongoza, lakini katika mioyoyao wakiumwa na
uharibifu wa mazingira uliofanywa na ujenzi wa hoteli hiyo, Idara ya Mazingira ikaona ni vyema
pia kuitumia ziara ya Mheshimiwa Makamo wa Kwanza wa Rais iliyofanyika katika eneo la
mradi tarehe 19/06/2011, na Kamati nayo inaona ni vyema tukapata maelezo ya mnasaba wa
hoja hii na ziara hiyo.
4.3.2 Taarifa Iliyotolewa na Idara ya Mazingira Juu ya Ziara ya Mhe. Makamo wa
Kwanza wa Rais Kwenye Hoteli ya Pemba Misali:
Taarifa imeeleza kuwa Mheshimiwa Makamo wa Kwanza wa Rais alichukua juhudi ya
kuzungumza na wadau mbali mbali kuhusiana na mambo kadhaa ikiwemo changamoto za
kimazingira zilizopo kwenye eneo hilo ambalo limeambatana na eneo Bandari ya Wesha.
Changamoto kubwa zilizoelezwa ni pamoja na ujenzi wa hoteli ya Misali uliofanywa bila ya
kuzingatia sheria ya mazingira ya 1996, na eneo hilo kukosa mpango wa kukabiliana na
145
umwagikaji wa mafuta (oil contingency plan). Kufuatia hali hii, Mhe. Makamu wa Kwanza wa
Rais, alitoa maagizo yafuatayo kwa Hoteli ya Misali:
i. Kufanya ukaguzi wa mazingira (environmental audit);
ii. Kufanya mpango wa kukabiliana na umwagikaji wa mafuta wa eneo la Wesha (oil
contingency plan); na
iii. Kulipia Gharama zote zinazostahiki kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo hayo.
Kwanza ifahamike wazi wkamba, pamoja na Idara ya Mazingira kueleza kwamba Sheria yao
haiwapi mamlaka makubwa kwa waharibifu wa mazingira, tunapenda tufahamishe kwamba, hata
hayo maazigo ya Mhe. Makamo wa Kwanza wa Rais yemezingatia matakwa ya Sheria, No.2 ya
mwaka 1996. Hapa tunazidi kueleza kwamba, maelezo ya Idara ya Mazingira pamoja na ukweli
wake, hayangestahiki kutolewa na kuelezwa kama hoja ya msingi ya kutomchukulia hatua
mwananchi anaekiuka taratibu za kimazingira. Basi ni vyema tuone, vipi maagizo hayo ya
Makamu wa Kwanza wa Rais yameweza kutekelezwa.
4.3.3 Ufuatiliaji wa Maagizo ya Mheshimiwa Makamo wa Kwanza wa Rais:
Katika kufatilia utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Makamo wa Kwanza wa Rais, Idara ya
Mazingira ilimuandikia mmiliki wa Hoteli ya Misali barua yenye kumbu kumbu
IM/29/2/8/VOL.XV/30 ya tarehe 22/07/2011 kumpa taarifa kamili ya maagizo ya Mheshimiwa
Makamo wa Kwanza wa Rais (Kielelezo Na.171).
Baada ya taarifa hiyo, Idara ya Mazingira ilituma wataalamu kufanya tathmini ya kuangalia upeo
(scoping) ambayo ilihitajika kwa ajili ya kutayarisha mwongozo wa ukaguzi wa mazingira, na
mpango wa kukabiliana na umwagikaji wa mafuta. Hadidu za rejea kwa ajili ya tathmini ilikuwa
ni pamoja na:
a) Kuangalia endapo mradi huo umekidhi matakwa yote ya sheria kitaifa na kimataifa;
b) Kuangalia matatizo yanayoweza kusababisha athari za mazingira kutokana mradi
wenyewe na ambayo pia yanaweza kuiathiri ardhi inayotumika kwa ajili ya mradi huo;
c) Kupima kikamilifu athari za mazingira katika sehemu zote za mradi – ardhini, baharini,
masuala ya afya, masuala ya kiusalama, n.k;
d) Kuchunguza mwenendo wa hoteli yenyewe kuhusuana uimarishaji wa mazingira kwa
kutumia taratibu, desturi na njia zinazokubalika kitalamu;
e) Kuangalia utaratibu ulioandaliwa na hoteli yenyewe, kama upo, katika kutunza
mazingira;
146
f) Kutoa mwongozo au maelekezo ya kufatwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira kwa siku
za baadae;
g) Kubuni mpango maalum utakaotumiwa na hoteli yenyewe kwa ajili ya utunzaji wa
mazingira; na kuwasiliana na wadau wengine wa mazingira katika kukuza hadhi ya hoteli
yenyewe.
Kwa kutumia hadidu hizi za rejea, kazi ya tathmini ya mazingira ilianza siku ya 14 August 2011
na kukamilika siku ya tarehe 17 August 2011. Kwa ajili ya kiutendaji ya tathmini hiyo, hadidu za
rejea zilizoelezwa hapo juu zilichambuliwa katika mambo au vipengele kadhaa yanayoorodhesha
hapa chini33
.
4.3.4 Mambo Ambayo Kamati ya Tathmini ya Mazingira Iliyafanyia Kazi
Mambo ambayo Kamati ya tathmini ya mazingira iliyafanyia kazi kutokana na hadidu za rejea
zilizo ainishwa hapa juu ni kama ifuatavyo:-
Kwa nini ujenzi wa hoteli hiyo uliweza kufanywa bila ya kuwepo tathmini ya mazingira
kabla ya ujenzi wenyewe kuanza kufanyika, jambo ambalo ni kinyume na sheria?
Jee ardhi ambayo majengo ya hoteli hiyo sasa yameshajengwa, ilipatikanwa kwa taratibu
ziliopo kisheria na kufanyiwa upembuzi yakinifu?
Ni nani waliokuwa wanaitumia ardhi hiyo ya kujengwa kwa hoteli hiyo; na jee
walifidiwa ipasavyo;
Jee kuna uharibifu wowote wa mazingira uliosababishwa na kuwepo kwa hoteli hiyo?
Jee kuna jitihada zo zote ambazo hoteli hii ilizichukua angalau kupunguza athari za
mazingira?
Jee kuna malalamiko yoyote ya msingi kuhusiana na „uvamizi‟ uliofanya na hoteli
kwenye ardhi iliyohusika?
Ni malalamiko gani ambayo wadhamini wa „Wesha Fuel Depot‟ wanayo dhidi ya Hoteli;
na Jee malalamiko hayo ni ya msingi?
Jee kuna athari zo zote za kimazingira kutokana na Jetty mbili zilizojengwa kwenye
hoteli hiyo?
33
Angalia ukurasa wa 14 1na 15 wa taarifa juu ya tathmini ya mazingira ya Hoteli hii iliyotolewa na Idara ya
Mazingira, Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, Zanzibar mnamo September 2011.
147
Jee kuna hatua zo zote za kimazingira zilizochukuwa na wamiliki wa Hoteli kuhusiana na
„waste management‟, „biodiversity conservation‟, „sewage disposal‟, „occupational
safety‟, na „enviromental management system‟?
Jee watu wa Wesha wameridhika na mradi wa Hoteli hiyo? Kama hawaridhiki na Mradi
huo ni kitu gani wanachohitaji au kutarajia?
Haya ndio mambo ambayo Kamati au Timu ya kufanya tathmini ya kimazingira iliyazingatia
katika hatua zake za kukukutana na wadau kuhusiana na kadhia hii.
Mnamo tarehe 22 Julai 2011, Idara ya Mazingira ilituma taarifa rasmi kwa Muwekezaji juu ya
azma ya Idara hiyo ya kuifanyia tathmini ya mazingira Hoteli ya Pemba Misali Sunset Resort
Co. Ltd. Barua ya taarifa hiyo imepokelewa na Kamati kama (Kielelezo Na.172) na mnamo
mwezi wa Septemba 2011, tathmini hiyo ilifanywa na maswala muhimu ya kimazingira
kugunduliwa, kama inavyoonekana hapa chini.
4.3.5 Mambo Yaliyongunduliwa Kutokana na Tathmini Iliyofanywa ya Kimazingira:
Kwa mujibu wa taarifa ya maandishi ya tathmini ya mazingira ambayo nakla yake ilipokelewa
na Kamati kama (Kielelezo Na.173), maelezo ya mambo yaliyogunduliwa katika tathmini
yenyewe yameelezewa kwenye ukurasa wa 18. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, timu iliyofanya
tathmini hiyo ya mazingira imesita kusema moja kwa moja juu ya athari nzuri (positive impacts)
na athari mbaya (negative impacts) zinazojitokeza kwenye mradi huo wa hoteli. Sababu ya kusita
huko imeelezwa kuwa ni kutokana na haja kubwa ambayo bado ipo ya kuifanyia ukaguzi
kamilifu Hoteli hiyo „complete external auditing‟ ambayo hadi wakati Kamati inapokea maelezo
haya bado ilikuwa haijafanyika.
Kamati ilielezwa kuwa tathmini hiyo hatimae ilifanywa na wataalamu ya Idara ya Mazingira ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa ufupi sana, mambo ambayo taarifa hiyo ya tathmini ya
mazingira imeonyesha kuwa yamegunduliwa ni kama ifuatavyo:-
Tayari Hoteli imeonekana kuanza kufanyia kazi matatizo ya kimakaazi (occupational
risks) ambayo yalilalamikiwa na „Depot‟ ya Mafuta ya Wesha inayomilikiwa na Gapco;
kwamba tayari ameanza kuondoa paa la makuti kwenye Jetty iliopo karibu na „Depot‟
kama ilivyodaiwa na Gapco;
Katika maoni ya watu ya Shehia ziliopo, ni Shehia moja tu ya Kilindi ndio imeonyesha
kutoridhika kwa kiasi Fulani na uwepo wa Hoteli ya Pemba Misali Beach Resort. Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, wananchi wa Shehia ya Kilindi walitoa masharti mawili ili
waridhike kuwepo kwa Hoteli hiyo hapo Wesha. Kwanza ni Hoteli kutowaruhusu
wageni wake kukoga kwenye Diko Kuu la Kilindi kutokana na mahitaji ya wananchi
kwenye eneo hilo, badala yake watumie ng‟ambu ya pili ya Diko hilo. Pili, Muwekezaji
148
atimize ahadi yake ya kuweka boti ya mashine ya kusafiria kati ya Kilindi na Wesha ili
kuwasaidia wananchi wa hapo kupata usafiri wa uhakika.
Hata hivyo, wakaazi wa Shehia mbili zilizobaki (za Ndagoni na Tibirinzi)
wameonyesha kuridhika kabisa na kuwepo na mradi huu wa Hoteli hii ya Pemba Misali
Beach Resort.
Hali halisi ya mikoko pahali ilipo Hoteli ni kuwa ina afya nzuri, na hivyo hivyo
inategemewa itakuwa sahihi kwa viumbe wanaoendesha maisha kwenye mikoko.
Taarifa hiyo imeonyesha pia kuwa watu wanaopita kwenye maoneo ya „Beach‟ ya Hoteli
hiyo (ambao wengi wao ni wanawake na watoto wanaotafuta chaza na kaa) wanafanya
shughuli zao kwa uhuru mkubwa na bila ya kukerwa na mtu yeyote. Pia wataaalamu
waliofanya tathmini hii ya mazingira wameeleza kushuhudia kwao wavuvi na watu
wengine kadhaa wanaosafiri kati ya bandari ya Chake Chake, bandari ya Wesha, na
watu wengine wanafanya shughuli zao baharini, wakifanya shughuli zao za kawaida
baharini bila ya kuwepo kwa kero yoyote.
Mbali na mambo yaliyoelezwa katika taarifa ya mazingira (kama inavyoonekana kwenye nukta
hizi hapa juu), tathmini hii iliyofanywa na wataalamu wa Idara ya Mazingira imeonyesha kuwa
Mradi huu wa Hoteli umepokelewa vizuri sana na washikadau kadhaa wa shughuli zao ambao
walihojiwa na wataalamu wa mazingira. Hata hivyo, taarifa hiyo ya mazingira imeonyesha pia
kuwa bado kuna mambo yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka sana. Baadhi ya mambo
yanayohitajika yapo nje ya uwezo wa Hoteli kuyatekeleza (ambayo kwenye taarifa ya maandishi
hayakutajwa). Hata hivyo taarifa imependekeza kuwa wamiliki wa Hoteli, wafanye „external
environmental audit‟ ili waweze kujua hali halisi ya „enviromental and socio-economic
performance‟ ya Hoteli yenyewe.
Ili tathmini hii iweze kufanyika, imeelezwa kuwa, ni lazima hadidu za rejea zifanywe kitaalumu
kwa ajili ya kufanyiwa kazi katika ufanyaji wa tathmini yenyewe; na ni matokeo ya tathmini
hiyo ambayo yaliiwezesha Idara ya Mazingira kufanya maamuzi ya kutoa au kutokutoa kibali
rasmi cha mazingira (environmental clearance). Pia kwa ajili ya kuiwezesha Idara ya Mazingira
kutoa mapendekezo juu ya hatua za kimazingira zinazofaa kufanyiwa kazi na Muwekezaji
husika.
Katika taarifa ya Idara ya Mazingira iliyokabidhiwa kwa Kamati, pia imeonyeshwa hadidu za
rejea ambazo Idara ya Mazingira imezifanya kwa ajili ya „external environmental audit‟ ambayo
bado inapaswa kufanywa na Wawekezaji wenyewe. Kamati ilielezewa pia kuwa katika taarifa
hiyo aina ya wataalamu wanaohitajika wameelezewa pamoja na mahitaji mengine kwa ajili ya
kukamilisha tathmini hiyo.
4.3.6 Taarifa ya ZIPA Juu ya Mradi wa Hoteli Pemba Misali Divers Co. Ltd
149
Baada ya kufahamu namna gani Idara ya Mazingira imehusika katika Mradi huo, ni vyema sasa
tukapata taarifa za Mamlaka ya Uekezaji na Vitega Uchumi (ZIPA) ili na wao tufahamu kwa
kiasi gani wameruhusu kujengwa kwa hoteli ama Mradi huu wakati ni wazi kwamba wamekiuka
taratibu za Kimazingira. Ili kupata ufafanuzi mzuri, Kamati iliwataka watendaji wakuu wa ZIPA
kutoa taarifa yao. Na hivyo basi, taarifa iliyotolewa kwa Kamati na Mkurugenzi Mkaazi wa
ZIPA ilieleza kuwa kuna wakati walipokea maombi ya Pemba Misali Divers Co. Ltd. Kwa
mujibu wa maombi yaliyofanywa ZIPA, wamiliki wa mradi huo walikuwa ni Wakanada wawili,
Bw. Alnoor Jinaa na Bibi Shahida Jinaa. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waombaji
waliambatanisha na maelezo ya mradi ambao walikuwa wanakuja kuwekeza, ambao haukuwa ni
hoteli. Kimsingi ZIPA ilikubaliana na maelezo ya mradi huo, na ikaiandikia Idara ya Mazingira
kuwapelekea maelezo ya mradi wenyewe ili waweze kuufanyia tathmini ya kimazingiza. Mradi
ulioombwa ulielezwa kuwa unaombwa ufanywe kwenye maeneo ya Wesha, lakini katika hatua
hiyo ilikuwa bado wawekezaji hao wanatafuta mahali halisi katika eneo la Wesha pa kufanyia
mradi huo. Kwa bahati, wawekezaji hao hawakurudi tena ZIPA kwa hatua nyengine yoyote ya
kuendeleza azma yao.
Kwa mradi huu wa sasa (yaani Hoteli ya Pemba Misali Divers Company Ltd), ZIPA haina taarifa
nao yoyote. Mradi huo haukuwahi kupitia ZIPA na kama ungepitia ZIPA, kwa vyovyote vile,
usingekubalika kwa vigezo vya uwekezaji wa hoteli mahali ilipo hoteli hiyo. Hata hivyo,
Mkurugenzi Mkaazi wa ZIPA alionyesha kuwepo kwa uwezekano wa miradi midogo midogo ya
uwekeazaji katika mambo yahusuyo utalii kuidhinishwa na Idara ya Utalii, ingawa hapakutolewa
ufafanuzi wa wazi juu ya kukubalika kwa mradi wa hoteli kama hii kuwa ni mradi mdogo wa
kitalii.
Alieleza pia kuwa taarifa rasmi ya ZIPA juu ya kutokubalika kwa mradi huu uliopo sasa ipo, na
alizieleza miongoni mwa sababu za kutokubalika kwa mradi huo mahali hapo ni kuwa, pamoja
na athari kubwa za kimazingira, usalama wa hoteli hiyo uko mashakani kutokana kuwepo na
depot katika maeneo ya karibu sana na hoteli hiyo; na kwamba mafuta yanayomwagika
yanaweza kusababisha maafa kwa hoteli hiyo. Mbali na yote hayo, eneo hilo halihusiki
kuekezwa kwa sababu ni eneo ambalo Serikali imeliwacha wazi makusudu (reserved area) kwa
ajili ya shughuli za kiSerikali za utafiti au uvumbuzi wa mafuta. Vile vile eneo lenyewe ni finyu
kwa mradi mkubwa kama huu uliopo sasa. Kwa vyovyote vile, kwa vigezo vya ZIPA mradi huu
haukubaliki kuwepo pale, na ZIPA imeainisha maelezo yote hayo katika taarifa yake rasmi
iliyoipeleka Serikalini kuhusiana na mradi huu.
4.3.7 Taarifa ya Kamisheni ya Utalii
Katika kikao chake hicho hicho cha tarehe 31/10/2011, Kamati ilipokea pia taarifa kutoka kwa
Kamisheni ya Utalii kuhusiana na Mradi wa Pemba Misali Diver. Taarifa ya Kamisheni ya Utalii
ilikuwa ni muhimu sana kwa Kamati ili kuweza kutathmini namna ambavyo Mradi huu, ambao
tayari ulionekana haukubaliki kabisa kabisa katika mtazamo ya ZIPA, ulikubalika katika
mtazamo wa Kamisheni ya Utalii.
150
Taarifa ya Kamisheni ya Utalii (Pemba) kwa Kamati Teule ilielezea kuwa‟ mnamo April 2010,
Kamisheni ilipokea ombi la Kampuni ya Pemba Misali Divers Ltd la kuwekeza kwenye eneo
hilo la Wesha. Pamoja na barua ya maombi, Kamisheni ya Utalii (Pemba) ilipokea pia
viambatanisho ambavyo vifuatavyo:-
i. Land Lease (yaani Hati ya Ukodishwaji Ardhi) iliyotolewa na Wizara ya Maji, Ujenzi,
Nishati na Ardhi kwa Kampuni ya Pemba Misali Divers Co. Ltd, mnamo tarehe
10/02/2010. Nakla ya Mkataba huo wa Ukodishaji ambayo ilipokelewa na Kamati
Teule imeambatanishwa (Kielelezo Na.174) cha taarifa hii. Mkataba huo unaonesha
kuwa eneo lililokodishwa lipo Ndagoni katika Mkoa wa Kusini, Pemba. Ni muhimu
pia ifahamike kuwa, Mkataba wenyewe wa ukodishwaji umeweka wazi kwenye
kijifungu cha „iv‟ kuwa, Mkodishwaji haruhusiwi kujenga mpaka awasilishe – a)
„Site Layout Plan, b) Topographical Map, c) Water supply network diagram, c) Plans,
sections and elevations of all all proposed structures‟ (zenye viwango maalum
vilivyoainishwa, n.k. Kati ya masharti yote haya hakuna lolote lililotekelezwa,
Kamati ilijulishwa.
ii. Feasibility Study (yaani, maelezo yakinifu kuhusiana na Mradi wenyewe) iliyotayarishwa
na Muwekezaji mwenyewe juu ya Mradi anaoomba. Hata hivyo, kinyume na
ilivyoelezwa kwenye taarifa ya Kamisheni ya Utalii kwa Kamati, Maelezo yakinifu
ambayo nakala yake imepokelewa na Kamati na Kufanywa Kielelezo Na.174 cha
taarifa hii hayahusiani na eneo la wesha; na kwamba yanahusiana na eneo (Project
location) la Vitongoji, Chake Chake, Pemba. Hapa inaonekana wazi kuwa hata
Wawekezaji na Watendaji wenyewe hawakuelewana katika jambo hili la msingi
kabisa.
iii. „Memorandum na Articles of Association‟. Haya ni maandiko (documents)
yanayoyoonyesha mambo yanayoelezea kuhusu Kampuni yenyewe inayowekeza.
Nakla za „Memorandum na Articles of Association‟ hizo zimepokelewa na Kamati
na kufanywa Kielelezo Na.175 cha Taarifa hii. „Memorandum na Articles‟ hizi
zinaonyesha kuwa wamiliki wa Kampuni hii ni (wanne ambao ni)
Ndg. Amani Ibrahim Makungu (40%);
Ndg. Ghania Khalfan Muhamed (25%);
Ndg. Asha Omar Ali (25%); na
Mhe. Machano Othman Said (10%).
Baada ya Kamisheni ya Utalii (Pemba) kupokea ombi la Muwekezaji lililoambatanishwa na
viambatanisho vilivyoainishwa hapa juu, ilipanga kufanya ukaguzi kwenye eneo liilikusudiwa
kujengwa Hoteli hiyo (kwa wakati huo) hapo Wesha (na sio Ndagoni kama ilivyoelezwa kwa
151
Mkataba wa Ukodishaji (Lease), wala Vitongoji palipoelezwa kwenye maalezo yakinifu ya
Mradi wenyewe).
Ukaguzi ulifanywa kwa kuwashirikisha wadau kutoka taasisi nyengine za Serikali ambazo ni
Idara ya Mazingira; Idara ya Upimaji na Mipango ya Miji; Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake
Chake; na Sheha wa Shehia ya wesha. Katika ukaguzi huo alikuwepo Mwakilishi wa
Wawekezaji (Ndg. Ahmed Muhammed Nassor). Aidha, kufuatia ukaguzi huo, taasisi
zilizoshiriki zilitoa taarifa zao na ushauri kwa Kamisheni ya Utalii (Pemba) na nakla zake
kupokelewa na Idara ya Mazingira na afisi ya Mkuu wa Wilaya, Chake- Chake.
4.3.8 Taarifa ya Idara ya Mazingira kwa Kamisheni ya Utalii Kufuatia Ukaguzi
Uliofanywa.
Taarifa iliyotolewa kwa maandishi na Idara ya Mazingira mnamo mwezi Aprili 2010 na
kupelekwa kwa Kamisheni ya Utalii kufuatilia ukaguzi huo, imepokelewa na Kamati na
kufanywa Kielelezo Na.176 cha Taarifa hii. Taarifa hiyo imeonyesha, pamoja na mambo
mengine, kuwa mambo yafuatayo ndio yalizingatiwa zaidi na Idara ya Mazingira katika kutoa
maoni yake. Mambo yenyewe ni:-
Eneo linaloombwa lina maumbile ya kisiwa kidogo.
Baadhi ya maeneo ya kisiwa hicho yamekuwa na aina tofauti za miti ya mikoko.
Kuna eneo linaloambatana na mwamba wenye dalili ya maporomokounaosababishwa na
maji ya bahari.
Fukwe ndogo ya mchanga.
Maeneo jirani na eneo hilo yamekuwa na aina na viwango tofauti za miti ya mikoko, hali
inayoashiria kuwa maeneo yanategewa kwa maisha ya viumbe wa aina mbali mbali.
Kutokana na hali hii, taarifa imeedelea kueleza, Idara ya Mazingira iliona kuwa -
Kwa mujibu wa kifungu 38(1) cha Sheria ya Nam. 2 ya 1996, Mradi huu utalazimu
kufanyiwa tathmini ya athari za kimazingira (EIA) kabla ya kuanza kufanya shughuli
yoyote ya Mradi; na
Kwa mujibu wa kifungu 38(2) cha Sheria Nam. 2 ya 1996, Mamlaka inayohusika na
utoaji wa leseni, kibali, cheti au ruhusa yoyote haitoweza kufanya hivyo kabla ya
muombaji kufanya tathmini ya athari za kimazingira na kupata Cheti cha Uchunguzi wa
Kimazingira (Environment Impact Audit – EIA) kwa mradi husika.
152
Kwa kuzingatia mambo yaliyoelezwa hapa juu na pia uchambuzi yakinifu uliowasilizwa (kwa
wakati ule), Idara ya Mazingira ilitoa maoni yafuatayo, juu ya maombi ya Mradi wa Pemba
Misali Divers Co. Ltd:-
Kwa sababu uchambuzi yakinifu uliotolewa haukuwa unajitosheleza, Wawekezaji
waandae “UCHAMBIUZI YAKINIFU” yenye maelezo ya kina kuhusiana na Mradi
unaoombwa yanayojitosheleza katika hatua za uchambuzi wa miradi.
Taarifa mpya za uchambuzi huo yakinifu za Mradi ziwasilishwe kwa wadau wote kwa
hatua za uchambuzi wa Mradi utaofanywa na Wadau wote kama inavyotakiwa kufanyika
na kama ilivyofanyika katika hatua ya awali.
Maombi ya Mradi yazingatiwe baada ya uwasilishaji wa taarifa mpya za uchambuzi
yakinifu kuwasilishwa kwa wadau na ripoti za wadau kuwasilishwa kwa taasisi husika.
Ukubwa wa kila bangaloo na ujenzi mwengine uelezwe ili uweze kuzingatiwa iwapo yale
yote yaliyodaiwa kujengwa katika eneo hili yatakuwa na nafasi za kutosha au kuweza
kutoa ushauri mwengineo (ikiwa „building plan‟ iwe ni sehemu ya vielelezo vya
uchambuzi yakinifu).
Suala la EIA ni matakwa ya kisheria hivyo halina budi kuzingatiwa kwa uzito wake.
Haya ndio baadhi ya maelezo ya msingi yaliyomo katika taarifa ya maandishi ambayo Kamati
ilielezwa kuwa yalitolewa na Idara ya Mazingira kwenda kwa Kamisheni ya Utalii kuhusiana na
Mradi wa Pemba Misali Divers Co. Ltd.
Taasisi nyengine ambayo ilishiriki katika ukaguzi huo na kutoa taarifa yake kwa Kamisheni ya
Mazingira ni Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Pemba.
4.3.9 Taarifa ya Afisi ya Mkuu wa Wilaya kwa Kamisheni ya Utalii Kufuatia Ukaguzi
Kamati pia ilipokea (na kuifanya Kielelezo Na.177 cha taarifa hii) taarifa ya maandishi ambayo
Kamisheni ya Utalii iliipokea kutoka Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake kuhusiana na
ukaguzi uliofanywa kwenye eneo lililoombewa kujengwa hoteli kwa Vitongoji, na eneo la kituo
cha kupigia mbizi (Diving Center) la Wesha.
Taarifa hiyo, ambayo tarehe zote za kuandikwa na kupokelewa kwa barua iliyoambatanishiwa
zinaonekana wazi wazi kubadilishwa, inaonyesha (pamoja na mambo mengine) kuwa katika
ukaguzi wao walipata maelezo ya wamiliki wa eneo la Wesha kuwa Mradi wanaomba kufanya
kwenye eneo hilo ni mradi wa Uzamiaji, isipokuwa zitakuwepo pia vyumba za kulala wageni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya maandishi, ushauri uliotolewa na Afisi ya Mkuu wa Wilaya ni
kuwa, kutokana na mapunguvu ya taarifa ya mmiliki wa eneo hilo, mapungufu hayo
yakamilishwe kwanza. Baada ya kukamilishwa mapunguvu hayo, Afisi ya Mkuu wa Wilaya
153
ilieleza haitakuwa na pingamizi ya kuwekezwa kwa Mradi huo. Kutokana na taarifa yenyewe,
inaonekana kuwa, mambo ambayo Afisi ya Mkuu wa Wilaya iliyaona kuwa Muwekezaji katika
utayarishaji wa „uchambuzu yakinifu‟ wa miradi yake ni haya yafuatayo:-
a. Lengo kuu la mradi husika;
b. Mazingira;
c. Maji;
d. Umeme;
e. Takataka;
f. Maji machafu
g. Maslahi ya wanajamii;
h. Suala la ajira hakuliweka wazi;
i. Kima cha Mishahara;
j. Matumizi ya ufukwe;
k. Idadi ya wafanyakazi 60 kwa hoteli ya vyumba 60; na
l. Kiwango Fulani cha kipato ambacho kitaingia kwa shehia husika.
4.3.10 Maamuzi ya Kamisheni ya Utalii Kutokana na Taarifa na Ushauri Iliopata
Afisa Mdhamini wa Kamisheni ya Utalii aliiambia Kamati Teule kuwa kutokana taarifa zote
hizo walizopokea, na pia ushauri wote ambao wamepewa, waliamua kutoa ruhusa kwa
Muwekezaji kuanza ujenzi wake. Uamuzi huo hasa ulichukuliwa baada ya Kamisheni ya Utalii
kuridhika kuwa hakuna mdau yoyote ambae aliuona Mradi huu kuwa haufai au ambae alisema
moja kwa moja kuwa mradi huu usiruhusiwe. Jambo kubwa ambalo wadau wote walihitaji
lifanyike ni kwa Muwekezaji kufanya mambo muhimu ya kuufanya mradi wake ukubalike, na
mambo hayo ndio aliyafanya kuwa ni masharti ya kutekelezwa kwa uwekezaji anaoruhusiwa
kufanywa. Nakla ya barua hiyo ya ruhusa iliyotolewa na Kamisheni ya Utalii kwa Muwekezaji
ilitolewa na kupokelewa na Kamati kama Kielelezo Na.178.
Kwa mujibu wa barua hiyo (Rejea Kielelezo Na.178), ruhusa ya kuendelea na uwekezaji
ulioombwa ilitolewa tarehe 28/04/2010 na kunyesha masharti ambayo kama hayakutekelezwa na
Muwekezaji, Kamisheni ya Utalii italazimika kufuta ruhusa hiyo. Ingawa masharti yenyewe
yameandikwa kwa lugha ya Kiingereza, yametafsiriwa kwa Kiswahili kuwa ni:-
Kwamba Mradi wenyewe uandikwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Makampuni.
154
Kwamba ruhusa iliyotolewa ni kwa ajili ya Muwekezaji mwenyewe na
haitauzwa wala kuahaulishwa kwa namna nyengine yoyote ile bila ya ruhusa
ya Kamisheni.
Kwamba Muwekezaji awasiliane na Mamlaka ya kodi ili kupata maelekezo
juu ya kukamilisha taratibu za kodi.
Kwamba jina la Mradi liwekwe mahali wazi sehemu ya mbele ya kuingilia
kwenye majengo ya Mradi wenyewe.
Kwamba Muwekezaji apeleke taarifa za kila mwezi na kila baada ya miezi
mitatu kuhusiana na hatua za kimaendeleo anazochuka kwenye Mradi wake.
Kwamba vyumba vya wageni viwe vinajitegemea (self-contained) na kwa
vyovyote vile pasiwe na vyoo vya pamoja na wahudumiwa wengine wa Mradi
huo, kwa kizingatia uchambuzi yakinifu uliofanywa.
Kwamba Kila mwaka Muwekezaji akate leseni mpya ya biashara kutoka
Kamisheni ya Utalii.
Kwamba Muwekezaji aajiri Wazanzibari na kuwaendeleza kielimu ili
kuwawezesha kufanya kazi za kitaalamu na pia katika ngazi za utawala.
Muwekezaji anatakiwa atoe taarifa kila mwaka kwa Kamishenmi ya Utalii na
pia kwa Kamisheni ya Kazi kuhusu mipango na maendeleo ya rasilimali watu
na mbinu zinazotumika ili kuhakikisha kuwa hatimae wazalendo wanachukua
nafasi za wageni.
Kwamba Mradi uzingatie Kanuni na taratibu zinazoongoza shughuli za utalii
na shughuli nyengine kama zilivyowekwa na Serikali.
Kwamba Mradi ni lazima uwe na akaunti katika benki yoyote hapa Zanzibar.
Kwamba Mradi hautaajiri wageni wala kuwashirikisha katika uendeshaji wa
shughuli zake bila ya kupata vibali vinavyohitajika.
Kwamba muwekezaji atamruhusu Afisa wa Serikali kufanya ukaguzi wa
mradi ikiwa ni pamoja na mahali pa ofisi, vifaa au zana za kufanyia kazi ikiwa
ni pamoja na mashine, vitabu vya kumbu kumbu kama vile vitabu vya usajili,
vitabu vya akaunti, risiti, na kumbu kumbu nyengine za mahesabu.
Kwamba Muwekezaji awasiliane na Idara ya Ardhi na Usajili na Idara ya
Mazingira kwa ajili ya kupata maelekezo yanayohusiana na shughuli zao.
Kwamba pasiwe na uwekaji rehani, ukodishaji wa Mradi, wala uhaulishaji
kwa njia nyengine yeyote bila ya ruhusa ya taasisi zinazohusika na uwekezaji
na utalii.
Kwamba Muwekeziji apeleke „site plan‟ na michoro mengine ya mradi
wenyewe kabla ya kuanza ujenzi.
Baada ya barua ya ruhusa yenye masharti hayo kutolewa kwa Muwekezaji siku ya tarehe
28/04/2010, Kamisheni ya Utalii ilitoa barua nyengine tarehe 29/04/2010 kuwataka Wawekezaji
kuwasilisha michoro na tathmini ya Mazingira kwa ajili ya Mradi wao kabla ya kuanza ujenzi
155
uliokusudiwa. Nakla ya Barua hiyo ilipokelewa na Kamati kama Kielelezo Na.179 cha taarifa
hii.
Hata hivyo baada ya uchunguzi, Kamati imepata mashaka na ukweli wa kuwepo kwa barua hiyo
kwa sababu ikiwa ni kweli kuwa barua ya ruhusa ya ujenzi iliyotolewa tarehe 28/04/2010
ilikuwa na kumbu kumbu Nam. KU/P/M.10/VOL.I/60 (kama inavyoonekana kwenye barua
yenyewe), haielekei kwa taratibu za kawaida kuwa barua iliyotolewa kesho yake (yaani tarehe
29/04/2010) iwe na kumbu kumbu Nam. KU/P/M.10/VOL.I/88, ambayo inaonekana kuwa ni ya
nyuma. Kamati imeona kuwa hapa kuna uwezekano wa udanganyifu uliofanyika.
Taarifa iliyotolewa na Afisa Mdhamini wa Kamisheni ya Utalii kwa Kamati Teule ilionyesha pia
kuwa mnamo tarehe 21/05/2010 uongozi wa Kamisheni ya Utalii Pemba ulitembelea kwenye
eneo la Mradi huu hapo Wesha na kugundua kuwa Muwekezaji alikuwa anaendelea na ujenzi,
bila ya kuwasilisha michoro na tathmini ya kimazingira na hatimae kupata idhini ya ujenzi. Kwa
barua yenye kumbu kumbu Nam. KU/P/PMDCL/198/13 ya tarehe hiyo hiyo 21/05/2010
Kamisheni ya Utalii ilimtaka Muwekezaji kusitisha hatua za ujenzi ambazo alikuwa anaendelea
nazo hadi hapo atakapowasilisha michoro na tathmini ya kimazingira (EIA) na hatimae kupata
idhini ya ujenzi (Kielelezo Na.180).
Kamati ilielezwa pia kuwa pamoja na Muwekezaji kupewa amri mbili (amri nyengine ni ile
iliyotolewa na Idara ya Mazingira mnamo tarehe 28/05/2010) ya kusitisha ujenzi wake,
hakustisha ujenzi aliokuwa anaendelea nao. Badala yake, kufuatia amri hizo za kuzuia ujenzi,
ujenzi uliendelea kwa kasi zaidi usiku na mchana mpaka hoteli (na sio kituo cha kuzamia)
ilipokamilika. Imeelezwa pia kuwa hata baada ya kuhamia upanuzi wa majengo ya hoteli hiyo
umekuwa unaendelea siku hadi siku, na bila ya kujali amri zilizotolewa na mamlaka
zinazohusika kwa mujibu wa sheria.
Akijibu masuala ya Waheshimiwa Wajumbe, Afisa Mdhamini wa Kamisheni ya Utalii Pemba
alieleza kuwa kwa kawaida ruhusa huwa zinatolewa kwa wawekezaji ambao hawajakamilisha
taratibu kwamba wakamilishe taratibu na baadae watekeleze mipango yao ya uwekezaji. Ruhusa
ya aina hii ndio ilitolewa kwa Pemba Misali Divers Co. Ltd, lakini akapuuza na kuanza ujenzi
bila ya kuzingatia masharti aliyopewa. Na hata baada ya kuanza ujenzi na kupewa amri ya
kuzuia, alikiuka amri hiyo na akaendea na ujenzi kadiri alivyopenda.
Wajumbe walipotaka kujua juu ya kuwepo kwa leseni ya biashara ya Muwekezaji, walielezwa
kuwa leseni anayo lakini Kamisheni ya Utalii Pemba haikutoka kwao (yaani Pemba) na hata
hawaelewi ilipatikana vipi kwa sababu hawakushirikishwa. Kilichotokea ni kuwa, baada ya
Muwekezaji kuanza kufanya biashara zake, Kamisheni ya Mazingira ilikwenda kwa ukaguzi wao
wa kawaida na walipouliza kuhusu leseni ya biashara, Muwekezaji alieleza kuwa leseni anayo.
Alipotakiwa kuionyesha, Muwekezaji alionyesha leseni yake ambayo inaonekana kuwa
imetolewa Makao Makuu ya Kamisheni huko Unguja.
156
Walipotaka kujua kuhusu utaratibu wa kutoa leseni, Wajumbe wa Kamati walijulishwa kuwa
kwa utaratibu wa kawaida leseni huwa zinatolewa baada ya tathmini ya mradi iliyopaswa
kufanywa na mamlaka ya Kamisheni huko huko Pemba, hata kama leseni ingeweza kutolewa
Unguja. Lakini tathmini hiyo ndio ambayo kimsingi ingewezesha maamuzi kufanywa hata juu ya
kiasi cha kulipwa kama ada ya leseni. Kamati imeelezwa kuwa tathmini hiyo haikuwahi
kufanyika. Ilielezwa pia kuwa hakuna Mradi mwengine wowote kama huu ambao leseni yake
ilitoka Unguja bila ya tathmini kufanywa kwanza huko Pemba.
4.3.11 Taarifa ya Idara ya Ardhi Juu ya Mradi wa Pemba Misali Divers:
Taarifa iliyopokelewa na Kamati Teule kutoka kwa Idara ya Ardhi Pemba, ileelezea kuwa kabla
ya ruhusa ya matumizi ya ardhi kutolewa kwa Muwekezaji, Idara ya Ardhi inatakiwa kuandaa
matumizi ya ardhi. Maandalizi ya matumizi ya ardhi huwa yanajumuisha hatua nyingi za
kitaalamu ikiwa ni pamoja na upimwaji wa ardhi na kuwekwa kwenye ramani ya mji. Baada ya
matumizi ya muwekezaji kukubalika kwenye ardhi husika, jukumu la kutoa „lease‟ ni la Waziri
mwenye dhamana juu ya mambo ya ardhi.
Taarifa iliendelea kuonyesha kuwa hati ya matumizi ya ardhi inayojadiliwa (yaani „lease‟)
ilitolewa tarehe 10/02/2010. Hati hiyo ya matumizi ya ardhi ilitolewa ilizingatia masharti yale
yale yaliyotolewa na Kamisheni ya Utalii. Nakla ya „lease‟ hiyo ilipokelewa na Kamati na
kufanywa Kielelezo Na.181 cha taarifa hii.
Alieleza Ndg. Januari Fusi ambaye ni Mkurugenzi, Idara ya Ardhi na Usajili kuwa
kinachojitokeza ni kuwa Muwekezaji hakufata maelekezo ya Serikali. Aliendelea kueleza kuwa
wakati akiwa ni Afisa Mdhamini wa Idara ya Ardhi Pemba, alitoa taarifa hiyo kwenye mkutano
wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa. Kufuatia taarifa hiyo, Mhe. Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba alitoa
amri ya kuzuiwa kwa ujenzi wa mradi huo uliokuwa umeanza bila ya kufata taratibu za Serikali.
Amri ya kuzuia ujenzi huo ilipotolewa ndio ujenzi uliendelea kwa kasi kubwa zaidi.
Ilielezwa kuwa kabla ya muwekezaji kupewa „lease‟ kwenye kiwanja hicho, kiwanja hicho
kilimilikiwa na Ushirika wa „Nanga Nzito‟ ambao waliitumia ardhi hiyo kwa kupanda mikoko.
Mnamo mwaka 2008 wanaushirika hao walipeleka ombi la kupimiwa ardhi hiyo ili waweze
kupata ruhusa rasmi ya matumizi ya ardhi hiyo kwa matumizi yao ya kilimo cha mikoko.
Upimwaji huo ulifanywa na ramani kutolewa, lakini hati rasmi ya matumizi ya ardhi hiyo
haikuwahi kutolewa kwa wanaushirika waliopimiwa. Katika mazungumzo ya Idara ya Ardhi na
Kamati ramani hiyo ilitolewa na kupokelewa kama Kielelezo Na. 182.
Mnamo mwaka 2009, Kamisheni ya Ardhi ilijuulishwa kuwa, Mhe. Machano Othman Said na
Ndg. Amani Ibrahim Makungu (wanaofanya biashara kwa jina la Pemba Misali Divers Co. Ltd)
wamenunua ardhi inayomilikiwa na ushirika wa Nanga Nzito. Baadae taarifa hiyo ililetwa rasmi
kwa ajili ramani waliyochorewa Nanga Nzito kuchorwa upya kwa ajili ya Mradi huu mpya.
Ramani ile ile iliyokuwepo (Rejea Kielelezo Na. 182), kwa vipimo vyake vile vile, ilichorwa
157
upya na ndiyo ambayo ilitumika kupewa „lease‟ Kampuni ya Pemba Misali Divers. Ramani hiyo
iliyochorwa upya imepokelewa na Kamati kama Kielelezo Na. 183.
Taarifa ya Idara ya Ardhi imeendelea kuonyesha kuwa Idara hiyo haina kumbu kumbu zozote
zinazohusiana na Mradi huo, isipokuwa ni ramani na „lease‟ pekee. Hata hivyo, katika ukaguzi
ambao watendaji wa Idara ya Ardhi walifanya kwenye eneo hilo waligundua kuwa Muwekezaji
huyo amejenga sehemu kubwa zaidi ambayo alinunua kutoka kwa wanaushirika wa Nanga
Nzito.
4.3.12 Ziara ya Kamati kwenye Hoteli ya Pemba Misali Divers:
Katika ukaguzi ambao Kamati Teule ikishirikiana na taasisi zote zilizohojiwa, zilifanya ukaguzi
kwenye eneo la Mradi huo mnamo tarehe 01/11/2010. Katika ukaguzi huo, wafanyakazi wa
Idara ya Ardhi na Upimaji waliionesha Kamati eneo la Mradi ambalo Muwekezaji alinunua
kutoka kwa ushirika wa Nanga Nzito. Baadhi ya vikuta vilivyowekwa na watumishi wa Idara ya
Ardhi kwenye eneo ambalo waliwapimia wanaushirika wa Nanga Nzito vilikuwa havionekani
wakati wa ukaguzi huo ama kwa sababu vimefunikwa na majengo au vimeng‟olewa. Hata hivyo,
kutokana na baadhi ya vikuta vilivyoonekana na pia vipimo vyengine ambavyo wataalamu wa
Idara ya Ardhi walivifanya, Kamati iliweza kuonyeshwa eneo ambao Muwekezaji alinunua
kutoka kwa ushirika wa Nanga Nzito.
Kilichoonekana katika ukaguzi huo ni kuwa eneo ambalo Muwekezaji alinunua kutoka kwa
Ushirika wa Nanga Nzito si zaidi ya robo ya sehemu yote ambayo Muwekezaji ameitumia kwa
majengo ya nyumba za Hoteli na Jetty mbili. Kutokana na ukaguzi huo, nyumba zenye vyumba
vya hoteli nambari 101 hadi 115, nyumba yenye vyumba vya hoteli 311 hadi 316, „Restaurant,
Reception‟, Ukumbi wa Mikutano, Vyoo viliopo karibu na „reception‟, vibanda cha walinzi na
eneo lote la kuingilia kwenye Hoteli hiyo. Kwa tathmini ya makisio iliyofanywa na wataalamu
wa Idara ya Ardhi, eneo lenye majengo ya nyumba tofauti za Hoteli nje ya lile eneo lililopimwa
na Muwekezaji kupewa „lease‟, limekisiwa kuwa lina wastani wa urefu wa mita 160 na upana wa
mita 40. Pia kuna sehemu yenye „jetty‟ mbili. „Jetty‟ iliyojengwa kutoka maeneo ya mapokezi
kuelekea baharini imekisiwa kuwa na urefu wa mita 60; na ile iliyojengwa kutoka usawa wa
barabara kuu kuelekea mapokezi imekisiwa kuwa na urefu unaozidi mita 120.
Maeneo yote haya yaliyoainishwa hapa juu yamejengwa na Muwekezaji bila ya ruhusa ya tasisi
yoyote ya Serikali na bila hata ya kufanyiwa vipimo. Kwa taarifa ya wataalamu wa Idara ya
Ardhi na Upimaji matumizi ya namna hii ya ardhi hayakubaliki kabisa kabisa. Wameeleza kuwa
kwa mujibu wa sheria, ili muwekezaji apewe ruhusa ya matumizi ya ardhi ni lazima ardhi hiyo
ipimwe, iwekewe vikuta, ipigwe ramani, na ramani yake iingizwe kwenye ramani ya mji. Pia
matumizi ya Muwekezaji kwenye ardhi iliyopimwa ni lazima yakubalike kitaalamu.
Baada ya hapo ndio Muwekezaji anaweza kuomba kupewa „lease‟ na, hata baada ya kupewa
„lease‟, hataruhusiwa kujenga mradi wake mpaka pale ambapo uchambuzi yakinifu wa mradi
158
wake, michoro ya ujenzi anaohitaji kufanya, tathmini ya athari za kimazingira za mradi wake, na
taratibu nyengine za kitaalamu zinazosimamiwa na taasisi tofauti za Serikali zitakapo kamilika.
Katika Mradi huu, Kamati imejulishwa, taratibu zote hizi hazikufatwa. Kibaya zaidi ni kuwa,
hata pale alipositishwa kuendeleza ujenzi wake kinyume na utaratibu, Muwekezaji huyu hakujali
kabisa na akaendelea na mipango yake kama vile Serikali haipo.
Matatizo mengine ambayo wataalamu wa Idara ya Ardhi waliyaelezea kuhusiana na Mradi wa
Hoteli hii ni kuwa, ujenzi kufanywa mpaka kwenye ufukwe (beach) kwa zile sehemu zenye
ufukwe, pamoja na kuwepo kwa matakwa ya sheria kuwa ujenzi uanze umbali wa mita 30
kutoka kwenye ufukwe. Vile vile, baadhi ya majengo yako kwenye mikoko kabisa, wakati sharia
inaelekeza kuwa ujenzi uanzie kwenye umbali wa angalau mita 30 kutoka kwenye mikoko au
„coral‟.
Kwa namna yoyote ile tabia za ya Wawekezaji wa aina hii haiwezi kukubalika, kwa maslahi ya
nchi. Na hivyo, Kamati inasisitiza kwamba sio sahihi kwa Serikali kuruhusu watu kufanya
mambo kinyume na utaratibu. Hata hivyo Kamati ilipanga kufanya mahojiano na wananchi
anaoishi kwenye maeneo ya Mradi wenyewe, na baadae kukutana na Muwekezaji ili kupata
maelezo yake binafsi kutokana na malalamiko ambayo Kamati imeyakusanya dhidi yake.
4.3.13 Majadiliano kati ya Kamati na Wanachi
Katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la Hoteli ya Pemba Misali Divers hasa kutokana
na manung‟uniko ambayo yalisemekana yanatokana na wananchi wa sehemu hiyo, Kamati Teule
ilikutana na wananchi siku ya tarehe 01/11/2011.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika hapo hapo kwenye Hoteli ya Pemba Misali Divers,
Kamati ilipokea historia fupi ya mahali hapo ambapo ilielezwa kuwa kabla ya ujenzi wa Hoteli
hii, mahali hapo patikuwa ni fungu, yaani palizungukwa na maji. Lipo katika pwani ya bandari
ya Wesha umbali ya kadiri mita 250-300 nyuma ya matangi ya mafuta ya kampuni ya Gapco.
Eneo hilo kwanza lilimilikiwa na Wizara ya Kilimo ambayo baadae iliwapatia wanaushirika wa
vikundi tofauti ukiwemo ushirika wa „Nanga Nzito‟, ushirika wa „Taratibu‟, na vikundi vingine
kadhaa vya wananchi. Baadae wamiliki wa vikundi tofauli waliuza sehemu zao (kwa mikataba
tofauti) kwa Ndg. Amani Ibrahim Makungu ambae ni mmoja wa wamiliki wa Hoteli hiyo.
Taarifa hiyo ya utangulizi ilitolewa na Sheha wa Shehia ya Wesha (Bw. Juma Bakar Junga).
Baada ya kupokea taarifa hiyo, ndio Kamati ilipata nafasi ya kujadiliana na wananchi kutoka
vikundi tofauti ambavyo vilikuwa na sehemu za kufanyia shughuli zao kwenye sehemu
iliyojengwa Hoteli hiyo.
Kikundi cha kwanza ambacho kilikabiliana na Kamati ilikuwa ni kikundi cha „Nanga Nzito‟.
Maelezo ya kikundi hicho yalitolewa kwa Kamati na Ndg. Mariam Hassan Jabir, ambaye ni
Katibu wa Kikundi hicho. Alielza kuwa kikundi chao ni cha ushirika uliosajiliwa kilikuwa
159
kinaendeleza kilimo cha miti kwenye eneo fulani (ambalo alionyesha) ndani ya majengo ya
Hoteli. Eneo hilo waliruhusiwa na Wizara ya Kilimo wapande mivinje. Baada ya kuendeleza
kilimo hicho kwa muda hivi, waliomba Serikalini wapimiwe eneo hilo ili waweze kupata ruhusa
rasmi ya kulitumia kwa shughuli zao. Walipimiwa na kupewa ramani ya sehemu yao, lakini
hawakuwahi kupewa hati rasmi ya umiliki wa sehemu hiyo.
Baada ya kipindi kama cha mwaka mmoja hivi kupita, ndio walifatwa na Ndg. Amani Ibrahim
Makungu akawaomba wamhaulishie yeye sehemu yao kwa ajili ya uwekezaji ambao alipanga
kuufanya kwenye ardhi hiyo. Aliielezea Kamati hiyo pia kuwa kwa hiari yao walimuhalishia
sehemu yao ya ardhi kwa Ndg. Makungu ambaye aliwalipa fedha zote Shilingi Milioni Kumi
(Tshs.10,000,000/=) ambazo walikubaliana. Kwamba waliandikiana mkataba unaoonyesha
hivyo, na hawana pingamizi wala tatizo lolote na Muwekezaji huyo. Hata hivyo, alieleza kuwa,
wao walimuuzia sehemu ya eneo lililojengwa Hoteli ambalo lilikuwa limepandwa mivinje.
Kikundi kingine kilikutana na Kamati ni Jumuiya ya Hifadhi ya Mikoko ambacho Katibu wake
ni Ndg. Salim Juma Mwadini. Kikundi hiki kilianza baada ya kuona kuwa mikoko inakufa
kutokana na mafuta yanayomwagika kutoka „depot‟. Maamuzi yalifanywa kuwa ili kuepuka
mikoko kutoweka kwenye baadhi ya sehemu yao waliamua wachukue juhudi maalum za
kupanda mikoko. Jumla ya Vikundi 11 viliitikia wito huu, vikiwemo vikundi vya wanafunzi wa
skuli. Kazi ikaendelea vizuri na mikoko ikaota vizuri.
Baada ya muda ndio walikuta watu wanajenga majengo ya hii Hoteli, na katika ujenzo wao
walikuwa wanakata mikoko bila ya hata ya wao wenyewe kujuulishwa. Kwa sababu
hawakuridhika na hatua hiyo, walilalamika mpaka kupitia kwenye vyombo vya habari. Hata
hivyo hakuna msaada wowote walioupata kutoka Serikalini au kwa mtu mwengine yeyote.
Adhari za ukataji huo wa mikoko zipo kwa viwango tofauti wengine wameathirika sana lakini
wengine sio kwa kiasi kikubwa. Lakini hakuna mtu miongoni mwao aliewahi kulipwa fidia.
Jambo linalokatisha tamaa kwa Serikali, kikundi hicho kilieleza, ni kuona kuwa walihamasishwa
kutunza mazingira kwa kupanda mikoko, lakini ilipotokea mtu akawa anaikata mikoko hiyo na
wao kulalamikia kwa nguvu zote juu ya suala hilo, bado Serikali ilikaa kimya kama vile haipo.
Hivi sasa ndio Kamati imekuja kufanya uchunguzi. Sasa basi uchunguzi huo ni wa kitu gani
wakati mikokoyetu imeshakatwa na watu wenye fedha zao wameshajenga Hoteli. Wanakikundi
hao walihoji kuwa Serikali ilikuwa wapi wakati wote huo?
Wakijibu suali lililoulizwa na Wajumbe wa Kamati, wanakikundi hao walieleza kuwa hakuna
mtu miongoni mwao ambae amewahi kulipwa fidia kutokana na mikoko iliyokatwa.
Walipoulizwa juu ya kuridhika kwao kwa kuwepo Hoteli hiyo mahali hapo, walieleza kuwa
hoteli hiyo sasa inaonekana kuwa ni hatua nzuri ya maendeleo katika maeneo yao. Kwamba
kuna watu wengi miongoni mwao ambao wanafaidika moja kwa moja (kwa ajira au kwa mamna
nyengine) kutokana na kuwepo kwa Mradi huo. Kwa hivyo, hawataki mradi huo uondolewe,
lakini pia hawaridhiki na uharibifu wa mazingira unaotokea kwenye mazingira ya Hoteli hiyo.
160
Wakielezea uharibifu wa mazingira unaoendea walisema kuwa kuna baadhi ya mikoko
inaendelea kukatwa katwa, kuna maji machafu yanayoingia baharini yanahitaji kudhibitiwa,
kuna maji pia yanayoingia baharini kutoka vyooni. Wanachohitaji ni kuona kuwa wanashirikiana
na Muwekezaji kudhibiti uharibifu wa mazingira na kusaidia kwa njia moja au nyengine kuinua
hali ya maisha kijijini pao.
Kikundi chengine cha ushirika ambacho Kamati ilizungumza nacho ni ushirika wa ufugaji kuku
wa „Mtarazaki Hachoki‟. Ushirika huu ulianza kwa ufugaji wa ng‟ombe. Baada ya baadhi ya
ng‟mbe kupata ugonjwa, waliobaki waliwauza na kugawana fedha. Kila mmoja wao akaamua
kufanya juhudi zake mwenyewe za ufugaji wa kuku.
Bibi Ashura Moh‟d Said alieleza kuwa yeye alifuga kuku na ikawa anapata mafanikio mazuri.
Wakati mradi wake wa kuku unaendelea vizuri ndio alijitokeza huyu Muwekezaji wa Mradi wa
Hoteli na kuomba aachiwe hiyo nafasi. Ameeleza pia kuwa, baada ya kukubaliana, Muwekezaji
huyo aliwalipa kile walichokubaliana kuwa ni thamani ya mradi wake wa kuku. Pia aliruhusiwa
kuchukua kuku wake wote. Kwa hivyo, na yeye ameridhika na wala hana mashaka yoyote na
Mradi ambao Muwekezaji anaendelea nao.
Mfugaji mwengine wa kuku ambaye Kamati ilizungumza nae ni Bibi Mariam Said. Aliielezea
Kamati Teule kuwa nae alikuwa na mifugo ya kuku kwenye eneo hilo. Kwamba, Muwekezaji
alipomuomba, alimuuzia kuku wake na fedha zote walizokubaliana alilipwa. Na yeye pia hana
pingamizi na Muwekezaji huyu.
Kwenye eneo lilijengwa Hoteli pia kulikuwa na ufukwe (ambapo sasa pamejengwa jetty) ambao
ulitumika kama uwanja wa vijana kuchezea mpira wakati maji yanapotoka. Mbali ya sehemu ya
uwanja huo iliyojengwa „jetty‟, kuna sehemu ambayo pamewekwa kokoto kwa ajili ya
kutengenezea barabara ya kuweza kupita gari.
Wameeleza kuwa walimuuliza Muwekezaji juu ya hicho alichowafanyia lakini akawa hana jibu.
Wakati huo walikuwa wanaendelea kucheza sehemu hiyo ingawa ni kwa mshaka mashaka. Hivi
sasa huwa wanakatazwa kabisa kuwepo kwenye sehemu hiyo. Walienda kulalamika ZFA, lakini
walijibiwa kuwa ZFA haina la kufanya. Walirudi tena kwa Muwekezaji na kumlalamikia ili
aweze kuwasaidi kuwapatia sehemu nyengine na pia jazi za kuchezea, lakini inaonekana hakuna
dalili za kuweza kusaidiwa.
Wachezaji hawa wameeleza kuwa hawaridhiki na kitendo hicho ambacho Muwekezaji huyu
amewafanyia, na kwamba hawana imani nae mpaka atakapotekeleza ahadi zake au kuwapa
sehemu yao ya kufanyia mazoezi.
4.3.14 Mazungumzo Kati ya Kamati na Muwekezaji
Baada ya kumaliza ziara yake kwenye Hoteli ya Pemba Misali Sunset Beach na kupata nafasi ya
kuzungumza na baadhi ya wanakijiji wa Wesha ambao kwa njia moja au nyengine wameguswa
161
na uwepo wa Hoteli hiyo, Kamati ilifanya mazungumzo na kiongozi mkuu wa wawekezaji wa
Hoteli hiyo ambae ni Ndg. Amani Ibrahim Makungu.
Wakati wa mazungumzo na muwekezaji huyo, Kamati tayari ilikuwa imejikusanyia taarifa
ambazo zilionyesha kuwepo kwa maeneo nanne ambayo ufafanuzi wa Muwekezaji huyo
ulionekana kuwa unahitajika. Maeneo yenyewe ni haya yafuatayo:-
i. Ruhusa ya ujenzi ilitolewa kwa masharti ambayo baadhi yake Muwekezaji alitakiwa
kuyatekeleza kabla ya kuanza ujenzi, lakini alianza mpaka kukamilisha ujenzi na kuanza
biashara bila ya kutekeleza baadhi ya masharti muhimu aliyopewa;
ii. Muwekezaji aliruhusiwa kujenga kituo cha uzamiaji (chenye nyumba chache za kulala
wageni), lakini badala yake aliamua kujenga hoteli bila ya kujali kuwa mradi wa hoteli
haukubaliki kwenye sehemu finyu iliopo mahali penyewe;
iii. Baadhi tu ya sehemu yenye mradi huo ndio imepimwa (na ilipimwa kwa ajili ya
shughuli za ushirika wa wapanda mivinje, baadae ikauzwa kwa Muwekezaji), lakini
Muwekezaji amepanua mradi wake katika eneo kubwa zaidi ambalo halikupimwa, na
wala hana ruhusa ya Serikali ya matumizi ya eneo hilo;
iv. Hapakuwa na taratibu zozote zilizochukuliwa na Muwekezaji kutafuta idhini ya ujenzi
wa majengo aliyojenga, jambo ambalo ni kinyume na sheria ya mipango miji;
v. Katika ujenzi wake, muwekezaji amejenga majengo mpaka kwenye ufukwe, na hiyo
kukiuka sheria inayoelekeza iwepo sehemu ya wazi kati ya majengo na kwenye ufukwe;
vi. Baada ya muwekezaji kuonekana kuwa ameshindwa kufata masharti ya uwekezaji,
alipewa amri za kusitisha ujenzi huo. Hata hivyo, aliendelea na shughuli zake za ujenzi
na baadae kuendelea kufanya biashara katika hali ya kudharau amri hizo;
vii. Leseni ya biashara ambayo mwekezaji anayo imetolewa bila ya mradi wake kufanyiwa
tathmini ambayo ingewezesha kujulikana baadhi ya masharti ya kuingizwa kwenye leseni
yenyewe; na
viii. Kwenye maeneo ya Hoteli hiyo kuna „jetty‟ mbili zimejengwa bila ya kuzingatia sheria
inazohusiana na ujenzi wa „jetty‟.
Haya ndio baadhi ya mambo ambayo Kamati ilihitaji kujirisha ilipokutana na muwekezaji.
Katika maelezo yake, Ndg. Amani Ibrahim Makungu alieleza kuwa yeye ni mfanyabiashara wa
hoteli kwa muda mrefu, na ana hoteli Nungwi, Kiwengwa na Kilimani, Mjini Unguja. Kuna
wakati alipata hamu ya kuwekeza na baada ya kuwaelezea rafiki zake, alionyeshwa eneo hilo la
Wesha. Alisaidiwa kuwapata watu ambao walimiliki sehemu hizo, na kwamba yeye alinunua
kutoka kwao. Nakla za mikataba ya unnunuzi wa vipande vidogo vidogo vya ardhi zilipokelewa
na Kamati na kufanywa kielelezo Na 184.
162
Baada ya hatua hiyo ndio alifatilia „lease‟ na alifanikiwa kupata. Hata hivyo, amekiri kuwa eneo
ambalo lilipimwa na yeye kupewa „lease‟ ni lile alililonunua kutoka kwa ushirika wa kupanda
mivinje. Sehemu alizojenga, ingawa alinunua kutoka kwa watu waliozimiliki kabla ya kuuziwa
yeye, lakini hakuwahi kuzitafutia „lease‟.
Kuhusiana na tuhuma za kutofuata taratibu za kisheria, alieleza kuwa ni kweli kuwa baadhi ya
mambo alilazimisha tu katika kufanikisha tama zake. Alitoa nasaha kuwa, katika hili, watendaji
wa Serikali hawapaswi kulaumiwa kwa sababu yeye kama mfanyabiashara anajua namna ya
kufanya mambo yake yaende, na ndivyo alivyofanya. Lakini sio wafanya biashara tu, lakini
hata wanasiasa wana namna zao za kuhakikisha kuwa wanashinda uchaguzi, kwa hivyo
watendaji wasilaumiwe.
Alipoulizwa namna ambavyo aliweza kupata leseni ya biashara katika hoteli ambayo ujenzi
wake ulizuiwa na ikaendelea kujengwa kwa mabavu, alieleza kuwa alifanikiwa kuipata kutokana
na msaada wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, wa wakati huo ambaye alimtoleshea
leseni hiyo kutoka Unguja baada ya taratibu zake kushindikana huko kwenye Kamisheni ya
Utalii Pemba.
Alipoulizwa kuhusu umiliki wa Kampunu ya Pemba Misali Sunset Beach Ltd, alisema kuwa
Kampuni hiyo inamilikiwa na – yeye mwenyewe, Ndg. Amani Ibrahim Makungu (40% ya hisa);
Ndg. Ghania Khalfan Mohammed (25%); Ndg. Asha Omar Ali (25%); na Mhe. Machano
Othman Said (10%). Aliendelea kueleza kuwa wahusika wote wamelipa hiza zao, isipokuwa
Mhe. Machano ambae hizo 10% amepewa tu kwa ajili ya mchango wake pale mambo
yanapokuwa magumu kwa upande wake. Alitoa mfano kuwa, wakati Mheshimiwa Mkuu wa
Mkoa wa Kusini Pemba alipozuia hatua za ujenzi wa hoteli hiyo, Mhe. Machano ndiye aliesaidia
kupatikana kwa ruhusa ya Mhe. Mkuu wa Mkoa na hivyo kuwezesha ujenzi wa hoteli hiyo
kukamilika na kuanza biashara.
4.3.15 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii ndogo, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
4.3.15.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Kuna Uvamizi Mkubwa wa Maeneo ya Fukwe na Uharibifu wa Mazingira na
Kamati imejiridhisha kwamba, Ujenzi wa Miradi ya Mahoteli Zanzibar
hauzingatii matakwa ya Sheria zinazoelekeza juu ya masuala ya ardhi na
mazingira.
(ii) Idara ya Mazingira imeshindwa kuisimamia ipasavyo Sheria zinazohusiana na
Mazingira kwa kutowachukulia hatua za kisheria Wawekezaji hawa na matokeo
163
yake wanaendelea kufanya uharibifu bila ya kujali mamlaka yoyote ama athari
kubwa ya kimazingira na kiustawi wa wananchi, inayoweza kutokezea.
(iii) Kamisheni ya Utalii pamoja na Taasisi nyengine za Serikali zinazohusika na
Uwekezaji wa Miradi ya Utalii zimehusika kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa
mazingira na uvamizi wa fukwe uliofanywa na Wawekezaji hawa.
(iv) Aliekuwa Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar, Mhe.
Machano Othman Said, kwa kumuliki kwake 10% katika Kampuni iliyomiliki
Hoteli ya Misali Sun set Beach ya Wesha, ametumika kusababisha kasoro
tulizozizungumzia katika Mradi wa Hoteli ya Misali Sun set Beach, iliyopo
Wesha.
(v) Watendaji Wakuu wa Serikali (ikiwa ni pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya
Utunzaji na Uhifadhi wa Barabara (UUB)) wameshiriki katika uharibifu wa
mazingira kwa kushirikiana na Muwekezaji kwa kufanya ufukiaji wa Bahari
katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa, kinyume na utaratibu.
(vi) Wawekezaji wa Miradi ya Utalii kwa makusudi na kwa jeuri kabisa hawaheshimu
sheria zinazohusiana na uwekezaji wa Miradi ya Kitalii huku Serikali inakaa
kimya na kuwatizama na bado wanapewa leseni za biashara hali ya kwamba
Serikali inafahamu uharibifu unaofanywa na Miradi yao. Hii inaonesha kuwa
kuna harufu ya rushwa katika maeneo hayo.
4.3.15.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:
(i) Serikali ndani ya miezi 3 (kuanzia tarehe ya kuwasilishwa ripoti hii) iunde Kamati
itakayofuatilia suala la uvamizi na uharibifu wa mazingira katika miradi yote ya
hoteli Zanzibar na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika
kukiukwa na kadhia hiyo, huku pia ikizichukulia hatua za kisheria hoteli zote
zitakazobainika kikiuka taratibu za Uwekezaji. Iwapo baada ya kumaliza muda
huo wa miezi 3, Serikali imeshindwa kufanya hivyo (kuunda Kamati hiyo),
Baraza la Wawakilishi litekeleze jukumu hilo la kuunda Kamati Maalum ya
Muda, ya kufuatilia suala hili na ripoti yake iwasilishwe Barazani.
(ii) Aliekuwa Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Machano
Othman Said awajibishwe kutokana na kushiriki kwake kwa kiasi kikubwa katika
uharibifu uliofanywa na ujenzi wa Mradi wa Pemba Misali Sunset Beach Hotel,
wakati yeye ni kiongozi wa Serikali.
(iii) Kwa kuwa Sheria Namba 2 ya mwaka 1996 imewapa mamlaka yanayofaa Idara
ya Mazingira ya kumchukulia mtu anaekengeuka sheria hiyo, hatua za kisheria,
jambo ambalo halikufanyika, Kamati inapendekeza Watendaji wakuu wa Idara ya
Mazingira wanaohusika na kusimamia mazingira, wachukuliwe hatua za
kinidhamu kwa kushindwa kwao kuisimamia sheria.
164
(iv) Watendaji Wakuu wa Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara (UUB)
walioshiriki katika ufukiaji wa ardhi (reclamation) katika hoteli ya Maruhubi
Beach Villa wachukuliwe hatua za kinidhamu ili iwe ni funzo kwa watendaji
wengine.
(v) Maagizo ya Idara ya Mazingira iliyoyatoa kwa wawekezaji hao kuhusiana na
uvamizi wa fukwe na uharibifu wa mazingira walioufanya kufuatia ujenzi wa
miradi yao (ikiwa ni pamoja na kuvunja majengo ya Mikahawa iliyojengwa ndani
ya fukwe, katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View pamoja), yasimamiwe na
Serikali Kuu huku ikihakikisha yanatekelezwa ndani ya miezi 2 (tokea tarehe ya
kuwasilishwa kwa ripoti hii) na taarifa za utekelezaji wake ziwasilishwe katika
Baraza la Wawakilishi.
(vi) Serikali isimamie ndani ya mwezi mmoja (baada ya kuwasilishwa kwa ripoti hii)
ikihakikisha kwamba, malipo yote ya leseni za biashara ya Utalii ambazo
hazikukatwa na Wawekezaji hao tokea kuanza kwa miradi yao, yalipwe mara
moja kama sheria zinavyoelekeza huku ikihakikisha kwamba, Wawekezaji hawa
wanafuata ipasavyo matakwa ya sheria zinazohusika na uwekezaji kabla ya
kupewa leseni na vibali vyengine vyovyote vinavyohusika na miradi yao.
(vii) Hatua za kisheria zinahohusiana na Mazingira na Uwekezaji wa Miradi ya Utalii
kwa ujumla zichukuliwe mara moja dhidi ya Wawekezaji hawa na taarifa ya hatua
hizo ziwasilishwe katika Baraza la Wawakilishi katika Mkutano wa Nane wa
Baraza, unaotarajiwa kuanza mwezi wa September/Octoba 2012.
HADIDU REJEA YA NNE:
5.0 KUHUSU UHAULISHWAJI WA KIWANJA KINACHOPAKANA NA LIVING
STONE HOUSE.
5.1 Utangulizi:
Katika Hadidu hii rejea, Kamati ilitakiwa kuchunguza umiliki halali wa kiwanja kinachopakana
na Living Stone, jengo ambalo hivi sasa linatumiwa na Kamisheni ya Utalii. Katika uchunguzi
wake, Kamati ilitakiwa iangalie historia ya umiliki wa kiwanja hicho na sababu za kuhaulishwa
kutoa kwa mmiliki mmoja hadi mwengine huku ikijiridhisha juu ya usahihi wa taratibu za
kisheria kama zimefuatwa katika uhaulishwaji wake. Aidha, Kamati ilitakiwa ichunguze maslahi
ya Umma kama yamezingatiwa katika uhaulishaji wake na hatimae itoe ushauri wake kwa
Serikali.
Kamati imeifanyia kazi hadidu hii rejea kwa mazingira tofauti. Imefanya mazungumzo ya
pamoja na Wizara ama Taasisi husika siku ya Jumatatu, tarehe 28/11/2011 katika kikao
kilichofanyika Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati huku Wizara hii ikiwa ni mwenyeji
wa Kamati na Taasisi zilizobakia, yaani Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB); Ofisi ya Rais,
Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na Idara ya Ardhi na Usajili. Lakini pia ilifanya
mahojiano na Mhe. Waziri aliehusika na suala hili tarehe 07/12/2011 lakini pia ilikutana na
165
Mmiliki wa Kampuni iliyohaulishiwa kiwanja hicho na Serikali, Mama Fatma Karume tarehe
06/12/2011, pamoja na kwamba anamiliki hisa 33% katika Kampuni wakati Ndg. Khalid Iddi
Mabrouk akimiliki hisa 51%. Kamati imefanya hivi kwa sababu ya kutokuwepo kwa
mawasiliano ya uhakika na Ndg. Khalid katika wakati husika. Aidha, ilifanya mahojiano na Ndg.
Ramadhan Abdalla Songa anaemiliki hisa 8 katika Kampuni hiyo tarehe 29/12/2011. Pamoja na
mazingira yote hayo, Kamati pia ilifanya ziara katika eneo husika kwa mashirikiano na Idara ya
Ardhi na Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati. Katika kufanya kazi suala hili, Kamati
imeona ni busara kupata uchanganuzi huo kwa mnasaba wa hadidu hizo ndogo ndogo kama
ifuatavyo:
5.2 Kuchunguza iwapo Taasisi iliyokuwa inakimiliki kiwanja hicho ilikirejesha
Serikalini kabla uhaulishaji huo kufanyika:
Kwanza ifahamike kwamba, kiwanja kilichopo Kinazini mkabala na Living Stone chenye namba
za usajili 186 na ukubwa wa mraba 750.00 kilikuwa na mali ya Serikali chini ya Wizara ya
Kilimo na Maliasili ambapo Wizara hii ilifikia hatua ya kujenga maghala yake katika kiwanja
hicho. Hata hivyo, Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) ilikihitaji kiwanja hicho kwa ajili ya
ujenzi wa afisi yake na kwa kuwa kulikuwa na majengo yaliyotumika kama ni maghala ya
Wizara ya Kilimo, ZRB ililazimika kupata ridhaa ya Wizara ya Kilimo ya kukitumia kiwanja
hicho. Katika mnasaba huu, ZRB ilipokea barua ya tarehe 2.1.2002 yenye kumbu kumbu namba
UMM/AU/MUN/N.10/11 VOL.IV kutoka kwa Mkurugenzi, Idara ya Ardhi na Usajili ambapo
Mkurugenzi alikiri kwamba Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati ilipokea ombi kutoka
ZRB kuomba kiwanja hicho kwa lengo la ujenzi wa afisi ya Bodi ya Mapato, Unguja. Hata
hivyo, Idara ya Ardhi na Usajili iliwashauri ZRB kuwasiliana na Wizara ya Kilimo na Maliasili
ili waweze kupata maafikiano ya matumizi mapya ya kiwanja hicho (Kielelezo Na. 185).
Aidha, kwa kupitia barua ya tarehe 21/1/2002, Bodi ya Mapato iliiomba Wizara ya Kilimo na
Maliasili kupatiwa kiwanja hicho (Kielelezo Na. 186). Hata hivyo, suala la msingi ni pamoja na
kujiuliza iwapo ZRB iliridhiwa na Wizara ya Kilimo na Maliasili kutumia kiwanja hicho kwa
malengo iliyoyakusudia na kwa kuzingatia barua ya tarehe 28/08/2002 yenye kumbu kumbu
namba WKMMU/29/5/4/1/72 iliyotoka Wizara ya Kilimo na Maliasili na kwenda kwa Katibu
Mkuu, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati inathibitisha kwamba, Wizara haikuwa na
pingamizi na ilikubali ZRB kulitumia eneo hilo. (Kielelezo Na. 187), kwa kuzingatia barua ya
tarehe 9/09/2002 yenye kumbu kumbu namba MUNA/34/14/378 VOL.1 mbayo Wizara ya Ardhi
ilimuandikia Kamishna ZRB kumkabidhi eneo hilo na kuwa tayari kushirikiana nao katika ujenzi
wa afisi ya ZRB. (Kielelezo Na. 188).
Baada ya juhudi zote hizo, ZRB ilifanikiwa kupewa Shahada ya Muda ya Haki ya Matumizi ya
Ardhi (Provision Certificate of a Right of Occupancy) mnamo tarehe 4/4/2003 kwa mujibu wa
166
kifungu cha 11 na 33 cha Sheria ya Umilikaji wa Ardhi, Namba 12 ya 1992 kwa lengo la
kujenga Afisi ya ZRB Unguja na kwa kuzingatia masharti, ikiwa ni pamoja na kutayarisha
michoro ya jengo/majengo lililokusudiwa ambalo/ambayo yamekusudiwa kujengwa kwenye
kiwanja kwa mujibu wa Kanuni za Mipango Miji; kuhakikisha kwamba michoro imepitishwa na
kibali cha ujenzi kimetolewa na Mamlaka husika kabla ya kuanza ujenzi, kwamba ZRB ifuate
taratibu za Mamlaka ya Mipango Miji katika upangaji wa Jengo/Majengo, matumizi ya kiwanja
na urefu wa jengo ama majengo yaliyokusudiwa kujengwa pamoja na kulinda na kuhifadhi kwa
muda wote alama zote za mipaka ya ardhi hiyo (Kielelezo Na.189).
Baada ya hatua hii, ZRB ilifanikiwa kupata kiwanja chengine cha kujenga Ofisi yake sehemu ya
Mazizini, na hivyo kubadilisha uamuzi wa kujenga Ofisi yake katika kiwanja cha Kinazini. Hata
hivyo, tunapaswa tujiulize, baada ya ZRB kuamua kujenga afisi zake Mazizini, badala ya
Kinazini, Je, ilikirejesha kiwanja hicho Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati au iliendelea
kukimiliki na hatimae kukihaulisha kwa taasisi nyengine ama mtu binafsi? Suala hili jawabu
yake ni nyepesi mno, ambapo Kamati ilipomhoji Kamishna wa ZRB Ndg. Mohammed Hashim,
yeye aliithibitishia Kamati kwamba, taasisi yake ilikirejesha Serikalini, kwa maana ilikirejesha
Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kwa kuandika barua ya tarehe 26/8/2009 yenye
kumbu kumbu namba ZRB/M.1/VOL.1/141 (Kielelezo Na.190) na tunapenda kunukuu sehemu
ya barua hiyo kama ifuatavyo:
“Kutokana na ZRB kukabidhiwa hati miliki ya kiwanja kilichopo Mazizini Unguja, ZRB inarudisha rasmi
hati miliki ya kiwanja cha Gulioni kwa matumizi mengine ya Serikali”
Mbali na ZRB kuandika Barua hiyo, lakini pia wameambatanisha na Shahada ya Muda ya Haki
ya Matumizi ya Ardhi, ambayo awali ilikabidhiwa kwake na Wizara husika. Kwa hoja hizi,
inatosha kusema kwamba, Kamati inakubaliana na maelezo ya ZRB kuhusiana na kiwanja hicho
kilivyo haulishwa kutoka mikononi mwa Wizara ya Kilimo hadi kukabidhiwa kwa ZRB kwa
lengo tulokwisha kulieleza. Hata hivyo, kuna haja ya kujiuliza juu ya Wizara ya Ardhi, baada ya
kukabidhiwa kiwanja hicho, je ilitoa taarifa Serikalini kufuta Umiliki halali wa ZRB, au inatosha
kwa barua ya ZRB kuifanya Wizara ya Ardhi, isiwe na sababu nyengine ya kutoa tangazo
angalau katika Gazeti Rasmi la Serikali juu ya ufutwaji wa umiliki wa kiwanja hicho na hatimae
kiwanja kikahaulishwa na kwenda kwa mtu binafsi!
Kamati haikupata ufasaha wa jawabu ya suala hili, katika vikao vyote ilivyofanya na Wizara ya
Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati vilivyokuwa vinasimiwa na Naibu Katibu Mkuu kwa upande
wa Wizara hiyo, wala suala hili halikowazi katika sheria za Ardhi isipokuwa kuna haja ya
kuangalia utendaji wa Wizara (practice). Katika kikao cha tarehe 27/12/2011, Kamati iliweza
kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ndg. Mwalim Ali
Mwalim baada ya juhudi kubwa kupita za kukutana nae na kutoa ufafanuzi wa masuala ambayo
Wizara yake ilishindwa kuyafafanua wakati wote wa Kamati ilipokutana na Wizara yake. Ndg.
Mwalim Ali Mwalim aliieleza wazi Kamati kwamba, kwa uzoefu na wanavyotekeleza Wizara
yake ni kwamba, baada ya kupokea kiwanja kilichorejeshwa na Taasisi yoyote ya Serikali, wao
167
kama Wizara, wanafanya Utambulisho (Aknowledgement) kwa taasisi hiyo kwamba
wamekipokea na baadae hufanya taratibu za kuihaulisha ardhi hiyo kwa mtu mwengine
inapotokezea haja ya kufanya hivyo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa majibu wa utafiti wa Kamati, hakuna Utambulisho wowote uliotoka
Wizarani kuwajuilisha ZRB, jambo ambalo limepelekea utatanishi mwingi ikiwa ni pamoja na
fikra kwamba kiwanja hicho kitaendelea katika uhalali wa matumizi ya ZRB kwa kuwa
walikuwa wamiliki wa awali; kitakuwa chini ya Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kwa
sababu ndio wasimamizi wakuu wa masuala ya ardhi na tayari kiwanja hiki kimesharejeshwa
kwao au Taasisi nyengine yoyote ya Serikali itakuwa na haki ya matumizi yake? Pamoja na hali
hii, utatanishi mkubwa zaidi unakuja kutokana na kiwanja hicho kilichokuwa mali ya Serikali,
kuhaulishwa kwa Kampuni binafsi, wakati Taasisi nyingi za Serikali hazina Ofisi. Suala jengine
la msingi ni kujiuliza, iwapo baada ya kiwanja hicho kurejeshwa Wizarani, je, Wizara ya Ardhi,
Makaazi, Maji na Nishati ilihusika vipi katika kukihaulisha kwa Kampuni hiyo binafsi. Ndg.
Mwalim Ali Mwalim, Katibu Mkuu wa Wizara hii, aliieleza Kamati kwamba, kwa kawaida
Maombi ya matumizi ya ardhi yanatakiwa yapitie kwake kama Katibu Mkuu wa Wizara. Hata
hivyo, watu wengi kwa kutofahamu utaratibu huu, huwa wanayapeleka maombi yao moja kwa
moja kwa Mhe. Waziri na hivyo, kuhusiana na kiwanja hiki, yeye wala Ofisi yake, haina taarifa
yoyote ya kupokea maombi na taratibu zilizofuatwa, isipokuwa Mhe. Waziri, ndie aliyehusika.
Kwa maana nyengine, yeye wala ofisi yake haikuhusika katika umilikishwaji wa kiwanja hiki
kwa Kampuni hiyo.
Majibu haya yanaweza yakakushangaza kidogo, unaweza ukajiuliza: „Inawezekanaje Katibu
Mkuu wa Wizara awe hajahusika na suala hili, tena hana taarifa yoyote kuhusiana na
uhaulishwaji wa kiwanja hicho, wakati Wizara anayoiongoza ndio msimamizi mkuu wa masuala
ya ardhi nchini? Suala kama hili Kamati imeshangazwa nalo kwa muda mrefu, tokea katika
kikao cha pamoja baina yake na Uongozi wa Wizara hii ya Ardhi, hadi wakati wa kukutana na
Katibu Mkuu mhusika, Ndg. Mwalim Ali Mwalim. Aidha, baada ya Kamati kupokea maelekezo
hayo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hii, Ndg. Tahir M.K. Abdullah, katika kikao
hicho, kwamba hata yeye kama Naibu Katibu Mkuu hajui lolote kuhusiana na suala hili, alisema
Naibu huyo kwamba, Katibu Mkuu ndie anaefahamu suala hili katika ngazi ya utendaji, Lakini
kwa bahati mbaya wakati Kamati inafanya majadiliano na Katibu Mkuu huyu, nae kama
alivyojibu Naibu Katibu Mkuu wake, akaeleza kwamba hakuhusika, na ni Mhe. Waziri ndie
mhusika Mkuu.
Kama ni hivyo basi, ni vyema angalau kidogo tukapata maelezo ya Mhe. Waziri wa wakati huo,
aliehusika na masuala ya Ardhi, Mhe. Mansour Yussuf Himid. Mhe. Waziri alipoitwa na Kamati
aliweza kutoa ufafanuzi uliohitajika kwamba, “ni kweli kiwanja hicho hapo kabla kilikuwa cha
Wizara ya Kilimo na baadae wakapewa ZRB, lakini baada ya ZRB kupewa kiwanja chengine
cha Kilimani Bar, ambapo pamoja na kwamba hakikuwafaa walipata kiwanja chengine eneo la
Mazizini, na hivyo kiwanja hiki cha Living Stone wakawa hawana haja nacho, na ndipo
kilipokuja kuombwa na Mama Fatma Karume kwa lengo la kufanya biashara, nae aliamua
168
kumpa Mama Fatma Karume ambae nae baadae aliamua kukiuza kwa Ndg. Ali Shaibu” Mhe.
Mansour alipoulizwa kuhusiana na tatizo la Mama Fatma kukiuza kiwanja hicho ndani ya mwezi
mmoja, akaeleza kwamba yeye hilo halioni kuwa ni tatizo.
Aidha, kuhusiana na utaratibu wa maombi ya kiwanja hicho kama ulifuatwa ama laa, Mhe.
Waziri aliieleza Kamati kwamba utaratibu umefuatwa kwani kulikuwa na maombi rasmi ya
kukiomba kiwanja hicho, ingawaje alishindwa kuwasilisha kwa Kamati ushahidi huo baada ya
kutakiwa kufanya hivyo, na kama Kamati ilivyokwisha eleza hapo kabla, kwamba pamoja na
maneno haya, kwa kuwa hakukuwa na ushahidi, Kamati haiwezi kuyategemea maneno pekee
bila ya ushahidi (mere statements without evidence). Hivyo basi, baada ya kujiridhisha juu ya
umiliki wa kiwanja hicho hapo kabla ya kuhaulishwa kwa Kampuni binafsi, na taarifa za
kiserikali juu ya urejeshwaji wake, ni vyema sasa tukaangalia sababu zilizopelekea kuhaulishwa
kutoka ZRB kwenda Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati na hatimae kikapewa kwa
Kampuni ya F & K Interprises Ltd kama ifuatavyo:
5.3 Kuchunguza sababu zilizopelekea kuhaulishwa kwa kiwanja hicho.
Baada kiwanja hicho kukabidhiwa Wizara yenye majukumu ya kusimamia ardhi, baada ya
mwezi mmoja tu, kilihaulishwa kwa kupewa Kampuni binafsi iitwayo F& K Enterprises
inayomilikiwa na watu wanne wafuatao:
1. Ndg. Khalid Iddi Mabrouk mwenye hisa 51%
2. Ndg. Fatma Karume mwenye hisa 33%
3. Ndg. Vuai Ameir Vuai mwenye hisa 8%; na
4. Ndg. Ramadhan Abdalla Songa mwenye hisa 8%.
Lakini ukifanya marejeo ya mahojiano ya Kamati na aliyekuwa Waziri wa Wizara hii, alisema
kwa uhakika kwamba alikuja kuombwa na Mama Fatma Karume nae aliamua kumpa baada ya
kujiridhisha kwamba yuko sahihi kisheria. Ukitafakari kwa kina na kwa mnasaba wa umiliki wa
Kampuni hiyo ya F & K interprises Ltd, unatapa maswali mengi ya kujiuliza.
Suala la kwanza utajiuliza, kwamba je kiwanja hicho kimepewa mtu binafsi au Kampuni? Lakini
kwa nini kama Kampuni suala hili lisifuatiliwe na Mmiliki Mkuu wa Kampuni hiyo na zaidi
Ndg. Khalid Iddi Mabrouk au kwa taratibu za Kikampuni ambazo ni mawasiliano rasmi (na sio
mtu kusema amefuatwa) na badala yake yeye kama Mhe. Waziri alifuatwa na Mama Fatma
Karume! Je hii haitoshi kuonesha kwamba alipokuwa anafanya maamuzi ya kukitoa kiwanja
hicho, Mhe. Waziri (kama alivyokuwa) amezingatia zaidi heshima ya Mama Fatma Karume na
wala sio Kampuni hiyo? Basi mashaka yako na wasi wasi ulionao, unazidi pale unaposikia
kwamba, mara tu baada ya kupewa kiwanja hicho, tena hata Mhe. Waziri alikiri kwa maelezo
yake mbele ya Kamati kwamba, baada ya mwezi tu kiwanja hicho Mama Fatma, kaamua
kukiuza! Basi ni vyema wasi wasi wako ulionao ukazidi kutoshelezwa na majibu yanayohusiana
na ufafanuzi wa hadidu hii rejea kama inavyoendelea kufafanuliwa.
169
Kwa ufupi, Kamati imefahamu bila ya shaka yoyote kwamba kiwanja hicho kimehaulishwa
kutoka Serikalini kwenda kwa Kampuni binafsi. Hata hivyo, pamoja na kuhaulishwa huko, kuna
masuala ya msingi ya kujiuliza kisheria. Je, kuna sababu zipi zilizopelekea Mhe. Waziri,
Mansour Yussuf Himid, kukihaulisha kiwanja hicho kutoka katika umiliki wa ZRB na kwenda
kwa Kampuni binafsi? Tukianza kulijibu suala hili, ni vyema pia tukajiuliza, Je, kuna ulazima
wowote wa kisheria wa kumtaka Waziri anehusika na ardhi kuwa na sababu maalum za
kuhaulisha ardhi ya Serikali kwenda kwa Mtu ama Kampuni binafsi? Jawabu ya masuala yote
haya ni mfululizo wa vifungu vifuatavyo vya kisheria.
Kwa mujibu wa kifungu cha 3(4) cha Sheria ya Umilikaji wa Ardhi, kama ilivyofanyiwa
marekebisho katika mwaka wa 2003 na mwaka 2010, kimempa mamlaka Waziri
anaeshughulikia masuala ya ardhi kwa kufuata masharti ya Sheria hiyo, kuigawa ardhi ambayo
iko katika mamlaka ya Serikali kwa kuimilikisha kwa watu ama kufuta haki hiyo kwa namna
itakavyofaa. Kifungu hiki kimempa mamlaka kamili (absolute power) Waziri, kwa kuona kwake
inafaa kuhaulisha ardhi yoyote ya umma kwenda kwa mtu yoyote, kwa sharti tu kwamba awe
amefuata masharti ya Sheria hii, na ni kusema kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 23 (a) cha
Sheria hiyo hiyo, kinamtaka Waziri ahaulishe ardhi hiyo kwa aidha kupitia Hati ya Matumizi ya
Ardhi, jambo ambalo amelifanya (Kiambatanisho Nam. 191). Ni kusema tu kwamba, hakuna
ulazima wa kisheria wa kumtaka Waziri husika kutoa sababu za kuhaulisha ardhi hiyo.
Hata hivyo, bado ipo haja ya kulijibu suala hili kwani ni miongoni mwa Hadidu Rejea ndogo
ndogo iliyokabidhiwa kwa Kamati. Kamati ilipohoji sababu za kuhaulishwa kwake katika kikao
chake cha siku ya Jumatatu tarehe 28/11/2011, Uongozi wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na
Nishati kama kawaida yake, ulishindwa kutoa sababu yoyote ya kuhaulishwa kwake kwa
kusisitiza kwamba, suala hili Uongozi wa Wizara hauna taarifa nalo, ni Waziri pekee ndie
aliehusika. Hivyo basi tarehe 07/12/2011 Kamati ilipofanya mahojiano na Mhe. Waziri huyu,
aliieleza Kamati kwamba aliamua kumpa Mama Fatma Karume kwa vile alikiomba kwa
madhumuni ya kufanya biashara. Na kwa hali hii, sababu kuu ya kumpa ni hiyo na sio
nyengineyo.
Bila ya shaka sababu hii inatosha kukuridhisha kufahamu udhati wa suala hili, lakini kwa upande
wa Kamati inaona pia ni busara kupata majibu ya Mama Fatma Karume ambae aliitwa kabla ya
Mhe. Mansour, yaani tarehe 06/12/2011, katika kikao chake na Kamati kilichofanyika katika
Afisi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mama Fatma alieleza kwamba, Kampuni yao ( na
wala sio yeye kama Fatma Karume) walikiomba kiwanja hicho kwa madhumuni ya kutanua
Ofisi yao ya Kampuni.
Ukifanya mahusiano ya majibu haya, baina ya Mhe. Waziri na Mama Fatma Karume, utaona
kwamba, majibu haya yanapingana ingawaje yote yana lengo moja la kibiashara. Aidha, pia nani
alifuatilia suala hili na kama kuna taratibu za maombi na nyenginezo, pia ni suala la utata, iwapo
utayarejea tena majibu ya watu hawa wawili. Mama Fatma Karume alijenga hoja zake zaidi
Kikampuni wakati Mhe. Waziri alijibu kwa mnasaba wa Heshma ya Mama Fatma Karume. Kwa
170
vyovyote vile, Kamati inapenda ifahamike wazi kwamba, suala hili lina shaka nyingi ndani yake.
Aidha, Kamati ilipomuuliza Mama Fatma kwa nini Kampuni yao ilikiuza kiwanja hicho ndani ya
mwezi mmoja tu baada kuhaulishiwa, alijibu kwamba kwa sababu Kampuni yao ilishindwa
kutekeleza madhumuni ya kukiomba kwao, yaani wameshindwa kujenga Ofisi kama
walivyokusudia awali. Hapa pia unazidi kupata mashaka juu ya uhalisia wa kuhaulishwa kiwanja
hicho, kwamba, inawezekana sana sio tu kwamba kimetolewa Serikalini na kupewa mtu binafsi
kwa sababu ya heshima yake, lakini pia inawezekana yale majibu ya Mhe. Waziri ya kuamua
kumpa Mama Fatma Karume kwa sababu ya biashara, ikawa inakusudiwa kwamba, hatua ya
Mama Fatma (ikiwa ni yeye ama Kampuni yake) kuamua kukiuza ndani ya mwezi mmoja, ndio
biashara yenyewe (yaani yeye kapewa bure na Serikali nae akapata faida ya juu kwa juu kwa
kukiuza mamilioni ya Shilingi).
Kamati haikutosheka tu na maelezo ya Mama Fatma Karume kwamba Kampuni yao ilikiomba
kiwanja hicho kutoka Serikalini kwa kufuata taratibu zote (yaani kwa kufata taratibu za
maombi), ilimtaka Mama Fatma awasilishe „Documents‟ zote zinazohusiana na suala hili siku
mbili baada ya kikao hicho. Lakini kwa masikitiko makubwa, mpaka tunatoa taarifa hii, hakuna
ushahidi wowote aliouwasilisha pamoja na kuahidi kwamba angeliwasilisha ushahidi huo kama
alivyotakiwa, haraka iwezekanavyo. Aidha, Kamati ilipokutana na Ndg. Ramadhan Abdalla
Songa ambae pia ni mmiliki wa hisa 8% katika Kampuni hiyo tarehe 29/12/2011, ilimtaka pia
awasilishe „Documents‟ hizo nae aliahidi tayari walikwisha ziandaa na kesho tu, yaani tarehe
30/12/2011 angeliziwasilisha. Kwa bahati mbaya sana, hakuna uthibitisho wowote uliofika
mbele ya Kamati. Basi kwa mnasaba huu, ni vyema sasa tukafahamu namna gani Kamati
imelichunguza suala hili kisheria.
5.4 Kuchunguza iwapo taratibu za kisheria zilifuatwa katika uhaulishaji wa kiwanja
hicho:
Baada ya kujiridhisha kwamba kiwanja hicho kimehaulishwa na Mhe. Waziri kupitia uwezo
aliopewa na sheria Namba 12 ya 1992, suala la kujiuliza je, uhaulishwaji huo umefuata taratibu
za sheria? Ili kujibu suala hili ni vyema tukafuata utaratibu ufuatao:
5.4.1 Maombi ya Kiwanja hicho kutoka kwa F & K Enterprises hadi kwa Waziri:
Kwa kawaida inatarajiwa kuwepo na muongozo wa sheria kumtaka mtu yoyote anaetaka kupewa
ardhi kupitia uwezo wa Waziri anaeshughulikia masuala ya ardhi, kuomba kwa njia ya
maandishi na kuipeleka barua hiyo kwenye Wizara inayoshughulikia masuala hayo. Suala kama
hili hufanyika sana hapa Zanzibar kwa wananchi wote wanaotaka kupatiwa viwanja
vilivyokatwa chini ya usimamizi wa Wizara inayoshughulikia ardhi, hupeleka barua zao
zinazoainisha ombi la kupatiwa ardhi na sababu za kuomba. Hata hivyo, suala hili halijaelezwa
moja kwa moja katika sheria za ardhi wala hakuna ufafanuzi wake katika Kanuni zilizotungwa,
juu ya suala hili. Kama ni hivi, ni vyema tukajiuliza, Je, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na
Nishati inapotumia muongozo huu imefanya makosa kisheria na kuna ubaya gani kwa Wizara hii
171
kuweka utaratibu mzuri kama huu ili kumsaidia Waziri kutekeleza majukumu yake aliyopewa
kisheria?
Jawabu ya suala hili ni kwamba, hakuna kifungu chochote cha sheria kilichoikataza Wizara
inayoshughulikia masuala ya ardhi kuanzisha utaratibu wa kuwataka wananchi kufanya maombi
ya ardhi ikiwa ni pamoja na kueleza sababu za kuomba na matumizi ya ardhi wanayoiomba na
hivyo, kitendo (practice) cha Wizara inayoshughulikia ardhi kuweka utaratibu wa maombi ni
kizuri na kinakubalika. Aidha, kwa upande wa sheria, ni vyema tukafahamu kwamba, suala
lolote ambalo halijakatazwa kisheria, hakuna ubaya wa kulifanya na kitendo cha kulifanya hadi
kuzoeleka na kuwa ni sehemu ya utaratibu, „impliedly‟ kinapelekea kuwa ni sehemu ya sheria na
hivyo ni lazima kifuatwe. Kwa maana hii, pamoja na uwezo aliopewa Mhe. Masour Yussuf
Himid, Waziri aliekuwa anashugulikia masuala ya ardhi 2005-2010, suala la kuangalia iwapo
kiwanja hicho kiliombwa na F & K Interprises ni jambo la msingi sana.
Aidha, Kamati ilipomwita Mhe. Mansour Yussuf Himid, tarehe 07/12/2011, kwa ajili ya
kuthibitisha namna alivyohusika na uhaulishaji wa kiwanja hicho, alikiri mbele ya Kamati
kwamba, kwa mujibu wa utaratibu uliokuweko Wizarani (Wizara iliyoshughulikia masuala ya
Ardhi) ili mwananchi aweze kupewa ardhi, ni lazima atangulize maombi ya ardhi hiyo. Kwa
maana hii, Mhe. Waziri anakusudia kusema kwamba, kama sio utaratibu huu, yeye kama Waziri
anaeshughulikia masuala ya ardhi, kamwe asingeliweza kuitowa ardhi hiyo kutoka Serikalini na
kuwapa Kampuni ya F& K interpreses. Zaidi ya hayo, utaratibu wa ZRB kama Taasisi ya
Serikali kufanya maombi ya kiwanja hicho kwa Wizara iliyokuwa inashughulikia masuala ya
ardhi, hakitakuwa na maana yoyote iwapo mtu binafsi asifanye hivyo, kwamba apewe tu kwa
utashi wa Waziri, jambo ambalo litaendelea kuleta shaka kubwa.
Baada ya hoja hizo, sasa ni wakati wa kujiuliza, Je, kiwanja hicho kimehaulishwa kutoka
Serikalini hadi kwa Kampuni binafsi kupita utaratibu wa maombi ama ni utashi wa Mhe. Waziri
pekee? Ili kulijibu suala hili ipasavyo, ni lazima kuwe na ushahidi wa maombi na namna maombi
hayo yalivyoshughulikiwa na kujibiwa. Aidha, Kamati ilipotaka kupatiwa ushahidi huo wa
maombi katika Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati ilichokuwa kinawakilishwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hii, Ndg. Tahir M.K. Abdullah, tarehe 28/11/2011, lakini kwa bahati
mbaya kama tulivyokwisha eleza hapo kabla kwamba, watendaji hao wa Wizara kwa pamoja na
kwa msisitizo, wakaieleza Kamati kwamba, masuala yote ya jambo hili yanajuulikana na Mhe.
Waziri Mhe. Mansour Yussuf Himid na Katibu Mkuu wa Wizara Ndg. Mwalim Ali Mwalim,
ambae ni Katibu Mkuu wa sasa na kipindi cha uhaulishwaji wa kiwanja hicho. Aidha, Kamati
ilipomwita Mhe. Waziri Mansour, alikiri mbele ya Kamati kwamba, kulikuwa na maombi
yaliyofanywa na F& K Enterprises na barua hizo zote zilikuwepo kwenye faili la barua hizo
lilikuwepo ofisini na anashangazwa kwamba sasa zimetoweka, hazijulikani zilipo.
Hata hivyo, Kamati pia ilimwita Shareholder mmoja wa Kampuni hii, Mama Fatma Karume
tarehe 06/12/2011, alieleza kwamba Kampuni yake ilifanya maombi ya kupewa ardhi hiyo,
lakini alishindwa kuthibitisha ushahidi wa maombi hayo na hivyo, Kamati kwa kauli moja
inathibitisha kwamba hakuna ushahidi wa kuombwa kiwanja hicho na hivyo, ina wasi wasi
172
kwamba, Mhe. Waziri ametumia vibaya madaraka yake, kwamba ameamua kukimilikisha
kiwanja cha Serikali kwa mtu binafsi bila ya maombi yoyote, kinyume na practice iliyopo.
5.4.2 Malipo yoyote yaliyofanyika juu ya uhaulishwaji wa Kiwanja hicho:
Kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Umilikaji wa Ardhi, No. 12 ya mwaka 1992 kinaeleza wazi
kwamba, Mzanzibari hatalipia gharama zenye thamani sawa na ardhi aliyopewa na Mhe. Waziri
anaeshughulikia masuala ya ardhi kwa njia ya „grant‟ lakini atalazimika kulipa gharama ndogo
ndogo zinazoambatana. Aidha, kwa kufuata masharti ya kupewa ardhi hiyo, mwananchi
hutakiwa alipie gharama za uombaji wa ardhi hiyo (Fees Applicable) kama ilivyoelezwa katika
kifungu cha 25 cha Sheria hiyo. Kwa kuzingatia masharti haya, Kamati pia imeona ili
kujiridhisha kwamba kiwanja hicho kimehaulishwa na kupewa F & K Enterprises kwa taratibu
za sheria, ni vyema ikathibitishiwa ama na Wizara inayoshughulikia masuala ya ardhi ama na
Kampuni ya F& K Interprises juu ya malipo yoyote waliyoyafanya ikiwa ni pamoja na gharama
za maombi yao, ili angalau lile lengo la kuisaidia Serikali kuongeza pato lake liweze kuonekana
na kuthibitika kufikiwa.
Kwa bahati mbaya sana, kama Kamati ilivyokosa ushahidi wa maombi ya F & K Enterprises
kupitia kwa Mhe. Waziri, Mama Fatma Karume na hata Ndg. Ramadhan A. Songa ni hivyo
hivyo, ushahidi wa malipo yoyote yaliyofanywa kuhusiana na kuhaulishiwa kiwanja hicho
hayakuweza kuthibitishwa, na kwa maana hii, Serikali imetoa kiwanja chake bila ya kupata faida
yoyote ya kifedha.
5.4.3 Uhaulishwaji wa Kiwanja hicho chini ya Mamlaka inayohusika:
Kama tulivyokwisha eleza awali ni kwamba sheria imezitambua njia tano kuu za umiliki wa
ardhi kwa Mzanzibari ikiwa ni pamoja na Waziri anaeshughulikia masuala ya ardhi kupewa
mamlaka ya kutoa ardhi hiyo kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 7 cha Sheria ya Umiliki wa
Ardhi ya mwaka 1992 pamoja na marekebisho yake yanayohusika. Aidha, kifugu cha 8 cha
sheria hiyo, kimeweka masharti ya namna mamlaka inayohusika, inavyopaswa kuzingatia
usahihi wa masharti ya utoaji wa ardhi hiyo. Kwa mnasaba wa hoja yetu hii, Mhe. Waziri
aliyekuwa akishughulikia masuala ya Ardhi, alitumia vifungu vya 7 na 8 vya Sheria hii, kutoa
Shahada ya Haki ya Matumizi ya Ardhi (Certificate of Right of Occupancy) yenye namba No. Z-
53/S.178/2010/186 na R.O No. Z-135/2010 ambapo Kamati haina pingamizi na uwezo wake
kisheria. Hata hivyo, Kamati inaamini kwamba, mamlaka hayo yametumika vibaya kwanza kwa
Mhe. Waziri kuipa Kampuni F & K interprises kiwanja hicho bila ya maombi yoyote wala
malipo yoyote kinyume na taratibu za sheria zinavyoelekeza, lakini pia kinyume na taratibu za
kiutawala kuhusiana na suala hili, Ofisi yake haikutoa taarifa yoyote ya kukipokea na kwa hatua
zinazofuata kwa ZRB.
5.5 Kiwanja hicho kuuzwa kutoka F& K Interprises hadi kwa Mfanyabiashara binafsi
Ndg. Ali Shaib Khamis:
Ifahamike wazi kwamba, baada ya kiwanja hicho kutoka Serikalini hadi kwa Kampuni ya F & K
interprises katika mwezi wa July 2010, mwezi mmoja tu baadae, yaani mwezi wa August 2010,
kiliuzwa na kwa thamani ya Shiling 150,000,000/ kwa Ndg. Ali Shaib Khamis, mfanya biashara
binafsi. Hapa Kamati inapata masuala mengi sana ya kuhoji ikiwa ni pamoja na nia ya F & K
173
Interprises kupewa kiwanja hicho kama ilikuwa ni kufanya biashara kama ilivyoelezwa na
Mhe.Waziri aliehusika na kuhaulisha kiwanja hicho, au ni kwa ajili ya kufungua Ofisi ya
Kampuni hiyo kama ilivyoelezwa na Bi Fatma Karume, Shareholder wa hisa 33% katika
Kampuni hiyo na baada ya kushidwa kujenga Ofisi yao ndio waliamua kukiuza kwa thamani
hiyo. Au Kamati inaweza kuhoji kwamba kitendo hiki cha kuuzwa kiwanja hicho ndani ya
mwezi mmoja tu ilikuwa ni udalali tu, kwa maana kupewa kiwanja Serikalini kwa njia ya bure
na wao ndio wauze kwa fedha nyingi, fedha ambazo zingelisaidia sana pato la nchi iwapo
zingeliingia Serikalini. Labda tuanze na sababu za Kamati kuwa na shaka juu ya matumizi
yaliyopelekea kiwanja hicho kupewa Kampuni hiyo.
Kwa kawaida, Shahada ya Haki ya Matumizi ya Ardhi inayotolewa na Wizara inayoshughulikia
masuala ya ardhi huwa na masharti yanayomtaka aliyepewa kukitumia kiwanja hicho kama
alivyoomba na kama Wizara inavyoona inafaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Hili
limefanyika pale ZRB walipokabidhiwa Hati hiyo, ambapo kuna masharti matano walilazimika
kuyafuata, ingawaje wakati Wizara inawakabidhi Hati Kampuni hiyo, hakuna masharti yoyote
yaliyotolewa na hivyo, ni sawa na kusema kwamba nia thabiti ya kupewa Kampuni hiyo haiwezi
kuonekana katika Hati. Hata hivyo, kwa kuwa Kamati ilipata maelekezo kutoka kwa mmiliki wa
Kampuni Bi Fatma Karume kwamba, wao F & K waliomba kwa matumizi ya kuanzisha Ofisi na
kuendeleza biashara yao, jawabu ambayo pia ilitolewa na Mhe. Manosur Yussuf Himid alipoitwa
na Kamati alikiri kukitoa kiwanja hicho na kumpa mama Fatma Karume kwa madhumuni ya
kuendeleza biashara zake.
Hata hivyo, Kamati inashangazwa kwa nini Kampuni hiyo ndani ya mwezi mmoja tu ilikiuza
kiwanja hicho kwa fedha nyingi, je kama wao waliomba kwa madhumuni maalum, ni kwanini
tena wauze kwa muda mfupi kiasi hicho? Je, hawakujua kama wasingekihitaji kwa kuwa
hakiwafai katika matumizi waliyokusudia ama tokea mwanzo walikuwa na nia ya kukiuza na
hivyo, walichotaka ni Waziri atumie mamlaka yake kisheria kuwapa ardhi ambayo wao
hawaihitaji bali wanahitaji fedha za kuendeshea na kuendelezea biashara zao? Masuala yenye
muelekeo huu yalipohojiwa kwa Bi. Fatma Karume, yeye alieleza kwamba, baada ya kushindwa
kujenga Ofisi na kuendeleza biashara zao kama ilivyokuwa nia yao ya kuomba, ndipo waliamua
kukiuza kama Mzanzibari yoyote anavyouza mali zake. Aidha, Mhe. Mansour yeye pia haoni
tatizo kwa F & K Interprises kukiuza kiwanja hicho kwani ni haki yao kisheria, lakini kwa
upande wa Kamati hili linatia mashaka, na zaidi baada ya kuuzwa kiwanja hicho, Waziri huyo
huyo alitoa hati nyengine yenye namba L.O.No. Z-53/S.178/2010/186 na R.O.No. Z-150/2010
kumpa Ndg. Ali Shaibu Khamis, Shahada ya Matumizi ya Ardhi iliyotolewa kwa mujibu wa
vifungu vile vile vya 7 na 8 vya Sheria ya Umilikaji Ardhi, Namba 12 ya mwaka 1992.
Suala jengine linaloipa mashaka Kamati ni juu ya ushughulikiwaji wa hati hizi, je kulikuwa na
maslahi ya umma ama maslahi binafsi; na je hakutoi shaka ya kuamini kwamba, mchakato huu
umekwenda kwa haraka mmno kwa kuzingatia maslahi binafsi zaidi kuliko ya umma? Suala hili
linawiyana na hadidu ndogo rejea iliyokabidhiwa kwa Kamati hii, kuchunguza iwapo kuna
maslahi binafsi ama maslahi ya Umma katika uhaulishwaji wa Kiwanja hicho. Tukianza na
kutafuta ufafanuzi wa masuala haya, ni vyema pia tuanze kujikumbusha kwamba, hakukuwa na
maombi ya kuombwa kiwanja hicho kutoka kwa Kampuni ya F & K Inteprises Ltd kwenda
Serikalini, na hivyo, kama tulivyokwisha eleza hapo awali, Kamati haina uwezo wa kusema ni
lini nia ya Mama Fatma Karume na wenzake ilianza utekelezaji wake, Kamati inachofahamu ni
174
tarehe 27/7/2010 Kampuni hiyo ilikabidhiwa rasmi uhalali wa umiliki ama matumizi ya kiwanja
hicho na ilipofika tarehe 13/8/2010 takriban siku 18 baadae F & K Enterprises waliingia
Mkataba wa kuuziana kiwanja hicho kwenda kwa Ndg. Ali Shaib Khamis (Kiambatanisho
namba 192) na siku nne baadae, yaani tarehe 17/8/2010 F & K Inteprises waliomba kubadilisha
jina la Hati yao kwenda kwa Ndg. Ali Shaib Khamis, (Kielelezo Na. 193) na siku hiyo hiyo,
tarehe 17/8/2010 Mhe. Waziri alitoa hati ama alibadilisha jina hilo kwa haraka na utendaji wa
ajabu kabisa. Pia, kwa mnasaba wa barua hii ya F & K Interprises kuomba kubadilisha jina la
hati yao, Kamati inapata mashaka na usahihi wa tarehe iliyoombwa ambayo ni 17/8/2010 na
tarehe ya kupokelewa barua hiyo katika Idara ya Ardhi na Usajili, tarehe 19/8/2010 na
iliposhughulikiwa tarehe 19/8/2010. Kwa maana hii, Mhe. Waziri alithubutu kushughulikia hati
ya Ndg. Ali Shaibu Khamis ama kubadilisha jina la hati ya F&K Interprises kwenda kwa mtu
mwegine kabla ya kuombwa kufanya hivyo, yaani yeye alitoa hati hiyo kwa Ndg. Ali Shaibu
Khamis tarehe 17/8/2010 wakati maombi yamepokelewa ofisini siku mbili baadae, yaani tarehe
19/8/2010.
Kwa bahati nzuri, wajumbe wa Kamati hii pia ni wajumbe wa Kamati za Kudumu za Baraza la
Wawakilishi, ikiwa ni pamoja na Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali
(P.A.C), Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa, Kamati ya Maendeleo ya
Wanawake na Ustawi wa Jamii na Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na Habari, ambapo
wanashuhudia kwamba, wananchi wengi wanyonge pamoja na Taasisi nyingi za Serikali
kukoseshwa hati miliki ikiwa ni pamoja na Shahada ya Haki ya Matumizi ya Ardhi, kwa muda
zaidi ya miaka 10, 5 n.k, na jambo linalosikitisha ni kwamba, taasisi hizi hupeleka maombi
Wizarani hapo na kufuata taratibu zote zinazoelekezwa na Wizara husika, ila matokeo yake
hupewa taarifa za kushughulikiwa maombi yao bila ya utakelezaji wowote, leo Kampuni binafsi
inapewa kiwanja bure bila ya maombi yoyote wala kulipia gharama zozote tena kwa maslahi
binafsi ya kuuza baada ya siku 18 kwa gharama kubwa Tsh. 150,000,000/- na mnunuzi kupewa
hati ndani ya siku nne, hili ni jambo la kuishangaza Kamati na kuipa wasi wasi mkubwa huenda
Mhe. Wazir alitumia mamlaka yake kwa kufahamu matokeo ya kukitoa kiwanja hicho kutoka
Serikalini hadi kwa mtu binafsi.
5.6 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari wa
mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali juu
ya hatua za kuchukuliwa.
5.6.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Kamati imebaini kwamba, kuhaulishwa kwa ardhi hii kumezingatiwa kibiashara
zaidi na sio kwa haja halisi ya matumizi ya ardhi husika.
Yaani, Kamati inakusudia kwamba, kwa kawaida Serikali inapofanya uhaulishaji wa
ardhi kwa wananchi wake hufanya kwa kuzingatia hali halisi ya maisha na haja ya
matumizi ya mwananchi huyo, kwa maana, huwasaidia wananchi wake wanyonge.
Lakini ardhi hii haikuhaulishwa kwa msingi huo.
175
(ii) Pamoja na Sheria ya Ardhi kutoa mamlaka makubwa kwa Mhe. Waziri
anaehusika na masuala ya ardhi kuweza kuihaulisha ardhi ya Serikali kwa
mwananchi, ni wazi kwamba mamlaka hayo yalitumika vibaya kwa kuzingatia
zaidi maslahi ya biashara na maslahi binafsi na sio maslahi ya umma.
(iii) Uhaulishaji wa ardhi hii umezingatia zaidi maslahi binafsi na wala sio maslahi ya
umma.
5.6.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo tuliouonesha hapo juu, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo
zichukuliwe:
(i) Uhaulishwaji wa kiwanja hicho haukuzingatia masharti ya utolewaji wake kama
yalivyokusudiwa na Sheria, hivyo, Kamati inapendekeza kiwanja hicho kirudi
Serikalini mara moja.
(ii) Kuna haja ya kuifanyia marekebisho Sheria ya Umiliki wa Ardhi, Namba 12 ya
mwaka 1992, ili isitoe mamlaka yasiyo na mipaka ya Mhe. Waziri kuhaulisha
Ardhi ya Serikali.
(iii) Kuna haja ya kufanya marekebisho ya Kanuni zinazohusiana na masuala ya ardhi
ili zitoe utaratibu wa Maombi ya matumizi ya ardhi kwa mtu yoyote anaehitaji na
yawe kwa kupitia Katibu Mkuu wa Wizara inayohusina na masuala ya ardhi.
HADIDU REJEA YA TANO:
6.0 UHALALI WA MIKATABA YA NYUMBA YA SERIKALI ILIYOPO KIPONDA
INAYODAIWA KWAMBA ALIPEWA MWANANCHI NA KUIUZA KWA MTU
MWENGINE.
6.1 Utangulizi:
Katika Hadidu hii rejea, Kamati ilitakiwa kuchuguza juu ya uhalali wa Nyumba ama gofu
Namba 755/756 iliyopo Kiponda iliyodaiwa kwamba ni milki ya mwananchi na aliamua kuiuza
kwa Ndg. Amina Aman Abeid Karume. Katika uchunguzi wake Kamati iliagizwa iangalie kama
Nyumba hiyo bado ni milki ya Serikali na kwa utaratibu gani uliotumika kuimiliki Nyumba hiyo.
Aidha, iangalie ni kwa utaratibu gani iliihaulisha nyumba hiyo kwa mwananchi vipi mwananchi
huyo ameiuza kwa mwananchi mwengine, lakini kubwa zaidi kuangalia uhalali wa Mikataba
hiyo kisheria na athari zake. Na mwishowe kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukua katika
kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Katika kuifanyia kazi hadidu hii rejea, Kamati ilikutana na Taasisi zinazohusika ikiwa ni pamoja
na Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati pamoja na Idara ya Nyumba, Afisi ya Mrajis
Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo. Aidha, kwa
mujibu wa madadiliano na haja ilipojitokeza, Kamati ilimwita Sheha wa Shehia ya Kiponda siku
176
hiyo hiyo na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja. Aidha tarehe 06/12/2011, Kamati ilimwita Ndg.
Amina Amani Abeid Karume katika Afisi za Baraza la Wawakilishi na kufanya mahojiano nae,
kama ilivyomwita Ndg. Juma Ali Kidawa, mwananchi anaedaiwa kuuziwa nyumba hiyo tarehe
27/12/2011. Vile vile baada ya Kamati kupata taarifa za kuhusika kwa Ndg. Ramadhan Abdalla
Songa, iliamua kumwita tarehe 29/12/2011 na hatimae Kamati imepata ufafanuzi uliohitajika.
Hivyo, ili kufikia lengo tulilolikusudia, ni vyema sasa tukafanya uchambuzi wa masuala
yafuatayo:
6.2 Umiliki halali wa Nyumba hiyo, Namba 755/56 Kabla ya Kutaifishwa na Serikali:
Kamati imepokea taarifa tatu tofauti kuhusu wamiliki wa asili wa Nyumba hiyo kabla
haijataifishwa na Serikali. Tukianzia na barua iliyowasilishwa kwa Kamati na Mzee Juma Ali
Kidawa, alipokuwa akiomba hati miliki ya nyumba hiyo kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji,
Ujenzi, Nishati na Ardhi tarehe 13/10/200334
alisema kwamba, nyumba hiyo ilikuwa inamilikiwa
na Mhindi aitwae Bi Fatu Balu na alipofariki alirithiwa na mtoto wake Bi Katija Gulam Hussein
Bhanji Punja, ambae pia wakati huo alikwisha tangulia mbele ya haki. Aidha, Ndg. Amina Aman
Abeid Karume nae aliwasilisha ushahidi wa kimaandishi kwamba nyumba hiyo mmiliki wake
alikuwa ni Baniani wa kabila la Bhatia alieitwa Ebji Siwji na alipofariki mwaka 1946, nyumba
hiyo aliuziwa Ndg.Sharadchandra Rattansi tarehe 30/06/1952. Na kwa ushahidi wa tatu ni barua
ya Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati ya tarehe 30/4/2004 yenye kumbu kumbu namba
MUNA/18/24/C.73/94 VOL.V iliyopelekwa kwa Mrajis Mkuu wa Serikali ikitoa ufafanuzi wa
usahihi wa umiliki halali wa Nyumba hiyo, kwamba kwa mmiliki wake wa asili alikuwa ni Ndg.
Saerad Chandra R. Jivandas. (Kielelezo Na. 194)
Hakuna ulazima kwa Kamati kuamua ni nani alikuwa mmiliki halali wa Nyumba hiyo, kutokana
na kwamba, tayari ilikwishataifishwa na Serikali, ila barua ya Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji
na Nishati tuliyoinukuu hapo juu, iko sahihi zaidi kisheria ukilinganisha na ushahidi mwengine
uliotolewa. Hata hivyo, ili Kamati iweze kuchambua uhalali wa mikataba iliyohusika na uuzwaji
wa nyumba hii, ni vyema pia kumfahamu Ndg. Juma Ali Kidawa na kufahamu uhusiano wake na
Ndg. Amina Aman Abeid Karume, ambao ndio walioonekana kuhusika na mkataba wa uuzwaji
wa Nyumba hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ilizozipokea, Kamati inakubaliana na ukweli kwamba, Ndg. Juma Ali
Kidawa alikuwa mfanyakazi ama mtumishi wa Mhindi aliyeaminika kuwa ni mmiliki halali wa
nyumba hiyo, kabla ya nyumba hiyo kutaifishwa na Serikali. Na katika utumishi wake, alikuwa
amekabidhiwa mali nyingi za Boss wake na kuzisimamia. Alipofariki Boss wake, Mzee Juma
Ali Kidawa aliiambia Kamati kwamba jamaa wa marehemu walimtaka awaoneshe mali za ndugu
yao na yeye alifanya hivyo. Alipewa fursa ya kuchagua mambo mawili, ama apewe sehemu ya
mali hizo ikiwa ni pamoja na nyumba zilizopo Katika Shamba la Marehemu, katika eneo la
Jumbi au apewe Nyumba hiyo iliyopo Kiponda, Namba 755/56, na kwa bahati nzuri alichagua
kupewa nyumba hiyo tunayoizungumzia. Hata hivyo, pamoja na maelezo mazuri ya Ndg. Juma
Ali Kidawa, Kamati haikupata ushahidi wowote wa kupewa Nyumba hiyo, ama kutoka kwa
Mmiliki wa asili ambae ndie Boss wake wala kwa ndugu wa Marehemu, ispokuwa ametoa Hati
34
Barua hii haina saini ya muandikaji, hivyo Kamati haiichukui kama ushahidi bali baadhi ya taarifa zilizomo
zinaweza kuisaidia Kamati kupata ufafanuzi wa baadhi ya mambo.
177
ya Zawadi (Deed of Gift) (Kielelezo Na. 195) ambayo haijasajiliwa wala haina uhusiano na
maelezo yaliyotolewa mbele ya Kamati (Collaborative Evidence) na pande nyengine
zilizohojiwa.
Aidha, katika hati hiyo saini ya Ndg. Ali Juma Ali iliyopo sehemu ya Mtoaji Zawadi (Donor)
inaleta utata juu ya usahihi wake, kwa sababu yeye hakutajwa kama ni Donors. Aidha, sehemu
ya mashahidi hazijatiwa saini, pia hati hii imefanywa mwaka 2005, wakati tayari nyumba hiyo
imeshataifishwa na Serikali. Kwa ujumla hati hii haiwezi kuwa kielelezo sahihi kwa Kamati.
Aidha, Ndg. Juma Ali Kidawa ameeleza kwamba alikuwa na ushahidi kamili wa umiliki wa
Nyumba hiyo isipokuwa vielelezo hivyo vimeungua moto kutokana na nyumba yake iliyokuwa
Fuoni kuungua moto. Kwa bahati mbaya sana Kamati haiwezi kuyachukua maelezo haya kuwa
ni ushahidi wa umiliki halali wa Nyumba hiyo kwa Bw. Juma Ali Kidawa. Zaidi ya hayo, Ndg.
Juma Ali Kidawa aliwasilisha barua ya tarehe 7/5/2003 kutoka kwa mdogo wa Marehemu Bi.
Khatoom Lalji Nanji Punja wa Migombani Zanzibar na Ndg. Nasim Lalji Nanji Punja wa Vuga
Zanzibar kwa lengo la kuthibitisha kwamba nyumba hiyo ni ya ndugu yake. Hata hivyo, Kamati
haiwezi kutegemea ushahidi huu kwa sababu hauna sifa za kuwa ushahidi sahihi wa kisheria
ikiwa ni pamoja na kukosa saini yoyote, pia inaleta utata juu ya mwandishi wake wakati anuani
ya alieandikiwa barua hiyo haionekani. (Kielelezo Na. 196)
6.3 Utaifishwaji wa Nyumba hiyo kwenda Serikalini:
Kamati imekubaliana na ushahidi uliotolewa mbele yake, kwamba Nyumba hiyo imetaifishwa na
kuwa mali ya Serikali, kupitia „Legal Notice‟ No. 5 ya mwaka 1978 na kutiwa katika gazeti
rasmi la Serikali tarehe 15/5/1978. Aidha, kwa mnasaba huu, Kamati pia ilipata maelezo kutoka
kwa Mzee Juma Ali Kidawa kwamba alipokuwa akifuatilia hati miliki ya nyumba hiyo kupitia
Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali, hakuweza kupatiwa kwa sababu nyumba tayari ilikuwa
imeshataifishwa. Aidha, maelezo haya Kamati iliyapata katika kikao cha pamoja na Wizara ya
Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati pamoja na watendaji wa taasisi nyengine zinazohusika na suala
hili tarehe 29/11/2011. Aidha, pia kupitia Sheha wa Shehia ya Kiponda aliyeitwa na kutoa
ushahidi wake mbele ya Kamati. Hivyo basi, Kamati inajiridhisha kwamba, suala la umiliki wa
nyumba hiyo ikiwa ni kwa mhindi yoyote anaesadikiwa kuwa ni mmiliki wa asili au baada ya
mmiliki huyo kumpa Bw. Juma Ali Kidawa kwa njia yoyote ile, iwe kwa Hiba“Gift” ama
vyenginevyo, hakuwezi kusimama kisheria kwani Tangazo la kutaifishwa nyumba hiyo
linaondosha uhalali wa umiliki wa nyumba hiyo kwa mwananchi yoyote aliyeimiliki hapo kabla.
Kwa maana hii, Bw. Juma Ali Kidawa hawezi kuwa mmiliki wa nyumba hii isipokuwa kwa njia
nyengine inayokubalika kisheria.
6.4 Uuzwaji wa Nyumba hiyo baada ya kutaifishwa na Serikali:
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati aliihakikishia Kamati kwamba,
baada ya Ndg. Juma Ali Kidawa kushindwa kupatiwa hati miliki ya nyumba hiyo kutokana na
ukweli wa kutaifishwa kwake, na baada ya nyumba hiyo kuanguka na kubaki gofu, alipokea
maombi yake kutaka kuuziwa gofu hilo na kwa hali hii, Katibu Mkuu, Ndg. Mwalim Ali
Mwalim alikwenda kumshauri Mhe. Waziri wa Ardhi naye alikubali kuuzwa nyumba hiyo kwa
Ndg. Juma Ali Kidawa. Tarehe 23/4/2007, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na
Nishati, alitoa hati ya umiliki wa kiwanja ama gofu hilo na kuwa milki halali ya Ndg. Juma Ali
178
Kidawa. Na kwa kupita hatua hii, tarehe 22/06/2007 Ndg. Juma Ali Kidawa aliuza gofu hilo kwa
Ndg. Amina Aman Abeid Karume kwa thamani ya Tsh. 15,000,000/-. Hata hivyo, kuna haja ya
kujiuliza juu ya uhalali wa Mikataba hiyo ya Uuzaji, je ni kweli ilihusika na wahusika (parties)
waliotajwa katika mikataba hiyo na je mikataba hiyo imefuata vigezo vya kisheria katika
kufungwa kwake? Ili kupata ufafanuzi wa masuala haya, ni vyema sasa tukafuatilia vipengele
vifuatavyo:
6.5 Mamlaka iliyohusika na kutoa Hati Miliki hizo (Sale Deed):
Kama tulivyokwisha eleza hapo awali kwamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi,
Maji na Nishati Ndg. Mwalim Ali Mwalim alikwishakiri kwamba ni yeye aliyetoa hati hiyo
kupitia Wizara yake kama ushahidi wa saini unavyoonekana katika hati hiyo (Kielelezo Na. 197)
kwa maana hii, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati ndio iliyohusika na uuzaji wa
nyumba hiyo kwa thamani ya Tsh. 5,000,000/-. Aidha, kwa upande wa Hati miliki inayoonesha
kuuzwa tena kutoka katika umiliki wa Juma Ali Kidawa kwenda kwa Amina Aman Abeid
Karume, Kamati imehakikishiwa kwamba hati hiyo imefanywa na Afisi ya Mrajis Mkuu wa
Serikali, wakati huo ndio iliyokuwa inahusika na hati hizo. Kwa maana hii, kuna kila haja ya
kuangalia namna ya Ofisi hizi mbili za Serikali zilivyohusika na uhalali ama ubatili wa hati hizi.
6.6 Uhalali wa Hati Miliki ya Uuzwaji wa Nyumba hiyo kwa Ndg. Juma Ali Kidawa:
Suala la awali ambalo kila mtu angejiuliza, je, hati miliki aliyopewa Ndg. Juma Ali Kidawa
kutoka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati ina mapungufu yoyote ya kisheria? Kamati
pia imelichunguza suala hili na kujiridhisha kwamba, Hati hiyo imekamilika kisheria na iko
sahihi. Hata hivyo, baada ya kupata shaka kuhusu uhalali wa saini ya Juma Ali Kidawa ambae
katika Nyaraka zote alizotia saini yake na kuwasilishwa kwa Kamati, ikiwa ni pamoja na
kitambulisho chake cha Mzanzibari, baadhi ya barua alizoandika, zinaonesha kwamba hatii saini
ya dole gumba inayoonekana katika hati hiyo ya ununuzi wa Nyumba hiyo. Kwa maana hii, saini
ya Mnunuzi wa Nyumba hiyo sio ya Ndg. Juma Ali Kidawa kama inavyoonekana. Aidha, ili
kujiridhisha zaidi, Kamati ilimhoji Ndg. Amina Aman Abeid Karume nae alisema kwamba
anakumbuka kuna kijana anaitwa „Songa‟ yaani Ndg. Ramadhan Abdalla Songa, ambae alidai
kuwa ni mtoto wa Juma Ali Kidawa na kwamba yeye ndie aliemtaka amshughulikie katika
ununuzi wa nyumba hiyo na hata kuiuza kwake. Kwa maana hii, yeye Ndg. Amina Aman Abeid
Karume hapo awali hakumjua Ndg. Juma Ali Kidawa, isipokuwa alimjua huyo mtoto wake na
kwa kuwa kijana huyu ana uhusiano wa karibu na mama yake, yaani Mama Fatma Karume, huku
akiamini kwamba ni kweli yeye ni mtoto wa Mzee Juma Ali Kidawa na katumwa na baba yake
na hiyo saini ni saini ya Juma Ali Kidawa.
Kuhusu Ndg. Ramadhan A. Songa, Kamati iliwahi kufanya mahojiano na Mama Fatma Karume,
ambae alimtambua Ndg. Ramadhan A. Songa kuwa ni fundi wake wa masuala mbali mbali na
alimtumia hata kusimamia ujenzi kadhaa wa masuala yake. Mbali na hayo, alimtambua kama ni
Mmiliki wa Hisa katika Kampuni yake ya F&K Interprises Ltd. Kuhusu kuhusika kwake na na
suala hili, Mama Fatma alieleza kwamba, Kijana huyu Songa alimfuata akimwambia kwamba
kuna babu yake anaitwa Juma Ali Kidawa, ni mmiliki wa Nyumba Namba 755/56 aliyopewa na
Mhindi na anataka amsaidie kupata Warka wa Nyumba hiyo. Suala hili lilimfanya aone ipo haja
ya kumsaidia na ndipo alipokwenda Mambo Msiige kwa ajili ya kumtafutia Warka huo. Kwa
179
bahati nzuri alikwenda na huyo Mzee Juma A. Kidawa, lakini hakuingia ndani na yeye Mama
Fatma aliingia ndani na kufuatilia Warka huo. Hata hivyo, aliambiwa kwamba nyumba hiyo
imeshataifishwa ni lazima auziwe, na ndipo Mama Fatma aliendelea kumsaidia kwa utaratibu
huo, lakini ilipofikia kwamba atoe Tsh. 5,000,000/- ili auziwe, Mzee huyu masikini hakuwa nazo
na ndipo alipomtafuta Amina Aman Abeid Karume, aliyemsaidia pesa hizo kwa kumkopesha na
alifanikiwa kuinunua kwa bei hiyo ya Tsh. 5,000,000/-.
Ni vyema pia tukapata muendelezo wa maelezo haya kupitia kwa Ndg. Songa. Kamati pia
ilimwita Ndg. Ramadhan Abdalla Songa tarehe 29/12/2011 na kumtaka atoe ufafanuzi wa
masuala mengi ikiwa ni pamoja na suala hili, nae kwa kuendeleza hapa tulipofikia, alieleza
kwamba, yeye si Mjukuu wala Mtoto wa Mzee Ali Juma Kidawa, lakini anakumbuka kuna watu
wanne walifika nyumbani kwa Mama Fatma kuomba msaada wa kusaidiwa kutengenezewa
warka na siku ya pili alikwenda huyo Bw. Juma Ali Kidawa ambae alimtaka msaada wa
kumuona Mama Fatma kwa ajili hiyo ya kupata warka. Mzee Juma alikubaliwa kusaidiwa na
ndipo wakapanga kukutana Mambo Msiige ambapo yeye Ndg. Songa na Mama Fatma waliingia
ndani kufuatilia warka, huku Mzee Juma Ali Kidawa akiwa nje. Kwa bahati nzuri walipokutana
na Ndg. Rajab Khatib, Msaidizi Mrajis wa Mrajis Mkuu wa Serikali alishindwa kuwasaidia
kwani alifanya mawasiliano ya kiutedaji na Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi na kupata taarifa
kwamba nyumba hiyo imetaifishwa.
Mama Fatma alikwenda kwa Katibu Mkuu (Ndg. Mwalim Ali Mwalim) na kuongea nae ili
amsaidie Mzee Juma kuimiliki nyumba hiyo, lakini alimzungusha kwa muda mrefu sana na
ndipo siku moja Ndg. Songa alizungumza na Ndg. Amina kuhusu tatizo hilo ambapo Ndg.
Amina alimpigia simu Katibu Mkuu kumuomba amsaidie Ndg. Juma Ali Kidawa, kwa bahati
nzuri alifanya hivyo kwa kuwauzia kwa Tsh. 5,000,000/-, ambazo alitoa Ndg. Amina. Ikafika
wakati fedha hizo zinahitajika kwani msaada ule wa fedha ulikuwa ni mkopo, hali iliyomfanya
Mzee Juma Ali Kidawa na wale watu wanne waliomfata Mama Fatma kuhusu nyumba hiyo, kwa
khiyari zao kuamua kumuuzia Ndg. Amina kwa Tsh. 25,000,000/- ambapo Amina pia alitoa Tsh.
10,000/- kumpa Songa awape wazee hao wakalipie kwa Sheha. Ndg. Songa alipewa Tsh.
25,000,000/- kutoka kwa Ndg. Amina kama mauziano halali ya nyumba hiyo, nae alitoa Tsh.
5,000,000/- kulipia deni la Ndg. Amina, Tsh. 3,000,000/- alilipwa yeye kwa kazi nzuri ya udalali
na kuwaachia Tsh. 17,000,000 wazee wote wanne na Mzee Juma kwa idadi ya wazee watano.
Anachoamini Ndg. Songa ni kwamba, wazee hao wanne waligawana fedha hizo bila ya kumpa
kitu Mzee Juma A. Kidawa ama walimlipa fedha kidogo na ndio Mzee huyu hakuridhika na
matokeo yake akatafuta njia ya kudai hajauza nyumba ili apate fedha nyingi zaidi na hili
analifanya kwa kusaidiwa na vijana wengine.
Kutokana na utatanishi baina ya majibu haya, Kamati ikamuita Ndg. Juma Ali Kidawa siku ya
Jumanne, tarehe 27/12/2011 ili kupata uhakika wa namna alivyohusika na mkataba huo, ambapo
yeye alikana kuhusika kwake katika mikataba hiyo, kwamba hakuwa mnunuzi wa Nyumba hiyo,
na saini iliyotiwa sio yake na wala hakuwahi kumtuma mtu yoyote kununua nyumba hiyo, wala
kutengeneza hati miliki. Maelezo kama haya aliyakiri Ndg. Juma Ali Kidawa katika barua yake
aliyoipeleka kwa Mhe. Abubakar Khamis Bakari, Waziri wa Katiba na Sheria tarehe 15/07/2011
baada ya suala hili kujadiliwa kwa mara ya kwanza katika Baraza la Wawakilishi, ambapo kama
tunavyomnukuu kwa muhtasari hapa chini, hakuwahi kuomba hati miliki ya gofu hilo:
180
“Nazidi kusisitiza kwamba, sijaomba wala sijadai kisheria ghofu iliyotajwa hapo juu (yaani ghofu
lililokuwa Nyumba Namba 755/756) kwa sababu ghofu hilo lilitaifishwa na Serikali na sina nyaraka na
ushahidi wowote kuwa nina haki na ghofu hilo” (Kielelezo Na 198)
Maelezo kama haya pia yaliwahi kutolewa na Sheha wa Kiponda Ndg. Issa Gwisa Issa kwamba,
baada ya suala hili kujadiliwa katika Baraza la Wawakilishi, Ndg. Juma Ali Kidawa aliwahi
kufika kwa Sheha huyo na kuthibitisha kwamba, yeye baada ya kufuatilia suala hilo Serikalini na
kuambiwa Nyumba hiyo tayari ilitaifishwa, basi hakuwahi tena kujihusisha nalo na hivyo,
hahusiki na sahihi za mikataba yote ya kuuzwa na kununua kwake.
Pamoja na maelezo hayo, kutokana na hali hii, Kamati ilihitaji kujiridhisha zaidi juu ya uhalali
wa saini iliyotiwa na Mzee Juma Ali Kidawa katika hati hiyo ya ununuzi, na kwa kutumia
mlinganisho wa saini anazotia katika maandishi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kitambulisho
chake cha Mzanzibari chenye namba 290133628 (Kielelezo Na. 199) na kwa kuzingatia Nyaraka
nyengine zilizowasilishwa kwa Kamati, ikiwa ni pamoja na barua aliyoiandika na kuisaini na
kumtumia Mhe. Abubakar Khamis Bakary, (Rejea Kielelezo Na.198) Kamati imejiridhisha
kwamba, hati hii haikupata saini ya Ndg. Juma Ali Kidawa bali ilisainiwa na mtu mwengine
asiyekuwa yeye kupitia jina lake.
6.7 Uhalali wa Hati Miliki ya Uuzwaji wa Nyumba hiyo kwa Ndg. Amina Aman Abeid
Karume:
Hapa tunakusudia kusema, kama alivyoeleza Ndg. Songa, na kama awali ilivyothibitishwa na
Ndg. Amina Aman Karume kwamba aliuziwa nyumba hiyo na Ndg. Juma Ali Kidawa. Kwa
mnasaba huu, ipo haja ya kuangalia uhalali wa Mkataba huo wa Mauziano baina ya Ndg. Juma
Ali Kidawa kama Muuzaji na Ndg. Amina Aman Abeid Karume kama Mnunuzi wa Nyumba
hiyo Namba 755/56. Bila ya shaka jawabu ya suala hili inategemeana sana na usahihi wa umiliki
wa hati ya awali tuliyoieleza hapo awali. Kwa maana hii, kwa kuwa hati ya awali ya tarehe
23/4/2007 imemhusisha Mnunuzi, Ndg. Juma Ali Kidawa ambae ununuzi wake umehusika na
udanganyifu na kwa kuwa udanganyifu ni moja kati ya mambo yanayoufanya Mkataba wowote
wa kisheria kuwa batili (void) ni wazi kwamba, ununuzi wa Nyumba hii kutoka kwa Juma Ali
Kidawa kwenda kwa Amina Aman Abeid Karume nao ni batili.
Aidha, miongoni mwa sababu nyengine zinazoufanya Mkataba huu (Warka) baina ya Juma Ali
Kidawa na Amina Abeid Aman Karume uwe na alama za udanganyifu ni utambulisho wa Mzee
Juma Ali Kidawa ambapo kwa mujibu wa Hati hiyo Juma Ali Kidawa amejitambulisha kuwa ni
Mzanzibari mwenye Kadi namba 030060722. Kwa kuwa suala la usahihi wa kadi yoyote ya
Mzanzibari linasimamiwa na Afisi ya Usajili na Kadi za Utambulisho-Zanzibar, tarehe
06/12/2011 Mwenyekiti wa Kamati alimuandikia barua Mkurugenzi wa Afisi hii yenye kumbu
kumbu namba BLW/K.10.18/47 (Kielelezo Na.199) kuomba Kamati ithibitishiwe juu ya usahihi
wa mwenye namba hiyo kwamba ni Juma Ali Kidawa, ambapo siku hiyo hiyo na kwa
uwajibikaji mzuri, Ndg. Mohammed Juma Ame, Mkurugenzi wa Usajili na Kadi za Utambulisho
alimjibu Mwenyekiti kwamba kwa mujibu wa uchambuzi walioufanya, Afisi yake imegundua
kuwa mwenye namba ya kitambulisho 030060722 ni Ndg. Khamis Khalid Makame na sio Ndg.
Juma Ali Kidawa (Kielelezo Na.200). Kwa maana hii, utambulisho wa Ndg. Juma Ali Kidawa
kwamba ni Muuzaji wa Nyumba hiyo una mashaka kisheria na umekusudia kumhadaa Mnunuzi
181
wa Nyumba hiyo na kwa mujibu wa maelekezo ya kifungu cha 17(b) cha Sheria za Mikataba,
Sura ya 149 ya Sheria ya Zanzibar kinavyobainisha kwamba, Udanganyifu pia hutokea pale
ambapo Mtu mmoja katika Mkataba ameamua kuficha ukweli anaoujua ama kwa kadiri ya
usahihi wa jambo anavyoamini dhidi ya mtu mwengine kwa lengo la kumfanya mtu huyo aingie
katika Mkataba husika.
Sasa tunaamini katika hali kama hii, kwamba Taasisi iliyohusika na Utengenezaji na hatimae
kutoa warka ama Mkataba huo, nayo haikutekeleza majukumu yae ipasavyo. Kwa mfano, leo
watu wawili waliouziana Nyumba, inakuwaje Warka ama Mkataba huo ushughulikiwe na
upande mmoja na sio wote wawili. Ama kwa mfano, baada ya kufika kwa taarifa zinazohusika
na upande huo ama pande zote mbili, kwa nini Taasisi hii isifuatilie ikafahamu ukweli na udhati
wa taarifa zilizowasilishwa? Ni wazi kama hili lingelitendeka, udhaifu huu wa taarifa za Ndg.
Juma Ali Kidawa ungelifahamika mapema na hivyo Afisi ya Mrajis kama Msimamizi wa
Serikali katika usajili wa Warka kwa wakati huo isingejiingiza katika aibu hii isiyovumilika.
Pamoja na Mkataba uliotajwa hapo juu kuwa ndio uliotambuliwa na Wizara ya Ardhi, Makaazi,
Maji na Nishati pamoja na Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali ambayo katika miaka ya 2007
ilikuwa inahusika na Uratibu wa Warka za Nyumba, Kamati imeshtushwa na hatua ya Ndg.
Amina kuwasilisha mbele ya Kamati Shahada ya Muda ya Haki ya Matumizi ya Ardhi yenye
Namba L.O.No. Z.53/S.34/2007/1 & 2 na P.C.R.O.No. Z.90/2007 iliyotolewa tarehe 17/04/2007
(Kielelezo Na.201), inayoonesha kwamba Nyumba hiyo hakuuziwa na Ndg. Juma Ali Kidawa
wakati maelezo yake aliyoyatoa mbele ya Kamati pamoja na maelezo ambayo Kamati imeyapata
kutoka kwa Wizara husika. Aidha, Kamati pia ilihakikishiwa na Bi Fatma Karume kwamba Ndg.
Amina aliuziwa nyumba hiyo na Ndg. Juma Ali Kidawa na sio vyenginevyo. Pamoja na maelezo
haya, Ndg. Amina aliwasilisha kwa Kamati hati hiyo ya umiliki wa ardhi aliyoipata kupitia
Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Mansour Yussuf Himid iliyotolewa kwa
kutumia kifungu cha 11 na 33 cha Sheria ya Umilikaji Ardhi, Namba 12 ya mwaka 1992,
inayompa uwezo Mhe. Waziri anaeshughulikia masuala ya ardhi kuhaulisha ardhi na
kummilikisha mwananchi kwa mujibu wa masharti yaliyotajwa katika kifungu cha 8(1) cha
Sheria hiyo.
Tunalotaka lifahamike hapa ni kwamba, Ndg. Amina amewasilisha hati mbili tofauti za umiliki
wa Nyumba Namba 755/56 , moja ni kuuziwa na mwananchi mwengine ambae ni Ndg. Juma Ali
Kidawa kama maelezo ya kifungu cha 7 (d) cha Sheria Namba 12 ya mwaka 1992
yanavyoruhusu umiliki wa ardhi kwa njia hii, kwa sharti tu kwamba muuzaji awe ni mmiliki
halali wa ardhi hiyo ambayo pia imesajiliwa kisheria na njia nyengine ni kuhaulishiwa na Mhe.
Waziri anaeshughulikia masuala ya ardhi ambayo inatambuliwa katika kifungu cha 7(a) cha
Sheria hiyo. Hata hivyo, jambo hili haliwezekani kufanyika pamoja, yaani kwa Ndg. Amina
kumiliki Nyumba moja kwa warka mbili zilizotolewa na wahusika wawili tofauti wenye hadhi
tofauti kisheria, ni sualaambalo haliyumkiniki. Isipokuwa pawe na tatizo ambalo yeye
mwenyewe Ndg. Amina analifahamu (yaani kujihami kwa namna yoyote). Hivyo, ni wazi
kwamba amedanganya Kamati kwa kuleta ushahidi wa kuhaulishiwa ardhi ya nyumba
inayohusika na hoja hii. Hata hivyo, kwa mujibu wa Shahada ya Muda ya Haki ya Matumizi ya
Ardhi, kilichomilikishwa kwa Ndg. Amina ni ardhi ya kiwanja Namba 1&2 chenye ukubwa wa
mita za mraba 212.94 ambacho kina sifa zote zilizotambulika katika Nyumba Namba 755/56.
Kwa lugha nyengine, pamoja na tofauti ilioyopo baina ya warka wa Uuzwaji wa Nyumba (Sale
Deed) ambayo Ndg. Amina aliupata Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati baada ya
182
kuamini kuinunua nyumba hiyo kutoka kwa Ndg. Juma Ali Kidawa na Shahada ya Muda ya
Haki ya Matumizi ya Ardhi(Provisional Certificate of a Right of Occupancy) ambayo imetolewa
na Mhe. Manshour Yussuf Himid, aliekuwa Waziri wa masuala ya ardhi, Kamati inaamini
kwamba hati hizo mbili zimekusudiwa katika jambo moja, likiwa ni Nyumba Namba 755/56 ama
kiwanja namba 1&2.
Baada ya kupata ufafanuzi kuhusu Hati ya Uuzaji wa Nyumba Namba 755/56, sasa ni vyema
kuendelea kuzungumzia kuhusu hii Shahada ya Muda ya Haki ya Umiliki wa Ardhi
iliyowasilishwa kwa Kamati na Ndg. Amina Aman Abeid Karume, ambapo kama tulivyokwisha
eleza awali kunako hoja zinazowiana na hii, kwamba, pamoja na uwezo mkubwa aliopewa
Waziri anaeshughulikia masuala ya ardhi kuhaulisha ardhi yoyote ya Serikali kwa Mzanzibari
mwenye sifa zinazokubalika na Sheria, miongoni mwa utaratibu husika wa kupata ardhi hiyo ni
mwananchi huyo kutakiwa kuomba kwa Waziri na kueleza sababu za kuomba kwake, jambo
ambalo halikufanyika kwa Ndg. Amina. Pamoja na kupewa ardhi hiyo, Kamati haikupata
ushahidi wowote wa kuombwa na hatimae kutunukiwa kwake ardhi hiyo. Aidha, Hati hii
haikuwahi kuwasilishwa katika kikao chochote cha Kamati na wala haikuwahi kujadiliwa wala
taarifa za kuwepo kwake hazikuwahi kuelezwa katika kikao chohote, isipokuwa baada ya
Kamati kuagiza kuletewa nakla zozote zinazohusika na suala hili kwa Ndg. Amina, ndipo kopi
ya hati hii ikaambatanishwa na kwa maana hii, Kamati inaichukua kama ushahidi uliokuja bila
ya maelezo yoyote.
6.8 Hatua alizozichukua Ndg. Amina Aman Karume katika kutafuta uhahali wa
Umiliki wa Nyumba aliyoinunua baada ya kufahamu Ubatili wa Mikataba ya
Awali: Baada ya Ndg. Amina kufahamu kwamba, ameuziwa Nyumba kinyume na taratibu za kisheria,
suala la kwanza ni kutafuta uhalali mpya wa umiliki wa Nyumba hiyo, ambapo mnamo tarehe
17/04/2007, Ndg. Amina Aman Karume alipata Shahada ya Muda ya Haki ya Matumizi ya Ardhi
iliyotolewa na aliyekuwa Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mhe. Mansour Yussuf
Himid, kwa kutumia mamlaka aliyopewa kisheria chini ya kifungu cha 11 na 33 vya Sheria ya
Umilikaji wa Ardhi Namba 12 ya mwaka 1992, ambapo Kamati haipingani na mamlaka ya
Waziri, isipokuwa namna ya utumiaji wa madaraka hayo kwa mazingira ya suala husika,
inaifanya Kamati kuendelea kujiuliza masuala mengi na kutaka kufahamu zaidi.
Suala hili Kamati ilifahamishwa na Ndg. Amina kwamba, baada ya Mhe. Mansour kupata taarifa
kwamba Ndg. Amina ameinunua nyumba hiyo kupitia kwa Ndg. Juma Ali Kidawa wakati
nyumba hiyo tayari ilikwisha taifishwa na Serikali, wakati huo huo akifahamu kwamba Mkataba
wa Ndg. Juma Ali Kidawa na Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi hauna uhalali wowote
wa kisheria, Mhe. Mansour aliwasiliana na Ndg. Amina na kumshauri kwamba hakukuwa na
haja ya kuinunua nyumba hiyo kupitia taratibu alizozifanya awali, na ndio maana Kamati
inafahamu kwa namna yoyote kwamba, Hati hii aliyopewa Ndg. Amina na Mhe. Waziri ni
kielelezo kikubwa cha uhusiano wa kifamilia baina ya Mhe. Waziri na Ndg. Amina Aman
Abeid Karume katika suala hili.
Jambo kubwa ambalo Kamati inaona linatia mashaka, ni kuwepo kwa Hati Mbili tofauti
zinazoonesha umiliki wa Nyumba moja, jambo ambalo halipo kisheria wala kimazoea (practice).
183
Kifungu cha 7 cha Sheria ya Ardhi ya mwaka 1992, kimeitambua njia moja tu, kati ya njia
ilizozitaja kuwa ni halali kwa mtu kuimiliki ardhi ambacho kinasema:
“Haki ya kumiliki ardhi kwa Mzanzibari yoyote inaweza kuwepo kutokana na njia
moja35
kati ya njia zifuatazo:
(a) Kupewa na Waziri (anaehusika na masuala ya Ardhi);
(b) Kutambuliwa haki sahihi ya umiliki wa ardhi kufuatia Usajili wa ardhi
iliyofanywa na Sheria ya Usajili wa ardhi ambayo itakuwa imesajiliwa chini
ya Sheria ya Usajili wa Ardhi;
(c) Kurithi kwa haki sahihi (ya ardhi) iliyosajiliwa;
(d) Kununua haki sahihi (ya ardhi) iliyosajiliwa; au
(e) Zawadi ya haki (ardhi) iliyosajiliwa kutokana na nia njema ya mmiliki wa
haki ya matumizi ya ardhi36
.
Hii ina maana, kwa mujibu wa Sheria ya Umiliki wa Ardhi, haiwezekani mtu mmoja kumiliki
ardhi kupitia njia mbili tofauti ambazo zote zimetambuliwa kisheria. Kwa Ndg. Amina ambae
anadai ni mmiliki halali wa Nyumba Namba 755/756 kwa sababu ameipata Nyumba hiyo kwa
kuuziwa na Ndg. Juma Ali Kidawa, yaani kupitia kifungu cha 7 (d) cha Sheria ya Namba 12 ya
mwaka 1992, wakati huo huo anadai ni mmiliki halali wa Nyumba hiyo kwa sababu ameipata
kwa kupewa na Waziri, kupita kifungu cha 7 (a) cha Sheria ya Namba 12 ya mwaka 1992, ni
jambo lisiloyumkinika kisheria na halina uzito wowote (Kielelezo Na.202) na Kamati
haikubaliani na uthibitisho uliotolewa wa umiliki mpya wa Nyumba hiyo kwa sababu
unapingana na taratibu za sheria.
6.9 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari wa
mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali juu
ya hatua za kuchukuliwa.
6.9.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Mikataba yote ya Umiliki wa Nyumba hiyo ni batili na haina nguvu za Kisheria.
Kamati imebaini kwamba, Mikataba yote ya mauziano iliyofungwa baina ya Serikali na
Ndg. Juma Ali Kidawa na baina yake na Ndg. Amina Aman Abeid Karume ni batili na
ya udanganyifu. Aidha, Hati ya Matumizi ya Ardhi aliyopewa Ndg. Amina Aman
Abeid Karume na Mhe. Mansour Yussuf Himid imekiuka taratibu za kisheria na
kiutawala.
(ii) Mzee Juma Ali Kidawa sio Mmiliki halali kisheria wa Nyumba iliyokuwa imefuatiliwa
35
Msisitizo ni wetu. 36
Tafsiri na Msisitizo ni wetu.
184
na wala hakuhusika na Uuzaji wa Nyumba hiyo kwa mtu yoyote na hakuwahi kufuatilia
Utengenezaji wa Warka wa Nyumba hiyo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa nia njema na mazingira halisi yalivyojitokeza yanaonesha
Mzee Juma Ali Kidawa alihusika na kufanya kazi kwa Mhindi aliyeimiliki nyumba
hiyo kabla ya kutaifishwa na Serikali.
(iii) Ndg. Ramadhan Abdalla Songa na Mama Fatma Karume walishiriki katika
Udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano uliofungwa baina ya Serikali (Wizara ya
Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati) na Ndg. Juma Ali Kidawa.
(iv) Ndg. Mwalimu Ali Mwalimu kama Katibu Mkuu, amechangia kufanyika kwa
udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano baina ya Wizara yake na Ndg. Juma Ali
Kidawa.
(v) Afisi ya Mrajis haikutekeleza majukumu yake ipasavyo hali iliyopelekea kuwepo kwa
Mkataba wa Mauziano batili baina ya Ndg. Juma Ali Kidawa na Ndg. Amina Aman
Abeid Karume.
6.9.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:
(i) Nyumba hiyo ambayo sasa imeshajengwa Hoteli ya Ndg. Amina Aman Karume,
Kamati inapendekeza hati zote hizo za umiliki wake zifutwe na apatiwe tena hati
ya umiliki wa ardhi husika na baadae atakiwe (Ndg. Amina Aman Abeid
Karume) amsaidie Ndg. Juma Ali Kidawa kwa kiwango cha fedha kisichopungua
Milioni Ishirini (20,000,000/) ili kumsaidia kujinasua na maisha. Kwa sababu
kwa mujibu wa ushahidi wa kimazingira, inaonesha wazi kwamba mwananchi
huyu alikusudiwa kuimiliki nyumba hiyo kutokana na uhusinao wake na mmiliki
wa Nyumba hiyo kabla ya kutaifishwa na Serikali.
(ii) Hatu za Kisheria zichukuliwe dhidi ya Wananchi wote waliohusika katika
udanganyifu uliojitokeza katika Upatikanaji wa Mikataba ya Mauziano kutoka
katika Mamlaka ya Serikali na kumuuzia Ndg. Juma Ali Kidawa na mauziano
baina ya Ndg. Juma Ali Kidawa na Ndg. Amina Aman Abeid Karume.
(iii) Hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa watendaji wakuu wa Wizara ya Ardhi,
Makaazi, Maji na Nishati waliohusika na upatikanaji wa Mkataba wa Mauziano
ya Nyumba Namba 755/56 kwa thamani ya Tsh. 5,000,000/- baina ya Wizara hii
na Ndg. Juma Ali Kidawa.
Hatua za nidhamu kama hizi zichukuliwe dhidi ya watendaji wa Afisi ya Mrajis
Mkuu wa Serikali walioshiriki katika upatikanaji wa Mkataba wa Mauziano
baina ya Ndg. Juma Ali Kidawa na Ndg. Amina Aman Abeid Kaurume.
HADIDU REJEA YA SITA:
7.0 KUTAFUTA UKWELI KUHUSU MATATIZO KWENYE UJENZI WA JENGO
JIPYA LA WIZARA YA FEDHA-CHAKE CHAKE PEMBA:
185
7.1 Utangulizi:
Katika kufuatilia Hadidu hii rejea, Kamati ilitakiwa kuchunguza iwapo kuna matatizo ya ujenzi
wa jengo jipya la Wizara ya Fedha, ambayo sasa ni Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya
Maendeleo ambapo imethibitishwa kwamba jengo hilo limetumia fedha nyingi za umma lakini
bovu la lina mwelekeo wa kupotomoka hata kabla ya kukamilika kwa ujenzi wenyewe. Kwa
ujumla tatizo la ujenzi huo limeeleweka zamani kiasi ambacho kila Mjumbe wa Baraza hili
analifahamu suala hili, kubwa zaidi lililotumwa kwa Kamati ni kuangalia chanzo cha matatizo
hayo lakini pia kuisaidia Serikali juu ya hatua za kuchukua kufuatia tatizo hilo.
Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati imekutana na Katibu Mkuu na wafanyakazi wengine
wa Wizara ya Nchi (AR) Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo katika jengo la Wizara hiyo
Chake- Chake, Pemba. Pia kukutana na wakandarasi walioendesha ujenzi huo pamoja na
kutembelea jengo hilo kwa ajili ya kufanya ukaguzi. Kamati ilifanya kazi hiyo siku ya Jumatano
tarehe 02/11/2011. Aidha, Kamati iliwaita pamoja Wajumbe wote wa Bodi ya Zabuni ya Wizara
hii, (Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo) pamoja na Idara ya ya
Uhakikimali na Mitaji ya Umma tarehe 06/12/2011 katika Afisi ya Baraza la Wawakilishi,
Unguja kwa lengo la kupata ufafanuzi zaidi wa masuala ambayo hayakujibika katika kikao cha
awali.
Kwa mujibu wa taarifa ya maandishi iliyosomwa mbele ya Kamati na Katibu wa Bodi ya Zabuni
ya Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, ujenzi wa jengo hilo ni moja wapo
ya hatua za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za utekelezaji wa „Programu ya Ujenzi wa Ofisi
ya Serikali ya Mapundizi ya Zanzibar‟. Utekelezaji wenyewe ulifanywa katika hatua zifuatazo:
7.2 Namna ya Kumpata Mkandarasi kwa Ajili ya Michoro na Usimamizi:
Mchakato wa utekelezaji wa ujenzi huo ulianza kwa Serikali kutafuta kiwanja ambacho
kilipatikana kwenye mtaa wa Mguye, Tibirinzi, Chake Chake, Pemba. Baada hatua hiyo, Serikali
ilitoa zabuni kwa ajili ya kupata Kampuni inayofaa kufanya michoro na kusimamia ujenzi
wenyewe (design and construction supervision). Matangazo kwa ajili ya zabuni hiyo
yalichapishwa kwenye magazeti mbali mbali yakiwemo magazeti ya „Zanzibar Leo‟, „Daily
News‟ na „The Guardian‟ yote ya tarehe 05/04/2007. Lakini, kivuli kimoja kilichotolewa kwa
Kamati na kuelezewa kuwa ni kivuli cha tangazo la zabuni kwa ajili ya Mkandarasi wa michoro
na usimamizi wa jengo, hakina dalili yoyote ya kuonyesha kuwa ni kivuli cha taarifa
iliyochapishwa kwenye gazeti na kutolewa nakala. Katika mazungumzo hayo, nakla ya
kikaratasi hicho kilitolewa na kupokelewa na Kamati kama Kielezo Na. 203 cha taarifa hii.
Jumla ya Makampuni 10 yaliitikia mwaliko kwa ajili ya zabuni hiyo. Kati ya hayo, Makampuni
2 yalitoka Zanzibar na nane yalitoka Dare s Salaam. Miongoni mwa Makampuni hayo ni
Makampuni 7 ambayo yalikidhi vigezo katika uchunguzi wa awali (preliminary examination).
Majina ya Kampuni hizo 7, ambazo baada ya kufaulu vigezo ziliarifiwa kuleta mapendekezo yao
ya „kiufundi na kifedha‟, yameorodheshwa kwenye taarifa ya maandishi iliyotolewa kwenye
186
Kamati. Katika tathmini ya mwisho, Kampuni ya K&M ARCPLANS ya Dar es Salaamu ndio
ilionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya michoro na kusimamia ujenzi uliokusudiwa na,
kwa hivyo, mnamo tarehe 29/11/2007 iliingia kwenye mkataba na Wizara ya Fedha, kwa ajili ya
ujenzi huo.
7.3 Namna ya Kumpata Mkandarasi kwa Ajili ya Ujenzi
Katika hatua ya pili, Kampuni ya Ushauri ya K&M ARCPLANS ilitayarisha michoro na baadae
kutayarisha nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi huo na kuziwasilisha Wizarani. Lengo
lilielezwa kuwa ilikuwa ni kuwapata Wakandarasi yenye sifa za daraja la I au la II kwa ajili ya
zabuni ya jengo hilo.
Mnamo tarehe 08/03/2008, ilielezwa kuwa tangazo kwa ajili hiyo lilitolewa kwenye magazeti
kadhaa yakiwemo „Daily News‟, „Zanzibar Leo‟ na „The Guardian‟. Katika mazungumzo hayo,
vivuli viwili vya matangazo yanayoonyesha kutolewa kwenye magazeti ya „Daily News‟ na
„Zanzibar Leo‟ vilitolewa, na kupokewa na Kamati kwa pamoja kama Kielelezo Na. 204.
Kutokana na tangazo hilo, Makampuni kadhaa yaliomba kupewa kazi hiyo ya ujenzi wa jengo la
Wizara ya Fedha, Pemba. Mnamo Machi 03, 2009 mnamo saa 04.30 za asubuhi zabuni
zilifunguliwa kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha, na kushuhudiwa na wawakilishi wa
Makampuni yote ambayo zabuni zao zilipokelewa. Makampuni yenyewe (pamoja na thamani ya
zabuni zao) ni kama ifuatavyo:
i. Mazrui Building Contractors Ltd (Zanzibar) Tshs 2,292,641,162/=;
ii. Masasi Construction Company Ltd (Dar es) Tshs 2,077,946,634/=;
iii. Salem Construction Co. Ltd (Zanzibar) Tshs 1,536,790,825/=; na
iv. Jansons Construction Co. Ltd (Zanzibar) Tshs 1,400,000,000/=.
Kamati ya Tathmini iliundwa na kufanya uchambuzi juu ya mkapuni manne yaliyoorodheshwa
hapo juu, na baadae kupendekeza. Kamati ya Tathmini ilifanya kazi hiyo kwa kuzingatia vigezo
vilivyoweka ndani ya „Tender Document‟, ambavyo ni:
i. Usajili wa Kampuni;
ii. Uthibitisho wa kulipa kodi;
iii. Ukamilifu wa kujaza nyaraka za zabuni;
iv. Zana za ujenzi kwa mujibu wa jengo lenyewe;
v. Wataalam wa ujenzi pamoja na uzoefu wao;
vi. Uzoefu wa Kampuni katika kazi za ujenzi; na
187
vii. Kazi zilizowahi kufanywa kabla.
Kamati ya Tathmini, katika uchambuzi wake, ilifikia uamuzi wa kuipendekeza Kampuni ya
Janson Construction Ltd ya Zanzibar (inayomilikiwa na raia wa Kenya) kwa ajili ya ujenzi huo.
Bodi ya Zabuni ya Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ilikubaliana na
tathmini hiyo, na kuomba idhini ya Katibu Mkuu (Accounting Officer) kwa ajili ya utekelezaji.
Baada ya idhini hiyo kutolewa, Mkandarasi aliechaguliwa aliarifiwa juu ya kushinda kwake
zabuni (tender) hiyo; nae alijibu kwa barua kuikubali kazi hiyo. Hatimae Mkataba kwa ajili ya
ujenzi huo ulifungwa. Nakla ya Mkataba huo iliolewa, na kupokelewa na Kamati kama
Kielelezo Na. 205. Baada ya Mkataba huo kupitiwa, unaonekana na dosari moja kubwa ambayo
athari yake inawezekana ikawa ni kubwa sana katika mazingira halisi ya utekelezaji wake.
Dosari yenyewe ni kuwa imeelezwa kwenye kifungu (7) kuwa -“(7) This contract is valid for
Forty Seven (47) weeks from the date of signing this contract”. (Yaani, Mkataba huu ni halali
kwa wiki arubaini na saba (47) tokea tarehe ya kusainiwa). Kwa kifungu hiki ni vigumu kufikiria
kuwa Mkataba huu wa Ujenzi uliosainiwa tarehe 13/05/2009 bado una nguvu za kisheria leo hii,
wakati wiki 47 tayari zimepita.
7.4 Maelezo Juu ya Hatua za Ujenzi
7.4.1 Maelezo ya Mwajiri
Katibu wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Fedha na Uchumi alieleza kuwa katika hatua ya baadae,
makabidhiano ya kiwanja yalifanyika baina ya Wzara ya Fedha na Uchumi- Zanzibar (ambae ni
muajiri/Client), Janson Constructions Ltd (ambae ni Mjenzi/Contractor) na K&M ARCHPLANS
(T) LTD (ambayo ni Kampuni ya Ushauri).
Baada ya hapo Mjenzi alilipa fedha ya dhamana ya kazi (performance Security) na mwajiri
kulipa kitangulizi cha malipo (advance payment) kwa mujibu wa Mkataba, na hatua za ujenzi
ikawa zimeanza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na baadae nakla yake kutolewa kwa Kamati (kwenye kikao
cha Kamati na watendaji wa Wizara ya Fedha siku ya tarehe 06/12/2011), hatua za ujenzi
zilienda vizuri, vikao mbali mbali kuzungumzia maendeleo ya ujenzi vikawa vinafanyika penye
eneo la ujenzi (site meeting, malipo yakawa yanaidhinishwa na Mshauri na kulipwa na Mwajiri
kwa Mjenzi kwa mujibu wa Mkataba, na hapakuwahi kutokea tatizo lolote kabla ya mkutano wa
Mwezi Machi 2010. Lakini maelezo hayo yaliachana kwa kiasi kikubwa na yale maelezo
yaliyotolewa na Katibu wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Fedha, kwamba ujenzi ulianza bila ya
Mjenzi kuwa na Mkandarasi Mkaazi (local engineer) ambae katika ujenzi anapaswa kuwepo
kusimamia ujenzi katika kila hatua. Lakini alieleza pia kuwa Mshauri wa ujenzi alitakiwa aweke
Mkandarasi wake (resident engineer) kwa ajili ya kujiridhisha juu wa umakini wa shughuli za
ujenzi zinavyoendelea. Aliendelea kueleza kuwa, waliwasiliana na Mshauri Mwelekezi zaidi ya
mara tatu kumtaka aweke Mkandarasi wake kwenye ujenzi, bila mafanikio. Hatimae baada ya
188
ujenzi kuanza kwa karibu miezi mitatu, ndio Mshauri alimleta „resident engineer‟ kwenye ujenzi
huo.
Ilielezwa katika taarifa ya maandishi kuwa, ni katika mkutano wa Machi 2010 kati ya Mjenzi,
Mshauri na Mwajiri ndio taarifa rasmi ya kutitia kwa jengo ikatolewa. Mnamo tarehe 09/04/2010
ndio Mshauri alitoa amri ya kusimamisha ujenzi (stop order) kwa kazi za ndani ya jengo; lakini
kazi za nje ya jengo zikawa zinaendelea. Mnamo tarehe 15/04/2010 Mshauri alitoa mbinu
kwamba Mjenzi arekebishe matatizo yaliyojitokeza kwa gharama zake kwa kutumia utaratibu
uitwao „under pinning‟. Lakini kabla ya „under pinning‟ kufanyika, „canopy‟ za jengo hilo nazo
ziliporomoka.
Taarifa ya maandishi iliyotolewa na Wizara kwa Kamati imeonyesha pia kuwa pamoja na vikao
kadhaa vya makubaliano kufanywa kati ya Mwajiri, Mshauri na Mjenzi, hapakuwa na
makubaliano yoyote ya msingi yaliyofanyika. Kwamba, Mshauri ameshauri kuwa matatizo
yaliyojitokeza yanaweza kutibika bila ya shaka yoyote kwa utaratibu wa „under pinning‟, ushauri
ambao unakubaliwa kimsingi na Mjenzi. Hata hivyo, alipoulizwa na Kamati kuwa endapo
ushauri wake utakubaliwa na Serikali yupo tayari kuwajibika kwa hitilafu yoyote itayotokea,
Mshauri hakuwa tayari kuwajibika kwa hilo.
Kwa upande wa Serikali (taarifa inaeleza kuwa), uamuzi uliopo hadi sasa ni kuwa jengo hilo
halifai, na Mkandarasi anapaswa kuliondosha kwa gharama zake na pia kurudisha gharama zote
za Mwajiri. Kamati ilijulishwa pia kuwa hadi wakati wa kikao cha Kamati na Wizara cha tarehe
06/12/2011, jengo lilikuwa halijakabidhiwa kwa Serikali, na kwamba bado jengo hilo lipo
kwenye dhamana ya Mjenzi, pamoja na Mshauri. Nakla ya taarifa ya maandishi ambayo imebeba
maelezo yote haya imetolewa, na kupokelewa kama Kielelezo Na. 206.
Kuna vyanzo vingine vitatu vya taarifa zilizopokelewa na Kamati kuhusiana na ujenzi wa jengo
la Wizara ya Fedha (Pemba), ambavyo ni: (i) taarifa ya Mshauri; (ii) taarifa ya Mjenzi; na (iii)
taarifa mtaalamu kutoka Idara ya Majenzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7.4.2 Maelezo ya Mshauri Mwelekezi (Consultant):
Taarifa ya Mshauri ilitolewa kwa Kamati na Engineer Arch Yared Dondo wa Kampuni ya K&M
Archplans (T) Ltd ya Dar es Salaam ambayo ndio iliingia Mkataba na Wizara ya Fedha na
Uchumi ya Zanzibar kufanya michoro na kusimamia ujenzi wa jengo la Wizara hiyo kisiwani
Pemba. Kwa mujibu wa Mkataba huo ambao nakla yake ilipokelewa na Kamati na kufanywa
Kielelezo Na. 207 cha taarifa hii.
Mkataba huo unaoonyesha kuwa malipo ya pamoja kwa kazi za uchoraji na ushauri ni
Tshs.81,552,000/=, bila ya kuwepo na mgawanyiko wa malipo. Lakini katika maelezo ya ziada
yaliyotolewa na Engineer Dondo kwa Kamati, asilimia sabini na tano (75%) ya malipo hayo ni
kwa kazi ya michoro; na 25% ndio malipo ya ushauri na usimamizi wa jengo. Hadi kufikia hatua
189
hii, tayari Mshauri Mwelekezi ameshalipwa Tshs.65,344,470/= na hivyo kubakia malipo ya
Tshs. 16,207,530/=.
Katika hali hii, Kamati imebaini ukosefu wa wazi wa umakini ulioonyeshwa na Wizara ya Fedha
katika hatua hii kwa kuzingatia kuwa ujenzi bado upo katika hatua za awali, wakati sehemu
kubwa ya malipo yameshafanywa kwa Mshauri Mwelekezi.
Katika taarifa yake, Engineer Dondo alieleza kuwa wakati wanakabidhiwa kazi walipewa
angalizo juu ya ubaya wa ardhi hapo penye kiwanja chenyewe. Ingawa hawakuipima ardhi hiyo
kwa sababu mara nyingi huwa wanapima ardhi kwa jengo la kuanzia ghorofa tano, lakini
walichukua tahadhari ya kutosha kwenye michoro waliyochora kiasi ambacho wana hakika kuwa
kama maelekezo yao yangefatwa vizuri basi hakuna uwezekano wa tatizo lolote kutokea.
Katika utekelezaji wa shughuli zao, michoro ya kwanza waliyochora kutokana na maelekezo
waliyopewa ulifanya gharama za ujenzi kuwa ni zaidi ya Tshs.2b/=. Gharama ya ujenzi
ikaonekana ni kubwa, na kutakiwa wafanye michoro ambayo gharama zake za ujenzi hazitozidi
Tshs.1.5b/=. Baadae ndio Mkandarasi akapatikana kwa thamani au gharama ya
Tshs.1,460,000,000/=, na ujenzi ukaanza. Hata hivyo, alieleza kuwa katika mchakato wa
kumpata Mkandarasi, Mshauri Mwelekezi hakushirikishwa. Hali hii hakuiona yeye kuwa ni
tatizo kwa sababu katika Mkataba wao haikuonyeshwa kuwa anatakiwa kushiriki katika kumpata
Mkandarasi (Mjenzi). Lakini alikubali kuwa kimsingi kwa sababu yeye ndiye anapaswa
kumsimamia kuhakikisha kuwa ujenzi unafanywa kitaalamu, basi ni vyema kujiridhisha kuwa
Mjenzi anayepewa Mkataba wa kujenga anao uwezo wa kufanya hivyo. Ila ni bahati mbaya
kuwa yeye hakushirikishwa.
Ameeleza pia kuwa bahati mbaya zaidi ni kuwa mmiliki wa Kampuni iliyopewa kazi ya ujenzi
sio mtaalamu wa ujenzi (yaani Civil Enginer). Wala sio Engineer wa fani yoyote ile, isipokuwa
kazi yake ya kawaida anayofanya ni fundi bomba (yaani, plumber). Kwa hivyo, kazi ambayo
yeye mwenyewe angeweza kuifanya ni hiyo ya mabomba tu na sio nyengine yoyote.
Vile vile, Kampuni yake haikuajiri hata „engineer‟ mmoja. Mafundi wawili ambao aliwahi
kuwaajiri katika kazi hii wote „technicians‟, ambao sifa yao kubwa ya elimu ya ujenzi ni FTC‟.
Wa kwanza alipoondoka, wa pili aliyetetwa ni mwalimu wa shule; hakuwa na uzoefu wa kutosha
wa kujenga. Kwamba ukweli ni kuwa hadi wakati mazungumzo haya yalifanywa kwenye
Kamati, Mjenzi alikuwa hana hata ofisi, na kwamba wakati Mshauri alipotaka kuona ofisi yake
(baada ya matatizo ya kiufundi kutokea) aliwaonyesha chumba alichokodi kwenye hoteli kuwa
ndio ofisi yake.
Akielezea sababu za jengo kutitia, Engineer Dondo alieleza kuwa matatizo ya kiufundi ndio
sababu pekee iliyopelekea athari zilizopatikana kwenye ujenzi huu, jambo ambalo wao walikuja
kilielewa baadae. Kwamba ujenzi ulianza bila ya kuwepo „local engineer‟ kwenye ujenzi (mpaka
kufikia kufukiwa msingi); wao walielekeza kila kitako kiwe cha 250mm, badala yake akafanya
190
vitako vya 200mm, na kuna baadhi ya nguzo hazikuwekwa vitako kabisa kabisa; msingi
ulipokuja kubeba mzigo, nguzo zikatitia kwenye matope. Ameeleza pia kuwa ametoa ufafanuzi
wa mambo yote haya katika taarifa aliyoituma kwa Wizara ya Fedha na Uchumi kufuatia
matatizo yaliyotokea ya kutitia kwa jengo, taarifa ambayo nakala yake imepokelewa na Kamati
na kufanywa Kielelezo Na. 208 cha taarifa hii.
Katika taarifa yake Kielelezo Na. 209, Mshauri Mwelekezi ameeleza pia kuhusu mambo
mengine kadhaa, yakiwemo haya yafuatayo:-
a. Mkataba kati ya Mwajiri na Mjenzi haukuzingatiwa. Kwamba katika ukurasa wa 1 na 2,
Mkataba unamtaka Mkandarasi awe na uwezo wa kiufundi, vifaa na wataalamu wa
kutosha, mambo yote haya hana;
b. Katika maelezo yenyewe ya „Tender‟, sifa za Kampuni zilielezwa kuwa ni pamoja na
uzoefu wa miaka mitano (See Part III item 9/12.5(a)). Kampuni hii ya ujenzi ilisajiliwa
Zanzibar mnamo mwaka 2007, kwa hivyo haikuwa na sifa zilizohitajika;
c. Ujenzi ulianza tarehe 30/05/2009 na mara tu baada ya ujenzi kuanza Mshauri aligundua
mapungufu mengi ya kiutaalamu kwa upande wa Mjenzi ikiwa ni pamoja na kushindwa
kufata baadhi ya maelekezo ya kiufundi aliyopewa na Mshauri. Taarifa ya matukio hayo
ilitolewa kwa maandishi na Mshauri kwenda kwa Mwajiri na kumbu kumbu za
maandishi zipo?;
d. Matokeo yake ni pamoja na kutitia kwa jengo na kuanguka kwa „canopy‟ kutokana na
kuchanganya saruji kwa viwango hafifu (angalia, lakini pia kwa kuondoa nguzo za zege
kabla ya siku 21 (kinyume na alivyoelekezwa na Mshauri; n.k.
Alipokuwa anajibu hoja za Kamati, Engineer Dondo alieleza kuwa kwenye ujenzi kama ule
panatakiwa pawe na Mkandarasi au Wakandarasi kwa upande wa Mjenzi, na vile vile kwa
upande wa Mshauri. Lakini, katika hatua za awali za ujenzi, wakandarasi wa pande zote mbili
hawakuwepo. Lakini tatizo kubwa ni kuwa Mjenzi hana uwezo; hafai kabisa kabisa kiasi
ambacho hata kusema umfukuze nchini ni hasara, aliendelea kueleza. Hata hivyo, ushauri wa
Mshauri Mwelekezi ni kuwa bado athari zilizojitokeza kwenye jengo hili zinaweza kutibika kwa
kutumia utaratibu wa „under pinning‟.
7.4.3 Maelezo ya Mkandarasi (Mjenzi):
Ndg. Arvinder Singu Jandu aliielezea Kamati kuwa yeye ni raia wa Kenya, anamiliki Kampuni
ya Jansons Construction Co. Ltd ambayo imesajiliwa. Kampuni hii ndio imeingia kwenye
Mkataba wa ujenzi na Wizara ya Fedha.
Ameelezea kuwa mambo yote ya ujenzi yamefata taratibu zote zilizokubaliwa kwenye Mkataba.
Kampuni yake inae „local engineer‟ na Mshauri Mwelekezi nae ameweka „resident enginner‟.
191
Kila hatua ya ujenzi huwa wanafanya kazi kwa kushuriana. Maelekezo yote ya Mshauri
Msimamizi huwa yanatekelezwa, na tatizo sio kuwa nguzo hazikuwa na vitako.
Tatizo ni kuwa vitako vya nguzo vimeliwa na maji ya bahari. Hili ni jambo linalojulikana. Hata
„resident engineer‟ alitujulisha mapema kuwa pale chini maji ya bahari yanafika, kwa hivyo
lazima saruji iwe ya kiwango cha juu. Walitekeleza maelekezo yao yote, lakini kwa bahati
mbaya sana maji ya bahari ikawa yameuwa ile saruji ya zege waliyoweka kwenye vitako vya
nguzo. Hii ndio sababu pekee ya nguzo kutitia. Akijibu maswali ya wajumbe wa Kamati, Ndg.
Jandu alieleza kuwa Kampuni yake imesajiliwa na Msajili wa Makampuni, na sio na Bodi ya
Wakandarasi. Kampuni yake haina mkandarasi aliyesajiliwa na Bodi hiyo. Yeye mwenyewe
hajasajiliwa na Bodi yoyote ya Wakandarasi popote pale, na wala sio Mkandarasi. Anakubali
kuwa hana sifa za kuwa mkandarasi, lakini akipata kazi anatumia wataalamu.
Wakati anapewa kazi hakuulizwa chochote kuhusu utaalamu wake wa kujenga, na anavyooamini
yeye kuwa hapana masharti kama hayo katika kupewa kazi ya ujenzi hapa Zanzibar. Anavyojua
mtu yeyote anaweza kuingia kwenye Mkataba wa ujenzi. Kama masharti hayo ya sifa yapo basi
inawezekana ni kwa wenyeji tu, wageni hatuulizwi masharti hayo. Yeye alitoa taarifa zake sahihi
wakati anapewa hii kazi, mtu yeyote anaweza kuangalia taarifa alizotoa – ndio hizi hizi,
ameeleza. Anavyoona sasa ni kuwa jambo la msingi ni makubaliano tu kwa sababu penye
makosa panahitaji kurekebishwa.
7.4.4 Maelezo ya Mtaalam Kutoka Idara ya Majenzi ya SMZ
Katika mazungumzo waliyofanyika kati ya Kamati, Mjenzi na Mwajiri, alialikwa pia mtaalam
wa mambo ya ujenzi kutoka Idara ya Majenzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na ni
Engineer Sabra Ameir Issa ndiye aliyehudhuria.
Katika maelezo aliyotoa mbele ya Kamati, Engineer Sabra alieleza kuwa baada ya hii hitilafu
kujitokeza, Idara ya Majenzi ilitakiwa kutoa ushauri juu ya tatizo lililojitokeza. Yeye alishiriki
katika kikundi cha wataalamu wa Idara hiyo waliotakiwa kuishauri Serikali. Ili waweze kufanya
kazi hiyo walipatiwa hati na kumbu kumbu zote muhimu kuhusiana na suala zima la ujenzi huo.
Baada ya kuzipitia kumbu kumbu hizo kwa makini sana, waliuliza maswali kupata ufafanuzi
pale ambapo palihitajika maelezo zaidi, na pia walifanya ukaguzi kadri palivyohitajika.
Katika uchunguzi wao, Engineer Sabra alieleza, waligundua kuwa jengo limetitia kiasi ambacho
limezuiwa zuiwa tu ili lisidondoke. Kwa ufupi jengo hili tunalozungumzia halifai kabisa kabisa,
alieleza.
Alitaja matatizo yaliyosababisha hali hiyo kuwa ni paoja na ubunifu mbaya wa jengo, usimamizi
mbovu, ujenzi uliokosa utaalamu, na uwezo mdogo wa Mjenzi kitaaluma. Alieleza kuwa kabla
ya ujenzi kuanza waliletewa „design‟ kwa ajili ya ushauri nao wakaeleza kuwa ujenzi wa
„design‟ ile haufai kwa udongo wa Pemba, lakini inaelekea ushauri ule haukutiliwa maanani
192
baada ya „designer‟ kubishia na kusema kuwa amefanya utafiti wa kutosha na hana wasi wasi
kuwa „design‟ ile inawezekana.
Tatizo jengine ambalo ni kubwa vile vile ni kuwa Mjenzi hakuwa na utaalamu unaohitajika kwa
ajili ya kazi kubwa kama hile. Mwenye Kampuni ya ujenzi mwenyewe si mtaalamu wa kujenga;
ni fundi bomba wa kawaida. Pia Kampuni yake haina hata Mkandarasi mmoja mwenye leseni ya
ujenzi ambapo hapa Tanzania zinatolewa ama na Bodi ya Wakandarasi ya Tanzania (kwa
Tanzania Bara) au ile ya Zanzibar (kwa upande wa Zanzibar).
Katika Kampuni hii ya ujenzi hamna mtaalam aliyesajiliwa na yoyote kati ya Bodi mbili hizi.
Kwa mantiki hii, ni wazi kuwa Mkandarasi wa jengo hili hana sifa za kufanya kazi ya ujenzi
hapa Zanzibar. Kwa maana nyengine ni kuwa hata kupewa kwake kazi hii ya ujenzi ni kinyume
na sheria za nchi, alieleza engineer Sabra.
Alipoulizwa Katibu wa Bodi ya Zabuni kuhusu uhakika wa maelezo ya Engineer Sabra alisema
kuwa walipokaa kwenye Bodi ya Zabuni mambo haya hawakuwahi kuyazingatia.
7.5 Ufafanuzi wa Kisheria Kutokana na Kadhia Iliyojitokeza
Kutokana na mzozo kuonekana kuelekea kwenye mkondo wa sheria, Kamati iliwaagiza
makatibu wake ambao ni wanasheria kufanya utafiti kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa kisheria
kuhusiana na tatizo hili.
Sheria ya Zanzibar inayosimamia shughuli za ukandarasi ni Sheria ya Usajili wa Wakandarasi,
Sheria Nam. 6 ya 2008. Chini ya kifungu chake cha 20, sheria hii inaelezea sifa za mtu au
Kampuni kuweza kuomba kusajiliwa kama Mkandarasi. Sifa hizo huwa zinatangazwa na Bodi
chini ya kijifungu 20(1)(a). Maombi ya mtu au kampuni kusajiliwa kama Mkandarasi
yanafanywa chini ya kifungu 18 cha Sheria hii. Chini ya kifungu hiki cha 18, baada ya mtu au
Kampuni kusajiliwa usajili wake unatangazwa kwenye Gazeti rasmi. Baada ya hapo ndio mtu au
kampuni iliyosajiliwa inaweza kuomba na kufanya kazi za ukandarasi ndani ya Zanzibar.
Kinachoonekana dhahiri hapa ni kuwa Kampuni ya Jansons Construction Company Ltd haikuwa
hata na nafasi ya kuomba kufanya shughuli za ukandarasi hapa Zanzibar. Ndg. Jandu ameeleza
mwenyewe kuwa hana sifa yoyote ya ukandarasi. Pia Kampuni yake haina mwajiriwa mwenye
sifa ya kuwa mkandarasi. Kwa maana hiyo Ndg.Jandu na pia kampuni yake, hawakutakiwa hata
kuomba kazi hiyo; na alivyoomba hakutakiwa kupewa. Ndio kusema kuwa kazi hiyo ilipewa
Kampuni ya Jansons Construction Co. Ltd kwa makosa; ni kinyume kabisa na maamrisho ya
Sheria ya Kusajili Wakandarasi ya Zanzibar ya mwaka 2008.
Tukizungumzia hatma au athari ya makosa haya kisheria, jibu lipo wazi kwa mujibu wa sheria za
mikataba; kwamba mkataba wowote uliofanywa kinyume na sheria za nchi unakosa nguvu za
kisheria – ni batili kuanza mkataba huo ulipofanywa. Kwa lugha ya sheria za kimikataba,
tunasema ni „void ab initio‟. Kilichobaki ni kuwa kila upande urudishe kwa mwenzake faida
193
iliyopata kupitia mkataba huo „fuiza‟. Yaani, hali ibakie kama vile hawangeingia kwenye
Mkataba.
Kwa maelezo haya ni kuwa ile rai ya Mshauri Mwelekezi kuwa jengo linaweza kutengenezeka
kwa mbinu ya „under pinning‟ haina nafasi kwenye Mkataba fuiza. Ingawa rai hiyo inaonekana
kuwa haina nafasi pia kwa kuzingatia ushauri wa Idara ya Majenzi ya SMZ jengo lililojengwa
pale halifai kabisa kabisa. Kamati inaona kuwa ushauri huu nao ni vyema kupewa nafasi yake
isije kutokea kama ule ushauri uliotolewa mapema na Idara hii kuhusu „design‟ na kupuuzwa,
ambao kama Mkandarasi (Mjenzi) angekuwa na uwezo wa kuwaelewa, na Mshauri Mwelekezi
angeacha ubishi, huenda hatua zote hizi za sasa zingeweza kuepukika.
Lakini, kwa upande wa Mkandarasi (Mjenzi), kifungu cha 33 cha Sheria ya Kusajili
Wakandarasi kinamuweka kwenye nafasi mbaya zaidi. Kijifungu 33(1)(d) cha Sheria hii
kinamfanya mtu au kampuni ambayo imeomba kufanya kazi za ukandarasi, wakati haikusajiliwa
chini ya Sheria hii kwa ajili ya kufanyakazi hizo, kuwa atakuwa ni mkosa wa kosa la jinai.
7.6 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii rejea, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
7.6.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Taratibu za kumtafuta Mkandarasi wa Ujenzi wa Jengo hili hazikuzingatia muongozo
na matakwa ya sheria zinazohusika.
(ii) Mkandarasi wa Ujenzi wa Jengo hili hakuwa na sifa zinazohitajika kisheria za
kumfanya achaguliwe kufanya kazi hiyo.
(iii)Viongozi Wakuu wa Wizara hii (Mhe. Waziri aliehusika na masuala ya fedha wakati
huo) na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na Bodi zao za
Zabuni hawakausimamia ipasavyo majukumu yao kama wanavyohitajika kisheria.
(iv) Kitendo cha kutokuwepo kwa Mshauri Mwelekezi Mkaazi (Local Consultant)
kimechangia sana kumfanya Mkandarasi ashindwe kutekeleze majukumu yake kwa
usimamizi wa karibu wa Mshauri huyo kama ilivyohitajika.
(v) Hakukuwa na mashirikiano ya karibu baina ya Mshauri Mwelekezi na Mjenzi, hali hii
pia imesababishwa na kutoshirikishwa kwa Mshauri Mwelekezi (ambae alikuwa
ameshapatikana kabla ya kupatikana Mjenzi) wakati wa kumtafuta Mjenzi.
194
(vi) Suala la hatua za kuendelea na Ujenzi ama Mkandarasi kwa gharama zake abomoe
jego hilo kwa kushindwa kulijenga katika kiwango kinachofaa, linahitaji maamuzi ya
haraka iwezekanavyo.
(vii) Wizara ya Fedha na Uchumi (kama ilivyokuwa) ilifanya malipo makubwa kwa
Mshauri Mwelekezi na Mjenzi huku ujenzi husika ukiwa katika hatua za awali.
Hali hii inapelekea (iwapo kutatokezea kutorejeshwa kwa fedha hizo na Mkandarasi)
ugumu wa kupata uhakika wa kushinda kesi iwapo suala hili watalipeleka katika
vyombo vya Sheria kutokana na wao wenyewe hawakuwajibika kisheria katika
kumpata Mkandarasi kwa mujibu wa Sheria zinazohusika (contributory negligence).
7.6.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo tulionesha kapo juu, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo
zichukuliwe:
(i) Viongozi na Watendaji wote waliohusika na kadhia hii wawajibishwe kisheria,
kwa sababu imethibitika kwamba, Wizara hii (Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo) imechangia kutokezea kwa tatizo hili.
(ii) Ujenzi wa Jengo hilo usiendelee tena na Serikali isimamie kurejeshwa kwa fedha
zote zilizotumika kujengea jengo hilo ndani ya miezi 3 tokea tarehe ya
kuwasilishwa kwa ripoti hii.
Aidha, taarifa ya hatua iliyochukua Serikali kuhusiana na suala hili ziwasilishwe
katika Baraza la Wawakilishi.
HADIDU REJEA YA SABA:
8.0 UHAULISHWAJI WA MAJENGO YA MAMBO MSIIGE NA STAREHE CLUB:
8.1 Utangulizi:
Moja kati ya Hadidu Rejea zilizotolewa kwa Kamati ni suala la ukodishwaji wa majengo ya
Mambo Msiige na Starehe Club. Katika kufuatilia Hadidu hii rejea, Kamati ilitakiwa ichunguze
sababu zilizopelekea kuhaulishwa kwa jengo la Mambo Msiinge na Starehe Club huku
ikichunguza athari zilinazopatikana baada ya kubadilishwa matumizi ya jengo hilo kihistoria na
na kihifadhi kwa mujibu wa hadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar, bila ya kusahau namna gani
taratibu za kisheria zimefuatwa katika uhaulishwaji na ubadilishwaji wake wa matumizi kama
upo. Aidha, Kamati imetakiwa kuchunguza juu ya ubovu na uvujaji wa jengo hilo kiasi ya
kuhamishwa kwa ofisi za Serikali zilizokuwa zinalitumia jengo hilo kabla ya kuhalishwa na
athari za kuhama kwa ofisi hiyo kwa mnasaba wa mazingira ya kuhama huko.
Katika mkutano ambao Kamati iliuitisha kwa ajili ya kuzungumzia swala hili, iliwaalika pia
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ardhi, Makaazi Maji na Nishati, na watendaji wa taasisi nyengine zinazohusika,
katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo.
195
Kamati pia ilikutana na Ofisi zilizohamishwa katika jengo hilo na ilibahatika kukutana na
Mwakilishi wa Aga Khan ambae ameisaidia sana Kamati kupata ufafanuzi wa masuala mbali
mbali ya historia na maendeleo ya majengo hayo na uhusiano wake na Serikali kuhusiana na
hoja hii.
Kikao hicho kilifanyika Afisi ya Baraza la Wawakilishi tarehe 25/11/2011, huku Kamati kwa
busara na haja ya kupata taarifa za suala hili kwa mnasaba wa historian a hifadhi, (mbali na
kukutana na Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe), ilikutana na Mkurugenzi anaehusiana na
Nyaraka na Hifadhi za Taifa Zanzibar. Na kwa utaratibu huu, Kamati ilikutana na aliekuwa
Waziri wa masuala ya ardhi wa wakati huo, Mhe. Mansour Yussuf Himid, ilikutana pia na
aliekuwa Waziri anaeshughulikia nasuala ya Fedha, Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini na
hata mmiliki wa Kampuni ya Kempiski, ambayo ndio inaaminika imekodishwa majengo hayo.
Mikutano yote hii ilifanyika katika Afisi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kwa siku na
wakati tofauti. Ili kupata ufafanuzi wa kina kuhusiana na hadidu hii rejea, ni vyema sasa tufuate
utaratibu wa taarifa ufuatayo:
8.2 Mkutano wa Kamati na Watendaji mbali mbali Taasisi za Serikali zinazohusika na
suala hili:
Katika maelezo yake kwa Kamati, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango
ya Maendeleo Ndg. Khamis Mussa alieleza kuwa jengo la Mambo Msiige bado ni mali ya
Serikali, na kwamba kilichotokea ni kulikodisha tu jengo hilo kwa wawekezaji wa nje. Kampuni
ya ASB Holdings Ltd ndio wakodishwaji. Ukodishwaji ulifanyika mnamo mwezi Oktoba 2010.
Aidha alipoulizwa na Wajumbe kuhusiana na amri ya Serikali iliyokuwapo wakati huo ya
kutouza mali za Serikali, Katibu Mkuu huyu alieleza kuwa amri iliyokuwepo ni ya kutauza mali
ya Serikali, lakini sio amri ya kukodisha. Ukodishwaji wa ardhi ya Serikali haukuzuiwa hadi
sasa, kwa sababu uhaulishwaji kwa njia ya kukodishwa umekuwa unaendelea bila kusita.
Akielezea kuhusu utaratibu unaopaswa kufatwa na Serikali katika ukodishaji wa mali zake,
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo alielezea kuwa
hakuna sheria yoyote inayoweka utaratibu wa kufatwa na Serikali katika kukodisha ardhi.
Maamrisho ya sheria yaliyopo ni yale tu yanayompa mamlaka Waziri kukodisha ardhi ya
Serikali. Alieleza pia kuwa mazoea yaliyopo ni kwa mtu kuonyesha nia yake ya kutaka kukodi
ardhi ya Serikali ama kwa kuzungumza na Waziri au kwa namna nyengine yoyote ile; na
kuonyesha lengo lake la kuwekeza katika ardhi inayohusika. Endapo mpango wake wa
kuwekeza umekubalika na ardhi anayoomba imeonekana inafaa kwa mradi anaotaka kuwekeza,
basi taratibu zinafatwa kwa ajili ya kukamilisha ukodishwaji huo.
Akizungumzia kuhusu ukodishwaji wa Majengo ya Mambo Msiige na Starehe Club, Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati alisema kuwa Wizara yao ilipokea
agizo kwa njia ya barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya
Maendeleo, kuwa Serikali imepata mwekezaji na imeamua kumkodisha (yaani apewe „Lease‟)
196
majengo ya Mambo Msiige na Starehe Club. Akiunganisha na maelezo yaliyotolewa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango
ya Maendeleo alielezea kuwa Ofisi yake ndio iliyotoa barua kupeleka Wizara ya Ardhi baada ya
kupokea maagizo kwa njia ya barua kutoka kwa Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anaeshughulikia Masuala ya Fedha.
Kwa mujibu wa barua hiyo yenye Kumbukumbu Namba IKL/TS/MUN-18/VOL.13/111 ya
tarehe 18 Oktoba 2010. Mhe. Waziri alimuarifu Katibu Mkuu kuwa Serikali imepokea ombi la
kukodishwa majengo ya Starehe Club na Mambo Msiige kutoka Kampuni ya ASB Tanzania Ltd
(ambao ni wamiliki wa Kilimanjaro Hotel Dar-es-Salaam; Zamani Zanzibar Kempiski; na Bilali
Lodge Kimpiski iliyoko Serengeti) kwa ajili ya kujenga Hoteli mpya ya Nyota Tano. Ombi
liliwasilishwa Serikali imekubali ombi hilo la kuyakodisha majengo hayo kwa kipindi cha miaka
99. Bei ya ukodishaji ni Dola za Kimarekani Millioni Moja na Laki Tano (US$ 1.5) ambazo ni
sawa na Tsh. Bilioni mbili, Milioni mia mbili khamsini (Tsh. 2,250,000,000/=). Fedha hizo
ziwekwe Benki katika Account Maalum kwa madhumuni ya kujenga jengo jipya la Afisi ya
Mrajis hapo Mazizini. Barua hiyo imeendelea kuelezea kuwa „grace period‟ isizidi miaka 10; na
kwamba taasisi ziliopo katika jengo la Mambo Msiige zihamie kwa muda katika jengo la zamani
la benki ya Watu wa Zanzibar hapo Forodhani. Mwisho Mhe. Waziri aliagiza kuwa hatua
zichukuliwe za makabidhiano kama ilivyoelekezwa. Barua hiyo iliyosainiwa na Mhe. Waziri wa
Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (Dr. Mwinyihaji Makame) nakala
yake ilitolewa kwa Kamati na kupokelewa kama “Kielelezo Na. 210”.
Kwa kufuata agizo la Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Ardhi,
Makaazi, Maji na Nishati ilitayarisha hati ya ukodishwaji, pamoja na kumbukumbu nyengine
zilizohitaji kwa ajili ya kufanikisha ukodishwaji huo. Hatimae hati ya ukodishwaji wa ardhi
ilisainiwa na Mhe. Waziri na kukabidhiwa kwa mwakilishi wa Kampuni ASB Holdings Ltd.
Nakala ya waraka inayohusika imetolewa na kupokelewa kama Kielelezo Na. 211 cha taarifa hii.
Alipotakiwa na Wajumbe wa Kamati kuhusiana na nakala zingine zinazohusina na ukodishwaji
huu, Naibu Katibu Mkuu wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati alieleza kuwa Ofisi yao haina
kumbukumbu yoyote ya ziada. Hizi hati mbili (barua ya kuidhinisha ukodishaji kutoka
Serikalini na hati „Lease‟ yenyewe). Hati (i.e. documents) nyengine zote kama zitakuwa zipo
katika hatua zetu (za kiutendaji). Hata hivyo aliendelea kueleza kuwa Kamati ikapata maelezo
zaidi kutoka kwa Katibu Mkuu mwenyewe. Katika utafiti wao kwenye kumbukumbu za Ofisi,
(kwenye mafaili ya Ofisi) hakuna hata barua ya maombi ya ukodishwaji yaliyofanywa na
Mwekezaji mwenyewe. Kwa ufupi hata faili lenye kumbukumbu za „lease‟ ya majengo ya
Mambo Msiige na Starehe Club.
Alipoulizwa sababu zilizopelekea Serikali kuweza kuamua kulikodisha jengo hilo, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha alieleza kuwa analojua yeye ni kupata agizo kuwa Serikali imeamua
kuyakodisha majengo haya, na hakuelezwa wala hakuuliza sababau za kukodishwa majengo
hayo. Agizo nyengine ni kuwa taasisi ambazo zinafanya shughuli za Serikali ni kua wahame na
197
wahamie kwenye jengo ambalo lilikuwa la PBZ na ambalo kwa sasa wamehama. Kwa maelezo
yaliyotolewa mbele ya Kamati na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na
Nishati hadi majengo hayo kukodishwa kwa Mwekezaji aliyepo, haikuwahi kutokea mwekezaji
kuomba akodishwe majengo hayo. Alieleza pia kuwa utaratibu wa kukodishwa majengo upo
wa aina mbili (i) ukodishwaji wa nyumba za Wizara; na (ii) ukodishwaji wa majengo ya Serikali
ambayo hayamilikiwi na Wizara fulani. Kuhusiana na ukodishwaji wa majengo ya Mambo
Msiige alieleza kuwa pale ni kama panapimwa upya na iliyokodishwa ni ardhi. Na hata
alipojulishwa kuwa tafsiri ya neno “ardhi” inajumuisha majengo, alieleza kuwa Wizara yao ina
uwezo wa kukodisha ardhi tupu na sio na majengo. Na kwamba kama majengo yamekodishwa
itakuwa yamekodishwa na Ofisi nyengine.
8.3 Taarifa ya Idara ya Mazingira:
Katika utangulizi wa taarifa yao ya maandishi kwa Kamati Teule, Idara ya Mazingira, ilieleza
kuwa inayo taarifa ya kutaka kujengwa kwa Hoteli ya Nyota Tano (Five Star Hotel) kwa jina la
„Hoteli ya Mambomsiige‟, au „Zamani Palace‟. Kwamba mradi huu utakuwa ndani ya Mji
Mkongwe wa Zanzibar uliomo kwenye Urithi wa Dunia (World Heritage) unaotambuliwa na
UNESCO. Mradi huo ni Hoteli ya vyumba 60 na unatarajiwa kutoa huduma ya kulala wageni,
chumba cha mikutano, huduma za afya ya mwili (GYM), michezo mbali mbali (spa), bwawa la
kuogolea, n.k. Mradi ambao unategemewa kutumia wastani wa Dola la Marekani Millioni 25 –
30.
Taarifa hiyo ambayo ilisomwa kwenye Kamati na Mkurugenzi wa Mazingira Ndg. Sheha Mjaja
Juma, ilionyesha kuwa Idara ya Mazingira iliipata taarifa rasmi kupitia barua yenye
kumbukumbu Nam. AMMN/29/9/C76/136/Vol. XX1 ya tarehe 14/09/2011 ambayo Katibu
Mkuu, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishari alimuandikia Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamo
wa Kwanza wa Rais juu ya Mradi huo kwa lengo la kutaka mradi huu ufanyiwe tathmini ya
Athari za Kimazingira.
Kabla ya kuendelea na maelezo ya kimazingira juu ya Mradi huo, Kamati imegundua kuwa
taarifa kuwa Wizara ya Ardhi haina kumbukumbu yoyote isipokuwa “Lease” haiwezi kuwa ni ya
kweli kwa sababau Idara ya Mazingira imeambatanisha katika taarifa yake barua ikiyotoka
kwenye Wizara hiyo na ambayo Wizara hiyo imekataa kuwepo kwa kumbukumbu yoyote
kwenye Ofisi yake. Hii ni ishara ya wazi kuwa zipo kumbukumbu ambazo Wizara ya Ardhi
imekataa kuzitoa. Nakala ya barua hiyo iliyotoka kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, makaazi,
Maji na Nishati kwenda kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais imo kama
kiambatisho I kwenye taarifa ya maandishi iliyotolewa kwa Kamati Teule tarehe 24/11/2011.
Nakla ya taarifa hiyo ya Idara ya Mazingira imepokelewa na Kamati na kufanywa Kielelezo Na.
212
198
Katika taarifa yake Idara ya Mazingira imeonyesha kuwa mnamo tarehe 28/09/2011 Ofisi ya
makamo wa Kwanza wa Rais ilitoa majibu ya barua hiyo na kueleza hatua zinazofaa
kuchukuliwa, pia na majina mawili ya wataalamu na anuani zao kwa ajili ya kufanya uchunguzi
wa awali (scoping exercise) ambao utabainisha mambo muhimu ya kimazingira na kijamii
yanayofaa kuzingatiwa wakati wa kufanya tathmini ya kijamaa na kimazingira kwa ajili ya mradi
huo. Aidha uchunguzi huo wa awali ndio ungepaswa kutoa Hadidu za Rejea zitakazotumika
wakati wa kufanya tathmini halisi ya kimazingira kwa ajili ya mradi huo, Kamati ilielezwa.
Katikati ya mwezi wa Novemba 2011, Idara ya Mazingira ilipokea maelezo mafupi ya ukurasa
mmoja kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya ASB (Tanzania) Ltd ya Dar-es-Salaam (Bw. A.S.
Rajab yanayoelezea ufupisho wa uchambuzi yakinifu (feasibility study) wa Mradi huo. Nakla ya
maelezo hayo (ambayo ni Kimbatisho 3 katika Ripoti ya Idara ya mazingira) yamepokelewa na
Kamati na kufanywa Rejea Kielelezo Na. 212 cha taarifa hii.
Mnamo tarehe 17 Novemba 2011, Idara ya mazingira ilijibu maelezo hayo kwa kuelekeza kuwa
kilichotakiwa kufanya katika hatua ya awali ni „scoping exercise‟, na wala sio „feasibility study‟,
kama ilivyoonekana kufanywa. Nakla ya barua ya Idara ya Mazingira iliyoelekeza hivyo
iefanywa Kiambatisho 4 cha Taarifa ya Idara hiyo iliyotolewa kwa Kamati kwa njia ya
Maandishi (Rejea Kielelezo Na. 212).
Kamati ilielezwa kuwa kuanzia wakati huo hadi sasa hapakuwa na mawasiliano mengine yoyote
yaliyopokelewa na Idara ya Mazingira. Kinachohitaji na ndio ambacho Idara ya Mazingira
inakisubiri ni “scoping report” na Hadidu Rejea ili iweze kuzipitia na baada ya kukubaliwa, ndio
zitafanywa kuwa ni mwongozo halali kwa ajili ya mradi huo.
8.4 Taarifa ya Mamlaka ya Mji Mkongwe:
Mkurugenzi Mtendaji (Ndg. Issa S. Makarani) wa Mamlaka ya Mji Mkongwe aliieleza Kamati
kuwa walipata ombi la Kampuni ya ASB Holdings Limited kwamba kufuatia kukodishwa kwao
jengo la Mambo Msiige, wanaomba waruhusiwe kufanya ujenzi wao wa Hoteli ya Nyota Tano
waliokusudia. Katika barua yao waliambatanisha pia na nakla ya Hati ya Kukodishwa ardhi.
Nakla ya barua ya ASB Holdings Limited kwa Mamlaka ya Mji Mkongwe imepokelewa na
kufanywa Kielelezo Na. 213 cha taarifa hii. Kufuatia kupokelewa kwa ombi hilo la ASB
Holdings Limited, Mamlaka ya Mji Mkongwe iliwasiliana na UNESCO kwa kujua kuwa kwa
sababu jengo la Mambo Msiige liko katika kiwango cha Daraja la Kwanza cha Urithi, inatakiwa
kwa yale mambo yanayoruhusiwa kurekebishwa basi ruhusa itoke UNESCO. Matakwa ya
UNESCO yalitumwa moja kwa moja kwa ASB Holdings Ltd ili yatekelezwe.
Hata hivyo, miongoni mwa kumbukumbu zilizotolewa kwa Kamati ni nakla ya barua kutoka
UNESCO kwenda Mamlaka ya Mji Mkongwe inayoonyesha kuwa UNESCO wamepata taarifa
kupitia vyombo vya habari kuwa jengo la mambo Msiige la Zanzibar limekodishwa kwa
Muwekezaji kwa kipindi cha miaka 99. Taarifa waliyoipata pia ni kuwa jengo hilo litafanyiwa
matengenezo makubwa ili lifae kwa huduma za hoteli. Barua hiyo imeonyesha kuwa madhumuni
199
ya kuwaandikia Mamlaka ya Mji Mkongwe ni kuwatanabahisha kuwa jengo hilo lina umuhimu
mkubwa na thamani yake ni maalum kuwa ni urithi wa ulimwengu mzima, na sio kwa Zanzibar.
Barua hiyo imenukuu Aya ya 172 ya “Operational Guidelines”, kwamba inahitaji Nchi
wanachama kuitambulisha Kamati ya Urithi (ya UNESCO) kwa matengenezo yoyote ambayo
kufanywa kwake kunaweza kuathiri thamani au hadhi ya urithi wa jengo linalohusika. Barua
hiyo ilimalizia kwa kutaka kujua hali au msimamo wa Serikali kuhusiana na matengenezo
yanayokusudia kufanywa kwenye jengo hilo. Nakla ya barua ya UNESCO kwa Mamlaka ya Mji
Mkongwe imepokelewa na kufanywa Kielelezo Na. 214. Barua hii inaonyesha iliandikwa tarehe
22/12/2010.
Lakini kabla ya barua hiyo, kumbukumbu zinaonesha kuwa tayari Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe aliandika barua mnamo tarehe 14/12/2010 (Ref.
STCDA/4 VOL.II/2010/237) kuiruhusu Kampuni ya ASB Holdings Ltd kufanya mambo
yafuatayo kwenye sehemu aliyokodishwa:-
a) Kujenga uzio kuzungushia sehemu yote ya Mambo Msiige, Starehe Club na
sehemu ya wazi iliopo kuelekea Hoteli ya Tembo.
b) Vipimo na maelekezo mengine juu ya namna ambavyo uzio huo unatakiwa uwe
vimeonyeshwa katika ramani iliyoambatanishwa.
c) Sehemu ya wazi iliopo upande wa Mashariki patajengwa bustani ambayo
itajengwa kufuata maelekezo ya Mamlaka ya Mji Mkongwe na itamilikiwa na
Mamlaka hiyo; na sehemu ya wazi iliopo upande mwengine pataendelezwa kama
itakavyoshauriwa na Wataalam wa Mamlaka hiyo.
d) Wakati hatua hizi zinaendelea, Mamlaka ya Mji Mkongwe inaomba Wahandisi na
Wataalamu wengine kutoka ASB Holding Ltd wakae pamoja na Wataalamu wa
Mamlaka hii ili kujadili kitaalamu maendeleo ya shughuli hizi.
e) Mamlaka ya Mji Mkongwe inasisitiza kuwa hatua nyengine yoyote isiendelezwe
nje ya hizo hatua zilizoelekezwa bila ya kutoa taarifa ya awali kwa Mamlaka hii.
Ilielezewa pia kuwa kibali hicho kitatumika kwa muda wa miezi sita (6); na malipo kwa ajili ya
ruhusa hiyo imeelezwa ndani ya barua hiyo kuwa ni Tshs. 1,500,000/=.
Taarifa zinaonyesha kuwa maagizo ya Mamlaka ya Mji Mkongwe kwa Kampuni ya ASB
Holdings Limited yalifanywa na taarifa inayoonyesha hivyo ilitumwa kwa Mamlaka hiyo
mnamo tarehe 22 Disemba 2010 na kupokelewa kwenye Mamlaka hiyo siku hiyo hiyo ya tarehe
22/12/2010. Cha msingi kinachoonekana hapa ni kuwa, idhini ya Mamlaka ya Mji Mkongwe
kuhusu hatua kuanza kuchukuliwa katika Mradi huu ilitolewa tarehe 14 Disemba 2010 bila
kuwashirikisha UNESCO; na hii inaonekana ndio sababu ya msingi kwa UNESCO kulalamikia
utaratibu katika barua yake ya tarehe 22/12/2010 (Kielelezo Na. 215)
Jambo moja ambalo limetia shaka katika uono wa Kamati hii ni kuwa, barua ya UNESCO
kulalamikia mwenendo wa Mamlaka ya Mji Mkongwe kutowashirikisha katika maamuzi mazito
yanayohusu hatma ya hadhi ya urithi iliyonayo Mji Mkongwe wa Zanzibar, iliandikwa tarehe
22/12/2010 (Barua ya ASB Holdings Limited) kuijulisha Mamlaka ya Mji Mkongwe kuwa tayari
200
imeshatekeleza maelekezo iliyopewa ya kujenga uzio kwenye sehemu iliyokodishwa nayo ikawa
imetoka tarehe hiyo hiyo 22/12/2010; na barua hiyo ikapokelewa tarehe hiyo hiyo kwenye
Mamlaka ya Mji Mkongwe.
Kitu kingine ambacho Kamati inapaswa kukizingatia ni maamuzi ya Kamati ya Urithi wa Dunia
(World Heritage Committee) katika mkutano wake wa 35 uliofanyika kwenye Makao Makuu ya
UNESCO huko Paris, kuhusiana na Mji Mkongwe wa Zanzibar. Katika taarifa hiyo ambayo
inaonekana kuchapishwa tarehe 7/7/2011, nakla yake imepokelewa na Kamati hii na kufanywa
Kielelezo Na. 216, kifungu cha 6 kinaonesha kuwa Kamati ya Urithi wa Dunia imeridhika na
namna nchi husika (the State Party) inavyotathmini maendeleo yanayokusudiwa kufanywa kwa
Hoteli ya Tembo hapo mambo Msiige Zanzibar; na imeshauriwa kuwa hatua zaidi za ushirikiano
zichukuliwe baina ya Nchi husika na Kituo cha Urithi wa Dunia, pamoja na IGOMOS ili
kuhakikisha kuwa maendeleo ya ujenzi wa Hoteli na matengenezo ambayo yatafanywa kwenye
majengo ya kihistoria yaliopo, pamoja pia sehemu ya wazi itayokuwepo hayataathiri hadhi ya
Urithi wa Dunia iliyopo.
Maamuzi pia yamefanywa (kama ni Aya ya 7 ya Maamuzi ya Kamati hiyo) kuwa Nchi husika
ipeleke taarifa kwa “World Heritage Centre: na kwa Mamlaka nyengine za kiushauri juu ya
marekebisho yanayopangwa kufanywa kwenye maeneo ya Kaskazini kwa Bandari; kuhusiana na
Awamu ya Pili ya matengenezo mbele ya “House of Wonders” na kwenye “Tippu Tip House”,
chini ya maamrisho ya Aya ya 172 ya “Operational Guidelines” kwa ajili ya kufanyiwa
mazingatio kabla utekelezaji wake haujaanza katika kila hatua.
Aya ya 8 ya maamuzi hayo imeitaka Nchi Husika kupeleka kwenye Kituo cha Urithi wa Dunia
(World Heritage Centre) mnamo tarehe 1 Februari 2012 taarifa endelevu juu ya namna ambavyo
Urithi wa Dunia unalindwa katika hatua za maendeleo zinazochukuliwa kwenye maeneo ya
Mambo Msiige ili kujithibitishia wenyewe kuwa hakuna athari yoyote ambayo itatokea dhidi ya
Urithi wa Dunia uliopo hapo; kinyume na hivyo ipo hatari ya kuuingiza Mji Mkongwe wa
Zanzibar katika orodha ya sehemu za Urithi wa Dunia ambazo zipo hatarini kuweza kuathiri
hadhi ya “Urithi wa Dunia” katika sehemu hiyo.
Kumbukumbu zinaendelea kuonyesha kuwa pamoja na tahadhari zote hizo za UNESCO,
maelekezo yaliendelea kutolewa kwa Muwekezaji kutoka kwa Mamlaka ya Mji Mkongwe.
Mnamo tarehe 23/12/2010 Mamlaka ya Mji Mkongwe iliiandikia Kampuni ya ASB Holdings
Limited kuiruhusu Kampuni hiyo kubomoa sehemu nyengine iliyobaki kwenye jengo la Starehe
Club. Barua hiyo yenye kumbukumbu No. STCDA/4 VOL.II/2010/239 inaelezea kuwa baada
ya Mamlaka hiyo kutembelea na kuona kuwa tayari Kampuni ya ASB Holdings Limited
imekamilisha ujenzi wa uzio, na kwamba iko mbioni kutoa taarifa yake, Mamlaka ya Mji
Mkongwe inatoa ruhusa kwa Kampuni ya ASB Holdings Limited kubomoa na kuondosha
mabaki ya jengo la Starehe Club, kwa kufuata maelekezo ya Mamlaka hiyo. Kilichosisitizwa
katika barua hiyo ni kuwa ubomoaji usiende zaidi ya ile sehemu iliyoidhinishwa. Nakla ya barua
hii imepokelewa na Kamati na kufanywa Kielelezo Na. 217.
201
Ruhusa za ubomoaji kwenye jengo la Starehe Club lililokodishwa ziliendelea kutolewa katika
hali inayoashiria hata kutokuwepo na maombi kutoka kwa Kampuni ya ASB Holdings Limited
yenyewe. Barua ya tarehe 25/03/2011 yenye kumbu kumbu No. STCDA/4 VOL.II/426 ilitoka
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mkongwe kwenda kwa Kampuni ya ASB
Holdings kuiruhusu Kampuni hiyo kumalizia kubomoa sehemu ya ukuta uliobakia wa jengo la
Starehe Club ambayo imeshikana na jengo la Mambo Msiige. Msisitizo uliendelea kuwekwa
kwa kutoendelea uvunjwaji katika sehemu zilizoidhinishwa Nakla ya barua hiyo imepokelewa na
kufanywa Kielelezo Na. 218.
Katika mtiririko wa ruhusa za ubomoaji katika eneo lililokodishwa hazikusita hapo. Ipo barua
nyengine ya tarehe 29/03/2011 yenye kumbukumbu STCDA/4 VOL.II/2011/247. Barua hii
inahusu ubomoaji wa chumba cha stoo kwenye jengo la Starehe Club. Msisitizo imewekwa vile
vile kuwa ubomoaji usihusishe sehemu yoyote ambayo ruhusa yake ya matengenezo haijatolewa.
Nakla ya barua hiyo nayo imepokelewa na Kamati na kufanywa Kielelezo Na. 219. Jambo
linaloonekana wazi hapa ni kuwa pamoja na msisitizo kupatikana kuwa majengo ya Mambo
Msiige na Starehe Club yamo kwenye urithi wa Dunia na kwamba mawasiliano ya moja kwa
moja kwenye Ofisi za UNESCO kwa matengenezo yanayokusudiwa kufanywa, pia mabadiliko
yenyewe, kumbukumbu hizi zinaonyesha taratibu zimekiukwa. Yaani, hapaonekani kuwepo
mawasiliano kati ya Mamlaka ya Mji Mkongwe na UNESCO.
Hata hivyo, mtazamo wa UNESCO kuhusiana na Mradi huu wa Uwekezaji kwenye majengo ya
Mambo Msiige na Starehe Club umewekwa wazi kwenye maamuzi ya Kituo cha Urithi wa
Dunia (World Heritage Centre) kuwa taarifa rasmi ya maendeleo yaliyojitokeza kwenye Mradi
huu inatakiwa ipelekwe na Nchi husika kwenye kituo hicho mnamo tarehe 1 Februari 2012 ili
taarifa hiyo iweze kuzingatiwa kwenye Mkutano wa 36 wa kituo cha Urithi wa Dunia (World
Heritage Committee) ambacho kitachunguza hali halisi ilivyo; na baadae kuamua hatma ya
Mradi huu katika mustakbali mzima wa Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Akielezea malipo ambayo Serikali ilipata kutokana na ukodishwaji huo wa ardhi, Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ardhi alisema kuwa ni US$ 1,500,000.00 Alielezea kuwa kiwango hicho
cha malipo ni kwa ajili ya kodi ya ardhi tu, yaani haikujumuisha kodi ya majengo. Kodi ya
majengo itajulikana baada ya Muwekezaji kujenga majengo na kutengeneza yale yaliopo sasa.
Baada ya hapo ndio Wizara yenye mamlaka ya kukodisha majengo hayo ndio itakuja kutoa bei
ya kodi ya majengo. Hata hivyo aliweka wazi kuwa Wizara yake siyo inayohusika na ukodishaji
wa majengo ya Serikali. Mamlaka ya Waziri anaeshughulikia maswala ya ardhi ni kukodisha
ardhi tu. Na hata baada ya kujulishwa kuwa kwa mujibu wa sheria ya ardhi inajumuisha pia
majengo, alieleza kuwa kodi ambayo Mhe. Waziri anaeshughulikia mambo ya ardhi amekuwa
anatolesha kodi ya ardhi peke yake bila ya kujumuisha majengo.
Akijibu swali juu ya kunyimwa “Lease” Kampuni ya Aga Khan Foundation ambayo iliomba
muda mrefu kabla ASB Holdings, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha alieleza kuwa uwezo wa
Aga Khan unaonekana ni mdogo kuweza kuimarisha vizuri sehemu ile. Aga Khan Foundation
202
wamekodishwa eneo kubwa Mangapwani na wamekaa nalo miaka nenda miaka rudi bila ya
kulifanyia maendeleo yoyote ya msingi. Kwa hivyo hata kama Aga Khan Foundation nao
waliomba, uamuzi wa Serikali wa kulikodisha eneo hilo kwa ASB Holdings ni la msingi zaidi.
Uwezo wa ASB Holdings unaonekana wazi kupitia Hoteli ya Kempiski wanayoimiliki,
aliendelea kueleza.
8.5 Maelezo ya Ziada Kuhusu Ukodishwaji wa Majengo ya Mambo Msiige na Starehe
Club:
Baada ya kupokea maelezo hayo ya msingi, Kamati ilipata maelezo pia kutoka kwa aliyekuwa
Waziri wa Wizara inayohusika na ardí,Mhe. Mansour Yussuf Himid, na Waziri aliekuwa
anashughulikia masuala ya Fedha Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini, Wamiliki wa
Kampuni ya ASB Holdings Ltd iliyokodishwa majengo hayo; na Kampuni ya Aga Khan
Foundation ambayo imedaiwa kuomba kukodishwa jengo na ikakataliwa katika hali
isiyoeleweka. Pia ilifanya mahojiano na mmiliki wa Kampuni ya ASB Hoilding, iliyokidishwa
majengo hayo, na hivyo, ni busara sasa tukafahamu namna wahusika hawa walivyoeleza kuhusu
hoja hii:
8.5.1 Maelezo ya Mhe. Mansour Yussuf Himid:
Mhe. Mansour alieleza kuwa ni kweli Serikali imeyakodisha majengo ya Mambo Msiige na
Starehe Club kwa Kampuni ASB Holdings Ltd ambayo inamiliki hoteli ya Kempeski. Yeye
mwenyewe kama Waziri anaehusika ndio aliyekodisha majengo hayo. Taratibu zote za kawaida
za ukodishwaji zilifuatwa katika ukodishwaji huo. Taratibu zenyewe ni kuanzia kwa maombi ya
kukodishwa kutoka kwa Kampuni inayohusika, tathmini ya kitalamu ya eneo linalotaka
kukodishwa kwa lengo la kuweza kuamua kodi, kuingia kwenye Mkataba wa “Lease”, na
mambo mengine ya kawaida ya kiofisi. Aliendelea kuielezea Kamati kuwa, mambo haya yote
yalifanyika na kumbukumbu juu ya mambo hayo, yote anahakika zipo kwenye Wizara husika
kwa sababu yeye aliziwacha kumbukumbu hizo zote zipo.
Alipopewa taarifa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yake ameiambia Kamati kuwa ofisini
kwao hakuna kumbukumbu yoyote ya ukodishwaji huo isipokuwa “Lease” yenyewe tu, Mhe.
Mansour alisema kuwa hayo yatakuwa ni maajabu makubwa ni lazima yapatikane maelezo ya
kina kuhusiana na upoteaji huo wa kumbukumbu. Akitoa mfano wa kumbukumbu ambazo yeye
mwenyewe alikuwa nazo, Mhe. Mansour alieleza kuwa ASB Tanzania Ltd waliandika kuomba
kukodishwa majengo haya na eneo lake. Mhe. Mansour aliitoa kwa Kamati nakala ya barua hiyo
ya tarehe 3/7/2010 ambayo haina nambari za kumbukumbu na haionyeshi kupokelewa popote,
imepokelewa na Kamati kufanywa Kielelezo Na.220, pia ametoa nakla za “Dokezo” la tarehe
11/10/2010 kutoka kwake kwenda kwa Mhe. Rais na “Dokezo” la tarehe 13/10/2010 kutoka kwa
Mhe. Rais kwenda kwake, Madokezo ambayo yanazungumzia ukodishwaji wa majengo ya
Mambo Msiige na Starehe Club, lakini hayaonyeshi kuwa yamewahi kupokelewa kwenye ofisi
yoyote. Madokezo hayo yamepokelewa kwa pamoja na kufanywa “Kielezo Na. 221”.
203
Kumbukumbu ya tatu iliyotolewa na Mhe. Mansour ni taarifa ya tathmini ya eneo lenyewe la
Mambo Msiige na Starehe Club. Nakla ya taarifa hiyo ya tathmini ambayo inajionyesha kuwa
imefanywa na Idara ya Ardhi na Usajili haina jina wala sahihi ya aliyeifanya na wala muhuri wa
taasisi husika, jambo ambalo sio la kawaida kwa taarifa rasmi kama hii. Nakla ya Taarifa hiyo
ya tathmini imepokelewa na Kamati na kufanywa “Kielelezo Na. 222.”
Alipoulizwa kuhusiana na kuwepo kwa maombi mengine ya kukodisha majengo hayo
yaliyotangulia, Mhe. Mansour alieleza kuwa hana kumbukumbu vizuri kuhusiana na hilo.
Alipotajiwa Aga Khan Foundation alieleza kuwa anawafahamu Aga Khan ambao ni maarufu
sana katika utunzaji wa Mji Mkongwe. Kwamba ni kweli Aga Khan walionyesha nia ya
kuwekeza kwa kutumia jengo la Mambo Msiige, lakini hawakuwahi kuleta ombi rasmi. Hata
hivyo alionyesha wasi wasi wake kuwa hata kama wangeomba, uwezekano wa Aga Khan
kukodishwa eneo hilo ni mdogo kutokana na kukosa uwezo wa kuliendeleza vizuri.
Alikumbushia kuwa Aga Khan amekodishwa eneo la Mangapwani kwa zaidi ya miaka 25 bila
kufanya maendeleo yoyote.
8.5.2 Maelezo ya Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini
Maelezo ya Mhe. Dr. Mwinyihaji yalikuwa ni machache sana kuhusiana na ukodishwaji wa
Majengo ya Mambo Msiige na Starehe Club. Alieleza kuwa yeye ndiye aliyepokea agizo kwa
wino mwekundu kutoka kwa Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
(wakati huo alikuwa Mhe. Dr. Amani Abeid Karume). Agizo alilopewa ni kuwa Serikali
imepata Muwekezaji ambaye ni Kampuni ASB Holdings Ltd inayomiliki hoteli ya Kempiski.
Katika agizo alilopewa lielezwa pia kuwa thamani ya ukodishwaji huo wa ardhi ni US$
1,500,000.00 na kodi yenyewe itakuwa ni ya kipindi cha miaka 99. Yeye alichotakiwa ni
kusimamia utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais. Katika kutekeleza agizo hilo, Mhe. Dr.
Mwinyihaji aliandika barua (Rejea Kielelezo Na. 210) kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na
Uchumi Zanzibar ambae alimtaka apokee fedha US$ 1,500,000.00 na azifungulie “account”
maalum kwa madhumuni ya kujenga jengo jipya la Afisi ya Mrajis hapo Mazizini. Katika barua
hiyo imeonyeshwa pia kuwa maombi ya ASB Tanzania Limited yalipokelewa tarehe 05 Oktoba
2010, wakati ile barua iliyotolewa na Mhe. Mansour kuwa ndio barua ya maombi ya ASB
Tanzania Limited inaonyesha kuwa iliandikwa tarehe 3/7/2010 na haina muhuri wakupokelewa.
Alipoulizwa na Kamati juu ya usahihi wa kuuza au kukodisha ardhi kwa ajili ya kupata fedha za
kujengea jengo la Ofisi ambayo inapaswa kujenga kwa fedha za bajeti, Mhe. Mwinyihaji
makame alisema kuwa yeye alitekeleza agizo alilopewa na Mhe. Rais na hakuwa na sababu ya
kuhoji jambo lolote. Alieleza kuwa hayo ni mamlaka ya Mhe. Rais, ambae bila ya shaka
anafanya maamuzi kwa maslahi ya nchi.
Alipotakiwa alete mbele ya Kamati Dokezo alilopewa na Mhe. Rais alirudia kusema kuwa
anavyoamini yeye ni kuwa Dokezo lililotolewa na Mhe. Rais kwa wino mwekundu ni siri ya
Serikali na hapaswi kulileta mahali pengine. Alipoelezwa kwamba Kamati Teule ina mamlaka
204
ya kupata taarifa hiyo kama kifungu cha 9 cha Sheria Namba 4 ya mwaka 2007 invyoelekeza, na
kukubali maelekezo hayo ya sheria lakini Kamati kwa abusara zake baada ya kikao hicho cha
Kamati kumalizika, Mwenyekiti wa Kamati aliagiza kwa Katibu wa Baraza barua rasmi
iandikwe kwa Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame na inukuu misingi ya sheria inayoonyesha kuwa
Kamati ya Baraza ina uwezo wa kisheria za kuitisha kumbukumbu yoyote ambayo inahitajika
kwa ajili ya shughuli za Baraza. Barua hiyo yenye kumbukumbu Namba BLW/10/18/50,
iliandikwa na kusainiwa na Katibu wa Baraza mnamo tarehe 08/12/2011 (Kieleelzo Na. 223) na
kupelekewa Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini, lakini mpaka wakati huu tunawasilisha
ripoti hii, “Dondoo” hilo lililodaiwa na Mhe. Dr. Mwinyihaji kuwa lipo bado halikuwasilishwa
kwa Kamati. Kubwa alilolifanya Mhe. Waziri ni kujibu tarehe 22/12/2011 kwa barua yenye
kumbu kumbu namba IKL/TS/BLW/-41/VOL, kwamba kama hapa tunavyonukuu:
“Napenda kukujuulisha kuwa, agizo la Mheshimiwa Rais nililopewa nimeshawajulisha Kamati katika
kikao chetu cha tarehe 7 Disemba 2011, hapo Afisi ya Baraza la Wawakilishi.
Hivyo, sina zaidi ya kuongeza kwa kuwa Mheshimiwa Rais Mstaafu alieniagiza yuhai na yupo nchini.
Nashauri aulizwe ili “Kamati iweze kujiridhisha yenyewe juu ya kuwepo kwa agizo hilo kwangu”
(Kielelezo Na. 224).
Kwa uwazi kabisa lugha hii inathibitisha kwamba, hata Serikali haina taarifa yoyote rasmi sio tu
ya maombi ya Mwekezaji huyu, lakini hata agizo la kutekeleza ukodishwaji huo wa majengo ya
Mambo Msiige na Starehe Club.
8.5.3 Maelezo ya ASB Tanzania Ltd:
Baada ya kuona kuwa kuna tofauti kubwa ya kimaelezo kati ya Watendaji wa Serikali na pia
Mawaziri wawili waliotoa maelekezo yao mbele ya Kamati, Kamati iliwaita wamiliki wa
Kampuni ya ASB Tanzania Ltd ili kupata maelezo zaidi juu ya namna ukodishwaji wa majengo
ya Mambo Msiige na Starehe Club ulivyofanywa. Msemaji wa ASB Tanzania Ltd alikuwa ni
Ndg. Hasu Masrani ambaye alijitambulisha kwa Kamati kuwa ni Mwenyekiti wa Kampuni hiyo
ambayo pia inamiliki Hoteli ya Zamani Zanzibar Kiempiski. Alieleza kuwa wakati hoteli yao ya
Zamani Zanzibar Kempiski inafunguliwa mnamo 12/1/2006, Mgeni Rasmi alikuwa ni Mhe. Rais
wa Zanzibar. Risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa ASB Tanzania Ltd mbele ya Mhe. Rais
ilieleza kuwa ili Kampuni yao iweze kufanya biashara yake vizuri ni vyema wapatiwe eneo kwa
ajili ya kujenga hoteli nyengine kwenye maeneo ya Mji Mkongwe. Yaani, maombi kwa ajili ya
ukodishwaji huu waliyafanya kwa njia ya risala, na hawakuwahi kutuma barua yoyote.
Baada ya muda mrefu kupita, mnamo Oktoba 2010 ndio walipigiwa simu kuulizwa kuwa bado
walikuwa wanahitaji eneo la kujenga hoteli kwenye maeneo ya Mji Mkongwe, na baada ya
kuonesha kuhitaji ndio waliitwa waje kupewa eneo. Walipofika Zanzibar walikutana na Mhe.
Mansour Yussuf Himid aliekuwa Waziri anaehusika na masuala ya ardí na Mhe. Dr. Mwinyihaji
Makame Mwadini, aliekuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, anaeshughulikia Fedha na Uchumi.
kwamba watu wawili hawa ndio ambao waliwapokea hapa Zanzibar na ndio walifanya nao
205
mazungumzo yote kuhusiana na ukodishwaji wa majengo ya Mambo Msiige na Starehe Club.
Alieleza Ndg. Hasu.
Jambo la msingi waliloitwa ni kujulishwa tu kuwa Serikali imezingatia ombi lao la kupatiwa
eneo la kujenga hoteli kwenye Mji Mkongwe. Walionyeshwa eneo na ikawa wameridhika nalo.
Baadae wakaelezwa kuwa watatakiwa kulipa US$ 1,500,000/= kwa ajili ya kuzihamisha Ofisi
zilizokuwa zinafanya kazi kwenye jengo la Mambo Msiige. Baada ya kulipa fedha hizo (US$
1,500,000/=), ambazo walilipa kwa mujibu wa Mkataba, pia walitakiwa walipe kodi ya US$
10,000/= kwa mwaka, kwa kipindi cha miaka 99. Hata hivyo, kodi hiyo ilikubaliwa ianze
kulipwa baada ya kumalizika kipindi cha miaka 10 ya “Grace Period”. Alitoa nakla ya Mkataba
wa “lease” ulioonyesha makubaliano hayo kama ambavyo Kamati iliipokea katika kikao cha
pamoja na Watendaji wa taasisi husika.
8.5.4 Maelezo ya Aga Khan Trust.
Baada ya Kamati kupokea maelezo yanayotia mashaka kwa kiasi kikubwa juu ya namna
ambavyo ukodishwaji wa Majengo ya Mambo Msiige na Starehe Club umefanywa, iliamua
kuwaita wamiliki wa Aga Khan Trust ili kupata maelezo ya namna ambavyo walijitokeza
kuomba kukodishwa eneo hilo na namna walivyokataliwa. Msemaji wa Aga Khan Trust
aliyepatikana ni Ndg. Moh‟d Baloo ambae alieleza kuwa alikuwa na Aga Khan katika Ofisa
ushirikiano (Co-ordinator) kuanzia 1984.
Ndg. Baloo aliielezea Kamati hii kuwa mnamo Machi 1997, Kampuni ya Zanzibar Serena Inn
ilipatiwa nafasi ya uhifadhi yenye kujumuisha majengo mawili ambayo kabla ya kuunganishwa
na kufanywa Hoteli ya Serena yalikuwa ni majengo ya kihistoria ambayo ni Jengo la Zamani
Extelcoms na Jengo lililotumika kama Nyumba ya Madaktari wa Kichina. Majengo hayo ndio
yamesarifiwa na kufanywa Hoteli ya vyumba 51 ya Serena Inn.
Mnamo mwezi wa April 1999 Kampuni ya Zanzibar Serena Inn iliandika barua kwa Katibu
Mkuu wa Afisi ya Waziri Kiongozi kuomba eneo lenye nyumba zinazotumika kama Ofisi ya
Wakfu na Mali ya Amana, Jengo la Mambo Msiige na Starehe Club, lakini hapakuwa na jibu
lililopatikana. Manamo mwaka 2001 Mkuu wa Taasisi ya Aga Khan Foundation alikuja
Zanzibar kwa lengo la kuomba kukodishwa majengo hayo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
ilimuomba kwanza asaidie kutengeneza “Conservation Master Plan” ya Mji Mkongwe. Aga
Khan iliifanya “Master Plan” hiyo mnamo mwaka 2004, na imeelezewa kuwa ni kutokana na
juhudi hiyo ndio Mji Mkongwe wa Zanzibar ukaingizwa katika Ramani ya Urithi wa Dunia
unaosimamiwa na UNESCO.
Mnamo June 2004 Mwakilishi wa Aga Khan alikutana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri
Kiongozi (kwa wakati huo) kuzungumzia uwezekano wa kupatiwa Aga Khan majengo
yaliyokuwa yanatumiwa na Ofisi ya Mufti, mambo Msiige na Starehe Club. Mnamo Julai 26,
2004 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikubali kufanya makubaliano (Memorandum of
Understanding) na Aga Khan Development Network. Watu watano walitoka Geneva walikuja
206
Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria utiwaji saini wa makubaliano hayo. Utiwaji saini ulipangwa
kufanyika siku hiyo ya tarehe 26 Julai 2004 mnamo saa 4.00 asubuhi, wajumbe kutoka Aga
Khan (Geneva) walikaa kwenye mahali walipowekwa kusubiri utiwaji saini lakini hawakuelezwa
kitu chochote cha msingi mpaka kufikia majira ya saa 7.00 baadae ndio wakajulishwa kuwa
sherehe ya utiaji saini imeahirika mpaka itapotolewa taarifa nyengine. Hata hivyo, imeelezwa
kuwa, taarifa hiyo nyengine haikuwahi kutolewa. Hatimae ndio ikaja kupatikana taarifa kupitia
UNESCO kuwa majengo hayo sasa yamekodishwa kwa Kampuni ya ASB inayomiliki Hoteli ya
Kempiski.
Jambo linalowashangaza Aga Khan ni kwamba pamoja na gharama nyingi walizoingizwa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiwa ni pamoja na ufanyaji wa “structural survey” kwa ajili
ya extension ya hoteli yao (structural survey ambayo imekubaliwa na UNESCO); majengo hayo
yamekodishwa Kampuni ambayo haijafanya hatua yoyote kati ya hatua zinazohitajika kwa
mujibu wa taratibu za UNESCO kwa ajili ya uwekezaji kwenye eneo liliomo kwenye urithi. Pia
SMZ wamefanya hivyo bila kujali mashirikiano yaliyopo kati yake na Aga Khan na zaidi, bila
kujali mchango wa Aga Khan katika uendelezaji wa Mji Mkongwe.
Akijibu swali la Mjumbe wa Kamati juu ya madai ya uwezo mdogo wa Aga Khan yaliyotolewa
na Watendaji wa idara ya Ardhi na pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, au hata Mawaziri,
kuhusiana na namna ambavyo Aga Khan wameshindwa kwenye eneo walilopewa na Serikali
muda mrefu uliopita, Ndg. Moh‟d Bhaloo wa Aga Khan alieleza kuwa matatizo yaliyosababisha
Kampuni yake kuwekeza kwenye Kiwanja cha Mangapwani ni pamoja na ucheleweshwaji wa
miaka mitatu uliofanywa katika kutolewa “lease”. Kulikuwa na kazi ya kuondoa Kambi ya Jeshi
katika eneo linalohusika. Pamoja na gharama ya TShs. 4.5 millioni kutumika kwa ajili hiyo,
uhamishaji wa Jeshi ulikamilika mnamo Oktoba 2000 kuanzia Mei 1992 “lease” ilipotolewa. Pia
kuwa maswala ya umeme na barabara inayopitika wakati ule, yote haya hayakuwa
yametekelezwa ipasavyo na Serikali. Matatizo na wananchi yaliyojitokeza baadae nayo
yalikuwa na athari kubwa kwa uanzaji wa harakati za uwekezaji kama tulivyopanga.
Kwa ujumla tarehe 21/6/2004 ndio Aga Khan walipewa orodha ya mahitaji ambayo baada ya
kuyakamilisha ndio wangeruhusiwa kuchukua hatua kuendeleza uwekezaji waliokusudia.
Mzozo wa wanakijiji ulikuja kumalizika mnamo tarehe 18/01/2005. Baada ya hapo, shughuli ya
kujenga ukuta wa fensi ilipangwa ianze tarehe 27/02/2012 na mipango hiyo ilijumuisha namna
ya kuendeleza hatua nyengine uwekezaji. Hata hivyo mnamo tarehe 11/01/2012 ndio barua
ikatolewa na Wizara ya Maji, Ujenzi na Ardhi kuwa “lease” iliyotolewa na Aga Khan kuhusiana
na eneo hilo la Mangapwani. Hivyo ndivyo hali halisi ilivyo, lakini bado Aga Khan
Development Network bado ina uwezo na inataka ipewe eneo lake, Ndg. Bhaloo alimalizia.
8.6 Athari za Ukodishwaji wa Jengo la Mambo Msiige kwa Ofisi zilizokuwa zinafanya
kazi kwenye Jengo hilo:
207
Kufuatia ukodishwaji wa majengo ya Mambo Msiige na Starehe Club uliofanywa na Serikali
kwa Kampuni ya A.S.B. Holdings Limited, Mkodishwaji ambae Mkataba wake ulisainiwa
mnamo tarehe 18/10/2010, siku ya tarehe 25/10/2010, Serikali ilitoa agizo kwa Ofisi zote
ambazo zilikuwa zinafanya kazi kwenye jengo la mambo Msiige zihame na kukabidhi ofisi hizo
tupu kwa Serikali. Uhamishaji huo ulihitajika ili kuiwezesha Serikali nayo ikabidhi jengo hilo
kwa Mkodishwaji (yaani ASB Holdings Limited) na badala yake Ofisi hizo ziende kuhamia
kwenye jengo ambalo hapo awali lilikuwa linatumika kwa makao makuu ya PBZ. Mapendekezo
yaliyofanywa wakati huo ilikuwa ni Ofisi ya Wakfu na Mali ya Amana ihamie na kuendelea na
kazi zake kwenye sehemu ya chini ya jengo hilo (ground floor); na ghorofa ya pili itumike kwa
pamoja kati ya Shirika la Meli, Zanzibar na Ofisi ya Utawala na Ofisi ya Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali. Nakla ya barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na
Uchumi kwenda kwa Mrajis Mkuu wa Serikali, imeambatanishwa na kufanywa Kielelezo Na.
224 cha taarifa hii.
Taarifa iliyotolewa kwa Kamati Teule na Mrajis Mkuu wa Serikali inaonyesha kuwa wakati ofisi
yake inapata taarifa hiyo ikiwa imo katika harakati za kuanzisha “Modern Registry System”,
lakini ikaonekana hata kwenye lile jengo la Mambo Msiige “System” isingeweza kuanzishwa
bila ya kufanyiwa matengenezo makubwa. Wakati Ofisi inafikiria namna ya kuwesha system
hiyo kuanza ndio agizo lilitolewa kuwa Ofisi hiyo sasa ihamie kwenye jengo lilikuwa Makao
Makuu ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambalo kwa utunzaji wa nyaraka linaonekana
halifai zaidi kwa sababu sehemu nyingi linavuja.
Lakini jambo jengine ambalo Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali ililiona ni kuwa ilihisi
haiwezekani na kuzihamisha salama nyaraka zote muhimu ambalo walikuwa nazo ndani ya
mwezi mmoja waliopewa. Lakini ili kupata usaidizi juu ya kueleweka kwa msimamo wao huo,
Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali iliomba ushauri kutoka kwa Idara ya Nyaraka, makumbusho
na Mambo ya Kale kuhusiana na uhamishaji huo. Barua No. IMS/JFV/3/VOL.IV/39 ya Mrajis
Mkuu wa Serikali ilijibiwa kwa barua No. NM/07/9/VOL.V/138 ya Mkurugenzi wa Idara ya
Makumbusho na Mambo ya Kale. Nakla za barua zote hizi mbili zinaambatanishwa na
kufanywa Kielelezo Na. 225 cha taarifa hii. Maelezo yaliyomo kwenye taarifa
iliyoambatanishwa na barua ya Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale
inaonyesha kuwa katika ukaguzi walioufanya, nyaraka nyingi sana ziko katika hali mbaya. Kati
ya hizo ni kumbukumbu zinazohusiana na vizazi na vifo, mikataba ya kibiashara, nyaraka za
majumba na mashamba, na vyeti vya ndoa na talaka.
Taarifa iliendelea kuonyesha kuwa, kumbukumbu zote hizo ni za umuhimu sana na nyengine ni
za muda mrefu sana kiasi ambacho kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi wa Kumbukumbu ya
mwaka 2008, zinapaswa kuwepo chini ya uangalizi na uhifadhi wa Taasisi ya Nyaraka,
Makumbusho na Mambo ya Kale. Taarifa hiyo ilielezea ushauri wa Idara ya Makumbusho na
Mambo ya kale kuhusiana na uhamishaji wa nyaraka hizo kunatokana na hali halisi ya nyaraka
hizo:-
208
(a) Mchakato huu wa uhamaji na uhamishaji wa nyaraka na kumbukumbu usipungue
muda wa miezi miwili; na
(b) Kwa zile kumbukumbu ambazo hazistahili kuwepo zihamishiwe Idara ya Nyaraka
kwa ajili ya uhifadhi wa kudumu. Taarifa hiyo imezitaja nyaraka hizo kuwa ni
pamoja na ........ (i) nyaraka za nyumba na mashamba; (ii) vyeti vya ndoa na talaka;
na (iii) „Index‟ – za kuanzia 1800 hadi 1980.
8.6.1 Jinsi ya Kuhama:
Kuhusu jinsi ya kuhama, kulingana na hali halisi ya nyaraka zilivyo, ushauri ulitolewa
unaonyesha kuwa mambo yafuatayo yalikuwa na umuhimu mkubwa wa kuzingatiwa:-
(a) Nyaraka zihamishwe kwa mujibu wa “Groups” na “Class” zake. Kamati ilielezwa
kuwa utekelezaji wa suala hili haukuwezekana kutokana na ukubwa wa zoezi
lenyewe na muda mfupi ulitolewa.
(b) Katika zoezi la uhamishaji yatumike maboksi ambayo nyaraka na kumbukumbu hizo
zinapangwa vyema na bila ya kushindiliwa. Tahadhari kubwa ilitolewa kuwa mapolo
na magunia yasitumike. Utekelezaji wa ushauri huu nao haukuwezekana. Wakati
Kamati Teule iliotembelea mahali nyaraka hizo zimepelekwa baada ya kuhama,
ilikuta baadhi ya nyaraka bado ziko kwenye mapolo. Nyaraka nyengine zimewekwa
kwenye mafungu mafungu chini zikiwa katika hali ya vipande vipande, na baadhi
yake zinamungunyuka. Kwa hali inavyoonekana, ni dhahiri kuwa lazima zitakuwepo
nyaraka nyingi ambazo haziwezi tena kupatikana hata kwa kuunganisha vipande
vipande.
(c) Uhamiaji na uhamishaji uwe chini ya usimamizi wa wataalamu wa Utunzaji na
Uhifadhi Nyaraka na Kumbukumbu.
(d) Isiwe siku ya mvua na kuwepo na uhakika wa usalama.
8.6.2 Hali ya Jengo lililohamishiwa Nyaraka:
Taarifa imeonyesha pia kuwa mnamo tarehe 04/11/2010 wataalamu wa Nyaraka, Makumbusho
na Mambo ya Kale walipata nafasi ya kufanya ukaguzi kwenye jengo linalohusika, kabla ya
uhamishwaji nyaraka kufanyika. Tathmini ya ukaguzi wao huo (taarifa inaonyesha kuwa) ni
kama ifuatavyo:-
(a) Vyumba vinavyotarajiwa kutumika ni finyu (uchache wa hewa, joto, unyevu, n.k.);
(b) Hali halisi ya jengo ilikuwa ni chafu sana. Hivyo ulihitajika muda wa kutosha ili
kulisafisha kulingana na unyeti wa Nyaraka na Kumbukumbu hizo.
(c) Kutokana na sababu hizo ilionekana kuwa jengo hilo halistahiki (yaani, halifai) kutokana
na unyeti wa Nyaraka na kumbukumbu hizo.
(d) Idara ya Nyaraka, Makumbusho na Mambo ya Kale iliomba Serikali ifikirie uwezekano
wa kuipatia Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali jengo jengine ambalo litaendana na vigezo
stahiki vya utunzaji na uhifadhi wa Nyaraka na Kumbukumbu zake.
(e) Na hata kama italazimika kuhama na kuhamisha kumbukumbu na Nyaraka hizo katika
hilo jengo jipya (PBZ ya zamani), idara ya Nyaraka ilipendekeza mambo yafuatayo:-
209
Kutengenezwa chumba maalum (Strong Room/Repository Room) kwa ajili ya
kuhifadhia Nyaraka na Kumbukumbu hizo. Chumba hicho kinatakiwa kiwe na
air conditions zisizopungua 5; “Shelves” zilizopangwa vizuri; Taa zenye mwanga
mkali; na kabla ya kuhamiwa jengo lifukizwe dawa (fumigation).
Kwa taarifa ambayo Kamati Teule iliipata wakati ilipotembelea kwenye jengo la PBZ ya zamani
ambapo Ofisi ya Mrajis wa Serikali ndipo ilipo sasa, kwa ufupi ni kwamba ushauri uliotolewa
hapo juu na Idara ya Nyaraka haukuzingatiwa na Serikali katika kulazimisha uhamishaji wa
Nyaraka na Kumbukumbu zake kutoka Mambo Msiige. Kwa tathmini ya Kamati Teule ni
vigumu kuelewa ni jambo gani kubwa ambalo liliweza kuipelekea Serikali katika kulazimisha
uhamishwaji huu wa ofisi na Nyaraka zilizohusika bila kuzingatia ushauri wa kitaalamu ambao
ulizingatia kwa kina utunzaji na uhifadhi wa rasilimali na urithi huu muhimu.
Mbali na taarifa hiyo ya Idara ya Nyaraka, Makumbusho na Mambo ya Kale iliopinga kitaalamu
kuhamishwa kwa nyaraka muhimu za Serikali kutoka Mambo Msiige kwenda Jengo la Zamani
la PBZ hapo Forodhani, pia kuna barua yenye kumbukumbu WN/KUB/IMS/54/VOL.II/139
(ambayo nakla yake imeambatanishwa kama Kielelezo Na. 226 cha taarifa hii) kutoka kwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Nchi (AR), Katiba na Utawala Bora kwenda kwa Katibu Mkuu, Wizara
ya Fedha na Uchumi ambayo inahusika kikamilifu na suala la uhamishwaji wa Nyaraka hizo.
Barua hiyo inaonesha, pamoja na mambo mengine kuwa, baada ya kupata agizo la Ofisi ya
Mrajis Mkuu wa Serikali, kuhama Mambo Msiige na kuhamia kwenye jengo lililokuwa Makao
Makuu ya PBZ Ltd hapo Forodhani, Ofisi ya Katibu Mkuu wa WN(UB) ilifanya ukaguzi katika
jengo hilo lililokuwa la PBZ ya zamani. Katika tathmini ya Wizara yake, jengo haliwezi na
halifai kutumika kwa shughuli za usajili pamoja na shughuli mbali mbali zinazofanywa na Ofisi
ya Mrajis Mkuu wa Serikali sababu ambazo Katibu Mkuu wa Utawala Bora alizieleza katika
barua yake ni pamoja na:-
(a) Afisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali ni miongoni mwa taasisi nyeti za Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kutokana na huduma muhimu inazotoa kwa Wazanzibari na pia
wageni. Aidha, Afisi hii ina jukumu na kuhifadhi na kutoa taarifa mbali mbali na
baadhi ya taarifa hizo ni za muda mrefu kuanzia mwaka 1912.
(b) Kumbukumbu zote hizi zinahitaji kutunzwa kwa utaratibu maalum ili ziweze
kuendelea kudumu kwa muda mrefu zaidi. Ili kufikia hali hiyo, uhifadhi wa
kumbukumbu hizo unahitaji chumba maalum chenye nafasi ya kutosha ili
zisiharibike.
(c) Usalama wa kumbukumbu hizo nao ni kitu muhimu cha kuzingatiwa kiasi ambacho
kuhamishwa kwake kunahitaji kuwekewa utaratibu maalum.
(d) Wingi wa kumbukumbu na nyaraka hizo unaohitaji nafasi ya kutosha angalau kwa
kuanzia isipungue ukubwa wa nafasi iliopo sasa.
(e) Afisi ya Mrajis inahudumia wananchi wengi kwa wakati mmoja, hivyo kuna
umuhimu wa kuwa na eneo la kutosha kuwezesha huduma hizo zitolewe kwa urahisi.
Msongamano wa watu utakaokuwepo kwenye ofisi mpya unaweza kusababisha
210
huduma zinazotolewa na ofisi hiyo kuzorota au kushindikana kabisa, hasa shughuli za
usajili.
(f) Afisi ya Mrajis imekuwa ikienda na utaratibu wa kufanya mabadiliko ya kuelekea
kwenye mfumo wa usajili kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa lengo la kuhakikisha
utoaji mzuri zaidi wa huduma na hivyo kuwaondoshea wananchi usumbufu. Katika
kukabiliana na mabadiliko hayo, jengo la Mambo Msiige lilionekana halifai lakini
jengo hilo la sasa linaonekana halifai zaidi. Kwa maana hiyo, kulazimisha Afisi ya
Mrajis kuhama Mambo Msiige na kuhamia jengo la zamani la PBZ ni kudumaza au
kuuwa kwa makusudi jitihada zinazokusudiwa kwenye mabadiliko hayo.
(g) Kutokana na sababu zote hizo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi (AR) Katiba na
Utawala Bora (kwa wakati huo) aliomba kuwa kama suala la kuhama kwenye jengo
la Mambo Msiige ni lazima, basi Afisi hiyo ipatiwe jengo ambalo lilikuwa linatumika
kama Afisi ya Baraza la Wawakilishi la zamani.
Pamoja na tahadhari zote hizo zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi (AR) Katiba na
Utawala Bora, Wizara ya Fedha iliamua kufumbia macho athari zote hizo na kuendelea
kulikodisha jengo lake na kulazimisha Afisi zote zenye Ofisi kwenye jengo la Mambo Msiige
kuhamia kwenye jengo la zamani la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
Kumbukumbu ambazo Kamati Teule ilizipokea kutoka kwa wahusika zinaonyesha kuwa barua
ya tahadhari zilizotajwa hapo juu zilitolewa kwa barua ya tarehe 4/11/2010, lakini siku ya pili
yake tu (tarehe 5/11/2010) Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akatoa barua kumbukumbu No.
MFEA AC/H-60/1/VOL.ii/40 kumuagiza Katibu, Wizara ya Katiba na Utawala Bora kwamba
kinachotakiwa ni Afisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali kutoa ratiba ya kuhama na si kitu kingine.
Kwamba hilo ni agizo la Serikali, na kwamba kazi ya kuhama inatakiwa iwe imekamilika ndani
ya mwezi mmoja. Nakla ya barua hii imepokelewa na Kamati Teule na kufanywa Kielelezo Na.
227 cha taarifa hii.
Kama agizo au karipio hilo halitoshi, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi alitoa barua
nyengine yenye Kumbukumbu namba WN/KUB/IMS/54/VOL.II/141 ya tarehe 8/11/2010
(ambayo nakla yake imefanywa Kielelezo Na. 228) inayodai Afisi ya Mrajis itoe ratiba ya
kuhama kutoka Mambo Msiige kwenda jengo la zamani la PBZ. Barua iliambatanishwa na ile
ya tarehe 5/11/2010, bila shaka, kwa kutilia msisitizo. Hata hivyo kutokana na mazingira
magumu, uhamishwaji huo haukuwezekana kwa muda wa mwezi mmoja uliotolewa. Lakini
baada ya Afisi ya Mrajis Mkuu kuomba kuongezewa muda na Mheshimiwa Makamo wa Pili wa
Rais kuingilia kati, muda wa kuhama uliongezwa na hatimae Afisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali
ikahamishwa kama ilivyotakiwa pamoja na Afisi nyengine zote ambazo zilikuwa zinafanya kazi
kwenye jengo la Mambo Msiige.
8.7 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
211
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii rejea, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
8.7.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Ukodishwaji wa Majengo ya Mambo Msiige na Starehe Club haukufuata taratibu za
uwekezaji zinazoelekezwa na sheria zinazohusiana na Uwekezaji Zanzibar.
(ii) Kamati haikupata kumbu kumbu zozote Serikalini zinazoonesha kuombwa kwa
majengo hayo ya Mambo Msiige na Starehe Club na Mwekezaji na hivyo, haiwezi
kuthbitika kwamba taratibu za kisheria na kiutawala zimefuatwa.
(iii) Kamati haikupata uthibitisho wowote wa kutoka agizo Ikulu juu ya ukodishwaji wa
majengo hayo (kwa mujibu wa taratibu zilizopo) na hivyo ni sawa na kusema kwamba,
Ukodishwaji wa Majengo hayo umezingatia zaidi amri ya mdomo ambayo iko kinyume
na taratibu.
(iv) Sio Mamlaka ya Mji Mkongwe wala Idara ya Nyaraka na Kumbu Kumbu za Taifa
iliyoshirikishwa ipasavyo katika Ukodishwaji wa majengo hayo wakati vyombo hivi ni
sehemu muhimu ya kutoa ushauri unaofaa juu ya suala hili.
(v) Kulikuwa hakuna haja ya Uharaka wa kuhama kwa Ofisi za Serikali zilizokuwa
zinatumia Majengo hayo na hivyo, hoja ya kuvuja kwa majengo hayo haina msingi
wowote na ni wazi kwamba sehemu waliyohamia ndio inavuja kabisa.
(vi) Nyaraka za Serikali zilizopo katika Afisi ya Mrajis wa Serikali, zipo katika hali mbaya
zaidi ukilinganisha na awali kutokana na jengo zilikohamishiwa sasa (Jengo la PBZ ya
zamani) kuwa katika hali mbaya na linavuja kabisa. Aidha, jengo hilo halina mazingira
wala hadhi ya kuhifadhia kumbu kumbu hizi muhimu, hali ambayo inahatarisha kumbu
kumbu hizo kupotea.
(vii) Serikali imetumia nguvu na ubabe katika kuzihamisha Ofisi zilizokuwa zinatumia
majengo hayo bila ya kuzingatia athari zitakazopatikana baada ya kuhama kwa Ofisi
hizi kwa mnasaba wa utaratibu huo.
(viii) Ukodishwaji wa Majengo hayo haukuzingatia maslahi ya umma na umefanywa zaidi
kwa maslahi binafsi ya Kampuni huku Serikali ikifunga mkataba wa miaka 99 bila ya
kujali mabadiliko ya kiuchumi na kihistoria ya Mji wake.
(ix) Licha ya Majengo hayo kukodishwa kwa USD 1,500,000/, Serikali haijafaidika na
fedha hizo kwa kiasi kilichotarajiwa kutokana na fedha nyingi hivi sasa zinatumika
kugharamia safari za kwenda na kurudi UNESCO kufuatilia hadhi ya Mji Mkongwe na
athari za kukodishwa kwa majengo hayo, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa michoro
husika.
212
8.7.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:
(i) Mkataba wa Kodi kwa Mwekezaji huyu (ASB Holdings Ltd) aliyekodishwa Majengo
hayo usitishwe mara moja kwa Serikali kurejesha Fedha za kodi iliyokwisha zipokea, na
Majengo haya yarudi Serikalini huku Serikali ikiona ipo haja ya kuyakodisha, ni Lazima
Majengo hayo yakodishwe kwa kufuata taratibu za kisheria kwa maslahi ya Taifa.
(ii) Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali itafutiwe eneo jengine kwa matumizi ya Ofisi
itakayokidhi haja na hifadhi bora za kumbu kumbu za Taifa, huku jengo hilo la PBZ ya
zamani lifanyiwe ukarabati liwe halivuji na kuwepo mahitaji yote muhimu ya Ofisi,
ikiwa ni pamoja na matumizi ya maji salama na ya uhakika na zibakie Taasisi zilizopo
baada ya kuondoka Ofisi ya Mrajis.
(iii) Mamlaka ya Mji Mkongwe na Idara ya Nyaraka na Kumbu Kumbu za Taifa
zishirikishwe ipasavyo katika hatua zote za ushauri na maelekezo juu ya uhifadhi wa
Majengo hayo ili yasipoteze haiba na historia yake.
HADIDU REJEA YA NANE:
9.0 UKODISHWAJI WA KISIWA CHA CHANGUU.
9.1 Utangulizi:
Katika kuchuhguza juu ya suala la ukodishwaji wa kisiwa cha Changuu, Kamati ilitakiwa
ichunguze suala zima la ukodishwaji wa kisiwa hicho kwa mnasaba wa taratibu za Uwekezaji wa
Mradi huu wa Utalii. Katika uchunguzi wake, Kamati ilitakiwa iangalie iwapo ukodishwaji wa
kisiwa hicho umefuata taratibu za kisheria, vipi Shirika la Utalii lilihusika katika ukodishwaji
wake na kuchunguza iwapo ukodishwaji huo una tija kwa Serikali kiasi cha kuuruhusu uendelee.
Kamati imeifuatilia hadidu hii rejea katika kisiwa chenyewe cha Changuu kwa kukutana na
Watendaji wa Wizara na Taasisi zinazohusika na Uwekezaji, tarehe 30/11/2011, ambapo ilifanya
mahojiano na watendaji hao ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Watendaji
wa idara ya Mazingira, Idara ya Ardhi na Usajili, na Watendaji wa ZIPA. Aidha, ilikutana na
Mkodishwaji wa Kisiwa hicho na kupata muda wa kufanya ziara katika kisiwa husika. Ili tupate
ufafanuzi unaohitajika, ni vyema sasa tufuate utaratibu ufuao:
9.2 Maelezo yaliyotolewa na Watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali kuhusiana
na Ukodishwaji huo:
Katika maelezo yake aliyotoa mbele ya Kamati Teule, Meneja wa Shirika la Utalii alisema kuwa
shirika lake lilikabidhiwa kisiwa hiki mnamo mwaka 1984, na iliendelea kukihudumia mpaka
mwaka 2002 ambapo kilikodishwa mnamo mwezi wa Disemba. Waliokodishwa ni Kampuni ya
Leizure Hotels LTd. Mkataba wa Ukodishwaji huo umeambatanishwa kama Kielelezo Na. 229
cha taarifa hii.
213
Katika ukodishwaji huo uliofanywa na Serikali, Shirika la Utalii lilipewa Shilingi za Tanzania
Milioni Arobaini (TShs. 40,00,000/-) ili waondoshe mkono wao kwenye kisiwa hicho. Mbali ya
fedha hizo, Leizure Hotels Ltd wakatakiwa walipe kodi ya Dola Elfu Moja (US$ 1,000.00) kwa
mwezi. Kodi ya US$ 1,000.00 iliendelea kulipwa mpaka mwaka 2004 ambapo, katika shughuli
zake za kawaida, Kamati ya Baraza la Wawakilishi ilitembelea Kisiwa hicho na kufanya
mazungumzo na taasisi za Serikali zinazohusika na ukodishwaji huo. Kamati ya Baraza
haikuridhika na kiwango cha kodi ambacho kilikuwa kinalipwa na wakodishwaji hao. Baada ya
hapo kodi iliongezeka kufikia US$ 3,500.00, na kima hicho ndio kiliendelea kulipwa mpaka
wakati Kamati Teule inafanya mazungumzo haya.
Katika kujibu hoja za Wajumbe, Meneja wa Shirika la Utalii aliielezea Kamati kuwa wakati wao
wanasimamia biashara kwenye kisiwa hicho walikuwa wanakusanya wastani wa US$ 5,500.00
kwa ujumla ambazo kiasi kikubwa zilikuwa zinatumika kulipiwa gharama. Alieleza kuwa, hata
hivyo, wao walihusika katika kukodisha biashara tu, lakini ukodishwaji wa Kisiwa chenyewe
umefanywa na Idara ya Ardhi kwa mashirikiano na ZIPA.
Alieleza pia kuwa uamuzi wa kukodishwa biashara ambayo Shirika lake ilikuwa inafanya
kwenye Kisiwa hicho, ulitolewa na Serikali kwa maana ya Wizara ya Biashara nao wao (Shirika
la Utalii) kupewa taarifa tu kuwa Serikali imeamua hivyo. Hii pia ndio sababu kuwa Shirika la
Utalii halikupata nafasi ya kuzungumza na mwekezaji kuhusu kuingia kwenye ubia wa biashara
kwa sababu maamuzi ya ukodishwaji hayakuwa ya Shirika lenyewe bali ni maamuzi ya Serikali,
wao walijulishwa tu. Akielezea kuhusu makobe, alisema kuwa makobe bado ni mali ya Shirika
lakini wameyakodisha kwa Wawekezaji hao kwa kupitia mikataba maalumu iliyoidhinishwa na
Idara ya Uhakiki Mali, Makobe hao bado wanashughulikiwa na wafanyakazi wa Shirika la Utalii
lakini wanalipwa na muwekeaji. Kwenye mkataba wa kisiwa hivyo kuna masharti ambayo
yaliingizwa baadae kuhusiana na makobe. Alieleza pia kuwa hakuna makobe ambao
wameondoshwa kwenye kisiwa hicho kupelekwa Zanzibar Park. Ni kweli kuwa Shirika lilitaka
kukodisha makobe kwa Zanzibar Park lakini kutokana na hisia tofauti za wananchi kulikataa
suala hilo, Serikali iliamrisha kuachana na mkataba huo.
Kuhusu wafanyakazi ambao Shirika ilikuwa nao kwenye Kisiwa hicho wakati biashara
zinafanywa na Shirika lenyewe imeelezwa ilikuwa ni wafanyakazi 25. Wakati wa ukodishwaji
mwekezaji alikubali kuajiri wafanyakazi 11 miongoni mwao. Kwa hivyo wafanyakazi 14
walistaafishwa. Akijibu maswali ya wajumbe kuhusiana na uhai wa Shirika la Utalii, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari alieleza kuwa Shirika la Utalii linapigwa vita ikiwa ni pamoja na
wafanyakazi na Viongozi wa Shirika lenyewe. Alitoa mfano kuwa Shirika linaajiri mtu kuwa
“Tours Operator”, lakini mtu huyo huyo anafungua biashara yake binafsi ya “Tours Operators”
na huko ndiko wageni wanakoshughulikiwa.
9.3 Taarifa ya ZIPA kuhusiana na Mradi huu:
214
Kamati ilipokea pia taarifa ya ZIPA kuhusiana na mradi wa Kisiwa cha Changuu. Katika
maelezo ya ZIPA yaliyotolewa mbele ya Kamati Teule, ilielezwa kuwa Leisure Hotels Changuu
Island Zanzibar Ltd ndio ambayo imekodishwa kisiwa hicho. Kwamba walipeleka maombi
mnamo mwaka 2002 na ukodishwaji ukafanyika mwishoni mwaka 2002; na kukabidhiwa rasmi
kisiwa hicho mnamo Agosti 2003. Nakla ya maelezo ya ruhusa waliyopewa imefanywa
Kielelezo Na. 230 cha taarifa hii.
Katika maelezo yake ya mradi, Leisure Hotels walieleza kuwa watakuwa na vyumba vya kulala
wageni. Hivi sasa wana vyumba 27 ambavyo wamejenga wenyewe. Walieleza kuwa mradi wao
utakuwa na thamani ya ujumla ya US$ 1.1 milioni. Hata hivyo haieleweki kuwa ni kiasi gani
wameweza kuwekeza hadi sasa.
Ilielezwa pia kuwa tatizo moja kubwa la Kampuni ya Leisure Hotels ni utoaji wa taarifa za
shughuli zake. Kwa mujibu wa sheria wanatakiwa kutoa taarifa kwa kila robo ya mwaka (yaani
kila miezi mitatu). Lakini Kampuni hii wamekuwa na tatizo kubwa sana la kupata utaratibu juu
ya swala hili. Tokea kuanza biashara zao mpaka mwaka 2007 hawakuwahi kutoa taarifa yoyote.
Mnamo mwaka 2008 waliwahi kutumiwa barua tatu na ZIPA ndio baadae wakatoa taarifa moja
tu na ndio hiyo hiyo ambayo wamewahi kutoa katika muda wote wa shughuli zake. Barua
ambazo wamewahi kuandikiwa ni barua yenye Nam. ZIPA/HT/2001/L.14/36 ya tarehe
15/02/2008; barua yenye Nam. ZIPA/HT/2001/L.14/39 ya tarehe 25/11/2008 (Kielelezo Na.
231)
Maelezo yaliyotolewa na watendaji wa ZIPA kwa Kamati Teule yameonyesha kuwa Leisure
Hotels Ltd waliwahi kuzuiliwa vibali vinavyotolewa na ZIPA ndio baadae wakatoa taarifa
mnamo mwaka huo wa 2008, na hadi wakati Kamati inakusanya taarifa hizi hawakuwahi kutoa
taarifa nyengine. Jambo ambalo Kamati hii ilionyesha kutoridhika na namna ambavyo Serikali
inavumilia wawekezaji ambao hawatekelezi majukumu yao kisheria. Kwa mujibu wa taarifa
hiyo ya ZIPA ukiukwaji wa sheria kwa wawekezaji hapa Zanzibar ndio changamoto kubwa
inayoikabili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa kuhusiana na shughuli za utalii. Kamati
ilishauri Serikali ihakikishe kuwa inasimamia ipasavyo kuona kuwa masharti yote ya kisheria
yanatimizwa na kila muwekezaji.
Katika kujibu maswali ya Kamati, Watendaji wa ZIPA walieleza pia kuwa hadi sasa hakuna
takwimu yoyote inayopatikana Serikalini kiutendaji kwa Leizure Hotels Ltd inayoonyesha idadi
ya wageni wanaingia kwenye Kisiwa cha Changuu, si kwa siku, kwa mwezi wala mwaka. Pia
haieleweki ni kiasi gani cha mapato ambacho mwekezaji anaingiza kutokana na biashara
anazofanya kwenye Kisiwa hicho. Lakini kibaya zaidi ambacho Kamati Teule ilipewa taarifa
yake ni kuwa hakuna hatua inayochukuliwa wala taarifa yoyote inayopatikana ya kiulinzi na
usalama kwenye Kisiwa cha Changuu.
9.4 Taarifa ya Idara ya Mazingira:
215
Taarifa ya Idara ya Mazingira kwa Kamati Teule ilitolewa kwa maandishi, na nakla ya taarifa
imepokelewa na kufanywa Kielelezo Na. 232 cha taarifa hii. Taarifa hiyo inaonyesha kuwa
mnamo tarehe 01/10/2002 Idara ya Mazingira ilipokea barua kutoka ZIPA ambayo
iliambatanishwa na „Maelezo Yakinifu‟ ya mradi ambao Kampuni ya Leizure Hotels Ltd ilikuwa
inauombea vibali vya ZIPA. Idara ya Mazingira ilitakiwa itoe maoni yake juu ya maswala ya
kimazingira kuhusiana na Mradi huo uliopangwa kufanyika kwenye Kisiwa cha Changuu.
Idara ya Mazingira ilizingatia maelezo yaliyotolewa kuhusiana na mradi huo na ikatoa
mapendekezo yake kwenye barua iliyoituma ZIPA mnamo tarehe 09/10/2002. Katika barua
hiyo, Idara ya Mazingira imependekeza mambo yafuatayo yafanyike:-
(a) Kuitishwa kikao maalum cha kujadili mwekezaji katika visiwa. Ilishauriwa kikao
hiki kishirikishe viongozi wa taasisi zote zinazohusika ikiwemo Mazingira, Utalii,
Uvuvi, Misitu, Ardhi na ZIPA.
(b) Wawekezaji katika visiwa wasipewe vibali mpaka wafanye tathmini kamili ya
kimazingira na kijamii.
(c) Mradi wa Mwekezaji kwenye kisiwa ni lazima ueleweke wazi wazi. Hii inasaidia
Serikali kuweza kujua mapema namna ambavyo mradi unaoanzishwa unapaswa
kusimamiwa.
Kwa maelezo yaliyotolewa kwa maandishi na Idara ya Mazingira, mambo yote muhimu
yalizingatiwa ipasavyo katika kutathmini maelezo ya Mradi wa Leisure Hotels Ltd wa Changuu.
Katika tathmini ya kimazingira yalikuwepo mapungufu machache ambayo, baada ya
kusawazishwa, mwekezaji alipewa vibali vya kuendesha biashara zake ikiwa ni pamoja na kibali
cha mazingira.
Hata hivyo, katika ukaguzi wa kimazingira uliofanywa baada ya Leisure Hotel Ltd kuanza
shughuli zake iligundulika kuwa Leisure Hotel Ltd wamejenga „jetty‟ kinyume na utaratibu.
Utaratibu uliopo ni kuwa ili mwekezaji aruhusiwe kujenga „jetty‟ ni lazima apate vibali na afate
ushauri kutoka taasisi za mazingira, uvuvi na taasisi ya sayansi ya baharini.
Baada ya kugundua tatizo hilo Idara ya Mazingira ilitoa barua yenye kumbukumbu
IM/29/2/8/VOL.XV/61 ya tarehe 02/08/2011 kumtaka mwekezaji huyu afike Idara ya Mazingira
kuonyesha vielelezo vinavyomruhusu kujenga „jetty‟ lakini mpaka wakati Kamati imefanya
mazungumzo haya na watendaji wa Idara ya Mazingira, Mwekezaji huyo alikuwa hajatekeleza
agizo la kwenda kwenye Idara ya Mazingira kuonyesha vibali vyake na kupata maelezo zaidi
yanayohusu mazingira kutokana na jetty iliyojengwa.
Akijibu swali la Mjumbe wa Kamati, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira alieleza kuwa sio rahisi
kutaja athari yoyote ya mazingira inayotokana na ujengaji wa „jetty‟ kama hakuna utafiti maalum
uliofanywa. Hata hivyo vibali maalum vinahitajika kuhusiana na ujengaji wa „jetty‟ ili kuzipa
taasisi husika nafasi maalum ya kuweka tahadhari kwa kuzingatia matatizo ambayo yanaweza
kujitokeza katika ujengaji wa „jetty‟. Kwa mfano „jetty‟ inaweza kujengwa na ikawa inazuia
216
mwenendo wa maji. Kwa kuepuka tatizo hili, „jetty‟ inaporuhusiwa kujengwa, Idara ya
Mazingira huwa inaweka masharti kuwa „jetty‟ ijengwe juu ya nguzo. „Jetty‟ inapokuwa juu ya
nguzo, tatizo la kuzuiwa kwa mwenendo wa maji inakuwa halipo zaidi. Tatizo jengine ujenzi wa
„jetty‟ ambapo huwa tunalizingatia wakati wa kuruhusu ujenzi wa „jetty‟ ni endapo hapatokuwa
na usumbufu wowote kwa wananchi. Yaani, ikiwa „jetty‟ inayoombewa kujengwa haitazuia
mwenendo wa maji, na ikawa pia haitosababisha uzumbufu wa watu wanaotumia fukwe, basi
kwa kawaida Idara ya Mazingira huwa haina pingamizi ya kuruhusu ujengwaji wa „jetty‟.
Kuhusiana na „jetty‟ iliyojengwa kwenye, Leisure Hotels imeelezewa na inaonekana kuwa
haizuii mwenendo wa maji, na pia hakuna usumbufu wowowte ambao unaopatikana kwa watu
hasa kwa sababu kisiwa cha Changuu ambapo hoteli hiyo ipo, ni mbali na makaazi ya kawaida
ya watu.
9.5 Tarifa ya Idara ya Ardhi:
Taarifa ya watendaji wa Idara ya Ardhi ilizingatia zaidi namna ambavyo ukodishwaji wa Kisiwa
cha Changuu ulifanywa na mambo mengine yanayohusiana na hayo. Taarifa hiyo ilionyesha
kuwa baada ya mwekezaji kukubaliwa na ZIPA, taarifa huwa inapelekwa Idara ya Ardhi kwa
ajili ya upimaji na taratibu nyengine za upatikanaji wa „lease‟. Katika upimaji uliofanywa katika
kisiwa cha Changuu kilikutikana kuwa kina ukubwa wa hekta 11.27. Baada ya taratibu
kukamilika, Idara ya Ardhi ilitoa „lease‟ (Kodi), kiwango cha kodi kinacholipwa kutokana na
kodi hiyo kimefanyiwa mapitio (review) kila baada ya miaka mitatu. Hata hivyo chini ya Sheria
ya Ardhi ya 1992 (kifungu cha 46(6)), wakati kodi inafanyiwa mapitio, ongezeko la kodi kama
litakuwepo halitozidi 10%, na hata kama ardhi inakuwa imeendelezwa sana kiasi gani.
Akijibu swali la Mjumbe wa Kamati, Mkurugenzi wa Idara ya Ardhi alieleza kuwa wakati kodi
inapangwa kwa mara ya kwanza kwenye ukodishaji wa Kisiwa hicho hapakuwa na tathmini
yoyote ya ardhi iliyofanywa, na hadi sasa ardhi hiyo haijafanyiwa tathmini hasa ya kitaalamu.
Kwa upande wao, wajumbe wa Kamati walifurahishwa na namna Mwekezaji wa Kisiwa cha
Changuu alivyofanikiwa kukiendeleza kisiwa hicho na kukiweka katika hali ya kuvutia kabisa.
Kamati Teule ilimpongeza sana Mwekezaji katika Kisiwa cha Changuu (yaani „Leisure Hotels
Ltd) na kumtaka aendelee kukitunza kisiwa hicho pamoja na makobe aliokabidhiwa kwa maslahi
ya Zanzibar kwa ujumla.
9.6 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii rejea, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
217
9.6.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Serikali (kupita kwa Mamalaka ya Uwekezaji Zanzibar na vyombo vyengine
vinavyohusika), haina takwimu yoyote inayoonyesha idadi ya wageni wanaingia kwenye
kisiwa cha Changuu, si kwa siku, kwa mwezi wala mwaka. Pia haieleweki ni kiasi gani
cha mapato ambacho mwekezaji anaingiza kutokana na biashara anazofanya kwenye
Kisiwa hicho. Lakini kibaya zaidi, hakuna hatua inayochukuliwa wala taarifa yoyote
inayopatikana ya kiulinzi na usalama kwenye Kisiwa cha Changuu.
(ii) Tathmini ya Ardhi iliyokodishwa kwa Mwekezaji bado haijafanywa na Idara ya Ardhi,
kitu ambacho kinakengeuka taratibu zilizopo.
(iii)Shirika la Utalii halikushirikishwa kwa ukamilifu katika ukodishwaji wa biashara ya
utalii ambayo walikuwa wanaifanya kabla ya kisiwa hicho hakijakodishwa kwa
Mwekezaji.
(iv) Mmiliki wa Hoteli hiyo iliyopo katika kisiwa hicho hafuati ipasavyo sheria zinazongoza
masuala ya uwekezaji wa miradi ya kitalii ikiwa ni pamoja na kutoa tarifa za mapato
yake, wageni wanaoingia na kutoka Hotelini hapo. Aidha kwa upande wa Serikali,
Mamlaka husika haziwajibiki kikamilifu katika kufuatilia suala hili.
(v) Kamati imegundua ukiukwaji wa taratibu za kimazingira kuhusiana na ujenzi wa „jetty‟
katika Hoteli hiyo.
9.6.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:
(i) Serikali (kupitia ZRB) ifanye ukaguzi maalum wa kupata taarifa sahihi za wageni
wanaoingia kwenye kisiwa hicho na ni kiasi gani cha mapato huwa kinakusanywa
kutokana na biashara yote inayofanyika bila ya kusahau mapato yanayotokana na
makobe. Na ripoti ya tarifa hizi ziwasilishwe katika Baraza la Wawakilishi si zaidi ya
miezi 3 kuanzia tarehe ya kuwasilishwa kwa ripoti hii.
(ii) Serikali ihakikishe kuwa inafanya tathmini ya ardhi inayotaka kukodishwa kabla
haijakodishwa ili iweze kupatikana tathmini halisi ya kodi inayostahiki kulipwa kwa
thamani ya ardhí hiyo. Aidha, Tathmini ya ardhi pia ifanywe wakati wa kufanya mapitio
ya kodi kwa ajili ya kujua uongezo sahihi la thamani ya ardhi hiyo na kuweza kutoa picha
halisi juu ya ongezeko la kodi kutokana na mapitio ya kodi yanayofanyika.
(iii)Kuna haja ya kufanya marekebisho ya ongezeko la kodi kwamba lisiishie 10% ya kodi ya
awali kama ilivyo kwenye mikataba yote ya ukodishwaji ardhi ya Serikali hivi sasa. Na
kwa hivyo basi, kifungu 46(6) cha Sheria ya Ardhi (No. 12) ya 1992 inafaa kiangaliwe
upya ili kitoe nafasi ya ongezeko la kodi la zaidi ya 10% ya kodi ya awali endapo
218
kutakuwa na ongezeko kubwa la thamani ya ardhi iliyokodishwa, pamoja na kiasi
kikubwa cha mapato kinachokusanywa na Mwekezaji kwenye ardhi husika.
(iv) Serikali ichukuwe hatua za makusudi za kulinda usalama kwenye maeneo ya visiwa
kama Changuu; na Serikali inapaswa kulitafakari suala hili kwa kuzingatia namna ya
kuzitumia Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya.
(v) Serikali ihakikishe inamsimamia ipasavyo Mwekezaji huyu ili azifuate kwa ukamilifu
sheria zinazohusiana na uwekezaji na hatua hii pia ifanywe kwa wawekezaji wote nchini.
(vi) Idara ya Mazingira na Taasisi nyengine zinazohusika, ifanye utafiti wa tathmni ya
mazingira kuhusiana na ujenzi wa „jetty‟ iliyojengwa kisiwani humo na ikiridhika kuna
uaharibifu mkubwa wa mazingira, Kamati inapendekeza hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi ya Mmiliki wa Hoteli hiyo.
HADIDU REJEA YA TISA:
10.0 USAMBAZAJI WA MAJENERETA YALIYOKUSUDIWA KUSAIDIA
USAMBAZJI WA MAJI:
10.1 Utangulizi:
Katika kufuatilia hadidu hii rejea, Kamati imetakiwa kuchunguza iwapo kuna majenereta 12
yaliyotolewa na UNICEF na kusambazwa katika vituo vya maji ili kusaidia usambazaji wa maji
wakati umeme unapozimwa. Na kama yapo, jee yapo katika maeneo yaliyokusudiwa na
yanafanya kazi au tayari yameshapotea katika mazingira yoyote ile. Kamati ililifanyia kazi suala
hili kwa siku mbili, baada ya Kikao cha pamoja na Watendaji wakuu, Wizara ya Ardhi, Makaazi,
Maji na Nishati na hatimae hufanya ziara ya kuyatambua majenereta hayo, ikiwa ni pamoja na
kufika katika Ofisi za UNICEF kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa majenereta hayo. Ili kupata
ufafanuzi wa suala hili, ni vyema tukapata maelezo yafuatayo:
10.2 Taarifa ya Majenereta kutoka kwa Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji
na Nishati:
Taarifa ya majenereta ilitolewa kwa Kamati na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Ndg.
Mustafa Ali Garu ambae alieleza kuwa majenereta yanayouliziwa na Kamati idadi yake ni 12.
Majenereta haya yalipokelewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mnamo 2008 kutoka
UNICEF ili yaweze kutumika kwa ajili ya operesheni wakati wa matatizo ya umeme hapa
Zanzibar. Baada ya majenereta hayo kumaliza kutumika kwenye operesheni yaliwekwa mahali
maalum kwa ajili ya kutunzwa. Hata hivyo, wakati mwengine majenereta hayo huwa yanatumika
kwa ajili ya huduma za maji endapo pametokea tatizo la umeme kwenye visima vya maji.
Ilielezwa kuwa wakati wa mazungumzo ya Kamati na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Maji, majenereta yote 12 yapo katika kutoa huduma kwenye visima vya maji. Wajumbe wa
Kamati waliomba wapelekwe kwenye visima ambapo jenereta hizo zipo ili waweze kujionea
219
wenyewe na kuweza kuthibitisha kuwepo au kutokuwepo kwa jenereta. Hata hivyo, kabla safari
ya Wajumbe kwenda kuona jenereta hizo kuanza, wajumbe walitaka wapate maelezo ambayo
yangewawezesha kuyatambua hayo majenereta watapokwenda kuyaona. Jibu la awali ambalo
wajumbe walipewa ni kuwa kwa kawaida majenereta huwa hayana nambari za utambulisho
(serial numbers) kwa hivyo ni vigumu kuweza kuyatambua kuwa haya ndio majenereta
yaliyotolewa msaada na UNICEF isipokuwa wangeweza kuyatambua kupitia tarifa za watu
ambao wanayatambua kutokana na kukabidhiwa majenereta hayo.
Taarifa hiyo ilisababisha mshangao kwa Waheshimiwa Wajumbe ambao walishindwa kuamini
kuwa kifaa cha gharama kubwa kama jenereta linaweza lisiwe na nambari ya utambulisho.
Kufikia hatua hii Kamati ilifanikiwa kupata orodha ya mahali ambapo jenereta hayo 12 ilidaiwa
yapo (kwenye visima). Hata hivyo, Wajumbe wa Kamati waliamua kuwa haitasaidia sana
kwenda kwenye visima kuangalia jenereta ziizotolewa msaada na UNICEF wakati hawana
maelezo yoyote yanayofanya majenereta hayo yatambulike. Wasi wasi huu uliwafanya
Wajumbe wa Kamati waende kwenye UNICEF kuweza kupata taarifa za makabidhiano ya
majenereta hayo, taarifa ambazo zilielezewa kuwa hazipo kwenye Ofisi ya ZAWA.
Kwenye Ofisi ya UNICEF, hapo Kinazini Zanzibar, Wajumbe wa Kamati walifanikiwa kupata
orodha kamili ya majenereta yaliyokabidhiwa kwa ZAWA na UNICEF. Baada ya kupata taarifa
hiyo muhimu, Wajumbe wa Kamati walifanya safari siku za tarehe 01/12/2011 na 02/12/2011
kuyatembelea majenereta hayo kwenye visima mbali mbali ambapo walielezwa kuwa majenereta
hayo yapo kwa ajili ya kutoa huduma. Taarifa kamili juu ya majenereta hayo na mahali ambapo
Kamati iliyakuta ni kama ifuatavyo:-
No. AINA YA JENERETA NAMBARI YA
UTAMBULISHO
MAHALI ILIPOONEKANA
1. 100KVA Perkins Diesel Engine U413961P Mwembe Mapapai, Donge
2. 60KVA Perkins Diesel Engine 4093005N Machui
3. 42KVA Perkins Diesel Engine 4080470N Jendele
4. 20KVA Perkins Diesel Engine 09301399N Chau
5. 60KVA Perkins Diesel Serial No. 11606591 Saateni
6. 60KVA Perkins Diesel Serial No. 11606778 Bambi
7. 45KVA Perkins Diesel Serial No. 11603576 Unguja Ukuu
8. 45KVA Perkins Diesel Serial No. 11603575 Dimani
9. 27KVA Perkins Diesel Serial No. 117703691 Dimani
220
10. 27KVA Perkins Diesel Serial No. 11702954 Lililoonekana Kandwi ni Serial
No. 11702754
11. 27KVA Pekins Diesel Serial No. 11603576 Iliyopo Mombasa ni Serial No.
11703837 (Baada ya Kufuatiliwa,
imegunduliwa kuwa Halipo)
12. 100KVA F.G. Wilson Serial No. FGWPEP 04AE-
0A16360
Saateni
Kulingana na taarifa inavyoonekana hapa juu, miongoni mwa majenereta 12 yaliyotolewa
msaada na UNICEF ni majenereta 10 (Namba 1 – 10) ambayo yalionekana bila ya kuacha wasi
wasi wowowte. Jenereta ambalo limeorodheshwa namba 11 Kamati ilikubaliana na Watendaji
wa Mamlaka ya Maji kuwa huenda ikawa nambari yake ilikosewa. Nambari iliyomo kwenye
jenereta ni 11702954 wakati nambari ya kwenye orodha inasomeka kuwa ni 11702754. Kamati
imekubaliana na hoja kuwa kuna uwezekano mkubwa tofauti iliopo huenda imetokana na
makosa ya kibinadamu tu wakati wa kuorodhesha nambari ya jenereta halisi.
Hata hivyo, jenereta lililoainishwa kwenye orodha kama namba 11603576 na kuelezewa kuwa
lipo kwenye kisima cha maji cha Mombasa kwa Mchina, Wajumbe wa Kamati hawakuliona
kabisa jenereta hilo. Jenereta lililokuwepo Mombasa kwa Mchina wakati Kamati Teule
ilipofanya ziara yake mahali hapo ni lenye nambari 11703837.
Maelezo haya kwa ujumla yake yameonyesha kuwa kati ya majenereta 12 yaliyotolewa msaada
na UNICEF kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Jenereta moja limekosekana na wala
halijulikani lilipo.
10.3 Matatizo Mengine yanayohusu Majenereta:
10.3.1 ZAWA Kutumia Watu wasio Waajriwa:
Jambo moja ambalo ni maarufu sana katika visima kadhaa vya maji vinavyomilikiwa na ZAWA
ni kuwa kuna watu ambao wafanyakazi wa ZAWA bila ya wao wenyewe kuajiriwa. Kibaya
zaidi, walio wengi hawapewi hata kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya malipo ya kazi
wanayofanya. Kamati imeiona hali hii inaweza kuhatarisha usalama wa jenereta hizo, kwani
katika hali kama hii, inawezekana sana watu wasiolipwa wakati wanafanya kazi, kunawafanya
wasijali uzima na thamani ya majenereta hayo.
10.3.2 Hali ya Majenereta yenyewe:
Katika ziara yake Kamati Teule ilijionea yenyewe kuwa miongoni mwa majenereta haya 12,
hakuna hata jenereta 1 ambalo lilikuwa lina uwezo wa kufanya kazi. Yaani, hapakuwa na
jenereta hata moja ambalo liliweza kuwashwa na kushika moto, wakati Wajumbe wa Kamati
ilipotembelea kwenye majenereta hayo.
221
Maelezo ya jumla ambayo Wajumbe wa Kamati Teule walipewa kwenye sehemu ambapo
majenereta hayo yapo ni kuwa ZAWA huwa hawapeleki hata mafuta kidogo kwa ajili ya
kuyapiga moto hayo majenereta. Kutokana na kukosa angalau kupigwa moto (kuwashwa)
majenereta yote ambayo Kamati ilipata nafasi ya kuyakaguwa ilikuwa hayawaki. Baadhi yao
tulielezwa kuwa ni mazima lakini Kamati haiwezi kuthibitisha kuwa majenereta hayo ni mazima
kwa sababu hayana mafuta hata ya kuweza kupigwa moto (kuwashwa). Baadhi ya majenereta
yalielezewa kuwa hayawezi tena kuwaka kwa sababu yamekaa muda mrefu bila ya kuwashwa.
Kwa ufupi, Kamati haikuona lolote kati ya majenereta hayo 12 ambalo linafanyakazi. Kwamba
yameharibika kutokana na kuachwa muda mrefu bila ya kufanyiwa uangalizi na bila ya
kutumika. Hali ilivyo sasa ni kuwa kwenye visima vyote ambavyo Kamati ilivitembelea hakuna
uwezekano wa majenereta kufanyakazi endapo umeme ungekatika. Tunaomba Baraza hili
tukufu lielewe hivyo.
10.4 Kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukuliwa kutokana na matokeo ya
uchunguzi huo.
Katika kutoa maelezo juu ya Hadidu hii rejea, Kamati imeona ni vyema kwanza itoe Muhtasari
wa mambo iliyoyagundua (Observation) na hatimae ndio itoe mapendekezo yake kwa Serikali
juu ya hatua za kuchukuliwa.
10.4.1 Muhtasari wa Mambo yaliyobainika na Kamati kufuatia Uchunguzi wake wa
Hadidu hii Rejea:
(i) Mamlaka ya Maji (ZAWA) imeshindwa kuzitambua mali zake (Majenereta hayo 12)
hali inayoonesha toka mwanzo kwamba hawakuwa na uchungu na kuharibika kwake.
(ii) Kitendo cha ya ZAWA kuwatumia watu ili kufanyakazi bila ya kuwalipa wala
kuwaajiri kinakiuka haki za binaadamu na wala hakivumiliki na Kamati imegundua
kuwa ni miongoni mwa sababu zinazopelekea watu hawa kutokuwa na uchungu wa
mali za ZAWA (ikiwa ni pamoja na majenereta) na matokeo yake uharibifu
unapotokezea, hakuna wa kuchukua hatua.
(iii)Kamati imegundua kuwa majenereta yote 11 iliyoyaona hayafanyi kazi na hii
imesababishwa na uzembe wa ZAWA kutopeleka mafuta ili majenereta hayo
yakaweza kutumika .
(iv) Lengo la kutolewa majenereta hayo halikufikiwa ipasavyo kwa sababu
hayajakusudiwa yatumike kwa muda mdogo na kuharibika mapema kama hali ya
majenereta hayo ilivyo hivi sasa.
10.4.2 Hatua za Kuchukuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo.
Kutokana na uchunguzi huo tulionesha kapo juu, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo
zichukuliwe:
222
(i) Mamlaka ya Maji (ZAWA) ilitafute jenereta ambalo Kamati imeshindwa kulitambua
ndani ya miezi mitatu tokea tarehe ya kuwasilishwa kwa ripoti hii na ikishindwa,
Mkurugenzi Mkuu wa ZAWA anawajibika kulilipa kupitia mshahara wake.
(ii) Majenereta yote 11 yaliyotambuliwa na Kamati yafanyiwe matengenezo ya haraka ndani
ya mwezi na yapatiwe mafuta ili yaweze kutumika kama ilivyokusudiwa.
(iii)Watu wanaotoa huduma vituoni(kwenye visima vya maji) watafutiwe utaratibu wa
kuajiriwa na katika kipindi chote hiki cha kusubiri ajira zao, ZAWA iwalipe posho za
kufanya kazi hiyo na suala hili litekelezwe mara moja.
SEHEMU YA TATU:
11.0 HITIMISHO:
Kamati inapenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mhe. Spika na Wajumbe wote wa Baraza la
Wawakilishi kwa maamuzi yao ya kuunda Kamati Teule ili kuchunguza mambo mbali mbali
yaliyohitaji kuchunguzwa kwa kina ili usahihi wake ufahamike kwa wananchi, lakini hatua ya
kwanza ni kuwasilishwa katika Baraza hili, hali hii imekuja kufuatia ufafanuzi wa mambo hayo
ulipotolewa na Serikali, haukuwaridhisha wajumbe waliowengi, na suluhisho la tatizo hili, kwa
busara zao, waliona ni kuunda Kamati hii, ili ikayafanyie utafiti yakinifu na matokeo ama taarifa
ya utafiti huo yawasilishwe Barazani. Kamati inatoa shukurani zake za dhati kwa Serikali na
zaidi kwa taasisi zote zilizohusika na kazi za Kamati, kwa mashirikiano yao ya muda wote
waliyoyaonesha kwa Kamati. Hata hivyo, Kamati inasisitiza haja ya kuwaelimisha watendaji wa
Serikali kwamba, Baraza hili tukufu la Wawakilishi ni chombo kinachoaminiwa na wananchi na
moja kati ya dhima walizokipa, ni kusema ukweli bila ya kificho kwa maslahi ya umma.
Pamoja na pongezi zetu kwa taasisi nyingi za Serikali na watendaji wake, tunasikitika kwamba
kuna baadhi ya watendaji hawakutoa ushirikiano mzuri kwa Kamati, mpaka pale Kamati
ilipolazimika kutumia uwezo wake wa sheria na kanuni mbali mbali. Jambo baya zaidi ambalo
halitaendelea kuvumilika, ni ile tabia ya baadhi ya watendaji na baadhi ya wakati hata viongozi
wa Taasisi hizi, kutaka kuipotosha Kamati kwa makusudi kwa kuipa taarifa zisizo za kweli ili
Kamati isifikie lengo ililotumwa na Baraza hili Tukufu. Lakini kwa umakini mkubwa sana wa
Kamati, tatizo hili limedhibitiwa na mara zote Kamati imehakikisha inaipokea taarifa yao kwa
upande mmoja, lakini kwa kutumia kila aina ya uwezo wake, ilifuatilia kwa undani na
kufanikiwa kupata ukweli ambao kwa ukamilifu wake tumeshaueleza katika ripoti hii.
Kamati inachukua fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru zaidi wananchi mbali mbali
wasiokuwa wafanyakazi wa Serikali ambao kwa namna moja ama nyengine walihusika na wito
wa Kamati, kwa mashirikiano yao mazuri waliyoyatoa, (ingawaje kwa baadhi ya waliisumbua
Kamati) kwa ujumla Kamati inawapongeza na kuwashukuru. Shukurani za pekee zim uendee
Ndg. Aman Ibrahim Makungu, Mkurugenzi wa E.A.Media, Mwakilishi wa Aga Khan Trust na
223
wengine wengi ambao walikuwa wawazi sana katika majibu yao kiasi ambacho kiliisaidia sana
Kamati kupata taarifa ilizozitafuta kwa wepesi mkubwa, hali ilosaidia sana kukamilika kwa kazi
hii.
Kwa ujumla wake, Kamati inashukuru kumaliza kwa salama kazi hii nzito iliyotumwa kuifanya
huku ikifahamu kwamba, Serikali na kila aliehusika atapata kioo cha kujimurika na kujifahamu
na hatimae atafanya marekebisho makubwa kwa kasoro ambazo kwa ukamilifu wake, Kamati
imezionesha na kuzitolea mapendekezo yanayofaa. Kamati inaamini kwamba ripoti hii itaisaidia
sana Serikali katika utelezaji bora wa majukumu yake, huku ikiheshimu haki na wajibu wa
Baraza la Wawakilishi katika kuisimamia kwa maana ile ile ya kuishauri, kuielekeza, na hata
kuikosoa panapohaja ya kufanya hivyo, lakini jambo la msingi zaidi ni kuisifu na kuipongeza
pale inapowajibika kwa maslahi ya wananchi wake.
Ripoti hii ni elimu tosha na ufahamu uliofikia kilele cha mafanikio kwa wananchi wote wa
Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na wasomaji wote wanaoutumia muda wao vizuri kwa
kujisomea taarifa mbali mbali ili kupata elimu na ufahamu wa kuwaongezea maarifa. Kwa
kupitia ripoti hii, mambo mbali mbali ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ni kilio kwa wananchi
kwa kukosa ufasaha wake au wamekuwa wakiyalalamikia kwa kuyajua kwa kiasi, basi watapata
upeo wa ufahamu na uelewa mzuri kwa kuisoma ripoti hii.
Kubwa zaidi, baada ya maelezo yote hayo ni kwamba, Kamati imetoa mapendekezo kadhaa kwa
kila hadidu rejea iliyoifuatilia. Tumefanya hivyo kwa lengo la kurahisisha ufahamu na ufasaha,
lakini kwa kuweka wepesi wa kutekelezwa kwake kama inavyostahiki kufanywa hivyo. Pamoja
na kwamba tayari tumeshaeleza maoni na mapendekezo yetu katika kila mwisho wa hadidu rejea
husika, kwa kuwa tunatakiwa kwa maelekezo ya kanuni ya 119(5) ya Kanuni za Baraza la
Wawakilishi Toleo la 2011, kutoa ripoti yetu na sehemu ya tatu ya hitimisho, tutoe maoni na
mapendekezo yetu kwa Baraza, ni vyema tukarejea kwa ufupi kuitaka Serikali iyapokee na
kuyatekeleza kwa vitendo mapendekezo yote tuliyoyatoa kwa mnasaba wa ripoti yetu hii, kwa
lengo moja kuu, nalo ni kuijenga nchi yetu na kuifanya izidi kuwa ni sehemu ya furaha kwa kila
mtu anaeishi katika nchi hii.
Kwa kuwa Kamati hii ilitumwa kufuatilia mambo hayo tuliyoyaeleza kwa upana wake katika
ripoti hii, na kwa kuwa ilitakiwa ilete ripoti yake Barazani, tunashukuru kwa kutekeleza vizuri
majukumu yetu na matakwa ya sheria na kanuni za Baraza lakini tunazidi kulitaka Baraza la
Wawakilishi liipokee ripoti hii kwa ukamilifu wake na kwa pamoja kuyasimamia mapendekezo
ya ripoti hii kama Baraza linavyowajibika kuisimamia Serikali, basi usimamizi huu uendelee
kuisaidia Serikali kuyatekeleza mapendekezo ya ripoti hii kivitendo bila ya kujali maslahi binafsi
lakini maslahi ya wananchi na nchi yetu yakipewa kipaumbele cha juu kabisa.
224
Tunapendekeza zaidi kwa manufaa ya wananchi wetu kwamba ripoti hii baada ya kupitishwa
Barazani, iwe rahisi na rafiki kwa kila mtu anaeihitaji. Kwa maana, isiuzwe lakini iwe inatolewa
bure na kila anaetaka afike katika Afisi ya Baraza la Wawakilishi ili aweze kuipata angalau kwa
njia ya „soft copy‟. Aidha, kwa kuwa Baraza la Wawakilishi lina tovuti yake (web site),
tunapendekeza ripoti hii iwekwe katika web site hiyo, na iwekwe katika hali ya kuhifadhiwa
isiharibiwe wala kuandikwa chochote (auditing), lakini iwekwe katika hali ya kuwezekana
kupatikana (down loading) kwa kila mtumiaji wa tovuti hiyo kwa njia ya urahisi kabisa.
Tunazidi kupendekeza kwamba, ripoti hii na ibakie katika Maktaba ya Afisi ya Baraza la
Wawakilishi, ili iwe rahisi kwa kila mtumiaji wa maktaba hiyo kuipata ripoti hii kwa wepesi.
Tunapendekeza hivi kwa sababu, moja kati ya dhima za Kamati hii ni kutafuta taarifa za kweli
ambazo kwa ukamilifu wake tumezipata, basi kwa kila mwenye elimu na kufahamu jambo moja,
ni wajibu wake aitoe elimu hiyo kwa wengine, kwa maana ni wajibu wetu sasa kuwaelimisha
wananchi wetu wafahamu kwa usahihi mambo yote ambayo wao ndio waliowatuma wawakilishi
wao kuyasimamia.
Mwisho kabisa, Kamati inaliomba Baraza hili tukufu liitake Serikali iyatekeleze mapendekezo
ya ripoti hii ndani ya miezi 3 kutoka tarehe ya kuwasilishwa kwa ripoti hii na hatimae Serikali
iwasilishe taarifa ya utekelezaji wake katika Baraza hili tukufu.
ORODHA YA WAJUMBE NA MAKATIBU WA KAMATI TEULE YA BARAZA LA WAWAKILISHI-
ZANZIBAR.
S.NO. JINA WADHIFA SAINI
1. Mhe. Omar Ali Shehe Mwenyekiti
2. Mhe. Asha Bakari Makame Mjumbe
3. Mhe. Hamza Hassan Juma Mjumbe
4. Mhe. Hija Hassan Hija Mjumbe
5. Mhe. Mbarouk Wadi Mussa (Mtando) Mjumbe
6. Ndg. Yahya Khamis Hamad Katibu
7. Ndg. Othman Ali Haji Katibu