processing the issues of your heart (swahili)

24
Kutengeneza Masuala ya Moyo Wako

Upload: fresh-start-for-all-nations

Post on 23-Jul-2016

264 views

Category:

Documents


8 download

DESCRIPTION

 

TRANSCRIPT

Page 1: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

Kutengeneza Masuala

ya Moyo Wako

Page 2: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

Scripture quotations marked (KJV/NKJV) are taken from the HOLY BIBLE, KING JAMES VERSION

- Public Domain

Where indicated (NASB): "Scripture quotations taken from the New American Standard Bible®,

Copyright © 1960, 1962, 1963, 1968, 1971, 1972, 1973, 1975, 1977, 1995 by

The Lockman Foundation - Used by permission." (www.Lockman.org)

Scripture quotations marked (NIV) are taken from the HOLY BIBLE, NEW INTERNATIONAL

VERSION®. NIV®. Copyright© 1973, 1978, 1984 by International Bible Society.

Used by permission of Zondervan. All rights reserved.

Je, umewahi kujisikia ukiwa chini

au katika hali ya kushindwa,

au kukwama katika hali yako ya sasa?

Je, uhusiano wako huonekana ukiwa

na dhiki na mvutano kila wakati?

Je, umekubwa na hasara hivi karibuni?

Haujachelewa kamwe kuanza MWANZO MPYA!

Page 3: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 1

Kama moyo wako ulikuwa chemchemi tu (chanzo cha maji) ambayo wengine wangeweza kunywa, je, wangekuwa na afya jinsi gani?

Swali inayotisha, si hivyo? Ni nani ambaye moyo wake haujawahi kuathirika kwa sababu ya mtu au kitu? Lakini, hata kama chemchemi yetu “imechafuliwa” na ukosefu wa msamaha au uchungu, bado tunaweza kuwa na "mwanzo mpya" kwa moyo wetu!

Ni maombi yetu kwamba unapotengeneza masuala ya moyo wako kwa kuandika majibu yako ya maswali katika kurasa zifuatazo, utakuwa huru kutokana na maisha yako ya hapo awali, si kuishi tu bali kustawi wakati huu, na kuwa na matumaini katika maisha yako ya baadaye!

Pia, tafadhali kumbuka Ultimate Fresh Start (Mwanzo Mpya wa Msingi) katika ukurasa wa 20. Kwa ajili ya mchakato wako ukuongoze katika uhuru wa kweli, na maisha ya kusamehewa na kusamehe, itakuwa ni muhimu kuwa na uzoefu wa Mwanzo Mpya ywa Msingi kabla ya Sehemu ya V - KUSAMEHE. Vinginevyo, huwezi kupeana kile ambacho haujapewa.

Kumbuka, HAUJACHELEWA KABISA!

Kusamehewa, mwenye kusamehe na kuwa huru,

Mchungaji Steve na Mindy Peterson

Kutengeneza Masuala ya Moyo Wako

Mchakato na njia katika kukusaidia kutatua masuala ya kosa, uchungu, na hasara

"Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo, maana

ndiko zitokako chemchemi za uzima," Mithali 4:23

Page 4: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 2

I Kosa / Uchungu / Hasara

NININI AU NANI AMEKUKOSEA AU KUKUUMIZA? AU ... UMEPOTEZA NANI AU NINI? “Ee BWANA, unijaribu, uupime moyo wangu na nia yangu,.” Zaburi 26:2

Anza kwa kutambua sehemu za makosa, uchungu au hasara katika maisha yako.

(a) Orodhesha makosa maalum au machungu, na mtu (watu) waliohusika:

· Watu waliokukataa kwa namna fulani, na jinsi walivyokukataa · Watu au mazingira ambapo haki zako zimekiukwa au

ulidhulumiwa · Migogoro inayo washirikisha marafiki, familia, kazi, kanisa au

mambo mengine · Talaka au kutengana

· Nyingine

Page 5: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 3

(b) Orodhesha hasara kubwa zilizokukabili katika maisha yako:

· Kupoteza kazi · Kudhoofika kiafya · Kupoteza uhusiano kutokana na ugomvi, talaka, kutengana, au

kifo · Kupoteza ndoto kwa ajili ya maisha yako au maisha yako ya

baadaye kuhusu ndoa, watoto, au kazi · Mengineo

(c) Chagua kosa moja hapo juu, machungu au hasara ili

utengeneze wakati huu.

Kosa, uchungu au hasara ni:

Mtu aliyekosa ni:

HAUJACHELEWA KABISA!...

Page 6: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 4

II ATHIRI

JE, UMEATHIRIWA KWA NJIA GANI?

“Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu.” Zaburi 139:23 Ni jinsi gani kosa hii maalum, uchungu au hasara ilikuathiri?

(a) Mawazo yako yamekuwa gani?

(b) Mawazo yako yamekuwa gani kwa mtu aliyehusika (kama inafaa)?

Page 7: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 5

(c) Je, hisia zako zimekuwa gani? Ifuatayo ni orodha ya

maneno ya kukusaidia kutambua vile unaweza kuwa unahisi kutokana na kosa maalum, uchungu au hasara. Ifuatayo ni orodha ya maneno ya kukusaidia kutambua vile unaweza kuwa unahisi kutokana na kosa maalum, uchungu au hasara.

Weka mviringo katika mambo yanayokugusa:

Kukataliwa Kushindwa Kukosa matumaini Machungu Kuhukumiwa Mwenye Hasira kali Hasira Kutelekezwa Aliye na hatia Asiojiweza Bubu Asiyetakikana

Asiyeambilika Mchafu Mwenye mashaka

Mpumbavu Mpweke Mwenye haya nyingi Asiyeamini Mwoga Asiye na thamani Mwenye chuki Mwenye matusi Mwenye wasiwasi Asiye pendwa Mwenye kuchukia Asiye na usalama

Mwenye huzuni Asiyevutia Mwenye mafadhaiko

Mpungufu Asiyelindwa Mwenye kutumiwa vibaya Mnene Aliye salitiwa Mwenye kupoteza

Mtu duni Aliye naswa Mwathiriwa na janga Mlaaniwa Mshutumiwa Mwenye wivu

Kwa kutumia maneno uliyo zungushia hapo juu, au maneno mengine ambayo yanahusu, andika jinsi kosa hili maalum, uchungu au hasara imekuathiri wewe mwenyewe.

HAUJACHELEWA KABISA!...

Page 8: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 6

III JIBU

JE, UMEJIBU VIPI KUHUSU KOSA HILI MAALUM, UCHUNGU, AU HASARA?

“Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele.” Zaburi 139:24 (a) Umesema nini?

Page 9: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 7

(b) Umefanya nini?

(c) Umeamua kufanya nini kuhusu jibu lako katika kila kosa, uchungu, au hasara ambayo unatengeneza?

HAUJACHELEWA KABISA!...

Page 10: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 8

IV MIMINA MOYO WAKO

Mimina MOYO WAKO KWA BWANA

Enyi watu, mtumainini Yeye, wakati wote, mmiminieni Yeye mioyo yenu, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.” Zaburi 62:8

“Namlilia BWANA kwa sauti kubwa, nainua sauti yangu kwa BWANA anihurumie. Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu.” Zaburi 142:1-2

(a) Mimina moyo wako kwa Bwana. Andika katika nafasi iliyo hapo chini hasa vile unajisikia

Bwana, hivi ndivyo ninajisikia:

Page 11: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 9

(b) Eleza Bwana mambo unayotamani lakini hayajatimizwa.

Bwana, hii ni njambo ambalo limenivunja moyo au linalonifadhaisha, au natami lingetokea hivi (au kuwa halingetokea hivi)

HAUJACHELEWA KABISA!...

Page 12: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 10

(c) Eleza Bwana mambo unayotamani sasa: Bwana, ninatamani:

Page 13: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 11

(d) Mshukuru Bwana:

“Shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.” 1 Wathesalonike 5:18

“…. sikuzote mkimshukuru Mungu Baba katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo kwa kila jambo.” Waefeso 5:20

“Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana na uniiite siku ya taabu nami nitakuokoa nawe utanitukuza…. Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi, naye aiandaaye njia yake jinsi ipasavyo nitamwonyesha wokovu wa Mungu.’’ Zaburi 50:14-15, 23 “Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la BWANA.” Zaburi 116:17

“Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.” 1 Wakorintho 1:18 “Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi Lake. Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe, ili Yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.” Warumi 8:28-29

Andika umwambie Bwana kwa maneno yako kwamba wewe unatoa shukrani kwa ajili ya hali na mazingira, na ya kwamba wewe uko tayari kukubali chochote mradi tu anataka kukitumia katika maisha yako kwa madhumuni yake, na kwa ajili ya mema kwako.

Bwana, nimechagua kutoa shukrani kwa ajili ya:

HAUJACHELEWA KABISA!...

Page 14: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 12

V KUSAMEHE

SAMEHE YULE AMBAYE AMEKUJERUHI AU AMEKUKOSEA.

Mfano wa Mtumishi asiyesamehe….

“Ndipo Petro akamjia Yesu na kumwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?” Yesu akamjibu, ‘‘Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.’’ ‘‘Kwa hiyo Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu zake za fedha na watumishi wake. Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta 10,000, aliletwa kwake. Kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake akaamuru kwamba auzwe, yeye, mkewe, watoto wake na vyote alivyokuwa navyo, ili lile deni lipate kulipwa. ‘‘Yule mtumishi akampigia magoti, akamsihi yule bwana akisema, `Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’’ Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake. “Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa memkopesha dinari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’ “Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’ “Lakini akakataa. Badala yake, alienda akamtupa gerezani hata atakapolipa hilo deni. ”Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia. “Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu! Mimi nilikusamehe deni lako lote uliponisihi. Je, haikukupasa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhurumia wewe?’ Kwa hasira yule bwana wake akamtia yule mtumishi mikononi mwa askari wa gereza ili ateswe mpaka atakapolipa yote aliyokuwa anadaiwa. “Hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ikiwa hatamsamehe kutoka moyoni kila mmoja ndugu yake aliyemkosea.’’

Mathayo 18:21-35

Page 15: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 13

(a) Andika maneno yako ya kukiri kwa ajili ya ukosefu wa

msamaha - "Lipa deni langu!" - kwa Bwana, pamoja na mitazamo isiyofaa na /au majibu mabaya.

HAUJACHELEWA KABISA!...

Page 16: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 14

(b) Chagua kumsamehe yule aliyekujeruhi au aliyekukosea.

KUFUTIA MADENI!

(c) Andika maombi yako kwa Bwana ukielezea uamuzi wako

wa kusamehe mtu ambaye amekujeruhi au amekukosea. Elezea makosa au mauchungu hayo kwa undani na jinsi yalivyokuathiri katika hapo awali, sasa, na katika siku zijazo.

Page 17: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 15

HAUJACHELEWA KABISA!...

Page 18: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 16

VI ACHILIA

ACHILIA KOSA, UCHUNGU AU HASARA YAKO KWA BWANA!

“Mtwike BWANA fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke. Lakini Wewe, Ee Mungu, utawashusha waovu katika shimo la uharibifu. Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila, hawataishi nusu ya siku zao. Lakini mimi, ninakutumaini Wewe.”

Zaburi 55:22-23

“Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu. Msimlipe mtu ye yote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Kisasi ni juu Yangu, Mimi nitalipa, asema Bwana.” Badala yake: “adui yako akiwa na njaa, mpe chakula, akiwa na kiu, mnyweshe. Maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto yanayowaka kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushindeni ubaya kwa wema.”

Warumi 12:16-21 “Meneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu na Mkombozi wangu.”

Zaburi 19:14

Page 19: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 17

(a) Kabidhi mtu na / au hali kwa Bwana.

(b) Andika katika sehemu iliyohapo chini, kwa mfano wa maombi, mtu au hali unayo kabidhi Bwana:

(c) Bariki na uombee mtu aliyekukosea au aliyekujeruhi.

“Yesu akasema, ‘Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!’” Luka 23:34

“Lakini mimi ninawaambia : Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi,”

Mathayo 5:44

HAUJACHELEWA KABISA!...

Page 20: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 18

———– MAONI ———–

Page 21: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 19

———– MAONI ———–

HAUJACHELEWA KABISA!...

Page 22: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

©2000 Fresh Start For All Nations 20

MWANZO MPYA ULIO WA MWISHO

Mwanzo Mpya Ulio wa Mwisho (The Ultimate Fresh Start) unahusu KUBADILIKA kwa moyo kabisa - kugeuka kutoka kwa maoni kwamba "yangu kwanza" na kufanya mambo yangu mwenyewe, hadi "Yesu ndiye wa Kwanza" na ninahamu ya kufanya mapenzi yake.

“....La hasha! Ninyi nanyi msipotubu, mtaangamia vivyo hivyo.” - Luka 13:3

“Ee Mungu wangu, natamani kufanya mapenzi yako, sheria yako iko ndani ya moyo wangu.’’ Zaburi 40:8

Kama nasikitika kwamba uchaguzi wa "mimi kwanza" umesababisha madhara mabaya, na lengo langu ni juu ya taabu yangu, ambayo Biblia huiita huzuni ya kidunia. Lakini, kama mtazamo wangu ni moja ya hukumu ya makosa yangu - makosa ya kuweka manufaa yangu mwenyewe kwanza, bila kujali matokeo yake, Biblia ingeiita taabu ya kiungu.

“Kwa maana huzuni ya kimungu huleta toba iletayo wokovu na wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti.” 2 Wakorintho 7:10

Mwanzo wako mpya ulio wa mwisho unaweza kuanza sasa hivi…

· Ungama kila kosa ya aina ya "mimi kwanza" ambayo umegundua katika maisha yako: kiburi, wivu, kufuru, ukosefu wa msamaha, na haki ya kuendesha maisha yako mwenyewe ...

· Mwambie Mungu umekuwa na makosa na umetenda dhambi dhidi Yake - katika njia zote ambazo hali ya "mimi kwanza" imekuwa ikifanya kazi katika mawazo, maneno, ama kwa vitendo katika maisha yako (eleza bayana)...

· Shukuru Mungu kwa sababu ya kutoa Mwanawe, Yesu, ili afe kwa ajili ya dhambi zako zote ...

· Mwambie Mungu unatubu – (kugeuka kutoka) kwenye dhambi hizi zote · Omba Mungu akusamehe – dhambi ya kila aina dhambi hizi... · Mwambie Mungu kuwa unajitoa Kwake kabisa - maamuzi yakumfanya

Bwana wa maisha yako, kama Bwana wako, wewe unajitoa Kwake ili afanye mabadiliko yoyote ambayo angetaka kufanya katika maisha yako.

· Sasa, mshukuru kwa msamaha Wake na kwa maisha Yake mapya ndani yako!

“Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha toka kwenye udhalimu wote.” 1 Yohana 1:9

“Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba ‘‘Yesu ni Bwana.’’ na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu.”

Warumi 10:9-10

Kwa habari zaidi kuhusu The Ultimate Fresh Start (Mwanzo Mpya ulio wa Mwisho) tembelea: www.stepuptolife.com

SWAHILI

Page 23: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

Printed and Distributed By:

Body Life Ministries

Publishing Sponsored in Part By:

Trans/Mid-America

For Additional Resources Contact:

Fresh Start For All Nations www.freshstartforallnations.org

or

Body Life Ministries (800-860-7125)

_______________________________________

In Kenya-

For additional copies and/or questions:

CISTERN MATERIALS TRANSLATION

AND PUBLISHING CENTER

P.O. Box 113-00220

Kijabe, Kenya

Email: [email protected]

Tel. (+254) 721 330 253 / 724 780 807

Translated in Swahili by Cistern Materials

Translation and Publishing Center

Page 24: Processing The Issues Of Your Heart (Swahili)

Swahili

Translated in Swahili by Cistern Materials

Translation and Publishing Center