kanuni za utumishi wa umma 2014

128
39 YALIYOMO Ukurasa Sheria ya Utumishi wa Umma. Nam 2 ya 2011 Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2014 chini ya Kifungu cha 37(4)................................................ 39 SEHEMU YA SHERIA Tangazo la sheria lililotajwa hapo chini limetangazwa katika Gazeti Rasmi hili. Tangazo la Sheria Nam. 41:- Kanuni za Utumishi wa Umma 2014 TANGAZO NAM. 28 KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA 2014 SHERIA ILIYOTUMIKA NAMBA 2 YA 2011 KANUNI hizi, zimetungwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma, Zanzibar, kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya kifungu 37(4) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Nam. 2 ya 2011. YALIYOMO: SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI 1. Jina fupi na kuanza kutumika. 2. Matumizi ya Kanuni. 3. Ufafanuzi wa maneno

Upload: letuong

Post on 29-Jan-2017

2.598 views

Category:

Documents


212 download

TRANSCRIPT

Page 1: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

39

YALIYOMO Ukurasa

Sheria ya Utumishi wa Umma. Nam 2 ya 2011Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2014chini ya Kifungu cha 37(4)................................................ 39

SEHEMU YA SHERIA

Tangazo la sheria lililotajwa hapo chini limetangazwa katika GazetiRasmi hili .

Tangazo la Sheria

Nam. 41:- Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

TANGAZO NAM. 28

KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA 2014SHERIA ILIYOTUMIKA

NAMBA 2 YA 2011

KANUNI hizi, zimetungwa na Waziri mwenye dhamana yaUtumishi wa Umma, Zanzibar, kwa kutumia uwezo aliopewa chiniya kifungu 37(4) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Nam. 2 ya2011.

YALIYOMO:

SEHEMU YA KWANZAUTANGULIZI

1. Jina fupi na kuanza kutumika. 2. Matumizi ya Kanuni. 3. Ufafanuzi wa maneno

Page 2: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

40

SEHEMU YA PILITARATIBU ZA UAJIRI NA UPANDISHAJI DARAJA

4. Watumishi wa Umma. 5. Uajiri. 6. Ujazaji wa nafasi zilizowazi. 7. Tangazo la Ajira na utaratibu wa usaili. 8. Kamati ya ushauri wa utaalamu kuhusu suala la ajira. 9. Muda wa majaribio na kuthibitishwa kazini.10. Masharti ya Uajiri.11. Ajira ya mkataba baada ya kustaafu.12. Watumishi wa kuazimwa.13. Ulipaji mishahara.14. Mamlaka ya kupandishwa daraja na kubadilishwa kada.15. Kupandishwa daraja kwa watumishi wa umma.16. Sababu zinazopelekea kupandishwa cheo.17. Kukubali au kukataa cheo.18. Muda wa kupandishwa cheo.19. Uteuzi katika utumishi.20. Taratibu za kushikilia wadhifa.21. Kusita kwa ajira.22. Uajiri kwa aliyewahi kuachishwa kazi au kuingia hatiani kwa

kosa la jinai.23. Kustaafu kwa hiari.24. Kustaafu kwa lazima.25. Muda wa kutoa taarifa ya kuacha kazi.

SEHEMU YA TATUMASHARTI YA AJIRA KWA MAKUNDI MAALUM

26. Hifadhi kwa watumishi wajawazito na wanaonyonyesha.27. Kazi za usiku kwa watumishi wa kike.28. Uajiri kwa watu wenye ulemavu.29. Ajira kwa mtu mwenye VVU/UKIMWI.

Page 3: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

41

30. Kipaumbele cha ajira kwa watu wenye mahitaji maalumu.SEHEMU YA NNE

MAADILI YA WATUMISHI WA UMMA

31. Viwango vya kimaadili.32. Miiko ya watumishi wa umma.33. Matumizi ya vileo.34. Kivazi katika sehemu za kazi.35. Vitendo vya ukosefu wa nidhamu.36. Udhalilishaji wa kijinsia.37. Mkataba wa huduma.38. Mgongano wa maslahi katika Utumishi wa Umma.39. Kutoa au kuchukua Zawadi.40. Kupokea au kutoa hongo.41. Uwajibikaji kwa Uongozi.

SEHEMU YA TANOTARATIBU ZA KIOFISI NA MAWASILIANO

42. Saa za Kazi.43. Watumishi wanaoingia kwa zamu.44. Mahudhurio kazini.45. Daftari la mahudhurio.46. Marufuku kutohudhuria kazini.47. Mawasiliano kuwa katika lugha ya Kiswahili.48. Mawasiliano rasmi ya Taasisi za Umma.49. Mawasiliano katika Afisi za Utumishi wa Umma50. Mawasiliano kati ya Waziri na Mtumishi wa Umma51. Mawasiliano nje ya Taasisi.

SEHEMU YA SITAUSIMAMIZI WA TAARIFA NA KUMBUKUMBU

52. Masjala katika utumishi wa Umma.

Page 4: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

42

53. Upatikanaji wa kumbukumbu binafsi.54. Udhibiti wa kumbukumbu za Serikali.55. Kuondoa, kuharibu au kubadilisha kumbukumbu.56. Kuchapisha taarifa za Afisi kwa asiyehusika.

SEHEMU YA SABAVIWANGO VYA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI

57. Muda wa zaidi katika kazi.58. Likizo la mwaka.59. Likizo ya dharura na Muda.60. Likizo ya Maradhi.61. Likizo ya uzazi.62. Likizo la Mume wa Mke aliyejifungua.63. Likizo bila ya malipo.64. Hatua zitakozochukuliwa likizo bila ya malipo inapomalizika.65. Utekelezaji wa makubaliano ya pamoja.66. Masharti ya kuingia katika Makubaliano.67. Mambo ya kuingia kwenye makubaliano.68. Chombo cha majadiliano.69. Muundo wa chombo cha majadiliano.70. Kazi za chombo cha majadiliano.71. Taratibu za kuwasilisha malalamiko kwa muajiri.72. Hatua za uwasilishaji wa lalamiko.73. Kushughulikiwa kwa lalamiko.

SEHEMU YA NANEMAFUNZO

74. Nafasi za Mafunzo katika Kazi.75. Uchunguzi wa afya.76. Mkataba wa mafunzo.77. Taratibu za udhamini wa Mafunzo.78. Posho la mafunzo ya muda mfupi nje ya nchi.

Page 5: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

43

79. Posho la mafunzo ya ndani ya nchi.80. Kutoa taarifa kwa Ubalozi wa Tanzania.81. Mafunzo baada ya saa za kazi.82. Marekebisho ya mshahara kwa aliyerudi masomoni.

SEHEMU YA TISAFURSA ZA WATUMISHI WA UMMA

83. Fursa ya kupata Mshahara wa likizo.84. Mkopo wa Mshahara.85. Posho la safari za kikazi86. Posho la kukaimu na kushikilia nafasi87. Posho la mazingira hatarishi.88. Posho la kazi maalum89. Posho la uhamisho90. Maposho mengineyo

SEHEMU YA KUMIUSIMAMIZI WA RASIMALI WATU

91. Mpango wa Rasilimali Watu.92. Ufuatiliaji na tathmini.93. Tathmini ya utendaji kazi.94. Uhamisho wa mtumishi wa umma.

SEHEMU YA KUMI NA MOJAMASHARTI YA AJIRA KWA RAIA WA KIGENI

95. Ajira kwa mtumishi wa kigeni.96. Mkataba.97. Likizo ya mwaka.98. Likizo ya dharura.99. Kuambatana na familia wakati wa safari.100. Utaratibu wa usafiri.

Page 6: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

44

101. Malipo ya ushuru na kodi nyenginezo.102. Uchunguzi wa Kiafya.103. Mkopo kwa mtumishi wa kigeni.104. Shughuli za kisiasa.105. Kumalizika mkataba.106. Kifo cha mtumishi wa kigeni.

SEHEMU YA KUMI NA MBILIUTARATIBU WA MAKOSA YA NIDHAMU NA JINAI

107. Utaratibu wa Makosa ya kinidhamu.108. Utaratibu wa Makosa ya jinai.109. Mwenendo wa kinidhamu kuwa siri.110. Adhabu kwa mujibu wa uzito wa kosa.111. Utaratibu wa hukumu ya makosa ya kinidhamu.112. Taarifa ya rufaa.113. Rufaa.114. Muda wa kusikiliza rufaa.

SEHEMU YA KUMI NA TATUMATIBABU YA WATUMISHI WA UMMA

115. Matibabu pamoja na uchunguzi wa afya ya mtumishi wa umma.

SEHEMU YA KUMI NA NNEMENGINEYO

116. Makabidhiano.117. Ruhusa za safari kwa mtumishi wa umma.118. Utaratibu wa uombaji wa likizo kwa wateuliwa.119. Vyeti vinavyotambulika na Serikali.120. Kukabiliana na maafa.121. Gharama za maziko.

Page 7: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

45

122. Matumizi ya simu.123. Ununuzi wa Vifaa vya kazi.124. Vipando vya Serikali.125. Huduma ya kwanza kwa watumishi.126. Vifaa vya kiusalama.127. Nyumba na samani za Serikali.128. Muhuri wa Afisi.129. Hakimiliki.130. Nishani.131. Kuagwa kwa watumishi wa umma.132. Gazeti rasmi la Serikali.133. Kushiriki katika siasa.134. Wafanyakazi wa kujitolea.135. Kutokuwepo kwa watumishi wa kutwa.136. Kanuni za utumishi zinakerebishika.

ORODHA YA VIAMBA TANISHO

KIAMBA TISHO "A" Ardhilhali ya kuingia kaziniKIAMBATISHO "B" Upimaji wa kidaktari.KIAMBA TISHO "C" Mkataba wa kuingizwa kazini.KIAMBA TISHO "D" AhadiKIAMBATISHO "E" Mkataba wa Uajiri baada ya kustaafu.KIAMBA TISHO "F" Mkataba wa ajira Maalum kwa uteuzi

wa Mheshimiwa RaisKIAMBA TISHO "G" Shahada ya Utumishi (Certificate of

Service)KIAMBA TISHO "H" Muongozo wa utengenezaji wa

mkataba wa utoaji wa hudumaKIAMBATISHO “I” Mkataba wa Udhamini wa Masomo

au mafunzo kwa watumishi ummaKIAMBA TISHO "J" Mkataba wa Uajiri wa Kutwa.

Page 8: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

46

DIBAJI

Kanuni hizi, zinachukua nafasi ya Kanuni za Utumishi waBaraza la Wawakilishi 2005, Maadili ya Utumishi waMahakama 1985 na Kanuni za Utumishi Serikali 1997.

Kanuni hizi zina lengo la kutoa ufafanuzi wa masharti ya Sheriaya Utumishi wa Umma ili kutoa muongozo wa uendeshajiwa masuala hayo. Vile vile zina madhumuni ya kuzibamapengo ambayo yangejitokeza katika utekelezaji nauendeshaji wa utumishi.

Kwa kuwa Kanuni hizi haziwezi kuelezwa kuwa ni zaukamilifu. Watumishi wa umma wanasisitizwa wanapoonaupungufu wowote au haja yoyote ya kufanya marekebisho,kuchangia na kutoa maoni yao Afisi Kuu ya Utumishi waUmma ili kuweza kuziimarisha zaidi. Waziri wa Utumishi,baada ya kuzingatia maoni hayo atapaswa kuchukua hatuazinazostahiki.

Page 9: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

47

SHERIA YA UTUMISHI WA UMMA,NAMBA 2 YA 2011

KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA ZAMWAKA 2014,

(Chini ya kifungu cha 37(4))

KWA UWEZO niliopewa chini ya kifungu 37(4) chaSheria ya Utumishi wa Umma, Namba 2 ya 2011, Mimi ,HAROUN ALI SULEIMAN Waziri Wa Nchi (OR) Kazina Utumishi wa Umma Zanzibar natunga Kanuni zifuatazo:

SEHEMU YA KWANZAUTANGULIZI

1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Utumishi waUmma za mwaka 2014, na zitaanza kutumika mara baadaya kutiwa saini na Waziri na kuchapishwa katika Gazeti Rasmila Serikali.

2. Isipokuwa kama itaelekezwa vyenginevyo, Kanuni hizizitatumika moja kwa moja katika usimamizi wa Utumishi waUmma na ndizo zitakazodhibiti muundo, uendeshaji nausimamizi wa Taasisi zote za Umma kama ilivyoelezwa katikakifungu 2 cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Namba 2 ya2011.

3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama maelezo yatahitajivyenginevyo:-

"Afisa katika utumishi wa Umma" maana yake nimuajiriwa katika Utumishi wa Umma mwenye

Jina fupina kuanzakutumika.

MatumiziyaKanuni.

Tafsiri yamaneno.

Page 10: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

48

wadhifa au daraja linalotambuliwa chini yamuundo wa utumishi unaohusika.

"Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma" maana yake ni AfisiKuu ya Utumishi wa Umma ya Utumishi wa ummainayosimamia masuala ya utumishi wa ummaZanzibar.

"Bodi ya Madaktari" maana yake ni Bodi iliyoundwachini ya Sheria ya Madaktari na Madaktari waMeno, Namba 12 ya 1999.

"Daktari wa Serikali" maana yake ni Daktarialiyeteuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afyakwa kufanya uchunguzi na matibabu kwawatumishi wa umma.

"Familia" kwa madhumuni ya Kanuni hizi maana yakeni:-Baba; mama; mke; mume; mtoto; kaka; dada;mamamkwe na babamkwe.

"Gazeti" maana yake ni Gazeti Rasmi la Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar.

"Idara" maana yake ni kitengo chini ya,Wizara, Taasisiinayojitegemea au Uwakala ulioanzishwa kwa jinahilo na kwa kawaida inaongozwa na Mkurugenziau Afisa wa cheo kama hicho kwa jina lolote.

"Jamaa" maana yake ni ndugu wa karibu waliyomondani ya familia ya mtumishi.

"Kamisheni" maana yake ni Kamisheni ya Utumishiwa Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 116cha Katiba ya Zanzibar.

Page 11: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

49

"Katibu Mkuu Kiongozi" maana yake ni Kiongozi waUtumishi wa Umma wa Zanzibar kwa mujibu wakifungu cha 49 (2) cha Katiba ya Zanzibar.

"Katibu Mkuu" " maana yake ni Afisa Mtendaji Mkuuwa Wizara.

"Kinyume cha Utaratibu" maana yake ni kinyume chasheria, Kanuni na miongozo.

"Kumbukumbu" maana yake ni taarifa yoyote yamaandishi bila kuzingatia ipo katika muundo ganiinayotumika kama ushahidi, iliyopokelewa nakuhifadhiwa na taasisi yeyote katika utekelezajiwa majukumu ya taasisi husika.

"Mamlaka ya Usimamizi wa Nidhamu" maana yakeni mtu yeyote au mamlaka iliyopewa uwezo chiniya Katiba, Sheria ya Utumishi wa Umma auSheria nyengine yoyote kuchukua hatua zakinidhamu dhidi ya mtumishi yeyote wa ummaaliyeteuliwa au aliye chini yake.

"Mahakama ya Kazi" maana yake ni kitengo chaMahakama Kuu ya Zanzibar iliyoanzishwa kwaSheria ya Mahusiano Kazini, Namba 1 ya 2005.

"Makundi maalumu" kwa madhumuni ya Kanuni hizimaana yake ni wanawake, watu wenye ulemavuna watu wanaoishi na Virusi VinavyosababishaUgonjwa wa Ukimwi au kuathirika na ugonjwawa UKIMWI.

"Mafunzo ya muda mrefu" maana yake ni mafunzoyanayoanzia kipindi cha miezi tisa na kuendelea.

Page 12: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

50

"Mamlaka ya Rufaa" maana yake ni mamlakailiyopewa uwezo wa kusikiliza rufaa dhidi yamalalamiko au hatua za kinidhamuzitakazoombwa na mtumishi wa umma au Serikalichini ya Sheria ya Utumishi wa Umma.

"Mavazi ya heshima" maana yake ni kivazikinachokubalika katika maadili ya kizanzibari.

"Mkuu wa kazi" maana yake ni Mkuu wa Idara auAfisa yeyote ambaye amepewa majukumu yakusimamia watumishi wengine.

"Mkuu wa Taasisi maana yake ni Afisa Mtendaji Mkuuwa Taasisi zinazojitegemea za Utumishi wa umma.

"Mtumishi wa kigeni" maana yake ni mtumishi waumma ambaye si raia wa Tanzania.

"Mtumishi wa Umma" maana yake ni mtu yoyotealieajiriwa katika Utumishi wa Umma.

"Nyaraka za Serikali" maana yake ni kumbukumbuzinazopatikana na kutathminiwa pamoja nakuhifadhiwa katika jengo la uhifadhi wa nyarakala taifa.

"Rais" maana yake ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi.

"Serikali" maana yake ni Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar.

"Sheria" maana yake ni Sheria ya Utumishi wa Umma,Namba 2 ya 2011, iliyoanzishwa chini ya kifungucha 1 cha Sheria hiyo.

Page 13: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

51

"Taasisi" maana yake ni chombo au Afisi huruinayojitegemea katika Utumishi wa Umma.

"Tume ya Utumishi husika" maana yake ni Tume zaUtumishi zilizoanzishwa chini ya kifungu cha 33cha Sheria ya Utumishi wa Umma.

"Upandishwaji daraja" maana yake ni kupandishwadaraja kwa mtumishi wa umma kutoka nafasindogo kwenda kubwa.

"Usiku" kwa madhumuni ya kanuni hizi maana yake nikuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 12:00 za asubuhi.

"Vileo" maana yake ni vinywaji au kitu chochotevinavyoweza kubadilisha akili ya mtu.

"Visiwa" maana yake ni visiwa vya Unguja na Pembana visiwa vidogo vidogo vilivyomo kwenye eneola Zanzibar.

"Watumishi wa muda" maana yake ni watumishiwanaoajiriwa kwa muda maalum kuanzia miezisita hadi miaka mitatu.

"Watumishi wa kutwa" maana yake ni watumishiambao wanalipwa malipo yao baada ya kumalizakazi kwa siku.

"Waziri" maana yake ni Waziri mwenye dhamana yautumishi wa umma.

"Wizara" maana yake ni Wizara iliyoanzishwa kwanamna iliyoelezwa chini ya kifungu cha 51 chaSheria ya Utumishi wa Umma.

Page 14: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

52

SEHEMU YA PILITARATIBU ZA UAJIRI NA UPANDISHAJI

DARAJA

4.-(1) Kutakuwa na watumishi wa umma watakaogawikakatika makundi yafuatayo:-

(a) Watumishi wa kudumu watakaokuwa na hakiya kupata likizo la malipo, kiinua mgongo namalipo ya uzeeni watakapostaafu baada yakumaliza muda wao wa utumishi auwatakapoachishwa kazi kwa sababuzinazoruhusu kupata mafao, endapo muda wautumishi wao kazini unaruhusu kupatiwamalipo hayo.

(b) Watumishi wa muda maalum watakaokuwana fursa ya kupata likizo na kupata maslahiyao kwa mujibu walivyokubaliana katikaMkataba.

5.-(1) Kwa kuzingatia kifungu cha 57 cha Sheria yaUtumishi wa Umma, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiatalazimika kuangalia vigezo vinavyohitajika kwa uajiri wanafasi yoyote ile kwa mujibu wa nafasi husika na atahakikishayafuatayo:-

(a) Mtu yeyote atakayeingia katika Utumishi waUmma atalazimika kujaza fomu ya aridhilihali(KIAMBA TISHO A) na kufanyiwauchunguzi wa afya yake na kuthibtishwaiwapo afya yake inaruhusu kufanya kazihusika na Daktari wa Serikali katika Hospitaliiliyokubalika na Serikali (KIAMBATISHO

WatumishiwaUmma.

Uajiri.

Page 15: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

53

B), atalazimika kufunga mkataba wa ajira(KIAMBA TISHO C) na kujaza fomu yaahadi ya kiapo inayokataza kutoa siri zaSerikali (KIAMBATISHO D).

(b) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiatahakikisha kuwa watumishi wanaoingiakatika ajira ya utumishi wa umma kwa maraya kwanza wanapatiwa mafunzo ya awali yakazi ndani ya muda wa majaribio.

(c) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiatahakikisha kuwa watumishi wanaoingiakatika ajira ya utumishi wa umma wenyemikopo katika Bodi za Mikopo za Elimu yaJuu anawatolea taarifa kwa Bodi husika kwaajili ya hatua za kurejesha mikopo hiyo.

(2) Baada ya muajiriwa kuridhia masharti yaliyomokatika mkataba wa ajira na kusaini, Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi au Afisa yeyote aliyepewa mamlaka kwa niabayake nae atasaini mkataba huo utakuwa umekamilika, nakalaya aridhililhali, fomu za uchunguzi wa afya, mkataba wa ajirapamoja na fomu ya ahadi ya kiapo ya kutunza siri zitatumwakatika Tume ya Utumishi husika, Afisi Kuu ya Utumishi waUmma, Wizara ya Fedha na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waSerikali.

6.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu cha 57 chaSheria, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi iwapo kuna nafasizilizowazi na zinazohitajika kujazwa na ikiwa bajeti inaruhusuatawasilisha ombi la kujaza nafasi hiyo Afisi Kuu ya Utumishiwa Umma.

Ujazajiwa nafasizilizowazi.

Page 16: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

54

(2) Siruhusa kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisikumuombea ajira mtumishi wa umma aliyeacha kazi kutokataasisi moja ya Serikali kwenda taasisi nyengine au mashirikaya umma.

(3) Mtumishi aliyeacha kazi chini ya kanuni ndogo ya(2) ya kanuni hii iwapo akihitaji kuajiriwa tena atalazimikakupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

7.-(1) Tume ya Utumishi husika itahakikisha nafasizilizokuwa wazi katika Idara zinatangazwa katika vyombovya habari kama vile redio, televisheni, magazeti pamoja namitandao.

(2) Tangazo la nafasi ya kazi litaainisha mahitaji namasharti ya kazi hiyo, cheo, kazi zake na ngazi ya mshahara.

(3) Tume ya utumishi husika itaandaa usaili kwa njiaya maandishi na njia ya mdomo kwa ajili ya kupata waajiriwawenye sifa.

(4) Tume ya utumishi husika itahakikisha inatoa kibalicha ajira kwa wasailiwa waliotimiza sifa za ajira.

(5) Mtu asiyeridhika na jinsi mchakato wa usailiulivyoendeshwa anaweza kupeleka malalamiko yake kwaKamisheni ya Utumishi wa Umma ndani ya miezi mitatukutoka mchakato huo ulipofanyika.

(6) Tume ya Utumishi husika na Taasisi za Umma kwakushirikana na Afisi ya Usalama wa Serikali (GSO)zitalazimika kumfanyia muajiriwa uchunguzi wa kiusalamakabla ya kutoa kibali cha kumuajiri ndani ya muda wa mwezimmoja baada ya hatua za usaili kukamilika.

Tangazola Ajira nautaratibuwa usaili.

Page 17: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

55

(7) Bila ya kuathiri kanuni ndogo ya (6) ya kanunihii, Afisi ya Usalama wa Serikali (GSO) itazingatia mamboyafuatayo wakati wa kumfanyia muajiriwa uchunguzi wakiusalama:

(i) vyeti vya masomo vya muajiriwa;

(ii) mahala anapoishi muajiriwa;

(iii) cheti cha kuzaliwa;

(iv) kitambulisho cha mzanzibari; na

(v) mwenendo na tabia zake katika jamii

8. Tume ya Utumishi husika inaweza kuteua Kamati yawataalamu katika fani husika kwa lengo la kutoa ushauri juuya kujaza nafasi za kazi.

9.-(1) Bila ya kuathiri kifungu cha 60 cha Sheria ya Ajira,Namba 11 ya 2005, mtumishi yeyote ambae ameajiriwa kwamara ya kwanza atalazimika kuwemo katika majaribio yautumishi kwa muda wa miezi kumi na mbili kuanzia tarehe yakuajiriwa.

(2) Ili kuhakikisha mtumishi aliyekuwemo katika mudawa majaribio anapata nafasi ya kuthibitishwa katika nafasiyake, ni wajibu kwa muajiri kuhakikisha yafuatayo:-

(a) Mtumishi wa umma anafahamu taarifa zautendaji wake na mahitaji mengine yakumuwezesha kuthibitishwa;

(b) Mtumishi wa umma atalazimika kupewataarifa ya maandishi ya robo mwaka juu yautendaji wake wa kazi;

Kamatiyaushauriwautaalamukuhususuala laajira.

Muda wamajaribionakuthibiti-shwakazini.

Page 18: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

56

(c) Mtumishi wa umma atalazimika kupatiwamafunzo ya awali ya kazi;

(d) Ikihitajika, mtumishi wa umma atakua na hakiya kupewa mafunzo, ushauri au msaadawowote ili aweze kuthibitishwa;

(e) Iwapo mtumishi wa umma atakuwaamekamilisha masharti ya majaribio KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi atatoa taarifa kwaTume ya Utumishi husika ambayo itachukuahatua za kumthibitisha kazini mtumishialieajiriwa kwa mara ya kwanza;

(f) Iwapo muda wa majaribio uliotolewamwanzoni umekamilika bila ya mtumishi waumma kukamilisha masharti ya majaribio,ataongezewa muda wa majaribio kwa kipindikisichozidi miezi sita; na mtumishi huyoatapewa taarifa ya hatua hiyo kwa maandishi;

(g) Endapo baada ya kuongezwa muda wamajaribio kwa mujibu wa kanuni ndogo (2)(f) ya kanuni hii, mtumishi wa umma ambaeataonekana bado hajatimiza masharti yakuthibitishwa katika Utumishi wa Umma,Taasisi itachukua hatua za kupelekamapendekezo katika Tume ya Utumishihusika kwa ajili ya kumuachisha kazi mtumishiwa umma alieajiriwa kwa mara ya kwanza.

(3) Mtumishi ambaye hakuthibitishwa baada yakumalizika kwa vipindi vyote vya majaribio ataombakuthibitishwa kazi kwa muajiri wake na ikiwa hajathibitishwaatapeleka malalamiko yake katika Tume ya Utumishi husika.

Page 19: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

57

(4) Mtumishi wa umma aliye katika muda wa majaribioatakuwa na haki na fursa zifuatazo:-

(a) Kulipwa mshahara na posho anazostahikikwa mujibu wa kazi yake;

(b) Kumkumbusha muajiri wake ili amthibitishebaada ya kumaliza muda wa majaribio;

(c) Kuomba likizo la kawaida la mwaka.

(5) Mtumishi wa umma aliyekuwepo katika muda wamajaribio hatoruhusika kwenda katika mafunzo ya mudamrefu mpaka baada ya kutimiza miaka miwili ya ajira yake.

10. Bila ya kuathiri masharti ya kifungu cha 59 cha Sheria,Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi:

(a) haruhusiki kabisa kumuajiri mtu aliye chini yaumri wa miaka 18 katika utumishi wa umma;

(b) atalazimika kumpangia kazi mtumishi wa ummainayolingana na hali yake ya afya, endapomazingira ya kazi husika yanahitaji kufanyahivyo.

11.-(1) Mtumishi wa umma aliyekwisha kustaafu nakupata kiinua mgongo chake na pencheni hatoajiriwa tenakwa masharti ya kudumu katika nafasi itakayoweza kumpatiapencheni kwa mara nyengine, isipokuwa anaweza kuajiriwakwa mkataba maalum na nafasi inayohitaji kujazwa lazimaiwe imetangazwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishiwa Umma katika Gazeti Rasmi la Serikali.

(2) Mtumishi aliyetajwa katika kanuni ndogo ya (1)ya kanuni hii, atalazimika kuridhia na kujaza mkataba(KIAMBA TISHO E).

Mashartiya Uajiri.

Ajira yamkatababaada yakustaafu.

Page 20: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

58

(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki watumishiwakatakaoteuliwa na Rais baada ya kustaafu watajazamkataba (KIAMBATISHO F).

12.-(1) Mtumishi katika utumishi wa umma Zanzibaranaweza kufanya kazi kwa kuazimwa katika utumishi waSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jumuiya zaKikanda, Taasisi au Mashirika ya Kimataifa baada ya kupataridhaa kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

(2) Mtumishi yeyote anaweza kuazimwa kwa kipindikisichozidi miaka miwili na kipindi hicho kinaweza kuongezwakwa muda wa miaka miwili mengine iwapo Mkuu wa Taasisi/Katibu Mkuu wake atakapoona inafaa.

(3) Baada ya kumalizika kwa muda wa vipindi viwili,Wakuu wa taasisi wanaohusika na mtumishi huyo watalazimikakuamua ama mtumishi huyo abakie katika sehemualiyoazimwa au kurudi katika sehemu aliyotoka na endapoakirudi atalazimika kulipwa mshahara unaoendana na taasisiyake kwa mujibu wa cheo au elimu yake.

(4) Masharti yaliyotajwa katika kanuni ndogo ya(2) na (3) ya kanuni hii, yatafuatwa kwa watumishi waMuungano, Jumuiya za Kikanda pamoja na Mashirika yaUmma wanapohitajika kufanya kazi katika nafasi yoyote yaSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar isipokuwa kwa nafasi yaUteuzi wa Rais.

(5) Endapo mtumishi wa umma ataazimwa kutokautumishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenda katikautumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana wakati anaondoka katika utumishi wa Serikali ya Zanzibaramekwishatimiza kipindi cha miezi sitini (60) cha kuchangia

Watumishiwakuazimwa.

Page 21: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

59

katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii atalipwa kutegemeana naalichochangia katika mfuko huo atakapofikia muda wake wakustaafu.

(6) Mtumishi yeyote anaweza kufanya kazi kwakuazimwa katika utumishi wa umma wa Zanzibar kutokaWizara au Taasisi moja kwenda nyengine kwa kipindikisichozidi mwaka mmoja. Endapo kipindi cha mwaka mmojakitazidi, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimika kufuatataratibu za uhamisho au kumrejesha anakotoka.

(7) Mtumishi wa kuazimwa atapaswa kulipwamshahara ule wa sehemu anayotoka au unaolingana nawadhifa wa sehemu ile aliyoazimwa kama anakokwendamshahara ni mkubwa atalipwa tofauti ya mshahara wake bilaya maposho.

(8) Mtumishi wa kuazimwa atakuwa na haki yakupandishwa cheo, kupata nyongeza ya mshahara pamaojana kupata haki nyenginezo zote zinazoambatana na mashartiya utumishi katika sehemu aliyoazimwa.

13.-(1) Mishahara yote italipwa kila mwisho wa mwezikwa fedha za Kitanzania, isipokuwa waajiriwa wa mikatabaambao malipo yao yanafuatana na masharti yaliyomo katikamikataba yao.

(2) Kila Mtumishi wa umma atastahiki kulipwamshahara wa mwezi alioutumikia.

(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki hesabu ya malipoya mwezi mmoja itaanzia siku 15 katika mwezi husika.

Ulipajimishahara.

Page 22: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

60

(4) Mtumishi wa Umma hatoruhusika kupokeamshahara zaidi ya mmoja katika taasisi za umma isipokuaanaweza kupokea posho kwa kazi aliyoifanya katika Taasisinyengine.

(5) Nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa mtumishiwa umma itaongezwa kulingana na tathmini ya utendaji wakewa kazi.

(6) Mtumishi wa umma wa ngazi ya uteuzi wa Rais,akiondoshwa katika uteuzi, mshahara wake wa mwezi utabakikama ulivyo isipokuwa posho aliyokuwa akipokea wakatiwa uteuzi litapangwa kulingana na matoleo ya Afisi Kuu yaUtumishi wa Umma.

14. Mamlaka ya kupandishwa daraja, kubadilishwa kadakwa mtumishi pamoja na kuthibishwa cheo ambachomtumishi anapewa, yatakuwa kwa Tume za Utumishi.

15.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 64 chaSheria, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi, atapendekezakwa Tume ya Utumishi husika kumpandisha daraja mtumishiyeyote wa umma mwenye sifa na ujuzi wa nafasizinazotarajiwa kujazwa kwa masharti yafuatayo:-

(a) nafasi hiyo iwe inafahamika katika miundoya kada za utumishi na mtumishi wa kujazanafasi hiyo achaguliwe kwa mujibu wamasharti ya Sheria.

(b) bajeti ya kutosha, zikiwemo fedha za kipindikilichobaki cha matumizi ya mfumo wa

Mamlakayakupandi-shwadaraja nakubadili-shwakada.

Kupandi-shwadarajakwawatumishiwa umma.

Page 23: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

61

muda wa kati kwa ajili ya kujaza nafasihusika;

(c) ripoti za tathmini za utendaji kazi waMtumishi kwa kipindi kisichopungua miakamitatu.

(2) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi hatokuwa nahaki ya kumpandisha daraja Mtumishi wa umma mpaka nafasihiyo iwe imethibitishwa kwa maandishi na kwa kuzingatiakuwa nafasi hiyo ijazwe kwa malengo ya kupata utendajimzuri na ufanisi katika Wizara au Taasisi; na kwamba nafasihiyo kabla ya hapo ilishikiliwa na mtumishi ambae wakati wamahitaji ya kujazwa nafasi hiyo amepandishwa cheo katikanafasi nyengine au ameondolewa kwa sababu zozotezilizoainishwa katika Sheria au Kanuni hizi.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni hizi,kupandishwa cheo kutafanyika kwa Mtumishi atakayethibitikakuwa anao uwezo wa kushika madaraka katika nafasizilizowazi inayohitaji kujazwa.

(4) Mtumishi wa ngazi ya juu na mwenye sifa yakushika nafasi zilizowazi atapewa kipaumbele katika kujazanafasi hiyo. Endapo Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiatathibitisha kwamba mtumishi wa ngazi ya juu hawezikutekeleza majukumu yake, nafasi hiyo italazimika kujazwana mtumishi mwengine wa chini yake na mwenye sifa.

16. Nafasi kwa ajili ya kupandishwa cheo mtumishi waumma, inaweza kuwepo katika hali zifuatazo:-

(a) iwapo mwenye kushika nafasi hiyo amefariki,ameacha kazi, amepandishwa cheo, amepewa

Sababuzinazopel-ekeakupandi-shwacheo.

Page 24: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

62

wadhifa mwengine au iwapo nafasi itakua wazikwa sababu nyengine kwa mujibu wa Sheria;

(b) iwapo nafasi mpya itakua imeundwa na Wizaraau Taasisi husika na imethibitishwa na Afisi Kuuya Utumishi wa Umma na kuidhinishwa naKamisheni.

17. Mtumishi wa umma aliyepandishwa cheo atalazimikakutoa taarifa kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi yamaandishi ya kukubali au kukataa dhamana aliyokabidhiwakatika muda usiozidi mwezi mmoja baada ya kuarifiwa rasmijuu ya kupandishwa cheo.

18.-(1) Mtumishi aliyepandishwa cheo atakuwa katikamajaribio ya cheo chake kipya kwa muda wa miezi sita.

(2) Endapo baada ya kumalizika miezi sita mtumishialiyepandishwa cheo ataonekana kutokuyamudu majukumuyake mapya, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atatoa taarifakwa Tume ya Utumishi husika juu ya mtumishi huyo; Tumeinaweza ikamrudisha mtumishi huyo katika cheo alichokuwanacho kabla ya kupandishwa cheo.

19. Uteuzi katika utumishi kwa watumishi wawalioteuliwa na Rais, ni lazima utangazwe katika Gazeti rasmila Serikali.

20.-(1) Iwapo mtumishi wa ngazi ya uteuzi wa Rais,atakuwa hayupo katika nafasi yake ya utumishi nafasi yakeitashikiliwa na mtumishi mwenye wadhifa sawa na wake auanayemfuatia kwa idhini ya Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiau Katibu Mkuu Kiongozi kulingana na wadhifa waanayeondoka.

Kukubaliaukukataa

Uteuzikatikautumishi.

Taratibuzakushikiliawadhifa.

Muda wakupandi-shwacheo.

Page 25: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

63

(2) Afisa atakayekuwa na haki ya kukaimu nafasiya uteuzi ni yule Afisa Mwandamizi atakayeidhinishwa naKatibu Mkuu Kiongozi.

(3) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi baada yakushauriana na Waziri husika atapendekeza kwa KatibuMkuu Kiongozi majina ya watumishi watatu na atakaeteuliwakushika dhamana hiyo awe mwenye uzoefu wa kutosha nakuzimudu dhamana hizo.

(4) Iwapo mtumishi wa umma atateuliwa kushikilianafasi hiyo ya ngazi ya uteuzi wa Rais atapewa barua rasmiya kukaimu itakayoonesha tarehe ya kuanza kukaimu naitapofikia muda wa kumaliza kukaimu, mtumishi huyoatapewa barua yake ya kusitisha kukaimu .

(5) Mtumishi wa umma ambaye hayumo katika uteuziwa Rais, nafasi yake itakaimiwa na mtumishi mwengine wangazi ya chini yake anayemfuatia kwa idhini ya Katibu Mkuuau Mkuu wa Taasisi.

(6) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu hiki hakunanafasi ya kukaimu kwa muda wa miezi kumi na mbili mfululizokutoka tarehe ya uteuzi wa kukaimu isipokuwa mhusikaatathibitishwa katika wadhifa huo au mwenye dhamanaatakaporejea.

(7) Mtumishi anayekaimu nafasi atastahiki kupataposho la kukaimu kwa mujibu wa matoleo yatakayotolewana Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

21.-(1) Bila ya kuathiri kifungu cha 68 cha Sheria,Mtumishi wa umma atasita kuwa mtumishi kwa sababuzifuatazo:-

Kusitakwa ajira.

Page 26: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

64

(a) kama ni mtumishi wa muda, baada yakumaliza Mkataba wake;

(b) kama ni mtumishi aliyeajiriwa kwa mkatabamaalum baada ya kumaliza mkataba wakeau atakaposhindwa kutimiza mashartiyaliyomo katika mkataba huo;

(c) kama ni mtumishi aliyeajiriwa kwa mara yakwanza atakapokuwa ameshindwakutimiza masharti ya majaribio;

(d) iwapo Rais ataamuru kuachishwa kwakekazi kwa mujibu wa uwezo alionaoKisheria.

(2) Mamlaka za kinidhamu inapopendekezakumuachisha kazi mtumishi wa umma italazimika kupelekamaombi katika Tume ya utumishi husika, isipokuwa kwawateuzi wa Rais; maombi yatapelekwa kwa Katibu MkuuKiongozi.

(3) Mtumishi wa umma atakayemaliza utumishi wakekwa sababu yeyote ile atalazimika kupewa Cheti cha kumalizautumishi (Certificate of Service) (KIAMBATISHO G).

22. Mtumishi aliyefukuzwa kazi katika utumishi wa ummakwa kosa la kinidhamu au kufukuzwa kazini kwa sababu yakuingia hatiani na kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa mudawa miezi sita au zaidi, au faini inayolingana na adhabu hiyo,hatoweza kuajiriwa kwa mara ya pili bila ya kupatikana idhiniya maandishi kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Uajirikwaaliyewahikuachishwakazi aukuingiahatianikwa kosala jinai.

Page 27: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

65

23.-(1) Mtumishi yeyote anaweza kustaafu kwa hiariatakapofikia umri wa miaka 55 baada ya kukubaliwa naTume ya Utumishi husika na kwa mteuliwa wa Rais anawezakustaafu kwa hiari baada ya kuwasilisha ombi lake kwa Raiskupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

(2) Mtumishi anayetaka kustaafu kazi kabla yakufikia umri wa kustaafu kwa lazima atapaswa kutoa taarifaya miezi mitatu kabla ya tarehe ya kustaafu ili kutoa nafasi yakutayarishiwa haki zake kufuatana na masharti ya uajiri wake.

24.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu 44 cha Sheriaya Ajira Nam. 11 ya 2005. mtumishi wa umma atatakiwakustaafu kazi kwa lazima atakapofika umri wa miaka 60.

(2) Muajiri atatoa taarifa ya miezi sita ya nia yake yakumstaafisha mtumishi huyo au atamlipa mshahara wa miezisita ikiwa hakumpa taarifa hiyo.

25. Mtumishi wa umma anayetaka kuacha kaziatalazimika kutoa taarifa ya miezi mitatu kabla ya kuachakazi au kutoa taarifa ya saa 24 na kulipa fedha itayolinganana kima cha mshahara wake wa mwezi mmoja; na atalazimikakusubiri kufikia umri wa kulipwa mafao kama ulivyoelezwakatika Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Namba 2 ya2005.

SEHEMU YA TATUMASHARTI YA AJIRA KWA MAKUNDI

MAALUM

26.-(1) Ni marufuku kwa Katibu Mkuu au Mkuu waTaasisi baada ya kupata uthibitisho kutoka kwa Daktari kwausalama na kwa afya ya mtumishi mjamzito kumpangia kaziza usiku au za ziada.

Kustaafukwalazima.

Muda wakutoataarifa yakuachakazi.

Kustaafukwa hiari.

Hifadhikwawatumishiwajawazitonawanaonyo-nyesha.

Page 28: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

66

(2) Ni marufuku kuajiri au kumpangia mtumishi wakike kufanya kazi katika eneo lolote lenye kutumika madawaya kemikali za sumu, benzino au mionzi ambayo yatapelekeakuathiri uzazi au ujauzito wake.

27. Ni marufuku kuajiri, kutuma au kumpangia kazimtumishi wa kike wakati wa usiku kwenye shughuli yoyoteya kazi isipokuwa mtumishi mwenye majukumu yafuatayo;

(a) Mtumishi wa kike ambae atakua na majukumuya uongozi;

(b) Mtumishi wa kike ambae anacheo katikauongozi;

(c) Mtumishi wa kike katika huduma za afya nahuduma nyengine za ustawi ambazo si hatarikwa afya na usalama wa mtumishi huyo;

(d) iwapo kazi husika inahitaji hivyo.

28.-(1) Mtu ambae ana ulemavu wa aina yoyote atakuwana haki sawa ya ajira kwenye aina yoyote ya kazikutegemeana na viwango vyake vya elimu, ujuzi na uwezona ataajiriwa kwa masharti sawa na kufaidika na haki na fursasawa katika Mkataba wa kazi.

(2) Ni marufuku kwa Muajiri yeyote kumnyima mtumwenye ulemavu ajira kutokana na ulemavu wake.

(3) Ni marufuku kwa Muajiri kumfukuza kazi mtumwenye ulemavu kwenye ajira kabla ya kumaliza mkatabawa kazi kutokana na sababu za ulemavu wake.

(4) Muajiri hatompangia kazi za usiku mtumishimwenye ulemavu na atampatia afisi muafaka, mazingira na

Kazi zausiku kwawatumishiwa kike.

Uajirikwa watuwenyeulemavu.

Page 29: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

67

vifaa rafiki, kazi mbadala na ratiba za kazi zitakazomuezeshakutelekeleza majukumu yake ya kazi.

29.-(1) Hakuna mtu ambaye ametimiza sifa za kuajiriwana akakoseshwa ajira au kunyanyapaliwa kutokana na kuishina Virusi Vinavyosababisha Ugonjwa wa Ukimwi aukuathirika na ugonjwa wa UKIMWI.

(2) Hakuna Mwajiri atakae mzuia mtumishi anaeishina VVU/UKIMWI kuhudhuria kliniki kwa ajili ya kujuamaendeleo ya afya yake.

(3) Kila Taasisi ya Umma itakua na mtumishi ambayeanashughulika na kutoa ushauri nasaha kwa watumishiwanaoishi na VVU/UKIMWI.

30. Itakapotokezea watu wa makundi maalumu wana sifasawa na watu wengine katika masharti ya ajira kipaumbelecha ajira kitatolewa kwa watu wa makundi maalumu.

SEHEMU YA NNEMAADILI YA WATUMISHI WA UMMA

31. Bila ya kuathiri kifungu cha 7 cha Sheria ya Utumishiwa Umma, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atahakikishakwamba Mtumishi wa umma anawajibika :-

(a) kuzingatia kiwango cha juu cha maadili yakitaaluma na nidhamu katika kutekelezamajukumu yake ya utumishi;

(b) kumuhudumia kila mtu wakiwemo watumishiwenzake na wananchi kwa nidhamu, heshima,usawa na bila ya upendeleo;

Ajira kwamtumwenyeVVU/UKIMWI.

Kipaumbelecha ajirakwa watuwenyemahitajimaalumu.

Viwangovyakimaadili.

Page 30: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

68

(c) kuonesha mwenendo mzuri na juhudi katikamajukumu yake ya kazi na kutoa maelekezona huduma kwa namna itakavyokuwa inafaa;

(d) kufanya kazi kwa kuzingatia wakati, ubora nakwa ufanisi;

(e) kutekeleza majukumu ya kazi kwa bidii nauaminifu;

(f) kuwatii viongozi na Serikali iliyopo madarakani.

32. Bila kuathiri kifungu cha 5 cha Sheria ya Utumishiwa Umma, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atahakikishakwamba Mtumishi wa umma atalazimika kuepukana namambo yafuatayo:-

(a) Kutumia Afisi kwa maslahi binafsi;

(b) Kuishusha hadhi Afisi au cheo chake;

(c) Kufanya matendo ambayo yatapelekeakujivunjia heshima;

(d) Kufanya matendo yatakayopelekea kushushahadhi na heshima ya Serikali;

(e) Kufanya biashara katika sehemu za kazi aukumkaribisha mtu mwengine kufanya biashara;

(f) Kufanya matendo yoyote yanayokwendakinyume na majukumu na misingi ya utumishi;

(g) Kujiingiza katika madeni atakayoshindwakuyalipa aliyodhaminiwa na mwajiri wakeambayo hayatozidi theluthi mbili ya mshaharawake.

Miiko yawatumishiwa umma.

Page 31: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

69

33.-(1) Ni marufuku kwa mtumishi wa umma kuvutasigara, kutumia madawa ya kulevya au aina yoyote ya vileokatika sehemu ya kazi.

(2) Ni marufuku kwa mtumishi wa umma kufanyamajukumu yake akiwa katika sehemu ya kazi au nje ya sehemuya kazi akiwa amelewa.

(3) Iwapo mtumishi atakiuka masharti yaliyoelezwakatika kanuni ndogo ya (1) na (2) ya kanuni hii , mtumishi waumma atachukuliwa hatua za kinidhamu kama zilivyoelezwakatika Sheria.

34.-(1) Mtumishi wa umma analazimika kuvaa kivazikilichosafi chenye kuhifadhi heshima yake na kinachokubalikakatika maadili na utamaduni wa Kizanzibari wakati akiwakazini.

(2) Iwapo mtumishi wa umma atahitajika kuvaa sareakiwa katika sehemu yake ya kazi, sare hiyo itatolewa kwagharama za Serikali.

(3) Bila ya kuathiri kanuni ndogo ya (1) na (2) yakanuni hii, Mtumishi wa umma atavaa mavazi yafuatayo.

(i) Kwa mtumishi mwanamme atavaa:-

(a) Kofia ya kiutamaduni wa Mzanzibari, kanzuna "sandals" au makubadhi;au

(b) Suti kamili ya Kitaifa ya rangi moja yenyeukosi wa kukata au isiyo na ukosi wakukata au isiyo na ukosi, na buti;

(c) Shati na suruali refu ya rangi yoyote nabuti.

(ii) Mtumishi mwanamke atavaa kamaifuatavyo:

Matumiziya vileo.

Kivazikatikasehemuza kazi.

Page 32: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

70

(a) Vazi refu la Kitaifa la Tanzania au vazi lolotela heshima lenye mikono, lisilobana nalinalofunika magoti.

(b) Kilemba au mtandio vinaweza kuvaliwa.

(c) Viatu vya buti au "sandals" za rangi nyeusiau rangi nyengine.

35. Mtumishi wa umma akiwa katika kituo chake chakazi au nje, atajiepusha na vitendo ambavyo vinakiuka maadiliya jamii yakiwemo ujeuri, matusi na lugha chafu au ainayoyote ya udhalilishaji wa kijinsia ambao utapelekea ukiukwajiwa Haki za Binadamu.

36.-(1) Nimarufuku kwa muajiri au mtumishi wa ummakufanya aina yoyote ya udhalilishaji wa kijinsia.

(2) Kwa madhumuni ya Kanuni hizi udhalilishaji wakijinsia katika uajiri utakua na maana ya :-

(a) Muajiriwa atakapotakiwa kufanya tendo landoa au kufanya aina yoyoteitakayopelekea kufanyika tendo la ndoaambalo :-

(i) Linaashiria au linaeleza ahadi yakupendelewa kazini;

(ii) Linaashira au linaeleza vitishoambavyo vitaathiri katika ajira;

(iii) Linaashiria au linaeleza vitisho haliya maslahi ya sasa au ya baadaekatika ajira au

Vitendovyaukosefuwanidhamu.

Udhalili-shaji wakijinsia.

Page 33: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

71

(b) Muajiri kwa kutumia lugha isiyostahikiikiwa ya maandishi au matamshi ambayoyanaashiria tendo la ndoa.

(c) Kwa kuonesha tabia ya wazi ya kufanyatendo la ndoa ikiwa kujishishika sehemuya siri au kufanya kitendo chochotekinachoashiria ufanyikaji wa tendo la ndoaamabcho kitaathiri ajira ya muajiriwa,utendaji au ufanisi wa kazi.

(3) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (1) na (2) yakanuni hii, Mtumishi wa umma atakapofanyiwa kosa laudhalilishaji wa kijinsia anaweza kulichukulia kama ni kosa lakinidhamu au la jinai. Ikiwa kosa hilo atalichukulia kuwa nikosa la kinidhamu hatua za kinidhamu zitachukuliwa kamazilivyofafanuliwa katika kanuni hizi. Ikiwa kosa hilo ni la jinaiatachukua hatua za kumuarifu muajiri wake kwa maandishina baadae ataripoti katika vyombo vya sheria.

(4) Ikibainika kuwa Mtumishi wa umma ametoamalalamiko ya uongo juu ya udhalilishaji wa kijinsiaatachukuliwa hatua za kinidhamu kama zilivyoelezwa katikaSheria.

37.-(1) Kila Taasisi italazimika kuandaa mkataba wahuduma kwa umma kwa muongozo uliopo katika(KIAMBA TISHO H).

(2) Mtumishi wa umma atatoa huduma kwa uadilifu nauaminifu, usawa, uwazi na kwa haraka ili kuifanya jamiikujenga imani na utumishi wa umma.

(3) Mtumishi wa umma katika kutoa hudumaatalazimika:-

Mkatabawahuduma.

Page 34: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

72

(a) Kuzingatia vigezo vya mkataba wa hudumakwa umma;

(b) Kutoa kipaumbele kwa watu wenyemahitaji maalum;

(c) Kujibu maombi kwa haraka, uwazi naufanisi;

(d) Kujenga mashirikiano katika kazi kwa ajiliya utoaji huduma bora kwa umma.

38.-(1) Ni marufuku kwa mtumishi wa umma kulifanyiakazi jambo ambalo lina mgongano wa maslahi katika utendajiwake wa kazi.

(2) Endapo maslahi yake binafsi yatagongana namajukumu yake ya kazi atalazimika kulitolea taarifa mapemasuala hilo kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi ambayeatachukua hatua zinazostahiki.

(3) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anawezakumruhusu mtumishi wa umma kuingia Mkataba na Taasisiya Serikali kufanya kazi mbali na anayoipatia mshahara, kwakazi maalumu na wakati maalumu kwa kipindi kisichozidimiezi mitatu na inapozidi mtumishi huyo anatakiwa achukuelikizo bila ya malipo.

39.-(1) Ni marufuku kwa Mtumishi wa Umma au mtuyeyote wa familia yake kuomba au kupokea zawadi, ihsaniau faida nyenginezo kwa ajili ya kushawishi au kuharakishamaamuzi ya jambo.

(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kutoa zawadi kwaajili ya kushawishi maamuzi au jambo ili kupelekea kupatamahitaji binafsi.

MgonganowamaslahikatikaUtumishiwaUmma.

Kutoa aukuchukuaZawadi

Page 35: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

73

(3) Endapo katika kutekeleza majukumu yakemtumishi wa umma atapokea zawadi au faida yoyote kwakiwango kitakachotolewa muongozo kwa toleo maalum naAfisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

(4) Zawadi inayotokana na Tunzo inayotolewa kwamtu binafsi kwa mchango wake utakaothaminiwa Kitaifa auKimataifa kama vile "nobel prize" inaruhusiwa.

(5) Mtumishi anaweza kukubali zawadi au mchangobinafsi kutoka kwa rafiki au jamaa, iwapo kufanya hivyo nidesturi.

(6) Iwapo atakiuka masharti yaliyoelezwa katikakifungu cha hapo juu, mtumishi wa umma atachukuliwa hatuaza kinidhamu kama zilivyoelezwa katika Sheria.

40.-(1) Mtumishi wa Umma ambaye kibinafsi au kikazi,ameomba, amepokea au ametoa hongo au ni wakala wa mtuambaye analengo la kumshawishi mtumishi mwenginekupokea au kutoa hongo, atakuwa amekiuka masharti yaKanuni hizi.

(2) Endapo mtumishi atakiuka masharti ya kanunindogo ya (1) ya kanuni hii,atakuwa ametenda kosa naakipatikana na hatia ataadhibiwa kwa mujibu wa Sheria zaZanzibar.

(3) Kwa madhumuni ya Kanuni hizi, hongo maanayake ni fedha au kitu chochote ambacho kitatolewa kwa ajiliya kushawishi au kuharakisha maamuzi ya jambo.

41. Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi au Idaraatawajibika kusimamia mambo yote yanayopaswakutekelezwa katika sehemu yake ya kazi na katika utoaji wamaamuzi.

Kupokeaau kutoahongo.

Uwajibika-ji kwaUongozi.

Page 36: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

74

SEHEMU YA TANOTARATIBU ZA KIAFISI NA MAWASILIANO

42.-(1) Isipokuwa kama itaelezwa vyenginevyo, mudawa saa za kazi utakuwa ni saa nane kwa siku sawa na masaaarubaini kwa wiki kwa utaratibu ufuatao:

(a) Jumatatu - Ijumaa : saa 01:30 asubuhi -saa 09:30 mchana; isipokuwa:

(b) Mwezi mtukufu wa Ramadhani:Jumatatu - Ijumaa: saa 01:30 asubuhi - saa08:30 mchana.

(c) Saa za kazi hazitobadilika hadi Waziriatakapoidhinisha mabadiliko hayo,

(2) Mtumishi wa umma atalazimika kuzingatia mudawa saa za kazi na atakapochelewa kufika kazini Katibu Mkuuau Mkuu wa Taasisi atalazimika kumchukulia hatua zakinidhamu ikiwa hajatoa sababu za msingi.

(3) Siku za Jumamosi na Jumapili na sikuzitakozoidhinishwa na Serikali kuwa ni siku za sikukuuzitakuwa ni siku za mapumziko.

43.-(1) Watumishi wanaoingia na kutoka kazini kwa zamupamoja na sehemu nyengine za kazi ambazo kwa mujibu washughuli zao za kazi hawawezi kufuata mpangilio wa kazikama ulivyotajwa kwenye kanuni ya 42 cha Kanuni hizi,wataingia na kutoka kazini kufuata mpangilio kadiriutakavyopangwa na Mkuu wa sehemu ya kazi inayohusika;kwa vyovyote vile uingiaji wao kazini hautozidi saa nane zakazi kwa siku na yasipungue masaa arubaini kwa wiki.

Saa zaKazi

Watumishiwanaoingiakwa zamu

Page 37: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

75

(2) Kikomo cha saa za kazi kilichoelezwa katikaKanuni hizi kinaweza kuzidi iwapo kutatokezea ajali, majangaau kazi za dharura zinazolenga kuokoa maisha ya watu, malina vifaa muhimu.

44.-(1) Kwa kuzingatia Kanuni za Utumishi wa Umma,kila mtumishi atalazimika kuwepo kazini wakati wote wa saaza kazi.

(2) Mtumishi wa umma atalazimika kuzingatia masaaya kazi katika kutekeleza majukumu ya kazi.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya ujumla ya Kanunihizi, Mtumishi wa umma atalazimika kufanya kazi wakatiwowote atakapohitajika kufanya hivyo.

(4) Iwapo kama mtumishi wa umma atakiukamasharti yaliyoelezwa katika kifungu hiki, mtumishi wa ummahuyo atachukuliwa hatua za kinidhamu kama zilivyoelezwakatika Sheria.

45.-(1) Kutakuwa na daftari la mahudhurio ambalolitatumika kuweka kumbukumbu ya muda wa mahudhuriokwa watumishi wa umma katika Wizara, Idara na vituo vyotevya kazi.

(2) Kila mtumishi, atajaza katika daftari la mahudhuriomambo yafuatayo:

(a) jina kamili;

(b) muda aliofika kazini na atakaotoka kazini;

(c) iwapo amechelewa atabainisha sababu zakuchelewa kwake;

(d) saini ya mtumishi.

Mahudhu-rio kazini

Daftari lamahudhu-rio

Page 38: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

76

(3) Taarifa za mahudhurio zilizoainishwa chini yakanuni ndogo ya (2) ya kanuni hii, zitahifadhiwa katika daftarila mahudhurio na kuthibitishwa na Mkuu wa Idara.

(4) Bila kuathiri kanuni ndogo (2) ya kanuni hii,Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atasimamia mahudhuriokwa ajili ya viongozi (Kwa madhumuni ya kifungu hikiviongozi maana yake ni wateuliwa), waliyomo chini ya taasisiyake.

(5) Itakuwa ni jukumu la Mkuu wa Idara kupitiadaftari la mahudhurio kila siku ya kazi na kuchukua hatuazilizoelezwa katika Sheria.

(6) Kutakuwa na daftari la kuondoka kazini wakatiwa saa za kazi ambalo litatumika kuweka kumbukumbu yamuda wa kutoka na kuingia kazini wakati wa kazi. Daftarihilo litajumuisha taarifa zifuatazo:-

(a) Jina kamili;

(b) Tarehe;

(c) Muda aliotoka kazini na kurudi kazini;

(d) Sehemu anayokwenda;

(e) Sababu za kuondoka kwake;

(f) Saini ya mtumishi.

(7) Kwa masharti ya ujumla ya kanuni hii kila Idaraitakuwa na daftari la mahudhurio na daftari la kutoka nakuingia kazini wakati wa saa za kazi.

(8) Kunaweza kuwekwa utaratibu mwengine wakushughulikia mahudhurio ya watumishi ya kutoka na kuingiakazini kwa njia ya elektroniki.

Page 39: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

77

46.-(1) Ni marufuku kwa mtumishi wa ummakutohudhuria kazini muda wa saa za kazi.

(2) Mtumishi wa umma atawasiliana na Mkuu wakewa kazi atakapokuwa mgonjwa au atakapokuwa na sababuzisizoepukika mapema siku ya kwanza kutohudhuria kwakekazini.

(3) Endapo mtumishi wa umma atahitajika kusafirinje ya Zanzibar au baina ya visiwa vya Zanzibar, kikazi auvyenginevyo atatoa taarifa kwa maandishi kwa Mkuu wakewa kazi, siku mbili kabla ya safari yake isipokuwa kamakutatokezea dharura maalumu.

(4) Iwapo atakiuka masharti yaliyoelezwa katikakanuni ya hapo juu, mtumishi wa umma atachukuliwa hatuaza kinidhamu kama zilivyoelezwa katika Sheria.

47. Mawasiliano ya kiserikali, kadiri itavyowezekana,yatakuwa katika lugha ya Kiswahili na pale itakapolazimikalugha nyingine inaweza kutumika.

48.-(1) Mawasiliano yote yanayoingia katika Taasisi zaumma lazima yafikie kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisina yanayotoka lazima yapate idhini ya Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi.

(2) Mawasiliano hayo yatalazimika kuwa kwa njiaya maandishi.

(3) Wakuu wa Taasisi wanapotaka kuwasilianawatalazimika kupelekeana barua rasmi.

(4) Kwa kadri itakavyowezekana barua pepe yaafisi ndio itatumika kwa ajili ya mawasiliano ya kiafisi.

Mawasili-ano kuwakatikalugha yaKiswahili

Mawasili-ano rasmiya taasisiza umma

Marufukukutohudhu-ria kazini

Page 40: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

78

(5) Mawasiliano yatakayofanywa kwa njia zaelektroniki yatalazimika kutolewa nakala na kuwekwa katikakumbukumbu za kiafisi.

(6) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atahakikishakwamba tovuti ya taasisi inashughulikiwa na inakwenda nawakati.

(7) Matumizi ya nukushi (fax) yasipelekwe mpakakwa idhini ya Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi na zipelekwekwa shughuli muhimu tu na zitiwe saini na Katibu Mkuu auMkuu wa Taasisi au Afisa aliyeruhusiwa kuipeleka nukushihiyo.

49.-(1) Mawasiliano katika Afisi za Utumishi wa Ummayatakuwa kwa utaratibu ufuatao:-

Mawasiliano ya wazi - Ni mawasiliano ya kilasiku yanayoendesha shughuli za taasisi ambazotaarifa zake zinashughulikiwa na masjala yabayana.Siri - Ni mawasiliano yenye taarifa zisizotakikanakutambulikana na watu wasiohusika katikamuda maalumu.

Siri sana - Ni mawasiliano yenye taarifazinazopaswa kutambulikana na Katibu Mkuu auMkuu wa Taasisi.

Siri kabisa - Ni mawasiliano yenye taarifazinazopaswa kutambulikana na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi au Kiongozi wa juu hasawanaohusika na vyombo vya ulinzi na Usalama.

50. Itakapotokea Waziri amewasiliana na mtumishi waumma kwa shughuli za kikazi mtumishi huyo atalazimikakuripoti kwa Mkuu wake wa kazi.

Mawasili-ano katikaAfisi zaUtumishiwa Umma

Mawasili-ano katiya WazirinaMtumishiwa umma.

Page 41: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

79

51.-(1) Ni marufuku kwa mtumishi wa umma kutoataarifa za Serikali kwa mtumishi wa umma wa Wizaranyengine, Idara, mtu binafsi au chombo cha habari, Kampuniau Shirika la kibinafsi bila ya kupata ruhusa kutoka kwaKatibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi.

(2) Taarifa katika vyombo vya habari zitatolewa namsemaji Mkuu wa Serikali, Waziri au Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi kwa kuzingatia uzito wa taarifa yenyewe.

(3) Iwapo mtumishi wa umma atakiuka mashartiyaliyoelezwa katika kanuni ndogo (1) ya kanuni hii, mtumishiwa umma atachukuliwa hatua za kinidhamu kamazilivyoelezwa katika Sheria.

SEHEMU YA SITAUSIMAMIZI WA TAARIFA NA KUMBUKUMBU

52.-(1) Bila ya kuathiri kifungu cha 95 cha Sheria yaUtumishi wa Umma na kifungu cha 13 cha Sheria yaKuanzishwa Uhifadhi wa Kumbukumbu na NyarakaZanzibar, Namba 3 ya 2008, Kila taasisi ya umma itakuwana masjala ya siri na bayana ambazo zitahifadhi kumbukumbuzote za Taasisi husika kwa utaratibu ufuatao:-

(i) Masjala ya siri itahusika na uhifadhi wanyaraka zote za siri zinazoingia na kutokandani ya taasisi;

(ii) Masjala ya bayana itahusika na uhifadhi wanyaraka zote za wazi zinazoingia na kutokandani ya taasisi;

(iii) Barua zinazoingia katika taasisizitapokelewa na kupelekwa kwa KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi kwa ajili yakuzifanyia kazi.

Masjalakatikautumishiwa Umma

Mawasili-ano nje yaTaasisi

Page 42: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

80

(2) Mkuu wa masjala atahusika na ufunguaji wamajalada kwa mujibu wa maada za barua zinazoingia,kuzisajili, kuzitia katika majalada na kuziwazilisha kwa Afisaanaehusika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

(3) Barua zote, kumbukumbu za mikutano,madokezo, ripoti na marejesho pamoja na viambatishovikiwepo, lazima ziwe na tarehe, namba ya kumbukumbu nasaini kwa ajili ya kuwekewa kumbukumbu.

(4) Majalada yote ya watumishi wa ummayatalazimika kuhifadhiwa katika masjala ya siri nahayatoruhusika kupewa mtumishi yeyote isipokuwa kwaruhusa ya Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi.

(5) Kumbukumbu za mawasiliano yoyote lazimazihifadhiwe kwenye majalada yanayohusika. Katibu Mkuuau Mkuu wa Taasisi atalazimika kuzishughulikia kwa wakatibarua zote zinazopokelewa katika taasisi yake.

53. Isipokuwa ikiwa ni lazima kwa ajili ya kutekelezamajukumu yake rasmi, mtumishi yeyote hatoruhusikakuchukua jalada lake binafsi.

54. Ni marufuku na hairuhusiwi kwa mtumishi yeyote waumma kutoa kumbukumbu za taasisi zilizomo ndani yamajalada bila ya kupata kibali cha Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi.

55. Ni marufuku na hairuhusiwa kwa Mtumishi wa ummakuharibu au kubadilisha kumbukumbu za umma isipokuwakwa idhini ya taasisi inayosimamia masuala ya uhifadhi wanyaraka.

56. Ni marufuku na hairuhusiwi kwa Mtumishikuchapisha taarifa za Serikali katika makala, kufanya tamthiliaau vyenginevyo bila ya kupata idhini ya Katibu Mkuu auMkuu wa Taasisi.

Upatika-naji wakumbuku-mbubinafsi

Udhibitiwakumbuku-mbu zaSerikali

Kuondoa,kuharibuaukubadilishakumbuku-mbu

Kuchapishataarifa zaAfisi kwa

asiyehusika

Page 43: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

81

SEHEMU YA SABAVIWANGO VYA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI

57.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria ya Utumishiwa Umma muajiri hatomtaka au kumruhusu mtumishi waumma kufanya kazi katika muda wa ziada na itakapobidimuda wa ziada hautozidi saa tatu kwa siku.

(2) Kazi itakayolazimika kufanywa katika muda wasaa za ziada na ikapelekea kulipwa posho la kufanya kazihiyo lazima ipatikane idhini ya Katibu Mkuu au Mkuu waTaasisi kabla ya kazi hiyo kufanyika.

(3) Kiwango cha masaa ya kazi kilichowekwa chiniya kanuni ndogo (1) ya kanuni hii, kinaweza kuongezwa iwapokutatokezea dharura au haja ya kufanya hivyo.

(4) Pale saa za kazi za ziada zitapofanywa mtumishiatastahiki malipo ya muda wa ziada kama ifuatavyo.

(a) kwa siku za kazi za kawaida mtumishi waumma atalipwa mara mbili ya kiwangoanacholipwa kwa saa katika siku yakawaida ya kazi (mshahara wa mwezi xsaa za ziada x 2/22 igaiwe kwa 8).

(b) kwa siku za mapumziko na mapumziko yakitaifa. Mtumishi wa umma atalipwa marambili na nusu ya kiwango anacholipwa kwasaa kwa kufaya kazi katika siku isiyokuwaya mapumziko ya kitaifa, ila malipo hayayatakuwa ni kwa saa nane (mshahara wamwezi x saa za ziada x 2.5 /22 igaiwe kwa8).

Muda waziadakatikakazi .

Page 44: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

82

(5) Kwa madhumuni ya kifungu hiki watumishi wangazi ya uteuzi wa Rais na wale watumishi watakaoainishwakatika muongozo utakaotolewa na Afisi Kuu ya Utumishi waUmma,hawatostahiki kupata malipo baada ya saa za kazikwa kuzingatia kwamba shughuli za kikazi baada ya saa zakazi, ni moja kati ya majukumu yake ya kazi.

58.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya kanuni yoyote yaKanuni hizi.

(a) Mtumishi wa umma atastahiki kupewalikizo la siku ishirini na nane za kazi ndaniya miezi kumi na mbili na atastahiki poshola likizo kila baada ya miaka mitatu au kamaitakavyofafanuliwa katika matoleo kutokaAfisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

(b) Mtumishi wa umma, atakaetumia likizoyake pahala ambapo sipo penye maskaniyake ya kawaida atapaswa kutoa anuaniya pahala hapo kwa Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi yake kabla ya kuanza likizoyake. Mabadiliko yoyote ya hapo baadaelazima ayaeleze.

(c) Siruhusa kwa mtumishi wa ummakuakhirisha likizo yake ya mwaka kwamadhumuni ya kulimbikiza siku zake zalikizo ili achanganye na za mwakamwengine, isipokuwa kwa dharura maalumiliyokubalika na kwamba kwa vyovyote vilehakuna likizo itakayolimbikizwa kwa njiaya kuaghirisha zaidi ya miaka miwili. Likizoitakayozidi miaka miwili itakuwa imepotea.

Likizo lamwaka.

Page 45: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

83

(d) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anawezakumzuilia mtumishi wa umma kwenda likizokwa maandishi na kwa dharura maalumukwa muda usiozidi miezi sita.

(e) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anawezakumruhusu mtumishi wa umma aliezuiliwalikizo lake kwa mujibu wa kanuni ndogo(d) ya kanuni hii, kwenda likizo wakatiwowote dharura hiyo itakapomalizika nakama miezi sita imepita tokea mtumishi huyoazuiliwe likizo lake na udhuru aliozuiliwalikizo hilo bado unaendelea, Katibu Mkuuau Mkuu wa Taasisi anaweza kuinunualikizo hilo la mtumishi huyo kwa thamaniya mshahara wa mwezi mmoja bila yaposho.

(f) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anawezakukatisha likizo la mtumishi wa ummayeyote wakati wowote ikitokea haja yakufanya hivyo na mtumishi huyoatawajibika kurudi kazini katika tarehealiyopangiwa na Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi. Isipokuwa kwamba, mtumishialiyekatishwa likizo lake chini ya kijifunguhiki anaweza kukubaliana na Katibu Mkuuau Mkuu wa Taasisi kuendelea na likizoyake udhuru huo utakapomalizika.

(2) Mtumishi wa umma aliyekuwepo masomoni kwamafunzo ya miezi tisa na kuendelea hatochuma likizo lolotekatika kipindi atakachokuwa masomoni.

Page 46: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

84

(3) Mtumishi wa umma ambaye atasimamishwa kazina kulipwa nusu mshahara kwa mujibu wa kifungu 84 chaSheria hatochuma likizo lolote katika kipindialichosimamishwa kazi.

(4) Kwa madhumuni ya kanuni hii, hesabu ya likizoitaanzia pale mtumishi wa umma atakaporipoti kazi baada yakumaliza likizo lake.

59.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi, kilamtumishi wa umma atastahiki likizo la dharura ya muda mfupikwa malipo kamili katika hali zifuatazo:

(a) ikitokea kifo cha mume, mke atastahikikupata likizo ya miezi minne na siku kumi;

(b) ikitokea kifo cha mke, mume atastahikikupata likizo la muda wa siku saba;

(c) ikitokea kifo cha baba au mama au mtotoau dada au kaka, mtumishi atapata likizola muda wa siku tatu;

(d) ikitokea kifo cha baba au mama mkweatastahiki kupata likizo la siku tatu.

(2) Bila ya kuathiri kanuni yoyote katika Kanuni hizi,Mtumishi wa umma anaweza kuomba siku za ziada za likizoya dharura iwapo atakuwa bado anahitaji kufanya hivyo,isipokuwa kwamba likizo hiyo isizidi siku ishirini na nane katikamiezi kumi na mbili.

(3) Likizo iliyotolewa katika kanuni ndogo (2)ya kanuni hii, Mtumishi atalazimika kukatwa likizo hilo katikalikizo lake alilochuma la mwaka.

Likizo yadharurana yaMuda.

Page 47: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

85

60.-(1) Taasisi italazimika kutafuta taarifa za mtumishialiyekuwa hajahudhuria kazini siku tano mfululizo na ikigunduakuwa mtumishi huyo ni mgonjwa taasisi ifanye utaratibu wakumpatia matibabu.

(2) Mtumishi wa umma atakapopata maradhiatastahiki likizo ya maradhi baada ya kupata idhini ya Daktariwa Serikali kwa muda usiozidi siku 60 za kazi kwa mwakammoja kwa malipo ya mshahara kamili bila ya kuathiri likizoya kawaida ya mtumishi huyo.

(3) Iwapo baada ya siku 60 kumalizika itaonekanabado mtumishi anahitaji muda zaidi wa kupumzika kutokanana hali mbaya ya afya yake, Daktari wa Serikali anawezakuidhinisha kwamba mtumishi anayehusika apewemapumziko mengine ya muda usiozidi siku 60 kwa malipoya mshahara kamili ambapo zitakatwa katika likizo yake yakawaida.

(4) Ikiwa baada ya kutolewa siku 120 za mapumzikokutokana na maradhi kwa mujibu wa kanuni ndogo (2) yakanuni hii, mtumishi atakuwa bado hajapata nafuu yakumuwezesha kuendelea na kazi, atastahiki kufanyiwauchunguzi wa afya yake na Bodi ya Uchunguzi wa Afya zaWatumishi, kufuatana na mapendekezo ya Bodi hiyo, mtumishiatapewa likizo ndefu ya maradhi ambayo haitopindukia siku180 kwa malipo ya mshahara kamili. Likizo hii itolewe paleitakapoonekana kuwa upo uwezekano wa mtumishianayehusika kupata nafuu katika muda huo, na kwamba nusuya likizo ndefu ya siku 180 za mwanzo italipwa kutokana nalikizo yake ya kawaida.

(5) Mtumishi aliye katika likizo ndefu ya maradhiatapaswa kuangaliwa afya yake na Daktari wa Serikaliangalau mara moja kwa mwezi na pale atakapoonekana

Likizo yaMaradhi.

Page 48: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

86

amepata nafuu kiasi cha kuweza kuendelea na kazi atapaswakuendelea na kazi tarehe ambayo Daktari ataidhinisha hatakama muda wake wa likizo ya maradhi haujamalizika.

(6) Mtumishi hatostahiki kuchuma likizo katikakipindi cha likizo ndefu ya ugonjwa.

(7) Ikiwa hata baada ya likizo ndefu ya ugonjwa yasiku 300 kwa malipo ya mshahara kamili mtumishi atakuwahajapata nafuu kiasi ya kuendelea na kazi anaweza iwapoDaktari wa Serikali ataona kuwa kuna uwezekano wamtumishi anaehusika kupata nafuu kiasi cha kumuezeshakuendelea na kazi, kuomba likizo bila ya malipo kwa mudausiopungua miezi sita.

(8) Ikiwa hata baada ya kumalizika muda uliotajwahapo juu wa likizo ya maradhi, mtumishi anayehusika atakuwabado anaendelea kuumwa kiasi ya kutozimudu kazi zake,mtumishi huyo hatostahiki muda wowote zaidi wa likizo yamaradhi. Inapotokezea hali hiyo Katibu Mkuu au Mkuu waTaasisi atapaswa kuchukua hatua za kuitaka Bodi yaUchunguzi wa Afya za Watumishi iidhinishe mtumishi huyokustaafishwa kwa sababu ya maradhi.

(9) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni hizi, Mtumishialiyekuwemo katika kipindi cha majaribio anastahiki kupatalikizo ya maradhi.

(10) Ni jukumu la Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisikufuatilia taarifa za ugonjwa za mtumishi aliyekuwepo katikalikizo ya maradhi.

61.-(1) Mtumishi wa umma anapojifungua atastahikilikizo ya uzazi ya miezi mitatu kwa siku za kalenda.

Likizo yaUzazi.

Page 49: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

87

(2) Likizo ya uzazi ya miezi mitatu itatolewa maramoja kila baada ya miaka miwili na miezi tisa kwa watumishiwanawake waliojifungua ambao wamo katika masharti yakudumu. Likizo hiyo haitaathiri likizo ya kawaida ya mwakaya mtumishi.

(3) Pindipo mtumishi wa kike atajifungua kabla yakutimiza muda uliotajwa chini ya kanuni ndogo (2) ya Kanunihii, atastahiki kupata mapumziko ya wiki sita za kalenda.

(4) Taarifa ya uzazi itatolewa na Mtumishialiyejifungua au mtu wake wa karibu kwa Katibu Mkuu auMkuu wa Taasisi kwa ajili ya kustahiki likizo ya uzazi yamtumishi huyo, taarifa hiyo lazima iambatanishwe nakitambulisho cha kuzaliwa kwa mtoto kitakachotolewahospitali, Sheha au Kiongozi wa Mtaa au Kijiji.

(5) Itakapotokea mtumishi amejifungua mapachakipindi cha likizo kitaongezwa mpaka siku mia moja.

(6) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni hizi,itakapotokea kuharibika kwa mimba au kufa kwa mtoto,mtumishi huyo atapewa likizo ya wiki sita kutoka tarehe yakujifungua au kuharibika kwa mimba.

(7) Mtumishi ambaye likizo yake imekatishwa kwasababu ya kifo cha mtoto mchanga, akipata ujauzito kablaya kutimiza miaka miwili na miezi tisa kuanzia tarehe yakujifungua au kuharibika kwa mimba, mtumishi huyo atastahikilikizo kama ilivyoelezwa katika kanuni ndogo (1) ya kanunihii.

(8) Hakuna mtumishi atakayefukuzwa, kuhamishwaau kuachishwa kazi kwasababu za ujauzito au kujifungua.

Page 50: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

88

(9) Mtumishi atakayejifungua atapewa saa moja yakunyonyesha kwa kila siku kwa kipindi cha miaka miwili.Mtumishi huyo atachagua aidha kuitumia nafasi hiyo asubuhikabla ya kuja kazini au mchana saa moja kabla ya muda wakuondoka kazini.

(10) Mtumishi wa kike mjamzito na aliyejifunguaatahudhuria kliniki kwa mujibu wa maelekezo ya Daktari waSerikali na mahudhurio hayo hayatoathiri malipo yake yamshahara na stahiki nyengine.

(11) Mtumishi wa umma atakaejifungua katika mudawa majaribio hatostahiki likizo iliyoelezwa katika kanunindogo (1) ya kanuni hii, isipokuwa atastahiki kupatamapumziko ya wiki sita za kalenda.

62.-(1) Mtumishi wa umma ambae mkewe amejifungua,ataruhusika kupewa likizo ya malipo kwa muda wa siku tanoza kazi ikiwa:-

(a) Likizo hilo litachukuliwa ndani ya siku sababaada ya mtoto kuzaliwa na halitoathirilikizo yake ya mwaka;

(b) Likizo hilo litatolewa kila baada ya miakamitatu.

(c) Taarifa ya kustahili likizo iwasilishwe kwaMkuu wake wa kazi na iambatanishwe nakitambulisho cha kuzaliwa kwa mtotokitakachotolewa hospitali, Sheha auKiongozi wa Mtaa au Kijiji.

(2) Bila ya kuathiri kanuni ndogo (1)(b) ya kanunihii, mtumishi wa umma mwenye mke zaidi ya mmoja atastahiki

Likizo laMume waMkealiyejifu-ngua.

Page 51: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

89

kupata likizo kwa kila mke atakapojifungua. Hata hivyo,endapo atakaekuwa anajifungua kila mwaka ni mke huyohuyo mmoja atastahiki likizo hilo kila baada ya miaka mitatu.

63.-(1) Likizo bila ya malipo zitaidhinishwa na KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi kwa kuzingatia mambo yafuatayo;kwa jambo ambalo halikuorodheshwa hapo chini; Tume yaUtumishi husika ndio itakayohusika na kuidhinisha likizo hiyo.

(a) ikiwa Mtumishi wa umma atapata kazikatika Mashirika ya Kimataifa.

(b) ikiwa mtumishi atamfuata mume au mkembali na kituo chake cha kazi ama kwalikizo au kwa kupata uhamisho.

(c) ikiwa mtumishi wa umma anatakakujihusisha na siasa.

(d) ikiwa mtumishi anataka kuhudhuria mazikoau maombolezo ya jamaa yake nje yaZanzibar.

(e) ikiwa mtumishi wa umma mwanawe, babayake, mama yake au mtu anaemtegemeani mgonjwa na mtumishi anatakakumshughulikia mgonjwa huyo.

(f) ikiwa mtumishi wa umma anataka kumfuatamume au mke aliyepata nafasi ya masomo,nje ya nchi.

(g) ikiwa mtumishi wa umma mwanamme aumwanamke ameoa au ameolewa na mumeau mke anaeishi nje ya Zanzibar.

Likizobila yamalipo.

Page 52: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

90

(h) Wake au waume wa Viongozi wa ngazi zajuu (Rais na Makamu wa Rais) ambao niwatumishi wa umma wanaweza kuchukualikizo bila malipo.

(i) ikiwa mtumishi atamfuata mume au mkealiyepewa uhamisho na Serikali aualiyeazimwa kwa kazi za nje ya nchi.

(2) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo (1) ya kanunihii, muda wa likizo bila ya malipo hautopungua mwezi mmojana hautozidi miaka mitatu isipokuwa kwamba likizo hiyoinaweza kuongezwa kwa kipindi cha pili ikitokezea haja yakufanya hivyo. Baada ya kipindi cha pili kumalizika na akihitajikuengezwa muda mtumishi huyo atalazimika kuacha kazi.Isipokuwa kwa mtumishi atakaejiunga na siasa.

(3) Kipindi ambacho mtumishi wa umma atakuwaamechukua likizo bila malipo, hakitohesabiwa wakati wamatayarisho yake ya mafao ya uzeeni katika taasisi yake.

(4) Mtumishi wa umma yeyote ambae ana mkopona amechukuliwa dhamana na Katibu Mkuu au Mkuu waTaasisi hatoruhusika kuchukuwa likizo bila ya malipo hadihapo ataporejesha mkopo huo.

(5) Mtumishi wa umma anapomaliza likizo bila yamalipo atalazimika kuripoti kazini na Taasisi ikiona inafaainaweza kumuongezea muda mtumishi anaeomba kwa kipindicha pili.

(6) Mtumishi wa umma hatoruhusika kuchukua likizobila ya malipo katika taasisi moja ya umma na kwendakufanya kazi katika taasisi nyengine ya umma.

Page 53: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

91

(7) Mtumishi wa umma aliyerudi likizo bila ya malipoatalipwa mshahara wake kwa mujibu wa muongozoutakaotolewa na Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

64.-(1) Mtumishi wa umma ambae hajaripoti kazini baadaya likizo bila ya malipo kumalizika, Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi atalazimika:

(a) kumkumbusha mtumishi anayehusikakuripoti kazini;

(b) endapo mtumishi wa umma atashindwakuripoti kazini hatua za kinidhamuzitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria.

(2) Mtumishi wa umma atakayechukua likizo bila yamalipo atalazimika kujaza fomu itakayopaswa kujazwa namtumishi huyo atakaporejea kazini baada ya kumaliza likizobila ya malipo pamoja na kujazwa na Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi husika; muongozo wa fomu hiyo utatolewa na AfisiKuu ya Utumishi wa Umma.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni hizi, mtumishiwa umma aliyejiunga na siasa akachukua likizo bila ya malipoatawajibika yeye mwenyewe kurudi kazini baada ya kumalizashughuli za siasa bila ya kusubiri kukumbushwa kufanya hivyona Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi wake.

65. Makubaliano ya pamoja yatakayofikiwa baina yapande zote za vyama vya wafanyakazi na waajiri, yatalazimikakutekelezwa na kufanyiwa kazi.

66. Haki ya kuingia katika makubaliano itafanya kazikwa watumishi wote isipokuwa wale wasioruhusiwa na wale

Hatuazitakazo-chukuliwalikizo bilaya malipoinapoma-lizika.

Utekelezajiwamakubalianoyapamoja.

Mashartiya kuingiakatikaMakuba-liano.

Page 54: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

92

waliotolewa katika Sheria ya Uhusiano Kazini, Namba 1 ya2005, kifungu cha 54.

67. Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi kwa mujibu waKanuni hizi, ataingia kwenye makubaliano na vyama vyawafanyakazi kati ya moja ya mambo yafuatayo:-

(a) kufanya tathmini ya hali ya kazi na mazingiraya utumishi;

(b) kuweka utaratibu wa mahusiano kati ya KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi na mtumishi;

(c) kuweka utaratibu wa mahusiano kati ya KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi na Vyama vyaWafanyakazi;

(d) kuweka utaratibu au kufanya tathmini juu yajambo lolote lililoruhusiwa kufanyiwa tathminina Sheria ya Utumishi wa Umma, Sheria yaAjira, Namba 11 ya 2005 au Sheria yaUhusiano Kazini, Namba 1 ya 2005 au Sherianyenginezo zinazohusiana na hayo;

(e) kufanya tathmini na kuweka utaratibu juu yamambo ambayo pande zote mbili wataonakuna umuhimu.

68.-(1) Kwa kuzingatia kifungu cha 80 cha Sheria yaUtumishi wa Umma kutakua na chombo cha juu cha kitaifacha majadiliano kitakacho wahusisha waajiri na waajiriwa.

(2) Chombo cha kitaifa cha majadiliano kitakuwachini ya Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

Mamboya kuingiakwenyemakuba-liano.

Chombochamajadi-liano.

Page 55: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

93

69. Chombo cha Majadiliano kitakuwa na wajumbewafuatao:-

(a) Mwenyekiti na Makamo Mwenyekitiwataoteuliwa na Waziri baada ya kushaurianana Vyama vya Wafanyakazi.

(b) Wajumbe wanne (4) wataoteuliwa na Chamacha wafanyakazi.

(c) Wajumbe wanne (4) wataoteuliwa na Wazirikufanyakazi kwa niaba ya Serikali.

(d) Katibu atateuliwa na Waziri.

70. Chombo cha majadiliano kitakuwa na kazi yakuishauri Serikali kuhusu mambo yafuatayo:-

(a) Mazingira mazuri ya kazi;

(b) Mahusiano mazuri baina ya waajiri nawaajiriwa;

(c) Kutoa mapendekezo kwa Serikali kuhusu tijana ufanisi na utowaji wa huduma bora kwawatumishi wa umma;

(d) Kufuatilia rufaa itakayoletwa kutokana nashauri lililofikiwa na vyombo vingine vyakisekta vya majadiliano juu ya maslahi yawatumishi;

(e) Kukubaliana kuhusu suala jengine loloteambalo washiriki wa makubaliano wataonainafaa.

Muundowachombochamajadi-liano.

Kazi zachombochamajadi-liano.

Page 56: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

94

71. Malalamiko ya mtumishi wa umma yanawezakuwasilishwa na mtumishi mwenyewe au kupitia Chama chaWafanyakazi, ambacho yeye nimwanachama kwa utaratibuufuatao:-

(a) Malalamiko yatawasilishwa kwa muajiri kwanjia ya maandishi yakieleza misingi ya lalamiko,yakiwemo mambo yafuatayo:-

(i) Jina la mlalamikaji na mlalamikiwa;

(ii) Chanzo cha lalamiko;

(iii) Aina ya lalamiko; na

(iv) Tarehe ya tukio.

(b) Lalamiko lazima lishughulikiwe ndani ya sikutano (5) baada ya kuwasilishwa kwa Taasisihusika;

(c) Lalamiko litasikilizwa wakiwepo wajumbewafuatao:-

(i) Mkuu wa Idara,

(ii) Mlalamikaji; na

(iii) Mwakilishi kutoka vyama vyawafanyakazi; ikiwa ipo haja ya kufanyahivyo.

72-(1). Endapo mlalamikaji hakuridhika na maamuzi yaMkuu wa Idara atawasilisha lalamiko lake kwa Katibu Mkuuau Mkuu wa Taasisi yake.

Taratibuzakuwasi-lishamalalamikokwamuajiri.

Hatua zauwasilishajiwalalamiko

Page 57: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

95

(a) Lalamiko lazima lishughulikiwe ndani ya sikutano (5) baada ya kuwasilishwa kwa Taasisihusika.

(b) Lalamiko litasikilizwa wakiwepo wajumbewafuatao:-

(i) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi,

(ii) Mlalamikaji; na

(iii) Mwakilishi kutoka Vyama vyaWafanyakazi ikiwa ipo haja ya kufanyahivyo.

(2) Endapo mlalamikaji hakuridhika na maaamuzi yaKatibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atawasilisha lalamiko lakekwenye Tume ya Utumishi husika na lalamiko hilo lazimalishughulikiwe ndani ya siku kumi na nne (14) baada yakuwasilishwa Tume ya Utumishi husika.

(3) Endapo mlalamikaji hakuridhika na maamuzi yaTume ya Utumishi husika atawasilisha lalamiko lakeKamisheni ya Utumishi wa Umma. Lalamiko lazimalishughulikiwe ndani ya siku kumi na nne (14) baada yakuwasilisha Kamisheni.

73. Lalamiko lolote litakalopelekwa katika mamlakahusika lazima lishughulikiwe na lijibiwe kwa maandashi nakwa wakati uliowekwa.

Kushughu-likiwakwa

lalamiko.

Page 58: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

96

SEHEMU YA NANEMAFUNZO

74.-(1) Taasisi zote za Serikali zitalazimika kuandaaMpango Maalumu wa Mafunzo pamoja na kutenga fedhakwa ajili ya maafunzo. Mpango huo utazingatia mahitaji yaTaasisi husika kama itakavyoainishwa katika bajeti ya mwaka.

(2) Mtumishi ataomba nafasi ya masomo kwa KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi ambaye ndiye mwenye idhini yakumruhusu mtumishi husika kuhudhuria masomoyanayoombwa.

(3) Maombi ya masomo yanaweza kukataliwa kwamsingi ifuatavyo:-

(a) iwapo nafasi hiyo haimo katika mpango wamafunzo ya Taasisi;

(b) iwapo nafasi ya masomo inayoombwaitakosekana;

(c) iwapo masomo yanayoombwa hayatakuwakwa manufaa ya Taasisi husika;

(d) iwapo mtumishi hajatimiza miaka miwili tanguarudi masomoni;

(e) iwapo hakutokuwa na fedha za kugharamiamasomo hayo.

(4) Mtumishi wa Umma atalazimika kusoma katikaVyuo vinavyombuliwa na Serikali.

(5) Kipaumbele kitatolewa kwa Watumishi wakudumu katika kuhudhuria mafunzo nje ya nchi.

Nafasi zaMafunzokatikaKazi.

Page 59: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

97

6) Ni wajibu wa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisikuwahamasisha na kuwaunga mkono watumishi wa ummakujiendeleza wao wenyewe kimafunzo au kitaaluma.

75. Bila ya kuathiri masharti ya Sheria yeyote ya nchiMtumishi wa umma atakayepata fursa ya kuhudhuria mafunzoyatakayozidi miezi sita nje ya nchi au ndani ya nchi atalazimikakuchunguzwa afya yake na Daktari wa Serikali kabla hajendamasomoni.

76.-(1) Mtumishi wa umma aliyepata ruhusa ya kujiungana masomo atalazimika kufunga mkataba na Taasisi yake(KIAMBA TISHO I).

(2) Mtumishi wa umma hatolazimika kufungamkataba iwapo:-

(a) atahudhuria mafunzo chini ya miezi sita;yasiyokuwa na gharama ya mafunzo yadiploma na kuendelea.

(b) atachukuwa likizo bila ya malipo.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya kanuni hizi, mtumishiwa umma baada ya kupata idhini kutoka kwa Katibu Mkuuwa Taasisi, anaweza kupangiwa sehemu nyengine ya kazikwa manufaa ya Taaifa ikitokezea kwamba taaluma aliyoipatahaiwezi kutumika katika taasisi yake ya awali.

(4) Mtumishi wa umma anaporudi masomoniatalazimika kuitumikia taasisi yake kwa muda wa miaka miwlindipo ataruhusiwa kwenda tena kusoma.

77.-(1) Kwa kutegemea uwezo wa Muajiri udhaminiwa mafunzo utajumuisha gharama zifuatazo:-

Uchunguziwa afya.

Mkatabawamafunzo.

TaratibuzaudhaminiwaMafunzo.

Page 60: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

98

(i) Usajili;

(ii) Mitihani;

(iii) Ada ya masomo;

(iv) Vitabu;

(v) Mahitaji yote ya kitivo husika;

(vi) Posho la utafiti;

(vii) Posho la usafiri la kwenda na kurudikutoka sehemu yake ya kazi hadisehemu anayoondokea;

(viii) Posho la kujikimu;

(ix) Ada ya viza pale itakapohitajika;

(x) Ada ya kodi ya uwanja wa ndegeitakapohitajika;

(xi) Posho la matibabu.

(2) Mtumishi wa umma aliyechaguliwa kuhudhuriamafunzo atalazimika kupatiwa ruhusa ya kuhudhuria mafunzohayo kwa maandishi pamoja na kulipwa mshahara wake.

(a) Mtumishi wa umma atakayekuwamasomoni kwa zaidi ya muda wa miezi tisahatopewa nyongeza ya mwaka yamshahara kwa kipindi atachokuwamasomoni.

(b) Endapo mtumishi wa umma aliyekwendamasomoni alikuwa akiishi katika nyumbaya Serikali ataendelea kuishi katika nyumba

Page 61: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

99

hiyo bila ya kuhamishwa wakati akiwepomasomoni. Hata hivyo akishindwa kurudimasomoni atalazimika kuhamishwa katikanyumba hiyo.

(c) Mtumishi aliyepata ruhusa ya kwendamasomoni atalazimika kuvikabidhi kwamaandishi vitendea kazi na vyombo vyamoto vya Serikali kwa Mkuu wa Taaasisi.

(3) Mtumishi atakaerudi kutoka kwenye mafunzoyaliyochukua muda usiopungua miezi tisa iwe mafunzo hayoyamefanyika hapa nchini au nje ya nchi, atapewa likizo yawiki mbili za kalenda kabla ya kuendelea na kazi. Na iwapomtumishi atakuwa katika mafunzo yaliyochukuwa muda wachini ya miezi tisa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atakuana uwezo wa kumpa likizo isiyozidi wiki moja ya kalenda.

78.-(1) Mtumishi wa umma aliyepata fursa ya kuhudhuriamafunzo ya muda mfupi nje ya nchi na kudhaminiwa na taasisizinazoendesha mafunzo hayo atalazimika kulipwa posholisilozidi muda wa siku 60. Utaratibu wa malipo ya poshohilo utatolewa na Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

(2) Mtumishi aliyetajwa katika kanuni ndogo (1) yakanuni hii,atastahiki kupatiwa:-

(i) Posho la mavazi mara moja kila baadaya miaka mitatu.

(ii) Posho la usumbufu wa njiani kilaanapohudhuria mafunzo.

(3) Mtumishi wa umma ambaye aliyepata nafasi yamafunzo mafupi ambayo hayakudhaminiwa na taasisi

Posho lamafunzoya mudamfupi njeya nchi

Page 62: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

100

zinazoendesha mafunzo hayo, Katibu Mkuu au Mkuu waTaasisi anaweza kumlipia gharama hizo kwa kadiri hali yauwezo itakavyoruhusu.

(4) Endapo mtumishi wa umma atapata nusu yagharama za malipo au atapata malipo kamili kutoka kwamfadhili lakini hayatokidhi kufidia gharama za maisha, KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi anaweza kuongeza kiwango chagharama hizo.

79. Mtumishi wa umma aliyepata fursa ya kuhudhuriamafunzo ya muda mfupi ndani ya nchi atalazimika kulipwaposho kwa mujibu wa muongozo utakaotolewa na Afisi Kuuya Utumishi wa Umma.

80. Endapo mtumishi wa umma atahudhuria mafunzo njeya nchi, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atatoa taarifa zamtumishi husika, kabla ya kuondoka katika Ubalozi waTanzania, ukiwa upo, ndani ya nchi husika. Mambo yafuatayoyatajumuishwa katika taarifa hiyo:-

(a) Jina na anuani ya Taasisi anayotoka mtumishiwa umma;

(b) Jina kamili na anuani ya mtumishi wa umma;

(c) Namba ya pasi ya kusafiria;

(d) Umri;

(e) Jinsia;

(f) Hali ya kindoa;

(g) Nafasi yake ya kazi;

(h) Jina kamili na anuani ya mtu wake wa karibuanaeishi Zanzibar;

Posho lamafunzoya ndaniya nchi

KutoataarifakwaUbaloziwaTanzania

Page 63: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

101

(i) Mafunzo anayohudhuria mtumishi wa umma;

(j) Tarehe ya kuanza na kumaliza mafunzo hayo;

(k) Jina kamili na anuani ya Chuo anachohudhuria

81. Bila ya kuathiri kanuni ya 76 ya Kanuni hizi, Mtumishiwa umma anaweza kutumia muda wake baada ya saa zakazi kujiendeleza na masomo. Katibu Mkuu au Mkuu waTaasisi anaweza kumlipia gharama za mafunzo hayo.

82.-(1) Mtumishi atakaefaulu katika masomo ya juuatastahiki kurekebishiwa mshahara wake baada yakuwasilisha vyeti vya masomo kwa kufuata moja ya njiazinazooneshwa hapa chini kwa kutegemea njia ile ambayoitayompatia mtumishi anayehusika mshahara mkubwa zaidikuliko ule aliokuwa nao kabla ya kwenda masomoni. Njiazenyewe ni:-

(i) Kurekebishiwa mshahara wakekulingana na kiwango cha elimualichosomea.

(ii) Kurekebishiwa mshahara wake kwakupewa nyongeza moja na nusu kwakila mwaka wa masomo ikiwamshahara alouacha umefikiakiwango cha fani aliyosomea.

(2) Mtumishi asiyefaulu masomo yake ya mwaka wamwisho na kuachishwa masomo katika fani inayoambatanana kiwango maalum cha mshahara atalipwa mshaharautakaokuwa mpungufu kwa nyongeza mbili za mshahara wakuanzia katika fani aliyosomea.

(3) Mtumishi wa umma atalazimika kuripoti kwamaandishi kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi baada yakumaliza masomo yake.

Mafunzobaada yasaa zakazi.

Mareke-bisho yamshaharakwaaliyerudimasomoni.

Page 64: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

102

(4) Bila ya kuathiri kanuni ndogo (1) ya kanuni hii,Mtumishi wa umma atastahiki kulipwa malimbikizo yamshahara wake kuanzia tarehe aliyotakiwa kuripoti kazinibaada ya kumaliza masomo na baada kuwasilisha vyeti vyakevya masomo.

SEHEMU YA TISAFURSA ZA WATUMISHI WA UMMA

83. Mtumishi anayekwenda likizo ya kawaida atakuwana fursa ya kutanguliziwa malipo ya mshahara wake wa likizo,iwapo atafanya maombi kwa Katibu Mkuu au Mkuu waTaasisi yake kabla ya kuanza likizo yake.

84.-(1) Mtumishi yeyote wa umma atakapofikwa namaafa makubwa atakuwa na haki ya kuomba kwa KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi husika mkopo usiopindukiamshahara wake wa miezi sita.

(2) Mkopo huo utatolewa baada ya kupatikanaushahidi madhubuti kama vile taarifa ya polisi, Sheha nakadhalika.

(3) Mkopo utatolewa iwapo mtumishi madeni yakehayatozidi theluthi ya mshahara wake.

85.-(1) Mtumishi wa umma atakayekwenda safari katikamoja ya visiwa vya Unguja na Pemba, Tanzania Bara au njeya Tanzania kwa shughuli za kazi atalipwa posho la kujikimukwa kutwa kwa kile kipindi ambacho atakuwa safarini.

(2) Safari za kikazi kwa kawaida zisipindukie wikimbili, isipokuwa pale Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiatakapoamua vyenginevyo.

Fursa yakupataMshaharawa likizo.

Mkopowamshahara.

Posho lasafari zakikazi.

Page 65: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

103

(3) Muongozo wa ulipaji wa posho la safari utatolewana Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

86.-(1) Posho la kukaimu litalipwa wakati ambapomtumishi anaendelea kukaimu nafasi kwa muda wa kipindikisichopungua mwezi mmoja. Posho hilo halitolipwa iwapomtumishi aliyeteuliwa kukaimu nafasi hiyo hatohudhuria kazinikwa sababu yoyote ile.

(2) Mtumishi anayepata posho kwa nafasi yake yakazi akiwa hayupo kazini kwa sababu zinazokubalika kisheria,hatokatwa posho lake hilo na anayeshikilia nafasi hiyoatastahiki kulipwa posho hilo kwa ile nafasi anayoishikilia kwakipindi chote anachoshikilia nafasi hiyo.

87.-(1) Mtumishi wa umma atakayepangiwa kazi katikamazingira hatarishi atalazimika kulipwa posho la mazingirahatarishi kama muongozo utakavyotolewa kutoka Afisi Kuuya Utumishi wa Umma.

(2) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo (1) ya kanunihii, watumishi watakostahiki kulipwa posho la mazingirahatarishi miongoni mwao ni watumishi wa kada za afya,madaktari wa wanyama, wanaohusika na madawa ya mionzi,wanaowahudumia wazee, wachimbaji mafuta na gesi asiliana watumishi wengine kama watakavyoainishwa katikamatoleo ya Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

88. Watumishi wa umma watakaopangiwa kazi maalumuwatastahiki kulipwa posho wakati wa utekelezaji wa kazihiyo.

89.-(1) Mtumishi atakaepewa uhamisho kutoka Ungujakwenda Pemba, Tanzania Bara au kinyume chake, atapaswa

Posho lakukaimunakushikilianafasi.

Posho lamazingirahatarishi.

Posho lauhamisho.

Posho lakazimaalumu.

Page 66: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

104

kulipwa posho la usumbufu litakalokuwa sawa na posho lasiku saba pamoja na usafiri wa ndani wa kufidia usumbufuatokaoupata katika kutekeleza amri hiyo ya uhamisho.

(2) Mtumishi aliyepewa uhamisho kwa njia yakuazimwa kwenda Tanzania Bara kwa mujibu wa kanuni ya12 ya Kanuni hizi na vile vile atapotakiwa kurejea Zanzibar,atalipwa posho la usumbufu litakalokuwa sawa na posho lasiku saba. Posho hilo litalipwa na yule aliyesababisha mtumishianayehusika kupewa uhamisho huo.

(3) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo (1) na (2) yakanuni hii, mtumishi huyo atastahiki kugharamiwa uhamishajiwa familia na mizigo yake.

(4) Posho la uhamisho halitolipwa kwa:

(a) Mtumishi ambae anaepelekwa Afisinyengine kwa kazi za muda kwa kipindikisichozidi miezi mitatu;

(b) Mtumishi anayeomba uhamisho kwamatakwa yake mwenyewe.

90. Kutakuwa na maposho mengine kwa watumishi waumma kwa mazingira maalumu kama itakavyoamuliwa na AfisiKuu ya Utumishi wa Umma kwa kadri itakavyoonekana inafaa

SEHEMU YA KUMIUSIMAMIZI WA RASIMALI WATU

91.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu 56 cha Sheriaya Utumishi wa Umma, Taasisi zote za umma zitalazimikakutayarisha Mpango wa mwaka na miaka mitano waRasilimali Watu, mpango huo utajumuisha mambo yafuatayo:-

Maposhomengineyo

MpangowaRasilimaliWatu.

Page 67: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

105

(i) Jina kamili la mtumishi;

(ii) Umri wa mtumishi;

(iii) Jinsia;

(iv) Elimu na fani ya mtumishi;

(v) Wadhifa wa Mtumishi;

(vi) Kima cha mshahara anacholipwamtumishi.

(2) Bila ya kuathiri kanuni ndogo (1) ya kanuni hii,Mpango wa Rasilimali Watu wa Taasisi, pia utazingatia mamboyafuatayo:-

(a) Maombi ya nafasi mpya za kazizinazopendekezwa na taasisi za umma;

(b) Maombi ya nafasi zitakazowachwa wazikwa sababu zozote zile;

(c) Idadi ya wastaafu wanaotarajiwa kutokakatika utumishi wa umma;

(d) Urithishaji uongozi kwa kuzingatia ukubwawa kuingia kazini (seniority list);

(e) Bajeti ya watumishi wanaotarajiwakupandishwa daraja;

(f) Bajeti ya mishahara kwa watumishi waumma;

(g) Bajeti zote za mahitaji ya Rasilimali Watuziendane na mpango Mkakati wa taasisi;

(h) Mahitaji ya mafunzo kwa watumishi waumma;

Page 68: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

106

(i) Ziada na upungufu wa watumishi wa ummakwa kuchukua hatua za kuwapanga;

(j) Bajeti ya watumishi wanaotarajiwa kwendamasomoni kwa kufuata mpango wamafunzo wa taasisi;

(k) Takwimu za ajira, mafunzo, uteuzi,upandishwaji vyeo na wastaafu.

(3) Bila ya kuathiri kanuni ndogo (1) na (2) ya kanunihii, mpango wa Rasilimali Watu utazingatia miundo ya taasisina majukumu yake. Muongozo wa mpango wa RasilimaliWatu utatolewa na Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

92. Bila ya kuathiri masharti ya ujumla ya Kanuni hizi,kila Taasisi ya umma itatayarisha ripoti ya Mpango wa Miakamitano sambamba na mwaka mmoja mmoja na kuwasilishaAfisi Kuu ya Utumishi wa Umma. Ripoti hizo zitapitiwa nakufanyiwa tathmini juu ya hali ya Rasilimali Watu katikautumishi wa umma.

93.-(1) Kila taasisi ya umma italazimika kumfanyiatathmini ya utendaji wa kazi mtumishi wake kila mwaka.Fomu ya tathmini itatolewa na Afisi Kuu ya Utumishi waUmma.

(2) Tathmini hiyo itamuwezesha mtumishi kupatiwa:-

(i) Nyongeza ya mwaka;

(ii) Kupandishwa daraja;

(iii) Barua ya pongezi;

(iv) Tunzo kwa utendaji mzuri.

Ufuatiliajinatathmini.

Tathminiyautendajikazi.

Page 69: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

107

(3) Tathmini hiyo pia itampelekea mtumishi huyo:-

(i) Kushushwa cheo;

(ii) Kupatiwa mafunzo;

(iii) Kuzuiliwa kupata nyongeza yamshahara;

(iv) Kupatiwa uhamisho; au

(v) Kubadilishwa katika nafasi yake;

(4) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atawasilishamapendekezo yaliyotajwa katika kanuni ndogo (2) na (3) yakanuni hii, kwa Tume ya Utumishi husika kwa hatua.

(5) Ikiwa mtumishi anaondoka katika sehemu yakeya kazi kwa likizo, safari au kwa uhamisho kwenda sehemunyengine, na iwapo kuondoka kwake kutakuwa katikakipindi ambacho tathmini ya utendaji wake inahitajika, KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimika kuikamilisha tathminihiyo kabla mtumishi huyo hajaondoka katika sehemu yakeya kazi. Iwapo tathmini hiyo itamhusu mtumishi aliyehamishwaitalazimu ipelekwe katika sehemu aliyohamishiwa.

94.-(1) Utaratibu wote wa uhamisho wa mtumishi waumma utafanywa kwa kuzingatia kifungu cha 65 cha Sheriaya Utumishi wa Umma.

(2) Mtumishi aliyepewa uhamisho, atahamishiwa nataarifa zake za kiutumishi katika sehemu aliyohamishiwa.

(3) Iwapo mtumishi wa umma atakaidi uhamishoutakaoidhinishwa kwa ajili yake na Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi, atakuwa amefanya kosa na ikithibitika hatua zakinidhamu zitachukuliwa dhidi yake, kama ilivyoelezwa katikaSheria.

Uhamishowamtumishiwa umma.

Page 70: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

108

SEHEMU YA KUMI NA MOJAMASHARTI YA AJIRA KWA RAIA WA KIGENI

95.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu 59 cha Sheria,Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi kama itamuhitaji raia wakigeni inaweza kumuajiri kwa masharti yafuatayo:-

(i) ikiwa hakuna mzalendo mwenye sifakatika nafasi hiyo;

(ii) ipatikane shahada ya polisi yakuthibitisha kutokuwa na makosa yajinai;

(iii) zipatikane taarifa zake kwa muajiriwake;

(iv) zipatikanae taarifa zake binafsi (CV);

(v) kuwe na makubaliano baina yake naSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

(2) Taarifa zitakazokusanywa katika kanuni ndogo(1) ya kanuni hii, zitalazimika kuwasilishwa kwa Katibu MkuuKiongozi.

(3) Kwa madhumuni ya Kanuni hizi, mgeni aliyefungandoa na mzanzibari na ambaye ni mkaazi wa kawaida waZanzibar hatochukuliwa kama ni mgeni ikizingatiwa kwambandoa imedumu kwa angalau miaka mitatu na endapo ndoaitavunjika haki iliyotolewa itaondolewa.

96. Mkataba wa kazi kwa mtumishi wa kigeniatakayeajiriwa katika taasisi za umma utaeleza mashartiyafuatayo:-

(a) Jina kamili la muajiri na muajiriwa;

Ajira kwamtumishiwa kigeni.

Mkataba.

Page 71: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

109

(b) Anuani kamili ya muajiriwa na nchi anayotoka;

(c) Uraia wa muajiriwa;

(d) Sifa na wadhifa wa muajiriwa pamoja na ainaya kazi anayoajiriwa kufanya;

(e) Majukumu ya kazi ya muajiriwa;

(f) Muda wa mkataba ambao hautokwendakinyume na masharti ya Kanuni hizi;

(g) Mshahara na marupurupu anayostahikimuajiriwa;

(h) Ukomo wa ajira;

(i) Stahiki atakazozipata baada ya kumalizamkataba;

(j) Warithi wa muajiriwa;

(k) Masharti mengine ambayo yatawekwa katikakanuni hizi.

97. Mtumishi wa kigeni, atastahiki kupata likizo yamwaka ambayo atatakiwa aiombe kwa maandishi kwaKatibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi. Iwapo atahitaji kusafirinje ya nchi katika kipindi cha likizo, atalazimika kupata ruhusakutoka kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi husika.

98.-(1) Iwapo mtumishi wa kigeni atalazimika kusafirinje ya nchi kwa sababu ya ugonjwa au dharura nyenginekwa mtu yeyote wa familia yake, maandalizi ya safari hiyoyatafanywa na yeye mwenyewe au familia yake.

Likizo yamwaka.

Likizo yadharura.

Page 72: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

110

(2) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anawezakuidhinisha likizo ya dharura kwa mtumishi wa kigeniitakapotokezea kifo cha mzazi wake, mke, mume au mtotona atastahiki kupata posho la usafiri kama itakavyoelezwakatika Mkataba wake.

(3) Likizo ya dharura itahesabiwa katika likizo yakeya mwaka.

99. Mtumishi wa kigeni wakati wa kuja Zanzibar gharamaza usafiri wake zitalipwa na Taasisi husika isipokuwaanapotaka kuambatana na familia yake gharama za usafiriwa familia yake atagharamia mwenyewe.

100. Ikiwa mtumishi wa kigeni atahitajika kusafiri kikazi,gharama zote za usafiri zitalipwa na Serikali kamaitakavyoelezwa katika Mkataba wake.

101. Iwapo mtumishi wa kigeni ataingia nchini na vifaavyake vya kufanyia kazi atalipa ushuru na kodi nyenginezokwa mujibu wa Sheria na taratibu za nchi.

102.-(1) Kabla ya kuwasili Zanzibar, mtumishi wa kigeniatalazimika kufanya uchunguzi wa afya yake, ili kuthibitishakwamba ana uwezo wa kufanya kazi Zanzibar. Ikiwaataambatana na familia yake, pia itawalazimu kufanyauchunguzi wa afya zao. Nakala za ripoti za uchunguzi waafya itaambatanishwa katika mkataba wake.

(2) Ajira ya mtumishi wa kigeni itakataliwa endapoitabainika kuwa afya yake sio salama kumuwezesha kufanyakazi Zanzibar. Endapo mmoja kati ya watu wa familia yakeatabainika kuwa hayuko salama kiafya, atashauriwaasiambatane nae na kama kuna ulazima wa kuambatana nae,basi ajira yake itakataliwa

Kuambatanana familiawakati wasafari.

Utaratibuwausafiri.

Malipoya ushuruna kodinyenginezo.

UchunguziwaKiafya.

Page 73: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

111

103. Mtumishi wa kigeni haruhusiki kuchukua mikopokatika taasisi za kifedha nchini.

104. Kwa namna yoyote ile, mtumishi wa kigenihatoruhusiwa kujishughulisha katika mambo ya kisiasa.

105. Mtumishi wa kigeni anapomaliza mkataba wakeatalazimika kuondoka nchini kurudi nchini kwao.

106.-(1) Endapo mtumishi wa kigeni atafariki Zanzibar,Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi kwa kushirikiana na Afisiya Mambo ya nje pamoja na Ubalozi wa nchi ya mtumishihusika kushughulikia taratibu zote zinazohusiana na mali zamarehemu pamoja na kuusafirisha mwili wa marehemu.

(2) Jamaa wa marehemu atalazimika kufanyamakabidhiano kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi hati,nyaraka na mambo yote yanayohusiana na utendaji wa kaziwa marehemu.

SEHEMU YA KUMI NA MBILIUTARATIBU WA MAKOSA YA NIDHAMU NA

JINAI

107.-(1) Mtumishi wa umma anapofanya kosa kuhusianana kazi yake, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi au Mkuuwa Idara husika atapaswa kuzingatia kama kosa hilo ni lajinai au ni la uvunjaji wa nidhamu za kazi au aina zote mbili.

(2) Iwapo mtumishi atafanya kosa la kinidhamu,Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi au Mkuu wa Idara atampataarifa ya dai hilo mtumishi husika na kupewa nafasi yakujieleza na baadae kuchukuliwa hatua muafaka. Taarifa ya

Mkopokwamtumishiwa kigeni.

Shughuliza kisiasa.

Kumalizikamkataba.

Kifo chamtumishiwa kigeni.

UtaratibuwaMakosayakinidhamu.

Page 74: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

112

mtumishi huyo itawasilishwa kwa maandishi kwa Katibu wachama cha wafanyakazi au mwakilishi wa wafanyakazialiyomo katika Kamati ya Uongozi.

(3) Iwapo Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi auMkuu wa Idara ataona kwamba mtumishi amefanya kosakubwa na ambalo hana mamlaka ya kulitolea maamuziatawasilisha malalamiko hayo katika Tume ya Utumishi husikaambayo itamtaka mtumishi anayelalamikiwa kutoa maelezokuhusiana na shutuma hizo, na kama ni kosa ambalo linawezakumalizwa na Tume ya Utumishi husika basi litalimaliza maramoja.

(4) Iwapo mtumishi huyo atakataa kosaanalotuhumiwa, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi au Mkuuwa Idara husika atatakiwa kutoa maelezo yake na mashahidikama anao na mlalamikiwa atapewa fursa ya kuwahojimashahidi hao.

(5) Iwapo Tume ya Utumishi husika itaona kwambahakuna kesi ya kujibu itapitisha azimio hilo mara moja nakama mtumishi huyo alikuwa amesimamishwa kazi basiatamriwa kuendelea na kazi mara moja.

(6) Tume ya Utumishi husika inapokaa kwa shughuliinayohusika na hatua za kinidhamu kwa mtumishi inawezakuwaalika mwenyekiti na katibu wa tawi la chama chawafanyakazi ambalo anatoka mfanyakazi huyo ambaowatashiriki katika kuchangia utatuzi wa suala linalojadiliwalakini unapofika wakati wa maamuzi Tume ya Utumishi husikandio itakayotoa maamuzi.

108.-(1) Mtumishi wa umma anapofanya kosa la jinai,Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi au Mkuu wa Idara atatoataarifa kwa maandishi kwa Katibu wa chama cha

UtaratibuwaMakosaya jinai.

Page 75: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

113

wafanyakazi na kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiambaye ataliripoti au atawezesha kuripoti Polisi kwauchunguzi na hatua.

(2) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atapaswakuijulisha Tume ya Utumishi husika juu ya hatua hiyoiliyochukuliwa dhidi ya mtumishi huyo.

(3) Mtumishi wa umma anayefanyiwa uchunguzi napolisi kwa kosa alilolifanya kuhusiana na kazi yakeatasimamishwa kazi na kulipwa nusu ya mshahara wakepamoja na maposho yake kwa kipindi cha mwaka mmoja,isipokuwa kwamba nusu mshahara utasitishwa atakapopewalikizo bila malipo kwa mujibu wa kifungu 84 cha Sheria yaUtumishi wa Umma.

(4) Malipo ya asilimia 10 ya mfuko wa hifadhi wajamii kwa mtumishi anayelipwa nusu mshahara yataendeleakulipwa na taasisi na asilimia 5 ya mshahara kamili wamtumishi itakatwa kutoka nusu ya mshahara atakaolipwa.

(5) Mtumishi anayelipwa nusu mshahara na ambayeanadaiwa na taasisi yoyote ambapo taasisi yake ni mdhaminiwake ataendelea kukatwa deni lake katika hiyo nusu yamshahara anayolipwa kama ilivyo katika mkataba huo.

(6) Iwapo kesi itamalizika na kuonekana hana hatiamtumishi huyo atapaswa kurejeshwa kazini na kulipwa tofautiya mishahara yake bila maposho kwa kipindi chotealichosimamishwa kazi.

(7) Iwapo atapatikana na hatia na kupewa adhabuya onyo, kifungo cha nje, faini au kifungo cha chini ya miezisita, atatumikia adhabu yake ya kifungo na akimalizaatarudishwa kazini lakini hatolipwa tofauti ya mishahara.

Page 76: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

114

(8) Haki za Mtumishi aliyepatikana na hatia kamailivyo katika kanuni ndogo za kanuni hii zitasita kwa kipindichote ambacho alikuwa hahuhdhurii kazini na zitaendelea tenaatakapoanza kurudi kazini. Kwa madhumuni ya kanuni hiisiku ambazo amekuwa nje ya kazi hazitahesabiwa katikakuchuma likizo na nyongeza ya mwaka.

(9) Pale ambapo kosa alilolifanya mtumishi ni lajinai na la kinidhamu, hakuna hatua za kinidhamuzitakazochukuliwa mpaka zimalizike hatua za jinai.

(10) Iwapo mtumishi aliyefanya kosa hilo atatiwahatiani na mahkama hatochukuliwa tena hatua za kinidhamu,lakini kama mahakama itamuachia huru hatua za kinidhamuzinaweza kuchukuliwa dhidi yake.

109. Isipokuwa kama itahitajika vyenginevyo na mamlakaza kinidhamu au mamlaka nyengine za kisheria mwenendowote wa kesi, hati na nyaraka zitakazotumika katika kesihiyo vitakuwa ni siri kwa mtu asiyehusika.

110. Bila ya kuathiri masharti ya kanuni zilizoelezwa hapojuu, adhabu hizi zitatolewa kulingana na uzito wa kosalilofanywa na mtumishi wa umma kama ilivyoelezwa katikaSheria.

111.-(1) Hukumu yoyote itakayotolewa kwa mtumishiwa umma itatolewa kwa maandishi ikijumuisha sababu yauamuzi wa hukumu husika na kujumuisha mambo yafuatayo:-

(a) Tarehe ya kosa la kinidhamu;

(b) Jina la mtumishi wa umma alietenda kosala kinidhamu na nafasi yake;

Mwene-ndo wakinidhamukuwa siri.

Adhabukwamujibuwa uzitowa kosa.

Utaratibuwahukumuyamakosayakinidhamu.

Page 77: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

115

(c) Maelezo ya kosa la kinidhamu alilolifanyamtumishi wa umma na vifungu vya Sheriaau Kanuni vilivyotumika;

(d) Ioneshwe kwamba mtumishialiyeadhibiwa alipewa haki ya kusikilizwana kuita mashahidi kama alikuwa nao;

(e) Maamuzi yaliyotolewa;

(f) Maamuzi ya rufaa kama yalitolewa;

(g) Sababu ya maamuzi;

(h) Taarifa zinazohusiana na makosayaliyopita kwa mtumishi wa umma hadikutolewa kwa hukumu kama zipo;

(i) Tarehe ya utoaji hukumu iliyotolewa;

(j) Mamlaka iliyotoa hukumu.

(2) Kwa madhumuni ya kanuni hii, kila hukumuinayotolewa na Mamlaka husika italazimika kuwekewakumbukumbu ambayo itajumuisha mambo yafuatayo:-

(i) Tarehe;

(ii) Mlalamikaji na Mlalamikiwa;

(iii) Aina ya kosa;

(iv) Mamlaka iliyotoa uamuzi;

(v) Maamuzi yaliyofikiwa.

112. Mtumishi yeyote alokuwa na nia ya kukata rufaaatatoa taarifa ya maandishi kwa mamlaka ya nidhamu husika

Taarifa yarufaa.

Page 78: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

116

kuelezea nia yake ya kukata rufaa itayoelezea sababu zakukata rufaa ndani ya siku 14 baada ya kutolewa maamuzi.

113.-(1) Mtumishi asiyeridhika na uamuzi wa KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi yake, atawasilisha rufaa yakeTume ya Utumishi husika kwa maandishi ndani ya siku 14kuanzia siku ya kuarifiwa kwake maamuzi hayo.

(2) Mtumishi asiyeridhika na uamuzi wa Tume yaUtumishi husika atawasilisha rufaa yake Kamisheni ndani yasiku 14 kuanzia siku ya kuarifiwa uamuzi huo.

(3) Mtumishi asiyeridhika na uamuzi wa Kamisheniatawasilisha rufaa yake Mahkama ya Kazi ndani ya mwezimmoja kuanzia tarehe ya uamuzi huo. Ambapo uamuzi wakeutakuwa wa mwisho.

(4) Nakala ya rufaa itapelekwa kwa kile chomboambacho maamuzi yake yanaombewa rufaa ambacho baadaya kupata nakala hiyo kitawasilisha kumbukumbu zotezinazohusiana na kosa la mtumishi huyo pamoja na vielelezokama vipo kwa chombo kinachotarajiwa kusikiliza rufaa hiyondani ya wiki moja.

114. Rufaa yoyote itakayoombwa italazimika kusikilizwandani ya siku 30 baada ya kupokea taarifa ya maombi yarufaa husika na kwamba rufaa hiyo italazimika kutolewauamuzi ndani ya kipindi cha siku 60 kuanzia siku iliyoombwa.

Rufaa

Muda wakusikilizarufaa.

Page 79: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

117

SEHEMU YA KUMI NA TATUMATIBABU YA WATUMISHI WA UMMA

115.-(1) Kila mtumishi atakuwa na haki ya kupatamatibabu katika hospital za Serikali. Mtumishi wa ummaanayetaka kwenda hospitali kwa matibabu atalazimikakwenda na fomu ya ugonjwa (sick sheet). Iwapo daktariataona ipo haja ya kumpa mapumziko mtumishi huyoatatakiwa kuainisha katika fomu ya ugonjwa na atalazimikakuwekewa kumbukumbu katika jalada lake.

(2) Kwa masharti ya kanuni ndogo (1) ya kanunihii, Katibu Mkuu wa Afya atalazimika kuteua madaktariambao watashughulikia matibabu ya watumishi wa umma.

(3) Mtumishi yeyote yule ambaye ataenda kinyumena utaratibu wa kanuni ndogo (1) ya kanuni hii, atakuwaametenda kosa na hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yamtumishi huyo.

(4) Kwa madhumuni ya masharti ya Kanuni hizi,kutakuwa na Bodi ya Uchunguzi wa Afya za Watumishi waUmma wanaosumbuliwa na maradhi ambayo yanaathiriutendaji wa kazi. Bodi itakuwa na lengo la kuchunguza nakushauri kama watumishi hao wanaweza kusaidiwa matibabuna taasisi zao au wastaafishwe kutokana na maradhiwaliyonayo au wabaki katika nafasi za utumishi walizonazohuku wakiendelea kusaidiwa matibabu.

(5) Itakapokubalika na Katibu Mkuu au Mkuu waTaasisi wa mtumishi ambaye afya yake itatakiwakuchunguzwa na Bodi ya Uchunguzi wa Afya za Watumishiwa Umma kufuatana na kanuni ndogo (4) ya kanuni hii, ombila uchunguzi litapaswa kupelekwa kwa Katibu Mkuu waWizara ya Afya ambaye ndio atakayeiarifu Bodi kwakutekeleza shughuli hiyo haraka iwezekanavyo.

Matibabupamoja nauchunguziwa afyayamtumishiwa umma.

Page 80: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

118

(6) Bodi itapaswa kutoa mapendekezo yake kuhusuafya ya mtumishi anayehusika katika nakala tatuzitakazopelekwa kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiinayohusika kwa kuzishughulikia ipasavyo. Iwapo Bodiitapendekeza kwamba mtumishi huyo astaafishwe kutokanana kutoweza kuzimudu kazi zake kwa sababu ya ubaya waafya yake, mtumishi huyo atastahiki kustaafishwa pamoja nakupewa haki zake zote.

(7) Kwa madhumuni ya Kanuni hizi, kila mtumishiwa umma atakuwa ni mwanachama wa Mfuko wa bima yaafya kama muongozo utakavyotolewa na Afisi Kuu yaUtumishi wa Umma.

SEHEMU YA KUMI NA NNEMENGINEYO

116.-(1) Mtumishi wa umma atalazimika kuandika baruaya makabidhiano wakati anapoondoka katika wadhifa wakekwa sababu yeyote ile.

(2) Mtumishi huyo atakabidhi barua yake yamakabidhiano kwa mujibu wa ngazi za kiungozi ndani sikuthelathini kwa utaratibu ufuatao:-

(i) Afisa atakabidhi kwa Mkuu waSehemu;

(ii) Mkuu wa Sehemu atakabidhi kwaMkuu wa Idara;

(iii) Mkuu wa Idara au Mkuu waTaasisi atakabidhi kwa KatibuMkuu;

Makabi-dhiano.

Page 81: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

119

(iv) Katibu Mkuu atakabidhi kwaKatibu Mkuu Kiongozi.

(3) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimikakuandaa fomu ya makabidhiano inayoonyesha orodha ya vifaaau nyaraka alizozitumia wakati wa kutekeleza majukumu yake.

(4) Utaratibu wa kanuni ndogo (1), (2) na (3) yakanuni hii, hautoathiri masharti ya jumla ya kifungu 68 chaSheria.

117. Mtumishi wa umma atalazimika kuandika barua yakuomba ruhusa ya kusafiri kati ya visiwa vya Unguja naPemba, Tanzania Bara au nje ya Tanzania ndani ya wiki mbilikabla ya kusafiri kwa utaratibu ufuatao:-

(i) Afisa ataomba ruhusa kwa KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisi kupitiakwa Mkuu wa Idara;

(ii) Mkuu wa Idara au Mkuu waTaasisi ataomba ruhusa kwaKatibu Mkuu;

(iii) Katibu Mkuu ataomba ruhusa kwaKatibu Mkuu Kiongozi baada yakutoa taarifa kwa Waziri wa wizarahusika.

118.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika uteuzi wa Raisatalazimika kuandika barua ya kuomba ruhusa ya likizo ndaniya mwezi mmoja kabla ya likizo hilo kwa utaratibu ufuatao:-

(i) Mkuu wa Idara au Mkuu waTaasisi ataomba ruhusa ya likizo

Ruhusaza safarikwamtumishiwa umma.

Utaratibuwauombajiwa likizokwawateuliwa.

Page 82: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

120

kwa Katibu Mkuu na Katibu Mkuuatamuombea kwa Katibu MkuuKiongozi;

(ii) Katibu Mkuu ataomba ruhusa yalikizo kwa Katibu Mkuu Kiongozibaada ya kutoa taarifa kwa Waziriwa wizara husika.

(2) Mtumishi huyo atastahiki posho la likizo kilabaada ya miaka mitatu, kama itakavyofafanuliwa katikamatoleo kutoka Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

119.-(1) Vyeti vinavyotambuliwa na Serikali kwa ajili yamfumo wa marekebisho ya mshahara na muongozo wautumishi ni kama vifuatavyo:-

(a) Shahada: ambayo itajumuisha Shahada yaUzamivu, Shahada ya Uzamili, Stashahadaya Uzamili na Shahada ya kwanza.

(b) Stashahada: ni cheti cha mafunzo ambachokimepatikana kwa muda angalau wamiaka miwili, baada ya kumaliza kidato chasita au kidato cha nne na cheti cha mafunzoau sifa nyengine inayofanana na hiyoambayo inatambulika na Serikali.

(c) Cheti cha Kidato cha sita.

(d) Cheti cha kidato cha nne.

(e) Cheti (Certificate).

(2) Utaratibu wa kuangalia maslahi ya watumishiwanaohudhuria mafunzo ya muda mfupi utawekwa na Tumeza Utumishi husika.

Vyetivinavyota-mbulikanaSerikali.

Page 83: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

121

(3) Kwa madhumuni ya masharti ya kanuni hizi,vyeti vya kitaaluma ambavyo vitakavyotambuliwa na Serikalini vile vyeti vinavyotolewa na vyuo vilivyosajiliwa na taasisiza taaluma.

120.-(1) Kila Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiatalazimika kuhakikisha kunakuwepo na vifaa vya awali vyakukabiliana na maafa na kujitaarisha na Mpango Mkakatiwa kukabiliana na maafaa kama utakavyotolewa muongozona taasisi inayosimamia masuala ya Maafa.

(2) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atahakikishakwamba hakuna jengo lolote linahusiana na taasisi yakelitakalojengwa bila ya kujali utaratibu mzuri wa kukabilianana maafa.

(3) Taasisi zote za umma zitaanzisha na kuweka Afisamaalum kwa madhumuni ya kuhakikisha utekelezaji na ufuatajiwa udhitibi wa maafa katika taasisi zao.

(4) Katika kuhakikisha kwamba Mpango wa Taifawa kukabiliana na maafa unatekelezwa kila taasisi itahakikishakatika mipango yake kunatengwa fungu maalumu kwa ajiliya kukabiliana na maafa.

(5) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atahakikishakuwa watumishi wote katika Taasisi yake wanafahamumpango na taratibu zote za kukabiliana na maafa na wanapatafursa ya kuhudhuria mafunzo ya kukabiliana na maafa.

121.-(1) Iwapo Mtumishi wa umma atafariki Taasisi yakeitagharamia gharama za maziko kama itakavyotolewamuongozo na Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

(2) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimika

Kukabilianana maafa.

Gharamazamaziko.

Page 84: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

122

kuwasilisha jina la mtumishi huyo kwa Katibu Mkuu Kiongozikwa ajili ya kutoa tangazo la tanzia katika Gazeti la Serikali.

(3) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimikakuwalipa mshahara wa miezi minne kwa watuwanaomtegemea marehemu.

(4) Ikiwa mtumishi wa umma au mwanafamilia wakeatafariki akiwa katika kituo cha kazi alichohamishiwa, aukutumwa kwa kazi taasisi italazimika kugharamia usafirishajiwa mwili wa marehemu.

(5) Ikiwa mtumishi atafiwa na mzazi wake (babaau mama), mume au mke au mtoto wa kumzaa atapatiwamalipo ya ubani. Ikiwa kifo hicho kimetokea nje ya kituochake cha kazi lakini ndani ya Tanzania, Taasisi inawezakumsaidia nauli ya usafiri ya kwenda na kurudi msibani.

122.-(1) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimikakuhakikisha kuwa simu zote za afisi zinatumika kwa matumiziya afisi tu. Simu za moja kwa moja ndani ya afisi (direct line)watastahiki viongozi wafuatao:

(i) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi;

(ii) Naibu Katibu Mkuu;(iii) Na wengine wanaofafana na hadhi

au wadhifa ya waliotajwa hapo juu.

(2) Mawasiliano ya simu zote za nje yatalazimikakupata kibali cha Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi.

(3) Endapo mtumishi wa umma atakiuka mashartiya kanuni hii, atakuwa amefanya kosa na ikithibitikaatachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria.

Matumiziya simu.

Page 85: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

123

123. Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimikakufanya manunuzi ya vifaa vya afisi kwa kufuata Sheria yaManunuzi, Namba 9 ya 2005 na kufanya usambazaji wa vifaahivyo kwa utaratibu ufuatao:-

(i) kuingizwa ndani ya ghala ya afisikwa ajili ya kuhifadhiwa;

(ii) kutolewa kwa ajili ya matumizi kwakufuata taratibu za ghala; na

(iii) kwa vifaa vilivyochakaa KatibuMkuu au Mkuu wa Taasisiatawasiliana na taasisi inayosimamiamasuala ya Mali chakavu kwakuchua hatua zinazofaa.

124.-(1) Watumishi wafuatao watakuwa na fursa yakupatiwa usafiri kwa shughuli zao za kazi kwa utaratibuufuatao:

(i) Katibu Mkuu Kiongozi;

(ii) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali

(iii) Waheshimiwa Majaji wa MahkamaKuu

(iv) Mrajis wa Mahkama Kuu

(v) Katibu wa Baraza la Wawakilishi

(vi) Mkurugenzi wa Mashtaka

(vii) Naibu Mwanasheria Mkuu

(viii) Kadhi Mkuu

Ununuziwa Vifaavya kazi.

VipandovyaSerikali.

Page 86: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

124

(ix) Mufti Mkuu(x) Mhasibu Mkuu wa Serikali

(xi) Katibu Mkuu

(xii) Naibu Katibu Mkuu

(xiii) Na watendaji wengine kamaKatibu Mkuu Kiongozi atavyoonainafaa kwa mujibu wa kazi zao.

(2) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atahakikishavyombo vyote vinavyotumika katika taasisi yake vinakuwana buku linaloonyesha matumizi ya safari ya chombo hicho.

(3) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atahakikishavyombo vyote vilivyomo katika taasisi yake vinafanyiwamatengenezo katika Karakana Kuu ya Serikali au sehemu(gereji) zitakazothibitishwa na Serikali.

(4) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anawezakumdhamini mtumishi wa umma kupatiwa fursa ya mkopowa vyombo vya usafiri kwa mujibu wa dhamana zao.

(5) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atahakikishavyombo vya usafiri vya Serikali vilivyo chini ya mamlaka yakevinapasishwa na kukatiwa bima.

(6) Kwa madhumuni ya kanuni hii, mtumishialiyepata fursa ya kupatiwa usafiri kwa shughuli za kaziatalazimika kukabidhi vipando hivyo kama masharti ya kanuniya 116 ya Kanuni hizi kinavyoeleza.

125.-(1) Kila Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiatalazimika kuhakikisha ndani ya taasisi yake kunakuwa naupatikanaji wa huduma ya kwanza ya afya na vifaa vyahuduma ya kwanza kwa watumishi.

Hudumayakwanzakwawatumishi.

Page 87: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

125

(2) Kila taasisi itakuwa na mtumishi atakaekuwa najukumu la kusimamia vifaa vya huduma ya kwanza na aliyepatamafunzo ya huduma ya kwanza.

126. Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimikakuhakikisha kuwa Mtumishi anayefanya kazi katika mazingirayanayohitaji vifaa maalumu vya kutendea kazi anapatiwa vifaahivyo vya kiusalama kwa afya yake ambavyo vitakuwa nimali ya Serikali.

127.-(1) Watumishi wafuatao watakuwa na fursa yakupatiwa nyumba za Serikali kwa mujibu wa wadhifa waokwa utaratibu ufuatao:

(i) Katibu Mkuu Kiongozi;

(ii) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali

(iii) Waheshimiwa Majaji wa MahkamaKuu

(iv) Mrajis wa Mahkama Kuu

(v) Katibu wa Baraza la Wawakilishi

(vi) Mkurugenzi wa Mashtaka

(vii) Naibu Mwanasheria Mkuu

(viii) Kadhi Mkuu

(ix) Mufti Mkuu

(x) Mhasibu Mkuu wa Serikali

(xi) Katibu Mkuu

Vifaa vyakiusalama.

Nyumbana samanizaSerikali.

Page 88: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

126

(xii) Naibu Katibu Mkuu

(xiii) Na watendaji wengine kamaKatibu Mkuu Kiongozi atavyoonainafaa kwa mujibu wa kazi zao.

(2) Kwa mtumishi mwenye wadhifa wa uteuzi waRais, Katibu Mkuu Kiongozi atalazimika kumuandikia baruamtumishi aliyemaliza uteuzi wake kuhama na kukabidhinyumba ya Serikali ndani ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja.Kwa mtumishi wengine atakayemaliza utumishi wake kwasababu yoyote ile Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisiatalazimika kumuandika barua mtumishi huyo ya kuhama nakukabidhi nyumba ya Serikali ndani ya kipindi kisichozidimwezi mmoja.

(3) Mtumishi atakayepelekwa kufanya kazi mbalina sehemu yake anayoishi kikawaida atastahiki kupatiwanyumba kwa njia ya kupangishwa kwa kadiriitakavyoyumkinika.

(4) Mtumishi anayehama katika nyumba ya Serikali,atapaswa kukabidhi nyumba kwa Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Katibu Mkuuau Mkuu wa Taasisi atamuarifu Mdhibiti Mkuu wa thamaniza Serikali, ambaye atapaswa kuangalia nyumba hiyo kablaya mtumishi anayehusika hajahama kwa madhumuni yakutazama usafi na uzima wake. Mtumishi anaehusika atapaswakugharamia matengenezo yote yatakayoonekana yanastahilikugharamiwa nae kwa mujibu wa Kanuni hizi kabla yakuihama nyumba hiyo.

128.-(1) Kutakuwa na muhuri wa Afisi au Wizara, ambaoutawekwa katika mazingira ya kiusalama na matumizi yakeya kiafisi lazima yafanywe kwa idhini ya Katibu Mkuu au

Muhuriwa Afisi.

Page 89: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

127

Mkuu wa Taasisi, na ihakikishwe kuwa hautumiki kwamatumizi binafsi.

(2) Muhuri wa Afisi au Wizara utakuwa chini yadhamana ya Mkuu wa Masjala ya Siri.

(3) Endapo mtumishi wa umma atakiuka mashartiya kanuni hii, atakuwa amefanya kosa na ikithibitikaatachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria.

129.-(1) Kazi yoyote ya ubunifu itakayofanywa namtumishi wa umma kama ni sehemu ya wajibu wake wa kaziitakuwa ni hakimiliki ya Serikali na ikihitajika kwa matumiziya jamii haitaruhusika kuuzwa kwa lengo la kujipatia faida.

(2) Kwa kuzingatia Sheria ya Hakimiliki, Namba14 ya 2003, Mtumishi wa umma atakayevumbua kazi yeyoteile atalazimika kulipwa haki yake kwa ajili ya kuthamini kaziyake hiyo.

(3) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anawezakumuajiri mtu mwengine yeyote kwa ajili ya kutengeneza kaziya ubunifu kwa kuzingatia Sheria ya Hakimiliki, Namba 14ya 2003.

130. Mtumishi wa umma anaweza kutunukiwa nishanikwa utaratibu ulioelezwa katika Sheria ya Shughuli za Rais,Namba 5 ya 1995.

131. Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anawezakuandaa sherehe ya kumuaga na utaratibu wa kumpatiazawadi mtumishi aliyemaliza muda wake wa utumishi.

Kuagwakwawatumishiwa umma.

Hakimiliki.

Nishani

Page 90: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

128

132.-(1) Kutakuwa na Gazeti Rasmi la Serikalilitalosimamiwa na Afisi inayoshughulikia masuala ya Barazala Mapinduzi. Mambo ya kiutumishi yafuatayo yatapaswakutangazwa katika Gazeti Rasmi:-

(i) Miswada yote;

(ii) Sheria;

(iii) Tanzia;

(iv) Wastaafu;

(v) Watumishi wapya;

(vi) Wanaohamishwa;

(vii) Watumishi watakaofukuzwa katikautumishi; na

(viii) Mambo mengine yote ya kiutumishiyatakayoamuliwa na Afisi Kuu yaUtumishi wa Umma.

(2) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimikakuwasilisha taarifa zinazotaka kuingizwa ndani ya GazetiRasmi kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ataidhinishakuchapishwa katika gazeti rasmi.

(3) Uchapishwaji wa jambo lolote katika GazetiRasmi, utakuwa ni taarifa tosha na ni sawa na kutolewa taarifarasmi kwa Taasisi yoyote ya Serikali inayohusiana na taarifahiyo.

(4) Kabla ya kutangazwa katika Gazeti Rasmi,taarifa zote zinazohusiana na matangazo ya Sheria zitalazimikakuwasilishwa katika Afisi ya Mwanasheria Mkuu.

Gazetirasmi laSerikali.

Page 91: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

129

133.(1) Mtumishi wa umma hatoruhusiwa kushiriki katikashughuli za siasa muda wa kazi, kifungu hiki hakitamzuiamtumishi kupata haki yake ya msingi ya kupiga kura na kuwamwanachama wa chama cha siasa akipendacho.

(2) Kwa madhumuni kanuni ndogo (1) ya kanunihii, hakuna mtumishi wa umma atakayeruhusiwa kufanyayafuatayo :-

(a) kufanya kampeni, kuonyesha hisia , kutoamatusi kwa chama au kiongozi wa chamaau kujihusisha mwenyewe katika mamboya siasa katika jamii; au

(b) kuvaa sare za chama, picha, kielelezoambacho kinaonyesha hisia zake zachama anachokipenda; au

(c) kushiriki katika maadamanoyaliyotayarishwa na chama; au

(d) kufanya kampeni ya chama cha siasa aumgombea wa chama na kuhudhuriamkutano wa siri wa chama cha siasa; au

(e) kutoa hotuba katika mkutano wa siasa,kuandika mitazamo yake kisiasa aukuandika barua za wazi dhidi ya kiongoziyeyote wa chama cha siasa.

(3) Ni marufuku kwa Afisa yeyote mwenye ngaziya juu kumruhusu au kumuelekeza mtumishi kushiriki katikashughuli za siasa muda wa kazi na pindipo akitiwa hatianiatachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za nchi.

Kushirikikatikasiasa.

Page 92: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

130

(4) Mtumishi wa Umma ambaye anashikililia ngaziya uteuzi na mtumishi ambaye ana wadhifa nyeti wa uongozikama ilivyoelezwa katika Sheria ya Watumishi wa UmmaKushiriki Katika Siasa, Namba 3 ya 2003 anawezakugombea au kushika nafasi katika siasa kwa mashartiyafuatayo-

(a) Mtumishi atatoa taarifa kwa Katibu Mkuuau Mkuu wa Taasisi husika angalau sikukumi na nne kuonesha nia ya kugombeaau kushika nafasi katika siasa.

(b) Mtumishi huyo wa umma atahesabikakuwa yupo likizo bila ya malipo baada yakumalizika taarifa ya siku kumi na nne nawakati wote wa kugombea nafasi katikachama na atakapopata nafasi hiyoatahesabika kuwa ameacha kazi.

(5) Mtumishi wa Umma aliyechukua likizo bilamalipo chini ya masharti ya kanuni ndogo (4) ya kanuni hii nahakupata uteuzi ndani ya chama chake atatoa taarifa ya niaya kurejea kazini kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisihusika na Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atamuarifu sikuya kurejea kazini kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake.

(6) Mtumishi wa Umma yeyote ambaye hakutajwachini ya kanuni ndogo (4) ya kanuni hii, anaweza kugombeaau kuwa na cheo kisiasa, kwa masharti yafuatayo:-

(a) Mtumishi atatoa taarifa kwa Katibu Mkuuau Mkuu wa Taasisi husika angalau sikukumi na nne kuonesha nia ya kugombeaau kushika nafasi katika siasa

Page 93: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

131

(b) Ndani ya siku saba (7) ya uchaguzi wakewa ubunge au uwakilishi, atachukuwalikizo bila malipo au kutoa taarifa yakuacha kazi.

(7) Iwapo mtumishi wa umma atakiuka masharti yakanuni hii, hatua za kinidhamu dhidi yake zitachukuliwa kamaifuatavyo:

(i) Karipio; kwa kosa la kwanza;

(ii) Karipio kali; kwa kosa la pili;

(iii) Kusimamishwa kazi; kwa kosa latatu;

(iv) Na hatua nyengine zozote zilezilizoelezwa katika Sheriainayohusuhu mtumishi wa ummakushiriki katika siasa.

134. Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi hatoruhusikakuweka wafanyakazi wa kujitolea katika taasisi yake.

135.-(1) Hakutakuwa na utumishi wa kutwa katikautumishi wa umma, kama kuna ulazima Katibu Mkuu auMkuu wa Taasisi atalazimika kuomba kibali kwa Tume yaUtumishi husika na kumjazisha mkataba (KIAMBATISHOJ).

(2) Utumishi wa mtumishi wa kutwa hautozidi miezisita na atalipwa pale ambapo anamaliza kazi yake kwa siku.

(3) Mtumishi wa kutwa hatakuwa na fursa yakupata likizo na wala hana haki ya kudai kiinua mgongo namafao ya uzeeni.

Wafanya-kazi wakujitolea.

Kutoku-wepokwaWatumishiwakutwa.

Page 94: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

132

136. Kanuni za utumishi zinaweza kutengenezwa aukurekebishwa kadiri inavyoonekana kuna haja ya kufanyahivyo na Waziri. Muongozo au marekebisho yatayofanywayatakuwa na uhalali pamoja na uzito sawa na Kanuni zautumishi zilizotangulia.

Kanuni zautumishizinareke-bishika.

Page 95: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

133

KIAMBA TISHO "A"(Chini ya kanuni ya 5(1)(a))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Makao Makuu/ Idara ya…………………….....................................

ARDHILHALI YA KUINGILIA KAZINI

1. Aina ya kazi……………………………….……………....

2. Kiwango cha mshahara…………………..………………..

3. Jina la muombaji kazi..…………..………………………...

4. Tarehe na pahala pa kuzaliwa………………………………

5. Uraia……………………..…………………...………….

6. Elimu…………………………...………………………...

7. Shahada ya juu- ikiwa anayo ….………………………….

8. Jee umewahi kuajiriwa kabla?

9. Ndiyo Hapana

Page 96: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

134

10. Kama jawabu ni ndiyo taja sababu ya kuiacha kazi hiyo.

…………………………………………………………………………

………………………………….……………………………………

Tarehe ……………..20……Saini ya muombaji kazi…….............

Kazi zote za Serikali ulizoajiriwa zamani lazima uzitaje pamoja nasababu zake mbalimbali ulizoachia au ulizoachishwa.

Kwa Daktari, Zanzibar

Tafadhali mpime huyu anaekuja na Ardhilhali hii yeye ni muombaji kazikatika Wizara/ Idara ya…………………………………………....kama...................…………… na utuletee matokeo yake hapa chini.

Tarehe ……………………. ………………………….. Mkuu wa Wizara/ Idara

Kwa ……………………………………………..

Mimi leo nimempima muombaji kazi aliyetajwa juu na nimemuona yakuwa yeye anafaa/ hafai kufanya kazi kama…………………………………. katika Wizara/Idara ya…………………………………….

Tarehe………………………….. ……......…….………. Daktari aliyepima

Page 97: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

135

KIAMBA TISHO "B"(Chini ya kanuni ya 5(1)(a))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBARREVOLUTIONARY GOVERNMENT OF ZANZIBAR

UPIMAJI WA KIDAKT ARIMEDICAL EXAMINATION

Ijazwe na yule anayepimwaTo be filled in by person being examined

Jina Kamili ……………………………………………………………………………………….Full name

Umri ……………… Mume Mke

Age Sex

Uliwahi kuchanja Ndio Hapana MwakaHave you been vaccinated (if so when)

Katika jamaa zako wapo waliougua kifua kikuu……………………Has any relative suffered from Tuberculosis

Baba yu hai………...…….Sababu ya kifo………………...………Is father alive Cause of death

Page 98: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

136

Umri aliofia……………………………… Age of death

Umepata kuugua ugonjwa gani mkubwa? …........ Taja tarehe…….…What kind of serious illness have you suffered? State approximatedates

Uliwahi kuugua kifua kikuu…………………………………………Have you suffered from: Tuberculosis

Magonjwa ya uasharati…………Homa ya baridi yabisi……………Venereal diseases Acute rheumatism

Kisukari……………… Ugonjwa wa akili……………....………...Diabetes Mental Disorder

Mafigo………………… Pumu ……………………….…..Kidneys diseases Asthma

Nahakikisha kwa dhati yangu kuwa yaliyoelezwa hapo juu ni kwelikwa nijuavyo mimi.(I certify that the above information is correct to the best of my knowledgeand belief).

Tarehe…………………………………………..Date

Saini…………………………………………..Signed

Ijazwe na DaktariTo be filled by the Medical Officer

Umri……………………………………………Apparent age

Page 99: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

137

Kiwiliwili…………………………………Physique

Mapafu…………………………………………Lungs

Moyo………………………………………Heart

Tumbo………………………………………….Abdomen

Mkojo uzito……………………………….Urine S.G

Alka ya hisia…………………………………..Nervous System

Ute…………………………………………Albumen

Ngiri …………………………………………..Hernia

Sukari……………………………………...Sugar

Meno………………………………………….Teeth

Mwendo wa damu…………………………Blood Pressure

Page 100: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

138

Nuru ya macho………………………………..Vision

Kusikia…………………………………….Hearing

Mapendekezo ya Daktari…………………………………………Recommendations of Medical Officer

Tarehe………………………………….Date

Saini…………………………………..Signed

Page 101: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

139

KIAMBA TISHO "C"(Chini ya kanuni ya 5(1)(a))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR_____________________

MKA TABA WA KUINGIZW A KAZINI

WIZARA YA……………………………………………………....

IDARA YA…………..……………………...………. ZANZIBAR.

Kwa …………….........................................................................

1. Nimeamriwa kwamba ikiwa umezikubali shuruti zilizomo katikaMkataba huu, unaingizwa kazini kwa kujaribiwa kwenye Wizaraya ......................................................................................Zanzibar, Tanzania, kuanzia tarehe..............................................

2. Mshahara utakaolipwa katika kazi yako niShilingi................................... kwa mwezi katika daraja ya................................. lakini itabidi usite kwenye vizingiti vyauwekevu.

3. Itakulazimu uzifuate Kanuni zote za Serikali zilizopo sasa nazitakazofanywa na Serikali muda baada ya muda, kwa msingi

Page 102: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

140

wake. Kanuni hizo hazitobadili shuruti zako za kazi kamazilivyoelezwa katika Mkataba huu wa kuingizwa kazini.

4. Utatakiwa uwe tayari kufanya kazi katika Wizara/ Idara yoyotena pahala popote katika Visiwa vya Unguja na Pemba au sehemunyengine yoyote ambako kuna afisi za SMZ.

5. Muda wa kujaribiwa kwako kazini ni miezi kumi na mbili, kuanziatarehe ……………………………….

6. Ikiwa baada ya kupita miezi kumi na mbili tangu kumalizika mudawa kujaribiwa utakuwa bado hujathibitishwa kuwa uendeleekazini au hujaarifiwa kwamba muda wako wa kujaribiwaumeongezwa itakupasa upeleke kwa Katibu Mkuu au Mkuuwa Taasisi yako ombi lako kutaka kuthibitishwa kuwemo kwakokazini.

7. Katika muda huu wa kujaribiwa, unaweza kutolewa kazini kwakupewa taarifa ya mwezi mmoja au wewe unaweza kutoka kazinivile vile kwa kutoa taarifa ya mwezi mmoja au kwa kulipamshahara wa mwezi mmoja, kwa kukosa kutoa taarifa hiyo.

8. Ikiwa muda wako wa kujaribiwa na kabla ya kuthibitishwakuwemo kwako kazini, umeonekana kuwa huna uwezo wa kazi,au umefanya kosa au umepinga amri za kazi, basi unawezakuachishwa kazi hapo hapo (yaani bila ya kupewa taarifa).

9. Kuhusu mwenendo na adabu ya kiserikali utapaswa kufuataSheria zote za Nchi, na matokeo na maamuzi yoyote ya Serikalikuhusu mambo hayo.

....................................................... Katibu Mkuu /Mkuu wa Taasisi

Page 103: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

141

Mimi nimekubali kuingizwa kazini kwa mujibu wa shuruti zilizomo katikaMkataba huu.Pia nakubali nihesabiwe ni Mzanzibar mwenye kitambulishoNamba………………

.................................. ................................ Tarehe Mtumishi

Page 104: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

142

KIAMBA TISHO "D"(Chini ya kanuni ya 5(1)(a))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR(Sheria inayokataza kutoka Siri za Serikali)

AHADI

WATUMISHI WA SERIKALI WOTE WATIYE SAINIWANAPOAJIRIW A

1. Nimefahamishwa na kuelezwa kuhusu Sheria ya Usalama waTaifa na utunzaji wa Siri za Serikali (The National Security andOfficial Secret Act) Nambari 5 ya 1983.

2. Natambua madhara yatakayonifikia pindi nitakapoivunja aukuipuuza Sheria hiyo.

3. Najua ipo Sheria inayomtaka mtumishi kuzuia Siri za Serikali nakwamba Sheria hiyo inafanya marufuku kutoa Siri za Serikalikwa kutoa makala katika magazeti, kuandika buku, kuhadithiana kumueleza aliyekuwa hahusiki kuambiwa au kuelezwa habarihizo bila ya kupata idhini ya Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisihusika.

4. Natambua kuwa shuruti hizi ni lazima kwangu wakati nikiwamtumishi wa umma na hata nitakapokuwa si mtumishi wa umma.

Page 105: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

143

Saini........................................ Saini........................................

Jina...................................... Jina .........................................Shahidi Muajiriwa

Tarehe ......................................

Page 106: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

144

KIAMBA TISHO "E"(Chini ya kanuni ya 11(2))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

MKA TABA WA UAJIRI BAADA YA KUSTAAFU

WIZARA……….…………….………………………….…...….

IDARA YA ……………..………..…………….………………….

ZANZIBAR.

KWA: …….……………..…………………..........

Nimeamriwa kwamba ikiwa umezikubali shuruti zilizomo katikaMkataba huu, unaingizwa kazini katika nafasi...............................……kuanzia tarehe ………………………… kwa masharti yafuatayo:-

MAJUKUMU

Katika kutekeleza wajibu wako, utapaswa kutekeleza majukumuyafuatayo:

(i)............................................................................................................

(ii)…………………………………………………………………........

Page 107: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

145

(iii)………………………………………………………………………

(iv)………………………………………………………………………

(v)………………………………………………………………………

(vi) Na majukumu mengine utakayopangiwa na Mkuu wakowa kazi.

MUDA WA MKA TABA

Muda wa Mkataba huu ni wa miezi/mwaka/miaka ……………kuanzia tarehe …………….. hadi tarehe …………………Unawezakuajiriwa tena baada ya kumaliza muda huo wa uajiri wako pindipoikihitajika kufanya hivyo.

MASHARTI YA AJIRA

Utawajibika kuzifuata, kuzitii na kuzitekeleza Sheria, Kanuni, miongozona matoleo ya kazi yaliyopo sasa na yatakayotolewa na Serikali mudabaada ya muda.

STAHIKI

n Utakuwa na haki ya kulipwa mshahara katika wadhifawako Shilingi..................................................kwa mwezisawa na Shilingi............................................kwa mwakana hautokuwa na nyongeza.

n Utastahiki kulipa kodi ya Mapato kutoka kwenyemshahara wako.

n Pindipo baada ya kuajiriwa ulikuwa tayari ushafikia umri

Page 108: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

146

wa kustaafu utalipwa asilimia 25% ya mshahara wakowote uliouchuma kwa kipindi ulichofanyia kazi bila yamalipo ya uzeeni.

n Safari zote za Kikazi za ndani na nje ya Tanzaniazitagharamiwa na Wizara husika.

KUMALIZIKA MKA TABA

n Endapo Serikali itaamua kusitisha Mkataba wakoutastahiki kulipwa mshahara wa mwezi mmoja aukuarifiwa mwezi mmoja kabla na kutengenezewa stahikizako kwa mujibu ya makubaliano ya Mkataba.

n Unaweza kuacha kazi baada ya kutoa taarifa ya mwezikabla au kuacha mshahara wa mwezi mmoja badala yake.

n Unaweza kuachishwa au kufukuzwa kazi kabla yakumalizika muda wa kazi ikiwa utaonekana umeshindwakutekeleza majukumu uliyopangiwa.

n Na endapo Serikali ikisitisha mkataba wako kwasababu ya kinidhamu hutostahiki kulipwa kiinuamgongo cha asilimia 25% cha mshahara wako.

LIKIZOUtastahiki kupata likizo la siku 28 kwa mwaka.

UTHIBITISHOMimi nakubali kuingizwa kazini kwa mujibu wa Shuruti zilizomo katikaMkataba huu.

......……………………MUAJIRIW A

Page 109: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

147

Tarehe ……………………

……………………………………..........KATIBU MKUU/MKUU WA TAASISI

Tarehe..............................

Page 110: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

148

KIAMBA TISHO "F"(Chini ya kanuni ya 11(3))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

MKA TABA WA AJIRA MAALUM KW A UTEUZI WAMHESHIMIW A RAIS

MKA TABA HUU, umetengenezwa leo tarehe …......, Mwezi wa……..., Mwaka………Baina ya KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI NA KATIBUMKUU KIONGOZI kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama Muajiri).

NA

Ndugu ........................................wa S.L.P ………………., Zanzibar;(ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama Muajiriwa).Kwamba, kufuatia Uteuzi wako uliofanywa na Mheshimiwa Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi siku ya tarehe .............Mwezi wa............. Mwaka............Na kwamba, ikiwa utakubali masharti yaliyomo ndani ya Mkatabahuu, utatumikia Wadhifa wa ……………..……..................................katika Wizara/Idara/Taasisi………………………. kwa mujibu wamasharti yafuatayo:-

MUDA WA UTEUZI

Kwamba, Uteuzi wako utakuwa kwa kipindi cha miaka ........... kuanzia

Page 111: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

149

tarehe ya kutangazwa uteuzi wako na unaweza kuteuliwa tena kuendeleana wadhifa wako kwa muda mwengine wa miaka..........kwa mashartiya mkataba huu au kwa masharti mengine kama ambavyo Serikaliitaamua.

MUDA WA MKA TABAMkataba huu utakuwa wa muda wa miaka ............. kuanzia tarehe yaUteuzi na utamalizika mara tu muda wa uteuzi wako utakapomalizikaau utapofutwa.

MASHARTI YA UTEUZI

n Muda wote wa Uteuzi wako utawajibika kwa Katibu waBaraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi na kwaWaziri/Katibu Mkuu wa Wizara…………………, kamaitavyoamuliwa na Katibu Mkuu Kiongozi.

n Muda wote wa Uteuzi wako utalazimika kuzifuata, kuzitiina kuzitekeleza Sheria, Kanuni, Matangazo na Matoleoyote ya Serikali yaliyopo na yatakayotolewa na Serikalikila baada ya kipindi.

n Muda wote wa Uteuzi wako utawajibika kutumikiaWadhifa wako kwa bidii, nidhamu na kwa heshima yaSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

STAHIKI ZA WADHIFA

n Katika kipindi cha Uteuzi wako utapokea Mshahara waShillingi ............ kwa mwezi, sawa na Shillingi .......... kwaMwaka, na hautokuwa na nyongeza (Fixed Salary).

n Utawajibika kulipa kodi ya Mapato kutoka kwenye

Page 112: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

150

Mshahara wako wa kila Mwezi kwa muda wote wa Uteuziwako.

n Kwamba Serikali haitochangia malipo ya Mfuko waHifadhi ya Jamii kwa kipindi chote cha Uteuzi wako.

n Safari zote za Kikazi za ndani na nje ya Tanzaniazitagharamiwa na Serikali kupitia Wizara husika.

STAHIKI BAADA YA KUMALIZA UTEUZIMara baada ya kumaliza Uteuzi wako, utastahiki kulipwa kiinuamgongo cha asilimia 25% cha mshahara wako wote uliochuma kwakipindi ulichofanyia kazi.

KUFUTWA KWA UTEUZI

Endapo Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi ataamua kufuta Uteuzi wako na kupelekea kuvunjika kwaMkataba huu, utastahiki kulipwa mambo yafuatayo:-

n Asilimia ishirini na tano (25%) ya mshahara wote uliochumakwa kipindi ulichotumikia wadhifa wako wa Uteuzi; na

n Mshahara wa mwezi Mmoja au kuarifiwa kusitisha kwamkataba wako mwezi mmoja kabla.

Na endapo Serikali ikisitisha mkataba wako kwa sababu yakinidhamu hutostahiki kulipwa kiinua mgongo cha asilimia 25%cha mshahara wako.

LIKIZO

Utastahiki kupata siku 28 za Likizo kwa kila mwaka kwa muda wotewa Uteuzi wako, na utastahiki kulipwa na Serikali posho ya likizokwa kiwango kitachoamuliwa na Katibu Mkuu Kiongozi.

Page 113: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

151

UTHIBITISHO

Mimi ………………………….nimekubali kuingizwa kazini katikanafasi ya ……………………………………….. kwa mujibu wamasharti ya Mkataba huu kama ilivyoelezwa hapo juu.……………………………SAHIHI YA MUAJIRIW A

MKA TABA HUU, Umetiwa saini leo tarehe ......... Mwezi wa .......Mwaka...........na

……….……………………MUAJIRI;KATIBUBARAZA LA MAPINDUZINA KATIBU MKUU KIONGOZI

Tarehe………………….

Page 114: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

152

KIAMBA TISHO "G"(Chini ya kanuni ya 21(3))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBARREVOLUTIONARY GOVERNMENT OF ZANZIBAR

SHAHADA YA UTUMISHICERTIFICATE OF SERVICE

Jina la Mtumishi…………………………………………….......… Name of Officer

Cheo na Idara ……………………………………………………Position held and department

Muda wa kuanza Ajira …………………………………………...Period of service from

Sababu ya kumaliza muda wa Ajira…………………………………Cause of termination of engagement

Ufanisi……………………………........………………………….Efficiency

Maadili ……………………………………………………………General conduct

…………….................… Mkuu wa Idara Head of Department

………………………..Mkuu wa Taasisi

Head of Institutiontarehe …………………….Date

Page 115: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

153

KIAMBA TISHO "H"(Chini ya kanuni ya 37(1))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

MUONGOZO WA UTENGENEZAJI WA MKA TABA WAUTOAJI WA HUDUMA

VIPENGELE VYA MKA TABA WA UTOAJI WA HUDUMA:

Mkataba wa Utoaji wa Huduma hutengenezwa kwa kuwa na vipengelevifuatavyo:-

1. Jina na nembo ya Taasisi: Sehemu hii huonesha Jina nanembo ya Taasisi.

2. Dira: Sehemu hii inaonesha wapi taasisi inataka kufika.

3. Dhamira: Sehemu hii huonesha huduma gani Taasisi inatakakutoa au kuwafanyia wateja wake.

4. Mamlaka: Sehemu hii huonesha uwezo au haki ya kisheriaya kuanzisha shirika / taasisi / kampuni.

5. Maadili ya taasisi: Sehemu hii huonesha maadili ya taasisikwa mfano, ubora, ufanisi, kujali wakati, uaminifu na ubunifu.

Page 116: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

154

6. Wataka huduma: sehemu hii huorodhesha na kuweka waziaina ya watu au taasisi ambazo zinatarajiwa kupata hudumaau watahusika na taasisi hiyo kwa mfano mashirika ya watubinafsi, wananchi, taasisi za Serikali n.k.

7. Wajibu na Kazi za Taasisi: Sehemu hii huoredhesha kazi zakila siku za taasisi ambazo lazima ziwe wazi kwa kila mdaukuzielewa. Ni vyema mkataba kuonesha kazi hizo na viwangovya huduma vinavyotolewa. Hii itategemea uwezo wa taasisihusika katika kutoa huduma.

8. Ahadi na Viwango vya Utoaji wa huduma: Sehemu hiiitaonyesha kwa uwazi jinsi, au wakati gani hudumazitapatikana.

9. Huduma: Sehemu hii itaonyesha idadi ya hudumazinazotolewa au zilizopangwa kutolewa. Lengo hasa lamkataba wa utoaji wa huduma ni kugundua wajibu wa taasisina huduma itolewayo baina ya taasisi na wataka hudumawake. Hali hii huoneshwa na vigezo vifuatavyo;-

n Malengo (targets) na vigezo (indicators)vinavyoweza kufikiwa na taasisi ambavyo mtakahuduma anavitarajia.

n Uhakika wa huduma ( viwango ambavyo vitakuwavinafikiwa kwa Nyanja zote)

10. Haki na Wajibu wa Mtaka huduma: Sehemu hii hutajahaki na wajibu wa mtaka huduma kwa taasisi hiyo. Kwamfano:

10. 1 Haki za Mtaka huduma

n Kuhudumiwa kwa heshima na bila upendeleo nakwa wakati

Page 117: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

155

n Kuwasilisha malalamiko;

n Kupitia na kukata rufaa kwa kuzingatia taratibuzilizowekwa;

n Kutunziwa siri katika masuala yao;

n Kuona taarifa zinazowahusu kwa kufuata taratibuzilizopo;

n Kushauri njia bora ya kuongeza ufanisi.

10.2 Wataka huduma wetu wana wajibu wa:-

n Kutoa ushirikiano kwa watumishiwanaowahudumia;

n Kutoshawishi watumishi kutoa huduma kwaupendeleo;

n Kuhudhuria mikutano au miadi kwa wakatiuliopangwa;

n Kutoa taarifa sahihi kwa taasisi na kwa wakatiunaotakiwa; na

n Kuzingatia taratibu za kisheria kwa huduma zozotewanazostahiki kupatiwa.

11. Faragha na usiri: Kama kuna haja ya faragha na usiri,Mkataba wa Huduma lazima uonyeshe jinsi gani Taasisiitahifadhi siri hizo kwa usalama wa wataka huduma, taasisina wadau wengine.

12. Uwezo wa Taasisi kifedha: Uwezo wa kifedha na vyanzovya mapato vya taasisi hulazimika kuoneshwa. Taarifa hiihumpelekea mtaka huduma kujenga matumaini na kukubalikuingia kwenye mkataba wa huduma na taasisi hiyo.

Page 118: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

156

13. Mawasiliano ya Taasisi: Mkataba wa huduma hujengamawasiliano baina ya Taasisi na mtaka huduma. Kwa hivyo,huhitaji kuelezwa namna ambavyo wataka huduma na wadauwatawasiliana na Taasisi kwa urahisi kwa mfano huduma zasimu, huduma za mapokezi, wovuti, tovuti, barua pepe, simupepe au mawasiliano mengine yoyote. Ni muhimu kwa mtakahuduma kujua wapi taasisi hiyo inapatikana.

Page 119: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

157

KIAMBA TISHO "I" (Chini ya kanuni ya 76(1))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

MKA TABA WA UDHAMINI WA MASOMO AUMAFUNZO KW A WATUMISHI WA UMMA.

MKA TABA HUU WA UDHAMINI WA MASOMO AU

MAFUNZO

umefungwa leo tarehe ………….… mwezi …………….…….

mwaka ……………..………

BAINA YA

Wizara/Idara/Ofisi ya ……………….….……………………….…iliyopo……………………………...……..……..… (ambayoitajulikana kama Muajiri) kwa upande mmoja;

NA,

Bwana/Bibi ………………………...……..…… wa Idara ya…………………………… Wizara ya ……………………………(ambaye atajulikana kama Muajiriwa) kwa upande wa pili.

Muajiri na Muajiriwa wanakubaliana kama ifuatayo:

Page 120: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

158

1. Muajiri kwa gharama zake au kupitia msaada wa Muajirikutoka kwa muhisani atagharamia masomo ya Muajiriwa kwamuda uliokubaliwa wa masomo kama ilivyoelezwa katikaMkataba huu.

2. Muajiriwa atahudhuria masomo katika ngazi ya cheti/diploma/ stashahada/shahada ya fani ya ……………katikachuo cha ………………………………… kiliopo (anuanikamili ya chuo) ………… ……………………………….yatayochukuwa muda wa mwaka/miaka …………………..na gharama ya masomo kwa muda wote wa masomozitakuwa TZS. …………………………….…………….na/au Fedha za kigeni (USD $ au …………………………)zenye thamani sawa na TZS.........….. na kufanya jumla yagharama za masomo kuwa TZS…………………….…………………………………………………...……………………………………

3. Malipo ya Ada na gharama nyengine ambazo zinawezakulipwa moja kwa moja katika Chuo au Taasisi zaUsafirishaji, zitalipwa moja kwa moja na Muajiri naMuajiriwa hatopewa fedha hizo mkononi isipokua katikamazingira ambayo kulipa moja kwa moja haitowezekana.

4. Bila kuathiri makubaliano mengine na Muajiri, Muajiriwaataendelea kuwa mtumishi wa umma na Muajiri atamlipamshahara wake wa kila mwezi kwa kipindi chote chamasomo.

5. Muajiri hatolazimika kulipa gharama nyengine zozote zamasomo ya Muajiriwa zaidi ya gharama za masomozilizotajwa katika Mkataba huu.

6. Muajiriwa anakubali kuwa endapo atabadilisha fani yamasomo, chuo au taasisi ya elimu bila ya ruhusa ya Muajiri

Page 121: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

159

udhamini wake utafutwa mara moja na Muajiriwa atatakiwakurejesha kwa Muajiri gharama zote zilizokwisha kutumika.

7. Muajiriwa anakubali kuwa kwa kipindi chote cha masomoatawasilisha maendeleo ya kila muhula au mwaka ya masomoyake kwa Muajiri.

8. Endapo Muajiriwa hatofanya vizuri katika masomo yakena ikibidi kurudia mwaka/miaka kinyume na mkataba huuMuajiri hatolazimika kumlipia gharama za ziada, ingawajeanaweza kumlipia iwapo ataona kufanya hivyo ni kwamanufaa ya Taasisi hiyo.

9. Muajiriwa wakati akiwa masomoni hatoshiriki na kujihusishana shughuli zozote ambazo ni kinyume na Sheria za Nchihusika, Chuo/Taasisi.

10. Muajiriwa baada ya kumaliza masomo atarudi kazini nakuendelea na kazi atazopangiwa na Muajiri wake na endapohatorudi kazini, yeye au mdhamini wake au wote kwa pamojawatawajibika kurejesha gharama zote za masomo/mafunzozilizoainishwa katika mkataba huu kwa Muajiri wake.

11. Muajiriwa anakubali kuwa hatoacha kazi wakati akiwamasomoni au baada ya kurudi masomoni na ataendelea nakazi kwa kipindi ambacho hakitopungua mara mbili ya mudawa masomo/mafunzo uliokubaliwa ndani ya mkataba huu,na iwapo atafanya kosa la kinidhanu litakalopelekeakufukuzwa kazi, Muajiriwa au Mdhanini wake watalazimikakurejesha kwa Muajiri, gharama za masomo/mafunzozilizokubaliwa na kulipwa kwa mujibu wa mkataba huu.

Page 122: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

160

12. Muajiriwa hatokwenda tena kwenye masomo mengine yamuda unaozidi miezi sita hadi awe ametimiza miaka miwilitokea tarehe ya kurudi masomoni kwa mara ya mwisho.

13. Endapo Muajiriwa ataamua kuvunja masharti ya vifungu vyamkataba huu atalazimika kurejesha gharama zote za masomoyake zilizogharamiwa na Muajiri katika kipindi kisichozidimiezi mitatu au iwapo kuna sababu za kutosha Maujirianaweza kumkata mshahara wake kwa kiwangokinachokubalika kisheria na hatopata udhamini wa Muajirikatika kipindi cha miaka mitano baada ya kuvunja mashartiya vifungu vya mkataba.

14. Gharama za masomo zitakuwa kama ifuatavyo(futaisiyohusika na makubaliano):-

(a) Nauli ya ndege/meli/usafiri mwengine.

Hapana/Ndiyo TZS USD

(b) Ada ya masomo

Hapana/Ndiyo TZS USD

(c) Posho la kujikimu

(d) Posho la vitabu

Hapana/Ndiyo TZS USD

Hapana/Ndiyo TZS USD

Page 123: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

161

(e) Posho la njiani

(f) Mshahara.

(g) Ada ya Viza

(h) Malipo mengine …………………………….…………………………...................................………….

I: MUAJIRIW A:

Jina: …………………………Cheo: ……………..……….……

Tarehe ya kuajiriwa……………… Mwaka wa kuzaliwa….............

Nam. ya ajira….……… ZSSF………....Nam. ya kitambulisho(ZanID)…......….

EMAIL:……… SIMU…………………..………………………

Hapana/Ndiyo TZS USD

Hapana/Ndiyo TZS USD

Hapana/Ndiyo TZS USD

Hapana/Ndiyo TZS USD

Page 124: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

162

Nathibitisha kwamba nimeusoma Mkataba huu na kukubalianana masharti yote yaliyomo ndani ya Mkataba huu.

SAINI: …………………………….……………

TAREHE: ……….…………………….……….

II: MDHAMINI WA MUAJIRIW A:

Jina: ……………..………….. Kazi: ………………...…………

Anuani…………...…..Mwaka wa kuzaliwa……….....……..…….

Shehia (anapoishi) ……......…. Nam. kitambulisho (ZanID) …..…..

Email:…………….........… Simu……………………………

Nathibitisha kuwa nimeusoma kwa makini mkataba huu nanakubali majukumu yote yanayoniwajibikia kwa kumdhaminiMdhaminiwaBw./Bi…………………….………………

SAINI: ……………………………………

TAREHE: ………..……………..……….

PICHA YARANGI

PICHA YARANGI

Page 125: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

163

III: MKUU WA IDARA

Jina: ………………..………. Cheo: ……………………………

Idara:..………………………. Wizara:…………………………..

Saini: ………………………. Tarehe: ………………….………

IV: IDHINI YA KATIBU MKUU WA WIZARA.

Mimi ……………………………………………..……..……

Katibu Mkuu naidhinisha udhamini wa masomo/mafunzo

yaliyotajwa hapo juu kwa Bwana/Bibi…………....................

katika fani ya …….............................................ambayo jumla ya

gharama zake ni TZS/USD……………...................………

……………………………………………….. kuanzia tarehe

…………………………………….na idhini hii imetolewaleo

tarehe …… mwezi wa …………mwaka ………………….

…………………………..………….KATIBU MKUU WA WIZARA

Page 126: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

164

KIAMBA TISHO "J"(Chini ya kanuni ya 135(1))

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

MKA TABA WA UAJIRI WA KUTWA

WIZARA……….…………….…….....………………………….

IDARA YA ……………..………..…........….……………………

ZANZIBAR.

KWA: …….……………..…………………..........

Nimeamriwa kwamba ikiwa umezikubali shuruti zilizomo katikaMkataba huu, unaingizwa kazini katika nafasi ya ..................................kwa muda wa ……………..kuanzia tarehe ………………………

(1) Katika kutekeleza wajibu wako, utapaswa kutekelezamajukumu yafuatayo:

(i).......................................................................................................

(ii).......................................................................................................

Page 127: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

165

(iii).......................................................................................................

(iv).......................................................................................................

(v).......................................................................................................

(vi) Na majukumu mengine utakayopangiwa na Mkuuwako wa kazi.

(2) Utawajibika kufuata masharti ya kazi na taratibu zote zakisheria wakati wote wa kutekeleza majukumu yako.

(3) Unaweza kuacha kazi wakati wowote utakapoamua.

(4) Unaweza kuachishwa au kufukuzwa kazi kabla ya kumalizikamuda wa kazi ikiwa utaonekana umeshindwa kutekelezamajukumu uliyopangiwa.

(5) Malipo yako yatakuwa kwa siku mara baada ya kumalizamajukumu yako.

(6) Hutokuwa na fursa ya kupata likizo, malipo ya kiinua mgongona mafao yauzeeni.

(7) Kuhusu mwenendo na adabu za kiserikali utapaswa kufuataSheria zote za nchi na matokeo ya maamuzi yoyote ya Serikalikuhusu mambo hayo.

Mimi nakubali kuingizwa kazini kwa mujibu wa Shuruti zilizomo katikaMkataba huu.

Page 128: Kanuni za Utumishi wa Umma 2014

166

……..................… ……….……..................……. Mtumishi Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi

Tarehe ………………………………

IMETIW A SAINI tarehe 29 mwezi wa Mei, Mwaka 2014

(MHE. HAROUN ALI SULEIMAN)WAZIRI WA WN (OR) - KAZI NA

UTUMISHI WA UMMA ZANZIBAR