kuhusu afrodad - afrodad.files.wordpress.com · mchakato wa mkataba wa mkopo ilifanyika kulingana...

32

Upload: others

Post on 27-Oct-2019

43 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

KUHUSU AFRODAD

Dira ya AFRODAD

AFRODAD inalenga mchakato sawa na endelevu wa

maendeleo kuelekea Afrika yenye mafanikio.

Dhamira ya AFRODAD

Kupata sera zitakazorekebisha migogoro ya madeni

ya Afrika kulingana na thamani ya mfumo wa haki za

binadamu.

Malengo ya AFRODAD ni pamoja na yafuatayo:

1. Kuongeza ufanisi na usimamizi wenye tija na matumizi

ya rasilimali ya serikali za Afrika;

2. Kupata/kuleta mabadiliko katika dhana ya kimataifa ya

kijamii na kiuchumi na mpangilio wa kidunia wa kisiasa

kwenye mchakato wa maendeleo unaotambulisha

mahitaji na matakwa ya watu wengi duniani;

3. Kuwezesha mazungumzo kati ya vyama vya kiraia na

serikali kwenye masuala yanayohusiana na Madeni na

maendeleo Afrika au sehemu nyingine.

MKATABA WA KUKOPAKanuni na Miongozo ya Ukopaji huru wa fedha kwa nchi

za AfrikaToleo Lililorekebishwa

Hatimiliki © 2013 AFRODAD Haki zote zimehifadhiwa

ISBN 978-0-7974-4509-3EAN 9780797445093

YALIYOMO

DIBAJI 6

1. UZINGATIAJI WA BUSARA NA DESTURI ZA

UKOPAJI NA USIMIMIAJI WA MADENI YA UMMA 8

2. UWEPO WA SHERIA NA KANUNI

ZINAZOTABIRIKA 11

3. MIUNDO NA WAJIBU ZINAZORATIBIKA NA

MADHUBUTI 13

4. UWEPO WA OFISI HURU YA USIMAMIZI WA

MADENI 18

5. USHIRIKI WA UMMA, UJUMUISHWAJI NA

KUWEKA TAARIFA HADHARANI 20

6. KUHESHIMU UBINADAMU NA HAKI ZA

WATU ZA KIIKOLOJIA 23

7. KUHESHIMIANA NA USAWA KATIKA UBIA NA

WAKOPESHAJI NA WAFADHILI WA KIMATAIFA 25

MAREJEO NA USOMAJI WA ZIADA 27

MKATABA WA KUKOPA

6

DIBAJI

Nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara zinakabiliwa na

changamoto kubwa katika michakato ya kuingia mikataba

ya madeni na usimamizi wa madeni ya umma. Changamoto

hizo zinatokana na vyanzo vya fedha za maendeleo,

michakato ya kuidhinisha mikopo, hali na masharti ya

mikopo, uchumi mkuu na sera za udhibiti, uwezo wa

kitaasisi kwa ujumla, na uwezo wa nchi kukopesheka.

Majeraha ya Migogoro ya madeni ya miaka ya 1970,

1980 na 1990 yanatokana na udhaifu wa michakato ya

uingiaji wa mikataba ya mikopo na usimamizi wa madeni

ya umma. Migogoro hii ya madeni ilichangia kwa kiasi

kikubwa matatizo ya kiuchumi na kijamii katika nchi za

Kusini mwa jangwa la Sahara kwa kuathiri uimara wa

uchumi na uwezo wa kukopesheka kimataifa. Madeni ya

muda mrefu yalidumaza uwekezaji, ukuaji wa uchumi na

biashara. Kulipia madeni kuliyasonga matumizi ya serikali

katika elimu, afya na mahitaji mengine ya kijamii katika

nchi nyingi zilizokuwa zinadaiwa.

7

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

Mkataba huu wa Kukopa una Kanuni na Miongozo ya

Ukopaji huru wa fedha. Unataka kutoa mwongozo na

kujulisha ukopaji huru kwa lengo la kuchangia uboreshaji

wa utawala dhaifu wa sasa, michakato ya kitaasisi na

kisheria ya mikataba ya mikopo na usimamizi wa deni

la umma. Kwahiyo, AFRODAD inazihimiza nchi zote

zinazokopa hasa zile zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara

kufuata kanuni na miongozo, ili kuhakikisha ufanisi na

utumiaji wenye tija wa rasilimali madeni na vifaa, kuzuia

kujirudia kwa migogoro ya madeni na kuzifanya serikali

kuwajibika kwa wananchi wao.

Mkataba huu una kanuni na miongozo saba pana

zifuatazo:

1. Uzingatiaji wa busara na desturi za ukopaji na

usimimiaji wa madeni ya umma

2. Uwepo wa sheria na kanuni zinazotabirika

3. Miundo na wajibu zinazoratibika na madhubuti

4. Uwepowaofisihuruyausimamiziwamadeni

5. Ushiriki wa umma, ujumuishwaji na kuweka taarifa

hadharani

6. Kuheshimu ubinadamu na haki za watu za kiikolojia

7. Kuheshimiana na usawa katika ubia na wakopeshaji

na wafadhili wa kimataifa

MKATABA WA KUKOPA

8

1 UZINGATIAJI WA BUSARA NA DESTURI ZA UKOPAJI NA USIMIMIAJI WA MADENI YA UMMA

1.1 Msaada wa Kisiasa: Serikali za Kitaifa zinahitaji

kutumia busara na kuupatia msaada umuhimu wa

kisiasa ukopaji na usimamizi wa madeni ya umma ili

kuhakikisha uendelevu wa madeni.

1.2 Mazingira imara ya Kiuchumi: Serikali za Kitaifa lazima:-

1.2.1 Zihakikishe kuwa mkakati wa madeni ya

Umma unaendana na sera kuu ya uchumi kwa

kuhakikisha kwamba kiwango cha ukuaji wa thamani

ya sasa ya deni jipya linalotolewa ni sawa au ni pungufu

ya kiwango cha ukuaji wa mauzo ya nje ya nchi, kwa

ajili ya uendelevu wa deni la nje.

1.2.2 Angalia kama mkopo mpya wa mradi

unaendana na sera ya maendeleo ya uchumi kwa

ujumla kabla ya kuidhinishwa.

9

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

1.2.3 Kuhakikisha kuwa mkopo ni kwa ajili ya sekta

zilizo kipaumbele na lazima kuimarisha uwezo wa

sekta ya Umma hasa katika usimamizi wa uwekezaji

wa umma ili kuongeza thamani ya fedha kwenye

miradi inayofadhiliwa na mkopo.

1.2.4 Kuhakikisha uthabiti wa uchumi mkuu,

uendelevu wa fedha, viwango vya chini vya riba, na

usimamiaji wa viwango vya athari za ukopeshaji taasisi

huru.

1.3 Vifungu vya Katiba: Serikali lazima zianzishe

mifumo sahihi na yenye nguvu kisheria na miundo

itakayowajibika kuratibu na kusimamia madeni ya

Umma.

1.4 Ridhaa ya Umma na Uwazi: Serikali lazima zichukue

hatua za Kisheria kuhakikisha kwamba ukopaji wote

wa Umma na usimamizi wa madeni unapata idhini ya

Bunge na Umma kwa ujumla.

1.5 Kujenga Uwezo: Serikali ni lazima zihakikishe kuwa

nchi zao zina uwezo wa kina, endelevu na wa muda

mrefu wa kusimamia madeni. Hii ni pamoja na:

MKATABA WA KUKOPA

10

1.5.1 Kuwa na fungu la zana za usimamizi wa madeni:

Kumbukumbu sahihi na rekodi za kisasa za madeni

yote na madeni yote ya nje yaliyohakikiwa wazi wazi,

ratiba ya majukumu ya malipo ya madeni ikiwa ni

pamoja na masuala ya dharura; uwezo wa kukadiria

athari za maamuzi ya kukopa ya taasisi nyingi za ndani

kwenye wasifu mzima wa deni la nchi; bajeti ya Taifa

na uwiano wa malipo.

1.5.2 Kuhakikisha kwamba wafanyakazi wote wa

Umma wanaoshughulika na kuingia mikataba ya

mikopo na usimamizi wa deni la Umma wanalenga

katika ufanisi wa kazi na majukumu yao:

1.5.2.1 Hakikisha mafunzo zaidi kwa walioshika

ofisi zinazohusika kwenye mikataba ya mikopo na

usimamizi wa deni la Umma – wakaguzi wa hesabu,

wahasibu, wachumi na wanasheria.

1.5.2.2 Hakikisha kwamba wafanyakazi wenye uzoefu

na motisha wanabakia na kupatiwa msaada wa

miundombinu muhimu, teknolojia na rasilimali fedha.

1.5.2.3 Hamasisha ushirikishaji wa wataalamu wa

nje ili kujenga ujuzi wa rasilimali watu waliopo

inavyotakiwa au hitajika.

1.5.2.4 Hamasisha kaguzi za pamoja na Taasisi

nyingine kubwa za Ukaguzi zilizoendelea.

11

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

2 UWEPO WA SHERIA NA KANUNI ZINAZOTABIRIKA

2.1 Mfumo wa Sheria: Mikataba yote ya mikopo ya

Umma na sheria na kanuni za usimamizi wa madeni

lazima zifungamane na vifungu vya katiba na sehemu

nyingine halisi za sheria zinazofafanua jinsi gani mikopo

ya Umma ipatikane, itumike na kulipwa.

2.1.1 Mfumo wa Sheria lazima pia utoe muda

maalum ambamo maombi ya mkopo yatafanyika na

kuidhinishwa ili kuepuka kupunguza kasi ya michakato

ya uidhinishaji ili kuhakikisha utekelezaji kwa wakati

na ufuatiliaji wenye ufanisi.

2.1.2 Mikataba mipya ya mikopo itakuwa ndani ya

muktadha wa mkakati mzima wa deni la serikali na

kulingana na programu/mipango ya maendeleo ya

Taifa. Mipango ya kukopa ya serikali inabidi kuendana

na uendelezaji wa muda mrefu wa deni.

2.2 Mamlaka ya Kukopa: Mfumo wa Kisheria lazima

uweke wazi ni nani mwenye mamlaka ya kukopa kwa

niaba ya serikali.

MKATABA WA KUKOPA

12

2.2.1 Kuna haja ya kuwa na miongozo iliyowazi

ya kisheria/kikatiba kuhusu majukumu na uwajibikaji

kati ya wakala wa serikali wanaohusika kwenye

usimamizi wa madeni, hasa kwa upande wa Wizara

ya Fedha, Benki Kuu na wakala tofauti au yeyote wa

usimamizi wa madeni na majukumu ya wafanyakazi

yaliyoainishwa vizuri ikiwa ni pamoja na sera bayana

za udhibiti na ufuatiliaji na mipangilio ya utoaji taarifa.

2.3Kiwango cha juu cha Kukopa: Inabidi ziwepo sheria,

kanuni na sera ambazo zitaainisha mipaka ya ukopaji

wa madeni ya Umma ya nje. Hii lazima ilandane na

uchambuzi endelevu wa deni la nchi.

2.4 idhini ya Kukopa: Muhimili wa kutunga sheria wa

serikali – Bunge litaidhinisha mikopo kabla mikataba

haijasainiwa. Hii itawezesha na kuhakikisha kwamba

mchakato wa mkataba wa mkopo ilifanyika kulingana

na miongozo na sheria zilizowekwa, na inaweza

kulipwa katika bajeti ya Taifa.

2.5 Mchakato wa Kuidhinisha: Sera ya Kukopa ambayo

inaainisha taratibu za kuidhinisha, muundo wa kamati

ya majadiliano na maandalizi ya majadiliano lazima

zianzishwe.

13

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

3 MIUNDO NA WAJIBU ZINAZORATIBIKA NA MADHUBUTI

3.1 Muundo wa Taasisi, Uratibu na Mawasiliano: Serikali

zitaanzisha Ofisi ya Usimamizi wa Madeni yaTaifa

(OUMT) kuhakisha uratibu na mawasiliano mazuri

kati ya wadau mbalimbali kwenye kuingia mikataba ya

mikopo na taratibu za usimamizi wa madeni.

3.2 Wizara ya Fedha: Wizara husika (mf. Wizara ya

Fedha) itawasilisha mahitaji ya serikali kukopa kwa

ajili ya idhini bungeni ili kupitishwa kama inavyotakiwa

kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

3.2.1 Wizara ya Fedha: Itasimamia fedha za nchi

ili kuhakikisha kuwa uwajibikaji kamili unafanyika

kwa Bunge na kwamba udhibiti wake wa fedha

unaimarishwa.

3.2.2 Wizara husika: Wizara husika zita:

3.2.2.1 Toa taarifa za mara kwa mara za maendeleo

ya programu zote zinazofadhiliwa na mikopo ya nje/

miradi kwa Wizara ya Fedha.

MKATABA WA KUKOPA

14

3.2.2.2 Shiriki katika majadiliano na mashauriano yote ya mikataba yote ya mkopo kwa ajili ya miradi na programu chini ya mamlaka yao.

3.2.2.3 Tekeleza, fuatilia na tathmini miradi na programu zote kwenye mamlaka yao kwa kushirikiana kwa karibu na wafadhili, Wizara ya Fedha, asasi za kiraia na walengwa.

3.3 Uangalizi wa Bunge: Bunge litasimamia jukumu muhimu la kuhakikisha uwajibkaji katika kuingia mikataba na michakato ya usimamizi wa madeni.

3.3.1 Bunge madhubuti na linalowajibika hukabiliana na athari za ukopaji uliokithiri kwa kushinikiza mifumo ya uwajibikaji wa serikali na uchunguzi wa kisheria, na kuishinikiza serikali kuboresha utendaji wa kifedha na

kibajeti. 3.3.2 Mwanasheria Mkuu: Mwanasheria Mkuu wa

Serikali atatoa ushauri wa kisheria wakati mchakato wa mkataba wa mkopo ili kuhakikisha kwamba unaenda sambamba na sheria za nchi.

3.4 Ukopaji wa Makampuni ya Umma: Serikali lazima ianzishe utaratibu na vigezo kwa ajili ya kutoa dhamana kwa makampuni ya Umma. Hii ni muhimu kwasababu endapo makampuni ya Umma yatashindwa kulipa riba

na gharama za madeni, serikali itatakiwa kulipa.

15

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

3.5 jukumu la Benki Kuu: Benki Kuu itapaswa kufanya kazi

kama mshauri wa kifedha wa serikali kwenye masuala

ya mikataba ya mikopo na kusimamia madeni.

3.5.1 Sheria ya nchi inatakiwa ionyeshe wazi

madaraka ya Benki Kuu, uhusiano wake na Wizara

ya Fedha, uhuru wake, uwajibikaji wake kwa Bunge

na Taifa, tahadhari lazima ichukuliwe ili kuepuka

udhalimu/matumizi mabaya ya madaraka kama hayo.

3.5.2 Benki Kuu inatakiwa kudumisha mfumo

salama na madhubuti wa malipo na ulipaji.

3.5.3 Benki Kuu itapaswa kupata maelezo yote ya

mali fedha za serikali na taasisis zake kutoka kwenye

taasisi za fedha na kuziwasilisha kwenye Ofisi ya

Madeni na Wizara ya Fedha.

3.5.4 Benki Kuu itapaswa kuwezesha ulipaji wa

madeni kwa kufuata ushauriwaOfisi yaUsimamizi

wa Madeni.

3.6 Mkaguzi Mkuu wa hesabu:OfisiyaMkaguziMkuuwa hesabu itawajibika kukagua taarifa za madeni ya

umma zilizowekwa wazi kwenye taarifa za fedha za

serikali au nyaraka nyingine ambazo kiasi cha deni

la Umma limeonyeshwa na kuhakikisha kuwa kiasi

kimeonyeshwa/wakilishwa katika misingi sahihi.

MKATABA WA KUKOPA

16

3.6.1 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu lazima awezeshwe

vizuri na aripoti kwa wakati kuhusu akaunti ya umma

ya nchi.

3.6.2 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atafanya uchambuzi

huru na kuhakikisha kwamba taarifa zinawekwa

bayana kwa umma na bodi muhimu au makundi ili

kuwezesha usimamizi wa madeni ulioboreshwa na

uelewa wa athari za kujifunga kifedha za sasa na za

baadaye. Mkaguzi Mkuu wa Hesabu lazima afanye

kaguzi kuhakikisha ufuatiliaji wa vigezo vya biashara za

kifedha vilivyowekwa kwenye usimamizi wa madeni.

3.7 Mhasibu Mkuu: Ofisi ya Mhasibu Mkuu itatoamiongozo na taratibu kwa ajili ya usimamizi wa fedha

za umma.Ofisi yaMhasibuMkuu inapaswa kuweka

mfumo wa jumla wa udhibiti na utumiaji wa rasilimali

za umma.

3.8 Taasisi za Fedha za Kimataifa/wakopeshaji: Taasisi

za fedha za Kimataifa kwa kutumia Miongozo ya

Usimamiaji wa Madeni ya Umma ya Kundi la IMF/

Benki ya Dunia lazima ziwezeshe ushauri wa kitaalamu

kwa nchi, mara kwa mara kusisitiza haja ya madeni

endelevu na kuwezesha utekelezaji wenye ufanisi wa

mipango ya uchumi.

17

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

3.8.1 Uwezo wa ufadhili wa ndani: Taasisi za Fedha

za Kimataifa zisaidie katika kujenga na kuimarisha

uwezo wa ndani wa kufanya tafiti ambazo zitaarifu

mchakato wa kutengeneza sera.

MKATABA WA KUKOPA

18

4 UWEPO WA OFISI HURU YA USIMAMIZI WA MADENI

4.1 Mfumo wa Usimamizi wa Madeni: Kwa madhumuni ya kuwa na mfumo mzuri wa uratibu wa mikataba ya mikopo na usimamizi wa madeni serikali inabidi ianzisheOfisi yaUsimamiziwaMadeni. Shughuli zaUsimamiziwaMadenilazimaziwekwechiniyaOfisimoja ya Usimamizi wa Madeni yenye majukumu ya nyuma, kati na ya mbele ya kiofisi.Wakati ofisiya mbele itashughulika na sera za madeni, sera za kukopa, taratibu na mbinu za kujadiliana, uelewa wa kitaaluma, ofisi ya kati itajikita kwenye kitengo chauchambuzi/upembuzi na athari, umuhimu wa mkopo uliopendekezwawakatiofisiyanyumaitajishughulishana utunzaji wa takwimu, ukuaji wa mikopo, uthibitishaji wa taarifa za madeni, misaada na masharti.

4.2 Uratibu wa Madeni yote: Ofisi ya Usimamizi waMadeni inaiwezesha nchi kuunganisha, kupanga na kuimarisha shughuli zote za usimamizi wa madeni kwenye chombo kimoja maalumu kilicho huru. Hii inaruhusu mpangilio mzuri wa udhibiti na inaondoa mwingiliano na kujirudia kunakohusiana na ushirikishwaji wa mawakala wengi, na ambapo usambaaji wa habari ni dhaifu na unaratibiwa vibaya.

19

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

4.3 Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Madeni: ShughulinajukumulaOfisiyaUsimamiziwaMadenivinapaswa kuwa vimeandikwa vizuri na kuwekwa kwenye nyaraka, ikiwa na kitabu cha muongozo, ikiwa ni pamoja na program muhimu za usimamizi za komputa.

4.4 Uwepo wa huduma za Kitaalamu: Ofisi huru yaUsimamizi wa madeni ya umma (DMOs) itoe faida za kipekee za kiutawala na utumishi na ubadilikaji ambao siowa kawaida kwaofisi/vitengo vya usimamiziwamadeni ambavyo ‘vimeingizwa’ kwenye wizara za fedha na/Benki Kuu.

4.5AinayaOfisiyaUsimamiziwaMadeni: Jukumu la Ofisi yaMadeni linategemeana na shughuli zake zausimamizi wa madeni, kama majukumu inayopangiwa na sheria na taratibu, kwenye mkakati inayochagua kuufuata na kwenye njia ilizowekewa kuyafikiamalengo yake. Ili kuhakikisha kwamba michakato ya usimamizi wa madeni, kama vile ulipaji wa madeni inafanyika kwa ufanisi zaidi; wajibu na majukumu lazima yawe wazi na taarifa za madeni lazima ziwe zimeimarishwa.

MKATABA WA KUKOPA

20

5 USHIRIKI WA UMMA, UJUMUISHWAJI NA KUWEKA TAARIFA HADHARANI

5.1 Umiliki na Uwajibikaji: Umiliki wa Kitaifa ni muhimu

kwa mafanikio ya miradi yote ya maendeleo

inayofadhiliwa kwa mikopo na ruzuku. Watu, ambao

wanapaswa kuwa walengwa wa mwisho wa mikopo

iliyochukuliwa kwa jina lao, lazima wawe na haki ya

kushiriki katika mchakato wa kufanya maamuzi ya

yanayohusu kukopa kwa umma. Hili lifanyike kupitia

uwakilishi wa bunge, ushiriki wa raia wa moja kwa

moja au ushiriki wa raia kupitia asasi za kiraia au

uwakilishaji. Asasi za kiraia, hasa waangalizi na makundi

yenye maslahi, yanapaswa kutambuliwa kama njia za

kuimarisha umiliki wa fedha za umma na uwajibikaji.

5.2 Uwazi na ushirikishaji wa wananchi kikamilifu: Mchakato wa mkataba wa mkopo lazima uwe wa

uwazi na shirikishi, ukiwashirikisha wananchi na

jamii zinazoathirika kwa kuwapa taarifa na muda wa

kutosha kujadili uchukuaji wa mkopo, ikiwa ni pamoja

na kusudi na masharti ya mkopo kwa mujibu wa

katiba ya nchi.

21

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

5.3 Kutambuliwa asasi za Kiraia Kisheria na Kitaasisi: Serikali zilizokubaliana na Mkataba huu zianzishe

mabaraza na taratibu ambazo wananchi kwa kupitia

hayo mabaraza na hizo taratibu wanaweza kujadili

na kushawishi mapendekezo ya sera za kiuchumi

kuimarisha umiliki wa umma wa mikakati ya uchumi

na madeni. Sheria za serikali lazima zionyeshe wazi

kwamba hii asasi ya kiraia ita:

5.3.1 Kuwa na jukumu la kushauri katika mchakato

wa mkataba wa mkopo na usimamizi wa madeni

ikifanya kama wataalamu ikifanya kazi kwa karibu na

wanaoongoza majadiliano na serikali kwa kushawishi

maamuzi ya kisera, kwa kutoa ushauri wa kisheria,

kitaalamu au kiufundi.

5.3.2 Fanya tafiti na uhamasishaji wakati wa

kutengeneza mapendekezo ya mradi/programu

na kwenye hatua za majadiliano ya makubaliano ya

mkopo.

5.3.3 Fuatilia miradi na mipango ya maendeleo,

ikiwa ni pamoja na namna inavyofadhiliwa. Hii

inaruhusu asasi za kiraia kufuatilia matokeo ya miradi

na programu zinazofadhiliwa na mikopo, pamoja na

fedha zilizotolewa kama matokeo ya mipango ya

msamaha wa madeni.

MKATABA WA KUKOPA

22

5.3.4 Hamasisha umma na ongeza ufahamu juu ya

masuala ya mikopo, ruzuku na masuala ya fedha za

maendeleo.

5.4 Utoaji wa taarifa kwa umma: Sheria ya Serikali ya

Fedha za Umma na uwajibikaji ieleze bayana kuwa

taarifa za matumizi ya fedha za mikopo ziwekwe

wazi kwa umma, hasa makundi ya kiraia, yenye nia

ya kufuatilia mikopo na ruzuku za serikali. Mkataba

wa mkopo uwekwe wazi kwa umma na usambazwe

kwa wadau mbalimbali kwa kutumia njia sahihi za

mawasiliano na zinazopatikana chini. Hii inaweza kuwa

kupitia kwa wabunge, matangazo kwa njia ya tovuti,

vyombo vya habari vya taifa, radio na/au televisheni.

5.5 Lugha: Mkataba upatikane kwa lugha kuu za Taifa

(ikiwa ni pamoja na lugha za jumuiya zilizoathirika).

Matoleo yote mawili toleo kuu na lililotafsiriwa yawe

na uhalali sawa mahakamani.

23

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

6 KUHESHIMU BINADAMU NA HAKI ZA WATU ZA KIIKOLOJIA

6.1 haki ya Umma ya Maendeleo endelevu: Sambamba

na mkataba wa Afrika Haki za Binadamu serikali

zihakikishe kuwa wananchi wanayo haki ya kupata

kikamilifu haki yao ya maendeleo endelevu kutoka

kwenye rasilimali madeni. Haki ya maendeleo na

uchumi zisitengwe na haki za kijamii, kisiasa na

kitamaduni.

6.2 Kukabili madhara ya Kukopa: Serikali ihakikishe

kwamba madhara ya kukopa na athari zozote za

utekelezaji wa miradi ya maendeleo vinapunguzwa

mpaka kiwango cha chini kwa watu wa kawaida hasa

makundi maalumu kama vile wanawake na watoto.

Miradi inayofadhiliwa kwa madeni lazima isikiuke haki

za binadamu na wala isichangie ukiukwaji wa haki za

binadamu. Haki hizi zimebainishwa kwenye Mikataba

na makubaliano yanayotambulika kimataifa ya Haki

za Binadamu ambayo wakopaji au wakopeshaji

wamesaini.

MKATABA WA KUKOPA

24

6.3 Uhamishaji: Miradi mikubwa ya maendeleo kwa hali

yoyote ile lazima iepuke kuwa chanzo cha uhamishaji

wa wazawa, masikini wa vijijini na wale wa kwenye

makazi duni mijini kwenye ardhi yao, chanzo cha

kipato na jamii. Iwapo miradi ya maendeleo kwa

sababu yoyote itasababisha uhamishaji wa watu

kutokakwenyemakaziyaofidiastahiliitatolewakwa

jamii zilizoathiriwa.

6.4 Uharibifu wa Mazingira: Ukopaji wowote wa Umma

ni lazima usikubali miradi inayokiuka viwango vya

chini vinavyokubalika kimataifa vya utunzaji/ulinzi wa

jamii, kazi na mazingira.

25

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

7 KUHESHIMIANA NA USAWA KATIKA UBIA NA WAKOPESHAJI NA WAFADHILI WA KIMATAIFA

7.1 Kuheshimiana: Serikali zitahakikisha kuwa uingiaji

wa mikataba ya mikopo na masuala ya usimamizi wa

madeni na wakopeshaji yanafanyika kwa kuheshimiana

na utu. Kanuni za msingi za Ufanisi wa Msaada

kwenye Azimio la Paris ya mwaka 2005, Ajenda ya

Accra ya mwaka 2008 na Ushirikiano wa Busan kwa

Ushirikiano Madhubuti wa Maendeleo ya mwaka 2011

lazima zitumike kuhakikisha usawa katika ushirikiano

kati ya wafadhili na mataifa yanayokopa.

7.2 Kukataa Masharti: Nchi wanachama wa Mkataba huu

lazima wakatae utumiaji wa masharti wa wafadhili na

taasisi za fedha za kimataifa wanapokopa fedha. Hii

huwasababishia kuwajibika kwa wakopeshaji na sio

kwa wananchi wao.

MKATABA WA KUKOPA

26

7.3 Kuheshimu na Kuwezesha Taasisi za ndani: Wafadhili

na Wakopeshaji wote wanapaswa kuvipatia vyombo

vya uangalizi vya serikali na mabunge msaada wa

kifedha na kitaalamu kuviwezesha kushiriki kikamilifu

katika kujadili na kufuatilia mikopo ya nje.

7.4 Usuluhishi wa haki na Uwazi: Mkataba wa mkopo

lazima uwe na kifungu kwa ajili ya utaratibu wa

usuluhishi huru na wazi iwapo kutakuwa na ugumu

katika ulipaji au mgogoro (kwa ombi la mkopaji au

mkopeshaji). Kutakuwa na usubirishaji wa ulipaji

wa deni wakati majadiliano yakiendelea. Mkopaji

asifunguliwe kesi mahakamani wakati majadiliano

yanaendelea. Wakopaji na Wakopeshaji lazima

wakubaliane na uamuzi wa msuluhishi huru na kuna

haki ya kukata rufaa.

27

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

MAREJEO NA USOMAJI NA ZIADA

1. AFRODAD (2007) “The Loan Contraction Process in Africa: Making

Loans Work for the Poor: The Case of DRC,” Study Report

2. AFRODAD (2007) “The Loan Contraction Process in Africa: Making

Loans Work for the Poor: The Case of Malawi,” Study Report

3. AFRODAD (2007) “The Loan Contraction Process in Africa: Making

Loans Work for the Poor: The Case of Tanzania,” Study Report

4. AFRODAD (2007) “The Loan Contraction Process in Africa: Making

Loans Work for the Poor: The Case of Mozambique,” Study Report

5. Borresen P and Pascal E.C (2001); “Role and organization of a debt

office”,Proceedingsofthesecondinter-regionaldebtmanagement

conference, United Nations Conference on Trade and Development,

pp33-53.

6. Chadambuka. Z.T. (2009) A Critical Review of the Legal Framework

of the Public Loan Contraction and Debt Management System in

Zimbabwe. ZIMCODD, Harare.

7. Mutasa, C. (2007) ‘Operationalizing debt sustainability’ in UNCTAD

(2007) Proceedings of the Fifth Inter-regional Debt Management

Conference, UN, Geneva.

MKATABA WA KUKOPA

28

8. De Renzio, P and Krafchik,W. (2007) “Lessons from the field:

The impact of Civil Society Budget Analysis and Advocacy in Six

Countries”, A Practitioners’ Guide, International Budget Project,

Washington D.C. International Budget Project.

9. Fyson, S (2009) “Sending in the Consultants: development agencies,

theprivatesectorandthereformofpublicfinanceinlow-income

countries,” International Journal of Public Policy, Vol.4 n. ½.

10. Krafchik, W (2003) “What role can Civil Society and Parliament

Play in Strengthening the External Auditing Function?” International

Budget Project, Washington D.C. International Budget Project.

11. Maruping. A.M. (2003) ‘ Public Debt Sustainability and the

development of domestic markets’ in UNCTAD (2003) Proceedings

of the Fifth Inter-regional Debt Management Conference and

WADMO conference, UN, Geneva.

12. MEFMI (2004) Towards an Effective national debt management

strategy in Tanzania, Workshop on Debt Management, Dar es Salaam,

United Republic of Tanzania.

13. MEFMI (2005) MEFMI, Public Debt Management Procedures Manual

vol 1. Sable Press (PVT) Ltd, Harare.

14. Meja,V.(2008)ThePublicLoanContractionProcess-AkeytoDebt

Management and Economic Governance, AFRODAD. Harare.

15. OverseasDevelopmentInstitute(2007)“Reformingpublicfinancial

management when the politics aren’t right: A proposal,” Opinion

Paper 89, London.

29

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

16. UNCTAD (2007) Proceedings of the Fifth Inter-regional Debt

Management Conference, UN, Geneva.

17. UNCTAD (2003) Proceedings of the Fifth Inter-regional Debt

Management Conference and WADMO conference, UN, Geneva.

18. United Republic of Tanzania (2004) Governments Loans, Guarantees

and Grants Act, 1974 and Amendments 2004

19. UNITAR (2002) Institutional Framework for Public Sector

Borrowing, UNITAR Training Programmes in the Legal Aspects and

Financial Management, Document No.17. Geneva.

MKATABA WA KUKOPA

30

KWA TAARiFA zAiDi WASiLiAnA nAAfrican Forum and Network on Debt and

Development (AFRODAD)

31 Atkinson Drive, Hillside

S.L.P. CY1517, Causeway

Harare, Zimbabwe

Simu: +263 4 778531/6

Nukushi: +263 4 747878

Tovuti: www.afrodad.org

Barua pepe: [email protected]

31

KAnUni nA MiOngOzO yA UKOPAji hURU WA FeDhA KWA nchi zA AFRiKA

African Forum and Network on Debt and Development

31 Atkinson Drive, Hillside

S.L.P. CY1517, Causeway

Harare, Zimbabwe

Simu: +263 4 778531/6

Nukushi: +263 4 747878

Tovuti: www.afrodad.org