nacopha swahili newsletter 005 final low res

18
BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA WALK THE TALK TOLEO NO. 005 JUNI - SEPT 2020 Mwitikio wa NACOPHA dhidi ya COVID 19 Meneja wa kanda ya Dar es Salaam Victoriah Huburya akigawa vifaa kinga dhidi ya COVID 19 kwa konga ya Chamanzi, Mbagala Dar es Salaam Uk 6-7 Ziara ya ukaguzi wa vikundi wezeshi mkoani Lindi na Mtwara Washiriki wa uchaguzi mkuu wa konga H/Wilaya Nachingwea katika picha ya pamoja Mara baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Nachingwea tar 9/06/2020. Uk 9 Mwenyekiti NACOPHA atembelea vikundi wezeshi HEBU TUFIKIE 95-95-95 Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, NACOPHA itakuwa inatekeleza mradi mpya unaofadhiliwa na USAID unaojulikana kwa jina la HEBU TUYAJENGE. HEBU TUYAJENGE ni maneno ya kiswahili yanayo maanisha mazungumzo kati ya makundi mbalimbali ya watu (marafiki, familia, watunga sera n.k) yakiwa na lengo la kufikia makubaliano au maamuzi yenye kuleta tija kuhusu jambo fulani. Katika mtazamo wa mradi HEBU TUYAJENGE ni mazungumzo yanayohusu masuala ya UKIMWI Tanzania katika kufikia 95-95-95 mwaka 2030. www.nacopha.or.tz NACOPHA Tanzania NACOPHA Tanzania nacophatz NACOPHA 3 ZEROS Uk 6-7 Uk 6-8 Ushirikishwaji kamili wa WAVIU BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA NYP+ wakutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Mhe. Jenista Mhagama Ziara ya viongozi wa NACOPHA ofisi ya Waziri Mkuu - Dodoma Mwenyekiti wa NACOPHA Bi. Leticia Mourice alitembelea shughuli za kiuchumi za kikundi cha WAVIU cha Jitume mkoani Morogoro. Uk 4-5

Upload: others

Post on 23-Oct-2021

15 views

Category:

Documents

0 download

TRANSCRIPT

Page 1: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

WALK THE TALK TOLEO NO. 005 JUNI - SEPT 2020

Mwitikio wa NACOPHA dhidiya COVID 19Meneja wa kanda ya Dar es Salaam Victoriah Huburyaakigawa vifaa kinga dhidi ya COVID 19 kwa konga yaChamanzi, Mbagala Dar es SalaamUk 6-7

Ziara ya ukaguzi wa vikundiwezeshi mkoani Lindi na MtwaraWashiriki wa uchaguzi mkuu wa konga H/WilayaNachingwea katika picha ya pamoja Mara baada yauchaguzi mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauriya Nachingwea tar 9/06/2020. Uk 9

Mwenyekiti NACOPHA atembeleavikundi wezeshi

HEBU

TUFIKIE 95-95-95

Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, NACOPHA itakuwa inatekeleza mradi mpyaunaofadhiliwa na USAID unaojulikana kwa jina la HEBU TUYAJENGE. HEBU TUYAJENGE ni maneno ya kiswahili yanayo maanisha mazungumzo kati yamakundi mbalimbali ya watu (marafiki, familia, watunga sera n.k) yakiwa na lengo lakufikia makubaliano au maamuzi yenye kuleta tija kuhusu jambo fulani. Katika mtazamowa mradi HEBU TUYAJENGE ni mazungumzo yanayohusu masuala ya UKIMWI Tanzaniakatika kufikia 95-95-95 mwaka 2030.

www.nacopha.or.tzNACOPHA Tanzania NACOPHA Tanzania nacophatz NACOPHA

3 ZE

ROS

Uk 6-7

Uk 6-8

Ushirikishwaji kamiliwa WAVIU

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

NYP+ wakutana na Waziri wa Nchi Ofisiya Waziri mkuu Mhe. Jenista Mhagama

Ziara ya viongozi wa NACOPHA ofisi yaWaziri Mkuu - Dodoma

Mwenyekiti wa NACOPHA Bi. Leticia Mourice alitembeleashughuli za kiuchumi za kikundi cha WAVIU cha Jitumemkoani Morogoro. Uk 4-5

Page 2: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

HEBU

TUFI

KIE

95-9

5-95

KANDA YA DAR ES SALAAM

1. Ilala H/Manispaa

2. Temeke H/Manispaa

3. Masasi H/Wilaya

4. Masasi H/Mji

5. Mtwara H/Manispaa

6. Newala H/Wilaya

7. Newala H/Mji

8. Lindi H/Wilaya

9. Lindi H/Manispaa

10. Nachingwea H/Wilaya

11. Ruangwa H/Wilaya

12. Tanga H/Jiji

13. Moshi H/Wilaya

14. Moshi H/Manispaa

15. Chalinze H/Wilaya

KANDA YA MWANZA

1. Nyamagana H/Manispaa

2. Musoma H/Manispaa

3. Shinyanga H/Manispaa

4. Igunga H/Wilaya

5. Nzega H/Wilaya

6. Nzega H/Mji

7. Sikonge H/Wilaya

8. Tabora H/Manispaa

9. Urambo H/Wilaya

10. Uyui H/Wilaya

11. Bukoba H/Manispaa

12. Kigoma Ujiji H/Manispaa

KANDA YA DODOMA1. Bahi H/Wilaya2. Chemba H/Wilaya3. Dodoma H/Manispaa 4. Kondoa H/Wilaya5. Kondoa H/Mji 6. Kongwa H/Wilaya7. Gairo H/Wilaya8. Ifakara H/Mji9. Kilombero H/Wilaya10. Kilosa H/Wilaya11. Malinyi H/Wilaya12. Morogoro H/Manispaa13. Ulanga H/Wilaya14. Ikungi H/Wilaya15. Iramba H/Wilaya16. Manyoni H/Wilaya17. Mkalama H/Wilaya18. Singida H/Wilaya19. Babati H/Mji 20. Simanjiro H/Wilaya21. Arusha H/Jiji22. Arusha H/Wilaya23. Ngorongoro H/Wilaya

Konga za utekelezaji

KANDA YA MBEYA

1. Mbeya H/jiji

2. Rungwe H/Wilaya

3. Ludewa H/Wilaya

4. Makambako H/mji

5. Makete H/Wilaya

6. Njombe H/Wilaya

7. Njombe H/Mji

8. Wanging'ombe H/Wilaya

9. Iringa H/Wilaya

10. Iringa H/Manispaa

11. Kilolo H/Wilaya

12. Mafinga H/Mji

13. Mufindi H/Wilaya

14. Sumbawanga H/Manispaa

15. Songea H/Manispaa

KAGERAMARA

ARUSHA

SINGIDADODOMA

MANYARA

TANGA

KILIMANJARO

PWANI

DAR ES SALAAM

LINDI

MTWARA

RUVUMA

IRINGAMOROGORO

MBEYARUKWA

MWANZASIMIYU

GEITA

SONGWE

KATAVI

SHINYANGA

TABORA

KIGOMA

Shinyanga MC

Kigoma Ujiji MC

Nzega DC

Nzega TC

Igunga DC

Uyui DCUrambo DC

Tabora MC

Sikonge DC

Chemba DC

Kondoa TC

Dodoma MCKongwa DC

Kilosa DC

Ifakara TC

Kilombero DC

Morogoro MC

Gairo DC

Ulanga DC

Malinyi DC

Manyoni DC

Ikungi DC

Iramba DC

MkalamaDC

Singida DC

Babati TC

Ngorongoro DC

Arusha CC

Arusha DC

Simanjiro DC

Rungwe DC

Ludewa

Makambako

Iringa MC

Njombe TC

Kilolo DC

Mbeya CC Sumbawanga MC

Wanging'ombe DC

Songea MC

Mufindi DC

Mafinga TC

Makete DC

Masasi DC

Mtwara MC

Newala

Lindi DC

Lindi MC

Masasi TC

Nachingwea

Ruangwa DC

Tanga CC

Moshi DC

Moshi MC

Chalinze DC

Temeke MCIlala MC

Njombe DC

Bahi DC

KENYA

UGANDA

MOZAMBIQUE

MALAWI

ZAMBIA

NJOM

BE

Bukoba MCMusoma MC

Nyamagana MC

Mradi wa Hebu Tuyajenge – Konga za utekelezaji

Mikoa ambayo haifikiwi na mradi

Ufunguo:

ENEO LA UTEKELEZAJI WA MRADI WA HEBU TUYAJENGE

Konga za utekelezaji Halmashauri 65 zilizopo katika mikoa 22 ya Tanzania bara

DISEMBA 10, 2019 – DISEMBA 9, 2024

Page 3: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Mwenyekiti NACOPHA atembeleashughuli za kiuchumi za WAVIUmkoani Morogoro na Arusha

Katika toleo hili

Bodi ya wahariri

Uk.

2 - 3

Mafunzo ya Wakiri tiba

4 - 5

6 - 7Unyanyapaa ni kikwazo kufikia95-95-95

8

Ziara ya ukaguzi wa vikundiwezeshi mkoani Lindi

9

10

12 - 13

Simulizi za mafanikio 14 - 15

NYP+ wakutana na Mhe. JenisterMhagama Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira,Kazi na wenye Ulemavu

11

Lulu Kansary | Pantaleon ShokiRose Olotu | Last Mlaki

Msanifu ubunifuRobert Salala

MwandishiGrace Mollel

MshauriDeogratius Rutatwa

1

3 ZE

ROS

Bi. Leticia Mourice

Deogratius Rutatwa

Ujumbe kutoka kwaMwenyekiti wa Barazala watu wanaoishi naVirusi vya UKIMWITanzania (NACOPHA)

Ujumbe kutokakwa MkurugenziMkuu Mtendaji

Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA) tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara yaAfya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa juhudi na mikakati mbalimbali dhidi ya mwitikio wa UKIMWI nchini. Tumekuwa tukishirikiana na Wizara ya Afya katika kuhakikisha huduma ya VVU na UKIMWI inawafikia wananchi kuanzia ngazi ya jamii sambamba na utolewaji wa elimu ya UKIMWI ili kuwa na Taifa imara. Pia tunaishukuru Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) kwa kuendelea kutufadhili kupitia mradi HEBU TUYAJENGE (HT) katika kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa ya 95 95 95 ifikapo 2030.

HT ni moja ya miradi tunayoitekeleza ikiwa moja ya malengo ni kulifikia kundi la wasichana balehe, wanawake wa umri wa kati pamoja na WAVIU ambao kiujumla ndio wamekuwa walengwa wakuu ambapo tukiangalia takwimu za Wizara ya Afya za mwaka 2016/2017 zinaonyesha maambukizi mapya ni vijana wa kati ya miaka 15 -24 ambapo ni 40% (wanawake 80% na wanaume 20%). Tuna imani kupitia mradi wa HT tutachangia kuzifikia 95-95-95 ili vijana wetu na jamii kwa ujumla waweze kufikia ndoto zao na kutengeneza kizazi salama.

HEBU TUYAJENGE ni moja ya miradi inayote-kelezwa na NACOPHA kwa kipindi cha miaka mitano kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani USAID. Mradi huu unalenga kufikia malengo ya juhudi za kitaifa ya 95 95 95 na utatekelezwa kwenye kata 325 katika Halmashauri 65 Tanzania bara, utahamasisha katika kuongeza huduma za upimaji, tiba na matunzo, uzazi wa mpango, pamoja na utetezi na uraghibishi kwa watu wanaoishi na VVU.

Kimsingi, mradi huu unafanywa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, Kamati za Bunge, Wizara ya Fedha, Mamlaka ya serikali za mitaa, Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) pamoja na kamati za uangalizi wa konga za WAVIU, mashirika mbalimbali yanayotekeleza afua za UKIMWI kama vile, FHI 360, AGPAHI, BMF, PACT Tanzania, JSI, JHPIEGO na EGPAF.

Mradi huu unatekelezwa katika mikoa 22 ambayo ni Dar es salaam, Mtwara,Tanga, Lindi, Kilimanjaro, Pwani, Dodoma, Morogoro, Singida, Manyara, Arusha, Shinyanga, Mwanza, Mara, Kagera, Tabora, Kigoma, Mbeya, Njombe, Iringa, Rukwa na Ruvuma.

Napenda kuwakumbusha kwamba, tunapaswa kuendelea kujikinga na ugonjwa wa COVID-19 kwa kufuata elimu na miongozo inayotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ili tuweze kuendelea kuchapa kazi na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Barabara ya Whitesand 86, Mtaa wa Keni Close/Kilongawima,Nyumba Na KUN/KIL/83. SLP 55811, Dar es Salaam, Tanzania.Simu: +255 22 2618518, Barua Pepe: [email protected]: nacopha.or.tz

Mwitikio wa NACOPHA dhidi yaCOVID-19

Serikali mkoani Tabora yaviwezeshavikundi vya WAVIU

Ziara ya viongozi wa NACOPHAOfisi ya Waziri Mkuu - Dodoma

Page 4: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

2

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Kwa kuitikia wito wa kuonana na Mhe. Waziri Mkuu Mtandao wa Vijana

Wanaoishi na Maambukizi ya virusi vya UKIMWI (NYP+) kupitia Baraza la

Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) walipata fursa ya

kuonana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na

watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Joackim Mhagama na kuwasilisha

maombi yao katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mkoani Dodoma.

Nafasi hiyo waliipata Katika mkutano wa maazimio ya viongozi wa dini

katika kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya Watu wanaoishi na virusi

vya UKIMWI ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mhe. Kassimu

Majaliwa na ulihudhuriwa na NACOPHA, Mhe. Job Dungai Spika wa Bunge,

Wabunge, Viongozi wa Kitaifa wa dini na wadau mbalimbali.

Vijana walipata nafasi ya kuwasilisha maombi yao kwa Mh. Mhagama

kupitia kwa Mwenyekiti wao Pundensia Bwiliza ambapo aliwasilisha

maombi matatu. Moja ya Maombi hayo ni kuhusu mpango endelevu wa

uwezeshwaji kiuchumi, kiujuzi (stadi) na kiuzalishaji mali kwa Vijana

wanaoishi na VVU, kujadili uwezekano wa suala la UKIMWI kupewa nguvu

ya kipaumbele cha upekee ili iwe ni agenda inayojitegemea katika mipango

ya maendeleo ya nchi yetu tunapoelekea 2025 na 2030 ili kuutokomeza

mapema UKIMWI.

Pia waliwasilisha ombi la kumuomba Waziri Mkuu awe mlezi wa Vijana kwa

Ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma

kutambua heshima na mafanikio aliyonayo Kitaifa ya kuwa ni Balozi wa

kampeni ya “Furaha Yangu” inayohamasisha wanaume kupima VVU.

Mheshimiwa Mhagama alipokea maombi ya vijana hao na aliahidi kuyafanyia

kazi yale yaliyo ndani ya uwezo wake na mengine kuyawasilisha kwa

Waziri Mkuu.” Naomba niwahakikishie sitawaangusha yatakuwa kati ya

mambo muhimu ya kupewa kipaumbele na nitayafanyia kazi nawaahidi”

Mhe. Muhagama alinukuliwa akisema “Maombi yenu mengine ambayo

mmeyaomba yako kisera na mmeomba sehemu sahihi maana hii ndio ofisi

inayoratibu masuala yote ya UKIMWI, na leo sikujua tu ilikua ni siku muhimu

ambapo tulikua na uzinduzi wa mfuko ambao unawezesha vijana wa aina

zote ila kwa kuwa tuko pamoja tutaangalia ni jinsi gani tutazitatua

changamoto za vijana kwa kuwajengea uwezo kiuchumi”.

Kutokana na changamoto wanazozipitia vijana WAVIU suala hili kuna haja

ya kulitazama kwa jicho la kipekee, “mimi ndiye nashughulikia Sera na

Uwezeshaji Kiuchumi, na pia ndiye Waziri anayeshughulikia mifuko yote ya

uwezeshaji upande wa Elimu, Ajira na Uwezeshaji. Naomba kuwahakikishia

kuwa suala la uwezeshwaji liko ndani ya uwezo wangu”.

Katika programu aliyozindua Mhe. Waziri ambayo aliyepewa jukumu la

kuratibu na kusimamia ni SIDO na VETA , aliomba watu wote hasa vijana

kuitumia fursa hii kwa kuzingatia masharti yaliyopo ili kupata mkopo. Aidha

aliwapongeza vijana kwa moyo wa ushupavu na jitihada walizonazo kwani

wao ni mfano wa kuigwa katika jamii zetu. Alizidi kuwatia moyo kutokata

tamaa kwani Serikali iko bega kwa bega na inatambua uwepo wao.

NYP+ wakutana na Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama

Mhe. Mhagama alisema, imefika wakati tujue sisi hatuishi kisiwani na hii

inapelekea tufanye kazi kwa kushirikiana na wadau wote wanaotekeleza

Afua za UKIMWI ili kuleta matokeo chanya.

Kwa mujibu wa takwimu za Kitaifa za viashiria vya UKIMWI 2016/2017,

asilimia 40% ya maambukizi mapya ya VVU nchini Tanzania yako kwa

vijana, asilimia 80% ya maambukizi haya yako kwa vijana wa kike. Mhe.

Mhagama alisema” Tumejiunga na harakati za kidunia, kikanda katika

kupambana na kuangalia ustawi wa suala hili kwa undani na tuna chombo

makini katika kuyatekeleza haya kupitia Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi

TACAIDS na tume hii kwakweli imefanya kazi nzuri na imesaidia kwa kiasi

kikubwa kupambana na ugonjwa huu na kuwaondolea watu hofu.”

Mhe. Jenister Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi na wenye Ulemavu akifungua mkutano na baadhi ya wawakilishi wa Jukwaa la vijana wanaoishi na VVU Tanzania

Picha ya Pamoja; waliokaa Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuuu Sera, Bunge, Ajira Kazi na wenye ulemavu wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya Pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS Dk. Leornard Maboko wa tatu kutoka kushoto, Mwenyekiti wa NACOPHA Bi. Leticia Mourice wakwanza kulia, Mkurugenzi Mtendaji wa NACOPHA Deogratius Rutatwa wa kwanza kushoto na Mwenyekiti wa

Jukwaa la Vijana wanaoishi na VVU Pudensiana Bwiliza. Waliosimama ni baadhi ya wawakilishi wa jukwaa la vijana wanaoishi na VVU kutoka mikoa mbalimbali Tanzania.

Page 5: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

3

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Kwa kuitikia wito wa kuonana na Mhe. Waziri Mkuu Mtandao wa Vijana

Wanaoishi na Maambukizi ya virusi vya UKIMWI (NYP+) kupitia Baraza la

Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) walipata fursa ya

kuonana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na

watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Joackim Mhagama na kuwasilisha

maombi yao katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mkoani Dodoma.

Nafasi hiyo waliipata Katika mkutano wa maazimio ya viongozi wa dini

katika kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya Watu wanaoishi na virusi

vya UKIMWI ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mhe. Kassimu

Majaliwa na ulihudhuriwa na NACOPHA, Mhe. Job Dungai Spika wa Bunge,

Wabunge, Viongozi wa Kitaifa wa dini na wadau mbalimbali.

Vijana walipata nafasi ya kuwasilisha maombi yao kwa Mh. Mhagama

kupitia kwa Mwenyekiti wao Pundensia Bwiliza ambapo aliwasilisha

maombi matatu. Moja ya Maombi hayo ni kuhusu mpango endelevu wa

uwezeshwaji kiuchumi, kiujuzi (stadi) na kiuzalishaji mali kwa Vijana

wanaoishi na VVU, kujadili uwezekano wa suala la UKIMWI kupewa nguvu

ya kipaumbele cha upekee ili iwe ni agenda inayojitegemea katika mipango

ya maendeleo ya nchi yetu tunapoelekea 2025 na 2030 ili kuutokomeza

mapema UKIMWI.

Pia waliwasilisha ombi la kumuomba Waziri Mkuu awe mlezi wa Vijana kwa

kutambua heshima na mafanikio aliyonayo Kitaifa ya kuwa ni Balozi wa

kampeni ya “Furaha Yangu” inayohamasisha wanaume kupima VVU.

Mheshimiwa Mhagama alipokea maombi ya vijana hao na aliahidi kuyafanyia

kazi yale yaliyo ndani ya uwezo wake na mengine kuyawasilisha kwa

Waziri Mkuu.” Naomba niwahakikishie sitawaangusha yatakuwa kati ya

mambo muhimu ya kupewa kipaumbele na nitayafanyia kazi nawaahidi”

Mhe. Muhagama alinukuliwa akisema “Maombi yenu mengine ambayo

mmeyaomba yako kisera na mmeomba sehemu sahihi maana hii ndio ofisi

inayoratibu masuala yote ya UKIMWI, na leo sikujua tu ilikua ni siku muhimu

ambapo tulikua na uzinduzi wa mfuko ambao unawezesha vijana wa aina

zote ila kwa kuwa tuko pamoja tutaangalia ni jinsi gani tutazitatua

changamoto za vijana kwa kuwajengea uwezo kiuchumi”.

Kutokana na changamoto wanazozipitia vijana WAVIU suala hili kuna haja

ya kulitazama kwa jicho la kipekee, “mimi ndiye nashughulikia Sera na

Uwezeshaji Kiuchumi, na pia ndiye Waziri anayeshughulikia mifuko yote ya

uwezeshaji upande wa Elimu, Ajira na Uwezeshaji. Naomba kuwahakikishia

kuwa suala la uwezeshwaji liko ndani ya uwezo wangu”.

Katika programu aliyozindua Mhe. Waziri ambayo aliyepewa jukumu la

kuratibu na kusimamia ni SIDO na VETA , aliomba watu wote hasa vijana

kuitumia fursa hii kwa kuzingatia masharti yaliyopo ili kupata mkopo. Aidha

aliwapongeza vijana kwa moyo wa ushupavu na jitihada walizonazo kwani

wao ni mfano wa kuigwa katika jamii zetu. Alizidi kuwatia moyo kutokata

tamaa kwani Serikali iko bega kwa bega na inatambua uwepo wao.

Picha ya pamoja kutoka kulia Mwenyekiti wa NACOPHA Bi Leticia Mourice, Mkurugenzi wa TACAIDS Dk. Leonard Maboko, Pudensia Bwiliza, Mwenyekiti wa Mtandao wa vijana wanaoishi

na Virusi vya UKIMWI na Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA Bw. Deogratius Rutatwa.

Mhe. Mhagama alisema, imefika wakati tujue sisi hatuishi kisiwani na hii

inapelekea tufanye kazi kwa kushirikiana na wadau wote wanaotekeleza

Afua za UKIMWI ili kuleta matokeo chanya.

Kwa mujibu wa takwimu za Kitaifa za viashiria vya UKIMWI 2016/2017,

asilimia 40% ya maambukizi mapya ya VVU nchini Tanzania yako kwa

vijana, asilimia 80% ya maambukizi haya yako kwa vijana wa kike. Mhe.

Mhagama alisema” Tumejiunga na harakati za kidunia, kikanda katika

kupambana na kuangalia ustawi wa suala hili kwa undani na tuna chombo

makini katika kuyatekeleza haya kupitia Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi

TACAIDS na tume hii kwakweli imefanya kazi nzuri na imesaidia kwa kiasi

kikubwa kupambana na ugonjwa huu na kuwaondolea watu hofu.”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi na wenye Ulemavu Mhe. Jenister Mhagama, akifurahia jambo na washiriki wa mkutano wa mtandao wa vijana wanaoishina Virusi vya UKIMWI wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma

Page 6: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

4

Mwenyekiti wa Baraza la watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania

(NACOPHA), Bi Leticia Mourice alifanya ziara ya kutembelea vikundi wezeshi

vya watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) Ikiwa ni ziara maalum ya

kuratibu na ufuatiliaji wa maendeleo ya vikundi hivyo, ziara hiyo ilifanyika

mwaka huu 2020 katika mkoa wa Morogoro.

Aidha katika ziara hiyo mkoani Morogoro aliweza kutembelea Konga ya

Morogoro MC, Kilombero DC na Gairo DC ambapo katika ziara hiyo aliambata-

na na viongozi kutoka Halmashauri za Serikali CHAC/DAC ambapo alifanikiwa

kuona shughuli mbali mbali zinazofanywa na vikundi hivyo pamoja na

changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli zao.

Wanavikundi hao wameweza kuanzisha miradi mbalimbali ya ujasiriamali ili

kujikimu kiuchumi na kuendesha maisha yao. Hii ni hatua mojawapo kubwa

kwa WAVIU kwani hapo mwanzo vikundi hivi vilitambulika kama vikundi vya

misaada na sasa hivi vinatambulika kama vikundi wezeshi.Wanavikundi

wamekuwa wakijiendesha wenyewe kupitia viongozi wao wa Konga ambapo

katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Konga ya manispaa ya Morogoro Kareen

Mpesa aliwasilisha ripoti kwa Mwenyekiti wa Baraza Bi Leticia Mourice

ambapo alishukuru kwa motisha ya kazi wanayoipata na mchango wao

kutambulika kwa Serikali kupitia ngazi ya Halmashauri kwani wamekuwa

wakifanya kazi karibu na CHAC/DACC. Aidha alishukuru kwa Mwenyekiti wa

Baraza kuwatembelea na kuwatia moyo katika shughuli zao.

Katika Konga ya manispaa ya Mororogo kuna Vikundi wezeshi 20

ambapo katika vikundi hiyo jumla ya wanachama ni 591 (291

wanawake na 300 wanaume). Vikundi hivyo vimekuwa vikijishughulisha

na kuuza batiki na vito vya asili kama shanga. Mwenyekiti wa Konga ya

manispaa ya Morogoro alisema wameweza kuendesha maisha yao

kupitia vikundi wezeshi na kuweza kuzingatia suala zima la utumiaji wa

dawa, kufuatilia/kupima kinga za mwili, uhamasishaji na kurudisha

walioacha kutumia dawa. Aidha alizungumzia suala zima la Ugonjwa wa

COVID-19 ambalo ni hatari kwa WAVIU na kusisitiza kufuata kanuni na

taratibu za Wizara husika ili kujikinga.

Katika Konga ya halmashauri ya wilaya ya Kilombero kuna vikundi

wezeshi 42 ambavyo vinaongozwa na viongozi wa konga. Mwenyekiti

wa Konga Bi Halida Kumba alielezea kwa undani jinsi vikundi vinavyo-

endesha shughuli zao na changamoto wanazokabiliana nazo. Shughuli

kubwa wanazojishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji ambavyo vimeku-

wa vikiwasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku aidha alisema

changamoto kubwa wanayokutana nayo ni katika suala zima la uchuku-

aji wa dawa na ufuatiliaji. Alibainisha ya kuwa kipindi cha mavuno eneo

hilo limekuwa likipata wageni wengi na kusababisha huduma za Afya

kuzorota. Alizungumzia pia suala la wanaume kutojiunga na vikundi

wezeshi kutokana na suala zima la kujinyanyapaa.

Katika Konga ya Gairo kuna kata 18 na vikundi wezeshi 20. Mwenyekiti

wa Konga Abeli Bigambo alimshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Watu

Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kwakuwa sehemu ya ufuatiliaji

katika vikundi wezeshi vya Gairo. Aidha alizungumzia suala la unyanyapaa

ambalo wameweza kukabiliana nalo ambapo alibainisha kikwazo

kikubwa kimekuwa ni ushirikina ambao umekuwa ukikwamisha

shughuli za maendeleo katika eneo hilo.

Aidha katika ziara hiyo alifanikiwa kutembelea Kikundi cha CHICHI

ambacho kipo katika kata ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo jina la

kikundi CHICHI lina maana kwa lugha ya kigogo “Chipimile chimanyile”

ambayo kwa lugha ya Kiswahili ina maana NIMEPIMA NA NINAJUA AFYA

YANGU. Kikundi hiki ni kati ya vikundi vinavyofanya vizuri katika Konga ya

halmashauri ya wilaya ya Dodoma.

Kikundi hicho wameweza kujiendesha chenyewe na kuweza kujipatia

mahitaji muhimu ya kila siku ikiwa ni pamoja na suala zima la ufatiliaji wa

afya zao. Katika ziara hiyo Mwenyekiti aliwasihi kuacha dhana ya

kujinyanyapaa na badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo

ya 95 95 95

Mwenyekiti wa NACOPHA atembeleashughuli za kiuchumi za WAVIUMorogoro na Arusha

Timu ya usimamizi wakijadili namna bora ya uendeshaji vikundi wezeshi wakati wa ziara ya mwenyekiti waNACOPHA alipotembelea vikundi wezeshi mkoani Morogoro

Mwenyekiti wa NACOPHA akiangalia bidhaa za batiki zilizotengenezwa na kikundi chaJitambue cha H/Manispaa Morogoro

Page 7: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

5

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Mwenyekiti wa Baraza la watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania

(NACOPHA), Bi Leticia Mourice alifanya ziara ya kutembelea vikundi wezeshi

vya watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) Ikiwa ni ziara maalum ya

kuratibu na ufuatiliaji wa maendeleo ya vikundi hivyo, ziara hiyo ilifanyika

mwaka huu 2020 katika mkoa wa Morogoro.

Aidha katika ziara hiyo mkoani Morogoro aliweza kutembelea Konga ya

Morogoro MC, Kilombero DC na Gairo DC ambapo katika ziara hiyo aliambata-

na na viongozi kutoka Halmashauri za Serikali CHAC/DAC ambapo alifanikiwa

kuona shughuli mbali mbali zinazofanywa na vikundi hivyo pamoja na

changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli zao.

Wanavikundi hao wameweza kuanzisha miradi mbalimbali ya ujasiriamali ili

kujikimu kiuchumi na kuendesha maisha yao. Hii ni hatua mojawapo kubwa

kwa WAVIU kwani hapo mwanzo vikundi hivi vilitambulika kama vikundi vya

misaada na sasa hivi vinatambulika kama vikundi wezeshi.Wanavikundi

wamekuwa wakijiendesha wenyewe kupitia viongozi wao wa Konga ambapo

katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Konga ya manispaa ya Morogoro Kareen

Mpesa aliwasilisha ripoti kwa Mwenyekiti wa Baraza Bi Leticia Mourice

ambapo alishukuru kwa motisha ya kazi wanayoipata na mchango wao

kutambulika kwa Serikali kupitia ngazi ya Halmashauri kwani wamekuwa

wakifanya kazi karibu na CHAC/DACC. Aidha alishukuru kwa Mwenyekiti wa

Baraza kuwatembelea na kuwatia moyo katika shughuli zao.

Katika Konga ya manispaa ya Mororogo kuna Vikundi wezeshi 20

ambapo katika vikundi hiyo jumla ya wanachama ni 591 (291

wanawake na 300 wanaume). Vikundi hivyo vimekuwa vikijishughulisha

na kuuza batiki na vito vya asili kama shanga. Mwenyekiti wa Konga ya

manispaa ya Morogoro alisema wameweza kuendesha maisha yao

kupitia vikundi wezeshi na kuweza kuzingatia suala zima la utumiaji wa

dawa, kufuatilia/kupima kinga za mwili, uhamasishaji na kurudisha

walioacha kutumia dawa. Aidha alizungumzia suala zima la Ugonjwa wa

COVID-19 ambalo ni hatari kwa WAVIU na kusisitiza kufuata kanuni na

taratibu za Wizara husika ili kujikinga.

Katika Konga ya halmashauri ya wilaya ya Kilombero kuna vikundi

wezeshi 42 ambavyo vinaongozwa na viongozi wa konga. Mwenyekiti

wa Konga Bi Halida Kumba alielezea kwa undani jinsi vikundi vinavyo-

endesha shughuli zao na changamoto wanazokabiliana nazo. Shughuli

kubwa wanazojishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji ambavyo vimeku-

wa vikiwasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku aidha alisema

changamoto kubwa wanayokutana nayo ni katika suala zima la uchuku-

aji wa dawa na ufuatiliaji. Alibainisha ya kuwa kipindi cha mavuno eneo

hilo limekuwa likipata wageni wengi na kusababisha huduma za Afya

kuzorota. Alizungumzia pia suala la wanaume kutojiunga na vikundi

wezeshi kutokana na suala zima la kujinyanyapaa.

Katika Konga ya Gairo kuna kata 18 na vikundi wezeshi 20. Mwenyekiti

wa Konga Abeli Bigambo alimshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Watu

Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kwakuwa sehemu ya ufuatiliaji

katika vikundi wezeshi vya Gairo. Aidha alizungumzia suala la unyanyapaa

ambalo wameweza kukabiliana nalo ambapo alibainisha kikwazo

kikubwa kimekuwa ni ushirikina ambao umekuwa ukikwamisha

shughuli za maendeleo katika eneo hilo.

Aidha katika ziara hiyo alifanikiwa kutembelea Kikundi cha CHICHI

ambacho kipo katika kata ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo jina la

kikundi CHICHI lina maana kwa lugha ya kigogo “Chipimile chimanyile”

ambayo kwa lugha ya Kiswahili ina maana NIMEPIMA NA NINAJUA AFYA

YANGU. Kikundi hiki ni kati ya vikundi vinavyofanya vizuri katika Konga ya

halmashauri ya wilaya ya Dodoma.

Kikundi hicho wameweza kujiendesha chenyewe na kuweza kujipatia

mahitaji muhimu ya kila siku ikiwa ni pamoja na suala zima la ufatiliaji wa

afya zao. Katika ziara hiyo Mwenyekiti aliwasihi kuacha dhana ya

kujinyanyapaa na badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo

ya 95 95 95

Mwenyekiti wa NACOPHA Bi. Leticia Mourice akifurahia na kupongeza shughuli za kilimo cha mpungazinazofanywa na kikundi cha WAVIU cha Jitume kilichopo kata ya Malimba mkoani Morogoro alipotembelea

kujionea shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazofanywa na WAVIU

Mwenyekiti wa Baraza la watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI NACOPHA Bi. Leticia Mourice alifanikiwa kutembelea Kikundi cha wanaume Wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI (KIWAWARU) kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Arusha, mkoani Arusha lengo likiwa kuwawezesha wanakikundi pamoja na kuwahamasisha wanaume kujiunga na huduma za UKIMWI.

Katika ziara hiyo ambayo ilikuwa na jumla ya wanachama 40, ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali Mratibu wa Ukimwi wa Halmashauri (CHAC) na Afisa Mtendaji wa Kata (WEO). Mwenyekiti wa Konga Bw.Francis Temu alielezea changamoto na mafanikio ya kikundi akisema jumla ya wanaume wanachama ilikuwa 165 ambao waliacha mahudhurio ila tuliwarudisha kupitia ushauri nasaha na huduma za kiafya. Pia tuliweza kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana na huduma za upimaji na waliobainika wana maambukizi kuanza huduma stahiki za tiba na dawa.

Mwenyekiti atembelea kikundi chawanaume WAVIU - KIWAWARU, Arusha

Page 8: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

6

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam Victoriah Huburya akigawa vifaa kinga dhidi yaCOVID 19 kwenye Konga ya WAVIU Chamanzi Mbagala

Dk. Martha Macha - DACC Temeke na Heriet Kamara - CHACC Temeke wakikabidhi vifaa kinga dhidi ya COVID 19 kwa mwenyekiti wa Konga ya Chamanzi , Mbagala, Dar es Salaam

COVID-19 iliripotiwa kwa mara ya kwanza Tanzania Machi 17 mwaka

huu 2020 na Aprili 9 iliripotiwa wagonjwa 12, ambapo Serikali ya Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania ilichukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na

kufunga shule zote kuanzia ngazi ya chini mpaka vyuo vikuu. Ugonjwa

huu ni wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi vya

corona havikuwa vikifahamika kabla ya sayansi ya tiba, na vilianzia

Wuhan, Hubei China January 2020 ambapo Shirika la Afya DunianI

(WHO) lilithibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo.

Dalili kubwa za COVID-19 ni pamoja na homa kali, mwili kuchoka,

kikohozi, kubanwa mbavu, kupumua kwa shida, vidonda kooni na

kuumwa kichwa. Kutokana na tafiti za Shirika la Afya Duniani (WHO)

linadai watu wenye athari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ni wazee

na watu wenye magonjwa ya kudumu kama shinikizo la damu, Figo,

kisukari pamoja na watu wanaoishi na VVU ambao kwa takwimu za

Tanzania kwa mwaka 2019 idadi ya WAVIU imefikia milioni 1.6.

Serikali kupitia Wizara husika, katika kudhibiti maambukizi ilianzisha

utaratibu maalum kwa WAVIU katika suala zima la uchukuaji wa dawa

pamoja na huduma nyingine za afya. Baadhi ya taratibu hizo ni pamoja

na utolewaji wa dawa za muda mrefu ambapo vituo vya kutolea dawa

(CTC) walihakikisha wanakuwa na mawasiliano na mpokea huduma ili

kama ikitokea tatizo kabla ya tarehe ya kurudi kuna utaratibu wa kufuat-

wa, kuhudumiwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa na wizara husika

ikiwa ni pamoja na kuepuka msongamano wakati wa kusubiri huduma,

kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kutumia vitakasa mikono

mara kwa mara pamoja na uvaaji wa barakoa zenye viwango

vilivyodhibitiwa. Hata hivyo mpaka sasa ugonjwa huu hauna chanjo wala

tiba ya moja kwa moja, hivyo kama yalivyo magonjwa mengine yanayos-

ababishwa na virusi, matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo na

ufuatiliaji wa karibu.

NACOPHA kupitia mradi wa HEBU TUYAJENGE unaofadhiliwa na Shirika la

Maendeleo la watu wa Marekani USAID limekuwa bega kwa bega katika

kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mwitikio wa NACOPHA dhidiya COVID-19

Page 9: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

7

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Baadhi ya washiriki kutoka konga ya Temeke jijini Dar es Salaam wakionyesha vifaa kinga walivyopokea dhidi ya COVID -19

katika kupambana na ugonjwa wa COVID 19 ikiwa ni pamoja na kutoa

vifaa kinga pamoja na elimu ya kujikinga katika mabaraza ya watu

wanaoishi na virusi vya UKIMWI ngazi ya jamii.

Utaratibu wa utoaji wa vifaa kinga pamoja na elimu ya kujikinga dhidi ya

COVID 19 ulitolewa kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na

Wizara husika ili kuhakikisha zinawafikia walengwa, ambapo nia na

madhumuni ni kufikia Halmashauri 65 zilizoko katika mikoa 22 nchi

nzima kwenye ngazi ya jamii. Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na barakoa,

sabuni, ndoo, vitakasa mikono pamoja na elimu ya jinsi ya kutumia vifaa

hivi ili kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

Kanda ya Dar es salaam ugawaji wa vifaa kinga dhidi ya COVID-19

ulifanyika katika Konga ya Ilala na Temeke ambapo zaidi ya WAVIU 900

tuliwafikia. Katika Konga ya Ilala jumla ya vikundi vilivyopokea 44 mbele

ya Mratibu msaidizi wa kudhibiti UKIMWI kutoka Manispaa ya Ilala Bi.

Anna Kagya na Mwenyekiti wa Konga ya Ilala Bw. Emanuel Msinga

pamoja na Katibu wa Konga Zawadi Bahenge ambao waliongoza zoezi

zima la ugawaji wa vifaa hivyo kwa kuhakikisha kila MVIU anapata na

kupatiwa elimu ya jinsi ya kujikinga, ambapo afisa ufuatialiaji na tathmini

wa NACOPHA Bi. Victoria Huburya pamoja na Meneja wa Kanda ya Dar

es saam Bw. Maligo Raphaeli wakiwa mstari wa mbele kuhakikisha

zoezi linaenda kama lilivyopangwa.

Katika Konga ya Temeke jumla ya vikundi vilivyopokea ni vikundi 8

ambapo zoezi hilo liliendeshwa mbele ya Mratibu wa UKIMWI wa

Halmashauri ya wilaya ya Temeke Bi, Martha Macha pamoja na mratibu

msaidizi upande wa jamii Bi.Herieth Kamara wa Manispaa ya Temeke.

Aidha Kanda ya Mwanza sehemu tulizoweza kuzifikia ni kata 60,

Halmashauri 12 ambapo ni katika mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga,

Kagera,Tabora na Kigoma, ambapo tulipata ushirikiano kutoka kwa

Viongozi wa Serikali akiwema Mkuu wa mkoa wa Kigoma Bw. Samson

Anga, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri pamoja na viongozi

kutoka manispaa na viongozi wa Konga.

Page 10: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

Mwenyekiti wa Baraza la watu Wanaoishi na virusi vya UKIMWI Bi. Leticia Mourice amezungumzia suala la unyanyapaa kama kikwazo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU) katika malengo ya kitaifa na kimataifa kufikia 95 95 95. Aliyasema hayo Mwezi Juni Mwaka huu 2020, katika mjadala na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za NACOPHA jijini Dar es salaam.

Unyanyapaa unaohusishwa na Virusi ya UKIMWI unaweza kuelezewa kama ni mchakato wa kupunguza thamani ya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI, takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha ya kuwa kiwango cha unyanyapaa nchini ni kwa asilimia 49.7 ambapo katika utafiti huo ulionyesha unyanyapaa umeathiri kwa kiwango kikubwa kwa watu kupata huduma za upimaji, tiba na matunzo na hata kubaki kwenye tiba kwa usahihi, katika jitihada za kupinga unyanyapaa kila mwezi Machi 01, kila mwaka jamiiinaazimisha siku hiyo.

Aidha katika mjadala huo Bi. Leticia alizungumzia suala la unyanyapaa kama kikwazo na tatizo kubwa kwa Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) ambapo aliomba jamii kuondokana na dhana potofu ya unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na VVU. Alielezea unyanyapaa uliopo katika jamii yetu ni wa aina mbili, aina ya kwanza ni unyanyapaa binafsi na aina ya pili ni ule wa mtu kunyanyapaliwa na mtu, kikundi au jamii kwa ujumla.

Bi Leticia alieleza ya kuwa unyanyapaa binafsi ni ile hali ya mtu kujinyanyapaa mwenyewe pale anapojihisi hana thamani na kujihisi watu watanionaje. Aina ya pili ni ile hali ya Jamii kumnyanyapaa mtu, kushindwa kuthamini utu kwasababu anaishi na VVU wakati yapo magojwa mengine ambayo yanapelekea hata mtu kukatwa viungo vya mwili mfano Kisukari

Hata hivyo katika suala zima la unyanyapaa vijana wameku-wa wahanga ambapo asilimia kubwa ya vijana wanajin-yanyapaa wenyewe hali inayopelekea wengi wao kuacha kutumia dawa kwa kuhofia kuonekana katika sehemu za kuchukulia dawa (CTC) na hivyo kusaba-bisha madhara kama kupoteza kizazi kijacho.

Katika utekelezaji wa Mradi wa HEBU TUYAJENGE, vijana ikiwa ni sehemu ya walengwa wakuu katika kuwahimiza utumiaji sahihi wa huduma za UKIMWI, pamoja na kuwajengea uwezo wa kujitambua na kusimama kwa kujiamini ili kuweza kutimiza ndoto zao.

Hata hivyo, Bi Leticia alishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanza-nia kupitia Wizara ya Afya Maendelo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto kwa mchango mkubwa katika mwitikio wa UKIMWI nchini, ikiwa ni pamoja na kushusha umri wa vijana kupima kutambua afya zao kwa ridhaa yao kutoka miaka 18 iliyokuwa awali na sasa imekuwa miaka 15, hii itamsaid-ia kijana kujua afya yake mapema na kama ana maambukizi aanze tiba mapema ili aweze kutimiza ndoto zake na kutengeneza Taifa la kesho.

Mwe

nyek

iti wa

Bar

aza

la wa

tu W

anao

ishi n

a vir

usi v

ya U

kimwi

Tanz

ania

Bi. L

etici

a M

ouric

e

Unyanyapaa ni kikwazo kufikia95-95-95

8

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Page 11: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

9

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

(NACOPHA) Bw. Deogratius Rutatwa pamoja na wajumbe wa bodi walifanya

ziara ya ukaguzi wa vikundi vya Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

(WAVIU) pamoja na shughuli mbali mbali katika utekelezaji wa mradi wa

HEBU TUYAJENGE unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu wa

Marekani USAID katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Ziara hii ilifanyika kwa

siku tano kuanzia mnamo mwezi Juni 2020.

Lengo la ziara ilikuwa kukagua shughuli zinazoendeshwa na vikundi vya

WAVIU na shughuli zinazoendelea katika Konga hususani uimarishaji na

uundwaji wa Vikundi. Katika ziara hii wajumbe waliweza kutembelea

Konga za Manispaa ya Mtwara Mikindani na Halmashauri ya Wilaya ya

Newala ambapo waliweza kukutana na wawakilishi wa Vikundi 14 vya

WAVIU Mkoani Mtwara. Mkoani Lindi Konga ya Nachingwea ilitembelewa

na wajumbe waliweza kuhudhuria mkutano mkuu wa Uchaguzi wa

Konga uliofanyika mapema Tarehe 09/06/2020.

Aidha wajumbe walitembelea Ofisi za Makatibu tawala mikoa ya Lindi na

Mtwara kwa ajili ya kutambulisha mradi katika ngazi ya Mkoa. Katika utambulisho huu wajumbe walionana na Makatibu tawala pamoja na maafisa maendeleo ya jamii wa mkoa.

Ziara hii imekuwa jukwaa muhimu la kuleta chachu ya mabadiliko kwa

kuwataka WAVIU mmoja mmoja na katika vikundi kuondokana na dhana

ya kuwa watu au vikundi vya misaada na badala yake wawe na mtizamo

Ziara ya ukaguzi wa vikundi wezeshimkoani Lindi na Mtwara

wa kujiamini, kujengana na kujasirishana Katika ngazi ya Konga,

Mtendaji mkuu wa Baraza aliwaagiza viongozi wa Konga

kufanya juhudi za makusudi za kuunda vikundi vya WAVIU pamoja

na Konga kata kwenye kila kata.

Ofisi ya Kanda ya Dar es Salaam ambayo ndio inaratibu Mikoa ya

Lindi na Mtwara tunatoa shukrani za dhati kwa Afisa Mtendaji Mkuu

pamoja na wajumbe wa bodi kwa jitihada za kutembelea Konga na

vikundi vyetu. Ziara hii imeleta mwamko mkubwa wa kujiamini na

kujijenga miongoni mwa WAVIU.

Afisa mtendaji mkuu (NACOPHA) Deogratius Rutatwa akielezea mradi wa Hebu Tuyajenge kwa WAVIU konga ya Newala vijijini alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli za vikundi wezezeshi mkoani

Mtwara 8/6/2020.

Afisa mtendaji mkuu wa NACOPHA na wajumbe wa bodi ya Baraza pamoja na wawakilishi wa vikundi vya WAVIU katika picha ya pamoja alipowatembelea wanavikundi hao kwenye ofisi yaHalmashauri ya wilaya ya Newala Vijijini tarehe 8/06/2020

Page 12: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

10

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Serikali mkoani Tabora yaviwezesha vikundi vya WAVIU

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiongea na wanakikundi chaFaraja pamoja na wananchi katika kata ya Nkinga Wilayani Igunga katika ziara ya kuhamasisha

kufikia malengo ya 95-95-95 pamoja na uanzishwaji wa Vikundi wezeshi vya WAVIU.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora ametoa milioni 12 kwa vikundi vya watu

wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) katika ziara yake alipotembelea

katika vikundi wezeshi kuona shughuli zinazofanywa na Konga kupitia

vikundi vya WAVIU ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji na utekelezaji wa

Mradi wa Hebu Tuyajenge unaotekelezwa na NACOPHA na kufadhiliwa na

Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambapo ziara hiyo

ilifanyika kwa siku saba June 22/06/2020 mpaka 28/06/2020 mkoani

Tabora.

Aidha amevutiwa na jitihada zinazofanywa na WAVIU katika vikundi vyao

na kuahidi kutoa kiasi cha Shilingi milioni moja katika kila kikundi ambapo

kiasi cha milioni 12 zilitolewa kwa vikundi kumi na mbili alipotembelea

katika vikundi mbali mbali ikiwemo Halmashauri ya Sikonge, Urambo,

Igunga, nzega mji, pamoja na Nzega Wilaya, ikiwa ni zoezi endelevu katika

utekelezaji wa mradi ambalo limeanza katika kanda ya Mwanza na

kujumuisha washiriki 42, wanawake 22 na wanaume 20.

Mkuu wa mkoa amesema fedha hizo zitaingizwa katika akaunti za vikundi

moja kwa moja kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao ili kujikwamua

kiuchumi. Hata hivyo Mwanri amewataka wakurugenzi wa halmashauri

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akipokea zawadi ya Kuku na Mafuta kutoka katika kikundi cha Upendo kilichopo Wilayani Sikonge wakati alipofanya ziara ya kutembelea vikundi wezeshi

zote za mkoa wa Tabora kutoa kipaumbele kwa vikundi vya watu Wanaoishi

na Virusi vya UKIMWI katika fedha za mikopo zinazotolewa na Halmashauri kwa makundi maalum.

Bwana Zakaria Matope, mjumbe wa Konga ya Nzega na Bi. Neema Samweli mjumbe wa Konga ya Igunga wamepongeza jitihada zinazofanywa na NACOPHA kupitia USAID kwa kuwapa kipaumbele katika miradi ya kuhakikisha inatokomeza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi, pia wameshukuru NACOPHA kwa kuwaunganisha na Serikali na jitihada zinazofanywa na mkuu wa mkoa kwa kuwathamini ikiwa ni pamoja na kuwatembelea na kuwapa moyo katika shughuli mbalimbali wanazojishughulisha nazo kama sehemu ya kujipatia kipato.

Page 13: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

11

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Mafunzo ya Wakiri tiba ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa HEBU TUYAJENGE( HT), ambayo hutolewa kwa kuzingatia utaratibu maalum ili kufikia walengwa na kuleta matokeo chanya. Utolewaji wa mafunzo haya umefanyika katika Kanda nne za mradi, Kanda ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya ambapo kabla ya utolewaji wa mafunzo kulikuwa na mafunzo ya Timu ya Uratibu wa Konga (CCT) ambayo walijengewa uwezo katika suala zima la kusimamia na kuendesha shughuli za mafunzo kwa wakati kwa kuzingatia taratibu zilizopo ili kuhakikisha ujumbe unafika kwa jamii ipasavyo.

Katika kanda Kanda ya Dar es Salaam, mafunzo yalifanyika kwa kipindi tofauti katika konga 15 ambapo jumla ya wakiri tiba 150 walipatiwa mafunzo hayo ambayo yanalenga namna ya utekelezaji wa shughuli za mradi katika kutoa huduma za UKIMWI ngazi ya jamii, ambayo yalikuwa yanatolewa kwa nyakati tofauti kwa kila konga na yalifanyika takriban siku sita na yalihusisha WAVIU na wawakilishi kutoka Halmashauri husika kama, Mratibu wa Ukimwi wa Wilaya(CHACC), Mratibu wa Afya (DACC) na Mratibu wa huduma za Afya majumbani (CBHSCO).

Aidha mafunzo haya yalitolewa na Wataalamu kwa kutumia mifano stahiki na kulikuwa na wasaa wa maswali na majibu ili kuhakikisha upokeaji wa taarifa unawafikia walengwa na kupata matokeo chanya ili kuweza kuzifikia 95 95 95 ifikapo 2030. Kanda ya Dar es Salaam Konga zilizoshiriki katika mafunzo ni H/wilaya Ilala, H/wilaya Temeke, H/wilaya Masasi, H/mji

Mafunzo ya wakiri tiba katikautekelezaji wa mradi

Timu za uratibu wa mradi wa Hebu Tuyajenge (HT) wakiwa katika mafunzo elekezi ya utekelezaji wa mradi yaliyofanyika katika kanda ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya

Masasi, H/wilaya Mtwara, Newala H/wilaya, Newala H/wilaya, H/wilaya Lindi, H/mji Lindi, H/wilaya Nachingwea, H/wilaya Ruangwa, H/mji Tanga, H/manispaa Moshi, H/wilaya Moshi na H/wilaya Chalinze.

Aidha katika Kanda ya Mbeya, mafunzo ya wakiri tiba yalitolewa katika konga 15 ambayo yalihudhuriwa na wawakilishi kutoka Manispaa (CHACC na DACC) ambapo utaratibu wa utolewaji wa mafunzo uliendeshwa na wataalamu kwa ufanisi na kwa kutumia njia mbali mbali ili kuhakikisha ujumbe unafika kwa jamii ipasavyo.

Konga zilizoshiriki katika mafunzo hayo ni Konga ya Makambako halmashauri ya Mji, Makete h/wilaya, Mafinga h/mji, Ludewa h/wilaya, Iringa h/wilaya, Songea h/manispaa, Sumbawanga h/manispaa, Rungwe h/wilaya, Mbeya h/jiji, Njombe h/mji, Kilolo h/wilaya, Iringa h/manispaa, Wanging’ombe h/wilaya Mufindi h/wilaya, na Njombe h/wilaya.

Kanda ya Dodoma jumla ya Konga zilizopatiwa mafunzo ni konga 23 ambayo yalihudhuriwa na wawakilishi kutoka Serikalini CHACC na DACC ambapo mafunzo hayo yalitolewa kwa ufanisi wa hali ya juu na kwa kutumia njia mbali mbali ili kujenga uelewa na kupata matokeo ya stahiki.Hali kadhalika kanda ya Mwanza mafunzo yaliendeshwa na wataalamu na waliendesha mafunzo hayo kwa awamu tofauti na kwa kuzingatia utolewaji wa mafunzo wa kiwango cha juu ambapo jumla ya Konga 15 zilishiriki katika mafunzo ambayo yalilenga kuwajengea uwezo wa kuwa mabalozi wazuri katika Konga zao.

Timu za uratibu zikiwa kwenye mafunzo elekezi ya utekelezaji wa mradi kanda ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Upland Changanyikeni

Page 14: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

12

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Ziara ya viongozi wa NACOPHAOfisi ya Waziri Mkuu - Dodoma

Baraza la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA)

mwezi wa Agosti mwaka huu 2020 waliweza kuwasilisha taarifa ya

utendaji wa shughuli za Baraza kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,

Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Doroth Mwaluko katika Mkutano uliofanyika

Ofisi ya Waziri Mkuu, mkoani Dodoma.

Katika mkutano huo ambao mgeni rasmi alikuwa Bi. Doroth Mwaluko,

pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI

(TACAIDS) Dr. Leornard Maboko, Pundensia Mbwiliza, Mwenyekiti wa

Mtandao wa Vijana wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI (NYP+), Ms.

Leticia Mourice Mwenyekiti NACOPHA, Bw. Deogratius Rutatwa Afisa

Mtendaji Mkuu NACOPHA, pamoja na wawakilishi wengine kutoka Ofisi

ya Waziri Mkuu.

Aidha Mwenyekiti wa NACOPHA Bi. Mourice alishukuru Serikali ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tawala za mikoa na serikali

za mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee

na Watoto (MoHDGEC) kwa kazi nzuri ambayo wanaendelea kuifanya

na hasa kuhakikisha watu wanoishi na VVU wanapata huduma stahiki.

Pia alishukuru Serikali kwa kuendelea kuitambua NACOPHA na

kufanya nayo kazi kwa ukaribu sana, hali kadhalika aliishukuru Serikali

ya Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la watu wa

Marekani USAID kwa kuendelea kuwezesha NACOPHA dhidi ya

mwitikio wa VVU NA UKIMWI na kuunganisha sauti za WAVIU nchini. Bi.

Leticia alielezea kuwa “NACOPHA inafanya kazi kwa kuzingatia sheria

na miongozo ya nchi kwa kuanzia ngazi ya jamii kupitia vikundi

wezeshi, konga kata na konga wilaya”. Bw. Rutatwa alielezea historia

ya NACOPHA kuwa ilianzishwa na Tume wakati wa NMSF II kwa lengo

na kuratibu WAVIU nchini, hivyo mwaka 2003 NACOPHA iliundwa na

kupata usajili rasmi mwaka 2005. Alielezea dira, dhima na lengo kuu la

NACOPHA, na alitaja tunu za NACOPHA kuwa ni uwajibikaji, utamaduni

bora, uadilifu, usawa wa kijinsia, kujitoa na kuheshimu utu na misingi

ya utawala bora.

Aidha, Bw. Rutatwa pia alibainisha kuwa hadi sasa NACOPHA ina jumla

ya konga 175 kati ya 185 za Tanzania Bara, pia ina wanachama

640,483 (406,838 wanawake na 233,645 wanaume) ambao ni 43%

ya WAVIU wote nchini. Vile vile aliwataja wanufaika wakuu wa

NACOPHA kuwa ni WAVIU kupitia ushiriki wao katika ngazi ya jamii

kutoka kwenye vikundi na konga za WAVIU.

Wakati wa wasilisho pia alipata wasaa wa kuelezea maeneo makuu ya

kimkakati ambayo ni:- Ushirikishwaji jamii na Uwezeshaji wa WAVIU;

Kuhamasisha uhitaji na utumiaji wa huduma za VVU; Utetezi na ushaw-

ishi wa kisera; Taarifa za kimkakati, Utafiti na mawasiliano; Kujengea

uwezo taasisi, vikundi na konga za WAVIU. Vile vile alielezea miradi

mbalimbali inayotekelezwa na NACOPHA ambayo ni pamoja na mradi

wa HEBU TUYAJENGE unaofadhiliwa na USAID, Mradi wa COMPASS

Africa unaofadhiliwa na AIDS Vaccine Advocacy Coalition (AVAC),

Pamoja na mradi wa Ushirikishwaji wa makundi maalum na WAVIU

katika ushawishi wa huduma mbadala zinazoshirikisha WAVIU

kikamilifu unaofadhiliwa na Global Network of People Living with HIV

and AIDS (GNP+)

Kwa kumalizia wasilisho lake Afisa Mtendaji mkuu wa NACOPHA

alielezea fursa mbalimbali kwa ajili ya maboresho ya baadaye ambazo

ni:- Upungufu wa rasilimali kwa ajili ya kuboresha uratibu na msaada

wa kitaalamu kwa Konga za WAVIU, Kuendeleza juhudi za kutokomeza

unyanyapaa na ubaguzi ili kuchagiza utumiaji wa huduma za upimaji

wa hiari, kujiweka wazi, utambuzi wa watoto na Wanaume dhidi ya

kinga ya maambukizi ya VVU, Mwitikio mdogo wa Wanaume, vijana na

Watoto, Uhamasishaji mkubwa wa utumiaji huduma usioendana na

huduma zilizopo katika baadhi ya vituo vya huduma za UKIMWI, Ukweli

ni kwamba lipo kundi kubwa linalohitaji kukingwa/ kujikinga na

maambukizi ya VVU.

Katibu mkuu alieleza ya kuwa, Watu wanoishi na virusi vya UKIMWI ni

wengi tu lakini hawajaamua kuwa wazi, hivyo alipongeza viongozi wa

NACOPHA kwa kuweza kupata ujasiri wa kuwa huru na kusema kuwa

wanaishi na maambukizi ya VVU. Aidha alielekeza kuwa ifike mahala

neno unyanyapaa wadau wote ikiwemo NACOPHA waachane nalo

kwani kadri linavyotamkwa ndivyo linavyokomaa, hivyo fikra zetu

zikiondokana na hili neno na mambo mengine yatakaa sawa.

Alihitimisha kwa kusema kuwa amefurahishwa kuona NACOPHA

inawajibika ipasavyo, lakini pia aliahidi kutafuta nafasi ya kutembelea

Ofisi za NACOPHA ili kujionea shughuli za WAVIU na kuendelea

kushirikiana, na pia alisisitiza kuwa NACOPHA ndiyo chachu kubwa ya

kuhakikisha kuwa mipango iliyopangwa inatekelezeka ili kuweza

kufikia malengo ya kitaifa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA Deogratius Rutatwa akiwasilisha utekelezaji wa shughuli za barazakwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Mhe. Dorothy Mwaluko

Mkurugenzi wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko akifurahia jambo wakati wa mkutano wa wasilisho la utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWII (NACOPHA) kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Mhe. Dorothy Mwaluko, katika

ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma

Page 15: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

13

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Baraza la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA)

mwezi wa Agosti mwaka huu 2020 waliweza kuwasilisha taarifa ya

utendaji wa shughuli za Baraza kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,

Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Doroth Mwaluko katika Mkutano uliofanyika

Ofisi ya Waziri Mkuu, mkoani Dodoma.

Katika mkutano huo ambao mgeni rasmi alikuwa Bi. Doroth Mwaluko,

pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI

(TACAIDS) Dr. Leornard Maboko, Pundensia Mbwiliza, Mwenyekiti wa

Mtandao wa Vijana wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI (NYP+), Ms.

Leticia Mourice Mwenyekiti NACOPHA, Bw. Deogratius Rutatwa Afisa

Mtendaji Mkuu NACOPHA, pamoja na wawakilishi wengine kutoka Ofisi

ya Waziri Mkuu.

Aidha Mwenyekiti wa NACOPHA Bi. Mourice alishukuru Serikali ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tawala za mikoa na serikali

za mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee

na Watoto (MoHDGEC) kwa kazi nzuri ambayo wanaendelea kuifanya

na hasa kuhakikisha watu wanoishi na VVU wanapata huduma stahiki.

Pia alishukuru Serikali kwa kuendelea kuitambua NACOPHA na

kufanya nayo kazi kwa ukaribu sana, hali kadhalika aliishukuru Serikali

ya Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la watu wa

Marekani USAID kwa kuendelea kuwezesha NACOPHA dhidi ya

mwitikio wa VVU NA UKIMWI na kuunganisha sauti za WAVIU nchini. Bi.

Leticia alielezea kuwa “NACOPHA inafanya kazi kwa kuzingatia sheria

na miongozo ya nchi kwa kuanzia ngazi ya jamii kupitia vikundi

wezeshi, konga kata na konga wilaya”. Bw. Rutatwa alielezea historia

ya NACOPHA kuwa ilianzishwa na Tume wakati wa NMSF II kwa lengo

na kuratibu WAVIU nchini, hivyo mwaka 2003 NACOPHA iliundwa na

kupata usajili rasmi mwaka 2005. Alielezea dira, dhima na lengo kuu la

NACOPHA, na alitaja tunu za NACOPHA kuwa ni uwajibikaji, utamaduni

bora, uadilifu, usawa wa kijinsia, kujitoa na kuheshimu utu na misingi

ya utawala bora.

Aidha, Bw. Rutatwa pia alibainisha kuwa hadi sasa NACOPHA ina jumla

ya konga 175 kati ya 185 za Tanzania Bara, pia ina wanachama

640,483 (406,838 wanawake na 233,645 wanaume) ambao ni 43%

ya WAVIU wote nchini. Vile vile aliwataja wanufaika wakuu wa

NACOPHA kuwa ni WAVIU kupitia ushiriki wao katika ngazi ya jamii

kutoka kwenye vikundi na konga za WAVIU.

Wakati wa wasilisho pia alipata wasaa wa kuelezea maeneo makuu ya

kimkakati ambayo ni:- Ushirikishwaji jamii na Uwezeshaji wa WAVIU;

Kuhamasisha uhitaji na utumiaji wa huduma za VVU; Utetezi na ushaw-

ishi wa kisera; Taarifa za kimkakati, Utafiti na mawasiliano; Kujengea

uwezo taasisi, vikundi na konga za WAVIU. Vile vile alielezea miradi

mbalimbali inayotekelezwa na NACOPHA ambayo ni pamoja na mradi

wa HEBU TUYAJENGE unaofadhiliwa na USAID, Mradi wa COMPASS

Africa unaofadhiliwa na AIDS Vaccine Advocacy Coalition (AVAC),

Pamoja na mradi wa Ushirikishwaji wa makundi maalum na WAVIU

katika ushawishi wa huduma mbadala zinazoshirikisha WAVIU

kikamilifu unaofadhiliwa na Global Network of People Living with HIV

and AIDS (GNP+)

Kwa kumalizia wasilisho lake Afisa Mtendaji mkuu wa NACOPHA

alielezea fursa mbalimbali kwa ajili ya maboresho ya baadaye ambazo

ni:- Upungufu wa rasilimali kwa ajili ya kuboresha uratibu na msaada

wa kitaalamu kwa Konga za WAVIU, Kuendeleza juhudi za kutokomeza

unyanyapaa na ubaguzi ili kuchagiza utumiaji wa huduma za upimaji

wa hiari, kujiweka wazi, utambuzi wa watoto na Wanaume dhidi ya

kinga ya maambukizi ya VVU, Mwitikio mdogo wa Wanaume, vijana na

Watoto, Uhamasishaji mkubwa wa utumiaji huduma usioendana na

huduma zilizopo katika baadhi ya vituo vya huduma za UKIMWI, Ukweli

ni kwamba lipo kundi kubwa linalohitaji kukingwa/ kujikinga na

maambukizi ya VVU.

Katibu mkuu alieleza ya kuwa, Watu wanoishi na virusi vya UKIMWI ni

wengi tu lakini hawajaamua kuwa wazi, hivyo alipongeza viongozi wa

NACOPHA kwa kuweza kupata ujasiri wa kuwa huru na kusema kuwa

wanaishi na maambukizi ya VVU. Aidha alielekeza kuwa ifike mahala

neno unyanyapaa wadau wote ikiwemo NACOPHA waachane nalo

kwani kadri linavyotamkwa ndivyo linavyokomaa, hivyo fikra zetu

zikiondokana na hili neno na mambo mengine yatakaa sawa.

Alihitimisha kwa kusema kuwa amefurahishwa kuona NACOPHA

inawajibika ipasavyo, lakini pia aliahidi kutafuta nafasi ya kutembelea

Ofisi za NACOPHA ili kujionea shughuli za WAVIU na kuendelea

kushirikiana, na pia alisisitiza kuwa NACOPHA ndiyo chachu kubwa ya

kuhakikisha kuwa mipango iliyopangwa inatekelezeka ili kuweza

kufikia malengo ya kitaifa.

Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa wasilisho la utekelezaji wa shughuli za NACOPHA wakiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwezeshaji Mhe. Dorothy Mwaluko aliyekaa katikati

Makamu Mwenyekiti wa NACOPHA Yusufu Marere aliyekaa katikati akiwa na wajumbe wa Bodi ya NACOPHA kulia; Pudensiana Mbwiliza na kushoto; Eliasi Charles wakati wa mkutano wa wasilisho la utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWII (NACOPHA) kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Mhe. Dorothy Mwaluko, Dodoma

Page 16: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

14

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

SIMULIZI ZA MAFANIKIO

Kurudiana kwa wanandoaambao mmoja anaishi na VVU

Bi. Kanisia Kadege aliachwa na mumewe Bw. Fisto Kisakali baada ya kufahamu anaishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Bw. Kisakali aliamua kuitelekeza familia yake na kuhamia sehemu nyingine na kumtuhumu mkewe kwa kutokuwa muaminifu katika ndoa yao.

Hali hiyo ilibainika katika kipindi cha ujauzito wa pili wa Kanisia ambapo mumewe alitaka waende katika kituo cha afya kwa ajili ya kujua hali ya afya yake ndipo alipogundulika anaishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI lakini hakuwa muwazi kwa mumewe ambaye hanamaambukizi.

Bi. Kadege ana umri wa miaka 42 na ni Mwanachama wa Konga ya Njombe anayeishi katika Kijiji cha Iyendela, katika kata ya Matembwe Mkoani Njombe. Anaishi na maambukizi toka mwaka 2014 na anafata taratibu za utumiaji wa dawa katika vituo vya utoaji wa huduma CTC.

Aliolewa na Bw. Kisakali kama mke wa pili na walifanikiwa kupata Watoto wawili. Mtoto wa kwanza ana miaka minne na wa pili ana mwaka mmoja ambapo watoto wote hawana maambukizi kutokana na mama kufuata taratibu za utumiaji wa dawa za kinga dhidi ya mama na mtoto (PMCT)

Mwezi wa tano mwaka huu 2020, Bw. Christopher Gwivaha na Bi. Evarista Hongoli wa kata ya Matembwe walihudhuria mafunzo ya

wakiritiba kupitia mradi wa HEBU TUYAJENGE na kujifunza jinsi ya kuwarudisha waliotoroka katika dawa, huduma za upimaji, upimaji wa wenza (index testing) na upimaji wa wingi wa virusi. Kupitia mafunzo ya wakiritiba waliamua kuwatembelea Bi Kanisia na Bw.Kisakali kila mtu katika makazi yake na walipata muda wa kuongea nao kuhusi-ana na mgogoro wao. Waliwashauri waende kupima katika kata ya Matembwe na baada ya matokeo wakiritiba walikaa nao na kuanza kutoa ushauri wa jinsi ya kuishi pamoja na kukubaliana na hali hiyo na walimueleza kwakuwa mkewe anafuata huduma za tiba (ART) hawezi kumuambukiza na pia walimsisitiza Bw. Kisakali kurejea nyumbani.

Baada ya jitihada hizo kikao kilifanyika Julai 07, 2020 ambapo Bw.

Kisakali alikubali kurudi nyumbani kwake na kumuomba mkewe

msamaha pamoja na wote waliohusika katika upatanishi. Hata hivyo

ili kuhakikisha amani na upendo unazidi kujengeka na kuleta furaha

baina yao, wawakilishi wetu katika sehemu husika wako karibu na

familia hii ili kujenga Taifa Imara.

Ni muhimu kwa jamii kutambua ya kuwa, kuishi na maambukizi ya

UKIMWI haiondoi haki ya kuolewa, kwani kuna asilimia kubwa ya

Watu wanaoishi na Maambukizi ya VVU na wameoa/kuolewa na watu

wasio na maambukizi na kuzaa Watoto wasio na maambukizi.

NinamshukuruBw. Christopher Gwivaha na Bi. Evarista, sasa hivi tuna furaha na tunatambua jinsi ya kuishi ikiwa mmoja ana maambukizi na mwingine hana na tunaahidi tutakuwa mabalozi wazuri na kusaidia wengine Said Fisto

Bi, Kanisia Kadege na mumewe Bw. Fisto

Kisakali pamoja na Watoto wao Chesco na Editoni Kisakaliwakiwa nyumbani kwao

baada ya kupatana

Page 17: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

15

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Konga ya Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga wamekuwa na uhaba

wa ofisi kwa muda mrefu na kufikia maamuzi ya kupanga ofisi toka

mwaka 2018. Konga hii ni miongoni mwa konga zinazotekeleza mradi wa

HEBU TUYAJENGE kanda ya Mbeya ambao unatekelezwa na NACOPHA

kwa ufadhili wa USAID.

Kumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya Konga na Halmashauri ya

Manispaa Sumbawanga kwa muda mrefu, tunathamini mchango na

ushirikiano mzuri kutoka kwa Serikali.

Mnamo tarehe 15/07/2020 jumla ya konga 18 za Halmashauri ya

Manispaa Sumbawanga zilitumwa kwa wawakilishi kushiriki katika

mafunzo ya Wakiri tiba yaliofanyika katika ukumbi wa Sambala katika

Halmashauri ya Manispaa Iringa, Pia walihudhuria wawakilishi kutoka

Halmashauri za wilaya (CHAC/DACC),Mwenyekiti wa Konga, Makamu

mwenyekiti, Katibu, Karani na mwakilishi wa Vijana, ni kati ya watu

walioshiriki katika mafunzo hayo pamoja na Wakiritiba kutoka katika kata

tano Mazwi, Majengo, Chanji, Pito and Ntendo.

Malengo ya mafunzo haya nikuwaunganisha WAVIU na huduma za

upimaji, upimaji wa wenza, Ufuatiliaji wa wingi wa virusi kwenye damu,

kuwarudisha katika dawa na kuwaunganisha na vikundi wezeshi.

Baada ya mafunzo Viongozi wa Konga kwa kushirikiana na mratibu wa

Ukimwi wa Wilaya na Mratibu wa Afya wa Wilaya wa Halmashauri ya

Manispaa ya Sumbawanga waliutambulisha mradi wa HEBU TUYAJENGE

malengo na sehemu zinazofikiwa na mradi na pia waliwatambulisha

wakiritiba waliopata mafunzo kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa

wilaya(DCDO) na Afisa Tawala wa Wilaya (DED) ili kupata ruhusa ya

kuwatambulisha katika kata na sehemu za utolewaji wa huduma za Afya

(CTC) kwa ajili ya shughuli za utekelezaji wa mradi. Hata hivyo Viongozi

wa Konga wana nafasi ya kuainisha changamoto wanazokabiliana nazo

katika utendaji.

Afisa Tawala wa wilaya anatambua juhudi zinazofanywa na Konga katika

utekelezaji wa mwitikio wa Ukimwi. Hivyobasi katika kuunga mkono

juhudi na utekelezaji yakinifu dhidi ya UKIMWI Afisa tawala wa wilaya

ametoa kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 900 katika Kijiji cha

Masufa street kilichopo kilomita saba kutoka mjini na ameagiza Afisa

Serikali bega kwa bega na konga H/ManispaaSumbawanga katika mwitikio wa UKIMWI

mipango miji wa Halmashauri kuhakikisha nyaraka zote ikiwepo Hati za

viwanja zimekamilika ili ujenzi wa Ofisi za Konga uanze pamoja na ufanyaji

wa shughuli nyingine za kiuchumi.

Pia aliahidi kutoa usafiri katika shughuli za utekelezaji wa mradi ili kusaidia

suala zima la kupambana na ugonjwa wa UKIMWI kwa wakazi wa eneo

husika.

“Kwa niaba ya NACOPHA Konga ya Halmashauri ya Manispaa ya

Sumbawanga, Ningependa kutoa shukrani kwa uongozi wa NACOPHA kwa

kutushirikisha katika mradi wa HEBU TUYAJENGE katika Halmashauri zetu.

Katika konga yetu huu ni mradi wa kwanza ambao tutautekeleza katika

Halmashauri yetu.Tunawashukuru uongozi wa Halmashauri ya Manispaa

ya Sumbawanga kwa msaada tulioupokea na msaada tunaoendelea

kupokea katika shughuli za utekelezaji wa UKIMWI na tunaahidi kuongeza

juhudi kwa lengo la kuokoa kizazi na maambukizi mapya,kuondoa

unyanyapaa katika jamii na kuhakikisha WAVIU wanapata huduma za tiba

na matunzo (ART). Ni matumaini kipindi cha utekelezaji wa shughuli za

mradi, unyanyapaa katika jamii utapungua na tutarudisha waliotoroka

katika dawa na kuwaunganisha WAVIU katika huduma za tiba na matunzo”

alisema mwenyekiti wa Halmashauri Manispaa ya Sumbawanga Bi.

Christina Mulisa.

Nimatumaini ya kwamba,kipindi cha utekelezaji wa shughuli za mradi

katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga,WAVIU wapya watapati-

kana,watoro wa dawa watarudishwa,Utolewaji wa huduma za afya katika

jamii, kuwaunganisha WAVIU na vikundi wezeshi pamoja na huduma za

ufuatiliaji wa wingi wa virusi katika damu.

Viongozi wa Konga ya Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga pamoja na Wakiri tiba katika ofisi za Afisa Tawala wa Wilaya wakati wa utambulisho wa mradi wa HEBU TUYAJENGE.

SIMULIZI ZA MAFANIKIO

Page 18: NACOPHA SWAHILI NEWSLETTER 005 FINAL low res

3 ZE

ROS

BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA

Baraza la Taifa la watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA)Barabara ya Whitesand 86, Mtaa wa Keni Close/Kilongawima, Nyumba Na. KUN/KIL/83 S. L. P 55811. Dar es Salaam, Tanzania. Simu: +255-22-2618518,

Barua pepe: [email protected], Tovuti: www.nacopha.or.tz