kuna tatizo la ujifunzaji duniani kutafuta ......kuna tatizo la ujifunzaji duniani licha ya...

2
WITO WA KUCHUKUA HATU Ndani ya miaka kumi iliyopita, familia inayoongezeka ya mashirika ya kiraia imeanzisha tathmini kubwa ya ujuzi wa watoto kusoma na kuhesabu inayofanyika kwenye kaya katika nchi tisa barani Asia, Afrika, na Amerika ya Kusini. Tofauti na tathmini nyingine kubwa zinazopima matokeo ya kujifunza, tathmini hizi zinafanyika kwenye kaya na hufanywa na wananchi wa kawaida. Hii inawapa fursa watu mbalimbali pamoja na wazazi, kujionea wenyewe nini watoto wao wanaweza kufanya. Upimaji wa ujuzi wa watoto kwenye kaya unasaidia kutathmini watoto WOTE, waliopo nyumbani siku ya utafiti siyo wale tu walioko shuleni. Tunaamini kwamba hii ni njia pekee ya kujua kama watoto WOTE wanapata stadi za msingi za kusoma na kuhesabu, ambazo huweka msingi muhimu wa maendeleo ya mtoto shuleni hapo baadaye. Pia ni njia muafaka ya kuwashirikisha watu wengi kufikiria kwa pamoja kuhusu ubora wa elimu. Ni pale tu watu wengi wanapoona kuna tatizo ndipo ufumbuzi unaweza kupatikana. KUNA TATIZO LA UJIFUNZAJI DUNIANI Licha ya kuongezeka kwa uandikishaji, takriban watoto milioni 250 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu, hata kama wameandikishwa na wanakwenda shule. Duniani kote, vijana wadogo milioni 200 humaliza shule bila kuwa na stadi za msingi wanazohitaji kufanikiwa maishani. KUTAFUTA UFUMBUZI WA TATIZO HILI HUANZA NA KULIELEWA TATIZO LENYEWE

Upload: others

Post on 24-Jan-2020

15 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: KUNA TATIZO LA UJIFUNZAJI DUNIANI KUTAFUTA ......KUNA TATIZO LA UJIFUNZAJI DUNIANI Licha ya kuongezeka kwa uandikishaji, takriban watoto milioni 250 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu,

WITO WA KUCHUKUA HATU

Ndani ya miaka kumi iliyopita, familia inayoongezeka ya

mashirika ya kiraia imeanzisha tathmini kubwa ya ujuzi

wa watoto kusoma na kuhesabu inayofanyika kwenye

kaya katika nchi tisa barani Asia, Afrika, na Amerika ya

Kusini.

Tofauti na tathmini nyingine kubwa zinazopima matokeo

ya kujifunza, tathmini hizi zinafanyika kwenye kaya na

hufanywa na wananchi wa kawaida. Hii inawapa fursa

watu mbalimbali pamoja na wazazi, kujionea wenyewe

nini watoto wao wanaweza kufanya. Upimaji wa ujuzi

wa watoto kwenye kaya unasaidia kutathmini watoto

WOTE, waliopo nyumbani siku ya utafiti siyo wale tu

walioko shuleni.

Tunaamini kwamba hii ni njia pekee ya kujua kama

watoto WOTE wanapata stadi za msingi za kusoma

na kuhesabu, ambazo huweka msingi muhimu wa

maendeleo ya mtoto shuleni hapo baadaye. Pia ni njia

muafaka ya kuwashirikisha watu wengi kufikiria kwa

pamoja kuhusu ubora wa elimu. Ni pale tu watu wengi

wanapoona kuna tatizo ndipo ufumbuzi unaweza

kupatikana.

KUNA TATIZO LA UJIFUNZAJI DUNIANI Licha ya kuongezeka kwa uandikishaji, takriban watoto milioni 250 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu, hata

kama wameandikishwa na wanakwenda shule. Duniani kote, vijana wadogo milioni 200 humaliza shule bila kuwa

na stadi za msingi wanazohitaji kufanikiwa maishani.

KUTAFUTA UFUMBUZI WA TATIZO HILI HUANZA NA KULIELEWA TATIZO LENYEWE

Page 2: KUNA TATIZO LA UJIFUNZAJI DUNIANI KUTAFUTA ......KUNA TATIZO LA UJIFUNZAJI DUNIANI Licha ya kuongezeka kwa uandikishaji, takriban watoto milioni 250 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu,

1 Hufanywa kwenye kaya, siyo shuleni. Kama lengo

ni kutoa elimu kwa watoto WOTE, basi ni lazima

tathmini ihakikishe kuwa watoto wote wanawakilishwa

kwenye sampuli. Katika nchi nyingi zinazoendelea, hili

haliwezekani kama tathmini inafanyika shuleni.

2 Hufanywa kwa mazungumzo ya mdomo, mtu mmoja

kwa kila mtoto. Matokeo ya tafiti za zamani huficha

ukweli kwamba watoto wengi hawawezi kusoma.

Kuwapima watoto kwa kuhojiana, mtoto mmoja baada

ya mwingine ni njia pekee ya kutambua kama mtoto

anaweza kusoma.

3 Hutumia zana rahisi ambazo ni rahisi kuzitumia. Mara

nyingi tatizo la matokeo duni ya kujifunza halionekani

dhahri. Tathmini hizi huwawezesha wazazi, walimu, na

watu wa kawaida kuelewa matokeo na kuwa sehemu ya

mchakato. Ni pale tu watu wengi wanapoona kuna tatizo

ndipo, ufumbuzi unaweza kujadiliwa na kutekelezwa.

4 Huyafikia maeneo mengi makubwa, ili matokeo yawe

na uwakilishi wa kitaifa na kimkoa. Kukadiria ukubwa

wa eneo la kufikia na mtawanyiko wa tatizo ni muhimu

sana katika kubuni ufumbuzi mwafaka.

TATHMINI ZINAZOFANYIKA KWENYE KAYA

JIUNGE NA HARAKATI HIZINina amini kwamba tathmini zinazofanyika kwenye kaya ni njia pekee ya kupima kujifunza kwa watoto wote.

Ungana nasi kwa kusaini Wito wa Kuchukua Hatua kupitia www.palnetwork.org AU tuma jina lako, shirika na nembo ya shirika lako kwa Hannah-May Wilson kupitia [email protected]

WWW.PALNETWORK.ORG