nipe moyo wako - gospel truth · kanisa la mungu. ————————— the gospel truth, po...
TRANSCRIPT
-
NIPE MOYO WAKO
moyo, akasimama polepole huku moyoni
akiwa amejaa masumbuko makubwa.
Alipatwa na majonzi mengi kwa sababu
alitaka sana kumfuata Bwana, lakini alikuwa
na utajiri mwingi na basi hakuwa tayari kuuza
mali yake. Basi huzuni kubwa ikionekana hata
kwenye macho yake kijana huyu alitingiza
kichwa chake na kuondoka kwa mwendo wa
taratibu. Nayo macho ya Yesu yakaonekana
kujaa machozi alipomtaza kijana huyo
akiondoka.
Hata ingawa Yesu alijua sifa nzuri za
mwanaume huyo Yeye alitambua kwamba
sifa hizo hazingemwezesha kijana huyo
kuingia Mbinguni. Kuingia mbinguni
kungemgharimu kijana huyo kutoa moyo
wake na kumpenda Mungu kuliko kingine
chote maishani mwake. Mungu alitaka kuwa
mtawala wa shauku zote za kijana huyo. Naye
Yesu alijua kwamba wakati utakuja ambapo
upendo wa kijana huyo kwa mambo ya dunia
kungevurugana na shauku lake la kumfuata
Bwana. Basi Yesu alishughulikia msingi na
maana ya kumfuata Yeye.
Mtu kuwa na tabia nzuri na kudumisha
nidhamu sio mambo yatoshayo kumfanya
mtu kupata uzima wa milele; pia mtu kuwa
na na shauku ya mambo ya Mungu silo jambo
ambalo linatosha. Inambidi mtu kujitoa
mhanga kwa upendo wa kumfuata Bwana
(Endelea kwa ukurasa 2)
huyu wa kuvutia alikuwa amejinyenyekeza,
na alikuwa na shauku ya kumpendeza
Mungu. Ndipo (huku sauti yake ikiwa imejaa
upendo) akamwambia, “Umepungukiwa na
neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo
vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na
hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.”
Uso wa kijana huyo ukakunjamana kwa
maana maneno ya Yesu yalimfanya kufa
“Mtu kuwa na tabia nzuri
na kudumisha nidhamu
sio mambo yatoshayo
kumfanya kupata uzima
wa milele.”
BIBLICAL INSTRUCTION AND ENCOURAGEMENT FOR THE
MISSION FIELD WORLDWIDE.
Toleo 3
(Marko 10:17-23; Luka 18:18-24)
Jua lilikuwa limewaka sana katika sehemu
hiyo ya mlima ambako kulijaa mawe wakati
Yesu alikuwa akitembea kwenye barabara
hizo zilizojaa vumbi. Siku hiyo ilikuwa ndefu
na wanafunzi hawa walikuwa wamechoka
sana kutokana na kushughulikia makusanyiko
ya watu ambao kila wakati waliwaandama.
Lakini kwa ghafla bwana mmoja ambaye
alikuwa amevaa nguo za kitajiri akatokea
huku akikimbia kwenye barabara hiyo
kuwaelekea. Na hapo akipunga pumzi kwa
nguvu alisujudu mbele yake Yesu na kwa
sauti ambayo ilijaa matarajio akamuuliza
Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili
nipate kuurithi uzima wa milele?”
Yesu akasimama na kumtazama bwana huyu
kwa huruma nyingi na akamjibu: “Wazijua
amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie
uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako
na mama yako.” Lakini huku moyo wake
ukiwa umejaa ukweli kijana huyu
akamwambia Yesu, “Haya yote nimeyashika
tangu utoto wangu.”
Yesu naye akageuza uso wake upande akiwa
amejaa mawazo na kutafakari kuhusu
mwanaume huyo ambaye alikuwa mbele
zake. Alijua kwamba huyu alikuwa kiongozi,
na kwamba alikuwa na utajiri mkubwa. Basi
akaguzwa sana moyoni kuona kwamba kijana
Tahariri
3
Kujifunza Biblia:
Uhusiano Unaoongozwa
wa Upendo
4
Shauka kubwa ya Mungu
5
Je, Wajua?
Sio kwa Ufasaha wa
Maneno
8
Swali na Jibu
7
MAFUNDISHO YA BIBLIA NA HIMIZO KWA
KAZI YA KIMISHENI ULIMWENGUNI KOTE
-
Inafundisha Kuhusu...
BIBLIA
Ukurasa wa 2
Yesu ili yeye aweze kurithi Mbingu. Tunaweza kuwa na shauku kwa Mungu, tunaweza
pia kuwa na kiwango fulani cha upendo, tunaweza pia kuwa wake au waume wazuri
(kwa watu ambao tulioa), hata tunaweza kuwa wananchi wazuri, na pia kuwa majirani
bora; lakini tunahitaji kuwa zaidi ya hayo.
Mungu anataka kwanza kabisa awe mtawala wa shauku zetu: “Mwanangu, nipe moyo
wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu” (Mithali 23:26). Maneno hayo yangali
ndio kilio chake Mungu kwa mwanadamu— “Nipe moyo wako.” Shauku zetu zote
zinapokuwa kwake Mungu ndipo ambapo tunaweza kumpenda kwa mioyo yetu yote,
nafsi zetu, mawazo yetu na nguvu zetu zote. Ni wakati ambapo Mungu amepata
mioyo yetu ndipo anapata shauku zetu, wakati wetu, pesa zetu, ndoto zetu na hata
mipango yetu. Wakati huo ndipo anakuwa nambari moja katika kila fani ya maisha
yetu.
Watu wengi katika siku zetu huja kanisani huku wakitaka kujua kuhusu Mbingu kama
ambavyo kiongozi huyo tajiri alifanya. Lakini wengine wao huondoka kwa sababu
hawako tayari kumpa Mungu shauku zao zote. Wengine nao washirika wa kanisa—
huku wakiimba, wakiomba, wakifunza biblia na hata wakati mwingine wakihubiri;
lakini wao huwa hawampatii Mungu “kitu hicho kimoja” ambacho hunabaki kuwa
kizuizi cha upendo wao kwa Mungu.
Je, upendo wako uko wapi leo? Je, umebakisha kitu kimoja? Je, umejitolea mhanga
kwa Mungu? Hebu mpe moyo wako. Chochote ambacho utahitaji kuachilia basi
kiachilie ili umfuate Bwana Yesu nawe utalipiwa kwa zawadi kuu katika maisha haya
na hata katika siku zijazo.
—mws
(Endelea kutoka ukurasa 1)
Neno la Mungu
2 Tim. 3:6, 2 Pet. 1:20-21, Mt. 24:35
Uhusiano wa Upendo
Mt. 22:37-40, Yn. 14:21-23, 1 Yoh. 4:7-21
Toba
Mdo. 3:19, 17:30, 2 Kor. 7:10
Uzao Mpya
Yn. 3:3-7, 2 Kor. 5:17, Rum. 6:1-4, Efe. 2:1, 5-6
Uhuru Kutokana na Dhambi
1 Yoh. 5:18, Mt. 1:21, Yn. 8:11
Ujazo wa Roho Mtakatifu
Mdo. 19:2, 15:8-9, 1:8
Utakatifu
Lk. 1:73-75, Ebr. 12:14, 1 Pet. 1:15-16,
Tit. 2:11-12, Rum. 6:22
Ufalme wa Mungu
Lk. 17:20-21, Rum. 14:17, Yn. 18:36
Kanisa
Mdo. 2:47, Efe. 4:4-6, 1 Kor. 12:12-13,
Kol. 1:18
Umoja
Yn. 17:20-23, Gal. 3:28, Ufu. 18:2-4
Kanuni za Kanisa
Mt. 28:19-20, 26:26-30, I Kor. 11:23-27,
Yn. 13:14-17
Uponyaji wa Kiungu
Lk. 4:18, Isa. 53:4-5, Yak. 5:13-16
Utakatifu wa Ndoa
Mt. 19:5-6, Lk. 16:18, Rum. 7:2-3,
I Kor. 7:10-11
Urembo wa Nje
I Tim. 2:9-10, I Kor. 11:14-15, Kum. 22:5
Mwisho wa Nyakati
2 Pet. 3:7-12, Yn 5:28-29, 2 Kor. 5:10, Mt.
25:31-46
Kupenda Amani
Lk. 6:27-29, 18:20
Ibada
Yn. 4:23-24, Efe. 5:19, 2 Kor. 3:17
Wajibu Mkuu
Mk. 16:15
Gazeti a Ukweli wa injili linachapishwa katika mataifa mbalimbali ili kusambazwa katika maeneo hayo. Kazi hii na zingine za kimishenari ambazo sisi hufanya huwezekana kupitia kwa matoleo ya kujitolea yanayotolewa kwa jina la
Kanisa la Mungu.
—————————
The Gospel Truth, PO Box 2042, Nixa, MO 65714 USA
Gazeti la ‘Ukweli wa Injili’ huchapishwa kwa jina la Bwana kwa matumizi ya watu wa mataifa yote
kwa kusudi la kuimarisha na kuwahimiza watu wote katika ukweli wa neno la Mungu. Gazeti hili hufundisha na kueneza ukweli wa Biblia ambao umethibitishwa tangu nyakati za Yesu Kristo na
mitume.
Neno la Mungu ndio mwongozo halisi na wa kipekee wa imani. Linafundisha wokovu na ukom-bozi kutokana na dhambi unaoletwa na utakaso wa Yesu Kristo; ambao hufuatiwa na ujazo wa
Roho Mtakatifu anayemwongoza mhudumu, kumwonyesha njia, na kumpatia nguvu; pia unam-letea mtu utakatifu halisi katika kila fani ya maisha yake; na pia kuleta umoja na utangamano wa watu wa Mungu. Huduma inayokubalika na Mungu inatokana na mtu kuwa na uhusiano wa kibin-
afsi na wa upendo ambao msingi wake ni ukweli.
Waandishi: Michael na René Smith
Ukweli wa Injili ni gazeti la kieletroniki linalochapishwa kila robo ya mwaka kwa jinsi Mungu
anavyotuongoza. Tutembelee katika tovuti yetu ya www.thegospeltruth.org ili uagize jalida hili kupitia kwa orodha yetu ya anwani pepe na upokee toleo lako la wakati huu. Hebu jisikie huru kututumia orodha ya majina na anwani pepe za watu wengine ambao wangependa kupokea toleo
hili kutoka kwa mwandishi wa jalida la Ukweli wa Injili.
UKWELI WA INJILI
UAGIZAJI
WASILIANA NASI
-
Tutembelee katika
www.thegospeltruth.org
ili uagize na uweze
kupata toleo za
hapo mbeleni.
Tahariri
Ukurasa wa 3
Haleluya. Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. Kwa
maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote —Zaburi 116:1-2
Nikiwa mtoto mdogo niliutoa moyo wangu kwa Mungu na kujisalimisha kwa utunzi
wake. Mimi ninakumbuka sana jinsi nilivyodondokwa na machozi kwa vile ambavyo
Roho Mtakatifu alifanya kazi yake ya kunihakikishia moyoni mwangu. Hapo katika
chumba cha nyuma katika Shule ya Jumapili mama yangu aliomba nami ili Yesu aingie moyoni mwangu.
Hata ingawa sikuwa nimejiingiza sana dhambini nilihitaji neema ile ya wokovu wa Mungu ambayo
humwokoa mwanadamu iingie katika maisha yangu kama jinsi ambavyo mshiriki wa madawa ya kulevya
hata mlevi wa pombe anahitaji. Na nilipokuwa nikikua na kukomaa mimi nilipitia na “uchungu wa kukua
kiroho” hata wakati mwingine nikakosa kufikia malengo ya maisha ya Kikristo—kama ambavyo hutokea
kwa watu wengi ambao wanaokoka wakiwa wangali wadogo. Lakini kamwe sikuwahi kupoteza shauku
langu la kumtumikia Mungu, hata ingawa nilifanya safari nyingi madhabahuni ili kuombewa kuokoka
tena. Hadi leo mimi ninamshukuru Mungu kwa ajili ya uaminifu wa Roho wake. Kama wimbo
unavyosema, “Roho ndiye aliyeniongoza hadi mahali nilipo sasa.” Mimi nilikuwa (na ningali) na shauku
kubwa sana ya kuwepo na uwepo wa Mungu maishani maishani mwangu kila siku, kwa maana nikifuata
njia zangu mwenyewe nitapotea.
Mimi nampenda Bwana na ninatilia umuhimu swala la uwepo wake maishani mwangu hata kuliko uhai
wangu mwenyewe. Mungu amekuwa mwaminifu kusikia sauti yangu na kujibu maombi yangu. Yeye
ameponya mwili wangu na akaniokoa kutoka mautini, na pia amenipatia familia ya ajabu, na kukutana
na mahitaji yangu ya kila siki; zaidi ya yote Yeye aliniokoa kutokana na minyororo na utumwa wa
dhambi. Amenipatia amani yake na uwepo wa Roho wake Mtakatifu. Kwa kweli ninayo mengi ya
kumshukuru Mungu. Hata ingawa wewe unakumbana na majaribu na masumbufu ya aina nyingi kama
unampenda Bwana maishani mwako una hazina kuu zaidi kuliko ingine ulimwenguni mote. Tolea hili la
Ukweli wa Injili linatilia umuhimu amri ambayo ni kuu zaidi na mafundisho ambayo ni makuu zaidi
katika Biblia, maanake—Upendo.
Unapokazana na mwaka huu mpya uwe na uhakika kwamba Mungu ataendelea kuwa mwaminifu
kwako. Kama jinsi ambavyo amekutana na mahitaji yako hapo mbeleni na kukuwezesha kupitia
mabonde na hata motoni ndivyo ambavyo atakuwa nawe mwaka huu. Ewe msafiri pamoja na Yesu,
endelea kuwa mwaminifu na uendelee kumtumaini Bwana wako. Ushindi mpya wakungoja na
ukiendelea kushikamana naye Yesu siku moja utatembea naye Mbinguni.
Ombi langu ni kwamba toleo la jalida la Ukweli wa Injili litaendelea kuwa na himizo na msaada mkuu
kwa kila msomi hapa kwetu nyumbani na hata katika nchi za kigeni. Kama gazeti hili limekuwa la
msaada kwako sisi tutapata kujengwa katika kazi hii ikiwa utaweza kutuandikia kuhusiana na swala hilo.
Basi jisikie huru kuniandikia kwa njia ya moja kwa moja kupitia kwa barua pepe:
Basi ni ombi letu kwamba Mungu atakubariki na kukupatia mwaka wa ajabu kupitia kwa uwepo wake.
Ninaomba kwamba tutembee katika mwanga na utakatifu wa Neno lake Mungu ili tuweze kudumu
katika amani.
—Michael W. Smith
Januari 2013.
mailto:[email protected]
-
MAFUNZO YA BIBLIA
Somo la Biblia: Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo
Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo,
naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu,
na Mungu hukaa ndani yake. Katika hili pendo
limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika
siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo,
ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.
– 1 Yohana 4:16-70
Maana ya upendo: Kuvutiwa na mtu, kumtakia
mema, kumfanyia mema, kushikamana na mtu.
Tendo la mtu analochagua kufanya.
I. Mawazo ya Mungu kwa Mwanadamu
A. Yeremia 31:3 Kuvutiwa na fadhili zake.
B. Yeremia 29:11-13 Mawazo ya amani.
II. Shauku la Mungu la Kuwa na Uhusiano na
Mwanadamu
A. Mwanzo 3:8-9 Mungu alikuwa na shauku la
ushirika.
B. Ufunuo 3:20 Tazama nasimama mlangoni.
C. 2 Wakorintho 5:17-18 Kupatanishwa na
Mungu.
III. Mungu Anapenda Nani?
A. Yohana 3:16 Ulimwengu.
B. Warumi 5:8 Watu wenye dhambi.
C. Waefeso 5:25 Kanisa.
IV. Dhihirisho la Upendo wa Mungu
A. 1 Yohana 4:9-10 Mungu alimtuma Mwanawe
wa pekee.
B. 1 Yohana 3:1,16 Tazameni ni pendo la
namna gani.
V. Upendo Ndio Amri Kuu Zaidi
A. Kumbukumbu 10:12 Upendo umeamriwa.
B. Mathayo 22:36-38 Mpende Bwana wako.
C. 1 Wakorintho 13:1-3 Bila upendo.
VI. Upendo ni Kipawa cha Mungu
A. 1 Yohana 4:7-8 Upendo unatokana na
Mungu.
B. Warumi 5:5 Upendo unatolewa na Roho
Mtakatifu.
JINSI YA KUTILIA
NGUVU UPENDO WAKO
KWA MUNGU
TUBU
Kubali kwamba umekuwa mlegevu na
kwamba umepoteza ari yako na bidii kwa
Mungu. Tubu na umwombe Mungu
msamaha na kwamba akurudishe mahali
ambapo ulikuwa hapo mbeleni kwa
mambo yako ya kiroho.
MTAFUTE MUNGU Anza kujifunza maandiko tena kwa bidii.
Mwombe Mungu akurudishie shauku ya
kuupenda ukweli na haki.
KUWA MTIIFU Jitenge kutokana na mambo ambayo
yatakuvuta mbali na Mungu na
kukupeleka mbali na makusudio yake
maishani mwako. Utiifu ni jambo ambalo
hutokana na mtu kufanya uchaguzi wa
wazi wa kumpenda Mungu zaidi ya
mambo mengine yote.
USIPUUZE USHIRIKA Usiache kutilia maanani swala la
kuhudhuria ibada. Andaa moyo wako na
uweke kando kila jambo ambalo
linakusumbua wakati ambapo umeingia
nyumbani mwake Mungu.
WATUMIKIE WENGINE Usiuruhusu ubinafsi ufanye uwe na uvivu
wa kiroho. Mwombe Mungu akuonyeshe
jinsi utakavyomtumikia kwa kuwatumikia
wale ambao wako karibu nawe.
KUWA NA FURAHA YA WOKOVU Dumu ukiwa na moyo ambao una
shukrani kwa ajili ya baraka zake Mungu.
Kila siku mwonyeshe Mungu upendo
wako (kwake) kwa mambo yote
unayofanya.
Ukurasa wa 4
Somo: Uhusiano Unaoongozwa na
VII. Upendo Ni kwa Matendo
A. 1 Yohana 3:18 Tupendane kwa matendo
na kweli.
B. Mathayo 15:8 Wengine huniheshimu kwa
mdomo.
VIII. Jinsi Upendo Wetu kwa Mungu
Unavyojidhihirisha
A. Yohana 14:15, 23-24 Atadumisha maneno
yangu.
B. 1 Yohana 5:3 Atadumisha amri zake.
C. 1 Yohana 4:20-21Twawapenda ndugu.
IX. Haiwezekani Kumpenda Mungu na
Ulimwengu
A. Mathayo 6:24 Huwezi kutumikia mabwana
wawili.
B. 1 Yohana 2:15-17 Usiupende ulimwengu.
C. Kumbukumbu 13:3 Bwana hujaribu
upendo wetu.
X. Sifa za Upendo wa Kweli
A. 2 Wakorintho 6:6 Hauna unafiki.
B. 2 Wakorintho 8:8 Wenye unyoofu.
C. 1 Timotheo 1:5 Unaotokana na moyo safi.
XI. Ukamilifu Unaotokana na Upendo
A. Waefeso 3:17-19 Utimilifu wa Mungu.
B. Yohana 15:10-11 Ili furaha yenu itimizwe.
XII. Nguvu za Upendo
A. 1 Yohana 4:18 Upendo ulio kamili hutupa
hofu nje.
B. 2 Wakorintho 5:14-15 Upendo hubidisha.
XIII. Ni Nini Hutenganisha Mwanadamu na
Upendo wa Mungu?
A. Warumi 8:35 Ni nani atatutenganisha?
B. Yohana 14:23-24 Kutofuata amri.
XIV. Kupoteza Upendo
A. Mathayo 24:12 Upendo utakuwa baridi.
B. Ufunuo 2:4 Kuacha upendo wa kwanza.
C. Ufunuo 3:15-17 Si moto si baridi.
XV. Kipawa kwa Wale Wampendao Mungu
A. Yakobo 2:5 Warithi wa ufalme.
B. 2 Timotheo 4:7-8 Taji la haki.
-
Ukurasa wa 5
What is Truth?
SHAUKU KUBWA YA MUNGU Nakala ya kuandamana na Mafunzo ya Biblia
MUNGU AMTAFUTA MWANADAMU Tangu kuumbwa kwa ulimwengu Mungu amekuwa na
shauku ya kuwa na uhusiana na mwanadamu. Tunasoma
jinsi Mungu alitembea katika Shamba la Edeni wakati wa
kupunga hewa ya mchana huku akiwa na shauku la kuwa na
ushirika na Adamu na Hawa (Mwanzo 3:8-9). Ingawa Biblia
ni historia na kitabu cha thiolojia kusema kweli biblia ni
nakala ya shauku la Mungu na juhudi zake za kutafuta
uhusiano wa upendo na wanadamu.
DHAMBI YAVUNJA UHUSIANO NA MUNGU Mungu aliumba wanadamu na shauku lake kuu ni kuwa na
uhusiano na viumbe wake—sio kwa njia
ya kushurutishwa bali kwa upendo.
Adamu na Hawa walikosa kumtii
Mungu na dhambi yao ikawatenganisha
na uhusiano wa karibu ambao
walikuwa nao na Mungu hapo mbeleni.
Daima dhambi huvunja uhusiano kati ya
mwanadamu na Mungu. Lakini Mungu hakurusu utengano
ulioletwa na dhambi, ukosefu wa utakatifu, na hukumu ya
kifo iliyokuwa juu yetu kuendelea kututenganisha naye.
MUNGU ALIMTUMA MWANAWE ILI
TUPATANISHWE NAYE
Mungu alitupenda sana hata akamtuma Mwanawe wa
pekee duniani ili tuweze kuokolewa (Yohana 3:16).
Msukumo ambao Mungu alikuwa nao ulikuwa ni wa
upendo na upendo huo ungaliko hawa wakati wa sasa:
“Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda
kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa
fadhili zangu” (Yeremia 31:3).
MATENDO YOTE YA MUNGU HUTOKANA NA
UPENDO
“Mungu ni upendo”(1 Yohana 4:8) na hiyo ndio nguzo ya
mahusiano yake na wanadamu. Wengine humwona Mungu
kama Mungu wa kufanyisha watu kazi ya sulubu—ambaye
ana matakwa mengi na ambaye ni vigumu kumpendeza.
Lakini picha hii inamwakilisha Shetani, haimwakilishi
Mungu. Mungu ni Mungu wa upendo ambaye hujali kuhusu
mambo yote ambayo huadhiri maisha yetu. Yeye anajaribu
kumfikia kila mwanadamu kwa upendo haijalishi hali yake.
Kamwe sisi hatustahili upendo wa Mungu na hakuna
chochote ambacho tumefanya cha kustahili upendo huo.
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu
sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa
tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8).
UPENDO UKIPATANA NA UPENDO HUWA
UPENDO ULIOKAMILIKA Kama upendo haupewi upendo huwa basi haujakamiika.
Mungu anatupenda lakini upendo huo haukamiliki hadi
hapo tunapompenda bila kujibakishia
chochote na kwa moyo wetu wote.
Mwanasheria mmoja alimuuliza Yesu,
“Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo
kuu? Akamwambia, Mpende Bwana
Mungu wako kwa moyo wako wote, na
kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia,
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa
roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo
kuu, tena ni ya kwanza.” Mafundisho mengine yote huwa
bure iwapo msingi wake sio sheria hii ya kwanza na iliyo kuu
zaidi. Watu wengi humtumikia Mungu kutokana na woga au
kwa kujitolea kwa kanisa au kwa thiolojia fulani. Lakini
uhusiano wa upendo huwa wenye kina zaidi na utajiri
mkubwa. Uhusiano wa upendo huleta utoshelevu wa kweli
kwa maana sasa uhusiano huwa umekamilika. Hii ndiyo
chanzo cha amani ya kweli na furaha ya kumtumikia
Mungu.
UPENDO WA KWELI HAUPATIKANI KWA NJIA
YA MABAVU
Kulikuwa na jamaa mmoja ambaye angemfungia mkewe
kwa nyororo jikoni mwao kila siku alipokuwa akitoka
kwenda kazini. Yeye alikuwa na hofu kwamba mkewe
angemwacha na asirudi. Uhusiano wao ulikuwa wa uongo
na utumwa. Ingekuwa afadhali zaidi kama mume
(Endelea kwa ukurasa 6)
-
Ukurasa wa 6
angeondoka kwenda kazini huku akifahamu kwamba mkewe
angekuwa tu hapo nyumbani atakaporudi kwa sababu mke
huyo alimpenda. Huu ndio uhusiano ambao Mungu
anatamani—uhusiano ambao mtu hashurutishwi kuishi kwa
utakatifu lakini ambao mtu anaishi kwa utakatifu kutokana na
moyo wake wa upendo. Nguvu za upendo ndizo husukuma
watoto wa kweli wa Mungu kuishi maisha matakatifu
(2 Wakorintho 5:14).
USHAHIDI WA UPENDO WETU NI UTIIFU WETU
Watu wengi humkaribia Mungu kwa vinywa vyao na
kumtukuza kwa midomo yao huku mioyo yao ikiwa mbali naye
(Mathayo 15:8). Lakini upendo wa kweli haudhihiriki kwa
maneno tunayonena bali kwa tabia za maisha yetu. “Yesu
akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno
langu” (Yohana 14:23). Huu ndio ushahidi wa kweli wa upendo
katika ulimwengu ambao wengi humkiri Kristo lakini ni
wachache ambao hutii Neno la Mungu. Mahali ambako hamna
utiifu hapana upendo. Hakuna chochote ambacho kinaweza
kututenganisha na upendo wa Mungu (Warumi 8:35)
isipokuwa kutokutii kwetu (Yohana 14:23-24).
HAKUNA UPENDO MWINGINE ISIPOKUWA
“UPENDO WA KWANZA” “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili” (Mathayo
6:24). Hakuna nafasi katika uhusiano na Mungu wa mtu
kufuata ulimwengu wenye dhambi na wakati huo huo
kumfuata Mungu. Mtu akipenda ulimwengu upendo wa Baba
haumo ndani yake (1 Yohana 2:15-17).
UPENDO HUFANYA MTU KUJITOA MHANGA
Wakati watu wawili wanapendana kwa kweli wao huwa tayari
kujinyima wakati na uwezo wao ili wawe pamoja. Shauku yao
kubwa huwa ni mmoja kumpendeza mwingine. Jambo hili
huwa la kweli hata kwa upendo wa kweli kwa Mungu utokao
moyoni mwa mtu. Upendo humfanya mtu kumwabudu Mungu
kwa hiari yake mwenyewe na kumtumikia. Basi utiifu unakuwa
si kazi ngumu ya sulubu bali huwa ni dhihirisho la upendo.
Upendo huleta furaha, kutoshereka, na nguvu katika utumishi
kwa Bwana.
APENDAYE MUNGU HUPENDA NDUGU YAKE
Watu wanapopata ujuzi wa upendo wa Mungu upendo wak
humwagwa mioyoni mwao kupitia kwa Roho Mtakatifu
(Warumi 5:5). Uhusiano huo huonekana sio tu kupitia kwa mtu
kuwa mtiifu kwa Mungu bali pia kwa upendo ambao mtu
huonyesha ndugu zake kanisani. Kwa maana mtu asipopenda
ndugu yake basi upendo wa Mungu haumo ndani yake
(1 Yohana 4:20-21).
UPENDO MKAMILIFU HUTUHAKIKISHIA UZIMA
WA MILELE
Sio tu kwamba uhusiana wa upendo na Mungu hutuletea
amani na uhusiano wa karibu na Mungu bali pia
unatuhakikishia uzima wa milele. “Baada ya hayo nimewekewa
taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa
siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda
kufunuliwa kwake (1 Timotheo 4:8).
SHAUKU KUU LA MUNGU NI KUWA NA UHUSIANO
NAWE Shauku kuu la Mungu ni wewe kuwa na uhusiana na urafiki wa
karibu naye. Mungu angetaka kuwa sehemu ya maisha yako.
Yeye ana shauku kwamba utatumia wakati wako na Yeye na
pia kwamba utawasiliana na Yeye. Kuna ushirikia wa karibu na
wa ajabu ambao unapatikana katika uhusiano kama huo.
Uhusiano na Mungu ambao msingi wake ni upendo utapatia
maisha yako maana na kusudi la kuishi.
—mws.
(Endelea kutoka ukurasa 5)
-
Ukurasa wa 7
Kikristo yenye uchovu mwingi ya kuwa na msimamo dhabiti kwa mafundisho ya Kikristo lakini bila upendo wa kupatia maisha hayo uhai. Uhusiano huchukuwa wakati wa mtu. Pia unahitaji kulindwa dhidi ya mambo ambayo yanaweza kuingilia kati.
“Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa” (Mathayo 24:12). Wengi wamepoteza upendo wao wa kwanza kwa maana wametoa upendo wao kwa mambo ya ulimwengu huu huku wakidumisha msimamo ambao kimsingi unaambatana na mafundisho ya Kikristo. Mungu basi anakuwa na wa kiwango cha pili kwa upendo wao au hata anakuwa ni wa kiwango cha chini zaidi. Wakati wao, uwezo wao, umakini wao, na mvuto wa upendo wao unakuwa kwa mambo mengine.
Jambo hili huleta uvivu kwa maisha ya mtu kumwishia Mungu na kunakuwa na ukosefu wa bidii ya kueneza injili. Kunakuwa tu na aina ya utauwa. Basi ni jambo muhimu kwetu kuchunguza tena maisha yetu ili kuhakikisha kwamba maisha yetu na bidii yetu ili kuhakikisha kwamba hatupotezi upendo wa kwanza.
Kama ambavyo mke na mume wanahitaji kuwasiliana na kutumia wakati pamoja ili kudumisha upendo wao ukiwa wenye nguvu ndivyo hivyo ilivyo kwa Mungu. Ni jambo muhimu kwetu ni kufanya bidii kudumisha “upendo wa kwanza” kwa kusoma Neno la Mungu, kuomba, kudumisha mahusiano, na kumweka Mungu mwanzo katika maamuzi yote tunayofanya. Zaidi ya yote tunahitaji kuufanya upendo kuwa ndio msukumo wa huduma yetu na sababu yetu ya kufanya mambo yafaayo.
Ni katika ujuzi huo wa upendo wa kwanza ndipo utakapopata bidii ya kushiriki injili na upako wa maisha ya kila siku. Upendo huo hufanya mafundisho ya Kikristo kuwa hai na kutoa sababu na furaha ya maisha.
—mws
upendo wao huwa limetokomea. Na mambo pia huwa hivyo kwa watu wengi katika uhusiano wao na Mungu. Waokovu wapya huwa na wakati mzuri wakiwa katika hali hiyo ya kujihisi wamesamehewa dhambi zao na wako kwenye maisha yaliyojaa amani na neema. Lakini ikiwa uhusiano huo haudumishwi mtu huyo anaweza aidha kuirudia dhambi ama kuendelea kufanya mambo “ya haki” lakini bila ukakamavu wa upendo huo wa kwanza.
Wale ambao wamepoteza upendo wa kwanza wameamuriwa kutubu. Kunao watu wengi na makusanyiko mengi ambayo wamesimama wima dhidi ya
uovu lakini wamepoteza moto wa upendo ambao ulikuwa ukiwaka hapo mbeleni. Wao wamepoteza kile kitu ambacho Mungu alitaka wawe nacho toka mwanzo—uhusiano wa upendo.
Upendo mkuu kwa Mungu ndio huleta joto katika huduma ambayo mtu anamfanyia Mungu. Basi tusianguke kwenye mtego wa kuwa na maisha ya
SWALI: Je, ni nini maana ya mtu kupoteza upendo wa kwanza?
JIBU: Swahili hili linaambatana na andiko la Ufunuo 2:4 ambalo linasema: “Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.” Roho wa Mungu alikuwa akizungumza kuhusu kusanyiko la Efeso.
Zingatia kwamba kusanyiko hili lilikuwa limesimama wima dhidi ya uovu na walikuwa wakifanya mambo mengi yaliyokuwa mazuri na ya haki. Ingawa walikuwa watiifu kwa mambo ya thiolojia na mafunzo ya kanisa Waefeso walikuwa wamepoteza uhusiano wa upendo uliowaambatanisha na Mungu ambao walikuwa nao hapo mbeleni. Nakala ya mafafanuzi cha JFB inasema: “Joto lao la upendo lilikuwa limeondoka na badala yake wakapatwa na maisha ya kushikilia mafundisho ya Kikristo kwa nguvu na ambayo hayakuwa na uhai.”
Wakati mwingi Maandiko hulinganisha uhusiano kati ya mwanadamu na Kristo kuwa kama ule wa kati ya bwana na mkewe. Hebu fikiria kuhusu wapenzi ambao walioa majuzi na ambao wanapendana sana na kujitolea mmoja kwa mwingine kwa uhusiano ulio hai. Wao hutaka kutumia wakati mwingi pamoja na kujinyima mambo mengi mmoja kwa ajili ya yule mwingine. Ndoa yao huwa na moto sana na pia uhai mwingi.
Lakini kama inavyokuwa wakati mwingi kwenye ulimwengu huu wenye dhambi wapendanao hupoteza ule upendo wao wa mmoja kwa mwingine na ndoa yao inakosa uhai. Wao huanza kuishi tu kwenye nyumba moja lakini joto la
“Wengi wamepoteza
upendo wao wa kwanza . . .
Wakati wao, uwezo wao,
umakini wao,
na mvuto wa upendo wao unaku-
wa kwa mambo mengine . . .
Mungu basi anakuwa na wa
kiwango cha pili kwa upendo
wao au hata anakuwa ni wa
kiwango cha chini zaidi.”
MASWALI
MAJIBU na
-
The Gospel Truth
P.O. Box 2042
Nixa, MO 65714
USA
Email:
Anwani
Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa
maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo,
naye amesulibiwa. Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko
mengi. Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye
kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika
hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. —1 Wakorintho 2:1-5
Jumapili moja mhubiri Charles Haddon Spurgeon ambaye
anajulikana kama “mhubiri wa wahubiri” alijihisi kwamba
amehubiri kwa njia dhaifu sana hivi kwamba akajionea aibu.
Alipokuwa akiondoka kutoka mle kanisana mwake lililokuwa
katika mji wa London na ambalo lilijulikana kama Metropolitan
Tabernacle yeye aliduwazwa na swali kama kwamba kutakuwa
na jambo lolote nzuri ambalo lingetokana na ujumbe kama huo
wake. Alipofika nyumbani akapiga magoti na kuomba, “Ewe
Bwana Mungu, waweza kufanya kitu bila kuwa na chochote.
Naomba ukaubariki ujumbe huo wangu ambao ni hafifu sana.”
Kwa muda wa miezi kadhaa iliyofuata watu 41 wakasema waliamua kumwamini Kristo
kama mwokozi kutokana na ujumbe huo “dhaifu.” Katika Jumapili iliyofuata na ili kufuta
“makosa” yake Spurgen aliandaa ujumbe “kemkem” lakini ng’o hakuna mtu aliyeokoka.
Ujuzi ambao Spurgeon alipata unatilia mkazo masomo mawili muhimu kwa watu wote
wamtumikiao Bwana. Kwanza kabisa tunahitaji baraka za Mungu kwa juhudi zetu zote.
Sulemani alisema katika Zaburi 127:1, “BWANA asipoijenga nyumba waijengao wanafanya
kazi bure.” Pili, udhaifu wetu huwa nafasi kwa Mungu kudhihirisha nguvu zake. Mtume
Paulo akasema, “Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na matusi, na matatizo, na adha, na
shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”
(2 Wakorintho 12:10).
Mkate Wetu wa Kila Siku, Mei 18, 1992.
Utakatifu kwa Bwana
Sio kwa Ufasaha wa Maneno
Ukurasa wa 8
• Yehova (Yahweh – Kiebrania) ni jina la kibinafsi la Mungu katika Maandiko. Mungu yule
ambaye ana uhai wake wa kibinafsi, asiyebadilika, wa milele, muumbaji na Bwana wa yote.
• Yesu ni jina lenye maana ya “Mwokozi.”
• Imanueli ni jina lenye maana ya “Mungu pamoja nasi.”
• Masihi nalo linatokana na Kiebrania na maana yake ni “kupakwa mafuta.”
• Kristo ni neno la Kiyunani lenye maana ya “aliyepakwa mafua.” Jina hili lina
maana moja na Masihi.
• Alfa na Omega ni herufi za kwanza na za mwisho za alfabeti ya Kiyunani. Maana yake ni kumwakilisha Yesu
kama “mwanzo na mwisho, maana yake ni wa kwanza na wa mwisho.”
Je, Wajua?
Neno Katika
Majira Yake