maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai · kilimo endelevu tanzania (sat) na...
TRANSCRIPT
Maelezo ya msingi kuhusu Mboji/Mbolea
Vunde/Mbolea Hai
Utayarishaji na matumizi
Mwandishi: Janet Maro
Wachoraji: Godwin Chipenya na Emmanuel Grieshaber
Toleo la kwanza
Mei 2011
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 2
Yaliyomo
1. Namna ya kutayarisha Mboji/Mbolea Vunde/Mbolea Hai....................................................... 3
1.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa kwenye mboji ................................................................................ 3
1.2 Mfano wa vitu ambavyo vyaweza kutumiwa kutengeneza mboji ....................................... 5
2. Namna ya kutengeneza mboji ya mimea .................................................................................. 6
2.1 Hatua ............................................................................................................................................ 6
2.2 Zingatia ........................................................................................................................................ 7
3. Wadudu wenye manufaa na mazingira yanayohitajika kwenye Biwi.................................... 8
3.1 Wadudu ambao husaidia kufanya biwi kuoza ....................................................................... 8
3.2 Mazingira yanayohitajika kwenye biwi .................................................................................... 9
4. Matunzo ya Biwi .......................................................................................................................... 10
4.1 Maji ............................................................................................................................................. 10
4.2 Kupindua/kugeuza ................................................................................................................... 11
5. Muda wa kukomaa na matumizi ya mboji ............................................................................... 13
5.1 Muda wa kukomaa ................................................................................................................... 13
5.2 Matumizi ya mboji .................................................................................................................... 13
6. Faida za Mboji/Mbolea Vunde .................................................................................................. 14
Vitabu vya Kurejelea ............................................................................................................................. 16
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 3
1. Namna ya kutayarisha Mboji/Mbolea Vunde/Mbolea Hai
Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku)) ambayo
imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama
majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa huku
ni tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya
hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri.
Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye
udongo ili kuinua mazao ya shamba.
Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani
bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda
mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini kama muda ukitengwa ili
kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni
yanatumika katika kutengenezea mboji.
Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji
huchemka hata kiasi cha kuua magonjwa ya mimea na mbegu za magugu.
Majani makavu ya ndizi ni mazuri kwa kutunza vifaa vya mbolea na kuweka ukavu. Hali hii
huwa huzuia kupotea kwa maji kabla ya kujenga lundo la mboji na wakati mbolea inapokuwa
inaiva.
1.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa kwenye mboji
Sehemu za mimea ambazo zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua wadudu (viuatilifu) na
kwekwe juzijuzi (Pesticide/herbicides).
Vipande vya nyama kwa sababu vinavutia panya na wadudu wengine.
Sehemu nyingi za Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku))
ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu
kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa
huku ni tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya
hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 4
Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye
udongo ili kuinua mazao ya shamba.
Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani
bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda
mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini kama muda ukitengwa ili
kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni
yanatumika katika kutengenezea mboji.
Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani.
Mboji huchemka hata kiasi mimea na majani ambazo ziliambukizwa ugonjwa.
Vifaa vilivyo na ncha kali kama mwiba ambavyo vyaweza kujeruhi mikono na miguu.
Magugu ambayo yanarudiarudia kila mwaka. Magugu kama hayo huuliwa kwa kuanikwa
kwenye jua kali ili yakauke baadaye huchomwa ili yasienee na jivu lake laweza
kuongezwa kwenye lundo la mbolea.
Vitu visivyo kua na uhai kama plastiki na chuma.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 5
1.2 Mfano wa vitu ambavyo vyaweza kutumiwa kutengeneza mboji
VIFAA MAANDALIZI MUHIMU KUFAHAMU TAHADHARI
Nyumbani
Maganda ya
matunda
Huoza haraka
Jivu la kuni Kuna madini ya Potassium
(K) na chokaa (Lime)
Tumia kiwango
kidogo
Takataka za
kufagia
Viwango na ubora tofauti
Shambani
Mabaki ya mimea
baada ya kuvuna
Katakata vitu
vigumu. Kama ni
vikavu nyunyuzia
maji
Vitu vigumu huoza
pole pole
Usitumie vile
vilivyowekwa
dawa juzijuzi
Majani makavu/
yaliokauka
Kama ni makavu
fanya kama hapo juu
Mimea/majani ya
kijani au mabichi
Katakata kama ni
kubwa
Jamii ya kunde
hupendekezwa
Magugu Katakata kama ni
kubwa
Usitumie mizizi
ya magugu ama
mbegu za magugu
Asili
Samadi Ina rotuba nzuri sana
Mkojo Vigumu kukusanya
hupatikana kwenye
zizi la ng’ombe
Nyunyuzia kwenye
biwi/lundo la mbolea.
Hufanya mbolea kuoza
haraka
Tumia viwango
vidogo
Udongo Tumia udongo
kama sentimita 10
kutoka tabaka la juu
ya shamba
Hutumika kufunika
Biwi/lundo la mbolea
Magugu ya
baharini (Mwani)
Yafaa yakaushwe na
hutumiwa na majani
yaliyo kauka
yana madini muhimu
kwa wingi
Samadi kutoka kwa mifugo na mabaki ya mimea ni nzuri sana katika kutengeneza mbolea hai.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 6
2. Namna ya kutengeneza mboji ya mimea
Kusanya vitu na vifaa vinavyohitajika katika utengenezaji wa mboji ambayo ni;
Majani mengi mabichi/kijani na makavu. Majani jamii ya mikunde ni mazuri sana kwani
hutengeneza kirutubishi cha naitrojeni (N) kwa wingi.
Mabua ya mahindi au vitawi vya miti
Udongo wa kawaida wa juu
Samadi, mbolea yoyote ya wanyama au mboji ya zamani
Majivu au vumbi la mkaa
Maji
2.1 Hatua
1) Chagua sehemu karibu na eneo ambalo mboji itaenda kutumika na ambapo kuna hifadhi ya
kutosha kukinga dhidi ya upepo, jua na mvua.
2) Katakata majani yawe madogo madogo ili yaweze kuoza haraka. Tengeneza msingi kama mita
sita (6) urefu na upana wake mita 2 kwa kutumia majani magumu kama matawi/vijiti. Hii
itahakikisha maji yanatiririka na hewa ina zunguka vizuri. Hakikisha kuna nafasi ya kutosha
kufanyia kazi kwenye biwi bila kulikanyaga.
3) Weka sentimita 10 ya majani ambayo hayaozi haraka kwa mfano mabua vya mahindi au
mimea mibichi/kijani.
4) Weka sentimita 10 ya vifaa ambavyo huoza haraka kwa mfano maganda ya mboga na
matunda.
5) Weka sentimita 2 ya samadi (mbolea-hai ya wanyama), mabaki ya mbolea ya zamani kama
yaweza kupatikana.
6) Weka udongo wa juu sentimita 10 kutoka kwenye shamba ambalo hulimwa.
7) Majivu na mkojo vyaweza kunyunyuziwa juu ili kufanya biwi/lundo kuoza haraka.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 7
Kukatakata majani
8) Nyunyizia maji kwenye biwi mpaka lilowe.
9) Rudia mpangilio huu kuanzia namba nne (4) mpaka lundo lifike mita moja (1.m) hadi moja na
nusu (1.5m) kwenda juu isipokuwa vijiti/matawi ya kwanza.
2.2 Zingatia
Biwi/lundo cha mboji kinatakiwa kifunukwe ili kupunguza/kuzuia mvuke ama mvua
nyingi ambayo hubeba rotuba kutoka kwenye mbolea. Weka gunia, nyasi ama matawi ya
ndizi yaliyokauka.
Kila tabaka/kunjo/safu yafaa kupangwa kuanzia kwenye ukingo ili lundo la mbolea
lisiporomoke.
Namna nyigine ya kuzuia lundo kuporomoka ni kwa kuweka vipande vya mbao kando ya
biwi. Wavu wa nyuzi za chuma utafanya biwi kukauka.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 8
Katika sehemu zenye ukavu mwingi. Mianzi iliyo na mashimo husaidia kufanya hewa
kuingia na kuzunguka kwa urahisi.
3. Wadudu wenye manufaa na mazingira yanayohitajika kwenye Biwi
3.1 Wadudu ambao husaidia kufanya biwi kuoza
Viumbe wengi wanaohusika na kazi hii ya kuoza ni wadogo hawaonekani kwa macho
matupu. Ila viumbe hawa huhitaji maji, hewa na vipande/sehemu ya viumbe wengine ambazo
kwao ni chakula. Viumbe hawa hula vipande hivyo na hutoa hewa ya carbon dioxide, maji na
joto.
Kuna hatua tatu kubwa wakati biwi linapooza; hatua ya kupanda joto, hatua ya kupoa/kuwa
baridi na hatua ya kukomaa.
Wakati ya hatua ya kupanda joto, joto hufikia kiwango cha juu sana katikati mwa biwi.
Uzuri wa joto hili ni kwamba magonjwa yaliyokuwa kwenye viungo vya biwi na mbegu za
magugu huchomwa hadi kufa.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 9
Hatua ya pili ya kuwa baridi; uyoga (fungi) huwa na faida nyingi kwa sababu kazi yake ni
kuzisaga nyuzi ngumu ambazo zimo kwenye viungo vya mimea au majani.
Kwenye hatua ya tatu, ‘hatua ya kukomaa’ viumbe wakubwa kama mchwa na
nyungunyungu husaidia kusaga na kuchanganya mbolea.
Hali ya anga ikiwa na joto jingi viumbe hawa hufanya kazi haraka kuliko wakati ambapo hali
ya anga ni baridi. Aina ya viungo vilivyotumika kujenga/kukuza biwi na ukali/uchungu (pH)
wa udongo pia huathiri kiwango cha mbolea kuoza.
3.2 Mazingira yanayohitajika kwenye biwi
Biwi huhitaji vitu vitatu: hewa, maji na joto.
Hewa
Viumbe wadogo kwenye biwi huhitaji hewa ili waweze kuishi. Hewa ya carbon dioxide
(CO2) ambayo imetolewa na wadudu hawa huhitaji kutolewa nje. Ikiwa hewa safi
itakosekana, viumbe wengine wasiohitajika huingia na kutoa harufu mbaya na pia kufanya
mbolea isioze haraka.
Maji
Kazi ya viumbe wadogo huwa polepole ikiwa biwi ni kavu. Aidha ikiwa biwi litalowa maji
basi viumbe wadogo watakufa na kufanya biwi kuwa na uchachu badala ya kutengeneza
mbolea. Hivyo basi kukagua kiwango halisi cha maji huhitaji ujuzi fulani.
Joto
Biwi hutoa joto wakati linaoza. Lundo likiwa na joto jingi viumbe wadogo hutoka, kisha
huweza kurudi pindi linapopoa.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 10
4. Matunzo ya Biwi
Ili kupata mbolea nzuri, biwi linapojengwa yafaa lishughulikiwe kwa utaratibu. Biwi hilo
litahitaji maji, kupinduliwa, joto na muda unaofaa wa kukomaa.
4.1 Maji
Wakati wa kiangazi biwi/lundo la mboji huhitaji kumwagiliwa maji kila wiki. Maji katika
lundo la mbolea hupimwa kwa kuweka fungu dogo la nyasi na kulitoa baada ya dakika tano.
Nyasi isipoonyesha majimaji au unyevu itabidi maji yamwagwe kwenye lundo hilo.
Kuna njia kadha za kuzuia mvuke kuinuka kutoka kwenye biwi, hali kadhalika kiwango cha
maji yanayomwagiliwa:
Funika lundo kwa majani ya ndizi ama nyasi.
Funika lundo kwa udongo.
Lundo lisigeuzwegeuzwe
Biwi likilowa maji itabidi kifunuliwe na kuachwa kikauke kwenye jua kabla ya kujengwa
tena.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 11
4.2 Kupindua/kugeuza
Katika muda wa wiki tatu (3) baada ya kujenga/kukuza biwi/lundo ukubwa wake utakuwa
umepungua sana. Kupindua biwi uhakikishe ya kwamba majani yaliyo kando yameoza pia
hewa safi imerejeshwa. Kupindua biwi huchanganya majani yaliyotengenezwa na kukijenga
upya. Majani yalivyo kando huwekwa katikati, ikiwa kuna ukavu, maji mengi na
majani/viungo vikavu huongezwa. Kupindua kunatikiwa kufanyike kila baada ya wiki tatu.
Hali ya joto na kiwango cha maji yafaa kupimwa siku chache baada ya kupinduliwa.
Kupinduliwa kwa mara ya tatu kutahitajika ikiwa viungo havitakuwa vimeoza kikamilifu.
Muda wa kugeuza mboji baada ya kuitengeneza
Mbolea yaweza kutengenezwa bila kupinduliwa ila viungo vilivyo kando havitaoza. Mbegu
za magugu na viungo na magonjwa ya mimea hayatakufa. Viungo vilivyobaki hutengwa na
kutumiwa kwenye biwi lingine. Japokuwa kugeuza hakuna lazima, kunapendekezwa ili
kupata mbolea nzuri.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 12
4.3 Kiwango cha Joto
Kupima kiwango cha joto kwenye biwi kunahitaji kijiti kirefu kichomwe ndani ya lundo siku
kumi (10) baada ya kujengwa. Kijiti yafaa kionyeshe joto la kutosha kinapoguswa kwa
mkono, la sivyo kuoza bado hakujaanza kufanyika. Katika hali kama hii, maji ama hewa
itahitajika kwenye biwi na biwi kuachwa kwa muda. Ikiwa biwi lina joto jingi, biwi linaoza
basi viumbe hai wanaweza kufa. Katika hali hii, hewa na maji itabidi kuongezwa ili kufanya
biwi lipoe. Kiasi cha joto yafaa kupimwa mara kwa mara kwa kutumia kijiti.
Joto linalotakiwa ili mboji iweze kuiva
Chini ya 57C
Joto hili linaweza kuivisha mboji lakini haliwezi kuua mbegu za magugu na magonjwa.
57-71C
Joto muafaka kwaajili ya kuivisha mbojj na kuua mbegu za magugu na magonjwa. Katika
kiwango hiki cha joto, mbegu zote na vijimelea vyote vya magonjwa vilivyoko kwenye
mchanganyiko wa mboji hufa na hivyo kutokuwepo pale mboji inapokuwa imeiva.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 13
Zaidi ya 71C
Joto hili ni kali sana na huweza kusababisha madhara mengineyo kama vile kuzalishwa kwa
gesi zenye madhara pia wadudu wenye manufaa ambao husaidia mboji kuiva huweza
kukimbia.
Muhimu kuhakikisha kuwa joto halizidi sana ili kuweza kuwa na mboji nzuri yenye
virutubisho.
5. Muda wa kukomaa na matumizi ya mboji
5.1 Muda wa kukomaa
Lundo la mbolea yafaa liachwe likomae baada ya joto kupoa. Mbolea yaweza kutumiwa mara
tu viungo vya kwanza vinapokosa ama vinapopoteza utambusho, na rangi yake ikageuka
kuwa nyeusi na harufu ikawa ya kuvutia.
Hata wakati huu mbolea yahitaji kufunikwa ili isilowe kwa maji ya mvua ama kukauka kwa
ajili ya jua bali ibakie na unyevunyevu. Mboji ikikawia muda mrefu kabla ya kutumiwa,
hupoteza rotuba na wanyama wadogo huifanya makazi yao.
5.2 Matumizi ya mboji
Umuhimu mkuu wa mboji ni kuongeza mazao ya shamba kwa kusaidia udongo kushikilia
maji kwa muda mrefu na kufanya udongo kuwa na afya bora. Pia mbolea hufanya udongo
kushikamana hivyo hupunguza mmomonyoko wa udongo.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 14
6. Faida za Mboji/Mbolea Vunde
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 15
Mbolea hutumiwa mara nyingi kwenye shamba lililoko karibu nyumbani na mbali na
nyumba. Wakati shamba huandaliwa kwa kupanda mbegu, mbolea huchanganywa kwenye
udongo wa juu. Mbolea haifai kuwekwa ndani ya udongo kiasi cha kwamba mizizi ya mimea
haitaifikia. Njia bora ni kuweka mbolea kidogo kwenye shimo ambamo mmea utapandwa.
Kwenye sehemu za ukame, mitaro huchimbwa kisha mbolea ikawekwa ambamo maji
hukusanyika na kutumiwa na mimea.
Hupunguza magonjwa na wadudu waharibifu wa mimea yalioko udongoni hivyo basi mimea
huwa na nguvu, afya na hustahimili magonjwa na wadudu waharibifu.
Mbolea za kemikali japo hutoa rutuba kwa mimea, hazitengenezi mpangilio au hali ya
udongo. Pia ni ghali na huongeza mazao kwa muda mfupi tu. Mboji huwa haibebwi na maji
ya mvua kama ilivyo mbolea za kemikali ama za viwandani na faida yake hudumu kwa muda
mrefu.
Mimea ambayo hupandwa kwa kutumia mbolea za kemikali huvutia wadudu, kwa sababu
rangi yake humetameta na matawi yake ni mwororo mno.
Mbolea vunde pia yaweza kutumiwa ili kufunika udongo usipoteze maji mengi. Mbolea
ambayo haiko tayari hasa kutumika kwa kazi kama hii iwekwe udongoni ili iendelee kuoza na
kuchanganyika kwenye udongo. Mbolea inapotumika kwa kuzuia maji kwenye udongo, yafaa
ifunikwe kwa majani madogo (matandazo). Hii itazuia mbolea isipoteze rotuba kwa sababu ya
joto jingi na miale ya jua.
Mboji pia hutumika kukuza miche na hata kwa kuwalisha samaki.
Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) na Swisscontact 16
Vitabu vya Kurejelea
Baadhi ya maelezo na michoro iliyomo humu imenakiliwa na kutafsiriwa
kutoka;
Henry Doubleday Research Association – HDRA (2005). “Composting in the
Tropics”. United Kingdom.
Kenya Institute of Organic Farming –KIOF (1994). “Field Notes on Organic
Farming”. Edited by Njoroge, J. P.O. Box 34972, Nairobi, Kenya.