kuwanusuru wakina mama -...

48
Kuwanusuru Wakina Mama Utokaji damu baada ya kujifungua MWONGOZO KWA WATOA HUDUMA Mafunzo kwa vitendo katika vikundi

Upload: duongngoc

Post on 06-Feb-2018

297 views

Category:

Documents


7 download

TRANSCRIPT

Kuwanusuru Wakina MamaUtokaji damu baada ya kujifungua

M W O N G O ZO K WA WAT O A H U D U M A Mafunzo kwa vitendo katika vikundi

2

© 2015 Shirika la Jhpiego

Haki zote zimehifadhiwa

ISBN 978-1-943408-08-5

20-09266 Rev A

3

Wanaowahudumia wakina mama wakati wa kujifungua ................................................... 5Kuokoa maisha wakati mama anapojifungua .......................................................................... 6Mawasiliano baina ya watoa huduma na mama ...................................................................... 7Jiandae kwa uzazi salama na safi .................................................................................................... 8Utokaji damu baada ya kujifungua ................................................................................................ 10Kutoka damu nyingi baada ya kujifunguaSababu za kutoka damu nyingi baada ya kujifungua ............................................................ 11Kufanya uamuzi na vitendo sahihi haraka kwa ajili ya mama na mtoto ......................... 12Huduma muhimu kwa mama na mtoto ...................................................................................... 13

Kutoa dawa ili kupunguza utokaji damu nyingi – ( Oksitosin au misoprostol) ............ 14Kukata kiunga mwana kati ya dakika 1-3 .................................................................................... 16Kufanya mvuto wa kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma na kudhibiti kizazi kisitoke ............................................................................................. 17Namna ya kulitoa kondo la nyuma ................................................................................................ 18Kuangalia kama kizazi kimesinyaa ................................................................................................. 19Kukagua kama kondo la nyuma limetoka lote ......................................................................... 20Kuangalia kama kizazi ni kigumu ................................................................................................... 21Je utokaji wa damu ni wa kawaida?............................................................................................... 22Huduma muhimu kwa mama na mtoto ...................................................................................... 23

Mazoezi ya kujifunza ............................................................................................................................ 24

Ikiwa kondo la nyuma halijatoka ................................................................................................... 26Rudia uniti 10 za oksitosin na vuta kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma na uthibiti kizazi kisitoke ..................................................................................................... 27Ikiwa kondo la nyuma halijatoka, limetoka au siyo kamili ................................................... 28Kupata huduma ya ziada .................................................................................................................... 30Rufaa kwa ajili ya huduma ya ziada ............................................................................................... 31Kuangalia kama kuna michaniko .................................................................................................... 32Kugandamiza michaniko ................................................................................................................... 33Kusugua kizazi ........................................................................................................................................ 35Kusugua kizazi, na kurudia dawa .................................................................................................... 36

Kugandamiza kizazi .............................................................................................................................. 38Huduma ya dharura na usafiri .......................................................................................................... 40

Mazoezi ya mafunzo ........................................................................................................................... 41Faharasa .................................................................................................................................................... 44Marejeo ...................................................................................................................................................... 45

Yaliyomo

4

Shukurani

Mwongozo wa mafunzo ya kudhibiti utokaji damu nyingi baada ya kujifungua iliasisiwa na kusanifiwa na timu iliyopo katika ofisi ya uongozi wa kiufundi ya Jhpiego kwa msaada wa

MCHIP timu ya afya ya uzazi ikiongozwa na Cherrie Evans na Peter Johnson

Tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa washirika wetu na wafanyakazi wenzetu waliopo kote duniani waliofanya kazi nasi ili kupunguza matukio yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya wakina mama wazazi na utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua. Tunapenda kutoa

shukurani za pekee kwa wale waliotoa mwongozo katika kufanikisha majarida haya, Shirikisho la Kimataifa la Wakunga (ICM), Shirikisho la Kimataifa la Madaktari bingwa wa wanawake

na uzazi( FIGO), Mfuko wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Shirika la Afya Duniani ( WHO), Mpango Shirikishi wa Afya ya Uzazi na Mtoto MCHIP) na Shirika la Taaluma la Watoto la Amerika (AAP). Tunapenda kuwashukuru washirika

na wafanyakazi wenzetu wa India, Malawi, na Zanzibar walioshiriki kujaribisha nyenzo hizi. Shukurani kubwa kwa Harald Eikeland, Mhariri sanifu wa Mafunzo, na Anne Jorunn

Svalastog Johnsen, mchoraji wa Laerdal kwa msaada wake usio na kifani kwa kuwezesha kufanya majarida haya yaeleweke kwa wote

.

Kazi hii imewezeshwa kupitia msaada kutoka kwa Laerdal Foundation for Acute Medicine na Jhpiego, mshirika wa Johns Hopkins University.

Jhpiego ni shirika la Afya la kimataifa, lisilo la kiselikali na kibiashara, lililo mshirika wa chuo kikuu cha Johns Hopkins. Kwa miaka 40, Jhpiego imewezesha wafanyakazi walio mstari wa mbele katika kutoa huduma ya afya kwa kubuni na kutekeleza kwa ufasaha, kwa gharama ndogo, na kwa namna rahisi ya kutatua matatizo yao ili kuimarisha huduma za afya kwa wakina mama na familia zao. Kwa kuweka ubunifu unaotekelezeka wa afya katika utendaji wa kila siku. Jhpiego inafanya kazi ya kushanganua

vikwazo ili kuwapatia huduma bora ya afya watu walio wepesi kuathirika duniani.

5

Mafunzo ya utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua ni jumla ya mafunzo yaliyopangwa kwa vikundi vilivyo mstari wa mbele katika kutoa huduma ya afya ya uzazi kwa wakina mama na vichanga. Mafunzo haya ni muhimu kwa watoa huduma wote wa afya wanaohudumia wazazi. Mafunzo haya yanawajumuisha wahudumu wenye ujuzi (wakunga, madaktari pamoja na wafanyakazi wengine) wanoweza kuitwa kufuatana na hali halisi.

Mafunzo ya utokaji damu nyingi baada ya kujifungua yameandaliwa ili kuwasaidia watoa huduma kupata stadi na ujuzi wa kufikia umahiri unaohitajika kumudu kwa usalama na ufanisi kuzuia, kutambua na kuhudumia utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua.

Vitini kwa ajili ya mafunzo haya ni Mpangokazi, mchoro wa utendaji ili kuwasaidia wahudumu katika kuhudumia hatua ya tatu ya uchungu, Bango Kitita, hutumika kutoa maelekezo na Mwongozo huu kwa Watoa Huduma. Mwongozo kwa Watoa Huduma ni kwa wote wawezeshaji na wanaojifunza. Mwongozo huu una taarifa zinazohitajika kuendeshea mafunzo yanayoendelea ikiwa ni pamoja na maelezo ya awali ya vitendo/somo pamoja na usuli wa maudhui.

Moduli hii imebuniwa ili itumike kufundishia watoa huduma wa afya vituoni mwao kwa muda wa siku moja, tumia mifano halisia (kifani cha mjamzito na mtoto mchanga) ili kuwezesha mazoezi. Baada ya mafunzo, malengo ni wahudumu waendelee kufanya mazoezi kwa kutumia mifano halisia, wakiongozwa na mmoja wao mwenye ujuzi zaidi katika kuhudumia uzazi. Kwa kutambua kuwa yeyote aliyejifunza anauwezo wa kuratibu mafunzo kwa wenzake kituoni mwake baada ya mafunzo ya awali. Mwongozo huu wa watoa huduma una faa kutumiwa na wawezeshaji na wanaojifunza.

Ni muhimu kufahamu kuwa katika nchi nyingine wahudumu waliopata mafunzo ndio wanaruhusiwa kufanya aina fulani za huduma, kwa mfano, kufanya kuvuta kiunga mwana, kuongeza njia ya uzazi, kutoa kondo la nyuma lilokwama kwa mkono au kuweka mpira wa kutoa mkojo. Angalizo kwa huduma ya ziada inabainisha ni kwa jinsi ipi bora zaidi ya kuwahusisha wale wote walioidhinishwa kufanya ujuzi husika.

Kama wanamafunzo wanaweza kupata mtandao wa mawasiliano, wanaweza kujifunza kwa kutumia moduli ya eleningi ya utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua iliyoandaliwa na Jhpiego, UNFPA, WHO na Intel inayopatikana:http://reprolineplus.org/learning-opportunities/course/managing-postpartum-hemorrhageWanamafunzo watafanya mazoezi ya aina mbili, yote kwa kizazi ambacho hakijasinyaa na kondo la nyuma lililokwama.Wanamafunzo watafuatilia kesi ya Bibi M. na Bibi B. wakifanya tadhimini ya awali, kugundua mahitaji, kutoa huduma na kutathimini huduma iliyotolewa, video fupi zilizotengenezwa na Medical Aid Films na zinajumuishwa kwenye mpango wa mafunzo. Video za Kutoka Damu Nyingi Baada ya Kujifungua ikijumuisha kuondoa kondo la nyuma lililokwama kwa mkono na kumsaida mtoto mchanga kupumua zinapatikana katika webu saiti ya Medical Aid Films http://medicalaidfilms.org/our-films/emergency-obstetric-newborn-care-skilled/.

Kwa wanaowahudumia wakina mama wakati wa kujifungua

6

Mtoa huduma anatakiwa kufahamuWakati wa ujauzito, uchungu, kujifungua na baada ya kujifungua kunawatu wawili wanaohitaji huduma- mama na mtoto. Afya na uhai wa wote unategemeana. Endapo

mama anapopoteza uhai na mtoto mchanga anaweza asiishi pia watoto wake wengine wapo hatarini.

- Programu za mafunzo ya utokaji damu baada ya kujifungua na ya kusaidia watoto kupumua zinatumika pamoja kwa kujenga ujuzi na maarifa kwa ajili ya kuwahudumia wote wawili mama na mtoto wakati na baada ya kujifungua

- Kutoka na damu baada ya kujifungua inalenga kukinga, kutambua, na kuhudumia utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua.

- Kusaidia watoto kupumua inafundisha huduma ya kawaida ya watoto wakati wa kuzaliwa na namna ya kumsaidia mtoto asiyepumua.

- Maamuzi yamtoa huduma yanaweza kuleta uhai au kifo kwa mama na mtoto.

- Ujuzi aliofundishwa katika mafunzo haya – kuhudumia kwa vitendo hatua ya tatu ya kujifungua, kukadiria kwa haraka upotevu wa damu, kutambua chanzo cha kutokwa na damu nyingi, na kutoa tiba sahihi ya utokaji wa damu nyingi – itaokoa maisha.

- Mafunzo yote yatajumuisha mifano halisia, kujenga ujuzi, na majadiliano.

MazoeziKufanyia mazoezi ujuzi uliojifunza kwenye mafunzo haya itakusaidia kuokoa uhai. Kabla ya kufanya zoezi lolote au drili, hakikisha mahitaji yote yapo tayari. Angalia orodha ukurasa wa 8.

Kunusuru maisha wakati mama anapojifungua

Matarajio ya utendaji1. Kutoa huduma makini ya hatua ya

tatu ya uchungu (AMTSL), ambazo ni mfululizo wa hatua tatu za afua zinazoshauriwa kwa kila uzazi na zilizothibitishwa ili kupunguza utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua (PPH) na vifo vya uzazi.

2. Kutambua na kuhudumia utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua

kwa kutumia mpangilio ulio kubalika.

Dondoo muhimu- Kuna watu wawili wanaohitaji

huduma, mama na mtoto- Uhai wa mtoto unategemea uhai wa

mama- Kila mafunzo yatajenga ujuzi na

maarifa ili kutoa huduma zinazofaa kwa mama na mtoto

- Ni muhimu kufanya mazoezi ya ujuzi uliopata baada ya mafunzo

Jiulize

Kuna umuhimu gani huduma ya mama kwa afya na uhai wa mtoto?

7

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa:Kushindwa kuwasiliana kutasababisha matatizo makubwa kwa wakina mama na watoto

- Fahamu nani wa kumwita na itakuwaje kama huduma ya ziada au rufaa inahitajika.

- Hakikisha mama na wanafamilia wake wanafahamishwa kinachoendelea

- Kama upo mwenyewe, wanafamilia wanaweza kuwa timu yako

- Wanatimu wako ni pamoja na watu unaofanya nao kazi kituoni kwako, wale wa kituo cha rufaa na ndugu wa mama.

- Ni vizuri kuwa na mazoezi ya vitendo ya mara kwa mara kujenga kujiamini ndani ya timu yako

- Kuweka mpango wa dharura mapema kutafanya mawasiliano yawe rahisi.

- Wasiwasi na woga ni hali ya kawaida wakati wa dharura, lakini vinaweza kuzuia mawasiliano.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya nini:- Kuwatahadharisha wanatimu wake kadiri

uzazi unavyokaribia ili wasaidie kama dharura ikitokea

- Kuwasiliana kwa sauti kwa kujiamini na kwa ufasaha – usidhani wengine wanafahamu unachokifikiri

- Mawasiliano yaliyokamilika yatahakikisha kuwa kila mmoja anajua kitu gani kinapaswa kufanyika na yatasaidia kuwatoa hofu mama na wanafamilia wake.

Mawasiliano baina ya watoa huduma na mama

Matarajio ya utendajiMhudumu ataweza kuwasiliana kwa ufasaha na wanatimu wakati wa dharura.

Dondoo muhimu- Mawasiliano mazuri yanaweza

kuokoa maisha- Mfahamu nani wa kumwita kwa

msaada- Toa majukumu kwa kila mwanatimu - Uwe tayari kwa dharura - Wajulishe wengine pale uzazi

unapokaribia

8

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa: Ahakikishe eneo la uzazi ni faragha, safi, lina joto na mwanga vya kutosha.

- Sabuni na spiriti/dawa ya kunawia – kunawa mikono ni muhimu kwa kuwakinga mama, mtoto, na mhudumu. Ni lazima kunawa kabla ya kuvaa glovu na baada ya kuzivua

- Glovu – iliyotakaswa ili kupunguza hatari ya maambukizo kwa mhudumu, mama, na mtoto. Kama inawezekana vaa glovu jozi mbili ili kupunguza hatari ya maambukizo kwa mtoto kwa kuvua jozi ya juu kabla ya kufunga na kukata kiunga mwana.

- Mikasi au nyembe – iliyotakaswa kwa ajili kukatia kiunga mwana

- Kitambaa safi – kikavu cha kumkaushia na kumpatia mtoto joto, msafishe mama, na futa damu kuona kama kuna michubuko.

- Kibana kiunga mwana, – kabla ya kukata, baada ya kukata, vuta kiunga mwana ili kutoa kondoa la nyuma na mkono mwingine kuzuia kizazi kisitoke

- Kinga binafsi kwa mtoa huduma – aproni, barakoa , miwani , buti na kofia, weka sehemu ya kuzalishia safi na punguza hatari ya maambukizo.

- Madawa – kabla ya kila uzazi oksitosin inapaswa kunyonywa kwenye bomba la sindano au vidonge vya misoprosto tayari kutolewa.

- Penguin Sakshin – kusafisha mdomo na pua ya mtoto pale inapohitajika

- Barakoa na mfuko wa kupumua – kumsaidia mtoto kupua inapohitajika.

- Stetoskopu – kwa kupima mapigo ya moyo ya mtoto kama msaada wa kupumua unahitajika.

- Saa – kwa kufuatilia muda gani kila hatua ya uzazi inachukua, kuweka muda wa kuzaa, na dakika ya kwanza baada ya kujifungua

Matarajio ya utendajiMhudumu atatambua viashirio vya uzazi safi na salama

Dondoo muhimu- Weka eneo la uzazi faragha lenye joto na mwanga wa kutosha- Ni lazima uwe na vifaa sahihi, safi na tayari kwa kutumika kabla ya kujifungua- Kwa kila uzazi, mara zote uwe umenyonya dawa ya msinyao kwenye bomba la sindano tayari kutolewa- Jaribisha ufanyaji kazi wa mfuko na barakoa (mask)- Uoshaji mikono na kutumia glovu na vifaa vilivyotakaswa au kuwekwa kwenye dawa kutapunguza hatari ya maambukizo- Andika muda wa kujifungua- Mama na mtoto mara zote wanapaswa kuwa pamoja

Jiandae kwa uzazi safi na salama

9

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;Kutayarisha vifaa vyote kabla ya mzazi kufika.- Kutumia mbinu safi kupanga vifaa na mahitaji.- Kutumia vifaa vyote vinavyotakiwa na kwa

usalama.- Kutengeneza vifaa na mahitaji kwa kutumia

vitu vilivyopo kama vitahitajika.- Kunawa mikono au apake dawa kabla na

baada ya kuvaa glovu.- Kutupa taka zote kwa namna inayostahili. - Kuweka vitu vyenye ncha kali kwenye

chombo kisichoruhusu vijitokeze nje. kutakasa mikasi, vibanio na vifaa vingine kwa mashine ya kutakasa au kwa dawa, zitumbukizwe kwenye mmumunyo wa klorini ya asilimia 0.5 kwa dakika10.

- Awasiliane na mama na “timu” ya uzazi.

- Awaweke mama na mtoto pamoja baada ya kujifungua.

Ni muhimu sana kwa oksitosin kunyonywa kwenye bomba la sindano au misoprostol kuwa tayari kwa kutolewa KABLA YA MTOTO KUZALIWA. Hii itakuwezesha kutoa dawa kwa haraka na kuwa na muda wakuzuia mama kutoka damu nyingi na kupunguza ucheleweshaji wa huduma ya kumwokoa kama mtoto hapumui.

Sabuni ya maji na spiriti ya kunawia

Glovu iliyotakaswa

Mikasi au wembe

Vitambaa visafi

Kibana kiunga mwana, vibanio, vifungio

Miwani kwa mtoa huduma

Oksitosin/Misoprostol

Penguin Sakshin

Barakoa au mfuko wa kupumua

Stetoskopu

Saa

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu Yafuatayo;- Wazazi wote wako hatarini kutokwa na damu

nyingi baada ya kujifungua- Utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua

unaweza kuwa taratibu, mfululizo wa mfululizo wa matone, kidogo kidogo au mbubujiko mkubwa. Aina zote hizi zinahatarisha maisha

- Damu inaweza kuwa maji au mabonge- Kupoteza damu yenye ujazo wa ml 500 au

mara pengine kidogo kunaweza kuhatarisha maisha ya mama

- Wazazi wagonjwa, wenye upungufu wa damu, au wenye lishe duni wanaweza kuugua hata kwa utokaji kidogo wa damu baada ya kujifungua.

- Kuna hatua ambazo mtoa huduma anaweza kuchukua ili kusaidia kupunguza utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua.

1 0

Matarajio ya utendajiMtoa huduma atatambua kwamba akina mama wote wapo hatarini kwa utokaji damu nyingi baada ya kujifungua na umuhimu wa kuzuia na kuchukua hatua za haraka.

Dondoo muhimu- Mzazi yeyote anaweza kutokwa na

damu nyingi baada ya kujifungua- Utokaji wowote wa damu nyingi

unahatarisha maisha

Utokaji damu nyingi baada ya kujifungua

Jiulize

Je, wazazi wote wapo hatarini kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua?

Ni mama yupi yupo hatarini kutoka damu nyingi?

Mtoa huduma anatakiwa kuwa;Kwa kiasi kikubwa utokaji mwingi wa damu baada ya kujifungua ni kwa sababu kizazi kushindwa kusinyaa au kuwa laini baada ya kujifungua.

- Mishipa midogo ya damu kwenye kizazi hupatia kondo la nyuma mahitaji wakati wa ujauzito.

- Kizazi lazima kisinyae ili kufunga mishipa midogo ya damu.

- Kama kizazi hakisinyai, mishipa midogo midogo (veseli) itaendelea kusukuma damu kwenye kizazi kitupu.

- Hii ndiyo sababu kubwa ya utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua.

- Kumkagua mama mara kwa mara baada ya kujifungua ili kuona kama kizazi ni kigumu inasaidia kutambua ikiwa ndiyo sababu ya kutokwa na damu nyingi.

Kubaki kwa kipande cha kondo la nyuma au kipande cha membrini husababisha utokaji wa damu nyingi. - Kama kipande cha kondo la nyuma au

membrini kimebaki, kizazi hakiwezi kusinyaa na mama atatokwa na damu nyingi.

- Ni muhimu kukagua kondo la nyuma baada ya kutoka ili kuhakikisha kama limetoka lote

Utokaji damu nyingi kunaweza kusababishwa na michaniko. Michaniko inaweza kuwa mikubwa au midogo, ndani au nje ya uke- Uongezaji wa njia ya uzazi kutaongeza

michaniko na utokaji wa damu nyingi, ikatwe tu kwa sababu maalum na mtoa huduma mwenye ujuzi

- Wanawake waliokeketwa wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuchanika

- Kufuta damu kwa taratibu kunaweza kukusaidia kuona wapi pamechanika

Mtoa huduma anatakiwa yafuatayo;- Mtoa huduma ana wajibu wa kumpima

mama mara kwa mara kwa mabadiliko ya utokaji wa damu.

- Mtoa huduma anatakiwa aangalie kizazi kutambua kama kinasinyaa.

Angalizo kwa huduma zaidi Kama wanamafunzo wana mafunzo ya ziada na idhini ya kutoa huduma ya kiwango cha juu, wafanye kazi ndani ya mawanda yao. Hii ni pamoja na kuongeza njia ya uzazi kama mama amekeketwa.

1 1

Sababu za utokaji damu nyingi baada ya kujifungua

Matarajio ya utendaji Mtoa huduma atatambua sababu za kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua na kuzitibu kwa usahihi.

Dondoo muhimu- Msinyao hafifu, michaniko, na kubaki

kwa kipande cha kondo la nyuma ni sababu kuu tatu zinazosababisha kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.

- Utokaji mwingi wa damu baada ya kujifungua husababishwa na kizazi kushindwa kuwa kigumu (msinyao hafifu).

- Kipande cha kondo la nyuma au membrini iliyobaki ndani ya kizazi huweza kusababisha damu nyingi kutoka.

- Michaniko inaweza pia kusababisha kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.

Uongezaji wa njia ya uzazi na ukeketaji unaongeza hatari ya michaniko.

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Baada ya kujifungua, hali ya mama na mtoto

inaweza kubadilika ghafla. Kufuatilia kwa makini dalili hizi ni muhimu sana.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;

Kwa mama- Kuangalia kwa umakini utokaji mwingi

wa damu tangu kujifungua, na kadiri unavyosubiri kondo la nyuma kutoka, na kila dakika 15 ndani ya saa mbili za kwanza baada ya kujifungua.

- Kagua kizazi kuona kama kinakuwa kigumu kama paji la uso wako kadiri kinavyosinyaa na kusitisha utokaji mwingi wadamu.

- Mchunguze mama kama ana dalili ya kupoteza damu nyingi kama vile; kuongezeka mapigo ya moyo, kushuka kwa msukumo wa damu, kupauka ngozi na mwili kuwa wenye baridi na unyevunyevu

Kwa mtoto - Sikiliza mtoto anavyolia wakati

unapomkausha vizuri- Dakika ya kwanza ya uhai kwa kichanga

ni muhimu sana. Kama mtoto halii, mfunike kwa nguo kavu ili apate joto, na mtomasetomase /mwanzishie kupumua. Fuata miongozo ya kuwasaidia watoto kupumua.

Kwa mama na mtoto- Kumweka mtoto kwenye kifua cha mama

kutakusaidia kuwafuatilia wote kwa wakati moja

- Kutumia ukionacho, ukihisicho, na unachokisikia kwa kuchukua uamuzi makini kujua hatua bora inayofuata kwa mama na mtoto

- Kuchukua hatua za haraka huokoa maisha

1 2

Fanya uamuzi makini na wa haraka kwa ajili ya mama na mtoto

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kutambua tatizo na kufanya uamuzi wa haraka unaofaa kwa ajili ya mama na mtoto

Dondoo muhimu- Dalili za kubadilika kwa hali ya mama

na mtoto lazima zifuatiliwe- Dalili kama kupoteza damu nyingi,

msinyao wa kizazi na upumuaji wa kichanga ni muhimu visaidie katika uamuzi wa nini cha kufanya .

- Kuchunguza dalili kwa makini, kufanya maamuzi, na kuchukua hatua haraka ni muhimu kwa ajili ya kuwasaidia mama na mtoto kuishi.

- Chukua hatua haraka kuokoa maisha!

Jiulize

Ni mara ngapi utamuangalia mama katika masaa mawili ya kwanza baada ya kujifungua

1 3

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa; - Katika kipindi hiki, kizazi kinasinyaa na kuwa

kidogo.- Hii hufanya kondo la nyuma kujitenga na

ukuta wa kizazi- Mchakato huu huchukua dakika 8-9, lakini

huweza kufikia hata saa.- Shirika la Afya Duniani linashauri huduma

makini kwa wazazi wote ili kupunguza hatari ya utokaji wa damu nyingi baada ya

kujifungua kwa asilimia 60 hadi 70- Kati ya dakika 1 hadi 3 baada ya kujifungua,

ni wakati wa kubana au kufunga na kukata kiunga mwana.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;Wakati mama na mtoto wote wanaendelea vizuri, huduma ya kawaida kwa wote inaweza kuendelea .

Fanya ya fuatayo Mzalishe mtoto na umweke tumboni kwa

mama. Mkaushe mtoto vizuri na uangalie

anavyolia, kupumua mfunike kwa kitambaa kikavu.

Angalia kama kuna mtoto mwingine tumboni, kama hayupo endelea na huduma ya hatua ya 3 (kwa mama) wakati huo huo ukiendelea kumwangalia mtoto.

Mpatie mama oksitosin au misoprostal ndani ya dakika moja baada ya mtoto kuzaliwa.

Wakati unasubiria kondo la nyuma kutoka, vua glovu ya juu kama umevaa jozi mbili, au badili glovu na ukate kiunga mwana cha mtoto ndani ya dakika 1-3 baada ya kujifungua.

Vuta kiunga mwana wakati wa misinyao. Gusa kizazi mara tu kondo la nyuma

linapotoka na sugua kizazi kama ni laini. Kagua kama kondo la nyuma limetoka lote.

Angalia kiasi cha utokaji damu. Angalia michaniko.

Endelea kuwaagalia mama na mtoto kwa ukaribu na toa huduma za kawaida.

Jiulize

Je, ni zipi sehemu tatu za huduma za kima- tendo za hatua ya tatu ya uzazi?

Je, ni wakati gani mama anachomwa sindano ya oksitosin

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kutoa hudumaza kawaida kwa mama na mtoto mara tu baada ya kujifungua.

Dondoo muhimu- Hatua ya tatu ya uchungu - ni muda

kati ya kujifungua na kutoka kwa kondo la nyuma.

- Hatua ya tatu ya uzazi ni: kutoa dawa ya kusinyaisha kizazi, kuvuta kiunga mwana na kuangalia msinyao wa kizazi.

- Huduma makini ya hatua hii inaweza kupunguza kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua

- Hakikisha mtoto anapumua vizuri katika dakika ya kwanza ya maisha

Huduma za kawaida kwa mama na mtoto

Jiulize

Dawa ipi inahitaji kuhifadhiwa penye nyuzi joto pungufu ya 25?

1 4

Kutoa dawa ili kupunguza utokaji wa damu nyingi- Oksitosin au Misoprostol

Matarajio ya utendaji Mtoa huduma ataweza kutoa kwa usalama na ufasaha oksitosin na misoprostol baada ya mtoto kuzaliwa.

Dondoo muhimu- Oksitosin na misoprostol zinasababi- sha kizazi kusinyaa.- Papasa kama kuna mtoto mwingine kabla ya kutoa dawa- Oksitosin hutolewa kama sindano na ni lazima ihifadhiwe penye nyuzi joto 25 au pungufu. Fuata maelekezo ya mtegenezaji. Dozi ni uniti 10.- Misoprostol ni vidonge na humezwa. Havihitaji kuhifadhiwa kwenye ubaridi. dozi mcg 600 (vidonge 3 vya mcg 200).- Kutoa dawa ndani ya dakika moja baada ya mtoto kuzaliwa

Ni muhimu sana kwa oksitosin kunyonywa kwenye bomba la sindano au vidonge vya misoprostol viwe tayari kwa kumezwa KABLA YA MTOTO KUZALIWA. Hii itakupa nafasi ya kutoa dawa kwa uharaka ili kumkinga mama kutokwa na damu nyingi na kupunguza ucheleweshaji wa uokoaji kama mtoto hapumui.

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Oksitosin na misoprostol zote ni dawa

zinazosababisha kizazi kuwa kigumu au kisinyae.

- Wakati kizazi kinasinyaa kinabana mishipa midogo ya damu na kusitisha utokaji wa damu nyingi.

- Oksitosin inatolewa kwa njia ya sindano kupitia kwenye msuli. Inatakiwa kuhifadhiwa katika nyuzi joto 25 au pungufu.

- Oksitosin ni chaguo la kwanza la dawa mujarabu iliyokubalika na Shirika la Afya Duniani.

- Misoprostol hutolewa kwa vidonge kwa jumla ya mcg 600 (mcg 200 kwa kidongex3) na inafanyakazi vizuri hata kama ikitunzwa sehemu ya joto na mwanga.

- Kabla ya kutoa dawa yoyote hakikisha hakuna mtoto mwingine tumboni. Mweleze mama kuwa anadungwa sindano au anapewa vidonge ili kuzuia utokaji wa damu nyingi.

- Toa ndani ya dakika moja baada ya kuzaliwa mtoto ili kizazi kisinyae na kisukume nje kondo la nyuma. Hii itazuia utokaji wa damu nyingi.

- Ergometrine inaathiriwa zaidi kwa mwanga na joto na inaongeza hatari ya kondo la nyuma kubaki. Isitolewe kwa mzazi yeyote mwenye shinikizo la juu la damu. Vilevile ina madhara makubwa yasiyotarajiwa kwa baadhi ya wazazi kama vile kutapika na shinikizo la juu la damu. Kwa hiyo, asipewe mama kwa ajili ya kuzuia utokaji wa damu nyingi pale oksitosin inapokuwapo

Oksitosin- Kutoa dozi sahihi: hakikisha kuwa uniti 10

ya oksitosin imenyonywa kwenye bomba la sindano kabla ya mama kujifungua.

- Mweleze mzazi kuwa anadungwa sindano kupunguza utokaji wa damu nyingi.

- Dunga sindano kwenye msuli mkubwa (kwa kawaida kwenye paja la mama).

MISOPROSTOL- Kutoa dozi sahihi: Andaa vidonge vitatu vya

mcg 200 kila kimoja kwa jumla ya mcg 600 tayari kabla ya kujifungua.

- Hakikisha mama amemeza vidonge baada ya mtoto kutoka

- Mnasihi mama kuhusu madhara yasiyotarajiwa ya dawa ya misoprosto.kama kutetemeka, kichefuchefu, kuharisha, na homa ambayo inaweza kutokea lakini hayana athari.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo:- Kabla ya mtoto kuzaliwa, aandae dawa tayari

kutolewa ndani ya dakika moja baada ya kujifungua.

- Apapase kama kuna mtoto wa mwingine.- Toa dawa na kiasi sahihi ndani ya dakika

moja baada ya mtoto kuzaliwa

Jiulize

Je, ipi ni dozi sahihi ya oksitosin?

Ni ipi dozi sahihi ya misoprostol?

1 5

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Muda maalumu wa kukata kiunga mwana

unategemea hali ya wote, mama na mtoto. Kusubiri angalau kwa dakika moja kubana na kukata kiunga mwana hukupa muda wa kutoa dawa ili kuzuia utokaji wa damu nyingi na muda wa mzunguko wa damu kutoka kondo la nyuma hadi kwa mtoto.

- Usafi wa kiunga mwana ni muhimu kuzuia maambukizo. Vifaa vyote vilivyotumika vitakaswe au viwekwe kwenye mmumunyo wa dawa.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kata kiunga mwana kati ya dakika moja

hadi tatu baada ya kujifungua kama mama na mtoto wanaendelea vizuri. Kama mama anatokwa na damu nyingi na mtoto hapumui vizuri, kata kiunga mwana mapema na omba msaada.

- Ili kukata kiunga mwana weka vibanio viwili au vifungio kwenye kiunga mwana. Weka kibanio cha kwanza au kifungio kwenye kiunga mwana umbali wa upana wa vidole 2 kutoka tumbo la mtoto. Weka kibanio kingine umbali wa upana wa vidole 5 kutoka tumbo la mtoto.

- Vaa jozi mbili za glovu kabla ya kuzalisha ili uvue moja kabla ya kukata kiunga mwana.

- Wakati unakata kiunga mwana, jihadhari na damu inayoweza kuruka, funika sehemu hiyo kwa kipande cha gozi iliyotakaswa .

1 6

Kata kiunga mwana kati ya dakika 1-3

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kukata kiunga mwana kwa usahihi katika muda mwafaka na kwa namna ambayo itapunguza hatari ya maabukizo kwa mtoto.

Dondoo muhimu- Kama mtoto anapumua vizuri, kata

kiunga mwana kati ya dakika 1-3 baada ya kujifungua.

- Kabla ya kukata kiunga mwana, vua jozi ya juu.

- Funga sehemu mbili au zibane na ukate katikati yake

1 7

Mtoa huduma anatakiwa - Kubana kiunga mwana karibu na msamba.- Msubiri mama apate uchungu, au kizazi kiwe

kigumu.- Tumia mkono moja kuzuia kizazi kwa

kuuweka juu ya mfupa wa kinena wa mama na kusukuma juu ili kupata msukumo kinzani.

- Wakati wa msinyao au uchungu, tumia mkono mwingine kuvuta kiunga mwana chini kwa taratibu. Endeleza msukumo kinzani kwenye kizazi juu ya mfupa wa kinena.

- Kama unahisi ugumu, acha na fanya tena wakati wa msinyao unaofuata.

- Acha kuvuta kiunga mwana kati ya misinyao.- Endelea kuvuta kiunga mwana wakati

wa misinyao mpaka pale kondo la nyuma litakapoonekana kwenye njia ya uzazi.

- Inaweza kuchukua misinyao kadhaa kwa kondo la nyuma kutoka.

- USIVUTE wakati unahisi ugumu au kama hakuna msinyao kwa sababu unaweza kukata kiunga mwana au ukatoa kizazi nje. Hali hii inaweza kumuua mama.

Angalizo kwa huduma ziada Wanamafunzo wanapaswa kushugulika ndani ya mawanda yao ya kazi. Hii ni pamoja na kuvuta kiunga mwana kama ilivyoelezwa hapa.

Matarajio ya utendajiMkunga mzoefu ataweza kufanya kwa usalama kuvuta kiunga mwana.

Dondoo muhimu- Uvutaji wa kiunga mwana ili kutoa

kondo la nyuma ufanywe tu na mkunga mwenye stadi na ujuzi.

- Uvutaji wa kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma unapaswa kuwa taratibu.

- Vuta kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma wakati kizazi kinasinyaa.

- Hakikisha mkono mwingine umezuia kizazi kisitoke wakati unavuta kiunga mwana

- Usivute kabisa kiunga mwana kama unahisi ukinzani.

- Kuvuta kwa nguvu au uhisipo ukinzani kutamuumiza mama.

- Vuta kiunga mwana taratibu, kuelekea chini tu. Usivute kwa mwelekeo tofauti.

Vuta kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma na mkono mwingine kuzuia kizazi kisitoke

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;Kama kipande cha kondo la nyuma au membrini zimebaki ndani ya kizazi, mama atatokwa na damu nyingi na anaweza kupata maambukizo- Kama kondo la nyuma likijitenga kutoka

kwenye kizazi, litasogea kwenye uke.- Wakati wa kutoa kondo la nyuma, ni muhimu

kuchukua hatua ya kupunguza uwezekano wa kuchana kondo la nyuma au membrini.

- Kama mtoa huduma atatumia mikono yote miwili kushika kondo la nyuma na kulizungusha kwa taratibu, membrini zitajisokota kama kamba, ambayo ni imara na vigumu kukatika.

- Kama kipande kidogo cha membrini kikikatika au kimebaki kwenye shingo ya kizazi inaweza mara nyingi kuondolewa kwa kuzungusha kipande kuwa kama kamba na kuivuta taratibu.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kadiri kondo la nyuma linavyotoka, tumia

mikono yote miwili kulipokea na kwa taratibu zungusha kondo la nyuma kuzuia kukatika kwa membrini.

- Kondo la nyuma na membrini ziwekwe kwenye chombo ili kuzikagua baadaye.

- Kwa haraka angalia kwa kugusa kizazi na sugua kama ni laini.

1 8

Namna ya kutoa kondo la nyuma

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kutoa kondo la nyuma lote na membrini zote.

Dondoo muhimu- Kipande cha kondo la nyuma

kilichobaki ndani ya kizazi usababisha kutokwa na damu nyingi na maambukizo.

- Kuzungusha taratibu kondo la nyuma kadiri linavyotoka inasaidia membrini zitoke zote.

Jiulize

Kwanini hutakiwi kuendelea kuvuta kiunga mwana wakati unahisi kuna ugumu?

Kupokea kondo la nyuma kwa mikono na kulizungusha kunasaidiaje kutokubaki kwa membrini ndani ya kizazi?

1 9

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu yafuatayo;- Kizazi kisichosinyaa au kilicho laini baada ya

kondo la nyuma kutoka, ni sababu kubwa ya utokaji damu nyingi baada ya kujifungua

- Mishipa midogomidogo iletayo damu kwenye kondo la nyuma na kwa mtoto wakati wa ujauzito itaendelea kutoa damu mpaka pale kizazi kitakaposinyaa

- Wakati kizazi kinasinyaa, mishipa midogo midogo itabanwa na hii itasimamisha damu kutoka

- Kuhisi upande wa juu wa kizazi (fandasi) ni namna nzuri ya kutambua kama kizazi ni kigumu au laini

- Usuguaji wa kizazi kunaweza kufanya kizazi laini kiwe kigumu na kusitisha utokaji wa damu nyingi.

- Mabonge ya damu yanaweza kutoka, ambayo pia itasaidia kizazi kisinyae.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kukagua kama kizazi ni laini- Kutambua kizazi kilipo kwa kugandamiza

kutumia kingo ya kiganja kwenye tumbo la mama kwa uthabiti juu ya kinena.

- Kukunja kiganja kuelekea chini ili kukihisi kizazi kwa juu au fandas.

- Kuangalia kama kizazi ni kigumu kama paji lako la uso au laini kama pua yako.

- Kama ni laini, sugua kwa nguvu kwa mwendo wa mzunguko mpaka ukihisi kuwa kigumu kama paji la uso na tazama kama damu inapungua

- Mfundishe mama namna ya kusugua kizazi chake.

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kupima msinyao wa kizazi na kusugua kizazi kama itahitajika.

Dondoo muhimu- Kizazi laini ni kisababishi cha kwanza

cha utokaji damu nyingi baada ya kujifungua.

- Kusugua kizazi kikiwa laini kutaifanya kisinyae au kuwa kigumu.

- Kusugua kizazi wakati kikiwa laini ni hatua muhimu katika kuzuia utokaji mwingi wa damu.

Angalia kwa kugusa msinyao wa kizazi

Jiulize

Kwanini ni muhimu kugusa na kuangalia kusinyaa kwa kizazi mara kwa mara?

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa; Kipande cha kondo la nyuma iliyobaki ndani ya kizazi inaweza kumfanya mama atokwe na damu nyingi. Na inaweza kusababisha kizazi kipate uambukizo ambao utamfanya mama augue sana. Vyote hivyo, kutokwa na damu na uambukizo kwaweza kumsababishia mama kifo- Upande wa kondo la nyuma ulioshikiza kwa

mama ni mweusi mwekundu na huonekana kama nyama. Umetengenezwa kwa ndwe nyingi.

- Upande mwingine ni angavu na wa kijivu, umefunikwa kwa membrini.

- Kama limetoka lote, ndwe kwenye kondo la nyuma yamekaa vizuri kama fumbo.

- Membrini ni lazima zikaguliwe pia kuona kama kuna vipande vimebaki.

- Wakati kipande cha kondo la nyuma au membrini ikibaki kwenye kizazi, kizazi hakiwezi kusinyaa vizuri na mama anaweza kutokwa na damu nyingi sana.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kukagua pande zote za kondo la nyuma

kama ni kamilifu.- Kushika upande angavu kwa viganja vya

mikono yote miwili yenye glovu iliyokunjwa ili kondo la nyuma lionekane kama bakuli

- Kuangalia kama ndwe zote zipo au kuna vipande vinakosekana.

- Nyanyua kondo la nyuma juu kuona kama membrini ni kamilifu.

- Angalia mishipa midogo ya damu inayozunguka ukingo wa kondo la nyuma kwani hii inaweza kuonyesha kuna kipande ndani.

- Kama inaonekana vipande havipo angalia mama anavyotokwa damu na msinyao wa kizazi na apate msaada wa ziada.

- Kama kila kitu kiko sawa, huu ndio muda muafaka kuangalia msamba kwa michaniko

2 0

Kagua kondo la nyuma kama limetoka lote

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kutoa kondo lote na membrini zote.

Dondoo muhimu- Pande zote za kondo la nyuma na

membrini lazima zihakikiwe kama zimekamilika.

- Kipande cha kondo la nyuma kilichobaki ndani ya kizazi cha mama inaweza kusababisha kutokwa damu nyingi na maambukizo.

Jiulize

Je, ni wakati gani salma wa kushika na mikono kondo la nyuma na kulitoa?

Kama kipande cha kondo la nyuma kimebaki ndani ya kizazi kwanini mama anatokwa na damu nyingi?

2 1

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Kizazi laini ni kisababisha kikuu cha utokaji

wa damu nyingi baada ya kujifungua.- Kizazi kinaweza kuwa laini mara tu baada ya

kondo la nyuma kutoka au kinaweza kuwa kigumu na kuwa laini baadaye

- Wakati wowote kizazi kinapokuwa laini baada ya kujifungua, mama hutokwa na damu nyingi.

- Kibofu kilichojaa mkojo kinaweza kusababisha kizazi kiwe laini hata kama kilikuwa kigumu hapo awali.

- Kugusa kizazi ni namna bora zaidi kuelezea kama kizazi ni kigumu au laini.

- Wazazi wasioangaliwa kila baada ya dakika 15 wanaweza kufariki kutokana na kutokwa na damu nyingi kwa kuwa hakuna aliyeona.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo; - Angalia kwa kugusa msinyao wa kizazi kila

dakika 15 kwa saa mbili za kwanza.- Kama kizazi ni laini, kisugue mpaka kiwe

kigumu.- Kama kizazi kilikuwa kigumu, baadae kikawa

laini, angalia kujaa kwa kibofu.- Msaidie mama akojoe kama kibofu kimejaa.- Mweleze mama akujulishe kama ataona

utokaji mkubwa wa damu au matone yasiyoisha.

Angalizo kwa huduma ya ziadaKama wanamafunzo wana mafunzo ya ziadana idhini, watende kazi ndani ya mawanda ya utendaji wao; hii ni pamoja na kuweka katheta kwenye kibofu cha mama kama hawezi kukojoa.

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kuangalia msinyao wa kizazi na kutambua kwa nini ni laini.

Dondoo muhimu- Kizazi kinaweza kubadilika kutoka

hali ya ulaini kwenda hali ugumu au ugumu kwenda ulaini

- Kukagua mara kwa mara kizazi na utokaji wa damuni muhimu sana kwa saa 24 ya kwanza, na lazima ifanyike kila dakika 15 kwa saa mbili za kwanza.

- Kibofu cha mkojo kilichojaa kinaweza kufanya kizazi kiwe laini.

- Mweleze mama akujulishe mara aonapo mbubujiko wa damu au matone endelevu

Angalia kwa kugusa kama kizazi ni kigumu

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Utokaji mwingi wa damu isiopungua ni wazi

kuwa unahatarisha maisha.- Mchirizi mdogo wa damu isiopungua

unahatarisha maisha pia.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kuangalia utokaji wa damu wakati

unaangalia msinyao wa kizazi.- Kuangalia damu kitandani, kwenye nguo za

mama na sakafuni.- Kama kizazi kimesinyaa na utokaji damu ni

mdogo, endelea kuangalia kwa ukaribu.- Mweleze mama akujulishe kama anahisi

damu zinatoka kwa wingi au matone yasiyoisha.

- Sasa ni wakati wa kuangalia michaniko

2 2

Je, utokaji wa damu ni wa kawaida?

Matarajio ya utendajiMtoa huduma atajiamini zaidi katika kupima kama utokaji wa damu baada ya kujifungua ni wa kawaida au mwingi.

Dondoo muhimu- Utokaji damu kunaweza kuwa ki-

dogo kidogo au mwingi- Utokaji wowote wa damu, kama

umezidi, unahatarisha maisha.- Damu inaweza kunyonywa kwenye

nguo au kumwagika chini.- Kukagua mara kwa mara msinyao wa

kizazi na utokaji wa damu ni muhimu kwa masaa mawili ya kwanza.

- Mwambie mama akujulishe aonapo utokaji wa damu nyingi.

Jiulize

Je, ni utokaji gani wa damu ni hatari kwa maisha ya mama?

Kwanini ni muhimu kwa mtoa huduma kuangalia utokaji wa damu kwa mama mara kwa mara?

2 3

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Kuwaweka mama na mtoto pamoja na katika

hali ya joto ni muhimu kwa afya ya wote.- Kama mama na mtoto wana afya nzuri,

unyonyeshaji uanzishwe mapema iwezekanavyo baada ya kujifungua.

- Unyonyeshaji pia unatoa oksitosin, na inaweza kusaidia kizazi kusinyaa.

- Kukagua mara kwa mara kusinyaa kwa kizazi cha mama na utokaji wa damu ni sehemu muhimu ya huduma ya kawaida kwa saa 24 za kwanza.

- Kibofu cha mama kikijaa, kinaweza kuzuia kizazi kusinyaa.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kama mtoto analia na kuhema kwa kawaida,

mweke mtoto kwenye ngozi ya mama mapema iwezekanavyo.

- Wasaidie mama na mtoto kuanza unyonyeshaji

- Waweke mama na mtoto katika hali ya joto.- Wakague mara kwa mara mama na mtoto

kwa saa 24 za kwanza.- Angalia msinyao wa kizazi na kuangalia

utokaji wa damu kila dakika 15 ndani ya saa mbli za kwanza.

- Mhimize mama akojoe mara kwa mara.

Matarajio ya utendajiMtoa huduma atakuwa na uwezo wa kutoa huduma ya kawaida kwa mama na mtoto baada ya kujifungua.

Dondoo muhimu- Muda wote waweke mama na mtoto

pamoja.- Mama aanze kunyonyesha mapema.- Kuwakagua mara kwa mara mama

na mtoto ni muhimu katika kipindi hiki.

- Angalia msinyao wa kizazi na utokaji wa damu kila baada ya dakika 15 kwa saa mbili za kwanza baada ya kujifungua.

Endeleza huduma za kawaida kwa mama na mtoto

Ukisiaji wa utokaji wa damu- Ni rahisi kufanya makadirio ya chini.- Utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua

ni upoteaji wa damu unaozidi mililita 500.- Ni muhimu kupima maendeleo ya mama.

Hata kama utokaji wa damu ni kidogo , dalili za kuonyesha kuwa damu nyingi imepotea kwa mama inajumuisha kutokwa kwa jasho, kuhema kwa nguvu, kuwa na wasiwasi, kiu, na kizunguzungu. Kwa kuongezea, mapigo ya moyo ya zaidi ya 110, au kipimo cha shinikizo la damu la juu kuwa chini ya 100, ni dalili za upotevu wa damu nyingi na hapo huduma ya ziada itahitajika.

MazoeziFanya mazoezi ya hatua ya tatu ya uchungu katika vikundi vya watu sita au pungufu vikiwa na mwezeshaji mmoja. Fanya mazoezi ya kuzalisha mtoto na uendelee mpaka hatua ya tatu ya uchungu AU tayarisha igizo la jinsi mtoto anavyokaa tumboni mwa mama wakati kiunga mwana hakijakatwa. Fanya mazoezi ya hatua ya tatu ya uchungu kana kwamba unamfanyia mzazi halisi. Kila mwanamafunzo atachukua zamu yake ya kuhudumia hatua ya tatu ya uzazi.

Toa mwongozo kadiri unavyohitajikana uwaeleze wanamafunzo kupitia hatua zinazooneshwa kwenye mpangokazi. Ni muhimu kutoa mrejesho kwa wanamafunzo wapi wamefanya vizuri na nini kifanyike kuboresha zaidi.

2 4

Dondoo muhimu- Kumbuka kuwa utokaji wa damu

unaweza kuwa kwa mbubujiko mkubwa, au kidogokidogo kwa matone ya endelevu, na aina zote ni hatari.

- Ni vigumu kukisia utokaji wa damu kwa macho.

- Uamuzi unapaswa uongozwe na dalili za mama.

- Kufanyia mazoezi hatua ya tatu ya uzazi ni muhimu ili kukusaidia kukumbuka mtiririko mzima.

MAZOEZI YA KUJIFUNZA

Mahitaji kwa mazoezi- Mahitaji ya uzazi (uk 9)- Vitambaa- Gozi - Mfano wa damu- Kifani cha mjamzito na mtoto mchanga

Angalizo kwa uwezeshajiTayarisha kila kitu kabla ya mazoezi. Vifaa hivi vitatumika wakati wa maonyesho.

2 5

au

Kuwanusuru Wakina Mama Utokaji damu baada ya kujifungua

Uzazi (angalia mpango kazi wa Kusaidia Watoto Kupumua)

Mpatie dawa ndani ya dakika 1

Kata kiunga mwana ndani ya dakika 1-3

Vuta kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma na dhibiti kizazi

Rudia kuvuta kiunga mwana dhibiti kizazi

Limetoka

Limetoka

Halijatoka ndani ya dakika 60

Halijatoka ndani ya dakika 30 Mhamasishe akojoe

Rudia 10 IU ya Oksitosin

Je, kondo limetoka?

Angalia kama kizazi kimesinyaa

kondo la nyma ni kamili ?

kizazi ni kigumu?

utokaji wa damu ni wa kawaida?

Sio kamili

KigumuKigumu

Kigumu

Ni Kamili

Laini

Laini

Mpatie huduma ya ziada

Sugua kizazi

Sugua kizaziRudia dawa

Kawaida

Endelea na huduma:Mhamasishe mama kunyonyesha

Angalia msinyao wa kizazi Fuatilia utokaji wa damu

Angalia hali ya mtoto na mama

Gandamiza mchaniko

Gandamiza kizazi

Huduma ya ziadaMfunike mama apate joto

KigumuDamu nyingi

LainiDamu nyingi

KigumuDamu ya kwaida

Sugua ikiwa ni laini

MPANGO KAZIJiandae kwa uzazi

© 2015 Jhpiego Corporation

All rights reserved

ISBN 978-1-943408-07-8

10 IU 200mcg x 3 = 600 mcg

Je,

Je,

Je,

20-09268 Rev A

Dakika yadhahabu

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Kondo la nyuma linapaswa kutoka baada

ya dakika nane hadi tisa baada ya mtoto kuzaliwa, lakini linaweza kuchukua hadi saa moja.

- Kama kondo la nyuma halijatoka ndani ya dakika 30, rudia uniti 10 za oksitosin. USIRUDIE misoprostal.

- Inaweza kuchukua misinyao kadhaa kwa kondo la nyuma kutoka.

- Kama kondo la nyuma halijatoka ndani ya saa moja, hatari ya kutokwa na damu nyingi na uwezekano wa maambukizo unaongezeka.

- Kama mama anatokwa na damu nyingi wakati wote, msaada wa ziada unahitajika kwa haraka hata kama kondo la nyuma limetoka au la.

- Kama kondo la nyuma halijatoka ndani ya dakika 30 na utokaji wa damu wa mama ni wa kawaida, mtoa huduma anaweza kusubiri kwa dakika zingine 30, lakini aanze kuwasiliana na msaada wa ziada.

- Kondo la nyuma likikwama linaweza lisisababishe damu nyingi kutoka mwanzoni, lakini inaweza kuwa hatari sana kwa mama.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kuandika muda wa mtoto kuzaliwa- Kutambua kama utokaji wa damu ya mama

ni wa kawaida au mwingi.- Kama mama anatokwa na damu nyingi,

omba msaada wa ziada.- Kama utokaji wa damu ya mama ni wa

kawaida na ni chini ya nusu saa tangu mtoto azaliwe, omba msaada wa ziada

- Msaidie mama kubadili namna ya ulalaji, kunyonyesha, na kukojoa, vyote hivi vinaweza kusaidia kondo la nyuma kutoka.

2 6

Kama kondo la nyuma halijatoka...

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kutambua kondo la nyuma lililokwama na kuchukua hatua za kupata msaada wa ziada.

Dondoo muhimu- Kondo la nyuma kwa kawida linatoka

ndani ya dakika 10, lakini linaweza kuchukua hadi saa moja.

- Kama kondo la nyuma halijatoka ndani ya dakika 30 na mama hatokwi na damu nyingi unaweza kusubiri kwa muda wa saa moja.

- Kama kondo la nyuma halijatoka baada ya saa moja na mama ana-tokwa na damu nyingi, omba msaada wa ziada.

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Kama kondo la nyuma halijatoka ndani ya

dakika 30 na utokaji wa damu ni wa kawaida mtoa huduma anaweza kusubiri hadi saa moja kabla ya kuomba huduma ya ziada.

- Kuvuta kiunga mwana kwa nguvu au wakati unahisi ukinzani ni hatari! Unaweza kutoa kizazi nje au kukatika kwa kiunga mwana na kufanya kuwa vigumu kutoa kondo la nyuma na kusababisha damu nyingi kutoka.

- Kama utokaji damu unaongezeka, msaada wa ziada unahitajika

- Kama kondo la nyuma halijatoka ndani ya saa moja, msaada wa ziada unahitajika.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kama kondo la nyuma halijatoka ndani ya

dakika 30, mhamasishe mama akojoe,na kama kondo la nyuma halijatoka,rudia uniti 10 za oksitosin, USIRUDIE misoprostol

- Wakati wa msinyao, kwa taratibu na uangalifu vuta kiunga mwana kuelekea chini kwa kila msinyao kwa kulisaidia kondo la nyuma kutoka.

- Zuia kizazi kwa mkono mmoja juu ya mfupa wa kinena

- Kama ugumu ukihisiwa, acha na ujaribu tena wakati wa msinyao unaofuata.

- Endelea kuvuta kiunga mwana huku ukiendelea kuzuia kizazi wakati wa KILA msinyao mpaka kondo la nyuma litakapojitokeza kwenye uwazi wa njia ya uzazi.

- Endelea kuangalia utokaji wa damu wa mama na wasiliana kwa msaada wa ziada kwa uwezekano wa kusaidiwa

- Wasiliana na msaada wa ziada ikiwa kondo halijatoka ndani ya saa moja au kama mama anatokwa na damu nyingi

Angalizo kwa huduma ya ziadaWanamafunzo wafanye ndani ya mawanda ya utendaji wao; hii inaweza kujumuishakuvuta kiunga mwana na kurudia dawa ya oksitosin kama ulivyooneshwa kurudia hapa.

2 7

Matarajio ya utendajiMtoa huduma mwenye ujuzi ataweza kuvuta kiunga mwana kutoa kondo la nyuma lililokwama ili kupunguza utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua.

Dondoo muhimu- Endelea kuvuta kiunga mwana

wakati wa kila msinyao, lakini kamwe isiwe wakati hakuna msinyao

- Uvutaji wa kiunga mwana lazima uwe wa uangalifu.

- Mara zote tumia mkono mwingine kuzuia kizazi kisitoke wakati unavuta kiunga mwana

- Kamwe usivute kiunga mwana kama ukihisi ugumu au ukinzani.

- Kuvuta kwa nguvu au ukihisi ukinzani unaweza kuchana/kata kiunga mwana au ukatoa nje kizazi.

- Kama kondo la nyuma halijatoka baada ya dakika 30, rudia kuchoma uniti 10 oksitosin kwenye msuli.

Rudia oksitosin uniti 10

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa- Kama mama anatokwa na damu nyingi wakati

wote, msaada wa ziada unahitajika haraka hata ikiwa kondo la nyuma limetoka au la.

- Kama kondo la nyuma halijatoka ndani ya saa moja, msaada wa ziada bado utahitajika hata kama mama hatokwi na damu.

- Kondo la nyuma lililobaki linaweza lisisababishe damu nyingi kutoka kwa wakati huo, lakini inaweza kuwa hatari sana.

- Kondo la nyuma lisilokamilika linaweza kuwa vigumu kulitambua

- Utokaji wa damu endelevu, wa matone au mwingi ulio mwekundu mwangavu inaweza

ama kipande cha kondo la nyuma kimebaki kwenye kizazi na kitasababisha utokaji wa damu uendelee.

- Kama kizazi kimepanda juu ya kitovu, inaweza kumaanisha kuwa mabonge ya damu yanajiunda ndani yake.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kufuatilia ni muda gani umepita tangu mtoto

alipozaliwa- Kagua kondo la nyuma kama limekamilika .- Kupima kusinyaa na kimo cha kizazi cha

mama, wakati huohuo akiangalia utokaji wa damu.

- Kufuatilia mapigo ya moyo na shinikizo la damu ya mama kwa kuangalia dalili za shoku (mapigo ya moyo juu ya zaidi ya 110, na ya chini yakiwa chini ya 100)

- Kuwasiliana na watoa huduma wenyeji wanaoweza kutoa huduma ya ngazi ziada.

- Kama msaada waziada haupatikani hapo, usafiri kwenda kituo cha huduma ya ziada unahitajika.

Angalizo kwa huduma ya ziadaKama wanamafunzo wana mafunzo ya ziada na mamlaka ya kutoa huduma ya kiwango cha juu, wafanye ndani ya mawanda ya utendaji wao. Hii ni pamoja na kumtoa mama mkojo kwa mpira na kutoa kwa mkono sehemu au kondo lote la nyuma.- Kama kondo la nyuma limetolewa

kwa mkono, mama atahitaji antibiotiki kupunguza hatari ya maambukizo.

- Utoaji wa kondo la nyuma kwa mkono isijaribiwe HATA MARA MOJA bila mafunzo kamili na mamlaka.

- Utoaji wa kondo la nyuma kwa mkono inamuumiza mama na inaweza kuwa hatari

- Mafunzo stahiki na ya juu yanahitajika ili kufanya hili kwa usalama na ufasaha.

2 8

Kama kondo la nyuma halijatoka au halijakamilika

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kutumia ujuzi wa maamuzi kwa kutambua kondo la nyuma lililokwama au lisilokamili na kuchukua hatua ipasayo.

Dondoo muhimu- Kondo la nyuma lisilokamili au

lililokwama linahitaji msaada wa ziada- Msaada wa ziada unahitajika kwa.

mama yeyote ambaye kondo la nyuma halijatoka ndani ya saa moja hata kama mama hatokwi na damu nyingi.

au

Kuwanusuru Wakina Mama Utokaji damu baada ya kujifungua

Uzazi (angalia mpango kazi wa Kusaidia Watoto Kupumua)

Mpatie dawa ndani ya dakika 1

Kata kiunga mwana ndani ya dakika 1-3

Vuta kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma na dhibiti kizazi

Rudia kuvuta kiunga mwana dhibiti kizazi

Limetoka

Limetoka

Halijatoka ndani ya dakika 60

Halijatoka ndani ya dakika 30 Mhamasishe akojoe

Rudia 10 IU ya Oksitosin

Je, kondo limetoka?

Angalia kama kizazi kimesinyaa

kondo la nyma ni kamili ?

kizazi ni kigumu?

utokaji wa damu ni wa kawaida?

Sio kamili

KigumuKigumu

Kigumu

Ni Kamili

Laini

Laini

Mpatie huduma ya ziada

Sugua kizazi

Sugua kizaziRudia dawa

Kawaida

Endelea na huduma:Mhamasishe mama kunyonyesha

Angalia msinyao wa kizazi Fuatilia utokaji wa damu

Angalia hali ya mtoto na mama

Gandamiza mchaniko

Gandamiza kizazi

Huduma ya ziadaMfunike mama apate joto

KigumuDamu nyingi

LainiDamu nyingi

KigumuDamu ya kwaida

Sugua ikiwa ni laini

MPANGO KAZIJiandae kwa uzazi

© 2015 Jhpiego Corporation

All rights reserved

ISBN 978-1-943408-07-8

10 IU 200mcg x 3 = 600 mcg

Je,

Je,

Je,

20-09268 Rev A

Dakika yadhahabu

2 9

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Kufahamu muda gani na wapi pa kupata

msaada ni muhimu sana inaokoa maisha.- Watoa msaada wa ziada wanaweza kutoka

kwenye jamii au wanaweza kufika kituoni haraka.

- Watoa msaada wa ziada wenye mafunzo na ujuzi zaidi kwa vitu kama kuweka /dripu na kutoa kondo la nyuma kwa mkono.

- Ni muhimu kuwafahamu wanaoweza kutoa huduma hii kabla ya dharura kutokea.

- Watoa huduma wa afya wa ziada wanajumuisha, wakunga, baadhi ya madaktarii, wauguzi na baadhi ya watoa tiba wasio matabibu.

- Taarifa za mawasiliano na watoa huduma wa ziada lazima ziwepo.

- Kama msaada wa ziada haupatikani kwa haraka, mama lazima asafirishwe kwenda kwenye huduma ya ngazi ya juu.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kutoa huduma zile ulizofundishwa tu. Kutoa

huduma bila mafunzo stahiki ni hatari.- Kuwa na mawasiliano (namba ya simu au

anuani) za watoa huduma wenyeji - Mchague mwanafamilia ili kwenda pamoja

kupata msaada wa ziada.- KAMWE usimwache mama peke yake.- Kama msaada wa ziada haupatikani kwa

haraka andaa mpango wa usafari.

3 0

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kuandaa mpango ili kupata msaada wa ziada ukihitajika

Dondoo muhimu- Kupata huduma ya ziada kwa haraka

kunaweza kuokoa maisha ya mama.- Usimwache mama peke yake ili

kutafuta msaada.

Pata huduma ya ziada

Jiulize

Je, ni kwanini huduma ya ziada inahitajika?

Je, ni wakati gani mtoa huduma anatakiwa afikirie kuomba huduma ya ziada?

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Kuchelewa kupata huduma inayohitajika ni

moja ya sababu kubwa za vifo vya wazazi kwa kutokwa na damu nyingi.

- Kujua wapi mama apelekwe na namna ipi ya kumfikisha kutapunguza ucheleweshwaji

- Kujulisha kituo cha rufaa kwamba unampeleka mama ili wajiandae kwa dharura.

- Kumsafirisha mama wakati ana nguvu ni salama kuliko kusubiri mpaka ifikie hali ya dharura.

- Kuwa na mpango mbadala wa usafiri ni muhimu ikitokea gari kuharibika au barabara kutokupitika.

- Mama na mtoto lazima wawekwe pamoja.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Aandae mpango madhubuti wa usafiri

kwenda kwenye hudumaya ziada - Mipango ijumuishe namna mbadala ya

usafiri, njia ya kupitia, watu wa kuwasiliana nao, na vituo kadiri inavyowezekana.

- Kuwaweka mama na mtoto pamoja na kuhakikisha wanapata joto wakati wote wa safari.

- Kufuatilia mabadiliko ya kutokwa na damu,shinikizo la damu, upumuaji,joto la mwili, mzunguko wa damu na kama kondo la nyuma limetoka wakati wa safari.

3 1

Rufaa kwa huduma ya ziada

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kuandaa mpango madhubuti wa usafiri.

Dondoo muhimu- Wajulishe kituo cha rufaa kuwa

unampeleka mama.- Ni vizuri umsafirishe mama wakati

ana nguvu badala ya kusubiri.- Mama na mtoto lazima wawekwe

pamoja.- Endelea kumwangalia mama kwa

mabadiliko ya hali yake njia nzima ni muhimu

Angalizo kwa wawezeshajiKama sehemu ya mazoezi yanayoendelea pitia mpangokazi wa usafiri wa kituoni kwako pamoja na wafanyakazi na hakikisha kila mmoja anafahamu mpangokazi huo. Hii ni lazima ijumuishe mipango mingine ikiwa barabara imefungwa au gari imeharibika. Kama hamna mpango, anzisha sasa.

Jiulize

Je, ni nani wa kuongozana na mama na kwa sababu gani?

Je, ni vitu gani muhimu vya kumuangalia mama wakati wa usafiri?

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Michubuko au michaniko ni kisababishi cha

pili kikubwa cha utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua.

- Mama anaweza kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua kwa sababu zaidi ya moja ikiwa michaniko na kizazi ni laini.

- Mama aliyekeketwa au aliyeongezewa njia ana uwezekano mkubwa wa kutokwa na damu nyingi kutokana na michubuko/michaniko.

- Uongezaji njia ya uzazi usifanywe kwa mama yeyote isipokuwa kama kuna ulazima

- Uongezaji njia ya uzazi ufanywe tu na mtoa huduma mwenye ujuzi.

- Kama michaniko iko ndani zaidi kwenye uke au kwenye shingo ya kizazi, unaweza ushindwe kuona.

- Kama kizazi ni kigumu na mama anaendelea kutokwa na damu, lakini huoni mchaniko wowote, msaada wa ziada na wakati mwingine usafiri vitahitajika.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kupunguza hatari ya maambukizo, endeleza

usafi kwa tahadhari zinazokubalika wakati unapoangalia michaniko ya mama.

- Futa damu kwa umakini kwenye msamba wakati wa kuangalia michaniko.

- Kwa umakini kagua michaniko- Endelea kupima kizazi kila dakika 15 kwa saa

mbili za kwanza baada ya mama kujifungua, kuwe au kusiwe na utokaji wa damu nyingi kutoka kwenye michaniko

- Pata msaada wa ziada kama kizazi ni kigumu na huoni michaniko na mama anatokwa na damu sana.

Angalizo kwa huduma ya ziadaKama mwanamafunzo ana mafunzo ya ziada na mamlaka ya kutoa huduma ya ngazi ya juu zaidi, ni lazima wafanye ndani ya mawanda ya kazi zao; hii ni pamoja na kukagua shingo ya kizazi kwa michaniko.

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kumkagua mama kwa michaniko na kuamua hatua sahihi ya kuchukua ili kuweza kudhibiti utokaji wa damu kutoka kwenye michaniko.

Dondoo muhimu- Kama kizazi ni kigumu na mama

bado anazidi kutokwa na damu nyingi, uwezekano ni michaniko hata kama haionekani. Pata msaada wa ziada haraka.

Angalia michaniko

3 2

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Kugandamiza kwa muda mrefu, kunasaidia

damu kuganda na kupunguza utokaji wa damu.

- Michaniko na michubuko vinaongezea uwezekano wa mama kupata maambukizo. Mbinu safi na tahadhari zinazokubalika kutapunguza maambukizo na kumlinda mama.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo- Kuvaa glovu na aendeleze usafi na tahadhari

zilizokubalika ili kupunguza hatari ya maambukizo kwa mama.

- Gandamiza kwenye michaniko kwa kutumia kitambaa safi au kilichotakaswa

- Gandamiza na kushikilia kwa muda mpaka pale damu inapopungua au iachapo kutoka.

- Wakati damu ikipungua au kuacha kutoka, acha kitambaa hapo na mlaze mama upande. Miguu yake iliyobanwa itaendeleza kubana michaniko.

- Kama damu imelowanisha kitambaa, usikiondoe. Weka kitambaa kingine juu ya kilicholowana, endelea kushikilia na kungandamiza omba msaada wa ziada.

Angalizo kwa huduma ya ziadaKama wanamafunzo wana mafunzo ya ziadana ana mamlaka, ni lazima wafanye ndani ya mawanda ya utendaji wao ikiwa ni pamoja na kushona michaniko.

Gandamiza michaniko

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kuthibiti utokaji wa damu kutoka michaniko inayoonekana.

Dondoo muhimu- Gandamiza michaniko kupunguza utokaji wa damu - Tumia kitambaa kisafi au kilichotakaswa kugandamiza ili kupunguza hatari ya maambukizo

3 3

au

Kuwanusuru Wakina Mama Utokaji damu baada ya kujifungua

Uzazi (angalia mpango kazi wa Kusaidia Watoto Kupumua)

Mpatie dawa ndani ya dakika 1

Kata kiunga mwana ndani ya dakika 1-3

Vuta kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma na dhibiti kizazi

Rudia kuvuta kiunga mwana dhibiti kizazi

Limetoka

Limetoka

Halijatoka ndani ya dakika 60

Halijatoka ndani ya dakika 30 Mhamasishe akojoe

Rudia 10 IU ya Oksitosin

Je, kondo limetoka?

Angalia kama kizazi kimesinyaa

kondo la nyma ni kamili ?

kizazi ni kigumu?

utokaji wa damu ni wa kawaida?

Sio kamili

KigumuKigumu

Kigumu

Ni Kamili

Laini

Laini

Mpatie huduma ya ziada

Sugua kizazi

Sugua kizaziRudia dawa

Kawaida

Endelea na huduma:Mhamasishe mama kunyonyesha

Angalia msinyao wa kizazi Fuatilia utokaji wa damu

Angalia hali ya mtoto na mama

Gandamiza mchaniko

Gandamiza kizazi

Huduma ya ziadaMfunike mama apate joto

KigumuDamu nyingi

LainiDamu nyingi

KigumuDamu ya kwaida

Sugua ikiwa ni laini

MPANGO KAZIJiandae kwa uzazi

© 2015 Jhpiego Corporation

All rights reserved

ISBN 978-1-943408-07-8

10 IU 200mcg x 3 = 600 mcg

Je,

Je,

Je,

20-09268 Rev A

Dakika yadhahabu

3 4

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Kizazi kisichosinyaa au kilichobaki laini baada

ya kutoka kwa kondo la nyuma, huwa ni sababu kubwa ya utokaji wa damu nyingi baada ya kujifungua.

- Kizazi kinaweza kuwa kigumu baada ya kujifungua, lakini kikabadilika kuwa laini.

- Kizazi na utokaji wa damu upimwe kila dakika 15 ndani ya saa mbili za kwanza baada ya kujifungua na mara kwa mara kwa

saa 24. Hii ni muhimu sana.- Kama utokaji wa damu wa mama ulikuwa

wa kawaida lakini ukaongezeka, kizazi chake kiguswe kama ni kigumu.

- Kusugua kizazi kunaweza kufanya kizazi laini kuwa kigumu; kunaweza pia kufanya mabonge ya damu yatoke, ambayo hupunguza utokaji wa damu.

- Kuangalia jinsi mama anavyotokwa na damu wakati ukisugua kizazi ni muhimu kwa kuona kama damu inapungua kadiri kizazi kinavyokuwa kigumu.

- Kibofu kilichojaa kinasababisha kizazi kuwa laini pia.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo- Kugusa ili kuona kama kizazi ni laini na kama

utokaji wa damu ni zaidi.- Gandamiza kwa uthabiti kwenye tumbo la

mama, chini ya kitovu kukihisi kizazi.- Kama ni laini, sugua kwa mwendo wa

mzunguko mpaka ukihisi kizazi ni kama mpira mgumu na damu kupungua. Kitakuwa kigumu kama paji lako la uso.

- Kama kibofu kimejaa, msaidie mama akojoe.- Mweleze mama akujulishe mara anapohisi

utokaji wa damu unaongezeka.

Angalizo kwa huduma ya ziadaKama mwanamafunzo ana mafunzo ya ziada na mamlaka, ni lazima wafanye ndani ya mawanda ya kazi zao. Ikiwa pamoja na kuweka katheta pale mama anaposhindwa kukojoa.

Jiulize

Je, ni dalili gani zinazoonyesha usuguaji wa kizazi kisichosinyaa unasaidia?

Je, kwanini ni muhimu kuangalia kizazi na utokaji wa damu kwa mama baada ya kujifungua?

3 5

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kutambua msinyao wa kizazi na kusugua kizazi laini ili kukifanya kigumu.

Dondoo muhimu- Kizazi laini ni sababu namba 1 ya

kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.

- Kusugua kizazi kutakifanya kisinyae.- Kizazi kinaweza kuwa kigumu,

baadaye kuwa laini. Kukagua mara kwa mara ni muhimu.

- Kibofu kilichojaa chaweza kukifanya kizazi kuwa laini.

- Kusugua kizazi na kuangalia utokaji wa damu ufanyike kila dakika 15 ndani saa mbili za kwanza baada ya kujifungua.

Sugua kizazi

Angalizo kwa huduma ya ziada;Kama mwanamafunzo ana mafunzo ya ziada na mamlaka, ni lazima wafanye ndani ya mawanda ya kazi zao. Ikiwa pamoja na kuweka dripu

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Wakati kizazi kinaposhindwa kusinyaa,

mama anakuwa kwenye hatari ya kutokwa na damu nyingi.

- Kama kizazi kikibaki laini, mama ataendelea kutokwa na damu nyingi kwa sababu mishipa midogo ya damu itaendelea kutoa damu.

- Kwa kutoa dozi ya pili ya dawa kunaweza kusaidia kizazi kusinyaa, kupunguza au hata kukatisha utokaji wa damu.

- Mwendelezo wa kusugua kizazi kunasaidia kizazi kusinyaa

- Kama kizazi hakisinyai kwa usuguaji na dawa, usafiri wa haraka kwenda kwenye huduma ya ziada utahitajika.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kuangalia utokaji wa damu wa mama wakati

akisugua kizazi- Kutathmini kama usuguaji unasaidia- Kama kizazi hakiwi kigumu na damu

haipungui ongeza dozi ya pili ya dawa ya oksitosin

- Endelea kusugua kizazi na angalia utokaji wa damu.

- Kizazi laini kinachotoa damu nyingi bila kukoma ni hatari! Wakati ukisubiri kuona kama dozi ya pili ya dawa na usuguaji zinafanya kazi, fikiria kuhusu mkakati wa usafiri. Kama mzazi anatokwa na damu nyingi, iwe kizazi kimesinyaa au la, atahitaji kwa haraka huduma ya ziada.

3 6

Sugua kizazi. Rudia dawa

Matarajio ya utendajiMtoa huduma atathibiti utokaji wa damu baada ya kujifungua kutokana na kizazi kutosinyaa.

Dondoo muhimu- Kusugua kizazi na kurudia uniti 10

oksitosin inasaidia kizazi kusinyaa. Kama oksitosin haipo, unaweza kutoa mcg 200 sawa na kidonge kimoja cha misoprostal.

- Kama kizazi hakiwi kigumu baada ya kusugua na kutoa dawa, usafiri wa haraka unahitajika.

- Anzisha dripu

Dozi ya mara ya pili yaOKSITOSIN unit 10 na mcg 200 au kidonge 1 ya MISOPROSTOL.

au

Kuwanusuru Wakina Mama Utokaji damu baada ya kujifungua

Uzazi (angalia mpango kazi wa Kusaidia Watoto Kupumua)

Mpatie dawa ndani ya dakika 1

Kata kiunga mwana ndani ya dakika 1-3

Vuta kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma na dhibiti kizazi

Rudia kuvuta kiunga mwana dhibiti kizazi

Limetoka

Limetoka

Halijatoka ndani ya dakika 60

Halijatoka ndani ya dakika 30 Mhamasishe akojoe

Rudia 10 IU ya Oksitosin

Je, kondo limetoka?

Angalia kama kizazi kimesinyaa

kondo la nyma ni kamili ?

kizazi ni kigumu?

utokaji wa damu ni wa kawaida?

Sio kamili

KigumuKigumu

Kigumu

Ni Kamili

Laini

Laini

Mpatie huduma ya ziada

Sugua kizazi

Sugua kizaziRudia dawa

Kawaida

Endelea na huduma:Mhamasishe mama kunyonyesha

Angalia msinyao wa kizazi Fuatilia utokaji wa damu

Angalia hali ya mtoto na mama

Gandamiza mchaniko

Gandamiza kizazi

Huduma ya ziadaMfunike mama apate joto

KigumuDamu nyingi

LainiDamu nyingi

KigumuDamu ya kwaida

Sugua ikiwa ni laini

MPANGO KAZIJiandae kwa uzazi

© 2015 Jhpiego Corporation

All rights reserved

ISBN 978-1-943408-07-8

10 IU 200mcg x 3 = 600 mcg

Je,

Je,

Je,

20-09268 Rev A

Dakika yadhahabu

3 7

3 8

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa; - Mara nyingine misuli ya kizazi haikubali

kusinyaa kwa dawa na kusugua.- Kizazi kinaweza kuwa laini na kuendelea

kutoa damu nyingi sana.- Ni muhimu kuchukua hatua za haraka ili

kupunguza kiasi cha damu kinachopotea.

- Kugandamiza kizazi katikati ya mikono yako kunabana mishipa midogo ya damu na inaweza kusaidia kizazi kusinyaa na kuacha kutoa damu nyingi.

- Ugandamizaji wa kizazi unaongeza hatari ya maambukizo.

- Mtoa huduma ni lazima awe na mikono misafi sana na glovu ndefu zilizotakaswa ili kukinga kusababishia maambukizo ndani ya kizazi cha mama.

- Wakina mama wanaohitaji afua hii tayari wameshapoteza damu nyingi na wana uwezekano wa kutokwa na damu tena.

- Wazazi hawa wanahitaji kuangaliwa kwa karibu zaidi na kwa muda mrefu kuliko wakina mama wasio na utokaji mwingi wa damu.

- Wazazi hawa wanahitaji kusafirishwa kwenye ngazi ya juu zaidi ya huduma kwa vile wapo hatarini kwa maambukizo na upungufu wa damu.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kunawa mikono yake na avae glovu zilizo

takaswa ambayo zinafikia kwenye kiwiko. Tumia dawa ya kusafisha mikono kama maji hayapatikani kwa urahisi.

- Mweleze mama kwa kifupi kitu unachotaka kumfanyia.

- Kwa taratibu ingiza mkono ukeni. Uingizaji uwe wa taratibu na kwa makini kwa vile huduma hii inaleta maaumivu kwa mama.

- Ingiza mkono wako ndani kabisa ukeni mbele ya kizazi. Usiingize mkono wako ndani ya kizazi.

- Weka mkono wako mwingine juu ya tumbo la mama na ubane kizazi katikati ya kiganja na ngumi.

- Wakati kizazi kitakapoanza kusinyaa na damu kuacha kutoka kwa polepole achia msukumo kwa mkono wako ulio tumboni.

- Fungua ngumi na pole pole toa mkono wako ukeni, ukitoka na mabonge ya damu yaliyopo.

- Kama inawezekana mwombe mtu mwingine kufanya mpango wa usafiri wakati wewe unamhangaikia mama.

Matarajio ya utendaji- Mtoa huduma anataweza kufanya kwa usalama na kwa ufasaha ugandamizaji wa kizazi kinachotoa damu nyingi kwa mikono miwili.

Dondoo muhimu- Kukandamiza kizazi hufanyika kwa

dharura pale ambapo mbinu zingine zimeshindwa kuzuia damu nyingi kutoka

- Kuweka kitu chochote ukeni kunaweza kusababisha

maambukizo.- kunawa mikono vizuri na uvaaji wa

glovu zilizotakaswa zinazofikia us- awa wa kiwiko ni muhimu ili kupun- guza uwezekano wa maambukizo.

- Kandamiza kizazi kwa ngumi iliyo ndani kabisa ya uke na mkono ulio juu ya tumbo, mpaka pale damu itakapoacha na kizazi kuwa kigumu –angalau dakika 5.

- Baada ya hapo usafiri utahitajika.

Kandamiza kizazi

au

Kuwanusuru Wakina Mama Utokaji damu baada ya kujifungua

Uzazi (angalia mpango kazi wa Kusaidia Watoto Kupumua)

Mpatie dawa ndani ya dakika 1

Kata kiunga mwana ndani ya dakika 1-3

Vuta kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma na dhibiti kizazi

Rudia kuvuta kiunga mwana dhibiti kizazi

Limetoka

Limetoka

Halijatoka ndani ya dakika 60

Halijatoka ndani ya dakika 30 Mhamasishe akojoe

Rudia 10 IU ya Oksitosin

Je, kondo limetoka?

Angalia kama kizazi kimesinyaa

kondo la nyma ni kamili ?

kizazi ni kigumu?

utokaji wa damu ni wa kawaida?

Sio kamili

KigumuKigumu

Kigumu

Ni Kamili

Laini

Laini

Mpatie huduma ya ziada

Sugua kizazi

Sugua kizaziRudia dawa

Kawaida

Endelea na huduma:Mhamasishe mama kunyonyesha

Angalia msinyao wa kizazi Fuatilia utokaji wa damu

Angalia hali ya mtoto na mama

Gandamiza mchaniko

Gandamiza kizazi

Huduma ya ziadaMfunike mama apate joto

KigumuDamu nyingi

LainiDamu nyingi

KigumuDamu ya kwaida

Sugua ikiwa ni laini

MPANGO KAZIJiandae kwa uzazi

© 2015 Jhpiego Corporation

All rights reserved

ISBN 978-1-943408-07-8

10 IU 200mcg x 3 = 600 mcg

Je,

Je,

Je,

20-09268 Rev A

Dakika yadhahabu

3 9

4 0

Mtoa huduma anatakiwa kufahamu kuwa;- Uchelewaji wa kupata huduma inayopaswa

ni sababu mojawapo ya vifo vya wakina mama vinavyotokana na utokaji wa damu nyingi.

- Kufahamu wapi pa kumpeleka mama na namna ya kumfikisha hapo kutapunguza ucheleweshwaji huu.

- Kuwasialiana na hospitali au kituo cha afya kabla ya kufika kutapunguza muda wa kusubiri mnapofika.

- Kuwa na mpango mbadala wa usafiri ni muhimu pale gari linapoharibika au barabara kutokupitika.

- Mama na mtoto wawekwe pamoja.- Kuwaweka mama na mtoto katika hali ya

joto na kufuatilia mabadiliko yoyote ya alama muhimu au utokaji wa damu nyingi ni muhimu wakati wa safari.

- Kuendelea kusugua kizazi wakati wa safari ni muhimu kupunguza utokaji wa damu nyingi.

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Watoa huduma wote wanapaswa waweze

kuelezea mkakati wa kituo wa usafiri kwenda kwenye huduma ya ngazi ya juu.

- Mipango inapaswa kujumuisha aina mbadala za usafiri, njia za kupita, mawasiliano, wahusika, na vituo pale inapowezekana.

- Waweke mama na mtoto pamoja na katika hali ya joto wakati wa safari.

- Fuatilia mabadiliko ya utokaji damu, dalili muhimu au kutoka kwa kondo la nyuma wakati wa safari.

4 0

Huduma ya dharura na usafiri

Matarajio ya utendajiMtoa huduma ataweza kumsafirisha mama salama.

Dondoo muhimu- Kama mama anaendelea kutokwa

na damu nyingi, usafiri wa dharura ni lazima.

- Iwapo mkandamizo wa mikono miwili umefanyika, usafiri kwenda huduma ya ziada unahitajika hata kama damu imepungua au imekoma kutoka .

- Mama na mtoto wawekwe pamoja.- Kumwangalia mama kwa mabadiliko

ya hali ni muhimu sana kwa wakati wote wa safari.

- Mpango mbadala wa usafiri unapaswa kuwapo pale itakapotokea barabara imefungwa au gari kuharibika.

Jiulize

Je, ni kitu gani cha kukipanga katika mpango wa usafiri?

Je, ni vitu gani muhimu vya kufanya kabla ya usafiri ili kupunguza utokaji wa wa damu nyingi?

MAZOEZI WAKATI KUNA TATIZOFanya mazoezi katika timu ya watu sita au pungufu na mwezeshaji mmoja kwa kila kikundi.

Kondo la nyuma limekwama:Anza kuigiza baada ya kiunga mwana kukatwa. Mwezeshaji azuie kondo la nyumalisitoke wakati wa misinyao lakini anamweleza mtoa huduma muda tangu kujifungua (dakika 30 na 60).

Utokaji wa damu nyingi kwa ajili ya kizazi kushindwa kusinyaa:Wakati kondo la nyuma limetoka, funga shingola kizazi la mfanano kwa kamba. Anza mfanano wakati mama amepata huduma ya hatua ya tatu ya uchungu pamoja na kupewa dawa za kusinyaisha kizazi na kondo la nyuma limetoka lote. Mwezeshaji atafungua tanki la damu na ataacha kizazi laini.

FANYA VISAMKASA VYOTE VINAVYOWEZEKANAWakati bado mkiwa kwanye vikundi vya watusita au pungufu, fanya senario bila kufuata mpangilio. Mwezeshaji atachagua senario bila ya kuwaeleza wanamafunzo lakini atafanya mfanano kuonyesha hatua ya kawaida ya tatu ya uzazi, au kondo la nyuma lililokwama, au kutokusinyaa kizazi kwa hatua mbali mbali. wanamafunzo wasiofanya kisamkasa (scenario) wafuatilie kinachotokea kwenye mpangokazi ndani ya kitabu chao cha Mwongozo wa Mtoa Huduma na watoe mrejesho kwa mwanamafunzo anaefanya mazoezi.

4 1

Dondoo muhimu- Utokaji wa damu nyingi baada ya

kujifungua unaweza kuzuiwa kwa ufasaha na kutibiwa kwa kuelewa vizuri kisamkasa (scenario)

- Kufuata hatua za mpangokazi kutamwongezea kila mmoja uwezo wa kuzuia na kutibu utokaji wa damu nyingi.

- Mazoezi ya mara kwa mara ni wajibu wa timu nzima.

- Mazoezi ya mara kwa mara kutawezesha kupata ujuzi makini na wamtiririko.

MAZOEZI YA VITENDO

Angalizo kwa huduma ya ziada- Kama sehemu ya mwendelezo wa

mazoezi, panga mpango wa usafiri wa kituo chako, na hakikisha kuwa kila mmoja ana ufahamu na mpango mbadala, Kama hakuna, anzisha sasa.

- Mazoezi ya kutumia kifani cha kuzalishia mtoto ni muhimu sana kwa wanamafunzo ili kupata ujuzi. Wakati wa mazoezi ya kugandamiza kizazi kwa viganja kwa kutumia kifani ni lazima ufunge shingo ya kizazi kwa utepe. Angalia uk. 9 wa “Mwongozo wa matumizi” ya mfano wa kuzalishia.

- Kwenye kituo, mtoa huduma anayefanya kazi kwenye timu anawajibu wa kuongoza mazoezi ya kawaida yaliyopangwa kwa kutumia: kifani, bango kitita na mpangokazi

4 2

Fuatilia matukio sita(chati hii ipo kwenye Bango Kitita)

Mtoa huduma anatakiwa kufanya yafuatayo;- Kabla ya kufanya mazoezi na kifani, fuatilia

visamkasa hivi kwenye mpangokazi. Fanya kisamkasa kingine ambacho ungeweza kukiona na ukifuatilie pia.

- Wakati wanatimu wako wanafanya mazoezi, fuatilia visamkasa wanavyofanya kwenye mpangokazi.

- Toa msaada kwao kama wanavyoomba. Toa mrejesho wenye kutia moyo.

4 3

4 4

Faharasi

Fandas Fandas ni sehemu ya juu ya kizazi. Fundas ni sehemu nzuri zaidi kutambua kama kizazi ni kigumu

Hali ya msinyao Ugumu au ulaini wa kitu fulani. Kuangalia msinyao wa kizazi ni kuangalia jinsi gani misuli ya kizazi ilivyo migumu au laini.

Kibofu Kibofu ni sehemu ya mwili ambapo mkojo huhifadhiwa.

Kinzani Kinzani ni kani inayosukuma dhidi yako wakati ukitumia kani upande mwingine.

Kituo cha rufaa Ktiuo cha rufaa ni hospitali yoyote au kituo cha afya au kliniki pale ambapo huduma ya ngazi ya juu zaidi inapotolewa kwa mama.

Kizazi Kizazi ni organi ndani ya mama ambapo mtoto hukua. Inaitwa pia tumbo la uzazi.

Kondo la nyuma Kondo la nyuma ni organi ndani ya kizazi cha mama kinachomlisha mtoto wakati anapokua tumboni.

Kubaki/Kukwama Kubaki/Kukwama inamaanisha kubaki, au kushindwa kuachia. Kondo la nyuma limebaki/kwama pale kizazi kinaposhindwa kuiachia.

Kuimarisha Kuimarisha ni kufanya kitu kisisogee. Wakati unafanya mvuto wa kiunga mwana uliodhibitiwa, tunaimarisha kizazi kwa kutumia mkono kusukuma juu dhidi ya mvuto ili isisogee.

Kukeketwa Mama atakuwa amekeketwa iwapo sehemu zinazozunguka mlango wa uke zimeondolewa

Kuongeza njia ya uzazi Kuongeza njia ya uzazi ni pale mlango wa uke unapokatwa ili kuuongeza/kuupanua wakati wa uzazi

Kusinyaa Kusinyaa inamaana ya kuwa kidogo, wakati kizazi kinasinyaa, kinakuwa kidogo na kigumu.

Kusugua Kusugua ni kusugua kwa nguvu sehemu ya mwili. Baada ya kujifungua tunasugua kizazi kwa kusugua fundus ambayo husaidia kizazi kuwa kigumu

Mamlaka Mamlaka ni ruhusa kutoka serekalini au kwa mwajiri inayomruhusu mtoa huduma kufanya tendo la ujuzi au stadi

Mawasilano ya kimatendo/ ufasaha Mawasilano fasaha hutokea pale wahudumu katika timu wanapoweza kusikiliza

na kuongea wao kwa wao kwa uwazi na moja kwa moja, ili kila mmoja aelewe na wafanye kazi pamoja na mlengwa (mama na mwenzi/ndugu).

Michaniko Michaniko ni mipasuko kwenye nyama au ngozi

Msamba Msamba ni eneo kati ya mlango wa uke na mlango wa wa aja kubwa/mkundu

Msinyao Msinyao ni ile hali inayofanya kizazi kuwa kidogo, wakati misuli inapobana na kuwa ngumu.

4 5

MrejeshoAnderson, J., Etches, D. 2007. Prevention and management of postpartum hemorrhage. Am Fam Physician Mar 15;75(6): 875-882. http://ukpmc.ac.uk/abstract/MED/17390600

Hofmeyr, G.J., Abdel-Aleem H., Abdel-Aleem, M.A. 2008. Uterine massage for preventing postpartum hemorrhage. The Cochrane Collaboration. http://apps.who.int/rhl/reviews/CD006431.pdf

Pathfinder International. 2010. Clinical and Community Action to Address Postpartum Hemorrhage. http://www.pathfinder.org/publications-tools/pdfs/Clinical-and-Community-Action-to-Address-Postpartum-Hemorrhage-The-Pathfinder-International-Model.pdf?x=94&y=31

Prevention of Post Partum Hemorrhage Initiative (POPPHI). 2007. Implementing Active Management of the Third Stage of Labor. http://www.path.org/publications/files/MCHN_popphi_amtsl_ref_man.pdf

World Health Organization. 2009. WHO Guidelines for the Management of Postpartum Haemorrhage and Retained Placenta. http://whqlibdoc.who.int/publications/2009/9789241597906_eng.pdf

World Health Organization. 2009. WHO Statement Regarding the Use of Misoprostol for Postpartum Hemorrhage and Treatment. http://whqlibdoc.who.int/hq/2009/WHO_RHR_09.22_eng.pdf

World Health Organization. 2012. Recommendations for the Prevention of Postpartum Hemorrhage and Treatment. http://www.who.int/maternal_child_adolescent/documents/postpartum_haemorrge/en/

World Health Organization. 2000. Managing Complications in Pregnancy and Childbirth: A Guide for Midwives and Doctors. http://whqlibdoc.who.int/publications/2007/9241545879_eng.pdf

World Health Organization and International Confederation of Midwives. 2010. Managing Postpartum Haemorrhage. Midwifery Education Modules. 2008. http://www.who.int/maternal_child_adolescent/documents/2_9241546662/en/

Yetter, J. 1998. Examination of the Placenta. American Academy of Family Physicians.http://www.aafp.org/afp/980301ap/yetter.html.

Kuvuta kiunga mwana Kuvuta kiunga mwana ni tendo la kutoa kondo la nyuma kwa kuvuta kwa utaratibu kuelekea chini nyakati za misinyao wakati huo huo ukizuia kizazi kisitoke nje

Njia ya kutoa dawa Njia ya kutoa dawa ni namna mgonjwa anavyo patiwa dawa. Njia ya kutoa oksitosin ni kwa sindano kwenyo misuli mikubwa

Nyingi/zaidi Nyingi ina maana ya zaidi, kwa wingi, zaidi ya kawaida. Kama mama anatokwa na damu nyingi ana tokwa na damu zaidi au nyingi kuliko kawaida

Tojo Mfuko wa tojo ni angavu, nyama nyembamba inaoyoshikilia mtoto na imeshikizwa kwenye kondo la nyuma. Tojo ni yale maji maji yaliyojaa ndani ya mfuko wa tojo/chupa. Tojo ni maji yanayotoka chupa ikipasuka.

Wasiwasi Wasiwasi ni ile hali inayopata watu pale wanapoogopa, au anapotishika. Wahudumu wanaweza kuwa na wasiwasi kwa namna ya kumhudumia mama anayetokwa na damu na damu nyingi kama hawajui la kufanya

4 6

Maelezo

4 7

au

Kuwanusuru Wakina Mama Utokaji damu baada ya kujifungua

Uzazi (angalia mpango kazi wa Kusaidia Watoto Kupumua)

Mpatie dawa ndani ya dakika 1

Kata kiunga mwana ndani ya dakika 1-3

Vuta kiunga mwana ili kutoa kondo la nyuma na dhibiti kizazi

Rudia kuvuta kiunga mwana dhibiti kizazi

Limetoka

Limetoka

Halijatoka ndani ya dakika 60

Halijatoka ndani ya dakika 30 Mhamasishe akojoe

Rudia 10 IU ya Oksitosin

Je, kondo limetoka?

Angalia kama kizazi kimesinyaa

kondo la nyma ni kamili ?

kizazi ni kigumu?

utokaji wa damu ni wa kawaida?

Sio kamili

KigumuKigumu

Kigumu

Ni Kamili

Laini

Laini

Mpatie huduma ya ziada

Sugua kizazi

Sugua kizaziRudia dawa

Kawaida

Endelea na huduma:Mhamasishe mama kunyonyesha

Angalia msinyao wa kizazi Fuatilia utokaji wa damu

Angalia hali ya mtoto na mama

Gandamiza mchaniko

Gandamiza kizazi

Huduma ya ziadaMfunike mama apate joto

KigumuDamu nyingi

LainiDamu nyingi

KigumuDamu ya kwaida

Sugua ikiwa ni laini

MPANGO KAZIJiandae kwa uzazi

© 2015 Jhpiego Corporation

All rights reserved

ISBN 978-1-943408-07-8

10 IU 200mcg x 3 = 600 mcg

Je,

Je,

Je,

20-09268 Rev A

Dakika yadhahabu