mamlaka ya kilimo na chakula kitengo cha ... - tea …
TRANSCRIPT
MAMLAKA YA KILIMO NA CHAKULA
KITENGO CHA CHAI
MKATABA WA HUDUMA
YALIYOMO
Utangulizi...................................................................................... 3
Wajibu ......................................................................................... 3
Maono ......................................................................................... 3
Lengo .......................................................................................... 3
Maadili Makuu .............................................................................. 3
Majukumu Makuu ......................................................................... 4
Wateja/Wadau/Washirika ............................................................... 5
Haki za Wateja/Wadau .................................................................. 5
Majukumu Ya Wateja/Washika Dau ................................................ 6
Wajibu na Majukumu Yetu ............................................................. 6
Maadili ya Kitaifa na Misingi ya Usimamizi ....................................... 6
Suluhu ya Malalamishi ................................................................... 7
Tathmini ya Mkataba wa Huduma ................................................... 7
Uchunguzi wa Utenda Kazi ............................................................. 7
Utoaji Maoni ................................................................................ 8
Huduma zinazotolewa na vikezo vya huduma ................................. 9
Vituo vya huduma na Anwani ........................................................12
1
2
Dibaji
Kitengo cha Chai chini ya Mamlaka ya Kilimo Na Chakula kina mamlaka na
jukumu la kusimamia, kustawisha na kuendeleza kilimo cha mmea wa chai.
Kupitia sheria ya AFA (Sheria Nambari 13 Ya 2013), Sheria Ya Mimea (Sheria
Nambari 16 Ya 2013) na sheria muhimi nyinginezo, pia kupitia ushirikiano na
mashirika mengine ya serikali na ya kibinafsi, Kitengo cha Chai kinaendelea
kusimamia sekta ya Chai kikizingatia lengo, maono, maadili makuu na vikezo
vilivyowekwa kuhakikisha utoaji wa huduma bora.
Dhamira yetu imara ya kutoa huduma bora inaambatana na kuzingatia sheria, uadilifu, uwajibikaji, taaluma, ushirikiano na ufanisi. Pia tunaongozwa na kumthamini mteja, nidhamu na kujitolea kutoa huduma bora kwa mteja, kuzingatia usawa tunapotoa maamuzi, uvumbuzi na ubunifu, utunzaji bora wa mazingira na kushirikisha umma. Lengo letu kuu ni kuendeleza utoaji huduma unaozingatia heshima ya kiutu kupitia usawa, haki za kijamii, kushirikisha wengine, usawa, haki za binadamu, kutobagua na kuwalinda wanyonge.
Mkataba huu wa huduma ni dhamira ya Kitengo Cha Chai chini ya Mamlaka ya
Kilimo na Chakula kutoa huduma ya hali ya juu kwa wateja wetu, washirika
na umma kwa jumla. Tunatazamia maoni yenu ili kutuwezesha kuendelea
kuboresha huduma zetu.
Msimamizi, Kitengo Cha Chai
3
1. Utangulizi
Kitengo Cha Chai chini ya Mamlaka Ya Kilimo Na Chakula kilibuniwa kupitia
Sheria Ya AFA (Sheria Nambari 13 Ya 2013) kutekeleza Sheria Ya Mimea
(Sheria Nambari 16 Ya 2013). Kitengo hiki kina majukumu ya usimamizi,
ustawishaji na ukuzaji wa sekta ya chai nchini Kenya.
Madhumuni ya mkataba huu wa huduma ni kujulisha na kutoa utaratibu wa
kupokea maoni ya wadau wetu kuhusu jukumu letu kwa sekta ya chai, wajibu
wetu, maono yetu, lengo, maadili na majukumu makuu. Kitengo cha Chai
kinakusudia uboreshaji wa utenda kazi kwa wadau wetu. Dhamira ya
Kitengo Cha Chai kutekeleza yote yaliyotajwa inapatikana kwa mkataba
huu wa huduma.
Mkatabu huu vile vile umewianishwa na Katiba ya Kenya, Sheria Ya
AFA (Sheria Nambari 13 Ya 2013), Sheria Ya Mimea (Sheria Nambari 16 Ya
2013) na Ruwaza Ya 2030.
2. Wajibu
Wajibu wa Kitengo Cha Chai ni kudhibiti, kustawisha na kukuza sekta ya chai
nchini Kenya.
3. Maono
Kuwa mthibiti wa kimataifa kwenye sekta ya kilimo
4. Lengo
Kuendeleza na kukuza viwango vya uzalishaji wa majani chai kisheria kupitia
uthibiti kamilifu ili kukuza uchumi
5. Maadili Makuu
1. Utaalamu
2. Uadilifu
3. Kumthamini mteja
4. Kufanya kazi pamoja
5. Ubunifu
4
6. Majukumu Makuu
Kuwezesha utayarishaji wa sera na kanuni mwafaka kwa
madhumuni ya kustawisha sekta ya chai (ikiwemo usajili/utoaji
leseni kwa wahudumu katika sekta ya chai: Wakulima/Wakuzaji;
Viwanda vya usagaji wa chai; Wapakiaji wa chai; Wauzaji wa chai
katika nchi za nje/Waagizaji wa chai kutoka nchi za nje; Madalali;
Maajenti wa Usimamizi; Maghala/Mabohari; Mwandalizi wa
Minada);
Kuwezesha uuzaji na usambazaji wa chai kwa kuangazia habari za
soko, pamoja na kutambua hali ya soko ikiwemo upatikanaji wa chai
na mahitaji ya soko, kuangazia soko la humu nchini na kuendeleza
ujasusi wa masoko ya nchi za nje na uendelezaji wa ratiba za uuzaji;
Kuendeleza ushirikiano na idara za utafiti za serikali na za kibinafsi,
ikiwemo Shirika La Utafiti wa Kilimo na Mifugo La Kenya (KALRO),
hasa Taasisi Ya Utafiti Wa Chai (TRI) ili kufanya utafiti unaolenga
kustawisha ukuzaji, uuzaji na utengenezaji wa chai
Kuuendeleza ufundishaji wa wakulima kwa ushirikiano na taasisi za
mafunzo kwa minajili ya kuongeza ujuzi wao kuhusu teknoljia za
ukuzaji wa chai na utafutaji wa soko;
Kuanzisha na kuhakikisha viwango vya ubora, sampuli na ukaguzi,
vipimo na uchambuzi, vipimo, vitengo vya kupima, mwongozo
wa maadili na upakiaji, utunzaji, uhifadhi na usafirishaji wa chai ili
kuhakikisha afya njema na biashara bora;
Kukuza na kushauri kuhusu mbinu za kuongeza thamanai kwa
bidhaa za chai kabla ya kusafirishwa kwa masoko ya nje.
5
7. Wateja wetu/Wadau/Washirika
Kitengo Cha Chai kinahudumia:
Wakulima/wakuzaji chai.
Viwanda vya usagaji wa chai
Wauzaji wa chai kwa masoko ya nje/Wanunuzi wa chai kutoka nchi za
nje
Madalali
Wapakiaji wa chai
Maghala/Mabohari
Maajenti wa usimamizi
Mabaraza ya Chai na Mashirika yanayohusika na biashara ya chai
Wizara na Idara za Serikali
Serikali Za Kaunti
Mashirika Ya Kiserikali
Taasisi za utafiti
Mashirika ya kiraia na vyama vya wafanyikazi
Watoaji huduma na vifaa
Washirika wa kimaendeleo
Wanahabari na taasisi za habari za humu nchini na kimataifa
Watumiaji wa bidhaa za chai
Umma
8. Haki Za Wateja/Wadau
Wateja wetu wana haki zifuatazo:
a) Kuhudumiwa kwa heshima
b) Kupokea majibu kwa muda ufaao
c) Usiri na faragha
d) Kupokea habari
e) Huduma na bidhaa bora
f) Mazingira mwafaka
g) Mawasiliano kamilifu
6
9. Wajibu wa wateja/wadau
Ili kutuwezesha kuwahudumia vyema na kudumisha ushirikiano, wateja wetu
wanatakiwa kutimiza yafuatayo:
a) Kuonyesha heshima na adabu;
b) Kutoa taarifa kamilifu;
c) Kutoa maoni kuhusu huduma zetu;
d) Kuzingatia sheria, taratibu na sera zilizopo;
e) Kuzingatia uadilifu;
f) Kukubali mbinu za kisasa na bunifu katika sekta ya
chai.
10. Wajibu na majukumu yetu
Kitengo Cha Chai kimejitolea kutimiza yafuatayo:
Kuendelea kuboresha mara kwa mara ujuzi, maarifa, uzoefu na
tajriba kwa wafanyikazi wetu ili kuhakikisha utoaji wa huduma
bora;
Utoaji wa huduma bora kwa wakati ufaao kwa wateja wetu;
Kutosheleza mahitaji ya wateja;
Kutojihusisha kamwe na ufisadi;
Kufuata mwongozo wa sheria;
Kuweka siri habari za mteja na nyinginezo za kibinafsi;
Kusuluhisha mizozo bila mapendeleo;
Kufanya uamuzi bila kuegemea upande.
11. Maadili Ya Kitaifa Na Misingi Ya Uongozi
Kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha Katiba Ya Kenya 2010, tunazingatia
maadili ya kitaifa na misingi ya uongozi ambayo inajumuisha mashirika ya
umma, maafisa wa kitaifa, wafanyikazi wa umma na watu wote. Maadili Ya
Kitaifa Na Misingi Ya Uongozi tunayozingatia ni:
(a) Uzalendo, umoja wa kitaifa, kugawana na ugatuzi wa utawala,
uzingatiaji wa sheria, demokrasia na kushiriki kwa umma;
7
(b) Hadhi ya kiutu, haki za kijamii, ushirikishaji, usawa, haki za
kibinadamu, kutobaguliwa na ulinzi kwa wadhaifu;
(c) Uongozi bora, uadilifu, uwazi na uwajibikaji
(d) maendeleo dhabiti
Iwapo maadili na misingi hii itakiukwa wakati wa utoaji huduma, waweza
kuwasilisha malalamiko kupitia kwa taratibu ambazo zimewekwa.
12. Suluhu ya malalamishi
Hakikisho la kuweka siri mlalamishi na malalamishi yake ni lazima ili
kulinda haki za wateja/wadau na pia watoaji wa huduma. Hata hivyo,
walalamishi wanahimizwa kujitambulisha ili kurahisisha majibu na pia
ufuatiliaji wa lalama zao. Kitengo Cha Chai kitatoa ithibati ya kupokea lalama
katika muda wa siku saba, na kisha kutathmini na kuyashughulikia
malalamishi hayo kwa mujibu wa sheria.
13. Tathmini ya Mkataba wa Huduma
Ili kuendelea kuwaridhisha zaidi wadau wetu, mkataba huu wa huduma
utakuwa ukifanyiwa tathmini kila mwaka. Tathmini hii itazingatia
mapendekezo na maoni ya wateja na maswala chipuka.
14. Uchunguzi wa utenda kazi
Kitengo Cha Chai kitahakikisha kuwa ahadi za mkataba huu zinatekelezwa
kikamilifu kupitia utafiti wa mara kwa mara kutathmini kuridhishwa kwa
wateja. Pia, kutakuwa na tathmini za kuchunguza utenda kazi na kuwasilisha
ripoti za mara kwa mara na machapisho.
8
15. Kutoa maoni
Kwa maswali zaidi, pongezi au malalamishi, tafadhali wasiliana na afisi
ifuatayo:
Mamlaka Ya Kilimo Na Chakula – Kitengo Cha Chai (Tea
Directorate)
Tea House, Naivasha Rd, off Ngong Rd
S.L.P 20064—00200
City Square, NAIROBI
Rununu: 254-722-200556/734-600994
Simu: 254-20-2536869/2536886
Tovuti: www.teaboard.or.ke; www.agricultureauthority.go.ke
Barua pepe: [email protected];
au
Tume Ya Haki Za KiutawalandWest End Towers, 2 Floor, Waiyaki Way Westlands
S.L.P 20414 – 00200 Nairobi. Simul: +254 020 2270000
Ba rua pepe : c e r t i f c a t i o n p c @ o m b u d s m a n . g o . ke Tovu t i :
www.ombudsman.go.ke
Waweza pia kuwasilisha maoni yako kupitia visanduku vya maoni/ulalamishi
vinavyopatikana katika maofisi yetu au uwasilishe kupitia kwa tovuti yetu ua
kwa kujaza vijikarasati/kitabu cha kuweka kumbukumbu katika vituo vyetu
vya huduma.
9
HUDUMA MAHITAJI/MASHARTI MALIPO/ADA MUDA
Maswali yaliyoandikwa Maswali yaliyoandikwa Bila malipo Siku saba za kazi
tangia kuwasilishwa
Maswali kupitia simu Maswali kuwasilishwa na
mteja kupitia simu
Bila malipo Muda usiozidi masaa
24 tangia kuwasilishwa
Maswali kupitia
barua pepe
Maswali kuwasilishwa na
mteja kupitia barua pepe
Bila malipo Muda usiozidi masaa
12 tangia kuwasilishwa
Malalamishi ya umma Lalamiko/malalamiko
kuwasilishwa na mteja
Bila malipo Muda usiozidi siku
saba za kazi tangia
kuwasilishwa
Maswali kutoka
vyombo vya habari
Swali/Maswali kuwasilishwa
na vyombo vya habari
Bila malipo Muda usiozidi siku
mbili za kazi tangia
kuwasilishwa
Malipo ya bidhaa au
huduma
Kuwasilishwa kwa bidhaa au
huduma inayoridhisha vigezo
vilivyowekwa pamoja na
ankra (invoice) asilia
Bila malipo Muda usiozidi siku 30 za
kazi tangia kuwasilishwa
kwa bidhaa au huduma
zinazotimiza vigezo
vilivyowekwa pamoja na
ankra (invoice) asilia
Utoaji mafunzo na
usaidizi wa kiufundi
kwa makaunti na wadau
‐ Ombi kutoka kwa mteja
‐ Ukadiriaji wa mahitaji ya mafunzo
Bila malipo Wakati mafunzo/usaidizi
wa kiufundi
unapohitajika
Usambazaji wa habari kuhusu uuzaji/masoko
Ombi kutoka kwa mteja Bila malipo Habari zinapohitajika
Kutathmini
shughuli/mipangilio ya
maswala ya uuzaji
kuhusu masoko ya humu
nchini na ya kimataifa
Ombi kutoka kwa mteja Bila malipo Mawasiliano/maongezina
wadau miezi miwili kabla
ya mwaka wa fedha
kukamilika/Mipangilio
kukamilika katika robo ya
kwanza ya mwaka wa
fedha
16. HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA VIGEZO VYA UTOAJI HUDUMA
HUDUMA MAHITAJI/MASHARTI MALIPO/ADA MUDA
Usimamizi wa taratibu za
kushiriki kwa wadau
katika utafutaji wa masoko
Usambazaji wa habari kuhusu usalishaji na biashara
Habari sahihi na iliyothibithishwa Bila malipo Tarehe/Siku ya 26 kila mwezi/Habari za kila mwakaa
Ukaguzi Ushirikiano Bila malipo Hakuna kujulishwa kwa ukaguzi wa ghafla/ Kujulishwa majuma mawili kabla ya ukaguzi ulioratibiwa/Kurudia ukaguzi kulingana na ratiba ya marekebisho
Malipo kwa watoaji
huduma/bidhaa
Ankra (invoices) asilia, stakabadhi za kuwasilisha bidhaa/huduma zilizotiwasahihi, Mkataba uliotiwa sahihi/LPO/LSO
Bila malipo Hundi ya malipo kwa
muda usiozidi siku 14
Usajili wa wakulima “Fomu A/A1” iliyojazwa kikamilifu na kurudishwa kwenye kiwanda cha kukabidhi majani chai
Uamuzi kwa muda usiozidi mwezi mmoja
Usajili wa Maajenti wa Usimamizi
“Fomu S” iliyojazwa kikamilifu kwa
kuzingatia mahitaji yaliyomo
‐ Usajali wa kwanza: 50,000/=‐ Usajili wa kila mwaka: 25,000/=
Mawasiliano ya kuthibitisha upokeaji wa ombi katika muda usiozidi juma moja; Uamuzi wa mwisho katika muda usiozidi miezi 3
Wafanyi biashara wa chai
waliosajiliwa
Bila malipo Mawasiliano kuhusu safari za kibiashara kufanywa miezi miwili kabla tarehe ya safari/Usambasaji wa habari kila robo mwaka juu ya matokeo ya safari zaKibiashara
10
Bila malipo
(a) Leseni ya kiwanda cha kawaida cha majani chai
“Fomu C” iliyojazwa kikamilifu
kwa kuzingatia mahitaji yaliyomo
‐ Leseni ya mara ya kwanza: 10,000/=‐ Leseni ya kila mwaka: 7,500/= Mawasiliano ya kuthibitisha
upokeaji wa ombi katika muda usiozidi juma moja; Uamuzi wa mwisho katika muda usiozidi miezi 3
b) Leseni ya kiwanda kidogo cha majani chaii
‐ Leseni ya mara ya kwanza: 5,000/=‐ Leseni ya kila mwaka: 3,000/=
HUDUMA MAHITAJI/MASHARTI MALIPO/ADA MUDA
11
Usajili wa madalali
Usajili wa wapakaji chai “Fomu M” iliyojazwa kikamilifu
kwa kuzingatia mahitaji yaliyomo
Usajili wa mabohari “Form K” iliyojazwa kikamilifu kwa kuzingatia mahitaji yaliyomo
Usajili wa msimamizi
wa Udalali
“Fomu X” iliyojazwa kikamilifu kwa kuzingatia mahitaji yaliyomo
‐ R Usajali wa kwanza:: 10,000/=‐ Usajili wa kila mwaka l: 10,000/=
Mawasiliano ya kuthibitisha upokeaji wa ombi katika muda usiozidi juma moja; Uamuzi wa mwisho katika muda usiozidi miezi 3
Usajili na uhakiki wa majani chai ya kuuzwakwa masoko ya nje
“Fomu V” iliyojazwa kikamilifu
kwa kuzingatia mahitaji yaliyomo
Katika muda usiozidi siku moja (1)
Usajili na uhakiki wa
majani chai ya kuagizwa
kutoka masoko ya nje
“Fomu W” iliyojazwa kikamilifu
kwa kuzingatia mahitaji yaliyomo
“Fomu I” iliyojazwa kikamilifu
kwa kuzingatia mahitaji yaliyomoMawasiliano ya kuthibitisha upokeaji wa ombi katika muda usiozidi juma moja; Uamuzi wa mwisho katika muda usiozidi miezi 3
‐ Usajali wa kwanza: 20,000/=‐ Usajili wa kila mwaka: 10,000/=
‐ Usajali wa kwanza: 5,000/=‐ Usajili wa kila mwaka: 2,000/=
Mawasiliano ya kuthibitisha upokeaji wa ombi katika muda usiozidi juma moja; Uamuzi wa mwisho katika muda usiozidi miezi 3
‐ Usajali wa kwanza: 20,000/=‐ Usajili wa kila mwaka: 10,000/=
Mawasiliano ya kuthibitisha upokeaji wa ombi katika muda usiozidi juma moja; Uamuzi wa mwisho katika muda usiozidi miezi 3
Bila malipo
Katika muda usiozidi siku tatu (3)
Bila malipo
Usajili wa wanunuzi wa
chai (Wanaouza kwa
masoko ya
nje/Wanaoagiza chai
kutoka masoko ya nje)
“Fomu G” iliyojazwa kikamilifu
kwa kuzingatia mahitaji yaliyomo
Mawasiliano ya
kuthibitisha upokeaji wa
ombi katika muda usiozidi
juma moja; Uamuzi wa
mwisho katika muda
usiozidi miezi 3
‐ Usajali wa kwanza: 20,000/=‐ Usajili wa kila mwaka: 10,000/=
17. VITUO VINAVYOTUMIWA NA KITENGO CHA CHAI (TEA DIRECTORATE) KUTOA HUDUMA NA ANWANI ZA VITUO HIVYO
Pongezi, malamishi na maoni ya kutuwezesha kuboresha huduma zetu yanaweza kuwasilishwa kwa Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Chai kupitia anwani zifuatazo:-
Ofisi Ya MombasaTea House, Ngonyo Rd, Off Moi AvenueS.L.P 90346 - 80100, MOMBASASimu: +254-41-2314668/2313089
Barua Pepe: [email protected]; [email protected]
Tovuti: www.agricultureauthority.go.ke
Ofisi Ya Eneo La Magharibi mwa Bonde La Ufa (West of Rift)stNdege Chai House, 1 Floor, Kericho-Nakuru Highway
S.L.P 1615-20200, KERICHOSimu: +254-52-30056; +254-202440652
Barua Pepe: [email protected]; [email protected]
Tovuti: www.agricultureauthority.go.ke
Ofisi Ya Eneo La Mashariki mwa Bonde La Ufa (East of Rift)rdCylet Plaza, Kubukubu Rd, 3 Floor, Rm4
S.L.P 2745, EMBUSimu: +254-202440652
Barua Pepe: [email protected]; [email protected]
Tovuti: www.agricultureauthority.go.ke
12
Mamlaka Ya Kilimo Na Chakula – Kitengo Cha
Chai (Tea Directorate)
Tea House, Naivasha Rd, off Ngong Rd
S.L.P 20064—00200
City Square, NAIROBI
Rununu: 254-722-200556/734-600994
Simu: 254-20-2536869/2536886
Tovuti: www.teaboard.or.ke;
www.agricultureauthority.go.ke
Barua pepe: [email protected];
au
Tume Ya Haki Za KiutawalandWest End Towers, 2 Floor, Waiyaki Way Westlands
S.L.P 20414 – 00200 Nairobi. Simul: +254 020 2270000
Barua pepe: [email protected] Tovuti:
www.ombudsman.go.ke