ki 214 ufundishaji kiswahili kwa wageni mbinu za ... · v. kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na...

19
1 KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI I. Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni Lengo kubwa ni kwamba ili mwanafunzi aweze kujua lugha hiyo kwa stadi zote za lugha ile. Stadi za lugha ni 1. Kusikiliza 2.kuzungumza 3. Kusoma 4.kuandika 5. Sarufi 6. Utamaduni wa lugha ile Malengo ya jumla ya kufundisha ili ni pamoja na:- 1) Kumwezesha mwanafunzi ili aweze kumudu lugha. 2) Kumwezesha mwanafunzi aweze kuwasiliana na wazawa wa lugha husika LUGHA YA KWANZA Stern (1983) anasema kwamba “lugha ya kwanza lugha ambayo mtoto hupata kutoka kwa mama yake mzazi angali mchanga. LUGHA YA PILI Stern (1983) anasema kwamba “ lugha ya pili si lugha ambayo mtoto/mtu aliipata alipoanza kukua na kupata lugha. Hii ni lugha ya kujifunza,kwa maana ya kwamba mtu huyu huwa tayari ana lugha nyingine.mfano. hapa Tanzania Kiswahili ni lugha ya pili kwa watu wengi LUGHA YA KIGENI Ni ile lugha ambayo unajifunza na kuitumia lakini wazungumzaji wake wako nje ya nchi au mbali na jamii anapokaa mwanafunzi huyo. Mfn lugha ya kiingereza ni lugha ya kigeni hapa Tanzania MALENGO YA JUMLA YA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI WA LUGHA YA KIGENI Mara nyingi hii hutegemea taaasisi yenyewe lakini kuna malengo ambayo ni ya jumla: 1) Kutaka kuwasiliana na wenyeji wa sehemu /nchi husika 2) Kujiandaa kusafiri kwenda nchi nyingine kwa shughuli mbalimbali 3) Kwa ajili ya kufanya biashara 4) Kukidhi vigezo vya masomo 5) Kufanya utafiti katika taaluma husika 6) Ili kupata ajira nchi za ng‟ambo KITU GANI KIANZE KUFUNDISHWA SASA? Onyo: usijaribu kumfundisha mwanafunzi sarufi za lugha hiyo kwanza, utamfundisha ikibidi lakini isiwe kipaumbele chako Anza na salamu za kawaida, salamu katika utamaduni wa mwafrika ni kitu cha muhimu sana, hivyo fundisha salamu,maana lengo ni kwamba huyo mtu aweze kuwasiliana.

Upload: others

Post on 04-Feb-2020

51 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

1

KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI

MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI

I. Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni

Lengo kubwa ni kwamba ili mwanafunzi aweze kujua lugha hiyo kwa stadi zote za lugha ile.

Stadi za lugha ni 1. Kusikiliza 2.kuzungumza 3. Kusoma 4.kuandika 5. Sarufi 6. Utamaduni

wa lugha ile

Malengo ya jumla ya kufundisha ili ni pamoja na:-

1) Kumwezesha mwanafunzi ili aweze kumudu lugha.

2) Kumwezesha mwanafunzi aweze kuwasiliana na wazawa wa lugha husika

LUGHA YA KWANZA

Stern (1983) anasema kwamba “lugha ya kwanza lugha ambayo mtoto hupata kutoka kwa mama

yake mzazi angali mchanga.

LUGHA YA PILI

Stern (1983) anasema kwamba “ lugha ya pili si lugha ambayo mtoto/mtu aliipata alipoanza

kukua na kupata lugha. Hii ni lugha ya kujifunza,kwa maana ya kwamba mtu huyu huwa tayari

ana lugha nyingine.mfano. hapa Tanzania Kiswahili ni lugha ya pili kwa watu wengi

LUGHA YA KIGENI

Ni ile lugha ambayo unajifunza na kuitumia lakini wazungumzaji wake wako nje ya nchi au

mbali na jamii anapokaa mwanafunzi huyo. Mfn lugha ya kiingereza ni lugha ya kigeni hapa

Tanzania

MALENGO YA JUMLA YA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI WA LUGHA YA

KIGENI

Mara nyingi hii hutegemea taaasisi yenyewe lakini kuna malengo ambayo ni ya jumla:

1) Kutaka kuwasiliana na wenyeji wa sehemu /nchi husika

2) Kujiandaa kusafiri kwenda nchi nyingine kwa shughuli mbalimbali

3) Kwa ajili ya kufanya biashara

4) Kukidhi vigezo vya masomo

5) Kufanya utafiti katika taaluma husika

6) Ili kupata ajira nchi za ng‟ambo

KITU GANI KIANZE KUFUNDISHWA SASA?

Onyo: usijaribu kumfundisha mwanafunzi sarufi za lugha hiyo kwanza, utamfundisha ikibidi

lakini isiwe kipaumbele chako

Anza na salamu za kawaida, salamu katika utamaduni wa mwafrika ni kitu cha

muhimu sana, hivyo fundisha salamu,maana lengo ni kwamba huyo mtu aweze

kuwasiliana.

Page 2: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

2

MALENGO YA UJUMLA YA UFUNDISHAJI LUGHA YA KISWAHILI KWA

WAGENI

a) Ili mwanafunzi wa Kiswahili ajue mambo yafuatayo:

i. Aweze kumudu lugha ya Kiswahili

ii. Aweze kuwasiliana na watumiaji wa lugha ya Kiswahili

iii. Ili wanafunzi waweze kung‟amua mambo yafuatayo:- Namna ya kusema jambo

gani? Mfano anataka kwenda chooni Asemee wapi? Kwa nini aseme? Kwa nani

aseme? Mazingira gani aseme?

iv. Ili kuwapa wanafunzi mbinu mbalimbali za kujifunza lugha ya Kiswahili.

Wanafunzi wafanye kwa vitendo ili waweze kujichukulia misamiati ya kutosha

v. Wanafunzi wang‟amue umuhimu wa lugha wanayojifunza

b) ili wanafunzi waweze kutimiza malengo haya, mwalimu ni lazima wape wanafunzi:

kuchunguzakugunduakutalii kuhusu lugha ya Kiswahili

c) wape uwezo wa kukuza lugha ya Kiswahili kila siku aweze kuongeza msamiati kwa

kusoma vitabu mbalimbali vya hadithi

d) wape nafasi kutumia mbinu mbalimbali lugha ili kukuza uelewa wao

e) wape uwezo wa kukuza fikra zao na kudadisi

f) wasaidie kufanya utumbuizi wa vipengele vya mfumo na utamaduni wa lugha ya

Kiswahili

NADHARIA KUU ZA UJIFUNZAJI LUGHA

Kuna mambo mawili ambayo waalimu tarajili wanapaswa kujua

1) mbinu za kujifunza lugha ya pili ni nyingi kama ilivyo waalimu wengi

2) manzingira halishi wakati wa ujifunzaji. Rogers (2001) anasema kwamba “ wakati

wa ufundishaji wa lugha ya kigeni hutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya

kuwasaidia wanafunzi wafikie malengo yao”

kuna nadharia kuu nne (4)za ujifunzaji lugha:

1) NADHARIA YA UHULKA

Mwasisi wake ni Noamy Chomsky (1957)

Wazo kuu lake ni kwamba: binadamu huzaliwa akiwa na uwezo lugha. Yaani kwenye

ubongo wake ana mfumo ambao huzaliwa nao kwa ajili ya kujifunza lugha. Ana kifaa

kinachoitwa LAD (Kifaa cha upataji lugha)

Naye Brown (2000) aliunga mkono mawazo haya. Mwingine aliyeunga mkono ni

Ellis (1997) walikuwa na hoja kwamba kuna kipindi mtu akifikia umri Fulani

hawezi kupata lugha sawasawa na wazawa wa lugha husika. Umri huo ni kuanzia

0-miezi 18. Kwa mujibu wa wataalamu hawa mazingira hayana msaada wowote

katika ujifunzaji lugha.

2) NADHARIA YA UTABIA (BEHAVIORISM)

Mwasisi wa nadharia hii ni J.B Watson. Wengine wanaoshadidia nadharia hii ni

Leornald Bloomfied, O.N Mowrer, B.F Skinner na A.W Staats

Edward Thorndike (1935) alikuwa wa kwanza kabisa kutafiti zaidi. Kwa mujibu

wa wanatabia ujifunzaji wa lugha ni mwigo kwa maana ya kwamba huiga kile

kinachosemwa na watu wanaomzunguka

Page 3: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

3

Aliyetafiti zaidi katika nadharia ya ujifunzaji ni Burrhus Frederic (B.F) skinner ,

Huyu alikubali ni mwigo lakini akaongeza kuwa ni uimarikaji wa tabia, hivyo

mtoto mdogo hazaliwi na lugha bali huichota kutoka kwa wazazi wake

Wilga Rivers (1968)anasema mtoto hujifunza kupitia kujaribu na kukosea “trial

and error’ huendelea kufanya hivyo mpaka anapofikia matamshi ya jamii nzima.

Nadharia hii inayapa mazingira nafasi kubwa katika ujifunzaji lugha

Je mtu akitengwa na jamii anaweza kuwa na lugha?

3) NADHARIA YA UTAMBUZI

Nadharia hii iliasisiwa na Jean Piaget (1954)

Alidai kuwa binadamu anapozaliwa kuna kipindi maalum cha kupata lugha

Alidai kuwa kujifunza lugha ni sehemu ya makuzi ya binadamu, kwa kadiri

unavyokua ndivyo unavyozidi kupata lugha

Alidai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa.

Arth(2003) anadai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa,kuanzia 0-miezi

18

Nadharia hii haipingani na umuhimu wa mazingira katika ujifunzaji lugha

4) NADHARIA YA UUMBAJI

Nadharia hii iliasisiwa na Jerome Brunner

Wazo kuu la nadharia hii inasisitiza nafasi ya mama katika upataji lugha ya

kwanza

Mtoto hutengeneza lugha kutegemeana na mawasiliano ambayo mama yake

anayatumia

Alidai, ili mtoto aweze kupata lugha ni lazima mambo yafuatayo yatimizwe

Muktadha

Tajiriba (experience)

Upangilifu (organization)

Kujenga mazingira ya upekuzi (udadisi_

Hukaza zaidi kuhusu mazingira katika ujifunzaji lugha

Mwalimu awatie moyo wanafunzi kugundua mfumo wa lugha wao wenyewe

Mwalimu na wanafunzi wanapaswa kutumia sana majadiliano

NJIA ZA UJIFUNZAJI LUGHA YA KISWAHILI

Njia za ufundishaji Kiswahili ni nyingi kama na waalimu nao walivyo wengi, lakini njia hizi

itatengemea hali ya wanafunzi, hata hivyo njia zifutazo zinapendekezwa zitumike.

1. Njia ya majadiliano-njia hii haifai kwa mwanafunzi ambaye ndio kwa mara ya

kwanza anasikia Kiswahili. Lakini ni njia nzuri kwa mwanafunzi ambaye

amewahi kusikia habari za Kiswahili

2. Njia ya mahojiano. Mfano mwalimu aandae maswali, awaambie wanafunzi

wajipe vyeo mfano mmoja anakuwa daktari mwingine anakuwa mgonjwa n.k

3. Mchezo wa maswali. Kwa mfano. Kama wewe ungekuwa rais wa marekani

ungefanyaje kuhakikisha unakomesha ugaidi duniani? Watajibu na kujipatia

msamiati kibao

4. Njia ya uigizaji-mwli awape wanafunzi mwongozo wa maigizo

Page 4: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

4

5. Njia ya maswali ya papo kwa papo (ana kwa ana) mfano: mimi ni Seni, wewe

ni nani?

6. Njia ya uwandani. Mfano ukitaka kuwafundisha misamiati ya sokoi wapeleke

sokoni.

7. Njia ya kutumia mazingira mbalimbali. Mfano kama mwalimu anataka

kuwafundisha michezo wapeleke uwanja wa mpira

8. Njia ya usomaji. Mfano kusoma pande nne za dunia,kuwapa matini mbalimbali

wanafunzi

9. Njia ya majadiliano funge. Yaani wanafunzi wanajadili vitu ambavyo

vimewekewa mipaka

Angalizo:uteuzi wa njia ipi itumike itategemea aina ya wanafunzi na kazi zao!

HULKA/TABIA YA UANAFUNZI KUJIFUNZA LUGHA

Wanafunzi hutofautiana kulingana na hulka zao, mwalimu anahitaji kuangalia mielekeo ya

wanafunzi wake. Baadhi ya tabia zao ni kama vile: ucheshi, hasira, aibu, hasira za kutojua,

hapendi kusahihishwa, mkimya nk

ATHARI ZA KIJAMII KUHUSU LUGHA/WANALUGHA

Kila jamii ina mtazamo wake kuhusu ujifunzaji lugha, mtazamo hasi ndio ambao huathiri

ujifunzaji lugha na kupelekea kutopata motisha wa kujifunza lugha. Baadhi ya mambo

yanayoathiri ni kama vile

i. Nia au lengo la kujifunza lugha hiyo

ii. Jinsia; inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha kuliko wanaume

iii. Umri; umri mdogo ni rahisi kupata lugha kuliko umri mdogo

iv. Mazingira; mazingira mazuri yanavutia mwanafunzi kujifunza haraka

v. Umilisi wa lugha kama akiwa na umilisi mdogo

Malengo ya mwalimu ni kuhakikisha anafanya mambo yafuatayo:

i. Kuwatia motisha wa kujifunza lugha

ii. Kumsaidia kuondokana na hasira

iii. Kuondoa dhana potofu ya ujifunzaji lugha. Mf. Kuna wanaoamini kwamba

Kiswahili ni lugha ya kiislamu

iv. Kuondoa utata katika vipengele vya kisarufi

v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika

Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara zinazotumika katika jamii.

Hivyo mwalimu anapaswa awaeleze mambo yafuatayo;

i. Baadhi ya utamaduni huangalia usoni, tabasamu na kujiamini

ii. Matumizi ya mkono wa kushoto au wa kulia

iii. Kuonyesha vidole-jamii zingine haziruhusu kabisa

iv. Namna ya kusimama na kuelezea jambo

Ili kutimiza hayo yote mwalimu lazima awe na sifa zifuatazo:

i. Awe muwasilishaji mzuri

Page 5: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

5

ii. Awe na mpangilio mzuri

iii. Awe mstahimilivu

iv. Awe na ujuzi wa kufundisha

v. Awe na uhusiano mzuri na wanafunzi

vi. Awe na maarifa ya somo

SIFA ZA MJIFUNZAJI LUGHA

a) Awe na utayari wa kujifunza lugha ya Kiswahili bila kulazimishwa

b) Afanye mazoezi ya kuitumia lugha hiyo

c) Atumie akili kupambanua dhana mbalimbali ili kugundua mambo ambayo jamii

Fulani inayafanya

d) Awe na uhuru wa kuzungumza lugha hiyo

e) Awe na ratiba ya kujifuza

f) Aweze kulinganua na kulinganisha lugha anayojifunza

g) Awe na ukarimu ili aweze kuwa na uhusiano na jamii husika

h) Awe mtendaji

i) Azingatie ubora ili aweze kujifunza zaidi

MOTISHA

Ni tabia au msukumo katika kutimiza malengo fulani. TUKI (2004) wanadai kuwa motisha ni

kitu kama fedha inayotolewa ili kumtia mtu hamasa kujifunza jambo.

Hata hivyo, si lazima umpe kitu bali unamtia moyo mwanafunzi na kumsaidia. Mwalimu

anapaswa kutumia motisha chanya sio hasi. Mfn hutakiwi kuchapa fimbo

Brown (1994) anasema kuwa motisha;

a) Ni kiwango cha uchaguzi ambacho unafanya kuhusu lengo unalotaka kufikia

b) Jitihada atumiazo mtu kufikia malengo hayo

SKINNER &WATTSON-hawa wanaangalia zawadi na uhimizaji kwa wanafunzi

pamoja na adhabu ili kufifisha na kujenga hali fulani

AINA ZA MOTISHA

1. Mwamko wa mjifunzaji mwanyewe

2. Mazingira mazuri ya kufundishia Kiswahili mfano, darasa, nje n.k

3. Jamii inayomzunguka ni motisha pia

4. Mwalimu anaweza kuwa motisha kwa mwanafunzi

5. Zana/vifaa vya kujifunzia pia ni motisha

MOTISHA IPO KATIKA MAKUNDI MIWILI

1. Motisha wa ndani-

Haitegemei vitu vya nje ya yenyewe

Hiki ni kile kinachoonekana kwa mjifunzaji lugha mwenyewe

Hii haibadiliki kulingana na muktadha wowote ule

2. Motisha wa nje

Ni aina ya motisha ambayo mwanafunzi hutegema kupewa, kupata, kusikia au kuona

Page 6: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

6

Hivi vitamsaidia katika kujifunza lugha

Mwalimu wasaidie wanafunzi kutumia lugha kulingana na muktadha. Hapa kuna

mambo ya kuzingatia:-

a) Akili ya mwanafunzi: lazima utambue tofauti zao katika akili zao ili kujifunza lugha

b) Kipaji chao-kuna wengine wana vipaji vya kujifunza lugha

c) Umri-watu wazima huchelewa kujifunza lugha

d) Jinsia-inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha haraka kuliko wanaume

UFUNDISHAJI LUGHA KIMAWASILIANO

Ni muhimu kuhakikisha kwamba katika kujifunza lugha ufundishaji uwe wa mawasiliano

Ni mbinu ya kufundisha lugha ngeni na lugha ya pili

Husisitiza mwingiliano maathiriano kama mbinu ya kujifunza lugha

KAZI ZA LUGHA

Van (1975) anasema kuwa kazi ya lugha ni:

a) Kutoa habari

Kusimulia

Kuuliza

Kutoa taarifa

b) Kutafuta taarifa za kitaaluma

c) Kuelezea mihemuko na misisimko. Mfno mapenzi, misisimko

d) Kuelezea masuala ya uadilifu.mfn kuomba msamaha, ibada etc

e) Kwenye mambo ya ushirikiano. Mfn kuamkia watu, kujitambulisha nk

Angalizo: hata kama mwanafunzi ana malengo mengine ya kujifunza lugha hiyo ni

lazima umfundishe umuhimu wa lugha hiyo kulingana na muktadha

MASHARTI YA KUZINGATIA

a) Azingatie majukumu ya kijamii mfn ataanzaje kuzungumza na mtu

asiyemjua? Watu wengine ni wenye mamlaka Fulani, hivyo kuna namna ya

kuzungumza nao

b) Majukumu ya kisaikolojia-mfano asipendelee upande wowote mfn

CHADEMA CUF na CCM

c) Mazingira ya lugha ilipo. Je ni lugha ya taifa? Watu wanaokuzunguka

wanatumiaje?

Angalizo: lugha sio sarufi tu au fonolojia bali ni chombo cha mawasiliano, hivyo

inahitaji kufundishwa kimawasiliano zaidi

MUKTADHA WA UFUNDISHAJI LUGHA

Haya ni mazingira halisi ambapo tukio la ufundishaji lugha hufanyika kwa kuzingatia

wadau wakuu watatu

a) Mwanafunzi

b) Mwalimu

Page 7: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

7

c) Jamii

Pamoja na motisha ufundishaji uzingatie sana mambo yafuatayo:

Utoaji wa kazi na mazoezi mengi

Tumia lugha katika mazingira halisi na yanayostahili ukilenga kwenye stadi nne

za lugha

Matumizi ya lugha kwa kuzingatia muktadha

Utumizi wa mazingira halisi ya darasa.mfn picha, katuni. Nk

Himiza ushirikiano miongoni mwa wanafunzi baina yao na baina yako mwalimu

Tumia mbinu zaidi ya moja. Mfn vikundi, majibizano nk (rejea mbinu)

Fafanua kwa uangalifu masuala ya kisarufi

Ajue maono ya mwanafunzi. Mfn huzuni, ucheshi nk

Kuunda mazingira ya utani darasani

UFUNDISHAJI WA DARASA MSETO

TUKI (2013) Mseto ni hali ya kuwa na mchanganyiko wa makabila mbalimbali

kutengeneza kitu fulani

Hapa ni mchanganyiko wa darasa lenye wanafunzi wanaotoka sehemu mbalimbali na

wenye umri tofauti, malengo tofauti nk

Hivyo mwalimu inakubidi utofautishe sana katika ufundishaji wako na uwe makini ili

usije ukawakwaza wanafunzi wengine

NAMNA YA UFUNDISHAJI DARASA MSETO

a) Lazima mwalimu uwe na maarifa ya wanajamii mfn utamaduni wao. Kama ni wazungu,

wachina nk jua utamaduni wao

b) Uwe na usisitizaji wa lugha lengwa. Kama ni Kiswahili basi pendelea kutumia Kiswahili

ili usiwakwaze sana. Hata hivyo lazima wawe na lugha ambayo wewe unaijua

c) Tumia vitendo halisi, ishara nk

d) Arika wageni mbalimbali waje waeleze kuhusu lugha na mazingira

e) Puuza(ignore) malengo ya wanafunzi

f) Ufundishaji wa masuala ya utamaduni lazima ufungamane na muktadha husika

SIFA ZA MPATAJI LUGHA

Mpataji lugha ni lazima awe na sifa kuu mbili tu:

1. Umilisi wa kiisimu

Ni uwezo alio nao mjifunzaji lugha ambao unamwezesha kutofautisha viambo,

miundo tofauti ya lugha na msamiati wa lugha

pia kuweza kutamka lugha ile.

2. Umilisi wa kiisimujamii

Ni umilisi ambao mtumiaji wa lugha hupata lugha inayomwezesha kujifunza lugha na

kuzingatia muktadha

NADHARIA /MBINU /MIKABALA ZA KUJIFUNZA LUGHA YA KIGENI

Nadharia ni mkondo wa mawazo unaotumika kuelezea jambo

Page 8: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

8

Mtesigwa(2009) anasema “ nadharia ni kiunzi cha mitazamo, mawazo au vitendo

vinavyohusisha uchunguzi, mpangilio na uchanganuzi wa matukio katika kukabili suala

fulani kisayansi

®kuna mambo mawili ambayo lazima tujikumbushe:

a) Njia za ufundishaji lugha ya kigeni ni nyingi kama waalimu walivyo

wengi

b) Kumbuka hali ya darasa. Tumia njia mbinu zaidi ya moja darasani,

usitumie njia moja tu.

Rogers&Richards (2001)wanasema kuwa tunapojiandaa kwenda kufundisha tunahitaji

kujiuliza maswali yafuatayo:-

a) Malengo ya ufundishaji lugha lengwa(LL) ni yapi? Mfano labda lengo lao

linaweza kuwa wanataka kuzungumza tu.

b) Upi ni msingi asili wa lugha lengwa na unaathiri vipi njia za kufundisha. Mfn

kaida za lugha ya Kiswahili ni zipi?

c) Ni misingi ipi inatumika kuchagua mambo katika ufundishaji lugha?

d) Ni misingi ipi ya upangiliaji wa mada. Mfano kwa kuzingatia suala la utamaduni,

mfano salamu nk

e) Je lugha mama ya mwanafunzi ina jukumu gani katika kujifunza lugha? Mfano

miundo ya lugha mama inafanana na lugha lengwa?

f) Je wanafunzi binafsi watumie mbinu zipi katika kujifunza lugha hiyo?

g) Je ni mbinu na vitendo vipi hufanikisha vizuri ujifunzaji lugha ya pili (kigeni)?

1. Mbinu ya tafsiri sauti

2. Mbinu ya moja kwa moja(direct method

3. Mbinu ya usomaji(reading approach method)

4. Kusikia na kusimulia (audiolingual method)

5. Kushirikisha jamii (community language learning method)

6. Mbinu ya ukimya (silence method)

7. Mbinu ya mawasiliano (communicative language approach)

8. Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)

9. Mbinu ya utambuzi (communitive code method)

10. Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)

wakati mwingine hujulikana kama mbinu ya kimapokeo. Huu ni mkabala ambao

ufundishaji wa lugha ya kigeni umejiegemeza katika sarufi ya lugha ya Kiratini.

Iliasisiwa/anzishwa na Meidinger (1783) na Ploetz (1849) wakati ule iliaminika kwamba

lugha ya kiratini ndiyo lugha pekee.

Nafasi ya lugha mama ilipuuzwa kwa kiasi kikubwa na ilijikita katika sarufi ya Kiratini,

na hivyo mwalimu alipaswa kujikita katika kufundisha sarufi ya Kiratini na vipengele

vingine vilipuuzwa

Huu ulikuwa ni mkabala elekezi-yaani unawaelekeza watu namna ya kutumia lugha na

sivyo wanajamii wanavyotumia lugha hiyo

Page 9: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

9

Iliasisiwa na Gouin(1880)

Nadharia hii inazingatia uzungumzaji wa lugha husika

Mbinu zilizopaswa kufundishia ni zile zilizohamasisha wanafunzi kuzungumza. Mfn

mbinu ya majadiliano,uigizaji,maswali katika vikundi

Masomo yalianza kwa hadithi fupi halafu wanafunzi wanauliza maswali kuhusu hadithi

waliyosimuliwa na mwalimu aliwaambia watoe maoni yao kuhusu hadithi hiyo.

Matumizi ya vielelezo vilitumika zaidi. Mfano picha, ramani, katuni n.k

Kipengele vya sarufi kilifungushwa kwa kufuata muktadha halisi ambamo lugha

inatumika

Kipengele cha utamaduni kilifundishwa kwa uchache sana

Mbinu hii inatumika kufundishia kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya

kigeni ambao hawatarajiwi kutoka nje ya nchi ambapo lugha hiyo

inatumika

Malengo yake huwa kuendeleza uwezo wao wa kusoma ile lugha

Vipengele vinavyofundishwa ni vile vinavyohusu usomaji, hivyo

vipengele vingine havihusiki. Mkazo wake ni kwamba anayejifunza lugha

aweze kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja.

Mbinu hii haimpi mjifunzaji lugha uwezo wa kuzungumza lugha husika

bali ni kuisoma tu.

4.

Nadharia hii ilitokana na haja ya ukarimani nchini marekani miaka 1940.

Iliasisiwa na Bloomfield (1942) na Fries (1945)

Msingi mkubwa wa nadharia hii ni kile kinachosemwa

Maandishi hayakupewa fursa kubwa bali kile kilichosemwa ndicho

kilikuwa cha muhimu sana. Bloomfield alisema kuwa lugha si katika

maandishi bali ni kile ambacho kinasemwa.

Inahusisha kusimulia mada mbalimbali na kupima uwezo wa kusikia

Walipenda sana kutumia miziki, nyimbo, usimulizi na ughanaji

Walisisitiza stadi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika

Waliongeza kitu kingine cha kuona

Iliasisiwa na curran (1976)

Dai la nadharia hii ni lugha ni watu, kwa maana ya kwamba huwezi

kutenga jamii na lugha

Walidai kwamba ili uweze kumfundisha mwanafunzi mgeni basi nenda

kwenye jamii husika

Walidai pia kwamba kama utaamua kufundishia darasani bali darasa lako

lifanye angalau lifanane fanane na jamii ya lugha husika

Ili uweze kufundisha watu ni lazima ushirikishe watu wanaotumia lugha

hiyo.

Page 10: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

10

Mwanafunzi atapata vichocheo vya aina nyingi katika jamii na kubaini ni

mambo gani yanafaa na mambo gani hayafai

Nadharia hii inaipa kipaumbele jamii kama chombo muhimu katika

kujifunza lugha

Nadharia hii inaamini kwamba kila lugha ina mfumo wake tofauti na

lugha nyingine, hivyo ufundishaji wa lugha ya pili ulenge kumfanya

mjifunzaji wa lugha kuwa mmilisi au kukaribia kuwa mmilisi wa lugha

anayojifunza

Nadharia hii inadai kwamba ujifunzaji wa aina yoyote ile unahusisha vitu

viwili.

Kichocheo Mwitikio mgeuko

(Mwalimu) (mwanafunzi)-(anabadilika)

Ili kuweza kutimiza hili, mwalimu anahitaji kujenga mazingira ya utani

katika darasa jambo ambalo litaleta matokeo mazuri ya umilisi wa lugha

husika

Nadharia hii inamhitaji mwalimu kufanya tathimini kwa wanafunzi

wake ili kubaini kama kuna badiliko

Nadharia hii inatokana na ukosoaji/udhaifu wa nadharia ya mbinu ya

sarufi na ile ya moja kwa moja

Ilianzishwa mwaka 1970

Wanadai kwamba mwanafunzi apewe vipengele vyote vya lugha kwa

ujumla mwanafunzi kumpa maarifa mapana kuhusu lugha, kumpakanuni

za msingi kuhusu lugha, halafu yeye mwenyewe kulingana na utambuzi

wake aweze kuielewa lugha.

Uwafundishe kanunu za msingi. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili ni

lazima ujue ngeli za majina-hii itakusaidia kutumia nomino katika

mazingira tofauti tofauti, vitenzi-waeleze namna ambavyo vinaweza kukaa

peke yake kama sentensi

Nadharia hii pia hujulikana kama mkabala asilia.

Iliasisiwa na James Asher 1969

Inatilia mkazo mfumo na muundo wa lugha.

Kama ilivyo nadharia ya usikizi nadharia hii pia inasisitiza umuhimu wa kumudu

mazungumzo kama sehemu ya umilisi wa lugha

Ufundishaji uhusishe mazoezi ya kurudia rudia ambayo angalau unamfanya mwanafunzi

kumudu anachojifunza

Nadharia hii inasisitiza matumizi ya vitendo na ishara mbalimbali kama nyenzo mojawapo

katika kujifunza lugha.

Ilianzishwa na Lonzano georgi (1979)

Page 11: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

11

Nadharia hii inayapa mazingira bora ya ujifunzaji lugha kama nyenzo muhimu mojawapo

katika kujifunza lugha. Hii inamaanisha kwamba mazingira yanayotumika kujifunzia

lugha ni lazima yamkumbushe mwanafunzi kile alichojifunza jana yake

Wanaelezea namna ya mkao wakati wa kufundisha wanafunzi wageni. Mkao katika darasa

uwe ni wa kutazamana, maana yake vikae kwa duara.

Wanasisitiza matumizi ya mziki laini na mziki nyororo

Inasisitiza maingiliano na maathiriano katika ya mwalimu, mwanafunzi na jamii

Wanakaza kwamba kujifunza lugha ni kujifunza kuwasiliana.

Kujua lugha kwa hakika sio kujua kanuni za lugha ile bali ni kujua namna ya kuwasiliana

na watu wa jamii ile kwa kuzingatia mikitadha mbalimbali ambamo lugha hiyo inatumika

Ni nadharia ambayo imeshaididiwa na wataalam wengi akiwamo Noamy Chomsky

Hii ndiyo nadharia ambayo inafaa kutumia kwa ajili ya kujifunza lugha

Hapa inamaanisha uwezo alio nao mtu wa kutumia lugha Fulani.

Viwango hivi viliwekwa na shirika/taasisi moja isiyokuwa ya kibiashara wala kiserikali

liitwalo Interagence Language Round Table (ILRT)

Kulingana na shirika hili wajifunzaji lugha wako katika viwango vitatu

a) Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level

b) Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level

c) Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level

a) Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level

Daraja limegawanyika katika viwango hivi

Kiwango cha 0-mwanafunzi hawezi kabisa kuzungumza lugha

Kiwango cha +0-mwanafunzi amekaririshwa tu mahitaji muhimu

akibadilishiwa tu basi Amepotea

Kiwango cha 1-mwanafunzi anaweza kusitahimili mazungumzo ya ana kwa ana ila hawezi

kuanzisha mazungumzo

Kiwango cha +1-huyu anaweza kuanzisha mazungumzo yeye mwenyewe, hata hivyo ni

kwa ajili ya kukidhi matarajio yake

b) Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level

Daraja la 2-lugha si kamilifu lakini anaeleweka kwa urahisi

Kiwango cha 3-anaweza kuzungumza lugha kwa muundo sahihi, ana msamiati wa mazingira

fulani fulani tu ili kukidhi mahitaji ya kitaaluma

Anaweza kukithi mahitaji ya kitaaluma

2+Lugha yake si kamilifu lakini anaweza kueleweka kwa urahisi

3mwanafunzi ana uwezo wa kuzungumza lugha kwa usahihi, ana msamiati toshelevu kwa

mazingira fulani fulani tu.

3+mwanafunzi ana uwezo wa kuzungumza lugha kwa muundo sahihi na ana uwezo wa

kukidhi mahitaji ya kitaaluma

4mwanafunzi ana uwezo wa kutumia lugha kwa usahihi na ufasaha katika viwango vyote

vya lugha. Yaani fonolojia-matamshi, sintakisia-miundo, mofolojia-maumbo

Page 12: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

12

Huweza kutoa maana ya viambo mbalimbali kulingana na muktadha

4+uwezo wa mzungumzaji wa kiwango cha juu kabisa katika mawanda yote lugha: yaani

fasihi na isimu

Ana uwezo wa kutumia kwa kuzingatia utamaduni wa lugha husika

Anaelekea kulingana na wazawa wa lugha husika

5usitadi wa lugha alio nao ni wa kiwango cha mmilisi wa lugha aliyeboboea

Ana sifa za kudhihilisha wakati wa lugha anayojifunza.

Suala la uteuzi wa vitabu vya kufundishia lina ugumu unaotokana na mambo yafuatayo:

Yaani malengo tofauti ya:

Malengo tofauti ya wanafunzi

Malengo tofauti ya taasisi

Malengo tofauti ya waajiri

Malengo tofauti ya waalimu

Malengo tofauti ya wazazi/walezi

Tutafafanua utofauti huo kwa namna ifuatayo:

Malengo tofauti ya mwanafunzi:-mfano viwango tofauti vya wanafunzi

kitabia, kiuchumi, kiuelewa, kiutamaduni,kiumilisi

viwango tofauti za wanafunzi mfano kiwango cha kati,juu nk

tofauti za kimaamzi. Mfano taasisi moja tu ihusike katika uandaaji wa vitabu vya

kufundishia mfano wizara ya elimu

uzingatizi tofauti wa vitabu. Mfano,bei, mwonekano, upatikanaji wake

Malengo ya kozi inabidi yaangaliwe

Wanafunzi walengwa ni akina nani?

Mkabala utakaotumia kufundishia

Stadi za lugha. Je kitabu kimekidhi stadi zote za lugha?

Ubora wa mazoezi yaliyotolewa ndani ya kitabu

Mfuatano wa masomo/mada. Ngumu? rahisi? Nk

Msamiati

Hali ya jumla ya kiisimu jamii. Je kitabu kimetumia lahaja, lugha rasmi, vigezo vya

kiutamaduni

Muundo mzima wa kitabu. Chapa yake ni ndogo au kubwa?

a) Kila somo/kitabu kiwe na lengo mahususi la kumsaidia mwanafunzi kuwasiliana

b) Kila kitabu kiwe na matini ya lugha kama izungumzwayo na wazawa

c) Kila kitabu kiwe na kielelezo cha mazingira halisi. Mfano salamu

d) Msamiati na sarufi ukidhi matakwa ya wanafunzi

Page 13: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

13

e) Utumizi wa vilelezo halisi kama vile picha,magazeti, tangazo, kadi nk

f) Kila kitabu lazima kiorodheshe sauti zilizo katika lugha husika ili aweze

kuzielewa.

UCHAMBUZI WA DOSARI

Maana yake:

Uchambuzi wa dosari ni njia ya kuainisha, kupambanua na kufafanua dosari mbalimbali

za wajifunzaji wa lugha ya kigeni/lugha ya pili

Suala la uchambuzi wa dosari liliasisiwa na Corder (1967) ambapo yeye anaeleza maana

ya dosari kuwa ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za lugha lengwa

Mambo yanayoshughulikiwa na wanausasanyuzi; wanashughulikia mambo makuu

manne

a) Jinsi mjifunzaji anavyoilewa lugha ya kigeni anayojifunza

b) Jinsi mjifunzaji anavyojifunza lugha ya kigeni/mbinu anazotumia

c) Matatizo anayokabiliana nayo wakati anajifunza lugha ya kigeni

d) Kung‟amua mchakato/kutambua michakato inayotumiwa katika kujifunza lugha

ya kigeni

UMUHIMU WA DOSARI/DHIMA YA DOSARI KWA WAJIFUNZAJI

LUGHA YA PILI

Dosari zinazofanywa na wanafunzi wanaojifunza lugha ya kigeni hutumiwa kama kioo

kinachoakisi hali halisi iliyofikiwa na wajipatiaji wa lugha ya pili.

Dosari hizi humpatia mwalimu nafasi ya kutathimini jitihada zilizofikiwa na wanafunzi

wake kwa minajili ya kuboresha au kuendeleza mbinu za ujifunzaji lugha na humsaidia

mwalimu kubadilisha vifaa anavyotumia katika ufundishaji.

Kwa ujumla umuhimu wa dosari unaangaliwa katika namna kuu nne

a) Kwa upande wa mwalimu

Huonyesha jitihada zilizofikiwa na wanafunzi na kusaidia kuboresha

b) Kwa watafiti

Huonyesha jinsi lugha inavyopatikana/inavyoamiliwa

c) Kwa mwanafunzi

Humsaidia mwanafunzi kujua ruwaza/partern ya maendeleo ya

mwanafunzi alipofikia

d) Kwa waandaa mitalaa

Huwasaidia kuboresha uandaaji wa vitabu na machapisho mbalimbali kwa

kujifunza

AINA ZA DOSARI

Aina hizi za dosari zimeainishwa kutokana na mbinu wanazotumia wanafunzi kujifunza lugha.

1. Dosari majumui/majumuisho

Hizi ni dosari ambazo mwanafunzi hutumia kanuni ya jumla ya lugha ya kwanza na

kuitumia katika lugha ya pili. Hii inasabisha kukiuka matumizi ya lugha lengwa.

Mfano katika lugha ya kiingereza vitenzi vingi huongeza “ed” mwanafunzi wa

Page 14: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

14

mswahili wa kiingereza anaweza kupata shida kwani anaweza kuwa anaongeza ed

katika kila kitenzi jambo ambalo sio sahihi.

2. Uepukaji/avoidance

Ni ule utaratibu wa mjifunzaji lugha ya kigeni kujaribu kuepuka matumizi ya

kanuni/maumbo/miundo fulani ya lugha. Kwa mfano mwanafunzi anajaribu

kuepuka matumizi ya neno fulani anatajaribu kuliepuka hilo neno na kutumia neno

lingine jambo ambalo litasababisha makosa.

Hata hivyo si rahisi kujua kama mtu fulani amekwepa matumizi ya neno fulani

3. Urahisishaji

Mwanafunzi anapoamua kurahisisha muundo wa lugha fulani hujikuta katika

dosari

4. Uhawilishaji

Uhamishaji wa miundo na kaida za lugha ya kwanza kwenda lugha ya pili.

Miundo hii inapohamishwa basi hukiuka miundo ya lugha ya pili.

Kwa mfano baadhi ya jamii ya watanzania hukiuka sana kanuni za Kiswahili.

Mfano Wanyakyusa wa hawawezi kusema “chama” bali “kyama” pia Wakinga

hawawezi kusema “viatu” bali wanasema “fyatu”

5. Utumizi ziada/over use

Ni kuongeza matumizi yasiyohitajika katika utumizi wa lugha

MISINGI YA UAINISHAJI WA DOSARI

Hapa ni kwa kuzingatia Nyanja kuu za lugha:

a) Dosari za kifonolojia/ukiushi wa matamshi-lugha zingine zina toni zingine hazina.

b) Dosari ya kimaumbo/kimsamiati-yaani upangaliaji wa vipashio vinavyounda maneno.

Mfano uwingi wa nomino za kiingereza hupachikwa mwisho tofauti kabisa na lugha

ya Kiswahili ambapo haitabiliki. Mfano pia katika lugha ya Kiswahili neno moja

linaweza kuwa na sifa ya kuwa sentensi, mfano “ninasoma” jambo ambalo kwa

kiingereza haiwezekani kuwa neno moja “ I read”

c) Dosari za kimuundo-taratibu tofauti tofauti zinazotumika kuunda vipashio. Kila lugha

ina utaratibu wake. Mfano. My brother-yangu kaka-mfumo huo hauwezekani kuwa

sawa

d) dosari za kimaana/kisemantiki- maana huwa ni tofauti tofauti

e) Dosari za kipragmatiki-hii ni miktadha mbalimbali mfano sokoni, kanisani

dosari kulingana na athari za kimawasiliano

Ni uainishaji wa dosari kulingana na uelewekaji/kutokueleweka kwa ujumbe

uliotolewa na mjifunzaji lugha. Kwa kuzingatia kigezo hiki tunapata aina mbili za

dosari.

1. Dosari za kimalimwengu/global errors-ni dosari ambazo zinafanya usemi

uliotolewa na mjifunzaji lugha kutoeleweka kabisa

2. Dosari za kienyeji/local errors-ni semi zinazotolewa na mjifunzaji wa lugha ya

pili ambazo haziko sahihi lakini zinaeleweka na msikilizaji. Mfano “I angry”

mfano mwingine ni “ninataka kura”-akiwa jikoni au akiwa katika jukwaa

anasema “ninataka kula”- hizi zinaeleweka na wasikilizaji japo haziko sahihi.

USHUGHULIKIAJI WA DOSARI ZA WANAFUNZI

Page 15: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

15

Kila mwanafunzi wa lugha ya pili huwa ana dosari katika kujifunza lugha ya pili. Ni

jambo la msingi kushughulikia dosari za wanafunzi, lakini angalia ni wakati gani

ushughulikie dosari hizo, hii ni kulingana na muktadha wa darasa: aina ya wanafunzi;

haiba yao, mihemko, aina ya dosari, umri n.k. Hata hivyo ikiwezekana dosari hizo ziweze

kushughulikiwa ili kusaidia zisijirudie rudie.

Wataalamu wengine wanaona kwamba dosari zisishughulikiwe. Mfano Krashen na

Terrell(1983) husema kuwa mwanafunzi aachwe mwenyewe atazidi kugundua dosari

hizo na atashughulikia mwenyewe.

Kathleen Bailey (1985)anapendekeza uamuzi wa aina saba

a) Puuza dosari hizo

b) Dosari zishughulikiwe papo kwa papo

c) Kuhusisha wengine katika kurekebisha dosari hizo. Mfano miongoni mwa wanafunzi hao

hao unaweza kuhusisha na wakakosoana wenyewe

d) Kuhusisha wanafunzi mahususi-yaani kumtumia mwanafunzi wa karibu na mwenzake

kumsahihisha mwingine.

e) Kumrudia mfanyaji dosari/ mfano unaweza kumwambia “unaweza kufikiri zaidi juu ya

hilo?”

f) Kuwaruhusu wanafunzi wengine kutoa tathmini.

g) Kumpa nafasi ya kujaribu tena na tena mfanyaji wa dosari baada ya vitendo fulani

kufanyika ndani ya darasa.

Mwisho wa yote lazima vitu vifuatavyo viwe vimejitokeza:-

1. Usahihi na uhalali wa dosari uwe umedhihilika

2. Sehemu na mahali dosari imefanyika iwe imebainishwa wazi wazi. Mfano kama ni

kwenye neno, tungo nk

3. Nafasi ya kurudia na kujirekebisha kwa mfanyaji dosari iwe imetolewa

4. Mifano mbalimbali ya dosari na usahihi wa semi uwe umetolewa na kuonyeshwa kwa

uwazi

5. Aina ya dosari iwe imeonyeshwa. Mfano kama ni dosari ya kimpangilio, kimatamshi nk

6. Marekebisho yawe yamefanywa kwa mifano anuai

7. Mhusika awe amesifiwa/kama ameepuka hizo dosari

MAMBO YANAYOATHIRI UJIFUNZAJI/UPATAJI LUGHA YA PILI/KIGENI

Mambo hayo ni yale ama yanayomwezesha au yanamkwamisha mpataji lugha kupata lugha.

Tutaangalia kwa mujibu wa Martland (1997)

1. Umri

Mtu mwenye umri mdogo ana ahueni zaidi katika kujifunza lugha kuliko mtu ambaye

umri umeenda. Mtoto ambaye hajabalehe mfano miaka kabla ya tisa (9). Hii inatokana

na kwamba mtu mzima tayari anakuwa na lugha nyingine ambayo inasigana na lugha

anayojifunza

2. Hali ya kiuchumi ya mjifunzaji lugha:

Mtu wa tabaka la chini hawezi kutumia vitu vya kisasa ili kupata lugha, maana vifaa

hivyo ni vya gharama kubwa.

Page 16: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

16

3. Hali ya darasa:

Darasa ambalo limejengewa mazingira ya utani, wanafunzi wanamudu haraka sana

kupata lugha.

Hii inajumuisha michezo mbalimbali katika darasa hilo

4. Msaada wa kifamilia/community support:

Ikiwa mwanafunzi lugha anayojifunza inatumika ndani ya jamii hiyo, atapata haraka

sana lugha kuliko mwanafunzi ambaye anajifunza lugha ambayo wazungumzaji wake

hawako hapo.

Mfano: Mtanzania anayetaka kujifunza kiingereza anapata shida kwa sababu

wazungumzaji wake wako nje ya nchi

5. Motisha:

Motisha ni kipengele muhimu sana katika ujifunzaji lugha

Mwanafunzi aliye na motisha ya ndani atapata lugha haraka kuliko anayepata motisha

ya nje. Ref. motisha

6. Kiwango cha elimu:

Mtu mwenye kiwango kikubwa cha elimu ana uwezo mkubwa sana wa kupata lugha

kuliko mtu ambaye hana elimu kabisa.

7. Matarajio:

Kama mjifunzaji lugha ana lengo la kufanya utafiti sehemu fulani, matarajio yake ni

kujifunza lugha na kuimudu ili akafanye kazi yake.

Kama mwanafunzi hana matarajio yoyote basi itakuwa ngumu kupata lugha.

8. Haiba

Wanafunzi wacheshi hupata lugha haraka kuliko wanafunzi ambao sio wacheshi.

Wachesi hupenda kujichanganya sana.

9. Mtazamo wa utamaduni wa ujifunzaji lugha ya kigeni/pili.

Mwanafunzi kama ana mtazamo hasi na lugha anayojifunza basi itakuwa ngumu sana

kupata lugha.

Mtazamo chanya ndio utakaomsaidia mjifunzaji lugha kupata lugha.

10. Uwezo wa kumudu lugha ya kwanza:

Uwezo wa lugha ya kwanza una kawaida ya kuathiri umuduji wa lugha ya pili, hasa

inapotokea kwamba lugha ya kwanza ni tofauti kabisa na mfumo wa lugha ya pili.

(Nozalle (2012) 11. Viigwa (role models in the community)

Hii ni kwamba kuna mtu gani katika jamii ambaye ni mtu maarufu unataka uzungumze

kama yeye? Hii itakusaidia kwa sababu mjifunzaji lugha atajaribu kujitahidi

azungumze kama mtu huyo.

12. Muktadha/mazingira

Mazingira ni muhimu katika upataji lugha

TOFAUTI ZA UPATAJI WA LUGHA YA KWANZA NA LUGHA YA PILI/KIGENI

Kuna tofauti kubwa kati ya upataji wa lugha ya kwanza na lugha ya pili. Kila mtu ana lugha ya

kwanza. Wataalam wanaokuwepo hapa kushadidia hili ni Ellis (1994) na Bley Vroman (1988)

Hawa wanabainisha hoja tisa, kama ifuatavyo:

Page 17: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

17

1. Mafanikio kwa ujumla: mtoto anapopata lugha ya kwanza huipata lugha ile kwa usahihi

katika Nyanja zote, japo anaweza asiweze kutofautisha uchambuzi kiisimu lakini

wapataji lugha ya pili hupata mafaniko katika maeneo fulani fulani tu katika lugha

wajifunzayo.

2. Kushindwa(failure): katika upataji wa lugha ya kwanza kushindwa hakupo labda kama

ana ulemavu fulani lakini kwa wapataji lugha ya pili kushindwa ni jambo la kawaida

3. Utofauti baina ya wajifunzaji/wapataji lugha (variation): wajipatiaji wa lugha ya kwanza

hawana tofauti yoyote katika upataji lugha, yaani wakifikia umri fulani labda kama miaka

3 hivi wote watakuwa wamepata, kama atakuwa hajapata lugha mpaka miaka 9 basi huyo

atakuwa na matatizo (msukuku-kukoma kujifunza lugha (fossilization )lakini lakini

wajifunzaji wa lugha ya pili kuna tofauti kubwa sana, utakuta mwishoni mwa kozi mmoja

amemudu na mwingine bado

4. Malengo/goals: lengo la mjipatiaji lugha ya kwanza ni umili wa lugha hiyo katika

viwango vyote lakini lengo la mjipatiaji lugha ya pili ni kupata maudhui na umilisi

kidogo

5. Usukuku(ukakamaaji): suala la usukuku halipo kwa mtoto anayejipatia lugha ya kwanza

lakini kwa mjipatiaji lugha ya pili hii ni hali ya kawaida kabisa(soma Han1998-2013).

6. Uvumbuzi/ughamuzi: wajipatiaji wa lugha ya kwanza huendelea kujipatia lugha ya

kwanza katika ughamzi bwete (kujisahihisaha dosari pasipo kujua) lakini mpataji lugha

ya pili huwa katika ughamzi tambuzi.

7. Maelekezo/instruction: ujipatiaji wa lugha ya kwanza hauhitaji maelekezo, labda kidogo

kwa ajili ya kuchochea lakini mjipatiaji wa lugha ya pili anahitaji maelekezo ya kina na

sahihi na kwa utaratibu maalumu.

8. Uthibitisho hasi:katika ujipatiaji wa lugha ya kwanza usahihishaji wa dosari haumsaidii

mpataji wa lugha ya kwanza kupata lugha ile lakini katika upataji wa lugha ya pili ni

muhimu kufanya masahihisho ili kumpa mwelekeo sahihi.

9. Athari hisivu (affective factor): mjipatiaji wa lugha ya kwanza hakuna kitu

kinachomwathiri kujipatia lugha ya kwanza, mfano hafikilii kwamba atakosea,

atachekwa bali yeye hutamka tu lakini katika ujipatiaji wa lugha ya pili athari hisivu zina

msaada sana katika kupata lugha. Mfano mwanafunzi mcheshi, hucheka atapata lugha

haraka kuliko mkimya.

10. Muda: mtoto huchukua muda mfupi kati ya miezi 36 anakuwa mmilisi wa lugha lakini

mjipatiaji wa lugha ya pili hutumia muda mrefu sana. Inachukua miaka kama tisa

UTAYARISHAJI WA MBINU ZA UFUNDISHAJI

A. UTAYARISHAJI WA SOMO:

Hapa tunaangalia muundo wa andalio la somo (lesson plan) unahitaji kuangalia mambo haya:

1. Muda

2. Mada

3. Malengo-ie kitu gani kitokee katika somo hilo. Mfano mwisho

wa somo mwanafunzi aweze kutaja aina ya „nomino‟

4. Mazingira/muktadha-darasa, aina ya wanafunzi.

Shajala

Logbook

Mhitasali

Page 18: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

18

MUUNDO WA ANDALIO LA SOMO

Andalio la somo linatakiwa kuwa na mambo yafuatayo

1. Malengo ya jumla (main objective)-haya ni mabadiliko ya muda mrefu yanayotakiwa

kutokea kwa muda mrefu. mfanoMwanafunzi aweze kutathimini….mwanafunzi aweze

kufahamu…

Mara nyingi malengo haya hayabadiliki

2. Malengo mahusus/malengo wezeshi

Haya ni malengo ya muda mfupi

Haya ni malengo ambalo ni la kudumu lakini lengo lake ni kusaidia lengo la

jumla

Tofauti kati ya malengo mahusus na malengo ya jumla ni kwamba malengo ya

jumla hayapimiki ilhali malengo mahusus yanaweza kupimika

Malengo mahususi ni mabadiliko ya muda mfupi ilhali malengo ya jumla ni

mabadiliko ya muda mrefu

Mwanafunzi aweze kutaja viungo vya binadamu vilivyo katika

kichwa…mwanafunzi aweze kulinganisha na kulinganua

Mwanafunzi aweze kuonyesha viungo vya mwili..

Kubainisha viungo vya mwili

3. Mada kuu.

Kila unapoenda kufundisha lazima kunakuwa na maada. Mfano wa mada ni Usafiri

wa Anga

4. Mada ndogo:

Kama mada yako itakuwa hapo juu, mfano Usafiri wa Anga, mada ndogo inaweza

kuwa,kuwasili kwa ndege, kukata tiketi, kufika uwanja wa ndege, mahali uwanja

wa ndege ulipo, hali ya miundombinu kwenda uwanja wa ndege nk

Kama ikiwa mada kuu ni familia: basi mada ndogo yaweza kuwa aina za familia

5. Zaka za kufundishia

Hakuna somo lisilo na zana za kufundishia. Mfano kama ni usafiri wa anga.

Unaweza kuchora picha ya mwanza, kuwapa ramani nk.

6. Utaratibu wa somo/yaani darasani

Somo lolote linakuwa na:

a) Utangulizi-tanguliza somo lako, kama sio mara ya kwanza wape chemsha bongo,

kama ni kwa mara ya kwanza unaweza kuanza na hadithi. Hii itakusaidia kuvuta

usikivu wa wanafunzi. Pia unaweza kuwaruhusu wanafunzi wakuulize maswali

kuhusu wanaelewa nini kuhusu kile unachoenda kukifundisha

b) Uwasilishaji wa kiini cha somo:- unaweza kuandaa maswali, unaweza kuandaa

makundi ya wanafunzi wachache wachache.

c) Utumizi/utendaji wa wanafunzi. Hapa mwalimu unategeneza mazoezi, kazi binafsi,

mazoezi mengine ambayo watafanya wenyewe, maswali ya papo kwa papo au

mazungumzo

7. Kazi ya nyumbani

Haifai hata kidogo kuwafundisha wanafunzi wageni kumaliza kuwafundisha na

kuwaacha bila kuwapa zoezi lolote la kufanya

Zoezi hilo lihusishe vile ambavyo mwanfunzi amesoma darasani.

Mfano wa zoezi: Mtafute mtu yeyote kule mitaani muulize maswali haya. Wewe ni

nani, unasoma? Umeoa? Je unapenda nini? Nk

Hii itakusaidia sana kujua wapi palipo na udhaifu ili uwee kuwasaidia wanafunzi

kama hajaelewa.

8. Tathmini/

Page 19: KI 214 UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI MBINU ZA ... · v. Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara

19

Ni lazima kujitathimini wenyewe kama wameelewa au la.

UONGOZI WA DARASA/UTHIBITI WA DARASA 1. Upangaji wa darasa/ je darasa limepangiliwaje? Je watu wote wako sana?

2. Mbinu za ufundishaji/mbinu zinazopendekezwa ili uweze kulitawala darasa ni mbinu shirikishi.

Usiwe mwongeaje tu wewe mwenyewe. Pia tumia mbinu za kuona.

3. Uimara wa mwalimu/lazima mwalimu ujiamini katika ufundishaji wako. Usionyeshe kuyumba

hata kidogo, kumbuka mara utakapoyumba hawatakuamini tena hata kama ukifundisha vizuri.

Kama wakikuuliza swali ambalo hulijui jaribu kuwashirikisha, kama na wao hawajui basi

waambie utawapata jibu siku nyingine. Unahitaji kuwa msafi. Uwe mbunifu.

4. Mwonekano wa darasa/ lazima darasa liwe linaonekana. Kusiwepo na sauti nyingine inayoingia

ndani

5. Matumizi ya ubao au power point. Vionekane vizuri

6. Sauti ya mwalimu-je sauti yako inasikika vizuri? Hakikisha sauti yako inasikika kwa wanafunzi

wote. Uwe na uwezo wa kuimudu lugha vizuri.

7. Ukubalifu wa mambo ambayo hukufundisha/hukupanga kuyafundisha..kama wanafunzi wakitaka

kufundishwa kitu Fulani ambacho wewe hukujiandaa kuwafundisha, itategemea hali ya darasa

UTAYARISHAJI WA MITIHANI

Huu ni mchakato wa upimaji wa maarifa/ujuzi ambao wanafunzi wameupata tangu mwanzo wa kozi hadi

mwisho wa kozi. Kipengele hiki ni cha muhimu sana hivyo lazima lifanyike kwa ustadi na ubunifu

mkubwa.

Malengo ya mitihani lazima yalenge kupima mambo manne

1. Ulenge kupima maarifa na ujuzi aliyopata mjifunzaji lugha.

2. Kupima mbinu mbalimbali alizotumia mwalimu kufundishia kama zimeeleweka au la.

3. Mitihani imelenga kupima mitaala

4. Mitihani inapima uwezo wa kuchochea kujifunza maarifa mapya.

AINA ZA UPIMAJI

1. Upimaji rasmi-huu ni upimaji unaofanyika mwisho mwa kozi na hufanyika mara moja tu.

Hupima viwango vyote ambavyo alijifunza mwanafunzi.

2. Upimaji usio rasmi-mwanafunzi anapimwa wakati somo linaendelea,mfano mazoezi, mitihani nk.

Mara nyingine upimaji huu huitwa upimaji umbaji KANUNI ZA UPIMAJI

1. Kuwapa wanafunzi muda wa kujiandaa-wape muundo wa mtihani ulivyo

2. Hakikisha jaribio lako linapima wanafunzi kitu walichojifunza

3. Hakikisha kwamba jaribio lako lina uhalisia/reality

4. Hakikisha kwamba jaribio lako/mtihani wako linachochea utendaji

***ili kutimiza haya, unapaswa

1. Hakikisha unaondoa utata katika mtihani huo/maswali yawe bayana/yawe wazi.

2. Muda wa kufanya mtihani huo uzingatie

3. Kuwepo na umakini katika uandishi/ avoid typing errors.

4. Hakikisha haurudii majaribio

5. Hakikisha wanafunzi wako hawaibii/kuangaliziana katika mtihani/cheating

***mwisho wa somo la Kiswahili kwa Wageni***