kujenga kwa uadilifu - lafargeholcim...kanuni za maadili ya biashara za lafargeholcim 11 1.2...

44
Kujenga kwa Uadilifu Kanuni Zetu za Maadili ya Biashara

Upload: others

Post on 27-Feb-2020

5 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Kujenga kwa UadilifuKanuni Zetu za Maadili ya Biashara

Page 2: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Utendakazi wa juu pamoja na uadilifu wa juu ni muhimu kwa mafanikio endelevu.

Kutenda kwa uadilifu hujenga imani, hulinda sifa zetu, hupunguza gharama yetu ya kufanya biashara, na huboresha thamani ya washika dau wetu.

Kutenda kwa uadilifu kunahusu kufanya jambo sahihi kila wakati na kunaanza na kutenda kwa kuzingatia Kanuni zetu.

Ni jukumu letu kutenda kwa uadilifu na kuwawezesha wengine kufanya vivyo hivyo.

02 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 3: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Jedwali la Yaliyomo

05 Ujumbe kutoka kwa CEO

06 Utangulizi

09 1. Uadilifu kazini10 1.1 Afya na Usalama (A & U)12 1.2 Utofauti, haki, na heshima14 1.3 Ulindaji wa mali ya kampuni yetu16 1.4 Mifumo ya taarifa, barua pepe, na mitandao ya kijamii

19 2. Uadilifu katika uendeshaji wa biashara20 2.1 Dhidi ya ruswa na ufisadi22 2.2 Zawadi na ukarimu24 2.3 Ushindani wa haki26 2.4 Kurekodi na kuripoti kwa usahihi28 2.5 Migongano ya Maslahi30 2.6 Biashara haramu ya hisa32 2.7 Adhabu na vikwazo33 2.8 Kuzuia ulaghai wa pesa

35 3. Uadilifu katika jamii36 3.1 Mazingira37 3.2 Haki za binadamu38 3.3 Uhusishaji jamii

40 Ushauri, mwongozo, na kuripoti

03Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 4: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

“Sote tuna wajibu wa kudumisha hadhi ya LafargeHolcim. Ninaamini kuwa mnaweza kudumisha uadilifu na maadili ya kazi katika kila jambo mnalofanya.”

04 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 5: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Ujumbe kutoka kwa CEOKwa Wafanyakazi,

Kwa kuwa kampuni yetu inaongoza ulimwenguni katika sekta ya nyenzo na vifaa vya ujenzi, ni lazima kila mfanyakazi awe mwadilifu. Kila mmoja wetu anatakiwa kutii sera zetu. Huu ndio wajibu wetu kwa mamilioni ya wateja ulimwengni kote, wauzaji wa bidhaa zetu na wenzetu wanaofanya kazi nyanjani na ofisini. Wafanyakazi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa njia inayofaa ili kudumisha ufanisi wa kampuni hii. Hadhi na idhini yetu ya huduma yanatuelekeza kufanya kazi kwa uadilifu ili kufanikiwa katika kila hatua.

Mwongozo wetu wa Maadili ya Kazi unafafanua mienendo ya kila mfanyakazi. Ingawa mwongozo huu haubainishi hali zote za kazi, lakini unatoa vielelezo na hali ambazo tunatakiwa kufuata. Tunatarajia kila mfanyakazi awe mwadilifu kila wakati. Tunajivunia bidhaa, ubora wa kazi na waajiri wetu. Tumebainishwa kwa njia ya kipekee kuongoza katika sekta hii na sote tunatakiwa kuzingatia fursa na majukumu ambayo tunapaswa kutekeleza.

Tafadhali soma na uhakikishe kuwa umeelewa sheria zilizo katika Mwongozo wa Maadili ya Kazi. Ikiwa huna uhakikia kuhusu jambo lolote, muulize msimamizi wako. Ninatarajia kila mtu afanye kazi kulingana na nia na lengo la Mwongozo wa Maadili katika hali zote, kila wakati.

Sote tuna wajibu wa kudumisha hadhi ya LafargeHolcim. Ninaamini kuwa mnaweza kudumisha uadilifu na maadili ya kazi katika kila jambo mnalofanya.

Asanteni,

Jan JenischMtendaji Mkuu wa Kampuni

Keith CarrMwanasheria Mkuu wa Kampuni

05Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 6: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

UtanguliziSheria zetu zinatoa mwongozo na kutoa mifano ili kukusaidia wakati unapokumbana na hali tata katika kazi yako ya kila siku. Pia zina marejeo kwa sera za LafargeHolcim, sheria husika, na kanuni kwa sababu hizi hutoa mazingira kwa ajili ya mada nyingi zilizojumuishwa katika Sheria zetu na Mpango wetu wa Uzingatiaji.

LafargeHolcim itaendelea kuwakilisha na kuendeleza sera mpya za kampuni zitakazotoa mwongozo zaidi, kwa hivyo tafadhali kagua Mtandao wako wa ndani kwa ndani na pia mandhari ya kiulimwengu ya sera za LafargeHolcim mara kwa mara kwa mambo mapya.

Kutenda kwa UadilifuLafargeHolcim inajitahidi kuunda mazingira ambayo uaminifu na uwajibikaji , uzingatiaji unafanikiwa kuwa ni lengo kuu. Kwa kutumia maarifa ya kawaida na uamuzi sahihi pamoja na Sheria zetu na sera na maelekezo ya LafargeHolcim kwa hakika utatosha kuhakikisha biashara inaendeshwa kwa uadilifu. Sheria zetu haziwezi kutazamia kila hali tunayoweza kukumbana nayo katika mahali pa kazi, lakini zitatusaidia kufanya maamuzi ya busara na kimaadili. Tunawatarajia wafanyakazi wetu kuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi sahihi kimsingi na kanuni kimaadili na kuziinua, hata wakishinikizwa.

Kila mtu, kila mahaliKila mfanyakazi, mkurugenzi, na afisa (“wafanyakazi”) katika kampuni zote zinazomilikiwa kikamilifu na LafargeHolcim na biashara zote za pamoja zilizo chini ya udhibiti wetu ni lazima wafuate Sheria hizi nyakati zote wakati wanawakilisha au kufanyia kazi LafargeHolcim. Katika kampuni ambazo hatuna udhibiti, tunataka utumiaji viwango vya tabia vinavyoonyeshwa katika Sheria hizi. Watu wote, ikijumuisha watoa huduma, wakandarasi wadogo, na washirika wa biashara, watahitajika kutenda kila wakati kwa Sheria zetu wakati wanatenda kwa niaba yetu au kwa jina letu.

Elimu na mafunzoWafanyakazi wote wanapokea mafunzo ya utangulizi na maadili ya kawaida na uzingatiaji. Vipindi hivi ni fursa kwako kuuliza maswali na kujadili jinsi ya kufanya Sheria hizi kuwa sehemu ya kazi yako ya kila siku katika utendaji.

Viwango vya juu zaidi kwa wasimamiziWasimamizi katika viwango vyote wana majukumu ya ziada chini ya Sheria zetu ambayo yanajumuisha kuunda mazingira wazi ambayo wafanyakazi wetu wanajihisi huru kuuliza maswali, kuibua wasiwasi, na kuripoti tabia mbaya. Viongozi wenye uadilifu wa kitabia wanathaminiwa na kupandishwa cheo katika shirika.

Ukiukaji Sheria zetuNi lazima sote tuzingatie Sheria zetu. Ukiukaji Sheria zetu, sera zetu, maelekezo, au sheria za nchi unaweza kuwa na madhara mabaya, yakijumuisha hatua ya nidhamu na hadi usitishaji uajiri, na pia adhabu zinazowezekana za kisheria na kijinai zote mbili kwa kampuni na kwa watu binafsi.

Wasimamizi wanatarajiwa

• Kuongoza kwa mfano – kwa maneno mengine, waonyeshe kwa tabia zao kinachomaanisha kutenda kwa uadilifu.

• Kuwasiliana na wale wanaowajibika kwao ili kuhakikisha wafanyakazi wanaelewa mahitaji ya Sheria zetu na wana rasilimali za kuyatimiza.

• Kuwasaidia wafanyakazi ambao, kwa imani njema, wanaibua maswali na wasiwasi.

• Kutekeleza Sheria hizi kila wakati.

Kabla ya kutenda, jiulize kila wakati, je, tabia yangu inaweza

• Kuonekana kama isiyoaminifu, isiyo ya kimaadili, au hatia ya kisheria?

• Kuharibu LafargeHolcim au sifa zake ikiwekwa hadharani?

• Kusababisha LafargeHolcim kupoteza imani na wafanyakazi wake, wateja wake, washika dau wake, au jamii zake?

• Kuwaumiza watu wengine, kama vile wafanyikazi wenzangu, wateja, au washika dau?

Ikiwa jibu kwa yoyote ya maswali haya ni “NDIO” au hata “PENGINE”, umetambua suala linalowezekana na unafaa kutafuta mwongozo miongoni mwa rasilimali nyingi zinazopatikana kwako, kama vile msimamizi, Idara ya Rasilimali Watu, Kisheria, Dhibiti za Ndani, Usalama wa Ndani, na pia afisa wako wa uzingatiaji wa ndani.

06 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 7: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

07Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 8: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Ni muhimu kukumbuka: Wakati kuna tofauti kati ya hitajiko la ndani la kisheria na Sheria zetu, kila wakati tunatumia kiwango kilicho cha juu zaidi. Ikiwa uzingatiaji Sheria unaonekana kutoambatana na sheria husika za ndani, unafaa kutafuta ushauri kutoka kwa afisa wako wa ndani wa uzingatiaji.

Timu za mauzo na biashara za LafargeHolcim zimefanya kazi kwa muda mrefu katika matumaini ya kujishindia tenda nyingi za uuzaji katika kampuni ya ujenzi. Wiki inayotangulia kabla ya zabuni kutoka, CFO anapokea simu kutoka kwa wakili anayemweleza kwamba anaweza kuhakikisha LafargeHolcim imeshinda zabuni ile ikiwa LafargeHolcim itamuajiri wakili mwenza ambaye ana wasiliano mazuri katika kampuni hiyo ya ujenzi. Kwa sababu kushinda zabuni hiyo ni kwa manufaa bora ya LafargeHolcim, CFO anahisi jaribio la kukubali. Je, anafaa kufanya nini?

Hali hii inaibua tatizo. Hali ushindi wa zabuni ni manufaa kwa LafargeHolcim, sio kwa manufaa yake ikiwa inakuja kutokana na kukiuka sheria au kudhuru sifa za LafargeHolcim. Hafai kuendelea bila kushauriana na afisa wake wa ndani wa uzingatiaji.

08 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 9: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

1. Uadilifu kazini

09Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 10: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

1.1 Afya na Usalama (A& U)Katika LafargeHolcim tunajitahidi kuunda mazingira ya kiafya na salama kwa wafanyakazi, wakandarasi, wateja, na washika dau wetu. Hakuna mtu anayefaa kuumia akifanya kazi pamoja nasi au kwa ajili yetu. Lengo letu ni madhara sifuri kwa watu. Ili kufanikisha hili, tunahitaji jitihada za kila mtu.

Kupitia michakato yetu ya usimamiaji na utendaji kazi, tunahakikisha kwamba kila mfanyakazi anaelewa kile anachowajibikia, na ni usaidizi upi unaweza kutegemea ilikupata mafanikio. Tunalenga kutoa mazingira salama na yenye afya na pia kufanya kazi na wafanyakazi na wakandarasi ili kuendeleza utamaduni unaohimiza uwajibikaji wa kibinafsi au pamoja kwa A&U.

Tunajumuisha A&U katika michakato yote ya biashara na kuhimiza utamaduni ambao wasiwasi unaibuliwa na kutatuliwa ndani ya kitengo cha biashara na kwa usaidizi wa utendaji wa A&U.

Afya na Usalama ni maadili ya msingi kwa LH na hivyo kila mfanyakazi au mkandarasi yeyote anayefanyia LH lazima ajue nini cha kufanya kuzuia majeruhi au vifo vitokanavyo na ajali.

Sheria za Afya na Usalama:

Sheria ya 1 Ninatathmini na kudhibiti hatari kabla ya kuanza kazi yoyote.

Sheria ya 2 Ninafanya tu shughuli ambazo nimeidhinishwa kufanya.

Sheria ya 3 Siruhusiwi kutumia vibaya vifaa vya afya na usalama, na nitumie PPE inayohitajika kila wakati.

Sheria ya 4 Nisifanye kazi nikiwa mlevi wa pombe au dawa.

Sheria ya 5 Ninaripoti matukio yote.

Kuishi kwa sheria hizi ni sharti la kazi

Sera Husika ya LafargeHolcim• Sera ya Kikundi ya Afya na

Usalama (A&U)

10 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 11: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Unafika mapema kazini asubuhi moja na unamuona mfanyikazi mwenzako akimeza tembe kadhaa pamoja na kinywaji kilicho chupani. Baada ya kumsalimu mfanyikazi mwenzako katika chumba cha matayarisho, unagundua harufu ndogo ya pombe kwenye pumzi yake. Ukimuuliza kama amekunywa pombe, anakwambia la, na kwamba ni dawa tu ya kuosha mdomo. Je, unafaa kufanya nini?

Unafahamu tukio linalihusiana na A&U katika shirika lako na unahisi kwamba halijaripotiwa kulingana na sheria. Je, unatakiwa kufanya nini?

Unapowasili katika mahali pako pa kazi na ugundue kwamba mfanyikazi mwenzako hatumii zana mwafaka za kazi. Je, unafaa kufanya nini?

Ili kuhakikisha kila mtu yuko salama katika mahali pa kazi, ni muhimu kwamba uibue wasiwasi kuhusu mfanyikazi huyo na msimamizi au Idara ya Rasilimali Watu. Mfanyikazi mwenzako huenda akawa ana tatizo ambalo anahitaji usaidizi, na kufanya kazi akiwa mlevi wa pombe au dawa kunaweza kuathiri usalama wa watu wengi sio tu yeye mwenyewe.

Hakikisha msimamizi wako anafahamu tukio hilo na uthibitishe naye kwamba suala hilo limeripotiwa. Ikiwa hauko huru kuzungumza moja kwa moja na msimamizi wako kuhusu suala hilo, zungumza na msaidizi wako wa A&U wa ndani, afisa wako wa uzingatiaji wa ndani, au mmoja wa rasilimali zingine nyingi za ndani zinazopatikana kwako. Ikiwa chaguo hizi hazionekani kuwezekana, huu unaweza kuwa muda mzuri wa kutumia Simu ya Uadilifu.

Hakuna anayeruhusiwa kutumia vibaya au kuhitilafiana na kanuni yoyote ya usalama (ambayo inajumuisha tathmini za hatari na kutumia zana mwafaka). Kwa hivyo unafaa kuibua wasiwasi wako na wa mfanyakazi mwenzako na umuulize kama anahitaji usaidizi wako ili kuhakikisha kazi ile inafanywa kwa usalama.

11Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 12: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

1.2 Utofauti, haki, na heshimaKama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000 na kuendeshwa kwa vituo vya uzalishaji katika zaidi ya nchi 80 kote ulimwenguni, LafargeHolcim ina bahati kuwa na wafanyikazi wa aina mbalimbali kiutendaji.

Tunaamini tuna wajibu wa kuchukuliana kwa hadhi inayomaanisha kufurahia utofauti, iwe utofauti huo upo kwa sababu ya rangi, dini, jinsia, mwelekeo wa kimapenzi au tofauti yoyote nyingine. Tofauti zinaweka wazi mitazamo tofauti ya ulimwengu, inayoboresha mtazamo wa LafargeHolcim wa ulimwengu na kutuwezesha kuwa bora tuwezavyo. Hivyo basi, tunathamini na kukuza mahali pa kazi ambapo panajumuisha na ni pa haki na ambapo panakuza heshima kwa wafanyakazi, wateja, na washirika wetu wa biashara.

Sote tunajitahidi kuunda mazingira ambayo hadhi, faragha, uhuru wa kutangamana, kujadiliana jumla wa kibinafsi, na haki na usalama wa kibinafsi wa kila kila mtu binafsi ni sehemu ya uzoefu wetu wa kazi wa kila siku. Tunaamini heshima katika mahali pa kazi ni msingi kwa utendaji kazi na uhusiano.

Wafanyakazi wote bila kujali cheo au kiwango cha kazi watachukuliwa kwa haki katika masuala yanayoathiri utendaji mafunzo, uajiri, fidia na kufutwa kazi.

Hakuna matisho au vitendo vya vuruguIli kuweka mazingira yetu ya kazi bila vurugu, tabia mbaya, wala kuogopeshwa, wafanyakazi wote wanafaa kuonyesha heshima sio tu kwenye mali ya LafargeHolcim, lakini pia wanapoendesha biashara ya LafargeHolcimc – iwe ni wakati wa mkutano na wateja, kuendesha lori la LafargeHolcim, au kutangamana na jamii ya ndani. Kila wakati tenda kwa utaalamu.

Ubaguzi Tunafanya kazi pamoja na watu binafsi wa kutoka makabila mbalimbali, tamaduni, dini, umri, ulemavu, hali za kimatibabu, rangi, utambulisho wa kijinsia, jinsia, mitazamo ya ulimwengu, na mahusiano kwa makundi ya kisiasa, mashirika, au makundi ya walio wachache. Kwa kuambatana na kuheshimiana kwetu na pamoja na sheria za uajiri za nchi nyingi ambako tunafanya kazi, hatuvumilii ubaguzi dhidi ya mtu yeyote kwa misingi ya yoyote ya vipengele hivi au tabia yoyote nyingine ya kuudhi inayolingana. Kanuni hizi zinaenea kwa maamuzi yote ya uajiri ikujumuisha uajiri, mafunzo, tathmini, kupandishwa cheo, na tuzo.

Dhuluma“Dhuluma” ni aina ya ubaguzi unaojumuisha tabia isiyo ya kufurahisha na ina dhumuni au athari ya kutengenza mazingira ya kuogopesha, uhasama, au mabaya. Dhuluma inaweza kuja kwa mifumo mingi, ikijumuisha matendo ya kimwili, maoni kwa matamshi au maandishi, au maonyesho ya kuonekana. Dhuluma ya kimapenzi inashuhudiwa kwa majaribio ya kimapenzi yasiyo furahisha, maombi ya mapendeleo ya kimapenzi, na tabia zingine za kimatamshi au kimwili zenye hali za kimapenzi yanayojaribu kutengeneza mazingira ya uhasama au mabaya ya kazi. LafargeHolcim inazuia vikali aina yoyote ya dhuluma, iwe inafanywa na mfanyakazi au mtu asiye mfanyakazi.

12 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 13: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Mmoja wa wafanyikazi wenzako mara kwa mara anashiriki utani na jirani yake anayeketi karibu naye. Kila mtu ofisini anaweza kusikia utani huo na maoni wanayotoa. Nyakati zingine utani huu una marejeo ambayo watu wengine wanayasikia kuwa cheshi lakini wengine hawayapendelei au kusikia yanawaudhi. Utani unaoleta ucheshi wa mwelekeo wa watu wa kimapenzi yanaonekana kuwa ya kuudhi haswa kwa mtu mmoja. Je, unafaa kufanya nini?

Wakati wa ziara kwenye kiwanda, unagundua kalenda ya ukutani inayoonyesha uchi wa mwanamke. Ingawa haupendezwi nayo, hautaki kushughulika kwani, hakuna wafanyikazi wanawake katika eneo hili la kiwanda.

Unatafuta mgombeaji wa kuajiri kama meneja wa mauzo wa idara ya mauzo. Unaamini kwamba bishara ya mauzo ni “biashara ya wanaume” na kujiuliza kama unaweza kuzingatia watumaji maombi wanaume peke yao kwa nafasi ya meneja wa mauzo.

Unafaa kuzungumza na mfanyikazi mwenzako na umueleze kwamba hata kama atafurahishwa na utani huo sio kila mtu ofisini anafurahishwa nao na kwamba baadhi ya utani huo unawakosea wengine. Ikiwa haachi kutoa maoni yale, unafaa kuripoti suala hilo kwa msimamizi wako au Idara ya Rasilimali Watu.

Unafaa kuripoti. Uonyeshaji picha ua michoro ya hali ya kingono katika yoyote ya mahali pa kazi pa LafargeHolcim unazingatiwa kuwa dhuluma ya kuonekana kwa macho na unapigwa marufuku kabisa. Unafaa kuripoti unachopata kwa msimamizi au meneja wa kiwanda ili kalenda ile iondolewe.

Hauruhusiwi kutafuta tu watumaji maombi wanaume wala hauwezi kukataa maombi kutoka kwa wanawake kwa msingi tu wa jinsia; huu ni ubaguzi kwa misingi ya jinsia. Utafutaji wako ni lazima uangazie uhitimu, ujuzi, na uzoefu wa wagombeaji na jinsi wanavyotimiza majukumu ya nafasi hiyo.

13Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 14: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

1.3 Ulindaji mali ya kampuni yetuWafanyakazi wote wanawajibika kwa kulinda mali ya kampuni na kutumia uamuzi mzuri ili kuhakikisha kwamba mali ya kimwili na kiakili na pia mali ya kifedha haiharibiwi, kuibiwa, kutumiwa vibaya wala kupotezwa ovyo ovyo.

Kulinda mali ya kimwiliMali ya kimwili ya LafargeHolcim, kama vile vyombo, nyenzo na vituo, ni muhimu kwa kufanya kazi zetu za kila siku. Mali hii imekusanywa kupitia kazi ya bidii ya watu walioko kote ulimwenguni. Kwa kufanyia kazi LafargeHolcim, kila mmoja wetu anawajibikia mali hii na ni lazima ailinde kutokana na wizi, hasara, utumizi mbaya, na ubadhilifu. Kwa ziada, ni lazima tuhakikishe kwamba rasilimali zote zinatumiwa kwa madhuni mwafaka ya biashara.

Kulinda mali ya kiakiliKatika LafargeHolcim, mara kwa mara tunazalisha dhana, mikakati na aina nyingine za taarifa ya kibiashara zenye thamani na zisizo za umma, tunazomiliki na tunazohitaji kulinda kama mali ya kiakili. Taarifa kama hiyo ni sehemu kubwa ya kinachotuweka kifua mbele katika ushindani. Ufichuaji usiofaa wa taarifa kama hiyo umepigwa marufuku, na ni lazima tuzingatie hatari za ufichuaji usiofaa wa taarifa ya faraghani.

Taarifa ya faraghani ya wafanyakazi na watu wa tatuUfikiaji kwa rekodi au data ya kibinafsi ya mfanyakazi mtarajiwa, wa sasa au wa zamani, ikijumuisha tathmini za utendaji kazi, mishahara, pensheni na manufaa, unaruhusiwa tu kwa watu wenye mamlaka mwafaka na kulingana na sheria za faragha wa data. Kwa ziada, tunawajibika kwa kulinda taarifa ya faraghani tuliyopewa kwa uaminifu na wateja, wauzaji, na washirika wetu wengine wa biashara kwa uangalifu kama tunavyolinda taarifa yetu binafsi.

Katika biashara ya kawaida, taarifa inahitajika kuhusu kampuni zingine, ikijumuisha wateja, wauzaji, na washindani. Hata hivyo, kuna mipaka ya kisheria na kimaadili katika kupokea taarifa ya ushindani:

• Hatufai kupata taarifa kupitia njia zisizofaa, kama vile kupitia rushwa au kuchunguza washindani wetu kwa siri.

• Kwa jumla hatufai kuomba au kupokea taarifa ya ushidani kutoka kwa vyanzo visivyo vya hadharani. Shauriana na afisa wako wa uzingatiaji wa ndani ili akufafanulie maana ya “visivyo vya hadharani” katika hali fulani ikiwa una wasiwasi wowote.

• Hatufai kuajiri mfanyakazi wa mshindani ili kupata taarifa ya faraghani kuhusu muajiri wake wa zamani.

• Hatufai kukubali taarifa iliyotolewa kuhusu mshindani inayoweza kuwa ya faraghani. Unafaa kuuliza kama ni ya faraghani, jinsi ilivyopatikana, na kama nyenzo inayotolewa ina ainisho kama “siri”, “faragaha”, “kiakili”, au “kwa macho yako pekee”.

14 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 15: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Wakati wa safari yangu kuelekea ofisini kwenye gari la abiria, nyakati zingine ninapiga simu zinazohusiana na kazi. Je, hili ni tatizo?

Je, unafaa kufanya nini mshindani akikutumia barua pepe yenye waraka wa faraghani ukiwa umeambatishwa kimakosa, kutokana na yeye kuchanganya jina lako na la mtu mwingine?

Ni lazima uwe mwangalifu kutojadili taarifa iliyo ya faraghani ya kampuni katika maeneo ya umma, kama vile ndani ya magari ya abiria, lifti, au katika kongamano na maonyesho ya biashara. Wakati ni muhimu kupiga simu katika eneo la umma, kuwa mwangalifu wa mazingara yako.

Ukigundua kwamba ni kosa na unajua ambatisho ni la faraghani, usilifungue, usilitumie mwingine, kulichapisha wala kulishiriki. Ikiwa umefungua waraka ule, ufunge, usifanye chochote kuhusiana na taarifa ile, na uwasiliane na afisa wako wa ndani wa uzingatiaji maramoja. Katika tukio lolote, usifute barua hiyo kabla ya kuzungumza na afisa wako wa ndani wa uzingatiaji.

15Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 16: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

1.4 Mifumo ya taarifa, barua pepe, na mitandao ya kijamiiTeknolojia katika mahali pa kazi inatuwezesha kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi zaidi. Tunaitegemea kusaidia michakato na mahusiano yetu kote ulimwenguni.

Ufikiaji wa mtandao, barua pepe na programu-tumizi zingine zinatolewa kwa madhumuni ya biashara. Mawasiliano yote ya biashara na ushirikiano wa ndani pamoja na wafanyakazi wengine na vyombo vingine vya nje vya LafargeHolcim ni lazima yafanywe kwa kutumia mawasiliano ya kielektroniki na akaunti za barua pepe zilizoidhinishwa za LafargeHolcim Group. Katika kutuma na kupokea mawasiliano ya barua pepe na ambatisho ni lazima utumie viwango sawia vya uangalifu kama zinazotumiwa katika mawasiliano ya nakala za karatasi. Kufichua nje (ikijumuisha vyombo vya habari, wawekezaji au wenegine) au kuchapisha kwa tovuti za mitandao ya kijamii, taarifa au mawasiliano ya ndani ya LafargeHolcim bila idhini umepigwa marufuku.

Ni lazima usitumie vibaya mifumo ya IT, Mtandao, akaunti za barua pepe, au taarifa na habari za LafargeHolcim kwa madhumuni yasiyo ya kisheria au kimaadili. Kutafuta, kupakua, au kutuma mbele taarifa yenye matusi au inayokosea wengine kunaweza kupelekea hatua za kinidhamu. Ni lazima pia ufahamu kwamba hauruhusiwi kutumia wala kunakili programu au data kutoka kwa mifumo ya IT ya LafargeHolcim kwa madhumuni ya kibinafsi isipokuwa kwa idhini ya kipekee kutoka kwa idara ya IT ya kufanya vile.

Mitandao ya kijamii inaturuhusu kuwasiliana papo hapo na kwa upana. Fikiri kwa makini kabla ya kusambaza picha au jumbe zinazohusu wafanyikazi wenzako au mahali pako pa kazi. Madhara ambayo hayakuonekana awali yanaweza kujumuisha kuharibu sifa za watu binafsi au kwa LafargeHolcim.

Sera Husika ya LafargeHolcim• Elekezo kwa Mtumiaji Mifumo

ya Taarifa

• Mapendekezo ya Mitandao ya Kijamii

16 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 17: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Unaweka nakala ya faili kiwekaji programu ya Microsoft Word kwenye kifaa cha USB na kupanga kuiweka kwenye tarakilishi ya nyumbani. Unahisi kwamba LafargeHolcim haiwezi ikapata madhara kwa sababu faili asilia inasalia kwenye mifumo yake. Je, unaweza kufanya hivyo?

Sio Sahihi. Wakati LafargeHolcim inaponunua programu, kwa kawaida iko chini ya makubaliano ya leseni na kampuni ya programu ile. Kutumia programu hiyo kwa madhumuni ya kibinafsi sana sana kutakiuka makubaliano hayo ya leseni na LafargeHolcim itawajibika kwa utumizi huo ambao haujaidhinishwa. Utahitaji ruhusa kutoka kwa idara ya IT ili ufanye hivyo.

17Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 18: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

18 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 19: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

2. Uadilifu katika utendaji wa biashara

19Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 20: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

2.1 Dhidi ya rushwa na ufisadiLafargeHolcim inauza bidhaa na huduma zenye msingi wa ubora, kuaminika, na mambo mengine mengi, lakini haitoi rushwa kamwe.

Tunajitoa kusaidia na kuwezesha ukuaji wa jamii kwa namna ambayo kunajiendeshea. Tunaona hili kama jukumu msingi linalokuja na leseni ya kujiendesha katika zaidi ya nchi 80. Kufuata amri ya sheria na kuweka mfano kuhusu jinsi ya kuendesha biashara ya kimaadili ni njia mojawapo kwetu ya kutekeleza jitihada hii kwa matendo.

Tunajua kwamba kupeana rushwa – hata zile ndogo – kunasababisha madhara makubwa kwa jamii, mara nyingi kukisababisha unyang'anyaji kutoka kwa watu wa tabaka la kati na kutengwa kwa maskini kutoka kwa huduma za serikali. Tunajua kwamba kupeana rushwa hakujawahi kuwa kuzuri kwa biashara, bila shaka sio biashara ya kudumu, na kwamba rushwa ya aina yoyote haifai katika utamaduni wa LafargeHolcim wa uadilifu.

Sheria za kimataifa dhidi ya ufisadi zinatumika kwa operesheni zetu zote kote ulimwenguni. Haikubaliki kutoa, kupeana, kuidhinisha aina yoyote ya rushwa au Marupurupu, ikijumuisha kupokea au kutoka kwa afisa yoyote wa umma au mtu wa kibinafsi. Pia hatuajiri watu wa tatu kufanya mambo ambayo sisi wenyewe haturuhusiwi kufanya, kama kupeana rushwa. Vyombo vingine vinavyotenda kwa niaba ya LafargeHolcim havitakiwi kutoa wala kupokea hongo kamwe.

Neno “watu wa tatu” linaweza kujumuisha washauri, wakandarasi wadogo, watoa leseni, mawakala wa mauzo, wauzaji , mawakala wa mipaka, kampuni za uhasibu au sheria, au kampuni zinazotoa usaidizi wa kupata visa, vibali, au hati za ukaguzi, na washirika wa pamoja wa biashara. Bila kujali aina ya chombo kingine, ni muhimu kwa watu wa tatu wanaoendesha biashara au kutoa huduma kwa LafargeHolcim au kwa niaba yake kuchaguliwa na kuhusishwa kwa kuzingatia Mwongozo wa Kazi Kamili ya Watu wa Tatu wa LafargeHolcim au, mara tu inapoanza kufanya kazi katika kampuni yetu, Elekezo ka Kazi Kamili ya Watu wa Tatu.

Malipo ya UwezeshajiNyakati zingine malipo kwa maafisa wa serikali yanaitwa “malipo ya uwezeshaji” ikiwa ni malipo madogo yaliyofanywa ili kupata huduma za kawaida za serikali ambazo mtu anayelipa ana haki kupata. LafargeHolcim inapiga marufuku wafanyakazi wake kufanya malipo kama hayo. Ubaguzi wa kipekee kwa sheria hii ni wakati mfanyakazi anaamini maisha yake, usalama wake wa kibinafsi, au afya yake iko katika hatari halisi na anahisi ni lazima alipe. Katika tukio ambalo mfanyakazi anafanya malipo hayo chini ya tishio la usalama au afya ya kibinafsi, maelezo yote muhimu ni lazima yaripotiwe kwa uzingatiaji wa ndani katika fursa ya mapema zaidi, na malipo hayo ni lazima yarekodiwe kwa usahihi katika vitabu na rekodi za LafargeHolcim.

Rushwa zinaweza kuwa za aina nyingi, sio pesa taslimu tu lakini pia fadhili za thamani kama vile kupewa usafiri, karo ya shule, michango ya kimisaada, na aina zingine za manufaa.

20 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 21: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Unapanga ujenzi wa kiwanda kipya cha kuzalisha saruji cha LafargeHolcim katika nchi yako. Katika majadiliano na mamlaka za ndani gavana wa mkoa anakuarifu kwamba kliniki mpya inahitajika katika mji ulio karibu na mahali kiwanda kitakapojengwa. Anabainisha wazi kwamba usaidizi wa LafargeHolcim katika ujenzi wa kliniki mpya hautasaidia tu ruhusa ya upangaji wa LafargeHolcim wa kiwanda chake kipya, lakini pia utasaidia mipango yake ya kuchaguliwa tena. Je, unafaa kufanya nini?

Chombo kingine kinakueleza kwamba “anawajua watu wote mashuhuri” na kwamba anaweza kuharakisha kutiwa sahihi kwa kandarasi mpya akipewa kiwango cha awali kwenye ada yake. Anakwambia kwamba kinahitajika kwa gharama za usafiri lakini hauna uhakika ni usafiri upi unahusika. Je, unafaa kufanya nini?

Ombi hili linaweza kukiuka sheria husika za dhidi ya ufisadi. Unafaa kuwasiliana na afisa wako wa uzingatiaji wa ndani na msimamizi wako kuhusu hali hii na uelekezwe vifaavyo.

Malipo kwa watu wa tatu ni lazima yafanywe dhidi ya ankara inayoainisha huduma halisi zilizotekelezwa mwa maelezo tosha kwamba umetosheka kwamba ni za halali na busara. Kulipa chombo kingine awali kwa ombi lake kunafaa kukufanya ujiulize mbona na uwe makini sana kuhusu kukubali sababu bila kukagua zaidi. Pia unafaa kupitia kazi kamili na sifa za chombo hiki kingine.

21Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 22: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

2.2 Zawadi na ukarimuHusiano nzuri za biashara zinajengwa kwenye imani na nia nzuri, na kwa sababu tunawathamini na kuwaheshimu wateja na washirika wetu wa biashara, kila upande unaweza ukataka kutambua hili mara kwa mara kwa kutoa zawadi na ukarimu.

Kwa kutumia akili ya kawaida, hiari, na uamuzi wa busara kabla ya kutoa au kupokea zawadi au ukarimu wowote, tunaweza kuepuka nia nzuri zinazofafanuliwa kimakosa. Zawadi na ukarimu ni lazima kila wakati ziwe wastani na hazifai kamwe kutumiwa ili kuweka ushawishi usiofaa au kuunda dhana ya mgongano au mgongano halisi wa maslahi.

Kuhusiana na zawadi na ukarimu kwa maafisa wa umma, unafaa kuwa makini. Maafisa wa umma ni wa aina nyingi na wanajumuisha mtu yeyote anayefanya jukumu la umma kwa nchi husika (watumishi wa umma), ambao wanaweza kujumuisha shirika la umma au kampuni inayomilikiwa na serikali. Serikali na taasisi zingine za serikali zina sheria maalum kuhusiana na kupeana zawadi na ukarimu kwa maafisa wake wa umma ambazo kwa kweli huenda zikawa zimekaza kamba zaidi kuliko kinachoruhusiwa na sera na maelekezo ya LafargeHolcim. Ikiwa unapanga kutoa zawadi au ukarimu kwa afisa wa umma na hauna uhakika, rejelea sheria zako za zawadi na ukarimu za ndani au afisa wako wa ndani wa uzingatiaji.

Hauwezi kutumia pesa au rasilimali zako binafsi ili kuepuka sheria za sera zetu, maelekezo yetu, au kama ilivyobainishwa katika Sheria hizi. Zawadi zote na ukarimu zilizopeanwa au kutolewa kwa wengine kwa niaba ya LafargeHolcim ni lazima zionyeshwe vifaavyo katika vitabu na rekodi za LafargeHolcim.

UkarimuUkarimu unajumuisha milo na vinywaji, na pia matukio ya kitamaduni, burudani, au michezo ambapo angalau mfanyakazi mmoja wa LafargeHolcim anatenda kama mwenyeji na anahudhuria. Ikiwa hakuna mfanyakazi wa LafargeHolcim anayehudhuria basi ukarimu huo ni “zawadi” na uko chini ya sheria zinazohusu zawadi.

ZawadiZawadi zinaweza kujumuisha bidhaa au huduma na pia vitu vingine vya thamani, kwa mfano, mikopo, karo za shule, gharama za huduma ya kimatibabu, na safari au tiketi kwenda kwa matukio ya kitamaduni, burudani, au michezo. Zawadi za pesa au sawia (kama vile vocha za zawadi) na marupurupu haziruhusiwi, kukiwa na ubaguzi mchache sana wa ndani ambao umeidhinishwa awali na Uzingatiaji wa Kundi.

Kurejesha ZawadiZawadi ikizidi viwango vilivyowekwa katika sera na maelekezo ya LafargeHolcim, mweleze msimazi wako, rekodi upokezi wake kulingana na sheria na maelekezo husika, na kwa ukarimu urejeshe zawadi hiyo na uelezee kwamba sheria za ndani za LafargeHolcim haziruhusu kukubali zawadi za kama hiyo. Ikiwa kurudisha zawadi hakuwezekani kwa kweli au kutamkosea aliyetuma vikubwa, ni lazima ichangwe bila kupeana jina la anayechanga kwa mashirika ya misaada, na kama hilo haliwezekani, itakubaliwa kwa niaba ya kampuni na kugawanywa kati ya wafanyakazi, huku Idara ya Rasilimali Watu zikiamua jinsi hilo litatekelezwa.

Mwongozo msingi Jiulize kama zawadi au ukarimu huo ni halali au kana kwamba inakiuka aidha sera au maelekezo ya watu wa tatu. Kisha ujiulize kana kwamba ungeaibika au kuweka kampuni katika nafasi mbaya ikiwa zawadi au ukarimu huo umechapishwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti. Ikiwa jibu kwa yoyote ya maswali hayo ni “ndio” basi zawadi au ukarimu huo ni lazima zisipeanwe wala kukubaliwa.

22 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 23: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Wakati wa kujadiliana bei na mmoja wa wauzaji wetu walinipa tiketi ya kwenda kutazama mechi ya kadanda ambayo ningependa sana kuhudhuria. Je, ni vyema kukubali tiketi hiyo?

Mteja mkuu wa LafargeHolcim anaandaa sherehe ya jioni ili kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya kampuni yake. Watu wengine muhimu wa biashara na maafisa wa serikali watakuwa kule. Nimealikwa. Je, ninaruhusiwa kukubali mwaliko huo?

La. Wafanyakazi wa LafargeHolcim hawaruhusiwi kukubali zawadi au burudani kutoka kwa watu binafsi au kampuni wakati wa majadiliano ya biashara, michakato ya zabuni, na mambo kama hayo. Unafaa kumshukuru muuzaji wako lakini umuelezee sababu kwa nini hauwezi kukubali zawadi yao.

Ndio, bora umealikwa kama mwakilishi wa LafargeHolcim na msimamizi wako ametoa idhini yake.

23Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 24: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

2.3 Ushindani wa hakiLafargeHolcim inaamini katika soko huru na ushindabi wa haki kwa sababu hii inahakikisha wateja wetu wanapata bidhaa na huduma bora kwa masharti bora.

Ukiukaji sheria dhidi ya imani na ushindani haujawahi kuwa nia ya LafargeHolcim na hauvumiliwi. Katika kanda na nchi zote ambako tunafanya biashara, tunajitahidi kushindania wauzaji na wateja vikali lakini kwa haki.

Wafanyakazi wetu ni lazima wasiwahi moja kwa moja au vinginevyo:• Kuingia katika makubaliano,

maelewano au kuratibu shughuli na washindani halisi au wanaowezekana kuhusiana na:

− bei zisizobadilika, ada, au vipengele vingine muhimu ili;

− Kupunguza au kuwekea vikwazo aina au kiasi cha bidhaa au huduma zinazouzwa

− Kugawa masoko kijiografia au kulingana na washirika wa biashara, sehemu za wateja, au aina za bidhaa;

− Kujihusisha katika mwasiliano yoyote na washindani kuhusu zabuni;

− Kupanga masharti au matoleo ya mchakato wa kushindania zabuni;

− Kususia wauzaji au wateja kama njia ya kuzuia muuzaji au mteja kujihusisha na mshindani.

• Kutumia vibaya nafasi ya ubabe katika soko fulani

• Kuingia katika makubaliano na mipango na vyombo vinavyoendesha viwango tofauti vya uzalishaji au usambazaji kama vile wauzaji, wasambazaji au wauzaji rejareja, ambayo yanadhalilisha au kuondoa ushindani huru na wa haki.

• Kubadilishana taarifa nyeti ya ushindani

• Kujihusisha katika tabia yoyote nyingine ambayo inaweza kupunguza ushindani kwa kukiuka sheria na kanuni husika.

Kuna aina nyingi za tabia zinazoweza kulengwa na sheria dhidi ya imani. Ni lazima uzingatie sheria hizi na pia sera za ndani za LafargeHolcim na kutafuta mwongozo kutoka kwa afisa wako wa uzingatiaji wa ndani na wataalamu wa sheria za ushindani wa Kundi, ikiwa una maswali au wasiwasi zozote.

Kanuni na sheria dhidi ya imani ni ngumu na ni nyingi na utekelezaji wao unaweza kutegemea vipengee mbalimbali. Ni vyema kuwa makini na kuuliza maswali badala ya kudhania hatua fulani itakubalika – uamuzi mbaya zio kijisababu.

24 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 25: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Mwakilishi kutoka kampuni nyingine ya saruji anakupigia simu na kukualika kwa mkutano katika nchi nyingine ili kujadili “uboreshaji” soko la bidhaa ambayo nyinyi wawili mnauza. Mkutano wa “uboreshaji” utafanyika nje ya nchi ambako “uboreshaji” huo utatendeka. Je, unafaa kujiunga na mkutano huo?

Mshindani anakujia mkurugenzi wa biashara wa LafargeHolcim na kupendekeza kudumisha bei kwa miezi kumi na miwili ijayo. Kampuni iko katika shinikizo la kutimiza lengo lake la EBITDA na meneja anafikiri kukubali pendekezo la mshidani huyo. Je, anafaa kuchukua fursa hiyo?

La. Unafaa kuwasiliana na afisa wako wa ndani wa uzingatiaji maramoja. Kuhudhuria mkutano wa “uboreshaji” kunaweza kuwa tabia mbaya sana ya kijinai . Usidanganywe na maneno ya kifumbo kama “uboreshaji”. Kuwa na mkutano katika nchi nyingine hakuwezi kubadilisha matokeo kwani mkutano huu bado unaweza kuvunja sheria husika dhidi ya imani.

La. Hii inaweza kuhitimu kama “genge”, ambalo ndilo aina mbaya zaidi ya makubaliano yasio ya kisheria (kwa mfumo wowote, kwa matamshi au maandishi). Kutenda kwa kukiuka sheria za ushindani sio nia njema ya LafargeHolcim. Kutenda kwa uadilifu kunakuhitaji kuzingatia sheria na pia sera na maelekezo ya LafargeHolcim, hata kama uwezekano wa kugunduliwa ni mdogo na kwanza fursa ya kutimiza lengo la biashara inaonekana kuongezeka. Kila wakati kumbuka akilini kwamba ukiukaji sheria za ushindani unaweza kuharibu sifa zetu vibaya sana na unaweza kuwa na athari mbaya ya kijinai na kifedha kwa Kampuni na watu binafsi.

25Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 26: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

2.4 Kurekodi na kuripoti sahihiKatika shughuli zetu zote za biashara na katika kila mfumo wa mawasiliano tuko kamili na wenye ukweli.

Huu ndio msingi wa jinsi tunavyotangamana na wengine, na hicho ndicho kinachotarajiwa kutoka kwetu katika mahusiano yetu na wawekezaji, wateja, wafanyakazi, na washirika wa biashara, na pia pamoja na umma na ofisi zote za serikali. Ugushi au uhitilafianaji usiofaa wa rekodi umepigwa marufuku. Kamwe usimwelekeze mtu mwingine kutayarisha au kuidhinisha rekodi ya uwongo au potofu au kufanya hivyo wewe mwenyewe kwa kuelekezwa na mtu mwingine. Wakati wa kutayarisha rekodi, ni lazima sote tutende kwa uadilifu ili taarifa isishikiliwe, kutokuwa kamili au kupotosha kimakosa. Kasoro katika rekodi zozote ni lazima zisuluhishwe kwa marekebisho mwafaka na kuwekwa wazi kwa watu wanaohitaji kujua kuhusu marekebisho kama hayo.

Uhifadhi rekodiRekodi za kampuni ni lazima zihifadhiwe kulingana na sheria husika na sera na miongozo ya LafargeHolcim. Kuharibu, kuficha au kuhitilafiana na rekodi yoyote ambayo umeelekezwa kuweka kumepigwa marufu. Ikiwa unajua au unaamini kuna uwezekano wa madai ya kisheria au uchunguzi wowote wa ndani au nje unaohusu rekodi yoyote uliyo nayo au iliyochini ya udhibiti wako, ni lazima uhifadhi rekodi hiyo na uitoe kwa haraka unapoelekezwa kufanya hivyo.

Kurekodi kwa wakati na kwa uaminifu taarifa ya kifedha na isiyo ya kifedha na uhifadhi unaofaa wa nyaraka na rekodi zetu ni muhimu kwa biashara yetu na ni muhimu kwa:

• Uaminifu na sifa zetu;

• Majukumu yetu ya kisheria na kiudhibiti;

• Uwezo wetu wa kufanya utabiri na maamuzi kamili ya biashara; na

• Wajibu wetu kwa washika dau na wakisha dau wengine wa nje.

26 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 27: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Ni wiki ya mwisho katika kipindi cha kuripoti cha robo mwaka. Msimamizi wako anataka kuhakikisha kwamba timu yako imetimiza hesabu za robo mwaka, kwa hivyo anakuuliza urekodi mauzo ambayo hayajathibitishwa ya bidhaa hivi sasa, hata kama mauzo hayo hayatakuwa yamehitimishwa mpaka wiki ijayo. Unafikiri hii haitadhuru mtu yeyote katika kampuni. Je, unaweza kufuata agizo hilo?

Umeteuliwa tu kama mtawala wa kifedha katika nchi fulani na umegundua kwamba idadi halisi ya klinka ghalani ni ya chini zaidi kuliko katika rekodi. Hasara iwezekanayo ni kubwa. Unazungumza na CEO wako anayejibu kwamba hawezi kugharamia ununuzi wowote mwaka huu kwani tayari yuko nyuma ya malengo yake. Anatoa maoni kwamba hasara hiyo inafaa kugawanywa katika miaka ijayo. Je, hii ni sawa kwako?

La. Gharama na mapato ni lazima yarekodiwe katika kipindi sahihi cha wakati. Mauzo hayo bado hayajakamilika. Inaweza kuwa uwakilishi mbaya na unaweza kuwa ulaghai ukiyajumuisha katika kipindi cha awali.

La, licha ya jibu la msimamizi wako, una jukumu la kuhakikisha kwamba ripoti ni kamili, ya haki, sahihi, na ya wakati. Ikiwa utafuata elekezo hili, utakuwa una weka rekodi za uwongo.

27Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 28: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

2.5 Migongano ya MaslahiSote tunahitajika kufanya maamuzi ya biashara kwa nia bora za LafargeHolcim, na sio kimsingi na nia za kibinafsi.

Mgogoro wa nia huenda ukaibuka wakati nia zetu za kibinafsi zinapohitilafiana, au zinaweza kuonekana kama zinahitilafiana, na uwezo wetu wa kufanya kazi zetu kwa ufanisi na haki. Tunapoweza, tunaepuka uhusiano au shughuli yoyote inayoweza kulemaza, au hata kuonekana kulemaza, uwezo wetu wa kufanya maamuzi muhimu na ya haki tunapofanya biashara kwa niaba ya LafargeHolcim.

Wakati husiano au shughuli kama hio haziwezi kuepukika, ni lazima uzifichue kwa wakati kwa msimamzi wako na afisa wako wa uzingatiaji wa ndani. Kwa ziada, vivyo hivyo unafaa kufichua nia yoyote ya kibinafsi inayoweza kuonekana kama ina uhusiano na utekelezaji mujukumu yako ya kitaalamu. Ikiwa una wasiwasi, kufichua husiano au shughuli kama hizo ni kwa nia maslahi yako. Uwazi mara nyingi unaondoa mtazamo wowote wa shughuli zisizofaa.

Husiano za njeHuenda ukaalikwa kuhudumu kama mkurugenzi, mshauri au mmoja wa usimamizi wa shirika la nje. Kwanza unafaa kukagua kana kwamba uhusiano huo unaruhusiwa chini ya mkataba wako wa uajiri, na kwa ziada hakikisha kwamba hautahitilafiana na kazi yako kwa LafargeHolcim. Zaidi, ikiwa shirika hili ni mshindani, huendesha biashara na LafargeHolcim, au kampuni inayomilikiwa na umma au taifa, uhusiano huo ni lazima uidhinishwe na afisa wako wa ndani wa uzingatiaji na msimamizi wako. Idhini sawia zinahitajika kwa wafanyakazi wanaotaka kuwania ofisi ya umma. Huku ikiwa haijapigwa marufuku kikamilifu, nafasi nyingi rasmi za umma zitaleta migogoro halisi au inayowezekana ya nia kwa mshikiliaji ofisi hiyo na bishara ya LafargeHolcim.

Hatutumii mali au taarifa ya LafargeHolcim kwa manufaa ya kibinafsi au kujinufaisha kibinafsi na fursa yoyote inayoibuka katika kazi yetu kwa LafargeHolcim.

28 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 29: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Muuzaji vyombo vya kiufundi amefikisha kinachoonekana kama mashine yenye kasoro na unagundua hili baada ya kusanikishwa. Baba-mkwe wako anamiliki kampuni inayouza, na kwa hivyo unazingatia kasoro hiyo kutorekebishwa.

Nimekujiwa na marafiki ili kuwekeza katika kampuni ambayo inazalisha malighafi ya kuuzwa katika soko la LafargeHolcim. Je, hii inajumuisha mgogoro wa maslahi nikichukua tu sehemu ya kifedha, bila mamlaka yoyote katika usimamizi?

Ufanyaji maamuzi wako haufai kuathiriwa na uhusiano wa kibinafsi na muuzaji. Ni jukumu lako kutenda kwa nia bora za LafargeHolcim. Unafaa pia kuripoti mgogoro huo kwa msimamizi wako na umfahamishe afisa wako wa uzingatiaji wa ndani kuhusu kweli kwamba una uhusiano wa kibinafsi na anayemiliki muuzaji.

Angalau ni mgogoro unaowezekana. Kana kwamba ni mgogoro halisi inategemea vipengele mbalimbali, ikijumuisha:

• Nafasi unayoshikilia katika LafargeHolcim;• Ushawishi ulio nao katika uchaguaji wauzaji wa LafargeHolcim;• Kiwango cha uwekezaji wako na hisa husika;• Umuhimu wa LafargeHolcim kama mteja mtarajiwa.

Katika tukio lolote, unafaa kumfahamisha msimamzi wako na afisa wako wa uzingatiaji wa ndani kabla ya kuwekeza katika kampuni hiyo ili kupata mwongozo na ushauri mwafaka. Kwa ziada, kunaweza pia kukawa na vipengee vinavyohusiana na ushindani vya kuzingatiwa.

29Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 30: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

2.6 Biashara haramu ya hisaLafargeHolcim inaunga mkono soko za hisa zilizo wazi na za haki kwa sababu ni muhimu kwa kujenga uaminifu na imani ya wawekezaji.

Biashara haramu ya hisa inatokea wakati hisa za kampuni zinaunzwa na kununuliwa kwa msingi wa taarifa muhimu, isiyo ya hadharani ambayo inaweza kuathiri pakubwa uamuzi wa mtu kuhusu kana kwamba atanunua au kuuza hisa hizo.

Taarifa ni “muhimu” ikiwa mwekezaji wa busara atazingatia taarifa hiyo kuwa muhimu wakati anazingatia kununua, kuuza au kushikilia hisa za kampuni hiyo. Taarifa ni “isiyo ya hadharani” mpaka wakati imefichuliwa na muda wa kutosha umepita wa soko za hisa kuchambua taarifa hiyo. Mifano ya taarifa muhimu, isiyo ya hadharani inajumuisha:

• Ilani ya awali ya mabadiliko katika usimamizi mkuu;

• Muunganiko au manunuzi ambayo bado hayajatangazwa;

• Madai ya kisheria yanayosubiri au yanayotishiwa;

• Matokeo ya kifedha isiyo ya hadharani;

• Uendelezaji wa bidhaa mpya muhimu;

• Mgawanyiko wa hisa ambao haujatangazwa.

Hatununui wala kuuza hisa za LafargeHolcim, kampuni yoyote ya LafargeHolcim, au kampuni yoyote nyingine iliyoorodheshwa hadharani kwa msingi wa taarifa ya ndani iliyopatikana wakati wa kufanya kazi na LafargeHolcim.

Sera Husika ya LafargeHolcim• Elekezo la Ufichuaji Biashara

na Soko

Sheria za biashara haramu ya hisa haipigi marufuku tu kununua au kuuza hisa kwa msingi wa taarifa ya ndani lakini pia kushiriki taarifa hiyo na watu wa tatu.

30 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 31: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Muuzaji vyombo vikubwa vikubwa anakukujia kwa faragha kuhusu mashine mpya wanayopanga kuleta upya sokoni. Tayari umeshaamua kwamba LafargeHolcim haiwezi kutumia bidhaa hiyo, lakini unafikiri kwamba inaweza kufanya vizuri sana kwa sekta zingine. Mara tu muuzaji anapopata wateja, una uhakika bei ya hisa za kampuni inaongezeka kiajabu. Je, unaruhusiwa kununua hisa za muuzaji huyu?

La. hauruhusiwi kununua hisa zozote za muuzaji mpaka umma ujue kuhusu bidhaa hiyo mpya. Hii ni “taarifa ya ndani” kwa sababu ililetwa kwa faragha. Hakujakuwa na ufichuaji kamili na wa haki kwa umma. Taarifa hii ni “muhimu” kwa sababu mwekezaji wa busara anaweza kuzingatia taarifa hii kuwa muhimu katika kufanya uamuzi wa uwekezaji kuhusu kampuni hiyo.

31Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 32: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

2.7 Adhabu na vikwazoLafargeHolcim inawakilishwa katika soko nyingi na kanda nyingi kote ulimwenguni, na kwa hivyo inaendeshwa chini ya sheria na kanuni za mifumo tofauti ya kisheria.

Tunafikisha bidhaa, huduma na teknolojia yetu kote ulimwenguni. Hivyo basi, tunajitoa kuambatana na sheria zote za uuzaji nje ya nchi na uletaji ndani nchin, ikijumuisha adhabu za biashara, vikwazo, na sheria, kanuni, na amri au sera zingine za serikali zinazoathiri biashara.

Kana kwamba bidhaa, huduma, au teknolojia inaweza kuuzwa nje ya nchi kutoka nchi moja hadi nyingine inategemea vipengele vingi ikijumuisha hali ya kipengee hicho, nchi yake asilia, utumizi wake hatimaye na mtumizi wake hatimaye. Adhabu na vikwazo zinawekea vikwazo shughuli za biashara na nchi, watu fulani

waliotajwa, na vyombo fulani, na kwa matumizi fulani ya hatimaye. Ni lazima basi tufahamau kuhusu vikwazo hivi na tupate rekeodi zote zinazoweza kuhitajika kabla ya kujihusisha katika shughuli ya biashara au kuuza bidhaa zetu nje ya nchi.

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Unaombwa na mteja kufikisha saruji kwa kampuni ambayo hauijui iliyoko katika nchi jirani. Nchi hii imewekewa vikwazo na UM. Haujui kama unaweza, au unafaa, kutimiza ombi la mteja huyo. Je, unafaa kufanya nini?

Unafaa kumuuliza afisa wako wa uzingatiaji wa ndani jinsi ya kushughulikia ombi hilo. Uwezo wa kusafirisha hutagemea vipengele vingi, ikijumuisha nchi ambayo mteja angependa usafirishe, bidhaa inayouzwa nje ya nchi, jinsi bidhaa hiyo itakavyotumiwa na nani.

32 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 33: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

2.8 Kuzuia ulaghai wa pesaNi lengo letu kufanya biashara na washirika wa biashara wenye sifa nzuri wanaoendesha shughuli halali za biashara na ambao fedha zao zinatoka kwa vyanzo halali.

Ulaghai wa fedha ni tendo la kijinai linalohusu kuficha ukweli kuhusu chanzo cha pesa kinachohisiana na shughuli ya kijinai, kama vile ugaidi, ulanguzi wa dawa za kulevya au rushwa. Tendo hilo la kijinai linatokea wakati pesa zilizopatikana kwa matendo ya kijinai zinajumuishwa katika biashara ili zionekane kuwa halali au chanzo chake cha kweli au mmliki wake hawezi kujulikana.

Ili kuzuia LafargeHolcim kutotumiwa kama njia ya ulaghai wa pesa, wafanyakazi wetu wanafuata mahitajio yote husika ya uhasibu, uwekaji rekodi na ripoti za kifedha kwa malipo ya pesa taslimu na aina nyingine ya malipo zinazohisiana na shughuli za biashara.

Kama wafanyakazi wa LafargeHolcim, tuko waangalifu kuhusiana na kugundua hatia za malipo na tabia zisizo za kawaida za wateja na wengine.

Ikiwa una tuhuma au maswali kuhusu shughuli iliyopendekezwa ya biashara, ibua maswali na msimamizi wako au afisa wako wa uzingatiaji wa ndani.

33Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 34: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

34 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 35: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

3. Uadilifu katika jamii

35Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 36: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

3.1 MazingiraKama raia wanaowajibika sote tunafahamu majukumu yetu endelevu kwa mazingira, na hitaji la kujihisisha kwa uamilifu ili kulinda na kuboresha maliasili yetu. Tunajitoa kupounguza athari hasi na kuongezea athari chanya kwa asili.

LafargeHolcim inajitoa kulinda mazingira katika nchi ambako inaendesha biashara, na ili kufanikisha hilo imeendeleza sera zenye malengo kuu kwenye:

• Utoaji gesi chafu; • Uhifadhi nishati; • Uhifadhi maji; • Kupunguza na kutupa takataka

vizuri katika mchakato wa utengenezaji;

• Kuongezea thamani, kutengeneza upya, kurejesha na kutumia tena takataka katika mchakato wa uzalishaji;

• Utumizi wa maliasili na mazoea ya kudumu;

• Urekebishaji/urejeshaji timbo na usimamiaji utofauti wa viumbe;

• Uzingatiaji sheria za kimazingara na mahitajiko ya watu wa tatu;

• Kufuatilia na kuripoti uzingatiaji na utendakazi wa kimazingara.

LafargeHolcim pia iko chini ya mahitajiko mengi ya serikali na sheria nyingi za kimazingara zinazoweka viwango vya chini zaidi. Katika LafargeHolcim tunajitahidi kwa kiwango cha juu zaidi cha tabia.

Mara kwa mara tunakagua utendakazi katika maeneo haya na kuendeleza mipango ya hatua ili kuboresha utendakazi wetu kwa uendelevu.

Tunakutia moyo kusaidia utumizi wa kudumu wa maliasili, ikijumisha uhifadhi maji, upunguzaji na urejeshaji wenye manufaa, utengenezaji upya na utumiaji tena wa takataka, uhifadhi nishati, na usimamiaji utofauti wa viumbe. Shauriana na mratibu wako wa kimazingira ili kujufunza mengi zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kusaidia LafargeHolcim na kuhakikisha tunatimiza malengo yetu.

Sera Husika ya LafargeHolcim• Sera ya Kimazingira

• Sera ya Nishati na Rasilimali Mbadala (NRM)

36 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 37: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

3.2 Haki za binadamuTunajitahidi kuheshimu na kulinda haki za binadamu popote tunapoendesha biashara.

Tunapiga marufuku maozea yafuatayo na hatutafanya biashara na mtu yeyote binafsi au kampuni yoyote tunayojua inashiriki katika yafuatayo:

• Utumiaji watoto vibaya, ikijumuisha wafanyikazi watoto;

• Adhabu ya kimwili;• Dhuluma kwa wafanyakazi, haswa

yenye msingi wa jinsia, asili, dini au mwelekeo wa kimapenzi;

• Kazi ya kulazimishwa;• Ubaguzi usio wa kisheria katika

mazoea ya uajiri;• Kukua na hali zisizosalama za kazi;

• Malipo (au mapunguzo) ya mshahara ambayo yanamuacha mfanyikazi chini ya mshahara wa chini zaidi; na

• na kanuni zisizohalali a muda wa ziada.

Jitihada yetu kwa haki za binadamu zipo katika Sera yetu ya Jukumu la Kampuni kwa Jamii ( JKJ) na kutiwa nguvu na ushiriki wetu katika Umoja wa Ulimwengu wa UM (UN Global Compact). Mfumo wa Usimamiaji Haki za Binadamu wa LafargeHolcim unatumiwa katika kampuni zote za Kundi. Mfumo huu unaangalia tabia

yetu binafsi na pia ile iliyo katika mnyororo wa thamani, haswa tabia ya wauzaji, wakandarasi wadogo na watoa huduma wengine wa watu wa tatu.

Ikiwa una sababu ya kufikiria kwamba LafargeHolcim au mmoja wa washirika wetu anakosa kuzingatia sheria na kanuni zilizoundwa kulinda haki za binadamu, shiriki wasiwasi zako na afisa wako wa uzingatiaji wa ndani.

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Sera Husika ya LafargeHolcim• Sera ya Jukumu la Kampuni kwa

Jamii ( JKJ)

Ninafanya kazi na muuzaji. Ninasikia uvumi kwamba muuzaji huyu anawaajiri watoto na wakati mwingine kufungia watu korokoroni katika maeneo yao ya kazi. Je, ninafaa kufanya nini?

Unafaa kuripoti uvumi huo kwa afisa wako wa uzingatiaji wa ndani ambaye ataanzisha hatua mwafaka na wafanyikazi wa JKJ ili kuthibitisha kana kwamba uvumi huu una ukweli wowote. LafargeHolcim inachukua masuala ya haki za binadamu kwa makini sana na itafanya kila juhudi kuhakikisha wauzaji wake wanafanya vivyo hivyo.

37Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 38: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

3.3 Uhusushaji jamiiLafargeHolcim inajitahidi kuwa raia kampuni anayeaminika na kutimiza majukumu yake kwa jamii ambazo anajiendeshea.

Tunajitahidi kufanya hivi kwa kuchangia kupitia uwekezaji na ujihusishaji, na kujenga husiano zenye msingi wa kuheshimiana na kuaminiana pamoja na washika dau wote katika jamii.

Tunaonyesha heshima kwa watu na sayari hii na kuwaomba wafanyakazi wetu wote kuzingatia, wanapofanya maamuzi ya biashara, athari za muda mfupi na muda mrefu kwenye jamii na mazingira.

Michango ya kisiasa LafargeHolcim kama kampuni haiegemei upande wowote wa kisiasa. Michango kwa vyama vya kisiasa, wanasiasa au wagombeaji ofisi ni mambo ya kibinafsi kwa wafanyakazi wetu. Majengo na mali ya LafargeHolcim haiwezi kamwe kutumiwa kuchangisha fedha wala kufanya kampeni za chama fulani cha kisiasa wala mgombeaji ofisi. Misaada ya kisiasa haiwezi kufanywa kwa jina la LafargeHolcim isipokuwa kama imeruhisiwa chini ya sheria za ndani na sera na miongozo husika ya LafargeHolcim, ambayo ni lazima ihitaji rekodi wazi na sahihi za michango kama hiyo na kupiga marufuku misaada kama hiyo kupeanwa ili kupata manufaa yasiyofaa.

Sera Husika ya LafargeHolcim• Sera ya Jukumu la Kampuni kwa

Jamii ( JKJ)

38 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 39: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, hii inamaanisha nini kwangu?

Katika uwezo wako kama mfanyakazi wa LafargeHolcim unaalikwa kuhudhuria sherehe ya jioni kwa ambayo sera za vyama vya kisiasa zitaangaziwa katika hotuba kabla ya shughuli za uchangishaji pesa kuanza. Tiketi yako kwa sherehe hii inataja mada ya hotuba na kwamba kwa kuinunua, chama hicho kitanufaika. Je, unafaa kufanya nini?

Uhudhuria wako katika sherehe hii ya kisiasa unaweza kuonekana kama LafargeHolcim ina uunga mkono wa chama hicho cha kisiasa. Ni lazima uwe mwangalifu katika kukubali mwaliko wowote kama huo na ushauriane na afisa wako wa uzingatiaji wa ndani kabla ya kukubali. Katika tukio lolote, ukihudhuria basi ni lazima iwe kama mtu binafsi.

39Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 40: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Ushauri, mwongozo, na kuripoti

Punde au baadaye wakati unafanyia LafargeHolcim kazi huenda ukakabiliwa na hali ambayo inaleta mshangao wa kimaadili. Wakati hilo linapotendeka, usisite kuripoti, uliza maswali kuhusu majukumu yako, na uripoti wasiwasi na tabia isiyo kubaliwa wakati inapohitajika. Kila wakati jaribu kuzungumzia maswali au wasiwasi kwa msimamizi wako wa karibu au wengine wanaoweza kusaidia, kama vile Idara ya Rasilimali Watu, Watu wa Kisheria, Ukaguzi wa Ndani, Dhibiti za Ndani, Usalama na afisa wako wa uzingatiaji wa ndani.

Simu ya UadilifuIkiwa hauko huru au haujafanikiwa katika kujadili suala na mojawapo ya chaguo zilizotolewa hapo juu, unafaa kufahamu kwamba Simu ya Uadilifu ya LafargeHolcim ni mbadala nyingine ya kupata ushauri au kuibua wasiwasi kwa nia njema kuhusu hali yoyote ambayo unajua au unashuku inakiuka Sheria zetu au sheria za taifa.

Simu ya Uadilifu inazinduliwa kote katika Kundi la LafargeHolcim katika miaka ya 2015/2016. Wakati inapatikana nchini mwako, ripoti kwa Simu ya Uadilifu ya LafargeHolcim zinaweza kufanywa kwa kupigia simu nambari ya simu iliyotolewa kwa nchi yako au kwa kujaza ripoti katika https://integrity.lafargeholcim.com.

Pia unaweza kufikia Idara ya Uzingatiaji ya Kundi moja kwa moja kwa kupiga simu kwa +41 58 858 8700 au kwa kutuma barua pepe kwa [email protected].

Ripoti yako itasomwa na timu ya wafanyikazi wa uzingatiaji na uchunguzi wa LafargeHolcim Group Compliance katika Uzingatiaji wa Kundi la LafargeHolcim, watakao shughulikia ripoti yako kwa namna ya utaalamu. Ripoti na taarifa husika zitashuhulikiwa kwa faragha na kushirikiwa na wale watu tu wanaohitaji kujua kuhusiana na kulinda maslahi ya kampuni.

Ushirikiano na chunguzi, kaguzi, na shughuli za udhibiti wa ndani Kuzuia na kugundua ukiukaji wa Sheria na sheria za taifa zinachukuliwa kwa makini sana katika LafargeHolcim. Vivyo hivyo, ukiukaji Sheria au sheria za taifa wowote unaowezekana unachunguzwa kwa wakati. Vile vile, wafanyakazi wote wanahitajika kushirikiana kikamilifu na kwa uaminifu katika uchunguzi, ukaguzi au shughuli yoyote ya udhibiti wa ndani, inayojumuisha kutoa majibu kwa wakati kwa maombi yote ya taarifa. Nyaraka zote, ikijumuisha lakini sio tu nakala za karatasi, kielektorniki na faili za barua pepe, ni mali ya kampuni na huenda zitapitiwa mara kwa mara katika kuzingatia sheria husika ya

faragha wa data na kulingana na sera na maelekezo ya LafargeHolcim kwa madhumuni ya chunguzi, kaguzi au shughuli za udhibiti wa ndani au kuhakikisha uambatano na sheria.

Ulinzi dhidi ulipizaji kisasiLafargeHolcim haivumilii ulipizaji kisasi dhidi ya mfanyakazi yeyote anayeripoti wasiwasi fulani kwa nia njema. Watu binafsi wanaochukua hatua dhidi ya mtu kwa kuibua wasiwasi au kushiriki katika uchunguzi atachukuliwa hatua ya kinidhamu, hadi na ikijumisha kufutwa kazi.

Sera Husika ya LafargeHolcim• Elekezo la Kuripoti Uzingatiaji

+41 58 858 [email protected]://integrity.lafargeholcim.com

40 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 41: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

Je, ninafaa kukosa kukimya lini?

Msimamizi wako anakuamrisha kubadilisha ripoti ya gharama, kitendo ambacho unajua ni ukiukaji sera za LafargeHolcim na Sheria hizi. Una wasiwasi kwamba msimamizi wako atafanya kazi yako kuwa ngumu ukikataa kufanya alichokwambia ufanye. Je, unafaa kufanya nini?

Umetambua kinachoweza kuwa suala tata. Kwa kawaida msimamizi wako ndiye angekuwa mtu bora zaidi wa kuzungumza naye mara ya kwanza. Badala yake, inaweza kuwa mwafaka kujadili suala hili na meneja wa msimamizi wako. Kwa ajili ya kuhusika kwa msimamizi wako, hata hivyo, kupigia simu Simu ya Uadilifu ni chaguo nzuri katika hali hii.

41Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 42: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

42 Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 43: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

43Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim

Page 44: Kujenga kwa Uadilifu - LafargeHolcim...Kanuni za Maadili ya Biashara za LafargeHolcim 11 1.2 Utofauti, haki, na heshima Kama kampuni ya kiulimwengu inayowaajiri zaidi ya watu 80,000

LafargeHolcim LtdZürcherstrasse 1568645 JonaSwitzerlandwww.lafargeholcim.com

© 2018 LafargeHolcim Ltd