mem bullettin 20

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 03-Jun-2018

268 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 8/12/2019 MEM Bullettin 20

    1/8

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbalikwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbalikwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    oleo No.20 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe Juni 13-19, 2014

    Gesi zaidiyagunduliwaGesi zaidiyagunduliwaUgunduzi uliofanyika katika kisima chaTaachui 1 unaendeleza mfululizo wa

    mafanikio ya uchimbaji kwa asilimia 100%katika kitalu namba 1,3 na 4 na vilevilekuongeza rasilimali zaidi kuwezeshautekelezaji wa mradi wa LNG nchiniTanzania.

  • 8/12/2019 MEM Bullettin 20

    2/8

    2 | MEM News Bulletin

    NISHATI

    FIVEPILLARS

    OF

    REFORMS

    TEL 2110490

    FAX 2110389

    MOB 0732999263

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUUBadra Masoud

    MSANIFUEssy OgundeWAANDISHI

    Veronica SimbaAsteria MuhozyaGreyson Mwase

    Teresia MhagamaNuru Mwasampeta

    INCREASE EFFICIENCY

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFICATION OFTHE CLIENT

    SATISFICATION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFICATION OFSHAREHOLDERS

    Na Veronica Simba Dar es Salaam

    Serikali ya Icelanditashirikiana na seri-

    kali ya Tanzania katikakuendeleza jotoardhi

    (geothermal) hapa nchini.Akizungumza na Waziri

    mwenye dhamana ya Nishatina Madini, Prof. SospeterMuhongo, Rais wa Iceland,Olafur Grimsonn amesemaserikali yake na kampuni zakeziko tayari kupokea wataala-mu kutoka Tanzania mapemamwezi Julai kwenda kujifunzamasuala ya jotoardhi nchinihumo.

    Waziri Muhongoameuelezea utayari wa Icelandkushirikiana na Tanzania kamafursa hususani kipindi hikiambapo serikali imedhamiriakutumia njia mbalimbali zakuzalisha umeme ikiwemojotoardhi, ili kupunguza naikiwezekana kuondoa kabisatatizo la upatikanaji wa nishatihiyo kwa wananchi wake.

    Nchi ya Iceland ndiyobingwa duniani kwa nishatiya jotoardhi, hivyo utayariwao kushirikiana nasi ni fursa

    kwetu kujifunza kutoka kwao

    namna walivyofanikiwa ilinasi tunufaike ipasavyo na jo-toardhi yetu, amesema Prof.Muhongo.

    Aidha, Waziri Muhongo

    amesema ili kunufaika ip-asavyo na fursa hiyo, wataala-mu kutoka Tanzania wataka-okwenda nchini Iceland kwaziara ya mafunzo, watatumiafursa hiyo kutafuta nafasi zauwekezaji kutoka huko.

    Kwa upande wake, Kam-ishna Msaidizi anayeshu-ghulikia masuala ya nishatimbadala, Bw Edward Ishen-goma amesema fursa hiyoimekuja kwa wakati muafakakwani sekta yake imejiwekeamikakati kuhakikisha uwepowa jotoardhi nchini unai-nufaisha jamii kwa kuzali-sha umeme na hivyo kukuzauchumi wa wananchi na taifakwa ujumla.

    Tanzania iko katika maan-dalizi na inatarajiwa kuwamwenyeji wa kongamano latano la jotoardhi kwa nchi zaAfrika Mashariki na Kati zi-lizo katika bonde la ufa.

    Kongamano hilo linatara-jiwa kufanyika mwishoni mwamwaka huu na litahudhuriwana nchi zinazounda umoja huoambazo ni Kenya, Uganda,

    Tanzania, Djibouti, Ethiopia,Rwanda na Eritrea.

    Katika hatua nyingine, Wa-ziri Muhongo amesema Tan-zania ni nchi ya mfano baraniAfrika kutokana na uwazi nautekelezaji wa miradi mbalim-bali ya maendeleo ikiwemo yanishati vijijini ambayo baadhiyake inafadhiliwa na Serikaliya Marekani kupitia Mfukowa Changamoto za Millenia(MCC).

    Ameyasema hayo kufua-tia ziara yake ya kikazi nchiniMarekani aliyoifanya hivi kar-ibuni na kukutana na serikali yaMarekani ambayo ameielezeakuwa ya mafanikio makubwa.

    Kwa mujibu wa Prof.Muhongo, Tanzania ni nchiinayopewa kipaumbele sanabarani Afrika kutokana namiradi mablimbali ya maende-leo ikiwemo ya nishati vijijinikusifika kwa kuwa na kiwangocha juu na yenye kutekelezeka.

    Amewataka Watanzaniakuacha tabia ya kujidharauwenyewe na kuwahakik-ishia kwamba miradi iliyochini ya wizara yake, hususanya umeme vijijini itazalishaajira kwa wananchi na itafuta

    umaskini.

    Serikali ya Iceland kuisaidia Tanzania jotoardhi

    Gesi zaidi yagunduliwaNa Malik MunisiKampuni ya Ophir EnergyPlc imetangaza ugunduzi wagesi asilia katika kitalu namba1 katika kisima kilichopewajina la Taachui 1. Kampuni hii

    inamiliki asilimia 20% ya hisakatika kitalu namba 1,3 na 4huku wabia wao BG Groupwakimiliki asilimi 60% ya hisakatika vitalu hivyo.

    Kisima cha Taachui1 kilichimbwa upande wa

    magharibi wa kitalu namba 1 nameli ya uchimbaji ya Deep seaMetro 1. Kisima hiki kilichimb-wa katika kina cha urefu wamita 4,215.

    Gesi iliyogundulika ilion-ekana katika kina cha mita 289

    ndani ya eneo ambalo lililengwakuwa na hifadhi ya nishati hiyo.Tabia ya mashapo katika malihifadhi iliyogundulika inafananakabisa na ile iliyogunduliwa ka-tika kisima cha Mzia ambachopia kipo katika kitalu namba 1.

    Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto) naRais wa Iceland, Olafur Grimsonn

  • 8/12/2019 MEM Bullettin 20

    3/8

    MEM News Bulletin | 3

    MADINI

    Nuru Mwasampeta na

    Teresia MhagamaWizara ya Nishatina Madini inatoawito kwa wananchikutembelea bandala Wizara ya Nishati katika viwanjavya Mnazi Mmoja jijini Dar es Sa-laam ambapo Wizara ikiungana naTaasisi nyingine itashiriki Maoneshoya Wiki ya Utumishi wa Ummayatakayofanyika katika viwanja hivyokuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2014.

    Wito huo umetolewa na

    Msemaji wa Wizara ya Nishati naMadini, Bi. Badra Masoud jijiniDar es Salaam wakati akiongea namwandishi wa habari hii.

    Gesi zaidiyagunduliwa

    Karibuni Wiki ya UtumishiBi.Badra amesema kuwa hii

    ni nafasi muhimu kwa wananchikupata elimu ya mojamoja kuhususekta za Nishati na Madini, kwakuwa wataalam waliobobea katikasekta za Nishati, Madini, Mazingira,sheria, na utawala watakuwepo kati-ka banda hilo ili kutoa elimu pamojana kutatua changamoto mbalimbalizitakazotolewa na wananchi katikakipindi chote cha Maonesho.

    Kuhusu kauli mbiu ya maone-sho hayo, Bi. Badra amesema kuwaMaonesho ya Wiki ya Utumishi waUmma 2014 yamebeba kauli mbiuinayosema Mkataba wa Msingi na

    Kanuni za Utumishi wa Umma Ba-rani Afrika ni chachu ya KuimarishaUtawala Bora na Uendeshaji washughuli za Serikali kwa Uwazi.

    Naomba niseme kwamba

    Wizara ya Nishati na Madini naTaasisi zake tunatekeleza kwavitendo kauli mbiu hiyo hasa sualala uwazi kwani tunaamini rasilimalitunazosimamia ni mali ya wananchihivyo ni haki yao kupata mrejeshowa kile tunachokitekeleza. Ali-sisitiza Bi. Badra.

    Aidha aliwataka watanzaniakufika katika banda la Wizara yaNishati na Madini na Taasisi zake iliwaweze kuhoji na kuuliza masualambalimbali ya kiutendaji ambayobado wananchi hawajayaelewa ikiwani pamoja na masuala ya uombaji wa

    leseni za utafutaji na uchimbaji wamadini, utafutaji na uchimbaji wagesi asilia na masuala yote mtam-buka yanayosimamiwa na Wizara.

    Makadirio ya rasilimaliambayo inaweza kuvunwakutokana na ugunduzi huoni futi za ujazo trilioni 1.0(1.0 TCF). Ukubwa wa eneoambapo gesi ipo umekaakatika namna ambayoinaruhusu ugunduzi kue-ndelea katika eneo la piliupande wa magharibi ambapoinaweza kuwa na ukubwasawa. Kisima cha tathmini nilazima kichimbwe ili kuthibi-tisha uwezekano huu na hililimezingatiwa na wabia hawa.

    Majaribio ya uzalishaji yana-tarajiwa kufanyika mwishonimwa mwezi Juni ili kutathmi-ni ugunduzi huu katika kisimacha Taachui.

    Mkurugenzi Mtendaji waOphir Energy Plc Ndg. NickCooper akiongea wakati wakutangaza ugunduzi huu alise-ma Ugunduzi uliofanyikakatika kisima cha Taachui 1unaendeleza mfululizo wamafanikio ya uchimbaji kwaasilimia 100% katika kitalunamba 1,3 na 4 na vilevile ku-

    ongeza rasilimali kuwezeshautekelezaji wa mradi wa LNGnchini Tanzania. Matokeohaya ni mazuri kwa Ophirkwa sababu mbili; kwanzainaongeza kiasi cha rasilimaliiliyogunduliwa katika upandewa mashariki na hivyo ku-punguza uhatari wa kibali chaOphir katika kitalu cha EastPande ambapo kisima chaTende 1 kitachimbwa hapobaadae mwaka 2014; pili,kiasi cha ujazo wa gesi asiliakilichogunduliwa cha 16.7

    TCF sasa kinakaribia kiasikinachotakiwa kuendelezaLNG Train ya tatu kutokakatika kitalu cha 1,3 na 4.

    Kaimu Mkurugenziwa Shughuli za Utafiti waTPDC, Dr. Emma Msackyamesema kuwa ugunduzi huuunazidi kuiweka Tanzaniakatika ramani ya nchi zinaz-ovutiwa na wawekezaji kwawingi hasa katika sekta ndogoya gesi. Aliongeza kuwaTPDC ipo katika mchakatowa kutathmini wawekezaji

    walioomba katika duru ya nneya ugawaji vitalu, ugunduzihuu unatia moyo kwani nidalili nzuri kwa makam-puni ya kimataifa na ya kitaifayanayotaka kuwekeza katikasekta hii.

  • 8/12/2019 MEM Bullettin 20

    4/8

    4 | MEM News Bulletin

    Matukio Pichani

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa SospeterMuhongo akinena jambo na Msemaji wa Wizara,Bi Badra Masoud pamoja na Mkurugenzi MtendajiTANESCO Eng. Felchesmi Mramba mjini Dodoma.

    Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia kwa ukaribumkutano uliokuwa ukijadili namna bora ya kutekelezasheria ya madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (katikati) akiongea jambo na baadhi ya wajumbewaliohudhuria mkutano uliokuwa ukijadili namna bora ya kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010.

  • 8/12/2019 MEM Bullettin 20

    5/8

    MEM News Bulletin | 5

    Mmoja wa wadauwa shughuliza utafutaji nauzalishaji gesiakitoa maoni yakekuhusu namna yakuboresha rasimuya Sera ya Petroli.Wanaofuatia nibaadhi ya wadaukutoka Kampunimbalimbalizinazofanyashughuli hizo nchini.

    Baadhi ya Maafisakutoka Wizara yaNishati na Madini naTaasisi mbalimbaliza Serikali

    wakifuatilia kikaowakati wa warshaya kupata maoniyatakayosaidiakuboresha Rasimuya Sera ya Petroli.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamojana Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti waHalmashauri, Viongozi wa Dini na baadhi ya Watendaji wa Wizara, mara baada ya kufungua mkutano uliojadiliutekelezaji wa Sheria ya Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto (waliokaa) ni Mkuu wa Mkoawa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadik, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mwantumu Mahiza, Mkuu wa Mkoa waMbeya Mhe. Abbas Kandoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati naMadini, Eliakim Maswi na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Deodatus Mtesiwa.

  • 8/12/2019 MEM Bullettin 20

    6/8

    6 | MEM News Bulletin

    nMasele aeleza inachangia zaidi ya 50% yamapato fedha za kigeninNi mwajiri mkubwa wa pili baada ya Kilimo

    Sekta ya

    Madini nchiniyapiga hatua

    Sekta ya Madini imepatamafanikio makubwa katikakuchangia ukuaji wa uchu-mi nchini kwa kipindi chamiaka 10 iliyopita kuanzia

    mwaka 2004-2014.Hayo yamebainishwa na

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini

    anayeshughulikia Madini, Mhe. Ste-phen Masele wakati akifungua se-mina ya siku moja iliyowashirikishaWakuu wa Mikoa yote ya TanzaniaBara, baadhi ya Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri, We-nyeviti wa Halmashauri na Viongoziwa Dini, kwa lengo la kuelimishanakuhusu masuala muhimu yanayohu-u sekta ya madini ikiwa ni pamoja

    na kujadili namna bora ya utekelezjiwa Sheria ya madini ya mwaka2010 na kanuni zake.

    Mhe. Masele aliyataja baadhi yamfanikio hayo kuwa ni pamoja nakuongezeka kwa ukuaji wa uchumikatika sekta ya madini kutokaasilimia 2.1 kwa mwaka 1997 hadikufikia asilimia 7.8 mwaka 2012;kuongezeka kwa mchango wa sektaya madini kwenye pato la taifa ku-oka asilimia 1.2 mwaka 1997 hadi

    asilimia 3.5 mwaka 2012; kuongeze-ka kwa mauzo ya madini nje ya nchikutoka Dola za Marekani milioni26.66 mwaka 1997 hadi Dola bilioni2.3 mwaka 2012.

    Aidha, ameongeza kuwa, ajiraasmi kwenye migodi mikubwameongezeka kutoka chini ya wa-fanyakazi 1,700 mwaka 1997 hadiakribani wafanyakazi 13,500 mwa-

    ka 2012 na kuongezeka kwa mapatoya Serikali kutokana na uchimbajimkubwa wa madini kutoka shilingibilioni 2 mwaka 1997 hadi kufikiahilingi bilioni 605 mwaka 2012 na

    hivyo kuiwezesha sekta kuchangia

    zaidi ya asilimia 50 ya mapato yafedha za kigeni nchini.

    Vilevile, ameeleza kuwa,takwimu zinaonesha kuwa, sekta yamadini ni mwajiri mkubwa wa pilinchini baada ya sekta ya kilimo am-bapo zaidi ya watanzania 1.5milioni

    wanajishughulisha moja kwa mojana shughuli za uchimbaji madini

    wengi wao wakiwa ni wale waishiovijijini wakijumuisha wanawake nawanaume.

    Kutokana na mafanikio hayo,Masele amewataka viongozi haokutimiza wajibu wao kutokana nanafasi kubwa waliyonayo katikautekelezaji wa sera ya madini huku

    wakizingatia kulinda maslahi ya

    Taifa na ya wawekezaji. Aidha,Mhe. Masele amewataka viongozihao kutumia mamlaka waliyonayokuchochea uwekezaji, kulinda rasili-mali za madini, kudumisha hifadhi

    ya mazingira na kusimamia sheriazilizopo.

    Awali, Katibu Mkuu wa Nishatina Madini, Bw. Eliakim Maswi

    alieleza kwamba, lengo la Wizara naSerikali ni kuhakikisha inawatendeahaki Watanzania kwa kuhakikisha

    wanafaidika na rasilimali madini,hivyo, amehimiza uzalendo katikakutekeleza majukumu mbalimbalikupitia sekta hiyo.

    Pamoja na hayo, Maswiamehimiza ushirikiano kati ya

    watendaji hao na viongozi wa dinina kuongeza kuwa, watendaji waHalmashauri , Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Viongozi wa Dini ni

    wadau muhimu katika utekelezajiwa majukumu ya wizara.

    Wakati huo huo, Mkuu waMkoa wa Mbeya ambaye pia niMwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa,

    Mhe. Abbas Kondoro amewatakawatendaji hao kuhakikisha am-ani na utulivu vinatawala katikamaeneo hayo ili kuwezesha shughulimbalimbali zinazohusu sekta yamadini kufanyika katika mazingira

    ya utulivu kutokana na umuhimu wasekta ya madini na mchango wakekwa maendeleo ya taifa.

    Na Asteria Muhozya,Dar es Salaam

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (wa pili kutoka kushoto) akiwasili katikaukumbi wa mikutano Kilimanjaro Hotel (Hyatt) , kwa ajili ya kufungua rasmi mkutano wa kujadilinamna bora ya utekelezaji wa sheria ya madini ya mwaka 2010. Wa kwanza kushoto ni NaibuKatibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, Wa kwanza kulia ni Kamishnawa Madini Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja, na wa pili kutoka kulia ni Mkuuwa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Said Mwambungu.

  • 8/12/2019 MEM Bullettin 20

    7/8

    MEM News Bulletin | 7

    NISHATI

    MUHIMU KUZINGATIA

    UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII

    TUFANYE KAZI KWA UADILIFU, BIDII, WELEDI,NA USHIRIKIANO BILA KUKATA TAMAA

    DAIMA TUSONGE MBELEKURUDI NYUMA NI MWIKO!!

    Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

    Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishatina Madini MhandisiNgosi Mwihavaameeleza kuwa, nia ya

    serikali ni kuwafikia wadau wengiili waweze kushiriki kutoa maoniyatakayosaidia kuboresha Rasimuya Sera ya Petroli.

    Ameyasema hayo wakatialipokuwa akifungua warsha yawadau wa masuala ya gesi namafuta jijini Dar es Salaam kwaniaba ya Katibu Mkuu, EliakimMaswi iliyowahusisha wadau washughuli za uzalishaji na utafutajigesi na mafuta na kuongeza kuwa,adhma ya serikali ni kuhakikishainapata maoni mengi na borayatakayosaidia kuboresha sekta hiyoambayo inakua kwa kasi kutokanana ugunduzi wa kiasi kikubwa chagesi katika kina kirefu cha bahari .

    Aidha, Mwihava ame-wataka wadau wa sekta ya gesi naPetroli kuhakikisha wanatoa maoniambayo yatakuwa na mchangomkubwa katika ukuaji na maende-leo ya sekta hizo kwa lengo lakuhakikisha kwamba pande zotezinanufaika.

    Ameongeza kuwa kutokanana ukuaji wa sekta na ugunduzihuo, serikali imeona ni muhimukuwa na Sera mahsusi ambayoitatoa mwongozo wa namna yakusimamia sekta hiyo, hivyo,uwepo wa kanuni, taratibu nasheria zitasaidia kusimamia sektavizuri hali ambayo itatoa fursa kwawadau kushiriki kikamilifu ikiwa

    ni pamoja na kuhakikisha kwambarasilimali hiyo inakuwa na manufaakwa watanzania.

    Aidha, ameeleza kuwa, kuto-kana na shughuli za utafutaji nauzalishaji gesi kuhitaji utaalamuwa hali ya juu serikali itahakikishainashirikiana na wadau hao katika

    shughuli hizo ili kuwawezeshawataalam wa ndani kuwezakujifunza na kupata uzoefu washughuli hizo na hivyo kuiwezesha

    sekta hiyo kusimamiwa na wata-alam wa ndani.Wataalam wetu wa ndani

    wanatakiwa kupata uzoefu washughuli hizi ili waje kusimamiawenyewe badala ya kutegemeawataalamu wa nje. Lakini kutokanana ugeni wetu katika jambo hili,

    tunahitaji ushirikiano na wadauhawa. Ameongeza Mwihava.

    Katika hatua nyingine,Mwihava amezitaka Hamshauri

    ambazo zinanufaika na mapatoyanayotokana na rasilimali za gesikuhakikisha wanayatumia mapatohayo kwa shughuli za maendeleokatika maeneo yao.

    Kwa upande wake KamishnaMsaidizi wa Umeme, MhandisiInnocent Luoga , ameongeza kuwa,

    rasilimali za gesi na mafuta ni zawazawa hivyo, ni wazi kuwa watan-zania ndio watanufaika kwanza narasilimali hizo.

    Aidha, ameongeza kuwa, serahiyo inatarajia kugusa maeneomengi katika sekta husika ilikuweka mazingira bora ya shughulizinazohusiana na sekta hiyo ku-fanyika kwa ubora ikiwa ni pamojana nchi ya Tanzania kunufaika narasilimali hiyo.

    Tunataka maoni bora Sera ya Petroli - Mwihava

    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati)akifuatilia kwa karibu wadau wakitoa maoni wakati wa warsha ya wadauwanaoshughulika na shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta ili kupatamaoni yatakayosaidia kuboresha Rasimu ya Sera ya Petroli. Wa Kwanza kushotoni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Umeme Mhandisi InnocentLuoga, wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi Nishati, anayeshughulikia Petroli MhandisiStanley Marisa na wa kwanza kulia ni Mjiolojia Mwandamizi Wizara ya Nishati naMadini, Adam Zuberi.

  • 8/12/2019 MEM Bullettin 20

    8/8

    8 | MEM News Bulletin

    NISHATI/MADINI

    Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano SerikaliniWasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    Huduma za madini

    kusogezwa kwa wananchi

    Na Veronica Simba Dar es Salaam

    Jumla ya Ofisi tano zamadini zinatarajiwakufunguliwa hivikaribuni katika sehemumbalimbali nchini

    hususan ambazo hazikuwana ofisi husika ili kuboresha

    huduma kwa wadau wa sektaya madini na wananchi kwaujumla.

    Hayo yamebainishwa naKamishna wa Madini nchiniMhandisi Paul Masanja marabaada ya kushuhudia utiajisaini makubaliano maalumuya mauziano ya majengoyatakayotumika kwa Ofisi hizouliofanyika wiki hii, MakaoMakuu ya Wizara ya Nishati naMadini, jijini Dar es Salaam.

    Akizungumzia madhumuniya kufungua Ofisi hizo,Kamishna Masanja amesema

    ni kuwaondolea adha wananchiwenye kuhitaji hudumambalimbali za madini kwakuwapelekea huduma hizokaribu.

    Madhumuni yetu nikuboresha huduma zetukuwa za kiwango cha juu namojawapo ya mikakati yetu nikupeleka huduma hizo kwa

    wananchi ili kuwapunguziaadha ya kusafiri umbali mrefukufuata huduma husika,amesema Mhandisi Masanja.

    Amesisitiza kuwa wadauna wananchi wenye kuhitajihuduma yoyote inayohusianana madini wafike kwenyeofisi hizo katika maeneoyao na watahudumiwa kadriinavyotakiwa.

    Maeneo ambayo ofisimpya za madini zinatarajiwakufunguliwa ni Njombe, Bariadi,Songea, Nachingwea na

    Kigoma.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishatina Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wakwanza kulia) akitiliana saini na Bw. FidelisLumato, mmiliki wa jengo litakalokuwa ofisiya madini mjini Njombe. Wanaoshuhudiani Kamishna wa Madini nchini MhandisiPaul Masanja (wa kwanza kushoto) naMwanasheria wa Wizara Bw. DamianRenatus.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishatina Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia),akibadilishana hati ya mauziano ya jengo

    na Bw. Mohamedbashir Hasham, ambaye nimmiliki wa jengo litakalotumika kama ofisiya madini katika wilaya ya Nachingwea.