presentation on biogas technology
TRANSCRIPT
Biogas Ni nini?• Ni gesi inayotokana na
uchachukaji wa vinyesi vya wanyama au masalia ya Mashambani / jikoni katika mazingira yasiyo na hewa ya Oksijeni (anaerobic digestion).
Kinyesi + maji/mkojo(Wanga + mafuta + protini + maji)
Biogesi Mbolea tope chujio
Uchachukaji/uvundaji Pasipo na hewa
Post treatment Mimea
Nishati
Bio-gas kama Teknolojia ilitoka wapi?
• Teknolojia ya biogas imekuwepo duniani kwa muda mrefu sana. Iliingia nchini Tanzania kupitia shirika la SIDO takribani miaka ya 1970 kutokea nchini India. Kwa wakati huu India walikuwa wanatumia muundo wa pipa linaloelea (Floating Drum) na ndiyo muundo SIDO walioeneza hapa nchini.
Historia inaendelea…• Muundo huu ulionekana kuwa na changamoto
ya pipa la chuma kupata kutu kutoboka na kumwongezea mteja gharama kubwa ya ukarabati.
• Baada ya kuzaliwa kwa Tasisi ya CAMARTEC (Centre of Agriculture Mechanization And Rural TEChnology-1983) Wataalamu walifanyia marekebisho muundo wa mtambo wa kichina uitwao “Chinese Fixed Dome” na hivyo kuzalisha aina ya mtambo uitwao “ CAMARTEC FIXED DOME PLANT”.
Miaka michache baadayemaboresho yalifanyika tenakatika harakati za kupunguzagharama za ujenzi wa mitambona kuzalisha aina mpya inaoitwa“ MODIFIED CAMARTEC DOME -
MCD”. Aina hii ya mtambo ambayondiyo tunayoineza kwa sasainaweza kupatikana kwa ujazowa kiwango cha 4m3, 6m3, 9m3
na 13m3 na rahisi kujenga.
Historia inaendelea…
Historia inaendelea…• Kwa kushirikiana na Tasisi ya SNV mwaka 2011
Watafiti walibuni aina ya mtambo unaostawi maeneo ya wafugaji yaliyokithiri kwa ukame. Mtambo huu unaitwa, “SOLID STATE DIGESTER- SSD”. Mitambo hii imepata umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na ubora wake katika uzalishaji wa gesi. Juhudi hizi zimetoa fursa kwa kila Mtanzania (mfugaji) mwenye nia kujenga Mtambo unaoendana na mazingira anamoishi.
Chemba Ya Kukorogea
CHEMBA YA KUINGIZIA MBOLEA
Chemba ya
majaribio
Chemba Mtanuko
Mdomo wa kutoleambolea
Nini kinachosababisha bio-gas iwake?• Kinachoiwezeshesha bio-gas kuwaka ni
gesi aina ya “Methen”ambayo ndiyo nyingi katika aina tatu za gesi zinazozaliwa wakati wa uchakachukaji.
- Methene (CH4) ………….…70 – 75%
- Hydrogen Sulphide (H2S) ..1 – 5% - Carbon Dioxide (CO2)…..25 – 30%
SIFA ZA GESI-VUNDE(BIOGAS)
• Haina moshi• Hailipuki kama ikivuja ndani ya chumba• Ina nguvu ya kupika chakula kwa muda
mfupi• Haisababishi masizi kwenye sufuria• Inamwondolea mteja gharama za
kununua gesi kila wakati.
FAIDA ZINGINE ZA TEKNOLOGIA YA BIO-GAS
Utunzaji wa mazingira na kupunguza uharibifu wa utando ulioko angani
“ozone layer”
Jinsi miyele ya jua inavyopozwa na utando angani (Ozone layer)
Mbinu za kupunguza gharama za ujenzi.
• Ruzuku kutoka kwa mfadhili (200,000)• Kuchagua aina ya mtambo mtambo unaolingana na uwezo
wa familia.• Kutafuta taarifa za upatikanaji wa vifaa.• Kuunganisha wateja kwa baadhi ya vifaa, mf. Chicken wire,
wire mersh, mchanga, nk.• Mafunzo ya mafundi wapatikanao maeneo husika. (Hadi
sasa tuna mafundi 56 ambao wameunda vikundi 11 vya ujasiriamali- BCEs)
• Kuunganisha wateja na tasisi za kutoa mikopo, mf. SACCOS, BANK (MRCB-Mwanga).
TOPE CHUJIO NININI??
”Ni mabaki ya Samadi
yanayopatikana yakiwa katika hali ya tope/uji mzito baada ya mtambo wa bio-gas kuzalisha gesi”.
CHANGAMOTO ZA TOPE-CHUJIO
• Upatikanaji wake si rahisi inapohitajika.• Inapokuwa katika hali ya uji-uji ina usumbufu
katika kusafirisha kwenda shambani.• Baadhi ya wafugaji wanajiskia kinyaa
kutumia Tope-chujio lililounganishwa na choo.
• Hakuna tekinolojia ya kutosha iliyopo kuhusu matumizi bora ya tope-chujio.
CHANGAMOTO ZA MRADI WA BIOGAS kwa ujumla.
• Baadh ya Wateja kushindwa kununua vifaa vinavyohitajika katika ujenzi kwa wakati.
• Baadhi ya wateja kushindwa kurejesha mikopo yao kwa taasisi husuka. Mf. Mwanga Bank(MRCB)
• Wateja wengi kutokuwa na taarifa za kuwepo kwa mradi katika maeneo yao (lack of Awareness).
• Kupunguzwa kwa ruzuku kutoka kwa Mfadhili.• Ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu matumizi sahihi
ya tope-chujio.• Mwitikio wa serikali ni mdogo kiushirikiano.